ufafanuzi wa agano jipya luka - african pastors …taratibu habari za yesu kabla ya luka. alitumia...

203
Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka www.africanpastors.org Na Dorothy Almond mwisho na Askofu Francis Ntiruka

Upload: others

Post on 08-Jan-2020

217 views

Category:

Documents


57 download

TRANSCRIPT

Page 1: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

Ufafanuzi WaAgano Jipya

Luka

www.africanpastors.org

Na Dorothy Almondmwisho na Askofu Francis Ntiruka

Page 2: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

Ufafanuzi WaAgano Jipya

LukaDorothy Almond

© African Pastors Fellowship 2010

Kimetolewa na:AFRICAN PASTORS FELLOWSHIP

Station House, Station Approach, AdishamCanterbury, Kent CT3 3JE

United Kingdom

www.africanpastors.org

Page 3: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

DIBAJIAliyeandika kitabu hiki cha ufafanuzi ni Sista Dorothy Almond aliyeishiTanzania kwa miaka 31, na sasa yu Uingereza hali amestaafu. Alikuwamwalimu katika Chuo cha Theologia, Kongwa kwa miaka 16 na katikaShule ya Biblia, Morogoro kwa miaka 6 na katika Shule ya Biblia, Msalatokwa miaka 4.

Mchoraji ni Peter Kasamba. Yeye ni Mwuganda anayeishi huko Kampala.Kwa muda mrefu amechora picha zote kwa vitabu vya APF. Anaongozapia Kwaya ya AYF.

Kitabu hiki chatolewa kwa msaada wa African Pastors Fellowship. Lengo nikuwasaidia watumishi wa Kanisa wanaosoma katika Shule za Biblia na

Page 4: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

.

RAMANI YA PALASTINA WAKATI WA KRISTO

Page 5: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 295

UTANGULIZI

(a) MwandishiInakubalika na wataalamu wengi kwamba Injili hiyo iliandikwa na Luka, ambayepia aliandika kitabu kingine kilichomo katika Agano Jipya, yaani, Matendo yaMitume. Ni yeye tu, katika waandishi wa Injili nne, ambaye aliandika kitabukingine chenye habari zilizotokea baada ya Yesu kuondoka duniani. Twapatakujua jambo hilo kwa kulinganisha utangulizi katika Luka (Lk.1:1-4) nautangulizi wa Matendo (Mdo.1:1). Vitabu vyote viwili vilipelekwa kwa mtualiyeitwa Theofilo, na katika Mdo.1:1 mwandishi ametaja kwamba amekwishakumwandikia kitabu kingine.

Waandishi wa kwanza wa maandiko ya Kikristo wameunga mkono wazo hilo laLuka kuwa mwandishi. Watu kama Marcion, Justin Martyr, Ireneo, Tertulliano,Origen, Klementi wa Iskanderia, na andiko liitwalo Muratorian Fragment.

Ni vigumu kufikiri habari hiyo kuwa haiwi kweli kwa sababu Luka hakuwaMtume, wala hakuonekana kuwa mashuhuri katika Kanisa, kwa hiyo ni nenoambalo lisingalikubalika kwa urahisi. Afikiriwa kuwa Mmataifa, wala hakuwashahidi wa mambo yaliyoandikwa katika Injili yake. Alisema kwamba alizipatahabari hizo kutoka kwa wale waliokuwa mashahidi na wahubiri wa kwanza wahabari za Yesu. Kwa hiyo, kwa jina lake kubandikwa katika vitabu viwili virefuvya Agano Jipya, vinavyochukua karibu robo ya maandishi yake yote, nakumfanya kuwa mwandishi aliyeandika zaidi ya wengine wote, haiwazikikwamba jambo hilo halikuwa kweli.

Tunajua mambo gani kumhusu Luka? Habari zake zapatikana katika Nyarakaza Paulo. Alikuwa mjoli wa Paulo na mtu aliyesafiri pamoja naye mara kwamara. Katika WaKolosai 4:11,14 Paulo amemwita ‘tabibu mpendwa’ naamemtaja tofauti na ‘wale wa tohara’ yaani waumini wa Kiyahudi, hivyoamefikiriwa kuwa Mmataifa si Myahudi. Ametajwa tena katika Filemoni 24 na 2Tim. 4:11; akiwa na Paulo wakati Paulo alipofungwa Rumi hali akitazamiakuuawa.

Habari nyingine inapatikana katika Matendo ya Mitume; viko vifungu kadhavinavyotumia neno ‘tu’ kama dalili ya mwandishi kuwapo wakati ule(Mdo.16:10ku. 20:5-16; 21:1-18; 27:1-28:16). Kwa hiyo, alikuwa na nafasi nzuriya kupata habari nyingi za mambo ya Kanisa, mitume, na wakristo, walipoanzakuhubiri Injili.

Inafikiriwa alipata nafasi ya kukusanya habari za Yesu wakati alipokuwaYerusalemu na Kaisaria. Wakati fulani walikaa na Filipo Mwinjilisti. Pauloalipotelemka kwenda Yerusalemu alikamatwa na kupitishwa katika hukumumbalimbali, kuanzia kwa Wayahudi, hadi mpaka kwa Warumi. Baada ya miakamiwili yeye na Paulo walianza safari ya kwenda Rumi ili Paulo ahukumiwe

Page 6: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

huko. Muda huo wote Luka alipata nafasi ya kuonana na viongozi na Wakristowaliokuwa wa kwanza kuamini, wale walioshirikiana na Yesu kabla ya KupaaKwake. Bila shaka alizuru mahali mbalimbali, kama Gethsemane, na Golgotha,miji ya Galilaya n.k. Hivyo alipata nafasi ya kutafuta, kutafiti, na kuhakiki habarializoziandika.Pamoja na hayo alipofuatana na Paulo alikutana na watu kama Sila, Agabo,Yakobo na wazee wa Kanisa la Yerusalemu (Mdo.21:17ku).

Twaweza kuona dalili ya Luka kuwa daktari kwa jinsi alivyoandika juu ya watuwaliokuwa wagonjwa, kwa mfano, mkoma ‘alijaa’ ukoma; mwenye homaalikuwa na ‘homa kali’ n.k.

Aliandika machache juu ya majadiliano kati ya Yesu na Mafarisayo, walahakutaja mambo yenye mvuto kwa Wayahudi. Alipotaja Agano la Kale alitumiaTafsiri la Kiyunani la Septuajinta.

Pengine alitoka Antiokia wa Shamu, ila hatuna uhakika. Wazo lingine nikwamba alitoka sehemu za Makedonia, na ya kwamba kutokana nakuzungumza na Paul, Paulo alipata maono ya kumwita Makedonia.

(b) Tarehe ya KuandikwaYafikiriwa kuwa kati ya B.K.60-63 kabla ya Paulo kufungwa huko Rumi. Hatahivyo, wako wataalamu wanaofikiri kwamba Injili hiyo haikuandikwa kabla yaB.K.75 na wengine hata baadaye. Ni vigumu kufikiri ni wakati wa baadaye,ikiwa Kitabu cha Matendo kiliandikwa baada ya Injili ya Luka, na Kitabu chaMatendo kinamalizika bila kutaja habari za matokeo ya kesi ya Paulo nakuuawa kwake.kama B.K.64. Pia Luka haonyeshi dalili yoyote ya kujuamaandiko ya Nyaraka za Paulo.

(c) AliyeandikiwaLuka amemtaja kuwa ‘Theofilo’ na wengi hufikiri huyo Theofilo alikuwa mtukweli, huenda alikuwa mwenye cheo, mheshimiwa. Yawezekana alikuwamfadhili wa Luka aliyemwezesha kuchapisha hicho kitabu. Ilikuwepo desturikwa wenye uwezo kuwasaidia wengine kwa njia hiyo. Baadhi ya wataalamuhufikiri kwamba hakuwa mtu kweli ila kwa sababu jina lake lina maana ya‘mpenda Mungu’ Luka alilenga kuwasaidia wale wote waliovutwa kumwaminiKristo na kumpenda Mungu. Yafikiriwa kwamba shabaha yake ilikuwakuwasaidia wenye elimu na ustaarabu kuelewa habari za maisha, matendo namaneno ya Yesu, na kupata picha kamili juu yake. Wakati ule Wakristowaliwazwa vibaya na wengi kwa jinsi ilivyoonekana hawakupenda watu, kwavile walivyojitenga na wenzao kwa kuwa iliwawia vigumu kujiihusisha nao katikadesturi za kipagani na imani za jadi n.k.

Page 7: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 297

(d) Mahali ilipoandikwaAma ni Rumi au liko wazo la kufikiri iliandikwa Akaya.

(e) Mtindo wa Injili ya LukaLuka aliandika kwa lugha ya Kiyunani. Utangulizi umeandikwa kwa Kiyunanisafi sana, ila baadaye, kwa kuwa alikuwa akisimulia mambo yaliyotokea kati yaWayahudi, Kiyunani kilipata kuwa na harufu ya Kiebrania. Alitaka kuonyeshakwamba Yesu ni Mwokozi wa ulimwengu mzima, mwenye kupenda na kusaidiakila aina ya wanadamu na kuwaokoa na kuwaponya shida zao. Lukaameonyesha Yesu kuwa Mwokozi wa ulimwengu mzima, wa Wayahudi, naWasamaria, na WaMataifa. Katika Injili yake Luka amependa kumwonyeshaYesu akijihusisha na wanawake pamoja na wanaume, watu huru na wafungwa.Amesisitiza jinsi Yesu alivyojihusisha na maskini, wajane, watoza ushuru,wenye dhambi, na wale wasiopendwa na jamii n.k.

Hivyo Luka ameingiza habari za mtu mmoja mmoja wa aina mbalimbalialiyehudumiwa na Yesu.Amesisitiza tabia ya kuomba ya Yesu.Alikaza jambo la upendo wa Mungu na jinsi Mungu alivyotekeleza mapenziyake katika maisha na huduma ya Yesu, na baadaye katika maisha ya Kanisa(Matendo ya Mitume). Alipenda kutumia neno ‘pasa’ na ‘budi’ kuonyesha jambohilo. Yesu alisukumwa kuonyesha upendo wa Mungu kwa watu mbalimbali(2:49; 4:43; 9:22; 13:16,33; 17:25; 19:5; 22:37; 24:7,26,44).

Mathayo alisisitiza ‘ufalme’ wa Yesu na jinsi Yesu alivyotimiza unabii wa Aganola Kale. Marko ameonyesha ‘uwezo’ wa Yesu, na Luka ‘upendo’ wa Yesu aliyeMwokozi, Mkombozi wa kila mwanadamu. Hivyo Injili yake imekuwa na mvutomkubwa kwa watu wengi.

1:1-4 Luka aeleza sababu zake za kuandikaLuka ameanza Injili yake tofauti na Mathayo, Marko, na Yohana. Yohanaalianza kwa kutaja Umilele na Uungu wa Yesu kabla ya kuja kwake duniani.Mathayo alianza na orodha ya ukoo wa Yesu akirudi mpaka baba wa Taifa laWayahudi Ibrahimu kwa kupitia kwa Daudi, mfalme wake mashuhuri. Markoalianza kwa habari za Yohana Mbatizaji na kuacha habari zote juu ya kuzaliwakwa Yesu. Luka alianza kwa kushuhudia jinsi alivyojua kwamba wenginewameandika habari za Yesu kabla yake na kukiri kwamba yeye hakuwa wakwanza kuziandika. Ila yeye alikuwa amejibidiisha kutafuta na kutafiti habarizake kwa kuzungumza na wale waliokuwa mashahidi ambao pia walikuwawahubiri wa kwanza wa habari hizo.Katika Kiyunani vifungu hivi vyote vinne ni sentensi moja tu.

k.1 Kifungu hicho chashuhudia kwamba wengi walikuwa wameziandika kwataratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha

Page 8: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi ya Mungu, maana yakeYesu aliutekeleza mpango wa Mungu wa ukombozi wa ulimwengu.

k.2 Habari hizo zilipatikana kwa kizazi cha pili cha Wakristo. Hao wa kizazihicho walikuwa wamehadithiwa habari hizo kutoka wale mashahidi waliokuwawamemwona Yesu, wamemsikia na kushirikiana naye, wakiyaona matendoyake makuu, na hasa Kuuawa Kwake, na kumwona yu hai baada ya KufufukaKwake na kabla ya Kupaa Kwake. Hao mashahidi wa kuona walitumwa naYesu kutangaza habari zake (Mdo.l:8 ‘mtakuwa mashahidi wangu’). Mwanzonihaikuwepo haja ya vitabu, wala hawakuona vema kuyaweka mambo hayo kwautaratibu, walisema kadiri walivyoyakumbuka hayo na kwa kulingana namahitaji ya wasikilizaji wao. Ila baadaye, kizazi cha pili cha Wakristowalitambua kuna umuhimu wa kuziweka habari hizo katika maandishi, nakuzipanga kwa utaratibu mzuri, ili watu wapate kuzisoma habari za maisha yaYesu hapa duniani tangu mwanzo mpaka mwisho wake.k.3 Hivyo, Luka pia, alivutwa kuziandika na amedai kwamba ameandika kwausahihi hali amezihakiki ukweli wake. Alifanya bidii sana kutafiti habari hizo.Tena ameziweka katika utaratibu mzuri. Katika neno hilo Luka amekuwa hodari,tukikumbuka kwamba yeye ni Mmataifa na mtu asiyekuwa na cheo katikaKanisa. Ila tusifikiri kwamba alitaka kuzihukumu kazi za wale waandishiwengine waliomtangulia, la, siyo. Aliona kwamba ipo nafasi ya mikazo mingineambayo italenga kuitimiza shabaha yake ya kuwavuta watu kama WaMataifawenzake. Kama Mmataifa bila shaka alivutwa na mambo mengine katikahuduma ya Yesu yaliyokuwa tofauti na yale yaliyowavuta Wayahudi (Mathayoaliandika yale mambo hasa yaliyowavuta Wayahudi). Pamoja na hayo alianzanyuma kwa wazazi wa Mbatizaji ili atayarishe njia ya kuandika kwa kirefu habariza kuzaliwa kwa Yohana pamoja na kuzaliwa kwa Kristo. Alikusudia kuwapawasomaji wake habari ya mizizi ya Ukristo kwa kurudi nyuma kabla ya kutokeakwa Yesu mpaka kuzaliwa kwa Mbatizaji. Luka aliyaangalia maandishiyaliyokuwepo pamoja na kuchunguza mapokeo ambayo hayakuandikwa iliaandike Injili pana sana. Aliposema aliandika kwa utaratibu, tusifikiri kwambayote yameandikwa katika mfuatano wa kutokea kwake, ila amepanga mambokwa utaratibu mzuri.

Ndipo alimtaja Theofilo mtukufu kuwa yule wa kuandikiwa. Wengi walikuwa najina hilo, tafsiri ‘mpenda Mungu’. Kwa neno ‘mtukufu’ amedhaniwa kuwa mtu wamaana, kama mwenye cheo katika serikali ya Kirumi, au mstaarabu mwenyesifa na uwezo. Alitaka Theofilo awe na uhakika wa yale aliyofundishwa. Kwamaneno hayo, ama Theofilo B alihitaji msaada wa kuendelea katika imani kwasababu ya wengine kusema vibaya juu yake. Pia mafundisho ya uongo yalianzakuzuka yakitolewa katika jina la Kikristo. Hatujui hasa, ila ni wazi kwamba Lukaalitaka Theofilo awe na habari sahihi juu ya Kristo. Pengine alimfadhili Luka nakumsaidia katika uchapishaji wa kitabu hicho.

Page 9: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 299

Majumlisho ya 1:5-2:52

Kabla ya kutazama kila kifungu ni vema kuangalia kwa ujumla mambo yasehemu hiyo. Inazo habari za unabii juu ya kutokea kwa Yohana Mbatizaji naYesu Kristo. Habari hizo zapatikana katika Luka tu.

Kwa kurudi nyuma mpaka unabii wa kuzaliwa kwa Mbatizaji Luka amejengadaraja kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. Kwa muda wa miaka mia nnehakutokea nabii katika Israeli. Katika tangazo la kuzaliwa kwa Mbatizaji Mungualifufua kipawa cha unabii na ukimya wa miaka hiyo mia nne ulikwisha. Lukaalitaka kuuonyesha uzuri wa Nyakati za Masihi na jinsi Roho Mtakatifualivyofanya kazi kwa nguvu. Pia alitaka kuonyesha kwamba Mbatizaji alikuwana mahali pa maana na pa kipekee katika jambo hilo. Ijapo haikuwepo hatari yawatu kumchanganya na Masihi mwenyewe (1:17) hata hivyo, haikuwezekanawatu wakose kuutambua umuhimu wake katika mpango wa Mungu.

Katika sehemu hiyo yote twaona mambo yasiyo ya kawaida - malaika, unabii,na miujiza.Yohana na Yesu walichukuliwa mimba bila kutazamiwa na isiyo kawaida; kwaupande wa Yohana wazazi walikuwa wazee na mama yake alikuwa tasa. Kwaupande wa Yesu, Yusufu na Mariamu walikuwa bado hawajaoana walakukaribiana kimwili. Malaika Gabrieli alitumwa kwa mzazi mmoja, Zakaria kwaupande wa Yohana na Mariamu kwa upande wa Yesu. Wote wawiliwalihangaika walipoambiwa habari. Wote wawili walipewa ahadi ya kuzaamwana. Wote wawili waliambiwa jina la kumpa mwana atakayezaliwa. Wotewawili waliambiwa kwamba wana wao watakuwa wakuu. Wote wawiliwalipoambiwa waliuliza ni kwa njia gani ambayo jambo hilo litatokea. Wotewalisikia furaha kubwa.

Baada ya kutahiriwa, jirani za Mbatizaji walisikia hofu wakitambua uhakika waMungu kuwemo katika jambo hilo. Kwa Yesu, wazee wawili, Simeoni na Ana,walitambua kwamba Mungu amejibu maombi yao ya kumpata Mwokozi. Ndiponyimbo za sifa ziliimbwa. Watoto wote wawili walikua na kuwa na nguvu (1:80;2:40). Hata hivyo ijapokuwa Mbatizaji alichukuliwa mimba wakati tofauti nakawaida za kuzaa ni Yesu aliyezaliwa kipekee kabisa, tofauti na wanadamuwote, kwa kuwa alizaliwa na bikira. Yohana atakuwa mkuu ‘mbele za Bwana’ ilaYesu ni Bwana (2:11).

Tofauti moja ni kwamba Zakaria alipewa adhabu kwa sababu aliuliza swali lakekatika hali ya kutokuamini ila Mariamu hakupewa adhabu kwa sababu aliulizaswali katika hali ya kuamini.

Mbatizaji na Yesu pamoja walikuwa wajumbe wa wokovu wa Mungu. Yohanaalimtangulia Yesu katika kuchukuliwa mimba, kuzaliwa, na kufanya huduma ilaYesu aliyemfuata baada ya muda mfupi alimzidi kwa cheo akiwa mkubwa

Page 10: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kabisa. Yohana, kama mtengenezaji wa njia, alikuwa na kazi ya kuwaandaawatu waipokee huduma ya Yesu iliyokuwa kubwa zaidi.

1:5-25 Kutabiri kuzaliwa kwa Yohana Mbatizajik.5-7 Luka ametaja wakati wa mambo hayo kutokea kihistoria. Herode Mkuualikuwa mfalme wa Yudea (pia Galilaya, Samaria, na sehemu kubwa ya Perea).Alitawala tangu K.K.37 hadi K.K.4 na wakati huo ulielekea mwisho wa maishayake. Walikuwepo makuhani wengi nao walifanya kazi hekaluni kwa zamu. Kwakawaida waliishi shambani nje ya Yerusalemu. Tangu zamani (1 Nya.24:1-6)walipangwa kwa utaratibu, walitoka kwa ukoo 24, na waliitwa kuja hekalunimara mbili kwa mwaka na kuhudumia pale kwa juma moja. Shughulizilitofautiana, na shughuli moja ya maana kuliko yote ilikuwa kufukiza uvumba.Waliruhusiwa kufanya mara moja tu na wengine hawakufanya hata mara mojamaisha yao yote. Walipiga kura kuona ni yupi atakayefanya hiyo kazi. Zakariaalikuwa na baraka kubwa kuwa na mke ambaye pia alitoka katika ukoo waukuhani. Makuhani walitakiwa kumwoa mwanamke bikira ila si lazima awe waukoo wa ukuhani.

Hao wawili, Zakaria na Elisabeti walikuwa watu wazuri sana, waliishi kwakutimiza matakwa ya Torati, tena walifanya ‘mbele za Mungu’ neno lakuonyesha nia yao safi ya kumpendeza Mungu hasa. Siyo kusema kwambahawakufanya dhambi, ila walijitahidi kuwa waaminifu kwa Mungu. Walikuwa nahuzuni moja kubwa katika maisha yao. Hawakuwa na mtoto, wala kwa umriwao, halikubakia tumaini la kupata. Jambo hilo kwa watu hawa waaminifulilikuwa vigumu kufahamu kwa sababu kwa kawaida ilidhaniwa kwamba watuwaaminifu watajaliwa na Mungu kupata baraka kubwa ya watoto. Tena walijuakwamba kwa sababu hiyo hawataweza kupata heshima ya kumzaa yule Masihiwala kwa kukosa uzao Masihi hatazaliwa katika familia yao. Walewaliompenda Mungu sana na kutarajia kuja kwa Masihi walitamani kwambahuyo Masihi atoke viunoni vyao, hali wakimwaza kwa kimwili tu. Katika kutajautasa na uzee wa Elisabeti kuna ukumbusho wa watu wa zamani Sarai,Rebeka, Raheli, Hana n.k (Mwa.18:11; 25:21; 29:31; 1 Sam.1:1-2; Waa.13:2).Maana ya majina yao: Zakaria - ‘Mungu anakumbuka’ (yaani agano lake) naElisabeti - ‘Mungu wangu ni kiapo’ (yaani ni mwaminifu).

k.8-10 Wakati ulifika kwa zamu ya Zakaria kufukiza uvumba baada ya kurakumwangukia. Bila shaka alijaa furaha sana kuwa yule wa kufanya hivyo, nikama amefikia upeo wa kazi ya ukuhani. Aliingia mle hekaluni, mahalipatakatifu, waliporuhusiwa makuhani tu. Wengine waliandaa vitu tayari, halafuwaliondoka na kumwachia yeye nafasi ya kujinyenyekeza mbele za Mungu,huko watu wamekusanyika nje kwa sala. Mambo hayo yalitokea katikamazingira ya maombi ya waaminifu katika Israeli. Uvumba ulifukizwa asubuhina jioni, na saa za sala zilikuwa tatu, mbili wakati wa kufukiza uvumba na mojakatikati ya mchana.

Page 11: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 301

k.11-17 (Ni vema kulinganisha sehemu hiyo na Danieli 9.20ku. kwa kuwamambo kadha hufanana – maombi, saa ya dhabihu ya jioni, Gabrieli (ambayeametajwa katika Danieli tu; pia majuma 70 (Dan.9.24) ni sawa na majuma 70tangu Zakaria kupewa ufunuo huo mpaka Yesu kuletwa hekaluni). Malaika(Gabrieli 1:19) alimtokea bila kujitambulisha mpaka baadaye. Luka hakuelezahali yake ila alitaja kwamba alisimama upande wa kuume, dalili ya kuonyeshakwamba analeta ujumbe mzuri. Zakaria alipomwona alifadhaika na kuogopa.Bila shaka alijaa mawazo mengi, ila malaika alimtuliza kwa kumwambiaasihofu. Kwa nini asihofu? Ni kwa sababu dua yake imesikiwa na Munguanajibu ombi lake. Ni dua gani ambayo ameomba? Alipoingia mle ndani bilashaka, kama Mwisraeli wa kweli, hali analiwakilisha taifa lake, aliomba kwa ajiliya tumaini la Israeli la kujaliwa kupata huyo Masihi aliyeahidiwa ili taifalikombolewe na shida zake. Ni vigumu kufikiri kwamba aliomba kwa ajili ya nafsiyake, huko, wakati huo, amekuwa mjumbe wa kuliwakilisha taifa lote. Bilashaka mara kwa mara yeye na Elisabeti waliomba sana kumpata mtoto,yawezekana wameacha kuomba kadiri muda wa uwezekano wake ulipozidikupungua. Kumbe, Mungu anajibu dua yake na ya wengine katika Israeli (akinaAna na Simeoni 2:25,38) ya kumpata Masihi na jibu lake lafungamana na jibu lamaombi yao ya kibinafsi ya kupata mtoto. Hivyo, malaika alimwambia wazikwamba, mkewe atamzalia mtoto wa kiume na itampasa amwite Yohana(maana ya jina la Yohana ni Bwana ni mwenye fadhili/neema). Tukiunganishajina hilo na majina yao ni kwamba Mungu analikumbuka Agano lake na kuwaMwaminifu kabisa kwa Israeli katika neema yake ya kumtuma Yohana,atakayekuwa mtangulizi wa Masihi ambaye hivi karibuni atazaliwa baada yaYohana kuzaliwa.

k.14 Jambo hilo litasababisha furaha kubwa sana. Kwa upande wao kujaliwakuwa wazazi, ila zaidi kwa sababu ni chanzo cha kutimizwa kwa ahadi yaMungu ya Israeli kupewa Masihi. Luka amependa kutaja jambo la furaha (2.10;10.17; 24.41).

k.15 Halafu malaika aliendelea kumwelezea Zakaria kazi ambayo huyo mwanawake Yohana atakayoifanya. Kwanza alimwambia atakuwa ‘mkuu mbele zaBwana’; ukuu wa kweli kabisa kwa sababu ni ‘mbele za Bwana’. Ni Mungu,peke yake, aliye na ukuu, ila Yohana atakuwa mkuu kwa sababu ya upekee wamahali pake katika historia ya Kuja kwa Kristo duniani. Pia atajitoa kabisakatika kuutimiza utume wake wa kuwaandaa watu tayari kwa kutokea kwaMasihi. Atafanana na Eliya kwa roho na nguvu (2 Waf.2:9,15; Dan. 12.3;Mal.3:1; 4:5ku). Atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.Nyakati za Agano la Kale Roho alikuja juu ya watu kwa muda fulani nakuwawezesha kutimiza jambo fulani, hakukaa juu yao moja kwa moja; ila kwaYohana sivyo itakavyokuwa. Katika maisha yake yote ataongozwa na kutiwanguvu na moyo na Roho. Hatahitaji kunywa divai wala kileo (Efe.5:18). Hakunanabii aliyefanana na Eliya kuliko Yohana. Wote wawili walifanya kazi jangwanina wote wawili walitangaza kwa nguvu hukumu ya Mungu bila upendeleo.Ukuu

Page 12: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

wa Yohana umeonyeshwa katika mambo mawili; la kwanza, yeye alitimizaunabii wa zamani; na la pili alilingana na Eliya.

k.16-17 Kazi yake hasa itakuwa kuwarejeza Waisreli wengi kwa Mungu wao.Kwa maneno hayo ni dhahiri kwamba wakati huo wengi walikuwa wamemwasiBwana na itampasa yeye awalete kwenye toba na kuwatahadharisha juu yahukumu ya Mungu. Ina maana gani maneno ‘kuigeuza mioyo ya babaiwaelekee watoto’? huenda maneno hayo yaliashiria hali ya mafarakano katikafamilia nyingi wakati ule. Hata hivyo, wako wanaofikiri kwamba ‘baba’ nimababa mashuhuri wa zamani, akina Ibrahimu na wengine, ambao kwakuitazama hali ya taifa kutoka mbinguni walichukizwa sana. Kwa baraka yawengi kuitikia mwito wa Yohana wa kutubu hata hao mababa watageuzamawazo yao na kuifurahia hali mpya nao watasikia ushirikiano mwema kati yao(Isa.29:22ku).

Kazi hizo zote zililenga jambo moja kuu, lile la kutokea kwa Masihi Mwenyewe,Mwana wa Mungu, Yesu Kristo. Ni matayarisho kwa ajili yake. Manabii wazamani walitangaza Kuja Kwake, ila jambo lenyewe lilikuwa bado. Yohanaalikuwa nabii wa mwisho katika safu ya manabii wa kale, ambaye atatangazakutimia kwa Kuja kwa Masihi, ambaye ameisha kufika, yu kati yao. Yohanaalikuwa nabii kweli aliyefanya kazi ya nabii ya kweli akiwaita watu wamrudieMungu wao (Yer.3:7,10; Eze. 3:19; Dan.9:13).

(Ni ajabu kuona kwamba Luka ameandika habari hizo za mambo ya Kiyahudina kueleza mazingira yake kwa kirefu, kwa Theofilo, Mmataifa, ambayoyalikuwa mageni kabisa kwake. Ni kuonyesha kwamba katika matendo yaMungu, malezi ya mtu si kitu).

k.18-20 Zakaria aliitikia ujumbe wa malaika kwa kutokuamini. Ikiwa alikuwaameomba dua ya kupata mtoto wakati huo ni vigumu kujua kwa nini alishtuka.Alikuwa na maulizo yaliyoonyesha kwamba hakuamini. Kutokewa na malaikakungalimtosha, ila alitaka uhakika zaidi, na pengine alifikiri kwamba alikuwa nahaki ya kuwa na mashaka kutokana na hali ya uzee wao ulio kizuizi kikubwakatika kutimiziwa jambo hilo. Ila ilimpasa akumbuke historia ya watu kamaIbrahimu, Hana, Gideoni, ambao pia walikuwa na kizuizi kama wao, naowaliambiwa habari kama hizo, na ingawa walikuwa na maulizo, hata hivyo,hayakuwa maulizo ya mashaka. Ilimbidi ayashinde mashaka yake.

k.19 Malaika hakumwachia nafasi ya kujitetea. Alijitambulisha kwake kuwaGabrieli, na kumjulisha cheo chake na utume wake. Yeye ni yule asimamayembele za Mungu ambaye amemtuma na habari hizo njema. Ni mheshimiwakweli kweli, kwa hiyo, Zakaria alikuwa amejaliwa fadhili kubwa kuambiwa habarihizo na malaika huyo. Kwa hiyo, kutokumwamini yeye wala ujumbe wake nisawa na kutokumwamini Mungu aliyemtuma, na kwa sababu hiyo, ijapokuwajambo lenyewe litatimizwa kwa wakati wake, yeye mwenyewe atapata adhabu

Page 13: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 303

ya kuwa bubu kwa muda huo wote wa kati, huenda alikuwa kiziwi pia (k.62).Alitaka ishara, naye alipewa, ishara ya adhabu, ili asiwe na mashaka tena. Kwahali hiyo habari ya ufunuo huo hazitaenezwa.

k.21-25 Tukio hilo lilimchelewesha ndani ya hekalu na watu waliokuwa njewalikuwa wakimtazamia ili aitoe baraka. kumbe amechelewa humo ndani.Kutoka kwa kuhani kulijulisha watu kwamba Mungu hakuwa na neno juu yao.Alipotoka akashindwa kutoa baraka (Hes.6:24-26) wala hakuweza kutoamaelezo. Watu walitambua kwamba ameona maono mle hekaluni ilahawakuelewa hasa ni nini iliyompata.

Baada ya kumaliza juma lake la huduma akarudi nyumbani kwa mkewe, nahata kwa Elisabeti Zakaria alishindwa kumweleza kwa midomo yaliyompata, ilabila shaka aliziandika habari zake ili mkewe afahamu sababu ya ububu wakena kumjulisha jambo kubwa litakalompata la kumzaa mtoto. Aliendelea kuwabubu.

Elisabeti akachukua mimba kwa kawaida ya wanadamu, tofauti na Mariamuambaye alichukua mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu tofauti na wanadamu.Elisabeti alijificha nyumbani kwa muda wa miezi mitano. Mwanzoni isingalikuwadhahiri kwamba alikuwa na mimba. Kwa nini alijificha? Pengine alisikia haja yakutulia na kuzingatia jambo hilo kubwa la neema ya Bwana katikakumwondolea aibu mbele za watu. Ilihesabiwa kama adhabu ya Mungu, nawanawake tasa walisikia aibu na mara kwa mara wenzao waliwalaumu(Mwa.21:6; 30:23). Alishangaa kama Sarai na Raheli walivyofanya zamani zakale.

1:26-38 Unabii/Tangazo juu ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristok.26-27 (Ling.na Dan.10:11.12). Malaika Gabrieli alitumwa kwa mwanamke jinalake Mariamu, aliyeishi Nazareti, mji katika eneo la Galilaya. Miezi mitanoilikuwa imepita tangu alipotumwa kwa Zakaria. Ujumbe wake kwa huyo, iwapoulifanana na ule kwa Zakaria juu ya kuzaa mtoto, hata hivyo, mtotoatakayezaliwa kwa Mariamu atampita yule atakayezaliwa na Elisabeti. HuyoMariamu alikuwa bikira, aliyeposwa na Yusufu wa ukoo wa Daudi, hivyo, kwaupande wa ukoo alistahili Masihi atoke kwake. Kwa desturi ya Kiyahudi,kuposana kulikuwa patano la nguvu sana, walioposana walihesabiwa mume namke, na wakiaachana walihesabiwa wazinzi na budi talaka ikatwe(Kum.22:13ku; 23ku). Wasichana wengi wa umri kama miaka 13 waliposwa.Kuposwa kwa Mariamu na Yusufu wa ukoo wa Daudi kulimhalalisha Yesuahesabiwe wa ukoo wa Daudi kupatana na unabii juu ya Masihi. Yusufuhatajwi tena, ni kama hahusiki tena katika habari hiyo.

k.28-29 Malaika Gabrieli alimsalimia Mariamu kwa maneno ya ajabuyaliyomfadhaisha. ‘uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe’. Maana yake nikwamba katika tukio hilo Mariamu amejaliwa neema ya Bwana. Amepewa

Page 14: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

mwito mkuu wa kuwa mama mzazi wa Mwokozi wa ulimwengu. (Ling. Nasalaam kwa wengine walioitwa na Mungu kufanya jambo kubwa Dan.9:23;10:11,19; Waa.6:12; Joe.2:21; Sef.3:14; Zek.9:19). Inaonekana maneno hayondiyo sababu ya fadhaa zake kuliko kumwona malaika. Alitafakari maana yake.Ni kama maneno ya heshima sana, ya kumkuza sana. Bila shaka alijisikiakwamba hakustahili hizo salaam. Ni neema gani ambayo amepewa. Neema yakumzaa Mwana wa Mungu, Masihi, Mwokozi wa ulimwengu. Hii ndiyo heshimayake kuu, inayozidi heshima ya wanawake wote, hata ile ya Elisabeti,atakayemzaa mtangulizi wa Masihi. (Neno hilo halina maana kwamba Mariamumwenyewe aweza kutoa neema na kujibu maombi n.k. ‘alipewa’ si ‘atatoa’).

Jambo la ubikira wa Mariamu umesisitizwa, likitajwa mara mbili katika k.27 nakudokezewa katika k.34,36,37. Ipo tofauti kubwa kati ya ubikira wa Mariamu nautasa wa Elisabeti. Bila shaka Luka alitaka kuonyesha ukubwa wa mwujiza waMariamu, bikira, kuzaa mtoto. Jambo la kuwa bikira, peke yake, si la maanawala haliwi ishara ya unyenyekevu wa kiroho.

k.30-31 Malaika alimwambia Mariamu kama alivyomwambia Zakaria ‘asiogope’kwa sababu neema ya Mungu ni pamoja naye. Ndipo Gabrieli aliendeleakumwambia habari njema kwamba atamzaa mtoto wa kiume na itampasa ampejina la Yesu (Bwana ni wokovu Mt.1:21).

k.32-33 Halafu malaika alipanua habari kuhusu mtoto atakayezaliwa. ‘atakuwamkuu’ kwa kuwa ataitwa ‘Mwana wa Aliye juu’. Huyo ni tofauti na watu wenginewote. Ni mwana pekee wa Mungu. Atapewa kiti cha enzi cha Daudi na kumiliki,si kwa muda fulani tu, bali kwa milele. Yeye ni timizo la unabii wa 2Sam.7:12ku. 2 Nya.22:9,10; Zab.2:7; 89:26ku. Atatoka katika ukoo wa Daudi(Mwa.49:10; Isa.9:1-7; 11:1-3). Ufalme wake hasa si wa kijiografia wala si wamuda. Maelezo hayo yalimfunulia Mariamu ukuu wa huyo mwanaatakayezaliwa.

k.34 Iwapo swali la Mariamu halilingani na maneno ya k.27, hata hivyo Mariamualitaka kujua jinsi jambo hilo litakavyofanywa. Inaonekana itatokea hivi karibunihuku yeye hana uhusiano wa kindoa na Yusufu, walikuwa katika muda wakuposana, muda usiowaruhusu kukaribiana kimwili. Hivyo, neno hilo litatokeakwa njia gani? Kwa mtindo wa Wayahudi neno ‘kujua’ lilikuwa na maana yakulala na mwanamume (Mwa.4:1; Waa.11:39; Hes.31:17,18). Hakuombaishara, wala hakukataa; aliamini ila alitaka kujua ni kwa njia gani yeyeatakayemzaa mtoto akiwa bikira na kabla ya kuolewa na bila kushirikiana namwanamume.

k.35 Kwa uchaji na heshima Gabrieli alimweleza kwamba ni kwa uwezo waRoho Mtakatifu, kwa kuwa Roho atamfunika kama wingu. Kwa maneno hayohakuna nafasi ya kuwaza kwamba Roho atashirikiana na Mariamu kimwili kamailivyo kawaida kwa wanadamu katika kuzaa. La, jambo hilo litatokana na uwezo

Page 15: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 305

wa Roho wa Mungu na mtoto atakayezaliwa atauchukua ubinadamu wake kwaMariamu (Gal.4:4) pia atakuwa mtakatifu bila dhambi ili awe anao ustahili wakuwaokoa wanadamu na dhambi zao. Atakuwa mwana wa Mariamu kwakuzaliwa na Mwana wa Mungu kwa asili. Jinsi habari hiyo ilivyoandikwa Lukaamesisitiza kwamba Mungu alitangulia katika tukio hilo na uwezo wa uumbajiwa Roho Mtakatifu ulimwezesha Mariamu kuchukua mimba, Yesu hakutokakatika ubinadamu uliopo.

k.36-38. Ndipo Gabrieli alimweleza Mariamu habari za Elisabeti kuzaa mtoto.Wengine wametatizwa kwamba Mariamu hakujua habari hiyo kwa sababuwalikuwa binamu na miezi mitano ilikuwa imepita tangu alipochukua mimba.Huenda shabaha yake ilikuwa kumtia moyo juu ya uwezekano wa mamboaliyoambiwa kutokana na uwezo wa Mungu uliodhihirika katika Elisabeti,ambaye tayari amechukua mimba. Lisilowezekana hasa ni bikira Mariamukuzaa mtoto kuliko Elisabeti, mtasa. Ni ukumbusho wa Mwa.18:13 naRum.4:17. Kwa njia hiyo Mariamu alipandikizwa wazo la kwenda kumsalimiaElisabeti.

Mariamu aliyaitikia hayo yote vizuri sana. Alijinyenyekeza na kwa imani alikubalineno hilo litendeke. Alikuwa tayari, kama mjakazi, kumtii Bwana wake. Haikuwarahisi kwake, kwa kuwa Yusufu aliyemposa ataonaje habari hiyoatakapoambiwa na Mariamu, naye atachukua hatua gani, maana alikuwa nahaki ya kukata talaka, na ndivyo alivyokusudia mpaka Mungu alimsaidia(Mt.1:18). Tena katika Torati (Kum.22:23ku) ilisema kwamba mtu aliyeziniauawe, kwa hiyo Mariamu alikuwa katika hatari hiyo; ila inafikiriwa kwambaamri hiyo haikufuatwa mara nyingi (Yn.8:1ku).

1:39-45 Mariamu aenda kumsalimia ElisabetiUwiano wa mpango wa Mungu kumhusu Yohana na mpango wake kumhusuYesu umedokezewa katika matangazo hayo mawili kufuatana ndipoumethibitishwa katika mama zao kukutana.

k.39-45 Bila kukawia Mariamu alisafiri mpaka mji mmoja wa Yudea, kusini yaGalilaya, mashambani walipoishi Zekaria na Elisabeti jamaa yake. Alifanyabidii, kwa sababu ilikuwa safari ndefu na yeye na Elisabeti wanalishiriki tukiohilo la kuja kwa Masihi . Hatujui kama alikuwa ameisha kumjulisha Yusufuhabari zake au siyo. Wala hatujui kama Yusufu alijua kuwa ana mimba. Alikaamiezi mitatu na Elizabeti ila hatusikii kwamba alikuwepo wakati Elizabetialipomzaa mtoto (k.56)

Alipomwamkia Elisabeti, kitoto katika tumbo la Elisabeti aliruka (Mwa.25:22,23).Iwapo kwa upande mmoja, kitoto kuruka tumboni si jambo geni ila kwa jinsiElisabeti alivyojisikia aliona kwamba ni ishara ya mambo makubwa. AlijazwaRoho Mtakatifu na kwa msaada wa Roho alitambua mapenzi ya Mungu nakujua kwamba huyo mtoto aliye tumboni mwa Mariamu ni Masihi (Zab.110:1)

Page 16: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kwa sababu alimwita Mariamu ‘mama wa Bwana wangu’. Hakumbariki Mariamuila aliukiri uheri wa Mariamu na wa mtoto wake. Iwapo yeye mwenyeweametendewa neno kubwa sana, naye atamzaa mtangulizi wa Masihi, hatahivyo, hakusikia wivu wala hakusumbuka kwamba huyo aliye mdogo kwa umri,aliyemo tumboni mwa Mariamu, amepewa heshima kuu na baraka kubwa.Tendo la mtoto Yohana kuruka tumboni mwa Elizabeti limetajwa tena (k.44)lilionyesha umuhimu wa huyo atakayezaliwa na Mariamu, ni itikio lake kwakuwepo kwa Mungu na utendaji wake (ling.k.41,43,44,56 na 2 Sam.6:2-19).

Elisabeti aliisifu imani ya Mariamu akikumbuka kutokuamini kwa mume wake(k.18,20,38,45). Wakati huo twaona Luka ameandika nyimbo za hao wahusika,nyimbo za sifa sana, zenye ufunuo wa mambo yatakayotokea. Wimbo wakwanza ni huo mfupi wa Elisabeti, alipopaza sauti yake kwa kuongozwa naRoho Mtakatifu. Zakaria bado angali bubu, na jambo hilo laonyesha kwambakwa kutokuamini kwake alikosa kushirikiana kwa midomo mpaka baada yakuzaliwa kwa Mbatizaji. Kutokana na ujuzi wake wa maisha Elisabeti aliaminikabisa kwamba ni Kristo anayezaliwa.

(Nyimbo zilizoimbwa katika muda huo wa kuzaliwa kwa Yohana na Yesu ni zaElisabeti, Mariamu, Zakaria, Simeoni, na wachungaji. Kuzaliwa kwa Masihi namtangulizi wake kulisababisha shangwe za muziki na shairi).

1:46-55 Wimbo wa Sifa wa MariamuMariamu aliimba wimbo huo baada ya binamu wake Elisabeti kumwita ‘mamawa Mungu wangu’ (k.43) si wakati wa kuambiwa habari na malaika Gabrieli.Elisabeti aliimba wimbo mfupi katika hali ya kusisimua na Mariamu aliimbawimbo wake katika hali ya utulivu. Huenda katika muda wa siku nne hivi yakusafiri alikuwa amezingatia sana mambo hayo yote na hasa jinsi zamani zakale Hana alivyojaliwa kuzaa mtoto Samweli baada ya muda wa kawaida yawanawake kuzaa. Wimbo wa Mariamu unafanana na ule wa Hana katikamambo kadha, ila hali yake ni tofauti (1 Sam.2:1ku). Hana alikuwa na shida yautasa ila Mariamu hakuwa na shida hiyo, shida yake hasa ilikuwa ile yawaaminifu wote katika Israeli waliomngojea kuja kwa Masihi. Hana alitumiamaneno ya ushindi juu ya adui zake, ila Mariamu alionyesha unyenyekevumkubwa alipotafakari rehema za Mungu kwake.

k.46-48 Alianza wimbo wake kwa kuonyesha nia yake ya kumwadhimishaMungu. Wimbo ulitoka moyoni na rohoni mwake, kama nafsi yake yoteilishirikiana katika kumfurahia Mungu na kumsifu kwa sababu ya habari njemailiyoletwa na malaika. Alikiri kwamba, ingawa atakuwa mzazi wa Masihi, hatahivyo yeye ni mhitaji, mwenye dhambi anayehitaji Mwokozi ‘Mungu, Mwokoziwangu’. Alijua kabisa ni mnyonge (k.38) ambaye amechaguliwa na Mungukumbeba Mwana wa Mungu tumboni mwake. Mariamu mwenyewe alitambuauheri wake, kama Elisabeti alivyoutambua (k.42, k.45) na vizazi vyotevitakavyofuata watautambua uheri huo.

Page 17: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 307

k.49-50 Ndipo Mariamu alitaja tabia za Mungu, uwezo wake (k.37), utakatifuwake, na rehema zake kwa wale wanaomcha. Iwapo yeye ni mjakazi, asiye nasifa wala uwezo, Mungu wake ndiye Mwenye uwezo ambaye amemwangaliamjakazi wake katika unyongwe wa hali yake akiwa binti katika mji mdogo waNazareti na kumfanyia makubwa (Isa.42:13; Sef.3:17). Tendo lake kwaMariamu si kwa ajili yake tu, ni kwa ajili ya vizazi vyote vinavyofuata, kwaoMungu ataendelea kuonyesha rehema zake kutokana na Kuja kwa Kristoduniani.

k.51-53 Huyo Mungu mwenye uwezo atafanya upya kila kitu kwa njia ya Masihiyake. Mapinduzi makubwa yatokea. Mungu amewaweka kando wenye kiburi,watawala, wakubwa, na matajiri, naye amemchagua mwanamke mnyongekuwa mzazi wa Masihi. Mungu ameishaonyesha tabia yake alipomchaguaElisabeti, ndipo Mariamu, na mtindo huo utaendelea Masihi atakapotokea.Mariamu ameyataja matendo ya Mungu kama yamekwisha-fanyika. Matendosita yametajwa katika k.51a, 51b, 52a, 52b, 53a, 53b. Yawezekana katika rohoya unabii Mariamu alikuwa akiyatabiri matendo makuu yatakayotendeka nahuyo Masihi kama yamefanywa tayari kwa sababu ya uhakika wake, kamamanabii wa zamani walivyotabiri.

k.54-55 Halafu Mariamu alitaja uaminifu wa Mungu kwa watu wake. Mungualiwarehemu Ibrahimu na mababa wa Israeli na ataendelea kuwarehemu watuwake kwa njia ya Masihi wake.

Mariamu alikaa na Elisabeti miezi mitatu. Je! aliondoka kabla ya YohanaMbatizaji kuzaliwa au baadaye. Pengine aliondoka kabla ili awaachie Zakariana Elisabeti kushangiliwa na wote waliofurahia kuzaliwa kwake. Katika mudahuo wa hao wanawake kuongea mengi na kushirikiana kwa ukaribu sanaZakaria hakuweza kushiriki katika maongezi yao ila bila shaka waliandikamengine ili awe na ufahamu kuhusu hayo makubwa yanayotendeka, dalili yayeye kushirikishwa ni katika k.67-69 maneno ambayo aliyasema mara baada yaMbatizaji kuzaliwa ambayo ni vigumu kufikiri angalielewa bila msaada wa Rohona kujulishwa mapema. Labda Mariamu aliondoka baada ya Yohana kuzaliwana Luka ametaja habari ya kuondoka kwake kabla ya kuziandika habari zakuzaliwa kwa Yohana ili sehemu hiyo iliyomhusu Mariamu ifungwe kwa sababuyafuatayo hayamhusu hasa.

1:56-66 Kuzaliwa kwa Yohana MbatizajiElisabeti alimzaa mtoto wa kiume na jirani na jamaa zake walikuja kufurahipamoja naye. Hatujui kama walifahamu kwamba Elizabeti alikuwa na mimbakwa sababu alijificha nyumbani miezi mitano ya kwanza. Wote walitambuakwamba amejaliwa rehema za Mungu.. Rehema za Mungu ni kwa taifa zima sikwa jamaa moja kwa sababu huyo aliyezaliwa ni mtangulizi wa yuleatakayekuwa Mwokozi wa ulimwengu.

Page 18: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.59 Wayahudi waliwatahiri watoto wa kiume siku ya nane baada ya kuzaliwa.Tohara iliingizwa wakati wa Abramu (Mwa.17:12; Law. 12:3). Zamaniinaonekana mtoto alipewa jina siku alipozaliwa (Mwa.21:3, 25:25,26) ilabaadaye inaonekana mtoto alipewa jina wakati wa kutahiriwa. Yohana na Yesuwalipewa jina siku ya kutahiriwa. Kwa jinsi Paulo alivyosema (Flp.3:5)inaonekana mtu alihesabiwa Myahudi halisi ikiwa alitahiriwa siku ya nane,wakati alipoingizwa katika Agano la Mungu na watu wake. Kwa kawaida mtotoalipewa jina mojawapo la jamaa ile. Lakini Elizabeti alikazana kabisa kwambalazima aitwe Yohana, jina ambalo halikuwepo katika jamaa zake. Alikaza jinahilo kwa sababu inaonekana Zakaria aliandika habari kadha za mamboyaliyotokea wakati wa kujiwa na Gabrieli hekaluni. Kama siyo, alifunuliwa naMungu kwamba ilimpasa amwite Yohana. Mpaka hapo Zakaria alikuwa bubu napengine kiziwi kwa sababu walimwashiria ili apate kuliidhinisha jina la mtoto.Bila kusita aliandika kwenye kibao walichomletea ‘Jina lake ni Yohana’. Kwawazi kabisa alifanya hivi. Hakutumia maneno kama ‘tumekata shauri jina liwe...’au budi ‘tumwite ....’ la. Ameishapewa jina na malaika na kwa sababu hiyo jinalake ni Yohana. Wote walishangaa kwa jinsi mama na baba walivyosema kwauhakika na kulitaja jina hilo lililo geni katika familia yao. Maana ya Yohana ni‘Mungu ni mwenye rehema’ au ‘ni kipawa cha rehema ya Mungu’. Majinayalikuwa muhimu sana katika Agano la Kale, Mungu ametajwa na majinambalimbali kufuatana na tabia na matendo yake. Vivyo hivyo watu walipewamajina kufuatana na wito wao, na Yesu atakapozaliwa atapewa Jina lenyemaana ya ‘Mungu huokoa’ au ‘Mungu ni wokovu’ (Mt.1:21,23).

k.64 Mara moja, baada ya kulitaja jina la mtoto, kinywa na ulimi wa Zakariavilifunguliwa, na mara alianza kumsifu Mungu. Wale waliokuwepo walishikwana uchaji wa Mungu, na kuzitangaza habari hizo katika nchi ya milima yaUyahudi. Katika kumtii Mungu alimbariki na kumrudishia uwezo wa kusematena.

k.66 Watu hawakupiga umbeya bali waliyaweka hayo yote mioyoni mwao nakuitafakari maana yake wakielewa kwamba huyo mtoto si wa kawaida na kwasababu hiyo Mungu anayo shabaha juu yake ya kufanya kazi fulani maalumkwa njia yake. Mara nyingi Luka amependa kutaja jinsi watu walivyoshikwa nauchaji wa Mungu wakishangaa matendo yake makuu (5:26; 7:16; 8;37 n.k).Hapo watu wameguswa sana juu ya kuzaliwa kwa mtoto huyu, kwanza kwasababu ya Elizabeti kuchukua mimba katika uzee wake; katika Elisabeti naZakaria kukazana juu ya kumpa jina lisilotazamiwa apewe; pamoja na jinsiZakaria alivyoweza kusema tena mara baada ya kutaja jina la Yohana. Hayoyote yalisababisha hofu watu wakitambua kwamba hayo yote ni dalili yaKuwepo kwa Mungu na utendaji wake. Hofu iliwashika wale waliokuwa karibundipo ikaendelea mpaka kwa wale walioambiwa habari hizo baadaye.Mungu alimlinda Yohana katika utoto wake, na kumtia nguvu, na kumwongozatayari kwa kazi yake ya baadaye.

Page 19: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 309

1:67-80 Wimbo wa Zakariak.68-70 Roho Mtakatifu alimjaza Zakaria na kumwongoza atabiri kwa njia yawimbo wa sifa. Alianza wimbo kwa kusema juu ya Masihi atakayezaliwa, sikwa mtoto wake. Alimshukuru Mungu sana kwa Kuja kwa huyo Masihi. KatikaYesu Mungu anawajia na kuwakomboa watu wake. Mungu alipokusudiakutenda kazi kubwa ilisemwa kwamba ‘anawajia watu wake’ (Kut.4:31;Jer.15:15). Neno ‘komboa’ linadokezea gharama ya ukombozi utakaofanyika.Baraka ya Mungu ni katika Yeye kuwajia watu wake katika Kristo na Kuja KwaKristo kumefungamana na ukombozi. Hivyo Mungu ameanza wokovu wa watuwake.

k.70 ‘pembe ya wokovu’ nguvu za mnyama zilihesabiwa kuwa katika pembeyake na nguvu za Mungu zitaonekana katika huyo Mwokozi hodariatakayefanya wokovu mkubwa wa kuwaokoa watu na dhambi zao. HuyoMwokozi ni wa ukoo wa Daudi (Zab.132: 17) kama manabii wa zamaniwalivyotabiri, neno linaloonyesha kwamba Mungu anayatekeleza makusudialiyoyakusudia tangu zamani. Inaonekana Mariamu alikuwa wa ukoo wa Daudikwa sababu wakati huo Yusufu hakutajwa na Mariamu bado hajaolewa naYusufu, wala haikuwa wazi atakavyomfanyia Mariamu atakapojua habari zakewala jinsi Mariamu atakavyotendewa kufuatana na sheria za Kiyahudi.

k.71-75 Halafu Zakaria aliendelea kusema juu ya huyo Masihi na kazi zake.Kwa njia yake watu wataokolewa na adui zao, pengine aliwaza kuokolewakimwili kutoka utawala wa Kirumi ila zaidi alilenga watu kuokolewa na dhambizao. Mungu ni mwaminifu kwa agano lake hasa lile alilolifanya kwa Ibrahimu,Mungu alifanya kwa kiapo akilitia muhuri hata asiweze kurudi nyuma asilitimize.Mwishowe watu wake watamwabudu bila hofu, wataishi maisha mazuri ya hakina utakatifu, kutokana na rehema zake. Maneno ya sehemu hiyo yahusu halizao za kiroho, kuliko kuokolewa na waliowatawala, wokovu hautakuwa wanamna ya siasa.

k.76-77 Habari hii huleta pamoja Yohana na Yesu na Zakaria alitabiri juu yauhusiano wao katika huo mpango wa Mungu wa wokovu wa ulimwengu. Baadaya kuzungumzia Masihi Zakaria alitaja mahali pa mtoto wake katika mpangohuo wa Mungu. Bila shaka alisikia fahari kubwa juu ya mwana wake na alisemanaye moja kwa moja. Mtoto wake, ataitwa nabii wake Aliye juu; Yesu ni Mwanawa Aliye juu, yaani Mwana wa Mungu. Yohana ni nabii atakayemtangulia nakutayarisha njia zake (Mal.3:1). Manabii walitangaza habari za Kuja kwa Masihi,ila hawakumwona kwa uso. Atatayarishaje njia za Masihi? Yeye hana uwezowa kuwaokoa watu ili atahubiri kwa nguvu juu ya dhambi zao na hukumu yaMungu na kuwaita wazitubu kwa kweli ili wajiandae kumpokea yule mwenyeuwezo wa kuwaokoa na dhambi. Mara zote Luka amesisitiza rehema za Mungukuwa chemchemi cha matukio hayo.

Page 20: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.78-79 Katika tukio hilo kubwa la kutokea kwa Kristo giza litaondoka namwanga utawaangazia watu nao wataongozwa kwenye njia ya amani.Watapatanishwa na Mungu, na kupatanishwa wao kwa wao. Ni ukumbushokwamba ulimwengu ulikaa katika giza mpaka Kristo alipofika (Isa.9:1-2; 60:1;Mal.4:2). Hapo tena mkazo ni juu ya mambo ya kiroho kuliko mambo ya siasa.

k.80 Mstari huu umejumlisha habari za Yohana katika kukua kimwili na kiroho,kulindwa na kuongozwa na Mungu. Pengine wazazi wake wazee walikufa kablahajawa mtu mzima. Kutaja majangwani Luka amedokezea kwamba hakukaamahali pamoja, tena ‘jangwani’ ilifikiriwa kuwa mahali pa kupata uvuvio wakinabii, na ni dalili ya Yohana kuwa nabii halisi tangu mwanzo.

MASWALI:

1. Kuna ushuhuda gani wa kufikiri kwamba Luka alikuwa mwandishi wa Injilihiyo?

2. Eleza hali ya Injili hiyo na kuonyesha ni mambo gani yaliyomvuta Lukakatika maisha na huduma ya Bwana Yesu?

3. Roho Mtakatifu alifanya kazi kubwa nyakati za Yohana Mbatizaji na YesuKristo Kuzaliwa:(a) Eleza kazi yake kwa upande wa Yohana?(b) Eleza kazi yake kwa upande wa Yesu?

4. Eleza umuhimu wa Yohana katika mpango wa Mungu na uhusiano wakena Kristo?

2:1-7 Kuzaliwa kwa Yesu KristoHabari hii imeandikwa kwa urahisi na bila mapambo kwa kutaja jambo lenyewetu, jambo ambalo ni tukio kuu katika historia ya ulimwengu, la Mungu kufanyikamwili na kuja kuishi kati yetu sisi wanadamu akikaa nasi kwa muda wa miakakama thelathini na mitatu hivi, akiitwa Yesu Kristo.

k.1 Luka aliiweka habari hii katika mazingara ya historia ya siku zile. Nchi yaPalestina ilikuwa katika jimbo la Shamu katika Dola ya Kirumi. Kaisari alipangamambo yaliyohusu majimbo yote yaliyo chini yake. Wayahudi walikuwa naMfalme wao, Herode, aliyewekwa na Kaisari ili amsaidie katika mambo yapalepale yaliyowahusu wenyeji.

Kaisari Augusto alitawala dola zima kwa muda mrefu (K.K.27-B.K.14). Nchinyingi. zilijisikia nafuu hatika hali zao, vita nyingi vilikwisha, na amani na utulivuvilikuwepo katika maeneo mengi. Aliiweka mipango mizuri ya kutawala dolayake vizuri. Ilibidi watu walipe kodi na mara kwa mara orodha za majinaziliandikwa ili afahamu uwezo wa wananchi, mapato yao, mali yao, na utajiriwao, ili apange kima cha kodi kufuatana na uwezo wa wananchi.

Page 21: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 311

k.2 Luka ametaja kwamba Kirenio alikuwa liwali wa Shamu. Si hakika kamaalikuwa liwali wakati huo, kuna ushuhuda wa uandikaji wa majina mwaka B.K.6(Mdo.5.37). Tena iwapo kuna habari za orodha za majina kuandikishwa marakwa mara katika majimbo mbalimbali hakuna habari moja ya kuandikwailiyohusu ‘ulimwengu’ yaani nchi zote za Dola.

k.3 Yawezekana mpango wa uandikaji huo uliongozwa na Mfalme Herode kwaajili ya Kaisari. Ilipangwa watu waende kwenye miji yao ya asili, penginekupunguza shida za watu waliochukia jambo hilo, maana kutozwa kodi kulikuwadalili ya kutawaliwa na watu wageni.

k.4 Mpango huo ulimsababisha Yusufu aondoke Nazareti na kwenda mpakaBethlehemu maili 6 hivi kusini ya Yerusalem, kwa kuwa alikuwa wa mbari yaDaudi, na Bethlehemu ndio mji alipozaliwa Daudi, Mfalme wao maarufu(1.Sam.16; 17:12, 58; 20:6). Hasa katika Agano la Kale Yerusalemu umeitwaMji wa Daudi (2 Sam.5:7; 6:10, 12, 16; 2 Waf.9:28; 12:22). Hatuna habari yaYesu kuzuru Bethlehemu baadaye ila siyo kusema kwamba hakwenda palekabisa.

k.5 Yusufu aliondoka na Mariamu, mja mzito, ambaye amemposa. ameitwamkewe (Mt.1:24) ila bado hawajakaribiana (Mt.1:25) ndiyo sababu ya kusemaamemposa. Je! Mariamu alikuwa na haja ya kwenda? Huenda si lazima aendekutokana na hali yake ya kukaribia kuzaa. Pengine ilifaa aende kwa sababuamekuwa mbali na Yusufu miezi mitatu hivi alipomtembelea Elizabeti na kukaanaye. Huenda watu wa Nazareti walikuwa wakimsemea vibaya walipoonakwamba ni mja mzito naye amekuwa hayupo kwa muda. Hayo yote ni mawazotu. Iwapo ilimbidi Yusufu aende Bethlehemu kwa ajili ya kuandikishwa, Mariamuapaswa kuwepo kwa sababu ya Yesu kuzaliwa pale ili atimize unabii wa Mika(Mik.5:1,2). Luka alitaka kuonyesha kwamba ni Mungu anayetawala katikamipango ya wanadamu, Kaisari ameagiza uandikishaji wa majina, na Munguameamua tangu zamani za kale kwamba Masihi atazaliwa Bethlehemu. (Mikaalitabiri miaka mia minane kabla ya tukio hilo).

k.6-7 Labda walichelewa kuondoka Nazareti na kwa sababu hiyo walipata shidaya kupata mahali pazuri pa kukaa. Kutaja hori imedhaniwa kwamba walikaakatika mahali pa wanyama. Huenda walikaa katika nyumba ya mtu maskini nawanyama waliishi pembeni katika chumba walimoishi watu na hori ilikuwemomle chumbani. Labda chumba walichotazamia kupata kilichukuliwa na wengine,au yawezekana watu hawakutaka kuwakaribisha. Inaonekana Mariamu alikuwapeke yake alipozaa akikosa msaada wa wanawake wengine maana twasomakwamba yeye alimvika kitoto na vipande vya nguo. Yote hayo ni dalili zaumaskini, kutokujulikana, na kukataliwa.

Tumepata wapi tarehe ya 25 Desemba kuwa siku ya kuzaliwa kwa Kristo.Katika Maandiko na katika maandishi ya zamani ya Kikristo neno hilo

Page 22: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

halikuandikwa, na hatujui kama hii ndiyo siku yake hasa, au ikiwa Wakristowaliongozwa kuchagua siku hiyo walipoamua kuadhimisha Kuzaliwa Kwake.Twajua kwamba Sikukuu hiyo iliadhimishwa Rumi kwa mara ya kwanzaB.K.354; Constantinople B.K.379 na Antiokia wa Shamu B.K.388. Miji hiyomikubwa ilikuwa vituo vikubwa vya Kanisa zamani zile. Baadaye tarehe hiyoilikubalika na Wakristo wengi.

2:8-20 Wachungaji walikuja kumwabuduYesuk.8 Kwa kawaida wachungaji hawakuwa na sifa njema kwa sababu katikakusafiri hapa na pale wakitafuta malisho kwa wanyama wao hawakujali mali yawatu. Pia ilikuwa vigumu wavishike viigizo vya sheria kwa sababu ya hali yakazi yao. Hawakutegemewa wala hawakuruhusiwa kutoa ushuhudamabarazani. Pengine hao wa Bethlehemu walitunza wanyama ili watu wapatewanyama kwa dhabihu zilizotolewa hekaluni. Kwa kawaida waliruhusiwakuchunga mashambani tu. Hatujui hao walikuwa wa tabia gani, penginewalikuwa watu wazuri.

Daudi, mfalme mashuhuri wa zamani, aliyezaliwa Bethlehemu alikuwamchungaji (1 Sam.16:11; 17:34,35) na katika Zaburi alimtaja Mungu kuwaMchungaji wa watu wake (Zab.23:1; 28:9; 100:3). Nabii Ezekieli alisisitizahabari za Mungu kuwa mchungaji wa Israeli (Eze.34:23).

k.9 Ghafula malaika aliwatokea wakati wa usiku, walipokuwa nje wakitunzakundi lao kwa zamu. Hatuambiwi jina la malaika, huenda ni Gabrielialiyemtokea Zakaria na Mariamu na kuwajulisha habari njema. Pamoja namalaika waliangaziwa ‘utukufu wa Bwana’ (Kut.16:7; 24:17) mwanga mkubwaulionekana juu yao. Si ajabu kwamba waliingiwa na hofu kuu.

k.10 Mara malaika aliwatuliza kwa kusema ‘msiogope’ kama alivyosema kwaZakaria na Mariamu (1:13,30) ndipo akaendelea kutoa sababu ya kutokuhofu.Tendo kuu limetendeka na Mungu alitaka kuwajulisha watu mbalimbali habarizake kwa sababu ni habari njema kabisa, ni habari za furaha nyingi, ni habariza kuzaliwa kwa Mwokozi wa ulimwengu.

k.11‘Leo katika mji wa Daudi amezaliwa....’ Hao ndio wa kwanza kuambiwahabari ya tukio hilo ambalo limefanyika ‘leo’. Ni habari mpya. Mtoto mchangaamezaliwa, na huyo mtoto ni Mwokozi, ni Kristo, ni Bwana. Ana sifa kuu kabisa.Ni yule ambaye ametiwa mafuta, ni Mfalme, Kuhani Mkuu, Nabii; yulealiyeahidiwa tangu zamani, pia ni Mungu Mwana (Kut.3:14). Amezaliwa ‘kwaajili yenu’ ni habari njema kwa watu wote. Tendo kuu limetendeka ambalolilihitaji kuelezwa na malaika, ili watu wafahamu kwamba huyo mtoto ni nanihasa na utume wake ni nini hasa. Hao wachungaji, waliotoka katika kundi lawatu waliodharauliwa, ndio waliofunuliwa siri ya huyo mtoto. Bila malaikakufunua neno hilo wasingaielewa habari yake, wala kuelewa maana na cheocha mtoto huyo, kwa sababu hawatamkuta katika jumba la kifalme, wala katika

Page 23: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 313

fahari za wakuu, bali watamkuta amelazwa katika hori ya wanyama kwa wazazimaskini.

k.12 Ndiyo sababu malaika aliwapa ishara. Waliyaamini maneno yake ilawatakapofika Bethlehemu watamtambuaje mtoto maana watoto wachangawengine watakuwa wamezaliwa wakati huo, ila ni mmoja tu ambaye atakuwaamelazwa horini. Kwa njia hiyo maneno ya malaika yatathibitishwa kuwa yakweli.

k.13-14 Mara jeshi la malaika wa mbinguni lilitokea (1 Waf.22:19) na kwa faharihiyo walijulishwa ukuu wa huyo watakayemkuta Bethlehemu. Ijapokuwawalikuwa jeshi, walikuwa jeshi la kutangaza amani si vita. Walitaja jinsimbinguni kulivyovutwa na kupendezwa na tendo hilo la Mungu. Pia duniaimepewa msingi wa kuipata amani na hali njema kwa wale ambao Munguamekusudia kujihusisha vema nao. Kwa tendo hilo Mungu amewafadhiliwanadamu.

k.15 Kisha hao malaika waliondoka na wachungaji walibaki peke yao. Bilakukawia waliamua kwenda kumwona huyo mtoto mchanga, ambaye makuuyamesemwa juu yake. Tumaini la miaka yote iliyopita limetimiziwa katika kujakwake.

k.16 Walisafiri kwa haraka, wakiwa na hamu kubwa sana. Ila hali watakazokutazitahitilafiana sana na utukufu ambao wao wenyewe walijaliwa kuuonawalipoambiwa habari zake. Hamna malaika, hamna fahari, hamna makuu.Wako Yusufu na Mariamu na mtoto mchanga sawa na jinsi walivyoambiwa,Mtoto aliye Mwokozi, Masihi, Bwana alikuwa amelala horini. Wasingaliambiwahabari hizo na malaika bila shaka wasingaliweza kuyaamini yaliyosemwa juuyake, ila kwa sababu yote yalipatana na maneno ya malaika walikubaliyaliyosemwa juu yake.

k.17-18 Waliwashirikisha Yusufu na Mariamu habari za kutokewa na malaika najeshi la malaika na maneno yaliyosemwa na malaika. Pia waliwaambiawengine, majirani n.k. Walikuwa wa kwanza kumwona na walikuwa wa kwanzakutoa habari zake. Watu walistaajabu walipousikia ujumbe wa wachungaji. Bilashaka waliamini kwamba Masihi amezaliwa.

k.19 Mariamu, tofauti na wachungaji waliosema habari zake, aliyaweka manenoyao moyoni mwake na kuyatafakari. Yalitia muhuri juu ya yale aliyoambiwa namalaika kabla ya kuchukua mimba. Luka alipataje habari hizo? twaelekezwakufikiri kwamba yalitoka kwa Mariamu mwenyewe (k.51).

k.20 Wachungaji walirudi kazini, huku wakiendelea kumsifu Mungu. Bila shakawalishangaa kuona kwamba wamejaliwa kuambiwa habari za tukio hilo kuukabla ya wengine wote. Mambo hayo yote yaliweka msingi mzuri kwa watu

Page 24: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kufikiri sana juu ya huyo Masihi ya kwamba atakuwa wa namna ganiyakiwadokezea kwamba hatakuwa mtu wa vita wala siasa, wala hatatakamakuu.

Katika habari hiyo twaona unyenyekevu mkuu wa Mungu.

2: 20-24 Yesu kutahiriwa, kupewa jina, na kuwekwa wakfuk.21 Ijapokuwa Yesu ni Masihi iliwabidi wazazi watimize sheria na desturi zaKiyahudi. Alitahiriwa siku ya 8 kama ilivyokuwa desturi tangu wakati wa Abramu(Mwa.17:12). Wakati huo alipewa jina la Yesu, lile ambalo malaika alikwishakumpa kabla Mariamu hajachukuliwa mimba (v.21).

k.22 Ndipo wakaenda hekaluni kutimiza sheria nyingine. Sheria moja ilimhusuMariamu kutakaswa. Kwa siku 40 mwanamke aliyezaa mtoto wa kiumealihesabiwa najisi mbele za sheria (Law.12:2ku) halafu mtoto wa kiumealiyekuwa kifungua mimba alitolewa kwa Bwana kwa kazi yake, akihesabiwamali ya Bwana (Kut.13:2; Hes.18:15). Yusufu na Mariamu walikuwa Wayahudiwaaminifu wakiyatimiza matakwa ya sheria. Walitoa ndege, ni maskini tuwalioruhusiwa kutoa ndege badala ya mnyama (Law.12:6).

2: 25-35 Simeoni na Wimbo wake ‘Nunc Dimittis’Hatujui mengine juu ya Simeoni ila hayo tunayoambiwa hapo. Wengi walikuwana jina hilo.

k.25 Aliishi Yerusalemu na amepewa sifa kubwa ya kuwa mtu mwenye haki namcha Mungu mwenye hamu sana ya kuona taraja kuu la Israeli kupata Masihilikitimizwa. Inaonekana kwamba alikuwa mzee kutokana na maneno ya‘hataona mauti kabla ya kumwona Kristo na Bwana..’. Walikuwepo kundi dogola watu waliompenda Mungu sana nao walisikia hamu sana ya kupata Masihina hamu hiyo ilizidi walipoona taifa lao linateswa chini ya utawala wa Kirumi.

Luka amesema kwamba Roho Mtakatifu alikaa juu ya Simeoni na hapo twaonajinsi Roho Mtakatifu alivyomjulisha kwamba atamwona Kristo kabla ya kufa,halafu Roho alimwongoza afike hekaluni wakati uleule ambapo Yusufu naMariamu na mtoto mchanga walipofika ili wayatimize matakwa ya sheria.

k.28 Simeoni alimpokea mtoto mchanga mikononi mwake na kumshukuruMungu na kutoa maneno ya unabii juu yake.

k.29 Alionyesha kwamba amekuwa tayari kufa kwa sababa sasa amemwonaMasihi, alijisikia kwamba ameutimiza wajibu wake wa kumsubiri na sasa nikama anaruhusiwa na Bwana wake kuondoka. Shabaha ya kungojea kwakeimetimizwa, sasa yu tayari kuondoka.

Page 25: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 315

k.30 Katika kumwona Kristo, amemwona Mwokozi wa ulimwengu, alikuwaameuona wokovu ambao Mungu mwenyewe ameuandaa.

k.31-32 Wokovu ni kwa ajili ya watu wote, kwa WaMataifa na kwa Taifa laIsraeli. Kristo ni ‘nuru ya kuwaangaza WaMataifa’. Simeoni hakushikwa na haliya utaifa kama Wayahudi wengi walivyoshikwa wakati ule. Wale waliosomaAgano la Kale bila upendeleo, walifahamu kwamba ahadi ya Mungu kwaAbramu ilikuwa ‘katika wewe Mataifa yote yatabarikiwa’ (Mwa.12). Pamoja nahayo Masihi ni ‘utukufu wa Israeli’. Hivyo, Masihi ataleta mwanga mkuu kwaulimwengu wote na kuondoa giza lake. Wokovu wake ni kwa watu wote.

k.33 Simeoni alisema mambo makubwa kumhusu Yesu yaliyozidi yaleyaliyosemwa na wachungaji. Mariamu ameishaambiwa makuu kumhusu mtotowake, na wachungaji waliongeza sifa zake walipokuja kumwona. Sasa Simeonialiwapokea na kumchukua mtoto mikononi mwake akaongeza sifa zaidi kwakushuhudia kwamba huyo ndiye Mwokozi wa ulimwengu atakayeukomboaulimwengu mzima. Jambo hilo liliwafanya Yusufu na Mariamu kuyastaajabiahayo yaliyonenwa juu yake.

k.34 Kisha Simeoni aliwabariki na kusema maneno ya unabii kwa Mariamukuhusu matokeo ya Kuja kwa Masihi katika Israeli pamoja na kusema jinsi yeyemwenyewe atakavyoguswa na hayo. Amewekwa kwa kuanguka na kuinukakwa wengi katika Israeli. Atasababisha farakano katika Israeli kati ya walewatakaompokea na wale watakaomkataa. Watu watapaswa kuamua kuwaupande wake au kuwa kinyume chake. Wale watakaompokea budi waachekiburi chao na kujinyenyekeza Kwake na kumpokea. Wasiokubalikujinyenyekeza wataangushwa. Maneno hayo yanadokezea habari za Matesona Kufa Kwake.

k.35 Kisha Simeoni alisema habari ya ‘upanga’ kuingia moyoni mwa Mariamu(neno lililotumika kwa upanga ni lile kwa upanga mkubwa). Yeye atashirikikukataliwa kwa mwana wake, kukataliwa kiasi cha kutundikwa msalabani.Hivyo, upanga utaingia moyoni mwake.

2: 36-38 Ana, alifika hekaluni na kumwamkia YesuLuka ameandika habari za huyo mwingine, kama shahidi wa pili, aliyefikahekaluni saa ileile Yesu alipoletwa. Yeye alikuwa mama mzee sana, aliolewakwa miaka saba ndipo akafiwa na mume na tangu hapo, kwa miaka themaninina minne (au miaka 88 ni umri wake) alitumia wakati wake wote, mchana nausiku, akifunga na kuomba na kutoa unabii. Pengine alikuwa na chumba chakeau nyumba yake katika eneo la hekalu. Bila shaka aliongozwa na kufunuliwa naMungu kwamba Yesu ameletwa hekaluni ili wazazi wazitimize taratibu zao zasheria. Alitoa shukrani zake kwa Mungu na kutoa habari zake kwa wale

Page 26: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

waliokuwa wakimtarajia Masihi. Viongozi wengi wa dini, akina Mafarisayo,Masadukayo, Makuhani n.k. walikosa uaminifu kwa Mungu, hata hivyowalikuwepo watu wachache waliodumu waaminifu nao walitamani sana Munguatimize ahadi yake ya kuwaletea Mwokozi atakayewatoa katika shida zao. Anaalistahili kuwa shahidi wa Kristo kwa sababu alikuwa nabii, pili alikuwa mpendaMungu sana. Katika Agano la Kale tunazo habari za wanawake waliokuwamanabii, Miriamu (Kut.15:20) Debora (Waa.4:4) Hulda (2 Waf.22:14) mke waIsaya (Isa.8:3).

Ni neno la kutia moyo kuona jinsi hao watu walivyofunuliwa na kuongozwa naMungu ili wapate kumwona Kristo hali akiwa mtoto mchanga na jinsi habarizake zilivyotangazwa kwa wengine.

Nabii hakutokea katika Israeli kwa muda wa miaka mia nne tangu nabii Malakimpaka Yohana Mbatizaji alipotokea. Hata hivyo, twaona kwamba Mungualikuwa amemwinua Ana kuwa nabii mke, kabla ya Yohana Mbatizaji kuwa mtumzima na kufanya kazi yake.

2: 39-52 Ujana wa Bwana YesuTunayo hiyo habari moja tu ya maisha ya Yesu alipokuwa kijana na ilitokeaalipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili.

k.39-40 Baada ya kuzitimiza taratibu zao huko Yerusalemu wote walirudimpaka Nazareti pamoja na Yesu. Kama mtoto awaye yote Yesu alipitia katikakila hatua ya kukua, kutoka hali ya kuwa mtoto mchanga, halafu akajifunzakusema, kutembea; ndipo akawa kijana mdogo, mwishowe akawa mtu mzima.Alikua kimwili katika kima chake, alikua katika akili zake akizidi kujua nakufahamu mambo mbalimbali, na alikua kiroho akijaliwa neema ya Mungukatika kupambana na majaribu ya utoto na ujana wake.

k.41 Ilimpasa kila Myahudi wa kiume ahudhurie hekaluni pale Yerusalemu,mara tatu kwa mwaka, kwa Sikukuu za Pasaka, Pentekoste, na Vibanda(Kut.23:14-17; Kum.16:16). Watu wa mbali walioshindwa kufika mara hizo zotewalijitahidi kufika kwenye Pasaka. Yusufu na Mariamu walishika sheria hiyo nakusafiri mpaka Yerusalemu kwa Pasaka. Bila shaka watu wa Nazaretiwalijiunga na kusafiri pamoja. Kwa desturi, akina mama na watoto walitangulia,ndipo wanaume na vijana walifuata nyuma.

k.42 Yawezekana Yesu amewahi kwenda pamoja nao kabla ya wakati huo.Sasa alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili, akianza polepole kuingia hali yamtu mzima na kujitwika wajibu zake kuhusu Torati n.k. Yafikiriwa kwambakijana wa miaka kumi na mitatu alifanywa ‘mwana wa sheria’ na mshiriki wasinagogi. Jambo la kwenda kwa Pasaka kulimzoeza katika wajibu zake zakidini.pengine walikuwa na shabaha ya kumzoeza katika mambo ya Pasaka.

Page 27: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 317

Atakapofika umri wa miaka kumi na mitatu atafanywa kuwa ‘mwana wa sheria’na kuingizwa kuwa mshiriki wa synagogi.

k.43-44 Shida ilitokea wakati wa kurudi. Walisafiri kwa muda bila kutambuakwamba Yesu hakuwa miongoni mwao. Pengine mama alidhani kwambaamekuwa na baba katika kundi la wanaume na baba alidhani kwambaamekuwa na wanawake na watoto. Watu walikuwa wengi na bila shaka njianivijana walichezacheza na kukimbia huko na huko. Huenda walitambuakutokuwepo kwake wakati wa jioni walipoandaa chakula au kwenda kulala.

k.45 Walipokosa kumwona wakaamua kurudi Yerusalemu na kumtafuta pale,hali wakiwa na wasiwasi na kuona mashaka kama amepatwa na madhara auvipi.

k.46-47 Kumbe, walimkuta hekaluni, hali amekaa na waalimu akiwasikiliza nakujifunza kwao, pamoja na kuwauliza maswali. Hata ilionekana kwamba alipatanafasi ya kutoa maoni yake kwa sababu twasoma kwamba hao waalimuwalistaajabia ufahamu wake na majibu yake.

k.48 Mariamu, mama yake alionyesha jinsi alivyokuwa amesumbuka kwakumkosa njiani. Ni kama alimkemea kwa kuwaletea shida hiyo kama amewaasiau kuwadanganya. Kama mama yeye alisikia wasiwasi na aliwahi kusemanaye.

k.49 Yesu akamjibu kwa maneno ya ajabu. Maneno hayo ni ya kwanza tuliyonayo ya Yesu kusema. Yote yaliyotangulia yalikuwa maneno juu yake. Hayo nimaneno yake mwenyewe. Ni kama alishangaa kwa vile walivyosumbukakumtafuta, ni kama alifikiri kwamba wasingalikuwa na haja ya kusumbuka nakumtafuta. Kama hawi pamoja naye si atakuwa na ‘Baba yake’ hekaluni?Alidokezea kwamba anao baba wawili, moja wa duniani na moja wa mbinguni,na katika maisha yake hana budi kuwa mwaminifu kwa wote wawili. Manenoyake huuonyesha uthabiti wake akiwa bado angali kijana wa miaka kumi namiwili. Aliendelea kutaja jinsi alivyojisikia. Ilimpasa awe katika nyumba ya Babayake. Maneno hayo ni makubwa. Kwanza yanaonyesha kwamba Yesuamesikia nafsini mwake kwamba anao uhusiano wa kipekee na Mungu, ni Babayake na yeye ni Mwana wake. Tena alijua kabisa kwamba kumtumikia Munguni jambo muhimu sana, ni neno linalompasa. Wao walisikia shidawalipomwona mahali alipo, yaani hekaluni, ila yeye hana shida yoyote, nyumbaya Baba yake ndiyo mahali pake hasa. Alikuwa na kiu sana kumjua Mungu namapenzi yake na alisikia msukumo wa wito wake ambao hatua kwa hatuaatazidi kuutambua.

k.50 Wazazi wake walishindwa kuelewa jambo hilo. Iwapo mengi makubwayamesemwa juu yake, ametajwa kuwa Mwokozi wa ulimwengu, Masihi wa ukoowa Daudi, n.k. Malaika alisema, wachungaji walisema, Simeoni alisema, na

Page 28: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

sasa yeye mwenyewe amesema. Kwa hiyo iliwachukua muda mrefu ili waelewemaana halisi ya ‘uana wake’ na kufahamu yaliyomo katika hayo yoteyaliyosemwa.

k.51 Yesu na wazazi wake walirudi nyumbani na Yesu aliwatii. Iwapo Mariamuhakufahamu maana ya maneno ya Yesu, hata hivyo, hakuyasahau na kamaalivyofanya na maneno ya wachungaji (k.19) aliyaweka moyoni mwake nakuyazingatia.

k.52 Hapo tena twapewa habari za Yesu kukua kimwili, kiakili, kiroho, na katikahali ya kushirikiana vizuri na watu pamoja na kuwa mwaminifu kwa Mungu kwakadiri alivyofahamu wajibu wake. Tukumbuke ya kwamba Yesu alilelewa katikanyumba ya kawaida, baba alifanya kazi ya useramala au ufundi fulani, naalikuwa na ndugu zake wa kike na kiume (Mk.6:3).

MASWALI:1. Ni mambo gani makuu yaliyosemwa kumhusu Kristo kwa watu

mbalimbali kama malaika kwa wachungaji na kwa Mariamu, Zakariakatika wimbo wake, Simeoni na Ana n.k.?

2. Ukuu na upekee wa Yesu Kristo ulidhihirishwa katika mambo gani nakwa njia gani?

3. Twajifunza nini kutokana na habari ya Yesu kuwa hekaluni alipokuwa naumri wa miaka 12?

3: 1-20 Yohana Mbatizaji na huduma yakeKama alivyofanya hapo nyuma Luka aliweka habari ya huduma ya Yesu katikamazingira ya historia ya sehemu zile. Inaonekana alipenda kufanya hivyo kwasababu alitaja historia wakati wa kuandika habari za kuzaliwa kwa Mbatizaji(1:5) na kuzaliwa kwa Kristo (2:1). Kwa hiyo, alisisitiza umuhimu wa huduma yaYohana nabii aliyetokea baada ya muda mrefu wa kukosa manabii. Wayahudiwalikuwa chini ya watawala wa kipagani waliokuwa wameigawa nchi sehemusehemu.

Tiberio alikuwa Kaisari B.K.14-37 na Pilato alikuwa liwali wa Uyahudi B.K.26-36. Herode alikuwa Mfalme wa Galilaya, huyo ni Herode Antipa, mwana waHerode Mkuu. Alitawala sehemu hiyo tangu K.K.4 hadi B.K.39, na karibu mudahuo wote Yesu aliishi na kufanya huduma yake katika eneo hilo. Filipo alitawalaeneo la kaskazini mashariki ya Galilaya tangu K.K.4 hadi B.K.34. Lisaniaalitawala sehemu iliyo kaskazini ya eneo la Filipo na hatujui kwa nini Lukaalimtaja kwa sababu sehemu yake haikuhusika na habari za Yesu. Kufuatanana habari hizo inafikiriwa kwamba Yohana alianza huduma yake kama B.K.27au B.K.28.

k.2 Halafu Luka alitaja habari za makuhani wakuu waliokuwepo. Ni mmoja tualiyekuwa kuhani mkuu ila wakati huo inaonekana Anasi aliendelea kuwa na

Page 29: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 319

sauti iwapo Kayafa, mkwewe alikuwa kuhani mkuu hasa (Yn.18:13; Mdo.4:6).Anasi alikuwa kuhani mkuu B.K.6-15 mpaka alipoondolewa na Warumi, ndipowana wake watano kwa mfuatano walishika cheo hicho kwa muda kishamkwewe Kayafa aliwekwa B.K.18-36. Kwa sababu waliwekwa na Warumiilikuwa vigumu wafanye kazi zao kwa unyofu wa moyo, iliwabidi waridhiane naokatika mambo mengi.

k.2b Hapo Luka ametaja jambo la maana sana. ‘Neno la Mungu lilimfikiaYohana..... jangwani’. Kwa maneno hayo Luka alisisitiza kwamba Yohanaalikuwa nabii halisi aliyelingana sawa na wale waliomtangulia, akina Isaya,Yeremia, Ezekieli n.k. Aliupata ujumbe wake kama wao walivyoupata, kutokaMungu mwenyewe, na wito wao uliwajia nyakati za watawala mbalimbali(Yer.1:1-2; 13:3; Isa.1:1; 6:1; 38:4; Eze.1:1-3). Yohana hakujitokeza mwenyewebali alingoja mpaka aliposikia msukumo wa Mungu.

k.3 ‘Akaja’ maana yake alifika karibu na mto Yordani na karibu na watu iliahubiri na kuwabatiza watu, huenda alikuwa akivuka ng’ambo na kurudi tena.Kwa sababu ya kubatiza alihitaji kuwa karibu na maji. Luka hakutaja habari zamavazi yake wala kula kwake kama Mathayo na Marko walivyofanya. Moja kwamoja alitaja habari za ujumbe wake. Neno kubwa kwa Luka ni kuhubiri kwakekuliko kazi yake ya kubatiza. Hakutaja habari za Ufalme wa Mungu kamaMathayo alivyofanya (Mt.3:2). Alihubiri kwa nguvu kwamba iliwapasa watuwatubu dhambi zao na kujiandaa tayari kwa kumpokea Masihi, na katika nenohilo alikuwa akiashiria aina ya wokovu utakaofanywa na Masihi, si wokovu wasiasa bali ni wa kiroho. Ili wauthibitishe ukweli wa toba lao watu walitakiwakubatizwa katika maji. Toba lao ni kumrudia Mungu, kumtegemea, na kufanyamapenzi yake. Yohana na Yesu walikuwa wajumbe. Yohana alitazama mbelekwa huduma ya Yesu akitoa nafasi kwa watu kuonja msamaha wa dhambiiwapo watu hawatajua msamaha kamili mpaka Kristo amekufa kwa ajili yakuwasamehe.

k.4-5 Mambo hayo yote yalikuwa na msingi katika unabii wa Isaya. Unabii waIsaya ulihusu nyakati zake, ila si zake tu, pia ulihusu wakati wa Yohana kablaya kutokea kwa Masihi. Injili zote zimetaja habari ya Yohana kuwa ‘sauti’ ni yuleambaye Mungu atamtumia ili aseme na watu wake. Kwa njia yake Mungualiwaita watu wajiweke tayari kwa Mfalme wao. Kama ilivyo katika nchi nyingizilizo na barabara zisizo nzuri, mkuu fulani atakapozuru mahali fulani watuhuzitengeneza barabara ziwe nzuri kwa mkuu kupitia pale. Ila njia iliyosemwahapo ni njia ya maisha, watu wayanyoshe maisha yao yaliyopotoka, yaaniwatubu. Ilikuwa kama amri iliyotoka kwa Mungu kuhusu mwenendo wao. Ndipomatokeo mazuri yataonekana, watu watakuwa tayari kwa Masihi Mwenyewe.Ujumbe huo uliwagusa watu wengi nao walibatizwa na Yohana, wakishukamajini na kuziungama dhambi zao (Eze.36:25ku. Zek.13:1).

Page 30: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

Kuhusu ubatizo, neno hilo lilikuwa geni kwa Wayahudi, walikuwa na maoshombalimbali yaliyoandikwa katika mapokeo yao. Wenyewe hawakubatizwa ilawaliwabatiza WaMataifa waliogeukia dini yao na kujiunga nao (hao waliitwawaongofu na baadaye wengi wao walimwamini Kristo). Kwa hiyo, Yohanaalikuwa akiwafanyia Wayahudi kuwa sawa na WaMataifa ambao Wayahudiwaliwahesabu ni ‘wachafu’. Katika jambo hilo alionyesha kwamba mtualiyezaliwa Myahudi hawi salama mbele za Mungu kwa sababu amezaliwaMyahudi.

k.6 Wokovu huo si kwa ajili ya Wayahudi tu bali ni kwa WaMataifa pia. ‘Wotewenye mwili’ watakaozitubu dhambi zao kwa kweli watapokelewa na Masihianayekuja. Watu walishtuka sana. Hapo twaona jinsi Luka alivyopenda kuwekawazi kwamba, Mungu kwa njia ya Mwana wake, alikuwa akiutengeneza wokovukwa ulimwengu mzima. Tena ametaja ‘wokovu’ kama kuleta nafuu katikaujumbe wa Yohana ambao katika k.7-17 ni ujumbe wa kuwatahadharisha nahukumu ya Mungu akisema kwa ukali. Makusudi ya Mungu hasa ni kuwaokoawanadamu si kuwahukumu.

k.7. Wengi walimwendea Yohana kwa sababu waliona kwamba nabii ametokeana kufanya kazi jangwani. Pia baadhi walikumbuka jinsi alivyozaliwa na wazaziwazee na maneno yaliyosemwa wakati ule, iwapo miaka 26 ilikuwa imepita.

Yohana hakudanganywa alipoona umati wa watu wakimjia, hakuwabembelezakwa maneno matamu ya kuwaridhisha, bali alisema kwa nguvu na kwa ukali juuya toba la kweli. Aliwaita ‘wazao wa nyoka’ pengine maneno hayo yaliwalengaMafarisayo na Masadukayo (Mt. 3:7). Watu walizoea kumwona nyoka akikimbiamajani yalipowaka moto. Hivyo, Yohana alitilia mkazo hukumu ya Mungu kamaambavyo manabii wa zamani walivyofanya. Aliwaonya wale waliokuja kwaubatizo wake watubu kwa kweli si kwa kukubali tendo la nje tu la kushukamajini.

k.8 Lazima maisha yao yapatane na toba lao. Wengine walifikiri kwambayatosha kwamba wawe wamezaliwa Wayahudi na kuwa watoto wa Ibrahimu.Ijapokuwa ilikuwa kweli Mungu alimpenda Ibrahimu na kumteua kuwa baba wataifa lao, hata hivyo, siyo kusema kwamba, kwa sababu hiyo, hawezikuwakataa wale waliotoka viunoni vyake. Yohana alilibomoa tegemeo hilo.Mungu aliyeumba kila kitu kutoka pasipo kitu, na kufanya taifa litoke kwaAbramu na Sarai walipokuwa kama wafu kwa upande wa kuzaa, awezakujipatia watoto wengine wasio wa uzao wa Ibrahimu; watoto wa imaniwanaofuata kielelezo cha Ibrahimu cha kumwamini na kumtegemea Mungu.

k.9 Ni wakati wa kukata shauri, hakuna kukawia, kwa sababu shoka limewekwatayari kuukata mti, maana yake, Mungu yu tayari kuleta hukumu juu yao(Isa.6:13; 10:33-34; Yer.6:6; Lk.13:6ku). Kutokea kwa Yohana, na baada yake,

Page 31: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 321

kutokea kwa Yesu, kutasababisha mgawanyiko katika watu ili mawazo yamioyo yao yapate kudhihirika.

k.10 Viongozi wa dini walilikataa shauri la Yohana (7:30) Katika makutanowalikuwapo wale waliotia maanani maneno yake nao walimwuliza jinsiilivyowapasa kutenda. Labda walifikiri iliwabidi wafanye jambo kubwa, ila kwamajibu yake kwa vikundi mbalimbali, mashauri yake yalihusu maisha ya kilasiku akiwaelekeza katika yale yaliyowezekana wayafanye.

k.11 Kwa wote aliwakumbusha wajibu wa kuwatunza watu waliokosa mahitajiya nguo na chakula, na kuwapenda jirani kama nafsi yao. Wawe na hurumu nawawe wakarimu katika kuwasaidia watu kutoka mali yao.

k.12-13 Halafu walimjia kundi la watoza ushuru. Walimwita mwalimu kamaYesu alivyoitwa baadaye. Hao hawakupendwa na watu kwa sababu walikuwatayari kuwasaidia watawala wa kigeni kukusanya kodi. Mtoza ushuru alipewaeneo fulani na kima fulani kwa sehemu hiyo. Hali hiyo ilimwachia nafasi yakuwadhulumu watu na kuwatoza zaidi. Wengi walifanya vibaya na walitajirikawakiwatoza watu zaidi na kuweka ziada mfukoni mwao. Jibu la Yohana lilikuwawazi kabisa ‘msitoze kitu zaidi....’ Watoza ushuru watubu kweli, wakubali kuishibila kuwadhulumu watu na bila kujitajirisha kwa njia zisizo halali.

k.14 Askari (yadhaniwa kuwa askari wa Kiyahudi si wa Kirumi, penginewalikuwa aina ya ‘polisi’) walimwuliza Yohana kuhusu wajibu wao. Mara kwamara maaskari waliwasaidia watoza ushuru kukusanya kodi kutoka walewaliokataa kulipa. Hivyo, kwa kufanya kazi pamoja na watoza ushuru ilikuwarahisi wajiunge nao katika kuwadhulumu watu. Kwa kuwa walikuwa na cheokilichowapa mamlaka ilikuwa rahisi wawashtaki watu kwa uongo na kwakutafuta rushwa. Yohana aliwaambia kwamba wasiwadhulumu watu walawasiwashtaki kwa uongo. Pamoja na hayo aliwashauri wawe radhi na mapatoyao, huenda hawakupata mapato mazuri ikitegemewa kwamba watawezakuongeza mshahara kwa njia zisizo halali zilizotajwa hapo juu.

Katika sehemu hiyo twaona jinsi Yohana alivyolenga maisha ya kila siku yawatu. Hakuwashauri watoza ushuru na askari waache kazi zao, ila aliwagusajuu ya majaribu yaliyowajia kwa njia ya kazi zao.

k.15 Kwa jinsi wengi walivyoitika wito wa Yohana na kubatizwa katika mtoYordani watu walianza kujiuliza kama Yohana ndiye Masihi. Ni dhahiri kwambataifa limeamshwa na kuwa katika hali ya kusisimua wakitambua kwamba jambokubwa linafanyika (Yn.1:20ku).

k.16 Ila Yohana aliyajibu mawazo na maulizo yao kwa kukana kabisa kuwaMasihi. Katika majibu yake alisisitiza ukuu na nguvu ya yule anayekuja nyumayake akijinyenyekeza sana sana. Alionyesha jinsi yeye mwenyewe asivyostahili

Page 32: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

hata kulegeza gidamu ya viatu vyake. Wakati ule wanafunzi walikuwa tayarikumfanyia mwalimu wao kazi ndogondogo, zisizo za maana wala sifa. Ila, hiyoya kulegeza gidamu hawakuwa tayari kufanya kwa sababu ilihesabiwa kaziduni kabisa. Inasemekana kwamba hata mtumwa hakutakiwa kufanya hivi.Kazi ambayo mwanafunzi na mtumwa hawakuwa tayari kufanya Yohanaangalifurahi kufanya akihesabu ni heshimu kubwa sana na kwa lugha hiyoalimwadhimisha Kristo na kujinyenyekeza kabisa. Pamoja na hayo alibainishakati ya ubatizo wake na ubatizo wa Masihi. Yeye hutumia maji ambayohusafisha kwa nje mwili wa mtu, hayana nguvu ya kumgusa mtu kwa ndani nakumbadilisha, iwapo alikuwa ametubu. Lakini Masihi atabatiza kwa Roho namoto. Yaani watu watapewa Roho wa Mungu atakayewagusa na kuwabadilishamioyoni mwao na kuwafanya upya kwa ndani. ‘moto’ ama ni dalili ya utakaso auya kupima mtu (1 Kor.3:13; Mal.3:1ku). Si kwamba kuna ubatizo wa aina mbili,wa Roho na wa moto, ni ubatizo mmoja tu. Roho wa Mungu atawajaribu nakuwapima na kuwatakasa. Kwa hiyo Yohana aliyashinda majaribu makali yakujiinua, aliwatazamisha watu kwa Masihi atakayetokea hivi karibuni na kwakazi za Masihi. Yeye na kazi zake ni matayarisho tu. Masihi atakapotokeaatakuta watu wameandaliwa tayari wakielewa kwamba Yesu amekuja kufanyamambo ya kiroho, kusimama upande wa haki na kweli. Yohanahakuwatazamisha wajiandae kwa vita ya kuwafukuza Warumi. Tusifikirikwamba ubatizo wa Yohana na Yesu unapishana, la, zote ni za maana, ila ulewa Yohana uliotangulia ulikuwa na shabaha ya kuwatayarisha watu kumpokeaYesu.

k.17 Masihi ataendeleza kazi ya kuhukumu, kuwatakasa watu wake, namgawanyiko utatokea. Itadhihirika wazi ni akina nani walio ‘ngano’ na akinanani walio ‘makapi’. Hukumu itakuwa kamili na hakika. Neema na ghadhabu nisehemu mbili katika Injili, zinawiana; msamaha, uhai mpya wa ndani, nautakaso kwa wengine, na hukumu ya adhabu kwa wengine. Wayahudiwalidhani kwamba Masihi atakapokuja atawahukumu WaMataifa tu, lakini siyo,haidhuru mtu ni wa kabila gani, au cheo gani, au tabaka gani, kila mtuatafanyiwa kufuatana na itikio lake kwa Yesu. Watu walipaswa kuhamia upandewa ‘haki’ katika maisha yao si kupitia katika maji ya ubatizo tu (Isa.66:24;Mk.9:48).

k.18-20 Yohana alitoa maonyo mengi kwa watu, ambayo yalikuwa sehemukatika habari njema aliyohubiri. Bila maovu kuangamizwa hamna habari njema.

k.19 Yohana hakuwaogopa watu, hata wakuu na wenye cheo. Hakuwa naupendeleo. Alimkaripia Herode Antipa kwa dhambi yake ya kumchukua mke wakaka wa kambo Filipo pamoja na kumwonya juu ya maovu menginealiyoyafanya.k.20 Jambo hilo lilimgharimu Yohana maisha yake. Herode alichukizwa sana,akamtia gerezani, na baadaye akamkata kichwa (Mt.14:3-4; Mk.6:17-18). Luka

Page 33: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 323

ametaja jambo hilo hapo ingawa halikufanyika mpaka baadaye. Ndipoaliendelea na habari za Yohana na kazi alizozifanya kabla ya kutiwa gerezani.

3: 21-22 Yesu alibatizwa na Yohana (Mt.3:13ku.Mk.1:9-11;Yn.1:31-34)Luka ametaja habari hii kwa ufupi, Mathayo kwa kirefu. Luka hakutaja kulekubatiza kwenyewe kana kwamba jambo la maana zaidi ni Kushuka kwa Rohona Tangazo la Baba; mambo hayo mawili yalimshuhudia Yesu kuwa Mwanapekee wa Mungu.

k.21 Katika k.20 Luka ameacha habari za Yohana Mbatizaji na kuanzakuziandika habari za Yesu, ni kama Yohana ameishamaliza kazi zake, wengiwamebatizwa, pia Yesu amebatizwa. Yesu alisubiri kumwendea Yohana iliabatizwe mpaka Yohana ameelekea kumaliza huduma yake. Siyo kusema wotewalibatizwa kwa sababu tunajua kwamba aliendelea kuwabatiza watu, ilawakati umetimia kwa Yesu kuanza huduma yake hadharani.

Wakati huo ulikuwa muhimu sana kwa Yesu kwa sababu katika ubatizoalikubali kabisa wito wake wa kuwa Masihi na Mwokozi wa ulimwengu.Maandalio yamekwisha na sasa ilimbidi ajitokeze mbele za watu na kuanzahuduma yake. Alianza kwa unyenyekevu kabisa akishuka majini na kubatizwana Yohana.

Ni Luka tu ambaye amesema kwamba Yesu alikuwa akiomba. Katika Injili yakeLuka alipenda sana kutaja habari za Yesu kuomba. Ilikuwa kawaida ya Yesukuomba kila wakati na hasa katika hatua kubwa za maisha yake alipokabiliwana mambo makubwa na magumu. ‘mbingu zilifunuka’ ilikuwa lazima mbinguzifunuke ili Roho ashuke halafu sauti ya Baba isikike, jambo hilo liliashiriaufunuo wa Mungu. Yesu aliona utukufu na adhama ya Baba yake na kujua kwahakika kwamba anao uhusiano wa kipekee naye, ni Mwana wake halisi.

Katika ubatizo Yesu alijitoa na kujiweka wakfu kwa kufanya mapenzi ya Babayake, alikubali kuwa yule atakayekufa kwa ajili ya dhambi za watu wote nakutoa nafsi yake kuwa fidia ya dhambi. Hivyo katika ubatizo alijiweka upandewa wenye dhambi, akipokea ubatizo wa toba ijapokuwa Yeye Mwenyewehakuwa na dhambi kwa hiyo hakuwa na sababu ya kutubu. Kwa tendo lakuushiriki ubatizo wa toba alikuwa akikataa dhambi kabisa, kwa kuwa mtuakitubu anakataa dhambi.

k.22 Roho alimshukia katika umbo lililoonekana kwa macho, kwa mfano wahua. Siyo kusema kwamba Roho ni hua au analo umbo fulani. Yesu alimwonana Mbatizaji alimwona (Yn.1:33, 34). Luka hasemi juu ya ubatizo mwenyeweuliofanywa na Yohana. Kwake neno kubwa ni kule kushuka kwa Roho naTangazo la Baba katika kusema na Yesu. Hayo ndiyo mambo makubwa na

Page 34: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

muhimu. Alitiwa mafuta na kusimikwa rasmi na Baba yake, kama Wafalme naMakuhani walivyofanyiwa (1 Sam.10:1ku. Isa.61:1).Sauti ilikuwa ya Baba yake, akimpa utume wake. Waamuzi na manabiiwalipewa Roho kwa kazi zao. Je! Utume wa Yesu ni nini? Yeye atafanya kazigani hasa? Kwa tangazo lake Mungu alimfunulia Yesu utume na kazi yakepamoja na kumhakikishia kuwa Mwana wake halisi, mpendwa wake, mwenyeuhusiano kamili naye. Yeye ni tofauti na wengine wote, ana asili katika MunguMwenyewe. Bila shaka neno hilo lilimtia Yesu nguvu na moyo wakati wakuanza huduma yake. ‘nimependezwa nawe’ Maneno hayo yana maana gani?Tangu alipozaliwa mpaka hapo akiwa mtu mzima wa miaka kama thelathiniamempendeza Mungu. Amepitia salama katika utoto na ujana wake, sasa yutayari kwa yote hata mazito yaliyo mbele yake. Ni kama Mungu alimwambia ‘juuyako mpango wangu wa kuuokoa ulimwengu umekaa’. Maneno hayo yalitokaZab.2:7 na Isa.42:1, sehemu zilizokubaliwa zilimhusu Masihi. (Uana wake piayadokezewa katika Mwa.22:2; Kut.4:21-23; 2 Sam.7; Isa.61:1). Hivyo, namnaya huduma yake imeamuliwa na tangazo la Baba yake. Yeye ni Mwana waMungu na Mtumishi ateswaye (Isa.53) ambaye atatimiza mapenzi ya Mungu yakuuomboa ulimwengu. Mungu alitia kibali chake kwa Utume wa heshima sanawa Yesu kuwa Mwokozi wa ulimwengu. Yesu aliisikia tena sauti ya Baba wakatialipogeuka sura mlimani (Lk.9:35) na kabla ya kuteswa kwake (Yn.12:28).

Kwa jinsi ambavyo Luka aliandika habari hizo kwa ufupi alisisitiza kwambajambo muhimu ni ule ufunuo wa utume wa Yesu kutokana na manenoyaliyosemwa na Baba pamoja na kushuka kwa Roho atakayemwezeshakuutekeleza utume huo. Hayo ni ya maana kuliko kubatizwa na Yohana.Tusiwaze kwamba Yesu hakuwa na Roho kabla ya hapo. Alizaliwa kwa uwezowa Roho Mtakatifu, alijazwa na Roho tangu kuchukuliwa mimba. Ila hapoalipewa vipawa rasmi vya Roho kuhusu utume wake wa kuwa Masihi naMwokozi. Kwa kushukiwa na Roho wakati huo Yesu alihakikishiwa kwambaanao uwezo wote wa kuutimiza wito wake.

3: 23-38 Orodha ya wazazi wa YesuKabla ya kuendelea na habari za Yesu Luka alipenda kumtambulisha Yesu nakumweka katika safu ya wanadamu tangu Adamu. Wayahudi walipenda sanakutunza orodha za koo zao na hasa zaidi wale wa ukoo wa Daudi. Yeyotealiyedai kuwa Masihi lazima aweza kuonyesha kwamba ametoka kwa Daudi.

k.23 Luka ametaja umri wa Bwana Yesu, yawezekana alitaka kuonyeshakwamba Walawi wa zamani waliruhusiwa kuanza kazi zao wakiwa na miakathelathini na zaidi. Hivyo Yesu, mtumishi wa Mungu, kwa kufuatana na mtindowa Walawi alikuwa na umri huo alipoanza huduma yake (Hes.4:47). Alikuwamtu mzima. Hapo nyuma Yusufu ameitwa ‘mwana wa Daudi’ (1:27,32,69) kwasheria ya Kiyahudi alikuwa hivyo ijapokuwa mwenyewe hakuwa baba mzazi waYesu. Shabaha ilikuwa kumwonyesha Yesu kuwa mwana na mrithi halali waDaudi.

Page 35: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 325

Wataalamu wengine hufikiri kwamba orodha hii inafuata ukoo wa Mariamu nawengine ukoo wa Yusufu. Tofauti na orodha ya Mathayo amerudi nyuma yaIbrahimu mpaka Adamu. Sehemu tangu Ibrahimu hadi Daudi kwa jumlainafanana na Mathayo. Ila tangu Daudi ni tofauti. Mathayo alifuata ukoo waYusufu akilenga kumthibitisha Yusufu kuwa mwana halali wa Daudi machoni pasheria, tena alifuata ukoo wa Wafalme na Luka alifuata watu wenyewe, ilatusifikiri kwa kutumia ‘mwana wa’ ni mwana hasa. Katika nchi mbalimbali mtuhumwita mtu ‘ndugu’ iwapo si ndugu halisi.

k.23b ‘akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu’ kwa maneno hayo Lukaamelinda neno la Yesu kuzaliwa na Mariamu, si Yusufu. Alizaliwa na bikira kwahiyo habari hii haiwezi kulingana na orodha za wengine.

Marko hakuandika orodha ila Mathayo alianza Injili yake na nasaba. Alianza naIbrahimu baba wa taifa la Kiyahudi, kwa sababu aliandika kwa ajili yaWayahudi.Luka alianza na jamaa ya Yusufu na Mariamu na kurudi mpaka Adamu, nakumaliza na maneno, ‘wa Mungu’. Hivyo Luka alisisitiza kwamba Yesu ni kwamataifa yote. Yesu ni Mwokozi wa ulimwengu kwa hiyo hakuna haja ya kukazahabari za Daudi na Ibrahimu n.k. Yesu alikuwa mwanadamu kweli aliyezaliwakatika taifa fulani na kabila fulani na ukoo fulani na aliishi Nazareti, mjiuliokuwepo. Kama sisi, alitoka kwa Adamu, yule aliyeumbwa katika sura yaMungu na kuwa mwanadamu wa kwanza. Ila tofauti na Adamu yeyehakuanguka. Alishuka kutoka mbinguni, kwa Mungu, kusudi amtii Mungu tofautina Adamu aliyemwasi (Flp.2:6-8). Yesu alistahili kuwa Masihi kwa sababualikuwa mwanadamu halisi. Hivyo Luka alimpa Yesu mahali katika familianzima ya wanadamu.

Kwa nini Luka aliweka orodha hiyo hapo kati ya mambo yanayofuatana.Yohana amefanya kazi yake, Yesu amebatizwa, yu tayari kuanza kazi, ila kablaya kufanya hivi ilimbidi ajaribiwe. Huenda Luka ameweka ukoo wa kibinadamukabla ya kuweka habari ya majaribu yake ili ambainishe na Adamu wa kwanza,ambaye alipojaribiwa alianguka. Kristo ni Adamu wa mwisho aliyekuja kutangualaana iliyosababishwa na Adamu wa kwanza (Rum.5:12ku; 1 Kor.15:22,45).

4: 1-13 Yesu alijaribiwa (Mt.4:1-11; Mk.1:12-13; Lk.4:1-13)Alipobatizwa Yesu alithibitishwa na Baba yake kuwa Mwana wake mpendwaambaye juu yake mpango wa ukombozi wa ulimwengu ulikaa. Wakati huoalijazwa Roho Mtakatifu ili awe na vipawa vyote vya kuutekeleza mpango huowa wokovu. Alikuwa tayari kuanza huduma yake, ila kabla ya kuanza alikaajangwani muda wa siku arobaini au zaidi na huku alipata utulivu wa kuuzingatiawito wake na namna ya Umasihi wake, na jinsi atakavyovitumia vipawaalivyopewa na uwezo alio nao kwa shabaha hiyo. Ilikuwa mpango wa Mungu

Page 36: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

akabili neno hilo kubwa kwa sababu katika neno hilo kuweko kwa Ufalme waMungu kunakaa. Mungu amekusudia kumweka Yesu awe kichwa chaubinadamu mpya aichukue ile nafasi ambayo Adamu aliharibu alipomwasi.Akifaulu kuukomboa ulimwengu, Mungu kwa njia ya Kristo, ataweka utawala wahaki mioyoni mwa wanadamu na Ufalme wake hautakuwa na mwisho. Katikakuyazingatia hayo yote Ibilisi aliona anayo nafasi ya kumjaribu kwa njia yakuyapandikiza mawazo yaliyohitilafiana na mapenzi ya Baba yake. Yesuhakuwa na dhambi kwa hiyo mawazo hayo yalitoka nje yake (kama yale yaAdamu wa kwanza). Iwapo hayo majaribu yalitoka nje yake yalimvuta kwasababu yalihusu jinsi atakavyotimiza lengo la kuja kwake. Yeye, zaidi yamwanadamu awaye yote, alisikia nguvu ya majaribu hayo, kwa sababu ni yuletu asiye na dhambi ambaye asikia nguvu ya majaribu kupita wenye dhambi,kwa kuwa wenye dhambi hawamtii Mungu kwa asilimia mia.

k.1 Yesu alijaa Roho akaongozwa na Roho mpaka jangwani, na wakati wotealipokuwapo huku Roho alimwongoza. Alikuwapo mahali pagumu, pa ukimya,pa upweke, pa shida kwa mahitaji ya mwili, hakula kitu kwa sababu alijitoakabisa kutafakari wito wake (yawezekana alikula vitu vidogo vilivyokuwapokama mizizi na mbegu za miti). Mwisho wa siku hizo arobaini alisikia njaa.

k.2 Ibilisi alifahamu kwamba Yesu amedhoofika kimwili, na amechoka baada yakupambana na mawazo mbalimbali ndipo Ibilisi akamletea aina tatu zamashauri makali sana.

k.3 Ni wazi kwamba Shetani alikuwepo ila kama alionekana katika umbo fulani,au kwa maono, au kwa kiroho, ni vigumu kujua, wala si neno kubwa kamaalikuwa na umbo fulani au siyo, jambo kubwa ni uhalisi wa kuwepo kwake kwahali fulani.

Neno ‘ukiwa’ ni kama kusema ‘kwa kuwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu’uthibitishe jambo hilo kwa kuligeuza jiwe hili liwe mkate. Ni kama alitaka Yesuafikiri kwamba kwa nini asumbuliwe na njaa ikiwa yeye ni Mwana wa Mungu nakwa nini asumbuliwe na njaa ikiwa anao uwezo wa kuondoa njaa kwa njia isiyokawaida na isivyowezekana kwa wanadamu wengine. Je! kama mwana, hanahaki ya kufanya hivi? Je! kama mwana, hana heshima hiyo ya kuutumia uwezowake jinsi atakavyoamua mwenyewe? Shetani alilenga kuutikisa uhusianowake na Baba, asiwe radhi na hali yake, asiwe tayari kusubiri msaada waMungu, na ayainue mapenzi yake kinyume cha mapenzi ya Baba yake. Nidhahiri kwamba Yesu alijua kwamba alikuwa na uwezo wa kipekee na uhusianowa kipekee na Baba na wito wa kipekee au asingalisikia kujaribiwa kwa njiahiyo.

k.4 Jesu hakujadiliana na Ibilisi, akamjibu kwa ufupi, kutoka Maandiko. Alijuahakika kwamba yale yasiyopatana na Maandiko hayatoki kwa Mungu.Wanadamu si kama mnyama anayeishi kwa kimwili tu. Mwanadamu

Page 37: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 327

ameumbwa ili ashirikiane na Mwumba wake. Wanadamu hataishi kwa mkate tu.Neno ‘tu’ ndilo la maana. Sehemu ya maisha yetu ni ya kimwili ila si yote. Kitukikubwa si mkate bali ni Mungu mwenye kutoa na kuhifadhi maisha yetu. Jibu laYesu lilitoka Kum.8:3 wakati watu wa Mungu walipoishi jangwani kwa miakakama arobaini. Katika kuupima utiifu wao kwa Mungu mara kwa marawalipatwa na shida za kimwili ili wajifunze kumtegemea Mungu. Yesu simfanyakazi wa huduma za jamii tu. Neno muhimu kwa Yesu lilikuwa kuutunzauhusiano wake na Baba kwa kumwamini na kujinyenyekeza Kwake. Bilakuujenga uhusiano huo hawezi kuwa Masihi halisi (Yn.4:34). Adamu, mwanawa Mungu (Mwa.3:38) na Israeli ‘mwana wa Mungu’ walijaribiwa kuhusu utiifuwao wa Mungu, nao wakaanguka. Yesu ‘Mwana’ tofauti na hao alimtii Mungu,Baba yake.k.5-8 Yesu alikuja ulimwenguni ili amshambulie Shetani na enzi yake (1Yoh.3:8; 5:19). Alikuja kuuleta Ufalme wa Mungu ili watu wamtawaze awemfalme wao na kumpaa utiifu wao. Hivyo atawezaje kufaulu kuwavuta watuKwake ili wampe utiifu wao? Hivyo Ibilisi alileta jaribu lingine kali sana lililogusakabisa shabaha hiyo. Alimshauri Yesu aridhiane naye, ndipo yeye atampa milkizote za ulimwengu. Awe tayari kuacha njia ngumu za mateso na shida, atumienjia za mkato, asijali mambo ya haki, na utakatifu, na rehema, na upendo.Atumia njia yo yote mradi awavute watu. Je! enzi hizo zilikuwa zake? La, hatakidogo, ila kwa njia fulani zilikuwa zake? Kwa njia gani? Kwa sababuwanadamu walikuwa wamempa utiifu wao, Adamu, na baada yake wanadamu,wamekuwa tayari kukubali mashauri yake ya uongo na kumwasi Mungu. Yesualimwita ‘mkuu wa ulimwengu huu’ (12:31; 14:30; 16:11) lakini si mkuu halisi, ilaamegusa sana maisha ya ulimwengu huo, uovu umeenea sana katika maishaya wanadamu wanaoishi kwa kujipendekeza bila kumjali Mungu na mapenziyake. Ni mkuu kwa sababu wanadamu wenye dhambi wamemruhusu aongozena kutawala maisha yao. Hata hivyo, si mkuu hasa. Ibilisi ni mwongo namdanganyifu mkubwa, akitumia nusu ya kweli na kuidai kuwa kweli yote. LakiniYesu alikuwa Mfalme tofauti (Yn.18:36) ufalme wake si wa namna za duniahiyo, siyo wa kijiografia, wala wa siasa n.k. bali ni ufalme wa haki ambao eneolake ni katika mioyo ya wanadamu. Kwa maneno machache Yesu alilikataakabisa shauri hilo la Ibilisi akitegemea Neno la Mungu kutoka Kum.6:13, nenolinaloonyesha kwamba wanadamu wote wapaswa wamsujudie na kumwabuduMungu peke yake. Mungu haushirikishi utukufu wake na mwingine awaye yote.Katika kumkataa Ibilisi Yesu alikuwa ameyakataa mawazo ya Kiyahudi juu yaMasihi kuusimamisha utawala wake pale Yerusalemu na kuliweka taifa lao liwejuu ya mataifa mengine. Yeye ni Mtumishi ateswaye atakayeingia ufalme wakekwa njia ya kufa Msalabani, atavikwa taji ya utukufu, ya miiba, pale Msalabani.Fahari ya Ufalme wake si ya dunia hii, bali ni fahari ya tabia njema za upendo,haki, utakatifu na rehema.

Ilikuwa haki Yesu apate chakula, ilikuwa haki Yesu apate milki za ulimwenguhuu, ila yalimpasa apate kwa njia halali zilizopatana na mapenzi ya Baba yake.

Page 38: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.9-12 Shetani, iwapo ameshindwa mara mbili, hakukata tamaa, aliona vemaalete jaribu lingine kali sana. Kama Yesu alikwenda mpaka Yerusalemu aukama alikwenda kimawazo si neno kubwa. Shabaha ya Ibilisi ilikuwa kumfanyaYesu ajiweke mahali pa hatari ndipo amlazimishe Baba yake amwokoe.Wayahudi walikuwa watu waliotaka ishara, mara kwa mara katika historia yaAgano la Kale tumeona hali hiyo. Kwa njia hii ya ajabu Shetani alitakakumdanganya Yesu na kumfanya aamini kwamba watu watavutwa kumpokeaawe Masihi wao (Mal.3:1ku). Katika Isa.35 ilitabiriwa kwamba Masihi atafanyamaajabu, lakini si maajabu yasiyo na lengo la kuwasaidia watu. Jaribu hilo lakujitupa chini halitasaidia watu, ni kama bure. Kwa sababu Ibilisiameishatambua kwamba Yesu huongozwa na Neno la Mungu, yeye naye,alitumia madondoo kutoka Zaburi 91:11ku. Akitaka kumhakikishia Yesuusalama wake, kutokana na ahadi ya Mungu juu ya ulinzi. Yesuhakudanganywa na hila yake, alijua kwamba Ibilisi ameyaacha maneno yamaana sana ‘atakulinda katika njia zako zote’ maana yake atamlinda hataatakapokanyaga njia ya mateso na kufa. Yesu alimjibu tena kwa ufupi sanaakirudia Kitabu cha Kumbukumbu, 6:16. Hakuna aliyeruhusiwa kumjaribuBwana Mungu, hata yeye, ingawa ni Mwana pekee wa Mungu, hana hakikufanya hivyo. Yesu alijua kwamba haja kubwa ya wanadamu ni kupatamsamaha na ushindi wa dhambi. Yampasa atoe nafsi yake kuwa fidia yadhambi, mashauri hayo yote ya Ibilisi hayaleti jibu kwa haja kubwa ya wenyedhambi ya kutibiwa dhambi zao..

Majibu yote ya Yesu yalitoka katika sehemu fupi ya Kitabu cha Kumbukumbukati ya 6:13 - 8:3. Ni kama alikuwa ameyazingatia sana mambo yaliyowapataWaIsraeli walipojaribiwa kumwasi Mungu. Yesu hakuingia katika majadiliano naShetani na ni fundisho kubwa kwetu. Ikiwa Yeye aliyejaa hekima na ufahamukamili hakuona vema kujadiliana na Shetani, si zaidi sisi?

(Mawazo kuhusu Kitabu cha Kumbukumbu: maana ya ‘Kumbukumbu’ ni Toratiya pili, ni kitabu kinachoweka tena sheria ya Mungu aliyopewa Musa. Ni sheriailiyotoka kwa Mungu kuwa kanuni ya maisha ya wanadamu. Kwa kifupi majibuya Yesu yalikuwa ‘wewe unasema mambo ya mwili yatangulie utii wangu kwaMungu. Lakini Mungu amewaambia wanadamu ‘wasiishi kwa mkate tu; kwahiyo hata mimi sitaishi kwa mkate tu. Wewe unanipa enzi zote, ikiwa nitakubalikukusujudu. Lakini Mungu amewaambia wanadamu kwamba wasikiabudu kituchochote kingine isipokuwa Yeye, kwa hiyo, hata mimi, sitakusujudu. Weweunanishauri kwamba nizitegemea ahadi zake kwa faida yangu ya binafsi. IlaMungu amewaambia wanadamu wasimjaribu kwa namna hiyo, kwa hiyo, hatamimi nami sitamjaribu. Hivyo Yesu aliweka kando utukufu na uwezo wake(Mt.26:53) na kujiweka mahali pa mwanadamu aliye chini ya sheria ya Mungu(Flp.2:7-8). Amerudi kuwa badala ya Adamu wa kwanza, yeye ni Adamu wamwisho. Katika bustani ya Adeni Ibilisi alimkabili Adamu wa kwanza, na Adamuwa kwanza aliyasikilizi mashauri yake, akaanguka, na katika kuangukaaliwaongoza wanadamu wote kwenye njia ya uasi. Adamu wa pili, Yesu alikuwa

Page 39: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 329

mtii wa mapenzi ya Baba yake. Hapo jangwani alimshinda Shetani na kupigahatua kubwa katika kupambana naye ambako upeo wake utafikiwa paleGethsemane na Msalabani. Tangu hapo wanadamu wanalo tumaini la ushindi).

Kwa sababu Yesu alikuwa jangwani peke yake, ni Yeye aliyewajulishawanafunzi wake habari hizo.

k.13 Shetani alishindwa kabisa. Nasi twaweza kuyashinda majaribu yetutukifuata kielelezo chake. Yeye hakuwa na silaha ila ile ambayo sisi nasitunayo, yaani neno la Mungu pamoja na nia iliyokazwa kumpendeza Baba.Mara kwa mara uaminifu wetu wa Mungu utapimwa, hakuna wakati ambapohatutajaribiwa katika maisha yetu ya hapa duniani.Shetani alimwacha Yesu ‘kwa muda’ baada ya kushindwa kwa kila njia yaanikwa kuleta kila aina ya jaribu, alikuwa ametumia mbinu zake zote zakumdanganya na kuutikisa uhusiano wake na Baba, akashindwa. Alimwachakwa muda, kwa sababu katika huduma yake yote Shetani aliendelea kumjaribukwa kutumia watu mbalimbali. Na Yesu aliwaonya wafuasi wake juu ya hilazake 8:12,13; 10:18; 11:14,16,18; 13:16; 22:3,28,31). Yesu aliishiwa nguvu naMungu alimtuma malaika aliyemtia nguvu, kwa hiyo, Mungu alimsaidia kwawakati wake (Mt.4:11). Maana ya neno ‘Ibilisi’ ni yule anayemkashifu Mungu;neno ‘Shetani’ lina maana ya mpinzani. Kwa hiyo anamshtaki Mungu kwetu nakumshtaki sisi kwa Mungu. Ni vema kusoma Ebr.2:14ku; 4:15-16; 5:7-8 kuhusumajaribu. Hatuwezi kuishi bila majaribu katika maisha yetu, hasa tukiwa wafuasiwa Yesu.

Huduma ya Yesu katika Galilaya 4:14 - 9:50

4: 14-15 Yesu alianza kuhubiri (Mk.6:1-6; Mt.4:17)Maneno hayo yanajumlisha huduma yake katika eneo la Galilaya. Lukaamesisitiza tena jinsi Yesu alivyofanya kazi yake katika nguvu za RohoMtakatifu. Shughuli mojawapo kubwa ilikuwa kuwafundisha watu juu ya Ufalmewa Mungu akizungukia vijijini na mijini. Alichukua nafasi alizopewa katikamasinagogi pamoja na kuhubiri hadharani. Iwapo hapo Luka hakutaja jambo lakutoa pepo na kuwaponya wagonjwa, tunajua kwamba Yesu alifanya hayoyote. Habari zake zilienea na wengi waliona huduma yake kuwa njema.

4: 16-30 Yesu alihubiri Nazareti na kukataliwa (Mk.6:1-6; Mt.13:53-58)k.16 Yafikiriwa Yesu hakwenda Nazareti mara alipoanza huduma yake katikaGalilaya ila Luka ametanguliza habari hii na kuiweka hapo mwanzoni. Nazaretini mahali alipolelewa na mahali walipoishi jamaa zake, wazazi na ndugu zake.Wengi walimwelewa kwa kuwa alikuwa ameishi kati yao kwa miaka thelathini,akiwa mtoto, ndipo kijana, kisha mtu mzima na mfanyi kazi kama wengi wao.Ilikuwa desturi yake kusali katika sinagogi siku ya Sabato (k.15) akitafuta nafasiya kuhubiri. Wakati huo alipewa nafasi ya kusoma Maandiko na kutoa

Page 40: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

mafundisho juu yake. Katika sinagogi hawakuwapo ‘pasta’ kama katikamakanisa yetu. Wazee waliangalia na kupanga wasomaji na wahubiri, naowalizoea kuwapa marabi wazungushiane nafasi ya kufundisha, Yesu nayealihesabiwa kuwa rabi.

k.17 Walimpa Yesu chuo cha Isaya, kwa kawaida somo moja lilitoka katikaTorati na lingine lilitoka katika Vitabu vya Manabii. Hatujui kama hilo somolilikuwa somo rasmi kwa siku ile au ikiwa Yesu Mwenyewe alilichagua. Neno‘akatafuta’ linatuelekeza kufikiri kwamba Yeye alilichagua.

k.18-19 Somo hilo lilihusu Masihi aliyeahidiwa na Mungu. Wakati ule wengiwalimtazamia kwa hamu, hasa kwa sababu walichukizwa na utawala waKirumi. Yesu alisema wazi kwamba unabii huo wa Isaya ulikuwa ukitimizwapale pale na wakati ule ule katika Yeye Mwenyewe. Yeye ametiwa mafuta,yaani kusimikwa rasmi (wakati wa ubatizo wake) naye ametumwa na Mungukutangaza habari njema kwa watu wenye shida, kwa maskini, wafungwa,vipofu, na waliosetwa (Isa.58:6; 61:1ku). Hakuna neno la siasa au utaifa,hakutumwa kuwafukuza Warumi. Aliacha maneno machache yanayoonekanakatika (Isa.61.2b) kuhusu ‘kisasi cha Bwana’ (Luka akaza kwamba wokovu nisasa, hukumu ni baadaye). ‘Mwaka wa Bwana uliokubaliwa’ maana yake simwaka fulani hasa, ila tangu wakati huo wokovu hupatikana. Kwa tangazo hiloYesu alionyesha jinsi alivyojisikia nafsini mwake, akiwa na uhakika wa wito nautume wake. Yeye alionyesha madaraka yake pale sinagogini, akiwa kati yamambo yaliyotokea pale. Maneno yake yaliashiria Jubilee, Yeye aleta wokovu.Yeye si mfanyakazi wa huduma za kijamii, wala yeye si mwana siasa aumwana mapinduzi, Yeye haingii eneo la siasa, hata hivyo, ana mzigo mkubwajuu ya mahitaji ya kimwili ya watu pamoja na mzigo juu ya haja zao za kiroho.

k.20 Baada ya somo akamrudishia mtumishi chuo cha Isaya, akaketi, hukuwote waliokuwamo sinagogini walimkazia macho, wakiwa na hamu sana yakusikia atakayosema. Bila shaka, aliposoma somo, mamlaka yake ilitambulikakatika sauti yake.

k.21-22 ‘Leo, Maandiko hayo yametimia ...’ ‘Leo hii’ yaani wakati huohuoMungu anatenda kazi kubwa kwa njia ya Yesu. Yale yaliyotabiriwa na Isayamiaka mia saba na zaidi iliyopita, sasa yametimia katika Yeye Yesu waNazareti. Waliyastaajabia maneno yake, kwa kuwa yalikuwa maneno yaneema, kwa njia yake Mungu huwakirimia watu neema ya msamaha wadhambi. Ila walipokumbuka asili ya yule aliyesema nao walisikia shida, walianzakusitasita. Walikumbuka malezi yake kati yao, baadhi yao walikuwawamecheza naye alipokuwa mtoto na kijana, walikuwa wamezungumza nayesokoni na kazini. Waliwajua baba na mama na ndugu zake akina Yakobo,Yose, Yuda na Simeoni, na maumbu yake. Walitatizwa kiasi cha kushindwakumwamini. ‘Huyu si mwana wa Yusufu?’ Kwa swali hilo walitaka kuuepaujumbe wake. Jibu ni ndiyo ila zaidi ya kuwa mwana wa Yusufu Yeye ni Mwana

Page 41: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 331

wa Mungu’. Pamoja na hayo katika mawazo yao walitaka ayathibitishe madaiyake kwa kufanya ishara kama kuwaponya watu n.k. kama walivyosikia alikuwaamefanya Kapernaumu.k.23 Yesu alitambua mapema swali lao na kabla hawajapata nafasi ya kuliuliza,Yesu alilisema. Walitaka ishara, dalili ya kutokumwamini, na kwa kuitumiamithali Yesu alionyesha kwamba ni vigumu sana mtu mkubwa apate kibalimahali alipotoka na kwa watu waliomjua hapo nyuma. Hata manabii wa zamanihawakupokelewa vizuri, akina Isaya, Yeremia, Ezekieli, Mika, Amosi ambaobaadhi yao waliuawa.

k.25 Kisha aliwakumbusha habari za manabii wawili mashuhuri, walioishizamani. Njaa kubwa ilipoingia nchini kwa sababu mvua haikunywa kwa miakamitatu na nusu Eliya alitumwa na Mungu aende kwa mmojwapo wa wajanealiyeishi nchi nyingine, si katika Israeli. Alitumwa kwa Mmataifa, tena mjane tu,na alihifadhiwa huko (1 Waf..17:8-16). (Watu walidhani kwamba Eliya atakujakabla ya Masihi (Mal.3:1; 4:5-6) (Yesu alisema kwamba Yohana Mbatizajialikuwa huyo ‘Eliya’ aliyesemwa na Malaki).

k.27 Wala si hivyo tu, hata Elisha alimponya mtu wa Shamu, mpagani,aliyeshikwa na ukoma. Alikuwa jemadari wa jeshi la adui zao WaShamu. KatikaIsraeli wenye ukoma walikuwepo, lakini Elisha hakutumwa kwao (2 Waf.5:1-14).Yesu alikuwa akidokezea kwamba habari njema si kwa Wayahudi tu, bali nikwa WaMataifa pia. Baraka zake hazina mpaka. Kumkataa pale Nazaretihakutamzuia. Wao walidhani Masihi atawabariki Wayahudi na kuwaangamizaadui zao, kumbe, Masihi yu tayari kuwabariki wote bila ubaguzi.

k.28-30 Maneno ya Yesu yaliwaghadhibisha. Hawakutaka kusikia zaidi. Haliyao ilibadilika sana, na tukichunguza sababu yake, ni ukosefu wa imani kwaupande wao. Walimtoa nje ya mji, dalili ya kumkataa kabisa, nao walikusudiakumdhuru au hata kumwua, ila kwa mwujiza au kwa fujo za msukumano, alipitakati yao na kwenda zake. Hatuna habari ya Yesu kurudi Nazareti.

4: 31-37 Yesu alimponya mtu mwenye pepo (Mt.8:14-17; Mk.1:21ku)Yesu alitoka Nazareti kwenda mpaka Kapernaumu, mahali alipoweka kituochake, pengine kwa nyumba ya Simoni Petro na Andrea. Ameanza kujulikanakama rabi/mwalimu na alipewa nafasi ya kufundisha katika masinagogi. Hivyosiku ya sabato alikwenda kuhubiri katika sinagogi la pale Kapernaumu.Alifundisha tofauti sana na marabi waliotegemea mawazo ya waalimumashuhuri, wakizoea kusema, ‘kama Rabi fulani alivyosema..’ ila Yesuhakutegemea wengine kwa mafundisho yake, yalitoka Kwake mwenyewe, tenamaneno yake yalikuwa na nguvu ya kugusa watu mioyoni mwao. Watuwalishangaa mno. Kwa kadiri alivyoendelea kusema, huku watu wamekaakimya na kumsikiliza, ndipo mtu mwenye roho ya pepo mchafu alipaza sautiyake na kwa nguvu alilia ‘Acha! tuna nini nawe Yesu wa Nazareti? Umekujakutuangamiza? Nakujua u nani, Mtakatifu wa Mungu’. Yule mtu alisumbuka

Page 42: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

sana alipokutana na Yesu, enzi ya uovu ilikutana na enzi ya utu mwema, nahamna patano kati yao. Ndiyo sababu pepo alisema ‘Acha, tuna nini nawe’.Katika kusema ‘Umekuja kutuangamiza?’ si kwamba pepo alikuwa akiulizaswali tu bali alikuwa akiitangaza kazi ya Yesu. Kazi ya Yesu yahusu ulimwengumzima wa uovu si kutoa pepo katika mtu mmoja tu. Pepo alimtambua Yesukuwa Mtakatifu wa Mungu ambaye mbele yake uovu huangamizwa. Yesuhakujadili na pepo bali alimkemea na kumnyamazisha, na kumtoa. Yesuhakutumia maneno ya apizo au laana, kama waganga walivyozoea kuyatumia.Pepo alimtoka yule mtu kwa kumwangusha chini bila kumdhuru akionyeshajinsi ambavyo hakupenda kutolewa, ila ilimlazimu amtii Mwana wa Mungu.Katika jambo hilo twaona vita iliyopo kati ya Yesu na enzi za uovu, kwa sababuYesu alikuja ulimwenguni aziharibu kazi za Shetani (1 Yoh.3:18). Pepowalimfahamu Yesu kuwa Mwana wa Mungu ila walikosa kumwamini (Yak.2:19).Watu waliokuwemo sinagogini walishangaa kwa kuona uwezo na nguvu yatendo hilo la Yesu lililoandamana na uwezo wa Neno lake alipowafundisha. Sikana kwamba alifanya mara moja au mara chache, walisema ‘awaamuru’ kamailikuwa kawaida yake kufanya hivyo. Kutokana na jambo hilo habari zakezilienea kila mahali katika eneo kubwa. Watu waliuona uwezo wa Roho katikahuduma yake.

4: 38-44 Yesu alimponya mkwewe Simoni na wengine wengiBaada ya shughuli zake pale sinagogini alirudi nyumbani kwa Simoni naAndrea, na Yakobo na Yohana waliandamana nao (Mk.1: 29). Walimkutamamaye mkewe Petro ni mgonjwa, ameshikwa na homa kali. Luka aliyekuwadaktari alisema homa ilikuwa kali. Walimwomba Yesu amsaidie. Yesuakasogea karibu naye na kuikemea ile homa, na mara moja ikamwacha,akaweza kuwatumikia. Neno kukemea ni lile lililotumika kwa kukemea pepo.Kukemea homa ni sawa na kukemea pepo, na homa humwacha mtu sawa napepo kumwacha mtu. Je! Yesu aliona kwamba Shetani yu nyuma ya homayake na kwa sababu hiyo ilimbidi aikemea hiyo homa, au vipi? ni vigumu kujua.Iliyopo ni kwamba huyo mama amewekwa huru mbali na homa yake. Lukaalitaka tufahamu kwamba aliponywa ugonjwa mkali na kwa mara moja. (Katika1 Kor.9:5 twasoma kwamba Petro alikuwa na mke ambaye alikwenda pamojanaye katika safari za kuhubiri; pengine mke wake alizungumza na akina mamana kuwahudumia Petro na wenzake kwa mambo ya kimwili kama kupika, kufuanguo n.k).

k.40 Yesu alikuwa amejishughulisha sana Sabato hiyo, pale sinagogini naaliporudi nyumbani. Bila shaka alisikia uchovu na alitaka kupumzika. Jualiliposhuka na sabato imekwisha, ndipo watu waliruhusiwa kubeba vitu n.k. Kwasababu wengi wamepata kusikia habari zake walileta wagonjwa wao naaliwahudumia mmoja mmoja na kuwaponya. Pia wenye pepo walikuja kutolewamapepo. Kama ambavyo tumeona hapo nyuma mapepo walimtambua nakupiga kelele wakilia ‘Wewe u Mwana wa Mungu’. Aliwakemea nahakuwaruhusu kunena kwa vile walivyomjua ni Masihi. Yesu hakutaka

Page 43: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 333

atambulishwe kwa njia hiyo, alitaka watu wenyewe wamtambue katika hayoyote aliyokuwa akiyafanya. Pia hawatamjua kwa ukamilifu mpaka atakapokuwaamekufa Msalabani, kwa kuwa mawazo yao juu ya Masihi yalihitilafiana naUtume wake. Twaona kwamba aliwaponya watu kwa kuwagusa mmoja mmojaila pepo walitolewa kwa neno lake bila kuguswa, na bila kudai watu wakiri imaniyao.

k.42-44 Ndipo baada ya shughuli hizo zote hakurudi nyumbani bali alikwendamahali pasipokuwa na watu. Yawezekana alijaribiwa kufikiri kwamba atatimizaUtume wake katika huduma ya kuwaponya watu bila mateso. Marko ametajakwamba alikuwa akiomba. Lakini hakuweza kujificha, watu walimtafutatafuta nawalipojua alipo wakaja kwake, nao walijaribu kumzuia asiondoke Kapernaumualijua kwamba alitumwa kuhubiri Habari Njema katika eneo kubwa la Galilayana Yudea, katika miji na vijiji vyake. Kazi yake ilikuwa kusafiri hapa na pale, bilakukaa mahali pamoja. ‘imenipasa’ alitambua ni mapenzi ya Mungu kufanyahivyo. Kwa njia ya Huduma yake ya kufundisha na kuponya na kutoa mapepoUfalme wa Mungu uliletwa kati ya watu na watu walizionja nguvu zake.

MASWALI:1. Eleza uzuri wa Yohana Mbatizaji, tabia yake na kazi zake.2. Kwa nini Luka alirudi mpaka Adamu alipoandika orodha ya ukoo wa

Bwana Yesu?3. Eleza umuhimu wa Yesu kujaribiwa na Shetani; na shabaha yake.4. Kwa upande wa Yesu, Yesu alipimwa kuhusu nini hasa?5. Kwa njia gani Yesu aliyashinda majaribu yake?6. Alipoanza huduma yake Yesu alifanya kazi za aina gani?7. Kwa nini alikataliwa alipohubiri katika sinagogi la Nazareti?8. Katika mahubiri yake alisema nini kuhusu utume wake, alitumwa kufanya

nini? na utume huo ulitofautiana na matazamio ya watu kumhusu Masihikwa njia gani?

5:1-11 Kuvua samaki wengi na wito wa Petro na wenzake(Mt.4:18-22; Mk.1:16-20; Ling.na Yn.21.lku)Mathayo na Marko wameandika habari hiyo bila kutaja habari ya mwujiza wakuvua samaki wengi. Kwa sababu hiyo wengine wamewaza kwamba jambo laYesu kuwaita hao lilitokea mara mbili na wengine wamewaza kwamba ni habarimoja na Mathayo na Marko waliacha kutaja habari ya mwujiza wa kuvuasamaki wengi.

Twajua kwamba Simoni Petro na Andrea na Yohana walikuwa wamekutana naYesu wakati wa huduma ya Yohana Mbatizaji (Yn.1: 35-52). Yesu alikuwaameanza kufundisha katika eneo la Galilaya na kufanya miujiza ya uponyaji na

Page 44: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kutoa pepo (Lk.4:33-35, 40) na umati wa watu walikwenda kumsikiliza (4.42).Simoni Petro na wenzake wameishajua habari zake.

k.1 Hapo twamkuta Yesu amesongwa na umati wa watu waliokuwawakimsikiliza alipokuwa akitoa Neno la Mungu; yaani ujumbe wa Mungu, Nenolisemalo juu ya Mungu. Walikuwa na hamu sana kumsikia kwa sababu Nenolake lilikuwa na nguvu na Yeye alilifundisha kwa mamlaka. (Neno hilo limeitwaInjili na katika Injili limeitwa habari njema ya Ufalme wa Mungu).

Mara zote Luka alitumia neno ‘ziwa’ kwa bahari ya Galilaya, watu walizoeakuiita ‘bahari’. Liliitwa ‘Ziwa la Chinneroth’ katika Agano la Kale. Yohana aliitaBahari ya Tiberia (Yn.21). Ilikuwa maili 13 kwa maili 7 na futi mia saba chini yausawa wa bahari.

k.2-3 Yesu aliona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, alichagua kile chaSimoni Petro, akaketi na kufundisha watu. Wavuvi walikuwa wakizitengenezanyavu zao tayari kwenda kuvua tena. Iwapo hawakupata kitu usiku ule,hawakukata tamaa, walikuwa wakiziandaa nyavu zao kwenda kuvua tena. Yesualikitumia chombo hicho kwa ‘kuvua watu’ yaani kwa njia ya kuhubiri alikusudiakuwaingiza wasikilizaji wake katika Ufalme wake akiwasihi kutubu nakumwamini.

k.4-5 Baada ya kumaliza kufundisha alimwambia Simoni aende kuvua samakitena. Lakini Simoni alisikia shida sana kulipokea neno hilo. Kwanza, kwasababu walikuwa wamevua usiku bila kupata kitu na bila shaka walisikiauchovu. Pili, kwa sababu haikuwa saa nzuri kwa uvuvi. Petro alikuwa mvuvi naalifahamu kazi hiyo sana pamoja na kufahamu tabia ya bahari na samaki namahali pa kupatikana kwa samaki. Yawezekana nafsini mwake alifikiri huyoYesu ni nani hata ajiingize katika ufundi wangu na kuniagiza hivyo? Si ameishimbali na bahari na hapo nyuma amekuwa seremala! Ajuaje mambo ya uvuvikiasi cha kuniongoza mimi aliye mvuvi halisi? Petro hakusikia shida Yesualipokitumia chombo chake kwa kuwahubiri watu, lakini kumwamuru juu yachombo chake na kwenda kuvua samaki, hili ni neno jingine! Ijapokuwapohakupenda wazo la kwenda kuvua hata hivyo, alikubali. ‘Bwana mkubwa...lakinikwa neno lako nitazishusha nyavu’. Neno la Kiyunani kwa ‘bwana mkubwa’limetumika na Luka tu, mara 7, na mara zote kwa Bwana Yesu. Ni neno lakumkiri Yesu kuwa mtu mwenye mamlaka. Hawawezi kutokujali neno lake, hatalile linalohusu uvuvi wa samaki. Kwa kawaida, wavuvi walifanya kazi usikukatika maji yaliyopungua. Yesu aliwaamuru waende mchana mpaka kilindini,tofauti kabisa na mazoea yao. Chombo kilichotumika kwa kuwavua samakililitumika na Yesu kwa kuwavua watu.

k.6-7 Tokeo la kulitii neno la Yesu lilikuwa kubwa. Waliposhusha nyavu zaowalivua samaki wengi mno, kuliko uwezo wa nyavu zao kuwabeba, hatailiwabidi wapungie mikono washirika wenzao, Yakobo na Yohana, ili waje na

Page 45: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 335

kuwasaidia kwa kuwaweka samaki wengine katika chombo chao. Ilionekanakwamba hata vyombo vyote viwili vilitaka kuzama majini. Ni kama mwujizaulifanyika si katika kuwavua samaki wengi tu, bali, pia katika vyombo na samakiwengi kufikishwa salama mpaka pwani.

k.8 Na tokeo kubwa zaidi liliwahusu wavuvi wenyewe. Petro amekuwa kati yahabari hiyo na alipoona tukio hilo alianguka chini miguuni pa Yesu na kusema‘Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana’. Aliitika kamamtu aliyejisikia yuko mbele za Mungu. Alitambua kwamba yeye ni mwenyedhambi, asiyestahili hata kidogo kukaa na huyo Yesu. Alifahamu kwamba wingiwa samaki haukuwa na maelezo nje ya uwezo wa Mungu. Alifanana na watuwa Mungu wa zamani, akina Ibrahimu, Ayubu, Isaya, na Wana wa Israeli, jinsiwalivyojisikia Mungu alipojifunua kwao (Mwa.18:27; Ayu.42:6; Isa.6:5;Kut.20:19; Dan.10:16). Alimwita ‘Bwana’ neno tofauti na lile la k.5.

k.9 Luka amesisitiza tena ‘wingi wa samaki’ na ushangao wa Petro nawenzake, Yohana, Yakobo (Andrea hatajwi kwa jina, alikuwa ndugu wa Petrona mshiriki kikazi).

k.10b-11 Yesu alimwambia Petro kwamba hakuna haja ya kuhofu na yakwamba tangu hapo maisha yake na ya wenzake yanabadilika sana. Wataachakuvua samaki, kitu cha kufa, nao watavua watu walio hai. Walielewa mbinu zakukamata na kuvua samaki, na tangu hapo watajifunza kwa Yesu mbinu zakuukamata usikivu wa watu na kuwaleta kwa Yesu. Watajifunza kwakushirikiana naye. Marabi walikuwa na wanafunzi walioandamana nao, ilatofauti na Yesu hawakuwashirikisha kazi yao, waliwafundisha mafunzo yao tu.Yesu aliwafundisha wanafunzi wake pamoja na kuwashirikisha huduma yake ilibaadaye awaachie hiyo huduma kuiendeleza.

Mwishowe, walipomaliza kushughulikia vyombo na samaki, wakaviacha,wakamfuata Yesu. Ule ujuzi waliopata kumhusu Yesu na uwezo wake ulikuwawa thamani sana kupita thamani ya samaki wengi. Inaonekana hapo nyumawamekwenda kumsikiliza na kufuatana naye mara kwa mara, ila tangu hapo,walikuwa wanafunzi wake wakamilifu, wakiandamana naye kila wakati.

Yesu na Simoni waliletwa pamoja kwa njia ya chombo. Wanafunzi haowalijifunza kwamba Yesu ni mtawala wa bahari na mawimbi yake na utajiriuliomo baharini. Wingi wa samaki ulikuwa ahsante yake kwa nafasi yakukitumia chombo chao. Siku ya Pentekoste Petro alivua watu wengi, kama elfutatu, alipohubiri kwa mara ya kwanza habari za Yesu baada ya Yesu kuwaamepaa na kurudi mbinguni.

Page 46: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

5:12-16 Yesu alimponya mwenye ukoma (Mt.8:1-4; Mk.1:40-45)Habari katika Luka inafanana na ile ya Mathayo na Marko na tofauti ni chachetu. Wenye ukoma walitawaliwa na sheria zilizoandikwa katika Walawi sura 13na 14. Hawakuruhusiwa kushirikiana na jamaa zao wala jamii ya watu.Hawakuruhusiwa kuingia mjini wala kusogea karibu na watu; wakisikia kishindocha watu iliwabidi wapaze sauti na kujitangaza ‘mimi ni mchafu, mimi ni mchafu’ili watu wajihadhari nao, wasije wakanajisika. Ukoma ulikuwa wa ainambalimbali, aina moja ilikuwa mbaya sana na wa hatari, mtu aliharibiwa sura,mara nyingine vidole vya mikono na miguu, hata pua, vilikatika. Jamii ya watuwalikabili shida hiyo kwa kuwatenga ili waishi kambini pamoja na wenye ukomawengine. Hawakuweza kufanya kazi na kupata mapato. Watu waliogopa sanawasije wakaambukizwa ukoma.

Hasa shida ilikuwa katika watu kuwaza kwamba ukoma ni zaidi ya kuwaugonjwa pia ni ‘uchafu/unajisi’ ulioweza kuwaambukiza watu na kuwanajisi.Ndiyo sababu imeandikwa kwamba walioponywa walitakaswa, yaaniwaliponywa kimwili pili waliondolewa unajisi. Hatari ilikuwa kwamba ugonjwahuo ulienea upesi katika watu.

k.12 Mtu alimjia Yesu hali amejaa ukoma; maana yake alishikwa sana naugonjwa huo. Ni Luka, daktari, aliyetumia neno ‘amejaa’ Mathayo na Markowaliacha kusema hivyo. Hatujui kwa nini huyo mtu alikuwa mjini. Huendaamesikia habari za Yesu kuwemo na alitaka kusema naye, inaonekanaameishasikia habari za Yesu na matendo yake mema kwa wagonjwa. Mkomaalipokutana na Yesu alifanya kama Petro alivyofanya mbele za Yesu (5.8)alianguka kifudifudi miguuni pake. Kwa maneno ‘Bwana, ukitaka, wawezakunitakasa’ alijifunua mawazo yake ya ndani, alikuwa na imani hata hakuwa namashaka juu ya uwezo wa Yesu kumponya, ila hakuwa na hakika kwambaYesu alipenda kumhurumia. Twaona mkazo juu ya utakaso ‘’ukitaka’ wawazakunitakasa’, mtu alijisikia ni mchafu. Neno ‘ukitaka’ ni dalili ya mtu aliyezoeakukataliwa na watu, amezoea maisha ya kutengwa na watu, kwa hiyo, hakujuakama Yesu alifanana nao na wengine, naye atamkataa pia. Hakuona vemakumdai amponye ila aliamini kabisa kwamba anao uwezo.k.13 Yesu akamjibu wazi kwa maneno ya kumtumainisha ‘nataka’ ‘takasika’akitangulia kumgusa. Yesu na mwenye ukoma wamesogeana hata kiasi chaYesu kumgusa. Bila shaka jambo hilo lilimtia moyo na furaha. Kwa miaka kadhaameishi bila kuguswa isipokuwa na wenye ukoma wenzake. Lilikuwa tendorahisi, ni nani asiyeweza kuunyosha mkono? ila lilikuwa tendo kubwa la ajabu,la upendo mwingi, lilisema zaidi ya maneno. Kwa tendo hilo Yesu aliyabomoamapokeo ya miaka mingi ya nyuma. Pia kwa tendo hilo alimkaribisha arudikuishi katika jamii, awe na uhuru wa kuishi kati ya watu tena. Ukomaukamwacha mara.

k.14 Ajabu ni kwamba Yesu alimkataza kwa nguvu asizitangaze habari hizo.Kwa nini? Yesu alitaka kuonyesha kwamba Yeye hawi kinyume cha Torati

Page 47: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 337

(neno ambalo Mafarisayo walizidi kumshtaki) alikuwa na mzigo kwambamatakwa ya Torati yatimizwe. Haikuwa vema utakaso wake kutangazwa kablahaujahakikishiwa na kuhani, kwa sababu ilikuwa haki ya kuhani kuupelelezaukweli wa uponyaji wa wenye ukoma, ni kama yeye alikuwa mtakasaji wakekwa upande wa kutoa hati ya utakaso. Yesu hakupenda kujiingiza katika kaziyake. Baada ya kuhani kutoa cheti ndipo mtu alikuwa na uhuru wa kuishi tenakati ya watu. Pia Yesu hakutaka kuamsha hamu za watu waliotaka kumfanyaawe Masihi wa namna ya siasa, mtu wa kuwafukuza Warumi na kuuwekautawala wake pale Yerusalemu na kuingia urithi wa ufalme wa Daudi, kamawengi walivyodhani Masihi atakavyofanya. La! alikuwa amekataa neno hilo palejangwani alipojaribiwa na Shetani. Pia hakutaka watu wamwaze kuwa mponyajina mfanya miujiza tu bila kujali mafundisho yake. Kwa upande wake nenokubwa ni kwamba watu kutubu na kutengeneza maisha yao na kuishi kwakumpendeza Mungu. Katika kuuhakikikisha ukweli wa uponyaji huo kuhanialishuhudiwa uwezo wa Yesu. Twaona Yesu aliivunja sheria juu ya kumgusamkoma maana ilikuwa sheria baridi iliyomkatisha mtu tamaa. Ila aliishika sheriailiyohusu kutoa shukrani kwa Mungu. Budi yule mtu amwendee kuhani na kutoasadaka iliyoamriwa. Katika habari hiyo twaona uwezo, mamlaka, na upendo waYesu.

k.15-16 Lakini yule mtu hakumtii Yesu, alizidi kuzitangaza habari zake na wengiwalikusanyika ili wamsikilize Yesu wakiwaleta wagonjwa wao ili wapatekuponywa. Yesu alitambua kwamba viongozi watazidi kumwonea mashaka nakushikwa na wivu juu yake kwa jinsi alivyowavuta watu wengi. Kwa sababu hiyoYesu aliwaepa, akaenda mahali pasipokuwa na watu na kuomba. Yawezekanaalisikia kujaribiwa sana kufanya jinsi watu walivyotaka. Hakutaka kutawaliwa.namatakwa yao, kwa vyovyote ajiweka chini ya matakwa ya Baba yake. Lukaamesisitiza desturi yake ya kuomba. (Tukilinganisha na 4:27 alipokuwaNazareti, alitaja jinsi Elisha alivyomponya Naamani mkoma, Mmataifaaliponywa huku Waisraeli wenye wakoma hawakuponywa. Hapo matumainiyapo kwa Waisraeli wenye ukoma kwa kuwa Yesu amemponya Mwisraelialiyemwamini kwa kweli).

5:17-26 Yesu alimponya mwenye kupoozwa (Mt.9:1-8; Mk.2:1-12)k.17 Luka hakusema mahali ambapo jambo hili lilitokea. Marko na Mathayowametaja Kapernaumu. Yesu alikuwa aliwafundisha watu na kuwaponya (k.15).Kabla ya kuendelea na habari yenyewe Luka ametaja kuwepo kwa Mafarisayona Waalimu wa Torati (vikundi vilivyoheshimika katika Israeli) nao walitokaGalilaya, Uyahudi, na Yerusalemu. Kutokana na sifa za Yesu kuenea mahalipengi viongozi wa dini waliwajibika kumpeleleza Yesu, kusikia mafundisho yakena kuyaona matendo yake, ila hawakuwa na nia safi. Watu walikuwawamekusanyika ndani ya nyumba, huenda katika ua la ndani. Luka ametajakwamba ‘uwezo wa Bwana ulikuwepo apate kuponya’. Kabla ya kuanzahuduma yake, alipobatizwa, Yesu alipewa Roho Mtakatifu (4:14) na wakati wotealifanya kazi katika nguvu zake, katika kuwaponya watu, katika kufanya miujiza,

Page 48: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

pia katika kuwasamehe watu dhambi zao, kazi hizo zote ziliyathibisha madaiyake ya kuwa Mwana wa Mungu. Tusiwaze kwamba Roho alimjia na kuondokana kumjia tena, la, alikuwa kama ghala ambayo Mungu aliweka hazina ya Rohondani yake. Wakati huo uwezo wa Roho ulidhihirika wazi katika matendo yaajabu aliyoyafanya Yesu.

Mafarisayo walikuwa kundi la walei, walioshikilia dini yao kwa bidii, wakijitahidikuyatimiza matakwa yote ya Torati, amri zilizomo katika Agano la Kale, pamojana mapokeo yaliyotungwa na waandishi katika kuifafanua Torati. Waalimu waTorati walikuwa kundi rasmi la wataalamu walioishughulikia Torati na kuifafanuana kuifundisha.. Wengi wao walikuwa Mafarisayo, na baadhi Makuhani. Watuwa vikundi hivi walijitokeza mara kwa mara katika huduma ya Yesu, wakizidikuhojiana naye hata wakaanza kumpinga. Walimfikiria Yesu kuwa kinyumechao kwa vile alivyokuwa na mikazo tofauti na yao. Wao walikaza mambo yanje, Yesu alikaza mambo ya ndani. Yesu alifundisha kwa mamlaka ya nafsiyake, wao walifundisha kwa kutegemea mafundisho ya marabi mashuhuri.Yesu alifunua viini vya Torati, wao walifundisha maneno yake tu bila kuchimbachini yake na kupata maana na lengo lake. Yesu alifanya huduma yake katikahali ya kuchunguzwa sana na hao watu, wakitaka kuupima uhalisi wa madaiyake.

k.18-19 Watu kadha (Marko ametaja wanne) walitokea hali wanambebakitandani mwenye kupoozwa wakitaka kumfikisha kwa Yesu ili aponywe.Walikuwa na imani na bidii. Waliposhindwa kumpitisha kati ya watu,hawakukata tamaa, bali walipanda ngazi na kutoa matofali ya dari nakumshusha mbele za Yesu. Yesu hakusikia shida alipoingiliwa wakati wakufundisha, wala hakujali kishindo chao na mavumbi ambayo huendayalimwangukia. Watu hawakuwazuia wala hatusikii kwamba mwenye nyumbaaliwanung’unikia kwa kuharibiwa dari ya nyumba yake. Labda ilikuwa nyumbaya rafiki.

k.20 Halafu Yesu, alipoiona imani yao, wale waliombeba na pengine imani yamgonjwa pia, alimgeukia mgonjwa na kwa maneno ya kumtia moyo nakumtumainisha alimwamkia ‘Ee rafiki’ ndipo akaendelea na kusema‘umesamehewa dhambi zako’. Kumbe! amekuja kwa ajili ya kuponywa kimwilina Yesu ametangulia kusema habari ya kutibu roho yake na dhambi! Kwa nini?Wayahudi wengi waliamini kwamba upo uhusiano mkubwa kati ya dhambi naugonjwa. Tunajua Yesu hakuunga mkono mtindo huo wa kuwaza kwao(Yn.9:2). Yawezekana huyo mtu amefanya dhambi fulani iliyosababishaugonjwa wake wa kupooza; au pengine alishikwa na mawazo ya Kiyahudi nakuyaweka mambo hayo mawili pamoja. Wengi waliokuwapo wangaliaminikwamba amefanya dhambi kwa sababu ya hali yake mbaya. Inaonekana Yesualifanya kwa kusudi la kuwachokoza Mafarisayo na Waalimu wa Torati akiwapachangamoto kali ili wamzingatie Yeye Mwenyewe kuwa nani hasa. Kwa jinsiambavyo Luka ameiandika habari hiyo inaonekana kwamba alitaka kusisitiza

Page 49: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 339

changamoto hiyo kuliko uponyaji wa huyo mtu na kuliko hoja juu ya uhusianokati ya dhambi na ugonjwa. Huyo mtu alionja nafsini mwake msamaha wadhambi zake kabla hajapona kimwili.

k.21 Mafarisayo na wenzao walichukizwa sana na maneno ya Yesu, masikionimwao yalikuwa kashfa. Yesu hakutangulia kusema ‘Mungu akusamehe’ balialimsamehe kwa mamlaka ya nafsi yake. Wote waliamini kwamba ni kazi yaMungu tu, peke yake, kusamehe dhambi, tena si kwa wakati huo, bali katikasiku ya mwisho ya hukumu. Kumbe Yesu alisema ‘umesamehewa’ siutasamehewa. Hivyo Yesu alileta msamaha wa dhambi katikati ya maisha yaulimwengu wa sasa. Walihojiana wao kwa wao na Yesu aliyatambua mawazoyao (4.23). Haikuwa vigumu ayatambue kwa vile alivyoelewa msimamo wao nakujua mtindo wa mawazo ya Kiyahudi. Tatizo lao ni Yesu Mwenyewe, ‘Ni nanihuyo?’.

k.22-23 Yesu aliwakabili na kuyajibu mawazo yao. Yesu hakuogopa watu, walahakusita kuweka wazi msimamo wake wala hakuacha kudai mamlaka kubwa.Hivyo, aliwapa changamoto ya kupima kati ya mambo mawili makubwa. Uwezowa kumponya kimwili, na uwezo wa kumponya kiroho. ‘Lililo jepesi ni lipi?’ amakumponya ama kumsamehe? Kwa kusudi, Yesu aliyaweka hayo mawili pamoja,moja likiwezekana, la pili lawezekana. Ikiwa moja ambalo linaonekanalimefanyika, na lingine ambalo halionekani, limefanyika pia. Lilikuwa jaribiokubwa kumponya yule mtu machoni mwa wote waliokuwemo, kwa kuwa ukweliwake utadhihirika wazi ila ukweli wa kumsamehe hautaonekana wazi, ilakumsamehe kwamfaa zaidi.Mtu aliye mponyaji wa kimwili tu hawezi kusamehe dhambi. Yesu alikuja kwashabaha ya kuwaokoa wenye dhambi na ndiyo sababu alikaza jambo hilo nabaadaye kidogo atawaambia kwamba ndiyo shabaha ya kuja kwake (5.31-32).Msingi wa kusamehe dhambi ni katika Kifo chake kitakachotokea mbeleni, naalikuwa na uthabiti wa kujua hakika kwamba Baba atamlinda katika mamboyote ili mwisho wa mwenendo wake ayatimize mapenzi ya Baba katika kutoanafsi yake kuwa fidia ya dhambi.

k.24 Ndipo Yesu alitilia mkazo neno hilo kwa kusema ‘ili mpate kujua yakwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi...’ amriyake si kwa huyo mtu mmoja tu, bali anayo amri katika dunia nzima kusemehedhambi. Pengine alidokezea kwamba anayo amri ya kufanya mambo mengi sihilo tu la kusamehe dhambi. Mwana wa Adamu ni jina ambalo Yesu alipendakulitumia, nalo limetumika sana katika Injili hiyo. Maneno yenyewe yatokaDanieli 7:13-14. Yamhusu Masihi ila si jina la kuamsha mawazo ya siasa kamajina la ‘Mwana wa Daudi’.

k.24b-25 Uhakikisho wa uwezo wa Yesu kumponya mwenye kupoozaulionekana mbele ya wale watu waliokuwepo. Yesu alimwamuru mgonjwaajitwike kitanda chake na kuondoka na kurudi nyumbani. Mara moja alifanya

Page 50: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

hivyo, huku akimtukuza Mungu. Hivyo, wote waliokuwepo walifahamu kwambaYesu alikuwa na uwezo wa mambo mawili, wa kumsamehe, kamaalivyotangulia kufanya, na wa kumponya, kama alivyofanya baada ya kuhojianana wapinzani wake. Kwa wale waliowaza kwamba ugonjwa husababishwa nadhambi walipata kujua kwamba ugonjwa unaosababishwa na dhambi unawezakuponywa na dhambi inayosababisha ugonjwa unaweza kusamehewa.

k.26 Watu wote walifahamu kwamba maneno ya Yesu hayakuwa maneno yahewani tu, bali yalikuwa na uwezo wa Mungu ndani yake. Watu walishikwa naushangao na kujaa hofu kwa sababu walikuwa wameuona uwezo wa Munguukifanya kazi kwa njia ya Yesu Kristo. Bila shaka madai ya Yesu ya kusamehedhambi yalikaa mawazoni mwao. Yesu alikuja duniani kwa shabaha ya kufanyaupatanisho wa dhambi ili awapatie wanadamu wote msamaha na uzima wamilele.

5:27-32 Mwito wa Lawi (Mt.9:9-13; Mk.2:13-17)Katika kumwita Lawi mtoza ushuru Yesu alitaka kuonyesha kwamba alitakakuwaita watu tofauti tofauti kuwa wanafunzi wake. Pia amefanya neno safi, kwakuwa amefanana na daktari ambaye husogea karibu na wagonjwa ili apatekuwashughulikia akiwagusa penye maumivu yao na kuwatibu na kuwapatiadawa za uponyaji.

Watu waliwachukia watoza ushuru kwa ajili ya kazi yao. Walikusanya kodi naushuru kutoka Wayahudi wenzao, kwa ajili ya Warumi, waliotawala nchi yao.Mara nyingi, walitajirika kwa sababu walitoza watu zaidi ya kima kilichotakiwana kuweka ziada hiyo mfukoni mwao. Walihesabiwa wanajisi na akinaMafarisayo kwa sababu ya kuwasaidia watawala wa kigeni walio WaMataifa.

k.27-28 Siku moja Lawi alikuwa ameketi forodhani akifanya kazi ya kutozaushuru kwa bidhaa iliyopitishwa pale. Alikaa Kapernaumu, mahali ambapoYesu ameweka kikao chake, kwa hiyo yawezekana alikuwa amemwona nakumsikia, hata pengine alikuwa amemwona akiwaponya watu .Ndipo siku moja Yesu alifikia pale forodhani na kumwita kwa maneno ambayoalitumia wakati wa kuwaita wanafunzi wengine ‘Nifuate’. Kama walivyofanyaPetro na wenzake (5.11) Lawi naye aliitika mara na kuacha vyote, akaondokaforodhani na kuambatana na Yesu. Hakusita, alijitoa kabisa, tena kwa furahakubwa. Haikuwa rahisi, kwa sababu, alipoondoka forodhani asingaliwezakurudia hiyo kazi tena tofauti na wavuvi ambao wangaliweza kurudi kwenyeuvuvi. (Lawi amefikiriwa kuwa ‘Mathayo’ (Mt.9:9) na baadaye Yesu alimwekakatika kundi maalum la Mitume. Jina la Mathayo laonekana katika orodha zaMitume katika Injili za Mathayo, Marko, Luka na katika Kitabu cha Matendo.

k.29 Kwa furaha kubwa Lawi aliandaa karamu kubwa nyumbani mwake.Aliwaita watoza ushuru wenzake, na wengine, Yesu akiwa mgeni wa heshima.Pengine Luka ametumia neno ‘wengine’ kwa sababu ya kuwepo kwa wanafunzi

Page 51: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 341

wa Yesu. Ila ni wazi kwamba walikuwepo pia ‘wenye dhambi’ wale ambaohawakushika sawasawa sheria na hasa mapokeo ya wazee, pamoja na walewenye maisha mabaya. Alitaka wote wafahamu kwamba ameamua kumfuataYesu, pia alitaka wakutane na rafiki yake mpya. Alijaa furaha nyingi sana, walahakuwaza kwamba amepata hasara ya mapato.

k.30 Mafarisayo na waandishi wao walikuwa karibu. Wasingaliweza kufikandani na kushiriki katika karamu kwa kuwa walidhani kwamba wakijihusisha nawatu wa namna hii wangenajisika. Walisema na wanafunzi na kuwanung’unikiakwa sababu ya kula na akina watoza ushuru na wenye dhambi. Walishindwakukubali kwamba Yesu ni Rabi au Masihi kwa sababu hiyo ya kujihusisha nawatu hao na kuwakaribisha katika Ufalme wake. Machoni mwao amevukampaka. Katika dini yao walijitenga na watu wa namna hiyo ili wawe ‘safi’machoni mwa sheria na mapokeo yao. Dini ya Yesu ilikuwa dini ya kushirikianana wenye dhambi bila kushiriki dhambi yao.

k.31-32 Yesu alikuwa ameyasikia manung’uniko yao, akawajibu kwa kutumiamfano wa daktari na wagonjwa. Wanaohitaji daktari ni wale wanaojisikiakwamba wana shida kimwili. Katika kuwatibu daktari husogea karibu nao nakuwagusa penye maumivu yao, ili awatibu na kuwapatia dawa za uponyaji.Daktari hamlaumu mgonjwa, eti, ni mgonjwa; la! Ila awalaumu wagonjwawasiotafuta matibabu. Tena shabaha ya daktari ni kuwaponya wagonjwa, ndiyosababu yu tayari kusogea karibu nao na kuwagusa ili afahamu shida zao. Walewalio katika hatari kubwa ni wale wagonjwa wasiotambua kwamba niwagonjwa. Ndipo Yesu alijidai kuwa daktari, mganga wa kutibu wagonjwa wakiroho, wale walioshindwa maisha. Aliwaita waje Kwake kwa toba na imani,kusudi awaponye. Tena aliwatafuta, hakungoja mpaka wamekuja Kwake,‘aliwaita’. Haina maana kwamba wako wenye haki wasiohitaji daktari aumatibabu, la, hakuna mwenye haki hata mmoja, kama isemavyo Warumi 3:10.Ila wako wanaojidai kuwa na haki, haki ambayo haitoshi machoni mwa Mungu(Mt.5:20; Flp.3:5-6).

Katika habari hiyo Yesu alifunua msingi wa huduma yake, amekujaulimwenguni ili awatafute na kuwaokoa wenye dhambi. Iko tofauti kubwa katiyake na Mafarisayo hasa katika jinsi walivyojihusisha na wenye dhambi. Yeyealiwatazama kwa huruma akitaka sana kuwasaidia. Mafarisayo waliwatazamakwa kuwahukumu. Waliogopa kujihusisha nao kwa ukaribu, wasijewakanajisika, na kwa sababu hiyo, walijitenga nao. Zaidi ya yote Yesu alijuakwamba anayo ‘dawa’ ya kutibu shida zao za rohoni, Yeye atakufa ili awapatiemsamaba wa dhambi zao na uzima wa milele. Kwa hiyo, jinsi Yesu naMafarisayo walivyohudumia watu ilitofautiana kabisa. Mafarisayo walikazamambo ya nje, ushikilaji wa visheria vidogo vidogo bila huruma na bila kujalihali za watu. Yesu alijaa huruma akiwapenda. Alisisitiza hali ya moyo, nakutazama nia na sababu za ndani. Manung’uniko ya Mafarisayo na swali laokwa wanafunzi yalimpa Yesu nafasi ya kutoboa wazi shabaha yake ya kuja

Page 52: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

ulimwenguni. Wala isifikiriwe kwamba Yesu hakuhesabu dhambi kwa uzito;hakubembeleza dhambi, aliwaita watu watubu dhambi zao, sawa na daktariambaye huwaza ugonjwa kwa uzito, akitaka watu watafute matibabu.

5:33-35 Habari ya kufunga (Mt.9:14-17; Mk.2:18-22)Luka hakutaja ni akina nani waliouliza juu ya kufunga. Mathayo amesema niwanafunzi wa Mbatizaji. Luka ameweka mazungumzo hayo kama ni maendeleoya mazungumzo yaliyotokea wakati wa karamu ya Lawi. Yohana Mbatizajialifanya huduma ya kuwaita watu kutubu na kubatizwa ndipo aliwafundishakufunga. Wanafunzi wa Mafarisayo pia walifundishwa kufunga ila sivyoilivyokuwa kwa wanafunzi wa Yesu. Yesu na wanafunzi walionekana kuwa watuwa furaha wakila na kunywa bila kufunga na hali hiyo ilifikiriwa kuwa si haliiliyofaa kwa watu waliotilia maana dini yao. Bila shaka walitatizwa kwa sababuYesu kama Yohana aliwaita watu watubu. Wayahudi waliwekewa siku moja,Siku ya Upatanisho, kuwa siku ya kufunga (Law.18:12). Wakati wa YesuMafarisayo walifunga siku mbili kwa juma (Lk.18:12). Yesu alifunga wakatimaalumu alipojaribiwa jangwani kabla ya kuanza huduma yake. Yawezekanaalifunga kwa siri nyakati zingine. Aliposema juu ya kufunga (Mt.6:16-18)hakukataa jambo lenyewe ila alihukumu hali ya watu waliofunga kwakujionyesha mbele za watu.

k.33 Walipouliza swali walitaja kufunga mara nyingi na kuomba dua. Huendawalifunga pamoja na kuomba. Twajua Yesu na wanafunzi wake waliomba sanana hapo Yesu hakusema juu ya kuomba. Pengine wanafunzi wake hawakuwana mazoea ya kuhudhuria saa maalum zilizowekwa kwa sala.

k.34 Yesu alijibu kwa kuwaambia kwamba wakati mpya umefika, wakati waarusi na Bwana Arusi yupo, kwa hiyo, si wakati wa kufunga bali ni wakati wakufurahi jinsi ilivyo wakati wa arusi. Pengine watu walitatizwa kwa sababuwaliitwa kutubu, huku walifurahi badala ya kuhuzunika. Katika Yesu, Ufalme waMungu uliletwa karibu na watu, na watu walipewa nafasi ya kuuingia, hivyohaikuwezekana watu wahuzunike. Hata Wayahudi walifananisha Kuja kwaMasihi kuwa kama Arusi na wakati wa sherehe kubwa kufanyika (Isa.25:6-9;35:1ku). Hapo nyuma, Yesu alijifananisha na daktari aletaye matibabu nauponyaji; hapo amejifananisha na Bwana Arusi aletaye badiliko kubwamaishani mwa watu (Mt.15:1ku. Yn.3:29). Neno ‘Bwana Arusi’ laashiria upendowake mkubwa kwa bibi arusi wake, yaani waumini, na umoja uliopo kati yao.

k.35 Hata hivyo, Yesu alidokezea kuondolewa kwake, kama ataondolewa kwanguvu kwa njia isiyo ya kawaida, ndipo kwa sababu ya huzuni wanafunzi wakewatafunga. Ni muda ule tangu Yesu alipokamatwa hadi siku alipofufuka(Yn.16:16ku). Baadaye Kanisa lilizoea kufunga wakati wa kuamua mambomakubwa (Mdo.9:9; 13:2-3; 14:23).

Page 53: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 343

k.36-39 Yesu alifuata mafundisho ya kufunga kwa kutoa mithali iliyoelezamabadiliko makubwa yanayosababishwa na Kuja Kwake na tofauti kubwa katiya dini ya Kiyahudi, na imani mpya ya Kikristo. Alionyesha jinsi isivyowezekanamambo hayo mapya yaingizwe katika mipango ya Kiyahudi. Mtu akijaribukufanya hivyo itakuwa sawa na kutia kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu.Mtu akikata kiraka katika nguo mpya huharibu ile nguo mpya. Tena akikitiakiraka cha nguo mpya kwenye vazi kuukuu lile vazi litaharibika zaidi, kwasababu nguo mpya bado haijarudi wala hailingani na ile nyingine. Alitilia mkazojambo hilo kwa kusema mfano mwingine wa divai mpya na viriba vikuukuuambavyo havina hali ya kunyumbulika na kupokea divai mpya. Divai mpyahuhitaji viriba vipya. Kwa mafundisho hayo Yesu alitoboa wazi kwamba hakujaili aitengeneze dini ya Kiyahudi bali alete imani mpya, hata hivyo, upo uhusianomkubwa kati ya mambo ya kale na mambo mapya. Ya kale yalikuwamatayarisho kwa hayo mapya. Badala ya mtu kuhesabiwa haki kwa sheria, mtuatahesabiwa haki kwa imani katika Kristo na kuongozwa na Roho Mtakatifu, sikwa andiko baridi la sheria (2 Kor.3:6). Katika habari hiyo nenolinalozungumzwa lahusu huo ‘upya’ utakaofanywa. Yesu ameonyesha kwambahuo upya unao uadilifu ulio na haki ya kusimama peke yake, bila kufanywakuwa kiraka tu wala usiwekwe katika viriba vikuu vitakavyouzuia huo upyausipumue vizuri.

k.39 Yesu alijua kwamba ni vigumu sana mtu alipokee neno hilo kwa upesi,kwa kawaida mtu huridhika na mazoea yake wala hawi tayari kujaribu jambojipya. Huenda alikuwa akidokezea tena kukataliwa na kuondolewa kwake. Swalilipo ‘wafanya nini na huo upya wakati ambao ya kale yangalipo? Katika sehemuifuatayo twaona mgongana juu ya Sabato.

6:1-5 Habari ya kuitunza sabatoMwisho wa sura ya tano tuliona jinsi Yesu alitoboa wazi tofauti kubwa kati yakena Mafarisayo na Waandishi. Alidokezea kwamba haitawezekanakuyapatanisha mafundisho yake na mafundisho yao. Neno hilo lilidhihirikakatika hali ya kuwaza na kufanya siku ya Sabato. Yesu alisema kwambaviongozi wamepotosha lengo la Torati kwa njia ya mapokeo yao. Kwa mapokeoyao walitaka watu waelewe namna ya kufanya siku ya Sabato.Yesu alionakwamba kwa njia ya mapokeo yao wamepotosha shabaha ya Sabato mpakaSabato imegeuzwa siku ya kuwalemea watu badala ya kuwa siku ya baraka.Ili awasaidie kuelewa matumizi halali ya Sabato Yesu, kwa kusudi, alitumiaSabato kwa kufanya kazi za rehema za uponyaji n.k. Alifahamu kabisa kwambakwa kufanya hivyo viongozi watachokozwa, lakini afadhali wachokozwe iliwalazamishwe wajihoji na kujirekebisha.

Katika mapokeo yao ya ufafanuzi wa Sabato Mafarisayo na Waandishiwaliandika aina 39 za kazi zilizokatazwa katika Sabato, tena aina hizo 39zilikuwa na matawi. Katika aina hizo moja haikumruhusu mtu kuvuna nakupukuchua masuke, kwa sababu kufanya hivi kulihesabiwa sawa na kuandaa

Page 54: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

chakula! Katika Agano la Kale (Kum.23:25) mtu aliyesikia njaa aliruhusiwakuyavunja masuke.

k.1 Yesu na wanafunzi walikuwa wakipita shambani na wanafunzi walivunjamasuke. Ndipo Mafarisayo waliwashambulia.

k.2 Yesu aliposikia kwamba Mafarisayo wamewashambulia wanafunzi wakealichukua jukumu la kuwatetea. Mbele yake walikuwa wamesikia uhuru wakuyavunja masuke.

k.3-4 Katika kuyajibu mashtaka yao Yesu aliwaambia Mafarisayo na waandishikwamba hawakujua Maandiko sawasawa ‘hamkulisoma....’ Aliwakumbushahabari za Daudi na jinsi alivyofanya wakati aliposikia njaa yeye na watuwaliokuwa pamoja naye. Aliichukua mikate ya Wonyesho na kuila na kuwapawenzake wale pia (1 Sam.21:1-6). Hakuna aliyemshtaki kwamba amevunjasheria iwapo wameula mkate wa kipekee ambao ni makuhani tu walioruhusiwakuula. Alifanya hivyo kwa sababu ya njaa, ilikuwa njia yake ya kuwahurumia nakuwapatia chakula. Tendo lake halikuhesabiwa kosa. Kwa kusema hivyo, Yesualisisitiza kwamba katika Agano la Kale haikuwa lazima sheria ishikwe jinsiilivyoandikwa bila kujali mahitaji ya watu. Katika kushikilia sheria zao bilahuruma walikuwa wamekosa kuelewa shabaha ya Torati. Hasa Sabato ilikuwasiku ya kufanya kazi za rehema, si kwamba ziruhusiwe tu, bali zilipaswakufanywa siku hiyo (Yn.7:23).

k.5 Kama Daudi alivyoidhinisha mkate wa Onyesho utumiwe vivyo hivyo naYesu aliye Mwana wa Adamu (Masihi) aliye Mwana na Bwana wa Daudi awezakuwaruhusu wanafunzi wake wayavunje masuke na kuyala. Yeye anayomamlaka ya kuamua iliyo halali na isiyo halali katika kushika Sabato. Neno lakuwaongoza ni huruma kwa watu. Kwa kudai kuwa Bwana wa Sabato alijiwekasawa na Mungu aliyeamuru iwepo Sabato wakati wa Uumbaji na kukazakuwepo kwake alipoiweka kuwa amri katika zile Amri Kumi. Mafarisayo nawazee walipoziweka sheria zingine za mapokeo yao juu ya Amri Kumi walikuwawamejifanya kuwa mabwana wa waamuzi wa Torati.

6:6-11 Yesu alimponya mtu mwenye mkono uliopooza siku ya SabatoLuka aliendelea kwa kutoa habari ya jambo jingine lililotokea siku ya Sabato.Yesu alikuwa akifundisha sinagogini, dalili ya kuwa alikubalika kuwa rabii.k.6-7 Kwa jinsi Luka alivyoiandika habari hiyo, huenda huyo mtu mwenyemkono uliopoozwa aliwekwa kwa kusudi mahali ambapo Yesu atamwona.Waandishi na Mafarisayo walitaka kuhakikisha kama ni desturi ya Yesukuponya siku ya Sabato ili wapate neno la kumshtaki baadaye, kwa kuwawalidhani kwamba ndio mwelekeo wake. Hivyo walingoja ili waone ni nini Yesuatakavyofanya. Hawakuwa na mzigo juu ya huyo mgonjwa bali juu ya sheria namapokeo yao na hasa walikuwa wakimwinda Yesu.

Page 55: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 345

k.8 Mara kwa mara Luka ametaja uwezo wa Yesu kujua mawazo ya watu.Isingalikuwa vigumu ayatambue mawazo ya hao Mafarisayo na wenzao kwakuwa alijua msimamo wao juu ya sheria, na nia yao ya kumwangusha. Hatahivyo Yesu hakuwaogopa wala hakuwa tayari kuridhiana nao. Haidhuruwanamwazaje Yeye atamponya yule mtu wazi mbele za wote. Ndipo alimwitaaje mbele na kusimama katikati, ili kila mtu aone linalotendeka.

k.9 Halafu Yesu aliwakabili wapinzani wake ambao wamejiweka kuwamabwana wa waamuzi wa sabato akawauliza moja kwa moja ‘Je! ni halali sikuya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya.. kuponya roho au kuangamiza?’Hakuna njia ya kati, ama ni kutenda mema, ama ni kutenda mabaya;kutokuponya ni sawa na kuangamiza. Waandishi na Mafarisayo walifundishakwamba mgonjwa aweza kushughulikiwa akiwa katika hatari ya kufa auikidhaniwa kwamba aweza kufa. La, siyo, budi angojee siku nyingine. Ni wazikwamba mwenye mkono wa kupooza asingalikufa siku ile. Yesu aliwazakwamba mtu ye yote aliyeugua au aliyekuwa na msiba kama huyo mtu, alihitajiasaidiwe bila kukawia. (Kwa sababu mkono uliopoozwa ulikuwa wa kiume,mkono ulliofikiriwa kuwa wa nguvu kuliko wa kushoto huenda alishindwakujipatia mahitaji yake mengi). Waandishi na Mafarisayo walitilia mkazo mamboambayo yasingefanyika siku ya Sabato, kwa hiyo, mapokeo yao yalijaa miikomingi. Kinyume chao Yesu alitilia mkazo mambo ambayo yangefanyika, hasaya kurehemu watu.

k.10 Kisha Yesu alitazama pande zote (Marko amesema kwa hasiraakishangaa ugumu wa mioyo yao) akiwapa nafasi ya kumjibu, lakiniwakanyamaza. Kisha Yesu akamwagiza yule mgonjwa kufanya lile ambaloameshindwa kufanya, yaani kuunyosha mkono wake. Alilitii neno la Yesu naalipojaribu kuunyosha akaona aliweza kuunyosha, na mkono wake ukawamzima. Yesu aliunganisha amri ya kumpenda Mungu na kumpenda jiranipamoja kuwa jumlisho la Amri zote. Kwake kutokumpenda jirani kwa kukosakumhurumia ni sawa na kutokumpenda Mungu, ni kosa kumwacha jirani katikashida yake. Yesu alikataa mawazo yaliyokaza mambo ya kutokufanya, nikutenda mema na kutokutenda mema ni sawa na kutenda mabaya. Yesu alionakwamba kuhifadhi maisha kunazidi matakwa ya Sabato. Pamoja na hayo,Waandishi na Mafarisayo walikuwa na mawazo ya kumwua Yesu, ambayo Amriya Mungu ilikataza kabisa (Mk.3:5-6).

k.11 Luka hakutaja njama ya wakuu kumwua ila alisema kwamba walijaauchungu na kushauriana wao kwa wao kuhusu watakavyomtenda.Hivyo twaona ufa unazidi kati ya Yesu na Mafarisayo na wenzao. Haohawakubali divai mpya, wataendelea na viriba vikuukuu na vazi kuukuu.Mawazo yao yalikuwa yameganda kabisa, hata walishindwa kutafakari mambokwa upya.(Habari nyingine za kuponya siku ya Sabato zapatikana katika 13:10ku na14:1ku).

Page 56: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

MASWALI1. Kwa nini Yesu aligongana na Mafarisayo na Waandishi? Walikuwa

wameandika nini kwa shabaha ya kuitunza Sabato?2. Yesu aliona shabaha ya Sabato ilikuwa nini hasa? Alipokuwa

akiwaponya watu siku ya Sabato alitaka kufanya nini? Machoni mwaMafarisayo alikuwa akifanya nini kuhusu Amri ya Mungu? Na Mapokeoyao? Fafanua.

3. Yesu aliposema juu ya kiraka kutiwa katika nguo mpya na divai mpyakuwekwa katika viriba kuukuu alikuwa na maana gani hasa?

6:12-16 Yesu aliwachagua Mitume 12 (Mt.10.1-4; Mk.3.11-13-19)Wakati huo Yesu alichukua hatua maalum katika huduma yake. Alielewakwamba wapinzani wake wamezidi kumchukia hata wameanza kuwazakumwondoa na Yeye bado hajamaliza kupitia katika miji na vijiji vya Galilaya nakuhubiri na kuwafundisha watu juu ya Ufalme wake. Hivyo aliona vema auwekemsingi maalum ili utakapofika wakati wa kuondolewa kwake wengine wawetayari kukabidhiwa kazi na kuendeleza utume wake. Kama Yeye alivyotumwana Baba, ndivyo Yeye atakavyowatuma hao. Ameisha kuwaita baadhi yaowafuatane naye (5.1ku).

k.12 Hali akijua ni hatua kubwa ya maana sana alipanda mlimani na kuomba iliapate uongozi wa Baba juu ya wale atakaowachagua kuwa Mitume. Watatokakatika kundi la wanafunzi wake ambao wameandamana naye kwa muda. Alikaamuda mrefu, usiku kucha, katika kuomba. Luka amependa kusisitiza desturi yaYesu kuomba wakati wa hatua kubwa katika maisha na huduma yake (3:21;5:16; 9:18, 28, 29; 11:l; 22:41).

k.13 Kulipokucha alikuwa tayari kuwaita kwa majina baadhi ya wanafunzi;aliwachagua watu kumi na wawili na kuwaita Mitume, watu wa kutumwa naujumbe maalum. Simoni Petro amewekwa kuwa wa kwanza katika orodha zotezilizopo (Mathayo, Marko, Matendo ya Mitume) na Yuda Iskariote mara zoteamekuwa wa mwisho na kutajwa kuwa msaliti. Hakuchaguliwa ili awe msaliti,alichaguliwa awe Mtume sawa na wale wengine, ila baadaye, iwapo aliendeleakatika kundi la Mitume, alianza kuteleza na kukosa uaminifu, mwishowe kwahiari yake mwenyewe aliamua kumsaliti Yesu. Iwapo twaweza kuhisi sababuzake hatujui kwa hakika zilikuwa nini hasa. Jina lake lina maana ‘mtu mwongo,au mtu asiye mkweli; na pengine jina limetoka kwa mahali ambapo penginealitoka ‘Kerioth’ kusini ya nchi. Simoni alipewa jina la Petro na Yesu, maanayake ‘jiwe’. Mbeleni ataimarika ndipo atafaa kuwa kiongozi kati yao (si juu yao).Jina lake kwa Kiaramaiki ni Kepha. Andrea alimleta Simoni Petro ndugu yakekwa Yesu (Yn.1:41). Yohana na Yakobo walikuwa ndugu, baba yao aliitwaZebedayo. Katika Marko 3:17 wameitwa ‘wana wa ngurumo’ pengine kwakulingana na tabia yao iliyoonekana wakati walipotaka Mungu alete moto juu yaWaSamaria ambao hawakuwa tayari kumkaribisha Yesu alipokuwa akipitia katiyao. Petro na Yohana na Yakobo walionekana kuwa karibu na Yesu kuliko wale

Page 57: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 347

wengine; walikuwa mlimani wakati Yesu alipogeuka sura; Yesu aliwachukuapamoja naye alipoingia chumbani ambamo binti wa Yairo alikuwa amelala,wakati Yesu alipomfufua, na usiku ule kabla ya Kufa Kwake alipoingia bustaniya Gethsemane hao watatu waliruhusiwa kwenda naye mle ndani zaidi.

Filipo ni jina la Kiyunani, ametajwa katika Injili ya Yohana (1:43-45; 6:5; 12:21-22; 14:9). Bartolomayo ametajwa katika orodha za Injili tatu ila katika Yohanajina lake halionekani na adhaniwa kuwa Nathanieli (Yn.1:45-46; 21:2). Mathayoadhaniwa kuwa Lawi, mtoza ushuru (Mk.2:14). Tomaso, maana ya jina lake ni‘pacha’ ametajwa katika Injili ya Yohana (11.16; 20.24; 21.2). Hatuna habari juuya Yakobo wa Alfayo. Simoni aitwaye Zelote ama alikuwa na maelekeo yasiasa akiwa mmojawapo wa kundi waliotaka kuipindua serikali ya Kirumi amaalikuwa amejitoa sana akiwa na bidii katika mambo ya kiroho. Yuda wa Yakobo,labda ni huyu aliyemwuliza Yesu swali katika Yohana 14:22. Pengine ni yuleaitwaye Thadayo katika Mt.10:3 na Mk.3:18. Marko ametaja makusudi mawiliya kuchaguliwa kwao; kwanza, wawe pamoja na Yesu ili wajifunze Kwake, nakuwa karibu naye kila wakati; na pili, Yesu apate kuwatuma kufanya mazoezi iliwafanye kama alivyofanya Yeye Mwenyewe, kuhubiri, kuponya watu, na kutoapepo, hasa kuhubiri (Mk.3.14). Aliwapa mamlaka yake na kuwashirikisha uwezowake.

Tunapozingatia jambo hilo la kuwekwa kwa Mitume twatambua hekima kubwaya Yesu katika kuandaa kwa mambo ya baadaye. Hao Mitume watakuwakiungo muhimu cha kuunganisha wakati wake na wakati wa kutokea kwaKanisa na kuhakikisha kwamba ukweli wote wa Yesu unaletwa katika maishaya Kanisa. Hao ni kama dhamana ya mambo yote ya Yesu katika mabadilikoyatakayotokea wakati wa Kuondolewa Kwake.

Hotuba ya Tambarare 6:17-49(ling. na Hotuba ya Mlimani Mt.5–7)

6:17-19 Watu wengi walikusanyika mahali tambarareAlipomaliza kuwaita na kuwaweka Mitume Yesu alishuka mlimani pamoja naompaka mahali tambarare pale mlimani ambapo watu wengi walikuwawamekusanyika. Neno ‘bondeni’ ni tofauti na lile lililotumika hapo. Katika umatihuo wa watu walikuwapo Mitume, na wanafunzi wake wengine wengi, walewalioandamana naye kila wakati, pamoja na makutano makubwa ya watu.Baadhi yao walitoka mbali, sehemu za Tiro na Sidoni, na wengine walitokakaribu. Huenda hao waliotoka Tiro na Sidoni walikuwa Wayahudi walioishi katiya WaMataifa, na kwa sababu hiyo, walikuwa wepesi wa kuyapokea mawazomapya. Yesu alikuwa amepata wanafunzi na hapo ni mara ya kwanza waitwewanafunzi (5:1 - 6:16). Sasa anawaambia hao wanafunzi waliopatikana hali namambo wanayodaiwa hali wakiwa wanafunzi wake.

Page 58: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.17b-19 Kwa nini hao wote walimjia? Walikuja wakitafuta mambo mawili, lakwanza; kuyasikia mafundisho yake, kwa sababu Yesu alifundisha kwamamlaka ya nafsi yake tofauti na waandishi waliotegemea mawazo yawataalamu wa dini ya Kiyahudi. La pili: kuwaleta wagonjwa wao ili waponywemaradhi yao na wenye pepo wabaya watolewe mapepo yao. Ni dhahiri kwambauwezo wa Yesu ulikuwa uwezo halisi na watu walitaka kumgusa ili wakutane nahuo uwezo (5.13; 7.14; 8.44; 18.15; 22.51). Wengi wao walivutwa na Yesu ilabado hawajakabidhi kwake na kumpa utiifu wao.

Je! hotuba tuliyo nayo hapo, ambayo ilitolewa penye tambarare ni ile yaMathayo ambayo tumezoea kuiita Hotuba ya Mlimani. Huenda tambarare hiyoilipatikana kati ya miinuko ya milima. Hotuba ya Luka ni fupi kuliko ile yaMathayo, mengine yafanana, na mengine yatofautiana. Bila shaka Yesualirudiarudia kusema mambo kadha na Luka ameyaweka mengine mahalimbalimbali katika Injili yake. Mathayo, kwa sababu alipenda kupanga mambopamoja amekusanya pamoja mafundisho ya Yesu katika mafungu makubwa.Zamani Mungu alitoa Torati kwa watu wake, wakati wa Musa. Hapo Yesu,kama Musa wa pili anatoa, si Torati nyingine, bali Mwongozo wa maadili kwawatu wake. Mwongozo huo ni kwa wale ambao wameisha kuwa wanafunziwake, hao wamo katika Ufalme wake kwa sababu wamejihusisha naye, aliyeMfalme wa huo Ufalme wa Mungu. Amekuja kuusimamisha utawala wakemioyoni mwa watu. Kwa hiyo, katika hotuba hiyo ametaja tabia na mwenendovilivyo muhimu kwa wafuasi wake. Taz.k.20 ‘akainua macho yakeakawatazama wanafunzi wake, akasema, Heri ninyi...’ Ijapokuwa wenginewalikuwepo lengo la kwanza la Yesu lilikuwa hao ambao wameishaamuakumfuata. Wengine watayasikia, kwa sababu katika makutano makubwa yawatu bila shaka wako wale waliovutwa kuitikia wito wake kuwa wanafunzi(Ling.Mt.5:1 na 7.28). Kwa hiyo, hapa hatuna masharti ya kuingia Ufalme wakebali ni maelezo ya maadili kwa wale waliomo katika huo Ufalme.

6:20-26 Baraka na OleMaana ya neno heri ni ‘pongezi’ ‘hongela’ na maana ya neno ole ni ‘sikitiko’ na‘wa kuhurumiwa’. Watu wa aina nne wametajwa kwa upande wa heri na wannekwa upande wa ole, na Luka alifanya ulinganifu kati yao.Wa aina nne wa kupongezwa ni maskini; walio na njaa sasa; waliao sasa; nawanaochukiwa na kushtumiwa na kutengwa kwa ajili ya jina lake. Kwa mawazoya kibinadamu watu wasingalikubaliana na Yesu katika kuwataja hao maskinina wenye njaa n.k. kuwa heri na watu wa kupongezwa. Wala watuwasingalikubaliana na Yesu katika kuwataja wenye mali na wanaoshiba n.k.kuwa watu wa kupewa ole. Hivyo Yesu aliyapindua mawazo ya kawaida yawatu jinsi wapimavyo mambo. Tukumbuke ya kuwa Yesu alisema maneno hayokwa wanafunzi wake. Wao wako katika hali ya heri kwa sababu wametambuaumuhimu wa kuwa wanafunzi wake, wamekaribishwa katika Ufalme wake nakushirikishwa baraka za Ufalme na kujua kwamba Mungu yu upande waoakifanya kazi katika ulimwengu huu. Wao wametambua kwamba mali na

Page 59: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 349

mafanikio ya kimwili huweza kuwa mtego ulio na hatari ya kuwaondoa katikauaminifu wao kwa Mungu. Uheri wao ni katika kumtegemea Mungu wala sikatika kutegemea mali zao na sifa za watu. Katika Agano la Kale walionakwamba Mungu alikuwa upande wa maskini na wajane na walioonewa nakuwashughulikia ili wapate haki zao. Injili ya Yesu huwa Habari Njema kwawatu wa namna hiyo maana hali yao huvuta usikivu wa Mungu. Yesu hakutakakusema kwamba umaskini na ukosefu wa mahitaji ya lazima, na huzuni kwa ajiliya shida ni hali za heri la, hata kidogo, hii si maana yake, kwa sababu hali hizosi nzuri, ila hali hizo ni afadhali kuliko kumwasi Mungu na kwa vyovyote hali zaozitageuzwa baadaye kuwa za furaha na baraka. Walio na mali, ambao hushibadaima na kucheka kwa kuwa wasikia raha hawatambui hatari waliyo nayo yakunaswa na kupofushwa macho hata kiasi cha kuyapenda mambo hayo kulikokumpenda Mungu na kuutamani Ufalme wake (18.23) na kuwa waaminifuKwake. Mara nyingi watu kama hao hawatambui kwamba haiwezekanikumtumikia Mungu na mali (16.13). Katika Injili hiyo Luka ametoa habari nyingijuu ya matajiri na wajibu wao wa kuwa wakarimu kwa Mungu na wanadamu(12.32-34; 16.9-12; 12.21).

Mara nyingi wafuasi wa kweli wa Yesu wachukiwa na kutengwa na wenzao nakushutumiwa kwa sababu wamempa Yesu utiifu wao. Yesu aliwaita wapokeemateso na dhiki kwa furaha kubwa, hataki wasikitike na kujiwaza vibaya; la,hata kidogo. Siyo kusema kwamba dhiki na mateso na kusemwa vibaya nimambo mazuri, la hata kidogo, ila ni heri kwa sababu asili yake ni katikakumfuata Yesu. Wapaswa wafurahi sana wakati wa kuteswa, hata kurukaruka,kwa sababu thawabu kubwa inawangojea huko mbinguni. Tena wamo katikaushirika mzuri sana wa watu waaminifu wa Mungu wa tangu awali, wamo katikasafu ya manabii wa kweli waliokataliwa na wenzao zamani. Kuteswa kwa ajili yaYesu ni heshima kubwa sana. Katika siku ya hukumu ya Mungu itadhihirikawazi kwamba walikuwa wanafunzi wa kweli wa Yesu wenye kibali cha Mungu.

Wale ambao waliepa shida kwa sababu walisita kumpa Yesu utiifu wao walahawakuwa waaminifu kwake watakosa kupata kibali cha Mungu. Ni hatari sanakusifiwa na watu wote, neno la maana ni wote. Si vibaya baadhi ya watukusema vema juu yetu ila ni hatari ikiwa wote watafanya hivyo. Itaonekanakwamba tumeridhiana nao katika mengine ambayo tulipaswa tusingeridhianenao.

6:27-36 Kupenda aduiKatika sehemu hiyo Yesu alisema kwa wale waliokuja kumsikia akiwafundishajinsi ya kumfuata. Alifikia kiini cha hotuba yake na kuchimba chini akisisitizaumuhimu wa upendo. Si upendo ya kimapenzi, wala si upendo kati ya rafiki aukati ya jinsia, wala si upendo wa hewani, wa mawazo tu, bali ni upendokiutendaji, utokao moyoni, tena ni upendo kwa wasiostahili. Kupenda aduililikuwa neno lililowashtua wasikilizaji wake. Yesu alikuwa na maana ganialiposema adui? Huenda alikuwa akiwawaza wale wanaowapinga Wakristo, na

Page 60: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

alionyesha kwamba Wakristo hudaiwa upendo wa hali ya juu, isiyo kawaida yawanadamu. Wema wao uwe na nguvu ya kupambana na uadui na chuki yawapinzani wao na licha ya kuwatendea vibaya wawafanyie mema.Wasiuangalie utendaji wao mbaya wala wasitawaliwe na nia ya kurudishianaubaya kwa ubaya, bali watende mema wakati wote, wasiweke mipaka katikaupendo wao kwa kuchagua wale wa kupendwa na wale wa kutokupendwa.Kuwapenda wale wanaowachukia ni jambo gumu sana. Tusisahau kwambawakati huo nchi ilitawaliwa na wageni, Warumi, waliokuwa wapagani.

k.28 Upendo waliodaiwa si upendo wa juujuu. Licha ya kuacha kuwatendeamabaya lazima wawafanyie mema. Wawabariki waliowalaani, na kuwaombeawale waliowaonea. Katika maneno yao waonyeshe upendo, wapunguze hali yauadui na chuki kwa kutokurudisha maneno mabaya bali wanene maneno memaya baraka. Katika kuwaombea adui zao kwa Mungu wanaonyesha nia yao yakumpendeza Mungu na kumtii Yesu na kutakia heri hao adui..

k.29-30 Vilevile kwa upande wa matendo wawe tayari kuyapokea mabayakama kupigwa shavu bila kurudisha pigo. Katika kurudishiana kila mtu hujitahidikuzidi mwenzake, hivyo mambo huzidi kuwa mabaya. Kwa kunyenyekea nakukubali kupigwa mtu hupunguza hali ya uadui. Mtu aweza kufanya nini zaidiikiwa mtu hukubali kuyapokea mabaya anayofanyiwa bila kulaumu na bilakukasirika? Kwa kufanya hivyo amekataa kuchokozwa. Wafuasi wake wawetayari kutoa na kutoa tena na tena, wawe na tabia ya utoaji kuliko kupata. Mtuanapoombwa msaada vema afikiri ni kwa njia gani aweza kuonyesha upendowa kweli na kumpa msaada utakaomjenga hasa. Wakati mwingine yafaa mtuapewe msaada wa vitu, wakati mwingine si msaada kumpa vitu, ni afadhaliatafutiwe msaada mwingine, kama kumpatia kazi, au mahali pa kukaa, aukumchukua kama rafiki n.k. . Kitu cha kumwongoza ni upendo halisi. Asiwekempaka katika utoaji wake.

k.31 Hapo Yesu alitoa kanuni nzuri sana. Hata zamani za kale watu walisemakwamba ni vema mtu asimtendee mwenzake lile asilotaka afanyiwe namwingine. Neno hilo lilikuwa na upungufu kwa kuwa lilihusu upande wakutokufanya. Yesu alisema kwa upande wa kufanya, hivyo alipanua jambo hiloliwe pana sana. Ni mengi ambayo twapenda tufanyiwe. Hivyo Yesu asemayapo mengi ambayo ni vema tuwafanyie wengine.

k.32-34 Wafuasi wake wapaswa wazidi wengine katika kutenda mema kwasababu hata watu wasiomwamini huwapenda na kuwasaidia wenzao. Wakotayari kuwakopesha n.k. ila wafuasi wa Yesu wadaiwa kuwazidi, wakiwa tayarikukopesha hata wale wasio jamaa wala rafiki zao. Wasikate tamaa juu ya mtu,wala katika kutenda mema; wasitazamie kurudishiwa kitu, wasifanye ulinganifuna kufanya kama walivyofanyiwa, la. Iwapo hawarudishiwi katika ulimwenguhuu, thawabu hufuata baadaye. Wanapofanya hivyo wafanana na Baba yao naBwana wao ambao huwafanyia mema walio waovu na wasioshukuru. Katika

Page 61: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 351

kuwapokea, Mungu alikuwa amewahurumia sana, vivyo hivyo na wao wapaswawawahurumie wengine kwa jinsi walivyohurumiwa na Baba yao wa mbinguni.Kwa njia hiyo watazidi kushirikiana na Baba katika ushirika unaoendelea nakuzidi hata mpaka uzima wa milele.

6:37-45 Kuwahukumu wengineHalafu Yesu aliendelea kupanua mafundisho yake juu ya kuwapenda watu kwakusema juu ya jinsi ipaswavyo wafuasi wake kuwawaza, kuwapima, nakuwathamini watu. Wasiwe wenye tabia ya kuhukumuhukumu nakuwalaumulaumu wengine. Yesu alikuwa akisemea hali ya wengi wanaoangaliamambo madogomadogo na makosa madogomadogo wakikosa hali ya ukarimukatika kusema juu ya wengine. Tunapofanya hivi tunaushusha uthamini waomachoni mwetu na machoni mwa watu wengine. Mungu atatumia kipimokilekile tunachotumia katika kuwapima wengine anapotupima sisi. Tena katikakuachilia kudai watu juu ya vitu twawaweka huru na mambo yaliyopita, wasilipemadeni n.k. Hata hivyo, Yesu alifundisha kwamba haitoshi kuwaachilia tu, balini vema kuwakirimu katika vitu tulivyo navyo. Ni hatua nyingine kabisa. KatikaYesu Mungu ametukirimia upendo na neema nyingi, hakuangalia upungufuwetu mwingi, na kwa sababu hiyo twapaswa kuwafanyia wengine kwa jinsiambavyo Mungu alivyotufanyia sisi. Kama Mungu angetupima na kutuhukumukwa haki kamili hakuna ambaye angestahimili. Katika kusema hivyo Yesuhakuwa na maana kwamba ni kosa kupima watu wakati wa kuchagua wafanyakazi, au wakati wa kuchagua watu kwa cheo fulani n.k. la, nyakati kama hizo nibusara kupima watu ili wafaao zile kazi au vyeo.

Katika kutaja vipofu Yesu alikuwa akiwaonya watu wasikubali kuongozwa nawaalimu waliotoa mawazo kwamba hakuna haja kutilia maanani mafundisho yaYesu juu ya kuwapenda adui na kuwa wakarimu katika kukaribisha watu. Haowaalimu walikuwa wepesi wa kuhukumu watu. Mwalimu si mtu wa kutoa ujuziau fundisho tu, kwa kuwa kwa kazi yake yeye hugusa maisha ya wanafunziwake. Iko tofauti kubwa kati ya boriti na kibanzi. Mtu hupaswa kuangalia sanamambo mazito yahusuyo maisha yake na kuyatilia maanani mafundisho yaYesu na kuyaweka maishani mwake, ndipo aweza kuwasaidia wengine katikamaisha yao kwa sababu mwenyewe anaona vema kwa kuwa ameangaliamaisha yake kwanza. Ajihukumu kwa ukali ndipo aweza kuhukumu kwahuruma maisha ya mwenzake. Asipofanya hivi mtu ni mnafiki akidai kuwamfuasi wa Yesu kumbe siye.

k.43-45 Halafu Yesu alitoa mwongozo wa kumsaidia mtu autambue ukweli waimani ya mwenzake. Ni kutazama maisha yake na kuyaona matunda yake. Kilamti hutambulikana kwa matunda yake, hii ndiyo kanuni katika miti na mimean.k. Kila mti huzaa kwa aina yake. Tena shabaha ya mti ni kuzaa matunda.Neno hilo twalifahamu na kanuni hiyo inahusu wanadamu na maisha yake.Mema hutoka katika moyo mwema wa mtu na mabaya hutoka katika moyomwovu wa mtu mwovu. Wema asemaye Yesu ni huo wema wa kuwapenda

Page 62: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

adui na kuwa wakarimu katika kuwawaza wengine. Ubaya una maana yakutokufaa na kutokuweza kutumiwa. Mara nyingi mtu hutambulikana kwamaneno yake yanayofunua yaliyomo ndani yake..

6:46-49 Misingi miwiliKisha Yesu aliwashtaki wale waliodai kuwa wafuasi wake huku wamekatashauri wasitimize matakwa yake ya kuishi kama alivyofundisha. Kwa kusema‘Bwana, Bwana’ Yesu alionyesha mamlaka yake ya kuwa mwalimu mwenyekutoa mafundisho halisi, yaliyo kanuni kabisa kwa wafuasi wake kwa sababundani yake mapenzi ya Mungu yalifunuliwa kwa maisha ya wanadamu. Katikak.47 alieleza hali ya mtu aliye mwanafunzi wa kweli. Kwanza amemjia Yesu, piaameyasikia na kuyajali mafundisho yake na kuyatia maishani mwake. Huyoamefanana na mjenzi wa nyumba ambaye aliuweka msingi wa nyumba kwauangalifu sana, akichagua kujenga juu ya mwamba na kwa kuchimba chinisana. Mfuasi wa Kristo apaswa afanane na mjenzi wa namna hiyo kwakuchukua kwa uzito mafundisho ya Yesu na kuyatenda. Matokeo ya nyumbailiyojengwa na mjenzi wa namna hii ni mazuri sana, hata gharika ikija na mtoukiishukia kwa nguvu, hata hivyo, nyumba husimama. Ndivyo itakavyokuwakwa Mkristo ajengaye maisha yake juu ya mafundisho ya Yesu, katika hukumuya Mungu atapita salama. Lakini sivyo ilivyo kwa mfuasi wa Yesu ambayeamefanana na mjenzi aliyejenga bila kuangalia anaiweka nyumba yake wapi,bila kuushughulikia msingi wake. Wakati wa gharika nyumba hiyo huchukuliwana maji. Ndivyo itakavyokuwa kwa Mkristo ambaye huyasikia mafundisho yaYesu bila kuyatia katika maisha yake, hakubali kuishi kwa kanuni ya zile heri(k.20-23) na kwa kuwapenda adui (k.27ku), wala hataki kuwahurumia watu baliapenda kuwahukumu na kuwalaamu kwa upesi sana (k.37). Mtu ambayeamesahau alivyotendewa na Mungu kwa huruma sana. Huyo mtu hatasimamakatika hukumu ya Mungu. Atakuwa ameishi bure akibaki bila kitu. Jambomuhimu ni msingi unaowekwa, misingi hutofautiana sana, mwingine ni imara,mwingine hauwi imara. Lakini siku ya mwisho itajulikana ni upi uliowekwa (1Kor.3:11ku). Twaona uthabiti wa Yesu kuhusu mafundisho yake, alijua asiliyake ni katika mapenzi ya Baba yake.

Msingi ni mafundisho yake, ni msingi bora. Tukiyawaza jinsi alivyozitaja zile herina ole n.k. ni vema tuyazingatie sana mafundisho yake, kwa sababu hayawimepesi, yaenda kinyume cha mawazo ya wengi na kama Yesu asingaliyafunuahayo sisi tungeshindwa kuyafikiri ni hivyo.

7:1-10 Yesu alimponya mtumishi wa akida (Mt.8.5-13)k.1 Luka alitaja kwamba hapo ni mwisho wa hotuba akidokezea kwamba hayoyaliyotangulia yalitolewa kwa wakati mmoja, ndipo Yesu pamoja na wanafunziwake na kundi la watu walishuka mlimani kisha Yesu alirudi Kapernaumu kituochake.

Page 63: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 353

k.2 Akida alikuwa askari mwenye mamlaka juu ya askari kama mia hivi, yeyepia alikuwa chini ya askari walio na mamlaka zaidi yake na kuwa juu yake.Hakuwa Myahudi (k.3,9) pengine alikuwa Mrumi, au Mmataifa, huendaalitumika katika jeshi la askari wa Mfalme Herode Antipa aliyetawala eneo laGalilaya kwa ajili ya Dola ya Kirumi. Pengine walikuwa kama polisi waliosaidiashughuli za kukusanya ushuru na kuulinda usalama wa eneo hilo.

Kutokana na yaliyoandikwa hapo huyo akida ameonekana kuwa mtu mzurisana kwa vile alivyomthamini na kumshughulikia mtumwa wake wakatialipougua vibaya. (Mt.8:6 amepooza). Hali yake ilikuwa mbaya hata kiasi chakukaribia kufa.

k.3-4 Akida alikuwa na uhusiano mzuri na Wayahudi. Twasoma kwambaaliwapenda (si kawaida kwa Wayahudi kujihusisha na wageni na hasa walewaliowasaidia Warumi katika utawala wa nchi). Alionyesha upendo wake kwakuwajengea sinagogi. Kwa kawaida maakida hawakuwa na uwezo wa kufanyahivyo. Pengine alikuwemo katika kundi la wacha Mungu waliovutwa na dini yaKiyahudi na kujiunga nao katika ibada. Wayahudi waliona kwamba amestahilikusaidiwa. Akida alikuwa amesikia habari za Yesu jinsi alivyowaponya watuwengi wenye ugonjwa mbalimbali. Aliishi Kapernaumu mahali ambapo Yesuameweka kituo chake na kutoka hapo alikwenda huko na huko akihubiri mijinina vijijini.

Akida aliwatumia viongozi wa Wayahudi, wazee waliotegemewa kwa mashauriyao. Aliwaomba wamwendee Yesu na kumwita aje nyumbani kwake kwashabaha ya kumponya mtumishi wake aliyempenda sana.

k.5-6 Walimfikia Yesu na Yesu akakubali kwenda nao mpaka nyumbani pahuyo Mmataifa. Hakusita kujihusisha na huyo Mmataifa kwa sababu Wayahudiwamejiweka kati yake na huyu Mmataifa, kwa hiyo, hawezi kushtakiwa kwambaamejihusisha na Mmataifa. Ila kabla hawajafika kwake, yule akida alikuwaamebadili mawazo yake. Katika kutafakari jambo hilo alijiona kwamba yeyehastahili hata kidogo huyo Yesu aingie nyumbani kwake. Sababu moja nikwamba Yesu ni Myahudi na yeye ni Mmataifa na kwa kawaida hawashirikiani.Pili katika kumwaza Yesu Mwenyewe katika uwezo wake wa uponyajialitambua kwamba hakuna haja akutane naye kwa kuwa yeye hastahili mbelezake. Yesu ni mstahili kuliko yeye. Hivyo alituma baadhi ya rafiki zake kwaYesu na kumpa ujumbe ‘asije’ tofauti na na ule wa kwanza wa ‘njoo’.

k.7 Kwani amebadili mawazo yake? Katika kuwaza kwake amezingatia jambola ‘mamlaka’. Katika cheo chake cha kuwa akida alikuwa na mamlaka yakuwaagiza askari walio chini yake, kwa kuwa aliposema neno walipaswa utii.Vivyo hivyo alipaswa awatii wakubwa wake walipomwagiza neno. Twaonaunyenyekevu wake, alisisitiza kuwa chini ya mamlaka kuliko kuwa na

Page 64: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

mamlaka juu ya wengine. Hivyo, hakuna haja awepo, ilitosha neno lisemwe,na kwa vyo vyote lile neno litatimizwa.

Halafu alipofanya ulinganifu kati yake na Yesu na kati ya mamlaka yake namamlaka ya Yesu alitambua kwamba Yesu alikuwa na mamlaka kuu katikamambo ya uponyaji na ya kwamba mamlaka hiyo ameipata kutoka mkuu wake,Yeye aliye juu, yaani Mungu Mwenyewe, akiwa na uhusiano wa ukaribu sananaye. Kwa sababu hiyo iwapo mwanzoni hakusikia shida katika kumwita Yesuaje kwake nyumbani isipokuwa alisita kiasi fulani kwa sababu alikuwa Mmataifana Wayahudi hawakupenda kujihusisha nao kwa ukaribu. Wazee wa Kiyahudiwaliona amestahili (k.4) ila yeye baada ya kuyazingatia hayo yote alijiona kuwahastahili hata kidogo Yesu aje kwake, wala hakuna haja ya kuonana naye walahakuna haja mtumwa wake mgonjwa akutane naye na kuguswa naye n.k.Ilitosha Yesu atamke neno tu na mtumishi wake atapona.

k.9 Jumla ya hayo yote ni kwamba Yesu hakuwa na haja ya kuja kwake, walaya kuonana naye, wala Yesu hakuwa na haja ya kumwona na kumgusamtumwa wake; jambo moja tu lilihitajika; Yesu aseme Neno tu. Uwezo ni katikaNeno la Yesu. Mtu huyo hakuwa na shaka lo lote kwamba mtumishi wakeataponywa (k.7). Kama imani yake ilibaki katika uponyaji tu au alizidi kujikabidhikwa Yesu, hatujui maana alikuwa amemwita Bwana (k.6). Yesu alimstaajabia,na alitaka mkutano wa watu waliomfuata wajue hivyo na sababu ya kustaajabukwake, ili hao nao washirikiane naye katika kushangaa kwake, hivyo,akawageukia na kusema wazi ‘Nawaambia, hata katika Israeli sijaona imanikubwa namna hii’. Hakutaka kuwalaumu kwa sababu katika Israeli walikuwepowaliomwamini, ila wengi walikuwa hawajamkubali, na imani ya huyo ilizidi imaniyao. Alimsifu Mmataifa, tena askari aliyefanya kazi ya kuwasaidia wakoloni.Katika Injili ni mara mbili tu tumesikia habari za Yesu kushangaa. Mara mojahapa kuhusu imani ya Mmataifa na mara moja kuhusu kutokuamini kwa wenyejiwa Nazareti walio Wayahudi (Mk.6:6). Ila tusifikiri alistaajabu kwa mara hizombili tu.

k.10 Luka amemaliza habari hiyo bila kutaja kwamba Yesu alitamka Neno lauponyaji. Pengine alitaka kuonyesha kwamba Yesu alimponya (au aliwezakumponya) hata bila kusema Neno. Kitu cha shangaa ni kuona kwambaMmataifa asiyestahili, aliye nje ya ‘watu wa Mungu’ alimtambua Yesu kupitawale ambao wangemtambua. Yesu alikuwa na uwezo katika nafsi yakeMwenyewe kumponya mtu bila kumwona na kusema naye. Kwa jinsi Wayahudiwalivyohusika na habari hiyo Yesu hakulaumiwa kwa vile alivyomshughulikiaMmataifa.

(Katika Mathayo habari imetofautiana kidogo, Mathayo ameacha kutaja wazeena ujumbe wa rafiki, na alisema habari za Yesu kuonana na akida. Huendaamefupisha habari na kuacha habari za wajumbe na kusema kama Yesu naakida walionana, ila hasa Yesu hakuonana naye. Luka alisisitiza habari za

Page 65: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 355

wazee na imani kubwa ya akida. Luka alivutwa na mambo ya WaMataifa naalitaka kuonyesha uzuri wao. Kwake neno kubwa lilikuwa si uponyaji balimamlaka kuu ya Yesu na asili yake katika uhusiano wa ukaribu sana naMungu, Baba yake.

7:11-17 Yesu alimfufua mwana wa mjane wa Naini(ling. Na Waf.wa kwanza 17:8ku)Mji wa Naini ulikuwa kama maili 25 kutoka Kapernaumu, mwendo wa siku mojahivi na kama maili 6 kutoka Nazareti. Yesu alikuwa pamoja na wanafunzi wakena mkutano mkubwa waliomfuata. Hapo nyuma tumeona kwamba alimponyamtu aliyekaribia kufa hapo kijana ameishafariki dunia.

k.12 Yeye na wale waliokuwa pamoja naye walikaribia mji tayari kuingia ndanina hapo walikutana na maandamano ya watu waliokuwa wakitoka nje kwendakumzika mtu. Aliyekufa alikuwa kijana, mwana pekee wa mama mjane ambayeameishafiwa na mumewe. Hivyo alikuwa peke yake, bila mwanaume wakumtunza na kumpatia riziki. Siku zile ilikuwa vigumu kwa wanawake kupatakazi. Pia ni mwisho wa ukoo wake, jambo muhimu kwa upande wake.

k.13 Yesu alifanyaje alipokutana na huyo mjane, na maiti, na wabebaji wajeneza? Alivutwa na dhiki ya huyo mama, akamhurumia, akiwaza hali zake zashida, huzuni ya kufiwa, upweke wake, na shida atakazopata kutokana na kifocha mwana wake. Kwa desturi ya mazishi huyo mama alilitangulia jenezaambalo lilikuwa wazi bila kifuniko. Hatujui kama wapiga filimbi walikuwepo, kwakawaida hao waliajiriwa, ila maskini walishindwa kuwaajiri. Yesu alisema mojakwa moja kwa mama huyo ‘Usilie’. Maneno ya kumtumainisha na kumdokezeakwamba hakuwa na haja ya kulia. Ndipo akaligusa jeneza, hakujali jambo lakunajisika iwapo kwa sheria ya Kiyahudi mtu alivyofanya hivi alinajisika(Hes,19.11,16).

k.14 Waliolichukua jeneza wakasimama, hali wakitazamia ni nini litakalotokea.Kisha Yesu akasema na maiti ‘Kijana, nakuambia, Inuka’. Tazama jinsialivyosema kwa mamlaka ya Nafsi yake ‘nakuambia’. Kijana akainuka, nakuketi, na kuanza kusema, dalili za kuwa uhai tena.

k.15 Akamrudisha kwa mama yake aliyemhitaji akae naye nyumbani nakumtunza; Yesu hakumwomba huyo kijana afuatane naye.

k.16-17 Watu waliitikiaje? Waliitika kama watu waliokuwa mbele za Mungu.Walihofu, maana yake, walimcha Mungu, nao wakamtukuza Mungu, si Yesu.Walimwonaje huyo aliyetenda tendo hilo kubwa la kumfufua kijana kutoka wafu.Walimwona kuwa nabii mkubwa ambaye ametumwa na Mungu kuwabariki,kama Zekaria alivyotabiri (1.68,78). Amefanana na Elisha na Eliya, manabii wazamani, ambao pia waliwafufua wafu (1 Waf.17:17ku. 2 Waf.4. 18ku). Mungu

Page 66: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

angali akitenda kazi kama alivyofanya zamani zile. Kweli sifa hiyo haikutosha,ila polepole, hatua kwa hatua, watu walizidi kumtambua jinsi Alivyo hasa,Mwana pekee wa Baba. Sifa zake zilienea mbali sana. Luka alimwita Bwana(k.13). Yesu alifanya tendo hilo bila kudai lo lote, hata imani, kwa wahusikawala kwa wale waliokuwepo. Alifanya tu bila kumdai mtu ye yote jambo lo lote.Mwana alipata uhai wake tena na mama alimpata mwana wake hai tena,baraka kubwa sana kwa wote wawili.

7:18-35 Yohana MbatizajiMatazamio ya Yohana yalionekana kuwa tofauti na hali ya huduma ya Yesu.Yohana alifungwa, yadhaniwa katika ngome ya Machaerus, mashariki yaBahari ya Chumvi. Wanafunzi wake walimwendea na kumpasha habari za Yesuna matendo yake. Alifahamu kwamba Yesu amewavuta wengi kumfuata.Haikosi walimweleza juu ya matendo makuu ya kuwaponya watu, kutoa pepon.k. Pamoja na hayo yawezekana walimwambia juu ya upinzani mkali waviongozi wa dini. Yesu alijihusisha na watu kwa urahisi, alijaa upendo nahuruma hasa kwa wanyonge, maskini, waliowekwa kando ya jamii n.k. Ila tatizokwa upande wa Yohana ni moja, matendo ya kuhukumu kama alivyotabirikwamba Masihi atayafanya yako wapi? Hamna dalili ya shoka kuwekwa penyeshina la mti wala ya pepeto la kuusafisha uwanda, na hasira inayokuja?(Mt.3.7,10,12). Neema imetangulia, neema nyingi, ambayo Yohanahakutazamia. Yeye alihubiri habari ya toba ya kuepa hukumu kali ya Mungu.Imekuwaje? Je! Yesu ni Yule ajaye? Au vipi? Pamoja na hayo hamna dalili yavita ya kupigana na Warumi na kuwaweka watu huru mbali na utawala waKiMataifa. Katika upweke wake Yohana alitatizwa na huduma ya Yesu.

k.17-18 Kwa hiyo aliwatuma wanafunzi wake wawili kwa Yesu ili wamwulizeYesu swala maalum ‘Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?’ Je!alikuwa akiwaza na kusema ni nani atakayefanya hizo kazi ya hukumu? Nivigumu kujua kwa hakika alikuwa na maana gani. Je! Yohana alipungua imani?ni vigumu kufikiri hivyo, ila katika hali ya mateso na upweke si rahisi mtu awemkakamavu, hasa ikiwa matazamio yake ni tofauti na yale yaliyokuwayakitokea. Huenda alihitaji subira.

k.20-22 Walipofika kwa Yesu wakamwuliza swala sawa na jinsi Yohanaalivyowaagiza. Kwa kutaja swala mara mbili Luka amelitilia mkazo. Yesu alijibukwa njia mbili, kwanza kwa kutenda matendo makuu ndipo kwa maneno yakuelezea.

k.21 ‘saa ile ile aliwaponya ...’ Mbele ya wanafunzi wa Yohana Yesu alifanyakazi za rehema kwa wagonjwa na wenye misiba, akitoa pepo na kuwajaliavipofu kuona n.k. Hizo kazi za rehema zilionyesha uwezo mkubwa wa Yesunazo zilipatana na utabiri wa Nabii Isaya juu ya nyakati za wokovu. Siyokusema kwamba Yesu hakutaja hukumu ya Mungu, aliitaja, ila mkazo wakeulikuwa rehema na neema. Hata Nabii Isaya alitaja hukumu wakati uleule

Page 67: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 357

alipozitaja kazi za rehema. Twaweza kusema kwamba huduma ya Yesu ilijaarehema kuliko alivyotazamia Yohana. Ni ukumbusho wa Nabii Yona aliyehubiriWaNinawi watubu, ndipo walipotubu, akasikitika sana (Yon.4:1; Yak.2:13).

k.22-23 Ndipo Yesu aliwaelekeza hao wanafunzi wa Yohana kurudi kwake nakumweleza waliyoona na kuyasikia, akitaja aina mbalimbali za kazi zake zahuruma. Aliongeza kusema kwamba maskini wanahubiriwa habari njema.Yohana akitafakari hayo yote atakumbuka kwamba Nabii Isaya alitabiri kwambaMasihi atayafanya hayo (Isa.26:19; 29:18ku. 35:5ku. 61:1). Jibu lake lililinganana hotuba yake katika sinagogi la Nazareti (4:18). Kwa hiyo aliwajibu kwakufanya uponyaji n.k. na kuyathibitisha kwa maelezo yake. Hizo ndizo kazimaalum za Masihi, kazi za Yule Ajaye. Kisha alisema ‘heri mtu ye yoteasiyechukizwa nami’ maana yake amebarikiwa yule anayetambua kwambaimepaswa kuwa hivyo.

k.24-28 Katika k.18-23 Yesu na matendo na huduma yake vilielezwa kwa jinsivilivyokuwa tofauti na matazamio ya Yohana. Katika k.24ku. Yohana nahuduma yake vimeelezwa katika nuru ya kuja kwa Yesu na Ufalme wa Mungu.Katika sehemu hiyo jambo linalozungumziwa ni mahali pa Yohana Mbatizajikatika huo wakati mpya ambao umeletwa na Yesu, wakati wa kuja kwa Ufalmewa Mungu. Wanafunzi wa Yohana walimrudia Yohana ndipo Yesu aliona vemaaseme juu yake watu wasije wakamwelewa vibaya na kufikiri kwamba Yohanaalikuwa amekosa wala hakufaa kuwa nabii. Kwa njia ya kuyauliza maswali nakuyajibu alitoboa wazi mawazo yao juu ya Yohana. Walipomwendea jangwanina kubatizwa naye, Je! walikwenda kumwona mtu wa namna gani? Mtu hafifu?mtu mwepesi? La! Hata kidogo! kinyume chake Yesu alisisitiza ukakamavu nauthabiti wa Yohana aliyeishi jangwani kwa shida sana, bila kujali kula kwakewala kuvaa kwake. Pia hakujali cheo cha mtu wala hakuogopa watu, hataMfalme Herode.

k.27 Ndipo Yesu aliendelea kumsifu sana Yohana, na kuonyesha mahali pakekatika mpango wa Mungu. Katika historia yote mpaka wakati huo hakunaaliyempita Yohana, alikuwa nabii mkuu kupita wote waliomtangulia. Alikuwayule ambaye Malaki alitabiri kwamba atakuja na kumtangulia Masihi (Mal.3:1).Alizidi manabii wote, kwa njia gani? Aliwazidi kwa sababu wao walitabiri kwambali kuja kwa Masihi bila kumwona; ila Yohana ndiye aliyemwona uso kwauso na kutangaza kufika kwake. Alipewa huduma ya heshima kubwa yakunyosha njia zake. Kwa hiyo hakuna aliyemzidi Yohana katika historia iliyopita,ila katika dahari mpya ya Agano Jipya, Agano la neema, na katika huo Ufalmeambao umeletwa na Yesu, hata muumini mdogo wa Yesu ni mkuu kuliko yeye.Si kwa kuwaza mtu kibinafsi, bali kwa kulingana na dahari yake na dahari mpyailiyoingizwa na Yesu. Ni kama kusema kwamba mtu aliye mkubwa wakati wautawala wa kigeni ni mkubwa kweli, ila mwananchi mdogo katika utawala wawenyeji baada ya kupita kwa utawala wa kigeni ni mkubwa kuliko mkubwa waenzi za nyuma. Ni Yesu atakayeutekeleza mpango wa Mungu wa kuwaokoa

Page 68: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

wanadamu na dhambi zao, hana mpango wa kuwatoa Waisraeli chini yautawala wa Kirumi. Yesu alifundisha kwamba Ufalme wa Mungu ni kwa‘wadogo’ (Mt.10:12; 18:10,14; Mk.9:42; Lk.9:48) pamoja na maskini nawaliowekwa kando na jamii, na wasiopendwa, n.k. (4:18; 7:22). Ufalme waMungu huwapa heshima na ukuu wale wasio na haki yo yote ya kudai wawehivyo.

k.29-35 Katika sehemu hiyo Yohana amewekwa sambamba na Yesu. Kuja kwaYesu kulileta mgawanyo katika watu. Walikuwepo wale waliojiweka upandewake ambao waliona kwamba Mungu amefanya iliyo haki, nao walikuwawameupokea ubatizo wa Yohana. Pia walikuwako wale waliokuwa kinyumechake, hasa Mafarisayo na Wana-sheria waliompinga Yohana na katikakumpinga walikuwa wamempinga Mungu pamoja na mpango wake wakuwaokoa wanadamu. Hapo tena jambo hilo limeonyesha maelekeo ya Yesukwa watu wanyonge na wale waliowekwa kando ya jamii, kama watoza ushuru.Wao ambao walidhaniwa watakuwa wa kwanza kupokelewa wamejiondoa kwasababu walitaka wokovu wa kisiasa si wa kiroho.

k.31 Kisha Yesu aliuliza maswali juu ya watu wa kizazi chake, wale ambaowamemwona Yohana pamoja na wale ambao wanamwona Yeye Masihi.Alifanya ulinganifu kati yake na Yohana na kuonyesha kwamba, hata Yohanaangalikuwa wa tabia gani, watu wasingalikuwa radhi naye. Walisema ‘ana pepo’kwa sababu aliishi jangwani na kula vitu vya shambani n.k. Vivyo hivyo na Yeyepia, hata angalifanya nini, wasingalimkubali. Yeye tofauti na Yohana aliishikama kawaida ya watu, hakujinyima chakula, hakujiwekea nadhiri yakutokunywa divai n.k. Hata hivyo walimwita mlafi na mnywaji wa divai. Pia, rafikiwa watoza ushuru na wenye dhambi, mtu ambaye alipenda kujihusisha na watuwa aina zote. Katika kufanya hivi watu walifanana na watoto katika michezoyao. Kundi moja wakisema ‘tufanye kiigizo cha harusi?’ wa kundi linginewakakataa; wengine wakisema ‘na tufanye kiigizo cha mazishi?’, wa kundilingine wakakataa. Hata wakisema tufanye kiigizo cha aina yo yote, baadhiwatakataa.

k.35 Iliwapasa watu wawe na hekima ya kutambua kwamba Mungu alikuwaakifanya kazi kwa njia ya Mbatizaji pamoja na kufanya kazi kwa njia ya Yesu.Watu wa hekima watatambua neno hilo, wala hawatakwazwa na Yohana walana Yesu. Kila mmoja alikuwa ishara kamili ya Kuja kwa Ufalme wa Mungu nakila mmoja alipewa fungu lake. Kwa kusema hayo yote Yesu alimheshimu sanaYohana na ilibidi watu wamheshimu pia. Wote wawili waliwiana katika mpangowa Mungu.

7:36-50 Yesu alipakwa mafuta katika nyumba ya Farisayo na Mfano wawadeni wawilik.36 Mara kwa mara Yesu aliitwa na Mafarisayo kwa chakula (11:37; 14:1) ilamara nyingi walikuwa na shabaha ya kumpeleleza. Hapo nyuma (5:29)

Page 69: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 359

alikwenda kula na mtoza ushuru na wenzake. Huyo Farisayo aliitwa Simoni(k.40). Yesu aliingia na kuketi chakulani. Kwa desturi meza ilikuwa ndefu nafupi na watu waliegemea mkono wa kushoto na kichwa kilielekea ndani namiguu ilinyoshwa kuelekea nje.

k.37 Watu waliweza kuingia na kuzungumza na waliokuwapo chakulani.Mwanamke mmoja, pengine alikuwa kahaba, hali amewahi kuandaa kufanyahivyo, akaja ndani na kusogea karibu na Yesu. Alikuwa na chupa ya marimariyenye marhamu (ya bei kubwa) ndipo akaivunja miguuni pake (kwa jinsiwalivyokaa mezani ilikuwa rahisi kuigusa miguu yake). Alilia akisikia nafsinimwake mchanganyiko wa huzuni na furaha ndipo akaipangusa miguu kwanywele za kichwa chake na kuibusu-busu na kuipaka marhamu (ilikuwa mwikokwa mwanamke kulegeza nywele zake mbele za watu). Alikuwa jasiri kweli,maana huyo Farisayo angalichukizwa kwa mwanamke wa sifa mbaya kuingiana kufanya alivyofanya, bila kujali watu. Tena alishangaa kuona kwamba Yesuamekubali huyo mwanamke amfanyie hayo yote bila kusema neno lo lote. bilakumkemea na bila kumzuia. Iliruhusiwa watu waingie ndani ya nyumba, hatawakati wa kula, kwa hiyo, si neno geni kwa huyo mama kupata nafasi ila ni kwasababu ya sifa zake Simoni hakufurahi.k.39 Farisayo hakusema wazi mawazo yake lakini Yesu aliyajua. Yesualifahamu kwamba Simoni ametatizwa na mambo mawili. Ameshindwakumkubali Yeye kuwa nabii kwa sababu(a) amekubali kufanyiwa hivyo(b) angekuwa nabii angalitambua ya kuwa huyo mwanamke hakuwa na maishamazuri.

k.40-43 Mfano wa wadeni wawili. Yesu alimkabili Simoni na kumwambiakwamba alikuwa na neno la kuzungumza naye, na Simoni alikubali Yesuaseme. Ndipo Yesu alitoa mfano wa wadeni wawili, mmoja mwenye denikubwa, na mwingine mwenye deni dogo. Kwa sababu wote wawili walishindwakulipa, mkopeshaji aliamua kuwasamehe wote wawili. Halafu Yesu alipomalizamfano akamwuliza Simoni swali ‘katika hao wawili ni yupi atakayempendazaidi?’ Alitaka Simoni amjibu, na Simoni, alijibu ‘Nadhani ni yule ambayealisamehewa nyingi’. Huenda kwa kusema ‘nadhani’ Simoni hakupenda kujibukwa sababu alitambua kwamba mwenye deni kubwa ni huyo mwanamke.Yesualiunga mkono jibu lake na kusema kwamba ameamua haki. Mwenye denikubwa aliyesamehewa ndiye atakayempenda mkopeshaji zaidi.

k.44ku. Ndipo Yesu alitafsiri mfano huo kwa Simoni na kwa mwanamke.Alimgeukia mwanamke na kusema na Simoni, akitaka Simoni amfikirie huyomwanamke na hali yake kwa makini sana. Ni nani kati yao ambayeamempokea Yesu vizuri, na kumfanyia kwa heshima impasayo mgeni rasmi. SiSimoni, kwa maana yeye hakufanya kama ilivyompasa kwa mgeni wa heshima.Hakumpa maji ya kuosha miguu yake, wala kumpaka mafuta kichwani, wala

Page 70: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kumpa busu la salaam za kumkaribisha. Lakini huyo mwanamke amefanyahayo yote yaliyompasa Simoni afanye.

k.47ku. Lakini si hivyo tu, yapo matokeo makubwa zaidi. Kwa nini huyo mamaamefanya hayo yote? Kwa sababu amesamehewa dhambi zake nyingi. Alijaaupendo na alitaka kuonyesha shukrani zake kwa Yesu kwa jinsi ambavyoamesaidiwa kuyashinda maovu yake. Aliyesamehewa kidogo ni nani? pengineni Simoni ambaye alidhani kwamba dhambi zake ni chache tu au pengine inamaana kwamba mtu asipokubali ni mwenye dhambi awaza kwa kosa la kufikirikwamba hana la kusamehewa. Tusifikiri kwamba huyo mwanamke alistahilikusamehewa kwa sababu ya kumpaka Yesu mafuta n.k. Chanzo cha hayo yotekilitokea katika kuwahi kusamehewa kwanza.

Ndipo kwa tangazo rasmi Yesu alimthibitishia msamaha. Kwa wote waliodhanikwamba huyo mama ni mwenye dhambi sasa wajue kwa hakika kwambadhambi zake zimesamehewa. Hapo tena Yesu amedai kuwa na mamlaka yakusamehe dhambi (5:20-26).

k.49-50 Halafu watu walioketi chakulani walianza kuwaza mioyoni mwao nakujiuliza ‘huyo ni nani hata asamehe dhambi’ kwa kuwa watu wote walikubalikwamba hii ndiyo kazi ya Mungu peke yake. Kisha Yesu akarudi kusema nayule mwanamke kwa kuwa ni huyo aliyetawala mawazo yake, akamwambia‘Imani yako imekuokoa’ imani iliyodhihirika katika tendo lake la kuthubutukuingia katika nyumba ya Farisayo, na kulia na kumimina mafuta n.k. ‘enendazako kwa amani’ Tukio la kusamehewa sikuzote ni amani, amani kwa Munguna amani ya Mungu moyoni.

MASWALI1. Eleza sababu za Yesu kuwachagua Mitume kumi na wawili?2. Katika hotuba ya tambarare Yesu alionyesha tofauti kati ya mawazo

yake na mawazo ya kawaida ya watu kwa kutamka baraka na ole.Tofauti hizi ni nini?

3. Eleza mikazo mingine ya Yesu katika hotuba hiyo.4. Mfano wa Misingi Miwili ni njia ya Yesu ya kuonyesha umuhimu wa kitu

gani?5. Eleza mambo makubwa katika habari ya Yesu kumponya mtumishi wa

akida.6. Eleza mambo makubwa katika habari ya Yesu kumfufua mwana wa

mjane wa Naini.7. Eleza shida ya Yohana Mbatizaji kumhusu Yesu na jinsi Yesu

alivyokabili hiyo shida.8. Yesu alisema nini kuhusu uwiano kati yao? Alitoa sifa gani juu ya

Yohana.9. Eleza mambo makubwa katika habari ya Yesu kupakwa mafuta katika

nyumba ya Farisayo. Alitumia mfano gani katika kumsaidia Farisayo?

Page 71: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 361

8:1-3 Wanawake waliomhudumia Bwana Yesuk.1-3 Katika sehemu hiyo fupi tumeambiwa jinsi Yesu na Mitume walivyotunzwawakati wa kuzunguka-zunguka vijijini na mijini. Tangu alipoondoka nyumbani nakuacha kazi yake ya ufundi Yesu alikuwa maskini, yeye mwenyewe hakuwa namali, wala hakuutumia uwezo wake wa KiMungu kujipatia riziki zake. Hapotumepewa habari za wanawake kadha wa kadha waliojitoa kumsaidia Yeye naMitume wakiwahudumia na kuwasaidia kutoka mali zao.

k.1 Yesu alihubiri hadharani, alipitapita mijini na vijijini akihubiri habari zaUfalme wa Mungu. Aliwafundisha watu jinsi ambavyo Mungu amejiingiza katikamaisha ya wanadamu na kuleta mpango mpya. Kwa njia yake Munguamesogea karibu na watu na kuwapatia nafasi ya kujihusisha naye bila shida.Badala ya kuyatimiza masharti yote ya Torati ndipo wapokelewe vema, iliyoposasa ni kwamba watu wazitubu dhambi zao na kuwa tayari kuishi maishamapya kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Mungu huwapokea kwanza ndipowatatiwa moyo wa kumpenda na kufanya mapenzi yake. Hawatahitajikakuyatimiza masharti yote ya Torati ndipo kupokelewa vema na Mungu. Munguatawapokea ndipo watatiwa moyo wa kumtii. Luka ametaja Mitume kuwapamoja na Yesu, wakijifunza kwa Bwana wao.

k.2 Yesu alitofautiana sana na marabi ambao hawakuwathamini wanawake,hawakuwafundisha kwa sababu waliwaona kuwa wa chini na watuwasiofundishika. Ila Yesu aliwavuta Kwake, aliwathamini sana, alikuwa tayarikuwatumia katika kazi yake, na baadaye, katika Kanisa walipewa nafasi nzuri.Baadhi yao waliandamana naye kutoka Galilaya hadi mpaka Yerusalemu,wengine walikuwepo pale Msalabani na kushuhudia Kufa Kwake, baadhiwalishuhudia Kuzikwa Kwake (ni wanawake tu ambao walipaona mahalialipozikwa) na Siku ya Ufufuo walikuwa wa kwanza kuliona kaburi li wazi natupu na Mariamu Magdalene alitumwa na Yesu kwenda kwa Mitume nakuwaambia habari njema ya Kufufuka Kwake; hivyo walistahili kuwa mashahidiwa kweli (23:55; 24:22-23,33).

Katika hao wanawake alikuwepo Mariamu Magdalene ambaye ametajwa maranyingi katika Injili. Huenda alitoka kijiji cha Magdala, maili chache kutokaKapernaumu. Si vizuri kumwaza kuwa kahaba, mwenye maisha mabaya.Kuwa na pepo saba ni kuonyesha kwamba aliishi kwa shida sana ya kuonewana mapepo. Kwa kawaida kuwa na pepo ni dalili ya shida ya akili si shida yamaisha machafu. Kutaja pepo saba ni dalili ya kuonewa sana. Haowaliomhudumia Yesu walifanya kwa moyo na kwa shukrani kwa sababu Yesualiwaponya ama kwa ugonjwa fulani au kwa kutolewa pepo.

k.3 Yoana ametajwa tena (Lk.24:10). Bwana wake alikuwa wakili wa HerodeAntipa, kwa hiyo, twajifunza kwamba baadhi yao walikuwa na uwezo wa mali.Wengine wamewaza kwamba huyo Kuza aweza kuwa yule aliyetajwa katikaYohana 4:46ku. wakifikiri kwamba ndiyo sababu ya kumfuata Yesu na ya Kuza

Page 72: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kukubali kwamba mkewe aandamane na Yesu katika safari zake. Ni mawazo tuambayo yanatusaidia kutatua tatizo la kufikiri juu ya huyo wakili kumruhusumkewe amwacha kwa muda mrefu hasa kwa sababu ya kumhudumia Yesualiyepingwa na wakubwa. Ni hapo tu Susana ametajwa.

Kwa sehemu hiyo fupi twajifunza kwamba Yesu alifanya kazi kwa bidii bilakujihurumia. Hakutafuta makuu, alikubali kujihusisha na watu wa kila aina,maskini kwa wenye mali, wanaume kama Mitume, na wanawake kamaMariamu Magdalene na wenzake. Tumepewa mwanga kuhusu jinsi Yesualivyopata riziki zake. Kundi la Mitume walikuwa na mfuko wa kununua chakulana kutoa vipawa kwa maskini (Yn.13:29) ila hatuambiwi fedha hizo zilitoka wapi.Hapo twajulishwa kwamba ni hao wanawake waliowasaidia.

(Luka amependa kuweka pamoja habari za wanaume na wanawake: Zakariana Elizabeti (Lk.1 na 2); Mjane na Naamani (4:25-27; Mwenye pepo namkwewe Simoni Petro (4:31-39; Akida na mjane wa Naini (7:1-17) mtumwenye kondoo na mwanamke mwenye shilingi (15:3-10); Mjane aliyepatahaki na mtoza ushuru aliyehesabiwa haki (18:1-14).

Hatusikii habari za Yesu kuingia tena katika masinagogi, pengine alichaguakuhubiri hadharini kwa sababu ya upinzani wa viongozi. Hata hivyo, wengiwalihudhuria mikutano yake. Katika Injili hatuna habari yo yote ya mwanamkealiyemfanyia Yesu vibaya, hasa, adui zake walikuwa wanaume. Pengine sivizuri kusema hakuna mwanamke, hata mmoja, ila kwa jumla wanawakewalivutwa sana kwa jinsi walivyojisikia kuthaminiwa sana na Yesu.

8:4-8 Mfano wa mpanzi (Mt.13:1-9; Mk.4:1-9)k.4 Yesu alitoa mfano huo wakati wengi walipokuja na kumsikiliza, ijapokuwaviongozi walimpinga, umati wa watu walimpenda sana. Ila Yeye alitaka wajitoeKwake kweli wasiwe wasikilizaji tu bila waonyeshe mabadiliko maishani mwao.

k.5a Alifananisha huduma yake na kazi ya kupanda mbegu. Mbegu yake ni yakipekee, ina nguvu ya Mungu ndani yake, ni mbegu halisi. Katika mfano mpanzialisambaza mbegu zake kwa ukarimu sana hali akitambua kwamba zinginezitaanguka mahali pasipofaa nazo zitakosa kuzaa vizuri. Mpanzi alikuwamkarimu sana, na mwenye matumaini makubwa katika uwezo wa zile mbeguzilizopandwa. Zingine zitapotea ila zile zinazoota penye udongo mzurizitasababisha mafanikio ya mavuno mengi (Isa.55:11).

k.5b Mbegu zingine zilianguka njiani, zikakanyagwa na watu, halafu ndegewakazila. Katika umati wa watu waliomsikiliza wengine walifanana na udongomgumu wa njia. Maisha yao yalikanyagwa na mambo mengi kwa kuwawaliruhusu mambo mengi kupitia maishani mwao. Hivyo, walipolisikia Neno laYesu hawakujali. Ilibaki kwamba wamemsikia tu.

Page 73: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 363

k.6 Halafu mbegu zingine zilianguka penye miamba. Hapo udongo ulikuwamchache, na mbegu zilipoanguka pale, mara ziliota, ndipo kwa kukosa rutubazikakauka. Mfano wa baadhi ya wasikilizaji wake, waliolipokea Neno lake kwafuraha, ila walikosa kina maishani mwao, muda si muda, hawakuendeleakumfuata Yesu.k.7 Mbegu zingine zilianguka katika miiba, na miiba na mbegu ziliota pamoja.Mbegu hazikuwa na uhuru wa kutosha kumea vizuri, zikasongwa na miiba, daliliya watu waliokuwa na mambo mengi katika maisha yao. Walikuwa tayarikumsikiliza Yesu na kulipokea Neno lake maishani mwao, ila kwa sababuhawakutia maanani jambo hilo moja hawakuzaa kitu.

k.8 Mpanzi aliendelea kupanda bila kujali mahali ambapo mbegu zakezilianguka. Zingine zilianguka penye udongo mzuri, zikamea, zikazaa vizurisana. Luka amesema zilizaa mia kwa mia. Ni kama amefupisha habari hiimaana Mathayo na Marko walitaja 30 kwa mia, na 60 kwa mia, na mia kwa mia.

Yesu alimaliza kwa kuwataja wasikilizaji wake; hayo aliyoyasema yaliwahusu,ni ujumbe kwao na ni juu yao kujiuliza ‘maana yake nini mfano huo kwangu?’.Yesu alitaka hao wasikilizaji waliopo walizingatie Neno lake, wasimwangalieYeye mbali na ujumbe wake.

Mfano huo unaonyesha kwamba Ufalme wa Mungu utakua kati ya upinzani wawengine, na uzembe wa baadhi ya wasikilizaji wake n.k. Chanzo cha Ufalmewa Mungu ni kidogo, mfano wa mbegu, ila mwishoni mavuno yatakuwa mengi.Yesu alisisitiza umuhimu wa Neno lake na wajibu wa kulitii. Neno lake linaouwezo wa kipekee, ni Neno lake, mbegu ni yake. Ni Yeye anayelipanda. Kwanjia ya mfano huo walibainika wale waliomtafuta kwa kweli, na wale waliotakakumsikia tu.

8:9-18 Maelezo ya Mfano wa Mpanzi (Mt.13:10-23; Mk.4:10-20)Wanafunzi walimwuliza Yesu maana ya mfano huo. Mathayo alisemawalimwuliza sababu ya kuitumia mifano (Mt.13:13).

k.10 Yesu aliwafunulia uheri wao kwa sababu wamejaliwa kupewa ujuzi kuhusuUfalme wa Mungu. Katika kushirikiana naye walizidi kuyafahamu makusudi yaMungu, ‘siri zake’ kuhusu njia zake katika kuuleta Ufalme wake kati yawanadamu. Siri hii ni Yesu na huduma yake na utume wake. Jambo hilolilikuwa limefichwa katika nyakati zilizopita na sasa lafunuliwa. Je! linafunuliwakwa akina nani? Kwa wale walioitika wito wake na kukubali kumfuata kwa dhati,hao ndio hufunuliwa mambo ambayo wanadamu hawawezi kuyajua kwa mbinuna akili zao wenyewe. Ila kwa wale ambao wamekosa kuitika vema wito waMungu hao wamejinyima nafasi ya kuzijua siri hizi. Wengi walikuwa wakimfuataYesu kwa juujuu bila kujitoa Kwake. Hivyo Yesu aliamua kuanza kuwafundishakwa njia ya mifano. Baadhi yao wakiizingatia hiyo mifano hao nao watajaliwa

Page 74: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kuzijua hizo siri, ila wasipotia bidii na wakikosa kuwa na unyofu wa moyo nakujitoa Kwake, watabaki bila kuelewa. Kwa hiyo, mifano ilikuwa njia ya kuifichasiri ya Ufalme wa Mungu pamoja na kuwa njia ya kuifunua. Katika jambo hiloneno la Nabii Isaya lilitimizwa (Isa.6:9-10).

Yesu alikuwa amefikia hatua kubwa katika huduma yake, wengi walimfuatapasipo kujitoa Kwake. Hivyo, ataendelea kuvumiliana nao na kuwapa nafasi ilamatokeo yatakuwa sawa na matokeo ya mpanzi katika mfano. Matokeo hayopia ni hukumu juu ya uzembe na kutokujali kwa wengi wa wasikilizaji wake. Ilakwa wale waliojitoa Kwake aliwafunulia siri za mifano faraghani.

k.11 Yesu alisema wazi kwamba mbegu ni Neno la Mungu. Neno la Mungu nisawa na mbegu, zote zina nguvu ya uhai ndani, zikipandwa zina nguvu yakuota, ila Neno la Mungu lina nguvu ya pekee. Kwa Neno la Mungu, yaaniujumbe unaohubiriwa, wakati ule na Yesu, na baadaye na Mitume na wenzao,halafu mbeleni na wahubiri Injili mpaka wakati wetu, Ufalme wa Mungu huletwakaribu na watu, na wale wanaoupokea huzionja nguvu zake maishani mwao.

k.12 Mpanzi katika ukarimu wake alisambaza mbegu zake mahali tofauti tofauti.Zingine zilianguka njiani, mahali pagumu palipokanyagwa na watu. Mbeguzilishindwa kuingia na ilikuwa jambo jepesi kwa mbegu kunyakuliwa kablahazijapata nafasi kupenya ndani. Adui wa Neno la Mungu ni Shetani, aliye aduimkubwa wa Mungu na Yesu. Wale wanaolisikia bila kujali, hilo Nenolasahauliwa na kupotea.

k.13 Wako wanaoipokea Injili kwa furaha ila hawastahimili wakati wa shida namajaribu. Kabla Neno halijapata nafasi kuota vizuri na kumea watu wanakuwawamekata tamaa na kuiacha imani yao.

k.14 Halafu wako wanaoipokea Injili vizuri ila kwa sababu wanayo mambomengi katika maisha yao, Neno la Mungu halipati hewa ya kupumua vizuri,yaani kumea na kuzaa. Masumbufu ya maisha, shughuli za mali, anasa, n.k.zasonga lile Neno hata halipati nafasi ya kuuonyesha uwezo wake wa kuzaa.Maisha yamejaa mambo mengi, imani ikiwa jambo mojawapo katika hayomengi, lakini imani haiwezi kukua pasipo kupewa nafasi ya kwanza katikamaisha ya mtu.

k.15 Hata hivyo, wako wanaolipokea Neno kwa furaha, na kwa moyo mnyofu,wakijitahidi kulitunza na kulipa nafasi katika maisha yao. Kwa imani na subirawao huzaa vizuri sana.Jambo linalosisitizwa ni kulisikia Neno la Mungu vizuri. Kwa njia ya huduma yaYesu watu walipewa nafasi tele kuitika wito wake na kujitoa Kwake. Kwa mfanohuo wanafunzi walifunuliwa mambo yaliyokuwa yakitokea wakati wa Hudumaya Yesu.

Page 75: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 365

Katika mfano huo Yesu alionyesha kwamba huduma yake inasababishamatokeo mbalimbali. Alijua kwamba wako watu wenye mioyo migumu,alifahamu kwamba wengi hawamkubali ila alikuwa na hakika kwamba Mungualijua mapema ndivyo itakavyokuwa na katika mipango yake akayaweka nafasikwa matokeo hayo. Makusudi yake hayazuiliwi na itikio la watu.

k.16-18 Yesu aliendelea kusisitiza umuhimu wa wasikilizaji kutilia maanani yalewaliyoyasikia. Hayo aliyosema juu ya mifano hayakuwa na maana kwamba siriya Ufalme wa Mungu iendelee kufichwa. Wanafunzi wake walizidi kuielewa nabaadaye itakuwa juu ya wahubiri Injili katika ulimwengu wote kuifunua. Taahaina kazi nyingine isipokuwa kung’aa. Hakuna awashaye taa na kuiwekauvunguni. Pia alisisitiza kwamba katika hukumu ya mwisho mambo yote ya kilamtu yatajulikana. Kila mtu amewajibika kutumia vizuri ujuzi alio nao wa Neno laMungu. Watakaovitumia vipawa vyao vizuri wataongezewa uwezo na ufahamuwao. Vivyo hivyo wasiotumia vizuri ufahamu wao, wakikosa kutilia maananiNeno lake watakuta kwamba uwezo wao wa kufahamu mambo ya kirohoutapotea.

8:19-21 Ujamaa wa kweli (Mt.12:46-50; Mk.3:31-35)Wakati fulani mama wa Yesu na ndugu zake walikuja kumwona Yesu.Yawezekana wamekosa kumwona kwa muda mrefu kutokana na shughuli zakenyingi katika kuzungukazunguka mijini na vijijini. Pengine walimhurumiawakitaka kumwomba apunguze shughuli zake. Walishindwa kumfikia kwasababu ya wingi wa watu. Halafu Yesu aliambiwa kwamba mama na nduguzake walikuwa wamefika karibu, nao walitaka kumwona. Ndipo Yesu alichukuanafasi hii kusisitiza tena umuhimu wa kulisikia Neno la Mungu. Hawezikuwatanguliza familia yake na kuipunguza huduma yake. Walisikiao Neno lakena kulitii ni ndugu zake. Kwa Neno lake anaunda jamii mpya ya watuwanaoshirikiana pamoja naye na kuishi kama familia yake. Tusifikiri kwambaYesu alikuwa akijiondoa kwa familia yake au ya kuwa aliwadharau. Iliwabidi haopia walipokee Neno lake. Neno la Mungu lina uwezo wa kuunda vifungo vyakuunganisha watu zaidi ya vifungo vya familia. Jamaa ya kimwili si neno kubwala mwisho. (Inaonekana Mariamu aliwazaa watoto wengine baada ya Yesu;Yesu alikuwa kifungua mimba (2:7). Kwa jinsi wanavyotajwa kwa majina katikaMathayo na Marko wataalamu wengi hufikiri kwamba hao ndugu walikuwawatoto wa Yusufu na Mariamu; ila wachache wafikiri kwamba maana ya neno‘ndugu’ ina maana pana kuliko hiyo (Mt.12:46; 13:55ku. Mk.3:33; 6:3; Yn.2:12).

Iliyo dhahiri ni kwamba mtu haingii katika Ufalme wa Mungu kutokana naukabila wake, kama Wayahudi walivyodhani, ambao walifikiri kwamba ilitoshawawe wazao wa Ibrahimu tu. Imani katika Yesu Kristo ndiyo kanuni ya kuuingiaUfalme wake, na wote wanaoingia ni ndugu zake na ndugu wao kwa wao.

Page 76: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

8:22-25 Yesu alituliza dhoruba (Mt.8:23-27; Mk.4:35-41)Bahari ya Galilaya ilikuwa futi 700 chini ya usawa wa bahari. Ilizungukwa namilima na upepo ulishuka kwa kasi katikati ya milima, hivyo dhoruba kalizilitokea kwa ghafula. Baadhi ya wanafunzi waliokuwa wavuvi waliizoea hiyobahari na kujua tabia yake.

k.22-23 Pengine Yesu aliomba wavuke mpaka ng’ambo ya ziwa ili apate utulivuna nafasi ya kupumzika baada ya shughuli zake nyingi.k.23 Yesu alikuwa mwanadamu kweli na kusikia uchovu mwingi. Baada yakupanda chomboni akashikwa na usingizi mzito, hata dhoruba ilipotokea nachombo kiliyumbayumba majini Yeye aliendelea kulala. Maji yalianza kujaachomboni, na wanafunzi walijisikia kwamba wamo hatarini. Hawakuwa watu wakuogopa upesi bila sababu kubwa. Yesu aliendelea kulala hali amemtumainiMungu, Baba yake, akijua ni Yeye atawalaye mawimbi na upepo.k.24 Kisha, wanafunzi walipomwona Yesu bado amelala, kama hana habari yadhoruba, wala ya hatari iliyopo, wakamwendea na kumwamsha na kumwambiashida yao. Walifikiri kwamba hakika wataangamia. Mara Yesu akaamka nakuukemea upepo na msukusuko wa maji, kukawa shwari kuu. Yesu alimwaminiBaba atamtunza potelea mbali itatokea nini.

k.25 Ndipo mwishowe Yesu aliwauliza juu ya imani yao, imekuwaje waliogopa?Imani yao ilikuwa wapi hasa? Ni kama wameiweka kando walipokabiliwa nashida kubwa. Waliitikia tendo hilo kubwa la Yesu kama wako mbele za Mungu.Waliogopa, wakashangaa, wakaulizana wao kwa wao kumhusu huyu Yesukuwa nani hasa, huyo ambaye wamejitoa kumfuata. Amesema na upepo namaji kwa mamlaka ya nafsi yake, navyo vimemtii. Wameuona uwezo wa Mungukatika tendo hilo la Yesu. Walijua kwa hakika kwamba ni Mungu anayetawalamaumbile; kumbe Yesu pia anayatawala (Zab.89:8ku. 93:3ku. 106:8ku.107:23ku. Isa.51:9). Walikosa kumwamini Mungu, yule anayeyatawalamaumbile. Wayahudi walidhani kwamba nguvu za uovu zimo katika maji naupepo n.k. hata wengine walidhani pepo wamo, hivyo Wayahudi hawakupendabahari hasa. Ukweli wa mwujiza huo ni katika kutokea kwa shwari mara baadaya neno la Yesu. Wanafunzi walipaswa wafahamu kwamba wasingalipata shidahata ikiwa Yesu angaliendelea kulala, hata ikiwa hakuwepo. Walipaswawamwamini Mungu anayetawala maumbile. Jambo kubwa ni kumhusu YesuMwenyewe, yu nani hasa? Yesu aliendelea kufanya maajabu yaliyomfunuakuwa sawa na Mungu.

8:26-39 Yesu alimponya mwenye pepo (Mt.8:28-34; Mk.5:1-20)k.26-27 Baada ya dhoruba kutulia Yesu na wanafunzi walifika kwenye pwani yanchi ya Wagerasi, mahali walipoishi WaMataifa wengi na hapo akatokeamwenyeji mmoja wa pale, mwenye pepo. Alikuwa katika hali mbaya sana,kama hakuwa mwanadamu bali alikuwa kama mnyama, hakuvaa nguo, walahakukaa nyumbani wala hakushirikiana na watu, bali aliishi kati ya wafu

Page 77: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 367

makaburini. Watu walikuwa wamejaribu kumtawala, walimfunga miguuni namikononi, ila kwa nguvu za pepo alizivunja. Watu waliogopa kupita mahali alipo,hivyo aliishi kwa shida sana. Hali yake ilisababishwa na jeshi la pepo waliokuwawamejisitiri ndani yake.

k.28ku. Labda aliona ile dhoruba kali na jinsi ilivyonyamishwa na mtualiyesimama na kuukemea upepo na msukosuko wa maji. Yesu hakuogopakumkaribia. Ajabu ni kwamba, alipomwona Yesu, Kuwepo kwa Yesu kulimtulizakiasi cha kumfanya aanguke mbele zake. Pepo aliye ndani ya yule mtu akapigakelele na kwa sauti kuu aliuliza ‘Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliyehai? Nakusihi usinitese’. Pepo alimtambua Yesu na kufahamu kwamba Yesualikuwa na mamlaka juu yake (4:34,41) na katika hukumu ya mwishoataangamizwa, ila ajabu ni kwamba Yesu amewahi kufanya hukumu kabla yawakati uliodhaniwa (ling.na Mt.8:29).

k.30ku. Ndipo Yesu akamwuliza ‘Jina lako nani?’ pengine Yesu alitaka yule mtuatambue kwamba anayo nafsi yake mwenyewe mbali na pepo zake. Katikakujibu, yule mtu alijitambulisha kwa kutaja pepo kuwa wengi, hivyo jina lake ni‘Jeshi’ kulingana na jinsi alivyotawaliwa na pepo wengi. Yule mtu alikuwa kamasi mwanadamu kwa jinsi alivyolemewa na hao pepo, hata katika maulizano nivigumu kuona kama ni yeye anayesema au ni pepo wanaosema.Pepo walifahamu kwamba hawana la kufanya ila kulitii neno la Yesu, na kwasababu hiyo walimwomba Yesu awaruhusu kujisitiri katika nguruwe (11:24);Yesu akakubali. Neno hilo linawatatiza wengi, kwa nini Yesu aliwaruhusuwaingie nguruwe? Ni vigumu kujua, ila siku ya hukumu yao ilikuwa haijaja bado.Tukumbuke kwamba katika mawazo ya Kiyahudi nguruwe hawakuwa nathamani yo yote, walihesabiwa ni ‘najisi/wachafu’ sawa na pepo (Law.11:7;Kum.14:8).

k.33ku. Yesu alikuwa katika nchi walioishi WaMataifa wengi, yawezekana huyomtu alikuwa Mmataifa. Ilikuwa mwiko kwa Wayahudi kufuga nguruwe ilahuenda mipakani na mahali pa WaMataifa wengi, hawakushika vizuri amri hiyo.Yesu alikubali wamtoke yule mtu na kuwaingia nguruwe. Yesu Mwenyewehakusababisha nguruwe wapotee majini. Labda kwa bahati mbaya pepowaliwatoka nguruwe kwa kelele na kuwashtusha nguruwe na kwa sababuwalikuwa kwenye mtelemko walikimbia kwa kasi na kuingia majini. Pepowalitumia nguvu zao za uharibifu kuwaharibu nguruwe. Kwa Yesu neno kubwalilikuwa uzima na usalama wa huyo mtu aliyekuwa amelemewa mno nao kwamuda mrefu. Katika hayo yote tukumbuke kwamba mtu aliponywa na ni pepowaliosababisha vifo vya nguruwe, si Yesu. Wachungaji waliyaona hayo yote nakwa haraka walikwenda kuwaambia wenyeji habari hizo.

k.35ku. Ndipo wakaja wenyeji ili walione tukio hilo. Bila shaka kwa huzuniwalitazama wale nguruwe wengi waliokuwa wamekufa majini. Pia walimwonayule mtu waliyemfahamu tangu siku nyingi, ambaye wamejaribu kumtawala,

Page 78: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

nao wakashindwa; kumbe ametulia vizuri miguuni pa Yesu, amevaa nguo, naalikuwa ana akili zake. Mabadiliko makubwa sana. Itikio lao lilikuwa kuogopa.Wale watu waliokuwa mashahidi wa hayo yote waliwaelezea wengine jinsi yulemtu alivyoponywa.

k.37ku. Kundi kubwa la wenyeji walifika nao wakamwomba Yesu aondokekwao. Walihofu kwamba akiendelea kukaa miongoni mwao atafanya mambogani kati yao. Walisukumia mbali nafasi yao ya ajabu. Katika kupima kwaowaliangalia nguruwe na kuhesabu thamani yao na hasara iliyotokea bila kufikirikwamba kwa upande wa wanadamu, mwenzao mmoja aliyelemewa sana,aliyepoteza akili, aliyekuwa mkali kuliko uwezo wao wa kumtawala,aliyeshindwa kuishi kati yao, sasa yu mzima kabisa. Jambo hilo lilimfaidia mtumwenyewe, wala si yeye tu, hata familia yake, hata jamii ya wenyeji.Walithamani nguruwe kuliko mwanadamu mwenzao!!

k.38ku. Aliyeponywa alitaka kuandamana na Yesu ila Yesu alikataa, alitakaakae katika nchi yake na kuwaambia wenyeji habari za makuu alivyofanyiwa naMungu (Yesu). Na ndivyo alivyofanya. Ikiwa alikuwa Mmataifa alifaa sanakuwashuhudia WaMataifa wenzake walioishi sehemu zile. Yesu hakuwezakubaki, ila yeye alibaki, na kumshuhudia.

8:40-56 Yesu alimfufua binti wa Yairo na kumponya mwanamke mwenyeugonjwa wa kutoka damu (Mt.9:18-26; Mk.5:21-43)k.40 Yesu aliporudi Kapernaumu watu waliokuwa wakimngojea walimkaribishakwa furaha.

k.41-42 Yairo, mkuu wa sinagogi, akaja, na kwa unyenyekevu akaangukamiguuni pake na kumwomba aje nyumbani kwa sababu binti yake, mwanapekee, wa umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa katika hatari ya kufa. Yesuakakubali kwenda naye, na watu wengi walifuatana nao. Yairo, alikuwamstahivu, mwenye wajibu wa kuzipanga ibada za sinagogi. Katika haja yakekubwa Yairo alijinyenyekeza kwa Yesu na kuomba msaada kwa ajili ya bintiyake.

k.43-45 Walipokuwa njiani jambo lilitokea lililowachelewesha na bila shakaYairo alianza kuwa na wasiwasi juu ya hali ya binti yake, ila hatusikii kwambaalinung’unika. Mwanamke mmoja alikuwa ameugua miaka kumi na miwili naugonjwa wa kutoka damu na katika kutafuta msaada alikuwa amezitumia malizake zote bila kupata nafuu. Tena ugonjwa huo ulimfanya asiweze kushirikianana wengine, kwa kuwa, kwa sheria ya Kiyahudi (Law. 15:25ku) alikuwa najisi naalinajisi kila kitu alichogusa. Hakuweza kuhudhuria ibada n.k. Kwa sababu yahali hiyo aliamua kusogea karibu na Yesu, nyuma yake, kwa siri, na kuugusaupindo wa vazi lake (Hes.15:38-40). Alikuwa na imani kwamba akifanya hivyoitatosha, ataponya, bila kusema lo lote wala kujidhihirisha mbele za Yesu na

Page 79: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 369

watu. Ndipo akaugusa upindo wa vazi la Yesu na mara akajisikia mwilinimwake kuwa amepona, akaanza kuondoka.

Lakini Yesu alitaka kumpa baraka zaidi ya uponyaji, alitaka kumrudisha kwenyejamii ya watu, ili watu wote wajue hakika kwamba unajisi wake umeondoka naamepona kweli. Pia awe na hakika kwamba ni Yesu aliyemponya, si vazi laketu. Budi ajihusishe na Yesu Mwenyewe, isiwe amekutana na nguvu zake tu bilakujitambulisha. Katika kujenga uhusiano naye atamwamini na kupata barakazaidi ya kuponywa. Hivyo Yesu aliliuliza swali ambalo lilionekana kama halinamaana yo yote. ‘Ni nani aliyenigusa?’. Wengi walikuwa wamemgusa, ila si kwakusudi, wala si kama huyo mama alivyomgusa, maana alimgusa kwa shabahaya kuponywa. Watu wote walikana kwamba wamemgusa, na Petro alimwambiaYesu kwamba amezungukwa na watu wengi, haikosi watu wamemgusa.

k.46 Yesu alisisitiza kwamba mtu alikuwa amemgusa, tena kwa kusudi, kwasababu alisikia kwamba nguvu zimemtoka. Hapo twajifunza kwamba uponyajiulimgharimia Yesu nguvu, tena hizo nguvu hazikumtoka moja kwa moja bilaYeye kuamua zimtoke.

k.47-48 Huyo mwanamke alitambua kwamba hakuweza kujificha, Yesualifahamu ni nani aliyemgusa, na sababu zake za kumgusa na matokeo yakumgusa, na alitaka ajitokeze wazi. Ndipo akajitokeza hali akitetemeka,pengine alihofu kwamba katika kuugusa upindo wake amekosa au labdaataondolewa uponyaji wake, au pengine aliogopa jinsi watu watakavyomfikiria.Alianguka mbele za Yesu na kumwambia yote, sababu yake ya kumgusa, naalishuhudia jinsi alivyoponywa mara. Kisha, akaisikia sauti ya Yesu akisemakwa upendo ‘Binti, imani yako imekuponya; enenda zako kwa amani’. Hivyo,Yesu alimthibitishia uponyaji wake na kumwongezea baraka ya amani. Hivyo,aliweza kurudi nyumbani na kuishi kwa amani kati ya watu, huku wote wakijuahakika kwamba ameponywa, wala hana unajisi tena.

k.49-50 Wakati huo wote Yairo aliendelea kumsubiri Yesu aje nyumbani. Ndipomtu akamjia na kusema kwamba hana haja ya kumsumbua Yesu, maana bintiyake ameishafariki dunia. Bila shaka, hapo kati, imani yake ilijengwa alipoonayule mwanamke ameponywa na Yesu, ila sasa habari hiyo ilimkatisha tamaa,hakuwaza kwamba Yesu aweza kumsaidia mtu baada ya kufa. Yesu alikuwaameusikia ujumbe, akamwambia Yairo kwamba hana haja ya kuhofu, yampasaaamini tu, na binti ataponywa.

k.51ku. Walipofika nyumbani ilikuwa dhahiri kwamba binti ameishakufa maanawapiga filimbi wameishafika na kuanza kuongoza maombelezo kamailivyokuwa desturi ya Kiyahudi. Kila mtu aweza kutambua kama mtu amekufaau siyo. Yesu aliwaagiza watu wasilie kwa sababu binti hakufa ila amelala tu.Hakuwa na maana kwamba binti alikuwa bado angali hai, ila kwa sababu alijuahakika atamrudishia uhai wake, alihesabu ni kama amelala tu. Mtu aliyelala

Page 80: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

ataamka, mtu aliyekufa, haamki tena. Wakristo walala tu kwa sababu baadaye‘wataamka’ yaani watafufuka (Yn.11: 11-14; 1 The.4:14). Dalili ya watu kuwa nauhakika wa kifo chake ilikuwa kwamba walimcheka Yesu sana kwa dharau,wakidhani kwamba ameshindwa kutambua kama mtu amekufa au siyo ‘maanawalijua si walidhani ya kuwa amekwisha kufa’.

Yesu alionyesha mamlaka yake hata kwa wakati wa kifo, wakati mgumu.Hakuwaruhusu wengine kuingia chumbani chenye maiti ya huyo msichanaisipokuwa mama na baba na wanafunzi watatu, Petro, Yohana na Yakobo.(Hao walikwenda naye tena alipopanda mlimani na kugeuka sura, na waliingiandani ya Bustani ya Gethsamane).

k.54 Yesu alifanyaje alipofika ndani kwa maiti ya huyo binti. Alimshika mkono,na kupaza sauti, na kusema ‘Kijana, inuka’ na mara akasimama, na roho yakeikamrejea. Yesu alimwagiza afanye yale ambayo hakuweza kufanya hatakidogo. Yesu hakutaka watu wengi wamkazie macho kwa hiyo yeye na wazaziwatulie nyumbani, wampatie chakula na kuendelea kama kawaida.Alipowakataza wasiseme habari hizo si kama wanyamaze kabisa, ilawasisemeseme, watu watajua yaliyotokea, ila wao wenyewe hawana haja yakuzitangaza habari hizo. Yesu hakutaka kuwachokoza viongozi na wale ambaowalikuwa wakitafuta kumpinga. Watu walistaajabu sana, dalili ya kuonyeshakwamba walijua hakika Yesu amemfufua binti huyo kutoka wafu. Hivyo Yesualionyesha mamlaka juu ya ugonjwa wa siku nyingi wa yule mama, na kifo chaghafula cha kijana.

MASWALI1. Yesu alitaka kufundisha mambo gani alipotoa Mfano wa Mpanzi?

Mafundisho hayo yatakuwa msaada gani kwa Mitume na Kanisabaadaye?

2. Wanafunzi walijifunzi nini kumhusu Yesu kutokana na Yesu kutulizadhoruba?

3. Kwa njia mbalimbali Yesu alitaka kuongeza ufahamu wao juu yake =Eleza kwa kutaja njia hizo.

9:1-6 Yesu aliwatuma Mitume kwenda kuhubiri(Mt.10:5-15; 14:1-12; Mk.6:7-29)k.1 Katika 8:1 tuliona kwamba Yesu alipanua huduma yake akienda kuhubirikatika miji na vijiji vya Galilaya. Mpaka hapo Mitume wamekuwa watazamajihalafu hapo twaona kwamba Yesu aliwaingiza katika huduma yake kwakuwatuma peke yao kwenye safari ya kutangaza Ufalme wa Mungu. Maneno‘Ufalme wa Mungu’ huonyesha kwamba wameshirikishwa huduma ileile yaYesu Mwenyewe, pia walitumwa kuwaponya wagonjwa na kutoa pepo.Aliwashirikisha uwezo na mamlaka yake. Aliwapa mwongozo kwa safari hii.Huenda Mitume hawakukaa na Yesu moja kwa moja bila kurudi nyumbani, kwa

Page 81: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 371

sababu wengine walikuwa na wake na watoto na iliwabidi wawaangalie nakuwapatia mahitaji yao. Hivyo twaona kwamba Yesu aliwaita, ndipoakawatuma, akiwapa vyote vilivyohitajika kwa huduma yao. Walipewa uwezona mamlaka juu ya pepo wote, na maradhi. Walikwenda wawili wawili (Mk.6:7).Kwa njia hiyo Mitume walipata ujuzi wa kazi ambayo Yesu atawaachiabaadaye, na kwa njia hiyo habari zake zilizidi kuenezwa. Waliitwa wawe ‘wavuviwa watu’ na katika safari hiyo ndivyo watakavyokuwa.

k.2 Kazi yao ilikuwa kuueneza ujumbe wake wa Ufalme wa Mungu, kuwaambiawatu kwamba, Mungu ni Mfalme mkuu, na kwa njia ya Yesu atakakuusimamisha utawala wake maishani mwa watu. Utume wao ni kuwasaidiawatu kiroho na kimwili, wale wenye pepo na wenye maradhi waponywe. Nenohilo linamthibitisha Yesu kuwa zaidi ya mwanadamu, aliweza kuwapa Mitumeuwezo wake wa kipekee na kuwashirikisha ile mamlaka aliyopata kwa Babayake.

k.3 Kwa sababu ni safari ya mara moja yenye haraka, waliambiwa wasipotezemuda katika kuiandaa vitu vingi. Waende bila kitu cho chote. Waende tu!. Yesualitaja fimbo, mkoba, mkate, fedha, kanzu mbili, akitoboa wazi kwamba nikwenda bila kitu (Mk.6:8 inasema ‘isipokuwa fimbo’ ni vigumu kueleza tofautihiyo). Vitu vilivyotajwa vilikuwa vya kawaida kwa safari. Wamtegemee Munguambaye ataona kwamba watayapata mahitaji yao ya lazima. Kwa hali hiyowataweza kujitia kabisa na kutimiza shabaha ya kwenda kwao bila kufikiriamambo mengine, tena watu wataelewa kwamba hawana shabaha nyingine ilaile ya kazi wazifanyazo. Itawasaidia kujihusisha na maskini ikiwa wao wenyewehawana vitu.

k.4 Wataishije? Watategemea kupokelewa na watu. Katika kukaa na watu,waridhike na mahali walipokaribishwa na hali za wale waliowakaribisha,wasibadilibadili mahali pao. Tena walipaswa wasikae mahali pamoja tu baliwaende mpaka vijiji vingine. Katika kukaa kwa muda mfupi hawatalemea watu.

k.5 Itakuweje wakikataliwa na wenyeji wa mahali fulani? Yesu aliwaambia kutoaishara kwao, ishara itakayowalazimisha kulizingatia tendo lao la kuwakataawale walioleta ujumbe maalum wa kuhusu Ufalme wa Mungu. Iliwaashiriakwamba wametenda tendo zito, wamejitenga na kujiweka nje ya kazianazofanya Mungu kwa njia ya Kristo na kusukumia mbali mwito wa Mungu wakutubu na kumwamini Masihi aliyetumwa na Mungu wao ambaye sasa yumomiongoni mwao. Pia ishara hiyo ilikuwa mwito wa mwisho wa kutubu, uliokuwana haraka wa kuitiwa (Mdo.13:51).

k.6 Mitume walimtii Bwana Yesu, wakazunguka vijijini na kuhubiri nakuwaponya watu kila mahali walipofika. Kwa njia hiyo eneo kubwa lilipatakuisikia Injili. Baadaye Yesu aliwatuma wengine, watu sabini, waliokwenda

Page 82: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kuandaa watu tayari kwa Yeye Mwenyewe kufika kwao (10:1ku). Twajifunzakwamba uinjilisti ndiyo shughuli za kwanza kwa Kanisa.

9:7-9 Shaka ya Herode (Mt.14:1-12; Mk.6:14-29)Kati ya kuwatuma Mitume na kurudi kwao Luka ameingiza habari za MfalmeHerode. Yesu alifanya sehemu kubwa ya huduma yake katika eneo la Galilayalililotawaliwa na Herode kwa ajili ya Dola ya Kirumi. Hapo nyuma alikuwaamemkata kichwa Yohana Mbatizaji, kwa sababu Yohana alimkemea kwadhambi ya kumchukua mke wa ndugu yake. Bila shaka dhamiri yake ilimshtakina aliposikia habari za Yesu na Mitume na jinsi walivyozungukazunguka katikaeneo lake na kuhubiri na kufanya maajabu, Herode alifadhaika, asielewe ni nanihasa ambaye anayafanya hayo yote. Alitaka kujua maoni ya watu, naowaliwataja watu mbalimbali. Wengine walisema kwamba Mbatizaji amefufukakutoka wafu; wengine walisema kwamba Eliya ametokea (taz.Mal.4:5 watuwalidhani yeye atatokea kabla ya Masihi). Wengine walidhani ni mmojawapowa manabii wa zamani (Kum.18:18). Herode angali alitatizwa, hakuwa tayarikuyapokea mawazo hayo. Alijua amemkata kichwa Yohana, kwa hiyo, ilikuwavigumu akubali ni Yohana, kwa hiyo, alibaki akisema ‘ni nani huyu’ - akatakakumwona, ili ajihakikishie kwamba huyo si Yohana.

9:10-17 Kuwalisha wanaume elfu tano (Mt.14:13-21; Mk.6:30-44; Yn.6:1-14)Ni mwujiza huo mmoja tu ambao umeonekana katika Injili zote nne na kwasababu hiyo unadhaniwa kuwa muhimu sana machoni mwa Wakristo wakwanza.

k.10 Mitume walimrudia Bwana Yesu baada ya mazoezi yao, naowakamweleza yote waliyoyatenda. Yesu aliwahurumia na alitaka kuwapatiautulivu pamoja naye, kwa hiyo, waliondoka Kapernaumu kwenda ng’ambo yaBahari mpaka eneo la Bethsaida, mji mashariki kaskazini ya Ziwa la Galilaya,mahali walipotoka Petro, Andrea, na Filipo (Yn.1:44).

k.11 Ila walishindwa kuupata huo utulivu, makutano walipoona kwamba Yesuamevuka, wao nao walimfuata, hata wengine waliwahi kufika kabla yake. Yesuhakuudhika, aliwapokea vizuri, na kuwafundisha na kuwaponya wagonjwa.

k.12 Aliendelea kufanya hivyo mpaka jua lilipoanza kushuka. Mitume walikuwana wasiwasi kuhusu hao watu, watakula nini na kulala wapi? maana palewalipokuwapo hapakuwa na kitu. Wao wenyewe hawakuwa na chakula chakutosha; walikuta mtoto aliyekuwa na mikate mitano na samaki wawili (Yn.6:9)tena hawakuwa na fedha za kutosha kwenda kutafuta chakula (Yn.6:7).Walimshauri Yesu awaage watu ili wajitafutie malazi na chakula.

k.13 Yesu aliwapa Mitume changamoto ya kuwalisha hao watu. Hapo nyumawalikwenda kuhubiri na kutoa pepo na kuponya wagonjwa kwa uwezo wake.

Page 83: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 373

Tena walipokwenda bila kitu hali wakimtegemea Mungu walitunzwa vizuri nawatu. Yesu alitaka wautazame uwezo wao na kujifunza ‘utupu’ wao, hawawezikuzikabili shida za watu kwa uwezo wao na mbinu zao peke yake. Walikuwa namikate michache tu na samaki wawili tu, visivyotosha kuwalisha hao watu.

k.14-15 Ndipo Yesu aliwaongoza la kufanya. Wafanye lile waliloweza, yaaniwawaketishe watu kwa safu za hamsini hamsini ndipo wataweza kuwahudumiavizuri na kwa taratibu. Walimtii Bwana Yesu.

k.16-17 Yesu aliitwaa ile mikate waliyokuwa nayo na wale samaki na mbele yaoalimshukuru Mungu kwa ajili yake. Wayahudi walizoea kutoa shukrani kabla yakula wakisema ‘Ubarikiwe Wewe Bwana Mungu wetu, Mfalme wa Ulimwengu,unaoleta mkate kutoka nchi’. Huenda Yesu alisema maneno hayo au manenoyaliyofanana na hayo. Ndipo akaimega ile mikate kisha akawapa wanafunzivipande vilivyomegwa nao walipitia katika safu za watu na kuwapa. Wotewalishiba, si kama walipata kidogo tu. Hata vilibaki vipande ambavyovingaliwatosha wengine. Vipande vilivyobaki viliushuhudia ukarimu wa Mungu.Huenda swali lilikuwepo Je! wafanye nini na mabaki, ikiwa mikate mitanoiliwatosha umati wa watu, Je! mikate iliyojaa vikapu kumi na viwili itafanya nini?Kwa mwujiza huo wanafunzi walizidi kufunuliwa uwezo wa Yesu. Katika Kristohaja za hao watu zilitoshelezwa kwa njia ya wanafunzi wake kumtii Bwana wao.Wanafunzi walijifunza kwamba wawe na huruma na wawe wepesi wa kusikiashida za watu na kuwatafutia msaada. Wakileta kwake vile vidogo walivyonavyo watafanya makubwa, kwa kuwa Yeye hadharau vile vidogo tulivyonavyo, ila budi viletwe Kwake kwa kupata baraka yake.

Je! watu walielewa tendo hilo la Bwana Yesu? Hatusikii kwamba walisema lolote, Pengine hawakujua chakula kilitoka wapi.

Katika 8:25 Yesu alipotuliza upepo na mawimbi ya bahari walijiuliza ‘ni nanihuyu?’, Herode pia amejiuliza ‘ni nani huyu?’, ndipo mara baada ya kuwalishawatu hao Yesu alipeleka Mitume faraghani na kuwahoji juu ya swala hilo,maana wamepewa nafasi za kutosha kumtambua vizuri.

9:18-27 Petro alimkiri Yesu kuwa Kristo (Mt.16:13-28; Mk.8:27- 9:1)Jambo hilo lilitokea karibu na Kaisari Filipi, chini ya Mlima Hermon, walipoishiWaMataifa, waliomwabudu mungu Pan (Mt.l613) hapo Yesu alipata nafasi yakutulia na wanafunzi wake, nafasi aliyoshindwa kupata alipovuka mpakaBethsaida (9:10).

k.18 Yesu alikuwa mtu wa maombi, alipenda kushirikiana na Baba yake kilawakati na zaidi alipofika hatua kubwa katika huduma yake. Wakati huo Yesuamefika kwenye njia panda katika huduma yake, watu wengi katika eneo laGalilaya wameishapata nafasi ya kumsikia na kumwona na kuona matendoyake makubwa. Ila pia alijua kwamba viongozi wameishaamua kumwondoa,

Page 84: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

hali hawawi tayari kumvumilia kwa vile alivyouvuta usikivu wa watu wengi, naowalimwonea wivu. Hivyo, ilimbidi azidi kuwaandaa wanafunzi wake tayari kwawakati wa kuondolewa kwake, ila kwanza ilikuwa lazima wawe wamemwelewavizuri. Je! wamemfahamu kuwa nani?

Baada ya kumaliza maombi yake Yesu aliwageukia wanafunzi na kuwauliza ‘Jemakutano hao wanasema ya kuwa mimi ni nani? Walimpa majibu yaliyolinganana majibu ya watu wakati Herode alipotaka kujua ni nani aliyekuwa akifanyamambo makuu katika eneo lake (9:9). Walijua maoni ya watu – ama ni YohanaMbatizaji au Eliya au mmojawapo wa manabii n.k. Lakini hasa Yesu hakutakakujua watu wasemavyo ila wao, Mitume wake, wasemavyo, maana hii nimuhimu kwake.

k.20 Moja kwa moja aliwauliza ‘Nanyi mwasema ya kwamba mimi ni nani?’Neno ‘nanyi’ linatawala sentensi hiyo. Petro, bila kukawia, aliwahi kujibu kwaniaba ya wenzake kama ilivyokuwa hali yake. ‘Ndiwe, Kristo wa Mungu’.Wamefikaje kwenye uamuzi huo? Kwa kuandamana naye kwa muda wakutosha kumwangalia vizuri. Wamemwona katika kila hali, ya shida na ya raha.Wamemwona akitenda mambo makuu ya kuponya wagonjwa, kutoa pepo,kutawala bahari, kuwalisha watu wengi na vitu vichache, kumfufua binti Yairon.k. Pia walionja uwezo wake wa kutoa pepo na kuponya maradhi walipotumwanaye kufanya hayo. Pia katika mambo madogo madogo ya kila siku, unyofu naunyenyekevu wake, utayari wake wa kutumika na uvumilivu wake walipokosaraha ya mahali pa kulala au kukosa riziki n.k. Hivyo walikuwa wamejihakikishiakwamba Yeye ni Masihi wa Mungu, yule aliyeahidiwa katika Maandiko. Yesualijua kwamba hawakufikia uamuzi huo kwa uwezo wao wenyewe bali kwamsaada wa Roho Mtakatifu (Mt.16:16-17).

k.21-22 Bila shaka, Yesu alitiwa moyo alipousikia ukiri huo. Ila ilimpasaayanyoshe mawazo yao kuhusu huyo Masihi. Yeye ni Masihi wa aina gani?Wayahudi walizoea kuwaza kwamba Masihi atakuwa mwanadamu hodari,kama Daudi, Mfalme wao wa zamani. Atawaokoa mikononi mwa watawala wao,atawaweka huru, ataliweka taifa lao kuwa la kwanza kati ya Mataifa. Ila Yeye siwa namna hiyo, Yeye si shujaa wa vita kama watu walivyotamani. Ufalme wakesi wa vita, wala hakuja kuliinua taifa lao juu ya mataifa mengine. La, hatakidogo. Yeye amekuja kuuondoa utawala wa dhambi mioyoni mwa watu wote,Wayahudi kwa WaMataifa.

Wanafunzi waliyashiriki hayo mawazo ya Kiyahudi, ila ni vigumu kujuawaliyashiriki kiasi gani, ila itikio la Petro wakati Yesu alipowafunulia kwambaatateswa linaonyesha kwamba mawazo yao hayakulingana na yale ya Yesu(Mt.16.22). Kwa hiyo, mara moja Yesu aliwaonya wanafunzi wake nakuwakataza kabisa kwamba wasimwambie mtu habari ya Yeye kuwa Masihi.Amekubali kuwa Masihi, ila hakutaka wengine, nje ya wanafunzi, walifahamuneno hilo. Hakutaka watu waje na kumshika kwa nguvu, na kumsimika kuwa

Page 85: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 375

Mfalme, kwa sababu wakifanya hivyo wataharibu shabaha ya Kuja Kwake.Kisha akawafunulia yaliyomo katika Yeye kuwa Masihi wa Mungu. Yaliyomo nimateso mengi, kukataliwa rasmi na wakuu (Baraza la Taifa watamhukumu nakumwona kuwa hafai), na kuuawa, na kufufuka kutoka wafu. Hayo ndiyoyaliyomo katika furushi la kuwa ‘Masihi’. Neno ‘imempasa’ laonyesha kwambahayo yote si bahati nasiba, wala ajali, bali ni wito na utume wake. Ilichukuamuda kwa wanafunzi kulipokea neno hilo na Yesu alirudia kulitaja tena na tena.

k.23-27 Kuna msalaba kwa Yeye, pia, kuna msalaba kwa wanafunzi wake. Siyokusema kwamba msalaba wao ni sawa na wa Kwake, si kana kwamba, kilamfuasi wa Yesu atatundikwa kwenye mti, la. Tena mateso yao hayatakuwa kwaajili ya kufidia dhambi za ulimwengu la. Yatatokana na chuki ya watuwasiomtaka Kristo.Msalaba wao ni nini hasa? Ni kuishi kwa kufanya mapenzi ya Mungu simapenzi yao, waseme ‘la’ kwa matakwa yao, wasiishi kwa raha na kwakujipendekeza, bali waishi kwa kumpenda Mungu na kuwapenda jirani zao.Wakubali kugharimiwa maisha yao katika kutumika kama Bwana wao Yesualivyofanya. Yeye alisema ‘sikuja kutumikiwa bali kutumika’; wao vile vilewafuate kielelezo chake. Wakifanya hivi watagundua siri kubwa ya maisha,katika kuipoteza nafsi yake mtu ataisalimisha. Kinyume chake, mtu apendayekuisalimisha nafsi yake na kuitunza hali akiangalia matakwa yake tu, basi, huyomtu atajikuta kwamba ameipoteza. Hii ni siri ya maisha ya kila mwanadamu.

k.25 Hapo Yesu aliuliza swala kubwa ‘yamfaa nini mtu kuupata ulimwenguwote, kama akijipoteza mwenyewe?’. Yampasa mtu azingatie sana maana yakuishi hapo duniani akikumbuka mwisho wake katika uzima wa milele. Hataakipata nini wakati huo ikiwa atabaki mikono mitupu baadaye, itamfaa nini?

k.26 Yesu alitaka kuwatia moyo kwa kuwakumbusha juu ya siku za baadaye,wakati wa hukumu ya mwisho. Katika siku hiyo, Yeye atamkiri kuwa wake kilammoja aliyethubutu kumkiri mbele za watu wakati wa kuishi hapo duniani.Kinyume chake, wale wote waliomwonea haya hapo duniani, waliokosakuonyesha msimamo wao, hao Yesu atawakana mbele za Baba na malaikawatakatifu. Itakuwa thawabu kubwa sana na siku ya fahari kuu kwa wale wotewaliomkiri Yesu hapa duniani. Itakuwa hasara na aibu kubwa kwa wale wotewaliomwonea haya hapo duniani. Mwana wa Adamu ni jina ambalo Yesualipenda kulitumia. Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni wa mbinguni (Dan.7:12ku).

k.27 Kifungu hicho kinatatanisha sana. Watu wamekitafsiri kwa njia nyingi.‘wauone kwanza ufalme wa Mungu’, maneno hayo yanahusu wakati gani?Wengine wafikiri yahusu ‘Ugeuko wa Yesu Mlimani’; wengine ‘Kufa na KufufukaKwake’; wengine ‘Kuja kwa Roho Mtakatifu’; wengine ‘Mwanzo wa Uenezi waInjili’; wengine ‘Anguko la Yerusalemu la B.K.70'. Ni vigumu kujua. Katikamatukio hayo yote, Ufalme wa Mungu ulizidi kusimamishwa katika dunia hiyo.

Page 86: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

9:28-36 Ugeuko wa Bwana Yesu (Mt.17:1-8; Mk.9:2-8)k.28 Luka ametaja kwamba tukio hilo lilitokea kama juma moja baada ya Yesuna wanafunzi wake kuwako huko Kaisaria Filipi. Wakati ule Yesu aliwauliza juuya utambuzi wao kumhusu Yeye Mwenyewe ndipo aliwafunulia habari yaKuteswa, Kufa, na Kufufuka Kwake. Kisha aliwaambia juu ya ‘msalaba’ wao,yaani jinsi itakavyowapasa kuteswa na kuvumilia mengi katika kumfuata kwaukamilifu. Twajua habari hiyo iliwashtua kabisa na kuwa kinyume cha mawazoyao walipomkiri kuwa Masihi.

Baada ya juma moja alitwaa watatu miongoni mwao, Petro, Yohana, naYakobo, nao walipanda mlimani pamoja naye. Ilidhaniwa mlima ni Mlima Tabor,ila shida ni kwamba mlima huo ni mbali sana na Kaisaria Filipi, kwa hiyo,huenda ni mlima Hermon ulio karibu na Kaisari Filipi. (Hao watatu walikwendana Yesu mpaka nyumba ya Yairo Yesu alipomfufua binti yake na baadayewalikwenda naye ndani ya Bustani ya Gethsemane). Yesu alikuwa amefikiahatua kubwa katika huduma yake, wakati umekaribia wa kuanza safari yake yakwenda Yerusalemu mahali ambapo atakataliwa na wakuu na kuuawa. Kwahiyo, alitumia muda huo katika kuomba, alihitaji kushirikiana na Baba na kutiwamoyo na nguvu ya kuukaza uso wake na kushika njia ya kwenda Yerusalemu iliayatimize mapenzi ya Babake. Hivyo, muda huu ulikuwa wa maana sanaKwake.

k.29 Wakati wa kuomba mabadiliko makubwa yalitokea katika sura na haliyake. Kwa muda alirudishiwa ule utukufu wake wa asili aliokuwa nao kabla yakuja duniani. Uso wake uling’aa, na mavazi yake yalimetameta.

k.30 Halafu watu wawili wa zamani, Musa na Eliya, walitokea nao walionekanakatika utukufu. Hao waliishi zamani za Agano la Kale, walikuwa mashuhurukatika historia ya Israeli. Musa ni yule aliyepanda mlimani na kupewa maweyenye Amri Kumi, pia alikuwa kiongozi aliyewaleta Waisraeli kutoka utumwanihuko Misri. Eliya alikuwa nabii wa maana sana. Hivyo walikuwa wakiwakilishaTorati na Manabii na ule ufunuo wa Mungu katika kipindi cha Agano la Kale,tangu Adamu wa kwanza hadi kuzaliwa kwa Adamu wa mwisho. Hatujui ni kwanjia gani wanafunzi waliwatambua, pengine Yesu alipozungumza nao aliyatajamajina yao au walifunuliwa na Mungu. Wote wawili walikuwa wamekutana naMungu mlimani, zamani za kale (Kut.24; 34; 35; 1 Waf.19) walitajwa pamojakatika Malaki 4:4,5).

k.31 Hao walikuwa wakizungumza na Yesu, na ni Luka tu ambaye ametuambiahayo mazungumzo yalihusu jambo gani. Yalihusu Kifo cha Yesu. KufarikiKwake, neno lililotumika ni lile kwa Kitabu cha Kutoka; ishara ya kwamba katikaKifo Chake Yesu atawakomboa wanadamu kutoka utumwa ulio mbaya kulikoule wa Misri, utumwa wa dhambi. Maneno ‘Atakakotimiza Yerusalemu’ yanamaana kwamba atakapokufa Yesu atakuwa anafanya kazi kubwa na kutimizajambo muhimu kabisa kwa maisha ya wanadamu, atazibeba dhambi zao na

Page 87: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 377

kuzifidia na kuwaweka uhuru mbali nazo (1 Pet.2.24). Jambo hilo litafanyikapale Yerusalemu, mahali halisi, na katika siku moja halisi, na litafanyika namwanadamu halisi, Yesu Kristo. Katika mwili wake halisi Yesu ataukomboaulimwengu. Hilo ni neno ambalo lilizungumzwa na Musa na Eliya na Yesu. Nidhahiri kwamba neno hilo ni kubwa mno katika mpango na mapenzi ya Munguna katika huduma ya Yesu. Utukufu na Mateso huwiana hayawi mambo mawiliyasiyopatana. Ilikuwa vigumu kwa wanafunzi na wengine kukubali neno hilo,hao walidhani kwamba Masihi atakuwa shujaa, kumbe ni Mwana Kondoo waPasaka.

k.32-33 Luka baada ya kusema juu ya Yesu na wale wawili alieleza habari zaPetro na wenzake ambao walikuwa wamelala. Walipoamka, walikuta mambohayo, wakatekewa, hawakujua maana yake wala kuelewa ni nini yanayotokea.Petro hakutaka hali hiyo ya utukufu itoweke, wala wale wawili waondoke,afadhali wakae, na yeye na wenzake wawajengee vibanda vitatu ili waendeleekuwepo. Pengine walitaka kuwaheshimu, au walitaka wakae zaidi. Ila Petroalisema tu, hali hakujua la kusema au la kufanya. Ila wakikaa, hakuna safari yakwenda Yerusalemu na kuteswa. Shauri hilo ni kama shauri la kumzuia Yesuasiende Yerusalemu.

k.34-35 Kisha wingu likawatia uvuli, katika historia ya Wayahudi wingu liliashiriaKuwepo kwa Mungu, wakati wa matukio makubwa kihistoria. Waliogopa sana.Ndipo Mungu alisema na wanafunzi kutoka katika wingu hilo. Mungualimshuhudia Yesu kuwa Mwana wake, mteule wake, ambaye iliwapasawamsikie. Tumeona kwamba swala la Yesu kuwa nani liliulizwa na wanafunziwakati wa Yesu kutuliza dhoruba (8:25) halafu liliulizwa na Herode (9:9) ndipoYesu aliwauliza wanafunzi swali hilo nao walimjibu vizuri (9.20). Sasa Munguametia muhuri wake kwenye jibu lao. Yesu ndiye Mwana wake, ni mteule wake,yule aliyechaguliwa kuwa Masihi wa kweli, ambaye kwa Kifo chake ataukomboaulimwengu. Wao walikuwa tayari kumkubali kuwa Masihi, lakini si Masihi wakuuawa, kwa hiyo, maneno ya Mungu, ‘msikieni Yeye’ ni kemeo kwa uzito waowa kupokea neno la kuuawa (Mt.16:22). Msalaba ni kiini cha huduma ya Yesu,ni kazi yake kubwa kupita yote. Pia msalaba wao, wa kujikana na kujitoa kabisaKwake, hata kiasi cha kugharimiwa maisha, ndio wito wao maalum. Katikaubatizo Baba alimhakikishia Yesu kuwa Mwana wake, mpendwa wake naalipogeuka sura ni wanafunzi waliohakikishiwa neno hilo.

k.36 Baada ya Baba kumaliza maneno yake, na Musa na Eliya kuondoka nakurudi mbinguni, ndipo Yesu alibaki pamoja na wanafunzi wake watatu, akiwana hali ya kawaida. Ni mwisho wa kipindi cha Agano la Kale, cha Torati naManabii, na ni mwanzo wa kipindi kipya cha Agano Jipya, cha neema (16:16).Waliondoka mlimani, wala hawakuzungumza jambo hilo na mtu ye yote.Utukufu wa mlimani ulipita na ulibaki mbele ya Yesu njia ya kwendaYerusalemu na kukutana na yote yatakayompata huko, kwa sababu ni kwa njiaya mateso ataingia utukufu wake utakaodumu.

Page 88: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

9:37-43 Yesu alimponya mvulana mwenye kifafa na pepo(Mt.17:14-21; Mk.9:14-29)k.37 Siku ya pili yake Yesu na wanafunzi watatu walishuka mlimani nawalipofika bondeni walikutana na watu wengi sana. Miongoni mwaowalikuwemo wale wanafunzi tisa walioachwa chini.

k.38-39 Katika umati huo wa watu walikuwepo mtu na mwana wake pekee,aliyesumbuliwa na ugonjwa na kifafa na mara kwa mara pepo mchafualimshambulia. Yule mtu aliipaza sauti yake ili Yesu amsikie, akamwomba Yesuamwangalie mvulana wake kwa sababu hali yake ilikuwa mbaya sana, huyobaba alimwelezea shida zake ya kupagawa, ya kupiga kelele, kuwa na kifafa nakutokwa na povu, na jinsi pepo alivyomchubuachubua wakati wa kumwacha.

k.40 Huyo baba alikuwa ameishaomba msaada kwa wanafunzi wa Yesu, ilawalishindwa. Bila shaka hao wanafunzi ni wale tisa waliobaki chini. Haponyuma walipewa uwezo na mamlaka ya kutoa pepo na kuwaponya wagonjwa(9:1). Kwa nini walishindwa? Ni vigumu kujua sababu yake, huenda walipewauwezo kwa ile safari moja tu; au pengine walikosa kuomba (Mk.9:29) auhuenda walikuwa na imani haba. Potelea mbali sababu ilikuwa nini, lililopo nikwamba walishindwa.

k.41 Yesu aliposikia habari ya kushindwa kwao alisema maneno magumu sana‘Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa nanyi na kuwachukulia hatalini?’. Maneno hayo yaliwahusu akina nani? Kwa sababu alitumia neno ‘kizazi’ni kama alikuwa akiwalenga watu kwa jumla, watu wake ambao, muda si muda,watamwondoa. Watu waliitazama miujiza yake bila kuzingatia maana yake,miujiza inayoashiria Nafsi yake na Cheo chake cha kuwa Mwana wa Mungu,Masihi. Walipaswa kutubu na kumpokea hata bila kuyatazama matendo yakemakuu. Pia yawezekana yaliwahusu wanafunzi ambao wamemkiri kuwa Mwanawa Mungu, Masihi. Kama waliamini kwamba ndivyo Alivyo, iliwabidiwamwamini, wakati wa kuwepo na wakati wa kutokuwepo. Kusema ‘hata lini’Yesu alidokezea kwamba anaelekea kumaliza huduma yake na ya kwambajambo linalomsumbua ni ukosefu wa imani.

k.42 Ndipo Yesu aliomba aletewe huyo mvulana, na mara moja pepo mchafualifanya matata yake kwa huyo mvulana, akitambua kwamba ni nafasi yake yamwisho, mbele za Yesu, kwa kuwa Yesu atakapomwamuru amtoke, kwavyovyote lazima atoke.Yesu alimtoa pepo mchafu, na kumponya mtoto na kifafachake, kisha akamrudisha kwa baba yake, hali yu mzima.

k.43 Watu wote wakashangaa kwa sababu walikuwa wameuona ukuu waMungu. Wakati wote Yesu alimtukuza Baba yake, huenda katika maneno hayotwaona dokezo la Yesu kuwa Mungu. Pale mlimani utukufu na ukuu wakeulifunuliwa, na hapo tena, ulionekana, alipomponya huyo mvulana.

Page 89: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 379

9:43b-45 Onyo la pili kuhusu Mateso yakek.43b Iwapo ukuu wake umedhihirika, hata hivyo, baada ya muda mfupi Yesuatakutana na watu waliokaza nia zao kumwondoa, kwa hiyo, alitaka kuuvutausikivu wa wanafunzi wake wasiendelee kuyastaajabu matendo yake makuubali waanze kulizingatia jambo kuu lililo mbele yake, yaani, mateso yake.Amewaambia wazi habari hiyo mara baada ya wao kumkiri kuwa Masihi (k.22).Kwa sababu neno hilo ni geni kabisa kwao, pia ni wazo wasilolipenda, ilimbidiYesu arudie kulisema tena.

k.44-45 Aliwaomba wayashike maneno kuhusu mateso yake. Yesu hakutoboawazi mambo yenyewe yaliyofichwa katika ‘Mwana wa Adamu anakwendakutiwa mikono ya watu’ kwa sababu ameisha kuyasema (k.22). Walikuwawazito sana na waliogopa kumwuliza maana yake. Luka ameandika kanakwamba ilikuwa mapenzi ya Mungu wasilitambue neno hilo. “kutiwa mikono yawatu” maneno hayo yanaashiria mambo mawili. (a) ni mpango wa Munguambao watu hawana habari nao (b) wapo wahusika, watakaomtia kwawahukumu, kama Yuda Iskariote, na viongozi wa taifa ambao watamkabidhikwa Pilato ili atoe hukumu ya kufa kwa kusulibiwa. Mpango wa Mungu namapenzi ya wanadamu hukutana katika Msalaba wa Kristo.

9:46-50 Yesu alitoa mafundisho juu ya unyenyekevu(Mt.18:1-14; Mk.9:33-37)k.46 Yesu alishikwa na mawazo ya mateso yaliyo mbele yake ila wanafunziwalikuwa mbali naye, wao walikuwa wakiwaza ukubwa na ni nani atakayekuwamkuu wao.

k.47 Yesu hakusikia maongezi yao ila alijua yaliyomo mioyoni mwao, na kablaya kusema maneno aliwapa mafundisho kwa njia ya kumtwaa mtoto nakumweka karibu naye. Bila shaka walishtuka kumwona akifanya hivyo, maanawatu hawakuwajali watoto, walidhani kwamba hawana maana, ni dhaifu tu,wenye kuhitaji msaada.

k.48 Mbele yao walimwona Yesu na mtoto kuwa kama ni watu wawili sawa.Halafu Yesu aliendelea kuwaonyesha kwamba kiini cha ukubwa ni kufanana namtoto mdogo. Mtu akitaka kumpokea Yesu hana budi kujinyenyekeza na kuwakama mtoto mdogo. Asiwe na mawazo marefu juu yake mwenyewe. Kilaatakayempokea mtoto kwa Jina lake, atakuwa amempokea Yeye, na zaidi yakumpokea Yeye, atakuwa amempokea Mungu Baba aliyemtuma. Mtu akijifanyakuwa mtoto hatajali mambo ya ukubwa. Atakuwa tayari kutumika, hatatakakuwa mkubwa na kutumikiwa. Yesu alijaa mawazo ya kudhiliwa kwake namateso yake, wao walijaa mawazo ya ukubwa na kukuzwa kwao. Piakumpokea mtoto ina maana ya kumpokea ye yote aliye na hali isiyoheshimiwana kukubalika na watu. Hata mpaka leo, baadhi ya Wakristo husumbuka sana

Page 90: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

juu ya ‘ukubwa’ hata miongoni mwa viongozi, wako wanaojiona eti ‘mimi niaskofu’, au ‘mimi ni mchungaji’, wanapenda kuandika ‘Revd. Fulani’ n.k.wengine wafikirie sana cheo chao, na wengine huwaza kundi lao au dhehebulao, mimi ni Mwanglikana, mimi ni Mkatholiki, mimi ni Mpentekoste n.k. Hatawasio na cheo waweza kujifikiria kwamba kazi wanazozifanya katika mitaa nashirika zina maana kuliko zingine. Hayo yote ni kinyume cha Kristo. Neno hilolinaonyesha jinsi wanafunzi walivyokuwa mbali sana na nia na tabia ya Bwanawao.

k.49-50 Yawezekana mafundisho hayo ya Yesu yalimchokoza Yohana naalikumbuka kwamba wakati fulani yeye na wenzake walimkataza mtu fulaniwaliyemkuta anatoa pepo katika jina la Yesu kwa sababu hakujiunga nao.Labda walimwonea wivu, hatujui. Ila Yesu alimjibu Yohana na kumwambiakwamba hawakuwa na haki ya kumkataza kwa sababu anayetoa pepo kwa Jinalake yu upande wake, wala si kinyume chake. Wawe wanyenyekevu, wawetayari kukubali wengine. Katika 11:23 Yesu alisema kinyume cha maneno hayo‘mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamojanami hutawanya’ ila tukichunguza mazingira ya maneno hayo ni tofauti. Katikavita na Shetani yampasa mtu akate shauri kabisa la kuwa upande wa Yesu.

Yesu alisafiri mpaka Yerusalemu 9:51 – 19:44

Sehemu hiyo ndefu ina habari ya safari ya Yesu kwenda Yerusalemu. HapoLuka ameachana na Injili ya Marko na kuweka mengi ambayo hayamo katikaInjili ya Marko. Luka ameonyesha kwamba Yesu hakwenda moja kwa mojampaka Yerusalemu. Twamkuta katika njia ya mkato, akipitia kati ya Wasamaria.Wakati mwingine twamkuta Yeriko ng’ambo ya Yordani katika eneo la Perea,njia ndefu ya kufika Yerusalemu kutoka Galilaya. Katika 17:11 twamkuta kati yaSamaria na Galilaya. Wataalamu hutoa mawazo mbalimbali katika kufafanuasehemu hiyo. Wako wanaofikiri kwamba Luka amekusanya mambo yaliyotokeawakati mbalimbali bila kujali mfuatano wake. Wengine wawaza kwambazilikuwepo safari mbili, moja ya Yesu kuhudhuria Sikukuu ya Vibanda (Yn.7) nanyingine baadaye alipoanza safari yake ya mwisho kwenda Yerusalemu. (Kwamarejeo kuhusu safari ya kwenda Yerusalemu tazama 9:51, 53; 13:22, 33;17:11; 19:11, 28 pia wazo la njia 9:57; 10:1, 38; 14:25)

Huenda ni vema kujumlisha kwa kusema kwamba hapo twamwona BwanaYesu ambaye anakwenda Yerusalemu kwa mateso yake kulingana na mapenziya Mungu hali akiwafundisha wanafunzi wake na kuwaandaa kwa kazi yao yakuhubiri Injili baada ya Kufa Kwake na Kufufuka Kwake. Yesu yu njiani yakuyatimiza mapenzi ya Mungu na utume wake, na wanafunzi wamo njiani, naowatapewa utume wao. Hapo kati Yesu huwapa mafundisho juu ya kumfuatakwa ukamilifu. Hapo nyuma katika Injili hiyo Luka amesisitiza matendo ya Yesuna katika sehemu hiyo amesisitiza mafundisho yake.

Page 91: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 381

9:51-56 Yesu katika SamariaYesu alikuwa ameandaa tayari kwa safari hiyo. ‘siku za Kupaa Kwake’ nimaneno ya kujumlisha yote yaliyomo mbele zake, Kuteswa na Kuuawa Kwake,Kufufuka na Kupaa Kwake. Hapo nyuma wakati wa Kugeuka sura, Musa naEliya walizungumza naye juu ya Kutoka Kwake, yaani Kifo chake cha Ukombozi(9:31). Atakapopaa na kurudi kwa Baba yake atakuwa ametimiza kwa ukamilifuUtume wake aliopewa na Baba. Kusudi afaulu kuyatimiza mapenzi ya Babailimbii aukaze uso wake kwenda Yerusalemu. Alianza kufanya hivyoaliposhuka mlimani baada ya Kugeuka sura, bila shaka alijaribiwa kurudi mojakwa moja kwenye utukufu wake wa asili, ila alishuka. Kwa sababu paleYerusalemu atakataliwa na kusulibiwa haikuwa rahisi aelekee Yerusalemu,ilimbidi ‘aukaze uso wake’ (Eze.21:2-3). Katika jambo hilo Yesu alikuwa shujaana mkakamavu.

k.52 Kwa sababu Yeye na wanafunzi walikuwa wakipita Samaria walihitajimalazi na chakula. Hatujui wanafunzi walikuwa wangapi, ila bila shaka Mitume12 walikuwepo, na kwa sababu hiyo, waliona vema kuwatuma wajumbe mbeleyao ili watayarishe malazi yao n.k.

k.53 Wayahudi na Wasamaria walikuwa adui, tangu zamani za Ezra naNehemia. Walikuwa wamelijenga hekalu lao huko Gerizimu ili wasiendeYerusalemu kwa Sikukuu. Mara kwa mara Wagalilaya hawakusikia shida,walizoea kupita Samaria kwa sababu ilifupisha safari yao kwenda Yerusalemu.Wayahudi walioshikilia sana dini yao walizoea kuvuka Yordani ili wasipite katikaSamaria wasije wakanajisika. Yawezekana ule uadui wao kwa Wayahudi nineno lililowaongoza kuwakataa Yesu na wanafunzi wake, na hasa walipoonakwamba wanapita tu wala hawatakaa nao kwa muda.

k.54 Lakini wanafunzi walichukizwa sana walipoona Bwana wao amekataliwana wenyeji wa kijiji hicho cha Wasamaria, nao walimtaka Yesu aagize motoushuke na kuwaangamiza. Jambo ambalo nabii Elisha alilifanya zamani za kale(2 Waf.2:10,11). Walimpenda Yesu sana na walisikia wivu kwa ajili yake naheshima yake. Yohana na Yakobo walipewa jina ‘wana wa ngurumo’ na Yesu,huenda walikuwa wakali au waliwaka hasira kwa upesi.

k.55-56 Yesu alifanya nini alipokataliwa? hakutaka kuwalipiza kisasi haowaliomkataa, wala hakutaka wanafunzi wake wawe na tabia ya namna hiyo.Maneno kadha yaliyowekwa katika mraba hayaonekani katika nakala zakwanza za Injili hiyo, hivyo imedhaniwa yaliingizwa baadaye. Hata hivyo,maneno yenyewe yanalingana na mawazo ya Yesu wakati huo. Shabaha yakekuja duniani ilikuwa kuwaokoa wanadamu wote. Yesu hakuudhika, Yeye nawanafunzi waliondoka na kwenda mpaka kijiji kingine.Hivyo Yesu aliwafundisha wanafunzi tabia iliyotakiwa katika huduma yao yabaadaye, watakapowafikia watu mbalimbali na Injili. Haidhuru amekataliwamahali fulani, budi aendelee na safari yake na kufika mahali pengine.

Page 92: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

9:57-62 Watatu walitaka kumfuata Yesu (Mt.8:19-22)Wengi walitaka kumfuata Yesu, hatujui kama hao watatu walitokea wakatimmoja au kila mmoja alitokea wakati fulani na Luka ameziweka habari zaopamoja ili aonyeshe mafundisho ya Yesu juu ya uanafunzi na jinsi Yesualivyosema kwa hao waliotaka kumfuata.

k.57-58 Mmoja alijitoa kumfuata Yesu, akisema kwamba atamfuata ko koteatakakokwenda. Bila shaka ndivyo alivyokusudia. Ila Yesu hakukaa mahalipamoja, alisafiri kutoka hapa mpaka hapa wala hakuwa na mahali pa kukaa nakuhesabu ni nyumbani. Hakuishi kwa raha na utulivu. Kwa hiyo alipomjibu yulemtu, hakumkataa, ila alitoboa wazi gharama ya kumfuata, ajue yaliyomo katikakumfuata vizuri. Twajua Yesu alihudumiwa na kukaribishwa na walewaliompenda, ila maneno hayo yadokezea kwamba Yesu ni yule wakukataliwa, ni mtu aliyekuja kwa watu wake wala hawakumpokea ((Yn.1:11).Budi yule mtu azingatie hayo anapokata shauri la kumfuata.

k.59-60 Halafu Yesu alimwita mtu fulani amfuate. Yule mtu hakukataa ilaaliomba ruhusa arudi nyumbani na kumzika baba yake kwanza. Yesuhakukubali atoe udhuru. Je! baba yake alikuwa maiti nyumbani na Yesualikataa asirudi kumzika? Ni vigumu kufikiri hivyo, maana ilikuwa wajibu wa kilaMyahudi mwanamume kushughulikia maziko ya babake. Hata katika dini yaKiyahudi hakuna wajibu uliotangulia huu, hata ule wa kuhudhuria Hekalu aukuchinja kondoo wa Pasaka. Pengine baba alikuwa amezeeka na muda simuda ilitazamiwa atafariki dunia. Hivyo yule mtu alitaka asubiri nyumbanimpaka baba amefariki, ndipo atakuja kumfuata bila masumbufu yakumwangalia baba, yaani, aiahirishe siku ya kumfuata. Kwa jibu lake Yesualionyesha umuhimu na haraka ya kazi ya kuhubiri habari za Ufalme waMungu. Hakuna jambo lo lote linalostahili kuwekwa kabla yake. Tusimaanishekwamba kukaa nyumbani, na kufanya wajibu za kila siku, kumekatazwa, ilakusiwekwe kuwa sababu ya kumchelewesha mtu katika kumfuata Yesu. Ikiwababa wa yule mtu alikuwa ameishafariki dunia Yesu amezidisha haraka naumuhimu wa kumfuata. ‘acha wafe wazike wafu wao’ wafu hao ni wafu wakiroho, hao waweza kushughulikia mambo yanayotokea katika maisha ya kilasiku. Wako wachache walio hai kiroho wawezao kuendeleza kazi za Mungu.

k.61-62 Halafu tumepewa habari ya mtu mwingine aliyejitoa kumfuata Yesu. Ilaalitaka kwanza awaage watu wa nyumbani mwake. Labda katika kusema hivyokuna hali ya kusitasita. Ila Yesu alimwambia wazi kwamba mtu ambayeamejitoa kumfuata si vema atazame nyuma. Mtu anayelima kwa plau hana budikutazama mbele yake ili alime kwa mstari sawasawa. Hakuna nafasi yakutazama nyuma mtu anapotaka kwenda mbele. Huenda mtu alikumbukahabari za Elisha na Eliya, Eliya alipotwishwa kazi ya Elisha aliomba arudikuwaaga nyumbani, Elisha akakubali. (1 Waf.19:21ku). Lakini Yesuhakumruhusu huyo mtu afanye kama Eliya alivyofanya.

Page 93: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 383

Yesu alisisitiza umuhimu wa kumweka Yeye na kazi yake kabla ya shughulizote zingine, hata shughuli za halali. Yesu alitaka kuonyesha kwamba ikiwa kitufulani kinazidi utayari wa mtu kukiacha, basi atakuta kwamba kumfuata Yesukutazidi uwezo wake. Luka hakutuambia itikio la kila mtu kwa mwito wa Yesu.

10:1-12 Yesu aliwatuma wanafunzi sabini (Ling.Mt.37-38; 10:7-16; 11:21-23)Safari ya kwenda Yerusalemu iliendelea na Luka alitaka kuonyesha umuhimuwa uinjilisti. Ingawa Yesu alikuwa ameukaza uso wake kwenda Yerusalemuhata hivyo hakuweka kando shughuli za uinjilisti, kazi ambazo ni malimbuko yakazi ya Kanisa zilizoandikwa katika Matendo ya Mitume. Alitoa habari ya watusabini waliotumwa na Yesu, ni habari inayopatikana katika Luka tu. Inafananana kutumwa kwa Mitume (9:1-6) na mengine yanafanana na habari yaKuwatuma Mitume katika Mathayo. Muda ulikuwa ukiendelea na miji mingibado haijafikiwa. Hao sabini walikwenda mbele yake ili watayarishe watu kwakufika kwake. (Ama walikuwa 70 au 72 - nakala zingine za zamani zasema 70na zingine 72. Nambari hii inalingana na wakati wa Musa (Kut.24:1-9;Hes.11:16ku.24ku) wazee sabini walipanda na Musa na wawili walibakikambini). Wengine huona hesabu hiyo inalingana na majina ya mataifa 70(Mwa.10). Wazo ni kwamba walitumwa ng’ambo ya pili ya Yordani, mahali paWaMataifa wengi. Yesu amekwisha kuzunguka katika Galilaya na kupitia katikaSamaria. Walikuwa akina nani? Je! Mitume walikuwa miongoni mwao? Hatujui.

k.1 Luka amemwita Yesu ‘Bwana’. Kuwatuma wawili wawili ni kuuthibitishaushuhuda wao na uhalali wao wa kuwa mashahidi wa Yesu. Sheria ya Kiyahudiilisema kwamba ni lazima mashahidi wawe wawili, tena ushuhuda waohupatana (Law.19:17; Kum.19:15).

k.2 Sababu ya kwenda ni uhaba wa watumishi; kulingana na wingi wa mavuno,watenda kazi ni wachache. Iliwapasa watu wamwombe Bwana mwenyemavuno hayo awatume watenda kazi katika mavuno yake. Neno ‘mavuno’linaleta wazo la haraka, maana mavuno hayawezi kusubiri mpakawamepatikana wavunaji. Wakati wote watumishi wa Mungu wapaswakukumbuka kwamba kazi ni Yake hasa. Yesu alitaja mavuno katika Mt.9:37;Yn.4:35

k.3 Aliwaambia hao sabini waende na aliwatahadharisha juu ya upinzaniwatakaokuta, nao wapaswa kufanana na wanakondoo, hawana nguvu yakuwakabili wale waliotaka kuwadhuru. Aliwaonya juu ya hatari iliyo mbele yao,hatari itakayokuwapo kwa watumishi wa Mungu kila wakati na kila mahali.k.4 Kwa sababu safari yao ina haraka, maana Yesu alikuwa anakuja nyumayao, iliwabidi wasilemewe na vitu vingi, waende upesi bila kubeba mifukomizito. Huenda maana yake kuhusu viatu ni kwamba wasichukue njozi ya pili, sikwamba wasivae viatu. Mfuko ulihusu fedha, mkoba ulihusu ubebaji wa vitu vyasafari. Tena njiani wasipoteze muda katika kuwaamkia watu kwa maneno

Page 94: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

mengi. Si kwamba wakose adabu, bali wasikawie, maana wanazo shughuli zaharaka. Kujitoa na haraka vimewekwa pamoja (9:60).

k.5-6 Watakapoufikia mji fulani watafute mahali pa kukaa, na mtu akiwa tayarikuwakaribisha wamsalimie kwa salaam za amani na yule mtu akiwa mtu waamani ndipo amani itamkalia; la, siye, amani itamrudia yeye aliyeitoa salaam.Inaonyesha kwamba maneno ya salaam yalikuwa na nguvu, hayakuwa manenomatupu tu, yalileta baraka kwa aliyeyapokea. Tena ilikuwa na maana kubwakwamba katika salaam zao zimefichwa amani na wokovu wa Yesu.

k.7-8 Waridhike na chakula na malazi waliyopewa, wasiulize maswali juu yachakula n.k. hasa ikiwa walikaa kwa watu wa Mataifa (Wayahudi walikuwa namiiko juu ya vyakula fulani). Wajue kwamba, kama wafanya kazi, wamestahilikupewa riziki zao, ila wasitafute kula kwa anasa, wala wasitumie muda katikakutafuta mahali pazuri zaidi. Wakifanya hivi watakosa kuuonyesha mzigo juu yautume wao, watu watadhani kwamba wamekuja kwa faida ya binafsi tu. Lazimahali zao zote ziwasaidie watu kufikiri kwamba wameletewa ujumbe maalumkabisa, ujumbe wa Ufalme wa Mungu.

k.9 Walipewa uwezo wa kuwapoza wagonjwa, dalili ya kuwa Ufalme wa Munguumekuja kwa nguvu. Ni wakati wa nafasi ya kuingia katika Ufalme wa Mungukwa njia ya kuupokea ujumbe wa wanafunzi hao. Budi watu waujali ujumbewao.

k.10-12 Wafanye nini kwa wale waliokataa ujumbe wao, ambao hawatampokeaBwana Yesu atakapofika kwao? Wapitie katika njia za mji ule na kuyakung’utamavumbi yaliyogandamana kwenye miguu yao, wakisema kwa wazi kwamba,hata ikiwa watu wamekataa kuwapokea, hata hivyo, walipaswa wajue hakikakwamba Ufalme wa Mungu umewakaribia. Ilikuwa ishara ya kuwaashiriakwamba wametenda tendo zito litakalosababisha hukumu ya Mungu. Si kanakwamba wamewakataa wanafunzi bali tu pia wameukataa Ufalme wa Mungu, nikama kusema kwamba hawakutaka kujihusisha na Ufalme unaoletwa na Yesu.Zamani za kale hukumu ya Sodoma ilijulikana sana na kusemwa sana katikahistoria ya Israeli, ila wale watakaomkataa Yesu na wajumbe wake watastahilihukumu kubwa zaidi (Mwa.19:13,24ku).

Katika habari hiyo twaona Yesu amesisitiza tena jinsi ambavyo wafuasi wakewapaswa kujitoa kabisa Kwake, wakubali kufanya kazi kwa bidii, wawe tayarikukabili hatari na shida, wawe na nia iliyokazwa na watoe kwa wazi ujumbe waInjili. Yesu alikuwa mtu wa shughuli nyingi pia alikuwa tayari kuwashirikishawengine kazi na uwezo wake.

Page 95: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 385

10:13-16 Yesu alitamka ole juu ya miji iliyomkataak.13-16 Yesu alitaja miji mitatu hasa, miji katika eneo la Galilaya, ambaowenyeji wake hawakuitikia vema Yesu alipofanya kazi kati yao. Hatuna habariyo yote ya Yesu kuwepo Korazini, mji uliokuwa karibu na Kapernaumu. Hivyo,katika Injili Nne hatuna habari zote za Yesu na huduma yake. Bethsaidaumetajwa kidogo, na Kapernaumu ni mahali ambapo Yesu alifanya shughulinyingi za uponyaji n.k. ni hapo alipoweka kituo chake (Mt.9:1). Iliyopo nikwamba miujiza iliyofanyika ilikuwa na shabaha ya kuwaleta watu kwenye tobana kumwamini Kristo. Watu walipouona uwezo mkuu wa Yesu walipaswakumwamini na kujikabidhi kwake, ila haikutokea hivyo kwa wengi waliomsikia.

Je! itakuwaje kwa miji hiyo? hali yao ya mwisho itakuwa mbaya kuliko ile yaTiro na Sidoni, miji ya zamani iliyoukataa ujumbe ulioletwa na manabii. Kwasababu gani itakuwa hivyo? Ni kwa sababu kama wenyeji wa Sodoma naGomora wangalijaliwa kuiona miujiza iliyofanywa na Yesu, wangalitubu kweli.Ni vema kukumbuka kwamba Kapernaumu na miji mingine sasa imekuwamagofu tu.

k.16 Yesu alisisitiza tena uhusiano mkubwa kati yake na ujumbe wake na walewanaotumwa kuutangaza. Katika kuwapokea wanafunzi watu walikuwawamempokea Yeye, wala si Yeye tu, hata na Baba aliyemtuma. Vivyo hivyowaliowakataa, walikuwa wamemkataa Yeye aliyewatuma pamoja na kumkataaMungu Baba, aliye asili ya utume wote. Mara kwa mara Yesu alirudia kusemajambo hilo (Mt.10:10; Yn.13:20).

10:17-24 Kurudi kwa wale sabini (Mt.11:25-27; 13:16ku)Hatujui wale sabini walikwenda kwa muda gani, yawezekana Yesu aliwapamuda wa kufanya hiyo kazi na kusema mahali pa kukutanika baadaye. Walirudikwa furaha sana, hali wamefanikiwa katika safari zao. Walipata ujuzi wa ajabuwa nguvu za kiroho, hasa walivutwa na uwezo wa kutoa pepo kwa Jina la Yesu.Hatusikii lo lote juu ya mahubiri yao. (Yesu alipowatuma hatukusikia kwambaaliwaagiza juu ya kutoa pepo).

k.18 Yesu alifurahi sana aliposikia habari zao, aliona kwamba katika mafanikioyao ya kutoa pepo, ipo dalili ya Shetani kushindwa, enzi yake kushambuliwa,kama kwa ghafula na bila enzi zile kutazamia itakuwa hivyo.k.19 Ndipo Yesu alisisitiza kwamba ameishawapa amri juu ya nguvu zampinzani wake mkuu Shetani. Nyoka na nge ni lugha ya kuelezea nguvu kali naza hatari za yule mwovu. Wamepewa amri na uwezo wa kutoa pepo.

k.20 Hata hivyo, Yesu hakutaka waijenge furaha yao juu ya jambo hilo ambalolina muda. Waijenge katika jambo lidumulo hata milele, wafurahi kwa sababumajina yao yameandikwa mbinguni. Kipaumbele cha kwanza ni hicho. Hatawengine watatoa pepo bila majina yao kuwa yameandikwa mbinguni (Mt.7:11).

Page 96: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

Shabaha ya kwanza ya Yesu ni kuwarudisha watu kwa Mungu ili wapate mahalipa usalama katika Ufalme wa Mungu.

k.21 ‘Saa ile ile’ maneno hayo yanaonyesha uhusiano mkubwa na habari yawanafunzi sabini kurudi kutoka safari zao hali wakiwa na furaha kubwa kwaujuzi wa kibinafsi waliopata katika huduma yao. Maneno yafuatayo ni itikio laYesu kwa yote waliyomwambia. Kwa msukumo wa Roho Mtakatifu alishangilia,yaani furaha yake ilizidi, na alisema moja kwa moja na Mungu Baba yake,Mungu wa rehema na Mungu mwenye nguvu, atawalaye mbingu na nchi.Alisema nini? Alimshukuru. Alimshukuru kwa ajili ya nini? Kwa sababu katikampango wake ameamua kuwatumia wale wanaojinyenyekea, watu wasiojiona,walio tayari kuupokea ufunuo wa kweli juu yake. Akina Mafarisayo na waandishikwa sababu ya kiburi chao wamenyimwa ujuzi huo kwa kuwa walidhanikwamba walijua mambo ya Mungu.Yesu amewafunulia wanafunzi wake, watuambao hawakusoma katika shule za marabi. Walijitoa kwake kwa imani, naalipowatuma walikwenda na kufanya kama alivyowaamuru, nao walionja uwezowake wa kuwatoa pepo na kuwaponya wagonjwa. Yesu alisikia radhi nampango huo wa Mungu. Hakuudhika, eti, viongozi wa dini na mashuhuri katikaTaifa hawakumpokea. Akakubali huo mpango wa Mungu kwa kuwawamepatikana wale waliompokea na kumtii. Hapo twaona mgongano kati yahekima ya dunia hii na hekima ya Mungu.

k.22 Halafu Yesu alishuhudia jinsi alivyokabidhiwa yote na Baba. Maana yakeamepewa ujuzi kamili na wa kipekee kwa njia ya uhusiano wake wa ukaribusana na Baba, Yeye na Baba wanao umoja mkamilifu, kwa hiyo Yesu anaoujuzi wa ndani (Yn.3:35; 13:3). Ufunuo huu Yesu ameruhusiwa kuwashirikishawale wenye hali ya unyenyekevu wa kuupokea. Uhusiano kati ya Baba naMwana ni wa kipekee, hakuna awezaye kuingia kati, hakuna awezayekuwavamia. Hayo yote ni mikononi mwa Baba na Mwana. Ni Mwana, pekeyake, awezaye kumfunua Baba. Kweli iliyo muhimu ni kwamba Mungu ni sawana jinsi Yesu alivyomfunua (Yn.14:7,9). Ujuzi huo ni wa kibinafsi si wa akili.Inaonekana wanafunzi wake walikuwa wameshika kweli za kumhusu Kristo naUfalme wake kutokana na safari zao.

k.23 Inaonekana maneno ya k.21 na k.22 yalisemwa masikioni mwa watu ndipoYesu aliwageukia wanafunzi na kuwaambia hayo ya k.23 wakiwa faraghani.Hasa alitaka kusisitiza baraka na uheri wao katika kuishi na kushirikiana nayekwa ukaribu. Manabii na wafalme walimtazamia kwa mbali, ila wao wamejaliwakumwona kwa macho yao na kumsikia kwa masikio yao. Walijaliwa heshima yahali ya juu.

Page 97: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 387

10:25-28 Mwana sheria aliuliza juu ya uzima wa milelek.25-26 Yawezekana Yesu alikuwa katika kufundisha kwa sababu huyu mwanasheria alikuwa ameketi ndipo akasimama na kumwuliza Yesu swali kuhusuuzima wa milele.Neno ‘amjaribu’ huenda nia yake haikuwa safi alipomwuliza Yesu swali hilo.Yawezekana alidhani kwamba Yesu atashindwa kutoa jibu sahihi ndipoataonekana kuwa mtu asiyestahili kuitwa ‘rabi’. Twaweza kusema kwambaalitaka kuona Yesu atasema nini kuliko kujibiwa swali lake. Lilihusu utendaji‘nifanye nini’, swali la maana sana, hakuna swali la maana kuliko hilo, na bilashaka mara kwa mara Yesu aliulizwa swali la namna hiyo. Alitaka kujua mtuafanye nini ili aurithi uzima wa milele. Kwa sababu alikuwa mwana sheria Yesualimrudisha kwenye Torati ambayo aliijua na kuipenda sana, daima ilikuwa kaziyake ya kuichunguza hiyo Torati. Yesu alitaka kujua amefika wapi katikauchunguzi wake, na kuona kama amepata mwanga wo wote wa kumsaidiakuelewa jinsi uzima wa milele upatikanavyo.

k.27-28 Kwa kweli huyo mwana sheria alikuwa ameelewa vizuri sana kiini chaTorati. Alijua kwamba Torati humwelekeza mtu kumpenda Mungu kwa hali zakezote, na kumpenda jirani yake kama nafsi yake. (Hata Yesu alitoa jibu la namnahiyo kwa mtu mwingine aliyemwuliza juu ya amri ipi iliyo kubwa Mt.22:37;Mk.12:29-31). Twaona kwamba baadhi ya Wayahudi walikuwa wameunganishamaneno ya Kum.6:5 na Law.19:8 kama Yesu alivyofanya. Kumpenda jiraniyako kama nafsi yako ni kumpenda jirani kwa jinsi unavyojipenda, haina maanaumpende kwa kiasi kile unachojipenda. Yesu aliunga mkono jibu lake nakumwambia kwamba amejibu vema. Kuishi maisha ya upendo ni kiini cha Toratina njia ya kupata uzima wa milele. Kisha Yesu alimwambia ‘fanya hivi naweutaishi’. Ni katika kufanya, si katika kujua, mtu hujaliwa kufika kwenye uzima wamilele.

(Ila tusifikiri kwamba Yesu alifundisha kwamba mtu huokolewa kwa matendomema, la! Maandiko yote huonyesha kwamba haiwezekani mtu ayatimizematakwa hayo ya Torati. Ndiyo sababu Yesu alikuja duniani ili kwa neema yakeatujalie nguvu ya kuitimiza Torati. Yeye anatupokea kwanza ndipo anatazamiatuishi maisha ya upendo. Kwa Torati mtu hapokelewi mpaka amezitimiza sheriazake).

10:29-37 Mfano wa Msamaria mwema(Mfano huo hupatikana katika Luka tu)k.29 Yawezekana yule mtu alitekewa na jibu la Yesu na dhamiri yake ilimshtakikwamba ameshindwa kumpenda jirani kama nafsi yake, hivyo aliendeleakuzungumza na Yesu akitaka kujua ‘Na jirani yangu ni nani?’. Alitaka Yesuatoboe wazi ni yupi hasa aliye jirani yake. Tukumbuke ya kwamba katikamawazo yao walikuwa na mpaka katika kupenda watu. Waliwapenda Wayahudiwenzao huku waliwachukia WaSamaria na WaMataifa.

Page 98: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.30 Yesu alimhadithia habari ya Myahudi fulani aliyepatikana na mabayakatika safari yake ya kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Njia hiyo ilijulikanasana kuwa mahali pa wanyang’anyi waliojificha miambani, maanahapakukaliwa na watu. Ilikuwa maili 17 kutoka Yerusalemu mpaka Yeriko,kwenye mtelemko wa futi 3,300. Makuhani wengi walikuwa na nyumba zaohuko Yeriko, wakija na kurudi Yerusalemu kila wakati. Huyo Myahudi alivamiwavibaya na wanyang’anyi, zaidi ya kuchukua mali yake, walimdhuru sana hataalielekea kufa.

k.31 Kwa bahati nzuri yeye hakuwa msafari peke yake siku ile. Mwinginealikuwa kuhani, na bila shaka Myahudi mwenzake aliyejeruhiwa angejipa moyoakitazamia atamsaidia. Ila alipofika pale na kumwona, hakumjali, akapitiakando. Hakumfanyia msaada. Bila shaka ilitazamiwa kwamba atamsaidiamwenzake aliye katika hali mbaya, kama sheria ilivyosema ‘mpenda jirani kamanafsi yake’. Kwa nini hakumsaidia? Yawezekana alihofu kwamba walewanyang’anyi wangalipo karibu nao watamvamia yeye pia. Yawezekana piaalidhani huyo mtu amefariki dunia na akiigusa maiti yake atanajisika(Law.21:1ku). Au, pengine alikuwa na shughuli zilizomhitaji aendelee na safariyake bila kukawia. Potelea mbali alikuwa na sababu gani alikosa kuitimiza toratiiliyosema ‘mpende jirani yako kama nafsi yake’.

k.32 Lakini, baada ya hapo, akaja msafiri mwingine, yeye naye mtu wa dini,Mlawi. Bila shaka mjeruhiwa alijipa moyo tena akitazamia msaada kutoka huyomaana huyo naye aliifahamu hiyo sheria juu ya kumpenda jirani kama nafsiyako. Yeye naye alifanya kama yule kuhani alivyofanya, akapita kando bilakutoa msaada wo wote. Pengine kwa sababu zile zile za kuhani.

k.33-35 Bila shaka mwana sheria alitazamia kwamba hapo Yesu atataja mtu watatu kuwa Myahudi, asiye kuhani, wala Mlawi, ambaye ni raia tu akidhanikwamba ni desturi ya Yesu kusema dhidi ya wahusika na dini. Kumbe! ajabu nikwamba alimtaja Msamaria, ambaye hakujua hiyo sheria juu ya kumpendajirani kama nafsi yako. Tofauti na wale waliojua sheria, alimhurumia,akamkaribia na kumshughulikia, hata kiasi cha kumpandisha juu ya mnyamawake kwa vile alivyoshindwa kutembea, huku yeye alitembea chini, wakafikakwenye nyumba ya wageni. Hata hakumwacha kwa haraka, akakaa naye kwasiku ndipo kesho yake aliendelea na safari yake, huku amemkabidhi mwenyenyumba pesa za kutosha kumtunza huyo Myahudi na kuahidi atalipa zaidiikitakiwa, atakapopitia pale tena. Kama asingalikuwa katika shida sana bilashaka huyo Myahudi asingalikubali ahudumiwe na Msamaria, ila kwa sababuya kushindwa kuendelea na safari alifurahi kuhudumiwa na huyo. Mawazo yakemabaya juu ya WaSamaria yalibadilika, akajifunza kwamba huyo amekuwamwema kwake, ameitimiza torati ya Kiyahudi. Basi, jambo hilo lilikuwa la ajabusana. Alionyesha upendo usio na mpaka wa utaifa au tabaka. Hakuchaguaamhurumie nani na nani, alipomkuta mwanadamu mwenzake katika shidaalimhudumia.

Page 99: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 389

k.36 Kisha Yesu alimwuliza mwana sheria jinsi alivyojisikia kuhusu habari hiyo,na ni yupi katika hao watatu aliyekuwa jirani, Myahudi, kuhani; Myahudi, Mlawi,au Msamaria? Hasa swali ni ‘Nani alitimiza Torati ya kumpenda jirani?’.Msamaria, asiye safi machoni mwao ndiye ametimiza Torati. Yesu hakumjibukwa kusema ‘Fulani na Fulani’ ni jirani yako bali alimwonyesha kwamba budiyeye mwenyewe awe jirani mwema. Ahitaji kufanyiwa upya moyoni mwake iliaonyeshe upendo wa aina hiyo.

k.37 Mwana sheria, alijua hakika ni nani aliyekuwa jirani, ni yule aliyemwoneamwingine huruma. Hakusema ‘yule Msamaria’ kwa sababu angalisikia shidakutaja Msamaria. Yesu alimwambia aende zake na kuwa jirani mwema nakuonyesha upendo kwa mtu ye yote bila ubaguzi. Yesu hakutaka abaki na‘ujuzi’ bali awe mtekelezaji wa yale anayoyajua. Lazima atazame mambo kwaupande wa wale wanaopata shida.

10:38-42 Yesu nyumbani mwa Martha na Mariamu(Habari hii ni katika Luka tu)Yafikiriwa kwamba habari hii ilitokea wakati mwingine, wala si katika mfuatanowa matukio ya sura hiyo. Twajua Martha na Mariamu waliishi katika kijiji chaBethania, maili mbili tu kutoka Yerusalemu (Yn.11:1) ila katika 17:11 Yesualikuwa angali mbali na Yerusalemu. Yawezekana jambo hilo lilitokea katikasafari mojawapo alipokwenda Yerusalemu, si safari yake ya mwisho.

k.38-39 Yesu alikaribishwa na Martha nyumbani kwake, inaonekana ni yeyemwenye nyumba, na Mariamu huenda alikuwa mdogo wake. Katika kumpendaYesu na kumtumikia Martha aliona vema afanye shughuli nyingi na kuandaliachakula cha aina aina, maana alihangaika kwa utumishi mwingi. Ila Mariamukatika kumpenda na kumtumikia Yesu aliona vema aketi miguuni pake kamamwanafunzi na kumsikiliza.

k.40 Lakini Martha hakupendezwa na umbu lake, akanuna, kwa sababu alikuwaamemwacha kuandalia chakula. Pengine Mariamu alikuwa amemsaidiamwanzoni na kumwacha alipoona kwamba shughuli zimezidi na Yesuameachwa peke yake. Pamoja na kununa juu ya Mariamu alinunu pia juu yaYesu ambaye alikubali Mariamu aketi muda huo wote miguuni pake bilakumwelekeza amsaidie. Kwa maneno ‘huoni vibaya’ ‘basi mwambie anisaidie’alikuwa akimkemea Yesu hata kumshauri aseme na mdogo wake. Hivyotwaona tofauti kati ya hao wanawake, mmoja akimwambia Yesu afanye nini namwenzake anamsikiliza Yesu na kuona asemavyo.

k.41-42 Kwa upole na kwa nguvu Yesu alimsahihisha Martha. Alimwonyeshakwamba alikuwa amepata shida kwa sababu ya ‘vitu vingi’ huenda maana yakeni kwamba alikuwa akiandaa vyakula mbalimbali, na Yeye angaliridhika nachakula kimoja tu. Ndipo alionyesha kwamba Mariamu hakuwa na kosa katika

Page 100: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kukaa miguuni pake. Alikuwa ameishika nafasi ya kijifunza mambo ya kirohomaadamu nafasi ipo, kwa sababu nafasi za namna hiyo ni chache. Katikautambuzi wa kiroho Mariamu alikuwa amelichagua fungu jema ambalo barakazake ataendelea kuwa nazo. Chakula hakilingani na kusikia Neno la Mungu.Kuwa mkaribishaji wa mgeni ni vema lakini pia budi mtu aukaribishe huoujumbe unaoletwa na mgeni hasa kwa sababu mjumbe huyo ni Mwana waMungu, mwenye kuleta wokovu nyumbani wa mtu (19:1ku).

Wote wawili walitaka kumheshimu Yesu, kumtumikia na kumwonyesha upendo.Kila mmoja alichagua njia yake ya kufanya hivyo. Kosa la Martha halikuwakatika kuandaa chakula bali kuhangaika na vyakula vingi, aina aina, ambavyoYesu hakuvihitaji. Yesu alikuwa radhi na chakula kimoja tu. Alitaka kuwasaidiawanawake hao na mafundisho yake si kula kwa anasa. Katika utulivu wanyumba hiyo aliweza kutulia vizuri na kuwafundisha. Jambo muhimu nikumsikiliza kuliko kuandaa karamu kubwa. Twajifunza kwamba shughuli zetuzisizidi kiasi kile ambacho kitatunyima nafasi ya kuomba na kusoma Neno lake.Twapaswa kujifunza uwiano ufaao kati ya ibada na shughuli, wala tusifikirikwamba ni ‘ama’ kuketi miguuni pa Yesu’ ama ‘kuandaa chakula’ la! vyotevyahitajika kwa uwiano ufaao.

MASWALI:1. Eleza kwa ufupi ni jambo gani lililotokea Yesu na wanafunzi walipokuwa

katika nchi ya Wagerasi. Yesu alikuwa na uwezo gani? Kwa niniWagerasi walimwomba aondoke mipakana mwao?

2. Kwa Yairo na familia yake Yesu alionyesha uwezo gani?3. Kwa nini Yesu aliwaingiza Mitume katika mwujiza wake wa kuwalisha

watu wengi na chakula kidogo? Alitaka wajifunze nini hasa?4. Eleza umuhimu wa Mitume kumtambua Yesu kuwa nani? Yesu alikuwa

amewasaidia hatua kwa hatua kumwelewa kwa njia gani?5. Mara baada ya Petro kumkiri kuwa Kristo Yesu aliwafunulia jambo gani

ambalo lilikuwa geni kabisa kwao.Ni nini siri ya maisha ya Kikristo? Mkristo atakiwa kuishi kwa hali na tabiagani?

6. Yesu alipogeuka sura mlimani ni nani waliotokea na kuzungumza naye?Eleza maana ya hao kumtokea. Pia walikuwa wakizungumza neno gani?

7. Wakati huo Mungu alitoa ushuhuda gani juu ya Yesu kwa Mitume nakuwaambia wafanye nini?

8. Wale Mitume tisa waliobaki chini walishindwa kufanya nini? Yesualisema sababu ya kushindwa kwao ilikuwa nini?

9. Kwa nini Wasamaria hawakuwa tayari kumkaribisha Yesu? Yohana naYakobo walitaka kufanya nini? Yesu aliwajibuje?

10. Twajifunzi nini kuhusu kuwa mfuasi wa Yesu kutokana na majibumbalimbali ambayo Yesu alitoa kwa wale watatu waliotaka kumfuata?

Page 101: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 391

11. Yesu aliwatuma wale sabini kufanya nini? Walipaswa wawe na hali gani?Kwa nini watoe ishara ya kuyakung’uta mavumi kwa miji iliyowakataakupokea ujumbe wao?

12. Wale sabini waliporudi kwa Yesu na kutoa habari za mafanikio yao, Yesualifanyaje?

13. Alitaka wajenge furaha yao katika jambo gani? Kisha alijishuhudia ninijuu yake na uhusiano wake na Baba?

14. Yesu alisemaje kwa mwana sheria aliyetaka kupata uzima wa milele?Eleza kwa ufupi.

15. Kwa nini Yesu alitoa Mfano wa Msamria Mwema? Alitaka kufundisha ninihasa?

16. Twajifunza nini kutokana na habari ya Martha na Mariamu?

11:1-13 Mafundisho ya Yesu kuhusu MaombiLuka alikuwa na moyo wa kupenda maombi na kila wakati katika Injili yakeametaja jambo hili. Katika sehemu hiyo ametoa mafundisho ya Yesu juu yamaombi. Alianza kwa kutoa ‘Sala ya Bwana’. Sala hii imeonekana pia katikaMathayo (6:9-13) katika Mathayo ni ndefu kuliko hiyo ya Luka. Yadhaniwakwamba Yesu alifundisha Sala hiyo zaidi ya mara moja, pengine hakutoamaneno yale yale kila wakati. Katika Mathayo Yesu alipinga desturi ya ‘unafiki’na jinsi WaMataifa walivyoomba kwa kurudiarudia maneno bila maana(Mt.6:5,7) kwa hiyo Yesu alisema ‘Bali ninyi salini hivi’. Katika Mathayo ilitolewamapema katika huduma ya Yesu, wakati wa Hotuba ya Mlimani. na katika Lukani baadaye.

Sala hii ni kuombewa na waumini wa Yesu kwa sababu ni hao tu wenyekumwita Mungu ‘Baba’ (Rum.8:15; Ga.4:6). Ni sala ya kutumiwa na wauminiwakiwa pamoja, maneno ni katika ‘wingi’ k.m. ‘yetu’ ‘utupe’ ‘zetu’ n.k.

k.1 Wanafunzi walikuwa na nafasi nzuri ya kuangalia maisha ya Yesu naowalimwona kuwa mtu wa maombi, maisha yake yote yalitegemea maombi, nakwa njia hiyo alijenga uhusiano wake wa ukaribu sana na Baba yake.Wanafunzi walivutwa na kielelezo chake nao walitaka awafundishe kuomba.Marabi waliwapa wafuasi wao mfano wa kuomba na Yohana Mbatizaji aliwapawafuasi wake mfano pia. Hivyo, wanafunzi, kama kundi maalum, ambaye Yesuni kiongozi wao, walitaka awape mfano pia, wawe na sala yao ya kipekee.

k.2 Yesu akakubali na kuwaambia ‘Msalipo, semeni..’ Je! alitaka wasememaneno yale yale kila wakati? Huenda, siyo. Maana alikuwa amewaonya juu yaunafiki na umuhimu wa hali ya uhalisi wa kuomba kwa maana. Ila kwa jinsialivyoandika Luka ni kama aliwapa maneno yenyewe ya kutumia. Ila zaidialitaja mambo waliyopaswa kuyaombea. Kwa vyovyote hakutaka wasememaneno tu bila kuyazingatia maana yake.

Page 102: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

Neno la kwanza ni ‘Baba’. Wamkaribie Mungu kwa hali gani? Wamkaribie sawana mtoto amjiavyo baba yake, kwa upendo na tegemeo. Wajue kwamba Munguyu karibu nao kabisa kama alivyo baba na mtoto wake. Wayahudi hawakufanyahivi katika maombi yao. Maneno katika mraba yaonekana katika Mathayo sikatika nakala za asili za Luka. ‘Uliye mbinguni’ ni ukumbusho ya kuwa Yulewanayemwita Baba ni yule wa juu kabisa mwenye madaraka juu ya yote. Kwahiyo, hapo tunao ‘ukaribu’ (kama Baba) na ‘umbali’ (uliye mbinguni) wa Mungu,yule anayeombewa.

‘Jina lako litakaswe’ katika mawazo ya watu wa zamani jina lilijumlisha yoteyaliyomhusu mtu, tabia na hali zake. Kwa hiyo ni kama kuomba ‘Mungu aweMungu’ kufuatana na jinsi alivyojifunua na anavyojulikana. Apewe heshima zotezinazolingana na jinsi alivyojifunua kwa wanadamu. Yaani Mungu ajulikaneAlivyo hasa.‘Ufalme wako uje’ Yesu alisisitiza kwamba alikuwa ameleta Ufalme wa Mungukaribu na watu. Wote waliokubali kujitia chini yake walikuwa wamemruhusuMungu awatawale. Kwa ombi hilo waumini hutaka Mungu azidi kuusimamishautawala wake juu ya uumbaji wake wote mpaka ufikie utimilifu wake Yesuatakaporudi tena.

‘Mapenzi yako...’ sehemu hiyo haipo katika Luka ila inaonekana katikaMathayo. Ni kuomba kwamba Mungu azidi kutawala maisha ya wanadamu, nawanadamu wazidi kujitia chini yake na kufanya Atakavyo Yeye.

k.3 Hapo ni kuomba juu ya maisha ya kila siku. ‘Utupe siku kwa siku riziki yetu’Baada ya kuomba yale yamhusuyo Mungu ndipo twajiombea kwa sababuMungu anao mzigo juu ya maisha yetu mazima, si kwa roho zetu tu. Yesualituelekeza kuomba kwa mahitaji yetu ya kila siku, chakula n.k. Tuombe tupatevitu vya kutosha tunavyohitaji hasa. Kwa ombi hilo twakiri kwamba tu wahitaji,tena daima tu wahitaji. Hakutufundisha kuomba tupewe vingi vya kutosha kwasiku nyingi, ili tusiwe na haja ya kuomba kila siku, la. Twapaswa kumtazama nakumtegemea Mungu kila siku.

k.4 Kama ambavyo tu wahitaji wa riziki zetu za mwili, vivyo hivyo, tu wahitaji wakusamehewa kila siku. ‘Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasitunamsamehe kila tumwiaye’. Katika ombi hilo twakiri kwamba tu wenyedhambi wenye haja ya kusamehewa. Tiririko la msamaha kutoka kwa Mungulinazuiliwa tukishindwa kuwasamehe wengine ila tusifikiri kwamba kuwasamehewengine ni msingi wa Mungu kutusamehe sisi. La! Mungu hutusamehe kwaneema yake, ila twapaswa kuuonyesha ukweli wa ombi letu kwa njia ya kuwatayari kuwasamehe wengine. Ni hali inayotupasa tukitaka kuufurahia msamahawa Mungu. Pia ina maana kwamba, ikiwa sisi, tulio wenye dhambi,twawasamehe wengine, twaweza kuwa na ujasiri na tumaini kwamba Munguwa rehema atatusamehe sisi. Neno ‘deni’ limetumika, likileta maana yakuachiliwa.

Page 103: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 393

‘usitutie majaribuni’ Mungu haleti majaribu ya kutuingiza katika dhambi(Yak.1:13) ila pengine aruhusu shida na magumu yatupate, ambayo ni kawaidaya wanadamu, ili imani yetu ijengwe (Yak.1:2-4) Magumu yawezakutukandamiza hata twasikia ni vigumu kuwa waaminifu kwa Mungu. Tu dhaifu,na tunapaswa kuwa na tahadhari juu ya dhambi, tuwe na tabia ya kukimbiamajaribu, tusicheze na moto. Hasa tunaomba tusiwekwe mahali pafinyu, tusijetukashindwa.

‘utuokoe na yule mwovu’ ni maneno yaliyomo katika Mathayo tu si katika nakalaza asili ya Luka. Kwa ombi hilo tunaonyesha nia ya kuachana na dhambi.Tunaomba Shetani asitunase kwa hila zake.

k.5-13 Yesu baada ya kuwapa wanafunzi mfano wa Sala ya Bwana aliendeleakutoa mafundisho juu ya maombi na kuwatia moyo wa kuomba ili wawe nahakika kwamba maombi yao yatajibiwa.

k.5 Ndipo Yesu alitoa mfano wa mtu aliyemjia rafiki yake usiku. Ilikuwa desturikwa watu kusafiri usiku ili waepe jua kali. Wengine waliishi katika nyumbayenye chumba kimoja cha kulala wazazi na watoto pamoja. Kwa mfano huoYesu alitaka wanafunzi wake wawaze jambo la urafiki. Swali la Yesu lilianzakatika k.5 na kuendelea hadi k.7 akiwa na shabaha ya kuwafikirisha wanafunzijuu ya rafiki aliyetajwa. Alisema juu ya msafiri aliyemfikia rafiki yake usiku wamanane (huenda kijijini hakuwepo hoteli wala duka la kujipatia riziki) akamkutahana kitu cha kumpa. Watu walizoea kutengeneza vyakula asubuhi vya kutoshasiku ile. Lakini rafiki aliona vema amwendee rafiki yake na kumwomba msaada.Alifanya hivyo kwa sababu ya haja yake si kwa kumsumbua rafiki yake.Akamkuta ameishalala pamoja na watoto wake. Huyo rafiki aliyejiwa na rafikiyake hakutaka kumshughulikia kwa vile itambidi yeye atoke kitandani nakufungua mlango, ndipo watoto wataamka n.k. Lakini yule mtu aliendeleakumwomba bila kusikia haya, maana alihitaji kula. Mwishowe huyo rafikialiondoka kitandani na kumpatia rafiki yake mahitaji yake. Alimsaidia iwapoilimsumbua kufanya hivyo na bila nia safi, hakutaka kusikia haya na kujulikanakuwa mtu aliyekosa kumsaidia rafiki yake. Tazama jinsi neno ‘rafiki’ limerudiwakatika vifungu hivi. Kutokumsaidia kulikuwa jambo lisilowazika. Ikiwa rafikiambaye si rafiki mzuri yu tayari kumsaidia mwenzake si zaidi sana Munguatayajibu maombi yetu? Tena si kawaida ya rafiki kufanya kama ilivyoelezwakatika k.5-7. Haina maana kwamba tumsumbue Mungu ndipo atatupa yaletunayomwomba, la; ila kwa upande wetu budi tukazane katika kuomba halitukijua kwamba Mungu yu tayari kuyajibu maombi yetu. Kama tunahitaji kitukiasi cha kukiombea mara moja tu, ina maana kwamba hatukihitaji hasa. Tuoneya kuwa walikuwa ‘rafiki’ uhusiano ulikuwepo kati yao. Mungu ni rafiki yetu wambinguni, rafiki mkamilifu na mwaminifu.

k.9-13 Yesu aliendelea kusema juu ya maombi akisisitiza mtu kumwombaMungu kama mwana anavyomwomba baba yake.Yesu alisisitiza neno la

Page 104: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kudumu katika maombi na kuwa jasiri wa kumwomba Mungu kama mwana kwababaye. Ikiwa rafiki asiye bora alimsaidia rafiki mwenzake wakati wa shidazake, si zaidi, Mungu aliye rafiki na zaidi ya rafiki ni Baba yetu, atayajibumaombi yetu. Iliyotakiwa tuwe na ujasiri wa kumwomba. Yesu alitoachangamoto hiyo kwa njia ya kusema ‘ombeni’ ‘tafuteni’, ‘bisheni’ maneno hayomatatu ni kitenzi ya njeo. Tuthubutu kumjia Mungu kama mwana kwa babayake na kwa vyo vyote Mungu ataitikia vema, atafanya zaidi ya baba zetu wamwili, ambao huwapatia watoto wao vitu vyema, iwapo wenyewe ni dhaifu.Yesu alirudia kusema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mtu binafsi na kwawanafunzi wote kwa pamoja ‘kila aombaye hupokea’ n.k. Mungu ni mkarimusana na wa kutegemewa kabisa naye ajua kutoa kinachotufaa. Yesu alifuatachangamoto ya k.9 na ahadi ya k.10. Ni kama kutoa mwito wa kuomba,kutafuta, na kubisha, ndipo thawabu itaonekana, hivyo wapaswa kuomba n.k.Kipawa chake bora ni Roho Mtakatifu, ila Roho si badala ya chakula na mahitajiyetu, ila pamoja na mahitaji yetu Mungu atatupa Roho wake, msaada mkubwakwa upande wa maisha yetu ya kiroho.

Kwa njia ya mafundisho hayo Yesu aliwatia wanafunzi wake moyo wa kudumukatika maombi, wazidi kuomba kila wakati kwa kila kitu, katika tumaini la kujuakwa hakika kwamba Mungu atayajibu maombi yao. Mungu hujua mahitaji yetu,pia hutambua ni kitu gani kitufaacho na kitu kisichotufaa. Kwa hiyo, awezakujibu ‘ndiyo’ au ‘siyo’ au ‘bado’ yote ni majibu.

11: 14-23 Yesu alishtakiwa kuwa anasaidiwa na Shetani(Mt.12:22-30, 43-45; Mk.3:22-27)

k.14 Ilikuwa desturi ya Yesu kutoa pepo katika wale waliolemewa. Ilikuwasehemu katika vita yake ya kupambana na nguvu za yule mwovu. Pepoalimtawala huyu mtu hata hakuweza kusema (Mathayo alisema alikuwa kipofupia). Yesu alimtoa pepo, ndipo mtu aliweza kusema tena na watu walijua hakikakwamba pepo amemtoka kwa vile alivyoweza kusema tena. Makutanowalistaajabu kwa kuwa waliathirikia sana na jambo hilo.

k.15 Hata adui zake hawakukana kwamba Yesu ametoa pepo. Ila walisemaamefanya kwa nguvu za Shetani, si kwa nguvu za Mungu. Inaonekana niMafarisayo na waandishi waliotoka Yerusalemu walioleta mashtaka hayo(Mt.12:24; Mk.3:22)

k.16 Wengine walitaka ishara ya kipekee, pengine sababu yao ilikuwa kuondoamashaka yote juu ya uwezo huo kuwa umetoka wapi. Hawakutosheka naishara ya Yesu kutoa pepo walitaka afanye neno kubwa zaidi kwakuyathibitisha madai yake ya kuwa yule mwenye kuuleta Ufalme wa Munguambao nguvu zake zimedhihirika katika kazi hizo.

Page 105: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 395

k.17 Yesu aliyajibu mashtaka kwa kukana kabisa kwamba alikuwa amepatanana Shetani katika kutoa pepo. Ndipo aliendelea kwa kuonyesha upuzi na utupuwa kusema hivi. Katika ufalme au katika nyumba ikitokea farakano basifarakano hilo litasababisha ufalme huo au nyumba hiyo kuanguka. Shetani nimwerevu, hawezi kukubali fitina itokee katika enzi yake, kwa sababu ikitokea,basi ajua hakika kuwa mwisho wake umefika. Shetani huharibu utu wema,haharibu watumishi wake, pepo wabaya na enzi za uovu. Kwa hiyo, ilibakikuuliza, kama si Shetani, ni kwa nguvu gani Yesu hutoa pepo?(Beelzebuli - Yesu alimwita Shetani. Lafikiriwa kwamba ‘Beelzebuli’ lina asilikatika kuwa Jina la mungu wa Ekroni. Wayahudi walilitafsiri kuwa ‘mungu wamainzi au mavi’. wakionyesha dharau kwa huyo mungu aliyeabudiwa na watuwa Ekroni (2 Waf.1:2,3,6,16).

k.19 Pamoja na hayo, walikuwapo wengine waliokuwa na uwezo wa kutoapepo. Je! wao waliwezeshwa na Shetani? Hakuna aliyesema hivi. Wote walijuakwamba uwezo huo watoka kwa Mungu peke yake tu. Wapaswa wasiwe navipimo viwili, maana wale wengine waliotoa pepo watawahukumu wamekosakatika kusema pepo hutoka kwa uwezo wa Shetani.

k.20 Lakini vita ya ndani haijatokea katika enzi za Shetani ila kinyume chamashtaka yao, ukweli uliopo ni kwamba Yeye ametoa pepo kwa ‘kidole, yaaniuwezo wa Mungu’ (Kut.8:19). Mathayo alitaja kwa ‘Roho Mtakatifu’ (Mt.12:28).Ni dalili ya kuwa Ufalme, yaani utawala wa Mungu umewajia watu nao wazionjanguvu za Mungu katika maisha yao kwa njia ya kujikabidhi kwa Yesu. Sawa nailivyotokea kwa huyo mtu aliyetolewa pepo maana aliwekwa huru akawezakusema tena.

k.21-22 Yesu aliendelea kusisitiza habari hiyo kwa kutumia mfano wa nyumbailiyolindwa na mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake. Vitu vyake vilikuwasalama. Hamna shida mpaka alipotokea mwenye nguvu kuliko yeye, ambayealimshambulia na kumnyang’anya silaha zake, na kuruhusu mateka wake kuwahuru. Maelezo hayo yaliweka wazi madai ya Yesu kuwa yule mwenye nguvuambaye amemnyang’anya Shetani nguvu zake, na kuwafungulia mateka wake(kama yule bubu). Shetani halingani naye kwa nguvu, katika vita ya kirohomshindi ni Yesu. Kwa kusema hivi Yesu alikuwa akidai mamlaka na uwezomkubwa kabisa na ameuthibitisha ukweli wake katika huduma yake ya uponyajina kutoa pepo. Shetani hana uwezo wo wote mbele za Mungu, hawezikusimama.

k.23 Kama ilivyo katika vita mtu hupaswa kuamua yu upande gani, ni vigumuakae bila kufanya uamuzi. Ndivyo ilivyo kwa wakati huo. Yesu ameuleta Ufalmewa Mungu, budi mtu aamue awe upande wa Yesu au awe kinyume chake, nivema mtu ajiunge naye. Ufalme wa Mungu si katika maneno bali ni katikanguvu za kuushinda uovu. Huo Ufalme upo katika Kuwepo kwa Bwana Yesu.

Page 106: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

11: 24-28 Habari ya pepo kumwacha mtu na kumrudia tenak.24ku. Habari hii inahusika na ile iliyotangulia. Pepo atolewapo mtu hutafutamahali pa kujisitiri. Ni picha ya pepo aliyesafiri akitafuta mahali pa kukaa.Akakosa kupapata, kwa hiyo, alirudia mahali alipokuwepo, na kwa bahati nzurialipakuta pametengenezwa vizuri sana. Hivyo akaamua kurudi pale pamoja napepo wengine, kama jamii, kisha mahali pale palikuwa pabaya hata kulikopalivyokuwa mwanzoni. Ni mfano wa mtu aliyekuwa na nyumba ya kupangia,naye alikuwa amempangia mtu ambaye hakuitunza vizuri. Ndipo mpangajialiamua kuondoka, na mwenye nyumba alipata nafasi ya kuipaka chokaa nakutia rangi n.k. na nyumba yake ilikuwa safi tena. Kisha akarudi yule mpangajiambaye alikuwepo mwanzoni pamoja na rafiki zake saba, nao wakakaa humona kuichafua nyumba ile.Ina maana gani mfano huo? Ni kuonyesha hatari ya mtu kudanganywa nanafuu zinazopatikana mara kwa mara katika maisha yake. Hazitadumumaadamu yule ‘mwovu, mwenye nguvu’ ni bwana. Ni Yesu tu ambaye awezakuleta manufaa ya kudumu katika maisha ya mtu, na ndivyo ilivyotokea katikahuduma yake. Watu walisaidiwa kweli, si kwa muda tu, na ndiyo sababualisema juu ya umuhimu wa kujitoa kwake k.21-22.

Yawezekana habari hii inadokezea huduma ya Yohana Mbatizaji. Wakati wakewengi walizitubu dhambi zao na kubatizwa ubatizo wa toba, tayari kwa hudumaya Bwana Yesu, ya Roho Mtakatifu, na kwa kuzipokea nguvu za Ufalme waMungu. Kwa hiyo, ni neno kwa wote waliotengeneza maisha yao wakati waYohana, budi waendelee na kumkubali Kristo na kumpokea maishani mwao.Bila kufanya hivyo, hali yao itakuwa mbaya kuliko hali yao kabla ya kutokeakwa Yohana. Na ndivyo ilivyotokea katika historia yao. Kwa maneno hayo Yesualidai uwezo mkubwa wa kuuondoa uovu na kutia moyo mpya wa kumpendaMungu kweli. Ni hatari ya ‘toba’ la kuacha mabaya bila kuchukua hatua yakuweka mema badala yake. Moyo wa kibinadamu si ombwe, umeumbwa uwena ‘mkazi’ ndani yake.

k.27-28 Ndipo Yesu aliendelea kwa kuonyesha ni akina nani waliobarikiwa.Mwanamke mmoja alipoyasikia maneno ya Yesu alivutwa sana, akaipaza sautiyake na kumwita heri mama wa Yesu kwa kumzaa mtu mzuri wa namna hiyo.Huenda alifikiri kwamba ‘Je! si lingalikuwa jambo zuri ikiwa mimi ningalikuwa namwana kama huyo?’. Yesu hakuukana uheri wa mama yake ila alimjibu kwakumwonyesha kwamba walio heri hasa ni wale wanaojihusisha naye kwa njiaya kulisikia na kulishika neno lake, si wale walio na uhusiano wa kimwili naye tu(6:46ku). Jambo muhimu kuliko yote ni watu kulipokea Neno lake. Kuvutwa nakupendezwa naye hakutosha, bali ni kujitoa kwake na kubadilika.

11: 29-32 Maonyo juu ya kutafuta isharaWatu wengi walikuwa wamemkusanyikia Yesu. Alisema juu ya wale waliokuwawamekataa kulishika neno lake kinyume cha wale waliotajwa k.27,28. Hapo

Page 107: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 397

nyuma watu walikuwa wameishaomba wapewe ishara itokayo mbinguni (k.16)na hapo ni jibu lake kwa ombi lao. Walikuwa wameziona ishara nyingi za uwezowake katika huduma yake na hasa katika uwezo wake wa kumtoa pepo mtububu. Ni kama walitaka ishara ya kipekee mfano wa kitu cha kutoka mbingunimoja kwa moja. Yesu aliwaambia wazi kwamba wamekuwa kizazi kibaya kwasababu hawakutaka ishara kwa shabaha safi ya kumwamini na kujikabidhikwake. Ombi lao lilificha kutokuamini kwao, kwa sababu, wameishaona nguvuna uwezo wa Yesu kwa njia ya matendo na mafundisho yake yaliyotoshakuwasaidia wenye nia safi. Matendo yake ya ajabu yalifunulia tabia njema zaMungu, huruma zake kwa wanyonge na wenye shida za kimwili kama uwete,ububu, maradhi mbalimbali, ukoma n.k. Kwa kazi hizo walifundishwa jinsi AlivyoMungu. Ila wao walitaka Mungu wa kuwatiisha adui zao na kuwahukumu kwaukali kama kuleta umeme na gharika n.k. Yesu alikataa kabisa ombi lao, maanaombi lenyewe si baya ila ni baya katika mazingira ya huduma yake, kwa hiyo,watapewa ishara moja tu, ya Yona.

k.30 Yona alitumwa kuwahubiri WaNinawi juu ya hukumu ya Mungu, ilaaliogopa kuwaendea, akaenda mahali pengine. Mungu alimhukumu, mabahariawalimtupa majini walipogundua kwamba wamepata shida katika safari kwa ajiliyake. Ila Mungu bado angali alitaka awaendee WaNinawi, hivyo aliokokabaharini kwa njia ya ajabu ya kumezwa na samaki mkubwa, ndipo samakiakamtapika kwenye pwani, naye akaokoka. Vivyo hivyo, Yesu atauawa, nabaada ya siku tatu Atafufuka katika wafu, ndipo itajulikana na watu wotekwamba Yeye ni yule aliyetumwa na Mungu. WaNinawi walipoyasikia mahubiriya Yona walitubu. Ingawa Yesu ametumwa na Mungu watu kwa jumlahawakumwamini, hata Atakapofufuka kutoka katika wafu, wengi wataendeleana hali ya kutokuamini (Mt.12:40; Yn.2:19). Yesu ni ishara kwa kizazi chakesawa na Yona alivyokuwa kwa Waninawi. Ishara ilikuwa ya mahubiri ya kuletawatu kwenye toba na itikio hilo liliwapasa wale walioyasikia mahubiri ya Yesuna kuona huduma yake yaliyodhihirisha uwezo na upendo na huruma yaMungu. Katika kutokutubu watu walionyesha ukaidi wao wa kukataa kutambuayaliyokuwa yakifanyika machoni pao. Katika huduma ya Yona Mungualionyesha huruma yake kwa WaMataifa na hata Yesu alionyesha huruma kwawengi waliowekwa kando na jamii.k.31 Halafu Yesu alimtaja mwingine ambaye ni hukumu kwa watu wa kizazichake. Malkia wa Kusini alizisikia habari za Sulemani na hekima yake. Alitakakumsikia mwenyewe hivyo alifanya bidii na kukata shauri kwenda mpakaYerusalemu, safari ndefu sana, na ya gharama, ili amwone na kumsikia (1Waf.10:1ku). Lakini Yesu alikuwa katikati ya hao watu wa ‘kizazi kibaya’walimwona kwa urahisi, bila gharama, bila taabu za usafiri, lakini wengi waohawakumjali. Hekima yake ilizidi ile ya Sulemani (7.35).

Yesu alikuwa mkubwa kuliko Sulemani na hekima yake ilipita ile ya Sulemani.Alikuwa mkubwa kuliko Yona. Watu wa nyakati za Sulemani na za Yonawatasimama katika siku ya hukumu na kuwahukumu watu wa kizazi cha Yesu

Page 108: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kuwa na hatia kwa kuwa walijaliwa kuona makuu mengi kupita watu wa zamanizile, lakini hawakuitika vema, hawakutubu toba la kweli. Wakati wa Yesu niwakati wa Ufalme wa Mungu kuletwa karibu na watu, ni dahari mpya, dahari yaRoho Mtakatifu, dahari ya watu kuonja nguvu za Mungu kwa ndani. Yesu ndiyeishara kamili kwa wale wote wenye nia safi na utambuzi wa kweli. Yeye ni ileishara moja tu kwa wale wa kizazi kibaya, ishara yenyewe ni tangazo lahukumu itakayowajia wote ambao hawakulipokea na kulitii neno lake.

11: 33-36 Mafundisho kwa taa (Mt.5:15; 6:22ku)Katika sehemu hiyo Yesu alisema juu ya kazi ya ‘taa’ ambayo ni kuangaza. Mtuawashaye taa huiweka mahali pazuri pa kuangaza vizuri. Mtu hupata kuonakwa njia ya jicho lake, nalo likiwa na afya njema yeye hupata kuona vizuri kwamwanga ulioko. Ila jicho lake likiwa baya, yaani, halina afya, hata mwangaunapoangaza yeye hukosa kuona vizuri. Hivyo, maisha yote ya mtu huguswana hali ya afya ya jicho lake. Huduma ya Yesu ni mfano wa taa, imekuwa wazi,Yesu ametembea huko na huko na kuhubiri na kufundisha watu hadharani,wengi wamepata kuona matendo yake ya ajabu, hivyo Yeye na huduma yakevimekuwa taa iliyowekwa mahali pazuri pa kuwaangaza watu. Mara kwa marawatu walimwomba Yesu afanye ishara ya kipekee ili wasaidiwe kumtambuakuwa Masihi, naye akakataa. Kuona kwao kulizuiliwa kwa sababu yakutokuamini kwao na ukaidi wao, walikuwa na ‘jicho baya, lililokosa afya’.Huduma yake ilikuwa changamoto kwao, nao waliwajibika kwa itikio lao lakutokubali mwanga wake uingie maishani mwao. Yesu alileta ufunuo kamili juuya Baba na mapenzi yake ila watu wengi hawakuupokea kwa imani na utii.Shida haikuwa katika ukosefu au upungufu wa mwanga bali katika hali yamioyo yao. Hawakuwa na nia safi. Yesu alitoa onyo kwa wale waliofikirikwamba wanao mwanga huko mwanga walio nao ni giza tupu. Bila Kristo mtuhawezi kuona vizuri, hawezi kutambua maana na shabaha ya kuishi kwake,wala hakubali kuongozwa na mapenzi ya Mungu. Mwanga wa Kristo huangazawakati wote ila inategemea hali ya upokezi. Maisha ya mtu hujaa mwangaanapomkubali Kristo kwa nia safi, bila unafiki na bila kuwa na nia mbili, maanaunafiki na kuwa na nia mbili ni ‘ugonjwa’ wa macho.

11: 37-44 Yesu aliwashtaki MafarisayoMafarisayo na wanasheria walikuwa vipofu kwa mwanga ulioletwa na Yesu kwasababu ya hali ya maisha yao, walikuwa wamepotoka, hawakuishi maishamema, pia walikosa unyofu katika maisha ya dini.

k.37-38 Wakati fulani Yesu alipomaliza kufundisha, Farisayo mmoja alimwalikakwa chakula. Mara kwa mara Yesu alialikwa kula nao. Walikuwa na desturi yamaosho mengi. Wakati wa kutoka safarini na kabla ya kula walizoea kuoshamikono yao kwa shabaha ya kuuondoa unajisi wo wote ambao huendawalikuwa wameupata katika kukutana na wenye dhambi na WaMataifa.Maosho hayo yalihusu unajisi si afya. Yesu hakujali desturi hiyo na huyoFarisayo aliyemwalika alishangaa. Hatusikii kwamba alisema lo lote ila kwa hali

Page 109: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 399

yake alionyesha kwamba alishtuka kwa sababu alidhani kwamba huyo rabimashuhuri atanawa kabla ya kula.

k.39 Yesu alichukua nafasi hiyo na kusema juu ya usafi wa kweli na usafi usiowa kweli. Alitaka kutoboa wazi unafiki wa hao Mafarisayo waliokaza mambo yanje bila kujali mambo ya ndani. Walishughulikia sana mambo ya nje, wakiwekasheria nyingi ndogondogo zilizosisitiza vitendo vya nje huku waliyaacha mambomakubwa ya ndani, ya moyo, upendo wa Mungu na kutenda haki. Walishikasheria za nje huku wameendelea na unyang’anyi na uovu, ilikuwa kanakwamba walishikilia sana mambo ya nje kwa shabaha ya kuyaficha maovu yaoya ndani. Hali hizo za ndani hazikuwa wazi kwa watu kuziona, ila Yesualizifunua, kwa kuwa ni hali halisi ambayo pia ni mwelekeo wa ubinadamu wetu.

k.40 Yesu aliwaita ‘wapumbavu’ kwa sababu vyote viwili, vya nje na vya ndani,vyaenda pamoja. Haswa, hali ya ndani ikiwa safi ndipo hata ya nje itakuwa safipia. Wingi wa maji yanayomwagwa katika mikono hautoshi kutengeneza halimbaya ya ndani.

k.41 Ina maana gani ‘sadaka vile vya ndani’? Pengine yaliyomo ndani yakikombe na sahani ni lugha ya kuashiria chakula kwa maskini; au pengine inamaana ya kusema juu ya wajibu wa mtu kutoa katika mali aliyo nayo; aupengine inasisitiza hali ya moyo wakati wa kutoa, mtu atoe kwa upendo na kwania safi si kwa kuuvuta usikivu na sifa za watu. Neno la utoaji lilikuwa muhimukatika dini ya Kiyahudi na ni neno linalosafisha undani wa mtu na kumwokoa nachoyo na kujipenda.

k.42 Halafu Yesu aliendelea kusema juu ya makosa ya Mafarisayo akitumianeno ‘ole wenu, Mafarisayo’. Ni neno la kuonyesha sikitiko pamoja na huzunijuu ya hali zao, si neno la kutaka walipiwe kisasi, ila ni neno la kuonyesha jinsiYesu alivyotamani sana wayatambue makosa yao na kuyatengeneza. Aligusajambo la kutoa zaka, neno lililotakiwa kwa wote walioshika sheria zilizoagizwakatika Agano la Kale (Law.27: 3-33; Kum.14:22-29, 26:12-15). Walizidiilivyotakiwa kwa upande wa kutoa zaka katika mboga na mimea ya viungo n.k.kwa kuwa sheria haikusema watoe katika vitu hivi. Lakini shida yao haikuwakatika kutoa zaka ila katika kuyaacha mambo makubwa ya adili na upendo waMungu. Iliwapasa wautangulize upendo kwa Mungu na maadili bila kuachakutoa zaka. Walitoa zaka bila kumpenda Mungu na bila kuwapenda watu nakuwapatia haki zao. Walitanguliza yasiyo ya maana na kuacha yaliyo muhimu.

k.43 Ndipo Yesu aligusa hali nyingine ya Mafarisayo. Hali ya kupendakuonekana mbele ya watu ili watambuliwe kuwa watu wazuri wa dini, tenawafanyiwe kwa upendeleo na kupewa viti vya mbele na kupewa salaam nyingiwalipokutana na watu sokoni n.k. Walifanya matendo ya dini kwa nia mbaya, sikwa kumpendeza Mungu bali kwa kuuvuta usikivu wa watu. Hata walijionyeshasana mbele za watu kusudi hali yao ya unyang’anyi n.k. isionekane. Walivaa

Page 110: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

dini kama mavazi ya kuyaficha mabaya yao. Walikuwa wanafiki, wakiwa kamawachezaji katika viigizo, mtu hufanya kuwa ‘fulani’ bila kuwa yule hasa. Ilatusifikiri ni Mafarisayo tu walio na hali hiyo, hata imekuwa daima jaribu kwawatu wa dini yo yote.

k.44 Yesu aliwafananisha na makaburi yasiyoonekana, mtu alihesabiwa kuwaamenajisika ikiwa aliigusa maiti n.k. kwa hiyo ilikuwa hatari kupita juu yamakaburi yasiyoonekana, maana mtu alinajisika bila kutambua na bilakukusudia kwamba anajisike. Yesu alisema kwamba wale waliofuatamafundisho na njia za Mafarisayo waliambukizwa uovu wao. Ndani ya makaburiimo mifupi ya wafu, na ndani ya Mafarisayo ipo hali ya ufa kiroho. Walikuwahatari kwa watu. Makaburi yasiyoonekana wazi ni picha ya Mafarisayo ambaohatari yao haigunduliki kwa urahisi. Yesu mwenye kusoma mioyo ya wanadamualielewa na kufunua hali zao halisi.

11: 45-52 Makemeo ya Yesu kwa Wana-sheriaMafarisayo walikuwa kama dhehebu katika dini ya Kiyahudi na Wana-sheriawalikuwa jamii ya watu walioshughulika sana na ufafanuzi wa Sheria,wakihesabiwa mabingwa wa sheria. Kazi yao ilikuwa kuwasaidia watu waelewematakwa ya sheria katika maisha yao ya kila siku, kwa hiyo kazi yao ilikuwanjema, ila kosa lilitokea katika kuuzidisha uzito wa matakwa hayo bila kutoamsaada na bila kuwatia moyo, hivyo watu walikatishwa tamaa. Wana-sheriawalikuwa Mafarisayo (ila Mafarisayo wengine hawakuwa Wana-sheria) na ndiyosababu mara nyingi twakuta kwamba Mafarisayo na Wanasheria wametajwapamoja.

k.45 Yawezekana huyo mwana-sheria alishangazwa na jinsi Yesualivyowashambulia Mafarisayo. Hakufikiri kwamba hayo aliyosema Yesu kwaMafarisayo yaliwahusu hao Wana-sheria pia. Ila Yesu hakuhofu kusema juuyao na kuwaonyesha makosa yao. Machoni mwa mwana-sheria Yesu alikuwaamewashutumu Mafarisayo.

k.46 Ni nini makosa ya wana-sheria? Kosa moja kubwa lilikuwa kuuongezauzito wa madai ya matakwa ya sheria kwa watu. Katika kuifafanua sheriawalijenga juu ya sheria iliyotoka kwa Mungu na kuweka visheria vingi vingi,vidogo vidogo, ambavyo walifundisha watu kwamba iliwapasa wavifanyewakitaka kuitimiza ile sheria iliyotoka kwa Mungu. Kwa hiyo hivi visheriavimekuwa mzigo mzito uliowalemea watu. Tena, kwa upande wao, hawakuwana huruma yo yote. Wao wenyewe walijiwekea vipengele vya kuupunguza uzitowake kwao. Badala ya kutoa mwanga juu ya sheria, walikuwa wameificha.Iliwapasa, kwa maelezo yao, kuwasaidia watu na kuwatia moyo, badala yake,waliwakatisha tamaa. Ndiyo sababu Yesu alitumia neno ‘ole’ maanaalisikitishwa sana na hali yao (ling. na wito wake Mt.11:28).

Page 111: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 401

k.47ku. Ndipo Yesu aligusa hali nyingine ya wana-sheria. Walipenda kujengamaziara ya manabii na kupamba makaburi yao, kana kwamba, walikuwaupande wa manabii na msimamo wao wa kuuleta Ujumbe wa Mungu uliowaitawatu watubu. Lakini hawakuwa katika safu ya watu wa zamani waliokuwawaaminifu kwa Mungu, waliolipenda Neno lake na kulipokea maishani mwao.Walikuwa upande wa wale waliowakataa manabii na ujumbe wao wa kweli.Neno hilo limethibitishwa katika kumkataa Yesu, Mwana wa Mungu, aliye mkuukuliko manabii wote, kwa kuwa hawakuwa tayari kuupokea ujumbe wake. Kwahiyo tokeo halisi ya kujenga maziara ya manabii lilikuwa kulifuta kumbukumbula manabii si kuwashangilia.

k.49-51 Mungu alijua ndivyo itakavyokuwa, hata hivyo, kawaida yao na tabiayao ya kuwakataa waliotumwa na Mungu, haitamfanya Mungu aache kutumakwao wajumbe wake, hata watakapomwua Yesu, hali hiyo itaendelea,watawakataa Mitume na Injili, hata hivyo, Mungu hakati tamaa. Walewaliowakataa wajumbe wa Mungu, kutoka mwanzo hata wakati wa Yesu,walikuwa na hatia na hukumu itawaangukia. Kukataa kwao kulikuwa na hatia.Hasa upeo utafika watakapomwua Mwana wa Mungu. Mungu ataleta hukumukali juu ya taifa la Kiyahudi, yote yatajumlishwa, tangu kuuawa kwa Habeli(Mwa.4:8) hadi kuuawa kwa Zakaria (2 Nya.24:2ku) damu yao italipizwa kisasi.Desturi hii ya kuwakataa na kuwaudhi hata kuwaua wanaotumwa kwaoilidhihirisha ukweli wa hali yao iliyoanza zamani za kale nayo itaendelea hatabaada ya Yesu kuondolewa.

k.52 Kisha Yesu alitaja ole mwingine juu ya Wana-sheria kwa kosa lakuwanyima watu ujuzi wa kweli wa Neno la Mungu na badala yake kuwapaujuzi wao, usio wa kweli, maana walikosa kuwafundisha kweli za Mungu.Walifundisha matakwa yaliyohusu mambo ya nje waliyoyatungwa wenyewe bilakusisitiza kwamba Mungu hutazama moyo, na Mungu, kabla ya mambomengine yote, hutaka watu wampende kwa moyo na kwa dhati. Ilitokeakwamba ujuzi wa Mungu ulishikwa na ‘mabingwa wa sheria’ na watuwalishindwa kuwaelewa. Hata katika Kanisa wametokea wachache ambao kwa‘theolojia’ yao wamezipotosha imani za watu. Iliwapasa wafundishe watumaana ya ndani ya Maandiko. Hawakumkubali Yesu na mafundisho yake, piawalijaribu kuwazuia watu wasijiunge na Yesu. Kwa hali yao Wayahudiwalipoteza sababu ya kuwepo kwao kama wateule wa Mungu, kwa hiyo,haikubaki sababu waendelee kuwepo katika hali ya kuwa taifa teule. Nyakati zakutayarisha njia ya Masihi zilikuwa zimetimizwa katika Kufika Kwake.

k.53 Matokeo ya mashutumu hayo kwa Mafarisayo na Wana-sheria ilikuwakwamba hao walimsonga vibaya, walimchokoza kwa maswali mengi, walikuwakama wanyama waliotafuta mawindo, wakitaka kudaka neno litakalotoshakumshtaki mbele ya viongozi. Yesu alikuwa na mzigo juu ya ukweli kulikousalama wake.

Page 112: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

MASWALI1. Wanafunzi walikuwa wameona nini katika maisha ya Yesu iliyowaongoza

kumwuliza awafundishe kuomba?2. Eleza matumizi ya Sala ya Bwana

Kwa Sala hii twajifunza ni mambo gani muhimu ya kuombewa?3. Ni jambo gani linalotutia moyo wa kuomba katika Mfano wa mtu aliyemjia

rafiki yake usiku?4. Yesu alidai mambo makubwa gani alipojibu shtaka la kuwa mtu

ametolewa pepo kwa msaada wa Shetani?5. Mtu apaswa afanye nini baada ya kutolewa pepo? Asipofanya hivi

itakuwaje kwake?6. Kwa nini Yesu alisema kwa nguvu watu walipotaka ishara? Ukaidi wao

ulionekanaje?7. Yesu alifananisha huduma yake na taa. Kwa nini watu washindwa

kumtambua sawasawa?8. Yesu alisema kwa ukali juu ya Mafarisayo na Wana-sheria. Alitoboa wazi

makosa yao na tabia yao kuwa nini?

Kuwa tayari kwa hukumu inayokuja 12:1-13:912:1-12 Wanafunzi wake wasiwe wanafiki, wamwogope Mungu tuYesu alisisitiza kwamba wanafunzi wake walipaswa kuonyesha wazi mbele zawatu uaminifii wao Kwake. Upo uhusiano kati ya sehemu hiyo na surailiyotangulia hasa juu ya mashutumu ya Yesu kwa Mafarisayo na Wanasheriawaliokaza mambo ya nje bila kuyajali mambo ya moyo na maadili.

k.1-3 Watu wengi sana walikuwa wamekusanyika hata kiasi cha kukanyagana.Kwa Luka mwandishi lilikuwa jambo muhimu kwa umati wa watu kuyasikiamaneno hayo ambayo Yesu alisema kwa wanafunzi masikioni mwao.Yesualiona vema awaonye wanafunzi juu ya Mafarisayo na hatari ya unafiki, kwasababu, unafiki ni jaribio linalowapata watu wa dini. ‘chachu’ ni kitukinachoenea kwa upesi na kwa siri, haionekani wazi na kuwemo kwakehakujulikani mpaka donge limevimba (Mt. 13:33). Watu walielewa neno lachachu kwa sababu waliitumia katika upishi wao.

Unafiki ni upuuzi kwa sababu ni wa muda tu. Wanafiki hawafikiri juu ya wakatiujao, wakati wa mambo yaliyofichwa kujulikana. Wanafiki ni mfano wa watuwasioona mbali, kwa sababu katika siku ya hukumu mambo yote yatadhihirikawazi na kujulikana, na hata kabla ya siku hiyo ‘mambo mengine yatadhihirika.Baadaye mambo yote yatajulikana kabisa. Hivyo, ya ndani, ya siri, hayatakaahali hiyo ya kufichwa wakati wote. Yaliyofichwa hayawezi kupona uchunguzimakini wa hukumu ya Mungu.

Yawezekana maneno ya k.3 yahusu utangazaji wa Injili. Wanafunzi wakewapaswa wasiogope kuhubiri Injili hadharani mwa watu. Wasiufiche utiifii wao

Page 113: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 403

kwa Yesu. Wakiitangaza Injili kwa wazi ndipo unafiki wa watu wa dini isiyo kwelipamoja na unafiki wa nia zao zitadhihirika. Unafiki wa Mafarisayo na wenzaouliwapofusha macho hata wakashindwa kutambua Kuwepo kwa Mungu katikahuduma ya Yesu.

k.4-12 Wamwogope nani? Yesu aliendelea kusema na wanafunzi wake,akiwaita ‘rafiki zangu’. Ni hapa tu, katika Injili tatu zinazowiana, ambapoamewaita hivyo (Yn.15:14). Yawapasa kufahamu ni kipambele kipi kilicho chakwanza. Ni kumcha Mungu si wanadamu. Kwa nini ni hicho? Ni kwa sababuwanadamu wanao mpaka katika uwezo wao, upeo wa uwezo wao unafikawanapouua mwili, ila baada ya kuuua mwili hawana la kufanya. Ila sivyo ilivyokwa Mungu. Baada ya kufa Mungu anao uwezo wa kumtupa mtu katikaJehanum. Kwa hiyo, ipo hatari kwa wanafiki, pia ni hatari kuwa waoga. Nikawaida ya wanadamu kuhofu kuuawa ila ni vema wakumbuke ya kuwa uwezowa Mungu unaendelea baada ya kifo. Kwa hiyo wamwogope Mungu kulikowapinzani wao kwa sababu ni jaribu kubwa kwa waumini kumwasi Kristo wakatiwa shida.k.6-7 Tena Mungu ayajua mambo yote, hata madogo yanayowapata, tenaanao mzigo juu yao. Yesu aliwatia moyo kwa kuwataja mashomoro, ndegewalio wadogo na wengi. Maskini walikula nyama yao nao waliuzwa sokoniwatano kwa senti mbili. Mathayo amesema waliuzwa wawili kwa senti 1, kwahiyo, kwa senti 2 mtu alipata wanne na mmoja kama zawadi, kwa hiyo, hatayule bure Mungu alijua habari zake. Si hivyo tu, Mungu ajua hesabu za nyweleza vichwa, tusifikiri kwamba hesabu yenyewe ndiyo neno la maana, ila ni usemiwa kuonyesha kwamba Mungu hujali hata mambo madogo madogo yakawaida. Jambo kubwa ni kwamba wao ni bora kabisa kuliko hao ndege ambaoMungu ajua habari zake. Kwa hiyo, kumwogopa Mungu ni kumcha katika haliya kumpenda na kumwamini. Mungu hawezi kuwaacha. Katika imani yaowashike makubwa mawili kwa uwiano; ukuu na uwezo wa Mungu Mwumbaji; nauhifadhi na uangalizi wake wa viumbe vyake. Hawana haja ya kuogopa.

k.8-9 Mbele yao, wakati wa kuletwa barazani, ama wawe watiifu kwa Bwanawao na kumshuhudia, potelea mbali, tokeo lake ni nini hata kufa. Ama wawe nahofu na kuogopa kukiri kuwa wafuasi wa Yesu.Uamuzi wao utatiwa muhurikatika siku ya mwisho, utaidhinishwa katika baraza la mbinguni na mbele zaMungu Mwenyewe. Yesu atamkiri au kumkana kila mtu kuwa wake kwakulingana na uamuzi wa yule mtu hapa duniani. Ni heshima ya hali ya juu Kristokumkiri mtu kuwa wake mbele za Baba na malaika na jeshi lote la mbinguni.Kinyume chake ni kanusho la upeo na la mwisho kwa Yesu kumkana mtu kuwasi wake mbele za Baba. Kwa hiyo mambo yanayotokea hapa dunianiyanatawala matokeo katika uzima wa milele. Tukumbuke kwamba twawezakumkana Yesu kwa njia mbalimbali, si wakati wa kuletwa barazani tu.Twamkana tunapokataa kupokea mamlaka yake na upekee wa mafiindishoyake; au tunapodhani na kufanya kwamba twajua zaidi yake juu ya neno fulani.Twamkana tunapotoa maelezo yanayopunguza mamlaka ya Neno lake, au

Page 114: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

tunapoukana Uungu wake na kuyapuuza madai yake juu ya maisha yetu. Hayoyote hutokana na kiburi chetu na kijitegemea kwetu. Hatuna haja yakumwogopa Shetani, hana uwezo wa kuigusa roho, wala kutawala mwishowetu. Wajibu wetu ni kumpinga (Yak.4:7; 1 Pet.5:9).

k.10 Ina maana gani, mtu aweza kusamehewa akisema neno juu ya Yesu, ilaakimkufuru Roho Mtakatifu hawezi kusamehewa. Yawezekana maana yakekwa wakati ule ni kwamba wale waliomkataa Yesu alipokuwa duniani, kablahajafufuka na kutukuzwa, waliweza kusamehewa baadaye ikiwa walikubalikutubu. Wale ambao baada ya Yesu kufufuka na kutukuzwa, na Roho Mtakatifukufanya kazi mioyoni mwa wengi, hao wakimsukuma mbali huyo Roho, haliwameiona kazi yake katika maisha ya waumini ni vigumu kuwaleta kwenye tobakwa sababu ya hali yao ya kutokuwa tayari kutubu na kuamini (Mdo.7:51). Nikama, kwa kusudi, wamefumba macho yao wasione na wameziba masikio yaowasisikie, kwa hiyo, hakuna njia ya kuwasaidia, ikiwa hawasikii kwambawamefanya dhambi watawezaje kutubu? Ni dhambi zito, haina msamaha.Dhambi hiyo yahusu mwenendo wa mtu, si kusema maneno fulani. Mtuakiendelea na hali ya kuikataa Injili na kupata mazoea ya kukataa, mwishoweatashindwa kutubu na kuamini. Yawezekana wazo ni kwamba Roho ni kamakidole cha Mungu (11.20). Ni kukana Kuwepo kwa Mungu wakati ambapoKuwepo Kwake kumekuwa wazi. Hivyo mtu hujiweka mbali na msamaha. Kuwana hali ya kutokuamini bado inasameheka, ila kuasi hakusameheki.

k.11-12 Roho Mtakatifu atawasaidia wanafunzi watakaposhtakiwa kwa sababuya imani yao katika Kristo.Yesu alikuwa akiwatahadhari kwamba mbele yao,baada ya Yesu kuondoka duniani, watateswa na kushtakiwa, wa kwanzakuwatesa watakuwa Wayahudi na baadaye wakati wa Injili kwenda kati yaWaMataifa hata viongozi wa WaMataifa watawashtaki pia. Roho Mtakatifuatawasaidiaje? Atawapa maneno ya kuyatumia katika utetezi wao, si kabla yakufika barazani ila wakati uleule wa kuwepo barazani. Tena atawafundishamaneno yanayowapasa kusema, si maneno ambayo yatasababishakufunguliwa kwao. Ndipo kwa maneno yao watamtukuza Mungu na kumtumikia(Mdo.4:8). Mungu yu pamoja nao wakati wote na hasa wanapoteswa nakushtakiwa. Watajaribiwa kujisumbua wakipenda kusalimisha maisha yao ila nivema wakaze nia zao kuvumilia. Kuanguka ghafula kama Petro alivyofanya(22:54-62) si jambo la kumkufuru Roho. Kumkufuru Roho ni mwenendo wa sikunyingi si jambo la mara moja.

12: 13-21 Mafundisho juu ya mali (Mt.6:19-21, 25-33)k. 13-14 Yesu alitoa onyo juu ya choyo pamoja na mfano wa tajiri mpumbavu.Mtu fulani katika makutano waliokuwa wakimsikiliza Yesu na mafundisho yakealimwomba aamue jambo la urithi kati ya yeye na ndugu yake. Wayahudiwalikuwa na sheria kuhusu urithi (Kum.21:17). Alimwita Yesu ‘Rabi’ na ndivyo

Page 115: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 405

wengi walivyomwaza. Lakini Yesu hakufikiri kwamba amewekwa kuwamwamuzi rasmi kwa kazi hiyo ya kutoa maoni juu ya mambo kama urithi. Kaziyake ilikuwa kuwaleta watu kwa Mungu si kuleta mali kwa watu. Aliwekwa kuwamwamuzi na mwenye mamlaka katika mambo ya kiroho si katika mambo hayoyaliyoweza kuamriwa na wengine waliowekwa kwa kazi hiyo. Huyo mtu alikuwaakijaribu kumtumia Yesu na urabi wake na mamlaka yake ya kiroho kwakujifaidi mwenyewe (ling.na Kut.2:14).

k. 15 Yesu aligusa kiini cha shida ya wengi aliposema juu ya choyo, ambayo nitamaa ya mtu kupata zaidi na kutokuridhika na alivyo navyo. Tena alisisitizakwamba yampasa mtu ajihadhari na kujilinda na choyo, ashindane na tabia hiyokama mtu ashindavyo na adui. Siyo kusema kila mtu mwenye choyo anaonawivu juu ya mwenzake, la, ila ni hali ya kutokuridhika. Hali hiyo huingiza mtukatika ugomvi n.k. Ndipo Yesu alitamka neno muhimu sana juu ya maisha yamwanadamu, uzima wake haumo katika wingi wa vitu alivyo navyo. Mtuajengaye maisha yake juu ya mali na hamu ya kuzidisha mali hujenga juu yamsingi usio imara. Mali si msingi bora, maana haiwi muhimu kiasi cha mtukufanya juu chini kuipata. Tangu zamani Mungu alisema kwamba mtu hataishikwa tnkate tu. Kwa nyakati zetu za watu kuwa na matakwa mengi Wakristowahitaji kutilia maanani hilo onyo la Yesu kuhusu mali kwa sababu jinsitunavyokabili jambo hilo ndivyo utayari wetu wa kuongozwa na Yesu utaguswapia.

k.16 Yesu aliendelea kusisitiza fundisho hilo kwa kutoa mithali juu ya mtummoja, tajiri, aliyefanikiwa sana katika ulimaji na kupata mavuno mengi.Alikuwa tajiri kisha akaongezeka utajiri kwa mafanikio katika kilimo chake,pengine kuliko alivyotazamia.

k.17-18 Huyo tajiri alipowaza atafanya nini na hayo mavuno yaliyozidi,akaamua kuzivunja ghala zake na kuzijenga nyingine kubwa zaidi, ili ayatunzehayo mavuno.

k. 19 Kisha aliamua kwamba apumzike, na kujifurahisha, hali akijua anayoakiba ya vyakula na mali, kiasi cha kutosha maisha yajayo.

Tunaposoma habari hiyo twaona kwamba lugha yote ilimzungukia yeyemwenyewe, alijaa umimi, alijiwaza mwenyewe tu. Tazama maneno ya umimi‘nifanye nini? Nita....’ ‘yangu, vyangu, nafsi yangu, ulivyojiwekea’ ‘ule n.k.’

k.20 Kumbe! alikuwa amemsahau Mungu! ‘Mungu akamwambia....’ Alidhanikwamba yeye mwenyewe ni mtawala wa maisha na mali yake, kumbe, sivyoilivyo. Usiku ule Mungu alimwita aondoke duniani, hakuna kupumzika wala kulawala kunywa wala kufurahi hapa duniani. Mali yake itakwenda kwa wengine.Mungu alimwita ‘mpumbavu’ (si mbaya). Katika kufikiri kwake na kuamuakwake amesahau maisha ya baadaye baada ya kuondoka hapa duniani.

Page 116: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

Ijapokuwa aliweza kuamua juu ya vitu vyake, hakuweza kuamua juu ya urefuwa maisha yake, neno hilo limo mikononi mwa Mwumba wake. Mali yakehaikumfaa lo lote kwa maisha ya baadaye. Mipango yake yote ilikuwa bure.Wajibu wake haukwisha alipofikia hatua ya kuwa salama kwa upande wamaisha ya hapo duniani, ilimbidi awafikirie wengine baada ya kuwa na vyakutosha mwenyewe. Akiba yake ilienea kwa miaka mingi lakini maisha yakekwa saa chache

k.21 Kujitajirisha kwa Mungu ni nini? ni kutumia mali kwa ajili ya maskini,wahitaji na wenye shida (k.33). Mali yenyewe na kuwa na mali si kosa, ila nimatumizi yake. Mtazamo wa huyo mtu kuhusu mali ulikuwa mbovu. Kila mtuhupaswa kuwa na mtazamo wa hekima juu ya mali yake. Ijapokuwa Yesualikataa kuwa mwamuzi kuhusu urithi wa yule aliyesababisha mazungumzohayo, hata hivyo ni mwamuzi wa mitazamo yetu na tabia zetu. Huyo mtualijipenda sana, wala hakumpenda jirani yake, wala Mungu, Mwumba wakealiye asili ya vitu vyote. Vitu tulivyo navyo tumejaliwa kuwa navyo kwa neemaya Mungu, ni kama tumeazimiwa vitu hivi kwa ule muda wa kukaa hapoduniani. Tena ni ukumbusho kwamba twaweza kuondoka duniani wakati wowote, hata kwa ghafula na bila kutazamia. Hatuna madaraka juu ya jambo hilo.

12: 22-34 Kuwa huru na masumbufuHayo yanayofuata ni mafundisho ya Yesu kwa wanafunzi wake na yanafuatamaoni yake juu ya utajiri.

k.22 Yesu aliongeza mafundisho yake juu ya choyo n.k. kwa kuwatahadharishawanafunzi juu ya kosa la kujisumbua hasa juu ya chakula na mavazi. Huendawalikuwa na wasiwasi kwa maisha yao ya mbele, wameacha kazi zao, nafamilia zao, kwa hiyo, wataishije? Choyo ni hali ya mtu kudhani kwamba hanavya kutosha; kusumbuka ni hali ya mtu kuogopa kwamba hatakuwa na vyakutosha. Yesu aliwaambia wazi kwamba ‘msisumbukie maisha yenu, mtakulanini...’

k.23 Ndipo alitoa sababu ya kuonyesha kwamba hawana haja ya kusumbuka.Haswa maisha yao ni bora kabisa kupita chakula na mavazi. Haiwaziki kwambaMungu aliyewaumba na kuwapa uzima hatakosa kuwapa mahitaji ya lazimakuendeleza maisha yao.

k.24 Yesu aliwaelekeza kuwaza juu ya ndege na maua, viumbe wengine waMungu, wasiolingana na wanadamu kwa thamani yao au ubora wao, hatahivyo, Mungu huwatunza. Viumbe hivi hawana uwezo wa kulima n.k. hata hivyowanaishi kwa neema ya Mungu. Kunguru walihesabiwa ndege najisi (Law.11:15) hata hivyo, Mungu huwatunza. Yesu alisisitiza ubora kabisa wawanadamu.

Page 117: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 407

k.25-26 Halafu Yesu alionyesha kwamba ni kazi bure kujisumbua kwa sababuwanadamu wanao mpaka katika uwezo wao. Hawawezi kuziongeza siku zaoduniani (kumbuka tajiri mpumbavu ambaye alipoitwa na Mungu aondokeduniani, hakuwa na la kufanya ila kuondoka). Wala mtu hawezi kukiongezakimo chake, kama amezaliwa mfupi atakuwa mfupi, kama amezaliwa mrefu,atakuwa mrefu. Kama tumeshindwa kuongeza siku au kimo, hata tukijisumbuakiasi gani hatutafaulu. Ikiwa jambo dogo linatushinda, Je! habari ya jambokubwa?

k.27-29 Yesu aliendelea kusema juu ya maua, ambayo muda wao wa kumea nimfupi sana, hata hivyo, Mungu huwavika kwa fahari, maumbo yao na rangi zaohuwa nzuri ajabu iwapo hayana uwezo wa kusokota kama sisi wanadamu. Hatahivyo, wamevikwa vizuri sana na Mungu. Tusifikiri kwamba Yesu alifundishakwamba sisi wanadamu hatuna haja ya kufanya kazi na kushughulikia kupatachakula n.k. La, Hakusema msifanye kazi, bali msijisumbue. Yatupasa tuwazena kupanga tutapataje chakula na mavazi yetu, ila hayo yasitawale maishayetu. Neno hilo lahusu vipaumbele vya maisha yetu.

k.30-31 Kisha Yesu alifika kwenye kiini cha habari hiyo. Waumini wanaye Babamwenye uwezo wote, aliyejaa upendo juu yao, Baba mkarimu, mtoaji. Yeyehujua kabisa kwamba wanayo mahitaji hayo ambayo ni lazima kwa kuishi kwao.Wajibu wao ni kumtumikia Mungu na kutanguliza shughuli za Ufalme wake.Kipambele cha kwanza katika maisha yao kiwe Ufalme wa Mungu na Yeye kwaupande wake ataangalia neno la riziki zao. Neno ‘kwanza’ laonyesha kwambamambo ya mahitaji yao yatafuata. WaMataifa hawashughulikii mambo yaMungu, mawazo yao yote huzungukia shughuli za chakula na mavazi na malin.k. Waumini wasifanane nao.

k.32 Yawezekana wanafunzi wake, kundi dogo, waliogopa walipofikiri maishaya baadaye. Itakuwaje? maana wameacha kazi zao, na nyumba zao. Penginewaliwaza utunzaji wa familia n.k. Yesu aliwaambia ‘msiogope’. Baba Munguamewapa ufalme wake, kitu kikubwa mno, nao wamewajibika kuutafuta kwanzashughuli za ufalme huo. Watazame vitu walivyo navyo na kuhesabu kwambahavina maana kwa kuvilinganisha na huo ufalme. Wawe tayari kutoa na kutoa,tena na tena, kwa sababu mali yao ya dunia ni ya muda tu, tena inawezakushambuliwa na kutoweka ghafula. Ila hazina ya mbinguni ni ya thamani mno,wala haishambuliwi na kitu cho chote, kimetunzwa salama. Kwa hiyo,wasitawaliwe na mali. Haina maana kwamba kila muumini asiwe na mali yoyote, la. Hilo ni neno kwa wachache. Twajua Martha alikuwa na nyumba nakumkaribisha Yesu nyumbani kwake, wala Yesu hakumwambia aiuze (10:38).Kabla ya kufa Yesu alimkabidhi mama yake kwa Mtume Yohana ambayealimpeleka nyumbani kwake na kumtumza (Yn. 19:27). Kama waumini wotewatakosa mali watakuwa maskini watakatifu wanaowalemea wanadamuwenzao. Kutegemea mali kunazuia kumtegemea Mungu. Maisha yetu yabaadaye ni muhimu kuliko maisha yetu ya sasa. Kila mtu ajua kwamba kile

Page 118: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

anachohesabu cha maana ndicho kinachomtawala, kwa hiyo, Yesu ametoachangamoto kwamba Ufalme wake uwe kitu cha kwanza katika maisha yetu.

12:35-48 Kurudi kwa Mwana wa Adamuk.35-44 Katika sehemu hiyo Yesu amesema juu ya watumishi waaminifu nawatumishi wasio waaminifu. Alisema moja kwa moja na wanafunzi wake. Kwamaneno ‘vyenu... zenu... ninyi’ amesisitiza mambo yanayowahusu waowenyewe. Hapo nyuma amesema juu ya haja yao ya kutanguliza mambo yaUfalme wa Mungu katika maisha yao, na maneno hayo yanayofuata yasemajuu ya zile hali zinazotakiwa kwa mambo ya mbele na hasa kwa tukio kuu laYesu kurudi na kuuhukumu ulimwengu na kuuingiza Ufalme wake kwaukamilifu.

k.35-36 Budi wawe wamejiandaa kwa ajili yake. Nyakati zile Wayahudi wakiume walivaa kanzu ndefu ambayo walizoea kuifunga kiunoni wakati washughuli. Hivyo wanafunzi nao wawe na hali ya kufanya kazi kwa bidii na kuvaakulingana na wakati uliopo. Pia wawe na taa zinazowaka, wawe na utambuzimaishani mwao na kuona vizuri ili wapime lililo muhimu na lisilo muhimu kwao.Wawe tayari kumpokea Bwana wao wakati wo wote atakapotokea, hata akijausiku sana wawe tayari. Haina maana kwamba wasilale, bali wawe tayarihaidhuru kama imeonekana Bwana amechelewa sana. Kuwa tayari nikuendelea kwa bidii katika shughuli za Ufalme wake. Wasipoe katika maishayao ya Kikristo.

k. 37-38 Hao walio tayari wana heri, na ajabu ni kwamba Yeye, Bwana wao,atajifunga na kuwahudumia chakulani. Katika Ufalme wa Mungu upinduzihutokea, mambo hayawi kama yalivyo katika falme za dunia hii. Wakiwa huruna masumbufu yaliyotajwa na Yesu kuhusu chakula na mavazi watakuwa nanafasi ya kujiweka tayari na kuwa macho kwa siku ile kuu ya Kurudi kwa Yesu,Bwana wao.

k. 39-40 Ila kama hawatakuwa tayari watafanana na mtu ambaye hakujaliusalama wa nyumba yake, akaja mwivi na kuivunja. Mwivi hatoi taarifa, hatumikadi ya kusema anafika saa fulani. Kama mtu angalizingatia usalama wanyumba yake angalichukua hatua za kuangalia kwamba nyumba yakeisivamiwe. Kutokuwa tayari kwa Kuja kwa Mwana wa Adamu kwasababishahasara kwa yule asiyejali. Ijapokuwa ni hakika Yeye atakuja hakuna ajuaye saa.Iwapo saa yake haina uhakika, jambo lenyewe lina hakika, na kwa sababu hiyo,wajiweke tayari.

k.41 Petro alitaka kujua kama hayo aliyosema Yesu juu ya watumishi kuwatayari yaliwahusu wao tu au yaliwahusu watu wote. Wakati unaosemwa nibaada ya Ufufuo wa Yesu na kabla ya Kurudi Kwake, wakati wa Injili kuhubiriwana Kanisa kuwepo.

Page 119: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 409

k.42-44 Yesu hakumjibu moja kwa moja ila alimwambia kwamba yalimhusuyeye na wale watakaowekwa kuwa viongozi katika Kanisa. Alisisitiza tena hajaya watumishi wake kuwa waaminifu, na wenye hekima ya kuutambua umuhimuwa kazi za Bwana. Alisema juu ya wakili aliyepewa wajibu mkubwa wauangalizi wa kuwapatia watumishi wengine posho lao na kuziendesha shughuliza shamba la bwana wake vizuri. Bwana wake atakapomkuta anafanya vizurindipo atapata heshima na thawabu ya kupewa madaraka makubwa zaidi.

k.45-46 Ndipo Yesu alisema juu ya watumishi wasio waaminifu. Ikiwa wakilialiyesemwa katika mfano amedhani kwamba Bwana wake harudi kwa vilealivyochelewa kuonekana na kwa sababu hiyo hajali wajibu wake wa kuangaliamanufaa ya watumishi, na yeye mwenyewe alegea na kuishi kinyume cha witowake. Hukumu kwa huyo wakili mbaya itakuwa kali sana, kwa sababu alijuayaliyompasa wala hakuyafanya. Atashiriki hali ya wasioamini.

k.47-48 Kanuni ya hukumu ya watumishi ni kiasi cha ufahamu wao wa mapenziya Bwana wao. Mitume walioshirikiana na Yesu na wale waliofundishwa naMitume walijua kabisa mapenzi ya Bwana wao, na sisi nasi, kwa kusoma Nenola Mungu kwa uangalifu, twaweza kujua mapenzi ya Mungu kwa maisha yetu.Hukumu ni kali kwa wale wenye ufahamu wa mapenzi ya Mungu. Ila kwa waleambao hawajui mapenzi ya Mungu, hukumu yao ni ndogo. Kuhukumiwawatahukumiwa, kwa sababu kukosa kufahamu ni kuwa na hatia kiasi fulani,kwa sababu kutokujua kwa mtu ni sehemu katika hali yake ya kuwa mwenyedhambi (Yak.4:17).

Kuna uwiano kati ya ufahamu wetu wa mambo ya Mungu na wajibu wetu wakufanya mapenzi ya Mungu. Ni muhimu sana kufanya mapenzi ya Mungu, sikuyajua tu. Inaonekana zipo tofauti katika thawabu na hukumu kulingana nanafasi zao. Kwa hiyo maneno ya Yesu yaliwahusu watu wote ila ni wafuasiwatakaohukumiwa vikali zaidi wakikosa katika kuutimiza wajibu wao.

12:49-59 Ishara za majira (Mt. 10:34-46; 16:2ku. 5:25ku)Yesu alisema habari hii kwa makutano pamoja na wanafunzi. Alisisitizaumuhimu wa nyakati zake, na kutoa shabaha ya Kuja Kwake. Kutokana na KujaKwake taifa la Israeli limefikishwa kwenye wakati wa kufanya uamuzi mkubwajuu yake, ama kumpokea, ama kumkataa. Ameendelea na huduma yake nawatu wamepewa nafasi nyingi za kumwona na kukata shauri juu yake.Amefananisha huo wakati na ule wa mtu aliye njiani kwenda hukumuni, ambayeinambidi akate shauri ama aendelee kwenda kwa hakimu na kuhukumiwa,ambapo mbele yake ni shida kubwa, ama atafute kupatanishwa na mshtakiwake na kuepa hukumu itakayomletea shida.

k.49 Yesu aliwaambia makutano kwamba shabaha ya Kuja Kwake duniani1ilikuwa kuleta watu kwenye njia panda ya kufanya uamuzi juu yake.Alifananisha jatnbo hilo kuwa kama moto kutupwa duniani, yaani hukumu kali

Page 120: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kuletwa juu ya kutokuamini kwao. Kwa nguvu ya Neno lake na Roho wake,moto huo unazidi kuwaka.

k.50 Ila jambo hilo linamwingiza Yeye Mwenyewe katika dhiki na mateso, paleMsalabani atazamishwa na dhiki kama mtu anavyozamishwa katika maji wakatiwa ubatizo naye alitamani sana wakati ufike wa Kufa Kwake ili hayo yoteyatokee. Yeye ataibeba hukumu ya Mungu juu ya dhambi za wanadamu. Hapotwajifunza jinsi Msalaba ulivyoweka kivuli chake juu ya Yesu hata kablahaujatokea, daima aliishi katika ufahamu wa kujua kwamba atateswa vikalisana katika kutoa fidia ya dhambi (Mk. 10:38; Zab.69:1-3; 2 Kor.5:14; Flp.1:23).Alilipokea neno la Msalaba hali akijua ni jambo lisiloepukika, hata hivyo,hakuvutwa wala kupendezwa na habari yake.

k.51-53 Halafu aliwauliza watu swali ‘Je! mwadhani ya kwamba nimekuja kuletaamani duniani?’ na alitoa jibu kwamba ‘La, sivyo, bali mafarakano’. Iwapo Yeyeni Mkuu wa Amani na amekuja kuufanya upatanisho kati ya Mungu namwanadamu, hata hivyo, Kuja Kwake kwasababisha matengano hata katikafamilia, kwa sababu ujumbe wake unawasukuma watu kukata shauri juu yake,ama kumpokea, ama kumkataa, kwa hiyo, hata katika nyumba wenginewatamkubali na wengine watamkataa. Inaashiria kwamba kuna mengineambayo ni muhimu kuliko amani, na ujumbe wake wa wokovu ndio mwenyeumuhimu huo. Ila mwishowe kabisa amani itakuwepo, wakati wa kutimizwa kwaUfalme wake.

k. 54-57 Ndipo Yesu aliendelea kusema na makutano juu ya hali yao. Walikuwamabingwa wa kusoma hali ya hewa na kujua kama mvua itanyesha au jualitaangaza. Ila ajabu ni kwamba, iwapo katika historia yao wamefundishwakumtazamia Masihi, na Yesu kwa huduma yake amewapa changamoto yakuwa Yeye ndiye huyo Masihi, akitenda maajabu ya kuyathibitisha madai yake,hata hivyo, hawakuwa tayari kukubali kwamba wakati huo ndio wa maana sanakatika historia yao, ni majira ya Masihi. Aliwaita ‘wanafiki’ kwa sababu ya halizao, walishughulikia mambo madogo kama hali ya hewa, ila mambo makubwaya kumhusu Yeye, hawakujali. Kwa kibinafsi hawakuwa watu wa kutaka haki.

k. 58-59 Katika upofii wa kutokuamini kwao, na katika hali yao ya kutokuwatayari kumpokea, wameshindwa kuona mawingu mazito ya hukumu ya Mungu.Baadaye, B.K.66-70, mawingu hayo yalileta juu yao hukumu kali ya Mungu,Warumi walikuja na kuuteka Mji wao mtakatifii, na kuulaza chini, pamoja nahekalu lao. Iliwapasa wajiweke tayari na kukata shauri la kupatana na Munguwao kabla hazijaja siku hizo za taabu. Nafasi hii ya kufanya patano ni katikakumpokea Yeye Wakiwa na hekima watatambua wakati huo ndio wakati wakuamua juu yake, baadaye watakuwa wamechelewa. Wafanye patano iliMungu asilete hukumu yake wakati huu katika ulimwengu wa sasa na wakatiwa baadaye katika ulimwengu ujao. Wafanye juu chini kupatana na mshtakiwao, wasipofanya hivyo hawatatoka salama barazani.

Page 121: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 411

13:1-5 Mikazo juu ya kutubuChangamoto wa kujiweka tayari kwa hukumu inayokuja unafikia upeo katikamwito wa kutubu kabla ya msiba kutokea.

k. 1-5 Katika sehemu hiyo tunayo habari ya ukatili wa siasa uliofanywa na Pilatona habari ya msiba fulani kutokea kama tendo la Mungu. Habari za mambohayo hazionekani katika maandishi ya historia ya nyakati zile.Watu walimpasha habari ya matukio hayo. Hatuambiwi sababu zao zakumwambia Yesu. Yawezekana walifikiri matukio hayo ni aina ya hukumualizozitaja Yesu katika mazungumzo yaliyotokea (12:58,59). Kwa mtindo waowa kuwaza Wayahudi walifikiri kwamba ikitokea shida au msiba fiilani sababuyake ni dhambi (Yn.9:1-2). Pilato alijulikana sana kuwa mkatili na inaonekanakwamba wakati fulani Wagalilaya waliofika Yerusalemu kwa kumwabuduMungu waliuawa kwa ukatili, wakati wa kutoa sadaka zao hekaluni. Si wazikama damu yao ilichanganyishwa na damu ya sadaka, ila ni hakika kwambawaliuawa wakati walipokuwapo Yerusalemu kwa shabaha ya kumtolea Mungusadaka zilizoamriwa. Pengine wao wenyewe walipatikana katika jambo lakuchochea siasa kinyume cha Warumi. Ni vigumu kujua kwa nini haikutokeaghasia katika watu, kwa sababu inaonekana kwamba Pilato alifanya kwa ukatilisana na tendo lake la kuchanganywa damu yao na damu ya sadaka lilikuwabaya mno. Watu walifikiri kwamba hao waliopatikana na uuaji huo bila shakawalikuwa wamefanya dhambi kubwa. Lakini Yesu hakuunga mkono wazo hilo.Yeye aliona watu wote ni wenye dhambi na wote walipaswa kutubu dhambizao, haidhuru zikiwa ndogo na chache, au zikiwa kubwa na nyingi.

k.4-5 Ndipo wengine walipatwa na msiba pale Yerusalemu wakati wa mnarahuko Siloamu kuanguka juu yao. Watu walidhani kwamba hao watu, bila shaka,wametenda dhambi kubwa iliyosababisha waangamizwe hivyo. Tena, Yesualikataa wazo hilo na aliendelea kusisitiza haja ya watu wote kutubu. Watu woteni wenye dhambi na watu wote wamepaswa kutubu, nao wasipotubuwataangamia, pengine si kwa njia ya uuaji mbaya au msiba, hata hivyo,watapatwa na hukumu ya Mungu mwisho wa maisha yao. Hivyo, Yesualisisitiza umuhimu wa watu kutubu bila kukawia. Maana hao walioangamizwahawakupata nafasi ya toba kwa vile walivyokufa ghafula bila kutazamia.Huenda Yesu alikuwa akiwaza wakati Warumi watakapokuja na kuwaangamizaWayahudi kwa sababu ya ukaidi wao wa muda mrefu.

13:6-9 Mfano wa mtini usiozaa matundak.6 Yesu aliendelea kusisitiza umuhimu wa kutubu bila kukawia. Alitumia mfanowa mtu mwenye shamba la mizabibu, na ndani yake alikuwa amepanda mtini.Mtini na mzabibu zilikuwa ishara ya taifa la Israeli (Hos.9:10; Isa.5:lku). Huyomtu aliona kwamba wakati umefika hata umepita kwa mtini wake kuzaamatunda maana umekaa muda wa kutosha. Kwa miaka mitatu ametazamiaatapata matunda.

Page 122: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.7-9 Kwa sababu ya kukosa kupata matunda aliona vema mtini ukatwe iliaweza kupanda mti mwingine mahali pake. Hivyo, akamwagiza mtunzaji washamba kuukata. Lakini huyo mtu akamshauri auache kwa mwaka mwingine,na yeye ataupalilia na kutilia samadi, na kufanya yote ya kuusaidia mtini kuzaa.Ndipo, ukikosa kuzaa baada ya huo mwaka mmoja, basi ukatwe. Hapo tenaYesu amesisitiza haja ya taifa la Israeli kuzaa matunda, yaani kutubu na kukatashauri la kumpokea kuwa Masihi wake wa kweli. Kwa kuwa Yesu alikuwaamefanya huduma yake kwa muda mrefii na mpaka hapo watu kwa jumlahawajampokea, hivyo ilionekana kwamba mashaka yapo ya kuwa wataendeleana hali hiyo. Ikiwa wataendelea hivyo basi, muda utafika, ndipo uamuziutatolewa kwamba taifa halifai kuendelea, liondolewe mahali pake kwa sababulimekosa kutambua shabaha na umuhimu wa uteule wake. Katika mfano huotwaona uvumilivu, subira, na rehema za Mungu aliye mzito wa kuleta hukumuakipenda kuwapa watu muda mrefu wa kutosha kuja kwenye toba nakumwamini Kristo. Kama ilivyokuwa wakati huo kwa taifa la Israeli, ndivyo ilivyo,kila wakati, na kwa kila mtu. Mtu akiendelea kumkataa Kristo hujiweka mahalipagumu pa kuingojea hukumu ya Mungu.

13:10-17 Yesu alimponya mwanamke siku ya SabatoHabari hii yapatikana katika Injili hiyo tu. Yahusu matumizi ya halali ya Sabato,jambo ambalo limeonekana hapo nyuma. Yesu alizoea kufundisha katikasinagogi (4:15,16,31,41; 6:6) na mara kwa mara aliponya watu siku ya Sabatokama kuchokoza Wayahudi ili watafakari sana juu ya mambo yaliyo halali yakufanywa siku hiyo. Sinagogi ilitokea kama mahali pa upinzani na sabato jambola kumpinga Yesu kwa jinsi viongozi hawakuwa tayari kuyabadili mawazo yaokuhusu Sabato. Baada ya habari hiyo hakuna habari za Yesu kuwa sinagoginitena kwa vile ilivyokuwa hatari aendelee kuchochea moto upinzani wao.Wataendelea kumpinga ila Yeye alihitaji nafasi ya kuwaandaa wanafunzi kwamgongano wa mwisho utakaotokea Yerusalemu utakaosababisha KuuawaKwake.

k. 11 Alipokuwemo sinagogini akifundisha Yesu alimwona mwanamkealiyelemewa mno, alikuwa amepindana asiweze kujiinua, tena alikuwaameonewa hivyo kwa miaka kumi na minane. Twaona tabia ya Yesu ilikuwakuwaona watu wenye shida na kutaka kuwahudumia. Ugonjwa wakeumesababishwa na kazi ya Shetani. Luka ametaja pepo wa udhaifu.Mwanamke mwenyewe hakuwa mbaya, wala hakuwa na maisha mabovu, la.Alikuwa ndani ya sinagogi akimwabudu Mungu, na Yesu alimwita ‘uzao waIbrahimu’ maana yake alikuwa akimwamini Mungu kweli. Ila kutokana na kaziya Shetani alikuwa ameonewa na udhaifu wa kupindana miaka hiyo yote. Nivigumu kuelewa uhusiano kati ya magonjwa na Shetani, ila hapo Yesualimponya akionyesha kwamba ni Yeye mwenye uwezo wa uponyaji na uwezowa kumshinda Shetani.

Page 123: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 413

k.12 Yesu alipomwona huyo mwanamke akamwita na kumwambia moja kwamoja ‘Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako’. Yesu alianzishia jambo hilo.Hatusikii kwamba yule mama alifanya lo lote. Yesu alitumia neno‘umefunguliwa’ kwa sababu alitaka kutumia neno hilo katika kujadiliana naviongozi (k.15).

k.13 Ndipo Yesu aliweka mikono yake juu yake akiukamilisha uponyaji wake.Yawezekana pepo wa udhaifu alitolewa (k.12) ndipo kwa kuwekewa mikonoakanyoka na kuponywa, kisha akamtukuza Mungu. Sifa ilienda kwa Mungu.Yesu hakujivutia sifa kwake.

k. 14 Ilipotokea hivyo, ni wazi kwamba hakuna aliyeweza kuukana ukweli wauponyaji huo ila hoja ilitokea juu ya jambo hilo kufanywa siku ya Sabato. Mkuuwa sinagogi na baadhi ya waliokuwepo hawakufurahia uponyaji wa huyo mamakufanyika katika Sabato nao walitaka kuuliza juu ya uhalali wake. Mkuuhakusema moja kwa moja na Yesu ila alisema na watu akiwakumbushakwamba walikuwa na siku sita za kuleta wagonjwa wao, hakuna haja yakuitumia siku ya Sabato kwa kazi hiyo. Huenda mkuu wa sinagogi alionakwamba ni yeye mwenye madaraka ya kuongoza mambo yanayofanyikasinagogini na Yesu alikuwa amemwingilia. Pengine aliogopa kwamba fujoitatokea mle sinagogini.

k.15-16 Yesu akamjibu kwa kumwuliza yeye na wale waliokuwa upande wake.Iwapo yule mkuu hakusema moja kwa moja na Yesu hata hivyo alikuwaamemlenga Yeye. Yesu aliwaita ‘wanafiki’ kwa sababu wao wenyewe katikautunzaji wa wanyama wao waliwafungulia siku ya sabato ili wapate maji n.k. Je!mwanamke si bora kuliko wanyama wao? Je! hana haki ya kufunguliwa siku yaSabato? Je! Shetani aendelee kumwonea? Wanyama hufunguliwa siku hiyomoja baada ya kufunguliwa kila siku nyingine. Huyo mwanamke Je! hawezikufunguliwa siku hiyo baada ya kufungwa miaka kumi na minane? Mnyamahaachwi hata kwa siku moja! Mbona mwanamke haachwi kwa siku moja? Yesualiona kwamba mwanamke huyo alikuwa na haki kabisa kufunguliwa siku hiyo‘haikupasa afunguliwe?’. Yesu hakuwaza kwamba uponyaji huo ni kaziisiyoruhusiwa kufanywa siku ya Sabato. ambayo ingeweza kungojea sikunyingine. Sabato ilikuwa siku ya kupata ushindi juu ya Shetani. Ni halali kufanyamema siku ya Sabato. Ni tendo la Mungu, la uwezo, ambalo huitakasa hiyoSabato. Badala ya kuwa tendo lisilofaa, lilikuwa tendo lililofaa sana kwa Sabato.Wapinzani walikuwa wanafiki kwa sababu hawakufuata kanuni moja katikakupima mambo. Walikuwa na kanuni moja kwa wanyama wao na kanuninyingine kwa mwanamke.

k.17 Wale waliokuwa wamempinga, mkuu na wenzake walisikia aibu namkutano wa watu walifurahi sana, si kwa jambo hilo tu, bali kwa mambomatukufu yote yaliyotendwa na Yesu.

Page 124: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

13:18-21 Mifano ya punje ya haradali na uchachuk.18 Inaonekana Yesu alisema mifano hiyo miwili baada ya yale mamboyaliyotokea sinagogini. Potelea mbali wengine wampinga, wapo wale wakumfuata. Huduma yake iliwagusa watu na kwa njia yake Mungu anauendelezaUfalme wake hapa duniani. Yesu aliamsha mawazo ya watu kwa kuuliza swali‘Ufalme wa Mungu umefanana na nini? nami niufananishe na nini?’ Ndipoaliendelea kutoa jibu.

k.19 Aliufananisha Ufalme wa Mungu na punje ya haradali, mbegu ndogoambayo ilipopandwa ilikua haraka ukawa mti ambao ndani ya matawi yakendege walitulia. Wayahudi walikuwa na mithali iliyotaja punje ya haradaliwalipotaka kusisitiza udogo wa kitu fulani. Kwa hiyo, iwapo chanzo cha Ufalmewa Mungu chaonekana kuwa kidogo sana, mwisho wake huwa mkubwa.Chanzo kilionekana kuwa kidogo; Yesu Mwenyewe hakuwa na mali, walamadaraka serikalini au sinagogini, hakuwa na ukubwa jinsi ulimwenguuwazavyo ukubwa. Wanafunzi wake walikuwa akina yahe, hawakutoka katikatabaka za juu wala hawakuwa na hali au uwezo wa kugusa mambo makubwaya siasa au dini. Walakini, mwisho huwa mkubwa sana ukilinganishwa nachanzo chake kidogo. Injili itakapohubiriwa ulimwenguni itawavuta watu wa kilataifa, kila tabaka, na kila hali. ‘ndege wa angani’ pengine maneno hayoyaashiria WaMataifa ambao wataingia katika Ufalme wa Mungu (Eze. 17:23;31:6; Dan.4:12, 21) au pengine ni maneno tu ya kuashiria uimara wa huo mti.Ufalme huo utakuwa wa walimwengu wote si kwa Wayahudi tu. Katika mfanohuo Yesu alisisitiza ukuaji wa nje wa Ufalme wa Mungu. Matukio matukufu nayenye uwezo yalitokea katika huduma ya Yesu hata hivyo ingalikuwa vigumukusema kwamba hayo yalionyesha Kuja kwa Ufalme wa Mungu kwa nguvu, ilayale yaliyokuwa yakitokea yalikuwa malimbuko yake na kuhakikishia kwambambeleni huo Ufalme utakuja kwa utimilifu na ukamilifu. Mwishowe ulimwenguwote utamezwa na huo Ufalme.

k.20 Yesu alirudia kuuliza swali Niufananishe na nini ufalme wa Mungu?’. Ndipoakaufananisha na chachu inayotiwa ndani ya unga mpaka unga woteunachachishwa. Chachu ni ndogo, unga ni mwingi, ila chachu inapotiwa ndaniya unga hufanya kazi kwa siri na kwa ukimya na kuenea katika unga wote,mpaka umekuwa tayari kwa kupikwa. Chachu hufanya kazi kwa ndani, kamaambavyo Roho Mtakatifu afanyavyo mioyoni mwa watu mpaka wamebadilishwakwa ndani. Uwezo wa kubadilika ulitoka nje, unga haukuweza kujibadilishamwenyewe. Kwa mfano huo Yesu alisisitiza ukuaji wa ndani wa Ufalme waMungu. Kuna uwezo mkubwa katika huduma ya Yesu na Injili yake na uwezohuo ni uwezo unaodumu hata mpaka milele.

Jambo kubwa linalofundishwa kwa mifano hiyo miwili ni chanzo kuwa kidogo namwisho kuwa mkubwa. Chanzo katika nchi moja na kwa mtu mmoja na watukadha waliojiunga naye, mpaka wengi kuja kumwamini na kubadilika kimaisha,hata kuugusa na kuubadili mwenendo wa ulimwengu na kuleta mabadiliko

Page 125: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 415

makubwa katika maisha ya watu wengi. Wa kwanza hawakuwa na rasimali,wala elimu ya juu, wala mamlaka katika tasisi n.k. ila walipewa kipawa chaRoho Mtakatifu ambaye alifanya kazi ndani yao na kwa njia yao. Pia Rohohufanya kazi ya kuwahoji watu katika dhamiri na mioyo yao kabla hawajamjiaKristo. Yesu afaulu kuuingiza Ufaline wa Mungu katika ulimwengu huo.

13: 22-30 Maingilio membamba ya uzima (Mt.7:13ku; 22ku; 8:llku)k.22 Luka ametukumbusha kwamba Yesu alikuwa akienda Yerusalemu,alipenda sana kutaja hiyo safari. Hakwenda moja kwa moja bali alipitia vijijini namijini na kuwafundisha watu, akiwapatia wengi nafasi ya kumsikia.

k.23 Njiani mtu fulani alimwuliza juu ya idadi ya watu watakaookolewa nakuingia katika Ufalme wa Mungu. Yawezekana swali lake liliulizwa katikamazingara ya huduma ya Yesu. Ijapokuwa wengi waliguswa na huduma yake siwote ambao watakuwemo katika Ufalme wa Mungu. Kama watakuwa wengi auwachache hutegemea itikio la wale waliomsikia na hapo Yesu alisisitiza wajibuwa watu kuitika vema. Si wengi walioitika mafundisho yake kwa kuyashika nakutia maishani mwao. Wayahudi walifikiri kwamba karibu Wayahudi wotewataingia Ufalme wa Mungu isipokuwa baadhi yao wachache kama watendamabaya sana na wazushi.

k.24 Yesu akamjibu yule mtu aliyemwuliza hilo swali ila hakumpa idadi ya watu.Badala yake alimpa yeye na watu wote changamoto ya kujitahidi, yaaniwafanye juu chini ili wapate kuingia katika huo Ufalme, kwa sababu mlangowake ni mwembamba. Si wote watakaoingia ila wale tu wenye kutubu kweli nakujikabidhi kwa Yesu. Haikuwa rahisi watu wafanye hivyo katika hewa yaupinzani na dharau iliyokuwepo kwa Yesu. Haina maana kwamba mtu awezakujistahilisha ili apate kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa jitahada zake, la,hakuna aliye na ustahili wa kutosha wa kuingia, ila yampasa mtu awe na nia yakuingia. Twaweza kufananisha na mchezo wa mpira, uwanja ni mkubwa namlango wa kupitisha mpira ni mdogo. Shabaha ya mchezo ni kuuingiza mpirakwenye nafasi ndogo. Vivyo hivyo, mlango wa wokovu ni mwembamba, ni YesuMwenyewe, Yeye ndiye mwenye madaraka juu ya wale wa kuingia, na ye yoteapendaye kuingia budi ajihusishe vema na Yesu.

k.25-27 Iwapo idadi haina mpaka, ni nafasi ambayo ina mpaka, kwa sababuitafika siku ya kufungwa mlango, ndipo nafasi itakwisha, na tangu hapohaitawezekana mtu ye yote aingie, potelea mbali adai nini (Mt.25:10). Ni kazibure kudai kwamba walimwona na kumsikia, ikiwa hawakuyapokea mafundishoyake, wala hawakuwa tayari kumpokea kwa dhati. Iliyotakiwa ni kumfahamukibinafsi kwa kujihusisha naye. Majadiliano ya kitheologia ya idadi n.k. hayanamaana yo yote. Jambo kubwa ni mwenye nyumba kuwatambua. Utafika wakatiwa mlango kufungwa, na nafasi ya kuingia kupita. Wakati huo wa sasa niwakati wa wokovu na wakati wa kujitahidi. Baadaye kutafuta kuingia ni kazi

Page 126: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

bure, maana ni kuchelewa. Wa kuingia ni wale wenye kutubu kweli na kuachamaisha mabaya.

k.28-30 Halafu Yesu alisema juu ya huzuni na kukata tamaa ya walewalioshindwa kuchukua nafasi ilipokuwepo. Watasikia shida sanawatakapowaona watu wa zamani, akina Ibrahimu, na manabii, n.k. wamo ndanina wao wamefungiwa nje. Tena, pamoja na hao wa zamani, kumbe watuwengine ambao walidhani kwamba kamwe hawatakuwemo watakuwemo pia,hao ni WaMataifa wakishiriki pamoja na akina Ibrahimu n.k. Watu watatokapande zote za dunia (Zab. 107:2-3). Kwa hiyo, hakuna atakayeingia moja kwamoja bila kumwamini Kristo. Ye yote atakayempokea Kristo atakuwemo, ikiwaalitangulia kuamini au aliamini baadaye, kama ni Myahudi au ni Mmataifa, sikitu, jambo kubwa ni uhusiano wake na Yesu. Wokovu na hukumu vinawiana.Changamoto kali ni kutokuwemo katika waliofungiwa nje. Luka amekaza wajibuwa mtu. Katika 14:15-15:24 atakaza upande wa pili, neema na ukarimu waMungu.

13:31-33 Uadui wa Herodek.31 Baadhi ya Mafarisayo walimwendea Yesu na kumwonya juu ya nia yaHerode kumwua. Huyo Herode alimwua Yohana Mbatizaji na alisikia wasiwasiwingi alipojulishwa habari ya matendo makuu ya Yesu na jinsi ambavyo watuwengi walikwenda kumsikiliza. Hao Mafarisayo walimwonya Yesu na kumshauriaondoke katika eneo la Herode na kwenda penginepo. Yesu alikuwa katikasafari ya kwenda Yerusalemu, ila hakuwa na haraka, akigeukia hapa na pale.

Kwa nini walimwonya? Kwa kawaida Mafarisayo walimpinga Yesu kwa nguvuila hawakumpenda Herode. Wazo moja ni kwamba walitumwa na Herode kwasababu alipenda Yesu aondoke mpakani mwake kwa sababu alijua kwambaakimwua dhamiri yake itamshtaki sana kama ilivyoendelea kumshtaki juu yakumkata kichwa Yohana Mbatizaji. Alikuwa na shabaha ya kumtisha Yesu iliaondoke kwenye eneo la utawala wake. Wazo lingine ni kwamba walifikirikwamba Yesu akienda Yerasalemu huko atashikwa na kuhukumiwa kufa.Kama si hivyo, wazo ni kwamba, ingawa Mafarisayo hawakumpenda Yesu,walikuwa upande wake kuliko kuwa upande wa Herode, hivyo, walitakakumhifadhi Yesu. Hatujui kwa hakika walitoa shauri hilo kwa shabaha gani.

k.32 Lakini Yesu hatishiki, iwapo anakwenda Yerusalemu haina maanakwamba anamkimbia Herode, kwa kuwa Herode hawezi kufanya lo lote lakuibadili mipango yake. Ataendelea na kazi zake za kutoa pepo na kuponyawagonjwa mpaka wakati wake utakapotimia, wakati ambao umeamriwa naMungu. Huduma yake ina muda usiotawaliwa na Herode, wala na mwingineawaye yote, ila na Mungu, Baba yake tu. Hivyo, hawezi kujali ujumbe waMafarisayo wa kuondoka alipo. Alimwita Herode, ‘yule mbweha’ mbweha nineno la dharau, na ni hapo tu, katika Injili zote, ambapo Yesu alionyeshadharau kwa mtu (Lk.23:8). Lina maana ya mjanja, mwenye hila, pia lina maana

Page 127: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 417

ya mtu asiye na maana wala thamani, mtu asiye na ukuu wala heshima. NdivyoYesu alivyomwona Herode, ila Herode mwenyewe asingejiona kuwa hivyo.Yesu alifanya kazi yake katika mpango maalumu, alitawala ‘wakati’. Kazi zakezilikuwa muhimu tena zenye haraka kwa sababu katika siku ya tatu atakamilika,maana yake ni, ama atakuwa amemaliza huduma yake katika eneo la Herode,ama ametimiza ukombozi wa ulimwengu aliokuja duniani kuufanya. (siku 3 sisiku tatu hasa, ni kusema juu ya vipindi mbalimbali vya ufuatano).

k.33 Yesu alisisitiza jambo hilo tena akitumia mfano ule ule wa siku tatu,akionyesha kwamba ilimpasa ashike njia yake, asikubali kupelekwa kando yashabaha yake ya Kuja duniani, kwa sababu njia yake ni ile iendayo Yerusalemu(9:51 aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu) mahali atakapofanya huoukombozi. Yerusalemu ni kitovu cha taifa na ni pale ‘mwisho’ wake (yaani kufakwake) utakapotokea.

13:34-35 Maombolezo juu ya Yerusalemuk.34 Yesu alisema moja kwa moja na Yerusalemu, akiuwaza kama mama(Isa.54; 62:4). Alishikwa na huzuni nyingi alipokumbuka historia yake mbayaambayo ilikuwa uzoefu wa kuwakataa wajumbe waliotumwa na Mungu nakuleta mwito kwa taifa kutengeneza njia zake na kutubu na kumrudia Munguwake. Yesu alikuwa katika mfuatano wa manabii na wenzao. Haohawakupokelewa vizuri, na upeo utafika hivi karibuni, Yesu atakapowaita kwamara ya mwisho. Alikuwa amefikia Yerusalemu mara kwa mara akileta mbeleyao madai yake ya kweli ya kuwa Masihi wao wa kweli, Mwana wa Munguambaye ametumwa kuwasaidia, na kuwaahidi ulinzi na usalama. Alikuwa mpolena mwenye huruma, alikuja kwa shabaha ya kuwakusanya na kuwapa amani,mfano wa kuku na jinsi kuku hukusanyavyo na kuwahifadhi vifaranga wake.Yeye angaliwapatia yote yaliyohitajika kwa usalama wao. Ila shida ilikuwaupande wao, hawakumtaka. Walimkataa, nao wataendelea kumkataa, kishawatamwua.

k.35 Ila si mwisho wake, ila kwa namna fulani ni mwisho wao katika kuwa taifeteule. Watabaki peke yao bila ulinzi wa Mungu, Mungu hatawashughulikia kamahapo nyuma. Baada ya miaka kama arobaini Warumi watakuja (B.K.70) naowatauteka mji wao mtakatifu nao watakosa nguvu za kujisalimisha. Watatekwana mwishowe mji wao utalazwa chini. Ila wasifikiri kwamba Mungu hana mzigojuu yao tena, anao, ila kwa sasa wamewekwa kando ya mpango wake wakuipeleka Injili ulimwenguni, kazi hiyo ya heshima ambayo WaMataifawamekadhibiwa. Yesu alipowaza hayo mawili mazito; kukataliwa kwake, nakuangamizwa kwao, mawili yaliyowiana, ndipo akauombolezea Yerusalemu.Watatamani Masihi wao atokee, kumbe! ameishatokea, nao hawakumtambua,wala hawakumtaka. Atakaporudi kwa mara ya pili ndipo watakapokuwa tayarikumpokea. Waliwajibika kwa yote yatakayowapata. Katika kumkataa Yesuwalikuwa wakifuata mazoea yao.MASWALI

Page 128: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

1. Yesu aliwaonya wanafunzi wake juu ya ‘chachu’ Chachu hiyo ilikuwa ninihasa? Na kwa nini Yesu alisema ni upuuzi?

2. Kwa nini Yesu aliwaonya wanafunzi wake kuhusu kuogopa?Aliwafundisha nini juu yake?

3. Katika mafundisho yake juu ya mali Yesu alitoa onyo gani kwa wanafimziwake?

4. Yesu alitoa Mfano gani kuhusu mali? Tajiri alifanya kosa gani hasa?5. Kwa nini ni kosa kuwa na masumbufu? Eleza jinsi Yesu alivyotilia mkazo

mafundisho yake?6. Watumishi waaminifu wahitajika kufanya nini katika muda wa Bwana

wao kuwa hayupo?7. Eleza maana ya maneno ‘Je! wadhani kwamba nimekuja kuleta amani

duniani....’8. Watu walipomwuliza Yesu juu ya tukio la Pilato kuchanganya damu ya

watu na dhabihu na Tukio la mnara kuangukia watu kadha Yesualisemaje juu ya dhambi za watu hao kulingana na dhambi za watuwengine?Alisisitiza jambo gani linalopasa watu wote?Ndipo alitoa Mfano gani kutilia mkazo fundisho hilo?

9. Yesu alitofautiana na viongozi kuhusu Sabato. Eleza tofauti kubwa katiyake na viongozi

10. Kwa mifano ya punje ya haradali na uchachu Yesu alitaka kufundishanini?

11. Yesu allmjibuje yule mtu aliyetaka kujua idada ya watu watakaookolewa?Eleza

12. Kwa nini Yesu aliomboleza juu ya Yerusalemu? Alijua nini itakayotokeana sababu yake?

14:1-6 Yesu alimponya mtu mwenye safurak.1 Baada ya ibada katika sinagogi Yesu alialikwa ale chakula katika nyumbaya mkuu mmojawapo wa Mafarisayo. Wakuu wengine walikuwepo pamoja nawana-sheria, nao walikuwepo ili wamvizie kuona atafanya nini kwa sababuilikuwa siku ya Sabato. Mara kwa mara Yesu alikuwa amewachokoza kwakuwaponya wagonjwa siku ya sabato.

k.2 Pamoja na hao alikuwepo mtu mwenye safura, pengine alialikwa au huendahakualikwa, maana mara baada ya habari hiyo Yesu alitoa mfano juu ya wageniwalioalikwa karamuni (k. 13,21). Ikiwa alialikwa inaonekana aliwekwa palekama mtego kwa sababu Mafarisayo walijua tabia ya Yesu ya kuponyawagonjwa siku ya Sabato, nao walitafuta sababu ya kumshtaki. Labda aliingiaakitamani kwamba Yesu amwone na kumponya. Ni vigumu kusema kwa hakikani kwa njia gani alipata kuwemo.

Page 129: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 419

k.3 Yesu atafanyaje katika mazingara hayo ya kuwepo kwa wapinzaniwanaomvizia na huyo mgonjwa anayehitaji kuponywa. Hakuna aliyesema nenoila Yesu hali akijua mawazo ya mioyo yao akahojiana nao kwa kuwaulizaWanasheria na Mafarisayo juu ya uhalali wa kuponya siku ya Sabato. Swalilake lilikuwa jepesi ila liliwabana. Aliacha kutaja ‘kazi’ maana Sabato ilisema‘usifanye kazi yo yote’ na wakuu waliona uponyaji ni aina ya kazi isiyoruhusiwa,ila Yesu alitaja ‘kuponya’. Watawajibika wakikataa mtu asiponywe siku yaSabato. Kwa jinsi alivyowauliza itaonekana kwamba wakijibu ‘la, si halali’wamekosa huruma na upendo.

k.4 Wakashindwa kumjibu, kwa sababu walihofu kusema ni halali, jibu lililokinyume cha mapokeo yao waliyotunga wenyewe. Katika Sheria ya Musahakuna neno lililoukataza uponyaji. Wakijibu ‘si halali’ itaonekana wamekosahuruma na upendo kwa wanadamu wenzao. Hivyo, walibanwa, wasiwe tayarikutamka wazi walivyoamini kutokana na mapokeo yao. Kwa hiyo, Yesualimshughulikia yule mgonjwa, akamponya na kumruhusu arudi nyumbanikwake.

k.5 Kisha Yesu akarudia kusema na wale wapinzani akiwauliza juu ya kawaidayao. Kati yao ni yupi mwenye wanyama ambaye atakosa kumshughulikiang’ombe au punda wake akitumbukia kisimani. Je! atamwacha taabuni? Hatakidogo, potelea mbali, mapokeo yao yasema nini juu ya kazi, watamhurumiamnyama na kumtoa. Kwa hiyo, si zaidi, imempasa Yesu amshughulikiemwanadamu aliye taabuni, ambaye, ingawa hayumo hatarini ya kufa, hatahivyo amesumbuliwa mwilini mwake. Kuna nakala za zamani ambazo badalaya neno ‘ngombe’ zina neno ‘mwana’. Kwa hiyo, ikiwa mwana wao kwa bahatimbaya atatumbukia kisimani, au kuanguka gengeni, Je! watamwacha? Hakikahawatamwacha, wala Yesu hatawaacha wagonjwa waugue kwa siku mojazaidi. Kwa hoja hiyo Yesu alitoboa wazi kwamba walikuwa na tabia yakuwahurumia wanyama wao kuliko wanadamu wenzao.

k.6 Wakashindwa kumjibu, kwa sababu walifahamu kwamba Yesu ameelewadesturi yao ya kuwaokoa wanyama wao siku ya Sabato. Kwa hoja zake Yesualikuwa amewaaibisha na kuwanyamazisha, na mmoja mmoja alikuwa akionjabaraka za kuwekwa huru na shida zake siku hiyo ya Sabato.

14: 7-14 Mfano juu ya unyenyekevu na ukarimu

k.7 Hapo Yesu alisema na wageni alipoona jinsi walivyofanya walipoalikwachakulani hasa katika kujitafutia viti vya mbele, hata wengine walikosa adabuwakisukumana ili wawe mbele. Hapo nyuma Luka ametaja jinsi Mafarisayowalivyokuwa na tabia ya kupenda viti vya mbele (11:43).

k.8-9 Itakuwaje wakati wa kufika kwa wenye heshima walioalikwa. Kwa kawaidawaheshimiwa hufika baada ya wengine. Mwenye madaraka ni mkuu wa karamu

Page 130: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

naye atawaomba wale waliotangulia kufika na kushika viti vya mbele warudinyuma na kuketi katika viti vya nyuma.

k.10 Kwa hiyo ni afadhali kuketi mahali pa nyuma, ndipo baadaye ikipatikananafasi mbele, mtu apate kuitwa kukaa mbele na badala ya kuaibishwaataheshimiwa mbele ya wenzake. Neno hilo lapatana na shauri la Mithali 25:6-7. Yesu alifundisha kwamba watu wapaswa wawe na unyenyekevu wa kweli.Hakutaka watu wawe na unafiki wa kujifanya kuwa wanyenyekevu. Kuketinyuma ili aitwe mbele si unyenyekevu! Mtu yumo karamuni kwa sababuamealikwa, hana sababu ya kiburi wala ya kujiona. Kwa sababu ni mfano, ndaniya maneno yake Yesu alikuwa akifundisha habari za Ufalme wa Mungu.Mafarisayo walidhani kwamba wamestahili kuwemo katika Ufalme wa Mungu,tena walijiona kuwa bora kuliko wengine walioitwa. Ila hakuna astahiliye kuingiakatika Ufalme wa Mungu, ni kwa neema na rehemu za Mungu tu mtu huitwakupitia katika mlango mwembamba na kuingia. Kwa hiyo, katika mfano huo,Yesu, pamoja na kutoa shauri hasa alikuwa akiusemea Ufalme wake ambaoameuleta karibu na watu. Mtu akiwa na unyenyekevu wa kweli, ambaye yutayari kuketi nyuma bila shida, huyo amefaulu kuepa hali zote za kumzuiaasiletwe mbele.

k. 11 Kisha Yesu alisema kanuni kimsingi kwa watu wote. Iwapo ni mfano ndaniyake ni mashauri makali kuhusu jinsi tunavyofanya hapo duniani ambayoinaashiria jinsi tunavyofanya mbele za Mungu.

k. 12-14 Baada ya kusema na wageni walioalikwa chakulani Yesu aliendeleakwa kusema na Farisayo mkuu ambaye alikuwa amemwalika kwenye chakula.Si kana kwamba alitaka kumhukumu ila alitaka kumpa yeye na wenzake wotemwongozo kuhusu kanuni ya kuwaalika watu chakulani. Hapo tena, ndani yamaneno yake, ni mafundisho kuhusu Ufalme wa Mungu ambayo yalihusu walewanaoalikwa kuingia ndani yake.

Hakuwa na maana kwamba wakati wote mtu asiwaite rafiki na jamaa zake, la.Ila yampasa mtu awakumbuke na kuwakaribisha wale wasio na uwezo wakumrudishia ukarimu wake. Hao ni akina maskini, vilema, viwete, vipofu, watuwaliodhaniwa kuwa wamekosa baraka za Mungu, ambao walidhaniwa kuwa njeya Ufalme wa Mungu na baraka zake. Kwa kawaida watu huwaita wenzaohalafu wanatazamia kwamba baadaye wenzao watawarudishia ukarimu waokwa kuwaita kula nao. Lakini Je! habari za wale wasio na uwezo wa kuandaakaramu na kuwaita wengine? Je! waachwe kando ya jamii? Yesu alihukumudesturi hiyo kwa sababu haipatani na tabia ya Mungu. Wakitaka kuwawakarimu na kufanana na Mungu wapaswa kuwa kama Yeye ambaye kwa njiaya huduma ya Yesu anawaita vilema, vipofu, maskini, n.k. waingie katikaUfalme wake. Ni vigumu kwa watu kuwa na wema usio na raghba. Si ukarimuhasa kuwapa wale wenye uwezo wa kuurudishia ukarimu; kurudishianaukarimu kwa kanuni hiyo si ukarimu hasa.

Page 131: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 421

k.14 Uheri wa kweli na baraka ya kweli ni katika kuwapa wale wasio cha kulipandipo watalipiwa baadaye katika ‘Ufufuo wa wenye haki’. ‘Upo ufufuo wa wasiohaki’ ambao umetajwa katika Mt.25:46; Mdo. 24:15.Hivyo katika mazungumzo hayo Yesu alitoa mwongozo kwa maisha ya wakatihuo, pia alitoa fundisho kubwa kuhusu Ufalme wa Mungu na hali yaunyenyekevu inayotakiwa katika wale wanaoalikwa kuingia. Hakuna aliyestahilikuingia, ni kwa neema na kwa rehema za Mungu mtu hujaliwa kuingia, mlangoni mwembamba, si mlango wa kupitia kwa watu wenye mabega mapana.

14: 15-24 Mfano wa karamu kuuYesu aliendelea na mfano mwingine kuhusu Ufalme wa Mungu. Wayahudiwaliwaza huo Ufalme kuwa ‘karama kuu’ itakayosababisha furaha kuu. Baadaya Yesu kutaja ufufuo wa wenye haki mtu mmoja aliyekuwemo chakulanialivutwa kutoa maoni yake juu ya uheri wa wale watakaoshiriki katika Ufalmewa Mungu, yaani wale watakaoshiriki ufufuo wa wenye haki. Bila shaka yeyealifikiri kwamba yeye mwenyewe atakuwa mmojawapo wa hao wenye heri hiyo.

k. 16 Ndipo Yesu alitoa changamoto ili watu wajihoji juu ya akina naniwatakaoshiriki katika Ufalme wa Mungu. Ni nani atakayekuwapo? Je! kwelihuyo mtu atakuwepo? na wengine waliokuwepo pia, Je! watakuwepo? Maanahao wote walidhani kwamba kwa hakika watakuwepo. Ndipo Yesu alitoa mfanojuu ya mtu mmoja, yaani Mungu, ambaye aliandaa karamu kubwa na kuwaalikawengi. Karamu kubwa ni dalili ya nafasi tele; kualikwa ni kuonyesha kwambamtu huingia kwa kualikwa, si kwa ustahili wake, wala kwa kujiingiza.

k.17 Ndipo baada ya taarifa ya kuwemo kwa karamu, watu walisubiri hadiwapate kujulishwa kwamba saa ya karamu imefika kwa sababu yote ni tayari.Ni rahisi kufikiri kwamba Yesu alisemea mambo ya baadaye, ila hasa alikuwaakisemea mambo yaliyokuwa yakitokea wakati wa huduma yake. Wakati huowa huduma yake ndio wakati wa kukubali mwito wake, kwa sababu kwa njiayake Mungu anasema ‘ Njooni...karamu yangu ni tayari...’.

k.18 Kumbe! Watu walifanyaje? Waliitikiaje mwito wa Mungu katika huduma yaYesu? Walitoa udhuru mbalimbali, ijapokuwa udhuru zao zilikuwa tofauti tofauti,nia zao zilifanana, hawakuwa na nia ya kufika. Udhuru zilizotajwa zilikuwakama sampuli tu, udhuru kuhusu ununuaji wa shamba na ng’ombe, shughuli zahalali, za kawaida. Udhuru mwingine ulihusu wajibu wa mtu kwa mkewe,huenda alikuwa ameoa hivi karibuni, jambo la uhusiano wa binafsi. Penginehizo zilitoka kwa watu wenye maisha mazuri. Zilionyesha kwamba walionawanayo mambo mazuri kufanya kuliko kujitoa kwa Yesu na kumfuata.Walimezwa katika maisha ya kila siku. Kwa hiyo, karamu ya Mungu, yaaniUfalme wa Mungu, haikuwa kipambele cha kwanza katika maisha yao. Yesualisema ‘tafuteni kwanza ufalme wa Mungu... ‘ (Mt.6.33)

Page 132: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.21 Mtumishi aliporudi na kumjulisha bwana wake habari ya watu kukataa kujakaramuni, bwana wake alikasirika, ila hakuona vema akate tamaa, akaamuakuwaita wengine ambao hawakualikwa mwanzoni. Waitwe wale ambaohawakuwa na matumaini kwamba watashiriki katika karamu hiyo; hao ni akinanani? Ni vilema, vipofu n.k. wale waliotajwa katika k.13. Hawakuwa na udhurukwa sababu hawakushikwa na mambo mazuri ya maisha hayo, ilikuwa rahisiwakubali kuja. Hao ni wale ambao Mafarisayo na Wana-sheria walidhanikwamba hawatapata nafasi katika Ufalme wa Mungu, lakini ni hao walioguswana kubarikiwa na huduma ya Yesu.

k.22 Hata hivyo, bado ingaliko nafasi katika karamu, nafasi ni tele, bado zikonafasi kwa wazururaji na wasio na kwao, watu waliohesabiwa kuwa mbali sanana Ufalme wa Mungu. Itambidi mtumishi awashurutishe, haina maana kwambaatumie nguvu, ila awahakikishie ukweli wa kukaribishwa karamuni. Ilikuwavigumu sana watu wa namna hii kufikiri kwamba wanaweza kuingia katika huoUfalme, kumbe waweza. Ni picha inayoonyesha matokeo ya huduma ya Yesuiliyozidi kupanuka na kuwaingiza watu wa kila aina. Ndipo baadaye Mitumewatahubiri Injili kwa WaMataifa katika nchi nyingine mpaka Imani ya Kikristoitakuwa imeenea kotekote ulimwenguni. Lazima karamu yake ijae watu.Makusudi ya Mungu hayazuiliki, potelea mbali baadhi ya watu waudharau witowa Injili.Watu hupewa nafasi ya kuukataa mwaliko wa kuuingia Ufalme wa Mungu, ilahawatazuia kusudi la Mungu kwa huo Ufalme. Watu wakipenda, wasipende,Ufalme wa Mungu upo nao utadumu kuwapo. Ufalme hautakosa kuwa na watu.Twajifunza kwamba uteule wa Mungu umekuwepo tangu milele; mtu hawezimwenyewe kujiamuria kuingia Ufalme wa Mungu, budi aitwe, hakunaatakayeuingia bila wito wa Mungu; ila hakuna atakayekuwa nje pasipo kuamuamwenyewe kuwa nje. Mtu hawezi kujiokoa mwenyewe ila mtu aweza kujilaanimwenyewe. Jambo kuu la kwanza ni kujitoa kwa Yesu, jambo hilo latanguliahata mambo ya familia, ya biashara, ya kazi n.k.Yesu alisisitiza umuhimu wa kuitika mara wito wa Injili na kuupokea wokovuwake bila kukawia. Baa kuu kuliko yote ni kukataa wito wa Mungu wakukipokea kipawa chake cha wokovu, kwa sababu Mwana wa Adamu alikujakuwatafuta na kuwaokoa waliopotea.

14: 25-35 Gharama katika kuwa mwanafunzi wa Yesu(Mt.5:13; 10:37ku. Mk.9:50)

Katika sehemu hiyo Yesu alimwita kila mmoja katika umati wa watu waliokuwawakifuatana naye kwenda Yerusalemu aache kila kitu kinachomzuia asiwetayari kujitoa Kwake kabisa kwa kulingana na kielelezo chake Mwenyewe chakutoa nafsi yake Msalabani kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu. Alifikirikwamba katika umati huo wapo wale walioweza kuwa wanafunzi wake.

k.25 Pengine Yesu alikuwa katika eneo la Perea katika safari yake ya kuelekeaYerusalemu. Watu wengi walikuwa na hali ya udadisi wakitaka kumwona na

Page 133: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 423

kumchunguza huyo rabi aliyetoka Nazareti. Kama ambavyo tumeishaona maranyingi, watu walidhani kwamba kule Yerusalemu litatokea jambo kuu la Yesukusimika kuwa Mfalme wa Wayahudi, hivyo wengi walikuwa tayari kuandamananaye wakitaka kushiriki katika tukio hilo.

k.26 Ila Yesu alitaka watu waliojitoa Kwake wajitie chini yake na kuwa tayarikufanya mapenzi yake, wasiwe watazamaji tu, mfano wa wale waendaokutazama mchezo wa mpira. Hivyo, alisema maneno magumu sana kwa umatiwa watu waliokuwa wakiandamana naye. Alitoa mwito wa kibinafsi kwa kilamtu. Kwanza katika uanafunzi wa kweli mtu apaswa amtangulize Yesu namatakwa yake na kuwa mtiifu kwake hata kabla ya kujali jamaa ya karibu(baba, mama, wanawe na ndugu) na matakwa yao. Hakuwa na maana kwambawawachukie hasa ila kwa kumtanguliza Yeye itaonekana kana kwambaamewachukia. Ni kuchukia katika maana ya ‘kuliko’ (Mwa.29:30-31 ling. na Mal.1:2-3). Yesu alidai apewe utiifu wa kwanza. Pamoja na hayo yampasa mtuamtangulize Yesu na matakwa yake kabla ya kwake binafsi. Ni kujitoa Kwakekwa ukamilifii na kwa moyo wote, si kwa nusunusu. Alisema wazi kwa sababupasipo kufanya hivyo mtu hawezi kumfuata sawasawa. Mtu anayechukiahafungwi na vifungo vya uhusiano wake na jamaa na kwa sababu hiyo yu hurukufanya lo lote ambalo Kristo amwite kulifanya, hajiwekei mpaka, aweza kuniamamoja tu, yaani kufanya mapenzi ya Mungu.

k.27 Ndipo aliendelea kutaja sharti lingine katika ufuasi wa kweli. Mtu ajitoeKwake kiasi cha kuwa tayari kupata dhiki na mateso kwa ajili yake. Walipopitanjiani watu walizoea kuona misalaba ya wale waliouawa kwa uhalifu wao. Kifohicho kilikuwa cha maumivu makali na aibu kubwa (9:23). Yesu alipotajakusulibisha walielewa maana yake. Katika kumfuata Yeye wanamfuata Yuleambaye hivi karibuni atatundikwa msalabani kwa kufidia dhambi zawalimwengu wote. Kwa hiyo hadai kwamba mfuasi wake afanye zaidi ya YeyeMwenyewe. Hata ikiwa mtu hafi kwa ajili yake, budi maisha yake yawe kamadhabihu iliyo hai (Rum.l2:lku). Msalabani Yesu alifika upeo kabisa katika kujitoakwake, na hata kabla ya kusulibishwa alikuwa akiwahudumia watu bilakujihurumia. Budi wafuasi wake wafuate kielelezo chake, wachache kwa kufakimwili, na wengi kufa kwa kujikana, wakikataa kufanya mapenzi yao ili wafanyemapenzi yake. Kwa hiyo, bila kuchukia na bila msalaba mtu hatafaulu kuwamwanafunzi wake halisi.

k.28-30 Halafu Yesu alitoa mifano miwili ya kuwasaidia watu kufahamu kwambaYeye hakutaka wanafunzi ambao hawakuzingatia hizo gharama za kumfuatazilizotajwa hapo juu. Kweli alitaka wanafunzi, ila alitaka wale ambao walitambuani mambo gani yaliyomo katika kumfuata nao wamekuwa tayari kuendelea bilakukata tamaa, na bila kushindwa njiani.

Mfano wa kwanza ulilenga wale watu walioandamana naye ‘ni nani katika ninyi,kama akitaka ....’ Alitumia mfano wa mjenzi ambaye kwanza inambidi aketi chini

Page 134: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

na kufanya hesabu ya gharama ili aone kama anazo fedha za kutosha kumalizajengo lake, ili asije akashindwa na kuaibika mbele za watu nao wakamdhihaki.Asifanye haraka, asichukuliwe na hewa iliyopo kwa sababu ya umati wa watu,asikate shauri bila kutafakari kwanza. Mambo ya kufikiriwa ni neno la kuchukiajamaa, yaani kumtanguliza Yesu na matakwa yake kabla ya familia, pamoja naneno la msalaba, yaani awe tayari kumfuata Yesu hata ikiwa ni kwa kupatahasara na dhiki n.k.

Mfano wa pili ulihusu hali fulani iliyokuwapo. Alikuwepo Mfalme aliyeonakwamba mfalme mwingine alitaka kuja kupigana naye. Kabla ya kuondokakwenda kupigana naye budi ahesabu na kuona kama anao askari wangapi naadui anao askari gani, na kama akiona atashindwa, afadhali atafute kupatananaye kabla hajaja yule mwingine na kumshinda. Fundisho lake ni sawa namfano wa mjenzi. Budi katika kujiunga na Yesu mtu atambue kwambaameingizwa katika vita iliyopo kati ya Yesu na Shetani, na katika vita hiyo mtuhuweza kujeruhiwa na kupata hasara. Watu watakaomfuata Yesu lazimawajiandae kwa vita hiyo, wasiingie vitani hali macho yao yamefumbwa wasionekwamba kumfuata Yesu ni kuvuta upinzani mkali wa adui kama ilivyotokea kwaYesu. Pengine mifano hiyo miwili inaashiria huduma ya Yesu, ameanzakujenga, na ni hakika kwamba ataimaliza, hajengi mnara ambao atashindwakuumaliza, na Yeye anao wanajeshi wa kutosha kumshinda adui wake bila hajaya kufanya patano naye.

k.33 Yesu aliyajumlisha maonyo hayo kwa makutano kwa kusema kwambayampasa kila mtu aache vyote alivyo navyo, pasipo kufanya hivyo, hawezikuwa mwanafunzi wake. Neno hilo alilitamka mara tatu (k.26b; 27b; 33).Tazama neno ‘hawezi’ hakuna kuridhiana, hakuna nafasi kwa ‘ikiwa’ ‘bali’ aumasharti mengineyo. Budi mtu awe huru mbali na tamaa ya vitu, asiwe nachoyo, wala hali ya kujipenda n.k. Haina maana kwamba mtu hawezi kuwa namali ila awe huru moyoni mwake kiasi cha kuwa tayari kuiacha mali yake aukuitumia kama Mungu atakavyomwongoza. Kwa hiyo, Yesu alitoboa wazikwamba, kila mtu atakayekuwa mwanafunzi wake wa kweli hana budikuyatafakaria mambo matatu; Kwanza, jambo la ‘kuchukia’ yaani kumtangulizaYesu na matakwa yake kabla ya jamaa na matakwa yao. Pili, jambo la‘kuchukua msalaba’ yaani kujikana nafsi yake kwa kumtanguliza Yesu namapenzi yake hata ikitokea dhiki, mateso, n.k. Tatu; jambo la ‘kuwa uhuru mbalina masumbufu’ yampasa mtu asiwe na masumbufu ya mali na vitu, awe nauhuru wa kufanya mapenzi ya Mungu bila kuzuiliwa na uangalizi wa vitu vyake.

k. 34-35 Kisha Yesu alisema habari ya chumvi ambaye ina kazi maalumu yakukolea, kuzuia maozo, n.k. Chumvi ina ukali wake, na ikipoteza hali hiyo ya‘kichumvi’ haina kazi tena, haifai kitu, hata kuwekwa nchini au kuwa jaa. Maanayake ni kwamba mwanafunzi ye yote wa Yesu akikosa hali ya kujitoa kabisakwa Yesu na kumtii hafai kuwa mwanafunzi wake, hatafaulu! Atashindwa tu!

Page 135: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 425

Mafundisho hayo yalikuwa magumu na makali, na Yesu alitaka watuwayazingatie kweli, maana kule aendako, Yerusalemu, si mahali pa kutawazwakwa fahari katika kiti cha enzi cha hapo duniani, bali atatundikwa msalabani nakutawazwa na Mungu pale penye aibu nyingi na dharau ya hali ya juu, na kwamaumivu makali.

Sura ya 15 inahusika na habari ya Karamu kuu iliyotajwa katika 14:15-24. Yesualionyesha kwamba karamu hiyo itakuwa na wageni ambao ilidhaniwa kwambahawatakuwepo, na wale waliodhaniwa kwamba watakuwepo, hawatakuwepo.Katika sura ya 15 Yesu alitoa mfano ulio na sehemu tatu, mfano uliosema juuya mtazamo wa Mungu kwa wale ambao walionekana kuwa hawastahilikuwepo katika Ufalme wa Mungu. Ulitokana na mambo mawili yaliyotajwakatika k.1 na k.2.

15: 1-2 Ukaribishaji wa furaha kwa wenye dhambiLuka ametaja kwamba wale waliokuwa na hamu ya kumsikiliza Yesu walikuwawatoza ushuru na wenye dhambi, watu ambao hawakupendwa walakukaribishwa na viongozi wa dini ya Kiyahudi (14:35b). Watoza ushuruwalichukiwa kwa sababu waliwasaidia Warumi kukusanya kodi kutokawananchi. Wenye dhambi ni wale ambao baadhi yao walikuwa na maishamabovu pamoja na wale ambao hawakushika vizuri vile visheria vidogo, vingi,ambavyo vilitungwa na waandishi na kuitwa ‘mapokeo’. Pengine walishindwakuvishika kwa sababu ya aina za kazi zao, tena viliwalemea watu.

k.2 Mafarisayo na Waandishi walipomwona Yesu anajihusisha na hao watu nakuwakaribisha, akienda kula nao bila kujali kula vyakula vilivyohesabiwa nimwiko na vya kumtia mtu unajisi. Wala hakuogopa kuonekana kama anadharauhayo mapokeo n.k. Watu hao hawakukaribishwa katika shirika zao na ibada zasinagogini. Hali ya Yesu iliwafanya wafikiri kwamba Yesu hawezi kuwa Masihikwa sababu angekuwa Masihi angeweza kutambua hali za hao watu na kujuakwamba ni wenye dhambi. Daima walimhukumu Yesu kwa hali yake yakujihusisha na kila aina ya watu, akionekana kuwa anawapenda na anatakawajiunge naye. Andiko lao moja lilisema ‘msijihusishe na waovu hata kwakuwaleta kwa Torati’.

15:3-32Mfano wa Kondoo aliyepotea, shilingi iliyopotea, na mwanaaliyepoteak.3-7 Kondoo aliyepoteaNdipo Yesu alitoa mfano, ulio na sehemu tatu, kwa shabaha ya kuwaelimishajuu ya mitazamo ya Mungu kwa watu kama hao watoza ushuru na wenyedhambi, mitazamo tofauti kabisa na ile ya viongozi.

Sehemu ya kwanza ya mfano ilisema juu ya mchungaji mwenye kondoo miaambaye mmoja miongoni mwao aliondoka zizini kwenda nje, akapotea bila

Page 136: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

mchungaji kujua alipo. Huyo mchungaji afanye nini? Aridhike na wale tisini nakenda waliokuwa salama? Akifanya hivi inaonekana amemhesabu yule mmojaaliyepotea kuwa hana thamani machoni mwake. Au, pengine, hatakikujisumbua na kuumia kwa ajili yake katika kumtafuta? Ila, Yesu alijua kwambasi kawaida ya mchungaji kumwacha yule mmoja bila kumtafuta. Aliuliza swali ‘ninani kwenu .... asiyewaacha .... aende amtafute yule aliyepotea hata amwone’?Kisha atakapomwona na kumrudisha nyumbani huwaita rafiki na jiraniwafurahini pamoja naye. Picha ni ya tajiri, mwenye kondoo mia, ambayealipopotewa na mmoja tu katika hao mia, hakuweza kuridhika na mali aliyonayo, alijitoa kabisa na kufanya bidii amtafute yule aliyepotea. Kwa muda ule,huyo mmoja alitawala mawazo yake na shughuli zake. Ndipo, huyo kondoommoja, alipopatikana, alisababisha furaha kubwa kiasi cha yule mchungajikuwaita wengine wafurahini pamoja naye.

Hayo yote ni picha ya Mchungaji Mwema, Yesu Mwenyewe, ambaye amekujakuwatafuta na kuwaokoa wale waliopotea. Iliwapasa viongozi, badala yakumhukumu, kufurahi pamoja naye wanapowaona watoza ushuru na wenyedhambi wakija kumsikiliza na kuwa tayari kutubu. Wayahudi walizoea kumwazaMungu kuwa Mchungaji wa Israeli (Isa.40:11; Eze.34:4,11-31; Zab.23).

Kila mwanadamu ni wa thamani machoni mwa Mungu na machoni mwa Yesu.Katika sehemu hiyo Yesu alikuwa akisemea huduma yake na utume wake nakuonyesha kwamba kipambele chake cha kwanza ni hicho cha kuwatafutakondoo za Mungu waliopotea.. Mchungaji hakujihurumia, walahakumnung’unikia kondoo aliyepotea, wala hakuzisikitikia taabu zake katikakumtafuta, bali alifurahi kwa kuwa mali yake iliyopotea ilipatikana tena. Nyumaya habari hiyo ni Msalaba wa Kristo na gharama itakayotolewa ili watu wapatekuokolewa.

Yesu alisema kwa hakika juu ya hali halisi ya mbinguni na jinsi ilivyo kwaMungu Baba yake, wakati wa mtu awaye yote kuziacha njia zake mbovu nakumrudia Mungu wake. Kila mwanadamu amethaminiwa kiasi cha Yesu kutoamaisha yake yote kwa ajili ya kumpata. Neno hilo lasababisha furaha kubwambinguni, na hapo duniani watu hupaswa kufurahi sana wanapomwonamwenye dhambi anatubu na kumwamini Kristo. Furaha hii ilikuwa dhidi yamanung’uniko ya viongozi wa dini wakati wa Yesu. Andiko moja la Kiyahudililisema ‘Ipo furaha mbele za Mungu wakati wa wale wanaomchokozawanapoondoka duniani’. Huenda si wote waliofikiri hivyo.

Yesu hakutaka kusema wala tisini na kenda hawakuwa na thamani machonimwake, la, alitaka kusisitiza furaha yake juu ya yule mmoja aliyepatikana baadaya kupotea. Wala siyo kusema kwamba wako tisini na kenda ambao hawahitajikutubu. Kila mwanadamu ni mwenye dhambi mwenye haja ya kutubu nakumwamini Kristo.

Page 137: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 427

k.8-10 Shilingi iliyopoteaYesu aliendelea kusisitiza habari ya furaha ya mbinguni juu ya mtu mmojakutubu na kumrudia Mungu akisema juu ya mwanamke mmoja mwenye shilingikumi, mali ndogo, ambaye alipotewa na shilingi moja. Tofauti na mchungaji tajirialiyekuwa na kondoo mia aliyepotewa na mmoja huyo mama alikuwa maskininaye alipotewa na shilingi moja katika kumi, hasara kubwa, kwa kuwainawezekana shilingi hizo ziliwekwa kwenye ukufu na kuwa kama kinga kwasiku za shida. Alifanya juu chini ili aione hiyo shilingi iliyompotea ambayohaikuwa na uwezo wo wote wa kurudi kwake, haikuwa na uhai, haikuweza kuliakama kondoo, haikuwa na nguvu yo yote, itabaki pale ilipo hadiitakapoonekana. Yesu alisisitiza bidii ya huyo mwanamke, hakuweza kutuliampaka alipoipata. Kama mchungaji, yeye naye, alifurahi sana alipoiona,akawaita jamaa na rafiki wafurahini pamoja naye. Fundisho ni lile lile la kondooaliyepotea, ni furaha ya Mungu kwa mwenye dhambi mmoja anayetubu.Huenda inaashiria kazi ya Roho Mtakatifii, ambaye, kama taa, anaangazamioyoni mwa wanadamu na kuwatia nuru ya Injili. Haja ya wanadamu ni tobana kumrudia Mungu.

Kwa sehemu hizo mbili za mfano Yesu ameonyesha kwamba kipambele chakwanza cha Mungu na mzigo wake ni juu ya wale waliopotea. Ndiyo sababukuu ya Kuja kwake duniani, alikuja kutafuta na kuwaokoa waliopotea. Kwa hiyoviongozi hufanya kosa kubwa wanapomhukumu juu ya kuwakaribisha akinawatoza ushuru na wenye dhambi. Ni kama hawakuelewa vema Mungu wao nashabaha ya kuja kwa Masihi wao.

k. 11-31 Mwana aliyepoteaYesu alizidi kusisitiza habari ya furaha ya mbinguni juu ya mmoja atubuye kwakusema juu ya baba aliyekuwa na wana wawili. Mmoja aliomba apewe sehemuya mali inayomwangukia, ndipo baada ya kuipata akamwacha baba nakuondoka nyumbani na kuishi kwa mbali na kwa vibaya. Mkubwa wake alibakina baba pale nyumbani na kufanya kazi.

k.11ku. Ni vema kuona kwamba habari inahusu wana wawili, si mwana mmojatu. Mdogo alimwomba baba amgawie mapema sehemu ya mali. Kwa desturi yaKiyahudi baba aliweza ama kuandika hati ya wasia ama aliweza kutoa vipawa.Ilikuwa kawaida mkubwa apate theluthi mbili (Kum.21:12). Baba aliweza kupatamapato ya shamba huku wana wawe na mali hiyo. Baba alimpa mwana mdogokipawa cha mali iliyokuwa haki yake, haikuwa kawaida kufanya hivyo, ndipobaada ya muda mfupi ilidhihirika sababu ya mwana mdogo kutaka urithi wakemapema, alitaka awe huru mbali na baba yake na kazi na wajibu za nyumbanin.k. Aliondoka nyumbani kwenda mbali sana bila kuachia cho chotekitakachomvuta arudi nyumbani baadaye. Hakumjali baba na wajibu wakumtunza katika uzee wake. Alitaka kwenda tu. Kwa kufanya hivyo hakufanyavizuri, kwa sababu alivunja umoja wa familia. Isingalihesabiwa kosa kamaangetaka sehemu kwa ajili ya kuoa au kitu cha namna hiyo, ila hasa alitaka awe

Page 138: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

huru mbali na baba. Kosa lake lilionekana alipoanza maisha mabovu, akiishikwa anasa na kwa kujifurahisha, akitapanya mali yake kwa kuishi ovyo. Wakatihuo hakukosa kuwa na marafiki wengi, wala hakusikia shida yo yote.

k. 14-16 Ila baada ya muda alipatikana na shida mbili, moja iliyosababishwa nakosa lake, na moja iliyotokea tu, bila kosa lake. Aliishiwa fedha, pia ilitokea njaakatika nchi ile iliyozidisha shida zake, hata akakosa mahitaji ya lazima, chakulana mavazi. Marafiki walitoweka, huenda hao nao walipata shida kwa sababu yanjaa. Chakula kiliadimika na bei yake ilipanda. Ilimbidi atafute kazi, lakinialishindwa kupata kazi nzuri, kisha hana la kufanya ila kukubali kazi iliyokuwachukizo kwa Wayahudi, kazi ya kuwatunza nguruwe, wanyama waliohesabiwakuwa wachafu kwa Torati (Law.ll:7; Kum. 14:8). Tena kwa namnaalivyoangaliwa kwa ukali hata ilikuwa shida apate chakula cha kutosha ingalaukilikuwa cha nguruwe. Zaidi ya yote yeye Myahudi ilimbidi afanye kazi kwamgeni asiye Myahudi. Jambo la aibu sana. Alikuwa amefikia hali ya chinikabisa, nguruwe walithamaniwa hata kuliko yeye aliye mwanadamu si mnyama.

k.17 Ndipo kutokana na shida zake alianza kuyazingatia maisha yakeakikumbuka hali ya nyumbani na kulinganisha hali yake ya sasa na ile yawatumishi wa baba yake.

k.18ku. Kisha akakata shauri la kurudi nyumbani, akiwaza atakavyosema kwababaye, atakiri kosa lake kwa Mungu na kwa baba na jinsi asivyostahili kuitwamwana wake, yu tayari kuwa mtumishi tu sawa na wale wengine. Alijiondoakatika haki zote za uana.

k.20ku. Akarudi kwa babaye na njiani alimkuta baba. Kabla hajafika nyumbanibaba alikuwa akiangalia ile njia katika tumaini la kumwona mwana akirudi.Huenda ilikuwa desturi yake kila wakati kufanya hivyo, kwa vile alivyotamanisana sana kumwona tena. Baba alichukua jukumu la kumrudisha katika familiana kinyume cha alivyodhani, baba alimkaribisha vizuri mno, akamwangukiashingoni na kumbusu sana. Kwa jinsi baba alivyomfanyia ilizidi yotealiyotazamia, maana, alipomwona alimhurumia sana kwa hali yake yote.Mwana alianza kumwambia maneno aliyokuwa ameyatunga tayari kusema, ilababa hakumwachia nafasi ya kusema yote.

k. 22-24 Baba aliwatuma watumishi wake walete nguo nzuri, na pete, na viatu;pia wachinje ndama aliyetunzwa tayari kwa wakati maalumu, waandae karamuiliyostahili mtu ambaye alikuwa kama amekufa na sasa yu hai tena. Nguo napete na viatu, vitu hivi vyote vilionyesha kwamba anapokelewa kama mwana nakupewa heshima na mamlaka kama mwana. Kuchinja ndama kulionyeshakwamba hakuna wakati mzuri wa kushehereka unaozidi huo wa sasa. Ndipowakaanza kushangilia. Mwana alipata ile raha na furaha ambayo alitafuta katikanchi ya mbali, akaikosa; sasa ameipata nyumbani mwa baba, mahali alipodhanikwamba haipatikani.

Page 139: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 429

Hayo yote yalitoa mwanga juu ya jinsi ambavyo Mungu huwapokea wenyedhambi wanaotubu dhambi zao.

k.25 Ila, Je! habari ya mwana mkubwa aliyebaki nyumbani wakati wote wamdogo wake kuwa mbali. Yeye alikuwa akiendelea kutumika, na alikuwashambani wakati wa kufika kwa mdogo wake hata sherehe ya kumkaribishailikuwa imeanza. Alipokaribia nyumbani alisikia sauti ya nyimbo n.k. akamwulizamtumishi sababu yake. Naye akamwambia kwamba ndugu yake amerudi nababa amemchinjia ndama kwa sababu amerudi yu mzima, mtumishi alisemakama alikubali alivyofanya baba.

k.28 Aliposikia hayo mwana mkubwa akakasirika sana, akakataa kuingia nakushehereka pamoja nao. Hata hivyo, kwa baba, yeye ni mwana wake, na kwasababu hiyo baba alimwendea nje na kumsihi aingie ndani. Lakini akamjibubaba kwa kuonyesha jinsi alivyojisikia ndani. Alitoa maneno mengi ya kudaihaki yake na uzuri wake, na ya kuwa amekuwa mwana mwaminifu. Alitumianeno ‘nimekutumikia’ maneno yenye harufu ya utumwa. Ameishi nyumbanikama mtumwa si kama mwana na ndiyo sababu hakuelewa maana ya neno‘baba’ na sababu ya furaha ya baba yake. Baba aliona kwamba amempatamwana wake tena ila mwana aliyekaa nyumbani hakuona kwamba amempata‘ndugu’ yake’ yaani mdogo wake tena.

k.30 Alijilinganisha na ndugu yake, ila hakumwita ‘ndugu’ alimwita ‘mwanawako aliyekula vitu vyako’ hakutaka kujihusisha naye hata kidogo. Baba likuwaamemkaribisha ila yeye akakataa kumwona kama ni ndugu yake. Ni kama huomkubwa ‘amepotea’ nyumbani mwa babaye.

k.31 Baba alimwacha aseme hayo yote hali akiendelea kumpenda, ndipoakasema naye kwa upendo sana ‘Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote,na vyote nilivyo navyo ni vyako’. Alikuwepo wakati wote na iwapo mdogo wakeamerudi hakuna kubadilisha hati ya wasia, yeye ataendelea kuwa mrithi wa vituvyake vyote, mdogo wake ameishapata na kupoteza ya kwake. Kuja kwamdogo wake haleti badiliko lo lote juu ya mali ya baba. Ila baba alisisitiza jinsiilivyokuwa haki wafurahi na kushangilia kurudi kwa ‘ndugu yake’ kwa sababujambo kubwa limetokea, ni kama aliyekufa amefufuka na kuwa hai tena, na yulealiyekuwa amepotea, hayupo nyumbani, ameonekana, yu nyumbani tena.Mungu hufurahi sana kwa mwenye dhambi awaye yote atubuye na kurudiKwake. Wenye haja ya toba ni watoza ushuru na wenye dhambi pamoja naMafarisayo na Waandishi.

Katika huduma ya Yesu waliopotea hukutana na upendo mkuu wa MunguBaba. Kwa neema yake Yeye hupokea kwa furaha kubwa wale watubuo nakuacha maisha yao mabaya.Wale ambao wameishi maisha mema kwa haki nautakatifu hawana haja ya kuhofu. Afadhali watambue kwamba wanapata‘ndugu’ na hii ni jambo la kusherehekea.

Page 140: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

Hadithi iliishia hapo kama hewani, hatujui kama mwana mkubwa alikubalikuingia ndani; wala hatujui kama mwana mdogo aliendelea kuishi vizurinyumbani. Imebaki kama changamoto kwa Mafarisayo na wenzao kuungamkono huduma ya Yesu na kuyafurahia mafanikio yake katika kuwavuta walewaliohesabiwa nje ya neema ya Mungu.

Kwa Kanisa ni ukumbusho jinsi itupasavyo kuwa tayari kuwakaribisha waleambao wamekuwa nje na kujihadhari na hali yo yote ya kuwahukumu aukujiona kuwa bora kwa sababu tumekuwa waumini wa siku nyingi.

Mafundisho mbalimbali juu ya mali 16:1-31

16: 1-9 Mfano wa wakili dhalimuk. 1 Yesu alitoa mfano huo kwa wanafunzi wake. Mafarisayo walikuwepo nakuusikia nao walimdhihaki Yesu kwa ajili yake (k.14).Palikuwa na tajiri mmoja aliyemwajiri wakili kuangalia mali yake. Baadaye tajirialisikia habari isiyo nzuri juu ya huyo wakili kwamba alikuwa akitapanya malizake, kama alivyofanya mwana mpotevu katika mfano uliotangulia (15:13).

k.2 Kwa hiyo tajiri alimwita ili ahakikishe kama ni kweli hiyo habari anayosikia.Akamwomba atengeneze hesabu kuhusu uwakili wake. Kwa njia hiyo atapatakujua ni kwa kiasi gani huyo wakili amemnyang’anya mali zake. Bwana wakealielekea kuamini kwamba habari aliyosikia ni kweli. Alimjulisha wakili kwambaikiwa ni kweli, basi hataendelea na uwakili wake. Inaonekana wakili alikuwa nawajibu mkubwa uliohusu fedha nyingi na alikuwa na madaraka ya kutegenezahati n.k.

k.3 Wakili alijua kwamba akiondolewa kazi atapata shida sana, atakosa mahalipa kukaa na fedha za kupata riziki, kwa hiyo, katika muda aliopewa na bwanawake kuleta hizo hesabu aliwaza juu ya kuondolewa kazi na namnaatakavyoishi mbeleni. Hajazoea kazi za mikono na hakuwa tayari kuaibika kwakuomba, kwa hiyo, aliutengeneza mpango mzuri wa kujisalimisha. Alijuakwamba itakuwa vigumu apate kazi tena kwa sababu ya sifa yake mbaya.

k.4-7 Akaamua kujihusisha vema na wadeni wa bwana wake. Kwa sirialimwendea mtu mmoja mmoja na kumwomba ararue hati yake ya kwanza nakuandika nyingine badala yake na kuipunguza hesabu yake. Ni vigumu kujuakwa njia gani aliweza kufanya hivyo na mawazo mbalimbali yametolewakueleza alivyofanya. Wazo moja lahusu desturi ya Wayahudi ambao kwamasharti ya dini yao hawakuruhusiwa kutoza wenzao ushuru. Yawezekanandani ya hesabu ijapokuwa haikuandikwa wazi, ushuru ulikuwepo, na wakilialiwaomba wadeni wa bwana wake kuandika hati isiyo na hesabu ya ushurundani yake, na kwa njia hiyo deni lilipungua. Ama, yawezekana katika hati yakwanza ilikuwa hesabu ya asilimia fulani kwa ajili ya wakili, kama ilivyo desturikatika kampuni za bidhaa. Wakili alikata shauri aondoe sehemu hiyo iliyo yake

Page 141: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 431

ndipo deni lilipungua na yeye atakosa asilimia yake. Kama si hivyo, yeyemwenyewe alijichukulia madaraka ya kupunguza hesabu, potelea mbali tajiriwake ataonaje. Pengine shughuli zilihusu kuazimu ardhi na malipo yalikuwakutoa asilimia fulani ya mazao au kima fulani kilichowekwa. Pengine hesabuiliyoandikwa ilikuwa juu kuliko ilivyokuwa hasa kwa kusudi la kuficha jambo laushuru.

Ni wazi kwamba tajiri alipata hasara kubwa, asilimia hamsini kwa upande wamafuta na asilimia ishirini na tano kwa upande wa ngano. Kama tajiri wakealikuwa akitoza gharama kubwa huyo wakili alifaulu kufunulia choyo yake. Nivigumu kujua hakika jinsi biashara hiyo ilivyokuwa.

k.8-9 Ni kifungu hicho kinachotatanisha watu. Kwa nini bwana wake amsifu kwatendo lake la kuyapunguza madeni ya wadeni wake? Kitu alichosifu ni busarayake, alikuwa mwepesi wa kung’amua hali zilizopo na kuchagua njiaitakayompatia rafiki katika wale wadeni wa bwana wake. Ilikuwa kawaida mtukumrudishia mwingine fadhili ikiwa alikuwa amepata fadhili kwake. Huyo wakilialitaka mahali pa kuishi, pengine kwa muda, mpaka atakapoona kama atawezakupata kazi au njia nyingine ya kuishi. Kitu kilichomshangaza tajiri wakekilikuwa uwezo wake wa kupata njia ya kumdanganya tena baada yakumnyang’anya mali yake mara ya kwanza. Wakili alikuwa mjanja kiasi chakumtia tajiri wake mahali pafinyu. Hakuweza kusema lo lote ikiwa yeyemwenyewe alipatana na wakili wake kuingiza ushuru katika hesabu ya deni,maana haikuwa haki kufanya hivyo. Au ikiwa alikuwa amelipiza wadeni wakegharama iliyozidi yeye mwenyewe ataonekana kuwa bepari. Au wakilialimshinda tu kwa ujanja wake.

k.8b-9 Hapo ni neno kwa wanafunzi wa Yesu. Wasiwe wajanja kama yulewakili, wala wasifanye udhalimu, la, hata kidogo! Hata hivyo, katika kazi zaMungu watumie busara, wawe na bidii na kutumia mali waliyo nayo kwakumpendeza Mungu. Yeye atawakaribisha Kwake mwishoni, watakapoachanana dunia hiyo, wakati ambapo mali haiwezi kuwa msaada tena. Katikakumtumikia Kristo ni afadhali kukosa kitu sasa, kama wakili alivyokosa asilimiayake, kwa ajili ya faida ya baadaye ya kukaribishwa mbinguni. Katika kusema‘mali ya udhalimu’ Yesu alidokezea kwamba mali yote ina harufu ya udhalimu.‘wawakaribishe’ ina maana ya kusema Mungu. Tukumbuke mazingara yamaneno hayo, Kuja kwa Yesu na Ufalme wake kulifikisha watu kwenye njiapanda ya kufanya uamuzi wa maana sana, yenye matokeo makubwa. Budiwatu wakate shauri juu yake, kwa sababu mwisho wa kila mtu hulingana nakumpokea au kumkataa Yesu. Washike nafasi ya kumtumikia Kristo hatayakiwapo matisho mengi. Mali ni sehemu katika mfumo wa dunia hii na kwasababu hiyo huwa na mvuto mkubwa. Utupu wa mali huonekana hasa, siwakati wa kukosa kuwa nayo, bali wakati wa kufa na kuondoka duniani, wakatiambao mali haina kazi tena.

Page 142: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

16:10-13 Matumizi mema ya malik. 10-12 Katika vifungu hivi Yesu alisisitiza kwamba uaminifu si bahati nasibu.Alivyo mtu ndivyo alivyo hasa; akiwa mwaminifu atakuwa mwaminifu katikamadogo na makubwa na katika mali yake na katika mali ya mwingine. Vivyohivyo, mtu akiwa dhalimu atakuwa dhalimu katika madogo na katika makubwana katika mali yake na katika mali ya mwingine. Wanafunzi wake wapaswawawe na mtazamo mzuri kuhusu mali, waitumie vema na kwa busara, kamwewasiruhusu mali ichukue nafasi ya Mungu katika maisha yao. Madogoyanayosemwa yahusu mali, makubwa yanayosemwa yamhusu Mungu. Malihaina thamani kubwa, ila mali aliyo nayo mtu amepewa kama dhamana kutokakwa Mungu na akiitumia vema itageuka kuwa baraka si laana. Mtu kwakumtumikia Mungu kwa moyo wake wote atayakinga majaribu ya kuvutwa namali.

k.11b. ‘ni nani atakayewapa amana mali ya kweli?’. Baada ya Yesu kuondokawanafunzi walikabidhiwa dhamana ya Injili, mali ya thamani sana, mali ya kweli.Iliwapasa waihubiri katika ukweli wake wote wakiwa na mzigo juu ya ueneziwake. Mungu ni mwema ambaye humdhamini mtu ‘mali yake’ mali hiyo nitofauti sana na mali ya dunia hii. Zaidi ya kumdhamini, Yeye humpa hiyo maliiwe yake. Mali hiyo ni mambo ya kiroho. Mpaka hapa mali imewazwa kama‘amana’ na ‘hazina’ ya kutumiwa kwa ajili ya maskini na wenye shida ndipoYesu aliendelea kuonyesha kwamba mali huweza kuwa mtego, bwana wakumtumikisha mtu. Hapo Luka anawatayarisha wasomaji wake kwa mfanokuhusu Lazaro na Tajiri fulani.

k.13 Yesu alionyesha hatari ya mali ambayo hutaka kuwa bwana wa kutawalamaisha ya mtu. Mali huwa bwana mkali inayomtumikisha mtu. Yesu alisemakwamba mtumwa hawezi kuwatumikia mabwana wawili. Kila bwana hudai utiifuwote, na ni mmoja tu ambaye aweza kuupata. Mali humdai mtu; Mungu humdaimtu; kila mtu apaswa ampe Mungu utiifu wake wote na kudumu kuwamwaminifu Kwake. Hakuna maafikiano kati ya Mungu na mali.

16:14-18 Yesu aliwakemea MafarisayoMafundisho hayo ya Yesu kuhusu mali yaliwatisha Mafarisayo ambao walijengausalama wao na kibali chao katika watu kwa kuangalia sana kwamba watuwawaone kuwa watu wazuri wa dini, huku kwa ndani sana walikuwa watu wakupenda fedha. Kwa hiyo waliposikia hayo mafundisho ya Yesu walimdhihaki.Wayahudi walidhani kwamba mali ni dalili ya baraka za Mungu, kwa hiyohawakusikia shida katika kutafuta mali. Wakubwa walificha choyo yao ya malichini ya ‘mavazi’ ya dini; kwa mfano, walitembelea wajane na kusali sala ndefuwakijionyesha kuwa wapenda Mungu, huku walikamua huruma za akina mamawakitumaini kupewa fedha. Walifunga, na kuomba, na kutoa sadaka, iliwatazamwe na watu, kusudi watu wawaone kuwa wapenda Mungu kweli(Mt.6:1-18). Walitafuta sifa za kuwa wapenda Mungu lakini hawakumpenda

Page 143: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 433

hasa, walijifanya kuwa waadilifu mbele ya wanadamu, lakini Yesu, hali akijuamioyo yao, aliwakemea na kusema kwamba yale ambayo wao waliyadhanikuwa safi na ya sifa mbele za Mungu, licha ya kuwa hivyo ni chukizo Kwake. Ilasi Mafarisayo tu walio na hali hii, ni kawaida ya wanadamu wengi. Munguhuangalia sababu na nia za mtu, si matendo yake ya nje tu. Machoni mwaMafarisayo Yesu na wanafunzi wake walionekana kuwa maskini, na kwasababu hiyo, walishindwa kufikiri kwamba wamebarikiwa na Mungu.

Halafu Yesu aliendelea kusema juu ya mambo ya ‘wakati’. Katika historia yaoiliyotangulia walikuwa na Torati na Manabii, navyo viliendelea hadi kufika kwaYohana Mbatizaji. Tangu kufika kwa Yohana wakati mpya umeanza, na sasa niwakati wa kuingia kwa Ufalme wa Mungu na kwa sababu hiyo hali kamailivyokuwa haipo tena, wakati wa Torati na Manabii umeishapita na badala yakeMungu ameleta karibu na watu utawala wake Mwenyewe kwa njia ya YesuKristo, Yeye atatawala maishani mwa mtu kutoka ndani si kwa sheria za nje.

Maneno ‘kila mtu hujiingiza kwa nguvu’ yana maana gani? Si wazi maana yakeni nini hasa. Pengine ni maneno ya kuashiria kwamba kila mtu apaswa afanyejuhudi ili apate kuingia katika Ufalme wa Mungu ulioletwa na Yesu. Awe nabusara ya kung’amua ni wakati mpya, afanane na yule wakili dhalimu ambayealitambua kwamba ilimbidi afanye mpango wa kujisalimisha, vivyo hivyo, kilamtu awe na hekima ya kukata shauri la kumpokea Yesu, wala asiwajaliwapinzani, kama hao akina Mafarisayo na wenzao ambao walijitahidikumshusha Yesu machoni mwa watu.

k.17 Hata hivyo, watu wasifikiri kwamba kwa kuwa wakati mpya umeanzamadai ya Torati yameondolewa kwa upande wa maadili. La! Siyo! Torati ingaliimesimama katika hali ya kuwa mwongozo wa maadili na ufunuo wa tabia zaMungu. Uasherati ungali ni uasherati, uwongo ungali ni uwongo, zote nidhambi. Tena madai yake yamenyolewa kuwa makali zaidi. Neno hilolaonekana wazi katika mafundisho ya Yesu katika Mathayo 5 na 6. Upungufuwa Torati ulikuwa katika hali yake ya kutokutoa uwezo wa kutimiza amri zakeingawa amri zenyewe zilikuwa safi. Kwa sababu hakuna awezaye kutimiza amrizake haiwezekani ibaki kuwa njia ya kupata haki. Yesu alileta njia mpya yakupata haki, njia ya neema, ya kuhesabiwa haki kwa njia ya kumwamini Yeye,muumini hujaliwa kipawa cha Roho Mtakatifu atakayemsaidia moyoni na kumtianguvu kwa ndani. Torati ilikuwa kama kibao cha kumwelekeza mtu kwenye njiabila kumpa uwezo wa kutembea katika njia ile.

Yesu alifafanua mafundisho hayo kwa kutoboa wazi mafundisho juu ya amri ya‘usizini’. Waandishi walipunguza uzito wa amri hii kwa kuweka vipengele.Waliruhusu wanaume watoe talaka kwa wake zao, huku wanawakehawakuruhusiwa kutoa talaka kwa mume zao. Pamoja na hayo, waliruhususababu hafifu kuwa zilitosha kwa kutoa talaka, si sababu kuu ya uzinifu tu.Yesu alitoa mafundisho makali hata alisema mtu ni kama amezini ikiwa

Page 144: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

amemtazama mwanamke kwa kumtamani. Alikataa sababu zote isipokuwa ileya uzinifu. Alijua kwamba mara nyingi mtu hutaka kuachana na mkewe kwashabaha ya kumwoa mwingine.

Maana ya Ufalme wa Mungu ni utawala wa Mungu juu ya maisha yote.

16:19-31 Mfano wa tajiri na mwombaji maskini LazaroYesu alimaliza mafundisho yake juu ya matumizi mema na mabaya ya mali kwakutoa mfano huu ambao umepatikana katika Injili hiyo tu. Huenda alikuwaangali akiwalenga Mafarisayo waliotajwa kuwa wapenda fedha pia mfano ulitiliamkazo maneno yake ‘lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele zaMungu’ (k.15). Mafundisho hayo yalikuwa dhidi ya mawazo ya Kiyahudiyaliyowaelekeza watu kufikiri kwamba utajiri ni dalili ya baraka za Mungu naumaskini ni dalili ya laana au ukosefu wa baraka za Mungu.

Yesu hakusema ni mfano ila haifikiriwi kwamba watu hao ni watu halisi, iwaponi katika mfano huo tu ambao Yesu ametaja mtu kwa jina. Lazaro, ni Eliesarikwa Kiebrania na maana yake ni aliyesaidiwa na Mungu. Tajiri ameitwa Diveskatika nakala za KiLatini, na ni tafsiri ya neno ‘tajiri’.

k. 19-21 Yesu alipambanua hali za hao wawili, tajiri na maskini. Tajiri alikuwana yote aliyoyataka, na maskini alikosa kila kitu. Tajiri alivaa vizuri sana, nguoza rangi ya zambarua na kitani safi viliashiria upeo wa uzuri. Rangi yazambarau ilikuwa ghali sana, ilitoka kwa samakigamba. Pia alikula kila siku kwaanasa, kwa furaha sana, akiwaita watu waliokuwa na hali kama yake ili walepamoja naye. Kwa jumla aliishi kama mtu wa tabaka yake, ila angeweza kuwatajiri mfadhili aliyewasaidia wengine. Hatusomi kwamba alifanya dhambi kubwa,ila aliishi kwa ajili yake mwenyewe, alijipenda sana, wala hawakuwaangaliawengine na mahitaji yao.

Kinyume chake maskini alikosa chakula, hata alitamani ale makomboyaliyoanguka katika meza ya tajiri ambao mbwa waliyapata. Alitegemea kilealichopewa na watu waliomhurumia. Hakuvaa vizuri, alikuwa na vidondovisivyotibiwa, vilivyorambwa na mbwa waliokula makombo kutoka meza yatajiri. Hali za tajiri na maskini zilikuwa mbali mno. Hata hivyo, hatusikii kwambamaskini alimlaumu Mungu, wala hakuinung’unikia hali yake, alikaa kimya tu,kama mtu aliyemtumaini Mungu tu.

k.22-23 Alipokufa maskini alipokelewa vizuri mbinguni na kukaa kifuani mwaIbrahimu, lugha ya kuashiria kwamba alipata raha sana akiwa na ushirikianomwema na mababa wa zamani. Wayahudi, walitegemea sana neno la kuwawazao wa Ibrahimu. Tajiri alikufa na hakupokelewa mbinguni bali alikwendakukaa mahali pa wafu walioweka tumaini lao kwa mali zao si kwa Mungu.Wayahudi hawakutazamia watakwenda kwenye mateso. Mapinduzi makubwayalitokea kwa kila mtu, tena shida aliyopata maskini hapa duniani ndiyo

Page 145: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 435

aliyopata tajiri baada ya kufa, tena zaidi yake; pia raha aliyopata tajiri hapaduniani ndiyo aliyopata maskini baada ya kufa, tena zaidi yake. Hapo dunianitajiri alilipwa vizuri sana katika maisha ya raha na maskini alikosa hata sentimoja, lakini hayo yote yamebadilika. Bila shaka tajiri aliumia zaidi alipomwonaLazaro amekaa karibu na Ibrahimu katika raha kubwa na yeye yuko mbali naye.

k.24-26 Ndipo tajiri akalia kwa Ibrahimu, akimwita baba, akamwombaamhurumie na kumtuma Lazaro amburudishe kwa kumpa maji kwa ajili yamateso yake. Tajiri amekuwa mwombaji, kama Lazaro alivyokuwa alipokuwaduniani. Bado angali akimwangalia Lazaro kwa kiburi cha kufikiri kwambaaweza kumhudumia, huku yeye hakumhudumia hapo nyuma. Iwapo Ibrahimualimwita mwanangu alimkumbusha ‘mema yake’ aliyopata alipojipenda nakuangalia ya kwake tu. Huku Lazaro alipata mabaya, ambayo yalimjia tu, bilayeye kuyatafuta. Yalikuwa kama fungu lake, naye alilipokea bila kumlaumuMungu. Haki imetendeka, mambo yamepinduliwa, na hayo matokeo ya maishayao ya duniani, yatakaa, hakuna kubadilishana mahali, hakuna kupita kutokahali moja mpaka hali nyingine. Kila mtu apaswa ayakubali matokeo hayo, kwasababu, matokeo si bahati nasibu. Tajiri alichagua kuishi kwa ajili yakemwenyewe, hata alipomwona Lazaro mlangoni mwake alimwacha katika shidazake, asiinue hata kidole chake cha kumsaidia. Maskini alichagua kuendeleakumtumaini Mungu ingalau hali yake ilikuwa mbaya hata kiasi cha kumkatishatamaa.

k. 27-31 Kisha tajiri alianza kuwawaza wengine, ila si maskini, bali ndugu zakewaliobaki duniani. Bila shaka aliogopa kwamba hao nao watafika matesoniwasipotubu hali zao za kujipenda kama yeye alivyojipenda. AlimwombaIbrahimu amtume, ama Lazaro, au mmoja aliyekufa na kuwa hai tena, iliawaonye ndugu zake juu ya hatari waliyo nayo. Lakini Ibrahimu akamjibukwamba ilitosha wasome na kufuata mafundisho ya Maandiko ya Agano laKale, hakuna haja ya mtu atoke katika wafu na kuwaonya. Katika Maandikoyamo mafundisho ya kuwaelekeza kuishi kama Mungu atakavyo, kumpendaMungu na kuwapenda jirani. Kwa hiyo, katika kusema hivi, Ibrahimu alidokezeakwamba tajiri alifika mahali alipo, si kwa sababu ya utajiri wake hasa, bali kwasababu ya kukosa kutia maanani Maandiko ambayo yangemwelekeza kuutumiautajiri wake katika kuwasaidia wenye shida. Hivyo, utajiri ni hatari, utajiri sidhambi. Ni matumizi ya fedha ambayo yataleta mtu kwenye raha au kwenyetaabu ya kukosa raha ya mbinguni. Hapo twakumbushwa habari ya wakilidhalimu ambaye alipoona amepotezewa kazi alifanya juu chini ajisalimishemaisha yake. Twaweza kuitumia mali yetu kwa kuwasaidia wahitaji au twawezakuitumia mali kwa kujifaidi mwenyewe ambao mwisho wake ni kuhukumiwaadhabu ya milele. Hakuna jambo litakalomsaidia mtu asiyeyajali mafundisho yaNeno la Mungu. Kila daima Wayahudi walidai ishara, kama tajiri alivyodaindugu zake wapewe ishara ya mtu aliyetoka katika wafu. Hata wakijiwa namgeni huyu au hata wakifunuliwa uzito wa mateso ya baadaye, hakunakuwasaidia. Hata Yesu atakapofufuka kutoka kwa wafu wengi hawatamwamini.

Page 146: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

Katika hayo yote Lazaro alikaa kimya, hakusema neno lo lote; hakunung’unika;hakuchekelea hali mbaya ya tajiri; hakutaka alipizwe kisasi; la: alipokea yotekatika kumtumaini Mungu.

Tusifikiri kwamba Yesu alitaka kutufunulia hali zote za baadaye. Ya kujifunza nikwamba kila mtu anao ‘mwisho’ wake katika raha au katika dhiki; na mwisho wakila mtu hutegemea jinsi alivyoishi hapa duniani. Kila mtu hana la kufanya ilakuupokea mwisho wake unaolingana na alivyochagua kuishi hapa duniani najinsi alivyotumia mali yake.

MASWALI1. Wakati wote Yesu alifanya huduma katika mazingira ya upinzani.

Aliwakabili wapinzani gani kwa hali gani? Eleza2. Kwa mfano wa karamu Yesu alihukumu hali zipi na kukubali hali zipi?3. Aliposema juu ya wale ambao hawakuitikia vema wito wa kufika

karamuni alikuwa Akisemea mambo ya wakati gani?Je! kutokufika kwa waalikwa rasmi kutasababisha karama isiwepo?Eleza Watu huwa na udhuru zipi wanapomkataa kumpokea Kristo?

4. Yesu alikuwa na shabaha gani alipotaja gharama katika kuwamwanafunzi wake?Watu wapaswa kufanya nini kabla ya kuamua kuwa wanafunzi wake?Kwa nini iwe hivi?

5. Ni nini iliyosababisha Yesu atoe mfano ulio na sehemu tatu?Alitaka kusisitiza mambo makubwa yapi?Alifundisha nini juu ya Mungu Baba?

6. Twajifunza nini kwa Mfano wa wakili dhalimu? Eleza7. Twajifunza nini kwa Mfano wa Tajiri na Mwombaji Lazaro?

Eleza uhusiano kati ya maisha ya sasa na maisha ya baadaye.

17:1-10 Maneno kadha wa kadha wa Bwana YesuKatika sehemu hiyo Yesu alitoa mafundisho mbalimbali, pengine kwa wakatimbalimbali, na Luka ameyakusanya na kuyaweka pamoja.

k.1-4 Yesu alifahamu kwamba katika ulimwengu huu vikwazo hutokea nawafuasi wake huwajibika wajihadhari ili wasisababishe wengine kukwazwa.Alitaja ‘kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa’. Wadogo hawa huwa akinanani? Pamoja na kuwa watoto ni wadhaifu wa imani, walio katika hatari yakudhuriwa, watu wa hali ya chini, waumini wapya n.k. Hao waweza kutiwamajaribuni kwa upesi au waweza kudhuriwa kwa upande wa kiroho kwamtazamo au matendo ya waumini wenzao. Yesu aliona jambo hilo kuwa zitosana hata alisema kwamba atakayemsababisha muumini kukwazwa apaswahukumu kali, ambayo itakuwa mbaya kuliko mtu kutupwa baharini na kupoteamoja kwa moja.

Page 147: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 437

Kwa upande wa yule aliyekosewa afadhali awe na mzigo juu ya yulealiyemkosea, kwa kumwonya juu ya kosa lake, na shabaha yake iwe yakumleta kwenye toba, si kumhukumu; ndipo akikubali kutubu, amsamehe. Hataikiwa atamkosea mara saba katika siku moja, akitubu, basi asipime kama tobalake ni la kweli au siyo, yeye amsamehe tu. Awe mkarimu wa kutoa msamaha,asiwe na mpaka, hata ikiwa ana shaka. Awe na huruma, ila asiwe dhaifu wakutokujali kosa, maana daima kosa ni kosa na daima Mkristo huwa kinyumecha dhambi. Yesu alisisitiza umuhimu wa msamaha usio na mpaka.

k.5-6 Bila shaka Mitume waliona kwamba walihitaji imani nyingi katikakuyatimiza hayo aliyoyaagiza Yesu. Walimwomba awaongezee imani. Yesualiwaelekeza kuwaza ‘uhalisi’ wa imani kuliko ‘wingi’ wake. Wakiwa na imani haikatika Mungu mwenye uwezo wote, hata ikiwa imani ile ni ndogo kabisa,wakiitumia tu, Mungu wanayemwamini ni mkubwa mno, basi, yote huwezekana.Maneno kama ‘chembe ya haradali’ na ‘ng’oka, ukapandwe baharini’ ni lughaya mithali na ya kipicha. Ilisemekana mkuyu ulikuwa na mizizi yenye nguvusana, hata ulikaa ardhini kwa miaka mia sita. Ni picha ya mambo magumusana, ambayo kwa imani ya kweli katika Mungu mwenye uwezo wote,wanafunzi wa Yesu wataweza kuyatimiza mapenzi yake hasa ya kuieneza Injiliyake duniani pote.

k.7-10 Watakapofaulu kufanya makubwa kwa ajili ya Mungu baada ya Yesukuondoka duniani, itawapasa kujihadhari na kiburi cha kujiona kwambawamekuwa watumishi bora, kana kwamba, Mungu analo deni kwao.Aliwakumbusha jinsi ilivyo kawaida katika watu. Mtumishi hatumikiwi na bwanawake, wala hasifiwi na bwana wake, kwa sababu ni wajibu wake kufanya ilekazi anayoagizwa na bwana wake. Wawe na mtazamo unaowapasa kuhusuutumishi wao. Katika siku zile wapo watumwa wengi waliokuwepo kwa kufanyakazi tu wakifanana na punda. Wawe na shukrani kwa heshima kubwa yakujaliwa nafasi za kumtumikia Bwana Yesu. Wasiwe na kiburi na kujiona.Twaitwa kuwa na uaminifu na utiifu wa hali ya juu. Hii ni picha moja ya Mungukana kwamba Yeye ni mkali kwa watumishi wake, ila tukumbuke kwamba kunapicha nyingine, tukimkumbuka Yesu na jinsi alivyosema juu ya wanafunzi wakena kuwafanyia alipowatawadha miguu na kuwaita ‘rafiki’ (Yn.13:1ku; 15:15;17.23).

17:11-19 Yesu aliwaponya wenye ukoma kumiHabari hii inapatikana katika Injili ya Luka tu. Kama ambavyo tumeishaonaYesu alikuwa akienda Yerusalemu na alipita kati ya Samaria na Galilaya.Hatuambiwi ni kijiji kipi alichoingia alipokutana na wakoma kumi. Kufuatana namaagizo ya Torati iliwabidi wakoma watangaze kuwepo kwao ili watuwajihadhari nao. Walipofahamu kwamba Yesu yu karibu nao, wakapaza sautizao na kumwomba awarehemu. Hawakumwomba awaponye, ila bila shaka,walitumaini kwamba ndivyo atakavyofanya. Amewatakasa wenye ukomawengine (5:14). Yesu hakusogea karibu nao, wala hakuwagusa, ila alipowaona

Page 148: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

alitambua shida zao na kuwapa nafasi ya kuonyesha imani na utii wao kwakuwaambia waende kwa makuhani na kujionyesha kwao. Maana yake, wafanyekama ni kweli wametakaswa. Makuhani walipewa kazi ya kuuhakikishia utakasowa wenye ukoma ili wailinde afya ya jamii katika eneo lao (Law.14:2-4). Wenyeukoma wote walimtii Yesu kwa vile hakuna hasara katika kwenda kwao kamautakaso ukifanyika au sio. Wote walitakaswa na mmoja wao alipotambuakwamba ametakaswa aliacha kwenda kwa makuhani akamrudia Bwana Yesuna kumshukuru. Njiani alimtukuza Mungu kwa sauti kuu akitaka watu wotewajue habari zake na jinsi alivyotendewa na Bwana Yesu. Alimpomfikia Yesu,akaanguka kifudifudi miguuni pake na kumshukuru. Kumbe! Huyo alikuwaMsamaria, mgeni asiyehesabiwa kuwa mshiriki katika jamii ya watu wa Mungu.Kwa kawaida Wayahudi na Wasamaria hawakushirikiana pamoja, ila kwasababu ya shida za ukoma hao kumi walikuwa wamejiunga pamoja. Shida hiyoilivunja kiambaza cha ukabila.

k.17 Yesu alishangaa alipoona kwamba ni mmoja tu, tena Msamaria, ambayeamerudi kutoa shukrani. Inaonekana yeye ni wa kwanza, na ni yeye tu,aliyerudi. Iliwapasa wote, na hasa Wayahudi, wamtukuze Mungu, wakiri wazikwamba ni Mungu aliyewatendea makuu, kumbe wamemsahau yulealiyesababisha utakaso wao, waliendelea kwa makuhani, hali wameshikwa nafuraha yao tu. Ila huyo Msamaria alipata baraka kubwa kwa kuwa aliujengauhusiano wa kibinafsi na Yesu, alitaja wazi shukrani zake, na imani yake ilitiwanguvu. Yawezekana maneno ‘imani yako imekuokoa’ yamaanisha kwambaaliponywa kiroho pamoja na kimwili, wale tisa walibaki hali wameponywa kimwilitu, huku walikosa kuujenga uhusiano wa kibinafsi na Yesu ambaye ni asili yabaraka zote za kimwili na za kiroho.

17: 20-37 Kuja kwa Ufalme wa Munguk.20-21 Mafarisayo walimwuliza Yesu habari za Ufalme wa Mungu na wakatiwa kuja kwake. Inaonekana swali lao lilikuwa kama ‘tutajuaje kama Ufalme waMungu umeisha kuja au wakati wa kuja kwake?’ Hatujui kama walimwuliza kwashabaha ya kutaka kujua hasa au vipi. Mara kwa mara Yesu alitoa mafundishokuhusu Ufalme wa Mungu, na hiyo ndiyo sababu yao ya kutaka kujua zaidi.Aliwajibu kwa kukanusha mambo fulani. Kwanza alisema kwambahaitawezekana watu watambue kwamba Ufalme wa Mungu umefika kwakusoma hali zilizopo. Kwa utaalamu wa nyota na mambo mengine hawatawezakujua (k.23). Hamna ishara maalumu. Wala si jambo la kuwa mahali maalamuwakati maalumu, la siyo. Ndipo alisema kwamba huo Ufalme wa Munguhauonekani wazi, haiwezekani kusema mahali ulipo, kwa kuwa hauwi ufalmewa kijiografia, wala wa siasa, ila uwezo wake huonekana kati yao katikahuduma na nafsi ya Yesu, yule Masihi mwenye ufalme huo. Kwa hiyo, huoufalme umeishafika katika Yesu na kuwa kati yao.

Page 149: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 439

k.22ku. Halafu Yesu aliendelea kusema na wanafunzi wake juu ya huo Ufalmewake. Watahitaji kuvumilia katika hamu yao ya kumwona Yesu tena. Mbeleni,watapenda kumwona Yeye kama wanavyomwona sasa, ila haitawezekana, aupengine watatamani sana aje kwa mara ya pili. Hawana haja ya kudakamashauri ya wavumishaji ambao watasema amefika hapa au pale. Hakunahatari yo yote ya watu kukosa kufahamu kwamba Amerudi. Kwa hiyo, hawanahaja ya kusumbuka katika kumtafuta, maana atakaporudi, atakuja kwa ghaflana bila kutazamiwa, hata hakuna awezaye kutabiri wakati wake. Kabla ya hayoyote, jambo zito litatokea, Yeye atateswa na kakataliwa, nao vilevile, baada yaYeye kuondoka watateswa. Itawapasa wawe na subira, wasiende huko na hukokwa kufuata mashauri ya wadanganyifu wanaotumia nyakati za shidakutangaza wakati na mahali pa kutokea kwake. Watamkuta yupo! basi!

k.26ku. Alitoa mfano wa wakati wa Nuhu na wa Lutu. Katika siku zao watuwaliishi bila tahadhari na bila kujali kwa sababu mamba yalikwenda kwamifuatano yake kama kawaida, wakila, wakioana, wakipanda, wakijenga,wakifanya biashara, n.k. Mambo ambayo si mabaya, wala dhambi hasa, ilawalifanya hayo yote bila kumjali Mungu, wakiridhiana na hali zilizopo,wakimweka Mungu nje ya mipango yao. Mungu hakuwepo katika mawazo yao.

Lakini katikati ya raha na starehe zao hukumu ya Mungu iliwafikia, naohawakuwa tayari, walipotea isipokuwa wale wachache walioujali ujumbe waNuhu na ujumbe wa Lutu. Nuhu na Lutu hawakuwa bila makosa na udhaifu, ilawote wawili walitia maanani habari za hukumu ya Mungu na kuandaa kuikabiliili wasalimike. Nuhu aliingia ndani ya safina, mahali pa usalama na Lutuakatoka Sodoma ili awe salama nje yake. Hata atakapokuja Mwana wa Adamu,watu hawatakuwa tayari, watamezwa katika shughuli za kila siku bila kumjaliMungu, nao watapotea kama wale wa zamani walivyopotea.

k.31 Ndipo Yesu alionyesha kwamba haitakuwepo nafasi yo yote ya kufanya lolote la kujiandaa, siku itakapofika, hata nafasi ya kurudi nyumbani kutokashambani, wala ya kushuka kutoka darini juu mpaka chini. Yesu alimtaja mkewa Lutu ambaye alitoka Sodoma pamoja na mumewe, alikuwa karibu kabisakusalimika, ila alitazama nyuma na kuangalia Sodoma, kana kwambaamesikitika kuondoka, akafa palepale. Wakati itakapokaribia hukumu,inayotakiwa ni haraka, mtu asijaribu kujiokoa wala kuviokoa vitu vyake, afadhaliapate hasara na kuiponye nafsi yake.

k.34ku. Atakaporudi Mwana wa Adama utengano utatokea kati ya watu, katikajamaa walioishi pamoja na katika wale waliofanya kazi pamoja. Yesu hakutajawatachukuliwa wapi ila bila shaka ni watakwenda Kwake (1 The.4:17).

k.37 Kisha wanafunzi baada ya kutaka kujua ni lini, walitaka kujua wapi. Yesualiwapa mithali. Jangwani upo uhakika wa kuwepo kwa mzoga ikiwa taianazunguka juu. Vivyo hivyo, itakuwa dhahiri alipo Mwana wa Adamu, watu

Page 150: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

wake watajua na kukusanyika Kwake, watamnusa kama tai anavyounusamzoga au mfano wa uvutano kati ya sumaku na chuma.

18:1-14 Yesu alitoa mifano miwili kuhusu maombi, mmoja juu ya mjane nakadhi dhalimu; na wa pili juu ya Farisayo na mtoza ushuru.

18:1-8 Mfano wa mjane na kadhiKatika k.1 Luka ameeleza shabaha ya mfano huo, fundisho lake ni kwambawaumini wawe na tabia ya kumwomba Mungu bila kukata tamaa. Yawezekanafundisho hilo linahusika na habari iliyotangulia juu ya Kurudi Kwake. Utakuwepomuda mrefu wa kungojea Kurudi Kwake, kwa hiyo, watu wake wasikate tamaawala kupoa katika imani yao. Msaada wao ni katika kuomba.

k.2 Yesu alitoa picha ya kadhi ambaye alikuwa tofauti sana na jinsi ilivyompasaawe. Hakumcha Mungu wala hakuwajali watu. Hakuwa na mzigo wa kuwapatiawatu haki. Huenda alikuwa mvivu, hakuwa tayari kuwashughulikia watu.Pengine alitegemea kupewa rushwa kabla ya kukata kesi.

k.3 Halafu Yesu alitoa picha ya mjane aliyekuwa amedhulumiwa na kwasababu hiyo alimwendea huyo kadhi ili ampatie haki yake. Hakuwa na uwezowa kutoa rushwa, hakuwa na mtu wa kumsaidia, alionekana kama hanamsaada. Hata hivyo, alikuwa na silaha mbili; haki ilikuwa upande wake, naalikuwa mvumilivu, hakukata tamaa, alizidi kumsumbua kadha kwa kumwendeadaima; hakuwa tayari kuachilia kesi yake.

k.4-5 Ilitokeaje? Yule kadhi alilazimika kumshughulikia huyo mjane iwapohakuwa na nia ya kufanya hivyo, alihofu kwamba ataaibika mbele za watuwanapoona jinsi mjane anavyomjia kila wakati. Pia alijua kwamba huyo mamaataendelea kumsumbua mpaka amepata haki yake. Hakuwa na la kufanya ilakumjali, dhidi ya tabia yake ya kutokujali watu.

k.6-8a Hapo Yesu alimlinganisha Mungu na huyo kadhi kwa kuonyesha tofautikubwa kati yao. Mungu si kama yule kadhi. Mungu huwajali wateule wake,anawapenda, ana mzigo juu yao, naye atawapatia haki, tena kwa upesi, yaanikwa ghafla bila kutazamiwa. Kuna tofauti kati ya maombi na hali yakuombaomba. Hata ikiwa inaonekana kwamba Mungu bado hajayajibu maombiyao, hata hivyo, hakika atayajibu. Hakuna haja ya kumsumbua kwa sababuMungu hana tabia kama yule kadhi. Ikiwa mara kwa mara watu wabayawafanya mema, hata bila nia safi, Je! Si zaidi Mungu? Yeye atafanya haki.Mungu ni Mungu mwaminifu na waumini wahitaji kudumu katika kuomba iliimani yao itiwe nguvu na nia yao isafishwe.

k.8b Maneno hayo hayana maana kwamba hawatakuwepo Wakristo dunianiBwana Yesu atakaporudi. Watakuwepo, maana wateule wake humlilia usiku na

Page 151: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 441

mchana, ila kwa jumla watu wataendelea katika kutokujali na kutokuaminikwao. Ikiwa Mungu amechelewa ni kwa sababu anataka kuwapatia watu wenginafasi ya kutubu na kumwamini, si kwa sababu hajali. Luka amependa kutajawajane na kuonyesha jinsi Yesu alivyokuwa na mzigo juu yao (2:37; 4:25-26;7:12; 20:47; 21:2-3).

18:9-14 Mfano wa Farisayo na Mtoza UshuruHapo Yesu ametoa mafundisho tena juu ya maombi kwa njia ya mfano wa watuwawili; mmoja Farisayo, mtu wa dini; na mmoja mtoza ushuru. Mambo hayawikama yanavyoonekana kuwa. Ilidhaniwa kwamba Farisayo, mcha Mungu, huwana kibali cha Mungu huku mtoza ushuru hana tumaini mbele zake. Wote wawili,Farisayo na mtoza ushuru, walikwenda hekaluni kuomba. Luka ametajakwamba shabaha ya mfano ni kuonyesha hali inayokubalika na haliisiyokubalika katika kuomba. Hali isiyokubalika ni ya mtu kuudai uzuri wakembele za Mungu na kuwadharau wengine. Hali inayokubalika ni mtu kukiri jinsiasivyostahili kumkaribia Mungu akikubali kwamba hana jambo zuri la kumdai ilaategemee rehema za Mungu tu.

k.10-12 Hao wawili wametajwa; ndipo Yesu alisema juu ya Farisayo. Ilikuwadesturi kwa Wayahudi kusimama wakati wa kuomba. Huyo Farisayo alisimamambele, mahali ambapo watu watamwona. Tena mbele za Mungu alijisemeasana, ni kama alimtupia jicho Mungu halafu alijiangalia mwenyewe sana.Alimshukuru Mungu kwamba hakufanana na wenye dhambi kama wadhalimu,wazinzi, n.k. Huyo Farisayo aliishi maisha safi, hata akajiona kuwa safi sana.Pia alifanya yale mema yaliyodaiwa na sheria ya Kiyahudi. Alifunga mara mbilikwa juma (Torati ilitaka Myahudi afunge mara moja kwa mwaka) kwa hiyoalizidi iliyotakiwa na Torati. Kuhusu zaka, alizidi iliyotakiwa na Torati(Kum.14:22). Hivyo, kwa mengi; kwa kutokufanya dhambi; na kwa kutimizamatakwa ya Torati, hakuwa na kosa. Ila shida yake ilikuwa alijaa ‘umimi’hakuwa na hali ya kusikia dhambi au upungufu wala haja ya msaada waMungu. Aliutegemea uzuri wake. Katika kujisifu kwake aliwadharau wengineakitaja na huyo mtoza ushuru ambaye pia alikuwa akiomba wakati huo.

k.13 Ndipo Yesu alieleza hali ya mtoza ushuru katika kuomba kwake. Kwanzaalikaa nyuma, kana kwamba hakusikia amestahili kusogea karibu. Hakuinuamacho yake mbinguni, alijisikia kama hana haki ya kumtazama Mungu.Alijipigapiga kifua chake dalili ya mtu aliyejiona kwamba hastahili jambo lo lote.Hakuwa na hali yo yote ya kuzificha dhambi zake, alijifahamu kuwa ni mwenyedhambi, mkosaji, na alimwomba Mungu amsamehe. Hakuwa na majivuno walahakudhani kwamba aweza kumdai Mungu jambo lo lote ila rehema zake. Hatani ajabu kuona kwamba amekuwemo hekaluni hali akimwomba Mungu.Hakumtaja Farisayo na unafiki wake.

k.14 Kisha Yesu alisema kwa wazi kwamba huyo mtoza ushuru alipata kibalicha Mungu, alihesabiwa haki, yaani alisamehewa dhambi zake (14:7-11). Kwa

Page 152: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

mfano huo Yesu alisisitiza kwamba Injili ni kwa walio nje, kwa wale waliowekwakando na viongozi wa dini ya Kiyahudi. Hao Mungu huwajali na kuwapokea. IlaMafarisayo na wote wanaofanana nao, wanaojiona kuwa bora, hao hukosakibali cha Mungu, hawahesabiwi haki. Haki yao wanayoidai na kuisifu haitoshimbele za Mungu. Mtu hupaswa kujihusisha na Mungu kwa kujidhili si kwakujikweza. Jambo muhimu si hali ya maisha ya nyuma bali hali ya sasa namtazamo wa mtu kwa Mungu wake. Farisayo katika dhana yake ya kumpendaMungu alikosa kuwahurumia wengine na haki yake haikuvuta watu wamkaribieMungu. Kwa hiyo, watoza ushuru na wenzao wanayo matumaini wakimgeukiaMungu na kutubu dhambi zao na Mafarisayo hawana matumaini ya kukubalikana Mungu wakiendelea kujiona na kujivuna na kufikiri kwamba ni bora kulikowengine.Kwa muda mrefu, tangu 9:51 Luka ameandika mambo mengi yasiyopatikanakatika Injili za Mathayo na Marko. Hapo amerudia kuandika mamboyanayoonekana katika Injili hizo.

18: 15-17 Yesu aliwabariki watoto wadogo (Mt.19:13-15; Mk.10:13-16)k.15 Si wazi ni akina nani walioleta watoto, neno katika Kigriki lina tenzi yakiume, kwa hiyo yawezekana mama na baba waliwaleta. Watu walikuwawamemwona Yesu aweke mikono juu ya wagonjwa nao walibarikiwa, hivyowaliona vema wawalete watoto wao kwa Yesu ili awabariki. Yasemekanakwamba Wayahudi walikuwa na desturi ya kuleta watoto kwa wazee iliwaombewe baraka, jioni ya Siku ya Upatanisho. Luka amewataja kuwa watotowachanga, Mathayo na Mark wamesema walikuwa watoto wadogo. PengineLuka alitaka kusisitiza jinsi ambavyo waliwategemea kabisa wazazi na wenginekwa maisha yao. Wanafunzi walichukizwa na jambo hilo na waliwakemea walewaliowaleta (Mk.10:14). Kwa nini? Pengine waliwaza kwamba ni kupotezamuda wa Bwana Yesu kana kwamba anazo shughuli nyingine za maana kulikohiyo; au walifikiri kwamba Yesu alihitaji kupumzika. Labda hawakupenda watuwaje kati yao na Yesu na kumjia kwa urahisi kama kuingia nafasi ambayowalidhani ni yao tu. Yawezekana chini kabisa katika mawazo yao hawakuonakwamba watoto wadogo wana maana ya kutosha kwa Yesu kuwashughulikia.

k.16-17 Yesu aliwaita wale watu na watoto waje Kwake, wasizuiliwe. Kwamaneno hayo Yesu alionyesha nia yake juu ya watoto na jinsi alivyowaonakuwa wa thamani sana. Ndipo alitoa mafundisho muhimu juu ya Ufalme waMungu, mtu akitaka kuingia Ufalme wa Mungu hana budi kuwa na tabia zawatoto wadogo. Hizo tabia ni nini hasa? Tabia ya kuwa wazi na tayarikumwamini mtu, kuwa bila unafiki au kujifanya kuwa mzuri kuliko walivyo hasa.Kuwa tayari kukiri udhaifu na haja ya kumtegemea Mungu na wengine kulikokujiona na kujitegemea. Hali hizo ni lazima kwa ye yote apendaye kuingiaUfalme wa Mungu. Ni kufanana na mtoza ushuru aliyesali hekaluni ambayeametajwa hapa juu. Ni hali ya mtu aliye tayari kuupokea huo Ufalme kamakipawa asichostahili. Inahusu mwelekeo wa mtu jinsi anavyojiwaza na jinsianavyomwaza Mungu.

Page 153: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 443

Habari hiyo ni ya maana kwa Kanisa na huduma yake kwa watoto, jinsi watotowanavyokaribishwa katika ibada na shughuli zake. Je! Tunawaona kuwa wathamani kiasi cha kuwawekea nafasi katika mipango na shughuli za Kanisa?Au, Je! tunawaona kama hawana thamani, na kwa sababu hiyo, wamekuwa njeya mipango na shughuli zetu. Tukisema kwamba tunawathamini bilakuwawekea nafasi ni kama tunasema bure.

18: 18-30 Kijana tajiri alimwomba Yesu apate Uzima wa Milele(Mt.10:16-22; Mk.10:17-22)

k.18. Huyo aliyemjia Yesu alikuwa kijana (Mt.19:22) tena ‘mtu mkubwa’ hatujuimaana ya maneno hayo kama alikuwa na cheo katika sinagogi au vipi. Alikuwana maisha safi, naye alikuwa tajiri. Alimjia kwa mbio, mwenye hamu sana yakujua njia ya kuupata uzima wa milele. Alionekana kuwa mkweli ambaye badohajasikia raha kamili maishani mwake. Alimjia Yesu kwa adabu akimwita‘Mwalimu mwema’ jina ambalo halikutumika kamwe na marabi. Wao waliona nijina linalomhusu Mungu peke yake, hakuna mwanadamu aliyestahili kuitwahivyo. Hatujui sababu ya huyo kijana kumwita Yesu hivyo, huenda alitumia jinahilo bila kutafakari maana yake.

k.19. Yesu alitaka kujua kwa nini amemwita hivyo? Alitaka azingatie yalemaneno aliyoyatumia. Je! Kama ni Mungu, peke yake, aliye Mwema, mbonabasi amemwita Yeye ‘Mwema’? Je! Amemwona kuwa sawa na Mungu au vipi?Katika Agano la Kale (Kum.6:4) ni Mungu peke yake aliyejaa wema. Kamaameona wema huu katika huduma ya Yesu Je! ametambua kwamba Ufalme waMungu umekuja? Je! kuna uhusiano kati ya mwalimu huyo mwema na Mungualiye chemchemi ya wema wote? Huenda ametumia bila kufikiri. Pia alizingatiehilo ombi lake la kuupata uzima wa milele. Je! Anafahamu ni jambo ganianaloliomba? Uzima wa milele ni kuishi katika Kuwako Kwa Mungu aliyeMtakatifu. Je! Amestahili kuishi mbele za Mungu Mtakatifu. Si itambidi amlilieMungu amrehemu? Hapo huyo mtu hakuonyesha nia ya kuyatafakari kwamakini mambo hayo.

k.20-21 Alikuwa ameomba afanye jambo fulani na Yesu alimjibu kwa kusemajuu ya kufanya. Ajipime kuhusu utendaji wake wa Amri za Mungu, na Yesualimwelekeza kwa amri zilizohusu utendaji wake kwa wanadamu wenzake.Alipomjibu Yesu hakuona kwamba kuna hali ya upekee katika amri hizo,alikuwa na hakika kwamba amezishika sawasawa tangu utoto wake. Marabiwalifundisha kwamba iliwezekana mtu aitimize Torati yote. Kwa hiyo, huyokijana katika kudai kwamba amezishika hakudai jambo la kigeni au la ajabu.Huenda alifikiri kwamba Yesu atampa jambo kubwa la kipekee kufanya si hilo lakuzishika amri. Amri kumi zilijumlishwa katika Kumpenda Mungu kwa moyowote na nguvu zote na akili zote na kumpenda jirani kama nafsi yako. Huendaalidhani kwamba anasema kweli alipodai hivyo, ila swali lipo; mbona amekuwana mali nyingi ikiwa anampenda jirani kama nafsi yake?

Page 154: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.22-23 Ndipo Yesu alimpa changamoto kali kwa shabaha ya kumwonyeshajinsi alivyokuwa amepungukiwa katika kumpenda Mungu na katika kumpendajirani. Amri ya kwanza ilisema juu ya kutokuwa na Mungu mwingine ila Yeye.Kumbe! huyo Kijana alikuwa na mungu mwingine ‘mali’. Yesu alimwambiaaviuze vitu vyake na kuwapa maskini ndipo amfuate. Hataweza kumfuatasawasawa mpaka kizuizi cha mali kimeondolewa maishani mwake. Ataishije naYesu aliyesema ‘ni bora kutoa kuliko kupata’ na kuendelea kuishi kwa msingiwa ‘kupata ni bora kuliko kutoa’? Alishindwa kufanya kwa jinsi Yesualivyomwambia, naye akaondoka kwa huzuni nyingi. Yesu alimwacha aendezake. Hatujui kama mbeleni alibadili uamuzi wake au vipi.

k.24ku. Kisha Yesu alisema juu ya shida ya wenye mali. Mali inapozidi shida yakujitoa kwa Yesu huzidi pia. Ni Mungu peke yake awezaye kuzivunja pingu zamali zinazoshika matajiri hata na wengine. Ni vema tuwaze mali kuwa zaidi yavitu na fedha, ipo mali ya elimu, ya cheo, ya hali, n.k. mali ni kitu cho chote auhali yo yote ambayo mtu huitegemea sana badala ya kumtegemea Mungu.Wayahudi walihesabu kwamba mali ni dalili ya baraka za Mungu na kwamafundisho yake Yesu alikuwa dhidi ya mawazo yao. Kwa mfano wa ngamiakupenya tundu la sindano Yesu alitaka kuonyesha jinsi isivyowezekana mtu yeyote, licha ya matajiri, kuingia katika Ufalme wa Mungu. Wokovu ni kwa matajirina kwa maskini. Kwa mtu ye yote kuokoka, potelea ni nani, ni mwujiza waMungu, ni kwa neema yake tu, ni kipawa chake kwa wale wanaojidhili nakukipokea kama watoto wadogo.

k.28 Maneno ya Yesu yaliwafanya wanafunzi wafikiri juu ya madai ya Ufalmewa Mungu na kujitoa kwao na jinsi ambavyo walikuwa wameacha familia nakazi zao kwa ajili ya kumfuata Yesu. Petro, kwa niaba yao alitaja jambo hilokwa Yesu. Yesu aliwaambia kwamba watapata familia kubwa kuliko waleambao wamewaacha pamoja na baraka nyingine nyingi. Ila tusiwaze kwambaYesu alibadili jinsi itakavyombidi mtu ahesabu gharama kabla ya kumfuata, ilakwa mtu yeyote ambaye katika ukweli wa moyo wake anajitoa kumfuata Yesuhatakosa baraka za kiroho wala mahitaji ya lazima kwa maisha ya kila siku(Flp.4:19). Hatumfuati Yesu kwa faida, lazima sababu zetu ziwe safi.

18: 31-34 Onyo la tatu kuhusu Kifo chake (Mt.20:17-19; Mk.10:32-34)Yesu alitoa onyo la kwanza na la pili alipoanza safari yake ya kwendaYerusalemu (9:21-22; 43b-45) na hili la tatu alisema alipokuwapo Yeriko karibukufika Yerualemu. Hayo yote ambayo tumesoma kati ya onyo la kwanza hadihilo la tatu yasomwe katika mwanga wa Kifo chake pale Yerusalemu. Iwapotumesema ni onyo la tatu, hasa Yesu alidokezea Kifo chake mara saba (5:35;9:21-22; 43-45; 12:50: 13:32ku. 17:25; 18:31). Katika onyo hilo aliongezahabari za Kifo chake, kwa kutaja kwamba hayo yote yameandikwa mapemakatika Maandiko ya Agano la Kale. Alitaja kwa mara ya kwanza kutiwa mikononimwa WaMataifa pamoja na kuyaeleza mateso yake kwa kutaja jinsiatakavyovunjiwa heshima yake na kushushwa hadhi yake na kunyenyekezwa

Page 155: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 445

mno. Ila siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. Hayo yote yamepangwa katikaumilele nayo ni kwa ukombozi wa ulimwengu nayo yatatimizwa hivi karibuniatakapofika Yerusalemu. Kwa hiyo, wakati wake unazidi kukaribia.

k.34 Wanafunzi hawakuelewa hata kidogo mambo hayo. Hawakuwezakulipokea neno la Masihi kuuawa kimwili. Wala hawataelewa mpaka Yesuatakapofufuka. Yawezekana walizuiliwa wasiyatambue hayo kwa mapenzi yaMungu au ni kwa sababu mambo hayo ni mageni kabisa kwao walishindwakuyapokea. Kila alipotaja Kifo chakeYesu alitaja pia Kufufuka kwake siku yatatu akionyesha kwamba Kifo chake ni njia ambayo kwayo ataupata ushindi.

18: 35-43 Yesu alimponya mtu kipofu (Mt.20:29-34; Mk.10:46-52)Mathayo ametaja vipofu wawili; huenda walikuwa wawili ila Luka amemtajammoja kwa sababu pengine alijulikana katika jamii ya Wakristo baadaye; Markoamemwita Bartimayo. Mathayo amesema Yesu alikuwa akitoka Yeriko, Lukaamesema alikuwa akiingia Yeriko. Palikuwa Yeriko, mji wa zamani na Yerikomji mpya uliojengwa karibu yake. Kwa hiyo, yawezekana Yesu alikuwaameondoka Yeriko wa zamani, akielekea kuingia Yeriko mpya. Hayo yote nimawazo tu. Huyo kipofu alikuwa njiani, akiomba sadaka, mahali pazuri kwasababu wasafiri wengi walipitia pale njiani kwenda kumwabudu Mungu hukoYerusalemu. Alisikia kishindo cha watu wengi, akataka kujua sababu yake.Aliambiwa kwamba Yesu wa Nazareti anapita. Wengi walikuwa wamesikiahabari za Yesu na uwezo wake wa kuwaponya watu, hata vipofu, na vilema, nawakoma n.k. Hivyo aliona kwamba hii ndiyo nafasi yake ya kumwomba Yesuamrehemu. Akapaza sauti akisema ‘Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu’. Kwamaneno hayo alimkiri Yesu kuwa yule Masihi aliyetazamiwa na Wayahudikufuatana na ahadi ya Mungu na ahadi ilitolewa kwamba huyo Masihi atawapavipofu uwezo wa kuona (Isa.35.1ku).

k.39 Wale watu waliokuwa mbele katika umati wa watu walioandamana naYesu walijaribu kumnyamazisha. Walimkemea na kumwambia anyamaze,yawezekana walidhani kwamba si vizuri kumchelewesha Yesu katika safariyake au pengine walifikiri kwamba Yesu ni mtu mkubwa ambaye hatamjali huyomtu, au ni wao wenyewe waliomwona kipofu mwombaji kuwa hana thamani yoyote machoni mwao. Ila yeye aliona hii ndiyo nafasi yake, kwa hiyo, hakunaatakayemzuia asiseme na Yesu. Pengine walichukizwa na maneno ‘Mwana waDaudi’ au walifikiri amekosa adabu. Lakini yeye mwenyewe alizidi kupaza sautiyake. Alionyesha imani kwa jinsi alivyokazana akutane na Yesu uso kwa usohaidhuru watu wanampinga.

k.40-41 Ijapokuwa Yesu alizungukwa na watu wengi alikisikia kilio cha huyokipofu, wakati wote alikuwa na mwelekeo wa kutambua wale waliomhitaji hasa.Akasimama na kuamuru aletwe kwake. Ndipo akamwuliza moja kwa moja ninini alichotaka hasa, alipenda atamke wazi haja yake kubwa. Kipofu hakusita,akamjibu Yesu kwa kumwambia kwamba alitaka kuona.

Page 156: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.42-43 Yesu alisema neno kwa mamlaka ya nafsi yake ‘upewe kuona, imaniyako imekuponya’. Maana yake imani imekuwa mfereji wa kumletea baraka yauwezo wa kuona. Ni njia ambayo kwayo atapata kuona. Mara moja akajaliwakuona. Kwa furaha alimfuata Yesu akiandamana naye katika safari ya kuelekeaYerusalemu, huku akimtukuza Mungu, ili watu wote wajue habari za uponyajiwake. Kisha watu wote walijiunga naye katika kumsifu Mungu. Kila mara Lukaametaja jinsi watu walivyomtukuza Mungu baada ya matendo makuu ya Yesu.Yesu hakujichukulia kwake sifa, daima aliwaelekeza watu kwa Mungu, Babayake (2:13,20; 5:26; 7:16; 9:43).

19: 1-10 Habari za Zakayo, mtoza ushuru

k.1-2 Yesu alikuwa akipita katikati ya Yeriko, akiwa kama maili 17 kutokaYerusalemu. Ndipo huyu Zakayo, kiongozi wa watoza ushuru katika eneo hiloalitamani sana kumwona. Yesu alijulikana kuwa ‘mpenda watoza ushuru nawenye dhambi’ (15:2). Hao watu hawakupendwa na watu. Mara nyingiwalitajirika kwa njia ya kazi yao. Warumi walitoa nafasi kwa mtu kununua hakiya kukusanya kodi katika eneo fulani, wakiweka kima walichotaka, na ilikuwajuu ya yule mtu kufanya mbinu za kupata kima hicho. Iliacha njia wazi kwadhuluma. Mara nyingi, kwa sababu haikuwekwa kima halisi kwa mtu kibinafsikutoa, watoza ushuru walidai zaidi ya haki na kuweka iliyozidi mifukoni mwao.Inaonekana Zakayo alikuwa mtoza ushuru katika eneo la Yeriko, mahali pamafanikio, tena njia kutoka mashariki ilipita pale, kwa hiyo watu walipaswakulipa ushuru juu ya bidhaa. Yesu alikuwa amemwita mmoja wao kuwa katikakundi la Mitume (Mathayo/Lawi). Hakuwaonyesha dharau kama watu wengine.Kwa hiyo, Zakayo alisikia mvuto mkubwa wa kumwona.

k.3-4 Alikuwa mfupi na watu walikuwa wengi, hivyo alishindwa kumwonasawasawa kwa hiyo akaamua kwenda mbio mbele na kupanda mkuyu iliamwone. Jambo hilo laonyesha jinsi alivyosikia hamu sana ya kumwona Yesu.Ijapokuwa alikuwa mkubwa, tajiri, hata hivyo hakuogopa kuchekwa. Twawezakusema alikuwa mdadisi ila pamoja na hayo ndani yake alitamani sanakumwona huyo ambaye amesikia habari nzuri juu yake na jinsi ambavyoanawahurumia watu.

k.5 Yesu alipofika pale Yesu alitazama juu na kumwona. Tena alimwita kwa jinalake, Zakayo, akamwambia kwamba imempasa ashinde nyumbani kwake kwaile siku. Neno imenipasa inaonyesha kwamba Yesu alihesabu kwamba kukaanaye ni sehemu ya utume wake na lengo la kazi yake, kama alivyosema katikak.10. Yesu hakuwa mtu wa kufuata desturi za watu za ubaguzi wakiwawekakando watu fulani, Yeye amekuja hasa kwa shabaha ya kutafuta na kuwaokoawaliopotea (Eze.34).

k.6-7 Zakayo hakukawia, akashuka upesi, tena kwa furaha, akamkaribishaYesu nyumbani mwake. Watu wote wakastaajabu na kunung’unika, kwa vile

Page 157: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 447

Yesu amechagua kukaa na mtu wa namna hiyo badala ya kukaa na wakubwawa dini n.k.

k.8 Ni vigumu kujua maneno hayo ya Zakayo yalisemwa wakati gani, ila neno‘akasimama’ linaonyesha kwamba ni tamko rasmi la uamuzi wake kwa wakatihuo, hakusema ‘nita..’ bali ‘na..’. Alikata shauri kubadili maisha yake bilakukawia. Wayahudi walifundishwa ama kurudisha mara nne (Kut.22:1; 2Sam.12:6) na mara nyingine waliamriwa kutoa kiasi kile kile na mara nyinginekiasi cha mara saba. Baadhi ya wataalamu hufikiri kwamba Zakayo alikuwaakiwajibu makutano waliomnung’unikia na kumshtaki amewadanganya watu.Kwa jinsi alivyosema alikataa kwamba amekuwa mnyang’anyi ‘nawapamaskini...’ Iliyo wazi ni kwamba tangu wakati huo wa kukutana na Yesu maishayake yamebadilika.

k.9 Yesu alitamka wazi kwamba wokovu umefika katika nyumba hii, wala si kwayeye tu hata familia yake wameguswa katika kufika kwa Yesu nyumbani mwao.Yesu alimhakikishia kwamba alikuwa Myahudi halisi sawa na Wayahudiwengine, kuwa mtoza ushuru hakumfanya asiwe Myahudi. Ila zaidi, amekuwamwana wa Ibrahimu, kwa sababu amefanana na Ibrahimu kwa kuwaamemwamini Yesu (Mwa.17:6; Rum.4:12).

k.10 Kisha Yesu alitoa tamko rasmi juu ya utume wake akisema kwamba alikujaduniani kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. Ni mchungaji mwema atafutayekondoo zake, kama alivyofanya kwa Zakayo, alipochukua hatua ya kwanza nakumwita ashuke mkuyuni (15:3-7; Eze.34:16). Zakayo alitubu kweli na kufurahisana. Wokovu wa Yesu ni wa kiroho, si wa kisiasa, pasipo watu kubadilikamoyoni, siasa yo yote haitafaulu katika kuuleta Ufalme wa Mungu.

19: 11-27 Mfano wa Mafungu kumi ya fedha (ling. na Mt.25:14ku)Inaonekana Yesu alitoa mfano huu baada ya watu kusikia yale aliyosema kwaZakayo. Pia kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu na wengi walikuwa namatazamio makubwa kwamba huko Yerusalemu mambo yatafikia upeo katikaYeye kusimikwa rasmi kuwa Mfalme wao. Lakini upeo hautakuwa kamawalivyodhani, badala ya kusimikwa rasmi kuwa Mfalme wao atakataliwa nao nakutundikwa msalabani. Ila Baba yake atamsimika rasmi baada ya kudhiliwakwake na kwa sababu ya kudhiliwa kwake (Flp.2:9,10). Kwa hiyo, Yesu atafikaYerusalemu kama mtu ambaye yu tayari kuanza safari ya kuondokaYerusalemu na kwenda mbali sana ili apate Utume wa Kutawala kama Mfalme.Katika siku zile wakati wa Dola ya Kirumi ilikuwa desturi kwa yule aliyetakakutawala, kwanza ilimbidi aende Rumi kwa Kaisari na kupewa Tume ya Ufalme.Ndivyo ilivyokuwa kwa Herode Mkuu na baadaye Arkelau mwana wakealipokwenda Rumi ujumbe ulipelekwa na raia kwamba hawakumtaka kwasababu alikuwa mkali sana. Basi, Kaisari alikubali atawale ila hakumruhusuajiite Mfalme.

Page 158: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.12 Katika mfano, Yesu alitaja kwamba ‘kabaila alisafiri kwenda nchi ya mbaliili ajipatie ufalme na kurudi’. Kwa maneno hayo Yesu alidokezea kwambaanaondoka wala hatarudi mara. Hapo kati watumishi wake wanapewa mafungukumi ya fedha ili wayafanyie kazi. Wakati uo huo wapinzani wake wanaendeleakumkataa wakijaribu kumzuia ili Tume yake isithibitishwe. Halafu, baada yamuda mrefu, Yeye atarudi na kuwapa thawabu watumishi waaminifu nakuwaadhibu wale waliomkataa kuwa Mfalme wao.

k.13 Akawaita watu kumi na kuwapa kila mmoja mafungu kumi ya fedhaakimwambia kila mmoja aifanyie biashara hiyo fedha ndipo atakaporudiwamrudishie hiyo fedha na faida yake. Watumishi walipewa uhuru wa kuchaguajinsi watakavyoitumia hiyo fedha katika muda huo wa kati.

k.14 Ndipo Yesu aliingiza habari za watu ambao hawakumtaka awe juu yao.Jambo hilo lafanana na historia ya wakati wao wa watu kwenda Rumikuthibitishiwa utawala wao na kupewa tume yao.

k.15-19 Yesu alirudia kutaja watumishi waliopewa mafungu ya fedha. Wakatiwa kurudi kwake kila mmoja aliitwa atoe habari ya utumishi wake. Wa kwanzaalikuwa amefanya vizuri sana, akaleta faida ya mafungu kumi, na bila kujisifualisema ‘fungu lako limeleta faida’, alikiri kwamba mafanikio yote yalitokana nakipawa alichopewa na nafasi ya kukitumia. Wa pili naye alikuwa amefanikiwaakaleta faida ya mafungu matano. Aliitwa mwema kama yule wa kwanzaalivyoitwa, naye akapewa uongozi juu ya miji mitano. Jambo muhimu lilikuwauaminifu wao si kiasi cha mafanikio yao. Kila Mkristo aweza kuwa mwaminifupotelea mbali anao uwezo mkubwa au mdogo.

k.20-23 Akaja mtumishi mwingine ambaye badala ya kuifanyia biashara fedhaaliyopewa aliitunza katika leso. Alitoa sababu kwamba alihofu bwana wake kwasababu alimdhani kuwa mkali, pia alimwaza kuwa mtu aliyetafuta faidakutokana na juhudi za wengine, hivyo hakuona vema afanye lo lote na ile fungualilopewa. Hukumu yake ililingana na jinsi alivyomwaza bwana wake. Mungualiyatumia maneno yake kuwa kanuni ya hukumu yake. Ikiwa alimfikiria kuwamkali, mbona hakuiweka fedha ili ipate riba? Mawazo yake juu ya bwana wakesi udhuru wa kutokufanya lo lote bali yangemwongoza kufanya kitu kamakuiweka fedha benkini ambayo ni shughuli ndogo tena hakuna hatari ya fedhakupotezwa. Maana pesa zenyewe hazikuwa zake. Hakufikiri kwamba bwanawake amekuwa mwema kiasi cha kumkabidhi mali yake. Je! ina maanakwamba tutamkuta Bwana Mungu kwa jinsi tunavyomwaza? Tusimaanishekwamba Mungu anayo tabia ya ukali, la, ila hukumu yake ni ya kweli na ni nzito.Ni picha ya wengi walio tayari kujihusisha na Yesu bila kuwa tayari kujitwikawajibu wa kujitoa kwake.

k.24-26 Watu wa karibu waliambiwa wayaondoe yale mafungu kumi ya fedhakwa yule mtu na kumpa yeye ambaye tayari anayo mafungu kumi maradufu.

Page 159: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 449

Hao watu walisita kufanya hivi kwa vile alivyokuwa na mafungu ishirini. HalafuYesu alieleza kwamba yule mwenye mafungu atazidishiwa kwa sababu kuwana mafungu huonyesha kwamba ametumia vizuri yale aliyopewa.Kumnyang’anya yule ambaye hakuleta faida yo yote huonyesha kwamba hatakile alicho nacho kitaondolewa. Ni muhimu kutumia kiasi cho chote, haidhuru nikidogo. Kutokuifanyia biashara si udhuru utakaokubalika na Mungu. Yesuhakutaja watumishi wengine walipewa mafungu kumi. Watumishi wotehugawanyika katika makundi mawili tu, kundi la wale waliotumia mafungu yaona kundi la wale wasiotumia mafungu yao. Kiasi cha faida kilichopatikana sikitu.

k.27 Baada ya kutoa hukumu juu ya watumishi Yesu alitaja hukumu ya aduizake ambao kamwe hawamtaki kuwa mfalme wao. Wao watapata hukumu kalisana. Huenda hukumu hiyo ilitokea wakati wa Warumi kuuteka na kuuangushaYerusalemu (B.K.68-70). Wakati huo wenyeji waliteseka sana. Wakati wote wakati watumishi wake huendelea kumtumikia kwa uaminifu wakisubiri KurudiKwake ndipo kila mmoja atapata thawabu yake kulingana na alivyofanya.

19: 28-40 Yesu aliingia Yerusalemu kwa shangwe(Mt.21:1-10; Mk.11:1-10; Yn.12:12-19)

k.28 Baada ya kutoa mfano wa mafungu kumi Yesu alikazana kushikamwenendo wake wa kwenda Yerusalemu. Tangu sura 9 Luka ametaja safarihiyo mara kwa mara na kila mara alionyesha jinsi Yesu alivyokuwa na nia sanaya kufika Yerusalemu kama lengo lake hasa ni kufika pale. Yerusalemu ulikuwamji mkuu na wa kwanza kwa Wayahudi na mahali pa hekalu. Sinagogi zilikuwakatika miji na vijiji ila hekalu lilikuwa moja tu na watu walitakiwa kuhudhuria palemara tatu kwa mwaka kwa Sikukuu zilizoamriwa

k.29 Kijiji cha Bethania kilikuwa maili mbili hivi kutoka Yerusalemu na Bethfage,kijiji kingine, kilikuwa karibu yake. Walipofika hapa Yesu aliwatuma wanafunziwawili ili wamletee mwana-punda ambaye atampanda na kuingia Yerusalemukwa wazi na kwa ujasiri. Aliwaelekeza hao wawili mahali watakapomkuta huyomwana-punda, na aliwapa maneno ya kuwaambia wenye punda wakiulizwasababu ya kumchukua. Inaonekana Yesu alikuwa na ujuzi wa kipekee maanaalijua mahali pa mnyama, na ya kwamba alifungwa, pia alikuwa badohajapandwa, na alijua hakika kwamba wenye punda watamruhusuwatakapoyasikia maneno ya wanafunzi. Luka amependa kutaja jinsi Yesualivyokuwa na ujuzi wa kipekee. Baadhi ya watu hufikiri kwamba alikuwaameishapanga na hao watu kabla ya wakati huo. Haidhuru ilikuwaje, iliyopo nikwamba ilitokea kwa jinsi walivyoambiwa na Yesu. Huyo mwana-punda alikuwabado hajapandwa na mtu ye yote na katika Torati mnyama wa namna hiyoalifaa sana utumishi wa Mungu (Hes.19:2; 1 Sam.6:7). Neno hilo laonyeshauwezo wa Yesu kumpanda na kumtawala mnyama ambaye hajazoea badokupandwa tena wakati wa kuzungukwa na umati wa watu na kelele nyingi.

Page 160: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.35ku. Walimfikisha punda kwa Yesu na wanafunzi walichukua hatua yakwanza wakizitandika nguo zao juu yake, kisha wakampandisha Yesu juu yake.Njiani watu walizitandaza nguo zao. Luka hakutaja habari za watu kukatamatawi na kuyatandika njiani. Hayo yote yaliashiria jinsi watu walivyomwazaYesu kuwa Masihi wakimshangilia kwa shangwe za Kifalme (2 Waf.9:13). Yesuhakusita kuzipokea sifa zao. Walipofika kwenye matelemko ya mlima waMizeituni na kuuona mji mkuu katika uzuri wake na hekalu likimetameta juaniwatu walizidi kuwa na shauku kuu. Walimsifu Mungu kwa ajili ya matendomakuu yote ambayo Yesu alikuwa amefanya (pale Yeriko alimjalia Bartimayokipofu uwezo wa kuona na hivi karibuni alikuwa amefufua Lazaro, mfu wa sikunne Yn.11:1ku). Hayo yote yalimdhihirisha Yesu kuwa anao uwezo wa kipekee,wa Mungu.

k.38 Watu walimkaribisha kwa maneno ya Zab.118:26, maneno yaliyotumikakatika kuwakaribisha wasafiri waliokuja Yerusalemu kwa Sikukuu ya Pasaka,maneno yaliyomhusu Masihi, na Luka aliingiza neno ‘Mfalme’ kwa kusisitizajambo hilo. Kwa kusudi, na kwa wazi, na kwa shangwe kuu, Yesu aliingiaYerusalemu kama kudai atawazwe kuwa Mfalme wao. Ila tukumbuke kwambakatika 19:11-28 alisema juu ya mtu aliyeondoka ili ajipatie ufalme ndipo atarudibaada ya muda mrefu. Kwa jinsi alivyoingia, hali amepanda mwana-punda, nakwa jinsi alivyofundisha kila wakati ya kuwa Ufalme wake si wa siasa, wala wavita, alitaka kuonyesha kwamba hakuwa na shabaha ya kufanya mapinduzi.Yeye ni Mfalme tofauti na wengine waliojidai kuwa wafalme, hata ilimbidiaazimu punda tofauti na wale waliokaa kwa raha na punda zao chini ya mitinina mizababu yao. ‘Amani mbinguni’ ni maneno ya kuithibitisha shabaha yakeya kuleta amani, amekuja afanye upatanisho kati ya Mungu na wanadamu nakwa ajili yake atatundikwa msalabani akiwa fidia ya dhambi. Ni ukumbusho wamaneno ya 2:14; 19:42. Kutokana na jumla ya Wayahudi kumkataa hao watuwatakosa kuwa na amani hiyo. Katika hayo yote Mungu hutukuzwa.Mafarisayo waliokuwemo miongoni mwa watu waliomshangilia Yesu,hawakupendezwa na shauku za watu. Ila waliona ni vigumu kusema namkutano wa watu, kwa hiyo, walimwomba Yesu awanyamazishe. Penginewalihofu kwamba Warumi watachukua hatua kali juu yao ikitokea ghasia mjiniwakati wa Sikukuu. Hasa walisikia wivu na kuchukizwa kwa vile Yesualivyopendwa sana na watu. Lakini Yesu aliwajibu kwamba, hata ikiwa watuwatanyamaza, mawe yatapiga kilele (Hab.2:11). Yawezekana ilikuwepo mithaliyenye maneno hayo. Zaidi ya yote tendo kuu linatendeka na uumbaji ulivutwakulishuhudia, mwumba wao anaingia Yerusalemu ili atundikwe msalabani kwaukombozi wa ulimwengu.

19: 41-44 Yesu aliomboleza juu ya YerusalemuHabari hii inapatikana katika Luka tu. Yesu alipoukaribia Yerusalemu na kuuonauzuri wa mji na hekalu likimetameta juani, maana lilipakwa na dhahabu, namarimari ilitumika katika ujenzi wake, alilia sana kwa sababu alijua mwisho

Page 161: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 451

wake utakuwa mbaya ikiwa wenyeji wake wataendelea kumkataa. Twaonatofauti kubwa kati yake na umati wa watu waliomsindikiza mpaka mjini. Waowalijaa furaha kubwa wakimshangilia sana, huku Yeye anaulilia sana mjimtakatifu. Kwani aliulilia huo mji? Aliulilia kwa sababu katika kumkataawatakuwa wamekosa nafasi njema sana ya kumpokea. Ni katika Yeye amanihupatikana, amani iliyo dalili ya uhusiano mwema kati ya watu na Mwumbawao. Lakini hayo yote hawakuyatambua, ni kama wamepofushwa macho.Alitamani sana wayabadili mawazo yao juu yake kabla ya nafasi kupita; wawetayari kumpokea kama Masihi wao.

k.43-44 Ndipo Yesu alitaja habari za kuangamizwa kwa Yerusalemu akielezamambo kadha yatakayotokea mbeleni. Mambo hayo yalitokea kweli, wakati waWarumi kufanya vita na kuangamiza Yerusalemu B.K.68-70. Boma ambalowatalijenga ili wajilinde na adui litatumika na adui na kuwa msaada kwaowanapouzunguka mji na kuuteka. Watu walishindwa kutoroka. Yesu alirudiakutaja sababu ya hayo yote ‘kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako’.Katika kuja kwa Yesu, Mungu alikuwa ameujia mji mkuu na wateule wake naohawakumtambua. Walipaswa kumtambua kwa sababu katika matendo makuuya Yesu waliuona uwezo mkuu wa Mungu na kwa sababu hiyo kwa vyo vyotewalipaswa kumpokea. Yesu alijua hali yao na mipango yao, jinsi wakuuwalivyoendelea kutafuta njia ya kumwondoa, kwa hiyo, alitamka wazi kwamba,kulingana na uamuzi wao wa kutokutaka mtu wa amani, vita wataipata, na kwavita watashindwa. Nabii Malaki alitabiri habari ya Yesu kulijia hekalu lake(Mal.3:1ku). Yesu aliwajia akileta wokovu na baraka kama Nabii Zekariaalivyotabiri zamani (Zek.9:9ku).

19: 45-48 Yesu alilitakasa hekalu (Yn.2:13-33; Mt.21:12-17; Mk.11:15-19)Luka ameandika habari hii kwa ufupi. Yohana aliweka habari hii mwanzoni mwaInjili yake. Je! Yesu alifanya tendo hilo mara mbili, mwanzoni na mwishoni mwahuduma yake? Wataalamu wengi hukubali kwamba alifanya mara mbili. Ilawako wengine ambao wanafikiri kwamba Yohana aliweka habari hii mwanzonimwa Injili kwa sababu alitaka kufanya tendo la Yesu la kumfufua Lazaro kuwalile lililowachokoza Wayahudi kufanya mipango ya kumwondoa.

Watu walitakiwa kutoa fedha ya kipekee hekaluni, hivyo nafasi iliwekwa kwawatu kubadili fedha. Wanyama wa sadaka walihitajika na watu waliwezakuwanunua pale Yerusalemu badala ya kuwaleta wanyama kutoka mbali.Nafasi hizo za kubadili fedha na kununua wanyama ziliwasaidia watu, ila Je!kwani shughuli hizo zifanyike pale hekaluni, katika ua la WaMataifa, mahali paopamoja tu pa ibada, kati ya kelele zake? Bila shaka zingeweza kufanyika mjiniau kandokando yake. Hilo ndilo jambo ambalo lilimsumbua Yesu aliposema‘Imeandikwa, nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala, lakini ninyi mmeifanyakuwa pango la wanyang’anyi’ kama Yeremia alivyotabiri (Yer.7:11; Isa.56:7).Mara nyingi watu walidhulumiwa katika shughuli hizo, wanyama waliuzwa kwabei kubwa na mara nyingine ikiwa watu waliwaleta kutoka nyumbani, wa kwao

Page 162: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

katika ukaguzi walikataliwa. Marko ametaja kwamba tendo hilo lilifanyika sikuiliyofuata ile ya kuingia Yerusalemu, lakini Yesu hakukamatwa, walimwachakuendelea mpaka baadaye kidogo.

k.47-48 Kila siku Yesu alifika hekaluni na kuwafundisha watu. Alikuwa jasiri,hakuogopa wakuu na wakati huo huo wakuu walizidi kuchukizwa nao wakazidikuikamilisha mipango ya kumkamata, ila walishindwa kwa sababu umati wawatu walikuwa wakimpenda Yesu na kuwa upande wake dhidi yao. Katikawakuu, walikuwa wakuu wa makuhani, hao walikuwa matajiri na wenye sautikatika siasa ya nchi. Walijitahidi kuridhiana na Warumi. Pamoja nao walikuwapowaandishi, wafafanuzi wa Torati. Wengine waliotajwa ni ‘wakuu wa watu’ na nimara ya kwanza hao kutajwa. Walikuwa akina nani? Huenda walikuwa viongoziwalei katika Baraza kuu la nchi lililoitwa Sanhedrin. Hao wote walitakakumwangamiza Yesu. Walichukizwa sana na matendo makuu ya Yesu kuingiaMji wao kwa shangwe kuu na kulitakasa hekalu bila kuomba idhini yao walakupitia kwao na kupata ruhusa yao. Ilionekana amewaweka kando bila kuijalimamlaka yao. Kwa hiyo, kwa siku chache katika juma hilo Yesu aliachiwanafasi ya kuwafundisha watu na wakuu walishika nafasi ya kumpinga kwa njiaya kumwuliza maswali makali.

Uhasama uliotokea katika 19:47-48 ulizuka tena nao uliendelea katika sura yoteya 20 viongozi wa makundi mbalimbali wakipambana na Yesu wakijaribukumwaibisha mbele za watu na kumnasa katika maneno yake.

MASWALI1. Yesu alitaka kufundisha nini kuhusu maombi alipotoa Mfano wa Mjane

na Kadhi na Mfano wa Farisayo na Mtoza Ushuru?2. Alipowabariki watoto wadogo Yesu alitaka kuonyesha nini kuhusu

huduma kwa watoto: pamoja na hayo alifundisha nini kuhusu Ufalme waMungu?

3. Eleza kwa nini ilikuwa vigumu kwa kijana tajiri kumfuata Yesusawasawa? Atapata shida gani? Ndipo eleza shida ya kuwa na mali.

4. Kipofu wa Yeriko alionyesha tabia gani nzuri alipojua Yesu anapitamahali alipo?

5. Fafanua habari za Zakayo ukionyesha jinsi Yesu alivyojihusisha naye?6. Twajifunza nini kutokana na Mfano wa Mafungu kumi ya fedha?7. Kwa nini Yesu aliingia Yerusalemu hali amepanda punda na

kushangiliwa na watu?8. Alipopata kuuona Mji Mkuu kwa mbali, Yesu alifanya nini? na kwa

sababu gani?9. Kwa nini Yesu alilitakasa hekalu? Ni mambo gani yaliyomwudhi?

Page 163: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 453

20: 1-8 Swali juu ya mamlaka ya Yesu (Mt.21:23-27; Mk.11:27-53)

k.1 Yesu alikuwa amefanya makuu bila ruhusa yao na bila kupata idhini yao.Jambo moja kubwa lilikuwa kuingia Yerusalemu kwa shangwe, la pili lilikuwakulitakasa hekalu, na lingine lilikuwa kuendelea kufundisha katika makumbi yahekalu. Alikuwa akihubiri habari njema ya kuwa Mungu amekuja karibu naokatika huduma yake. Ndipo ghafla wakatokea kundi rasmi la watu kumhoji,wakuu wa makuhani pamoja na waandishi na wazee, hao wazee bila shakawalikuwa waheshimika walei. Yaonekana hao walikuwa wajumbe waliotumwana Baraza kuu la Sanhedrin.

k.2 Moja kwa moja walimwuliza swali kuhusu mamlaka yake. ‘Mambo hayo’ nijumla ya yote aliyokuwa akiyatenda, nao walitaka kujua ni kwa mamlaka ganianayafanya, na ya kuwa hiyo mamlaka ilitoka kwa nani? Sehemu ya pili yaswali ilikuwa na shabaha ya kumnasa, kwa sababu akijibu ‘kwa Mungu’ marawatamshtaki kuwa amekufuru. Ilikubalika kwamba, ni Masihi, peke yake,ambaye alikuwa na mamlaka ya kufanya jinsi Yesu alivyofanya bila kupataruhusa yao.

k.3-4 Yesu hakuepa swali lao ila alijibu kwa njia ya kuuliza swali ambaloliliunganisha huduma yake na ile ya Yohana Mbatizaji. Yohana alifanya kazi bilakupata ruksa yao. Watu walimkubali kuwa nabii aliyetumwa na Mungu, ambayealifanya kazi kwa mamlaka ya Mungu. Yeye alifanya jambo geni kwa Wayahudi,wale waliotubu aliwabatiza. Ilikuwa desturi ya Kiyahudi kuwabatiza WaMataifawalioongokea dini yao, si Wayahudi wenzao. Yohana alisema wazi kabisakwamba yeye hakuwa Masihi, ila alitumwa kutayarisha njia yake. AlimshuhudiaYesu kuwa mkuu kuliko yeye ambaye yeye hakustahili kuilegeza gidamu yaviatu vyake. Kwa hiyo swali la Yesu lilikuwa halali, kwa sababu, katika kulijibuwatakuwa wamepata jibu sahihi la swali lao.

k.5-6 Waliona kwamba kwa jinsi Yesu alivyowauliza wamebanwa kabisa.Walijua kwamba wakijibu kwamba Ubatizo wa Yohana ulitoka kwa watu tu, basiwatu watawapiga, maana wote walikubali kwamba Yohana alitumwa na Mungu.Wakijibu ulitoka mbinguni ni dhahiri kwamba walipaswa kuukubali ule ushuhudawa Yohana alioutoa juu ya Yesu na kumpokea Yesu kuwa Masihi aliyetumwana Mungu.

k.7 Kwa sababu hawakutaka kuwa watu wa kweli na kuuzingatia ukweliuliofichwa ndani ya swali la Yesu kuhusu mamlaka itokayo kwa Mungu,wakamjibu ‘hatujui’ jibu la ajabu sana likitolewa na viongozi ambao walipaswakuamua mambo ya kiroho na ya Mungu. Wamekuwa kama viongozi vipofuwasiofaa kuwa viongozi kwa sababu ya unafiki wao.

k.8.Yesu akakataa kuwaambia wazi ni kwa mamlaka gani aliyofanya mamboyake. Hakusema kwamba hakuwa na mamlaka, wakati wote Yesu alifanya

Page 164: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

mambo yake yote kwa mamlaka ya Mungu na kwa kulingana na mapenzi yaBaba yake. Wangalipata jibu kama wangalijibu swali lake sawasawa.

20: 9-19 Mfano wa Shamba la Mizabibu (Mt.21:33-46; Mk.12:1-21)Katika mfano huu Yesu alitoa changamoto kwa viongozi baada ya waokumwuliza juu ya mamlaka yake. Viongozi walitambua maana ya mfano huo naya kuwa Yesu alikuwa amewalenga. Katika historia yao mara nyingi viongozihawakuwa tayari kuwajibika kwa Mungu.Katika Agano la Kale taifa la Israeli lilifananishwa na Shamba la Mizabibu.Katika Isa.5:1-7 nabii alimsifu sana mwenye shamba, yaani Mungu,aliyelipenda na kulishughulikia sana taifa hilo (Yer. 2:21; Zab.80:8; Eze.15.1-6;19:10ku. Hos.10:1; Yoe.1:7). Wote waliosikia mfano walifahamu, bila shida,kwamba Yesu alikuwa akilisemea taifa lao teule. Hasa Yesu aliwalengaviongozi (wakulima) ambao katika historia yao yote wamewakataa wajumbe(manabii) waliotumwa na Mungu. Ila wakati huo ni tofauti, upeo umefikiwa, kwasababu Mungu amemtuma Mwana wake, si nabii. Kwa hiyo ni juu yao amakumpokea, ama kumkataa, na matokeo yatakuwa mafanikio au hukumu kali.

k.9-13 Ilikuwa desturi ya mwenye shamba kuwapangisha watu ili walimeshamba na kumpatia mwenye shamba mavuno, ndipo mtumwa alitumwakupata hayo mavuno na kumletea. Ilitokea kwamba, kila alipotumwa mtu wakupata hayo mavuno alifanyiwa vibaya na kukataliwa. Hivyo, mwenye shamba,hakupata cho chote na watumishi waliotumwa walifanyiwa isiyo haki. Bila shakalilikuwepo patano kati ya wakulima na mwenye shamba juu ya sehemuiliyokuwa haki yao kwa kazi yao na sehemu yake. Kila mtumwa alifanyiwavibaya kuliko mwenzake aliyemtangulia.

k.13-15a Lakini, kwa sababu mwenye shamba ni mzuri ambaye analipendasana shamba lake, yaani Mungu alipenda sana taifa la Israeli, badala yakuwachukulia hatua na kuwahukumu, aliamua kuwapa nafasi nyingine tena.Badala ya kumtuma mtumwa aliamua kumtuma Mwana wake mpendwa,akitumaini kwamba watautambua upendo wake kwao, nao watamstahi huyoMwana wake na kumpa matunda ya shamba.

Ajabu ni kwamba, walipomwona Mwana, waliona ni nafasi yao ya kulishika hiloshamba. Kwani waliwaza hivyo? Huenda walidhani kwamba mwenye shambaamefariki dunia na ndiyo sababu Mwana amewajia. Au, yawezekana walifikiriBaba amemkabidhi mwana shamba lake. Pengine waliona mwenye shamba yumbali, atashindwa kuwachukulia hatua, au huenda walidhani kwamba mwenyeshamba atakata tamaa, wala hataendelea kutazamia matunda ya shamba. Yotehayo ni ndoto tu. Iwapo Mwana huonekana kama hana usalama, ni wakudhuriwa tu, hata hivyo, Yeye ni mwamba imara ambao ukigongana na mtu,au mtu akigongana na huo mwamba, kwa vyo vyote, hasara kubwa itampatayule mtu. Walipomwona Mwana walimtupa nje ya shamba na kumwua.

Page 165: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 455

Hawakutaka shamba linajisike na damu yake, kwa sababu likinajisika,watashindwa kuyauza mazao yake.

k.15b-16 Hao wakulima walikosa kuutambua ushupavu wa mwenye shamba.Yeye hataachilia hilo jambo zito la kumwua mwana wake. Wahusika katikakumkataa mwana wataadhibiwa vikali. Neno hilo liliwakwaza sana walewaliolisikia; ila walikwazwa zaidi waliposikia kwamba, baada ya waokuondolewa shamba, wengine watapangishwa shamba. Hao ni akina nani?Kumbe ni WaMataifa, watu waliodharauliwa sana na taifa la Israeli. Walifikiriwakuwa mbali sana na nje ya mipango ya Mungu. Ila ilikuwepo sharti moja tu,iliwapasa WaMataifa pia wampatie mwenye shamba, yaani Mungu, matunda yashamba, jambo ambalo hao Wayahudi walishindwa kufanya. Viongozi,waliposikia habari hiyo, walisema ‘Hasha, yasitukie haya!’ waliona ni kitisho chaukatili sana.

k.17-18 Kisha Yesu alionyesha kwamba neno hilo lilikuwamo katika Maandiko(Zab.118:22-23). Yesu ni Jiwe la heshima, la uwezo, na la maana sana katikajengo, na iliwapasa wajenzi wa taifa la Israeli waliweke mahali pake pa juu. Nijiwe muhimu katika makusudi ya Mungu juu ya Israeli. Jambo kubwa ni kwambani Yesu aliye na kibali cha Baba, ametumwa naye, naye hufanya mapenzi yakena kwa njia yake makusudi ya Mungu hutekelezwa. Wao watabaki wakiteseka.Yesu kwao ni kikwazo. Haitakuwa rahisi kumwamini Yeye aliyekataliwa nakuuawa, ila Mungu atamtukuzwa baada ya kudhiliwa kwake, kwa njia yakumfufua kutoka wafu.

k.19 Wakuu wa makuhani na waandishi waliomsikia walijua kwamba Yesuamewasema, pia ameonyesha kwamba anaijua mipango yao ya kumwondoa.Palepale na saa ileile walitaka kumkamata na kumwondoa. Ajabu kabisa.Hawakuwa tayari kuuzingatia huo mfano na kujihoji na kujirekebisha mwenendowao. Kwa njia ya mfano huo Yesu alikuwa amelijibu swali lao juu ya mamlaka.Yeye ni Mwana mpendwa wa Baba, ambaye ametumwa na Baba kwa shambalake, taifa la Israeli. Yesu alijua kwa hakika kwamba Yeye ni Mwana wa Baba,pia alijua mwisho wake ni kuuawa hivi karibuni.Viongozi walichukizwa sana na mfano wa shamba la mizabibu, ni kama ulikuwakuni ya kuwasha moto chuki yao. Walitafuta njia nyingine ya kumnasa Yesu.Walizidi kutafuta ushahidi pamoja na kumsumbua na maswali ili akose fadhili zawatu. Mpaka wakati huo wameshindwa kufanya walivyotaka kwa sababu watuwengi walikuwa upande wa Yesu. Walijaribu kuvuta serikali ya Kirumi waonemashaka juu yake na kumfikiria kuwa mwanamapinduzi, ndilo lengo la swalihilo.

20: 20-26 Swali juu ya kumtolea Kaisari kodi (Mt.22:15-22; Mk.12:13-17)k.20 Wakuu wenyewe hawakumjia Yesu ila waliwatuma wanafunzi wao ambaowalijifanya kuwa walitaka kujua wafanye nini hasa kuhusu malipo ya kodi kwaDola ya Kirumi. Maneno ya kifungu hicho yaonyesha nia yao mbaya.

Page 166: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

‘wakamvizia-vizia’ ‘wapelelezi’ ‘waliojifanya’ ‘ili wamnase’ ‘wapate kumtia katikaenzi na mamlaka ya liwali’. Kwa hiyo, kifungu hicho chatoboa wazi chuki yaokubwa na hila yao na shabaha yao.

k.21 Waliposema na Yesu waliyatumia maneno ya kumpaka mafuta ili asiwena tahadhari anapowajibu. Maneno yenyewe yalikuwa kweli ili sababu yao yakuyatumia ilikuwa ya hila, ni kama kumbembeleza aseme mawazo yake kwauhuru na kwa wazi.

k.22 Ndipo walimwuliza moja kwa moja swali la kuhusu uhalali wa kulipa kodikwa serikali ya Kirumi. Walidhani kwamba jibu ama litakuwa ndiyo au siyo.Akijibu ‘ndiyo’ ni kama ameridhiana na utawala wa Kirumi ni kujiweka mbali nahamu ya Wayahudi wenzake waliokazana kupata uhuru mbali na Rumi.Akifanya hivyo basi wataweza kuziamsha nia za watu na kuonyesha jinsiasivyofaa kuwa Masihi wao. Dhidi yake akijibu ‘siyo’ ni kama haungi mkonoutawala wa Kirumi, basi, watakuwa wamepata neno la kumshtaki kwa serikali.Neno la kodi liliwachukiza sana Wayahudi, kwa kuwa ilikuwa dalili yakutawaliwa na wageni. Wao walijiona kuwa taifa huru, ambalo mtawala wao niMungu peke yake. Warumi waliingiza kodi kama B.K.6-7 na ghasia ilitokea, namara kwa mara watu waliinuka waliofanya kampeni ya kukataa kulipa kodi(Mdo.5:37). Hao walioleta swali hilo walitaka kujua kama ilikuwa halali mbele zaMungu, walijua kwamba ilikuwa halali kwa sheria ya Kirumi. Ni swali lililojadiliwasana kati yao.

k.23-25 Je! Yesu atajibuje? Atatokaje katika mtego wao? Yesu aliwaombawamwonyeshe dinari, fedha ya Kirumi, yenye sanamu ya Kaisari, fedhawaliyotumia katika maisha ya kila siku pamoja na sarafu za aina nyingine.Ndipo aliwauliza ‘ina sura na anwani ya nani?’ Ama Yesu hakuwa na fedhamfukoni au alitaka wao wailete ili iwe dhahiri kwamba wakiwa na fedha hiyo niishara ya kuwa wamepaswa kulipa kodi kwa huduma na fadhili walizopatakutokana na utawala wa Kirumi. Wakipenda, wasipende, kwa kuitumia fedhayenye sanamu ya Kaisari wamekiri kwamba wamedaiwa kodi, tena hawaonishida katika kuitumia fedha hiyo kwa biashara na maisha yao kwa faida yao.Mbona basi, wakatae kulipa kodi? Iliwabidi watamke wazi kwamba anwani nasura zilikuwa za Kaisari.

Kisha Yesu aliendelea kwa kutamka neno muhimu kabisa kuhusu uhusiano waserikali na uhusiano wao na Muumba wao. ‘vya Kaisari mpeni Kaisari’ maanayake, hawakuweza kujiondoa na kuishi kana kwamba hawakuwemo chini yaDola ya Kirumi wakati ule. ‘vya Mungu mpeni Mungu’ vilevile Mungu anayo hakiyake ya kupewa utiifu wao, kwa kuwa, vyote walivyo navyo vyatoka Kwake.Wanadamu wote ni raia chini ya utawala fulani, ama ya nchi yao wakiwa huru,au ya nchi nyingine ikiwa hawawi huru. Pia, wakati wote, wanadamu ni raia wambinguni. Hivyo Yesu hakukubili kutenganisha wajibu wa mtu kwa utawala wahapo duniani na wajibu wake kwa utawala wa Mungu. Ila siyo kusema kwamba

Page 167: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 457

tawala hizo mbili ni sawa. Utawala wa Mungu na utiifu wetu kwa Mungu huzidiule wa serikali, ila haiwezi kuwekwa nje yake. Katika utiifu wetu kwa Mungu,sehemu mojawapo ni utiifu wetu kwa serikali. Serikali ina haki yake ila hainahaki ya kuingia eneo la maisha ya mtu linalomhusu Mungu. Si sawa kugawamaisha katika sehemu mbalimbali. Mwishowe sehemu zote zamhusu Mungu.(Ling.Rum.13:1-7; 1 Pet.2:13-17). Wayahudi waliingiza kodi ya hekalu, na kilaMyahudi alipaswa kuilipa.

k.26 Jibu lake liliwashangaza watu, nao waliouliza swali wakanyamaa,hawakuweza kumshtaki Yesu kwa njia yo yote. Badala ya kumwaibisha mbeleza watu na kuipunguza sifa zake, watu walizidi kumpenda.

20: 27-40 Swali juu ya Ufufuo (Mt.22:23-33; Mk.18-27)k.27 Vikundi mbalimbali waliendelea kumwuliza Yesu maswali yenye shabahaya kumnasa au kumwaibisha, ili aonekane kuwa mtu asiyejua mambo yaMungu sawasawa. Hao Masadukayo hawakuwa kundi kubwa, walitoka katikatabaka ya makabaila nao walikuwa na sauti kuu katika utawala wa nchi chini yaWarumi. Walijiunga na kundi la makuhani, matajiri, waliokuwa radhi na mambojinsi yalivyo, wakiwa tayari kujipendekeza kwa Warumi ili waendelee katikavyeo vyao. Mafarisayo na makundi mengine hawakuwapenda ila katikakumpinga Yesu walikuwa tayari kujiunga nao. Kwa upande wa dini Masadakayowalishika mambo juujuu, hawakuwa na hali ya kiroho, wala hawakuyakubalimapokeo ya waandishi. Inafikiriwa kwamba kwa upande wa Maandikowalikubali vitabu vitano vya Musa. Kutokana na Mdo.23:8 twaona kwambahawakuamini neno la ufufuo, kuwapo kwa malaika na roho. Yafikiriwa walitokakwa Sadoki, kuhani wa zamani (1 Waf.1:8; 2:35).

k.28-33 Walimwuliza Yesu swali juu ya ufufuo, wakilenga kuonyesha ni upuzikuamini kuwepo kwa ufufuo. Walitunga mfano wa ajabu sana, wa ujinga.Walitaja ile ruhusu ya Musa kwa ndugu ya mtu aliyekufa bila kuzaa watotokumchukua mkewe ili azae mtoto, kusudi jina la huyo mume aliyekufa lisipotee.Katika mfano wao walisema kwamba walikuwepo ndugu saba ambao mmojabaada ya mwingine alimchukua huyo mama, mpaka saba wamekuwa naye,kisha wote walifariki dunia bila kuzaa naye. Ndipo wakataka kujua ni yupiatakayehesabiwa kuwa mume wake katika ufufuo wa watu, maana wote sabawalikuwa ‘mume’?.

k.34-36 Yesu aliwajibu kwa kuonyesha kwamba maisha ya baadaye ni tofautisana na maisha ya sasa. Wakati huo Mungu ameamuru ndoa iwepo kwashabaha ya watoto kuzaliwa na pengo linaloletwa kwa watu kufa lizibwe. Kwanjia hiyo wanadamu hupata kuendelea kuwepo duniani. Katika ulimwengu ujaohakuna kifo, watu wataishi milele na milele, na kwa sababu hiyo hakuna haja yawatu kuzaliwa, na ikiwa hakuna haja ya watu kuzaliwa basi, hakuna haja yakuwepo kwa ndoa na uhusiano wa kimwili kati ya mume na mke. Yesu alisemakwamba watu watakuwa kama malaika ambao hawafi, nao watakuwa ‘wana’

Page 168: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

wa Mungu kwa sababu wamekuwa ‘wana’ wa ufufuo. Maisha yao yatakuwa nahali ya utukufu na uhuru mbali na shida za kimwili kama kuzeeka, kuugua, nakupatwa na ajali. Hayo yote yatatoweka. Watu watazidi kufanana na ‘Baba’ yaowa mbinguni (Yn.1:12ku. 1 Yoh.3:1ku). Uzima wa milele si kuendelea kuishi tukatika mazingira mapya, kama Wayahudi walivyodhani na hata leo ndivyowengi wawazavyo bali ni kuishi katika mabadiliko ya hali, katika ‘mwili wa roho’.Kwa hiyo, wale waliouliza swali walikosa katika kuwaza kwamba maisha yabaadaye yatafanana na maisha ya sasa.

k.37 Kisha Yesu alisisitiza neno hilo na uhakika wa kuwepo kwa Ufufuoakiyatumia maneno ya Musa wakati alipokuwapo jangwani na kuitwa na Mungukutoka kijiti kilichowaka moto (Kut.3:6) Mungu alijitaja kuwa Mungu waIbrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo, watu ambao walikuwawameishafariki dunia. Mungu hakusema wa marehemu Ibrahimu n.k. Kwa jinsialivyosema hao mababa walikuwa wangali hai mbele zake.

k.38 Yesu alikaza neno hilo kwa kusema kwamba Mungu si Mungu wa wafubali wa walio hai, kwa kuwa wote huishi kwake. Wale watakaoushiriki uzima wamilele, baada ya kufa, wako hai kwa Mungu, uhusiano wao haukatiki wakati wakufa, bali unaendelea na kuzidi. Ndipo katika Siku ya Ufufuo miili yao itafufuliwana kuungana na roho zao, watapewa miili mipya ifaayo maisha ya baadaye,kisha wataishi mbele za Mungu milele na milele. Hilo ndilo tumaini la waumini.

k.39-40 Waandishi kadha waliona kwamba Yesu amewajibu vizuriMaSadukayo. Yawezekana hao waandishi waliamini jambo la ufufuo. Baada yahapo watu hawakuthubutu kumwuliza swali tena. MaFarisayo walishindwakumnasa, MaSadukayo walishindwa kumpuuza mbele za watu.Yesu alisema kwa mamlaka juu ya neno la ufufuo kwa sababu alitoka kwaMungu na kujua yaliyopo juu, na katika hali ya kuwa Mungu Mwana alielewayatakayotokea baadaye.

20: 41-44 Swali juu ya Kristo (Mt.22:41-46; 23:6; Mk.12:35-37)Baada ya vikundi mbalimbali kumshambulia Yesu na maswali yao YesuMwenyewe alishika nafasi ya kuwauliza swali moja muhimu, la maana sana, juuya Nafsi yake, swali ambalo wakijibu sawasawa watamwelewa vizuri. Swalililihusu jinsi walivyomwaza Masihi. Je! Masihi ni ‘Mwana wa Daudi’ tu,aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi? Au Je! Masihi ni zaidi? Ana asili katikaMungu, Je! ni Mwana wa Mungu?’ Wengi walimkubali kuwa ‘mwana wa Daudi’wakijua alizaliwa katika ukoo wa Daudi (1:27,32,69; 2:4; 18:38 ku). Mara nyingialiitwa hivyo. Katika kumwaza kuwa ‘mwana wa Daudi’ walimlinganisha naDaudi, aliyekuwa Mfalme wao mashuhuri, mtu wa vita aliyewashinda adui zaona kuliinua taifa lao kuwa na sifa kati ya Mataifa. Katika kutaka Masihi walikuwawakitamani kupata mtu kama Daudi atakayefanya sawasawa na Daudialivyofanya, hasa walitaka mtu atakayefanya vita na kuwashinda adui zao, hasaWarumi waliowatawala.

Page 169: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 459

Kwa kuuliza swali hilo Yesu alitaka kuyatikisa mawazo hayo ya watu nakuusahihisha ufahamu wao juu ya Masihi na kazi zake. Yesu aliyatumiamaneno aliyoyatumia Daudi katika Zaburi 110 akionyesha kwamba Daudimwenyewe alifahamu kwamba Masihi atamzidi kwa sababu asili yake ni katikaMungu si katika wanadamu. Ndiyo maana ya ‘Bwana (yaani Bwana Mungu)alimwambia Bwana wangu (yaani Masihi) uketi mkono wangu wa kuume hataniwaweke adui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako’ Hivyo Daudi alimwitaMasihi ‘Bwana wake’ na kusema kwamba Mungu amemwambia Masihikwamba atamweka mkono wake wa kiume…’ Kwa kusema hivi Yesu hakukanakwamba kimwili ametoka viunoni vya Daudi, ila alidai kwamba, kwa asili,ametoka kwa Mungu na atarudi kwa Mungu, na ya kwamba Kufufuka Kwakekutathitibisha neno hilo (Mdo.2:36). Iwapo hakusema wazi, Yeye, kamaalivyodokezea mara nyingi, si mtu wa vita. Kazi yake na utume wake sikuwafukuza Warumi, Yeye huhusika na maadui makubwa zaidi, dhambi,Shetani, na mauti, katika Kufa Kwake atawashinda hao adui za wanadamuwote si wa Wayahudi tu.

20: 45-47 Maonyo juu ya waandishi wa sheriaYesu alitoa onyo hilo kwa wanafunzi wake wakati wa watu wengi kuwepo nakumsikiliza. Alifahamu kwamba baadaye wanafunzi watakuwa na vyeo naheshima kati ya watu. Katika Kanisa watakuwa viongozi, nao watajaribiwakujiona na kutaka kuwatawala waumini kwa nguvu. Ikitokea hivyo basi, Ukristoutaganda na kufanana na dini ya Kiyahudi ukikaza mambo ya nje badala yamambo ya ndani, ya moyo. Hii ni hatari mojawapo iliyo mbele ya Kanisa. Lukaameachia neno hilo bila kusema lo lote juu ya itikio la watu au la wakuu, ilaMathayo alisema kwamba tangu hapo watu hawakuweza kumjibu walahawakuthubutu kumwuliza maswali tena (Mt.22:46).Katika kuwaonya wanafunzi Yesu alitaja waandishi wa sheria na kielelezo chaokibaya. Walitumia nafasi yao ya dini wakitafuta kuheshimwa na watu. Walivaanguo zao tofauti na kujionyesha kuwa tofauti, lakini walifanya hivyo kwa kuifichachoyo na udhalimu wao. Hasa waliwanyang’anya wajane mali zao hukuwakisali sala ndefu sana ili waifiche choyo yao. Waliwanyang’anya kwa njiagani? Yesu hakusema wazi, ila siku zile waandishi walikuwa wanasheria.Yadhaniwa kwamba walitoza fedha kwa huduma hiyo ijapokuwa haikuruhusiwakufanya hivi; pengine walikuwa wadhamini kwa mali ya wajane, na kutumianafasi hiyo kwa kula fedha zao. Huenda waliwashurutisha watu dhaifu kamawajane kutoa vipawa vikubwa, wakinyonya rehema zao. Hasa walikuwawanafiki, walivaa nguo za dini na kujifanya kuwa wacha Mungu lakini sivyowalivyo. Yesu alisema kwamba hukumu yao itakuwa kubwa zaidi, maanawalitazamiwa kuwa wema. Hayo yote ni maonyo kwa wanafunziwatakaowaongoza waumini baadaye. Tusifikiri kwamba waandishi wotewalikuwa wabaya, la sio, ila kwa jumla ndiyo hali yao (Mk.12:28-34).

Page 170: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

MASWALI1. Kwa nini Yesu aliulizwa juu ya mamlaka yake? Ni mambo gani

yaliyosabibisha swali hili?2. Katika Mfano wa Shamba la Mizabibu Yesu alidai kuwa nani? Na

alitumwa kwa shabaha gani? Matokeo ya kuja kwake yatakuwa nini?Mwishowe itakuwaje?

3. Kwa nini Yesu aliulizwa swali juu ya kodi? Katika jibu lake alitoamafundisho gani muhimu kuhusu wajibu wa mtu kwa serikali yake nawajibu wake kwa Mungu? Eleza uhusiano kati yao.

4. Kwa nini Yesu aliulizwa swali juu ya ufufuo? Katika jibu lake alitoamafundisho gani muhimu kuhusu jambo la ufufuo?

5. Yesu alipouliza swali juu ya Masihi kuwa Mwana wa Daudi alitakakuonyesha nini hasa?

21:1-4 Sadaka ya mjane maskini (Mk.12.41-44)Yesu alikuwa angalipo katika eneo la hekalu ambapo ‘hazina’ palikuwapo,mahali pa watu kuweka matoleo yao, (Yn.8.20) masanduku 13 yaliyochongwakwa sura ya tarumbeta yalikuwepo. Kila sanduku kwa sadaka fulani.Yesu alikuwa ameketi ndipo akainua macho yake na kuwaona matajiri wakitoasadaka zao katika masunduku ya hazina. Kwa jinsi alivyosema inaonekanawalikuwa wakitoa kwa ukarimu, ila kwa kulingana na mali yao matoleo yaohayakuwa makubwa, walikuwa hawakujitoa kama ilivyowapasa kwa shughuli zaMungu zilizofanyika pale. Ndipo alimwona mjane mmoja, maskini, yeye aliwekafedha kidogo sana katika sanduku, ila toleo lake lilikuwa kubwa kulingana namali aliyokuwa nayo, yeye alikuwa amejitoa kabisa kwa kazi za Mungu(Lk.2:36-38).k.3-4 Kisha Yesu alitoa mawazo yake kuhusa utoaji wa hao watu mbalimbali.Alisema kwamba huyo mjane, ijapo ameweka kidogo sana, hata hivyo ametoakuliko jumla yote ya hao matajiri wote walioweka fedha nyingi. Sababu yake nikwamba hao, baada ya kutoa walibaki na fedha nyingi, huyo mjane hakubaki nachochote, kwa kuwa alikuwa ametoa vyote alivyokuwa navyo. Pamoja na hayo,ilikuwa vigumu kwa wajane kuishi vizuri katika mazingira ya wakati ule, maranyingi walishindwa kupata fedha ya kutosha kwa riziki zao, ila, kwa sababualimpenda Mungu kwa moyo, alikuwa tayari kumtegemea kwa riziki zake.Huenda Luka aliweka habari hiyo hapo akitaka kuonyesha tofauti kubwa sanakati ya huyo mjane na waandishi waliotajwa mwisho wa sura ya 20 ambao kwachoyo ya mali walilenga wajane na kuny’onya huruma zao.

21: 5-24 Matabiri juu ya maagamizo ya Yerusalemu na hekaluk.5 Watu kadha walikuwa wakiongea juu ya uzuri wa hekalu ambao ulitokanana sadaka za watu. Hasa walivutwa walipotazama mawe yake makubwayaliyochongwa vizuri. Ni kama kudai kwamba bila shaka Mungu amependezwana taifa lake teule na yote yanayofanyika hekaluni. Lakini Yesu hakuvutwa nauzuri wa jengo hilo, lililohesabiwa ajabu mojawapo katika ulimwengu wa siku

Page 171: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 461

zile. Yeye aliweza kuona mbele na kujua mwisho wake utakuwa mbaya,utaangamizwa, hata jiwe moja halitasalia juu ya lingine. Kwani litapatwa nahukumu hiyo? Yeye alikuja Yerusalemu na kwa hekalu ili atakase ibada namaisha ya taifa teule, kusudi Mungu aweza kuwapenda watu wake tena. Watuwengine hufuata dini kwa desturi na mazoea ya kufanya mambo kadha nabadala yake wengine wafanye kwa moyo wa kumpenda Mungu na kuzitimizaamri zake kwa furaha. Lakini imekuwa dhahiri kwamba viongozi hawakutakakuirekebisha mienendo yao, wangali walitaka kuyashikilia mambo ya nje bilakuyajali mambo ya ndani. Kwa sababu hiyo Yesu hawezi kukubali hekaluliendelee kuwepo. Hivi karibuni wao watamwangamiza Yeye, ila jambo hilo sineno la mwisho, Mungu ataliangamiza jengo lao na mji wao utatekwa nakuangamizwa, ila si sasa, watapewa nafasi ya kumwamini, baada ya KufufukaKwake. Lakini hali yao ya kutokumwamini iliendelea, ni baadhi tu waliomwaminibaada ya Kufufuka Kwake. Hao walijiunga na Kanisa (Ling. Yn.2:19,21). Kablaya Kuja kwa Ufalme wa Mungu na Mwana wa Adamu kurudi, Mungu atamwagahasira yake katika hukumu.Tukilinganisha na Mathayo 24.1-3 na Marko 13.1-4 twaona ni wanafunziwaliomwuliza habari ya wakati wa mambo hayo kutokea. Waliunganishamambo mawili, maangamizo ya hekalu na mwisho wa ulimwengu, ila Luka hasaamesisitiza neno la maagamizo ya hekalu.

k.7 Wanafunzi walimwuliza Yesu kuhusu ishara zitakazothibitisha ukaribu wamatukio hayo na Yesu alitaja ole zijazo.Katika hayo yafuatayo si rahisi kujua kama ishara na mambo yanayotajwayahusu maangamizo ya hekalu na Yerusalemu, au mwisho wa ulimwengu.Katika Injili za Mathayo na Marko mambo yamechanganyana zaidi kulikoyalivyo katika Luka (Mt.24.1ku. na Mk.13.1ku).

k.8 Katika kutoa habari za ishara Yesu alitoa onyo kwa wanafunzi wake juu yahatari ya kudanganyika kwa sababu watatokea watu kadha watakaodai kuwaMasihi, pia watadai kwamba wakati wa ukombozi wa taifa lao umekaribia. Kwajinsi walivyozidi kukandamizwa na Warumi Wayahudi walizidi kutamani sanahuyo Masihi atokee. Hata tukitazama Mdo.1.6 wanafunzi wenyewe walikuwa namawazo kama hayo, ndipo baada ya kumpata Roho Mtakatifu walielewamambo kwa tofauti. Masihi wa uongo wataamsha fitina ya kupindua serikalilakini Wakristo wasivutwe kujiunga nao katika mambo kama hayo.

k.9-11 Yesu alitaja kwamba vita na fitina itatokea, na ndivyo ilivyotokea, mpakaWarumi walipokuja na kufanya vita kuu juu ya Yerusalemu kuanzia B.K.66 hadiB.K.70. Wasitishwe na mambo hayo kwa sababu huo mwisho ni bado. Hata njeya Yudea, katika WaMataifa, vita na mapigano yatatokea. Pamoja na misibambalimbali, kama njaa na tauni, hata yatatokea mabadiliko katika sayari pia.Mambo kama hayo yatazidi, hata hivyo, hayo yote si ishara za mwisho.

Page 172: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.12-19 Hata kabla ya misiba na vita n.k. jambo moja kimsingi litatokea. Yesualitaja wanafunzi kupatwa na mateso na kukataliwa na watu. Katika nchi yaowenyewe, na kwa watu wao, watakamatwa na kuudhiwa, baadhi watapelekwambele ya viongozi wa masinagogi na kuhukumiwa adhabu, hata adhabu ya kifo.(Pamoja na kuwa mahali pa ibada na mafundisho, shughuli za uhakimuzilifanyika sinagogini na mengi yaliyohusu maisha ya watu walioishi vijijini namijini kushindwa). Watasalitiwa na jamaa na marafiki, wala si hivyo tu,watateswa na WaMataifa. Katika Matendo ya Mitume twaona kwamba hayoyote yalitokea (Mdo.4: 5.17ku.40; 6.8ku. 12:1-2, 15:1ku. 16:1ku. 27:1ku).Watateswa kwa sababu ni wafuasi wa Kristo. Ila si hasara kabisa kwa sababuwatapata nafasi ya kutoa ushuhuda. Watakapojitetea mbele za wakuu hawanahaja ya kusumbukia waseme nini, maana kwa msaada wa Roho watapewa lakusema, hata wapinzani wao watashangaa na kushindwa na hekima na uwezowao (Mdo.4.13; 7.2-53). Neno hilo halihusu habari ya kuandaa mahubiri,twapaswa kuandaa vizuri mahubiri yetu. Katika kutoa ushuhuda waowatatangaza matendo makuu aliyofanya Mungu kwa njia ya Yesu maishanimwao.

Inaposema watachukiwa na watu wote haina maana kwamba kila mtuatawachukia, ila katika kila mahali na kila wakati wasitegemee kwamba wataishikwa usalama. Wanapoteswa wanafunzi waweza kutazamia kwamba Munguatawalinda katika hatari (Mdo.4:21,29; 9:23-25; 12:6ku). Maneno ‘hautapoteahata unywele mmoja wa vichwa vyenu’ yanaonekana kama yanapinga hayoyaliyotangulia kuhusu wengine kuuawa kwa ajili ya Kristo. Huenda maana yakeni kwamba Mungu hutawala mambo hayo yote na ya kuwa hawatapatwa namadhara bila Mungu kukubali. Potelea mbali yatokee nini, wawe na hakikakwamba Mungu yu juu ya yote. Wengine wataishi, wengine watateswa,wengine watauawa, ila kwa vyo vyote Kanisa zima halitashindwa, wauminiwataendelea kuwepo. Kila Mkristo huhitaji subira na kuvumilia hadi mwisho bilakukata tamaa, kwa sababu katika ulimwengu huu ni vigumu kuishi maisha yaKiKristo kwa uaminifu bila kupingwa.

Halafu Luka aliendelea kuutaja mwisho wa Yerusalemu. Alirudi kwa k.11 namambo yaliyotajwa katika k.9-11 na kuonyesha kwamba yataendelea na kuzidihata baada ya mwisho wa Yerusalemu. Hukumu juu ya Yerusalemu ni hatuammojawapo tu katika shida na dhiki za ulimwengu na upeo utafika katikahukumu ya Mungu juu ya ulimwengu, ndipo Ufalme wa Mungu utakuja naMwana wa Adamu atarudi.

Yesu alitoa habari ya ishara itakayowajulisha kwamba ‘mwisho’ wa Yerusalemuumefika. Watajua kwa hakika watakapoona Yerusalemu umezungukwa namajeshi ya Dola ya Kirumi. Si wakati wa kufikiri kwamba Masihi atatokea, kamawaliyodhani wenyeji wake, wakitazamia kwamba Masihi atatokea nakuwaokoa. La, sivyo. Ni wakati wa uharibifu wake. Wengi watauawa kwaupanga, na wengi watatekwa na kuchukuliwa mpaka nchi zingine. Watu

Page 173: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 463

watapata shida sana, hawataweza kwenda nje kulima, watakosa chakula naitakuwa dhiki kubwa kwa akina wenye mimba na watoto wachanga, hata Yesualisikia kuwahurumia. Wale walio nje wasithubutu kuingia ndani. Zamani watuwa mashambani walipoona vita, walizoea kukimbilia miji yenye boma ili wawesalama, lakini hawatakuwa salama ndani ya Yerusalemu.

Wakati huo yawapasa wafuasi wake wakimbie. Yesu alitoa mwongozo kwawaumini, mara watakapoona majeshi yameanza kuzunguka mji, wakimbiliemilimani, ng’ambo ya Yordani. Yasemekana kwamba Wakristo walifanya hivyo,walitii neno la Yesu, wakaenda mpaka mji ulioitwa Pella katika eneo laDekapoli, ng’ambo ya Mto. Yordani.

Yusufu, Mwandishi wa historia ya Kiyahudi, hakuwa Mkristo. Alipoandika habarihizo alisema kwamba watu 97,000 walitekwa na watu wengi sana waliuawa.Yafikiriwa alitia chumvi hesabu hizo, hata hivyo, ni dalili ya wengi mnokudhuriwa sana. Maneno ‘mapatilizo’ na ‘yatimizwe yote yaliyoandikwa’huonyesha kwamba mambo hayo si bahati nasibu, bali ni hukumu ya Mungujuu ya taifa la Israeli, kwa sababu ya kumkataa Yesu, ndipo baadaye,waliendelea kuwatesa wafuasi wake. Ni wachache tu, mmoja mmoja,waliompokea Yesu, si taifa kwa jumla.

Maneno ‘hata majira ya Mataifa yatakapotimia’ yana maana gani? Huendamaana yake ni kwamba WaMataifa watatawala nchi kwa muda wote ulioamriwana Mungu. Mungu atawatumia WaMataifa kuyatekeleza makusudi na hukumuzake. Katika muda huo Injili itahubiriwa na watu watapewa nafasi ya kumwaminiKristo, nafasi ambayo Wayahudi walikuwa wameisukumia mbali. MbeleniWaMataifa pia watapatikana na hukumu ya Mungu.

21: 25-28 Matabiri juu ya Mwisho wa ulimwengu (Mt.24.29-31; Mk.13.24-27)Baada ya kuzungumzia ‘mwisho wa Yerusalemu’ ambao ulikuwa karibu kabisa‘watakapoyaona’ majeshi ya Kirumi, ndipo Yesu aliutaja ‘mwisho waulimwengu’ utakapokuwa karibu kabisa ‘watakapomwona’ Mwana wa Adamuakija kwa nguvu na utukufu mwingi. Ishara zitatokea katika maumbile ya asili,pengine lugha hiyo inatumiwa kueleza shida na ghasia zitakazotokea katikanchi mbalimbali na kati ya WaMataifa au pengine ni kuonyesha kwambamabadiliko makubwa yatakayotokea kwa ghafula katika hali ya maisha ya watu(Isa.34.4). (Zamani watu waliwaza bahari kuwa ishara ya machafuko kati yawatu Zab.46:3). Watu watakapopatikana na mabadilliko hayo makubwawatatishwa sana, wakiwaza sana ni nini inayoupata ulimwengu.

Lakini Wakristo hawana haja ya kuogopa, ni watu wa kuviinua vichwa vyao nakufurahi, kwa sababu, hivi karibuni watapata matimizo ya wokovu wao, shidazao zote zitakwisha, nao watakwenda kuishi na Kristo kwa milele. Watajua ni‘mwisho’ watakapomwona’ Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu.Wakitegemea neno hilo hawatadanganywa na watu wasemao tofauti na kudai

Page 174: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

kwamba Kristo atatokea hapa au pale, katika siku fulani na mambo kama hayo(Ling.Dan.7:13).

(Baadhi ya wataalamu hufikiri kwamba k.25-28 yasema juu ya Kuanguka kwaYerusalemu, ila si rahisi kukubali wazo hilo)

21: 29-38 Haja ya kukesha (Mt.24.32-35; Mk.13.28-31)Yesu alimaliza sehemu hiyo yote juu ya mwisho wa Yerusalemu na mwisho waulimwengu kwa kutoa tahadhari kwa wanafunzi.k.29-33 Alitoa mfano wa mtini na miti mingine ambayo inapochipua huashiriakukaribia kwa majira ya kutazamia mavuno. Vivyo hivyo, watakapoona mamboyaliyotajwa katika k.28 wajue kwa hakika kwamba, Ufalme wa Munguumekaribia kutimizwa. Ishara ni dalili ya kuwatumainisha kwamba Munguatachukua hatua zile za kuuondoa uovu wote na kumhukumu yule mwovu nawatumishi wake na kuleta utawala wake juu ya mambo yote. Kwa hiyo, dhiki,shida, misiba na misukosukuo katika ulimwengu si sababu ya kutishwa bali nisababu ya kufurahi na kujua kwamba Mungu anatekeleza makusudi yakemema juu ya uumbaji wake wote.

k.32 Kifungu hicho kinatatanisha, ni nini maana yake? ‘kizazi hiki’ ni kipi? Na‘haya yote’ ni mambo gani? Je! Yahusu kizazi cha wale waliokuwepo Yesualiposema maneno hayo, na kama ni hivyo, ‘haya yote’ ni yale mamboyaliyotajwa kuhusu Anguko la Yerusalemu. Pengine jambo hilo linafanana naunabii wa zamani. Manabii walitabiri mambo yaliyohusu wakati wao na maranyingine yalihusu wakati wa baadaye pia, ni kama kusema yalikuwa namatimizo mawili, ya wakati wa karibu na wakati wa baadaye. Lakini, wenginewatauliza, kwa nini Luka ameweka neno hilo hapa wakati Yesu alipokuwaakizungumzia mambo ya mwisho wa ulimwengu na Kurudi Kwake? Kwa hiyobaadhi ya watu hufikiri kwamba ‘kizazi hiki’ ni kile kitakachoziona zile isharazinazotangulia wakati wa karibu Kurudi Kwake Yesu. Twaweza kusemakwamba mambo hayo yote huwiana kwa sababu yahusu hukumu za Munguhaidhuru hukumu hizo zitatokea kwa wakati tofauti.k.33 Hapo Yesu aliwathibitishia uimara wa Neno lake, ni Neno litokalo Nafsinimwake, yaani kwa Mwana wa Mungu, mwenye usawa na Mungu Baba naMungu Roho. Ni Neno la kutegemewa kabisa, la kweli, lifaalo kuwaongoza watukatika imani na mwenendo wa kila siku. Lina hali ya umilele, vitu vingine vitapitaila Neno linadumu.

k.34-36 Katika mwanga wa mafundisho hayo juu ya uhakika wa Kurudi Kwake,Yesu aliwatahadharisha wafuasi wake juu ya maisha yao ya kila siku. Mudaunaendelea kupita, hata hivyo, siku moja Yesu atarudi, kwa ghafula, bilakutazamiwa. Hakusema mara, bali ghafula, iko tofauti kati ya maneno hayomawili. Waweza kuwa na mitazamo miwili kwa maisha yao. Waishi kamawapendavyo, wakifanya hivyo watakuwa kama vipofu. Afadhali wasivutwe namazingira na tabia za watu wengine, ambao kawaida yao ni kula na kunywa

Page 175: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 465

kupita kiasi na kuwa na masumbufu mengi. Kuja Kwake ni mfano wa mtegoambao hufyatuka ghafula, ni mtego utakaowanasa wanadamu wote wa kilamahali na kila hali. Mtazamo unaowapasa ni kukesha na kuomba, wawe tayarikila siku, ndipo itakapofika watakuwa salama, kisha watamwona na kuishimbele za Mwana wa Adamu. Huku wale ambao hawakujali, wala kujiandaatayari, watahukumiwa, hawataishi mbele za Bwana.

k.37-38 Yesu aliendelea kufika hekaluni kila asubuhi na kuwafundisha watu,ndipo jioni akatoka mjini kwenda kulala kwenye mlima wa Mizeituni. Wageniwaliokuwepo kwa ajili ya Sikukuu walikuwa wengi na ilikuwa vigumu kupatamalazi. Marko alisema kwamba alikwenda Bethania, kijiji cha maili mbili nje yaYerusalemu (Mk.11.11). Waliokuja kumsikiliza walikuwa wengi, wakiamkamapema na kufika hekaluni wakiwa na hamu sana kuyasikia mafundisho yake.Bila shaka walifikiri kwamba, muda si muda, Yesu atafanya jambo kubwa lakuushika utawala na kuusimamisha Ufalme wake pale pale wakati ule. LakiniYeye alielewa hali zao zitabadilika na mwishowe, badala ya kumchagua Yeye,watamchagua Baraba, ndipo Yeye atasulibiwa. Mpaka hapo mambo hayoyamefichwa watu wasiweze kuyatambua.

22: 1-6 Usaliti wa Yuda (Mt.26.1-5; Mk.14.lku.10ku. Yn.11.45-53)k.1 Hapo Luka ametaja kwamba wakati ulikuwa karibu na Sikukuu ya mikateisiyotiwa chache, iliyoitwa Sikukuu ya Pasaka. Zamani Sikukuu hizi zilikuwatofauti ila baadaye ziliwekwa pamoja (Hes.28.16ku). Watu waliuondoa chachuyote iliyokuwamo nyumbani kabla ya kuila Pasaka. Chachu ilikuwa dalili yauovu. Wayahudi walihesabu siku kuanza wakati wa jua kuchwa, kwa hiyo,Pasaka ilianza jioni tarehe 14 Nisan na Siku za mikate isiyotiwa chachuziliaanza 15 hadi 21 Nisan.

k.2 Tumeishaona kwamba wakuu wamekata shauri la kumwondoa Yesu wakatiwowote watakapopata nafasi (19.47; 20.19ku). Wamelenga wakati wa Pasakawalijua Yesu atafika Yerusalemu wakati huo. Kwa kawaida aliishi na kufanyahuduma yake katika eneo la Galilaya na kufika Yerusalema wakati wa Sikukuumbalimbali. Ila walitatizwa na jambo moja. Mpaka wakati huo watu wengiwalikuwa upande wa Yesu wakienda kumsikiliza. Watawezaje kumkamata bilafujo kutokea? Walijua kwamba fujo ikitokea Warumi watakuja na kuwaondoakwenye vyeo vyao. Iwapo Mafarisayo walimpinga Yesu tunaona kwamba niwakuu wa makuhani na waandishi waliochukua hatua juu yake, maana waowalitawala mambo yaliyotokea Yerusalemu na hasa kuhusu hekalu, kwa hiyo,hao ndio viongozi katika mipango ya kumkamata Yesu.

k.3-6 Ndipo, bila kutazamiwa, msaada ulitokea uliorahisisha na kuwasaidiakatika mipango yao ya kumkamata Yesu. Mmojawapo wa wanafunzi aliamuakumtia Yesu mikononi mwao. Walijua kwamba kwa msaada wake watawezakumshika bila fujo, maana ataelewa mahali alipo, wakati wa usiku, wakati wawatu kuwa wamelala. Huyo aliyemtia mikono mwao ni Yuda Iskariote. Yeye

Page 176: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

aliyejitokeza kwa wakuu na kuzungumza nao na kupatana nao kiasi cha fedhawatakachompa kwa msaada wake, walifurahi sana.

Ila nyuma ya mipango ya Yuda ni Shetani, maana yeye ndiye mpinzani mkuuwa Yesu. Tangu Yesu alipozaliwa alikuwa amejaribu kumwondoa. Kwa njia yaHerode wakati alipokuwa angali mdogo; tena wakati wa majaribu yakejangwani; wakati mwingine baada ya kuhubiri katika sinagogi la Nazareti,wenyeji walichukizwa na hotuba yake walitaka kumtupa chini. Yesu alimchaguaYuda ili awe mwanafunzi wake akamweka katika kundi la Mitume.Hakumchagua kwa shabaha ya kumsaliti. Yuda alimkaribisha Shetani nakumruhusu apandikize mawazo ya kumsaliti Bwana wake. Hata hivyo, ni Yudamwenyewe aliyemsaliti Yesu kwa hiari yake mwenyewe.

Ila nyuma ya yote ni Mungu, Yuda kumtia Yesu mikononi mwa adui ni matimizoya mapenzi ya Mungu, bila Yuda kutambua hivyo (Lk.9:44; 22:21-22;Mdo.2:23). Kwa sababu Mungu ametupa sisi wanadamu hiari ya kuchaguamema au mabaya, nafasi imewekwa kwa sisi kufanya mabaya. Ajabu nikwamba Mungu anao uwezo wa kukubali haya mabaya yafanyike, hatakuyatumia, ili makusudi yake ya kuukomboa ulimwengu yatimizwe. Siyokusema kwamba lazima mabaya hayo yafanyike ili mapenzi ya Munguyatimizwe, ila kama hakuna njia nyingine, basi, Mungu hawezi kushindwa namabaya ya wanadamu, wala na upinzani na hila za Shetani, la. Daima Munguhuleta mema kutoka mabaya. Ndivyo ilivyokuwa katika Kusulibiwa kwa Yesu. Sivigumu kwa neno hilo kutabiriwa mapema; hata sisi twaweza kujua itatokea ninipaka akiachwa ndani ya chumba pamoja na panya, nani atabaki asubuhi?Vilevile nuru ikija ulimwengu na kuangaza mahali pa giza, si ajabu gizalitaipinga hiyo nuru, na ndivyo ilivyokuwa Nuru ya Ulimwengu, Bwana Yesualipokuja duniani (Yn.8:12; 3:19ku).

22: 7-23 Karamu ya Mwisho (Mt.26.17-19; Mk.14.12-16; Yn.13.1ku)

k.7-13 Yesu alitamani sana kuila Pasaka hii na wanafunzi wake kwa utulivu nakwa sababu hii alificha habari ya mahali n.k. kusudi watu wasijue mipangoyake. Yeye alitawala mambo hayo.Ilipofika siku ya kuila Pasaka, Yesualiwatuma Petro na Yohana kwa ajili ya maandalizi yake. Bila shaka kwasababu Yesu aliufahamu mpango wa Yuda aliificha mipango yake juu ya mahalipa kuila Pasaka ili Yuda asiwe na habari mapema. Pengine alikuwaameishapanga na mtu fulani wa mjini kupata chumba kwa ajili hiyo. TukumbukeYerusalemu ulijaa wageni na ilikuwa vigumu kupata chumba. La, sivyo, kwaujuzi wake wa kipekee alifahamu mapema habari hizo

Page 177: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 467

.

k.9-13 Waliotumwa walitaka kujua ni wapi watakapoiandaa Pasaka. Yesualiwapa ishara kadha ambazo zitawasaidia. Watakapoingia mjini watakutana namwanamume akichukua mtungi, huyu wamfuate na kuingia nyumba anayoingiayeye. Ndipo waseme maneno fulani kwa mwenye nyumba, ndipo yeyeatawaonyesha chumba kikubwa chenye vifaa kama meza na humo waiandaaPasaka. Walihitaji divai, miche michungu, mkate usiotiwa chachu namwanakondoo.

Ilikuwa si kawaida kwa mwanamume kuchukua mtungi wa maji nainasemekana kwamba kama mwanamume alibeba maji alitumia chupa yangozi. Wengine hufikiri kwamba nyumba ilikuwa ya Mariamu, mama wa Marko.Kutoka Mdo.12.12 twajua kwamba baadaye Wakristo walizoea kukutana pale.Labda ni chumba walichotumia wakati wa kumngojea Roho Mtakatifu, ila hatujuikwa hakika, maana wengine wanafikiri kwamba wakati huo walikuwa katikaukumbi wa Hekalu (Mdo.1.13). ‘Mwalimu akuambie’ huenda mwenye nyumbaalikuwa mfuasi au rafiki wa Yesu ambaye amefahamiana naye kabla ya wakatihuo. Mpaka saa ya mwisho Yuda hakujua mahali ambapo Yesu amepangakuila Pasaka pamoja nao.

Karamu ya mwisho

Page 178: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.14-23 Yesu na wanafunzi waliila Pasaka pamoja (Mt.26.20,23-29;Mk.14.11,14-17, 20-25; Yn.13.21-30)k.14-16 Maandalio yote yalikuwa tayari na saa ilifika kwa Yesu kuketi chakulanipamoja na wanafunzi wake. Aliwaambia kwamba alikuwa ametazamia kwahamu kuila Pasaka pamoja nao kabla ya kuteswa kwake. Yeye aliyajua yoteyaliyo mbele yake, na kama yasingalikuwa mapenzi ya Mungu angaliwezakuwa mbali na Yerusalemu. Alitaka kushiriki nao chakula hicho cha maanasana na kukipa maana mpya, maana ambayo inatokana na Kifo chake kwa ajiliya kuwaokoa watu na dhambi zao. Ukombozi wake ni wa kiroho sio wa kimwiliau siasa. Wayahudi katika Sikukuu hiyo waliadhimisha kutolewa kwaoutumwani mwa Misri, kwa mkono hodari wa Mungu. Yesu alifahamu kwambamwisho wa mpango wa zamani wa Agano la Kale umefika na sasa ni mwanzowa mpango mpya, wa Agano Jipya, na kwa sababu hiyo alitaja Ufalme waMungu. Ni wakati wa dahari mpya, wakati wa kusimamishwa kwa Ufalme waMungu mioyoni mwa wanadamu.

k.17-19 Ilikuwa desturi katika karamu hiyo ya Pasaka kutoa baraka na kuomba,ndipo watu walikinywea kikombe cha kwanza cha divai pamoja na sahani yamimea ya viungo na mchuzi. Ndipo watu walihadithiwa habari ya Pasaka yakwanza. Waliimba Zab.113, halafu walikinywea kikombe cha pili cha divai.Baada ya ombi la shukrani walikula mlo mkubwa wa nyama ya kondooiliyokokwa pamoja na mkate usiotiwa chachu na mimea michungu. Baada yamaombi, walikinywea kikombe cha tatu cha divai na Zab.114-118 ziliimbwa.Ndipo kikombe cha nne cha divai kilifuata. Hivyo walikunywa divai mara nne. Sirahisi kujua ni mara ipi katika hizo mara nne ambayo Yesu alisema maneno juuya damu yake alipochukua kikombe cha divai. Haikuwa kawaida kushirikikikombe kimoja. Kutaja Agano Jipya ni ukumbusho wa unabii wa Yeremia(Yer.31-34) kuhusu msamaha wa dhambi na maisha mapya. Agano la Kalelilitiwa muhuri na damu (Kut.24:8).

Yesu alitaja tena Ufalme wa Mungu akisema kwamba hatakunywa tena divaimpaka Ufalme wa Mungu utakapokuja. Si rahisi kufahamu maana yake. Ni wazikwamba alifahamu hali mpya inaanza, na ni wakati wa kupita kwa mipango yakale. Wakati wa Pasaka watu walitazama nyuma na kukumbuka jinsi mababazao walivyotolewa utumwani Misri. Yesu alitazama mbele kwa jinsi watuwatakavyotolewa katika utumwa wa dhambi na kuja kwa Ufalme wa Mungu.

k.19 Mpaka hapa mambo yalifuata kawaida ya Kiyahudi. Halafu Yesualipochukua mkate na kuumega na kuwapa alisema maneno yaliyotia maanampya kwa karamu hiyo. ‘Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu’.Alikuwa angali na mwili wake, kwa hiyo mkate si mwili wake hasa. Tukumbukekwamba alisema ‘Mimi ni mlango’ ‘Mimi ni Mzabibu wa kweli’ n.k. hakuwa vituhivi hasa, ila vilimwashiria kuwa kama vitu hivi. Vivyo hivyo, mkate ni ishara yamwili wake unaotolewa na kuvunjwa msalabani, na kwa sababu hiyo, na kwanjia hiyo, uzima wa milele hupatikana. Aliwaagiza wafanye hivi kwa ukumbusho

Page 179: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 469

wake. Kwa hiyo, alitaka Wakristo wamkumbuke hasa kwa vile alivyotoa nafsiyake kuwa fidia ya dhambi. Twaona uthabiti wa Yesu, alikuwa na uhakika juuya yote yaliyokuwa yakitokea. Alijua kwamba kwa kifo chake ulimwenguunakombolewa na wanadamu wanapata ondoleo la dhambi na uzima wamilele.

k.20 Ndipo alikichukua kikombe na kuwapa akisema maneno yaliyotia maanampya. Damu yake inamwagika kwa ajili yao. Katika yote yanayotokea mpangowa Mungu wa kuuokoa ulimwengu unafanyika. Yesu hafi kwa sababu ya chukiza wakuu tu, wala hafi kwa sababu ya hila ya Yuda tu, wala hafi kwa kigeugeucha watu, wala hafi kwa upinzani wa Shetani, adui wake mkuu; la, hata kidogo.Mara nyingi Shetani alijaribu kumwondoa Yesu katika shabaha yake ya kwendamsalabani na hata alipokuwa msalabani alimjaribu kwa jaribu kali sana yakushuka msalabani hali akijua kwamba Yesu akifa kwa wenye dhambi yeyeamepata mshindi wake na wanadamu wameupata wokovu wa roho zao. Haponyuma alitaka awahi kufa, lakini hakutaka afe msalabani kwa ajili ya kufidiadhambi. Hao wote waliompinga walikuwa na sehemu yao katika mamboyanayofanyika, na kila mtu au kundi la watu walifanya kwa hiari yao wenyewe,ila wasingaliweza kufanya lo lote bila kibali cha Mungu. Mungu aliwaruhusuwafanye hayo waliyotaka, huku Yeye aliyachukua mabaya yao yote na ‘kufumasweta’ la wokovu. Yesu aliamini kabisa kwamba, baada ya Kufa Kwake, Kanisalitainuka, wanafunzi watapewa nguvu ya Roho Mtakatifu, nao watafanywa kuwajamii mpya ya watu wa Mungu. Katika karamu ya Ushirika Mtakatifu/KuumegaMkate/Eukaristi (waumini huiita karamu hiyo kwa majina mbalimbali) wafuasiwake hukumbuka dhabihu aliyotoa Msalabani kwa ajili yao, iliyoashiriwa katikatendo la kuuchukua mkate na kuinywa divai. Kwa njia hiyo baraka zote zamateso yako yaletwa kwa wakati wa sasa katika maisha ya waumini.‘inayomwagika’ haina maana kwamba damu ya Yesu ilitiririka sana ila nimaneno ya kueleza kifo chake cha ukatili (Mwa.9:6; Eze.18:10' Isa.59:7).

k.21-22 Kisha Yesu alitamka kwamba yumo miongoni mwao yuleatakayemsaliti. Alisema neno hilo kwa wazi mbele yao. Huyo msalitiamekuwemo katika shirika la wale waliofuatana na Yesu kwa muda wa miakamitatu hivi. Ajabu ni kwamba, walipoambiwa hivyo, hawakujua ni nanialiyetajwa, wala hawakumnyoshea mikono Yuda kana kwamba wamehisi niyeye, ni kama hawakuwa na mashaka juu yake. Yuda alikuwa amejificha kweli,hakuna aliyetambua hila yake. Katika k.22 Yesu alitaja mambo mawili muhimu.Jambo la kwanza ni kwamba katika kwenda kuuawa Yeye anayatimiza mapenziya Mungu na jambo la pili ni kwamba Yuda anayemtia mikononi mwa adui,anafanya kwa hiari yake mwenyewe, na kwa sababu hiyo ana hatia juu yajambo hilo. Hakufanya katika hali ya kufikiri kwamba anafanya mapenzi yaMungu. Tendo hilo baya la kumsaliti Yesu halimpatii udhuru wa kudai kwambaamesaidia utekelezaji wa mapenzi ya Mungu. Yeye aliwajibika kwa tendo hilona Yesu aliweka neno hilo wazi. Wala tusiwaze kwamba kama asingalifanyawakuu wangalishindwa kumpata Yesu, hao wangaliendelea kupanga njia

Page 180: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

nyingine ya kumkamata Yesu, Yuda alirahisisha njia tu. Yesu aliposema ‘olewake’ hakusema katika hali ya kumlipiza kisasi, la, hasa maneno hayo yalikuwamchanganyiko wa huzuni na sikitiko, kwa kuwa mpaka dakika ya mwisho Yesualijaribu kumshawishi auache mpango wake. Wafanyao waovu wanayo hatiakwa maovu yao, potelea mbali, ikiwa Mungu akiyatumia na kuyageuza kuwamema, kama Alivyofanya katika Kifo cha Yesu (Mdo.2.22-23).

22: 24-30 Ukuu wa kweli (Mt.26.31-35; Mk.14.27-31; Yn.13.16-18)k.24 Mashindano yaliyotokea kati ya wanafunzi. Walitambua kwamba mamboyameiva nao wakadhani kwamba Yesu atausimamisha Ufalme wake paleYerusalemu nao watakuwa pamoja naye akiwapa vyeo mbalimbali. Kwa hiyowalitaka kujua ni nani ambaye atahesabiwa wa kwanza kati yao. Haikuwa maraya kwanza wajadili neno hilo (Mt.18.1-5; 20.24-28; Mk.9.33-37; 10.41-45;Lk.9.46-48) ila ni ajabu kuona kwamba walikuwa na mashindano hayo wakatihuo wa Yesu kukaribia kifo chake.

k.25 Hata hivyo, Yesu hakukata tamaa juu yao wala kuwakemea. Aliwavumiliana kuwafundisha kwamba itakuwepo tofauti kubwa kati yao na jinsi watuwafanyavyo katika uongozi na utawala wa hapa duniani. Katika dunia hii wenyemamlaka na vyeo hupenda kutumikiwa si kutumika, huufurahia ukubwa waokwa kuwatumikisha walio chini yao. Pia hupenda kujiona kuwa wanafanya vizurina wenye kufadhili raia wao.k.26 Haitakuwa hivyo kati yao. Mkubwa awe kama mdogo, asijione, asijiinue juuya wenzake, asipende kutumikiwa, bali awe wa kwanza kutumika. Ukubwa nauongozi utakuwepo kwa namna fulani, ila si kwa namna ya dunia hiyo.(Tukumbuke Yesu alisisitiza jambo hilo alipotoa kielelezo cha utumishialipowatawadha miguu Yn.13). Pengine majadiliano yalianza wakati hakunammoja wao aliye tayari kufanya kazi ya chini ya kuwatawadha miguu baada yasafari na pengine walijadili ni nani atakayekaa karibu na Yesu mezani.

k.27 Ndipo Yesu alitoa mfano wa mtu aketiye chakulani na mtumishi amletayechakula. Alisema wazi kwamba Yeye ndiye mkubwa, mwenye kuketi chakulani,hata hivyo, amekuwa tayari kutumika si kutumikiwa, kuleta chakula si kuletewa.Wale wanaomtumikia Kristo kwa uaminifu katika mambo madogomadogo ndiowale wenye ukuu wa kweli.

k.28 Kisha Yesu alikiri uaminifu wao, wamekuwa naye, wakienda huko na hukokatika vijiji na vijiji ya Galilaya, wakivumilia shida mbalimbali kama kukosachakula na malazi mara kwa mara. Yesu alikuwa amefarijika kwa ushirikianowao.

k.29 Iwapo watatumika, hali wakiwa viongozi walio na mamlaka yake yakuhubiri Injili, hata hivyo hawatakosa heshima. Watashiriki ufalme wa Mungu,kama Yesu alivyoushiriki na Baba yake. Watashiriki katika karamu ya Ufalmewa Mungu na kupewa kazi na mamlaka ya kuongoza mambo.Wamekuwa

Page 181: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 471

pamoja naye hapo duniani, na baadaye, watakuwa pamoja naye Ufalme waMungu utakapotimia. Kujinyenyekeza si jambo la mwisho, kufuatwa na jambo lakutukuzwa na Mungu mpaka juu sana. Kama ilivyokuwa kwa Yesu, ndivyoitakavyokuwa kwa wale waliojiunga naye. Yesu alisema kwamba watahukumu‘kabila kumi na mbili za Israeli’. Alikuwa amechagua Mitume kumi na wawili,nao wameshiriki naye katika kuutangaza ujumbe wake kwa Israeli nzima.Mbeleni ujumbe wake utatangazwa katika ulimwengu. Paulo alisema‘watakatifu (yaani Wakristo) watahukumu ulimwengu’ (1 Kor.6:2). Shabaha yaahadi hizo ni kutia moyo na nguvu wafuasi wa Yesu wanaomtumikia kwaunyenyekevu, kwa sababu wengine hawatawajali, watawaudhi na kuwatesa, ilabaadaye watainuliwa juu. Kwa hiyo, unyenyekevu na kutumika si kinyume chaukubwa bali ni tabia zinazotakiwa katika wale wenye ukubwa na uongozi. Yesualikuwa na uhakika kwamba amepewa mamlaka na Ufalme na Baba yake na yakwamba kwa njia ya Kufa Kwake huo Ufalme utasimamishwa katika ulimwenguhuo.

22: 31-38 Yesu alitabiri mkano wa Petro(Mt.26.33-35; Mk.14.27-31; Yn.13.36-38)

k.31 Ni Luke tu ambaye ametaja jinsi Shetani alivyohusika katika habari hiyo.Yesu alisema wazi kwa Petro akitumia jina lake la asili, ukumbusho wa udhaifuwake, wakati huo hatakuwa mwamba kama Yesu alivyotumaini alipobadili jinalake hapo nyuma. Lakini Yesu hakusema kwamba Shetani anamtaka yeye tu,bali alikusudia kuwaangusha kundi zima la wanafunzi, ila kwa sababu Petroameonekana kama kiongozi wao Shetani alimlenga yeye hasa hali akijuakwamba akimwangusha Petro atafaulu kuwaangusha wengine pia. Hapo Yesualikuwa akidokeza kipindi kigumu kilicho mbele yao, wakati atakapokamatwa nakuuawa. Shetani akifaulu kuwavuruga, basi Kanisa halitatokea wala kusimama.Yampasa ampinge Shetani ili Shetani asifaulu shabaha yake, Yesu alikuwaamemwonbea Petro hasa (si kwamba hakuwaombea wengine pia, ila alijua niPetro aliyehitaji msaada wa pekee). Habari hii inafanana na Ayubu 1 na 2.

k.32 Petro atateleza kwa muda mfupi, ndipo atajirekebisha na Yesuatakapomtokea baada ya Kufufuka Kwake, atarudishwa rasmi katika kundi laMitume na kusimama imara na kuwa msaada mkubwa kwa wenzake. Imaniyake haitatoweka kabisa, na makusudi ya Shetani yatazuiliwa.k.33 Hata hivyo Petro hakuutambua udhaifu wake, alifikiri kwamba atakuwamwaminifu hata kupita wenzake. Alikiri kwamba yu tayari kufungwa hatakuuawa kwa ajili yake,

k.34 Kisha Yesu akamfunulia jinsi atakavyojaribiwa na kuanguka. Tena siwakati wa mbali, bali usiku wa leo, kabla ya jogoo kuwika atakana kabisakwamba anamjua Yesu, tena si mara moja tu bali mara tatu. Hapo twaona ujuziwa kipekee wa Yesu, tena twaona uaminifu wa waandishi wa Injili ambaowaliweka habari za kuanguka kwa Petro ambaye baadaye alikuwa kiongozi

Page 182: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

miongoni mwa Mitume. Mshtuko wa jambo la Petro kumkana Yesu ulipunguzwakwa sababu Yesu aliwaambia mapema. Habari hii ni onyo kwetu sisi sote (1Kor.10:12).

k.35-38 Yesu aliwatazamisha nyuma na kuwauliza ikiwa walipungukiwa nachochote alipowatuma kuhubiri na kupona watu, wakati walipokwenda bilafedha na vifaa (9.1-6). Wakamjibu ‘La’. Lakini hali ya saa ni tofauti. Wakati ulehuko Galilaya watu walifuatana na Yesu kila mahali, wakimfurahia nakumsikiliza. Lakini sasa Yesu yuko Yerusalemu, kati ya watu wasiomtakaambao watamkataa na kumwua. Wao vilevile hawatapendwa na wingi wa watu,watakataliwa na kuteswa. Watapata shida nao watahitaji kuwa na fedha navifaa mbalimbali ili wazikinge shida hizo.

k.36b Kifungu hicho chatatanisha sana. Yesu aliwashauri kwamba wajipatieupanga. Neno la ajabu, kwa sababu Yeye mwenyewe amesisitiza kwambaUfalme wake si wa hapa duniani, wala hautasimamishwa kwa vita ya kimwili.Punde kidogo, Petro alipoutumia upanga wakati Yesu alipokamatwa, Yesuakamwambie asiutumie, akamponya yule aliyekatwa sikio. Yesu alikuwa namaana gani aliposema maneno hayo? Je! Alikuwa akisema ‘upanga’ au alikuwaakiwatahadharisha juu ya shida kubwa na ya kwamba watahitaji ujasiri mkuu?Lazima wajiandae katika mawazo yao tayari kupambana na dhiki na shida, siwajivike upanga.

k.37 Ndipo akataja yaliyo mbele yake - kule kuuawa kati ya wahalifu nakuhesabiwa mhalifu wa hali ya juu (hapo amedokezea unabii wa Isaya 53).Yesu alijua hakika kwamba mwisho wake ni kufa Msalabani, tena kifo chake nicha ukombozi, atakuwa fidia ya dhambi, ili wanadamu wapate msamaha nauzima wa milele. Hayo yote yameandikwa katika Maandiko, hayana budikutumizwa.

k.38 Walikuwa na panga mbili, huenda wamejiandaa tayari kumpigania Yesuwakidhani kwamba Ufalme wake utasimamishwa wakati huo. Katika mawazoyao huo Ufalme ni wa hapa duniani, wa siasa, si wa kiroho. Yesu alipoona yakuwa wamekosa kumwelewa na shabaha yake katika kutaja upangaakayakatisha mazungumzo.

22: 39-46 Yesu aliomba katika bustani ya Gethsemane(Mt.26.36-46; Mk.14:32-34)

k.39 Baada ya kushiriki Chakula cha Pasaka Yesu alitangulia kwenda mpakamlima wa Mizeituni na wanafunzi walimfuata. Alipokuwa Yerusalemu ilikuwadesturi yake kwenda hapa kila jioni. Yuda alifahamu jambo hilo, kwa hiyo alijuamahali pa kumpata Yesu ikiwa Yesu atafanya kama kawaida yake. Luka hatajiBustani ya Gethsemane kama Mathayo na Marko wanavyofanya. Pia

Page 183: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 473

amefupisha habari hiyo. Hasemi juu ya Yesu kwenda mbele ndani ya bustaniakiwachukua Petro, Yohana na Yakobo pamoja naye, ndipo akawaachakwenda ndani zaidi halafu akawarudia mara tatu.

k.40 Alipofika pale aliwashauri wanafunzi waombe ili wawe tayari kukabilimagumu yaliyo mbele yao, wakati atakapokamatwa na kuhukumiwa.

k.41-44 Ndipo Yesu aliomba, akipiga magoti dalili iliyoonyesha dhiki yake. Kwakawaida Wayahudi waliomba hali wamesimama na vichwa kuelekezwa juu.Wakati ulikuwa umefika kwa Yeye kukubali kabisa kuwa dhabihu ya dhambi nakatika kifo chake kuzibeba dhambi za ulimwengu wote na kuhukumiwa naMungu kwa ajili yake. Neno hilo ni zito mno, hasa kwa sababu Yeye hakufanyadhambi, hakujua dhambi, wala hakuwa na dhambi. Katika ubinadamu wakealisita, alitishwa sana na jambo hilo hata akaona vema kumwomba Babaamwondolee kikombe hiki. Kikombe kimejaa mateso na adhabu ya Mungu juuya dhambi. Inaonekana mapenzi yake yaliachana na mapenzi ya Baba, hatahivyo, mara moja akaweka mapenzi yake yakubaliane na mapenzi ya Baba(Zab.11.6; 16.5; Isa.51.17,22; Yer.25.15). Alijitoa kwa hiari yake mwenyewe,bila kushurutishwa, kwenda kuuawa kwa ukombozi wa wenye dhambi, tofautina wanyama waliotolewa dhabihu kwa dhambi, wao walipelekewa tu, bila idhiniyao na bila kutambua wafanyavyo. Tusifikiri kwamba Yesu aliogopa kufa, ilaalitishwa na jambo la kuachwa na Mungu na kufanywa kuwa dhambi (Mk.15.34;2 Kor.5.21). Katika Gethsemane Yesu hakukinywea kikombe bali alikubalikukinywea. Ulikuwa wakati wa vita kuu na alipotoka bustanini alikuwaameupata ushindi, yu tayari kuwakabili kwa ujasiri wale waliokuja kumkamatawakiongozwa na Yuda.k.43-44 Uzito wa vita yake umeonekana kwa jinsi alivyohitaji kutiwa nguvu namalaika ili asife kabla ya kuhukumiwa. Dhiki yake ilikuwa kubwa hata alitoa harikama damu. Mambo hayo huonyesha uzito wa jinsi alivyojisikia rohoni mwake.

k.45-46 Alipomaliza kuomba akawajia wanafunzi na kuwakuta wamelala. Niusiku na bila shaka walikuwa wamechoka, pia walijaa huzuni na kulemewa nahayo yote yaliyokuwa yakitokea. Yesu aliwashauri waombe kwa sababu mbeleyao ni mambo mazito nao walihitaji kuomba. Bila kuomba Shetani atapatanafasi ya kuwashambulia na kuwaangusha.

22: 47-54a Yesu alikamatwa (Mt.26.47-56; Mk.14.43-50; Yn.18.2-11)

k.47 Kwa wanafunzi shida ilikuwa karibu kuliko walivyodhani, kwa kuwa, Yesualipokuwa angali akisema nao, mkutano wa wale waliokuja kumkamatawalionekana, wakikaribia na taa zao za mienge zilikuwa zikiwaka gizani. Yudaalikuwa akiwaongoza kundi la watu, wakuu wa makuhani, maakida ya hekalu,wale waliolinda usalama wa hekalu, na wazee, yaani viongozi wa walei.Yohana ametaja kikosi cha askari, hao walitoka kwa Warumi. Walikuwa nasilaha, panga na marungu. Hayo yote ni dalili ya kuonyesha waliona kazi hiyo

Page 184: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

ya kumkamata Yesu ni muhimu na kwa vyo vyote wasikose kumpata. NdipoYuda, mmoja wa wale Thenashara akajitokeza na kumkaribia Yesu ili ambusu,Marko ametaja kwamba alimbusu. Ilikuwa kawaida kwa wanaume kutumia busukatika kuwasalimiana, na desturi hiyo ilimfaa Yuda katika kumtambulisha Yesuwakati wa usiku. Ilidhaniwa kwamba huenda mapigano yangetokea baina yaYesu na watu wake na wale waliokujwa kumkamata. Yesu alijaribu kumhojiYuda kwa mara ya mwisho akamwuliza ‘Wamsaliti Mwana wa Adamu kwakumbusu?’ na kwa kujiita ‘Mwana wa Adamu’ alikuwa akimkumbusha kwambaYeye ndiye Masihi aliyetoka kwa Mungu, si mtu wa kawaida tu. Ni jambo zitokuona kwamba Yuda aliyeishi katika jamii ya Mitume kwa miaka mitatualimsaliti Yesu kwa kutumia ishara ya upendo.

k.49-50 Wanafunzi walipotambua ni nini yanayotokea waliona njia ifaayo nikujiokoa kwa kupiga vita. Walimwuliza Yesu ikiwa alitaka wampiganie?Walikuwa na panga mbili, Je! Wazitumie? Kabla ya kungojea jibu Petro aliuvutaupanga na kumkata sikio la kuume mtumwa wa Kuhani Mkuu (Yn.18.10).Walionyesha utiifu wao kwa Yesu na ujasiri lakini hayo yote yalikuwa kinyumecha alivyowafundisha.

k.51 Yesu aliwazuia wasiendelee kumpigania, Yeye hakutaka mapigano, akawaradhi kukamatwa, hata alionyesha huruma kwa yule aliyeumia na kumponya.Hakutaka wakuu wapate neno la kumshtaki kuwa kiongozi wa watu wa vitakama mwana mapinduzi. Mbele ya Pilato alisema ‘Ufalme wangu sio waulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishiwangu wangenipigania, nisije nikatiwa ….Lakine ufalme wangu sio wa hapa’.

k.52-53 Ndipo Yesu alisema na wale waliokuja kumkamata. Inaonekanawalishtuka kwa jinsi hakuonyesha wasiwasi akikubali kukamatwa (Yn18.6).Aliwauliza sababu ya kuja wakati wa usiku wakiwa na silaha nyingi kanakwamba Yeye ni mnyang’anyi au mwanamapinduzi. Yeye ni mwalimualiyefundisha kila siku hekaluni, saa za mchana, bila kufanya matata, mbonabasi wamekuja usiku. Hapo nyuma wameshindwa kumpata kwa sababu watuwengi walikuwa upande wake. Kwa unafiki na woga wamekuja usiku ila ni ‘saayao’ wameruhusiwa na Mungu kufanya yale waliyokusudia kuyafanya na katikakufanya hivyo, watayatimiza mapenzi ya Mungu kwa wokovu wa ulimwengu.Kwa kutaja ‘mamlaka ya giza’ huenda Yesu alidokezea sehemu ya Shetanikatika hayo yote, yeye amechochea wivu na chuki katika wakuu kiasi cha waokufanya mipango ya kumwondoa (Kol.1.13; Efe.6.12).

k.54a. Kisha wakamkamata Yesu na wanafunzi wake walikimbia (Mk.14.50).Waliweza kujisalimisha kwa sababu ilikuwa usiku. Pia kwa jinsi Yesualivyojitokeza kwa wakamataji wake alikuwa amewalinda (Yn.18.8,9). Katikamatukio hayo yote Yesu ni mtawala.

Page 185: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 475

22: 54b-62 Petro alimkana Bwana Yesu mara tatu

(Mt.26.57-75; Mk.14.53-72; Yn.18.12-27)k.54b-55 Yesu alipelekwa mpaka nyumba ya Kuhani Mkuu na Petro alimfuatakwa mbali. Katika Yohana 18.15 tuna habari ya mwanafunzi mwingine, Yohanaambaye pia alifuata na ni yeye aliyempatia nafasi Petro aingie katika ualililozungukwa na vyumba mbalimbali. Hapo moto uliwashwa kwa sababu yabaridi na Petro alisogea karibu na kuketi kati yao.

k.56-57 Ndipo mjakazi mmoja mngoja mlango (Yn.18.15) kwa mwanga wamoto alimtambua, akamkazia macho Petro na kuwaambia watu waliokuwatayarai kumsikiliza kwamba huyo Petro alikuwa pamoja na Yesu. Petro akakanakwa kusema hakumjua.

k.58 Baada ya muda mwanamume mmoja alipomwona alimwambia Petro‘Wewe nawe u mmoja wao’. Petro akamjibu kwa kukana ‘Ee mtu, si mimi’.Petro aliogopa nini? maana Yesu alipokamatwa wakuu hawakuwakamatawanafunzi.

k.59-60 Muda ulipita, huenda Petro akadhani kwamba hatari imepita, lakini siyo.Baada ya saa moja kupita ndipo mtu mwingine alisema kwa nguvu kwamba‘Hakika na huyu alikuwa pamoja naye, kwa kuwa yeye pia ni Mgalilaya’. Kwamara ya tatu Petro akakana akasema ‘sijui usemalo’. Lakini Petro akasikiajogoo akiwika, akakumbuka jinsi alivyokuwa amedai kwa nguvu kwamba lichaya kumkana yu tayari kufa pamoja naye (22:33,34) akasikitika mno. Labdaalikumbuka maneno ya Yesu juu ya mtu kumkana (12:29). Je! Yesu atamkanambele za Baba?

k.61-62 Yesu alikuwa mahali alipoweza kumwona Petro. Pengine katikachumba cha orofani, ama alipita kutoka chumba kimoja mpaka kingine. Yesualigeuka na kumtazama Petro, bila shaka alisikitishwa na tendo la Petrokumkana mara tatu, iwapo alikuwa amemwonya, hata hivyo, Petro, tofauti naYuda, alikuwa tayari kutubu kosa lake, akatoka nje, akalia kwa majonzi.Tukilinganisha habari hiyo katika Injili zingine, habari nyingine inapatana nanyingine ni tofauti. Waandishi wote hukubaliana kwamba Petro alimkana maratatu, na mara ya kwanza kwa mjakazi na ya kwamba baada ya mara ya tatujogoo aliwika na Petro akajirudi. Katika Mathayo aliyemwuliza mara ya pilialikuwa mjakazi mwingine, katika Marko mjakazi yule yule, katika Lukamwanamume, na katika Yohana watu kadha. Kuhusu mara ya tatu Mathayo naMarko ametaja watu waliosimama pale; Luka ametaja mtu mwingine; naYohana ametaja ni mtumwa mmojawapo wa Kuhani Mkuu aliye jamaa wa yulealiyekatwa sikio, naye alitaja kumwona Petro bustanini pamoja na Yesu. Nivigumu kuzipatanisha habari hizo, ni vema tukumbuke kwamba neno likisemwana moja mara nyingi wengine walidaka na kulisemezana wao kwa wao. Yohanaamegawa habari hii kwa kuweka ulizo la kwanza ndipo habari ya hukumu

Page 186: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

mbele ya Ana, ndipo kurudia kutaja ulizo la pili na la tatu. Bila shaka Petrohakuulizwa kwa mfulizo, hata Luka ametaja muda kupita kati ya maulizo hayo,ila waliona vema kumaliza habari hiyo moja kwa moja. Mathayo na Markoametaja kwamba Petro alimkana Yesu kwa kulaani na kuapa.

22: 63-65 Yesu alidhihakiwa na kupigwaWakati wa kungojea hukumu, hali amelindwa na askari, wao walifanya michezoya kupoteza muda,. Walikuwa wamesikia kwamba huyo aliyekamatwa alikuwanabii, hivyo, walimdhihaki kwa kupima uwezo wake wa kutabiri. Walifunika usona kumpiga halafu kumwuliza atabiri ni nani aliyempiga. Pamoja na hayowalimdhihaki na kumtukana na kumpiga. Ila Yesu alikaa kimya, alijua haowameingizwa katika jambo hilo bila kuelewa sawasawa. Ilikuwa kawaida yakazi yao kulinda walioshtakiwa na kwao Yesu aonekana kuwa mtu sawa nawengine. Ni mwanzo wa kudhiliwa kwake.(Maelezo ya hukumu mbalimbali zilizotokea kati ya usiku ule na asubuhi yake.Kila Injili ina habari zake, kila mwandishi amechagua habari fulani na kuachanyingine. Kama kila mwandishi angaliandika habari zote, Injili yake ingalizidikuwa ndefu kupita kiasi. Kwa hiyo, ni vema kufanya ulinganifu kati yao. Hapotumejumlisha jinsi ambavyo twadhani mambo yalivyokwenda:

1. Hukumu ya uchunguzi ilifanyika mbele ya Anasi Kuhani wa nyuma ambayeangalikuwa akiwa na sauti kuu katika mambo yao (Yn.18.19-23)

2. Hukumu ya utangulizi mbele ya Kayafa na wajumbe kadha wa Baraza laolililoitwa Sanhedrin (Mt.26.57-68). Ilifanyika usiku.

3. Hukumu mbele ya Baraza Zima, asubuhi na mapema, wakati ulipowezekanakufanya hukumu ya halali (Lk.22.66-71). Haikuwa halali kufanya hukumu yajambo zito wakati wa usiku. Hata haikuwa halali kuitekeleza hukumu wakumwua mtu siku ile ya hukumu yake kutolewa, kwa sababu ya kuachia mudawa ushuhuda mwingine kutokea. Katika haraka yao ya kumwondoa Yesuhawakufuata sheria zao za kuhalalisha hukumu hiyo.

4. Hukumu mbele ya Liwali wa Kirumi, Pilato. Yohana ameandika kwa kirefuhabari hizo.

k.5.Hukumu mbele ya Mfalme wa Wayahudi, Herode iliyotajwa katika Luka tu(Lk.23.6ku).

22: 66-71 Yesu mbele ya Baraza kuu la KiyahudiKwa sababu walikuwa chini ya utawala wa Kirumi, Sanhedrin haikuwa namamlaka ya kutekeleza hukumu ya kufa. Kwa hiyo ilikuwa juu yao kuandaashtaka juu ya Yesu ambalo waliweza kuliweka mbele ya Pilato kusudiamhukumu Yesu adhabu ya kufa. Kwa hiyo, lazima shtaka lihusu siasa na

Page 187: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 477

usalama wa nchi, hivyo njia ni kumwambia Pilato kwamba huyo Yesu amedaikuwa Mfalme wa Kiyahudi, Masihi, ambaye ni hatari kwa serikali ya Kirumi, kwakuwa shabaha yake ni kufanya mapinduzi. Ndiyo sababu walimwuliza moja kwamoja ‘Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie?’ (Luka hataji habari ya wakuukutafuta mashahidi). Hawakuuliza kwa shabaha ya kutaka kujua wenyewe balikwa lengo la kupata neno la kumshtaki mbele za Pilato, hivyo walimtia hatarini,akijibu ni kama anajiandikisha cheti cha kufa. Kwa sababu hiyo Yesuhakuwajibu, ni kama kazi bure kujibu, kwa sababu hawatamsadiki na kamaakiwauliza maswali kuhusu Umasihi wake hawatamsikiliza kwa kupata kwelimaana wamekwisha kuamua kwamba kwa vyo vyote imempasa auawe, maanahawamtaki kabisa. Hapo nyuma alijaribu kuzungumza neno hilo pamoja naowakakataa (20.3ku. 41ku).

k.69 Hata hivyo, ijapokuwa hawawi tayari kupokea neno la Yeye kuwa Masihi,aliwahakikishia kwamba tangu wakati ule, hali akiwa Mwana wa Adamualiyewekwa na Mungu (Dan.7.13) atashiriki utukufu na uwezo wa Mungu, ndipoatawahukumu wale waliompa kisogo. Katika Zab.110 maneno hayo yalikubalikakuwa yalimhusu Masihi.

k.70-71 Walitambua kwamba Yesu alipotaja maneno ‘Mwana wa Adamu’alikuwa akijisemea mwenyewe na wote walijiunga pamoja na kumwuliza ‘Basi,wewe ndiwe Mwana wa Mungu?’. Walitaka sana athibitishe neno hilo, kwasababu kudai kuwa Mwana wa Mungu ni kufuru ya hali ya juu machoni mwasheria yao, na adhabu yake ni moja tu, kuuawa. Lakini shtaka la kufuruhalitasimama mbele ya Pilato, mpagani. Ila katika kutumia maneno ya Yesuwao wenyewe wamemkiri kuwa Mwana wa Mungu. Yesu akawajibu kwakukubali bila kusema ndiyo moja kwa moja, kwa kuwa jinsi Yeye alivyowaza najinsi wao walivyowaza yalihitalifana. Wakaridhika, wakaona kwamba hawanahaja ya ushuhuda mwingine, Yesu Mwenyewe amejishuhudia lile walilolitaka.Yesu alikuwa amedai kuliko walivyodhani kuhusu Masihi, alidai kuwa nauhusiano wa kipekee na Mungu, na katika mawazo yao hii ni zaidi ya mawazoyao kuhusu Masihi.

23: 1-5 Yesu mbele ya Pilato, liwali Mrumi(Mt.27.1-14; Mk.15.1-5; Yn.18.23-28)

Pilato, liwali wa Kirumi alikaa Kaisaria na ilikuwa desturi yake kuja Yerusalemuwakati wa Sikukuu, kwa sababu mara nyingi fujo ilitokea.

k.1 Wajumbe wote wa Sanhedrin waliafikiana na kwa nia moja walimpelekaYesu kwa Pilato katika hali ya kumsukuma liwali atimize matakwa yao ya kutoahukumu ya hatia yenye adhabu ya kusulibishwa. Hawataridhika na hukumunyingine.

k.2 Hivyo walipofika, mara wakaanza kutoa mashtaka ya mambo matatu, yoteya siasa, waliacha kutaja jambo la kufuru ambalo hasa machoni mwao lilistahili

Page 188: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

Yesu afe, ila walifahamu Pilato, mpagani hawezi kujali mambo ya dini yao.Mashtaka mengine hayakuwa na nukta ya kweli, hasa ile ya kuhusu kodi,maana Yesu mwenyewe alipoulizwa alisema ‘mpe Kaisari ya Kaisari’ (20.25).Shtaka la Yesu kuwa Kristo, mfalme, lilikuwa nusu kweli, maana Yesu hakuwaMfalme kwa jinsi ambavyo Pilato alivyofikiri, kwake Mfalme atakuwa mpinduziwa serikali ya Kirumi, na Yesu siye.

k.3 Bila shaka Pilato alipomtazama Yesu hakuweza kudhani kwamba huyoaliye mbele yake ni mpinduzi wa nchi, hali yake yote haikulingana na ile yamwanamapinduzi, wala hakuwa na silaha au jeshi au hali yo yote ya kuelekeavita. Hivyo alitambua kwamba mashtaka yao hayakuwa sawa, pia alitambuakwamba wamemleta kwa sababu ya husuda (Mt.27.18; Mk.15.10). AkamwulizaYesu moja kwa moja, ‘Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?’ ndipo Yesuakamjibu ‘Wewe wasema’. Hakuweza kukana, ila hakukubali moja kwa mojakwa vile jinsi alivyowaza Pilato ni tofauti na jinsi Yeye alivyo Mfalme. Lukaamefupisha habari hizo za Yesu kupelelezwa na Pilato, Yohana ameziandikakwa kirefu (Yn.18.33.-38 na 19.1ku).

k.4-5 Kisha Pilato alitoa uamuzi rasmi mbele ya makuhani wakuu na makutanoakitangaza kwamba hakuona neno ovu katika Yesu. Hapo ilimbidi amruhusuaende zake. Lakini wakuu hawakuwa tayari kuachilia mambo hapo, walizidikumshtaki Yesu kwa nguvu wakimwonyesha Pilato kwamba ameamsha watukatika eneo kubwa, kwa kuanzia Galilaya hadi Yudea.

23: 6-12 Yesu mbele ya Herodek.6-7 Habari hii ni katika Luka tu. Ilikuwa dhahiri kwamba Pilato hakutakakuhusika na kesi ya Yesu. Alijua mawili: la kwanza: Yesu si hatari kwa serikaliya Kirumi na la pili: Wayahudi wanakazana katika kumshtaki kwa nguvu sana.Yuko mahali pafinyu, atawezaje kuepa kutoa hukumu yenye adhabu ya kufa nakuafikiana na Wayahudi ambao waonekana kuwa hawatakuwa radhi nahukumu yo yote ila ile ya kusulibiwa. Kwa hiyo, aliposikia kwamba Yesuameanza kazi yake huko Galilaya akaona vema kumpeleka kwa Herode, iliyeye amhukumu. Ilikuwa sawa kwa mtu kuhukumiwa katika eneo la kosa lake.Pia Herode alikuwa pale Yerusalemu kwa Sikukuu. Hapo nyumawamegombana na kwa kumpa Herode fadhili hiyo ugomvi wao ulipatakutengenezwa (k.12).

k.8. Herode alifurahi sana kumwona Yesu, hapo nyuma alitaka kumwona,hakuweza. Hata wakati fulani aliposikia habari za miujiza yake alidhani kwambaYohana Mbatizaji amefufuka kutoka wafu. Herode alikuwa amemwua YohanaMbatizaji kwa sababu alimkemea kuhusu kumchukua Herodia kuwa mkeweambaye alikuwa mke wa ndugu yake. Hasa alitaka Yesu afanye miujiza mbelezake. Bila shaka aliwaza kwamba Yesu atakuwa tayari kufanya lo lote lakumpendeza ili amwachilie.

Page 189: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 479

k.9. Ila Yesu hakuwa tayari kujipendekeza mbele zake. Alimwona kama mtu wajuujuu asiyetia maanani jambo zito, hivyo hakumjibu hata neno moja. Yesualikuwa tayari kusema na kujitetea, ila ni kwa huyo tu hakusema neno lo lote.

k.10 Wakuu wa makuhani na waandishi walikuwepo na kumshtaki kwa nguvu,ila Herode hakujali mashtaka yao, yeye aliona ni nafasi ya kumfanyia Yesudhihaka na kumchezea. Bila shaka alichukizwa na hali ya Yesu na kumwoneahasira. Alijiunga na askari waliomvika Yesu mavazi ya kifalme na kumfanyaduni, na kwa michezo yao kupuuzia madai yake ya kuwa mfalme.Ila jambomuhimu ni kwamba Herode hakutoa uamuzi wa kusema Yesu alikuwa na hatia.Ikiwa aliona kwamba Yesu hana hatia, mbona basi, hakumfungulia? Badalayake alimrudisha kwa Pilato ili Pilato amhukumu. Pilato hakufurahi, walaWayahudi, kwa sababu bado hawajapata lile walilotaka.Kwa hiyo watawala wote wawili, yule aliyetawala Yudea, na yule aliyetawalaGalilaya, wote wawili walimwona Yesu kuwa hana hatia. Ila wote wawiliwalikosa nguvu katika nia zao ya kumruhusu Yesu moja kwa moja, wakiogopakufanya iliyo halali na haki kwa sababu ya kuwahofu viongozi wa Kiyahudi,wasije wakawashtaki kwa wakubwa wao huko Rumi.

23: 13-25 Pilato, Baraba, na Yesu (Mt.27.15-26; Mk.15.6-15; Yn.18.38-19.16)k.13 Kwa kuwa Herode hakutoa hukumu juu ya Yesu, akamrudisha kwa Pilato,ilimbidi Pilato awakutanishe wakuu wa makuhani pamoja na watu. Huendaalidhani kwamba watu wakiwepo watakuwa upande wake na kumsaidia katikakuwapinga wakuu waliozidi kumsukuma atoe hukumu ya kufa. Lakinihakutambua werevu wa wakuu na uwezo wao wa kuyabadilisha mawazo yawatu hata wamwombe Pilato awafungulie Baraba si Yesu.

k.14-15 Ni dhahiri kwamba aliwakutanisha wakuu na watu ili atoe tangazo rasmiya kumfungulia Yesu. Alionyesha kwamba ameyapeleleza mambo yake bilakukuta kosa lo lote lililostahili auawe. Pia alitaja jinsi Herode alivyoshindwakuona kosa lo lote liliompasa Yesu auawe.

k.16 Ndipo aliamua Yesu apigwe ili kumfundisha awe na tahadhari juu yamwenendo wake, ndipo atamfungua. Inasemekana kwamba ilikuwa desturi yakufanya hivyo. Pia ilikuwa desturi kuwapiga watu mijeledi kabla ya kwendakusulibishwa kwa shabaha ya kuwadhoofisha na kuharakisha kufawatakapotundikwa mtini. Bila shaka Pilato alidhani kwamba watuwatamhurumia Yesu watakapomwona amedhiliwa na kupigwa, naowataridhika. Lakini, sivyo.

k.17 Katika Mk.15.15.6 na Yn.18.39 desturi ya kumfungulia mhalifu mmojawakati wa Sikukuu imetajwa. Hatujui kwa nini Baraba alitajwa, alikuwa mhalifumashuhuri aliyeongoza fitina mjini na kufanya uaji. Inaonekana alikuwamwanamapinduzi.

Page 190: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.18-19 Katika kumweka Yesu ambaye Pilato amemtangaza kuwa hana hatiapamoja na mtu aliyekwisha kuhukumiwa kosa haikuwa sawa. Lakini Pilatoalikuwa tayari kukamata jambo lo lote ambalo alidhani kwamba litamwokoa nawajibu wa kutoa uamuzi wa Yesu kuuawa.

k.20 Pilato hakuwa tayari kuachilia jambo hilo bila kujaribu tena kumruhusuYesu, ila kama hakimu na liwali aliye na nguvu nafsini mwake na kwakutegemea cheo chake, angalimfungulia tu, hata bila kutafuta kuridhiana nawakuu, ila aliogopa fujo na ghasia na watu kumshtaki kwa Kaisari huko Rumimaana alikuwa na historia ya kufanya mambo yaliyowachukiza na ripoti zamambo hayo zimewahi kufika Rumi.

k.21 Ndipo kwa mara ya kwanza neno ‘msulibishe’ lilisikika. Hawataridhika nahukumu yo yote ila hiyo. Tena walizidi kupaza sauti zao, watu wote, pamoja naviongozi. Viongozi walikuwa wameshawishi watu kumwomba Baraba si Yesu.Yawezekana walifikiri kwamba kama tunafunguliwa mhalifu, tufunguliwe mhalifualiye mhalifu kweli kweli mwenye uwezo wa kuamsha moto wa siasa ya uhuru.Pia watu walipotoshwa katika mawazo yao kwa jinsi viongozi walivyotafsirivibaya Yesu na kazi zake.

k.22 Ndipo tena Pilato alitangaza jinsi alivyomwona Yesu kuwa bila hatia. Bilashaka hakupendezwa na ombi lao la kumpata Baraba, mtu aliye hatari kwaserikali ya KiRumi pia kwa salama na amani ya nchi. Akimhukumu Yesu afe naakimruhusu Baraba atafanya makosa mawili; kumfungulia mkosaji na kumwuaasiye mkosaji. Hii ni mara ya tatu Pilato kusema wazi mbele za watu kwambaYesu hakuwa na hatia machoni pake na machoni pa sheria (hasa tukijumlishana uamuzi wa Herode ni mara 4; k.4,14,15,22 Yn.18.38; 19.4,6).

k.23 Kama kipambele cha kwanza cha Pilato kingekuwa kufanya haki, na kwamamlaku yake ya uliwali, angalimfungulia Yesu mara bila kusitasita. Ila sasaalitamba kwamba pamoja na wakuu kuwa kinyume cha Yesu, watu pia, huwakinyume chake, kwa sababu wameshauriwa na viongozi wao. Kwa hiyo ni kazibure kuendelea kushindana nao. Hakuna jambo litakalowaridhisha watu,hawatatulia mpaka Yesu ameuawa, nao wakazidi kupiga kelele. Kisha sauti zawatu pamoja na sauti za makuhani wakuu zikashinda. Huenda Pilato alikuwana mashaka kwamba watu wako tayari kufanya ghasia mjini, jambo la hatariwakati wa Sikukuu na Yerusalemu kujaa watu. Ikitokea ghasia yeye ataulizwana wakuu wake huko Rumi (19.12) kwa hiyo bila kutaka, alikubali kumpa Yesuadhabu ya kusulibishwa. Alikuwa mwoga aliyeshindwa kufanya iliyo haki, hukuwakati wote akimshuhudia Yesu kuwa bila kosa na hatia.

Page 191: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 481

Bwana Yesu kusulibishwa23:26-49 (ling. Mt.27:32ku.Mk.15:21ku.Yn.19:17ku)

23: 26-31 Yesu alipelekwa kwa mahali pa kusulibiwaIlikuwa desturi kwa mtu kuubeba mti wa msalaba wake (Yn.19.17) nainaonekana Yesu alianza kuubeba ndipo akashindwa. Tukumbuke kwambaalikuwa amekosa usingizi, amekuwa na shughuli nyingi, pia alikuwa amepigwamjeledi, hayo yote yalimfanya akose nguvu. Warumi walimshurutisha mtu,aliyeitwa Simoni wa Kirene aliyekuwa akiingia mjini aubebe nyuma yake.Warumi kwa kuwa walikuwa watawala waliweza kumwagiza mtu afanye kamawalivyomtaka. (Inaonekana huyo mtu na familia yake walijulikana katika Kanisabaadaye (Mk.15.21; Rum.16.13)

k.27-31 Wengi walimfuata Yesu na kumwombolezea, huenda walikuwawachache waliolia ‘msulibishe’ wakiwa nje na mbali na mahali alipohukumiwa.Wengi walikuwa wangali wakimpenda na kusikitikishwa sana kwa hayoyaliyompata. Bila shaka walijaa mchanganyiko wa huruma na udadisi. Ilikuwadesturi ya watu kuhudhuria jambo la namna hiyo.Ni Luka tu ambaye amewataja ‘binti za Yerusalemu’ na maombolezo yao. IlaYesu hakutaka wamhurumie Yeye, hakuwa na hali ya kujihurumia, kwa sababualikuwa akiwaza yatakayowapata watu wa Yerusalemu na Wayahudi baadayewakati wa Mungu kuleta hukumu yake juu yao kwa tendo hilo kubwa lakumkataa na kumwua Masihi wao. Yesu aliweza kuona kwa mbali jinsi Warumiwatakavyouteka Mji mtakatifu. Wote watapata shida, ila hasa, akina mamawatapatwa na shida kubwa watakapokosa chakula cha kuwapa watoto wao nakuwaona wakifa kwa sababu hiyo. Ila hayo yote yalifichwa machoni mwao.(Hos.10.8; Ufu.6.16). Hakutaka huruma yao bali toba lao. Linalotokea ni msibamkubwa kwa taifa la Israeli zaidi ya kuwa msiba Kwake. Matukio ya baadayehusababishwa na hayo wanayomfanyia Yesu wakati huo. Katik dhiki yakekubwa Yesu alikuwa akiwakumbuka wengine kuliko kujihurumia.

k.31 Maneno ‘mti mbichi’ na ‘mkavu’ yana maana gani? Huenda maana yake nikwamba si kawaida kwa mtu kuukata mti mbichi kwa kuni, kwa hiyo, si kawaidakwa mtu asiye na kosa kuuawa. Ikiwa Yesu, aliyetangaziwa mara nyingi naWarumi kuwa mtu asiye na hatia anafanyiwa tendo hilo baya la kumwua,Warumi watawafanyia nini Wayahudi ambao machoni mwao wamewakosa nakuukataa utawala wao? Hakika watawaadhibu vikali sana. Na ikiwa Wayahudiwamfanyie Yesu namna hiyo, Yeye aliyekuja kuwaletea wokovu, watapatwa nahukumu gani kwa kumwangamiza? Yesu alikuwa akitazama mbele kwamatokeo ya dhambi ya taifa lake.

23: 32-38 Yesu alisulibiwa kati ya wahalifu wawiliWaandishi wote wa habari hizo hawakuzitilia chumvi wala kusisitiza maumivuya kimwili ya Yesu. Kifo hicho kilikuwa kikali sana, chenye maumivu mbalimbali

Page 192: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

ya kimwili kama kiu, njaa, uchovu, kupigwa na jua mchana na baridi usiku.Pamoja na maumivu hayo ipo aibu nyingi ya kukaa uchi na kutazamwa nawatu. Kwa kawaida mtu alikufa polepole, hata aliweza kukaa msalabani kwasiku kadha. Ila kwa Yesu yalikuwepo maumivu ambayo hayakuonekana,alihesabiwa laana na mwenye dhambi, alipozibeba dhambi za ulimwengu wotena kufanywa kuwa dhambi (2 Kor.5.21) akasikia nafsini mwake kutengwa naBaba yake kwa ajili hiyo. Hayo maumivu ya kiroho yalizidi yote kwa sababuroho yake ilikuwa laini sana kwa vile hakuwa na dhambi, hakufanya dhambi,wala hakujua dhambi, naye alijua kushiriki kibinafsi katika roho yake kila wakatina Baba yake bila ushirika wao kukatikakatika. Agano Jipya lakaza maana yaKifo chake na umuhimu wake kuliko shida za kimwili.

Waandishi wa Injili zote nne wametaja habari hiyo ila ni Luka tu ambaye asemajuu ya mmoja kubadili hali yake na kumwomba Yesu. Yesu alihesabiwa mhalifukweli akiwa kati yao na kwa mafundisho ya Kikristo ni kuonyesha kwambaalikuwa kufa kwa ajili ya wenye dhambi wote (Isa.53.9,12). Mtu alitundikwakwenye mti na kufungwa ama kwa kamba au kwa kupigiliwa misumari. Yohanaalitaja Yesu alipigwa misumari kwenye mikono yake na huenda kwenye miguuyake (Yn.20.25; 24.39). Mahali paliitwa Fuvu la Kichwa, wala si wazi palikuwamahali pa namna gani. Wengine wamewaza kwamba palikuwa mwinuko wenyesura ya fuvu la kichwa, lakini mwinuko haitajwi. Katika hadithi ya Kiyahudiimesemekana ni mahali pa mifupa ya Adamu, lakini hii ni hadithi tu. Afadhalituseme kwamba watu hawajui kwa hakika. (Kalvary ni neno la KiLatini;Golgotha neno la KiAramaiki). Katika habari hiyo Luka ameacha habarinyingine zilizomo katika Injili ya Marko. Luka amewataja wale wawili kuwawahalifu, Mathayo na Marko walisema walikuwa wevi; huenda walikuwa wanamapinduzi.

k.34 Ndipo Yesu alitamka neno la ajabu sana, alimwomba Baba yake,awasamehe kwa sababu hawakujua watendalo. Ombi hilo lilikuwa kwa ajili yaakina nani? Bila shaka lilikuwa kwa ajili ya askari ili wao watakaposikia kwambaYesu amefufuka kutoka wafu na hofu itawashika pengine kiasi cha kujiuawakidhani kwamba atawalipiza kisasi. Pengine si kwa ajili ya hao tu, bali kwawahusika wote kwa kuwa, iwapo kwa upande mmoja walifahamu kwa upandemwingine hawakuelewa kwa ukamilifu. Katika Sheria ya Kiyahudi haukuwepomsamaha kwa dhambi za kujua, kwa hiyo, Yesu aliachia mlango kwa msamahaakisema kwamba hawakujua wafanyalo (Law.4.2; Hes.15.25-29). Yesu alikujakufanya upatanisho kwa njia ya Kifo chake hivyo, alitoa wito wa kuupokeaupatanisho huo. Tendo hilo linaonyesha ufadhili wa Yesu kati ya maumivu yakena magumu yote aliyoyatendewa. Ilikuwa desturi kwa askari kupata nguo zawaliosulibishwa, kama zawadi kwa kazi hiyo ngumu. Yesu alinyang’anywa kilakitu, alidhiliwa mno (Yn.19.23ku. Zab.22:7,18).

k.35 Watu waliokuwepo walisimama na kuangalia huku wakuu kati yaowalimfanyia mzaha wakishuhudia kwamba aliwaokoa wengine; sifa nzuri sana.

Page 193: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 483

Katika huduma yake alikuwa amewainua wengi kuwa na hali njema. Ilawalishindwa kuelewa kwa nini hakujiokoa akiwa Kristo, mteule wa Mungu.Tofauti kati ya hali yake na madai yake ilikuwa kubwa hata haikueleweka kwanini amedhiliwa kiasi hicho. Pamoja na dhihaka za wakuu, askari pia walijiunganao. Walikuwa wamesikia maneno kuhusu madai yake kuwa Mfalme waWayahudi, pia walisoma anwani iliyotangaza neno hilo. Anwani iliandikwa naPilato, kwa kawaida anwani ziliwekwa juu ya misilaba kwa kutangaza kosa lamtu na kuwa onyo kwa watu. Yesu hakuwa na kosa, na Pilato, akitakakuwalipiza Wayahudi kwa kumlazimisha atoe hukumu ya kufa aliona vemaaweke neno hilo wazi. Iliandikwa kwa lugha tatu (Yn.19.20).Walipoanza kumsulibisha, Yesu alipewa divai yenye dawa ya kupunguzamaumivu (Mt.27.34; Mk.15.23) akakataa kunywa, maana alitaka awe nafahamu zake timilifu kwa sababu hakufa tu, bali katika kufa alikuwaakiupatanisha ulimwengu na nafsi yake. Askari walimdhihaki kwa kumletea siki.Baadaye alikubali kuinywa hiyo siki, ilikuwa divai hafifu, wakati huo alitakakupata sauti ili alie kwa nguvu na kuutangaza ushindi wake (Zab.69.21;Yn.19.29).

23: 39-43 Mhalifu mmoja alitubuMwanzoni wahalifu wote wawili walimtukana Yesu ila baadaye mmoja alibadilimawazo yake. Yawezekana maneno ya Yesu kuhusu msamaha, pamoja nadhihaka za watu zilizomtaja kuwa Masihi na Mfalme wa Wayahudizilimwongoza atafakari sana hali yake na hali ya Yesu aliye kati yao.Alipomtazama akamwona kuwa tofauti na wengine, hakuapa wala kulaani, balikwa upole na unyenyekevu na kwa kujiheshimu alikaa msalabani haliakiwawaza wengine na kutoa maneno ya maana sana. Hivyo akamkemeamwenzake na kumkumbusha habari za kumhofu Mungu, kwa sababu ilikuwahaki waadhibiwe, ila alishuhudia jinsi Yesu hakuwa na hatia wala kutenda lolote lililostahili awepo pale. (Pilato na Herode na sasa huyo wote wametajaYesu kuwa bila hatia). Kwa imani kubwa akitegemea anwani iliyosema ‘huyo niMfalme wa Wayahudi’, akamwelekea Yesu na kumwomba amkumbukeatakapoingia katika ufalme wake. Kama alidhani huo ufalme ni wa sasa au niwa baadaye, hatuwezi kujua alikuwa na mawazo gani.Ila Yesu akamjibu kwauthabiti akimwambia kwamba, leo atakuwa pamoja naye peponi. Neno peponini la KiAjemi kwa bustani, kama Edeni, bustani mbalimbali zimetajwa katikaAgano la Kale. Bustani iliashiria mahali pa baraka katika ulimwengu ujao, kwahiyo badala ya kwenda Sheol, mahali pa wale ambao hawatafika mahali pema,yeye atakwenda peponi, na kushiriki na Yesu pale. Alihesabiwa haki kwa imani,naye alikuwa malimbuko ya wokovu kutokana na kifo cha Yesu (2 Kor.12.3;Ufu.2.7). Hakuwa na nafasi ya kutenda lo lote isipokuwa kumwamini Kristo tu.Katika kufa Yesu alikuwa na nguvu za kuokoa.

Page 194: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

MASWALI1. Yesu alitabiri maagamizo ya hekalu na ya Yerusalemu. Alitoa sababu

gani kuu ya maangamizo hayo? Yalitokea lini na kwa njia gani?2. Kuhusu mwisho wa ulimwengu Yesu alisema ni nini itakayokuwa ishara

ya mwisho? Wafuasi wake wasidanganywe na mambo gani na kufikirikwamba mwisho umekuwa karibu?

3. Eleza habari za Yuda na kutoa mawazo yako juu ya usaliti wake nasababu zake.

4. Wakati wa kula Pasaka Yesu alitia maana gani upya kuhusu mkate nadivai. Katika kufanya hivyo Yesu alionyesha uthabiti gani?

5. Je! waonaje mafundisho ya Yesu juu ya ukuu wa kweli ? Je! KatikaKanisa mafundisho hayo yanafuatawa? Eleza.

6. Eleza umuhimu wa Yesu kuomba katika Bustani ya Gethsemane.7. Eleza hukumu ya Yesu mbele ya Pilato. Je! Pilato alifikiri Yesu alikuwa

na hatia? Kama jibu lake ni ‘la’ eleza ni nini iliyomshinda asimfungulieYesu.

8. Eleza habari ya Yesu kusulibishwa. Katika kufa kwake Yesu alikuwaakifanya nini hasa?

23: 44-49 Kifo cha Bwana Yesuk.44-45 Luka ametaja jambo lililotokea kuanzia saa sita hadi saa kenda, wakatiYesu alipokuwepo msalabani. Giza kuu lilifunika nchi yote, wakati wa juakuwaka sana na mwanga ni mkubwa. Ni vigumu kufikiri kwamba jua lilipatwakwa sababu Pasaka ilifanyika wakati wa mwezi mpevu. Hakuna maelezo yakuonyesha jinsi tukio lenyewe lilivyokuwa, ila twaweza kutafuta maana yake. Nitendo la Mungu na yawezekana shabaha yake ilikuwa kuuvuta usikivu wa watuili wafahamu kwamba wakati huo tendo kuu la ajabu lilikuwa likifanyika,ulimwengu ulikuwa ukikombolewa kwa njia ya kifo cha Yesu, dhambiilihukumiwa katika Yesu, akiwa dhabihu kwa dhambi za ulimwengu wote, naShetani alinyang’anywa haki yake ya kuwaonea wanadamu. Pamoja na hayo,huenda liliashiria kwamba uumbaji wote ulijiunga na Yesu katika huzuni nasikitiko nyingi kwa kosa hilo kubwa lililofanywa na wanadamu. Pia lilikujakufunika aibu ya Mwana wa Mungu akiwa uchi na kupigwa na jua n.k. Ndipotendo lingine lilifanyika na Mungu, pazia la hekalu lilipasuka katikati. Pazia hilolilitenga Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu. Hakuna aliyeingia ndani yaPatakatifu pa Patakatifu ila Kuhani Mkuu, mara moja kwa mwaka, siku yaUpatanisho, akiichukua damu ya dhabihu, kwa ajili ya kuufanya upatanisho katiya Israeli na Mungu. Kwa hiyo Mungu alitaka kufundisha watu kwamba njiaimepasuka na tangu hapo mtu ye yote, aweza kumwendea wakati wo wote,mahali po pote, hali akiitegemea dhabihu ya Yesu (Ebr.9.8-14; 10.19ku).

k.46 Mwisho wa saa hizo tatu za giza Yesu alilia kwa sauti kuu na kujikabidhikwa Baba yake kwa amani akitumia maneno ya Zaburi 31.5. Alionyesha imanikuu kwa Baba yake, hali akijua hakika kwamba atampokea. Ndipo alikata roho.Alikuwa akitawala hata katika kufa kwake. Luka hataji kilio kizito cha Yesu kabla

Page 195: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 485

ya kukata roho, kilio kilichoonyesha taabu za Kifo chake cha upatanisho, jinsialivyojisikia kutengwa na Baba wakati wa kuzibeba dhambi za ulimwengu nakuhukumiwa na Baba kwa ajili yake (Mt.27.46; Mk.15.34). Katika kuandikahabari hizo Luka amesisitiza amani ya Yesu na mamlaka yake, alimsamehemtu na kumhakikishia mahali pema baada ya kufa, na wakati wa kumalizakubeba dhambi alijikabidhi kwa Baba na kukata roho, kama kuisalimu. Alifanyamapenzi ya Baba yake, alikuwa na umoja naye na katika kufa alionyesha hivyo.

k.47-49 Ndipo Luka ameonyesha jinsi watu walivyojisikia walipoyatazamamatukio hayo. Akida, kiongozi wa kikundi cha askari wahusika katika shughuliza kumsulibisha Yesu na kumwangalia msalabani, alitoa ushuhuda wake.Alimsifu Mungu na kutangaza Yesu kuwa hana hatia, mtu wa haki ambayeametendewa isiyo halali. Ilikuwa siku ya huzuni sana kwa Israeliwalipomsulibisha yule asiyekuwa na hatia. Luka amependa kusisitiza neno laYesu kuwa bila hatia na kushuhudiwa na watu mbalimbali, kama Pilato na huyoakida, watu wasio Wayahudi, watu wapagani.

Umati wa watu walionaje? Wale waliokusanyika pale, wenyeji wa Yerusalemuambao walikwenda kutazama yaliyotendeka. Wao walisikitishwa sana,wakarudi makwao wakijipigapiga vifua. Huenda walianza kutambua kwambawalikosa walipojiweka upande wa wakuu wao na kuomba Yesu asulibiwe,wakitafakari kwa upya juu ya Yesu na tukio hilo. Mambo hayo yalisaidia nakuwa matayarisho kwa mahubiri ya Injili siku ya Pentekoste, wakati watu elfutatu walipokata shauri kumpokea Yesu (Mdo.2.37-38).

Je! Habari za wale waliomjua Yesu nao wamefuatana naye kutoka Galilaya. Piahao wanawake waliomfuata kutoka huko? Inaonekana walishikwa na huzuniwakishindwa kuelewa maana yake. Hao walisimama mbali. Mathayo ametajabaadhi ya wanawake kuwa karibu na msalaba na Yohana ametaja mama waYesu na Mtume Yohana kuwa pale (Yn.19.25). Mathayo ametaja kwambatetemeko la nchi lilitokea (Mt.27.51).

23: 50-56 Maziko ya Bwana Yesu (Mt.27.57-61; Mk.15.42-47; Yn.19.38-42)k.50-51 Injili zote zataja Yusufu wa Arimathayo kuwa yule aliyechukua jukumula kumzika Yesu. Kwa kawaida mwili uliachwa msalabani, ndipo ukatupwakatika kaburi la watu au kuachwa kwa ndege kula. Yusufu amepewa sifa nzurisana, alikuwa mjumbe wa Sanhedrin ila hakukubaliana na wale waliotoauamuzi wa Yesu kuuawa, pengine hakuwepo wakati wa kupitishwa kwa huouamuzi. Ameitwa mtu mwema, mwenye haki, mtu aliyekuwa akiutazamiaUfalme wa Mungu. Maana yake nini maneno hayo? Pengine ni njia ya Lukakusema kwamba alikuwa mfuasi wa Yesu, ingalau kwa siri, kama alivyokuwaNikodemo (Mt.27.57; Yn.19.39). Wayahudi wote walitazamia Ufalme wa Munguila bila shaka Yusufu aliuwaza kwa jinsi Yesu alivyoueleza. Alitoka Arimathayo,mji wa Kiyahudi uliokuwa karibu na Yerusalemu. Pengine Yusufu alikuwa

Page 196: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

amehamia Yerusalemu kwa sababu alikuwa amechonga kaburi lake pale tayarikwa maziko. Makaburi mazuri yalikuwa ghali (Mt.27.60).

k.52 Yeye hakusikia ni jambo jema kumwacha Yesu bila kumzika kwaheshima, ila mpaka ameruhusiwa na Pilato hakuweza kuuchukua mwili. Hivyoalimwendea Pilato na kumwomba apewe. Siku za Yesu kudhiliwa zimepita,amekufa kati ya wahalifu ila azikwa kwa fahari kama mfalme (Isa.53.9ku).

k.53-56 Yusufu aliuweka mwili wa Yesu katika sanda ya kitani kwa desturi yaKiyahudi. Hakuweza kufanya yote yaliyotakiwa kwa sababu jioni ile iliamkiaSabato ya Sikukuu. Wayahudi walihesabu siku kuanza saa moja ya jioni, Kwasheria mtu akifa siku iliyotangulia Sabato jamaa hawakuruhusiwa kufanya nenozaidi ya kumzika tu. Yohana katika Injili yake ametuambia kwamba Nikodemo,mtu mwingine wa Baraza na mwanafunzi wa siri wa Yesu alimsaidia Yusufu.Yeye aliyaleta manukato yenye uzito mkubwa. Wanafunzi walikuwawamekimbia kwa hofu ya kukamatwa au kwa huzuni ya kulemewa na kukosanguvu ya kufanya kitu. Ila wanawake walikuwa wakakamavu, walipatazamamahali Yesu alipowekwa, ili baada ya Sabato kupita, waje na kumfanyia Yesuhuduma za mwisho, za kutia manukato na marhamu. Wote walipumzikakwenye Sabato. Watu waliwaza kwamba mambo yaishia hapo.

24: 1-12 Kufufuka kwa Bwana Yesu (Mt.28.1-10; Mk.16.1-8; Yn.20.1-10)k.1 Wanawake walipumzika siku ya Sabato, siku ya saba kufuatana na kawaidaya Wayahudi kuhesabu juma. Kwa hesabu zetu siku ya saba ya juma huitwaJumamosi. Halafu baada ya Sabato kwisha hao wanawake walikwenda kaburinimapema sana wakiwa na manukato waliyokuwa wametayarisha ili wamalizekumzika Yesu kwa uzuri. Majina yao yametajwa katika k.10. Kamwehawakuwaza kwamba yawezekana watakosa kuikuta maiti ya Yesu, neno hilohalikupata nafasi mawazoni mwao.

k.2-3 Njiani walikumbuka jiwe lililowekwa kaburini na kuzungumzia namnawatakavyoliondoa, maana lilikuwa kubwa (Mk.16.3) ila walipofika pale walilikutalimeondolewa nao wakaweza kuingia mle kaburini bila shida. Kumbewalipotazama hawakuuona mwili wa Yesu.

k.4-5 Neno hilo liliwasumbua, hawakujua la kuwaza wala la kufanya;watafanyaje na manukato waliyoleta? Mwili utakuwa wapi? Hawakufikirikwamba Mungu atakuwa amemfufua Yesu ila labda watu wamefanya kitu.Wakati huo wa wasiwasi, watu wawili (malaika k.23) walisimama karibu nao,hali wamevaa nguo zilizong’aa. (Marko alitaja mtu mmoja si wawili, ila penginealitaja mmoja tu, yule aliyesema Mk.16.5). Luka amesema kwamba haowalisimama, na katika Injili nyingine waliketi, bila shaka mara nyingine walibadilihali yao ya kukaa. Hao wanawake waliogopa na kuinama kifudifudi kwaheshima mbele zao. Ndipo waliulizwa swali lenye lengo la kuwasaidia kubadili

Page 197: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 487

mawazo yao. ‘Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu? Yaani wasimwazeYesu kuwa mfu, kwa sababu yu hai, na mahali pake si katika wafu.

k.6-8 Ndipo waliwaambia wanawake ‘Hayupo hapa, amefufuka’. Yeyehakuondolewa na kuwekwa mahali pengine. La, bali amefufuka. Kisha malaikawaliwakumbusha jinsi ambavyo Yesu alikuwa amewahi kuyataja mambo hayowalipokuwa pamoja naye Galilaya. Alikuwa ametamka wazi kwamba atatiwamikononi mwa wabaya na kusulibiwa na kufufuka siku ya tatu (9.22; 17.25;18.33). Walijua hakika kwamba ameishatiwa mikononi mwa wabaya nakusulibiwa, kwa hiyo, imebaki jambo la kufufuka siku ya tatu. Sehemu yamwisho imetimizwa pia, ni siku ya tatu, naye amefufuka. Walikumbuka habarihiyo nao wakaridhika, sasa walijua maneno hayo yalihusu kufufuka kwa mwiliwake, si kufufuka kimawazo au siku za baadaye. Lilikuwa jambo muhimu kwawanawake kujua kwamba mambo hayo mawili, Yesu kutabiri habari hiyomapema, na kutimizwa kwake sasa, ni mawili yanayowiana.

k.9 Hivyo waliondoka kaburini na kurudi na kuwaarifu Mitume na wenzao habariza mambo waliyoyakuta kaburini na maneno ya malaika. (Yuda Iskariote alijiuakabla ya Ufufuo (Mt.27.3-10).

k.10 Hapo Luka ametaja majina ya baadhi ya wanawake waliokwenda kaburini.Kwa sheria ya Kiyahudi wawili walitosha kutoa ushuhuda wa kukubalika,walijulikana na Mitume nao walikuwa wameandamana na Yesu huko Galilayawakimhudumia, Luka aliwataja hapo nyuma, mwanzo wa huduma yao kwaYesu, sasa wanaitimiza (8:3; Mk.15:40,16:1,9. Mt.28:1, Yn.19:25).

k.11 Lakini hao Mitume hawakuwa na mwelekeo wa kusadiki yaliyosemwa nahao wanawake, hata waliyaona ni upuzi. Neno hilo linatuonyesha kwambahakuna aliyewaza kwamba Yesu atafufuka kutoka wafu, iwapo alikuwaamewahi kuwaambia habari hiyo. Walishtushwa sana na habari iliyoletwa nawanawake.

k.12 Petro aliona vema aende mbio mpaka kaburini ili ahakikishe yaliyosemwana wanawake, na alikuta mambo sawa na walivyomwambia (Ling.na Yn.20:3-10). Alistaajabia tukio hilo, ndipo akarudi nyumbani hali akingojea itakavyotokeasiku hii inapoendelea. Pale kaburini hakuwaona malaika, bali aliona vitu fulanimuhimu, vitambaa vya sanda vimelala mle ndani.

Mitume walisikia shida sana katika kuamini habari za Kufufuka kwa BwanaYesu, walikuwa wazito sana. Kwa hiyo, baadaye, walipozitangaza habari zaBwana Yesu na hasa Kufufuka Kwake, jambo hilo lilipata nguvu na kuwavutawatu wauzingatie ukweli huu.

Page 198: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

24: 13-35 Yesu aliwatokea wawili katika njia ya kwenda Emauk.13-14 Ilikuwa siku ile ile ya Ufufuo wa Yesu na wawili miongoni mwawanafunzi wa Yesu (si Mitume) ambao wamekuwepo Yerusalemu kwa Pasakana kuona yote yaliyotendeka walikuwa wakirudi, ama nyumbani, au kwa mahaliwalipokaa. Sikukuu ya Pasaka iliendelea kwa siku saba, siku za Mkate usiotiwachachu. Walifahamu mengi yaliyotendeka pale Yerusalemu, Yesu kuhukumiwa,kusulibishwa, na kuzikwa. Pia walifahamu kwamba siku hiyo, asubuhi namapema, wanawake kadha miongoni mwa wafuasi wa Yesu walikwendakaburini, wakakosa kuuona mwili wa Yesu nao wakasema kwamba walitokewana malaika waliowaambia kwamba Yesu yu hai. Jambo la ajabu! Jamboambalo halikutazamiwa. Bila shaka mchana huo wangedhani kwamba Yesuangetokea baadhi yao, hasa Mitume, lakina mpaka walipoondoka Yerusalemuhakuna habari nyingine. Petro na Yohana walikwenda kaburini na kuuhakikishaukweli uliosemwa na wanawake ila Yesu Mwenyewe hawakumwona. Hivyo,hao wawili walikuwa wameondoka Yerusalemu hali ya kuchanganyikana,wasijue waamini nini. Bado wangali wakisikia huzuni na uzito wa hali kwamabaya yaliyompata Yesu. Kwa sehemu, maneno ya wanawake yaliwafanyawaanze kutumaini, ila kwa kidogo tu. Kwa hiyo, njiani walikuwawakizungumzana jinsi walivyojisikia kuhusu hayo yote wakirudiarudia kusemajuu ya yale matukio.

k.15-16 Ndipo mgeni mmoja, aliyeonekana kama ametoka Yerusalemuakasogea karibu na kuandamana nao. Ila wakashindwa kumtambua. Kwa jinsiLuka alivyoandika inaonekana walizuiliwa wasimtambue. Pengine kwa tendo lakipekee la Mungu kusudi Yesu apate nafasi ya kuwafundisha kutoka Maandikokwanza kabla ya kujifunua kwao. Pengine uzito wa hali zao uliwazuiawasimtambue, au pengine Yesu alichukua sura tofauti (Mk.16.12). Twasomamahali pengine watu walishindwa kumtambua mara (Mt.28.17; Yn.20.14; 21.4).

k.17-18 Kwao huyo mgeni alionekana kuwa mtu asiyejua mambo maanaaliwauliza ni maneno gani waliyokuwa wakizungumza. Neno hilo liliwashtusha,wakasimama na kuzikunja nyuso zao. Pengine hawakupendezwa na huyomgeni kujiingiza katika mazungumzo yao mazito. Pia walishangaa kwa swalilake, ambalo lilikuwa la ajabu likitoka kwa mtu waliyedhani ametokaYerusalemu, maana Yerusalemu ulijaa habari za matukio ya Yesu kusulibiwana ndivyo Kleopa mmoja wa hao wawili alivyomjibu.Mambo yaliyompata Yesu yalikuwa dhahiri, yalifanyika machoni mwa watu,yaliweza kupelelezwa na habari zake kuhakikishiwa. Ila ni wao wasioyajuamambo, hawajui huyu anayewauliza ni Yesu Mwenyewe.

k.19ku. Yesu akawauliza hayo mambo kuwa mambo gani, kwa kuwa alitakawayamwage yale yaliyokuwemo mioyoni mwao. Ndipo walionyesha jinsiwalivyomwaza huyo Yesu kuwa nabii na yule wa kukomboa Israeli na utawalawa Kirumi. Walisema tumaini lao lilijengwa juu ya uwezo wa Yesu katikakutenda na kunena akionekana kuwa mtu mwenye kibali cha Mungu na watu.

Page 199: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 489

Halafu walitaja yaliyompata Yesu kutoka wakuu wao. Waliwalaumu wakuu waokwa kifo cha Yesu, si watu, wala si Warumi ambao waliitekeleza hukumu hiyo.Mawazoni mwao ni viongozi wa taifa lao ambao walikuwa sababu ya Yesukuuawa. Hao wawili walikuwa sawa na Wayahudi wenzao katika kufikirikwamba Masihi atawaokoa na utawala wa kimwili nao walikuwa wameaminikwamba Maandiko yasema hivyo. Maandiko yalisema Masihi atawaokoa watuna dhambi zao, na itampasa afe, hayo hawakufahamu. Kisha walitaja habari zawanawake kwenda kaburini na kutokewa na malaika waliowaambia kwambahuyo Yesu yu hai, hata mwili wake haukuwemo kaburini. Jambo hilo liliwapashida, walikuwa hewani, wakiwa na hofu na mashaka pamoja na matumaini.Bila shaka baada ya habari za wanawake walifikiri kwamba Yesu atawatokeabaadhi ya Mitume, ila mpaka walipoondoka Yerusalemu, hamna habari yanamna hiyo.

k.25ku. Ndipo Yesu baada ya kusikia hayo yote yaliyokuwemo mioyoni mwaoaliwakemea kwa uzito wao wa kufahamu Maandiko, maana kutoka Agano laKale na unabii wake walipaswa kujua kwamba Masihi atateswa. Jambo kubwalililokuwemo katika Agano la Kale lilikuwa kwamba ni mapenzi ya Mungu mmojaafe kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu na dhambi. Neno hilo lilikuwa lazima.Kweli Maandiko yalisema juu ya uwezo na uhodari wa Masihi na kumfananishana Mfalme Daudi mashahuru wao aliyewaokoa na adui zao. Dhabihu zote namipango yote ya Agano la Kale yaliashiria ukombozi wa dhambi kwa njia yakumwaga damu. Yesu aliwafunulia neno hilo kutoka sehemu zote za Maandikoakionyesha kwamba neno hilo lilikuwa lengo la Mungu tangu awali. KatikaAgano la Kale lilikuwa wazi kwamba Mungu alikuwa Mtakatifu aliyewazadhambi kwa uzito. Pamoja na hayo ilikuwa dhahiri kwamba Mungu ni Pendo,apendaye wanadamu upeo. Kwa sababu hiyo ilimbidi apate njia ya kuwaMtakatifu na kuhukumu dhambi na katika kumtoa Yesu Mwana wake mpendwakuwa dhabihu ya dhambi alionyesha upendo wa ajabu sana huku akidumukuwa Mtakatifu. Njia ilikuwa ya gharama kubwa ya Yesu kusulibishwa. Yesualiwaelimisha pamoja na kuigusa mioyo yao.

K.28 Walifika karibu na kijiji cha Emau na Yesu alifanya kama anatakakuendelea katika safari yake. Hao walimkaribisha na Yesu alikubali kukaa nao.Chakula kilipokuwa tayari wakaketi mezani na kwa desturi ya Kiyahudi shukraniilitolewa. Lakini badala ya mwenyeji kutoa shukrani, mgeni alifanya. Mgenialikuwa mkaribishaji! Akachukua mkate na kuubariki, akaumega na kuwapa.Tukumbuke hao hawakuwepo kwenye Chakula cha mwisho, ila huendawalikuwepo wakati wa kuwalisha watu zaidi ya elfu tano (9.10-17). Kwa njiafulani walimtambua huyo mgeni aliyeandamana nao njiani ni Yesu. PengineMungu aliwapa ufunuo huo au pengine kwa desturi yake ya kuuchukua mkatena kuumega n.k. walimtambua, akifanya kama mazoea yake. Penginewaliziona jeraha za misumari mikononi mwake. Hatujui hasa ni niniiliyowasaidia kumtambua, ila mara alitoweka mbele zao. Si kama aliondokakama kawaida ya mtu kuondoka, bali akatoweka.

Page 200: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

k.32 Walishuhudia jinsi walivyosikia alipowafunulia Maandiko, sasa waliaminikabisa kwamba huyo mgeni alikuwa Yesu na katika furaha yao hawakusikiauzito wo wote wa kimwili, wakaamua kurudi Yerusalemu kwa wenzao nakuwaambia habari hizo. Walipofika wakawakuta wenzao wamekaa pamoja.Hao pia wamejipa moyo kwa sababu mchana ule Yesu alikuwa amemtokeaPetro. Hakuna maelezo yo yote ya jinsi alivyomtokea (1 Kor.15.5) ila hayoyaliyathibitisha maneno ya wanawake. Walikuwa tayari kumwamini Petro,hawakuwa tayari kuwaamini wanawake! Halafu hao wawili walishuhudiayaliyowapata katika safari yao na wakati wa kula pamoja na Yesu.. Polepole,hatua kwa hatua, Yesu alikuwa akiwatumainisha wanafunzi na kuwaweka tayarikwa kuwatokea wakiwa wote pamoja.

24: 36-49 Yesu aliwatokea Mitume mle chumbani(Yn.20:19-23; Ling.Mt.28:16-20; Mk.16:14-20)

Luka ametutayarisha kwa habari hii. Hapo nyuma ametaja habari ya kaburikuwa tupu, ushuhuda wa malaika kwa wanawake, ujuzi wa kibinafsi wa walewawili waliposafiri kwenda Emau, na dokezo la Petro kumwona Yesu. Sasatwapata habari ya Yesu kukutana na Mitume na wanafunzi akitokea mlechumbani walimokuwa wamekusanyika. Alionyesha kwamba yeye si mtazamajitu bali Yeye yu hai katika mwili, akala samaki mbele yao.

k.36 Wale wawili na Mitume walikuwa wangali wakisema wao kwa wao ndipokwa ghafula Yesu alitokea na kusimama katikati yao. Yohana alisema milangoilifungwa (Yn.20.19). Yesu aliwaamkia kwa salaam za kawaida ya Kiyahudi‘Amani iwe kweni’ salaam za kuwatumainisha kwamba hawatakemewa kwa vilewalivyokimbia na kumwacha wakati alipokamatwa. Lakini hao hawakusikiaamani, hawakuwa tayari kumwona, walikuwa wazito kama wale wawiliwaliokwenda Emau.

k.37 Katika mchana huo mawazo yao yalivutwa kuamini kwamba Alikuwa hai,huku wakiwa na mashaka, kwa vile Yesu alikuwa bado hajawatokea. Asubuhiwanawake walileta habari ya kuwa Yesu yu hai, waliambiwa hivyo na malaika.Pia ilisemekana ametokea kwa Petro, ndipo wale wawili waliokwenda Emau,sasa hivi, wameleta habari kwamba wamemwona. Kwa hiyo walikuwa nusutayari kumwona, ila alipowatokea kwa ghafula, na kwa uwezo wa kipekee,walishituka na kuogopa sana. Twashangaa kusoma kwamba waliogopa hukuwameisha kuwaambia wale wawili kwamba ‘Bwana amefufuka kweli kweli’?Mbona imekuwa hivyo? Huenda ni kwa jinsi alivyotokea, kwa ghafula, piaalitokea katikati yao bila wao kujua ni kwa jinsi gani alivyoingia mle ndani hukumilango imefungwa.

k.38-40 Yesu aliwauliza sababu ya kufadhaika na kuwa na shaka? Ndipoaliwahakikishia ukweli wa kuwa ni Yeye Mwenyewe aliye mbele yao.Akawaonyesha mikono na miguu yake, bila shaka kovu za misumari

Page 201: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 491

zilionekana wazi kwa hiyo, aliye mbele yao ni Yeye aliyesulibiwa, si mwingine.Hata aliwaita wamguse na kujua kwamba Yeye si roho bali anao mwili kweli,mwili wenye uwezo mpya, usiozuiliwa kama hapo nyuma, hata hivyo ni mwili.Ufufuo si jambo la roho kuendelea kuishi bali ni kuishi kwa mwili wa roho aumwili wa ufufuo. Mwili utavikwa uwezo mpya utakaokanusha uwezo wa dhambina mauti. Alitaka Mitume na wenzao wajue uhalisi wa Yeye kuwa hai.

k.41-43 Kumbe! Mambo huwa mema kuliko walivyowaza nao wakafurahi sanana kuendelea kustaajabu. Yesu alizidi kuwahakikishia ukweli wa uahi wake nakuishi kwake katika mwili wenye uwezo mpya ambao pia aliweza kuufanyaupatane na mwili wa kawaida kwa kula akisikia kufanya hivyo. Mwili wakeuliweza kukipokea chakula bila kukihitaji. Kwa hiyo aliwaomba wampe chakula.Nao walimpa kipande cha samaki wa kuokwa na Yeye alikila kipande hichombele yao akisisitiza ukweli wa mwili wake (1 Kor.15.35-38).Kwa wawili waliokwenda Emau Yesu alijitambulisha kwao katika kula mkate, nahapo, kwa Mitume, kwa kula samaki. Ni ukumbusho wa mwujiza aliofanya haponyuma alipowalisha watu elfu tano na mikate mitano na samaki wawili, wakatiambapo wanafunzi walijengwa katika imani yao.

k.44-49 Kwa jinsi Luka alivyoandika sehemu hii tungedhani kwamba hayoyalitokea siku ile ya Yesu kufufuka, ila imefikiriwa kwamba hapo amejumlishahabari zilizofuata siku ile mpaka siku ya Kupaa Kwake.

k.44ku. Katika Injili yake Luka amesisitiza neno la Maandiko kutimizwa na hapotena aliwafundisha Mitume na wenzao kutoka kila sehemu ya Agano la Kalejinsi ilivyoandikwa kwamba ilikuwa lazima Masihi ateswe ndipo kufufuka kutokakwa wafu, kisha habari hizo ziletazo msamaha wa dhambi zihubiriweulimwenguni. Kutaja Torati, na Manabii, na Zaburi, mkazo ni kwamba hakunasehemu yo yote ya Agano la Kale inayokosa kuwa na neno hilo. Kamaalivyofanya njiani kwa wale wawili alifanya tena kwa Mitume na wanafunziwengine.

k.47 Kutokana na habari hizo Yesu aliwapa wajibu wa kutangaza neno la tobana ondoleo la dhambi. Watu wapewe nafasi ya kuamua juu ya kubadili maishayao na kumpokea Kristo. Watafanya kwa Jina lake, wakitangaza matendomakuu ya Kristo katika kuishi, kufa, kufufuka na kupaa Kwake. Habari hiyo nikwa WaMataifa wote nao wataanza pale pale walipo, Yerusalemu. Ilahawataanza mpaka wamevikwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Wasijaribu kufanyakwa juhudi zao wenyewe. Yesu alikuwa na mamlaka ya kumtuma RohoMtakatifu ambaye Baba alikuwa amewaahidi.

Kwa hiyo tumeona jinsi Yesu alivyowapa msingi imara wa Maandiko, msingi wakujenga juu yake huo ujuzi wa kibinafsi waliopata walipomwona baada yaKufufuka kwake, kuzungumza naye, kula pamoja naye, na kutumwa naye. Ni

Page 202: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

jambo muhimu kwa ujuzi wetu wa kibinafsi kupatana na mafundisho yaMaandiko, ndipo mtu huwa imara sana katika imani yake.

Kisha Yesu aliwapa ahadi ya kuvikwa na uwezo wa Roho Mtakatifu, kipawaatakachowaletea baada ya Yeye kupaa na kutukuzwa na Baba huko juu.Wapaswa wamsuburi huyo Roho wakikaa wote pamoja pale Yerusalemu.Iwapo wanazo habari kamili, wangeweza kuzitangaza habari za Yesu kwausahihi, hata hivyo, walihitaji uwezo wa kipekee kufanya hivyo.

24: 50-52 Yesu alipaa mbinguni(Mdo.1.9-11) Ling. Na Yn.20.19-23; Mt.28.16-20)

k.50ku Hapo mambo yafikia upeo. Yesu amejitambulisha kwao, amewaonyeshamikono na miguu na kula pamoja nao. Amewapa mafundisho yaliyo msingiimara. Sasa hali yao ni tayari kung’ojea Yerusalemu kwa furaha na matumaini,wakimwabudu Mungu. Yesu aliwatokea wanafunzi mara kwa mara kwa mudawa siku arobaini (Mdo.1.3) ndipo siku ilifika kwa Yesu kuwaacha na kurudi kwaBaba yake. Hivyo aliwakutanisha pamoja na kuwachukua mpaka kijiji chaBethani kwenye mlima wa Mizeituni. Aliinua mikono na kuwabariki, akiwawekakatika ulinzi wa Baba yake, mfano wa Kuhani Mkuu zamani za kale, ndipoaliondoka kwenda juu machoni mwao na wingu lilimpokea, wasimwone tena.Walijua kwa hakika kwamba amewaacha, wala hatawatokea tena mpakaAtakaporudi mwisho wa mambo yote.

Sasa wameelewa kabisa kwamba alitoka kwa Baba naye amerudi kwa Babawala hawakuhuzunika kwa sababu hiyo bali walijaa furaha na tumaini lakupewa Roho Mtakatifu. Walirudi mpaka Yerusalemu kama walivyoaagizwa, nakukaa humo, wakisubiri hiyo ahadi. Katika muda wa kungoja walifika hekalunikila wakati kwa kumsifu Mungu pamoja na kukusanyika katika nyumba, huendaile walipokuwemo wakati alipowatokea siku ya Ufufuo, ambayo yadhaniwakuwa ya Mariamu. Hapo walitumia muda katika kuomba huku wakiujengaumoja wao na ushirikiano wao. Siku za kugombania ukubwa zimekwisha, wotewalikuwa na hamu ya kuvikwa uwezo mpya wa Roho tayari kwa kufanyauinjilisti. Luka ametupa picha ya furaha yao na ibada yao. Luka hakuandikazaidi kwa sababu alikusudia kuandika kitabu kingine (cha Matendo) ambachokitaanza na habari hizo za Kupaa kwa Yesu.

Kupaa kwake kulifunga huduma yake hapo duniani. Atakapomtuma Rohoataanza huduma yake kutoka mbinguni, huduma itakayotekelezwa kwa njia yawanafunzi wake (Mdo.1:1).

Page 203: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Luka - African Pastors …taratibu habari za Yesu kabla ya Luka. Alitumia neno ‘kutimizwa’ kuonyesha kwamba aliamini kwamba habari hizo zilitimiza mapenzi

LUKA 493

MASWALI1. Jambo la pazia la hekalu kupasuka kutoka juu liliashiria nini?2. Yesu alisikia taabu mbalimbali aliposulibishwa. Taabu yake kubwa kuliko

yote ilikuwa nini?3. Eleza mambo yaliyowapata wanawake waliokwenda kaburi mapema

baada ya Sabato. Waliporudi kwa Mitume waliwaambia nini? na Mitumewalionaje?

4. Eleza jinsi Yesu alivyojihusisha na wale wawili waliokwenda Emau.Kabla ya kujifunua kwao aliwasaidiaje?

5. Kufika jioni ile ni mambo gani yaliyowatayarisha Mitume kufikiri kwambani kweli Yesu amefufuka kweli?

6. Kwa jinsi Yesu alivyowatokea walijifunza nini kuuhusu mwili wake? Nawalijuaje Yesu hajakata tamaa juu yao?

7. Kwa nini Luka aliandika machache kuhusu Kupaa kwa Bwana Yesu?

MASWALI KUHUSU KITABU KIZIMA CHA LUKA

1. Umejifunza mambo gani makubwa kumhusu Bwana Yesu kutoka Injiliya Luka?

2. Unafikiri Luka alitaka kutoa picha gani kumhusu Yesu Kristo?