taarifa ya utekelezaji wa mkukuta 2010/11

22
(CHANGAMOTO) MDAHALO KUHUSU SERA ZA KITAIFA TAREHE 26-27 JANUARI 2012: BLUE PEARL HOTELI UBUNGO PLAZA WIZARA YA FEDHA

Upload: amil

Post on 03-Feb-2016

160 views

Category:

Documents


1 download

DESCRIPTION

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKUKUTA 2010/11. (CHANGAMOTO) MDAHALO KUHUSU SERA ZA KITAIFA TAREHE 26-27 JANUARI 2012: BLUE PEARL HOTELI UBUNGO PLAZA WIZARA YA FEDHA. YALIYOMO. Utangulizi Utekelezaji wa MKUKUTA 2010/11 Hali halisi na Changamoto Hitimisho. UTANGULIZI - PowerPoint PPT Presentation

TRANSCRIPT

Page 1: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

(CHANGAMOTO)

MDAHALO KUHUSU SERA ZA KITAIFA TAREHE 26-27 JANUARI 2012: BLUE PEARL

HOTELI UBUNGO PLAZA

WIZARA YA FEDHA

Page 2: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

YALIYOMOUtanguliziUtekelezaji wa MKUKUTA 2010/11

Hali halisi na Changamoto

Hitimisho

Page 3: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

UTANGULIZI

Umaskini!!!!!!........ Ni nini?Ni hali ya maisha iliyo duni inayomfanya mtu kushindwa kumudu mahitaji

ya msingi. Umaskini ni matokeo ya mambo mengi yaliyochanganyika, ambayo hayakufanyika kwa tija kutokana na visababishi mbalimbali.Unapimwaje?

Kwa kuangalia viashiria vya: umaskini wa kipato; na ule usio wa kipato (mf.upatikanaji wa huduma za jamii).

Viashiria vinavyotumika kupima hali ya Umaskini ni vingi, vikiwemo: Ujinga; Huduma za jamii zisizotosheleza mahitaji (maji, afya na elimu); Vifo; Utapiamlo; Uharibifu wa mazingira; Tatizo la ajira; Kipato kidogo; na Makazi duni.

Page 4: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Sababu za UmaskiniZipo sababu nyingi za umaskini za ndani na nje.

Sababu za ndani ni pamoja na:-

Sera za Uchumi: Sera za fedha na matumizi ya Serikali kutotosheleza kukuza uchumi unaonufaisha wengi;

Huduma zisizotosheleza katika sekta ya kilimo;

Uwekezaji usiotosheleza katika viwanda mijini na vijijini;

Page 5: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Sababu za ndani… Inaend..Mapungufu katika uanzishaji na uendeshaji wa

Asasi za Kiraia zinazoanzishwa kuleta maendeleo vikiwemo vyama ushirika;

Teknolojia duni;Mila potofu na desturi zisizo na tija katika kuleta

maendeleo (ubaguzi wa kijinsia; ushirikina n.k.) Tabia ya uzembe na uvivu;Maradhi, na hasa magonjwa sugu (HIV&AIDS,

TB n.k;Idadi kubwa ya familia; Utoaji wa maamuzi usio na tija, Mila na desturi zisizo na tija.

Page 6: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Sababu za nje:Sababu za nje zinazoweza kuchangia

umaskini ni pamoja na: Kuwa na deni kubwa la Taifa;Urari mbaya katika biashara ya Kimataifa;Kuongezeka kwa wakimbizi;Mdororo wa Uchumi Duniani; na Mabadiliko ya Tabia ya nchi (Climate

change).

Page 7: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Jukumu kubwa la Serikali: Ni pamoja na kuweka mazingira bora ya kisera ili sekta

binafsi na mtu mmoja mmoja atumie fursa zilizopo kujiletea maendeleo (Maendeleo ya mtu huletwa na yeye mwenyewe).

Uandaaji na utekelezaji wa Sera na Mikakati ya kupambana na umaskini (Mkakati wa Kusimamia Sera za Kuondoa Umaskini 1998; PSRP 2000-2003; MKUKUTA I 2005 – 2010; MKUKUTA II (2010 – 2015);

Mikakati na Programu za kisekta na programu za maboresho;

Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP) (2011 – 2016);

Miongozo hii ya kisera hutoa vipaumbele kwa sekta na wadau wote kupanga na kutekeleza majukumu waliyopewa.

Page 8: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Jukumu kubwa la Serikali….InaendeleaKupitia Mfumo wa Ufuatiliaji hali ya umaskini,

mapitio ya mara kwa mara hufanyika na dosari (changamoto) zinazojitokeza huibuliwa na kujadiliwa na wadau kwa uboreshaji;

Taarifa ya Utekelezaji wa MKUKUTA na Ripoti ya Hali ya Umaskini na Maendeleo ya Watu ni miongoni mwa ripoti muhimu zitolewazo kuhabarisha wadau mafanikio na changamoto zilizopo;

Majadiliano pia hufanyika kila mwaka kama vile mapitio ya sekta za huduma ya jamii (Sector Reviews) elimu, afya na maji;

Utafiti kuhusu maoni ya wananchi (Views of the People Survey) juu ya wanayoyaona, na kupata maoni yao.

Page 9: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

2. UTEKELEZAJI MKUKUTA 2010/11MKUKUTA II ulioanza kutekelezwa mwaka jana ni

mwendelezo wa MKUKUTA I unaosisitiza: kukuza uchumi na kupunguza umaskini wa kipato, kuboresha huduma za jamii na ustawi wa jamii, na kuimarisha utawala bora na uwajibikaji;

Katika mapitio ya kila mwaka ripoti ya utekelezaji wa MKUKUTA huandaliwa kwa kushirikiana na sekta zote kuhabarisha wadau mafanikio na changamoto za utekelezaji;

Pia kupitia midahalo huu, wadau hujadili na kutoa maoni ya kuboresha utekelezaji wa malengo yaliyoainishwa katika MKUKUTA II na mipango mingine ya kisekta; na

Ripoti ya utekelezaji wa MKUKUTA 2010/11 imetoa mchango katika maandalizi ya Mwongozo wa mipango na bajeti kwa mwaka unaofuata.

Page 10: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Hali Halisi na Changamoto i. Pato la mwananchi kukua sambamba na Ukuaji

wa Uchumi Jumla; Umaskini wa kipato umepungua kwa kiwango cha 2.1%

kati ya mwaka 2001 na 2007; Ongezeko la idadi ya watu ni 2.9% kwa mwaka; Pato la Taifa (GDP) lilikua kwa 7.0% kwa mwaka 2010

ikilinganishwa na 6.0% mwaka 2009, Sekta zinazochangia kwenye GDP kwa kiasi kikubwa:

utoaji huduma 43.6%(2009) na 43.9%(2010); kilimo 24.6%(2009) na 24.1%(2010); uzalishaji viwandani 8.6%(2009) na 9%(2010);

Sekta zinazokua kwa kasi ni pamoja na mawasiliano (22.1%), sekta ya ujenzi (10.2%) sekta ya huduma ya fedha (10.1%), na sekta ya Viwanda (7.9%) mwaka 2010; na

Sekta hizo huajiri kiwango kidogo cha watu.

Page 11: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Hali Halisi na Changamoto..Inae i. Pato la mwananchi kukua sambamba na

Ukuaji wa Uchumi Jumla

Tafiti wa hali ya ajira (ILFS 2006) inaonyesha Sekta zinazokua kwa kasi, zinaajiri idadi ndogo ya watu, ikilinganishwa na sekta ya kilimo yenye kuajiri watu wengi, 74.7% ambayo inakua kwa kiwango kidogo, 4.2% mwaka 2010;

Ukuaji mdogo wa sekta zinazogusa Watanzania wengi kama vile kilimo, viwanda, mawasiliano,

Kuongeza uzalishaji, ajira, na pato la Taifa kuendelea kuimarika;

Page 12: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Hali Halisi na Changamoto..Inaeii. Upatikanaji wa nishati ya uhakika na

nafuu: Serikali imeendelea kupanua vyanzo vya

nishati ya umeme na kupanua wigo wa ushiriki wa sekta binafsi, ili kuzalisha na kusambaza umeme wa kutosha, wa uhakika na nafuu hususan kwa wazalishaji wadogo;

Kwa sasa uzalishaji wa nishati ya umeme ni pungufu ya mahitaji kwa 205Mw; mwaka 2010;(Mitambo mingi inatumia mafuta ambayo ni ghali) - gharama za nishati kuwa juu.

Page 13: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Changamoto....Inaendeleaiii.Kuimarisha usafiri wa reli na

barabara za Vijijini: Kuimarika kwa usafiri wa reli ni

muhimu kwa kipato cha watu maskini - kama njia nafuu ya kusafirisha mazao na bidhaa nyigine za biashara;

Kadhalika barabara za vijijini kuhakikisha zinapitika muda wote ili kuunganisha maeneo ya uzalishaji na masoko kwa njia endelevu zaidi, na hasa uwezo wa kujenga madaraja na barabara zenye viwango vya lami badala ya kuweka vifusi kila mwaka.

Page 14: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Changamoto.... Inaendeleaiv. Kuboresha huduma za jamii, Ubora

wa Maisha na Ustawi wa Jamii: Elimu:

Kiwango cha uandikishaji katika ngazi zote za elimu kinaendelea kuongezeka, pasipo kasi ya kutosha katika kuboresha viwango vya ubora wa elimu kwa makundi yote;

Kuimarisha mifumo ya elimu uendelezaji bora wa rasilimali watu, teknolojia na utashi katika ajira binafsi zenye tija.

Page 15: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Changamoto....Inaendeleav. Kuboresha huduma ya Afya na ustawi wa

watoto na wanawake:Idadi ya vifo vya watoto wachanga

imepungua kutoka watoto 58 (2007/08) hadi 51 (2009/10) kwa kila watoto 1000 wanaozaliwa hai (DHS 2009/10) - lengo ni 38 ifikapo mwaka 2015;

Idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua toka watoto 112 (2004/05) hadi 81 (2009/10) kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai (DHS 2009/10) - lengo ni 54 ifikapo mwaka 2015;

Page 16: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Changamoto....InaendeleaVifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi

vilipungua kutoka 578 (2004/05) hadi 454 (2009/10) kwa kila kina mama 100,000 waliojifungua watoto hai-lengo ni 265 ifikapo 2015;

Wastani wa Watoto kwa kila mama ni 5.4(2010) kutoka 5.7(2005). Lengo la MKUKUTA II ni watoto 5;

Kuendelea kuboresha kiwango cha ubora wa huduma ya afya hususan upatikanaji wa wataalam, miundo mbinu na vitendea kazi katika maeneo ya vijijini;

Page 17: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Changamoto....Inaendeleavi. Upatikanaji wa maji safi na salama na

nafuu, usafi wa mazingira na makazi bora;

Bado Serikali inayo kazi kubwa kuboresha upatikanaji wa maji safi nchi nzima, kuboresha mazingira na makazi bora. Watanzania wengi na hasa vijijini hawana maji safi na salama wengine makazi ni duni na mabadiliko ya tabia nchi kuwaathiri wengi (ukame, mafuriko n.k.)

Page 18: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Changamoto....Inaendeleavii.Kinga ya Jamii kwa Makundi maalum

Idadi ya Watanzania wanaoshindwa kumudu elimu au kujipatia ujuzi katika fani mbalimbali kuwawezesha kufanya shughuli ndogondogo za kujipatia kipato ni kubwa;

Jitihada mbalimbali za kulinda makundi maalum hazijafanikiwa vya kutosha. Sehemu kubwa ya makundi hayo haijafikiwa na huduma za msingi kuwawezesha kujimudu kimaisha, ambayo ni pamoja na:

Kuhudumia watoto yatima wasio na msaada na waishio katika mazingira magumu;

Kutoa huduma za kijamii na kiuchumi kwa watu wenye ulemavu; na

Watoto wa kike wengi wanapata ujauzito kabla ya kumaliza elimu ya msingi, au kupata watoto katika umri mdogo, na kushindwa kuwatunza.

Page 19: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Changamoto....Inaendeleaviii.Kuboresha Mifumo ya huduma za umma

Serikali imeendelea kuimarisha mifumo ya utawala katika taasisi za umma ikiwa ni pamoja na kuboresha utumishi wa umma, sekta ya sheria, kuimarisha usimamizi huduma za jamii kama vile kuunda kamati mbalimbali za kusimamia utekelezaji lakini bado maeneo mengi utekelezaji hauridhishi;

Kupeleka madaraka karibu na wananchi kwa kuimarisha Serikali za mitaa;

Kuimarisha mifumo ya usimamizi raslimali za umma; Kuimarisha mifumo ya ushirikishwaji wadau katika

kupanga mipango ya maendeleo; na Kuimarisha ufuatiliaji ikiwemo kuhakikisha fedha

zinapatikana kwa wakati, kutekeleza vipaumbele, kukusanya takwimu na kufanya tafiti za kupima mafanikio, na kutumia takwimu hizo kwa mipango ya maendeleo.

Page 20: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Hitimishoix.Kuimarisha Utekelezaji wa

mipango yetu Tunafahamu kero na changamoto zetu, Mikakati na mipango ya kutatua kero na

changamoto zetu ipo katika ngazi zote na nyingi zimo ndani ya uwezo wetu;

Tunayo amani, usalama na utulivu katika nchi,

Tunazo rasilimali watu, ardhi nzuri na maliasili za kutosha;

Sote tuchukue hatua sasa, kutekeleza yale tuliyokubaliana kwa dhati na kwa uadilifu;

Page 21: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Hitimishoix.Kuimarisha Utekelezaji wa mipango

yetu MKUKUTA II ni wetu sote, tujadili, tusimamie

kutekeleza vipaumbele na kutathmini mafanikio; Mifumo ya ufuatiliaji katika kila sekta kupewa

kipaumbele na kujengewa uwezo ; Wadau katika sehemu zote, tutafakari tulikotoka, tuko

wapi, na tunakwenda wapi na hatimaye kuchukua hatua stahiki, kila mmoja kwenye nafasi yake;

Kila mdau atambue wajibu na mchango wake, na kadri itakavyowezekana, kuongeza ufanisi;

ILI MALENGO YA MKUKUTA II YAFANIKIWE, HATUNA BUDI SOTE KUONGEZA BIDII, KUZINGATIA

UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI

Page 22: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA  MKUKUTA  2010/11

Asanteni kwa kunisikiliza,

A. Mwasha, Mkurugenzi (PED),

Wizara ya Fedha

……………MWISHO………..