ukuzaji wa asali africa (honey care africa) · ya mchavusho wa wadudu ni mara nne zaidi ya vile...

9
Miradi ya Equator Wanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii Kenya UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) Empowered lives. Resilient nations.

Upload: tranbao

Post on 02-Mar-2019

239 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) · ya mchavusho wa wadudu ni mara nne zaidi ya vile vinavyozalishwa bila mchavusho (Gallai N. et al., 2009) . Katika utafiti uliofanyika

Miradi ya EquatorWanafijiji na Maendeleo Himili ya Jamii

Kenya

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)

Empowered lives. Resilient nations.

Page 2: UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) · ya mchavusho wa wadudu ni mara nne zaidi ya vile vinavyozalishwa bila mchavusho (Gallai N. et al., 2009) . Katika utafiti uliofanyika

MIRADI YA UNDP EQUATOR Kote duniani, jamiii zinazidi kubuni mbinu zinazonuiwa kuyakidhi mahitaji yao ya kila siku na ya kimazingira. Kuna kazi chache ambazo zimechapishwa za kuelezea kinagaubaga hizo mbinu bunifu na vile zilianzishwa,vile ziliathiri wakaaji wa sehemu mbali mbali na vile zimekuwa zikibadilika pindi wakati unapotita. Wachache wamejitokeza kuelezea wazi wazi juu ya miradi yao, na hata wale ambao wamefanya hivyo ni wakuu wa vijiji ambao wamefanya kuelezea kufaulu kwao.

Mradi huu wa Equator Katika unadhamiria kujaza hili pengo kama njia moja ya kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake. Masimulizi juu ya huu mradi ni baadhi tu ya mingi ambayo imefaulu na kushinda tuzo za Equator baada ya kukaguliwa na kutathiminiwa katika kitengo cha makundi ya kijamii yanayo hifadhi mazingira na kuinua maisha ya wanafijiji. Miradi hii inakusudiwa kuwa mifano ya kuiwa na kuwatia shime kuzungumzia ilivyofaulu ili kuhamasisha ulimwengu juu ya uhifadhi wa mazingira.

Bonyeza katika ramani ya miradi ya Equator ili upate kupata habari zaidi

WahaririMhariri Mkuu : Joseph CorcoranMuhariri Meneja : Oliver HughesWahariri Waliochangia : Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Erin Lewis, Whitney Wilding

Wahandishi Waliochangia Edayatu Abieodun Lamptey, Erin Atwell, Toni Blackman, Jonathan Clay, Joseph Corcoran, Larissa Currado, Sarah Gordon, Oliver Hughes, Wen-Juan Jiang, Sonal Kanabar, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Rachael Lader, Patrick Lee, Erin Lewis, Jona Liebl, Mengning Ma, Mary McGraw, Gabriele Orlandi, Juliana Quaresma, Peter Schecter, Martin Sommerschuh, Whitney Wilding, Luna Wu

Uchoraji Oliver Hughes, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Amy Korngiebel, Kimberly Koserowski, Erin Lewis, John Mulqueen, Lorena de la Parra, Brandon Payne, Mariajosé Satizábal G.

ShukraniEquator ingependa kuwashukuru wanachama wa Honey Care Africa na haswa mwongozo mchango wa Madison Ayer. Picha zote ni za Honey Care Africa, ramani ni za CIA World Factbook na Wikipedia. Masimulizi juu ya mradi huu yalitafsiriwa kwa Kiswahili na Dr. Ken Ramani.

Nukuu ZiadaUnited Nations Development Programme. 2012. Honey Care Africa, Kenya. Equator Initiative Case Study Series. New York, NY.

Page 3: UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) · ya mchavusho wa wadudu ni mara nne zaidi ya vile vinavyozalishwa bila mchavusho (Gallai N. et al., 2009) . Katika utafiti uliofanyika

3

UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA)Kenya

MAELEZO KUHUSU MRADI HUUHoney Care Africa ni mradi wa kijamii ambao unajishughulisha na mbinu za kuinua mapato ya wakulima wa mashinani nchini Kenya kwa njia ya ufugaji nyuki. Huku mradi huu ukizingatia utamaduni wa ufugaji nyuki nchini kama njia moja ya kuzalisha chakula na pia kujitafutia riziki, washikadau wana lengo la kuimarisha kiwango cha mapato miongoni mwa familia masikini kama njia moja ya kupambana na uwindaji haramu, ukataji miti kwa ajili ya mbao na uchomaji makaa. Kupitia kwa njia ya kuuza mizinga maalumu ya nyuki, mpango huu umeimarisha njia za kuisambaza kwa wakulima kwa kukubali kununua asali yao kwa bei wastani na hivyo kusaidia wafugaji kununua kwa wingi mizinga hii ya kipekee na kuimarisha na kupanua uzalishaji asali. Asali hiyo utengenezwa na kupakiwa kwa hali ya juu ya usafi na kuuzwa chini ya anwani: “Honey Care Africa” na “Beekeepers Delight”. Kiwango kikubwa cha faida inayotokana na bishara hii inagaiwa jamii 15,000 ambazo zinashiriki ufugaji wa nyuki kwa sasa.

MUHTASARIULISHINDA TUZO YA EQUATOR: Mwaka 2002

ULIANZISHWA: Mwaka 2000

ENEO: Mikoa saba kati ya minane nchini Kenya

WANAOFAIDIKA: Watu katika kaya 15,000

MAZINGIRA: Manufaa ya mchavusho

YALIYOMOHistoria na Mandhari 4

Majukumu Makuu na Ubunifu 5

Matokeo ya Kimazingira 6

Matokeo ya Kijamii 6

Matokeo ya Kisera 6

Jinsi ya Kudumisha Mradi Huu 7

Maono 7

Wahisani 8

Page 4: UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) · ya mchavusho wa wadudu ni mara nne zaidi ya vile vinavyozalishwa bila mchavusho (Gallai N. et al., 2009) . Katika utafiti uliofanyika

4

Mradi wa Honey Care Africa ulianzishwa mnamo mwaka 2000 kama shirika la kijamii ili kuimarisha na kukuza ufugaji wa nyuki miongoni mwa jamii mbali mbali mashariki mwa Afrika. Shirika hili hufanya kazi na wakulima wadogo miongoni mwa jamii za mashinani nchini Kenya kwa kuwapa misaada ya kifedha, mafunzo na ushauri ili kuwapa nguvu na uwezo wa kujiinua kutokana na umasikini unaowakumba. Kwa kuziwezesha familia kufuga nyuki na kuuza asali kwa mapato ya juu, mpangilio huu umesaidia Wakenya wengi wa mashambani kugundua mbinu zaidi za kujipatia riziki.

Ufugaji nyuki: raslimali ambayo imesahaulika

Mwanzoni, ufugaji wa nyuki ulichukuliwa kama njia ya kujipatia riziki kwa watu wanaoishi sehemu kame za Kenya. Hii dhana ilitokana na maamuzi ya wakazi wa maeneo haya kulingana na hali ya mazingira, utamaduni, na mienendo ya kijamii. Dhana hizi zimekuwa zikinawiri kufuatia misukumo mbali mbali inayotokana na Serikali pamoja na mipangilio mbali mbali ya Kimsingi, wale wanaoishi katika sehemu zenye mvua nyingi, udongo wenye rutuba, na hali ya hewa baridi walijisghulisha na kilimo cha mimea na mazao ya kuuza, huku wale wanaoishi katika sehemu kame na sizizo na rutuba waliamua kufuga wanyama na kuhamahama kutoka sehemu moja hadi nyingine wakiwatafutia maji na malisho. Wengine katika sehemu kame walijishughulisha na ukuzaji wa mimea ambayo inahimili kiangazi huku wakifuga nyuki kama njia mbadala ya kuzalisha chakula.

Baada ya uhuru wa Kenya, serikali na mashirika yalihimiza watu kuendelea na mtindo huo huo wa ufugaji katika sehemu kame huku sehemu zenye mvua zikihimizwa kukuza mimea kwa ajili ya chakula na mapato ya kifedha. Mashirika ya kimataifa yalionekana yakisisitiza mpangilio wa zamani badala ya kuhimiza watu walioishi katika sehemu zenye mvua kushiriki katika mbinu mbadala kama vile ufugaji nyuki kwa ajili ya asali. Kwa hiyo, ufugaji nyuki na usalishaji asali ulinasibishwa na sehemu kame kama vile Ukambani.

Ni wazi kwamba sehemu ambazo zina uwezo wa kuzalisha asali ncini Kenya hazijahusishwa wala kutumika ipasavyo. Hali hii imekuwa mbaya kwa sababu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki hazijakumbatiwa na wakazi wa maeneo yanayoshughulikia ufugaji. Pia kunahitajika elimu kwa wafugaji ambayo itawawezesha kutumia mbinu mpya za ufugaji. Kwa sasa, wafugaji wengi nchini Kenya wanatumia mbinu za zamani ambapo mizinga ya zamani na mbinu za kuvuna asali kwa

kutumia moshi zinatumika badala ya ile ya kisasa. Mashirika mbali mbali yameshindwa kuhimiza mbinu za kisasa za kuzalisha asali, jambo linaloashiria kwamba utafiti katika sekta hii ni wa hali ya chini sana.

Mpangilio wa kufaidi wote

Mradi wa Honey Care Africa ulianzishwa na wafanyibishara watatu ambao ni Wakenya ili kuziba pengo hili la kushirikiana kati ya jamii na wafadhili wa kimataifa na mashirika ya kibinafsi.Wakulima hupewa mikopo midogo kununua mizinga ya kisasa na ya hali ya juu inayotengenezwa na Honey Care. Baadaye wakulima hao hupewa mafunzo bora kuhusu ufugaji wa nyuki na uzalishaji wa asali wa hali ya juu.

Mradi huu pia huwatafutia wafugaji nyuki soko ya asali kwa bei inayofaa. Honey Care huchukua asali kutoka kwa wafugaji na kuwalipa wakulima papo hapo, huitengeneza na kuipakia na kuitafutia soko kwa kuiuza katika maduka ya jumla nchini huku wakipata faida kidogo.

Asali hiyo ambayo inauzwa kwa anwani mbili za “Honey Care Africa” na “Beekeeper’s Delight” imejulikana kote eneo la Afrika Mashariki na imekubalika katika masoko ya eneo hilo. Kufikia sasa, mradi huu wa Honey Care umewafaa takriban watu 75,000 katika sehemu zenye umasikini mkubwa nchini Kenya. Mazingira pia yametunzwa kupitia kwa njia ya kutunza miti ili kufuga nyuki.

Mfano wa kimataifa ulitia fora

Biashara hii imefanikiwa kwa kupata msukumo kutoka kwa mashirika ya kibinafsi na wafadhili ambao wameungana na wenyeji kuleta maendeleo na kuhifadhi mazingira. Muungano huo umetambuliwa kwa manufaa yake nchini Kenya na mataifa mengine kote ulimwenguni. Muungano huo umepata sifa na hata kutuzwa na mashirika kama vile Benki ya Dunia na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP). Mnamo 2004, mpango Honey Care ulipeleka huduma zake nchini Tanzania, ikitumia mkopo kutoka kwa Kampuni ya Mikopo ya Kimataifa (AFC). Mipango ya shirika hili ni pamoja na kutafuta soko katika sehemu za mabanda katika miji mbali mbali.

Historia na Mandhari

“Mabadiliko ya hali ya anga na matokeo yake kwa kilimo ni janga kuu kwa kwa wakulima wadogo eneo la Afrika Mashariki – ni janga kuu kwa vile linahusu maisha ya binadamu. Jamii zimeenzi

ufugaji nyuki kama njia moja ya kujitarazaki.” Madison Ayer, CEO, Honey Care Africa

Page 5: UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) · ya mchavusho wa wadudu ni mara nne zaidi ya vile vinavyozalishwa bila mchavusho (Gallai N. et al., 2009) . Katika utafiti uliofanyika

55

Majukumu Makuu na Ubunifu

Majukumu manne makuu ya Honey Care ni pamoja na utengenezaji wa mizinga ya nyuki ya hali ya juu aina ya “Langstroth” ambayo husambaza katika jamii za mashambani, kutoa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa wenyeji na mawaidha ya kimsingi kuhusu ufugaji huo, kununua asali inayovunwa na wafugaji kwa bei bora na kutengeneza na kuuza asali hiyo. La muhimu katika njia hii yote ni kuiboresha asali, kuinua hali ya maisha kwa familia husika na kuwaelimisha umuhimu wa kuhifadhi na kuendeleza mazingira. Kwa vile ufugaji nyuki haukuwa jambo geni kwa wenyeji, vifaa vya ufugaji kwa mazao ya hali ya juu, ujuzi na elimu pamoja na soko ya asali hazikuwapo kwa wingi mnamo mwaka 2000. Katika hali hii, Honey Care huwapa wafugaji mbinu za kufuga nyuki, jinsi ya kuhakikisha kwamba asali inayotengenezwa ni ya hali ya juu, kutafuta soko na mafunzo kuhusu matumizi ya pesa na jinsi ya kupata mapato makubwa.

Mtindo mpya wa kuzalisha asali ya hali ya juu kupitia kwa mpango wa pamoja unaodhamiria kuhifadhi mazingira na wanaowaletea wenyeji mapato umefanikiwa kwa vile kulikuwa na misingi ya ufugaji wa nyuki katika jamii za Kenya. Mbinu za kitamaduni zilitumia mizinga ambayo iliundwa kutokana na miti au vyungu au mizinga duni. Kwa kawaida, kuvuna asali kulisababisha vifo vya nyuki wengi na kuacha moshi kwa asali. Mradi wa Honey Care ulianza kutengeneza mizinga ya kisasa ya Langstroth, ambayo inaweza kubomolewa na kuondoa asali kwa utaratibu bila ya kutawanya nyuki. Njia hii pia huchukua muda mfupi sana kuvuna asali kwa wiki ikiwa ni kati ya dakika 5 na 10. Kwa kuwahakikishia wafugaji soko, Honey Care imewapa motisha ili washiriki kwa wingi katika njia hii mpya ya uzalishaji mali.

Ushirikiano

Mafanikio ya mradi huu wa Honey Care yametokana na ushirikiano mkuu na mashirika mbali mbali huku lengo kuu likiwa ni kuwanufaisha Wakenya milioni 25 masikini ambao wanaishi mashinani. Hadi leo, mpango huu umeshirikisha makundi mbali mbali katika wilaya za Kitui na Taita Taveta huku yakipata msaada kutoka kwa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA) na Wizara ya Ufugaji na Uvuvi ya serikali ya Kenya. Mashirika mengine ambayo yanasaidia mradi huu ni kama Aga Khan Foundation kupitia kwa mpango wa Coastal Rural Support Programme ulioko wilaya ya Kwale; mpango wa kufuga nyuki na kuhifadhi mazingira katika msitu wa Kakamega kupitia kwa Community Action for Rural Development (CARD); na mipango minine mingi katika hifadhi ya wanyama pori ya Mlima Kenya na mpango wa kuhifadhi misitu uliogharamiwa na shirika la Global Environment (GEF). Pia kunao mpango wa kukopesha mizinga ya nyuki katika mikoa ya Nyanza, Magharibi, Rift Valley kupitia kwa K-Rep Development Agency (KDA), Africa Now, na IFC.

Mradi wa Honey Care pia hushirikiana na makundi madogo madogo, makundi ya wanawake na yale ya vijana ili kutoa huduma zao kwa wale wanaozihitaji. Kufikia sasa, zaidi ya 15,000 watu wameingia katika ufugaji nyuki. Idadi hii inasimamia karibu watu 75,000 ambao hutegemea ufugaji nyuki.

Page 6: UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) · ya mchavusho wa wadudu ni mara nne zaidi ya vile vinavyozalishwa bila mchavusho (Gallai N. et al., 2009) . Katika utafiti uliofanyika

6

MatokeoMATOKEO YA KIMAZINGIRAUfugaji wa nyuki una manufaa mengi kwa mazingira. Miradi ya Honey Care kila mara hulenga kupunguza visa vya uharibifu wa mazingira. Mpango huu umefanikiwa kupunguza visa hivi na kuimarisha mzingira bora kupitia maafisa wa mashinani.

Ukataji miti umekomeshwa

Mpango huu wa Honey Care hutoa fedha za matumizi kwa jamii husika ili wasijishughulishe na visa vy uharibifu wa mazingira kwa njia ya kukata miti kwa ajili ya kuchoma makaa. Mafunzo kuhusu ufugaji nyuki husisitiza umuhimu wa mazingira bora. Kupitia kwa mpango wao wa “Bees for Trees” yaani nyuki kwa miti, mradi huu unmetoa mizinga na vifaa vingine kwa wafugaji kwa makubaliano ya kutunza misitu na kupanda mingine ambapo mizinga hiyo itahifadhiwa.

Manufaa ya mchavusho kwa kilimo na mazingira

Ni dhahiri kuwa nyuki husaidia kwa kiasi kikubwa katika mchavusho (pollination) wa mazingira. Faida zinazotokana na mchavusho huonekana katika mazao ya vyakula na mimea mingine. Mnamo 2005, makadirio ya manufaa ya mchavusho kutokana na wadudu hasa nyuki ulimwenguni yalikuwa karibu dola za Amerika billioni 208. Hii ilikuwa karibu asilimia 9.5 ya vyakula vyote vilivyozalishwa ulimwenguni wakati huo. Ubora wa vyakula vinavyozalishwa kwa njia ya mchavusho wa wadudu ni mara nne zaidi ya vile vinavyozalishwa bila mchavusho (Gallai N. et al., 2009) . Katika utafiti uliofanyika nchini Kenya, faida zinazotokana na uchavusho ni asilimia 40 kutokana na mauzo ya mazao hayo (Kasina et al., 2009) . Faida hii inatokana na mazao ya kila mara ya kiwango na hali ya juu. Mimea kama malenge haiwezi kuzaa matunda bila mchavusho.

Mradi wa Honey Care umejaribu kukusanya habari kuhusu umuhimu wa ufugaji nyuki kupitia kwa maafisa wake walio mashinani. Kufikia sasa zaidi ya mizinga 30,000 imenasa nyuki wenye asili ya Kenya ambao ndio wanalengwa na mpango huu Honey Care. Hatua hii inalenga kupunguza uwezekano wa athari za kuleta nyuki kutoka nchi zingine. Miongoni mwa jamaa wanaofuga nyuki, 3,500 huishi katika maeneo kame na hivyo kurahisisha kazi ya ufugaji nyuki chini ya mradi huu kutokana na ujuzi walio nao wenyeji. Kwa vile wakulima sasa wana njia mbadala ya kupata riziki, ukataji miti kwa ajili ya kuchoma makaa umepungua kiasi kikubwa. Mizinga 5,000 inapatikana katika msitu wa kilomita tatu, mbuga za wanyama pori au sehemu tambarare ambapo wanahitajika kufugwa kwa njia ya kawaida. Kwa upande wa mimea, kumekuwa na uimarishaji kilimo kwa kati ya asilimia 15 na 30, huku mazao yakiongezeka kwa zaidi ya asilimia 100.

MATOKEO YA KIJAMIIMradi wa Honey Care kwa sasa unashirikiana na mikoa saba kati ya mikoa minane nchini Kenya na limeendeleza huduma zake kwa nchi jirani za Malawi, Tanzania, na Sudan Kusini. Nchini Kenya, wafugaji waliopata huduma hizi ni karibu 75,000, wote wakiwa ni wenyeji ambao wanaishi mashinani. Waliofaidika kutokana na mradi huu mnamo mwaka wa 2010 ni 32,250 ambao asilimia 43 ni wanawake.Mapato ya kila familia ambayo inashiriki mpango huu wa Honey Care ni dola za Amerika 250. Mapato haya hutokana na asali ambayo huuzwa katika soko mbali mbali na mapato yanayotokana na mavuno ya vyakula mbabi mbali yaliyoongezeka kutokana na mchavusho. Utafiti unaonyesha kuwa wakulima hutumia asilimia 33 ya mapato yao kutoka kwa asali kwa chakula na dawa, asilimia 25 kwa mbolea na mbegu, asilimia 18 kwa ada za elimu, asilimia 10 kwa nyumba na makao, na asilimia 5 biashara mbali mbali.

MATOKEO YA KISERAMradi wa Honey Care hujishughilisha na watu wa mashinani hata kama kwenye baadhi ya mipango umeshirikiana na Serikali ya Kenya. Kundi hili limenasibishwa na maendeleo ya kijamii na shirika la kukadiria ubora wa bidhaa nchini (Kenya Bureau of Standards). Kwa hiyo, kundi hili limetuzwa “Kenya Quality Award” katika kiwango cha bishara ndogo na za wastani mnamo mwaka wa 2004.

Shirika hili lilikuwa mojawapo ya mashirika anzilishi ya Kenya Honey Council mnamo 2003. Linawakilisha wahisani wakuu katika ufugaji nyuki nchini Kenya. Liliundwa kama shirika kuu la kuwezesha washikadau kukuza na kuendeleza malengo yao. Malengo mengine makuu ni pamoja na kukuza na kupanua ufugaji nyuki nchini Kenya, kuelimisha wananchi kuhusu manufaa ya asali na nyuki kwa jumla na kuhakikisha kwamba bidhaa zinazotokana na ufugaji nyuki ni za hali ya juu kwa kutoa mafunzo yanayohitajika, kwa wakulima na hata wanaotumia bidhaa hizo. Maazimio yao pia ni kujadiliana na Serikali ya Kenya ili kuibua sheria zinazostahili katika sekta hii. Pia, hujadiliana na serikali za mataifa mengine kutoa mwongozo bora wa biashara ya bidhaa zinazotoka nchini Kenya.

Shirika hili la Honey Care lingali likiunda muungano wa mashirika ya kibinafsi na serikali ili kukuza ufugaji nyuki wa kiasi kikubwa nchini Kenya. Mpango huo unaendelea kutumika katika maeneo mbali mbali nchini hasa maeneo ambayo yanafuga nyuki ambapo wakulima hupata mikopo inayojulikana kama “Asali Loan” kwa usaidizi wa wahisani kama vile Benki ya Equity. Kutoa mafunzo kwa maafisa wasaidizi mashinani kpitia kwa wizara ya Ufugaji na kituo cha ufugaji wa nyuki.

Page 7: UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) · ya mchavusho wa wadudu ni mara nne zaidi ya vile vinavyozalishwa bila mchavusho (Gallai N. et al., 2009) . Katika utafiti uliofanyika

7

Jinsi ya Kudumisha Mradi HuuJINSI YA KUDUMISHA MRADI HUUKwa miaka saba ambayo shirika la Honey Care limedumu, limekuwa shirika la manufaa kwa wengi. Mpango wa Honey Care unajikita katika misingi ya kuhimiza mbinu za uzalishaji mali ambazo zinahifadhi mazingira ambayo inaweza kudumu.Mpango huu unahakikisha kwamba kila mmoja wa washiriki anatoa mchango wake wa kimawazo. Kila mshiriki hufaidika kwa kushiriki kikamilifu.Wafuga nyuki mashinani huona manufaa ya uzalishaji asali ya hali ya juu, na manufaa mengine yanayotokana na shughuli zingine za kilimo mbali na ufugaji nyuki.

Mradi huu wa Honey Care hupata faida kutokana na ujuzi wao wanaoutumia wakati unahitajika. Asali iliyosafishwa huleta faida kubwa kwa washiriki wote katika uzalishaji na usafishaji wa asali na wale wanaouza bidhaa hizo. Mashirika wafadhili ambao hushirikiana na Honey Care katika ufugaji wa nyuki hufaidika kutokana na maendeleo haya ya kila wakati. Watu wengine pia hunufaika kutokana na ufugaji wa nyuki kwa njia ya mazingira bora.

Shirika la Honey Care huchukua jukumu la uongozi katika mashirika mbali mbali katika biashara hii. Washiriki wengine husaidia katika kuwainua washiriki kifedha kwa njia ya mikopo kwa wakulima ili kuanzisha mbinu hizi mpya za ufugaji wa nyuki. Hata kama wakulima hupata faida na kujitegemea, kuna wakati fulani ambapo wanahitaji pesa za kuwasaidia kuinua zaidi bishara yao. Mashirika wafadhili walio na ofisi katika maeneo mbali mbali pia husaidia. Honey Care kuwafikia wakulima wa mashinanii, na hivyo kupunguza gharama ya kupeleka huduma kwao.

MAONO Honey Care inaendelea kuungana na wahisani wengine kwa madhumuni ya kueneza habari na kuhimiza Wakenya kwamba ufugaji nyuki ni njia muhimu ya kujipatia riziki. Kuanzisha biashara hiyo huwa ni vigumu wakati mwingine kwa sababu ya ukosefu wa fedha kwa wakulima wengi wa mashambani. Shirika lenyewe linahitaji fedha za kuwahamazisha wakulima kuhusu mbinu mpya za ufugaji, kuyakusanya makundi ambayo yanahusika katika ufugaji nyuki, kuwapa mafunzo, vifaa na maafisa wa kuwaelekeza jinsi ya kutumia vifaa hivyo. Shirika hili pia linajishughulisa na mafunzo ya mbinu za kuvuna asali mahali ambapo inapokelewa na malipo. Honey Care pamoja na washirika wa serikali, mashirika ya kiserikali hutoa fedha za kuanzisha biashara hii. Ufugaji nyuki ni bisahara ambayo inapanuka kwa kasi baada ya misingi bora kuwekwa. Hii ni kwa sababu kuna wafanyakazi katika sekta hii, ardhi ndogo inayohitajika na kuwepo nyuki ambao hawanunuliwi.Wahisani wa kibinafsi huchangia kwa kuwasaidia wakulima kupanua biashara yao.

Shirika la Honey Care limeshiriki katika miradi mbali mbali ya ufugaji nyuki nchini Kenya, Tanzania, Malawi na Sudan Kusini. Miradi yake mikubwa, hata hivyo imo nchini Kenya. Honey Care Africa Tanzania, ilianzishwa 2005, na imekua hata kiwango cha shirika kubwa zaidi la kuzalisha na kuuza asali katika nchi zingine. Biashara hii nchini Kenya na Tanzania imeendelezwa sambamba, kila moja ikishughulikia changamoto zake kivyake. Lakini kwa sasa nchi hizo zinafanya bishara hii kwa ukuruba mkuu zikiwa na lengo la kuunganisha miradi yao ili kuunda ushirikiano wa kusambaza bidhaa zao katika eneo lote

Page 8: UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) · ya mchavusho wa wadudu ni mara nne zaidi ya vile vinavyozalishwa bila mchavusho (Gallai N. et al., 2009) . Katika utafiti uliofanyika

la Afrika Mashariki. Huku Kenya na Tanzania zikiwa nchi anzilishi za mradi huu, kuna mipango ya kujumuisha mataifa mengine ya Afrika Mashariki ili kuanzisha umoja wa ufugaji nyuki eneo zima.

Changamoto kuu ambayo inatarajiwa katika muungano mkuu wa aina hiyo ni jinsi ya kuwashrikisha wahusika wote katika eneo hilo pana. Sheria za ufugaji nyuki hutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine; pia kuna njia mbali mbali ambazo jamii tofauti zinalichukulia suala kama hilo. Washirika tofauti pia wana tofauti zao wenyewe kwa jinsi ambavyo yanatoa misaada na pia malengo yao makuu ambayo yanaambatahnishwa na ufadhili wao. Hata hivyo, kudumu kwa ufugaji nyuki kama njia moja ya uzalishajia mali utategemea pakubwa washiriki kutoka upande wa serikali na wafadhili ili kuweka misingi inayohitajika kwa wakulima kufuga nyuki. Mashirika ya kibinafsi yanahitajika kutoa misaada itakayowawezesha wakulima kupanua biashara yao.

WAHISANIWahisani wa Serikali na Mashirika ya Kiserikali• Wizara ya Ufugaji (Kenya)• Kituo cha Kufuga Nyuki (Kenya)• Wizara na Viwanda (Kenya)• Wizara ya Misitu na Wanyamapori (Kenya)• Wizara ya Misitu na Ufugaji Nyuki (Tanzania)

Mashirika ya Maendeleo• DANIDA / Serikali ya Kenya• Swiss Contact & Swiss Development Corporation• Belgian Technical Cooperation (BTC)/Wizara ya Mazingira na

Mali Asili• DFID, Dorcas Aid and Mama Mzungu Foundation• UNDP (GEF)• EU, DFID, Soros Foundation & World Bank (SME) • U.S. Ambassador’s Fund• Ubalozi wa Uingereza• Ubalozi wa Ujerumani• Ubalozi wa Finland • Swedish International Development Agency (SIDA)

Mashirika yasiyo ya Kiserikali• Aga Khan Foundation• Community Action for Rural Development (CARD) • German Agro Action• World Vision• Action Africa Help International (AAHI)• Wildlife Society for Protection of Animals (WSPA)• Biodiversity Conservation Programme (BCP)• Rotary Club of Stroud (UK) and Rotary Club of Hurlingham• Farm Africa• Africa Now

Sekta ya Kibinafsi• Kakuzi Ltd.• Business Alliance Against Chronic Hunger (BAACH)• Equity Bank• Bidco

8

Page 9: UKUZAJI WA ASALI AFRICA (HONEY CARE AFRICA) · ya mchavusho wa wadudu ni mara nne zaidi ya vile vinavyozalishwa bila mchavusho (Gallai N. et al., 2009) . Katika utafiti uliofanyika

Masimulizi kuhusu miradi mingine, bonyeza hapa:

Equator InitiativeEnvironment and Energy GroupUnited Nations Development Programme (UNDP)304 East 45th Street, 6th Floor New York, NY 10017Tel: +1 646 781-4023 www.equatorinitiative.org

Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ndio unaoendesha miradi ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni kwa kutoa mwito wa mageuzi na kuelekeza mataifa kwa maarifa, na malighafi ili kusaidia watu kujiimarisha kimaisha.

Mradi huu wa Equator huleta pamoja Umoja wa Mataifa , serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, wafanyibiashara na makundi ya mashinani ili kutambua na kuimaliza maendeleo himili kwa watu na jamii kwa jumla.

©2012 Haki Zote ni za Mradi wa Equator

MAREJELEO YA ZIADA

• Jiwa, F. 2003. Honey Care Africa’s tripartite model: an innovative approach to sustainable beekeeping in Kenya. XXXVIII Congress APIMON-DIA, Ljubljana, Slovenia. http://www.apimondia.com/apiacta/slovenia/en/jiwa.pdf

• Gallai N, Salles JM, Settele J, Vaissière BE, 2009. Economic valuation of the vulnerability of world agriculture confronted to pollinator decline. Ecological Economics (68), 810-821

• Kasina M., J. Mburu, M. Kraemer and K. Holm-Müller. 2009. Economic benefit of crop pollination by bees: A case of Kakamega small-holder farming in western Kenya. Journal of Economic Entomology, 102 (2): 467-473