· web viewtutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na...

23
1 HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, MHESHIMIWA DK. ALI MOHAMED SHEIN, KATIKA UZINDUZI WA UIMARISHAJI WA MFUMO WA WAKALA WA USAJILI WA MATUKIO YA KIJAMII NA OFISI MPYA ZA WILAYA, TAREHE 4 SEPTEMBA, 2018 Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi ; Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid ; Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Haji Omar Kheir ; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Waheshimiwa Mawaziri na Manaibu Waziri mliopo katika hafla hii, Mheshimiwa Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee ; Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Hassan Khatibu Hassan ; Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara mliopo katika hafla hii, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama,

Upload: others

Post on 28-Feb-2020

1 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

1

HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, MHESHIMIWA DK. ALI

MOHAMED SHEIN, KATIKA UZINDUZI WA UIMARISHAJI WA MFUMO WA WAKALA WA USAJILI WA

MATUKIO YA KIJAMII NA OFISI MPYA ZA WILAYA, TAREHE 4 SEPTEMBA, 2018

Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi ; Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,

Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid ; Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,

Mheshimiwa Haji Omar Kheir ; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,

Waheshimiwa Mawaziri na Manaibu Waziri mliopo katika hafla hii,

Mheshimiwa Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee ; Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,

Mheshimiwa Hassan Khatibu Hassan ; Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja,

Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara mliopo katika hafla hii,

Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama,

Wenyeviti wa Bodi za Taasisi mbali mbali,

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar,

Page 2:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

2

Viongozi mbali mbali wa Serikali na Vyama vya Siasa,

Ndugu Waandishi wa Habari,

Ndugu Wananchi,

Mabibi na Mabwana.

Assalam Aleikum.

Naanza kwa jina la Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Mwenye kumiliki uhai na uzima wetu, kwa kutuwezesha kukutana hapa kwa ajli ya Uzinduzi wa Uimarishaji wa Mfumo wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii pamoja na Ofisi mpya ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar ya Wilaya ya Kati iliyojengwa hapa Dunga.

Natoa shukurani zangu za dhati kwako Mheshimiwa Haji Omar Kheri Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kunialika kuwa mgeni rasmi katika shughuli hii muhimu kwa maendeleo yetu. Shukurani zangu maalum nazitoa kwenu wageni waalikwa na wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika hafla hii.

Page 3:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

3

Ndugu Wananchi, Nakupongezeni kwa juhudi mlizozifanya hadi mkaweza kufungua Ofisi katika Wilaya zote kumi na moja za Unguja na Pemba. Nakuhimizeni muyatunze vizuri majengo ya ofisi hizo pamoja na vifaa vyote, ili yaendelee kudumu. Tuzingatie hekima ya ule msemo wetu wa Kiswahili usemao ‘Kitunze Kidumu’. Ni dhahiri kwamba ofisi hii isipotunzwa, uzuri huu unaoonekana leo hautoweza kudumu.

Juhudi zenu hizi za kujenga majengo mapya na kuweka vifaa na mifumo mipya, zinathibisha kwamba mmefahamu vyema na mnathamini umuhimu wa Ofisi hii kwa maendeleo yetu. Taasisi hii ina historia kubwa inayolingana na umuhimu wake; nami mara nyingi nnapopata fursa ya kuwa Mgeni Rasmi katika shughuli zetu za maendeleo, hupenda sana kutanguliza historia yenye mnasaba na shughuli yenyewe. Nimekuwa nikifanya hivi kwa sababu nataka tujikumbushe wapi tulipotoka, tumefikaje hapa tulipo na jitihada zetu za maendeleo zinalenga tuelekee wapi.

Ndugu Wananchi,

Page 4:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

4

Historia ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar imeanza miaka mingi iliyopita, hadi tukafika hapa tulipo. Wengi tunaifahamu Ofisi ya Mrajis wa Vizazi na Vifo ambayo ilitokana

na Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu au ‘Administrator General Office’ iliyoundwa mwaka 1911. Makao Makuu ya Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu yalikuwa katika jengo maarufu la “Mambo Msiige” lililokuwepo katika Mtaa wa Shangani maarufu kwa jina la “Kelele Square” mjini Unguja. Leo si siku ya kuelezea maana ya Mambo Msiige na Kelele Square, bali ni kuyaelezea yaliyokuwa yakifanyika kwenye nyumba hio katika mtaa huo. Kiongozi wa Ofisi hiyo alijulikana kama ‘Administrator General’ na Msaidizi wake Mkuu aliitwa ‘Administrator General Agent’ aliyekuwa na ofisi yake huko Pemba. Kwa wakati huo, ‘Administrator General’ alikuwa akiongoza Idara sita (6) ikiwemo Ofisi ya Pemba. Katika kila idara kulikuwa na Msaidizi wake mmoja wakifuatiwa na wafanyakazi wengine wa chini yao. Majukumu Makuu ya Ofisi hii yalikuwa ni kusimamia masuala ya urithi na wakfu kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu pamoja na kufanya usajili wa mambo mbalimbali, yakiwemo matukio ya Vizazi, Vifo, Ndoa, Talaka na Usajili wa Mtoto wa Kulea (Child Adoption).

Page 5:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

5

Mbali na majukumu hayo, Ofisi hii vile vile, ilikuwa ikifanya Usajili wa biashara, makampuni na nyaraka mbalimbali kama za nyumba, vikataa na mashamba. Hapa tunaona jinsi Ofisi hii ilivyokuwa na shughuli za mchanganyiko wa mambo mengi.

Ndugu Wananchi, Baada ya Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964, Ofisi ya ‘Administrator General’ iliunganishwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, na ‘Administrator General’ akajulikana kwa kwa jina la ‘Registrar General’ au Mrajis Mkuu wa Serikali. Viongozi waliowahi kuiongoza Ofisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali baada ya Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964 Zanzibar ni pamoja na Bwana Sherali Champsi, Bwana Khalil Hassan Mirza, Bw. Ussi Khamis Haji, Bwana Rajab Baraka Juma na Bwana Abdulla Wazir Ramadhan. Baada ya mabadiliko hayo makubwa yaliyopelekea kuunganishwa Ofisi hizo mbili, Mwanasheria Mkuu akawa ndiye mwenye dhamana ya Ofisi zote mbili yaani; Ofisi ya Mrajisi Mkuu na ya Mwanasheria Mkuu. Miongoni mwa sababu za kuziunganisha ofisi hizo, ilikuwa ni tatizo la

Page 6:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

6

ukosefu wa wataalamu wa kutosha katika fani ya sheria, hasa baada ya wataalamu wengi wa fani ya Sheria waliokuwa wakiendesha Afisi ya ‘Administrator General’ kuondoka nchini baada ya Mapinduzi. Katika mwaka 1980, kwa sheria nambari 5 ya mwaka 1980, kiliundwa chombo maalumu cha kuyashughulikia masuala ya Wakfu na Mali ya Amana kwa Waislamu. Chombo hicho kiliundwa, ili kupunguza majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria na Mrajis Mkuu wa Serikali; na kiliitwa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana. Katika mwaka 1985, Ofisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali iliwekwa kama chombo na Ofisi iliyojitegemea peke yake na iliendelea kuyashughulikia masuala ya usajili wa vizazi, vifo, ndoa, talaka na mengineyo, isipokuwa yale ya Wakfu na Mali ya Amana; ambayo yalikuwa yakishughulikiwa na Kamisheni kama nilivyokwishaeleza.

Ndugu Wananchi, Mnamo mwaka 2006, Baraza la Wawakilishi la Zanzibar lilifuta sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo, Sura ya 90, iliyokuwa ikitumika zamani kabla ya Mapinduzi ya 1964, na kutunga sheria mpya nambari 10 ya mwaka 2006 ambayo pamoja na mambo mengine, iliainisha cheo maalum cha Mrajis wa Vizazi na Vifo ambaye Ofisi yake

Page 7:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

7

ndiyo iliyopewa jukumu la kuyashughulikia masuala hayo. Kwa hivyo, katika kuitekeleza sheria hiyo, nami nilipoingia madarakani, niliona haja ya kufanya mabadiliko kidogo. Kwa hivyo, mwaka 2012, nilifanya uteuzi wa Mrajis na Naibu Mrajis wa Vizazi na Vifo. Uteuzi huu ulikwenda sambamba na kuundwa kwa Ofisi ya Mrajis wa Vizazi na Vifo ambayo ilikabidhiwa majukumu yake ya Usajili wa Vizazi na Vifo peke yake. Mtakumbuka kuwa Ofisi ya Mrajis wa Vizazi na Vifo hapo awali ilipoanzishwa ilikuwa chini ya Wizara inayoshughulikia Mambo ya Sheria, lakini katika mwaka 2016, Ofisi hii tuliihamishia katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ. Katika mabadiliko hayo, Ofisi hii iliunganishwa na Ofisi ya Usajili wa Kadi za Utambulisho.

Vile vile, nataka nielezee historia fupi ya vitambulisho vya Mzanzibari, (ZAN ID) hasa kwa wale ambao hawalijui chimbuko lake. Katika mwaka 1966, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliona ipo haja ya kuweka utaratibu wa wananchi kuwa na vitambulisho vya Uraia na Ukaazi kwa dhamira njema kabisa ya kuwafikia kwa urahisi wananchi wake kwa ajili ya kupata huduma mbali mbali zilizostahiki. Kwa hivyo wananchi waliokamilisha masharti yaliyohitajika kwa wakati ule iliwalazimu kupatiwa

Page 8:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

8

vitambulisho hivyo. Kwa mantiki hiyo, katika mwaka huo huo wa 1966 ilitungwa Sheria namba 11 ya mwaka 1966 ambayo ilijulikana kwa jina la “Sheria ya Uraia na Ukaazi”. Sheria hii iliwekwa kwa lengo la kutekeleza haja ya kuwepo na kutumika vitambulisho vya Mzanzibari ambavyo kwa wakati huo vikijulikana kama ‘Kadi za Uraia’. Kutokana na muda tulionao, historia hii ya ‘Kadi za Uraia’ itaishia hapa kwa leo; ila ni muhimu kuelewa kwamba utaratibu huu wa kutoa vitambulisho, si mpya kama wengi wanavyodhania. Idara ya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari ilianzishwa rasmi kwa Sheria nambari 7 ya 2005, na chini ya sheria hiyo wananchi wanaendelea kupatiwa vitambulisho hivyo hadi sasa.

Ndugu Wananchi, Baada ya Mapinduzi ya 1964, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika awamu mbali mbali imekuwa ikifanya mageuzi ya mfumo wa Ofisi hii, ili kuimarisha utendaji na utoaji huduma kutokana na umuhimu wake kwa ustawi na maendeleo ya jamii. Kwa dhamira hii, Serikali iliifuta Ofisi ya Mrajis Mkuu wa Serikali mwaka 2013 na kuanzisha Ofisi nyengine mpya ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali (Business and Property Registration Agency - BPRA), na baada ya muda mfupi tu tangu kuanzishwa kwake, Serikali

Page 9:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

9

iliiongezea majukumu mengine zaidi ya kusajili ndoa na talaka. Katika kuziendeleza jitihada za Serikali za kuziundia shughuli za kijamii Taasisi zake maalum na kuimarisha mifumo ya utendaji kazi ya Taasisi hizo, mwanzoni mwa mwaka 2018, Sheria nambari 3 ya mwaka 2018 ilitungwa, ambayo ilianzisha rasmi kwa Ofisi ya Usajili wa Matukio ya Kijamii.

Ofisi hiyo ya Wakala ndiyo yenye majukumu makuu ya kusimamia shughuli za kijamii zilizokuwa zikifanywa na Ofisi ya Mrajis wa Vizazi na Vifo na Ofisi ya Usajili wa Kadi za Vitambulisho. Sambamba na uanzishwaji wa ofisi hii, mnamo mwezi Machi 2018, niliwateua Viongozi Wakuu wa Taasisi hii ambao ni Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Hussein Khamis Shaaban, pamoja na Manaibu Wakurugenzi Watendaji wawili ambao ni Ndugu Idrissa Shaaban Zahran anayeshughulikia Usajili wa Wazanzibari Wakaazi na Wageni na Ndugu Shaaban Ramadhan Abdalla anayeshughulikia usajili wa vizazi, vifo, ndoa na talaka. Viongozi hawa niliowateua wana elimu na uwezo wa kutosha na hapana shaka kwa kushirikiana na watendaji wote wa Ofisi hii watayatekeleza kwa ufanisi mkubwa majukumu tuliyowakabidhi.

Page 10:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

10

Ndugu Wananchi,Kama nilivyotangulia kusema kwamba tumekuwa tukiunda Taasisi mbali mbali na kufanya mabadiliko katika Taasisi hizo kila baada ya muda kutokana na kuongezeka kwa mahitaji yetu, lakini nataka muelewe kwamba kuongezeka kwa mahitaji ni miongoni mwa ishara ya kuongezeka kwa maendeleo yetu. Kwa hivyo, ili tuweze kuwa na maendeleo ya haraka zaidi na kwa kasi kubwa ni lazima tushirikiane katika kutimiza wajibu wetu. Natumia fursa hii kukuhimizeni na kukutakeni mzifanye kazi zenu kwa kuzingatia misingi ya utawala bora, sheria na kanuni zinazoongoza Taasisi yenu, mfanye kazi zenu bila ya upendeleo wowote na bila ya woga. Endeleeni kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na kutumia misingi ya haki.

Upatikanaji wa takwimu zilizosahihi ni muhimu sana katika maendeleo yetu na kwa hivyo, usajili mzuri wa takwimu za ndoa na talaka utaweza kuturahisishia uandaaji wa mikakati imara ya kukabaliana na changamoto hii. Aidha, utasaidia katika juhudi zetu za pamoja za kuimarisha haki za watoto na kina mama zinapovunjika ndoa, jambo ambalo linachangia kuongezeka kwa kesi na matukio ya udhalilishaji katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.

Page 11:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

11

Serikali inahitaji takwimu na usajili uliosahihi kutoka katika Taasisi mbali mbali, ili tuweze kupanga na kutekeleza mipango yetu ya maendeleo vizuri. Upangaji wa mipango ya maendeleo ni shughuli muhimu inayotegemea takwimu sahihi juu ya maisha ya wananchi, hali zao, umri wao, rasilimali zao, uwezo wao wa kiuchumi, sehemu wanazoishi na mambo mengine mengi, kama kila mmoja wetu anavyofahamu. Tunahitaji kuwa na takwimu sahihi zinazohusiana na watoto, vijana na wazee, ili zituwezeshe kujipanga vizuri katika kuendeleza na kuimarisha sekta ya afya na elimu. Tunahitaji kujua umri wa wananchi, ili tuweze kujiandaa vizuri katika utayarishaji wa nguvukazi na masuala ya pensheni. Kwa mfano, hivi sasa tunapata matatizo mengi katika utoaji wa pensheni jamii kutokana na ugumu uliopo wa kutambua umri halisi wa wazee katika sehemu mbali mbali Unguja na Pemba.

Ndugu Wananchi, Kwa upande mwengine, nakuhimizeni mtekeleze vizuri jukumu lenu la kulinda amani na usalama wa nchi kwa kuwa imara na makini katika usajili na utoaji wa vitumbulisho. Vitambulisho vya Mzanzibari ni kielelezo

Page 12:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

12

muhimu kinachohitajika katika utoaji wa huduma tafauti kwenye maeneo muhimu. Vitambulisho vinatumika katika benki kufanya miamala ya fedha, kufanya usajili katika mitandao ya simu na katika kutafuta ajira. Kwa hivyo kamwe tusiruhusu mianya yoyote kwa watu kughushi vitambulisho, kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa nchi pamoja na maslahi ya kila mmoja wetu.

Ni matumaini yangu kwamba kila mmoja atayaangalia masuala haya niliyoyaeleza kwa upana zaidi na kwa pamoja muongeze bidii katika kuyatekeleza majukumu yenu, ili kuulinda usalama wa nchi yetu na raia wake. Vile vile, naendelea kukuhimizeni kwamba katika kuwahudumia wananchi lazima muweke kipa umbele kwao, kwani wao ndio walengwa wakubwa. Lazima tuwajali tunaowahudumia na huo ndio msingi wa utawala bora. Tabia hii itakujengeeni mustakabali mzuri katika kazi zenu. Inapotokezea kuwa watu hawastahiki kupewa huduma wanazodai, wafahamisheni kwa kutumia lugha nzuri na kamwe msiwahamakie na msiwadharau, kwani Waswahili wanasema “Maneno mazuri humtoa nyoka pangoni”.

Ndugu Wananchi,

Page 13:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

13

Utendaji wa majukumu yenu, unagusa maslahi ya kila mmoja wetu kwa upana zaidi. Kwa msingi huo, natarajia kuwa mtafanyakazi kwa kushirikiana na Taasisi zote muhimu kama vile NIDA, ZSSF, ZRB, TRA, Mfumo wa e-Health, Ofisi za Wilaya na Mikoa, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali na kadhalika. Andaeni mikakati na taratibu nzuri za kushirikiana na kubadilishana taarifa na Taasisi hizi kwa kuzingatia sheria na kanuni za uhifadhi na utumiaji wa taarifa za wananchi na zinazoongoza Taasisi zenu.

Ndugu Wananchi, Nafahamu jitihada kubwa zilizofanyika katika kuwasajili Wazanzibari 712,982 na kukusanya mapato ya TZS 154,726,300 katika mwaka 2017/2018 kwa malipo mbali mbali. Naamini kuwa mmejipanga vizuri katika kuitekeleza Sera ya Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi ya mwaka 2008 na hapana shaka Mfumo wa Wakala wa Usajili na Matukio ya Kijamii utatuwezesha kupata takwimu mbali mbali za msuala ya kijamii zilizo sahihi na kuyadhibiti mapato ya huduma zitakazotolewa. Vile vile, tunataraji kwamba Ofisi za Wilaya zitaihamasisha jamii kuzitumia ofisi hizo, ili wananchi wapate huduma wanazozihitaji kwa ufanisi na kwa haraka.

Page 14:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

14

Ndugu Wananchi, Sote tunafahamu umuhimu wa masheha katika kutimiza wajibu wao katika kuwatumikia wananchi kwenye Serikali za Mitaa. Masheha wanafanya kazi nyingi na nzito zilizo kwenye mamlaka yao katika suala zima la usajili wa taarifa za vizazi, vifo, ndoa, talaka na utoaji wa vitambulisho. Barua wanazozitoa ikiwa na ridhaa yao katika kuyafanikisha mambo ya wananchi kwenye shehia zao, zinakidhi mahitaji ya kanuni na taratibu ziliopo. Hata hivyo, zipo taarifa zinazoelezwa kwamba baadhi ya Masheha hutoa barua hizo kwa kukubali kurubuniwa (rushwa). Yapo mengi yaliyosemwa kuhusu Masheha na utoaji wa barua kwa ajili ya kutengeneza hati mbali mbali bila ya kuzitii sheria na taratibu zilizowekwa. Natoa onyo kali kwa Masheha wenye tabia hio na Wakuu wa Mikoa wanaokubali kufanya nao kazi au kuwateua masheha wa aina hiyo. Uongozi wa Ofisi hii kwa kushirikiana na Wakuu wa Mikoa na Wilaya lazima muwachukulie Masheha hao hatua kali kwa mujibu wa sheria. Katika kulitekeleza agizo langu hili, vile vile zipo taarifa kwamba wapo watu wanamiliki vifaa kwa njia ya siri ya kuwa na mitambo yenye kutoa vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya masomo, vitambulisho, leseni na nyaraka nyengine za Serikali kwa

Page 15:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

15

njia ya kughushi. Watu hawa ni lazima watafutwe kwa njia yoyote na washughulikiwe haraka iwezekanavyo kutokana na uvunjaji wa sheria wanaoufanya.

Mifumo mipya tunayoianzisha inahitaji tuwe na vijana wenye elimu ya juu na uwezo wa kuhimili kazi. Kwa hivyo, nakusisitizeni muwaajiri vijana wenye taaluma, ujuzi, na maarifa pamoja na ari ya kizalendo kwa ajili ya kuendesha mifumo hii mipya. Wekeni utaratibu mzuri wa kuzilinda taarifa zote muhimu kwa kuzingatia sheria ziliopo ambazo mtapaswa mzitumie dhidi ya wale watakaojaribu kughushi na kutoa taarifa za wananchi bila ya kuzingatia sheria. Lazima muweke mipango imara ya kutoa mafunzo na kuwasomesha wafanyakazi mnaowahitaji. Kwa mara nyingine nakukumbusheni kwamba katika kutekeleza shughuli zenu kupitia Mfumo huu, watendaji mna dhima kubwa ya kuzitunza na kuzidhibiti taarifa mbali mbali za wananchi, ili zisitumike kwa njia zisizo halali. Uongozi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ una kazi kubwa ya kutoa elimu kwa wananchi, ili waifahamu vizuri Taasisi hii pamoja na kazi zake. Kwa kuwa hii Taasisi mpya kimuundo, ni wazi kwamba hivi sasa ni wananchi wachache tu ndio wanaofahamu vizuri majukumu yenu. Ongezeni juhudi

Page 16:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

16

katika kuwahamasisha wananchi, ili wavitumie Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi katika shughuli zao pale vinapohitajika.

Ndugu Wananchi, Nimefahamu kwamba Mfumo huu mpya tunaouzindua leo, utatuwezesha kuzidhibiti na kuzitunza kumbukumbu za Wazanzibari na wageni wanaokaa Zanzibar kwa madhumuni mbali mbali; kama vile utoaji wa Vyeti vipya vya Kuzaliwa vilivyo imara zaidi na vyenye alama mbalimbali za kiusalama pamoja na Kadi mpya ya Mzanzibari Mkaazi ya Kielektroniki (e-Card) ambayo itatengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa yenye ‘chip’ na yenye uwezo wa kubeba taarifa mbalimbali za mwombaji pamoja na alama nyingi za kiusalama. Kwa ujumla Mfumo huu utatoa vifaa katika hali ya juu ya mtindo wa kisasa yenye usalama na haitakuwa rahisi kughushi kwa wale wenye kupenda kufanya majaribio ya kihalifu ya aina hiyo.

Ndugu Wananchi, Nimezisikia na nimezifahamu changamoto mbali mbali nilizoelezewa. Naelewa kuwa panapo mafanikio hapakosi changamoto, na changamoto si ishara ya kurudi nyuma

Page 17:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

17

bali ni dalili muhimu za maendeleo. Serikali imepiga hatua ya maendeleo kwa kuunda Taasisi hii na kuimarisha mifumo yake kutokana na changamoto zilizohitaji kufanyiwa kazi na kutatuliwa, ili kuimarisha huduma zilizokuwa zikitolewa. Kwa hivyo, kama tulivyoweza kutatua changamoto mbali mbali mpaka tumefikia leo kuwa na Mfumo imara wa taarifa za kijamii, naamini kwamba miongoni mwa changamoto mlizozibainisha nyingi kati ya hizo, zinaweza kutatuka ikiwa nyinyi wenyewe mtazidisha kasi na ari ya utendaji. Nimeteua viongozi wa kuendesha shughuli za Taasisi hii nikiwa na imani kwamba ni wachapakazi ambao wana uwezo wa kufanya ubunifu, kama nilivyoeleza mwanzo wa hotuba yangu. Kwa hivyo, kwa mashirikiano ya pamoja na Taasisi mbali mbali za Serikali, changamoto hizo mlizowaziwasilisha na zitakazoibuka zinaweza kupatiwa ufumbuzi. Serikali nayo kwa upande wake tutashirikiana na wanaohusika, ili tuweze kufanikiwa. Tumuombe Mwenyezi Mungu aiongezee baraka nchi yetu, ili tuweze kuendesha shughuli zetu kwa ufanisi zaidi.

Ndugu Wananchi, Kabla ya sijamaliza hotuba yangu, natoa shukurani zangu maalumu kwa uongozi wa Kampuni ya “ZIT Solutions”

Page 18:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

18

kwa kukubali kushirikiana nasi katika kuandaa mfumo huu mpya. Aidha, shukurani za dhati ziende kwa kampuni mbali mbali za kizalendo zilizoshiriki katika ujenzi na uimarishaji wa Ofisi zenu katika Wilaya zote za Unguja na Pemba. Ni matumani yangu kwamba ushirikiano huu mzuri uliopo kati ya Uongozi wa Wakala na washirika wote hawa mtauimarisha kwa faida yenu na pande zote zinazohusika.

Kwa mara nyengine, natoa shukurani kwako Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa kunialika kuwa mgeni rasmi. Natoa wito kwa wananchi wote washiriki kikamilifu katika zoezi lililopangwa la usajili na uimarishaji wa taarifa kwa uharaka na ujumla, (Mass enrolment and update), ambalo litafanyika katika Wilaya zote za Unguja na Pemba. Nimeelezwa kuwa hivi sasa tayari ufungaji wa miundombinu na mifumo umekamilika. Nimefurahi sana kwa heshima mliyonipa ya kuwa mtu wa mwanzo wa kuziimarisha taarifa zangu katika mfumo huu mpya, tuliouzindua leo hii.

Page 19:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

19

Natoa tena shukurani kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, kwa mapokezi mazuri na kwa wananchi wote kwa kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa jengo hili na mfumo huu ambao ni muhimu katika uimarishaji wa haki, usalama pamoja na upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Namshukuru tena na

kumpongeza msomaji Kurani Tukufu yenye maudhui na mnasaba wa shughuli yetu hii, msanii aliyeghani utenzi uliobeba ujumbe muhimu, na wale waliotutumbuiza kwa ngoma nzuri ya kibati pamoja na burudani iliyoambatana na mafunzo katika mchezo wa kuigiza.

Ndugu Wananchi, Namalizia hotuba yangu kwa kusisitiza mashirikiano katika kuilinda na kuidumisha hali ya amani tuliyo nayo hivi sasa, ambayo kila mmoja wetu anaujua umuhimu wake. Ni wajibu wetu tuishi kwa amani na utulivu huku tukifanya shughuli zetu kwa bidii na mshikamano. Tutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona, tunasoma na tunasikia kwenye vyombo vya habari kila siku kutoka katika baadhi ya nchi za

Page 20:  · Web viewTutafakari sana kwamba hizi hatua za maendeleo tunazopiga ni matokeo ya kuwepo amani na utulivu tulio nao. Mahali pasipo na amani hapana maendeleo. Ushahidi wa haya tunauona,

20

wenzetu zenye migogoro. Namuomba Mwenyezi Mungu atuzidishie baraka, neema na audumishe umoja na msihikamano uliopo miongoni mwa wananchi na baina ya wananchi na wageni mbali mbali wanaotutembelea. Natoa wito kwa wananchi wenzangu na wageni wote wanaoingia na kuishi Zanzibar kuitumia vyema Ofisi hii ya Wakala katika kupata huduma zao.

Nakutakieni nyote afya njema na kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yenu. Mwenyezi Mungu akujaalieni mrudi nyumbani salama.

Baada ya kusema hayo, sasa natamka kuwa Uimarishaji wa Mfumo wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii umezinduliwa rasmi.

Asanteni kwa Kunisikiliza.