wimbo wa sakima · 2018. 12. 30. · wimbo wa sakima skrevet av: ursula nafula illustret av: peris...

20
Wimbo wa Sakima Wimbo wa Sakima Ursula Nafula Peris Wachuka Ursula Nafula swahili nivå 3

Upload: others

Post on 23-Jan-2021

0 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Wimbo wa SakimaWimbo wa Sakima

Ursula Nafula Peris Wachuka Ursula Nafula swahili nivå 3

Page 2: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Sakima aliishi na wazazi wake na dada yake wamiaka minne. Waliishi katika shamba la mtu tajiri.Nyumba yao ya nyasi ilikuwa mwisho wa safu yamiti iliyopendeza.

2

Page 3: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Sakima alipokuwa na umri wa miaka mitatu,aliugua na kupoteza uwezo wa kuona. Hata hivyo,Sakima alikuwa mvulana mwenye kipaji.

3

Page 4: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Sakima alitenda mambo mengi ambayo wavulanawengine wa umri wake hawakufanya. Kwa mfano,aliketi na watu wazima na kujadili mambomuhimu.

4

Page 5: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Wazazi wa Sakima walifanya kazi katika nyumbaya yule tajiri. Walitoka nyumbani asubuhi namapema na kurudi jioni. Sakima aliachwa nadada yake.

5

Page 6: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Sakima alipenda kuimba nyimbo. Siku mojamama yake alimuuliza, “Sakima, unajifunzanyimbo hizi kutoka wapi?”

6

Page 7: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Sakima alimjibu, “Nazisikia akilini mwangu kishanaziimba.”

7

Page 8: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Sakima alipenda kumwimbia mdogo wake hasaakihisi njaa. Dada yake alimsikiliza na kucheza.

8

Page 9: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

“Naomba uimbe tena na tena, Sakima,” mdogowake alimsihi. Sakima alikubali na kuimba maranyingine.

9

Page 10: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Jioni moja, wazazi wake waliporudi nyumbani,walikuwa kimya sana. Sakima alijua kwambalazima kulikuwa na jambo baya.

10

Page 11: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

“Kuna shida gani, mama, baba?” Sakima aliuliza.Sakima aligundua kwamba mwana wa tajiri waoalikuwa amepotea. Tajiri alihuzunika na kuwa naupweke mkubwa.

11

Page 12: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

“Labda atafurahi tena nikimwimbia,” Sakimaaliwaambia wazazi wake. Wazazi wake walidharauwazo lake. “Yeye ni tajiri sana. Wewe ni mvulanaasiyeona. Unadhani wimbo wako utamsaidia?”

12

Page 13: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Hata hivyo, Sakima hakukata tamaa. Mdogo wakealimpa moyo. Alisema, “Nyimbo za Sakimahunituliza mimi nikiwa na njaa. Zitamtuliza tajirivile vile.”

13

Page 14: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Siku iliyofuata, Sakima alimwomba mdogo wakeamwongoze hadi kwenye nyumba ya tajiri.

14

Page 15: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Alisimama chini ya dirisha moja kubwa na kuanzakuimba wimbo wake alioupenda. Pole pole,kichwa cha tajiri kilionekana dirishani.

15

Page 16: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Wafanyakazi waliacha kazi zao. Wakasikilizawimbo mzuri wa Sakima. Hata hivyo,mwanamume mmoja alisema, “Hakuna aliyefaulukumtuliza bwana. Je, huyu mvulana asiyeonaanafikiri atamtuliza?”

16

Page 17: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Sakima alipomaliza kuimba wimbo wake alianzakuondoka. Tajiri alitoka nje kwa haraka nakusema, “Tafadhali, imba tena.”

17

Page 18: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Wakati huo huo, watu wawili walikuja wakiwawamembeba mtu kwenye machela. Walimkutamwana wa tajiri akiwa amechapwa na kuachwakando ya barabara.

18

Page 19: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Tajiri alifurahi sana kumwona mwana wake tena.Alimzawadia Sakima kwa kumliwaza. Aliwapelekamwanawe na Sakima hosipitali ili Sakima awezekusaidiwa kuona tena.

19

Page 20: Wimbo wa Sakima · 2018. 12. 30. · Wimbo wa Sakima Skrevet av: Ursula Nafula Illustret av: Peris Wachuka Oversatt av: Ursula Nafula Denne fortellingen kommer fra African Storybook

Barnebøker for NorgeBarnebøker for Norgebarneboker.no

Wimbo wa SakimaWimbo wa SakimaSkrevet av: Ursula Nafula

Illustret av: Peris WachukaOversatt av: Ursula Nafula

Denne fortellingen kommer fra African Storybook (africanstorybook.org) og ervidereformidlet av Barnebøker for Norge (barneboker.no), som tilbyr barnebøkerpå mange språk som snakkes i Norge.

Dette verket er lisensiert under en Creative Commons Navngivelse 4.0 Internasjonal Lisens.

20