taasisi ya elimu tanzania (tet) - ukuaji na ujifunzaji ... ukuaji na...ukuaji na ujifunzaji wa mtoto...

63
Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli ya Pili Taasisi ya Elimu Tanzania MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 1 25/04/2019 10:18

Upload: others

Post on 23-Nov-2020

60 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali

Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini

Moduli ya Pili

Taasisi ya Elimu Tanzania

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 1 25/04/2019 10:18

Page 2: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

ii

© Taasisi ya Elimu Tanzania, 2018

Toleo la Kwanza, 2018

ISBN: 978 - 9976 - 61 - 800 - 6

Taasisi ya Elimu TanzaniaS.L.P 35094Dar es Salaam.

Simu : +255 22 2773005 / +255 22 277 1358Faksi: +255 22 2774420Baruapepe: [email protected]: www.tie.go.tz

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kutafsiri, kupiga chapa, kurudufu au kutoa andiko hili kwa namna yoyote ile bila idhini ya maandishi ya Taasisi ya Elimu Tanzania.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 2 25/04/2019 10:18

Page 3: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

iii

Yaliyomo

Ukurasa

Utangulizi................................................................................................ iv

Shukurani ............................................................................................... ix

Orodha ya majedwali .............................................................................. x

Vifupisho.................................................................................................... xi

Sura ya Kwanza Ukuaji na ustawi wa mtoto........................................................................... 1

Sura ya Pili Ukuaji wa ubongo na ujifunzaji .................................................................. 15

Sura ya Tatu Uchangamshi wa awali ................................................................................ 25

Faharasa...................................................................................................... 49

Marejeleo .................................................................................................... 50

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 3 25/04/2019 10:18

Page 4: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

iv

Utangulizi

UsuliMafunzo kazini kwa mwalimu ni jambo la msingi sana ili kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji kufanyika kwa ufanisi. Mafunzo humuongezea mwalimu maarifa na stadi kulingana na mabadiliko yanayotokea siku hadi siku. Hivyo, ni muhimu kwako mwalimu wa elimu ya awali kupata mafunzo uwapo kazini. Mafunzo hayo yatakusaidia kujenga umahiri katika kutekeleza mtaala wa elimu ya awali kwa ufanisi na hivyo kuboresha kiwango cha elimu katika ngazi husika na ngazi nyingine zinazofuata. Sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) 2012- 2016, vimebainisha kuwa Elimu ya Awali ni moja kati ya vipaumbele vya serikali. Aidha, kila shule ya msingi inatakiwa kuwa na darasa la elimu ya awali. Mwaka 2016, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) iliboresha mtaala wa elimu ya awali. Mtaala huo ulianza kutumika rasmi mwaka 2017. Baada ya uboreshaji, baadhi ya walimu wa elimu ya awali walipata mafunzo ya namna ya kutekeleza mtaala huo.

Hata hivyo, imeonekana kuwa kuna haja ya kuwajengea uwezo walimu wote wa elimu ya awali katika ufundishaji na ujifunzaji wa mtoto. Hivyo, TET kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Aga Khan Foundation (AKF) na Shirika la Umoja wa Mafaifa la Kuhudumia Watoto “UNICEF “ waliandaa moduli za mafunzo kazini kwa walimu wa elimu ya awali kwa kuzingatia mtaala wa elimu ya awali wa mwaka 2016.

Lengo la moduliLengo la moduli hii ni kukuwezesha kupata maarifa na stadi ili kuwa na ujuzi wa namna mtoto anavyokua na kujifunza.

Mlengwa Mlengwa mkuu wa moduli hii ni mwalimu wa elimu ya awali aliye kazini. Aidha, inaweza pia kutumiwa na walimu wakuu, maafisa elimu kata, wathibiti ubora wa shule, maafisa elimu wa wilaya na wadau wengine wa elimu ya awali.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 4 25/04/2019 10:18

Page 5: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

v

Jinsi ya kutumia moduliMwalimu unatakiwa kuisoma moduli hii na kufanya kazi mbalimbali zilizoainishwa. Utashirikiana na wenzako kama itakavyokuwa imeelekezwa. Aidha, unatakiwa kuwashirikisha walimu wenzako katika changamoto mbalimbali ulizokumbana nazo katika ufundishaji na ujifunzaji ili kujadiliana kwa pamoja namna ya kuzitatua. Muundo wa moduliModuli hii imegawanyika katika sura tatu. Sura ya kwanza ni ukuaji na ustawi wa mtoto. Sura ya pili ni ukuaji wa ubongo na ujifunzaji na sura ya tatu inahusu uchangamshi wa awali. Kila sura ina utangulizi, umahiri wa kujifunza na jaribio la awali ambalo utafanya ili kujipima uelewa wako kabla ya kuanza kusoma sura husika. Vilevile, kutakuwa na maudhui utakayojifunza katika sura husika, kazi za kufanya, tafakuri na jaribio baada ya kujifunza ambalo utalifanya ili kupima ulichojifunza katika sura husika. Aidha, katika vipindi tofauti, utafanya kazi mbalimbali zilizopo mwishoni mwa moduli katika jumuiya za ujifunzaji.

Utaratibu wa utoaji wa mafunzoMuda wa mafunzo kwa kutumia moduli hii pamoja na moduli nyingine zilizomo katika mpango huu ni mwaka mmoja. Mwalimu unatarajiwa kukamilisha moduli zote nne (4) za mafunzo husika. Moduli hizo ni Utoaji wa elimu ya awali, Ukuaji na ujifunzaji wa mtoto, Uchopekaji wa masuala mtambuko katika mtaala wa elimu ya awali na Utekelezaji wa mtaala wa elimu ya awali. Pamoja na kujifunza maudhui yaliyomo katika moduli hizi unapaswa kutumia maarifa na ujuzi unaopata katika muda wote unapokuwa kazini ili kuboresha ufundishaji wa ujifunzaji wa mtoto.

Mwalimu, utakabidhiwa moduli husika na utajifunza mwenyewe katika kituo chako cha kazi. Unapaswa kusoma na kufanya kazi zote zilizoainishwa katika kila moduli. Unatakiwa pia kujipangia utaratibu wa kuzisoma moduli hizo kwa ukamilifu kwa kuzingatia muda wa mafunzo uliopangwa. Sambamba na hilo, kutakuwa na jumuiya za ujifunzaji katika ngazi ya shule na vituo vya ujifunzaji ndani ya kata ambapo mtakutana kwa ajili kubadilishana uzoefu, mafanikio na changamoto mlizokutana nazo katika ujifunzaji. Ujifunzaji katika jumuiya utaongozwa na shughuli zilizoainishwa mwishoni mwa kila moduli.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 5 25/04/2019 10:18

Page 6: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

vi

Aidha, ili kuhakikisha kwamba jumuiya za ujifunzaji zinafanyika kwa ufanisi, mnapaswa kukutana angalau mara moja kwa wiki katika ngazi ya shule, mara moja kwa mwezi katika vikundi vya walimu vya ujifunzaji ndani ya kata na mara mbili kwa mwaka katika vituo vya walimu vya ujifunzaji ngazi ya kata.

Kabla hujaanza kusoma katika kila sura, unapaswa kufanya jaribio ambalo linaakisi maudhui ya sura husika. Baada ya kujifunza maudhui ya sura hiyo utafanya tena jaribio lile lile ili kupima uelewa wako baada ya kusoma sura husika ya moduli. Vilevile, utapewa kazimradi za kufanya ambazo zitajumuishwa katika upimaji utakaofanyiwa.

Upimaji wa mafunzoUpimaji wa mafunzo utafanyika ili kubaini kama umejenga umahiri kama ilivyokusudiwa na utahusisha mambo yafutatayo:

i. Mkoba wa kazi ambao utajumuisha vitu mbalimbali kama vile kazi za vikundi, zana za kufundishia na kujifunzia, machapisho mbalimbali uliyotumia katika kujifunza na majibu ya shughuli mbalimbali ambazo umezifanya katika moduli husika.

ii. Kazimradi itahusisha zana zinazogusa umahiri sita zilizopo katika mtaala na muhtasari wa elimu ya awali ambazo zitahakikiwa mwisho wa mafunzo.

iii. Uangalizi wa ufundishaji ndani na nje ya darasa utafanyika mara tatu (3) kwa muda wote wa mafunzo. Uangalizi utafanywa na mwalimu mkuu, afisa elimu kata na mthibiti ubora wa shule. Zana itakayotumika katika uangalizi itatoka kwenye kiongozi cha mthibiti ubora wa shule.

Upimaji wa mafunzo utafanywa na mwalimu mkuu katika ngazi ya shule na afisa elimu kata katika ngazi ya kata. Aidha, wathibiti ubora wa shule ngazi ya wilaya na kanda na maafisa elimu wa wilaya na mkoa watasimamia zoezi zima la ujifunzaji na upimaji ili kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa yana ubora uliokusudiwa.

Mwalimu unapaswa kusoma na kupimwa katika moduli zote nne na kufaulu kwa kiwango kisichopungua alama C ili kuweza kutunukiwa cheti cha kukutambua kama mwalimu wa elimu ya awali uliyefuzu mafunzo kazini. Mwongozo wa upimaji utakuwa kama inavyooneshwa katika Jedwali la 1 na la 2:

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 6 25/04/2019 10:18

Page 7: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

vii

Jedwali 1: Mwongozo wa upimaji

Mkoba wa kazi KazimradiUangalizi wa

ufundishajiJumla

20 20 60 100

Jedwali 2: Viwango vya ufauluAlama Daraja Kiashirio75 – 100 A Bora64 – 74 B Vizuri sana44 – 63 C Vizuri35 – 43 D Inaridhisha0 – 34 F Dhaifu

Ufuatiliaji na tathmini ya mafunzo Kwa kuwa mafunzo yatafanyika katika ngazi ya shule na vituo vya ujifunzaji ndani ya kata, walimu wakuu, maafisa elimu kata, wathibiti ubora wa shule na maafisa elimu wa wilaya ndio watakaokuwa wafuatiliaji wakuu wa mafunzo haya. Kutakuwa pia na ufuatiliaji katika ngazi ya taifa ikijumuisha TET, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) kitengo cha mafunzo ya ualimu na idara ya usimamizi wa elimu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI).

Tathmini ya utekelezaji wa Programu ya Mafunzo Kazini kwa walimu wa elimu ya awali itafanyika baada ya kumaliza mafunzo. Lengo la tathmini hii ni kuona kama mafunzo yametekelezwa kama yalivyopangwa na kubaini changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji kwa ajili ya kuboresha. Tathmini hii itahusisha wadau mbalimbali kuanzia ngazi ya shule hadi taifa. Zana za kufanyia tathmini zitaandaliwa na TET kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali. Baada ya tathmini kukamilika, maboresho yatafanyika katika maeneo yanayohusika na mafunzo yataendelea. Tathmini zitafanyika pale inapobidi kulingana na mahitaji.

Tafsiri ya alama Katika moduli hii kuna alama mbalimbali zinazokuwezesha kutambua shughuli zinazotakiwa kufanyika wakati wa usomaji.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 7 25/04/2019 10:18

Page 8: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

viii

Alama Maelezo

Lengo au malengo yanayopaswa kufikiwa na msomaji wa programu hii katika sura

Zingatia vidokezo au wazo muhimu na kulikumbuka

Maswali ya kujiuliza kabla au hata wakati wa kuendelea kusoma

Muhtasari uliotolewa kuhusu sura inayohusika

Marejeleo yaliyotumika ambayo yanapendekezwa uyasome ili kuelewa zaidi

Tafakuri ambayo utaifanya katika sura inayohusika

Kazi ya kufanya

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 8 25/04/2019 10:18

Page 9: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

ix

Shukurani

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inatambua na kuthamini mchango muhimu wa washiriki waliofanikisha uandishi wa moduli hii ya Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali.

TET inatoa shukurani za dhati kwa mchango uliotolewa na wataalamu wafuatao walioshiriki kutayarisha moduli hii:

Waandishi: Deborah Llewellyn, Vida Ngowi, Masumbuko Mpoli, Sharifa Majid, Sauda Hamis, Hanifa Mponji, Mathias Suwi, Flora Henjewele, Manjula Jogy, Christina Kamamba, Dkt. Richard Shukia, Davis Gisuka, Dkt. Daphina Mabagala, Rehema Mwawa, Nestory Mgimwa, Eric Kilala, Sr. Cecilia Boniface, Wesket Mlagulwa, Dkt. Tandika Pambas, Edith Mdoe na Lomitu Mollel

Wahariri: Dkt. Lyabwene Mtahabwa na Ambrose F. Maghanga

Msanifu: Rehema H. Maganga

Wachoraji: Alama Art and Media Production

Mratibu: Vida Ngowi

Aidha, TET inatoa shukurani za pekee kwa Shirikia la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ‘UNICEF’ na Aga Khan Foundation (AKF) kwa kufadhili uandishi na ujaribishaji wa moduli hii.

Mwisho, TET inatoa shukurani kwa Global Partnership for Education (GPE) chini ya mpango wa kuboresha ufundishaji wa stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) unaojulikana kama Literacy and Numeracy Education Support (LANES) kwa kufadhili uhakiki na uchapaji wa moduli hii.

......................................Dkt. Aneth A. Komba Mkurugenzi MkuuTaasisi ya Elimu Tanzania

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 9 25/04/2019 10:18

Page 10: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

x

Orodha ya Majedwali

Jedwali Na 1: Mwongozo wa upimaji ................................................... vii

Jedwali Na 2: Viwango vya ufaulu ....................................................... vii

Jedwali Na 3: Mabadiliko ya ukuaji wa mtoto (miaka 4-5) ..................... 8

Jedwali Na 4: Tabia za watoto na afua stahiki ........................................ 33

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 10 25/04/2019 10:18

Page 11: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

xi

Vifupisho

AKF - Aga Khan Foundation

GPE - Global Partnership for Education

KKK - Kusoma, Kuandika na Kuhesabu

LANES - Literacy and Numeracy Education Support

MMEM - Mpango wa Maendeleo ya Elimu Msingi

OR-TAMISEMI - Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

TET - Taasisi ya Elimu Tanzania

UNICEF - United Nations Chidren's Fund

WyEST - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 11 25/04/2019 10:18

Page 12: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 12 25/04/2019 10:18

Page 13: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

1

Sura ya Kwanza

Ukuaji na ustawi wa mtoto

Katika sura hii utajifunza dhana ya ukuaji wa mtoto, hatua za ukuaji wa mtoto, nyanja za ukuaji, changamoto za ukuaji na utatuzi wake. Vilevile, utajifunza juu ya mabadiliko ya ukuaji wa mtoto katika vipindi tofauti vya makuzi yake.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii, utaweza:i. kuelezea dhana ya ukuaji wa mtotoii. kubainisha nyanja za ukuaji na maendeleo ya mtotoiii. kueleza mambo yanayoathiri ukuaji wa mtoto.

Jaribio kabla ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo kabla ya kuanza kujifunza maudhui ya sura hii:1. Je, unaelewa nini kuhusu dhana ya ukuaji wa mtoto?

2. Kutokana na uzoefu wako, elezea hatua za ukuaji wa mtoto.

3. Fafanua nyanja za ukuaji wa mtoto.

4. Eleza changamoto za ukuaji wa mtoto na namna ya kukabiliana nazo.

1.1 1.1 Dhana ya ukuaji wa mtoto

Je, unaelewa nini kuhusu ukuaji wa mtoto?

Pamoja na majibu uliyonayo, dhana ya ukuaji wa mtoto inafafanuliwa kuwa ni mchakato ambao kila mtoto anapitia tangu kutungwa kwa mimba, kipindi cha mimba, na baada ya kuzaliwa kuelekea utu uzima. Ukuaji wa mtoto unahusisha kukua kiakili, kimwili, kihisia na kijamii ambavyo vyote huchochewa na mabadiliko ya kibaiolojia na mazingira. Ili mtoto aweze kukua vizuri kabla na baada ya kuzaliwa,

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 1 25/04/2019 10:18

Page 14: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

2

anahitaji lishe bora, malezi bora, uchangamshi wa awali, upendo, mazingira rafiki na huduma bora za afya. Hivyo ni muhimu kuelewa namna mtoto anavyokua na kujifunza ili uweze kukidhi mahitaji ya kila mtoto katika ufundishaji na ujifunzaji wake.

1.2 Nyanja za ukuaji wa mtoto

1.2 Baada ya kuifahamu dhana ya ukuaji wa mtoto, inakupasa pia kufahamu nyanja za ukuaji wa mtoto. Ukuaji wa mtoto umegawanyika katika nyanja tofauti.

Je, unaelewa nini kuhusu nyanja za ukuaji wa mtoto?

Pamoja na majibu uliyonayo, mtoto hukua katika nyanja za kimwili, kiakili, kijamii, kihisia na lugha.

1.2.1 Ukuaji wa mtoto kimwili

Ukuaji wa mtoto kimwili unahusisha ongezeko la mwili katika uzito na kimo pamoja na utendaji wa misuli mikubwa na midogo. Stadi za kukuza misuli midogomidogo inahusisha uwezo wa kuutawala mwili na uhusiano kati ya viungo na matendo anayofanya mtoto; kwa mfano, uhusiano wa macho na mikono ambayo inasaidia kufanya shughuli nyingi muhimu ndogondogo. Shughuli hizi kwa watoto zinajumuisha kufunga na kufungua kamba za viatu, zipu, vifungo, kufungua kurasa za kitabu, kuokota vitu, kushikilia vitu, kuchora, kudaka mpira mdogo na kupaka rangi. Shughuli nyingine zinazosaidia kukuza misuli midogomidogo ya watoto ni kama vile kukoroga, kupima, kumimina na kuchota. Matendo haya humwezesha mtoto kutumia na kukuza misuli midogo ya mikono na vidole. Mwalimu, unapaswa kuwapa watoto shughuli za ziada zitakazosaidia kukuza misuli hiyo kwa sababu inawajengea stadi za kuandika.

Ukuaji wa misuli mikubwa unajumuisha shughuli kama vile kutembea, kukimbia, kusukuma na kurusha. Mifano mingine ni kama kunyanyua, kutupa, kubiringisha na kucheza ndani ya maji. Aidha, shughuli kama kuruka, kukimbia, kurusha, kudaka, kucheza mpira wa miguu na mikono humsaidia mtoto kukuza misuli mikubwa.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 2 25/04/2019 10:18

Page 15: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

3

Mwalimu, unapaswa kuhakikisha kuwa kila siku unawapa watoto shughuli zitakazohusisha misuli mikubwa kwa ajili ya kujenga afya zao kimwili na kiakili.

1.2.2 Ukuaji wa mtoto kiakiliUkuaji wa mtoto kiakili ni uwezo wa mtoto unaohusisha kujifunza, kukumbuka, kufikiri, kutatua matatizo na kufanya maamuzi. Unapaswa kuandaa shughuli za watoto ambazo zitawasaidia kukua kiakili kwa kutoa vifaa vinavyoendana na umri na uwezo wao wa kuvitumia. Mfano wa shughuli hizo ni kupanga vibao vidogo, vibao fumbo na michezo ya bodi. Kadiri mtoto anavyoendelea kukua na kujifunza, mpatie shughuli zinazochochea udadisi na zinazomfikirisha zaidi ili kuendeleza ujifunzaji wake. Mfano, unaweza kuandaa shughuli zitakazomwezesha mtoto kutatua changamoto mbalimbali.Mtoto anapokua kiakili huonesha dalili zifuatazo:

i. kuongezeka kwa kiwango cha uwezo wa kufikiri ii. kutambua mambo mbalimbali iii. kuweza kutatua matatizoiv. kuongezeka kiwango cha udadisi v. kuwa na umakini katika kufikiri, kuamua na kutendavi. kutofautisha, kulinganisha na kukumbukavii. ukuaji wa lugha kwa kujifunza maneno na kuongezeka kwa msamiativiii. usikivu

1.2.3 Ukuaji wa mtoto kijamii na kihisia

Ukuaji wa mtoto kijamii na kihisia ni uwezo wa mtoto wa kuchangamana, kujenga uhusiano na wenzake, kufanya mambo mwenyewe bila msaada wa mtu mwingine na kujitawala. Ukuaji wa mtoto katika eneo hili hujengwa na silka na tabia inayotokana na kurithi, malezi na utamaduni. Unapaswa kuwapa watoto shughuli zitakazowasaidia kujenga tabia ya kubadilishana zamu katika michezo, kuvumiliana, kucheza kwa kushirikiana, kutengeneza marafiki na kujali wengine. Mfano wa shughuli hizo ni kama vile igizodhima, kusimuliana hadithi, michezo ya pamoja na kazi za vikundi.

Kumbuka kuwa nyanja hii ni muhimu sana katika kumjengea mtoto uwezo wa kujifunza, kufanya majaribio, kufanya uamuzi sahihi na kujiamini. Nyanja hii isipokuzwa vizuri inaathiri ukuaji wa nyanja nyingine. Hivyo, hakikisha kuwa

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 3 25/04/2019 10:18

Page 16: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

4

unatoa kazi mbalimbali zitakazomsaidia mtoto katika kukuza nyanja hii. Kwa mfano, watoto kucheza katika kona ya nyumbani, usimuliaji wa hadithi na michezo ya nje ya darasa humpa fursa ya kushirikiana na wenzake katika utendaji. Pia, inakupasa kujenga uhusiano chanya kati yako na watoto kwa kushirikiana nao katika kazi mbalimbali.

1.2.4 Ukuaji wa lugha

Ukuaji wa lugha ni mchakato wa mtoto kusikiliza kwa umakini, kuelewa, kuwasiliana au kuelezea hisia zake kwa kutumia lugha. Lugha ina nafasi kubwa katika ujifunzaji wa mtoto kwa sababu ukuaji wa lugha una uhusiano wa karibu na ukuaji wa ubongo. Lugha inamsaidia mtoto kuweza kuchangamana na jamii, kujifunza kutoka katika mazingira na kupokea maelekezo mbalimbali kutoka kwa wengine. Pamoja na kuwa Kiswahili ni lugha rasmi ya kufundishia Elimu ya Awali, kuna maeneo ambayo bado lugha ya asili ya eneo linalohusika inachukua nafasi kubwa. Hivyo, mwalimu una nafasi ya kutumia lugha inayozungumzwa katika eneo linalohusika pale inapobidi wakati wa ufundishaji na ujifunzaji, ili kuwasaidia watoto katika kipindi cha mpito kuelekea kujifunza lugha ya Kiswahili na kuzoea mazingira ya shule. Hii itawasaidia kujiamini na kuongeza msamiati katika lugha ya Kiswahili. Katika kukuza stadi ya lugha, mwalimu unatakiwa uzingatie stadi nne za lugha.

Wape watoto kazi zitakazosaidia kukuza stadi za lugha kama ifuatavyo:

i. Stadi ya kusikiliza: Stadi hii inajumuisha uwezo wa kusikiliza milio ya sauti za wanyama na vitu vilivyopo katika mazingira yao. Ni uwezo wa kubaini sauti na milio mbalimbali ya vitu, watu, na wanyama katika mazingira.

Je, ni mambo gani muhimu ya kuzingatia katika kujifunza na kukuza stadi ya kusikiliza kwa makini?

Ili kukuza stadi ya kusikiliza ni muhimu kuzingatia mambo mawili yafuatayo: a. Uwezo wa kiakili wa mtoto: Si rahisi kumfundisha mtoto kusikiliza

kwa makini iwapo uwezo wake wa kiakili ni wa chini.b. Uwezo wa kusikia wa mtoto: Ni vigumu kumfundisha mtoto kusikiliza

kwa makini iwapo uwezo wake wa kusikia ni wa chini au hasikii kabisa.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 4 25/04/2019 10:18

Page 17: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

5

Stadi za kusikiliza ambazo ni muhimu kuzikuza kwa mtoto ni:• Kusikiliza• Kutambua sauti• Kutofautisha sauti za aina mbalimbali• Kutafsiri sauti, ili kutambua aina ya ujumbe unaoelezwa.

1. Elezea namna mtoto anavyoweza kutambua sauti ili kumjengea Stadi ya kusikiliza.

2. Je, unafahamu nini kuhusu mbinu za kuwafundishia watoto kutambua sauti?

ii. Stadi ya kuzungumza: Stadi hii inajumuisha kujieleza, kuimba, kuuliza na kujibu maswali, kutoa maoni, kusimulia hadithi na kuelezea matukio.

Jinsi ya kukuza uwezo wa stadi ya kuzungumza

Ni muhimu sana kwa watoto wadogo kusaidiwa katika kukuza uwezo na stadi ya kuzungumza wanapokuwa katika darasa la elimu ya Awali. Kwa vile, wengi wao Kiswahili ni lugha ya pili ya mawasiliano hasa kwa watoto walio vijijini. Ukuaji wa stadi ya kuzungumza hutegemea mazingira ya sehemu husika na kiwango ambacho Kiswahili kinazungumzwa katika mazingira hayo.

Jinsi mtoto anavyojifunza kuzungumza

Mtoto hujifunza kuzungumza kwa njia zifuatazo:a. nyimbo b. hadithic. kusikiliza na kuelezea aliyoyasikiad. kuiga kuongea maneno anayoyasikiae. kuyasema anayoyasikia kwa kurudiarudia yeye mwenyewef. kusimulia anayoyaona au kuyasikia kwenye vyombo vya habari mfano

runinga, redio na video

Maneno anayoyasikia mtoto huweza kubakia katika kumbukumbu yake wakati atakapoweza kujenga dhana. Ukweli huu unabaki kuwa hivyo, hata anapojifunza

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 5 25/04/2019 10:18

Page 18: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

6

lugha ya pili. Kwa hiyo, unashauriwa kutumia zana za kufundishia kama vile vielelezo vya picha, vitu halisi na pia vitendo vya mara kwa mara. Kwa vile watoto wengi ambao umri wao haujafikia miaka mitano, wana uwezo mdogo wa kujifunza sarufi ya lugha, basi inashauriwa walimu au wazazi/walezi waanze kuwafundisha lugha watoto kwa kuwapa mazoezi madogomadogo ya kuzungumza hasa kwa njia ya michezo. Michezo hii inaweza kuwa ya mtoto mmoja au ya vikundi. Ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo katika kumsaidia mtoto kujenga stadi ya kuzungumza:

• kutenga muda wa kuzungumza na mtoto• kutumia miundo rahisi iliyo sahihi • kutoa majibu kwa maswali mbalimbali ya watoto• kusisitiza mazungumzo miongoni mwa watoto katika michezo na

ujifunzaji

iii. Stadi ya kusoma: Stadi ya kusoma hujumuisha kubaini chapa, kusoma picha, kusimulia hadithi kwa kuangalia picha na kujenga msamiati mpya. Stadi ya awali ya kusoma ni ujuzi ambao mtoto anatakiwa kuwa nao ili amudu kujifunza kusoma kwa urahisi. Mtoto huanza kujifunza stadi hii tangu anapokuwa nyumbani. Unapofika wakati wa kuanza kujifunza kusoma herufi, kasi hujengeka kwa urahisi zaidi. Hii ni kwa sababu anakuwa ameipitia misingi yote ya kusoma kwa njia ya matendo mengine na hivyo anapoanza kujifunza hakawii kuelewa kusoma herufi.

iv. Stadi ya kuandika: Stadi hii hujumuisha kuchora mistari, michoro mbalimbali, kuchora picha na kuzipaka rangi, kuandika namba na herufi.

Kuandika ni stadi ya kuweka dhana, wazo au ujumbe katika maumbo sauti yaitwayo herufi ili yaweze kusomwa na watu. Ujenzi wa stadi za awali za kuandika ni hatua ya kumjengea mtoto umahiri muhimu anaotakiwa kuwa nao ili aweze kujifunza kuandika kwa urahisi.

Mtoto hawezi kujua kuandika bila kujengewa uwezo. Tendo la kuandika kwa mara ya kwanza kwa mtoto si jambo rahisi. Kwa kawaida, ukimpa mtoto kalamu kwa mara ya kwanza anaweza kushika vibaya; hapo ndipo unagundua kuwa stadi hizi ni muhimu sana kwao.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 6 25/04/2019 10:18

Page 19: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

7

Kumbuka kuwa nyanja hizi za ukuaji zinategemeana. Hivyo, ni muhimu unapompa mtoto kazi uzingatie nyanja zote. Kwa mfano, katika kuwasomea watoto hadithi, watoto watakuza nyanja ya lugha na mawasiliano kwa kuelezea kile walichosikia au kilichowafurahisha. Pia, watakuza nyanja ya ukuaji wa kihisia na kijamii kwa kuonesha hisia zao kutokana na hadithi. Vilevile, nyanja ya ukuaji kiakili itamwezesha mtoto kuwa msikivu na kuweka kumbukumbu ya kile alichosikia. Kimwili, mtoto atashiriki katika matendo mbalimbali kutokana na hadithi iliyosimuliwa. Katika kuhakikisha mtoto anakuwa katika uhusiano mzuri na mwalimu, unatakiwa kuonesha upendo ili wajihisi kuthaminiwa. Kujenga mazingira rafiki ni jambo muhimu katika ukuaji wa mtoto katika nyanja zote.

1.3 Hatua za ukuaji wa mtoto

1.3 Ukuaji wa mtoto hupitia katika hatua mbalimbali. Hatua hizo ni kabla na baada ya kuzaliwa.

Je, unaelewa nini kuhusu hatua za ukuaji wa mtoto kabla na baada kuzaliwa?

Ukuaji wa mtoto kabla ya kuzaliwa huanzia pale mimba inapotungwa hadi mtoto anapozaliwa. Kipindi hiki ni cha miezi 9 au wiki 38. Ili mtoto aweze kukua vizuri, mama mjamzito anahitaji lishe bora, upendo, matibabu na mazingira safi na salama. Hivi vyote kwa pamoja huwezesha viungo vya mtoto kuundwa na kukamilika; ingawa viungo hivyo vinakuwa bado havijakomaa. Vilevile, ni vema wazazi watarajiwa wawe na afya njema na wafanye maandalizi mazuri ili mimba itakapotungwa, iwe yenye kumfanya mtoto aweza kukua vizuri.

Hatua za ukuaji wa mtoto baada ya kuzaliwa huanza mara tu mama mjamzito anapojifungua. Hatua hii hufahamika kama “Utoto uchanga” ambao ni kuanzia kuzaliwa hadi miaka miwili. Katika umri huu mtoto hufanya matendo kutokana na silka za kimaumbile kama vile kulia, kunyonya, kunusa, kugusa, kuchezesha miguu na mikono na kufumba macho. Katika umri wa miaka 3-6, kiwango cha kufikiri huongezeka; huanza kutofautisha matendo mema na mabaya na kutambua vitendo vya maadili mema katika jamii. Katika umri wa miaka 6-8 uwezo wa mtoto wa kudadisi mambo huongezeka. Pia, mtoto hujifunza na kufundishwa mambo

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 7 25/04/2019 10:18

Page 20: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

8

mbalimbali na kuyaelewa kwa urahisi. Mtoto katika umri huu anahitaji kuwa na marafiki ambao ni sehemu ya kundi rika. Lifuatalo ni jedwali linaloonesha mabadiliko ya ukuaji wa mtoto wa miaka 4-5

Jedwali Na 3: Mabadiliko ya ukuaji wa mtoto (miaka 4-5)

Umri Mabadiliko ya UkuajiMiaka Kijamii/Kihisia Kiakili Kimwili Lugha

4-5 • Kufanya matendo madogo madogo ya kihaiba

• Kujieleza mwenyewe (mahitaji yake na uzoefu katika mazingira yake ya kila siku)

• Kutambua majukumu ya watu wengine

• Kucheza kwa kuzingatia jinsi

• Kucheza na watoto wengine na kutengeneza marafiki

• Kuchukua idadi sahihi ya vitu

• Kutaja na 1-9 kuhesabu namba mpaka 20 kwa kukariri na kuelewa

• Kutofautisha vitu

• Kutambua rangi za msingi

• Kutambua nyakati na matukio

• Kuoanisha maumbo ya namba na idadi ya vitu

• Kupanga herufi kwa mfuatano

• Kuumba herufi • Kuandika jina lake

• Kutambua mahali kitu kilipo

• Kujaza kibao fumbo

• Kucheza michezo (ya hiyari ya pekee, jozi na vikundi)

• Kuigiza, kutupa na kudaka, kuruka, kukimbia, kumwaga na kujaza

• Kufunga na kufungua vifungo kwa usahihi

• Kuvaa na kuvua nguo mwenyewe

• Kuchora picha inayoeleweka mfano nyumba, mtu

• Kujaza kibao fumbo chenye vipande vingi

• Kupaka rangi kwa usahihi

• Kufinyanga

• Kuwa na msamiati wa kutosha wa lugha yake

• Kupenda masimulizi, hadithi na mikasa

• Kupenda kuuliza maswali

• Kujua nyimbo mbalimbali na kupenda kuziimba

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 8 25/04/2019 10:18

Page 21: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

9

Ni muhimu kutambua kwamba mabadiliko ya ukuaji wa mtoto hutofautiana kutoka mtoto mmoja hadi mwingine hata kama ni wa umri mmoja na kutoka jamii moja hadi nyingine. Vilevile, hatua za ukuaji zinaweza kuathiriwa na mambo mbalimbali ikiwamo magonjwa, kipato cha familia, lishe duni, mazingira au urithi. Kwa ujumla, mazingira yanayomzunguka mtoto yana nguvu kubwa katika kutoa mwelekeo wa ukuaji wa mtoto.

Je, kwa nini inampasa mwalimu kufahamu hatua za ukuaji wa mtoto?

Pamoja na majibu yako, ni dhahiri kuwa, unapaswa kuwa na ufahamu wa hatua za ukuaji wa mtoto ambao utakusaidia kuelewa uwezo wake kulingana na umri wa mtoto. Hivyo, utaweza kuwapa shughuli mbalimbali kwa kuzingatia mambo wanayoweza kuyatenda na kuendeleza ujifunzaji wao. Kumbuka kuwa kuna msemo usemao “Tambaa kabla ya kutembea na tembea kabla ya kukimbia”, hii ina maana kwamba ukuaji wa mtoto katika nyanja zote unapitia hatua moja baada nyingine.

1.4 Mambo yanayoathiri ukuaji na maendeleo ya mtoto

Siku 1000 za maisha ya mtoto tangu kutungwa kwa mimba ni hatua muhimu sana ya ukuaji wa mtoto. Kipindi hiki huhusisha ukuaji kimwili, kiakili kijamii na kihisia. Mambo yanayotokea katika kipindi hiki yana mchango mkubwa katika ukuaji na ujifunzaji wa mtoto. Mambo haya yanahusisha lishe, tabia za wazazi au walezi, malezi, mazingira, mambo ya kijamii na kiutamaduni.

Eleza umuhimu wa kila moja ya mambo hayo kwa ukuaji na maendeleo ya mtoto

Pamoja na majibu yako, maelezo yafuatayo yanafafanua umuhimu wa kila kipengele kilichobainishwa.

i. Lishe Lishe bora ni muhimu sana kwa mama mjamzito kabla na baada ya kujifungua kwa ajili ya ukuaji mzuri wa mtoto. Iwapo mama mjamzito hatapata lishe bora, mtoto

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 9 25/04/2019 10:18

Page 22: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

10

atakayezaliwa hatakua vizuri. Upungufu wa lishe bora na afya duni ya mama wakati wa ujauzito vinaathiri ukuaji wa ubongo wa mtoto.

Maziwa ya mama ni chakula bora kwa mtoto mdogo. Maziwa haya yanampa mtoto virutubisho muhimu vinavyohitajika katika ukuaji. Unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo ni muhimu sana kwa mtoto kwa kuwa unasaidia kuboresha afya na ukuaji wake. Maziwa ya mama yanasaidia katika ukuaji wa ubongo wa mtoto na hivyo kukuza uwezo wake kiakili. Hivyo ni dhahiri kwamba lishe bora kwa mtoto kabla na baada ya kuzaliwa ina mchango mkubwa katika ukuaji na ujifunzaji wake.

Baada ya miezi sita mtoto anapaswa kupewa chakula kingine pamoja na maziwa ya mama. Katika kipindi hiki mtoto apatiwe chakula stahiki, kinachotosheleza mahitaji yake na kwa muda muafaka. Mtoto anapoendelea kukua anapaswa kupata virutubisho stahiki na kwa kiwango kinachotakiwa ili kumsaidia katika ukuaji wake.

Umuhimu wa lishe katika kipindi cha utotoni Mambo muhimu katika maendeleo ya awali ya kukua kwa mtoto ni lishe stahiki ya kutosha, yenye mwendelezo na yenye mwitikio chanya.

Lishe ni jambo muhimu linalotakiwa kutiliwa mkazo katika kipindi cha utotoni. Lishe duni ni chanzo kikubwa cha magonjwa ambapo hudumaza ukuaji wa watoto kimwili na kiakili na hivyo kupunguza uwezo wa kufanya vizuri shuleni. Mfano wa madhara ya kiafya kutokana na lishe duni ni pamoja na utapiamlo, upungufu wa vitamin A, upungufu wa damu pamoja na upungufu wa madini joto. Lishe duni inaweza kuwa ni matokeo ya kipato kidogo, imani za kimila na desturi au ukosekanaji wa chakula bora. Kubadilisha imani za wazazi na mazoea yao kunahitaji mwitiko wa uhalisia wa mambo na ubunifu. Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa ukuaji wa mtoto:

a. Ni muhimu mtoto kupata kifungua kinywa chenye virutubishob. Watoto wanahitaji protini zaidi, mfano mayai, maharagwe na maziwac. Watoto wanahitaji vitamini A na E ambazo zinapatikana katika

machungwa na mbogamboga

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 10 25/04/2019 10:18

Page 23: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

11

Ni muhimu kufahamu uelewa wa wazazi na vipaumbele katika milo yao. Pia, ni muhimu kuwauliza ni kwa kiwango gani wanaweza kufikia malengo yao. Kufanya hivyo kutasaidia shule kuunganisha kile wanachojua wazazi na kusaidia kupata maarifa zaidi juu ya lishe. Kujua kwa kina madhara ya upungufu wa lishe bora kunahitaji mazungumzo na wazazi ili kujua matatizo yanayokwamisha upatikanaji wa lishe bora kwa watoto wao. Kwa mfano, wazazi wanaweza kuondoka mapema kwenda shambani wakawaacha watoto wajivalishe wenyewe na kujitafutia chochote cha kula kabla hawajaenda shule.

Walimu wazungumze na wazazi wakubaliane kwamba watoto wapate kifungua kinywa nyumbani kabla ya kwenda shule na wapate chakula cha mchana wakiwa shuleni. Wataalamu wa afya na lishe wana wajibu wa kushauri juu ya aina ya vyakula vinavyopatikana katika maeneo husika na jinsi ya kuviandaa. Ili kulinda afya za watoto himiza mambo yafuatayo:

• kuosha mikono kabla na baada ya kula• kula pamoja mahali pasafi • kula chakula kinachoandaliwa shuleni kwa pamoja• watoto kutoleta shuleni vitu vidogovidogo vya kula kwa mfano pipi

na biskuti kwa sababu huchangia kuharibu meno na kuambukizana magonjwa.

Katika maeneo ambayo kuna utapiamlo, kuna uwezekano wa

kushirikisha asasi za kijamii na zisizo za serikali kuchangia lishe bora shuleni hususani kwa watoto wa elimu ya awali. Katika mazingira ambayo chakula hutolewa shuleni, watoto wakatazwe kuleta vyakula au vitu vidogovidogo vya kula kutoka nyumbani.

Udumavu na jinsi unavyoathiri afya ya mtoto

Unaelewa nini kuhusu neno kudumaa?

Kudumaa ni hali ambayo inasababishwa na lishe duni ambapo humuathiri mtoto katika ukuaji wake kimwili na kiakili. Madhara ya lishe duni utotoni yanaweza kusababisha matatizo ya kiafya ya kudumu maishani. Familia nyingi hazina uelewa

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 11 25/04/2019 10:18

Page 24: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

12

kwamba mtoto aliyedumaa maisha yake huwa hatarini kama hatua za kumsaidia hazitachukuliwa. Lishe bora na ya kutosha ni haki ya mtoto. Wazazi/walezi wanatakiwa kutambua kwamba lishe bora ni jambo muhimu kwa maisha ya mtoto. Hivyo wazazi/ walezi wanatakiwa kuwapa watoto lishe bora.

Utajuaje kama mtoto amedumaa?

Ili kujua mtoto aliyedumaa, bainisha umri sahihi na mabadiliko ya ukuaji wake. Dalili za mtoto aliyedumaa mara nyingi zinaweza kuwa ni uzito mdogo na ukuaji mdogo wa umbo kulingana na umri wake, ukuaji mdogo wa akili unaosababisha maendeleo hafifu katika ujifunzaji wake na kushambuliwa na magonjwa ya mara kwa mara ikiwemo kuharisha.

ii. Tabia za wazazi/waleziTabia za wazazi/walezi zina athari katika ukuaji wa mtoto. Kwa mfano; uvutaji wa sigara wakati wa ujauzito au kukaa katika mazingira yenye moshi wa tumbaku una athari kwa mama na mtoto pia. Vilevile, utumiaji wa vileo wakati wa ujauzito una athari kubwa katika ukuaji wa mtoto kabla na baada ya kuzaliwa na hata katika ujifunzaji wake. Mtoto anayekulia katika familia ambayo ina watu walevi na wavuta sigara huathirika kisaikolojia. Vilevile tabia hizi za wazazi au walezi huathiri uwezo wa mtoto wa kujifunza na ukuaji wake kwa ujumla. Tabia za ulevi huchangia kukosa uangalizi na hivyo kuongeza uwezekano wa mtoto kutengeneza marafiki wabaya.

iii. Malezi ya wazazi/waleziUkuaji na ujifunzaji wa mtoto unategemea malezi anayopata kutoka kwa mzazi/mlezi wake. Ni wazi kuwa, ili mtoto aweze kujifunza, anahitaji kupata malezi mazuri kutoka kwa wazazi au walezi wake kama vile upendo, lishe, uchangamshi wa awali na usalama. Mtoto akikosa vitu hivi, anaweza kuathirika katika ukuaji wake kimwili, kijamii, kihisia, kiakili na hata katika ukuaji wa lugha. Vilevile, inaweza kusababisha msongo wa mawazo. Hivyo, ni vema kuyatambua mahitaji haya ili kumsaidia mtoto aliyekosa malezi bora aweze kushiriki katika ujifunzaji kama watoto wengine.

iv. Masuala ya kijamii na kiutamaduniIli kufanikisha tendo la ufundishaji na ujifunzaji kwa ufanisi ni muhimu, kuwajua

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 12 25/04/2019 10:18

Page 25: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

13

watoto wako ukizingatia masuala ya kijamii na kiutamaduni. Masuala haya yanaathiri ukuaji na ujifunzaji wa mtoto darasani. Kwa mfano, baadhi ya jamii huwakataza watoto kula baadhi ya vyakula kama mayai. Vilevile, kuna baadhi ya jamii mtoto mdogo hatakiwi kuongea au kuhoji kitu kwa wakubwa. Endapo mtoto atafanya hivyo huadhibiwa kwa utovu wa nidhamu. Hali hii ikikithiri huathiri uwezo wa mtoto kujiamini, kufikiri na kupenda kudadisi au kuuliza maswali.

v. Masuala ya kimazingira

Je, mazingira mazuri kwa mtoto ni yapi?

Suala la mazingira kwa mtoto ni muhimu sana katika ukuaji wake. Kwa mfano, eneo lililoathiriwa na uchafuzi wa mazingira kama vile machimbo ya madini, maeneo ya kutupa takataka ya viwanda vikubwa na yenye majitaka husababisha magonjwa ya kuambukiza na hivyo kuathiri ukuaji wa mtoto. Mazingira mazuri kwa watoto hujumuisha upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa na huduma za afya. Mpango wa Elimu ya Awali ni lazima uhakikishe upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa na kuhamasisha watoto wanywe maji mara kwa mara.

Je, utatumia mikakati gani endelevu itakayoshirikisha wazazi/walezi na jamii kuondoa changamoto za ukuaji wa mtoto?

Dhana ya ukuaji wa mtoto imefafanuliwa kuwa ni mchakato ambao kila mtoto anapitia tangu kutungwa kwa mimba, kipindi cha mimba, baada ya kuzaliwa kuelekea utu uzima. Ukuaji wa mtoto unahusisha kukua kiakili, kimwili, kihisia na kijamii ambavyo vyote huchochewa na mabadiliko ya kibiolojia na mazingira. Ili mtoto aweze kukua vizuri kabla na baada ya kuzaliwa, anahitaji lishe bora, malezi bora, uchangamshi wa awali, upendo, mazingira rafiki na huduma bora za afya. Hivyo ni muhimu kuelewa namna mtoto anavyokua na kujifunza ili uweze kukidhi mahitaji ya kila mtoto katika ufundishaji na ujifunzaji wake.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 13 25/04/2019 10:18

Page 26: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

14

Jaribio baada ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo baada ya kujifunza maudhui ya sura hii:1. Je, unaelewa nini kuhusu dhana ya ukuaji wa mtoto?

2. Kutokana na uzoefu wako, elezea hatua za ukuaji wa mtoto.

3. Fafanua nyanja za ukuaji wa mtoto.

4. Eleza changamoto za ukuaji wa mtoto na namna ya kukabiliana nazo.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 14 25/04/2019 10:18

Page 27: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

15

Sura ya Pili

Ukuaji wa ubongo na ujifunzaji

Katika sura hii utajifunza kuhusu uhusiano wa ukuaji wa ubongo na ujifunzaji. Mambo ambayo utajifunza ndani ya sura hii, ni dhana ya ukuaji wa ubongo katika ujifunzaji, mahitaji katika ukuaji wa ubongo, mambo yanayoathiri ukuaji wa ubongo na namna mtoto anavyojifunza kupitia vitendo mbalimbali.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utaweza:i. kufafanua dhana ya ukuaji wa ubongo katika ujifunzajiii. kueleza mahitaji ya ukuaji wa ubongo iii. kufafanua mambo yanayoathiri ukuaji wa ubongo na

ujifunzajiiv. kueleza namna mtoto anavyojifunza kupitia vitendo

mbalimbali

Jaribio kabla ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo kabla ya kuanza kujifunza maudhui ya sura hii:1. Je, unaelewa nini kuhusu ukuaji wa ubongo wa mtoto?2. Bainisha sababu zinazoweza kuathiri ukuaji wa ubongo wa mtoto.3. Fafanua mahitaji ya msingi yanayoweza kumsaidia mtoto katika

ukuaji wa ubongo.

4. Eleza uhusiano uliopo kati ya ukuaji wa ubongo na ujifunzaji wa mtoto.

2.1 Dhana ya ukuaji wa ubongo na ujifunzaji

Je, unafahamu nini kuhusu ukuaji wa ubongo na ujifunzaji?

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 15 25/04/2019 10:18

Page 28: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

16

Pamoja na majibu yako, ni vema kufahamu kwamba tafiti kuhusu ukuaji wa ubongo na ujifunzaji zimejikita katika kuangalia mambo mbalimbali yanayoathiri ukuaji wa ubongo na ujifunzaji. Tafiti hizi zinaonesha kuwa wastani wa uzito wa ubongo wa mtu mzima ni Kilogramu 1.4, uzito huu unakaribia asilimia 2-5 ya uzito wote wa mwili. Ubongo unakuwa tayari umeshaanza kukua tokea mtoto akiwa tumboni na unakuwa na robo ya uzito wa ubongo wa mtu mzima.

Uzoefu katika mazingira na uchangamshi wa awali unachochea ukuaji wa ubongo na ujifunzaji. Mtoto anapozaliwa anakadiriwa kuwa na nyuroni zipatazo bilioni 100, ila nyuroni hizi hazifanyi kazi mpaka ziunganishwe. Miunganiko ya nyuroni huchochewa na kutumika mara kwa mara katika kipindi cha awali cha makuzi ya mtoto. Pale nyuroni zinapokuwa hazijaunganishwa (kupitia uzoefu, uchangamshi) kwa kawaida huwa zinapotea. Katika miaka ya awali ya maisha ya mtoto nyuroni milioni moja zinaweza kuungana kwa kila dakika. Baada ya kipindi hiki, muungano wa nyuroni unapungua.

Kielelezo namba 1: Ukuaji wa nyuroni na maendeleo ya ubongo.

Chanzo: Corel, J.L (1975). The Postnatal Development of the Human Cerebral cortex. Cambridge,

MA: Havard University Presa)

Katika kipindi cha miaka ya awali ambapo nyuroni zinaunganishwa kwa kasi kubwa mtoto anatengeneza stadi za kutenda, hisia ya kujitambua, uhusiano na wengine, stadi za lugha, kudadisi na muendelezo wa kujifunza.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 16 25/04/2019 10:18

Page 29: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

17

Kituo cha Makuzi ya MtotoCHUO KIKUU CHA HARVARD

Muunganiko wa mishipa ya fahamu kwa kazi tofauti hukua kwa mpangiliaoUkuaji wa Ubongo wa Binadamu

-8-7-6-5-4-3-2-1

Kuzaliwa

Njia za mishipa ya fahamu(Kuona, Kusikia)

LughaUwezo mkubwa wa utendaji

(Miezi) (Miaka)

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19

MWAKAWA KWANZA

CHANZO: C.A. Nelson (2000)

Kielelezo namba 2: Mpangilio unaoonesha ukuaji wa mishipa ya fahamu kulingana na kazi tofauti.

Chanzo: C. A. Nelson (2000).

Ubongo wa mtoto unakua kutokana na mwitikio wa vinasaba na mazingira. Uhusiano uliopo kati ya vinasaba na uzoefu anaopata mtoto katika mazingira yake vinachangia ukuaji wa ubongo. Hivyo, ni vema kufahamu kuwa familia na jamii zina mchango mkubwa katika kuwezesha ukuaji wa ubongo wa mtoto ili aweze kujifunza. Kwa hiyo inakupasa kusoma na kujifunza juu ya tafiti za ukuaji wa ubongo.

Je, kuna umuhimu gani kujifunza kuhusu tafiti za ukuaji wa ubongo?

Pamoja na majibu uliyonayo, tafiti za ukuaji wa ubongo zinakusaidia kujua mahitaji ya ukuaji na ujifunzaji wa mtoto na kutoa afua stahiki. Vilevile, zinakusaidia kuandaa mazingira rafiki yatakayochochea ukuaji na ujifunzaji wa mtoto wa awali.

Ukuaji wa Ubongo wa BinadamuMuunganiko wa mishipa ya fahamu kwa kazi tofauti hukua kwa mpangilio

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 17 25/04/2019 10:18

Page 30: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

18

Ubongo unaanza kukua kabla ya mtoto kuzaliwa na huendelea kukua muda wote wa maisha baada ya kuzaliwa. Ipo tofauti ya ukuaji wa ubongo baina ya mtu mmoja na mwingine. Hii haishangazi, kwani hata miili yetu inakua tofauti.

Hii inatokana na tofauti iliyopo kuhusu namna ubongo unavyofanya kazi kati ya mtoto mmoja na mwingine. Kwa mfano, mtoto X anaweza kuwa na uwezo mkubwa katika kujieleza lakini ana uwezo mdogo katika namba. Wakati mtoto Y, ana uwezo mkubwa katika namba lakini ana uwezo mdogo katika kujieleza.

Pamoja na kwamba darasani kwako una watoto ambao umri wao unalingana, haimaanishi kwamba utayari wao wa kujifunza upo sawa. Tambua kwamba namna ubongo unavyofanya kazi kati ya mtoto mmoja na mwingine ni tofauti. Hivyo basi, ni muhimu kuelewa ukuaji wa ubongo wa mtoto ili uweze kuandaa shughuli na kupanga mbinu na mikakati ya kutumia wakati wa ufundishaji ukizingatia msingi wa tatu katika ufundishaji unaosisitiza kwamba kila mtoto anajifunza kulingana na uwezo wake.

2.2 Mahitaji katika makuzi ya ubongo

Kuna mahitaji gani muhimu yanayosaidia makuzi ya ubongo wa mtoto?

Kuna mahitaji mengi ya msingi anayopaswa kupata mtoto ili ubongo wake uweze kukua kikamilifu. Baadhi ya mahitaji hayo ni lishe bora, afya, uchangamshi wa awali, malezi bora, mapumziko, maji safi na salama. Kwa kawaida mtoto hujifunza mambo mengi zaidi kipindi cha umri wa miaka 0 hadi 5. Uzoefu wa utendaji wa kila siku husisimua hisia za mtoto na hivyo kuchochea kwa kiasi kikubwa makuzi ya ubongo.

Ubongo huendelea kubaki wazi ukisubiri ushawishi wa mazingira kadri mtoto anavyoendelea kukua. Namna ubongo unavyokua unafananishwa na jinsi mti unavyokua ukitegemea mwanga wa jua, maji na aina ya udongo. Vivyo hivyo, ili mtoto akue anahitaji mazingira rafiki yenye lishe na malezi bora.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 18 25/04/2019 10:18

Page 31: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

19

Kielelezo namba 3: Namna ukuaji wa ubongo unavyofananishwa na mti unavyoitikia mazingira yake katika kukua.

2.3 Mambo yanayoathiri ukuaji wa ubongo na ujifunzaji

Tafiti zinaeleza kuwa, ubongo unaweza kuchakata taarifa kwa haraka zaidi pale ambapo kutakuwa na muungano mkubwa zaidi wa nyuroni. Hata hivyo, ujifunzaji wa mtoto unaweza kuathiriwa na mambo mbalimbali kama vile lishe, malezi, mazingira, uchangamshi wa awali, mapumziko, msongo wa mawazo, vitisho na hisia. Yafuatayo ni maelezo mafupi kuhusu msongo wa mawazo na hisia.

2.3.1 Msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo unaathiri vipi ukuaji wa ubongo wa mtoto?

Ni dhahiri kuwa mwendelezo wa vitisho husababisha msongo wa mawazo na kuathiri amani na upendo wa mtoto. Mtoto anapokuwa na msongo wa mawazo na mwendelezo wa vitisho, huathirika katika ukuaji wa ubongo na ujifunzaji. Hali ya

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 19 25/04/2019 10:18

Page 32: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

20

msongo husababisha kuzaliwa kwa homoni ya msongo iitwayo ‘‘cortisol’’, ambayo huvuruga ukuaji wa neva. Msongo wa muda mrefu huharibu uwezo wa mtoto katika kujifunza na kudumaza afya ya mwili wake. Hii ni kwa sababu msongo unapunguza uchukuaji wa virutubisho katika chakula kwa ajili ya ukuaji wa ubongo.

Mazingira yanayosababisha msongo wa mawazo shuleni au nyumbani huathiri ujifunzaji wa mtoto. Msongo pia husababisha uchukuaji wa kiwango kidogo cha virutubisho kwenye chakula ambapo matokeo yake ni kupata utapiamlo na udumavu. Msongo wa kudumu au msongo sumu unaweza kujengeka kutokana na mambo kama vile:

i. Mazingira yenye vurugu ambayo huweza kumwathiri mtoto kimwili kiakili, kisaikolojia na kijinsia

ii. Shambulio la mwiliiii. Unyanyasaji wa kijinsiaiv. Kuonewav. Mtoto kutojaliwa na wazazi au familia yake. Hii humuathiri kihisia na

kimwilivi. Kifo cha mwanafamiliavii. Maumivu ya mwili ya muda mrefuviii. Kulazimishwa kufanya mambo na tabia zilizo nje ya uwezo wake

Kielelezo namba 4: Mtoto mwenye msongo wa mawazo.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 20 25/04/2019 10:18

Page 33: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

21

Unawezaje kumsaidia mtoto, kuzuia msongo wa mawazo ili aweze kujifunza kwa ufanisi?

Ili kuchochea ukuaji wa ubongo na ujifunzaji wa mtoto, unapaswa kuzuia msongo kwa kuandaa mazingira rafiki ya ufundishaji na ujifunzaji kama vile:

i. Kutotumia viboko au kutoa maoni yenye udhalilishaji kwa mtotoii. Kutumia michezo mbalimbali katika ufundishaji na ujifunzaji wa mtotoiii. Kuzingatia utulivu wakati wa kushusha pumzi ili watoto watulieiv. Kuwapa watoto motisha kwa kila shughuli wanayofanyav. Kushirikisha wazazi/walezi na jamii kwa kuwapa elimu juu ya athari ya

matumizi ya vitisho na adhabu kali kwa mtoto katika ujifunzaji wakevi. Uandaliwe utaratibu wa kupewa chakula

2.3.2 Hisia na ujifunzaji

Kuna uhusiano mkubwa kati ya hisia na ujifunzaji. Hisia huathiri kumbukumbu na urejeshwaji wa taarifa zilizohifadhiwa. Kwa kupitia mazingira wezeshi yenye kutia moyo, unaweza kuboresha ukuaji wa kihisia na kijamii kwa mtoto.

Je, unawezaje kudhibiti hisia za mtoto ili kuchochea ujifunzaji wake?

Mambo yafuatayo yanaweza kumsaidia mtoto kudhibiti hisia na kuchochea ujifunzaji. Mambo hayo ni:

i. Mazingira ya darasani ambayo yanakuza mtazamo chanya kati ya mtoto na mtoto, mtoto na mwalimu

ii. Hadithi kuonesha matokeo ya hisia iii. Lugha laini na nyepesi inayoonesha kujali wakati unapozungumza na

mtotoiv. Vikundi vidogovidogo ili kuhamasisha uhusiano chanya baina ya mtoto

na mtoto

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 21 25/04/2019 10:18

Page 34: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

22

2.4 Ujifunzaji kwa njia ya vitendo

Unaelewa nini kuhusu dhana ya ujifunzaji kwa vitendo?

Ujifunzaji ni mchakato wa kupata ujuzi unaopelekea kubadilika kwa mwenendo au tabia kutokana na uzoefu au kufundisha. Zifuatazo ni aina tatu za ujifunzaji:

i. Kujifunza kwa kuona na kusoma maandishiii. Kujifunza kwa kusikia sautiiii. Kujifunza kwa vitendo na mazoezi:

Mtoto hujifunza kwa kutumia vitendo au michezo mbalimbali bila yeye kujua. Kwa mfano, kwa kutumia kibao fumbo mtoto anajifunza dhana tofauti kama vile rangi, maumbo, wanyama na hesabu. Mtoto anapocheza michezo ya nje kama vile kuruka, kukimbia na kubiringika anajifunza stadi mbalimbali kama sayansi, lugha na dhana za kihisabati. Kushiriki katika shughuli mbalimbali kupitia kona za ujifunzaji. Vilevile kwa kupitia kona za ujifunzaji mtoto anashiriki katika shughuli mbalimbali.

Ili uhakikishe kuwa watoto wanajifunza kwa vitendo wakati wote, inabidi kutekeleza mambo yafuatayo:

i. kuwa mwezeshaji katika ujifunzaji wa mtoto ambapo utawapa fursa ya kuchunguza, kutafuta, kuhoji, kujaribu na kukuza uelewa wao wa dhana mbalimbali

ii. kuandaa mazingira ili watoto wahamasike kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali na kujenga stadi muhimu

iii. kuwapa watoto uhuru wa kuchagua michezo wanayopendelea na kuwapa majukumu, mfano kuwa kiongozi wa darasa, kikundi au katika shughuli nyingine

iv. kuwawezesha watoto kujenga umahiri wakiwa peke yao au na wenzao kwa kuzingatia uwezo wao ndani na nje ya darasa

v. kuwaongoza watoto kufanya kazi mmojammoja, wawiliwawili au katika vikundi kwa kujadiliana, kushirikiana na kuheshimu maoni ya wengine

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 22 25/04/2019 10:18

Page 35: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

23

vi. kupanga darasa kwa kuzingatia shughuli inayofanywa, idadi ya watoto na nafasi iliyopo

vii. kuandaa kona za ujifunzaji ili kutoa fursa kwa watoto kuzitumia na kujenga umahiri.

Unatakiwa kubuni mazingira stahiki ili kusaidia ufundishaji na ujifunzaji wa mtoto kwa lengo la kufikia umahiri unaokusudiwa. Vilevile, katika kufikia lengo la ujifunzaji wa mtoto, zingatia misingi ifuatayo ya ufundishaji na ujifunzaji:

i. ufundishaji na ujifunzaji katika Elimu ya Awali hufanyika kwa vitendo ii. ukuaji na ujifunzaji vinahusiana iii. maendeleo ya ukuaji wa mtoto na ujifunzaji yanategemea ushirikiano

wa mwalimu, familia na jamii inayomzunguka iv. kila mtoto anajifunza kulingana na uwezo wake v. kuzingatia usafi na usalama wa mtoto na mazingira ya kufundishia na

kujifunzia.

Fikiri kisha andika namna lishe, uchangamshi wa awali, mapumziko na maji safi na salama yanavyochangia katika ukuaji wa ubongo wa mtoto.

Eleza namna maudhui ya sura hii yalivyoweza kubadilisha fikra zako juu ya ukuaji wa ubongo na ujifunzaji wa mtoto wa Elimu ya Awali.

Umejifunza dhana ya ukuaji wa ubongo katika ujifunzaji, mahitaji katika ukuaji wa ubongo, mambo yanayoathiri ukuaji wa ubongo na ujifunzaji na namna mtoto anavyojifunza kupitia vitendo mbalimbali. Umeona kwamba ubongo unakuwa tayari umeshaanza kukua tokea mtoto akiwa tumboni na unakuwa na robo ya uzito wa ubongo wa mtu mzima. Aidha, uzoefu katika mazingira na uchangamshi wa awali unachochea ukuaji wa ubongo na ujifunzaji. Hivyo ni muhimu sana kwako mwalimu kuyaelewa masuala haya.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 23 25/04/2019 10:18

Page 36: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

24

Jaribio baada ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo baada ya kujifunza maudhui ya sura hii:1. Je, unaelewa nini kuhusu ukuaji wa ubongo wa mtoto?

2. Bainisha sababu zinazoweza kuathiri ukuaji wa ubongo wa mtoto.

3. Fafanua mahitaji ya msingi yanayoweza kumsaidia mtoto katika ukuaji wa ubongo.

4. Eleza uhusiano uliopo kati ya ukuaji wa ubongo na ujifunzaji wa mtoto.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 24 25/04/2019 10:18

Page 37: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

25

Sura ya Tatu

Uchangamshi wa awali

Karibu katika sura ya tatu inayohusu uchangamshi wa awali. Katika sura hii utajifunza dhana ya uchangamshi wa awali, matendo ya uchangamshi, utambuzi wa mapema wa mahitaji ya mtoto na utoaji wa afua stahiki kwa mtoto na namna utakavyoshirikisha jamii katika utoaji wa afua stahiki.

Baada ya kujifunza maudhui ya sura hii utaweza:i. kueleza dhana ya uchangamshi wa awali

ii. kubaini matendo ya uchangamshi

iii. kufanya utambuzi wa mapema na kutoa afua stahiki

iv. kushirikisha jamii katika masuala yahusuyo uchangamshi wa awali.

Jaribio kabla ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo kabla ya kuanza kujifunza maudhui ya sura hii.1. Eleza mambo yanayochochea uchangamshi wa awali.

2. Fafanua namna mtoto anavyoweza kujifunza kupitia michezo.

3. Ni mambo gani ambayo walimu na wazazi/walezi wanaweza kushirikiana katika kuchochea uchangamshi wa awali kwa watoto?

3.1 Dhana ya uchangamshi wa awali

Unaelewa nini kuhusu uchangamshi wa awali?

Uchangamshi wa awali ni jumla ya mambo yote yanayomwezesha mtoto kupata fursa za kushiriki kikamilifu katika kutenda mambo mbalimbali. Uchangamshi wa awali unahusisha matendo mbalimbali yanayofanywa na wazazi/walezi pamoja na walimu kwa mtoto. Matendo hayo ya ujifunzaji humjengea mtoto uwezo wa

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 25 25/04/2019 10:18

Page 38: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

26

kufikiri, kutatua matatizo, kuwa mbunifu, kujenga misuli, kupambanua vitu na kujenga uwezo wa kujieleza. Baadhi ya matendo changamshi ambayo wazazi/walezi, walimu na jamii wanapaswa kuyafanya ni pamoja na kuzungumza, kuimba, kusimulia hadithi, kucheza, kuonesha upendo na ukaribu, na kutumia vifaa mbalimbali vya kujifunzia. Pamoja na matendo hayo, uchangamshi wa awali unahusisha uwepo wa mazingira changamshi kwa watoto. Mazingira chamgamshi ni sehemu ya kujifunzia iliyoandaliwa ambapo ujifunzaji na udadisi wa mtoto huchochewa na mazingira hayo.

Kielelezo namba 1. Mazingira ya ndani ya Darasa la Elimu ya Awali.

3.2 Matendo ya uchangamshi

3.2 Matendo changamshi kwa watoto ni kama vile kuimba, kucheza, kuonesha upendo na faraja.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 26 25/04/2019 10:18

Page 39: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

27

3.2.1 Kuimba na watoto

Watoto hufurahia nyimbo na midundo kwa sababu inasisimua na kuvuta usikivu na hisia. Nyimbo huchangamsha ubongo na kutunza kumbukumbu na hivyo kuwezesha tendo la ujifunzaji. Mwalimu inakupasa kubuni nyimbo katika shughuli unazoandaa kwa watoto na wakati wa kuimba waongoze watoto kufanya matendo. 3.2 2 Kucheza na watoto

Tangu kuzaliwa mtoto hupenda michezo. Michezo humsaidia mtoto kuwa mtendaji mkuu pamoja na kuyaelewa mazingira na kuyatumia katika ujifunzaji wake.

Kwa nini michezo inasisitizwa katika ujifunzaji wa mtoto?

Michezo ni shughuli inayomwezesha mtoto kutenda na kuwa mbunifu katika kujenga taswira, kujenga dhana mbalimbali, kukua kimwili, kiakili na kijamii. Michezo kwa mtoto ni kazi kama zilivyo kazi nyingine. Michezo humjengea mtoto utayari wa kujifunza, moyo wa kujituma, kushirikiana na kupenda kujifunza. Mtoto anapocheza, ubongo wake hufanya kazi zaidi kwa sababu anaruhusu hewa ya oksijeni kuingia kwa wingi katika ubongo na hivyo kusababisha utendaji mzuri wa ubongo. Uchezaji wa mtoto ndiyo ujifunzaji wake. Michezo ya watoto imegawanywa katika aina tofauti kwa kutegemeana na muktadha wa uchezaji. Baadhi ya michezo hiyo ni:

i. Michezo huruMichezo hii, hujumuisha michezo yote ambayo watoto hucheza bila kuongozwa na mtu mwingine. Michezo huru hutokana na msukumo wa ndani wa mtoto kwa vile anaipenda na kuifurahia. Katika michezo hii mara nyingi mtoto huchezea vifaa ambapo hufanya majaribio, kuchunguza na kugundua kuwa vitu vilivyomo katika mazingira yake vinaweza kumsaidia kujifunza na kujenga dhana mbalimbali. Michezo hii hujumuisha michezo ya kujenga, kupanga vitu, kupaka rangi, kuchora, kuumba, kuwinda/kutega wadudu ambao si hatarishi, kuunda vitu pamoja na michezo ya burudani. Aidha, michezo hii haina kanuni na hailengi kwenye ushindani bali ni kwa ajili ya kumfurahisha mtoto na kumwezesha kujifunza.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 27 25/04/2019 10:18

Page 40: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

28

ii. Michezo ya kijamiiMichezo ya kijamii huchezwa na mtoto kwa ushirikano na wengine. Michezo hii huibua hisia, stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuhesabu. Mfano wa michezo hii ni kama vile kombolela, maigizo, ngoma, rede, mdako, maigizo dhima pamoja na nyimbo mbalimbali za watoto. Kumbuka kuwa michezo hii ni muhimu sana katika ukuaji na ujifunzaji wa mtoto; hivyo, hakikisha kila mtoto anashiriki katika michezo kwa kuwahamasisha na kuwapongeza hasa wale wenye aibu na wenye mahitaji maalumu.

iii. Michezo ya kutumia nguvu

Michezo hii mara nyingi huchezwa katika maeneo ya nje. Michezo hii husaidia ukuaji wa misuli mikubwa na midogo na hukuza mawasiliano kati ya vitendo na mwili. Pia, mtoto hujifunza baadhi ya kanuni za michezo kama vile kushirikiana, kuvumiliana, kusameheana, kukubali kushindwa, kucheza kwa zamu na kukubali kukosolewa. Michezo hii, husaidia kusisimua ubongo wa mtoto na kumfanya kuwa tayari katika ujifunzaji. Mifano ya michezo ya kutumia nguvu ni kukimbia, kucheza michezo mbalimbali inayohusisha mpira, kupanda na kuteleza, kurusha mpira, kuogelea, kulenga shabaha, kukimbia, kuruka na kuvuta kamba.

Pamoja na michezo hiyo, andaa vifaa stahiki vitakavyotumiwa na watoto katika michezo. Vifaa hivyo viwe na sifa stahiki ili viweze kuchochea ari ya watoto kuvitumia na hatimaye kuweza kujifunza. 3.2.3 Kuonesha upendo na faraja

Watoto wanahitaji kuoneshwa upendo na malezi mazuri kutoka kwa walimu, wazazi/walezi na jamii. Hali hii ina mchango mkubwa katika uchangamshi wa awali wa mtoto. Baadhi ya matendo yanayoonesha upendo kwa watoto ni kama vile kuwathamini, kuwasikiliza, kuwarekebisha kwa upendo na kuwapongeza pale wanapofanya vizuri. Vilevile, kuwapatia malezi bora ambayo ni chakula, mahali pazuri pa kulala, matibabu, kulindwa, maji safi na salama na mazingira salama. Kwa kufanya hivyo, watoto wanajihisi salama, huru na kujisikia wapo karibu na watu waliowazunguka. Kwa ujumla, hali hii inaongeza uwezo wa watoto kujifunza na kukua kiakili na kimwili.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 28 25/04/2019 10:18

Page 41: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

29

3.3 Utambuzi wa mapema na utoaji wa afua stahiki

Katika ufundishaji wa Elimu ya Awali, mwalimu unapaswa kuwa na uelewa wa kufanya utambuzi wa mapema na kutoa afua stahiki kwa watoto ili uweze kuboresha ukuaji na ujifunzaji wao.

3.3.1 Utambuzi wa mapema i. Dhana ya utambuzi wa mapema

Unaelewa nini kuhusu utambuzi wa mapema?

Utambuzi wa mapema ni utaratibu wa kubainisha na kutambua watoto wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye ulemavu na vipaji maalumu ili uweze kuwapa msaada unaostahili. Utambuzi wa mapema unasaidia kubaini watoto ambao wana matatizo ya ukuaji na ujifunzaji ambayo yanaweza kuleta kikwazo au kumweka mtoto katika hatari. Utambuzi wa mapema wa matatizo ya ujifunzaji ya mtoto unaweza kukusaidia kutoa msaada unaotakiwa mapema na kuwezesha mafanikio ya baadaye ya mtoto shuleni na nje ya shule. Unapaswa kujua dalili za mapema ambazo zinamweka mtoto katika hatari ya kupata matatizo ya ujifunzaji na pia kuelewa taratibu za ukuaji wa mtoto. Taratibu hizi, zitakusaidia kufanya utambuzi wa mapema na namna ya kutoa afua stahiki.

Je, utajuaje kama mtoto ana matatizo katika ujifunzaji?

Katika Elimu ya Awali, watoto wanajifunza katika viwango na mtindo tofauti. Iwapo mtoto ana matatizo katika kusoma picha, kutambua namba, herufi au ana shida katika baadhi ya matamshi, anaweza kuwa na matatizo ya ujifunzaji. Mfano, mtoto mwenye matatizo ya ujifunzaji anaweza kuelewa hadithi vizuri wakati inasomwa lakini baadae anashindwa kujibu maswali. Mtoto pia anaweza kuimba wimbo herufi a-z lakini ukimpa herufi moja kuisoma hawezi.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 29 25/04/2019 10:18

Page 42: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

30

Kwa kawaida watoto wenye matatizo ya ujifunzaji wana akili za kawaida au za ziada ila wanapata shida kueleza wanachoelewa. Kwa kuwa ni vigumu kwa watoto hawa kuweza kufanya shughuli fulani, hali hii huwafanya wawe na hasira, kuchanganyikiwa, kutojiamini na kupata msongo. Mtoto anaweza kujua kitu gani anataka kufanya, mfano kusoma, kuandika au kufanya tendo fulani lakini jinsi ya kufika hapo ni lazima ahangaike/azunguke, hawezi kwenda moja kwa moja.

Matatizo ya ujifunzaji yamegawanyika katika makundi matatu:a. Matatizo ya kuzungumza au lugha b. Matatizo katika stadi za kusoma, kuandika au kuhesabuc. Matatizo mengine ya kukosa utulivu, stadi za utendaji na kumbukumbu

Kwa kawaida, mtoto anaweza kuwa na tatizo moja la ujifunzaji, mfano tatizo la kusoma au kufanya hesabu. Lakini pia, mtoto anaweza kuwa na matatizo ya ujifunzaji zaidi ya moja. Matatizo ya kukosa utulivu sio tatizo la ujifunzaji lakini watoto wenye matatizo ya ujifunzaji mara nyingi wanakosa utulivu katika kujifunza.

Dalili zinazoonesha kuwepo kwa matatizo ya ujifunzaji kwa watoto ni pamoja na:i. kuchelewa kuongea

ii. matatizo ya matamshi

iii. tatizo katika kujifunza maneno mapya

iv. matatizo ya kujifunza kusoma

v. matatizo ya kujifunza namba, alfabeti, rangi na maumbo

vi. kutokuwa makini

vii. kutofuata maelekezo

viii. kushindwa kushika kalamu

ii. Namna ya kufanya utambuzi wa mapema Kuna mbinu mbalimbali za kufanya utambuzi wa mapema kwa mtoto. Hata hivyo, mbinu ya uchunguzi ndiyo inayopendekezwa kwako kuitumia. Ni muhimu kujifunza kuchunguza na kurekodi tabia na kuweka kumbukumbu kwa maelezo yenye mantiki nzuri. Taarifa za uchunguzi zinakusaidia katika mambo mbalimbali kama ifuatavyo:

a. Kubaini chanzo cha tatizo (sio tu la mtoto bali hata mazingira yake na watoto anaohusiana nao)

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 30 25/04/2019 10:18

Page 43: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

31

b. Kupata uelewa mzuri wa malengo, hisia na tabia ya mtotoc. Kupata taarifa kuhusu shughuli wanazofanya watoto na namna

wanavyofanyad. Kurudia kufanya uchunguzi kwa kipindi fulani kuona namna ukuaji wa

mtoto unavyoendeleae. Matokeo ya uchunguzi yanaweza kutumika wakati wa kujadili maendeleo

ya mtoto katika ujifunzaji ukiwa na wazazi/walezi au wataalamu.

Unapomchunguza mtoto ni vizuri kukaa, kumwangalia na kumsikiliza. Watoto wanaonesha hisia zao wakati wanapofanya shughuli. Wanawasiliana kupitia sauti, namna ya ukaaji, alama na muonekano wa uso. Wakati wa kufanya uchunguzi ni vizuri kuchunguza kila anachokifanya mtoto bila kumwingilia sana katika utendaji wake ili aone ni hali ya kawaida. Kitu cha msingi sana katika uchunguzi wa mtoto ni kuangalia kile anachofanya mtoto badala ya kile unachodhani anatakiwa kufanya. Unatakiwa kurekodi taarifa kutokana na matendo anayofanya na kugundua mabadiliko ya tabia ya mtoto.

Kwa kuwa ni vigumu kuchunguza kila mtoto anachofanya, unatakiwa kufikiria taarifa muhimu unazotaka kupata kuhusu mtoto. Yafuatayo ni baadhi ya maswali ambayo yanaweza kukuongoza wakati wa kufanya uchunguzi:

a. Je, mtoto anaishi katika mazingira gani? Ni shughuli gani nyingine zinafanyika katika mazingira hayo?

b. Mtoto anatumiaje vifaa katika shughuli anazotenda? Anachukua muda kuanza kuvitumia au anatumia mara moja? Je, anatumia vifaa kama kawaida au kwa namna nyingine, kwa kuvichunguza?

c. Je, mtoto anafurahia anachokifanya? Anazingatia anachokifanya au anaangalia wenzake wanachofanya? Anatumia muda gani kuzingatia? Anabadili shughuli mara ngapi?

d. Je, miondoko ya mtoto ikoje? Mwili wa mtoto unakakamaa au unalegea? Miondoko yake ina mpangilio gani?

e. Je, mtoto anaweza kufanya mazoezi kwa kutumia viungo kutoka kushoto kwenda kulia mfano kupeleka mkono kutoka kushoto kwenda kulia na kinyume chake na kudaka mpira?

f. Je, Mtoto anazungumzaje? Anaongea, anaimba na kutumia maneno yasiyo na maana akiwa anafanya shughuli? Anatumia sentensi au neno moja? Mtoto anawasilianaje na wenzake kwa maneno au ishara?

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 31 25/04/2019 10:18

Page 44: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

32

g. Je, mtoto anajisikiaje kwa anachokifanya? Anafurahia? Anaridhika? Anahitaji msaada au kuhimizwa? Anajaribu mambo mapya mwenyewe au anasubiri kusaidiwa?

h. Je, mtoto anaishije na wenzake? Anacheza mwenyewe, na baadhi ya watoto au na watoto tofauti? Yuko au hayuko tayari kushirikiana na wenzake kuchezea midoli? Anaanzisha wazo au anasubiri wenzake waanzishe? Anakuwa huru kumuuliza mwenzake kuhusiana na kile anachofanya?

i. Kuna mabadiliko gani kati ya mwanzo na mwisho wa shughuli? Je, hisia za mtoto zinabadilika kadiri anavyofanya kazi?

j. Mtoto ana uhusiano gani na wewe? Je, anapenda kukuona? Yuko tayari kukuambia alichokifanya au anachokifanya?

k. Mtoto ana uhusiano gani na wazazi wake? Je, anapenda kuwaona akirudi nyumbani? Yuko tayari kuwashirikisha anachofanya?

3.3.2 Utoaji wa afua stahiki

Afua stahiki katika muktadha huu ni utaratibu wa utoaji huduma maalumu stahiki zinazolenga kupunguza au kuondoa changamoto za ukuaji na ujifunzaji kwa mtoto mwenye mahitaji maalumu. Ni muhimu kutambua kuwa kila afua stahiki inayotolewa inapaswa iendane na mahitaji ya kila mtoto. Utoaji wa afua stahiki mapema unasaidia:

i. Kutatua matatizo ya ujifunzaji kabla hayajawa makubwa na kusababisha madhara mengine kama vile ya kitabia na kihisia

ii. Kufundisha stadi husika kwa kutumia mbinu zinazozingatia uwezo na kufanyia kazi uhitaji uliogundulika

iii. Kuboresha utendaji katika maeneo ya ujifunzaji.

Kwa uelewa zaidi, unaweza kupitia maandiko mbalimbali yatakayokuwezesha kubainisha watoto wenye mahitaji maalumu na afua stahiki zinazohitajika kutolewa.

Fikiri kisha andika namna utakavyobaini watoto wenye mahitaji maalumu na namna utakavyotoa afua stahiki.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 32 25/04/2019 10:18

Page 45: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

33

Jedwali lifuatalo linaonesha tabia mbalimbali za watoto wenye mahitaji maalumu na afua stahiki zinazoweza kutolewa.

Jedwali Na 4: Tabia za watoto na afua stahiki

Dalili/Tabia Afua stahiki

Ana uwezo mkubwa sana kuliko wengine katika kundi rika lake.

• Mpe kazi nyingi kulingana na uwezo wake• Mpe majukumu darasani

Anauliza maswali mengi • Msikilize kwa makini kisha mjibu kwa kumpa maswali ya kumfikirisha

• Mrekebishe bila kumvunja moyo na umsaidie kupata jibu sahihi

Huchagua vitendo ambavyo wenzake huona vigumu

• Mpe vifaa nyumbufu• Mpe nafasi ya kuwasaidia wengine

Huwa mkali na hupigana na wenzake

• Mpe nasaha mfano mwelekeze awe mvumilivu

• Mweleze athari za kupigana• Wasiliana na wazazi/walezi wake

Hapendi kushirikiana na wenzake na kuonekana kuwa na mawazo (dalili za msongo wa mawazo)

• Mwalimu kutembelea familia na kuona mazingira anayoishi mtoto

• Kujenga uhusiano wa karibu na mtoto ili uweze kutambua tatizo

• Wasiliana na mzazi/mlezi kuimarisha uhusiano na mtoto kwa kumjali

Kutojiamini • Kumpongeza katika jambo alilofanya• Kumpa nafasi ya kujieleza katika

shughuli mbalimbali darasani

Maendeleo duni katika nyanja zote

• Kujenga uhusiano wa karibu na mtoto ili uweze kutambua tatizo

• Mwalimu kutembelea familia na kuona mazingira anayoishi mtoto

• Ushirikiano kati ya shule na wazazi/walezi

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 33 25/04/2019 10:18

Page 46: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

34

Kulala kila wakati darasani • Mpe kazi za kumshughulisha.• Kujenga uhusiano wa karibu na mtoto na

mzazi/mlezi ili uweze kutambua tatizo

Uchokozi • Asomewe kanuni za darasani kila mara• Mpe kazi nyingi za kufanya• Aelezwe athari za uchokozi• Mpe majukumu ya uongozi

Kukosa utii • Kujenga mahusiano ya karibu na mtoto ili uweze kutambua tatizo

• Aelezwe athari za kukosa utii• Wasiliana na mzazi/mlezi wake

Maendeleo kimakuzi kuwa nyuma ukilinganisha na umri

• Kujenga uhusiano wa karibu na mtoto ili uweze kutambua tatizo na kushirikisha vyombo vinavyohusika inapobidi

• Mwalimu kutembelea familia na kuona mazingira anayoishi mtoto

• Ushirikiano kati ya shule na wazazi/walezi

Kukatisha masomo • Kushirikisha uongozi wa shule pamoja na wazazi/walezi na jamii kwa ujumla ili kujua tatizo na kuangalia namna ya kulitatua

Tabia na mielekeo isiyofaa • Kuweka uhusiano mzuri kati ya mwalimu na mtoto, mwalimu na mzazi/mlezi na kati ya mtoto na mzazi/mlezi

Hofu na mashaka ya kushirikiana na wengine

• Kufanya ufuatiliaji wa karibu kwa kipindi kirefu ili kupata taarifa zitakazosaidia kugundua tatizo na kisha kuchukua hatua

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 34 25/04/2019 10:18

Page 47: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

35

Kutozingatia maelekezo • Mpe maelekezo kwa ufupi, lugha nyepesi na motisha anapotimiza

• Pangilia kazi vizuri, mwambie unatarajia nini kwake na ondoa mambo yanayoharibu umakini wake

Kusahau haraka • Mpe maelekezo kwa ufupi, lugha nyepesi na motisha anapotimiza

• Mpe kazi mbalimbali kulingana na umri, shauku yake na utamaduni unaohusika

Kuchanganywa kwa urahisi na matukio mengine

• Mpe shughuli moja kwa wakati

Kukwepa kazi inayotaka umakini • Apewe shughuli kulingana na uwezo wake

Kupoteza vitu sana • Kufanya ufuatiliaji wa karibu• Kuongea na mtoto ili ajue jinsi ya

kujitawala na kutunza mali yake

Kutosikiliza unapoongea naye • Kujenga uhusiano wa karibu na mtoto kwa kujishusha

• Chunguza ili ujue kwanini hasikilizi unapoongea naye

Kutokuwa na subira katika kungoja zamu yake

• Kumpa shughuli zaidi zinazohusisha tabia ya kusubiri

• Msaidie ili ajenge tabia ya kusubiri na kufuata zamu

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 35 25/04/2019 10:18

Page 48: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

36

Kujitupa chini, kurusha miguu, kupiga kelele

Kulipa kisasi akikosewa

Kukataa kucheza na/au kuchukia wengine

Kujitenga na wenzake

• Wasiliana na wazazi kuhusu njia za kutawala hasira

• Kujenga uhusiano wa karibu na mtoto na familia ili kusadia katika kumaliza tatizo

• Kuwa wazi na mfano wa kuigwa katika kutawala hasira

• Chunguza chanzo cha tabia ya kulipiza kisasi kwa mtoto ni nini?

• Msadie ili aweze kujenga tabia ya kusamehe anapokosewa

• Tumia vitabu na hadithi kuhusu hasira na jinsi ya kuitawala

• Msaidie mtoto ili ajenge tabia ya kuwathamini na kuwapenda wenzake

• Mhamasishe mtoto ajenge tabia ya kuchangamana na kucheza na wenzie

Kushindwa kutumia vizuri viungo vya mwili

• Kufuatilia kwa karibu kujua tatizo ni nini

Kuongea kwa sauti ya juu sana • Kufuatilia kwa karibu kujua kama ana tatizo la usikivu

• Kumwelekeza namna ya kuongea taratibu kwa sauti ya kusikika

Kushindwa kujieleza kwa ufanisi kulingana na kiwango chake

• Kuwa karibu na mtoto na kumwekea mazingira ya kujieleza zaidi

• Kumpa shughuli zitakazomfanya ajieleze mara kwa mara

• Kumpa mazoezi ya kutamka maneno mengi ili kujenga msamiati wa lugha husika

Kujikwaa au kujigonga kila mara kwenye vitu mbalimbali darasani

• Kufuatilia kwa karibu kujua kama ana tatizo la uoni

• Kuliweka darasa katika mpangilio mzuri

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 36 25/04/2019 10:18

Page 49: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

37

Kuleta vitu karibu sana na macho wakati wa kusoma

• Kufuatilia kwa karibu kujua kama ana tatizo la uoni

• Kuwaweka watoto katika sehemu inayostahili kwa umbali kutoka sehemu ya kusoma

Hupenda kukaa peke yake kwa muda mrefu

• Mhimize kushiriki katika kazi za vikundi• Mpe majukumu katika vikundi

3.4 Kushirikisha jamii katika utoaji wa uchangamshi wa awali

Uchangamshi wa awali ni vitendo vinavyochochea, makuzi na maendeleo ya awali ya ujifunzaji wa mtoto.

Je, jamii inaweza kushirikishwaje katika utoaji wa uchangamshi wa awali kwa mtoto?

Jamii ina jukumu kubwa la kuhakikisha upatikanaji wa huduma za msingi kwa mtoto ili kuchochea uchangamshi wa awali. Huduma hizo ni lishe bora, kupatiwa vifaa vya kuchezea vinavyoweza kusaidia ujifunzaji wa dhana mbalimbali, kutoa nafasi ya kucheza na ulinzi wa kutosha kama ifuatavyo:

3.4.1 Lishe

Lishe ni chakula ambacho kina virutubisho vyote vinavyohitajika ili mwili uweze kukua ipasavyo. Ni muhimu mwalimu uhakikishe watoto wanapata lishe wakiwa shuleni na nyumbani. Lishe inachangia kwa kiasi kikubwa katika ujifunzaji wa watoto. Kama watoto watakosa lishe watadumaa na kuathiri ujifunzaji wao. Hivyo, uwashirikishe wazazi kwa kutumia mbinu mbalimbali kuhusu umuhimu wa lishe kwa watoto. Vilevile, ni muhimu kuhakikisha watoto wanapata maji safi na salama ya kunywa kwa sababu maji yanasaidia ubongo kufanya kazi zake vizuri, ikiwemo kufikiri, kukumbuka, kuwa makini na ubunifu.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 37 25/04/2019 10:18

Page 50: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

38

3.4.2 Michezo

Kumbuka kuwa michezo ni sehemu muhimu katika maisha ya watoto. Kwa kutumia mikutano ya wazazi, ni muhimu uwaelimishe wazazi/walezi kuhusu umuhimu wa uchangamshi wa awali kwa watoto wao. Ni vema uaandae siku ya michezo shuleni ili wazazi/walezi wote waweze kushiriki na kuona namna ambavyo watoto wanakuza stadi mbalimbali kupitia michezo. Hii itawapa wazazi/walezi maarifa juu ya umuhimu wa michezo; hivyo kuwapa watoto wao fursa ya kucheza michezo huru na kuchezea vifaa mbalimbali wakiwa nyumbani. Zifuatazo ni aina za michezo na mifano yake:

i. Michezo ya ndaniWakati mwingine, hali ya hewa inaweza ikawa sio salama kwa watoto, hivyo, tumia michezo ya ndani. Ifuatayo ni baadhi ya michezo inayohitaji nafasi ndogo; hivyo, inaweza kuchezwa ndani ya darasa:

a. Saba juu Jinsi ya Kucheza:

• Wagawe watoto kwa kuwapatia namba 1 hadi 7 kulingana na idadi yao

• Watoto wote waliotamka namba isiyo 7, wainamishe vichwa vyao na kufumba macho na kunyoosha vidole gumba juu

• Watoto waliotamka namba 7 watapita wakichagua mtoto mmoja mmoja wakimgusa kidole gumba

• Wote saba wakishapita wanasimama na kuita saba juu• Kila mtoto aliyeguswa anajaribu kukisia nani katika wale saba aliyemgusa• Wale saba waliogusa wenzao hawatoi jawabu mpaka watoto wote

wamebahatisha• Kila mtoto anabahatisha mara moja• Wale saba wanatoa jawabu• Wale waliobahatisha sawa wanaingia katika saba juu

b. Kioo Jinsi ya Kucheza:

• Mwalimu anawaambia watoto wafanye kila tendo alilofanya yeye mpaka aseme basi (mfano: mwalimu anaweza kusimama na watoto

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 38 25/04/2019 10:18

Page 51: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

39

wakasimama, kuketi na watoto wanaketi, kukuna kichwa na watoto wanakuna kichwa, n.k.)

• Watoto wakishaelewa wanaweza kufanya wawili wawili• Kila jozi inakaa sehemu yake• Mtoto mmoja anafanya kitendo na mwingine anaiga kama vile wanaakisi.• Mwalimu akihitimisha, watoto wanabadili nafasi zao• Jaribu njia nyingine ambapo watoto wanaiga hisia

Mtindo mwingine unaitwa “Solo amesema”. Watoto wanasimama katika mistari. Anawaambia warudie aliyosema Solo. Kiongozi anasema: Solo amesema “ruka ruka”, "piga makofi": Solo alisema watoto wafanye. Kiongozi anayeanza akiwaambia wafanye kitendo ambacho Solo hajasema. Yeyote anayefanya anatoka mpaka raundi nyingine ianze. Mchezo huu unasaidia kukuza stadi za kusikiliza na kuwapa mazoezi ya viungo.

c. Siri ya guniaWafunge watoto macho kwa vitambaa kisha waambie watambue vitu mbalimbali kwa kutumia hisia zao. Watoto wanaweza kutambua vitu hivyo kwa kupapasa, kunusa, kuonja na kusikiliza. Tumia vitu vinavyopatikana katika mazingira yanayowazunguka: mfano wa vitu vinavyoweza kutumika katika mchezo huu ni.

Kupapasa: unyoya, kauri au jiwe, chuma, nguo, sarafu.Kunusa: kahawa au chai, unga, kitunguu.Kuonja:, tunda linalofahamika, njugu, muwa, limau, chumvi au sukari.Kusikiliza: kengele, filimbi, ngoma, piano (kitu chochote kinachotoa sauti).

d. Chupa ina nini ndani? (Kwa watoto wadogo)Chukua chupa tupu kadhaa mbele ya darasa. Kila chupa tia kiasi cha mbegu za mazao mbalimbali kama vile maharagwe, mtama au mchanga na gololi. Funika chupa na karatasi ya rangi ili kilichokuwamo ndani kisionekane. Tikisa chupa mojamoja, waambie watoto wasikilize sauti itokayo kwa kila chupa na waseme ni kitu gani kilichomo ndani ya chupa.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 39 25/04/2019 10:18

Page 52: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

40

e. Kutembea kiimani/kihisia Mchezo huu huchezwa ndani au nje ya darasa. Watoto wacheze wawiliwawili, mtoto mmoja amfunge mwenzie macho kwa kitambaa kisha amtembeze nje na ndani ya darasa, kisha aliyefungwa macho aseme yuko wapi kwa hisia ya mazingira aliyomo.

ii. Michezo ya nje ya darasa Michezo hii huchezewa nje ya darasa. Usalama wa uwanja kwa ajili ya michezo ya nje unatakiwa kuzingatia yafuatayo:

• Hakikisha eneo ni safi na salama, liko wazi na hakuna vitu vinavyoweza kuleta athari kama vile mawe, vioo vilivyovunjika na vitu vyenye ncha kali

• Zingatia hali ya hewa kwa mfano mvua au jua

• Hakikisha eneo lina mipaka na linazingatia mahali watoto wanapoweza kuchezea na ambapo hawaruhusiwi kuchezea

• Kama uwanja unapakana na barabara weka uzio wa vijiti na kamba au mawe ambayo watoto wanaweza kuona

• Walimu wawe makini katika kuhakikisha watoto wasizagae. Iwapo wazazi watajitolea watakuwa ni msaada mkubwa.

Vifaa vya kujifunzia na kuchezea michezo ya nje vinavyouzwa vinaweza kuwa ghali sana. Hivyo, mwalimu unashauriwa kufanya yafuatayo ili kupata vifaa vya michezo:

• Kama hakuna vifaa vya michezo, tafuta vitu mbalimbali katika mazingira halisi kama vile magogo, magurudumu, kamba, mipira na vijiti. Shirikisha jamii kutengeneza vifaa vya michezo kwa kutumia malighafi zinazopatikana katika eneo hilo. Wadau wa Elimu ya Awali wanaweza kushirikiana na watu wengine kupata vifaa vya michezo kwa gharama ndogo au bure. Mfano wa vifaa hivyo vinaweza kuwa tairi za baiskeli kwa ajili ya kubiringisha. Pia, tairi za magari zinaweza kupangwa kwa kupandia na kuruka, vipande vya miti vinaweza kutumiwa kutengeneza mizani au bembea

• Hakikisha viwango vya usalama wa vifaa vya kuchezea. Michezo ya kuteleza ‘kuserereka’ ikiwa na miinuko mikali inaweza kuangusha

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 40 25/04/2019 10:18

Page 53: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

41

watoto. Ikiwa imetengenezwa kwa chuma hupata moto wakati wa jua. Ikiwa ni ya mbao inaweza kufanya ufa au kuwa vificho vya wadudu wadogo wenye kuleta madhara

• Mwalimu au wazazi/walezi wakague vifaa vya kuchezea kila siku kuhakikisha viko salama. Baadhi ya wazazi wanaweza kukubali kuchukua jukumu hilo.

Ifuatayo ni mifano ya michezo ya nje ya darasa:a. Mbio za kupokezana

Mbio za kupokezana zinawawezesha watoto kuwa makini;Jinsi ya kucheza:

• Wapange watoto katika mistari miwili• Mwalimu asimame mita kadhaa mbele yao• Watoto wawili waambiwe wakimbie wamshike mwalimu mkono• Wakimshika mwalimu wanarudi kumshika mwenzao halafu wanarudi

kusimama nyuma ya mstari• Wote wanapata fursa ya kumkimbilia mwalimu• Mstari wa kwanza kumaliza ndio utakaokuwa umeshinda• Kila mara mwalimu anatakiwa awe mbunifu wa mitindo mbalimbali

ya kukimbia mfano; kukimbia kwa mguu mmoja, kukimbia kinyume nyume, kurukaruka, n.k.

b. Mijongeo ya wanyama na ndegeWatoto hufurahi kuiga mijongeo ya wanyama kwa mfano; kobe, ngedere, kuku, bata, mbwa, paka, samaki, ndege, simba na chura.Vifaa: Ngoma.

Jinsi ya kucheza:• Mwalimu atamke jina la mnyama kisha aanze kupiga ngoma• Wakati ngoma inapigwa watoto wanatembea wakiiga mfano wa mnyama

aliyetajwa• Ngoma ikipigwa haraka watoto wanatembea haraka, ikipigwa polepole

watoto wanatembea polepole

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 41 25/04/2019 10:18

Page 54: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

42

c. Kurusha mpiraKurusha mpira kwenye mduara au kulenga walio kwenye mduara ni mchezo unaofurahisha. Watoto wanaweza kurusha au kudaka mpira kwa kupokezana. Watoto wanapenda kucheza mchezo wa kukwepa mpira.

Jinsi ya Kucheza• Watoto sita wasimame nje ya duara• Walenge kuwapiga na mpira wale walio katika duara (hairuhusiwi

kulenga kichwa)• Watoto walio ndani ya duara wanajaribu kukwepa • Kama mtoto akipigwa na mpira anatoka nje ya mduara awe ni wa kulenga

wale walio ndani ya mduara. Mchezo unaendelea hadi wanabaki watoto sita tu katika mduara

• Hao sita wanatoka nje ya mduara na mchezo unaanza tena. Mwalimu anaweza kubadili kanuni ili kunogesha mchezo.

d. Kamba Kamba ni nzuri kwa kuruka na kujisawazisha: Jinsi ya Kucheza:

• Tandaza kamba chini katika muundo tofauti, watoto wapite kufuatisha hizo kamba ili wasitumbukie katika mto

• Waruke kamba huku wakihesabu namba, au kuimba nyimbo

e. Kuvuka mto Jinsi ya Kucheza:

• Tandaza kamba mbili chini, ziwe kama kingo za mto• Watoto waruke kutoka ng’ambo moja mpaka nyingine• Ongeza upana wa mto kwa kusogeza kamba. Watoto waendelee kuvuka

mpaka pale watakaposhindwa.

f. Mistari na gololi Jinsi ya Kucheza:

• Waelekeze wachore duara kubwa kwenye mchanga au sakafu• Waelekeze watoto waweke gololi kati ya tano au kumi kwenye duara• Watumie gololi ambazo ni kubwa kwa ajili ya kulenga/ kupiga gololi

zilizopo katika mduara

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 42 25/04/2019 10:18

Page 55: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

43

• Mchezaji anapaswa kuwa nje ya duara wakati wa ulengaji• Mchezo huu ufanyike kwa zamu yaani mtoto mmoja baada ya mwingine• Waeleze watoto kuwa mchezaji ataendelea kucheza endapo atapata

kupiga gololi na endapo atakosa kupiga itabidi asubiri hadi zamu yake ifike tena

• Kama mtoto hajaweza kupiga gololi hata moja itabidi aache gololi ya kupigia katika duara hadi zamu yake ya kucheza itakapofika

• Watoto waendelee kucheza hadi gololi zote ziishe katika mduara• Mshindi katika mchezo huu ni yule ambaye amepata gololi nyingi zaidi.

Kuna michezo mingi ya watoto ya kuchora mistari chini na kutupa gololi. Kuwafundisha watoto michezo hiyo ni njia nzuri ya kukuza stadi za kufikiri.

g. Baridi au moto Jinsi ya Kucheza:

• Kitu kama kifutio cha ubao, daftari, kitabu n.k. kinachaguliwa na kufichwa

• Mtoto anaambiwa atoke nje• Kitu hicho kinafichwa• Mtoto aliyekuwa nje anaitwa kukitafuta• Akisogea pale kilipofichwa wenzake wanapiga makofi, akienda mbali na

kilipofichwa makofi yanapungua• Akishakipata inakuwa ni zamu ya mtoto mwingine kutoka nje na kurudi

kutafuta kitu kilichofichwa.

h. Kumbukumbu Jinsi ya Kucheza:

• Watoto wakae kwenye mduara• Mtoto mmoja aingie darasani na aguse kitu• Mtoto mwingine aingie aguse hicho kitu na aguse kingine• Mtoto wa tatu aingie aguse hivyo vitu viwili na kingine cha tatu.• Mtoto mwingine aingie aguse hivyo vitu vitatu na cha nne• Watoto wengine waangalie tu na wasitoe dokezo• Kosa likifanyika mchezo unaanza tena

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 43 25/04/2019 10:18

Page 56: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

44

• Mwalimu anaweza kuwasaidia watoto kuhesabu ni vitu vingapi walikumbuka na awatake kuongeza idadi ya vitu wanavyoweza kukumbuka.

i. Mduara wa mbio za kupokezana nafasi Jinsi ya Kucheza:

a. Watoto wanasimama katika mduarab. Watoto wananyoosha kidole kimoja kuelekea kwa wenzao walio upande

mwingine wa mduarac. Mwalimu akisema kimbia, wote wanakimbilia upande mwingine wa

mduara kushika ile nafasi ya yule uliyemlengad. Wakigongana wakati wakikimbia wanasema “pip”e. Lengo la mchezo ni kufanya mduara mwingine wakiwa katika nafasi

tofauti.

f. Vikundi vya herufi au namba Jinsi ya Kucheza:

• Watoto wajipange kwa vikundi vya wawili au watatu na kujaribu kuunda herufi hiyo. Mwalimu anaweza pia kutaja namba.

• Mwalimu anaweza kutambua walivyofanya na awatake watoto wengine wasimame na watazame jinsi vikundi vilivyofanya.

• Wajaribu tena herufi nyingine na mwalimu aeleze jinsi walivyounda herufi au namba.

g. Mchezo wa bata - bata bukini (bata mkubwa) Jinsi ya Kucheza:

• Watoto wanakaa katika mduara mkubwa.• Mtoto mmoja anazunguka akiwashika wenzake kichwani na kuwaita

bata, bata, bata.• Baada ya kuwashika mara kadhaa na kuwaita bata, bata, bata anamshika

mmoja anamwita bukini.• Bukini anamkimbiza aliyemwita bukini naye anakimbia kujaribu

kuchukua nafasi aliyoacha bukini.• Akishindwa anaketi katikati ya mduara.• Bukini anarudia mchezo• Akishikwa mwingine anaingia katikati ya mduara naye aliyekuwa

katikati anarudi kwenye mduara anaendelea na mchezo

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 44 25/04/2019 10:18

Page 57: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

45

iii. Michezo huria ya njeKatika kipindi cha michezo ya nje, tenga dakika chache za watoto kuwa huru kutembea, kuzungumza wao kwa wao na kucheza wenyewe. Muda huo watoto wanaweza wakataka kucheza na kamba, mipira, vijiti au kuumba vitu. Watoto wanaweza pia kutumia muda huo kurudia kazi waliyojifunza siku za nyuma kama kutunza bustani au kuchunguza wadudu

3.4.3 Kuhakikisha usalama wa kutosha kwa watotoMtoto anahitaji ulinzi tangu akiwa tumboni mwa mama na hata baada ya kuzaliwa. Ulinzi ni hali ya kushirikisha usalama wa mtoto na humwepusha na athari zinazoweza kujitokeza kwa mfano vitendo vya unyanyasaji. Mtoto anahitaji kulindwa na ni mojawapo ya haki ya msingi. Wazazi/walezi na jamii huandaa mikakati na sheria ndogondogo za kuweza kusimamia na kutoa huduma hii muhimu kwa kumpa mtoto ulinzi kutokana na hatari au majanga na vitendo vya ukatili.

Kumbuka kuwa matukio mengi ya ukatili yamekuwa yakifanywa kwa watoto na watu wa karibu kama vile ndugu au jamaa, walezi wao wa nyumbani na walimu. Matukio haya pia yamekuwa yakifanywa na watu wasiojulikana. Kutokana na hali hii, watoto wanahitaji kulindwa dhidi ya aina zote za ukatili, unyanyasaji, uonevu, majanga na hatari kwa nguvu zote. Ulinzi na usalama wa mtoto umo mikononi mwa wazazi/walezi, walimu, jamii na taifa kwa ujumla.

Ni vema ukatambua kuwa kuna aina tofauti za unyanyasaji kwa watoto, baadhi ya aina hizo ni unyanyasaji wa kimwili, kihisia, kijinsia na kisaikolojia. Ni muhimu kubaini dalili za mtoto aliyenyanyaswa na namna ya kumsaidia.

Je, ni dalili zipi zitakazokuonesha kuwa mtoto ananyanyaswa?

Zifuatazo ni baadhi ya dalali za mtoto aliyenyanyaswa:a. Kuwa na michubuko isiyoelewekab. Vidonda c. Kuvunjikad. Kuwa na hofu

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 45 25/04/2019 10:18

Page 58: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

46

e. Kuwa mgomvi (anagombana na watoto wenzake)f. Uvaaji wake sio sahihi, anakuwa anaficha vidondag. Kujitenga kabisa na wenzakeh. Kuwa katili kwa wenginei. Kupiga wengine bila hurumaj. kutembea au kukaa kwa shida

Jadili dalili zinazoweza kujitokeza kwa mtoto aliyenyanyaswa kihisia na kijinsia. Eleza utakavyoshirikisha familia yake katika kumsaidia.

Tendo la unyanyasaji linaathiri ujifunzaji kwa mtoto; hivyo, unashauriwa kuwa karibu na kuonesha upendo kwa watoto. Hii ni kwa sababu watoto wanakuwa huru na kumwamini mwalimu wao kuliko mtu mwingine yeyote. Mwalimu una fursa zaidi ya kuweza kubaini mtoto aliyenyanyaswa na kuchukua hatua za kumsaidia kwa kushirikisha uongozi wa shule na kuhusisha vyombo vinavyohusika na wazazi/walezi pale inapobidi.

Hivyo, unapaswa kuwaelimisha wazazi/walezi na jamii juu ya umuhimu wa utoaji wa huduma za msingi kwa watoto ili kuchochea uchangamshi wa awali kwa watoto wao.

Ushirikishwaji wa jamii katika kutoa huduma stahiki unawezeshwa na mwalimu mwenye stadi za uongozi na mawasiliano mazuri na wazazi/walezi na jamii ili kuweka mikakati ya kukabili changamoto zinazotokana na ukuaji na ujifunzaji wa mtoto.

Jamii inajukumu kubwa la kuhakikisha upatikanaji wa huduma za msingi kwa mtoto ambazo zinachochea uchangamshi wa awali. Huduma hizo ni lishe bora, kupatiwa vifaa vya kuchezea vinavyoweza kusaidia kujenga dhana mbalimbali, kutoa nafasi ya kucheza na ulinzi wa kutosha.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 46 25/04/2019 10:18

Page 59: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

47

Eleza changamoto ulizokutana nazo wakati wa kufanya utambuzi wa mapema na afua stahiki ulizotoa.

Dhana ya uchangamshi wa awali inahusisha jumla ya mambo yote yanayomwezesha mtoto kushiriki katika shughuli mbalimbali kwa uhuru. Kumbuka kwamba mtoto hujifunza vizuri katika mazingira changamshi yaliyoandaliwa na kuratibiwa vizuri. Uchangamshi wa awali ni muhimu sana kwa mtoto katika ukuaji na ujifunzaji wake. Baadhi ya matendo changamshi kwa mtoto ni kama vile kucheza michezo mbalimbali, kusimulia hadithi na kusikiliza, kuonesha upendo, kujali na kutumia vifaa mbalimbali katika kujifunza. Hivyo, unapaswa kuwa mbunifu kuhamasisha wazazi/walezi na jamii kwa ujumla kushiriki katika kufanya uchangamshi wa awali kwa mtoto katika nyanja zote za ukuaji na kuchochea ujifunzaji wao.

Jaribio baada ya kujifunza

Jibu maswali yafuatayo baada ya kujifunza maudhui ya sura hii.

1. Eleza mambo yanayochochea uchangamshi wa awali.2. Fafanua namna mtoto anavyoweza kujifunza kupitia michezo.3. Ni mambo gani ambayo walimu na wazazi/walezi wanaweza

kushirikiana katika kusaidia uchangamshi wa awali kwa watoto?

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 47 25/04/2019 10:18

Page 60: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

48

Jumuiya za ujifunzaji

Maswali yafuatayo, yataongoza majadiliano katika jumuiya za ujifunzaji:

1. Ni kitu gani ulichojifunza katika moduli hii ambacho kimekusaidia katika

kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa watoto wa Elimu ya Awali? Eleza

kwa kutumia mifano halisi.

2. Taja changamoto ulizokumbana nazo wakati wa ujifunzaji wa maudhui ya

moduli hii.

3. Ni mbinu gani ulizozitumia katika kutatua changamoto hizo?

4. Je, kuna uhusiano gani kati ya ukuaji na ujifunzaji wa mtoto?

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 48 25/04/2019 10:18

Page 61: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

49

Faharasa

Afua stahiki Ni utaratibu wa utoaji huduma stahiki kwa watoto wenye mahitaji maalumu unaolenga kupunguza au kuondoa changamoto za ukuaji na ujifunzaji.

Huduma Ni jumla ya mambo yote anayopatiwa mtoto kama haki zake za msingi ili kumwezesha kukua vizuri.

Kona za ujifunzaji Maeneo yaliyowekwa vifaa/zana mbalimbali za kujifunzia ambazo watoto wanaweza kuzitumia kwa muda wao wenyewe kulingana na vionjo vyao.

Mahitaji maalumu Uhitaji wa uangalizi na huduma za kipekee kwa mtoto kulingana na hali au utendaji wake.

Mazingira rafiki Ni maeneo yanavyovutia, salama na safi yenye kukidhi shughuli ya ujifunzaji wa mtoto ndani na nje ya darasa kwa kuzingatia mahitaji ya watoto wote.

Mkoba wa kazi Ni jalada au kifaa kinachotumika kuhifadhia kazi za mwalimu alizozifanya hatua kwa hatua katika nyakati tofauti za ujifunzaji ambazo zitatumika katika upimaji ili kutathimini maendeleo ya ufundishaji na ujifunzaji.

Tafakuri Ni ile hali ya kufikiri kwa kina juu ya ubora au udhaifu wa jambo fulani ili kujua kipi kilifanikiwa na kipi hakikufanikiwa na wapi panahitaji maboresho ili kuleta ufanisi.

Silka Mwenendo anaozaliwa na kukua nao kiumbe hasa wa jamii ya wanyama kama vile binadamu ambao huwa ni mwitikio wa baadhi ya vichocheo.

Uchangamshi wa awali Vitendo vinavyochochea malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya ujifunzaji wa mtoto.

Umahiri Ni uwezo wa kufanya jambo fulani kwa ufanisi.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 49 25/04/2019 10:18

Page 62: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

50

Bee, H. & Boyd, D. (2004). The Developing Child. (10th Edition), London: Allyn & Bacon.

Beith, K. & Tassoni, P. (2002). Diploma in child care and education (3rd Ed.), Harlow: Pearson Education Limited.

Corel, J.L (1975). The Postnatal Development of the Human Cerebral Cortex. Cambridge, MA: Havard University Presa)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (2013). Moduli ya Kwanza: Ujuzi wa Malezi Changamshi kwa Watoto Wadogo. Dar Es Salaam: Press “A”.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (2016). Mtaala na Muhtasari wa Elimu ya Awali. Dar es Salaam: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (2014). Sera ya Elimu na Mafunzo.

Dar es Salaam: WEU Press,

Kiango, J. G., Lodhi, A.Y., Ipara, I., & Nassir, A. (2008). Kamusi ya Shule za Msingi. Dar es Salaam: Oxford University Press.

Madrasa Early Childhood Programme, (2017). Material Development Facilitator Manual (Draft).

Madrasa Resource Centre. (2000). The Madrasa Pre School Curriculum. Madrasa Resource Centre East Africa Regional Office Mombasa, Kenya.

Nelson, C.A. (2000). The developing brain. In: Shonkoff, J.P. and Phillips, D.A. (eds) From Neurons to Neighborhoods: The Science of Early Child Development. Washington DC: National Academy Press.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 50 25/04/2019 10:18

Page 63: TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) - Ukuaji na Ujifunzaji ... UKUAJI NA...Ukuaji na Ujifunzaji wa Mtoto wa Elimu ya Awali Programu ya Mafunzo Endelevu ya Mtaala kwa Mwalimu Kazini Moduli

51

Taasisi ya Elimu Tanzania. (2003). Moduli ya Somo la Malezi ya Elimu ya Awali, Dar es Salaam: Inter Press of Tanzania Limited.

Taasisi ya Elimu Tanzania, (2003). Moduli ya Somo la Mbinu za Kufundishia Elimu ya Awali. Dar es Salaam: Inter Press of Tanzania Limited.

Taasisi ya Elimu Tanzania. (2010). Mwongozo wa Kufundishia Elimu ya Awali kwa Shule za Awali Tanzania, Dar es salaam: Navneet Publications (India) Limited.

Taasisi ya Elimu Tanzania,. (2013). Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti: Ualimu wa Elimu ya Awali, Dar es Salaam: Taasisi ya Elimu Tanzania.

Taasisi ya Elimu Tanzania. (2016). Mwongozo wa Mwalimu wa Kufundishia Elimu ya Awali. Dar es Salaam: Taasisi ya Elimu Tanzania.

Taasisi ya Elimu Tanzania. (2016). Mwongozo wa Michezo ya Kufundishia Elimu ya Awali. Dar es Salaam: Taasisi ya Elimu Tanzania.

Taasisi ya Elimu Tanzania. (2017). Mwambata wa Kufundishia Elimu ya Awali, Dar es salaam: Taasisi ya Elimu Tanzania.

Tassoni, P. (2002). Certificate in Child Care and Education. Glasgow: Pearson Education Limited.

MODULI UKUAJI NA UJIFUNZAJI 2017_icon 9.indd 51 25/04/2019 10:18