sera mpya ya elimu na mafunzo tanzania

Upload: muhidin-issa-michuzi

Post on 01-Jun-2018

1.786 views

Category:

Documents


89 download

TRANSCRIPT

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    1/77

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    2/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    i

    SERA YA ELIMU NA MAFUNZO

    2014

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    3/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    ii

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    4/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    iii

    YALIYOMO

    VIFUPISHO v

    DIBAJI vii

    SURA YA KWANZA 1

    1.0. UTANGULIZI 1

    1.1. Hali Ilivyo 8

    SURA YA PILI 18

    2.0. UMUHIMU WA SERA 18

    2.1. Dira, Dhima na Malengo ya Sera 19

    SURA YA TATU 21

    3.0. HOJA NA MATAMKO YA SERA 213.1. Mfumo, miundo na taratibu nyumbufu kumwezesha

    Mtanzania kujiendeleza kwa njia mbalimbali katikamikondo ya kitaaluma na kitaalamu

    21

    3.2. Elimu na mafunzo yenye viwango vya uboraunaotambulika kikanda na kimataifa na kukidhimahitaji ya maendeleo ya Taifa

    24

    3.3 Upatikanaji wa fursa mbalimbali za elimu namafunzo nchini

    40

    3.4. Mahitaji ya Rasilimaliwatu kulingana na Vipaumbelevya Taifa

    46

    3.5. Usimamizi na uendeshaji madhubuti wa elimu namafunzo nchini

    50

    3.6. Mfumo endelevu wa ugharimiaji wa elimu namafunzo nchini

    55

    3.7. Mfumo wa elimu na mafunzo unaozingatiamasuala mtambuka.

    57

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    5/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    iv

    URA YA NNE 604.0. MUUNDO WA KISHERIA 604.1. Utangulizi 60

    4.2. Sheria za kusimamia elimu na mafunzo 60SURA YA TANO 625.0. MUUNDO WA KITAASISI 625.1. Utangulizi 625.2. Ngazi ya Taifa 635.3. Ngazi ya Mkoa 655.4. Ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa 655.5. Ngazi ya Kata 665.6. Ngazi ya Shule na Vyuo 675.7. Ufuatiliaji na Tathmini 675.8. Hitimisho 68

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    6/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    v

    VIFUPISHO

    AZAKI Asasi za KiraiaCA Continuous Assessment

    IGC-POPC International Growth Centre – Presidents’Of ce Planning Commission

    MKUKUTA Mkakati wa Kukuza Uchumi na KupunguzaUmaskini Tanzania

    MMEM Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi

    MMES Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya

    SekondariMMEJU Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Elimu ya Juu

    MMEU Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi

    MEMKWA Mpango wa Elimu ya Msingi kwa WatotoWalioikosa

    MUKEJA Mpango wa Uwiano kati ya Elimu ya WatuWazima na Jamii

    OWM-TAMISEMI

    O si ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa

    SADC Southern Africa Development Community

    TEHAMA Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

    UNESCO United Nations Educational, Scienti c andCultural Organisation

    UKIMWI Upungufu wa Kinga MwiliniURT United Republic of Tanzania

    WyEMU Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

    VVU Virusi vya Ukimwi

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    7/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    vi

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    8/77

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    9/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    viii

    mafunzo ili uwe na tija na ufanisi, kuendelea kutoa fursa zaelimu na mafunzo kwa usawa na kuendelea kuinua uborawa mitaala ya elimu na mafunzo ili ikidhi mahitaji yamaendeleo ya Taifa. Aidha, Serikali itaendeleza matumiziya lugha ya Kiswahili, Kiingereza, Alama, pamoja na lughanyingine za kigeni katika elimu na mafunzo. Vilevile,itaendelea kuinua ubora wa mfumo wa upimaji, tathminina utoaji vyeti katika ngazi zote. Serikali itaimarisha uwezowa uongozi na utawala katika sekta ya elimu na mafunzona kupanua wigo wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo.

    Sera hii mpya inaweka Dira ya elimu na mafunzo nchinikuwa ni “ Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi,umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katikakuleta maendeleo ya Taifa” na Dhima yetu kuwa ni “ kuinuaubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibuzitakazowezesha kupata idadi kubwa ya Watanzania walioelimika

    na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katikaku kia malengo ya maendeleo ya Taifa letu”. Ili kufanikishautekelezaji wa Sera hii kwa ukamilifu, kunahitajikaushiriki wa wadau wote wa elimu na mafunzo katikangazi zote, ikiwemo sekta binafsi, Asasi za Kiraia (AZAKI)na washirika wengine wa maendeleo.

    Mwisho, napenda kuwashukuru wale wote walioshirikikwa namna moja au nyingine katika mchakato mzima wakukamilisha Sera hii.

    Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    10/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    1

    SURA YA KWANZA

    1.0. UtanguliziSera hii ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ni matokeo yakuhuishwa na hatimaye kufutwa kwa Sera ya Elimu na Mafunzo(1995), Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996), Sera yaTaifa ya Elimu ya Juu (1999) na Sera ya Teknolojia ya Habari naMawasiliano kwa Elimu Msingi (2007). Utekelezaji wa Sera yaElimu ya Ufundi na Mafunzo (1996) na Sera ya Taifa ya Elimuya Juu (1999) ulisimamiwa na iliyokuwa Wizara ya Sayansi,

    Teknolojia na Elimu ya Juu; na utekelezaji wa Sera ya Elimu naMafunzo (1995) na Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasilianokwa Elimu Msingi (2007) ulisimamiwa na iliyokuwa Wizaraya Elimu na Utamaduni. Mwaka 2006, Serikali ilibadilishamuundo wa iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni kuwaWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kujumuisha elimuya juu na baadaye mwaka 2008 kujumuisha elimu ya ufundi

    katika wizara hiyo. Sera hizo za elimu, kwa ujumla, zilitoamwongozo kuhusu kuongeza ushirikishwaji wa sekta binafsi;kuongeza fursa za elimu na mafunzo kwa usawa; kupanuawigo wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo; kuhuisha muundowa uongozi wa elimu kwa kupeleka madaraka na majukumukatika ngazi ya shule, jamii, wilaya na mikoa; kuinua ubora waelimu; kuimarisha uhusiano kati ya elimu rasmi na elimu nje yamfumo rasmi na kuwezesha ukuaji wa utamaduni wa elimu yakujiajiri na kubuni ajira.

    Katika miaka 19 ya utekelezaji wa Sera ya kwanza ya Elimu naMafunzo ya mwaka 1995 pamoja na Sera nyingine mahususiza elimu na mafunzo, Tanzania imepata mafanikio makubwakatika sekta ya elimu. Mafanikio haya ni pamoja na kupanuawigo wa elimu katika ngazi zote, kuanzia elimu ya awali hadi

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    11/77

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    12/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    3

    elimu na mafunzo ya ufundi, elimu ya vyuo vikuu, mfuko waelimu na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu piavimeanzishwa na vinafanya kazi nzuri ya kuendeleza elimu namafunzo nchini.

    Hata hivyo, changamoto nyingi zimejitokeza katika kipindi chautekelezaji wa Sera hizi, ambazo zimekuwa zikiathiri uborana usawa katika elimu inayotolewa kwenye ngazi mbalimbali.Changamoto hizi ni pamoja na upungufu wa miundombinu navifaa vya kufundishia na kujifunzia ikiwemo vitabu, maabara,maktabana madarasa;. upungufu wa walimu hususan walimuwa sayansi, hisabati na stadi za kusoma, kuhesabu na kuandika;kushuka kwa morali ya kufundisha miongoni mwa walimu kwasababu ya maslahi yasiyoridhisha na mazingira magumu yakazi; utambuzi ha fu wa wanafunzi wenye mahitaji maalumuna mazingira duni ya kujifunzia; kutokuwepo kwa utaratibu wautambuzi na uendelezaji wa wanafunzi wenye vipaji na vipawa;

    matumizi ha fu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) katika utoaji wa elimu na mafunzo; na walimu nawanafunzi kutomudu lugha ya kufundishia na kujifunzia katikangazi mbalimbali za elimu. Vilevile kiwango cha watu wazimawenye kufahamu kusoma, kuandika na kuhesabu kimeshukakutoka asilimia 85 mwaka 1992 hadi asilimia 77.9 kulingana naSensa ya Taifa ya mwaka 2012.

    Aidha, bado Sekta ya elimu na mafunzo inakabiliwa nachangamoto ya mfumo usiokidhi mahitaji ya elimu namafunzo nchini. Mfumo wa elimu na mafunzo umetawaliwana muundo wa kitaaluma wenye dhana ya kuchuja wahitimuili kupata wachache wenye uwezo mkubwa katika taaluma nawatakaosoma hadi kumaliza katika ngazi ya chuo kikuu. Hali

    hii inatokana na nafasi za elimu na mafunzo ngazi za juu kuwa

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    13/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    4

    chache kadri wanafunzi wanavyohitimu kuanzia ngazi ya elimuya msingi na kuendelea, hivyo kuwa na muundo wa kuchujabadala ya ule wa kutoa fursa kulingana na uwezo, vipaji navipawa. Hali kadhalika, muundo wa 2+7+4+2+3+ unachukua jumla ya miaka 18 kutoa rasilimaliwatu. Hii ina maana kwambamwanafunzi anayeanza masomo akiwa na umri wa miaka 7atamaliza elimu ya juu akiwa na umri wa takribani miaka 23.Umri huu ni mkubwa ikilinganishwa na nchi nyingine kama zaAfrika ya Kusini, Maurishasi, Malesia na U ni ambapo umri wakijana anayemaliza elimu ya juu ni takribani miaka 20 hadi 22.

    Vilevile, hakuna mwingiliano fanisi kati ya muundo wa elimuya ufundi na muundo wa elimu ya jumla na hivyo kushindwakuwawezesha wahitimu wa elimu ya ufundi kujiendelezakatika elimu ya juu. Pamoja na hayo, kuna ukosefu wa mfumoendelevu wa utambuzi wa sifa mbadala utakaowawezeshawatu waliopata ujuzi kwa njia mbalimbali za elimu na mafunzokujiendeleza kielimu na kuingia katika ulimwengu wa kazi.

    Vilevile, kumekuwa na changamoto katika kuinua uborawa elimu na mafunzo kutokana na mitaala katika ngazimbalimbali za elimu na mafunzo kutokidhi mahitaji yamabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na teknolojia nahivyo kutoa wahitimu ambao hawana umahiri wa kutosha

    kuhimili ushindani katika ulimwengu wa kazi. Aidha,Taasisina mashirika yanayotoa huduma za kielimu yaliyopo chini yaWizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo yana mamlakakamili ya uendeshaji wa shughuli za elimu bila kuwa namahusiano ya kisheria katika utendaji baina yao na wizarazinazosimamia elimu na mafunzo na hivyo kuathiri uborawa elimu itolewayo. Hali kadhalika, changamoto nyingine nikutokuwepo kwa ugharimiaji endelevu kutokana na mifuko ya

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    14/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    5

    elimu kutokidhi mahitaji ya elimu katika ngazi zote na hivyokuhitaji vyanzo vingine vya ugharimiaji endelevu wa elimu namafunzo.

    Utekelezaji wa Ibara ya 146(1) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania (1977) kuhusu ugatuaji umekuwa nachangamoto mbalimbali. Katiba inatamka katika Sura ya Nane(kuhusu madaraka kwa umma), kwamba, madhumuni yakuwapo Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchina hivyo kuwezesha Serikali za Mitaa kuwajibika kutekelezakazi zake katika eneo husika. Sheria za Serikali za Mitaa zinatoamajukumu kwa Halmashauri kuhusu elimu katika Kifungu cha55 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Miji) ya 1982. Nikwa mantiki hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakupitia Matangazo ya Serikali Na. 494 na 494A ya mwaka 2010aligatua na kuiweka katika usimamiaji wa OWM-TAMISEMIelimu ya awali, msingi na sekondari na kuacha Wizara ya Elimu

    na Mafunzo ya Ufundi kushughulikia Sera katika masuala yoteya elimu na mafunzo. Hata hivyo bado kuna changamoto zamuingiliano wa baadhi ya majukumu katika utekelezaji waugatuaji kwa upande wa utendaji na usimamiaji wa elimu kati yaWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na OWM-TAMISEMI.

    Katika miaka ya hivi karibuni, viwango vya ubora wa elimu

    vimekuwa vikishuka. Hali hii inadhihirishwa na ufaulu katikamitihani ya kuhitimu elimu ya msingi na elimu ya sekondaringazi ya kawaida kuwa na mserereko wa kushuka kutokaasilimia 54 mwaka 2007 hadi ku kia asilimia 31 mwaka 2012,kwa upande wa elimu ya msingi; na asilimia 90 mwaka 2007hadi asilimia 43 mwaka 2012 kwa elimu ya sekondari; wakatiidadi ya watahiniwa inaongezeka mwaka hadi mwaka.Maarifa na Ujuzi wa wahitimu katika ngazi hizo ni mdogo

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    15/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    6

    ikilinganishwa na ngazi ya elimu waliyo kia. Hali kadhalika,maarifa na ujuzi wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi na elimuya juu havikidhi mahitaji mbalimbali katika ulimwengu wa kazi.Tathmini zinaonyesha kwamba, ili kuimarisha ubora na ufanisiwa elimu na mafunzo nchini, kuna ulazima wa kuimarishamaeneo mbalimbali ambayo yanahusika na ubora wa elimu namafunzo.

    Katika harakati za kimaendeleo, yapo mabadiliko ya sera zakijumla na mipango ya kitaifa iliyojitokeza katika kipindicha utekelezaji wa sera hizi. Kutokana na Dira ya Taifa yaMaendeleo 2025 na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Mudamrefu 2011/12 hadi 2024/25, Serikali imelenga kujenga jamiiiliyoelimika na yenye kupenda kujielimisha. Pamoja na azmahiyo, Tanzania imeridhia Itifaki ya SADC (1997) kuhusu elimuna mafunzo inayozitaka nchi wanachama kuwa na elimumsingiya lazima kwa kipindi kisichopungua miaka tisa; Itifaki ya Dakar

    (2000) kuhusu Elimu kwa wote; Makubaliano ya Perth UNESCO(2007) kuhusu Elimu ya Sayansi na Teknolojia na mafunzo yaufundi na mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha,kuna baadhi ya masuala mtambuka yakiwemo mazingira, jinsia, VVU na UKIMWI na Ubia baina ya Sekta ya Umma naSekta Binafsi ambayo yamejitokeza na yanahitaji kujumuishwakatika Sera ya Elimu na Mafunzo.

    Sekta ya elimu na mafunzo ina jukumu la kuandaa na kuzalisharasilimaliwatu kwa ajili ya Taifa. Ripoti mbalimbali zinaonyeshakwamba kuna nakisi kubwa ya wataalamu walioelimika kwakiwango cha elimu ya juu wanaohitajika ili Tanzania i kie kuwanchi yenye uchumi wa kati i kapo mwaka 2025. Taarifa ya IGC-POPC (2011) inaonyesha kuwa, Rasilimaliwatu ya Tanzania,kwa kiasi kikubwa, ni wafanyakazi wenye ujuzi wa chini ambao

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    16/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    7

    ni asilimia 84, wakifuatiwa na wenye ujuzi wa kati ya asilimia13 na wenye ujuzi wa juu asilimia 3. Hata hivyo, kwa nchi zakipato cha kati ngazi ya chini, ulinganifu unaonyesha kuwanchi hizo zina wastani wa asilimia 55 ya wafanyakazi wenyeujuzi wa chini, asilimia 33 ujuzi wa kati na asilimia 12 ujuziwa juu. Hivyo, sekta ya elimu na mafunzo ina changamoto yakuinua mchanganyiko wa wafanyakazi wenye ujuzi katika fanimbalimbali ili ku kia mahitaji ya rasilimaliwatu kwa nchi yakipato cha kati i kapo mwaka 2025.

    Mfumo wa elimu na mafunzo wa sasa una changamotoya kuliwezesha Taifa kukidhi ongezeko la mahitaji yarasilimaliwatu kulingana na vipaumbele vya Taifa kwa sababutakwimu za elimu za mwaka 2000 hadi 2012, zinaonyesha kuwani wastani wa asilimia 5 tu ya wahitimu wa darasa la saba ndiyowanaofaulu na kuendelea hadi ku kia elimu ya sekondari ya juu; na wastani wa asilimia 4 tu ya wahitimu hao wa darasa la

    saba ndiyo wanaofaulu na kuendelea hadi elimu ya juu. Kwamwenendo huo ni dhahiri kwamba Taifa litaendelea kuwa nanakisi ya wataalamu kama hatua madhubuti za kuongeza fursana kuinua ubora wa elimu hazitachukuliwa.

    Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 imeandaliwa ilikutoa mwelekeo wa elimu na mafunzo nchini kwa kuzingatia

    mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na kiteknolojia nachangamoto za elimu na mafunzo kitaifa, kikanda na kimataifa,ili kuongeza fursa, ufanisi na ubora wa elimu na mafunzo nchinina ku kia viwango vya rasilimaliwatu kwa nchi yenye uchumiwa kati i kapo mwaka 2025.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    17/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    8

    1.1. Hali IlivyoUchambuzi wa tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Elimuna Mafunzo ya mwaka 1995, umeonyesha kuwa matamko59 kati ya matamko 149 ya Sera hayakutekelezwa. Kati yahayo, matamko 25 yalihusu elimu ya msingi na sekondari,18 yalihusu elimu ya ufundi na 16 yalihusu elimu ya juu.Tathmini ilibaini pia kuwa mpango mkakati wa kuelekezautekelezaji wa sera hizo haukuandaliwa mpaka mwaka 1997ulipoanzishwa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu, namwaka 2001 ulipoandaliwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu

    ya Msingi (MMEM). Tathmini ilibaini pia kuwa usimamizina uendeshaji wa elimu na mafunzo katika ngazi ya mkoa nawilaya unafanywa na mamlaka mbalimbali zinazoongozwana kanuni na taratibu tofauti pamoja na OWM-TAMISEMI.Walimu wanaandaliwa na kuajiriwa na Wizara ya Elimu naMafunzo ya Ufundi wakati haki zao za kiutumishi na nidhamuzinashughulikiwa na Idara ya Utumishi wa Walimu. Utaratibuhuu wa usimamizi wa walimu chini ya mamlaka tatu tofautiunafanya hali ya uwajibikaji na utawala bora kuwa mgumu.Kutokana na taarifa ya tathmini, inapendekezwa kuwa Serikaliiunde Bodi ya kitaalamu ya kusimamia maendeleo ya utaalamuwa ualimu. Vilevile walimu wawe chini ya mwajiri mmojaatakayeshughukia masuala ya ajira, nidhamu na maendeleo

    yao.

    Vyuo vya elimu ya ufundi stadi na vyuo vya ualimuhavikuwekewa muundo wa kitaasisi unaoviunganisha namaa sa elimu wa wilaya na mikoa kama ilivyoelekezwa kwenyeSheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na katika Sera ya Elimuna Mafunzo ya mwaka 1995. Taasisi zilizo chini ya Wizarazinazotoa huduma za kielimu hazina uhusiano wa kiutendaji

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    18/77

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    19/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    10

    elimu na mafunzo Serikali, sekta binafsi na wadau wenginewa maendeleo, wamekuwa wakichangia kuongeza fursa kwamakundi yote kwa usawa.

    Hali kadhalika, tathmini ilionyesha kuwa jitihada za Serikalizimeleta mafanikio ya kuongezeka kwa fursa katika ngazimbalimbali za elimu na mafunzo. Hata hivyo, kumekuwa nachangamoto ya wanafunzi kuacha shule kutokana na sababumbalimbali na wengi kutopata fursa ya kuendelea kutokana naufaulu mdogo.

    Vile vile, taasisi kama vile Taasisi ya Elimu Tanzania, Baraza laTaifa la Mitihani Tanzania, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi,Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Tume yaVyuo Vikuu Tanzania huratibu ithibati na uthibiti wa viwangovya ubora wa elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali. Kilataasisi ina bodi ya utendaji ambayo hutoa maamuzi kuhusumasuala ya utoaji na uendeshaji wa elimu na mafunzo katikamaeneo ya mamlaka zao. Tathmini ilibaini kuwa taasisi hizizinahitaji muunganiko fanisi wa utendaji kazi kisheria ilikuongeza ufanisi katika usimamizi wa ubora wa elimu namafunzo nchini.

    1.1.1 Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka

    1995Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995ulifanyika kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi(MMEM) na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari(MMES). Baadhi ya malengo ya Sera yaliyotekelezwa katikamipango hiyo ni:

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    20/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    11

    Kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji(i)wa elimu na mafunzo kwa kuhimiza kuanzisha nakuendesha shule na taasisi za elimu na mafunzo,

    Kutilia mkazo utoaji wa elimu bora kwa kuangalia(ii) upya mitaala, kuinua ubora wa usimamizi wawalimu na kutumia maendeleo ya mwanafunzi yakila siku katika upimaji,

    Kupanua upatikanaji wa fursa za elimu kwa(iii)kuzingatia usawa kwa makundi yote nchini, na

    Kupanua wigo wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo(iv)kwa kudhibiti matumizi ya Serikali pamoja nakuhimiza uchangiaji wa gharama.

    Katika kutekeleza mipango hiyo, kumekuwa na mafanikioyakiwemo kuongezeka kwa ushiriki wa sekta binafsi katikakutoa elimu na mafunzo, kuimarishwa kwa usimamizi wa

    walimu kwa kuundwa chombo cha kushughulikia masuala yawalimu kama vile usajili, kuthibitishwa kazini, kupandishwamadaraja na masuala ya nidhamu. Aidha, kumekuwa namafanikio katika maandalizi, uendelezaji, utoaji na ufuatiliajina tathmini ya mitaala ya elimu ya awali, msingi, sekondarina ualimu. Hali kadhalika, kumekuwa na ongezeko la fursambalimbali katika ngazi za elimu ya msingi, sekondari namafunzo ya ualimu. Idadi ya wanafunzi walioandikishwakatika elimu ya msingi iliongezeka kutoka 3,942,888 (wavulana1,992,739 na wasichana 1,950,149) mwaka 1996 hadi 8,247,172(wavulana 4,086,280 na wasichana 4,160,892) mwaka 2012ambayo ni ongezeko la zaidi ya mara mbili. Kwa upande waelimu ya sekondari ngazi ya kawaida, kumekuwa na ongezeko

    la wanafunzi walioandikishwa kutoka 185,119 (wavulana 98,435

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    21/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    12

    na wasichana 86,684) mwaka 1996 hadi wanafunzi 1,802,810(wavulana 954,961 na wasichana 847,849) mwaka 2012 ambaloni ongezeko la zaidi ya mara tisa. Aidha, Idadi ya wanafunzikatika elimu ya sekondari ya juu imeongezeka kutoka 13,974(wavulana 9,597 na wasichana 4,377) mwaka 1996 hadiwanafunzi 81,462 (wavulana 55,512 na wasichana 25,950) mwaka2012 ambalo ni ongezeko la zaidi ya mara tano. Mafanikio hayapamoja na mengine yamechangiwa na utaratibu wa Serikalikutoa ruzuku kwa shule za umma za msingi na sekondari.Aidha, wazazi na wanafunzi wameendelea kuchangia ada na

    michango mbalimbali katika shule za sekondari na vyuo kadriwanavyohitajika kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu zaelimu na mafunzo.

    Mafanikio hayo yamekuwa pia na changamoto katika maeneombalimbali yakiwemo ya mitaala kutokidhi mahitaji kutokanana mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na teknolojia.

    Vilevile, kutokana na upanuzi wa fursa za elimu katika ngazizote kumekuwa na ongezeko la mahitaji ya nyenzo, vifaa nazana za kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote.

    1.1.2 Utekelezaji wa Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya mwaka 1996

    Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya mwaka 1996 ilitekelezwakupitia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya utoaji waelimu katika sekta ya ufundi. Hata hivyo, kupitia Mpangowa Maendeleo ya Sekta ya Elimu, uliandaliwa Mpango waMaendeleo ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi StadiPamoja na masuala mengine, Sera ya Elimu ya Ufundi na

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    22/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    13

    Mafunzo ilikuwa na malengo yafuatayo:Kupata idadi ya kutosha ya mafundi na(i)wanateknolojia mahiri ili kukidhi mahitaji ya sektarasmi na isiyo rasmi;

    Kuanzisha na kuimarisha taasisi za mafunzo ya(ii)ufundi kwa kuziwekea vitendea kazi na wataalamuili kutimiza malengo;

    Kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uendeshaji(iii)na ugharimiaji wa elimu ya ufundi;

    Kuwa na mfumo fanisi na bora wa elimu na mafunzo(iv)ya ufundi ili kuleta usawa wa fursa za elimu namafunzo;

    Matumizi ya sayansi na teknolojia katika maendeleo(v)ya kijamii na kiuchumi; na

    Kuhimiza na kuratibu ubora wa matokeo ya(vi)wahitimu kupitia uanzishwaji wa Baraza la Taifa laElimu ya Ufundi.

    Utekelezaji wa Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yamwaka 1996 umeleta mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamojana: kukamilika kwa mfumo wa sifa linganifu za mafunzo yaufundi na ufundi stadi kutoka ufundi mchundo hadi uhandisi;

    kutekelezwa kwa mtaala unaozingatia umahiri wa stadi hususankwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Barazala Taifa la Elimu ya Ufundi; kujumuishwa kwa masomo yastadi za kazi katika mitaala ya elimu ya msingi; kuanzishwakwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi kwa sheria ya BungeSura ya 129; na kuongezeka kwa vyuo vya ufundi kutoka 695mwaka 2005 hadi 750 mwaka 2012 na kuwezesha ongezekola wanachuo kutoka 78,586 (wanaume 43,022 na wanawake

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    23/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    14

    35,564) mwaka 2005 hadi wanachuo 104,440 (wanaume 54,350na wanawake 50,190) mwaka 2012. Vyuo vya elimu na mafunzoya ufundi stadi viliongezeka kutoka vyuo 195 mwaka 2005hadi ku kia vyuo 260 mwaka 2011 na kuongeza udahili wawanachuo kutoka 39,759 (wanaume 30,123 na wanawake 9,636)mwaka 2005 hadi 85,040 (wanaume 46,342 na wanawake 38,698)mwaka 2011.

    Pamoja na mafanikio hayo, utekelezaji wa Sera ya Elimu yaUfundi na Mafunzo ulikuwa na changamoto zifuatazo:

    Ukuaji mdogo wa fursa za elimu ya ufundi na(i)mafunzo ya ufundi stadi ukilinganishwa na mahitajiya taifa na ulimwengu wa kazi;

    Mtazamo hasi kuhusu mafunzo ya ufundi;(ii)

    Fikra mgando za ujinsi katika dhana nzima ya(iii)mafunzo ya ufundi;

    Upungufu wa wakufunzi wenye sifa na kutokuwepo(iv)kwa mazingira mazuri ya kuwabakisha kazini;

    Kutokuwepo kwa mwingiliano fanisi kati ya mfumo(v)wa elimu ya ufundi na mfumo wa elimu ya jumla;na

    Mafunzo kutokidhi mahitaji ya ulimwengu wa kazi.(vi)

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    24/77

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    25/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    16

    Kutokuwepo kwa ugharimiaji endelevu wenye(ii)kuleta tija na hivyo kuendelea kuwa mzigo mkubwakwa Serikali, wazazi na wanafunzi;

    Kutokuwepo kwa ushirikiano bayana baina ya sekta(iii) ya elimu na viwanda katika utoaji wa elimu ya juu;

    Kutokuwa na mfumo endelevu na mpana wa(iv)utambuzi wa sifa mbadala unaoruhusu wahitimukatika ngazi mbalimbali za elimu kujiunga na elimuya juu;

    Kuendelea kuwepo kwa vikwazo mbalimbali(v)ikiwemo mitazamo hasi inayokwamisha maendeleoya elimu ya juu, u nyu wa rasilimali mbalimbali namatumizi duni ya TEHAMA katika maendeleo yaelimu ya juu; na

    Baadhi ya mitaala ya elimu ya juu kutotosheleza(vi)

    mahitaji ya maendeleo ya Taifa na ulimwengu wakazi.

    1.2 Changamoto za jumla katika Sekta ya Elimu naMafunzo Nchini

    Utekelezaji wa sera za elimu na mafunzo, unakabiliwa na

    changamoto mbalimbali za jumla zikiwemo:

    Kukosekana kwa mfumo nyumbufu unaoruhusu(i)elimu na mafunzo kupatikana na kutambulika kwanjia mbalimbali mbadala;

    Kuwepo kwa elimu na mafunzo yenye viwango(ii)vya ubora visivyotambulika kitaifa, kikanda nakimataifa;

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    26/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    17

    Kutokuwa na mfumo wa ajira unaowezesha(iii)upatikanaji wa wataalamu wa kada mbalimbaliwanaohitajika katika sekta ya elimu na mafunzonchini;

    Kukosekana kwa fursa zitolewazo kwa kila(iv)Mtanzania kulingana na mahitaji yake na sehemu namazingira aliyopo;

    Kutokuwa na mfumo wa ugharimiaji wa elimu na(v)mafunzo wenye wigo mpana na endelevu;, na

    Kutozingatia masuala mtambuka kikamilifu katika(vi)elimu na mafunzo.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    27/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    18

    SURA YA PILI

    2.0. UMUHIMU WA SERA

    Tangu kuanza kutekelezwa kwa Sera ya Elimu na Mafunzo (1995),Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996) na Sera ya Taifaya Elimu ya Juu (1999) kumekuwa na mabadiliko mbalimbaliya kisiasa, kijamii, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia ambayoyameleta changamoto na kuzifanya Sera hizo zipitwe na wakati.Mabadiliko ya kiuchumi duniani yameleta msukumo kwa nchizinazoendelea na zilizoendelea ama kubadilisha au kuimarishasera, programu na mikakati yake ili ziweze kuhimili ushindaniwa kiuchumi na kuleta maendeleo endelevu ya kijamii, kisayansina kiteknolojia. Tanzania ni moja ya nchi ambazo uchumi wakeumeendelea kukua na ku kia asilimia 7 mwaka 2012. Kukuahuku kunatokana na kuongezeka kwa uwekezaji katika sektambalimbali za kiuchumi. Azma ya Tanzania ni ku kia uchumi

    wa kati i kapo mwaka 2025 ambapo sekta ya elimu na mafunzoimepewa jukumu la kuandaa rasilimaliwatu ya kutosha kwaajili ya kukidhi mabadiliko hayo.

    Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ililenga elimu yamsingi na ya lazima iwe miaka 7, lakini kwa mujibu wa Dira yaMaendeleo ya Taifa 2025 ni kuwa na taifa la watu wenye elimuya kati na ya juu ili kuwa na watendajikazi wenye uwezo wakushughulikia kikamilifu changamoto za kimaendeleo. Halikadhalika, Sera ya Ajira na Utumishi wa Umma ya mwaka 1999inatamka kuwa sifa ya kuajiriwa katika utumishi wa ummakwa masharti ya kudumu ni kiwango cha elimu kisichopunguaelimu ya sekondari ya kidato cha nne.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    28/77

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    29/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    20

    2.2. Malengo ya Sera2.2.1. Lengo la Jumla:Kuwa na Watanzania walioelimika na wenye maarifa na ujuzikuweza kuchangia kwa haraka katika maendeleo ya Taifa nakuhimili ushindani.

    2.2.2. Malengo MahsusiMalengo mahsusi ya Sera ni kuwa na:

    Mfumo, miundo na taratibu nyumbufu kumwezesha(i)Mtanzania kujiendeleza kwa njia mbalimbali katika

    mikondo ya kitaaluma na kitaalamu;Elimu na mafunzo yenye viwango vya ubora(ii)unaotambulika kitaifa, kikanda na kimataifa;

    Upatikanaji wa fursa mbalimbali za elimu na(iii)mafunzo nchini;

    Ongezeko la rasilimaliwatu kulingana na vipaumbele(iv)vya Taifa;

    Usimamizi na uendeshaji madhubuti wa elimu na(v)mafunzo nchini;

    Mfumo endelevu wa ugharimiaji wa elimu na(vi)mafunzo nchini; na

    Mfumo wa elimu na mafunzo unaozingatia masuala(vii)mtambuka.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    30/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    21

    SURA YA TATU3.0. HOJA NA MATAMKO YA SERA

    3.1. Mfumo, Miundo na Taratibu Nyumbufu KumwezeshaMtanzania Kujiendeleza kwa Njia Mbalimbali katikaMikondo ya Kitaaluma na Kitaalamu.

    Suala

    Mfumo wa elimu na mafunzo

    Maelezo

    Serikali imejitahidi katika kufanikisha upatikanaji wa haki yaelimu kwa watoto wa jinsi zote kwa kuwezesha uandikishajiku kia asilimia 105.5 ya wanafunzi katika elimu ya msingi.Hata hivyo, elimu baada ya elimu ya msingi imeendeleakuwa na changamoto mbalimbali kwa sababu mfumo ulioposasa unategemea zaidi utaratibu wa kuchuja wanafunzi

    kwa ajili ya kuendelea na masomo badala ya kutoa fursa yakuwaendeleza kadri ya uwezo, vipaji na vipawa vyao. Mfumohuu pia umejikita katika taaluma na ulibuniwa wakati shule navyuo vikiwa vichache na ulilenga zaidi dhana ya kusoma nakumaliza katika ngazi ya chuo kikuu na hivyo kuwafanya walewanaoshindwa kuendelea kitaaluma kuchaguliwa kujiunga naelimu na mafunzo ya ufundi stadi au mafunzo ya ufundi. Hikini kiashiria cha mfumo kushindwa kutoa fursa anuai za elimuna mafunzo ambazo zingeweza kumfanya mhitimu apate ujuzina maarifa kwa ajili ya ulimwengu wa kazi.

    Hali kadhalika, kwa muundo wa elimu yetu wa 2+7+4+2+3+mwanafunzi anayeanza masomo akiwa na umri wa miaka 7atamaliza elimu ya juu akiwa na umri mkubwa, takribani miaka 23

    ikilinganishwa na nchi kama za Afrika ya Kusini, Maurishasi,

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    31/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    22

    Malesia na U ni ambapo umri wa kijana anayemaliza elimuya juu ni takribani miaka 20 hadi 22. Kwa mantiki hii, mfumonyumbufu unahitajika ili kuongeza idadi ya wanafunziwanaomaliza katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzokuendelea na masomo katika ngazi nyingine.

    Lengo

    Kuwa na mfumo nyumbufu wa elimu na mafunzo wenye tijana ufanisi na hivyo kuongeza idadi ya wananchi walioelimikana kuwa na maarifa kwenye fani mbalimbali.

    Tamko3.1.1 Serikali itaweka mfumo nyumbufu katika elimu na

    mafunzo ili kuwezesha wananchi wengi zaidi kujielimishana kuwa huru kutafuta elimu katika fani wanayopendahadi kufkia upeo wowote kulingana na stahili na uwezowao.

    Suala

    Umri wa elimumsingi na muda wa elimu na mafunzo

    Maelezo

    Muundo wa elimu na mafunzo uliopo unatoa fursa ya mtotomwenye umri wa miaka mitano kujiunga na elimu ya awali kwa

    muda wa miaka miwili. Mtaala wa elimu ya awali umeandaliwakwa namna ambayo unatakiwa ufundishwe kwa miaka 2lakini Tathmini ya Sera za Elimu na Mafunzo ya mwaka 2008inaonesha kuwa mtaala huo unaweza kufundishwa kwa mwakammoja kama ukifundishwa kwa ufanisi. Pia, Itifaki ya Dakar yamwaka 2000 ambayo ilitakiwa itekelezwe hadi i kapo mwaka2015 ambayo Tanzania imeridhia na kufuatana na UNESCO(ISCED, 1997), elimu ya awali inatakiwa kutolewa kwa watoto

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    32/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    23

    wenye umri kati ya miaka mitatu hadi sita.

    Kwa sasa, Elimu ya Msingi inatolewa kwa miaka saba (7) nani ya lazima kwa uandikishaji na mahudhurio kwa mujibu wa

    Sheria ya Elimu Sura ya 353 ya sheria za Nchi. Wahitimu waelimu ya msingi katika mfumo wa sasa wanakuwa na umri wamiaka 13. Baadhi ya wahitimu huendelea na elimu ya sekondarina mafunzo ya ufundi; waliokosa fursa hizo huingia kwenyeulimwengu wa kazi. Wahitimu hawa wanakuwa na umrimdogo na hawana maarifa na ujuzi unaotosheleza kujiunga naulimwengu wa kazi au kukabiliana na changamoto za maendeleo,iwapo watakosa fursa ya kuendelea na elimu ya sekondaringazi ya kawaida au elimu ya ufundi. Shirika la Kimataifa laKazi limeweka mkataba wa umri wa chini wa kuajiriwa kwabaadhi ya kazi kuwa ni miaka 15. Hali kadhalika, Itifaki yaSADC (1997) kuhusu elimu na mafunzo inasisitiza kutokomezakutojua kusoma na kuandika kwa kuweka juhudi ya kuwa

    na elimumsingi na ya lazima kwa wote angalau kwa kipindikisichopungua miaka tisa (9). Kutokana na makubaliano haya,kuna umuhimu wa kurekebisha muundo wa elimu ya awali namsingi ya sasa ili elimu ya awali iwe ya lazima na itolewe kwakipindi kisichopungua mwaka mmoja kulingana na mahitaji yamwanafunzi husika. Kila mtoto mwenye umri wa miaka 4 hadi6 na ambaye amepata elimu ya awali, kwa mujibu wa sheria,apatiwe elimumsingi itakayotolewa kwa muda wa miaka 10ili kumwezesha mwanafunzi kusoma, kuandika na kuhesabu,kuwa na ufahamu wa mambo ya ujumla na kupata maarifa naujuzi katika elimu, ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.

    Lengo

    Kurekebisha muda wa elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbaliili kuleta tija, ufanisi na matumizi bora ya rasilimali.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    33/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    24

    Tamko

    3.1.2. Serikali itaweka utaratibu wa elimu ya awali kuwa yalazima na kutolewa kwa watoto wenye umri kati ya

    miaka mitatu hadi mitano kwa kipindi kisichopunguamwaka mmoja.

    3.1.3. Serikali itaweka utaratibu wa elimumsingi kuwa yalazima kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne;na kutolewa kwa miaka kumi na umri wa kuanza darasala kwanza kuwa kati ya miaka minne hadi sita kulingana

    na maendeleo na uwezo wa mtoto kumudu masomokatika ngazi husika.

    3.1.4. Serikali itaweka utaratibu wa kuhakikisha muda wakukamilisha elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbaliza elimu baada ya elimumsingi unalenga mwanafunzikupata ujuzi stahiki kulingana na Mfumo wa Tuzo waTaifa.

    3.1.5. Serikali itahakikisha kuwa elimumsingi katika mfumowa umma inatolewa bila ada.

    3.2. Elimu na Mafunzo Yenye Viwango vya UboraUnaotambulika Kikanda na Kimataifa na Kukidhi

    Mahitaji ya Maendeleo ya TaifaSuala

    Uthibiti wa ubora wa elimu na mafunzo

    Maelezo

    Ubora wa elimu na mafunzo unatokana na ubora wa mitaala

    iliyopo, umahiri wa watekelezaji wa mitaala hiyo, uongozi,

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    34/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    25

    usimamiaji, mazingira ya kutolea elimu na mafunzo, tathmini narasilimali zilizopo. Taifa kwa sasa linakabiliwa na changamotombalimbali katika suala la ubora wa elimu na mafunzo katikangazi zote.

    Matokeo katika mitihani ya darasa la saba na kidato channe yamekuwa na mserereko wa kushuka kutoka asilimia54 mwaka 2007 hadi ku kia asilimia 31 mwaka 2012 kwaupande wa elimu ya msingi; na asilimia 90 mwaka 2007 hadiasilimia 43 mwaka 2012 kwa elimu ya sekondari, wakati idadiya watahiniwa inaongezeka mwaka hadi mwaka. Maarifa naUjuzi wa wahitimu katika ngazi hizo ni mdogo ikilinganishwana ngazi ya elimu waliyo kia. Halikadhalika, maarifa na ujuziwa wahitimu wa mafunzo ya ufundi na elimu ya juu hayakidhimahitaji mbalimbali katika ulimwengu wa kazi. Tathminizinaonyesha kwamba, ili kuimarisha ubora na ufanisi wa elimuna mafunzo nchini, kuna ulazima wa kuinua ubora wa mitaala,

    ukaguzi wa shule, tathmini, ithibati, na mamlaka zinazohusikana masuala hayo.

    Idara ya ukaguzi wa shule ina jukumu la kufuatilia uborawa elimu ya msingi na sekondari kwa kuzingatia mitaalana viwango vilivyowekwa. Utendaji wa idara hii umekuwaukikabiliwa na changamoto mbalimbali na hivyo kushindwakutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Changamoto hizo nipamoja na kuendelea kutumia falsafa ya ukaguzi iliyokuwa natija wakati shule zikiwa chache tofauti na sasa ambapo shuleni nyingi na hivyo kuhitaji ushirikishwaji zaidi wa wadau nambinu mbadala; upungufu katika muundo wa usimamizi nauendeshaji wa ukaguzi wa shule ambao umewaweka wakaguzimbali na shule ziliko pamoja na kushindwa kuzifanya Kamati

    na Bodi za Shule, Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule pamoja na

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    35/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    26

    wazazi kuwajibika vya kutosha katika suala la usimamizi nauthibiti wa ubora wa elimu itolewayo na shule zetu. Ukaguziha fu pia unachangiwa na kutokuwa na wataalamu mahiri nawa kutosha na ukosefu wa vitendea kazi.

    Kwa upande mwingine, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi lina jukumu la kuratibu ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu katikavyuo vya elimu ya ufundi; na Mamlaka ya Elimu na Mafunzoya Ufundi Stadi ina jukumu la kuratibu ithibati na uthibiti waubora wa mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo mbalimbalivya ufundi stadi. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania imepewamajukumu ya kuweka na kuratibu ithibati na uthibiti wa uborawa elimu ya juu katika vyuo vikuu nchini. Utendaji wa vyombohivi vya ithibati pamoja na vyombo vingine kama Taasisi yaElimu Tanzania, Bodi ya Huduma za Maktaba, Taasisi ya Elimuya Watu Wazima na Mamlaka ya Elimu Tanzania umekuwana changamoto katika kuinua viwango vya ubora wa elimu ya

    msingi, sekondari, vyuo vya ualimu, vyuo vya elimu ya ufundina mafunzo, vyuo vya ufundi stadi na vyuo vikuu. Uhusianobaina ya taasisi hizi na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundipamoja na OWM-TAMISEMI ni mdogo kwa kuwa hakunautaratibu madhubuti wa uratibu baina yao. Sheria za vyombohivi zinahitaji kutathminiwa upya ili kuleta mshikamano katikamfumo mzima wa usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini.

    Lengo

    Kuwa na ufanisi katika uratibu, usimamizi, ithibati na uthibitiwa ubora katika utoaji wa elimu na mafunzo.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    36/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    27

    Tamko

    3.2.1. Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarishausimamizi, ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu na

    mafunzo katika ngazi zote.3.2.2. Serikali itahakikisha vyombo vya usimamizi na

    uendeshaji wa elimu na mafunzo vinahusiana kiutendajikatika ngazi zote za elimu na mafunzo.

    3.2.3. Serikali itaimarisha mfumo, mbinu, dhana na falsafa yaukaguzi wa shule ili kuleta ufanisi zaidi katika uthibiti

    wa ubora wa elimumsingi nchini.Suala

    Mitaala ya elimu na mafunzo

    Maelezo

    Mtaala ni mwongozo wa elimu katika ngazi mbalimbali

    za elimu na mafunzo ambao ikiwa hautaandaliwa vizuri,kutekelezwa ipasavyo au kutathminiwa kwa umakini, mfumowa elimu utashindwa kufanya kazi na hautaweza kuletamatarajio yanayokusudiwa na jamii. Hadi mwaka 2005 mitaalailiyokuwepo kwa upande wa elimu ya awali, msingi na sekondariilijikita zaidi katika maudhui ya ufahamu na kuwa na msisitizomdogo katika kujenga ujuzi. Kuanzia mwaka 2005 mitaala hiyoilibadilika na kuwa ya kujenga ujuzi. Tathmini inaonyeshakuwa mabadiliko haya yalifanyika bila kushirikisha wadaumbalimbali wakiwemo walimu, wazazi, waajiri, wanafunzi,wakufunzi, wahadhiri, vyama vya kitaalamu, vyama vyakisiasa, taasisi za kidini, mashirika ya kiserikali na yasiyo yakiserikali, waratibu wa elimu na wakaguzi. Aidha, hapakuwa

    na maandalizi ya kutosha kwa watekelezaji wa mitaala. Hivyo,

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    37/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    28

    walimu kwa ujumla hawafundishi kwa namna iliyotegemewakatika mitaala iliyopo.

    Baadhi ya mitaala ya ngazi za ufundi, ufundi stadi na elimu

    ya juu imepitwa na wakati na haikidhi mahitaji ya ulimwenguwa kazi na hivyo wahitimu wa mitaala hiyo kutoajirika aukushindwa kufanya kazi kwa ufanisi pale wanapoajiriwa. Pia,kumekuwa na changamoto kwa wahitimu waliomaliza masomokatika mtaala wa ufundi kutotambulika kujiunga na mtaala wataaluma kwa baadhi ya fani; au mhitimu aliyemaliza katikamtaala wa taaluma kutotambulika katika mtaala wa ufundi.

    Tathmini pia zinaonesha kuwa mitaala ya baadhi ya vyuohaina ulinganifu katika maudhui na muda wa mafunzo kwaprogramu zinazolingana na kufanana. Kwa mantiki hii, kunaumuhimu wa kufanya tathmini ya mitaala iliyopo ili kuandaamitaala inayokidhi mahitaji ya elimu na mafunzo ya sasa na yabaadaye kuendana na mahitaji ya maendeleo na mabadiliko yasayansi na teknolojia kitaifa, kikanda na kimataifa.

    LengoKuwa na mitaala yenye tija, iliyofanisi na inayokidhi mahitajiya soko la ajira katika kuleta maendeleo ya Taifa na kuhimiliushindani.

    Tamko3.2.4. Serikali, kwa kushirikiana na wadau, itahuisha mitaala

    iliyopo katika ngazi zote za elimu na mafunzo ili iendena wakati na kukidhi mahitaji ya elimu na mafunzo yasasa na siku zijazo kwa kuzingatia mahitaji ya Taifa,walengwa na soko la ajira.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    38/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    29

    3.2.5. Serikali, kwa kushirikiana na wadau, itahakikishamitaala inazingatia stadi za msingi za mawasiliano,kusoma, kuandika na kuhesabu; kutafti; kuchambuataarifa; kutafsiri, kutathmini na kutumia maarifa,uvumbuzi, ubunifu na ujasiriamali katika ngazi zote zaelimu na mafunzo.

    3.2.6. Serikali itaimarisha usimamiaji na upimaji wa utekelezajiwa mitaala katika taasisi za elimu na mafunzo katikangazi zote, ili kuleta ufanisi wa elimu na mafunzoyatolewayo.

    Suala

    Elimu ya Sayansi na Teknolojia

    Maelezo

    Elimu ya Sayansi na Teknolojia ni muhimu katika kumwezesha

    mwananchi kumudu mazingira yake na kumwezesha kuchangiamaendeleo ya taifa. Watoto huanza kufundishwa somo lasayansi kuanzia darasa la III na katika elimu ya sekondari ngaziya kawaida wanafunzi wote husoma Fizikia, Kemia, Baiolojiana Hisabati hadi kidato cha pili (2). Aidha, wanafunzi wotehuendelea kusoma Baiolojia na Hisabati hadi kidato cha nne (4).Baadhi ya wanafunzi huchagua kuendelea na masomo ya Fizikiana Kemia kuanzia kidato cha tatu (3) hadi cha nne (4). Takwimuzinaonyesha kuwa, katika wanafunzi 100 ni wanafunzi kati ya30 – 35 tu ambao wanasoma masomo ya sayansi katika kidatocha tatu (3) na nne (4) ambao wakifaulu ndiyo wanaotarajiwakusomea fani mbalimbali za Sayansi na Teknolojia katika vyuovya elimu ya juu na vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo.

    Mitaala ya elimu ya msingi na sekondari inatakiwa kuweka

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    39/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    30

    mkazo katika elimu ya Sayansi na Teknolojia. Makubalianokuhusu Elimu ya Sayansi na Teknolojia (UNESCO-PERTH2007) yanasisitiza kufanya mapitio ya mitaala ya elimu yaSayansi na Teknolojia ili kuongeza hamasa ya wanafunzikutambua umuhimu wa Sayansi na Teknolojia katika jamii. Piakuna umuhimu wa kuweka mkazo katika matumizi ya Sayansina Teknolojia katika kufundishia na kujifunzia.

    Lengo

    Kuwa na idadi ya kutosha ya wananchi walioelimika katika

    Sayansi na Teknolojia na kukidhi mahitaji ya maendeleo yaTaifa.

    Tamko

    3.2.7. Serikali itaimarisha muundo na utaratibu wa ufundishajiwa masomo ya Hisabati, Sayansi na Teknolojia katikangazi zote za elimu na mafunzo.

    3.2.8. Serikali itahakikisha matumizi zaidi ya Sayansi naTeknolojia katika utoaji wa elimu na mafunzo katikangazi zote.

    Suala

    Nyenzo, vifaa, zana na mbinu za kufundishia na kujifunzia

    MaelezoUtekelezaji fanisi wa mitaala unategemea upatikanaji wanyenzo, vifaa na zana stahiki za kufundishia na kujifunziakulingana na mahitaji ya masomo na programu katika ngazimbalimbali za elimu na mafunzo. Nyenzo, vifaa, na zana hizoni pamoja na mihtasari, vitabu vya kiada na ziada, kemikali za

    maabara, mitambo na karakana. Kumekuwa na upungufu wanyenzo, vifaa na zana bora za kufundishia na kujifunzia katika

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    40/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    31

    ngazi zote za elimu na mafunzo ambapo, kwa mfano, uwianowa kitabu kwa wanafunzi katika elimu ya msingi ni takribanikitabu kimoja kwa wanafunzi watatu (3) na kati ya wanafunziwanne (4) hadi tisa (9) kwa shule za sekondari kulingana nasomo. Pia, baadhi ya vifaa, zana na nyenzo zilizopo, amazimepitwa na wakati au haziendani na mahitaji ya sayansi nateknolojia ya sasa. Hali hii imekuwa ikichangia kudhoo shautoaji wa wahitimu bora.

    Vilevile, mfumo huria wa uchapishaji wa vitabu na uandaajiwa zana na nyenzo nyingine za elimu na mafunzo umeathiriupatikanaji wa vitabu, zana na nyenzo bora na za kutosha katikashule na vyuo nchini. Pia, gharama za vitabu, zana na nyenzohusika imekuwa kubwa kuliko uhalisia wa gharama hizo.Katika hali ya aina hii, ni muhimu kuweka utaratibu mahususiwa upatikanaji wa vitabu, zana na nyenzo bora na za kutoshazinazokidhi mahitaji.

    Lengo

    Kuwa na mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.

    Tamko

    3.2.9. Serikali itahakikisha vifaa, nyenzo na zana stahiki zakufundishia na kujifunzia katika elimu na mafunzo

    zinatosheleza kulingana na mahitaji na maendeleo yasayansi, teknolojia na mbinu za kufundishia na kujifunziakatika ngazi zote.

    3.2.10. Serikali itahakikisha upatikanaji wa kitabu bora kimojacha kiada kwa kila somo kwa kila mwanafunzi katikaelimumsingi ambavyo vitaandaliwa kwa utaratibu

    maalumu.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    41/77

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    42/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    33

    kwa makundi yote katika ngazi zote za elimu namafunzo.

    Suala

    Mazingira salama na huduma muhimu shuleni na vyuoni.Maelezo

    Mazingira katika baadhi ya shule na vyuo nchini ni duni nahayana usalama wa kutosha. Takwimu kwa upande wa shuleza sekondari zinaonyesha kuwa ni shule 3,415 kati shule 4,528zenye huduma ya umeme. Zipo changamoto nyingi katikaupatikanaji wa huduma bora na muhimu kama chakula, majisa na salama, afya, umeme, mawasiliano na usa ri. Hudumahizi huchangia kuongeza ushiriki kwa walimu na wanafunzikatika mchakato wa elimu na mafunzo. Mazingira tulivu,salama na yenye kuvutia walimu na wanafunzi huongeza tijakatika ufundishaji na ujifunzaji. Kuna umuhimu wa kuwa na

    mazingira yanayokidhi mahitaji na huduma muhimu shulenina vyuoni ili kuinua ubora wa elimu na mafunzo.

    Lengo

    Kuwa na mazingira salama na huduma muhimu na endelevushuleni na vyuoni.

    Tamko

    3.2.13. Serikali itahakikisha kuwa huduma muhimu zikiwemoza chakula bora, mawasiliano, umeme, maji saf nasalama, na afya zinapatikana katika shule na vyuo.

    3.2.14. Serikali itahakikisha kuwepo kwa mazingira bora nayenye usalama katika utoaji wa elimu na mafunzo

    nchini.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    43/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    34

    Suala

    Ushauri na unasihi katika elimu na mafunzo.

    Maelezo

    Katika shule za msingi, sekondari na vyuo, huduma ya ushaurina unasihi haitolewi kama huduma ya msingi kwa wanafunzi.Huduma hii hutolewa na walimu wa malezi na nidhamu ambaopia siyo wataalamu wa ushauri na unasihi na huwajibikakufundisha masomo mbalimbali hali ambayo inasababishahuduma hiyo kutotolewa kwa ufanisi. Kukosekana kwa ufanisi

    katika utoaji wa huduma hii shuleni na vyuoni, kumechangiakuwepo kwa mmomonyoko wa maadili katika jamii.

    Huduma ya ushauri na unasihi inalenga kumwezeshamwanafunzi na jumuiya ya shule na chuo kwa ujumlakukabiliana na changamoto za maisha, ili kujenga mwelekeo,tabia na kuendeleza mila, desturi na maadili mema katika jamii.

    Pia, huduma hii inahitajika katika kumsaidia mwanafunzi kujuamustakabali wa masomo atakayoyachagua au aliyoyachaguana umuhimu wake katika maendeleo yake na ya Taifa.

    Vilevile, ushauri na unasihi unahitajika kwa wafanyakazikatika ngazi zote za elimu ili waweze kupata stadi za maishaza kujitambua na kufanya maamuzi sahihi katika kutekeleza

    wajibu wao kikamilifu kama walezi wa wanafunzi na jamii.Lengo

    Kuwa na huduma ya ushauri na unasihi inayokidhi mahitajikatika elimu na mafunzo.

    Tamko

    3.2.15. Serikali itaimarisha utoaji wa huduma ya ushauri naunasihi katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    44/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    35

    Suala

    Elimu yenye kudumisha amani.

    Maelezo

    Utandawazi, tofauti za kiuchumi na mwingiliano wa watu wenyetamaduni mbalimbali umechangia katika kuleta mabadiliko yamaadili na tabia na hivyo kuleta changamoto za amani katika jamii. Elimu katika taifa ni mhimili wa kudumisha amani katika jamii kwa kujenga stadi za kutatua migogoro, kujenga umojawa kijamii na mshikamano. Kuna umuhimu wa kuwa na elimu

    ya amani itakayolenga kuwasaidia wanafunzi kupata uwezowa kuzuia na kutatua migogoro kwa amani wakati inapotokeamiongoni mwa watu, kati ya watu au baina ya makundi, kitaifaau kimataifa. Mitaala ya elimu na mafunzo iandaliwe kwakuzingatia haki na kujenga Taifa lenye amani na utulivu.

    Lengo

    Kuwa na mhitimu mwenye stadi za kudumisha amani, kuhimilina kutatua migogoro katika jamii.

    Tamko

    3.2.16. Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha stadiza kudumisha amani, kuhimili na kutatua migogoro,uzalendo na maadili zinajumuishwa katika mitaala yaelimu na mafunzo kwa ngazi zote.

    Suala

    Matumizi ya Kiswahili, Kiingereza, lugha nyingine za kigeni nalugha ya alama katika mawasiliano.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    45/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    36

    Maelezo

    Lugha za Kiswahili, Kiingereza, lugha nyingine za kigenina lugha ya alama zinafundishwa kama masomo katika

    ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Pamoja na juhudi zakufundisha lugha hizo, bado kuna udhaifu wa kumudu lughasanifu katika mawasiliano. Sehemu kubwa ya udhaifu huoinatokana na miundombinu na mbinu duni za kufundishiana matumizi madogo ya lugha sanifu katika mazingira yakawaida.

    Lugha ya Kiswahili ni lugha ya Taifa na inatumika kama lughaya kwanza au ya pili miongoni mwa wananchi wengi. Lugha yaKiswahili imekua kwa kiwango cha kimataifa ambapo inawezakutumiwa na wananchi wengi kupata maarifa na ujuzi katikanyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Sayansi na Teknolojia.Lugha ya Kiingereza inatumika kama lugha ya pili na ya tatukwa baadhi ya wananchi. Kiswahili na Kiingereza ni lugha rasmi

    za kio si. Ufahamu mzuri wa Kiingereza na lugha nyingine zakigeni pia unamwezesha Mtanzania kuwa na mawasiliano nawatu wa mataifa mengine na kupata elimu, ujuzi na maarifa.Aidha, lugha ya alama hutumika kufanya mawasiliano baina yaviziwi na watu wengine. Wanafunzi hawa wanashindwa kupataelimu na mafunzo kwa ufanisi kutokana na kutokuwepo kwautaratibu mahsusi wa kufundisha na kutumia lugha ya alama.

    Lengo

    Kujenga uwezo wa kutumia lugha mbalimbali katikamawasiliano.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    46/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    37

    Tamko

    3.2.17. Serikali itahakikisha kuwa lugha ya Kiswahili, Kiingereza na nyingine za kigeni zinafundishwa kwa

    ufasaha na ufanisi katika ngazi zote za elimu namafunzo nchini ili kuleta ufahamu na umahiri kutokanana umuhimu wa lugha hizo katika masuala ya kitaifa,kikanda na kimataifa.

    3.2.18. Serikali itawezesha lugha ya alama na maandishi yanukta nundu kutumika katika ngazi zote za elimu na

    mafunzo.Suala

    Lugha ya kufundishia na kujifunzia

    Maelezo

    Kwa sasa, lugha za kufundishia na kujifunzia katika elimu na

    mafunzo ni Kiswahili na Kiingereza. Lugha ya kufundishia elimuya awali na msingi ni Kiswahili. Aidha, lugha ya Kiingerezainatumika kufundishia katika baadhi ya shule.

    Lugha ya Kiingereza hutumika kufundishia katika shule zasekondari, vyuo vya ualimu ngazi ya stashahada, vyuo vyaufundi na vyuo vya elimu ya juu. Aidha, lugha ya Kiswahilihutumika kufundishia katika vyuo vya mafunzo ya ualimungazi ya cheti na vyuo vya ufundi stadi. Matumizi ya lughaya Kiingereza yanazidi kupanuka ulimwenguni kutokana nautandawazi. Hali kadhalika, matumizi ya Kiswahili nchini nakatika mabara mengine yameongezeka. Pia, Tanzania imeridhiaItifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusiana na maendeleona matumizi ya Kiswahili, na Tanzania kuchaguliwa kuwa makao

    makuu ya Taasisi ya Kuendeleza Kiswahili katika Jumuiya.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    47/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    38

    Kwa hiyo, kuna umuhimu wa kuimarisha matumizi ya lughaza Kiswahili na Kiingereza kwa kuzifanya kuwa lugha zakufundishia katika ngazi mbalimbali.

    LengoKutumia lugha ya kiswahili katika ufundishaji

    Tamko

    3.2.19. Lugha ya Taifa ya Kiswahili itatumika kufundishia nakujifunzia katika ngazi zote za elimu na mafunzo naSerikali itaweka utaratibu wa kuwezesha matumiziya lugha hii kuwa endelevu na yenye ufanisi katikakuwapatia walengwa elimu na mafunzo yenye tijakitaifa na kimataifa.

    3.2.20. Serikali itaendelea na utaratibu wa kuimarishamatumizi ya lugha ya Kiingereza katika kufundishia nakujifunzia, katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

    Suala

    Upimaji, tathmini na maendeleo ya wanafunzi katika elimu namafunzo.

    Maelezo

    Upimaji na tathmini katika ngazi za elimu ya msingi, sekondari,vyuo vya ualimu, vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi, elimu yaufundi na vyuo vya elimu ya juu hufanywa na shule, taasisiau vyuo na wakati mwingine kuratibiwa na taasisi zilizopewadhamana hiyo. Muundo na taratibu za upimaji katika ngazihizi umekuwa na changamoto nyingi. Changamoto mojawapokatika eneo hili ni aina ya upimaji usiozingatia malengo ya

    mitaala ya kujenga ujuzi, na mfumo usiohusisha kikamilifuwakuza mitaala, watekelezaji, wapimaji na wasimamizi. Pia,

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    48/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    39

    kutozingatiwa muundo thabiti wa upimaji kwa kujumuishaalama za maendeleo ya mwanafunzi akiwa shuleni na alamaza mtihani wa mwisho unaotungwa na Baraza la Mitihaniinachangia kuto kiwa kwa malengo ya mtaala husika. Aidha,mfumo wa utoaji wa alama za A, B, C, D, E, S na F zinazotolewana Baraza la Mitihani hutofautiana mwaka hadi mwaka, nakatika masomo tofauti na kutofautiana katika tafsiri baina yashule na Baraza la Mitihani. Hali hii inasababisha baadhi yawanafunzi kushindwa kuendelea na elimu na mafunzo katikangazi za juu bila sababu za msingi. Kuna umuhimu wa kuwepo

    kwa muundo madhubuti ili kuleta ufanisi katika mfumo waupimaji na tathmini ya maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma.

    Kwa upande wa upimaji na tathmini katika elimu ya ufundina mafunzo, njia mbalimbali zinatumika ambazo hutofautianakulingana na fani na aina ya kozi. Upimaji huo hufanywa navyuo chini ya uratibu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

    na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi. Upimajina tathmini katika vyuo vya elimu ya juu hufanywa na vyuovyenyewe pamoja na taasisi zinazoratibu uendeshaji wa vyuohivyo. Aidha, vyuo vikuu vina mamlaka ya upimaji, tathmini nautoaji tuzo baada ya programu zao kupewa ithibati na Tume yaVyuo Vikuu Tanzania ambayo imetoa mwongozo wa upimajina alama kwa masomo mbalimbali.

    Kutokana na umuhimu wa upimaji na tathmini katika elimuna mafunzo, hakuna budi kuwa na utaratibu wa kitaifa wakudhibiti upimaji na tathmini katika ngazi na programumbalimbali za elimu na mafunzo.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    49/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    40

    Lengo

    Kuimarisha upimaji na tathmini ya maendeleo ya mwanafunzikitaaluma.

    Tamko

    3.2.21. Serikali itaweka mfumo wa upimaji na tathminikatika elimu na mafunzo utakaozingatia vigezovinavyotambulika vya upimaji wa kila siku wamaendeleo ya mwanafunzi na mitihani ya mwishoya kukamilisha ngazi husika ya elimu na mafunzo

    kulingana na mitaala iliyopo katika ngazi zote za elimuna mafunzo.

    3.2.22. Serikali itaweka na kusimamia mfumo wa kitaifawa sifa linganifu wa tuzo kwa ngazi zote za elimu namafunzo ili kurahisisha wahitimu kuweza kujiendelezakielimu na mafunzo.

    3.3. Upatikanaji wa Fursa Mbalimbali za Elimu na MafunzoNchini

    Suala

    Fursa kwa usawa katika elimu na mafunzo

    Maelezo

    Fursa za elimu na mafunzo zinapatikana kwa kila Mtanzaniabila ubaguzi wa jinsi, rangi, kabila, dini, ulemavu na hali yakijamii au kipato. Ingawa fursa hizo katika elimu ya msingizimeongezeka hadi ku kia asilimia 92 ya wanafunzi wa rikalengwa mwaka 2012, bado uandikishaji wa wanafunzi wa rikalengwa katika elimu ya sekondari ya kawaida ni asilimia 36.6

    tu na asilimia 2.7 ya wanafunzi wa rika lengwa kwa sekondariya juu. Takwimu za mwaka 2012 zinaonyesha uwiano sawa

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    50/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    41

    wa uandikishaji wa wasichana kwa wavulana katika elimu yamsingi, wakati katika elimu ya sekondari ya kawaida uwianoni 0.9 kwa maana ya kwamba uandikishaji wa wasichana nimdogo ukilinganishwa na wa wavulana. Uandikishaji wawasichana unazidi kupungua ukilinganishwa na wa wavulanakatika elimu ya sekondari ya juu ambapo uwiano wa wasichanakwa wavulana ni 0.5. Hali hii inaashiria kupungua kwa ushirikiwa wasichana katika ngazi za juu za elimu. Pamoja na hayo,kumekuwa na mdondoko wa wanafunzi katika ngazi za elimuya msingi na sekondari. Wanafunzi wengi wanaacha shule

    kutokana na sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu hizo niumbali wa kutembea kwenda shuleni na kurudi, ujauzito, ndoaza utotoni, ajira za watoto, utoro, umaskini, kukosekana kwamahitaji maalumu shuleni kwa baadhi ya wanafunzi, na baadhiya mila na desturi zinazokinzana na utoaji wa elimu kwa watotowa kike. Takwimu za mwaka 2012 zinaonyesha kwamba katikashule za msingi, jumla ya wanafunzi 69,015 (wavulana 37,578 nawasichana 31,437) kati ya 8,247,172 sawa na asilimia 0.8 waliachashule kwa sababu mbalimbali wakati kwa shule za sekondariwanafunzi walioacha shule ni 76,050 (wavulana 42,559 nawasichana 33,491) kati ya wanafunzi 1,884,272 sawa na asilimianne (4). Pamoja na juhudi za Serikali, sekta binafsi na wadauwengine wa maendeleo kutoa fursa za elimu kwa makundi yote,

    baadhi ya makundi bado hayaja kiwa kikamilifu kutokana nasababu za kijamii, kiuchumi na kijiogra a. Ili ku kia malengoya elimu na mafunzo kwa wote kuna umuhimu wa kuondoavikwazo vinavyosababisha wanafunzi kushindwa kukamilishamzunguko wa elimu katika ngazi husika, ikiwemo changamotozinazotokana na mahitaji maalumu kwa baadhi ya wanafunzi.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    51/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    42

    Lengo

    Kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanakamilisha mzungukowa elimu na mafunzo katika ngazi husika.

    Tamko

    3.3.1. Serikali itaendelea kuongeza fursa anuwai za elimu namafunzo kwa usawa kwa makundi yote ya kijamii katikangazi zote ikiwemo watoto wenye mahitaji maalumu.

    3.3.2. Serikali itaondoa vikwazo vinavyozuia fursa yawanafunzi kuendelea na masomo na kukamilisha mzungukowa elimu katika ngazi husika.

    Suala

    Usawa wa jinsi katika elimu na mafunzo

    Maelezo

    Uwiano wa uandikishaji wa wanafunzi katika elimu ya msingikwa wavulana na wasichana ni takribani 1:1; elimu ya sekondarini 1:0.9 wakati elimu ya juu ni 1:2. Takwimu hizi zinaonyeshakuwa mwendelezo wa mwanafunzi kutoka ngazi moja kwendangazi inayofuata kwa wasichana umekuwa ukipungua. Ingawakiwango cha mdondoko kinaathiri wavulana na wasichana,tathmini inaonyesha kuwa wasichana wana uwezekano

    mkubwa zaidi wa kukatisha masomo hususan wanapo kiakatika madarasa ya juu kuanzia darasa la tano. Halikadhalika,ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi mbalimbali zausimamizi na uongozi ni mdogo kutokana na dhana kwambawanawake hawana uwezo sawa na wanaume. Kuna umuhimuwa kuweka usawa wa ushiriki katika fursa za elimu na mafunzopamoja na nafasi za usimamizi na uendeshaji katika sekta yaelimu na mafunzo.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    52/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    43

    Lengo

    Kuwa na usawa wa kijinsi katika elimu na mafunzo

    Tamko

    3.3.3. Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha kuwausawa wa kijinsi katika elimu na mafunzo unazingatiwa.

    Suala

    Elimu na mafunzo kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo huriana masafa.Maelezo

    Serikali imeweka utaratibu wa elimu au mafunzo kwa ajili yawatoto, vijana na watu wazima waliokosa fursa katika mfumowa kawaida, ili kujiendeleza kielimu na kumudu changamotoza maisha au kuhitimu katika ngazi mbalimbali za elimu namafunzo. Utaratibu huo ni pamoja na kuwepo kwa Mpangowa Uwiano Kati ya Elimu na Jamii (MUKEJA) na Mpango waElimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa (MEMKWA). Fursa zaaina hii zinaweza kutolewa kwa ufanisi kwa kuweka miundostahiki katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo nchini.

    Elimu inaweza kutolewa vizuri zaidi endapo Teknolojia yaHabari na Mawasiliano (TEHAMA) na rasilimaliwatu wenyeujuzi stahiki vitatumika. Hii pia ni katika kutambua mafanikioya kujielimisha kwa njia mbalimbali zikiwemo elimu kwa njiaya posta, elimu kwa njia ya redio, televisheni, maktaba za taifana kisomo cha watu wazima. Kuna upungufu wa rasilimaliwatuwa kutoa elimu kwa njia ya masafa na pia vifaa vya TEHAMA

    ni vichache na havikidhi mahitaji ya utandawazi na ushindanipamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia, na hivyo, wakati

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    53/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    44

    mwingine kusababisha changamoto za ufanisi na viwango dunivya ubora wa elimu itolewayo.

    Lengo

    Kuimarisha elimu na mafunzo kwa kutumia njia mbalimbaliikiwemo ujifunzaji huria na masafa.

    Tamko

    3.3.4. Serikali itaweka utaratibu na mazingira wezeshikuhakikisha elimu na mafunzo ikiwa ni pamoja na elimuya watu wazima inatolewa kwa ufanisi katika ngazizote kwa njia mbalimbali ikiwemo ujifunzaji huria namasafa.

    3.3.5. Serikali itaweka utaratibu na kusisitiza matumizi yaTEHAMA katika utoaji wa elimu na mafunzo katikangazi zote.

    SualaKutambua na kuendeleza vipaji na vipawa

    Maelezo

    Mitaala ya sasa haitoi fursa ya kubaini na kukuza vipajina vipawa kwa kuzingatia mahitaji na kasi ya wanafunzikujifunza katika ngazi zote za elimu na mafunzo. Utaratibuuliopo unazingatia wale tu wenye ufaulu wa juu wa mitihanikuwa ndiyo pekee wenye vipaji. Hali hii, haitoi fursa yakubaini, kukuza na kuendeleza vipaji vya aina mbalimbali kwawanafunzi katika ngazi mbambali za elimu na mafunzo kamavile, muziki, ngoma, ufundi, uchoraji na michezo. Kutokana naudhaifu huu wa mitaala iliyopo, kuna haja ya kupitia mitaala hii

    ili izingatie wanafunzi wenye vipaji, kasi ya kujifunza, vipawana kuwaendeleza.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    54/77

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    55/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    46

    Lengo

    Kutambua na kurasimisha maarifa, ujuzi na stadi alizopatamtu nje ya mfumo wa shule ili aweze kujielimisha kwa njia

    mbalimbali.Tamko

    3.3.7. Serikali itaweka utaratibu na kuimarisha utambuzi wamaarifa, ujuzi na stadi zilizopatikana nje ya mfumo washule ili kupanua fursa za kujiendeleza kielimu.

    3.4. Mahitaji ya Rasilimaliwatu Kulingana na Vipaumbelevya Taifa

    Suala

    Upatikanaji wa walimu na rasilimaliwatu wengine mahiri kwaajili ya sekta ya elimu.

    Maelezo

    Uhitaji wa walimu katika ngazi mbalimbali za elimu namafunzo katika sekta ya elimu, umekuwa ukiongezekamwaka hadi mwaka. Hali hii imechangiwa na upanuzi wasekta ya elimu pamoja na kukosekana kwa vivutio ambavyovingewahamasisha wanataaluma mbalimbali kuingia katika faniya ualimu na kuwabakisha humo. Aidha, kufuatia kupanuka

    kwa sekta nyingine nchini, baadhi ya walimu wamekuwawakiacha kazi ya ualimu na kujiunga na sekta ambazo zinavutiazaidi kimaslahi na mazingira. Kutokana na hali hii kumekuwana uhitaji mkubwa wa walimu katika fani mbambali hasa zaufundishaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK),hisabati, sayansi na lugha. Kwa mfano, hadi ku kia Desemba2013, mahitaji ya walimu katika maeneo mbalimbali ya sayansina hisabati yalikuwa kama inavyooneshwa kwenye jedwali.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    56/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    47

    Somo Wanao-hitajika WaliopoUpungufu

    Idadi AsilimiaAgriculture 905 300 605 66.9Physics 10,203 3,748 6,455 63.3

    Computer Studies 1,108 433 675 60.9Electrical Engineering 69 29 40 58.0Basic Mathematics 13,478 5,896 7,582 56.3Chemistry 10,541 4,887 5,654 53.6Biology 11,144 5,561 5,583 50.1Engineering Science 47 24 23 48.9MechanicalEngineering 80 41 39 48.8

    Food and Nutrition 220 120 100 45.5Civil Engineering 100 60 40 40.0AdditionalMathematics 512 310 202 39.5

    Total 48,407 21,409 26,998 55.8Chanzo: Basic Education Statistics in Tanzania – BEST, 2013Katika elimu ya juu, takwimu za mwaka 2012/13 zinaonesha

    kuwa vyuo vya elimu ya juu vinahitaji jumla ya wanataaluma7,556 ambao wamebobea katika fani mbalimbali. Hivi sasa,vyuo hivi vina jumla ya wanataaluma 5,441 na hivyo kuwa naupungufu wa wanataaluma 2,115. Upungufu wa wahadhiri/wanataaluma unachangia katika kuathiri ubora wa elimu ya juu nchini. Kwa hali hii, kuna haja ya kuweka mazingira borayatakayohakikisha kwamba vijana wengi wenye umahiri wa juu wanajiunga na kubaki katika taaluma ya ualimu ili kukidhimahitaji ya nchi katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo.

    Lengo

    Kuwa na rasilimaliwatu mahiri na ya kutosha ili kukidhimahitaji ya sekta ya elimu na mafunzo.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    57/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    48

    Tamko

    3.4.1. Serikali itainua ubora wa mfumo wa ajira katika sekta yaelimu na mafunzo ili uwe mahsusi na kukidhi mahitaji,

    upatikanaji na usimamizi wa rasilimaliwatu kwa ajiliya maendeleo ya sekta ya elimu na mafunzo.

    Suala

    Upatikanaji wa rasilimaliwatu mahiri na ya kutosha katikasekta nyingine.

    Maelezo

    Taifa limejiwekea vipaumbele ambavyo vitaiwezesha Tanzaniaku kia kiwango cha nchi ya uchumi wa kati i kapo mwaka2025. Vipaumbele hivyo ni pamoja na miundombinu, kilimo,viwanda, rasilimaliwatu na huduma za jamii, utalii, biasharana huduma za kifedha. Kutokana na vipaumbele hivyo, sektaya elimu na mafunzo inatakiwa kuandaa rasilimaliwatu yakutosha kukidhi mahitaji ya sekta za vipaumbele na mahitajimengine kitaifa, kikanda na kimataifa. Kuna nakisi kubwa yawataalamu walioelimika kwa kiwango cha juu wanaohitajika iliTanzania ku kia kiwango cha nchi yenye uchumi wa kati. Ripotimbalimbali zinaonyesha kwamba rasilimaliwatu ya Tanzania,kwa kiasi kikubwa ni wafanyakazi wenye ujuzi wa chini ambao

    ni asilimia 84, wakifuatiwa na wenye ujuzi wa kati asilimia 13 nawenye ujuzi wa juu asilimia 3. Hata hivyo, kwa nchi za kipatocha kati ngazi ya chini, ulinganifu unaonyesha kuwa nchi hizozina wastani wa asilimia 55 ya wafanyakazi wenye ujuzi wa chini,asilimia 33 ujuzi wa kati na asilimia 12 ujuzi wa juu. Hivyo, Tanzaniaina changamoto ya kuinua mchanganyiko wa wafanyakazi wenyeujuzi katika fani mbalimbali ili ku kia mahitaji ya rasilimaliwatukwa nchi ya kipato cha kati ku kia mwaka 2025.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    58/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    49

    Mfumo wa elimu na mafunzo wa sasa hauliwezeshi Taifakukidhi ongezeko la mahitaji ya rasilimaliwatu kulingana navipaumbele vya Taifa kwa sababu takwimu za mwaka 2000hadi 2012 zinaonyesha kuwa ni wastani wa asilimia 5 tu yawahitimu wa darasa la saba ndiyo wanaofaulu na kuendeleahadi ku kia elimu ya sekondari ya juu; asilimia 4.3 hujiungana mafunzo ya ufundi stadi, asilimia 1.2 hujiunga na elimuya ufundi ; na wastani wa asilimia 4 ndiyo wanaofaulu nakuendelea hadi ku kia elimu ya juu. Kwa mwenendo huo, nidhahiri kwamba Taifa litaendelea kuwa na nakisi ya wataalamu,

    kama hatua madhubuti za kuongeza fursa na kuinua ubora waelimu hazitachukuliwa.

    Lengo

    Kuwa na rasilimaliwatu mahiri na ya kutosha ili kukidhimahitaji ya sekta mbalimbali kwa maendeleo ya Taifa.

    Tamko

    3.4.2. Serikali itaweka utaratibu nyumbufu wa maendeleo yawanafunzi kielimu na mafunzo na kufanya tathminiya mara kwa mara ili kujua mahitaji kamili yarasilimaliwatu na ujuzi unaohitajika ili elimu namafunzo yanayotolewa yaweze kukidhi mahitaji.

    3.4.3. Serikali itaweka mazingira bora na kuhakikisha kuwasekta ya elimu na mafunzo inatoa rasilimaliwatuya kutosha na mahiri ili kukidhi mahitaji ya sektambalimbali kwa maendeleo ya Taifa.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    59/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    50

    3.5. Usimamizi na Uendeshaji Madhubuti wa Elimu naMafunzo Nchini

    Suala

    Uongozi, usimamizi na uendeshaji katika sekta ya elimu namafunzo

    Maelezo

    Kumekuwa na changamoto katika uzingatiaji wa majukumuna uwajibikaji katika sekta ya elimu kutokana na mfumo wauongozi, usimamizi na uendeshaji kuanzia ngazi ya wizarazinazohusika na elimu na mafunzo, hadi ngazi ya shule, vyuona asasi mbalimbali ambazo umeathiri ufanisi wa sekta yaelimu. Sekta ya elimu na mafunzo imekuwa ikiongozwa naSera ya Elimu na Mafunzo (1995), Sera ya Elimu ya Ufundi naMafunzo (1996) na Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) kutokanana muundo wa wizara zilizokuwepo wakati huo pamoja na

    asasi zake. Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996) na Seraya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) zilikuwa zikisimamiwa nailiyokuwa Wizara Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu na Seraya Elimu na Mafunzo (1995) ilikuwa ikisimamiwa na iliyokuwaWizara ya Elimu na Utamaduni. Mafunzo ya ufundi stadiyalikuwa yakisimamiwa na iliyokuwa Wizara ya kazi. Kufuatiamabadiliko mbalimbali, na kuanzishwa kwa Wizara ya Elimuna Mafunzo ya Ufundi mwaka 2006, kumekuwa na haja yakuwa na sera inayosimamia elimu kulingana na majukumumapya ya Wizara. Ugatuaji wa majukumu katika sekta ya elimuna mafunzo kutoka ngazi ya Serikali Kuu kwenda Mamlaka zaSerikali za Mitaa katika maeneo ya usimamizi na uendeshaji washule za msingi na sekondari umesababisha mwingiliano wa

    majukumu na kutowajibika.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    60/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    51

    Pamoja na mabadiliko hayo, sheria, kanuni na miongozo yauongozi, usimamizi na uendeshaji hazikufanyiwa marekebishoili kukidhi mahitaji. Kwa mfano, Wizara ya Elimu na Mafunzoya Ufundi, OWM-TAMISEMI na Tume ya Utumishi waUmma Idara ya Utumishi wa Walimu kwa pamoja zimekuwazikishughulikia masuala ya ajira ya walimu bila kuwa namipaka iliyowazi na hivyo kuathiri ufanisi na uwajibikaji.Aidha, mipaka ya madaraka katika uongozi na usimamizikati ya OWM-TAMISEMI na Wizara ya Elimu na Mafunzo yaUfundi haiko bayana.

    Kutokana na mwingiliano huo, kuna umuhimu wa kuhuishasheria, kanuni, miongozo na majukumu ya WyEMU na OWM-TAMISEMI ili masuala ya kisera yafanywe na Wizara ya Elimuna Mafunzo ya Ufundi na ya kiutendaji yafanywe na OWM-TAMISEMI na hivyo kuleta ufanisi na uwajibikaji.

    Lengo

    Kuwa na uongozi, usimamizi na uendeshaji wenye tija nauwajibikaji katika sekta ya elimu na mafunzo.

    Tamko

    3.5.1. Serikali itahuisha mfumo na muundo wa uongozi,usimamizi na uendeshaji katika sekta ya elimu ili uwe

    na tija na uwajibikaji.3.5.2. Serikali itaweka utaratibu wa kuteua na kutambua

    nafasi za usimamizi wa utekelezaji wa sera ya elimu namafunzo katika ngazi ya mkoa, wilaya, kata, vyuo nashule ili ziwe na hadhi maalumu katika utumishi.

    3.5.3. Serikali itahakikisha maadili na haiba ya walimu nawatumishi wengine yanazingatiwa katika ngazi zote zaelimu na mafunzo.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    61/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    52

    Suala

    Ushirikiano wa elimu na mafunzo kati ya Tanzania Bara naZanzibar.

    Maelezo

    Elimu ya Juu ni suala la muungano, wakati ngazi nyingine zaelimu siyo za muungano. Hata hivyo, sekta za Elimu TanzaniaBara na Zanzibar zina uhusiano na ushirikiano katika maeneoya mitaala na upimaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundistadi. Hali kadhalika, katika ngazi ya elimu ya sekondari na vyuo

    vya ualimu kuna uhusiano katika maeneo ya mitaala, upimajina utoaji vyeti. Kwa kuzingatia suala hilo, kuna umuhimuwa kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kielimu baina yaTanzania Bara na Zanzibar.

    Lengo

    Kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kielimu kati yaTanzania Bara na Zanzibar.

    Tamko

    3.5.4. Serikali itaimarisha ushirikiano katika elimu na mafunzokati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

    Suala

    Ushirikiano katika elimu na mafunzo kikanda na kimataifa.Maelezo

    Umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika elimu namafunzo unazidi kuongezeka kutokana na maendeleo yauchumi unaotegemea maarifa na ujuzi. Kwa hiyo, ushirikianoni suala linalohitajika kwa kuwa maarifa na stadi hazinamipaka wala ukomo. Tanzania imeridhia mikataba, itifaki

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    62/77

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    63/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    54

    kipaumbele cha kutosha katika kutenga ardhi kwa ajili ya shule,vyuo na taasisi za elimu katika ngazi zote.

    Lengo

    Kutenga ardhi kwa ajili ya matumizi ya elimu na mafunzo.Tamko3.5.6. Serikali itahakikisha kuwa mahitaji ya ardhi kwa ajili

    ya elimu na mafunzo yanazingatiwa kwenye mipango yamaendeleo ya ardhi nchini.

    Suala

    Mfumo wa takwimu na taarifa za elimu na mafunzo.MaelezoSekta ya elimu na mafunzo ina mfumo wa kupata na kutoatakwimu za elimu na mafunzo katika asasi zake. Mfumo huounahitaji kuwa madhubuti ili utaratibu wa ukusanyaji nautunzaji wa takwimu na taarifa uwe sahihi na wa kuaminika

    na takwimu kupatikana kwa wakati. Kuna kumbukumbumuhimu ambazo zimewekwa katika mpangilio tofauti tofautina kufanya upatikanaji na matumizi yake kuwa magumu.Hatua zote za mipango ya elimu, zinahitaji taarifa zenyeubora. Kwa hiyo, mifumo ya taarifa inatakiwa iwe rahisikutumika kwa kuhakikisha ukusanyaji, uchambuzi, uhifadhina usambazaji wa takwimu na taarifa unakuwa fanisi. Kuwepokwa mfumo madhubuti wa menejimenti ya data kunachangiakwa kiasi kikubwa kuleta ufanisi katika uendeshaji wa elimuna mafunzo.LengoKuwa na mfumo wa hazina data unganifu katika elimu namafunzo.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    64/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    55

    Tamko

    3.5.7. Serikali itaimarisha mfumo wa menejimenti ya hazinadata unganifu za elimu na mafunzo kwa ngazi zote.

    3.6. Mfumo Endelevu wa Ugharimiaji wa Elimu na MafunzoNchini.

    Suala

    Ugharimiaji wa elimu na mafunzo.

    Maelezo

    Serikali inagharimia elimu na mafunzo kwa kushirikiana nawadau wa maendeleo ya elimu wa ndani na nje. Kutokana naongezeko la mahitaji ya elimu na mafunzo, jamii pia imekuwaikichangia katika ugharimiaji wa elimu na mafunzo kwa njiambalimbali ikiwemo ujenzi na uendeshaji wa shule na vyuo

    unaofanywa kupitia sekta ya umma na binafsi. Ada pamoja namichango mingine ambayo inatolewa na wazazi na wanafunzikatika shule na vyuo vya umma na binafsi pia zimekuwa nisehemu ya michango ya kuendesha shule na vyuo hivyo.Serikali hutenga kati ya asilimia 17 mpaka 23 ya bajeti ya Taifakwa ajili ya elimu na mafunzo ikiwemo mikopo na ruzuku kwaajili ya wanafunzi. Pia, fedha zinazotengwa katika bajeti yaelimu hazitoshelezi mahitaji halisi ya kuinua ubora wa elimuna mafunzo kutokana na changamoto za mfumo na muundowa rasilimali fedha kwa ajili ya elimu. Changamoto hizo nipamoja na fedha kutopatikana kwa wakati zinapohitajikaau kutolewa pungufu kuliko kiasi kilichoidhinishwa, hivyokushindwa kutekeleza majukumu yaliyopangwa katika

    kipindi cha mwaka wa fedha husika. Aidha, utaratibu wa

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    65/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    56

    upelekaji wa fedha kwenye shule ama taasisi za elimu unahitajikuwa bora zaidi ili kuhakikisha kuwa fedha zinazopelekwazina ka na kutumika kwa kazi iliyokusudiwa kuliko ilivyosasa ambapo kuna nyakati fedha zinazopatikana hutumikakatika malengo tofauti. Hali hii imechangia sekta ya elimukushindwa kutekeleza kikamilifu majukumu yake na hivyokuathiri u kiwaji wa malengo yaliyowekwa. Hali kadhalika,kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusukiwango cha ada na michango inayotolewa katika shule navyuo. Ada na michango hiyo katika baadhi ya shule ni kubwa

    kuliko matarajio na uwezo wa wananchi walio wengi na hivyokuwa sehemu ya kero katika mfumo wa elimu na mafunzo.Katika hali hii, kuna umuhimu wa kuweka utaratibu na kubunivyanzo mbalimbali vya fedha ili kuwa na mfumo endelevu waugharimiaji wa elimu na mafunzo. Aidha, uandaliwe utaratibumadhubuti wa kuhakikisha fedha zina ka shuleni na vyuonina zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

    Lengo

    Kuwa na mfumo endelevu wa ugharimiaji wa elimu namafunzo.

    Tamko

    3.6.1. Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kuimarishamfumo wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo, ikiwemomikopo na ruzuku, ili uwe endelevu na wenye vyanzoanuai.

    3.6.2. Serikali itaweka utaratibu wa ada na michangombalimbali katika shule na vyuo binafsi ili kusimamiakwa ufanisi masuala ya ada na michango katika shulena vyuo.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    66/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    57

    3.7. Mfumo wa Elimu na Mafunzo Unaozingatia MasualaMtambuka.

    Suala

    Elimu ya mazingira.MaelezoKuongezeka kwa idadi ya watu na shughuli mbalimbaliza huduma za kijamii na za uchumi zisizozingatia taratibuzinazofaa kumesababisha uharibifu wa mazingira nchini. Hiini pamoja na ukataji ovyo wa miti, uchafuzi wa hewa, uharibifu

    wa vyanzo vya maji, utupaji ovyo wa taka maji, ngumu na zasumu; na matumizi mabaya ya ardhi yaliyokithiri katika maeneomengi. Elimu ya mazingira itiliwe mkazo zaidi katika mitaalaya elimu na mafunzo katika ngazi zote ili kupata Watanzaniawenye stadi za kutunza mazingira. Elimu itolewayo shuleni navyuoni haina budi kumjengea mwanafunzi na jamii tabia nautamaduni wa utunzaji wa mazingira.

    LengoKuwa na wahitimu katika ngazi zote za elimu na mafunzowenye maarifa, stadi na utamaduni wa kutunza mazingira.Tamko3.7.1. Serikali itaweka utaratibu utakaohakikisha kuwa

    maudhui ya kutunza mazingira yanazingatiwa katikamitaala ya elimu na mafunzo katika ngazi zote.

    SualaMaambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI (VVU naUKIMWI).Maelezo

    Sekta ya elimu na mafunzo ni mojawapo ya sekta zilizoathirikana virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Maambukizi ya VVU na

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    67/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    58

    UKIMWI yamechangia kushuka kwa ubora wa elimu kutokanana maambukizi kuathiri walimu na wanafunzi. Kuongezekakwa mahudhurio duni na vifo vya walimu na wanafunzi ni tishiokubwa kwa maendeleo ya elimu. VVU na UKIMWI vinaathirikundi kubwa la rasilimaliwatu wakiwemo wanafunzi, walimuna wafanyakazi wenye umri unaotegemewa kutoa mchangomkubwa zaidi katika maendeleo ya Taifa. Mojawapo yamadhara ni upotevu wa walimu wenye uzoefu na wanafunzikushindwa kukamilisha mzunguko wa elimu na mafunzo.Hata hivyo, upatikanaji wa elimu ya kutosha ya kujikinga

    na kuzuia maambukizi ya VVU na UKIMWI ni changamotokubwa kwa wanafunzi na jamii inayozunguka shule na vyuo.Aidha, kutokana na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzikatika ngazi za elimu na mafunzo kumekuwa na upungufuwa washauri nasaha wenye ujuzi katika masuala ya VVU naUKIMWI na stadi za maisha.

    Ni jukumu la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushirikianana taasisi zake pamoja na taasisi nyingine zinazohusika na VVUna UKIMWI kuhakikisha upatikanaji wa taarifa za VVU naUKIMWI katika shule na vyuo. Taarifa hizi ni pamoja na madazisizotahiniwa zinazohusu VVU na UKIMWI katika shule navyuo. Elimu itolewayo shuleni na vyuoni haina budi kuzingatiaumuhimu wa kumwelimisha mwanafunzi katika umri mdogoili kumjengea tabia na mwenendo stahiki kuhusu kujikinga namaambukizi ya VVU na UKIMWI, pamoja na kutoa huduma nafaraja kwa walioathirika.

    Lengo

    Kutoa elimu kwa wanafunzi, walimu na jamii ili kupunguzakasi ya kuenea kwa maambukizi ya VVU na UKIMWI.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    68/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    59

    Tamko3.7.2. Serikali itajumuisha stadi za kujikinga na VVU na

    UKIMWI katika mitaala ya elimu na mafunzo katika

    ngazi zote.SualaUbia kati ya sekta ya umma na binafsi katika elimu namafunzo.MaelezoSekta ya elimu na mafunzo ni mojawapo ya maeneo muhimu ya

    uwekezaji kwa njia ya ubia baina ya sekta ya umma na binafsi.Sekta ya elimu ina mahitaji makubwa yakiwemo ya maabara zasayansi, karakana, madarasa, mabweni na nyumba za walimupamoja na miundombinu mingine muhimu ya ustawi wawanafunzi na walimu katika shule na vyuo.Kwa kutambua u nyu wa rasilimali za umma na mchango wasekta binafsi, kuna umuhimu wa kuweka mazingira wezeshikatika sekta ya elimu ili kutumia rasilimali na fursa za sektabinafsi kwa ajili ya kufanikisha uwekezaji kwa njia ya ubia.LengoKuongeza uwezo wa sekta ya elimu na mafunzo katika kupanuana kuimarisha miundombinu na huduma mbalimbali katikangazi zote za elimu na mafunzoTamko3.7.3. Serikali itaimarisha ubia baina ya sekta ya umma na binafsi

    katika upatikanaji wa miundombinu ya kisasa na hudumambalimbali katika ngazi zote za elimu na mafunzo.

    3.7.4. Serikali itapanua wigo na kuimarisha ushiriki fanisi wawadau mbalimbali katika sekta ya elimu na mafunzo

    katika ngazi zote.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    69/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    60

    SURA YA NNE4.0. MUUNDO WA KISHERIA

    4.1 Utangulizi

    Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo utazingatia muundowa kisheria utakaowawezesha wahusika kutekeleza majukumuyao. Kwa mujibu wa Sera hii, majukumu ya kila sehemu yasekta hayana budi yawekwe wazi ili kuondoa mkanganyikona migongano ambayo imekuwa ikijitokeza katika usimamiajina utekelezaji wa masuala mbalimbali ya elimu. Aidha, taasisi

    zilizo chini ya Wizara pamoja na zitakazoundwa zitatekelezamasuala ya elimu na kuwajibika kwa Wizara yenye dhamanaya elimu na mafunzo. Hali kadhalika, sekta za umma na binafsizinazoshughulikia utoaji wa elimu na mafunzo zitatakiwakufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayotolewakatika kuwezesha utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo.

    4.2 Sheria za kusimamia elimu na mafunzoUtekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo utafuata sheriambalimbali. Sheria zilizopo zitarekebishwa ili ziendanena mahitaji ya matamko ya Sera hii. Baadhi ya sheriazitakazorekebishwa ni pamoja na Sheria za Serikali za Mitaa(Sura ya 287 na Sura ya 288 ya Sheria za Tanzania) ili ziweze

    kukidhi mahitaji ya ugatuaji wa elimu ya awali, elimu ya msingina elimu ya sekondari. Mabadiliko ya sheria hizi yatalenga katikakuhakikisha kwamba kunakuwa na usimamizi na uendeshajithabiti wa elimumsingi na sekondari katika ngazi mbalimbaliza OWM-TAMISEMI. Aidha, sheria nyingine ambazo hazikidhimahitaji ya utekelezaji wa sera hii zitafutwa au kurekebishwa.Baadhi ya sheria hizo ni Sheria ya Elimu Sura ya 353, Sheria yaBaraza la Mitihani la Tanzania Sura ya 107, Sheria ya Taasisi

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    70/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    61

    ya Elimu Tanzania Sura ya142, Sheria ya Bodi ya Mikopo yaWanafunzi wa Elimu ya Juu Sura ya 178, Sheria ya Vyuo VikuuSura ya 346, Sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Suraya 129, Sheria ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya UfundiStadi Sura ya 82 , Sheria ya Bodi ya Huduma za MaktabaTanzania Sura ya 102, Sheria ya Mfuko wa Elimu Sura ya 412,na Sheria ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Sura ya 139.Vilevile, sheria nyingine mpya zinaweza kutungwa kufuatanana mahitaji ili kukidhi maelekezo na matamko mapya ya seraambayo hayawezi kutekelezwa kwa sheria zilizopo. Baadhi

    ya sheria zitakazotungwa ni pamoja na sheria ya elimumsingina sekondari. Sheria hii itaelekeza masuala mbalimbali yaelimumsingi na sekondari ikiwemo mitaala na upimaji wakitaifa katika ngazi hizi.

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    71/77

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    72/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    63

    Kwa upande wa OWM-TAMISEMI itakuwa na jukumu lakuandaa mipango, bajeti, usimamizi na uendeshaji wa shule zaelimumsingi na sekondari na kuhakikisha elimu inayotolewainakidhi viwango vya ubora wa elimu vinavyotambulikakikanda na kimataifa. Hali kadhalika, , Wizara pamoja nataasisi nyingine zenye kuhusika na utoaji wa elimu na mafunzozitawajibika kuhakikisha uwepo wa mipango, bajeti, usimamizina uendeshaji bora wa elimu katika maeneo yao. Aidha,utekelezaji wa Sera hii unahitaji muundo mahsusi wa kitaasisikatika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya taifa hadi ngazi za

    chini za utoaji wa elimu na mafunzo.5.2. Ngazi ya Taifa

    Katika kutekeleza sera ya elimu na mafunzo, Wizara ya Elimuna Mafunzo ya Ufundi itakuwa na muundo wa kitaasisiutakaojumuisha idara za uta ti na kumshauri Waziri juuya maendeleo ya Sera katika elimu ya awali, elimumsingi

    sekondari, elimu ya ualimu, elimu ya ufundi na mafunzo yaufundi stadi, elimu ya juu na mfumo wa Tuzo wa Taifa namahusiano ya kimataifa kuhusu elimu na mafunzo nchini.Idara nyingine zitakuwepo kwa mujibu wa kanuni na taratibuza o si za umma.

    Taasisi na Vyuo vilivyo chini ya wizara vitawajibika katika

    majukumu ambayo vitapangiwa na wizara kwa mujibu washeria na kutoa taarifa za utekelezaji kulingana na taratibu.Wizara, taasisi, mashirika ya umma na binafsi yenye shule,vyuo au taasisi za elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbalizitawajibika kuwasilisha taarifa na mipango iliyopitishwana shule, vyuo au taasisi hizo kwa mujibu wa taratibu ilikuiwezesha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutoataarifa juu ya mipango na maendeleo ya elimu na mafunzo

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    73/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    64

    kwa ujumla. Wadau wote wa maendeleo wanakaribishwa kwadhati kushiriki katika masuala mbalimbali ya elimu na ufundinchini. Katika kufanikisha hili, Wizara ya Elimu na Mafunzoya Ufundi itaweka utaratibu ambao utawapa fursa wadauwa maendeleo kuchangia kwa ufanisi maendeleo ya elimu namafunzo nchini.

    Pia mamlaka za kusimamia elimu na mafunzo katika ngazimbalimbali zitakuwa huru katika kutekeleza majukumu yakeili kuleta tija katika maendeleo ya elimu nchini. Mamlaka hizini pamoja na Mamlaka ya Ithibati na Uthibiti wa ubora wa

    Elimumsingi na Sekondari, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo yaUfundi, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Tume ya VyuoVikuu Tanzania, Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, Taasisiya Elimu ya Watu Wazima, Wakala wa Maendeleo ya Uongoziwa Elimu, Taasisi ya Elimu Mtandao Dakawa na nyinginezitakazoundwa kulingana na mahitaji. Aidha, Wizara ya Elimuna Mafunzo ya Ufundi na OWM - TAMISEMI zitashirikiana na

    wizara, taasisi na wadau wengine wanaojihusisha na utoaji waelimu na mafunzo nchini. Ushirikiano huo utahusu uchambuziwa Sera ya Elimu na Mafunzo, kuweka viwango na kuandaasheria, kanuni, miongozo na taratibu za utekelezaji wa Sera,kuandaa mipango mikuu ya elimu na mafunzo, kufuatilia,kupima na kutathmini utekelezaji wake.

    Kwa upande wa OWM-TAMISEMI, kutakuwa na O si yaMkuu wa Elimu OWM-TAMISEMI ambayo itasaidiwa naidara za elimu ya awali, elimumsingi, sekondari, elimu ya watuwazima na elimu nje ya mfumo rasmi. Idara hizi zitawajibikakuwa na wataalamu wenye ujuzi wa masuala ya mipango yaelimu ya awali, elimumsingi na sekondari pamoja na masualayanayohusu elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi,ili kupanga, kusimamia na kutekeleza ipasavyo majukumu yaOWM-TAMISEMI katika elimu na mafunzo. Idara nyingine za

  • 8/9/2019 SERA MPYA YA ELIMU NA MAFUNZO TANZANIA

    74/77

    Sera ya Elimu na Mafunzo

    65

    OWM-TAMISEMI zitaendelea kuwepo au kuundwa kulinganana majukumu mengine ya OWM-TAMISEMI.

    5.3. Ngazi ya Mkoa

    Jukumu la usimamizi wa utekelezaji wa Sera ya Elimu naMafunzo katika ngazi ya mkoa litakuwa la A sa Elimu Mkoa.A sa Elimu Mkoa atashauri kuhusu masuala mbalimbali yautekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika mkoa nakutoa mrejesho na ushauri kwa OWM-TAMISEMI kuhusumaendeleo ya elimu na mafunzo katika ujumla wake.

    5.4. Ngazi ya Mamlaka za Serikali za MitaaMamlaka za Serikali za Mitaa zitahusika kat