wordpress.com · web viewkwa kufanya hivi, “hakuna tena myahudi au myunani, mtumwa au mtu huru,...

44
Maisha ndani ya Kristo Utangulizi Kuwa mkristo ni kuwa na uhusiano na ushirika na Bwana Yesu Kristo. Swali ni, je uhusiano huu unawezekana kwa njia gani? Je, ikiwa mtu anajitahidi sana kuishi maisha mazuri, hii itamfanya kuwa mkristo? Biblia inasema kwamba, hakuna mtu ambaye anaweza kufanywa mkristo kwa kuishi maisha mazuri. Je, ikiwa mtu anamheshimu Kristo kwa sababu Biblia inasema kwamba lazima tumheshimu kwa sababu Yeye anastahili heshima zetu, hii itamfanya mtu huyo kuwa mkristo? Jibu ni la. Kwa sababu kumheshimu tu Kristo haiwezi kumwokoa mtu yeyote. Kile kila mtu anahitaji kufanya ni kufahamu kwamba Kristo Yesu alikuja hapa ulimwenguni kuishi na baadaye kufa kwa ajili ya wenye dhambi kama wewe. Mwamini Yesu kuwa Mwokozi wako na umtegemee Yeye pekee katika maisha yako yote ili ukubalike mbele za Mungu kwa ajili ya yale ambayo amekufanyia. Hivi ndivyo inavyomaanisha kuwa mkristo: ni yule mtu ambaye amemwamini Kristo na ambaye ana uzima wa milele (Yohana 3:16). Imani ambayo inaokoa huwa inatuleta katika uhusiano na ushirika ambao umejawa na furaha tele na utajiri mkubwa wa kiroho. Huwa tunamjua Kristo Yesu kama Mwokozi na Bwana, Kuhani na Mfalme, Rafiki na Ndugu wetu. Agano Jipya linatufafanulia vyema kuhusu uhusiano wetu na Kristo. Katika makanisa mengi jambo hili limesahaulika sana na wengi huwa hawalielewi kamwe. Jambo hili ni siri ambayo imefunuliwa kwetu leo na pia si gumu kufahamu. Tunapofahamu jambo hili, maisha yetu hubadilika kabisa na kusudi kuu la kitabu hiki ni kuwahimiza wale wote ambao ni wakristo kuhusu jambo hili. Pia ninaomba sana kwamba yale ambayo ninafundisha hapa yatawasaidia wengi kuvutwa na kuletwa kwa Kristo Yesu ili waweze kuokoka. Ninaomba kwamba Mungu atakupatia tamaa ya kuwa na uhusiano na ushirika na Bwana Yesu Kristo na kwamba hutapumzika hadi umeokoka. Je, uhusiano huu na Kristo ni wa aina gani? Huu ni uhusiano ambao umekuja kwa sababu ya kuunganishwa na Kristo Yesu. Mtume Paulo anazungumzia jambo hili kwa kutumia neno katika. Neno hili limetumika kama mara mia mbili katika maandishi ya Paulo. Kwa mfano kuna mahali ambapo anasema, katika Kristo, katika Yeye, na katika Bwana. Katika Kitabu cha Waefeso 1:1-14, anazungumza kuhusu kuwa katika Kristo Yesu kama mara kumi na moja. Wakristo katika mji wa Efeso walikuwa waaminifu katika Kristo. Vivyo hivyo, Wafilipi walikuwa watakatifu katika Kristo Yesu (Wafilipi 1:1) na Wakolosai walikuwa Watakatifu na ndugu waaminifu katika Kristo (Wakolosai 1:2). Kulingana na neno la Mungu, mkristo ni mtu ambaye ako katika Kristo. Hii ndiyo sababu kuunganishwa pamoja na Kristo ndiyo msingi mkuu wa mafundisho ya wokovu ambayo yanahubiriwa na makanisa matakatifu ya Mungu. Kuunganishwa na Kristo Yesu ni jambo kubwa sana kwa sababu lilifanyika kabla ya ulimwengu kuwepo na litaendelea hadi milele. Mafundisho haya ni makuu sana kwa sababu yamejawa na baraka zote za wokovu. Hata kama wengi wemesoma na kujaribu kuandika mambo mazuri kuyahusu mafundisho haya, wanadamu hawayafahamu kabisa hata kama wameamurishwa na Mungu wayatii kwa imani. Kwa hivyo msomaji wangu usitarajie nikueleze kila kitu kwa sababu hata mimi sijui kila kitu.

Upload: others

Post on 05-Nov-2020

1 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Maisha ndani ya Kristo

Utangulizi

Kuwa mkristo ni kuwa na uhusiano na ushirika na Bwana Yesu Kristo. Swali ni, je uhusiano huu unawezekana kwa njia gani? Je, ikiwa mtu anajitahidi sana kuishi maisha mazuri, hii itamfanya kuwa mkristo? Biblia inasema kwamba, hakuna mtu ambaye anaweza kufanywa mkristo kwa kuishi maisha mazuri. Je, ikiwa mtu anamheshimu Kristo kwa sababu Biblia inasema kwamba lazima tumheshimu kwa sababu Yeye anastahili heshima zetu, hii itamfanya mtu huyo kuwa mkristo? Jibu ni la. Kwa sababu kumheshimu tu Kristo haiwezi kumwokoa mtu yeyote.

Kile kila mtu anahitaji kufanya ni kufahamu kwamba Kristo Yesu alikuja hapa ulimwenguni kuishi na baadaye kufa kwa ajili ya wenye dhambi kama wewe. Mwamini Yesu kuwa Mwokozi wako na umtegemee Yeye pekee katika maisha yako yote ili ukubalike mbele za Mungu kwa ajili ya yale ambayo amekufanyia. Hivi ndivyo inavyomaanisha kuwa mkristo: ni yule mtu ambaye amemwamini Kristo na ambaye ana uzima wa milele (Yohana 3:16).

Imani ambayo inaokoa huwa inatuleta katika uhusiano na ushirika ambao umejawa na furaha tele na utajiri mkubwa wa kiroho. Huwa tunamjua Kristo Yesu kama Mwokozi na Bwana, Kuhani na Mfalme, Rafiki na Ndugu wetu. Agano Jipya linatufafanulia vyema kuhusu uhusiano wetu na Kristo. Katika makanisa mengi jambo hili limesahaulika sana na wengi huwa hawalielewi kamwe. Jambo hili ni siri ambayo imefunuliwa kwetu leo na pia si gumu kufahamu. Tunapofahamu jambo hili, maisha yetu hubadilika kabisa na kusudi kuu la kitabu hiki ni kuwahimiza wale wote ambao ni wakristo kuhusu jambo hili. Pia ninaomba sana kwamba yale ambayo ninafundisha hapa yatawasaidia wengi kuvutwa na kuletwa kwa Kristo Yesu ili waweze kuokoka. Ninaomba kwamba Mungu atakupatia tamaa ya kuwa na uhusiano na ushirika na Bwana Yesu Kristo na kwamba hutapumzika hadi umeokoka.

Je, uhusiano huu na Kristo ni wa aina gani? Huu ni uhusiano ambao umekuja kwa sababu ya kuunganishwa na Kristo Yesu. Mtume Paulo anazungumzia jambo hili kwa kutumia neno “katika.” Neno hili limetumika kama mara mia mbili katika maandishi ya Paulo. Kwa mfano kuna mahali ambapo anasema, “katika Kristo, katika Yeye, na katika Bwana.” Katika Kitabu cha Waefeso 1:1-14, anazungumza kuhusu kuwa katika Kristo Yesu kama mara kumi na moja. Wakristo katika mji wa Efeso walikuwa “waaminifu katika Kristo.” Vivyo hivyo, Wafilipi walikuwa “watakatifu katika Kristo Yesu” (Wafilipi 1:1) na Wakolosai walikuwa “Watakatifu na ndugu waaminifu katika Kristo” (Wakolosai 1:2). Kulingana na neno la Mungu, mkristo ni mtu ambaye ako “katika Kristo.” Hii ndiyo sababu kuunganishwa pamoja na Kristo ndiyo msingi mkuu wa mafundisho ya wokovu ambayo yanahubiriwa na makanisa matakatifu ya Mungu.

Kuunganishwa na Kristo Yesu ni jambo kubwa sana kwa sababu lilifanyika kabla ya ulimwengu kuwepo na litaendelea hadi milele. Mafundisho haya ni makuu sana kwa sababu yamejawa na baraka zote za wokovu. Hata kama wengi wemesoma na kujaribu kuandika mambo mazuri kuyahusu mafundisho haya, wanadamu hawayafahamu kabisa hata kama wameamurishwa na Mungu wayatii kwa imani. Kwa hivyo msomaji wangu usitarajie nikueleze kila kitu kwa sababu hata mimi sijui kila kitu.

Kile ninaweza kukuambia ni kwamba mafundisho haya yalinisaidia sana na yameendelea kunisaidia sana katika maisha yangu ya ukristo. Kwa hivyo ninaomba kwamba unapoendelea kuyasoma, kwa ujasiri, utasema kweli “mimi niko katika Kristo,” na kwamba maneno haya yatamaanisha jambo kubwa kuliko jinsi umekuwa ukiwaza.

Page 2: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Tutaona jinsi kuunganishwa kwa Kristo kunatuletea maisha mapya na pia tutaona jinsi tunafaa kumtegemea Kristo pekee katika maisha yetu tunapoishi katika ulimwengu huu mwovu. Tutasoma kuhusu jamii kubwa ya Mungu ambayo ni jamii yetu sasa. Tutaona jinsi mateso na shida ni moja ya njia ambazo Mungu anatumia kutuvuta karibu na karibu kwa Kristo Yesu na kutufanya tuwe kama Kristo mwenyewe.

Tutaanza na jinsi tunapoingia katika uhusiano na ushirika huu pamoja na Kristo.

Sura ya Kwanza

Imani ndani ya Kristo

Je, Kristo ni nani ambaye wakristo wote wameunganishwa Kwake? Jibu la Biblia ni kwamba, Yeye ndiye Mwana wa Mungu, Yeye ni yule yule ambaye kwa mamlaka na utukufu ako sawa na Mungu Baba. Yeye ndiye Mesiya, Yule ambaye amepakwa mafuta na ndiyo timizo la tumaini la watu wote wa Mungu. Yeye ndiye Mwokozi ambaye aliishi maisha matakatifu, akafa msalabani, alifufuliwa kutoka kwa wafu na alirudi mbinguni. Yeye ndiye Mfalme wa sasa na hakimu ambaye atahukumu ulimwengu. Yeye ni haya yote na mengine mengi sana. Kwa haya yote tutazingatia mambo mawili tu haswa yale ambayo Paulo anatumia katika 1 Wakorintho 15:45;47 akimfafanua Yesu Kristo, yaani “Adamu wa mwisho” na “Mtu wa pili.”

Adamu wa mwisho

Adamu alikuwa mwakilishi wa wanadamu wote. Paul anazungumza kuhusu Adamu na Kristo kuwa ndiyo watu muhimu kabisa ambao wamewahi ishi katika ulimwengu wote na kwamba hakuna mtu mwingine ambaye atawahi linganishwa nao. Swali ni, kwa nini Paulo katika kuandika kwake awaze hivi? Jibu ni kwamba, kuna wakilishi wawili kwa watu wote wa ulimwengu: Adamu na Kristo.

Hii inatuonyesha kwamba Mungu huwa hashuguliki tu na wanadamu kwa misingi ya kibinafsi bali anawaona wanadamu na kuwashughulikia kama kikundi kupitia kwa mpango Wake mwenyewe. Mpango huu ni agano ambalo Mungu mwenyewe ametengeneza na watu wake.

Katika agano hili, Mungu anamchagua mtu mmoja kuwa mwakilishi wa kikundi cha watu wengi. Uhusiano ambao Mungu ako nao na mwakilishi wa kikundi hicho, ndiyo ule ule ako nao na kila mtu ambaye anaakilishwa katika kikundi hicho. Kila shughuli ya Mungu juu ya kila mtu wa kikundi hicho anaifanya kupitia kwa mwakilishi wa kikundi hicho. Mungu katika mipango Wake amewaweka wakilishi wawili, yaani Adamu na Kristo, na kila mwanadamu amewakilishwa na Kristo au Adamu. Unaweza kufahamu hali yako ya dhambi ikiwa utafahamu kwamba wewe ulizaliwa katika Adamu na kwa hivyo yeye ndiye mwakilishi wako. Unaweza tu kufahamu na kufurahia wokovu wako ikiwa utafahamu kwamba umeondolewa katika Adamu na kwa hivyo yeye sasa si mwakilishi wako. Wewe sasa kuletwa katika Kristo na sasa ni mwakilishi wako. Paulo anazungumza juu ya jambo hili katika Warumi 5:12-21.

Kile ninamaanisha kwa mfano ni, mtu mmoja anaishi katika eneo la mbunge fulani ambaye ni adui wa Rais. Kwa hivyo eneo lake halifaidiki hata kidogo kutoka kwa serikali kwa sababu mbunge ni adui wa Rais. Lakini siku moja huyo mtu anahamia eneo lingine ambalo mbunge wake ni mtoto wa Rais. Ni wazi kwamba atafaidika sana kwa sababu mbunge wake ni mtoto wa Rais. Vivyo hivyo wale ambao

Page 3: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

hawajaokoka wako katika Adamu ambaye ni mwakilishi wao na ambaye alianguka dhambini. Kwa hivyo wao pia wanahesabiwa kuwa wenye dhambi na maadui wa Mungu. Lakini yule ambaye anaokoka anaondolewa kutoka katika Adamu na kuletwa katika Kristo ambaye ndiye Mwana wa Mungu. Kwa hivyo wao sasa wanapata baraka zote kutoka kwa Mungu kwa sababu Mwakilishi wao ndiye Mwana wa Mungu.

Mtu mmoja

Katika kifungu hiki cha Warumi 5, neno la kuzingatia sana ni “Mtu mmoja.” Kila jambo ambalo Adamu alifanya, kila mtu anahesabiwa amelifanya. Adamu baada ya kuanguka dhambini, hakuwa na uhusiano na Mungu, na kwa hivyo wale ambao wako katika Adamu pia hawana uhusiano wowote na Mungu. Kwa njia hiyo hiyo kila jambo ambalo Kristo alifanya akiwa mtu Mmoja, limehesabiwa kwa wale wote ambao anawakilisha, pia maisha Yake matakatifu yamehesabiwa kwa wale ambao anawakilisha. Kile ninamaanisha ni kwamba kulingana na mafundisho ya Biblia, wakati Adamu alitenda dhambi, kila mwanadamu alitenda ile dhambi. Hii ndiyo sababu Biblia inasema, “Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja na kupitia dhambi hii, mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi” (Warumi 5:12). Vilevile, wakati Kristo alitii sheria ya Mungu wale wote ambao wameokoka walitii pamoja naye. Hii ndiyo sababu Biblia inasema, “Kwa tendo la mtu mmoja la haki huleta kuhesabiwa haki kule kuletako uzima kwa wote...vivyo hivyo kwa kutii kwa mtu mmoja wengi watafanywa wenye haki” (Warumi 5:18,19).

Tunaona hapa hali ya mwanadamu kwamba yeye amenaswa katika dhambi. “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja...Kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:10;23). Je, kwa nini ikawa hivi? Je, ni kwa sababu kwamba kila mwanadamu mwenyewe amechagua kutenda dhambi? Biblia inasema, la. Jibu lile Biblia inapeana katika Warumi 3:10;23 ni kwamba, kila mwanadamu ni mwovu kwa sababu ya dhambi ya Adamu ambaye ndiye mwakilishi wa kizazi chote cha mwanadamu. Paulo anasisitizia jambo hili katika Warumi 5. Anasema, dhambi iliingia ulimwenguni kupitia “kwa mtu mmoja” (mstari wa 12), “Wengi walikufa kwa sababu ya kosa la mtu mmoja” (mstari wa 15), “Hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja” (Mstari wa 16), “Kwa maana ikiwa kutokana na kosa la mtu mmoja, mauti ilitawala” (Mstari wa 17), “Kwa hivyo kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa watu wote” (Mstari wa 18), “Kwa maana kwa vile kwa kutotii kwa yule mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi” (Mstari 19).

Je, unafahamu kusisitizwa kwa maneno haya: “Mtu mmoja”? Sisi sote ni watenda dhambi kwa sababu ya uhusiano wetu na Adamu. Kwa ufupi ni kwamba, “Wanadamu wote ambao wametoka kwa Adamu, kwa asili, wamefanya dhambi ndani mwake na wakaanguka naye katika dhambi ya kwanza.” Sisi sote tulikuwa ndani mwa Adamu wakati alipoanguka katika dhambi na mauti ilitufikia na hukumu kwa kupitia kwake. Dhambi ndiyo hali ya kila mwanadamu ulimwenguni kote kwa sababu sisi kwa asili ni watoto wa Adamu.

Hata katika hali hii, tunamshukuru Mungu kwamba huu siyo mwisho wa kila mwanadamu kwa sababu kuna wokovu ambao umeahidiwa pamoja na uzima wa milele na baraka tele tele. Je, wokovu huu unatufikia aje? Je, ni kwa njia gani mtu anaweza kupata wokovu huu? Hapa ndipo mtume Paulo anatueleza ukweli wote ambao unapatikana katika Biblia. Hapa ndiyo kuna mabishano ya wengi ambao wanawaza kwamba wokovu hupatikana kwa kufanya matendo mazuri na kwa kujitahidi kwao kuwa wazuri. Maoni ya watu hawa ni kwamba, Mungu ni kama ametengeza mtihani na kwamba mtu lazima ajitahidi kibinafsi apite mtihani huu. Na wanawaza kwamba ni juhudi za mtu ambazo zitamsaidia kupita mtihani huu. Ikiwa mtu atajitahidi sana kwa kufanya vizuri sana, basi atapita mtihani huu na ataokoka.

Page 4: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Lakini Paulo anauliza, je, ni namna hii tulipotea kwanza? Jibu ni la, kwa sababu tumepotea kupitia kwa mtu mmoja, yaani Adamu, ambaye ni mwalikishi wa kizazi cha wanadamu wote. Ikiwa tulipotea kwa njia hii, je, tutaokolewa aje? Jibu ni kwamba tunwaweza tu kuokolewa kupitia kwa Mtu Mmoja, kwa sababu tulianguka dhambini kupitia mtu mmoja.

Warumi 5 inaendelea kusema, “Neema ya Mungu na ile karamu iliyokuja kwa neema ya mtu mmoja, yaani Kristo imezidi kuwa nyingi kwa ajili ya wengi” (mstari wa 15), “Wale wanaopokea wingi wa neema ya Mungu na karamu Yake ya kuhesabiwa haki, watatawala katika uzima kwa njia ya huyo mtu mmoja, yaani, Yesu Kristo” (mstari wa 17), “Tendo la mtu mmoja la haki huleta kuhesabiwa haki kule kuletako uzima wa wote” (mstari wa 18) na “Kwa kutii kwa mtu mmoja wengi watafanywa wenye haki” (mstari wa 19).

Je, unaona hapa jinsi Mungu mwenye hekima yote anavyodhihirishwa? Yeye ni Mungu ambaye anajua mwanzo hadi mwisho na ambaye amepanga kila kitu kwa njia kuu zaidi. Njia tunapaswa kutumia kurudi kwa Mungu ndiyo ile ile ambayo tulitumia wakati tulitoka Kwake. Njia ya wokovu wetu ambayo ni kuu zaidi kuliko kuanguka kwetu dhambini, inaweza kudhihirisha jinsi tulianguka dhambini. Katika Adamu tulianguka dhambini. Katika Adamu tulikufa kiroho na tulihukumiwa, lakini katika Kristo tumetii sheria zote za Mungu na kwa hivyo tunaishi kiroho. Katika Kristo tumeishi maisha makamilifu, katika Kristo tumelipa deni la dhambi, katika Kristo tumefufuliwa na katika Kristo tunaishi milele. Kila kitu ambacho Kristo alifanya kwa wokovu wetu, Mungu Baba anahesabu kwamba sisi wenyewe tumekifanya. Mateso yake yote yanahesabiwa yetu na ushindi Wake msalabani ni ushindi wetu.

Hii ndiyo sababu Mungu anatazama wanadamu wakiwa katika vikundi viwili, yaani wale ambao wako katika Adamu, na wale ambao wako katika Kristo Yesu. Ukweli ambao uko katika Biblia ni kwamba kuna watu wawili ambao waliishi hapa ulimwenguni na kila maisha ya mwanadamu yanategemea hawa wawili. Biblia inasema kwamba, “Kwa maana kama vile katika Adamu watu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Kristo wote watafanywa hai” (1 Wakorintho 15:22). Mimi na wewe tuko katika Adamu au Kristo, na kwa hivyo mwishowe kuishi au kufa kwetu kunategemea ni nani mwakilishi wetu. Kwa hivyo sasa tunaweza kufahamu ni nini Paulo anamaanisha wakati anamwita mwokozi “Adamu wa mwisho au Mtu wa pili.” Kristo ndiye kichwa cha kila mtu ambaye ameokoka na amewafanya kuwa watu wapya. Yeye ndiye kichwa cha mwanamume na mwanamke ambao wako katika uhusiano na Mungu, na Mungu anawashughulikia kwa njia mpya kabisa.

Sasa kila mkristo ameondolewa kutoka kwa Adamu na ameletwa katika Kristo, ambaye ndiye mwakilishi wa Agano Jipya. Tumeunganishwa kwa “Mtu wa pili.” Kwa sababu ya Kristo Yesu kuna wanaume na wanawake wengi wapya, idadi ambayo isiyohesabika: “Umati mkubwa wa watu ambao hakuna ye yote awezaye kuuhesabu. Kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha” (Ufunuo 7:9). Kristo ndiye mwokozi ambaye tunaitwa kuamini. Kuungana na Kristo kunamaanisha kuwa sehemu ya mpango wa Mungu wa kufanya kila kitu kuwa kipya.

Mabadiliko makubwa

Wokovu ni kuondolewa katika Adamu na kuletwa katika Kristo Yesu. Haya ni mabadiliko makubwa sana ambayo yanaweza tu kufanywa na Mungu pekee. Wale wote ambao wameokoka sasa wanawakilishwa na Kristo mbele ya Mungu na wamefanywa watu wapya. Wokovu ni kuunganishwa

Page 5: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

kwa Kristo Yesu Mwenyewe. Ni Mungu Roho Mtakatifu mwenyewe ambaye anafanya kazi hii, ni Yeye mwenyewe ambaye anatuwezesha tuwe katika Kristo milele. Yeye ndiye anayetuondoa kutoka katika Adamu na kutuleta katika Kristo. Wakati Paulo anaandika kuhusu kanisa anasema, “Katika Roho mmoja wote tulibatizwa katika mwili mmoja” (1 Wakorintho 12:13).

Je, jambo hili linafanyika aje? Je, tunawezaje kujua kwamba mtu ameunganishwa kwa Kristo na Roho Mtakatifu? Ishara ni imani. Kile Roho Mtakatifu anafanya ni kwamba anatuleta katika wokovu wetu ambao uligharamiwa na Kristo Yesu Mwenyewe. Wakati Roho Mtakatifu anatufanya tuzaliwe mara ya pili, huwa anatuwezesha kumwamini Kristo na hili ndilo jambo muhimu sana kwetu. Ni kwa imani tunakuja kwa Kristo na bila imani hatuwezi kuja kwake na kuokolewa.

Haya ni mafundisho ya undani sana, na hakuna yeyote ambaye anaweza kuyaelewa kabisa, zaidi ya jinsi Mungu ameyafunua kwetu. Ukweli ni kwamba wateule wa Mungu wamekuwa katika Kristo kabla ya Mungu kuweka misingi ya ulimwengu (Waefeso 1:4). Kabla hajasulibishwa, Bwana Yesu Kristo alimwomba Baba, “Nimewajulisha Jina Lako wale ulionipa kutoka katika ulimwengu. Walikuwa wako, ukanipa Mimi, nao wamelitii Neno Lako” (Yohana 17:6). Wale wote ambao wataokoka milele, Mungu Baba aliwachagua kabla ya Yeye kuumba ulimwengu, na alimpa Kristo watu hawa. Hii ndiyo sababu wao wameunganishwa kwa Kristo tangu milele. Hii inamaanisha kwamba kabla ya Mungu kuweka misingi ya ulimwengu, Yeye aliwachagua wakristo wote wawe katika Kristo

Lakini pia hatuwezi kuingia katika ushirika huu au kufurahia baraka zake hadi wakati tunaamini. Paulo aliwakumbusha wakristo wa mji wa Efeso ambao walikuwa wamechaguliwa kwamba kulikwa na wakati ambapo wao walikuwa wafu katika makosa na dhambi zao ambazo walizitenda (Waefeso 2:1-2). Pia Paulo anasema hivi kuhusu Andronico na Yunia katika waraka wa Warumi kwamba, “walikuwa katika Kristo kabla yangu”(Warumi 16:7). Sababu ya Paulo kusema hivi haikuwa kwamba yeye hakuwa amechaguliwa na Mungu, bali ni kwa sababu yeye hakuwa ameamini wakati huo. Yaani mtu anaweza kuwa katika Kristo kwa sababu amechaguliwa na Mungu aokoka, lakini awe bado hajamwamini Kristo na kuokoka. Kuamini ni jambo muhimu sana, na hii ndiyo sababu Biblia inasema, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

Kuamini katika Kristo.

Je, inamaanisha nini kuamini? Huwa mara mingi tunaamini mambo ambayo tunaambiwa au kuona. Kwa mfano tunaamini kwamba Kampala ni mji mkuu katika nchi ya Uganda kwa sababu tumeambiwa jambo hili. Lakini kuamini jambo hili hakuwezi kubadilisha maisha yetu au kutuletea furaha. Hili ni jambo kweli lakini halileti mabadiliko maishani mwetu.

Hii siyo ukweli wakati tunazungumza kuhusu kumwamini Kristo. Kumwamini Kristo ni zaidi ya kukubali kwamba Yeye aliishi hapa ulimwenguni na akateseka na kufa kwa ajili ya watenda dhambi. Kumwamini Kristo ni kuishi ndani Mwake na kufanya yale ambayo yanamtukuza Yeye mwenyewe. Kunamaanisha kujitambulisha kwamba wewe ni mtu wa Kristo na kujitolea kabisa kwa ajili Yake pekee. Ikiwa unamwamini Kristo, basi wewe unategemea Yeye kwa kila kitu. Ni Yeye pekee ambaye unamtazama na kumtegemea kwa kila kitu. Wewe ni mmoja wa mwili Wake sasa na kwa milele yote. Yeye ni kila kitu kwako, uaminifu wako sasa ni Kwake. Wewe uko ndani Mwake na Yeye ndiye maisha yako ya milele. Ndani Mwake wewe ni kiumbe kipya. Waza juu ya mitume, je kumwamini kulimaanisha nini kwao? Kuamini kulimaansiha kubadilishwa kabisa kutoka ndani mwao. Walijitambulisha naye mbele za watu na walimsikiza na kuzungumza naye. Kila kitu ambacho aliwaambia waliamini na walijaribu kukitii. Yesu Kristo na wanafunzi wake walitembea nchini kote

Page 6: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

pamoja. Walitembea pamoja, wakafanya kazi pamoja na walitatizwa pamoja. Walikuwa pamoja naye na walisimama naye. Kwao kuamini kulimaaninisha kujitolea kabisa kwa ajili ya Bwana Yesu Kristo milele. Hii ndiyo sababu Petro alimwambia Kristo, “Tazama, sisi tumeacha kila kitu na kukufuata” (Mathayo 19:27).

Tunapokuja kwa Kristo Yesu kwa imani, tunaweza kukosa kujua kwamba tunafaa kujitolea kabisa. Bwana arusi huwa hafahamu kabisa siku ya ndoa jinsi maisha yake yatakavyobadilika, kwamba ujana wake unabadilika na mke ambaye anaoa ako na mipango mingi juu ya maisha yake. Sasa bwana arusi huyu hajui kabisa kwamba pesa ambayo alikuwa anatumia kwa starehe zake sasa mke wake atazitumia kwa mahitaji ya nyumba. Masaa ambayo alikuwa akimaliza kwa kutazama mpira kwa runinga, baada ya kuoa anapaswa kuyatumia kuwa pamoja na mke wake. Sasa yeye hayuko peke yake, na kwa hivyo ni lazima ajifunze kuishi kwa ajili ya mke wake. Lakini hata kama haelewi kabisa majukumu haya yote, ukweli ni kwamba majukumu haya yako hapo hadi afe. Aliapa kuyatekeleza kikamilifu katika hali zote za maisha. Hivi ndivyo ilivyo kujitolea kwa ajili ya Kristo Yesu.

Imani ambayo inayohubiriwa katika makanisa mengi leo ni imani ya kuwapotosha watu. Watu wanaambiwa kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na kile wanahitaji kufanya ni kukubali kwamba kweli jambo hili lilifanyika na kwamba dhabihu yake ilikuwa kwa ajili yetu. Wanaambiwa kwamba hii ni imani ya wokovu ambayo kila mtu anahitaji ili awe mkristo. Ni kama mtu ambaye ako na deni kubwa sana na siku moja anasikia kwamba kuna mtu ambaye ako tayari kumlipia deni hilo. Anaambiwa kwamba kile anahitaji kufanya ni kukubali kwamba ako na deni hilo na mara moja litalipwa hata kama mtu mwenye kulilipa hamfahamu. Yeye bora tu aelewe kwamba deni lake limelipwa na mtu mwingine.

Imani iletayo wokovu kulingana na Biblia ni tofauti sana na mafundisho haya. Imani iletayo wokovu kulingana na Biblia inafanya kazi na iko. Agano Jipya linazungumza kuhusu kuamini katika Kristo au juu ya Kristo. Maneno haya yote yanafundisha kwamba imani ya ukweli inatuleta katika uhusiano wa karibu sana na Kristo na inatuunganisha kwa Kristo. Kuamini kunamaanisha kuja kwa Kristo Yesu, kumpokea Kristo Yesu na kumwamini Kristo Yesu kwa wokovo wetu. Kristo alisema kwamba kumwamini ni kama kunywa damu Yake na kula mwili wake (Yohana 6:53). Kuamini kunamanisha kuingia ndani ya Kristo, kuwa Wake, kuwa pamoja naye na kuunganishwa Kwake milele. Imani ya wokovu si kupokea baraka za mtu ambaye hatumjui na hatujawahi kutana naye. Badala yake inamaanisha kuwa na uwezo wa kusema “Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo” (Wafilipi 1:21).

Hii ndiyo sababu maandiko yanatuonyesha kwamba uhusiano wetu na Kristo ni wa karibu sana. Sisi ndiyo mawe katika jengo na Yeye ndiye jiwe kuu (Waefeso 2:19-22; 1 Petro 2:4-8); sisi ni matawi na Kristo ndiye mzabibu (Yohana 15:1-8); sisi ni mwili wa Kristo na Yeye ndiye kichwa (Waefeso 4:15-16; 1 Wakorintho 12); Kristo ndiye Bwana Arusi na sisi ndiyo bibi arusi (Waefeso 5:30,32). Uhusiano wetu ni wa karibu sana na unatuhusisha sisi wenyewe na ni wa ushirika wa sisi kwa sisi. Hii inamaanisha kuwa na Kristo ambaye yupo karibu sana na ambaye ako pamoja nasi kila wakati.

Ukweli ni kwamba wokovu ni jambo kuu sana kuliko jinsi watu wengi wanavyowaza. Ni jambo ambalo hatuwezi kufafanua kwa njia za wanadamu kwa sababu wokovu si kuamua tu kumpokea Kristo, bali ni zaidi ya kufanya uamuzi. Je, inawezekanaje kwamba uamuzi wetu unabadilisha hali yetu mbele za Mungu? Ikiwa tunataka kufahamu kabisa wokovu, lazima kwanza tufahamu kwamba huu ni mpango na kazi ya Mungu kwa neema Yake. Wokovu ni kubadilishwa na kuwa kiumbe kipya na kuletwa katika uhusiano wa uaminifu na Kristo. Kristo anakuwa kila kitu kwa yote. Wokovu ni kuondolewa kutoka katika Adamu na kuletwa katika Kristo.

Page 7: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Uhusiano mpya

Je, kuwa katika Kristo kunamaanisha nini? Kulingana na Paulo kila kitu kinabadilika: “Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya” (2 Wakorintho 5:17). Uhusiano wetu na Mungu umebadilika. Wakati tulikuwa katika Adamu, tulikuwa mbali na Mungu, na tuliishi chini ya hasira Yake na mwisho wetu ulikuwa hukumu wake. Lakini sasa kwa sababu tuko katika Kristo, Mungu Baba anatushughulikia kupitia kwa Kristo Yesu pekee. Mungu Baba hakubali kuwa na uhusiano wowote na mtu yeyote kupitia kwa njia nyingine yeyote isipokuwa kupitia kwa Kristo Yesu. Kila neno analozungumza nasi, kila amri, kila ahadi na kila agizo, yote yanatufikia kupitia kwa Kristo Yesu. Kila baraka tunayopata, tunaipata kupitia kwa Kristo Yesu. Wakati Mungu Baba anatuadhibu, anatuadhibu kupitia kwa Kristo Yesu. Kila wakati Mungu hutulinda, hutupa nguvu, hutuongoza na kutusaidia, yote ni kupitia kwa Kristo Yesu. Kila kitu ambacho Mungu Baba anawafanyia watu wake, anakifanya kupitia kwa Kristo Yesu.

Paulo anatuambia, tunateseka Naye (Warumi 8:17); tumesulibishwa Naye (Warumi 6:6); tunakufa Naye (2 Timotheo 2:11); tumezikwa Naye (Warumi 6:4); tumefanywa kuwa hai Naye (Waefeso 2:5); tumefufuliwa Naye (Wakolosai 3:1); tuko na umbo moja Naye (Wafilipi 3:10); tumetukuzwa Naye (Warumi 8:17); tunaishi Naye (Warumi 6:8); tunaketi Naye (Waefeso 2:6) na tunatawala Naye (2 Timotheo 2:12). Katika kila kitu tuko katika Yeye. Kristo ni hekima yetu na Yeye ndiye haki yetu na utakatifu wetu na ukombozi wetu (1 Wakorintho 1:30). Tunatajirishwa katika Kristo (1 Wakorintho 1:5). Mungu ametubariki katika Kristo na kila baraka ya kiroho katika ulimwengu wa kiroho (Waefeso 1:3).

Maombi yetu yanajibiwa kwa sababu tuko katikaKristo Yesu. Bwana Yesu alisema wazi kuhusu maombi ambayo yatajibiwa: “Ninyi mkikaa ndani Yangu na maneno Yangu yakikaa ndani mwenu, ombeni lo lote mtakalo, nanyi mtatendewa” (Yohana 15:7). Kuungana kwetu na Kristo ni jambo la maana sana kwamba Yeye mwenyewe huwaongoza watu wake katika maombi yao. Hili ni jambo la furaha sana na ambalo linafaa kutuhimiza kuenda mbele za Mungu na kuomba. Kila jambo ambalo mkristo anafanya kwa ajili ya kumtukuza Mungu, analifanya kwa sababu Kristo mwenyewe ako ndani mwake. Mkristo hawezi kuwa na maisha ya tabia ya dhambi kwa sababu hii haitampendeza Kristo.

Kuungana kwetu na Kristo Yesu ni jambo la maana sana kwamba hata miili yetu huwa imeunganishwa kwake, viungo vya miili yetu pia huwa vimeunganishwa kwa Kristo Yesu. Paulo anazungumzia jambo hili kwa wazi kabisa wakati anawaambia Wakorintho kwamba kuchukua miili yao na kuitumia katika zinaa ni kuchukua “viungo vya mwili wa Kristo na kuviunganisha na mwili wa kahaba” (1 Wakorintho 6:15).

Watu huwa hawafahamu kwamba kuenda na kahaba ni kutumia viungo vya mwili wa Kristo na njia ya dhambi. Lakini Paulo anatuelezea kwamba njia moja tu ya kuepuka dhambi ni kufahamu kwamba tumeunganishwa kwa Kristo. Tunapotenda dhambi, huwa tunajiletea aibu na pia huwa tunatumia mwili wa Kristo vibaya sana. Paulo anatuelezea sababu ambayo tuko nayo ya kuepuka dhambi. Anasema, “Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungo vya Kristo?” (1 Wakorintho 6:15). Je, tutachukua viungo vya Kristo na kuviunganisha na mwili wa kahaba? Jibu ni la.

Hatufai kuwaza kwamba tumebarikiwa na Mungu kwa sababu Kristo ndiye chanzo cha baraka zote, bali ni kwa sababu tumeunganishwa kwake. Sisi sote tunajua kwamba Kristo ndiye chanzo cha baraka zetu. Kwa sababu ya jambo hili hatufai kuwaza kwamba Kristo ako mbali na baraka hizi. Baraka hizi zimenunuliwa na Kristo mwenyewe na ni zake. Hazina ya baraka hizi ni Kristo na kile tunahitaji kufanya ili tuzipokee ni kuja Kwake kwa imani. Tukija kwake, tutaunganishwa kwake, na hii ndiyo

Page 8: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

sababu tutapokea baraka hizi.

Unapokea baraka hizi zote kwa sababu tu uko katika Yeye. Msamaha wa dhambi zako, haki ambayo uko nayo, kukua kwako katika utakatifu, kuongozwa kwako, amani ya dhamira yako na furaha katika Roho Mtakatifu, yote yanatoka kwa Bwana Yesu Kristo na kukufikia kwa sababu uko katikaKristo Yesu. Usiwahi kusahau jambo hili kamwe. Tunaweza tu kuwa na uhusiano na Mungu Baba kupitia kwa Kristo peke yake. Tunafurahia baraka zetu kwa sababu tuko katika Kristo na tunazipokea kutoka kwa Kristo. Mwandishi mmoja alisema, “Tunatajirishwa katika Kristo kwa sababu sisi ni viungo vya mwili Wake na tumeunganishwa Naye. Kwa sababu sisi tumeunganishwa kwake, Yeye hutupatia kila kitu ambacho anapokea kutoka kwa Mungu Baba.

Hii ndiyo inavyomaanisha kuwa na uhusiano na Kristo mwenyewe. Kufahamu jambo hili vyema kutatusaidia sana kumpenda Kristo badala ya kupenda baraka zake zaidi kuliko Yeye. Baraka ambazo Bwana Yesu Kristo anapeana haziwezi kutenganishwa naye. Ili tuweze kufurahia baraka hizi, lazima kila siku tuwe katika ushirika wa karibu sana na wa kumtegemea Kristo pekee kwa kila jambo. Kristo pekee ndiye furaha ya kufurahia baraka Zake. Kwa sababu ya hii, tunafaa kumpenda na kumwabudu Kristo.

Ndani ya Kristo milele

Je, ni usalama gani ambao mkristo ako nao kutokana na kuunganishwa kwa Kristo? Katika kitabu cha Warumi 5, Paulo anazungumzia jambo hili. Paulo anasema hivi kwamba kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani, hakikisho na furaha. Hapa Biblia inahakikishia wakristo wote kwamba, wao wako na wokovu, na wokovu huu ni wa kweli na umehakikishwa. Biblia inafundisha jambo hili kwa njia hii: kwanza inatufundisha madhara ya kuwa katika Adamu.

Biblia inatufundisha kwamba madhara ya kuwa katika Adamu ni kifo. Je, kuna uwezekano wa kuepuka kifo? Jibu ni la. Je, kuna watu fulani ambao ni wema sana kuliko wengine na kwa hivyo wao hawatakufa? Jibu ni la. Je, kwa nini wanadamu wote mwisho wao ni kifo? Jibu ambalo Biblia inapeana ni, kwa sababu wote wako katika Adamu wote watakufa.

Je, inamaanisha nini kutolewa katika Adamu na kuletwa katika Kristo? Kama vile madhara ya kuwa katika Adamu ni kifo, vivyo hivyo matokeo ya kuwa katika Kristo ni maisha mapya. Je, kwa wale wote ambao wako katika Kristo, kunauwezekano wa kutokuwa na maisha mapya? Jibu ni la. Je, kuna uwezekano kwamba siku moja yule ambaye sasa ako katika Kristo atajipata kwamba ameondolewa katika Kristo na kurejeshwa katika Adamu? Jambo hili kulingana na Biblia haliwezekani kamwe. Ni Mungu mwenyewe ambaye ametuondoa katika Adamu na kutuleta katika Kristo Yesu. Tunaweza tu kuondoka katika Kristo ikiwa tunaweza kuyabadilisha mpango ya Mungu ambayo Yeye alipanga kabla ya kuumba ulimwengu. Jambo hili hakuna mtu yeyote ulimwenguni hata kwa maombi yake, anaweza kulifanya. Kwa hivyo kwa sababu Mungu ametuleta katika Kristo, tuko katika Kristo milele.

Ikiwa wewe ni mkristo unaweza kutazama kifo bila uoga. Unapotazama na kusikia kila wakati kwamba watu wanakufa, ukweli ni kwamba hii ni kwa sababu wanadamu wote wako katika Adamu. Tunaposoma Biblia, tunaambiwa kwamba tutakufa kwa sababu ya dhambi ya Adamu. Kwa mkristo jambo hili halifai kumwogopesha hata kidogo, badala yake tunafaa kusema, “katika Adamu watu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Kristo wote watafanywa hai” (1 Wakorintho 15:22).

Huu ndiyo utukufu wa uhusiano ambao tumeletwa ndani. Hivi ndivyo Mungu ametufanyia. Mtu yeyote akiwa katika Kristo, yeye ni kiumbe kipya. Ya kale yamekwisha, sasa ni mapya. Hii ndiyo

Page 9: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

sababu wakati wakristo wanakutana pamoja, huwa wanaimba. Ni kwa sababu ni jambo kuu kuwa katika Kristo Yesu! Haijalishi udhaifu wako au uoga wako, maisha yako, yako salama na ni ya furaha katika Kristo. Ikiwa uko katika Kristo uko salama milele. Je, wewe uko katika Kristo?

Njia ambayo haina tumaini

Msomaji, pengine wewe hujaokoka. Ikiwa hii ndiyo hali yako, huna tumaini la mbinguni. Kuwa mkristo siyo jambo dogo au chaguo tu, inamaanisha kuwa miongoni mwa watu tofauti ambao wanaitwa watu na watoto wa Mungu.

Ikiwa wewe hujaokoka, Biblia inasema wewe uko na shida kubwa sana. Je, shida ni gani? Pengine utawaza kwamba nitasema shida yako ni kwamba wewe ni mwenye dhambi. Lakini ukweli ni kwamba hii si shida yako ya kwanza. Ni kweli kwamba wewe ni mwenye dhambi ambaye anaelekea jahanum. Lakini kulingana na Biblia hii si shida yako ya kwanza. Kulingana na Biblia shida yako ya kwanza ni kwamba wewe uko katika Adamu, na Mungu anakushughulikia kupitia kwa Adamu. Mungu ataendelea kukushughulikia kwa njia hii hadi uje kwa Kristo. Kwa hivyo hii inamaanisha kwamba kile unatarajia kutoka kwa Mungu ni kifo, hukumu, jahanum na mateso ya milele. Wewe ni mmoja wa wale ambao watahukumiwa milele.

Kwa sababu hii ndiyo hali yako, kila kitu ambacho unajaribu kufanya ili umtukuze Mungu, ni bure machoni pa Mungu. Haijalishi juhudi zako ambazo unafanya kama kujitahidi kuwa mtu mzuri sana, kuishi maisha mazuri, kuwasaidia maskini, kuwa mkarimu na kuwa mtu mvumilivu. Kwa haya yote hakuna hata moja ambayo itabadilisha hali yako; wewe uko katika Adamu, haijalishi unafanya nini, hutawahi kufurahisha Mungu. Kila mtu ambaye bado ako katika Adamu atahukumiwa, hata kama atalia, “Mungu unionee huruma kwa sababu ninajitahidi kufanya mambo mazuri!” Lakini ukweli ni kwamba matendo yako mazuri hayatakubadilisha. Wewe huna tumaini na huna njia ya kuepuka na hakuna chochote unaweza fanya kujiondoa katika hali hii. Huna tumaini isipokuwa ghadhabu ya Mungu jahanum milele. Ukitaka, unaweza kumaliza muda wako wote ukijaribu kumfurahisha Mungu kwa juhudi zako mwenyewe hadi kifo chako, lakini ujue kwamba hutakuwa umejiletea tofauti yoyote ikiwa bado uko katika Adamu.

Kwa mfano mtu ambaye amehukumiwa kifo baada ya kutenda makosa makubwa sana. Hakimu katika mahakama anatoa hukumu ya kifo kwa mtu huyu. Baada ya kuhukumiwa, mtu anapelekwa mahali ambapo atangoja hukumu yake itekelezwe. Akiwa humo, anaweza kuwafanyia wengine mema na kuwasaidia wengine sana, lakini hata baada ya haya yote hawezi kuepuka hukumu yake kwa sababu amehukumiwa kifo. Vivyo hivyo, wale ambao wako katika Adamu tayari wamekwisha kuhukumiwa kifo. Kwa hivyo kuna njia moja tu kuepukua hukumu ya Mungu na hii ni kuondoka katika Adamu na kuja katika Kristo.

Huu ni mfano wa wale ambao wako katikaAdamu na jinsi inavyomaanisha kuwa katika Adamu. Hii ni hali ya kuogopesha sana. Kuna mgawanyiko miongoni mwa wanadamu ambao wanasoma kitabu hiki. Hata kama mgawanyiko huu hauonekani kwa macho, ukweli ni kwamba mgawanyiko upo na ni wa hatari sana. Katika ulimwengu huu kuna watu wawili wa kabila mbili. Wengine wenu wako katika Adamu na wengine wenu wako katika Kristo. Tumaini la yule ambaye ako katika Adamu ni kuondoka na kuingia kwa Kristo. Je, unawezaje kutoka na kuingia kwingine? Kwa nguvu na uwezo wako huwezi na hutawahi kuwa na tumaini lolote. Tumaini moja tu ambalo ninaomba kwamba utafanya ni, kumwamini Kristo. Mwombe Mungu akuhurumie. Mwombe, “Bwana ninakiri kwamba mimi ni mwenye dhambi. Nilizaliwa mwenye dhambi na niko na hali ya dhambi na ninajua jambo hili kwamba ikiwa sitasamehewa na kubadilishwa, nitaenda jahanum. Nimejua kwa kweli kwamba hata nikijaribu

Page 10: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

aje kwa uwezo na nguvu zangu, siwezi kujiokoa. Mungu ninakuomba niondoe katika Adamu na unilete katika Kristo Yesu. Nisaidie nimwite awe mwokozi wangu. Niondoe katika Adamu na uniunganishe kwa mwanao Kristo Yesu.”

Ikiwa utamwomba Mungu akufanyie hivi, atafanya hivyo. Yeye ni Mungu mwenye neema na huruma. Jambo hili linaweza kufanyika na huwa linafanyika kwa maelfu kila siku. Katika kitabu cha Matendo ya Mitume 16:30-31, mtu mmoja alijua kwamba yeye alikuwa mwenye dhambi na aliomba, “Je, nitafanya nini ili niokoke? Nitafanya nini ili niondoke katika Adamu na niingie katika Kristo?” Jibu lilikuwa wazi kabisa, “Mwamini Bwana Yesu Kristo na utaokoka, wewe na jamii yako yote.” Haijalishi wewe ni nani au yale ambayo umefanya. Haijalishi umekuwa mwovu kiasi gani, Mungu ni tajiri katika rehema.

Wakati Kristo alisulubishwa Kalivari, kulikuwa na mtu mmoja mwovu ambaye alikuwa na muda mdogo wa kuishi. Kwa sababu alijua kwamba hukumu ilikuwa mbele yake, alimwomba Kristo ambaye alikuwa pia msalabani amhurumie. Bwana Yesu Kristo hakumwambia kwamba kwanza alihitaji kuweka maisha yake vizuri na kuacha mambo fulani fulani au kujaribu kuishi maisha matakatifu. Pia hakumwambia kwamba alikuwa amechelewa sana. Maneno ya Mwana Mtakatifu wa Mungu kwa mtu yule yalikuwa, “Amin, nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso” (Luka 23:43). Ombo lake fupi kwa Bwana Yesu Kristo lilimfanya aondolewe kutoka jahanum na kuingizwa mbinguni.

Je, utamwomba Bwana Yesu Kristo akuokoe? Je, unajua inamaanisha nini kuwa katika Adamu? Je, unajua kwamba Mungu ako tayari kukutoa katika Adamu na kukuleta katika Kristo Yesu mwanawe? Hili ni jambo kuu sana kuliko jambo lolote ambalo linaweza kukutendekea katika maisha yako yote. Ninaomba kwamba Mungu atakuwezesha kufanya hivi.

Sura ya Pili

Sisi ambao tulikufa kwa dhambi

Waza kwamba unasoma mambo haya katika kitabu ambacho kinazungumza kuhusu utakatifu: “Shida kuu ambayo wakristo wengi wako nayo leo ni kwamba wanajaribu sana kwa uwezo wao kuishi maisha ya ukristo. Badala yake, wanapaswa kufahamu hali yao kwamba wao sasa wako katika Kristo. Kile wanahitaji kufanya ni kufahamu kwamba Mungu anawapenda na wanafaa kufurahia baraka ambazo Mungu amewapatia katika Kristo.” Je, utawaza nini? Pengine utawaza kwamba haya ni mafundisho ya uongo. Lakini ukweli ni kwamba haya ndiyo mafundisho ya Biblia.

Je, ni kwa nini sisi wakristo tunang'ang'ana sana katika maisha yetu ya ukristo? Sababu kuu ni kwamba wakristo hawajafahamu kabisa baraka ambazo ni zao katika Kristo Yesu. Mara nyingi huwa hatuelewi kazi ambayo Mungu ametufanyia na ikiwa tutaelewa tutakuwa watu tofauti kabisa.

Katika sura hii, ninataka kukufundisha kuhusu dhambi ambayo iko katika wale ambao wameokoka. Wale ambao wameokoka hawajakamilishwa, bali bado wako na dhambi ndani mwao. Ni jambo la kuhuzunishwa kwamba wengi ambao kweli wameokoka hawajali kwamba wao pia wanatenda dhambi. Wengi wao wanapuuza tu ukweli huu kwamba wanatenda dhambi, na wengi wengine wanatoa vijisababu ni kwa nini wanatenda dhambi. Hawa wote hawapigani vita dhidi ya dhambi bali wanaacha tu dhambi ikae ndani yao na iendelee maishani mwao.

Wengi leo wanatumia mstari wa Warumi 6:14 ambao unasema, “Kwa maana dhambi haitakuwa na

Page 11: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema” kusema kwamba wao sasa hawana haja ya kutii sheria ya Mungu. Wengi wengine wanasema, “Sisi wakristo hatujakamilika, lakini tumesamehewa dhambi zetu zote.” Hawa wote wanatumia mafundisho haya kuwa vijisababu ya kuendelea tu kutenda dhambi bila kujaribu kupigana vita dhidi ya dhambi ambayo bado iko ndani mwao.

Hii ndiyo sababu wengi ambao wameokoka hawaonekani kuwa tofauti na watu wa dunia. Tukichunguza maisha yao, tunaona wao wanatenda zile dhambi ambazo watu wa dunia pia wanazitenda. Wengi ambao wameokoka wanapenda sana anasa za dunia na pesa na vitu vya dunia, kama tu vile watu wa dunia wanavyovipenda vitu hivi. Wengi ambao wameokoka siku ya Jumapili (ambayo ni siku ya Bwana) wanafanya tu yale mambo ambayo watu wa dunia wanayafanya.

Katika kitabu cha Warumi sura ya saba, Paulo anafundisha kuhusu jambo hili la dhambi ndani ya yule ambaye ameokoka. Kulikuwa na watu katika kanisa la Roma ambao walisema, “Tuseme nini basi? Je, tuendelee kutenda dhambi ili neema ipate kuongezeka?” (Warumi 6:1). Yaani, wao walisema, “Wakati Mungu anamsamehe mwenye dhambi mkuu, watu wa dunia wote wanaona utukufu wake. Basi wacha tuendelee na dhambi ili wakati Mungu atatusamehe, wote wataona utukufu wake.”

Jibu ambalo Paulo aliwapatia linaonekana katika Warumi 6:2. Paulo alisema, “La hasha! Sisi tulioifia dhambi, tutawezaje kuendelea kuishi tena katika dhambi?”

Hali yetu mpya

Je, mkristo ni nani? Kama tulivyoona katika sura iliyopita, kwamba mkristo ni mtu ambaye ako katika Kristo, mtu ambaye ameondolewa katika agano moja na kuletwa katika agano lingine. Ni ukweli kwamba tunaingia katika Kristo kwa imani. Pia tumejifunza kwamba jambo hili linafanyika kwa nguvu za mwenyezi Mungu pekee. Si jambo ambalo linafanyika kwa nguvu zetu.

Wakati tumeletwa katika Kristo, tunakuwa na kiongozi mpya, sisi tunakuwa viungo vya mwili mpya. Tumeondolewa katika utawala moja na kuletwa katika utawala mwingine. Vile Paulo anavyoandika katika kitabu cha Wakolosai 1:13, “Kwa maana alituokoa kutoka katika ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana Wake mpendwa .” Sasa Mungu anashughulika na sisi kama watu wapya kabisa katika Kristo Yesu. Tunaishi maisha mapya tukiwa katika hali mpya, katika ulimwengu mpya. “Kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya” (2 Wakorintho 5:17).

Kwa ufupi, wakristo ni watu wapya na hii ndiyo sababu Biblia inasema kuokoka ni kuzaliwa mara ya pili (Yohana 3:13), na hali hii mpya ndiyo msingi wa utakatifu wetu. Je, kwa nini tuwe kama Kristo mwenyewe? Jibu ni kwa sababu tayari tuko ndani Mwake. Biblia inatueleza kuhusu hali yetu kwamba, tumechaguliwa na kutakaswa na Mungu mwenyewe. Maneno haya yanaweza kuwachanganya wengi kwa sababu tunajua sote kwamba tuko katika hali ya kutakaswa na siyo kwamba tumetakaswa tayari.

Maneno haya yanaweza kuwa mageni kwetu kwa sababu tunajua kwamba kazi ya utakaso ni ya muda na kwamba ni kazi ambayo inaendelea katika maisha yetu yote hapa ulimwenguni. Huu ni ukweli kabisa. Kwa nguvu na kazi ya Roho Mtakatifu tunawezeshwa kila siku kufa pole pole kwa dhambi na kuendelea kuishi katika utakatifu. Hii ni kazi ya kila siku na ya mwaka baada ya mwaka. Huwa tunaua matendo ya mwili (Warumi 8:13) na huwa tunabadilishwa katika mfano wa Kristo mwenyewe. Pia Agano Jipya linazungumzia kazi ya utakaso kuwa kazi ambayo Mungu anaifanya mara moja. Hii

Page 12: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

inamaanisha kwamba, Mungu mwenyewe anatuita kutoka kwa ulimwengu kwa kutuondoa kutoka katika Adamu na anatuleta katika Mwana Wake Kristo Yesu.

Kwa mfano wakati Paulo anawaandikia watu wa kanisa la Korintho anawaita “wale waliotakaswa katika Kristo Yesu” (1 Wakorintho 1:2). Lakini unapoendelea kusoma barua hii ya 1 Wakorintho, utaona kwamba hawa walikuwa watu ambao hawakuwa wamekamilika. Miongoni mwa washirika wa kanisa hili la Korintho kulikuwa na watu ambao walikuwa wamechanganyikiwa sana katika mawazo yao kuhusu ukristo wa kweli na wengine walikuwa wakizini. Pia katika kanisa hili kulikuwa na migawanyiko na washirika wengi walipenda anasa za ulimwengu huu. Je, kwa nini Paulo anawaita “wale waliotakaswa katika Kristo?” Kile Paulo anamaanisha hapa ni kwamba watu hawa walikuwa wameondolewa katika ufalme wa shetani na kuingizwa katika ufalme wa Mungu. Baada ya Mungu kufanya hii, Yeye anaanza kazi ya kuwabadilisha kutoka ndani mwao.

Kwa mfano, mtu anahama nchi fulani na anaenda nchi nyingine tofauti kabisa. Kufika katika nchi nyingine inaweza kumchukua masaa machache tu lakini baada ya kufika huko bado ana tabia ya nchi ile ambako alitoka. Hata kama anaishi nchi ngeni, bado atakuwa na tabia ya nchi alikotoka. Pole pole tabia zake zitaanza kubadilika na yeye ataanza kuishi kama watu wa nchi hiyo. Vivyo hivyo, yule ambaye ameokoka ameondolewa kutoka katika ufalme wa shetani kuingizwa katika ufalme wa Mungu. Wakati angali bado mkristo mchanga, atakuwa na tabia za dhambi nyingi. Lakini pole pole tabia hizi za dhambi zitaanza kuondoka na yeye ataendelea kukua kama Kristo mwenyewe. Hii ni kazi ambayo Roho Mtakatifu anafanya katika maisha yake yote hapa ulimwenguni.

Sisi Ambao tulikufa kwa dhambi

Je, hali yetu mapya inafafanuliwa aje? Biblia inasema, “Sisi ambao tulikufa kwa dhambi” (Warumi 6:2). Mkristo ni mtu ambaye amekufa kwa dhambi. Paulo anaendelea kuzungumza jambo hili katika mistari ya 3-10 wakati anazungumza kuhusu kuungana kwetu na Kristo katika kifo na kufufuka Kwake.

Biblia inasema, “Kristo aliifia dhambi mara moja” (Warumi 6:10). Kwa ufupi hali yake ya kuwa katika mazingira ya dhambi iliisha wakati Yeye alifufuka kutoka kwa wafu na kupaa mbinguni. Wakati moja Yeye alikuwa hapa ulimwenguni na alizingirwa na dhambi, lakini sasa ako mbinguni ambamo anazingirwa utukufu. Hii haimaanishi kwamba Kristo alikuwa mtenda dhambi au kwamba alikuwa na dhambi yoyote moyoni Mwake wakati alipokuwa hapa ulimwenguni. Kristo alikuwa Mtakatifu, bila hatia yoyote ya dhambi yoyote (Waebrania 7:26). Lakini hata hivyo alikuja hapa ulimwenguni na kuishi miongoni mwa watenda dhambi.

Wakati Kristo alikuwa hapa ulimwenguni, aliona dhambi na kusikia dhambi kila wakati. Katika kila miji aliingia na vijiji, Kristo aliona watu wakitenda dhambi na kuzungumza dhambi. Wanadamu walikuwa waovu wakati huo jinsi walivyo leo. Hata katika hali hii, hakujitenga na walevi, wezi, waongo na makahaba na kuishi peke yake. Mifano ya ukosefu wa haki, uovu wa wanadamu na uchoyo wa wanadamu, haya yote yalifahamika kwake kila wakati. Yeye mwenyewe alijaribiwa katika kila hali jinsi tunavyojaribiwa (Waebrania 4:15). Aliteswa na wanadamu, alichukiwa na alisengenywa pia. Inaonekana kwamba watu wa kijiji chake walijua kwamba wakati mamake alikuwa mimba, yeye hakuwa ameolewa. Hii ndiyo sababu maadui wake walimwambia, “Sisi si watoto wa haramu” (Yohana 8:41).

Je, hili si lilikuwa jambo la kuhuzunisha sana kwa mtu ambaye alikuwa Mtakatifu kamili kuishi katika hali ya aina hii? Ikiwa Lutu mwenyewe alihuzunika kila siku kwa sababu ya dhambi za watu ambao

Page 13: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

alikuwa anaishi miongoni mwao (2 Petro 2:7,8), je, ulikuwa huzuni wa aini gani kwa nafsi ambayo ilikuwa takatifu kuendelea kuishi miongoni mwa waovu na kuona na kusikia dhambi kila wakati? Kwa zaidi ya miaka 30, aliishi katika mazingira ya dhambi na jambo hili lilimgharimu gharama kubwa sana ambayo hatuwezi kuelezea kabisa.

Baada ya haya yote alikufa, akaziwka, akafufuka na akapaa mbinguni. Wakati huu aliondokoa kutoka katika mazingira ya dhambi milele. Aliifia dhambi mara moja. Hatawahi rudi kuishi katika ulimwengu huu wa dhambi. Pia ahatwahi pata mateso ambayo alipata katika ulimwengu huu wa dhambi. Bwana wetu Yesu Kristo aliifia dhambi na alishinda dhambi hiyo milele na kifo Chake kilikuwa kilele cha maisha Yake hapa katika ulimwengu wa dhambi. Wale wote ambao wako katika Kristo, wako katika uwepo ambao dhambi haina nguvu kamwe katika uwepo huo.

Je, hii inamaanisha nini kwa sisi ambao tuko katika Kristo? Inamanisha kwamba kwa sababu tumeunganishwa Kwake hata sisi tumekufa kwa ulimwengu na dhambi zake. Sisi sasa hatumo katika ufalme wa dhambi, tumo katika ufalme wa nuru. Tumeondolewa katika Adamu na hatutawahi kurudi humo tena. Bwana Yesu Kristo hakufa tu kwa ajili yetu, lakini pia hata sisi tumekufa katika Yeye. Paulo anasisitiza jambo hili sana anaposema: “Sisi tulioifia dhambi...sote tuliobatizwa kwa Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti Yake. Kwa hivyo tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika kifo..Tumeungana naye katika mauti Yake..kwa maana twajua kwamba utu wetu wa kale ulisulibiwa pamoja naye...Basi tulikufa pamoja na Kristo” (Warumi 6:2,3,4,5,6,8).

Hii ndiyo hali yetu sasa, tulikufa kwa dhambi. Paulo hasemi kwamba tungekuwa tumekufa au kwamba tunahitaji kufa au tunapaswa kujaribu kufa au kwamba siku moja tutakufa kwa dhambi. La hasha hasemi hivyo. Anasema, “tulikufa pamoja na Kristo.” Hatuwezi kuendelea katika ushirika wa zamani ambao tulikuwa nao na ulimwengu wa dhambi kwa sababu tumekufa kwa mambo haya. Mtu ambaye amekufa hawezi kuendelea katika ushirika na wale ambao wamebaki, kwa sababu kufa kunamaanisha mwisho wa ushirika kama huo. Je, kwa nini huwa tunahuzunika kwa ajili ya wapendwa wetu ambao wamekufa? Ni kwa sababu katika maisha haya hatutawahi kuwa na uhusiano au ushirika nao tena.

Bwana Yesu Kristo hakufa tu, lakini pia alifufuliwa katika utukufu na sasa anaishi katika utukufu. Paulo anasema, “Uzima alio nao anamwishia Mungu” (Warumi 6:10). Hili ni jambo la ukweli kutuhusu. Hata sisi baada ya kufa kwa dhambi, tumefufuliwa na kupewa maisha mapya katika ulimwengu mpya. Maisha haya tunayoishi, tunayaishi kwa nguvu na utukufu wa Mungu. Biblia inafundisha kwamba tunaunganishwa kwa Kristo katika kifo Chake, na pia tunaunganishwa kwa Kristo katika kufufuka Kwake. Hii ndiyo sababu Paulo anasema, “Kama vile Kristo alivyofufuka kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo sisi nasi pia tupate kuenenda katika upya wa uzima” (Warumi 6:4). Hiki ndicho kilele cha yale ambayo yametutendekea sisi. Wokovu ni kazi ya ajabu ya Mungu ambapo anatuondoa katika Adamu na kutuleta katika Kristo Yesu.

Watu wengi hawajawahi kuelewa kazi ya wokovu kabisa. Kuokoka kunamaanisha kuacha ulimwengu wa dhambi na kuingia katika maisha mapya ya Mungu. Hivi ndivyo wakristo walivyo. Hii ndiyo sababu wale ambao wameokoka hawawezi kuuliza swali hili, “Je, tuendelee kutenda dhambi ili neema ipate kuongezeka?” Yaani hatuwezi kuendelea kuishi katika ulimwengu ambao tulikombolewa kutoka ndani kwa sababu ulimwengu huu uko na anasa za mwili na tama za macho. Hili ni jambo la upumbavu kabisa kwa sababu kuwa mkristo inamaanisha kuondolewa kabisa katika dhambi. Je, kama tumeondolewa katika maisha ya dhambi, itakuwaje tena turudi katika maisha hayo? Hali yetu mpya inafanya swali hili kuwa la upumbavu kabisa. Inawezekanaje kwamba, “Sisi tulioifia dhambi kuendelea kusihi tena katika dhambi?”

Page 14: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Kwa mfano, mtu ambaye ameokoka na awe amepata safari ya kuenda mahali. Wakati ako huko rafiki wake mmoja anamwambia, “Si uko peke yako? Hukuja na mke wako. Kwa hivyo unaweza fanya chochote utakacho hata kuzini na mwanamke mwingine, mke wako ako mbali na hakuoni.” Je, mtu huyu atamjibu rafiki wake vipi? Kwa sababu mtu huyu anafahamu wokovu wake vyema, atajibu rafiki wake kwa huzuni na hasira kwamba, “Mke wangu ni mtu wa maana sana kwangu kuliko mtu mwingine yeyote. Yeye ni mfupa wa mfupa wangu na nyama ya nyama yangu. Ninampenda sana kuliko maisha yangu. Je, unafikiria kwamba kuna kitu katika ulimwengu huu ambacho kitanifanya ni zini dhidi ya mke wangu? Kwa sababu unanieleza mambo haya ni wazi kwamba wewe hujui kuwa mume inamaanisha nini. Na ukweli ni kwamba wewe hufahamu ndoa ni nini. Na hujui upendo ni nini. Ninakuhurumia sana.” Mkristo akiwa anaendelea katika dhambi, au maisha yake yawe ya hali ya kutomtii Mungu, basi nitamwuliza swali hili, “Je, wewe ni mkristo wa kweli?” Tuliona katika sura iliyopita kwamba wanadamu wako katika vikundi viwili: wale ambao wako katika Adamu na wale ambao wako katika Kristo Yesu. Lakini pia kuna kikundi cha tatu, wale ambao wanajiwazia kwamba wao wako katika Kristo, lakini kwa ukweli wao bado wako katika Adamu. Watu wengi wanakiri kuwa wakristo hata wengine wanasema kweli wao wamezaliwa mara ya pili. Kwao huu ni ukweli kabisa na watakasirika wakati mtu yeyote atawauliza kuhusu wokovu wao. Lakini watu hawa huwa hawaonyeshi ishara ya kubadilika hata kidogo. Ndani mwao hakuna ishara yoyote ya maisha mapya ndani ya Kristo. Ndani mwao huwezi kupata hakikisho la kweli kwamba wao wameondolewa katika Adamu na kuletwa katika Kristo.

Je, unaweza kusema ukweli kwamba hivi ndivyo ulivyo, kwamba wewe umeifia dhambi? Je, wewe umebadilishwa? Je, wewe ni mwanamke au mwanamume mpya? Je, unaishi katika ulimwengu mpya? Kuna wengi leo ambao wanadai wameokoka lakini hawaishi jinsi wakristo wanafaa kuishi, na wao wanawaza kuna kitu fulani wamekosa ambacho kitawawezeshea kuishi maisha ya ukristo. Hii ndiyo sababu wanatafuta njia nyingi ili wafaulu katika maisha ya ukristo. Lakini ukweli ni kwamba wengi wao hawajaokoka kamwe. Wanawaza kwamba wanahitaji jambo fulani ili waweze kuishi kama wakristo ilhali hawajawahi kuokoka. Watu hawa hawajawahi kuokoka na kufanywa viumbe vipya. Mkristo ni mtu ambaye amefanywa kiumbe kipya.

Jukumu letu mpya

Unaweza kuwaza kwamba, ni vyema sana kutueleza kwamba tumekufa kwa dhambi na tumeondolewa katika Adamu na kuletwa katika Kristo, lakini nini itafanyika na dhambi zetu ambazo tumetenda na zile ambazo tutatenda? Ninajua kwamba dhambi bado iko ndani mwangu, kwa hivyo nitafanya aje ikizingatiwa sana niko ndani ya Kristo. Je, nitawezaje kuishi maisha matakatifu? Je, ninawezaje kusaidika?

Katika Warumi 6:11-14, Paulo anaeleza jinsi tunafaa kuishi maisha yetu kama watu wapya katika Kristo Yesu.

Jihesabuni kuwa wafu

“Jihesabuni wafu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu” (Warumi 6:11).

Hitaji letu kuu kwa haya yote ni kufahamu msimamo wetu kwa sababu chanzo cha maisha mapya ni mawazo mapya. Katika kifungu hiki Paulo anasisitiza umuhimu wa kufahamu na kuelewa jambo hili. Anasema, “Au hamjui...tunajua....tunajua” (Warumi 6:3,6,9). Ni wazi kwamba kuna mambo ambayo tunahitaji kujua.

Page 15: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Watu wengi leo hawafahamu mafundisho ambayo yako katika Biblia. Huwa wanasema mafundisho haya, hayana maana kabisa. Yesu alisema kwamba, “Mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32). Ikiwa tutaweza kuishi jinsi tunafaa kuishi, tunafaa kufundishwa inamaanisha nini kuunganishwa kwa Kristo. Zaidi ya yote, Paulo anasema kwamba tunafaa kuwa na mazoea ya kila wakati kujiwazia hivi. Mfahamu kwamba mmekufa kwa dhambi. Kwa ufupi ni kwamba tuendelee kufahamu kwamba sisi tumekufa kwa dhambi na sasa tunaishi kwa ajili ya Kristo. Wacha haya yawe mazoea. Usiwahi sahau kuhusu hali yako ya sasa kwamba wewe uko katika Kristo.

Hili ndilo jambo la kwanza katika kitabu cha Warumi. Unaposoma kitabu cha Warumi utaona kwamba mara ya kwanza tunapewa amri ni baada ya sura 5 za kwanza. Kwanza Paulo anatuonyesha kwa urefu kwamba tunahitaji wokovu. Anatueleza kwamba Mungu kupitia kwa Kristo, amepeana wokovu huu. Anazungumza kuhusu amani na hakikisho mambo ambayo mkristo anapata baada ya kupata wokovu huu na amefafanua kuunganishwa kwa Kristo kunamaanisha nini. Kabla ya kutuonyesha majukumu yetu, kwanza anatuonyesha kile Mungu ametufanyia kupitia kwa Kristo Yesu Mwana Wake. Kwa hivyo barua hii ya Warumi ikiwa tutaifahamu, lazima kwanza kabisa tusikilize mafundisho yake. Lazima tumsikilize Mungu kwanza na tufahamu kabisa kile ambacho anasema halafu, tuamini na tutaanza kumwabudu jinsi inayofaa.

Mchungaji mmoja ambaye aliitwa John Owen alisema, sababu kuu ambayo inatuletea udhaifu katika mambo ya kiroho ni, kukosa kujua vyema baraka ambazo tuko nazo. Mchungaji huyu alifundisha sana kuhusu kupigana na dhambi na kujaribiwa na dhambi ambayo bado iko ndani mwa mkristo. Aliwahimiza wakristo kila wakati kwamba, “Ua dhambi, la sivyo, dhambi itakuua.” Alihimiza sana juu ya mambo kama haya na pia aliendelea kusisitiza kuhusu umuhimu wa kuwa waangalifu na kujitolea kabisa katika vita dhidi ya dhambi ambayo bado iko ndani mwetu. Ni lazima kila wakati tuishi kwa neema na imani. Kile Mungu ametufanyia, ndiyo msingi wa yale ambayo tunafaa kufanya.

Majaribu katika maisha ya ukristo.

Maisha ya ukristo yamejawa na majaribu mengi sana. Kila upande tumezingirwa na hatari mingi sana. Kwa upande mmoja tunajaribiwa kupuuza mambo ya Mungu, kutotii neno la Mungu, kupenda ulimwengu na kuwa na ukristo wa uongo. Katika sura hii tayari tumezungumzia kuhusu wale ambao hudai kwamba wao ni wakristo ilhali siyo wakristo kamwe. Mara mingi sisi huwa tunaona mambo haya lakini tunajaribu kuyaepuka. Lakini kwa kujaribu kuyaepuka, huwa pia kwa upande mwingine tunakuwa kama Mafarisayo ambao dini yao ilikuwa tu kufuata sheria, na hawakufahamu chochote kuhusu kutembea na Mungu. Kwa kufanya hivi, walipoteza maana ya neema na baada ya muda, kila kitu kwao kilikuwa sheria na majukumu tu. Badala ya kuwa wanyenyekevu na wenye shukurani kwa Mungu, walikuwa wenye kiburi na wenye kujiamini.

Paulo aliwaandikia wale wakristo ambao walikuwa katika hatari ya kuwa kama Mafarisayo akasema, “Ninyi Wagalatia wajinga! Baada ya kuanza kwa Roho, je, sasa mwataka kukamilishwa katika mwili?” (Wagalatia 3:1,3). Hawa Wagalatia walikuwa wanajaribu kujikamilisha kwa nguvu zao. Jambo hili linaweza kufanyika kwa haraka sana tusipojichunga. Je, wewe uko katika hatari ya kuregeza msimamo wako? Je, huenda mahubiri ambayo unayasikia kila wakati ni ya fanya hii, fanya hili, fanya hivi? Je, wewe ni mmoja wa wale ambao ukristo wao ni wa kujaribu na jaribu sana? Je, wewe ni mmoja wale ambao wanajikuta katika hali ya lazima nimfanyie Mungu jambo kubwa sana, kama, kusoma Biblia sana, kuomba sana na kuhubiri sana kuhusu Kristo?

Usiniwazie vibaya. Ukweli ni kwamba lazima sisi sote tujitahidi katika mambo haya. Lazima tumtumikia Kristo kwa maisha yetu yote. Mara nyingi huwa tunakuwa na nia mbaya katika kufanya

Page 16: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

mambo haya. Mara nyingi huwa tunaanza na kumaliza jambo tukiwa tunajiamini sisi wenyewe. Huwa tunageuza wokovu kuwa kazi ya mwanadamu kwa sababu tunasahau kuhusu neema ya Mungu na kusudi la Mungu la kuwabariki watu wake. Mara nyingi jambo hili hugeuka kuwa lazima nifanya bidii sana na mwishowe furaha hutuondoka ya kufurahia baraka za Mungu.

Mpangilio huu huwa haufaulu kamwe. Mara nyingi watu huumia au huwaumiza au huumizwa dhamira zao kwa kujiwekea malengo yao au kuwawekea wengine yale ambayo wanafaa kukamilisha. Kuna wale ambao hujaribu kulingana na jinsi wameambiwa, lakini baada ya muda mfupi, wao hukata tamaa. Mara nyingi badala ya kuwasaidia watu kama hawa, huwa tunawawekea mizigo mikubwa ambayo hawaweza kubeba. Tunawafanya wamwazie Mungu kama yule mtu ambaye katika Mathayo 25:24 alisemakana kuwa “mtu mgumu.”

Mungu siyo Mungu mgumu. Yeye ni Mungu mwenye huruma na mkarimu. Huwa hadharau juhudi zetu ndogo za kumtii au kutueleza kwamba sisi si watu wa maana. Badala yake, Yeye ni Baba ambaye anawatazama watoto wake wakijaribu kumtumikia, na anasema wakati huo, “mmefanya vyema sana watoto wangu. Siku moja utaweza kufanya vyema zaidi.”

Ni habari njema kwamba Kristo anatupatia wokovu wa bure kwa wote ambao watakuja Kwake. Shida yetu kuu si kwa sababu tunakosa kujitahidi, bali ni kujiamini na yale ambayo tuko nayo.

Kujaribu sana.

Nitatumia mfano wa mchezo wa mpira kukuonyesha kujaribu sana ni kufanya nini. Kuna wachezaji wengi ambao hucheza mpira na wanapata matokeo mabaya ambayo hawakutajaria. Na huwa wamejaribu sana kutia bidii. Ukitazama sana kwa nini wanapoteza michezo yao, utapata kwamba ni kwa sababu hawakufunzwa vyema jinsi ya kuucheza mchezo huo.

Kuna watu wengi pia ambao wanajaribu kuishi maisha ya ukristo kwa njia kama hii. Wanajaribu sana kuishi maisha ya ukristo lakini lengo lao si halali. Msingi wa kuishi maisha yetu ya ukristo siyo “Lazima nifanye,” badala yake inafaa kuwa “kwa saabu ya Kristo.” Kile Mungu ametufanyia ndani ya Kristo ndiyo jambo ambalo litatuletea utofauti. Mwandishi mmoja ambaye aliitwa Walter Marshall aliandika akisema kwamba, lazima kwanza tuokoke ndipo tutaweza kufanya majukumu ya sheria ambayo tunatarajiwa tufanye. Ni lazima tutekeleze majukumu ya sheria, lakini swali ni, tutayatekeleza aje? Jibu ni, kwanza lazima tuokoke.

Mara mingi tunasikia Kristo akizungumziwa kwamba Yeye ndiye mfano wetu. Huu ni ukweli, kwa sababu Yeye ndiye mfano bora na himizo kwetu. Kristo Yesu alisema, “Mimi niwawekea kielelezo kwamba imewapasa kutenda kama vile nilivyowatendea ninyi” (Yohana 13:15). Petro anawahimiza wasikilizaje wake wavumilie mateso. Anasema, “Kwa kuwa ninyi mliitwa kwa ajili ya hayo, kwa sababu Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachia kielelezo, ili mzifuate nyayo zake” (1 Perto 2:21). Hatuwezi kufanya jambo lingine lolote isipokuwa kufuata mfano wa Kristo na tabia Yake kila wakati.

Ikiwa Bwana wetu Yesu Kristo hangekuwa zaidi ya mfano kwetu wa kufuata, je tungekuwa na wa kutuhimiza? Kwa mfano, mtoto ambaye ako na baba ambaye ni mcheza kandanda lakini iwe mtoto wake hana uwezo ya kucheza mchezo huo. Kila wakati babake anapojaribu kumfunza, mtoto anakuwa hataki kabisa. Je, baba huyu atakakuwa na mfano gani kwa mtoto huyu? Je, ingekuwa aje ikiwa Kristo Yesu hangekuwa zaidi ya mfano kwetu? Lingekuwa jambo la huzuni kwetu kuwa na mfano mkamilifu ambao hata tukijaribu aje hatuwezi kufikia. Ukitazama, je, ni watu wangapi ambao wanajaribu

Page 17: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

kuufuata mfano wa Kristo kwa njia zao na kwa nguvu zao? Je, ni jambo la kushangaza kweli kwamba wanakosa kufaulu kwa jitihada zao?

Sababu kuu kwa nini wakristo wanaishi maisha bila furaha ni, kwa sababu hata baada ya kusikiza mafundisho ya Kristo na kuwaza juu ya mafundisho hayo, wao wanaishi maisha yao kwa kujitegemea wao wenyewe. Kwa kufanya hivi, wanajishusha moyo sana.

Shukurani kwa Mungu kwa sababu Bwana Yesu Kristo ni zaidi ya mfano tu kwetu. Yeye ndiye kichwa cha Agano ambaye ndani Mwake sisi ni viumbe vipya. Siri ya kuishi haya maisha mapya ni kuamini kwamba maisha haya ni yetu kupitia kwa Yesu Kristo. Wakristo wengi huwa hawafahamu thamana ya imani kwa sababu wanawaza kwamba imani haina maana.

Imani ina nguvu sana kuliko kitu kingine chochote. Paulo anasema kwamba, jueni kwamba mmekufa kwa dhambi na sasa mko hai kwa Mungu. Wakristo wote wanafaa kuishi maisha yao wakijua kwamba wao ni watu wapya ndani ya Kristo kwa neema ya Mungu. Kila mkristo anafaa kuwaza juu jambo hili na kila wakati kuomba juu ya jambo hili. Kila mkristo anafaa kuzama katika ukweli huu kwamba ikiwa mtu ako katika Kristo, Yeye amekufa kwa dhambi na sasa yeye ni kiumbe kipya. Yaani, yeye amekufa kwa dhambi na sasa ako hai kwa Mungu. Katika kila jambo ambalo mkristo analifanya, anafaa kujiwazia hivi.

Mkristo ni mtu ambaye kila siku anajitahidi kuishi maisha ambayo yanaonyesha kwamba yeye ako katika uhusiano na ushirika na Kristo Yesu. Uhusiano wake na Kristo unamfanya aishi maisha ambayo ni ya kumtukuza Mungu. Ni jukumu lake kuishi maisha haya lakini ukweli ni kwamba haya ndiyo maisha yake.

Ishi kulingana na maisha yako mapya.

Watu wa Mungu wanahitaji kila wakati kukumbuka yale ambayo Mungu amewafanyia na jinsi amewageuza kutoka kwa dhambi na kuwaleta Kwake. Kuondolewa katika utawala wa dhambi ndilo jambo muhimu ambalo linafaa kutufanya sisi wakristo tujitahidi kuishi maisha matakatifu. Kujua kwamba sisi ni watu wapya, ndicho chanzo chetu cha kuishi maisha kama watu wapya. Ni lazima tujue kwamba tumekufa kwa dhambi na tuko hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.

Paulo anaendelea kutueleza mambo kadhaa mengine.

Kataa dhambi

“Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii tamaa mbaya” (Warumi 6:12)

Kataa kumtumikia dhambi! Dhambi inadhihirishwa kuwa bwana ambaye “hutawala wanadamu” (mstari wa 12,14). Dhambi kila wakati huwa inajaribu kutunasa tena na huwa inatumia miili yetu ili iweze kututawala. Paulo anatuelezea kwamba hatufai kutii dhambi na kuiacha itushawishi kwa njia yeyote ile. Biblia inatueleza kwamba, tusiache shetani atudanganye. Usiache shetani akutawale jinsi alivyokuwa akitawala. Kataa nguvu za shetani ambazo umekombolewa kutoka ndani. “Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii tamaa mbaya. Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoe kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu Kwake kama vyombo vya haki” (Warumi 6:12-13).

Page 18: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Sura ya tatu

Kaeni ndani Yangu

Bwana Yesu Kristo aliwaambia wanafunzi wake kwamba, “Msifadhaike mioyoni mwenu” (Yohana 14:1). Bwana Yesu Kristo aliwaambia hivyo kwa sababu aliona kwamba walikuwa wamejawa na wasiwasi. Je, kwa nini walikuwa na wasiwasi? Ni kwa sababu Bwana Yesu Kristo alikuwa anaenda kuwaacha. Alikuwa amewaambia kwamba alikuwa anaenda kufa lakini wao hawakuona kwamba maneno Yake yalikuwa na umuhimu wowote. Wakati huu, ujumbe ulikuwa wazi kwao na walijua kabisa kwamba Bwana Yesu Kristo alikuwa anaenda kuwaacha. Aliwaambia, “Watoto Wangu, Mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo. Niendako, ninyi hamwezi kuja” (Yohana 13:33). Waliposikia haya, walijawa na wasiwasi.

Je, walikuwa waendelee aje wakati Bwana Yesu alikuwa hayuko pamoja nao? Kwa miaka mitatu alikuwa nao kila wakati. Walikuwa wamemsikiza akizungumza na kujifunza mengi kutokana Naye. Upendo Wake uliwagusa sana, maisha Yake matakatifu yalikuwa yamewapa changamoto kubwa sana na miujiza Yake ilikuwa imewaacha vinywa wazi. Aliwahimiza na kuwapa nguvu wakati walikuwa wadhaifu na pia aliwaongoza wakati walikuwa wamekosa mwelekeo. Je, wangeendeleaje wakati hakuwa nao tena?

Bwana Yesu alijua kwamba wamefadhaika na kwa hivyo alisema, “Kwa sababu nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni” (Yohana 16:6). Alifahamu jinsi walihisi na alitaka wafahamu kwamba anajua hali yao. Katika sura za Yohana 14-17, tunapata mazungumzo ya mwisho ya Bwana Yesu Kristo ya kuhimiza sana. Alisema, “Nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami. Sitawaacha ninyi yatima, naja kwenu..Yafaa Mimi niondoke kwa kuwa nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu” (Yohana 14:3,18; 16:7).

Maneno haya ya kaeni ndani mwangu mara mingi huwa yanapuuzwa. Haya yalikuwa maneno yakuwafariji wanafunzi wa Kristo. Kile Kristo anawaeleza ni kwamba, hawaachi peke yao. Wao walikuwa wake na walikuwa wameunganishwa kwake na hakuna chochote ambacho kingewaondoa Kwake, hata kiwe ni kifo. Kupitia kwa huduma wa Roho Mtakatifu, wangeendelea kupata kila baraka na kuwa katika uwepo Wake.

Hii ndiyo hali ambayo nitaka tuzungumzie. Kuwa ndani ya Kristo ni zaidi ya kujulikana tu na Mungu. Ni jambo la utajiri sana ikizingatiwa hali yetu mpya ambayo tumepokea kwa imani na hii ikiwa ndiyo msingi wa maisha yetu ya ukristo. Jambo hili limekusudiwa tulifahamu vyema kabisa; kwamba tuko katika Kristo Yesu. Kuna mchungaji mmoja ambaye alisema kwamba, Maisha ya imani ya kweli hayawezi kuwa maisha bila hisia. Ni lazima yawe maisha ambayo imejawa na upendo na ushirika kwa sababu ushirika na Mungu ndiyo kilele cha ukristo wa kweli. Kumfahamu Mungu na kumfurahia inapatikana katika maneno haya, “Kaeni ndani Yangu.”

Ukweli ambao Kristo anaeleza hapa

Nchi ya Palastina ilikuwa nchi ambayo ilikuwa na mizabibu mingi sana na kwa kila nyumba mti huu ulipatikana kwa kusudi la kuleta kivuli. Katika kivuli hiki watu wangeketi na kupumzika na kushirikiana na kupata chakula pamoja. Hakuna kitu ambacho watu wangefahamu sana kama mti huu, matawi yake na matunda yake. Maneno ya Kristo “Kaeni ndani Yangu,” yalikuwa mfano mwema ambao kila mtu angefahamu hata mtoto mdogo: “Mimi ni mzabibu wa kweli, ninyi ni matawi” (Yohana 15:5). Fundisho Lake lilikuwa wazi kabisa. Maisha ya tawi yalitoka kwa mti. Tawi halingeweza

Page 19: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

kuweko bila mti kuwepo. Bila mti, tawi hata kama lingekuweko, halingekuwa na maana yoyote, isipokuwa kuchomwa tu. Kila tunda zuri na lenye afya, limeweza kuwa hivyo kwa sababu mti umeendelea kuliwezesha kuwepo.

Jambo hili ni la kweli hata kwetu sisi wakristo. Kuendelea kwetu katika jambo lolote lile, kunategemea kuweko kwetu katika Kristo. Hatuwezi kukua au kuendelea katika maisha yetu ya ukristo kwa nguvu zetu, bali tunaweza tu kwa nguvu za Kristo. Hii inamaanisha kwamba kuunganishwa kwa Kristo si jukumu tu ambalo tumefanya, bali ni uhusiano mkubwa sana ambao tuko nao pamoja naye. Hii inamaanisha kwamba tunaendelea kupata nguvu katika maisha yetu ya kiroho kutoka kwa Kristo mwenyewe.

Kwa nguvu zetu au kwa uwezo wetu hatuwezi kuwa watu ambao Mungu anataka tuwe. Hatuwezi kujibadilisha kwa njia yoyote ile. Hatuwezi kujiokoa wala kuamua kuwa wazuri na kuanza kumpendeza Mungu. Kristo pekee ndiye anaweza kutufanyia haya yote. Kristo ndiye huwa anatubadilisha, Anatuwezesha kupigana na dhambi kwa neema, Anatutayarisha kwa ajili ya kufanya mapenzi Yake na Anatutumia kutekeleza mapenzi Yake katika ulimwengu huu. Paulo anasema kwamba “sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tupate kutenda matendo mema” (Waefeso 2:10).

Kwa hivyo kuna jukumu kwa kila mkristo kutenda matendo mema. Ni lazima tujitahidi katika ukristo wetu kutekeleza yale ambayo Kristo anaamuru katika neno lake. Biblia inasema, “kwa hiyo, wapenzi wangu, kama vile ambavyo mmekuwa mkitii sikuzote, si tu wakati nikiwa pamoja nanyi, bali sasa zaidi sana nisipokuwapo. Utimizeni wokovu wenu kwa kuogopa na kutetemeka, kwa maana Mungu ndiye atendaye kazi ndani yenu, kukata kwenu na kutenda kwenu kwa kulitimiza kusudi Lake jema” (Wafilipi 2:12-13).

Yesu Kristo ndiye mzabibu ambao huwezesha matawi kua na kuendelea.

Huwa hatutakaswi kwa sababu ya juhudi zetu pekee. Kuna watu wengi ambao wamejaribu kwa juhudi zao lakini wamekosa kufaulu. Martin Luther ni mfano mkubwa wa watu wale ambao walijaribu kwa juhudi zao kujitakasa. Kuna wakati ambapo alifunga kwa siku tatu lakini hakuwezi kujitakasa kutoka kwa dhambi zake. Alikiri dhambi zake kwa kuhani mara nyingi kila siku, na pia kulikuwa na wakati moja ambapo alikiri dhambi zake kwa kuhani kwa masaa sita. Kama angeweza kufanya mambo mengine, angefanya ili aweze kupata msamaha wa dhambi zake na kujiwezesha kuishi maisha matakatifu. Juhudi zake zote hazikumletea lolote zuri. Alihitaji kuelewa injili ya neema ya Mungu kupitia kwa Yesu Kristo. Alifahamu kwamba, kukua katika ukristo na kuzaa matunda, ni matokeo ya kazi ya Bwana Yesu Kristo ndani mwetu. Muungano kati ya Kristo na wafuasi wake ndiyo msingi wa maisha ya ukristo.

Kazi ya Bwana Yesu Kristo aliyefufuka

Hili ni jambo ambalo linaelezwa wazi katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Luka anamweleza Theofilo jinsi alivyowandikia katika kitabu chake cha kwanza kuhusu “mambo yote Yesu aliyofanya na kufundisha tangu mwanzo” (Matendo ya Mitume 1:1). Kile Luka anamaanisha ni kwamba katika kitabu hiki cha Matendo ya Mitume anaeleza yale ambayo Yesu Kristo aliendelea kufanya na kufunza baada ya kurudi mbinguni. Huduma ya mitume, hasa hasa Petro na Paulo, imepewa kipao mbele, lakini ni Bwana Kristo ambaye alikuwa anawatumia kufanya kazi yake.

Petro na mitume wengine walihubiri na kanisa likakua. Lakini hii ilifanyika ni kwa sababu Bwana

Page 20: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

“akaliongeza kanisa kwa wale watu waliokuwa wakiokolewa” (Matendo ya Mitume 2:47). Katika mji wa Filipi, Lidia alisikiza ujumbe wa Paulo wakati yeye aliwahubiria wanawake kando ya mto. Lakini Lidia aliokoka baada ya Mungu kuufungwa moyo wake (Matendo ya Mitume 16:14). Baada ya Petro na Yohana kutumika na Bwana Yesu Kristo kumponya kiwete ambaye alikuwa anaketi mlangoni mwa hekalu, Petro aliendelea kueleza jinsi muujiza huo ulivyofanyika. Alisema, “Enyi wanaume wa Israeli, kwa nini mnastaajabu kuhusu jambo hili? Mbona mnatukazia macho kwa mshangao kana kwamba ni kwa uwezo wetu au utakatifu wetu tumefanya mtu huyu kutembea? Mungu wa Abrahamu na Isaki na Yakobo, Mungu wa baba zetu amemtukuza Mwanawe Yesu ambaye ninyi mlimtoa ahukumiwe kifo na mkamkana mbele ya Pilato ingawa Yeye alikuwa ameamua kumwachia aende zake” (Matendo ya Mitume 3:12-13).

Wakati muujiza unatendeka, kanisa la kwanza lilieleza kwamba, ni Kristo Yesu ambaye alikuwa amefanya haya.

Jambo hili ni la ukweli kulingana na yale ambayo tumeshasoma. Tuko katika Kristo. Kristo ndiye kila kitu. Ni jambo la maana sana ikiwa tutakumbuka hili katika ulimwengu ambao umejawa na wanadamu ambao wanawaza kwamba kila kitu kinategemea wao. Hata katika makanisa huwa tunataka kufanya jinsi tunataka. Makanisa mengi huwa yanazingatia sana yale ambayo mwanadamu anaweza kufanya au kupata. Kile wanadamu huwa wanaonyesha ni kwamba wao ndio wanaendesha kila jambo katika ufalme. Lakini kile ambacho ni muhimu ni kile ambacho Kristo anataka kifanyike na kwamba sisi tumeunganika Kwake. Kristo Yesu ndiye chanzo cha maisha. Tunapoona matawi yamejawa na matunda, tunajua kwamba na tunafaa kujua kwamba hayatoki tu kwa matawai bali kwa mti.

Kile ambacho ni cha ajabu sana ni kwamba, Bwana Yesu Kristo ametuchagua tumfanyie kazi. Tukumbuke kwamba Bwana wetu Yesu Kristo ako mbinguni. Tumebarikiwa sana kuwa watu ambao Kristo anatumia kwa nguvu zake na neema yake katika ulimwengu huu. Sisi ni mwili wake hapa ulimwenguni. Sisi ndiyo chombo ambacho Kristo anatumia kuwaita na kuwaleta watu katika Ufalme Wake na kuwarejesha katika uhusiano mwema na Mungu wao. Kazi ambayo tumepewa ni kubwa mno na mavuno ya kazi hii ni makubwa ya ajabu.

Hakikisho ambalo Bwana Yesu Kristo anapeana

Kristo alisema, “Kaeni ndani yangu.” Kwa maneno mengine Yesu anasema, bakini ndani mwangu, unganeni kwangu, unganeni kwa nguvu Zangu na mwendelee kuishi katika uwepo Wangu. Je, hili si ni jambo la ajabu sana? Bwana Yesu Kristo ni Mungu mwenyewe, Mungu wa ajabu, mwenye kuishi katika utukufu wa kuogofya, Mungu Mtakatifu na mwenye nguvu zote. Kukaa ndani ya Kristo si ni jambo la kutuhimiza sana. Je, kuishi katika uwepo wa Kristo si ni jambo ambalo linawahitaji wakristo wote kuwa waangalifu? Kwa sababu ya udhaifu wetu na dhambi, kila wakati tutajihisi kuwa watu ambao hatustahili kamwe mbele za Kristo. Kuwa katika Kristo kila wakati ni jambo ambalo linastahili kuheshimiwa sana. Jukumu la kuendelea kuwa mkristo , si rahisi hata kidogo, lakini tunafaa kulifanya. Hii ni baraka kubwa sana kuwa katika Kristo, lakini si jambo rahisi kuliendelesha.

Kristo anaonyesha jambo hili kwa kusema kwamba, “Kama vile Baba alivyonipenda Mimi, hivyo ndivyo Mimi nilivyowapenda ninyi. Basi kaeni katika pendo Langu” (Yohana 15:9). Kristo anatupenda na huu ni ukweli. Je, sisi huwa tumnamshukuru kwa ajili ya jambo hili? Je, ni watu wangapi ambao wanakupenda kwa kweli? Ni jambo la furaha na la thamani sana wakati mtu anatueleza kwamba anatupenda. Hili ni jambo ambalo halifai kusahaulika kamwe. Upendo mkuu ndiyo Kristo ametudhihirishia sisi watu Wake. Wakati anasema, “Kaeni ndani Yangu” (mstari wa 4), na “Kaeni katika pendo Langu”, haya yote ni jambo moja kwamba Kristo ni upendo.

Page 21: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Aliwaambia wanafunzi wake, “Nimewapenda.” Ukweli ni kwamba alikuwa amewapenda wanafunzi Wake tangu kuumbwa kwa ulimwengu wakati alipojitoa kuwa Mwokozi wao. Aliwapenda wakati alipokuja hapa ulimwenguni kuteseka na kufa kwa ajili yao. Lakini hata wakati wa haya yote, wanafunzi Wake walifahamu mambo haya yote pole pole na pia hawakuwa wamekamilika, lakini aliwapenda. Hata katika maisha ya milele, upendo wa Kristo hauwezi kupimika ambao ako nao juu yetu.

Wakati anapofafanua jinsi anavyotupenda, anaeleza jinsi jambo hili lilivyo: “Kama vile Baba alivyonipenda Mimi, hivyo ndivyo Mimi nami nilivyowapenda ninyi” (mstari wa 9). Tukiwaza juu ya upendo wa Mungu juu ya Mwana Wake, tunaona jinsi Kristo anavyowapenda watu Wake. Katika maisha ya Kristo yote hapa ulimwenguni, Mungu Baba alikuwa naye na alimwongoza katika kila jambo. Wakati Kristo alipobatizwa katika mto Yordani, sauti ilisikika kutoka mbinguni ikasema kwamba, “Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa Wangu ambaye nimependezwa Nawe” (Marko 1:11). Vivi hivi ndivyo Kristo anavyowapenda watu wake. Hakuna jambo lolote katika ulimwengu ambalo linaweza kulinganishwa na upendo huu. Maneno haya yalitoka katika kinywa cha yule ambaye ni ukweli mwenyewe.

Je, huwa tunafahamu upendo mkuu ambao Kristo ako nao juu yetu watu wake. Je, jambo hili huwa linatuletea furaha na huwa linatuongoza kumwabudu Mungu? Je, huwa jambo hili linamaanisha lolote kwetu? “Ndipo Wayahudi wakasema, 'Tazama jinsi alivyompenda Lazaro'” (Yohana 11:36). Pia huenda jambo hili ndilo linawashangaza sana malaika mbinguni: Upendo wa Kristo kwa watu Wake.

Swali la kujiuliza

Bwana Yesu Kristo anasema, “Kaeni katika pendo Langu.” Je, hii inamaanisha nini? Je, kuna wakati ambapo tunaweza kujipata kwamba tuko nje ya upendo huu wa Kristo? Kristo anawapenda watu Wake na upendo mkubwa sana ambao hautawahi kubadilika. Kristo huwapenda watu Wake na haijalishi wao ni kina nani au wamefanya nini. Je, tunafaa kuogopa kwamba siku moja tutaondoka upendo wake? Je, kwa nini Bwana Yesu Kristo anatuambia “Kaeni”?

Ni ukweli kwamba hakuna siku hata moja ambayo Bwana Yesu Kristo atauondoa upendo Wake juu ya watu Wake. Biblia inasema, “Alikuwa amewapenda watu Wake waliokuwa ulimwenguni, naam, aliwapenda hadi kipimo cha mwisho” (Yohana 13:1). Upendo huu, huvumilia na haushindwi katika jambo lolote leo na hata milele. Je, amri hii kutoka kwa Kristo inamaanisha nini: “Kaeni katika pendo Langu.”

Wakati jua huwaka, sisi husema kwamba hewa ni mzuri sana kwa sababu hali ya anga huwa mzuri sana. Wakati jua linapotua, huwa tunahisi baridi kwa sababu joto la jua halipo tena. Hivi ndivyo ilivyo na upendo wa Kristo kwa watu Wake. Huwa mara kwa mara upendo huu hungaa juu ya watu Wake. Lakini tunaweza kujinyima na nafasi ya kufahamu upendo huu. Huwa dhambi zetu zinatutenga na Mwokozi wetu na kutuficha kutokana na upendo huu. Kuishi katika upendo Wake, ni kuishi katika nuru ya jua na kutokubali kivuli chochote kutuzuia. Ikiwa tunataka kuishi katika upendo huu, lazima tuishi katika upendo Wake.

Amri hii hutuletea furaha kubwa sana ikiwa tutaitii amri hii, “Kaeni katika upendo Wangu.” Tutafahamu jambo hili vyema na tutafurahi sana katika jambo hili si kwa wakati mmoja tu bali kila siku. Bwana Yesu Kristo anataka tufurahie pendo Lake kila wakati. Je, ni nani hatamani jambo hili? Upendo huu ni wa kweli na Kristo anataka tuufurahie sana. Swali ni, je, tutafurahia pendo hili aje?

Page 22: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++ Jukumu ambalo Bwana Yesu Kristo anatupatia

Jukumu kuu liko katika neno hili, “kaeni” ambalo linapatikana mara 10 katika sura ya 15 ya kitabu cha Yohana. Neno hili linamaanisha, bakini, ishini, dumuni au mtu kuendelea kuishi mahali fulani. Wale ambao wameokoka, wanaishi katika Kristo na katika pendo Lake,: “Kaeni katika pendo Langu.” Kaeni ni jukumu ambalo tunastahili kufanya na si jambo ambalo linatendeka tu. Si jambo ambalo linajitokeza tu au jambo ambalo linafanyika tu lenyewe. Hili ni jambo ambalo tunafanya wenyewe. Tunafaa kulizingatia sana na kufanya kila jambo ili tuweze kulikamilisha. Kile tunaihitaji kufanya ni kuhakikisha kwamba kuunagana kwetu na Kristo kuwe jambo ambalo ndilo msingi wa maisha yetu ya kila siku. Hili ni jukumu letu. Je, tunafaa kulitekeleza aje?

Huwa tunakaa ndani ya Kristo kwa imani.

Kama jinsi tumeona, tuliamini katika Kristo, tulikuja kwake kwa imani na kwa njia hiyo hiyo, tunafaa kuendelea kuishi ndani Mwake kwa imani. Hii inamaanisha kwamba kila wakati tunapaswa kukumbuka Kristo ni nani na yale ambayo ametufanyia. Tunafaa kufahamu vyema uhusiano wetu wa sasa ambao tuko nao na kujitahidi kuishi kulingana na nuru ya neno Lake. Kwa ufupi ni kwamba lazima tuendelee kwa imani tukimtazama tu Mwokozi wetu na kuendelea kumtegemea katika kila jambo.

Mtoto mdogo huwa anawategemea wazazi wake kwa njia hii. Huwa anajua kwamba kutoka kwao ataweza kupata kila kitu; chakula, mavazi, upendo na ulinzi. Kwa sababu ya udhaifu wake, mtoto huyu anajua kwamba hawezi kuendelea kuishi katika ulimwengu bila kuwa na mtu ambaye ako na nguvu nyingi, mtu mwenye hekima ambaye atamlinda na kutosheleza mahitaji yake yote. Vivyo hivyo tunamhitaji Kristo, na kwa ujasiri tunaweza kusema, “Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu” (Zaburi 23:1). Wakristo hawaitwi waamini bila sababu yoyote kwa sababu tusipoamini, basi hatuwezi kujulikana kuwa wakristo. Sisi wakristo ni watu ambao tuko na imani ndani ya Kristo Yesu si tu wakati tunapookoka, bali pia kwa kila hatua ya maisha ya ukristo wetu.

Huwa tunaendelea kuishi ndani ya Kristo kwa utiifu

Jambo hili limeonyeshwa wazi katika mstari wa 10: “Mkizishika amri Zangu, mtakaa katika pendo Langu, kama Mimi nilivyozishika amri za Baba Yangu na kukaa katika pendo Lake.” Bwana Yesu Kristo ni Mwokozi na pia ni zaidi ya Mwokozi. Yeye ni Bwana na ni Mungu ambaye huzungumza na mamlaka yote na ni Yeye ambaye tumeitwa tumtii katika kila jambo. Kukataa mapenzi Yake ni kuvunja ushirika naye na kujitenga na kusudi lake na baraka Zake. Ikiwa tunakosa kumtii Kristo kupitia kwa neno Lake, tunamkataa Yeye mwenyewe.

Wakristo wanapotii sheria ya Mungu, wao huishi katika ushirika wa karibu sana naye. Zaburi ya 1 huanza, “Heri mtu yule.” Maana ya neno hili katika lugha ya Kiebrania, ni baraka nyingi ambazo ni za kweli. Je, kubarikiwa huku ni kwa aina gani? Je, kubarikiwa ni hisia tu za moyo kwamba tuko karibu na Kristo? Ukweli ni kwamba hisia ni mzuri kwa sababu huwaletea wakristo furaha katika uhusiano wao na Mungu. Lakini kile ambacho kinazungumzwa katika Zaburi hii, ni kuhusu maisha ya mkristo ya kila siku.

“Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hafuati njia ya wenye dhambi au kukaa katika baraza la wenye mizaha. Lakini huifurahia sheria ya Bwana, nayo huitafakari mchana na usiku” (Zaburi 1:1-2).

Page 23: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Kwa hivyo furaha ni kuzitii amri za Mungu. Kuwa mtiifu kwa Mungu siyo tu njia ya kubarikiwa bali ni baraka yenyewe. Kumtii Kristo ni kuishi ndani Mwake na kufurahia upendo Wake kikamilifu.

Kuna zaidi ya kuishi ndani ya Kristo kando na imani na utiifu. Kristo huishi ndani ya mkristo (mstari wa 4,5). Pia tunaambiwa kwamba, ikiwa tutapendana, Mungu hukaa ndani mwetu (1 Yohana 4:12). Jambo la kuzingatia sana ni kwamba, Mungu Baba na Mungu Mwana hawatii wala hawategemei wale ambao Wao wanaishi ndani mwao. Pia kuna ushirika wa karibu sana kati ya Mungu Mwana na Mungu Baba kama Kristo anavyoeleza; “Mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani Yangu” (Yohana 14:10). Je, msingi wa uhusiano huu wote uko wapi?

Tunaendelea kuishi katika Kristo kwa kushirikiana naye.

Kuishi ndani ya mtu ni kuwa na ushirika wa milele wa ndani sana naye. Inamaanisha kuzungumza naye, kushirikiana naye na kujitoa kwa ajili yake na kuwa na ushirika wa karibu sana naye. Urafiki wa aina hii, ni wa utukufu mkubwa sana na unatosheleza. Urafiki huu ndio jukumu letu na kibali kikubwa sana ambacho tumepewa.

Mara nyingi wakristo wengi huwa hawafurahii majukumu yao na mwishowe wao huyafanya bila furaha yoyote. Kuna wakristo ambao wanasoma Biblia na kuomba kila siku kwa sababu wakati wao walikuwa wakristo wachanga, waliambiwa haya ni majukumu yao. Kwa hivyo wanafanya haya yote si kwa sababu wako na furaha kwa kuyafanya, bali kwa sababu haya ni majukumu yao. Lakini ni wachache ambao hufahamu umuhimu wa kusoma Biblia na kuomba kwa sababu wanajua kwamba haya ni mambo ya maana katika ukristo wao.

Wao wanafanya majukumu yao kwa furaha kwa sababu wanafahamu wao tawi ambalo linapokea maisha na nguvu kutoka kwa mzabibu. Maisha haya huingia katika mawazo na mioyo yetu kupitia kwa Neno la Mungu, na hii ndiyo sababu Kristo alisema, kaeni ndani Yangu. Aliendelea kueleza jinsi tunapaswa kukaa ndani Yake, ni kupitia kwa neno Lake ambalo linakaa ndani yetu (mstari wa 7). Kila wakati tunaposoma Biblia, huwa tunafungwa macho na mawazo yetu kwa maneno ya Kristo ambaye yako na uwezo wa kutubadilisha. Tunapokuwa tunasoma Biblia, huwa Bwana Yesu Kristo anazungumza nasi kwa nguvu ambazo ziko na uwezo wa kubadilisha maisha yetu. Neno Lake linaongoza maombi yetu tunapoomba kwamba atatubairiki, na kwamba baraka zake zitafika ulimwenguni kote kupitia sisi.

Wakristo wengi wanafahamu kwamba kuna kasoro katika maisha yao ya ukristo. Labda sababu ni hii kwamba wao hawajitahidi katika ushirika na uhusiano wao na Kristo. Ikiwa hatutajitahidi katika ushirika wetu na Bwana wetu Yesu Kristo, je, tutawezaje kufurahia upendo Wake? Je, tutawezaje kupewa nguvu na Kristo Yesu ambaye tunampuuza? Si kwamba aliacha kutupenda, lakini ni kwa sababu tumekosa kumpenda Kristo na kujitolea kwa ajili yake. Majuto ya wakristo wengine wakati maisha yao yanamalizika hapa ulimwenguni ni kwamba wao hawakujitolea kabisa katika ushirika wao na Kristo Yesu. Ikiwa hatutafaulu katika jambo hili, basi hatutafaulu katika mambo yote. Kasisi Ryle alisema, Kukaa ndani ya Kristo kunamaanisha kuwa na ushirika wa karibu sana na Kristo kila wakati. Kila wakati tuwe tunamtegemea Yeye, kuomba Yeye na kila wakati Yeye pekee awe ndiye chemichemi ya maisha na nguvu zetu. Kila wakati lazima awe msaidizi wetu mkubwa na rafiki wa dhati.

Pia katika makanisa yetu tunafaa kuwa na ushirika wa kila siku na Bwana Yesu Kristo. Lazima tumwabudu Mungu kwa maombi na kwa kusoma neno Lake kila siku. Wengi leo wanawaza kwamba ikiwa wanataka ukristo wao uonekane kuwa na nguvu, wanapaswa kuomba kwa sauti ya juu sana kwa

Page 24: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

masaa mengi, kuwa na vyombo vya muziki na kuhubiri kwa kelele. Lakini ukweli ni kwamba mkristo atapata nguvu katika maisha yake ya ukristo ikiwa atajitahidi kila siku kutembea na Kristo kama vile Kristo mwenyewe anafundisha.

Mitindo ya ulimwengu imewaingia wakristo wa sasa. Tunafaa kuondoa mambo yale ambayo hayaambatani na neno la Mungu ikiwa kweli tutaleta mabadiliko katika kanisa la Kristo. Mtu anafaa kuonyesha jinsi alivyo kwa matendo badala ya mazungumzo tu. Tunafaa kuwaonyesha watu kwamba msingi wa nguvu ni maisha ya milele. Tamaa ya kutaka kuwa watu wenye kutunga mambo ambayo hayaambatani na Biblia tunafaa kuiacha kabisa kwa sababu hakuna kile ambacho kimetungwa wanadamu kitaondoa kile ambacho Mungu ameweka tangu kuumbwa kwa ulimwengu huu.

Kutii na kufuata neno la Mungu, ni kujua ukweli na ahadi za Mungu. Biblia inasema kwamba, “Wale wamtumainiao Bwana watafanya upya nguvu zao. Watapaa juu kwa mbawa kama tai, watapiga mbio wala hatachoka” (Isaya 40:31). Kanisa ambalo linazingatia ushirika na Kristo kuwa jambo muhimu kabisa, litabarikiwa sana Naye na litazaa matunda mengi.

Matokeo ambayo Kristo anahidi

“Akaaye ndani Yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana” (mstari wa 5). Tawi ambalo limeunganishwa kwa mzabibu, litazaa matunda mengi sana kwa sababu tawi hilo linapokea mazao mazuri kutoka kwa mzabibu. Kukaa ndani ya Kristo husababisha kuwepo kwa matunda mengi wakati nguvu za Kristo zinapomiminika kwa watu Wake.

Je, mazao haya ni gani? Jibu ni, kila kitu ambacho Kristo hufanya ndani mwetu na kupitia kwetu. Kuwa kama Kristo mwenyewe ni tunda la Roho Mtakatifu ambalo tunaelezwa katika Wagalatia 5:22-23: “Upendo, furaha, amani, uvumilivu, upole, uzuri, uaminifu, ukarimi na kiasi.” Ni Bwana Yesu Kristo mwenyewe ambaye huwa anatubadilisha katika mfano Wake mwenyewe na tunda ambalo tunazaa huwa mara kwa mara tunakuwa kama Yeye mwenyewe. Haya ndiyo maajabu ya wokovu wetu. Mungu hajatusamehe tu dhambi zetu, pia hatukubaliwi tu kama wenye haki mbele Zake, bali huwa tunabadilishwa ili mara kwa mara tuwe kama Bwana Yesu Kristo: “Wale Mungu aliwajua tangu mwanzo, pia aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa Mwanawe, ili Yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi” (Warumi 8:29). Lengo letu ni kuwa kama Kristo Yesu mwenyewe. Je, ni nini tunahitaji ambacho kitatuletea furaha na tumaini?

Tunda hili pia ni huduma ambao uko na mazao. Tunda hili linajumlisha kuwaongoza wengi katika Ufalme wa Mungu, kuwasaidia kukua katika imani na pia kuwahimiza wengi ambao wako katika ufalme tayari. Mwito wa kwanza wa Kristo kwa wanafunzi Wake ulikuwa, waje na washiriki naye. Mwito huu baadaye uliwawezesha kuwa na huduma ambazo ziliwaleta wengi kwa Kristo. Kristo aliwaambia wanafunzi wake, “Njoni nifuateni nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu” (Marko 1:17). Jukumu lao lilikuwa kumfuata Kristo. Jukumu la Kristo lilikuwa kuwafanya wavuvi wa watu.

Wengi leo wengi wamebadilisha mpango na wamejifanya kuwa wavuvi wa watu. Kwa kufanya hivi tunamaliza muda mwingi tukiwaza, jinsi ya kujitayarisha, ni nini tutawaeleza watu na ni wapi tutaenda. Tunasahau kwamba ni kazi ya Kristo kutufanya wavuvi wa watu na tunafaa kumwachie kazi hii. Jukumu letu ni kujitolea kabisa kwa kumfuata na kukaa karibu Naye tukijifunza kutoka Kwake ili tuweze kuwa kama Yeye siku baada ya siku. Ikiwa tutazingatia kumfuata Kristo, Kristo atatufanya tuwe wavuvi. Kristo atatuletea fursa nyingi za kuhudumu na atusaidie kutumia fursa hizo na kuzaa matunda kwa Ufalme wa mbinguni. Majukumu yetu, yaani sisi na Kristo Yesu yamerudiwa katika Marko 3:14 wakati tunaambiwa kuhusu kutumwa kwa mitume. “Akawachagua kumi na wawili ambao

Page 25: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

pia aliwaita mitume, ili wapate kuwa pamoja naye na kuwatuma kwenda kuhubiri” (Marko 3:14). Kwanza lazima tukae naye halafu tutatumwa nje kuhubiri.

Kuzaa matunda mengi ndilo jambo la furaha sana kwa wakristo wote. Hatufai kuishi maisha ya ukristo ambayo hayazai matunda ndani mwetu. Kristo ako nasi na kwa sababu hii, maisha yetu yanafaa yawe ya kuzaa matunda, yawe na mwelekeo ili tuweze kuufikia ulimwengu na ujumbe wa injili ambao unageuza maisha ya watu milele. Wakati tunapoona matunda ambayo tumezaa, tusiwahi kujivuna na kuwaza kwamba sisi ni wa muhimu sana kuliko wakristo wengine. Mafanikio haya ni kwa sababu ya Kristo. Haya yatadhihirisha maneno haya ya Kristo: “Ninyi mkikaa ndani Yangu na maneno Yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtatendewa” (mstari wa 7). Ushirika wetu na Kristo hutuleta katika maombi ambayo sisi huomba kwa mapenzi Yake na siyo mapenzi yetu na kwa kufanya hivi, tunapata kwamba maombi yetu yanajibiwa. Wale wote ambao hufanya kazi jinsi Kristo anavyotaka, hugundua kwamba, wakati Kristo analijenga kanisa Lake, huwatumia wao katika kazi hii.

Pasipo Mimi hamwezi kufanya jambo lolote

Ikiwa mkristo anataka kukua katika ukristo wake au kukua katika huduma wake, ni lazima akae ndani ya Kristo. Hili ni jambo la maana sana kwa sababu Bwana Yesu Kristo anapeana onyo hapa: “Pasipo Mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote” (mstari wa 5). Ikiwa sehemu ambayo inaunganisha tawi na mzabibu imevunjwa au kuharibiwa, tawi hilo halitakuwa kwenye mzabibu na halitaweza kuzaa matunda. Ikiwa hatujaunishwa kwa Kristo hatutaweza tu kufanya mambo madogo au makubwa, bali ukweli ni kwamba hatutaweza kufanya chochote bila Kristo na nguvu Zake ndani mwetu, hatuwezi kufanya lolote jema.

Tunastahili kuzingatia jambo hili kwa makini sana. Je, tunazaa matunda katika maisha yetu ya ukristo? Je, ni mambo gani ambayo tunafanya katika maisha yetu ya ukristo? Je, kuna lolote ambalo tunafanya kwa ajili ya watu wa ulimwengu? Hatufai kuwaza kwamba Mungu anafanya mambo machache tu hapa na pale. Mungu ako anafanya kazi katika maeneo tofauti tofauti katika ulimwengu huu. Lakini ukitazama makanisa mengi leo, utaona kwamba kuna matunda machcahe ya kweli. Makanisa mengi leo yanakufa, kusanyiko za maombi hazihudhuriwi, mahubiri yanaleta mazao madogo sana na nguvu za Kristo hazionekani sana ndani mwa watu jinsi zinafaa kuonekana. Ikiwa kweli sisi husema ukweli, basi jambo hili tunaona likiwa la kweli kabisa. Ukosefu wa mazao haufai kuwa kisingizio kwamba Mungu hivyo ndivyo amependezwa. Mara nyingi wakristo wengi husema hivi. Lakini wanakosa kujua kwamba huenda makosa ni yetu.

Kwa wale ambao wanatazamia matunda mengi, suluhisho ni wazi; tunahitaji kuzingatia sana ushirika wetu wa kibinafsi na Kristo Yesu.

Ikiwa mapenzi ya Kristo hayatimiki ndani mwetu, ikiwa kuna jambo lolote jema ambalo tunafaa kufanya na halijafanywa, basi tunafaa kuchunguza sana ushirika wetu na Kristo. Tunapoona kwamba hatujali kabisa majukumu yetu kama wakristo na tunapuuza kuwasaidia wengine, kuna dawa kwa ugonjwa huu na dawa hii ni chunga sana ushirika wako na Kristo Yesu.

Himizo kubwa la kufanya hivi, linatokana na ikiwa sisi ni wakristo, basi hatujatenganishwa kabisa na Kristo Yesu. Ikiwa kuna hisia za kutengana naye, ni kwa sababu sisi tumekosa kufahamu neema na kufurahia uwepo Wake jinsi tunafaa kuufurahia. Ukweli ambao hakuna mtu anaweza kuondoa ni, milele na milele wakristo wote wameunganishwa kwa Kristo Yesu, Bwana wa utukufu na hakuna yeyote anaweza kuwaondoa katika mwungano huu. Kristo ndiye amepewa “mamlaka yote mbinguni

Page 26: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

na duniani” (Mathayo 28:18).

Kristo aliahidi kwamba, “nitalijenga kanisa” (Mathayo 16:18) na atafanya jambo hili kupitia kwetu kwa ajili ya furaha yetu ya milele. “Nimewaambia mambo haya ili furaha Yangu iwe ndani yenu na furaha yenu iwe kamili” (Yohana 15:11).

Sura ya 4

Wakristo wote wameunganika katika Kristo

Tumekuwa tukiangalia maisha katika Kristo tukizingatia sana mkristo. Lakini katika sura hii tutatazama matokeo makubwa kwa sababu ya uhusiano huu.

Kuwa ndani ya Kristo hutuleta katika jamii kubwa sana ya watakatifu wote. Paulo aliandika na kusema kwamba uhusiano katika Kristo huondoa kila aina ya kizuizi ambacho kimekuwepo kati ya Mungu na mwanadamu na kati ya mwanadamu ya mwanadamu. Kwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia 3:28).

Jamii hii ya Kristo ni moja ulimwenguni kote. Jamii hii huabudu Mungu Mmoja na wao husikiliza na kufuata Neno Lake. Wote wako ndani ya Kristo. Wakristo wanaweza kuwa wanaenda makanisa tofauti tofauti na wawe wanaishi manyumba tofauti tofauti na pia wanatoka katika nchi tofauti tofauti na wawe wanafanya kazi tofauti tofauti, lakini wote wako ndani ya Kristo na ni jamii moja hapa ulimwenguni na huko mbinguni.

Unapotazama ulimwenguni kote, utaona kwamba makanisa yamegawanyika katika vikundi fulani fulani chini ya madhehebu mengi sana. Kwa mfano kuna kanisa la Kibaptisti, Kiangilikana na Kipentekote na hata katika vikundi hivi, kuna wale ambao wameokoka kwa kweli na wao ni wa Kristo. Umoja wa kanisa ni muhimu sana katika kuuhubiria ulimwengu huu. Bwana Yesu Kristo mwenyewe aliomba, “Ili wawe na umoja kama vile Wewe Baba ulivyo ndani Yangu na Mimi nilivyo ndani Yako, wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa Wewe ndiye uliyenituma Mimi” (Yohana 17:21). Unapotazama kwa nje, inaonekana kwamba hakuna umoja ya wakristo, lakini ukweli ni kwamba wale ambao wameokoka wana umoja katika Yesu Kristo ulimwenguni kote. Wao ni jamii moja.

Pengine unawaza kwamba wakati wa Agano Jipya makanisa yote yalikuwa na umoja na hakukuwa na madhehebu. Pengine unawaza kwamba wakristo walikuwa wamoja kwa njia ambayo haionekani siku hizi na kwa sababu ya umoja huu, maneno ya Kristo katika Yohana 17:21, yalitimika wakati huo. Lakini kile tunafaa kufahamu ni kwamba, mambo hayakuwa jinsi tunavyowaza. Kwa mfano ni wazi kwamba katika kanisa la Korintho kulikuwa na mgawanyiko. Hii ndiyo sababu Paulo aliwaandikia “Nawasihi ndugu zangu, katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane nia zenu ninyi, ili pasiwepo na mtengano katikati yenu na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi. Kwa maana ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kleo kwamba kuna magomvi kati yenu” (1 Wakorintho 1:10-11).

Pia ni wazi kwamba makanisa katika miji ya Galatia na Kolose yalikuwa na walimu fulani wa uongo ambao walileta migawanyiko. Pia mtume Paulo aliwahimiza wakristo katika miji Roma kwamba wasiwe watu wakupingana juu ya mambo fulani au wawe watu wa kuwahukumu wengine (Warumi

Page 27: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

14:1,13). Pia aliwaonya wakristo huko Efeso kwamba baada ya yeye kuondoka, “mbwa mwitu wakali watakuja katikati yenu ambao hawatalihurumia kundi. Hata kutoka miongoni mwenu wenyewe watainuka watu na kupotosha kweli ili wawavute wanafunzi wawafuate” (Matendo ya Mitume 20:29-30).

Paulo aliwashukuru sana wale ambao walikuwa wamehubiri injili katika mji wa Roma, lakini wakati huo huo, yeye alijua kwamba wengine walikuwa wanahubiri Kristo kwa ajili ya faida zao za kibnafsi. Hii ndiyo sababu aliandika “Ni kweli kwamba wengine wanaomhubiri Kristo kutokana na wivu na kwa kutaka kushindana. Hao wa kwanza wanamtangaza Kristo kutoakana na tamaa zao mwenyewe wala si kwa moyo mweupe wanakusudia kuongeza mateso yangu katika huku kufungwa kwangu” (Wafilipi 1:15, 17). Wakati Paulo alikuwa anafikia mwisho wa huduma wake alisema kwamba, “watu wote katika Asia wameniacha” (2 Timotheo 1:15). Mtume Yohana akizungumza kuhusu wale ambao walikuwa wameacha imani alisema, “Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu hasa” (1 Yohana 2:19).

Hatufai kuwaza kwamba kanisa la kwanza lilikuwa kanisa ambalo halikuwa na dosari yoyote. Kanisa hili lilikuwa na matatizo kama tu kanisa la leo. Lakini hata wakati wa matatizo kama haya, Paulo alisema kwamba wakristo wote wako katika Kristo. Je, hii inamaanisha nini? Je, anamaanisha kwamba siku moja tutakuwa na umoja huko mbinguni? Huu ni ukweli lakini hakuwa akimaanisha hivyo hapa. Je, alikuwa akimaanisha kwamba haya ni mawazo tu ambayo tunafaa kusahau? Umoja ambao Paulo anazungumza juu yake ni ule ambao ni thabiti, wa kweli na ni wa kudumu.

Wale ambao wameokoka ndilo kanisa la Kristo.

Umoja wa Wakristo katika Kristo unamaanisha nini.

1. Wakristo wameunganika pamoja na Kristo hata kabla ya ulimwengu kuumbwa.

Jambo hili linatuelekeza kwa mafundisho ya kuchaguliwa na Mungu. Mungu amepanga kuwaokoa wenye dhambi kwa kutegemneza Agano ambalo la Ukombozi. Katika Agano hili la ukombozi, Mungu Baba kwa upendo aliwachagua watu fulani kuwa wake; Mungu Mwana alikufa kwa ajili yao msalabani na Mungu Roho Mtakatifu huwapatia imani ili waweze kupokea wokovu wao ambao umegharamiwa na Kristo Yesu. Agano hili la Mungu limekuwepo kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Biblia inasema kwamba Mungu alituchagua katika Katika kabla ya Yeye kuumba ulimwengu (Waefeso 1:4). Yesu Kristo anazungumza kuhusu jambo hili katika maombi Yake akisema, “Kwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale ulionipa. Nimewajulisha Jina Lako wale ulionipa kutoka katika ulimwengu. Walikuwa wako, ukanipa Mimi, nao wamelitii Neno lako. Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile Jina ulionipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa, ili Maandiko yapate kutimia. Baba, shauku Yangu ni kwamba, wale ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili waweze kuuona utukufu Wangu, yaani, utukufu ule ulionipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu” (Yohana 17:2,6,9,12,24). Kanisa ni mwili mmoja. Wakristo ndio wateule wa Mungu, wamechaguliwa na Mungu na ni wale ambao wamepewa Bwana Yesu Kristo.

Hii ni siri ambayo amefunuliwa kwetu. Umoja wa sisi wakristo ni jambo ambalo limekuwepo tangu zamani hata kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, umoja huu umekuwepo. Kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, kulingana na ushauri wa Mungu wa Utatu, wakristo wameungana katika Kristo Yesu.

2. Wakristo wameungana katika Kristo katika Agano la Kale lote.

Page 28: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Baada ya Adamu na Hawa kuanguka katika dhambi, Mungu alimlaani shetani na pia akatabiri hukumu na wokovu wakati alisema, “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, huo atakuponda kichwa nawe utamgonga kisigino” (Mwanzo 3:15).

Hapa Mungu anaanzisha uadui kati ya watu wawili, kati ya uzao wa mwanamke na wa shetani. Katika vita hivi, Mungu anasema kwamba uzao wa mwanamke utamshinda shetani kwa kumponda kichwa baada ya kuumizwa. Uzao wa mwanamke ni Mwokozi Yesu Kristo. Lakini pia watu wake wote wako pamoja naye na Agano la Kale ni hadithi ya kikundi hiki kimoja cha watu Wake, jinsi kikundi hiki kinavyowekwa pamoja, jinsi kinavyokombolewa na kuendelea kuwepo chini ya nguvu za Mungu. Watu katika kikiundi hiki wametoka katika mataifa yote ya ulimwengu na wao ni kizazi cha Abrahamu ambaye Mungu alimwambia kwamba, “kupitia kwako mataifa yote duniani yatabarikiwa” (Mwanzo 12:3). Paulo anazungumza kuhusu Abrahamu na anasema kwamba, Abrahamu ndiye baba wa wale wote ambao wanaokoka, yaani baba wa wakristo wote (Warumi 4:11,16). Wakati Paulo anazungumza kuhusu Israeli, hamaanishi watu wa inchi ya Israeli, bali anamaanisha wale ambao wameokoka duniani kote.

3. Wakristo wote waliunganika katika Kristo alipokufa msalabani.

Hapa kuna tukio la kihistoria. Mwana wa Mungu alikufa kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Lakini swali ni, je, Kristo alifia nani, watu wote au wengi miongoni mwa wote? Jibu ni kwamba alikufa kwa ajili ya watu Wake. Watu wake ni kina nani? Ukweli ambao Biblia inatupatia ni kwamba watu wake ni wale ambao Mungu Baba alimpatia aje afe kwa ajili yao. Hakufa kwa ajili ya kila mtu. Huu ni ukweli wa thamani ambao kila mkristo anafaa kuzingatia sana. Kama Paulo, tunampenda na kumwabudu Mwana wa Mungu ambaye alitupenda na akajitoa afe kwa ajili yetu (Wagalatia 2:20). Kristo aliwaona na huwaona watu Wake wakiwa wameungana pamoja. Biblia inazungumza kuhusu Kristo kuwaokoa watu wake kutokana na dhambi zao (Mathayo 1:21). Anasema, ninayatoa maisha yangu kwa ajili ya kondoo wangu (Yohana 10:15). Kristo alilipenda kanisa na akajitoa kwa ajili yake (Waefeso 5:25). Kristo alilipenda kanisa, kanisa ambalo ni moja na limeunganika pamoja ulimwenguni kote.

Wakati Kristo alikuwa anajitoa, alifahamu vyema kwamba watu wake wote wameunganika tangu mwanzo hadi mwisho watakuwa pamoja. Umoja huu ambao upo kulingana na kusudi la Mungu, umehakikishwa na damu ya Kristo Yesu. Tunapokuwa na imani ndani ya Mwana wa Mungu aliyekufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, tunaona kwamba sisi wakristo tumeungana ndani Mwake.

4. Wakristo wote wameunganika katika Kristo katika wokovu.

Sisi sote tumekuja kwa Kristo kwa njia tofauti tofauti. Wakristo wote wameletwa kwa Kristo kwa njia tofauti tofauti. Ni furaha kubwa sana wakati tunaposikia jinsi watu wamekuja kwa Kristo. Sisi sote tunaweza sema, “Njoni msikilize ninyi nyote manaomcha Mungu, nami niwaambie aliyonitendea” (Zaburi 66:16). Wokovu ni jambo la maana sana na kila mmoja wetu lazima awe na imani kuupata. Lazima tumwendee Kristo sisi wenyewe. Hatufai kumwamini mtu yeyote au jambo lingine lolote kutuletea wokovu.

Huwa tunakuja kwa imani kwa njia tofauti tofauti. Kuna wale ambao wamekuja kwa Kristo wakiwa watoto, wengine wakiwa vijana na wengine wakiwa wazee. Wengine huja baada ya mambo fulani fulani kufanyika katika maisha yao.

Lakini hata kama tunakuja kwa njia tofauti tofauti, kuna mwungano kati wakristo wote. Wakristo wote

Page 29: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

wamezaliwa mara ya pili na wakristo wote wametubu dhambi zao. Wakristo wote wamekuja kwa Mwokozi ambaye ni Kristo Yesu na wamepokea msamaha wa dhambi zao. Wakristo wote wamevalishwa haki Yesu Kristo na Roho Mtakatifu anaishi ndani mwao. “Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja. Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo moja, Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote” (Waefeso 4:4-6). Hata kama tumekuja kwa Kristo kwa njia tofauti tofauti, wokovu ni ule ule na tumeungana na Kristo Yesu.

5. Wakristo wote wameungana katika Kristo na kwa hivyo wanaongozwa na Biblia.

Yale ambaye yameandikwa katika Biblia ni ushuhuda wa umoja wa wakristo kwa sababu Biblia ni kitabu kimoja. Haijalishi sisi ni kina nani, tumezaliwa wapi, tumetoka wapi, kabila zetu ni gani, rangi zetu ni gani, ikiwa tumeokoka, sisi sote tunasoma kitabu kimoja; Biblia. Mahitaji yetu ni tofauti, lakini Biblia huwafaidi wakristo wote. Kando na maagizo kwa watu tofauti tofauti kama vile Baba na mama na watoto na wachunagaji, hakuna mtu ambaye anaweza sema kwamba Biblia haina mafundisho kwake. Biblia inatuzungumzia sisi sote haijalishi wewe ni nani na uko wapi na unapitia katika majaribu gani au unaishi maisha gani, Biblia inazungumza yote kwa wote. Sisi sote tumepewa amri zile zile na sisi sote tunabarikiwa kwa baraka zile zile. Sisi sote ni watu moja chini ya uongozi wa kitabu kimoja.

6. Wakristo wote wameungana katika Kristo kuishi maisha matakatifu.

Amri zote katika Agano Jipya zimelenga mwili mmoja na mwili huu ni kanisa. Mara nyingi huwa tunawaza kwamba amri hizi ni kwa mtu binafsi, lakini ukweli ni kwamba amri hizi zimelenga watoto wote wa Mungu. Maisha ya ukristo ni maisha ya kanisa zima. Ni maisha ambayo kila mmoja wa mkristo anaishi kwa sababu ameunganishwa kwa Kristo Yesu ambaye ndiye kichwa cha mwili huo.

Paulo anazungumza mara kwa mara kuhusu maisha haya ya ukristo ambayo tunaishi kwa umoja. Katika maandishi yake anatumia maneno kama, wafanyikazi wenzangu, mandugu wenzangu, watumishi wenzangu, wafungwa wenzangu (Warumi 16:3; Wafilipi 1:7; Wakolosai 1:7; Wafilipi 2:25; Warumi 16:7). Ndipo tunda la Roho Mtakatifu (Wagalatia 5:22-23) lidhihirike, tunahitaji ushirika wa wakristo wengine. Hatuwezi kuwa na upendo, uvumilivu, upole, uzuri, uaminifu, ukarimu, kiasi, ikiwa hatutaungana na wakristo wengine. Bila ushirika wa wakristo wengine, tunda hili la Roho Mtakatifu haliwezi kukua. Kwa ufupi ni kwamba hatuwezi kukua katika ukristo wetu bila kuungana na wakristo wengine.

Bila umoja huu, hatuwezi kutii amri kama, mpendaneni, ungamianeni makosa yenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa (Yohana 13:34; Yakobo 5:16). Mistari kama hii inahitaji tuwe tumeungana ikiwa tutaweza kutii amri hizi.

Majukumu ambayo yako katika Biblia yanahakikisha umoja wetu. Katika Waefeso 6 tunapewa vazi la ambalo mkristo anafaa kuvaa ili aweze kupinga mishale ya Shetani. Katika maneno haya, ujumbe ni kwa kila mkristo. Ni mfano wa askari mmoja ambaye anafaa kujitayarisha dhidi ya adui wake. Lakini hata kama maelezo yanaonekana kuwa ni kwa mtu mmoja, mfano mkuu ni ule ambao unadhihirisha jeshi la Kristo likiwa pamoja vitani. Huu ni mwili ambao ni watu ambao wamefunga kwa mshipi wa ukweli, wamevaa dirii ya haki na wamechukua chapeo ya wokovu na upanga wa Roho (Waefeso 6:14-17).

Kazi ya kanisa ambayo ni kumwabudu Mungu, kuomba kwa Mungu na kueneza injili, yote

Page 30: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

yanafanyika kwa umoja wa kanisa. Wakristo wengi wanaweza kushangaa wakati wanaposikia kwamba wakristo wa zamani waliona kukutana pamoja kuwa jambo la muhimu sana kuliko wakati wa maombi ya kipekee. Huu umoja ambao Agano Jipya linasisitiza na ni jambo la kuhuzunisha kwamba wengi leo wanataka kujitenga na wakristo. Maisha ya ukristo kulingana na Biblia yanawezekana tu ikiwa watu wa Mungu wataishi katika umoja.

7. Wakristo wote wameungana katika Kristo katika utukufu.

Wakristo wamekuwepo kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Wakristo wote walikuwa wameunganika katika Kristo kabla ya ulimwengu kuwepo na bado wataendelea kuwa katika Kristo hata ulimwengu utakapopita. Kwa pendo Lake, Mungu alituchagua kabla ya kuumba chochote na atatukusanya kwa upendo siku ile Kristo atarudi. Bwana Yesu Kristo alisema kwamba, “Haya ndiyo mapenzi yake Yeye aliyenituma, kwamba, nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali niwafufue siku ya mwisho” (Yohana 6:39). Maono ya Yohana katika kitabu cha ufunuo ya utukufu mkuu, yalikuwa “Baada ya kutazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna ye yote awezaye kuuhesabu. Kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema, 'Wokovu una Mungu wetu, Yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na Mwana-Kondoo!' (Ufunuo 7:9,10)

Hii si ndoto bali ni ukweli ambao utafanyika wakati Kristo atakaporudi. Umoja wetu katika Kristo ni jambo la ukweli na limedhihirishwa kwa njia tofauti tofauti. Umoja wa wakristo ni jambo kuu sana. Wakristo wanajulikana kwa alama moja na wako na uzoefu moja na mwisho wao ni mmoja. Sisi sote ambao ni wakristo tuko ndani ya Kristo Yesu. Lakini je, hii inamaanisha nini kuhusu jinsi tunavyofaa kuishi hapa ulimwenguni?

Matokeo ya sisi kuungana ndani ya Kristo.

Kuna matokeo kadhaa ya sisi kuwa katika Kristo. Tutaona haya yote kwa njia sita.

Kipimo cha maisha yetu.

Umoja huu uko na mipaka ya kiroho ambayo inafaa kuzingatiwa ikiwa mtu ataendelea kuwa mmoja wa umoja huu. Sisi tuko katika Kristo pekee. Hakuna umoja wowote nje ya Bwana Yesu Kristo. Yeye ndiye msingi wa umoja wetu na tumeungana na wale tu ambao wako katika Kristo Yesu. Yeye ndiye mzabibu na sisi ni matawi. Yeye ndiye kichwa cha mwili na sisi ni viungo. Maisha Yake yako ndani mwetu na Yeye ndiye hutuongoza. Hiki ndicho kipimo, 'katika Kristo.'

Kwa hivyo wale wote ambao hawako katika Kristo, hawako katika umoja nasi. Wao bado wako katika Adamu na kati yetu nao kuna kizuizi kikubwa sana. Wanaweza kudai kwamba wao wako katika umoja nasi hata kwa nje kutambuliwa kana kwamba wako nasi, lakini ukweli ni kwamba haiwezekana mtu kuwa ameunganishwa kwa mwili lakini siyo kwa kichwa.

Ukweli huu unaondoa madai ya wengi kwamba wao ni wakristo kwa sababu wanaenda kanisani au wanafanya mambo fulani ya kidini. Wengi huwa hawajiulizi swali hili, Je, mkristo ni nani? Je, tunawezaje kutofautisha mkristo wa kweli na ule wa uongo? Wao hupuuza maswali haya na hawajiulizi pia je, ishara za mkristo wa kweli ni gani? Wao hudhani kwamba yeyote ambaye anakiri kwamba yeye ni mkristo ameokoka. Pia wanadhani kwamba wakati Kristo aliombea umoja wa watu

Page 31: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

wake, ndio wao ambao aliombea (Yohana 17).

Kipimo cha wale ambao wako katika Kristo, kinamaanisha kwamba kwa wakati fulani lazima tufanye uamuzi ugumu sana. Kuna wakati ambapo tunapaswa kunajitenga na kutoka katika kusanyiko za makanisa ikiwa katika makanisa haya Kristo hahubiriwi. Tukifanya hivi, watu watasema maneno mengi kutuhusu lakini hatufai kufa moyo kwa sababu wote ambao wanakutana siyo wakristo na ikiwa tutakutana nao, jambo hili litakuwa la kumsaliti Bwana Yesu Kristo. Katika mambo ya ulimwengu, tunaweza kuungana na wale ambao hawajaokoka, lakini kuhusu mambo ya kiroho hatuwezi kabisa kumkubali mtu ambaye hajaokoka kuwa mmoja wa wale ambao wameokoka. Hii haimaanishi kwamba sisi tunajitenga, bali ni kwamba sisi tunazingatia umoja wa wakristo ambao wako katika Kristo.

Jambo hili ni la kuwaonya wakristo wote ambao wanabaki katika makongamano ambayo yanaendelea kukataa injili ya Kristo. Pia kuna watumishi ambao huregeza msimamo wao kuhusu mambo fulani fulani ya Biblia. Wao huwa haizungumzii kamwe na kuhusu dhambi na pia hawahimizi watu kuwaleta wengine katika Ufalme wa Mungu. Je, wakristo ambao wanabaki katika makanisa haya wanaweza kusema kwa ujasiri kwamba wao wanaishi maisha ya umoja wa wakristo? Paulo anawahimiza wakristo wachanga kwamba, “Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu ye yote atawahubiria injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele” (Wagalatia 1:9). Je, wewe huwaonaje walimu wa uongo? Wewe huwaona kama watu ambao wamelaaniwa? Ikiwa wewe unashirikiana nao, je, hiyo si ni kumsaliti Mungu?

Pia kunachangamoto kwetu binafsi. Lazima tujiulize maswali kama haya, Je, mimi ni mkristo wa kweli au bado mimi niko nje ya Bwana Yesu Kristo? Je, mimi niko katika umoja wa watu wa Mungu au la?

Fahamu yote.

Umoja wa wakristo unapatikana katika Kristo pekee. Umoja huu upo kila wakati. Hii ndiyo sababu Paulo anaandikia kanisa la Korintho na anawaita wale “walioitwa kuwa watakatifu, pamoja na wale wote ambao kila mahali wanaliita Jina la Kristo wetu Bwana wetu aliye Bwana wao na wetu pia” (1 Wakorintho 1:2). Kwa sababu ya uaminifu wetu kwa Bwana Yesu Kristo, wakristo wote ni ndugu na dada zetu. Kwa hivyo hatuwezi tukaungana na watu ambao hawajaokoka na kuwaita ndugu na dada zetu katika Kristo.

Hapa kuna utukufu wa umoja wa ukristo ambao unavuka mipaka ya rangi, nchi, lugha na kabila zote za ulimwenguni. Huwa umoja huu unaleta watu pamoja; wakubwa na wadogo, maskini na tajiri wote huitana mandugu.

“Hapa hakuna Myunani wala Myahudi, aliyetahiriwa wala asiyetahiriwa, asiyetaarabika wala aliyetaarabika, mtumwa wala mtu huru, bali Kristo ni yote na ndani ya wote” (Wakolosai 3:11).

Umoja wetu katika Kristo unavuka mipaka ya madhehebu. Ukweli ni kwamba tuko na mambo ambayo tunatofautiana kama wakristo. Lakini ikiwa sisi sote tuko katika Kristo, basi sisi ni madada na mandugu hata kama kuna tofauti hizi. Hatufai kuwatenga wakristo wenzetu kana kwamba wao ni watu ambao hawastahili kuwa miongoni mwetu. Tunafaa tuishi katika umoja kama wakristo. Tunafaa kutazama kanisa la Kristo jinsi Kristo mwenyewe anavyoliona. Wakati Petro alikuwa na shaka juu ya huruma wa Mungu, Mungu aliambiwa kwamba, “Usikiite najisi kitu cho chote alichokitakasa Bwana” (Matendo ya Mitume 10:15).

Page 32: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Kuna wakristo ambao ni vigumu sana kushirikiana nao kwa sababu ya jinsi wanavyofanya mambo yao na mafundisho yale ambayo wanafundisha. Tunaweza kuwaza haya yote na yawe ya kweli, lakini tunapaswa kukumbuka kwamba hata hawa Mungu anawapenda kwa sababu wameokoka. Kristo alikufa msalabani kwa ajili yao, na pia siku ya mwisho wataurithi ufalme wa Mungu pamoja nasi. Kama Eliya katika kitabu cha 1 Wafalme 19:10, ni rahisi kujiona kwamba kama kanisa, ninyi peke yenu ndiyo mnafundisha ukweli na ninyi ndiyo wateule peke yenu. Hata sisi binafsi kutokana na kiburi au kushushwa moyo, tunaweza kuzungumza hivi. Lakini hata wakati Eliya aliposema kwamba, “ni mimi peke yangu niliyebaki,” Mungu alimhakikishia Eliya kwamba kulikuwa na manabii elfu saba katika nchi ya Israeli ambao walikuwa waaminifu Kwake na hawakuwa wameziabudu sanamu za huku. Manabii hawa ambao Mungu alimwambia Eliya kuwahusu hakuwa anawajua hata kidogo. Hivi ndivyo ilivyo hata wakati wa leo mahali popote tulipo. Mungu ako na watu wake kila mahali ambao wanampeda sana jinsi tu tunavyompenda. Tukiwaza juu ya ukubwa wa kanisa la Kristo ulimwenguni kote, tunafaa kumshukuru Mungu sana na kujihimiza.

Tunafaa kukumbuka pia kwamba kila mmoja wetu ako na jinsi anavyofurahia kufanya mambo fulani fulani. Kuna wengine wetu ambao mioyo yetu ni migumu kuhusu mambo fulani na hatuwezi kukubali kushiriki na watu ambao wanakataa mambo hayo. Kuna wengine wetu ambao tuko na mioyo myepesi na tunamkubali yeyote ambaye anakiri wokovu. Ni vyema sana ikiwa tutafahamu udhaifu wetu na tuombe Mungu atusaidie turekebisha.

Watu wa aina tofauti tofauti

Hata kama kuna umoja wa watu katika Kristo, umoja huu uko na watu wa aina tofauti tofauti. Watu hawa ni wa aina mbali mbali. Kama tu jinsi Mungu alivyoumba ulimwengu, aliumba mimea tofauti tofauti na wanyama tofauti tofauti, vivyo hivyo, kuna watu wa aina mbali mbali na vipaji mbali mbali. Mwili wake Kristo umejawa na watu ambao wako na vipaji mbali mbali. Mwili wa Kristo haujajumlisha watu wa aina moja tu au watu wenye vipaji sawa, ni mwili ambao uko na kila aina ya watu ambao wameitwa na Mungu mwenyewe kutoka katika mataifa mbali mbali na kupewa vipaji mbali mbali. Huu ndiyo uzuri wa neema ya Mungu ambayo inadhihirika katika utofauti wa watu ambao katika mwili wa Kristo.

Hii ndiyo tofauti kubwa iliyoko kati ya kanisa la kweli na lile ambalo si la kweli. Katika makanisa mengine ambayo si ya kweli, washirika huongozwa tu kwa maneno ya mtu mmoja na huwa hawawezi fanya lolote isipokuwa wamrishwe naye. Lolote wanaloambiwa huwa wanalifuata tu bila kuuliza swali au kujiwazia wenyewe. Wao hukariri maandiko sawa na wao hufuata njia moja tu hata kama ni mbaya wao huwa hawaulizi. Pia kuna makanisa ambayo yanahubiri kweli lakini pia kuna baadhi ya wachungaji ambao huwazuia washirika wao kiwango kwamba washirika hawawezi kufanya lolote ikiwa mchungaji hajasema. Mchungaji huyu hutawala mawazo na maisha ya washiriki jinsi anavyotaka. Ukweli ni kwamba kanisa liko na watu tofauti tofauti ambao wamepewa vipaji tofauti tofauti ambavyo wanafaa kuvitumia kwa ajili ya kumtukuza Mungu. Huu ndio mojawapo wa ushuhuda wa kanisa kwa watu wa ulimwengu huu; Kanisa ni kikundi cha watu ambao wametoka mahali tofauti tofauti, katika kabila tofauti tofauti, wanazungumza lugha tofauti tofauti na wako na vipaji tofauti tofauti. Ni kwa nguvu na neema ya Mungu watu hawa wanaweza kuendelea kuwa na imani moja na kila mmoja kumkubali mwingine.

Utukufu wa utofauti huu miongoni mwa watu hawa unadhihirka wakati kanisa linakuwa moja ambalo limeunganika katika Kristo. Hivi ndivyo Paulo anavyosisitiza wakati anafundisha kuhusu mwili wa Kristo. Anasema, “Mwili si kiungo kimoja bali ni viungo vingi. Kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? Kama ulivyo, kuna viungo vingi, lakini mwili ni mmoja” (1

Page 33: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Wakorintho 12:14, 19-20). Tunahitaji miguu, mikono, masikio na macho ikiwa utaukamilika. Viungo hivi vyote ni vya aina tofauti. Vivyo hivyo, kila mkristo anamhitaji mwingine, hakuna yule ambaye amekamilika. Kwa hivyo umoja wetu unatusaidia kukamilishana. Umoja huu unatufanya tuweze kuwapenda wakristo wenzetu kwa kweli. Umoja wetu kama kanisa la Kristo unatufanya tupendane na kuona kwamba kila mmoja anamwihitaji mwingine. Mkristo hafai kujiona kwamba hahitajiki na wakristo wengine.

Kwa maongozo ya Mungu, kuwepo kwa madhehebu tofauti tofauti si jambo baya. Katika historia, Mungu ametumia madhehebu haya ili ukweli fulani uweze kudumishwa na mafundisho fulani ambayo yamepuuzwa na madhehebu mengine yaweze kuendeleshwa na madhehebu mengine. Hata kama hukubaliana nami kuhusu jambo hili, tumshukuru Mungu kwa sababu ya watu tofauti tofauti ambao wako na vipaji tofauti katika mwili wa Kristo. Nguvu za kanisa zinatokana na Mungu mwenyewe, lakini kanisa liko na nguvu kwa sababu ya utofauti wa watu na kwa sababu ya utofauti wa vipaji ambavyo wako navyo. Utofauti huu hautakoma hapa ulimwenguni bali pia mbinguni utakuwepo. Yohana anasema katika kitabu cha Ufunuo kwamba, “Baada ya haya nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna ye yote awezaye kuuhesabu. Kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo.” (Ufunuo 7:9). Mbinguni hatutabadilishwa kiwango kwamba hatutawezi kutambulika jinsi tulivyokuwa wakati, bali utofauti wetu katika mambo kama rangi, lugha, kabila na taifa tutakuwa navyo mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.

Msingi ambao ni Mungu mwenyewe.

Kuna wengi leo ambao wanaungana pamoja kwa ajili kutengeneza miungano ambayo itawezesha makanisa fulani kuwa katika kikundi kimoja. Haya yote yamefanyika kwa kusudi zuri sana. Wengi wamewaza kwamba tukifanya hivi umoja wetu utakuwa dhabiti sana katika Kristo.

Wale ambao wamefanya hivi, kwa maoni yangu, hawa wanawaza kwamba mwili wa Kristo umetengana na ni juu yetu kama wanadamu kuuleta pamoja. Lakini kulingana na jinsi tumeona, jambo hili haliwezekani kamwe. Tumezungumzia kuhusu yale ambayo Mungu amefanya ili kuuweka mwili huu pamoja. Kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu umoja huu wa wakristo uliwekwa na Mungu. Kalivari tulikuwa katika umoja huu na katika utukufu tutakuwa katika umoja huu. Mungu ametuondoa katika Adamu na kutuleta katika Kristo.

Hii haimaanishi kwamba basi hatufai kufanya lolote ili mwili huu uendelee katika umoja huu. Lakini inamaanisha kwamba hatufai kuona juhudi zetu kama jambo ambalo mwili wa Kristo unategemea kuwepo. Mungu ako na kusudi kuu la umoja huu katika ulimwengu huu ambalo ni “kuvitia vitu vyote vya mbinguni na vya dunia chini ya kiongozi mmoja, ndiye Kristo” (Waefeso 1:10). Kusudi hili liko linatekelezwa na litakamilishwa na Mungu mwenyewe. Tunafaa kuvumilia kwa imani tukifahamu kwamba Kristo Yesu ako analijenga kanisa Lake katika umoja. Hii ni kazi Yake.

Changamoto iliyoko

Hapa kuna mafundisho ya Biblia ambayo mara kwa mara yasipozingatiwa vizuri, huenda tukajichanganya. Hatufai pia kusahau kwamba tuko na jukumu la kufanya ili tuendeleze umoja wetu katika Kristo. Mchungaji mmoja alisema, hata kama tunakemea wale ambao wanataka kuendelesha umoja huu wa wakristo, sisi tunafaa kujitoa kuona kwamba umoja unaendelea kuwepo. Ikiwa kanisa la Kristo halitazingatia umoja, tutakuwa tunatenda dhambi dhidi ya Kristo. Mwili wa Kristo upo hapa ulimwenguni na hatufai kupuuza majukumu yetu ya kuendeleza umoja katika mwili huu hapa

Page 34: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

ulimwenguni. Kristo katika ombi lake (Yohana 17), aliombea mwili wake wote kwamba utakuwepo na utaendelea katika umoja. Ikiwa hatutazingatia umoja huu, tutakuwa tunapuuza ombi hili la Kristo na kumkosea heshima.

Tunafaa kuhuzunika sana wakati tunaona migawanyiko katika kanisa la Kristo. Tunafaa tuwe watu wa kutafuta suluhisho kwa yale ambayo ndiyo matatizo ya kanisa la Kristo. Je, tunafaa kufanya nini kuhusu makanisa ambayo yanagawanyika na yale ambayo yanapigana, madhehebu ambayo yanazozana kila wakati? Kwa sababu ya haya yote, ulimwengu unatuchekelea sisi wakristo. Wale ambao wanazozana wanasema kwamba migawanyiko hii ni kwa sababu ya kutoelewana, lakini ukweli ni kwamba ni dhambi ambayo utapata katika mizozo kama hii. Mambo kama kiburi miongoni mwa watumishi na kutaka kutawala kanisa kana kwamba ni afisi ya dunia, ndiyo moja ya mambo ambayo yanaleta migawanyiko hii. Mara kwa mara, utukuta kwamba kuna uzuri ambao unatokana na mizozo hii, lakini huwa mizozo hii inaliumiza kanisa la Kristo sana.

Lazima tuwe na lengo la kuleta amani katika kanisa la Kristo. Lazima tukubali kushuka chini kwa jinsi tunavyofanya mambo, lazima tuwasamehe wakristo wenzetu mara kwa mara. Lazima tukeshe kwa maombi kwa ajili ya kanisa. Tuombe kwamba tutakuwa na uvumilivu na tuamue kwamba hatutatatiza umoja huu na amani katika kanisa la Kristo. Mahali ambapo kuna migawanyiko, tujaribu sana kuleta amani.

Jinsi ya kuendeleza umoja kwa amani.

Je, tunawezaje kufikia umoja huu? Je, tunawezaje kuendeleza umoja huu? Jibu la maswali haya si rahisi kutekeleza. Je, ni nani aliye tuunganisha? Jibu ni Kristo. Je, tunawezaje kuishi katika umoja? Jibu ni, kwa kuja karibu sana kwa Kristo. Jinsi tunavyokua katika ukristo wetu, ndivyo tunavyokuja karibu sana na Kristo na kuimarisha umoja wetu kama ndugu na dada katika Kristo.

Ni lazima tumwombe Mungu ili atuwezeshe kuishi katika umoja. Tunapomkaribia Kristo sana na kumfanya Yeye kuwa msingi wa kila jambo katika maisha yetu, ndipo umoja wetu utakavyoendelea kuimarishwa. Tunavyozidi kukua katika upendo wa Kristo, ndivyo upendo wetu unavyokua juu ya wakristo wengine.

Tuhakikishe kwamba mioyo yetu inamtamani Kristo kila siku kwa sababu hii ndiyo sababu ambayo inaweza kutuwezesha kuishi maisha ya umoja kama wakristo. Wanadamu wameumbwa kuishi katika umoja. Kila mwanadamu anamhitaji mwingine na kwa sababu hii, Mungu alisema, “Si vema huyu mtu awe peke yake” (Mwanzo 2:18). Tumwombe Kristo atufunze jinsi ya kuwapenda wakristo wengine na upendo ukue zaidi na zaidi miongoni mwetu. Biblia inasema, “Tazama jinsi ilivyo vema na kupendeza ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!...Kwa maana huko ndiko Bwana alikoamuru baraka Yake” (Zaburi 133:1,3).

Ushirika wa mateso ya Yesu Kristo

Kuna mateso mengi hapa ulimwenguni. Hii ni kwa wanadamu wote na kwa sababu sasa tumeokoka tusitarajie kuishi maisha bila mateso. Paulo anatukumbusha kwamba, “Imetupasa kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kupitia katika taabu nyingi” (Matendo ya Mitume 14:22). Huwa tunateseka kimwili kutokana na magonjwa au maumivu fulani. Huwa tunateseka kimawazo kutokana na wasiwasi fulani au kutokana na mambo fulani ambayo hutuudhi. Pia huwa tunateseka kutokana na dhuruma za watu fulani fulani. Pia huwa tunapata mateso kutoka kwa wale ambao huwa hawatutakii mazuri hata wakati mwingine kutoka kwa marafiki. Hakuna hata mmoja ambaye ataepuka matatizo. Hivi ndivyo

Page 35: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

maisha yalivyo hapa ulimwenguni.

Je, huwa matatizo tunayawazia aje? Je, huwa tunakasirika na kulalamika? Je, huwa tunapoteza imani yetu ndani ya Mungu na kuwaza kwamba Mungu hakuwa mwaminifu kwetu? Je, tumekasirika Naye kwa sababu ya matatizo ambayo tumepitia? Je, tumeshawahi kujiuliza matatizo mengi ambayo tunakumbana nayo kama wakristo ni kwa sababu hatujitahidi sana kuhubiri Kristo kwa watu wa ulimwengu? Je, tumezingiriwa na mafundisho ya utajiri na afya ambayo yanaagiza kwamba tukiwa na imani kubwa matatizo haya yote yataondolewa? Watu ambao wanaamini mafundisho ya utajiri na afya huwa wanashushwa mioyo wakati vili vitu ambavyo wameagizwa kupata wanakosa kuvipata. Lakini hata kama wanahisi hivyo, wako na hatia ya kutoamini neno la Mungu. Kuna wakati mwanamke mmoja alikuja kwangu akilia machozi kwa sababu mtoto wake msichana alikuwa mgonjwa sana. Aliniambia kwamba kuna mhubiri mmoja ambaye alimwambia kwamba, mtoto wake alikuwa katika hali ambayo alikuwamo kwa sababu mwanamke huyu hakuwa na imani.

Je, sisi huvumilia matatizo ambayo tunapitia tukijua kwamba hii ni sehemu ya maisha yetu hapa ulimwengu? Himizo kwetu ni kwamba hata tukipitia matatizo hapa ulimwenguni, matatizo haya ya hapa ulimwenguni hatuwezi kuyalinganisha na utukufu ambao tutaupata mbinguni (Warumi 8:18). Ni makosa makubwa sana kuwaza juu ya matatizo kama jambo ambalo halifai kuwapata wakristo. Tunaweza kufurahia matatizo ikiwa tutamtazama Kristo pekee katika kila jambo. Je, kumtazama na kumtumainia Kristo hutusaidia aje katika matatizo yetu? Mara ya kwanza inaweza kuonekana kwamba jambo hili linazidisha matatizo na kuyafanya kuwa magumu sana. Kwa sababu tumeunganishwa na Bwana Yesu, je, sasa tunafaa kuwa wanyonge na kuacha kila tatizo litulemee kwa sababu ni lazima tupitie katika matatizo haya? Katika Biblia tunaelezwa kwamba matatizo yetu yameunganishwa kwa kuungana kwetu na Kristo Yesu. Petro anatumihiza “tufurahi kwa kushiriki mateso ya Kristo” (1 Petro:4:13). Paulo anaandika na anasema kwamba, sisi ni warithi pamoja na Kristo naam, tukiteswa pamoja naye tupate pia kutukuzwa pamoja naye (Warumi 8:17) na pia kwamba tunashirika kabisa katika mateso ya Kristo (2 Wakorintho 1:5). Paulo anaendelea na kutueleza kwamba hili ndilo kusudi lake; kushiriki katika mateso ya Kristo: “Nataka nimjue Kristo na uweza wa kufufuka Kwake na ushirika wa mateso Yake, ili nifanane naye katika mauti yake” (Wafilipi 3:10). Kuwa ndani ya Kristo ni kushiriki katika mateso Yake.

Je, kwa nini ikiwa hivi? Je, tukiungana na Kristo Yesu hutuwezesha aje kukumbana na matatizo yetu?

(a) Mateso haya ni ishara kwamba kweli tumeokoka.

Watu wengi huwa wanamtamani Kristo ambaye kwao ni mtu mzuri, mwalimu mwema na mtu ambaye kwao ni mfano wa kufuata tu. Wakati Kristo alipokuwa hapa ulimwenguni, ni wachache ambao walimtamani. Badala yake wengi walimchukia sana na mwishowe walimwua. Ikiwa angerudi hapa ulimwenguni kwa njia ambayo alikuja nayo, bado atachukiwa na wengi na hata atauliwa.

Mungu alisema kwamba uadui utakuwa kati ya kati Kristo na shetani tu, na pia kati watoto wao (Mwanzo 3:15). Uadui huu umekuwepo tangu kitambo. Shetani anamchukia Kristo na wale ambao wamemwamini. Bwana Yesu Kristo alituonya kwamba, “kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni kwamba ulinichukia Mimi kabla yenu...Kumbukeni lile neno nililowaambia, hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake. Kama wamenitesa Mimi, nanyi pia watawatesa, kama wamelishika neno langu, watalishika na neno lenu pia” (Yohana 15:18, 20).

Paulo alinukuu Zaburi akimlilia Mungu; “Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa” (Warumi 8:36). Kama wakristo hatuhitaji kutarajia kuheshimiwa na watu.

Page 36: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Lakini pia haimaanishi kwamba sasa tunafaa kujibu matatizo hayo kwa kupigana vita vya nyama na damu na wale ambao wanatutatiza. Tunafaa kuwa tayari na kujua kwamba ulimwengu hautatukaribisha kwa furaha. Watu wengi ulimwenguni haupendi ujumbe wa injili. Kizazi cha sasa ni kile ambacho kimeelimika sana, lakini hakifahamu neno la Mungu na kinachukia neno hilo. Si rahisi sana kupata watu wengine wakizungumza kuhusu madini mengine vibaya kama jinsi wanavyozungumza juu ya ukristo. Kuna uadui mkubwa sana dhidi ya wakristo ulimwenguni zaidi ya dini nyingine yoyote.

Paulo alizungumza kuhusu wakristo wote akisema, “tunaposingiziwa, tunajibu kwa upole. Mpaka sasa tumekuwa kama takataka ya dunia na uchafu wa ulimwengu hadi leo” (1 Wakorintho 4:13). Hivi ndivyo ulimwengu unavyotuona. Lazima tutarajie kuchukiwa, upinzani, mateso na hata kuuliwa. Lakini hatufai kushushwa moyo na haya mambo yote. Haya yote ni dhihirisho kwamba tumeokoka na tuko katika Kristo.

Ikiwa tunapendwa na ulimwengu sana, basi lazima tujiulize kama kweli imani yetu ni ya kweli. Kristo alisema, “Ole wenu watu watakapowasifu” (Luka 6:26). Sifa hizi ni ishara kwamba hatujadhihirishia ulimwengu kwamba sisi wa Kristo. Kwa yule ambaye ameokoka, sifa za ulimwengu ni aibu na ni za kumchukiza sana. Hii ndiyo sababu tunafaa kufurahia wakati wa matatizo kwa sababu hii ni hakikisho kwetu kwamba kweli sisi ni wa Kristo na kwamba tuko naye nje ya kambi (Waebrania 13:13).

Kuteseka kwa ajili ya Mwokozi wetu ni ishara kwamba sisi tuko katika kundi Lake na hili ndilo kundi ambalo Yesu alilihimiza kwamba “Furahini kwa kushangilia kwa maana thawabu yenu ni kuu” (Mathayo 5:12). Ni ishara kwamba tumeondolewa katika Adamu. Bwana Yesu Kristo alisema kwamba, “kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeliwapenda kama unavyowapenda walio wake. Kwa sababu ninyi si wa ulimwengu, lakini Mimi nimewachagua kutoka katika ulimwengu, ndiyo sababu ulimwengu unawachukia” (Yohana 15:19). Mateso ni ishara kwamba shetani ambaye ndiye anatutatiza anafahamu hali yetu ya kiroho kwamba sisi ni wakristo.

Kuteseka kwa njia hii ni ishara kwamba tutaurithi utukufu ujao ambao Petro alielezea wasomaji wake: “Furahini kuwa mnashiriki katika mateso ya Kristo, ili kwamba mpate kufurahi zaidi na kushangilia wakati utukufu wake utakapofunuliwa” (1 Petro 4:13). Paulo naye anasema, “Basi ikiwa sisi ni watoto, basi tu warithi, warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo, naam, tukiteswa pamoja Naye tupate pia kutukuzwa pamoja Naye” (Warumi 8:17).

Wakati Paulo anazungumza kuhusu mateso, anafahamu vyema yeye mwenyewe kuteseka inamaanisha nini. Paulo alisema haya kutokana na yale ambayo alipitia. Alisema, “Nimefanya kazi kwa bidii kuliko wao, nimefungwa gerezani mara kwa mara, nimechapwa mijeredi sana, nimekabiliwa na mauti mara nyingi. Mara tano nimechapwa viboko arobaini kasoro kimoja na Wayahudi. Mara tatu nalichapwa kwa fimbo, mara moja nilipigwa kwa mawe, mara tatu nimevunjikiwa na meli, nimekaa kilindini usiku kucha na mchana kutwa. Katika safari za mara kwa mara, hatari za kwenye mito, hatari za wanyang'anyi, hatari kutoka kwa watu wangu wenyewe, hatari kutoka kwa watu mataifa, hatari mijini, hatari nyikani, hatari baharini, hatari kutoka kwa ndungu wa uongo. Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, katika kukesha mara nyingi, ninajua kukaa njaa na kuona kiu, nimekaa mara nyingi bila chakula, nimesikia baridi na kuwa uchi” (2 Wakorintho 11:23-27).

Mwisho wa barua ya Paulo kwa Wagalatia, Paulo aliandika, “Tangu sasa mtu ye yote asinitaabishe, kwa maana nachukua katika mwili wangu chapa Zake Yesu” (Wagalatia 6:17). Katika makanisa ya Wagalatia kulikuwa na mjadala juu ya kutahiriwa. Walimu wa uongo walikuwa wameingia ndani na walikuwa wanamshituma Paulo kwa sababu alisema kwamba mtu hahitaji kutahiriwa ili aokoke.

Page 37: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Katika mstari huu wa Wagalatia 6:17, Paulo anawaelezea wale Wayahudi ambao walikuwa wanasisitiza kutahiriwa kwamba, “ninyi mnazungumza kuhusu kutahiriwa kama alama ya ukristo wa kweli, mimi nimepitia mambo magumu sana kwa sababu ya injili. Alama ambazo niko nazo ni ishara tosha ya uaminifu wangu kwa Bwana wangu Yesu Kristo.”

Mateso ambayo tunapatana nayo kwa ajili ya Bwana wetu ni alama za heshima kwamba sisi tumeungana na Yeye ambaye alidharauliwa na kukataliwa na wanadamu. Ni dhihirisho kwamba tuko katika Kristo.

Jinsi tumeunganishwa kwa Kristo Yesu

Bwana Yesu Kristo siyo Mwokozi pekee bali pia ni Yeye ambaye anatuongoza katika maisha yetu ya wokovu. Yesu Kristo alikuja hapa ulimwenguni na kufa ili atuokoke, na pia ili atuongoza katika maisha yetu ya wokovu. Alikuja hapa ulimwenguni, akafa juu ya msalaba, akazikwa, akafufuka na akarudi mbinguni katika utukufu. Hivi ndivyo wokovu wetu ulivyo. Tukiwa tumeunganishwa Kwake, tunakufa Naye, kufufuka Naye na tunaisha katika Yeye kiroho. Ili tuweze kuokoka, lazima tufahamu dhambi zetu na tutubu. Huwa tunanyenyekezwa zaidi na kuongozwa kutubu dhambi zetu. Hadi wakati tunapookoka ndipo tunapata tumaini na nguvu za kufufuka katika furaha na utukufu wa milele.

Wakati tumeokoka, kazi ya utakaso huanza ndani mwetu. Biblia inasema, “Jihesabuni wafu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu” (Warumi 6:11). Huwa tunatekeleza jambo hili kwa kuanza kuacha na kuanza kupigana na zile dhambi ambazo bado ziko ndani mwetu na kugeuka na kuanza kuishi maisha matakatifu. Mungu huwa anatutakasa kwa kutupitisha katika mateso mengi. Bwana Yesu Kristo alikuwa mtakatifu kamili lakini tunaelezwa kwamba, “Ingawa alikuwa Mwana, alijifunza utii kutokana na mateso aliyoyapata” (Waebrania 5:8). Maana ya hii si kwamba alihitajika kuwa mtiifu kwa sababu kulikuwa na wakati ambapo hakutii. Bali inamaanisha kwamba, kupitia yale mateso ambayo alipatana nayo hapa ulimwenguni, alifahamu kumtii Mungu inamaanisha nini. Hatuwezi kujifunza kutii kwa kusoma tu, bali lazima tutende.

Wakati tunapomwomba Mungu atufanye kuwa kama Kristo mwenyewe, lazima tufanye ombi hili kwa unyenyekevu sana. Kwa mfano, tukimwomba Mungu kwamba atusaidie tuwe na moyo wa kuwasamehe wengine, je, Mungu atajibu maombi hayo kwa njia gani? Je, atayajibu kwa kutuletea watu karibu nasi ambao ni wazuri na hawatukosei? Haiwezekani hivi, njia tu moja ambayo tunaweza kuwasamehe wengine ni kuwa na uwezo wa kusaheme. Mungu ataruhusu watu watukosee na wengine watushitumu. Ni wakati huu ambapo tutaweza kujifunza kuwasamehe watu kwa mioyo yetu yote. Wakati huu tutaweza kuomba Mungu na ataweza kujibu.

Huwa tunanyenyekezwa wakati wengine wanatudharau na hawajali yale ambayo tunafanya. Huwa tunajifunza uvumilivu kwa kuwa watu wenye subira kila wakati. Mungu hutuwezesha kuwa watu ambao wanawapenda wengine sana kwa kutuletea watu ambao ni wagumu kupendwa na mwanadamu. Imani yetu huwa inakua wakati tunapitia mambo kama haya magumu sana.

Mchungaji mmoja ambaye aliitwa John Calvin alisema, Yeyote ambaye Mungu amemfanya mwana wake, lazima mtu huyu ajiandae kupitia mambo magumu sana. Maisha haya yatajumlisha mateso na taabu nyingi kutoka kwa shetani na watu wake. Jinsi tu alivyoruhusu mateso katika maisha ya Yesu Kristo Mwanawe, vivyo hivyo, atayaruhusu katika maisha ya ndugu na dada Zake.

Page 38: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Hivi ndivyo tulivyo katika Kristo Yesu. Hivi ndivyo anavyotubariki na kujibu maombi yetu. Anayajibu haya yote kwa kutufanya tuwe kama Kristo mwenyewe. Tunaweza kua katika Kristo ikiwa tutakubali kupitia yale ambayo alipitia. Kwa sababu hii, Paulo aliwaandikia Wafilipi akisema, “Nataka nimjue Kristo na uweza wa kufufuka Kwake na ushirika wa mateso Yake, ili nifanane naye katika mauti Yake” (Wafilipi 3:10). Paulo hapa anatueleza kwamba tunapoendelea kuishi maisha haya mapya katika Kristo, anatueleza kwamba lazima tuwe tayari kushiriki katika mateso Yake ili mwishowe tuweze kupata kufufuka kutoka kwa wafu (Wafilipi 3:11). Huu ndio ukweli, lazima tufe Naye ikiwa tutafufuka Naye. Mafundisho mengi siku hizi kuhusu maisha ya ukristo ambayo yanafundishwa ni ya uongo. Mafundisho haya yanawahimiza watu kwamba maisha ya ukristo ni maisha ambayo hayana matatizo wala kusumbuka kokote. Lakini Biblia inafundisha kwamba ni kwa kupitia kwa mateso na matatizo, tunageuzwa na kuwa kama Kristo mwenyewe.

Ikiwa wewe ni mkristo, lazima utapata mateso kama Kristo. Kristo aliteseka kwa sababu ya kuishi maisha matakatifu na kuhubiri ujumbe wa injili. Vivyo hata sisi ambao tumeokoka tutateswa. Kama vile Kristo alikufa, sisi tumekufa kwa dhambi. Kama vile Kristo alifufuka, sisi pia tumefufuka ili tuishi maisha mapya katika Yeye. Kwa sababu Kristo ako katika utukufu tutakuwa Naye katika utukufu.

Tunahitajika kumhudumia Kristo

Kristo Yesu hakukataa kuteswa wakati alikuwa hapa ulimwenguni. Si hali kwamba mateso yalikuwa jambo ambalo hakulitarajia. Mateso yalikuwa moja ya mambo ambayo alifahamu kwamba alikuwa ayapitie. Hili ndilo lilikuwa kusudi lake alipokuwa anajinyenyekeza akiwa mtiifu hadi kwa mauti msalabani (Wafilipi 2:8).

Ni kupitia kwa mateso ndipo aliweze kutuletea msamaha wa dhambi zetu na kutununulia uzima wa milele. Akiwa uzao wa mwanamke, alikuwa amshinde shetani. Aliweza kumshinda kwa kumponda kichwa chake na pia naye kisigino chake kiliumia wakati huo (Mwanzo 3:15). Kalvari alishinda na alimaliza kazi ambayo Mungu Baba alikuwa amemtuma afanye. Msalaba ndiyo ulikuwa kilele cha mateso Yake yote. Ilionekana kwamba alikuwa ameshindwa. Lakini ilikuwa iwe hivyo ndipo apate kushinda. Mateso hayakuwa huduma wake, bali mateso Yake Kristo Yesu ndiyo yalikuwa msingi wa kazi yake hapa ulimwenguni na ushindi Wake.

Kanisa la Kristo linafaa kuendeleza kazi ya Kristo Yesu hapa ulimwenguni na tuifanye jinsi alivyoifanya, hata kama tutapata mateso mengi sana. Uchungu wa mateso haya unaanzia mioyoni mwetu wakati Roho Mtakatifu anapotusaidia kupigana na dhambi zetu ambazo bado ziko ndani mwetu na kuubeba msalaba wetu kila siku. Jambo hili si rahisi hata kidogo. Ni rahisi sana kwetu kuanguka katika majaribu ya shetani kuliko kujitahidi katika ukristo wetu. Lazima tujitahidi katika kila hali kugana vita hivi. Vita hivi ni vya maisha yetu yote hakuna siku ambapo tutapumzika. Lazima tupigane na dhambi ambayo bado iko ndani mwetu. Katika vita hivi kuna kuteseka ambako kunatoka mioyoni mwetu kwa sababu ya yale ambayo tunapitia wakati wa vita hivi. Hivi ndivyo kila mkristo anafaa kujitolea kabisa ili apigane na dhambi hii kwa ajili ya Kristo.

Wakati tunamtumikia Kristo, huwa tunakumbana na mateso makubwa. Kazi ya kanisa mara kwa mara ni ngumu sana na inambidi mtu ajitolea kabisa. Tunaweza kujitolea kabisa kwa sababu ya kazi ya kanisa kama kuhubiri neno la Mungu, lakini wakati mwingine inaweza kuwa tupate kwamba hakuna matunda mwngi. Kwa sababu ya hii huwa tunashushwa mioyo kabisa na pia tunachoka na hata wakati mwingine kuwaza kwamba tuache kazi hii kabisa. Lakini hatufai kuacha kazi hii kwa sababu si kazi ambayo tunafanya kwa hiari yetu. Ni kazi ambayo tunafanya kwa upendo na hivi ndivyo

Page 39: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

tunavyomtumikia Bwana wetu Yesu Kristo. Kuwahubiria wale ambao hawajaokoka kuna wakati linakuwa jambo ambalo linashusha moyo na hata wakati mwingine ni jambo la kuogofya sana. Kuwajali watu na kuhakikisha kwamba tunawasaidia kiroho, ni kazi ngumu sana na hata wakati mwingine ni jambo la kuvunja mioyo. Kuna wakati ambapo tunaweza kusema kwamba, 'nimechoka sitaendelea sasa.' Lakini huwa tunaendela hata baada ya kuwaza hivi. Kusimama imara kwa ajili ya Kristo, itawafanya watu wa ulimwengu watuchukie sana kwa sababu hawaipendi injili ya Kristo. Lakini hata hivyo hatufai kurudi nyuma au kuangalia nyuma au kufa moyo, bali tunafaa kuendelea kuwa waaminifu kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Hakuna njia rahisi ya kumtumikia Kristo. Lazima tuhesabu gharama. Kuwa mwanafunzi Wake Kristo ni kuubeba msalaba wake na hili ndilo jambo ambalo siku hizi halizungumziwi kamwe. Kuna wengi ambao wanakiri kwamba wao ni wakristo, lakini wao ni waongo sana na hawajitolei kabisa katika kazi ya Mungu. Wanaonekana kuwa wamejawa na upendo wa “anasa kuliko kumpenda Mungu. Wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje lakini wakizikana nguvu za Mungu” (2 Timotheo 3:4-5).

Kristo anapomwita mtu amfuate, huwa anamwita aje afe na akiwa hatachukua msalaba wake na kumfuata, basi hastahili kuitwa wa Kristo (Mathayo 1:38). Paulo alifahamu jambo hili na ndiyo sababu huduma na mateso yake aliyazungumzia akasema kwamba, “Sasa nafurahia kule kuteseka kwangu kwa ajili yenu na katika mwili wangu ninatimiliza yale yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, ambao ni kanisa” (Wakolosai 1:24). Wakristo hupatana na mateso makubwa sana wanapomhudumia Mungu.

Njia ambayo tunashiriki na Kristo

Ushirika na Kristo si jambo ambalo limepangwa na serikali. Hili ni jambo ambalo linafanyika kwa sababu tumeunganishwa kwa Kristo mwenyewe. Jambo hili hufanyika kupitia kwa kumwabudu Kristo, kumtii, kupitia kwa kujichunguza na zaidi kupitia kwa mateso. Paulo anazungumza juu ya jambo hili wakati anasema kwamba anashiriki katika mateso Yake (Wafilipi 3:10). Kwa ufupi anasema kwamba anajua kushiriki mateso mateso ya Kristo.

Kuna ushirika katika mateso. Wale wote ambao wamepitia mateso haya, wako na jambo la kuwaunganisha pamoja. Unapokutana na watu ambao wamepitia mateso sawa, wanaweza kuwa watu ambao hawajuani, lakini wanapoanza kuzungumza haitawachukua muda mwingi kabla ya kufahamiana na kuwa marafiki. Mateso yao huwaleta karibu sana na mwingine.

Kwa njia hiyo hiyo, mateso yetu hutuleta karibu sana na Kristo Yesu na huwa yanatusaidia kumfahamu vyema zaidi. Huwa mateso yanatufanya tukumbuke huduma wake wakati alipokuwa hapa ulimwenguni. Katika Zaburi 69:4,8,20, Yesu anasema kwamba, “Wale wanaonichukia bila sababu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu, wengi ni adui bila sababu, wale wanaotafuta kuniangamiza. Ninalazimishwa kurudisha kitu ambacho sikuiba. Nimekuwa mgeni kwa kaka zangu, mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe. Dharau zimenivunja moyo na nimekata tamaa, nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata yeyote, wa kunituliza, lakini sikumpata ye yote.” Labda huenda unaweza kusema maneno kama haya. Labda wewe ndiye mkristo wa pekee katika jamii yako na katika nyumba yenu wengi hawakuelewi na wameamua kukaa mbali sana nawe. Jambo hili huenda linakuacha ukiwa huna mtu wa kutegemea wala kukusikiza wala wa kucheka naye.

Kumbuka yale masaa wakati Kristo aliomba, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke” (Mathayo 26:39). Labda kuna wakati hata wewe uliomba ombi hili kwa moyo wako wote na kwa nafsi yake yote wakati ulikuwa umekumbwa na mateso. Katika Biblia tunasoma kwamba

Page 40: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Kristo aliomba kwa machozi sana kwa Yule ambaye alikuwa na uwezo wa kumwokoa kutoka kwa kifo (Waebrania 5:7). Unaweza kumbuka hata wakati wewe mwenyewe umelia sana na kwa sababu hii umemkaribia sana Kristo na kuelewa kabisa mwito wako wa kuwa mkristo.

Mateso haya huwa yanatufanya tumkaribie sana Mwokozi. Wakati wa mateso, sisi hujihisi sana kwamba tuko karibu na Mwokozi na tunahisi nguvu zake ambazo zinatuongoza maishani mwetu. Sasa tunaweza kufahamu kwa nini Paulo alisema, “Nataka nimjue na uweza wa kufufuka Kwake na ushirika wa mateso Yake” (Wafilipi 3:10).

Huwa matatizo yetu hayatuletei tu fahamu ya kumwelewa Mwokozi wetu vyema, lakini pia hutuonyesha jinsi Mwokozi wetu anavyotujali sana. Kristo huwa karibu nasi kila wakati. Huruma wake huwa unawafikia watu wake wote. Paulo alifahamu jambo hili wakati alipokutana na Kristo alipokuwa anaenda Damasku wakati Bwana Yesu alimwambia, “Sauli, Sauli mbona unanitesa?” (Matendo ya Mitume 9:4). Je, Sauli alikuwa anamtesa Kristo? Ukweli ni kwamba alikuwa anawaua watu ambao walikuwa wameokoka. Lakini kwa kuuliza swali hili, Bwana Yesu Kristo alikuwa anajitambulisha na watu Wake. Bwana Yesu Kristo anamaanisha hapa kwamba unapogusa watu Wake unamgusa Yeye mwenyewe. Unapowaumiza watu Wake, unamwumiza Yeye mwenyewe. Mateso yetu katika ukristo wetu ni mateso katika Kristo: “Ni Mimi Yesu unayenitesa” (Matendo ya Mitume 26:15).

Ushirika huu umetabiriwa katika karme zote. Wakati Isaya aliandika kumhusu Mwokozi alisema “Katika taabu zao zote naye alitaabika” (Isaya 63:9). Bwana Yesu Kristo akizungumza kuhusu yale ambayo yatatendeka siku ya mwisho, alisema “Amini, amini ninawaambia, kwa jinsi mlimvyotendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea Mimi” (Mathayo 25:40). Huu ndiyo ushiriki kati ya Kristo na watu Wake. Tunahitaji kufahamu jambo hili. Mara nyingi sisi hujiuliza swali hili, Je, Kristo anawapenda watu wake wote sawa? Bwana Yesu Kristo hawapendelei wakristo wengine zaidi kuliko wengine. Huwa anatupenda sisi sote sawa bila kutubagua. Kuna wakati ambapo upendo huu wa Kristo kwa watu wake unadhihirika kwa njia tofauti tofauti.

Kwa mfano, katika jamii ambapo kuna watoto wanne, wazazi wa watoto hawa wanawapenda wote sawa. Huwa hawawabagui hata kidogo. Lakini kwa wakati moja, mmoja wa watoto anagonjeka. Wakati huu wazazi watashughulikia sana yule ambaye ni mgonjwa. Hii haimaanisha kwamba hawawapendi wale watoto wengine. Lakini hata wakati wanafanya hivi, wale watoto wengine huwa hawakasiriki nao kwa sababu ya kumshughulikia yule mmoja sana.

Hivi ndivyo tunafaa kuwaza juu ya Kristo Yesu. Kitabu cha Waebrania kina tuhakikishia upendo wa Kristo wa kipekee kwa watu wake wakati wako na mahitaji: “Kwa kuwa hatuna Kuhani Mkuu anaweza kuchukuliana na sisi katika udhaifu wetu...Kwa kuwa Yeye mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wale wanaojaribiwa” (Waebrania 4:15; 2:18).

Ulimwenguni kuna wakristo ambao wanateseka sana. Wengi hawana watu wa kuzungumza nao, wengi wamevunjwa mioyo, wengi wako katika uchungu, wengi wanateswa na kuuliwa na wengi wamefungwa, wakati haya yote yanatendeka, moyo wa Kristo huwa unahuzunika na kuwa na huruma juu ya watu wake na kutoka kwake tunapata kijito ambacho kinatiririka na upendo na neema.

Ikiwa wewe ni mkristo, umehakikishiwa upendo wa Kristo. Dumu katika ukweli ukifahamu kwamba Kristo anafahamu uchungu wako na anakuhurumia. Ukiwa na imani katika mateso yako, mateso hayo yatakuleta karibu sana katika ushirika na Kristo. Kwa hivyo kwa ujasiri, tukaribie kiti cha neema ili tuweze kupokea huruma na neema wakati wa mahitaji (Waebrania 4:16).

Page 41: WordPress.com · Web viewKwa kufanya hivi, “Hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume au mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu” (Wagalatia

Ushirika na Kristo ni jambo la uhusiano wa karibu sana Naye kwamba hata wakati wa kufa bado Yeye huendelea kutupenda zaidi. Baada ya maisha hapa ulimwenguni, tunakufa katika Kristo (1 Wathesalonike 4:16). Huwa tunakufa katika Bwana (Warumi 14:8) na kwa Bwana (Ufunuo 14:13). Nafsi za wale ambao wameokoka huwa zinakamilishwa katika utakatifu wakati wa kifo hata kama miili yao inazikwa. Huwa wana tumaini la kufufuka katika utukufu. Je, faraja ya mkristo wakati anakufa ni gani? Faraja yake ni kwamba yeye ni wa Kristo milele na milele.

Tunaunganishwa kwa Kristo kwa sababu ya upendo wake juu yetu. Wakati tumeunganishwa kwa Kristo, huwa tumehakikishiwa ulinzi na furaha ya milele. Sisi tuko katika Kristo na Kristo ako ndani mwetu.

Je, ni nini ambayo imetuongoja mbeleni? Mbinguni ndiyo inatungoja na hili ndilo jambo moja tuko nalo kama hakikisho kwamba Bwana Yesu Kristo hatawahi kuwaacha wale ambao wameunganishwa Kwake.

“Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika kuwa wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yalio chini, wala kiumbe kingine cho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 8:38-39).