taarifa kwa vyombo vya habari.doc

Upload: ngabwe

Post on 09-Jan-2016

4.641 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Noves Moses

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

17/09/2015

BENKI YA POSTA TANZANIA (TPB) YAKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA AFYA UNGI MSUKA, KONDE.

Leo, tarehe 17 Septemba 2015, Benki ya Posta Tanzania (TPB) inakabidhi rasmi mradi wa kituo cha Afya cha Ungi, Ungi Shehia ya Msuka Mashariki Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, kituo ambacho Benki hiyo imedhamini ukamilishaji wake.

Kituo hicho cha afya kinatarajiwa kusaidia wananchi takriban elfu tano wanaoishi kijijini hapo, ambao wamekuwa wakitembea mwendo mrefu kuzifuata huduma hizo kwenye vijiji vya jirani.

Akiongea kwenye makabidhiano ya Kituo hicho Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba Moshingi alisema benki yake inadhamiria kuendelea kuisaidia jamii kuondokana na changamoto mbalimbali za kijamii, hususan huduma ya afya kwa mama na mtoto.

Mara baada ya kupata maombi ya kumalizia ujenzi wa kituo hiki cha Ungi kutoka Jumuiya ya Maendeleo Jimbo la Konde, tulichukua uamuzi wa haraka wa kusaidia, kwa kuelewa umuhimu wa afya kwa wananchi. Juhudi zetu hizi hazitaishia hapa, tunaahidi kuendelea kushirikiana nanyi ili kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa hapa zinawanufaisha wananchi wote kwa ajumla, alisema Moshingi.

Akizindua jengo hili, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Raisi Mhe. Mohammed Aboud Mohammed aliishukuru Benki ya Posta kwa msaada huo na kuipongeza kwa kuijali jamii. Alisema kuwa taasisi zote zinazotoa huduma ni muhimu zitambue kuwa bila wananchi huduma wanazozitoa haziwezi kuwa endelevu, hivyo akazitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa Benki ya Posta ya kuwajali wananchi wanaotumia huduma zao. Pia aliwasihi wanakijiji wa Msuka kukitumia vizuri kituo hicho kwa kukitunza.

Naye Katibu wa Jumuiya ya Maendeleo Jimbo la Konde ambao ndio watekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ungi ndugu Ismail.. Aliishukuru TPB kwa msaada huo mkubwa walioutoa na kuahidi kuwa watatumia na kutunza kituo hicho cha afya ambacho wanaamini kitakuwa mkombozi kwa wananchi wa Kijiji hicho cha Msuka na maeneo jirani.