wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 ·...

12
Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za kimungu na hali halisi katika maisha yao. Tunapendeza utumie kadi ili kuwazawadi wale watakaohudhuria, na kuwahimiza watoto wafike kila wiki ili kupata kadi za kucheza na wengine. Patia kila mtoto kadi ya Shujaa na kadi Maalum ambazo wamepata kutokana na kuhudhuria darasa kila wiki. Tunapendekeza uandike jina la mwanafunzi katika upande wa nyuma wa kadi yao. Ili kucheza mchezo, watoto wanakuwa katika jozi .Kisha kwa kila zamu ya mchezo, fanya yafuatayo: Mwalimu anasoma moja ya hali/maswali yaliyotolewa, lakini hasemi ni sifa ipi inayohitajika kwa hali hiyo. Wachezaji wanabashiri sifa inayohitajika katika hali hiyo na kutafuta kadi ya Mashujaa ambayo ina pointi zaidi katika sifa hiyo. Pia wanaweza kuchagua kadi Maalum ili kuwasaidia kushinda. Baada ya kila mpinzani kuchukua mchanganyiko wa kadi ya Shujaa na Maalum ambazo wanaamini zitawasaidia kushinda, utahesabu 1 hadi 3, nao wataweka kadi zao katikati ya meza mara moja zikiwa zimeangalia juu.Kumbuka: katika zamu za mwanzo, ruhusu muda zaidi ili waweze kujifunza jinsi ya kucheza. Baadaye, wahimize waamue haraka ili kuleta msisimko katika mchezo. Mchezaji atakayepata pointi zaidi katika sifa sahihi baada ya kujumlisha pointi kutoka kwa kadi za Shujaa na kadi Maalum anakuwa mshindi wa zamu hio.Hifadhi alama hii, na kujumlisha zamu ambazo kila mtoto atashinda. Kila kadi inaweza kuchezwa tu mara moja kwenye mchezo. Baada ya kila zamu, kila mchezaji anachukua kadi ambazo ametumia kucheza na kuziweka kando zikiwa zimeaangalia chini. Cheza zamu zaidi hadi watoto waishiwe na kadi. Mshindi atakuwa mchezaji atakayeshinda zamu nyingi. Wafanye watoto wabadilishe mpinzani na kucheza tena.

Upload: others

Post on 20-Jan-2020

9 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 · aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa

Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za kimungu na hali halisi katika maisha yao.

Tunapendeza utumie kadi ili kuwazawadi wale watakaohudhuria, na kuwahimiza watoto wafike kila wiki ili kupata kadi

za kucheza na wengine.

Patia kila mtoto kadi ya Shujaa na kadi Maalum ambazo wamepata kutokana na kuhudhuria darasa kila wiki.

Tunapendekeza uandike jina la mwanafunzi katika upande wa nyuma wa kadi yao. Ili kucheza mchezo, watoto

wanakuwa katika jozi .Kisha kwa kila zamu ya mchezo, fanya yafuatayo:

• Mwalimu anasoma moja ya hali/maswali yaliyotolewa, lakini hasemi ni sifa ipi inayohitajika kwa hali hiyo.

• Wachezaji wanabashiri sifa inayohitajika katika hali hiyo na kutafuta kadi ya Mashujaa ambayo ina pointi zaidi

katika sifa hiyo. Pia wanaweza kuchagua kadi Maalum ili kuwasaidia kushinda.

• Baada ya kila mpinzani kuchukua mchanganyiko wa kadi ya Shujaa na Maalum ambazo wanaamini zitawasaidia

kushinda, utahesabu 1 hadi 3, nao wataweka kadi zao katikati ya meza mara moja zikiwa zimeangalia

juu.Kumbuka: katika zamu za mwanzo, ruhusu muda zaidi ili waweze kujifunza jinsi ya kucheza. Baadaye,

wahimize waamue haraka ili kuleta msisimko katika mchezo.

• Mchezaji atakayepata pointi zaidi katika sifa sahihi baada ya kujumlisha pointi kutoka kwa kadi za Shujaa na kadi

Maalum anakuwa mshindi wa zamu hio.Hifadhi alama hii, na kujumlisha zamu ambazo kila mtoto atashinda.

• Kila kadi inaweza kuchezwa tu mara moja kwenye mchezo. Baada ya kila zamu, kila mchezaji anachukua kadi

ambazo ametumia kucheza na kuziweka kando zikiwa zimeaangalia chini.

• Cheza zamu zaidi hadi watoto waishiwe na kadi.

Mshindi atakuwa mchezaji atakayeshinda zamu nyingi. Wafanye watoto wabadilishe mpinzani na kucheza tena.

Page 2: Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 · aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa

Kuna aina mbili za kadi: kadi za Shujaa na kadi Maalum. Kila kadi ya

shujaa inaonyesha mtu kutoka kwenye Biblia na maadili ya sifa sita

zifuatazo: Nguvu, Uadilifu, Utiifu, Unyenyekevu, Huruma na Imani.

Kila shujaa wa Bibilia ana pointi 100 kwa kila moja ya sifa hizi,

kutokana na uchambuzi wa maisha yake. Ikiwa shujaa hakupata fursa ya

kuthibitisha sifa zake katika hali fulani, basi hatapata pointi zozote katika

hali hiyo. Mashujaa wawili hawawezi kuwa na idadi sawa ya pointi kwa sifa

sawa. Ikiwa shujaa alionyesha udhaifu katika hali fulani, atakuwa na pointi

chache kuliko yule shujaa ambaye kamwe hakuonyesha udhaifu katika hali

hiyo.

Mifano: Kwa sababu hatuoni Imani kubwa katika maisha ya Habili, atapata tu pointi 50 kwa sifa ya imani. Kwa kuwa

aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa Huruma, kwa sababu alimpa

Mungu yote aliyotaka na kuonyesha upendo wake kwa Mungu. Ibrahimu atapoteza pointi za Uadilifu kwa kudanganya

kuhusu mkewe, na kusema ni dadake. Nuhu atapoteza pointi za Huruma kwa sababu haijaandikwa kama aliwaombea

maelfu au mamilioni ya watu ambao walikuwa wanakaribia kuangamia au kama alijaribu kuwaokoa. Musa atapata pointi

100 kamili katika Unyenyekevu kwa sababu Biblia inasema kuwa alikuwa mtu mnyenyekevu zaidi kuwahi kuishi. Yosefu

hatapata pointi yoyote katika unyenyekevu kwa sababu aliwaarifu ndugu zake kuhusu ndoto wakati haikufaa, na pia

hatuoni unyenyekevu mwingi alipokuwa waziri mkuu. Ibrahimu anapata 97 katika Utiifu kwa sababu aliondoka nchi yake

na kufuata Mungu na alitii kwa kuondoka Sodoma na Gomora. Lakini hatapa pointi 100 kamili kwa sababu Nuhu alikuwa

na utiifu zaidi kwa kujenga safina kubwa, na kufanya kazi kwa takriban miaka 100 bila kuona dalili za mvua.

Kadi maalum hubadilisha thamani ya kadi zinazochezwa. Itakusaidia kushinda hata ikiwa wewe na mpinzani wako

mmechagua Shujaa sawa.

• Biblia: inaongeza alama kwa pointi zilizoonyeshwa katika ubora unaochagua.Hakikisha unatumia sehemu ya

Biblia ambapo Shujaa anapatikana.

• Dhahabu iliyofichwa: itaondoa pointi 10 kutoka kwa shujaa wa mpinzani wako.

Page 3: Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 · aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa

• Maombi: itaongeza pointi 10 kwenye Imani ya shujaa wako.

• Sanduku la Agano: itapunguza Nguvu za mpinzani wako hadi sifuri.

• Mti Ulioanguka: itapunguza Unyenyekevu wa mpinzani wako kwa pointi 20.

• Uumbaji: tumia hii kwenye hali ambayo unafikiria unaweza shinda. Ikiwa utashinda,

utaweza kukomboa kadi tatu ulizotumia hapo awali .

• Upanga wa Bwana: tumia kadi hii kushinda zamu kiotomatiki. Kadi hii inaweza

kutumika peke yake.

• Moto wa Mungu: mfanye mpinzani wako kuruka zamu.

• Ukoma: itakufanya upoteze zamu lakini itapunguza Nguvu ya mashujaa wa mpinzani

wako kwa pointi 20 katika mchezo wote.

• Utekwaji: Tumia kadi hii kushinda zamu yako. Pia chukua shujaa wa ghafla kutoka kwa

mpinzani wako, na kumlemaza kwa mchezo wote.

Katika mfano huu,

Mtoto 1 na Mtoto 2

wana kadi walizopata

kutokana na kuhudhuria

wiki tofauti.

Mtoto 1 Mtoto 2

Swali: "Dadako akikwambia udanganye, ni shujaa yupi atakusaidia?"

Sifa inayohitajika: Uadilifu (usiwaambie watoto)

Mwalimu anasubiri kwa muda ili watoto waweze kuwaza, kisha anahesabu hadi 3.

Mwalimu

Mtoto 1 Mtoto 1 anachagua Isaka na Biblia,

akidhania sifa inayohitajika ni

Uadilifu.

Mtoto 2 anachagua Ibrahimu na

Dhahabu iliyofichwa, akidhania sifa ni

Imani.

Mtoto 2

Kumbuka: lazima achague kadi ya Biblia

ya Torati kwa sababu hadithi ya Isaka

inapatikana katika kitabu cha Mwanzo. Pointi za Imani hazitahesabiwa kwa

sababu sifa inayohitajika sio Imani

lakini Uadilifu katika zamu hii.

Page 4: Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 · aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa

Mtoto 1 Mtoto 2

Page 5: Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 · aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa

1. Dadako akikwambia udanganye, ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

2. Rafiki yako anakuja na kukuambia kuwa jambo unalofanya ni kosa, na ndani yako unajua kwamba unakosea, na

unahitaji kukubali na kuomba msamaha. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

3. Uko shuleni na wanafunzi wenzako wanaanza kukucheka. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

4. Baba yako anakuomba uoshe gari na hutaki. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

5. Ulipokwenda dukani kununua peremende, muuzaji alikurudishia pesa zaidi. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uadilifu)

6. Mko shuleni kisha mwanafunzi mmoja anateleza na kuanguka chini na kila mtu anamcheka. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Huruma)

7. Siku moja msichana akakupa zawadi ambayo haikukupendeza, lakini alikupa kwa upendo mwingi. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Unyenyekevu)

8. Mjomba anakushauri ukunywe pombe. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

9. Shuleni, wanafunzi wenzako wanakuonya kuwa hupaswi kuwa Mkristo huko. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

10. Dada yako anavunja kichezeo chako unachopenda zaidi. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

11. Baba yako alikwambia kuwa Mungu hakupendi. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

12. Wazazi wako wanakuonya usicheze na rafiki yako kwa sababu yeye ni mtu mbaya. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Utiifu)

13. Mchungaji wako anakuomba mwende naye kuhubiri. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

14. Ni wakati wa chakula cha jioni na chakula kilichopo kinaweza kutosha tu wewe na familia yako, lakini wageni

wanaingia na wana njaa. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

15. Mchungaji wako anakuomba ufunge, lakini mama yako anatayarisha chakula kitamu sana siku hiyo. Ni shujaa

yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

16. Mama yako anatayarisha chakula ambacho hupendi, lakini anasema unahitaji kula ili uwe na afya njema. Ni

shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

17. Mama yako anakuambia uoge. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

18. Shuleni msichana anateleza na kukumwagia soda. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

19. Unavuka barabara na unakutana na nyanya aliyebeba mifuko mizito karibu kuiangusha. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Huruma)

20. Mama yako anakuomba uende nyumbani kwa mtoto ambaye hamsikizani ili umpe zawadi. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Huruma)

21. Mwanafunzi mwenzako anararua kitabu chako na unahisi kulipiza kisasi. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

22. Kila wakati dada yako anakwambia kuwa una sura mbaya na hili linakuhuzunisha. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Imani)

23. Mwalimu wako wa shule ya Jumapili hukuadhibu kila wakati na hili hukufanya ukasirike. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Utiifu)

24. Siku moja shuleni rafiki yako anakushauri uibe mfuko wa mwanafunzi mwingine. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uadilifu)

25. Shangazi yako hukuadhibu kwa sababu ya kufanya makosa, hivyo humpendi. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Unyenyekevu)

26. Siku moja ulihisi kwamba Mungu anakuita ili ufanye kitu ambacho hakutaka kufanya. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Imani)

27. Mtoto mwingine anakupa sigara uvute. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

28. Kanisani wanasema kuwa wewe ni mvivu, na hutaki kukubali. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

Page 6: Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 · aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa

29. Rafiki anakushauri uibe pesa za wazazi wako, na kama hutafanya hivyo, hatakuwa rafiki yako tena. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Uadilifu)

30. Mwalimu wako wa shule alisema kwamba mwanadamu alitoka kwa nyani, na sio kutoka kwa Mungu. Ni shujaa

yupi atakusaidia? (Imani)

31. Mwalimu alikupa alama zisizofaa na wazazi hawataki kuskia hili na wanataka kukuadhibu. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Uvumilivu)

32. Mwenzako alikuambia kuwa una sura mbaya. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

33. Ulimwambia dadako kitu kisichofaa na unajua hili na unapaswa kumwomba msamaha. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Unyenyekevu)

34. Mchungaji anakataa ujiunge na kundi la kuimba sifa. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

35. Shuleni mwalimu wako hajawahi kukusifu. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

36. Mama yako alikulaumu kwa kitu ambacho haukufanya. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

37. Nyanya yako alikuja kutembea na akawaletea wengine zawadi, lakini hakukuletea. Unajua unapaswa

kumsamehe na kusahau hili, ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

38. Uko kwenye basi na nyanya mzee anaingia. Umeketi na yeye amesimama, ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

39. Unacheza shuleni kisha unateleza na kuanguka. Kila mtu anaanza kukucheka. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uvumilivu)

40. Shuleni kila mtu ako kwenye mchezo, na unawaomba kujiunga ili kucheza nao. Wote wanakataa. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Uvumilivu)

41. Unaona mvulana akimpiga msichana mdogo. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

42. Hakuna mikasi ya kutosha shuleni kwa kila mtu kuwa na wake. Mwenzako anakuja na kuchukua mkasi wako na

kwenda. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

43. Msichana anakupenda na anataka umbusu. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

44. Umemwomba Mungu akupe baiskeli na bado huna. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

45. Mama yako anakutuma dukani na anakupa elfu moja, unaporudi anasahau kukuitisha pesa zilizobaki. Ni shujaa

yupi atakusaidia? (Uadilifu)

46. Mwalimu anauliza ni mwanafunzi yupi ambaye ni mwerevu zaidi. Unajua vizuri wewe ni mwerevu, lakini unajua

ni makosa kujigamba. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

47. Siku moja ulikuwa unatembea barabarani na mtu aliyekuwa mbele yako akaangusha kibeti na hakugundua. Ni

shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

48. Nyanyako yako alikuomba uende hotelini kumnunulia chakula lakini ukamletea chakula ambacho hakutaka,

hivyo akakasirika. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

49. Wazazi wako walikuacha na shangazi ambaye humpendi. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

50. Dada yako ni mkubwa kukuliko na kila wakati anakucheka. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

51. Dada yako anakutuma mara kwa mara na kujifanya mama yako, hivyo humpendi. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uvumilivu)

52. Mama yako anakuambia kwamba Mungu anakupenda. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

53. Wazazi wako wanakuambia kuwa unapaswa kuamini kuwa kila kitu kinawezekana. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Imani)

54. Mwalimu wako alikuomba usaidie kusafisha kanisa. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

55. Wazazi wako walikuambia usafishe chumba chako, lakini hutaki. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

56. Rafiki anataka kukuomba baiskeli yako, lakini hutaki kumpa. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

57. Una haraka kuvuka barabara, lakini kuna mwanamke katika kiti cha magurudumu na anakuomba umsukume ili

avuke. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

58. Wazazi wako wanataka kukununulia zawadi kwa sababu ulipita mtihani, lakini unajua kwamba ulidanganya

kwenye mtihani. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

59. Mwalimu wako amekuweka katika kundi ili kufanya shughuli fulani pamoja. Lakini kuna mtu ambaye

hamsikizani. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

60. Baba yako alikuomba uombe ili upate kazi mpya. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

61. Baba yako anakuomba ufanye kitu ambacho hupendi kufanya. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

Page 7: Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 · aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa

62. Mwalimu wako wa shule anasema kwamba Biblia ni kitabu cha kupotosha. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

63. Mchungaji wako anakuambia kuwa unaweza kuhudhuria tukio la kanisa hata kama wazazi wako hawakubali,

lakini unajua kwamba mamlaka ya kwanza ambayo Mungu ameweka ni wazazi wako. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uvumilivu)

64. Wazazi wako hawataki kukuruhusu uhudhurie tukio la kanisa. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

65. Wazazi wako wanakuambia kwamba hupaswi kutoka nje, lakini uko peke yako ndani ya nyumba, kisha marafiki

zako wanafika na kukuambia utoke ili mcheze. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

66. Unaenda dukani halafu unapatana na mtoto ambaye akakutusi, unajua hupaswi kumtusi, lakini unakasirika sana.

Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

67. Una mtihani muhimu sana ambao haujasomea na unapata nafasi ya kuiba wakati wa mtihani. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Uadilifu)

68. Mnafanya kufanya kazi kama kikundi shuleni, unajipata ni wewe pekee unashughulika na wengine hawafanyi

lolote, na lazima uwaambie wenzako wakusaidie. (Uvumilivu)

69. Mtoto anasema shuleni kwamba wewe ni mwongo. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

70. Wenzako wanakulaumu kwa kitu kilichopotea, na kila mtu anasema wewe ni mwizi. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Imani)

71. Mama yako anakuambia kuwa ulikosa, na unapaswa kukiri na urekebishe kosa lako. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Unyenyekevu)

72. Mama yako anakuambia kwamba anakupenda na hivyo unapaswa kumpenda, pia. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Huruma)

73. Rafiki yako anakwambia ukule kitu ambacho unajua hupaswi kula. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

74. Familia yako inajitayarisha kuhamia nyumba nyingine, hivyo unapaswa kwenda na kuishi na nyanya yako wakati

huu. Shujaa yupi atasaidia? (Imani)

75. Wazazi wako wanataka kukutuma dukani lakini jua ni kali na duka iko mbali sana. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Unyenyekevu)

76. Unagundua kwamba kaka yako aliiba pesa za baba yako. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

77. Baba yako anataka uondoe takataka nje, lakini ni usiku na kuna giza. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

78. Ulipokuwa na marafiki zako sokoni walikuambia uibe kitu dukani. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

79. Mwalimu wako shuleni anakuambia kuwa Mungu hayupo. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

80. Unataka kuomba ili uweze kupata udhamini kwa sababu ulipita mtihani. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

81. Marafiki zako wanakuambia uibe matunda kutoka kwa jirani. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

82. Marafiki zako wanataka upige kengele au ugonge mlango wa jirani na kisha utoroke, lakini wazazi wako

wamekuonya usifanye hivyo. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

83. Mwalimu wako anakuambia usome kitabu fulani, lakini wewe unataka kusoma kitabu tofauti. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Utiifu)

84. Mama yako anakuomba umwombee kwa sababu anaumwa na kichwa, na anakuambia kwamba Mungu

ataponya kwa maombi. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

85. Kuna mtoto shuleni ambaye ana huzuni kwa sababu hana chakula cha mchana na hana pesa. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Huruma)

86. Mchungaji wako alikuomba umsaidie kufundisha watoto lakini huna hakika ikiwa watakusikiliza. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Imani)

87. Shuleni mlienda kutembelea makao ya yatima ili kuona jinsi watoto hao huishi, na wakaomba kikundi chako

kiwasaidie watoto hawa. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

88. Siku yako ya kuhitimu inakaribia na mnahitajika kuvaa suruali nyeusi. Wazazi wako hawana uwezo wa

kukununulia suruali mpya, kwa hivyo unapaswa kumwomba binamu yako. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Unyenyekevu)

89. Mwenzako anataka kuongeza jina lako kwenye mradi, hata ingawa hukuchangia chochote. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Uadilifu)

90. Ulikwenda kanisani ili kusaidia lakini haukupewa chochote cha kufanya. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

91. Shuleni mtoto anakuomba umpe chakula chako cha mchana. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

Page 8: Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 · aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa

92. Unamwomba rafiki yako maji, lakini anakunyima. Unapaswa kuitikia maji hayo ni yake na kwamba yeye hataki

kukupa. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

93. Mwanafunzi ambaye ni mchafu sana na ananuka vibaya anataka kuingia katika kikundi chako. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Huruma)

94. Siku moja mvulana mtaani anakupa madawa ya kulevya. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

95. Msichana fulani darasani anasahau na kuacha pesa juu ya meza na hakuna mtu mwingine anagundua isipokuwa

wewe. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

96. Mwalimu anafundisha kitu kisicho sahihi darasani, kila kitu anasema sio sahihi hivyo kila mtu anamcheka, lakini

hujui cha kufanya. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

97. Wenzako wanasema wewe ni mwoga kwa sababu hupendi kwenda nje na wasichana, lakini unajua kwamba

unangoja wakati unaofaa wa kukutana na msichana, ambaye Mungu amekuchagulia. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Imani)

98. Kila mtu shuleni ananakili kazi ya nyumbani ya mwenziwe na leo unajipata haujafanya kazi yako ya nyumbani. Ni

shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

99. Watoto wa majirani wanafanya matendo yasiyofaa na baba yako alikushauri usicheze nao tena. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Utiifu)

100. Kuna huyu mtoto ambaye ni mjeuri sana na hupigana na wengine kila wakati, na anakuomba uwe rafiki

yake kwa sababu anahisi upweke. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

101. Mwenzako anakuita mwoga kwa sababu hupigani na wanafunzi wenzako.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uvumilivu)

102. Siku moja kiongozi wa kanisa lako anakuambia kuwa Mungu hawezi kukutumia kwa jambo lolote na

unahisi vibaya, kwa sababu inaonekana kwamba Mungu bado hajakuita kuhudumu.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Imani)

103. Mwalimu anachukua chingamu kutoka mdomoni mwake na kukupa ukule.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uvumilivu) HEHEHE!

104. Mchungaji alikuomba uwe unaenda kanisani mara moja kila wiki ili kufagia na hupendi kufanya hivyo.Ni

shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

105. Katika shule ya Jumapili mwalimu wako anapeana peremende, lakini mtoto mdogo kukuliko anakosa

kupata peremende yoyote.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

106. Mama yako alikuambia kuwa baba yako hakupendi. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

107. Marafiki zako wanataka muende pamoja na kuchora michoro kwenye kuta. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uadilifu)

108. Marafiki zako wanataka muende mvunje madirisha pamoja.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

109. Mwalimu wako wa shule ya Jumapili alikuambia kuwa wewe ni mvulana mzuri, lakini unastahili

kubadilika na kuboresha tabia fulani.Wewe hutaki kukubali maoni yake. Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Unyenyekevu)

110. Rafiki yako anakwambia mwende kusumbua jirani yako.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

111. Unagundua kwamba rafiki yako huwa anaiba fedha zako za chakula cha mchana.Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Uvumilivu)

112. Mchungaji wako anakuomba muende naye kwenye hospitali ili kuwaombea wagonjwa.Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Imani)

113. Mama yako alikwambia uende kutembelea shangazi ambaye humpendi na ambaye kila wakati

anakuzomea.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

114. Mama yako anajihisi mgonjwa na anakwambia umwombee.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

115. Mama yako anamgawia kaka yako mkubwa chakula kingi kukuliko, lakini anaelezea kuwa ni kwa sababu

yeye ni mtu mkubwa kukuliko, na unapaswa kuelewa mama yako.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

116. Rafiki wako anakuomba umsaidie kuiba mtihani. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

117. Unaenda onyesho na kugundua kuwa kichezeo chako ndicho kizee zaidi, lakini unajua kwamba wazazi

wako hawana uwezo wa kununua kichezeo kipya.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

118. Marafiki zako hawakujumuishi wanapocheza kandanda.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

Page 9: Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 · aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa

119. Rafiki anakuambia kwamba ili kupita mtihani unapaswa kuiba majibu kutoka kwa meza ya mwalimu.Ni

shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

120. Watoto wengine wanapiga mbwa mdogo na una waona.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

121. Kuna shilingi mia moja zilizoachwa kwenye dirisha la duka na hakuna mtu ameziona.Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Uadilifu)

122. Baba yako anakuomba uende uwape wanyama chakula, lakini kipindi unachopenda kwenye TV

kinakaribia kuanza.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

123. Mama yako anakuambia usaidie kusafisha vyoo vya kanisa, lakini hutaki kwa sababu ni vichafu.Ni shujaa

yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

124. Kwenye TV unamsikia mtu fulani akisema kuwa Mungu hayupo.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

125. Mnaenda kwa matembezi na familia yako na mnakutana na mlemavu akiomba msaada wa chakula.Ni

shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

126. Kanisani, mwenzako anasema uongo kukuhusu na huwezi kufanya chochote ila kusubiri mpaka ukweli

ujulikane.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

127. Rafiki ya kaka yako analala nyumbani kwenu, na wazazi wako wanakuomba umsongee kitandani

chako.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

128. Familia yako mnaomba Mungu ili ampatie nyumba mpya.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

129. Babu yako anakuomba umsaidie kusafisha bustani, lakini ni likizo na kuna jua jingi.Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Utiifu)

130. Unamwona mtoto wa jirani akiiba dukani.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

131. Mwenzako hana fedha za kutosha ili kununua kifungua kinywa chake.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Huruma)

132. Ni wakati wako wa kuhubiri kanisani na unahofia kufanya makosa mbele za watu.Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Imani)

133. Marafiki zako wanataka kukupeleka kwenye maonyesho bila ruhusa.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uvumilivu)

134. Hutaki kukamilisha kazi yako ya nyumbani kwa sababu unahisi uvivu.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

135. Kila mtu atakuwa amevaa nguo zinazopendeza kwenye karamu ya rafiki, lakini wazazi wako hawana

uwezo wa kununua nguo za bei ghali.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

136. Unaona muuzaji akimrudishia mtoto mdogo pesa zaidi.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

137. Mwenzako anakuambia umgonge mtoto mwingine.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

138. Ni Jumamosi asubuhi na babu na nyanya wanakuja kutembea.Wazazi wako wanakuomba usafishe

chumba chako kabla ya wao kufika. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

139. Marafiki zako wanataka kusumbua wanyama kwenye bustani ya wanyama.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uadilifu)

140. Kaka yako anakuambia kuwa wazazi wako hawakupendi kwa sababu kila wakati huwa wakakukemea.Ni

shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

141. Rafiki anakuomba mwende naye sehemu ambayo ina wanyama wengi na hupendi wanyama.Ni shujaa

yupi atakusaidia? (Huruma)

142. Unachelewa kufika katika darasa la kanisa kwa sababu haukuwa makini na mwalimu anapokuuliza

sababu ya kuchelewa unataka kumdanganya.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

143. Kulikuwa na mashindano ya uimbaji kanisani na mtu mmoja hakuimba vizuri na sasa kila mtu

anamcheka.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

144. Mko katika mkutano wa watoto na kuna huyu msichana anayekuomba umwombee ndugu yake kwa

sababu ni mgonjwa.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

145. Marafiki wako wanakualika kuogelea mtoni, lakini baba yako anakuonya kuwa kufanya hivyo ni hatari

sana.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

146. Wazazi wako walikuuliza uwaangalie ndugu zako wadogo, lakini kuna ndugu yako mdogo ambaye huwa

hatii unachomwambia.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

Page 10: Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 · aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa

147. Mwalimu anakuomba ufute bodi, lakini hupendi kufanya hivyo.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

148. Marafiki wako wanakuambia uwachezee mzaha majirani.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

149. Umepata kibeti na ulipokifungua ukapata maelezo ya mwenyewe.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

150. Unakutana na mzee akiwa amebeba mfuko mzito.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

151. Katika duka la shule wanakuomba usubiri mpaka waweze kuwashughulikia watoto wote wadogo.Ni

shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

152. Unaamini kuwa kutoa ni bora kuliko kupokea; lakini marafiki zako wanakuambia vinginevyo.Ni shujaa

yupi atakusaidia? (Imani)

153. Marafiki zako wanakuhimiza usiende kanisani Jumapili hii.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

154. Mpira wa jirani ulianguka upande wa nyumba yenu, lakini hawajui ulikwenda wapi.Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Uadilifu)

155. Familia ya rafiki yako iliibiwa kila kitu chao, na sasa wanahitaji msaada.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Huruma)

156. Baba yako anakuuliza uzime TV, kwa sababu programu inayoendelea ni mbaya kwako.Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Utiifu)

157. Umeketi sehemu nzuri sana kanisani, lakini unaambiwa usimame mtu mwingine aketi hapo.Ni shujaa

yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

158. Unajua kwamba wewe ni wa thamani, kwa sababu Biblia inasema hivyo; lakini kila mtu anakuambia

kuwa wewe ni bure.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

159. Marafiki wako wanakualika uangalie filamu iliyo na picha za ngono.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uvumilivu)

160. Shuleni unapata mfuko uliopotea.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

161. Wazazi wako wamekuuliza umwangalie dada yako mdogo, lakini unataka kwenda nje na kucheza na

marafiki zako.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

162. Huwa unaketi karibu na marafiki zako darasani, lakini mwalimu wako anataka ukae sehemu tofauti.Ni

shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

163. Wewe ni mgonjwa, na unamwomba mchungaji akuombee.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

164. Marafiki zako wana magazeti ya watu wazima na wanataka uyaangalie.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uvumilivu)

165. Mtu anakupea filamu haramu, za bei ya chini.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

166. Unaona jirani yako akisukuma gari lake, kwa sababu limekwama.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

167. Mnatazama TV pamoja na ndugu zako, na mama yako anataka wewe uende dukani.Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Utiifu)

168. Ulikuwa ukicheza mpira na ukaharibu mimea ya jirani.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

169. Katika darasa lako la Biblia, mwalimu anakualika umwombee mgonjwa.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Imani)

170. Marafiki zako wanataka umsumbue mwanafunzi ambaye hawampendi.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uvumilivu)

171. Unagundua kwamba mama yako aliacha pesa mezani, na ameshaondoka.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uadilifu)

172. Dada yako mdogo anataka kuchuna tunda mtini, lakini hawezi kufikia.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Huruma)

173. Mama yako anakuambia uondoe takataka nje, lakini hutaki.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

174. Wewe pamoja na dada yako mdogo mnataka peremende, lakini ni moja tu iliyobaki. Ni shujaa yupi

atakusaidia?(Unyenyekevu)

175. Baba yako anasema kuwa anataka kwenda nje kucheza na wewe.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

176. Marafiki zako wanataka muende kucheza katika eneo la jirani, lakini unajua jirani hapendi hilo.Ni shujaa

yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

177. Rafiki yako ana michezo mingi ya video, na unafikia kuiba mmoja.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

178. Unapata mama yako akiinua mbao nzito peke yake.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

Page 11: Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 · aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa

179. Mama yako anakuambia kuwa huwezi enda kucheza hadi umalize kazi yako ya nyumbani, lakini marafiki

zako tayari wanakungoja nje.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

180. Baba yako alikwambia ufanye kitu lakini hukufanya, sasa anakukemea.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Unyenyekevu)

181. Nyanyako amelazwa hospitalini, lakini kila mtu anakwambia kuwa atapata nafuu.Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Imani)

182. Unakutana na mtu mzima ambaye humjui na anakuambia uende pamoja naye kwa sababu ana zawadi

yako kwake nyumbani.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

183. Katika jokofu kuna kipande cha keki, unataka kukichukua, lakini unajua ni cha ndugu yako.Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Uadilifu)

184. Unaona mwanamke mzee akibeba mifuko mizito nje ya duka.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

185. Wazazi wako wamekupa saa moja uzime TV na uende kulala.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

186. Mwenzako anakusumbua, lakini hutaki kulipiza kisasi.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

187. Marafiki zako wanasema kwamba hupaswi kwenda kanisani.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

188. Marafiki zako wanataka uweke mnyama ndani ya mfuko wa mwanafunzi mwenzako. Ni shujaa yupi

atakusaidia?(Uvumilivu)

189. Mmoja wa ndugu yako amepoteza sanduku la krayoni, hujui ni nani, na unazihitaji.Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Uadilifu)

190. Mtoto mdogo kabisa shuleni ameshindwa kupanda juu ya kifaa cha kubembea.Unamwona akijaribu,

lakini anashindwa. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

191. Mama yako alikuambia kwamba unapaswa kutengeneza kitanda chako.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Utiifu)

192. Baba yako alikukemea, lakini sasa anataka umkumbatie na umbusu.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Unyenyekevu)

193. Marafiki zako wanasema kwamba Mungu amekuacha, lakini Biblia inasema kuwa Mungu atakuwa

pamoja nawe kila siku.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

194. Marafiki wako wanakuambia usiogope na upige kengele za kanisa.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Uvumilivu)

195. Unaona mtu akiangusha pesa wakati anafanya malipo dukani.Hakuna mtu anagundua isipokuwa

wewe. Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uadilifu)

196. Mtoto anaanguka akicheza uwanjani, lakini hakuna anayetaka kumsaidia.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Huruma)

197. Mama yako amekwambia ujifunge ukanda wa kiti wakati unapoingia kwenye gari, lakini unaona kwamba

watoto wengi hawafanyi hivyo.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

198. Baba yako alikuambia kuwa unapaswa kwenda na kumuomba msamaha jirani kwa kitu kibaya

ulichomfanyia.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Unyenyekevu)

199. Huamini kama unaweza kupita mtihani, lakini mama yako anakuambia umuombe Mungu na atakupa

hekima.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Imani)

200. Filamu uliokuwa ukingoja iko karibu kuanza kwenye TV, lakini ni wakati wa kwenda katika darasa lako la

Biblia.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Uvumilivu)

201. Katika duka la gazeti unaona gazeti unayopenda, lakini huna fedha.Unafikiri kuiba gazeti. Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Uadilifu)

202. Dada yako anakuja kwako akilia na kuomba msaada kwa sababu mnyama wake kipenzi ameumia.Ni

shujaa yupi atakusaidia? (Huruma)

203. Wazazi wako wamekuonya usizungumze na watu ambao huwajui.Ni shujaa yupi atakusaidia? (Utiifu)

204. Ndugu yako aliacha gari likiwa chafu sana, lakini baba yako amekuomba ulioshe.Ni shujaa yupi

atakusaidia? (Unyenyekevu)

205. Biblia inasema kwamba Mungu yu pamoja nawe na atakusaidia wakati wote.Ni shujaa yupi atakusaidia?

(Imani

Page 12: Wanafunzi wako wanaweza kucheza huu ili kujifunza jinsi ya kuhusisha sifa za … · 2018-11-09 · aliuawa akiwa na umri mdogo, anapata pointi 1 tu ya Nguvu. Anapokea pointi 90 kwa