shujaa katika africa - andy chande€¦ · 9 utangulizi kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya j.k....

281
1 Shujaa Katika Africa

Upload: others

Post on 18-Jul-2020

57 views

Category:

Documents


9 download

TRANSCRIPT

Page 1: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

1

Shujaa Katika Africa

Page 2: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

2

Picture of J.K.Chande

Page 3: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

3

Shujaa Katika Africa

SAFARI KUTOKA BUKENE

J.K.CGANDE

Page 4: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

4

PUBLISHER / PRINTER INFO

Page 5: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

5

DIDICATED TO

Page 6: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

6

BLANK

Page 7: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

7

CONTENTS IN KISWAHLI

Page 8: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

8

BLANK

Page 9: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

9

UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri na Dola ya Kiingereza. Simulizi inajaribu kutoa picha ya maisha ya mtu, na vile vile vituko vya wakati huo, yote mawili kwa ufasaha kabisa. Miaka ya mwanzo ya Karne ya Ishirini ikishuhudia kuhamia Afrika Mashariki wa Wahindi waliokuwa raia wa Kiingereza, baadhi yao kusaidia ujenzi wa reli za Afrika Mashariki, na wengine kujenga mtandao wa Biashara katika eneo hilo. Mmoja wa hawa, Kashavji Chande, baada ya kujitumbukiza katika safari ya hatari ya meli kutafuta utajiri, akaanzisha kitu ambacho, wakatu ule wa robo ya pili ya karne, kilionekana kuwa chombo kikubwa sana cha biashara, Kampuni iliyoitwa “Chande Industries Ltd.” Mwanawe, Jayantilal Keshavji Chande, maarufu kwa jina la mkato JK, au Andy, akawa ndiye nguzo ya Kampuni ile ya familia, ingawa kwa muda mfupi mno, kutokana na kunaswa katika wimbi la kutaifishiwa mali katika miaka ya ’60. Bila kukata tamaa, aliendelea mpaka akawa mtu mashuhuri katika uendeshaji wa Kampuni ya Viwanda na Biashara ambayo haikuwa yake tena, bali sehemu ya Makampuni ya Biashara na Viwanda yaliyomilikiwa na Serikali ya Tanzania. Hiyo ndiyo hadithi yenyewe, inasisimua, inasikitisha, lakini inatia hamasa. Maelezo tunayoyaona humu kuhusu kipindi kile cha kabla ya Uhuru yamesheheni vituko, mivutano kati ya watu, na matarajio ya mafanikio katika Uchumi., Wazazi wa JK walikuwa wamebobea katika fani ya Uhasibu, kukisia miradi inayoleta faida, kujitahidi kwa moyo wote kujenga uhusiano mwema na wakulima waliowauzia mazao, na kununua mali iliyosindikwa au iliyoingizwa kutoka katika nchi za nje. Ingawa hakuzipenda Taratibu za Elimu zilizokuwa na Ubaguzi wa Rangi, JK aliiitumia vema nafasi aliyopewa na familia iliyompenda sana. Akiutumia uzoefu wake, akisaidia katika kuhakikisha kuwa

Page 10: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

10

mipango katika kipindi kile cha mpito kuelekea kwenye Uhuru iliwashirikisha watu wote na wa rangi zote. Miaka sita baada ya Uhuru wa Tanganyika likaja wimbi la kutaifishwa kwa shughuli muhimu za Uchumi. Shughuli zote za Viwanda na Biashara za familia ya Chande, na za watu wengine, zikataifishwa na Serikali. Ni uvumilivu na uzalendo mkubwa wa familia ya Chande, siyo tu kwamba waliikiri hatua hiyo iliyochukuliwa na Serikali, lakini vile vile walikubali, kwa moyo mmoja, kusimamia mabadiliko ya kumiliki sehemu hii ya Uchumi wa Nchi. Kwa kuujua vema moyo na uwezo wa JK katika mambo ya biashara, Rais Nyerere akamkabidhi kwa miaka mingi Uenyekiti na Usimamizi wa Badi za Mashirika mengine ya Umma. Kwa kuwa, kwa miaka mingi, Mashirika hayo yamekuwa yakiendeshwa na yakisimamiwa na Watumishi wa Serikali Wastaafu, kazi hiyo iliviza uvumilivu wake, ujuzi wake na matumaini yake. Maelezo yake juu ya mabishano yaliyokuwapo kati ya wakubwa hao yanashangaza sana, ingawa hatimaye alifanikiwa. Pamoja na vizingiti alivyopambana navyo, ingawa alivaa madaraka makubwa, alitekeleza majukumu yake kwa ujasiri mkubwa, kwa busara na kwa mafanikio. Hakupata cheo cha maana cha siasa katika Tanzania Huru, lakini bado ushawishi wake katika mwelekeo wa siasa ulikuwa mkubwa; na kitabu hiki kinaeleza kirefu mafanikio hayo. Maelezo yaliyo humu hayako bayana, lakini matokeo yake hayana ubishi, kwa ngazi ya Taifa na ya Kimataifa. Mashirikiano yake peke yake, na watu wengi sana, ni ushahidi wa kutosha wa umaarufu wake. JK ni mtu mwenye vipaji vingi, habari ya maisha yake haitakamilika bila kutaja mambo anayoyapenda. Wengi wa mambo hayo anayoyapenda na madaraka aliyonayo yanashangaza kweli kweli. Nilimtambua mara ya kwanza kutokana na ari yake katika masuala ya elimu, aliponitumbukiza katika Bodi ya Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert. Baadaye nikagundua kuwa alikuwa kiongozi mashuhuri katika Shule ya Viziwi, na mambo mengine mengi sana ya kuchangia katika shghuli za Jamii za Rotary na Freemason. Huyo ni mtu asiyepumzika katika shughuli za kuisaidia

Page 11: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

11

Jamii siyo kwa kuchangia tu ila, muhimu zaidi, kwa kuwahamasisha kwa moyo wake wote. Lakini vile vile amekuwa mtu mwenye kuipenda mno familia yake: miaka hamsini ya ndoa yake nzuri na Jayli ilianza kwa mapenzi ya hofu-hofu, lakini ikaishia kwenye pingu za mahusiano na mapenzi makubwa. Ukizungumza na mmoja wao utatambua jinsi alivyo na mapenzi makubwa mno kwa mwenzake, pamoja na mapenzi yao, wote wawili, kwa watoto wao watatu, wote wa kiume. Kwa baba ambaye kazi zake na huruma yake ni kubwa mno, kiasi cha kukaribia kupotelewa na akili, mshikamano huu wa familia, mseto huu wa upendo na uvumilivu ni mfano wa kuigwa na kwa kweli unatia moyo. Kwa historia yake hiyo JK ameipa Tanzania nafasi ya pekee ya kukumbuka, kuhifadhi na kuchambua na, kama hapana budi, kuandika upya Historia ya Tanzania. Kumbukumbu za Wakoloni ni sehemu tu ya Historia yetu; lakini tunapaswa vile vile kuandika yale ambayo sisi wenyewe tunayakumbuka, kwa vigezo mbalimbali tunavyovijua sisi. Natumaini kuwa mawazo hayo yatawashawishi rafiki zake wa Mataifa yote nao kuandika wanayoyajua. Ametambuliwa, na kupewa Heshima, na Vyombo vya Taifa na vya Kimataifa, heshima ambayo anaistahili kabisa. Mimi nafurahi kuhusishwa na kutambuliwa kwa sifa na heshima anayopewa. Maisha ya JK yanadhihirisha zama, tangu Wahindi walipohamia Afrika Mashariki, na kuendelea wakati wa kudai Uhuru, na kuzaliwa kwa Taifa Huru la Tanganyika, mpaka kuzaliwa kwa Jamhuri na Muungano wa Tanzania. Na sasa tuko kizingitini tukitafuta namna nzuri ya kuiunganisha Afrika Mashariki, na hatimaye kuifanya dunia kuwa kitu kimoja. Nampa Heshima yake JK; Mtanzania mashuhuri, na mtu mashuhuru mwenye sifa ya Kimataifa. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika. Benjamin William Mkapa

Page 12: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

12

Rais, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

BLANK

Page 13: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

13

MAELEZO YA MWANZO Babu yangu, nasikia, alikuwa mtu mashuhuri. Alikuwa mashuhuri kwa sababu ya upendo wake mkuu wa familia yake; na vile vile kwa sababu alikuwa mkaribu mno kwa mtu yeyote aliyeomba msaada wake. Kadhalika alijulikana sana kutokana na huruma yake katika biashara ya minadani. Mara nyingi babu yangu alimpelekea Kadi Dalali wake aliyekuwa Rajpar, akimwelekeza katika masuala ya Hisa za Mafuta, za Nafaka na za Madini. Hatima yake, mara nyingi, aliishia kwenye kununua vitu kwa bei kubwa, na kuviuza kwa bei ndogo! Shamba dogo la familia, na biashara ndogo aliyokuwa anaifanya kule India ya Magharibi, visingeweza kuhimili hasara za mara kwa mara kama hizo. Misukosuko ilitokea kila mara, ambayo iliweza kutulizwa tu kwa njia za zimamoto. Kisha, mwanzoni mwa mwaka 1922, mkasa wa mwisho ukatokea ambapo baba yangu aliumwa na mbwa mwenye kichaa; akaugua mpaka akafa ! Hofu ya kufilisika iliyotuandama kwa muda mrefu sasa ikawa imedhihirika. Hata hivyo, mila zetu zilikuwa zinazuia kuuzwa kwa rasilmali peke yake ya maana iliyobaki ; eka 50 za shamba walilolilima kwa vizazi kadha. Hapo ndipo baba yangu ; Keshavji alipolazimika kufanya maamuzi muhimu. Wakati huo, akiwa na umri wa miaka 22 tu, akaamua kulipa madeni yote ya familia, siyo kule kwao India, ila kwa kupanda meli iliyokuwa inakuja Afrika, akimwacha huko mamaye mjane, ndugu zake watatu wa kiume, na wawili wa kike ; na mkewe aliyekuwa na umri wa miaka 18, na binti mdogo mmoja, wake mwenyewe. Miaka 45 baadaye, Februari 10, 1967, niliitwa na Mheshimiwa Waziri wa Tanzania wa biashara, kwa Taarifa ya saa mbili tu pale. Katika muda aliouchukua Mhe. Waziri kusoma ibara mbili tu za kurasa zilizochapwa kwa mashine, mali zote za familia zilizolimbikizwa Tanzania yote ya nyuma, zikachukuliwa ! Mali zangu zote kabisa zikawa zimetaifishwa na Serikali ya Tanzania. Kama ilivyomtokea baba yangu kabla yangu, nilikodoa macho kuuangalia mkasa huo, nikitambua kwamba vizazi vya familia

Page 14: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

14

yangu vilikuwa vinanitegemea mimi katika masuala ya fedha. Lakini, tofauti na alivyofanya baba, sikujitumbukiza kwenye meli kwenda katika nchi nisizozijua, nikitafuta ahueni katika Bara lingine. Mimi nilibaki Tanzania ; nchi niliyoipenda, na huku ndiko kwetu. Lakini saa ile niliona kama nchi yangu nayo imenitupa ! Hayo ndiyo maelezo yangu.

Page 15: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

15

SHUKRANI Kwa miaka mingi sasa ndugu zangu marafiki na wajoli wengine wamekuwa wakinishawishi niandike habari za maisha yangu. Ingawa ilikuwa dhamiri yangu wakati wote kufanya hivyo sikuupata muda huo kwa sababu ya kusafiri mno ili kukamilisha mahitaji niliyoahidi kuwatimizia. Nilipochapisha, mwaka 1995, makala nilizokusanya juu ya Kikundi cha Freemason, katika Jarida lililoitwa "Mwelekeo wako ni Wapi", nilikuwa nimeanza kuitekeleza ahadi hiyo kwa juhudi kubwa. Lakini vile vile, kusafiri kwangu mara kwa mara kukasababisha kazi hiyo kuwa ngumu. Mwaka huu uliopita, shinikizo za marafiki zangu zimenisukuma kutimiza Ahadi hiyo iliyochelewa sana, na wakanisaidia katika kazi ya kunakili matukio fulani. Limekuwa jambo la furaha iliyoje kupata maisha ya furaha namna hii nchini Tanzania. Nani aliyepata bahati kama niliyoipata mimi : kuwa na familia, mafariki na jamaa walioniongoza na kunichangamsha katika maisha yangu, na wakati wote mimi nikiwa mwenye kufaidika ? Baada ya kusema hayo, sina namna ya kuwashukuru watu wengi namna hiyo walio sehemu ya maisha yangu, pamoja na wale walionisaidia kuandaa kumbukumbu zangu. Mimi nawajua, na wao wananijua nao watafurahi kujua kwamba nitaendelea kuwashukuru daima kwa kunitia moyo ; nitawashukuru pia kwa uaminifu wao, kwa usafi wao wa moyo, na kwa misaada yao mingi. Kwao wote natoa shukrani zangu, na kuwahakikishia mapenzi yanayodumu. Nawashukuru, Mchapishaji wa Penembra Press, Dk. John Flood ; namshukuru Douglas Campbell, Mhariri wangu mvumilivu aliyepanga mwelekeo wa Kitabu changu ; na mchoraji hodari wa Penumbra, Mag Carson. Kukipa Kitabu hiki heshima ya kuwa kumbukumbu ya mke wangu Jayli, na ya familia yangu, ni hatua inayostahili. Kwa mara nyingine natambua kwa furaha bahati niliyokuwa nayo kwa kumpata Jayli kuwa mwenzangu kwa kipindi kirefu cha maisha

Page 16: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

16

yangu. Namnong’onezea penzi langu Jayli ambaye, miaka hamsini iliyopita, alinichagua mimi kuwa mumewe. Rais wa Tanzania, Mhe. Benjamin William Mkapa, kwa mapenzi makubwa ameniandikia Utangulizi, na kwa Heshima hiyo nawiwa shukrani nyingi kwake. Wakati wote ameijengea sifa Ofisi ya Rais, na Nchi yetu kadhalika. Kwa hakika kabisa, Rais Mkapa ni mmoja wa Viongozi mashuhuri kabisa katika Bara la Afrika.

Page 17: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

17

MOJA

BUKENE MJI WANGU UTOTONI Nilizaliwa Mombasa tarehe 7 Mei, 1928. Baba yangu, Keshavji na mama yangu Kanku waliishi Bukene, katika Wilaya ya Nzega ya Jimbo la Magharibi la Tanganyika. Huko ndiko nilikozaliwa. Mara baada ya mama yangu kupata nguvu za kuweza kusafiri, tukaenda Bukene. Kwa mujibu wa mila za kabila la Hindu, shangazi yangu ndiye aliyenipa jina, naye akanichagulia jina la Jayantilal, kutokana na herufi tatu za alfabeti zilizojitokeza katika ramli; ya kwanza ikiwa J. Lakini jambo ambalo halikuzingatia taratibu ni kwamba kuzaliwa kwangu duniani hakukuandikishwa rasmi kule Mombasa mpaka baada ya miaka mingi kupita; na hata wakati huo nikawa nimeandikishwa kwa mujibu wa kalenda ya Hindu; ndiyo sababu ya kuandikwa ndani ya Daftari kuwa nilizaliwa Agosti 27, 1929. Kwa hiyo kama alivyo Malkia wa Uingereza, nikajikuta nina tarehe mbili tofauti za kuzaliwa; kadhalika, sawasawa na Malkia wa Uingereza, kila tarehe ina mwaka wake tofauti. Bukene, mji wangu nchini Tanganyika, haukuwa zaidi ya kijiji katika mavumbi katika nchi ambayo, wakati huo, ilikuwa inaitwa Afrika ya Mashariki ya Wajerumani. Mji huo, ulio kiasi cha maili 50 Kaskazini ya Tabora, wenyewe ulikuwa maarufu kama Soko la Waarabu la Watumwa na, baadaye, Makao Makuu ya Mkoa wa Wakoloni. Watu wa Bukene walikuwa Jamii iliyoshikamana sana, iliyoelekeza nguvu yake kwenye kilimo cha mpunga na mahindi, hasa kwa ajili ya chakula chao wenyewe. Baba yangu, Keshavji, alikuwa na duka katika barabara kuu, iliyokuwa barabara peke yake mjini hapo, akiuza bidhaa mbali mbali, pamoja na mafuta. Lakini vile vile alifanya biashara ya mazao ya kilimo yaliyokuwa yanapatikana huko, akiwa kama dalali kati ya wakulima na wanunuzi waliokuwa wanahudhuria masoko ya Tabora na Dar es Salaam. Mara nyingine aliwapa fedha wakulima wa eneo hilo waliokuwa wametindikiwa, ingawa alipata faida kidogo sana zaidi ya uhusiano mwema.

Page 18: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

18

Mara nyingi zaidi faida aliyokuwa anaipata ilikuwa ndogo mno, si zaidi ya thamani ya kuuza gunia tupu au madebe matupu ya mafuta; faida peke yake ya maana aliyopata ilitokana na biashara kubwa alizofanya kwa kuuza mchele. Lakini, wakati mimi nazaliwa, biashara yake iliyokuwa inategemea misingi imara ya biashara ilianza kushamiri. Kama wale wengine waliofika Bukene, Keshavji naye alifika huko kwa njia ya kuzunguka. Kituo chake cha kwanza, baada ya kuondoka Kijijini kwake Ged Bagasara, ambako sasa ni Gujerati, kilikuwa Bandari ya Bombay. Hapo alipanda meli iliyoitwa S.S. Karagola, ya Kampuni ya Kiingereza ya Meli, iliyokuwa inakwenda Mombasa. Huko Mombasa, kwa kutumia mtandao alioujenga mkwewe, Manjibhai Damodar Ruparelia, aliyekuwa na biashara iliyoshamiri katika Pwani ya Waswahili, Makao yake Makuu yakiwa Mombasa, Keshavji akapata kazi katika Kampuni ya Mfanya-biashara wa Kihindi aliyebobea ambako, akisimamiwa vema na mwenye Kampuni, Haji Abdulrahman Issa, alifanya kazi kwa ujira mdogo sana. Akifikiria shida za watu wa familia yake kule India, huku akiitarajia siku ambayo mkewe na watoto wake wadogo watakuja kuungana naye, baba yangu alifanya kazi kwa bidii kubwa, huku akihangaika kutafuta kazi na Majukumu ya ziada. Mnamo kipindi cha mwaka mmoja akawa amewaridhisha mno Waajiri wake wapya kiasi cha kupewa Hisa zilizompa ubia katika Kampuni hiyo; lakini yeye akakataa. Hata hivyo, ingawa hakuwa tayari kuuza, kwa kigezo cha fedha, hatima yake katika Kampuni hiyo, wakati huo alikuwa amekwisha iweka familia yake katika hali nzuri. Baadaye, alipoamua kuishi Dar es Salaam badala ya Mombasa, ili kuepuka kutegemea ukarimu wa wakweze, kwa maisha yake, Baba yangu akaanza kufanya kazi ya biashara. Halafu, mwaka 1924, mkasa mwingine ukatokea; matatizo ya macho yake yakamlazimu kurudi India kutafuta matibabu; akakaa huko mwaka mzima kuimarisha afya yake, kufufua biashara za

Page 19: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

19

familia, na shughuli za shamba. Lakini wakati wote huo Afrika ilikuwa inamwita; na mwaka 1925 hakuweza tena kuahirisha kuuitikia wito huo. Mwishoni mwa Karne ya kumi na tisa, mmoja wa binamu zake, Jathalal Velji Chande, alisafiri kwa jahazi, pamoja na nduguze, kuja Dar es Salaam. Jahazi hilo la tanga moja: dogo, jembamba na chakavu, lilikuwa linatumiwa na wachuuzi wa Kiarabu miaka nenda miaka rudi; lakini lilikuwa linakwenda kasi sana. Kwa njia hiyo hiyo, Keshavji alisafiri mpaka Tanganyika, na kujiunga na Kampuni ya binamu yake iliyokuwa tayari imeshamiri. Wakati huo reli ya kuunganisha Mwanza na Tabora ndiyo kwanza imefunguliwa na, kwa njia hiyo, nafasi nyingi za biashara zikapatikana katika eneo hilo la Tanganyika ya Magharibi. Kwa sababu zisizojulikana labda ukereketwa wa Ofisa mmoja wa Kikoloni aliyekuwa Makao Makuu ya Jimbo, Tabora, Kijiji hicho kidogo cha Bukene, kilichokuwa katika njia hiyo ya reli, kikapata kujengewa stesheni. Keshavji akaja Bukene na, mnamo mwaka mmoja akafuatiwa na mkewe na binti yake. Baba yangu alipokuja Bukene mara ya kwanza barabara hiyo hiyo moja ya udongo mwekundu ndiyo iliyokuwako, tena ilikuwa na urefu wa yadi mia nne tu. Mwisho wake barabara hiyo, kila upande, ilikuwa inapotea, kila ulipofuata, kwenye mbuga isiyoeleweka kwa maili nyingi kupitia vichaka vyenye vijumba hapa na pale, vinavyozungukwa na miti ya matunda. Bukene ni mji uliokuwa na historia nchini Tanganyika ya kuwa na farasi, angalau mmoja; lakini mwaka 1925 badala ya farasi mmoja ikawako gari moja. Lakini bado Bukene walikuwako punda wengi, na kuku walioparura ardhi mbele ya nyumba zao. Na nyumba zenyewe: haikuwako wakati huo hata moja iliyokuwa na namba wala jina. Zilikuwa zinalingana hali, na zilikuwa zinawatosha kwa shughuli zao: kuta na sakafu udongo mtupu, kama ilivyokuwa desturi yao, lakini juu madebe yaliyochanwa au, kwa nasibu, mabati yaliyochakazwa na jua la kiangazi cha miezi sita.

Page 20: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

20

Katika moja ya nyumba za aina hiyo kiasi cha hatua 50 kutoka Shule ya Kijiji iliyokuwa na darasa moja, ndimo baba yangu alimoweka Ofisi yake ya kwanza, na ndimo mumo humo mlimokuwa duka lake. Baadaye mama na dada yangu walipofika, akaipata nyumba iliyokuwa jirani na duka, ambamo wote kabisa waliishi. Yeye hakuwa wa kwanza, wala hakuwa mfanyabiashara peke yake, aliyevutiwa kwenda kwenye sehemu hii ya Jimbo la Magharibi. Wafanyabiashara wengine, hasa Wahindi, ingawa Waarabu nao walikuwako, walivutiwa kwenda kwenye maeneo hayo kwa sababu ya reli mpya iliyotandikwa, na taratibu zilizokuwa zimepangwa za kupanua kilimo. Tukio la kwanza la utotoni ninalolikumbuka ni la duka, hasa ile mashine ya kukobolea mahindi iliyokuwa upande mmoja wa dirisha. Kama nina uhakika wa kitu chochote cha wakati ule basi ni ule udadisi unaokaribia wazimu, wa kutaka kujua vitu na watu wanavyoweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi nilioupata, nikiwa mtoto, kutokana na kukaa muda mwingi katika mazingira hayo. Kila kitu, kiwe kidogo namna gani: kifuniko cha kopo, au kipande cha dumu la mafuta, kimejikita kichwani mwangu kama kumbukumbu ya milele ambayo bado ninaifurahia hadi sasa. Katika kichwa changu bado naliona lile dumu la galoni nne za petroli lenye alama ya Kampuni ya Vacuum Oil ya Afrika Kusini, likiwa limetupwa kama takataka nje mbele ya duka. Ndani, yakiwa yamepangwa juu ya meza za mbao, yakawamo marobota ya pamba ambayo, kwa kuwa wanunuzi wetu wengi hawakujua kuwa ni pamba inayouzwa, yalikuwa ndiyo magodoro ya msaidizi wa familia, kijana asiyejali, ambaye baba alimleta kutoka India. Chini, sakafuni, ilikuwako mizigo ya sabuni za kufulia na za kuogea, zenye rangi za bluu na manjano, kila mzigo ukiwa na miche 24. Sabuni hizo zilikuwa zinauzwa katika vijiji vyote vya Jimbo la Magharibi: kwanza miche mizima mizima kwa Wafanyabiashara wa Vijijini, kisha na wao wanauzia familia za Wakulima baada ya kuikata vipande vipande, kila mche vipande vinane. Pamoja na mazao ya mpunga na mahindi, baba yangu vile vile alikuwa anashughulikia mazao ya alizeti, nyonyo, muhogo,

Page 21: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

21

njugumawe, mkonge, nta na asali; vyote hivyo vilikuwa vinaonekana katika duka hilo moja. Nta na asali ndivyo vilivyokuwa vipimo vya Hali ya Hewa katika maeneo ya Bukene na Tabora, maana mvua zilipokuwa hazitoshi ndipo Wakulima walipopata sababu ya kupambana na nyuki katika ‘makoloni’ yao. Hata hivyo, lilikuwako soko tayari kwa nta na asali yote iliyoweza kupatikana, kiasi kwamba katika miaka iliyofuata, wakati wa Vita Vikuu vya Pili, baba yangu alikuwa anauza asali mara kwa mara katika Kampuni iliyoitwa United Kingdom Commercial Corporation, mali ya Serikali ya Kiingereza, ambapo nta hiyo ilikuwa kiungo muhimu kwenye Kampuni ya kutengenezea mafuta ya kujipaka. Hata Serikali ya Jimbo nayo ilihimiza biashara ya masega ya nyuki, kwa kumteua Afisa wa Nyuki aliyeitwa Smith, na kumweka katika Ofisi iliyoanzishwa kwa madhumuni hayo mjini Tabora. Bwana Smith, akiwa na mahusiano ya karibu na wanunuzi wa nta ya baba yangu, alifurahiwa sana na yale aliyoyaona kwa wapakuaji wa asali katika Jimbo la Magharibi hata baadaye akaandika kitabu kuhusiana na shughuli hizo. Nilipokuwa na umri wa miaka sita nilibadili taratibu zangu za kila siku kuhudumia duka, Ofisi na nyumbani, nikajitumbukiza badala yake kwenda darasani katika shule ya kijiji. Wakati ule Bukene zilikuwako shule mbili: Shule ya Wahindi iliyokuwa na watoto wapatao arobaini, waliokuwa na umri wa kati ya miaka sita na kumi na tano; na Shule ya Halmashauri ya Wilaya, iliyojengwa na Serikali ya Wakoloni, kwa ajili ya watoto wa Kiafrika. Kwenye shule ya Wahindi mafunzo yalikuwa katika lugha ya Gujerati, na wote sisi tukawa chini ya mafundisho ya Bwana Jigjavan, Mwalimu aliyefundisha na kuishi kwenye nyumba hiyo hiyo moja, na yenye chumba kimoja. Kwa angalau sababu moja ya Kanuni, Jagjivan aliipuuza shida hiyo. Kwa sababu ambazo hazikupata kuwekwa wazi, Waingereza waliokuwa wanatawala Tanganyika hawakushabikia kabisa kujenga msingi imara wa Elimu katika mfumo uliowekwa na Wajerumani.

Page 22: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

22

Kwa hiyo, badala ya kudhamiria kusimamia mitaala na mafanikio ya Vituo vya Elimu vilivyokuwa sasa chini ya Himaya yao, kama walivyofanya Watawala wa Kikoloni kwingineko, katika maeneo yaliyoonekana katika ramani kuwa na dosari, hawa wa Tanganyika walifanya mambo yao bila kujali, wakiwaachia Wamisionari wa Kilutheri, waliokuwa wameenea nchi nzima kwa kuambatana na Utawala wa Wajerumani, kuendelea kupanga na kutoa elimu katika mzingira yasiyokuwa sawa. Usimamizi wa shule kama ile aliyokuwa anaiendesha Jagjivan ukawa kama kutimiza wajibu tu: kwa ukaguzi kutoka Tabora wa nusu saa kila mwaka. Lakini kama majukumu ya Mkuu wa Shule yalionekana kuwa mepesi kuliko kawaida, sisi wanafunzi ndio tuliofidia ugumu wa kazi yake kutokana na uwezo wetu katika umri tuliokuwa nao. Mpango wa Javjigan katika kukitegua kitendawili hicho ulikuwa kuwa na darasa la nje ambako wanafunzi waliokuwa na rika na bongo zilizokabiliana walijikusanya katika sehemu tatu au nne, zilizoonekana kuwa zinafaa kwa zoezi hilo. Inawezekana hakuna hata mmoja wetu aliyetoka kwenye shule ile ya chumba kimoja, Bukene, akiwa na uwezo wa kuendelea na elimu ya juu zaidi; lakini vile vile hakuna hata mmoja wetu aliyetoka bila alama nzuri, hata kama ya lugha ya Gujerati, katika masomo yote muhimu ya Mtihani wa Cambridge. Siku zangu za shule wakati ule sita kwa juma kama zilivyokuwa za watoto wengine wote wa siku zile, na pengine za watoto wengi wa siku hizi, zilikuwa na ratiba ngumu. Saa moja asubuhi mara baada ya jua kuchomoza, mama yangu aliniamsha kutoka katika chumba tulichoshirikiana na wenzangu wawili. Baada ya hapo nilipiga mswaki, siyo kama huu wa kizungu, ila ule wa miti unaotafunwa, uliofanya meno yangu kuwa meupe ajabu. Baada ya kwenda haja kwenye choo cha shimo na ndoo ya maji mkononi, nilioga maji yaliyokuwa kwenye gudulia la zamani la shaba, yaliyokuwa yamechemshwa kwa mkaa. Nilipokuwa mtoto sikutumia sabuni kuogea bali mbegu za mhalita ambazo, zikitumbukizwa kwenye maji, hutoa povu jembamba lenye harufu nzuri. Nikiwa safi, na nimevaa nguo zangu, nilikaa chini ukumbini na, nikitumia meza fupi, kupata chai aliyonipikia mama yangu,

Page 23: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

23

iliyokwishatiwa sukari. Baada ya hapo nilitembea kwa dakika tano kufika shule. Mchana nilirudi nyumbani, kula na kupumzika. Tulitakiwa shule tena saa nane mchana, wakati ambapo ukali wa jua la utosini ulipoanza kupungua; na tulimaliza masomo saa kumi na moja. Haikuwa kawaida kwa baba yangu kufunga duka lake kabla ya saa moja na nusu usiku. Kwa hiyo ili kujishikiza mpaka wakati wa chakula hicho cha usiku, ambapo watu wa familia tulikula pamoja, nilibugia haraka haraka maandazi machache, matamu, kabla ya kurudi kwenye uwanja uliokuwa kiasi cha nyumba nne kutoka kwetu, kucheza volleyball au marbles na marafiki zangu. Kusema kweli sikuwa hodari wa mchezo wowote kati ya hiyo; nilipoteza michezo kwa marafiki zangu wa shule kwa kiwango ambacho hata marafiki wa babu yangu wangevionea aibu. Lakini katika ulimwengu wa siku zile, ambapo hata magazeti hayakuwapo, wala radio, kilichokuwako tu ni gramafoni ya kunyonga ‘utumbo’, iliyotumiwa zaidi kuwafurahisha wazazi wetu kuliko sisi, kule kupoteza mchezo wa volleyball au marble na, kwa nasibu nilipopata bahati ya kuchungulia gazeti la vichekesho katika lugha ya Gujerati, ndipo nilijihesabu siku hiyo kuwa nimestarehe sana. Hiyo ilikuwa moja ya starehe; ya pili ni Treni iliyokuwa inasimama stesheni ya Bukene. Treni katika reli hiyo ya Mwanza-Tabora hazikuwa nyingi, na hizo za awali ndizo zilizoweka mwelekeo wa siku za mbele. Lakini thamani ya ile nadra ya msururu mrefu wa mabehewa ya mizigo, na zaidi sana wa mabehewa ya abiria, iliwafanya watu wa Bukene waone kwamba kuingia kwa Treni Bukene lilikuwa tukio la kufurahia. Nilipokuwa mtoto, Treni ya mizigo, ilipita Bukene kwa wastani wa mara moja kwa siku. Treni za abiria zilipita mara moja kwa juma, kila Jumatano majira ya saa mbili usiku; na Wananchi wengi walioongozwa na Steshenmasta Mhindi walifurahia kufika kwa treni hiyo kana kwamba wanaiona kwa mara ya kwanza. Steshenmasta mwenyewe alijitokeza akiwa amevaa suti ya kaki na kofia ya pama.

Page 24: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

24

Mtu peke yake anayeweza kuelewa, angalau kidogo, furaha tuliyokuwa tunaipata sisi watoto wadogo wote, katika wakati ule wa miaka ya 1930, ni yule aliyekuwa anaishi katika kijiji kile cha Bukene wakati huo, kwa wakati filimbi ya Treni iliyokuwa inapigwa iliposikika mawinguni, nyota zikionekana na waliosahau kukumbuka kuwa, kumbe, ni Jumatano usiku! Kuingia kwa Treni Bukene lilikuwa jambo la kufurahisha sana; maana kumpata mgeni wa kuingia nyumbani mwetu lilikuwa jambo la furaha na la kujivunia sana. Mwaka 1938, nilipokuwa na umri wa miaka kumi (ingawa kwa kumbukumbu za Mombasa miaka tisa) dada yangu mkubwa aliolewa Bukene. Mchumba wake, wa Madhehebu ya Hindu, alitoka Misungwi, karibu na Mwanza, ambako na yeye alikuwa na duka kama la baba yangu, lakini dogo zaidi. Waliomsindikiza Bi-Arusi, kiasi cha watu ishirini, walisafiri kwa barabara na kwa Treni kuja nyumbani kwetu Bukene. Sherehe iliendelea kwa siku tatu; na siku yenyewe ya arusi nakumbuka Kiongozi wa dini ya Hindu akighani wakati dada yangu amekaa kimya, mbele yake mwali wa moto kwa wa karibu saa tatu nzima. Katika seherehe hiyo nilivaa nguo mpya, pamoja na suruali: kwa mara ya kwanza. Siku ya pili baada ya arusi, ikawako sherehe nyingine ya Madhehebu ya Hindu iitwayo ‘Yognopavit’. Mimi na mdogo wangu ndio tuliokuwa walengwa. Ibada kama hii, ambayo mara nyingi huunganishwa na sherehe nyingine, kama arusi, kwa kawaida huanza na mwoaji kumuaga Mjomba wake na, katika tukio hilo, huyo kijana huombewa Baraka ya maisha kwa zawadi ya fedha. Baada ya mimi kupewa zawadi yangu, noti ya shilingi kumi, nilielekezwa kufika mbele ya huyo kiongozi wa dini aliyenipa zawadi ya kamba ndefu, unene wake kama kalamu, nijizungushie mwilini mpaka kiunoni. Yule Kiongozi alianza kwa kunionyesha namna ya kuizungusha ile kamba sikioni, kwa usalama, kila nilipokwenda haja ndogo. Ingawa ilikuwa inakera, niliizinga

Page 25: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

25

kamba hiyo mwilini, ikifunikwa na nguo zangu, mpaka nilipofikia umri wa miaka kumi na mitatu. Arusi ya dada yangu ilifanyika wakati ambapo biashara za baba yangu zilikuwa zinaanza kushamiri. Mwaka 1935 binamu yangu Juthalal Velji Chande alimuuzia baba yangu duka lake. Ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kwa baba yangu kupata mtaji kama huo, na ikawa ndiyo ngazi ya kuendeleza biashara zake kwa haraka. Mnamo mwaka mmoja Keshavji akawa amewataka wadogo zake, Ratansi na Amratlal, waliokuwa bado wanaishi India, kuja huku kushirikiana naye. Mara akaanzisha Kampuni iliyoitwa Keshavji Jethabhai and Brothers iliyokuwa inafanya kazi zake katika miji miwili, Bukene na Tabora. Mara likafuatia Shirika la Sukari kutoka Uganda, na ndilo lililoanzisha hapo Bukene biashara ya mpunga na mashine nne za kukobolea; bondeni kidogo, upande wa pili wa barabara ikatazamana na nyumba yetu; na hatimaye viwanda vya kukamua mafuta na kutengeneza sabuni. Mafanikio yake ya kupata nafasi ya Uwakala wa Kampuni ya Vacuum Oil ya Afrika Kusini, waliotangulia kabla ya Esso, na wa Motor Mart, waliokuwa Mawakala wa General Motors, ndiyo yaliyomfungulia mlango wa kazi za usafirishaji katika Tanganyika ya Magharibi. Wakati ule General Motors walikuwa wanauza, katika Afrika Mashariki, malori ya aina ya Bedford na Chevrolet. Baba yangu alifanya kazi hiyo kwa kuuza malori aliyokuwa ameletewa, akipeleka fedha kwenye Kampuni ya Motor Mart kama tu kulikuwako malori yaliyokuwa yameuzwa. Ofisi yake ya biashara ilikuwa Mtaa wa Livingstone, katikati ya mji wa Tabora, alipojitengenezea nafasi kwa ajili ya Kampuni hiyo mpya ya familia. Malori ya maonyesho kwa kila aina ya gari yaliyokuwa na bei ya sh. 3,000/= (au pauni 150), kwa lori la tani tatu, na sh. 5,000/= (au pauni 250) kwa lori la tani tano, yaliegeshwa moja kila upande mbele ya duka, ambako vile vile yaliwekwa, kwa maonyesho, madumu yaliyokuwa yamejaa petroli na mafuta ya taa matokeo yake, kwa jumla yakawa mtego wa kifo zaidi kuliko maonyesho ya

Page 26: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

26

biashara, au angalau ushawishi kwa vibaka kuiba! Hata hivyo, katika miaka yote baba yangu aliyofanya biashara ya malori mjini Tabora, haikutokea hata mara moja lori kuharibiwa, acha baki kuibiwa; na, pamoja mafuta yote yaliyokuwa nje, ambayo yangeweza kulipuka, kwa rehema za Mungu mikasa yote iliepukwa. Niliporudi Bukene nikachunguza maendeleo ya biashara za baba yangu, ambazo shughuli zake zilikuwa zimefurikia upande wa pili wa barabara. Kujengwa kwa Kiwanda cha Kusindikia Mafuta cha aina ya Maxoil iliyotoka Rosedowns, Uingereza, iliyokuwa na uwezo wa kukamua galoni ishirini na nne ya mafuta kila siku, mashine ya kukoboa mahindi iliyonunuliwa kutoka Kampuni ya Lehmann’s iliyoko Mtaa wa Acacia, Dar es Salaam, (Kampuni ambayo, la kushangaza, bado inaendesha shughuli zake katika Ofisi zile zile, ingawa sasa inamilikiwa na mtu mwingine). Mtambo wa kutengenezea sabuni ya kufulia, miche ya rangi ya manjano, nyeupe na bluu, yote hayo, na zaidi, yalimpa furaha ya kutosha kijana yeyote aliyekuwa anatamani kuona mambo mapya. Nashukuru kwamba kusikitishwa kwangu na matatizo ya jamii ya watu wa Bukene kukawa kumeyeyuka. Nilipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili nilikuwa nimechoshwa na kijiji hicho kilichokuwa na mtaa mmoja tu, na ile treni ya saa mbili usiku kila juma na, zito zaidi, mazingira ya shule ya Wahindi ya chumba kimoja. Baada ya kuhamishia sehemu kubwa ya biashara yake Mtaa wa Livingstone, Tabora, baba yangu akaamua kuwa na mimi, mwanawe mkubwa, niende kule kuendelea na masomo katika mji uliokuwa umejipatia, katika Tanganyika ya Wakoloni, sifa ya kuwa mji wa ajabu, lakini wenye jina kubwa katika mafanikio ya elimu.

Page 27: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

27

MBILI

KIPINDI CHA SHULE Wakati wa Kiangazi cha mwaka 1940 nilihamia Tabora, nikakaaa kwa baba yangu mdogo, Ratansi. Wakati huo Vita vya Hitler vilikuwa vinatikisa sehemu kubwa ya Ulaya Magharibi. Vita vya Waingereza vikawa ndiyo kwanza vinaanza lakini mapambano ya meli katika Bahari ya Atlantic yalikuwa yanapamba moto. Kwangu mimi niliyekuwa Tanganyika ya Magharibi niliyaona mambo hayo kuwa ni ya mbali mno. Tofauti na vile Vita Vikuu, vilivyosababisha nchi hii iliyoitwa Afrika Mashariki ya Wajerumani kuwa uwanja wa mapambano makali ya ardhini na baharini, mapambano yaliyopewa baadaye jina la Vita vya ‘Icecream’, Vita Vikuu vya Pili havikuleta misukosuko mikubwa. Hata hivyo ni kweli kwamba, ili kuweka Taratibu za kuendesha Dola kwa misingi ya Utawala unaolingana, bado mawimbi ya Vita hivyo vya mbali yalikuwa yanaonekana. Kwa raia wa kawaida kilichoonekana wazi ni kule kupata chakula kwa mgawo. Lakini tofauti na ilivyokuwa huko Uingereza, zoezi hilo lilikuwa la makaratasi tu, ambalo halikuwa na athari, au tuseme athari kidogo tu, katika maisha ya kila siku. Kwa familia yetu ya Wafanyabiashara kuanzishwa kwa udhibiti wa bei, na maghala ya kuhifadhi chakula Mikoani, ndizo hatua zilizokuwa za maana zaidi. Lengo la Sera zote mbili hizo ni kuhakikisha kuwa, kwanza, chakula kinapatikana na, pili, kudhibiti Walanguzi. Lakini katika nchi ambayo uchumi wake ndiyo kwanza unajijenga, inayofanya jitihada kubwa ya kujijengea masoko ya hakika, hatua hizo zilikuwa baraka kubwa isiyotarajiwa. Ghafla tukajikuta hatufungwi tena na bei zilizokuwa zinatawala Masoko ya Nje; badala yake yakawako mahitaji ya kudumu kwa mazao yetu yo yote au bidhaa zo zote tulizoweza kuzitengeneza. NOTE – SPACE FOR FOOT NOTE IN THIS PAGE

Page 28: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

28

Lakini hatua zile zilizochukuliwa wakati wa Vita hazikulenga mambo ya uchumi peke yake. Mji wa Tabora uliteuliwa, pamoja na Arusha, kuwa vituo vya kuhifadhi mateka wa Vita katika Tanganyika. Arusha walipelekwa Taliani, na haraka wakazoea mazingira kiasi cha kubuni mipango ya kupanua kwa haraka ujenzi wa barabara Nchini. Wakati huo huo Tabora wakapelekwa mateka wa Kijerumani, ambao walikuwa wachache; wakafichwa na kufungiwa katika nyumba Fulani Magharibi ya mji. Tofauti na Taliani kule Kaskazini, ambao mawazo pekee waliyokuwa nayo yalikuwa kujitafutia fedha, wala si kujaribu kutoroka, Wajerumani walijikalia peke yao, wakitumikia ufungwa usiokuwa na shughuli yoyote. Sikupata ushahidi hata mara moja wa Mfungwa wa Vita wa Kijerumani kuonekana mjini Tabora. Kwa kweli wanamji wa Tabora waliposikia habari zao hata hawakuwatia maanani. Hata katika ile Kamati ya kuwajadili mateka hao, alimotumbukizwa baba yangu mdogo, ili kushawishi Wahindi waingie katika Jeshi, iliyokuwa chini ya usimamizi wa Dk. S.B. Malick, Mkurugenzi wa Utumishi aliyekuwa Mwasia, Mateka Wajerumani hawakupata kuzungumzwa. Wakati huo baba yangu, biashara zake zikiwa zimeshamiri kwa haraka, alikuwa na wasiwasi kuliko mimi juu ya matukio ya vita vilivyokuwako Ulaya. Kwa hiyo alijinunulia redio ya aina ya Zenith, yenye umbo la ajabuajabu, aliyoitumia kusikiliza kwa hamu Taarifa za Habari za BBC kila jioni, hasa akifuatilia harakati za Vita hivyo vilivyokuwa vikali. Kila Vita vilivyoendelea, na yeye akaendelea kusikiliza matangazo ya jambazi moja lililokuwa linaitwa Lord Haw Haw. Lakini yote hayo kwa kiasi kikubwa hayakuathiri maisha yetu ya kila siku. Fujo za kampeni za upande mmoja zilizokuwa zinaendeshwa na Mussolini dhidi ya Ethiopia mwaka 1936 zilitikisa zaidi sehemu yetu hii ya dunia kuliko ambavyo Vita Vikuu vya Pili vilivyoweza kufanya. Kitendo cha kuvamiwa kwa Ethiopia, haramu kufikiria na hata kutekeleza, kiliwatetemesha sana watu wa Afrika wa Mashariki; wimbi la Wakimbizi lililofunika Kusini

Page 29: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

29

likawa jambo lingine baya kukumbuka, ya madhila makubwa ya dunia hii ndogo yanayosababishwa na Madikteta wa Kikoloni na Wafuasi wao. Lakini ingawa Historia ya dunia ilikuwa imenipita upande, ghafla Historia yangu mwenyewe ikaimarika nilipohamia mji mwingine kilometa themanini Kusini. Kwa kijana kama mimi niliyetoka kijijini, niliona Tabora kuwa mji wenye maajabu mengi. Mji umechangamka, mitaa imesambaa kila upande, siyo tena pande mbili tu za Kijiji; ulikuwa mji wenye mchanganyiko wa mataifa yote na dini zote, idadi ya Waislamu ikilingana na ya Walutheri, Wakatoliki na Waanglikana. Na, kama kabila la Wanyamwezi lilikua limeshamiri kama ilivyokuwa kule kwetu Bukene, idadi na shughuli za watu hao zilikuwa nyingi mno kuliko ambavyo ingeweza kuonekana Wilayani Nzega. Mazingira yangu yalikuwa yamebadilika, lakini vile vile yakabadilika malezi niliyokuwa nayapata kutoka kwa baba yangu. Kwake sasa nilikuwa natakiwa kuwa mtu mzima, Mfanyakazi anayeandaliwa; na sasa akanihimiza, kwa nguvu, kujihusisha na biashara ya familia, akinipa kazi ndogo ndogo kufanya niliporudi nyumbani kutoka shule, kama vile kuhesabu fedha iliyoingia, nikiwa nimejificha nyuma ya Ofisi. Lakini shule nayo ilikuwa tofauti mno, lakini bora zaidi kwa kiwango kikubwa. Inawezekana Shule iliyoitwa Haridas Ranchod Memorial School; iliyojengwa kwa ajili ya watoto wa Kihindi, iliyopo mpaka leo, haikuweza kufikia viwango vya elimu vilivyokuwa vinatolewa na shule nzuri za Wakristo zilizokuwa Tabora miaka ya 1930. Lakini, kwa kulinganisha na viwango vingine vyote vya Shule za Tanganyika ya Kikoloni, shule ile ilikuwa nzuri mno. Katika shule ile ya Haridas, elimu niliyokuwa nimeipata mpaka wakati huo ikaongezeka kupita kiasi. Ujuzi wangu wa Tanganyika, hasa jinsi ilivyokuwa inatawaliwa, ulipanuka vilevile. Tabora ndipo nilipouonja, kwa mara ya kwanza, Utawala wa Wakoloni kule Bukene, watu weupe niliowaona walikuwa wale tu waliokuja mara chache kuwakagua Watumishi wa Serikali, walioweka kambi zao mwisho wa barabara kuu kwa muda

Page 30: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

30

waliopewa kutafiti mambo yoyote waliyotumwa. Lakini Tabora, Makao Makuu ya Jimbo, Wazungu waliokuwa wanatawala hawakuwa wachache, wala hawakuweza kujificha. Baba yangu Mdogo, Ratansi, alyekuwa na nafasi ya kuwasiliana na Serikali mara kwa mara, alijenga mahusiano mema na Ma-PC na Ma-DC wote waliokuja. Vile vile alikuwa na mawasiliano na watumishi wa ngazi za chini, hasa Bwana Ambalal K. Patel wa Ofisi ya PC, aliyetunukiwa baadaye nishani ya MBE; na Bwana Ambalal B. Patel, aliyekuwa katika Ofisi ya DC. Majuma machache tu baada ya mimi kuanza masomo Tabora, kuwako kwa mikondo mitatu tofauti ya binadamu wa Kikoloni , ya weupe, wekundu na weusi, kukadhihirika wazi wazi kwangu. Mkondo wa Weupe, mwembamba lakini unakwenda kasi, ulihalalisha kuwako kwa kuviza ile mingine miwili. Katika nchi nzima, ule Mkondo wa Weusi ukawa umeelekezwa kwenye kilimo na kazi nyingine za mikono, ingawa pale Tabora wakati ule, bila kujua, ukawa mji peke yake ulionusurika na taratibu hizo kwa kuwa na shule nzuri sana kwa wanafunzi ambao baadaye walijidhihirisha kuwa Kizazi cha kwanza cha Viongozi wa Tanganyika. Mkondo mwekundu wa watu ambao wakati ule waliitwa Wahindi, walikuwa tayari wamejikita katika biashara pale sokoni, lakini kila ilipowezekana, watoto wao walielekezwa kuondokana na shughuli za biashara, na kutumbukia badala yake katika Utumishi wa Serikali. Maji ya Mikondo yote hiyo mitatu yalichanganyika kwa kiwango kidogo tu, na hata kuchanganyika kwenyewe kukawa na manufaa kwa Weupe; mfarakano wa Mikondo hiyo ukiwa umeanza mapema, tangu utotoni, kutokana na tabaka katika Taratibu za Elimu. Weupe waliwapeleka watoto wao kwenye shule za Waingereza, ili wajifunze Kiingereza; Wekundu kwenye Shule za Wahindi, ili wajifunze Gujerati, na Weusi, Waafrika, kwenye shule zilizoitwa “za Wenyeji,” wajifunze Kiswahili. Lakini wakati mwingine kama ilivyotokea katika sehemu nyingine za Dola ya Kiingereza, Masharti ya kujua Kiingereza na kucheza kirikiti yakawa muhimu

Page 31: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

31

katika Mikondo yote mitatu, na kutoa nafasi ya mawasiliano kati yao wote. Sikupata madhara yo yote nilipokuwa siwezi kucheza kirikiti. Sasa Wahindi, katika ujumla wetu, tulikuwa hodari katika mchezo huo tangu karne iliyopita; na, katika Tanganyika, timu zetu za Wahindi zilicharaza kwa kiwango kikubwa timu za Waingereza waliokuwako nchini. Katika michezo hiyo, na katika mazungumzo yaliyokuwa yanafuatia, tulipokuwa tunachambua kila kipengere cha mchezo, ubaguzi uliokuwako uliachwa pembeni. Katika mazungumzo kama hayo ndipo nilipojihisi kuwa na wajibu, au tuseme zawadi, ya kutamani kutafuta nafasi za mawasiliano yaliyotakiwa kuzungumzia mambo yaliyo zaidi kuliko haya ya starehe za pamoja. Katika Tanganyika inawezekana Mikondo hiyo mitatu inayotokana na rangi za watu ikaelekea kila mmoja upande wake; lakini kutokana na mazungumzo tuliyokuwa nayo wakati ule kuhusu mchezo wa kirikiti, na juu ya Biashara na Utawala katika miaka iliyopita, nilijihisi kuwa na shauku ya kweli, inayoonekana kuwa nadra kuipata, ya kuogelea kati ya Mikondo hiyo mitatu, na mara kwa mara kuyachanganya maji yake kwa faida kubwa zaidi. Kidogo kidogo maisha yangu ya Tabora yakaanza kupata mwelekeo. Kutoka nyumbani kwenda shule ni mwendo wa nusu saa tu. Mara nyingi nilicheza Volleyball na marafiki zangu, kama nilivyokuwa nafanya kule Bukene, na karata wakati wa jioni, au siku za mwisho wa juma. Vile vile ilikuwako senema Barabara ya Mabama, iliyoitwa ‘Tabora Talkies’, ambako tulilipa senti 50 kuangalia sinema ya Kihindi, wakati tukitafuna karanga tulizonunua kutoka kwa wachuuzi wa barabarani. Lakini mara nyingi nikitoka shule nilikuwa narudi nyumbani kwa baba yangu mdogo Mtaa wa Livingstone, nikisimama mahali kati ya duka letu na huko tulikokuwa tunaishi, kuchukua kazi isiyokamilika niliyokuwa nimeiacha usiku uliopita, au kukaa tu nikimsikiliza baba mdogo akichambua mambo ya biashara. Halafu, siku moja mchana, yapata miezi kumi na nane tangu nihamie Tabora, Baba yangu mdogo alikuwa mlangoni pa duka lake

Page 32: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

32

akinisubiri nirudi kutoka shule. Alikuwa amepigiwa simu, muda mfupi tu kabla, kutoka Bukene, akiagizwa kunitaarifu kuwa mama yangu amefariki! Mpaka sasa naona shida kuyaandika maneno hayo, na kisha niweze kuendelea kuandika. Asubuhi ya siku ile ya mwaka 1942, pale Tabora, mama yangu alikuwa hai, mzuri na bado ninaye. Mchana akawa kajiondokea; tena kujiondokea milele! Kutokea hapo haikupita siku bila kumkumbuka katika jambo lolote, liwe jepesi au zito. Pengine, laiti ningalijua wakati ule kuwa mama yangu alikuwa mgonjwa, tena anaumwa sana, mambo yangekuwa tofauti. Laiti ningalipata nafasi ya kugundua kuwa mkasa huo unakaribia kunikuta, kidogo uchungu wake ungalipungua. Lakini nina mashaka. Nilimpenda mama yangu kwa kiwango kile ambacho mzaliwa wa kwanza tu anaweza kukitambua; na, kumpoteza katika umri huo, akiwa kijana bado, wakati ujana wangu mimi ndiyo kwanza unaanza, lilikuwa tukio ambalo halikuweza kuvumilika wakati ule. Hata sasa, ingawa miaka 69 imepita, uchungu bado ni uleule, donda lile halijapoa bado; na hata muda uliopita, ambao kwa kawaida hupoza uchungu, muda huo haujanisaidia mimi! Katika muda uliofuata nikaelewa mazingira yaliyosababisa kifo chake. Aliumwa na mbu mmoja tu akapata ugonjwa wa malaria yaliyompanda kichwani: ugonjwa ule ulio tatizo la Tanganyika, toka zamani mpaka sasa. Dalili za kwanza zilizojitokeza siku chache tu kabla ya kifo chake na, kama ilivyo kwa maradhi hayo, hali yake ikazorota kwa haraka mno. Kwa kuwa kule Bukene hakukuwa na Daktari, wacha baki Hospitali, Mganga kutoka Hospitali ya Wilaya, Nzega, umbali wa kilometa 34, aliitwa aje kumhudumia. Mganga akafanya uchunguzi wake kwa haraka sana na, bila kubabaika, akaharakisha mipango ya kumkimbiza mama yangu kwenda Hospitali ya Nzega. Lakini kabla hata hajaondoka Bukene, uhai kidogo uliokuwa umebaki mwilini mwake ukayeyuka taratibu! Akiwa na umri wa miaka thelathini na mitano tu, alifariki akiwaacha watoto kenda, wavulana watatu na wasichana sita.

Page 33: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

33

Picha ya mwisho aliyopigwa mama, ambayo sasa inaning’inia katika ukuta wa nyumba yangu, inadhihirisha uzuri na uvumilivu wake kama ninavyoukumbuka. Lakini picha hiyo ni ukumbusho wa kudumu wa moja tu ya matukio mengi yanayokumbusha Upendo wa Mama ulioniunganisha wazi wazi mimi na yeye. Pamoja na mambo mengine, mama yangu alikuwa akijivunia sana nywele zake, na alikuwa na haki ya kujivunia, kwa vile zilivyokuwa nyingi na zenye kumeremeta; na yeye akajitahidi kuhakikisha kuwa na sisi pia tunakuwa nazo za kumeremeta vichwani mwetu. Mara moja kila juma mama yangu alivisugua vichwa vyetu kwa dawa aliyoingiza kutoka India, mafuta yaliyokuwa na harufu nzuri yaliyojulikana kwa jina la ‘Brahmi’. Mara baada ya kusingwa mafuta hayo vichwa vyetu vilifungwa na kitambaa cha bafta, kuhakikisha kuwa mafuta hayo yanaingia kichwani kucha nzima wakati tulipokuwa usingizini. Halafu kesho yake, kabla hatujanywa chai, aliziosha kwa zamu nywele za kila mmoja wetu, akituambia kwa sauti yake laini jinsi mafuta aliyoyasinga na kuyafungia kwa saa kumi na mbili kichwani, yalivyokuwa yanafanikiwa kuimarisha nywele zetu. Nywele zangu mwenyewe, ngumu zilizodumu mpaka nilipofikia umri wa miaka 70, zinaweza kuwa ushahidi wa kutosha wa manufaa haya ya ‘Brahmi’. Lakini kwangu mimi kumbukumbu ya zoezi hili haiko kwenye uzuri wa mafuta, ila kwenye zoezi la kutuosha nywele sisi wote kwa upendo mwingi, katika maisha yaliyokatika kwa ukatili mkubwa, na ghafla mno. Majuma yaliyofuatia zoezi la mwili wa mama yangu kuteketezwa kwa moto pale Tabora, yakaonekana sehemu ya maisha yangu yaliyokuwa ya upweke zaidi. Baba zangu wengine, watatu pamoja na Baba Liladhar, ambaye wakati ule alikuwa anaishi India, na Shangazi zangu wawili, wakiwa karibu zaidi na Baba yangu, kumliwaza kutokana na msiba uliompata. Na mimi, vile vile, nikalazimika kuwa karibu zaidi na familia, nikibeba majukumu ambayo kamwe sikuyatarajia, nikikomazwa haraka haraka hata wakati ule wa huzuni.

Page 34: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

34

Tulijitahidi kadiri tulivyoweza, lakini kila tulivyojitahidi mara nyingi haikuwezekana kufanikisha wakati wote majukumu yaliyosiana ya kuendesha biashara kwa mafanikio upande mmoja na kulea watoto tisa upande mwingine. Baada ya jitihada ya miezi sita ya kufanikisha mambo hayo familia ikaamua, kwa shingo upande kwamba watoto wawili kati ya hao, mtoto mkubwa wa kiume, na mmoja wa dada zake wadogo, hawana budi kuhamia Dar es Salaam, kilometa mia nane Kusini Mashariki ya Tabora, kuishi na Jamaa. Uamuzi huo ulipofikiwa, mimi nilikuwa na umri wa miaka kumi na minne tu. Kuingia kwangu katika mji wa Dar es Salaam wakati wa kiangazi cha mwaka 1942 kulikuwa tofauti sana na jinsi nilivyoingia katika mji wa Tabora, miaka miwili iliyopita. Tabia za ujana nilizokuwa nazo baada ya kuondokana na maisha ya Kijijini zilikuwa zimeniondoka zamani; badala yake yakaja mawazo ya kupanga mambo na kuwajibika. Sikuwa mwanamume kamili bado, lakini vile vile sikuwa tena kijana asiyejali, kama nilivyokuwa kabla ya hapo. Dada yangu mdogo akaenda kuishi na mjomba wangu Karandas Nanji Ruparelia; mimi mwenyewe nikaishi katika nyumba ya binamu yangu Ramji Velji Chande, ingawa huko nyuma yeye alikuwa amejitenga na baba yangu. Yeye alikuwa anaishi nyumba ya ghorofa mbili katika Barabara ya Bagamoyo. Mara baada ya kungia Dar es Salaam niliandikishwa kusoma katika Shule ya Tambaza, Shule ya Wahindi, iliyokuwa na sifa kuliko nyingine zote za Wahindi nchini; na Mwalimu wake Mkuu, H.D. Naik, akiongoza kwa sifa ya kusimamia nidhamu. Huko nilifanya vizuri kiasi, nikaweza kufaulu, kwa kiwango cha Cambridge School Certificate, masomo ya Hisabati, Kiingereza, Kemia, Jiografia, Historia na Elimu ya Jamii. Maisha yangu mjini Dar es Salaam yakaiga kwa haraka mambo mengi ya Taratibu nilizokuwa nazifuata nilipokuwa Tabora. Baada ya kutoka shule nilimsaidia binamu wa baba yangu, niliyemwita Mjomba, katika shughuli za Ofisi iliyokuwa katika ghorofa ya chini. Nilianza na kazi zile zinazosumbua sana: kupanga bahasha

Page 35: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

35

kulingana na mapendekezo yote yaliyokuwamo katika barua zilizopokelewa wakati wa Ukoloni na hata baada ya Ukoloni. Nilipewa meza, na gundi, niweze kubandika vipande vya karatasi nyeupe juu ya barua zilizokuwa zinaingia. Baada ya hatua hiyo nikapewa safari na, baadaye, kazi ya kudumu ya kuandika barua. Nilikuwa naishi katika chumba kimoja pamoja na binamu zangu. Jumapili au siku nyingine baada ya saa zile za shule, nilijikuta nafanya kazi na Mhindi mmoja, mtu mzima zaidi, aliyeitwa Dayalal Bhatt. Kwa sababu alizozijua yeye mwenyewe, Bhatt alipenda kuitwa jina la ‘Niranjan’, ambalo kwa kifupi maana yake ni ‘Mtu wa Furaha’ Niranjan akiwa kiumbe wa tabia hiyo ya mzaha, wala siyo kujifurahisha, alidiriki kuacha kufanya kazi saa saba na dakika kumi barabara; akapanda ghorofani na kuingia katika chumba kimoja. Kisha akavua pole pole suruali yake na kujitupa kitandani kulala kwa dakika hamsini barabara. Siku moja tukamfuatilia huko ghorofani, tukasubiri kwa kiasi cha dakika kumi ili kuwa na hakika kuwa keshalala kabisa; kisha tukasogeza mikono ya saa yake ya ukutani kufikia saa nane barabara. Kengele ya saa ilipogonga saa hiyo Niranjan akaamka, akavaa suruali yake, na kuteremka haraka chini, akibabaika na kushangazwa. Ilimchukua muda mrefu baada ya pale kujua kuwa, kuna sababu asiyoijua yeye, alipungukiwa dakika arobaini nzima za usingizi wake. Lakini hata hivyo, mimi na binamu yangu hatukuyaonea haya yale tuliyoyafanya. Miezi kadha baada ya mimi kuingia Dar es Salaam, ilidhihirika kwa mjomba wangu na kwangu mimi pia kuwa nisingeweza kamwe kuwa mwanafunzi nyota katika shule yoyote nitakayokwenda. Siku moja DC kutoka Tabora, Bwana Robinson, alimpa habari kwenda Ofisini kwake kupata Taarifa ya maendeleo ya masomo yangu hapa Dar es Salaam. Bwana Robinson alipofika, Mjomba wangu alikuwa amekaa katika kiti chake, kama kawaida, kwenye kona ya Ofisi. Bwana Robinson akakaribishwa, na Mjomba wangu akamwangalia kutoka utosi hadi

Page 36: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

36

unyayo. Ulikuwa mgogoro wa mila: Mhindi kavaa kibandiko cheupe kichwani, cha aina ya ‘Gandhi’, na kanzu ya Kihindi iliyombana inayoitwa ‘dhoti’, yule Mwingereza, Ofisa wa Kikoloni, kavaa kaputura yake ndefu, viatu na soksi. Akitambua kasoro iliyokuwako katika mazingira yale, Bwana Robinson akaenda kwa haraka kwenye Hoja iliyomleta. Alipoulizwa mafanikio niliyoyapata katika mitihani niliyofanya miezi michache iliyopita, Mjomba wangu akatetema na kuchezea vifungo vya shati lake. Hatimaye baada ya kuhisi kuwa alikuwa anahangaika kupata jibu, akatamka kwa majivuno kuwa mimi nilikuwa ‘miongoni mwa Vijana wa Mstari wa Mbele, lakini kuanzia upande wa kushoto’ Ni dhahiri kwamba, kwa kusema hivyo, alikuwa anahusisha kauli yake na maandishi ya ki-Gujerati, ambayo hutoka kulia kwenda kushoto. Lakini Mjomba wangu hakutambua kwamba Bwana Robinson alitafsiri vibaya kabisa jibu lake. Aliporudi Tabora alikivuruga kipimo cha chini Baba yangu alichokuwa nacho kwangu, alipomwambia kuwa nilikuwa nafanya vizuri sana shuleni, kiasi kwamba, kwa kweli, alikuwa anaupoteza bure uwezo wangu kwa kunitaka nifuate nyayo zake katika biashara ya duka. Mabishano hayo yakaibua wasiwasi wa Baba yangu alipohoji kama habari hizo nzuri ambazo hakuzitarajia kuhusu mafanikio yangu katika masomo kweli zilitoka kwa Mwalimu aliyehusika. Alipojua kuwa ni binamu yake, yaani Mjomba wangu, ndiye aliyeyasambaza maneno hayo, wasiwasi wa Baba ukapungua. Haukupita muda mrefu kabla ukweli haujagundulika kwamba, katika watoto wote waliofanya vibaya darasani, mimi ndiye niliyekuwa bora. Ingawa sikuwa na akili nyingi sana, bado nilifurahia kusoma kwangu mjini Dar es Salaam. Niliyafurahia masomo yenyewe, hasa Hisabati na Historia; na kwa haraka sana nikapata marafiki wengi. Wakati wa mapumziko tulikula machungwa kwa karanga, na kunywa Coca Cola. Wakati mwingine mbuzi wa mitaani walituibia chakula chetu, au ngedere wa porini waliibuka kutoka vichakani kula takataka. Dar es Salaam ndipo nilipoonja bia kwa mara ya kwanza: chupa moja ya IPA, iliyojulikana duniani kote kwa jina

Page 37: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

37

kamili la Indian Pale Ale. Na ni Dar es Salaam vile vile ambako, kwa mara ya kwanza, nilitambua uzuri wa Wasichana. Ilikuwa mwiko kabisa katika familia za Kihindi siku zile kwa wavulana kukaa karibu karibu na wasichana. Mwiko huo ulikataza hata kuwa na mazungumzo ya kawaida, hali iliyopelekea zile taratibu za watu kupendana kuwa ngumu zaidi kuliko ilivyo kawaida. Hata hivyo nashukuru kuwa na bahati ya kuishi katika mji mmoja na dada yangu mdogo Vijya, lakini bila wazazi wangu, nikapata bahati ya kukutana na wasichana wengi bila kuhalifu mila hizo: na bado nikampenda mmoja, rafikiye Vijya, msichana mchangumfu aliyeitwa Chandraprabha. Kwa bahati yangu, naamini na yeye alinipenda pia; lakini kwa bahati yetu mbaya sisi wote wawili, nafasi yetu ya kuendelea zaidi ya hapo ilikuwa ndogo, kwa sababu tu alikuwa rafiki wa dada yangu. Katika muda huo mfupi nilipomjua na kujisikia kumpenda sana msichana yule wa ajabu, hatukushirikiana kwa lolote zaidi ya maneno ya kawaida tuliyoyazungumza ovyo ovyo. Lakini, kama ilivyo kwa kila penzi la mwanzo, hata waraka wa kawaida uligeuzwa shairi; na, katika hali hiyo, kumbukumbu inabaki. Mwanzoni mwa mwaka 1944 Baba yangu alikwenda India kuoa mke mwingine; akarudi Tanganyika na mke mpya, jina lake Rumkunver; na, jambo la kawaida kwa wakati ule, Mama huyo alikuwa ameachika kwa mumewe wa kwanza. Kukutana kwetu na Mama huyo kwa mara ya kwanza kulileta shida, au tuseme hakuturidhisha wote sisi wawili. Nilikuwa mtu mzima wa kutosha kutambua matatizo Baba yangu aliyolazimika kukumbana nayo katika jitahada zake za kumridhisha katika mahitaji yake: akiwa peke yake, kazini au nyumbani. Kwanza kuja kwangu Dar es Salaam wakati nikiwa bado mdogo kulishinikizwa na vizingiti kama hivyo. Vile vile niliyatambua sana mahitaji ya wadogo wangu waliokuwa wadogo zaidi, waliohitaji upendo ambao mama peke yake ndiye anayeweza kuutoa. Ni sifa kubwa kwa mama huyo kupata heshima tokea mwanzo kutoka kwetu watoto wote sisi. Alionyesha kwa busara uvumilivu na upendo mkubwa hata tukatokea kumheshimu, na baadaye kumpenda sana. Aliuhuisha tena uhai wa Baba yangu, akiwalea

Page 38: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

38

watoto wote wadogo kama wake. Kubwa zaidi, alijijengea nafasi maalum katika mioyo ya watoto wakubwa bila kujaribu kufuta mioyoni mwetu kumbukumbu za Mama yetu tuliyempenda. Kutokana na Upendo na Upole wake, uamuzi wa Baba yangu kuoa tena ukamfikisha kwenye nafasi nzito zaidi, na yenye matumaini zaidi. Lakini kumbe siku zangu za kukaa Dar es Salaam, na hata Tanganyika, bila mimi kujua, zilikuwa zimekwisha. Mwishoni mwa mwaka 1944 shauku ya Baba yangu kuhusu maendeleo zaidi katika elimu yangu ilielekezwa India. Kama alivyohisi yeye, na alivyonieleza wakati ule, nafasi za kusomea digree kule India ni pana zaidi, na mafunzo yake ni mazuri zaidi kuliko Chuo chochote kilivyoweza kutoa katika Tanganyika ya Ukoloni. Isitoshe, kuhamia India kungesaidia kuongeza upeo wangu uliokuwa finyu wakati ule; na wakati huo huo ningepata nafasi ya moja kwa moja ya kujua na kuzingatia Mila na Desturi za Babu zangu. Lakini kiasi gani Baba yangu alinitaka nipige hatua katika safari yangu hiyo ya uvumbuzi wa binafsi wakati wote limekuwa swali lisilokuwa na majibu. Baba yangu alikuwa akichunguza, kwa majivuno na kwa wasiwasi pia, hamu yangu ya kujifunza Falsafa na Dini ya Kihindi ilivyoongezeka mwaka hata mwaka. Alitambua wazi wazi, zaidi sasa kuliko hapo mwanzo, kwamba nilibeba katika tabia yangu silka za mama yangu za kuchunguza na kutafiti mambo ya msingi. Lakini wakati huo huo alijua kuwa nilipaswa kuchanganya hayo na kutafuta Utaalam na Ubingwa, na jitihada ya kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu, hali iliyokuwa ya lazima kwangu ili kujenga juu ya msingi alioujenga katika shughuli zake nyingi za biashara. Kwa hiyo kwenda kwangu India kusoma ilikuwa kwake kama kujitosa, turufu ya aina iliyohusiana zaidi na marehemu baba yake kuliko inavyomhusu yeye mwenyewe. Nadhani yeye mwenyewe alitumaini kuwa endapo fikira zangu katika dunia hii ya utaalam zitachukua nafasi kubwa, siku moja ningetambua kwamba hatima yangu ya kweli, kama ilivyo hatima ya walio wengi wa Madhehebu ya Lohan, ambao ni Tawi la Hindu (asili yao Lohar Pradesh) walioenea katika sehemu kubwa ya nchi ambazo sasa ni

Page 39: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

39

Afghanistan, Pakistan, Kashmir na Hindu Kush; wale wengine ambao katika Karne ya kumi na moja walihamia Saurastra na Kutch, sasa hivi sehemu ya Mkoa wa Gujerati huko India. Hata kabla yangu watu hao walijihusisha na mambo ya biashara, siyo Misahafu wala Hadithi. Wakati ule mwaka 1945, nilipokuwa nakata tiketi yangu kwenda India, matatizo kama haya yalionekana kuwa bado yako mbali mno. Bado naikumbuka furaha ya ile safari ya kwanza kwenda kwenye nchi ya mama yangu. Bado naikumbuka meli iliyoitwa S.S. Takliwa, ya British-India Navigation, niliyoipanda Bandarini Dar es Salaam. Bado naikumbuka safari ile ya siku saba kufika Bombay kupitia Mombasa. Na, zaidi sana, naikumbuka ile siku nilipofika Bombay ambapo, baada ya fujo ya kumkiana na watu wa familia ya Baba yangu, nikatoka jioni na binamu, ambaye baadaye ndiye aliyetambuliwa kuwa mwenyeji wangu, tukaketi katika Mgahawa uliokuwa unamilikiwa na Mwirani, rafiki ya binamu wa baba yangu, tukinywa chai yenye manukato na kutafuna tambuu, tukizungumza hadi usiku juu ya mipango yetu ya baadaye kuanzia kesho yake, na hamu ya kuanza tena masomo kwa haraka kadiri itakavyowezekana. Binamu yangu alikuwa mtu makini kiasi kwamba ushauri wake kwangu, wa papo kwa papo, ukawa kuachana na masomo ya Sekondari, na badala yake kujiandikisha mara moja kwenye Chuo cha Uhasibu. Kwa kuwa nilirudishwa India kukamilisha mafunzo ya Elimu ya kawaida, nilipata kigugumizi kubadili Mpango wangu, saa ishirini na nne tu baada ya kufika Bombay; badala yake tukafikia maafikiano yaliyoniruhusu sasa kuomba nafasi kwenye Chuo cha Uhasibu, ili niweze kutumia kwa manufaa muda wowote utakaopita kabla sijaipata shule ya Sekondari inayofaa. Kati ya Vyuo viwili vilivyokuwa jirani vilivyonipa nafasi kujifunza Uhasibu, ‘Dovar’s College of commerce’ na ‘Batliboi’s Accountancy Training Institute’, nilichagua Batliboi’s, na familia yangu ndiyo iliyolipia gharama. Lakini sikukaa sana kule Batliboi’s. Majuma machache baada ya kufika India nilipata nafasi katika Chuo, chenye jina lisilofanana na hadhi yake, cha ‘Scottish

Page 40: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

40

Orphanaae Society’, katika Mtaa wa Mahim, nje kidogo ya Jiji. Kufika huko nililazimika kupanda treni kila siku asubuhi katika stesheni ya Churchgate, mwendo wa saa nzima kwa treni inayotumia umeme, mali ya Bombay Electric Supply and Tramways Ltd. Siku hiyo hiyo ya kwanza nikaujutia uamuzi wangu wa kuachana na Batliboi’s, siyo tu kwa sababu ya safari ndefu iliyoongeza muda wa shule uliokuwa mrefu mno, lakini pia hata shule yenyewe ilikuwa inazorota kwa haraka. Walimu wenyewe walikuwa mseto wa ovyo wa Wahindi na Wazungu. Wanafunzi kadhalika wakawa mchanganyiko wa aina hiyo hiyo, ari ikawa imevizwa na mafanikio duni katika shule hiyo. Badala ya kutafuta ushauri zaidi juu ya Mpango wangu wa Elimu, nikajiamulia mwenyewe la kufanya kuhusu yale masomo niliyoyataka. Sikuwa na jingine la kufanya ila kuondoka. Kwa bahati nzuri wakati ule nilikuwa nimekwisha kaa Bombay kwa kiasi cha miezi sita, hivyo nikawa najua namna ya kuepuka kufanya makosa mara mbili mbili. Safari hii, nikiwa nimepata ushauri sahihi, nikajiandikisha katika shule iliyoitwa St. Peter’s Boys High School, kule Panchgani, iliyoko kilimani katika Wilaya ya Sakara, yapata kilometa 256 Kusini Mashariki ya Bombay. Asili ya jina hilo Panchgani ni vilima vitano viliouzunguka mji. Ni mji uliochangamka, lakini vile vile mzuri kupindukia, ulio katika mwinuko wa kiasi cha mita 1,000, wenye mchanganyiko wa majengo yanayoshindana, bila mpangilio, ya Kihindi na ya Kikoloni, katika barabara zinazoelekea kwenye miteremko. Mlimani, umbali wa kilometa 18, mwisho wa barabara inayopitia Nyanda za Pwani na Mto Mtakatifu wa Krishna, ndipo ilipo stesheni maarufu ya Mahabhaleshwar, ambayo kwa kawaida wakati wa kiangazi, huvamiwa na watu wa Bombay; na tangu zamani ni kimbilio la Watawala wa Kihindi na wa Kikoloni. Mwendo wa saa u nusu kwa Basi kutoka hapo kuna mji wa Poona, sasa unaitwa Pune, ambako Agakhan alikuwa na kasir lake, na ambako vile vile Agakhan alipata kuwekwa kizuizini. Kufika huko,

Page 41: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

41

kutoka Bombay, ni mwendo wa saa tatu tu katika treni ya ‘Deccan Queen’. Mara nilipofika Panchgani nilitambua kuwa uamuzi nilioufanya ulikuwa sahihi. Mji wenyewe umechangamka, mahali pa kutuliza moyo baada ya joto Bombay. Shule yenyewe, yenye watu waliojaa ukarimu, ilikuwa inaendeshwa vizuri. Wanafunzi wenzangu wote walionekana kuwa na upendo, wenye bongo zuri na wanaosoma kwa bidii; na uhusiano kati ya Wanafunzi wa Shule nyingi za Bweni pale Panchgani ulikuwa wazi pamoja na, kwa mara ya kwanza katika kujua kwangu, kati ya wasichana na wavulani. Lakini lilikuwako tatizo moja kubwa. Wakati nilipokuwa najiandikisha, Mwalimu alisisitiza kama walivyosisitiziwa wanafunzi wote wa Bweni, kuwa Mzazi au Mlezi mwingine awe jirani, na aweze kupatikana, endapo tatizo lolote litatokea. Mwanzo nilidhani kuwa huo ulikuwa mfano mwingine wa umangimeza ambao, kwa namna moja au nyingine, ningeweza kuukwepa. Lakini haikuwa hivyo. Mara nilipofika Panchgani ikanidhihirikia kuwa hilo ni sharti muhimu lisiloweza kukwepeka. Fikira zangu za kwanza zikanisukuma kwenye kukata tamaa. Wazo la kurudi Bombay, mazingira ambayo ndiyo kwanza nimeondokana nayo, niliogopa sana. Wakati huo huo, Baba yangu alikuwa katika Bara lingine, Tanganyika, zaidi ya kilometa 3000 kutoka Panchgani, nafasi yangu ya kutimiza Sharti hilo la Shule ilikuwa ndogo. Katika hali ya wasiwasi mkubwa nilitafuta ushauri wa binamu yangu mwenye umri wa miaka kumi na minane aliyekuwa Bombay, ambaye hakupata kuniangusha wakati wowote nilipopata tatizo. Kwa kweli alimwandikia barua Mkuu wa Chuo hicho cha St. Peters siku iliyofuata akijitambulisha kuwa yeye ndiye Mlezi anayenidhamini. Kama mikasa ilivyo, kitendawili hiki kilikuwa kigumu kwangu kukitegua. Kwanza, kutokana na kubabaika baada ya kupewa sharti hilo la kujiunga na shule, nusura niliache zoezi lote kabisa. Lakini, kama kuna mtu aliyejitosa kuwa Mdhamini wa mtu mwingine mwenye umri unaolingana na wake, basi Binamu yangu alidiriki kufanya hivyo. Kielelezo cha kwanza cha tabia hii ya ‘usanii’

Page 42: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

42

ilionekana kwenye jina lake. Alikuwa anaitwa Satyavan Juthalal, jina ambalo tafsiri yake ni ‘kivuli cha ukweli’, au ‘mwongo wa kutupa’. Sababu hasa ya yeye kupewa mchanganyiko huo wa majina mimi siijui; lakini, iwe makusudi au bahati mbaya, alikuwa ananuia kufanana na tafsiri zote mbili hizo za jina lake. Kule kujipachika mwenyewe wadhifa wa kuwa Mdhamini wangu si kielelezo kikubwa kuliko vyote vya ukorofi wake. Baba yake aliitia familia yake katika matatizo kwa sababu ya kucheza kamari, binamu yangu asingeweza kuepuka kujenga tabia ya ‘bahati nasibu’ kila alipopata nafasi. Satyan akajijengea tabia ya kubadili shule kama mashati, akihama kila alipohisi kuwa mbinu zake za kudanganya zimegundulika. Kubwa kuliko zote lilihusu Cheti cha shule, chenye sifa kubwa. Katika Mtihani wake wa mwisho katika lugha ya Ardhamagadhi, aliamua kufanya mtihani huo katika Kituo cha mbali; huko akamwajiri mwenyeji aliyeijua lugha hiyo, kumfanyia huo mtihani. Dhahiri akafanya vizuri mno, kiasi cha kuwatia mashaka Viongozi wa Shule yake. Wakampelekea Postcard baba yake, moja baada ya nyingine, kumweleza wasiwasi wao kuwa binamu yangu amefanya hila nyingine mbaya kuliko zote. Lakini, wala si ajabu, zote hizo zikanaswa kabla ya kumfikia Baba yake; na vile vile majibu mazuri yakarudishwa, mpaka, hatimaye, kadi moja ikanaswa. Baba yake akajibu, kwa ukali wote, kwamba ameonana na mwanawe mara chache sana katika miezi michache iliyopita, na kwamba Taarifa zozote za mafanikio yake hayo “ya ajabu” zinawezekana. Binamu yangu huyo akaendelea kuwa Mlezi wangu mpaka nilipofikia umri wa kujitegemea. Wakati wote huo nilikuwa namwona kwa nadra sana, hata pale nilipokwenda kuishi naye Bombay. Saa zake za kazi zilianza wakati zangu zilipokoma; na mimi nilipokwenda kazini yeye yuko nyumbani. Baadaye akasafiri kwenda Afrika Mashariki, na kutoka hapo, akaenda Kongo. Wakati wote nimewiwa deni kwake, kwanza kwa kuniopoa shimoni wakati matumaini yangu yote yalipokuwa yamepotea, na pili kwa kunifundisha somo zuri la maisha kwamba wakati mwingine Imani na Utakatifu wa mtu haina budi kuvizwa na hali halisi inayochanganyika na ubunifu.

Page 43: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

43

Mara nilipokivuka kile kizingiti cha Udhamini, niliruhusiwa kushiriki kwa ukamilifu katika maisha na shughuli zote za Shule ile ya Wavulana ya St. Peters. Mimi nilipangwa katika Bweni Jekundu; ndiyo kusema kwamba nilikubaliwa kuishi katika Kijiji cha Lawrence, pamoja na wanafunzi wengine wa Bweni hilo wapatao thelathini. Wanafunzi watatu au wanne waliishi kwenye chumba kimoja; ila mimi na wanafunzi wangu wengine wawili tulilala ukumbini; Mwingereza mmoja, Edgar Glancey, mtu wa makamo, akiwa Mlezi wa Bweni letu. Glancey ambaye hatimaye alistaafu na kwenda kuishi Australia, alikuwa mtu wa huruma sana; naye alikuwa na mke aliyekuwa na huruma zaidi; hao wawili walihakikisha kuwa napata, kwa haraka sana, nafasi ya utulivu shuleni hapo. Mkuu wa Shule, Bwana O.O. Bason, Mwingereza mwingine, vile vile alikuwa mtu mwema; na heshima yangu kwake, iliyoanza pale aliposhindwa kumhoji vizuri Binamu yangu kuhusu umri wake na shughuli zake, zilizoongezeka kila miaka ilivyopita, kwa jinsi nilivyozijua na maarifa aliyokuwa anayatumia. Maana Benson aliiendesha shule ile katika kipindi cha msukosuko mkubwa katika historia ya India, kampeni zilipokuwa zimefikia kilele za kuwafukuza Waingereza, ambapo Mipango ya Wananchi kwa ajili ya Utawala wa ndani kama siyo Uhuru kamili, ilianza kudhihirika. Shule hiyo ambayo, kama nilivyokwisha kusema, zamani ilikuwa ikiitwa Shule ya Wavulana wa Kizungu, ilikuwa inaendeshwa kwa mpango wa kuingiza Wanafunzi kwa tabaka, ambapo asilimia kubwa ya wanafunzi ilikuwa ya Wahindi-Wazungu, nafasi zilizobaki ndizo walizopewa wengine: wengi wa hao wakiwa Watoto wa Watawala, Wana wa Wafalme; na wengine kama mimi, wanaotoka Nchi za Nje. Shule iliendelea kuwa na sura hiyo hata baada ya kubadili jina lake; na bado ikawa lazima kwa kila mmoja kuhudhuria ibada ya Jumapili katika Kanisa la Shule. Suala hili la Dini katika Shule lilinipa matatizo. Wanafunzi wenzangu wawili, Waislamu, wakamwomba Mkuu wa Shule wasamehewe kuhudhuria Ibada hiyo ya Wakristo ya Jumapili; badala yake Sheikh apatikane

Page 44: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

44

kuwafundisha Kuruani. Nikafanya kama walivyofanya wao; na mimi, nikashangaa, nikafanikiwa vile vile. Nilishangaa zaidi, kwa kweli nilistaajabu, kugundua kuwa Imam wa dini ya Hindu alipatikana kunipa Mafunzo ya Mwanzo wakati ule ule wa Ibada za Jumapili.! Dhahiri Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Shule lilikuwa ndilo jambo muhimu kwa idadi kubwa ya Wakristo katika Shule yetu. Kwa kuwa mabinti kutoka Shule ya Wasichana ya Kimmin iliyokuwa jirani waliruhusiwa kushiriki katika Ibada hiyo, jitihada kubwa kadiri ilivyowezekana zilifanywa kuhakikisha kuwa Wasichana wanatenganishwa na Wavulana, lakini, katika hali halisi, haikuwezekana kuwatenganisha. Kwa hiyo ikatokea kuwa, kama vile vile maombi yangu ya kuruhusiwa nisishiriki Ibada za Jumapili, yalivyokubalika, na mimi nikakutana, Kanisani, na msichana wa Kabila ya Parsee, jina lake Aloo Davar. Kwanza tulionana kwa mbali, wakati macho yetu yalipopenya kati ya vichwa vya wanafunzi wenzetu. Lakini haukupita muda kabla hatujatambulishana, kwa msaada wa msichana Chotara wa Kihindi/Kiingereza, Gloria Bright, aliyezitambua dalili za kupendana kwetu, na kuchukua hatua,. Ghafla Aloo aliubadili upeo wangu kuhusu Kanisa lile. Labda baada ya kusoma kidogo kitabu cha Binamu yangu, nilihama haraka kutoka kuwa adui, nikawa Badala yake muumini wake mkubwa. Nikiwa na imani kubwa na Aloo, kiasi cha kujitumbukiza kuimba Kwaya, ingawa hatimaye sikufanikiwa kuwa Mwanakwaya, nafasi ambayo ingaliniwezesha kumwona, bila kizuizi, Mpenzi wangu wakati wote wa Ibada. Nikiacha Mpango huo wa muda wa kutosheleza shauku yangu, mimi na Aloo tulikubaliana kujiandikisha kwa Mwalimu wa Zamu kuwa tu ndugu binamu, ili kuhakikisha kuwa kukutana kwetu baada ya Ibada ya Jumapili kunatambuliwa rasmi na Mamlaka inayohusika, kila mmoja kwenye Shule yake. Katika kujisaidia wenyewe tulikuwa tunawasaidia na wengine pia, kama vile vile sisi tulivyosaidiwa na Gloria Bright. Lakini

Page 45: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

45

ikadhihirisha upesi kuwa kila mabinamu sisi tulipozungumza katika eneo la Kanisani St. Peters tulipokea barua za uhasama kutoka kwa wenzetu waliokuwa na wivu kwa sababu ya kukosa ama ujanja ama bahati ya kutambulika mapema katika Kanisa la Shule kuwa mabinamu. Wakati huo masomo yangu yakawa yanaendelea vizuri. Nilikuwa na marafiki wengi miongoni mwa wanafunzi wenzangu shuleni hapo, waliotokana zaidi na familia za Madaktari, Wanasheria, Maafisa wa Wakoloni na wa Tawala za Dola za Zamani waliokuwa na sifa nchini India baada ya Utawala wa Mongul. Hapa nilikutana vile vile na watoto wa familia kubwa katika nchi za Afrika na Asia, pamoja na kijana mmoja wa familia tajiri kutoka Uganda, ambaye wakati wote aliagiza chakula alichokitamani kutoka Bombay. Kwa hiyo nilikula vizuri na, nadhani, nilisoma vizuri pia. Kama nilivyokuwa siku zote, sikuwa mwanafunzi wa kwanza-kwanza, hata ukihesabu kutoka kushoto. Lakini kwa kujitahidi kwangu nikafaidika na mafunzo ya kiwango cha juu yaliyokuwa yanatolewa. Vile vile, uzuri una namna yake ya kushinikiza usikivu. Labda mwalimu wetu kijana, Eunice Salisbury, alikuwa anatuvutia sana sisi vijana: umbile lake, nyweke zake, na macho yake ya bluu, yalitufanya sisi wote tumsikilize kwa makini, na hivyo wengi wetu tukaibuka na alama za juu. Miaka sitini baadaye, Desemba 4, 2004, nilirudi kwenye Shule hiyo ya Wavulana ya St. Peters; sikuwa na Aloo, ila nilikuwa na mke wangu Jayli, nimemshika mkono. Mimi na Jayli tukachanganyika na watu wengine wapatao 1,500, pamoja na Wanafunzi kadha wa zamani, wengi wao kutoka nje ya India katika dhifa iliyofaywa siku ya mwisho ya Sherehe ya kumaliza miaka 100 tangu Shule ianzishwe, mimi nilikuwa Mgeni Rasmi. Hivyo nikatakiwa kusimulia baadhi ya matukio wakati nilipokuwa Shule. Nilifurahi sana kupitia njia ile, nikakutana na Wanafunzi, wapya na wa zamani wa zaidi ya Vizazi viwili na hasa kukutana na mmoja wa Walimu wangu wa zamani, Bwana Davis. Nilifurahi kulikuta jengo lile likiwa limetunzwa vizuri, na bustani na mazingira yakiwa katika hali ya kuridhisha mno. Katika moja ya

Page 46: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

46

mabweni yaliyokuwa Lawrence Villa, nilikiona kitanda nilichokuwa nalalia yapata miaka sitini iliyopita, ingawa vitanda vyetu vilikuwa vinabadilishwa na kuwekwa vya ghorofa, ili kukidhi mahitaji ya nafasi yaliyokuwa yanaongezeka shuleni hapo. Na, katika picha ya Maonyesho ya Maika Mia, nikaikuta picha ya mchumba wangu wa zamani, Aloo. Baada ya Sherehe ya siku tatu, mimi na Jayli tuliporudi Bombay (sasa Mumbai) tukamwalika kwetu Katibu wa Bodi ya Shule na Mkewe kwa chakula cha jioni. Tulipomaliza nilijisikia kana kwamba maisha yangu kule shuleni yamekoma jana tu. Msisimko nilioupata St. Peters ulilingana na kuchangamka kwa moyo na kuongezeka kwa upeo wangu wa siasa. Kule Bukene, Tabora na Dar es Salaam masomo yangu yalikuwa na muelekeo wa Uingereza tu na mara chache, Historia ya Ulaya. Hata katika shule za Wahindi vitabu tulivyosoma karibu wakati wote vilikuwa na mwelekeo wa Uingereza tu na, mara chache, Historia ya Bara la Ulaya. Lakini hapa Panchgani mwelekeo wa masomo ukabidilika ghafla: nilipata vitabu vya Historia, vya Mila na vya dini za Kihindi. Macho yangu yalifunguka zaidi kuliko yalivyopata kuona zamani, na vitabu vya Mabingwa wa Historia kama Sir Vincent Smith na Padre James Gense, S..J., vilibadili upeo wangu wa kuijua dunia, na nafasi yangu duniani. Msigano mkubwa ukanibana moyoni kati ya shauku yangu mpya ya kujifunza mambo ya India na yale yaliyokuwa yananitokea kule India. Nikatumbukia katika kufurahia ile miezi kumi na minane kabla ya Uhuru. Katika shamra shamra za Vijana za Kampeni ya kuwaondoa Wakoloni nchini, na shauku la kuliona Taifa la India, katikati ya upinzani ulioshamiri wa Raj, Kibaraka wa Waingereza. Kwa nasibu nilipata nafasi ya kushuhudia hatua za Uhuru wa Nchi ya familia yangu, na Uhuru wa nchi yangu, mwenyewe. Tanganyika; na bila shaka uzoefu wangu kule India ukaelekeza fikira zangu katika maswala ya Uhuru, Dar es Salaam, miaka kumi na mitano baadaye. Kwa hiyo yule kijana aliyeandika barua kupitia gazeti la ‘Times of India’, akishinikiza kukoma mapema kwa Utawala wa Kiingereza nchini, akawa ndiye wa kukokotwa katika

Page 47: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

47

mkondo wa kuondoka ghafla kwa Waingereza kutoka Afrika Mashariki katika miaka ya mwanzo ya 1960. Katika nafasi zote mbili hizo, nchi kubwa kubwa ambazo, mpaka wakati huo, zilikuwa zinaendeshwa na idadi ndogo ya Waingereza waliokuwa na ujuzi mkubwa, wakajikuta sasa wanashughulikia mambo yao wenyewe. Katika nafasi zote mbili hizo, haraka hiyo ikaeneza sumu kali. Kule India, na katika nchi zote za kule, yakazaliwa makundi, mifarakano na mikasa, iliyodumu mpaka leo. Katika Tanganyika, haraka hiyo ikaacha Taratibu za Utawala zisizoandaliwa vizuri kwa Majukumu hayo makubwa ya Taifa, nchi iliyojengwa katika msingi wa kutegemea wengine, kulikojenga uwezo mdogo unaendelea kuviza hatima ya Nchi. Lakini fikira zozote ambazo ningalikuwa nazo juu ya kupatikana kwa Uhuru wa India zilitoweka katika lile wimbi la Utaifa lililozikumba nchi za sehemu ile. Aidha, nilikuwa na mengine kichwani mwangu yaliyokuwa muhimu zaidi kuliko yote, katika ujana wangu, ya kuufuta Ukoloni wa Kiingereza. Masomo yangu ya Sekondari yalikuwa yamemalizika kwa mafanikio mwishoni mwa mwaka 1948, nikapata cheti cha Juu cha Cambridge, kwa kufuzu masomo ya Historia, Kiingereza na Uraia. Wakati ulikuwa umefika sasa kuendelea na mazomo ya Chuo Kikuu. Kwa masomo hayo nilikwenda Poona; sasa hivi kunaitwa Pune, Nikajiandikisha katika Chuo cha Nawrosjee Wadia, kilicho Tawi la Chuo Kikuu cha Poona, kusoma shahada ya B.A. katika mchepuo wa Historia ya India. Tangu siku ya kwanza ilidhihirika kwangu kuwa masomo yangu yangenipa shida kubwa kuliko yoyote niliyopata kuikabili. Mkuu wa Chuo, Bwana Joeg alikuwa msomi makini; ili kusoma, acha baki kufanikiwa, katika mazingira yale ya wasomi nililazimika kufanya kazi kubwa zaidi kuliko nilivyowahi kufanya huko nyuma. Na, safari hii, hayakuweko yale macho ya bluu ya kunipa changamoto. Shida ya ziada ilikuwa kukosa mahali pa kukaa. Haikuwako nafasi katika hoteli ambayo Chuo kilipanga kuitumia; matokeo yake nikahamahama hoteli moja baada ya nyingine, nilipojibanabana kati ya Watalii na Wafanyabiashara. Hatimaye nikajenga urafiki na

Page 48: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

48

Bwana Homi Irani aliyekuwa na hisa katika Hoteli ya Napier pale Poona. Homi aliniruhusu kupata chumba kwa bei nafuu, kwa sababu ya kukaa hapo muda mrefu; ndipo hatimaye nikatulia. Nikanunua baiskeli na kuanza kutembea mjini: kwenda senema na sehemu nyingine za michezo. Nikiwa na Wanachuo wenzangu, pamoja na Homi, nikaanza kwenda kwenye Migahawa na kuvinjari mji. Mambo mengine yaliyonifurahisha, nilipopata nafasi, wala hayaelekezi kwa Wajukuu zangu, lakini yalikuwa ya kawaida miongoni mwa wenzangu. Pamoja na nafuu niliyopata kutokana na kiwango cha kodi nilichokuwa nalipa kule Napier, bado nilikuwa natafuta mahali pa kuishi ambapo ningeweza kupaita nyumbani. Hatimaye nikapata makazi mahali nisipopatazamia. Mfanyabiashara wa Kimarekani, John Aliyanak, mtu wa aina yake katika mji mzima wa Poona alijijenga miaka miachache iliyopita kama Mfanyabiashara wa magari; biashara yake ikawa inakaribia kuanguka toka wakati ule tulipokutana kule Naples. Alipopata habari za matatizo yangu ya siku nyingi ya kukosa mahali pa kuishi, yeye na mkewe, Eva, wakaamua kunichukua nyumbani kwao, nikae kwa malipo. Ingawa gharama ya kuishi nyumbani kwao, Na. 6 Barabara ya Staveley yangechukua asilimia 40 ya mshahara wangu wa juma, sikuchelea kukubali masharti yao. Baiskeli yangu na sanduku langu lililokaa katika nyumba kadha mjini Poona, hatimaye vikapata mahali pa kudumu pa kupumzikia. Hao akina Alyanak walikuwa wenyeji wangu wakarimu sana. Ingawa nyumba yao haikuwa ya fahari, yenye choo kilichoweza kusafishwa kutoka nje tu, wao na mtumishi wao wa Ki-Goa aliyeitwa Augustine, wakanikaribisha kama mmoja wa familia. John alikuwa anaamka mapema, mara nyingi akiondoka nyumbani kabla ya mapambazuko; hivyo nililazimika kunywa chai peke yangu. Lakini karibu siku zote jioni, tulikuwa tunakula pamoja kama familia. Kuishi na akina Alyanak kulinipa utulivu niliouhitaji, ili nifanikiwe katika masomo yangu ya Chuo Kikuu. Mwaka 1949 ulipopita kuja 1950, nilijihisi kuwa nilikwisha kujijenga kweli kweli mjini Poona .

Page 49: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

49

Kisha ghafla mwezi Januari 1950, nikapokea barua kutoka kwa baba yangu akinitaarifu kuwa mdogo wake, Ratansi anayeishi Dar es Salaam, alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu sasa amekuwa akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa; hatimaye akashauriwa kung’oa meno yake yote. Lakini hata baada ya kuikubali tiba hiyo ngumu bado maumivu yake Baba yangu mdogo yakaendelea; na ikakubalika kwamba alihitaji mapumzuko ya kutosha kujaribu kutatua tatizo hilo. Wakati huo shughuli za Dar es Salaam zilikuwa katika mpango wa haraka wa kupanuliwa, na mashine ya kusaga imejengwa kwa gharama ya shilingi milioni sita; hivyo ilikuwa lazima mtu apatikane kuendesha shughuli hizo, mpaka hapo Baba mdogo atakapopona na kurudi kazini. Kwa mujibu wa barua ya baba yangu, mtu huyo aliyekuwa anatafutwa, kumbe alikuwa mimi! Sikupenda kabisa kukatisha masomo yangu, wakati nimemaliza chini ya nusu ya mafunzo ya miaka minne. Lakini vile vile nilijua kuwa sikuwa na namna ya kukwepa, ila kutii tu ombi la Baba yangu. Kwa hiyo nikaenda kuonana na Bwana Joag, na Naibu wake Bwana Suni, kuwaelezea hali hiyo, na kuuliza kama ningeweza kuhifadhiwa nafasi yangu mpaka nitakaporudi. Bwana Suni akanitazama kwa jicho la wasiwasi, kwa kuwa alikwisha pata matatizo kama hayo yaliyoletwa na mwanafunzi wa Kihindi kutoka Afrika Mashariki, na hivyo akataka kujua zaidi. Akaniuliza, “Je, unatoka Zanzibar?” Nikajibu, “Tanganyika”, na ukali wake ukapungua. Hata hivyo, hakuweza kunihakikishia kuwa nafasi yangu ingekuwa wazi, na wote walisisitiza kuwa, endapo nitaruhusiwa kurudi, nitalazimika kurudia masomo ya mwaka wa pili mzima. Kwa hiyo niliagana na akina Analyak nikiwa na moyo mzito sana. Nikaenda Bombay moja kwa moja, kwa matumaini ya kupata meli mapema kwenda Dar es Salaam. Lakini bado bahati mbaya ilikuwa, inaniandama. Ulipita mwezi mzima kupata tiketi ya meli pale Bombay kwenda Dar es Salaam, na hata hivyo kwa shinikizo la Wakala wa Meli wa Dar es Salaam, Smith Mackenzie, ndipo hatimaye nilipopata nafasi hiyo. Hatimaye, Februaru 1950,

Page 50: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

50

nikaondoka na MV Vasna kwenda Tanganyika; nikiwa sijui hatma yangu, na nikiacha kazi niliyoianza ikiwa haijakamilika!

Page 51: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

51

TATU

BIASHARA ZA FAMILIA NA UZOEFU Nilirudi nyumbani nikijua kabisa kuwa huko Dar es Salaam nitatumbukizwa mara moja katika shughuli za biashara za familia ambazo wakati huo zilikuwa zimepanuka, na pia zimechukua bidhaa nyingi zaidi ukiacha nyonyo na alizeti. Kampuni sasa ilikuwa, inauza pia mawese, kunde na nafaka, na vile vile nta na asali; aidha ilikuwa inashughulikia ngozi na pamba. Kampuni hiyo ya familia ndio iliyokuwa mwuzaji mkubwa wa kahawa na asali katika nchi za nje. Lakini ikatokea kuwa, kumbe, Baba yangu alikuwa na Mpango mwingine. Labda kwa kuhofu kuwa, kwa upande wa Dini, tabia yangu ilikuwa imevurugika sana katika miaka sita iliyopita, akaona vema nirudi katika eneo la kazi zangu asilia kule Bukene, nijifunze biashara kuanzia chini, kutoka kwa Baba yangu mdogo mwingine, Amratlal. Mabadiliko hayo yalizidi kufanya kurudi kwangu nyumbani kunikatishe tamaa zaidi. Ilikuwa shida ya kutosha kwangu kuacha masomo yangu na marafiki zangu kule Poona, kuja Dar es Salaam. Kuyaacha hayo yote kisha kwenda Bukene kuanza maisha mapya kabisa lilikuwa pigo kubwa. Maisha ya Bukene yangenikumbusha mno maisha yangu ya utotoni, pamoja na Mama yangu. Lakini sasa yote hayo mawili yametoweka, wala hayatapatikana tena! Lakini uvumilivu na, pengine ari kubwa iliyoniwezesha kuvuka vizingiti vingi nilivyopambana navyo katika ujana wangu, ndio ulionifikisha katika sura hii ya mwisho. Nilipofika Bukene nikakuta mabadiliko kidogo tu katika miaka hii kumi tangu nilipoondoka. Bado treni ya abiria inasimama stesheni Bukene saa mbili jioni kila Jumatano; bado punda na kuku wa mitaani wanakwepakwepa magari katika barabara iliyo moja tu, tena haina lami. Na Bwana Jagjivan bado anaendesha madarasa yake katika shule ya zamani, karibu na duka letu la familia. Labda badiliko

Page 52: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

52

moja tu kubwa linaloonekana ni ukubwa wa mashine za familia za kukoboa na kusaga nafaka. Biashara ya Baba yangu ilikuwa imeshamiri zaidi toka nilipoondoka kwenda India kuanzia pale alipokuwa mmoja wa wanunuzi wakubwa wa mazao Wilayani Nzega, himaya yake katika biashara ya vyakula sasa ikawa imekua kiasi cha kuhesabika kuwa ya Kitaifa. Kule Bukene, pamoja na ile mashine ya awali ya kukoboa mpunga Baba yangu aliyoijenga miaka ya 1940, kumeongezeka kiwanda cha kutengenezea miche ya sabuni ya rangi za bluu na njano; kadhalika kiwanda cha kukoboa na kusaga mahindi kilichotoa unga wa dona, na kingine kilichosindika mafuta kutoka katika mbegu mbali mbali. Ukiziunganisha shughuli zote hizi, pamoja na zile za biashara zilizoenea katika Jimbo lote la Magharibi, ndio msingi wa kupanuka kwa biashaza za familia huko Tabora na Dar es Salaam. Uti wa mgongo ni kauli aliyoitumia Baba yangu mdogo mara kwa mara. Yeye na Shangazi yangu walinipenda mno; wala sikuwa na shaka na hilo. Lakini yeye Baba alikuwa msimamizi mkali, aliyenitarajia kushirikiana naye kwenye chai ya asubuhi, mara nyingi alifajiri, kama kitangulizi cha kazi ya siku hiyo ambayo kwa kawaida iliendelea mpaka zaidi ya saa moja na nusu usiku. Hayo ndiyo mafunzo ya shughuli za biashara niliyoyapokea haraka haraka. Ujuzi wangu wa Kiswahili uliokuwa tayari umeimarika, ukawa umeongezeka kwa kiwango kikubwa sana. Uliongezeka pia uwezo wangu wa kuandika Kiingereza na Gujerati. Kubwa kuliko yote, nilianza kuelewa yale yaliyoifanya biashara yetu ishamiri na jinsi utajiri unavyoweza kuongezeka kutokana na kazi ngumu, ujuzi wa masoko, uhusiano mzuri kati ya Wafanyakazi wote, toka juu mpaka chini na, kubwa kuliko yote, kufanya kazi kwa bidii zaidi. Katika ile miezi mitatu na nusu ya mwaka 1950, niliyokaa Bukene, muda wa kuondoka kazini na kupumzika ulikuwa shida kupatikana. Kwa kawaida, saa chache nilizopata kupumzika nilikwenda kwenye nyumba yetu ya zamani ya familia ambayo, kulingana na vile ilivyokuwa nilipokuwa mtoto, sasa ilikuwa imepanuliwa na kukarabatiwa. Lakini wakati mwingine nilipokuwa na nafasi, ndipo

Page 53: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

53

nilipotembelea kambi zilizokuwa katika sehemu nyingine, nje ya mji. Huko, kwa kawaida walipitapita Maafisa wa Kikoloni kutoka Idara za Ujenzi na Kilimo, Tabora, mmoja mmoja au wakati mwingine wawili wawili, waliokaa majuma kadha wakiangalia masuala ya upatikanaji na usafirishaji wa mazao, katika lengo la kuhakiki ubora wa mazao na upatikanaji wa chakula. Siku nyingine, wakati wa jioni, nilizungumza na Mabwana Shamba wa Kiingereza hadi usiku; wote tukiifurahia nafasi hiyo na mazungumzo, baada ya muda mrefu wa kazi ya kutwa. Mara nyingi, siku za Jumapili, niliwapelekea Maafisa hao vifurushi vidogo vya chakula cha Kihindi kutoka nyumbani kwetu, kuongezea chakula chao walichopikiwa pale kambini. Kadhalika, ilivyokuwa siku za mwanzo hapa Tanganyika na kule India, nilitokea kuwa na uwezo wa kujenga mahusiano mazuri na watu wa aina mbalimbali, katika misingi ya usawa na ushirikiano. Baada ya majuma kumi na manne, Baba yangu mdogo aliponiona kuwa sasa natosha kufanya kazi Dar es Salaam, nilijiuliza kama nafasi hiyo ingeniruhusu kurudi India kuendelea na masomo yangu. Lakini haikuwa hivyo, badala yake nikajikuta nimeunganishwa katika Timu ya Familia ya kufanya kazi Dar es Salaam. Siwezi kuficha kukata tamaa kwangu kutokana na uamuzi huo. Lakini wakati huo huo nilipata, kwa mara ya kwanza, kuonja harakati kamili za biashara. Uzoefu wa muda mfupi nilioupata kule Bukene, ulinidhihirishia kuwa hatima yangu haikuwa katika Historia ya kwetu India, ila katika biashara hapa Tanzania. Majukumu yangu ya kwanza, Dar es Salaam, yalikuwa ya ukarani. Biashara kama hii yetu, katika kipindi kile mara baada ya vita, ilitegemea sana simu na vitabu vya mwongozo kama Bentleys na Acmes. Jukumu langu lilikuwa kuandika Ujumbe uliotakiwa kupelekwa kupitia Cable and Wireless, na kuandika bili kulingana

Page 54: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

54

na bidhaa zilizouzwa. Nilitakiwa vile vile kuandaa orodha ya madai, nikitumia mashine ya chapa ya kizamani ya aina ya Imperial. Sina haja ya kusema kuwa hakuna hata moja kati ya kazi hizo iliyokuwa inanifurahisha sana, lakini zote zilikuwa msingi uliokuwa wa lazima kuuweka kabla ya kushika majukumu ya kusafirisha bidhaa nchi za nje kutokana na biashara yetu iliyokuwa imepanuka sana. Kampuni yetu ilikuwa inaagiza mbata kutoka Mafia, zilizokuwa zinakuja kwa jahazi, na lilikuwa jukumu langu kuhakikisha kuwa mwuzaji mkuu wa mbata hizo, Fazal Bhanji Jessa, anazipakia mbata hizo katika muda uliotakiwa, na kwamba mbata hizo zilipakuliwa bila kuchelewa katika Bandari ya Majahazi ya Kurasini, na kisha kuhangaikia Bima. Tukio moja tu lililokuwa na hadhi ya kukatiwa Bima lilikuwa “kupotea kwa bidhaa zote kutokana na kupotea kabisa kwa chombo”. Hakuna Kampuni yoyote ya Bima iliyokuwa tayari kubeba dhamana kwa tukio la aina nyingine yoyote. Siku moja, mchana, alinijia Ofisini mtu mmoja aliyekuwa na nguo zilizochanikachanika, akaniambaa kuwa yeye alikuwa Nahodha wa Jahazi M.65; kwamba alikuwa anatuletea mbata, lakini Jahazi lao limezama! Hapo nikakumbuka kuwa nilisahau kukata Bima. Nikampigia simu Bwana Pillai, aliyekuwa katika Ofisi ya Kampuni ya J.M. Jaffer and Co. Ltd, Wadhamini wao wa Bima, na Mawakala pekee wa Kampuni ya New Zealand iliyoitwa south British Insurance Company Ltd. Nikamwomba Bwana Pillai nilikuwa na jambo la dharura la kuzungumza naye, na kwamba nilikuwa njiani kwenda kwake. SPACE FOR FOOT NOTE MR KASA TO NOTE

Page 55: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

55

Nilipofika kule nikaeleza nilivyopitiwa kuchukua Bima kwa ajili ya shehena ile. Nikiwa papo hapo, akashika simu kuomba kuzungumza na Mkurugenzi wa South British Insurance Company, kwenye Makao Makuu yao, Mombasa. Ulipita muda kupata mawasiliano hayo, lakini alipompata akamweleza tatizo. Bwana Pillai akaagizwa kutoa Bima ya Muda, ada yake watozwe Chande Brothers Limited. Hayo yalifanywa na Makampuni yale ya Bima kwa hisani tu, wakitambua wingi wa fedha walizokuwa wanazipata kutoka katika Kampuni ya familia yetu. Nikaagizwa kumweka Nahodha Dar es Salaam, na kumfanyia mipango ya kula kiapo mbele ya DC, akieleza mazingira yaliyosababisha kuzama kwa Jahazi. Zoezi hilo lilihitaji uchunguzi wa Bandari zote za Afrika Mashariki ili kuthibitisha kama, kweli, Jahazi hilo lilizama. Hatimaye madai yetu yakaheshimiwa, tukalipwa. Kutokana na tukio hilo South British Insurance Company wakafanya mpango wa kutupatia bima kwa shehena zetu zote, mwaka mzima, na kutoa Taarifa kila mwezi ya shehena zilizosafirishwa kulingana na Bima hiyo. Baba yangu mdogo, Ratansi, hakupata kugundua ujanja nilioutumia. Kufika mwaka 1950 familia yetu ilikuwa inauza nchi za nje kahawa nyingi zaidi kuliko Kampuni nyingine yoyote ya Tanganyika. Treni nzima ilibeba nafaka toka Bukene mpaka gati la Princes Margaret, bandarini Dar es Salaam, na kahawa kutoka Moshi mpaka bandarini Tanga, ili kusafirishwa kwenda Uingereza na sehemu nyingine za Ulaya. Lakini, kama nilivyokwisha kusema mapema, sisi ndio tuliokuwa wasafirishaji wakubwa wa mawese, pamba, mashudu, mbegu za mafuta, hata alizeti na nyonyo, nta na asali. Lilikuwa jukumu langu kuhakikisha kuwa mazao yote hayo yanafikishwa kule yalikotakiwa kufika. Meli zote zilizokuwa zinakuja katika Pwani yetu hii zilikuwa zimeunganishwa katika Kampuni iliyoitwa East African Conference Lines ikiwa na Makao Makuu yake London, na Ofisi ya Kanda Mombasa, Kampuni hiyo ilikuwa inahudumia meli za Union Castle (Mawakala wao Smith Mackenzie), Lloyd Triestino (Mawakala wao Mitchell Coutts) na Clan Hall and Harrison (Mawakala wao African Mercantile Company Ltd.) Kila moja ya Kampuni hizi za Meli ilitoa punguzo la ada, kwa jina la punguzo lililocheleweshwa,

Page 56: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

56

la kiasi cha asilimia tisa; na kila Kampuni ikishindania kupata nafasi ya kubeba mizigo hiyo. Lakini hati ya ushirika wa Wamiliki Meli, iliyotoa nafasi ya kuchapisha noti pale ilipowezekana, vile vile ilijitahidi kusema vizuri na wenye mizigo kama sisi. Nakumbuka safari yangu ya awali ya London niliyoifanya mapema katika kazi yangu ilinipatia nafasi ya kula chakula cha mchana pale Ritz na Mwenyekiti wa Kampuni za Meli zao, kilichotanguliwa na kinywaji cha gin kwenye Klabu hiyo. Lakini fahari iliyodhihirika katika tafrija ile ilifunika umuhimu wa lengo zima la ziara yetu. Siku hizo shughuli za kusafirisha mizigo kuja Afrika Mashariki zilikuwa zinaendeshwa kwa uthabiti na uaminifu mkubwa. Uhakika katika kila hatua ya utekelezaji maana yake ilikuwa sisi, wasafirishaji wakuu, tuliweza wakati wote kutegemea uaminifu na umahiri wa Kampuni zote zilizokuwa Mawakala wa Meli. Kwa hiyo kazi kubwa kwetu sisi tuliokuwa katika nchi kama Tanganyika iliyokuwa na miundo mbinu mizuri katika usafirishaji, ni kuweza kupokea mizigo yetu bandarini kwa muda uliotakiwa, na ikiwa salama. Mnamo wakati huo huo ndipo Baba na Baba Mdogo walipoanza kufikiria kujenga upya mtandao wao wa biashara. Kitovu muhimu cha shughuli hizo kilikwishakuwa Dar es Salaam, sababu kubwa ni kwamba tulikwisha pata eneo kubwa la kufanyia biashara, na kiwanja cha kutosha, katika Barabara ya Pugu. Mwaka 1952, Baba akaamua kuhamia Dar es Salaam moja kwa moja na, ili kufanya hivyo, akaziuza nyumba zake za Tabora; moja ya duka, nyingine ya ofisi, zilizokuwa katika Mtaa wa Livingstone. Nyumba hizo zilinunuliwa na shemeji yangu, mume wa Vijya, aliyeipa biashara yake jina jipya la Tanna Brothers, kulingana na jina la duka lake la Mwanza. Kitendo cha Baba yangu kuhamia Dar es Salaam kiliniwezesha, labda kwa mara ya kwanza, kumwelewa vizuri. Nikatokea kutambua umahiri wake katika mambo ya biashara, utambuzi wake wa vita ndogo ndogo, na wa kupanga mikakati. Zaidi sana nikaweza kumtambua kuwa ni mtu mnyenyekevu na mwenye ari

Page 57: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

57

katika utekelezaji, na mtu mwaminifu kweli kweli . Keshavji hakunywa pombe wala hakuvuta sigara, na kwake nyama mwiko kabisa. Alikwenda Jamatini kila siku, kuabudu na kutoa zaka na misaada kwa ajili ya shughuli za Jamii, kule Magharibi ya Tanganyika na hapa hapa Dar es Salaam. Aliwalipa vizuri wafanyakazi wake, na kuwapa heshima iliyowastahili. Alikuwa mtu wa kawaida, aliyependa kutembea kwa miguu, na vile vile kukaa na familia yake; na, muhimu kuliko yote, alikuwa na busara ya kuishi na watu. Nikiutumia uhusiano mwema wa Baba na Baba Mdogo waliokwisha kuujenga na watu wengi katika Dola na katika Biashara, na halafu ule nilioujenga mimi mwenyewe, nilianza kujishughulisha na maisha ya Jamii niliyoishi nayo. Nilitumbukia katika Chama cha Utamaduni, njia pekee Jijini iliyowawezesha watu wa Mataifa yote kuchanganyika bila hofu wala upendeleo. Kwa kweli, pamoja na jina lake, mara nyingi utamaduni wenyewe haukupata kuzingatiwa. Tulikutana mara moja, siku ya Jumamosi, kila mwezi, Mwenyekiti akiwa J.F. Moffet, Kamishna wa Kikoloni wa Huduma za Umma katika maeneo ya British Council, kwa sababu haikuweko Hoteli iliyokuwa tayari kutumiwa na kikundi kama kile kisichoeleweka. Huko tulikunywa chai pamoja na kuzungumzia matukio ya wakati huo. Baadaye mimi nikajulikana sana katika Chama hicho, mpaka nikapigiwa kura kuingizwa kwenye Kamati, na baadaye nikachaguliwa Kaimu Katibu. Tuliwakaribisha watu mashuhuri kutupa nasaha zao. Kufika mwishoni mwa mwaka 1950 tulikuwa tumepata nafasi kuwasikiliza watu mashuhuri kama Aga Khan, aliyetoa Mada kuhusu “Vita katika Jiji” ambalo maana ya jina lake ni “Bandari ya Salama”, kitendawili ambacho Mtoa Mada hakubabaika kukielezea. Kadhalika wakaja Makamo wa Rais wa India, Dk. Radhakrishnan aliyetoa mada kwa dakika arobaini, bila kusoma mahali, juu ya Hatma ya Ustaarabu, kwa Hotuba ya kusisimua pale Avalon Cinema. Wengine walikuwa Mheshimiwa Bibi Indira Gandhi, Mheshimiwa Ian Macleod, Mheshimiwa Sana Bibi Golda meir,

Page 58: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

58

Mtukufu Askofu Mkuu wa Cantebury, Mchungaji Mkuu Arthur Michael Ramsey. Mpaka wakati huo nilikuwa naujua vema Ukumbi wa Avalon. Mwanzoni mwa mwaka 1950 nilikuwa na mazoea ya kwenda senema lakini si kwa kukatia tikiti, kama nilivyokuwa nafanya na marafiki zangu kwenye Nyumba za Senema ya Tabora Talkies ila kama Mjomba wa Bodi iliyokuwa na sifa sana ya kudhibiti Picha za Senema. Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuteuliwa katika Chombo cha Umma, niliyoipata kutokana na kujishughulisha sana na mambo ya Jamii mtaani; uwezo wangu ukapata kuonekana zaidi. Nikajikuta nikiwa mmoja kati ya Wadhibiti watatu tuliotakiwa kutoa ripoti kwa Bwana Percy Everet, Mdhibiti wa Filam wa Taifa, ambaye naye alitakiwa kufikisha taarifa zake kwa Bwana Barclay Leechman, Mjumbe wa Baraza la Utawala, aliyehusika na masuala ya Huduma za Umma. Percy Everet, mtu makini aliyetumia gari ya aina ya Austin kwa shughuli zake za kila siku, alikuwa Mkurugenzi katika Tawi la Mjini hapa la Chama cha Wafanyabiashara za Jumla wa Afrika Mashariki, Gailey and Roberts (sasa limechukuliwa na Uniliver) na hakufaa kwa lolote zaidi ya kuchekesha. Pamoja na mambo mengine Percy Everet aliwapenda sana kasuku, waliokuwa wameenea kiasi cha kuijaza nyumba alimokuwa anaishi na mkewe Queenie. Percy ndiye aliyekuwa Msimamizi wa Bodi ya kudhibiti Filam Tanganyika nzima kwa karibu miaka kumi, kabla hajapata nafasi nzuri zaidi ya kuwa Mstahiki Meya wa Kwanza kuteuliwa katika Jiji la Dar es Salaam, na kushiriki kwa ari kubwa katika Baraza la Biashara na Baraza la Viwanda. Wakati ule, katikati ya miaka 1990, Jiji la Dar es Salaam lilikuwa na majumba matano ya Senema. Pamoja na Avalon lililokwisha tajwa hapo mwanzo, kulikuwako Amana, Empire, Empress na Odeon na, katika hayo, ni Amana tu lililokuwa katika eneo linaloweza kuitwa la Wenyeji. Mwanzoni mwa kila mwezi, Wajumbe wa bodi ya Filam walialikwa kwa barua ya Katibu wa Bodi kuwajulisha ratiba yao katika majuma manne yanayofuata. Mara nyingi wito huo ulituhusu Wajumbe watatu, wa Bodi kuhudhuria na kutathmini picha, peke yetu, katika ukumbi mmoja

Page 59: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

59

kati ya hizo tano za Sinema Jijini; kazi tuliyoifanya kwa mzunguko kudhibiti filam zilizopangwa kuonyeshwa, Tulishauriwa kuwa tusichanganyike wote pamoja, ila tukae ukumbini kila mmoja peke yake, labda kwa sababu picha nyingine zinaweza kuonekana vizuri zaidi kutoka pembe fulani tu. Maelekezo tuliyoyapata kwa ajili ya uchambuzi wa Filam yalikuwa ya wazi wazi pia. Tulitakiwa kuangalia, na kutoa Taarifa, juu ya sehemu zozote katika filam zilizokuwa zinashawishi ngono, au vitendo vya uhalifu wa sheria, lakini hayakuweko maelekezo yoyote kuhusu ubaguzi, wa rangi wala wa Dini. Baada ya kutoa Taarifa zetu, filam ilipewa alama ‘U’, au “A” au ‘X’. Na, pamoja na kazi yote hiyo, hatukupata chochote zaidi ya shilingi ishirini kwa kila kikao kwa ajili ya usafiri. Mwanzoni niliyakabili majukumu hayo mapya kwa jitihada zilizostahili. Nilifika kwenye Kituo nilichopangiwa, na kukaa nikaangalia filam za Kihindi zisizokuwa na ujumbe wowote ambazo, kwa kawaida, zilikwenda kwa muda wa saa tatu nzima. Nilijitahidi kukaa na kuangalia mpaka mwisho kabisa picha za Abbott na Castello, mpaka hatimaye nikatokea kuwa bingwa wa picha zinazoshindaniwa za Alan Ladd, Tyrone Power na Stewart Granger. Katika mazingira hayo haukupita muda kabla ya kudhihirika upumbavu wa mambo yale niliyokuwa natakiwa kuyafanya. Kwanza kule Marekani, katika miaka hiyo ya 1950, biashara ya filam ilikuwa mno kutokana na vitendo vya Seneta McCarthy na genge lake waliofanya karibu kila filam ya Hollywood ilikuwa inatangaza ubabe, ujambazi, ngono na uzandiki. Wakati huo huo hata filam za Kiingereza hazikuwa bora zaidi, zikionyesha mielekeo mbali mbali ya maisha ya Waingereza. Na filam za Kampuni ya Bombay zilikuwa zinashurutisha kwa ukali kuzingatia Maadili ya Kihindi kiasi kwamba jitihada za kudumu za Wasambazaji kuulaghai umma kutumaini kuona vitu vya maana zaidi hazikufanikiwa siku zile hata kumbusu mtu ilikuwa haimo. Lakini ukweli ni kwamba hata kama vizingiti kama hivyo havingekuwako kabisa, bado zile filam zote zilizopenya kimya

Page 60: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

60

kimya kufika pwani ya mbali ya Tanganyika zingekuwa zimevuka machekecheke makali ya Serikali za Marekani, Uingereza na India. Wazo kwamba sisi tuliokuwa katika Bodi ya kudhibiti Filam hapa Tanganyika tungeweza, mchana mmoja katika Jumba la Senema, kugundua sehemu zilizokuwa zinachochea hisia za ngono ambazo Bodi zote hizo nyingine hazikugundua linatia mashaka sana. Kusema kweli Bodi yetu hii ndogo ya Filam ilikuwa mfano mwingine wa Taratibu za Ukoloni wa Kingereza wa kuoanisha miundo ya Utawala wa ndani duniani kote bila wenyewe kujiuliza : Kwa nini ! Labda kama sisi Watanganyika miaka miwili tu baada ya maasi ya Mau Mau katika nchi ya jirani ya Kenya, tungaliagizwa kutafuta Visa ambavyo vingeliweza kuvuruga utengamano uliokuwako katika ya Mataifa mbalimbali, kazi yetu ingalikuwa na manufaa kweli. Lakini haikuwa hivyo ; Kwa hiyo haikuwako faida yoyote. Hivyo haishangazi kwamba ari yangu katika shughuli hii ya kudhibiti filam ilififia. Nikishirikiana na Mameneja wa Majumba ya Senema, ambao mawazo yao yalikuwa tu katika kupanga filam walizokuwa wanatarajia kuzionyesha majuma yaliyokuwa yanafuata, niliweza kupenya katika giza la ukumbi nikajiondokea dadika kumi tu toka filam kuanza kuonyeshwa, na kurudi dakika chache tu kabla ya mwisho wake. Kwa mahusiano mema na Wamiliki wa Senema, na kwa vile tulivyokuwa tunatawanywa ndani ya ukumbi wenye giza, niliweza kupenya katika giza hilo nikajiondokea baada ya kama dakika 10 baada ya filam kuanza kuonyeshwa, na kurudi muda mfupi tu kabla ya mwisho wake. Kwa hisani ya wenye Senema, na kwa vile tulivyokuwa tunatawanywa gizani, niliweza kukwepa kwa miezi kadha majukumu mengine ya kudhibiti filam; mpaka mwishowe kwa bahati mbaya, mchana wa siku moja, mwenzangu, mke wa Wakili, akaugundua ujanja wangu huo. Haraka haraka nikashitakiwa kwa Percy Everett, na mara hiyo hiyo akanipigia simu. Everett akaanza mazungumzo kama kawaida, akieleza masikitiko yake juu ya malalamiko yaliyomfikia dhidi yangu, akaendelea kusema kwamba, kutokana na taarifa hizo, mimi nisingeweza tena kutekeleza majukumu yangu namna

Page 61: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

61

inavyotakiwa! Nikauliza, ili kulikwepa kosa na kupata muda wa kufikiri kwanza, “Siwezi vipi?” Baada ya kukaa kimya kidogo, kama mtu anayefikiria atakalojibu, Everett akanitobolea kwamba taarifa zimemfikia kusema kuwa nilikuwa naondoka kwenye ukumbi wa Senema kiasi cha dakika kumi tu toka filam kuanza; na kwamba yeye, Everett, ameelezwa kuwa mchezo huo nilikuwa naufanya mara kwa mara kama ndiyo tabia yangu. Ikawa zamu yangu kunyamaza kidogo, kisha nikakiri, “Ni kweli; mara moja au mara mbili, nilipokuwa naangalia moja ya zile filam ndefu za Kihindi, katika ukumbi usiokuwa na hewa ya kutosha, wala viyoyozi, nililazimika kutoka nje mara moja kuvuta hewa na, siku moja, nilifikia hali mbaya kiasi cha kutafuta msaada wa daktari. Lakini hayo ni matukio machache tu ukilinganisha na jinsi nilivyokuwa natekeleza majukumu yangu katika Bodi”. Nikaendelea, lakini ukitazama uzito wa mashitaka hayo, pengine ingefaa kupanga mkutano rasmi, mimi, wewe, na huyo mshitaki wangu kwa pamoja. Kwa nafasi hiyo angeweza kufafanua zaidi Sura na Aya, na mimi nikapata nafasi ya kujitetea kwa kuelezea ya upande wangu. Kufika hapo Everett akanyamaa kimya tena. Kwa vile nilivyomtamka mshitaki wangu kuwa ni mwanamke, akatambua kuwa utetezi wangu ni muhimu. Wote sisi, yeye na mimi, tuliusikia uvumi uliokuwa unaelezwa Jijini kuwa mwanamke mmoja alikuwa na shauku ya kupata nafasi ya ziada katika Bodi kwa ajili ya rafiki yake; kwa hiyo kuipata nafasi hiyo kwa kumtoa mtu mwingine lingekuwa jambo la manufaa kwake katika kutimiza azma hiyo; lakini gharama yake ni kuiumbua Bodi. Everett akakohoa kidogo, kisha akaniambia, kwa sauti isiyokuwa kali kama ile ya mwanzo, niendelee na shughuli zangu, lakini niwe muangalifu zaidi katika siku zijazo. Akaendelea, “lakini, kwa mbali, naendelea kuamini kwamba ulikuwa unayatenda hayo,” Wakati huo majukumu yangu ndani ya Kampuni ya familia yalizidi kuongezeka. Nilimtambua Baba yangu mdogo kuwa mtu mwenye uwezo mkubwa, na, nadhani, na yeye aliniona kuwa mtu aliyekuwa tayari kujifunza. Nilijifunza kwake namna ya kuwasimamia

Page 62: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

62

wafanyakazi na ya kuendesha Viwanda, nikaelewa matatizo ya kuendesha mashine za kusaga na za kukamua mafuta. Nikawa fundi wa mazungumzo na wanunuzi na wauzaji na, kwa njia hizo, nikaanza kujijengea sifa miongoni mwa wafanyabiashara wenyeji. Nawiwa deni kubwa na Baba zangu wadogo, wote wawili, waliochochea wakati wote ari yangu, sio tu katika shughuli zangu mwenyewe, bali vile vile katika kujifunza mbinu za biashara kwa namna nzuri, kule Bukene na hapa Dar es Salaam waliniamini, hatua kwa hatua, kwa kunikabidhi madaraka zaidi. Matokeo yake nikakabiliwa na mmoja wa wale niliokuwa nashirikiana nao zaidi katika biashara walionitaka niwasaidie kuanzisha chombo kilichoitwa ‘Round Table’ hapa Dar es Salaam. Utaratibu huo wa ‘Round Table’, chombo cha wakubwa kilichochipukia Uingereza, kikakua na kupatikana Round Table ya Ireland na Visiwa vyote vya Uingereza, wakati huo ulikuwa ndio kwanza unapenyeza mizizi yake katika Afrika na Asia. Katika Afrika Mashariki ‘Round Table’ ilikuwa imeanzishwa Mombasa na Nairobi. Na kufika mwaka 1954, zikawako nong’ono za Miji ya Dar es Salaam na Kampala kufuatia. Kwa ari na ushawishi mkubwa wa Alistair Niven, Wakala wa Meli za Union Castle, na Ron Hornsby, mkadiriaji wa kodi ya mapato Nchini, Mkutano wa kwanza ukafanyika Dar es Salaam, na mimi nikahudhuria. Mara baada ya hapo ‘Round Table’ ya Dar es Salaam ikazinduliwa rasmi na kupewa namba 4 kwa kuwapiku Kampala, waliopewa namba 3, na mimi nikatambuliwa rasmi kuwa Mwanachama wa kwanza duniani wa ‘Round Table’ asiyekuwa Mzungu. Siwezi kukana kuwa nilijivunia kutambulika kiasi hicho, lakini sikutaka kudumu katika kujipongeza. Dunia ilikuwa imesonga mbele tangu kuanzishwa kwa ‘Round Table’ na suala la kutambua mabadiliko hayo lilikuwa limekwishapitwa na wakati. Nafurahi kutamka kwamba mimi nilikuwa wa kwanza kati ya wengi, wasiokuwa Wazungu, kushika nafasi hiyo. Mara nikafuatiwa na Noorali Sayani, Mwanasheria wa kabila la Ismaili, Tony Almeida, Msanifu wa Majumba, Al Noor Kassim, Ismailia vile vile, Mwanasheria aliyekuwa katika Baraza la Mawaziri la Nyerere, na, baadaye Hamza Kasongo, Mtangazaji

Page 63: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

63

mahiri katika Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC. Hivi leo, kwa jitihada za waanzilishi waliomo katika miji kama Dar es Salaam, ‘Round Table’ ya dunia imekuwa kweli mwakilishi wa jamii ya Wafanyabiashara, na wa wale inaojitahidi kuwahudumia. Lakini, kwa masikitiko makubwa, uwakilishi wa dunia nzima kama ule wa vyombo vinavyofanana, pamoja na Freemasonry, unapungua. Harakati zangu katika ‘Round Table’ ziliongezeka kila miaka hiyo ya 1950 ilivyosonga mbele. Mwaka 1956, nilichaguliwa Katibu, Ron Hornsby akiwa Mwenyekiti. Kwa pamoja kazi yetu ikatuwezesha kupata ujuzi wa mambo mbali mbali tuliouhitaji katika utekelezaji wa majukumu yetu. Kwa sababu ya ugumu wa taratibu za Klabu yetu, nilijitahidi kubuni kumbukumbu za mkutano unaokuja sambamba na zile za mkutano uliopita. Nilipopeleka kwa Ron kwa mara ya kwanza, kumbukumbu zote mbili, Ron akaniangalia kama mtu ambaye ndio kwanza ameshuka kutoka katika Sayari nyingine, lakini alipokwisha kuuelewa utaratibu wangu huo tukaelewana vizuri. Mwaka uliofuata nikachaguliwa Makamu Mwenyekiti na hatimaye nikawa Mwenyekiti mwaka 1958. Katika mwaka ule niliokuwa Mwenyekiti wa Round Table tulipata fedha nyingi kwa ajili ya misaada kuliko zilizowahi kupatikana katika kipindi kingine chochote huko nyuma. Kivutio hicho cha mwaka kilichoingiza fedha nyingi kuliko zote ni kile kilichoitwa ‘Mannequin Parade’, kunadi mali za Aly Khan, mwana wa Mfalme, kule Oysterbay. Kwa ufadhili mkubwa wa Shirika la Ndege la Uingereza, BOAC, warembo watatu mashuhuri wa London wakaletwa Dar es Salaam, wakiwa na msuka nywele mashuhuri, Bwana Teasy-Weasy Raymond. Hakuna haja ya kueleza kwamba kipindi kile cha mwisho wa miaka ya 1950 Dar es Salaam kulionekana kuwa mbali mno na tabia za London, na tofauti hizo za utamaduni zikajidhihirisha pale pale uwanja wa ndege. Mara baada ya wageni hao kuteremka kwenye ndege, baada ya safari yao ndefu, wakazuiwa na Maofisa Forodha wa Tanganyika, pamoja na mavazi na vito walivyokuja navyo. Baada ya kubembeleza sana, nikisaidiwa na Meneja wa Dar es Salaam wa BOAC, ndipo ‘Teasy-Weasy’, pamoja na wale Warembo watatu na

Page 64: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

64

mizigo yao yote, waliporuhusiwa kukamilisha safari yao kwa kuingia mjini Dar es Salaam. Warembo hao wa London walikaribishwa wakiwa wageni wa Hoteli ya New Africa. Katika mikutano ya awali ya maandalizi, kabla ya kuja kwao, ilikubaliwa kwamba kusingekuwako tatizo la wenyeji kujitolea kuwasaidia Warembo hawa katika jambo lolote linalowezekana. Bwana ‘Teasy-Weasy’ akachukua jukumu la kusimamia jukumu lote la urembo na vyumba vya kubadilishia nguo, na wale wa Kamati hawakuwa na nafasi kubwa ya kuingilia. Siwezi kusema kuwa nilimwonea wivu Bwana ‘Teasy-Weasy’ majukumu yake. Mazingira yale ya kupokelewa kwao yaliwavuruga warembo wale, wakapata wasiwasi wa hali itakavyokuwa katika siku zilizobaki. New Afrika ikishuhudia mabishano yasiyoisha! Siku ilipowadia, nikampata bingwa kutoka kikosi cha wataalamu wa maigizo kiitwacho Dar es Salaam Players, mtu ambaye, kama nakumbuka vizuri, baadaye alijenga urafiki na mtaalamu wetu mashuhuri. Timu hiyo ya wataalamu wa shughuli hii iliandaa nafasi ya muda katika varanda ya nyumba kuwawezesha Warembo hao kufanyia mazoezi, wakaweka na viti na vinywaji kwa kile kilichotarajiwa usiku wa kukumbukwa na yenye furaha ambayo haijapata kutokea. Utaratibu wa huduma ulikuwa mzuri mno, kama zilivyoporomoshwa shukrani za Waalikwa, wakiwa pamoja na Gavana Mhe. Richard Turnbull, na Meya wa Dar es Salaam, Mhe. Richard Howarth. Kwa bahati mbaya, kitu ambacho hata mmoja wetu hakufikiria, ni hali ya hewa ya Dar es Salaam. Mtu yo yote aliyewahi kuishi Dar es Salaam, hasa eneo la Oysterbay, ataujua ule upepo mwororo, wa baridi, ambao mara nyingi hupuliza kutoka pwani. Asubuhi ya siku ile ya Mannequin-Parade, upepo ule mtamu wa baharini ukageuka Kimbunga, kilichotikisa vyombo muhimu katika nafasi iliyoandaliwa, kimbunga ambacho msuka nywele yeyote anayejulikana duniani hangeweza kuhimili. Hata sisi, Wanakamati, tulitaharuki, na kuwaza kuihamishia ndani shughuli ile, lakini wakati tulikuwa tumechelewa mno kupanga sherehe kwa plan B. Tulichofanikiwa kufanya tu ilikuwa kuwaficha habari hizo wageni waalikwa

Page 65: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

65

waliokuwako New Afrika ambako wakati huo hata subira ya Bwana ‘Teasy-Weasy’, ambaye kwa kawaida ni mtu mchangamfu, ilianza kuyeyuka. Jioni ya jana yake nilimshambulia muhudumu kwa ulegevu wake katika kumletea kinywaji cha Gin, nikitishia kumpeleka London kupata mafunzo yanayostahili. Kule kwenye nyumba ya Oysterbay tulikuwa tukiomba kwa matumaini ya kasi ya upepo ule kupungua. Majira ya saa kumi na mbili jioni, giza linaingia, upepo ukatoweka ghafla, kwa hiyo maonyesho yakaendelea kwa mafanikio yaliyotambuliwa na Waheshimiwa waliokaribishwa, yalikuwa mafanikio makubwa zaidi kuliko tulivyotarajia. Mara moja tu Bwana Gavana na wale aliofuatana nao, na Mkewe aliyevaa kofia ya manyoya na vidhibiti vyeupe vya viganja, walipata hisia ya yale tuliyokabiliana nayo mpaka kufanikisha shughuli ile, wakati kile kimya kilichokuwako kilipobadilika kuwa kelele za wasichana waliokuwa wanagombana katika chumba cha kuvalia tulichokitengeneza. Kesho yake tukaandikwa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Tanganyika Standard, na fedha tulizozikusanya zilituwezesha kuanzisha huduma ya Wauguzi katika Wilaya (wakati huo) ya Dar es Salaam, kuhudumia wagonjwa waliokuwa katika viunga vyake. Shughuli zangu za biashara zilinisukuma kuingia katika Chama cha Dar es Salaam cha Wanunuzi wa Mazao, ambacho mara moja kilinichagua kuingia katika Kamati yake ya utendaji, ambayo wakati mmoja Baba mdogo alikuwa Mwenyekiti wake. Vile vile nikawa Mwanachama wa Chama cha Dar es Salaam cha Biashara na Kilimo, kilichoanzishwa mwaka 1921 katika miezi ya mwanzo ya udhamini ya Waingereza. Kufika mwaka 1960, nikawa Rais wa kwanza wa Chama hicho asiyekuwa Mzungu ingawa, miaka minne kabla ya hapo niliitwa na Gavana Edward Twining kwa lengo la kuniingiza katika Baraza la kutunga Sheria kwa miezi sita, kujaza nafasi iliyokuwa wazi kutokana na mmoja wa wajumbe wa Kihindi aliyekwenda likizo ndefu.

Page 66: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

66

Baraza hilo lilianzishwa Tanganyika mwaka 1926, kumshauri Gavana katika mambo mbali mbali. Kufika mwaka 1948, kama ilivyokuwa katika Nchi zote za Jumuiya ya Madola, Wazawa wachache kutoka Mataifa makubwa Nchini, wakakaribishwa kushiriki. Hapa Tanganyika Baraza likapanuliwa kuingiza Wajumbe wapya wanne wa Kiafrika, na hao, pamoja na wale wa Kiasia, idadi yao ikalingana kabisa na wale Wawakilishi wa Waingereza waliokuwamo, na hivyo kujenga kile ambacho Ofisi ya Makoloni ilidhamiria kukiita “Uwakilishi Uliolingana”. Kama ilivyokuwa katika dola yote ya Kingereza iliyoitwa baadaye Jumuiya ya Madola, Baraza la kutunga Sheria lilifanya kazi sambamba na Baraza la Utawala, lililokuwa ndio kama Kabineti ya Gavana wa wakati huo. Kwa hiyo nafasi niliyopewa kuingia kwenye Baraza la Kutunga Sheria ilikuwa kama alama ya kuheshimiwa. Lakini kabla ya kukubali au kukataa, nilitafuta ushauri kutoka kwa Baba, kwa mshangao wangu, nikakuta anapinga vikali kuteuliwa kwangu katika nafasi hiyo, akisisitiza kuwa ingenifaa zaidi kuelekeza nguvu zangu katika biashara, na kukwepa vishawishi vyovyote vya kutumbukia kwenye Siasa. Akanidhihirishia, bila ya kutamka hivyo, hofu yake katika familia nikiteuliwa, kama zawadi, katika huduma ya utawala wa Kikoloni, kulinganisha na uhusiano unaokuwa wa familia na Viongozi wa Kiafrika wa Siasa na Biashara, kama John Rupia na Dossa Aziz ambao, kwao wao, Kampuni yetu inanunua Mpunga na, mara nyingi, baada ya kutoa malipo ya mwanzo. Sababu nyingine ya wasiwasi wa Baba yangu ilikuwa kwamba, kufikia mwaka 1956, mwelekeo wa Siasa katika Tanganyika ulikuwa umebadilika. Huko nyuma, katika miaka ya 1920, Serikali ya Uingereza ilipewa na Umoja wa Mataifa, jukumu la kutawala Tanganyika kwa lengo la kuiandaa Nchi kujitawala. Kizazi kipya cha Watanganyika weusi, kinachoongozwa na Mzalendo mwenye upeo mkubwa, Dk. Julius Nyerere, kilijibebea jukumu la kuiandaa Nchi yao kwa kujitawala. Msomi wa Chuo Kikuu cha Edinburgh, aliye kuwa na marafiki, na aliyesaidiwa, na kikosi kizima cha Fabian ndani ya Chama cha Leba cha Uingereza, Dk. Nyerere

Page 67: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

67

alianzisha, mwaka 1954 Chama cha Siasa cha TANU kilichojijengea sifa ya kimataifa na hapa Nchini pia. Nyerere alikuwa na moyo wa kibinadamu, asiyekuwa na hata kifupa kimoja cha ubaguzi mwilini mwake, ingawa walikuwako baadhi ya Viongozi Wakuu katika Chama chake waliokwisha anza kudai, sio tu kuondoka kwa dola ya Kikoloni, bali vile kukomeshwa kwa unyonyaji wa Wahindi wanaowafanyia wafanyakazi wao, Waafrika weusi. Labda sababu za hisia hizo katika masuala ya uchumi zinaweza kuelezeka. Wakati ule wastani wa mshahara wa Mzungu katika Tanganyika ulikuwa chini kidogo ya £1,800 (Sh. 36,000/=) kwa mwezi, ukilinganisha na wa Mwasia wa £500(Sh.10,000/=) na wa Mwafrika £75 tu (Sh. 1,500/=) Lakini jinsi takwimu hizi zilivyokuwa zinatafsiriwa katika uwanja wa siasa kwa kweli zilikuwa zinaudhi, kwa sababu wakati huo huo Mh. Gavana Edward Twining alikwishatoa kibali cha kuanzishwa kwa UTP kilichogharimiwa na fedha za Waasia wa hapa na Waingereza wa nje ili kushinikiza mawazo ya zamani ya kikoloni katika kitu kilichodhaniwa kuwa usawa wa Mataifa katika Tanganyika itakayokuwa huru. Wahimili wa UTP walikuwa familia mbili kubwa, za Waasia na watu binafsi waliokuwa na uwezo kama Tom Tyrell na Kanali Sterling, waliokuwamo baadaye katika Capricon Society. Haraka haraka Chama cha UTP kikaungwa mkono na baadhi ya Maafisa wa Kiingereza, pamoja na Gavana mwenyewe mwaka 1957, kwa kukishambulia Chama cha TANU kuwa ni cha kibaguzi, kwa sababu ya kuwazuia Waasia na Wazungu kuwa Wanachama wake, ingawa Wanachama wa TANU walioongozwa na Dk. Nyerere, walikuwa wanawashawishi kimya kimya, Waasia kujiunga na TANU. Kwa hiyo Wafanyabiashara wa Kiasia kama sisi walikuwa wakibamizwa pande zote, na wakati mwingine wakivutwa pande zote, za mabishano makali ya Kisiasa na ya ubaguzi wa rangi. Baba yangu aliijali zaidi kuliko wengi waliomtangulia hali ya kuenea kwa harakati hizo. Lazima niseme kuwa vile vile alikuwa mwangalifu mno katika masuala yoyote yaliyohusu Siasa, tangu

Page 68: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

68

alipohamia Dar es Salaam kutoka Tabora, alizidisha hamu aliyokuwa nayo toka zamani, ya kutumbukia katika shughuli za misaada katika jamii. Alikuwa akiniambia kuwa ninapotoa chochote, mkono wangu wa kushoto usijue kile kinachofanywa na mkono wangu wa kuume. Msimamo wake huo kuhusu utajiri ndio uliomfanya akatambulika na kuheshimiwa miongoni mwa jamii ya Waasia mpaka akachaguliwa Rais wa Lohana Mahajan. Mchango wake ulitambuliwa, vile vile miongoni mwa Waafrika weusi, hasa kutokana na ridhaa yake kuwa na ushirikiano wa dhati na wafanyabiashara wa Kiafrika, kama wale wakulima wa Mpunga, akina Aziz na akina Rupia. Lakini mawazo yake yalikuwa katika biashara na utajiri tu, sio katika Siasa, na alinitaka mimi niliyekuwa na mwelekeo wa kushika Biashara za Familia kumfuatisha katika msimamo wake usiokuwa wa Kisiasa, au, unaobeza au hata kupinga mambo ya Kisiasa. Baada ya Mkutano huo wetu sisi peke yetu nikautii ushauri wa Baba yangu, na kuukataa uteuzi wa Gavana kuniingiza kwenye Baraza la Kutunga Sheria. Lakini, kwa kufanya hivyo, nilitambua kwamba mimi na Baba yangu tutadumisha tofauti za misimamo katika vitendo vyetu wakati wa kuhudumia Wananchi, na kwamba kuhitilafiana huko kutapanuka kila siku zitakavyokuwa zinapita. Maana hata kama niliielewa hofu ya Baba kwangu kuchangamkia mno mambo ya Siasa, na kwamba ningedumu katika utenganisho huo kati ya Biashara na heka heka za Siasa maisha yangu yote, nilitambua kuwa kujishughulisha kwangu katika kuwahudumia watu kusingewezekana nchini mwangu bila ya kutumbukia kwenye hatari au kunipa gharama fulani. Iwe katika sura ya ushauri katika siku zile za mwisho katika utawala wa Kikoloni, au katika nafasi kama hiyo hiyo katika Serikali zitakazofuata za Tanganyika huru, wakati wote itapatikana nafasi ya watu wachache wasionijua vema kutafuta visa vya kunitafsiri au kunielezea vibaya shabaha zangu mwenyewe. Inawezekana kuwa mwaka 1956 usingeweza kuniona nikiapishwa kuwa Mjumbe wa muda wa baraza la kutunga sheria, lakini wakati huo nilikuwa nabeba madaraka yaliyokuwa yananitosha na kuzidi katika Kampuni ya familia. Kufika mwaka 1952 majukumu yangu

Page 69: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

69

katika kusimamia uuzaji wa bidhaa Nchi za nje yalinifanya nichaguliwe na Baba zangu kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Chande Brothers Ltd. Majukumu mengi ya uzalishaji yalikuwa bado yamekamatwa na Kampuni tofauti ya Chande Industries Ltd, ambayo kiwanja chake cha eka kumi na tano zilizoko barabara ya Pugu sasa kilikuwa kinaendelezwa kwa haraka. Tulinunua eneo hilo lilitarajiwa kuwa Makao Makuu ya National Milling Corporation kwa hati ya miaka tisini na tisa kutoka kwa Sheikh Ali Bin Saidi, ambaye naye alilinunua miaka ya 1920 kwa bei ndogo sana kutoka kwa msimamizi wa Mali ya adui (Yaani Wajerumani), na tulikwishajenga viwanda vingi vya kusaga na kukamua mafuta. Wakati huo Kampuni yangu, Chande Brothers Limited, ilikuwa siyo tu mwuzaji mkuu katika nchi za nje wa kahawa ya Tanganyika, lakini vile vile ilipanda na kushika nafasi ya pili kati ya wauzaji wa Nta, na kuwa miongoni mwa kumi wa kwanza katika Biashara iliyokuwa na faida kubwa kuliko zote ya mbegu za mafuta na mashudu, ikishindana na Makampuni makubwa yaliyokuwa Uingereza, kama Unilever, Gibson na Kampuni, ya Steel Brothers. Mwaka 1957 ukatokea mfarakano kati ya Baba zangu wa Bukene na hawa wa Dar es Salaam. Kwa mgongano katika familia kutokana na wivu kati ya wake wa ndugu au watoto wao, hasa kwa sababu ya mali, hali hiyo ya mgongano katika familia hutokea. Chimbuko la ugomvi lilikuwa Baba mdogo wa mwisho Amratlal, aliyekuwa Bukene, alijihisi kuwa anabaguliwa. Ingawa hakuwako hata mmoja kati yetu aliyeyajua hayo mpaka yalipolipuka, lakini yeye alijihisi tu kuwa amebaguliwa akiwa katika kile kijiji kilichoko mbali, Magharibi ya Tanganyika. Matatizo madogo madogo yaliyo ya kawaida katika maisha ya kule, kama ugumu wa kupata leseni, au kupata nafasi ya kupakia mizigo katika mabehewa, yaliachwa yakaongezeka kwa kiwango kikubwa kwa sababu ya kukosekana msaada na huruma kutoka kwa kakiye Ratansi aliyekuwa Dar es Salaam mpaka hatimaye Baba mdogo Amritlal akatamka azma yake ya kujitenga na Kampuni hiyo ya familia! Jitihada za Baba na za Baba mdogo Ratansi, kumshawishi aachane na fikira za kuchukua hatua hizo hazikufanikiwa; hivyo

Page 70: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

70

hatimaye ikakubaliwa mali za familia zigawanywe. Jambo hilo likawa jepesi kuliko yeyote kati yetu alivyofikiria. Shughuli za Bukene zililingana kwa kiwango na shughuli yoyote ya Kampuni ya Familia iliyoko Dar es Salaam, kwa hiyo akaachiwa Baba mdogo Amratlal. Baba mdogo Ratansi akaendelea kushika Chande Brothers Limited iliyoshughulikia uuzaji nchi za nje wa Kahawa na mazao mengine; na baba yangu akashika Chande Industries Limited, iliyokuwa inamiliki Viwanda vya kusaga unga na kukoboa mpunga mjini Dar es Salaam. Ndugu hao watatu wakaendelea kuwa Wajumbe wa Bodi za Kampuni zote tatu. Baba yangu mdogo, Ratansi akafunga biashara zake katika miaka ya mwanzo ya 1960, na kuanzisha biashara ya kuuza kahawa mjini Bangolore, India, akisaidiwa na watoto wake watatu wa kiume. Karibu wakati huo huo Baba yangu mdogo, Amritlal, akaondoka pia, na kuanzisha shughuli nyingine za biashara kule Secunderabad, India. Mwaka ule uliofuatia kugawana Kampuni, Baba yangu aliteuliwa Mkurugenzi Mkuu wa Chande Industries Limited. Wakati huo Kampuni mpya ya Dar es Salaam peke yake ilipangiwa awamu mpya ya kupanuliwa haraka haraka. Gavana mpya na, kwa mawazo yangu, mwerevu zaidi, Mhe. Richard turnbull, aliteuliwa kutawala Tanganyika. Haukupita muda kabla sijakabiliwa rasmi upya na kutakiwa, safari hii, kuingia katika Mabaraza yote mawili: la Kutunga Sheria na la Kutawala. Safari hii nikaazimia kukubali; lakini, kabla ya kufanya hivyo, nikataka kumshirikisha Baba yangu kwanza ili anikubalie. Kwa hiyo nikaanza kwa Baba mdogo, Ratansi, na yeye akashauriana na Baba mdogo mwingine wa Bukene. Vile vile nikazungumza na baadhi ya marafiki wa Baba yangu, ndipo hatua za kutafuta ridhaa ya baba zilipoanza. Safari hii jitihada ile ya pamoja ilizaa mafanikio kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Baba yangu akanipa baraka zake, lakini kwa sharti moja nililolikubali haraka, kwamba nisipokee mshahara wala posho, wala marupurupu mengine yoyote kutokana na kazi hizo. Kuingia kwangu katika Baraza la Utawala kulinitumbukiza katika mambo ya ndani kabisa ya Serikali ya Waingereza nchini

Page 71: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

71

Tanganyika. Kama ilivyo katika Baraza la Mawaziri kule Uingereza, tulikutana kila Alhamisi asubuhi, baada ya Mada kutawanywa mapema kwa uthibitisho wa Kitabu cha kukabidhi Barua kilichokuwa kinafungiwa sandukuni. Mwanzo nilidhamiria kuwa, baada ya Makabrasha hayo ya Serikali, niongeze mzigo kwa Katibu wangu wa Chande Industries Ltd; lakini Katibu wangu alipoikosa ridhaa ya Maafisa wa Usalama, ikabidi mke wa Mtumishi mmoja wa Hazina aletwe kufanya kazi kwa muda kuhangaikia hayo makabrasha yangu. Ndipo nilipoitambua kwa haraka bahati yangu ya kuongezewa msaada wa mikono miwili zaidi. Wingi wa Makaratasi ya Vikao vya Kamati hiyo ya Utawala yalikuwa mengi mno kiasi kwamba lazima yangemwelemea Katibu wangu wa upande wa Biashara. Aliponiteua kuingia kwenye Baraza la Utawala, Gavana alikuwa na matumaini kwamba ningalikubali kutetea masuala ya Biashara; lakini badala yake nikachagua kusimamia Kilimo. Mjumbe wa Baraza la Utawala hakuwa na nafasi kubwa ya kuboresha masharti na mazingira ya Biashara ndani ya Jumuiya ya Madola; lakini mengi yaliweza kufanyika kuboresha Kilimo ndani ya Tanganyika. Lakini ni muhimu kuzingatia funzo lililopatikana baada ya ule Mradi wa Karanga, mfano pekee wa mtaji mkubwa uliotolewa na Serikali ya Uingereza katika historia yake ya Ukoloni nchini Tanganyika. Hata hivyo, miezi michache tu baada ya kuanzishwa kwake mwanzoni mwa miaka ya 1950, karanga likawa jina baya lililoambatishwa na uzembe; na mwelekeo huo unadumu mpaka leo. Waziri wa Chakula wa Uingereza baada ya Vita, John Strachey, Mb., ndiye hasa aliyekuwa mtetezi mkubwa wa Mradi ule; lakini watekelezaji wenyewe walikuwa Wawakilishi wa Kampuni ya Uniliver, ambayo kushindwa kwake kutarajia mengi ya matatizo yaliyouandama Mradi tangu mwanzo ndiko kulikosababisha wengine wote kulaumiwa, kama siyo kulaaniwa. Kwanza ubora wa mazingira na ardhi kwa ajili ya Kilimo katika maeneo mapya ya Kusini-Mashariki ya Tanganyika hayakuwa yamechunguzwa kwa ukamilifu.

Page 72: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

72

Zaidi ya hayo, yalikuwako matatizo makubwa ya mawasiliano yaliyokuwa yanatakiwa kuyatoa mazao kutoka shamba na kuyafikisha kwenye masoko. Ikabidi ijengwe reli mpya kutoka huko vijijini hadi Bandarini Mtwara, iliyopata mara moja jina la “Reli ya Karanga” , kwa gharama kubwa mno. Kisha ilibidi mji wenyewe wa Mtwara ujengwe upya, Wahuni wa mjini wakaupa mji huo jina la utani la Stracheyville, kwa kumbukumbu ya Waziri wa Chakula wa Uingereza aliyekwishatajwa. Lakini, pamoja na gharama mpya yote hiyo, mapato madogo yaliyotoka katika hayo mashamba mapya wakati wote yalikuwa yakikabiliwa na vitimbi vikubwa vya wafanyabiashara wa karanga wenyeji waliokuwa na shauku la kulinda hisa zao za soko. Kama Unilver ndio waliotengeneza jeneza la kuzikia Mradi ule wa Karanga, basi Mfanyabiashara wa Kihindi aliye mwenyeji ndiye aliyelipigilia misumari ya mwisho. Lakini kabla sijaanza kuyakabili matatizo hayo mengi yaliyoko katika kilimo, nikajikuta nimerundikiwa majukumu mengine. La kwanza, na pengine ndilo lililokuwa gumu kuliko yote, lilikuwa kuchaguliwa kwangu kuingia kwenye Kamati ya Kupunguza Adhabu ya Wauaji. Katibu Mkuu wa Serikali, John Fletcher Cooke, Mtumishi wa Serikali aliyekuwa muhimu kuliko wote katika Tanganyika ya Mkoloni, ndiye aliyenikabili mwanzo, akitaka ruksa yangu kutumika kwenye Kamati hii ya watu wanne. Nikavuta muda, nikichelea kabisa kuhusika na kazi ya namna hiyo. Lakini kwa vile, kulinganisha na wengine, nilikuwa mgeni kabisa katika Baraza la Utawala, sikuwa na nafasi ya kubisha nilipoletewa ombi hilo mara ya pili. Katika kipindi kifupi cha miaka minne nilihama kutoka kudhibiti filam kwa niaba ya Serikali, na kufikia nafasi ya kufikiria upya Hukumu za Kifo. Nilikabili kazi hiyo nikiwa na wasiwasi kidogo. Hawakukosea. Majukumu ya Kamati yalikuwa kumshauri Gavana juu ya kila Hukumu ya kifo iliyotolewa na Mahakama. Mapendekezo yetu yalitolewa kutokana na Taarifa nne tofauti: toka kwa Kamishna wa Magereza, Afisa Ushauri wa Jamii, kutoka Mahakamani (pamoja na kumbukumbu za Kesi katika ngazi zote mpaka Mahakama ya Rufaa), na kutoka kwa Kiongozi wa Dini aliyeruhusiwa na

Page 73: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

73

Mahakama kumtembelea katika chumba chake cha kungojea kunyongwa. Zaidi sana kesi hizo zilihusu mauaji yaliyofanywa katika mazingira ya uchawi, ambapo mara nyingi ilikuwa vigumu kubainisha kile hasa kilichotokea, na kwa nini. Kwa hiyo tulitafakari kwa undani kabisa yale yote yaliyotokea na kuandikwa katika yale mabuku manne, tukijitahidi sana kupata msimamo mmoja ambao wote sisi tungeweza kuutetea, na msimamo huo ndio uliokuwa msingi wa mapendekezo yetu kwa Gavana. Mapendekezo yenyewe, yaliyopatikana mwisho wa taratibu hizo, yalikuwa rahisi na ya wazi; mtu anyongwe, au afungwe maisha. Matatizo yalitokea tu pale ambapo Gavana hakukubaliana na ushauri wetu, hapo alilazimika kupeleka London Taarifa yetu na mawazo yake yasiyoafiki: pamoja na ushahidi. Jambo moja linalolingana katika utaratibu wa Sheria, kati ya kazi yangu ya awali ya kudhibiti filam na hii mpya ni kukosekana kwa nafasi ya kutosha katika maamuzi. Kama ambavyo, katika kudhibiti filam, watengenezaji wa filam na Serikali za nje zilikwisha tuwekea msimamo, ndivyo ilivyokuwa katika taratibu za Sheria nchini Tanganyika kabla ya Uhuru. Nilitambua tangu mwanzo matarajio ya Watawala kwamba Kamati yetu ingeridhia Hukumu nyingi za kifo, kama si zote, zilizokuwa zinatolewa na Mahakama. Dhahiri kuwako katika Kamati Mwanasheria Mkuu wa Serikali, John Cole, kama mwanachama kamili, kuliimarisha lengo hilo; na mara nikatambua kuwa ingalituwia vigumu kuwapinga Wanasheria waliokuwa na imani na Taratibu zao wenyewe za kupima utekelezaji wa Sheria. Kwa hiyo muda wangu uliotumika katika Kamati hii ulinisononesha zaidi kuliko ilivyopata kuwa nilipokuwa katika nafasi nyingine yoyote niliyoshika kuhudumia Umma. Faraja ndogo tu niliyoipata katika Kipindi changu cha miaka miwili ni kule kuamini kwangu kuwa nilifanya kila nililoweza kuhakikisha kwamba hakuna uamuzi wa kuridhia mtu kunyongwa uliopitishwa kwa wepesi-wepesi, na kwamba tulifanikiwa mara nyingi zaidi, kuliko Serikali ilivyotarajia, kupendekeza kubadili Hukumu ya kifo kuwa kifungo cha maisha.

Page 74: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

74

Kazi nyingine mbili nilizopewa nilipokuwa Mjumbe wa Mabaraza mawili: la Kutunga Sheria na la Utawala. Niliteuliwa Mkaguzi na kupewa jukumu la kuchunguza hali ya Magereza Tanganyika nzima, na vile vile nikawa Mjumbe wa Baraza la ushauri la Jimbo la Mashariki, Mwenyekiti wake akiwa PC, lililokuwa linakutana Morogoro mara moja kwa mwezi. Katika Jukumu lile la kwanza nilifanikiwa kuleta mabadiliko kidogo katika mazingira ya Magereza, hasa katika taratibu mpya za kuwapa wafungwa mafunzo ya ufundi, (Kabla ya hapo wafungwa walikuwa wanatumikishwa kazi za hurubu tu zisizohitaji utaalam wo wote), na kupanuliwa kwa mashamba kadha ya Magereza. Katika hili la pili, nilihusika katika kusaidia kuharakisha ujenzi wa barabara mpya, hasa katika maeneo ya Vijijini. Kufika mwaka 1959 majukumu yangu yakawa yameongezeka mno. Pamoja na wajibu wangu rasmi katika Baraza la Kutunga Sheria, na Baraza la Utawala, nilikuwa nimejiongezea kazi nyingi zaidi za kila siku katika kuendesha shughuli za Chande Industries. Wakati huo Baba yangu alikuwa anashughulikia zaidi masuala ya mwelekeo, akinielekeza katika yale yaliyokuwa mazito zaidi, wakati yeye anadhibiti mitandao yetu Mikoani. Afya yake ikaanza kudidimia, siyo kama ilivyokuwa zamani; lakini kwa kufanya kazi pamoja, tukishirikiana na Baba mdogo, tukawa tunaneemeka katika biashara, na tunabarikiwa katika familia. Sikuwa hata na fununu kuwa, wakati ule, Baba yangu alikuwa mgonjwa sana; lakini ghafla akawa mahututi! Uchunguzi wa mwanzo, uliothibitishwa baadaye na Daktari Bingwa, ulionyesha kansa ya bandama, na kwamba ugonjwa ulikuwa umekwisha enea. Tukatambua kuwa hatukuwa na muda wa kusubiri; tukatafuta duniani kote Bingwa ambaye angeweza kuokoa maisha ya Baba yangu. Tukampata mmoja huko Boston, Marekani, bingwa anayetambulika dunia nzima, aliyekwisha fanikiwa kumponya Anthony Eden. Familia ikafanya mpango kumpeleka Baba yangu huko mara moja. Hatua ya kwanza ya safari yake ikatufikisha Nairobi, lengo likiwa kumpa Baba nafasi ya kupumzika kidogo katika hospitali liliyoitwa Parklands Nursing Home, kabla ya kupanda ndege kwenda Boston,

Page 75: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

75

kupitoa Roma. Lakini tulipofika kwenye huo mji mkuu wa Kenya, tukiwa tumepata hatimaye nafasi ya kufikiria zaidi baada ya juma zima la wasiwasi, kwa ushauri wa rafiki yetu Bwana Anderson, Baba yangu akabadili mawazo yake akaamua kwamba asingetoka tena kwenda Boston kwa matibabu. Alikuwa anajua fika jinsi ugonjwa ulivyokuwa umekwisha kumwenea; na hakupenda kabisa kubahatisha, asije akafa akiwa peke yake huko Marekani. Kwa hiyo akaamua kujirudia Dar es Salaam, kwenye familia yake. Baada ya hapo mwisho ukamfikia haraka. Aliweza kuona katika siku zake za mwisho akizungukwa na wale aliowapenda, akifarijiwa na rafiki zake wengi wa karibu. Wawakilishi wa Wafanyabiashara na wa Serikali, pamoja na Katibu Mkuu wa Serikali, walifika kumwona mara ya mwisho; na alikufa kwa amani na furaha, baada ya kuwa, katika siku zake za mwisho, karibu na mjukuu wake aliyempenda, Manish. Mwezi ule Baba aliofariki, Agosti 1959, kwa jumla ulikuwa na misukosuko mingi. Kulikuwa na vituko vilivyojirudiarudia, vilivyokuwa vinaelekeza hisia za baadhi ya Viongozi Wakuu wa TANU, kuchukia Waasia. Kwa mara nyingine sumu ya ubaguzi wa rangi ikawa inachemka katika Uwanja wa Siasa. Lakini, pamoja na hayo yote, mazishi ya Baba yangu yakawa kielelezo kingine cha kuwako nchini ushirikiano kati ya makabila yote, mataifa yote na Dini zote, hali ambayo, wakati wote, ndiyo iliyokuwa mhimili mkuu wa Jamii ya Watanganyika. Watu wa aina zote, wa Imani zote, kutoka Jamii zote, walimiminika kuja kwenye mazishi ya Baba yangu. Rambirambi zilifululiza kwa mamia kutoka kila pembe ya nchi; kutoka Wakulima aliokutana nao katika mashamba ya mpunga kule Jimbo la Magharibi, mpaka Gavana wa Tanganyika mwenyewe. Katibu Mkuu wa Serikali, John Fletcher Cooke, ndiye aliyehitimisha fikira za watu wengi katika barua aliyoniletea baadaye akisema, “Baba yako alijulikana sana Dar es salaam kutokana na haiba na utu wake, na kwa michango mingi aliyoitoa kuinua maisha ya watu Jijini. Najua kwamba watu wengi wanahuzunika sana kwa kifo chake, siyo tu wale wa familia na

Page 76: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

76

jamii yake, bali pia marafiki zake wengi aliowajua miongozi mwa aina zote za watu Tanganyika nzima. Keshavji alikuja Tanganyika miaka yote hiyo ya nyuma ili kukomboa Jina na Mali za Familia. Alifanya hivyo, lakini kisha akaendelea kufanya mengi zaidi. Ucha-Mungu wake, Busara zake, Maadili yake, na huruma zake nyingi zitaendelea kudumu katika mioyo ya wengi, na kwa miaka mingi; na sifa hizo ndizo zitakazoendelea kuwa dira yangu.

Page 77: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

77

NNE

NDOA NA JAYLI WA AJABU Kifo cha Baba kilikuwa pigo kubwa. Uhusiano wetu ulikuwa wa aina ambayo vijana wa leo, hata wale waliolelewa katika desturi za Lohana, wasingeweza kuuelewa. Upendo wangu kwa Mama yangu ulikuwa huru, usiokuwa na masharti. Kwa Baba dhahiri, hisia tulizokuwa nazo kati yetu hazikuwa na nguvu ile ile; lakini uhusiano kati yetu ulijengeka kutokana na vitu vilivyokuwa zaidi ya hisia, ulioimarishwa na mila, maadili, zaidi ya yote, kuzingatiwa kwa wajibu, kila mmoja kwa mwenzake, ulomfunga katika mila zetu, Baba na mwanawe wa kwanza. Kwa hiyo uhusiano huo hatimaye ulipokatika ukubwa wa hasara niliyoipata ukaingia katika moyo wa utu wangu. Kama nisingekuwa na mke niliyempenda sana, na mwana wangu mwenyewe wa kwanza, mdogo bado, kifo cha Baba yangu kingaliniachia pengo maishani mwangu, ambalo ingalikuwa vigumu sana kulijaza. Kisha kama ilivyonitokea mara nyingi maishani mwangu, upendo wa mke wangu Jayli ulinisaidia kuona matatizo yo yote katika sura yake halisi. Kufikia Agosti 1959, tulikuwa katika ndoa kwa zaidi kidogo ya miaka minne; na mwana wetu wa miaka mitatu, Manish, Mjukuu wa kwanza wa kiume katika familia ya Chande, tayari alikwisha neemesha majuma machache ya mwisho ya Baba yangu: kuwako kwake katika mazingira kulisaidia sana kupunguza makali ya lile rungu la mwisho. Sikuwa tena naishi na Baba yangu nyumbani kwake, Barabara ya Upanga, maana wakati huo tulikuwa na kwetu wenyewe, nyumba nzuri katika barabara ya Umoja wa Mataifa. Kama nilivyosema, mimi na Jayli tulikuwa katika maisha ya furaha ya ndoa kwa zaidi kidogo ya miaka minne, ingawa maisha ya kuoa yalikuwa kichwani mwangu muda mrefu sana kabla ya hapo. Miaka minane kabla ya kifo cha Baba yangu, na si muda mrefu baada ya kurudi Tanganyika haraka haraka kutoka India, wazo la mimi kuoa likaingia kwanza katika kichwa cha Baba yangu mdogo, Ratansi.

Page 78: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

78

Nasema wazo liliingia kichwani mwa Ratansi kwa sababu ndivyo alivyo Baba huyo, Kweli na mimi nilikuwa nawapenda wasichana lakini fikra zangu wakati ule kwa kweli haikuwa katika kuendeleza vizazi vya ukoo. Lakini Baba yangu mdogo, Ratansi, pamoja na kuwa mtu mwema na mcheshi, alikuwa vile vile mtu wa vitendo aliyependa taratibu, naye akawa wa kwanza katika familia kutambua, alipoinukia kutoka katika ugonjwa ulionilazimu kurudi nyumbani, kwamba mpwawe Andy amefikia umri katika maisha yake ambapo karibu atahitaji kuwa na familia yake mwenyewe. Yeye akiwa na Baba yangu, ndiye alilianzisha wazo la mimi kutakiwa kuoa toka mwaka 1951. Siku hizo mazungumzo kama hayo hayakuwa jambo la ajabu, maana ndoa za kupangwa zilikuwa ndio utaratibu, siyo kasoro, katika desturi za Kihindi. Ndugu hao wawili walitafakari kwa muda la kufanya, wakichambua mikakati mbali mbali, kabla ya kukubaliana, hatimaye, kwamba kwa kweli wakati umefika kunitafutia mke anayenifaa. Lakini kwanza wakajibebesha jukumu la kunichunguza kwa karibu mimi mwenyewe, ili kugundua kama nilikwisha jitumbukiza mahali popote maishani mwangu. Wakati ule nilikuwa na harakati nyingi sana za kijamii mjini Dar es Salaam, mara nyingi nikila chakula na kunywa na marafiki zangu, kinyume cha mapenzi ya Baba yangu; na kutoka, siku za Jumamosi na Jumapili, kwenda Zanzibar lakini katika kipindi chote hicho, sikuwa na rafiki maalum wa kike. Baadaye Baba yangu mdogo akapata habari za msichana wa Kihindi aliyekuwa anaishi Kisumu. Baba yake alikuwa anajulikana katika familia yetu, naye alikuwa mwanachama katika Jumuiya ya Lohana. Haukupita muda mrefu mawasiliano yakafaywa; na wote wawili, mimi na msichana, kila mmoja peke yake, tukaambiwa dhamiri za Baba zetu; kwamba tukutane. Lakini, wakati maandalizi yalipokuwa bado yanafanyika kwa ajili ya siku ile muhimu ya kukutana kwetu kwa mara ya kwanza, mkasa ukatokea. Wakati wa kuvuka mto uliojaa, yule msichana aliyetoka Kisumu akafagiliwa na kasi ya mafuriko, akazama. Mkasa huo ukasababisha kusitishwa kwa muda ile mipango ya familia.

Page 79: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

79

Lakini baada ya kipindi kirefu kidogo, miezi kadhaa baada ya ile ajali mbaya, Baba yangu na Baba mdogo wakajiona kuwa tayari kulirudia zoezi lile. Safari hii fikira zao zikaelekezwa Kaskazini zaidi. Kwa zaidi ya miaka thelathini Baba yangu alikuwa anaijua familia ya Madhvani waliokuwa wanaishi Jinja, Uganda. Akina Madhvani walikuwa watu wa biashara, tena biashara kubwa, wakiwa moja ya familia zilizokuwa na mafanikio makubwa nchini Uganda, kama siyo katika Afrika Mashariki nzima. Kama alivyokuwa Baba yangu, Muljibhai Madhvani alijulikana sana katika Jamii ya Lohana; na kwa kweli, zaidi ya hivyo, katika safari zake nyingi alizokuja Tanganyika, mara nyingi Muljibhai alifikia kwa Baba yangu kwenye nyumba ile ya Tabora. Baada ya muda uhusiano wao katika masuala ya biashara ukaimarika na kuwa urafiki wa dhati, uhusiano wenye upendo na kuaminiana uliodumu maisha yao yote, mpaka Baba yangu akateuliwa Wakala wa Kampuni ya Sukari ya Madhvani nchini Tanganyika. Baada ya muda na mimi pia nikapata kuwajua wachuuzi wa Madhvani, na nikajenga urafiki na mwana mkubwa wa Muljibhai, Jayant. Kama nilivyokuwa mimi, Jayant pia alitumbukia katika Baraza la Kutunga Sheria la Uganda. Si ajabu, kwa kuangalia vipaji vyao vilivyodhihirika katika biashara, mtu akasema kuwa familia ya Madhvani ni kama gurudumu la dhahabu katika biashara. Lakini kati ya akina Madhvani na akina Chande, mazungumzo yakawa yanaendelea katika kuunganisha udugu, na wakati huo huo kushirikiana katika biashara. Kwa hiyo haishangazi hata kidogo kuwa hatimaye masuala ya arusi yangu yalizungumzwa katika familia zote mbili. Kama ilivyokuwa desturi, hoja hiyo haikuanzishwa moja kwa moja na baba hao wawili, lakini ikapitia kwa mshenga. Lakini mara mambo hayo yalipowekwa bayana, Baba zetu hao wawili wakakubaliana kwa haraka kwamba niende Uganda na kuishi na familia hiyo, ili nikutane na binti wa tatu wa Muhjibhai, Jayalaxmi. Wakati huo nilikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano, na mmoja kati ya watoto watano; wakati Jayalaxmi alikuwa na miaka kumi na sita tu, na mmoja kati ya watoto kumi na wawili. Kabla sijaondoka kwenda Jinja, Baba yangu akanidokeza shabaha yenyewe ya safari

Page 80: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

80

yangu ya Uganda. Lakini jambo kubwa ni kwamba Jayalaxmi, au Jayli kama nilivyozoea kumwita, hakuambiwa! Kasoro hiyo ya kutojua yaliyokuwa yamepangwa ikafanya kitendo cha kukutana kwetu mara ya kwanza, bila ya kutia chumvi, kuwa cha kusisimua. Nilipotokea kujua, nikawa nagwaya kwa mawazo tu ya kukutana na Jayli, kiasi cha kukataa mwaliko wao wa kufikia kwenye maeneo ya shamba lao lililoko Jinja, nikaamua badala yake kufikia mjini Kampala, nilikokuwa tayari na marafiki wengi. Lakini angalau mimi nilipata nafasi ya kufahamu kile kilichokuwa kinatokea. Jayli hakuwa na fununu hizo za ndani na kwa jinsi nilivyojitokeza siku hiyo haikuwako nafasi kwake wala kwa familia yake kulitambua lengo hilo. Pengine nilizidiwa mno na shauku; au nilifadhaishwa kwa urahisi na utulivu wake uliojidhihirisha kwangu mara moja katika matukio mengi madogo madogo; lakini labda lililonibabaisha sana, kwa bahati mbaya, ni kuendesha gari lake mwenyewe katika umri mdogo kama ule. Labda nilishangazwa zaidi na ukubwa wa shamba la miwa la Kakira, lenye eneo la eka elfu ishirini katikati ya himaya ya biashara ya Madhvani. Kwa sababu yoyote ile jua lilichomoza na kuzama bila jambo lolote kubwa kujulikana. Wazazi wa Jayli hawakuweza kutambua niliyokuwa nayawaza juu ya Binti yao Jayli wala, lazima niseme, mimi mwenyewe sikuweza kuwa na hakika na mafanikio ya posa hiyo, ingawa niliridhika kwa haraka kuwa Jayli alikuwa binti mzuri mno. Kuhusu Jayli mwenyewe, nilikuwa na mashaka kama nilitokea kumfurahisha sana siku hiyo. Kwa kweli najua kuwa sikumfurahisha. Lakini, baada ya yote hayo, niliporudi Dar es Salaam nilianza kwa haraka kushabikia wazo la kumwoa Jayli. Mawazo yangu ya kwanza yaliyovizwa kwa namna fulani na matukio ya siku ile kule Jinja mara yakatulizwa na hali ya matumaini ya ndoa. Baba yangu mdogo, bila kutaharuki kwa taarifa za kutatanisha zilizokuwa zinamfikia kutoka katika familia ya Madhvani, mara akachipusha ari yake katika kutetea Muungano huo kati ya familia hizi mbili maarufu katika biashara; na mimi, kama kawaida, nikausikiliza ushauri wake kwa makini.

Page 81: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

81

Lakini ni baada ya kujitumbukiza kwa akina Ridley, marafiki wa Kiingereza wa familia zote mbili, ndipo hatimaye niliposaidiwa kuamua. Robert Ridley alikuwa ndiye mkuu wa Standard Bank of South Africa Limited katika Afrika Mashariki, na kwa nafasi hiyo alikuwa Meneja wa Benki na msiri aliyeaminika katika familia zote mbili za Chande na Madhvani. Mkewe, Mary, alikuwa vile vile rafiki mkubwa wa wote; na hao, mke na mume wakachanganya jitihada zao katika kukamilisha ndoa hiyo, kutokana na kutufahamu kwao vizuri mimi na Jayli. Hatua hiyo ikaondoa mashaka yoyote niliyokuwa nayo huko nyuma. Kwa msingi huo mimi na Jayli tukafunga uchumba rasmi Machi 28, 1953. Baada ya hapo familia zetu mbili zikaanza kufikiria tarehe na mipango ya arusi yetu. Lakini kabla hawajafika mbali sana taarifa ya wasiwasi ikaja kutoka Uganda kuwa uchunguzi wa daktari umegundua kuwa mamaye Jayli ana ugonjwa wa kansa. Kwa kuwa madaktari wa huko hawakuwa na uwezo wa kuzuia ugonjwa kuenea, mgonjwa akapelekwa kwenye hospitali moja mjini New York ambako, kwa bahati mbaya, mabingwa walithibitisha kuwa ugonjwa umefikia kiwango ambacho kinge mwezesha kuendelea kuishi kwa kiasi cha majuma mawili tu. Kwa hiyo akafariki huko, akiwa na familia yake. Tatizo hilo kubwa likavuruga mipango yote ya arusi kwa miezi kumi na miwili iliyofuata ya msiba rasmi katika familia, mpaka nusu ya pili ya mwaka 1954, pande hizo mbili zilipoanza kuweka mipango upya. Lakini, kwa mara nyingine, msiba mwingine wa familia ukasitisha mipango hiyo. Safari hii ulikua msiba wa upande wangu: kifo cha binamu yangu nchini Kongo kilichosababisha familia yangu kuingia kwenye taratibu rasmi za msiba kwa miezi sita mingine. Hatimaye, kufika mwanzoni mwa mwaka 1955, mimi na Jayli tukawa huru kuanza upya mipango yetu. Kwa bahati mbaya kipindi kirefu cha uchumba wetu kimekuwa cha huzuni kubwa, hasa kwa Jayli; lakini sisi wenyewe tukawa na mawasiliano katika miezi mingi yote hiyo, tukidumu katika azma yetu ya kuoana iliyokwisha sitishwa mara mbili. Lakini pengine marafiki zetu hawakuwa na

Page 82: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

82

matumaini makubwa juu ya mipango yetu, wakanitania kuwa arusi na Jayli ilikuwa ndoto zaidi kuliko ndoa, inayosonga mbele zaidi na zaidi kila mara tulivyokuwa tunaikaribia. Wengine walitamka hadharani wakishangaa, naamini kwa masihara, kuwa hatimaye familia ya Madhvani iligundua mifupa iliyokuwa imefichwa chumbani kwangu, na wasiwasi ukawa unawasukuma kufikiria upya. Kwa bahati nzuri, hatimaye kejeli zetu hizo zikayeyuka pale ilipotajwa tarehe 5 Mei, 1955 kuwa ndiyo siku ya arusi yetu kule Uganda. Waalikwa katika arusi hiyo walifika kwenye shamba la Madhvani, karibu na Jinja, kutoka maeneo mbali mbali, wakisafiri kwa ndege, kwa magari na hata kwa miguu. Baba yangu alikodi ndege ya aina ya DC-3, iliyokuwa na uwezo wa kubeba abiria ishirini na wanane, kutoka Shirika la Ndege la Afrika Mashariki; na familia yetu ikaruka na ndege hiyo kutoka Dar es Salaam mpaka kwenye Kiwanja kidogo cha Jinja. Kutoka hapo tulisafiri kwa magari yaliyoletwa na familia ya Madhvani kiasi cha kilometa kumi na nne kufika kwenye shamba lao. Nina kumbukumbu ndogo sana kuhusu safari zote mbili, kutokana na furaha iliyokuwa inabubujika kutoka katika mioyo ya wale wa familia yangu niliofuatana nao. Ninaloweza kukumbuka tu la siku ile ni umahiri wa mipango ya kupokelewa kwetu iliyoandaliwa kwenye Kiwanja cha Ndege cha Jinja; uhakika kama wa Kijeshi tulipokuwa tunasindikizwa mpaka kwenye magari yaliyokuwa yanangoja, magari ambayo yaliondoka kwa msururu mpaka kufika kwenye shamba la Madhvani: ashirio, kama ilivyotokea, ya mambo ya mbele; au utangulizi wa sherehe ya arusi ambayo mipango yake yote haikubadilika, ambapo kila tukio lililopangwa na kutekelezwa kwa uangalifu sana. Labda ufanisi ulioonekana katika kutekeleza vizuri kila kilichopangwa wakati wa kupokelewa kwetu ndio ulionisukuma kufanya maandalizi yangu na mimi mwenyewe. Labda ni vigumu kwa watu wa Imani kama yetu kuelewa urefu, wakati mwingine unaochosha, wa arusi za wa-Hindu. Uzoefu wangu mimi mwenyewe, hasa kutokana na arusi za dada zangu, umenikumbusha shida na furaha zinazoonekana katika sherehe zinazoendelea kwa

Page 83: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

83

siku tatu nzima, mchana na usiku. Lililonisumbua zaidi katika sherehe ile lilikuwa pale Maarusi walipolazimika kukaa wametulia kwa saa nzima juu ya vigoda vidogo sana mbele ya moto mwingi unaowaka. Kwa kuwa niliona jinsi dada yangu mkubwa na mumewe walivyohangaika ili kufanikiwa sehemu hii ya sherehe, nilitumia nafasi ya kwanza niliyopata kuzungumza na Imam wa Dini ya Kihindu, Bwana Keshavial Monji Joshi, aliyepangwa kuendesha ibada ile ya arusi yetu, kama angeweza kutafuta namna ya kuharakisha sehemu ile ya sherehe, nikisisitiza kuwa nilikuwa na hakika ya watu wengi wa familia zote mbili wangeweza, hatimaye, kutafuta namna ya kumshukuru. Lazima nikiri kuwa nilitiwa moyo sana na Imam yule baada ya kudhihirisha kwake kulielewa tatizo hilo, lakini sikufurahiwa sana na yale aliyoyafanya baada ya hapo. Haraka akamwendea Kaka mkubwa wa Jayli anayeitwa Jayant, na kumweleza kwa undani kile tulichokizungumza. Kama Jayant alivyonieleza baadaye, hoja aliyoizungumza Imam ni kwamba, eti, “shemeji yako mtarajiwa anatafuta njia za mkato.” Sina haja ya kueleza kuwa sikutumia “njia za mkato” siku ile; na kwa nasibu, shemeji yangu ninayemwamini, Jayant, alikwisha ridhika na mapendekezo yangu ya kubadili kidogo sherehe ile, bila kusema lolote zaidi. Arusi yenyewe ilikuwa na msisimko mkubwa, inayolingana na kishindo cha kuungana kwa watu wa familia mbili za Wahindi mashuhuri kabisa katika Afrika Mashariki. Watu wazito kabisa wa Uganda walialikwa na wakahudhuria. Ingawa Bwana Gavana mwenyewe hakuweza kufika, lakini alileta salaam za pongezi, kama vile vile alivyofanya Katibu Mkuu wa Serikali; lakini PC wa Jimbo la Mashariki alifika. Sherehe ilifanyika katika Bwalo Kuu la Shamba la Madhvani lililokuwa limepambwa kifahari kwa hariri na maua, na vibweka vingine vya kila rangi. Kule nje ya Bwalo, kulikoendeshwa sherehe yenyewe ya arusi, sehemu ambayo nadhani iliachwa kwa ajili ya kuegeshea gari, nayo ilipambwa vivyo hivyo kwa magudulia ya shaba na fedha yaliyokuwa na kila urembo katika kila pembe. Jayli

Page 84: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

84

mwenyewe alikuwa anameremeta wakati wote, akiwa amevaa sari za kifahari zilizopambwa, wakati Wageni waalikwa, Wanafamilia na marafiki zao, nao walikuwa wanapendeza. Katika tukio lililo tofauti na mila, Jayli alikabidhiwa arusini na Kaka zake wakubwa wawili, waliomdai Baba yao awape heshima hiyo. Jambo lingine la kushangaza lilionekana katika Hotuba ya Shukrani iliyotolewa kwa mbwembwe na dada yangu mdogo Vijya Tanna, kwa niaba ya familia yangu. Nasema ilikuwa ya kushangaza kwa sababu sijui kama alikuwako yeyote kati yetu aliyetarajia kuwa dada angeweza kusema hadharani vizuri namna ile, bila maandishi wala kunong’onezwa. Wakati huo marafiki zangu waliokuja Jinja kutoka Dar es Salaam kupitia Nairobi na Kampala, wote walifurahi sana, ingawa nilipata hisia kwamba walivutiwa zaidi na mazingira na nafasi waliyoipata kuona nchi, kuliko chochote kile kilichokuwa kinatokea katika arusi yenyewe. Zawadi zilitolewa kwa wingi mno; nyingi sana katika hizo, kama zilivyo zawadi za arusi duniani kote, zimenipotea katika mawazo ya kichwa changu. Moja tu: saa ya dhahabu ya aina ya Favre Leuba, na mkanda wake wa dhahabu, niliyopewa na familia ya mke wangu, ndiyo niliyonayo moyoni mwangu na mkononi mwangu tangu siku ile. Saa ile ya Kiswiss yenye umaarufu wa hali ya juu sana, tangu siku ile niliyoipewa, haijapata kufunguliwa wala kusafishwa; ingawa mara nyingi nimeuliza, bila mafanikio uwezekano wake angalau kusafishwa. Hata sasa hivi naivaa kila siku, ingawa kioo kimefifia kwa ukungu, na maandishi yanafifia kutokana na uzee; na mkanda wake asilia, wa dhahabu, umekwisha yeyushwa na kusanwa vifungo vya shati. Ninapokwenda nchi za nje tu ndipo ninapoivua saa ile ninayoipenda na kuiweka kabatini, na kuvaa badala yake saa inayofaa zaidi, yenye funguo mbili, ambayo wakwe zangu waliungana kuninunulia, saa isiyokuwa na ugumu katika kuitumia, toka siku zile kabla ya simu za kukoroga, ambapo simu zililazimika kuombwa saa za mchana hotelini kwangu kutoka sehemu moja ya dunia ili ijibiwe baadaye usiku, tena pengine usiku wa manane mjini London, Ukiacha saa ile ya mkono, bado tunatumia baadhi ya vikombe vya chai tulivyozawadiwa na akina Ridley, na saa ya ukutani tuliyopewa

Page 85: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

85

na wafanyakazi wetu, ambayo bado inapendezesha chumba chetu cha kulia. Lakini tukirudia masuala ya arusi yetu kule Jinja; hatimaye, baada ya kuahirishwa mara mbili, mimi na Jayli tukawa tumeoana, katika sherehe iliyofana na iliyojaa furaha kubwa. Kwa hiyo wakati ukafika tulipolazimika kufanya safari ya kurudi Dar es Salaam. Baba yangu mdogo akapanga utaratibu wa safari kwa uangalifu uliolingana na ule wa Madhvani, akidhamiria kufanya safari ya kurudi kama utalii zaidi kuliko safari. Badala ya kurudi moja kwa moja hadi Dar es Salaam, ndege yetu ya DC-3 tuliyokodi safari hii ilipangwa kupitia Kisumu, Nairobi na Mombasa, tukisimama katika kila Kituo kuwapa nafasi wenzetu katika familia na marafiki, ambao hawakupata nafasi kwenda Jinja, kukutana nasi wote, wakati bado tumepambwa na mavazi yetu ya arusi. Lakini wakati ndege ilipofika Nairobi, mpango ule wa Baba yangu mdogo ukawa umevurugika, pale Meneja wa Shirika la Ndege la Afrika Mashariki alipokataa kuutambua Mkataba wa kukodi ndege mara baada ya kutua uwanja wa Nairobi, ndugu na marafiki wakiwa tayari wamekusanyika karibu na ndege, tukaambiwa kwamba tulipaswa kupunguza baadhi ya wasindikizaji wa arusi, ili kutoa nafasi kwa abiria wengine, ambao hawakupata nafasi katika ndege nyingine ya kawaida. Hakuna haja ya kueleza kuwa hawakuwako hao wa ziada, na hapo tukalazimika wote kusimama ili kujitambulisha. Hatimaye, baada ya kucheleweshwa kwa saa kadha, wenye ndege wakatulia, na sisi tukaruhusiwa kuendelea na safari yetu. Lakini kwa kuwa, mpaka wakati huo, ratiba yetu ilikuwa imevurugika vibaya, na giza likawa linaanza kuingia, hatua ya mwisho ya kuelekea Mombasa ilibidi irukwe. Tukaenda moja kwa moja mpaka Dar es Salaam, na hivyo kuwakera wale wote waliokuwa wanatungoja kwa saa nyingi ili kutuona hawakuweza kutuona! Laiti Meneja wa Shirika la Ndege la Afrika Mashariki angalitambua kuwa alikuwamo katika ndege hiyo mtu aliyekuwa na tabia na

Page 86: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

86

hadhi kama ya Baba yangu mdogo Ratansi, angalifikiria mara mbili au mara tatu kabla hajatuchezea sisi siku ile. Mara tulipofika Dar es Salaam, Baba yangu mdogo akafungua Madai Mahakamani dhidi ya Shirika la Ndege kutokana na kuvunja Mkataba. Mahakama ya Dar es Salaam ikayaridhia madai hayo ya Baba yangu mdogo, na akalipwa gharama zake pamoja na fidia. Kufikia hapo Shirika la Ndege la Afrika Mashariki likaona kwamba hukumu ya Mahakama iliyompa haki Baba yangu mdogo ingetoa mwelekeo mbaya ambao ungaliligharimu sana Shirika katika siku za mbele. Maneja wake akakata rufaa mpaka kwenye Privy Council ya London: na huko akashindwa pia. Kwa hiyo ikatokea kwamba, kwa kosa la kutoa tikiti zaidi ya kiasi kinachotakiwa kulingana na viti vya ndege; uvumilivu wa Baba yangu mdogo Ratansi, na ndoa yangu na Jayli kule Uganda mwezi Mei 1955, ikawa sehemu ya Taarifa rasmi za Privy Council. Kurejea kwetu Dar es Salaam kukakumbwa na mambo yaliyokuwa zaidi ya mashitaka ya Mahakama. Baba yangu alipanga awamu nyingine ya tafrija ya fahari, ambapo Waheshimiwa wa Jijini, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Serikali, Bwana Rex Surridge, walihudhuria kikamilifu. Kisha, wakati Baba yangu mdogo anaelekeza mawazo yake kwa Wanasheria wa Dar es Salaam, mimi na Jayli tukaamua kuendelea na safari zetu za arusi. Kituo chetu cha kwanza kikawa Mbuga ya Wanyama ya Malkia Elizabeth iliyoko Uganda. Baada ya siku chache za kuangalia wanyama huko, tukahamia Rwanda, Burundi na Kongo ya Wabiligiji tukatumia huko sehemu iliyotufurahisha mno ya majuma mawili kuvinjari katika nchi ile ya ajabu lakini yenye vurugu nyingi. Wakati ule mawasiliano na sehemu ile ya dunia hayakuwa yanalingana na yale ya Dar es Salaam, na hivyo kukosekana kwa salaam zetu zozote kwenda kwenye shamba la Madhvani kule Jinja kukaibua wasiwasi kwao juu ya usalama wetu. Hatimaye Babaye Jayli akawasiliana na Baba yangu, kutaka kujua kama alikuwa na habari zozote juu yetu. Baada ya mapumziko yetu katika misitu na milima ile kumalizika, tuliibuka bila kudhurika kutoka katika ule msitu wa giza tukiwa tumeusahau kabisa wasiwasi

Page 87: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

87

wote tuliokuwa tumeusababisha sisi tukajirudia Dar es Salaam na kufikia kwenye nyumba ya Baba yangu, Barabara ya Upanga. Nyumba ile iliyokuwa katika eneo zuri karibu na Upanga Sports Club, na karibu sana na makaburi ya Jumuiya ya Madola yaliyokuwa yanatunzwa sana, kwangu mimi ilikuwa mahali pazuri pa kuishi. Lakini hapakuwa pazuri namna hiyo kwa watu ambao ndio kwanza wanaoana; na, pamoja na Baba yangu kutukaribisha tukae mle, hatukukaa Upanga kwa muda mrefu. Miezi kadha kabla ya arusi yetu nilikuwa nimepata nyumba katika Barabara ya Umoja wa Mataifa, karibu zaidi na katikati ya mji, na hayakupita majuma mengi kabla ya kupafanya mahali hapo kuwa nyumbani kwetu wenyewe. Katika Barabara hiyo ya Umoja wa Mataifa ndipo nilipobaini, mnamo miezi michache ya ndoa yetu, kwa nini akina Ridley walimsifia mno Jayli kuwa angefaa kuwa mke wangu. Familia yake ilikuwa mbali, kilometa nyingi katika nchi nyingine, wakati huo akiwa na umri mdogo wa miaka kumi na minane tu, asiyejua vema mambo ya dunia; amelelewa katika maisha ya raha, kama si ya anasa, akihudumiwa na watu wakati wote. Lakini bado akayakubali maisha mapya mjini Dar es Salaam kwa ari inayotia moyo, bila dalili wala nong’ono za malalamiko. Kwa haraka akazishika barabara hatamu za kuendesha maisha yetu, akitokea kuwa mpishi hodari sana, mchangamfu nyumbani, na mwenzi mwenye bongo zuri alilolidhihirisha tangu siku za mwanzo. Vile vile alikuwa na busara ya kufikiria neno la kuniambia ili kuniweka sawa, wakati wa raha na wakati wa matatizo. Kabla haujapita muda mrefu, akawa na mahusiano mazuri sana na mama yangu wa kambo, na halafu na dada yangu wa Dar es Salaam na mdogo wangu wa mwisho pia; wala haukupita muda kabla hajazifuta kasoro zangu za kuwa na mawasiliano na ndugu zangu walio wengi. Kwa kifupi nilitambua haraka jinsi nilivyokuwa na bahati ya kumwoa. Furaha yetu ilikamilika pale Jayli alipokuwa mjamzito, na kumzaa kule Kampala mtoto wa kiume mwenye afya tuliyempa jina la Manish. Usiku wa Februari 3, 1956, siku moja kabla ya kuzaa

Page 88: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

88

mtoto, Jayli alikaa muda mrefu na rafiki zake, akicheza karata kama kawaida yake, hali iliyowashawishi wenzake kuamini kuwa alikuwa amekaribia kumleta duniani mcheza-karata mzoefu. Kwa jinsi ilivyotokea, walikosea; ingawa Jayli mwenyewe hakupoteza hamu ya kucheza karata. Mara mama na mtoto walipoonekana kuwa na uwezo wa kusafiri, safari ya kurudi kwao Dar es Salaam kukawa kipindi cha sherehe kubwa kwangu mimi na kwa Baba yangu, maana hatimaye ametunikiwa mjukuu wake wa kwanza mwanamume, mwenye thamani kubwa katika Jamii yetu. Matukio hayo yaliashiria kuanzishwa kwa Kipindi cha Bahati, kwangu mimi, kwa Jayli na, kwa kweli, kwa familia yangu yote. Na, ingawa kifo cha Baba yangu, tarehe 19 April, 1959, kilifuta ghafla kipindi hicho, baada ya muda Kipindi Kipya kikafuata na hiki kipya kikawa kizuri vile vile.

Page 89: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

89

TANO

UHURU WA TANZANIA Kule India nilipata ahari ya kuwapo wakati wa kuzaliwa kwa Taifa hilo sasa, mwishoni mwaka miaka ya 1950 nilikuwa naona waziwazi kuwa nilikuwa nasubiri kuona kuzaliwa kwa Taifa lingine jipya. Pamoja na kwamba maandalizi ya Wakoloni kwa ajili ya Uhuru wa Tanganyika yalikuwa duni; pamoja na kwamba Mwalimu Nyerere, Kiongozi aliyekuwa na upeo mkubwa sana katika vuguvugu la Utaifa kwa Tanganyika, alikuwa akiutabiri tangu 1957, Kwamba ungepatikana baada ya kizazi kimoja kizima. Pamoja na kwamba uchumi wa nchi ulikuwa nyuma kwa kipindi kirefu, kwa kila kitu ukitegemea utaalam, masoko na mitaji ya watawala wa Kikoloni waliokuwa wanakaribia kuondoka; ukweli wenyewe uliokuwa rahisi kueleweka ni kwamba Harold MacMillan alikwisha dhamiria kuiachia upepo wa mabadiliko uangushe pole pole kuta za ubeberu wa Kiingereza katika Afrika. Zilikuwako zinapata nyufa pole pole; na kwamba angehakikisha hayo yanatendeka, pamoja na kwamba historia imemfunza manufaa wanayopata wahusika katika mabadiliko ya haraka namna hiyo, bali gharama zake vile vile. Labda Waziri hodari wa Makoloni wa Macmillan Ian Mcleod aliuelezea kwa kifupi mwelekeo huo mpya kule Whitehall aliponiambia wakati wa ziara yake nchini Tanganyika mwaka 1950 akisema, “Kama kosa linafanyika, basi afadhali lifanyike wakati mambo yanasonga mbele” Na Serikali ya Kiingereza ilidhamiria kabisa mambo yasonge mbele. Hatua ya kwanza ya zoezi hili ilikuwa Uchaguzi wa kwanza kabisa wa kidemokrasia uliofanyika Tanganyika. Gavana Richard Turnbull alipotangaza kwamba Awamu ya kwanza ya uchaguzi huo imepangwa kufanyika mwaka 1958, sehemu kubwa sana ya Wanachama wa Vyama vya Kizalendo vya Kiafrika walizipokea habari hizo kwa wasiwasi, si kwa sababu hawakutaka kujitawala; kwanza wazo la Uhuru lilikuwa linachemka katika damu yao kwa

Page 90: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

90

muda mrefu. Ukweli ni kwamba hawakuweza kuyaamini malengo yaliyokuwa yakitangazwa na Dola ya Wakoloni. Vibwagizo hivyo vinadhihirisha mfarakano uliokuwapo kati ya Wananchi na Watawala wao wa Kikoloni. Ingawa walikuwako miongoni mwa Watawala hao Watumishi wa Serikali waliokuwa wanamapinduzi na wafanyakazi hodari, mara moja moja walitokea baadhi wasiotaka maendeleo hayo, mwelekeo wao ukiwa kuulea Ukoloni. Siku moja nilimsikia kijana akighani shairi lifuatalo wakati wa shughuli moja mjini Arusha, ambako Walowezi walikuwa na kauli kubwa .

Joto halipungui katika nchi basi Muda kumwagika miguuni kirahisi Kunguru mgonjwa anaporuka kwa kasi Katika nchi ya Bado Kidogo. Shauri limeanza wako wapi waume Meza imeandaliwa kalamu tuitume Safari imewadia haiendeki kamwe Katika nchi ya Bado Kidogo. Lakini nifundishe zaidi kuamini Ongezeko la kasi faida yake nini Kuyajali yote hayo kwanza mimi ni nani Katika nchi ya Bado Kidogo,. Yafaa nini kwa mtu haraka ya daima Mashaka kuyakabili na huku akitetema Muda ungaliko mwingi wala hautasimama Katika nchi ya Bado Kidogo Anayekandamizwa yakini bado mjinga Anakuwa kichekesho maisha mbele kisonga Mengine yaachilie bada ya yako kupanga Katika nchi ya Bado Kidogo Jua livyokuwa jana pia na leo sawia

Page 91: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

91

Na la kesho tachomoza muda wake kifikia Uko wapi wasiwasi neno moja fikiria Katika nchi ya Bado Kidogo Ndivyo nijuavyo nchi joto halibadiliki Muda unavyoyoyoma miguu haishikiki Na mimi ninavyoishi ni kula kulikobaki Katika nchi ya Bado Kidogo

Kwa kusaidiwa na mkalimani, kati ya wanashamba wa Kifaransa na Mkulima aliyekuwa akijipumzikia chini ya mti: Mfaransa akaanza, “Kwa nini hutafuti mbolea, ukaongeza juhudi zaidi, na kushirikiana na Wakulima wenzako? Ukifanya hivyo, baada ya muda mfupi, mazao yako yataongezeka maradufu”. Mkulima akahoji, “Yatanisaidia nini mimi hayo?” Mfaransa akajibu, “Utapata maisha bora zaidi, utapata furaha zaidi na muda mwingi zaidi wa kupumzika!” Mkulima akamalizia, “Hayo ndiyo ninayoyafaidi hivi sasa!” Ni kweli kwamba tofauti za mila na silika za watu binafsi zilichangia katika kuvuruga fikira za pande zote mbili. Lakini matatizo mazito zaidi yalishinikiza kuzuka kwa hali ya kutoaminiana kati ya mataifa ya Tanganyika., Gavana Edward Twining, wakati huo ndiyo kwanza ameondoka, alikwisha fanya mengi yaliyovuruga uhusiano kati ya TANU na Utawala wa Kikoloni, wakati mwezi Mei, 1951 katika jeuri yake ya kawaida, alipokitangaza chama hicho cha Wanamapinduzi wa Kiafrika kuwa na Ubaguzi wa Rangi! Alikuwa ametoa hoja kuwa hatima ya viongozi wa Jadi ilikuwa inavizwa na wale waliokuwa wanajenga hoja zao kwa jazba za Uanamapinduzi unaopita kiasi, ambao kwa kweli si lolote zaidi ya ubaguzi. Kisha lilikuwako jambo ambalo si dogo, la Chama cha Siasa cha Twining Mwenyewe, UTP. Alichokiunda ili kiwe, na kwa kweli kikawa kinaifanya kazi hiyo, mpinzani wa malengo ya TANU ya muda mrefu. Maendeleo duni ya Waafrika katika Utumishi wa Serikali, na katika elimu, yakawa nongwa nyingine iliyoisukuma TANU kupoteza matumaini yake kwa uchaguzi uliokuwa umepangwa, wakipima kwa uangalifu dhamiri ya Utawala wa

Page 92: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

92

Kikoloni. Wakati Tanganyika inapata Uhuru walikuwako Waafrika weusi wachache sana waliokuwa na Shahada za Chuo Kikuu nchi nzima. Na mwisho lilikuwako tatizo la uwiano katika Vyombo vya Dola dunia nzima, Mabaraza ya Kutunga Sheria na ya Utawala, ambayo bado hayakuwapa Wanamapinduzi wa Kiafrika kauli yo yote juu ya namna ya kuziendesha nchi zao. Kwa hiyo halikuwa jambo la ajabu kwa Wanamapinduzi wengi wa Kiafrika kutokwa na imani kabisa na mafanikio ya uchaguzi. Walikuwa wamechoshwa na ahadi zisizotekelezwa za maafikiano yaliyokuwako kati yao na Utawala wa Kikoloni; na, kwa jumla, hawakutaka tena kutafuta suluhu na Waasia na Wazungu wengi waliokuwa wanaishi Tanganyika, ambao kwa makusudi walikataliwa kujiunga na TANU, mpaka kiasi cha mwaka mmoja tu kabla ya Uhuru. Katika hali hiyo, ngumu na ya hatari, ndipo umahiri wa Mwalimu Nyerere, kama Kiongozi mashuhuri wa Nchi, ulipodhihirika. Tofauti na Wanaharakati wenzake wengi wapigania Uhuru wa Afrika, Mwalimu alitambua wakati wote umuhimu wa kujenga msingi imara kadiri ilivyowezekana katika kuunga mkono Utaifa wa Tanganyika, bila kujali Sera ambazo Chama kilijipangia. Mfano mzuri wa mwelekeo huo ni pale alipokubali kuupokea msaada wa fedha kutoka katika Jamii ya Kiasia mwaka 1957 kwa ajili ya safari yake ya kwenda New York kutoa Msimamo wake katika Umoja wa Mataifa; au ushauri wa kitaalamu alioutafuta kutoka kwa Wanasheria wa Kiasia alipobambikiziwa kesi mwaka 1958. Maana, tofauti na walivyofanya Wanaharakati wenzake, Mwalimu alitambua haraka kwamba Mipango mipya ya Wakoloni kwa ajili ya Waafrika kujitawala wenyewe ingeweza kuwa kiini-macho kitakachowafungulia mlango wa kupenya Vyama tapeli kama UTP, ambavyo malengo yao kwa manufaa ya Watanganyika walio wengi yalikuwa ya mashaka. Tofauti na walivyokuwa Viongozi wengi wa Tanganyika wa wakati ule, Weusi, Wekundu na Weupe, Mwalimu akajidhihirisha mara moja kuwa mtu asiyekuwa na papara, aliyekuwa na msimamo usioyumba; akitafuta, bila kuchoka, kukomesha Ukoloni katika Afrika nzima, kwa kweli dunia nzima

Page 93: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

93

lakini, kila ilipowezekana, kwa amani bila machafuko wala kumwaga damu. Nimepata kumwona mtu kama huyo huko nyuma kule India katika miaka ya 1940, Mahatma Gandhi, aliyekuwa vile vile mtu mwenye msimamo imara, ambaye naye hakutaka kutumia mabavu kama silaha ya kufanikisha malengo ya kisiasa. Kama alivyokuwa Mwalimu, Gandhi akakazania vile vile kujenga jamii inayojiendesha kwa taratibu za sheria ambapo watu wote, wake kwa waume, wanapata haki na nafasi sawa. Yeye vile vile alilazimika kusaidia harakati za Uhuru ambazo, wakati mwingine, subira yake ya kuwavumilia ndumilakuwili wa Kikoloni, ilizaa matunda ya uwezo wake wa kuona mbali na kutoa uamuzi sahihi. Kule India nilielewa vema jinsi watu wa namna hiyo, wenye msimamo na wasiokuwa na pupa, walivyojitosa katika harakati za kutekeleza Sera zao madhubuti, lakini zisizotaka shari. Bado nakumbuka yale niliyoyasikia mjini Poona, kwamba Mahatma Gandhi aliuawa siyo kwa mikono ya Mkoloni Mwingereza, lakini na mwananchi mwenziwe wa kabila la Hindu, tena baada ya Uhuru kupatikana, kutokana na namna Chama cha Indian Congress kilivyokuwa kinawadekeza Waislamu. Lakini kama Mwalimu mwenyewe alikuwa anazitambua hatari hizo, hakutaka wasiwasi wake huo uvize uamuzi wake. Maana katika miaka hii muhimu ambapo Uhuru ulikuwa unakaribia, hali ya hatari mno ilipojidhihirisha kati ya Wakoloni na Wanamapinduzi, ndipo uhodari wa Mwalimu ulipojitokeza. Maana mtu huyu alikuwa na kipaji cha pekee, na uzoefu wa aina yake, ulioweza kuwafanya watu wa mataifa yote, wake kwa waume, siyo tu wajisikie salama kwa kuwako kwake, lakini vile vile kukubali kuyatekeleza, kichwa kichwa, maamuzi yake. Mtu ye yote aliyehudhuria Mkutano wa Mwalimu aliondoka uwanjani akiamini kuwa yeye, wala siyo Mwalimu, ndiye aliyetarajiwa kutoa mapendekezo ya maana. Kwa kuyachanganya mawazo mazuri kutoka kwa Wananchi, Mwalimu akafanikiwa kuwaelekeza wole waliokuwako kukubali kuwa walikuwa wanahusika na Mipango hiyo ya baadaye, na

Page 94: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

94

kwamba wote kwa pamoja walikuwa wanatoa mchango wao kuhusu Chama na Serikali, na kwa kweli katika mjadala mzima wa Taifa, Tanganyika nzima. Kwa njia hiyo ndivyo Mwalimu alivyoanza taratibu zake za kuwashawishi wana-TANU waliokuwa na msimamo mkali juu ya busara ya kushiriki katika Awamu ya Kwanza ya Uchaguzi uliopangwa na Gavana Richard Turnbull. Awamu hiyo ya kwanza ilipangwa kufanyika mwezi Septemba 1958; na ya pili miezi mitano baadaye, Februari 1959. Kwa mujibu wa taratibu alizoziweka Gavana, kila moja katika mataifa yetu matatu lingepata viti kumi kati ya thelathini vilivyowekwa kwa ajili ya wachaguliwa. Kwa kuwa mgawanyo huo wa viti haukushabihiana hata kidogo na uwiano wa mataifa yaliyokuwako Tanganyika (wakati ule Waasia na Wazungu, wote pamoja, walikuwa tu kati ya asilimia moja na moja u nusu ya watu wote wapatao milioni kumi) ilikuwa hapana budi suala hili la rangi kuzaa mabishano ya kwanza katika mijadala ya ndani ya TANU. Mwelekeo wa Mjadala huo ulikwisha wekwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Tangu pale Vyama vya Siasa vilipotambuliwa nchini Tanganyika miaka kadha ya nyuma, wasiwasi juu ya uwiano usiokuwa sawa katika mambo ya Uchumi na Siasa baina ya mataifa ya Tanganyika ulizaa malalamiko mazito katika Siasa za Ndani. Baadhi ya Wakereketwa wa TANU walizipinga shutuma za Twining za ubaguzi kwa kuonyesha mgawanyo usiokuwa sawa wa mali ya nchi kwa Waasia na Wazungu, wakisisitiza kuwa shida yao haikuwa katika rangi ya ngozi za watu, bali usawa katika mambo ya uchumi. Baadhi ya Viongozi wa Vyama wakafika mbali zaidi katika hoja hiyo, wakizungmzia hoja ya kuwarudisha watu walio wachache wa Jamii hizo kwenda kwao India, Pakistani na Uingereza, baada ya Uhuru kupatikana. Wengine walivuka hata hapo, wakiwalaani hadharani Wafanyabiashara wa Kiasia kuwa wanyonyaji wa Wakulima wa Kiafrika, kama kinga ya kushika kwa mabavu shughuli za biashara, kama ilivyotokea katika baadhi ya maeneo ya Usukuma, ambako Wachuuzi wa Kiasia walikuwa wanazuiwa katika masoko ya pamba.

Page 95: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

95

Katika mazingira hayo sehemu kubwa ya hasira na kukata tamaa ilieleweka kabisa. Lakini, kama Mwalimu alivyotambua waziwazi kuwa kama itashindikana kuelekeza hasira hii kwenye maslahi ya Sera, basi ungekuwako uwezekano mkubwa wa damu kumwagika bure na kupatikana kwa madhara mengine kwa muda mrefu. Kama tahariri ya gazeti la Kenya Weekly News ilivyochambua siku hiyo, pengine kwa kejeli, “Hakuna anayeamini kuwa Bwana Nyerere anawaunga mkono watu wahuni au wakaidi miongoni mwa wafuasi wake, lakini bado itabidi hatua kali zichukuliwe kama zoezi zima halitakiwi lionekane kuwa la utovu wa nidhamu na ni la hatari.” Matatizo ya Nyerere yalikuwa makubwa zaidi kutokana na taratibu zilizopangwa za uchaguzi uliokuwa unapendekezwa. Siyo tu kwamba Waafrika walio wengi wangalikosa haki ya kupiga kura, kutokana na tafsiri iliyokuwa inatakiwa na Gavana, bali Wagombea wote, bila kujali walitakiwa kushindania kura za mataifa yote; na Wapiga kura nao wakatakiwa kuwapigia kura Wagombea wa kila taifa. Hakuna hata moja ya hatua hizo iliyokuwa inalingana na taratibu za ushindani ulio sawa, pamoja na kwamba mipango iliyowekwa ilikuwa inatambua hali halisi ya uchumi katika siku zile Wazungu wa Tanganyika walipokuwa wanavuna mapato ya mwaka ya wastani wa pauni 1,560, Waasia pauni 654, na Waafrika pauni 75 tu! Wala haishangazi kwamba, katika hali hiyo, hata Mwalimu alilibeza mwanzoni wazo la kushiriki katika uchaguzi uliopangwa kwa misingi ya Utaifa. Lakini wakati mjadala huo wa ndani ulipokuwa unapoa, ghafla akabadili mawazo yake, kama alivyofanya mara nyingi alipokumbana na hoja nzito, na kuanza kutetea hoja mpya kuwa TANU haina budi kupambana katika Uchaguzi huo, hata kama mipango yake inaonekana kuwa na dosari kiasi gani. Kama alivyoeleza wakati fulani baadaye, “Chama changu kilikataa kushiriki katika Uchaguzi, wakisema, ‘Hata kama tutavichukua hivyo Viti ya Waafrika, bado tutaendelea kuandamwa na vile viti kumi vya Waasia, na kumi vya Wazungu’. Lakini mimi nikasema, ‘Msiwe Wapumbavu; msikae hapa mkiamini kuwa Waasia wote au Wazungu wote wanayapinga tunayoyatetea; wengi wao wanautaka Uhuru zaidi kuliko tunavyoutaka baadhi yetu hapa”.

Page 96: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

96

Mkutano wa Mwaka wa Wajumbe wa Chama ukajadili kwa siku nne suala hili la kushiriki katika Uchaguzi. Majadiliano yalikuwa makali wakati wote; lakini ukali haukuzidi kiasi wala hakukuzuka vurugu. Hatimaye Mwalimu akafanikiwa kuwashawishi walio wengi, “ijapokuwa wingi wao haukuwa wa kishindo (thelathini na saba kati ya sitini) kumuunga mkono. Lakini hasira za wale waliokuwa wakati wote wanadai wasishiriki katika Uchaguzi zikawa zinaendelea. Baada ya Mkutano huo, katika mabishano makali yaliyokuwa yanachochewa na wale vichwamaji waliokuwa wanaamini kuwa mawazo ya Nyerere ya kushiriki katika Uchaguzi yalikuwa yanashinikizwa na udhaifu wake, siyo Hoja, chama Kipya kikaibuka kilichokuwa kinawachukia Waasia na Wazungu. Chama hicho kipya kiliitwa African National Congress, au ANC, nacho kikamchagua mtu machachari mwenye makelele mengi, Zuberi Mtemvu, kuwa Kiongozi wake. Katika matamshi yake ya awali chama hicho kipya cha ANC kilisisitiza kwamba katika nchi yo yote ya Kiafrika, kama Tanganyika, maslahi ya Waafrika ndiyo yanayopasa kutawala, na lazima yazingatiwe kabla ya yale ya watu wa mataifa mengine., Inawezekana Mwalimu alipata dalili za ushindi ndani ya TANU; lakini sasa alikuwa katika hatari ya kuzidiwa na ANC. Matokeo ya mjadala ule wa Chama juu ya kushiriki katika Uchaguzi wa kwanza nchini Tanganyika ni moja tu kati ya mambo mengi yaliyombidi Mwalimu kuamua. Pamoja na mengine, ushindi wake katika hilo ukawa dalili ya mabadiliko kwa jinsi Wanamapinduzi walivyoufikiria Uongozi wake katika TANU kuhusu tabaka la Waasia na Wazungu nchini Tanganyika. Kabla ya hapo yalikuwako mashaka mengi ndani ya TANU, hasa kwa sababu ya hofu, chuki na kutokuelewa. Mwalimu vile vile aliongeza idadi ya hao waliokuwa na mashaka. Lakini mara taratibu zilizozaa uamuzi wa TANU zilipowekwa bayana, watu walipoanza kuelewa jinsi ulivyokuwa mgumu lakini wa kidemokrasia kabisa, mjadala wa Hoja ya Mwalimu, fikira za watu zikaanza kubadilika, tena kwa haraka. Kwa kuwa nilishiriki katika Vikao vya ndani vya Baraza la Kutunga Sheria na vya Baraza la Utawala, na kuchanganyika na

Page 97: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

97

Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki wa Kiasia na wa Kizungu, niliweza kutambua mara moja jinsi ushindi wa Mwalimu ulivyozaa mwelekeo. Wala haukuwa mwelekeo peke yake uliokuwa unabadilika. Ushindi wa Mwalimu uliweka msingi wa mabadiliko katika taratibu za kupiga kura: katika chaguzi mbili za Tanganyika wa 1958-1959, na ule uliofuata wa mwaka 1960. Katika Uchaguzi ule wa 1958-59, TANU ikaweka Wagombea katika Viti vyote vilivyokuwako, na ikavinyakua vyote, kwa kupata asilimia 67 ya kura zote zilizopigwa, baada ya Waasia na Wazungu wengi walipochagua kuhamisha kura zao na kuunga mkono Chama cha TANU. Wagombea wa Kiasia walioungwa mkono na TANU, Kama Sophia Mustafa, Mahamoud Rattansey, na rafiki mkubwa wa Mwalimu Amir Jamal, wote walishinda kwa kishindo katika majimbo yao. Kinyume chake, Wagombea wote wa UTP kilichokuwa kinaungwa mkono na Twining wakafagiliwa mbali katika Uwanja wa Siasa; wakati ANC, kwa kuwa walikataa kushiriki wakajipotezea nafasi ya kujipima nguvu. Kutokea wakati huo, na kuendelea, kasi ya mabadiliko ya Katiba ikaongezeka ghafla. Kamati ikateuliwa, chini ya uongozi wa Mhe. Richard Ramage, kuunda upya Sura za Baraza la Kutunga Sheria na Baraza la Utawala, ili kuongeza kiwango cha Uwakilishi wa Watanganyika Weusi. Gavana akaaanza kuutafuta ushauri wa Mwalimu mara nyingi zaidi juu ya mwelekeo wa baadaye katika mabadiliko ya Utawala na Siasa. Mwalimu akawateua Wajumbe Watano wa TANU kuingia katika Baraza la Utawala (lililoshabihiana na Baraza la Mawaziri) Derek Bryson, Solomon Eliufoo, Chifu Fundikira, Amir Jamal na George Kahama. Kisha Uchaguzi Mkuu ukapangwa kufanyika mwezi Agosti 1960, kwa lengo la kukabidhi Uhuru mwisho wa mwaka unaofuata. Ulipokaribia Uchaguzi huo ndipo nilipotambua jinsi TANU walivyokuwa wananihitaji. Siku moja, mchana, nikapokea ujumbe kutoka kwa Kiongozi mmoja wa TANU, Kasela-Bantu. Ujumbe wenyewe ulikuwa kwamba alipata salamu kutoka kwa Katibu Mkuu wa TANU, Oscar Kambona, kwamba yeye Kambona pamoja na Mwalimu walikuwa wananitarajia kutamka hadharani kuwa naunga mkono mapambano ya Waafrika, na kwa kuunga mkono jitihada

Page 98: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

98

hizo nikubali kuwa Mgombea wa TANU katika Uchaguzi Mkuu uliokuwa unakaribia. Nikatambua mara moja kwamba, nyuma ya ombi hili, ilikuwako dhamiri ya Uongozi wa TANU kuondosha hofu za Waasia wote waliokuwa bado na wasiwasi, na kuwahakikishia kwamba, katika Uongozi wa Mwalimu, Tanganyika Huru itakuwa nchi ambamo nafasi za biashara zitapatikana kwa watu wote sawia, bila kujali asili zao za rangi wala za dini. Nilitafakari sana, tena kwa muda mrefu, juu ya malalamiko ya Kambona. Lakini bado, pamoja na kuzingatia ushauri wa Baba yangu nisichanganye biashara na Siasa, hatimaye nilishindwa kuutekeleza uamuzi huo; siyo kwa sababu ya kutokuwa na imani kwa Mwalimu binafsi, au kwa yale ambayo yeye na Uongozi wa TANU walikuwa wanajitahidi kuyatekeleza. Lakini nilitenganisha kwa uangalifu kati ya kutumika kwangu katika Baraza la Kutunga Sheria na Baraza la Utawala kama Mwakilishi wa Jamii nzima, na kung’ang’ania kazi inayoambatana moja kwa moja na Chama cha Siasa. Mimi niliamini kabisa kuwa njia ambayo ingefaa zaidi kulisaidia Taifa la Tanganyika linalozaliwa ingekuwa kujitahidi kujenga misingi ya uchumi iliyo imara zaidi kuliko kutumbukia kichwa kichwa katika shughuli za siasa. Sidhani kwamba vipengere vya Hoja hiyo vilieleweka kwa urahisi kwa Mwalimu na Kambona. Kwanza walikuwa bado wanapambana na upinzani wa watu wachache, wana-TANU wanamapinduzi waliotaka kudumisha, kinyume cha mawazo ya Mwalimu, wazo la kuwakataa Waasia na Wazungu kuingia katika chama. Kwa kweli nilitambua kwamba, miezi sita tu tangu kupata mwaliko wa kugombea kiti kwa niaba ya TANU, Mwalimu hakufurahia kukataa kwangu kupokea Wajibu huo. Wote wawili tukakutana kwenye dhifa iliyoandaliwa Aquarian Restaurant, kwa heshima ya Waziri wa Kazi wa Kenya, Ibrahim Nathoo. Wakati wa dhifa hiyo, Mwalimu alimlalamikia Nathoo kwamba mimi nilifurahia zaidi kuingizwa kwenye Serikali ya Wakoloni kwa kukubali kushiriki katika Baraza la Kutunga Sheria na Baraza la Utawala, na kwamba

Page 99: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

99

sikudhamiria kutoa ushirikiano kwa TANU, wala kuitumia nafasi aliyotaka mimi niishike katika Tanganyika huru! Nilikuwa na nafasi ndogo ya kusema au kufanya lolote kumtuliza; nikajifanyia uamuzi wangu kutokana na yale niliyoyaona kuwa ya msingi, na ambayo ningeweza kuyatetea. Wakati huo nafasi yoyote ambayo ningaliweza kuipata kuingia katika Orodha ya TANU ilikwisha kupita. Mgombea mwingine wa Kiasia, Mahmoud Raltansey, akateuliwa kugombea Jimbo la Tabora, ambalo mwanzo nilipangiwa nigombee mimi. Kushindania nafasi hiyo hadharani kusingenisaidia chochote, na kungegongana na dhamira yangu. Kwa hiyo nikalazimika kuliacha hilo lipite, na kusubiri nafasi ya siku zijazo katika kuwasiliana na Mwalimu na Uongozi wa TANU, kujaribu kuwaelewesha msimamo wangu mwenyewe katika masuala ya Uhuru wa Tanganyika, na ridhaa yangu katika kulitumikia Taifa jipya endapo nitatakiwa kufanya hivyo. Kampeni za Uchaguzi wa mwaka 1960 zilitawaliwa na ghasia nyingi. Ingawa Mwalimu alitembea nchi nzima wakati huo wa Kampeni, akisisitiza wakati wote watu watulie, akiwakumbusha wapiga kura kwamba mara Uhuru utakapopatikana, Wawekezaji wa nchi za nje watatarajia kuwako nchini humu ikiwa na amani na utulivu; maana yalikuwako matukio ya fujo katika Jimbo la Kaskazini, na vile vile maoni ya Mhariri ya kibaguzi katika gazeti la Uhuru, yaliyowashambulia Waasia na Wazungu kuwa “Wanyonyaji wa Waafrika”. Lakini Kampeni haikuwa na vurugu kama Waasia na Wazungu wengi walivyohofia; na, kama Mwalimu alivyosisitiza mara nyingi katika Ujumbe wa Kampeni ambao dhahiri uliwalenga watu wa nje pamoja na wasomi wachache nchini, Tanganyika huru chini ya uongozi wake kamwe haitafikia kuwa Kongo nyingine. Ujumbe huo na maelekezo mengine mengi yaliyokuwa na lengo la kuwatia moyo wale watu wachache wa mataifa mengine lazima ulieleweka kwa Waasia na Wazungu, kwa sababu tarehe 30 Agosti, 1960, watu milioni 1.1 waliwapigia kura Wagombea wa TANU, kutokana na ule wito wa “Urafiki kwa wote”. Ushindi mkubwa

Page 100: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

100

mno! TANU ikazoa Viti sabini kati ya sabini na moja vilivyoshindaniwa. Ukitambua kwamba, kwa mujibu wa taratibu za Uchaguzi zilizokuwapo, Viti kumi na moja kati ya hivyo viliwekwa kwa ajili ya Waasia (Ratasey alishinda kwa kishindo kule Tabora), na kumi kwa ajili ya Wazungu, matokeo hayo yalidhihirisha Imani kubwa katika Sera za Usawa zilizokuwa zinasisitizwa na Mwalimu. Lakini bado, katika tukio lingine kubwa lililomkumbusha Mwalimu mivutano ya ndani ya TANU aliyoendelea nayo, Wakorofi wakaendelea kupinga jitihada za kuwaruhusu wale Wagombea ishirini na mmoja wa Kiasia na wa Kizungu kujiunga rasmi na Chama cha TANU. Septemba 2, 1961, siku tatu tu baada ya Uchaguzi, Dk. Julius Nyerere akaapishwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa kuchaguliwa katika Tanganyika. Katika Hotuba yake ya kwanza iliyotangazwa katika radio, alisema kwamba Utaifa ulikuwa umeungana na Utani na vicheko “Watu wa Tanganyika wamekuwa watetezi wakubwa wa Utaifa bila ya kuwa wabaguzi”. Pamoja na ushindi wake huo alikataa kutumbukia katika Serikali ya Muda, badala yake akawateua watu kuingia katika Baraza la Mawaziri (lililoitwa, kabla ya hapo, Baraza la Utawala. Wakati huo, katika mapatano aliyoyafanya na Mhe. Richard Turnbull, Wajumbe wote wa Baraza la Kutunga Sheria na wa Baraza la Utawala wa Kuchaguliwa na wa Kuteuliwa, kama mimi mwenyewe, wakaendelea na wadhifa wao mpaka Tanganyika ilipopata Uhuru wake Desemba 9, 1961. Mwaka ule wa mwisho wa kusubiri Uhuru ulipita mbio kweli kweli; matumaini, mwaka 1961 ulipokuwa unayoyoma, yakawa yanazidi kuongezeka. Kama wengine waliokuwa nje na ndani ya Mabaraya yale ya KUtunga Sheria na Utawala, nilikuwa na wasiwasi wangu mwenyewe juu ya muundo wa kuhuzunisha ambao Waingereza walinuia kulirithisha Taifa hili jipya. Lakini nilijua pia, kutokana na uzoefu wangu kule India na Dar es Salaam pia, kuwa Uhuru unaponukia hauwezi kuzuiwa wala kucheleweshwa. Uhuru wa Tanganyika usingeweza kupatikana kwa kumwaga damu, kama ilivyokuwa kule India miaka kumi na minne kabla; ingawa vile vile haukupatikana kirahisi.

Page 101: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

101

Bado nakumbuka waziwazi Sherehe zile za Uhuru za tarehe 9 Desemba, 1961. Usiku wa manane fataki zililipuliwa kwa maonyesho kuangaza Bandari ya Dar es Salaam, ambako watu waliokuwa na shauku kwa maelfu ya mamia walikusanyika kushuhudia. Muda mfupi sana kabla ya hapo, pale Ikulu, Bendera ya Kiingereza ilikuwa inashushwa pole pole mlingotini, na kupandishwa badala yake Bendera ya Tanganyika, yenye rangi ya kijani, njano na nyeusi. Watu walikuwa na shauku nchi nzima, wakicheza mabarabarani na kukumbatiana. Vijijini watu walikusanyana kumsikiliza Kiongozi huyo mpya akitangaza. “Sisi Watu wa Tanganyika tunataka kuwasha Mwenge na kuupandisha kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, uangaze mpaka nje ya mipaka yetu: kuwapa Matumaini waliokata Tamaa, Upendo palipokuwa na Chuki, na Heshima palipokuwa na Dharau.” Hatimaye Tanganyika, Nchi yangu, ikapata kuwa Taifa Huru.

____________

Page 102: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

102

SITA

MWALIMU NYERERE NA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Miaka arobaini na minne imepita tangu Tanganyika ilipopata Uhuru wake. Nikizikumbuka siku zile za mwanzo za kujitawala, kwa kupima amani, utulivu na neema inayoongezeka katika Tanzania ya leo, wakati mwingine naushangaa uvumilivu usioyumba na wema wa watu wa Nchi yangu hii. Mwalimu alitimiza Ahadi yake kwa watu wa nje kwamba kamwe Nchi hii changa, Tanganyika Huru, haitakuwa “Kongo nyingine”. Lakini bado, kulingana na nchi nyingi za Afrika, kama si zote, zilizoibuka kutoka katika kivuli cha ukoloni, sisi Watanzania, wote sisi, tulilazimika kuvumilia dharau na magumu mengi, hasa katika mawimbi ya miaka ile ya mwanzo. Hakikuwako kigezo cho chote cha kuiga ili kufanikisha kumng’oa mkoloni, wala mpango ambao wote sisi tungeweza kuuiga. Badala yake, pamoja na kuheshimu vigezo vyote vya utulivu na kukua kwa nchi, katika mwelekeo wa uchumi au wa ustawi wa Jamii, au hata wa ubinadamu tu, nchi changa ya Tanganyika ilizianza mbio za maendeleo nyuma mno kulinganisha na nchi zilizoendelea, kiasi kwamba mara nashangaa kuona tumemudu kuchechemea masafa marefu namna hii bila kutumbukia, hata mara moja, katika machafuko makubwa. Tuliingia katika dunia hii mpya tukiwa tegemezi, na kila sera tuliyoifuata toka tupate uhuru imetumika tu kuimarisha fikira za kutegemea kabisa watu wengine kwa maisha yetu yote. Kila Viongozi wetu walipotafuta msaada nchi za nje ili kutatua matatizo yetu, kama walivyolazimika kufanya wakati wote katika miaka arobaini ya kwanza ya Utaifa wetu, tulikuwa tunajitumbukiza katika mivutano ya Siasa za Wakubwa, na matakwa na mwelekeo wa Wasomi na Wanasiasa wastaafu, wanaonuia kudhibiti maendeleo ya Jamii. Au, labda linalouma zaidi, kushindwa kwa marafiki zetu wenye nia njema kutuamini kwa misaada inayodumu, isiyokuwa na

Page 103: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

103

masharti; badala yake wakatulazimisha kutumia fedha zao kukidhi mahitaji yao kwa namna yao, siyo kwa manufaa yetu sisi. Hata sasa, katika hali ya huzuni kabisa, najikuta nikiihofia Tanzania na nchi zote zinazoendelea kama Tanzania, tukirukaruka kama tufanyavyo wote katika mawimbi ya dunia; hatuzungumzwi tena kwa kutumbukizwa katika magomvi yoyote ya Mataifa makubwa, lakini bado tunavutwa na nguvu ambazo hakuna mtu duniani anayeweza kujidai kwamba anaweza kuzitawala, lakini bado vile vile ambazo zinaziwezesha nchi tajiri kuwa tajiri zaidi na masikini kuwa masikini zaidi. Lakini sasa hebu nirudi tena kwenye zile siku za mwanzo za Utaifa wetu. Kama nilivyokwisha kusema mapema, wasiwasi wangu katika kuutafuta Uhuru haraka haraka ulitokana na Uchumi dhaifu, kushindwa kwa Wakoloni kuwafunza na kuwaelimisha Waafrika kwa ajili ya kujitawala, na uwezekano wa kulipuka kwa ubaguzi wa rangi. Lakini tazama, siku chache tu baada ya Mwalimu kushika madaraka, hayo maovu mawili yakatishia kuusukuma Utawala wake mpya nje ya mwelekeo. Majadiliano ya kwanza kabisa ndani ya Baraza jipya la Kutunga Sheria yakatokea kuwa yale yale yaliyohusu uraia na rangi za watu: muswada wa Sheria uliopendekeza mwelekeo, hatua kwa hatua, wa kuwapatia uraia watu wote waliozaliwa Tanganyika, isipokuwa wale wa kizazi cha pili. Mapendekezo ya Serikali, yaliyoonekana kuwa mazuri, yalikuwa na mwelekeo wa kuwaruhusu, hatimaye, watu wote waliokaa nchini muda mrefu kupata uraia, yakakumbana mara moja na upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya Wajumbe wa TANU, waliotaka “Tanganyika ibaki kwa Watanganyika tu!” Jibu la Mwalimu likawa fupi na kali, akiwashutumu walalamikaji hao kuwa na tabia kama za wale Nazi wa Ujerumani. Kama alivyofafanua baadaye, “Kama sisi katika Tanganyika tunaupa uaminifu wetu katika masuala ya Uraia, na kuuoza kwenye Rangi, basi tujue hatutaishia hapo. Tutaendelea kuuvuruga Msingi huo…..tutaporomoka mpaka tufikie kuimegamega Nchi yetu. Sisi tunautukuza Ubinadamu, siyo Rangi.”

Page 104: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

104

Mara moja Majadiliano haya ya Baraza la Kutunga Sheria yakatoka nje ya Ukumbi wa Karimjee na kuenea nchi nzima kama moto wa mbugani, na Vyama vya Wafanyakazi vilivyokuwa vimesimama bega kwa bega na TANU wakati wote wa kupigania Uhuru vikaungana na Wakereketwa wa Baraza kupinga waziwazi Sheria hiyo ya Uraia. Baada ya majuma machache tu ya kushika madaraka, Mwalimu akaona umuhimu wa kuachia ngazi ya Waziri Mkuu na kumkabidhi madaraka hayo Makamu wake Rashidi Kawawa. Badala ya kuendesha Nchi kama Waziri Mkuu, Mwalimu sasa akajikuta amelazimika kurudi kule alikotoka: yaani kwenye Chama chake, akisafiri nchini kote, pamoja na watu wake, kuanzisha Mjadala mpya wa Kisiasa. Sababu kubwa ya Mwalimu kulazimika kufanya hivyo ilikuwa kushindwa kwa Serikali ya Uingereza kuwaandaa Waafrika kushika madaraka na kutambua mipaka ya madaraka hayo. Makada wa TANU wasomi waliokuwa wachache mno, wote walikuwa wamepewa madaraka makubwa Serikalini siku ya kwanza tu ya kupata Uhuru. Zoezi hilo likakinyang’anya Chama Wakereketwa wasomi na kukiacha, huko Mikoani na Vijijini, mikononi mwa Wanachama waliolazimika kuwa kiungo tu katika Siasa. Kwa hiyo Mwalimu akaona mamlaka yake yanavizwa moja kwa moja na watu kama hao, hivyo akalazimika kuiachia kwa muda nafasi yake, ili kuiunganisha Serikali yake na watu ambao sasa ilikuwa inawatumikia. Wakati Mwalimu alipokua anahangaika kusafiri nchi nzima, Sera ya kuwapa madaraka Waafrika sasa ikawa inasimamiwa na Serikali iliyokuwa inaendeshwa na Kawawa. Watumishi kadha wa Serikali, Wazungu, wakastaafishwa kwa lazima; lakini walilipwa fidia. Watumishi wengine 260 wa Serikali wasiokuwa Waafrika, zaidi sana Waasia, wakapoteza ajira zao; na Watumishi wapya 600 wa Kiafrika wakachukuliwa. Wakati huo huo mafunzo ya haraka haraka yakaanzishwa kwa ajili ya Watumishi wa Serikali wa Ngazi za Chini. Sera za aina hiyo hiyo zikatekelezwa katika Jeshi la Polisi. Kufikia mwezi Juni, 1962, kiasi cha asilimia arobaini ya watumishi wa kigeni wakawa wameondoka kazini. Hatua hizo zilisaidia sana kutuliza wimbi la malalamiko kati ya wananchi walio wengi

Page 105: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

105

waliokuwa wanadai Serikali ichukue hatua za haraka kurekebisha uwiano mbaya na dhuluma zilizokuwako wakati wa Utawala wa Wakoloni. Lakini haja ya kudhibiti zaidi ya vile ilivyowezekana katika ama mjadala ama mabadiliko madogo katika taratibu ikalazimu kupitisha katika Bunge Sheria mpya ya kusimamia madaraka ya Vyama vya Wafanyakazi mwezi Juni 1962, na kuikabidhi Serikali uwezo wa kuwaweka watu kizuizini. Kufikia wakati huo Mwalimu alikwisha kamilisha ziara zake nyingi nchini, akiwahakikishia wafuasi wake juu ya uaminifu wa Viongozi aliokuwa nao, na kujenga upya taratibu za TANU za kitaifa. Mwezi Agosti, 1962, akachaguliwa kwa kauli moja kuwa Mgombea wa TANU wa Kiti cha Rais, na akachaguliwa kwa kura nyingi ingawa waliojiandikisha na waliopiga kura walikuwa wachache. Mkasa wa kwanza ukawa umepita. Kwa kutumia mila za Kiafrika za mazungumzo na watu, na Sheria kali kali, Wapinzani wa yale waliyoyaeleza vibaya masuala ya Sera walizoamini kuwa zinawapendelea Waasia na Wazungu wakawa wamedhibitiwa. Lakini ikadhihirika kuwa hali hiyo ilikuwa kama kificho tu katika Kampeni ndefu zaidi Mwezi Agosti, 1962, Kiongozi wa zamani wa Chama cha Wafanyakazi Christopher Kasanga Tumbo akajiuzulu kazi yake ya Ubalozi kule London, ili aunde Chama kilichoitwa Peoples Democratic Party, PDP. Mwezi huo huo ukazuka mgomo katika mashamba ya mkonge ambayo kabla ya Uhuru yalikuwa yanaajiri zaidi ya asilimia thelathini ya Wafanyakazi wote wa Kiafrika. Hatua aliyoichukua Mwalimu kujibu matatizo yote hayo ilikuwa kufungua Uanachama wa TANU kwa watu wa Mataifa yote, na kisha kuanzisha mpango wa Chama kimoja. Chama cha Taifa cha Waislamu wote wa Tanganyika, AMNUT, kikadai bila mafanikio ipigwe Kura ya Maoni kuamua suala hili la Chama Kimoja. Sheria ya Kuwatia watu kizuizini ilitumika kuvirudisha Vyama vyote vya Siasa kwenye mstari: na Tumbo akakimbilia Kenya. Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi, hasa wale waliokuwa wanashinikiza migomo, wakatiwa ndani bila kufikishwa Mahakamani. Pamoja na Hatua hizo, bado viongozi wa vyama vya Wafanyakazi waliendelea kuchochea upinzani dhidi ya

Page 106: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

106

Serikali, wakitumia Hoja, kama walivyoiona wao, ya kasi ndogo katika kuwapa Waafrika madaraka, kama fimbo ya kupigia. Mwalimu na Serikali yake wakajitahidi kupambana na msimamo huo kwa kuongeza hatua za kuwatia watu kizuizini, wakichanganya na Sera zilizokuwa na lengo la kulinganisha nafasi za kazi. Kufika mwanzoni mwa mwaka 1964 jitihada za kulitatua tatizo hilo zikamchosha. Januari 7, 1964, akasambaza barua katika Wizara zote kutangaza. “Lazima Taifa litumie nguvu yote ya ujuzi na uzoefu, ngozi inayofunika ujuzi huo haidhuru kitu. Maana yake ni kwamba Ubaguzi katika utumishi Serikalini kuhusu ajira, mafunzo na kupandishwa vyeo lazima ukomeshwe mara moja. Hatuwezi kuruhusu kuneemeka kwa tabaka katika Uraia: daraja la kwanza na la pili. Mpango maalum wa kuwapa nafasi Waafrika sasa umefungwa.” Siku nne baadaye yakatokea Mapinduzi Zanzibar, kutokana na kutumbukia kwa raia wa Uganda ambaye hakuwa anajulikana sana, John Okello. Katika muda mfupi wa chini ya saa arobaini na nane, katikati ya machafuko makubwa katika mitaa ya Stone Town. Waarabu na Machotara wao wengi wakawa wameuawa. Serikali ya Sultani ikaomba msaada kutoka Serikali ya Uingereza, lakini haukupatikana, ingawa Serikali ya Uingereza ilipanga taratibu za kumwondoa Sultani, familia yake, na wengine aliokuwa na uhusiano nao wa karibu. Siku kumi na tatu baadaye, safari hii huku Bara, yakatokea maasi ya askari, na majengo muhimu yakazingirwa, pamoja na Ikulu ya Dar es Salaam. Maasi hayo yakaenea haraka kwenye Kambi ya Jeshi ya Tabora, ambako Viongozi wa Maasi walipinga wazi wazi jitihada za Mwalimu za kuleta mabadiliko, wakitumia kinga ya kudai nyongeza ya mishahara na kuondoshwa kwa Maafisa wa Kiingereza. Ilibidi Mawaziri wa Mwalimu wafanye kazi kubwa ya kubembeleza, na baadaye Jeshi la Waingereza likatumika kuzima maasi hayo ya siku sita. Matukio hayo mawili, Mapinduzi na kisha Maasi, yalidhihirisha udhaifu wa Utawala wa Ndani katika siku zilizofuatia kuondoka kwa Wakoloni. Hususan yale maasi yaliyolazimu kutafutwa

Page 107: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

107

Wakoloni wa zamani kuokoa Utawala wa Mwalimu, ndiyo yaliyotukumbusha mipaka ya madaraka hata ya Mwalimu mwenyewe, miaka mitatu baada ya kupata Uhuru. Mwalimu akajisikia kudhalilika pale alipolazimika kutafuta msaada wa Majeshi ya Kiingereza kuyazima maasi hayo; na baadaye kuwaomba Nigeria kutoa msaada wa ufundi Jeshini. Katika yote hayo, hakuna hata moja lililokaribia Machafuko ya Kongo. Lakini kwa Mwasia kama mimi, niliyekuwako Tanganyika katika siku hizo za wasiwasi, hali hiyo ya kusambaa kwa ghasia ilikuwa inatia mashaka. Sisi tuliokuwa tabaka la wachache tulitambua fika kuwa kuendelea kwetu kukaa Tanganyika kulitegemea moja kwa moja kukabiliana kwa busara na Suala la Utaifa uliokuwa unaenezwa na Uongozi wa TANU. Bahati nzuri kwetu katika suala hili na, kwa kweli, katika mambo mengine yote ya msingi, Mwalimu Nyerere aliendelea kusimama imara, ijapokuwa alisononeshwa na matukio ya Zanzibar na yale ya Kambi za Jeshi za Dar es Salaam na Tabora, bila kutetereka katika Imani yake juu ya usahihi wa kuwahesabu watu wote kuwa sawa. Wala hakukawia kuzinduka baada ya matukio hayo, kiasi cha kumwezesha kujijenga upya na kuongeza umaarufu wake katika Taifa. Akifanya kazi kwa karibu na Abeid Amani karume, Kiongozi mpya wa Zanzibar, alifanikiwa kuunganisha nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar kuwa Jamhuri mpya ya Muungano wa Tanzania, iliyozaliwa Aprili 26, 1964, kiasi cha miezi mitatu na nusu tu toka yale maasi yaliyoongozwa na Okello. Na, mara baada ya maasi ya askari huko Bara, akawastaafisha wale askari waliokuwa hawaridhiki. Yote haya, yakipimwa pamoja na tamko lake rasmi kwamba Sera ya kuwabeba Waafrika imekufa, yakatusaidia sisi raia wa Kiasia na wa Kizungu kujenga Imani katika nchi hii ambamo sasa tumekuwa raia wake. Wakati huo kushiriki kwangu katika mambo ya Taifa lililokuwa linainukia kulikuwa bado kudogo, lakini nikawa nafanya lile nililoweza kusaidia kutatua baadhi ya matatizo kwa upande wa Elimu. Mwaka 1963, baada ya utekelezaji wa Mpango muhimu wa Serikali uliotilia mkazo sana mahitaji ya elimu kwa wenyeji, watoto wa mataifa ya kigeni wakaachwa bila hata shule moja, nzuri,

Page 108: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

108

iliyokuwa inafundisha kwa lugha ya Kiingereza. Nililizungumza tatizo hilo na marafiki zangu wachache waliotoka nchi za nje, na hatimaye ishirini kati yetu tukaamua kuanzisha kitu kama Shule ya Kimataifa jijini Dar es Salaam. Fedha zikachangishwa, kwa kutumia zaidi Balozi chache, hasa Wakala wa Marekani kwa ajili ya Maendeleo ya Kimataifa, USAID, waliokuwa wa msaada mkubwa. Sam Butterfield, Mkurugenzi wa hapa wa USAID, na Balozi wa Sudan, Mhe. E.M. Elamin, wakawa ndio wachangiaji wa Kampuni hiyo. Kampuni za Kigeni zilizokuwako Tanzania, kama Caltex na Shell, vile vile zilisaidia katika kuchangia. Serikali iliunga mkono mradi huo, lakini ikasisitiza kuwa misaada yao ielekezwe kwa watoto wa Wageni tu. Kiwanja kikapatikana katika eneo zuri, na shule ikajengwa. Mimi nikateuliwa Mweka Hazina wa kwanza wa shule hiyo, na George Panayotopolous Katibu wa kwanza. Panayotopolous hakuwako nchini kwa kipindi fulani, na ikaniangukia mimi kufanya kazi zote hizo mbili, ya Katibu na ya Mtunza Hazina. Hatimaye nikapewa Uenyekiti wa Kampuni iliyotumika kuanzishia shule hiyo, lakini nikaukataa mzigo huo; kwa mawazo yangu niliona kuwa Uraia wangu wa Tanzania ulikuwa kizingiti. Lakini nikabaki katika Bodi kwa miaka ishirini, nikiwa mwakilishi pekee Mtanzania asiyekuwa na dhamana, na nikashiriki katika jitihada za shule zilizofanikiwa kupata matokeo yaliyotarajiwa kwa niaba ya Jamii ya watu wa nje waliokuwa wanaishi na kufanya kazi nchini Tanzania. Lakini kushiriki kwangu kikamilifu katika mambo ya Elimu hakukuishia kwenye shule hiyo ya kimataifa peke yake. Baada ya kuanzisha Shule ya Viziwi ya Buguruni, Dar es Salaam, ambayo hivi sasa inawahudumia wanafunzi 238, kati ya hao 70 wakikaa Bweni, na kushiriki katika shughuli za Chuo cha Elimu ya Biashara kama Mwenyekiti wa Bodi yake ya Mitihani, nimejihusisha vile vile, kwa karibu, na chama cha Dar es Salaam cha Elimu ya Sekondari ambacho nacho kilianzishwa mwaka 1963. Chama hiki ndicho kinachomiliki Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert, iliyopewa jina la huyo Mshairi maarufu ambaye mashairi yake yamesisimua maisha ya Watanzania kwa mamilioni, na

Page 109: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

109

wengine wengi nje ya mipaka yetu. Tokea mwanzo shule iliungwa mkono na Serikali na Umma wa Watanzania na wengi wengine walio nje ya mipaka yetu. Rais Benjamin Mkapa, aliyewahi kuwa Gavana wa shule hiyo aliwahi kusema siku moja, “Mimi nina hakika kabisa kwamba kutumika kwenye Bodi ya Shule ya Shaaban Robert kulinipa nafasi kubwa ya kuelewa matatizo ya elimu nchini mwetu, na jukumu kubwa wanalolibeba watu binafsi katika kuyakabili matatizo hayo.” Kwa mawazo yangu Shaaban Robert alikuwa mfano wa ushirikiano, nusu wa binafsi na nusu wa umma, ambao Mkapa aliwaelezea wenzi wangu; na nikatumia nguvu na muda mwingi kufanikisha ushirikiano huo. Tulikuwa na bahati ya kuwapata Wakuu wa Shule wawili, wazuri sana, Bibi Mary Koleth ambaye, kwa bahati mbaya, hayuko nasi tena, aliyeuweka msingi imara kweli kweli katika miaka ya mwanzo, alipounganisha kwa mafanikio nidhamu kali na ari ya kujifunza. Hivi karibuni zaidi Bwana Suryakant Ramji ameitumikia shule kwa mafanikio makubwa, akiwa kwanza Naibu wa Mkuu kwa miaka kumi na minne, na baadaye akiwa Mkuu mwenyewe. Nafarijika nikitambua kuwa mchango wangu mimi mwenyewe haukukosa kutambulika. Rais Mkapa alisema katika Mahafali ya mwaka 1968. “Andy ni mtu wa sehemu nyingi na idadi kubwa ya nafasi za madaraka; lakini pamoja na yote anayotarajiwa kuyafanya katika muda alionao, ameweza wakati wote kupata muda wa kushughulikia mambo mengine mengi mazuri, akitoa misaada kwa wenye shida na kupunguza machungu na mateso ya watu katika Jamii yetu. “Nilikuwa nawaambia rafiki zangu huko nyuma kwamba yeye ndiye mtu hodari kuliko wote nchini kwetu katika kutunza kumbukumbu. Ameweka nafasi maalum katika kitabu chake cha kumbukumbu kwa ajili ya Shaaban Robert katika miaka hii mingi. Mamia ya Wazazi na wengine wengi wanaonufaika na shule hii wanamuenzi sana”. Vile vile, katika mwaka 2003, katika sherehe ya kutimiza miaka arobaini ya Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert, Waziri Mkuu

Page 110: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

110

wa Tanzania Frederick Sumaye, wakati akinipongeza mimi, alisema, “Pamoja na kufurahia jitihada za wale wanaoshughulikia mambo ya kila siku ya Shule, ni muhimu kabisa kwetu kuwatambua wale wanaotimiza majukumu yao kimya kimya, na mmoja wa hao ni Dk. Chande, siyo tu kwa hatua alizochukua kufanikisha shule hii, lakini vile vile kwa tuzo la Ushujaa alilolipata hivi karibuni. Akiwa Mtanzania wa kwanza kupokea tuzo hilo linalopatikana kwa nadra siku hizi, ninajivunia kutamka kuwa Dk. Chande ameyapokea mafanikio yake kwa unyenyekevu, kazi ngumu na kujituma.” Jamii ya shule ikaamua kulipa jina langu Bwalo la Shule yao lililozinduliwa rasmi na Rais Mkapa mwaka 1997, na wakataka ridhaa yangu kufanya hivyo. Nikaipokea heshima hiyo, mradi tu hayo yatendeke baada ya mimi kufariki. Katika mwelekeo huo huo, wakati Mstahiki Meya wa Dar es Salaam, Mhe. Kitwana Kondo, aliponikabili mnamo miaka ya 1970 kuniomba niiruhusu Halmashauri ya Jiji kuupa mtaa mmoja jina langu, nikakataa, kwa maelezo kwamba kwa mila ya familia yetu hatutaki kuweka kumbukumbu za kutukuza majina yetu isipokuwa tu baada ya kufariki. Nikirudi kwenye yale mabadiliko makubwa ambayo Nchi ilikuwa inayapata, ingawa na mimi nilikuwa na wasiwasi ule ule waliokuwa nao Jamii ya Kiasia, kwa hakika kuzoeana kwangu na Rais Nyerere wakati huo kulinifanya niyaelewe mambo katika sura tofauti. Ingawa niliukataa uteuzi wa TANU mwaka 1960 kugombea kiti cha Tabora, hisia zo zote mbaya dhidi yangu hazikuendelea mpaka kufika Serikalini. Mara alipokishika Kiti, Rais Nyerere akanipa nafasi za kukutana naye kwa ajili ya mambo mazito, kuanzia uteuzi wa nafasi ndogo ya Mwenyekiti mpya wa Makumbusho ya Taifa (ambayo mpaka wakati huo yalikuwa na jina la Mfalme George V) mpaka kuteuliwa Mjumbe wa kwanza wa Serikali katika Bodi mpya ya TANESCO pale Serikali ilipotaifisha hisa za Balfour Beatty mwaka 1964. Lakini pengine, la muhimu zaidi, niliweza kuthibitisha ahadi yangu ya zamani kwa Mwalimu kwamba ningekuwa wa manufaa zaidi kulihudumia Taifa hili jipya kama Mfanyabiashara kuliko nikiwa Mwanasiasa.

Page 111: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

111

Pengine nafasi yangu pale Makumbusho, kabla na baada ya Uhuru, haikudhihirisha umuhimu wo wote, lakini ilinipa mimi fursa ya kutumbukia katika baadhi ya mambo muhimu ya kale yaliyokuwa yanagundulika mpaka wakati huo. Mwaka 1964 nikiwa Mwenyekiti wa Makumbusho, nilikuwa na wajibu wa kupatana na mmoja wa Wanamakumbusho mashuhuru duniani, Dk. Louis Leakey, ili turudishiwe lile fuvu la kale, Zinjanthropus, aliloliokota yeye, akiwa na mkewe Mary, katika pango ya Olduvai, Tanzania ya Kaskazini. Wala haishangazi kuwa kazi hii ilikuwa rahisi zaidi kuitamka kuliko kuitenda. Pamoja na kukubaliana masharti ya kulichimbua fuvu, yaliyotiwa saini na wote wawili, Leakey na Oscar Kambona, Waziri wa Tanzania wa Elimu, Mkataba huo ulieleza waziwazi kwamba Dk. Leakey hakuwa na uwezo wa kupata ushahidi wa maana au vitu bandia. Pengine inaelezeka kuwa Leakey hakuwa radhi kulirudisha fuvu Tanzania. Alisisitiza kuwa, pamoja na makubaliano yake na Kambona, alikuwa anabanwa na wajibu kwa Jamii ya Kimataifa ya Sayansi kulihifadhi fuvu lile kwa niaba ya vizazi vijavyo. Jukumu langu likawa kumsisitizia kwamba kulirudisha fuvu Tanzania, na kulihifadhi kwa salama milele, hayakuwa mambo mawili yanayogongana. Nilikutana na Dr. Leakey mara nyingi katika jitihada zangu za kumtuliza, mpaka hatimaye tukaweza kupata maafikiano yaliyouridhisha wasiwasi wake wa Kisayansi. Wasiwasi huo ukawa pamoja na kujengea, ndani ya makumbusho, kasha litakalowekwa ndani ya chumba chenye kiyoyozi, na kumwajiri Mtaalam atakayewarahisishia Wanasayansi kuendeleza Utafiti. Baada ya makubaliano hayo ya msingi na Dk. Leakey, kwa maelekezo yangu, Bodi ya Makumbusho ikaanza kutafuta njia za kupatia fedha ili kutekeleza mpango huo. Wakati huo Makumbusho ilikuwa chini ya Wizara ya Ustawi wa Jamii, Michezo na Utamaduni, na sehemu kubwa ya Bajeti ilielekezwa kwenye sehemu nyingine zisizokuwa za Utamaduni. Nikamwendea Waziri Mgonja; yeye akaniambia kuwa fungu alilopata kutoka Hazina lilikuwa dogo mno, kiasi kwamba isingaliwezekana kupata fedha zaidi za

Page 112: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

112

kuimarisha Makumbusho. Hivyo kilio changu cha kuhakikisha kuwa kumbukumbu za Tanzania zinalindwa hakikuweza kusikilizwa. Kwa hiyo nilikwenda, Waziri akijua, kuonana na Rais Nyerere, ambaye aliubariki ule Mkataba na Dr. Leakey, lakini akanishauri kuendeleza jitihada za kutafuta fedha kutoka katika Jamii ya Wafanyabiashara kuliko kuitumainia Serikali. Hatimaye jitihada hizo zikazaa matunda zilipoungwa mkono kwa nguvu na Kampuni za Williamson Diamonds, Gailey and Robets (Kundi la Uniliver), na Vyanzo vingine kadha. Michango hiyo siyo tu ilikidhi masharti ya mapatano na Dk. Leakey, lakini pia ililipia ujenzi wa “Ukumbi wa Mtu” uliobuniwa na Wajenzi wa Nchini, French and Hastings. Miaka kadhaa baadaye, katika sherehe ya ufunguzi wa Ukumbi huo uliofanywa na Rais Mwinyi, Dk. Richard Leakey, mwana wa Louis Leakey, akatoa hotuba nzuri sana katika lugha ya Kiswahili. Wakati huo kwa msaada wa Serikali ya Uholanzi, Bodi ya Makumbusho ikapata nafasi ya kumtumia Mtaalam wa Mambo ya Kale, Meyer Hasserbeg, aliyekuwa ndiyo kwanza amemaliza muda mrefu wa kazi yake kule Ghana. Ili kuharakisha kuja kwake, nikatafuta njia ya mkato. Badala ya kuomba msaada kutoka Hazina kwa Taratibu za kawaida, nikamwomba Dk. Wilbert Chagula, Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam, kufikisha maombi rasmi Ubalozi wa Denmark, ili Hesselberg aruhusiwe kukubali wadhifa wa Mhadhiri, katika Chuo Kikuu, wakati vile vile akifanya kazi katika Makumbusho. Chuo Kikuu, na Ubalozi, wote wakayakubali mapendekezo yangu. Kwa msaada wa Kamati ya Nyumba iliyokuwa chini ya Katibu Mkuu David Mwakosya, nyumba ikapatikana; wakati huo Bernard Mulokozi naye analihangaikia suala la Makumbusho. Kiasi cha miezi mitatu baada ya kufika kwake, Hasserbeg akaomba ruhusa Hazina kuingiza nchini gari yake bila kulipia ushuru. Ombi hilo ndilo hatimaye lililofanya Hazina kutambua kuwako kwa Hesselbert nchini Tanzania. Nikaitwa na Katibu Mkuu wa Hazina, Jacob Namfua, kuulizwa kwa nini Serikali nyingi zilikuwa zinaendesha nchi hii. Hatimaye, baada ya kueleza kila kitu, Mradi

Page 113: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

113

ukaonekana kama kitendawili kisichoisha; nikafanikiwa kutuliza hasira zote, na hatimaye Namfua, kwa unyenyekevu wote, akayakubali yale yaliyokwisha kutokea. Fuvu lingali kwenye chumba cha chini katika Jengo la Makumbusho mpaka leo, pamoja na lingine la mfano lililotolewa na ukoo wa akina Leakey, ili watu walione pale Makumbusho. Yako mengine mengi, pengine makubwa zaidi, yaliyovumbuliwa toka wakati huo kwenye Pango hilo na kwingineko, lakini siwezi kusahau nilipoliona mara ya kwanza fuvu la Zinjanthropus, lililokuwa limepauka na, kwa mawazo yangu, linalothibitika kuwa ni la mmoja wa binadamu wa mwanzo kabisa. Mwaka 1995 nilikuwa mmoja wa watu watatu tulioteuliwa katika Ujumbe wa kwenda Arabuni kujadili masharti ya Mkataba wa kwanza wa biashara na Utamaduni kati ya nchi zetu mbili. Ujumbe wa Tanzania ulikuwa Jerry Kasambala, Waziri wa Biashara na Ushirika; Osiah Mwambungu, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, na mimi mwenyewe. Nassor El-Buali aliuhudumia Ujumbe kama Katibu. Tulifika Cairo kwa ndege ya Waarabu, tukisindikizwa na Ahmed Shafik Mustafa, kutoka Ubalozi wa Waarabu mjini Dar es Salaam, mtu mwenye heshima zake aliyepanda ngazi mpaka kuwa Balozi wa nchi yake kule Uingereza. Kwa kuwa hatukutarajia mambo ya itifaki jioni ile, tukajipatia vinywaji vyote kwa uhuru ndani ya ndege; kwa hiyo lazima nikiri kuwa tulipofika Cairo tulikuwa taabani. Hapo Cairo tulipokelewa na Waziri wa Biashara za Nje, Bwana Shuke, lakini baada ya kusalimiana, tukaachiwa kufanya kila mtu alilolitaka kwa muda mrefu mno katika Ukumbi wa Waheshimiwa pale Uwanja wa Ndege. Hatimaye nikamwuliza yule msindikizaji wetu nini kinaendelea. Bwana Mustafa akaulizauliza, kisha akaja na jibu kwamba Waziri wa Tanzania hakuwa na cheti halali cha chanjo ya homa ya manjano; kwa hiyo Maafisa wa Afya walikuwa wanaleta matatizo, wakisema kuwa watatoa Cheti cha msamaha endapo tu watapata maelekezo kutoka kwa Waziri wa Afya mwenyewe, ambaye wakati huo alikuwa kwenye sherehe ya arusi, na hivyo hapatikani!

Page 114: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

114

Hatimaye muafaka ukapatikana, na tukaruhusiwa kuondoka Uwanjani. Kule tulikofikia, Shepherd’s hotel, nilishangazwa zaidi na nguvu za Waziri, asiyekuwa na Hati za Afya. Pamoja na safari ndefu angani, na muda mrefu tuliosubiri pale Uwanjani, na vyote vile alivyokula na kunywa tukiwa safarini, bado akakubali haraka haraka mwaliko wa mwenyeji wetu kuangaza macho kwa muda mfupi katika Klabu ya Usiku ya Sahara City. Wote tukalazimika kujikokota kurudi kwenye vyumba vyetu alfajiri, na kusinzia kidogo katika muda huo tulioupata. Saa 3.00 kamili asubuhi kesho yake, Waziri aliyeyafunika macho yake kwa mawani ya jua, baada ya kunywa haraka haraka majagi mawili ya maziwa, akatoa moja ya hotuba nzuri za papo kwa papo kuliko zote nilizopata kuzisikia, akifafanua kwa uzito wote Mapendekezo ya Tanzania katika Mazungumzo hayo. Baadaye siku hiyo, tulipoufikisha ujumbe wa Mwalimu Nyerere kwa Marehemu Rais Abdul Nasser, Waziri kwa mara nyingine tena akajitokeza kwa namna ya kusifiwa. Nasser mwenyewe alionekana kama mtu aliyevurugikiwa, akiwa na hamu ya kutusikiliza, labda kutokana na ujuzi mdogo aliokuwa nao kuhusu sehemu yetu ya dunia. Lakini, pamoja na hayo, wote tukatambua kuwa tuko mbele ya Kiongozi mwenye uwezo mkubwa kabisa. Siku tatu baadaye tukarudi Dar es Salaam, Mkataba ukiwa mfukoni mwa Waziri. Vile vile mwaka 1995 nilipokuwa natembelea Port of Spain, nilitakiwa kwenda Caracas, Venezuela, kwa ndege. Niliondoka hotelini mapema ili niwahi kufika Uwanjani, lakini nikacheleweshwa katika msongamano wa magari, na hivyo nikachelewa kuipata hiyo ndege ya Venezuela. Ndege ilikuwa haijaruka bado, lakini makarani wakakataa kunipokea. Nikamtafuta Meneja wa zamu; lakini na yeye, ingawa alilielewa fika tatizo langu, akasisitiza kwamba Orodha ya Abiria ilikwishafungwa, wala haitawezekana tena kuingiza jina langu. Akapendekeza niende na ndege ya KLM, iliyotarajiwa kuondoka kiasi cha dakika tisini baadaye.

Page 115: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

115

Nikamsisitizia kuwa nilikuwa na marafiki waliokuwa wananisubiri katika hoteli ya Caracas Hilton, nami sikuwa na hakika kama KLM ingepata ruhusa ya kuchukua abiria kati ya Trinidad na Venezuela. Meneja yule, akanihakikishia nisiwe na wasiwasi, kwa hakika ningepata nafasi katika ndege ya KLM. Akajitolea kuwajulisha marafiki zangu juu ya mabadiliko hayo ya ndege; hivyo nikampa majina yao, na namba zao za simu. Ndege ya KLM ikatua mara baada ya kuanza safari yangu ya Caracas. Nilipofika hoteli ya Hilton ikadhihirika kwamba marafiki zangu hawakupata taarifa juu ya mabadiliko hayo ya ndege. Lakini wakati wa mazungumzo ya jioni ikafahamika kuwa ndege ile iliyokuwa inakwenda Venezuela ilitekwa na magaidi na kulazimishwa kutua Cuba! Dhahiri Mwenyezi Mungu alikuwa upande wangu siku ile. Mfano mwingine wa kushiriki kwangu mapema katika harakati za Serikali ni hatua zile nilizofanikiwa kuzichukua katika kuviza uchochezi wa Wafanyabiashara katika hisia zilizokuwa zinawaka moto katika masuala ya kumiliki ardhi. Huku Tanganyika, tofauti na ilivyokuwa kwa majirani zetu Kenya katika miaka ile iliyofuatia kufutwa kwa Ukoloni, suala la kumiliki ardhi halikuguswa katika mazungumzo yaliyopelekea kukabidhiwa kwa Madaraka. Wakati Tewa Saidi Tewa, Waziri wa Ardhi katika Serikali ya Tanganyika, alipoufuta uratatibu wa zamani wa mtu kuhodhi ardhi milele, kama yake, na kuweka badala yake Utaratibu wa kumilikishwa na Dola hata kama ni kwa muda mrefu, hatua hiyo ikazaa uhasama mkali kutoka kwa Jamii ya Wafanyabiashara nchini. Wakati ule, na inafanana na Taratibu za Uchumi Huria za nchi nyingi nyingine Mabenki ya biashara yaliyokuwako Tanganyika yalitoa mikopo kwa Wafanyabiashara kwa dhamana za mashamba sambamba na Hati za nyumba. Sheria hii mpya ilitishia matukio ya watu kunyang’anywa mali kutokana na kushindwa kuilipa mikopo hiyo, na vile vile kusitishwa kwa mikopo ya baadaye. Kwa hiyo kwa nafasi yangu kama Mwanachama muhimu wa Vyama Vikuu vya Wafanyabiashara wa Dar es Salaam,

Page 116: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

116

nikawasiliana na Wakopeshaji Wakuu wawili: Standard Bank of South Afrika Ltd., na Barclays, na kuwasaili Mameneja wao kama Hati walizokuwa wanazishikilia kama dhamana zingepungua hadhi kutokana na kutekelezwa kwa Sheria hiyo. Nilipothibitishiwa kuwa mambo hayo hayahusiani, nikawa na ujasiri wa kutoa taarifa kwenye Vyama vya Wafanyabiashara nchini kwamba haikuwako hofu yo yote kwa madeni yaliyopo kulazimishwa yalipwe mapema. Matokeo yake, sehemu kubwa ya uhasama uliokuwako katika Jamii ya Wafanyabiashara nchini, dhidi ya Utaratibu mpya wa kumiliki ardhi, ukayeyuka. Uzoefu wangu mwingi katika biashara ya Afrika Mashariki, na mtandao wa uhusiano nilioujenga kutokana na shughuli zangu za biashara Mikoani, ulikuwa vile vile na manufaa kwa Taifa la Tanganyika, na baadaye Tanzania. Wakati wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, iliyounganisha Kenya, Tanzania na Uganda, mimi nilikuwa Mjumbe wa Jopo la kushughulikia Masuala ya Afrika Mashariki, BEAA, lililokutana Ikulu. Mara baada ya Ian Smith kujitangazia Uhuru wake kule Rhodesia, suala la Msaada wa Wachina katika Ujenzi wa Reli ya TAZARA likawa zito. Nikamshauri Dickson Nkembo, Mwenyekiti wa BEAA, kwamba Utaratibu ambao ungefaa ungekuwa ule ambao ungeiwezesha Tanzania kumiliki reli kutoka Dar es Salaam mpaka mpakani mwa Zambia, na Zambia kumiliki sehemu inayoingia katika nchi yake; kila nchi ikibeba sehemu yake ya kuwajibika katika kulipa ule mkopo uliotoka China. Nikashauri vile vile kwamba pengine Rais Kaunda, angependa kufikiria kutafuta fedha kutoka katika nchi rafiki kujenga gati katika Bandari ya Dar es Salaam, itakayomilikiwa na Serikali ya Zambia. Lakini hakuna hata moja kati ya hayo mawili lililozungumzwa Kikaoni. Baadaye nikateuliwa na Serikali kuwa Mjumbe katika Bodi ya Shirika la Reli la Afrika Mashariki, EARC; na Shirika la Bandari, EAHC; na Shirika la Huduma za Mizigo. Nilifurahia sana kuteuliwa kwenye Bodi ya Shirika la Reli na, baada ya kuvunjika kwa Shirika hilo, kuteuliwa Mwenyekiti wa Shirika la Reli la Tanzania, nafasi ambayo nimeitumikia kwa miaka kumi na miwili

Page 117: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

117

baadaye. Nafasi hizi zilinikumbusha uzoefu nilioupata nikiwa mmoja wa Washauri sita wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli na Bandari za Afrika Mashariki mwishoni mwa miaka 1950. Mara baada ya kuvunjika kwa Shirika hilo, nikateuliwa na Rais Nyerere kuwa Mwenyekiti wa Shirika la Ndege, na baadaye Mwenyekiti wa Mamlaka ya Bandari, akanikubalia ombi langu la kutumika kwenye Mashirika hayo nikiwa si Mwenyekiti Mtendaji. Shughuli zote hizi za kulitumikia Taifa zilikuwa dalili za mwelekeo wa Sera za Umma. Kufika katikati ya miaka ya 1960, yale malumbano makubwa juu ya rangi ya mtu yalikuwa yamemalizika, na ulimalizika vile vile mjadala juu ya uwezo wa binadamu, baada ya Serikali kuanzisha mpango mkubwa wa masomo yenye mwelekeo wa kazi; pamoja na mpango, uliokuwa umechelewa, wa kupanua sekta za Elimu ya Sekondari na ya Juu zaidi kwa ajili ya Waafika. Wasiwasi wangu wa mwisho kati ya tatu nilizokuwa nazo kabla ya Uhuru, yaani kasoro ya msingi katika uchumi, sasa ulikuwa unajitokeza. Rais Nyerere alikuwa anayatafakari yote hayo kwa miaka mingi. Miaka yake ya masomo katika Chuo Kikuu kule Uingereza, na mambo yaliyofuatia ya kushikamana sana na Tawi la Fabian la Chama cha Leba cha Uingereza, vilimpa changamoto ya kutafakari. Mara baada ya Uhuru akatoa tamko kuhusu filosofia yake ya uchumi iliyokuwa changa bado katika maandishi yaliyoitwa “Ujamaa wa Kiafrika”. Katika maandishi hayo alieleza Imani yake kubwa kwamba Ujamaa ndio ulio utaratibu wa kawaida katika Afrika, kabla ya kutawaliwa na Wakoloni. Katika siku zile, alisisitiza “Kila mtu alifanya kazi……..bepari au kabaila hakuwa anajulikana, lakini ……ubepari usingewezekana. Katika zama zile Mwafrika hakutamani kuhodhi mali yake binafsi, kwa lengo la kuwatawala wenzake wote. Kamwe hakuwa na vibarua wala “mikono ya kiwanda” kumfanyia kazi. Lakini baadaye wakaja Mabepari, wageni; walikuwa matajiri, na walikuwa na maguvu; hivyo, dhahiri, Mwafrika naye akaanza kutamani kuwa tajiri.”

Page 118: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

118

Fikira kama hizo ndizo zilizokuwa msingi wa kuwaelimisha upya Wana-TANU wenyewe kuanzia mwaka 1962 na kuendelea; akawafundisha kwamba Ujamaa wa Kiafrika ulijengwa juu ya misingi ya kuheshimiana, kushirikiana mali, na ridhaa ya watu wote katika Jamii kufanya kazi kwa manufaa yao wote. Ulipokwisha kubalika Tanganyika, aina hii ya Ujamaa ingeisogeza Jamii kwenye maendeleo ya usawa, kufikia hali ya kushirikiana inayoitwa “Ujamaa”. Kama alivyosema Mwalimu katika kitabu chake juu ya Ujamaa, kilichotolewa mwaka ule ule. “Ujamaa ni fikira za mtu…..Imani katika Umoja wa watu, na hatma ya Mwanadamu. Kwa maneno mengine, msingi wake ni usawa wa binadamu.” Dhana ya Ujamaa iliendelea kuenea katika miaka iliyofuata, ikichanua katika mawazo ya Mwalimu kila uwezo wake ulivyoongezeka katika Serikali na katika dunia. Katika mawazo yangu, matukio mawili yasiyohusiana ya mwaka 1965 yalitoa changamoto muhimu katika maendeleo ya baadaye ya Ujamaa. Mwaka ule Rais alifanya ziara yake ya kwanza, lakini hiyo ikazaa nyingine nyingi, kwenda China ya Mwenyekiti Mao. Karibu wakati huohuo, Ian Smith akafanya kufuru ya kujitangazia Uhuru kwa niaba ya watu wa Rhodesia, na hivyo kuitumbukiza Jumuiya ya Madola katika matatizo, na kuzaa mfarakano mkubwa kati ya nchi zilizokuwa zinatumia lugha ya Kiingereza Barani Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, na huyo Mtawala wao wa zamani. Hakuna mahali popote katika Afrika, labda ukiacha Rhodesia, ambako hatua za haraka-haraka za kutambua Utawala wa Smith zilikubalika. Lakini dhahiri hisia za Tanzania ndizo zilizokuwa kali kuliko zote, ilipodhihirika kuwa mazungumzo yale yaliyofanyika katika meli ya Tiger, na kwa kweli haukuwako uwezekano tena kwa kila jambo jingine ambalo Serikali ya Wilson ilikuwa ikifanya, ukiacha hasira za pamoja dhidi ya Sera hiyo kukubalika po pote. Mwalimu akaamuru mara moja kuvunja Uhusiano wa Kidiplomasia na Uingereza. Kwa kufika hapo Tanzania, nchi peke yake kati ya nchi zote za Afrika zilizokuwa zinatumia lugha ya Kiingereza, Mwalimu akasababisha kupungua zaidi kwa uwezekezaji wa Waingereza uliokuwa tayari unapeperushwa, na kwa biashara na Tanzania ambayo kwanza, lazima tukiri, ilikuwa ndogo tu. Kwa

Page 119: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

119

uchumi ulioimarika hatua kama hizo zisingelisumbua sana, ukitambua kwamba Waingereza hawakupata kushabikia Uchumi wa Tanzania kwa nguvu kama walivyofanya Kenya na hata Uganda. Lakini katika hali ya kutisha ya Uchumi wa Tanzania, katikati ya miaka ya 1960, nakisi iliyotokea katika miaka hiyo miwili ya kuvunja Uhusiano na Uingereza, na athari zake zilizoendelea kwa muda mrefu zaidi, hazikuweza kuondoka kwa haraka, pamoja na misaada yote iliyopatikana kutoka Nchi za Scandinavia, Uchina na Nchi za Mashariki, iliyotolewa kama fidia. Kuivunjika kwa Uhusiano kulifikisha Tanzania kwenye njia panda kati ya nchi inayoinukia, ambayo bado inategemea sana nguvu za Wakoloni, na nchi changa inayojiamini katika Ukanda wake; inayojiandaa kuchukua nafasi yake kama Nchi ya Mstari wa Mbele, na Shujaa wa Mfumo Mpya wa Uchumi wa Kimataifa. Lakini vile vile, kwa maoni yangu, ilikuwako tofauti kubwa mno kulinganisha na falsafa ya Mwalimu katika masuala ya Uchumi. Matokeo ya kufarakana na London yakamfanya atambue kwamba sasa hana cha kupoteza, na kama anacho kitakuwa kidogo mno kitakachotokana na hatua hizo kali za mikasa ya Taifa. Wakati Uingereza ilipokuwa inatoweka kabisa katika mawazo, Mwalimu hatimaye akawa huru kupanga mwelekeo wake wa Ujamaa katika usafi wake wote, bila ya hofu ya visasi vya kisiasa au vya kiuchumi kutoka London. Mazingira magumu yalidai hatua za kimapinduzi. Kwa hiyo, kwa mawazo yangu mimi, haikuzuka tu kwamba Azimio la Arusha lilizaliwa katika kile kipindi cha miaka miwili cha kuvunja uhusiano na London. Februari 5, 1967, baada ya Mkutano wa siku nne wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU, katika mji ule mzuri wa Kaskazini. Sehemu nyingi za mawazo ya Mwalimu kuhusu Ujamaa wa Mwafrika hatimaye zikaingia kitabu hicho kimoja cha Sera. Azimio lenyewe la Arusha lilikuwa na kurasa mbili tu, lakini kishindo chake kwa hatima ya Tanzania ikawa nzito kweli kweli; maana mnamo siku chache tu mawimbi yake yakawa tayari yanadhihirika Serikalini na katika shughuli za watu binafsi. Katika miaka michache iliyofuata, filosofia ya Taifa ya Kujitegemea

Page 120: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

120

iliyosisitizwa katika Azimio la Arusha ilianza kutekelezwa mfulilizo katika Sheria, Mipango ya Maendeleo, na mabadiliko makubwa ya Sera yaliyogusa maisha ya kila Mtanzania. Mtu akilisoma Azimio hilo sasa, miaka arobaini toka liandikwe hisia za kuunung’unikia umasikini wa Tanzania zinajitokeza katika kila mstari. Fedha hakuna; maendeleo ya Viwanda ni duni; watu wenye taaluma ya Ufundi ni wachache; nchi karibu ifikie hali ya kufilisika na kuwa tegemezi moja kwa moja; wala hakuwako mtu angalau aliyekaribia kuvumbua namna ya kuondokana na hali hiyo. Kwa mujibu wa Azimio la Arusha, kutegemea fedha halikuwa jibu la matatizo. “Ni dhahiri kwamba, huko nyuma, tulichagua silaha isiyofaa kwa Mapambano yetu, kwa sababu tulichagua fedha kuwa ndiyo silaha. Tunajaribu kuondoa udhairu wetu katika Uchumi kwa kutumia silaha za wale wenye nguvu za Uchumi”. Hata kutegemea misaada kutoka nje halikuwa jibu. “Tunakosea tunapodhani kuwa tutapata fedha kutoka katika nchi za kigeni, kwanza kwa sababu, kusema kweli, hatutaweza kupata fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo yetu; na pili kwa sababu, hata kama tutazipata, kutegemea misaada namna hiyo kutoka nje kungehatarisha Uhuru wetu na Sera nyingine za nchi yetu.” Wala maendeleo ya viwanda siyo jibu, “Hata kama tutapata misaada yote tunayoihitaji, pamoja na maendeleo ya Viwanda, kutegemea kwetu kwa misaada hiyo kungeweza kuathiri Sera yetu ya Ujamaa” Kwa hiyo, badala yake, Azimio lilielekeza Kazi kwa bidii, kutumia akili, na ardhi, kuwa ndizo Nguzo za Maendeleo ya baadaye ya nchi hii. Haya yote yalielezwa vizuri, kwa kifupi, katika Hotuba iliyosema, “Kuanzia sasa na kuendelea tutasimama wima na kutembea kwenda mbele kwa miguu yetu wenyewe, badala ya kuliangalia tatizo hili miguu juu kichwa chini. Viwanda vitakuja, na fedha kadhalika; lakini msingi wake ni Wananchi na jitihada zao katika kazi ngumu, hasa katika Kilimo. Hiyo ndiyo maana ya Kujitegemea”. Kishindo cha Azimio kilidhihirika nchini na duniani kote maana, ukiacha vuguvugu la ndani lililotokana na Sheria na amri

Page 121: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

121

zilizozaliwa na Azimio, maandishi hayo yakawa ndiyo hatua ya kwanza ya kuthibitisha fahari ya Mwalimu, au wengine wangesema utukufu wake, katika Mjadala wake wa kwanza kuhusu Utaratibu Mpya wa Uchumi wa Kimataifa. Nchi za Nodik waliokuwa, na ndio mpaka sasa, wanaoongoza duniani kwa kutoa Misaada ya Maendeleo, wakawa watu wenye ari zaidi ya kuisaidia Tanzania, baada ya Azimio la Arusha. Azimio lile liliimarisha mshikamano uliokuwapo na Nchi za Kijamaa za Ulaya na Asia, pamoja na Cuba. Mji wenyewe wa Arusha ukapanda hadhi kiasi cha ajabu; haukuwa tena uwanja wa senema za John Wayne kama ulivyokuwa mwanzoni mwa miaka ya 1960, lakini ukawa alama ya Haki za Jamii zilizokusanya maelfu ya Mikataba ya Wasomi, ikisukuma mbele mambo ya kuigwa duniani kote, na hata kusababisha kuwako kwa Kituo cha Arusha cha Haki za Jamii kinachodumu mpaka sasa huko Alberta, Canada. Lakini, dhahiri, nilihusika zaidi na matokeo ya Azimio huku karibu na nyumbani. Wafanyabiashara wakiwa tayari na wasiwasi, walikuwa sasa wanatangaza rasmi kuwa vurugu kubwa sana katika taratibu za Uchumi zilizokuwako sasa zinakaribia. Hali hiyo isingekuwa ya kushangaza; maana, wakati kipindi cha miaka ya 1960 kilikuwa angalau kipindi cha ongezeko kubwa la shughuli za ujenzi na chakula, pamoja na zangu mwenyewe za Chande Industries Limited, haiwezekani kuficha ukweli kwamba Taratibu za Soko, haki zile za nafuu zilizokuwa zinafanya kazi nchini Tanzania, zilikuwa kikwazo kwa Viongozi wa TANU na kwa Wanachama wao vile vile. Tayari, katika miezi iliyotangulia, nilipokea barua nyingi kutoka kwa Mawaziri wa Serikali kunikumbusha mwelekeo niliopaswa kuufuata katika kukodisha, kuanzisha au kuingiza bidhaa. Nawakumbuka sana Mawaziri wawili, wa Fedha na wa Viwanda, waliponishauri na kunisisitizia kwa nguvu kutafuta Biashara kwa mapana zaidi, yaani nising’ang’anie kununua vya Waingereza wakati nikiagiza Vinu vya kusagia kutoka ng’ambo. Mazungumzo yaliyokuwa yanazidi kuenea mjini Dar es Salaam yalikuwa na mwelekeo wa kutaifisha Sekta muhimu za Uchumi.

Page 122: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

122

Mnamo saa ishirini na nne baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha, nong’ono baada ya nong’ono zilizagaa mjini Dar es Salaam. Kabla ya hapo, mimi na Jayli tulipanga kusafiri kwenda Mauritius, kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Tulipokuwa huko nilipangiwa kusimamia Mkutano wa Chama cha Round Table katika Mashariki ya Afrika, lakini hali hii mpya ilinilazimu kufuta mipango hiyo. Ilikuwa bahati yangu kufanya hivyo, maana mchana wa Februari 9, siku nne tu baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha, nilitakiwa kupiga ripoti kesho yake katika Ofisi ya Waziri wa biashara, saa tano kamili.

________________

Page 123: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

123

SABA

MATATIZO YA UTAIFISHAJI Sikupata usingizi wa kutosha usiku wa Februari 9. Pamoja na kwamba nilikuwa nimechoka na mwenye wasiwasi, nilikwenda kazini asubuhi yake kama kawaida Ofisini kwangu kwenye eneo la Viwanda vya Kusindika, Barabara ya Pugu. Nikasimama kwenye zuria mbele ya meza yangu, nikiangalia maeneo ya barabarani yanayokabiliana na reli mpya ya TAZARA, nikitafakari nini kitakachotokea tena. Haukupita muda nikagundua. Muda mfupi kabla ya saa tano mchana nilifika kwenye lango la Wizara ya Biashara, nikaelekezwa kupanda ghorofani kwenye chumba cha Mikutano. Kule, upande mmoja wa meza, wakakusanyika wenzangu wengi waliokuwa wanahusika na Viwanda vya Usagishaji. Jack Jones, Msimamizi wa Makampuni yaliyokuwa makubwa kuliko mengine yote, na Kiongozi wa Kampuni hiyo moja tu iliyokuwa kubwa kuliko zote, alikuwako, kama walivyokuwako Wawakilishi wa Viwanda vingine sita vya kusaga. Upande wa pili wa meza vilikuwako viti viwili, vitupu. Mara viti hivyo vikajazwa na Abdulrahman Babu, Waziri wa Biashara, na Afisa mmoja kutoka katika Wizara ya Mambo ya Ndani. Wakati huo nje tu ya lango, mtu aliyekuwa na mavazi ya kawaida alionekana akizurura; alidhaniwa kuwa Polisi, lakini kwa hakika alikuwa Afisa Usalama. Mara baada ya mtu huyo kuingia na kukaa kitini, Waziri Babu akaufungua Mkutano bila kusubiri. Alitusalimia kwa Kiingereza, kisha akakamata Karatasi iliyokuwa mbele yake. Ilikuwa Hotuba fupi iliyoandaliwa kueleza kuwa, kuanzia saa sita mchana siku ile, Hisa zote za Kampuni zetu za kusaga zilikuwa mikononi mwa Msajili wa Hazina. Wanahisa waliokuwapo waliahidiwa kupewa fidia kamili na ya haki. Huo ndio ukawa mwisho; Babu akaufunga Mkutano ghafla, kama alivyoufungua. Kampuni zetu zote zikawa zimetaifishwa mnamo muda mfupi wa chini ya dakika moja. Upande wetu wa meza sisi sote tulikazana kuangalia mbele kwa mshangao, tukiwa kimya! Nikamwangalia Waziri Babu aliyekuwa

Page 124: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

124

amevaa shati la mikono mifupi, nami nikamwona anaangalia paketi ya sigara za Sportsman mbele yake, mezani. Kisha upande wangu wa kushoto, Jack Jones akasimama ghafla na kuanza kuzungumza, “Je, tunaruhusiwa kuuliza maswali?” Alionekana amefadhaika, kama pengine hakukasirika. Babu akajibu, kwa sauti ndogo, “Hakuna maswali,” huku akinyosha mikono yake kushika pembe za meza. Na mimi nikauliza, “Je, tunaweza kupata angalau nakala ya Tamko hilo? Mimi nitaitaka ili niweze kumweleza kwa usahihi Mhe. Janus Simpson, Mwenyekiti wa Kampuni yangu kule Uganda”. Babu akatazamana na wenzake kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, nao wakatazamana kwa muda, kama kupembua mawazo yao mbele na nyuma, kisha akamwinamishia kichwa pole pole Waziri mwenzake. Akaturudia sisi na kunijibu mimi binafsi akisema, “Vema.” Watu wawili waliokuwa upande mwingine wa meza wakasimama na kuondoka Mkutanoni, kuandaa makala za Tamko. Kwa kuwa walikwenda kwenye Ofisi ya Serikali ya Tanzania mwaka huo wa 1967, iliwachukua muda mrefu mno kuchapisha nakala hizo kuliko ilivyowachukua kuziandika na kuelezea Ujumbe wake. Wakati Babu na Ujumbe wake walipotoka katika chumba, mazungumzo yakawa machache sana kati yetu sisi wanane tuliokuwa bado tumeduwaa upande wa pili wa meza. Wote sisi tulishituka, na tena kila kitu ambacho mtu angalitaka kusema kilikwisha semwa. Ndipo hatimaye tulipoondoka katika Jengo la Wizara dakika chache tu kabla ya saa sita, wote tukizing’ang’ania bahasha zetu zilizokuwa na nakala za lile Tamko la Babu. Kila mmoja aliondoka na njia yake, bila kusimama au kubadilishana mawazo; na nilipofika Ofisini, nikawakuta Polisi wenye silaha wamepangwa kuzunguka jengo letu. Nilikuwa na hakika kabisa kuwa hawakuwako Polisi pale nilipoondoka saa nne na nusu; kuwapo kwao wakinizunguka sasa hivi, kimya kimya lakini ni bughudha, ilikuwa ishara nyingine ya kuthibitisha kwamba Serikali isingebahatisha kuachia Sera hii ya utaifishaji iende kombo.

Page 125: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

125

Jambo la kwanza nililofanya nilipofika Ofisini likawa kuzungumza na ndugu yangu, Chuni, kumweleza yote yaliyotokea. Kisha nikapiga simu Kampaka kwa Mhe. James Simson, aliyeijua vema Tanzania baada ya kazi katika viwanda vya Mafuta nchini Tanzania kabla ya Uhuru. Lakini majibu yake kwa simu niliyompigia siku hiyo yalidhihirisha kutoelewa kwake kabisa hali ilivyokuwa. Nilipomweleza asubuhi yake yote yaliyotokea, pamoja na kwamba Walinzi wenye silaha wamepangwa kulizunguka jengo, maneno yake ya kwanza yakawa, “Huu ni wizi wa moja kwa moja!” Baadaye akanishauri niende mara moja kuonana na Rais na kujua kutoka kwake hasa Sheria gani iliyompa haki ya kutaifisha moja kwa moja Kiwanda cha Kusindika. Kufika hapo, kwa kuelewa maandalizi makubwa Serikali iliyoyafanya, ambayo lazima ni pamoja na kutegea simu nilizokuwa napiga, nikafunga simu. Lakini mnamo muda mfupi wa kama dakika mbili, Mhe. Simson asiyechoka akapiga simu, akilalamika kuwa mazungumzo yetu yalikatishwa. Hapo nikamweleza kuwa, hata kama haiko Sheria inayoridhia wazi wazi kutaifisha kwa Kiwanda cha Kusindika, haitachukua muda mrefu kuitunga na kuipitisha. Nikazima simu tena na, badala yake, nikamtafuta Jayant, kakiye Jayli, aliyekuwa Uganda . Kama sifa kubwa mno kwao, yeye na mdogo wake Manubhai walielewa mara moja ukweli wa hali halisi. Kwanza Rais Milton Obote wa Uganda amekuwa akizungumzia kwa muda mrefu hatua kama hizo hizo alizoziita Mkataba wa Mtu wa Kawaida, ambao ungekusanya Nguzo zote za Uchumi na kuzifanya Mali ya Nchi. Akanihakikishia kuwa Ukoo wa Madhvani ungefanya kila wanachoweza kunisaidia; wangeleta ndege kutoka Uganda, angalau kuchukua vitabu vya Kampuni nyingine ndogo katika kundi lao zilizokuwa na Makao Makuu yao katika Jengo langu, kama vile Kilimanjaro Breweries. Vile vile angezungumza na Edgar Wadley, Mhasibu mwenye shahada aliyeko Uingereza, aliyemfanyia kazi huko nyuma. Kama lilikuwako lingine lo lote lililohitajika kutendeka kwa upande wa mtaji, pengine Edgar angetambua. Jayant akazima simu, nami nikafikiria namna ya kuhamisha makaratasi Ofisini kwangu. Nikagonga kengele ya mezani kwangu

Page 126: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

126

kumwita Karani wa Ofisi; hakuna aliyekuja. Nikagonga tena na, ilipokuwa hakuna aliyetokea ukweli wa yale yaliyokuwa yananikabili hatimaye ukadhihirika, ukilipuliwa, kama ilivyo mara nyingi, siyo na tukio lo lote kubwa, bali lililo la kawaida kabisa. Nikavuta pumzi na kusimama, nikachungulia tena dirishani mkabala na stesheni ya TAZARA. Mimi na ndugu zangu sasa tukawa katika hali moja ya fedha au, ukitaka, katika kijito hicho hicho bila makasia, maana hakuwako kati yetu aliyekuwa na akiba ya maana katika Benki, kwa jinsi tulivyozoea kuchukua fedha kutoka kwa Mhasibu wa Kampuni kila tulipozihitaji: Mhasibu wa Kampuni ndiye aliyekuwa Benki yetu, akipokea mishahara yetu ya mwezi na kulipa madeni kwa niaba yetu. Ndugu yangu alikuwa mdogo kwangu, hajaoa bado; pengine mjanja zaidi kuliko mimi. Lakini, tofauti na mimi, alikataa kutumia nafasi iliyotolewa baada ya Uhuru kuomba Uraia wa Tanzania, akapendelea kubaki raia wa Kiingereza, akiwa na Pasi ya Kiingereza ya kusafiria. Sasa, kwa chuki yake kutokana na Uamuzi wa Serikali kututaifisha, haikumchukua muda kuamua juu ya hatua inayomfaa kuchukua, akaamua kuondoka Tanzania kabisa. Baada ya kumpigia simu Jayli kumjulisha yaliyotokea, nikabaki katika Ofisi yangu Barabara ya Pugu, mpaka kiasi cha saa moja usiku, nikiyatenganisha makaratasi yangu binafsi na yale ya biashara za Kampuni zangu zilizokuwa na Makao Makuu yake kule. Nikitambua sana kuwako bado kwa Walinzi wenye silaha nje ya Jengo, sikufanya tena jitihada za kutoa makaratasi yangu Ofisini jioni ile, badala yake nikayarundika juu ya meza yangu. Nilitambua fika kwamba nilikuwa nachunguzwa, na kwamba rasmi nilikuwa nafuatiliwa. Lazima nikiri kwamba nilipofika nyumbani jioni nilikuwa karibu nakata tamaa. Akili yangu haikuwa imetulia, na aina zote za dhana za kipuuzi zikajaa kichwani mwangu. Picha moja iliyokuwa inanirudia mara kwa mara ilikuwa ile ya Baba yangu, na jinsi kila kitu alichokifanikisha nchini Tanzania, kwa niaba ya familia, kilivyoyeyuka. Katika kipindi cha zaidi ya miaka arobaini na saba,

Page 127: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

127

vizazi viwili vya familia yangu vilihangaika sana, vikijitahidi kuimarisha biashara kwa misingi ya uangalifu na kuwatendea haki Wafanyakazi na Wauzaji wa malighafi, katika hali ambayo leo ingeitwa nidhamu ya kushirikiana. Kama walivyo Wafanyabiashara wengi tulirudisha kwenye Kampuni karibu kila senti tuliyoivuna, tukiangalia kukua kwa biashara ya baadaye, kuliko mawazo yo yote ya matumizi yetu sisi wenyewe. Jitihada zetu zikazaa matunda mengi lakini nayo tena yakarudishwa kwenye biashara; na sasa mafanikio hayo yamenyakuliwa na Dola, kama tunda linaloning’inia! Nikajikuta nashangaa kama Imani yangu juu ya ridhaa ya Nchi ya Tanzania kuniacha niendelee na shughuli zangu bila kizuizi cho chote ilikuwa dalili ya ushamba wangu mkubwa. Kwanza, angalau ndugu yangu alikuwa na hisia kiasi cha kuweza kuhofia mikasa ya baadaye, mpaka akaing’ang’ania passport yake ya Kiingereza. Lakini, kinyume chake, mimi nikawa raia kamili wa Tanzania, bila kutegemea ngome yo yote ya siku zijazo. Hayo ndiyo yaliyokuwa mawazo yangu niliporudi nyumbani jioni ile; niliona kana kwamba dunia ilikuwa inanifunika. Sikuweza tena kuchambua nini hasa nilichokuwa nakifikiria. Lakini Jayli akanisaidia nisipoteze mwelekeo, nilipokuwa nikipiga hatua ovyo chumbani na kujitumbukiza katika wazimu usiokuwa na sababu. Alizungumza nami usiku kwa utulivu, kwa hakika na kwa akili na, kila saa zilivyokwenda, busara, ushawishi na uthabiti wake ukaweza kunirudishia Imani yangu. Wakati fulani katika mazungumzo yetu marefu ya usiku, alisema kwamba kile Mwenyezi Mungu alichopenda kukichukua lazima atakurudishia siku moja. Nikaanza kukumbuka kuwa, kumbe, maisha lazima yawe na sababu ambayo Mwenyezi Mungu ameipanga; kwamba nimekumbana na matatizo huko nyuma na nikayashinda, na kwamba ni muhimu kwangu sasa kutulia na kuepuka maamuzi ya papara yatakayonifanya nijute daima. Zaidi ya yote, Jayli alinisaidia kukumbuka kwamba elimu ya watoto wetu, iliyo muhimu sana duniani humu kwetu sisi wote wawili, tayari imedhaminiwa na Mfuko aliuouanzisha Baba Mkwe kwa madhumuni hayo. Kitu

Page 128: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

128

kingine cho chote chenye umuhimu mdogo zaidi kitawekwa kwenye nafasi yake kwa jinsi siku zinavyokwenda. Kwa kutulizwa hivyo, nikaenda kazini kesho yake kama kawaida, nikafika Ofisini mnamo saa tatu asubuhi bado nikakuta Jengo limezingirwa na Walinzi wenye silaha. Ndani Ofisini kwangu, mtu mmoja nisiyemjua alikuwa karibu na meza yangu, ameinama akichambua kwa uangalifu makaratasi niliyokuwa nimeyatupa kikapuni. Nilipofika mlangoni, wakati naingia, akasimama haraka na kuja kwangu kujitambulisha. Akataja jina lake kuwa ni Hieronimus Msefya, na kwamba ndiyo kwanza ameteuliwa na Rais kuwa Mwenyekiti wa Kampuni yangu! Nikamwuliza kama angetaka kutembeatembea na kukutana na Wafanyakazi, akajibu “Hapana, nataka kukutana na wewe kwanza.” Nikatumia muda mrefu wa saa nzima iliyofuata kuzungumza na Msefya; nikatambua mara moja kwamba Uteuzi wake ulikuwa wa Kisiasa akiwa Mbunge wa zamani asiyekuwa na uzoefu wo wote katika masuala ya Viwanda vya Usindikaji. Alikuwa mtu mcheshi, asiyeonyesha dalili zozote za uhasama, wake yeye mwenyewe au wa kushinikizwa, dhidi yangu. Baada ya kuondoka Ofisini siku ile, bila hata kujitambulisha kwa Wafanyakazi wengine, nilimwona kwa nadra sana kufika kwenye Jengo letu. Baada ya kuondoka kwake, nikaendelea na kazi ya kuyapanga makaratasi yangu kwa utaratibu. Wakati huo, katika Ukumbi wa Karimjee, Bunge lilikuwa linakutana na utabiri wangu niliompa Mhe. James Simpson jana yake ulikuwa unathibitika. Katika Mkutano wa dharura, Muswada wa Sheria mpya ya kutaifisha Viwanda vya Usindikaji ulikuwa unawasilishwa na Waziri wa Biashara Abdulrahman Babu. Muswada huo ulikuwa unamainisha, sawasawa na lile Tamko la jana yake, kwamba fidia kamili na ya haki, italipwa kwa Wanahisa wote wa Kampuni za Usindikaji. Ukaendelea kusisitiza kuwa mishahara na marupurupu ya wafanyakazi wa Viwanda vinavyotaifishwa hayatakuwa mabaya zaidi ya yale yaliyokuwako zamani. Muswada ukaishia kwa kuwaomba wenye Viwanda na Watendaji wakubaliane na mahitaji hayo ya Taifa kwa kuhakikisha makabidhiano mazuri kutoka Utawala wa zamani na kuingia huu mpya.

Page 129: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

129

Majadiliano ya Muswada huo yalikuwa kama kutimiza wajibu, na ukapitishwa kwa kauli moja siku ile ile kuwa Sheria. Niliposikia hivyo katika radio jioni yake, sikuweza kuficha tabasamu yangu ya kulazimisha. Laiti ningalipokea nafasi niliyopewa na Mwalimu kugombea kwa tikiti ya TANU Kiti cha Ubunge cha Tabora, ningalishiriki katika zoezi hili la kujifilisi mwenyewe. Siku iliyofuata nilikua tayari kuanza kazi yangu tena. Nikaitisha Mkutano wa Wafanyakazi kuzungumza nao juu ya Mipango yangu ya baadaye, lakini vile vile kusikiliza matatizo yao. Nikakuta kuwa wale Wafanyakazi wa Kiasia walikuwa bado na wasiwasi, wakihofia hatima yao nchini humu; lakini Waafrika walikuwa na matumaini zaidi: kwa kweli baadhi ya Wafanyakazi wa Kiafrika walizishangilia habari kwamba Serikali ilikuwa imeanza kushika hatamu za njia za uchumi, hivyo hawakuona tena sababu ya kufanya kazi zao za kila siku. Mchana wa siku ile, Jumatano nikaitwa Ikulu kukutana na Rais. Tofauti na ilivyokuwa huko nyuma nilipofika kwake, nyumbani au Ofisini, Mwalimu alikuwa amekaa kitini kwake katika Chumba cha Mkutano cha Baraza la Mawaziri, na kijana wa kuandika kumbukumbu yuko kitini kwenye kona. Na, isivyo kawaida kwa Rais huyo wa Tanzania, Mwalimu hakusimama nilipoingia, badala yake akanielekeza kukaa katika kiti kilichokuwa karibu naye. Akauanza Mkutano kwa kunitaka radhi, akiniambia jinsi alivyosikitishwa kwa kulazimika kufikia Uamuzi wa kutaifisha Kampuni yangu. Lakini nilipaswa kujua kwamba shughuli za Usagishaji za kununua nafaka kutoka kwa Wakulima ili kuwauzia watumiaji zilikuwa na nafasi kubwa katika kupatikana kwa chakula cha kawaida cha Watanzania. Kwa mujibu wa Azimio la Arusha, eneo hili la Uchumi lilipaswa kuwa chini ya umiliki wa Umma. Hiyo ndiyo sababu ya kutoa uamuzi wa haraka wa kutaifisha. Akaendelea kuniuliza juu ya Mipango yangu ya baadaye, akitaka kujua kama nilikuwa na mipango yoyote na, kama nilikuwa nayo, iko wapi!

Page 130: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

130

Nikajibu kwa kusema kwamba, kwa mawazo yangu, Mwalimu alikuwa amefanya kosa kubwa. Kutaifisha Makampuni halikuwa jibu la matatizo ya Uchumi wa Tanzania; lakini Historia itaamua nani kati yetu aliye sahihi. Dhahiri Mwalimu alisikitishwa na jibu hilo, akadakia, “Usijali Historia; wewe unataka kufanya nini? Kama unataka cheo Serikalini, labda katika Ubalozi; nina hakika hayo yanaweza kutekelezwa haraka” Ikawa zamu yangu kutoa jibu jepesi. Sikuwa nawazia kufanya kazi Ubalozini, kwanza siku chache zilizopita nilikataa kazi niliyoipewa katika UNIDO. Nikasema, “Nataka kuendesha Kampuni hii, kwa muda wowote nitakaoruhusiwa kufanya hivyo”. Mwalimu, akitabasamu kwa jibu hilo, akasema, “Endelea; kisha akaongeza kuwa hatua zitachukuliwa kuhakikisha kuwa madai ya familia kuhusu fidia yatashughulikiwa kwa ukamilifu, kwa haki na kwa haraka. Nikarudi Ofisini kwangu na kukuta Wafanyakazi wangali wanasherehekea Ubinafsishaji zaidi kuliko kurudi kufanya kazi. Nikaita mara moja Mkutano wa Wafanyakazi na kuwaambia, “Ndiyo, Kampuni hii sasa ni mali ya Umma, lakini maana yake ni kwamba ni mali yetu, ninyi na mimi. Kama Wafanyakazi watashindwa kufanya kazi kama walivyokuwa wanafanya zamani, basi nafasi yangu haitaweza kuthibitishwa; nami nitalazimika kurudi kuzungumza na Rais ambaye, labda, ataleta mtu mwingine kuendesha shughuli hizi. Nikawatuma Wanyapara kwenda kuzungumza na Wafanyakazi na kuwaeleza hayo yote. Wakaenda; na, tokea wakati huo, wafanyakazi wakanywea: wakafanya kazi kwa bidii, bila kungoja tena kukumbushwa Wajibu wao. Ulipofika mwisho wa siku nyingine, nikawa nimechoka tena; lakini, ingawa haikudhihirika kuwa tumerudi kazini kama kawaida, na pengine haitatokea tena kwa muda mrefu sana, angalau iliweza kuendelea kwa juma zima katika hali iliyokuwa karibu sana na hali ya kawaida. Siku iliyofuata kazi zangu zilikatishwa na wito mwingine, safari hii Waziri wa Fedha, Amir Jamal, Mtanzania mwenye asili ya Kihindi. Amir alikuwa swahiba mkubwa sana wa Rais, kutokana na urafiki

Page 131: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

131

ulioimarika baada ya Amir kugharimia Mawakili waliomtetea Mwalimu katika kesi yake ya mwaka 1958. Kuitwa kwangu na Amir kulichukua sura ya makaribisho ya kula naye chakula cha mchana mnamo saa tisa na nusu alasiri, nyumbani kwake Seaview. Nilimtaarifu kuwa nilikwisha kula, lakini hata hivyo ningehudhuria. Jitihada za Amir kuuanzisha Mkutano huo katika sura ya urafiki bila kuwa na urasimu mwingi hazikufanikiwa sana. Aliponiambia kuwa alisikia nilikwenda kuonana na Rais jana yake, nikamwambia kuwa niliitwa Ikulu, wala sikujipelekesha kupiga soga. Alipogundua kukasirika kwangu, Amir akageukia haraka kwenye shughuli aliyoniitia. Rais alimtuma kusimamia kwa haraka malipo ya fidia wanayostahili kupata familia ya Chande. Kamati ingeundwa kwa kazi hiyo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Amon Nsekela, atawasiliana nami haraka kunipa maelezo zaidi juu ya Uanachama, misamaha, na mambo kama hayo. Nikamshukuru Amir kwa Taarifa hiyo, na nikasubiri wito wa Nsekela. Lakini kitu ambacho Amir alishindwa kunidokezea ni kwamba yeye mwenyewe alikwisha kuwa Mhasibu Mkuu wa Chande Industries Limited kukataa kuwasilisha, kwangu au kwa ndugu yangu, fedha zozote mpaka atakapopata Amri nyingine. Maagizo kama hayo hayo yalikwenda kwa Wahasibu wa Kampuni nyingine zote za Usindikaji zilizotaifishwa. Haikunishangaza kuona ile Kamati ya kusimamia “malipo ya haraka” ya madai ya familia yangu ikiteuliwa mara moja. Hatimaye, baada ya kucheleweshwa kwa majuma kadha, Naibu Katibu wa Hazina akateuliwa Mwenyekiti, na Mwakilishi mmoja kutoka Wizara ya Fedha, na mwingine kutoka Wizara ya Viwanda, wakaongezwa kama Wajumbe. Mjumbe wa mwisho kuteuliwa alikuwa Steen Harisen, Mhasibu kutoka Denmark aliyeazimwa na Serikali ya Tanzania kutoka Serikali ya Uholanzi, na ambaye baadaye akawa Mkurugenzi Mkuu aliyelianzisha Shirika la Ukaguzi la Tanzania. Hizi hazikuwa habari nzuri kwangu, nikijua sifa ya Hansen iliyoenea kuwa mtu wa nadharia tu, mwenye mwelekeo wa visasi katika suala hili la fidia.

Page 132: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

132

Wakati huo Maagizo aliyopewa Bwana Fedha asinipe fedha zo zote yalikuwa yanazingatiwa kwa ukamilifu, na maana yake ni kwamba wala kaka yangu wala mimi mwenyewe hatukuwa na fedha zo zote kukidhi maisha yetu ya kila siku. Marafiki, hasa Waafrika na Wazungu, walikuwa upande wetu. Mwanzoni marafiki zangu wengi wa Kiasia, labda kwa hofu ya kutiwa hatiani, wakaepuka kushirikiana na sisi. Lakini jitihada za marafiki zisingeweza kuwaondoa mlangoni hao manyang’au wa fedha. Hapo, kwa mara nyingine, familia ya Jayli ikajitumbukiza tena kuokoa jahazi. Kaka zake wakaleta cheki mbili, kila moja shilingi elfu ishirini za Tanzania: moja yangu na moja ya ndugu yangu, kuchukuliwa kutoka Standard Bank ya Afrika Kusini kule Jinja. Fedha hizo, pamoja na misaada iliyokuwa inatolewa na marafiki zetu wengi wa Dar es Salaam, ndizo zilizoinusuru familia yetu mpaka hapo jibu la maana zaidi kuhusu mkasa wetu wa fedha lilipopatikana. Kabla haujapita muda mrefu, hatua zile zile za utaifishaji zilizoniumiza mimi, kwa mshangao mkubwa zikawa chanzo cha ajira yangu ya ziada. Hatua za kutaifisha Mabenki zilichukuliwa mara baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha na, kwa sababu ilizozijua Serikali ya Tanzania peke yake huenda kutokana na kuteuliwa kwangu mwaka 1966 kuwa Mwenyekiti mtarajiwa wa Bodi ya Afrika Mashariki ya Barclays Bank, DCO, nikaombwa kushika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki mpya, National Bank of Commerce. Niliikataa nafasi hiyo kwa hoja kwamba, mpaka muda mfupi tu uliopita, sikuwa na akiba yo yote katika Benki. Lakini Serikali ikang’ang’ania kunihitaji nishirikishwe, hivyo hatimaye nikakubali kuwa Mjumbe katika Bodi mpya, kwa Wadhifa wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mikopo. Kaimu Meneja Mkuu wa kwanza wa Benki mpya, Robert Scott, alifanya kazi katika Benki Kuu, hivyo hakuwa na uzoefu mkubwa katika masuala ya Biashara. Mara ikadhihirika kwamba Uingereza wake na uzoefu wake mdogo haukuiridhisha Serikali ya Tanzania, na haraka haraka Scott akawekwa pembeni, akachukuliwa badala yake mzoefu wa Benki Kuu, safari hii mtu wa Denmark , aliyeitwa Jacobson. Huyo alifanya kila aliloliweza katika mazingira hayo

Page 133: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

133

lakini, kama alivyokwama Scott kabla yake, akakuta maamuzi yake kila mara yanatiliwa mashaka na Bodi, ambayo wakati ule ilikuwa na watu kama Profesa Konradsen wa Scandinavia, ambaye mawazo yake katika Uchumi yalimsaidia Mwalimu kuonekana kuwa Bingwa wa mambo ya fedha, na Profesa Reginald Green; msanii, na wengine wangemuita tapeli, aliyetumika kwa miaka kadha kwa kuazimwa na Serikali za Afrika Magharibi na za Afrika Mashariki kwa ufadhili mkubwa wa Ford Foundation. Kuna Kitabu kilichoandikwa juu ya ushawishi wa watu kama Prof. Green kuhusu Afrika katika miaka ya 1960, lakini siyo hiki; wala mimi sitaki kabisa kuwa mtu wa kukiandika. Pengine inanitosha kudokeza hapa kwamba, angalau kwa mawazo ya Wafanyabiashara wa Dar es Salaam wa miaka ya 1960 na 1970, Wasomi kama Green, hodari lakini wasiokuwa na uzoefu, na wakati mwingine wanaopoteza mwelekeo, wametoa picha isiyokubalika kuhusu baadhi ya Hatua tulizokuwa tunazijaribu kwa jina la Ujamaa wa kiafrika. Matatizo yaliyokuwa yanaendelea kati ya Konradsen na Bodi iliyokuwa inaongozwa na mwenyekiti wake Nsekela, yalimsukuma Mwenyekiti huyo wa Bodi kunitafuta nimsaidie kumtafuta Mtendaji Mkuu mpya mwenye uzoefu. Nikawatumia marafiki zangu wa Marekani na Ulaya, pamoja na David Rockfeller wa New York, na Francois Gavotty wa Paris. Gavotty akapendekeza kwangu jina la Jacques Gerbier, Meneja wa Benki aliyepata uzoefu katika Banque Nationale de Paris, (Benki ya Taifa ya Paris) aliyeweza kukisema Kiingereza vizuri. Huyo Gerbier alikuwa ndiyo kwanza amemaliza Mkataba wake nchini Madagascar, kwa hiyo alikuwa tayari na uzoefu wa kufanya kazi Barani Afrika, lau kama katika nchi yenye watu wanaotumia lugha ya Kifaransa. Baada ya Gabier kusailiwa na Balozi wa Tanzania, Obedi Katikaza, mjini Paris, Nsekela akamkaribisha akutane nasi mjini Dar es Salaam; nasi tukamwita aje. Ingawa ni mtu wa ajabu ajabu kidogo, mwenye aibu isiyolingana na mafanikio aliyoyapata kiasi hicho, alithibitika kuwa hodari mno katika masuala ya Benki. Alitarajiwa kuwa mtu wa namna hiyo, maana Benki mpya ya biashara wakati ule ilikuwa ya tatu kwa umaarufu katika Afrika nzima.

Page 134: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

134

Baada ya kutumia ushawishi wangu kwa manufaa kiasi hicho juu ya Ubinafsishaji wa Kiwanda kimoja, mtu unaweza ukasamehewa kwa kudhani kuwa sasa Serikali ingekuhurumia ukiwa katika Kiwanda cha Usindikaji. Lakini kwa hilo utakuwa umekosea; maana mwezi Machi 1967, majuma manne tu toka kuingia kwa Uongozi mpya, nilipata ujumbe kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Hazina, Mayisela, kunitaka nionane naye mara moja. Haikuwa lazima kwangu kuwa Mtabiri kutambua kuwa mkutano huo usingehusu mipango yoyote ya baadaye ya shughuli za Usagishaji, ila bila shaka ulihusu fedha za huko nyuma za familia ya Chande. Hakuna haja ya kujitapa kwamba nilipatia. Nilipofika ofisini kwa Mayisela, hakuwa na wazo lo lote kuhusu shughuli zilizokuwa zinaendelea wakati huo; badala yake akatoa Maandishi ya Kampuni aliyoyapata kutoka katika Idara yetu ya Uhasibu, yaliyoonyesha kuwa huko nyuma mimi na ndugu yangu tulipewa na Kampuni ya Chande Industries Ltd. Mikopo ya riba ndogo kununua nyumba tulizonazo sasa. Mayisela akaendelea kusema kuwa utaratibu kama huo usingekuwa na kasoro wakati ule, lakini ukweli ni kwamba, kwa sasa, wote sisi tuko katika mchezo wa aina tofauti. Hapo mimi na ndugu yangu tukalazimika kuilipa mikopo hiyo mara moja, na mimi nikapewa kazi ya kumjulisha ndugu yangu. Kufikia hapo nikawa fundi zaidi wa kucheza mchezo huo mpya; nikajibu, “Vema, naelewa kabisa. Unaweza kukata fedha hizo za deni langu la zamani kutoka katika ile “fidia kamili na ya haki; ambayo karibu utanilipa kwa ajili ya kutaifisha rasilimali zangu”. Katika hili Mayisela, kusema kweli, alitabasamu akikubaliana na pendekezo langu. Kisha akaendelea kunieleza, kwa faragha, kwamba alipiga kelele kudai kurejeshwa mikopo kwa sababu tu ya kuagizwa kufanya hivyo. Ili kukamilisha mambo, sasa nilitakiwa kumwandikia Katibu Mkuu, nikitoa mapendekezo ya kulilipa deni kutokana na fidia niliyotarajia kuipokea karibuni. Hayo nilifanya, na wala sikushangaa sana kwamba sikusikia tena habari za mkopo ule. Lakini mwezi uliofuata Mayisela akaniita tena; safari hii akataka tuzungumzie gari ya Kampuni niliyokuwa naitumia, aina ya Toyota Crown. Hata katika siku zile haikuwa gari

Page 135: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

135

ya fahari, lakini ilikuwa ya raha zaidi kwa sababu ya kuwa na kiyoyozi ndani yake, na nyuma kisanduku kidogo cha barafu. Mayisela akaniambia kuwa gari hiyo ilikuwa mali halisi ya Taifa na lazima irejeshwe. Huko mwanzo niliyakubali maelekezo hayo, wakati Kampuni mpya ya Usindakaji ilipokubali kunipa gari mbadala kwa ajili ya kazi za Ofisi. Lakini lilikuwako wazo lingine, nilitamani kuwezeshwa kununua tena kutoka Serikalini gari ya aina ya Toyota kwa bei itakayopangwa na Serikali. Safari hii sikutaka kutumia lugha laini laini; nikamwelekeza Mayisela mahali ambapo angeweza kuliegesha gari lake. Majuma machache baadaye nikaamua kuachana na ile Toyota, na kupata gari nyingine iliyokuwa bora zaidi kuliko ambavyo ingekuwa kutokana na kuidhinishwa na Serikali. Nikitumia nafasi ya ukata katika Viwanda vya usagishaji, nikamnusuru Mhusika mwenzangu wa Utaifishaji, Jack Jones, kwa kununua gari lake la aina ya Mercedes, rangi ya maziwa, kwa bei ya kukubaliana kwa kutambua kuwa anamaliziamalizia mambo yake nchini Tanzania. Huku kuitwaitwa na Serikali kila mwezi hakukusaidia kuinua ari yangu. Baada ya kupata nyama yao katika duru la kwanza, sasa wakawa wanadai na mifupa vile vile. Wajoli wangu wengi wa zamani katika shughuli hizi wakatambua kuwa kuhangaishwa huku kulilenga kuwasukuma waondoke wenyewe nchini; na kwa kweli wengi wao waliondoka. Mnamo miaka mitatu ya kutaifisha Viwanda, hakuwako hata Mzungu mmoja aliyebaki katika Ngazi ya Utawala katika Viwanda vyote vya Usindikaji, hata Waasia wakabaki wachache sana. Lakini, kwa uamuzi wangu muhimu wa kung’ang’ania nafasi, mimi sikuwa na tatizo la kupangua mashambulizi hayo kila mwezi. Kwa kuwa nilikuwa nimeteuliwa Meneja wa Kampuni yangu ya zamani Juma moja tu kabla ya utaifishaji. Kwa mshahara wangu ule ule, nikaona akilini mwangu, kwa uwazi wote uliowezekana, kuwa Mwalimu alikuwa na nia njema kabisa aliponiambia, Endelea! Vile vile, huruma aliyoionyesha Mayisela inalingana na Sera ya kulikamua tunda mpaka likauke, lakini bila ya kukusanya makapi. Zaidi ya hivyo, kama hawakujua wakati ule

Page 136: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

136

kuwa wangenihitaji kuendesha shughuli hizi wakati ule wa Utaifishaji, kwa hakika sasa wanajua. Wafanyakazi walitaka kufanya kazi na mimi, bila ya kujali vyeo vyao wala rangi zao; na soko linanitangaza, hapa nyumbani na katika nchi za nje. Siku za mwanzo za Utaifishaji zilikuwa ngumu kwa Mtandao wetu wa biashara na nchi za nje, mara waliposikia yale yaliyotokea, ghafla wakawa na hofu kubwa ya kubahatisha. Huko nyuma, nilikuwa nanunua kila nilichokihitaji, kama mashine, kwa mikopo laini. Mwezi Februari 1967, siku chache baada ya Utaifishaji, ghafla njia kama hizo za mikopo zikafungwa, na Kampuni haikuwa na akiba ya kutosha kufidia upungufu huo. Zamani kauli yangu tu ilikubalika kuwa Mkataba; lakini sasa, katika hali hii mpya, Wauzaji hawakuwa tayari tena kuiamini kauli tupu wakihoji, kwa haki kabisa, kwamba kwa kuwa sasa mimi ni Mwajiriwa tu, ambaye inawezekana nisiweko baadaye bili zitakapoletwa, wasingekuwa radhi kuuza chochote kwa mkopo. Kwa kweli ilikua mpaka mwezi Oktoba, 1967, ambapo hatimaye Wauzaji walipoamini kuwa mimi nitakuwa katika Kiti hicho maisha, na kwamba nilikuwa na uwezo wa kuendesha biashara ya Kimataifa katika hali nzuri. Na wakati wote nilipojitahidi kuwashawishi juu ya busara ya kufanya biashara na sisi, vizingiti walivyoviruka, pamoja na kusikiliziwa simu zao havikukoma. Mwezi Oktoba, 1967, nilipoona hatimaye kuwa tatizo langu la biashara limekwisha kupita, mimi na mke wangu tulitakiwa kusafiri kwenda new York, tukiwa wageni wa Kampuni ya ndege ya Trans World Airlines, TWA, iliyokuwa ndiyo kwanza inatumbukia katika soko letu. Sikusita kuupokea mwaliko huo kwa sababu wakati huo nilikuwa natamani kupata nafasi ya mapumziko. Watanzania wengi walikuwa wamealikwa vile vile, pamoja na Mhe. Hasnu Makame, Waziri wa Utalii na Rasilimali Asilia, na wote tukasafiri pamoja kwa shangwe kubwa. Siku ya tatu ya safari yetu, mara baada ya kuwasili New York kupitia Athens, nikapokea Ujumbe kutoka kwa Katibu wa Rais, Dar es Salaam, kwamba Mwalimu alikuwa na haja ya kuonana nami kwa haraka. Nikamrudia Katibu na kumwomba amweleze Rais

Page 137: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

137

kwamba nilikuwa nje ya Nchi, na kwamba nitakwenda kuonana naye mara baada ya kurejea. Lakini, kama inavyotokea mara nyingi katika mazingira kama hayo, Katibu hakutaka kumpa Rais taarifa hiyo mbaya, kwamba nisingeweza kuonana naye kwa haraka namna hiyo, wacha baki kumweleza sababu. Nikiwa nimekata tamaa, nikapeleka tena ujumbe kwa Katibu Mkuu wa Ikulu kumweleza kuwa nilikuwa New York kama mwalikwa wa Trans World Airlines, TWA, na kwamba nilikuwa radhi kabisa kuondoka mara moja kurudi Dar es Salaam, ila ningelazimika kusafiri kwa ndege nyingine maana ndege za TWA zilikuwa zinakwenda huko mara moja tu kwa juma; na hivyo ningalilazimika kutumia fedha, ambazo sikuwa nazo, kulipa tena nauli kamili. Hatimaye, baada ya kungoja sana, nikamfikishia Ujumbe ulioniruhusu kuendelea kukaa New York, na kuonana na Rais nitakaporudi Dar es Salaam. Haishangazi kwamba siku zilizosalia za kukaa kwangu New York zilikuwa za wasiwasi mkubwa; hali iliyotarajiwa kuwa ya mapumziko zikawa siku nne za mateso. Pamoja na jitihada zangu zote, sikuweza kugundua kwa nini Rais alitaka kuonana nami kwa umuhimu huo, na kichwa changu kikajaa dhana za kutisha za kila aina. Hatimaye, juma lilipomalizika, nikasafiri kurudi Dar es Salaan nikiwa na wasiwasi mkubwa; na mara baada ya ndege kutua nikapiga simu Ikulu. Ikatokea kuwa Rais hakuwako; aliondoka Tanzania kwenda kwenye Mkutano wa Nchi zisizofungamana na Upande wowote. Lakini alikuwa ameacha maagizo Ofisini kwake kunitaka niende kuonana na Waziri wa Kilimo, Derek Bryceson. Nilipofika Ofisini kwa Bwana Bryceson nikakuta kuwa naye pia hapatikani alikuwa na mazungumzo na Balozi wa Sweden. Lakini Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, David Mwakosya, kwa kutambua wasiwasi wangu uliokuwa unaonekana wazi wazi acha baki uchovu wa safari yangu na ndege, akanikalisha kitako katika Ofisi ya nje na kuniarifu Rais alimwagiza Waziri kuniambia kuwa alikuwa anautarajia msaada wangu katika kujenga chombo kimoja kutokana na Viwanda vinane vilivyokuwako vya Kampuni za Usindikaji, na kukiendesha chombo hicho.

Page 138: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

138

Baada ya wasiwasi wote niliokuwa nao kule New York, taarifa hii iliniingia kama ndoto, baada ya miezi tisa ya kusumbuliwa, kukashifiwa na kufilisiwa, wakati sikuwa nimejiandaa kwa mikasa kama hiyo. Sikufikiria hata kidogo katika mawazo yangu kule New York sababu nyingine yo yote ya Rais kunitafuta zaidi ya kunikemea au kuninyanyasa. Badala yake, sasa nilikuwa natakiwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni mpya kubwa ya Taifa ya Usindikaji, masharti ya kazi yakiwa yamepangwa moja kwa moja na Rais mwenyewe. Nilipokaribishwa, hatimaye, kuonana na Waziri Bryceson, nilimwambia kuwa nilihitaji muda kidogo kutafakari juu ya kazi niliyokuwa napewa, kabla sijarudi kutoa majibu. Waziri alionekana kushangazwa, akaniuliza, “Kwa nini unahitaji muda kufikiria jambo kama hilo?” Nikajibu, “Kwa sababu nitalazimika kufikiria hilo wazo la kuunganisha Viwanda.” Akaniuliza tena, “Je, una jingile lolote la kuniuliza?” Nikaendelea, “Kiwanda changu kilikuwa cha pili tu kwa ukubwa kati ya Viwanda vyote vya Usindikaji. Kule kwenye Kiwanda kikubwa kabisa kuliko vyote bado kuna watu watano walioazimwa kutoka kwenye Kampuni zao asilia. Mara baada ya Kampuni zote hizo kuunganishwa, hao wataondoka, na hivyo ujuzi mwingi utapotea. Kwa mfano, mimi sijui lolote juu ya kusindika chakula cha ng’ombe, wala cha vinyama vidogo vya kufugwa. Ikawa sasa zamu ya Waziri Bryceson kuchanganyikiwa, akauliza, “Na nini tena?” Nikajibu, “Maelekezo yametolewa na Kamati ya Mashirika ya Umma, SCOPO, ambayo kwa kweli yanashusha mishahara ya Wafanyakazi wa Viwanda vilivyotaifishwa, kulingana na Sera mpya na Bei na Mapato. Endapo Waajiri watatekeleza yalivyo Maelekezo hayo, basi uwezekano wa kuwapandisha vyeo Wafanyakazi hautakuwako kabisa!” Bwana Bryceson akanyamaza; lakini Katibu wake Mkuu, Mwakosya, akadakia, “Kuna lingine zaidi?” Nikajibu, “Ndiyo.” “Nini?” Nikaendelea, “Idara za Kazi na Uhamiaji huchukua kati ya miezi minne na miezi sita kuchambua maombi ya Wageni wanaotaka ruhusa ya kufanya kazi nchini humu. Kwa utaratibu huo

Page 139: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

139

sitaweza kuwaajiri Wataalam ninaowataka” Mwakosya akadakia, “Niletee matatizo hayo, nami nitayashughulikia. Kuna jingine? “Nikajibu, “Bado nahitaji muda wa kutafakari zaidi!”. Uso wa Bwana Bryceson ukaporomoka zaidi! Niliporudi nyumbani nilikuwa na wasiwasi, nikakosa amani. Mwisho wa juma la matatizo, na mwisho wa safari ndefu ya ndege kuvuka Bahari ya Atlantic, akili yangu haikuwa imetulia kiasi cha kuweza kufanya maamuzi mazito. Katika wakati ambapo Maafisa wa Wizara kadha za Serikali walikuwa wananikwamisha kuendesha shughuli za Kiwanda changu mwenyewe cha Usindikaji, sasa natakiwa kubeba kazi ya ziada ya Kujenga upya na kuunganisha Sekta nzima ya Viwanda hivyo. Nikazungumza mambo hayo na Jayli, na hatua hiyo ikasaidia sana, ingawa akili zangu zilikuwa hazijatulia bado; na usingizi ukanihama mpaka hatimaye, saa nane za usiku, nilipolazimika kumeza vidonge vya usingizi. Siku iliyofuata, Jumamosi, sikuamka mpaka karibu saa sita mchana. Nilijisikia vibaya: miguu bado mizito, nikiwa bado nasinzia kutokana na vidonge vya usingizi nilivyovimeza, na ambavyo sikuwa nimevizoea. Lakini hatimaye, niliposimama kwenda kuoga, nilikuwa nimekwisha amua la kufanya. Kuna mithali ya Kihindi inayosema kuwa kama kinyozi amekwisha nyoa nusu ya kidevu, afadhali umwachie amalizie, bila kujali shida zozote zitakazokukabili. Kwa kweli sikuwa na namna ya kukwepa; sikuwa na lingine la kufanya ila kutekeleza yale ambayo Rais alinitaka niyafanye. Jumatatu iliyofuata Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo aliniita Ofisini kwake, akaniambia kuwa ameusikia wasiwasi wangu juu ya kuteuliwa kwangu, na kwamba alikuwa ananihurumia. Kisha akaendelea kueleza mambo kadha ambayo Serikali ilikuwa inafikiria kuyafanya kunisaidia. Kwanza walinitaka mimi, wala siyo mtumishi yeyote wa Serikali, kubuni Sheria ya kuanzisha Shirika hili la Muungano; wala wasingejali kama sikutumia lugha ya Kisheria, jambo muhimu ni kuhakikisha madhumuni yanakamilika kuiwezesha Sheria hiyo kuwa kama Msahafu wa Utendaji kazi, na kuwaachia wenyewe kuyaweka hayo katika lugha ya Sheria.

Page 140: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

140

Pili, Serikali itakaa kuzungumza nasi kwa kirefu kabla hayajapendekezwa majina yote ya watu watakaoingia katika Bodi ya Wakurugenzi. Tatu, Serikali itatumia kwa uangalifu Maelekezo mapya ya SCOPO kuhusu mishahara ya Wafanyakazi wa Viwanda vilivyotaifishwa. Kama hapana budi, itafanyika Mikutano Maalum na Wafanyakazi hao, lijulikane la kufanya kuboresha vivutio vya kupanda ngazi. Nikamshukuru kwa maelezo hayo na kumhakikishia kumpa msaada huo utakaohitajika. Hatimaye nikatamka kuwa nimeamua kukubali kazi hiyo. Ndivyo ilivyomalizika ile miezi tisa ya wasiwasi mkubwa maishani mwangu. Katika kipindi kile sikuwa na la kufanya wakati kila kitu familia yangu ilichokifanyia kazi kubwa sana kukijenga, kwa zaidi ya vizazi viwili, tumenyang’anywa kwa maandishi ya kalamu. Nilimwona ndugu yangu akifanya maamuzi muhimu ya kujiondokea Tanzania moja kwa moja. Niliiona familia yangu ikihangaika na hofu ya kutokujua jinsi ya kuendelea kuishi. Na, baada ya kupoteza kila kitu nilichomiliki, pamoja na Kampuni yangu mwenyewe, sasa najikuta nikikubali kuendesha shughuli zote za usindikaji, kwa niaba ya Serikali hiyo hiyo iliyotaifisha rasilimali zangu! Watu husema kuwa Uzoefu ndiye mwalimu bora. Vema, nimejifunza mengi mwaka ule: yangu mwenyewe, ya Jayli, na ya nchi changa ambayo mimi nimekuwa raia wake. Katika kutafakari mikasa hiyo, nimepata kutambua, kwa kina zaidi kuliko nilivyopata kujua huko nyuma, jambo gani ni muhimu kwangu, na jambo gani si muhimu. Katika mwaka mzima wa 1967 Jayli alitulia kimya, akiwa imara wakati mambo yote yalipokuwa yanakwenda kombo; na uimara huo wa tabia yake ukasaidia kunivusha. Na mimi pia, huko nyuma, nikaujenga msingi usiopimika wa uwezo wa kupambana na dhoruba bila kulegalega katika mambo ya msingi. Pengine, jambo kubwa kuliko yote, ni kule kutambua kuwa safari ile ndefu niliyoianza miaka yote hiyo kutokea Bukene haikuweza kuvunjika, hata kwa mkasa mkubwa kama huu. Tanzania ilikuwa ndiyo nyumbani, ndiyo kwetu kwa mema na mabaya; na, ile kukatizwa tena kuwa Mtanzania halisi, nilipaswa kuyakabili kwa

Page 141: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

141

shida, lau kama kwa miezi michache, maisha waliyokua wanaishi Wananchi wenzangu wengi tangu Ukoloni ulipoingia Afrika Mashariki. Kwa kushiriki katika magumu yanayowapata wengine, nikapata kuelewa kuwa hali halisi inachanganya hali halisi ya wasiwasi wa sasa na ile ya mashaka makubwa zaidi ya siku zijazo. Kama wenzangu hao, nilikubali kujifunza hayo niliyoandikiwa, yoyote yale, kwa uvumilivu, kwa heshima, lakini kwa uchungu mwingi, bila kukosa matumaini ya baadaye. Jambo moja la mwisho linalohusu matukio ya mwaka 1967 linastahili kutajwa. Kitu pekee cha maana tulichokuwa nacho Tanzania, ambacho hatukukubali Serikali itie mkono wake, ni vito vya dhahabu vya Jayli. Lakini vito hivyo vilikuwa na thamani kubwa ya mapenzi, na sisi wote tulidhamiria kuvitunza sana kwa usalama. Kwa hiyo tukakubaliana kuvipeleka viwekwe kwa Wazazi wa Jayli kule Uganda, wakavitunze mpaka tutakapokuwa tayari kuvirudisha. Hatukutarajia kabisa kuzuka kwa Idi Amin ambaye mwaka 1971 aliwafukuza Waasia wote kwa taarifa ya saa ishirini na nne tu, kila mmoja akichukua sanduku lake moja tu la nguo. Kwa njia hiyo vito vya Jayli vikapotea: ikawa kumbukumbu nyingine, kama ilihitajika kumbukumbu, ya usahihi wa filosofia ya Jayli ya Uwezo wa Mungu wa Kutoa na kuchukua.

_______________

Page 142: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

142

NANE

……….MVINYO NA MKATE NA MASANDUKU Mwishoni mwa miaka ya 1960, Wamarekani wawili mashahuri kwa kuandika nyimbo, Burt Bacharach na Hal David, walitunga wimbo mzuri wa mapenzi ulioitwa “Boti, Ndege na Treni”. Bila wenyewe kujua, pengine waliniandikia mimi wimbo ule, maana hata jina lenyewe lilikuwa na mwelekeo wa kuelezea matukio katika maisha yangu, wakati pilika za utaifishaji zilizokuwa zinashinikizwa na Azimio la Arusha zilipoanza kuota mizizi. Wakati Bacharach na David walipokuwa wanaghani wimbo wao huo uliopeperushwa hewani kusikika duniani kote, mimi nikajikuta nimetumbukizwa katika nafasi kubwa katika Bodi za Shirika la Bandari na Shirika la Reli. Kwa bahati mbaya, “Boti, Treni na Usindikaji” wa chakula cha wanyama hauendi katika mwelekeo huo kabisa. Bila Burt na Hal kujua, wakati huo nilipokuwa nashika madaraka ya kusimamia sehemu kubwa ya Mtandao wa Tanzania katika Usafirishaji wa Kimataifa, nilikuwa bado Mhusika vile vile katika Shirika la Usagishaji la Tanzania, kutokana na Sheria ya Bunge Na. 19 ya 1968 ambayo, kwa kuombwa na Mwalimu, nilishiriki kuiandaa Sahani yangu ikawa imejaa mpaka kufurika. Lakini bado ingaliweza kujaa zaidi kama nisingalikuwa na upeo wa kuingiza kwenye Sheria ya Shirika la Taifa la Usagishaji kifungu kilichowekwa mahsusi kuzuia kuingiliwa na Wizara mara kwa mara katika vitu vidogo vidogo vya shughuli za kila siku; kwa sababu, ingawa nilikuwa mtu mpya kabisa katika masuala ya Ujamaa wa Kiafrika, lakini miaka yangu mingi katika Biashara za Binafsi, na katika Mabaraza ya Utawala na ya Kutunga Sheria, nimejifunza zaidi ya jambo moja au mawili kuhusu namna Serikali inavyofanya kazi katika nchi kama Tanzania. Ushawishi ulioko kwa Maafisa Wakuu, acha baki Mawaziri, kutumbukia katika shughuli za kila siku za sekta muhimu za uchumi, hata zile zilizokuwa ndiyo kwanza zimetaifishwa, kwa kweli ulikuwa karibu hauwezekani kuzuilika. Ndiyo sababu

Page 143: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

143

niliandika pendekezo la kifungu cha Sheria kuzuia mianya ya Uendeshaji wa aina hiyo. Pengine nilifungua mlango kumuacha Waziri anayehusika, na kwa shughuli hizi ni Waziri wa Kilimo, angeweza katika mazingira fulani kuwa na haki, hata wajibu wa kutoa Maelekezo ya jumla. Lakini Sheria ikaendelea kufafanua kuwa maelekezo yoyote ya Wizara yenye lengo mahsusi yangekuwa batili. Wakati wa kutayarisha vifungu hivyo sikuwa namlenga mtu yeyote wala mazingira yoyote. Kwanza nilikuwa namfahamu kwa miaka mingi Waziri aliyehusila, Derek Bryceson, akiwa mjoli wangu na rafiki yangu, acha baki kufanya kazi naye pamoja katika kuliunda upya Baraza la Utawala, lililofanya kazi sambamba na Baraza la Mawaziri katika kile kipindi cha kuelekea Uhuru. Kifungu hicho, ukitaka kujua, kilikuwa kinaweka tahadhari ya jumla ili kukwepa maagizo maalum, wala siyo kukwepa yale ya jumla. Hata hivyo, mnamo mwaka mmoja tangu kushika madaraka ya kusimamia Viwanda vyote vya usindikaji, nilifurahi kuwa nilikuwa na upeo wa kuyawaza hayo mapema. Kama nilivyokwisha fafanua, sikutarajia kuwa na mawazo yaliyokuwa yanasigana na yale ya Waziri wa Kilimo, ingawa mawazo yangu mengi yalimfanya aondoke Ofisini, Derek Bryceson na mkewe wa kwanza, Bobbi, walikuwa marafiki zetu wakubwa, watu wa kufurahisha, lakini makini, wenye msimamo imara katika Taifa ambalo Mwalimu alikuwa katika harakati za kulijenga. Kwa kweli Derek alikuwa anajivunia kuwa karibu sana na Mwalimu, ambaye alitokea vile vile kuwa jirani yake kule alikokuwa anaishi. Uhusiano huo na jirani yake, aliyekuwa rafiki yake, na mjoli wake kwa miaka mingi katika mambo ya Siasa, ulinifanya mimi na watu wengine wa Dar es Salaam kuamini kabisa kuwa huo ndio uliokuwa uhusiano imara kuliko wa wengine wote kati ya Kiongozi huyo na Mtanzania mwingine yeyote asiyekuwa asilia. Kwa siku nyingi zaidi, hata awe na kazi nyingi kiasi gani, Derek aliweza kupata muda wa kubadilishana mawazo na jirani yake huyo maarufu; na mara nyingi akaweza kuimarisha umaarufu wa kuwa Kiongozi wa kwanza asiyekuwa Mwafrika mweusi katika Serikali. Maana katika siku zile ambapo watu walishirikiana katika siasa,

Page 144: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

144

uhusiano wake yeye na Mwalimu ulikuwa umeanza mbali sana huko nyuma katika TANU kabla ya Uhuru; na ukaribu wa uhusiano huo ukadhihirika katika ukweli kwamba Derek alikuwa Mzungu pekee aliyepata nafasi muhimu kabisa, mara baada ya kujitawala, na akateuliwa na Mwalimu kushika moja ya Wizara nyeti kabisa katika Baraza la Mawaziri. Kwanza, Derek ndiye aliyepata kura nyingi kuliko wengine wote katika Uchaguzi wa mwaka 1960. Kwa hiyo ilikuwa jambo la ajabu kabisa, wala tusiseme bahati mbaya, kwamba nilionekana tangu mwanzo kuwa nasigana na Derek. Mawasiliano yangu kwake yeye, kama yalivyokuwa na kwa wengine, mpaka na kwa Rais mwenyewe, wakati wote yalijengwa katika msingi wa uwazi kabisa, msingi nilioulea tokea siku za mwanzo kabisa nilipokuwa nafanya shughuli zangu binafsi. Kutoka siku ile niliyokabidhiwa shughuli za Usindikaji, nikiwa wazi mno wakati wote mbele ya Derek katika kuelezea hali ilivyo, lakini vile vile nilimweleza wasiwasi wangu juu ya uwezekano wa kupata mapema mafanikio yatakayotokana na kazi yenye vizingiti vingi katika kuunganisha Kampuni tisa za Viwanda vyenye ukubwa na ufanisi unaotofautiana. Nikifikiria ya huko nyuma, nadhani uwazi wangu kuhusu matatizo na matarajio ya mazingira hayo mapya ndio ulionifanya nifarakane na Waziri. Labda habari peke yake aliyokuwa anataka kuijua na kuisukuma mbele kuhusu Viwanda vya Usindikaji vilivyokuwa vimetaifishwa ni zile habari njema tu. Kwa sababu zozote zile, nilitambua haraka kuwa ufa ulikuwa unazidi kupanuka kati yetu. Hata kabla sijazianza shughuli za kuendesha Viwanda vya Usindikaji, vilivyokuwa vimetaifishwa, nilikwisha mwambia Derek kuwa nilikuwa na hofu ya uwezekano wa kuunganisha, kwa utaratibu mzuri, baadhi ya kazi za Usindikaji, kama vile kutengeneza mashudu, ambazo sikuwa na uzoefu nazo kabisa. Naye, kwa upande wake, akamnongoneza Katibu wake Mkuu kuwa nilikuwa na wasiwasi wa bure, akisema, Usindikaji ni usindikaji tu”. Nilisikia kwamba, kabla ya hapo, Derek alimpa kazi Mtaalam wa Kimarekani kuishauri Serikali namna ya kupanga upya Taratibu za Viwanda vya Usindikaji baada ya kuwekwa mikononi mwa

Page 145: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

145

Taifa; Mtaalamu huyo alikuwa amekaa karibu mwezi mzima katika Hoteli ya Kilimanjaro, akifanya uchunguzi fulani. Ukiacha Derek na Katibu wake Mkuu, hakuna mwingine aliyeiona taarifa ya Mtaalamu huyo, ambayo pengine inaingia vumbi katikati ya makabrasha ya Wizara. Nilipata nong’ono kuwa Mtaalamu huyo aliona kuwa uunganishaji huo wa Viwanda ungekuwa kazi ngumu mno, na vikwazo vyake vingi mno, kiasi kwamba lazima utahitaji ujuzi wa Wataalam wasiopungua kumi na wanne kutoka nje. Jambo ni la hakika: kwamba Mtaalam huyo aliongeza ufundi wake wa kucheza gofu katika kipindi alichokuwa Tanzania. Karibu kazi yangu ya kwanza kabisa baada ya kushika madaraka yangu mapya mwezi Januari, 1968, ikawa kumkumbusha Waziri wasiwasi wangu juu ya matukio yatakayovuruga kabisa yanayotokana na sera mpya ya Mapato na Mishahara, katika matarajio ya kupanda ngazi, kwa Wafanyakazi watakaokuwa wanaingizwa katika hiyo Kampuni mpya itakayokuwa imeunganishwa baada ya Utaifishaji. Yeye naye akamwelekeza Katibu wake Mkuu kuwa hilo lilikuwa tatizo kubwa alilopaswa kulishughulikia. Kwa bahati nzuri Katibu Mkuu akalielewa lile nililokuwa nikilidai; kwa hiyo akajichangamsha kunitoa katika dimbwi hilo, kufikia mahali ambapo muafaka unaofaa ulipatikana. Alifanya vivyo hivyo nilipokwenda kuomba msaada wake juu ya matatizo ya Vibali vya Wafanyakazi wageni, na kisha ukaja ule mvutano katika Kiwanda cha Mvinyo cha Dodoma, kilichokuwa kinaendeshwa na Serikali. Sasa Tanzania haimo tena katika hesabu ya watengenezaji wa mvinyo duniani. Afrika Kusini, ndiyo; Tanzania, Vema, lakini Hapana! Katika nyanda zetu kama za Dodoma, ambako zamani Wananchi wa Kabila la Wagogo walienea, kiwanda kidogo lakini muhimu cha kutengenezea mvinyo kilianzishwa na Wamisionari wa Kitaliani katika miaka ya 1950. Kwa kweli kule Dodoma hakuna zao lililokuwa linakubali zaidi ya zabibu na nyanya; na, nadhani, hizo ndizo sababu zilizowasukuma Wataalam kutumbukia. Lakini, kwa sababu yoyote ile, na kwa vigezo vingi, shughuli za Dodoma

Page 146: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

146

zilielekea kufanana na za kusindika mvinyo mahali pengine popote panapochipukia katika dunia inayoendelea. Ulikuwako utani ulioanzishwa na mabingwa wa mvinyo kubeza uzuri wa mvinyo ya mwanzo iliyotengenezwa. Watengenezaji walilazimika kutegemea sana Utaalam na vifaa vya Wazungu. Lakini katika shamba moja zabibu hizo za Dodoma likawa tofauti kabisa. Kinyume na ilivyo katika sehemu nyingine, tuseme Afrika Kusini, au Chile, au hata Australia, miche ya zabibu za Dodoma hazikupandwa chini ya vivuli katika miteremko ya milima iliyokauka na jua, bali ndani ya gereza, katika mashamba yaliyozingirwa uwigo yaliyokuwa sehemu ya jela la Isanga. Huu umaarufu wa zabibu usiokuwa wa kawaida haukuwa kwangu mimi jambo kubwa, wakati wazo la kutakiwa kuendesha Kiwanda cha Mvinyo cha Dodoma liliponong’onwa mara ya kwanza. Jambo lililonisumbua zaidi lilikuwa kukosekana uwiano kati ya kuendesha Shirika la Taifa la Usindikaji na kuanzisha upya, kwa kiwango kidogo, usindikaji wa mvinyo. Nilikwisha iruhusu Serikali kupanua tafsiri ya Usindikaji kujumlisha ukamuaji wa matunda na kutia mboga kwenye makopo. Sasa nilikuwa naombwa kuendeleza na kuboresha manufaa katika kiwanda ambacho sina ujuzi wowote nacho, na ambacho, huko nyuma, uhusiano wake na shughuli za usindikaji ulikuwa mdogo zaidi kuliko kutengeneza shira au kutia matunda kwenye makopo. Kama kawaida, sikujua lolote kuhusu Mipango iliyokuwa inabuniwa na Serikali mpaka siku nyingi zimeyoyoma, na hata hivyo nilitokea kuyajua hayo kwa bahati tu. Nikiwa ziarani mjini London, rafiki yangu mmoja aliponiambia kwamba Wizara ya Kilimo ilikuwa na maandalizi ya kuhamishia kwenye Kampuni yangu ya Usindikaji shughuli za Shamba la Zabibu la Dodoma. Kwa kuwa nilikuwa London, katika kipindi ambacho mawasiliano kati ya Uingereza na Tanzania hayakuwa mazuri sana, sikuweza kufanya lolote kurekebisha hali hiyo, zaidi ya kuendelea kuwa na wasiwasi. Lakini mara niliporudi Dar es Salaam, hata kabla sijaipata nafasi hiyo mimi mwenyewe, wasiwasi wangu ukaondolewa; nikapokea wito kufika mbele ya Waziri wa

Page 147: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

147

Kilimo kwa haraka kadri ilivyowezekana, kuzungumzia masuala ya Kiwanda cha Mvinyo cha Dodoma. Nilipofika Ofisini kwa Waziri kesho yake asubuhi, Waziri, labda kwa wasiwasi wake wa kuwa na uhusiano uliozidi kuwa mbaya kati yetu, hakupoteza muda wa kueleza chimbuko la pendekezo lake. Bila kutoa utangulizi wowote, akanipa hizo habari mbaya za uhamisho uliokuwa unapendekezwa; na, si hivyo tu, habari hizo alinipa si kwa mjadala kati yetu, lakini kama uamuzi uliokwisha kutolewa. “Kwa Amri ya Mwalimu, Baraza la Mawaziri limeamua kukukabidhi wewe Kiwanda cha Mvinyo cha Dodoma. Kama una tatizo lolote kuhusu uteuzi huo, basi nenda mwenyewe ukazungumze naye.” Kwa sababu za maana, sikupenda kutumia nafasi hiyo niliyopewa na Waziri Bryceson, nikipendelea zaidi kuliweka wazo hilo kama akiba. Badala yake nikaenda kwanza kuzungumza na Kamishna Mkuu wa Magereza. Tofauti na msimamo wa Waziri, Kamishna Obadia Rugimbana alikuwa radhi kabisa kunieleza kinaganaga shida na matatizo ya Zabibu zile zilizokuwa gerezani. Akanieleza kinaganaga mipango iliyokuwapo katika kulima, kupanda na kutunza mizabibu. Akanieleza tatizo la kupata Wataalam wanaotakiwa kutoka miongoni mwa wafungwa waliopo, na kutambua matatizo ya kweli wakati wa kusafirisha mavuno yaliyopatikana. Na wakati alipokuwa anazungumza, ilidhihirika wazi kwamba Rugimbana alikuwa anaamini kabisa kwamba Taratibu alizozianzisha pale Kingolwira haziwezi kudumu kwa sababu nyingi tu, pamoja na za usalama wa Gereza. Hoja hiyo ilinisaidia kuelewa, kwa uwazi zaidi, majukumu yasiyotabirika yaliyotokana na Mkuu wa Gereza wa hapo kuendesha Kiwanda cha Mvinyo. Acha baki hatari ya kupoteza wafanyakazi wake wengi muhimu kuondoka kwa mpigo, Chateos Checky hakuwa aina ya mtu aliyekuwa na mwelekeo ambao Mfanyakazi yeyote wa mvinyo mwenye adabu zake angeweza kuwataka awashawishi waamuzi. Tangu Baraza la Mawaziri lilipoamua kuhamisha mashamba ya zabibu na Kiwanda kipya cha mvinyo, Mwalimu akiwa kitini,

Page 148: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

148

nililazimika kulishughulikia suala hilo kwa uangalifu kidogo. Nilipoonana tena na Kamishna Rugimbana, nilimdokezea kwamba Watumishi wake wanaweza kukumbana na mazingira magumu wakijua kwamba Watumishi wa Shirika langu watakuwa wanaendesha shamba ambalo, kwa taratibu zilizoko, si mali ya Idara ya Magereza, lakini bado yangali chini ya himaya yake. Shirika langu lilikosa utaalamu katika kupanda mizabibu na kutengeneza mvinyo; maana yake ni kwamba nililazimika kwenda nje ya nchi kutafuta Wataalam. Vile vile nilikuwa nahofia mnunuzi atakapogundua kuwa zabibu hizo zimelimwa kwa nguvu za wafungwa. Nilihangaika kwa kutumia mtandao wa Chama Tawala mpaka hatimaye uamuzi huo ukaangaliwa upya na ikawa Kiwanda cha Mvinyo peke yake ndicho kilichochukuliwa na Shirika langu. Nilimwahidi Kamishna Rugimbana kuwa ningemsaidia kupata Shirika litakalotoa ufadhili kwa ajili ya mafunzo ya watumishi wake wachache katika fani ya kuzuia uharibifu wa mazingira. Nikamtafuta Balozi wa Ufaransa, Mhe. Andre Naudy, mtu aliyelelewa katika maadili safi, aliyeshitushwa alipojua kuwa Watanzania walikuwa wanajitahidi kutengeneza mvinyo! Akiwa amekaa katika ukumbi wake uliopambwa sana ndani ya Jumba lake la Ubalozi, Naudy alikaa kimya akinisikiliza nilipokuwa natamba na simulizi yangu juu ya namna ya kutengeneza mvinyo. Pengine ingekuwa sahihi zaidi kusema kuwa alikuwa kimya kabisa, mwenye uso ulioshupaa, baada ya kumweleza masuala yote yaliyoingia na kutoka kule Kingolwira: zaidi yaliyoingia, kwa kuzingatia mazingira ya mahali pale. Alikuwa mtu wa mashaka, au hata tuseme aliyejaa hofu, kwamba mtu yeyote aliye na hata chembe ya ujuzi wa biashara angeweza kufikiria kutengeneza mvinyo kibiashara katika sehemu kama Kingolwira, katika nchi kama Tanzania. Akakataa kutoa msaada wowote wa ufundi, lakini akakubali kuwapatia Watanzania wawili mafunzo nchini Ufaransa katika fani ya kuzuia uharibifu wa mazingira. Mnamo dakika chache za kukaa kwangu katika kiti cha Balozi, taswira yangu ya mradi wa watu Weusi unaopandikizwa katika mizabibu iliyoko Dodoma ikayeyuka

Page 149: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

149

ghafla. Nikamaliza kikombe cha chai niliyokuwa nakunywa; nikaomba radhi na kuondoka. Wakati huo Kamishna Rugimbana alikuwa anafurahia uwezekano wa kuendeleza shamba la Magereza, na kupanua mipaka yake. Majuma machache baadaye Mwalimu akalitembelea shamba hilo, na Kamishna akapata nafasi ya kuomba apatiwe matrekta mawili. Mwalimu akasema, “Kama unayahitaji, unastahili kuyapata.” Afisa Ugavi wa shamba akaenda kuyanunua matrekta mawili, lakini bila kufuata Taratibu zilizotakiwa, kama vile kuchunguza bei za matrekta hayo kutoka sehemu zaidi ya moja. Siku nyingi baadaye, kutokana na Hoja ya Serikali, Mwakilishi wa Kamishna akasema kuwa Mwalimu alitoa ruhusa ya kuyanunua. Lakini akaambiwa kuwa ingawa pengine Mwalimu aliidhinisha ununuzi huo, yeye asingalimwamuru mtu yeyote kupuuza Taratibu zilizopo za ununuzi wa mali ya Serikali. Kutoka hapo nikaenda kwa Balozi wa Italia; yeye kadhalika alikuwa Mwanadiplomasia wa zamani aliyestaarabika. Tayari Mapadre wa Kikatoliki kutoka Italia walikuwa wanatengeneza chupa chache za mvinyo nyekundu kule Bihawana; kwa hiyo angalau hapa, hatimaye, ingawa niliweka shinikizo kubwa kupita kiasi juu ya ufundi ule wa mwanzo katika kutengeneza mvinyo nyekundu kwa kiwango kidogo kule Bihawana, hivyo hatimaye na hapa, ingawa inawezekana nimeweka shinikizo kubwa mno katika shughuli za mvinyo katika maeneo ya Dodoma, nikawa nimeanza kupiga hatua. Balozi akanisikiliza, na mwelekeo wake ukawa wa kunikubalia, tena kwa furaha; akakubali kunitafutia Bingwa katika fani hiyo ya kutengeneza mvinyo; akakubali vile vile kugharimia kuletwa kwake. Na, kubwa kuliko yote, alikubali kutia saini Makubaliano yote hayo. Mnamo majuma machache Signor Tomosili alikuwa amepatikana na kuteuliwa, na, kwa baraka za Balozi wa Italia na zangu mimi mwenyewe, bado zilisikika masikioni mwake, akakubali kwenda kuchanganya mvinyo Dodoma. Kukamilisha zaidi furaha yake na yangu, akatembea katika maeneo ya Wagogo, akiwa na vijana wawili, Wataalam wa sayansi ya udongo walioteuliwa na Serikali ya Ufaransa kwa ajili ya kufundisha; maana kufikia wakati huo

Page 150: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

150

Mhe. Naudy alikuwa amekwishainukia kutoka katika mshituko alioupata baada ya kuwatembelea, kiasi cha kujitokeza na msaada wake mwenyewe uliokuwa unahitajika kweli kweli. Signor Tomosili ndiye mtengeneza mvinyo pekee wa Kiitaliano ambaye mtu angeweza kumtegemea; si tu kwa sababu ya kuipenda mno kazi yake bali pia kwa umahiri wake ulivyodhihirika katika kila hatua aliyoichukua katika shughuli hiyo. Lakini alikuwa kama Sultani, mwenye hasira zisizofanana na za Watanzania; zilizokuwa zinafumuka kila alipohisi kuwa heshima yake, aliyokuwa anailea kama zabibu, ilikuwa inatiliwa mashaka. Niligundua mara moja jazba ya mtu huyo, kutokana na taarifa nilizokuwa nazipokea kutoka kwa wafanyakazi wangu huko Dodoma. Sikuzitia maanani Taarifa hizo, labda kwa sababu, tulipofikia hatua ya kutia mvinyo katika chupa, wakati ule wa muhula wa kwanza wa Tomosili, niliwatuma Wahasibu wangu wawili kwenda dodoma kutathmini wenyewe gharama zilizokuwa zinatarajiwa katika Mradi huo. Lakini kwa bahati mbaya, katika kufanya hivyo, sikuzizingatia kiasi cha kutosha hisia za Signor Tomosili. Ingawa katika kuwatuma Wahasibu wale sikuwa na uhasama wowote, na laiti ningalikuwa nao ningaliukiri. Signor Tomosili akakitafsiri vibaya kitendo hicho kuwa dalili ya ukosefu mkubwa wa Imani katika ufundi wake. Kwa kuomba kuangalia tu vitabu vya kazi, Wahasibu hao wakajikuta katika mazingira tofauti ya kukemewa mpaka, hatimaye, Tomosili akampigia simu Balozi wa Italia, Dar es Salaam. Alihisi kuwa tulikuwa tunavuruga heshima yake kama bingwa wa kutengeneza mvinyo, kwa kujaribu kumwelekeza yeye, Tomosili, namna ya kuifanya kazi yake katika kipindi hiki muhimu cha mafanikio ya msimu wake wa kwanza wa zabibu, hapo Dodoma; kwa hiyo tulikuwa tunamwingilia kati. Hatimaye, kutokana na busara na uwezo mkubwa wa Balozi wa kushawishi, niliweza kumtuliza Tomosili, nikimhakikishia kuwa hatukuwa na inda hata kidogo dhidi ya maajabu ya utaalamu wake, wala hatukutaka kwa njia yoyote kuudhibiti Mradi wake, na kwamba tulichotaka tu ilikuwa kupata kitu kama makisio ya

Page 151: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

151

gharama ya kutengeneza mvinyo katika msimu ule. Akiridhishwa na juhudi zetu za pamoja, akarudi kazini kwake na kutengeneza chupa za kwanza za mvinyo nyekundu, kuwahi uzinduzi rasmi uliofanyika Makao Makuu ya Shirika la Maendeleo ya Taifa, NDC, Dar es salaam. Sitazama sana kuielezea shughuli hiyo, katika jitihada za kusitiri fadhaa yangu na ya wafanyakazi wenzangu. Hata kule kuiita shughuli ile kuwa ni uzinduzi ilikuwa sababu tu ya kutafuta kuaminika lakini, kwa kujitetea wenyewe, tulikuwa na busara ya kutambua mipaka ya yale tuliyokuwa tunayafanya. Haikuwako kamwe hatari yoyote kwamba tungebandika karatasi ya tarehe katika chupa yetu yoyote, wala kuitangaza mvinyo kuwa ni ya Tanzania; hata Tomosili, pamoja na jeuri yake, asingeweza kutetea Hoja hiyo. Hapana; hii mvinyo ya Dodoma iliyotengenezwa na Kampuni mpya ilikuwa mvinyo ya kawaida kabisa, na haukupita muda kabla haijatambulika na Wageni waliokuwa wanaishi Tanzania kuwa ni kinywaji cha mvinyo halisi. Nina mashaka sana kama mvinyo ya miaka miwili ya kwanza ilivuka majiko ya Oysterbay, na Msasani; lakini angalau tulifanikiwa kuweka msingi imara wa Kiwanda cha Mvinyo kilichoimarisha sana ubora wake baada ya miaka kupita; na kazi kubwa aliyoifanya Tomosili na wale waliokuja baada yake imewaziba midomo watu wengi waliokuwa na matarajio madogo katika Mradi huo. Hatimaye aina nyingine ya aina ya “Rose” ikaongezwa, kuwa pamoja na ile nyekundu, na kwa muda mrefu sasa aina hizo mbili za mvinyo zimekuwa zikinywewa sana. Hata kama, pengine, hazilingani na mvinyo za Afrika Kusini; lakini ukitambua na huko tulikotoka, ndani ya kuta za Gereza la Kingolwira, bado tumepata mafanikio yasiyokuwa yametarajiwa. Inawezekana sikupenda, katika shughuli zangu, kuongeza kazi hiyo ya kutengeneza mvinyo; lakini angalau haikuathiri hizo shughuli zangu za kila siku. Kisha, matukio mawili yaliyo mabaya zaidi, yaliyozuka haraka haraka, moja baada ya jingine, yakasababisha uhusiano wangu uliokuwa mbaya dhidi ya Waziri kufika ukomo wake. La kwanza lilikuwa mgogoro usiokuwa na madhara makubwa wa kusafirisha mpunga kutoka Morogoro kwenda Dar es

Page 152: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

152

Salaam. Bila kujulikana na mtu yeyote ndani ya Shirika, Wizara ikagundua matatizo mengi yaliyohusiana na usafirishaji, yaliyoonekana kuhitaji uchunguzi rasmi wa Bodi. Bodi hiyo ikaundwa, Mwenyekiti wake akiwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo; na ikaanza kukusanya ushahidi juu ya malalamiko ya utumiaji mbaya wa Madaraka. Lakini mara ya kwanza kabisa mimi kufahamu kuwa matatizo hayo yalikuwa yanajulikana, licha ya kuwa yanafanyiwa uchunguzi rasmi, ilikuwa pale Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo aliponipigia simu kunishitua kwamba Bodi ya Uchunguzi ilikwisha wasilisha Maoni yake kwa Waziri. Kwa mujibu wa maelezo ya Katibu Mkuu, matokeo yake yakawa, moja kwa moja, Waziri sasa ananitaka mimi niwafukuze kazi mara moja watumishi wangu watatu. Nikishitushwa na madokezo hayo, na nikitambua madhara yatakayonisibu katika Shirika langu, nikatafuta haraka haraka kuonana na Katibu Mkuu. Haikunishangaza kwamba Mkutano wangu kule Wizarani haukuwa mzuri kwa wote waliohusika. Nilipofika pale niliomba, na nikapata, maelezo ya msingi uliyotumiwa katika kuufanya Uchunguzi huo. Nikaambia jinsi mahojiano yalivyoendeshwa, na Uamuzi aliofikia Naibu Waziri. Katibu Mkuu akalalamika kuwa, katika mazingira hayo, mimi sikuwa na la kufanya ila kuwafukuza kazi hao Watumishi watatu walioonekana kuwa ndio chanzo cha matatizo. Nikajibu kwamba nisingeweza kufanya kitu kama hicho; badala yake nikahoji uhalali wa Madai hayo, na Taratibu zilizotumiwa na Waziri katika kupeleleza jambo hilo. Badala ya kuja kwangu tangu mwanzo, au kwa Wasaidizi wangu, wakati tuhuma hizi zilipotolewa, Wizara ikaona vema kuunda Bodi ya Utafiti. Bodi hiyo ikakaa na kufanya Utafiti wake bila mimi kujua; wala kupewa, mimi au Shirika langu, nafasi ya kuyasikiliza Mashitaka yenyewe, na ya kuyajibu. Zaidi ya hayo, Maagizo ya moja kwa moja ya kuwatimua watu watatu kati ya Wafanyakazi wangu inakwenda kinyume na Sheria iliyoruhusu kuundwa kwa Shirika la Usindikaji.

Page 153: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

153

Nikamkumbusha Katibu Mkuu kwamba Sheria hiyo, waziwazi, inamzuia Waziri au Afisa wake yeyote kutoa kwenye Shirika Maagizo yoyote yenye mwelekeo mahsusi. Endapo Waziri, au Naibu Waziri, au Maafisa wao Wakuu, kwa sababu yoyote ile, hawaridhiki na kazi za Shirika chini ya uongozi wangu, basi anachotakiwa kufanya Waziri ni kumwomba Rais aliyeniweka mimi kwenye nafasi hii kuniondoa. Majibu ya Bryceson kwa Hoja zote hizo, kama ililvyokuwa mara nyingi alipokuwa amebanwa, yakawa kunielekeza kwenda kuonana na Rais. Kwa mshangao, wake nililipinga wazo hilo pia. Derek Bryceson, siye Mwalimu, ndiye alishindwa kushauriana nami kuhusu mashtaka makubwa dhidi ya Maendeleo ya Shirika langu. Derek Bryceson, siyo Mwalimu, ndiye aliyevunja Sheria aliponitaka niwafukuze kazi Wafanyakazi wangu. Kwa hiyo lilikuwa jukumu lake pia kutafuta njia ya kuondokana na Tatizo hilo, wala si jukumu la Rais. Kwa sasa, na kwa sababu nilizokwisha kumweleza, haikuwako nafasi ya kukubaliana na Maelekezo yake. Kwa kauli hiyo, Mkutano wangu na Katibu Mkuu ukavunjika ghafla. Siku tatu baadaye, Katibu Mkuu Timothy Apiyo akaniita tena, akitarajia kuwa, safari hii, nitakuwa nimelegeza msimamo wangu. Akayarudia tena Maelekezo ya Waziri ya kuwafukuza wale Wafanyakazi watatu. Kwa mara nyingine nikakataa, ila safari hii nikamtaka alitie Agizo hilo katika maandishi, nikijua kabisa kuwa, kwa kufanya hivyo, nilikuwa nazikaza kamba za kumfungia Bryceson. Haukuwako uwezekano wowote kwa Wizara kunielekeza lolote kwa maandihi, kutokana na yale ambayo wote sisi tuliyajua kuhusu sheria ya Usindikaji. Kama nilivyotarajia, Waziri akalitafakari wazo langu hilo la mwisho kwa siku chache, na kisha akampigia simu Ernest Mulokozi, Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, aliyekuwa Mwenyekiti wa Shirika la Taifa la Usindikaji. Simu hiyo ikamsukuma, kwa haraka, Mwenyekiti kuniletea barua ya kunitaka niitishe kwa haraka Mkutano wa Dharura wa Bodi ya Shirika la Taifa la Usindikaji, na Waziri Bryceson angekaribishwa kwenye kikao hicho. Nikiwa na Maagizo kama hayo kutoka kwa Mwenyekiti, sikuwa na hiyari ila kutekeleza; na, katika kufanya

Page 154: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

154

hivyo, nikajitahidi kudhihirisha, kwa uchangamfu wangu mkubwa, kukubali kwangu. Katika jibu langu, nilidiriki hata kuainisha kuwa Mwalikwa Mahsusi wa Mwenyekiti atakaribishwa katika Mkutano huo Maalum wa Bodi. Lakini moyoni mwangu nilitambua kuwa sasa nilikuwa katika hatari kubwa ya kuzidiwa ujanja, au hata kutegewa. Lakini nilikwishafanya maandalizi ya kuikabili hali hiyo. Umahiri wangu wakati wa kubuni Mapendekezo ya Sheria ya Usindikaji wa Taifa ulizingatia mpaka Muundo wa Bodi ya Wakurugenzi. Sikuwa na uwezo wa kuelekeza suala la Uenyekiti wa shirika, lakini nilikuwa na bahati kutokana na kuteuliwa kwa mtu mwenye huruma nyingi, Mulokozi; nami nikahakikisha kuwa Wajumbe waliosalia wa Bodi wanakuwa watu ambao ningeweza kuwaamini, na ambao wangeweza kuniamini na mimi, katika karibu matatizo yote. Kwa watu hawa niliweza kujieleza, kuandaa Uwanja wa Mapambano dhidi ya Waziri. Siku ile ya Mkutano, Bryceson aliendesha gari lake mwenyewe kuja kwenye Ofisi zetu Barabara ya Pugu, kama alivyokwisha kufanya mara nyingi. Wakati alipokuwa anauvuta mwili wake kutoka katika kiti cha mbele cha gari yake, aina ya Mini Morris, mimi mwenyewe nilikuwa nimesimama nyuma ya gari yake nikisubiri kumpokea. Pamoja na kusononeka kwangu kutokana na jinsi alivyouchukulia uhusiano wetu kwa upande wa Utaalam, bado nilimhesabu kuwa rafiki zaidi kuliko kuwa hasidi; mtu ambaye kwa jumla, ni mwema na mnyenyekevu, aliyetamani Viongozi wetu wafanye mambo mazuri wakati wote. Baada ya kusalimiana, nikamtambulisha kwa Wakurugenzi waliosalia kisha tukaendelea na Kikao. Ilimchukua Waziri Bryceson dakika arobaini na tano tu kuitambua wazi wazi hali halisi. Kwa mshangao wangu, Timothy Apiyo, Katibu Mkuu wa Wizara, akiwa Mjumbe wa Bodi, aliniunga mkono, na dhahiri, kwa kufanya hivyo, alikuwa anajiweka katika mwelekeo uliokuwa unasigana moja kwa moja na ule aliokuwa nao alipokuwa Kiongozi wa Watumishi katika Wizara hiyo. Kwa hili nilimshukuru. Ghafla Waziri Bryceson akatangaza, “Basi, yanatosha! Naamini wote, pamoja na Andy, tumezingatia mafunzo tuliyoyapata kutokana na kitendo hiki; sasa tuachane na hayo”.

Page 155: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

155

Bila majadiliano zaidi, hivyo ndivyo tulivyofanya; wale wale Watumishi watatu miongoni mwetu waliokuwa wamelengwa kufukuzwa kazi hawakupata kamwe kujua kuwa Wizara ilikuwa imenuia kuwafukuza kazi; wala hawakuzijua jitihada zilizofanywa kwa niaba yao kuuepusha mkasa huo. Ningependa pia kusema kuwa Utetezi wangu kwa niaba ya hao watatu haukulenga mambo ya teknolojia peke yake wala haukushinikizwa na mapenzi matupu kwa Wafanyakazi wangu. Tulipoukaribia Mkutano wa Bodi niliwatuma watu wawili waaminifu katika Shirika kuchambua kinaganaga Tuhuma zote zilizokuwa zimefikishwa mbele ya Tume ya Uchunguzi, iliyoteuliwa na Wizara. Watumishi wangu mwenyewe waliona kwamba, kwa hakika kabisa, hazikuwako Tuhuma za kujibu, na kwamba orodha nzima ya Mashitaka ilikuwa imetengenezwa kulingana na uvumi mtupu na ushahidi wa kupangwa. Bado haijaeleweka kwangu, mpaka sasa, nini hasa wizara ilichotarajia kutokana na Uchunguzi ule. Kwa jinsi Sheria yenyewe ilivyotungwa, uwanja ulikuwa finyu mno kuweza kutumika kuhoji madaraka yangu. Lililokuwa linawezekana zaidi, kwa jinsi mambo yalivyokuwa yanakwenda nchini Tanzania siku zile, chuki binafsi dhidi ya mfanyakazi mmoja, au wote wale watatu wa Shirika, zimetumika kuwa ndio msingi wa harakati zote hizo za Uchunguzi. Kwa sababu zozote zile, msumari mwingine ulikuwa umegongomewa kwenye jeneza la urafiki wangu na Derek Bryceson. Kwa bahati mbaya, misumari ya mwisho kabisa ilikuwa karibu karibu; lakini ile Taarifa ilipokuja ikawa na makosa ya Waziri mwenyewe: makosa ya kutokujua kiwango cha uvumilivu wangu, na ya kutokujua kiwango cha umuhimu wake yeye mwenyewe mbele ya Rais. Akiwa karibu mno na Mwalimu kwa muda mrefu sana, Bryceson alikuwa anatambua fika shinikizo lililokuwa linambana Rais kujidhihirishia mwenyewe zaidi kuliko mtu mwingine yeyote kwamba Utawala wake unatekeleza mambo kulingana na Ahadi alizozitoa kwa Wananchi. Baada ya Azimio la Arusha, Dira ya Taifa na mbele ya Mataifa mengine, ukaja Ujamaa na manufaa

Page 156: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

156

yaliyotarajiwa kupatikana katika maisha ya Watanzania wa kawaida. Kwa hiyo ilieleweka kwamba utaifishaji wa shughuli za usindikaji ulimpa Waziri nafasi ya kufanya lolote aliloliweza kusaidia kutekeleza malengo ya Mwalimu. Hilo nililielewa pia, na ndiyo sababu hasa ya kukubali kwangu kuubeba Wajibu huo wa Taifa. Kwa hiyo tulipaswa Derek na mimi kuwa tunavuta kamba upande mmoja. Lakini yeye akang’ang’ania kutoa Maamuzi yanayohusu shughuli za Usindikaji alizozifikiria yeye kuwa na manufaa kwa Taifa, bila kunishirikisha mimi hata kidogo. Mgogoro ukazuka tena kuhusu masuala ya mchele. Safari hii kiini cha tatizo hakikuwa Usafirishaji, bali Bei. Derek Bryceson hakuwa ameelewa kikamilifu jinsi soko la zao hilo, na ya mazao mengine, yalivyojiendesha. Alidhani, na ikadhihirika baadaye kuwa makosa, kwamba lazima zile Kampuni nane za Usindikaji kabla ya kutaifishwa, zilikuwa zinapata faida kubwa mno kutokana na mpunga; hivyo moja ya manufaa ambayo Wananchi wangepaswa kuyapata kutokana na Ujamaa ingekuwa kushuka kwa bei ya mchele; na akatoa Maelekezo katika hilo. Hakutaka ushauri wa Shirika mapema; alijiendea tu kutangaza bei mpya, wakati huo huo akitoa Tamko kuwa bei ya mpunga atakayopewa Mkulima itabaki pale pale! Bei hizo zikathibitishwa na Kamati ya Uchumi ya Baraza la Mawaziri. Zikawako nong’ono kwamba wazo la kwanza la Bryceson lilikuwa kwamba bei hizo zitumike Dar es Salaam, eneo ambalo mchele unatumika zaidi, na Jimbo la Uchaguzi la Waziri mwenyewe. Mapunguzo hayo ya bei yalifanywa kwa kutegea manufaa makubwa ya kisiasa, kwa sababu kipindi chenyewe kilikuwa kinakaribia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Derek Bryceson alikuwa anajua fika kwamba Waislamu wa hapo walikuwa wanafuturu kila siku mwezi Ramadhani kwa kula wali mara moja tu jioni. Kwa hiyo punguzo hilo la bei katika msimu ule wa mwaka lingeongeza sana mahitaji: Kwa hiyo ningepata kuongeza faida kutoka ile ndogo sana kutoka katika kila kilo mia za gunia la mchele mpaka kupata hasara ya kati ya shilingi kumi na mbili hadi kumi na nne katika kila gunia. Vile vile nikakabiliana na mfumuko

Page 157: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

157

wa mahitaji ambayo hata sikutarajia kuyatimiza kutokana na malighafi iliyokuwa inapatikana, kwa sababu baada ya Usindikaji kutaifishwa, na mimi nililazimika kupanga upya kazi kwa kuunganisha Viwanda vyote. Mshituko uliotokana na Tangazo la Waziri ukanifanya nikose usingizi, nikatambua haraka kwamba nafasi yangu ya kufurukuta ni ndogo. Si kwamba tu Shirika lingepata hasara katika kila gunia litakalokuwa limekobolewa, lakini pia kutokana na kufungwa, majuma machache yaliyopita, kwa Viwanda vinne kati ya vinane vinavyokoboa mpunga nchini, ili kupunguza hasara; sasa ningelazimika kukodi; kwa gharama kubwa, wakoboaji wa nje ili kutosheleza mahitaji ya mchele yanayoongezeka, na hivyo kuongeza hasara kwa kiwango kikubwa sana. Shughuli hii ya Usindikaji wa Taifa ilikuwa ndiyo kwanza imetuliza mawimbi ya kuunganishwa kwa lazima. Uamuzi kama huo ukidumishwa utatulazimisha kusikia zoezi zima la utaifishaji linavurugika; kwa sababu Shirika lilikopa fedha kununua Viwanda kutoka Ujerumani, na limeomba mkopo mwingine kununua mitambo kutoka Uingereza; namna ya kulipa ilionekana kuwa ya wasiwasi. Maana yake sasa ni kwamba tutapaswa kujadiliana upya Taratibu za Malipo, na pengine matokea yake yatakuwa kupoteza Imani na Uongozi, na athari za jumla hatika hali ya biashara ya Tanzania. Nikatambua haraka kwamba, ili kudumu, nilipaswa kumwendea Waziri na kumwelezea wasiwasi wangu. Sikushangaa kwamba nilipomfafanulia matokeo ya Uamuzi wake, ambayo hakuyatarajia, alikuwa mbishi. Alieleza kwamba Wataalam wa Wizara waliomshauri, baada ya uchambuzi wa biashara ya mchele, walipendekeza bei ya mchele ipunguzwe; na Mapendekezo yaliyotokana na wazo hilo yakafikishwa mbele ya Kamati ya Uchumi ya Baraza la Mawaziri. Bila kuongeza Hoja nyingine yoyote, Waziri akanisisitizia kwamba, kwa mawazo yake yeye anayoyaamini kabisa, Uamuzi huo wa Baraza la Mawaziri ndio wa mwisho.

Page 158: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

158

Nikaondoka kwenye Mkutano ule katika hali ya wasiwasi. Ilinichukua miezi mingi kuwaridhisha Wakulilma wangu wa mpunga, toka siku zile za Viwanda vya Chande, kukubaliana nami bei nzuri tangu mwanzo. Nililazimika kwenda mwenyewe kubadilisha mitambo katika baadhi ya Viwanda nilivyolazimika kuvichukua. Gharama ya kuvilipia vifaa hivyo, ambavyo wakati wa Chande vilipatikana kwa mkopo bila kuulizwa maswali, sasa ni mkopo wa miaka mitano katika vitabu vya Shirika la Usindikaji. Badiliko hilo la ghafla katika biashara ya mchele, kutoka kupata faida ndogo mpaka kuangukia kwenye hasara kubwa mno likafanya mipango yangu yote kuwa hatarini. Hata kama matarajio ya ongezeko kubwa la mahitaji ya mchele yasingetokea, na dalili zote zilizokuwa zinaonekana zilikuwa kinyume cha hayo, hali katika Shirika kwa jumla ilikuwa ya mashaka. Kama Bryceson hakuusikiliza wasiwasi wangu, na Katibu wake Mkuu akarudi kwangu keshoye kuniambia kuwa hakuniunga mkono, basi nililazimika kulifikisha tatizo hilo kwa Rais. Na sasa, kwa mara ya kwanza toka wakati ule tulipofarakana kwa sababu ya kukataa nafasi ya kugombea kiti kwa niaba ya TANU, nimegundua kuwa Rais alikuwa anakataa kuonana nami. Nikaenda kwa Katibu wake Mkuu, Dickson Nkembo, kumweleza kwa undani sababu zangu za kutaka kuonana na Rais. Nilipokosa jibu la maombi yangu ya kwanza, nikapeleka barua nyingine tatu kukumbushia. Baada ya kukaa kwa mwezi mzima bila majibu, na wakati huo fedha zinatumika tu katika hesabu za Shirika, nikaenda kwa Nkembo tena, kumweleza hofu na masikitiko yangu, na jinsi ujanja unavyoniishia kwa kutokujua la kufanya. Nkembo akanisikiliza kwa utulivu, akiyaandika yote niliyoyasema; lakini hakutaka kutoa kauli yake mwenyewe. Jioni siku ile, kwa kuwa sikupata nong’ono yoyote kutoka Ikulu, nikashawishiwa na marafiki zangu kwenda kwenye starehe katika Klabu ya Usiku ya Simba, katika Hoteli ya Kilimanjaro. Mke wangu na marafiki zangu, wakiwa na wasiwasi mkubwa juu ya mambo mazito yaliyokuwa yananisumbua, wakadai tutoke, lengo likiwa kuniondosha kwenye fikra za bei za mchele, angalau kwa saa

Page 159: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

159

chache. Wakati huo Hoteli ya Kilimanjaro ndiyo iliyokuwa na sifa kubwa mjini Dar es Salaam; na mimi nikaifahamu vema nilipokuwa Mwenyekiti wa shirika la Utalii lililoimiliki Hoteli ya Kilimanjaro iliyokuwa inaendeshwa na Kampuni ya Kiyahudi Mlonot Ltd. Lakini starehe za pale Simba hazikuweza lolote usiku ule kutuliza wasiwasi wangu. Pamoja na upuuzi wote uliokuwa unanizunguka, na jitihada zote kubwa za marafiki zangu, nilikuwa nimezingwa mno na matatizo ya biashara kiasi kwamba sikuweza kustarehe, au angalau kupumzika. Kufika saa saba usiku, saa nyingi baada ya muda marafiki zangu waliotaka tuondoke, nikaondoka hapo wakati wenzangu wote walipokuwa bado wanataka kuendelea; tukashuka kupitia ukumbi wa hoteli mpaka chini tulipokuta vijana wamekusanyana kikundi barabarani. Mbele yao kijana mmoja alikuwa anauza gazeti la Jumapili, ndiyo kwanza linatoka mitamboni lina habari nzito katika ukurasa wake wa mbele ya mabadiliko ya Mawaziri. Nilipolinunua nikasoma kuwa Mwalimu ameamua kumwondoa Waziri wa Kilimo kutoka kwenye Baraza la Mawaziri na kumpa kazi ya Mkuu wa Mbuga za Wanyama; badala yake anakuja Joseph Mungai, Mbunge wa Mufindi, ambaye wakati huo alikuwa anasoma Kanada. Fikira zangu za kwanza baada ya kuzisoma habari hizo zikanielekeza kwenye huzuni. Pengine na mambo mengi yoyote watakayonifikiria watu wengine, Derek Bryceson alikuwa, kwa miaka mingi, rafiki yangu wa kweli; na sasa kupelekwa kwenye Mbuga za Wanyama ni kama ameteremshwa hadhi. Kweli hatukuwa tunakubaliana katika yote tangu niliposhika kazi ya Kitaifa katika Viwanda vya Usindikaji, lakini kuhitilafiana kwetu kulitokana tu na kukosekana kwa mawasiliano yaliyo wazi, na kushindwa kuelewa jinsi Kiwanda, hata hicho cha Taifa, kinavyoendeshwa, bila kukwepa jukumu la kujituma kutekeleza yale yenye maslahi kwa Tanzania. Hata kama mtu akiwa Mjamaa wa kweli kweli, anayelinda na kuendesha Uchumi wa kupangwa, bado Mashirika ya Umma yatalazimika kuendeshwa katika misingi ya Kibepari.

Page 160: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

160

Lakini dhahiri tofauti zilizojitokeza zilikuwa zinafanya kazi zetu, ama zake ama zangu, zisiwe na mafanikio. Kwa hiyo nilihisi kuwa mazungumzo yangu na Rais ilikuwa ndiyo chachu iliyoamua wazo la kubadili Mawaziri ghafla. Haukuwako uthibitisho wowote kwamba, kwa kuondoka kwake Derek, matatizo yangu yangekwisha. Lakini lazima nikiri kwamba habari ya mabadiliko hayo, baada ya matokeo yake kuonekana, iliniwezesha kupumzika kidogo, wakati nilipokuwa nangojea Waziri mpya Joseph Mungai kuchukua nafasi yake katika Baraza la Mawaziri. Hayo niliyafanya kwa majuma mawili, ingawa matatizo yaliyotokana na ukoboaji wa mchele yaliendelea kuongezeka. Mwishoni mwa mwezi, wakati Waziri Mungai alipokuwa amekwisha kukaa kwenye nafasi yake kwa karibu majuma matatu, bado halikuwako lolote lililosikika kutoka kwake, kwa hadhara wala kwa faragha, juu ya bei ya mchele wa walaji. Nikaanza kuwa na wasiwasi tena, wa aina ambayo hata kutembelea Klabu ya usiku ya Simba kusingeweza kuutuliza. Kwa hiyo nikatafuta namna ya kuonana na Waziri mpya. Kauli yake ya kwanza, mara baada ya kunisikiliza, ikawa ya kujikinga zaidi. Wakati alipochukua hatua ya kunieleza kwa kirefu kwamba yeye alikuwa mgeni katika kazi hiyo, na bado alikuwa anajifunza undani wa masuala ya kilimo nchini Tanzania; bado alikuwa anajijengea nguvu yake ya Kisiasa. Katika hali hiyo nisingeweza kumtarajia kugeuza maamuzi yote ya Baraza lililopita, na kutangaza mara moja kufuta Uamuzi wa Waziri aliyekuwako, hasa kwa vile Uamuzi huo ulipokelewa vizuri sana nchini. Nikamwambia kuwa nimeyaelewa matatizo yake, lakini na mimi hali yangu katika Viwanda vya Usindikaji ilikuwa inakatisha tamaa. Haikuwako haja ya utafiti wowote zaidi; watumishi wake wote wamekwisha elezwa msimamo huo wazi wazi. Nikamwambia pia kuwa nilikuwa natafuta nafasi ya kuonana na Rais kwa zaidi ya mwezi sasa, lakini bila mafanikio. Kutokana na yale ambayo Waziri alikwisha niambia, sikuwa na la kufanya zaidi ya kurudia ombi langu la kuonana na Mwalimu.

Page 161: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

161

Mungai akaonekana wazi kuwa mtu aliyekosa raha baada ya kusikia habari hizo; lakini, kwa sifa yake yeye, hakulipinga wazo langu la kuomba tena kuonana na Rais. Kwa kweli, nilitoa shukrani kwake na kwa Watumishi wa Ikulu, hatimaye nikapewa nafasi ya kuonana na Rais, saa nane mchana, katika siku moja ya juma lililofuata. Wakati huo miezi mitatu ilikuwa imepita tangu nilipolieleza tatizo hilo mbele ya Derek Bryceson. Nilikwenda kuonana na Rais, Ikulu, nikiwa na Timu nzito kutoka Shirika la Taifa la Usindikaji. Pamoja na Naibu wangu, walikuwamo Wakurugenzi wa Fedha na wa Uzalishaji. Tulipokaribishwa katika Ukumbi wa Baraza la Mawaziri, nilimwona Waziri Mungai upande mwingine wa meza, pamoja na Katibu Mkuu wake; alikuwako pia Katibu Mkuu wa Rais na Wasaidizi wake wawili, Vijana, kutoka Ikulu. Wote tulikuwa tumekaa, tukingojea Mwalimu afike. Mwalimu alipoingia, akakaa na kuuliza nani ataanza Mjadala. Nikajitokeza; lakini kabla sijaenda kwenye Hoja yenyewe, nilimwomba ruhusa nizungumze katika lugha ya Kiingereza. Akanikubalia. Nikaanza kwa kueleza mazingira yaliyokuwapo wakati nilipokubali kupokea jukumu la kuongoza Shirika la Taifa la Usindikaji. Niliukubali Mkataba wa miaka mitano kuendesha Kampuni hiyo kwa mujibu wa Sheria Na. 19 ya 1968 iliyoeleza wazi wazi kwamba nilipaswa kuiendesha Kampuni kwa misingi kamili ya biashara; lakini sasa inaonekana kuwa natakiwa kuiendesha Kampuni kama Chama cha Msalaba Mwekundu. Nilikuwa napata hasara haraka-haraka, na hatimaye mzigo wa hasara hiyo utakuwa mkubwa. Kwa hiyo nililazimika kusimamisha shughuli sasa hivi ili nifanye mahesabu; na kisha niamue kama mimi, pamoja na Kampuni yangu, bado tuna uwezo wa kuendelea kuendesha shughuli katika namna ilivyoanzishwa. Kufika hapo nikagundua kuwa Mwalimu alikuwa ananitaka nisitishe kuzungumza. Akashusha mawani yake, akanitazama; kisha akageuka pole pole kushoto kwake, kisha kulia kwake; hatimaye akawaangalia Wajoli wake waliokaa, wakihaingaika vitini mwao kwa wasiwasi. Akanigeukia mimi tena kuniuliza, “Nani anayekuambia uachane na Utaratibu wako wa kuendesha

Page 162: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

162

Kampuni?” Nikajibu, “Mawaziri,” wakati huo namfikiria Bryceson. Mwalimu akasema, “Basi hawajui wanachokisema. Nakutaka uzalishe faida, ukifikiria Taratibu za Uwekezaji baadaye.” Rohoni nikafurahi, maana Mwalimu mara nyingi aliposema “ziada,” alikuwa na maana ya “faida”. Mwalimu akaendelea, “Zaidi ya hayo nakutaka uangalie uwezekano wa kupata Viwanda vipya vya kusaga mahindi, Dodoma na Mtwara.” Kufika hapo, Mwalimu akamtaka Waziri Mungai afikirie upya suala hili la utaifishaji kwenye Kikao cha Baraza la Mawaziri. Kisha Mwalimu akasimama na kuondoka; Mkutano umekwisha. Nikakusanya makaratasi yangu na kushuka chini ambako nilimkuta Awinia Mushi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, akinisubiri karibu na gari yangu. Akitumia sasa lugha ya Kiswahili, Mushi akaanza kunishambulia kwa sababu ya maneno niliyoyasema katika Kikao kile, akihoji, “Lugha gani ile uliyotumia mbele ya Mkuu wa Nchi!” Nikamwangalia kwa utulivu; kisha nikamjibu, kwa taratibu, “Bwana Mushi, mimi siwezi kulala usiku huu. Ninao hapa mfukoni mwangu ufunguo unaofungua milango yote ya Ofisi ya Makao Makuu ya Shirika la Taifa la Usindikaji; ukitaka nitakukabidhi ufunguo huu sasa hivi, kwa sababu Kampuni inapata hasara kubwa sana ya fedha.” Akanibwatukia, “Kwani ni fedha zako!” Nikamjibu, “Najua; najua ni fedha za Umma, nami najihisi kuwajibika kwazo.” Baada ya hapo nikajiondokea. Siku mbili baadaye nikarudi tena Wizara ya Kilimo kuonana na Waziri Mungai na Katibu Mkuu wake. Wote wawili wakawa wametulia kiasi cha kutosha, na Mungai akaufungua Mkutano wetu kwa maelewano ambayo dhahiri alinuia kuyaendeleza. Akasema, “Vema, na tuanze ukurasa mpya!” Katika muda wa saa mbili zilizofuata tukaweka msimamo kati yetu kwamba wote tulikuwa tunataka tunufaike katika Uchumi na katika Siasa., Hakuwako yeyote Mkutanoni pale aliyefurahia kupunguzwa kwa bei anayolipwa Mkulima kwa mpunga wake, kutokana na yale tuliyoyajua ya hali mbaya ya kilimo cha Tanzania. Kwa hiyo wote tukakubaliana kwamba zilikuwa zinahitajiwa Taratibu za kuongeza,

Page 163: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

163

pole pole, bei za Wanunuzi, ili Shirika la Taifa lirudi katika hali yake ya kupata faida. Na Mungai akawa mwaminifu katika ahadi yake. Ingawa miezi mingi ilipita kabla mambo hayajaenda kwenye mwelekeo uliotakiwa, niliweza kutumia maelewano yangu mapya na Mungai kuwahakikishia wale wote tuliokuwa tunafanya nao biashara, wanaotuuzia na wanaotukopesha, kwamba hakukuwako sababu ya kuwa na wasiwasi katika Malengo yetu yaliyokuwamo katika Mpango wetu wa Miaka Mitano. Matatizo ya mpunga sasa yakawa yameondoka kabisa; lakini lilibaki la matanuru ya kuokea mikate. Nilikuwa nashangaa wakati wote kwa nini matanuru hayo hayajapata kutajwa katika orodha ndefu ya Viwanda muhimu vya kutaifishwa iliyotolewa siku zile baada ya Azimio la Arusha. Mpaka leo sijui sababu yake; lakini kwa sababu yoyote ya kurukwa kwake, pengo hilo la sera ya Serikali lilikuwa linakaribia kuzibwa. Mara ya kwanza mimi kuijua kasoro hiyo ilikuwa pale nilipopigiwa simu na Amir Jamal, Waziri wa Tanzania wa Fedha. Hiyo ndiyo iliyokuwa tabia yake siku zote; kumwuliza mtu moja kwa moja bila kubanwa na urasimu. Sababu zake za kunipigia simu nazo zikafafanuliwa haraka; na hiyo nayo ni tabia nyingine ya Jamal. Akaniambia, “Watu wetu” (yaani Wahindi)” walikuwa wanadanganya katika shughuli zao za kuoka mikate (wakati huo soko la mikate lilikuwa limehodhiwa na Wagiriki na Wahindi) Jamal akaendelea kusema kuwa ingawa matanuru ya mikate hayakutajwa Mkataba wangu wa mwanzo, lakini hiyo ni biashara ndogo katika usindikaji. Je, ningeweza kuyashughulikia matatizo yote ya mikate mibovu au yenye vipimo pungufu yaliyokuwa yameenea Tanzania nzima? Sikuweza kumpinga. Nimekuwa nikiitambua wakati wote haja ya kuwa na Taratibu nzuri katika shughuli za Usindikaji, ili zijumlishe na matanuru ya kuokea mikate. Kwa uzoefu wangu mwenyewe nilitambua jinsi matanuru hayo yalivyokuwa katika hali mbaya; nikatambua mara moja kwamba hata jitihada zilizokuwa zinaendelea kurekebisha hali hiyo hazikuwa bora zaidi. Kadhalika, Jamii zilizokuwa zinatoa misaada zilikuwa zimekwisha tambuliwa

Page 164: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

164

na Serikali ya Tanzania kuwa ndio msingi wa mafanikio yetu katika zoezi hilo. Miezi michache kabla Jamal hajanipigia simu, yalifanywa mawasiliano na Balozi wa Uholanzi, aliyekuwa wakati huo na mmoja wa Miradi mikubwa kabisa ya misaada ya maendeleo nchini Tanzania. Mara baada ya kupata habari hiyo ya madhambi yaliyokuwa yanatendeka katika shughuli za kuoka mikate, akakubali kugharimia ujenzi wa Kiwanda cha Mikate cha aina ya Baker Perkins, pamoja na kubeba gharama za kufundishia Wafanyakazi watakaokiendesha. Lakini majuma yale machache kabla ya Jamal hajapiga simu, mipango hiyo ya Waholanzi ikaanza kuvurugika, kutokana na mabadiliko ya kipaumbele cha Bajeti ya Wajerumani. Huko nyuma Wajerumani waliahidi kugharimia ujenzi wa Gati katika Bandari ya Tanga kwa ajili ya kushushia shehena za mbolea, angalau kwa mara ya kwanza lakini baadaye, kwa sababu zisizojulikana, ahadi hiyo ikafutwa dakika za mwisho. Kwa bahati Waholanzi wakajitokeza kuokoa jahazi; lakini matokeo ya hatua hiyo yakawa kuachana na ule Mpango wa kuleta Kiwanda cha kutengenezea mikate, maana isingewezekana kujenga gati na Kiwanda cha Mikate vile vile. Mchezo huo wa “kukata pua kuunga Wajihi” uliovuruga mipango ya nchi zilizokuwa zinatoa misaada toka siku za mwanzo za Uhuru mpaka sasa uliiweka nchi katika hali ya kuyumba. Katika kuhangaika kumpata Mfadhili mwingine wakaangukia kwa Wakanada. Wakati ule wa Waziri Mkuu Pierre Trudeau, Wakanada walikuwa wanatoa misaada kwa Tanzania kwa kiwango kikubwa mno kuliko walivyokuwa wanatoa kwa nchi nyingine yoyote katika Bara la Afrika. Haikumchukua Balozi wa Kanada aliyekuwako Dar es Salaam muda mrefu kuikubali dhamana hiyo; na Wakanada wakaja kuutekeleza Mradi huo. Kile Kiwanda cha Baker Perkins kilichotarajiwa kuletwa kutoka Uholanzi kilitarajiwa kupatikana kwa mkopo wa riba ndogo ambao ungelipwa, nusu kwa nusu, kati ya Waholanzi na Watanzania. Mkopo huo nao ungesukumizwa kwenye Shirika; lakini muda wa kulipa nao ungepunguzwa kufikia miaka saba hadi kenda, na

Page 165: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

165

Hazina ingetoza riba kwa viwango vya biashara vinavyohusu mikopo ya muda wa kati. Huo mtambo wa Wakanada, ambao naamini kwamba vile vile ungetengenezwa na wao hao Baker Perkins, ungaligharimu kiasi cha mara mbili mpaka mara tatu zaidi kuliko ule wa Waholanzi. Serikali ikaukamilisha Mkataba uliohusika na Shirika la Kanada la Misaada ya Maendeleo ya Kimataifa kwa maelewano na Shirika la Taifa la Usindikaji. Yalikuwako manung’uniko kutoka kwa baadhi ya Wasomi wa Kikanada, labda kwa kushinikizwa na Wataalam wao wasiofurahia misaada ya Wakanada kwa Watanzania, kwa kuhofu kwamba msaada wa Wakanada kwa Watanzania kulima ngano na kuoka mikate ungevuruga nafasi ya Wakulima wa Kanada! Kabla Kiwanda hakijajengwa, Wakanada wakakubali kutoa, bure, Huduma za Mtaalam; na wakakubali kutoa mafunzo kwa Watumishi wawili wa Shirika katika fani ya Waokaji Wakuu wa Mikate. Bila kuwasiliana kwanza na Serikali wala na Shirika, Wakanada wakapeleka kwenye Shirika Wasifu wa mtu wao aliyeitwa Bwana Thoroughgood. Nilipodai tupate wasifu wa angalau mtu mwingine mmoja, nikaambiwa tu kuwa huyo Bwana Thoroughgood, aliyekwishafanya kazi kama hizo huko India, ingawa katika Viwanda vidogo zaidi, ndiye hasa mtu aliyekuwa anafaa. Ikatokea tu kwamba, wakati wa mazungumzo hayo, nikakutana na Amir Jamal, Waziri wa Fedha, aliyenigombeza kwa kuchelewa bila sababu kumwajiri yule Mshauri wa Ki-Kanada, akinikumbusha kwamba Kanada ndiyo Nchi iliyokuwa inatoa misaada mikubwa sana kwa Tanzania; na kwamba Mawaziri Wakuu wake, Lester Pearson na Pierre Trudeau, walikuwa marafiki wakubwa wa Mwalimu. Kufika wakati nilipomkubalia Jamal, Wakanada walikuwa tayari wamekwisha jiandaa kutia saini Mkataba. Kwa bahati yangu mimi, Bwana Thoroughgood akatokea, kama jina lake linavyotafsiriwa, kuwa Makini na Mwema vile vile; na baada ya muda, tukaweza kuliweka sawa suala hilo la Kiwanda cha Mikate, kiasi cha kuwaridhisha Wananchi na Serikali pia.

Page 166: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

166

Miaka yangu iliyosalia, ya mkataba wangu wa miaka mitano kama Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Usindikaji, ilimalizika vizuri. Kusema hivyo maana yake siyo kwamba sikuwa tena na matatizo yoyote: kwa kweli nilikuwa nayo. Tabia zile za zamani za “liwalo na liwe”, zilizokuwa zimeenea katika shughuli nyingi za Viwanda vile vingi vidogo vidogo, zilichukua muda kufutika. Lakini hatimaye nikajikuta nina uwezo wa kutumia muda mwingi zaidi kwa sehemu hizo nyingine nilizoteuliwa na Serikali kuzishughulikia. Uzoefu wa Kiwanda cha Metal Box nao ukajitokeza wakati huo huo pia. Kabla ya kutaifishwa kwake, Metal Box Tanzania Limited kilimilikiwa mia kwa mia kama Kampuni Tanzu ya Metal Box PLC ya Uingereza. Baada ya kutaifishwa, Serikali ya Tanzania ikachukua asilimia hamsini ya hisa za hiyo Kampuni Tanzu, kuiachia hiyo Kampuni ya Kiingereza kuwa na Mkurugenzi mmoja zaidi ndani ya bodi, lakini Mwenyekiti wa bodi ateuliwe na Serikali. Mwenyekiti wa kwanza wa Bodi akawa Clement George Kahama, lakini akajiuzulu alipoiachia nafasi yake ya Mkurugenzi wa Shirika la Taifa la Maendeleo. Aliyeteuliwa badala yake hakukubali kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Metal Box. Akamteua badala yake mmoja wa Watumishi wa Shirika, Bi Rukia Hamisi. Kampuni ikaendelea kuendeshwa na ile Kampuni-Mama ya Uingereza, iliyokuwa inashika madaraka kulingana na ule Mkataba wa Msaada wa Ufundi. Lakini, kwa kupunguza chumvi, uhusiano kati ya Wakurugenzi wa Kitanzania na wale wa Kiingereza haukuwa mzuri; katika Mkutano mmoja Wakurugenzi wa Kiingereza walisimama na kuondoka kabla mkutano kumalizika, wakiwa na dukuduku zito. Baada ya hapo, Wakurugenzi wa Bodi walio wenyeji hawakukutana tena kwa zaidi ya mwaka mmoja, ingawa Kampuni iliweza kuendelea kufanya kazi chini ya Mkurugenzi wake Mwingereza. Dhahiri hali hii haikuwa ya kuridhisha, hata kwa Serikali ya Tanzania. Hatimaye akaja Ernest Mulokozi kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo, na Mwenyekiti wa Shirika langu mwenyewe la Usindikaji; akaniuliza kama ningekuwa radhi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Kampuni ya Metal Box Tanzania, kwa lengo la

Page 167: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

167

kusaidia kurejesha uhusiano mwema kati ya Kampuni asilia ya Kiingereza na Wakurugenzi wa humu nchini. Wakati huo nilikuwa na matatizo na Wanahisa wa Ki-Kanada katika Kampuni ya Viatu ya Bata Shoe, ambao huko nyuma nilikuwa najadiliana nao ili wabakize hisa zao asilimia tano katika Kampuni hii ya Tanzania. Kwa sababu hiyo, na kutokana na shughuli zangu nyingi katika Shirika la Taifa la Usindikaji, sikulikubali ombi la Mulokozi. Katika kufanya hivyo nilikuwa vile vile najua fika kwamba Serikali ya Tanzania ilikuwa imelipeleka jina langu tangu mwaka 1967 kuwa Mkurugenzi wa Kampuni, lakini Kampuni-Mama ilisema kuwa waliona maslahi yangegongana, wakati Shirika la Taifa la Usindikaji likiwa mnunuzi katika Metal Box Tanzania. Lakini Kampuni-Mama hiyo nayo ilijua fika kwamba, kutokana na mfarakano kati ya wakwe zangu akina Madhvani wa Uganda na Metal Box wa Kenya, Madhvani wakajenga Kiwanda chao wenyewe cha kutengeneza makopo huko huko Uganda, zaidi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya Kampuni zao wenyewe; kwa sababu hiyo hakuna hata moja kati ya hoja hizo mbili itakayotosha kugeuza msimamo wa Serikali. Baada ya kuhangaika sana, hatimaye nikashawishiwa na Waziri wa viwanda kushika kwa miaka miwili Uenyekiti wa Metal Box Tanzania. Kazi yangu ya kwanza, nikiwa Mwenyekiti ilikuwa kukutana na Wakurugenzi wa Kiingereza. Kwa hiyo nikapanda ndege kwenda London; na, nilipofika, nikamweleza Balozi wetu madhumuni ya safari yangu. Ofisi Kuu ya Metal Box ilikuwa katika Mji wa Reading, na nilipangiwa kupelekwa huko na dereva mmoja wa Kampuni hiyo, msichana aitwaye Pat Brown. Katika safari nzima nilikuwa nikihangaika kimya kimya, na wakati mwingine kwa wazi, kupata habari za ndani za Wenye hisa wa Kampuni hiyo. Lakini Pat alikuwa mfuga-mbwa, aliyeonekana kuwapenda kama mwehu; kwa sababu, iwe makusudi au kwa kupagawa, kila swali nililomwuliza alijibu kwa kibwagizo cha mmoja wa mbwa wake! Kabla ya kuamua kwenda Reading, kuonana na Wakurugenzi wa Kiingereza, nilitafuta msaada wa kifundi kutoka kwa watu wa Asia

Page 168: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

168

na Ulaya niliokuwa nafahamiana nao, lakini nikagundua kuwa Kampuni-Mama ya Kiingereza ilikuwa inafanya shughuli nyingi katika nchi hizo; na ilikuwa na kauli ya maana huko, hata ya kuziba midomo ya wale niliotarajia kuwa wangenipa habari. Lakini nikafanya mpango na Kampuni moja ya Finland kuleta msaada wa kifundi endapo, kwa bahati mbaya, mpango huo utashindikana. Jambo hilo lilikuwa muhimu kwa sababu mmoja wa wanunuzi wakubwa, Tanganyika Packers Limited, mali ya Libregs, ilikuwa inanunua makopo kutoka Metal Box Tanzania kutilia nyama waliyokuwa wanasindika na kusafirisha mpaka Ulaya, na tulilazimika kuhakikisha kuwa nyama nyingine yoyote mbadala sharti iwe na sifa ya kimataifa. Nilipofika Reading nilikuta Bendera ya Tanzania pale penye Ofisi Kuu, iliyokuwa ndani ya nyumba iliyoitwa Queen’s House, yaani Nyumba ya Malkia. Aidha nililakiwa na Wafanyakazi wawili wa cheo cha juu waliowahi kufanya kazi katika Bodi ya Kampuni yao Tanzu huko Tanzania. Mnamo saa nne asubuhi baada ya kunywa kahawa kwa kashata, tukaanza mazungumzo yetu. Upande wa Waingereza uliongozwa na Bwana Wills ambaye, ilionekana, alifanya kazi ya kusifiwa katika Jeshi la Kiingereza kule Mashariki ya Mbali. Namna zake zilikuwa za kijeshi, kama siyo za mapambano. Kwa mujibu wa mawazo ya Kampuni-mama, msimamo wa Tanzania ulikuwa kama wa mzaha-mzaha; ndiyo sababu waliendelea kudai kuwa na wingi wa Wajumbe katika Bodi ya Wakurugenzi. Wala hawakufurahi nilipodakia na kusema kuwa, kutokana na uzoefu wangu mimi mwenyewe, manufaa ya wingi katika hali hii ni kama mapambo tu, na kwamba lingekuwa jambo la maana zaidi kwa pande zote mbili kufanya kazi pamoja. Nikaongeza kutamka kuwa, kwa mawazo yetu ilikuwako bado nafasi kubwa ya maendeleo na upanuzi katika soko la nyumbani na la Kanda. Kisha nikagusia kwamba hata Taratibu za Wingi wa Wajumbe zingeweza kuangaliwa upya na Serikali ya Tanzania. Kufika hapo Bwana Wills akadakia kusema, “Hatutaki lugha ya namna hiyo hapa; wala hatutaki kutishwa”. Nikatabasamu, kisha

Page 169: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

169

nikajaribu kuyarudisha mazungumzo kwenye mstari. Lakini papo hapo Mkurugenzi wao wa Fedha akapendekeza tuahirishe kikao ili tukapate chakula cha mchana kilichokuwa kimeandaliwa na Mhe. Alex Page, Mwenyekiti wa Kampuni. Tukala na kunywa katika mazingira mazuri tu na, baada ya kunywa kahawa, tukarejea kwenye mazungumzo. Wakati huo jazba zilikuwa zimepungua, kila upande ukiwa umetambua mwelekeo na nguvu za Hoja za upande wa pili, haikupita muda mrefu kabla ya kupatikana maelewano. Tukamaliza kwa tabasamu na kupeana mikono; na, kama kusisitiza umuhimu wa yale tuliyokubaliana, nikarudishwa na mmoja wa Wajoli wa Wills, badala ya Pat mpenda-mbwa. Kiasi cha mwaka mmoja baadaye, Kampuni ilipokuwa inafikiria kuongeza mikondo, mimi na Meneja Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo, Arnold Kilewo, tulirudi Reading kama timu. Tukaangalia vile vile baadhi ya Makampuni ya kutengeneza makopo kule Uingereza. Tuliwekwa kwenye hoteli nzuri mtaa wa Marlow, na jioni tukakaribishwa kwenye Hoteli ya Vyakula inayoitwa French Hom. Nikatakiwa na Mwenyekiti wetu kuchagua mvinyo. Mimi si mnywaji sana wa mvinyo, na kwa kweli, sijui lolote la maana kuhusu mvinyo, ingawa wakati huo Shirika la Taifa la Usindikaji lilikuwa linatengeneza mvinyo isiyokuwa na sifa kubwa, aina ya Chateau Migraine. Nikaitazama orodha nzima ya mvinyo mpaka nikaangukia kwenye moja ambayo bei yake wakati ule ilikuwa kiasi cha shilingi 13,000/= na, nikitaka kujua mwenyeji wangu angenifikiriaje, nikaichagua! Ghafla ikaonekana kana kwamba yule Mjumbe kutola Metal Box alitaka kuzimia. Haraka nikamrudisha Mhudumu wa mvinyo na kutaka aniletee chupa ya mvinyo nyekundu badala yake. Kukata tamaa kwa Mhudumu kukajidhihirisha mpaka usoni kwake kwa kiwango ambacho sijapata kukiona. Vivyo hivyo inaweza kusemwa furaha ya yule mtu aliyetoka Metal Box. Mfarakano huu na Metal Box, acha baki hofu yao juu ya tabia ya “liwalo na liwe” kwa upande wa Watanzania, ukanipa upeo zaidi juu ya matatizo yanayoikabili Serikali ya Tanzania inayojitahidi kufanikisha siasa yake ya Ujamaa.

Page 170: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

170

Uko mfano mwingine mmoja unaopaswa kuzingatiwa. Shirika la Bandari lilikuwa limepungukiwa zana za kuhudumia mizigo; kwa hiyo likatangaza tenda kuwataka wenye uwezo kutaja bei zao kwa dola ya Marekani kuvileta vifaa, na ujenzi wa kuongeza uwezo uliopo; na sehemu kubwa ya malipo itapatikana kutoka Benki ya Dunia, Tenda ya Kampuni moja ya Ulaya ikaonekana kuwa ndiyo iliyofanikiwa, na nikazichukua karatasi zao za Tenda kwa uchambuzi. Nilipokuwa nayachambua makaratasi hayo nikafika mahali paliposema kuwa ingawa bei ilitangazwa kwa dola ya Marekani, lakini itapimwa kwa thamani yake ya sasa., Kwa maneno mengine, Shirika la Bandari lilikuwa linatakiwa kubeba gharama zo zote zitakazotokana na mabadiliko ya thamani ya dola. Nikiwa na wasiwasi juu ya jambo hilo, niliwashauri wenzangu katika bodi kwamba tuweke nafasi nyingi wazi endapo makubaliano na wenzangu yatavunjika kutokana na jambo hili dogo katika tenda. Mnamo muda wa saa mbili tu baada ya kulitamka tatizo hilo, Wazungu walikuwa tayari wanawanung’unikia Mawakala wao waliokuwa ndani ya Serikali ya Tanzaia kwamba, eti mimi nilikuwa naleta matatizo! Wakajaribu kunijia ili tuyazungumze, lakini nikaona kwamba uamuzi wa bodi ungeweza kutazamwa upya na Bodi yenyewe tu, kwa hiyo haikuwako faida yoyote ambayo ingepatikana kwa kukutana nao. Baada ya hapo wakaanza kuelekeza shinikizo zao ndani ya Benki ya Dunia. Shinikizo zilizoelekezwa kwenye Wizara ya Tanzania ya Mambo ya Nchi za Nje zilimsukuma Waziri wa Fedha Cleopa Msuya kumpigia simu Katibu Mkuu wa Wizara ya Usafirishaji, Paul Mkanga, kujaribu kutafiti kwa nini Maafisa wake katika Mamlaka ya Bandari walikuwa wanaiwekea ngumu Tenda hiyo. Majibu yangu mimi, yalipotakiwa, yakawa kwamba Bodi ilikuwa na wajibu wa kufanya kazi kwa haki na kwa uwazi, na kwamba wakati wote inazingatia maslahi ya Shirika na ya wale wanaohusika nalo. Katikati ya malumbano hayo yanayohusu Mkataba wa Kampuni ya Ulaya, nikachukuliwa ghafla kwenda New York. Nilikuwa

Page 171: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

171

nimeteuliwa Msaidizi wa Kiongozi wa Kamati ya Maandalizi kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliopangwa kufanyika Rio de Janeiro, na nilipaswa kuhudhuria vile vile Mkutano wa Kamati jijini New York. Kadhalika, nilikuwa nimechaguliwa na Kundi la G77 na China kutumika kama kiungo katika G8 kuhusu uwezeshaji wa fedha katika masuala ya Mazingira. Nilipokuwa New York, niliombwa na Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi kwenda Washington kukutana na Maafisa wa Benki ya Dunia, nikiwa bado naukumbuka ushauri muhimu kutoka kwa Waziri kwamba, kwa gharama yoyote ile, lazima niepuke kugombana na Benki. Wakati Balozi wa Misri alipokuwa ananiwakilisha katika mazungumzo kule New York, kwenye majadiliano yale ya G77-G8, mimi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari tulikaa hotelini kwangu mjini Washington; tukiwa na Charles Nyirabu, Balozi wa Tanzania Nchini Marekani, na kuzungumza msimamo gani tuukazanie katika kuzungumza na Benki ya Dunia. Nyirabu alikuwa mtu hodari sana katika masuala yote ya fedha za kimataifa, baada ya kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, kwa vipindi vitatu. Baada ya mazungumzo yetu yaliyotuwezesha sisi wote kuwa na makubaliano ya jumla akaniuliza kama nilimtaka afuatane nami keshoye katika shughuli zangu. Nikatarajia kuwako kwa duru lingine; nikamwomba ajiweke tayari tayari. Hofu yangu juu ya kuwako kwa mapambano ikathibitika kuwa ya msingi. Mapema katika kikao cha mwanzo, Mwakilishi wa Benki ya Dunia akang’ang’ania kuwa Tenda iliyotoka kwenye ile Kampuni ya Ulaya ilikuwa inajibu mahitaji yetu kwa kiasi cha kutosha. Kufika hapo nikaamua kuonana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki aliyekuwa anahusika katika eneo letu, ambaye alitokea Malawi. Maafisa wa Benki wakanituhumu kulipeleka suala hilo katika mwelekeo wa Siasa, lakini mimi nikatetea kwamba nilikuwa na kila haki ya kufanya hivyo kutokana na kukataliwa kwa msimamo wangu. Mkutano ukavunjika bila kuwapo kwa hoja zaidi. Jioni ile Nyirabu akaandaa hafla kwa ajili ya Ujumbe wangu, ambako Maafisa kadha wa Benki ya Dunia walikaribishwa. Kabla ya muda wa chakula Nyirabu akashauri yaweko makubaliano, akisema, “Kwa nini hamuyakubali yale ambayo Benki

Page 172: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

172

inayapendekeza?” Na jioni ile, wakati wa chakula, hatimaye nilikubali; lakini kwa maelewano kwamba kukubali huko kutaongezewa na mitaji ya ziada kwa Tanzania, pamoja na manufaa mengine yanayohusiana, ingawa hayajabainishwa. Kwa mara nyingine tena nikawa nimekidhihirisha kile ambacho siku zote nilikuwa namwambia Mwalimu kwamba, sikuzaliwa kuwa Mwanadiplomasia lakini mafunzo mengine muhimu zaidi yaliniingia, na kutokana na hayo niliyojifunza kutoka wakati huo katika fani ya diplomasia yamebaki kuwa ya manufaa kwangu sasa kama yalivyokuwa wakati ule. Yote yanaweza kujumlishwa katika Msingi mmoja usiobadilika, kuwa kamwe waombaji hawatapata nafasi ya kuchagua, hata kama mabadiliko ya maoni kimataifa juu ya dhamiri ya kujikwamua yatakudanganya ukafikiria vinginevyo. Nikakumbushwa yale aliyayasema Mwalimu, “Ni gharama kubwa kuwa masikini!” Tamko hilo halijapata kuwa wazi kuliko ilivyotokea kuwa wakati wa mtikisiko wa bei za mafuta mwanzoni mwa miaka ya 1970. Baada ya Vita vile vya siku sita vya 1967, na hasa baada ya vita vya Yom Kippur vya 1973 baadhi ya nchi za Kijamaa za Kiafrika zilivunja uhusiano wao na Israel. Kwa kutambua hivyo, nchi za Kiarabu zilizokuwa na mafuta zikaamua kutoa misaada kwa nchi zile za Afrika zilizokuwa katika hali ngumu kutokana na kupanda mno kwa bei za mafuta. Wakishirikiana na Jumuiya ya Waarabu, Mawaziri wa Mafuta wa nchi hizo za Kiarabu wakakubali, kwa kusimamiwa na Umoja wa Nchi huru za Afrika, Taratibu zilizoelekeza msaada wa fedha kwa nchi zile zilizoathirika. Kwa upande wake Umoja wa Nchi huru za Afrika ukakasimu majukumu ya kuandaa Mipango hiyo kwa Kamati ya Mawaziri wao watano wa Nchi za Nje, Mwenyekiti wao akiwa Waziri wa Nchi za Nje, Mansour Khalid, kutoka Sudan. Tanzania ikiwa mjumbe katika Kamati hiyo, iliwakilishwa na John Malecela, Waziri wa Nchi kwa ajili ya Mambo ya Nje. Kabla ya kuvunjika kwa uhusiano, Israel ilikuwa na shughuli nyingi nchini Tanzania. Walijihusisha katika Vyama vya Ushirika vya Walaji, COSATA, na Kampuni moja ya Tel Aviv, Mlonot Ltd., ikiwa inaendesha Hoteli ya Kilimanjaro, iliyo bora kuliko zote

Page 173: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

173

nchini Tanzania; pamoja na Beach Hotel ya Dar es Salaam. Waliingia Tanzania, na Afrika kwa jumla, kwa kuhurumiwa kutokana na lile wimbi la maangamizi, kwa kuhesabiwa kama wanyonge wenzetu, waliokumbwa katika hila za Mataifa makubwa ya Ulaya. Theodore Hezl, mmoja wa waanzilishi wa Dini ya Kiyahudi alisema kwa kelele katika kitabu chake Altneuland, “Kwa mara ya kwanza nimeuona Ukombozi wa Wayahudi, watu wangu; nitasadia vile vile Ukombozi wa Waafrika”. Kwa sababu hizo Waafrika wengi katika mila zao wanaihesabu Israel kuwa nchi inayodumu kwa ushujaa wakati ikiwa imezingirwa na majiraji walio mahasidi watupu. Vita vya siku sita vya mwaka 1967 vilianza kubadilisha fikira hizo, na vita vya Yom Kippur vikaimarisha mwelekeo huo. Fikra za Israel kuwa Nchi ya Kijamaa yenye lengo la kutokufungamana na upande wowote, na kukubalika kuwa sehemu ya Dunia ya Tatu, zimeyeyuka, na kuingia badala yake hali ya Nchi ambayo maslahi yake yamefungamana na yale ya Marekani, Uingereza, Ureno ya Sabzar pamoja na Afrika ya Kusini inayodumisha ubaguzi. Kuzinduka huko kwa Waisraeli, kwa kweli na kwa Nchi zote za Magharibi kwa jumla, ni matokeo ya kuimarishwa kwa Siasa Kali mlangoni mwa Viongozi wengi wa Afrika na Jamii walizokuwa wanazitawala. Yote hayo yakajumlishwa pamoja kuifanya nafasi ya Israel katika Bara hili kurudi kuwa ya wasiwasi. Kwa hiyo kuvunja uhusiano ilikuwa ndiyo njia rahisi kwa Nchi za Kiafrika kuelezea mashaka yao dhidi ya Nchi za Magharibi bila kukumbana na madhara yoyote. Baada ya kuundwa Kamati ya Mafuta ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika, Balozi Weidi Mwakasafyuka wa Wizara ya Nchi za Nje, Tanzania, akanipigia simu kunitaarifu kuwa Wizara ilipokea mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Muungano wa Nchi za Afrika akinitaka nitumike kama Mshauri wa Kamati ya Mansour Khalid. Fikira zangu za mwanzo zilinielekeza kusema, Hapana, mimi sikuwa najua lolote kuhusu mafuta. Balozi akayakubali maelezo yangu na kujiendokea, lakini baadaye akarudi na kusema kuwa Serikali ilinitaka nishike nafasi hiyo, kwa vile ilivyokuwa

Page 174: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

174

inahusiana zaidi ya kutoa fedha za kununulia mafuta, kuliko na mafuta yenyewe. Hivyo, dhahiri, nilipaswa kukubali, na mchana wake akaniletea nyumbani kwangu tikiti za ndege kwenda Addis Ababa, posho ya safari na makaratasi ya Maelekezo. Siku mbili baadaye nikapanda ndege kwenda Addis Ababa, pamoja na Waziri Malecela na timu yake kutoka Wizarani. Tulipofika hoteli nikapokea simu kutoka Ofisi ya Bwana Ekangaki, Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika, kuniambia kuwa alitaka kuonana nami; gari ilikuwa njiani kuja kunichukua, nami ningeambatana naye mpaka Uwanja wa Ndege, kumpokea Mwenyekiti wa Kamati. Tukiwa tunaelekea huko, Katibu Mkuu akanipa mawazo yake kuhusu uanzishaji wa Benki maalum itakayotumiwa kutoa fedha: mikopo ya muda wa kati na muda mrefu ya kulipwa bila riba, ila gharama ndogo ya huduma, ambayo ingepatikana katika nchi za Afrika kwa ajili ya kununulia mafuta. Nikamwuliza kwa nini hakutaka kutumia Benki ya Maendeleo ya Afrika ambayo, kwa mawazo yangu, ilikuwa inaendeshwa vizuri na, kwa ada kidogo tu, ingeweza kufanya kazi ile ile: ingewapatia fedha Waafrika na, wakati huo huo, ingeokoa gharama za kuanzisha Chombo kipya kabisa. pendekezo langu halikupokelewa vizuri, nikasikia baadaye kwamba njama zilikuwa zinatayarishwa kuipata Kampuni ya Kiingereza, Lornho, itambuliwe katika shughuli za kununua mafuta, na kufanya mipango ya kupata mikopo kutoka Benki hiyo iliyokuwa inapendekezwa. Lakini mpango huo haukufanikiwa. Baada ya Mkutano ule wa Addis Ababa wote tukaenda Cairo ambako kwa mpango wa Umoja wa Waarabu, Mawaziri wa pande zote mbili walikutana. Katika siku ya kwanza Waziri wa Ghana akawatupia hoja tangu mwanzo Mawaziri wa Kiarabu, akiwaonyesha yale aliyoyaona kuwa wanakubaliana na mawazo ya Mawaziri wa Afrika. Akaleta hoja ya bei nafuu za mafuta kwa ajili ya Nchi za Kiafrika; lakini wazo hilo likawaudhi Mawaziri kadha wa Mafuta, na hivyo pendekezo hilo likakataliwa.

Page 175: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

175

Ingawa nilikuwa naunga mkono mawazo yake katika hilo, nikachukua nafasi kumkumbusha yule Waziri wa Ghana, kwa lugha laini kadiri ilivyowezekana, kwamba uamuzi wa kuvunja uhusiano na Israel ulitokana na misingi ya maadili wala siyo ya uchumi. Lakini lazima niseme kwamba nchi nyingi sana za Afrika hazikutaka kuyaeleza mambo katika sura hiyo kwa sababu ya kuumizwa na bei za mafuta; na hilo linaeleweka. Wakatafuta kufidiwa na mafuta ya bei nafuu, wakati kwingine kote duniani watu walikuwa wanakamuliwa ili kupata bidhaa hiyo muhimu. Matokeo ya Mkutano huo yakawa kiasi kikubwa cha fedha kutengwa kwa matumizi ya Nchi za Afrika, fedha ambazo zingepatikana kupitia Benki ya Waarabu inayoshughulikia Maendeleo ya Afrika, BADEA. Uamuzi huo ukathibitishwa rasmi baadaye katika Mkutano wa sita wa Nchi za Kiarabu uliofanyika Aligers mwezi Novemba 1973, na Benki hiyo ikaanza kufanya kazi yake mjini Khartoum, Sudan, mwezi Machi 1975. Katika kipindi cha kiangazi cha mwaka 1972, wanangu wadogo wawili wakamfuata Manish kusoma kule Uingereza. Angalau Anuj na Rupen waliondoka wakiwa na umri wa miaka tisa, siyo saba; lakini kuondoka kwao kwenda nje ya familia kulituachia sikitiko vile vile. Kwanza walikwenda Stock House, Brunswick, Shule mpya ya msingi karibu na Ashhorst Wood. Baadaye wakamfuata Manish na binamu zao kule Charterhouse, ambako wote walipata makao ya pili katika nyumba iliyoitwa Lockites House, chini ya udhamini mzuri wa Mwalimu Mlezi Norman Evans. Evans alikuwa mtu wa huruma aliyekuwa na masikio mapana yaliyompa jina la utani la Dumbo; na yeye na mkewe Margaret wakafanya kila lililowezekana kuwafanya vijana wetu wote watulie. Hilo lilikuwa jambo kubwa kwa sababu fedha zilikuwa adimu tangu wakati ule wa utaifishaji. Kwa kushindwa kugharimia tikiti za ndege kati ya London na Dar es Salaam siku zile ambazo usafiri ulikuwa na gharama kubwa sana, vijana wale walitumia siku nyingi sana za likizo yao ama kwa dada yangu, Wembley, ama kwa Edna Gundle kule Chigwell, Essex. Tulikuwa na bahati kuwa na Edna, aliyekuwa anawapa vijana wetu wote raha ya maisha ya nyumbani.

Page 176: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

176

Alikuwa mtu mcheshi na mwenye huruma, lakini vile vile makini kwa kuzingatia Taratibu. Kabla ya kukubali kufanya chochote kwa niaba yetu, alinilazimisha kutia saini mkataba wa malezi, na nakala yake ninayo mpaka leo hii. Aliimarisha tabia njema za nidhamu kwa vijana waliokwisha zoea tabia mbaya za kudekezwa na Baba zao, Shangazi zao, na Wajomba zao. Nikitoa mfano mmoja; kama wakimwambia wanataka viatu vipya, lazima atawaambia wamletee kwanza vile vya zamani, avikague. Kwa njia hiyo na nyingine nyingi akasaidia kuimarisha Taratibu za kuthamini mali walizonazo mpaka leo. Kipindi changu cha miaka mitano, nikiwa Meneja Mkuu wa Shirika la Usindikaji kilikuwa kinakaribia kwisha, maana Mkataba wangu ulisema kuwa ningeliachia kiti hicho Desemba 31, 1972; wala mimi sikuwa na nia ya kuendelea zaidi, hata kama mtu angesema au angefanya nini kunishawishi kubadili mawazo yangu. Walikuwako watu ndani ya Serikali waliokuwa wanaamini kuwa mafanikio ya Shirika yalitegemea kuwako kwangu mimi pale. Hasa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, walikuwa na hofu zaidi, wakifikiria yale ambayo yangeweza kutokea mimi nikiondoka, na wakafanya kila hila waliyoiweza kumshawishi Rais akatae kuniachia. Hivyo ukawako ucheleweshaji wa kumpata mtu ambaye wangempendekeza kwa Rais ashike nafasi yangu, zoezi ambalo nilipenda likamilike kabla ya katikati ya mwaka 1972, ili kumwezesha huyo Mteuliwa kupata uzoefu katika kazi yake mpya. Lakini mimi lazima niseme kwamba sikuwa na mawazo kama hayo, eti hakuwako mwingine ambaye angeiweza kazi hiyo ila mimi tu! Kufika mwaka 1972 biashara ilikua imekwisha imarika; nilikuwa nimekwishaipanga Timu nzuri pamoja na Afisa ambaye dhahiri alikuwa na uwezo wa kuishika nafasi hiyo. Werner Kapinga, aliyekuwa vile vile Mjumbe wa Bodi kwa kuteuliwa na Rais. Nikahama kutoka katika Ofisi yangu na kumkaribisha Werner aingie. Hakutaka kufanya hivyo, akipendelea badala yake niendelee kuitumia Ofisi hiyo, na yeye atumie chumba kingine upande wa pili wa jengo. Wafanyakazi wakawa bado wananijia mimi kwa shida

Page 177: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

177

zao; wananiletea na mafaili kuchambua matatizo na kuelekeza maamuzi. Nilijua kwamba nilipaswa kuondoka kwa usalama; kwa hiyo nikangoja mpaka Kapinga alipokuwa kwenye livu fupi ndipo nilipohamisha kutoka kwenye nyumba hiyo vifaa vyangu vyote, nikaacha tu namba zangu za simu kujulisha wapi nitakapopatikana baada ya hapo. Aliporudi Kapinga akajikuta amekamata hatamu zote zinazomwezesha kuikabili hali. Bado tulikuwa tunakula chakula cha mchana pamoja mara kwa mara; sijamwona mtu kama Werner kwa kupenda kula. Na mimi nilikuwa nimeteuliwa Mjumbe wa Bodi na Mshauri asiyelipwa wa Bodi hiyo. Lakini kwa malengo yoyote yale, shughuli zangu ngumu za kila siku katika masuala ya usindikaji yalikuwa yamekoma kabisa, baada ya kuyahangaikia kwa miaka ishirini na miwili. Lakini lazima nitafute nafasi ya kutoa picha ya mwisho kutokana na shughuli zangu katika Shirika la Taifa la Usindikaji. Watanzania wanayo tabia ya ovyo ya utani ambayo wageni wanaokuja na kufanya kazi Tanzania hawaijui. George Anderson, Mwingereza aliyekuwa anafanya kazi katika Shirika la Usindikaji kule Arusha, alikuwa na matatizo na Wafanyakazi wawili wa Kitanzania kuhusu makato yao kulipa mkopo, na vile vile malipo ya uzeeni. Msingi wa tatizo ulikuwa kubadili-badili majina, uliompa matatizo mara kwa mara Karani wa kulipa mishahara. Hatimaye George akakerwa mno na kasoro hiyo kiasi cha kuwaambia, pale hasira zake zilipopanda, kwamba dawa pekee aliyoweza kuifikiria ilikuwa mmoja wao abadilishe jina lake. Alikuwa ameyasahau yote yale aliyozungumza nao mpaka mshahara mwingine ulipoletwa, ambapo ghafla na yeye akapata matatizo katika makato ya mkopo wake mwenyewe. Hapo akagundua kuwa mmoja kati ya wale Watanzania wawili aliowagombeza kwa kweli waliuzingatia ushauri wake na wakabadili jina lake. Jina jipya la mtu yule lilikuwa nani? Amini usiamini ni George Anderson.

Page 178: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

178

TISA

……..NA MAGAZETI Jina la Kampuni, “Lonrho”, wakati wote limekuwa na uzito maalum katika Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kipindi kirefu kabla Edward Heath hajazitaja Kampuni za kuchimba madini zilizokuwa na Makao Makuu yake Uingereza, na Kampuni Tanzu zao nyingi, kuwa “Hazikubaliki mbele ya Ubepari”; na hata zaidi kabla ya uhasama mkubwa wa kibinafsi ati ya Tiny Rowland, Mwenyekiti wa Lonrho, na Mohamed Ali Fayed, walipomwona papa aliyeanikwa aliyeitwa “Tiny” amening’inizwa kwenye chumba cha chakula kule Harrods, jina la Lonrho likatiliwa mashaka, kama si kuchukiwa, siyo tu na idadi kubwa zaidi ya Waafrika weusi, lakini vile vile na sehemu kubwa ya Wazungu Walowezi, walioamini kuwa Tiny hakuwa pamoja nasi. Watanzania hawakuwa tofauti katika mawazo hayo. Hata kama Lonrho ilikuwa Kampuni muhimu katika eneo lililokuwa linalilia uwekezezaji wa mitaji kutoka nchi za nje, lakini Mwenyekiti wa Lonrho alikuwa hatakiwi kabisa na kila mtu aliyekuwa ndani ya Chama Tawala nchini Tanzania, kutoka Rais mpaka mtu wa chini kabisa. Lakini bado, pamoja na hayo yote, miaka ya mwanzo ya 1970 ilishuhudia Lonrho wakiimarisha nguvu zao katika magazeti ya Tanganyika na kwa njia hiyo, wakanirithi mimi kama Mwenyekiti. Kutumbukia kwangu kwenye shughuli hizo kulianza mwaka 1959, nilipotakiwa kuingia katika Bodi ya Tanganyika Standard Ltd. Wakati ule Kampuni hii ilikuwa inachapisha magazeti mawili katika lugha ya Kiingereza; Tanganyika Standard na Sunday News. Kampuni ya Tanganyika Standard ilikuwako tangu miaka ya mwanzo ya 1930 na ilikuwa sehemu ya Kampuni mashuhuri ya East African Standard, iliyojumlisha vile vile gazeti la Uganda Argus la Kampala, na Mombasa Times na East African Standard ya Kenya. Kampuni hizo zote, kama kikundi, zilianzishwa na kumilikiwa na Rudolf na Claude Anderson Rudolf alikuwa rafiki yangu, niliyeshirikiana naye baadaye katika Chama cha Wafanya biashara.

Page 179: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

179

Wakulima wa Kenya, waliokuwa na dukuduku la kutangaza hadharani mawazo ya Wakoloni kwa karibu kila jambo walilohisi lilikuwa linawahusu sana, kutoka kilimo, utalii, viwanda na siasa, mpaka lile linalowagusa sana moyoni; nafasi ya Wazungu katika Afrika Walihusudu kampuni hiyo. Dhahiri maoni ya Mhariri katika Magazeti yote hayo yalikuwa yanaunga mkono sana utawala uliokuwako wa Kikoloni. Wahariri hao, na wasomaji wao, wakijihisi kuwa sehemu ya wasomi; na kweli Wahariri ndivyo walivyokuwa. Hakuna aliyeueleza msimamo huo vizuri zaidi kuliko Mhariri Mkuu wa Nairobi ; mtu mwenye ari, na wengine wanamwita dikteta, Kanali Kenneth Bolton. Kampuni ya Standard haikuwa peke yake katika soko la magazeti nchini Tanganyika, wala mimi sikuwa Mwasia peke yangu katika nafasi ya maana. Kwa kweli Jamii ya Kiasia kwa jumla ilikuwa inajishughulisha na magazeti ya nchini toka miaka ya 1930, ambapo Mhindi aliyeitwa V.R. Boal alipoanzisha gazeti la Tanganyika Herald katika lugha ya Kiingereza na Gujerati, likishindana moja kwa moja na lingine lililoitwa Tanganyika Opinion, ambalo nalo lilichapishwa katika lugha hizo mbili, na kuhaririwa na mtu wa ukoo maarufu wa Patel. Katika kipindi hicho gazeti moja la Kiingereza na lingine la Ki-Gujerati lilikuwa linatolewa kila juma, lakini baadaye yote yakashindwa kuendelea. Gazeti moja la Kiswahili la kila juma lilikuwa linatolewa na Idara ya Serikali ya Habari. Kufikia miaka ya 1960 magazeti yale ya lugha mbili yakasalimu amri mbele ya ushindani wa magazeti ya kundi la Standard, pamoja na yale mengine yaliyoingia katika soko. Hayo ni pamoja na yale yaliyokuwa yanaunga mkono Wanamapinduzi wa Afrika: Uhuru, gazeti rasmi la TANU; Ngurumo lililomilikiwa na kuendeshwa na Mhindi, Randhir Thakar, lakini pia likiunga mkono TANU, na Nationalist, lililokuwa na nguvu kubwa ya kibiashara katika ushindani wa magazeti ya kundi la Standard. Mwaka 1969 nilikuwa tayari nimeshiriki kikamilifu katika Mabaraza mawili ya Kutunga Sheria na Utawala; kadhalika katika Kamati ya Biashara, Klabu za Rotary na Freemasons. Lakini hakuna hata moja kati ya Kamati hizo iliyoniandaa kwa

Page 180: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

180

kukabiliana na mazingira ya Kikoloni yaliyokuwa yanatawala magazeti ya Kundi la Standard wakati ule. Kule Nairobi, Bodi nzima iliegemea Klabu ya Muthaiga, ambayo mawazo ya wanachama wake wote kuhusu Wakereketwa wa Kiafrika yanajulikana kwa urahisi. Lakini mwelekeo wa Waandishi wa Kundi lenyewe la Standard, wanaojiamini wenyewe kuwa watetezi wa Afrika, uliwasukuma kubakiza ghadhabu yao kwa Wazungu wenzao. Wengi katika Wazungu waliokuja Afrika kufanya kazi za muda mfupi, na wakaokota kidogo, au wakashindwa kabisa kuelewa mila za wenyeji, walionekana kuwa watu wa “ngazi ya juu”, au angalau wageni. Watu weupe walio Wajamaa wakereketwa, kama yule Msaidizi wa siku nyingi wa Mwalimu Nyerere, Mjamaa wa kweli Joan Wicken, walikuwa wanalaumiwa hadharani, kama vile vile walivyofanyiwa akina Tiny Rowland, kwa kutokuwa “mmoja wetu”. Waandishi wa Kizungu walioletwa Afrika Mashariki walikuwa labda wanaonekana kuwa watu wa kudharauliwa kuliko wote; wakiingia, kama walivyokuwa wakifanya katika ndege za Kiingereza za aina ya VC10, kuandika habari muhimu kwa ajili ya magazeti yao na Vyombo vingine vya Habari, kisha wanaondoka. Hawa “Wallah wa VC” kama walivyoitwa, walikuwa walionekana na Waandishi wa nchini kuwa kwanza hawana wanalojua kuhusu Afrika na pili, mbaya zaidi, hawajali. Lakini hakuna hata moja kati ya manung’uniko yaliyokuwa yanasikika Klabu ya Mthaiga, wakati wa chakula cha mchana au wa viburudisho vya jioni, yaliyoweza kupata nafasi katika habari za siku. Wajumbe wa Bodi ya gazeti la East African Standard walikuwa wajanja mno kutumbukia katika mtego wa kutoa gazeti litakalowapa mahasidi au washindani wao wengi nafasi ya kulalamika. Nilipoingia kwenye Bodi ya gazeti la Standara mwaka 1959, ilikwisha dhihirika kwa wale waliohusika upande wa Tanganyika kuwa Upepo wa Siasa ulikuwa umeanza kupuliza kwa kasi katika mwelekeo wa Uhuru. Kama mioyoni mwao walikua wanaifurahia hali hiyo, au hawakuifurahia, lakini walitambua haraka kuwa kuendelea kwao kufanya kazi kungetegemea kuepuka uhasama na Viongozi wa TANU.

Page 181: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

181

Lilikuwa jambo la kawaida kwa gazeti la Tanganyika Standard kujidhihirisha kuwa mtetezi wa Wazungu nchini humu, kama ilivyojitokeza katika kipindi kile baada ya Uhuru. Lakini lilikuwa jambo jingine kabisa kwa gazeti kuonekana kuwa na uhasama wa aina yoyote dhidi ya uongozi mpya wa Wanamapinduzi wa Kiafrika. Kwa hiyo mwelekeo wa Maoni ya Wahariri kabla ya Uhuru wa kutetea Utawala uliokuwako, na maendeleo ya soko ukaendelea vivyo hivyo mpaka wakati wa kupatikana kwa Taifa jipya la Tanganyika. Hali hiyo ikaisukuma Serikali mpya, iliyokuwa na shughuli nyingine nyingi, kuyapuuza magazeti yaliyokuwako; vile vile Watumishi wa Kizungu wakaachiwa uhuru wa kuendeleza juhudi zao za kudumisha utamaduni wao wakiwa Afrika, wakati huo huo wakiwatia moyo Waafrika na Waasia wengi kadiri ilivyowezekana, walioelimika, kutumbukia katika aina ya maisha wanayopenda. Katika miaka ya 1950, mwanzoni, nilikutana na A.J. Nevill, Mhariri wa kwanza niliyemjua; baada yake wakaja Bill Ottowill, Ken Ridley, na hatimaye rafiki yangu mkubwa Brendon Grimshaw, anayemiliki kisiwa cha Mayonne, karibu na Mahe, Shelisheli, ambaye bado nawasiliana naye mara kwa mara. Nevill, ambaye wakati wote alionekana nadhifu kwa kuvaa suti nyeupe, siku moja nilimwalika azungumze na Chama cha Utamaduni cha Dar es Salaam ambacho mimi wakati huo nilikuwa Kaimu katibu wake. Upande wa biashara wa Kampuni ya Gazeti ulikuwa unasimamiwa na Charles Thetford, na baada ya yeye kuondoka akashika Alan Nihill, mwana wa Mhe. Bareky Nihill, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki. Klabu ya Gymkhana ya mjini Dar es Salaam, ambayo haikuwa ya Wasomi wala yenye kung’ang’ania mno mila kama ile ya Muthaiga kule Kaskazini, lakini ilikuwa ndio uwanja mkuu wa kutekeleza yale malengo mawili. Mialiko ya kutembelea na kujiunga na Klabu hiyo, iliyokuwa na viwanja vyake vya gofu na kirikiti na, pamoja na hayo, nafasi nyingi zilipatikana za watu waliokuwa na fikira zilizolingana, Waafrika na Waasia, kukutana. Mara baada ya kutumbukia kwenye Bodi, haikupita muda kabla, mimi pia sijaalikwa kujiunga. Kwa kuwa Katiba ya Klabu iliruhusu kuingia watu waliokuwa na damu ya Kizungu tu, basi wakatengeneza

Page 182: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

182

tabaka la “Wanachama wengineo” nje ya Katiba; na hivyo mwaka 1961 nikawa mtu wa kwanza asiyekuwa Mzungu kuwa Mwanachama. Si jambo la kawaida kwa mtu kutamba kuwa na uwezo wa kujiingiza katika kundi lolote, lakini sikujisikia raha kabisa pale Klabu, na nilikwenda huko mara chache sana. Kwa kweli nilikwenda tu kwa ajili ya kukabidhi Vikombe vya michezo kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni kama International Computers Limited, wakati huo Kitegauchumi cha Kampuni ya Kiingereza ya IT. Baada ya uamuzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kusita kutoa leseni kwa Klabu zenye Ubaguzi wa Rangi, Wanachama, pamoja na mimi chini ya Uongozi wa Rais wa Klabu David Newton, wakaamua katika Mkutano Mkuu wa Februari 28, 1962, ambao na mimi niliuhudhuria, kubadili Katiba yao na kuruhusu huduma za Klabu kutumika na watu wa mataifa yote. Sababu yangu ya kutaka kujiunga na Klabu ya Gymkhana ilikuwa kujifunza kucheza gofu. Nilipokuwa naulizauliza David Newton akaniambia kuwa mtu mmoja, Bwana K.C. Fane, angeweza kunisaidia, lakini alikuwa kwenye likizo yake Uingereza, na alitarajiwa kurejea baada ya miezi miwili. Bwana Fane aliporejea akanipigia simu, na mazungumzo yetu yakawa kama ifuatavyo. “Nasikia unataka kujifunza kucheza gofu; tunaweza kukutana pale Klabu katika majuma mawili yajayo; saa 8 mchana kila Jumanne na Ijumaa?” Na mimi nikajibu, “Asante Bwana Fane, lakini itaniwia vigumu kutoka Ofisini wakati huo, na kwa vyovyote vile, joto litakuwa kali mno!” Naye akadakia, “Bwana Chande sahau habari ya gofu; hutaweza kamwe kujifunza kucheza mchezo huo.” Nilikuwa wa manufaa zaidi katika Kikundi hicho katika masuala ya biashara. Wakati nilipoingia katika Bodi, Tanganyika Standard ilikuwa Kampuni moja ya biashara iliyoshughulikia Magazeti, Ofisi ya Uchapishaji, na Utengenezaji wa Vifaa vya Kuandikia. Shughuli zikaongezeka baada ya muda, wala hakutokea mtu aliyehoji busara ya mrundikano wa shughuli kiasi hicho. Kama nilivyowadokezea Wakurugenzi mara baada ya kuingia katika Bodi, gazeti lilikuwa

Page 183: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

183

linabeba mzigo mzito mno, na hivyo Chombo kizima, kilikuwa kinashirikishwa mapungufu ya sehemu nyingine yoyote. Kwa hiyo nikapendekeza zianzishwe Idara nne, kila moja ijitegemee peke yake: Tanganyika Standard News-Papers Limited (ndio Wamiliki); Printpak Tanzania Limited (Uchapishaji), Standard Properties Limited (Wenye majengo); na Office and Stationery Supplies Limited (Wasambazaji wa Magazeti na Watunzaji wa Vifaa vya Ofisi). Pendekezo langu likakubaliwa na kushughulikiwa, na busara ya mgawanyo huo ikadhihirika zaidi kila miaka ilivyopita. Kuanzia mwaka 1962, ilipopitishwa Sheria ya kuwatia watu kizuizini, mpaka Februari 1967, mawazo yaliyokuwa yanatawala miongoni mwa Wazungu waliokuwa katika Bodi yakawa kwamba, pamoja na hali hiyo, bado utaifishaji haukuwa umechambuliwa vizuri. Lakini katika siku zile zilizofuatia Azimio la Arusha, ambapo wasiwasi wangu mwenyewe juu ya Utaifishaji wa Serikali ulifika kileleni, Mwalimu akatoa Hotuba juu ya Ujamaa mbele ya umati mkubwa sana mjini Dar es Salaam, iliyoutilia mashaka gazeti katika sehemu nyingi. Alikuwa katikati ya maelezo marefu kuhusu Hoja ya kuelekeza Msimamo wa Umma kwenye manufaa ya Ujamaa wa Kiafrika, wakati sauti ilpojitokeza katikati ya umati ule kupiga kelele, “Gazeti la Standard! Gazeti la Standard!”. Huyo hakuwa mmoja wa wauzaji wetu mahili, akilitangaza gazeti lake; alikuwa Mwana-TANU mkereketwa aliyekusanya mawazo hayo yaliyoibuka ndani ya Chama. Kwa haraka sana Mwalimu akayatambua matokeo ya yale ambayo yule mtu alikuwa anayatangaza, na akamkaripia mropokaji huyo kwa kelele zaidi, “Unaweza kulihariri?” Majibu yake yakapotea katikati ya vicheko vilivyofuata, lakini hayakuwapiga chenga Wajumbe wa Bodi kwamba suala hilo sasa anaulizwa Rais hadharani, katika aina ya uwanja ambao utazaa wasiwasi zaidi, na pengine wasiwasi wa hatari. Lakini katika ile miaka ya 1960 suala la Utaifishaji lilikuwa kama mwanga mdogo mbele ya jicho. Jambo zito zaidi kwangu lilikuwa uwiano wa madaraka katika kundi hilo. Mwaka 1959 nilipoingia katika Bodi mara ya kwanza, shuguli za kule Kenya zilikuwa

Page 184: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

184

ndicho kitovu; kwa kweli ulifika wakati ilipodhaniwa kuwa shughuli hizo pekee ndizo gurudumu la Bodi nzima. Wakati Kanali Kenneth Bolton alipokuwa anaelekeza kwa simu kutoka Nairobi Maelekezo ya Mhariri yaweje katika Magazeti yote, Mwingereza aliyeitwa Charles Thetford alikuwa amekaa katika Ofisi iliyokuwa karibu akipanga mikakati ya biashara katika gazeti. Hao wawili ndio waliokuwa wanaendesha yote ya Kampuni yaliyotendeka, wakitarajia vibaraka wao wa Dar es Salaam na Kampala kufanya si zaidi sana ya kuipigia saluti Bendera ya Kampuni, na kutii. Kama ilivyo silika yangu, nilizidhibiti tangu mwanzo taratibu hizi za kufanya kazi, pamoja na tofauti zilizokuwako za mahitaji na za utendaji katika masoko tofauti. Mara nilipoteuliwa Mwenyekiti wa shughuli za Tanganyika mwaka 1963, nikaanza kupunguza pole pole misimamo ya Nairobi katika dunia yetu, hatua ambayo lazima ingenigonganisha na yule Kanali mstaafu, msema kweli. Mfano mmoja halisi wa matatizo tuliyokuwa nayo ulitokea wakati Mhariri wetu Brendon Grimshaw alipokuwa katika likizo yake ya mwaka. Grimshaw alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa, na ni vigumu kumpata mwingine badala yake, hata kwa kipindi cha likizo, lakini nikamteua Kaimu, David Martin, kushika nafasi yake mpaka mwenyewe atakaporudi. Kanali Bolton alipoambiwa niliyoyafanya akalipuka na ghadhabu yake, akilalamika sana kuwa angalipaswa kushauriwa mapema, na kusisitiza kuwa David Martin hakuwa mmoja wetu. Mwishowe nikatokea kuwa mshindi katika malumbano hayo, kwa sababu tu hakuwako mwingine zaidi ya Martin ambaye angaliweza hata kukaribia kujaza nafasi ya Grimshaw. Lakini mpaka mwaka 1968 Bolton akawa bado na kauli nzito katika mapambano yetu yaliyo mengi, kwa sababu yeye alikuwa sehemu ya Wenye-hisa kule Nairobi walioonekana kama wa kudumu. Kisha akatumbukia Lonrho katika sura ya Mwenyekiti wake Tiny Rowland, na kufanya mabadiliko kwa kila mmoja wetu kulingana na vigezo vyake. Lonrho ilikuwa inaimezea mate kwa miaka kadha biashara ya magazeti katika maeneo ya Mashariki ya Afrika. Ulipokaribia Uhuru wa Zambia mwaka 1964 Tiny Rowland alikwisha kuyanunua

Page 185: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

185

magazeti ya Times of Zambia na Zambia News na gazeti lililokuwa na wasomaji wachache lililoitwa Livingstone Mail. Akamteua Mwingereza, bingwa wa magazeti aliyeitwa Richard Hall kuwa Mhariri Mkuu wa magazeti yake, na Hall akaanza kazi kwa kuteua Wasaidizi aliowaamini katika nchi hiyo iliyokuwa ndiyo kwanza imepata Uhuru wake. Akaisalimisha Pasi yake ya Uingereza ya kusafiria ili kupata Uraia wa Zambia na, kwa kutumia uhusiano wake na Utawala mpya wa Zambia, akaweza kwa haraka kujitenga na idadi kubwa ya Wazungu. Lakini kufika mwishoni mwa mwaka 1967, Chama cha UNIP kilichokuwa kinatawala Zambia kikamtupa mkono, kwa kumdhania kuwa kibaraka wa Ubepari wa Kiingereza. Hall akapanda ndege kurudi Uingereza, na kuendelea kuandika kitabu alichokiita “Gharama kubwa ya Maadili” juu ya yale yaliyomsibu, kilichomtenga zaidi na marafiki zake wa zamani katika Serikali. Wakati huo Rowland, baada ya kuharibikiwa kule Zambia, akaanza kutafuta nafasi nyingine katika nchi ya Afrika iliyokuwa imetulia zaidi ili kujitengenezea Chombo kizuri cha habari. Macho yake yakaangukia kwenye Kampuni za Standard, zilizomvutia Rowland kwa sababu mbalimbali. Kila gazeti lilikuwa katika nchi isiyokuwa na uhusiano mbaya kati yake na Serikali. Kila moja lilikuwa linaongoza katika soko la nchi yake; na, pengine lililo muhimu kuliko yote, kila moja lilikuwa katika nchi ambako Lonrho walikuwa wanatafuta nafasi ya kupanua biashara zao. Kwa hiyo Rowland akayanunua haraka-haraka kutoka kwa akina Anderson: East African Standard, Tanganyika Standard, na jingine lililokufa haraka, Uganda Argus; na hivyo mara moja akawa mmiliki wa magazeti mwenye nguvu kubwa kuliko mwingine yeyote katika nchi zote za Afrika Mashariki. Baadaye akanunua vile vile msururu wa mahoteli nchini Kenya, pamoja na ile inayojulikana sana Mombasa, ya Nyali Beach. Kila alivyojidhihirisha kutumbukia katika Vyombo vya Habari ndivyo Mheshimiwa Tiny Rowland alivyokuwa chukizo kwa wengi katika Afrika Mashariki. Kutokana na historia yake, Rowland akawapa sababu wakoloni wa Kizungu kufufua uhasama wao mkubwa wa toka zamani kwa Wajerumani. Akawavuruga

Page 186: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

186

wafanyabiashara, waliomwona kuwa anafanya mambo yake, kwa taratibu zake mwenyewe, siyo zile walizokuwa wanazijua wao; na alikuwa anatiliwa shaka na Wanamapinduzi wa Kiafrika, wakihofu matokeo ya kuwa na mtu miongoni mwao aliye tajiri mno na mwenye uwezo mkubwa akitamba bila wasiwasi ndani ya nchi zao masikini. Kiasi cha majuma mawili baada ya kuyakamata yale magazeti, Tiny Rowland akamleta mtu aliyeitwa Mheshimiwa Gerald Percy kuonana nami. Lengo la ujumbe huo lilikuwa kuchunguza kama ningekuwa tayari kuendelea na wadhifa wa Mwenyekiti wa Tanganyika Standard. Nikitambua jinsi Mwalimu asivyomwamini Rowland, na kwa kweli alivyomchukia; na jinsi Joan Wicken, Msaidizi wa Rais, Amir Jamal na Roland Brown, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, wote walivyokuwa wanayaunga mkono mawazo ya Rais kwa uzito ule ule, nikatambua mara moja umuhimu wa kusubiri kidogo. Nikamwambia Percy kuwa nilihitaji kutafakari mapendekezo yake kabla sijafikia uamuzi; na kwamba, kwa vyovyote vile, kwa kuwa nimekuwa nikikaimu nafasi ya Mwenyekiti kwa zaidi ya miaka minne, pengine lingekuwa jambo la busara kwa akina Lonrho kutafuta mtu mpya . Muda mfupi baada ya mkutano ule nikatoka kwenda kunywa soda na Katibu Mkuu wa Rais, Dickson Nkembo, niliyemwelezea mapendekezo ya Lonrho. Nikamwambia kwamba, kwa kweli, niliyakataa, kwamba sikutaka kuendelea na kazi ile kwa sababu “Hebu tuseme kweli, Tiny Rowland amepigwa marufuku nchini Tanzania”. Siku mbili baadaye Nkembo akaniita kuniambia kuwa Rais alinitaka niende kesho yake Ikulu kuonana naye. Baadaye, siku ile ile, Nkembo akapiga tena simu kusema kuwa ule mkutano haungekuwako tena, lakini badala yake Mwalimu amemwachia ujumbe, ambao maudhui yake ni kwamba Serikali ya Tanzania ingependelea zaidi mimi niikubali kazi ya Lonrho na kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi. Mwelekeo huo ni dhahiri, kwamba kama uhusiano wa baadaye kati ya Serikali ya Tanzania na Lornho haukwepeki, basi Mwalimu angehitaji mtu anayeaminika, yaani mimi, niwe ndani yake.

Page 187: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

187

Hapo sasa nikamrudia Gerald Percy na kumwambia kuwa nilikuwa tayari kuendelea na kazi kwa masharti mawili. Kwanza Bodi ya Wakurugenzi iwe na uhuru wa kibiashara; na pili Kanali Bolton apunguze kujitumbukiza kwake katika masuala ya uandishi na ajira katika gazeti. Percy akaridhika na kuyakubali yote mawili. Badiliko lingine, moja tu, lililotarajiwa kuafikiwa na upande wa Lonrho lilikuwa kuteuliwa katika Bodi wajumbe wengine wawili, wao wenyewe. Kwa kadiri ninavyokumbuka, hakuna hata mmoja kati ya hao wapya aliyewahi kuhudhuria kikao, kwa hiyo tukaendelea kuendesha Kampuni kama vile tulivyokuwa tukifanya zamani, ukiondoa wale tuliokuwa hatuwataki kutoka Nairobi. Sisi tukafurahi na, inaonekana, na Lonrho pia, hasa kwa nafasi ile ya kuwa peke yetu katika soko kujipatia faida nzuri. Kisha, mwishoni mwa mwaka 1969, nikapokea ujumbe kutoka kwa Paul Bomani, Waziri wa Mipango, kunitaka niende kuonana naye. Nilipofika ilidhihirika, kutokana na wasiwasi wake, kwamba ule haukuwa mkutano wa kawaida kati ya marafiki wa zamani. Akanielekeza kukaa kitako, kisha akaniambia kuwa alitaka kuzungumza nami kwa nafasi yangu ya Mwenyekiti wa Bodi ya Magazeti ya Standard: kwamba Serikali imeamua kuitaifisha na kuiweka chini ya usimamizi wa Shirika la Taifa la Maendeleo, NDC, kwa ajili ya shughuli za kila siku, na mimi nikibaki kwenye Bodi hiyo kama Mwenyekiti. Nikakaa kwanza na kuyatafakari yale aliyoyasema, ambayo mimi hayakunishangaza kutokana na yale yote yaliyotokea katika miaka miwili iliyopita. Wakati huo huo nikaamini kuwa kufanya hivyo ni kukosea, na nikamwambia Bomani vivyo hivyo. Nikamwuliza, Serikali ina sababu gani ya kutaka kudhibiti magazeti ambayo wakati wote yamekuwa yanaunga mkono Chama na Serikali. Kama sababu ni fedha, basi pengine kumiliki magazeti siyo njia inayofaa: hebu angalieni ufanisi wa Magazeti ya Chama. Kisha nikapendekeza, “Kwa nini hamteui Bodi ya Ushauri kusaidiana na Wahariri wa gazeti? Serikali ingeweza kuteua

Page 188: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

188

Wawakilishi kutoka, tuseme Wasomi, Wanasheria, Wafanyabiashara, pamoja na watu wengine wachache wenye busara, na hawa wangeweza kufanya kazi bega kwa bega na Mhariri”. Sasa ikawa zamu ya Paul kutafakari, hatimaye akaniuliza, “Unadhani Tiny Rowland atayakubali mapendekezo yako?” Nikamjibu kuwa sijui, lakini shinikizo la Lonrho ni nzito, kwa hiyo nilikuwa na hakika kabisa kuwa watalikubali jambo lolote lisilokuwa na uhusiano na faida watalikubali. Paul akakubali, akisema kwamba atanipigia simu baada ya siku chache. Baada ya majuma matatu Waziri Bomani akanipigia simu tena, kunitaarifu kuwa Serikali imeyatafakari kwa makini mapendekezo niliyoyatoa badala ya yale ya Serikali, lakini bado Serikali ikaamua kushikilia msimamo wake ule ule. Akaniomba radhi kwa hilo, lakini bado uamuzi wa kutaifisha ukabaki pale pale. Nikamjibu kuwa ni vema tu, kama huo ndio uliokuwa uamuzi wao. Nikaendelea, “Mnakijua barabara hicho mnachokitaifisha? Kama mnataifisha magazeti, mtapata mashine za kuchapia, madeski na viti; vifaa kadha vya kupigia picha, filam na mafaili,basi. Mitambo ya kuchapia gazeti si mali ya Kampuni, na majengo kadhalika!”. Majibu ya Bomani yakawa mafupi na ya wazi; akashituka na kusema, “Mungu wangu!” Kisha akapiga simu na, ilipokuwa hakupata jibu, akaacha na kuniambia atanitafuta tena baadaye. Majuma mengine sita yakapita kabla sijasikia lolote kutoka kwa Waziri. Mazungumzo ya safari hii yakawa mafupi zaidi kuliko yale ya safari iliyopita. Akanitaarifu kuwa Serikali itataifisha Kampuni zote nne, na kwamba mimi ningeendelea kuwa Mjumbe wa Bodi kama ilivyopendekezwa hapo mwanzo. Tiny Rowland kamwe hakupata kujua kuwa nililazimika kueleza Serikali ya Tanzania muundo wa Shirika lake, jambo ambalo, kwa vyovyote vile, Serikali yenyewe ingeweza kulipata kutoka kwa Msajili wa Makampuni. Pengine ilikuwa rahisi zaidi kwa Serikali kuamua kutaifisha Kampuni zote nne katika Kundi hilo, kuliko kutaifisha ile moja tu iliyokuwa inachapisha magazeti. Hiyo ilikuwa hatua iliyoweza kuchukuliwa kwa haraka zaidi, na ambayo ilikuwa na machungu kidogo zaidi kwa wote waliohusika.

Page 189: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

189

Utawala mpya ulipokuja ukanikuta nimesharudi kwenye Bodi, wakati Rais mwenyewe ndiye aliyekuwa Mhariri Mkuu. Mhariri Mtendaji, Brendon Grimshaw, aliyeponea chupuchupu kuyeyuka pamoja na Lonrho, akapelekwa kuongoza Idara mpya ya Uhusiano iliyopewa jukumu gumu la kusafisha hisia mbaya zilizokuwako dhidi ya Shirika la Taifa la maendeleo, NDC. Kwangu mimi ya kuagwa kwake kutoka gazeti la Standard ilikuwa, kwa vigezo vingi, mwisho wa kuwajibika kwa utawala wa Kikoloni nchini Tanganyika, ingawa hali hiyo ilijidhihirisha kiasi cha miaka kumi baada ya Uhuru wenyewe kupatikana. Tulipata vinywaji na vitafunio, tukiwa tumekusanyika katika vikundi vidogo vidogo, tukizungumza bila makelele, kama ambavyo mtu alipaswa kufanya kule Gymkhana saa za magharibi. Kisha baada ya wasimu kukamilika na hotuba za mwisho kutolewa, Brendom Grimshaw, muungwana kama desturi yake na bado rafiki yangu mkubwa, alipitapita akimuaga kila mfanyakazi mwenziwe, akiwapa mkono Wakusanyaji wa Habari, Waandishi Mahsusi, Wahariri Wasaidizi na Wapiga Picha, akiwaelekeza majukumu yao kuyatenda wakiwa waaminifu kwa Utawala Mpya; na kuwaongeza ari kwa kuwaambia wajihisi kama timu ile ile ya kirikiti iliyokuwa inashinda, hata kama wanabadili Kapteni. Giza likawa linaingia, na jua likawa linazama. Jua lilikuwa linazamia wapi ndilo swali ambalo hakuwako mmoja wetu katika gazeti aliyeweza kulijibu, lakini bado haikutuchukua muda kabla kuligundua jibu. Siku ile ya kuteuliwa kwake, nikapata habari kwamba Serikali ilikuwa imemweka Frene Ginwalla, raia Mhindi wa Afrika ya Kusini, kuwa Mhariri wa kwanza wa gazeti jipya la Standard lililotaifishwa na kupewa jina jipya la Daily News; na mara baada ya kuanza kazi akaligeuza gazeti hilo kuwa na mwelekeo wa siasa za Kimapunduzi. Moja ya vitendo vyake vya kwanza kikawa kunifuata London nilikokwenda kwa shughuli zangu, ili tuzungumzie mipango yake ya baadaye. Alipofika London akahangaika kukutana na watu wengi mashuhuri. Richard Gott alikuwa Mwandishi mashuhuri wa magazeti na vitabu aliyejipatia sifa kwa kuutetea Ujamaa katika Marekani ya Kusini wakati wa vurugu za kisiasa za miaka ya 1960.

Page 190: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

190

Kipindi kifupi kabla ya hapo. Muda mfupi kabla ya hapo aliandika kitabu kilichoitwa Vita vya Umma ndani ya Amerika ya Kusini; na alikuwa mtu wa akili nyingi sana na msimamo safi wa siasa uliowazidi mno Waandishi wenzake wengi wa Kiingereza, hata katika miaka ile ya 1960. Kwa nafasi yake ya Mhariri wa Mambo ya Nje, yeye alikuwa wa kwanza kuteuliwa na Frene Grinwalla, na kwa maoni yangu ndiye aliyekuwa bora kuliko wote; ila, pamoja na sifa zote hizo, hakuwa na uzoefu wowote katika mambo ya Afrika, wala yale ya Jumuiya ya Madola. Wala mabadiliko hayo yaliyoanzishwa hayakwishia kwa Richard Gott. Mnamo miezi michache akawa ameongezewa rafiki yake, Rod Prince, Mhariri wa zamani wa gazeti la Peace News, na Msaidizi wa Mhariri aliyefunzwa na Shirika la Magazeti ya Kifaransa, AFP, kule Paris. Mwajiriwa mwingine wa Kiingereza alikuwa Ian Christie, mwana wa mmiliki wa hoteli kule Edinburgh aliyewahi kwenda Msumbiji kuwasaidia Frelimo katika matangazo yao, mpaka baadaye akapata heshima ya kubandikwa jina Mh. Haw Haw na Wazungu waliokuwa wanalegalega kule Rhodesia kabla ya uhuru. Kisha, kama Frene Ginwalla alivyokuwa anaunga mkono ANC, Tony Hall naye akajitokeza, pamoja na Mwandishi hodari mwingine wa Kenya, Phillip Ochieng, mwandishi wa makala ya kila juma, kukosoa sana kitendo kiovu cha kila Mwanasiasa katika Afrika ya Mashariki. Kwa kigezo chochote kile, na hasa kwa kiwango cha gazeti la Standard, timu hiyo ilikuwa nzito; lakini vile vile ilikuwa imezidiwa na ubinafsi na ukereketwa, kiasi kwamba haukupita muda mrefu kabla ya mlipuko wa kwanza kuzuka. Cha kushangaza, lakini pengine ilitarajiwa, mlipuko huo ukawahusu watu wawili miongoni mwa wale wageni waliokuwa na ujuzi mkubwa kabisa. Wakati ule ilidhaniwa kuwa ni tofauti za mitazamo kati ya Ginwalla na Gott: Ginwalla aliupinga msimamo wake uliotokana na kutukuza mafanikio ya Mwenyekiti Mao dhidi ya Uongozi wa Kirusi, wa zamani na wa sasa. Wakati wote mwelekeo kama huo ulikuwa

Page 191: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

191

unamwudhi Ginwalla, kwa sababu tu Warusi wamekuwa wakiunga mkono Chama chake cha ANC. Kwa nje tatizo hilo lilionekana kuwa la kisiasa tu, lakini ubinafsi ukatumbukia na mji ukawa hauwatoshi wote wawili. Kwa hiyo Gott akatafuta nafasi ya kuonana na Mwalimu, akiwa anaanza taratibu za kujiondoa kwenye nafasi ile. Wawili hao wakakutana nyumbani kwa Mwalimu, Msasani, Kaskazini kidogo ya mji wa Dar es Salaam. Gott akajieleza kwa kirefu katika mazingira ya uhuru kabisa juu ya matatizo yaliyokuwa yanamsibu katika kutekeleza kazi zake mbele ya Mhariri aliyekuwa na amri kali kali. Akaendelea kusema kuwa, kwa hakika, wakati umefika kwa Mhariri Mkuu kuteua Mtanzania Mzaliwa kulihariri gazeti. Lazima hoja za Gott zilimridhisha Rais mwisho wa juma lile maana mnamo majuma mawili Mikataba ya Ginwalla, Gott, Hall na Prince ikawa imepanguliwa yote; wote wakaondoka mjini. Sammy Mdee, Mwandishi kijana Mtanzania, hodari sana wa lugha zote mbili za Kiswahili na Kiingereza, na aliyekuwa na uzoefu wa kutosha, akateuliwa Mhariri Mtendaji. Ulikuwa mwisho wa ajabu wa sura nzuri ya mwanzo katika historia ya gazeti la Standard katika muhula ule mpya baada ya Azimio la Arusha. Ulishusha pazia kufunga ushirikiano mzuri mno niliopata kuuona katika miaka mingi niliyokuwa katika gazeti la Tanganyika Standard. Lakini vile vile ulikwisha, kwa bahati nzuri, kuondolewa kwa mizigo mikubwa ya magazeti ya nyongeza yaliyokuwa yanatolewa nyakati zile za Ginwalla na Goff, nyongeza ambazo zinabaki kuwa historia, baada ya kutolewa aina moja ya kurasa mia kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Lenin, yaliyotupwa katika mifereji ya jijini kwa idadi kubwa mno kwa kutumia vijana wengi sana, kiasi cha kuziba mifereji ya maji machafu jijini Dar es Salaam. Dhahiri Gott alizikumbuka kwa hamu siku zake za kukaa Dar es Salaam. Akiziandika habari zake katika gazeti la London la Guardian karibu miaka arobaini baadaye kuhusu kifo cha Mwalimu, akayakumbuka mazingira ya kuajiriwa kwake na kuondoka kwake. “Nilipokaribishwa Dar es Salaam nilijikuta nikiwa Mhariri wa

Page 192: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

192

mambo ya nchi za nje katika Gazeti la Taifa ndani ya nchi ya Chama kimoja, na mara nikaingia matatani na Mabalozi wa Uingereza na marekani kwa kuwaandikia habari Reuters. Katika taarifa za Vietnam tulikuwa tunafuta maneno ya “Viet Cong; na kuandika badala yake Wapigania Uhuru wa Vietnam ya Kusini”. Gott akaendelea. “Nyerere hakuwa na wasiwasi katika majukumu yake kama Mhariri Mkuu, lakini akatusisitizia tusikwepe kuandika habari zinazohusu kasoro zinazodhihirika katika wizara mbali mbali, na mara moja tu aliingilia kati katika suala hili. Frene Ginwalla alinitaka niandike Maoni ya Mhariri kulaani vitendo vya Rais Nimeiri wa Sudan, aliyekuwa ndiyo kwanza amewanyonga wanachama kadha wa chama cha Kikomunisti cha Sudan. Nimeiri alikuwa mmoja wa Viongozi waliomwunga mkono Mwalimu Nyerere katika mapambano yake dhidi ya iddi Amin wa Uganda; na Maoni ya Mhariri, niliyoandika dhidi ya rafiki wa Tanzania wa wakati huo yakawa yanaaibisha sana. Frene akajiondokea nchini kwa ndege ya kwanza, na mimi nikafuata mara baada ya hapo”. Kuondoka kwa Ginwalla na Gott, Ginwalla akiwa amesonga mbele kuelekea kwenye kiti cha Spika katika Afrika ya Kusini baada ya kukomeshwa kwa Ubaguzi wa Rangi, kukawa kumewafungulia mlango Waandishi wa Kitanzania. Aliyetia fora katika hao akawa Ben Mkapa, aliyepata mafunzo yake katika gazeti la London la Daily Mirror, kutokana na msaada wa marehemu Barbara Castle la mumewe Edward. Ben, mwenye karama nyingi, hasa za ujuzi na matumizi ya lugha, aling’ara tangu mwanzo; na mimi au mwingine yeyote aliyemwona akifanya kazi zake pale Daily News, zamani Standard, hakushangaa kwamba maendeleo yake ya baadaye yangezidi hata yale ya Frene Ginwalla, mpaka pale alipopelekwa Wizara ya Nchi za Nje kuwa Waziri, na hatimaye kustahili kushika nafasi yenyewe ya Rais wa Tanzania. Mara nyingi tulikuwa tunakutana kama ndugu na, kabla hajawa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, yeye na mimi tulikuwa Wajumbe wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert. Katika kipindi kile alichokuwa Waziri wanchi za Nje, rafiki yangu wa toka zamani Malcolm McDonald, Rais wa Chama cha Nchi za Madola, aliyekuwa anaishi katika mtaa ulioitwa Seven Oaks, Kent

Page 193: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

193

ya Magharibi, alikuja kukaa nasi baada ya kutoa taarifa ya muda mfupi kidogo. Kwa taarifa ya muda mfupi vile vile nikamwalika Ben naye aungane nasi katika chakula cha jioni. Ilikuwa siku ya Jumapili, na hivyo dereva wake hakuwa kazini; lakini akaliendesha gari mwenyewe kuja kukutana na Malcolm, mwana wa Ramsay McDonald ambaye, naamini, alikuwa Waziri wa Nchi mdogo kwa umri kuliko wote alipoingia katika Serikali ya Kiingereza. Katika siku zilizofuata, nikawa Mwenyekiti wa Magazeti ya Standard, lilizuka jambo lililokuwa na utata maalum wa kisiasa. Kwa miaka kadha Mwalimu amekuwa akifanya jitihada ya kukomesha mawazo yaliyoufanya mji wa Dar es Salaam kuwa kitovu cha maisha ya Watanzania. Mwaka 1973 akachukua hatua yake kubwa kuliko nyingine zote zilizopita ya kuhamisha Makao Makuu ya Nchi maili mia nyingi mpaka Dodoma. Wakati majengo mapya ya Bunge na Makao Makuu ya Chama yalipokuwa yanajengwa akamwagiza Waziri Mkuu Salim Ahmed Salim kutafiti pamoja nami uwezekano wa kulihamishia Dodoma gazeti letu vile vile. Nikitambua kwamba nilipaswa kuyatoa matamshi yangu kwa uangalifu, kwa vile mwelekeo wa Siasa ulikuwa unajengeka mgongoni mwa Mradi wa Dodoma, nikatamka kwamba hatua kama hiyo ingeweza kuchukuliwa, lakini ingehitaji gharama kubwa kuikamilisha. Hivyo ingebidi upatikane mtambo mpya wa kuchapia magazeti upatikane na ujengewe; majengo yakodishwe, au yanunuliwe, au mapya yajengwe; nyumba zinazofaa kuishi wafanyakazi na familia zao pia zipatikane; na huduma zilizopo za mawasiliano ya simu ziimarishwe na kufanywa za kisasa zaidi. Labda haishangazi kuwa hakuna aliyehama; lakini kuondoka kwangu mimi mwenyewe kulikuwa kunakaribia. Reginald Mengi, mfanyabiashara hodari kutoka Mkoa wa Kilimanjaro,ambaye baadaye akawa kama nyota katika masoko ya habari, akateuliwa kuwa Mwenyekiti badala yangu. Nikaondoka na mambo mengi ya kukumbuka, lakini bila masikitiko. Siku za Wafanyakazi wacheza-kirikiti, na za akina Tiny Rowland, sasa zilikuwa zimeachwa nyuma. Tukiwa na watu kama Mkapa kileleni, na Mengi akajitokeza, nilikuwa sihitajiwi tena kwa nguvu ile ile kama nilivyokuwa nahitajiwa zamani.

Page 194: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

194

Maendeleo ya Magazeti ya Standard hayakutegemea tena matukio ya Nairobi na London; sasa Watanzania, kwa haki kabisa, hatimaye wanaubeba mzigo wote. Miezi michache baadaye nikasoma habari fupi iliyosema kuwa Mengi amejiuzulu nafasi ya Mwenyekiti, ili ahangaike kuanzisha Kampuni yake mwenyewe ya Habari.

_______________

Page 195: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

195

KUMI SHUGHULI ZA FREEMASON

Ingawa kipindi kile cha mwisho wa miaka 1960 kilikuwa cha wasiwasi kwa wengi wa jamii ya Kiasia nchini Tanzania, miaka ya mwanzo ya 1970 kilizaa wasiwasi wa aina nyingine, safari hii katika mpaka wa Uganda. Kuingia kwa utawala wa Jenerali Idi Amin kulizaa aina mpya ya misukosuko katika historia ya nchi hiyo; wala haukupita muda kabla ya kuuelekeza Utawala wake wa Waafrika watupu, na wa kikatili, kwenye maangamizi yake mwenyewe. Sheria mpya za Uraia zilizozingatiwa kama dini ziliwalazimu Wageni wengi mno , hasa Wahindi waliokuwa na Uraia wa Kiingereza, kuikimbia nchi na kuwasababashia matatizo makubwa wengi wa wale waliohusika. Miongoni mwa hao walioamriwa kuondoka kwa taarifa fupi sana, bila kuchukua mali zao zaidi ya sanduku moja tu la vifaa, walikuwa familia ya Jayli, pamoja na kwamba walikwisha kuwa raia wa Uganda; lakini Uraia wao ukawa umefutiliwa mbali kwa tangazo la Televisheni. Kakiye Jayli, Manibhai, alikuwa mmoja wa wale waliofutiwa Uraia wao, na keshoye akaitwa na Waziri wa Ndani kuambiwa kuwa anawekwa kizuizini. Dereva wa Manubhai akaamrishwa kuendesha gari, akisindikizwa, kutoka Ofisi ya Waziri mpaka kwenye lile gereza lenye sifa mbaya la Makindye. Wote wawili wakalala jela. Familia ya Manubhai ilijulishwa habari za kutiwa ndani kwake saa za jioni sana. Yule dereva akaachiliwa baada ya siku mbili, lakini Manubhai na gari lake Mercedes 500 wakaendelea kusota kizuizini. Askari Magereza wakawa wanalisafisha gari hilo kila siku, na Manubhai akatunzwa kwa heshima kubwa mno. Kikaletwa kutoka nyumbani chakula cha watu wasiokula nyama, pamoja na msahafu wa Hindu, Bhagvad Giba. Kuwamo gerezani humo Mwandishi wa Kiingereza, Sandy Gall, na wengine wachache katika vyumba vya jirani, na Taarifa za Habari zilizosikika mpaka Uingereza, ziliwapa matumaini ya kuishi wote waliokumbwa na janga hilo la kutisha. Manubhai mwenyewe, mtu wa Imani mpole na mwema, akafanikiwa kudhihirisha imani yake.

Page 196: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

196

Lakini gereza likabaki na kumbukumbu yake. Baadhi ya wanafamilia wakaihama nchi; na, baada ya kuwa kizuizini kwa majuma matatu, Manubhai naye akaachiwa na kutakiwa aondoke pia. Mabalozi wawili, wa Marekani na wa Uingereza, wakajitolea kumsaidia. Kama nilivyosema, matokeo ya mikasa kama hiyo kwa familia mara nyingi yakawa kukatishwa tamaa lakini vile vile uchumi wa Uganda ukawa umevurugika kwa kiwango kikubwa. Kwa mfano, familia ya Jayli iliharibikiwa katika biashara zao za kusindika sukari, kutengeneza bia, na bidhaa nyingine kama masanduku ya vioo, viberiti, vyuma kwa ajili ya ujenzi, chai na nguo. Wakati ule wa kuwafukuza Wahindi, shughuli hizo zilikuwa zinaingiza kiasi cha asilimia kumi ya Pato la Taifa la Uganda. Kwa hiyo vitendo vya Idi Amin kuwafukuza Wahindi havikuwa tu chuki na vya Kibaguzi, bali viliathiri hatima ya nchi ambayo wakati huo alikuwa anaitawala. Maoni yangu mimi ni kwamba aliyatambua hayo yote kabla ile amri haijatekelezwa, lakini azma yake ya kukabiliana na Serikali ya Kiingereza, ambayo ni sehemu ya uhusiano, wa pendo na chuki, na nchi iliyomfundisha mbinu za vita, ikalipuka wakati huo. Kwa sababu hiyo, naamini kabisa kwamba, laiti Serikali ya Kiingereza ingelionyesha huruma kwa Waasia waliokuwa wanaondoka, Amin angalipunguza ghadhabu zake dakika za mwisho, akalazimika ama kuifuta Amri yake ama kulegeza kamba kidogo kwa namna nyingine. Badala yake Serikali ya Kiingereza, kwa kumtumia Jim Callaghan ikamsihi Amin kufikiria upya uamuzi wake. Katika mazingira hayo ambayo hata hakuyaelewa; ikapatikana sababu nzuri ya kutoa amri ya kuwafukuza Wahindi ingawa hapo mwanzo hawakukubalika, lakini hatimaye Waasia walio wengi waliofukuzwa Uganda wakakimbilia Uingereza, ingawa wachache walikwenda Canada, na wengine nchi za Ulaya. Kuishi kwa Waasia hao nchini Uingereza kuliratibiwa na Kamati ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Gavana wa zamani wa Tanganyika, na rafiki yangu wa zamani, Mhe. Richard Turnbull. Historia inaonyesha jinsi uhamiaji huo ulivyowanufaisha wengi kati ya wale waliofukuzwa, na vile vile zile nchi zilizowapokea.

Page 197: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

197

Historia inaonyesha pia jinsi utawala wa maguvu wa Idi Amin ulivyoporomoka, kama zilivyoporomoka tawala za wote wale waliohalalisha mabavu, na hatimaye Mwalimu Nyerere akawa ndiye chimbuko la mabadiliko. Mwaka 1979, baada ya majeshi ya Idi Amin kuteka sehemu ya Mkoa wa Kagera wa Tanzania, Majeshi ya Tanzania, pamoja na kuwa na silaha duni, yalipambana kama simba na kuyafagilia majeshi ya Uganda nje ya Tanzania. Lakini Mwalimu hakuishia hapo; akizingatia hoja ya kupata mabadiliko ya utawala nchini Uganda, akayaamuru majeshi yake kusonga mbele moja kwa moja mpaka Kampala: na yakamwondoa Amin! Kukawako faraja na furaha kubwa baada ya kupatikana habari za kupinduliwa kwa Amin. Idadi ndogo ya wale Waasia waliofukuzwa wakarejea kushika tena mali zao walizokuwa wamenyang’anywa. Familia zilizomiliki Kampuni kubwa za Viwanda, kama akina Madhvani na akina Mehta, wakachukua tena mali zao na kuwekeza zaidi katika kuviimarisha Viwanda vyao, mwelekeo ulioendelezwa zaidi pale baada ya Lule,Binaisa na Obote, Rais Museveni aliposhika madaraka. Nilitokea kuwapo kwenye Mkutano uliofanyika Neasden, Uingereza, katika miaka ya 1980, Rais Museveni alipowahutubia Waasia kiasi cha elfu mbili waliokuwa wamefukuzwa kutoka Uganda, akiwahimiza kurudi kwenye nchi yao asilia ili kuchangia katika kujenga upya uchumi wa Uganda. Akiyaangalia madhara yaliyoletwa katika kipindi cha Amin, Rais Museveni akawaambia hao Wananchi wenzake, “Kipindi chote hiki sisi tulikuwa tunapambana maporini, wakati wenzetu ninyi mlipokuwa mnastarehe huku Shepherds Bush”. Akina Madhvani wakarudi Uganda, na hatimaye mmoja wao katika ukoo, Niirisha Madhvani Chandaria akateuliwa na Museveni kuwa Katibu wa Kwanza katika Ubalozi wa Uganda kule Washington, DC, kwa kazi ya kushawishi uwekezaji mpya. Yuko huko bado, akiwa kama Balozi Mdogo. Ghasia za Amin za kuwafukuza wenzake zilipotulia, mawazo yangu yakarudi haraka kwenye hatima ya kazi yangu mwenyewe. Nilipoiacha nafasi ya kuendesha Shirika la Taifa la Usindikaji mwishoni mwa Desemba 1972, sikuwa tena na ajira ya kudumu.

Page 198: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

198

Lakini kusema hivyo maana yake siyo kwamba sikuwa na kazi ya kufanya; haikuwahi kuwa hivyo na, naamini, haitapata kuwa. Lakini kwa kuwa nilitumbukiza nguvu zangu nyingi katika biashara za familia, na kisha kuziona mali zote hizo zinamezwa mara moja na Serikali, nikaamua kwamba shughuli zangu za baadaye zitaendeshwa kwa namna ninayoitaka mimi, kwa masharti yangu, na kwa kasi inayonifaa mimi. Zaidi ya yote, nilitaka sasa niwe na uhuru wa kuchagua utakaotokana tu na kuhangaika kwangu katika yale nitakayoyaona kuwa ni njia ya kuniongezea haraka miradi mbalimbali. Tangu mwanzoni mwa mwaka 1973, nimejitahidi kujithibitishia mwenyewe, na kuwathibitishia wengine kwamba, kwa kweli, ujuzi nilioupata katika biashara ya familia ungeweza kuhamishiwa kwa urahisi katika sehemu nyingine; na, katika kufanya hivyo, nilitaka kuendelea kutimiza ahadi niliyotoa mbele ya Mwalimu miaka mingi iliyopita, kuutoa utaalam na uzoefu wangu kwa manufaa ya Taifa letu changa. Sasa hatimaye, nilipokuwa mtu huru, nikaendelea kujihusisha na kazi nyingi za Serikali na za Mashirika zilizozuka wakati wa Azimio la Arusha. Kuanzia treni na meli, ndege na viwanda, na kisha mabenki na magazeti, majukumu yakaongezeka kujumlisha, nikitaja machache, Bahati Nasibu, Utalii, Barabara, Ujenzi, Hospitali, Maji na Hifadhi ya Mazingira. Ninayo ya kueleza juu ya kila moja ya shughuli hizo, lakini labda yale yanayohusu hifadhi ya mazingira ndiyo ninayoyaenzi zaidi moyoni mwangu. Lakini kabla sijayaeleza hayo yaliyo mazito sana ya uhusiano kati ya binadamu na mazingira yake, yaliyokuwa yanasumbua kichwa changu tangu nilipokuwa mtoto kule Bukene, nataka nirudie kuhangaika kwangu katika shughuli ninazoweza kuziita “zisizokuwa na faida”. Pengine neno hilo “zisizokuwa na faida” halieleweki vema, maana ingawa ni kweli, kwa tafsiri finyu, kwamba shughuli zile hazikuzaa fedha, lakini mafanikio yaliyopatikana kutokana na shughuli hizo kwa zaidi ya miaka hamsini iliyopita hayana mfano wake, wala thamani yake haipimiki, na hivyo bei yake ni kubwa kuliko binadamu anavyoweza kuikadiria.

Page 199: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

199

Nimekwisha andika kwa kirefu jinsi Baba yangu Keshavji alivyonilea katika maadili ya kazi ngumu. Jitihada zake zikafanikiwa mno, kiasi kwamba sikuthubutu kutegea katika kazi yoyote niliyoifanya, wala sikushirikiana na wengine waliokuwa wanategea kazi. Lakini Baba yangu alinipa zawadi kubwa zaidi, moja kutokana na uswalihina wake. Tangu utoto wangu alinishinikiza kutambua kwamba binadamu wote wana wajibu mkubwa zaidi; kwanza kabisa kwa Mwenyezi Mungu, lakini vile vile kwa binadamu wenzao wasiokuwa wamebahatika kama wao. Nasikitika kueleza kuwa haikuwamo ndani ya roho yangu ari ya kushika dini kama aliyokua nayo Baba yangu, ingawa bado naendelea kumwamini Mwenyezi Mungu. Lakini katika kipindi chote nilichofanya kazi nimezingatia kwa dhati misingi yote ya ubinadamu, na nikaitumia kila nilipoweza kwa uwezo wangu wote. Siku zangu za mwanzo katika kikudi cha Rotary nimekwisha zieleza. Lakini kabla sijajiunga na Rotary nilipata hamu ya kujiunga na Chama hiki cha kusaidiana cha Freemasonry. Ilitokea hivyo kwa sababu ya tabia na vitendo safi mno vya marafiki zangu wawili niliokuwa nao karibu sana wakati huo; Bob Campbell Ritchie, Mwingereza, na John Maclean Mkochi. Hapo mwanzo wala sikujua kiwango cha kujishughulisha kwao na Freemason; kwangu mimi walikuwa marafiki tu waliotokea kuwa Watumishi wa Serikali: mmoja wao mtumishi katika Makoloni na mwingine mfanyakazi wa Relwe. Lakini kila nilipoendelea kuwajua zaidi nikapata kugundua kwamba jioni ya kila Jumatatu, baada ya saa za kazi, Bob na John waliondoka pamoja kwenda kwenye mikutano ya ajabu-ajabu katika jumba lililokuwa karibu na bahari mjini Dar es Salaam. Pole pole, kwa kiasi wasiwasi wangu ulivyoongezeka, wakaanza kunieleza kidogo kidogo yale yaliyokuwa yanatendeka huko. Kumbe walikuwa tayari katika kundi hilo la Freemason, na haraka sana na mimi nikatamani kuwa mmoja wao pia. Kwa bahati mbaya wote sisi tulikuwa tunaishi katika Tanganyika ya Wakoloni katika miaka ya mwanzo ya 1950, wala haikuwako nafasi

Page 200: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

200

kabisa kwa ama Bob ama John kuwa na uwezo wa kunisaidia mimi kuingia katika jengo hilo la Pwani kama mwanafunzi; walikuwa wanatakiwa Wazungu watupu, tena Wazungu wa aina fulani. Lakini, wakiwa marafiki zangu, bado walitaka kunisaidia; kwa hiyo wakanitambulisha kwa Sheikh Mustafa na kwa Jivraj Patel, Wana-Mason wenzangu ambao baadaye walikuwa kama ndugu zangu. Mustafa na Patel ndio walionielemisha kuhusu madaraja yote ya makambi ya Mason yaliyokuwa yanatumika nchini Tanganyika wakati ule, kwamba madaraja hayo yaliwekwa kubainisha madaraja kati ya Wazungu wageni waliokuwako, na wengine waliokuwa chini ya ngazi hiyo, kwa mujibu wa taratibu za Wakoloni za kujitenga zilizokuwako nchini Tanganyika wakati huo, na kwamba taratibu hizo zilikuwa na mwelekeo wa ubaguzi uliokuwako miongoni mwa jamii ya Wazungu wageni, na, chini ya hapo, mwelekeo wa tabia, na kwa kweli Sera, ya ubaguzi kwa ajili ya kuendeleza matabaka. Maana yake hali hii ni kwamba, nafasi ya kwanza kabisa ya makazi mjini Dar es Salaam ilitengwa kwa ajili ya watu wa daraja la juu kati ya Jamii ya Watanganyika, Waingreza weupe walio wasomi. Nafasi ya pili ilitengwa kwa ajili ya Wazungu wafanyabiashara; na ya tatu ya Wazungu wengine, zaidi Waskochi, ingawa sikupata kujua kisa cha kuwaweka, katika ngazi hiyo. Na ilikuwako ngazi ya nne, Kambi ya Nyota ya Jaha; hiyo ilikuwa ya Wahindi kama akina Mustafa na Patel, na mimi mwenyewe. Haikuwako Ngazi ya Tano wakati ule; maana yake ni kwamba Waafrika weusi hawakuwa na nafasi yoyote ya kuingia. Aina hii ya ubaguzi haikunishangaza. Lakini lililonishitua ni shida niliyoipata kuingia ndani ya ile nyota ya Jaha. Hakuna aliyenitahadharisha mapema juu ya vizingiti vilivyopaswa kuvukwa katika kuwapima wanachama wapya, bila kujali uwezo wao wa fedha au wadhifa wao katika Jamii. Badala ya kupata mwaliko mapema wa kuungana nao, kama nilivyotarajia, nikalazimika kusubiri kwa karibu miaka miwili, wakati kufaa kwangu kuwa mwanachama wa Mason kulipokuwa kunachunguzwa.

Page 201: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

201

Katika kipindi hicho shughuli zangu za kila siku, kazini na nje ya kazi, zilikuwa zinachunguzwa kwa makini; kadhalika shughuli na mawazo ya ndugu zangu na marafiki zangu wa karibu. Ingawa mimi nilikuwa Kiongozi wa moja ya familia kubwa za wafanyabiashara wa Kihindi katika Afrika Mashariki, bado sikutafutiwa njia ya mkato, wala haikuniwia rahisi kuingia. Mpaka mwishowe tarehe 25 Oktoba 1954, ndipo nilipokaribishwa katika hiyo Nyota ya Jaha, kwa namba 5299. Zaidi kidogo ya miaka hamsini baadaye, kundi hilohilo likaamua kufanya hafla kubwa sana ya kumbukumbu ya miaka yangu hamsini ya Uanachama. Katika hafla ile, kikundi kikanipa zawadi nyingi nitakazozienzi daima; na shughuli za usiku ule zikaendeshwa kwa ratiba nzuri mno, pamoja na fataki na kitabu kilichotayarishwa rasmi cha kumbukumbu ya yale niliyoyafanya nikiwa ndani ya Chama cha Mason. Kikosi chetu hicho kikabaki kuwa cha Wahindi watupu kwa miaka kumi iliyofuata, mpaka hatimaye kilipozinduka na kutambua kuwa uhuru ulikwisha patikana miaka miwili iliyopita. Kwa kweli kilipita kipindi kirefu zaidi ya hicho kwa Kikosi hicho kilichokuwa mjini hapa na Ngazi nne wakati ule wa ukoloni kujiunda upya katika sura iliyolingana zaidi na Tanzania mpya isiyokuwa na ubaguzi: aina ya mabadiliko yaliyofanywa miaka kadha huko nyuma katika Klabu ya Rotary na Vyama vingine vya hiyari. Wanachama wachache wa Kambi ya Dar es Salaam, wote wakiwa wafanyabiashara wa Kizungu, waliotamani kuhamishia Kambi yao huko London, waliomba Kambi Kuu ya Uingereza kurekebisha Hati iliyowaruhusu Wanachama hao kukutania Dar es Salaam, lakini jitihada hizo hazikufanikiwa. Lakini kwa upande mwingine bado Wana-Mason walikuwa wamesonga mbele zaidi kuliko Watanganyika wengine wasomi, kama uzoefu wangu katika Tanganyika Standard ulivyonisaidia kutambua baadaye. Nilipoanza kutafuta uanachama wa Freemason nililazimika kutambua kuwa nilikuwa natumbukia katika mazingira ya kujitenga duniani ambayo sikuwa nayajua. Maana ingawa mpaka wakati huo Chama cha Freemason kilikuwa katika sura hiyohiyo kwa karibu

Page 202: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

202

miaka mia tatu (kambi hizo mbili ziliunganishwa Uingereza mwaka 1715), hali ya usirisiri wake unaokigubika imeongezeka sana katika miaka hii michache. Freemason walikuwako katika sehemu yangu hii ya dunia kwa muda wa miaka hamsini, Kambi ya kwanza ya Afrika Mashariki ikiwa imeanzishwa Zanzibar mwaka 1904, lakini ikachukua miaka mingine ishirini na minne kwa Kambi ya kwanza ambayo, kwa shamra nyingi, Gavana ndiye aliyeiwekea Jiwe la Msingi ili ijengwe huko Bara katika Mtaa ulioitwa wakati ule Main Avenue, sasa hivi Sokoine. Tangu miaka hiyo ya 1920 idadi ya Vikundi vya Mason nchini Tanzania, na Afrika Mashariki kwa jumla, imeendelea kuongezeka. Ongezeko kama lilo hilo limejidhihirisha katika Asia, Marekani ya Kusini, na baadaye Ulaya ya Mashariki baada ya kipindi kile cha kuingia kwa Ukomunisti. Lakini kwingine kote, hasa Ulaya ya Magharibi, Amerika ya Kusini na Australia, idadi ya Wanachama wa Mason wamekuwa wakipungua pole pole na kuacha pengo kubwa duniani kutoka milioni saba waliokuwako wakati wa Vita Kuu ya Kwanza kufikia milioni tano tu. Hata hivyo, mchango wanaodai ndugu hao milioni tano, kwa Chama chao na kwa Jamii, ni mkubwa sana. Wanatoa misaada kila mwaka, kulingana na kazi zinazotekelezwa na Vikundi vyao, kiasi cha dola milioni mia nne za Marekani. Huku Tanganyika, baadaye Tanzania, walisaidia Kituo cha Wakoma cha Kinditwi Wilayani Utete; Kituo cha Watoto cha Mama Theresa; Shule ya Vipofu ya Pongwe, Mkoani Tanga; Kituo cha Yatima cha Arusha, Hospitali ya Mnazi Mmoja kule Zanzibar; na Shule ya Viziwi ya Buguruni, ni machache tu kati ya Miradi mingi iliyogharimiwa na Vikundi vya Mason. Kati ya Miradi hiyo yote, ule wa Shule ya Buguruni ndio ninaouthamini sana moyoni mwangu; maana mimi ndiye Mwanzilishi na mchangishaji mkuu wa fedha; mhamasishaji na mtetezi mbele ya Viongozi Wakuu kwa niaba ya shule hiyo kwa muda wa miaka thelathini iliyopita. Lakini bado, pamoja na shughuli zote hizo za maana, kwa muda wote huo niliokuwa Mwanachama wa Freemason, mara nyingi wale

Page 203: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

203

Wanachama wa zamani wamenyanyaswa sana na magazeti ya nchi za Magharibi. Kutoka kuonekana kuwa Chama ambacho huruma na dhamiri zake katika kumwinua binadamu zinathaminiwa, kama ilivyokuwa katika kipindi kirefu cha karne za kumi na nane na kumi na tisa na mwanzo wa karne ya ishirini, sasa kimeporomoshwa hadhi kwa mashambulizi makali ya magazeti yasiyokuwa na msaada, kiasi cha kuigeuza Freemason kuwa kama kivuli tu, Kikundi cha wafitini wa ajabu-ajabu waliojaa hila! Freemason wenyewe walishiriki katika kujiangusha katika kipindi kile cha baada ya Vita. Mateso waliyokuwa wanafanyiwa Freemason makusudi wakati wa Vita katika nchi za Ulaya: kutoka Ufaransa ya Vichy kupitia Ujerumani ya Nazi na Italia ya Ufashisti, na kuendelea mpaka Urusi ya Kikomunisti na Vibaraka wake, ndio waliokuwa wahusika wakuu wa Maamuzi ya kushinikiza Freemason watoweke machoni mwa Umma. Uamuzi huo mgumu wa kuifanya Amri hiyo kuwa ya siri zaidi, maana ndiyo njia pekee ya kuwasalimisha Wanachama wao wengi waliokuwa hatarini zaidi, ukawaacha Freemason kwa jumla katika hatari ya kushambuliwa na wale waliokuwa wanataka kuikashifu, na hata kuihujumu kwa mabaya zaidi. Mfululizo wa simulizi chafu, nyingi ya hizo zilitoka kwa maadui wetu wa vita wa wakati ule, zikaenea katika sehemu nyingi maarufu miongoni mwa watu wa Nchi za Magharibi. Sababu moja ni Amri iliyokuwa imetolewa kuwakataza wote walioalikwa kutoa hadharani matamshi ya kusahihisha mengi ya madai hayo, yaliyokuwa yanashinikizwa na Kundi la Nazi, yalikuwa ama ni upuuzi mtupu, eti kwamba Freemason ilikuwa, kwa njia moja ama nyingine, sehemu ya njama za Uyahudi kutaka kuitawala dunia, au sababu ya kidunia zaidi, na hivyo yenye madhara zaidi, eti kwamba Freemason ni hatua ya mwanzo ya kudhibiti ajira kwa ajili ya Wanachama wa Freemason peke yao! Hakuna hata moja katika shutuma hizi mbili, wala hizo nyingine zilizotumbukia katikati, zilizokaribia ukweli wowote; lakini Amri hiyo, kwa jinsi ilivyonyamaziwa kimya katika muda wote toka mwisho wa 1940 mpaka miaka yote ya 1950, ikaachia shutuma hizo mbaya ziimarike mpaka kuonekana kuwa karibu na kweli. Matokeo

Page 204: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

204

mabaya yanayojitokeza kuhusu picha hii illiyokuwa inapindwapindwa yalijidhihirisha sana katika nchi za Ulaya na Marekani ya Kaskazini; kadhalika na huku Afrika, Asia na Marekani ya Kusini. Chama cha Freemason hakijapata misukosuko ya kutoeleweka kwa kiwango kile kile kama ilivyotokea kwingineko katika nchi zilizoendelea, pamoja na jitihada za Mapadre kadha wa Kikatoliki kuwashawishi Wakatoliki wao wasihudhurie Mikutano ya Freemason. Kwa kweli, nilipoanza kushika madaraka makubwa zaidi ndani ya Chama hicho, kwanza katika Ngazi ya Wilaya, na kisha Ngazi ya Kimataifa, ndipo nilipoelewa kwa ukamilifu ukubwa wa tofauti zilizokuwapo kati ya yale ambayo Freemason walikuwa wanayaamini na kuyatenda, na jinsi maneno na matendo yao yalivyokuwa yanadhihirika mbele ya watu walio nje ya nchi za Magharibi. Ili kuanza kuelewa vizuri zaidi chama hiki, na hivyo pengine kuanza kuoanisha dhana na hali halisi, lazima mtu arudi kwenye misingi ya Freemason. Itikadi yenyewe ya Wema na Maadili ndiyo iliyonitumbukiza katika mazungumzo yangu ya kwanza na akina Campbell Ritchie na Maclean, juu ya huruma kwa binaamu mwanzoni mwa miaka ya 1950. Wakati ule ndipo nilipoanza kutambua kuwa, kumbe, maana kamili ya Uanachama wa Freemason ni Sayansi ya maisha ambayo lengo lake ni kumtia moyo mwanadamu kwa kumwelekeza vile anavyotarajiwa kuwa: mtu mwenye ukamilifu katika vyote. Sehemu kubwa ya Hoja hiyo ya ukamilifu wa mtu inafichwa katika dhana, na pengine ndiyo maelezo ya uvumi unaoelekezwa kwenye shughuli za Freemason. Lakini Taratibu hizo zimejengwa kwa malengo ya makusudi, ambayo mimi nayaona kuwa mazuri tu, ya kuamua na kuboresha fikira, moyo na hadhi ya Binadamu. Kwa hiyo, katika hatua ya kwanza ya kuingizwa kwenye Freemason, Misingi mikuu ya Maadili na kusema kweli inayojenga Freemason inasisitizwa kiasi cha kutosha katika mawazo ya mtu anayetaka kujiunga na Chama au mtahiniwa.

Page 205: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

205

Hatua ya pili ya Freemason inasisitiza kuendelezwa kwa vipaji na ufundi katika sanaa na sayansi ili mtu aweze kuwa na manufaa makubwa kadiri inavyowezekana katika maisha. Hatua ya tatu inatoa nafasi kwa mtu kufikiria saa chache za mwisho wa maisha yake, lau kama hili litaonekana kuwa kama ndoto. Kwa njia hizo, huyo anayetaka kujiunga na Freemason anaelekezwa namna ya kuishi kwa kutumia nafasi zote kabisa zilizopo, katika namna inayooana na misingi mitatu ya Freemason, ambayo ni: Upendo wa Kindugu, Misaada na Ukweli, na kwamba Kifo ni Lazima. Misingi hii mitatu ikiisha kufafanuliwa katika maelekezo ya Wakufunzi yanayositiri mengi kati ya matunda ya Freemason, ndiyo iliyonivutia zaidi nilipopata kujua kwa undani, kwa mara ya kwanza, baadhi ya mambo katika Kikosi cha Antient. Katika Taratibu za Freemason, Msingi wa Upendo wa Kindugu unawaelekeza ndugu zetu wote kuwatambua binadamu wote kuwa familia moja iliyoumbwa na huyo Mwenyezi, lakini wakati huo “msaada” unatoa ujumbe kuelekeza Imani niliyofunzwa na Baba yangu, yaani kuwasaidia wenye shida: iwe katika kuwapunguzia umasikini, au kuwaliwaza wanaosumbuliwa na matatizo. Huo ni wajibu wetu sisi wote. “Ukweli,” msingi wa tatu na, pengine, ndio muhimu kuliko yote, ni dhana takatifu ambayo, kwa mwanachama wa Freemason, ndio msingi wa kila jema la binadamu. “Kuwa mtu mwema na mkweli” ni somo linalotolewa mapema kwa kila mtu anayetaka kuingia katika Freemason; hivyo ni Kauli inayotumiwa kila mahali kama zana ya kurekebisha na, kama lazima, kuelekeza njia ya maisha na vitendo vya mtu kulingana na Masharti yale manne muhimu ya Freemason: Kiasi, Uvumilivu, Busara na Haki. Na misingi yote hii ya Maadili ina umuhimu unaojumlisha siyo tu mafunzo ya falsafa za watu wa kale, kuanzia Wagiriki mpaka Budha mpaka Zaroaster, lakini hata za Dini zinazojulikana. Kinyume na propaganda zinazoenezwa za Mafashisti wa Kiitaliano, na wengine wengi zaidi ya hao, Freemason si chombo cha Dini, wala vile vile, kinyume chake, hakipingi Dini; kwa kweli Freemason wanawakaribisha watu wote bila kujali Imani zao za

Page 206: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

206

Dini, wala hawafanyi mbinu za kubadili Imani zao wala kuelekeza Ibada zao; wanachojaribu tu ni kuwafanya binadamu bora zaidi. Hivyo hiyo ndiyo dunia niliyoijua mwaka 1954, na ikawa sehemu muhimu ya maisha yangu kuanzia hapo. Katika kipindi hicho nimepata bahati ya kushuhudia kujitolea kwa Wanachama wa Freemason katika kuwasaidia wenye shida ndani ya Afrika Mashariki na hata nje ya hapo. Nimepata kutambua umuhimu wa mafunzo ya Freemason katika kujenga hisia za utu-wema na ukweli kwake mtu mwenyewe na kwa binadamu wenzake. Moyo wangu, mawazo yangu na roho yangu, vyote vimeimarika kutokana na kushiriki kwangu katika Freemason; na kuimarika huko kunatofautiana kabisa na hisia zinazotangazwa katika magazeti mashuhuri ya nchi za Magharibi. Kuwasaidia wenzetu kuwasaidia wengine ndiyo misingi niliyojifunza katika miaka yangu mingi ndani ya Freemason. Baada ya kushika nafasi za juu zaidi katika Kambi hii ya Nyota ya Jaha mnamo miaka ya mwisho ya 1950 na 1960, nikateuliwa Kiongozi Mstahiki mwaka 1967, wakati huo ndio kwanza nimeteuliwa Rais wa Muungano wa Vyama vya Round Table vya Afrika Mashariki. Mwaka uliofuata, kwa vile nilivyokuwa Mwanachama wa kwanza wa Round Table asiyekuwa Mzungu, nikawa Rais wa Kwanza wa Round Table na Vyama vinavyoambatana nayo duniani mwenye asili isiyokuwa ya Kizungu: ukweli ulioinua hadhi ya nafasi hii kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko ilivyokuwa kawaida. Kwa nafasi hiyo nikalazimika kusafiri sana, kuandamwa na Magazeti, na kuwa na shughuli nyingi za uwakilishaji kimataifa. Mwaka 1970 nikakamilisha kipindi changu cha uongozi kama Rais wa Kimataifa wa Baraza la Dunia la Klabu ya Huduma za Vijana; na mwaka uliofuata, baada ya kulazimika kustaafu kutoka katika chombo hicho kwa sababu ya umri, nikawa Makamu wa Kudumu wa Mwenyekiti wa Muungano wa Round Table katika Afrika Mashariki. Mwaka 1970 nikajiunga na Round Table ya Dar es Salaam, hatua ya kwanza kuelekea kwenye nafasi ya Gavana aliyewajibika na Klabu sabini na nane katika sehemu kubwa ya Afrika.

Page 207: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

207

Mwaka 1972 nikachukua hatua yangu ya kwanza kuelekea kwenye madaraka makubwa zaidi katika Freemason nilipochaguliwa Afisa Mkuu wa Wilaya wa kufanya kazi na Makao Makuu ya Freemason Mkoani kule Nairobi ambao wakati ule walikuwa wanasimamia Makambi kiasi cha ishirini na manane katika Afrika Mashariki nzima. Kila nilivyopata madaraka makubwa zaidi, ndivyo nilivyohakikisha kwamba nilifanya kila lililowezekana kutakasa Freemason mbele ya Umma. Kwa uzoefu wangu mimi watu kwa kawaida hutilia mashaka, na hata kuogopa, mambo wasiyoyaelewa. Kwa hiyo wakati wote nilipoulizwa habari za Freemason nikajitahidi kumweleza huyo mwulizaji misingi ya chombo hicho, nikisisitiza kwamba hakikuwa Chama cha Siri, na Wanachama wake wanajulikana wazi; na kwamba Mikutano yake haifanyiki katika sehemu za kujificha ila katika Kumbi za Mikutano zinazojulikana, zenye Hati za Serikali na zinazoweza kutambulika wazi wazi. Kama nilivyokwisha kusema mapema, Chama hiki na maajabu yake kiliingia wakati wa Vita Vikuu vya Pili, tulipokuwa tunajaribu kuwalinda Wanachama wetu waliokuwa Italia, Ufaransa na Ujerumani dhidi ya vituko vya Mataifa makubwa. Toka wakati huo tumejidhihirisha wazi wazi mbele ya umma, na kujitahidi wakati wote kuwaondolea mashaka, na kudhihirisha kuwa Chama chetu ni Chombo kinachomwingiza mtu mwema, na kujitahidi kumfanya mwema zaidi. Kwa bahati mbaya, si wote wanaozikubali hoja hizo. Kwa mfano, mwaka 1994, miaka minane baada ya kuteuliwa kwangu kuwa Msimamizi Mkuu wa Wilaya ya Afrika Mashariki nzima, Rais Moi wa Kenya akaunda Tume ya Serikali kuchunguza Tuhuma za kutumia uchawi kama njia ya kushinikiza msimamo wa Jamii ya Kenya. Kwa mshangao wangu, lakini wala sikushituka, nikaitwa mbele ya Tume hiyo, kwa nafasi yangu kama msimamizi wa Wilaya, kutoa Tamko kama shahidi. Nikumbukavyo mimi hii haikuwa mara ya kwanza kutolewa shutuma za njama za siasa dhidi ya Freemason. Watu wachache tu

Page 208: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

208

wakasahau kashfa ya P.2 kule Italia, ambako harakati haramu za wakorofi wachache ziliaibisha sura ya Kambi za Freemason dunia nzima ambayo mpaka wakati huo haikuwa ya kisiasa. Lakini kule Kenya nong’ono za Freemason kuunga mkono kabila moja lililokuwa na upinzani dhidi ya Serikali zilithibitika kuwa uvumi mtupu. Ingawa sikupata nakala ya mwisho ya Taarifa ya Tume, na wala haikuwako iliyotolewa hadharani, ukweli wa kutohusishwa kwetu uliweza kudhihirika katika vibwagizo tulivyokuwa tunavisikia kutoka Serikalini, pia kukosekana kwa kauli yoyote ya kutukosoa ndani ya Taifa hilo, na tabia ya Serikali ya Kenya kuepuka kuingilia Makambi ya Freemason yaliyokuwako nchini humo. Na, kwa upande mwingine, shutuma zilizokuwa zinaelekezwa kwa Freemason wa Kenya lilikuwa jambo la bahati njema, hata ikapatikana nafasi ya kueleza upya, kwa hadhara na pembeni, ukweli kwamba ndani ya Freemason Siasa ni jambo la mtu binafsi, na Dini kadhalika; si mambo ya kujadiliwa wala kushughulikiwa katika Kambi ya Freemason. Sijawahi kutumbukia katika tatizo la kisiasa la aina hii dhidi ya Serikali ya Shelisheli, au ya Tanzania, wala ya Uganda, hata wakati ule wa vuguvugu la Ujamaa wa Kiafrika baada ya Azimio la Arusha. Ilitokea hivyo kwa sababu Mwalimu alichunguza sana misingi ya vyama vya Hiyari vilivyokuwamo nchini Tanzania wakati wa Uhuru, na kubaini kwamba vyote hivyo, kwa kiwango fulani, vilikuwa vinaendeshwa kama vyama vya kusaidiana. Mara mbili tu niliona Kambi zetu zikiwa chini ya uchunguzi wa Serikali, na mara zote hizo zilikuwa za mashaka kabisa, na zikayeyuka haraka. Mara ya kwanza Afisa kutoka Idara ya Mambo ya Kale, aliyekuwa ndiyo kwanza amerudi kutoka Ziara ya Kirafiki nchini Urussi, akatafuta nafasi ya kuonana nami Makao Makuu ya Freemason mjini Dar es Salaam, ili apate Taarifa kuhusu chama chetu na shughuli zake. Akiwa Ofisini humo macho ya yule Afisa wa Kitanzania hayakuweza kukwepa kuangalia vile viti asilia vya kulala vilivyokuwa na mito myeupe, nyuma ya Ukumbi wa Freemason. Mara moja maswali yake yakahama kutoka viwango

Page 209: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

209

vya misaada tulivyokuwa tunatoa, na kuelekea kwenye hivi viti na mito yake. Akaanza kuulizia-ulizia habari zake, nami nikamweleza kuwa vile viti vilikuwako pale kwa miaka mingi, wala havikuhifadhiwa kwa matumizi ya Freemason peke yao, ila vilikuwa vinatumika vile vile, mara nyingi, katika Baraza la Kutunga Sheria, kwa kukodishwa. Hakuachia hapo; Kiongozi huyo alirudi Ofisini kwake na kuanza kuandika Taarifa ndefu juu ya hatima ya jengo lile na baadhi ya vifaa alivyoviona, taarifa ambayo hatimaye haikuzaa lolote, lakini nakala zake nikazihifadhi katika mafaili yangu mwenyewe, ili kunichangamsha wakati nitakapokuwa nimechoka. Mgongano wa pili na Maofisa wa Tanzania ulitokea wakati Kampuni ya Umeme, TANESCO, ilipofikiria kuanzisha Chuo chake cha mafunzo. Nikiwa mwenyewe Mjumbe wa Bodi ya TANESCO, pengine nilikuwa mtetezi mkubwa wa Chuo hicho kuliko Wajumbe wengine wote, bila kujua wakati huo kuwa wengine wazito zaidi ndani ya TANESCO walikuwa wanalimezea mate eneo hilo tulilolimiliki, lililokuwa na jengo la Makao Makuu yetu jijini Dar es Salaam. Ghafla, bila ya Taarifa yoyote, wakati wa moja ya ziara za wageni wetu kutoka nje, waliokuwa wanakuja mara kwa mara, TANESCO wakapewa Hati ya Kutaifishwa kwa manufaa ya umma kwa Jengo la Makao Makuu yetu pamoja na Eneo lake; na Amri hiyo hatimaye ikachapishwa katika Gazeti la Serikali. Amri hiyo ya kutaifishwa ilikuja na masharti kwamba waliohusika katika utaifishwaji huo walipewa siku tisini za kukata rufaa, wakipenda. Niliporudi Tanzania na kuelezwa habari za tukio hilo baya, na ingawa muda ulikwishapita, nikatayarisha haraka haraka maandishi yaliyohusika katika kukata rufaa, kwa sehemu kubwa nikiambatisha maelezo marefu ya historia ya Freemason katika Afrika Mashariki. Haukupita muda mrefu baada ya kukabidhi kwa Rais makala zilizohusika, na hata zisizohusika, Katibu Mkuu wa Rais akanipigia simu kusema kuwa ile Amri ya kutaifisha lile eneo ili wapewe TANESCO imebatilishwa na Mwalimu mwenyewe; TANESCO wameambiwa kutafuta kiwanja sehemu nyingine kujenga Chuo

Page 210: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

210

chao nilichokuwa nakidai, na sisi tukaruhusiwa kuendelea na mipango yetu. Na huo ukawa ndio mwisho. Kuwa Mwanachama wa Freemason maana yake ni mtu kujitolea kuingia katika safari ndefu isiyo na mwisho ya kujifunza na kuchunguza. Kwa muda wa miaka hamsini iliyopita mafunzo yangu ndani ya Freemason yameniwezesha kupata Shahada nyingi za ngazi na umuhimu unaozidiana, ukiacha Ukuu wa Wilaya nzima ya Afrika Mashariki, yaani Kenya, Shelisheli, Tanzania na Uganda kwa miaka kumi na tisa. Nikitaja nafasi chache tunilizoshika, nimekuwa Msimamizi, kwanza Mdogo kisha Mkuu, wa Kambi Kuu ya Viongozi wa Freemason wa Uingereza na Wales. Mara ya kwanza kabisa nafasi hiyo kushikwa na mtu asiyekuwa mkazi wa Uingereza. Nimepewa heshima ya kuwa Mstahiki Kamanda wa Kambi ya Donyo Sabuk ya Royal Ark Mariner, na nimeshika Uongozi wa Kambi hiyo toka mwaka 1990. Mimi ni Msimamizi Mkuu wa Afrika Mashariki wa Kikosi Kikuu cha Freemason cha Royal Ark cha Uingereza, nikiwa nimeshika nafasi hiyo tangu 1960, na Ofisi ya Wilaya toka 1972. Mwaka 2000 nikawa Naibu wa Mshika Upanga Mkuu wa Kikosi Kikuu, na bado mimi ni Mkufunzi Mkuu wa Heshima katika Kikosi Kikuu cha Uskochi. Mwaka 1987 nilipata Shahada ya Mtakatifu Lawrence, Shahada ya Shujaa wa Constantinopole, Hati Takatifu ya Kuhani Mkuu na ya Wawekezaji Wakuu wa Suleiman; nikapata vile vile Hadhi muhimu ya Ushujaa ya Msalaba Mwekundu wa Babeli. Mwaka 1968 nikaingia katika Halmashauri ya Wasimamizi Wakuu Namba 1 walioteuliwa na waliokuwa hodari mno nchini Uingereza na Wales, na nikapewa tuzo la shahada ya Msimamizi Bora kuliko wengine wote. Mwaka uliofuata nikaingia kama Mwanafunzi wa Mkataba katika Jamii ya Waabudu wa Freemasons, Tawi la Row Assemblage. Kwa mtu wa nje anayesoma simulizi hizi, mambo machache kama haya hayakuwa na maana yoyote lakini kwa Mwana-Freemason umuhimu wa vyeo hivyo vingi ukadhihirika haraka. Ila kwa wasomi wote, wana-Freemason na wale ngumbaru, Taratibu ndefu

Page 211: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

211

za mafunzo ya Freemason huzaa maswali mengi ya msingi. La kwanza kubwa katika maswali hayo, na ambalo ni dhahiri, ni vipi mtu kama mimi niliyeshika nafasi nyingi za Uongozi katika biashara, katika Jamii na katika vyombo, nitakuwa radhi kujitolea mara moja, na kwa ari hiyo, kutumia miaka hamsini na mitano ya mafunzo yanayohitajika. Ni swali la msingi ambalo wengi wanaotaka kuingia katika Freemason wamekaa na kujiuliza. Jibu lake linatokana na asili ya Chama chenyewe, na hali ya mtu huyo anayetaka kujiunga. Muda wa mafunzo wakati wote, tangu zama za kale kabisa za miaka ya kati ya Ulaya, umeunganisha mafunzo ya matambiko, nidhamu na unyenyekevu. Kwa jumla yale ya Freemason yanayotokana na Taratibu za Mazoezi ya Wajenzi wakuu wa zamani hayana tofauti. Nimekuwa nikiamini wakati wote kwamba, pamoja na mafanikio ya zamani ya binadamu katika maisha, katika sanaa, sayansi, jeshi na biashara, bado dhamiri ya kujifunza maisha yote mambo ya udugu, nidhamu ya tabia na vitendo, na unyenyekevu unaofaa, lazima yote hayo yatasaidia katika kuleta mafanikio zaidi. Kujishughulisha kwa ajili ya manufaa ya Jamii, hasa wale miongoni mwao wanaopatikana na matatizo, kama ambavyo Freemason na Rotary wanavyofanya, ni vizuri sana. Lakini kufanya kazi hiyo ya hiyari kwa msingi imara wa maadili na kweli ni kitu kingine kabisa, kunamsaidia zaidi yule mpokeaji, lakini kunamdai mtoaji gharama kubwa zaidi. Kinyume cha fikira za watu wengi, Freemason si Chombo watu wanachoweza kukitumia kujitukuza, haijapata kuwa na wala haitapata kuwa hivyo; na hiyo ndiyo sababu Taratibu za kuwasaili watu wanaotaka kuingia ni ndefu na za kuchokonoa sana. Kila ninapozungumza au ninapoelezea habari za Freemason, nasisitiza jambo hilo kwa nguvu kabisa. Vile vile Freemason inahusu Huduma kwa Jamii, na kwa binadamu kwa jumla, kutokana na utekelezaji wa Taratibu za Nidhamu ya Chama inayojulikana. Hatimaye majadiliano yanayohusu mchango wa Freemason katika Jamii yanafuata mwelekeo unaofaa. Mfano mmoja ulio dhahiri nilioushuhudia mimi mwenyewe hivi karibuni ni Hotuba iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa chakula cha jioni katika hoteli moja mjini Dar es Salaam, tarehe

Page 212: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

212

9 Oktoba 2004, kusherehekea mwaka wa mia moja wa kuanzishwa kwa Kambi ya Kwanza ya Freemason katika Afrika Mashariki. Rais Mkapa akanakili maneno ya Mwandishi na Mhariri mmoja wa Kimarekani, George Horace Lorimer, aliposema, “Ni vizuri kuwa na fedha, na vitu vile ambavyo fedha inaweza kuvinunua; lakini ni vizuri pia mara nyingine kuhakikisha kwamba hujavipoteza vitu vile visivyoweza kununuliwa kwa fedha.” Baada ya kujua kwamba, kwa kipimo cha Tanzania, Wanachama wa Freemason waliohudhuria walikuwa na fedha, Rais akawashauri kuwania malengo makubwa zaidi ya moyo wa huruma wenye uadilifu, upole, uvumilivu, busara na haki; na kuwa mfano mwema kwa wengine. Lakini kisha akawaandama hao Freemason na kuwataka kutafsiri kwa usahihi Imani yao hiyo hiyo ya kiasi, ushupavu, busara na haki, kulingana na matatizo yanayoikumba dunia ya leo; kwa lugha nyingine, kukumbusha yale ambayo Rais aliyaona kuwa matatizo makubwa ya leo: kutukuza ubinafsi, kujitafutia manufaa ya haraka haraka, na milipuko ya mawazo; vile vile na ung’ang’anizi katika masuala ya siasa, uchumi na dini. Kama inavyotokea siku zote, maswali aliyoyauliza Rais Mkapa yalikuwa yamefikiriwa vizuri na kuwasilishwa kwa usahihi. Kwa mwelekeo huohuo, Rais Mwai Kibaki wa Kenya naye akawaunga mkono Freemason katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake Septemba 25, 2004, kusema, “Wanachama wenu wamechangia kiasi cha kutosha, kwa niaba ya Serikali, katika kuinua hali ya maisha ya Wananchi.” Na katika sherehe iliyofanyika katika Ukumbi wa Freemason mjini Nairobi, Novemba 8, 2004, Makamu wa Rais wa Kenya, Moody Awori, alisema, “Kujitolea kuwasaidia watu wetu, hasa wale wenzetu wanaoonekana kupungukiwa na bahati, ndiyo ishara ya utekelezaji wa Imani yenu ya Kiasi, Uvumilivu na Kujitolea, ili kuinua hali ya maisha yao.” Sisi wa Freemason tunakumbushana kutimiza Wajibu wetu kwa Mwenyezi Mungu, kwa Mamlaka yaliyopo ndani ya nchi tunamoishi, na kwa familia zetu. Lazima dunia itakuwa mahali pema zaidi pa kuishi, endapo wote sisi tataapizana kwa dhati kuwa tutafanya hivyo. Mambo mengi yamebadilika tangu nilipoingia

Page 213: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

213

katika Freemason kwaka 1954. Baada ya kuuacha wadhifa wa Msimamizi Mkuu wa Wilaya ya Afrika Mashariki baada ya miaka kumi mfululizo katika nafasi hiyo, sasa naiangalia kwa faraja michango Wanachama wetu waliyoitoa kuendeleza shughuli hizo; lakini, kubwa zaidi, najivunia ari waliyoionyesha katika kuboresha maisha ya jamii zao. Wakati wote Wanachama wa Freemason wanazingatia mahitaji ya watu wanaokumbwa na matatizo. Hapa Tanzania ule mkasa mkubwa wa kuzama kwa meli ya M.V. Bukoba katika Ziwa Victoria mwaka 1996 uliwasukuma Freemason wa Afrika Mashariki na Uingereza kutafuta misaada kwa haraka. Lakini nikakumbuka vile vile gharama na hatari ya umasikini uliokithiri. Meli hiyo MV Bukoba ilikuwa mali ya Shirika la Reli la Tanzania, wakati huo mimi nikiwa Mwenyekiti. Nilipata habari ya kuzama kwa meli hiyo kwa televisheni, wakati mimi na marafiki zangu tulipokuwa tunazungumza Mjini Kano, baada ya chakula cha jioni, katika Hoteli ya Union Bank of Nigeria tulimokuwa tunakaa. Nikarudi haraka Tanzania, kupitia London, kujumuika na wenzangu, ili mipango ifanywe kusaidia familia za wale waliofariki au waliojeruhiwa. Idadi ya watu waliofariki ilipoongezeka kufikia mamia nikashituka na kupandwa na ghadhabu, nilipoambiwa kwamba haikuwako meli hata moja kati ya zile zilizomilikiwa na Shirika la Reli iliyokuwa na Bima ya aina yoyote. Jinsi mkasa wa M.V. Bukoba ulivyoendelea kueleweka, nikawa naambiwa na Viongozi wa Shirika la Reli kwamba bodi iliyokuwako huko nyuma iliamua Bima isiwekwe kwa meli yoyote, hata kwa kiwango cha kumkinga “mtu wa tatu”, kutokana na shida ya kukosekana fedha; kasoro kubwa niliyoithibitisha baadaye kwa kuangalia kumbukumbu za Bodi. Kwa hiyo umasikini ndio uliokuwa chanzo cha mkasa; lakini ndio uliozaa umasikini zaidi. Hatua kama hiyo hiyo ya kuukabili mkasa wa M.V. Bukoba ilichukuliwa baada ya kushambuliwa kwa mabomu kwa Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam na Nairobi mwaka 1998. Katika nafasi mbili hizo zote, msaada uliotolewa na Freemason ukawa na lengo la kusaidia familia za wale walioathirika zaidi, na mpaka sasa ada za watoto wa shule waliopoteza wazazi wao kutokana na mabomu ya

Page 214: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

214

1998 zinalipwa na Freemason walioko nchini. Sura kama hiyo hiyo inaweza kuonekana duniani kote, Mkasa wa Tsunami wa hivi karibuni uliwafanya Freemason kutoa rasmi pauni nusu milioni kati ya misaada iliyoombwa dunia nzima, zaidi ya mamilioni mengine yaliyochangishwa na Freemason moja kwa moja duniani kote. Majukumu yanayobebwa na Makambi yetu kwa misaada Wilayani, yawe makubwa au madogo, yanaendelea kutekelezwa kwa nguvu na kwa huruma. Jitihada zote hizo zinapaswa kutiwa moyo na kushangiliwa. Lakini bado, kama Rais Mkapa alivyotuasa sisi Freemason wa Afrika Mashariki katika dhifa ya miaka mia mjini Dar es Salaam mwaka 2004, hakuna sababu ya kujivuna tunapokabiliwa na vizingiti vya kujisahau na hadaa vilivyo vingi sana katika Karne hii ya ishirini na moja. Kama alivyosema yeye, na ni sahihi kabisa, “Hatutaki sadaka tupu, bali na kujali vile vile”. Hiyo ndiyo iliyokuwa sababu yangu kubwa ya kujiunga na Freemason na Rotary pia; na inafaa kubaki kuwa mfano kwa wote wale waliojiunga na Freemason, au wale ambao bado wanatamani kujiunga. Kama nilivyosema katika maandishi yangu ya hivi karibuni, Freemason ni aina ya maisha mtu anayotarajiwa kuyaishi; msingi wake ni dini inayomwelekeza kwenye maadili yanayooana na Ujirani Mwema, na kupata sura ya utu katika upendo na dhamiri ya kuhudumia wengine. Mafunzo ya Freemason faida yake si ya leo tu, bali ya siku zote hata milele; ni chimbuko la Wema na Utulivu unaowaelekeza Wanachama wake kwenye uvumilivu, uungwana na heshima kwa kila binadamu. Kwa sababu maisha yangu yote ya kufanya kazi nimeyatumia katika Afrika Mashariki, yanakotawala mawazo mepesi kwamba maisha ni “machungu, mafupi na yaliyojaa unyama” mawazo yanayovizwa uungwana wa ajabu wa Watu wa Tanzania na Viongozi wao, haja kubwa inayotakiwa ya kuwa na nidhamu kali inadhihirika wazi kwangu. Ninachoweza kuomba tu ni kwamba Freemason wenzangu waendelee kuyazingatia hayo wanapoendelea katika mazoezi yao, na katika maisha yao ya kila siku. Na, kwa jumla, hakuna mmoja wetu anayeweza kulikwepa shinikizo linalotulazimu kuwa binadamu bora zaidi kwa njia yoyote ile iliyo ndani ya uwezo

Page 215: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

215

wetu. Kukariri kwa kifupi yale aliyoyasema Rais, na George Lorimer, wakati mwingine tafuta na kuhakikisha kwamba hujapoteza mambo hayo, na yale Maadili ya Kibinadamu ambayo hayawezi kununuliwa kwa fedha.

Page 216: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

216

KUMI NA MOJA

BWANA MASHIRIKA Mashirika, Mashirika, Mashirika. Nchi yoyote ambayo msingi wake wa uchumi lazima usimamiwe na Dola, iwe kwa falsafa ya Marx, au ya Mao, au hata ya Ujamaa wa kawaida, itageuka haraka kuwa nchi iliyojaa “Mashirika”. Katika miaka ya 1970 na 1980, Tanzania haikuweza kuikwepa kasoro hiyo. Wakati ule wa kushamiri kwa biashara zake nchini Tanganyika, Baba yangu Keshavji alitambuliwa kwa upendo Tanganyika nzima kama “Bwana Usindikaji”. Kwa sababu ya ari yangu kubwa kutumikia Nchi yangu ya Kijamaa iliyokua inajengwa na Mwalimu Nyerere, jina langu la utani katika Tanzania huru lingepaswa kuwa “Bwana Mashirika”. Katika kipindi cha miaka michache nikajikuta nimeteuliwa na Rais kuwa Mwenyekiti wa Mashirika makubwa yafuatayo: Shirika la Ndege; Shirika la Utalii; Shirika la Bandari, Shirika la Reli; Shirika la Magazeti ya Tanganyika Standard; Shirika la Huduma za Usafiri, Shirika la Uwekezaji katika Mahoteli, Printpak Tanzania; Shirika la Taifa la Usambazaji, Kampuni ya Fedha za Maendeleo; Shirika la Kuuza nje Mazao ya Kilimo; Kampuni ya Viatu; Shirika la Mazao ya Misitu; Kampuni ya Filam; Mamlaka ya Maji Mijini; Kampuni ya Kutengeneza Vileo; Shirika la Bima Tanzania; na Shirika la Vifaa vya Elimu. Wala majukumu hayo hayakugusa nafasi zangu nyingi katika Bodi nyingine, wala Uenyekiti wangu katika Vyombo visivyozaa faida, kama Huduma za Maktaba na za Makumbusho, au za Mfuko wa Utafiti wa Dawa za Kiafrika. Haukuwako uchawi wowote katika kuendesha lolote kati ya Mashirika hayo kwa mafanikio. Kwa kweli shughuli hizo ni sawa na biashara nyingine yoyote inayohitaji uzoefu wa kutumia mitaji na watumishi wanaoweza kufanya kazi kwa ufanisi kadiri inavyowezekana. Wakati mwingine iko haja ya kutumia ufundi wa diplomasia wa aina nyingine ambao mtu ana mashaka ya kuwa nao. Mfano mzuri wa wakati ule ni pale tulipotakiwa kuchambua mfarakano uliozuka wakati wa kuanzisha Shirika la Ndege la Tanzania.

Page 217: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

217

Katika kipindi kile baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki Tanzania ikaanzisha Mashirika yake yenyewe kuendesha shughuli za Reli, Barabara, Bandari na Ndege. Rais Nyerere akaniteua Mwenyekiti wa Shirika la Ndege, wadhifa nilioukubali kwa masharti ya kutokuwa Mtendaji, wakati Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi akidhamiria kuwa na Mwenyekiti wa kukaa Ofisini muda wote. Kati ya Mashirika yote ya Afrika Mashariki yanayosimamia Mawasiliano na Uchukuzi, Shirika la Ndege ndilo lililorithi wafanyakazi waliokuwa wazoefu kuliko mengine yote baada ya kuvunjika kwa Shirika la Ndege la Afrika Mashariki. Kwa kweli wafanyakazi wachache wa ngazi ya juu, kama Silva Rwebangira, walikuwa wanajulikana katika Kampuni za Ndege za Kimataifa. Lakini wakati wafanyakazi walipokuwa wanajitolea kwa moyo wao wote kuiletea mafanikio Kampuni yao wenyewe, changa, wakajikuta wakihangaika wakifanya kazi katika mazingira magumu mno. Kwanza kabisa ilikuwako shida ya kurudisha familia za wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Afrika Mashariki kutoka Nairobi, pamoja na matatizo ya elimu ya watoto wao, na wasafirishaji wa vifaa vyao vya nyumbani, ikiwa pamoja na magari yao. Serikali ya Tanzania ikalielewa tatizo lao, lakini ikajikuta katika hali ngumu sana, na kulazimika kutafuta fedha za ziada kuubeba mzigo wote wa kusimamisha Mashirika mapya baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kabla ya mgawanyo wa mali za Shirika lililovunjwa, ambao dhahiri ulichukua muda mrefu zaidi kukamilika kuliko ilivyotarajiwa; ilibidi fedha nyingine nyingi zitolewe na Serikali ya Tanzania, na mimi nadhani kuwa gharama ya Serikali ya Tanzania, na ya moja kwa moja au ya kupitia Vyombo vingine, ilikuwa kiasi cha dola 900 milioni za Marekani. Dhahiri ulikuwako wasiwasi mkubwa sana, na kiasi fulani cha hasira kwa upande wa wafanyakazi, wakati mambo yote hayo yalipokuwa yanashughulikiwa. Nakumbuka kuitwa jioni moja kwenye mkutano wa marubani, mainjinia, wahudumu wa abiria na wafanyakazi wengine wa Shirika uliofanyika pwani ya Africana, nje kidogo ya Dar es Salaam,

Page 218: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

218

ambako wengi wao walipata malazi baada ya kurudishwa kwa mabavu kutoka Nairobi. Mimi nilikwenda huko na Michael Shirima, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania, ambaye kwa bahati sasa hivi ni mwanahisa muhimu na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege Precision inayoendelea vizuri; Kenya Airways wana hisa katika Kampuni hiyo. Baada ya kula chakula cha jioni na hao Watumishi Wakuu ambapo, kwa busara, tuliwapa waliohudhuria vinywaji vya bure, tukafanya Mkutano pamoja na wafanyakazi wengine wote. Mkutano huo ulikuwa mzuri, pamoja na shida zote wafanyakazi walizokuwa wamezipata. Hatimaye tukaufunga Mkutano mnamo saa nane za usiku; na, mimi na Michael tulipoondoka kurudi nyumbani, tulijihisi kuwa tulipata mafanikio makubwa sana. Hata hivyo, Kamati ya Kudumu ya Mashirika, SCOPO, ilitishia kuvuruga sehemu kubwa ya mafanikio yetu walipojaribu kuoanisha mishahara ya Wahudumu wa ndani ya ndege na ya wafanyakazi wa sehemu nyingine. Mpaka tulipofafanua adha wanazopata Wahudumu ndani ya ndege, na hatari wanazokumbana nazo kila siku: kwamba lazima wawe tayari kukabili dharura zozote, na hivyo lazima afya zao zichunguzwe kila baada ya miezi sita, ndipo SCOPO waliporidhia kuboresha mishahara yao. Hayo ndiyo baadhi ya matatizo, ambayo kutatuliwa kwake kulihitaji ufundi wa biashara na wa diplomasia, niliyotakiwa kuyatatua kwa niaba ya Serikali. Lakini, katika baadhi ya hayo, umahiri katika biashara na ari ya kuitumikia nchi yetu kwa kazi ngumu kwa kweli visingetosha. Kwa hayo ilihitajika moyo wa kujitolea, na huo ulidhihirika katika kazi zangu zilizohitaji “uvumilivu” wa kudumu. “Uvumilivu”, ufundi wa kuishi leo katika namna itakayohifadhi manufaa ya kesho, ni dhana iliyokuwamo mioyoni mwa kila mmoja kabla ya kuingia kwa Mapinduzi ya Viwanda. Wawindaji, Wadundulizaji, Wakulima wa zamani, na wengine wa makabila asilia; hakuna mmoja kati ya hawa aliyehitaji kuelimishwa namna ya kuyakabili mazingira yaliyokuwako. Hata kama maisha yao yote yalitegemea kilimo, lakini walifanya hivyo kwa namna isiyoviletea kasoro vizazi vilivyofuata.

Page 219: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

219

Mapinduzi ya Viwanda, na mabadiliko ya jamii yaliyoletwa na Mapinduzi hayo, yalibadili uhusiano uliokuwapo kati ya binadamu na mazingira yake. Haikuwezekana tena kwa watu wetu kudhani kuwa shughuli zao za uzalishaji zingeendelea kuoana na mazingira yake. Rasilimali, kwanza madini, kisha wanyama na mimea, zilianza kutumika kwa kasi iliyozaa matishio mawili ama ya kuchoka ama ya kutoweka kabisa. Ikazaliwa dunia yenye sura mbili; ambapo matajiri wakatokea kuwa matajiri zaidi, lakini masikini, wale waliokuwa na bahati, wakabaki pale pale. Na, katika dunia hiyo, matajiri wakanyakua rasilimali za wanyonge waliokosa kinga, wakitumia silaha za vita na ukoloni kupunguza gharama za ulafi wao. Kisha, baada ya muda, dunia ikabadilika tena, safari hii katika masuala ya siasa, na hatimaye misingi ya ulafi wa Wakoloni iliyokosa mipaka ikafagiliwa mbali. Lakini badala yake ukaja unyonyaji wa aina nyingine, ambao ngome yake haikuwa tena katika maguvu, bali katika unafiki, uliojidhihirisha katika mwelekeo wa nchi za viwanda, zilizojipa haki ya kutumia na kuvuruga bila kujali hatima ya watu wengine. Hasara ya mwelekeo huo wa kutowajibika ilidhihirika katika ushawishi wa nchi zilizoendelea dhidi ya nchi za Dunia ya tatu kujiwekea mipaka ya matumizi ya rasilimali zao wenyewe, kwa kisingizio kwamba walikuwa na majukumu maalum kuhifadhi mito yao, misitu na majani kama Mwenyezi Mungu alivyodhamiria. Maana yake Hoja hiyo ni kwamba ilikuwa haki kwa Pennsylvania, au Lancashire au Ruhr kubaki na mazingira asilia kuangaliwa na miungu ya Viwanda, mradi tu Tanzania, Brazil na Madagascar, nchi za dunia hii hii, zianzishwe kwa kuyaacha maeneo yao wenyewe yachakae kabisa, kusafisha hewa na kutoa uwanja utakaotumiwa na matajiri kuwinda wanyama wanaowaona wao kuwa na thamani kubwa. Mambo yote hayo yanaonekana kuwa ya kuchekesha, au tuseme yote hayo yanakaribia ukweli. Nikiwa mkazi wa Tanganyika mnamo miaka ya 1950, nilizoea kuwasikia Watawala wa Kikoloni wakitamba kwa kuiacha Tanganyika isiwe na viwanda, kwa kisingizio cha kudumisha mapori ya kuvutia Watalii. Lakini

Page 220: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

220

sikutarajia kuwa ulaghai wa aina hii ungeendelea mpaka karne ya ishirini na moja kwa kuweka mitego dhidi ya watetezi wazembe wa uchumi wa utalii, kwa kuimarisha Haki sawa kati ya Tajiri na Masikini, na kuwapa wale walio masikini mno miongoni mwetu Majukumu ya kuiokoa dunia kwa njia moja au nyingine kwa kubakia masikini milele. Miaka mingi iliyopita nilifahamu kidogo tu mvutano uliokuwako kati ya mahitaji ya wananchi wa nchi zinazoendelea na yale ya taratibu za uchumi wetu ulio dhaifu. Nilipokuwa bado kijana, kule Bukene, niliwaangalia watu waliokuwa wanafanya kazi katika Kampuni ya Baba yangu walipokusanyika jioni, nje, kupata chakula. Hawakuwa na majiko ya kisasa; si stovu, wala si oven, wala haukuwako umeme. Kuni tu na, wakibahatika, labda mkaa uliojazwa chini ya sufuria au chungu kikubwa. Hapa nikashangaa siyo tu kwa hasara ya kukata kuni katika misitu yetu, lakini na kasoro yenyewe katika mapishi; kuni nyingi sana au mkaa mwingi sana, ulitumika kupikia chakula cha watu wachache tu. Hatimaye wasiwasi huo uliokuwa unawasumbua wenye viwanda katika kuhudumia viwanda vyao ukageuka kuwa wasiwasi wa kudumu zaidi kuhusu mazingira. Nikaanza kutambua kwamba, hata kule Bukene, uhusiano kati ya binadamu na mazingira yale usingeweza kudumu milele. Hata bila kuwako viwanda vya maana, bado kuongezeka kwa idadi ya watu tu, uliokuwa mwelekeo wa Tanganyika katika karne ya ishirini, kulikuwa kunaelemea rasilimali zilizokuwako. Katika nchi iliyopungukiwa na hata maji safi ya kutosha, au miti ya kutosha karibu na maeneo wanakoishi watu, wala chakula cha kumtosha kila mtu, rasilimali za aina zote hazikuwa salama. Hata katika Tanzania, moja ya nchi zilizo chimbuko la ustaarabu, ambako mila za kutunza mazingira zimekuwa mmoja wa misingi muhimu ya maisha ya makabila yote, na ambako mila nzuri za Wahadzabe zinang’ara mpaka sasa kama dira duniani kote, na ambako ardhi haijapata kuwa na bei, lakini bado, hata nchini Tanzania misukosuko ya baadaye ingali inatunyemelea. Nikiwaza, “Hebu fikiria yatakayotokea, na yale yaliyokwisha kutokea

Page 221: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

221

kwingineko”. Fikira kama hizo zikawa za kutumbua sana, na hatimaye kuwa chimbuko la wito wa maisha., Nafasi ya kwanza niliyoipata; ya kuyaweka baadhi ya mawazo hayo katika vitendo, ilitokea nilipoteuliwa Mwenyekiti wa Shirika la Utalii la Tanzania. Wakati ule, mwishoni mwa miaka ya 1960, mwelekeo ulikuwa zaidi katika Utalii wa kuangalia wanyama. Lakini kwa nasibu uwezo mdogo wa Vyombo vya Tanzania, pamoja na ukweli kwamba uzito wa Makampuni ya Utalii ya Ulaya viliwekwa na kushughulikiwa kutoka Nairobi, faida zilizopatikana kwa kuwaangalia hao wanyama wa Tanzania hazikuingia katika mifuko ya Watanzania. Kwa hiyo kwa haraka-haraka mambo muhimu kwangu yakawa mawili: kwanza kushawishi Makampuni ya Utalii ya Nchi za Nje, na Wateja wao, waione Tanzania kuwa Kituo cha Utalii kwa nafasi yetu wenyewe na siyo kama sehemu ya Kenya, na kujaribu kuvunja ile Imani iliyokuwako ya vivutio vya Utalii katika pwani ya Shelisheli na Mombasa kuwa masoko ya Utalii ya Marekani na Uingereza peke yao. Halikuwako jepesi kati ya mambo mawili hayo. Kwa miaka mingi sasa mipango ya Watalii wa Marekani na Uingereza kuja Afrika Mashariki ilikuwa inafuata Taratibu zilizokwisha wekwa. Mapumziko ya Pwani yalikuwa Mombasa. Baada ya hapo Watalii walivushwa mpaka wa Tanzania kwa mabasi kuingia katika Mbuga za Wanyama za Tanzania ya Kaskazini. Serengeti, Ngorongoro mpaka Manyara, kuangalia wanyama kwa siku chache, kabla ya kurejeshwa tena kwa mabasi kwenye hoteli zao za Mombasa na Nairobi. Mara nyingi walirudi Namanga bila kutambua kwamba walikwisha vuka mpaka kuingia Tanzania; na mara chache mno, kama walijaribu, walitumia fedha zao zote nchini mwetu, kwa kuwa walipendelea zaidi kununua zawadi walizozitaka kupeleka kwao kutoka mitaa iliyokuwa karibu na Hoteli ya New Stanley mjini Nairobi. Kwa kuwa Shirika la Utalii la Tanzania lilikuwa na vitanda elfu moja tu katika nchi nzima, na lililazimika kutegemea Mikataba na Mashirika ya Kigeni kudumisha kiwango kilichotakiwa katika baadhi ya hoteli zenye sifa, kama Hotels Meru (Denmark), Kilimanjaro (Uyahudi), New Afrika (Uingereza), na

Page 222: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

222

kwa sababu zilikuwako nafasi chache mno katika Pwani ya Zanzibar, na chache zaidi huku Bara, na kwa sababu Kenya walikuwa hodari zaidi kwa Kampeni za Masoko ya Utalii, zilizopelekea watu wengi kuamini kuwa Mlima Kilimanjaro uko Kenya, na siyoTanzania, tulianza tukiwa nyuma mno! Lakini bado unyonge huo huo ulikuwa na manufaa makubwa katika kujenga sera iliyojaribu kuondoa msigano uliokuwako kati ya Maendeleo na kupatikana kwa Fedha zilizokuwa zinahitajika sana. Iliyumkinika kuwa tukiitangaza Tanzania kwa kelele ndogo, lakini kwa lengo la kunyakua fedha nyingi sana kutoka katika masoko makubwa ya Ulaya na Marekani ya Kaskazini, hatari ya Utalii kuvuruga, kwa njia yoyote ile, mazingira asilia yanayowaleta Watalii hao nchini Tanzania itapungua. Tukiwa na vyumba vichache katika hoteli zetu, na vivutio vichache zaidi, tunaweza tu kunuia kuchukua nafasi za kuanza katika soko, na kupandisha kiwango cha fedha tutakazozipata kwa kila Mtalii atakayekuja Tanzania, hata kama idadi ya Watalii watakaokuja itapungua. Kwa malengo hayo nilibuni na idara ya Uhamiaji kuchunguza uwezekano wa Maafisa wao kuwa katika ndege zinazowaleta Watalii, ili wagongewe mihuri ya kuwaruhusu kuingia nchini wakiwa bado wamo ndani ya ndege, ili kuwapunguzia muda watakaotumia kwa mambo hayo wanapoingia nchini. Ulipita muda kabla utaratibu huo haujazaa matunda. Umuhimu wa kwanza ukawa katika kuhamisha mapato kutoka katika Utalii wa wanyama wa Tanzania ili yaingie mifukoni mwa Watanzania wenyewe; maana Wafanya biashara Wazungu, wa Kenya na wa Ulaya, walikuwa na kauli kubwa katika Mbuga zetu za Wanyama. Kwa hiyo tukaweka vizingiti vipya kwa magari kuingia katika mbuga hizo, na wakati huohuo tukanunua, kwa mpigo, magari hamsini ya aina ya Volkswagen. Tukaanza kunyang’anya mara moja kazi hiyo Makampuni ya Watalii yasiyokuwa na huruma wala wajibu kwa Watanzania. Matokeo ya mambo hayo kisiasa yalikuwa muhimu vile vile. Jomo Kenyatta, baba Mwanzilishi wa Kenya ya sasa, alikuwa akitangazwa kwa sifa za kuwa Mwanzilishi wa Demokrasia katika Afrika. Kinyume chake, Mwalimu Nyerere anayetambulika na

Page 223: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

223

Wanasiasa wa Kenya, pamoja na Vyombo vyao vya Habari, kwa uwezo wake wa kushawishi, kabla na baada ya kushika madaraka, sasa akawa anatuhumiwa kuwa mtetezi wa Ukomunisti mwenye kuwahifadhi kila kikosi cha Magaidi wa Kiafrika cha Afrika Kusini na Afrika Magharibi uhusiano ukaanza kuvurugika, kwa hiyo haikushangaza kwamba, katika miaka ya 1970, Jumuiya ya Afrika Mashariki, iliyoanzishwa kwa matumaini makubwa mno mnamo miaka ishirini iliyopita, hatimaye ikaporomoka! Kuvurugika kwa uhusiano huo hatimaye kukaharibu pia shughuli za usafiri kati ya Kenya na Tanzania. Wakati mwingine hali hii iliyaweka maisha yangu katika hali ngumu. Wakati mmoja nililazimika kushawishi wapite salama kurudi Kenya watalii wa kigeni mia saba waliovuka mpaka visivyo halali katika kivuko cha muda kimoja kati ya vingi katika miaka ile ya 1970, shughuli nyeti na ngumu mno iliyodai makubaliano na madereva wa Volkswagen hamsini na wanane, Mameneja wa Hoteli za Kenya, Wanasheria, Swissair na, hatimaye, Mwalimu Nyerere mwenyewe majadiliano hayo lazima yamepunguza miaka yangu mingi niliyotarajia kuishi, na ambayo wakati mwingine yalidai ufundi wa usuluhishi au wa kutetea mateka uliounganishwa pamoja. Lakini zilikuwako faida pia. Kufungwa kwa mpaka kuliwalazimu wenye Kampuni za Utalii kutambua jitihada zetu zilizokuwa zinaendelea Marekani ya Kaskazini na London katika kuinadi Tanzania kuwa nchi inayojitawala inayostahili kofikiriwa kuwa Kituo cha Utalii kama haki yake. Na lolote ambalo ningeweza kufanya kumdhihirishia Rais na Mawaziri wake, kwamba kuongezeka kwa mapato ya fedha yanayotokana na utalii, kwa kuwaumiza majirani zao wa Kaskazini walio wagumu, litakuwa jambo jema linalopaswa kuhimizwa. Kazi ya kuendesha Shirika la Utalii sambamba na kusimamia Viwanda vya Usindikaji, pamoja na shughuli nyingine, haikunizuia kuendelea kutambua hatari iliyoko katika masuala ya mazingira duniani kote. Huko nyuma, mnamo mwisho wa miaka ya 1960, nilikuwa na uhusiano wa karibu na Paulo de Costa, Mwanachama wa Rotary, Mbrazil, aliyewahi huko nyuma kuwa Rais wa Rotary dunia nzima. Bado nakumbuka wazi wazi safari yetu sisi wawili

Page 224: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

224

mwaka 1984 kwenda kwenye Mkutano mjini Nashville, Tennessee. Wakati huo Rais wa Dunia wa Zamani wa Rotary, James L. Bomar, alinifanyia mpango wa kupata hadhi ya Mstahiki mjini Tennessee, heshima iliyonilazimu “kununua” kiasi cha futi za mraba kumi za ardhi katika Kata ya Moore. Mpaka leo bado napokea barua kutoka kwa Katibu wa Mji kunieleza hali halisi kuhusu kiwanja hicho Na. 655, na kinavyofyekewa au kutumiwa kwa malisho; nadhani wanyama wadogo wadogo, wala hawafikii kundi. Jioni siku moja, nikiwa barazani katika Hoteli iliyoitwa Nashville’s Opryland, mimi na rafiki yangu Mbrazil tulikuwa tukizungumza huku tukinywa kwa muda mrefu mpaka usiku wa manane juu ya haja ya kuoanisha kupatikana kwa riziki na kuondoa umasikini. Kauli yake, kwa nafasi yake kama Rais wa Rotary Duniani, ikawa, “Kuhifadhi Sayari inayoitwa Dunia”. Katika kufafanua jinsi alivyotaka kuyatangaza mawazo yake hayo kwa nguvu zake zote, akanirudisha kwenye Hoja inayohusu matumizi ya kuni kwa kupikia miongoni mwa wananchi wa Tanzania, wengi wao wakiwa masikini! Nikamwambia kwanza nilikuwa tayari kuzungumza masuala ya mazingira, kama changamoto tu, lakini kama hakuna njia nyingine ila kuangusha miti kupata kuni, basi wasiwasi kuhusu mazingira hauna nafasi. Paulo hakukubaliana nasi, akasema kwa ukali, “Huwezi kuyatengenisha mambo haya namna hiyo”, kisha akaendelea kuhoji, kwa imani yake kabisa, kuwa kuhifadhi mazingira na kuondoa umasikini ni pande mbili za shilingi hiyo hiyo: huwezi kufanikisha moja bila ya kuchukua hatua ya kulikabili la pili. Mawazo hayo yakachukua nafasi kubwa sana katika kichwa changu, wakati wa Uongozi wangu katika Shirika la Utalii mpaka katikati ya miaka ya 1970. Lakini mara nyingi matatizo mabaya zaidi yakawa yanajitokeza. Kubwa katika hayo, na inashangaza, lilikuwa kupatikana Ofisi! Ofisi za Shirika la Utalii zilikuwa katika nyumba ya kupanga: kijumba kidogo tu. Kwa vile hazikuwako nafasi za kuwatosha wafanyakazi wote, Kiongozi aliyenitangulia akalazimika kukodi sehemu kubwa ya ghorofa ya tatu ya Hoteli ya New Afrika iliyokuwa jirani iwe Ofisi za hao waliozidi. Matokeo

Page 225: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

225

yake yakawa Shirika kupoteza sehemu kubwa ya mapato ya fedha za kigeni. Bodi ikaamua kutafuta kiwanja kingine kilichoonekana kinafaa kujenga Ofisi mpya za Makao Makuu. Kwa kuwa tulikuwa na tatizo la kudumu la upugufu wa fedha, tukaamua kujenga kwa kushirikiana na Kampuni ya Kuuza Nje Mazao ya Kilimo, GAPEX, pamoja na Mfuko wa Pensheni wa Kampuni ya Upagazi ya Afrika Mashariki. Ingawa ilitarajiwa kwamba gharama zingepungua kutokana na utaratibu huo, bado Mashirika hayo yangeonekana kuwa ya ajabu; na ilikuwa bahati iliyotokea kwamba, pamoja na jitihada zetu zote kutafuta kiwanja hatukufanikiwa! Hapo ndipo Balozi wa Sweden nchini Tanzania, wakati wa dhifa aliyoiandaa nyumbani kwake, aliponieleza kwamba Ofisi yake ilikuwa inaendelea kufuatilia maslahi ya Israel baada ya Serikali ya Tanzania kuvunja uhusiano nayo kwa sababu ya Vita vile vya siku sita. Kwa kukosa matumaini ya kurudi tena, Serikali yao huko Tel Aviv ikaamua kuuza majengo ya Ubalozi wao mjini Dar es Salaam kwa dola za Marekani 80,000 kwa masharti kwamba fedha hizo ziwe zimefika kwa Balozi wao wa New York mnamo juma moja. Kwa nini hasa Israel walitaka kuharakisha mambo kiasi hicho haikueleweka, kwangu mimi na Balozi wa Sweden vile vile. Lakini kwa mawazo yangu nafasi waliyoipata kwa bei hiyo ilikuwa nzuri mno kwa mtu kuikataa. Nikatambua mara moja kuwa sikuwa na uwezo wa kupata fedha nyingi kiasi hicho mnamo juma moja, kwa hiyo nikaomba, na nikapata, muda wa juma moja zaidi; na nikaanza kazi ya kuishawishi Bodi kuachana na Mradi huo. Nikaitisha mara moja Mkutano wa Bodi ya Utalii ili kufafanua mapendekezo yaliyokuwapo, na manufaa ambayo tungaliyapata. Baada ya muda mfupi tu wa majadiliano Bodi ikanipa idhini ya kuendelea, mradi tu kupatikane kibali cha Wizara yetu ya Maliasili, na mradi tuwe na uwezo wa kupata fedha za kuugharimia Mradi, wenyewe, angalau kwa sehemu, kwa fedha zinazotokana na Utalii. Wizara nayo ikakubali haraka haraka, na fedha zikapelekwa New York ndani ya muda. Kwa hiyo nikakaa nikijipongeza kwa kazi nzuri niliyoifanyia nchi ya Tanzania. Majuma mawili baadaye

Page 226: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

226

Balozi wa Sweden akanijia tena; lakini hakuwa na furaha. Akanieleza kwamba alikuwa amejitumbukiza hatarini alipokubali kuniongezea juma moja kutafuta fedha za kununulia lile jengo, lakini nikashindwa kutimiza ahadi; hivyo Balozi wa Israel mjini New York hajalipwa. Nikamjibu kwamba lazima lilikuwako kosa; lakini utetezi wangu haukufaa kitu. Haraka sana nikamtafuta Dickson Nkembo, Katibu Mkuu wa zamani wa Ikulu, wakati huo akiwa pia Mwenyekiti wa Benki ya Taifa ya Biashara, iliyokuwa na jukumu la kuzifikisha hizo fedha New York. Dickson akaniambia kuwa yeye mwenyewe alisimamia zoezi hilo; lakini kwa kuwa Balozi wa Sweden amelalamika, ataliangalia tena suala hilo na kutoa taarifa. Maelezo ya tatizo hilo yakawa wazi kiasi cha kuchekesha. Karani wa Benki ya Morgan Guarantee ya New York alipata taarifa ya kuingia fedha kabla hajaondoka kwenda livu. Badala ya kushughulikia papo hapo, yeye akazihifadhi nyaraka hizo katika “safe”, pamoja na makabrasha mengineyo muhimu, mpaka atakaporudi livu. Benki ya Taifa ya biashara haikupata kujua hatua iliyochukuliwa dhidi ya karani huyo ingawa, kutokana na sifa ya uzembe katika Benki hiyo, mtu anashawishika kubuni. Lakini fedha zikatolewa haraka na hatimaye, lengo likatimia. Nikaamini kabisa kuwa nilifanikiwa kuzuia kitu kama mapinduzi. Lile jumba likanunuliwa kwa bei rahisi kwa vigezo vya bei za wakati ule. Kwa kweli rahisi mno, tukaokoa fedha zile za kupanga, na kunufaika na ile nafasi iliyopatikana katika Hoteli ya New Afrika. Naamini niliifanyia mema nchi ya Tanzania, ingawa wengine walifikiria vinginevyo. Kiasi cha mwezi mmoja baada ya makubaliano hayo nikapokea simu kutoka kwa Waziri wa Fedha, Amir Jamal, aliyetaka kujua nini hasa nilichokuwa nakifanya: badala ya kuimarisha Utalii kama nilivyoagizwa, sasa najitumbukiza katika ujenzi wa majumba! Nikamjibu Mheshimiwa Waziri kwamba lile lilikuwa tatizo la mara moja tu, lililokuwa la faida kubwa sana kwa Tanzania. Kwa nini? Nilikwisha kumpata mtu aliyetaka kulinunua jengo lile kwa dola za Marekani 104,000 baada ya kulipa dola 80,000 majuma manne yaliyopita. Kadhalika, nilitimiza hatua zote zilizotakiwa; niliita

Page 227: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

227

Kikao cha Bodi na kupata ridhaa yake; nikapata kibali cha Wizara Mama vile vile. Baada ya hapo mimi sikuona tatizo lolote. Baada ya hapo Amir Jamal akajinyamazia. Lakini baada ya miezi sita,kabla tu ya kuhamia kwenye Ofisi zetu mpya, nikakabiliwa na Naibu wa Balozi wa Marekani mjini Dar es Salaam, Herbert Levin. Nadhani alitaka kulinunua jengo hilo, lakini Kanuni za Serikali yao hazikumruhusu, badala yake akataka kulikodi. Nikadai dola 25,000 kwa mwaka, kulipwa mwanzo wa kipindi. Marekani wakalikodi jengo hilo, na kuliimarisha zaidi kwa kiwango kikubwa, kwa fedha zao wenyewe. Hatimaye walipoondoka jengo likarudi tena mikononi mwa Bodi ya Utalii iliyokuwa imeundwa upya. Na sasa, kutokana na matengenezo hayo, kodi ikaongezeka kwa dola 10,000. Tukio hilo dogo likanifunza mengi kuhusu mwelekeo wa Serikali ya Mwalimu katika masuala ya biashara. Si kweli kwamba hawakutaka kuweka mipango ya kuimarisha zaidi manufaa ya Tanzania, lakini hulka yao ya mashaka dhidi ya masoko, iliyo kawaida ya Wajamaa dunia nzima, ikawazuia kuwa na imani na mapatano yoyote yaliyoonekana kuzaa faida ya haraka haraka. Nakumbuka kwamba, katika miaka ya 1970, nililifanyia mpango wa mkopo shamba la miwa la Mtibwa, Kampuni iliyokuwa inamilikiwa wakati ule na Shirika la Taifa la Chakula NAFCO, kwa kushirikiana na Kampuni ya Madhvani; mkopo wa kiasi cha pauni millioni 2 uliotolewa na Benki ya Williams and Glyn ya Uskochi, kulipwa ndani ya muda wa miaka sita na riba ya asilimia 6 kwa mwaka, inayopungua kila malipo yanavyotolewa, kuiwezesha Mtibwa kununua zana kutoka Kampuni ya Fletcher and Stewart ya Derby. Waziri wa Fedha, Jamal akahofu kuwa ulikuwako mtego, vinginevyo Benki isingethubutu kutoa fedha kwa masharti laini kama hayo. Katika nafasi hizo, na nyinginezo, nilifanikiwa kuondoa hofu hizo, kisha wote wakaungana nami katika kufurahia matunda. Lakini, kwa kweli, hawakuwako Wawekezaji wa kutosha waliokuwa tayari kufanya kazi kwa Taratibu hizi mpya. Matokeo yake ukatawala wasiwasi, nadharia na silka ya kutothubutu!

Page 228: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

228

Nilipokuwa Mwenyekiti wa Shirika la Utalii Tanzania, Meneja Mkuu alikuwa Gabriel Mawala, mtu safi na mfanyakazi wa siku nyingi, aliyeendelea kuzingatia masuala ya Utalii mpaka alipofariki miaka michache iliyopita. Nakumbuka tukio moja la kuchekesha. Kutokana na pendekezo langu, Mawala akamwomba Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha kuliruhusu shirika la Utalii kupata fedha kutoka katika Mfuko wa kuimarisha Utalii uliokuwa unashikwa na Hazina, ombi hilo likakataliwa. Nafasi ya Mawala baadaye ikachukuliwa na Francis Byabato, aliyekuwa ndiye kwanza amestaafu kazi yake ya Naibu Katibu Mkuu wa Hazina, nami nikamwomba alitazame upya ombi lile, kwa vile nilivyoamini kuwa sasa tulikuwa na nafasi nzuri zaidi. Lakini, kiasi cha majuma sita baadaye, nikagundua kuwa huyo aliyechukua nafasi yake kule Hazina alikwisha mjibu kwamba asingeweza kufanya vizuri zaidi ya kunakili barua yake mwenyewe aliyoiandika wakati alipokikalia kiti cha Hazina. Jibu hilo halikumfurahisha Byabato. Kiasi cha miaka miwili baadaye Ezrom Maryogo, mmoja wa Wasaidizi binafsi wa Rais Nyerere, akaniambia kuwa Rais aliamua kumteua yeye kuwa Meneja Mkuu wa Shirika, akisema kuwa madhali hakuwa na uzoefu wowote wa kuendesha Mashirika ya Biashara, ningemsaidia. Kiasi cha mwaka mmoja hivi baada ya Maryogo kushika wadhifa huo, mimi nikaamua kujiuzulu Uenyekiti na, miezi minne baadaye, Chifu Adam Sapi, Spika wa Bunge akateuliwa badala yangu. Na Bodi yenyewe ikaundwa upya. Haikuwa rahisi hata kidogo kupata uwiano mzuri kati ya haja ya kuingiza fedha na kuhifadhi mazingira yetu. Kama ilivyotokea katika nchi nyingine za Afrika, sisi nasi tumesumbuliwa na wawindaji haramu pamoja na makampuni ya nje yanayokata magogo bila kibali. Lakini, kwa bahati nzuri, jitihada za pamoja za Mabwana Forodha hodari na Watunga Sera walioelimika zikapelekea kupatikana kwa Maamuzi yaliyo muafaka. Wananchi hawakushabikia kula manyama ya porini, kwa hiyo kutoweka kwa wanyama kunakodhihirika katika nchi kama Kongo hakukuweza kutokea Tanzania. Na Sera ya Utalii ya “wanyama kidogo, thamani kubwa” ikazaa fedha zote zilizokuwa zinatakiwa bila kuelemea mno

Page 229: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

229

Mbuga zetu za Wanyama. Lakini bado tahadhari ingali inatakiwa kila upande. Kwa jinsi Taratibu zetu hizo za kuvutia Watalii zinavyozingatiwa, sambamba na kuviimarisha Vijiji vyetu, hatari ya Kampuni za Utalii na Wanakijiji kuviza maendeleo, hata katika zile mbuga zenye majina makubwa kama Gombe, bado inasumbua maendeleo yao wenyewe tu. Bado kukata magogo bila kibali, hati miliki, ni tatizo kama lilivyo tatizo kwa vijiji kukata miti michache iliyosalia kuchoma mkaa au kutengeneza vinyago. Utalii wa Tanzania unajidhihirisha katika wasiwasi walionao Marekani na Waingereza; na, mpaka sasa katika soko la dunia nzima la thamani ya karibu dola trilioni 4 kwa mwaka, Afrika inaambulia asilimia nne tu ya Biashara ya Dunia ya Tatu, na chini ya asilimia mbili ya Biashara yote ya Utalii! Lakini, pamoja na yote hayo, sera zilizowekwa na Tanzania katika miaka ya mwisho ya 1960 na 1970, zilizolenga kufanya utalii wa uchumi udumu nchini Tanzania kwa vizazi vingi vijavyo, dhahiri zimefanikiwa kwa kiwango ambacho karibu sasa sekta ya Utalii itaingiza nchini fedha nyingi zaidi katika uchumi wa Tanzania. Kuiachia nafasi yangu ya Mwenyekiti wa Shirika la Taifa la Utalii hakukuwa na maana ya kusitisha kujihusisha kwangu katika masuala ya Mazingira. Shughuli za Rotary na Round Table zote zilikuwa zimetengenezea toka zamani taratibu zilizokuwa zinajulikana kwa muda mrefu kuhusu; mazingira, ya Nchi na ya Kimataifa. Tulikuwa na Klabu za Rotary katika Afrika, zilizokua zinafanya kazi kama Washirika katika kuhifadhi Mazingira, na kupata nafasi kubwa ya kuwa na ushirikiano wa karibu na Serikali na, Wafanyabiashara. Katika mawasiliano hayo ya kirafiki, au kupitia nafasi za mafunzo zinazotolewa na Mfuko wa Rotary uliokuwa unafanya kazi tangu 1947, na kupitia Mipango ya ushirikiano inayogharimu zaidi ya dola milioni 100 za Marekani kila mwaka kwa Vikundi vya aina zote, toka vile vinavyonuia kupunguza umasikini mpaka vile vinavyodhibiti maradhi, dhahiri Rotary wameonyesha mafanikio, Aidha wameweza kusaidia kwa kuwa chachu katika kujenga

Page 230: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

230

uhusiano wa karibu zaidi kati ya kuhifadhi mazingira na kufuta umasikini, masuala yaliyo muhimu mno ndani ya moyo wangu. Mwaka 1989 Dr. Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika, OAU. Rotary wakaomba mahusiano ya kideplomasia na Umoja huo, maombi ambayo Dk. Salim aliyakubali na kuvipokea Vitambulisho vyangu kama Mwakilishi wa kwanza wa Rotary ndani ya OAU. Mtumishi mashuhuri wa Afrika, Dr Salim alipoteuliwa mara ya kwanza alikuwa ndiye mdogo kwa umri kuliko Mabalozi wengine wote; sasa hivi yeye ndiye Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere. Mwishoni mwa miaka ya 1980, Serikali ilipogundua ari yangu kubwa katika kufanikisha masuala yote ya mazingira, nikateuliwa Naibu wa Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika Tume ya Maandalizi kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Dunia uliopangwa kufanyika Rio. Kutokana na nafasi hiyo, nikachaguliwa na kundi la nchi zinazojiita G77, pamoja na China, kuwawakilisha katika Kundi la nchi zinazojiita G7, au sasa G8, katika masuala ya Mazingira Duniani. Lengo la Mpango huo mkubwa lilikuwa kuhakikisha kuwa fedha zinarudishwa kwenye nchi zinazoendelea, kama fidia, kwa kulipia uharibifu unaoendelea wa mazingira ya dunia unaofanywa na nchi zenye Viwanda. Baada ya mvutano mgumu katika mabishano ya muda mrefu muafaka akapatikana. Kwa jumla ndivyo ilivyokuwa pia katika Mapatano ya Rio. Wakati Serikali ya Marekani ilipokuwa inajiondoa katika kundi la Watetezi wa Mazingira, lililodumu katika vipindi vyote viwili vya Utawala Reagan, na, wakati walipokuwa waeungana na Wazungu na watu wengine duniani kusherehekea kumalizika kwa Vita Baridi, Rio ikaonekana kuwa mwanzo wa jitihada za pamoja za kunusuru dunia. Sisi tuliokuwa Rio tulikuwa na matumaini kwamba Ujumbe wa Marekani ungalikuwa mzito sana, wa kuongozwa na angalau Makamu wa Rais Dan Quayle. Lakini, ilivyotokea, hata Mkurugenzi aliyehusika na Mazingira hakuwako. Tulipokutana kienyeji jioni moja, mtu mmoja alilalamikia ari duni ya Serikali ya Marekani. Waziri Kamal Wath

Page 231: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

231

wa India akasema, “Tusiwasumbue Rais Bush na Makamu Quayle; sisi tunasumbuliwa na vichaka na matetemeko!” Ni tukio lililokuwa na umuhimu mkubwa mno na, mpaka sasa, baada ya kasoro za waziwazi za kushindwa kuheshimu Makubaliano ya Kyoto, bado Rio imebaki imara kama kichocheo kwa wote wanaoheshimu kwa dhati matatizo ya Mazingira yetu. Sisi tulio Tanzania tunafahamu zaidi ya wengine wote ulivyo dhaifu uwiano kati ya mipango ya Mungu na uwiano wa binadamu. Sio suala la mbuga zetu peke yake na wale wanyama wa dunia tano wenye majina makubwa nchini Afrika, au wanyama wengine wanaovutia zaidi. Wala si suala la uzoefu wetu ambao, mara nyingi; tumeupata baada ya matatizo mengi katika kuoanisha mahitaji ya vijiji vyetu masikini na yale ya wanyama na miti iliyo katika mazingira yao. Masuala hayo yanadai uelewa, ambao Waafrika wanao kuzidi watu wengine wengi, kwamba hatimaye mambo yote hayo yanahusiana; na kwamba hatua zinazochukuliwa katika sehemu moja, bila kujua au kuwaza wasiwasi wa Bara hili kubwa, uwe wa siasa na Uchumi au wa Mazingira, mara nyingi zinatuathiri sana sisi tulio Afrika tunaobaki kuwa watazamaji tu. Katika dunia hii iliyounganika ambamo wachache tu ndio wanaoelekeza Sheria za kutawala wengi, kuna somo lililositirika la kujifunza katika hayo yote, kwamba iko haja ya kuzingatia majukumu ya dunia nzima; kwanza katika Afrika, ndiyo, lakini muhimu zaidi katika Serikali, Mashirika na Makampuni ya Mataifa makubwa yaliyoendelea.

Page 232: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

232

KUMI NA MBILI

MIAKA YA MWINYI Ilipokaribia miaka ya 1980 nilikuwa bado “Bwana Mashirika” wa Tanzania; kwa kweli jioni ya siku moja, tulipokuwa katika dhifa ya chakula cha jioni, Balozi mmoja alinitania kwa kuniita “Balozi wa Dunia ya Mashirika”. Lakini wakati huo nilikuwa tayari naamini kwamba jitihada za Tanzania za kujenga ujamaa zilikuwa zinashindwa vibaya. Zaidi sana, mwasisi wake mkuu, Mwalimu Nyerere, naye alikuwa na mawazo kama hayo hayo. Maana, pamoja na kutumbukiza msaada wa zaidi ya dola za Marekani bilioni 2, na kupanga upya Taratibu za uchumi, bila kusahau uzalishaji katika kilimo, na jitihada zote za chombo kama Benki ya Dunia kusaidia kujenga upya Taratibu zetu, bado Tanzania ya mwaka 1980 ilikuwa masikini kwa kiwango kile kile kama ilivyokuwa mwaka 1961! Kwa kigezo cha masafa ambacho Wanakijiji walilazimika kutembea kutafuta maji safi; kwa kigezo cha virutubisho katika vyakula wanavyokula; kwa vigezo vya matarajio ya miaka ya kuishi, na ya vifo vya watoto wachanga; kwa kweli kwa vigezo vingi vinavyotumika kulinganisha uchumi wa nchi mbali mbali duniani; dhahiri Tanzania haikuwa inaendelea. Kwa kweli, kwa vigezo vyote vya maana vya Umoja wa Mataifa, bado sisi tulikuwa chini kabisa, pamoja na nchi nyingine kama Bangladesh. Sababu za kasoro zote hizo haziwezi kudhihirika kwa uchambuzi mwepesi-mwepesi. Kwanza watu wenye akili nyingi sana duniani humu wameelekeza mawazo yao kwenye matatizo yetu. Mtu anaweza kuutaja upungufu wetu wa rasilimali, kama mafuta. Mwingine atataja matatizo ya sehemu kubwa ya mazingira yetu. Mwingine kuvurugika kwa Taratibu zetu za zamani katika biashara, ambazo mpaka sasa zimesitiri kasoro nyingi katika Mipango yetu ya Uchumi. Na bado mwingine anaweza kutaja kushindwa kwa Sera za Ujamaa dunia nzima. Lakini kasoro ambazo hatimaye zilivuruga fikira za Mwalimu za Ujamaa zilikuwa nzito zaidi kuliko zote hizo.

Page 233: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

233

Kwa muda wa miaka ishirini nimekuwa nikitafakari tatizo lilikuwa wapi. Kwa utafiti wangu yafuatayo, ambayo pengine hayakupangwa vizuri, ni baadhi ya mambo yaliyosababisha kasoro hiyo: Nchi yangu imeshindwa kuyakabili Mazingira ya Uchumi yaliyotokana na Ushindani katika hali ya Uhuru. Bila shaka Historia itatoa majibu ya swali hilo. Katika miaka 1960 na 1970, Waafrika wengi, hasa Watanzania, waliona ni rahisi kumimina lawama zote za matatizo yetu milangoni kwa Watawala wetu wa Kikoloni; na kwa kweli lawama nyingine bado zinawaandama mpaka sasa. Kama walivyo wakaidi wengi, wao nao hujaribu kutetea hoja zao, labda kama njia ya kujikosha wasiwajibike kwa yale yote yaliyotokea hapa katika miaka yote arobaini hivi iliyopita. Kwa kuzidisha chumvi, wamejitosa katika kupunguza uzito wa mashitaka ya msingi yanayoelekezwa kwao. Hapana, siamini kuwa Waingereza wanastahili kulaumiwa kwa matatizo yetu yote. Kama Ukoloni ni aina ya Udikteta, na kwa hakika ndivyo ulivyo, basi pengine Waingereza ndio peke yao, kati ya Watawala wote wa kigeni, waliojenga Utawala endelevu na wenye huruma. Lakini kama mtu atafanya utafiti wa kina juu ya sababu za kuvia kwa Ujamaa, hataweza kukubali kuwa Watawala wetu wa Kikoloni hawakuwa na Wajibu unaowaandama kutokana na baadhi ya matatizo yanayotokea sasa. Maana, kwa kweli, Utawala wa Mwingereza katika Tanganyika ulikuwa kama wa mzaha-mzaha ukilinganisha na tuseme Kenya au Zimbabwe. Pengine hali hiyo ilitokana na muda na namna Waingereza walivyodakia majukumu baada ya Vita Vikuu vya Kwanza. Pengine ndivyo yalivyokuwa Masharti ya Shirikisho la Mataifa. Pengine ni kwa sababu ya ugumu wa maisha katika maeneo yale yaliyo katikati ya Tanzania; au sababu ya mapambano ya kudumu dhidi ya magonjwa ya kuambukiza kama malale na malaria; au kuhangaika na hali ya kukosa mvua za kutosha; au masafa marefu kuyafikia mashamba kwenye ardhi inayolimika. Mazingira yote hayo yakawazuia Wageni kuwa na makazi ya kudumu nchini kuanzia mwisho wa karne ya kumi na tisa na kuendelea.

Page 234: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

234

Kwa sababu zozote zile, kukosekana kwa shauku na ari katika jitihada za Waingereza kulidhihirika kwa jinsi Nchi yetu ilivyokuwa mwaka 1961, wakati Mwalimu aliposhika madaraka. Wakati ule, kutokana na uwekezaji mdogo katika mipango ya elimu ya wananchi, walikuwako Waafrika wachache sana waliokuwa na Shahada za Chuo Kikuu miongoni mwa watu wasio 10 milioni. Hata Elimu ya Msingi, ambayo karibu gharama yake yote ilikuwa inabebwa na Wamisionari, pengine haikufanikiwa mwaka 1961 zaidi ya vile ilivyokuwa mwaka 1931. Wakati ule Tanganyika ilipokuwa inapata Uhuru, mipango yake ya kilimo ilikuwa ya ovyo ovyo, kiasi kwamba nchi haikuweza kutumia vema maarifa mapya, na hata hayo yaliyokuwako nchini, (na katika hayo miradi iliyosifiwa sana ya Kilimo cha karanga, ambayo kwa kweli ilitia aibu, ni mmoja tu wa mifano inayojulikana). Waingereza wakaturithisha taratibu za kupata chakula zilizolenga wakati wote uzalishaji uliowalenga walaji Wazungu wa nchini badala ya Wananchi waliokuwa wanalima. Tuliachwa tukiwa Utawala wa kubabaisha usiokuwa na uwezo wowote zaidi ya kutekeleza Sera za “liwalo na liwe”, Tukarithi miundombinu ya usafirishaji ambayo, kwa kuisifia sana, tunaweza kuiita ya ovyo ovyo tu; mawasiliano tuliyokua nayo na Nchi za Nje hayakutosha, na gharama yake ikawa kubwa mno kwetu. Msingi wa biashara zetu ukawa, na ukaendelea kuwa kwa muda mrefu baada ya Uhuru, wa kutegemea Kampuni za zamani na zisizokuwa na ufanisi za kuagiza na kuingiza bidhaa, zilizokuwa zinaendeshwa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya Taifa-mama. Vyombo vyetu vya habari vilikuwa vimekamatwa na Wazungu walowezi, na kumilikiwa na Wazungu wengine wasiokuwa wakazi wa humo; na hali ikaendelea kuwa hivyo kwa karibu miaka kumi. Uchumi wetu haukupata kuimarishwa na Wajerumani wala Waingereza. Haikuwako Sekta ya Viwanda yenye maana; na hiyo iliyokuwako ikabaniwa katika utamaduni uliokuwa umeenea wa “dukawalah”, yaani maduka yaliyokuwa yanamilikiwa na Wahindi, uliokuwa unakubalika kwa shida, na mara nyingi walikuwa wanadharauliwa. Na kadhalika.

Page 235: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

235

Lakini udhaifu wa Taratibu tulizorithishwa na Waingereza; kama nilivyosema hapo mwanzo, zenyewe kwa sehemu ni matokeo ya ugumu wa mazingira vijijini. Kudra haikuona vema kuibariki Tanzania kwa akiba kubwa kubwa za mafuta yanayochimbika, au za madini yanayoweza kufikiwa kwa urahisi. Wala kudra haikulipa Taifa hili jipya rutuba ya kutosha katika ardhi inayoweza kulimwa chakula cha kutosha. Inawezekana Tanzania kuwa nchi yenye eneo kubwa sana; lakini maeneo yake ya Kilimo, kama yalivyo, yamesambaa sehemu sehemu, na kuvurugwa na hali isiyotabirika ya rutuba ya ardhi yake, mvua zisizokuwa za hakika, na mashambulizi ya kudumu ya mbung’o na wadudu wengine. Kasoro hizo ndizo zinazodhihirisha sababu za kukosekana kwa Wawekezaji kutoka Jamii ya Watu wa Nje; ndizo vile vile zilizozaa vizingiti kwa yale ambayo Watanzania wenyewe wangaliweza kuyafanya katika kuendeleza kilimo nchini. Labda, kwa bahati mbaya, matatizo kama hayo hayakuweza kuweka kiwango cha mwisho cha ongezeko la watu. Kutokea mwanzo wa Utawala wa Waingereza, mpaka mwaka ule Mwalimu alipong’atuka kuacha nafasi yake ya Rais, idadi ya watu wetu iliongezeka mara tano, na hilo ni pamoja na kiwango kikubwa sana cha vifo vya watoto wachanga na matarajio madogo ya watu kuishi kwa muda mrefu. Kwa kwenda kinyume na mwelekeo wa hali yetu, kuongezeka huko kwa idadi ya watu kukazaa kasoro nyingine katika taratibu zetu za kilimo. Ili kulisha wingi wa watu hao walioongezeka, ambao zaidi walikuwa vijana, hasa wanaume, waliohamia mijini, ikabidi yale mazao asilia ya chakula kama mtama na uwele, yanayostahimili mazingira ya kilimo ya Tanzania, yaachwe, na kulimwa badala yake mimea inayotoa mazao mengi zaidi lakini yasiyoweza kuhimili ukame, kama mahindi. Kwa hiyo haishangazi kwamba wale Wananchi wa Vijijini waliokuwa wanasumbuka sana wakasalimu amri kutokana na hali hiyo. Kisha siasa za ukombozi wa Afrika hazina budi kuongezwa katika mjadala huu. Tanzania ikachipukia mbele ya harakati zilizozaa vita na mapambano ya kikabila yaliyoenea katika sehemu kubwa ya Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara. Hakuna hata moja kati ya nchi hizo, nyingi kati yake zikiwa zimeundwa, nje ya utaratibu, na

Page 236: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

236

Wakoloni waliokuwa wameziteka, ili kujenga kitu cha kuwatambulisha kama Mataifa. Athari zake mara nyingi zikawa kujenga utii na uaminifu kwa udogo kuliko kwa nchi. Kukiwa eneo kubwa sana la ardhi, na makabila mbali mbali mia na ishirini ndani yake, Tanzania ikawa na tatizo lililokuwa linanukia kuimarisha dhana ya kanda kama siyo ukabila. Wakati huo huo, ikiwa na mipaka na nchi nane, na mkondo mdogo wa bahari unaoelekea kwenye eneo la Ukoloni wa Waarabu, nchi mpya Tanganyika huru ikawa, na ndivyo ilivyo mpaka sasa, katika wasiwasi zaidi kuliko nchi nyingine nyingi kwa sababu ya matokeo ya vita na maradhi ya nchi za mipakani. Nchi changa kama Tanzania zimetumbukia vile vile katika mchezo mkubwa zaidi wa Siasa za Utawala, zilizozihesabu Nchi zinazoendelea kuwa zaidi kidogo ya vyombo vya kuweka rehani ya kuchezewa na Mataifa makubwa yaliyoshuhudia vile Vita Baridi vilivyopiganwa na Mawakala wao katika hizo nchi changa za Afrika. Na kisha, kujumlisha yote, mivutano ya hatua hizo mbili za kuuzika Ukoloni na kujenga Utaifa wa Mwafrika ilipositishwa ghafla katika mpaka wake wa Kusini, Tanzania, kama ilivyojulikana wakati huo ghafla ikajikuta, katika ile miaka ya mwanzo ya wasiwasi baada ya kujitawala, inalazimika kuchagua kati ya Watawala wake wa zamani wa Kikoloni na Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini, Msumbiji, Zambia na Zimbabwe; Uamuzi mzito wa Imani ulioambatana na matokeo mabaya ya Uchumi yasiyotarajiwa. Mwisho kuna masuala ya Maendeleo ya Kimataifa. Kwa jumla hilo lilikuwa zoezi lililopangwa kwa nia njema kwa ajili ya kuzisaidia nchi changa kama Tanzania kujisukuma kwa nguvu zake zenyewe. Lakini kwa sababu ilikuwa shughuli mpya, iliyoanzishwa wakati mataifa makubwa yalipokuwa yanacheza michezo inayohusu dunia nzima, hatari zinazozikabili nchi zile zilizokuwa zinasaidiwa hazikupata kuchunguzwa kwa makini kama ilivyostahili. Benki ya Dunia iliyokuwa inaongozwa na Robert McNamara ilikuwa sahihi kutambua kufaa kwa Tanzania kuwa Kituo kipya cha vielelezo vya maendeleo.

Page 237: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

237

Lakini, kama ilivyokuwa katika miradi mingi ya mwanzo ya kipindi kile, matokeo hayakulingana hata kidogo na yale yaliyopangwa. Mara nyingi mno tumeziona nchi zilizotoa misaada zikidai sifa zaidi kutokana na kutoa kwao kuliko kudumisha yale waliyotarajiwa kuyaanzisha. Fedha zilizotolewa kusaidia nchi kama Tanzania ziliingia kwa mpigo, na mara nyingi hazikutosha, kiasi kwamba mara nyingi kikawa cha kugombania. Masharti yaliyoambatana na matumizi ya fedha zilizotolewa, kununua bidhaa na huduma kutoka nchi hiyo hiyo inayotoa msaada, yakavuruga mafanikio ya mipango hiyo. Kadhalika Wafadhili wakayarudia makosa waliyoyafanya Waingereza; ya kuamua nini kifanyike, kifanyike wapi, na kwa namna gain, bila kuwashirikisha Watanzania wenyewe. Mara nyingi watu wanaoonekana kuwa Wataalam wa Mikataba iliyo wazi walighilibiwa juu ya Tanzania, kwa sababu watoa fedha walitaka kuwatafutia kazi sehemu nyingine. Katika mazingira hayo wala haishangazi kwamba kiasi kinachotamkwa mara kwa mara cha dola za Marekani bilioni 2 za Msaada wa Kimataifa kwa Tanzania kati ya 1961 na 1985 si sahihi. Kiasi halisi cha fedha zilizotolewa kwa Tanzania ni kidogo mno kuliko hivyo, isipokuwa katika namna moja muhimu, lakini ya hatari. Kiwango cha kutegemewa kilichonunuliwa huko na fedha zote hizo za Wafadhili kilikuwa na thamani iliyozidi sana dola bilioni mbili. Na, kwa masikitiko, baada ya miaka ishirini, fikira hizo zingali zinaandama mawazo ya Watanzania mpaka sasa. Tukiwa tumegeuzwa na Ubeberu kuwa Omba-omba, na kisha tegemezi wa fedha za Wafadhili, bado tunayakiri mpaka sasa maisha hayo ya Omba-omba, na vivyo hivyo katika vitendo vyetu. Mpaka hapo picha utakuwa umeipata. Nayaandika haya siyo kwa lengo la kumteta Mwalimu na watu wetu wasilaumiwe kwa kuviza Ujamaa, bali la kupunguza lawama zozote zinazoelekezwa kwao kutokana na yale yote tunayoyajua sasa. kwa kweli ni ajabu kwa Tanzania kuibuka kutoka siku zake za mwanzo kabisa bila kukumbana na majanga ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, au ya njaa, au Utawala wa maguvu wa Kijeshi, au maradhi ya kuambukiza ya halaiki. Dhahiri lawama zimekuwa zikituelemea

Page 238: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

238

sana sisi, kama inavyodhihirika kwa machafuko ndani ya nchi nyingi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Lakini bado hakuna haja ya kupuuza baadhi ya makosa yaliyofanywa katika ile miaka yetu ya mwanzo. Hekaheka za Vijiji vya Ujamaa walikohamishiwa, bila kuchagua, asilimia arobaini ya Wananchi kwenda kwenye maelfu ya Vijiji vipya, maili nyingi kutoka maeneo walikozaliwa, ni moja ya Sera za Uchumi za wakati ule zilizokuwa na utetezi mdogo kuliko zote. Na, kweli, uhamaji ulichangia katika kuwaunganisha watu wa nchi hii, kwa kuimarisha fikira muhimu za utaifa juu ya zile za zamani za U-kabila, U-kanda au hata U-Dini. Lakini matokeo mabaya ya kilimo kilichokuwa tayari kimevurugika yalikuwa mazito na yaliyodumu kwa muda mrefu. Watu walipelekwa kwenye maeneo wasiyoyaelewa, kufanya kazi katika Jamii mpya za wageni watupu; na matumaini makubwa ya Ushirika kuundwa kila mahali hayakupata kuungwa mkono kwa fedha za kutosha na Wataalamu. Kadhalika Uongozi ulishindwa kubaini haja ya wenye maduka kufanya biashara zao. Mawazo ya Mwalimu katika kujishughulisha kwangu na Viwanda vya usindikaji na kazi nyingine katika uchumi hayakuwa ya kawaida. Wafanyabiashara wengi mno, Waasia na Waafrika, walitumbukia katika mtego wa kushabikia nadharia za Siasa kuliko kufikiria fedha na maendeleo ya uchumi. Uchumi, hata kama sehemu yake kubwa inaendeshwa na Dola, lengo lake lazima liwe kutengeneza ziada. Vile vile ungelenga maeneo yale yenye mahitaji makubwa, na fedha chache kuliko zote zinazotoka nchi za nje; halisi na za matarajio. Lakini haikuwa hivyo. Hatimaye ikazuka hali ya kutegemea mno marafiki zetu, Wajamaa wa Kimataifa, ambao upeo wao wa Siasa ulikuwa wa juu sana, lakini mwelekeo wao wa Uchumi ulikuwa unazidi kudumaa. Inawezekana Wa-Cuba, Wajerumani wa Mashariki na Warussi walikuwa wajoli wetu wazuri wa kisiasa katika miaka ile ya matatizo, kutokana na fikira za ovyo za Waingereza zisizoweza kutetewa juu ya ubaguzi wa rangi wa Ian Smith kujinyakulia Uhuru wa Zimbabwe. Lakini, kwa kweli, uhusiano wa kidugu na Urussi

Page 239: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

239

na majirani zake usingeweza kutuinua kutoka chini ya aina yoyote ya Uchumi wa Dunia. Kama ilivyo sifa yake ya kudumu, Mwalimu vile vile alizitambua kasoro zake mwenyewe kila matatizo yalipozuka katika mazingira ama aliyoyarithi ama aliyoyatwikwa. Mtu wa ajabu miongoni mwa Viongozi wa Kiafrika wa rika lake, hakuwa na tamaa ya kuwa Rais wa Maisha, wala ya kuchafua jina lake kubwa kwa manufaa yake mwenyewe. Alikuwa mtu mkubwa mno mbele ya watu, na mkubwa zaidi kwa kukiri kwamba yeye naye ni mwanadamu. Na, mwishoni mwa miaka ya 1980, akabaini kuwa muda ulikuwa unakaribia kwa Mwenge wa Uhuru kukabidhiwa mtu mwingine. Katika Taifa jipya, kazi ya kumchagua Kiongozi anayekubalika sana na Wananchi walio wengi kamwe haitakuwa rahisi; na tatizo ni gumu zaidi katika nchi kama Tanzania ambako, kwa Historia, Bara ambayo watu wake wengi ni Wakristo imeungana na Zanzibar ya Waislamu. Katika Chama cha Mapinduzi, kilichochukua nafasi ya TANU kama Chama Tawala, walikuwako Wanasiasa wengi, vijana zaidi, waliokuwa wanatamani kuishika nafasi ya Mwalimu. Lakini katika hao walioruhusu majina yao yajitokeze katika kinyang’anyiro hicho, ni wachache tu walioonekana na Mwalimu kuwa na sifa ya kushika nafasi ya Rais. Kwa mawazo yake, malengo ya Utaifa, na hoja ya kudumisha jitihada zilizokuwa zinaendelea za kujenga Umoja wa Taifa, ndivyo vilivyostahili kuwa vigezo vikuu. Barabara ikawa inaelekea Zanzibar, na kwa Mwislamu. Vitabu vya Historia vikawa tayari vimejielekeza kwenye mchakato wa Uteuzi huo wa CCM uliokuwa unakaribia. Sioni sababu ya kuyarudia maelezo hayo, wala ya kuongeza tafsiri yangu mwenyewe. Kwa kuwa hakumwandaa mtu wa kushika nafasi yake, Mwalimu akawa huru kutumbukiza ushawishi wake kuhakikisha kuwa Uchaguzi unaelekezwa kwenye kuzingatia manufaa ya baadaye ya Tanzania kwa jumla. Hatimaye pendekezo la Chama, na la Mwalimu, la Mgombea Ali Hassan Mwinyi, likaupa Mkutano wa Uteuzi nafasi nzuri, pamoja na Baraka za Mwalimu, lakini vile

Page 240: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

240

vile likatoa changamoto katika kupanga dira mpya kwa mwelekeo wa Tanzania, kwanza katika Uchumi, lakini baadaye katika Siasa. Kuyafanya hayo yote bila Mwalimu ingekuwa kazi ya kutisha. Kujaribu kuyafanya mabadiliko makubwa namna hiyo wakati bado Baba wa Taifa letu ana kauli, na ni sehemu muhimu ya Ujenzi wa Nchi, licha ya kuwa ndiye Mwenyekiti wa chama Tawala, ni tukio lililohitaji tafakari nzito. Kwa sababu hiyo tu, kigezo chochote cha mafanikio ya Rais Mwinyi katika vipindi viwili vya utawala wake kunahitaji kuzingatiwa. Wachambuzi wengine wamependa kukipuuza kipindi cha utawala wa Mwinyi, baada ya mafanikio makubwa mno ya Urais wa Mwalimu. Lakini mimi sikubaliani nao; maana katika kipindi chote cha miaka ya sabini na, kwa kweli, mpaka pale mabadiliko yalipofanywa mwaka 1985, mafanikio makubwa zaidi yalikuwa katika Siasa. Lakini katika Uchumi Nchi ilikuwa chini ya maji, ingawa sehemu yake kubwa ilikuwa imezama. Pamoja na ufundi wake wote, Mwalimu hakuweza kuleta mabadiliko kutoka Uchumi wa Imla kwenda kwenye Uchumi Huria wakati alipokuwa kitini; badala yake kazi hiyo nzito akaachiwa Mwinyi na Wasaidizi wake. Kwa hiyo nimetosheka na Hoja za Umuhimu wa Urais wa Ali Hassan Mwinyi. Yeye ndiye aliyejitumbukiza katika kuthubutu, ndiye aliyeuweka msingi wa maendeleo ya Uchumi na ya Jamii yaliyopatikana kuanzia 1995, wakati Benjamin Mkapa alipochaguliwa Rais. Uhusiano wangu na Rais Mwinyi wakati wote ukawa tofauti na ule niliokuwa nao na Rais aliyeng’atuka. Ujamaa ulimfikisha Mwalimu kwenye mapambano dhidi ya wafanyabiashara wa nchini; na, ingawa Sera zake hazikupata kunitoa nje ya mstari, nilikuwa natambua wakati wote kuwa walikuwako wengine ambao hawakuwa na bahati hiyo. Mwalimu alikuwa mtu wa kuzingatia misingi, lakini aliyekuwa tayari wakati wowote kubadili mwelekeo wake endapo ushahidi mpya, na wa kutosha, utawasilishwa mbele yake. Hata kama Wapenzi wake mwenyewe wanahusika, kama ilivyokuwa kwa Derek Bryceson, hatasita kutekeleza yale anayoyaamini kuwa ya manufaa kwa nchi.

Page 241: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

241

Rais Mwinyi kadhalika alijitahidi kutekeleza nchini Tanzania yale aliyoyaamini kuwa sahihi. Yeye alikuwa, na ndivyo alivyo mpaka sasa, mtu mwungwana zaidi kuliko Mwalimu alivyopata kuwa; mtu mwenye silika ya usuluhishi, mwenye ujuzi wa asili wa jinsi ya kupata suluhu katika mahusiano baina ya watu wenye Imani tofauti na asili tofauti miongoni mwa Watanzania. Anaheshimika mno kutokana na namna anavyowahudumia wale wanaotafuta Ushauri wake. Inawezekana nimekutana naye mara chache zaidi kuliko nilivyokuwa nakutana na Mwalimu; lakini, kwa Rais Mwinyi, haikuwako haja kubwa ya kukutana naye. Rais Mwinyi alijikita kwenye Mpango wa Uchumi ulioelekea zaidi kwenye dhana na utekelezaji wa yale niliyokuwa nataka yatekelezwe miaka ishirini kabla. Kadhalika, naona si haki kabisa kumlinganisha na Mwalimu, kwa vile hayuko mtu nchini Tanzania ambaye angeweza kulinganishwa naye, au hata kuwa na haja ya kulinganisha uwezo wa mtu huyo mashuhuri kwa uzalendo wake katika masuala ya Taifa na ya Kimataifa. Lakini hata kama hakuwa mashuhuri Kimataifa kama Mwalimu, lakini Rais Mwinyi vile vile alipungukiwa uwezo wa Mwalimu wa mapambano. Kauli ya Mwalimu ya kumkosoa, kwamba aliisimamia Ikulu kama duka, ilikuwa inamkosoa Mwinyi na Nyerere kadhalika, kama si zaidi, maana Mwalimu alionekana, kwa wale wasiomjua vema kuwa mtu wa kusimamia misingi mwanzo mpaka mwisho, hata pale mara nyingi, ilipomdai afanye kitu tofauti cha manufaa zaidi. Wakati wa utawala wa Rais Mwinyi niliendelea kulitumikia Taifa kwa uwezo wangu wote, katika Mashirika kama kawaida, lakini vile vile katika shughuli za Serikali, na ushauri wa kimya kimya; na wakati huo nilikuwa nakitumikia Chama Tawala vile vile. Baada ya miaka mingi ya kuwashauri viongozi katika masuala ya biashara, nikateuliwa kuwa mjumbe katika Bodi ya Chombo chake cha Biashara, mkono uliowekwa kwa malengo maalum ya kukwepa kutegemea fedha za Serikali kuendeshea shughuli za Chama. Bado nilizoea kukutana na Mwalimu mara kwa mara, nikidumisha utamaduni wetu wa toka zamani wa kuambiana kweli na, naamini, kwa kuaminiana; na nikaendelea kunufaika na busara zake na upeo wake, kama alivyofanya mwenzake aliyeshika nafasi yake. Na,

Page 242: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

242

jinsi Utawala wa Mwinyi ulivyoshamiri, ndivyo uchumi wa Tanzania ulivyoanza kuzinduka pole pole kutoka katika usingizi wake. Lakini Utawala wa Mwinyi utakumbukwa siyo tu kwa sababu ya wakati ule yalipoanza Mapinduzi makubwa ya Uchumi. Maendeleo ya kutosha ya Siasa ndani ya nchi na nje ya mipaka yake yalitumika kuupa mtihani Utawala wake katika namna ambayo isingaliweza kutarajiwa wakati Rais mpya aliposhika madaraka mwaka 1958. Taifa linawiwa deni kubwa na Rais Mwinyi kwa kufanikisha mabadiliko ya Mwelekeo, na kuanzisha mabadiliko katika Taratibu za Uchumi. Mwanzoni yale matukio ya nchi za nje yalionekana zaidi kuwa nafasi mpya kuliko kuwa changamoto mpya, angalau kwa nchi masikini za dunia inayoendelea. Kumalizika kwa Vita Baridi mwishoni mwa mwaka 1980, na Mpango ulioitwa wa Jangwani mwanzoni mwa mwaka 1991, yote mawili hayo yalionekana kuwa dalili za mabadiliko makubwa katika Taratibu za Siasa za Kimataifa. Mazungumzo yote yaliyokuwa yanatoka Washington, na baadaye London, juu ya Taratibu mpya za Dunia, yaliashiria kuelezea kuwa pazia lilikuwa linakaribia kushushwa kuzifungia tabia za zamani za Vita Baridi za kuingilia bila kizuizi mambo ya ndani ya nchi zinazoendelea. Utaratibu huo mpya wa Dunia ulioonekana kama dalili za kurejea kwenye Misingi ya kwanza ya Umoja wa Mataifa, ila tu safari hii zimepata uhai mpya kwa kupewa fedha za kutosha kutoka Umoja wa Mataifa katika shughuli za kimataifa ambazo zingezaa matumaini makubwa, na kuwa nguvu kubwa, kwa nchi kama Tanzania. Tukiwa na Katibu Mkuu Mwafrika, na Mwafrika mwingine anayesimamia shughuli za Usuluhishi, hatimaye yakawako matumaini ya kweli kwamba Usawa na Utawala wa Sheria, wala siyo tena “mwenye maguvu ana haki,” sasa ungekuwa ndio msingi wa kutumika dunia nzima katika kuzuia na kusuluhisha mapambano, na kujenga upya nchi baada ya mapambano. Mwanzoni mipango hiyo mizuri ilitoa matumaini ya kweli kwa Viongozi na Watu wengine wenye kutafakari mambo katika karibu nchi zote zinazoendelea. Mwelekeo wa Kimataifa mintaarafu kuhusu matatizo ya Haiti, na baadaye Bosnia, mwanzoni mwa

Page 243: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

243

miaka ya 1990, ulidhihirisha ridhaa mpya ya Jamii ya Kimataifa lile lililotakiwa kuwalinda wanyonge na kutetea sheria katika sehemu zile za dunia ambazo zamani hazikuwa zinatambuliwa, au ambazo Umoja wa Mataifa haikuwa na shughuli nazo. Kisha vikazuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia mwaka 1992, na, pamoja na vita hivyo, zikawako dalili kwamba Mataifa makubwa, hasa Marekani, bado yalikuwa yanataka kujipatia sifa. Lakini mwaka 1994, baada ya kulipuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda, ndipo mataifa ya Dunia ya Tatu kwa jumla, na hasa Waafrika, walipoanza kutambua kwamba mawazo ya hali ya juu na maarufu mapya ya kusuluhisha magomvi ya wale wanaojiita Mfumo Mpya wa Dunia yanaweza kutumika katika maeneo machache tu, na kwamba vigezo vya kuyateua maeneo hayo vingewekwa kwa lengo la kuwaacha nje. Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda na Burundi, kama vile vilivyozuka katika Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia, vimekuwa vikiwaka na kuzimika kwa muda mrefu zaidi kuliko ambavyo watu walipenda kukumbuka. Serikali za Tanzania, moja baada ya nyingine, kutoka mwaka 1970 na kuendelea, zililazimika kubeba mzigo wa mawimbi ya wakimbizi mara kwa mara kutoka katika sehemu hiyo ya dunia, waliohangaika kwa maelfu katika maeneo ya mpakani; na mara nyingi hawakurudi tena kwao. Lakini vita vile vilivyozuka Rwanda mwaka 1994, kutokana na kuawa kwa Marais wa Rwanda na Burundi, walipokuwa wanarudi Kigali baada ya jitihada nyingine ya kutafuta usuluhishi nchini Tanzania, vilikuwa vya ukatili ambao hakuna mtu aliyewahi kuuona huko nyuma. Rais Mwinyi alilielezea tukio hilo kuwa kama Bosnia nyingine mlangoni kwake; na, kwa sababu nyingi, alikuwa sahihi. Lakini, katika jambo moja kubwa kabisa, hususan uharaka na kiwango cha hatua zilizochukuliwa na Jamii ya Kimataifa kule Rwanda kuzuia kuuwawa kwa raia wa Rwanda waliokosa namna yoyote ya kujitetea, kwanza kwa maelfu na kisha kwa mamia ya maelfu, kulikofanywa na jirani zao na rafiki zao, tofauti kati ya Bosnia na Rwanda ilikuwa kubwa mno.

Page 244: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

244

Nilipokuwa katika Mkutano wa Mkoa kule Kigali, uliohusu kutokomezwa ugonjwa wa polio, Waziri wa Afya wa Rwanda aliniuliza kama nilikwisha fika kwenye ule uwanja wa mauaji. Nilipojibu kuwa sijafika, yeye akanifanyia mpango wa kwenda huko. Gari ya Serikali iliyonipeleka ilipitia kwenye kijiji kilichopewa jina la Mandela. Nilipofika huko nikapewa kitabu cha Wageni na kutakiwa kuandika humo maoni yangu. Kwani niliweza kusema nini? Nikaandika tu, “Naamini Vizazi vilivyopo, na vijavyo, vya Wanyarwanda vitajifunza kutokana na hayo yaliyopo mahali hapa”. Mwaka 1992 kule Bosnia, baada ya kelele za vilio vya mwanzo, Wazungu na Marekani walitoa kiasi cha kutosha cha fedha na watu kuyazima mapigano kabla hayajapoteza maisha ya watu wengi mno. Hawakufanya kitu chochote kama hicho kule Rwanda; cho chote kabisa ila kusema tu! Matokeo yake Waafrika kwa jumla, lakini zaidi Watanzania, wakalazimika kubeba sehemu yo yote waliyoiweza ya mzigo wa Rwanda. Hawakuwa na uwezo wa kuyazima mauaji hayo, badala yake Serikali ya Mwinyi ikafungua mipaka kuwaruhusu Wakimbizi kwa mamia ya maelfu kufurika Tanzania, na wakati huo huo kuongeza jitihada zake katika mazungumzo yaliyokuwa yanafanyika mjini Arusha. Gharama ya fedha na katika Jamii ya kuwahifadhi Wakimbizi waliowekwa wakati ule kwenye mji uliokuwa wa pili kwa ukubwa katika Jamhuri ilikuwa kubwa mno. Hatimaye Jumuiya ya Kimataifa katika sura ya Umoja wa Mataifa, ikajitumbukiza na kuubeba mzigo huo wa mawimbi yasiyoisha wa shida za binadamu waliokuwa wanafurikia Tanzania na kuendelea kutoa fedha na baadaye Majaji wa kushughulikia kesi za mauaji hayo mjini Arusha. Kufikia wakati huo tayari imani kwa Umoja wa Taifa ilikuwa imekwisha potea. Kwa kweli, laiti ungalikuwako Umoja Mpya wa Dunia, na ukawako wakati huo huo ushahidi mdogo wa kuthibitisha dhana hiyo, basi lingekuwa suala la kurudia vitendo vya ubeberu wa zamani wa kuthamini maisha ya Wazungu zaidi kuliko yale ya Waafrika. Funzo hilo lingeendelea mpaka kuathiri mazungumzo yote yatakayofuata ambayo Serikali ya Mwinyi na ya Rais mwingine

Page 245: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

245

atakayekuja baada yake, pamoja na Mwalumu mwenyewe, wangefanya iwe katika maeneo ya Maziwa makuu, au hata kama ni Burundi. Msaada uliokuwa unatolewa ulikuwa mdogo mho, tena katika maeneo ya pembezoni tu. Wakati hali hiyo ya kukata tamaa ilipokuwa bado inachambuliwa, Serikali ya Mwinyi ilikuwa imechacharika kuandaa Uchaguzi Mkuu wa Kwanza wa Vyama Vingi baada ya Uhuru. Huko nyuma, mwaka 1992, Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Msanifu Mkuu wa Mabadiliko kutoka kwenye Mfumo wa Chama Kimoja, lakini Serikali ya Rais Mwinyi ndiyo iliyoandaa Uchaguzi huo nchi nzima mwaka 1995. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Chama Tawala kikalazimika kunadi Sera zake nchini kote na kuvibwaga Vyama vya Upinzani vilivyokuwa vinatafuta kutambuliwa na Umma. Bado Vyama vya Upinzani nchini Tanzania vikawa vinadai kwamba Uamuzi wa CCM wa mwaka 1992 kuachana na Utawala wa Chama Kimoja ulikuwa ni zoezi la kejeli tu. Nasikitika kusema kwamba sijauona bado usahihi wa Hoja hiyo. Hoja zinazolenga kuwashawishi watu kubadili msimamo zinapaswa kuwa wazi zaidi. Hebu itisha Uchaguzi mwingine wa Chama Kimoja, kama zilivyokuwa Taratibu za huko nyuma. Lakini badala ya kushikilia Taratibu zile za zamani, CCM ikawa na ujasiri wa kuanzisha Utaratibu mpya ulioleta sura mpya ya kisiasa, Kaskazini na Kusini; mwelekeo ambao, kutokea wakati huo, umefungua mlango kwa siku zijazo kwa Chama cha Upinzani kushinda katika Uchaguzi wa Zanzibar. Katika uzoefu wangu, hakuna mlaghai anayeweza kuwa na moyo wa kujitosa kiasi hicho. Kwa lolote lile ambalo Wapinzani watalisema, dhahiri uamuzi wa kufanya Uchaguzi wa Vyama Vingi nchini Tanzania mwaka 1995 ulianzisha vuguvugu jipya la kisiasa nchini. Lakini fikira hizo zikavizwa na mashindano yasiyotabirika kuhusu uteuzi wa Mgombea wa CCM wa Kiti cha Rais. Baada ya kuishika nafasi hiyo kwa vipindi viwili kamili, Rais Mwinyi hakuruhusiwa kugombea tena. Lakini kutoweka kwa jina la Mwinyi katika Orodha hiyo hakukupunguza idadi ya Wagombea. Kama

Page 246: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

246

ilivyokuwa mwaka 1985, kiasi cha majina kumi na mawili yalikuwa yananadiwa kushindania nafasi hiyo ya ngazi ya juu kabisa. Kabla ya uamuzi wa Mkutano wa CCM wa Uteuzi, kwa mara nyingine Mwalimu akadhihirisha siyo tu azma yake ya kusimamia misingi, bali vile vile uwezo wake wa kutoa uamuzi mzuri papo kwa papo. Kutokana na idadi kubwa ya Wanasiasa waliobobea akataka ijulikane kuwa yeye alikuwa anampendekeza mmoja kati ya wale wasiotajwatajwa sana. Aliyasema hayo baada ya kueleza mashaka yake makubwa kabla ya hapo juu ya usafi wa Wagombea waliokuwa wananadiwa na Magazeti. Viongozi waaminifu wa Chama na Waandishi wa Magazeti wakashituka; lakini, kama kawaida yake, misingi ya Taarifa hiyo ya Mwalimu ilikuwa mizito. Hatimaye chaguo la Mwalimu, Mgombea wa CCM ambaye baada ya muda mfupi atakuwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuwa mwingine ila rafiki yangu wa zamani Benjamin William Mkapa. Inawezekana hakuwa anajulikana sana wakati huo na Watanzania wengi, lakini mimi sikuwa na sababu ya kumshangaa wala kumtilia mashaka. Kutokea siku ile ya Uteuzi wake, kama vile vile ilivyokuwa alipoteuliwa kuendesha Gazeti la Tanganyika Standard miaka mingi nyuma, nilitambua kuwa Ben Mkapa ndiye aliyekuwa anafaa kwa kazi hiyo nchini Tanzania, na katika muda muafaka. Mwaka 2005 CCM, kwa mara ya kwanza, ikawa inamtafuta Mgombea wa Kiti cha Rais bila Mwalimu kuwapo. Walikuwako Wagombea kumi na mmoja, miongoni mwao Mabalozi wawili waliokuwa madarakani. Rais Mkapa, akiwa Mwenyekiti wa Chama, ndiye aliyekiongoza Kikao, na Chama kikamteua Jakaya Mrisho Kikwete, wakati huo akiwa na umri wa miaka 54, na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje toka mwaka 1995. Kutokana na uwezo wake wa kuwachangamkia Vijana, yeye akaonekana kuwa Mgombea anayefaa sana katika karne hii ya ishirini na moja. Mwisho wa Kipindi cha Mwinyi kilizuka kizingiti binafsi katika maisha yetu sisi wenyewe familia. Mnamo miaka ya 1980, na mwanzoni mwa miaka ya 1990, vijana wetu watatu wakawa watu wazima kwa kila kigezo. Kila mmoja akawa amepata mafanikio

Page 247: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

247

katika fani yake, na pengine mafanikio ya kujivunia. Baada ya kufuzu katika fani ya Uhasibu katikati ya miaka ya 1970, Manish akapanda ngazi kuwa Mhasibu wa sifa katika Kampuni kubwa ya Uhasibu kabla ya kuteuliwa Mkurugenzi wa Fedha na Mtendaji Mkuu wa Kampuni iliyoitwa Imry PLC, akielekeza jikuzi ya haraka (pamoja na kuanzisha Minada ya Hisa ya Miradi ya Kampuni hii) Baadaye akawa Mtendaji Mkuu wa Kampuni kubwa kuliko zote za Ulaya, Landmark Securities, na kisha akarejea kwenye kuendeleza biashara zake mwenyewe. Sasa hivi yeye ni Mwenyekiti wa NCP, Kampuni kubwa kuliko zote Ulaya nzima ya kuegesha magari. Akiwa Mjumbe wa Tume ya Mirathi ya Uingereza, Manish anapenda sana kujihusisha na Huduma za Jamii. Ametumbukia kabisa katika Chama cha Taifa cha Kuzuia Ukatili wa Watoto, na ni Mdhamini wa Mfuko unaoitwa Windser Leadership Trust, ulioundwa kwa madhumuni ya kawatia moyo watu kutumika katika shughuli za Jamii. Anuj, kama kaka yake, naye amehitimu katika fani ya Uhasibu; alifanya kazi katika Kampuni ya Uingereza ya Albright and Wilson, na pia katika Kampuni ya Marekani ya NCR Corporation kabla ya kuwa Mwanahisa mdogo kuliko wote katika Kampuni ya Grant Thornton. Amepata nishani ya Ufanisi Mkubwa ya Lloyd TSB, na ni Mjumbe wa Bodi ya SME ya Chama cha Taifa cha Waajiri, na vile vile ni Mwanachama wa Umoja wa Waajiri wa London. Ni Mshauri katika Mfuko wa Misaada wa Prince Trust, anayejishughulisha na mambo mengi ya misaada. Rupen, mwana wetu wa mwisho, alipata Shahada yake ya Pili ya Masomo ya Biashara kutoka Chuo Kikuu cha London, na Shahada ya MBA kutoka Chuo Kikuu cha Santiago, California. Lakini yeye hafanani na ndugu zake, maana aliamua kwenda kufanya kazi katika sehemu ambazo zisingeweza kumpatia faida, akihudumia Kampeni za Kimataifa za UNA na CARE, kabla hajaanzisha Ofisi ya Mfuko wa Agakhan, mjini Dar es Salaam, yeye akiwa Mtendaji Mkuu wa kwanza. Hivi sasa yeye ndiye Mkurugenzi wa Kituo cha Kujenga Utaalam; Chuo cha Maendeleo ya Elimu, Mashariki ya Afrika; na vile vile Chuo Kikuu cha Agakhan. Ni mwalimu mzuri, lakini vile vile Rupen ana silika ya kuhudumia Jamii.

Page 248: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

248

Lakini pamoja na kuongezeka huko kwa familia, bado Rupen hajaoa, ingawa hana upungufu wa marafiki wa kike. Manish, kaka yake mkubwa, alikutana na kupendana na Lucy Dickens, mwanafunzi mwenzake wa Charterhouse, ambaye ni mjukuu wa mwandishi aliyesifika sana kipindi cha Malkia Victoria; na wanao watoto wawili: binti Lonika, ambaye sasa hivi ana umri wa miaka kumi na minane, na mwanafunzi wa Charterhouse; wa pili kijana wa kiume Josha, mwenye umri wa miaka kumi na sita, anasoma Highgate. Walitalikiana mwaka uliopita; lakini kila tukifika London tunakutana na Lucy, Mhariri wa zamani wa Mitindo na Uzuri katika gazeti la Brides Magazine, Lucy amebahatika kuwa mwandishi na mchoraji mzuri wa fani zote. Kazi zake alizozionyesha zimeshangiliwa na wengi katika maonyesho ya London. Anuj, mwana wetu wa kati, alimwoa Nishma, msichana aliyekutana naye baada ya kutambulishwa na rafiki zake wa London. Amezaliwa Mombasa, Kenya; yeye ni Msanii wa kupamba kumbi. Fani yake ni pamoja na kutengeneza skafu zilizotiwa rangi kwa mikono. Wakati mwingine Nishma hutumia Studio za Lucy kwa kazi zake. Wanaye binti mmoja aitwaye Polomi, sasa ana umri wa miaka kumi na minne. Wajukuu wetu wote wamebarikiwa kwa kuwa na akili nyingi na wazuri wa sura, hali inayomfurahisha sana babu kuielezea; na, kama baba zao, mara nyingi wanadhihirisha tabia za zamani za familia zao. Bila ya kumbagua yeyote kati yao, maana kila mmoja ana kipaji chake mwenyewe, ninachukua nafasi ya kuutaja mfano mmoja. Alipokuwa na umri wa miaka sita tu, nilimpeleka mtoto Josha kwenye duka la vitu vya kuchezea watoto. Hamley’s Toy Department Store, mjini London. Kabla hatujaingia, Josha akanisimamisha; akaniangalia na kusema, “Babuji, kabla sijaanza kuchagua, nataka kujua kiwango cha matumizi yangu kitakuwa shilingi ngapi.” Hapa anasema Chande wa kweli.

________________

Page 249: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

249

KUMI NA TATU

URAIS WA MKAPA Wakati Rais Mkapa alipoapishwa kuwa Rais wa Tatu wa Jamhri ya Muungano mwaka 1995, mimi nilikuwa na umri wa miaka sitini na saba, au tuseme sitini na sita, kulingana na taarifa zilizopo kwenye Ofisi ya kumbukumbu, Mombasa. Bado nilikuwa na matamanio ya mtu wa nusu ya umri wangu, kwa namna yoyote ile utakayoifikiria. Lakini wakati mwingine mwili wangu ulinikatalia, baada ya kusumbuliwa sana katika kipindi cha miaka arobaini na mitano iliyopita. Pamoja na uzee niliokuwa nao, au nilioufikiria, bado nilikuwa na jukumu kubwa la kutekeleza katika masuala ya uchumi wan chi. Lakini, kwanza, kabisa, matatizo yaliyokuwa yanamkabili Rais aliyekuwa anaingia yalikuwa ya kisiasa zaidi. Si kwamba tu hakuwa anachangamkiwa, wala kwamba hakuwa na uwezo wa kuwadhibiti Wanachama wa Chama Tawala kama ile waliokuwa nao Wagombea wenzake wa nafasi hiyo; wala hakuwa na kauli iliyolingana na ya Mwenyekiti wa Chama Tawala, ambaye bado alikuwa nayo Rais wa zamani. Lakini kuingia kwa Vyama Vingi kukaviletea Vyama vya Upinzani tatizo kubwa. Benjamin Mkapa alishinda vizuri katika Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, alipojinyakulia asilimia 61 ya kura, kulinganisha na asilimia 27 tu alizopata Mshindani wake Mkuu, Augustine Mrema. Lakini kule Zanzibar Rais aliyekuwako Salmin Amour alibanwa kwa karibu sana na Mgombea wa CUF, Seif Sharif Hamad: karibu mno kiasi cha kumkosesha pumzi ya kisiasa. Kiwango hicho kidogo cha ushindi wa Rais Amour, wa chini ya asilimia moja, kiliashiria mwanzo wa misukosuko ya kisiasa iliyotumia muda mwingi wa kipindi chote cha miaka kumi ya utawala wa Rais Mkapa. Ushindi finyu katika matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, na ucheleweshwaji wa siku tatu katika kumtangaza mshindi baada ya nong’ono za mwanzo kuwa Hamad alikuwa ameshinda; na tofauti ya kura kati ya visiwa

Page 250: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

250

vikubwa viwili vya Zanzibar, CUF wakiongoza Pemba na CCM wakiongoza Unguja; kasoro zote hizo zikamfanya Rais wa Jamhuri ya Muungano atambue ugumu wa mchakato wa Siasa aliolazimika kukumbana nao. Wakati huo nikatambua, na bado najua mpaka sasa kutokana na uzoefu wangu binafsi nilioupata hata kabla ya Mapinduzi ya 1964, mlipuko unaoweza kutokea katika Jamii hizi za Zanzibar zenye mahusiano makubwa, endapo kisa chochote kitapatikana. Kutokana na Visiwa hivyo kuawanyika toka wakati ule wa Uchaguzi wa 1995, kama vilivyogawanyika katika mila tangu karne nyingi zilizopita, inadhihirika wazi wazi hoja ya Uzalendo na Utaifa kwa Rais anayeingia. Huko nyuma, mwaka 1985, Rais Mwinyi alikabidhiwa kazi ngumu ya kuanzisha Taratibu za kuleta mabadiliko ya kujenga upya Uchumi na, lazima tumsifie, akafanya hivyo. Lakini kwa kuwa Jamii ya Kimataifa ilikuwa bado inatoa misaada ya maendeleo katika namna ambayo hata haikukaribia kuonekana, na wakati huo huo Uchumi wa Tanzania ukilazimika kujisukuma utoke katika dimbwi ulimokuwa umetumbukia kwa muda mrefu; nafasi ya kurekebisha hali hiyo haraka haraka katika Kipindi hicho cha Rais Mwinyi ilikuwa ndogo mno, au pengine haikuwako kabisa. Kutokana na takwimu za Relwe na Bandari, nilijua kwamba thamani ya uzalishaji mali na ya mauzo ya bidhaa katika nchi za nje kwa muda wote kati ya mwisho wa miaka ya 1980 ya mwanzo wa miaka ya 1990, hasa katika kilimo, ilikuwa ndogo mno. Katika kipindi kile nchi jirani, kama Msumbiji, ilikwisha anza kuvutia kiasi kikubwa cha uwekezaji kutoka nchi za nje. Nyingine, kama Kenya, zilikuwa zimeanza kutumia mawasiliano yao ya kimataifa kutumbukia katika Soko la Kimataifa lililokuwa linashamiri la mboga na maua ya Afrika. Vile vile, kule Uganda, ilidhihirika kuwa, kutokana na mafanikio ya biashara za familia ya mke wangu, uchumi kule ulikuwa unaneemeka kwa kiwango kizuri. Lakini wakati huo huo Uchumi wa Tanzania ukawa unadorora huko chini. Vitu vikawa ghali mno, labda kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi yetu, na kuagiza kutoka nchi za nje bidhaa

Page 251: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

251

nyingi mno. Kukua kwa uchumi kukawa kudogo, ingawa tulianza kwenye kiwango kizuri; na kwa hakika kilikuwa kidogo mno kiasi kwamba isingewezekana kusambaza matunda yake kwa jamii zote za Tanzania. Akiba yetu katika Benki Kuu ikawa ndogo mno; na mafanikio ya shughuli za uzalishaji wa kilimo zilizoanzishwa zikavizwa kwa kukosekana kwa mtandao mzuri wa barabara kwenda kwenye vituo vya reli na kwenye miji. Maana yake kasoro hizo ni kwamba siyo tu kiwango cha faida ya mazao yote tuliyoyauza nje kilipungua sana, kwa sababu ya gharama za uzalishaji na uharibifu wa kawaida; lakini wazalishaji wa Tanzania, tofauti na wale wa, tuseme, Kenya, hawakuwa na uwezo wa kuthibitisha kwamba mazao yao yangefika mahali Fulani katika tarehe Fulani, kwa sababu ya misukosuko hiyo ya safari ndefu katika barabara za Vijiji zisizokuwa na lami. Dhahiri kipingamizi hiki cha mwisho cha kasoro katika usafiri wa barabara kitahitaji kushughulikiwa mapema na uongozi wa ngazi ya juu. Kwa hakika Rais Mkapa aliyajua masuala hayo, na akayapa umuhimu katika mawasiliano yake na Wafadhili wa Kimataifa, hasa wale wa Umoja wa Ulaya. Lakini alitambua vile vile kuwa lengo lake la uchumi katika kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano kilipaswa kuwa utengamano katika uchumi kwa jumla. Hakikuwako hata kigezo kimoja cha uchumi kilichodhihirisha kwamba mambo yalikuwa yanakwenda kama ilivyokuwa inatakiwa. Ilikuwa hapana budi kufanya hivyo, tena kwa haraka, kama alitaka kuwashawishi Wawekezaji wa Mataifa yaliyokuwa yanatoa misaada kuwa kila dola moja iliyotumika Tanzania ingeweza kuzaa matunda yaliyokuwa yanatarajiwa. Nijuavyo mimi Rais Mkapa ni mmoja kati ya Viongozi wawili tu wa Kitaifa waliokubali kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara nchini Tanzania. Aliongoza Mkutano wa Sita wa Wawekezaji wa Kimataifa; na kufuatia, yeye mwenyewe, kwa karibu sana, matokeo ya Maamuzi yao. Na pale ambapo, katika Mkutano mmoja kama huo, Wawekezaji walizingatia uswahiba wa Benki ya Dunia katika masuala ya uwekezaji, Rais James Wolfensohn alitamka kwamba kumpata mtu kama Mkapa kuwa Mkuu wa Nchi ni zawadi ya ziada kwa Wawekezaji.

Page 252: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

252

Katika kipindi hicho mimi nilikuwa Paris kwa kazi zangu kama Mwenyekiti wa Shirika la Reli la Tanzania. Usiku wa kwanza wa mkusanyiko huo wa Kimataifa wa wafanyakazi wa reli ilifanyika dhifa rasmi ambapo Kamishna wa Umoja wa Ulaya, na Kiongozi wa zamani wa Chama cha Leba, Neil Kinnock, alitoa hotuba ya msingi. Sasa hivi mwanangu, Manish, anayekiunga mkono Chama cha Mabepari, yuko tayari kuivuta bahari kuukwepa mgongano kama huo. Nilipangwa kufikia kwenye Hoteli ya Hilton, si mbali kutoka Ofisi ya Umoja wa Kimataifa wa Wafanyakazi wa Reli. Nilipokuwa bafuni, naoga, simu ikalia chumbani kwangu. Wakati huo Jayli alikuwa HongKong na, nikiamini kuwa yeye ndiye aliyekuwa anapiga, nikakimbia haraka kupokea. Niliposikiliza nikakatishwa tamaa kusikia kuwa, kumbe ni Karani wa Simu aliyetaka kuniambia kuwa gari la kunipeleka kwenye dhifa ya jioni ile lilikuwa limekwishafika. Nilipokuwa narudi bafuni nikatereza na kuanguka kwenye dimbwi la maji yaliyokuwa yanatiririka nilipokuwa nikioga. Ingawa niliumia, lakini niliweza kujikokota mpaka kuifikia simu na kumweleza Karani wa simu hayo yaliyonikuta. Dakika kumi baadaye, Daktari aliyekuwa anajua Kiingereza akawa amekwishafika chumbani kwangu, na kuniambia kuwa, pengine, ubavu mmoja ulikuwa umevunjika. Akaniuliza kama nilitaka kwenda kwenye hospitali ya Kiingereza ama ya Kimarekani. Nikiwa bado na maumivu, nikanong’ona, “Hospitali iliyo karibu kupita zote.” Nikapelekwa kwenye Hospitali ya Kiingereza, ambako daktari mwanamke alinitibu. Vipimo vya X-ray vikaonyesha kuwa ubavu wangu wa chini ulikua umepata ufa, na hivyo ikawa sababu ya kuikosa ile dhifa, na ya kuchelewa kurudi London. Baadaye, bila shaka kutokana na wasiwasi wa mwanangu wa kwanza, nikasikia kuwa Bwana Kinnock mwenyewe alitoa hotuba nzuri sana kuhusu hatima ya shughuli za usafirishaji duniani.

Page 253: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

253

Ni suala moja kutambua haja ya kuwa na mabadiliko katika masuala ya uchumi wa jumla; lakini ni suala lingine kabisa kuitekeleza dhana hiyo. Hata katika Nchi za Magharibi, ambako raia wa kawaida, kwa kulinganisha, anajua tofauti kubwa iliyoko kati ya starehe na ufukara, na ambako Dola inatoa msaada kwa ajili ya huduma zote, pamoja na usafiri, Sera zozote za Serikali zinazoelekea kupunguza matumizi ya Serikali, na wakati huo huo kupandisha kodi, lazima zitapambana na kelele za kupinga. Katika uchumi kama ule wa Tanzania wa mwaka 1995, ambapo watu walio wengi walikuwa wanaishi katika hali ya umasikini wa kutupa, na ambapo Utumishi Serikalini ulipojaza zaidi ya kiwango nafasi chache zilizojulikana kusaidia familia kubwa kubwa, sera hizo mpya zilikuwa kama mchezo mkubwa wa kamari ulioleta machungu. Lakini kama, hatimaye, mafanikio yangeonekana, basi Tanzania ingejenga uchumi wenye mwelekeo wa kuinukia. Lakini je, Watanzania walio wengi wangalikuwa radhi, au na uwezo, wa kuisubiri hiyo neema itakayoibuka? Hilo basi ndilo tatizo lililokuwa linamkabili Rais Mkapa. Kwa kweli hakulikwepa, badala yake akatambua kwamba usingekuwako mgogoro wowote. Hakuwa na la kufanya ila kuanzisha Mpango mkubwa wa marekebisho ya uchumi, bila kujali wananchi wangesema nini; bila ya hivyo Uchumi wa Tanzania ungedidimia. Katika miaka mitano iliyofuata Mpango wake wa kurekebisha Uchui ukaanza kudhihirika. Idadi ya Watumishi wa Serikali ikaanza kupunguzwa; katika Wizara nyingine wakapunguzwa sana. Taratibu zikaanzishwa, sambamba na hatua za kisheria kuweka wazi namna ya kununua vifaa, ili kuzuia uharibifu na udanganyifu. Hatua kama zizo hizo zikaanzishwa katika masuala ya Mikopo ya Serikali, na Kanuni zikaimarishwa za namna ya watumia fedha za Serikali, na zikazingatiwa. Mapato ya kodi walizokuwa wanalipa Wafanyabiashara na watu wengine ambayo yalikuwa madogo mno kulinganisha na yale ya nchi nyingine, yakaanza kupanda. Fedha nyingi sana zilizokuwa zimeelekezwa kwenye uchimbaji wa madini ya dhahabu zikarejeshwa kwenye uchumi kwa njia ya misaada, Rais akitetea, kwa kiwango cha kuridhisha, kwamba kwa njia hiyo tu rasilimali za nchi zingeweza kuendelezwa.

Page 254: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

254

Hatua zikachukuliwa kuzirejesha kwa wenyewe zile shughuli za uchumi zilizokuwa zimetaifishwa, ambazo wananchi wenyewe wangestahili kuzihangaikia kikamilifu, kama vile mawasiliano ya simu. Na Mpango wa kuzuia rushwa, ukaanzishwa uliokuwa na Ofisi zake zilizoenea nchi nzima. Kwa kukaa kwangu kama Mjumbe wa Vyama vya Biashara na katika Mashirika, niliweza kubaini kuwa mipango hiyo haikuwa inapokelewa kwa shangwe bali kwa shingo upande. Miaka karibu arobaini ya uchumi uliokuwa unalegalega, na baada ya hapo miaka mingine sabini ya unyonyaji wa uchumi uliokuwa unafanywa na Wakoloni waliokuwa hawajali, ikafanya Jamii ya Wawekezaji kuwa na wasiwasi mkubwa sana katika kuzingatia Mpango wa Mkapa. Mzigo kwa binadamu wa mwelekeo huo wa uchumi uliweza kueleweka kwa urahisi, lakini bado hakuwako mtu aliyekuwa tayari kuelezea manufaa yatakayopatikana. Nilikuwa na nafasi nyingine ya manufaa wakatu ule, katika ngazi ya kimataifa, iliyoniwezesha kuuchambua uchumi wa dunia nzima, na kubaini jinsi watu wengine waliokuwa na madaraka nchini Tanzania walivyokuwa wanaendelea. Mwaka 1995 nilikaribishwa na Rais wa zamani, Gorbachev kushiriki katika “Mjadala wa Hali ya Dunia,” ulioitishwa na Mfuko wa Gorbachev ulioundwa Marekani kwa ajili ya kuchambua matokeo ya misukosuko ya kipindi kile cha Vita Baridi. Kwa kuwa Mfuko huo ulikuwa Marekani, sehemu kubwa ya mjadala ikawa juu ya matokeo ya dunia ya upande mmoja kwa Marekani, Umoja wa Mataifa na dunia nzima kwa jumla. Lakini katikati ya mazungumzo hayo, na pia kule San Francisco mwaka 1997, katika Mkutano wa Kimataifa wa Viwanda uliogharimiwa kama kawaida na Chuo cha Utafiti cha Stanford, Menlo Park, California, wakishirikiana na Baraza la Mikutano la New York, mimi nikiwa mwanachama wa Bodi zote mbili hizo, na vile vile Mjumbe wa Baraza la Kimataifa kwa zaidi ya miaka ishirini, niliweza kupata picha ya mazingira ya kimataifa yalivyokuwa yanazibadilikia nchi zinazoendelea.

Page 255: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

255

Kutokana na kuhadaika kunakotokana na jitihada za Umoja wa Mataifa kulinda sehemu za dunia zilizokuwa na matatizo, hasa kwa sababu kushindwa kwa nchi kubwa kubwa kutimiza majukumu yao, majadiliano yaliyofanywa baada ya vile Vita Baridi, ndani na nje ya Serikali, yalikuwa tayari yanabadili mwelekeo wake. Mabingwa waliokuwa ndani ya Mabaraza ya Kimataifa, katika Serikali za nchi muhimu na Makampuni makubwa ya Kimataifa walikuwa wanazidi kuamini kwamba kukua kwa uchumi ndiyo njia iliyokuwa inaaminika zaidi ya kuepuka mapigano kuliko vizingiti au jeshi lolote ambalo Umoja wa Mataifa unaweza kuliweka. Hali kadhalika, walikuwa wameanza kuamini kuwa, angalau hatimaye, Soko la Dunia lilikuwa linajengwa, kutokana na kufunguliwa kwa bidhaa kutoka China na India, zinazozalishwa kwa wingi, kwa gharama ndogo, na zenye ubora unaoendelea kuwa wa hali ya juu siku hadi siku. Furaha hii inayozidi kuongezeka kutokana na matumaini ya mafanikio hayo, ambayo haraka haraka yakabatizwa jina la Uchumi wa Dunia, haikuzifikia nchi kama Tanzania. Kwa mara nyingine, kutoka mahali paliponifaa nje ya Nchi, nikaweza kuona kuwa Mapinduzi yaliyokuwa yanatekelezwa na Rais Mkapa yataipa Tanzania nafasi nzuri kabisa inayoweza kupatikana ya kuutumia huu mwelekeo wa Soko la Dunia. Wengine walio ndani ya Nchi bado hawajavutika kutokana na kuzama katika mwelekeo wa Sera za Wakati ule za Ujamaa. Kama ambavyo walitaka wakati ule kuudhibiti Uchumi kutoka katika Ofisi za Serikali, wanataka kufanya vivyo hivyo sasa hivi kwa kutumia nguvu za uchumi za dunia, na kwa njia Fulani kuziweka nguvu hizo nje ya mipaka ya Tanzania. Kwa bahati nzuri Rais Mkapa alikuwa mtu mwenye upeo mpana. Alitambua kwamba Soko la Dunia si uwanja ambao mtu angeweza kuchagua kuutumbukia au kuukwepa. Ni tatizo lililopaswa kushughulikiwa, na majibu yake kuandaliwa. Vile vile alikuwa mtu mwenye moyo mkubwa wa kuthubutu. Si mtu anayejipendekeza katika kutafuta umaarufu wake binafsi katika kipindi chake chote cha Uongozi wa Siasa hakuwahi kutumia mbinu za ulaghai:

Page 256: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

256

akakazania sana kuondoa malalamiko Nchini, akaendelea mpaka akaufufua uchumi na kujenga upya Mfuko wa Taifa. Na baada ya muda matunda yakaanza kuonekana: Mfumuko wa Bei ukashuka kutoka mamia mpaka makumi, na kisha ukaporomoka kufikia chini ya asilimia tano. Kukua kwa Uchumi kukapanda kwa kiasi cha asilimia tano. Akiba za Benki Kuu zikapanda kufikia kiwango cha kuridhisha, Mapato ya Serikali na Mikopo kwa Umma hayakushughulikiwa tena kwa Taratibu za zamani za maamuzi zilizokuwa hazielezeki. Na uwezekano sasa wa kuwa na Uchumi uliounganika wa Kanda ukajitokeza tena baada ya kipindi cha miaka ishirini, pamoja na mawazo ya kuirejesha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Matokeo ya haraka ya mafanikio hayo yakawa ya kimataifa zaidi kuliko ya hapa nyumbani. Kutokana na mawasiliano yangu na Serikali za nchi za nje na uwekezaji wao nikatambua kwamba mabadiliko yanayofanyika sasa yataonekana kuwa ya maana kubwa. Takwimu mpya za uchumi zimepatikana wakati muafaka ambapo jamii za wale wanaotusaidia zinatafakari upya ufanisi wa taratibu zao za zamani za kutoa misaada ya Kimataifa, na mafanikio ya Mkapa katika masuala ya uchumi wa jumla utaifanya Tanzania kuwa mbele ya nchi nyingine nyingi zinazopata misaada katika kufikiriwa kupata misaada mipya. Kwa mafanikio hayo Taratibu hizo mpya za kufikisha misaada katika mafungu yanayounganishwa katika ratiba ya miaka mingi na yanayopelekwa moja kwa moja kwa Mhasibu anayehusika, sasa yataongezwa nchini Tanzania. Umuhimu wa badiliko hilo, wakati ambapo mafungu yaliyozoeleka kwa nchi kama Kenya yanaanza kutoweka hauwezi kupuuzwa. Kwa mara ya kwanza kabisa Serikali ya Tanzania imeweza kuunganisha sehemu kubwa ya misaada inayotoka nje ndani ya Bajeti yake ya Taifa. Katika sura hiyo ya kutabirika, na misaada inayoletwa mapema katika fedha taslimu, na siyo katika ahadi zisizothibitika, au misaada mingine badala yake, ufanisi wa misaada kama hiyo utadhihirika haraka. Kutokana na mabadiliko hayo makubwa ya uchumi yaliyoletwa na Rais, taratibu za zamani za kutukuza ubinafsi kama ndiyo kigezo

Page 257: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

257

kikubwa cha kuingiza misaada nchini Tanzania hatimaye zikawa zimekomeshwa. Lakini ilikuwako kasoro ya wazi katika mambo yote haya. Dhahiri kujifunga mkanda kwa Serikali ya Tanzania kuliwaletea shida hizo hizo Wananchi wa Tanzania, walioona kwamba mikanda yao ilikuwa inawabana mno. Pengine Mpango wa Mkapa ungaliweza hatimaye kuvielekeza vigezo vya uchumi kwenye ufanisi, uliotakiwa, lakini bado vigezo vyote vya ustawi vikawa vimeganda pale pale; wakati mwingine huduma kama za afya au upatikanaji wa nafasi katika Shule za Msingi zikiwa zimedidimia zaidi. Kutokana na kuzungumza kwangu mara nyingi na Rais, najua kwamba na yeye kasoro hii inamuuma. Lakini, ingawa ilimuudhi kujua kuwa watu wa Tanzania walikuwa wanaendelea kuteseka, alikuwa na uwezo mdogo sana au tuseme hakuwa nao kabisa, wa kuyashughulikia matatizo yao mpaka atakapofanikiwa kuziweka sawa Kanuni za Fedha za Serikali. Kusema hivyo maana yake siyo kwamba hakuwa na mipango ya baadaye; huko nyuma, mwaka 1966, alikwisha weka misingi ya mabadiliko ya hali ya maisha, kwa lengo la kutafuta ustawi wa Taifa zima. Nililitambua hilo kutokana na kuongezeka kwa kushiriki kwangu katika sekta ya Afya nchini Tanzania. Wakati wote nimejihusisha na Huduma za Jamii nchini. Jitihada zangu katika kuanzisha Shule ya Viziwi, na kuendelea kwangu kushiriki kwa kiwango cha juu katika Halmashauri za Wananchi kwa ajili ya Mipango ya Fedha, Elimu ya Sekondari na ya biashara, mengi katika hayo kuanzia katikati ya miaka ya 1960 na kuendelea, yanadhihirisha ari yangu kubwa katika kuboresha Taratibu za Elimu katika ngazi zote na kwa Watanzania wote. Lakini kadiri miaka ile ya 1990 ilivyokuwa inakwenda nikaanza kushika madaraka makubwa katika Sekta ya Afya nchini: nikawa Mdhamini wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha Kimataifa cha Uganda na Teknolojia cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Chama cha Tanzania cha Wagonjwa wa Moyo; Chama cha Wauguzi wa Tanzania waliosajiliwa, Chama cha Tanzania cha Viziwi, na Chama cha Tanzania cha Wagonjwa wa Akili na Kupooza. Nimekuwa na uhusiano wa muda mrefu na baadhi ya

Page 258: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

258

Vyama hivi., Ukiacha uhusiano wangu na Shule ya Viziwi ya Buguruni, mimi nilikuwa mshiriki mkuu, kupitia Vyama vya Mason na Rotary. Katika kuanzisha Mpango wa Wauguzi wa Wilaya Tanzania. Lakini kuongezeka ghafla kwa majukumu yangu mengine katikati ya miaka ya 1990, na yanayoongezeka mpaka leo, kunadhihirisha hoja ya kuimarisha Sekta ya Afya ya Jamii iliyokuwa imezidiwa kazi., na ambayo haikuwa imeendelea sana kwa kukosa msaada wowote ambao ningeweza kuutoa. Siwezi kukataa kuwa sehemu hii ya kazi ilikuwa ngumu kuliko nyingine yoyote niliyopata kuifanya. Matatizo yaliyokuwako kwenye Hospitali ya Mifupa ya Muhimbili, ambayo mimi ni Mwenyekiti wake yakawa, na yakaendelea kuwa, na ugumu wa aina yake; na mara nyingi nimekata tamaa kwa kushindwa kutoa jibu rahisi kwa tatizo lolote lile lililojitokeza. Lakini vile vile sijapata kuyakwepa. Katika miaka yangu yote ya kazi ni mara moja tu nilipojiuzulu kutoka katika Sirika. Ka kweli sikuwa tayari kuiterekeza ile Sekta ya Afya wakati ilipokuwa inahitaji msaada wowote ambao ningeweza kutafuta. Kufikia mwishoni mwa miaka ya l990, Sekta ya Afya ikaanza kuwa chimbuko kubwa zaidi la shughuli za Serikali zilizokuwa zimeongezeka. Hatimaye Rais, akihangaika bega kwa bega na Jamii za humu nchini, zilizokuwa na mifuko ya fedha ka ajili ya Sekta maalum, akaweza kuelekeza mawazo yake katika kushughulikia zile kasoro kubwa katika kutoa huduma za Jamii nchini Tanzania. Lakini wakati kazi hii muhimu ilipokuwa inaanza kushamiri, manung’uniko ya kisiasa kule Zanzibar nayo yakawa yanaongezeka. Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa mwaka 2000 ukamrudisha kitini Rais Mkapa kwa ongezeko kubwa la kura, akimwangusha Mpinzani wake Mkuu, Profesa Lipumba wa CUF. Lakini kule Zanzibar matatizo yaliyojitokeza katika Uchaguzi wa 1995 yakajitokeza tena. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola wa wakati huo, Chifu Anyouku, alitumia sehemu kubwa ya

Page 259: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

259

mwisho wa miaka ya 1990 akitafuta suluhu kati ya CCM na CUF kula Zanzibar, na alikuwa karibu sana afanikiwe. Lakini hatimaye jitihada hizo ziliposhindikana katika kipindi kilichokuwa kinakaribia Kampeni za Uchaguzi wa mwaka 2000, uwanja ulikuwa tayari umewekwa kwa jaribio lingine la kupima nani zaidi kati ya CCM na CUF, ila safari hii Wapinzani wakawa wamejawa na uchungu mwingi. Mwaka 2000 CCM wakashinda katika Uchaguzi wa Rais kule Zanzibar, na Amani Abeid Karume, mwana wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, akakikalia Kiti wakati Wapinzani walipozua malalamiko ya udanganyifu. Mimi niliwahi kufanya kazi na Karume katika Bodi ya Shirika la Reli na Bandari mnamo miaka ya 1990, na tulikuwa tunashirikiana vizuri. Nimemwona wakati wote akiwa mkimya, na mtu mwenye heshima. Uchaguzi wa kugombea Viti vya Baraza la Wawakilisho nao ulikuwa unalalamikiwa kwa makelele mengi. Wapinzani walidai kuwa ulikuwako wizi wa kura, lakini Waangalizi wa Kimataifa wakasema tu kuwa zilikuwako kasoro. Wajumbe wa CUF waliochaguliwa wakagoma kukalia Viti vyao; na mwishoni mwa mwezi Januari, 2001, mivutano hiyo ikafikia kilele wakati Maandamano ya Wapinzani katika maeneo ya Stone Town mjini Unguja, na Pemba vile vile, yalipoishia kwenye vurugu na, katika jitihada za kuzizima vurugu hizo watu zaidi ya thelathini wakauawa, miongoni mwao askari wawili wa Polisi! Machafuko hayo ya Zanzibar yalimletea matatizo makubwa kweli kweli Rais Mkapa, aliyetumia miaka mitano iliyopita kujenga Sera za Uchumi wa Tanzania zilizokuwa zinakubalika machoni mwa Serikali na Makampuni ya Viwanda vya nchi zilizoendelea; wakati mauaji katika mitaa ya Zanzibar yalipokuwa yanaviza sehemu kubwa ya kazi, kama siyo kazi nzuri aliyoifanya. Hili lilithibitika zaidi wakati Vyombo vya Habari vya Nchi za Magharibi vilipokuwa vinadai maoni yao wao. Mahojiano ya Rais na Tim Sebastian wa BBC, ambapo Sebastian aliyalinganisha matukio ya Zanzibar na maeneo ya mauaji ya Pol

Page 260: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

260

Pot ni funzo gumu mno kwa Vyombo vya Habari vya Nchi za Magharibi. Vifo vya watu wa Zanzibar vilionekana kuwa tukio la aibu kwa Taifa, kama ambavyo ingalikuwa katika nchi nyingine yoyote iliyostaarabika. Lakini kutabiri kutokana na tukio hilo kwa kulilinganisha na mauaji makubwa ya Pol Pot kulionyesha tu jinsi ulivyokuwa mdogo uelewa wa mazingira, hata kwa chombo muhimu kama BBC. Kukiwa na msimamo wa kumwandama Mkapa kama ule ulioonekana katika Taarifa za Magazeti ya Kimataifa, nafasi ya kurudisha tena uhusiano na Watoa-misaada haikuwa nzuri. Katika miezi michache iliyofuata, Mipango mizuri ya Rais katika kuiendeleza Tanzania ilikuwa hatarini. Ni kweli kwamba misaada ya uchumi kwa maendeleo ya Tanzania haikupungua, ingawa vikwazo viliwekwa dhidi ya Zanzibar, lakini mpaka wakati mazingira mazuri yalipokamilika juu ya ushirikiano wa baadaye na Wafadhili yaliyokuwa yamevurugika huko nyuma. Rais Mkapa na washauri wake wa karibu sana wakaanza kazi ya kuziba tofauti zilizokuwako kati ya Vyama. Lakini kwa kufanya hivyo kujitosa kisiasa alikojitumbukiza hakukumpa sifa kama ile ile aliyoipata huko nyuma alipochukua hatua za kuokoa uchumi wa Taifa. Kwa kweli ulipita muda mrefu toka Muafaka kupatikana na CUF mwezi Oktoba 2001 ndipo hatua za kujenga Imani kati ya Rais na Wafadhili wake wa Kimataifa zilipozaa matunda. Ningeweza kuendelea kusema kuwa, kwa mawazo ya Mkapa juu ya Jumuiya zinazotoa misaada, matokeo ya machafuko ya Zanzibar yalikuwa kama kikwazo. Fikira hizo hazikuzuka ghafla ila zilitokana na nong’ono za muda mrefu. Wafadhili walizozifikisha kwa Rais, nyingine kwa mbwembwe. Watu walioathirika zaidi na machafuko ya Januari 2001 waliendelea kuthibitisha Imani yao kubwa kwa Rais wakati wa mazungumzo, wakati wa kutia saini, na kisha wakati wa kuutekeleza Muafaka wenyewe. Kitendo cha CUF kukubali kutumbukia kwenye mitego hiyo kinadhihirisha uwezo wa Rais, maana ni yule tu mwenye uadilifu usiotiliwa mashaka ambaya angeweza kurejesha mahusiano na CUF. Mpaka wakati huo, Wafadhili hawakuonyesha tena Imani ile

Page 261: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

261

ile kwa Rais katika kipindi chote kile cha matatizo, pamoja na hatua zote za hatari alizozichukua katika kusukuma Mpango wake wa kubadilisha mwelekeo wa Uchumi wa jumla. Ingawa mimi hakuniambia lolote katika hayo, hata kwa kuninong’oneza, naamini kwamba matukio yale ya mwaka 2001 yalinifunza kwa uwazi zaidi kuliko kitu kingine chochote upungufu wa uaminifu wao kwake, kiwango cha kuelewa wajibu wao katika kuitawala nchi kama Tanzania. Kwa hiyo haishangazi sana kwa Mwalimu kujikuta analazimika, katika miaka ile ya mwanzo ya kujitawala, kuihakikishia Jamii ya Kimataifa kuwa Tanganyika mpya iliyokuwa inajitawala kamwe haitakuwa “Kongo nyingine. Kauli kama hizo, na hoja kama hiyo ya kuuhakikishia umma mazingira mazuri ya siku za mbele, ndizo Taratibu zinazotumiwa na nchi zote zenye Viwanda kutoka wakati ule mpaka sasa. Pamoja na matatizo yoyote yaliyojitokeza katika mwaka ule wa Muafaka, bado Mpango wa kushirikiana na Jumuiya zinatoa misaada kwa ajili ya Huduma za Jamii iliimarishwa zaidi. Mpango wa dharura wa kujenga Shule za Msingi, na mafunzo ya Walimu, ikainua kwa haraka idadi, hata kama siyo ubora, wa watoto wanaopata Elimu ya Msingi nchini Tanzania. Kwa uongozi wa Waziri wa Elimu, Mungai, (wakati huo shughuli zake katika Kampuni za Sukari kama zilivyokuwa zangu, zilikuwa zimekoma) dhamira ya Rais ya kutoa Elimu ya Msingi bure kwa watoto wote ikawa imetimia. Mipango mingine mikubwa ya kupunguza maradhi ya malaria na maambukizi ya ukimwi, kwa kueneza kila mahali zana za kinga, kama vyandarua na kondom, sasa imekamilika, pamoja na hatua za kuinua viwango vya Huduma za Hospitali kwa Watanzania wote. Hatimaye umuhimu umewekwa kwa maji kupatikana karibu na maeneo wanakoishi watu na wakati huo huo mabomba ya kuondolea maji machafu yanatandikwa jijini. Kitendo cha kuwaachia watu binafsi kuhangaikia masuala ya mawasiliano kumeleta ongezeko kubwa mno la watu wenye simu za mikononi. Mpango wa kusambaza umeme Vijijini, na ujenzi wa

Page 262: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

262

mtandao mpya wa barabara, kubwa na za Vijijini, sasa hivi unaendelea; na Taratibu za kutumia Bandari ya Dar es Salaam sasa hivi zimebadilishwa kabisa, kiasi kwamba muda wa kuingiza na kutoa mizigo unaotumiwa sasa na Makampuni unalingana na ule unaotumiwa katika Bandari nyingine kubwa ya Pwani ya Afrika Mashariki. Popote unapoangalia kuna dalili za mabadiliko na za kusonga mbele, lakini Imani yangu mimi wakati wote imekuwa kujenga nchi inayojitahidi kuwa bora zaidi baada ya miaka mingi ya kuvia.

__________

Page 263: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

263

KUMI NA NNE

NISHANI Ile safari iliyoanzia Bukene miaka yote hiyo iliyopita imekaribia mwisho wake. Nayaandika haya si kwa sababu nimepata hivi karibuni hisia za kutoweka kwangu mimi mwenyewe, ila kwa sababu ya idadi kubwa ya zawadi na tuzo nilizoanza kuzipokea mnamo miaka michache iliyopita. Wanariadha tu, pengine na Waimbaji na Waigizaji wachache walio hodari kabisa ndio wanaopewa tuzo na Jamii wanapofikia kilele cha usanii wao. Sisi wengine, tukipata tuzo yoyote, tunaipata tu pale tunapofikia ukingo wa uchakavu. Mwaka 1995-96 nilipokea Tuzo la Rais la Hati ya Dhahabu ya Karne kupitia Rotary ya Kimataifa kutokana na msimamo wangu na kujitoa katika kusaidia maendeleo ya Rotary. Mwaka 1998 nikapokea tena tuzo la “Huduma zaidi ya Ubinafsi” kutoka Rotary ya Kimataifa kwa kutambua kazi yangu ya miaka yote hiyo niliyoitumikia Rotary, baada ya kupokea Tuzo mwaka 1993 kwa ajili ya Huduma iliyotukuka. Vile vile, mwaka 1958, nilipigwa butwaa kwa furaha baada ya kuteuliwa na Kituo cha Kimataifa cha Wasifu cha Uingereza kuwa Mtu wa Kimataifa wa Mwaka huo. Ilikuwa heshima kwangu kuonekana kuwa nilikuwa nastahili kiasi hicho. Mwaka 2003 nikateuliwa Mdhamini wa Mfuko muhimu wa Rotary uliokuwa na kiasi cha dola milioni tisini kila mwaka, unaotunzwa Illinois, Marekani. Wakati nayaandika haya, mimi ni mtu peke yangu kutoka Afrika na Mashariki ya Kati ninayeushika Wadhifa huo. Mwaka 2004 nikachaguliwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Rotary wa Uingereza. Tuzo hizo zilianza kumiminika kipindi cha Kiangazi cha mwaka 2003, ambapo kwanza nilipokea Tuzo muhimu inayoitwa “Hind Retna” kutoka kwa Waziri Mkuu wa zamani wa India, I.K. Gujral kisha ikatangazwa na Mkutano wa Kimataifa wa Wahindi wasioishi India, NRI, kuwa Mhindi wa Mwaka kwa wale wasioishi kwao.

Page 264: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

264

Mwaka huo huo nikapewa Nishani ya Dhahabu ya Kujivunia India katika mkutano ulioitishwa na NRI wa London. Muhimu kuliko zote nilitaarifiwa na Serikali ya Kiingereza kuwa Mtukufu Malkia Elizabeth II alinuia kunitunukia Nishani ya Heshima ya Mpiganaji wa Dola ya Kiingereza, K.B.E. Nishani kama hiyo, ilitolewa mara ya kwanza mwaka 1917 wakati wa Utawala wa Mfalme George V, ghafla imekuwa moja ya nishani maarufu sana kwa Waingereza, nami nikatambua thamani yake kwangu. Kwa mujibu wa maelezo yaliyoambatana na Tuzo hiyo, Nishani hiyo nilipewa kwa kutambulika kazi niliyoifanya kujenga uhusiano mwema kati ya Uingereza na Tanzania, na kwa kazi zangu za kujitolea dunia nzima. Nilipokuwa nataarifiwa juu ya Nishani hii, Ikulu ya Buckingham ilinipa nafasi ya kuchagua moja kati ya namna mbili za kuikabidhiwa: ama nisubiri nafasi katika moja ya Sherehe za kawaida, huko London wakati wa kiangazi, ama niipokee Tuzo mikononi mwa Balozi wa Uingereza aliyeko nchini Tanzania. Kwa vile nilivyo Mtanzania mwaminifu ninayejivunia Nchi yangu, mimi nilipendelea zaidi nafasi hii ya pili; lakini kabla sijautoa uamuzi wa mwisho, nikataka ushauri wa Jayli na wa watoto wangu. Wote tukakubaliana kuwa, katika mazingira hayo, Sherehe itakayofanyika Dar es Salaam itafana zaidi, siyo tu kwa kuthibitisha uhusiano wangu mkubwa na Nchi hii ambayo mimi ni raia wake, lakini vile vile itawapa nafasi rafiki zangu wengi walio Watanzania kushiriki katika sherehe hiyo ya kutunukiwa Uraia wa Kiingereza. Haraka haraka tarehe ya kupewa Tuzo hiyo ikapangwa kuwa Agosti 29, 2003. Nasema haraka haraka kwa sababu niligundua baadaye kuwa Balozi wa Uingereza alikuwa anakaribia kustaafu. Ikakubaliwa kuwa sherehe hiyo, ambayo ingekuwa ya mwisho kwa Balozi huyo, ifanyike nyumbani kwake Mtaa wa Kenyatta, inayoelekea Bahari ya Hindi, na ambayo hapo zamani ilikuwa nyumba ya Mgiriki aliyekuwa na mashamba ya mkonge. Baada ya hapo ingekuwako dhifa katika Viwanja vya nyumba hiyo, na jioni yake tafrija rasmi kwenye hoteli ya Royal Palm, ambayo sasa inaitwa Movenpick Royal Palm.

Page 265: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

265

Siku hiyo ya kutunukiwa Uraia ilikuwa ya furaha kubwa na shamrashamra nyingi. Jua lilichomoza vizuri na kwa bahati ya Mungu, upepo ulitulia na kugeuka badala yake hewa nzuri. Nyumbani kwa Balozi huyo wageni zaidi ya mia wakakusanyika, pamoja na Mawaziri, Viongozi wengine wa Serikali, Mabalozi, Wafanyabiashara, Wajoli wangu wengine na familia yangu, wakajumuika kushiriki kwenye Sherehe hiyo. Muhimu kuliko wote, kwa vigezo vyo vyote vya itifaki, vile vile vya urafiki wetu wa siku nyingi, Benjamin William Mkapa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mkewe; pamoja na Mama Karume, Mke wa Rais wa Zanzibar, walikuwako wakishiriki katika Sherehe hiyo. Katika hotuba aliyoitoa kabla mimi kutunukiwa heshima hiyo ya Ushujaa, Balozi Richard Clarke aliyekuwa anaondoka alieleza jinsi nafasi kama hizo zinavyojitokeza kwa nadra; kwa kweli hajakuwako Mtanzania mwingine yeyote aliyepata Tuzo kama hiyo tangu tupate Uhuru. Alieleza vile vile katika lugha rahisi lakini ya kusisimua, historia ya maisha yangu na kazi nilizozifanya kwa kujitolea, katika Tanzania yenyewe na katika kudumisha uhusiano kati ya Tanzania na Uingereza. Na; wakati alipokuwa anazungumza, sikuweza kujizuia ila kuacha mawazo yangu kutafakari mambo ya nyuma, ya furaha ya wazazi wangu wangalikuwapo, kuiona sherehe hii; na kisha deni la hivi karibuni ninalowiwa na Jayli na familia yangu hivyo nilipokaa na kumwangalia Jayli na wanangu wazuri watatu, Hotuba ya Balozi ghafla ikaelekea kwenye familia yangu, akimimina sifa nyingi za kujitolea kwa Jayli na watoto wangu katika kuhangaika pamoja nami katika shughuli hizo za dunia. Baada ya hapo Kipindi cha Hotuba kikaisha; nikatakiwa kusimama, na Balozi akanivisha kifuani kwenye koti langu nishani ndogo, nzuri inayometameta, kunitambulisha kuwa nimekuwa Shujaa wa Hali ya Juu kabisa. Zilikuwako tabasamu chache za kejeli kati ya Watanzania waliokuwapo yalipotamkwa maneno yale ya “Dola ya Kiingereza,” lakini sidhani kama alikuwako mtu aliyechukizwa, ila ni dalili ya furaha kwa Taifa kutokana na mimi kupewa heshima hiyo.

Page 266: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

266

Baada ya waandishi wa magazeti na marafiki zangu kupiga picha kikaja chakula cha mchana chini ya mahema katika uwanja mpana uliopambwa na mikoche na misonabari; mazingira ya kuzidi kuwa ya uhuru kabisa; nami nikatumia kiasi cha saa mbili nzima kuzungumza na Rais mbele ya ndugu zangu. Nikaona kwamba Rais Mkapa, kama walivyokuwa ndugu zangu, alizifurahia simulizi zile. Tulipoondoka kwenye nyumba hiyo, Balozi Clarke akanikabidhi Kitabu kilichotiwa saini na wale wote waliohudhuria, na ganda lake likiwa na nembo ya Serikali ya Malkia. Kwa bahati dhifa ya jioni ile kule Royal Palm ilihudhuriwa na rafiki yangu mwingine, Rais wa zamani Ali Hassan Mwinyi. Mazingira yote yakawa na shamra-shamra nyingi, na za kukumbukwa, kwa sababu nyingi. Kufika wakati wa chakula cha mchana, fikira zangu zote zikaelekea kwenye kutunikiwa nishani. Sasa, saa nyingi baadaye, kwenye ile dhifa ya Royal Palm, ikawa ndiyo nafasi ya kufikiria furaha ya familia yangu. Ninawapenda mno wanangu, upendo unaodhihirika katika uhusiano ulio tofauti sana na ule nilionao kwa baba yangu. Mimi na Jayli tuliwalea wana wetu katika mazingira tofauti, tukiwasisitizia adabu wakati wote, lakini kwa mkazo mdogo juu ya Wajibu na Mamlaka. Matokeo yake wanetu wana furaha, wala hawana wasiwasi, watu wa kisiasa kabisa. Kwa hiyo namna walivyojitokeza kwenye sherehe ile ya Royal Palm mimi ilinifurahisha sana, maana hawakuelewa kwa namna ya kuniona mimi kuwa kiumbe mwenye uwezo wote; ilinifurahisha zaidi kuona furaha yao ya kweli kumwona “Mzee” anatunukiwa Shahada ya Ushujaa: maana sauti ya Manish ilipaa kwa shangwe, machozi yakimlengalenga pale alipotoa Hotuba kwa niaba ya familia. Ikawako aina hiyo hiyo ya furaha kwa Anuj na Rupen, wakati wao na wajukuu zetu walipokusanyika mbele ya jukwaa. Kwa mafanikio yoyote ya mwanadamu, kuwapenda watoto bila mpaka, na kupendwa nao namna hiyo hiyo, ndiyo mafanikio yanayozidi mengine yote. Lakini furaha yangu katika kupokea Heshima kama hiyo haikukoma jioni ile. Kesho yake ikawako arusi ya mwana wa Rais Mkapa,

Page 267: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

267

Nicola; na mimi na shemeji yangu Manubhai Madhvani tukapata bahati ya kuwa miongoni mwa wenzetu, kwa mamia, walioalikwa baadaye kwenye Tafrija baada ya arusi. Katika Hotuba yake ya kuwakaribisha Maarusi, ghafla Rais akaitangaza arusi ile kuwa ni “siku ya pili ya kusherehekea, nilisherehekea jana kwa sababu ya kushuhudia Mtanzania Mashuhuri akitunukiwa Nishani aliyoistahili ya Ushujaa katika Dola ya Kiingereza. Alistahili kwa sababu iliashiria kukubalika kwa Huduma alizozitoa kwa muda mrefu Mkereketwa huyo wa Tanzania kwa wenzake Watanzania. Akaendelea kutoa pongezi kutokana na mafanikio yaliyotokana na urafiki wetu katika kuimarisha tabia yake: “uwezo wangu katika uchambuzi wa kisiasa; uelewa wangu wa hali halisi katika uchumi wa dunia ya leo, na katika kuinua hali ya maisha ya watu wetu …..Mtanzania mzito, mwaminifu, aliyehangaika sana kunisaidia mimi kujenga busara, upendo, ukarimu na unyenyekevu”. Hatimaye akawaomba wageni wote wanywe kwa heshima yangu. Siwezi hata kuanza kueleza matokeo ya kauli zile kwangu. Mimi kupokea tuzo kutoka Serikali ya Nchi ya Kigeni, na tuzo kubwa kama hiyo kutoka nchi mashuhuri kama Uingereza, hiyo peke yake ni heshima kubwa. Lakini kwa Mtanzania mwaminifu, aliyejitahidi sana kuitumikia Nchi yake kwa hali na mali, kupata sifa kama hizo kutoka kwa Rais mwenye hadhi kama ya Mkapa, ni suala lingine kabisa. Kwa kigezo cha Balozi wa Kiingereza aliyeondoka, Rais Mkapa ni mtu aliyebarikiwa kuwa maarufu; wachache waliofuatia mwelekeo wa Tanzania katika kipindi cha miaka kumi iliyopita wangethubutu kulipinga hilo. Mimi sidai kuhusika na yale aliyoyagusia katika Hotuba ile ya arusini, lakini kama Ben Mkapa ameridhika kuniona mimi kuwa rafiki mzuri wa kuaminika, na mzalendo wa kweli, mimi hayo yananitosha, na zaidi ya kunitosha. Orodha ya tuzo zangu mimi haiishii hapo. Mwaka 2005 Serikali ya India iliniridhia kunitunukia nishani kama hiyo ya Ushujaa. Januari 9, 2005 kule Mumbai, nilipokea kutoka kwa Rais wa India A.P.J. Abdul Kalam, nishani ya Pravasi Bharatiya Sam-man kwa kutambua mafanikio yangu makubwa katika Masuala ya Jamii, na kushiriki kwangu, kwa mafanikio, katika kuinua heshima na sifa ya India, na katika kuzingatia mahitaji ya Wahindi waliokuwa Nchi za Nje. Nishani kama hizo zilianzishwa miaka michache sana

Page 268: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

268

iliyopita, na inatolewa kila baada ya mwaka mmoja kwa watu kumi mashuhuri wenye asili ya India. Nilipokwenda India kupokea nishani hiyo, sikuwa na la kufanya zaidi ya kuzikumbuka siku zangu nilizoishi kwa furaha kule Poona na Panchgani. Baba yangu, Keshavji alilazimika kuondoka India ili kurejesha heshima ya familia, na mimi sasa nikawa nakwenda huko kukamilisha azma hiyo. Mwezi Julai, 2004, Dk. Andrew Pocock, aliyeshika nafasi ya Balozi Richard Clarke, aliniomba kupanda mnazi katika Viwanja vya nyumba yake rasmi, kuwa kumbukumbu ya kutunukiwa kwangu Nishani ya Ushujaa niliyokuwa nimepata siku za nyuma. Miongoni mwa watu waliokuwepo kwenye sherehe hiyo ni pamoja na Mke wa Rais, Mama Anna Mkapa, aliyekuwa ndiyo kwanza amerudi kutoka China mnamo muda wa saa mbili tu zilizopita. Na mwisho kuna ile zawadi muhimu mno ya kutambua miaka yangu mingi katika Freemason. Huko mwanzo nilitunukiwa Shahada, lakini hatua za kuitambua zilifikia kilele chake Machi 8, 2006, nilipopewa Tuzo ya Juu kabisa inayoweza kutolewa: Nishani ya kiongozi Mkuu ya Huduma katika Freemason. Nishani hii adimu na inayotolewa kwa nadra, ilianzishwa mwaka 1945 na Kiongozi wake Mkuu, Henry, Mtawala wa Sita wa Harewood; heshima aliyoipata kwa sababu ya kutambuliwa wale wanaotambuliwa kwa Huduma yao ya sifa kwenye chama. Nishani hiyo ilianzishwa maalum ili iweze kutumika nje ya Utaratibu na, kwa maana namna nyingi, inaweza kufananishwa na Nishani ya Sifa inayotolewa na Mfalme au Malkia wa Uingereza. Kwa kipindi chote imetolewa kwa Freemason wasiozidi 12 kwa wakati mmoja. Nilipoyasikia maelezo ya Katibu Mkuu wakati nilipokuwa napewa alama ya kutambuliwa kwangu, nilijisikia kutukuzwa na kunyongekea wakati huo huo: mimi nilikuwa Freemason wa saba niliyekuwa hai kupata tuzo hiyo. Sherehe ilifanyika katika Hekalu Kuu la Freemason mjini London, Uingereza, mbele ya Wanachama zaidi ya elfu moja. Familia nayo huleta heshima yake kubwa; na mwaka huu nikasherehekea mafanikio yaliyowashangaza Wazazi wa Jayli na

Page 269: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

269

vile vile Wazazi wangu mwenyewe. Ijumaa tarehe 6 Mei, 2005, mjini Dar es, Salaam tulisherehekea kumbukumbu ya arusi yetu iliyofanyika Mei 5, 1995. Watoto wetu wakapanga, kwa upendo, uangalifu na jitihada kubwa, shughuli nyingi za kusherehekea kwa muda wa siku nne. Mwana wetu wa pili, Anuj; mke wake, Nishma; na binti yao, Polomi walikuwa wamekuja Dar es Salaam kuandaa shughuli za chakula cha mchana na cha jioni; pamoja na matembezi, na kadhalika. Wana wetu wote watatu walishiriki katika majukumu ya kuandaa Sherehe kwa uhakika ule ule kama lilivyokuwa lengo la sherehe za awali. Mawazo yetu sisi wote wawili yalikuwa kwenye kutoa picha, kama walivyosema, ya maisha yetu, kama waliyoiwasilisha kwa ufundi mkubwa wakati wa dhifa ya jirani iliyoandaliwa mwishoni mwa sherehe zile za kuzaliwa. Dhifa ilihudhuriwa na Rais Mkapa, Rais wa zamani Mwinyi, na Rais wa Zanzibar Karume, kila mmoja na mke wake; kadhalika na Mawaziri Wakuu wa zamani, na Waheshimiwa Spika wa Bunge la Tanzania na la Afrika Mashariki. Picha zilizochaguliwa na wanetu na kuonyeshwa kwa watu zikanirudisha nyuma mimi na Jayli tulivyokuwa tunaifurahia pamoja, bila kuwasahau watoto wetu wapendwa, na wajukuu wetu. Katika hotuba yake ya kutukaribisha, Rupen alizungumza kwa heshima na furaha kubwa, kama vile vile alivyofanya Manish katika ile sherehe ya Tuzo la Ushujaa mwaka 2003, nami nikayafurahia sana maneno mazuri ya Rais Mkapa alipokuwa anatutakia heri. Kwa kuwa maneno yale yalikuwa na maana kubwa kwangu, nachukua nafasi hii kuyanukuu. “Wakati wote Mhe. Andy amekuwa Kiongozi mashuhuri katika masuala ya Uchumi wa Tanzania na ya Jamii ya Watanzania; na vile vile ametumikia Serikali kwa nafasi zote alizoshika katika Bodi za Mashirika ya Umma, na katika Tume na Kamati, baadhi yake akiwa Mwenyekiti. Mhe. Chande ni mtu mnyenyekevu, lakini mwenye uwezo mkubwa, siyo kiongozi dume kama wanaume wengi wanavyosemekana kuwa. “Tangu wakati wa ukoloni Mhe. Chande amekuwa katika misukosuko ya Siasa na ya mabadiliko ya Uchumi nchini mwetu;

Page 270: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

270

hata wakati wa harakati za kutafuta Uhuru; na Uhuru wenyewe, kutaifisha Mashirika na, hatimaye kubinafsisha Makampuni. Wakati wote huo yeye alikuwapo, na akayashuhudia yote hayo. Wala si kwa sababu aliyaona tu, ila wakati mwingine na yeye binafsi yalimkumba, kama wakati ule biashara za familia yake zilipotaifishwa. “Hakuna atakayepata kujua kamwe uzito wa mzigo na thamani halisi ya hasara mtu aliyoipata katika mazingira kama hayo. Labda tunaweza kujua, kwa hakika, hasara halisi inayopatikana katika Uchumi na kwa watu binafsi; lakini kwa hakika hatuwezi kupigia hesabu kiwango cha uchungu na cha saikolojia kinachotokana na uharibifu au hasara inayopatikana. “Ni dalili ya wazi ya uthabiti wa Mhe. Chande kwamba ameyahimili matatizo hayo kwa moyo mkuu, angalau machoni pa watu kama mimi tunaomwangalia kwa mbali. Mhe. Chande hakupoteza Imani wala ujasiri wake, wala hakutoroka nchini, badala yake akazinadi dunia nzima Hoja za Mwalimu Nyerere za kuhalalisha ubinafishaji, na bado akabaki Mtetezi wa biashara za Familia hata baada ya kutaifishwa. “Hakuna atakayejua milele matokeo kamili na hasara mtu anayopata katika mazingira hayo. Pengine tunaweza kufanya hesabu ya hakika hasara itakayopatikana katika Uchumi na upotevu wa vitu; lakini sisi, kwa hakika, hatuwezi kufanya hesabu sawasawa ya hasara ya mshtuko na ya saikolojia, au hata ya uharibifu. “Uimara wa Mhe. Andy unajidhihirisha kwa jinsi alivyoibeba mikasa yote hiyo kana kwamba ni mambo ya kawaida, angalau kwa watu kama mimi tunaomwangalia kwa mbali, Mhe. Andy hakupoteza Imani, wala Ujasiri wake hakutoroka; badala yake akazifanya za Kimataifa fikira za Mwalimu Nyerere katika Taratibu za Kutaifisha; na hata akaendelea kuwa kinara wa Biashaza za Familia baada ya kutaifishwa. Hakuthubutu kuivuruga; badala yake akachukua nafasi kubwa kuibadili: kutoka kuwa ya binafsi na kuifanya ya Umma.

Page 271: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

271

“Wanaume waaminifu wenye ndoa hapa watakuambia kuwa kila madaraka yanavyopanda katika Jamii ndivyo unavyomtegemea mkeo kukupa mkono na bega la kuegemea. Ni dhana ya zamani, lakini bado ni sahihi, kwamba mgongoni kwa mafanikio yake yuko mwanamke: kwa hiyo naungana nanyi katika kumpa sifa Jayli, mke wa Mhe. Andy”. Rais na Mama Mkapa wakatuunga mkono katika dansa baada ya chakula cha jioni; wote wawili, Jayli na mimi, tukajihisi tumeinuliwa hadhi na kupata heshima ya pekee. Ndoa imara ni kama biashara iliyo shamiri, inayodai kazi ngumu, uaminifu, na sehemu kidogo ya bahati. Lakini tofauti na biashara, ndoa inadai vile vile Upendo na Uvumilivu. Ile furaha tu ya kuoana na mtu aliye radhi kushirikiana nawe katika neema na katika shida; mtu atakayemsaidia mwenzi wake kwa uaminifu na kwa ukamilifu bila kuchoka. Jayli alikuwa mwari wangu miaka hamsini iliyopita, bado ni mwari wangu mpaka leo. Nimeyaona hayo yote, na zaidi. Na sasa, baada ya kusherehekea miaka hamsini pamoja ya furaha na yenye mazao mema, bado tunatarajia ya ziada kila mmoja kwa mwenzake, na kutoka katika neema ya maisha. Tunafurahi zaidi kwa sababu wana wetu vile vile wanajishughulisha na Huduma za Jamii, na kwamba wameirithi ile tabia ya kuneemesha Jamii Mwenyezi Mungu aliyowakabidhi, tabia ambayo na mimi nimeirithi kutoka kwa baba yangu mwenyewe. Wakati mwingine kuzeeka kunaweza kufananishwa na treni inayoanza kupamba moto. Miaka ya utoto inakwenda polepole sana kila siku na maajabu yake yanayojitokeza inaonekana kwa mtoto kama mwaka mzima. Lakini mara mtu akiufikia utu uzima, siku na kisha miaka inakimbia mno. Mimi naona kama jana tu pale Rupen mtoto wa nyumbani mwetu alipokuwa mchanga. Mwangalie sasa na ndugu zake pia, yote ni madume; na kizazi kilichofuata, yaani wajukuu, sasa ni watu wazima vile vile. Kwa hiyo nazikumbuka akilini mwangu siku zile zilizokuwa ndefu mno utotoni kule Bukene, na ile nyumba iliyoezekwa bati, na ile barabara nyembamba isiyokuwa na lami. Nilikuwa, nakimbia

Page 272: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

272

kutoka shule ili nirudi kukaa karibu na mama yangu: nakaa sakafuni nikimwangalia mama alivyokuwa anapika chakula cha jioni, akimung’unya halua alizosema alinipikia mimi tu; nikimsikiliza aliponisimulia habari za zama zake, na zama zangu pia. Sasa niko katika kituo cha treni cha Bukene, katika giza la jioni ya Jumatano, nikiwa mmoja kati ya kundi kubwa la Wanakijiji waliokuwa wanasubiri treni ya abiria ya kila juma; na katika hamu ya kusubiri huko honi inalia kwa mbali; nasimama nikimwangalia Steshenimaster akikung’uta nguo zake kwa mara ya mwisho. Juu nyota zinametameta katika anga la Afrika; hewa bado ya moto; lakini upepo umetulia. Na chini vumbi jekundu miguuni mwetu. Safari yangu ndefu kutoka Bukene sasa inakaribia kwisha. Lakini wakati mwingine, moyoni mwangu, najua kuwa sijapata kuondoka.

___________________

Page 273: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

273

INDEX

Page 274: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

274

INDEX

Page 275: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

275

INDEX

Page 276: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

276

INDEX

Page 277: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

277

INDEX

Page 278: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

278

INDEX

Page 279: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

279

INDEX

Page 280: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

280

INDEX

Page 281: Shujaa Katika Africa - Andy Chande€¦ · 9 UTANGULIZI Kitabu hiki ni simulizi ya maisha ya J.K. Chande, Mwanachama wa Klabu za Round Table na Rotary, aliyetunukiwa Nishani ya Ujasiri

281

LAST PAGE