warning for heavy rains/tahadhari ya mvua kubwa 20/01/2016 - 21/01/2016

Upload: muhidin-issa-michuzi

Post on 10-Mar-2016

36 views

Category:

Documents


0 download

DESCRIPTION

Warning for heavy rains/Tahadhari ya mvua kubwa 20/01/2016 - 21/01/2016.

TRANSCRIPT

  • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

    MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

    Simu: 255 22 2460735/2460706

    FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056

    Barua pepe: [email protected] DAR ES SALAAM

    Tovuti: www.meteo.go.tz

    Unapojibu tafadhali nakili:

    Kumb. Na.: TMA/1622 20 Januari, 2016

    Taarifa kwa Umma: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa.

    Taarifa Na. 201601-02

    Muda wa Kutolewa

    Saa za Afrika Mashariki Saa 9:00 Alasiri

    Daraja la Taarifa: Tahadhari

    Kuanzia:

    Tarehe 20 Januari, 2016 - Usiku

    Mpaka:

    Tarehe 21 Januari, 2016

    Aina ya Tukio

    Linalotarajiwa

    Vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa

    24 katika siku hizo vinatarajiwa.

    Kiwango cha uhakika: Wastani (80%)

    Maeneo yanayotarajiwa

    kuathirika

    Mikoa ya Lindi, Mtwara na kusini mwa mikoa ya Pwani na

    Morogoro

    Maelezo:

    Hali hii inatokana na kuendelea kuimarika kwa ukanda wa

    mvua katika maeneo yaliyotajwa hapo juu. Pia kutokana na

    mvua kubwa zilizonyesha katika maeneo hayo, mvua

    zinazotarajiwa zinaweza kusababisha mafuriko.

    Angalizo:

    Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa kujitokeza pia

    kwenye maeneo machache ya mikoa ya Arusha,

    Kilimanjaro, Manyara na Mara.

    Wakazi wa maeneo tajwa wanashauriwa kuendelea

    kuchukua tahadhari na hatua stahiki.

    Maelezo ya Ziada Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii

    na itatoa mrejeo kila itakapobidi.

    Imetolewa na

    Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.