sababu ya kuandika kitabu hiki cha permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya...

18

Upload: others

Post on 06-Nov-2019

89 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ya kiswahiliPermaculture nini? Ni nini kinawafanya watu kuendelea kuwa wategemezi?Nguzo 5 za Permaculture

Maadili na kanuni za Permaculture

Mambo ya msingi ya kupangilia eneo la PermacultureKuweka mpango katika utekelezaji

Rasilimali

Kuongeza uzalishaji wa mavuno yako

Mpangilio wa Bustani ya karibu na nyumba ya kuishiMifugo na mimea; Mchanganiko wa mazao bustanini; Konokono ya mimea ya viungo;Artemisia Annua Anamed; Solardryer ­ Kukausha majani na matunda kwa jua; Bustanindogo na kwenda juu; Bustani ya Mandala; Mbolea ya maji; Kutengeneza mbolea;Kuku trekta; Kugawanya uzio kwa kuku na mboga; Aquaponic; Ufugaji wa Nyuki

Mpangilio wa ujenzi wa nyumbaMifano ya ujenzi wa nyumba kwenye Permaculture; Kujengea kwa mifuko ya udongo; Nyumbazenye kusitahimili; majanga ya maji na upepo; Rasilimali zingine katika ujenzi wa nyumba;Ujenzi wa kutumia; matairi na udongo; Ujenzi kwa kutumia majani ya nafaka; Choo cha mboleaya mboji; Kutengeneza sabuni; Jiko Bora kwa matumizi kidogo ya kuni; Kutengeneza Tanuri

Maji na ardhi inavyopaswa kutumikaUvunaji maji ya mvua na kuyahifadhi; Technologia tofauti za kutega maji na kupanda mimea;Mbinu za utekaji maji; Kuchimba mifereji; Mfano wa mfumo endelevu wa kujipatia kuni mifugowakilishwa zizini; Jinsi ya kutumia A­Furemu; Kutengeneza mitaro; Grid and pit planting; Bustaniya msitu; Chinampa; Kilimo cha Azolla; Kilimo cha msituni /kupanda miti miongoni kwa mazao /kilimo cha mseto; Agroforestry ­ Ni mchanganyiko wa mazao ya kilimo na msitu; Zero­Grazing

Kutunza MitiKuanza bustani yako ya miche ya miti; Miti gani kukuza kwa bustani; Jinsi ya kutayarisha;mchanga; Miche ya vyungu; Vidokezo vya bustani ya miche

Mawasiliano ya Permaculture Afrika Mashariki

Page 2: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ya kiswahili

Tumegundua vitabu vingi vya Permaculture duniani kote,vingi vimeandikwa kwa kiingereza, kijerumani, na lughanyingine ambako zaidi ndiko kazi za Permaculture zilikoanziana zinakoendelea kuendelezwa.

Kwa kuzingatia kwamba wakulima wengi walioanza kujifunzakilimo kwa kufuata mfumo au maelekezo ya Permaculturewalioko katika nchi za Afrika mashariki wengi wao wame­fundishwa kwa Kiswahili, lakini pia Kiswahili ni lughainayoeleweka kwa urahisi zaidi kwao, kwa kuwa tungependaelimu na ujuzi uwafikie watu wengi na kwa muda mfupitumeona umuhimu mkubwa wa kukiandika kitabu hiki chaKiswahili cha Permaculture ili kiweze kutatua baadhi yachangamoto kwa wakulima wetu.

Permaculture

2

Kutokana na kupatikana kwa kitabu hiki chaKiswahili matarajio yetu ni kwamba kutakuwana mabadiliko makubwa sana kwenye mambo yaafya, na uhifadhi wa mazingira. Maana watuwengi wamepotea kwa kukosa maarifa. Elimu namafundisho yaliyomo katika kitabu hiki itawafikiawatu wengi zaidi na ikifanyiwa utekelezaji ­ Wengiwataepuka kilimo chenye kutumia kemikalikwa wingi kitu ambacho kimepelekea kuwa chanzokikubwa cha matatizo ya kiafya lakini pia uchafuziwa mazingira.

Kitabu tumekiandika kwa namna ambayo wewemwenyewe msomaji kinaweza kukuongoza katikakufanya utekelezaji katika kuanza kukibadilishakilimo chako, na mfumo mzima wa namna yako yakuishi na hivjo itapelekea wewe na familia yakowote kuwa na afya bora na pia kuwa na mazingiramazuri na salama.

Julai 2017, Wels / AustriaDr. Peter Feleshi Chairman anamed Tanzaniana Bernhard Gruber, President Austrian Foodforest­Institutena Franz Hörmanseder, Mtaalamu wa Maendeleo

Page 3: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

3

"Kuweka mfumo endelevu wa maisha"

"Ni wajibu wako kujenga mfumo wa kujitegemea mwenyewe katikakujiletea maendeleo, kuyatunza mazingira na kulinda pia viumbe wengine"

„Ni mjumusho wa jinsi ainambalimbali ya viumbe

Wanavyoweza kuishi pasipo kuletauharibifu na kukuza uchumi"

„Kuishi maisha kwa uhalisia wake"

Permaculture nini?

Page 4: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

PermakulturNi nini kinawafanya watu kuendelea kuwa wategemezi?

­ Ukosefu wa elimu

­ Utegemezi wa kutumia mbegu chotarana mbolea za viwandani zenye kemikali

­ Kutegemea maelekezo kutoka kwenyemakampuni ya biashara jinsi yakuendesha kilimo chako

­ Kutegemea kupata mikopo kutokakwenge makampuni ya biashara namabenki

Kusimamia kuwa na afya bora na kulima / kusitawisha mazao yako mwenyewe nisawa na kuchapisha / kuzalisha fedha zako mwenyewe.

4

Thamani ya mazao yako itadumu kwa muda mrefu!

Page 5: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

50% Wakulima

20% Wafanyakazi

10% wavuvina wafugaji(ambaowanatem­beatembea)

20%Wanakaamjini

Mgawanyo wa chakula kidunia:Nusu ya chakula chote duniani kinachopatikana huza­lishwa na wakulima wadodgowadogo ambao shambalao halizidi hekta mbili. (World food report 2009).

5

Ni muhimu kuvuna maji ya mvua na kuyatumia

Ni muhimu kuwa na mbegu zako mwenyewe za asili

Ni muhimu ardhi kuitunza na kuirutubisha

Ni muhimu kupanda mazao mchanganyiko

Watu wenye njaa duniani kote

Page 6: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

6

Maji

Ardhi

Moto

Hewa

Permaculture

JamiiUjenzi wa nyumbaya makaoChakula bora

Nishatiendelevu

Teknolojia naelimu

Ili kazi za Permaculture zifanikiwe na kuwaendelevu ni lazima kuzingatia nguzo 5 za

Permaculture ambazo msingi wake ni:

Kuwa na maji ya kutosha safina salama

Nguzo 5 za Permaculture

Kuwa na afya njema na pia kuwa naardhi yenye rutuba ya asili

Hewa safi isiyochafuliwa

Mazingira yenye kujitosheleza kutegemea uhitaji / matumizi yake

Page 7: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

7

Chakula bora

Kulinda vyanzo vya maji lakini piakutumia maji safi na salama.Ni vizuri kulinda mbegu zetu zaasili­ mwili unahitaji virutubisho.Ni vizuri kulinda vizazi vya mifugowanyama pamoja na mazao mengine

kama vile mbogamboga kutegemea mahali ulipo.Ni vizuri pia kubadilishana na kueneza kwa wenginembegu za asili zenye ubora.

55% chakula cha wangana sakri (carbohydrate):Mahindi, mtama, mchele,ndizi, mihogo, viazi, ngano(mikate), miwa, nafaka,magimbi, maharage, mbaazi(chakula jamii ya kunde)

30% mafuta:Mayai, maziwa, nyama,samaki, mbegu nafaka(mfano: alizeti, mchikichi,karanga, korosho, nazi, ufuta,mbegu za pamba, …)parachichi, mlongelonge,mbuyu

15% chakula cha kujengamwili (protein): Mayai,maziwa, nyama, samaki,wadudu (mfano: kumbikumbi,senene, …) mbegu zamchicha, ufuta, karanga(chakula jamii ya kunde)maharage, mlongelonge

Mwili pia unahitaji chakula cha vitamini nishati na madini pia chakula cha kuandoa / kupunguzasumu mwilini.

7

Kinavyohitajika mwilini na makundi yake:

Kwa vitaminiMfano: mboga za majani, matunda,karanga, samaki, kitunguu maji, kitunguusaumu, pilipili, asali

Kwa madiniMfano: chumvi, dagaa, mlongelonge,tangawizi, binzari, mchicha, asali

Kwa kuondoa / kupunguza sumu mwiliniMfano: matunda yote vitamini c,mchaichai, mlongelonge, Mayai, maziwa,nyama, samaki, tangawizi, binzari, na mint,asali

Ni muhimu sana kwa kila mmojakuweka mpango wa jinsi atakavyopatachakula kilicho na uwakilishi wamakundi yote ya chakula, kwa ajili ya afyanjema. Siyo vyema kula chakula cha ainamoja tu! Na hii ni bora zaidi kusitawishachakula / mazao yetu wenyewe bilakusahau kuistawisha / kuirutubisha ardhikwa kutumia mbolea za asili!

Siyo vyema mbegu ya mimea / nafaka kuzibadilisha kutoka katika uhalisia wake.

Page 8: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

8

Nishati endelevu

Tunapaswa kuwa na uwianokatika matumizi ya nishati.Kwa mfano: Iwapo unapikakwa kutumia kuni na haupandimiti mingine maana yake mitiyote utaimaliza kwenye eneo.

Kama una mifugo (wanyama) kinyesi chao unawezakukitumia kwa kupikia, biogas, umeme, lakinipia mbolea.

Kwa sababu ya kuongezeka kwa idadi ya watu na viumbe vingine duniani pamoja namabadiliko ya tabia ya nchi kuwa uwezekano mkubwa wa uhaba wa nishati zinazotengenezwakwa matumizi mbalimbali ya uendeshaji wa shughuli za siku kwa siku kama vile:

­ Mafuta (Petrol, Diesel, mafuta ya taa, oil,mafuta ya ndege, …)­ Gas­ Makaa ya Mawe­ Atomiki

Kwa maana hiyo ni muhimu sana kwanza kutafutanjia endelevu ya nishati ambayo itakuwa haihusikina uchafuzi wa mazingira na kuhatarisha afyaya binadamu na viumbe vingine kama vile.­ kutumia nishati ya jua (solar, kwa kupataumeme wa jua, jiko, pasi, …)

­ kutumia nishati ya upepo(kwa kusukuma maji, kuzalisha umeme, …)

­ kutumia nishati ya maji ya maporomoko(kwa kuzalisha umeme)

­ kwa kutumia nishati ya maji moto ya chemichemi(kwa kupikia)

­ kwa kutumia nishati ya kuni (miti mkaa wa kutengeneza;kuni za kutengeneza kutokana na vitu vingine.Kwa mfano: Takataka na vinyesi vya wanyama; biogesi– pia kutokana na vinyesi.

Page 9: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

9

Ujenzi wa nyumba ya makao (Usanifu)

Sehemu ya makao na jinsi yakujenga nyumba ya kuishi nimuhimu sana kuzingtia mamboyafuatayo:­ Nyumba ya kuishi inapaswa

kujengwa penye usalama na palipo na kivuli.­ Nyenzo zitokazotumika kujengea ziwezinapatikana kwa urahisi, na zilizo imara.­ Nyumba inapaswa kuwa na msingi imara.­ Mahali nyumba itakapojengwa kuwe nauhakika wa upatikanaji wa vyanzo vya maji.­ Ili kuepuka madhara ya moshi wakati wa kupika vyema jiko kutengwa nje ya nyumbaya kuishi / kulala na lijengwe jiko sanifu (ndilo lenye ubora).­ Kwa kuzingatia urutubishaji wa ardhi / udongo, ni vizuri pia kutengeneza choo chakutengeneza mboji (compost toilet)­ Nyumba inaweza kujengwa ikawa imara na ya kudumu kwa kutumia vitu vilivyokwisha

kutumika (kwa mfano: chupa za maji za plasticna za vioo, matairi ya magari yaliyotumika, mifukoya saruji kwa kuijaza mchanga na kishakuijengea nyumba).­ Pia unaweza kutumia matofali makuukuu(yaliyotumika na kutupwa).

Page 10: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

Teknolojia na elimu

Teknolojia na elimu ni nguzo muhimusana katika shughuli / kazi zapermaculture. Kutokana na mabadilikoya tabia nchi na maendeleo dunianikwa ujumla ni vizuri watu kujiendeleza

kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanyatafiti mbalimbali kujifunza kwa njia ya mitandao(internets).Katika shughuli / kazi za permaculture ni muhimusana kwa upande wa teknolojia pia kutumia mbinu

stahiki ili kuonyesha uhalisia wa uwiano wa utumiajiwa nyenzo, nguvu (rasilimali) lakini pia kufanyashughuli zote zinakuwa endelevu na pasipo kuletamadhara yoyote kutokana na mfumo wa uumbajiwa Mwenyezi Mungu.

­ Kuna teknolojia za zamani nzuri na teknolojia nyingimpya nzuri, tunapaswa zote kuziunganisha nakuzitumia kwa ajili ya kujiletea maendeleo yetusisi wenyewe.

­ Mabadiliko tutajiletea sisi wenyewe kwa kupanga vizuri namna ya kuishi, kuboresha afyazetu, kuyatunza mazingira na viumbe vingine.

Jamii ni nguzo muhimu katikakufanya utekelezaji wa shughuli/ kazi zote za permaculture nakuzifanya ziwe endelevu.Katika nguzo ya jamii umojaunahitajika, kwani jamii inapaswa

Jamii

kuishi, kufanya kazi, lakini pia kujiwekea taratibuza kuishi na kuweka mipango yake kwa pamoja.Jamii ni muhimu sana kuona kwamba waowenyewe wamechagua kuishi katika maeneo namazingira wanayoishi bila kujali ni mjini au ni kijijini, lakini pia ni muhinmu kuelewakwamba ni wao waliochagua kufanya kazi wanazozifanya. Ni vyema kutambua kwambaili kuiendeleza jamii ni lazima kuishi na majirani au watu wengine ambao wataishi pamojakatika eneo, kijiji, mtaa husika ambapo kwa pamoja kila mmoja atakuwa na uhalali waumiliki wa pamoja na hivyo ndiyo inayopelekea jamii kuwa na umoja katika kupanganamna ya kujiletea maendeleo ya pamoja katika eneo lao. Lakini pia kuweka kanuni yataratibu za kuishi.

10

Page 11: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

­ Jamii wanapaswa kufanya kazi kwapamoja, kuwa na nyenzo za pamojaza kufanyia kazi, kuweka mipangoyao na taratibu za kuishi pamoja.­ Jamii wanapaswa kuona ni jinsi ganiwatautumia muda wao kwa kufanyakazi pamoja.+ Wanaweza wakabadilishana mudawa kufanya kazi ­ kama vile kukopeshanamuda – kwa kufanya kazi.+ Wanaweza kubadilishana vitu kwa vitu.+ Nchi nyingine kama vile Austria upandewa Permaculture wanao mfumo katikajamii wa kutumia vocha – mtu anajitoakufanya kazi kwa muda fulani lakini piasiku atakapokuwa na kazi ya kufanyaanaweza kupatiwa mtu wa kufanya kazikwa muda kama vile yeye mwenyewealivyojitoa kwa kufanya kazi.

[-]N

amba

yaus

ajilim

atumi

zi....

........

.[+]

Namb

ayau

sajili

mfan

yaka

zi....

......

madh

umun

i:.....

........

........

........

........

.....

kuba

dilish

anaw

akati

........

........

........

....tar

ehe:

........

........

........

........

........

........

.sa

ini[+]

........

........

........

........

........

......

..

saini

[-]..

........

........

........

........

........

......

[-]N

amba

yaus

ajilim

atumi

zi....

........

.[+]

Namb

ayau

sajili

mfan

yaka

zi....

.......

madh

umun

i:.....

........

........

........

........

....ku

badil

ishan

awak

ati....

........

........

........

tareh

e:....

........

........

........

........

........

.....

saini

[+]....

........

........

........

........

........

....sa

ini[-

]......

........

........

........

........

........

.

[-]N

amba

yaus

ajilim

atumi

zi....

........

..[+]

Namb

ayau

sajili

mfan

yaka

zi....

.......

madh

umun

i:.....

........

........

........

........

.....

kuba

dilish

anaw

akati

........

........

........

....tar

ehe:

........

........

........

........

........

........

..sa

ini[+]

........

........

........

........

........

........

.sa

ini[-

]......

........

........

........

........

........

..

Coup

onma

kao

maku

uCo

upon

matum

iziCo

upon

mfan

yaka

zi

11

Page 12: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

Maadili na kanuni za Permaculture

Unapopata eneo ambalo unafikiria kuanzishashughuli / kazi zako za permaculture ni vyemakuzingatia mambo yote muhimu ikiwa pamojana maadili ya permaculture na kanuni zake.Kwa hatua ya kwanza unapaswa kufahamukwamba shughuli / kazi zote zitakazofanyikakatika eneo husika zitakuwa ni endelevu na zakudumu, pia ni lazima kufikiria kwamba kunaviumbe wengine ambao pia wanayo haki kamawewe kulitumia eneo hilo. Mtu wa permacultureanatakiwa kuzingatia maadili na kanuni katika kuweka mgawaniyiko wa eneo na kubuniuwiano, matumizi ya eneo ndiyo njia pekee itakayomsaidia kufanikisha mpango huo.

12

Kanuni na maadili – hufanya kazi kwapamoja kwa kutegemeana kama ifuatavyo:

Maadili ya Permaculture:

earth care ­ kuihudumia na kuilinda dunia

people care ­ kuwahudumia na kuwajali watu

fair share ­ uwiano sawa katika utumiaji na

mgawanyo sawa wa rasilimali zilizopona

kupunguza ongezeko la viumbe

Kuihudumia na kuilinda dunia

Ni wajibu wetu kuihudumia na kuilinda dunia kwakuweka mazingira endelevu kwa viumbe vyote;kuyalinda na kuyatunza mazingira, kuirutubishaardhi na pia kujali afya ya viumbe vyote.

Kuwahudumia na kuwajali watu

Kuweka mfumo mzuri jinsi ya kuwahudumia,kuwatunza watu wote kwa kuwajali kuhakikishamahitaji yote muhimu wanapata pasipo kujalitabaka zao (kwa mfano: kuwa na afya borakupata maji safi na salama, kupata hewa safi,

Page 13: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

kupata elimu, kupata ulinzi, kupata nyumba(makao), na pia kuhakikisha kwamba wanapatachakula bora na cha kutosha). Kuwahamasisha iliwaishi, na kufanya kazi kwa pamoja, kupatamuda wa burudani na kusherehekea kwa pamojamatukio mbalimbali.

Uumbaji ulifanyika mara moja na kumalizika kwa upande wa dunia na viumbe vyote,hivyo ni muhimu sana kwa kuifanya dunia iwe endelevu ni lazima kuwa na uwiano sawakatika utumiaji wa rasilimali kwa viumbe vyote na pia kudhibiti na kupunguza ongezeko:­ Kuweka mpango mzuri wa matumizi ya ardhi katika familia, mtaa na kijiji.­ Kuhakikisha kwamba watoto wanapatiwa elimu ya kutosha.­ Kuhakikisha kwamba ongezeko la ukuaji wa uchumi hauhatarishi maisha ya viumbevyote na mazingira yake kwa ujumla.

Maadili na kanuni za Permaculture

13

Chunguza, angalia nakisha chukua hatua

Kukusanya nakuhifadhi nishati

Kupata mavuno

Acha asili ifanyekazi yake

Tumia rasilimali ambazozinaweza kurejeshwa

Usizalishe taka

Anza na picha kubwakisha fuata maelekezo

Unganisha badalaya kutenganisha

Kutumia teknolojiandogo na yapolepole

Kazi za aina tofauti

Ongeza maeneo yapembeni / kando

Tumia ubunifu nakujali mabadiliko

kuihudumia na kuilinda dunia

kuwahudumia

na kuwajali watuuwiano sawa katika utumiaji

na kupunguza ongezeko laviumbe

Uwiano sawa katika utumiajina kupunguza ongezeko la viumbe

Page 14: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

14

Chunguza, angalia na kisha chukua hatua

Kwa mfano: Kuangalia na kuli­chunguza eneo itakusaidia kufanyamaamuzi sahihi kipi kukiwekawapi, na pia wapi kuepuka kufanyanini – mfano palipo na miamba

/ mawe hapafai kwa bustani, penye maji majipia hapafai kujenga nyumba. Panafaa kwa bustani.

Kukusanya na kuhifadhi nishati

Kwa mfano: Jinsi mti unavyoku­sanya nishati kutoka kwenye juana maji, mti unaihifadhi nishatihiyo na kwa baadaye inaweza kutu­mika kama vile matunda, kuni,mbao, ...

Kupata mavuno

Ili kupata mavuno ya kutoshaikiwezekana zaidi – unapaswakuweka mpango mzuri, kwakuzingatia nguvu iliyotumika

unapaswa kupata mazao mengi zaidi kwa kufanyakazi shambani, unatumia nishati shambani kwako,baada ya mavuno, utapata mazao mengi ambayoyatakupa nishati nyingi zaidi au hata sehemunyingine kuuza na kupata fedha kwa matumizi mengine.

Acha asili ifanye kazi yake

Katika ardhi kuna mimea mingiinaota kwa kutegemea mahaliulipo, kwa kufuata uhalisia wamahali fulani pia kuna miti inayootamahali hapo. Hivyo kwa mfano msitu wa chakulaunakuwa na mchanganyiko wa miti mbalimbaliambayo hutumika kwa chakula, hivyo ukishaipandaitakuwa tu yenyewe hautahitaji kufanya chochote

katika ukuaji, kazi ndogo itakayofanyika ni kuipunguzia matawi na uvunaji.

Page 15: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

1315

Tumia rasilimali ambazo zinaweza kurejeshwa

Kwa matumizi ya rasilimali mbali­mbali unapaswa kuona kwambakuna rasilimali zingine nguvu zakezinaweza kurejeshwa upya.Kwa mfano: Miti, wanyama, jua,

maji, upepo na kuni.Lakini kuna rasilimali zingine nguvu zakehaiwezekani kurejeshwa upya.Kwa mfano: Petrol, Gas, Atomic, madini, ...

Usizalishe taka

Asili haitambui kama kuna takana haizalishi, ukizalisha taka tafutauwezekano wa kuzifanya kuwarasilimali itakayotengenezwaupya na kutumika tena.

Unganisha badala ya kutenganisha

Tunazo rasilimali aina mbalimbaliambazo kila moja inafaa kutumikakwa kuzifanya kazi zetu kuwaendelevu, hivyo basi tunapaswakuzitumia rasilimali zote kwa

kuziunganisha kwa pamoja ili kuleta maanakatika utumiaji.Kwa mafano: Kama kuna jiwe kubwa liko shambanimwako, litatumika kukusanya maji na kuyaleta shambani, lakini pia kuna wakatilitatumika kwa kuweka kivuli, na kwa nchi za baridi litatumika kutunza joto.

Anza na picha kubwa kisha fuata maelezoNi vizuri kuanza na kitu kikubwana ndipo unafuata maelezo.Kwa mfano: wazo la kwanzaumepata ardhi hivyo haitajalishakuona kwamba unapaswa kufuatampangilio ulioko kwa vitu vidogo vidogo.

Page 16: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

16

Kutumia teknolojia ndogo na ya polepole

Kwa mfano: Ni vyema kuajiriwakulima watano badala yatrekta moja!Haraka haraka haina baraka!

Kazi kwa aina tofauti

Unapofanya kazi ya kilimo, nivyema kwanza kufikiri kwambakuna mambo mengi ya kuzingatia,ikiwa pamoja na uwepo wa viumbewengine ambao pia watatoa mchango wao katikakufanikisha kazi yako ya kilimo na pia ueleweumuhimu wa kuwa na mazao mchanganyiko kwenyeshamba lako.

Ongeza maeneo ya pembeni / kando

Ni muhimu sana maeneo yote yapembeni kutunzwa na hatakuongezwa ili kuweza kustawishaaina mbalimbali mazao mimea.

Tumia ubunifu na kubali mabadiliko

Kutokana na mabadilikombalimbali yanayosababishwa namabadiliko ya hali ya hewa duniani,unapaswa kutumia ubunifu na piakukubali mabadiliko.Kwa mfano: Hali ya ukame inapojitokeza ni lazimakubuni njia itakayowezesha utumiaji wa maji kidogo,ikiwa ni pamoja na kuweka matandazio ...

Page 17: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

17

Mambo ya msingi ya kupangilia eneo la Permaculture

Kwa mtu wa Permaculture mara tu anapopata eneo kwaajili ya kazi zake za Permaculture au hata kama alikuwa analoeneo lake lakini baada ya kuelimika anapenda kulibadilisha liwe kwamfumo wa Permaculture ni muhimu sana wakati wa kuanza kuweka mpango wa kulipangiliaeneo lake jinsi atakavyolitumia ni lazima kuzingatia mambo ya msingi katika kupangiliaeneo la Permaculture kama ifuatavyo.

Historia ya ardhi yako

Muhimu kufahamu historia ya eneo lako. Itakusaidiakujua kama labda hapo awali kulikuwa na viwanda,zizi la ngombe, kulikuwa na msitu mkubwa aujangwa hiyo itakusaidia kuweka mpango jinsiya kuliendeleza.

Jiolojia na Jiografia

Jiologia itakusaidia udongo wa ardhi yakokufanyiwa uchunguzi na kubaini mchanganyikouliomo – kwa mfano, kama kuna kemikali, miamba,mawe, …Jiografia itatusaidia kuona eneo lako limekaa vipi.

Hali ya hewa

Ni muhimu kujua hali ya hewa ya mahali lilipoeneo lako, kwani ni vyema kufahamu hata majiraya mvua, misimu ya kilimo …Hivyo itakusaidia kuweka ubunifu zaidi katikakuendeleza kazi zako za kilimo.

Page 18: Sababu ya kuandika kitabu hiki cha Permaculture kwa lughaa ... · makampuni ya biashara jinsi ya kuendesha kilimo chako Kutegemea kupata mikopo kutoka kwenge makampuni ya biashara

18

Permaculture kazi zake hufanyika miongoni mwa

Ni vizuri kuufahamu udongo wa ardhi yako hivyoitakusaidia pia kuona mazao ya kusitawisha katikaeneo lako. Kuna maeneo mengine udongo unatindikali au alkali nyingi, kitu ambacho hupelekeabaadhi ya mimea kutokusitawi vizuri hapo. Vilevile kuna viumbe vingine huishi kwenye udongolakini pia husaidia katika kuurutubisha kama vileaina mbalimbali ya minyoo na funza ambao ni wa

Udongo

muhimu katika mchakato wa urutubishaji wa udongo. Ni vyema kuwalinda.

Ni mimea gani imesitawishwa hapa

Ni muhimu kufanya utafiti kuona ni mazao /mimea gani imesitawi vizuri katika eneo hilohata kwa kuangalia kwa jirani zako kuona nimazao / mimea gani imesitawi vizuri.

Miundombinu na mambo ya kijamii

jamii. Ili kuzifanya zikubalike na kuzifanya kuwa endelevu ni lazima pia kujihusisha na mamboya kijamii kama vile mambo ya afya ya msingi, na afya kwa ujumla, elimu, mambo ya kiroho,mambo ya mila na utamaduni.Lakini pia ni pamoja na kuona mambo ya miundombinu pia yanapewa kipau mbele kama vile:mabarabara, mitandao ya mawasiliano, masoko, ...