sisal smallholders farmers training

17
SOKO LA MKONGE YUNUS A. MSSIKA and Laddy Swai* *Laddy Swai; ARI-Mlingano, Box 5088, Tanga, Tanzania Mobile phone: +255754921876 JULAI, 2012**

Upload: swaimanka

Post on 20-Jul-2015

99 views

Category:

Documents


8 download

TRANSCRIPT

Page 1: Sisal Smallholders Farmers Training

SOKO LA MKONGE

YUNUS A. MSSIKA and Laddy Swai**Laddy Swai; ARI-Mlingano, Box 5088, Tanga, TanzaniaMobile phone: +255754921876JULAI, 2012**

Page 2: Sisal Smallholders Farmers Training

YALIYOMO

Utangulizi

Uzalishaji wa Singa

Hali ya Soko la Mkonge

Nini kifanyike?

Hitimisho

Page 3: Sisal Smallholders Farmers Training

1.0 UTANGULIZIKilimo cha Mkonge kwa Wakulima wadogo ni moja ya mikakati ya Bodi ya Mkonge Tanzania katika kuhakikisha kuwa umiliki wa Sekta hii unakuwa mikononi mwa wa Tanzania walio wengi.

Utekelezaji wake unazingatia sera na mikakati

mbalimbali ya kitaifa na unalenga katika kuongeza uzalishaji na tija kwa Sekta ya Mkonge nchini na hivyo kupunguza umasikini.

Page 4: Sisal Smallholders Farmers Training

2.0 UZALISHAJI MKONGE

Tangu enzi za ukoloni na baada ya uhuru na hata sasa,

uzalishaji na mauzo ya Mkonge nchini kwa kiasi kikubwa

umekuwa ukitegemea wakulima wakubwa.

Kwenye miaka ya 1960-70 Sekta ya Mkonge ilikuwa ni

mhimili muhimu wa uchumi wa Tanganyika na baadaye

Tanzania huru.

Katika kipindi hicho, Sekta ilikuwa ikichangia zaidi ya

65% ya uzalishaji na mauzo ya mazao ya biashara nje ya

nchi.

Page 5: Sisal Smallholders Farmers Training

UZALISHAJI….

Mfumo wa kwanza wa kilimo cha Mkonge kwa

wakulima wadogo nchini ulianzishwa miaka ya

1960 baada ya Azimio la Arusha katika kijiji cha

Kabuku, wilaya ya Handeni.

Mfumo huu ulidumu hadi miaka ya 1980 na ukafa

kutokana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni

wananchi kutoandaliwa na kushirikishwa

kikamilifu kulima Mkonge kupitia mfumo huu.

Page 6: Sisal Smallholders Farmers Training

UZALISHAJI…..

Baada ya muda mrefu kupita, mfumo wa kilimo cha Mkonge

kwa wakulima wadogo nchini ulianzishwa tena mwaka

1,998.

Mfumo wa Kilimo cha wakulima wadogo nchini

umegawanyika katika makundi mawili; .i.e kilimo cha

Mkataba chini ya skimu ya SISO ( Sisal Smallholders and

Outgrowers) na wakulima nje ya SISO.

Kwa sasa kuna jumla ya wakulima wadogo 5,828 nchini.

Page 7: Sisal Smallholders Farmers Training

3.0 HALI YA SOKOHali ya soko la Mkonge duniani ni nzuri kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya singa za Mkonge duniani kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa mpya kama Composite na masuala ya mazingira.

Masoko ya Mkonge wa Tanzania ni Uchina, Saudi Arabia, Uingereza, Uhispania, Ujerumani,Nigeria, Kenya na Uganda.

Hata hivyo, uzalishaji wetu bado ni mdogo kuweza kukidhi mahitaji hayo ya soko.

Ongezeko hilo la mahitaji limesababisha kupanda kwa bei za madaraja ya singa za Mkonge kwenye soko la ndani na nje ya nchi. Mfano,bei ya singa za daraja la UG kwa sasa ni Dola1,400/tani ikilinganishwa na Dola 1,250/tani mwaka 2011.

Page 8: Sisal Smallholders Farmers Training

HALI YA SOKO….

Bei za Mkonge katika soko la dunia hupangwa na

Umoja wa Wazalishaji wa Singa Ngumu Duniani

(Inter-Govermental Group on Hard Fibre) ambao

hukutana kila mwaka kujadili masuala mbalimbali

yahusuyo maendeleo ya singa ngumu.

Bei hizo hubadilika kutokana na hali ya soko la

dunia ilivyo kwa kipindi husika.

Page 9: Sisal Smallholders Farmers Training

HALI YA SOKO….

Mahitaji ya Mkonge ndani ya nchi ni makubwa

ikilinganishwa na kiasi kinachozalishwa kwa sasa.

Hali hii imesababisha kupanda kwa bei ya Mkonge

kwenye soko la ndani ya nchi.

Mathalani Bei elekezi ya Mkonge wa daraja la UG

kwa sasa ni wastani wa Shilingi 1,900,000/tani.

Wanunuzi wakubwa wa singa kwa soko la ndani ni

viwanda vya kusokota kamba pamoja na makampuni

na wafanyabiashara mbalimbali.

Page 10: Sisal Smallholders Farmers Training

4.0 NINI KIFANYIKE…….

Ili mkulima wa Mkonge aweza kunufaika na bei

hizo nzuri za singa, hana budi kufuata kanuni

bora za kilimo cha Mkonge zitakazomwezesha

kuzalisha singa za daraja bora.

Lengo liwe kupata singa za madaraja ya juu na

hivyo kupata mapato zaidi na hatimaye kuboresha

maisha yake.

Page 11: Sisal Smallholders Farmers Training

5.0 CHANGAMOTO

Mitaji midogo

Uhaba wa Korona ndogo za kusindikia majani

Ukosefu kwa hati miliki kwa wakulima walio chini ya mfumo wa SISO

Uelewa mdogo wa mfumo wa ukadiriaji bei kwa kwa wakulima hususan walio chini ya mfumo wa SISO

Uhaba wa huduma za ugani kwa wakulima walio nje ya SISO

Page 12: Sisal Smallholders Farmers Training

6.0 HITIMISHO

Mkonge ni zao lenye matumizi mengi, kwenye nyanja

mbalimbali kama katika kilimo, nishati, ujenzi, famasia,

magari, meli, ndege,majumbani, ofisini na mazingira.

Ni zao ambalo kwa sasa soko lake ni la uhakika na mwelekeo

unaonesha litendelea kuwa hivyo kwa muda mrefu ujao na

hivyo kumuhakikishia mkulima kipato cha uhakika na kwa

muda mrefu.

Umuhimu wa zao la Mkonge kwa maendeleo ya nchi hasa

maeneo ya vijijini, sasa na baadaye unapaswa kupewa

kipaumbele kwani zao la Mkonge lina sifa za kustahimili hata

kwenye maeneo ambayo mazao mengine hayawezi kustawi.

Page 13: Sisal Smallholders Farmers Training

MKONGE KWENYE MAGARI

Page 14: Sisal Smallholders Farmers Training

MKONGE KWA UJENZI WA NYUMBA BORA

Page 15: Sisal Smallholders Farmers Training

KORONA NDOGO ILIYOBORESHWA

Page 16: Sisal Smallholders Farmers Training

AHSANTENI KWA

KUNISIKILIZA

Page 17: Sisal Smallholders Farmers Training