swahili swahili afya yangu ndani ya shepparton · pap-test ni kipimo kinachofanywa ili ... ikiwa na...

44
Afya yangu ndani ya Shepparton Muongozo wa huduma za kiafya Kitabu hiki kinaelezea huduma za kiafya zinazopatikana ndani ya Greater Shepparton yakiwemo maelezo kadhaa yanayoelezea Wakimbizi na Wahamiaji. SWAHILI

Upload: hathuy

Post on 05-Jun-2018

290 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

Swahili

Afya yangu ndani ya Shepparton

Muongozo wa huduma za kiafya

Kitabu hiki kinaelezea huduma za kiafya zinazopatikana ndani ya Greater Shepparton yakiwemo maelezo kadhaa

yanayoelezea Wakimbizi na Wahamiaji.

SWAHILI

Page 2: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

2 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Kitabu hiki kimeandaliwa na Goulburn Valley Health’s Kitengo cha kuinua na ushauri wa kiafya

na:

Halmashauri ya mji wa Greater Shepparton Kildonan UnitingCare Primary Care Connect

FamilyCare The Ethnic Council of Shepparton and District

Vision Australia Shirika la msalaba mwekundu Australia

Goulburn Ovens Institute of TAFE

Tunapenda kutoa shukrani zetu kwa wote walio tusaidia

The R E Ross Trust

© 2014 by GV Health — Health Promotion Department.

All rights reserved. Imechapishwa Juni 2014

Page 3: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

3 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Yaliyomo

Faharasa 4

Kanuni za Australia katika haki ya huduma za afya - Victoria 8 Mfumo wa huduma za kiafya Australia. 9

Vituo vya matibabu vya Shepptorn 15

Idara ya dharura (ED) 17 Garama za matibabu 18

Dawa 19

Ni nini vituo vya afya vya kijamii? 21

Huduma za afya kwa mama na mtoto 27 Huduma ya macho 32

Afya na maisha mazuri 37

Mkimbizi na mtafuta msaada 38

Msaada kwa walemavu 40

Kuweza kuunganishwa na na Shepparton 41

Wasiliana nasi 42

Page 4: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

4 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Misamiati A Wakili Ni mtu anayeongea na kusihi

badala ya mtu mwingine Masaa ya ziada Nihuduma inayotolewa na

wafanyakazi kabla ya saa 3 asubuhi na baada ya saa 11 jioni.

Afya washirika Hutoa huduma kama physiotherapy, occupational therapy, dietitian, speech pathologist and podiatry

B Maziwa ya mama Kutoa chakula cha mtoto kwa

kunyonyesha Kipimo cha matiti Nikipimo kinachotumika kupima

dalili ya kansa ya matiti Wingi wa bili Huruhusu bili za matibabu

kutumwa mojakwa moja kwa malipo ya utabibu.

C Mfuko wa uzazi Ni sehemu ya mfumo wa uke

ambayo ipo kwenye njia ya uzazi Muuguzi Mtaalamu wa afya Hali mbaya Inaonyesha kiasi cha hali mbaya

ya afya E Tahadhali Kitishio cha maisha F Virutubisho Makuzi ya mtoto tumboni

Page 5: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

5 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

G Daktari wa Huduma (GP) H Huduma ya afya Kuzuia, kutibu na kuondoa

ugonjwa. Huduma za afya za kulinda mwili, afya ya akili, matibabu na washirika wa afya, yote hayo ni muhimu katika timu ya huduma ya afya.

L Maabara Ni chumba au jengo linalotumika

kupimia magonjwa; Mshutuko wa kiafya

M Mammografia Nikipimo cha X-ray

kinachochunguza mfumo wa matiti (see Breastscreen)

Dawa Madawa husika kutoka kwa GP kwa kuimalisha afya itokanayo na kutokurutubishwa.

Kufunga kizazi Hakuna kizazi tena (Hasa kwa afya ya wanawake)

N Dawa bila maelezo Madawa yanayopatikana

kwenye duka la madawa ambayo hayahitaji maelekezo ya GP

O Optometristi Mtaalamu wa afya ya jicho.

Mabadiliko ya afya, yanayohitaji matibabu ya haraka (Piga 000)

Ni mganga wa matibabu ambaye amepitia mafunzo ya kutoa huduma

Page 6: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

6 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

P Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili

kufuatilia mabadiliko ya chembechembe katika uke (see Women’s Health)

Peri-natal Miezi mitano kabla ya kuzaa na mwezi mmoja baada ya kuzaa

Maelekezo Ni maandishi yanayotolewa na mtaalamu wa matibabu kwa lengo la kuimalisha afya.

S Mtaalamu Ni mjumbe wa timu ya huduma

ya Afya ambaye ana elimu na utaalamu katika sekta ya Afya. (kwa mfano. Jinaekologisti)

Dalili Ni alama au ishara inayo onesha dalili za ugonjwa

T Matibabu Njia au uwezo wa kumsaidia

mgonjwa, Mda - mhimu Matokeo ya vipimo

yanayoendana na mda Triage Uchunguzi wa kapaumbele

katika appointment na matibabu W Mjane Mwanamke/mwanaume

aliyefiwa na mwenza wake.

Page 7: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

7 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Utangulizi Hakuna kiasi cha mawasiliano kinacho weza kukufanya uwe na amani, hasa katika nchi mpya, hasa unapokuwa mwenyewe mji mpya. Mfumo wa huduma za Afya zinatofautiana dunia nzima.Utakuwa na mabadiliko mengi kwa namna maisha yalivyokuwa kabla ya kufika Shepparton hasa pale inapojitokeza afya yako na inaweza fahamike sana. ‘Afya yangu ndani ya Shepparton’ Malengo ya kitabu hiki ni kukusaidia wewe kwa kuhama ,kukusaidia kutunza muda na nguvu, na kukusaidia vitu muhimu katika maisha yako, kama vile, familia ,afya nzuri na kufurahiya jamii yako mpya. Piga 000 kwa msaada zaidi.

Page 8: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

8 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Kanuni za Australia katika haki ya huduma za afya - Victoria

Kanuni za Austraria za huduma za afya na haki zaelezea haki za mgonjwa, watuhumiwa na kuwasaidia kwa kutumia mfumo wa huduma za Afya. Hizi haki ni za muhimu sana popote na sehemu yeyote kuhakikisha kuwa huduma ya afya inayotoiewa ni salama na yakiwango cha juu.

Huduma zote za afya zilizoko ndani ya Shepparton hufuata mkataba na maelekezo ya haki zako. Haki zako zimeorozeshwa katika ‘Kanuni za Australia katika haki ya huduma ya afya ndani ya Victoria’. Hivi vitabu vinapatikana katika vituo vya huduma ya afya na katika mtandao kwa kutumia lugha 24 tofauti tofauti, ikiwemo braille version.Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti hii; http://health.vic.gov.au/patientcharter/publications Tunapendekeza wewe mwenyewe uwe karibu na hizi haki.

Page 9: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

9 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Mfumo wa huduma za afya za kiaustralia. Mfumo wa mfuko wa huduma ya afya kwa uma Australia unaitwa kadi ya mfuko wa afya. Kadi ya mfuko wa afya, huruhusu wa Australia

wote kupata huduma ya afya iliyo bora ambayo ni nafuu na upatikanaji wake ni rahisi. Unapo jiandikisha kwenye mfuko huu unatakiwa uwasilishe cheti cha kuzaliwa, au pasipoti ya kusafilia.Unapokuwa umejiandikisha utapewa kadi yenye namba, jina lako na majina mengine ya familia yako ambao wako chini ya miaka 16. Mfuko huu husaidia kumtofautisha mtu mmoja na mwingine, hupunguza gharama za kutibiwa kwa General Practitioner (GP), na kununua madawa kwa bei nafuu .Baadhi ya vituo vya afya hutangaza hizo bili nafuu. Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako, kwani mfuko huu utakulipia moja kwa moja. Baadhi ya vituo vingine utahitajika ulipie huduma hapohapo, kama ndivyo utahitajika kupeleka risiti kwenye mfuko huu ili urudishiwe fedha zako. Pia inategemea aina ya visa uliyonayo, cheo ulicho nacho, unaweza ukawa wa kawaida au wa thamani ya juu chini ya mfuko huu, kwa kununua madawa na

Page 10: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

10 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

huduma za hospitalini.Kadi utakayo pewa ndiyo itakuelezea wewe upo kundi lipi. Ofisi za kadi ya mfuko wa afya chini ya Shepparton zipo 298 mtaa wa Maude katika jengo moja ya Ofisi ya local Centrelink.. Pia kwa maelekezo zaidi tembelea tovuti hii. www.medicareaustralia.gov.au au piga namba hii 132 468; Kama unahitaji msaada katika lugha Fulani piga, 131 202. Wakalimani

Kila mmoja ana haki ya kupata taarifa ya huduma hii.kwa kujua Matibabu na gharama zinazotakiwa. Wakalimani wenye vibari wanapatikana maana wakalimani ni muhimu katika kujadili historia ya ugonjwa, matibabu, majibu

ya vipimo na majibu ya daktari au kulazwa. Kama GP wako au anayekuhudumia haongei lugha yako ni wajibu wao madaktari kukusaidia mkalimani. Unapokuwa na appointment na daktari au muhudumu lazima utoe taarifa mapokezi kama unahitaji mkalimani wa lugha husika. Mkalimani anaweza kukusaidia kwa njia ya simu au itategemea na yeye mwenyewe akusaidie kwa njia gani. Huu ni wajibu wa mtoaji wa huduma ya afya. Unaweza vile vile

Page 11: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

11 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

kumujulisha mtu wa mapokezi kama unahitaji mkalimni wa kiume au wa kike. Jitihada zote zitafanyika ili kukidhi matakwa yako. Huduma ya ukalimani ni bure kwa hospitari za uma na kwa GPs. Gharama ni kwa hospitali binafsi na kwa mganga kadhaa. Ni muhimu kutumia mkalimani kwa sababu atakusaidia kuwasiliana na waganga wa afya kadhaa.Wakalimani hawa wamejifunza kuelewa misamiati ya lugha za kiganga. Itakuwa ngumu kujadili na mlengwa kama utatumia rafiki au mwana familia kuwa mkalimani (na hasa kama mkalimani ni mtoto). Lakini huduma ya afya inasisitiza kuwatumia wakalimani wataalamu. Huduma ya Ukalimani na Utafisiri (TIS) Wanaweza kukupa wakalimani. Piga 131 450 kwa kufanya appoitment au kwa kupata huduma ya ukalimani haraka.

Page 12: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

12 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Daktari wa Familia (GP) Daktari wa Familia (GP) huchunguza afya ya mwili pia huitwa daktari wa familia au daktari wa ndani. Na kama una ugonjwa wa ghafla sehemu nzuri ya kwenda ni kwa GP. Muda unaweza kuwa ni kidogo sana kwa daktari ,ni vizuri kupanga muda binafsi kwa kila mmoja. Kama wewe na wengine katika familia nyingine mnataka kumuona daktari kwa wakati mmoja. Tafadhali muulize lini akupangie muda.

GPs wanaweza kukuelekeza kipi cha kufanya kuchunguza afya yako na namna ya kuzuia ugonjwa kama vile chanjo na kufanya upimaji kwa wanawake na wanaume. Kupima mara kwa mara humsaidia GPs kufahamu

zaidi juu ya afya yako. Hii inaweza tumika kwa maelezo au kwa kupima (mfano,kipimo cha damu au kipimo cha kumsikia mgonjwa hali yake). Wakati GP anachunguza afya yako, atakuuliza kuhusu afya yako kwa sasa na matibabu uliyopata nyuma. Kama ukiwa na imani na Daktari, kutamsaidia GP kukufahamu zaidi na,kujua historia yako ya matibabu pia kuwa karibu na wewe muda wote.

Page 13: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

13 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Tumia mtu katika familia, rafiki au mtoa huduma ya afya kuwa anamkumbusha GP wa eneo lako, inaweza kuwa msaada mkubwa kwako. Kadi ya punguzo au Kadi ya huduma ya afya Husaidia kupata huduma ya matibabu kwa gharama ndogo ya ugonjwa wa meno na gharama ndogo za kununua miwani ya macho. Kama unahisi GP wako hajakuhudumia vizuri una haki ya kubadilisha GPs au kulalamika kwake tena.

Page 14: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

14 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Vitu muhimu vya kukumbuka

Nenda na kadi yako ya mfuko wa afya kwa kila ahadi ya dactari.

Mueleze GP wako matatizo yako yote na jinsi unavyo jisikia kadri uwezavyo.

GP wako hana ruhusa kuzungumzia matatizo yako kwa mtu mwingine zaidi ya yako tu.

Kama unawasiwasi kunakitu huja kielewa kutoka kwa GP hakikisha unamwambia anakueleza tena au muulize mkalimani.

Kama unaona hutaweza kutimiza ahadi yako na Gp, unatakiwa upige simu kwenye ofisi ya GP haraka iwezekanavyo afute ahadi yako.

Page 15: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

15 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Vituo vya afya vya Shepparton

Kituo cha afya Anuani Namba ya simu

Archer Street Clinic 215 Archer Street, Shepparton

(03) 5821 7344

Family Medical Centre 174 Nixon Street, Shepparton

(03) 5822 2533

Kialla Medical Clinic Shop 21D 8025 Riverside Plaza Goulburn Valley Highway, Kialla

(03) 5823 5446

Lister House Medical Centre

60 Nixon Street, Shepparton

(03) 5831 2333

Market Place Medical Centre

Shop 31, 110 Benalla Road, Shepparton

(03) 5822 2677

Nixon Street Medical Centre

46 Wyndham Street, Shepparton

(03) 5822 1000

Primary Care Connect 399 Wyndham Street, Shepparton

(03) 5823 3200

Princess Park Clinic 172 Welsford Street, Shepparton

(03) 5821 9655

Sana Medical Centre 142 Nixon Street, Shepparton

(03) 5822 4000

Shepparton Medical Centre

49 Graham Street, Shepparton

(03) 5823 3100

The Old House 77 Wyndham Street, Shepparton

(03) 5831 1366

Tristar Medical Group 6–8 Waranga Drive, Kialla

(03) 5823 5977

Wyndham House Clinic

96 Maude Street, Shepparton

(03) 5821 5633

headspace 129 High Street, Shepparton

1800 551 800

Page 16: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

17 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Idara ya dharura (ED)

Idara ya dharura wana maajenti wa huduma ya afya wanaoshughulikia wagonjwa walio mahututi au walio jeruhiwa vibaya.

Katika Shepparton, ni sehemu ya GV Health zilizoko kwenye hospitali za kawaida mtaa wa Graham. Unapoenda Idara ya dharura utapata yafuatayo:

1. Muuguzi wa zamu atachunguza ugonjwa au ajari yako.

2. Utapangiwa wakuhudumie vipi kutokana na hali ya ugonjwa au ajali uliyo nayo.

3. Aina ya kwanza mgonjwa atahudumiwa haraka sana. Aina ya 2-5 wagonjwa watapelekwa kwenye sehemu ya kusubilia

4. Karani atachukuwa maelezo yako ili kukusaidia wakati wa kukutibu.

Muda wa kusubili utatokana na hali yako ilivyo kama umezidiwa sana utapewa muda mfupi kama sio sana muda mrefu kidogo. Wagonjwa wengine katika hii idara ya dharura watatibiwa na kurejeshwa nyumbani, kama unataka kulazwa hospitalini kwa matibabu zaidi.Hospitali hukutoa kwenye idara ya dharura na kukupeleka kulazwa hospitalini katika muda mahususi.

6

Swahili

Goulburn Valley (GV) Health - Idara ya afya yako

Hospitali ya Goulburn Valley (GV) ndio idara ya afya ya umma katika Shepparton na iko Graham street.

Hospitali ya GV hutoa huduma kwa wangonjwa wanaohitaji upasuaji, maatibabu kwa watoto, uzazi, magonjwa mahututi, na maatibabu ya ugonjwa wa akili.

Idara hii pia hutoa huduma za jamii kama vile elimu ya ugonjwa wa kisukari, kujizuia na huduma za wazee, huduma za afya zingine na utibabu wa kansa. Ili kupata huduma hizi lazima uwe na rufaa kutoka kwa daktari wako (GP).

Huduma zingine katika huduma hii ya GV ni za meno, utoaji wa damu na upigaji wa picha kwa nia ya kuangalia magonjwa.

Kama ugonjwa wako au kuumia ni mahututi lazima kwenda moja kwa moja idara ya dharura (emergency) ambayo ni sehemu ya GV afya.

Page 17: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

17 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Idara ya dharura (ED)

Idara ya dharura wana maajenti wa huduma ya afya wanaoshughulikia wagonjwa walio mahututi au walio jeruhiwa vibaya.

Katika Shepparton, ni sehemu ya GV Health zilizoko kwenye hospitali za kawaida mtaa wa Graham. Unapoenda Idara ya dharura utapata yafuatayo:

1. Muuguzi wa zamu atachunguza ugonjwa au ajari yako.

2. Utapangiwa wakuhudumie vipi kutokana na hali ya ugonjwa au ajali uliyo nayo.

3. Aina ya kwanza mgonjwa atahudumiwa haraka sana. Aina ya 2-5 wagonjwa watapelekwa kwenye sehemu ya kusubilia

4. Karani atachukuwa maelezo yako ili kukusaidia wakati wa kukutibu.

Muda wa kusubili utatokana na hali yako ilivyo kama umezidiwa sana utapewa muda mfupi kama sio sana muda mrefu kidogo. Wagonjwa wengine katika hii idara ya dharura watatibiwa na kurejeshwa nyumbani, kama unataka kulazwa hospitalini kwa matibabu zaidi.Hospitali hukutoa kwenye idara ya dharura na kukupeleka kulazwa hospitalini katika muda mahususi.

Page 18: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

18 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

PIGA 000 Piga 000 kama hali yako sio nzuri au umezidiwa sana au umepata ajari kubwa, Gari la dharura au askali au gari la zima moto zitakuja kutokana na dharura uliyo nayo. Piga 000 haina garama unaweza kupiga muda wowote na sehemu yoyote. Ni muhimu kuwa na hizi namba sehemu yoyote maana yaweza tokea dharura.

Page 19: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

19 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Gharama za Matibabu Kadi yako ndiyo inaweza kuwa na gharama zote za matibabu. Kuna gharama ambayo hulipwa siku ya ahadi ya kuonana kimatibabu. Kwa mfano malipo ya kuonana na Daktari, ikiwemo wataalamu wa matibabu, vipimo pamoja na upasuaji; vipimo vya macho hufanywa na wataalamu wa macho; matibabu pamoja na oparesheni katika hospitali za umma. Gharama zote hutolewa moja kwa moja kwenye kadi ya matibabu. Muda mwingine kunakuwepo utofauti wa gharama na gharama inayokatwa kwenye kadi. Utofauti wa gharama hizi hulipwa siku ya matibabu. Kama una Kadi ya punguzo au Kadi ya Huduma za Afya, hii inaweza kukufanya ulipie dawa kwa gharama nafuu, gharama ya chini ya matibabu ya meno pamoja na miwani.

Dawa

Katika Australia, kuna sheria ambayo inaruhusu baadhi ya dawa kununuliwa kwa wauza dawa bila maelezo yoyote ila kuna zingine mpaka zitolewe ufafanuzi na

Daktari.

Page 20: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

20 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Maduka ya dawa ni sehemu ambayo dawa hutunzwa na kuuzwa. Kinaweza kuwa kitengo fulani ndani ya hospitali au duka kwenye jumuiya. Kama ukipewa maelekezo ya dawa na daktari, zipeleke kwa muuzaji wa dawa. Watakuambia jinsi ya kutumia dawa hiyo andika jina lako kwenye boksi au juu ya chupa ya dawa. Ni muhimu kufuata maelekezo ya kutumia dawa mpaka itakapoisha. Dawa itumiwe na mtu aliyeandikwa kwenye Chupa au kwenye boksi la dawa na HAIRUHUSIWI kutumia na mtu zaidi ya mmoja. Ni kinyume cha sheria kumpatia dawa mtu au kumtumia nje ya nchi. Mgonjwa aliyepo Hospitali anaweza kupewa dawa na mfamasia wa hospitali. Kama umepewa maelekezo ya kutumia dawa na Daktari wa Hospitali, unaweza kupewa dawa kutoka kwa mfamasia wa kituo cha afya cha GV au kwa mfamasia anayetambuliwa na jamii. Unaweza kuambia uende kwenye maduka ya dawa ya kituo cha afya cha GV kwa dawa kuu ambazo hazipatikani kwenye maduka ya dawa ya ya kawaida. Maduka ya dawa ya kawaida hutoa dawa ambazo na zimeandikwa na Daktari. Maduka ya kawaida pia huuza dawa ambazo hazihitaji kumuona Daktari. Hifadhi dawa katika eneo salama lililo mbali na watoto.

Page 21: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

21 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Nini kituo cha afya cha jamii. Kituo cha afya cha jamii ni kituo kinachotoa ofa ya huduma ya afya na huduma ya ustawi wa jamii kiafya. Primary Care Connect ni kituo cha afya cha ndani cha jamii ambacho kipo mtaa wa Wyndham 399 huduma za Shepparton: o Mshauri wa wakimbizi au wakili (Refugee

Counsellor/Advocates) anaweza kupunguza msongo wa mawazo ambayo umeyapata wakati wa matatizo.Hasa mshituko ulioupata kabla ya kuja Australia.wanaweza pia kukusaidia kupata huduma muhimu kupitia wao.

o Muuguzi wa afya ya mkimbizi (Refugee Health Nurse) anaweza kutoa msaada wa taarifa na ustawi wa afya yako na kukuunganisha na GPs na huduma za hospitali.

o Dietician anatoa ushauri kuhusu chakula na vitamin ambavyo hujenga mwili na kulinda afya..

o Timu ta usimamizi wa fedha Financial Management Team inaweza kukusaidia kama unatatizo la kifedha na kukusaidia kupanga bajeti yako.

Kuna huduma nyingi ambazo hutolewa na Primary Care Connect . Kwa mawasiliano zaidi tafadhali wasiliana na (03) 5823 3200 au tembelea tuvuti yetu. www.primarycareconnect.com.au

Page 22: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

22 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Afya ya jamii katika Kituo cha Afya cha GV ni mpango unaotoa msaada kwa watu wenye matatizo ya kiafya na mahitaji mengine muhimu bila kujali umri ili kuweka mabadiliko mazuri katika kubadili hali za kitabia. Kuna huduma kama:

o Matibabu ya wagonjwa wa akili o Matibabu ya viungo vya mwili o Wataalamu wa lishe o Kazi za Kijamii o Wauguzi katika afya ya uzazi o Patholojia o Upasuaji wa viungo katika mwili o Msaada binafsi

Kuna huduma nyingine nzuri katika kituo hiki cha afya. Ulizia kuhusiana na huduma hizi kwa daktari au mtoa huduma au piga simu katika kituo cha afya cha kijamii kwa namba hii (03) 5832 3100. Ingawa hizi huduma hutolewa bure, lakini yaweza kuwepo gharama ndogo kwa baadhi ya huduma. Kama hauwezi kugharimia, tafadhali jadili na mtoa huduma wako.

Page 23: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

23 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Huduma kwa Wazee Watu wote huthaminiwa nchini Aaustralia. Huduma kwa wazee ni huduma ambayo hutolewa kwa watu walio na umri mkubwa. Kuna huduma mbalimbali ambazo hutolewa ndani ya mji wa Shepparton ili kutoa msaada wa mahitaji muhimu kwa wazee. Kwa taarifa zaidi kuhusiana na huduma hizi waweza kumuulizia muuguzi au ukampigia simu mshauri aliyekaribu kwa namba 1800 200 422 au ukatembelea tovuti hii http://www.myagedcare.gov.au/

Page 24: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

24 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Huduma za afya kwa Wanawake Katika Australia, kuna mipango madhubuti kwa ajili ya utoaji wa huduma za afya kwa Wanawake. Zifuatazo ni huduma na mipango muhimu ambayo hutolewa katika mji wa Shepparton: Kupanga familia na Afya ya uzazi: Kama ungependa taarifa au ushauri juu ya upangiliaji wa kupata mimba au juu ya mambo ya afya ya wanawake unaweza kumuona muuguzi wako. Muuguzi anao uwezo wa kukuandikia upelekwe: Afya ya Wanawake Kituo cha GV — Specialist Consulting Suites Mtaa wa Graham, Jengo I Simu: (03) 5832 3600 Vipimo vya Kansa Kipimo hiki husaidia kuangalia mabadiliko katika mfumo wa seli kwenye mfuko wa uzazi. Kama vikionekana mapema zaweza kupatiwa matibabu kwa haraka. Na kama havijapatiwa matibabu haraka husababisha kansa katika mfuko wa uzazi. Muuguzi huchukua mifano ya seli kutoka kwenye mfuko wa kizazi. Huduma hii haina madhara. Mifano iliyotolewa hupelekwa maabara kwa ajili ya kuchunguza kama kuna mabadiliko yoyote yaliyojitokeza. Wanawake wanashauriwa kupimwa kansa ya kizazi hata kwa mwaka mmoja baada ya

Page 25: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

25 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

kujamiiana au wakifikia umri wa miaka 18 hivi au waweza kupima kwa baadae. Pia wanawake wanashauriwa kupata kipimo hiki kila baada ya miaka miwili. Kwa mwanamke yeyote ambaye huwa anajamiiana mara kwa mara awe anapata kipimo hiki cha kansa ya kizazi mpaka kwenye umri wa miaka 70, hata kama wamefiwa waume, wametalakiwa au wamefunga kizazi. Kipimo hiki ni bure ila baadhi ya wataalamu hutoza gharama za ushauri. Unaweza kuulizia kabla ya kuweka appointment kwa muuguzi. Baadhi ya wanawake huona aibu kwa kupatiwa huduma hii, ni muhimu kuchagua vituo wanavyopenda na hawataona aibu. Unaweza kuchagua daktari au muuguzi wa kike. Vipimo hivi hupatikana kwa daktari wako na pia kwenye kituo cha afya ya wanawake cha GV. Kupima Matiti kwa kuchunguza kansa kwa wanawake Kipimo cha x-ray kwa wanawake hutolewa bure katika kituo cha kuchunguza kansa kwa wanawake Victoria. Kipimo hiki huweza kugundua kansa ya matiti wakati ikiwa bado changa sana. Kansa hii ikijulikana mapema yaweza kutibiwa kiufanisi.

Page 26: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

26 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Kansa hii huwa ya kawaida kwa wanawake wenye umri mkubwa. Kama una miaka zaidi ya 50 na hauna dalili zozote za kansa, unatakiwa kupata uchunguzi kwa kila miaka miwili. Wanawake wengi ambao wameshapimwa hukutwa hawana dalili za kansa. Kwa kuweka ahadi ya matibabu au ushauri piga: 132 050 Kama una dalili zozote za uvimbe au maumivu kwenye matiti ni muhimu kumuona mtaalamu.

Page 27: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

27 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Huduma za afya kwa Mama na Mtoto Vituo vya huduma za kiafya za mama na mtoto hutolewa na wauguzi waliobobea, ambao hutoa:

Ukuaji, afya na kuangalia maendeleo ya watoto Kusaidia wazazi kwa kuwalisha watoto, kitabia

na mambo mengine ya kitoto. Taarifa juu ya mambo ya afya kwa wanawake Kutoa ushauri na kufanya urejeshi kwa vituo

vya uzazi Makundi mengine hukutana na wazazi pamoja

na watoto Mipango ya chanjo Kuwatembelea nyumbani endapo ni ngumu

kwako kupata kituo Kupeleka kwa watoa huduma wengine kama

wanalishe

Hii ni huduma ya bure kwa familia zenye watoto kati ya miaka 0-6. Ulizia kwenye halimashauri ya mtaa wako kuwa ni wapi unaweza kupata kituo cha afya cha mama na mtoto kilichopo karibu au unaweza kupiga simu 5832 9700.

Wahudumu wa kituo cha afya cha Peri-natal emotional wanapatikana kwa kutoa msaada katika kituo cha afya cha GV. Je, kwa nini utoaji wa chanjo ni muhimu? Utoaji wa chanjo ni salama na huweza kukulinda pamoja na familia yako baina ya magonjwa mengi

Page 28: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

28 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

(kama vile surua) kabla ya kuwa karibu nao katika jamii. Utoaji wa chanjo si lazima, ila inashauriwa kupatiwa kwa kila mmoja. Chanjo inaweza kutolewa nchini mwako ila inashauriwa kumuona Daktari au mhudumu wa afya ya mama na mtoto kujiridhisha kama umepatiwa huduma hii dhidi ya magonjwa yote yanayolengwa na mpango wa utoaji chanjo nchini Australia. Ni jambo jema kwa watu wazima na watoto kuangaliwa kama kama wana chanjo. Je, ni wapi ninaweza kwenda kupata chanjo? Mpango wa Chanjo ya bure dhidi ya magonjwa ya watoto na watu wazima. Kuna baadhi ya chanjo ni za kulipia. Muda wa watoto kuanzia miaka 0–6 hufanywa na halmashauri za mtaa. Ulizia halmashauri ya mtaa au kituo cha afya cha mama na mtoto chenye kliniki ya chanjo. Watoto, wanafunzi na watu wazima pia wanaweza kupatiwa chanjo na daktari aliyepo karibu au Baraza la kikao cha chanjo Kama una swali lolote kuhusiana na chanjo, yawasilishe kwa daktari wa familia, au mhudumu wa afya ya mama na mtoto.

Page 29: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

29 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Unyonyeshaji

Maziwa ya mama ni chakula cha kawaida kwa mtoto, yametengenezwa kiuasilia sawa na mwili wa mtoto.

Ni chakula ambacho kimejumuisha virutubisho vyote vinavyohitajika kwa mtoto kwa miezi sita ya kuzaliwa kwake

Humuondolea njaa pia kiu, hahitaji maji ya Huongeza kinga ya mtoto dhidi ya maambukizi

ya magonjwa. Hupunguza hatari ya kuwa na mzio (allergy)

Unyonyeshaji pia ni muhimu kwa mama.

Yanapatikana wakati wowote, ni rahisi na yanapatikana muda huo huo yanapohitajika.

Ni safi na Salama. Humtuliza mtoto wakati akiwa hana raha nan i

msumbufu. Husaidia mfuko wa kizazi wa mama kurudi

katika hali ya kawaida mara baada ya kujifungu.

Humpa mama wakati wa kupumzika mchana wakati akimnyonyeha mtoto.

Akina mama wasionyonyesha huwa kwenye hatari ya kupata kansa ya matiti na ugonjwa wa moyo.

Unyonyeshaji husaidia kuleta upendo wa ukaribu pia ni dhamana yako na mtoto, pia

Page 30: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

30 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

yawezakuwa ni nafasi ya kuzoeana kiundani baina yenu wawili.

(Taarifa hii imetolewa kwenye Jumuiya ya Unyonyeshai ya Australia www.breastfeeding.asn.au)

Msaada wa Karibu akina mama wanaonyonyesha

Kituo cha Afya 26 Scoresby Ave, Shepparton (03) 5831 1370

Maternal and Child Health Nurse

Wasiliana na halmashauri ya mtaa (03) 5831 9312

Greater Shepparton Breastfeeding Cafe

Community Centre Riverside Plaza, Shop 21c 8025 Goulburn Valley Highway Kialla (03) 5832 9312

Australian Breastfeeding Association Shepparton Group

Huduma masaa 24 Piga: 1800 686 268 Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.facebook.com/ABAShepparton

Family Care Parent Child Program

(03) 5823 7000

Page 31: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

31 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Huduma ya Meno Je, ni mahali gani naweza kupata huduma ya meno? Unaweza kutafuta wataalamu wa huduma ya meno kutoka wataalamu wanaojitegemea au katika kliniki za umma za huduma ya meno. Wataalamu wanaojitegemea hawana muda mrefu wa kusubiria huduma ila ni ghari sana. Je, itakuwaje nisipokuwa na uwezo kwa ajili ya mtaalamu anayejitegemea? Kama una kadi maalumu ya matibabu au bima, serikali hutoa huduma ya matibabu ya meno kwa gharama ndogo katika huduma zifuatazo:

GV Health Idara ya Meno Graham Street, Shepparton 3630 Simu: (03) 5832 3050

Gharama ya chini kwa ushauri katika huduma hizi ni *$26.00. Hutegemea na matibabu yaliyotolewa, gharama zingine zaweza kuwa hadi *$104.00. Ugonjwa wa meno wa dharula waweza kuwa kama Meno kuumwa, uvimbe sehemu za mdomo au mdomoni hata usoni, au kutoka damu. *Gharama hizi ni za huduma unapoanza lakini zaweza kubadilika.

Page 32: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

32 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Huduma ya macho

Wapi naweza kupata vipimo vya tatizo la kutokuona? Unaweza kwenda kwa mtaalamu wa macho kupimwa kama unatatizo la macho.Huna haja ya kupata ruhusa kutoka kwa GP.

Ni wajibu kupimwa macho yako mawili kila baada ya miaka miwili. Wataalamu wengi hulipwa gharama za kupima kwa hiyo huna haja ya kulipia chochote unapoenda kupimwa. Lakini unaweza lipia Miwani na lesensi.Kama unakadi ya wasiojiweza au kadi ya huduma ya afya au ni mwanafunzi wa kutwa utatakiwa kulipia kiasi kidogo cha fedha katika huduma ya macho ikiwemo miwani ya macho na lesensi ya bei nafuu katika kliniki ya Chuo cha macho cha Victoria. Nifanye nini kama miwani haitanisaidia? Vision Australia Ni shirika linalotoa msaada kwa vipofu au watu wenye mwanga hafifu.. Huduma zao .zinalenga kusaidia watu wenye matatizo hayo kufanya vitu wanavyo hitaji kufanya. Huduma ni kama zifuatazo.

Page 33: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

33 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Kliniki ya muono hafifu hutoa maelekezo na mafunzo ya kuwasaidia wenye matatizo hayo kuzikabili hali zao na namna ya kutumia sehemu ya hiyo ndogo ya kuona iliyobaki, kwa mfano namna ya kutumia magifaya na mwanga ulio boreshwa.

Kutoa ushauri na mafunzo ya shughuli zao za kila siku kama vile kupika,kutumia vifaa na shughuli binafsi.

Kutathimini na kutoa ushauri namna ya kuwasaidia watu wenye matatizo ya kuona kuweza kuendelea kusoma kazi zao za kila siku na kufurahiya wanacho fanya.

Kutoa mafunzo ya muda mfupi na ujuzi mbalimbali, ili kuwasaidia kufanya kazi katika mazingira yao na maeneo ya mbali na kusafiri salama kwa kujiamini.

Ushauri na mafunzo ya tekinolojia ,kusaidia watu kujifunza komputa vifaa vingine.

Maabala huruhusu kuchukua vitabu na magazeti

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu hayo yote juu na huduma nyingine nyingi na Vision Australia, tafadhali wasiliana na 5831 9400 au 1300 84 74 66,au tembelea tuvuti yetu: www.visionaustralia.org.au

Page 34: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

34 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Huduma kwa viziwi Mwan Audiolojia, huthamini, hutibu na kukabili matatizo yote yatokanayo na kutosikia kwa watu wote na umri wowote GV Health hearing care hupatikana sehemu maalumu.

Wapi naweza kupata vipimo vya tatizo la kutosikia. Huduma uwezo Namna ya

kujiunga Huduma ya Kusikia ya Kitaifa

Hutoa huduma za bure kwa viziwi: Kwa watu wenye

kadi za wasiojiweza Watu ambao

wamejiunga na Centrelink

Huduma hii haihusiki na watu wenye kadi ya kipato kidogo.

Utahitajika kuchukua fomu aidha kwenye familia yako ya GP au; Ofisi zinazotoa huduma ya kusikia ya 1800 686 126

Page 35: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

35 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Huduma uwezo Namna ya kujiunga .

Australian Hearing

Huduma ya bure hutolewa kwa watoto na vijana chini ya miaka 21 ambao makazi yao ni Australia.

Kuwapata tumia simu namba; 131 797

H.E.A.R Services

Vipimo vya awali hutolewa bure kwa vijana

Hupatikana katika jamii ndani ya vituo vya afya.wasiliana na vituo nya ndani kama huduma hii ipo.

Page 36: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

36 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Faidika na Shepparton

Page 37: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

37 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Afya na Maisha Mazuri Tunafahamu kuwa watu wanaohamia Australia hukutana na upinzani baada ya kufika Australia, matatitzo ya kuelewa, usingizi, ndoto

mbaya na kujihisi wakosaji pia kuwa na hasira. Hivi vyaweza kuwa na usumbufu kidogo, hasa wakati unapotaka kutulia kimaisha ndani ya nchi hii. Endapo matatizo haya yanaingiliana na maisha ya kila siku, yanaweza kuwa rahisi kuongea na washauri, mtumishi katika jamii au msaikolojia ambaye anaweza kuongea na kupanga njia za kutatua matatizo hayo. Ili kupata msaada unaweza kuwasiliana na kituo cha Primary Care Connect kwa namba 5823 3200 au muulize GP wako kukusaidia kupata huduma. Kituo cha headspace Shepparton hutoa huduma kwa watu wenye umri kati ya miaka 12–25 kama unahisi una msongo wa mawazo wa kitu chochote. Ili kupata msaada zaidi piga 1800 551 800 au tembelea tovuti hii: www.headspace.org.au Kufanikisha huduma hii unaweza kuwawasiliana na shirika. GP wako atakuwa na uwezo wa kutambua huduma sahihi kwako.

Page 38: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

38 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Mkimbizi na mtafuta msaada Wengi wanaoingia Australia wana sumbuliwa na tatizo la mfanyakazi ambaye yupo tayari kuwasaidia au kuwaelekeza namna ya kuishi kutokana na viza au uhamiaji, wanatakiwa kusaidiwa kwa vitu vifuatavyo:

Makazi Kuwapangia madarasa ya kusoma kingeleza, Kuwaandikisha wanafunzi mashuleni Kujaza fomu za Centrelink Kupata vifaa vinavyotumika nyumbani kwako. Kutafuta watoto. Kukuweka karibu na jamii

Yafuatayo ni mashirika yaliyo katika Shepparton yameonesha muda wao na majukumu yao kwa watu binafsi au familia zinazo hitaji misaada kutoka kwao.

Kildonan UnitingCare 219–225 Wyndham Street, Shepparton 3630 Simu: (03) 5831 6157 Tuvuti: www.ucce.org.au

Page 39: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

39 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Ethnic Council Shepparton 158 Welsford Street, Shepparton 3630 Simu: (03) 5831 2395 Tuvuti: www.ethniccouncilshepparton.com.au Msalaba mwekundu 399 Wyndham Street, Shepparton 3630 Simu: 1800 811 700 Tuvuti: www.redcross.com.au GOTAFE 152–200 Fryers Street, Shepparton 3630 Simu: 1300 468 233 Tuvuti: www.gotafe.vic.edu.au

Page 40: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

40 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Msaada kwa walemavu Ulemavu unaweza kuwa wa upungufu wa akili,viungo, ukiziwi , bubu, upofu na kudumaa kimwili na akili. Katika Shepparton, Jamii

nyingi zenye mashirika ya kusaidia walemavu, hutoa msaada wa moja kwa moja kwa watu wenye ulemavu. Kama unasumbuliwa na ulemavu Centrelink wanaweza kupata msaada wa kifedha na misaada mingine. Husaidia watu wasiojua Kiingereza ila ni walemavu na misaada yao wataipata: FamilyCare 19 Welsford Street, Shepparton 3630 Simu: (03) 5823 7000 Primary Care Connect 399 Wyndham Street, Shepparton 3630 Simu: (03) 5823 3200 Tuvuti: www.primarycareconnect.com.au

Page 41: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

41 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Connect GV 12 Bowenhall Street, Shepparton 3630 Simu: (03) 5821 2466 Tuvuti: www.connectgv.com.au Vision Australia Mtaa wa Corner Archer na Channel Road, Shepparton 3630 Simu: (03) 5831 9400 Tuvuti: www.visionaustralia.org

Karibu Shepparton The Greater Shepparton City Council ina mengi ya kusaidia jamii. Kwa mawasiliano ya shughuli za kijamii kama: matukio, michezo na muziki tembelea www.greatershepparton.com.au pigal (03) 5832 9700.

Listi ya mashirika ya kawaida ya Shepparton yameandikwa nyuma ya hiki kitabu.Kila moja inaweza kusaidia matakwa ya mtu binafsi Kwa ushirika tunaweza kutoa huduma bora ambayo inaweza kuboresha maisha yako na ya salama ndani ya Shepparton

Page 42: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

42 A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

Wasiliana nasi

Shirika Anuani Namba ya simu GV Health Graham Street,

Shepparton (03) 5832 2322

Ethnic Council Shepparton

158 Welsford Street, Shepparton

(03) 5831 2395

Family Care 19 Welsford Street, Shepparton

(03) 5823 7000

GOTAFE 152–200 Fryers Street, Shepparton

(03) 5833 2686

Greater Shepparton City Council

90 Welsford Street, Shepparton

(03) 5832 9700

Primary Care Connect

399 Wyndham Street, Shepparton

(03) 5823 3200

Kildonan UnitingCare

219-225 Wyndham Street, Shepparton

(03) 5831 6157

Vision Australia Corner Archer Street and Channel Road, Shepparton

(03) 5831 9400

Red Cross Australia

399 Wyndham Street, Shepparton

(03) 5823 3268

headspace 129 High Street, Shepparton

1800 551 800

Page 43: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre
Page 44: Swahili SWAHILI Afya yangu ndani ya Shepparton · Pap-test Ni kipimo kinachofanywa ili ... Ikiwa na maana kuwa huwezi kutumia pesa yako toka mfukoni mwako , ... Family Medical Centre

Piga 000 Kama hali yako sio nzuri au unasumbuliwa na tatizo la kiafya

A f y a y a n g u n d a n i y a S h e p p a r t o n

For more information about services provided by GV Health, visit www.gvhealth.org.au

GV Health Publication – GVH0435 Prepared By: Health Promotion Department, GV Health For review: October 2017