serikali ya mapinduzi zanzibar hotuba ya waziri wa … · mheshimiwa hamad rashid mohamed kuhusu...
TRANSCRIPT
SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR
HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA
MHESHIMIWA HAMAD RASHID MOHAMED
KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI
KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 KATIKA
BARAZA LA WAWAKILISHI
ZANZIBAR
04 Juni, 2020
KAULI MBIU YA MWAKA 2020/2021
“KUIMARISHA MFUMO WA UGATUZI ILI KUFIKIA DHAMIRA
YA UPATIKANAJI WA HUDUMA BORA ZA AFYA
KWA WANANCHI WOTE”
YALIYOMO MAELEZO YA VIFUPISHO .................................................................................................... i
UTANGULIZI ..................................................................................................................... 1
MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/20 ............................................. 4
MUHTASARI WA MAFANIKIO YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 ............... 6
UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZILIZOPANGWA KATIKA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 ....... 7
PROGRAMU YA KINGA NA ELIMU YA AFYA ....................................................................... 8
Huduma za UKIMWI, Kifua Kikuu, Ukoma na Homa ya Ini .................................................... 9
Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto ......................................................................... 10
Huduma za Kumaliza Malaria Zanzibar ................................................................................ 13
Huduma za Maradhi yasiyo ya Kuambukiza ......................................................................... 14
Huduma za Maradhi Yasiyopewa Kipaumbele ..................................................................... 15
Huduma za Elimu ya Afya ..................................................................................................... 16
Huduma za Lishe .................................................................................................................. 16
Huduma za Afya ya Mazingira .............................................................................................. 17
Huduma za Afya ya Wafanyakazi ......................................................................................... 18
Huduma za Afya ya Msingi ya Akili ....................................................................................... 18
Huduma za Afya ya Msingi ya Macho .................................................................................. 18
Huduma za Ufuatiliaji wa Mienendo ya Maradhi ................................................................ 19
Huduma za Afya Bandarini na Uwanja wa Ndege ................................................................ 21
PROGRAMU YA HUDUMA ZA TIBA .................................................................................. 22
Programu ndogo ya Huduma za Matibabu .......................................................................... 22
Huduma ya Upatikanaji, Uhifadhi na Usambazaji wa Dawa, Zana na Vifaa vya Utibabu .... 23
Huduma ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ................................................................................ 24
Huduma za Damu Salama .................................................................................................... 24
Programu ndogo ya Huduma za Uchunguzi ......................................................................... 25
Huduma za Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi ............................................................ 25
UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO ...................................................................... 27
Mradi wa Ujenzi wa Bohari Kuu ya Dawa Pemba na Maabara ya Wakala wa Chakula, Dawa
na Vipodozi ........................................................................................................................... 27
Mradi wa Kupandisha Hadhi Hospitali za Vijiji na Wilaya .................................................... 27
Mradi wa Ujenzi wa Hospitali kisasa ya Rufaa na Kufundishia Binguni ............................... 28
PROGRAMU YA UENDESHAJI NA URATIBU WA WIZARA YA AFYA .................................... 29
Programu ndogo ya Uongozi na Utawala ............................................................................ 29
Programu ndogo ya Mipango, Sera na Utafiti...................................................................... 30
Taasisi ya Tafiti za Afya – Zanzibar Health Research Institute ............................................. 32
Programu ndogo ya Uratibu wa Shughuli za Afya Pemba ................................................... 32
Maabara ya Afya ya Jamii – Public Health laboratory Pemba ............................................. 33
PROGRAMU YA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA ................................................................ 34
Programu ya huduma za Uchunguzi na Matibabu ............................................................... 34
Programu ndogo ya Uongozi wa Hospitali na Utawala ........................................................ 35
Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ................................................................................... 36
CHANGAMOTO ............................................................................................................... 37
MWELEKEO WA BAJETI YA WIZARA YA AFYA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 ......... 38
SHUGHULI KUU ZITAKAZOTEKELEZWA NA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 40
Programu ya Tiba ................................................................................................................. 40
Programu ya Hospitali ya Mnazi Mmoja .............................................................................. 41
SHUKRANI ...................................................................................................................... 42
HITIMISHO ..................................................................................................................... 44
MAOMBI YA FEDHA KWA UTEKELEZAJI WA KAZI ZILIZOPANGWA KWA PROGRAMU ZA
WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21 .................................................................... 44
VIAMBATISHO ................................................................................................................ 45
i
MAELEZO YA VIFUPISHO
BOQ - Bill of Quantity
BOQ - Bill of Quantity
CCM - Chama cha Mapinduzi
CDC - Center for Disease Control
COSTECH - Tanzania Commission for Science and Technology
DANIDA - Danish International Development Agency
DFID - Department for International Development
DNA - Deoxyribonucleic Acid
DRC - Democratic Republic of Congo
EA - East Africa
EAC - East African Community
ECHO - Echocardiography
e-LMIS - electronic Logistic Management Information System
GF - Global Fund
GFATM - The Global Fund to Fight AIDS, Tuberculosis and Malaria
HIPZ - Health Improvement Project Zanzibar
HMIS - Health Management Information System
HPV - Human Papilloma Virus
HSSP IV - Health Sector Strategic Plan IV
IHI - Ifakara Health Institute
IHR - International Health Regulations
JHPIEGO - Johns Hopkins Program for International Education in Gynecology and Obstetrics
JKU - Jeshi la Kujenga Uchumi
JWTZ - Jeshi la Wananchi wa Tanzania
KMKM - Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo
KVZ - Kikosi cha Valantia Zanzibar
LLINs - Long Lasting Insecticide Nets
MKUZA III - Mpango Mkakati wa Kupunguza Umaskini III
MOI - Muhimbili Orthopaedic Institute
MOU - Memorandum of Understanding
MRI - Magnetic Resonance Imaging
NHA - National Health Accounts
NIMR - National Institute for Medical Research
PEPFAR - President’s Emergency Plan for AIDS Relief
PHCU+ - Primary Health Care Unit +
PITC - Provider Initiated Testing and Counseling
PMI - President’s Malaria Initiatives
RCH - Reproductive and Child Health
SDGs - Sustainable Development Goals
SMZ - Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
ii
TB - Tuberculosis
TEHAMA - Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
THPS - Tanzania Health Promotion Support
TV - Television
UAE - United Arab Emirates
UK - United Kingdom
UNDP - United Nations Development Program
UNFPA - United Nations Population Fund
UNICEF - United Nations International Children Emergency Fund
USAID - United States Agency for International Development
VVU - Virusi Vya UKIMWI
WHO - World Health Organization
ZAWA - Zanzibar Water Authority
ZBC - Zanzibar Broadcasting Corporation
ZFDA - Zanzibar Food and Drug Agency
ZOP - Zanzibar Outreach Program
ZU - Zanzibar University
1
UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Baraza lako likae kama Kamati ya
Matumizi kwa madhumuni ya kupokea, kujadili na hatimae kuidhinisha makadirio ya
mapato na matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa
rehema, muumba mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake, kwa kutujaalia
kukutana hapa tukiwa wazima wa afya na nchi yetu ikiwa hatika hali ya amani na
utulivu. Aidha, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwasilisha mbele ya
Baraza lako hotuba hii ya bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
3. Naomba nichukuwe nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa Dkt. Ali Mohamed Shein,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa jinsi ambavyo ameongoza
nchi yetu kwa busara, hekima na umahiri wa hali ya juu na kwa namna ambavyo Serikali
ya Awamu ya Saba chini ya uongozi wake umeiwezesha Wizara ya Afya kutekeleza
majukumu yake kwa ufanisi na mafanikio makubwa. Mheshimiwa Rais anastahiki
pongezi kwa juhudi anazozichukuwa katika kuhakikisha kwamba wananchi wa Zanzibar
wanafaidika na matunda ya Mapinduzi ya Januari 1964. Tumeshuhudia namna nchi
ilivyopata maendeleo makubwa katika sekta za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kwa
upande wa Sekta ya Afya, tumejionea mageuzi makubwa, ambapo huduma za kinga na
tiba zimeimarishwa kwa kiasi kikubwa kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa huduma
bora kwa wananchi. Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta ya afya chini ya
uongozi wake yanaelezewa kwa kina katika MAKALA MAALUM YA BAJETI, 2020/2021
inayoelezeautekelezaji wa Ilani ya CCM kuanzia mwaka 2010 hadi 2020. Mafanikio
haya yote yatabaki kuwa alama ya uongozi wake na utumishi wake kwa wananchi wa
Zanzibar. Tunamuomba Mwenyezi Mungu ampe afya njema na maisha marefu yeye na
familia yake, Amin.
4. Mheshimiwa Spika, natoa shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi,
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, kwa kusimamia vyema utekelezaji wa shughuli za
Serikali, kwa kuzingatia Ilani ya CCM na miongozo mingine iliyopo. Aidha, miongozo na
maelekezo yake yameisaidia sana Wizara ya Afya kutimiza wajibu wake wa kutoa
huduma bora za afya kwa wananchi. Hotuba yake aliyoitoa katika Baraza hili tarehe 6
Mei, 2020 wakati akiwasilisha bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka 2020/2021, nayo
imeonesha dira ya utekelezaji wa shughuli za Serikali kupitia Wizara mbali mbali kwa
mwaka wa fedha ujao wa 2020/2021.
2
5. Mheshimiwa Spika, nichukuwe fursa hii kukupongeza wewe mwenyewe binafsi, kwa
kuliongoza Baraza hili umakini mkubwa kwa kipindi chote cha miaka mitano, ambapo
sasa linakaribia kumaliza muda wake. Pia nawapongeza Naibu Spika, Mheshimiwa
Mgeni Hassan Juma na Wenyeviti wa Baraza hili Mheshimiwa Mwanaasha Khamis
Juma na Mheshimiwa Shehe HamadMattar kwa kukusaidia katika kuendesha mijadala
ndani ya Baraza hili, kazi ambayo wameifanya kwa umahiri mkubwa. Aidha,
nampongeza Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Ndugu Raya Issa Msellem kwa
kusimamia na kufanikisha shughuli za Baraza kwa ufanisi.
6. Mheshimiwa Spika, Wizara inathamini mchango mkubwa kutoka kwaKamati ya Ustawi
wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi, ambayo pamoja na mambo mengine, imejadili,
kushauri, kutoa maoni na kupitisha Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi
ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2020/2o21. Naomba niwapongeze na
kuwashukuru wajumbe wote wa Kamati hii pamoja na makatibu wake, kwa kazi kubwa
waliyoifanya katika kipindi chote cha utekelezaji wa shughuli zake. Kamati hii, chini ya
uenyekiti wa Mheshimiwa Mwanaasha Khamis Juma, Mwakilishi wa Wananchi wa
Jimbo la Chukwani, akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Nassor Salim
Ali(JAZEERA) Mwakilishi wa Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, imesaidia sana Wizara
kubaini na kuzishughulikia kero zilizokuwa zinawakabili wananchi katika kupata huduma
za afya. Aidha, michango yao imeweza kusaidia katika kuimarisha utendaji wa shughuli
za Wizara kwa jumla kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi.
7. Mheshimiwa Spika, naomba niishukuru kwa dhati kabisa Kamati ya Bajeti ya Baraza la
Wawakilishi chini ya Uenyekiti wa Mheshimiwa Mohamed Said (DIMWA), kwa kujadili
na kutoa ushauri katika mapendekezo ya Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha
2020/2021. Pia, Wizara inathamini michango ya Wajumbe wote wa Baraza la
Wawakilishi, kwani yalikuwa na dhamira ya kufanikisha azma ya Mwasisi wa Taifa hili,
Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume ya kuona huduma za afya zinaimarika na
kuwafikia wananchi wote, hususan wanyonge, bila ya ubaguzi wowote. Kwa kweli
katika utumishi wao wa miaka mitano ndani ya Baraza hili, Wajumbe hao wameonesha
ukomavu wa kisiasa na uwajibikaji mkubwa katika kuwawakilisha wananchi
waliowachagua. Hivyo, namuomba Mwenyezi Mungu awape ushindi mkubwa kwenye
majimbo yao katika katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba 2020 ili warejee tena
katika Baraza hili, Amin.
3
8. Mheshimiwa Spika, sote tunaelewa kwamba ulimwengu umefikwa na taharuki ya
kuibuka kwa ugonjwa wa Covid-19, tumuombe Mwenyezi Mungu atufanyie wepesi
katika janga hili. Aidha, nichukuwe fursa hii kuwaomba Wajumbe wa Baraza hili pamoja
na wananchi wote kwa ujumla kuchukuwa tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa
afya juu ya kujikinga na kufuata maelekezo ya Serikali. Niwaombe sana wananchi
tusifanye mzaha, maradhi haya ni mabaya na hayachagui mtu. Tujitahidi kufuata
masharti ya kiafya ili tuweze kuudhibiti ugonjwa huu usienee nchini mwetu. Nanukuu
maneno ya Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein“... Tusifanye masihara na maradhi
ya Korona, wananchi tusiwe wakaidi bali tufuate muongozo wa Serikali ...” mwisho
wa kunukuu.
9. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo sasa naomba nitoe maelezo ya mapato na
matumizi pamoja na utekelezaji wa shughuli za Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha
2019/2020.
4
MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/20
10. Mheshimiwa Spika, Kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichofanyika mwezi Juni 2019,
kilipitisha jumla ya matumizi ya Shilingi 88,613,900,000/= kwa ajili ya kutekeleza
shughuli mbali mbali za Wizara ya Afya. Kati ya hizo, Shilingi 17,202,000,000/=
ziliidhinishwa kwa ajili ya mishahara na maposho, Shilingi 35,002,500,000/= kwa kazi za
kawaida na Shilingi 2,270,602,000/= zikiwa ruzuku kwa taasisi zilizo chini ya Wizara.
Vile vile, Shilingi15,622,000,000/=ziliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya Hospitali ya Mnazi
Mmoja; ambapo Shilingi 10,954,800,000 ni kwa ajili ya mishahara na maposho na Shilingi
4,667,200,000 kwa matumizi ya kawaida. Kwa upande wa shughuli za maendeleo, Wizara
iliidhinishiwa kutumia Shilingi 34,138,798,000/=, kati ya hizo, Shilingi 17,896,000,000/=
kutoka Serikalini na Shilingi 16,242,798,000/= kutoka kwa Washirika wa Maendeleo.
11. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi wa Machi, 2020, jumla ya Shilingi
54,205,308,509/= sawa na asilimia77.7 ya fedha zilizotengwa (Shilingi
69,764,347,532/=) kwa kipindi cha robo tatu zilipatikana na kutumika. Kati ya hizo,
Shilingi 13,868,467,469/= (asilimia 115.7) zilitumika kwa malipo ya mishahara na
maposho; Shilingi 22,915,890,487/= kwa shughuli za uendeshaji (asilimia 80.4), na
Shilingi1,685,309,561/= kwa taasisi zinazopata ruzuku (asilimia94.1). Kwa upande wa
utekelezaji wa shughuli za maendeleo, jumla ya Shilingi15,735,640,992/= (asilimia
57.3) zilipatikana; Shilingi8,122,188,349/= kutoka Serikalini na Shilingi 7,613,452,643/=
kutoka kwa Washirika wa Maendeleo.
12. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, Hospitali ya Mnazi Mmoja iliingiziwa jumla ya
Shilingi 12,013,634,348/= sawa na asilimia 111.6 ya fedha zilizotengwa kwa robo tatu;
Shilingi 8,999,484,795/= sawa na asilimia 109.5 zilitumika kwa ajili ya mishahara na
maposho naShilingi 3,014,149,533/= (asilimia118.5) zilitumika kwa matumizi ya
kawaida (Kiambatisho namba 1).
13. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Afya (Fungu H01) ilipangiwa kukusanyajumla ya Shilingi
387,235,000/= na Hospitali ya Mnazi Mmoja (Fungu H02) ilipangiwa kukusanya Shilingi
560,471,000/= kutoka katika vyanzo vyake mbali mbali vya mapato. Hadi kufikia Machi
2020, Wizara imekusanya na kuingiza katika Mfuko Mkuu wa Serikali jumla ya
Shilingi208,717,044/= sawa na asilimia 53.9 naHospitali ya Mnazi Mmoja Shilingi
410,109,657/= sawa na asilimia 73.2 ya fedha zilizokadiriwa (Kiambatisho namba 2).
5
14. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa bajeti iliyoidhinishwakatika kipindi hicho cha
utekelezaji (2019/2020), matumizi ya Wizara ya Afya yalielekezwa katika kutekeleza
vipaumbele vifuatavyo:
i. Kuimarisha mfumo wa udhibiti wa ubora wa huduma za afya katika ngazi zote;
ii. Kuongeza huduma za upatikanaji wa kinga na elimu ya afya dhidi ya maradhi ya
kuambukiza na yasiyoambukiza ili kujenga uelewa na hatimae kubadili tabia na
mienendo;
iii. Kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi na huduma za mama na
mtoto kwa misingi ya usawa;
iv. Kuandaa mazingira ya utayari kwa ajili ya huduma za dharura ikiwemo
kipindupindu;
v. Kuimarisha huduma za tiba na uchunguzi;
vi. Kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu, vifaa na “reagents” zenye ubora na
usalama katika ngazi zote;
vii. Kuimarisha upatikanaji wa huduma za rufaa ili kupunguza idadi ya wagonjwa
wanaosafirishwa kwa ajili ya matibabu nje ya nchi;
viii. Kuimarisha nguvu kazi ya afya kwa kusomesha wafanyakazi katika kada za
kitaalamu na kuinua mafao ya wafanyakazi;
ix. Kuimarisha mifumo ya afya kwa kufanya tafiti mbali mbali;
x. Kuimarisha miundo mbinu ya hospitali na vituo vya afya ili kuendana na viwango
vya utoaji wa huduma; na
xi. Kuongeza na kuimarisha mashirikiano na washirika mbali mbali wa Sekta ya Afya
wakiwemo wa Sekta binafsi ili kuimarisha utoaji wa huduma za afya.
6
MUHTASARI WA MAFANIKIO YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
15. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa hapo juu, Wizara ya
Afya imepata mafanikio mengi katika kipindi cha mwaka 2019/2020. Baadhi ya
mafanikio yaliyopatikana ni kama yafuatayo:-
i. Kuongezeka kwa idadi ya wafanyakazi, ambapo jumla ya wafanyakazi wapya 602
(Unguja 445 na Pemba 157) wa kada mbali mbali wakiwemo madaktari, wauguzi na
wataalamu wa maabara wameajiriwa; Jumla ya wafanyakazi 133 wa kada mbali
mbali wamepelekwa masomoni ndani na nje ya nchi wakiwemo madaktari bingwa
31;
ii. Kukamilika kwa muundo wa utumishi wa kada za afya (Scheme of Service);
iii. Kukamilika kwa jengo la huduma za mama na mtoto katika Hospitali ya Kivunge;
iv. Kuendelea kuimarika kwa upatikanaji wa dawa muhimu katika hospitali na vituo
vya afya zikiwemo dawa za saratani na za kusafisha figo;
v. Kuanzishwa kwa kliniki maalum ya huduma za wagonjwa waliopandikizwa figo
(kidney transplant) katika hospitali ya Mnazi Mmoja, ambapo jumla ya wagonjwa
sita (6) wanaendelea na huduma ;
vi. Kukamilika kwa jengo la macho katika Hospitali ya Mnazi Mmoja;
vii. Kupatikana kwa CT Scan mpya yenye uwezo mkubwa wa uchunguzi wa maradhi
katika Hospitali ya Mnazi Mmoja pamoja na ufungwaji wa tanuri jipya la kuchomea
taka hatarishi (Incinerator) katika Hospitali ya hiyo ;
viii. Kupatikana vifaa muhimu vya huduma za mifupa ikiwemo kitanda maalum
(othopoedic bed) cha upasuaji wa mifupa na X-ray (C-arm) inayotumika wakati wa
upasuaji.
Kwa ujumla, mafanikio yaliyofikiwa kwa mwaka 2019/2020 yanaelezwa kwa kina kupitia
program husika katika vifungu vinavyofuata.
7
UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZILIZOPANGWA KATIKA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
16. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa taarifa kwamba,shughuli mbali mbali zilizoainishwa
katika hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2019/2020 zimeweza
kutekelezwa kwa kiwango kikubwa kwa mujibu wa bajeti iliyopitishwa. Hivyo, taarifa hii
inaelezea utekelezaji wa shughuli hizo, pamoja na maagizo mbali mbali ya Serikali
kupitia Programu mbali mbali za Wizara pamoja na Programu ya Hospitali ya Mnazi
Mmoja. Aidha, taarifa hii inagusia mafanikio yaliyopatikana katika maeneo
yaliyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2010/2015 na
2015/2020) katika kuimarisha huduma za afya hapa nchini kwa kipindi cha Serikali ya
Awamu ya Saba.
8
PROGRAMU YA KINGA NA ELIMU YA AFYA
17. Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa huduma za kinga na elimu kwa jamii ni muhimu
katika kuikinga jamii na maradhi mbali mbali, yakiwemo ya kuambukiza na yasiyo ya
kuambukiza. Katika kuhakikisha kwamba jamii inapata huduma na elimu ya afya juu ya
kujikinga na maradhi hayo, Wizara ilitenga jumla ya Shilingi 21,888,822,000/= kwa ajili
ya Program ya Kinga na Elimu ya Afya. Hadi kufikia mwezi wa Machi, 2020, jumla ya
Shilingi 10,665,847,157/=, sawa na asilimia 64.6 ya fedha zilizotengwa kwa robo tatu za
mwaka zilipatikana na kutumika kwa utekelezaji wa shughuli hizi. Shughuli
zilizopangwa kutekelezwa na program hii ni kama zifuatazo:-
i. Kukamilisha Mpango Mkakati wa miaka mitano wa kupambana na Homa ya Ini
Zanzibar (Viral Hepatitis Strategic Plan I (2019/2020 - 2023/2024);
ii. Kuendelea kudhibiti maambukizi ya VVU kwa kutoa huduma za ushauri nasaha,
upimaji na matibabu;
iii. Kuendelea kutoa huduma za tiba kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu, Ukoma na Homa
ya Ini;
iv. Kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto;
v. Kuendelea na utekelezaji wa mikakati ya kumaliza malaria Zanzibar;
vi. Kukamilisha matayarisho ya ‘Public Health Contingency Plan’;
vii. Kuendelea kutoa huduma za uchunguzi na tiba ya maradhi ya macho katika
hospitali, vituo vya afya na skuli;
viii. Kuendelea na mkakati wa kubadilisha tabia hatarishi zinazochangia kuenea kwa
maradhi ya kichocho, minyoo na matende hapa Zanzibar;
ix. Kuendelea na mikakati ya kupambana na maradhi ya kuambukiza na
yasiyoambukiza;
x. Kuendelea kufanya tafiti (operational research) zitakazotoa muelekeo sahihi wa
kupambana na minyoo na kumaliza maradhi ya Kichocho, Matende na Vikope
Zanzibar;
xi. Kushirikiana na programu ndogo ya Mipango, Sera na Utafiti katika kuimarisha
mfumo wa ukusanyaji takwimu za wagonjwa wa Saratani katika Hospitali ya Rufaa
na Hospitali za Mkoa na Wilaya na za watu binafsi; na
xii. Kufanya uchunguzi wa maradhi ya Shinikizo la damu, Kisukari na Saratani.
Utekelzeaji wa shughuli zilizoainishwa hapo unaelezewa kupitia huduma zinazotolewa
na programu husika kama ifuatavyo: -
9
Huduma za UKIMWI, Kifua Kikuu, Ukoma na Homa ya Ini
18. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha utekelezaji (Julai, 2019 - Machi, 2020), watu
185,437 (wanaume 80,841 na wanawake 104,596) walichunguzwa VVU katika hospitali,
vituo vya afya na taasisi mbali mbali zinazotoa huduma za ushauri nasaha na upimaji wa
VVU. Kati yao watu 1,254 (wanaume 422 nawanawake 812), sawa na asilimia 0.7 ya
watu wote waliochunguzwa waligundulika kuwa na VVU.
19. Katika jitihada za kuzuia maambukizi ya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,
jumla ya wajawazito 45,331 walipimwa VVU katika kliniki zinazotoa huduma ya
ujauzito; wajawazito 84, sawa na asilimia 0.2 waligunduliwa na VVU. Pia, watoto 263
waliozaliwa na mama wenye Virusi vya UKIMWI walichunguzwa damu zao ili kubaini
kama wana maambukizi kutoka kwa mama zao. Katika uchunguzi huo watoto watatu
(wa kiume mmoja na wa kike wawili), sawa na asilimia 1.1 waligunduliwa kuwa na
maambukizi.
20. Mheshimiwa Spika, huduma na tiba kwa wanaoishi na VVU ziliendelea kutolewa, jumla
ya watu wapya 864 wanaoishi na VVU (wanawake 875 na wanaume 279) walisajiliwa
katika kliniki zinazotoa huduma hizi Unguja na Pemba. Hadi sasa, jumla ya watu
wanaoishi na VVU 6,830 wamesajiliwa katika kliniki hizi tokea huduma hizi
zilipoanzishwa hapa nchini, ambapo wagonjwa 6,644 sawa na asilimia 97.3
wanaendelea kutumia dawa za kupunguza makali ya Virusi vya UKIMWI. Hivyo,
kiwango hiki kilichofikiwa tayari kimevuka shabaha ya kimataifa iliyowekwa ya kufikia
asilimia 90 ya watu wote waliogundulika kuwa na VVU wawe wanatumia dawa za
kupunguza makali ifikapo mwaka 2020.
21. Mheshimiwa Spika, huduma za uchunguzi wa maradhi haya ziliendelea kutolewa katika
kliniki iliyopo Mnazi Mmoja na maabara za Hospitali za Kivunge na Makunduchi kwa
Unguja na Abdalla Mzee, Chake Chake, Wete, Micheweni na Vitongoji kwa Pemba.
Katika kipindi kinachoripotiwa, jumla ya watu 50,204 walipimwa Homa ya Ini B; kati yao
watu 971 sawa na asilimia 1.9 waligunduliwa na maambukizi. Pia, watu 27,516
walipimwa Homa ya Ini C, ambapo watu 70 sawa na asilimia 0.3 waligundulika na Virusi
vya homa hiyo. Aidha, huduma za tiba kwa maradhi ya homa ya ini ziliendelea
kutolewa katika kliniki iliopo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, ambapo wagonjwa 147
10
walisajiliwa (wanaume 59 na wanawake 82); kati yao, wagonjwa 11 (wanawake 2 na
wanaume 9) wameanzishiwa dawa.
22. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwamba jamii inapata uelewa wa maradhi haya,
Wizara ilitoa mafunzo ya homa ya Ini kwa Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi. Aidha, kwa muendelezo huo huo wa kutoa elimu kwa jamii, vipindi vitano
(5) vya redio na matangazo 90 ya televisheni yalirushwa hewani, sambamba na
usambazaji wa vipeperushi vyenye kutoa elimu ya kutambua dalili na ishara za maradhi
hayo katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba, vipeperushi hivyo pia, vilielezea
jinsi maradhi ya homa ya ini yanavyopatikana pamoja na namna ya kujikinga.
23. Mheshimiwa Spika, kuanzia kipindi cha Julai 2019 hadi Machi 2020, sampuli za
makohozi 5,884 (Unguja 3,624 na Pemba 2,260) zilichunguzwa maradhi ya Kifua Kikuu;
sampuli 515 (Unguja 343 na Pemba 172) sawa na asilimia 8.8 ziligundulika kuwa na
ugonjwa huo. Hali ya wagonjwa wanaopata usugu wa dawa (Multi-Drug Resistance)
bado imeendelea kujitokeza kwa baadhi ya wagonjwa, hadi sasa jumla ya wagonjwa
watano 5 (Unguja wanne na Pemba mmoja) wenye kifua kikuu sugu wanaendelea
kutibiwa kwa dawa za daraja la pili na hali zao zinaendelea vizuri.
24. Mheshimiwa Spika, huduma za kupunguza makali ya athari za dawa za kulevya kwa
vijana walioathirika na dawa hizi zinaendelea kutolewa katika kituo cha Hospitali ya
Wagonjwa ya Akili Kidongo Chekundu. Katika kipindi hicho cha utekelezaji, wateja
wapya 909 (wanaume 845 na wanawake 64) wamepatiwa dawa za kupunguza uraibu
na utegemezi wa dawa za kulevya. Tokea huduma hizo zilipoanzishwa mwaka 2015,
kuna jumla ya wateja 651(wanaume 608 na wanawake 43) wanaoendelea kupatiwa
dawa hizo.
Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto
25. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 jumla ya wajawazito
40,177 walihudhuria katika kliniki angalau mara moja katika kipindi chote cha ujauzito;
kati yao, wajawazito 5,725 sawa na asilimia 14.2 walihudhuria kliniki kwa mara ya
mwanzo wakiwa na ujauzito wa chini ya wiki 12. Asilimia hii ni ndogo na inaashiria
kuwepo kwa muamko mdogo wa kuhudhuria kliniki mapema kwa ajili ya uchunguzi
miongoni mwa jamii. Wizara inaendelea kuchukuwa juhudi za kuhamasisha jamii
hususan mama wajawazito kuhudhuria kliniki mara tu wanapojihisi wamebeba ujauzito
kwa uchunguzi, ili kuweza kugundua mapema matatizo yanayojitokeza na kuchukua
11
hatua stahiki, hivyo kupunguza matatizo yanayopelekea vifo vya uzazi pamoja na
madhara mengine yanayoweza kuepukika.
26. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai,2019 hadi Machi, 2020 jumla ya wajawazito
28,068 (asilimia 40.1) wamejifungua katika hospitali za Serikali na binafsi pamoja na
vituo vya afya vya msingi vinavyotoa huduma za kuzalisha kwa Unguja na Pemba
(Kiambatisho namba 3); hata hivyo, idadi hii ni ndogo kulingana na wastani wa
wajawazito 69,902 waliotarajiwa kujifungua katika kipindi hicho. Hii inaonesha
kwamba bado mama wengi wanaendelea kujifungulia majumbani, jambo ambalo
linaweza kuhatarisha maisha ya mama mwenyewe na mtoto. Niendelee kuwasihi
wananchi kuzitumia huduma za afya wakati wa kujifungua kwani Serikali imefanya kila
lililowezekana kuziimarisha huduma hizi katika vituo vingi karibu na maeneo wanayoishi
wananchi.
27. Mheshimiwa Spika, Shirika la Afya Dunia linapendekeza wazazi wahudhurie kliniki kwa
ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kwa vipindi vinne; ndani ya saa 24 baada ya
kujifungua, siku ya tatu (3) hadi ya saba (7), siku ya nane (8) hadi ya 28 na siku ya 29
hadi ya 42. Katika kipindi cha utekelezaji wazazi 26,378 sawa na asilimia 94 walifanyiwa
uchunguzi mara tu baada ya kujifungua. Kati ya wazazi hao, akina mama 3,954 (asilimia
15) tu ndio waliorudi kufanyiwa uchunguzi katika hudhurio la pili. Wizara inaendelea
kuiomba jamii kutumia fursa zilizopo katika kuchunguzwa afya zao na kuwataka akina
baba kuwahimiza kinamama kurudi kliniki pamoja na watoto kwa mujibu wa ratiba
waliyopangiwa ili kuepuka matatizo ambayo yanaweza kugunduliwa mapema na
kuchukuliwa hatua stahiki.
28. Mheshimiwa Spika, Huduma za uzazi wa mpangilio zimeendelea kutolewa katika vituo
vyote vinavyotoa huduma za afya ya uzazi na mtoto, ambapo jumla ya wateja wapya
19,310 walijiunga na huduma hizo za njia mbali mbali; zikiwemo za muda mfupi, muda
mrefu na zile za kudumu. Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Idadi
ya Watu (UNFPA) kwa kutambua kwamba matumizi mazuri ya njia hizi yanaweza
kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga kwa asilimia 30, imechukua juhudi
kuhakikisha kwamba huduma hizi zinapatikana katika vituo vyote vya afya vinavyotoa
huduma za afya ya uzazi. Niendelee kuwaomba tena wananchi kuzitumia huduma za
uzazi wa mpango zinazopatikana katika vituo vyote vya afya vinavyotoa huduma za afya
12
ya uzazi Unmguja na Pemba. Aidha, huduma hizi zinatolewa bure bila malipo yoyote
kama sera ya afya inavyoelekeza.
29. Mheshimiwa Spika, pamoja na kuimarika kwa huduma, naomba nikiri kwamba bado
nchi yetu inakabiliwa na changamoto ya vifo vya watoto. Kwa kuliona hilo, Wizara
imewajengea uwezo wahudumu wa afya kwa kuwapatia mafunzo masafa ya utibabu wa
maradhi ya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano. Jumla ya wafanyakazi
227(Unguja 118 na Pemba 109) wa kada mbali mbali kutoka katika vituo vya afya
walipatiwa mafunzo hayo ili kupunguza idadi ya vifo vya watoto. Aidha, jumla ya watoto
38,889 wenye umri chini ya mwaka mmoja wamepatiwa chanjo za kukinga maradhi ya
kuambukiza (Kifua kikuu, Surua, Homa ya Ini, Homa ya Uti wa mgongo, Donda koo,
Kifuduro na Pepopunda); ambapo kiwango cha chanjo kwa watoto wenye umri huo
imefikia asilimia 83.3. Huduma hizo za chanjo zinatolewa katika vituo vyote vya afya
vya Unguja na Pemba, vikiwemo vituo vya afya vya binafsi vinavyotoa huduma za afya
ya uzazi na mtoto.
30. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoa huduma za chanjo ya kuzuia kansa ya
mlango wa kizazi kwa watoto wa kike wenye umri wa miaka 9 hadi 14. Hadi kufikia
Machi 2020, jumla ya wasichana 22,849 wenye umri huo wamepata dozi ya kwanza na
10,160 wamekamilisha dozi ya pili ya chanjo hiyo tokea ilipoanza kutolewa katika
mwezi wa Aprili 2018. Aidha, kwa mwaka huu wa fedha (2019/2020), jumla ya
wasichana 8,879 wamepatiwa dozi ya kwanza na wasichana 5,585 wamepatiwa dozi ya
pili ya chanjo hiyo.
31. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Shirika Linaloshughulikia Masuala ya
Idadi ya Watu (UNFPA) imefanya ukarabati wa vituo vitatu (3) vya kutolea huduma
zinazoendana na mahitaji ya vijana; Unguja vituo viwili (Nungwi na Bwejuu) na Pemba
kituo kimoja cha Konde. Kukamilika kwa ukarabati wa vituo hivyo kunafanya idadi ya
vituo vinavyotoa huduma hizo kufikia 10, ambapo jumla ya vijana 4,243 wanaendelea
kupatiwa huduma mbali mbali katika vituo hivyo.
13
Huduma za Kumaliza Malaria Zanzibar
32. Mheshimiwa Spika, baada ya kipindi kirefu nchi yetu kuripoti kuwa na idadi ndogo ya
wagonjwa wa malaria, sasa maradhi hayo yameanza kuonyesha dalili za kuongezeka.
Idadi ya wagonjwa wa malaria katika kipindi cha Julai 2019 hadi Machi, 2020 ni 8,872
(sawana asilimia 5 ya waliopimwa) ikiwa ni ongezeko la asilimia 60 ikilinganishwa na
kipindi kama hiki mwaka 2018/19, ambapo wagonjwa 3,463 sawana asilimia 1.2 ya
waliopimwa (4,671) waligundulika kuwa na vimelea vya malaria. Kati ya wagonjwa
8,872 waliogunduliwa kuwa na vimelea vya malaria, wagonjwa 4,636 sawa na asilimia
52 wamefuatiliwa majumbani kwa lengo la kuzuia maambukizi katika jamii. Takwimu
zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya waliogunduliwa na vimelea vya malaria
walikuwa na historia ya kusafiri nje ya Zanzibar katika kipindi hicho. Katika kudhibiti
suala hili, Wizara imeweka vituo vya upimaji wa vimelea Bandarini na katika viwanja vya
ndege kwa ajili ya kuwapima wasafiri wanaoingia. Aidha, vituo vya kutowa elimu ya
afya juu ya malaria vimeanzishwa katika boti za abiria zinazoingia na kutoka Zanzibar.
33. Mheshimiwa Spika, takwimu zinabainisha kwamba kati ya wagonjwa 25,252
waliolazwa katika hospitali za Serikali, wagonjwa 530 walikuwa wanaugua malaria na
wagonjwa sita sawa na asilimia 1.1 walifariki kutokana na malaria kali. Ongezeko
kubwa la ugonjwa huu limechangiwa na kuongezeka kwa mazalia ya mbu waenezao
malaria kulikosababishwa na mvua zilizonyesha kwa muda mrefu kuanzia Oktoba 2019 -
Januari, 2020. Katika kukabiliana na tatizo hili, Wizara imeendelea kuchukuwa hatua
mbali mbali zikiwemo upimaji wa damu kwa ajili ya kuchunguza malaria kwa wananchi
katika maeneo yaliyoathirika zaidi na kutoa matibabu kwa wagonjwa waliogundulikana
na vimelea; ugawaji wa vyandarua vyenye dawa; uhamasishaji katika jamii pamoja na
upigwaji wa dawa majumbani, ambapo jumla ya nyumba43,616 (Unguja37,797 na
Pemba 5,819) sawa na asilimia 96.7 ya makadirio (nyumba 45,107) zilipigwa dawa
katika Wilaya zote isipokuwa kwa Wizaya ya Mjini.
34. Mheshimiwa Spika, sambamba na hatua hizo zilizochukuliwa, shughuli za ugawaji wa
vyandarua zilifanyika, jumla ya vyandarua 152,962 vyenye dawa ya muda mrefu
viligawiwa kwa wananchi kupitia mpango endelevu wa ugawaji wa vyandarua. Aidha,
zoezi la kuua viluilui vya mbu katika sehemu zinazotuama maji na mabwawa liliendelea
kufanyika katika maeneo yaliyobainika kuwepo kwa wingi wa mazalio ya mbu; maeneo
hayo yanatoka katika Wilaya zote za Unguja na Wilaya za Wete na Micheweni kwa
14
Pemba. Sambamba na shughuli hizo, elimu ya afya juu ya kinga ya malaria iliendelea
kutolewa kupitia mikutano ya kijamii, vyombo vya habari (TV na Redio) za Serikali na
binafsi pamoja na usambazaji wa vipeperushi vyenye ujumbe wa kuelimisha jamii.
Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kuchukuwa juhudi hizo ili lengo la kumaliza
malaria Zanzibar ifikapo 2023 liweze kufikiwa.
Huduma za Maradhi yasiyo ya Kuambukiza
35. Mheshimiwa Spika, huduma za maradhi yasiyoambukiza zimeendelea kutolewa katika
vituo vya afya 50 Unguja na Pemba. Maradhi haya yasiyoambukiza yanaonekana
kushamiri na kushika kasi si kwa hapa Zanzibar tu, bali pia katika nchi nyingi za Bara la
Afrika. Katika kuendeleza mapambano dhidi ya maradhi haya, Wizara imezindua Mradi
wa miaka mitano wa “Universal Health Coverage Priority setting”, ambao unatekelezwa
kwa mashirikiano baina ya Wizara ya Afya na “University of Bergen”. Utekelezaji wa
Mradi huo umeanza katika mwaka huu wa fedha unaomalizika (2019/2020) chini ya
udhamini wa Bill na Melinda Gates Foundation. Lengo la mradi huu ni kudhibiti na
kupunguza ukubwa wa maradhi yasiyoambukiza na vichochezi vyake katika jamii.
36. Mheshimiwa Spika, ugonjwa mwengine ambao unaonekana kusumbua jamii yetu ni
maradhi ya saratani. Kwa kutambua madhara ya ugonjwa huu, Wizara inaendelea
utafiti wa kujua ukubwa wa maradhi haya kwa kufanya uchunguzi, utafiti huo
unafanyika kwa mashirikiano baina ya wataalamu wa ndani na wa nje kutoka katika
Jimbo la Nanjing nchini China. Katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020,
uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ulifanyika katika awamu mbili tofauti Unguja
na Pemba, ambapo jumla ya wanawake 9,198 (Unguja 5,181 na Pemba 4,017) sawa na
asilimia102.2 ya makadirio walichunguzwa. Kati ya wanawake waliochunguzwa; 341
(Unguja 79 na Pemba 262) waligunduliwa na dalili za awali za saratani; 235 (Unguja 34
na Pemba 201) walikuwa na maambukizi, ambapo walipatiwa matibabu stahiki na
wanawake 23 (Unguja 15 na Pemba 8) walibainika kuwa katika hatua za juu za ugonjwa
huo, hivyo walipatiwa rufaa kwa ajili ya matibabu zaidi katika Hospitali ya magonjwa ya
saratani Ocean Road huko Dar-es-Salaam.
37. Mheshimiwa Spika, ni wajibu wa Wizara kuhakikisha kwamba jamii inapata elimu na
uelewa juu ya magonjwa yasiyoambukiza. Kwa kutekeleza hilo vipindi 15 vya
kuelimisha jamii vilirushwa hewani kupitia vyombo vya habari vya ZBC redio na TV, Hits
FM, Assalamu FM, Coconut FM, Chuchu FM, Redio Al-Noor, Redio Istikama ya kisiwani
Pemba na Redio Adhana. Pia, elimu ya afya juu ya magojwa ya kisukari na afya ya
kinywa na meno ilitolewa kwa wanafunzi wa Skuli za Mwanakwerekwe “A” na “C”,
ambapo wanafunzi 416 (wanaume105 na wanawake 311) wa darasa la 1-6 katika skuli
hizo walipatiwa mafunzo hayo. Mafunzo mengine yalitolewa kwa wanafunzi wa Skuli
15
za Alhisani, Mwanakwerekwe “C” na Chuo cha Ufundi cha Karume juu ya kujichunguza
saratani ya matiti, mafunzo hayo yalitolewa wakati wa maadhimisho ya mwezi wa
uelewa wa Saratani ya Matiti, Oktoba 2019, katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil.
Aidha, makala maalum kuhusiana na magonjwa hayo zimetayarishwa na kuchapishwa
katika Gazeti la Zanzibar Leo.
38. Mheshimiwa Spika, katika kupata taarifa za suluhisho la maradhi yasiyoambukiza,
Wizara imeanza kufanya utafiti juu ya athari za shinikizo la damu kwa mama
wajawazito. Utafiti huo unafanyika katika Hospitali za Mnazi Mmoja, Kivunge na
Makunduchi kwa Unguja na Hospitali za Chake Chake na Wete kwa upande wa Pemba.
Pia, utafiti huo utahusisha baadhi ya maeneo katika Shehia za Unguja na Pemba.
Napenda nitoe wito kwa viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali na jamii kwa ujumla
kujenga utamaduni wa kupima afya zao angalau mwaka mara moja na kufuata maelezo
ya wataalamu wa afya katika kujikinga na kuepuka vichocheo vinavyopelekea maradhi
yasiyoambukiza.
Huduma za Maradhi Yasiyopewa Kipaumbele
39. Mheshimiwa Spika, Uchunguzi wa maradhi yasiyopewa kipaumbele ulifanyika katika
vituo vya Kinazini (Unguja) na Mkoroshoni (Pemba), ambapo jumla ya watu 965
walichunguzwa maradhi ya Kichocho, kati yao 584 (asilimia 60.5) waligundulika na
maradhi hayo. Aidha, Watu 560 ambao walikuwa na dalili za matende walichunguzwa
na wote walibainika kuwa na maradhi ya matende. Wananchi wote waliogunduliwa na
maambukizi walipatiwa matibabu stahiki.
40. Mheshimiwa Spika, Wizara pia, imefanya utafiti wa kuangalia kiwango cha maambukizi
ya maradhi ya kichocho katika Shehia 47 na skuli 47 za Unguja na Pemba. Matokeo ya
utafiti huo yameonesha kwamba kiwango cha maambukizi ya kichocho kitaifa ni
asilimia 0.9 (Unguja asilimia 0.5 na Pemba asilimia 1.3), kiwango hichi kinaashiria
kupungua kwa maambukizi ya maradhi hayo ikilinganishwa na asilimia 3 ya maambukizi
katika mwaka 2018. Vile vile, utafiti wa kuangalia uwepo wa konokono katika mito
minne (4) na mabwawa 25 katika mabonde ya Chambani, Ukutini na Kengeja ulifanyika.
Matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa mabwawa 13 (Chambani 12 na Ukutini moja)
yana wadudu wa konokono, hivyo hatua ya kunyunyizia dawa katika mabwawa hayo
zilifanyika.
41. Mheshimiwa Spika, kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Maliasili, jumla ya
wakulima wa mpunga 60 wanaolima katika mabonde ya Mwera, Mtwango na Kianga
walipatiwa elimu ya afya juu ya kujikinga na maradhi ya Kichocho. Aidha, mikutano ya
16
kuhamasisha jamii juu ya kubadilisha tabia zinazochangia maambukizi ya maradhi
yasiyopewa kipaumbele ilifanyika.
Huduma za Elimu ya Afya
42. Mheshimiwa Spika, elimu ya afya juu ya kujikinga na maradhi ya kuambukiza na
yasiyoambukiza inaendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari, makongamano,
mikutano ya kijamii na katika skuli. Kwa mashirikiano na Manispaa na Halmashauri za
Unguja na Pemba, jumla ya wanafunzi 22,520 kutoka katikaskuli 109 walifikiwa na
kupatiwa elimu ya afya juu ya maradhi ya kuharisha na kipindupindu, usafi wa
mazingira, afya ya kinywa na meno pamoja na afya ya uzazi. Pia, jumla ya walimu 94
kutoka katika skuli zote za Wilaya ya Magharibi “A” walipatiwa elimu juu ya ugonjwa wa
Ebola.
43. Mheshimiwa Spika, sambamba na juhudi hizo, jumla ya vipindi 28 (redio 19 na
televisheni 9) vya kuelimisha jamii kuhusiana na masuala mbali mbali, ikiwemo maradhi
ya kuharisha, maradhi ya malaria, homa ya Ini, homa ya Ebola, Mtoto Njiti na afya ya
uzazi vilirushwa kwenye vyombo mbali mbali vya habari vikiwemo vya sekta binafsi na
jamii. Uhamasishaji wa jamii kuhusiana na maradhi ya kuharisha na kipindupindu pia
umefanyika kupitia gari la matangazo, michezo ya kuigiza pamoja na mikutano ya
hadhara iliyofanyika katika shehia 105 za Unguja na Pemba.
44. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha huduma za afya katika jamii, Wizara ya Afya kwa
mashirikiano na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za
SMZ, imetayarisha Mkakati wa Afya ya Jamii Zanzibar (Zanzibar Community Health
Strategy). Mkakati huo umezinduliwa rasmi na Mheshimiwa Waziri wa Biashara,
Viwanda na Masoko, Balozi Amina Salim Ali katika mkutano wa 12 wa Mapitio ya Sekta
ya Afya uliofanyika mwezi Februari, 2020. Napenda kutoa wito kwa viongozi na
wananchi wote wa Zanzibar kutoa mashirikano ya kutosha kwa wahudumu wa kujitolea
wa jamii ili kuhakikisha kwamba mkakati huu unatekelezwa, kwani wao ndio walengwa
wakubwa.
Huduma za Lishe
45. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Afya inachukuwa juhudi mbali mbali katika kuhakikisha
kwamba inajenga taifa lenye wananchi wenye afya nzuri. Miongoni mwa hatua
zinazochukuliwa ni utoaji wa huduma za matone ya Vitamin “A” kwa watoto walio na
umri wa chini ya miaka mitano, ambayo hutoa kinga ya mwili na kuepusha uwezekano
wa kupata utapiamlo na udumavu pamoja na kuugua maradhi mbali mbali.
17
46. Mheshimiwa Spika, jumla ya watoto 221,949 (Unguja145,524 na Pemba 76,425) sawa
na asilimia 97.8 ya watoto 226,916 wenye umri wa miezi 6-59 waliokadiriwa,
wamepatiwa matone ya vitamin A. Kwa upande wa dawa za minyoo, watoto 197,487
(Unguja 129,154 na Pemba 68,333) sawana asilimia 94.8 ya watoto 208,211 wenye
umri wa miezi 12-59 waliokadiriwa walipatiwa dawa hiyo. Aidha, watoto 109
waligunduliwa na utapiamlo mkali na 1,063 utapiamlo wa kiasi. Watoto wote
waliogunduliwa na utapiamlo walipewa rufaa katika vituo vya afya vilivyo karibu nao
kwa uchunguzi zaidi pamoja na kuanzishiwa matibabu (Kiambatisho namba 4).
47. Mheshimiwa Spika kama tujuavyo, suala la lishe ni mtambuka (multisectoral), hivyo,
Wizara kwa kushirikiana na taasisi nyengine imeshiriki katika kuandaa mpango shirikishi
wa miaka mitano wa kupambana na suala la lishe duni nchini. Mpango huo, ambao
unaratibiwa na kusimamiwa na Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, utekelezaji wake
unahusisha sekta mbali mbali, zikiwemo Elimu, Kilimo, Afya, Tawala za mikoa,
wanawake na watoto na mazingira, ambazo zinazohusika kwa namna moja au nyengine
katika kuimarisha lishe ya jamii. Wizara ya Afya tayari imeandaa mpango wa
utekelezaji na kuingiza katika bajeti ya mwaka 2020/2021 kwa ajili ya utekelezaji.
Huduma za Afya ya Mazingira
48. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha ubora na usalama wa maji, Wizara imetoa
mafunzo ya usalama wa maji ya kunywa kwa wahusika wa masuala ya maji pamoja na
wanajamii, kupitia wajumbe wa kamati za afya na kamati za maji za Shehia na wenye
maduka. Jumla ya washiriki 403 (Unguja 268 na Pemba 135) kutoka katika Manispaa za
Mjini, Magharibi “A” na Magharibi “B” kwa Unguja, Wete na Micheweni kwa Pemba
walipatiwa mafunzo hayo. Mafunzo hayo yalienda sambamba na ugawaji wa dawa za
kutibu maji ‘water guard’ uliofanywa na Maafisa wa Afya kutoka katika vituo vya afya.
Aidha, mafunzo ya uchukuaji wa sampuli za maji na kuzifanyia uchunguzi yalitolewa
kwa washiriki 24 kutoka katika Manispaa za Wilaya ya Mjini, Magharibi “A” na
Magharibi “B”; Skuli ya Sayansi za Afya (SUZA); Mamlaka ya Maji (ZAWA); Baraza la Mji
Wete; na Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni.
49. Mheshimiwa Spika, Jumla ya vidonge 1,051,033 vya kutibu maji (water guard 0.67g)
viligawiwa katika Wilaya zote 11 Unguja na Pemba katika Shehia ambazo hazina maji
kutoka Mamlaka ya Maji (ZAWA). Aidha, uchunguzi wa sampuli 57 za maji kutoka
katika vianzio tofauti vya maji, vikiwemo mifereji (sampuli 15), visima (sampuli 10) na
18
maji yaliyotuwama katika madimbwi (sampuli 24) ulifanyika katika Shehia 20 zilizo
katika hatari ya maambukizi ya Kipindupindu (Mchangani, Uzini, Dunga, Kiembeni,
Binguni, Jumbi, Ubago, Kidimni, Shaurimoyo, Kinuni, Dimani, Bububu, Jang’ombe,
Migombani, Kipungani, Uwandani, Magogoni, Chunga, Pangawe na Kwarara). Matokeo
yameonyesha kwamba sampuli 11 za maji hayo hazikuwa salama kwa matumizi ya
binadamu; hatua za kutoa elimu kwa wanajamii, kugawa dawa za kutibu maji na
kunyunyiza dawa ya klorini katika mabwawa yaliyoonekana na viluilui vya maradhi
zilichukuliwa.
Huduma za Afya ya Wafanyakazi
50. Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanya uchunguzi wa afya kwa wafanyakazi 14,304;
ambapo wafanyakazi 658 (asilimia 4.6) walibainika kuwa na matatizo mbali mbali ya
kiafya, yakiwemo maambukizi ya mkojo, minyoo, homa ya matumbo, maradhi ya ngozi,
kisukari, UKIMWI, Homa ya Ini B na C, shinikizo la damu na kaswende. Wafanyakazi
wote waliogundulika na matatizo walipatiwa matibabu na huduma stahiki. Aidha,
wafanyakazi 60 wamepatiwa mafunzo juu ya usalama wa afya kazini.
Huduma za Afya ya Msingi ya Akili
51. Mheshimiwa Spika, jumla ya ziara 37 za kutoa huduma za masafa “outreach”za afya ya
akili zilifanyika katika vituo vya afya vya Uzini, Chwaka, Unguja Ukuu, Nungwi,
Matemwe, Bumbwini Misufini, Donge Vijibweni, Kombeni, Kendwa, Bumbwisudi,
Tumbatu Gomani na Hospitali za Makunduchi na Kivunge. Katika zoezi hilo wagonjwa
1,109 walipatiwa huduma za afya ya msingi ya akili. Aidha, wahudumu wa afya 103
(Unguja 53 na Pemba 50) kutoka katika vituo vya afya vya daraja la pili (PHCU+)
walipatiwa mafunzo ya kuwatambua wagonjwa wa afya ya akili. Vile vile, mafunzo ya
tiba ya mazungumzo ya afya ya akili yalitolewa kwa wahudumu wa kujitolea 80 kutoka
katika Shehia za Unguja zilizomo katika Wilaya za Kusini, Kaskazini A, Mjini, Magharibi A
na Magharibi B. Pia, mafunzo hayo yalitolewa kwa wanafunzi wa Skuli 22 za Sekondari
Unguja na Pemba; ambapo wanafunzi 1,500 na walimu 37 walifikiwa na kupatiwa elimu
hiyo. Sambamba na mafunzo hayo, vipindi vitatu (3) kuhusiana na afya ya akili
vilirushwa hewani kupitia redio za ZBC, Zenj FM na Assalam FM.
Huduma za Afya ya Msingi ya Macho
52. Mheshimiwa Spika, huduma za matibabu ya macho kwa njia ya masafa zilitolewa katika
vijiji saba (7) na kwenye vituo vya afya katika Wilaya zote za Unguja. Vijiji vilivyofikiwa
19
na huduma hizo ni Mwera, Kibeni, Chaani, Makunduchi, Kianga, Kiwengwa na Taveta.
Jumla ya wananchi 3,119 walichunguzwa, ambapo wananchi 782 (wanaume 252na
wanawake 530) waligunduliwa na matatizo mbali mbali ya macho. Wananchi 213
walipewa rufaa kwa ajili ya matibabu zaidi kutokana na matatizo mbali mbali,
wakiwemo wananchi 63 wenye matatizo ya mtoto wa jicho, 102 wenyeuhakiki mbaya
wa mwanga machoni na 48 waligundulika na matatizo mengine tofauti ya macho.
53. Mheshimiwa Spika, ili kupunguza upofu usio wa lazima, wanafunzi 506 wakiwemo wa
skuli zaKinuni na Kijitoupele walifanyiwa uchunguzi wa afya ya macho. Wanafunzi 32
waligundulika na matatizo ya uhakiki mbaya wa mwanga machoni, hivyo walipatiwa
rufaa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu zaidi. Nachukua fursa hii
kuishukuru Manispaaa ya Wilaya ya Magharibi B kwa mashirikiano makubwa waliyotoa
katika kufanikisha zoezi hili la uchunguzi wa afya ya macho katika skuli. Aidha,
wahudumu wa afya 80 (Unguja 50 na Pemba 30) walipatiwa mafunzo ya awali ya
uchunguzi wa afya ya macho. Mafunzo hayo yalilenga kupunguza msongomano wa
wagonjwa wa macho katika Hospitali za rufaa na kutoa uwiano wa huduma kwa
wagonjwa wa macho katika vituo vya afya ili kuzuwia upofu usio wa lazima.
54. Mheshimiwa Spika, kwa kushirikiana na shirika lisilo la Serikali la Sight Savers kutoka
Sweden, kambi ya upimaji na ugawaji wa miwani kwa wananchi wenye shida ya uhakiki
mbaya wa nuru zilifanyika katika Wilaya ya Kaskazini A na Wilaya ya Kusini Unguja.
Katika zoezi hilo jumla ya wananchi 1,330 (wanaume 403 na wanawake 833) walipimwa
na kupatiwa miwani bure.
Huduma za Ufuatiliaji wa Mienendo ya Maradhi
55. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Afya kwa mashirikiano na Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais imetayarisha Mpango wa miaka 10 wa kumaliza Kipindupindu Zanzibar (ZACCEP
2018 - 2027). Mpango huo shirikishi wenye lengo la kutokomeza kabisa maradhi ya
Kipindupindu hapa Zanzibar ifikapo mwaka 2027, ulizinduliwa na Mheshimiwa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein katika
Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil, tarehe 10 Septemba, 2019. Mpango huo
unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, utekelezaji wake unahusisha taasisi
zote zinazohusika kwa njia moja au nyingine katika kudhibiti maradhi ya kipindupindu,
Wizara ya Afya kwa upande wake inatoa ushauri na kusimamia shughuli za kitaalamu.
20
56. Mheshimiwa Spika, kama nilivyotangulia kueleza mwanzoni kwamba nchi yetu imepata
maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi aina ya Corona SARS-
Cov-2. Mgonjwa wa mwanzo wa maradhi hayo hapa Zanzibar aliripotiwa tarehe 18
Machi, 2020, ambaye alikuwa ni raia wa kigeni. Hadi kufikia tarehe 31 Machi, jumla ya
wagonjwa 105 wamegundulika kuwa na virusi vya Corona; kati yao, watatu (3) ni
wageni na 102 wenyeji. Mwenendo wa maradhi hayo kwa sasa, unathibitisha uwepo
wa maambukizi katika jamii, ikimaanisha kwamba tumeanza kuambukizana wenyewe
kwa wenyewe.
57. Mheshimiwa Spika, kufuatia hali hii kwa hatua za awali, Wizara imeandaa muongozo
wa utambuzi wa mgonjwa mwenye maambukizi ya COVID -19 (case definition), ambao
unatumiwa na watumishi wa afya katika hospitali na vituo vya afya. Aidha, fomu
maalumu za ufuatiliaji wa wageni wanaoingia kutoka nchi hatarishi zenye maambukizi
ya COVID-19 pamoja na wale wanaohisiwa kuwa na dalili za viruzi hivyo zimeandaliwa
na kusambazwa kwa Maofisa wa Afya wa Wilaya kwa ajili ya ufuatiliaji.
58. Mheshimiwa Spika, mpango maalum wa kudhibiti ugonjwa wa Covid-19 umeandaliwa
ambao tayari umeridhiwa na Serikali. Mpango huo unajumuisha sekta mbali mbali na
umebainisha majukumu ya kazi kwa wajumbe wa timu za dharura (Emergency
Response Teams - RRT). Vile vile, mafunzo juu ya ufuatiliaji wa ugonjwa wa Covid-19 na
Ebola yametolewa kwa watendaji 40 wakiwemo maofisa ufuatiliaji, wakurugenzi
wasaidizi wa afya kutoka katika Halmashauri na Manispaa na maafisa takwimu kutoka
katika kila Wilaya Unguja na Pemba. Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wa
kubaini na kugundua, kumfuatilia na namna ya kumripoti mgonjwa mwenye dalili za
magonjwa hayo. Aidha, mafunzo hayo pia yalitolewa kwa wahudumu 70 wa afya wa
kujitolea kwenye jamii kutoka Wilaya zote za Unguja.
59. Mheshimiwa Spika, mafunzo mengine maalum ya ugonjwa huu yameendelea kutolewa
kwa maofisa 25 wa kada za afya; wakiwemo madaktari, wauguzi, Maabara, Fundi sanifu
dawa, Wafamasia, Maofisa wa Afya na watoa elimu ya afya. Mafunzo haya pia,
yalitolewa kwa timu ya kukabiliana na maradhi ya mripuko katika Wilaya za Pemba. Vile
vile, wafanyakazi 39 wa huduma za afya bandarini walipatiwa mafunzo ya namna ya
kufanya ukaguzi kwa wasafiri wanaoingia kupitia bandarini na viwanja vya ndege kwa
lengo la kuchukuwa tahadhari ya kuenea kwa virusi vya Corona hapa nchini.
60. Mheshimiwa Spika, katika muendelezo wa kujenga uelewa kwa jamiijuu ya maradhi ya
Covid-19, Wizara imekuwa ikitoa taaluma kwa wananchi kupitia vyombo vya habari
kuhusiana na ugonjwa huo. Niwaombe Viongozi wote pamoja na Wajumbe wa Baraza
hili kuwahimiza wananchi katika majimbo yao kufuatilia kwa makini maelezo yote
yanayotolewa na wataalamu wa afya kuhusiana na janga hili la kitaifa lililoikumba dunia
nzima.
21
Huduma za Afya Bandarini na Uwanja wa Ndege
61. Mheshimiwa Spika, zoezi la ukaguzi wa vyombo na abiria wanaoingia nchini lilifanyika.
Jumla ya vyombo 2,749 vilivyowasili vilifanyiwa ukaguzi; vyombo 13 vilibainika kuwa na
wadudu waenezao maradhi (mende na panya). Hatua ya upulizaji dawa na uwekaji wa
mitego ilifanyika katika vyombo hivyo. Sambamba na ukaguzi wa vyombo, abiria
584,198 waliopitia bandarini na uwanja wa ndege walikaguliwa ili kubaini uwepo wa
maambukizi ya ugonjwa, hata hivyo hakukuwa na abiria aliyegundulika kuwa na
maradhi ya kuambukiza.
62. Mheshimiwa Spika, katika hatua nyengine, abiria 576 waliotoka nchi zenye mripuko wa
Ebola wamepimwa joto na kujazishwa fomu maalumu za ufuatiliaji. Aidha, wageni 117
walioingia kutoka Congo DRC na 66 kutoka Uganda wamerikodiwa na kuripotiwa
pamoja na kufuatiliwa kwa karibu kupitia maofisa ufuatiliaji wa Wilaya, ili kubaini kama
wana dalili za ugonjwa wa Ebola; pia, hakukuwa na mgonjwa yeyote aliyeripotiwa kuwa
na maambukizi ya ugonjwa huo. Aidha, huduma za utoaji wa chanjo kwa abiria
wanaosafiri nje ya nchi na wageni wanaoingia nchini ziliendelea kutolewa. Hadi kufikia
Machi 2020, wasafiri 2,218 walipatiwa chanjo za kuwakinga na maradhi mbali mbali
yakiwemo ya homa ya manjano.
63. Mheshimiwa Spika, nilieleza katika hotuba ya bajeti inayomalizika (2019/2020)
kwamba Wizara imepanga kutayarisha mpango wa dharura wa kukabiliana na miripuko
ya maradhi hatari ya kuambukiza (Public Health Emergency Contigency Plan) kwa
mujibu wa kanuni za afya za kimataifa (International Health Regulations - (IHR) 2005).
Napenda kuwaarifu Wajumbe wa Baraza hili kwamba tayari mpango huu umekamilika
na utekelezaji wake umeanza.
22
PROGRAMU YA HUDUMA ZA TIBA
64. Mheshimiwa Spika, programu hii inajumuisha shughuli za utoaji wa huduma za afya
katika Hospitali za ngazi ya Vijiji hadi Mkoa, pamoja na huduma zinazotolewa kupitia
mabaraza ya kitaaluma (Baraza la Madaktari na Baraza la Wauguzi na Wakunga) na Bodi
ya Hospitali Binafsi. Huduma nyengine ni zile zinazotolewa na Bohari ya Dawa, Ofisi ya
Mfamasia Mkuu wa Serikali na Mpango wa Damu Salama, pamoja na huduma za
uchunguzi zinazosimamiwa na Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi, Wakala wa
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Kitengo cha Huduma za Uchunguzi.
Programu hii pia, inasimamia shughuli za Kitengo cha Huduma za Mkono kwa Mkono.
Vile vile, inasimamia mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Kisasa ya Rufaa na Kufundishia
Binguni, pamoja na mradi wa Kuzipandisha Hadhi Hospitali za Vijiji Kufikia Ngazi ya
Wilaya na za Wilaya Kufikia Ngazi ya Mkoa.
65. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2019/20, Program ya Tiba ilitengewa jumla
ya Shilingi 49,296,254,000/=, kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbali mbali. Hadi kufikia
Machi 2020, Shilingi 29,970,488,324/= sawa na asilimia 76.2 ya fedha zilizotengwa kwa
robo tatu zilipatikana na kutumika kwa kutekeleza shughuli zilizopangwa, ambazo ni:
i. Kuanza ujenzi wa majengo ya huduma za dharura, huduma za uchunguzi na
huduma za upasuaji katika eneo lililotengwa kwa ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya
Rufaa na Kufundishia ya Binguni;
ii. Kukamilisha ujenzi wa jengo la ghorofa la wodi ya wazazi na watoto katika Hospitali
ya Wilaya ya Kivunge;
iii. Kuendelea na hatua za matayarisho ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi katika
Hospitali ya Abdalla Mzee, Mkoani Pemba;
iv. Kuendelea na ujenzi wa Bohari ya Dawa Vitongoji Pemba;
v. Kuendelea na ujenzi wa Maabara ya Wakala ya Chakula, Dawa na Vipodozi;
vi. Ununuzi na usambazaji wa dawa, vifaa vya utibabu na “reagents” katika hospitali na
vituo vya afya;
vii. Kukusanya damu ili kukidhi mahitaji yaliyopo pamoja na kuanzisha kituo cha
ukusanyaji damu katika Hospitali ya Wilaya ya Makunduchi;
viii. Kuimarisha mfumo wa upimaji damu wa automatiki (AUTOMATION)
Utekelezaji wa shughuli hizo kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Machi 2020, kwa mujibu
wa programu ndogo husika ni kama ifuatavyo:
Programu ndogo ya Huduma za Matibabu
66. Mheshimiwa Spika, shughuli za matibabu ziliendelea kutolewa kwa wagonjwa wote
waliohudhuria katika hospitali kwa ajili ya kupata huduma. Katika kipindi cha Julai 2019
23
hadi Machi 2020, jumla ya mahudhurio ya wagonjwa wa nje 352,131 (wanaume
149,798na wanawake 202,333) yaliripotiwa katika Hospitali za vijiji, Wilaya, Mkoa
pamoja na hospitali binafsi na jumla ya wagonjwa 36,036 (wanaume 6,502 na
wanawake 29,534) walilazwa katika hospitali hizo, ambapo wagonjwa 474 walifariki
dunia; Mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahali pema Peponi, Amin (Kiambatisho
Namba 5). Pia,jumlaya wagonjwa 118,858 waliripotiwa kuhudhuria katika kliniki za
huduma za maradhi maalumu (Kiambatisho namba 6). Taarifa hizi hazihusishi
wagonjwa waliopatiwa huduma katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
67. Mheshimiwa Spika, jumla yawagonjwa 328 walipitishwa na Bodi ya Madaktari kwa ajili
ya kupatiwa huduma za matibabu ya rufaa nje ya nchi. Kati yao, wagonjwa 225
walipelekwa Tanzania Bara na 76 walisafirishwa nje ya nchi (India) kwa ajili ya matibabu
zaidi. Jumla ya Shilingi 4,163,561,488/= zilitumika, ambazo ni sawa na asilimia 97.7 ya
fedha zilizotengwa (Shilingi 4,259,685,429/=) kwa ajili ya matibabu ya rufaa za
wagonjwa nje ya Zanzibar.
Huduma ya Upatikanaji, Uhifadhi na Usambazaji wa Dawa, Zana na Vifaa vya Utibabu
68. Mheshimiwa Spika, Ilani ya CCM ya mwaka 2010 - 2015 na ile ya mwaka 2015 - 2020
imesisitiza juu ya uimarishaji wa huduma za afya nchini. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
imeweza kufanikisha hilo, kwa kuhakikisha kwamba hospitali na vituo vya afya
vinakuwa na dawa, vifaa vya utibabu na “reagents” za kutosha ili wananchi
wasisumbuke kupata huduma za afya pale wanapohitaji. Jumla ya Shilingi bilioni15.8
zilitengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa katika bajeti ya mwaka wa fedha wa
2019/2020, ambapo hadi kufikia Machi 2020, Shilingi bilioni 10.0 zilitumika kwa ajili ya
ununuzi wa dawa muhimu, vifaa vya utibabu na “reagents”. Dawa, zana na vifaa vya
utibabu vilivyonunuliwa vimesambazwa katika hospitali na vituo vyote vya afya Unguja
na Pemba. Takwimu zinaonesha kwamba asilimia ya upatikanaji wa dawa muhimu
(tracer medicines) imeongezeka kutoka asilimia 90 mwaka 2018/2019 hadi asilimia 94
kufikia Machi, 2020. Hayo ni mafanikio makubwa yaliyopatikana katika eneo la
upatikanaji wa dawa, hali inayowapa wananchi faraja na unafuu wa kupata huduma za
afya. Uwepo wa dawa muhimu katika hospitali na vituo vya afya unaendeleza dhamira
ya Mapinduzi ya 1964 ya kutoa matibabu bure kwa wananchi wote bila ya ubaguzi wa
aina yoyote. Hatuna budi kuipongeza Serikali ya Awamu ya Saba, chini ya uongozi wa
Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kulitekeleza hili kwa vitendo.
69. Mheshimiwa Spika, zoezi la kufanya makisio ya mahitaji ya dawa (quantification) kwa
mwaka wa fedha 2020/2021 limefanyika, ambapo jumla ya Shilingi bilioni 19.3
zinahitajika kwa ununuzi wa dawa, vifaa vya utibabu na “reagents; zikiwemo dawa za
saratani na za huduma za kusafisha figo, pamoja na vifaa vya huduma za mionzi na
24
radiologia kwa hospitali zote Unguja na Pemba. Kwa mujibu wa bajeti iliyotengwa kwa
mwaka 2020/2021, Wizara ya Afya imepanga kutumia Shilingi bilioni 17.7 kwa ajili ya
ununuzi wa dawa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 12 ya bajeti ya dawa ya mwaka
2019/2020. Aidha, makisio ya dawa za Kifua Kikuu na Ukoma pekee yalifanyika na
kuonyesha kwamba kwa mwaka 2020/2021, Shilingi 396,036,962/= zinahitajika kwa
ajili ya ununuzi wa dawa za maradhi hayo. Fedha za ununuzi wa dawa hizi zimepangwa
kupitia msaada wa Global Fund.
Huduma ya Tiba Asili na Tiba Mbadala
70. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi kinachoripotiwa, Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala
limeweza kusajili waganga wa tiba asili 18, msaidizi mganga mmoja, kliniki moja (1) na
maduka ya dawa asili 12. Jumla ya waganga wa tiba asili na wauza dawa za asili 181
walifanyiwa ukaguzi kwa mujibu wa Sheria Namba 8 ya Baraza la Tiba Asili na Tiba
Mbadala ya mwaka 2008. Katika ukaguzi huo waganga 174 (asilimia 96.1)
wamegundulika kufuata miongozo na waganga saba (7) hawakufuata muongozo,
ambapo hatua stahiki za kuwafungia biashara zao zilichukuliwa.
Huduma za Damu Salama
71. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi hiki cha utekelezaji, jumla ya ‘uniti’ 10,458 za damu
zilikusanywa sawa na asilimia 65.4 ya lengo la kukusanya ‘uniti’ 16,000 kwa mwaka.
Uniti za damu zilizokusanywa baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kuangalia virusi vya
UKIMWI, kaswende na homa ya Ini B na C zimesambazwa katika hospitali zote za
Serikali na binafsi zinazotoa huduma ya tiba ya damu Unguja na Pemba.
Huduma za Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi
72. Mheshimiwa Spika, Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi ilifanya ukaguzi katika hospitali
na vituo vya afya vya binafsi 78. Vituo vitatu (3) vilisimamishwa kutoa huduma
kutokana na kasoro zilizogundulika; vituo hivyo ni Dr. Ali Amour Paediatric Clinic,
Rosath Medical Centre na Marie Stopes Dispensary. Hata hivyo, hivi sasa huduma katika
vituo hivyo zimerejeshwa baada ya kutekeleza maagizo waliyopewa. Aidha, jumla ya
maombi 11 ya kufungua vituo vipya yamepokelewa; ambapo kati yao maombi sita (6)
yalikubaliwa na kupatiwa usajili baada ya kukidhi vigezo na maombi matano (5)
yanaendelea na hatua za ukamilishaji wa vigezo vinavyohitajika.
Huduma za Baraza la Wauguzi na Wakunga na Baraza la Madaktari
73. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha huduma za uuguzi na ukunga, Baraza la wauguzi
na wakunga limeanza kutayarisha Mpango Mkakati wa Baraza la Wauguzi na Wakunga.
Katika kipindi cha utekelezaji, Baraza la Wauguzi na Wakunga limesajili na kutoa leseni
kwa wauguzi na wakunga 437 (wapya 245 na marudio192). Aidha, zoezi la ukaguzi wa
25
kuangalia shughuli za kazi za uuguzi limefanyika katika vyuo vitatu (3) vinavyotoa
taaluma ya uuguzi na ukunga (Zanzibar University - ZU, Zanzibar School of Health na
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar – SUZA), hospitali saba (7) na vituo vya afya 12.
Kutokana na umuhimu wa taaluma ya uuguzi Shirika la Afya Ulimwenguni limeutangaza
mwaka 2020 kuwa ni mwaka wa uuguzi, hivyo nachukua fursa hii kuwaomba sana
wauguzi wote nchini kufuata maadili ya uuguzi wakati wanapowahudumia wananchi.
Kwa upande wa Baraza la Madaktari, jumla ya madaktari wapya 294 wamesajiliwa na
kupewa leseni.
Programu ndogo ya Huduma za Uchunguzi
74. Mheshimiwa Spika, huduma za uchunguzi ziliendelea kutolewa kwa wagonjwa
waliohitaji huduma hiyo, ambapo jumla ya vipimo 203,362 vilifanyika vikiwemo; vipimo
vya maabara (167,360), X-ray (11,545) na ultrasound (24,457). Katika kuimarisha
huduma za uchunguzi, Wizara kupitia Kitengo cha huduma za uchunguzi, imefanya
ukaguzi katika hospitali saba (7) na vituo vya afya 41. Ukaguzi umebaini kuwepo kwa
ongezeko la wafanyakazi wa maabara katika hospitali zilizokaguliwa na kuwepo kwa
mashine ya Gene-Xpert katika Hospitali ya Wilaya ya Kivunge. Changamoto mbali mbali
zilibainika, ikiwemo ufinyu wa nafasi za kufanyia shughuli za maabara na kukosekana
kwa miongozo ya kazi (SOP); changamoto hizi zimeanzwa kufanyiwa kazi, ikiwa pamoja
na kufanya mapitio ya SOP na kuzisambaza katika maabara zote.
Huduma za Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali
75. Mheshimiwa Spika, Wakala ya Maabara ya Mkemia Mkuu imefanya ukaguzi katika
maeneo ya uhifadhi wa kemikali ya bandari, viwanda, skuli za Serikali na za binafsi,
pamoja na maghala. Katika ukaguzi huo, imebainika kwamba maeneo mengi yamefikia
kiwango cha kuhifadhi kemikali kwa mujibu wa miongozo iliyowekwa na maabara.
Aidha, zoezi la usajili wa wajasiriamali, wazalishaji na wasafirishaji wa kemikali
limefanyika, ambapo vibali 1,314 vya kuingiza kemikali nchini vilitolewa na maeneo 56
ya kuhifadhi kemikali yalisajiliwa. Vile vile, uchunguzi wa kesi 10 za vinasaba na sampuli
32 za matukio tofauti ikiwemo kesi za udhalilishaji, utambuzi wa vinasaba, na utambuzi
wa wazazi umefanyika. Pia, uchunguzi wa vielelezo 765; vikiwemo bangi (185), dawa
za kulevya (169), mkojo (107) na pombe (53)kutoka taasisi mbali mbali na watu binafsi
umefanyika kwa lengo la kusaidia kutoa ushahidi katika kesi zinazoendeshwa katika
mahakama.
Huduma za Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi
76. Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Wakala wa Dawa, Chakula na Vipodozi imefanya ukaguzi
katika maeneo 2,775 (Unguja 1,894 na Pemba 881)sawa na asilimia 96 ya maeneo
2,900 ya biashara za chakula, dawa, vipodozi na vifaa vya utibabu yaliyopangwa
26
kukaguliwa. Katika ukaguzi huo, maeneo 91 (Bucha 5, Bekari 20, mauka ya Chakula 7,
Famasi 5 na OTC 54) yalizuiwa kufanya biashara kutokana na kutokidhi viwango. Katika
hatua nyengine, tani 1,122 za bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu zilikamatwa;
tani 353.5 (chakula 329.5, dawa 18.5 na vipodozi 6.5) zimeteketezwa; na tani 1.5
inasubiri kuteketezwa baada ya kukamilika taratibu za kisheria. Vile vile, tani 496
zimerudishwa sehemu zilipotoka na tani 270 zinasubiri kurudishwa baada ya kukamilika
taratibu za kisheria. Takriban bidhaa zilizotekelezwa zinakadiriwa kuwa na thamani ya
Shilingi 330,050,000/=.
77. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa usajili, Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi
wameweza kusajili majengo 1,357 (Unguja 903 na Pemba 454) sawa na asilimia 59 ya
majengo 2,300 ya biashara ya kutoa huduma za chakula, dawa na vifaa vya utibabu
yaliyopangwa kusajiliwa. Kati ya majengo hayo, 356 yalikuwa maombi mapya na
majengo 1,001 ya uhuishaji wa vibali. Aidha, maombi mapya ya usajili wa bidhaa 150
yalipokelewa, ambapo maombi ya bidhaa 140 (asilimia 93) yamepatiwa usajili baada ya
kufanyiwa tathmini na kukidhi viwango vilivyowekwa na maombi yaliyosalia (47)
yanaendea kufanyiwa tathmini.
78. Mheshimiwa Spika, shughuli nyengine zilizofanywa na taasisi hii ni uchunguzi wa
sampuli 1,320 za chakula, dawa na vipodozi; Sampuli hizo zinahusisha 1,212 za
Chakula,74za dawa, 10za dawa za miti shamba na sampuli 16 za vipodozi. Kati ya
Sampuli hizo, sampuli 17 (asilimia 1.3)zachakula 13, dawa 3 na moja yadawa za
mitishamba hazikufaa kwa matumizi ya binadamu kutokana na kutokidhi viwango
vilivyoweka.
27
UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
Mradi wa Ujenzi wa Bohari Kuu ya Dawa Pemba na Maabara ya Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi
79. Mheshimiwa Spika, dhamira ya Serikali ya kujenga bohari ya dawa huko Pemba kwa
ajili ya kuondosha tatizo la uhifadhi wa dawa imetekelezwa. Ujenzi wa jengo hilo la
Bohari huko Vitongoji, Pemba umeanza katika mwaka wa fedha 2018/2019 na
tayarijengolimeshaezekwa na liko katika hatua za umaliziaji, linategemewa kukabidhiwa
ndani ya mwaka huu wa 2020. Kukamilika kwa Bohari hiyo huko Pemba kutasaidia sana
uhifadhi wa dawa kisiwani humo na kuongeza upatikanaji wa dawa; pia Serikali itakuwa
imetimiza ahadi yake kwa wananchi katika eneo hilo kwa mujibu wa Ibara 102 (k) ya
Ilani ya CCM (2015 – 2020) inayosisitiza suala zima la uhifadhi wa dawa.
80. Mheshimiwa Spika, mradi mwengine uliotekelezwa ni ujenzi wa maabara ya Chakula,
Dawa na vipodozi ulioanza katika mwaka wa fedha 2018/2019. Naomba kutoa taarifa
kwamba ujenzi huo unaendelea katika ghorofa ya tatu, ambapo hadi kufikia tarehe 26
Machi 2020, ujenzi huo tayari ulishafikia asilimia 52 naumepangwa kukamilika katika
mwaka wa fedha 2020/2021.
Mradi wa Kupandisha Hadhi Hospitali za Vijiji na Wilaya
81. Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kwamba katika mwaka wa fedha 2018/2019, Serikali
ilianza ujenzi wa jengo la ghorofa kwa ajili ya kupanua huduma za mama na mtoto
katika Hospitali ya Wilaya ya Kivunge, ikiwa ni katika kutimiza ahadi ya Serikali ya
awamu ya saba kwa wananchi ya kuifanya hospitali hiyo iweze kutoa huduma za ngazi
ya Mkoa. Jengo hilo la ghorofa mbili liliwekwa jiwe la msingi na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan tarehe 09 Januari,
2020 wakati wa shamra shamra za sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi
ya Zanzibar. Napenda kuwaarifu wajumbe na wananchi wote wanaofuatilia hotuba hii
kwamba jengo hilo limekamilika na tarehe 24 Aprili, 2020 limekabidhiwa rasmi kwa
Wizara. Baadhi ya vifaa vinavyohitajika kwa Hospitali hiyo vimeanza kupokelewa
kutoka kwa washirika mbali mbali, akiwemo mfanya biashara BOPAR, ambae ameahidi
kutoa vitanda 140, kiti kimoja cha kung’olea meno na mashine moja ya “ultrasound”.
Wizara inatoa shukrani za dhati kwa mfanya biashara huyo na tunaomba wengine
wajitokeze katika kusaidia azma hii njema ya Serikali.
28
82. Mheshimiwa Spika, katika hatua nyengine,Wizara imekamilisha taratibu za maandalizi
ya ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Chake-Chake Pemba; mkataba
wa ujenzi umesainiwa na mkandarasi ameshakabidhiwa eneo kwa ajili ya ujenzi
unaotarajiwa kuanza muda wowote kutoka sasa. Kwa upande wa ujenzi wa nyumba za
madaktari katika Hospitali ya Mkoa ya Abdalla Mzee, Wizara imekamilisha matayarisho
yanayohitajika, ikiwemo kusaini Mkataba wa Makubaliano na Serikali ya Jamhuri ya
Watu wa China, ambayo imeahidi kugharamia ujenzi huo. Wakandarasi kutoka China
walitarajiwa kufika Zanzibar katika mwezi wa Machi 2020 kwa ajili ya kuanza ujenzi huo,
lakini kutokana na hali ya sasa ya dunia ya kuzuka kwa maradhi ya Covid-19
wakandarasi hao wamezuiliwa kuja Zanzibar hadi hapo hali itakapotengemaa. Hata
hivyo, uongozi wa Wizara ya Afya umefanya mawasiliano na Balozi Mdogo wa China
aliyepo Zanzibar na amekiri kwamba makubaliano hayo ya ujenzi wa nyumba za
madaktari katika Hospitali ya Abdalla Mzee bado yapo pale pale na shughuli za ujenzi
zitaanza mara moja pale tu hali itakaporuhusu.
Mradi wa Ujenzi wa Hospitali kisasa ya Rufaa na Kufundishia Binguni
83. Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kwamba kiu ya walio wengi ni kuona azma ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ya kujenga Hospitali kisasa ya rufaa na ya kufundishia katika
eneo la Binguni Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja imefanikiwa. Serikali ilitegemea
kupata mkopo kutoka mfuko wa Saudi, Badea na Kuwait kupitia Serikali ya Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kwa ajili wa ujenzi wa hospitali hiyo. Kutokana na kuchelewa
kupatikana kwa fedha hizo, Serikali iliamua kutenga fedha kidogo kidogo kila mwaka ili
ujenzi huo uanze katika muda muafaka. Hivyo, katika bajeti ya mwaka 2018/2019,
Serikali ilitenga Shilingi Bilioni 3.97 kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi huo, ambapo
Wizara ya Afya iliajiri mshauri mwelekezi kwa ajili ya kuandaa michoro pamoja na
utayarishaji wa gharama za ujenzi (BOQ); kazi hiyo ilikamilika na kuwasilishwa Serikalini.
84. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa nia njema kabisa, imeamua kutumia Kampuni ya
Serikali ya Ujenzi, inayowahusisha wahandisi wa Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar na wataalamu wengine wa ujenzi. Maamuzi haya yamelenga kupunguza
gharama za ujenzi huo, hasa ikitiliwa maanani kwamba wahandisi hawa wameonesha
kuwa na uwezo wa kutosha kutokana na majengo ambayo tayari wameyajenga. Aidha,
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na mshauri mwelekezi itaendelea kuwa msimamizi na
itafanya ufuatiliaji wa karibu katika kuhakikisha ubora wa majengo na mahitaji yote
29
yanayotakiwa kuwepo katika hospitali ya aina hiyo. Katika bajeti ya mwaka 2019/2020,
Serikaliilitenga Shilingi Bilioni 6, kwa ajili yakuanza ujenzi wa majengo manne; jengo la
huduma za dharura, jengo la uchunguzi wa maradhi (Central pathology laboratory) na
radiolody; na jengo la huduma za upasuaji.
PROGRAMU YA UENDESHAJI NA URATIBU WA WIZARA YA AFYA
85. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa programu hii unahusisha shughuli za programu
ndogo za Uongozi na Utawala; Sera, Mipango na Utafiti pamoja na Uratibu wa shughuli
za Afya Pemba. Katika mwaka wa fedha 2019/2020, Wizara ilitenga Shilingi
17,428,825,000/= sawa na asilimia 19.7 ya bajeti ya Wizara. Hadi kufikia Machi, 2020
Shilingi 12,968,973,028/=, sawa na asilimia 97.5 ya fedha zilizotengwa kwa robo tatu
zilitumika kutekeleza kazi mbali mbali zilizopangwa, zikiwemo:
i. Kusomesha madaktari na wafanyakazi wa kada nyengine za afya zilizopewa
kipaumbele na Wizara kwa mujibu wa mahitaji;
ii. Kukamilisha utayarishaji wa Mpango Mkakati wa IV wa Afya;
iii. Kuendelea na utafiti wa mimea inayotumika kwa Tiba asili Zanzibar;
iv. Kuratibu vikao vya pamoja na washirika mbali mbali wa masuala ya afya;
v. Kutayarisha muongozo wa ukaguzi wa huduma za Afya (National Integrated
Supervision Guideline);
Taarifa ya utekelezaji wa shughuli hizo katika kipindi kinachoripotiwa inaelezewa
kwa kina kupitia programu ndogo husika kama ifuatavyo:
Programu ndogo ya Uongozi na Utawala
86. Mheshimiwa Spika, Wizaraimeajiriwafanyakazi 602 wa kada mbali mbali (Unguja 445
na Pemba 157), wakiwemo Madaktari (59), Wauguzi (31), Daktari wa Meno (15),
Wafamasia (5), Fundi Sanifu Maabara (59) na Fundi Sanifu dawa (39). Aidha,
wafanyakazi 128 wamerudi kutoka masomoni (Kiambatisho namba 7a na 7b).
Ongezeko hili la wafanyakazi katika mwaka 2020 linafanya idadi ya madaktari
wazalendo katika hospitali za Zanzibar kufikia 345 na wauguzi 1,328. Hadi kufikia Machi
2020, idadi hii ya madaktari inafanya daktari mmoja kuhudumia watu 4,445 (1: 4,445)
na muuguzi mmoja kuhudumia watu 1,258 (1: 1,258).
87. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha sekta ya afya inakuwa na watendaji wa
kutosha;wafanyakazi 133, wakiwemo madaktari bingwa 31 na wataalamu wengine wa
afya pamoja na wafanyakazi wa fani nyengine wamepelekwa masomoni katika kipindi
cha Julai 2019 hadi Machi 2020; hivyo,kufanya jumla ya wafanyakazi wanaoendelea na
30
masomo ya muda mrefu ndani na nje ya nchi kufikia 450. Katika kipindi hicho,
wafanyakazi 39 wamestaafu kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi na wafanyakazi saba
(7) wamefariki dunia Mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahali pema Peponi, Amin.
88. Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanya ufuatiliaji wa wafanyakazi waliopo masomoni katika
vyuo mbali mbali vya Tanzania Bara, vikiwemo Muhimbili University of Health and
Allied Sciences (MUHAS), Catholic University of Health and Allied Sciences (CUHAS),
University of Dodoma (UDOM) and Kilimanjaro Christian Medical University College
(KCMUCO) Moshi) ili kujua maendeleo na changamoto zinazowakabili. Katika ufuatiliaji
huo wafanyakazi 57 wa kada mbali mbali walifanyiwa uhakiki. Uhakiki huo umebaini
kwamba wafanyakazi wote wanaendelea na masomo kulingana na kozi zao, hakukuwa
na mfanyakazi aliyebadilisha kozi kama ilivyokuwa hapo kabla.
89. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuimarisha maslahi ya wafanyakazi kwa mujibu wa
ngazi za elimu na muda wa ajira, Wizara imeandaa mapendekezo ya muundo mpya wa
utumishi kwa kada za afya. Muundo huo tayari umewasilishwa Tume ya Utumishi
Serikalini kwa hatua za mazingatio. Ni matumaini ya Wizara kwamba utekelezaji wa
muundo huu utasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa malalamiko ya wafanyakazi wa
fanihizo.
90. Mheshimiwa Spika, kupitia programu hii mikataba na hati za mashirikiano (MoU) 50
imesainiwa, inayojumuisha Mikataba tisa (9) yenye thamani ya Shilingi 16,
863,910,060/= kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa vya utibabu na “reagents”. Aidha,
miswada ya Sheria ya Kuanzisha Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar na wa Kuanzisha
Baraza la Usajili na Usimamizi wa Wataalamu wa Maabara za Kuchunguza Maradhi ya
Binadamu imeandaliwa na tayari imepitishwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar cha mwezi wa Aprili, 2020. Vile vile, kanuni 11 za Wakala wa Chakula, Dawa na
Vipodozi (ZFDA) zimeandaliwa kwa kuwekwa masharti bora ya utekelezaji wa Sheria ya
Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2006 (na Marekebisho ya 2017). Kanuni hizo
tayari zimepelekwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.
Programu ndogo ya Mipango, Sera na Utafiti
91. Mheshimiwa Spika, kwa mashirikiano na washirika mbali mbali wa masuala ya afya,
Wizara imeandaa rasimu ya awali ya Mpango Mkakati wa Nne wa Sekta ya Afya pamoja
na kufanya mapitio ya Mpango Mkakati wa Taarifa za Afya (HIS Strategic Plan) ili
kuendana na mahitaji ya sasa. Uwepo wa Mpango Mkakati wa Taarifa za Afya
utarahisisha kazi ya ukusanyaji, uchambuzi na usambazaji wa taarifa ndani na nje ya
sekta pamoja na kuimarisha ubora wa taarifa zinazokusanywa. Aidha, miongozo mbali
mbali imetayarishwa ikijumuisha (i) Muongozo wa kitita cha utoaji wa huduma za afya
31
katika ngazi ya kati na ngazi ya rufaa “Essential Health Care Package for Secondary and
Tertiary Levels”, ambao umetayarishwa kwa mashirikiano na Wataalamu elekezi kutoka
Shirika la Afya Ulimwenguni na “Bergen Center for Ethics and Priority Setting”. Hatua
inayoendelea hivi sasa ni kuufanyia gharama (costing) za kila huduma kulingana na
ngazi ya utoaji wa huduma; (ii) Muongozo wa Ubora wa Viwango (Quality Assurence
Strategic Plan), ambapo rasimu ya muongozo huo imekamilika na kuwasilishwa kwa
washirika wanaohusika kwa ajili ya kupata maoni zaidi; na (iii) Muongozo wa ukaguzi
(National Intergrated Supervision Guideline) ulifanyiwa mapitio, muongozo huo ndio
utakaotumika katika kufanya ukaguzi kwenye hospitali na vituo vya afya.
92. Mheshimiwa Spika, ripoti mbali mbali zimetayarishwa zikiwemo za utekelezaji wa
Wizara kwa mwaka 2018/2019 (Annual Health Sector Performance Report), ripoti za
utekelezaji za kila robo mwaka zilizowasilishwa katika Kamati ya Ustawi wa Jamii ya
Baraza la Wawakilishi pamoja na ripoti ya utekelezaji ya maagizo ya Kamati ya Ustawi
iliyowasilishwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Aprili, 2020. Pia, ripoti za kila
robo mwaka za utekelezaji wa miradi ya maendeleo zinazowasilishwa Tume ya
Mipango, taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na ripoti za utekelezaji wa shughuli za
Wizara zinazowasilishwa kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi (Bango Kitita) zimeandaliwa na kuwasilishwa kama taratibu
zinavyoelekeza. Aidha, Wizara imeweza kukamilisha Kitabu cha Taarifa za Afya (Health
Bulletin, 2018), Jarida la Afya pamoja na Mpango wa Matumizi wa Wizara na Hotuba ya
Bajeti ya mwaka 2020/21, ambayo leo inawasilishwa katika kikao hiki.
93. Mheshimiwa Spika, shughuli nyengine zilizofanywa ni kuandaa mkutano wa 12 wa
mapitio ya utekelezaji wa sekta ya afya kwa mwaka 2018/2019. Mkutano huo
uliwashirikisha wadau mbali mbali wa afya wakiwemo Washirika wa Maendeleo, Asasi
zisizo za Kiserikali, Taasisi za Umma na Halmashauri za Wilaya. Katika mkutano huo
washiriki walipata nafasi ya kutoa mapendekezo yao juu ya uimarishaji wa huduma za
afya hapa nchini, ambayo yamezingatiwa katika uandaaji wa bajeti na Mpango wa
Utekelezaji wa Wizara kwa Mwaka 2020/2021.
94. Mheshimiwa Spika, katika kuhamasisha matumizi ya takwimu katika kupanga mipango
yenye kuleta matokeo, Wizara imepanua wigo wa uwekaji wa taarifa kwa kutayarisha
“Dashboard” zinazoonesha muhtasari wa taarifa mbali mbali za afya na viashiria
ambavyo vinasaidia katika kufanya uchambuzi kutokana na matokeo ‘Bottleneck
Analysis’. ‘Dashboard’ hizo zinapatikana katika mtandao uliounganishwa kwenye
mfumo wa DHIS2 ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa hizi kwa urahisi.
32
95. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia program hii ilifanya utafiti kwa lengo la kutathmini
mtazamo wa wananchi kuhusiana na huduma za afya wanazopatiwa katika hospitali na
vituo vya afya vya Serikali. Jumla ya hospitali tisa (9), vituo vya afya daraja la pili 34 na
vituo vya afya 32 vya daraja la kwanza vinavyotoa huduma za mama na mtoto, za
kujifungua na za wagonjwa wa nje vilihusika katika utafiti huo wa kuridhika kwa wateja
(Client Satisfaction Survey - CSS). Jumla ya washiriki 2,532 waliopata huduma walipata
fursa ya kutoa maoni yao, ambapo asilimia 97 ya waliopata huduma za matibabu ya nje
na asilimia 99 ya wajawazito wliohudumiwa katika kliniki za mama wajawazito na
wazazi waliripoti kuridhishwa na huduma walizopewa. Hata hivyo, wananchi hao
wameshauri kuimarishwa kwa baadhi ya huduma, hususan za uchunguzi katika vituo
vya afya vya msingi ili vipimo muhimu viweze kupatikana karibu na maeneo yao. Pia,
utafiti wa kutambua matumizi ya fedha za afya (National Health Accounts - NHA) kwa
mwaka 2017/18 umefanyika na ripoti ya awali imeshatayarishwa.
Taasisi ya Tafiti za Afya – Zanzibar Health Research Institute
96. Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Utafiti wa Afya, Zanzibar imeendelea kufanya tafiti mbali
mbali ikiwemo utafiti wa maradhi ya ngozi yaliyoibuka katika Wilaya ya Micheweni
huko Pemba. Aidha, rasimu ya Sheria ya Kuanzisha Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar
(Zanzibar Health Research Institute -ZAHRI) imeandaliwa na kupitishwa katika Baraza la
Wawakilishi katika kikao kilichofanyika mwezi Aprili 2020. Kwa upande wa ujenzi wa
majengo ya taasisi hiyo tayari jengo moja la ofisi limekamilika na kuhamiwa na hatua za
ujenzi wa jengo la maabara ya utafiti wa “Microbiology” zinaendelea na linategemewa
kukamilika mwishoni mwa mwezi wa Juni 2020. Jumla ya maombi ya mapendekezo ya
tafiti 52 yamepokelewa kutoka katia taasisi na vyuo mbali mbali (Kiambatisho namba
8). Tafiti zote zilipatiwa ruhusa ya kuendelea kufanywa baada ya kukidhi vigezo
vilivyowekwa, ambapo tafiti 12 zimekamilika na 40 zinaendelea na utafiti.
Programu ndogo ya Uratibu wa Shughuli za Afya Pemba
97. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki, Wizara ya Afya Pemba imefanya matengenezo
katika sehemu ya huduma za dharura katika Hospitali ya Abdalla Mzee. Vile vile,
matengenezo ya mfumo wa usambazaji maji katika Hospitali ya Micheweni yalifanyika
na matengenezo ya ‘generator’. Pia, Ofisi imesimamia ujenzi wa fensi katika Hospitali
hiyo ya Micheweni kwa mashirikiano na Jumuiya ya Maendeleo ya Jimbo la Micheweni.
Aidha, huduma za masafa zimetolewa katika vituo vya Kiuyu M’buyuni, Maziwa
Ng’ombe, Wingwi, Sizini na Konde kwa wiki mara mbili katika Hospitali ya Micheweni na
wiki mara moja katika Hospitali ya Wete.
33
Maabara ya Afya ya Jamii – Public Health laboratory Pemba
98. Mheshimiwa Spika, Kupitia Maabara ya Afya ya Jamii - Public Health Laboratory (PHL)
iliyopo Wawi, Chake Chake Pemba; tafiti mbali mbali za maradhi zimefanywa. Tafiti hizo
zimefanywa kwa mashirikiano na taasisi za ndani na nje ya Zanzibar. Miongoni mwa
tafiti zilizofanywa na Maabara hii katika kipindi hiki ni utafiti wa kuangalia ubora na
usalama wa matibabu ya minyoo ya tumbo kwa kutumia dawa za aina ya Mebendazo
(ChewableMebendazole)uliozishirikisha skuli nne za Pemba (Furaha, Wawi, Piki na
Bwagamoyo). Utafiti mwengine uliofanywa ni utafiti wa kuangalia ubora na usalama
wa matibabu ya minyoo ya tumbo kwa kulinganisha na utumiaji wa dawa ya aina ya
“albendazole”. Ripoti ya awali ya tafiti hizo tayari zimeandaliwa. Aidha, kwa sasa
utafiti unaoendelea kufanywa na maabara hiyo ni wa kuangalia ubora wa huduma
wanazopatiwa watoto wachanga, hasa wale wanaozaliwa kabla ya kutimia muda wao
(watoto njiti).
99. Mheshimiwa Spika, mbali nashughuli za utafiti, taasisi hii pia iliendesha mafunzo ya
uimarishaji wa uwezo wa uchunguzi wa kimaabara katika nchi za joto yaliyoratibiwa
kwa ushirikiano baina ya PHL, Wizara ya Afya Zanzibar, Shirika la Afya Duniani (WHO) na
taasisi ya Ivo de Carneri ya Italy. Jumla ya washiriki 27 kutoka Zanzibar, Kenya, Tanzania
Bara, Rwanda, Uganda, Somalia, South Sudan, Iran, Burkina Faso, Timor-Leste, Ethiopia,
India, Swaziland and Italy walishiriki katika mafunzo hayo yaliyofanyika hapa Zanzibar.
34
PROGRAMU YA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA
100. Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Mnazi Mmoja ni taasisi inayojitegemea (semi -
autonomous institution) katika Wizara ya Afya iliyoanzishwa chini ya Sheria namba 3 ya
mwaka 2016. Hospitali hiyo inaongozwa na Bodi ya Ushauri na shughuli za utendaji wa
kila siku zinasimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji. Aidha, Taasisi ya Hospitali ya Mnazi
Mmoja inatumika kwa kutoa huduma za tiba, mafunzo ya nadharia na vitendo
(Intenship) ya kada za afya kwa wanafunzi wa hapa nchini na wa kigeni pamoja kufanya
shughuli za utafiti. Bodi ya Afya ya Afrika Mashariki ya Baraza la Madaktari imeitambua
rasmi hospitali hii kutumika kwa kufundishia madaktari.
101. Mheshimiwa Spika, hospitali hii ina jumla ya Idara nane (8); Idara ya Tiba; Dawa na
vifaa tiba; Uchunguzi wa Maradhi; Uuguzi; Ufundi; Mipango na Fedha; Mafunzo na
Utafiti; na Idara ya Uendeshaji na Utawala. Hata hivyo, kwa mujibu wa utekelezaji wa
kiprogramu, utekelezaji wa shughuli za idara hizi zinaripotiwa kupitia programu kuu
mbili; (i) program ya huduma za uchunguzi na matibabu na (ii) program ya huduma za
uongozi na utawala.
Programu ya huduma za Uchunguzi na Matibabu
102. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuziimarishahuduma za uchunguzi katika Hospitali
ya Mnazi mmoja, Serikali imenunua mashine nyengine mpya ya CT Scan yenye slice
128, ambayo ina uwezo mkubwa wa uchunguzi wa maradhi mbali mbali. Kufungwa kwa
mashine hiyo kunaifanya Hospitali hiyo kuwa na mashine mbili za CT-Scan. Kuwepo
kwa mashine hizo za uchunguzi ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar ya kuifanya Hospitali hiyo iweze kutoa huduma za rufaa. Aidha, katika
kuimarisha huduma za uchunguzi, hospitali imeweka mfumo wa kielektroniki ambao
unawezesha picha za X-ray na CT Scan kuweza kusambazwa kwa wepesi kutoka kitengo
cha radiolojia hadi vitengo vyengine.
103. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2019 hadi Machi 2020, Hospitali ya Mnazi
Mmoja imefanya vipimo 198,271 (maabara 154,415; X-ray 18,654; ultrasound 20,651;
CT-Scan 2,572; na MRI 1,613). Aidha, vipimo vyengine vilivyofanyika ni uchunguzi wa
mfumo wa chakula kwa kutumia darubini kupitia njia ya mdomo “endoscopy” (299) na
njia ya haja kubwa “colonoscopy “(67). Kwa upande wa huduma za matibabu hadi
kufikia Machi 2020, jumla ya mahudhurio ya wagonjwa wa nje 100,961 (wanaume
41,915 na wanawake 59,046) yameripotiwa na wagonjwa 12,925 (wanaume 6,246 na
wanawake 6,679) walilazwa. Aidha, jumla ya mahudhurio ya wagonjwa 67,214
yaliripotiwa katika kliniki za huduma za maradhi maalumu zikiwemo meno, presha,
moyo, kisukari nakadhalika (Kiambatisho namba 9). Vile vile, wajawazito 10,950
35
walijifungua katika Hospitali ya Mnazi Mmoja na Mwembeladu, ambapo wazazi 1,220
walijifungua kwa njia ya upasuaji (asilimia 11.1)
104. Mheshimiwa Spika, jumla yaWagonjwa 64 wenye matatizo ya figo waliendelea
kupatiwa huduma za kusafisha damu na wagonjwa sita (6) waliopandikizwa figo
(transplant) wanaendelea na matibabu katika kliniki ya huduma za matibabu ya figo.
Pia,huduma za maradhi ya Saratani katika klinikiya maradhi hayo ziliendelea kutolewa,
ambapo jumla ya wagonjwa wapya 221 wa maradhi hayowamepokelewa na kufanya
wagonjwa wote wanaoendelea na matibabukufikia 924. Vile vile, wagonjwa 1,646
wamepatiwa huduma maalumu ya matatizo wa moyo.
105. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa huduma zinazotolewa kupitia kambi maalum,
jumla ya kambi 16 ziliendeshwa, ambapo wagonjwa 1,282 walichunguzwa na kupatiwa
matibabu wakiwemo wagonjwa 412 waliofanyiwa upasuaji wa maradhi mbali mbali
ikiwemoupasuaji wavichwa maji. Pia, vifaa mbali mbali vya matibabu vimepokelewa
kwa ajili ya kuendesha kambi ya upasuaji ya watoto wenye matatizo ya sehemu ya
kukojolea na wenye ulemavu unaotokana na kuungua (inteplastic Surgery); vifaa kwa
ajili ya wodi ya watoto pamoja na vifaa vya ICU pia vimenunuliwa.
Programu ndogo ya Uongozi wa Hospitali na Utawala
106. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Saba imepiga hatua kubwa ya kuongeza
madaktari bingwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja ili iweze kutoa huduma za ngazi ya
rufaa kama ilivyoelezwa katika ilani ya CCM. Kwa mwaka wa fedha 2019/2020, Hospitali
ya Mnazi Mmoja imepata jumla ya madaktari bingwa 10 wakiwemo daktari bingwa wa
mionzi, figo, ngozi, upasuaji wa masikio, pua na koo, matatizo ya kina mama na
madaktari bingwa wa maradhi mbali mbali, hivyo kufanya idadi ya madaktari bingwa
wazalendo kufikia 39. Pia, hospitali imepokea wauguzi bingwa wanane (8) wa huduma
za kina mama na watoto baada ya kurejea kutoka masomoni, hivyo kufanya idadi ya
wauguzi bingwa kufikia 28.
107. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2019 hadi Machi 2020 uzalishaji wa ‘oxygen’
uliendelea katika hali nzuri baada ya mtambo kufanyiwa matengenezo makubwa na
kuwezesha kuzalisha jumla ya mitungi 4,124 ya gesi, ambapo matumizi kwa ajili
yaHospitali ya Mnazi mmoja kwa kipindi hicho ni mitungi 4,325 naHospitali nyengine
zilihitaji mitungi 87. Hivyo, idadi hiyo iliyozalishwaimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa
kupunguza idadi ya mitungi iliyonunuliwa TOL. Sambamba na uzalishaji huo wa gesi,
uwekaji wa mtambo wa uzalishaji wa “liquid oxygen” umeendelea vizuri na uko katika
hatua ya mwisho kukamilika.
108. Mheshimiwa Spika, hospitali imeratibu mafunzo ya kujifunza kwa wanafunzi wa kigeni
(Elective Placement), ambapo jumla ya Wanafunzi 34 kutoka Australia (3), Denmark (3),
Ujerumani (8), Norway (13), Ureno (2), Ufaransa (1) na Uingereza (4) wamepokewa na
36
kujifunza. Pia hospitali imeendelea kupokea wanafunzi kutoka katika Vyuo vya Taaluma
za afya vya SUZA, ZU, SHA na KIUT kwa ajili ya mazoezi ya vitendo (intenship).
109. Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa mashirikiano na Chuo Kikuu cha
Gothernburg cha nchini Sweden imefanya utafiti wa matumizi ya dawa za ‘antibiotic’ na
upatikanaji wake kwa jamii ya Zanzibar. Tafiti nyengine zinazoendelea kufanywa ni za
kuangalia ukubwa wa tatizo la saratani ya mlango wa kizazi kwa kina mama, saratani ya
matiti natenzi dume kwa wagonjwa waliohudhuria katika hospitali ya Mnazi Mmoja
kuanzia mwaka 2017 hadi mwaka 2019. Utafiti mwengine uliofanyika ni wakuangalia
ukubwa wa tatizo la utapia mlo hatarishi kwa watoto walio chini ya umri wa miezi 6 na
utafiti wa tatizo la uhaba wa damu hatarishi kwa watoto wenye tatizo la selimundu.
Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
110. Mheshimiwa Spika, kupitia mradi wa maendeleo wa kupandisha hadhi Hospitali ya
Mnazi Mmoja,vyumba viwili vya CT Scan vimefanyiwa ukarabati na kufungwa mashine
(mpya na kongwe), ambayo moja imeanza kufanya kazi. Aidha, majengo mbali mbali
yameweza kufanyiwa ukarabati likiwemo jengo moja la macho na jengine kujengwa
upya. Nachukua fursa hii kuwaeleza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba
majengo ya huduma za matibabu ya macho yamekamilika na huduma zimerejea
kutolewa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja. Sambamba na hilo, vifaa mbali mbali
vimenunuliwa vikiwemo vifaa kwa ajili ya huduma za mifupa (kitanda cha upasuaji na
mashine ya C arm), Ct Scan na incinerator. Aidha, ujenzi wa jengo la Hospitali ya
wagonjwa wa akili iliyopo Kidongo Chekundu unaendelea vizuri, na hivi sasa tayari
jengo la ghorofa moja limeshaezekwa na jingine linaendelea kujengwa. Aidha, zabuni ya
kumtafuta mkandarasi kwa ajili ya ukarabati wa chumba cha upasuaji (theatre)
imeshatangazwa na mara tu mkandarasi huyo atakapopatikana kazi ya ukarabati
itaanza mara moja.
37
CHANGAMOTO
111. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio hayo yaliyoorodheshwa Wizara ilikabiliwa na
changamoto mbali mbali ambazo kwa kiasi ziliathiri utekelezaji wa baadhi ya shughuli
zilizopangwa. Changamoto hizo pamoja na (i) Upungufu wa wataalamu wa fani za afya;
(ii) Ongezeko la wagonjwa wa Malaria katika baadhi ya maeneo; na (iii) Kuibuka kwa
maradhi ya Covid-19, ambako kumeathiri utekelezaji wa shughuli za Wizara.
112. Mheshimiwa Spika, hatua mbali mbali zimechukuliwa katika kutatua changamoto
zilizoainishwa hapo juu, ikiwemo kupeleka masomoni wafanyakazi wa afya kusomea
fani zinazokosekana, kuchukua hatua za kudhibiti kikamilifu maambukizi ya ugonjwa wa
COVID-19 na kuendeleza mikakati ya kumaliza malaria.
38
MWELEKEO WA BAJETI YA WIZARA YA AFYA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021
113. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa huu ndio mwaka wa mwisho wa awamu ya saba ya
uongozi wa Zanzibar, yapo masuala muhimu na ya msingi, ambayo Serikali ijayo
itapaswa kuzingatia katika kuimarisha huduma za afya nchini, nayo ni:
i. Kuweka mfumo endelevu wa fedha kwa kugharamia huduma za afya,
utakaowezesha kuendeleza sera ya utoaji wa huduma bure za afya kwa wananchi
wote kama ilivyoasisiwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza
wa Zanzibar, mara baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964;
ii. Kuendeleza ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya rufaa na kufundishia Binguni;
iii. Kufanya ukarabati mkubwa wa Hospitali ya Wete pamoja na kuiimarisha Hospitali
hiyo kufikia daraja la Hospitali ya Mkoa;
iv. Kukamilisha ujenzi wa maabara ya utafiti wa uchunguzi wa maradhi
yanayosababishwa na virusi (Virology) katika eneo la Binguni;
v. Kujenga mazingira mazuri ya utendaji kazi kwa wafanyakazi wa afya, ikiwemo
kunyanyua maslahi yao na kuwapatia makaazi karibu na maeneo yao ya kazi;
vi. Kukamilisha ujenzi wa hospitali maalum ya kutibu wagonjwa wenye maradhi ya
kuambukiza (highly Infectious treatment Centre) katika eneo la Dunga;
vii. Kuanzisha Idara ya Uchunguzi wa Maabara; na
viii. Kuanzisha huduma za matibabu ya upasuaji wa Moyo.
Hivyo, Mpango wa Utekelezaji wa Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2020/2021
utayazingatia haya kuwa ni miongoni mwa vipaumbele katika kuimarisha huduma
za afya.
114. Mheshimiwa Spika, ili kufikia malengo yaliyowekwa na Shirika la Afya Ulimwenguni
kuhusiana na azma ya kufikia shabaha ya upatikanaji wa huduma za afya kwa watu
wote (Universal Health Coverage – UHC), Wizara ya Afya katika mwaka wa fedha wa
2020/2021, imepanga kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia mfumo wa ugatuzi.
Aidha, hili linakwenda sambamba na kauli mbiu ya mkutano wa 12 wa mapitio ya sekta
ya afya inayoelekeza juu ya haja ya kuimarisha mfumo wa ugatuzi ili kufikia dhamira ya
upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wote “Strengthening
Decentralization by Devolution for Effective Universal Health Coverage”. Katika
kufanikisha kauli mbiu hiyo, Wizara itaelekeza nguvu zake katika kutekeleza malengo
yafuatayo: -
i. Kuimarisha huduma za kinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza na yasiyoambukiza,
ikiwemo kuongeza kasi ya utoaji wa elimu ya afya ili kujenga uelewa na kupelekea
mabadiliko ya tabia miongoni mwa jamii;
39
ii. Kukamilisha Kitita cha Utoaji wa Huduma za Afya (Essential Health Care Package)
kwa ngazi zote ili iwe ni dira katika kutoa huduma sambamba na kuandaa makisio
ya gharama kwa utekelezaji wake;
iii. Kukamilisha Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (5) wa Wizara utakaozingatia
mpango wa muda mrefu wa maendeleo wa Zanzibar (Dira 2050);
iv. Kubuni na kutekeleza mbinu mbadala katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi
na vifo vya watoto wachanga;
v. Kuimarisha huduma za tiba na uchunguzi wa maradhi;
vi. Kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu, vifaa vya utibabu na “reagents” zenye
ubora na usalama katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya;
vii. Kuimarisha upatikanaji wa huduma za rufaa ili kupunguza idadi ya wagonjwa
wanaosafirishwa kwa ajili ya matibabu nje ya nchi;
viii. Kuimarisha nguvu kazi ya afya kwa kusomesha wafanyakazi katika kada za
kitaalamu pamoja na kuinua maslahi ya wafanyakazi;
ix. Kuimarisha mifumo ya taarifa za afya kwa kufanya tafiti mbali mbali; na
x. Kuongeza ushirikiano na washirika mbali mbali wa sekta ya afya zikiwemo sekta
binafsi na jamii.
40
SHUGHULI KUU ZITAKAZOTEKELEZWA NA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021
115. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwamba vipaumbele na malengo yaliyowekwa
yanafikiwa, Wizara kwenye mwaka wa fedha 2020/2021, kupitia programu husika,
itatekeleza shughuli zifuatazo:
Programu ya Kinga na Elimu ya Afya
116. Mheshimiwa Spika, katika kufanikisha utekelezaji wa malengo ya Wizara yaliyopangwa
kutekelezwa kupitia programu ya Kinga na Elimu ya Afya, Wizara imetenga jumla ya
Shilingi 28,664,931,000/= ambazo ni sawa na asilimia 28.6 ya bajeti ya Wizara kwa ajili
ya kutekeleza shughuli zifuatazo: -
i. Kuandaa Mpango Mkakati wa Maradhi yasiyo ya kuambukiza
ii. Kuhakikisha sera ya udhibiti wa tumbaku inafanyiwa kazi kikamilifu katika ngazi ya
taifa na jamii;
iii. Kufanya shughuli za ufuatiliaji wa maradhi;
iv. Kuandaa muongozo wa Maradhi Yasiyopewa Kipaumbele Zanzibar (Comprehensive
Guideline for Manangement of Neglected Tropical Diseases);
v. Kufanya utafiti wa kujua kiwango cha minyoo nchini;
vi. Kuendelea kutekeleza Mpango wa Kumaliza Kipindupindu Zanzibar; na
vii. Kutekeleza Muongozo wa Kimataifa wa Afya (Internation Health Regulation - IHR)
katika kudhibiti maradhi ya kuambukiza.
Programu ya Tiba
117. Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kwamba huduma za uchunguzi na matibabu
zinaimarika zaidi, Wizara imetenga Shilingi 51,258,210,000/= sawa na asilimia 51.1 ya
bajeti kuu ya Wizara kwa ajili ya programu hii, kwa ajili ya kutekeleza shughuli zifuatazo:
i. Kuendelea na ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya Rufaa na kufundishia ya Binguni;
ii. Kuanza ujenzi wa nyumba za wafanyakazi katika Hospitali ya Abdalla Mzee;
iii. Kuendelea na ujenzi wa wodi ya wazazi na watoto katika hospitali ya Chake Chake;
iv. Kufanya ukarabati mkubwa wa Hospitali ya Wete;
v. Ununuzi wa dawa, vifaa vya utibabu na ‘reagents’ kwa ajili ya hospitali na vituo vya
afya vya Serikali; na
vi. Kukamilisha Maabara ya Chakula, Dawa na Vipodozi.
Programu ya Uendeshaji na Uratibu wa Wizara ya Afya
118. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2020/21, Wizara imetenga Shilingi
20,312,959,000/= sawa na asilimia 20.3 ya bajeti ya Wizarakwa ajili ya kutekeleza
shughuli kuu zilizopangwa katika programu hii, ambapo Shilingi 7,149,122,000 /=
41
zitatumika kwa shughuli za utawala na uendeshaji; Shilingi 4,367,344,000 /= kwa
shughuli za uratibu wa mipango, Sera na Utafiti na Shilingi 8,796,493,000/= kwa kazi za
uratibu wa shughuli za afya Pemba. Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na: -
i. Kupeleka masomoni wafanyakazi wa afya wa kada zilizopewa kipaumbele na
Wizara kwa mujibu wa mahitaji;
ii. Kulipa mishahara na maposho ya wafanyakazi;
iii. Kutayarisha Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini (Monitoring & Evaluation
Framework) wa Mpango Mkakati wa IV wa Afya;
iv. Kuimarisha mifumo ya taarifa; na
v. Kuratibu shughuli za uandaaji wa sera, mipango, tafiti na taarifa mbali mbali
zinazohusu Wizara.
Programu ya Hospitali ya Mnazi Mmoja
119. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa 2020/21, Serikali imetenga Shilingi
18,233,200,000/=;Shilingi 12,243,200,000 kwa ajili ya mishahara na Shilingi
5,990,000,000 kwa matumizi ya kawaida ya Hospitali ya Mnazi Mmoja. Shughuli
zilizopangwa kutekelezwa kupitia Programu hii ni kama zifuatazo-
i. Kuimarisha upatikanaji wa huduma za uchunguzi kwa wagonjwa;
ii. Kuimarisha upatikanaji wa huduma za matibabu ya rufaa;
iii. Kuhamasisha utumiaji wa TEHAMA kwa wafanyakazi;
iv. Kuimarisha miundo mbinu ya Hospitali ikiwemo ukarabati wa ’theatre’ kuu ya
Hospitali ya Mnazi Mmoja na Kufanya matengenezo kwa baadhi ya wodi;
v. Kuanza ujenzi wa tangi la kuhifadhia ’oxygen’ (Liquid Oxygen); na
vi. Kununuwa baadhi ya vifaa vya utibabu muhimu ikiwemo mashine za uchunguzi na
za matibabu.
42
SHUKRANI
120. Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kwamba katika mwaka wa fedha 2019/2020, Wizara ya Afya
imepata mafanikio makubwa katika kutekeleza majukumu yake licha ya kukabiliwa na
changamoto mbali mbali, zikiwemo mripuko wa maradhi ya Covid -19. Mafanikio haya
yametokana na nguvu za pamoja na mshikamano uliopo baina ya Wizara na taasisi
nyengine za ndani na nje ya nchi na washirika mbali mbali wanaohusika na masuala ya
afya. Nachukuwa fursa hii kuwashukuru wale wote waliochangia mafanikio haya
pamoja na wale walioshirikiana na Wizara kwa njia moja au nyengine katika kuunga
mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha huduma za afya.
121. Mheshimiwa Spika, kwa dhati kabisa napenda kuwashukuru wafanyakazi wa afya walio
mstari wa mbele katika vita ya kupambana na Covid-19, najua wamejitolea mhanga
kwa kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya kuwahudumia jamaa na ndugu zao; huu ndio
uzalendo mkubwa kwa nchi yao na Insha Allah Mwenyezi Mungu atawalipa kwa kazi
yao. Niwashukuru pia baadhi ya wananchi, ambao wameanza kuchukuwa hatua za
kujikinga na maradhi ya Covid-19 na kuwanasihi sana wale ambao bado ni wakaidi
wachukuwe hatua za kujikinga. Corona bado ipo na kila mtu achukuwe tahadhari za
kujikinga ndipo tutaendelea kubaki salama.
122. Mheshimiwa Spika, hiini bajeti yangu yangu ya mwisho kama Waziri wa Wizara hii. Hivyo, napenda
kuchukuwa fursa hii kumshukuru Naibu Waziri wa Afya Mheshimiwa Harusi Said
Suleiman pamoja na watendaji wote wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Katibu Mkuu
Bi Asha Ali Abdulla, Naibu Katibu Mkuu Bi Halima Maulidi Salim, Mkurugenzi Mkuu
Dkt. Jamala Adam Taib, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dkt. Ali
Salim Ali, Afisa Mdhamini Pemba Bi Shadia Shaaban Seif, Mshauri wa Waziri wa Afya
Dkt. Mohamed S. Jiddawi na Wakurugenzi wote kwa mashirikiano makubwa
waliyonipatia katika kipindi chote nilichoongoza Wizara hii. Kwa kweli mashirikiano yao
ndio yamepelekea kupata mafanikio tuliyofikia. Aidha, nawashukkuru Wenyeviti na
Wajumbe wa Bodi za Taasisi zilizomo katika Wizara ya Afya.
123. Mheshimiwa Mwenyekiti,pia, nachukuwa fursa hii kuzishukuru nchi rafiki
zinazoshirikiana nasi katika kuimarisha huduma za afya hapa nchini. Shukurani ziende
kwa Serikali za Denmark, Jamhuri ya Watu wa China, Cuba, Uholanzi, Spain, Canada,
Israel, Norway, Ujerumani, Korea, Uturuki, India, Kuwait, Marekani, Italy, Saudi Arabia,
Oman, UAE na Uingereza. Aidha, nazishukuru Wizara na taasisi za Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar zikijumuisha Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum
za SMZ; Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali;
43
Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji; Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee,
Vijana, Wanawake, na Watoto; Wizara ya Kilimo, Maliasili na Uvuvi; Wizara ya Habari,
Utalii na Mambo ya Kale; Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji
na Nishati; Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA); Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO),
pamoja na sekta binafsi na asasi zisizo za Serikali.
124. Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua nafasi hii adhimu kumshukuru Mke wa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Mama Mwanamwema
Shein, na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais, Mheshimiwa Mama Asha Balozi kwa
mashirikiano makubwa waliyotupatia wakati wa utekelezaji wa shughuli mbali mbali za
Wizara ya Afya.
125. Mheshimiwa Spika, Sasa naomba uniruhusu kuyashukuru mashirika mbali mbali ya
Maendeleo, yakiwemo Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO, UNICEF, UNFPA, World
Bank, Danida, Mfuko wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (GFATM);
Haukeland University Hospital ya Norway, SAVE THE CHILDREN, Engender Health, D -
Tree International, World Diabetic Foundation, Sight Saver, HIPZ, JHPIEGO, Pharm
Access International, Measure Evaluation, Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kupambana
na Malaria (PMI), CDC, THPS, DFID, AMREF, JHPU, IHI, WATER AID, Rotary UK, PEPFAR,
ZOP, UNDP, EAC, Zanzibar Milele Foundation, kundi la G-20. Pia, nawashakuru wale
wote ambao sikuweza kuwataja katika orodha hii. Hata hivyo, watambue kwamba
michango yao tunaithamini sana.
44
HITIMISHO
MAOMBI YA FEDHA KWA UTEKELEZAJI WA KAZI ZILIZOPANGWA KWA PROGRAMU ZA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21
126. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2020/21 Wizara ya Afya (Fungu H01)
inakadiriwa kutumia kiasi cha Shilingi 100,236,100,000/=. Kati ya hizo Shilingi
19,351,500,000/= kwa ajili ya mishahara na maposho, Shilingi 35,313,100,000 /= kwa
kazi za kawaida na Shilingi 2,924,400,000 /= ni ruzuku kwa taasisi zilizo chini ya Wizara
ya Afya na Shilingi 42,647,100,000/= kwa shughuli za miradi ya maendeleo, kati ya hizo,
Shilingi 20,996,000,000/= kutoka serikalini na Shilingi 21,651,100,000/= kutoka kwa
washirika wa maendeleo.Pia, Hospitali ya Mnazi Mmoja (Fungu H02) imepangiwa
kutumia Shilingi 17,348,600,000/= kati ya hizo, Shilingi 12,249,400,000/= kwa ajili ya
mishahara na maposho na Shilingi 5,099,200,000/= kwa ajili ya matumizi ya uendeshaji
(Kiambatisho namba 10). Pia, wizara imepangiwa kukusanya Shilingi 360,505,000 /= na
Hospitali ya Mnazi Mmoja imepangiwa kukusanya Shilingi 675,000,000/= kutoka katika
vyanzo vyake mbali mbali vya mapato.
127. Mheshimiwa Spika, sasa naomba Wajumbe wa Baraza hili, waijadili hotuba hii ya bajeti
ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2020/2021, na hatimae wakubali kupitisha matumizi
ya Shilingi100,236,100,000/=kwa Wizara ya Afya (Fungu H01) na Shilingi 17,348,600,000/= kwa
matumizi ya Hospitali ya Mnazi Mmoja (Fungu H02). Aidha, waridhie makusanyo ya
Shilingi360,505,000 /= kwa Wizara ya Afya na Shilingi 675,000,000/=kwa Hospitali ya Mnazi
Mmoja kwa ajili ya kuingizwa katika Mfuko Mkuu wa Serikali.
128. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
HAMAD RASHID MOHAMED (MBLW, MBM)
WAZIRI WA AFYA
ZANZIBAR
45
VIAMBATISHO
Kiambatisho Namba 1: Muhtasari wa Mapato na Matumizi kwa Wizara ya Afya 2019/2020
FUNGU HO1: WIZARA YA AFYA Makisio ya
fedha 2019-20
Makisio ya
fedha Julai
2019 - Machi
2020
Fedha
zilizopatikana
Julai 2019-Machi
2020
Asilimia ya Fedha
zilizopatikana
(Julai 2019-Machi
2020)
Asilimia ya Fedha
zilizopatikana
kwa mwaka
2019/20
Matumizi mengineyo
(OC)
Unguja 33,488,637,155 27,303,682,677 21,997,044,745 81 66
Pemba 1,513,862,845 1,209,929,515 918,845,742 76 61
Jumla ndogo 35,002,500,000 28,513,612,192 22,915,890,487 80.4 65.5
Mishahara
Unguja 9,347,774,000 7,193,658,501 7,611,351,719 106 81
Pemba 7,854,226,000 4,795,029,999 6,257,115,750 130.5 80
Jumla ndogo 17,202,000,000 11,988,688,500 13,868,467,469 115.7 80.6
Ruzuku
Unguja 2,020,138,000 1,727,719,500 1,508,705,310 87.3 75
Pemba 250,464,000 62,616,000 176,604,251 282 71
Jumla ndogo 2,270,602,000 1,790,335,500 1,685,309,561 94.1 74.2
Jumla kuu kwa kazi za kawaida 54,475,102,000 42,292,636,192 38,469,667,517 91.0 70.6
Kazi za Maendeleo SMZ 17,864,000,000 14,188,000,000 8,122,188,349 57 45
Wahisani 16,274,798,000 13,283,711,340 7,613,452,643 57 47
Jumla kazi za maendeleo 34,138,798,000 27,471,711,340 15,735,640,992 57.3 46.1
JUMLA KUU WIZARA (FUNGU H01) 88,613,900,000 69,764,347,532 54,205,308,509 77.7 61.2
Hospitali ya Mnazi
Mmoja
Matumizi ya Kawaida 4,667,200,000 2,544,408,625 3,014,149,533 118.5 64.6
Mishahara 10,954,800,000 8,216,100,000 8,999,484,795 109.5 82.2
JUMLA (FUNGU H02) 15,622,000,000 10,760,508,625 12,013,634,328 111.6 76.9
JUMLA KUU WIZARA YA AFYA 104,235,900,000 80,524,856,157 66,218,942,837 82.2 63.5
46
Kiambatisho Namba 2: Taarifa ya Makusanyo ya Wizara ya Afya (Julai,2019 - Machi, 2020
ITEMS GFS CODE Maelezo
Makusanyo
halisi
2018/2019
Makisio ya
Makusanyo
2019/2020
Makusanyo
halisi Julai
2019 - Machi
20
Asilimia ya
Makusanyo
Makadirio ya
makusanyo
April - Juni
2020
Makadirio ya
makusanyo
2020 /20 21
H0101
Programu ya Kinga na Elimu ya Afya
142200 Administration Fees
1422035 Ada ya chanjo za Wasafiri 112,794,000 105,893,000 97,089,000 91.7 32,397,000 148,251,000
1422050 Uchunguzi wa vyombo vya usafiri
na Abiria 66,590,000 80,254,000 30,572,000 38.1 23,938,000 66,505,000
1422051 Malipo ya X Ray na uchunguzi wa
damu 46,656,700 62,976,000 40,736,748 64.7 21,928,000 79,000,000
Jumla ndogo 226,040,700 249,123,000 168,397,748 67.6 78,263,000 293,756,000
H0102
Programu ya Huduma za Tiba
142200 Administration Fees
Ada ya kibali cha Tiba Asili 17,936,000 36,705,000 19,620,296 53.5 9,176,250 36,240,000
Jumla ndogo 17,936,000 36,705,000 19,620,296 53.5 9,176,250 36,240,000
H0103
Programu ya Usimamizi wa Sera na Utawala
Administration Fees
Procurement Unit 8,683,000 10,073,000 6,400,000 63.5 6,936,748 18,509,000
Jumla ndogo 8,683,000 10,073,000 6,400,000 63.5 6,936,748 18,509,000
JUMLA UNGUJA 252,659,700 295,901,000 194,418,044 65.7 94,375,998 348,505,000
47
ITEMS GFS CODE Maelezo
Makusanyo
halisi
2018/2019
Makisio ya
Makusanyo
2019/2020
Makusanyo
halisi Julai
2019 - Machi
20
Asilimia ya
Makusanyo
Makadirio ya
makusanyo
April - Juni
2020
Makadirio ya
makusanyo
2020 /20 21
H01303
142200 Administration Fees
1422051 Malipo ya X Ray na uchunguzi wa
damu 11,049,000 75,969,000 14,299,000 18.8 6,276,260 12,000,000
JUMLA NDOGO 11,049,000 75,969,000 14,299,000 18.8 6,276,260 12,000,000
145000 Miscellaneous and Unified Revenue
1422073 Malipo mengineyo 4,874,000 15,365,000 0 0 0 0
JUMLA NDOGO 4,874,000 15,365,000 0 0.0 0 0
JUMLA PEMBA 15,923,000 91,334,000 14,299,000 15.7 6,276,260 12,000,000
JUMLA (FUNGU H01) 268,582,700 387,235,000 208,717,044 53.9 100,652,258 360,505,000
H02 Hospitali ya
Mnazi Mmoja
Huduma za haraka na huduma za
afya 621,547,305 560,471,000 410,109,657 73.2 150,361,343 675,000,000
JUMLA (FUNGU H02) 621,547,305 560,471,000 410,109,657 73.2 150,361,343 675,000,000
JUMLA KUU WIZARA YA AFYA 890,130,005 947,706,000 618,826,701 65.3 251,013,601 1,035,505,000
48
Kiambatisho Namba 3: Taarifa za Hali ya Uzazi katika Hospitali na Vituo vya Afya vya Serikali,
Hospitali za Binafsi, Julai 2019 hadi Machi 2020
Zoni Hospital Wajawazito
Waliolazwa
Waliojifungua Watoto
waliozaliwa Hai Wazazi
Waliofariki Kawaida Upasuaji W'me W'ke
Pemba
Chake Chake 3,140 2,228 281 1,347 1,150 2
Abdulla Mzee 2,367 1,321 215 847 835 2
Micheweni 1,853 1,279 78 734 625 2
Wete 2,409 1,545 208 886 902 8
Vitongoji 294 225 106 123
PHCUs+ 2,679 1,845 960 899
PHCUs 737 848 428 424
Jumla 13,479 9,291 782 5,308 4,958 14
Unguja
Mnazi Mmoja 8,941 7,111 1,220 3,696 3,616 23
Mwembeladu 2,678 2,619 1,320 1,296
Kivunge 3,140 1,985 103 1,168 1,065 3
Makunduchi 2,367 657 35 354 337
Bubbubu
Military 174 111 3 54 61
KMKM
PHCUs+ 2,974 2,377 1,137 1,225
PHCUs 589 534 281 257
Jumla 18,835 15,394 1,361 8,010 7,857 26
Binafsi
Al-Rahma 817 479 181 340 321
MIna 19 8 11 9 12
Global 217 147 70 119 99
Farham 22 21 13 8
Kitope RC 7 7 5 2
Tawaqal 318 228 88 150 160 1
Jumla 1,400 890 350 636 602 1
Jumla Kuu 33,714 25,575 2,493 13,954 13,417 41
Jumla ya Wazazi 33,714 28,068 27,371 41
49
Kiambatisho namba 4: Idadi ya Watoto Waliopatiwa Matone ya Vitamin A na Dawa za Minyoo, 2019
Mkoa/Wilaya
Watoto walopatiwa matone ya VIT A Walopatiwa dawa za minyoo Watoto waliopimwa Hali ya lishe
Jumla ya
waliokadiri
wa Miezi
6-59
Waliopewa
vitamin A
Asilimia ya
waliopewa
Jumla ya
waliokadiri
wa Miezi
12-59
Waliopewa
dawa za
minyoo
Asilimia ya
waliopewa
Julmla ya
wliopimwa Hali Nzuri
Wenye
Utapiamlo
wa kiasi
Wenye
Utapiamlo
mkali
Wenye
Uvimbe wa
miguu
Kaskazini Pemba
Micheweni 18,767 18,763 100.0 16,682 16,753 100.4 18,767 18,686 64 13 0
Wete 20,653 21,218 102.7 18,331 19,097 104.2 20,653 21,060 141 17 0
Jumla ndogo 39,420 39,981 101.4 35,013 35,850 102.4 39,420 39,746 205 30 0
Kusini Pemba
Chake Chake 19,365 19,177 99.0 17,213 17,126 99.5 19,365 19,070 100 7 0
Mkoani 17,837 17,267 96.8 15,855 15,357 96.9 17,837 17,140 113 14 0
Jumla ndogo 37,202 36,444 98.0 33,068 32,483 98.2 37,202 36,210 213 21 0
Jumla Pemba 76,622 76,425 99.7 68,081 68,333 100.4 76,622 75,956 418 51
Kaskazini Unguja
Kaskazini A 12,213 18,101 148.2 17,391 16,043 92.2 12,213 17,937 151 13 0
Kaskazini B 16,193 14,933 92.2 14,394 13,272 92.2 16,193 14,787 139 7 0
Jumla ndogo 28,406 33,034 116.3 31,785 29,315 92.2 28,406 32,724 290 20 0
Kusini Unguja
Kati 12,213 11,402 93.4 10,856 9,905 91.2 12,213 11,287 104 11 0
Kusini 6,465 6,344 98.1 5,747 5,570 96.9 6,465 6,290 52 2 0
Jumla ndogo 18,678 17,746 95.0 16,603 15,475 93.2 18,678 17,577 156 13 0
Mjini Magharibi
Mjini 33,180 33,274 100.3 29,493 29,441 99.8 33,180 33,168 98 8 0
Magharibi A 31,989 23,299 72.8 28,435 20,604 72.5 31,989 23,241 52 6 0
Magharibi B 38,041 38,171 100.3 33,814 34,319 101.5 38,041 38,111 49 11 0
Jumla ndogo 103,210 94,744 91.8 91,742 84,364 92.0 103,210 94,520 199 25 0
Jumla Unguja 150,294 145,524 96.8 140,130 129,154 92.2 150,294 144,821 645 58 0
Jumla Zanzibar 226,916 221,949 97.8 208,211 197,487 94.8 226,916 220,777 1,063 109 0
50
Kiambatisho Namba 5: Taarifa za mahudhurio ya wagonjwa wa nje, waliolazwa na waliofariki,
Julai 2019 - Machi 2020
Hospital Wagonjwa wa nje Waliolazwa Wliofariki
W'me W'ke W'me W'ke** W'me W'ke
Chake chake 22,596 27,485 780 4,132 20 18
Abdulla Mzee 15,201 21,604 1,188 3,191 85 52
Micheweni 37,797 49,089 740 2,932 41 35
Wete 23,051 36,253 1,461 4,269 61 43
Vitongoji 6,366 8,411 831 1,557 11 10
Kivunge 8,791 13,238 683 3,622 33 24
Makunduchi 7,324 13,017 389 2,893 12 17
Jumla kwa hospitali 121,126 169,097 6,072 22,597 263 199
Jumla Hospitali za Binafsi 28,672 33,236 430 587 8 4
Jumla ndogo 149,798 202,333 6,502 29,534 271 203
Jumla Kuu 352,131 36,036 474
** idadi ya wanawake inajumuisha waliolazwa kwa huduma za kujifungua
51
Kiambatisho Namba 6: Mahudhurio ya Wagonjwa katika Kliniki za Maradhi Maalum, Julai 2018 - Machi 2019
Klinik Mnazi Mmoja Chake Chake Makunduchi Wete Kivunge Abdula Mzee Micheweni Vitongoji
Jumla W'me W'ke W'me W'ke W'me W'ke W'me W'ke W'me W'ke W'me W'ke W'me W'ke W'me W'ke
Accupuncture 1,174 1,148 2,322
Cardiac 1,245 2,174 310 743 514 1,171 260 457 198 512 142 193 7,919
CTC 276 618 9 25 138 207 2,850 5,764 106 165 173 294 10,625
Dental 2,569 4,034 1,177 1,559 1,095 1,374 1,275 1,387 2,138 3,066 1,373 1,459 190 323 50 65 23,134
Diabetic 1,710 2,348 53 102 292 554 118 324 498 574 476 663 140 255 52 68 8,227
ENT 5,042 5,753 1,699 3,085 1,367 1,778 1,475 1,569 231 317 22,316
Eye 1,587 2,003 1,977 3,350 239 449 4,314 4,928 341 427 1,704 2,445 422 451 101 145 24,883
Eye Theatre 229 205 90 110 634
Gynacology 4,046 2,339 2,959 3,730 13,074
Major Theatre 901 793 318 586 52 36 240 266 209 123 246 420 56 141 4,387
Minor Theatre 4,899 1,880 674 1,063 113 37 1,547 1,018 1,426 606 2,127 1,597 769 401 18,157
Oncology 380 450 830
Orthopedic 2,231 1,637 121 128 2,717 2,705 9,539
Physiotherapy 2,051 2,574 1,528 1,500 168 218 141 173 8,353
Psychatric 5,309 5,571 596 736 98 164 1,172 1,329 157 231 602 819 16,784
STI 10 47 23 59 5 10 86 181 23 111 14 71 39 110 789
Surgical OPD 2,082 1,189 939 498 0 0 950 625 3,844 3,771 13,898
TB and Leprosy 44 31 15 4 26 18 16 16 9 6 5 1 6 4 201
Jumla 31,409 35,805 9,291 15,514 2,057 2,830 11,720 15,920 8,235 12,159 12,976 18,493 3,556 3,962 1,159 986 186,072
Angalizo: hospitali ya makunduchi haina wodi ya orthopedic, wagonjwa wanaooneka wamepatikana kwa njia ya outreach services
52
Kiambatisho Namba 7a: Idadi ya Wafanyakazi Walioajiriwa na
Waliorudi Masomoni, 2019/2020
Kada Walioajiriwa Waliorudi
masomo
Madaktari 59 15
Wauguzi 31 42
Daktari Msaidizi 0 1
Fundi Sanifu Maabara 59 8
Afisa Mazingira 4 11
Fundi Sanifu dawa 39 12
Daktari wa Meno 15 1
Afisa Viungo Bandia 7
Wataalamu wa ganzi na usingizi - 8
Wafamasia 5 -
Wakemia 5 -
Afisa Tabibu 101 -
Biochemistry 1 -
Psysiotherapy 10 -
Afisa mionzi 5 -
Food Inspector 4 -
Afisa Ustawi 1 -
Muhandisi Vifaa Tiba 1 -
Afisa Ugavi na Manunuzi 2 2
Afisa Sheria 1 -
Afisa miradi - 2
Afisa TEHAMA 2 6
Afisa umeme - 1
Afisa Utumishi 2 -
Msimamizi wa Fedha - 1
Katibu Muhutasi 3 -
Afisa Ushauri Nasaha 2 7
Afisa kumbukumbu 3 2
Wahudumu wa Afya 232 1
Afisa Rasilimali watu - 4
Dereva 6 -
Mlinzi 1 -
Special Gang 1 -
Social worker - 4
Jumla 602 128
53
Kiambatisho Namba7b: Madaktari Waliopelekwa Masomo kwa fani ya
Udaktari Bingwa na maafisa afya na watendaji wengine, 2019/2020
Fani ya Daktari bingwa Idadi
Mkojo (Urologist) 1
Mionzi (Radiologist) 1
Mtaalamu wa maabara (Pathologist) 1
Matibabu ya watoto (Paediatrician) 1
Wataalamu wa macho (Opthalmologist) 2
Mtaalamu wa Saratani (Oncologist) 1
Magonjwa ya kinamama (Obstetrics and Gynaecologist) 7
Neuro Surgeon’ 2
Upasuaji (General Surgeon) 8
Magonjwa ya ndani (Internal Medicine) 1
Emergency Medicine’ 2
Moyo (Cardiologist) 2
Ganzi na usingizi (Anaesthesiologist) 2
Jumla madaktari bingwa 31
Anaesthetic Officers’ 2
Biomedical Engineering’ 4
Clinical Psychologist’ 2
Fani nyengine zisio za afya 94
Jumla kuu 133
54
Kiambatisho Namba 8: Orodha ya Mapendekezo ya Tafiti zilizopokelewa 2019/2020
Namba Principal Investigator &/or
Co- Investigator Andiko (Proposal)
ZAHREC/PR/19/001 Mr. Said Mohammed Ali - PHL
** Feasibility study- The efficacy of video analysis as a supplementary objective tool to Criterion Based Clinical Audit (CBCA) in newborn emergencies
ZAHREC/PR/19/002 Ms. Shemsa Nassor Msellem -Milele Zanzibar Foundation
** Maternal and Child health in Zanzibar: Coverage, determinants and perceptions
ZAHREC/PR/19/003 Dr. Farhat J. Khalid - ZIHIVTB&LP
**Factors influencing provider- intiated HIV testing and counceling Uptake among clients attending outpatient Department in Zanzibar
ZAHREC/PR/19/004 Prof. Dr. Jennifer Keiser/ Said Ali - PHL
**Efficacy and safety of a new chewable tablet of mebendazole versus the swallowable standard tablet of mebendazole against hookworm infection in children’s randomized controlled trial
ZAHREC/PR/19/005 Saleh Talib Handhal Biomonitoring and environmental exposure assessment of Phthalates and their metabolites in Zanzibar population
ZAHREC/PR/19/006 Dr. B. Jacob/ Dr. Salma Abdi Mahmoud
**Improving care after life threating acute obstetric complications; evaluation of a primary care-based psychological intervention in Zanzibar
ZAHREC/PR/19/007 Dr Fatma Kabole - NTD **Parasitology survey for urogenital schistosomiasis in pre-school, school-aged children, adolescents and adults in Zanzibar (Unguja and Pemba Islands.
ZAHREC/PR/19/008 Hamisi M. Malebo - PHL/NIMR
**Understanding the menstrual hygiene management (MHM) challenges facing school girls in rural and urban areas in Tanzania.
ZAHREC/PR/19/009 Dr. Farhat J. Khalid ZIHIVTB&LP
**Reducing the burden of TB among people living with HIV: Evaluation of implementation of isoniazid preventive therapy in Zanzibar.
ZAHREC/PR/19/010 Dr. Ali Omar Ali -Engender Health
**Research Protocol for the Post abortion Care Family Planning project in Tanzania Protocol number: TAN-41.**
ZAHREC/PR/19/011 Dr. Ali Omar Ali - EAC **Regional Assessment of Integrated Reproductive Maternal Newborn child and Adolescent health and HIV/AIDS Services in the East African community
ZAHREC/PR/19/012 Dr. Alibina Chuwa - NBS 2016 Tanzania Population Based HIV Impact Assessment (2016 THIS)’’
ZAHREC/PR/19/013 Dr. B. Jacod Improving care after life threatening acute obstetric complications; evaluation of a primary care-based psychological intervention ’’Friendship Bench’’, in Zanzibar.
ZAHREC/PR/19/014 Dr. Farhat J. Khalid ZIHIVTB&LP
**Evaluation of Implementation of Isoniazid Preventive Therapy in Zanzibar.
ZAHREC/PR/19/015 Dr. Farhat J. Khalid ZIHIVTB&LP
Retention in PMTCT care Cascade and Associated Factors in Zanzibar.
ZAHREC/PR/19/016 Annette Onken Etiology of febrile illness in patients presenting at Mnazi Mmoja Hospital, Zanzibar, with focus on Bacteremia, malaria, dengue fever and other viral diseases.
ZAHREC/PR/19/017 Peter Furu, Dr. Haji Mwevura - SUZA
Environmental Sustainability of hotels on Zanzibar.
ZAHREC/PR/19/018 Shaaban Hassan haji - ZIHIVTB&LP
Regional baseline study to document the prevalence, sensitivity patterns, treatment guidelines, packages and standards for Sexually Transimitted Infections (STIs) in the East African community (EAC) region.
ZAHREC/PR/19/019 Jutta M. Adelin Jorgensen Using a prospective register-based study, qualitative research, and economic analysis to support evidence sysntheses for health policy and system change in Zanzibar
ZAHREC/PR/19/020 Dr. Mohammad Zaman/ Dr. Quantitative modeling and system-level analysis of maternity and obstetric care at Mnazi Mmoja Hospital FP improved
55
Namba Principal Investigator &/or
Co- Investigator Andiko (Proposal)
Maryam A. Silas - Chukwani University
health outcomes
ZAHREC/PR/19/021 Said Mohammed Ali Innovative Strategies in the management of new born emergencies in Low- and middle- income countries (LMIC)
ZAHREC/PR/19/022 Esther Ngadaya, Msafir iMarijani - NIMRI
End of project evaluation for the East Africa Public Health Laboratory networking Project In Tanzania
ZAHREC/PR/19/023 Dr. Mtumwa I. Kombo - Engender Health
Using standards-based audit to assess and improve the quality of emergency obstetric care and exploring functioning of the referral system during pregnancy, labour and the postpartum period in Mbeya and Zanzibar, Tanzania. An implementation research.
ZAHREC/PR/19/024 Mr. Ahmed Gharib Khamis Field-Testing of proposed food-based dietary guidelines amongst consumers in Tanzania
ZAHREC/PR/19/025 Dr. Beatrice K Mutayoba/ Ms Asha Ussi - ZIHIVTB&LP
Assessment of the economic burden incurred by tuberculosis patients and their households on diagnosis and treatment of tuberculosis in Tanzania
ZAHREC/PR/19/026 Mr. Sunil Sazawal/ Said Mohammed Ali -PHL
To find Programmatically feasible methods of accurate assessment of gestational age and to tes biological markers as predictors of important maternal and fetal outcomes
ZAHREC/PR/19/027 Dr. Henrik Sjovall/ Myinyi I. Msellem - MMH
Patterns of antibiotic consumption in Zanzibar. Adherence to guidelines, availability and the roles of patients complience. A discriptive pilot study.
ZAHREC/PR/19/028 Dr. Ali Hussein Kassam - Chukwani University
A 4 year follow up of patients attending the diabetic clinic of Mnazi Mmoja Hospital, Zanzibar with focus on dietary habits, metabolic status and frequencies of diabetic foot complication.
ZAHREC/PR/19/029 Dr. Naufal Kassim Mohammed - MMH
Iodine status in goiter patients attending Mnazi Mmoja Hospital, Zanzibar
ZAHREC/PR/19/030 Abass T. Makame/Elizabeth A. Agoye - Engender Health
Satisfaction and Perception Survey: Assessing quality of case on provision of reproductive health services in supported facilities
ZAHREC/PR/19/031 Dr. Honorati Masanja/ Ame M. Ame - ZAHRI/IHI
** Implementation of post measles-rubella campaing vaccination coverage survey Tanzania 2019
ZAHREC/PR/19/032 Dr. Stefanie Knopp/Said Ali - PHL
The last mile: novel tools and strategies for breaking schistosomiasis transmission
ZAHREC/PR/19/033 Dr. Esther Ngadaya/ Dr. Salma Masauni - NIMRI
Assessment of the knowledge, attitude and practice related to Ebola Virus Disease (EVD) in Zanzibar
ZAHREC/PR/19/034 Dr. Fatuma Manzi - IHI ** Evaluation of National Introduction of HPV Vaccine in Tanzania
ZAHREC/PR/19/035 Said Mohammed Ali -PHL Cholera situation analysis and epidemiological study of cholera Hotsport in Zanzibar to inform preparedness and response planning
ZAHREC/PR/19/036 Ngonidzashe Marimo/Mwanaaisha Juma Fakih -SUZA
Final evaluation of Afya Bora ya Mama na Mtoto project (2015-2018)
ZAHREC/PR/19/037 Lucas Matemba/Mayassa S. Ally/ Ame Masemo - ZAHRI/NIMRI
Situational analysis on the magnitude of xero derma pigmentosum disease and its associated factors in Pemba Zanzibar
ZAHREC/PR/19/038 Mr. Said Mohammed Ali - PHL
Novel tools and strategies for breaking schistosomiasis transmission
ZAHREC/PR/19/039 Dr. Farhat J. Khalid - ZIHIVTB&LP
Rapid assessment to certain the situation of HIV infected children in Zanzibar
56
Namba Principal Investigator &/or
Co- Investigator Andiko (Proposal)
ZAHREC/PR/2020/0001 Daphrosa lyimo/ Mangi J.ame masemo
Factors affecting uptake of childhood vaccination in urban communities of Tanzania
ZAHREC/PR/2020/0002 Omar Mwalimu Reducing burden of hypertensive disorders in pregnancy (hdp) in Zanzibar at Unguja and Pemba island in a selected health care facilities and community
ZAHREC/PR/2020/0003 Dr. Ester Ndagaya Baseline study for the GRREAT initiative for adolescent girls in Zanzibar: Mbeya and Songwe Regions
ZAHREC/PR/2020/0004 Halima Ali Khamis Assessment of knowledge, attitude, belief and practices related to cholera prevention and control in Zanzibar
ZAHREC/PR/2020/0005 RehemaKahando/ Dr. Mtumwa Kombo
Endline evaluation for the PACFP project in Tanzania
ZAHREC/PR/2020/0006 Rickard Ignell/Khamis Ameir Haji
Assessment of push-pull technology for the control of exophilic malaria mosquitoes
ZAHREC/PR/2020/0007 Shaali Makame Ame Comparative genomics of adult ecatorramericanusworms exposed to different levels of ALB: new insights into the mechanisms of anthelminthic resistance
ZAHREC/PR/2020/0008 Ester Ndagaya/ Halima ali Khamis
Assessment of knowledge, attitude and practice related to Corona virus disease (Covid-19) in Tanzania mainland and Zanzibar
ZAHREC/PR/2020/0009 Dr. Sanaa S. Said Chronic inflammatory joint disease in Zanzibar. Status quo and what to do A study of disease characteristics, treatment and follow-up
Angalizo ** Tafiti zilizokamilika
57
58
Kiambatisho Namba 9: Mchanganuo wa maombi kwa mwaka wa fedha 2020/2021
Maelezo ya Matumizi Wizara
ya Afya - HO1
Matumizi ya Shughuli za Maendeleo Matumizi ya
Kawaida kutoka
Serikalini
Jumla kuu Mchango wa
Serikali
Misaaada
washirika wa
Maendeleo
Mikopo
washirika wa
maendeleo
Jumla ya fedha
za Maendeleo
Programu ya Kinga na Elimu ya Afya
Huduma za Kinga na Elimu
ya Afya
7,417,831,000.00 7,417,831,000.00
Mradi Shirikishi wa Huduma
za Afya ya Uzazi wa Mama
na Mtoto
500,000,000.00 9,574,373,234.00
10,074,373,234.00
10,074,373,234.00
Mradi Shirikishi wa Kudhibiti
Maradhi wa Ukimwi, Kifua
Kikuu, Ukoma na Homa ya
Ini
248,000,000.00 5,090,361,742.00
5,338,361,742.00
5,338,361,742.00
Mradi wa Kudhibiti Malaria
Zanzibar
248,000,000.00 5,586,365,024.00 5,834,365,024.00
5,834,365,024.00
Jumla ndogo
996,000,000.00
20,251,100,000.00 21,247,100,000.00 7,417,831,000.00 28,664,931,000.00
Programu ya Tiba
Programu ndogo ya
Uchunguzi 29,129,268,000.00 29,129,268,000.00
Huduma Ndogo ya
Matibabu 2,728,942,000.00 2,728,942,000.00
Mradi wa Kupandisha Hadhi
Hospitali za Wilaya na Vijiji 5,000,000,000.00 5,000,000,000.00
5,000,000,000.00
Mradi wa Kupandisha Hadhi
Hospitali ya Mnazi Mmoja 1,500,000,000.00 1,500,000,000.00 1,500,000,000.00
Ujenzi wa Hospitali ya Afya
ya Akili 1,400,000,000.00 1,400,000,000.00 2,800,000,000.00 2,800,000,000.00
Ujenzi wa Hospitali ya Binguni 6,000,000,000.00 6,000,000,000.00 6,000,000,000.00
Ujenzi wa Bohari Kuu ya
Dawa Pemba 2,000,000,000.00 2,000,000,000.00 2,000,000,000.00
Ujenzi wa Maabara ya
Chakula na Dawa (ZFDA) 2,100,000,000.00 2,100,000,000.00 2,100,000,000.00
59
Maelezo ya Matumizi Wizara
ya Afya - HO1
Matumizi ya Shughuli za Maendeleo Matumizi ya
Kawaida kutoka
Serikalini
Jumla kuu Mchango wa
Serikali
Misaaada
washirika wa
Maendeleo
Mikopo
washirika wa
maendeleo
Jumla ya fedha
za Maendeleo
Jumla ndogo 18,000,000,000.00 1,400,000,000.00
19,400,000,000.00 31,858,210,000.00 51,258,210,000.00
Programu ya Usimamizi wa Sera za Afya na Utawala
Utumishi na Uendeshaji 7,149,122,000.00 7,149,122,000.00
Sera Mipango na Utafiti 2,367,344,000.00 2,367,344,000.00
Usimamizi wa Huduma za
Afya Pemba 8,796,493,000.00 8,796,493,000.00
Ujenzi wa Maabara ya Taasisi
ya Utafiti wa Afya 2,000,000,000.00 2,000,000,000.00
2,000,000,000.00
Jumla ndogo 2,000,000,000.00 2,000,000,000.00 18,312,959,000.00 20,312,959,000.00
Jumla (Fungu (H01) 20,996,000,000.00 21,651,100,000.00
42,647,100,000.00 57,589,000,000.00 100,236,100,000.00
Programu ya Hospitali ya
Mnazi Mmoja Fungu H02
Matumizi ya Shughuli za Maendeleo Matumizi ya
Kawaida kutoka
Serikalini
Jumla kuu Mchango wa
Serikali
Misaaada
washirika wa
Maendeleo
Mikopo
washirika wa
maendeleo
Jumla ya fedha
za Maendeleo
Programu ya Uchunguzi na
Matibabu
3,454,523,050.00 3,454,523,050.00
Programu ya Uongozi na
Utawala
14,394,076,950.00 14,394,076,950.00
Jumla (Fungu (H02) 17,848,600,000.00 17,848,600,000.00
Jumla Kuu - Wizara ya Afya
H01 na H02 20,996,000,000.00 21,651,100,000.00
42,647,100,000.00 75,437,600,000.00 118,084,700,000.00