ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona...ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona...

7
https://covid-no-mb.org Adopted from COVID-19 myth busters compiled by the World Health Organization (WHO) Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona (maelezo kutoka WHO) 1. Kukaa juani au mahali penye nyuzijoto zaidi ya sentigredi 25 HAKUWEZI kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya korona (covid-19). 2. Unaweza kupona ugonjwa wa virusi vya korona (COVID-19). Kupata virusi vipya vya korona HAKUMAANISHI kwamba utakuwa navyo katika maisha yako yote. 3. Kuwa na uwezo wa kuzuia pumzi yako kwa sekunde 10 au zaidi bila kukohoa au kujisikia vibaya HAINA maana kuwa huna ugonjwa unaosababishwa na virusi vya korona (COVID-19) au ugonjwa mwingine wowote wa mapafu. Swahili

Upload: others

Post on 18-Jul-2020

13 views

Category:

Documents

0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona...Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona (maelezo kutoka WHO) 1. Kukaa juani au mahali penye nyuzijoto zaidi ya sentigredi 25 HAKUWEZI

https://covid-no-mb.orgAdopted from COVID-19 myth busters compiled by the World Health Organization (WHO)

Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona(maelezo kutoka WHO)

1. Kukaa juani au mahali penye nyuzijoto zaidi ya sentigredi 25 HAKUWEZI kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya korona (covid-19).

2. Unaweza kupona ugonjwa wa virusi vya korona (COVID-19). Kupata virusi vipya vya korona HAKUMAANISHI kwamba utakuwa navyo katika maisha yako yote.

3. Kuwa na uwezo wa kuzuia pumzi yako kwa sekunde 10 au zaidi bila kukohoa au kujisikia vibaya HAINA maana kuwa huna ugonjwa unaosababishwa na virusi vya korona (COVID-19) au ugonjwa mwingine wowote wa mapafu.

Swahili

Page 2: Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona...Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona (maelezo kutoka WHO) 1. Kukaa juani au mahali penye nyuzijoto zaidi ya sentigredi 25 HAKUWEZI

https://covid-no-mb.orgAdopted from COVID-19 myth busters compiled by the World Health Organization (WHO)

Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona(maelezo kutoka WHO)

4. Unywaji wa pombe HAUWEZI kukukinga dhidi ya COVID-19 na unaweza kuwa hatari.

5. Virusi vya korona COVID-19 VINAWEZA kuambukizika katika maeneo yenye hali ya hewa ya joto na yenye unyevu.

6. Hali ya hewa yenye baridi na theluji/barafu HAIWEZI kuua virusi vipya vya korona.

7. Kuoga kwa maji ya moto HAKUSAIDII kukukinga kupata virusi vipya vya korona.

Swahili

Page 3: Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona...Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona (maelezo kutoka WHO) 1. Kukaa juani au mahali penye nyuzijoto zaidi ya sentigredi 25 HAKUWEZI

https://covid-no-mb.orgAdopted from COVID-19 myth busters compiled by the World Health Organization (WHO)

Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona(maelezo kutoka WHO)

8. Virusi vipya vya korona HAVIWEZI kuambukizwa kwa kuumwa na mbu.

9. Mashine za kukausha mikono HAZINA uwezo wa kuua virusi vipya vya korona.

10. Kujinyunyizia pombe au klorini katika mwili wako wote HAKUWEZI kuua virusi vipya vya korona.

11. Chanjo dhidi ya nimonia HAIKUKINGI dhidi ya virusi vipya vya korona.

Swahili

Page 4: Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona...Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona (maelezo kutoka WHO) 1. Kukaa juani au mahali penye nyuzijoto zaidi ya sentigredi 25 HAKUWEZI

https://covid-no-mb.orgAdopted from COVID-19 myth busters compiled by the World Health Organization (WHO)

Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona(maelezo kutoka WHO)

12.Kusafishapuayakokwamajiya chumvi mara kwa mara HAKUSAIDII kukukinga na maambukizo ya virusi vipya vya korona.

13. Kula vitunguu saumu HAKUSAIDII kukinga maambukizo ya virusi vipya vya korona.

14. Je, taa ya ultravioleti (UV) inayoua viini vya magonjwa inaweza kuua virusi vipya vya korona?

Taa ya UV haipaswi kutumiwakusafishamikonoau sehemu nyingine ya ngozi kwani mionzi ya UV inaweza kusababisha kuwasha kwa ngozi.

Swahili

Page 5: Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona...Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona (maelezo kutoka WHO) 1. Kukaa juani au mahali penye nyuzijoto zaidi ya sentigredi 25 HAKUWEZI

https://covid-no-mb.orgAdopted from COVID-19 myth busters compiled by the World Health Organization (WHO)

Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona(maelezo kutoka WHO)

15. Je, themo skana (skana yamafua) ina ufanisi gani katika kugundua watu walioambukizwa virusi vipya vya korona?

Themo skana ina ufanisi katika kugundua watu wenye homa (yaani homa kali) inayosababishwa na maambukizi ya virusi vipya vya korona. Lakini haiwezi kugundua watu ambao wameambukizwa ambao bado hawajaanza kuugua na kupata homa, kwa sababu dalili za ugonjwa na homa kali kwa watu walioambukizwa virusi vya korona huanza kuonekana kati ya siku 2 hadi 10.

Swahili

Page 6: Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona...Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona (maelezo kutoka WHO) 1. Kukaa juani au mahali penye nyuzijoto zaidi ya sentigredi 25 HAKUWEZI

https://covid-no-mb.orgAdopted from COVID-19 myth busters compiled by the World Health Organization (WHO)

Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona(maelezo kutoka WHO)

16. Je, virusi vipya vya korona vinaambukizika kwa wazee pekee, au je vijana pia wanaambukizwa?

Hapana! Watu wa umri wowote wanaweza kuambukizwa virusi vipya vya korona (2019-nCoV).

17. Je, kiuavijasumu (antibiotiki) ina uwezo wa kukinga au kutibu virusi vipya vya korona?

Hapana! Kiuavijasumu au antibiotiki haiwezi kutibu virusi, isipokuwa vijidudu vya bakteria tu.

Swahili

Page 7: Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona...Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona (maelezo kutoka WHO) 1. Kukaa juani au mahali penye nyuzijoto zaidi ya sentigredi 25 HAKUWEZI

https://covid-no-mb.orgAdopted from COVID-19 myth busters compiled by the World Health Organization (WHO)

Ukweli juu ya tetesi kuhusu virusi vya korona(maelezo kutoka WHO)

18. Je, kuna dawa yoyote maalumu ya kukinga au kutibu virusi vipya vya korona?

Kwa sasa hakuna dawa maalumu ambayo imehakikishwa kuwa inaweza kukinga au kutibu virusi vipya vya korona.

Swahili

COVID19 Myth Busters in World Languages

· Maintained by ICU Linguistics Lab and Dr. Seunghun J. Lee in Tokyo, Japan.· Translated by Daisuke Shinagawa & Chrispina Alphonse.· Designed and illustrated by Daehan Won of Studio C-clef in Seoul, Korea.