tume ya uchaguzi ya zanzibar sheria ya …zec.go.tz/en/wp-content/uploads/2015/08/kanuni.pdf ·...

30
1 TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR SHERIA YA UCHAGUZI, NAM. 11 YA 1984 KANUNI ZA UCHAGUZI [Chini ya Kifungu cha 130(1)] _______________ KWA UWEZO iliopewa chini ya kifungu cha 130(1) cha Sheria ya Uchaguzi Nam. 11 ya 1984, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inatunga Kanuni zifuatazo: SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI Jina fupi na kuanza kutumika. 1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Uchaguzi, 2015 na zitaanza kutumika mara baada ya kutangazwa katika Gazeti Rasmi la Serikali. Ufafanuzi. 2. Katika Kanuni hizi isipokuwa kama itaelezwa vyenginevyo:- “Chama cha Siasa” maana yake ni chama cha Siasa kilichosajiliwa chini ya Sheria ya Vyama Vya Siasa Nam. 5 ya 1992; “Daftari” maana yake ni Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililotayarishwa na kutunzwa kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha Sheria; ”Eneo la Uchaguzi” maana yake ni eneo au sehemu ya Jimbo iliyowekwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 6 cha Sheria. ”Hakimu” maana yake ni Hakimu wa Mahakama ya Mkoa. “Jimbo” maana yake ni kuhusiana na uchaguzi wowote isipokuwa wa Rais, ni jimbo kwa madhumuni ya uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi au Serikali za Mitaa na kwa uchaguzi wa Rais ni Zanzibar yote; “Karatasi ya kura” maana yake ni karatasi ya kura inayotayarishwa na Tume katika hali ambayo inaweza kutumiwa na mpiga kura kwa ajili ya kupiga kura; “Katiba” maana yake ni Katiba ya Zanzibar ya 1984 pamoja na marekebisho yake; ”Kiongozi wa Serikali ya Mtaa” maana yake ni Diwani “Mgombea” maana yake ni mtu ambaye amekubali kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar au Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi au Uongozi wa Serikali za Mitaa; “Mgombea Urais” maana yake ni mtu yeyote aliyeteuliwa wadhifa wa Urais;

Upload: vuongdang

Post on 31-Jan-2018

419 views

Category:

Documents


10 download

TRANSCRIPT

1

TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR

SHERIA YA UCHAGUZI, NAM. 11 YA 1984

KANUNI ZA UCHAGUZI

[Chini ya Kifungu cha 130(1)]

_______________ KWA UWEZO iliopewa chini ya kifungu cha 130(1) cha Sheria ya Uchaguzi Nam. 11 ya 1984, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inatunga Kanuni zifuatazo:

SEHEMU YA KWANZA

UTANGULIZI

Jina fupi na kuanza kutumika.

1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Uchaguzi, 2015 na zitaanza kutumika mara baada ya kutangazwa katika Gazeti Rasmi la Serikali.

Ufafanuzi.

2. Katika Kanuni hizi isipokuwa kama itaelezwa vyenginevyo:- “Chama cha Siasa” maana yake ni chama cha Siasa kilichosajiliwa chini ya Sheria ya Vyama Vya Siasa Nam. 5 ya 1992; “Daftari” maana yake ni Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililotayarishwa na kutunzwa kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha Sheria; ”Eneo la Uchaguzi” maana yake ni eneo au sehemu ya Jimbo iliyowekwa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 6 cha Sheria. ”Hakimu” maana yake ni Hakimu wa Mahakama ya Mkoa. “Jimbo” maana yake ni kuhusiana na uchaguzi wowote isipokuwa wa Rais, ni jimbo kwa madhumuni ya uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi au Serikali za Mitaa na kwa uchaguzi wa Rais ni Zanzibar yote; “Karatasi ya kura” maana yake ni karatasi ya kura inayotayarishwa na Tume katika hali ambayo inaweza kutumiwa na mpiga kura kwa ajili ya kupiga kura; “Katiba” maana yake ni Katiba ya Zanzibar ya 1984 pamoja na marekebisho yake;

”Kiongozi wa Serikali ya Mtaa” maana yake ni Diwani “Mgombea” maana yake ni mtu ambaye amekubali kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar au Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi au Uongozi wa Serikali za Mitaa; “Mgombea Urais” maana yake ni mtu yeyote aliyeteuliwa wadhifa wa Urais;

2

“Mkurugenzi wa Uchaguzi” maana yake ni Mkurugenzi aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 7 cha Sheria na inajumuisha mtu atakayeteuliwa kufanya kazi kwa wadhifa huo wa Mkurugenzi; “Mpiga Kura” maana yake ni mtu yeyote ambaye kwa wakati huo anazo sifa za kupiga kura katika uchaguzi wowote kwa mujibu wa Sheria; “Msimamizi wa Kituo” maana yake ni Msimamizi wa kituo cha kupigia kura aliyetuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 63 cha Sheria; “Msimamizi wa Uchaguzi” maana yake ni Msimamizi wa Uchaguzi aliyeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Sheria na inajumuisha Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi.

“Mwangalizi” maana yake ni Mwangalizi wa Uchaguzi wa ndani au wa nje ambaye amekubaliwa na Tume. “Mwenyekiti” maana yake ni Mwenyekiti wa Tume aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 119 cha Katiba na inajumuisha Makamo Mwenyekiti au mtu mwengine yoyote atakayeteuliwa kufanya kazi za Mwenyekiti; “Sanduku la kura” maana yake ni sanduku la kura lililotayarishwa na Tume kwa kuruhusu kuingiza ndani yake karatasi ya kura katika hali ambayo mtu hatoweza kuitoa; “Shahada ya Mpiga Kura” maana yake ni shahada inayotolewa kwa mujibu wa Sheria kumuwezesha mtu kupiga kura; “Siku ya Uchaguzi” maana yake ni siku ambayo imeteuliwa kwa ajili ya upigaji kura chini ya kifungu cha 51 cha Sheria na inajumuisha uchaguzi mdogo; “Siku ya Uteuzi” maana yake ni siku iliyowekwa kwa ajili ya uteuzi wa wagombea; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Uchaguzi Nam. 11 ya mwaka 1984 pamoja na marekebisho yake;

“Tume” maana yake ni Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iliyoanzishwa chini ya kifungu cha 119 cha Katiba ya Zanzibar, 1984; “Uchaguzi” maana yake ni:-

(a) Kuhusiana na uchaguzi wa kumchagua Rais, basi ni

uchaguzi wa Rais; (b) Kuhusiana na uchaguzi wa Wawakilishi basi ni Uchaguzi wa

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi;

(c) Kuhusiana na uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa basi ni Uchaguzi wa Serikali za Mitaa;

na inajumuisha uchaguzi mdogo.

3

“Uteuzi” maana yake ni uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi wa nafasi ya Urais au Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi au nafasi ya Udiwani; ”Wakala wa kuhesabu kura” maana yake ni mtu aliyeteuliwa kama ni wakala wa kuhesabu kura chini ya kifungu cha 77 cha Sheria. “Wakala wa upigaji kura” maana yake ni mtu aliyeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 64 cha Sheria.

SEHEMU YA PILI

ELIMU YA WAPIGA KURA

Mamlaka ya utoaji wa elimu ya wapiga Kura

3. (1) Bila ya kukiuka masharti ya kifungu cha 5 (b) cha Sheria, Tume itakuwa na dhamana ya kukuza, na kuratibu utoaji wa elimu ya wapiga kura.

(2) Kwa madhumuni ya Kanuni hii, elimu ya wapiga kura inajumuisha utoaji wa elimu, taarifa na uhamasishaji juu ya mwenendo wa uchaguzi na taratibu zake.

(3) Katika utekelezaji wa jukumu la kukuza na kuratibu elimu ya wapiga kura, Tume inaweza kushirikiana na Asasi za kijamii na Taasisi za kiserikali.

Kibali cha utoaji wa elimu ya wapiga kura

4. (1) Asasi au Taasisi inaweza kuomba kupatiwa kibali cha kutoa elimu ya wapiga kura katika hatua yoyote ya uchaguzi kwa muda na wakati utaotangazwa na Tume.

(2) Tume inaweza kutoa kibali cha elimu ya wapiga kura, au kuthibitisha na kuidhinisha matumizi ya vielelezo vya elimu ya wapiga kura kwa Asasi za kijamii na Taasisi za kiserikali zitakazoomba kutoa elimu ya wapiga kura.

(3) Tume itakuwa na haki ya kukubali au kukataa matumizi ya vielelezo ambavyo vimewasilishwa kulingana na masharti ya Kanuni ndogo ya (2) ya Kanuni hii.

(4) Endapo Tume haitokubaliana na vielelezo vilivyowasilishwa itavirejesha kwa Asasi au Taasisi husika ili kufanya masahihisho iwapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo.

(5) Taasisi au Asasi iliyopewa kibali cha kutoa elimu ya wapiga kura, itawajibika kushirikiana na Ofisi za Tume ya Uchaguzi za Wilaya husika katika utoaji wa elimu ya wapiga kura .

Vielelezo vya elimu ya wapiga kura.

5. Kwa madhumuni ya sehemu hii, vielelezo vya elimu ya wapiga kura vinajumuisha vitini, vipeperushi, mabango, vijarida na vipindi vya redio na televisheni pamoja na vifaa vyengine vinavyobeba ujumbe wenye elimu ya wapiga kura.

4

Kukiuka vifungu vya Kanuni.

6. Taasisi au Asasi yoyote itakayokiuka masharti ya sehemu hii itakuwa imetenda kosa na ikipatikana na hatia itanyang’anywa kibali cha kutoa elimu ya wapiga kura.

SEHEMU YA TATU

UTEUZI WA MAAFISA WA UCHAGUZI

Uteuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi au Wasaidizi Wasimamizi wa Uchaguzi.

7. (1) Kutakuwa na Msimamizi wa Uchaguzi na Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi kwa kila jimbo la uchaguzi ambao watateuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Sheria na watakuwa na dhamana ya kuendesha, kuratibu na kusimamia uchaguzi katika majimbo waliyoteuliwa.

(2) Tume, wakati wowote kabla ya uchaguzi, itawaelekeza Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasaidizi Wasimamizi wa Uchaguzi kwa maandishi mambo yafuatayo:-

(a) tarehe ya kuanza kwa utekelezaji wa majukumu yao na muda

wa kumalizika kwake; (b) maelekezo na masharti ya kazi; na

(c) miongozo mengine kama Tume au Mkurugenzi wa Uchaguzi

watakavyoona inafaa.

(3) Msimamizi wa Uchaguzi au Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi atakayeteuliwa chini ya Kanuni hii mara tu baada ya kupata barua ya uteuzi atamjuulisha kwa maandishi Mkurugenzi wa Uchaguzi kukubali kwake uteuzi huo.

Kuondolewa kwa Msimamizi wa Uchaguzi au Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi.

8. (1) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni ya 7, Tume pale ambapo itajiridhisha kuwa Msimamizi wa Uchaguzi au Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi kwa sababu zozote hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake ipasavyo:-

(a) itasitisha uteuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi au Msaidizi

Msimamizi wa Uchaguzi na itamfahamisha kwa maandishi sababu za kusimamishwa kwake; na

(b) itateua mtu mwengine kuwa Msimamizi wa Uchaguzi au

Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi.

(2) Msimamizi wa Uchaguzi atakayeteuliwa au Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi mara tu baada ya kupata barua ya uteuzi atamjuulisha kwa maandishi Mkurugenzi wa Uchaguzi kukubali kwake uteuzi huo.

(3) Pale ambapo Msimamizi wa Uchaguzi au Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi aliyeteuliwa, bila ya sababu ameshindwa kutekeleza masharti ya Kanuni ndogo ya (2) ya Kanuni hii, Tume inaweza kumteuwa mtu mwengine kuwa Msimamizi wa Uchaguzi au Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi.

5

(4) Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi katika kutekeleza majukumu ya kazi zake, atakuwa chini ya uangalizi wa Msimamizi wa Uchaguzi.

Msimamizi wa kituo.

9. (1) Kwa kufuata maelekezo yatakayotolewa na Tume, kila Msimamizi wa Uchaguzi atawateuwa kwa maandishi Msimamizi wa kituo na Wasaidizi Wasimamizi wa vituo, kwa kila kituo kwa shughuli za uchaguzi katika majimbo anayoyasimamia.

(2) Tume itaamua idadi ya wasimamizi wa vituo au Wasaidizi Wasimamizi wa vituo wanaohitajika kwa kila kituo cha kupigia kura.

(3) Mtu yeyote aliyeteuliwa chini ya Kanuni hii atatakiwa kuweka saini yake katika mkataba wa ajira yake katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi kama itakavyoelekezwa na Tume.

(4) Kila Msimamizi wa kituo atakuwa ni dhamana wa kituo cha kupigia kura.

(5) Kwa kuzingatia masharti ya Sheria, Kanuni hizi na miongozo itakayotolewa na Tume, kila Msimamizi wa kituo na au Msaidizi Msimamizi wa kituo watafanya kazi zao chini ya usimamizi wa Msimamizi wa Uchaguzi au kama itakavyokuwa.

Taratibu za uteuzi wa watendaji wa kituo.

10. (1) Kwa kufuata maelekezo yatakayotolewa na Tume Msimamizi wa Uchaguzi atafanya uteuzi wa Wasimamizi wa vituo na Wasaidizi Wasimamizi wa vituo kwa,

(a) kutangaza nafasi na kuwataka watu wenye sifa kuomba; (b) kufanya uteuzi wa awali wa waombaji na kubandika majina

yaliyopitishwa katika Ofisi yake au katika ubao wa matangazo kwa madhumuni ya kuwaita katika usaili walioteuliwa katika jimbo;

(c) kutangaza tarehe, muda na pahala pa usaili; na

(d) kufanya usaili wa waombaji.

(2) Msimamizi wa Uchaguzi mara baada ya kufanya usaili atateua waombaji wenye sifa kuwa Wasimamizi wa vituo, na kadri itakavyokuwa, Wasaidizi Wasimamizi wa vituo.

Kiapo cha kutunza siri

11. (1) Msimamizi wa Uchaguzi na Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi, kabla ya kuanza rasmi utekelezaji wa majukumu yake, atakula kiapo cha kutunza siri mbele ya Hakimu katika Fomu Namba FK. 1A na Fomu Namba FK. 1B kwa Msaidizi Msimamizi kama ilivyotayarishwa na Tume

(2) Msimamizi wa kituo na Msaidizi Msimamizi wa kituo kabla ya kuanza rasmi utekelezaji wa majukumu yake, atakula kiapo cha kutunza siri mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi katika Fomu Namba FK. 2 kama ilivyotayarishwa na Tume.

6

Mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi.

12. (1) Tume katika wakati wowote baada ya uteuzi wa watendaji wa uchaguzi na kabla ya uchaguzi, itapanga na kuendesha mafunzo kwa watendaji hao juu ya taratibu zake, Sheria na Kanuni za Uchaguzi.

(2) Msimamizi wa Uchaguzi, kwa miongozo ya Tume, ataendesha mafunzo kwa Wasimamizi wa Vituo na Wasaidizi Wasimamizi wa Vituo juu ya taratibu za uchaguzi, Sheria na Kanuni zitakazotumika katika uchaguzi.

SEHEMU YA NNE

UTEUZI WA WAGOMBEA Siku ya uteuzi na Utoaji wa fomu za uteuzi.

13. (1) Tume kupitia katika Gazeti Rasmi la Serikali itatangaza siku maalumu ya uteuzi ambayo itaanza saa 10 za jioni ya siku ya mwisho ya tarehe ya kurejesha fomu za uteuzi hadi saa 10 za jioni ya siku inayofuatia.

(2) Tume itapanga na kutangaza kupitia katika Gazeti Rasmi la Serikali tarehe ya kuanza kutolewa na tarehe ya mwisho ya kurejesha fomu za uteuzi kwa ajili ya uteuzi wa wagombea.

Uteuzi wa Wagombea

14. (1) Kwa mujibu wa masharti ya Katiba na Sheria, kutakuwa na uteuzi wa wagombea kama ifuatavyo:-

(a) Uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi wa Rais;

(b) Uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi;

(c) Uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa; na

(d) Uteuzi wa Viti maalumu vya Wanawake kwa wagombea wa

Uwakilishi.

(2) Uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi wa Rais utafanyika kwa mujibu wa masharti ya Sura ya tatu ya Sheria;

(3) Uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi utafanyika kwa mujibu wa masharti ya Sura ya nne ya Sheria;

(4) Uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika kwa mujibu wa masharti ya Sura ya tano ya Sheria; na

(5) Uteuzi wa Viti maalumu vya Wanawake kwa wagombea wa Uwakilishi utafanyika kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 67 cha Katiba.

Uwasilishaji wa majina ya wagombea Urais.

15. (1) Kwa uchaguzi wa Urais kila chama cha siasa kinachokusudia kushiriki katika uchaguzi huo kitawasilisha jina la mgombea wake kwa Tume.

(2) Tume baada ya kupokea jina la mgombea Urais kama ilivyoelezwa katika Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii, itatoa fomu za uteuzi kama zilivyotayarishwa na Tume.

7

(3) Kulingana na maelekezo ya Sheria, fomu za uteuzi wa wagombea wa Urais zitawasilishwa kwa Mwenyekiti katika siku na tarehe kama itakavyoelekezwa na Tume.

(4) Mgombea yeyote wa Urais wakati wa kuwasilisha fomu za uteuzi kwa Tume, atalazimika kuambatanisha picha zake nne zilizopigwa ndani ya siku tisini (90) zenye ukubwa wa “Post Card” na ataweka dhamana ya fedha kama itakavyoelekezwa na Tume.

Fomu za Uteuzi 16. (1) Fomu za Uteuzi za mgombea zitakuwa na taarifa muhimu

zifuatazo:- (a) Maelezo binafsi ya Mgombea; (b) Tamko la mgombea kuwa anazo sifa za kugombea uchaguzi

kwa mujibu wa Sheria; (c) Uthibitisho wa Chama cha Siasa kuwa mgombea huyo ni

mwanachama wake na kimetoa ridhaa kwa yeye kugombea; (d) Tamko, majina, saini na namba za kujiandikisha za wadhamini

wa mgombea; (e) Kiapo cha Mgombea; na (f) Uthibitisho wa Tume au Msimamizi wa Uchaguzi kuwa

mgombea huyo anazo sifa za kugombea.

(2) Ili mgombea aweze kuteuliwa na Tume au Msimamizi wa Uchaguzi, kwa kadiri itakavyokuwa, atalazimika kujaza fomu kwa usahihi na kuziwasilisha Tume au kwa Msimamizi wa Uchaguzi.

Tume Kuthibitisha kupokea fomu za uteuzi.

17. Tume baada ya kupokea fomu za uteuzi, itathibitisha kwa maandishi kupokea fomu hizo.

Fomu za uteuzi kubandikwa katika eneo la wazi la Ofisi

18. Mkurugenzi wa Uchaguzi atabandika kwenye eneo la wazi la Ofisi Kuu ya Tume ya Uchaguzi fomu za uteuzi za wagombea wa Urais zilizopokelewa kabla ya saa kumi kamili za jioni ya siku ya uteuzi

Pingamizi dhidi ya fomu za uteuzi.

19. (1) Mkurugenzi wa Uchaguzi au Mgombea wa Uchaguzi wa Urais anaweza kuweka pingamizi dhidi ya karatasi ya uteuzi ya mgombea wa Urais.

(2) Mgombea wa Urais ambaye ataweka pingamizi dhidi ya fomu za uteuzi za mgombea yeyote, atapeleka pingamizi yake kwa Mkurugenzi ndani ya saa 24 tokea uteuzi wa wagombea ulipofanyika kwa kujaza Fomu Namba PUR 1A iliyowekwa na Tume.

(3) Tume kabla ya kuthibitisha juu ya uhalali wa pingamizi yoyote, bila ya kuchelewa:-

(a) itamjuulisha kwa maandishi mgombea ambaye fomu zake za

uteuzi zimewekewa pingamizi na kumtumia nakala ya fomu ya pingamizi na taarifa nyengine inayoonesha tarehe, pahala na muda ambao pingamizi hiyo itasikilizwa.

8

(b) itampa mgombea au wakala wake nafasi ya kujieleza. Wakala wa mgombea atatambulishwa Tume kwa maandishi yaliyowekwa saini na mgombea mwenyewe.

(4) Pale ambapo Tume imetoa uamuzi juu ya pingamizi yoyote, itazijuulisha kwa maandishi pande zinazohusika, sababu za uamuzi ilioutoa na uamuzi wa Tume utakuwa wa mwisho.

(5) Pale ambapo Tume itakubaliana na pingamizi iliyowekwa dhidi ya mgombea, italiondoa jina la mgombea huyo katika orodha ya wagombea walioomba kuteuliwa.

Uteuzi wa wagombea wa Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi.

20. (1) Endapo Uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi umepangwa kufanyika katika jimbo la uchaguzi, kila chama cha siasa kinachokusudia kushiriki katika uchaguzi huo kitawasilisha barua ya utambulisho inayoelezea kwa ukamilifu jina la mgombea wake katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi.

(2) Msimamizi wa Uchaguzi baada ya kupokea jina la mgombea wa Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kama ilivyoelezwa katika Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii, atatoa fomu za uteuzi kama zilivyotayarishwa na Tume kwa mujibu wa Sheria

(3) Kwa mujibu wa masharti ya Sheria, fomu za uteuzi wa wagombea wa Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi zitawasilishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi katika siku na tarehe kama itakavyoelekezwa na Tume.

(4) Mgombea yeyote wa Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wa kuwasilisha fomu za uteuzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi atalazimika kuambatanisha picha zake nne zenye ukubwa wa “post card” zilizopigwa ndani ya siku tisini (90) na ataweka dhamana ya fedha kama itakavyoelekezwa na Tume.

(5) Msimamizi wa Uchaguzi baada ya kupokea fomu za uteuzi atathibitisha kwa maandishi kupokea kwa fomu hizo.

(6) Msimamizi wa Uchaguzi atazihakiki fomu alizozipokea kuona kama zimejazwa vizuri, na iwapo kuna eneo linalohitaji kurekebishwa atamshauri mgombea kurekebisha sehemu hiyo. Iwapo Mgombea hatafanya marekebisho husika Msimamizi hatamteua mgombea huyo.

Kubandika Fomu za wagombea wa Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi.

21. Msimamizi wa Uchaguzi atabandika nakala za Fomu za uteuzi za kila mgombea pahala wazi nje ya Ofisi ya Uchaguzi ya Wilaya kwa kipindi cha saa 24 baada ya uteuzi wa wagombea.

Pingamizi dhidi ya karatasi za uteuzi za mgombea wa Ujumbe wa Baraza la

22. (1) Mkurugenzi, Msimamizi wa Uchaguzi au mgombea anaweza ndani ya kipindi cha saa 24 baada ya uteuzi wa wagombea kuweka pingamizi kwa kujaza Fomu Namba PUW 2A kwa uteuzi wa Mwakilishi au Fomu Namba PUD. 2A kwa uteuzi wa Diwani na ataiwasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi.

9

Wawakilishi au Diwani.

(2) Msimamizi wa Uchaguzi mara baada ya kupokea Fomu ya pingamizi kutoka kwa mpingaji na kabla ya kutoa uamuzi juu ya uhalali wa pingamizi yoyote atafanya yafuatayo:-

(a) atamjuulisha kwa maandishi mgombea ambaye fomu zake za

uteuzi zimewekewa pingamizi pamoja na nakala ya fomu ya pingamizi na taarifa nyengine zinazoelezea tarehe, pahala na muda ambao pingamizi hiyo itasikilizwa.

(b) atampa mgombea au wakala wake nafasi ya kujieleza. Wakala wa Mgombea atatambulishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi kwa maandishi yaliyowekwa saini na Mgombea mwenyewe.

(3) Pale ambapo Msimamizi wa Uchaguzi ametoa uamuzi juu ya pingamizi yoyote iliyowekwa chini ya Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii, atawajuulisha wahusika uamuzi na sababu za uamuzi huo.

(4) Pale ambapo Msimamizi wa Uchaguzi amekubaliana na pingamizi iliyowekwa dhidi ya mgombea, ataliondoa jina la mgombea katika orodha ya wagombea walioteuliwa.

Pingamizi iliyowekwa na Msimamizi wa Uchaguzi

23. (1) Msimamizi wa Uchaguzi atamuekea mgombea ambaye hakutimiza masharti ya uteuzi kwa kukataa kumteuwa mgombea husika. Katika kutoa uamuzi huo wa kutomteuwa mgombea Msimamizi wa Uchaguzi ataelezea sababu za kutomteuwa mgombea huyo. (2) Tume ndani ya saa 48 itasikiliza pingamizi hiyo na kuitolea uamuzi.

Rufaa

24. (1) Mgombea yeyote ambaye hakuridhika na uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi, anaweza kukata Rufaa kwa Tume ndani ya kipindi cha saa 48 tokea uamuzi ulipotolewa kwa kujaza fomu ya rufaa Fomu Namba. RUW 2A kwa rufaa ya Uwakilishi na Fomu Namba RUD. 3A kwa rufaa ya Udiwani.

(2) Kwa mujibu wa Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii, mkata Rufaa atawasilisha fomu ya Rufaa yake kwa Mwenyekiti na nakala ya Rufaa hiyo itawasilishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi.

Usikilizwaji wa Rufaa.

25. (1) Tume inaweza kabla ya kuisikiliza Rufaa, kumwita mtu yeyote au kutaka taarifa au ufafanuzi kutoka kwa mtu yeyote.

(2) Kushindwa kutokea kwa mtu yeyote ambaye ameitwa na Tume chini ya Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii katika muda na pahala alipotakiwa hakutaathiri usikilizaji wa Rufaa au kutolewa uamuzi na Tume.

(3) Tume itasikiliza rufaa iliyopelekwa mbele yake na kuitolea uamuzi.

10

(4) Baada ya Tume kutoa uamuzi wa rufaa iliyowasilishwa itaziarifu pande zinazohusika kwa maandishi juu ya uamuzi wake na sababu za uamuzi huo.

(5) Uamuzi utakaotolewa na Tume chini ya Kanuni hizi utakuwa ni wa mwisho.

Uteuzi, pingamizi na rufaa za wagombea kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

26. Utaratibu unaotumika juu ya uteuzi, pingamizi na Rufaa kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ndio utakaotumika kwa uteuzi, pingamizi na Rufaa zinazohusiana na Wagombea wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Isipokuwa kwamba pale ambapo neno Wagombea wa Uwakilishi limetumika katika Kanuni hizi litahesabiwa kuwa ni Wagombea wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uthibitisho wa Uteuzi

27. Tume au Msimamizi wa Uchaguzi, kwa kadiri itakavyokuwa, mara baada ya kumteuwa mgombea itamthibitisha mgombea huyo kwa kumpa shahada ya uthibitisho wa uteuzi kama ilivyotayarishwa na Tume.

SEHEMU YA TANO

KUJIONDOA, KUFARIKI AU KUTOKUWEPO KWA MGOMBEA

Kujiondoa kwa mgombea wa Urais, Uwakilishi na Udiwani

28. (1) Mgombea wa Urais anaweza kujiondoa kwa kutoa taarifa ya maandishi aliyoitia saini mwenyewe atakayoiwasilisha kwa Mwenyekiti si zaidi ya saa 10 za jioni ya siku ya uteuzi. (2) Mgombea wa Uwakilishi au Udiwani anaweza kujiondoa kwa kutoa taarifa ya maandishi aliyoitia saini mwenyewe atakayoiwasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi si zaidi ya saa 10 za jioni ya siku inayofuatia ya siku ya uteuzi na kama siku hiyo si siku ya kazi basi siku ya kazi inayofuatia.

(3) Taarifa ya kujiondoa iliyotolewa chini ya Kanuni ndogo ya (1) au (2) ya Kanuni hii, iambatanishwe na tamko la kisheria lililotolewa na kutiwa saini na mgombea mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu kwa Mgombea wa Urais au Hakimu kwa mgombea wa Uwakilishi au Udiwani.

(4) Kwa mujibu wa masharti ya Sheria na Kanuni hizi mgombea yeyote atakaeondoa jina lake nje ya utaratibu uliyoekwa na Kanuni ndogo (1) na (2) dhamana yake aliyotoa kwa Tume wakati wa uteuzi itachukuliwa na kupelekwa Serikalini.

(5) Pale ambapo mgombea amejiondoa baada ya uteuzi, chama cha siasa husika hakitakuwa na haki ya kumteua mgombea mwengine badala yake.

Kufariki kwa Mgombea.

29. (1) Pale ambapo baada ya siku ya uteuzi na kabla ya kufungwa kwa upigaji kura siku ya uchaguzi, mgombea Urais akafariki, Tume baada ya kuthibitisha taarifa za kifo cha mgombea huyo itaahirisha uchaguzi.

11

(2) Endapo, baada ya siku ya uteuzi na kabla ya kufungwa upigaji kura katika uchaguzi wa ujumbe wa Baraza la Wawakilishi au uchaguzi wa Serikali za Mitaa mgombea akafariki, Msimamizi wa Uchaguzi baada ya kuthibitisha taarifa za kifo hicho, ataahirisha uchaguzi na haraka ataiarifu Tume juu ya uamuzi huo.

(3) Endapo uchaguzi wowote utaahirishwa chini ya Kanuni ndogo ya (1) au (2) ya Kanuni hii, Tume katika kipindi kisichozidi siku thelathini baada ya uahirisho huo itateua siku nyengine ya uteuzi wa mgombea na taratibu za uchaguzi katika Jimbo hilo zitaanza upya.

(4) Mgombea yeyote aliyeteuliwa kwa uchaguzi huo ulioahirishwa atahesabiwa kuwa ameteuliwa kihalali na ataendelea kugombea nafasi hiyo isipokuwa ambapo atatoa taarifa ya kujiondoa.

Kufariki kwa mgombea baada ya siku ya uteuzi na kurejeshwa kwa dhamana.

30. (1) Pale ambapo Mgombea amefariki baada ya siku ya uteuzi na kabla ya kufungwa kwa zoezi la upigaji kura, dhamana aliyolipa kwa Tume wakati wa uteuzi, itarejeshwa kwa mwakilishi wake wa kisheria na Tume au Msimamizi wa Uchaguzi.

(2) Kwa mujibu wa Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii Mgombea hatapewa dhamana aliyoweka iwapo baada ya kutangazwa kwa matokeo amepata chini ya asilimia 10 ya idadi ya kura zote halali zilizopigwa na dhamana hiyo itawasilishwa Serikalini.

Kutokuwepo kwa mgombea

31. (1) Endapo baada ya Siku ya Uteuzi wa wagombea, kutokana na sababu ya kufariki, kujiondoa au sababu nyengine yoyote hakutakuwepo na mgombea katika Jimbo, Tume kwa kutoa tangazo katika Gazeti Rasmi, itaahirisha uchaguzi huo na itateua siku nyengine si zaidi ya siku thelathini tokea kuahirishwa huko.

(2) Baada ya Tume kuahirisha uchaguzi, na kutangaza siku mpya ya uteuzi, kutokana na sababu zilizoainishwa katika Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii, taratibu zote za uchaguzi zitaanza upya.

(3) Iwapo uteuzi unafanyika kutokana na sababu za kujiondoa kwa wagombea, Tume haitamruhusu mtu aliyejiondoa kugombea tena katika uchaguzi huo.

SEHEMU YA SITA

KAMPENI ZA UCHAGUZI

Kipindi cha Kampeni

32. (1). Kutakuwa na kipindi cha kampeni kwa kila uchaguzi kama ambavyo itatangazwa na Tume.

(2) Kipindi cha kampeni kitaanza mara baada ya uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi unaogombewa na kumalizika saa 12 jioni kabla ya kuanza upigaji wa kura.

(3) Muda wa kuendesha mikutano ya Kampeni kwa wagombea wote utaanza saa 2 asubuhi na kumalizika saa 12 za jioni.

12

Ratiba ya pamoja ya mikutano ya kampeni za Rais

33. (1) Mkurugenzi anaweza kabla ya kuanza kwa kampeni kwa uchaguzi wa Rais, kukitaka kila chama cha siasa kinachohusika kupeleka kwake ratiba ya mikutano ya kampeni ambayo chama kinakusudia kuifanya kwa ajili ya uchaguzi.

(2) Ratiba inayopendekezwa ya mikutano ya kampeni ieleze kwa ukamilifu tarehe, wakati, mkoa, wilaya na eneo ambalo mikutano hiyo inakusudiwa kufanyika.

(3) Mkurugenzi anaweza, baada ya kupata ratiba hizo kutoka kila chama cha siasa kilichotajwa chini ya Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii, kuitisha mkutano wa vyama vyote vya siasa au wagombea wanaohusika ili kuandaa ratiba ya pamoja ya mikutano ya kampeni.

(4) Baada ya kuandaa ratiba ya pamoja chini ya Kanuni hii, Mkurugenzi atasambaza nakala za ratiba hiyo kwa:-

(a) Vyama vyote vya siasa ambavyo vinashiriki katika uchaguzi wa

Rais; (b) Wasimamizi wa Uchaguzi;

(c) Msajili wa Vyama vya Siasa;

(d) Wakuu wa Mikoa kwa taarifa;

(e) Wakuu wa Wilaya kwa taarifa na

(f) Makamanda wa Polisi wa Mikoa kwa ajili ya kuweka ulinzi.

Kubadilisha ratiba ya pamoja ya mikutano ya Kampeni za Urais

34. (1) Pale ambapo chama chochote cha siasa kina nia ya kufanya mabadiliko ya sehemu ya mkutano wake wa kampeni au ratiba, kitalazimika kumjulisha Mkurugenzi kwa maandishi kikielezea sababu za mabadiliko hayo saa 48 kabla ya kufanyika kwa mkutano huo wa kampeni.

(2) Mkurugenzi mara baada kupokea taarifa ya aina hiyo, kabla ya kufanya mabadiliko anaweza kuitisha mkutano wa pamoja na vyama vya siasa au wagombea wanaohusika kujadiliana juu ya mabadiliko hayo.

(3) Kwa mujibu wa Kanuni ndogo ya (1) na (2) ya Kanuni hii, pale ambapo ratiba ya pamoja itahitajika kufanyiwa marekebisho, Mkurugenzi atarekebisha na atavifahamisha vyama vya siasa vinavyohusika na Maafisa ambao wametajwa chini ya Kanuni ya 33 (4) ya Kanuni hizi.

Ratiba ya pamoja ya mikutano ya kampeni za uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la

35. (1) Msimamizi wa Uchaguzi anaweza kabla ya kuanza kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa, kuvitaka vyama vya siasa vinavyohusika kuwasilisha kwake mapendekezo ya ratiba zao za mikutano ya kampeni wanayokusudia kuifanya kwa ajili ya uchaguzi.

13

Wawakilishi na Serikali za Mitaa

(2) Mapendekezo ya ratiba za mikutano ya kampeni yaelezee tarehe, muda na sehemu ambapo mikutano hiyo inakusudiwa kufanyika.

(3) Msimamizi wa Uchaguzi baada ya kupokea mapendekezo ya ratiba za mikutano ya kampeni kutoka kila chama kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii, ataitisha mkutano wa pamoja wa vyama vya siasa au wagombea wanaohusika, kwa lengo la kukubaliana juu ya ratiba moja ya mikutano ya kampeni.

(4) Baada ya kuandaa ratiba ya pamoja ya mikutano ya kampeni chini ya Kanuni ndogo ya (2) ya Kanuni hii, Msimamizi wa Uchaguzi atazisambaza nakala za ratiba hiyo kwa:-

(a) Vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi wa ujumbe wa

Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa katika jimbo;

(b) Mkuu wa Wilaya kwa taarifa; na

(c) Kamanda wa Polisi wa Wilaya kwa ajili ya kuweka ulinzi wa mikutano ya kampeni.

Mabadiliko ya ratiba ya pamoja ya kampeni za Wagombea wa Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa.

36. (1) Pale ambapo chama cha siasa kina nia ya kubadilisha ratiba yake au eneo la mikutano yake, kitalazimika kumuarifu Msimamizi wa Uchaguzi kwa maandishi na kuelezea sababu za mabadiliko hayo saa 48 kabla ya kufanyika kwa mkutano huo wa kampeni.

(2) Msimamizi wa Uchaguzi mara baada ya kupokea mapendekezo ya mabadiliko anaweza kuitisha mkutano wa vyama vinavyohusika kwa kujadiliana juu ya mabadiliko yaliyopendekezwa.

(3) Endapo kampeni za uchaguzi za Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi au Serikali za Mitaa zitaingiliana au kugongana na ratiba ya pamoja ya wagombea wa Uchaguzi wa Rais, Msimamizi wa Uchaguzi atavijuulisha vyama vyote vya siasa na kuvitaka kufanya marekebisho muhimu katika ratiba ya pamoja ya kampeni za wagombea Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi au Udiwani.

(4) Endapo katika kutekeleza masharti ya Kanuni ndogo ya (2) na (3) ya Kanuni hii, ratiba ya pamoja imefanyiwa marekebisho na chama cha siasa, Msimamizi wa Uchaguzi anaweza kuthibitisha au kutothibitisha mapendekezo ya mabadiliko hayo.

(5) Pale ambapo Msimamizi wa Uchaguzi amethibitisha au kutothibitisha marekebisho yaliyokusudiwa katika Kanuni ndogo ya (4) ya Kanuni hii atalazimika kuelezea sababu za kuthibitisha au kutothibitisha.

(6) Kwa mujibu wa Kanuni hii, Msimamizi wa Uchaguzi baada ya kufanya marekebisho ya ratiba ya pamoja atatoa taarifa kwa:-

(a) Vyama vya siasa vinavyohusika;

(b) Mkuu wa Wilaya; na

14

(c) Kamanda wa Polisi wa Wilaya.

Kampeni katika nyumba za ibada, taasisi za elimu na majengo ya umma.

37. (1) Kwa madhumuni ya uchaguzi, vyama vyote vya siasa havitaruhusiwa kufanya kampeni katika nyumba za ibada, taasisi za elimu na majengo ya umma.

(2) Kwa madhumuni ya Kanuni hii, nyumba za ibada zinahusisha eneo lolote lililoandikishwa kwa madhumuni ya kufanya harakati mbalimbali za kidini.

(3) Kwa madhumuni ya Kanuni hii, majengo ya taasisi ya elimu ni pamoja na eneo lolote linalotumika kwa madhumuni ya kutoa elimu. Isipokuwa Tume inaweza kuzuia matumizi ya viwanja vilivyo nje ya majengo ya elimu kwa ajili ya mikutano ya kampeni za uchaguzi endapo kutakuwa na shughuli za kielimu zinazoendelea katika majengo hayo.

(4) Kwa madhumuni ya Kanuni hii, majengo ya Umma ni pamoja na Ofisi za Serikali zinazotoa huduma kwa jamii.

Kuidhinisha vifaa vya kampeni

38. (1) Tume itaidhinisha matumizi ya vifaa vya kampeni kwa ajili ya kampeni za vyama vya siasa.

(2) Kila chama cha Siasa, kabla ya kuchapisha vifaa vya kampeni kwa ajili ya matumizi yake kitawajibika kuwasilisha Tume mchoro wa awali wa kifaa husika kwa ajili ya kuidhinishwa.

(3) Tume baada ya kuridhika na mchoro wa awali uliowasilishwa na chama husika kwa ajili ya kampeni zake itauthibitisha na kuidhinisha kutumika kwake kwa ajili ya kampeni.

(4) Kwa madhumuni ya Kanuni hii vifaa vya kampeni vinajumuisha; mabango, picha, fulana, kofia, kanga, vitenge na vifaa vyengine vitakavyoidhinishwa na Tume.

(5) Chama chochote kitakaekwenda kinyume na masharti ya Kanuni hii kitakuwa kimetenda kosa na kikipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tano.

SEHEMU YA SABA

SIKU YA UCHAGUZI Siku ya Uchaguzi.

39. Kwa mujibu wa vifungu vya Katiba na Sheria, kutakuwa na siku ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na viongozi wa Serikali za Mitaa kama ambavyo itatangazwa na Tume.

Taarifa ya Uchaguzi

40. (1) Tume itatoa taarifa ya uchaguzi wa Rais kwa umma kabla ya kuanza upigaji kura.

(2) Msimamizi wa Uchaguzi atatoa taarifa ya uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na viongozi wa Serikali za Mitaa kwa wananchi wa eneo lake kabla ya kuanza upigaji kura.

15

(3) Taarifa ya uchaguzi iliyotajwa chini ya Kanuni hii itaelezea mambo yafuatayo:-

(a) Tarehe na muda wa kufunguliwa na kufungwa kwa upigaji

kura; (b) anuani ya kila kituo cha kupigia kura katika jimbo;

(c) majina na nambari za usajili za wapiga kura ambao watapiga

kura katika kila kituo;

Kufutwa kwa siku ya uchaguzi na kutangazwa kwa siku nyengine

41. (1) Pale ambapo kabla ya siku ya uchaguzi kwa uchaguzi wowote, kutatokea tukio ambalo litasababisha uchaguzi kutofanyika, Tume itaifuta siku ya mwanzo ya Uchaguzi na itatangaza siku nyengine kwa ajili ya Uchaguzi husika.

(2) Pale ambapo katika siku ya uchaguzi, uchaguzi utashindwa kufanyika katika jimbo la uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi haraka atatoa taarifa kwa Tume ambayo itateua siku nyengine ya uchaguzi kwa jimbo hilo.

(3) Iwapo siku ya uchaguzi iliyopangwa awali imefutwa, Tume itatangaza siku nyengine kwa uchaguzi husika na itatoa taarifa ya uchaguzi kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya 40

Wakala wa upigaji kura.

42. (1) Kila Chama cha siasa kinachoshiriki katika uchaguzi, kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 64 cha Sheria, katika kipindi cha siku kumi na nne kabla ya upigaji kura, kinaweza kuwasilisha jina moja la wakala wa Mgombea Urais, ikiwa kimeweka mgombea, na jina jengine kwa ajili ya wagombea wa Uwakilishi na udiwani kwa Msimamizi wa Uchaguzi majina na anuani za mawakala na vituo ambavyo wamepangwa.

(2) Jina la wakala na anuani ya kituo anachosimamia vitawasilishwa pamoja na picha mbili za ukubwa wa picha za ”passport” kwa ajili ya utaratibu wa kupatiwa kitambulisho cha uwakala.

(3) Msimamizi wa Uchaguzi baada ya kupokea taarifa chini ya Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii, atawajuulisha Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura mawakala walioruhusiwa kuwemo katika vituo vya kupigia kura.

(4) Kila wakala wa upigaji kura atatakiwa kabla ya kuanza shughuli zake ndani ya kituo cha kupigia kura, kula kiapo cha kutunza siri mbele ya Hakimu katika Fomu Namba FK. 3 kama ilivyotayarishwa na Tume. (5) Kila wakala wa upigaji kura atatayarishiwa kitambulisho kwa ajili ya kumtambulisha. Kitambulisho kilichotayarishwa atapatiwa wakala iwapo atakuwepo katika kituo tu.

16

Majukumu ya wakala wa upigaji kura

43. (1) Wakala wa upigaji kura atatekeleza majukumu yafuatayo:- (a) kugundua watu wanaojifananiza kwa kutizama jina la mpiga kura

katika daftari la wapiga kura alilopatiwa na Tume. (b) Kumuwakilisha na kulinda maslahi ya mgombea katika kituo cha

upigaji kura kwa kuhakikisha taratibu za kiuchaguzi zinakwenda kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za uchaguzi.

(c) Kushirikiana na Msimamizi wa kituo na wasaidizi wa vituo

kuhusiana na masuala ya upigaji kura na uchaguzi katika kituo cha upigaji kura.

(2) Wakala wa upigaji kura anaweza kuomba kwa msimamizi wa kituo kuona kitambulisho cha mpiga kura kwa ajili ya kugundua wanaojifananiza.

Usambazaji na ulinzi wa vifaa vya uchaguzi na upigaji kura.

44. (1) Tume itakabidhi Vifaa vyote vya uchaguzi na upigaji kura kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, pamoja na kutoa miongozo ya utumiaji, usambazaji na ulinzi wa vifaa hivyo.

(2) Msimamizi wa Uchaguzi siku moja kabla ya tarehe ya upigaji kura, atasambaza au atatoa amri ya kusambazwa vifaa vya uchaguzi kwa kila kituo cha kupigia kura.

(3) Kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii, usambazaji wa vifaa vya uchaguzi utafanyika kwa maandishi, kwa kujaza Fomu Namba PS. 1 ya orodha ya vifaa, na vifaa vyote vitakuwa chini ya usimamizi wa Msimamizi wa kituo cha kupigia kura.

Matayarisho ya upigaji kura

45. (1) Kabla ya kuanza upigaji kura, msimamizi wa kituo atafanya yafuatayo:- (a) Ataandaa mazingira ya kupanga kituo kama ilivyoelekezwa na

Tume na atajaza Fomu Namba PS. 2 ya mahudhurio ya kituo;

(b) atajaza fomu za kufungua kituo cha kupigia kura kwa kujaza Fomu Namba PS. 3;

(c) atajaza fomu za kumbukumbu ya vifungio vya masanduku ya

kura na mihuri kwa kujaza Fomu Namba PS. 4

(d) ataonesha sanduku tupu la kupigia kura kwa walioruhusiwa kuwapo kituoni;

(e) atalifunga sanduku la kura kwa kutumia vifungio maalum na

kuwaruhusu wagombea au mawakala waliopo kama watahitaji kufanya hivyo na kujaza Fomu Namba PS. 5A kwa uchaguzi wa Rais, Fomu Namba PS. 5B kwa uchaguzi wa Uwakilishi na Fomu Namba PS. 5A kwa uchaguzi wa Udiwani za kumbukumbu ya vifungio vya masanduku ya kura;

(f) ataliweka sanduku la kupigia kura sehemu linapoonekana kwa

kutumbukiza karatasi za kura; na

17

(g) atatoa tamko la kufungua kituo na kuanza upigaji kura.

Kuridhika au kutoridhika na matayarisho ya kituo cha upigaji kura.

46. (1) Pale ambapo Wakala yeyote wa upigaji kura ameridhika au hakuridhika na matayarisho ya kituo cha kupigia kura, atapaswa kabla ya kuanza kwa upigaji kura kujaza Fomu Namba PS. 3 ya ufunguaji wa kituo cha kupigia kura.

(2) Msimamizi wa Kituo atayatolea uamuzi malalamiko ya wakala na kueleza sababu za maamuzi hayo.

Upigaji kura.

47. (1) Kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 68(3) cha Sheria, Msimamizi wa kituo cha kupigia kura au Msaidizi Msimamizi wa kituo cha kupigia kura iwapo ataridhika kuwa jina la mpiga kura limo katika Daftari la kituo hicho:-

(a) ataiangalia shahada ya mpiga kura pamoja na maelezo yake

na kulinganisha na maelezo yaliyomo katika Daftari;

(b) Atasoma kwa sauti jina la mpiga kura huyo;

(c) ataweka alama katika jina la mpiga kura huyo katika daftari kuonesha kuwa mpiga kura huyo tayari amepatiwa karatasi ya kura.

(d) Atamuelekeza mpiga kura kwa Msaidizi Msimamizi wa kituo ili

ampatie karatasi ya kura.

(2) Msaidizi Msimamizi wa kituo baada ya kuelekezwa na msimamizi wa kituo kumpatia mpigakura karatasi ya kupigia kura atafanya yafuatayo:-

(a) Ataichana karatasi ya kupigia kura kutoka katika kitabu cha

karatasi za kura;

(b) Ataikunja kwa utaratibu ambao kura iliyopigwa haitaweza kuharibika na kumfahamisha mpiga kura utaratibu wa kuikunja karatasi husika baada ya kupiga kura;

(c) ataipiga muhuri maalumu uliotayarishwa na Tume karatasi ya

kura; na

(d) atampatia mpiga kura karatasi ya kura.

(3) Mpiga kura baada ya kupatiwa karatasi ya kura atakwenda kwenye kituturi cha kupigia kura na:-

(a) Atachagua mgombea mmoja tu ambaye amependelea

kumpigia kura yake kwa kuweka alama ya vema (√) au alama yoyote inayoonesha nia ya mpiga kura;

(b) ataikunja karatasi ya kura kwa utaratibu aliyoelekezwa;

18

(c) ataitumbukiza karatasi ya kura iliyokunjwa ndani ya sanduku husika la kura; na

(d) atakwenda kwa Msaidizi Msimamizi wa kituo kutia wino

usiofutika katika kidole chake cha shahada cha mkono wa kushoto kabla ya kuondoka kituoni.

Kupiga kura eneo la faragha

48. (1) Mpiga kura atapiga kura yake kwa siri katika eneo la faragha kama itakavyoelekezwa na Tume.

(2) Msimamizi wa Kituo atakiweka kituturi cha kupigia kura katika sehemu ya faragha itakayomuwezesha mpiga kura kupiga kura yake kwa siri.

Upigaji kura kwa wenye mahitaji maalumu

49. (1)Tume inaweza kuweka kifaa maalum cha kupigia kura kumuwezesha mtu mwenye mahitaji maalum kupiga kura bila ya usaidizi.

(2) Iwapo mpiga kura hawezi kupiga kura mwenyewe kwa sababu ya mahitaji maalumu yanayotokana na ulemavu, kutokujua kusoma na kuandika au sababu nyengine yoyote, anaweza kusaidiwa kupiga kura yake na mtu aliyemchagua kama jamaa yake wa karibu.

(3) Msimamizi wa Kituo atamruhusu mtu huyo kumsaidia mpigakura aliyeomba kusaidiwa kupiga kura yake baada ya kuridhika na maelezo ya mpiga kura huyo kwa kuorodhesha taarifa za mpiga kura huyo katika Fomu Namba PS. 6 ya wapiga kura waliosaidiwa.

(4) Iwapo Mpiga kura hana mtu wa kumsaidia anaweza kumuomba Msimamizi wa kituo kumsaidia kupiga kura yake.

(5) Mtu yeyote anayemsaidia mpiga kura kabla ya kutekeleza wajibu huo atakula kiapo cha kutunza siri. Isipokuwa, kiapo cha msimamizi wa kituo alichokula awali kwa utekelezaji wa majukumu kitachukuliwa kuwa ni kiapo kwa madhumuni ya kifungu hiki.

Ufungaji wa kituo cha kupigia kura

50. (1) Mara baada ya kukamilika upigaji kura, Msimamizi wa Kituo atatangaza kufungwa kwa kumalizika kwa upigaji wa kura katika kituo na atalifunga sanduku la kura katika kipenyo cha kuingizia kura mbele ya wanaoruhusiwa kuwemo katika kituo cha kupigia kura.

(2) Msimamizi wa kituo kabla na baada ya kumaliza kupiga kura, ataweka kumbukumbu za karatasi za kura kwa kujaza Fomu Namba PS. 7A kwa uchaguzi wa Rais, Fomu Namba PS 7B kwa uchaguzi wa Uwakilishi na Fomu Namba PS. 7C kwa uchaguzi wa Udiwani zinayoonyesha yafuatayo:-

(a) karatasi za kura alizokabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi;

(b) vishina vya karatasi za kura zilizotumika;

(c) karatasi za kura ambazo hazikutumika; na

19

(d) karatasi ya kura iliyoharibika.

(3) Kwa madhumuni ya Kanuni ndogo ya (2), karatasi ya kura iliyoharibika maana yake ni karatasi ya kura iliyoharibika kabla ya mpiga kura kuiingiza katika sanduku la kura; kutokana na ama kuchanika vibaya, au mpiga kura kukosea kupiga kura hiyo na kuomba kupatiwa karatasi nyengine au sababu nyengine yoyote itayosababisha karatasi hiyo isiweze kuingizwa katika sanduku la kura; (4) Mara baada ya kukamilika kwa uwekaji wa kumbukumbu za karatasi za kura katika fomu husika, atakifunga kituo cha kupigia kura kwa kujaza Fomu Namba PS 8.

Kuahirishwa kwa upigaji kura.

51. (1) Iwapo siku ya upigaji kura, zoezi hilo litaingiliwa na vurugu au limezuilika kwa vurugu au ghasia za wazi, au tukio linalosababisha uchaguzi usiendelee, Msimamizi wa kituo cha kupigia kura atafanya yafuatayo:-

(a) kama kutakuwa na wapiga kura ambao wamebakia, ataahirisha

upigaji kura mpaka hali itakapotengamaa na iwapo hali haikutengamaa ataahirisha hadi siku inayofuata na kituo kitafunguliwa saa zile zile za upigaji kura kama ilivyokuwa siku ya kwanza;

(b) iwapo wapiga kura wote waliomo katika daftari wamekamilisha

kupiga kura, upigaji kura utahesabiwa kuwa umekamilika.

(2) Iwapo upigaji kura utaahirishwa kwa mujibu wa Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii, Msimamizi wa kituo cha kupigia kura haraka atamjuulisha Msimamizi wa Uchaguzi au Msaidizi Msimamizi wa Uchaguzi. Msimamizi wa Uchaguzi au Msaidizi Msimamizi haraka iwezekanavyo ataiarifu Tume kuhusu suala hilo.

SEHEMU YA NANE

KUHESABU, KUJUMLISHA KURA NA KUTANGAZA MATOKEO

Kuhesabu kura.

52. (1) Baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji kura, mawakala wa upigaji kura watahesabiwa kuwa ni mawakala wa kuhesabu kura, isipokuwa pale tu ambapo mgombea amewasilisha mawakala maalumu kwa ajili ya kuhesabu kura. (2) Msimamizi wa Kituo cha kuhesabu kura kabla ya kuanza kuhesabu kura atafanya yafuatayo:- (a) Ataandaa mazingira ya kituo cha kuhesabu kura;

(b) Atajaza fomu ya kuridhika au kutoridhika na ufunguzi wa kituo

cha kuhesabia kura;

(c) Atatoa tamko la kuanza kwa zoezi la kuhesabu kura na atahesabu kura kwa utaratibu ufuatao:-

20

i. Atakata vifungio vya plastiki vilivyofungwa pembeni mwa sanduku la kura;

ii. Atamimina karatasi za kura katika sehemu iliyotayarishwa

kwa ajili ya kuhesabia kura; iii. Atahesabu kura moja moja kwa sauti ili kujiridhisha na idadi

ya karatasi za kura zilizopigwa; iv. Ataandika idadi ya kura zote zilizopatikana kutoka katika

sanduku la kura;

(d) Baada ya kurikodi idadi ya kura zilizopatikana kutoka sanduku

la kura atafanya yafuatayo:- i. Ataikunjua karatasi ya kura moja moja na kuionesha

mgombea aliyepigiwa au kama imeharibika na

ii. Ataiweka kura aliyoikunjua kwa mujibu wa mgombea aliyepata kura hiyo au eneo la kura zilizoharibika;

(e) Msimamizi baada ya kukamilisha hatua ya upembuzi wa kura kwa mujibu wa wagombea au upande wa kura zilizoharibika atafanya yafuatayo:- i. atahesabu kwa sauti kura za kila mgombea na zile

zilizoharibika au zenye mgogoro;

ii. ataandika idadi ya kura zilizopatikana kwa kila mgombea na kulinganisha na hesabu ya kura zilizopatikana kutoka kwenye sanduku la kura;

iii. atazifunga kura hizo na kuziweka katika bahasha tofauti

kama ifuatavyo:-

(a) Bahasha ya kura halali,

(b) Bahasha ya kura zilizoharibika, na

(c) Bahasha ya kura zenye mgogoro.

(f) Atajaza fomu ya matokeo na kuibandika nakala moja sehemu ya wazi ya kituo, nakala nyengine ataiwasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi na nakala zilizobakia atazigawa kwa mawakala na waangalizi waliomo katika kituo.

Kuridhika au kutoridhika na matayarisho ya kituo cha kuhesabia kura

53. (1) Pale ambapo wakala wa kuhesabu kura ameridhika au kutoridhika na matayarisho ya kituo cha kuhesabia kura, atapaswa kabla ya kuanza kwa zoezi la kuhesabia kura kujaza maelezo yake katika Fomu Namba PS. 9.

21

(2) Msimamizi wa Kituo atasikiliza maelezo hayo na kupitia fomu hiyo ataeleza namna alivyoyashughulikia maelezo hayo.

Matokeo ya kituo cha kuhesabia kura.

54. (1) Msimamizi wa kituo cha kuhesabia kura, baada ya kuhesabu kura zote kwa mujibu wa Sheria na Kanuni hizi, ataweka kumbukumbu za matokeo ya uchaguzi ya wagombea Urais katika Fomu Nam MUR 12A, wagombea Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Fomu Nam 22A, na viongozi wa Serikali za mitaa katika Fomu Nam 32A.

(2) Fomu za matokeo kwa kila uchaguzi zitatiwa saini na Msimamizi wa kituo, mgombea au wakala wa kuhesabu kura na kila wakala au mgombea atapatiwa nakala ya matokeo.

(3) Msimamizi wa kituo mara baada ya kuweka kumbukumbu za matokeo katika fomu husika atafanya yafuatayo:-

(a) atabandika nakala ya matokeo ya uchaguzi ya kituo katika eneo la wazi nje ya kituo.

(b) atafunga pamoja na kuweka vifungio katika sanduku la kura

bahasha zote za karatasi za kura.

(c) atajaza Fomu Namba PS 10 na atatoa tamko la kufunga kituo cha kuhesabia kura

(4) Msimamizi wa kituo baada ya kufunga kituo cha kuhesabia kura atawasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi yafuatayo:-

(a) fomu za matokeo ya kituo cha kuhesabia kura ziliyojazwa;

(b) taarifa ya kituo cha kupigia kura ambayo itakuwa na

yafuatayo:-

(i) fomu zilizojazwa kama zilivyotayarishwa na Tume.

(ii) tamko la mpiga kura kama lipo ambalo limefanywa kama ilivyoelekezwa na Tume;

(iii) fomu zenye malalamiko ya mpiga kura kama zipo kuhusu

mchakato wa uchaguzi na maelezo ya jinsi ambavyo yameshughulikiwa;

(iv) fomu ambazo hazikutumika;

(v) fomu zenye hesabu za kura; (vi) karatasi za kupigia kura zilizokuwa hazikutumika au

zimeharibika kama zipo; (vii) Daftari la wapiga kura;

(c) sanduku la kupigia kura na kura; na

22

(d) kifaa chengine chochote cha uchaguzi au kupigia kura

alivyokabidhiwa kwa ajili ya kazi za uchaguzi.

Taarifa ya majumuisho ya kura.

55. Msimamizi wa Uchaguzi, siku saba kabla ya upigaji kura, atavijuulisha kwa maandishi vyama vya siasa au wagombea siku, wakati na pahala pa majumuisho ya kura ndani ya jimbo.

Majumuisho ya kura za wagombea urais.

56. (1) Msimamizi wa Uchaguzi mara baada ya kupokea matokeo na kabla ya kufanya majumuisho ya vituo katika Jimbo lake, atatolea uamuzi kura zenye malalamiko zilizowasilishwa kwake na Msimamizi wa kituo kama zipo.

(2) Kutakuwa na wakala wa majumuisho ambaye atateuliwa na mgombea kwa madhumuni ya kumwakilisha mgombea katika majumuisho ya kura katika jimbo. (3) Msimamizi wa Uchaguzi atafanya majumuisho ya kura kutoka vituo vyote katika jimbo la uchaguzi mbele ya wagombea au mawakala wa majumuisho ya kura kama watakuwepo.

Matokeo ya kura za uchaguzi wa Rais kwa majimbo.

57. Msimamizi wa Uchaguzi baada ya kufanya majumuisho ya kura kwa uchaguzi wa Rais:-

(a) ataweka kumbukumbu ya matokeo ya vituo kwa wagombea

Urais kwa jimbo katika Fomu Namba MUR 12A iliyotayarishwa na Tume;

(b) atatoa kwa kila mgombea au wakala nakala ya fomu ya

matokeo hayo;

(c) mara moja atawasilisha kwa Tume fomu ya matokeo ya wagombea Urais kwa jimbo pamoja na fomu zote za vituo.

Kujumlisha na kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Urais

58. (1) Tume itavijulisha kwa maandishi vyama au wagombea wa Urais pahala, muda na tarehe ya majumuisho ya kura za Urais siku saba kabla ya upigaji kura, ambapo majumuisho yote yatafanyika.

(2) Tume itafanya uhakiki wa matokeo ya majimbo yote itakayoyapokea na kuyatangaza kwa kila Jimbo.

(3) Kwa mujibu wa Kanuni hii, Tume itajumlisha matokeo ya urais kwa majimbo yote kama yalivyowasilishwa kwake na Wasimamizi wa Uchaguzi.

(4) Tume baada ya kufanya majumuisho ya hesabu za matokeo ya majimbo chini ya Kanuni hii:-

(a) itaweka kumbukumbu za matokeo ya urais kwa majimbo yote;

(b) itatangaza matokeo ya jumla ya Urais na itamtangaza

mgombea ambaye amepata wingi wa kura halali zilizopigwa;

23

(c) itatoa kwa kila mgombea au wakala wake au chama kinachohusika nakala ya matokeo; na

(d) itabandika nakala ya matokeo katika ubao wa matangazo wa

Ofisi za Tume.

(5) Tume haraka baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Rais chini ya Kanuni hii, itatoa shahada kwa mshindi wa Uchaguzi kwa kujaza Fomu Namba SUR 15A kama iliyotayarishwa.

(6) Shahada ya mshindi wa Urais iliyoelezwa chini ya Kanuni ndogo ya (5) itakuwa na maelezo yafuatayo:-

(a) jina kamili la mgombea aliyeshinda;

(b) tarehe ya uchaguzi;

(c) nafasi aliyochaguliwa mgombea; na

(d) saini ya Mwenyekiti.

(7) Tume itachapisha matokeo ya uchaguzi wa Rais katika Gazeti Rasmi.

Kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Viongozi wa Serikali za Mitaa.

59. Msimamizi wa Uchaguzi baada ya majumuisho ya kura kutoka katika vituo vyote vya kupigia kura katika jimbo:-

(a) Atajaza matokeo ya uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la

Wawakilishi na Viongozi wa Serikali za mitaa katika Fomu MUW 22B na Fomu Namba MUD 32B kama ziliyotayarishwa na Tume.

(b) atawataka wagombea au mawakala wao kama watakuwepo kuweka saini zao katika fomu hizo;

(c) Haraka, atamtangaza mgombea ambaye amepigiwa kura nyingi

halali kuwa ndiye aliyeshinda katika jimbo;

(d) atatoa kwa kila mgombea au mawakala wao kama watakuwepo nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi; na

(e) atabandika nakala ya fomu ya matokeo katika sehemu ya wazi

nje ya kituo cha majumuisho ya jimbo.

(2) Msimamizi wa Uchaguzi mara baada ya kutangaza matokeo chini ya Kanuni hii, atatoa shahada kwa mgombea aliyechaguliwa ambaye maelezo yake yatakuwa katika Fomu Namba SUW 15B iliyotayarishwa na Tume, kuwa mshindi wa ujumbe wa Baraza la Wawakilishi na Fomu Namba SUD 15C kwa mshindi wa uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

(3) Shahada ya ushindi wa uchaguzi iliyoelezwa chini ya Kanuni ndogo ya pili itakuwa na maelezo yafuatayo:-

(a) jina kamili la mgombea aliyechaguliwa;

24

(b) tarehe ya uchaguzi;

(c) nafasi ya mgombea aliyechaguliwa; na

(d) saini ya Msimamizi wa Uchaguzi.

(4) Msimamizi wa Uchaguzi baada ya kutangaza matokeo ya jimbo, atatuma matokeo kwa Tume, na Tume itayachapisha matokeo hayo katika Gazeti Rasmi la Serikali.

SEHEMU YA TISA

KUTANGAZWA KWA WAJUMBE WA VITI MAALUM VYA

WANAWAKE KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI

Viti Maalum vya Wanawake.

60. (1) Kutakuwa na Viti Maalum vya Wanawake katika Baraza la wawakilishi kama inavyoelezwa chini ya kifungu cha 67(1) cha Katiba.

(2) Kwa mujibu wa Kanuni ndogo ya (1) ya Kanuni hii, kila chama cha siasa ambacho kimeshiriki katika uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, kinaweza kupendekeza majina ya wanawake wenye sifa za kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Viti Maalum vya Wanawake.

Taratibu za uteuzi.

61. (1) Kwa mujibu wa Vifungu vya 67 na 68 vya Katiba, Tume itataja idadi ya wagombea wanawake ambao watateuliwa na kila Chama cha Siasa.

(2) Kila Chama cha siasa kinachowadhamini wagombea wa viti maalum vya wanawake kwa mujibu wa masharti ya Katiba na Kanuni hizi, kinapaswa kuwasilisha Tume orodha ya majina ya wagombea hao kabla ya siku ya uteuzi iliyotangazwa na Tume.

(3) Kila mgombea wa viti maalum vya wanawake ambaye jina lake limewasilishwa Tume chini ya Kanuni ndogo ya (2) ya Kanuni hii, atatakiwa kujaza Fomu Namba UM 01 kama zilivyotayarishwa na Tume. (4) Fomu za uteuzi zitatakiwa kuwa na yafuatayo:-

(a) maelezo binafsi ya mgombea wa viti maalum vya wanawake; (b) tamko maalum la mgombea mwanamke;

(c) uthibitisho wa chama cha siasa kuwa mgombea mwanamke ni

mwanachama na anadhaminiwa na chama hicho.

(5) Baada ya kupokea orodha ya majina ya wagombea wa viti maalum vya wanawake na kujiridhisha kuwa wanazo sifa za kuwa wagombea, Tume itafanya uteuzi na kuviarifu Vyama vyao.

25

(6) Kila chama cha siasa kitachoshinda zaidi ya asilimia kumi (10%) ya viti vya majimbo ya Baraza la Wawakilishi, ndani ya saa 48 baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, kitawasilisha orodha ya majina ya wagombea wanawake iliyopangwa kwa umuhimu wake.

(7) Masharti ya kifungu cha 68 cha Katiba yatatumika kwa kila mwanamke ambaye amedhaminiwa na chama cha siasa kama ni mgombea.

(8) Tume kwa mujibu wa masharti ya vifungu vya 67 na 68 vya Katiba, Kanuni hizi na kwa mujibu wa mpangilio wa umuhimu wa majina katika orodha za wagombea zilizowasilishwa na kila chama cha siasa, itawatangaza wagombea wanawake kutoka kila chama kinachohusika.

(9) Tume itapeleka taarifa ya uteuzi kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi na chama cha siasa kinachohusika.

(10) Tume itachapisha katika Gazeti Rasmi majina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Wanawake wa Viti Maalum.

SEHEMU YA KUMI

MASHARTI MENGINEYO

Kutokuwepo kwa wakala wa upigaji kura au mgombea.

62. Kutokuwepo kwa Wakala wa kupiga kura au kuhesabu kura au Mgombea katika muda uliopangwa na pahala pa kupigia kura hakutasababisha kusimamishwa, kuchelewa au kutohalalishwa kwa mchakato wa uchaguzi.

Kura halali 63. (1) Ili kura ihesabiwe kuwa ni kura halali, mpiga kura atatakiwa apige kura yake kwa kuweka alama ya vema (V) katika chumba maalumu kilichowekwa chini ya mgombea anayemchagua.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni hii, Tume itaihesabu alama nyengine yoyote kuwa ni alama halali ikiwa tu itaonesha dhamira ya mpiga kura.

Kura iliyoharibika 64. (1) Kura itahesabiwa kuwa imeharibika iwapo mpiga kura atafanya yafuatayo katika karatasi ya kura:-

(a) Kuweka maandishi yoyote au alama inayoweza kumtambulisha;

(b) Kuchagua zaidi ya mgombea mmoja;

(c) Kutochagua mgombea yoyote;

(d) Kuweka alama nje ya eneo la mgombea katika karatasi ya kura.

(2) Kura itahesabiwa kuwa imeharibika iwapo haikupigwa muhuri maalum wa Tume.

Kutolewa kwa Fedha za uchaguzi na matumizi ya

65. (1) Mkurugenzi anaweza kuidhinisha fedha kwa ajili ya malipo ya watendaji wa uchaguzi au masurufu kwa Wasimamizi wa Uchaguzi kwa madhumuni ya kurahisisha na kuendesha uchaguzi.

26

fedha na taarifa za matumizi

(2) Matumizi ya fedha za uchaguzi yanayofanywa na Wasimamizi wa Uchaguzi yatafanyika kwa mujibu wa Kanuni za Fedha na Kanuni za Manunuzi ya Umma.

(3) Kila Msimamizi wa Uchaguzi mara baada ya kukamilisha shughuli zote za uchaguzi na katika kipindi kisichozidi wiki mbili baada ya kutangazwa kwa matokeo atatayarisha na kuwasilisha kwa Mkurugenzi ripoti ya utekelezaji na taarifa ya matumizi ya fedha alizokabidhiwa kwa ajili ya kuendesha uchaguzi.

Kushindwa kufuata masharti ya Kanuni.

66. Pale ambapo Msimamizi wa Uchaguzi ameshindwa kufuata maelekezo ya Kanuni ya 65 (2) na (3) ya Kanuni hizi, Mkurugenzi atachukua hatua za kinidhamu dhidi ya Msimamizi wa Uchaguzi kama zililivyoainishwa katika Kanuni za Fedha

Taratibu nyengine za uchaguzi.

67. Maafisa wa Uchaguzi, Watendaji wa Uchaguzi, Wagombea, vyama vya siasa pamoja na wadau wa uchaguzi, watalazimika kufuata masharti ya Katiba, Sheria na Kanuni pamoja na miongozo mingine yoyote itakayotolewa na Tume.

Makosa na adhabu.

68. Mtu yeyote ambaye atakwenda kinyume na masharti ya Kanuni hizi atakua ametenda kosa na akipatikana na hatia atapewa adhabu kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi.

ZANZIBAR, Imetiwa saini leo tarehe ____, Mwezi wa _______, 2015.

_________________ Jecha Salim Jecha

Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar

27

JADWELI LA KWANZA

KURA HALALI NA KURA ZILIZOHARIBIKA

MIFANO YA KURA HALALI

KURA HALALI HALALI

Jina na Anuani Jina na Anuani Jina na Anuani

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Chama Chama Chama

Kura halali inayokubalika ambayo imewekewa alama ya vema katika chumba cha mgombea aliyechaguliwa na mpiga kura kama inavyoelekezwa na Sheria.

Jina na Anuani Jina na Anuani Jina na Anuani

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea ///

Chama Chama Chama

Alama iliyowekwa kwenye picha ya mgombea kinyume na maelekezo (uso wa mgombea): nia ya mpiga kura inaeleweka

Jina na Anuani Jina na Anuani Jina na Anuani

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Chama

√ Chama Chama

Alama ya √ (vyema) imewekwa katika alama ya chama (logo) nia ya mpiga kura inaeleweka, kura hiyo itahesabiwa.

Jina na Anuani Jina na Anuani Jina na Anuani

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Chama √

Chama Chama

28

Alama ya √ (vyema) imewekwa katika alama ya chama (logo) na chumba cha kuweka alama ya mpiga kura, nia ya mpiga kura inaeleweka, kura hiyo itahesabiwa.

Jina na Anuani Jina na Anuani Jina na Anuani

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Chama

Chama Chama

Alama ya √ (vyema) iliyowekwa imevuka eneo la mgombea aliyekusudiwa. Hata hivyo, nia ya mpiga kura inaeleweka, kura hiyo itahesabiwa kuwa ni halali kwa mgombea wa mwanzo. MFANO WA KURA ZILIZOHARIBIKA

Kuweka alama √ (vyema) katika chumba kinachokubalika na alama ya X katika sura au picha ya mgombea. Kura hii haikubaliki kwa sababu nia ya mpiga kura haiko wazi.

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Chama Chama Chama

√ Alama ya √ (Vyema) imewekwa nje ya eneo lote la kupigia kura (iko nje chumba kinachopendekezwa); haitahesabiwa

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Chama Chama Chama

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

X

CHAMA CHAMA CHAMA

29

Alama za VYEMA (√) ziko kama ilivyoelekezwa chini ya picha za wagombea wote, kura hiyo haikubaliki kwani mpiga kura hakumpigia mgombea moja kama anavyotakiwa na Sheria.

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Chama Chama Chama

Karatasi ya kura haikupigwa muhuri wa kituo sehemu ya nyuma kama inavyoelekezwa na Sheria, karatasi hiyo haifunguliwi na haihesabiwi.

Jina na Anuani Jina na Anuani Jina na Anuani

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Picha ya Mgombea

Chama

Chama Chama

Hasara

Karatasi ya kura imetiwa maandishi yanayomtambilisha mpiga kura

30

JADWELI LA PILI

FOMU ZA KANUNI ZA UCHAGUZI