umuhimu wa umwagiliaji katika uzalishaji wa mboga … aina gani ya umwagiliaji tunakutana nao?....

8
OKTOBA - DISEMBA, 2017 #6 Nakala ya bure Umuhimu wa umwagiliaji katika uzalishaji wa mboga mboga kibiashara Umwagiliaji ni jambo muhimu sana linalohitajika katika uzalishaji wa mboga mboga kibiashara. Pamoja na soko, mbegu bora na utunzaji mzuri wa mazao, upatikanaji wa maji na udhibiti wake unaleta mabadiliko katika biashara ya mboga mboga. Ni vyanzo gani vya maji vinapatikana Tanzania? . Wakulima wengi hupata maji kutoka kwa mamlaka zao za mitaa hasa kwa njia ya mifereji. Kwa mfano, hili ni kawaida katika mashamba binafsi katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha. . Wakulima hutumia mito midogo na mikubwa kwa umwagiliaji. Ambapo mito ni ya msimu, wakulima huchimba mashimo kwenye ukingo wa mto ili kupata maji. Hii ni ya kawaida katika maeneo ya Dodoma, Morogoro, Mwanza, Shinyanga na Tabora. . Ambapo kuna mabwawa na maziwa wakulima hutumia vyanzo hivi vikubwa vya asili au vya kutengeneza kwa kuyavuta maji moja kwa moja kutoka ziwani au kulima pembezoni mwa vyanzo hivo, hii ni katika maeneo kama Mkoa wa Mwanza, Kikore na Iringa. . Kuchimba visima vya mkono au mashine ni muhimu kwa uzalishaji wa mboga mboga. Visima hivi vinaweza kumililikiwa na jumuiya au mtu binafsi. . Wakulima wengine hutegemea maji ya mvua kwa umwagiliaji, hasa wakati wa mvua za masika. 1 Umwagiliaji kwa njia ya matone katika shamba mkoani Karatu Ikiwa rasilimali zinapatikana, ni bora kutumia umwagiliaji kwa njia ya matone kwa mavuno mengi, yenye ubora na ufanisi

Upload: phungtuong

Post on 09-Mar-2018

693 views

Category:

Documents


46 download

TRANSCRIPT

OKTOBA - DISEMBA, 2017 #6

Nakala ya bure

Umuhimu wa umwagiliaji katika uzalishaji wa mboga mboga kibiasharaUmwagiliaji ni jambo muhimu sana linalohitajika katika uzalishaji wa mboga mboga kibiashara. Pamoja na soko, mbegu bora na utunzaji mzuri wa mazao, upatikanaji wa maji na udhibiti wake unaleta mabadiliko katika biashara ya mboga mboga.

Ni vyanzo gani vya maji vinapatikana Tanzania? . Wakulima wengi hupata maji kutoka kwa mamlaka zao za mitaa hasa kwa njia ya mifereji. Kwa mfano, hili ni kawaida katika mashamba binafsi katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

. Wakulima hutumia mito midogo na mikubwa kwa umwagiliaji. Ambapo mito ni ya msimu, wakulima huchimba mashimo kwenye ukingo wa mto ili kupata maji. Hii ni ya kawaida katika maeneo ya Dodoma, Morogoro, Mwanza, Shinyanga na Tabora.

. Ambapo kuna mabwawa na maziwa wakulima hutumia vyanzo hivi vikubwa vya asili au vya kutengeneza kwa kuyavuta maji moja kwa moja kutoka ziwani au kulima pembezoni mwa vyanzo hivo, hii ni katika maeneo kama Mkoa wa Mwanza, Kikore na Iringa.

. Kuchimba visima vya mkono au mashine ni muhimu kwa uzalishaji wa mboga mboga. Visima hivi vinaweza kumililikiwa na jumuiya au mtu binafsi.

. Wakulima wengine hutegemea maji ya mvua kwa umwagiliaji, hasa wakati wa mvua za masika.

1

Umwagiliaji kwa njia ya matone katika shamba mkoani Karatu

Ikiwa rasilimali zinapatikana,

ni bora kutumia umwagiliaji kwa

njia ya matone kwa mavuno mengi, yenye ubora na

ufanisi

Ni aina gani ya umwagiliaji tunakutana nao?. Umwagiliaji kwa njia za asili kutoka kwenye mirefeji au mabonde: Njia hii ikiwa ni ya kawaida kutokana na mfumo wa upatikanaji maji (mifereji ya maji), hupoteza maji mengi kupitia kuingia ardhini na uvukizi na mazao hayawezi kukua kwa usawa.

. Wakulima hutumia ndoo na kikombe, hasa kwenye udongo kichanga kama vile Bagamoyo. Kuchota maji kutoka kwenye mfereji na kumwagilia juu ya tuta ni kawaida kwa maeneo kama Ilemala, Mwanza. Kwa bahati mbaya,vitendo hivi ni kazi kubwa sana na huleta upotevu wa maji.

. Umwagiliaji wa Sprinkila: Maji yananyunyizwa kwa msukumo wa juu kutoka kwenye bomba na mfumo wa Sprinkila. Pampu yenye nguvu na mfumo wa bomba vinahitajika. Njia hii ina hasara: unyevu mwingi hupotezwa kwa upepo na uvukizi, na unyevu wa majani kwa muda mrefu husababisha magonjwa.

. Umwagiliaji kwa njia ya matone ni wa gharama nafuu na wenye matokeo mazuri. Kila tundu hutoa kiasi sawa cha maji na hivyo kuna usawa wa umwagiliaji. Matundu haya hupunguza upotevu wa maji kwa kumwagilia moja kwa moja usawa wa mizizi ambako maji huletwa kwenye mmea wenyewe. Kuna faida nyingine ya nyongeza ya kunyweshea mbolea kwa kutumia njia ya matone (fertigation).

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine mwaka 2016 ulionesha uchambuzi wa gharama-faida wa njia za umwagiliaji:

Uchambuzi wa gharama/faida wa nyanya kwa kutumia njia tofauti za umwagiliaji

Njia ya umwagiliaji Gharamaza kudumu

Gharama zamuda/Ekari

Gharama ya jumla

Mapato Faida Uwiano(Faida /gharama ya jumla)

Mfereji 0 2,267,000 2,267,000 3,040,000 773,000 0.34

Pampu na mpira 360,000 2,887,000 3,237,000 4,960,000 1,713,000 0.59

Umwagiliaji kwa njia ya matone + pampu 4,500,000 4,192,000 8,692,000 17,440,000 8,748,000 1.01

Umwagiliaji kwa njia ya matone + Kisima 9,800,000 4,192,000 13,992,000 17,440,000 3,448,000 0.25

*Mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone hudumu kwa muda wa miaka 3-5

Unatambua njia za kuhifadhi maji? . Ni muhimu kuhifadhi maji kwa kutumia matenki au mabwawa. Tandaza kwenye mabwawa nyenzo ambazo hazipitishi maji ili kuzuia kupoteza maji kwa kuzama ardhini.

. Kuhifadhi maji ya mifereji katika mabwawa au matenki inaweza kuwa njia ya kuvuna maji, ambayo hasa inamaanisha kuvuna maji ya mvua kwa matumizi ya baadaye. Hii ni kawaida kwa nchi kama Botswana ambapo mvua / maji hayapatikani kwa urahisi. Hata hivyo, kila mtu lazima azingatie uhitaji wa maji ya mazao, ambao unaweza kuwa 3-4 mm (au 1-2 inch) kwa siku. Kwa ekari moja mahitaji ya kila siku ni takribani lita 15.000 au 15 m3.

. Matumizi ya matandazo (kama ya majani) yatapunguza upotevu wa unyevu kutokana na uvukizi. Matandazo haya yana faida ya kuongeza rutuba kwenye udongo pale majani yatakapooza. Matandandazo ya plastiki yanaweza kutumika hasa ambapo umwagiliaji kwa njia ya matone unatumika kwenye hali ya baridi. Katika mazingira ya joto sana Tanzania matandazo ya plastiki hayapaswi kutumika kwasababu yataathiri ukuaji wa mazao!

Ni wakati gani mzuri katika siku kumwagilia mboga mboga?Wakati mzuri ni mapema asubuhi, hasa kati ya saa 10 alfajiri na 4 asubuhi, ambapo maji hupoteza kiasi kidogo kutokana na uvukizi. Wakati huo pia mimea hutoa unyevu unaohitajika kujitengenezea chakula kwa ajili ya siku nzima. Wakati mwingine mzuri ni jioni: kati ya saa 10 na 11 jioni. Kumwagilia katikati ya siku husababisha kuunguza mazao kwa upotevu wa unyevu unaotokana na uvukizi, isipokuwa kwa njia ya matone inaweza kuwa tofauti. Kumwagilia usiku kunaweza kusababisha magonjwa ya ukungu. Mbali na hivyo maji hayatumiki kikamilifu kwani mmea utakuwa haujitengenezei chakula chake, au utafanya hivyo kwa kiwango kidogo, kwasababu hupumua wakati wa usiku.

Uliza SEVIA!Kwa mafanikio ya uzalishaji wa mazao ya mboga mboga kibiashara, wakulima wanatakiwa kutumia rasilimali za maji zilizopo, kutafuta vyanzo vipya na kuhifadhi maji. Waulize Maafisa Ugani wa SEVIA kuhusu kilimo cha umwagiliaji: wanaweza kutoa ushauri wao, kwa kuzingatia bajeti na mazingira yako.

2

Kuvuna maji

Matikiti maji yamefunikwa na matandazo ya majani

Kukusanya maji ya mvua na kuyahifadhi ni muhimu kwa baadae maji yatakapopungua

Kuvuna maji

Kamwe hatuachi nyuma dhima yetu ‘Kuona ni kuamini’: huwa tunatoa huduma zetu kupitia mashamba darasa ambayo huanzishwa miezi kadhaa mapema. Hakuna aliechwa wakati huu. Wafanyakazi walipangwa katika timu ya kuhudumia maelfu ya wakulima wanaotarajiwa.

Wakulima walianza kufika kwa uchache kwenye tarehe 1 na 2 ya Agosti, hapa Dodoma. Hata hivyo, mwishoni mwa wiki na hadi 8 Agosti, wakulima walikuja kwa wingi. Timu ya Mwanza ilikuwa karibu kuzidiwa na wakulima zaidi ya 4000 ambao walikuja kupata huduma za SEVIA na kuona aina na teknolojia, iliyoonyeshwa na banda jipya la SEVIA kwenye

maonyesho haya. Wakulima ambao walitembelea walijifunza jinsi maeneo madogo ya ardhi yanavyoweza

kutumika vizuri, faida za mbegu nzuri, usimamizi wa mazao bora na upatikanaji wa huduma za ugani bila malipo. Uzalishaji ndani ya nyumba kitalu na nje ulielekezwa.

Mbali na mahudhurio makubwa, jambo lingine la Nanenane mwaka huu ilikuwa ni ziara ya shamba darasa la SEVIA iliyofanywa na Dr Charles John Tizeba (Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi). Meneja Ugani Epaphras Milambwe alimpa maelezo mafupi jinsi SEVIA inavyochangia kuboresha uzalishaji wa mboga mboga, uwiano wa uzalishaji na mapato ya wakulima wadogo. Waziri aliipongeza SEVIA kwa kazi yake. “Endeleeni kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa kwa uendelevu wa kazi zenu”, alisema kwa kusisitiza.

Tunatarajia kuendeleza ushirikiano wetu na wakulima tuliokutana nao huko Nanenane na wengine wengi. Mwaka 2018 SEVIA itarudi tena Nanenane !

Inaonekana kila mkazi wa Mwanza alikuwa karibu kutazama shamba la SEVIA

Mary Maganga wa SEVIA anaelezea uzalishaji wa nje wa pilipili hoho mkoani Morogoro

SEVIA IMEWAFIKIA ZAIDI YA 6,000 KATIKA NANENANEMwaka huu tena SEVIA ilishiriki katika maonyesho yetu maarufu ya kitaifa ya kilimo: Nanenane. Lilikuwa ni tukio letu la tatu na kubwa hadi sasa. Tulishiriki katika vituo vinne: Arusha, Dodoma, Morogoro na Mwanza. Kwa Mwanza ilikuwa ni mara ya kwanza. Kwa ujumla tuliweza kufikia wakulima 6,070 ambao wanaume 4,428 na wanawake 1,642.

3

Katika jarida la kwanza la Mkulima wa SEVIA (mwaka 2015) tulionesha malengo tunayotarajia kufikia ndani ya mradi huu. Tukiwa nusu ya kipindi cha mradi mpaka sasa, tunafuraha kukuonesha muhtasari wa maendeleo yetu.

SEVIA katika ufanisi mkubwaKituo cha SEVIA kimeanzishwa Lambo Mferejini, Wilaya ya Hai (karibia na Moshi Mjini), kikiwa na majengo kwa matumizi ya ofisi, maeneo kwa ajili ya majaribio/ mashamba darasa, mifumo ya umwagiliaji, vifaa vya kuvunia maji, wafanyakazi na vifaa vingine ili kusaidia uendeshaji wa taasisi. Kufikia Agosti 2017, SEVIA imekuwa ikifanya kazi kwa ufanisi mkubwa: imehusika katika maendeleo, utekelezaji na usambazaji wa tekinolojia bunifu mashambani na uchunguzi wa mbegu bora za mboga mboga hapa Tanzania. Kituo kimetambulika kwa taaluma na ubunifu wa uzalishaji wa mboga mboga.

Zaidi ya wakulima 23,000 wamefikiwaKujenga uwezo kwenye taaluma ya uzalishaji wa mboga mboga, ambalo ni lengo kuu la SEVIA! Tangu kuanzishwa, mafunzo 18 yalifanyika SEVIA na mengine mengi nje ya kituo. Mafunzo haya yamewasaidia wakulima kuiga na

kubadilisha uzalishaji wa mboga mboga. Mpaka sasa tumewafikia wakulima zaidi ya 23,000. Maudhui ya mafunzo hayo ni kwa mf. Kuzuia magonjwa/wadudu kwenye mazao, matumizi sahihi ya mbolea, umwagiliaji kwa njia ya matone, kulima kwenye nyumba kitalu na utunzaji na uhifadhi wa mazao baada ya kuvuna. Mradi wa SEVIA umeongeza maarifa kwa wakulima wa mboga mboga na wataalamu katika sekta hii.

Mashamba darasa 600: ‘Kuona ni kuamini’ Kupitia SEVIA, wakulima katika Wilaya 19 nchini Tanzania wametambulishwa katika mbegu chotara na njia bora za utunzaji wa mazao. Tumeanzisha zaidi ya mashamba darasa 600 kama sehemu ya mkakati wa SEVIA, ‘Kuona ni kuamini’, kwa kuzingatia maudhui kuanzia utunzaji wa kitalu hadi shughuli za shambani. Kupitia mpango wa Afrisem wa mbegu chotara, aina 20 za nyanya chungu na pilipili kali zilitambulishwa kwenye soko.

4

Nukuu kutoka kwa wakulima:

“Nimekua nikipata hasara. SEVIA walinifundisha kilimo cha nyanya katika ardhi yenye ukubwa wa 250m2.

Kutokana na eneo dogo hilo nimetengeneza kiasi cha 400,000 tsh ndani ya miezi miwili na nusu kwa gharama za uzalishaji wa 50,000 tsh. Kabla ya hapo ningetumia 200,000 tsh kwa mapato ya 20,000 tsh. Ilifika hatua ya kukata tamaa katika biashara ya kilimo na kufanya kazi

machimbo. Ila sasa nimebadili mawazo nitategemea kilimo cha mboga mboga. Asante sana SEVIA.”

SEVIA: Kuona ni kuamini

TUKO WAPI SASA? Imeandikwa na Elijah Mwashayenyi

Kuunganisha masokoIngawa SEVIA wamekuwa hawanunui wala kuuza mazao ya wakulima. Wanatoa baadhi ya taarifa kuhusu masoko na kutengeneza uhusiano wa masoko. SEVIA inafanya kazi na taasisi zingine kama Tanzania Horticulture Association kuhusu maswala ya upatikanaji wa masoko.

Kukuza uchumi wa vijijiniSEVIA imekuwa ikitetea kilimo kizuri cha mboga mboga, ambacho kitatoa ajira nzuri. SEVIA haitoi fedha kwa wakulima. Ingawa inashirikiana na taasisi kama EFTA ambayo inatoa mkopo wa vifaa vya kilimo bila dhamana yoyote na NMB Bank ambayo pia inatoa mikopo. SEVIA inatambua kwamba, kama kilimo cha mboga mboga kitakuwa ni biashara yenye faida kubwa kwa wakulima, hivyo itachangia kupunguza umasikini vijijini na watu kuhama makazi zaidi iwe kwa kupenda kwao.

Matokeo ya kudumuKulingana na hali iliyoko sasa, tulilenga kuanzisha mashamba darasa 1000, kufundisha wataalamu 1000, kuwa na mbegu chotara za aina tofauti 30, kufikia wakulima 30,000,ingawa malengo haya yatafikiwa na zaidi hadi mwaka 2020. Hata hivyo, SEVIA haifanyi kazi kwa kuangalia idadi tu, bali ubora. Tunaamini kuwa jitihada zetu zitaleta matokeo ya kudumu kwa wakulima na wadau wengine ndani na nje ya Tanzania.

Jumla kwa sasa Hadi kufikia 2020

Muhtasari wa maendeleo dhidi ya malengo ya mradi

0 200 400 600 800 1,000 30,000

30,00023,575

1,000562

1,000698

3020

100144

5031

3011

104

11

Wilaya 19 ndani ya mikoa 10

15,729 7,846

SEVIA ina jumla ya wafanyakazi 45Idadi ya vituo vya SEVIAvilivyoanzishwa

Idadi ya vitabuvya kitaalamu

Idadi ya miongozoya mazao

Idadi ya miradi na taasisiza taaluma/utafiti

Idadi ya aina ya mazaoyaliyofanyiwa jaribio

Idadi ya mbegu chotarazilizozalishwa (Afrisem)

Idadi ya shambadarasa (maeneo)

Idadi ya wakulimawaliofikiwa

Idadi ya wataalamuwaliofundishwa

“Binti yangu sasa anajivunia kilimo cha mboga mboga. Sio tu

kwa sababu tuna chakula cha kutosha ila pia

tunauza mboga mboga! Tunatengeneza pesa za

kutosha, kutimiza mahitaji yetu na kuhifadhi kiasi

kinachobaki. Binti yangu hatafuti tena kazi

za ofisisni”

“Pesa ni pesa. Uipate ukiwa Dar es Salaam au

hapa kijijini kwangu. Uipate ukiwa daktari, mwalimu, mhandisi au

yoyote… Napata mshahara wangu kupitia

kilimo cha mboga mboga.. kipato changu ni

kikubwa kuliko mshahara wa

wafanyakazi wa serikali walioko maeneo ya mjini….. najihimili mimi mwenyewe”

5SEVIA ni timu!

VIDOKEZOJifunze aina ya mazao ya kupanda ndani ya kibanda kitaluJifunze aina ya mazao ya kupanda ndani ya nyumba kitalu je unajua mafanikio ya kilimo cha nyumba kitalu yanategemea taaluma yako katika aina ya mazao, na hasa utunzaji wa mazao? Nyumba kitalu haitakufanya kuwa mkulima bora isipokuwa taaluma yako, ujuzi na taarifa utakazozipata.

Unajua kuwa...

Matumizi ya nyumba kitalu yanaweza kuwa tofauti kulingana na mazingiraNchi za ukanda wa baridi mboga mboga kama nyanya, tango na pilipili hoho zinalimwa ndani ya nyumba kitalu. Katika maeneo hayo nyumba kitalu husaidia kuongeza joto. Hata hivyo, katika mazingira ya joto hatutarajii kuongeza joto na dhumuni la nyumba kitalu Tanzania ni kuzuia mvua, wadudu na vimelea vya magonjwa.

Kufahamu mazao yanayoweza kupandwa ndani ya nyumba kitalu ni muhimuTunapendekeza mazao ya muda mrefu wa joto/yanayotambaa yanayoweza kuvunwa kwa muda mrefu (miezi 6-8) chini ya utunzaji mzuri wa mazao. Nchini Tanzania nyanya, tango na pilipili hoho ni mazao yanayolimwa ndani ya nyumba kitalu kwa ajili ya biashara. Usipande kabichi au sukumawikindani ya nyumba kitalu kwa sababu mapato yake hayatatosha kurudisha gharama za uwekezaji ulizotumia.

Nyanya ndani ya nyumba kitalu zinaweza kuvunwa zaidi ya miezi 8 Unapopanga kulima nyanya ndani ya nyumba kitalu lazima kwanza ufikirie aina ya mbegu. Kuna aina mbili za nyanya: Nyanya fupi na Nyanya ndefu Kama Monteazul F1 na Moyo F1, ni chaguo zuri kwa kilimo cha nyumba kitalu na inaweza kuvunwa zaidi ya miezi 8. Zinakuwa ndefu zikipogolewa shina kuu moja au mawili. Kwa kilimo cha nje, nyanya fupi aina ya Jarah F1 na Kipato F1 zinapendekezwa.

Aina ya tango la nje na la nyumba kitalu ni tofauti Kuna aina mbili ya tango, ambayo ni tango linalojichavusha na lisilojichavusha. Tango linalojichavusha kama Mydas F1 ni nzuri kulima ndani ya nyumba kitalu kwa sababu halihitaji wachavushaji. Mavuno yanaweza kwenda miezi 4 -6. Tango lisilojichavusha ni tango la kulimwa nje, kama Monalisa F1, linahitaji wachavushaji (kama nyuki) kwa ajili ya uzalishaji. Kwa sababu hii haliwezi kupandwa ndani ya nyumba kitalu (au wachavushaji wawekwe ndani).

Unapenda pilipili hoho za rangi au za kawaida? Fanya chaguo sahihi mapema!Kuna aina mbili ya pilipili hoho katika soko la Tanzania: za rangi

(nyekundu na njano) na pilipili hoho za kawaida. Ingawa kila aina itatoa matunda ya rangi yasipochumwa yakiwa ya kijani, lakini mavuno ya pilipili hoho za kawaida sio mazuri kwa kuzalisha matunda ya rangi. Kwa hiyo ni muhimu kuchagua mapema unataka kupanda aina

ipi. Kwa kilimo cha nyumba kitalu tunapendekeza pilipili hoho za rangi, kama Pasarella F1 na Ilanga F1. Chini ya uangalizi mzuri wa mazao unaweza kuvuna miezi 6-8. Unatakiwa kutoa maua ya kwanza ili kusaidia ukuaji imara ambao utatoa matunda yenye ukubwa sawa na mengi.

Je unapenda pilipili hoho za kawaida? Zinapendekezwa kulimwa katika mashamba ya wazi pekee, kwa sababu zinatumia muda mfupi kukomaa na kutoa matunda hivyo hupunguza hatari ya kuvamiwa na wadudu na magonjwa. Kwa kilimo cha nje tunapendekeza aina kama Red Jet F1 na Kaveri F1. Ambayo yanaweza kuvunwa mpaka miezi 4.

6

SIMULIZI KUTOKA MASHAMBANI

Bw na Bi Hendry Mchau ni wakulima wa nyanya, kabichi, tango na sukuma wiki kutoka Mbokomu- Manyire, Arusha. Hivi karibuni wamejenga jokofu la asili kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya mboga mboga, wamejifunza teknolojia hii kutoka SEVIA baada ya kuhudhuria maonyesho ya shamba darasa. Jokofu la asili linawasaidia kuhifadhi mazao yao (hasa nyanya) baada ya mavuno, kwa kipindi cha wiki 2 hadi mwezi mmoja na nusu. “Nina uwezo wa kuhifadhi mazao yangu mpaka bei ya soko ipande”, alisema Bw Mchau. “Baadhi ya majirani na marafiki zangu wamegundua hili na wana mpango wa kujenga majokofu yao.”

Bw Salima Tamimu (57) kutoka kijiji cha Mrua wilayani Kondoa amekuwa akijihusisha na kilimo cha mboga mboga kwa miaka 30. Amekuwa akilima nyanya, pilipili hoho, kabichi, vitunguu, tango, nyanya chungu na bamia.

“Sikuwa na sehemu ya kuomba ushauri, kila ninapopata changamoto ya kudhibiti wadudu na magonjwa. Sikujua ni aina gani ya mbolea nitumie”, alisema. Mwezi wa 3 mwaka 2017 alikutana na Afisa ugani wa SEVIA, Paschal Lusolela. Bw Tamimu alikuwa na nia ya kuandaa shamba darasa kulinganisha uzalishaji wa mbegu chotara na za asili za kabichi na pilipili hoho kwa kuondoa tunda la kwanza. Baada ya hapo alitangaza kwamba,” sasa najua umuhimu wa kuchagua aina nzuri ya mbegu, kuzipanda kwa kuacha nafasi sahihi na wakati wa kuweka mbolea katika mazao yangu. Ninatarajia kupanda Mapema F1 (kabichi) mwezi wa 10”. Akiwa amehamasishwa na SEVIA katika maonesho ya mashamba darasa mwezi wa 7 anategemea kununua vifaa vya umwagiliaji kwa njia ya matone kwa ajili ya robo ekari.

Bw Felicion Marko (52) ni mkazi wa kijiji cha Bukumbi kata ya Misungwi (Mwanza). Alianza kilimo cha mboga mboga mwaka 1985. Amekuwa akilima nyanya, pilipili hoho, kabichi, tikiti maji na tango.

SEVIA ilianza kufanya nae kazi mwezi wa pili 2017, aligundua kuwa anatakiwa kuongea ujuzi katika njia zake za kilimo, hasa baada ya kujifunza kupitia shamba darasa la SEVIA lililowekwa shambani kwake. Shamba darasa lilielekeza uwekaji wa mbolea kwenye pilipili hoho na kufungia kamba na waya kwenye zao la nyanya.

Hivi sasa amekuwa akipanda nyanya kwa kutumia muongozo huo wa kuweka mbolea na kufunga kamba na waya, utaalamu wote ni kutokana na SEVIA. “Mimi ni mkulima mwenye furaha”, alisema.

7

Bw Marko akielezea shamba darasa kwa majirani zake

Shamba la Bw Tamimu lenye kabichi za asili (Utukufu wa Enkhuizen)

Salimu Tamimu alikua na shamba darasa la mbegu chotara za kabichi na pilipili hoho mwezi wa 4 mwaka 2017

Zingatia kununua miundombinu ya umwagiliaji kwa njia ya matone

Hujachelewa kujifunza

Tunza nyanya mpaka bei ipande

WATU WA SEVIAKutana na timu yetu ya uganiSEVIA sasa ina maafisa ugani wanaojumuisha wilaya 19 katika mikoa 10. Kila afisa ugani anafanya kazi na wakulima kwa kutumia shamba darasa katika uzalishaji wa mboga mboga kwenye wilaya. Mashamba darasa hayo ni katika aina bora na teknolojia. Mafunzo, ushauri,

kutembelea mashamba na maonesho ya shamba darasa ni sehemu ya kazi ya afisa ugani. Huduma hizi hazina malipo. Timu hii inasaidiwa moja kwa moja na Epaphras Milambwe (Meneja Ugani) na Mary Maganga (Afisa ugani mwandamizi, mwenye wajibu wa mafunzo na kudhibiti mazao dhidi ya magonjwa na wadudu waharibifu), ambao wapo katika kituo cha SEVIA kilichopo Lambo Mferejini, lakini husafiri mara kwa mara kwa usimamizi. Angalia afisa ugani alie karibu na wewe, anaweza kuwa na shamba darasa karibu na wewe. Au labda unataka kuwa na shamba darasa la SEVIA wewe mwenyewe?

8

AJENDADISEMBAOKTOBA NOVEMBA

Mafunzo kwa wakulima

Kupanda mazao ya majaribio na shamba darasa

Mkutano wa SEVIA

Mafunzo kwa wataalamu wa kilimo kutoka Uganda Mkutano wa mwaka wa wafanyakazi

Mafunzo kwa wataalamu wa kilimo

WahaririElijah Mwashayenyi Anita van Stel

UbunifuMooizo Design

Michango ya jarida hili ni kutoka kwa• Halima Jumanne• Ikunda Marandu• Epaphras Milambwe• Clara Mlozi• Elijah Mwashayenyi• Herman de Putter• Anita van Stel

• Wageningen UR • SEVIA • Communications consultant

Anuani ya posta SEVIA, P.O. Box 7211, Moshi

Anuani ya kutembeleaLambo, MferejiniTanzania+255 685 942 364www.sevia.biz

WACHANGIAJI

Je, unataka kupokea nakala za bure za awali za jarida hili? Tafadhali tuma barua pepe au soma jarida katika tovuti yetu www.sevia.biz

Ruwuma

Iringa

Mbeya

Rukwa

Kigoma

Tabora

Singida

Dodoma

Mtwara

Lindi

Pwani

Tanga

Kilimanjaro

Manyara

Arusha

Mara

Shinyanga

Mwanza

Kagera

Morogoro

Dar es Salaam

Lewis MlekwaMorogoro (Vijijini na Manispaa Mvomero), [email protected]

Nurdin MndoholeleBagamoyo, [email protected]

Paschal LusolelaKondoa, [email protected]

Theophilo NyigagaHai, [email protected]

Frank MazengoRungwe, [email protected]

Andrew NyambegaMbeya Vijijini na Manispaa, [email protected]

Mseti MwitaDodoma, [email protected]

Ladislaus MkufyaBabati, [email protected]

Thobias MkamateMoshi Vijijini na [email protected]

Franco KajunaMisungwi na [email protected]

Wilfred MakangeIringa Vijijini na Manispaa, [email protected]

Joseph MasethyaLushoto, [email protected]

Iddi Haridi Arusha Manispaa na Meru, [email protected]

Athumani IssahMonduli na KaratuArusha and [email protected]