zanzibar daima online

32
Zanzibar Daima Septemba 2013, Toleo 03 Ufisadi waila SUK “Matusi ya Komba Wapya” Makala Maalum Mimi ni Mansoor Yussuf Himd Uhafidhina wa Kiswandui, Ukoloni wa Dodoma JAMVI LA BARAKA Tumejifunza nini kutoka Zimbabwe Tembelea mtandao wetu wa www.zanzibardaima.net kwa habari moto moto

Upload: hassan-mussa-khamis

Post on 30-Nov-2015

5.713 views

Category:

Documents


0 download

DESCRIPTION

Zanzibar ina safari ndefu ya kwenda kabla ya kuwa nchi iliyostawi kiuchumi kwa vile mfumo wake wa kiutendaji umebomoka kabisa, licha ya kuongozwa na serikali yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa.

TRANSCRIPT

Page 1: Zanzibar Daima Online

Zanzibar Daima OnlineSeptemba 2013, Toleo 03

Ufisadi waila SUK

“Matusi ya Komba Wapya”

Makala MaalumMimi ni MansoorYussuf Himd

Uhafidhina wa Kiswandui, Ukoloni wa Dodoma

JAMVI LA BARAKA

Tumejifunza ninikutoka Zimbabwe

Tembelea mtandao wetu wa www.zanzibardaima.net kwa habari moto moto

Page 2: Zanzibar Daima Online

08 Hakuna asiejuwa ya kuwa Elimu imeshuka kiwango kikubwa 10 “Mimi ni Mansoor Yussuf Himid”

Nina hisia zangu kama binadamu...

04 Ufisadi waila SUK

08Ili Zanzibar iendelee itilie mkazo ICT

10 Kutoka Magazetini

12 Makala Maalum

17 Ngurumo la Mkama Ndume

19Matusi ya ‘Komba Wapya’ wa CCM

24 Jamvi la Baraka

28Bado Mansoor anao uhai wa kisiasa

32 Kauli ya Mwinyi Mkuu

36Mkeka wa Mwana wa Mwana

38 Wanafacebook wasemavyo

40Uhafidhina wa Kisiwandui, Ukoloni wa Dodoma

48 Ladha ya Beti

50 Tufungue kitabu

53Hivi ndivyo Kriketi ichezavyo

44 Tartiiib, CCM bye bye 16 Naam, Napinduzi Daima

58 Tutachimba mafuta, lakini tutayari? 60 Taifa gani lisilokumbuka msiba wa watu wake?

2

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

3

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

YaliomoWajumbe wa Baraza la Wawakilishi walitaja upotevu wa fedha kutokana na usajili wa meli za kigeni ambapo mapato yanayotokana na uwakala wa kampuni ya Philtex ya Dubai, inayosajili meli za kimataifa, hayakuwa wazi.

>

MAKALA yanayoongoza toleo hili yanajaribu kuligusa dondandu-gu lenye kuula watani wetu. Ni

ufisadi uliokithiri na unaoshamiri hata ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Ni banguzi linaloambukiza na linaloweza kuufanya uchumi wa visiwa hivi uwe ni wenye kudumaa hata tufanyeje kujaribu kuukwamua.

Ufisadi ni ufisadi lakini una sura tafauti. Unabandikwa majina mbalimbali kutege-mea namna unavyojitokeza. Hakuna ufi-sadi unaoweza kutoa udhuru. Au unao-weza kuwa safi.

Daima huwa muovu, nauwe wa kuzila fedha za umma au wa maadili.

Ufisadi ni ufisadi. Ule wa madaraka, wa kuzitumia vibaya nguvu za utawala ni ufi-sadi wa kisiasa.

Ufisadi wa aina hii aghalabu hufanywa na wakuu wa serikali kama vile Rais na mawaziri wake au na watumishi wa seri-kali kuanzia ngazi ya makatibu wakuu na kuteremka kwendea chini. Hawa huya-tumia madaraka yao kujinufaisha binafsi ima kwa kujipatia mali kwa njia haramu au kwa kuwarahisishia walio wao mambo yao yawaendee.

Ni uovu. Ni uharibifu. Ni ubadhirifu. Ni kula rushwa. Ni kutoa rushwa. Ni kulish-ia. Ni kutoa hongo. Ni kutoa au kupokea

chauchau. Ni kula mrungura. Ni kuto mrungura. Ni kutoa kilemba. Ni kupewa kilemba. Yote hayo yamo katika istilahi ya ufisadi.

Ufisadi ni uhalifu, ni kitendo cha jinai. Wanaofumaniwa nacho wanastahili wa-tiwe nguvuni na wapandishwe mahaka-mani. Hakuna kuoneana muhali. Hakuna kulindana. Wenye hatia waadhibiwe.

Katika sekta ya uchumi binafsi ufisadi unaongeza gharama za kufanyia biashara.

Ubaya mwingine ni kwamba mirungu-ra inayakinga makampuni yenye kutoa huduma mbovu.

Katika sekta ya umma ufisadi unapotosha uchumi kwani serikali hutumia fedha za umma kuwekeza kwenye miradi mikubwa kama ya miundombinu.

Aidha, ufisadi una tabia ya kuwafanya wa-jenzi wa miundombinu wasifuate kanuni za mazingira.

Tunawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walioonyesha uzalendo kwa kufichua ufisadi. Wananchi lazima tuwapige darubini wanaofanya ufisadi wa kuuhujumu uchumi. Na serikali nayo inapaswa iwachukulie mafisadi hatua zin-azohitajika.

UJUMBE KUTOKA KWA

SERIKALI LAZIMA IWACHUKULIE HATUAMAFISADI

MhaririAhmed Rajab

Page 3: Zanzibar Daima Online

kikazi” ambayo yamekuwa yakishughu-likiwa ipasavyo.

“Hakuna pahala pasipokuwa na mapun-gufu. Sio sahihi kusema hakuna ushughu-likiaji. Mambo yanatekelezwa kama ilivyo kawaida,” alisema Waziri huyo anayetokea CUF, chama ambacho kimekuwa kikipin-gana na ufisadi tangu kilipokuwa kwenye upinzani.

Rashid alisema si jukumu la wizara kud-hibiti ubadhirifu kama upo, bali “kwa mu-jibu wa taratibu za nchi kuna chombo maalum kinaitwa CAG (Chief Auditor Gen-

eral, mdhibiti mkuu na mkaguzi wa mali za Serikali). Hicho ndicho chombo kina-choshughulikia udhibiti wa mali za Seri-kali.”

“Kama wao (Wawakilishi) wameona kuna ripoti iliyosema (pametokea ubadhirifu) halafu wizara haikuchukua hatua, ndio ili-kuwa waseme. Lakini tuliwaambia haya mambo hayako tena. Kama yalifanyika, ilikuwa hapo nyuma. Tokea mamlaka iun-dwe, kila kitu kiko kwenye order (sawasa-wa).”

Hata hivyo, uchunguzi wa Zanzibar Dai-

Kulindana Kwingi

Mtandao wa E Government unashukiwa kula fedha nying kuliko kazi iliofanywa. Mradi wa wa uwanja wa Ndege Zanzibar umefeli baada ya zaidi ya dola 60 za mkopo kuingizwa humo. Mradi wa mkonga wa taifa umegharimu dola milioni 19 na Wawakilishi wanataka tume iundwe.

Miongoni mwa taasisi zilizotajwa kuoza kwa ufisadi ni zile zinazotege-mewa kuendesha uchumi kama vile bandari, viwanja vya ndege na utalii

N A M AUA M O H A M M E D

4

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

5

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Zanzibar ina safari ndefu ya kwenda kabla ya kuwa nchi iliyostawi kiu-chumi kwa vile mfumo wake wa kiu-

tendaji umebomoka kabisa, licha ya ku-ongozwa na serikali yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa.

Uchunguzi uliofanywa na Zanzibar Daima Online katika taasisi mbalimbali za seri-kali pamoja na mitaani, umegundua kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoundwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) inakabiliwa na ufisadi wa kutupwa.

Ubaya zaidi ni kuwa kunakosekana hatua zozote za kinidhamu dhidi ya wanaohusi-ka ambao baadhi ya wakati wakiwa wa-najulikana hata na watu walio nje ya taa-sisi hizo.

Miongoni mwa taasisi zilizotajwa kuoza kwa ufisadi ni zile zinazotegemewa kuen-desha uchumi kama vile bandari, viwanja vya ndege na utalii.

Baraza la Wawakilishi lililoahirisha vi-kao vyake mwezi uliopita lilimalizika kwa shutuma za wazi za ufisadi serikalini uliobuliwa na Wawakilishi kadhaa. Lakini Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, analaumiwa kuwa alihitimisha ho-tuba yake ya kuliahirisha Baraza hilo kwa kukemea kufichuliwa huko kwa ubadhir-

ifu wa fedha za umma, akitishia kutumia sheria inayolinda siri za Serikali dhidi ya utolewaji wa taarifa kama hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa, Balozi Iddi alihoji kwamba ni kosa la jinai kutumia hoja za siri za Seri-kali kuibua maovu Serikalini.

“Ni mtu huyu huyu juzi tu aliliambia Baraza kwamba eti yeye anachukia rush-wa na wizi Serikalini na kwamba hawezi kuvimilia vitendo hivyo. Leo anakuja na vitisho kwa wale wanaofichua uovu huo,” alisema Jussa akiongeza kwamba ikiwa walioko Serikalini hawapendi “kufichuli-wa uovu, wizi na ufisadi unaofanyika basi waache uovu, wizi na ufisadi huo”.

Zanzibar Daima Online imefahamishwa na vyanzo kadhaa vya habari ndani na nje ya Serikali kwamba kiwango cha kulin-dana bado ni kikubwa ndani ya mamlaka zinazohusika na usimamizi na uendeshaji Serikali, kiasi ya kwamba uwepo wa Seri-kali ya Umoja wa Kitaifa haujabadilisha kabisa “utamaduni wa kula na kusaza.”

Lakini Waziri wa Miundombinu na Ma-wasiliano wa Zanzibar, Rashid Seif, amemuambia mwandishi wetu kwamba tuhuma za ufisadi zinazotajwa kuiandama Serikali yake ni “mambo ya kikawaida ya

Ufisadi wailaSUK Zanzibar

Page 4: Zanzibar Daima Online

ma Online umegundua kwamba ubadhirifu na ufisadi Serikalini unachochewa sana na watendaji wakuu, wakiwemo makatibu na wakurugenzi, na hasa kwa misingi ya siasa.

Ali Nassor Ali, mfanyabiashara kisiwani Unguja, aliliambia jarida hili kwamba kuna mifano mingi ambapo makatibu wana-kosa kuwajibika kwa mawaziri wao “kwa kuwa hawakuteuliwa na mawaziri hao bali (wameteuliwa na) Rais.”

“Kwa vile katibu mkuu huyo na mkurugen-zi haoni sababu yoyote ya kuwajibika kwa waziri kwani hana uwezo wa kumfuta kazi, hasa kwa kuwa waziri anayehusika hayuko mrengo mmoja (wa kisiasa) na Rais inaku-wa vigumu kwa katibu mkuu au mkurugenzi kusikiliza amri ya waziri huyo.”

Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, Zan-zibar haitapiga hatua za maendeleo kwa kuwa “siasa imewekwa mbele kuliko masla-hi ya nchi.”

Hivi karibuni Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mo-hammed Shein alifanya mageuzi katika baadhi ya wizara zake. Alizifumua wizara tano nyeti na kuziunda upya.

Shein alifanya mabadiliko katika wizara hizo, siku chache baada ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoa tuhuma kad-haa nzito za ufisadi katika wizara hizo, huku wakitaka Serikali ichukue hatua za haraka na kali dhidi ya watumishi wanaotuhumiwa kufanya ufisadi.

Baadhi ya watu wanasema kuwa Shein amefanya mabadiliko ili kupunguza mianya ya ufisadi, japo baadhi ya wengine wana mtizamo kuwa hakuna mabadiliko ya ku-shtua yaliyotokea kwa sababu mawaziri ni walewale, na watendaji ni walewale.

Wizara zilizofumuliwa ni Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la

Mapinduzi iliyokuwa ikiongozwa na Dk Mwinyihaji Makame Mwadini; na Wizara ya nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora iliyokuwa chini ya Haji Omar Kheri.

Dk Mwinyihaji sasa anaongoza wizara mpya ya ‘Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Uta-wala Bora’, na Haji Omar Kheri amepewa ju-kumu la kuongoza Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais –Tawala za Mikoa na Idara Maalum (vi-kosi).

Wizara nyengine zilizopata mtikisiko ni Wi-zara ya Nchi Ofisi ya Rais - Fedha, Uchumi, na Mipango ya Maendeleo iliyokuwa iki-ongozwa na Omar Yussuf Mzee; na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika chini ya Haroun Ali Suleiman.

Katika muundo mpya, Omar Yussuf Mzee sasa ni Waziri wa Fedha; na Haroun Ali Suleiman ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Kazi na Utumishi wa Umma.

Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake, na Watoto, waziri wake akiwa Zainab Mohammed Omar pia ilifumu-liwa na kuundwa upya. Baada ya kuundwa upya Mama Zainab sasa anaongoza wizara mpya, kubwa, ya ‘Ustawi wa Jamii, Uwezes-haji wa Wananchi Kiuchumi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake, na Watoto.

Ufisadi ulitajwa katika wizara na taasi-si nyingi za serikali, lakini ufisadi mkubwa umebainika katika Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, hasa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini (Zanzibar Maritime Authority - ZMA), na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (Zanzibar Airports Authority - ZAA).

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walitaja upotevu wa fedha kutokana na usajili wa meli za kigeni ambapo mapato yanayoto-kana na uwakala wa kampuni ya Philtex ya Dubai, inayosajili meli za kimataifa, hayaku-wa wazi.

“Hii ni dhahir kuna ubababaishaji, haku-na utaratibu wa mapato hayo... imekuwa hayaeleweki na ripoti za fedha zinaashiria kuna upotevu mkubwa wa fedha, na meli zinaposajiliwa makubaliano, kwa mujibu wa maelekezo ya Shirika la Kimataifa la Usafiri katika Maji - International Maritime Organization (IMO), kila meli iliyosajiliwa in-atakiwa itoe nafasi tano za ajira za ubaha-ria kwa nchi husika, je, hili linafanyika?” alihoji Hamza Hassan Juma, Mwakilishi wa Kwamtipura (CCM).

ZMA, kupitia wakala wake Philtex, imeku-wa ikisajili meli tangu mwaka 2009, laki-ni nafasi za ubaharia hazionekani, wakati Zanzibar inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Hija Hassan Hija, Mwakilishi wa Kiwani (CUF) pia alilalamika kuwepo kwa ukwe-paji mkubwa wa ulipaji wa ushuru katika bandari ya Zanzibar akitoa mfano wa tuhu-ma kuwa makontena mia tatu hayalipiwi kila mwezi. “Inatakiwa kwa kila kontena moja, ada ya Bandari ni [shilingi] elfu sitini (60), lakini ada hiyo imekuwa haionekani.”

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pia wa-liibua ufisadi katika mradi wa mkonga wa taifa ambao baada ya kukamilika, utawe-zesha taasisi za Serikali kuwa na mtandao wa mawasiliano.

Mtandao wa kwanza unaolengwa ni ku-ziunganisha taasisi za serikali, ‘E-Go-vernment’, halafu baadaye itafuatiwa na mtandao wa afya ‘E-Health’, na mengineo, lakini Wawakilishi wametilia shaka kubwa kuwa fedha zilizotumika ni nyingi kuliko kazi iliyofanywa.

Mradi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar, umefeli na kukera wajumbe wengi wa Ba-raza la Wawakilishi ambao wamehoji kwa nini hali hiyo ikatokea na kusababisha ha-sara kubwa kwa Serikali, wakati fedha zili-

zotumika ni fedha za mkopo zaidi ya dola za Marekani milioni 60.

Mradi wa mkonga ambao haujakamilika umegharimu dola milioni 19 za Marekani (sawa na zaidi shilingi bilioni 31), wajumbe walitaka tume iundwe kuchunguza sakata hilo, lakini Spika wa Baraza na Serikali ha-wakuridhia.

Spika alishauri tuhuma hizo zichunguzwe na Serikali, na Balozi Seif Ali Iddi ameahidi kufanya uchunguzi kubaini kama tuhuma za ufisadi katika mradi wa mkonga ni za kweli.

Katika mfululizo wa malalamiko ya ufisa-di katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wa-wakilishi pia walionyesha wasiwasi wao kuhusu matumizi ya fedha katika miradi ya ujenzi wa barabara, Unguja na Pemba.

“Ukiangalia barabara nyingi visiwani humu zimesita, mfano ujenzi wa barabara za: Amani/Mtoni, na Wete-Gando-Wete-Ch-ake, umesita bila sababu zinazoridhisha,“ alisema Mwakilishi mmoja.

Pia matumizi ya pesa kwa ajili ya barabara sita za kusini Pemba yanatia shaka kwani, barabara hizo zimekosa viwango ambapo tokea zifunguliwe sasa ni mwaka mmoja tu lakini zimeshaanza kuharibika, kwa mujibu wa kumbukumbu za Baraza la Wawakilishi.

Barabara hizo zilizinduliwa kwa sherehe za Mapinduzi lakini haijafika sherehe ya Mapinduzi nyingine barabara hizo tayari zimeshaanza kuchimbika hii ni kukosa vi-wango va ubora vya barabara.

Na licha ya wajumbe wa Baraza la Wawa-kilishi kuitaka serikali ichukue hatua dhidi ya ufisadi unaotokea Serikalini, wasiwasi mkubwa ni kwamba utamaduni wa kulin-dana na kudharauliana utaendelea kuita-funa sekta ya umma na ya binafsi visiwani Zanzibar kwa siku kadhaa zijazo.

6

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

7

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 5: Zanzibar Daima Online

Ili iendelee, Zanzibar yahitaji kutilia mkazo ICTKALAMU YA BIN RAJAB

MARA nyingi, kama si zote, tu-napokuwa tunazungumzia mustakbali wa nchi yetu, tu-

nakuwa tunasisitiza sana juu ya vigezo vya maendeleo vinavyojikita kwenye siasa au uchumi. Ni nadra kuitupia macho elimu na hasa elimu ya mambo ya ufundi na hasa zaidi ile inayohusu teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT).

Elimu hii imekuwa muhimu sana katika miaka ya hivi karibuni kote duniani na ushahidi unaonyesha kwamba zile nchi zilizoipa kipaumbele elimu hiyo zimepa-ta mafanikio makubwa katika maende-leo yao ya kiuchumi na ya kijamii katika muda usio mrefu.

Kwa kutoitia sana maanani elimu ya teknolojia ya mawasiliano tunakuwa tunajipunja wenyewe kwani elimu hiyo siku hizi ndiyo yenye kusakwa kote du-niani kwa vile ni muhimu kwa maende-leo ya mataifa — makubwa na madogo.

Nchi kama yetu ina nafasi nzuri ya kunufanika kutokana na elimu aina hiyo. Tunaipata nafasi hiyo nzuri kwa sababu hatunayo elimu hiyo. Hatu-wezi, kwa hivyo, kufanya makosa kama yanayofanywa na nchi zilizo na uzoefu wa elimu ya aina hiyo na zenye kutaka kujiendeleza katika nyanja hiyo.

Elimu ya watoto haihusiki na kusoma tu na kupata maksi nzuri klasini tu. Elimu ni njia ya kuvumbua vitu vipya tusivyovi-jua na pia njia ya kuongeza maarifa

yetu.

Hakuna asiyejua kwamba ikilinganishwa na nchi nyingine duniani hata baadhi ya zilizo barani Afrika Zanzibar imetupwa nyuma katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kwa kiwango kikubwa wa kulaumiwa ni sisi wenyewe.

Zamani tulijitupa wenyewe nyuma kwa kutoipa elimu umuhimu unaostahiki. Haitukhalis kukaa na kushika tama huku tukilalamika na kuwahusudu wen-zetu walioendelea. Tunaweza, tukitaka,

kuwafukuzia na kuwapata. Lakini tutahi-taji kwanza tuwe na moyo, ari na dhamira ya kukubali kwamba hatuna njia ya ku-wafikia wenzetu ila kukamia kuipata elimu hiyo ya teknolojia ya mawasiliano.

Ni rahisi bila ya shaka kukaa na kusema tunataka hiki na tunataka kile. Ni vigumu kuandaa mkakati utaobadili namna tu-livyozoea kufikiri na tukazibirua fikra zetu.

Itatubidi kwanza tuwe na mpango wa kuitumia elimu hiyo kwa kuzipindua akili

zetu na fikra zetu ili tuwe na namna mpya ya kufikiri. Pili, itatubidi tuwe tayari kuyatumia maarifa tut-ayoyapata kwa ubia kwa manufaa yetu sote, bila ya kubaguana.

Katika hili Serikali, bila ya shaka, ina dhima kubwa. Ninavyosikia ni kwamba Wizara ya Elimu inajitahidi kuwa na mfumo wa aina mpya wa elimu utaoweza kukuza uwezo wake we-nyewe na wa walimu pamoja na wanafunzi wa kuitumia hiyo teknolojia ya mawasiliano.

Pa kuanzia kwanza ni ka-tika klasi, darasani. Wizara ya elimu inapaswa iwe na mkakati wa kuzifanya skuli ziwe na jukumu la kuwa-

fanya Wazanzibari wawe na uwezo wa kuitumia teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT).

Haitoshelezi kwamba wenye kujifunza kuhusu matumizi ya ICT wawe na uwezo wa kujua namna ya kuitumia tu teknolojia hiyo. Watahitaji pia wawe na uwezo wa kujua namna ya kuisarif hiyo teknolojia na pia waidhibiti vilivyo lugha ya teknolojia hiyo.

Hiyo si kazi ndogo kwa sababu kila uchao

Inaendelea Uk.27

8

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

9

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 6: Zanzibar Daima Online

KUTOKA MAGAZETINI

Ndege ya Shirika la Ndege la Oman (Omanair) iliigonga ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethi-

opian Airlines) iliyokuwa imeegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aman Abeid Karume mjini Zanzibar siku ya Jumatatu (tarehe 2 Septemba) wakati ndege hiyo ilipokuwa inaanza safari yake kuelekea Dae es Salaam, liliripoti gazeti la Mwananchi siku ya Ju-manne.

Ndege hiyo ya Omanair iliyokuwa na abiria 150 iliigonga sehemu ya bawa la ndege ya Ethiopian Airlines, jambo am-

balo lilizua taharuki kwa abiria walioku-wemo kwenye ndege hizo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Miundom-binu na Mawasiliano wa Zanzibar, Rashid Seif Suleiman, chanzo cha ajali hiyo hakikufahamika mara moja, hivyo akawataka wananchi kuiachia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ku-fanya uchunguzi wake.

Hata hivyo, ndege hiyo iliruhusiwa kue-ndelea na mipango yake ya safari baada ya kubainika kuwa haikuwa na tatizo la kupelekea kuahirisha safari yake.

Ndege zagongana Zanzibar

Jela miaka 60 kwa kubaka

Mahakama ya Wilaya ya Chake Chake, Pemba, imemuhukumu Abubakar Mkulu Bakar (28)

kifungo cha miaka 60 gerezani kwa kosa la kuwabaka watoto mapacha, liliripoti gazeti la Zanzibar Leo siku ya Jumatano (tarehe 4 Septemba).

Kikao cha Mahakama hiyo kilichoogozwa na Hakimu Khamis Ramadhan kiliridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka dhidi ya mshitakiwa huyo mkaazi wa Wambaa na kuamua kwamba anapaswa kutumikia

kifungo cha miaka 30 kwa kila mtoto aliyembaka.

Sambamba na adhabu hiyo mshtakiwa pia alitakiwa kulipa faini ya shilingi 200,000 taslimu kutokana na kuwasababishia maumivu makali watoto hao, ili iwe ni fundisho kwa watu wengine.

Abubakar aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana familia inayomtegemea, lakini mahakama ilitupilia mbali maombi hayo.

Mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu, Sheikh Khalid

Azzan Hamdan, amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja tangu Septemba 1 huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa dhidi yake, liliripoti

Kiongozi wa Uamsho yu hoi

Kamati ya Maridhiano yaibua mazito

Kamati ya maridhiano Zanzibar imetoa pendekezo la kufanyiwa marekebisho jina la Jamhuri ya muungao wa Tanzania na

badala yake iwe jamhuri za muungano wa Tanzania, kwa lengo la kuleta usawa wa kutambulika kwa nchi mbili hizo ambazo ziliungana tangia mwaka 1964, liliripoti gazeti la Sura ya Mtanzania la tarehe 5 Septemba 2013.

Pendekezo hilo lilitolewa na mmoja ya mjumbe wa Kamati hiyo, Ismail Jussa Ladhu, wakati wa mkutano wa kujadili rasimu ya katiba huko Bwawani mjini Zanzibar, Agosti 31 mwaka huu.

Sambamba na pendekezo hilo la kufanyiwa marekebisho jina la Jamhuri ya muungano, kamati hiyo pia iliitaka tume ya marekebisho ya katiba

kuyaondoa mambo yote ambayo si ya muungano na ambayo yamo kwenye rasimu ya katiba, kwa madai kuwa hayakustahili kuwekwa kwenye rasimu hiyo.

Aidha wametaaka pawepo na usawa kwenye Taasisi za Muungano ikiwa ni pamoja na Mahakama, Bunge, pamoja na Barazala mawaziri, sambamba na kubadilishana nafasi ya uraisi kwa washirika wa muungano.

Hata hivyo wameitaka tume ya mabadiliko ya katiba kuyaondoa mambo matatukati ya yale saba ambayo yameanishwa na rasimu ya katiba na badala yake yabakie mnne kati ya hayo ikiwa ni pamoja na Sarafu na Benki Kuu, Mambo ya nje, usajili wa vyama vya siasa, Uraia na uhamiaji.

gazeti la Mwananchi siku ya Jumatano (tarehe 4 Septemba)

Sheikh Khalid amefikishwa hospitalini hapo kufuatia kuugua ghafla na ugonjwa ambao hadi sasa haujabainishwa wazi na madaktari wanaomshughulikia.Kamishna wa Magereza Zanzibar, Khalifa Hassan, alibainisha kuwa huko nyuma Sheikh Khalid Azzan alishawahi kuumwa wakati akiendelea kusota katika gereza la Kiinua Miguu, lililopo kando kidogo ya kitovu cha Unguja Mjini.

Wakili wa viongozi hao wanaokabiliwa na

kesi ya uharibifu wa mali na kuhatarisha amani ya nchi, Abdalla Juma, alisema kuwa Sheikh Khalid Azzan anaugua ugonjwa wa kibofu cha mkojo ugonjwa ambao unampasa mteja wake apelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo Katibu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Omar Abdalla Ali, amesema kwa sasa hawajajua ni maradhi gani aliyonayo mtuhumiwa huyo, ila walishaanza kumfanyia vipimo na kusisitiza kuwa wanaendelea kumfanyia matibabu.

10

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

11

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 7: Zanzibar Daima Online

MAKALA MAALUM

“Mwenyezi Mungu amlaze pema Marehemu Abeid Karume, yeye na wen-ziwe, Awasamehe kwa

makosa yao, na sisi atupe kauli thabiti. Tufuate nyoyo na misingi yao iliyolenga katika mustakabali wa Zanzibar na kizazi chake.

“Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Subhana Wata’ala, Mwingi wa

Ujuzi na Mwenye kuelewa kipi kipo nda-ni ya kila nafsi ya kiumbe alichokiumba, kilicho hai leo na kinachokuja. Atujaalie hikma na busara na atuepushe na fitna. Aujaalie mkusanyiko wetu huu uwe wa manufaa na tija kwa Wazanzibari wenze-tu na kizazi chetu. Atujaalie pia tumalize kwa salama na kuelekea kwetu kwa sa-lama.

“Mengi yameshasemwa. Mimi leo sina

“Mimi ni Mansoor Yussuf Himid”

mengi ya kuyasema, lakini ninayo ya kuyasema. Na nitasema wa udhati wa moyo wangu. Siogopi. Mapinduzi Daima. Ndio maana siogopi. Mapinduzi. Siogopi. Kwa maana, maana sahihi ya mapinduzi naielewa. Ni freedom. Uhuru. And I am a free man (mimi ni mtu huru). Mimi na nyinyi, sote ni watu tulio huru. Free.

“Ninawaombeni pia munistahmilie. Pengine mliyoyatarajia kutoka kwangu hamtayasikia. Inaweza kuwa hivyo, lakini nakuombeni mlihishimu hilo na mni-stahmilie na nikikosea mnisamehe, ma-ana tangu ninatoka nyumbani kwangu ninamuomba Mwenyezi Mungu anijaalie kauli thabiti. Na anijaalie niwe na kauli ya ukweli, na anijaalie nisiwe na kauli za fitna, wala uchochezi, wala ubaya. Kwa hivyo, nawaombeni mnistahmilie na pia ikiwa yale mliyotarajia hayakuwa, basi

muendelee kuwa wavumilivu.

“Ninaanza kwa kuwashukuru sana sana wananchi wa jimbo la Kiembesamaki kwa heshima kubwa na imani kubwa waliyonipa kuwa Mwakilishi wao tan-gu mwaka 2005. Ninawashukuru sana sana. Hishima haikuwa ndogo, ni hishima kubwa. Imani haikuwa ndogo, ni imani kubwa. Nawashukuru sana na kuwata-kia maisha yenye salama na mafanikio pamoja na familia zao. Na namuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuyafanya maisha yao kuwa mepesi na kuyafanya kila la kheri.

“Hakuna binaadamu aliyekamilika. Nina-waomba sana, kwa unyenyekevu mkub-wa, wanisamehe pale nilipowakosea. Mimi hawajanikosea, ila nawashukuru kwa mema waliyonifanyia.

12

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

13

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

TANBIHI: Jumamosi ya tarehe 31 Agosti 2013, Kamati ya Maridhiano ya Zanzibar iliitisha kongamano kwenye Ukumbi wa Salama, Bwawani Zanzibar, kutoa msimamo wake kuhusu Rasimu ya Katiba mpya, lakini pia mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Mansoor Yussuf Himid, ambaye alifukuzwa kutoka Chama cha Mapinduzi hivi karibuni, alitoa hotuba ya kwanza hadharani tangu afukuzwe. Ifuatayo ni sehemu ya hotuba hiyo.

Page 8: Zanzibar Daima Online

“Ninawashukuru pia wote nilioshiri-kiana nao katika maisha yangu ya ki-siasa – ndani ya Serikali katika wizara zote nilizozitumikia, ndani ya Baraza la Wawakilishi – nawashukuru wawakilishi wenzangu wote. Namshukuru Mheshim-wa Spika na watumishi wa Baraza kwa namna tulivyoishi kwa wema. Mwenye-zi Mungu awajaalie na wao wote kila la kheri.

“Nimekuwa nikiulizwa maswali men-gi sana na waandishi wa habari kutoka kila pembe ya dunia – Marekani, Ulaya, Uchina, yaani nchi nyengine ambazo ndio kwanza nimezisikia kipindi hiki, mpaka simu inakataa mwisho wake inaganda, inanibidi kutafuta mafundi kuja kuiwe-ka sawa. Nataka niyajibu baadhi ya yale ambayo ninayakumbuka, ili yaishe hapa. Sioni sababu ya kuendeleza jambo.

“Nikaulizwa sa-babu za kufu-kuzwa. Sizijui. Mtawauliza we-nyewe walionifu-kuza. Lakini nili-sikia kwa mbali, kwamba walise-ma kwenye kikao kwamba huyu ndiye aliyesema juu ya suala la mafuta na gesi asilia, Muungano huu ni wizi wa mchana.

“Mwenziwe “Sita-ki“? Basi (Inajibu hadhira). Nimeulizwa, je nitakwenda mahakamani? Siendi. Sa-babu kubwa ni kuwa nilichaguliwa kwa

mapenzi na hishima kubwa na wananchi wa Kiembesamaki, sitaki kuwa Mwakilis-hi wa mahakama. Sitaki. Pili, sina pesa ya kuchezea na mshahara ndio ushakatika hivyo. Kisha, ya nini malumbano? Haku-na haja. Waungwana hawalumbani hata kidogo.

“Nimeulizwa na waandishi wa habari, uchaguzi mdogo nitagombea? Sigom-bei. Ya nini kuendeleza machungu ya wananchi wa jimbo la Kiembesamaki? Ya nini tuendeleza malumbano na siasa za matusi? Hapana. Mwaka 2015 nikiwa hai, nikiwa mzima na bado nikiwa nina dhamira na moyo wa kuwatumikia watu, ninaweza nikafikiria vyenginevyo.

“Naulizwa umechukizwa na kufukuzwa? Una ugomvi na CCM? Sina. Na nitak-wambieni kwa nini. Binaadamu daima

mwenye ukweli wa nafsi yake, muungwana hatizami moja. Hili si dogo. Kwangu mimi ni kubwa, tena sana, na ndio maana tu-lipokuwa tunaimba “Sisi Sote“, miye nililia, kwa sababu si dogo hili.

“Miye naitwa Mansoor Yussuf Himid. Nilitaka mwenyewe kuji-unga na Chama cha Mapinduzi. Sikulazimishwa na mtu. Na ki-nyume inavyosemwa nilikwenda mwenyewe kuitafuta hiyo kadi yangu ya mwanzo mwaka 1987. Lakini madhali Mwenyezi Mungu amewapa wanadamu midomo, wana haki ya kusema, basi waa-

che waseme. Ukweli wa nafsi na ukweli wa hali halisi naujuwa mimi.

“Kwa hivyo mimi sina ugomvi na Chama

cha Mapinduzi. Nimejenga historia ya udugu na kifamilia ndani ya Chama cha Mapinduzi. Nina wenzangu mle ambao tumeishi kwa hisani kubwa na mapenzi makubwa. Na mikono ya pole mingi sana iliyonifika mimi kwa watu kunitafuta imetoka humo humo ndani ya CCM. Kwa hivyo, yale kwangu mimi hayatafutika. Nitaendelea kuwaenzi wenzangu na ni-taendelea kuwaheshimu. Maamuzi ya kisiasa ndio maamuzi ya kisiasa kama tulivyosema Sitaki Basi.

“Wenzangu wamenipa, wameniona sifai kuwa miongoni mwao. Ni haki yao kwa sababu ni chao. Ni chao. Miye simo tena. I am a free agent (ni wakala huru). Wapo washaanza kunitafuta: “Tutakufanya mwenyekiti wa chama chetu weye!“

“Lakini kama nilivyosema, mimi mtu huru. Wala wasidhani – wala wasidhani – kama nikiamua kufanya maamuzi yoyote yale yaliyokuwa ndani ya misingi ya kati-ba na sheria, kwamba nitakhofia. Nitafa-nya. Kama kutukana tena hapo, haya tu. Kila mmoja atajijuwa mwenyewe.

“Nikaulizwa utakata rufaa? Mimi sikati rufaa. Sikati rufaa. Ya nini? Tunarudi pale pale, sitaki mwenziwe basi. Wenzio was-hakupima, hawakutaki tena, namkatia rufaa nani? Hapakaliki tena eti pale. Miye siye. Miye si mwenziwao. Kwa hivyo, hapana. Nilimsikia mmoja wao akisema “Sisi na yule yashatuishia“ (huku aki-kung’uta mikono). Na mimi yashaniis-hiya.

“Ninazo hisia zangu kama binadamu, zin-aungana na historia yangu na historia ya wazee wangu. Lakini sasa si pahala pake, si wakati wake. Pengine miezi ya mbele,

miaka ya mbele, tukiwa tumetulizana, kama nitakuwa nalo la kusema, nitalise-ma. Sitokhofia kusema.

“Lakini kwa sasa niseme tu, kwamba na-washukuru sana wenzangu. Mimi naen-delea kuenzi historia ya udugu na matu-maini niliyojenga kule. Ninawashukuru wenzangu wengi sana.

“Tena mtashangaa, mikoa mingi sana ya Bara, viongozi wengi wamenipigia simu, wengine wakiwa wameshangaa, wengi-ne wakiwa na huzuni kubwa, lakini wote lengo lilikuwa ni kunipa pole, kunitaka nitulizane na kumshukuru Mungu. Na Alhamdulillah, nishamshukuru Mwenye-zi Mungu, na ninaendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu Ndiye wa kutegemewa na Ndiye wa kushukuriwa.

“Riziki itatoka kwengine kama ipo. Kama haipo, ndiyo mipango ya Mungu.

“Nikaulizwa na waandishi wengi, je uko salama kwa maana hakuna aliyenitisha? Alhamdulillah. Lazima niseme ukwe-li. Mbali ya kupata faraja na kuungwa mkono kwa wingi, hakuna aliyenitukana, hakuna aliyenibughudhi. Niko salama kama raia wanavyopaswa kuwa salama. Alhamdulillah, namshukuru Mwenyezi Mungu. Kusema vyenginevyo, nitakuwa nasema uongo na miye sitaki kusema uongo.“

Bonyeza hapa uisikilize hotuba kamili:

MAKALA MAALUM

14

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

15

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 9: Zanzibar Daima Online

Naam, Mapinduzi Daima, Zanzibar DaimaNGURUMO LA MKAMA NDUME

Wazanzibari na Watanganyika wana malezi tafauti kuhusi-ana na sura ya Muungano. Ambapo Watanganyika wa-

nauangalia huu kuwa ni Muungano wa Serikali Moja, Wazanzibari wanauangalia kuwa ni wa Shirikisho la Serikali Tatu.

Hata kama si Serikali Moja wala Tatu iliyoandikwa popote katika sheria kuu zinazoongoza nchi hizi mbili, bado tabia, matendo na maono ya watu wa pande hizi yanasomeka hivyo.

Ndiyo maana, si rahisi kwa Mtanganyika kumkuta anajiita kwa jina hilo, maana kwa wengi wao Tanganyika imeshapo-

tea, lakini kila mara utamkuta Mzanzibari akijiita na akijinasibisha kwa Uzanzibari wake.

Huu ni uamuzi wa kimapinduzi kwa pande zote mbili za Muungano. Kwa Tanganyika ni wa kimapinduzi kwa kuwa umeweza kupindua fikra za takriban vi-chwa milioni 40 na kuvifanya viamini kitu kimoja.

Kwa Zanzibar ni wa kimapinduzi kwa kuwa vichwa milioni moja tu, ambavyo ni chini ya asilimia 3 tu ya Watanzania wote na vinavyokaa katika chini ya asil-imia moja tu ya ardhi yote ya Tanzania, vimeweza kuhimili hisia za kutokuridhika

kwa miaka 50 ya Muungano huu.

Lazima tukiri kwamba ni ujasiri tu ndio unaomwezesha mwanadamu kuweza kukaa na fundo la moyo kwa miaka mingi kama hii.

Kubwa zaidi kwetu ni kukiri kwamba kuna kutokuridhika huko kwa upande wa Zanzibar, ndipo tuweze kusaidiana kuya-geuza mateso yetu kuwa faraja. Kukubali huko kutayaendeleza Mapinduzi ya kweli ya Zanzibar kwa kuyapa maana katika maisha ya kila siku na ya kila mmoja wetu.

Mapinduzi hasa ni matokeo ya kutokurid-hika, ambako husababishwa na mgogoro kati ya njia ambazo watu wanaouona ukweli na njia ambazo wangelipenda uk-weli huo Zanzibar inauona ukweli kuwa Muungano huu, katika hali uliyo, ni tatizo kwake na, sasa, ingelitaka kuuona kuwa ni sehemu ya utatuzi wa tatizo hilo.

Huko hakuwezekani ila kwa Mapinduzi; na hayo si mapinduzi ya mapanga na marungu, wala bunduki na mizinga, bali ya fikra na mkakati. Haya ni Mapinduzi ambayo yanatakiwa yapitie hatua tano za matayarisho kwa ajili ya mapinduzi ya kuporomoka kwa mfumo mkongwe, ya kuharibika kwa mahusiano makon-

N A M O H A M M E D

G H A S S A N I

17

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

16

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

Page 10: Zanzibar Daima Online

gwe, ya kujenga mahusiano mapya; na ya kuuimarisha mfumo mpya.

Ama kwa kujijua au kutojijua, tayari tu-meshapita kipindi cha kwanza cha ma-tayarisho kwa ajili ya Mapinduzi, kipindi ambacho kilitawaliwa na woga wa wa-nanchi na mateso ya watawala.

Kilikuwa ni kipindi ambacho, ingawa palikuwa na kiwango kikubwa cha ku-tokuridhika na jinsi Muungano huu una-vyoikandamiza Zanzibar, si Wazanzibari wengi waliothubutu kueleza kutokurid-hika huko. Bali hata wale wachache wali-othubutu, walisemea vibuyuni ambako ama walichokisema kilimalizwa huko huko au wenyewe walimalizwa kwa njia zao za kumalizana.

Sasa tulipo, kwa maoni yangu, ni ka-tika hatua ya pili ya Mapinduzi, ambapo mfumo mkongwe wa Muungano usio na maslahi kwa Zanzibar unaelekea kuporo-moka.

Kawaida kipindi hichi ni matokeo ya ku-potea kwa uongozi ndani ya kundi la wa-tawala, ambapo mgawanyiko wa makun-di humfanya kila mmoja kutenda vyake. Mara nyingi hatua hii haifikiwi mpaka aji-tokeze kiongozi anayejiona kuwa mwa-namageuzi kutaka kuunusuru mfumo

mkongwe; na akafeli.

Mwanasiasa wa Kifaransa na mtaalam wa uchumi Anne-Robert-Jacques Tur-got na mwanasiasa na waziri mwenzake Jacques Necker walijaribu kuunusuru ufalme wa Ufaransa kabla ya mwaka 1798 na Waziri Mkuu wa zamani wa Urusi Pyotr Arkadyevich Stolpyin alifanya jaribio kama hilo nchini Urusi kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia, lakini wote walishindwa.

Huo huwa ni wakati ambapo, kutokana na mtikisiko wake, mfumo mkongwe huwa kama tayari umeshakufa kitambo, lakini kwa kuwa watu wanaothubutu kuyathibitisha mauti yake hawajatokea, basi huendelea kuwepo tu ukiendea up-epo na kudura ya Mungu.

Nabii Suleiman (A.S) alikuwa amefari-ki siku nyingi, lakini watumishi wake waliendelea kutumika wakidhani bosi wao amekaa kitini akiwasimamia, hadi mchwa alipokuja kuila fimbo yake. Kuna watu waliojua kuwa Awamu ya Tatu ya Serikali ya Ufaransa imeshakufa tangu mwaka 1934, lakini maziko yake yalifany-wa mwaka 1940.

Wazo ninalojaribu kuliwasilisha hapa ni kwamba, sasa umefika wakati wa yale

yale matakwa ya Wazanzibari, kama yalivyoelezwa kupitia Ripoti za Tume za Jaji Nyalali, Jaji Kisanga na sasa kupitia Tume ya Jaji Warioba ndiyo yatakayouon-goza Muungano wa Tanzania na wala sio Katiba hii ya Serikali Mbili ambayo Chama cha Mapinduzi inadhani kwamba itabakia milele.

Na viashiria vya utabiri huo vimeanza kujengeka sasa. Changamoto iliyo mbele yetu kwa sasa ni ukweli kwamba hatua za tatu, nne na tano zinakuja kwa kasi na, yumkini, hatuna matayarisho mazuri kuzikabili.

Kwa mfano, hatua ya tatu, ambayo ni ya kuharibika kwa mahusiano makon-gwe, kwa mintarafu ya kuharibika kwa muundo wa sasa wa Muungano, ina ma-tatizo yake. Mojawapo ni kwamba, wenye maslahi na mahusiano haya hivi sasa, wameanza kutumia nguvu zao za ziada kuzuia yasiharibike.

Na ingawa, kutokana na matakwa ya kiwakati hawatafanikiwa, lakini kama ilivyo kawaida ya mti mkubwa unapoan-guka, husababisha maafa kwa pale unapong’okea (panaweza kuchimbika shimo kubwa) na kule unakoangukia (unaweza kuelemea nyumba au wapita njia na kuwajeruhi kama si kuwatoa roho zao).

Lakini mara tu kipindi hiki kinapoanza, hutanguliwa haraka sana na kipindi cha ujenzi wa mahusiano mapya. Huu ni mfano wa ujenzi wa nyumba mpya juu ya kongwe, ambapo mwenye nyumba huen-delea kujenga nyumba mpya, huku yeye akiwemo ndani.

Huvunja kiambaza kimoja kwanza na kusimamisha kipya mahala pa kilicho-vunjwa, kabla hajakwenda katika kiam-baza chengine. Ingawa huweza kuchukua muda mrefu kwa nyumba kukamilika, kutegemea na uwezo wa kifedha, kiu-fundi na mazingira ya ujenzi. Lakini ni staili ya yenye faida moja kubwa: hakuna wakati ambapo mwenye nyumba analaz-imika kulala nje, hata kama katika kipindi cha ujenzi huwa hakai katika makazi ma-zuri sana.

Hapo ndipo, kwa maoni yangu, nchi hii inapoelekea. Muungano huu utaanza kuvunjika na mpya kuundika kwa wakati mmoja. Ninachoeleza ni kwamba tunak-wenda katika kipindi ambacho hatutas-ema kuwa hatuna Muungano moja kwa moja, lakini pia hatutakuwa na Muun-gano huu.

Mwisho tutaingia kwenye kuimarisha mahusiano mapya tutakayoyajenga. Uk-weli ni kwamba Zanzibar na Tanganyika, bali pamoja na mataifa mengine yaliyo jirani, yataendelea kuwa na mahusiano dumu daima. Lakini tafauti na sasa, ma-husiano yajayo kwa sababu ya Mapin-duzi haya, yatakuwa na sura nyengine na matakwa mengine.

Hata hivyo, tuzinduke Wazanzibari, kwamba jambo pekee linaloweza kutu-fikisha hapo ni moja tu. Nalo ni mkono mmoja kuyashikilia Mapinduzi yetu na mwengine kuishikilia Zanzibar yetu. Yaani isiwe tu Mapinduzi Daima, lakini iwe pia Zanzibar Daima; maana Mapin-duzi Daima hayana maana ikiwa hatuna Zanzibar.

NGURUMO LA MKAMA NDUME

19

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

18

BOXED CREATIVE MAGAZINE TEMPLATE 03>

WWW.YOURDOMAIN.COM ISSUE 03 - WINTER 2012>

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03

Page 11: Zanzibar Daima Online

Kukua kwa kasi kwa vuguvu-gu la watu wa Zanzibar la kutaka mamlaka kamili ndani ya Muungano kunaonekana

kukitia kiwewe chama cha CCM. Hivi sasa viongozi wake, badala ya kuji-bu hoja zinazotolewa juu ya suala hilo, wameamua kuropokwa matusi ya nguoni na kujipapatua kama ana-vyofanya farasi anapokuwa katika sakaratil maut ( anapokuwa anakata roho).

Hali hii ya kusikitisha na inayoche-fua roho na ambayo ni kinyume na ustaarabu wa Wazanzibari uliojen-geka tokea dahari na enzi kutokana na misingi ya dini, utamaduni, silka na khulka ilionekana katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofa-nyika mwishoni mwa wiki mjini Un-guja.

Baadhi ya viongozi wa CCM wa-liopanda jukwaani ka-

tika uwanja unaoitwa Kombawapya uliweza kuwalinganisha na komba waliolewa kwa kutamka maneno ya kashfa ambayo ni nadra kuyasikia hadharani kutoka katika mdomo wa Mzanzibari, awe nyumbani au nje.

Waliokuwa hasa wakiongo-za katika matusi ya nguoni ni viongozi wenye nyad-hifa za juu katika CCM na Jumuiya yake ya Vijana (UVCM), hasa Mwenyekiti mpya wa taifa wa UVCM Sadifa Juma Kha-mis na Mwe-nyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini, Bo-r a f y a

MATUSI YA ‘KOMBA WAPYA’ WA CCMLA KUSEMWA LISEMWE

N A S A L I M S S A L I M

20

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

21

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 12: Zanzibar Daima Online

Silima.

Wawili hao waliugeuza mkutano huo kuwa darasa la masuala ya kaumu Lut na bila ya kuona haya wala vibaya waliwahu-sisha baadhi ya viongozi na wanasiasa maarufu wa chama cha CUF, wakiwemo waliokuwemo ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na vitendo vya liwat.

Matusi hayo mazito yaliojaa uhuni pia ya-liporomoshwa kwa ahli na marafiki wa vi-ongozi hao wa CUF, kama vile waliokuwa wakitamka uchafu huo hawakuzaliwa na mwanamke.

Baya zaidi na ambalo linakwenda kinyu-me na maadili na uwajibikaji katika taalu-ma ya tasnia ya habari matusi haya hay-akukatishwa na yaliendelea kutangazwa moja kwa moja na baadhi vituo vya tele-visheni na radio.

Watu wengi waliokuwa wakifuatilia ma-tangazo haya majumbani na hata sehe-mu zenye watu wa rika tafauti walilazimi-ka kuzima radio na televisheni zao.

Mmtu mmoja aliyehudhuria mkutano huo ambaye naye alilazimika kuondoka baada ya muda alisema: ’’Siku hii itaingia katika kurasa chafu za historia ya Zanzibar. Ili-kuwa aibu , fedheha na ushenzi uliokithiri kipimo chochote kile cha unyama“.

Kinachoshangaza walipokuwa watu hawa wakitukana viongozi wenzao waliopo we-nye hiyo sehemu ya wageni wa heshima walitulia kama kunguru waliotiwa maji na hakuna aliyethubutu kuwkemea:“ Hivyo sivyo“.

Wengine waliokuwepo hapo wakiwa na watoto na wajukuu zao nao walishanga-za watu kwa uamuzi wao wa kufurahia na kushangilia matusi.

Askari polisi waliopelekwa hapo kuha-kikisha mkutano unafanyika kwa mujibu wa sheria na hapatolewi kauli za kuha-tarisha amani au kuchochea fujo walikaa kimya na hakuna hatua yoyote iliyochu-kuliwa, wakati wa mkutano wala baada ya mkutano, dhidi ya hao waliokuwa wakib-wabwaja matusi.

Habari za uhakika zimeeleza kwamba siku iliofanyika mkutano ule viongozi wa juu wa CCM/Zanzibar na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, walikuwepo Zanzibar.

Kinana ambaye huelezwa kama ’‘muung-wana aliyetimia“ aliondoka Zanzibar siku ya pili yake bila ya kutoa tamko la kulaani au kukemea uhuni ule. Hii imetoa tafsiri kwa baadhi ya watu kwamba walichofa-nya wahuni wale kimepata baraka ya vi-ongozi wa juu wa chama chao.

Baadhi ya wakuu wa Jeshi la Polisi Zanzi-bar wamekuwa na kigugumizi na wengine wamejifanya mabubu wanapoulizwa kwa nini wanaruhusu uhuni wa aina ile na kitu gani kinachowazuia kuhakikisha sheria zilizopo zinachukua mkondo wake katika kuwawajibisha kisheria watu wanaotuka-na watu hadharani.

Baadhi ya wazee wa Zanzibar ambao wa-lishuhudia mikutano ya chama kilichoju-likana kama cha Haki za Binaadamu kili-chokuwepo Zanzibar kabla ya Mapinduzi na kilichopata umaarufu kwa lugha yake ya matusi wanasema matusi yaliokuwa yakisikika kwenye mikutano ya Haki za Binaadamu ni kichuguu tu kwa matusi ya-liosikika hivi karibuni.

Wadadisi wa mambo ya kisiasa wanau-liza : Je, Polisi ingelikaa kimya na kufunga pingu zake kama matusi yale yalielekezwa

kwa viongozi wa CCM?

Watu wengi waliohojiwa wanasema usi-ku ule ule yangefunguliwa mashitaka dhi-di ya walioyatamka matusi, wale walio-wakaribisha juu ya jukwaa na walioomba kibali cha kufanyika mkutano.

Uchunguzi wa jarida hili umebaini kuwa mmoja wa waliofurutu ada ya kutoa ma-tusi siku ile amekuwa akitibiwa baada ya kila kipindi kwa matatizo ya akili katika hospitali ya wagonjwa wa akili iliopo Zan-zibar.

Nini kilichotokea hata akaweza kukabidhi-wa nafasi ya juu ya uongozi wa UVCM hivi karibuni ni swali ambalo labda viongozi wa CCM wenyewe watalijibu.

Lakini jibu linalosubiriwa kwa hamu ni lile la swali linaloulizwa kwa shauku kubwa, nalo ni: Je, CCM itawachukulia hatua watu

hawa au chama hicho kina ilani mpya ya uchaguzi ambayo inashajiisha makada wake kutukana watu?

Kwa sasa kiwewe hiki cha kutaka watu wasishindane kwa hoja bali kwa matu-si na kuvifanya viwanja vya mikutano ya kisiasa viwe maeneo ya kufanya utafiti wa kuandika kamusi la matusi la lugha ya Kiswahili kinaipeleka Zanzibar pabaya.

Wapo pia wanaouliza je, CCM imebadi-li jina kutoka Chama cha Mapinduzi na kuwa Chama cha Matusi au hayo matusi ndio mapinduzi yanayokusudiwa?

Historia haitawasahau wahuni hawa wanaoshabikia kutukana watu ovyo ma-tusi ya nguoni na wale wote wenye uwe-zo wa kuwadhibiti na walioamua kuwa-nyamazia.

LA KUSEMWA LISEMWE

22

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

23

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Natoa pongezi zangu kwako binafsi pamoja na waandishi wenzio mliojitolea kulisimamisha Zanzibar Daima OnLine. Matumaini yetu, Wazanzibari, ya siku nyingi yametimia.

Nimepata fursa ya kuyapitia majarida yote mliyotoa. Naamini kwa dhati kabisa Wazanzibari watalikaribisha kwa moyo mkunjufu. Mchangayiko wa mada katika toleo la pili ni mfano mzuri wa kuliendeleza.

Nilifurahi kuyasoma makala ya mwandishi wenu wa michezo. Alinikumbusha wakati wa utoto wetu pale Abdul Majham akin'gara katika timu ya Taifa na Vikokotoni. Naam yeye na Marhemu Shioni Mzee walikuwa wakicheza kama roho zao "zimeunganishwa" pamoja. Akiwa na mpira mmoja anajua wa pili atampasia vipi.

Wakati huo mabeki ndio akina Mtumwa Mwenda (Police), Chifu (Miembeni), Abdulla Azan (Police) nk. Tunatarajia kusoma mengi ili vijana wetu wafahamu tunakotoka na sisi wazee kukumbushana yaliyopita. Kwa pamoja tutaweza kuendelea kuijenga Zanzibar ya wote.

A. Abdalla - Denmark

Kopenhagen, Denmark

Heko Ahmed Rajab

Page 13: Zanzibar Daima Online

Uchaguzi mkuu uliofanywa Zimbabwe mwishoni mwa Julai ulihitimisha mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa

kama ulioko Zanzibar,ingawa huo si wa mpito kama wa Zimbabwe kwa vile umo ndani ya Katiba. Uchaguzi huo wa Zimbabwe una somo kwa Zanzibar.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zim-babwe ,iliyoundwa baada ya mzozano wa uchaguzi wa 2008, ilidumu kwa miaka mitano hadi uchaguzi wa Julai licha ya misukosuko mingi.

Katika uchaguzi wa Julai Robert

Gabriel Mugabe aliibuka mshindi akipata asilimia 61 ya kura na chama chake cha ZANU-PF kikashinda the-luthi mbili ya viti vya bunge. Ushindi huo uliwashangaza wengi ndani na nje ya Zimbabwe.

Wengi wanaamini kulipita mizen-gwe iliyoendeshwa kitaalamu.

Uchaguzi wa Zimbabwe um-ezusha swali: wengine wanaji-funza nini ?

Katika nchi nyingi migogoro ya kisiasa in-ayoibuka baada ya kufanywa chaguzi

husababishwa kwa sehemu kubwa na

Tume ya Uchaguzi ku-tokuwa huru.

Tatizo hili lilikuwa donda ndugu katika chaguzi zote

za Zanzibar tangu ulipoan-za mfumo wa demokrasia ya

vyama vingi 1992.

Katika chaguzi zote zilizofanywa Zanzibar chini ya mfumo huo wa

vyama vingi Tume ya Uchaguzi (ZEC) ilikuwa ikikosa uwiano kati ya

wadau wahusika na ilikuwa mateka

Tumejifunza nini kutoka

Zimbabwe

Ingawa Wazanzibari tumekubaliana kuwa na maridhiano na tumeona haja ya kuondoa uhasama wa kisiasa, bado vizingiti vipo

wa chama kinachotawala cha CCM.

Kuna dhana kwamba kwa vile mwenyekiti wa Tume huteu-liwa na Rais basi daima huwa mtiifu kwa Rais aliyemchagua na hawi mtiifu kwa sheria na kiapo alichoapa cha kuiheshimu na kuitii sheria hiyo.

Ingawa Wazanzibari tumekubaliana kuwa na Maridhiano na tumeona haja ya kuuondoa uhasama wa kisiasa, bado vizingiti vipo:

- Mizengwe na wizi wa kura;

- Tume kuwa ndiyo yenye kauli ya mwisho na uamuzi wake kutoweza kup-ingwa;

- Wanaoshindwa kutoweza kupinga matokeo ya uchaguzi wa Urais mahaka-mani;

- Na hata Jumuiya za kikanda na bara la Afrika kama Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Muungano wa Afrika (AU) ambazo viongozi wake

wamekuwa na tabia ya kushindwa kue-lezana ukweli na kuendelea kulindana, kukubaliana na matokeo.

Haya Zanzibar ina uzoefu nayo tangu 1995 .

Ni takriban miaka mitatu sasa tangu uchaguzi uliopita. Mbali na kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) baina ya CCM na CUF, hakuna hatua kubwa ili-yochukuliwa na Rais Ali Mohamed Shein kuonyesha kuwa kweli amenuia kuiona Zanzibar inafungua ukurasa mpya. Ahadi alizotoa wakati alipozungumza Hoteli ya Bwawani siku yalipotangwa matokeo ya uchaguzi uliopita,kuhusu dosari ziliopo hakuzitekeleza. Alitamka,

JAMVI LA BARAKA

N A M O H A M E D A B D U L R A H M A N

24

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

25

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 14: Zanzibar Daima Online

nikimnukuu vyema: “ Nimeyasikia na kwa kweli ni mazito.Nitazungumza na wenzangu ili kuyarekebisha. “ Ha-tuna uhakika ikiwa alizungumza na wenzake lakini hadi sasa ni wazi kuwa hakuyarekebisha.

Kwa sehemu kubwa mazingira yalio-sababisha utata miaka ya nyuma bado hayajabadilishwa.

Uteuzi wa wakuu wa mikoa, wa wilaya na wa nyadhifa mbalimbali Serikalini hadi leo bado unazingatia u-CCM. Zaidi ya yote Tume ya Uchaguzi bado inateuliwa pasina kuwepo uwiano na hali ya kuwari-dhisha wadau wote wanaokhusika CCM na CUF na hata vyama visivyo na uwakili-shi katika Baraza la Wawakilishi lakini vilivyosajiliwa rasmi kuwa ni vyama vya kisiasa.

Aidha wale wasio wana CCM wanaende-lea kunyimwa vitambulisho kuanzia vya ukaazi , vya Uzanzibari hadi vya kupigia kura. Si hasha wakati wa kukaribia ucha-guzi ujao litaongezeka na la daftari la ku-pigia kura.

Rais Shein ameunda Tume mpya hivi karibuni kuchukua nafasi ya ile iliomaliza muda wake mwezi Januari mwaka huu na iliyoundwa na mtangulizi wake Amani Karume 2008. Kazi nzuri kubwa iliofany-wa na Tume hiyo ilikuwa ni kusimamia kura ya kwanza ya maoni katika historia ya visiwa hivi kuhusu uundwaji wa Seri-kali ya Umoja wa kitaifa . Lakini katika ripoti yake ya kutathmini utendaji wake katika kipindi cha miaka mitano, Tume hiyo ilieleza kwamba ilishindwa kukamili-sha kazi ya kupitia upya mipaka ya ma-jimbo ya uchaguzi.

Katika mkutano mmoja wa chama chake

huko Pemba mwezi mmoja uliopita, ka-tibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamadi aliionya Tume mpya dhidi ya fununu zilizozagaa kwamba ina mpango wa kuyapunguza majimbo ya uchaguzi Pemba hadi kufikia 14. Pindi hilo likiwa na ukweli bila shaka lit-atafsiriwa kuwa sehemu ya mizengwe ya mapema kabla ya uchaguzi wa 2015.

Yote hayo hayayafanyi mazingira yawe mazuri na ni kikwazo cha maende-leo, haki za binaadamu na demokrasia .Madosari kama hayo ndiyo yaliyoisibu demokrasia nchini Zimbabwe. Alau wa-jumbe wawili wa Tume ya Uchaguzi Zim-babwe walijiuzulu baada ya kutangazwa matokeo. Hatua yao ilikuwa na ujumbe mzito.

Hapana shaka wahafidhina wa Zanzibar, wapinga mageuzi, wapinga maendeleo na wasioitakia mema wamo mbioni. Miz-engwe na hila za aina zote ndio nguzo zao za kuhakikisha wanaendelea kuwepo kwenye madaraka .

Ni matarajio ya Wazanzibari kwamba uchaguzi wa 2015 hautaandamwa na jin-amizi la Zimbabwe na kina Mugabe.

Maridhiano ndiyo dira lakini dira hiyo itatimia tu pindi hitilafu zilizokuwa kik-wazo miaka mingi zitaondolewa. Hayo yanapaswa kuanza kufanyiwa kazi sasa.

Ikiwa wanasiasa na watunga sheria (Wawakilishi) wamelewa madaraka na wamelala fofofo, umma ambao ndiyo uliowaweka madarakani una jukumu la kuyapigania kwa nguvu zote, ili 2015 Zanzibar ipige hatua nyingine mbele baada ya Maridhiano yalioidhinishwa na asilimia 66 ya umma wa Wazanzibari.

JAMVI LA BARAKA

wa kujua namna ya kuitumia tu teknolojia hiyo. Watahitaji pia wawe na uwezo wa kujua namna ya kuisarif hiyo teknolojia na pia waidhibiti vilivyo lugha ya teknolojia hiyo.

Hiyo si kazi ndogo kwa sababu kila uchao kunapatikana maendeleo mapya katika teknolojia hiyo na lugha yake pia inabadi-lika — au kama haibadiliki sana — basi angalau hukua kulingana na maendeleo mapya yanayopatikana.

Kuna natija moja kubwa ambayo walimu wa Zanzibar wataipata. Nayo ni ku-wawezesha wawe na chombo kita-choweza kwa kiwango kisichofikiriwa kabla kuwa na fursa za kuwapatia wana-funzi elimu iliyoongezeka na pia itawapa walimu wao fursa ya kujiendeleza katika kazi zao za ualimu.

Kwa mujibu wa takwimu nilizoziangalia kwa haraka haraka kasoro ya asilimia 20 ya skuli 298 zilizo katika wilaya 10 za Un-guja na Pemba zina kompyuta. Hii ni ida-di ndogo sana. Na inazidi kua ndogo kwa vile kila skuli kati ya hizo ina kompyuta moja au mbili tu.

Inasikitisha zaidi kusikia kwamba ni skuli 13 tu, kama asilimia 5 ya skuli zote, zinaz-owafunza wanafunzi masomo ya teknolo-jia ya mawasiliano na kasoro ya asilimia 3 ya walimu wanatumia teknolojia ya ICT kufundishia.

Takwimu zinazidi kusikitisha ukisikia kwamba miongoni mwa walimu 7,534, ni 268 tu, kasoro ya asilimia 5 walio-

fundishwa namna ya kutumia ICT na we-nye uwezo wa kuitumia teknolojia hiyo. Miongoni mwa skuli 47 zenye kompyuta ni 17 tu zenye waratibu wa teknolojia ya ICT.

Na si kompyuta zote zilizo katika maskuli zenye kufanya kazi. Nyingi zimeharibi-ka. Ukienda kutembelea skuli utazikuta kompyuta zilizojaa mavumbi kwa vile ha-zitumiwi.

Vyombo vingine vyenye kusaidia katika masomo ya ICT navyo pia utavikuta havi-fanyi kazi. Kwa mfano, mitambo ya kutia hewa baridi katika vyumba vya kompyuta haifanyi kazi. Takriban asilimia 73 ya skuli za Unguja na Pemba hazina umeme. Kama asilimia 3 zinatumia majenereta na asilimia 2 ya skuli zinapata nguvu za umeme kutoka miale ya jua.

Kwa hakika, naitoshe nikisema kwamba takwimu kuhusu nyenzo za kufundishia masomo ya teknolojia ya mawasiliano zi-nahuzunisha.

Nimegusia juu ya dhima ya Wizara ya Elimu katika kunyanyua somo la teknolo-jia ya habari na mawasiliano visiwani Zanzibar. Lakini ninajua kwamba tuna magwiji wa fani hii walio ughaibuni na wengine waliostaafu na waliorudi nyum-bani. Nadhani kuna haja ya kuzingatia jinsi gani watavyoweza kuchangia ili ku-saidia elimu hii muhimu iweze kupenya kwa urahisi katika skuli zetu za Unguja na Pemba.

Inatoka Uk. 09

Ili Zanzibar iendelee haitaji ICT

26

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

27

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 15: Zanzibar Daima Online

WARAKA KUTOKA BONN

Bado Mansoor ana uhai wa kisiasaKufukuzwa Mansoor Yussuf Himid,

mwakilishi wa Kiembesamaki, ku-toka Chama cha Mapinduzi (CCM),

ni jambo la kawaida. Wazanzibari wa-sishangae. Iko mifano mingi kama hiyo duniani.

Swali ni: vipi chama cha CCM kimepiga moyo konde na kumtema mwanakinda-kindaki huyo aliyekitumikia chama kwa muda mrefu, na aliyewahi kukamata nyadhifa kadhaa za uwaziri serikalini?

Jina la Mansoor kwa Zanzibar si kama langu; lake linaambatanishwa moja kwa moja na Mapinduzi ya nchi hiyo ya Janu-ari 12, 1964. Usiku wa kuamkia tarehe hiyo baba yake, mwanamapinduzi Yus-suf Himid, alikuwa miongoni mwa watu wa mstari wa mbele walioiteka kambi ya kijeshi ya Ziwani, kitendo kilichosaba-bisha Mapinduzi hayo yafanikiwe.

Yussuf Himid alikuwemo katika Baraza la Mapinduzi la mwanzo na baadaye akawa mkuu wa mwanzo wa jeshi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar akiwa na cheo cha ubrigadia. Binafsi, kwa Manso-or kuyakana ‘Mapinduzi Daima’ ni sawa na kumkana marehemu baba yake. Hat-hubutu kamwe.

CCM, lakini, imehisi haiwezi kumstaha-milia Mansoor, licha ya jina lake zito lenye kuvutia. Lakini sifikiri kwamba sa-babu hasa ya kufukuzwa Mansoor ni ile iliotolewa Dodoma kwamba amekwenda kinyume na ilani ya CCM yenye kutaka Tanzania iendelee na mfumo wa sasa

wa Muungano wa serikali mbili, ambapo yeye Mansoor anataka Muungano wa serikali tatu, Zanzibar ikiwa na mamlaka kamili. Mansoor ni muumini wa Muun-gano, lakini ulio chini ya msingi wa kuh-eshimiana, usawa na haki.

Wako wanasiasa kadhaa ndani ya CCM huko Tanganyika na Zanzibar wenye mawazo sawa na ya Mansoor, lakini hawajapewa kadi nyekundu au hata ya manjano. Makamu mwenyekiti wa CCM, Philip

Mangula, amekwenda mbali zaidi na ku-sema yeye ni muumini wa serikali MOJA ya Muungano. Tamko hilo lilinyamaziwa kimya ndani ya CCM, mshipa watu hau-jawapiga.

Lakini sababu hasa ninayoiona mimi ni kwamba Mansoor ana bashasha ya kimaumbile, anamiliki haiba ya baba yake. Kwake yeye ‚Mapinduzi Daima’

ni karata ya kutaka kuyapindua daima mawazo ya Wazanzibari wasikubali fikra mgando. Chama cha Wananchi (CUF) siku hizi nacho pia kinalipiga baragumu linalo-nadi Mapinduzi Daima. Hoja ya Mapinduzi Daima yaonyesha sasa imewaunganisha Wazanzibari na kuwa vuguvugu linalo-geuka kuwa wimbi lisilozuilika kutaka nchi yao iwe na mamlaka kamili.

Pia Mansoor yaonyesha ana ule moyo wa kujiamini, sifa aliyokuwa nayo Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid

Karume, kwamba Wazanzibari wanataka na wana uwezo wa kujiamulia wenyewe mambo yenye maslahi nao, tena bila ya kuwajali watu wengine, ikiwa ni wa mado-la makuu au madogo.

Hofu ya CCM ni kwamba lau Mansoor angeachiliwa ndani ya chama hicho aen-delee kutetea anachokiamini angeweza kuzidi kuwaambukiza kifikra baadhi ya viongozi wengine chamani.

CCM hivi sasa iko mashakani huko Tan-

N A M O H A M E D A B D U L R A H M A N

28

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

29

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 16: Zanzibar Daima Online

ganyika kutokana na upinzani unaopata nguvu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kwa hivyo, CCM haiko tayari kuachia safu zake Visiwani zikiwa zinadhoofika zaidi. Kumfukuza mwanasiasa huyo ni jaribio la chama kutaka kujinusuru. Hiyo ni haki ya cha-ma chochote, hata cha mpira, seuze tena chama kikubwa cha kisiasa.

Hilo, kwa bahati nzuri, Mansoor ameli-tambua, na ndio maana amewataka Wa-zanzibari wote waheshimu mawazo ya watu wanaotafautiana nao. Malumbano hayafai, tena hasa katika wakati huu mu-himu utakaoamua mustakbali na hatima ya Zanzibar.

Kuna wenye kufikiri kwamba ingekuwa vizuri Mansoor angejiengua mwenyewe kwanza kutoka CCM kabla ya kungojea afukuzwe. Yaonyesha hajataka kulipa fadhila nyingi alizofanyiwa na chama hicho kwa kujigeuza kuwa „msaliti“ wa chama hicho na kuwafungulia njia wazi wale watu wasiokubaliana naye wazidi kumsakama kisiasa.

Mwishowe ilidhihirika wazi, na kama ali-vyoungama mwenyewe, kwamba kwake yeye Zanzibar ni muhimu zaidi. Zanzibar KWANZA na chama baadaye, ndio kau-li mbiu yake. Ninahisi kwamba chama kumtema kabla ya yeye kukitema ku-memjengea sifa zaidi. Ni taabu sasa yeye kutuhumiwa kwamba amekisaliti chama.

Uamuzi wa Mansoor kutokata rufaa mahakamani na kuupinga uamuzi wa CCM wa kumfukuza unamaanisha ame-kubali kupoteza kiti chake katika Baraza la Wawakilishi. Uamuzi wake huo huenda ukang’arisha zaidi nyota yake ya kisiasa katika siku za mbele. Kwa vyovyote , kwe-li ametumwa huko Barazani na wapiga kura wa Kiembesamaki, lakini isisahauli-ke kwamba amekwenda huko pia kupitia tiketi ya chama cha CCM. Ilivyokuwa sasa CCM haina imani naye, kwa hivyo amefa-nya uungwana pia kutobisha kuenguliwa kutoka Baraza hilo. Hapa amechangia vi-zuri kuendeleza moyo wa kustahamiliana kisiasa Visiwani Zanzibar.

Lakini, hata hivyo, ilivyokuwa Katiba mpya ya Tanzania inayotarajiwa huen-da ikaruhusu wagombea binafsi katika uchaguzi, mimi sitoshangaa kumuona tena Mansoor akirejea katika ulingo wa siasa, na wala sitostaajabu kukiona cha-ma kingine kikimuomba agombee uwaki-lishi kwa tiketi ya chama hicho.

Mansoor Yussuf Himid yu bado kijana. Anaweza akawa na mustakbali mpana katika siasa za Zanzibar, pindi akitaka. Yu huru, kama anavyoamini yeye kwamba Wazanzibari wote pia ni huru katika ku-waza na kuamua. Siasa si mama yao. Ni mama tu ndiye asiyeweza kumkana mwanawe na ni mwana tu asiyeweza kumkana mama yake.

WARAKA KUTOKA BONN

30

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

31

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Uzanzibari wetu ni kiungo cha kuzishinda fitina za mahasidi

‘Ni upuuzi kuwagawa watu kwa kutafuta asili yao, hasa kwa Wa-zanzibari ambao karibu wote wa-mechanganya damu zao hata ha-wajitambui wenyewe. Mtu kujiita kabila gani, au kabila gani, ni kwa mapenzi yake, ikiwa ukabila ndio mila. Lakini Waislamu wame-katazwa kujifadhilisha kwa mak-abila na asli. Na ustaarabu unat-wambia hivyo hivyo. Mmarekani mweusi, mwekundu, mweupe na

wa manjano wote ni Wamarekani. Kadhalika Waingereza, na kadha-lika Waomani au Wamisri, au Wa-hindi. Huku kuchanganyika kwe-tu kumetunufaisha sana, katika malezi, na tabia, na maingiliano. Uzanzibari wetu ni kiungo am-bacho kitaweza kushinda fitna za mahasidi waliotugawanya ili wat-uteke, na watutawale. InshaAllah hatimaye mahasidi watahayari.’

DonDoo kutoka kitabu ‘Mzanzibari asiMlia HaDitHi Yake’ kilicHoanDikwa na sHeikH sHaaban saleH FarsY.

Soma Jarida la ZanZibar daima online kila wiki mbili

Unaweza kutangaza biashara yako kupitia Zanzibar Daima Online, jarida la kila wiki mbili lenye wasomaji wengi wenye kuzungumza lugha ya Kiswahili duniani kote.

Page 17: Zanzibar Daima Online

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinapita katika kipindi kigumu sana. Wengi wa viongozi wake wana uchovu wa ki-

wango cha juu.

Kadiri ninavyopima staili zao za ku-tenda, nataasaf kwamba wamecho-ka kufikiri na hawatendi tena kwa muala. Hawatendi baada ya kuwa wamefikiri. Wanatenda pasina kuta-fakari.

Tatizo zaidi hutokea inapoonyesha kuwa siku hizi viongozi wakubwa wa chama hichi wanatenda bila ya ku-fikiria athari za wanachokitenda.

CCM imekuwa ni chama tafauti na asili yake. Zamani ukiona viongozi wake wamefanya jambo au wame-amua jambo fulani, basi huwa wali-ifikia hatua hiyo baada ya kuangalia kila hali.

Wananchi walizoea kuwaona vion-gozi wa chama hichi wakituliza akili

KAULI YA MWINYI MKUU

N A J A B I R I D R I S S A

zao kwa wakati wote. Hichi ni chama ki-ongozi kwa hivyo haikuwa rahisi kukikuta kimekurupuka.

Kwa vile kilikuwa chama kiongozi enzi zile, vyama vya upinzani vilihitaji kujipan-ga vilivyo kumudu kujibu kauli zake. Hali-kuwa jambo rahisi kujibu hoja ya viongozi wa CCM. Wakitafakari.

Kweli, zile zilikuwa zama za aina yake; na Rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi, wakati akiwa Ikulu, alikuwa akipenda sana kusema “kila zama na kitabu chake.”

Zama za viongozi wa CCM kutenda kwa utulivu zimekwisha kabisa. Na nionavyo zimepita kama upepo, si rahisi kurudi tena. Zilikuwa ni zama maalum zile, na kitabu chake kilifaa tu kwa wakati ule. Si leo.

Siku hizi viongozi wa CCM wanaonekana wakiamua mambo bila ya nadhari. Siku hizi watu hawa wanaamua mambo bila ya kuangalia athari za maamuzi yao. Ma-tokeo yake, kila wanapotoa uamuzi, wa-najikuta wameadhirika.

Maamuzi mengi ya CCM siku hizi huwa hayatekelezeki. Haichukui muda mrefu CCM wakishaamua kitu, kinawarudia wenyewe. Ubaini kuwa viongozi wa CCM wametenda makosa tena yakawa ni ma-kosa ya ovyo. Zamani haikutarajiwa kuwa hivyo, siku hizi ndiyo kawaida. Kila uchao, viongozi wa CCM wanakosea katika wa-nayoyatenda.

Nitoe mfano hai hapa. Kamati ya Marid-

hiano inayoongozwa na Mzee Hassan Nassor Moyo, ilianzishwa 2009. Miaka mitano hivi imeshapita tangu ianzishwe kamati hii yenye wajumbe sita mchan-ganyiko – kutoka CCM na kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Kamati hii ilianzishwa kutafuta namna ya kuiondoa Zanzibar katika siasa za chuki, za fitna, za uhasama, za ugomvi, siasa za inda na za kuchusha. Kupitia kamati hii, siasa za kibaguzi zimepita.

Katika muda wote huo, ingawa mengi yamefanywa ili kuidhoofisha, hatujawahi kuwasikika viongozi wa CCM wakifun-gua midomo yao kuilia njama Kamati ya Maridhiano. Tena, wakati ule, wakiogopa hasa kutenda jambo lolote ambalo lingei-ingiza kamati hii kwenye mtihani. Vion-gozi wa CCM wakihofia kuadhirika.

Lakini leo, viongozi hao wanahoji maamuzi ya Kamati ya Maridhiano. Inau-lizwa, inahojiwa, inasakamwa, inasham-buliwa, inaguswa watakavyo CCM. Ina-julikana namna walivyokuwa wanajaribu kuihangaisha kamati hii isitekeleze mi-pango yake kwa utuo.

Kamati ya Maridhiano imefika pahali inavuta kulia na kushoto, mashariki na magharibi, kaskazini na kusini. Usiku na mchana kamati hiyo inaundiwa mizaha, inakejeliwa, inabezwa kwamba haina inalo. Wajumbe wake wanafedheheshwa ili waonekane na umma kuwa si lolote si chochote.

Viongozi wakubwa wakubwa wa CCM

Kamati ya Maridhiano ni zaidi ya Waride/CCM

32

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

33

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 18: Zanzibar Daima Online

wanatangaza leo kuwa hawaitambui Ka-mati ya Maridhiano. Ofisi Kuu ya CCM/Zanzibar hapo Kisiwandui, inathubutu leo, miaka mitano baada ya kuundwa kwa Kamati ya Maridhiano, kuhoji ni lini chama hicho kilitoa baraka zake kuianzi-sha kamati.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Waride Bakari Jabu anaandika tamko lisemalo kitendo chochote cha kamati hiyo kulihusisha jina la CCM (katika mambo yake) kihesabiwe na wananchi kuwa ni utapitapi, choko-choko na ukorofi wa kisiasa.

Eti wana-CCM waliokuwa wajumbe wa NEC, wajumbe wa Baraza la Mapinduzi leo ni “watapitapi” na “wakorofi wanaotia chokochoko.”

Waride anasema katika tamko lake hilo, kuwa CCM ina utaratibu na kanuni zake za kuunda kamati na “si kuundiwa au kusemewa na kundi lolote.” Anasema in-apotokea haja ya kuunda kamati yoyote ile, wajumbe wake hutokana na “maazi-mio ya vikao halali vya kikatiba na si ku-kurupuka kama ifanyavyo inayojiita Ka-mati ya Maridhiano.”

Kwa CCM, Moyo sasa anakurupuka na anaongoza kamati isiyotambuliwa na Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Kwa CCM, Moyo pamoja na Mohamed (Eddi) Ahmed Riyami na Mansoor Yus-suf Himid ambao ni wajumbe wa kamati yake, ni wavurugaji wenye malengo ya kukidhi tamaa zao.

Viongozi wa CCM wametokwa na haya siku hizi. Wanatupa tu buu kama vile wa-navyopiga ndege gizani. Wanabahatisha.

Chama hicho kinawataka leo wanaume hawa waeleze kule walikopata ruhusa au walikotumwa na ni nani aliwatuma miongoni mwa viongozi wa juu wa chama washiriki katika kamati hiyo.

Sasa basi, tamko la Waride linawahenye-sha Moyo na wenzake kuwa hawaja-tumwa kwa vyovyote vile kushiriki katika Kamati ya Maridhiano na ieleweke kuwa wajumbe wamejipeleka wenyewe “ili ku-potosha na kuwahadaa wananchi kwa manufaa yao.”

Moyo ni mtu wa umri. Isitoshe, umri wake ni tafauti kabisa na alionao Waride, mtoaji wa tamko la CCM, chama ambacho Moyo kakitolea jasho lisilo kiasi. Chama ambacho Eddi Riyami kakihenyea na chama ambacho Mansoor hakijitoa kuki-jenga.

Waride, katika tamko hilo ambalo ameli-toa kwa niaba ya uongozi wa juu wa CCM/Zanzibar, hawezi kusimama kwa kigezo chochote kile sambamba na Moyo wakapanga siasa na namna ya kuziche-za. Kisiasa, kiumri, kihadhi, kiungwana na kizalendo Moyo na Waride ni kama lila na fila – hazitengamani.

Anavyofikiri Moyo hawezi kufikiri Waride. Vile anavyoyaona mambo Moyo sivyo anavyoyaona Waride pamoja na wengi wa hao waliomtuma aipinge Kamati ya Maridhiano. Ni watu wasiofanana kwa namna yoyote ile. Wakati Waride ni wa leo, Moyo ni mtu wa taarikh.

Badala ya kuwa Moyo na wenzake ndio waliokurupuka, ukweli ni kwamba Wa-ride na wenzake katika CCM ndio wenye upungufu wa kuyajua mambo. Hawaji-tambui wapi wametoka, wapi wapo na wapi wanakwenda.

KALAMU YA MWINYI MKUU

34

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

35

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 19: Zanzibar Daima Online

N A R I Z I K I O M A R

MKEKA WA MWANA WA MWANA

Siasa za Muungano huipetea ‘kumvini’ Zanzibarhuu, kama yalivyo mawazo ya wenzetu wengi wa Tanzania Bara. Utatanishi wa pili unazalisha malalamiko kwamba Se-rikali ya Muungano inafanya hila za ma-kusudi kuinyang’anya Zanzibar kila kile kilichokuwa chake.

Ukweli ni kwamba huu ni utatanishi wa kimtego na wa kufunika kombe, ambao azma yake kubwa ni kufifilisha ile hoja ya ulazima wa Serikali ya Tanganyika kuja juu, ionekane na ifanye kazi zake rasmi kuwakilisha na kusimamia matakwa na maslahi ya Watanganyika yasiyokuwa ya Muungano.

Bila ya kuwa na chombo cha kutunga sheria cha Tanganyika kama kulivyo na chombo cha kutunga sheria cha Zanzibar na bila ya kuwa na mamlaka tafauti ya

utawala ya Tanganyika kama kulivyo na mamlaka ya utawala ya Zanzibar, tutaen-delea kuwa mbali kabisa na uhalisia wa

Muungano kama yalivyo matakwa ya Mkataba.

Kuudharau kwengine uhalisia wa Muun-gano ni kulidogosha suala zima linalo-husu Muungano wenyewe. Angalia, kwa mfano, Muungano mzima umewekwa ni idara tu ndani ya Ofisi ya Makamu wa Rais, ambayo ina idara nyengine kadhaa.

Wakati Rais Jakaya Kikwete aliona um-uhimu wa kuunda wizara maalum kus-hughulikia Afrika ya Mashariki, hakuona kabisa umuhimu wa kuwa na wizara kamili kushughulikia Muungano. Hili lina-onyesha namna Serikali inavyoudharau Muungano kama kwamba ni suala dogo tu.

Labda hapa linakuja suala la ufundi na

la kimantiki kwa wakati mmoja: kwamba katika mjengeko wa utawala serikalini, majina ya vyeo vya wakuu wa vitengo

Tunapozungumzia Muungano wetu, kuna mambo mawili ambayo ndiyo uhalisia wake: kwanza, huu ni

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, nchi mbili zilizokuwa na mamlaka kamili na ambazo zilisalimisha baadhi ya mam-laka yake hayo kwenye chombo kimoja, huku kila upande ukibakia na sehemu nyingine ya mamlaka yake.

Huu si Muungano baina ya mkubwa na mdogo panapohusika hadhi ya nchi zili-zoungana, maana eneo la kijiografia wala idadi ya watu havikuwa vitu vilivyoamua kuwepo na kutokuwepo kwa Muungano, kwa hivyo haviwezi leo kuamua uendes-hwaji wa Muungano wenyewe.

Pili, ni ukweli kwamba huu Muungano ni kitu kikubwa na muhimu sana kwa pande zote mbili za Muungano.

Wakati huo ndio uhalisia kuhusu Muun-gano, siasa za Serikali ya Muungano zi-naonyesha vyengine. Angalia, kwa mfano, mjengeko wa Serikali hii katika uwiano wa nafasi zinazoshikiliwa na watu kutoka pande hizi mbili kwenye wizara za Muun-

gano.

Uwakilishi wa Zanzibar ni wa kulazimisha kama kwamba Zanzibar ni mwalikwa tu na sio mwenza wa Muungano wenyewe. Inapotokea Mzanzibari amepewa nafasi katika wizara hizo, huwa ni kwa kukari-bishwa na, au, kukirimiwa tu. Hata Idara ya Muungano iliyo chini ya Ofisi ya Maka-mu wa Rais, mambo ni hayo hayo.

Jambo hili linakwenda sambamba na utatanishi wa makusudi unaofanywa na Serikali ya Muungano. Utatanishi wenye-we ni kwamba, kwa upande wa Serikali ya Muungano, imefanya mara nyingi huko nyuma, kumpa Mzanzibari kuongoza wizara ambayo si ya Muungano; ikijua fika kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha mantiki ya Muungano wenyewe na kwamba kunachochea malalamiko ya haki kutoka kwa Watanzania wa Bara.

Si jambo la haki hata kidogo, kwa mfano, kwa Mzanzibari kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, au Maliasili na Nishati, maana hayo si mambo ya Muun-gano. Wako Watanzania wa Bara wenye uwezo mkubwa kuongoza wizara hizo.

Na hata Bungeni, si haki kwa wabun-ge kutoka Zanzibar kujadili na kuamua mambo ya Tanzania Bara ambayo si ya Muungano. Si haki pia kwa Serikali ya Muungano kuunda wizara ambazo zi-nachanganya mambo yaliyo na yasiyo ya Muungano katika kapu moja, kama ilivyo, kwa mfano, katika suala la elimu ya juu, sayansi na teknolojia.

Utatanishi wa kwanza unazalisha mal-alamiko kwamba Wazanzibari wanafai-dika na kudekezwa sana na Muungano

37

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

36

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

Page 20: Zanzibar Daima Online

hunasibiana na vitengo vyao, kwa mfa-no mkuu wa kurugenzi ni mkurugenzi na mkuu wa wizara ni waziri.

Kutokana na kupuuzwa na kudharauli-wa kwa makusudi kwa matatizo ya Mu-ungano huu, hakujawahi kupita muongo ambapo Muungano hautikiswi na ku-tikisika. Kwa bahati mbaya ni kwamba, kila Muungano unapotikisika, macho-ni mwa wakubwa huonekana kama kwamba unatikisika kwa kuwa hauna mambo ya kutosha.

Na, hivyo, kama vile Mfalme Jeta wa Shaaban Robert alivyokuwa akila na kunywa kila kili-chopo, basi nao wakub-wa huzi-di kuu-miminia Muun-gano kila cha Zanzibar na kila cha Tanzania Bara tumboni mwake.

Hilo ni kosa kubwa katika sayansi ya utatuzi wa migogoro. Wapemba hu-sema: ”Ganga shina, matawi hayag-angika!” kwa maana ya kuwa, kutibu maradhi ni kukitibu chanzo chake na sio dalili zake.

Ni kosa kutokujiuliza kwa nini Muun-gano huu unatikisika (haushibi) na kujiuliza tu vipi unatikisika (unalilia

njaa na kiu). La kujiuliza ni ikiwa hivi kweli Muungano huu uliumbwa na roho ya kushiba na kukinai au uli-umbwa na uroho wa kufakamia na kusaza kila kitu? Ikiwa hivyo ndivyo, kuna siku kutakuwa na cha Zanzibar tena na, au, cha Tanzania Bara peke yake?

Baadhi ya wakati Wazanzibari hu-kumbushwa na wenzao wa Bara ule msemo wa Kiingereza usemao: ”You cannot eat your cake and have it!”

kwa maa-na ya kuwa mtu ha-wezi kuila keki yake na bado akaende-lea kuwa nayo. Ni ama aile imalizike na asiwe nayo au

asiile kabisa ikiwa anataka kubakia nayo.

Lakini kuna upande mwengine wa ukweli katika suala hili la keki: nao ni kuwa kuna mtu asiyeila keki yake na bado asiwe nayo na mwengine anayeila keki yake na akaendelea kuwa nayo. Ndivyo siasa za Muunga-no kuelekea Zanzibar zilivyothibitisha kwa nusu karne hii ya kuwepo kwa-ke.

MKEKA WA MWANA WA MWANA

Abdul Hamid Zanzibar na Tanganyika ziliungana kama nchi mbili huru bila ya kuzingatia ukubwa na wingi wa watu wake, hivyo ni vyema kama kweli viongozi wanataka kuuenzi Muungano huu ni lazima waondoshe fikira za udogo wa Zanzibar na watu wake katika maamuzi na migao ya fedha kama mshirika sawa wa muungano.

Akili Idd Tuliza Nadhani huo utakuwa ndio mwisho wa CCM kutawala Zanzibar.

Abdul Hamid Huu ni udhaifu wa kisiasa ulioneshwa na viongozi wa CCM/Zanzibar baada ya kushindwa kujibu hoja za Mh.Mansoor na badala yake kuanza kutoa maneno machafu na matusi ya nguoni. Jambo muhimu ni kumuomba Mh.Mansoor kupuuza matusi yao ili kutowapa mwanya wahafidhina kuendeleza siasa zao za chuki na husda katika Zanzibar yetu.

Ustaadh Harith naam jina la ccm bado linaendelea kuwa baya zanzibar katika vichwa vya wasomi na wenye akili maana huwezi kusikiliza mkutano wa ccm wewe na familia yako. mi nawaomba wajirekebishe kinyume chake watakimbiwa na wanachama kila siku.

Rajab Juma Othman Hii ni mbegu walioipanda wenyewe walipata nafac ya utawala na wakashindwa kuitetea nchi walikua wanadili na cuf tu hebu ikumbuke kauli ya kiung-wana iliotolewa na maalim Seif NITAKUA NANYINYI NIKIWA NDANI YA CCM NA NJE YA CCM

Abdul Hamid Huu ni udhalilishwaji kwa viongozi wetu wa Zanzibar kwani wakiukaji wa sera ya Muungano wapo wengi sana akiwemo yeye Naibu Spika wa Bunge la Muunga-no, aliyerikodiwa akipigia debe muundo wa serikali tatu lakini ccm dodoma hawakumfu-kuza na wala hawakumletea maneno yasio na maana.

Inaendelea Uk. 47

38

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

39

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 21: Zanzibar Daima Online

Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete [kushoto] na Makamo Mwenyeki wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.

Kadhia ya kufukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapin-

duzi (CCM) mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mansoor Yussuf Himid, imewagu-sa Wazanzibari wengi.

Wapo waliofurahishwa na kufukuzwa kwake na walioona kuwa wame-pata ushindi. Hawa ni wale tunaowaita siku hizi kuwa ni wahafidhina, waliokuwa wakikerwa na kukereketwa kwa kazi aliyokuwaakiifanya.

Wako waliosikitishwa na kuvunjwa moyo na uamuzi huu wakilalami-ka wakiiona CCM kama

ni adui wa Zanzibar na maslahi yake. Hawa wa-naamini kuwa kilichom-fukuzisha Mansoor ni kusimama kwake kidete kuitetea nchi yake ya Zanzibar na maslahi yake ndani ya Muungano. Wanavyoona ni kwamba Mansoor ameponzwa na juhudi zake za kuleta maridhiano, umoja na heshima miongoni mwa Wazanzibari na za kuh-akikisha kuwa wanaun-gana katika kusimamia mambo yenye maslahi na taifa lao la Zanzi-bar na vizazi vyake vya baadaye.

Lakini kuna kundi maalum la Wazanzibari

ambalo limeathirika zaidi na moja kwa moja kuto-kana na sakata hili. Nalo ni la wananchi wa jimbo la Kiembesamaki ambalo mwakilishi wake alikuwa Mansoor.

Ijapokuwa CCM ndiyo iliyomdhamini Mansoor kubeba bendera yake na kusimama kama mgombea wa nafasi ya uwakilishi katika jimbo hilo, lakini ni juhudi za wanajimbo ndizo zili-zompeleka mwakilishi wao huyo katika Baraza la Wawakilishi, na si CCM kama CCM. Ni wanan-chi ndio waliohimizana, wakapigana kampeni na hatimaye wakasimama

misusuru kwa misururu kupiga kura zao na kuh-akikisha wanamchagua mwakilishi wanayemta-ka.

Hawakujali mvua wala jua, njaa wala kiu, lakini walichokuwa wakikitaka ni kumuona Mansoor anakuwa mwakilishi wao. Na haya hayaku-tokea mara moja. Mara zaidi ya moja, wananchi wa jimbo hilo, tokea pale alipoingia ka-tika ulimwengu wa siasa, walimrid-hia na

UHAFIDHINA WA KISIWANDUI, UKOLONI WA DODOMAM

wan

dish

i Maa

lum

N A M U S TA FA S H A R I F .

40

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

41

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 22: Zanzibar Daima Online

kumpa imani na kura zao ili awe kiongozi wao wa jimbo.

Hata katika uchaguzi wa 2010 na ulio-fanywa baada ya Mansoor na wenzake kufanikiwa kuleta Maridhiano ya Wa-zanzibari – jambo ambalo liliwakera sana wanaCCM wahafidhina na pengine ikawa miongoni mwa vyanzo vya kumfika ya-liyomfika – wananchi hawakusita kumpa kura zao na kukubali kuongozwa naye.

Vyereje leo wakatoke watu wachache na sababu zao tu, wakaseme wanamfu-kuza mwakilishi wa watu eti kwa sababu amekwenda kinyume na sera ya chama (kama kweli amekwenda kinyume), bali si matakwa ya wananchi waliomchagua na anaowaongoza? Kwa imani yangu, si kila aliyempigia kura Mansoor alikuwa mwanaCCM, bali wanachama wa vyama vyengine na wale wasiokuwa na vyama pia walimtilia voti zao.

Kwa hali hii, watu wa Kiembesamaki wamenyang’anywa haki yao waliyoipata kidemokrasia, wamepotezewa kiongozi mpenda watu wote wa jimbo lake, vija-na, wazee, kike kwa kiume. Watu hawa wameondolewa mwenzao anayependa maendeleo yao na aliyekuwa na msaada mkubwa wa hali na mali kwao.

Kwa kukurupuka huku walikokurupu-ka CCM bila ya kuwasikiliza wananchi wa Kiembesamaki, naona kwa maneno ya vijana wa kileo “itakula kwao”, kwani wana wa Kiembesamaki wanamjua nani Mansoor na wako tayari kumsikiliza ata-kachokisema na kumfuata popote pale atakapokwenda, kwani yeye ndiye ki-ongozi wao waliyemchagua na kumridhia.

Nasema “itakula kwao” wahafidhina wa CCM Zanzibar, ambao kwa kusaidiana na wakoloni wa Dodoma wamefanikisha wa-

lichokifanikisha, lakini hawakujua kuwa “ukiujuwa huu, huu huwiji.”

Ni dhahiri kwamba viongozi wa CCM Kisi-wandui Zanzibar ndio waliokuwa wakis-hadidia na kuisukuma CCM Makao Makuu Dodoma kumfukuza Mansoor kwa saba-bu wakati wote wao wenyewe wameku-wa wakilisema hili. Ni wao waliolianza na walihakikisha kwamba watafanikiwa.

Wahafidhina wa Zanzibar wamekuwa na chuki dhidi ya Mansoor na kutokana na kufanikiwa kwake katika mengi. Nasema kufanikiwa, maana tafsiri ya jina “Man-soor” niliyoipata kwenye mtandao wenye majina ya watoto wa Kiislamu ni “mshin-di”.

Na, naam, Mansoor amewashinda kwa mengi. Miongoni mwao ni hili la kusima-ma pamoja na Kamati ya Maridhiano ya Mzee Hassan Nassor Moyo kuhakikisha Wazanzibari wanazika tafauti zao ili waweze kusimamia mambo yao na kuji-funza kukubaliana pale wanapotafautia-na. Jambo hili kwa kiasi kikubwa limefi-nikiwa, Alhamdulillah.

Lakini la ushindi wa Mansoor na wenzake limekuwa mwiba mkali kwa wahafidhina na wasioitakia mema Zanzibar, ambao siku zote wanataka kuiona ikiwa nyuma tu kwa hali yoyote. Ndipo wakaamua kumuwekea kisasi cha kumuadhibu, na kama wasemavyo wenyewe, “hata bado”, kwa maana ya kwamba hawataishia hapo. Uvumi ni kwamba sasa wanam-pikia jungu Rais Mstaafu Amani Karume ili naye wamuadhirishe kama alivyowaa-dhirisha wao, kwa kuwaletea Maridhiano na Serikali ya Umoja wa Kitaifa wasiyoi-taka.

Dodoma, kwa upande wake, licha ya kuri-potiwa kwamba ilikuwa inapingana na

matakwa haya ya wahafidhina awali, lakini ukweli ni kwamba ilikuwa inafu-rahia. Mzanzibari yeyote anayesimama dhidi ya Muungano, kichwa chake ni ha-lali ya Chimwaga.

Si siri kwamba Mansoor amekuwa mstari wa mbele katika kusimama na kutetea Mfumo wa Muungano utakaoirejeshea heshima yake Zanzibar. Hivyo, ni wazi kwamba kwa kujitangaza alivyojitangaza, mbele ya CCM Dodoma Mansoor alisha-saini hati yake ya kifo, nao wakawa wa-nasubiri apelekwe tu wamnyonge.

Sababu ni kwamba alitishia maslahi ya Tanganyika ambayo inajiona kama mko-loni ambaye ametawalishwa na Zanzibar milele.

Kama historia inavyotuonyesha, kudai maslahi ya Zanzibar ndani ya Muungano ni kugombana na mkoloni. Na madha-li Mansoor amethubutu kulifanya hilo, ameingia kwenye ugomvi na mkoloni.

Imani yangu kubwa ni kuwa mkoloni naye yumo katika kupika jungu hili au kama hajapika japo kwenye kulila hatoki kwani nnachokiamini mimi migogoro ndani ya CCM haipo Zanzibar tu, na kama kusalitiwa CCM haisalitiwi Zanzibar tu.

Tanganyika ndiko inakosalitiwa zaidi kuanzia kwenye maagizo yake, sera zake mpaka mali zake lakini hujasikia kufu-kuzwa mtu.

Lakini kwa sababu mshtakiwa alikuwa Mzanzibari, tena aliyeshtakiwa na ma-wakala wa ukoloni, kwa kosa la kupinga-na na ukoloni basi mkoloni hakuona uzito wa kushusha hukumu yake. Hukumu hii, hata hivyo, haitashushwa kwa akina Phillip Mangula anayetaka Serikali Moja, wala Job Ndugai na wenziwe wanaotaka pia Serikali Tatu kama Mansoor. Hawa ni wenyewe.

Nimalizie kwa kujumuisha nukta zangu mbili: moja, uhafidhina ndani ya CCM Ki-siwandui ulilipika jungu la Mansoor na utayapika na ya wengine, maana hau-taki mabadiliko. Lakini na ukoloni ndani ya White House Dodoma nao umetumia fursa hiyo kumpoteza mmoja wa wale wanaopingana na ukoloni.

Na madhali wahafidhina, vibaraka wa ukoloni wapo na wakoloni wenyewe bado wana nguvu, basi tutaona mengi sana mwaka huu. Sababu ni kuwa sisi Wazan-zibari tumeamua kuvunja mahusiano makongwe na mtawala.

42

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

43

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Unaweza kutangaza biashara yako kupitia Zanzibar Daima Online, jarida la kila wiki mbili lenye wasomaji wengi wenye kuzungumza lugha ya Kiswahili duniani kote.

Page 23: Zanzibar Daima Online

Tartiib CCM bye bye

“Ndugu wajumbe wa Mku-tano Mkuu wa CCM, tupatieni mgombea atakayekidhi mata-

rajio ya wananchi na sio matarajio yako wewe mpigakura. Tupatieni mgombea atakayekidhi matarajio ya Watanzania. Watanzania wanahitaji mabadiliko, wa-sipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM.’’

Hii ilikuwa ni kauli ya Mwalimu Julius Nyerere, wakati huo akimpigia debe mgombea wake wa urais abebe bendera ya CCM katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, mwaka 1995.

Nyerere aliuacha wasia huo na kila siku wanaCCM hujidai kuukariri, lakini ukweli ni kuwa wameisahau maana yake. Na ni kuusahau ama kuupuuza kwao ndiko kunakowafanya warudi nyuma badala ya kwenda mbele.

Ukweli ni kuwa Tanzania inaenda mbele na CCM inarudi nyuma. Binafsi nilid-hani yale ya 1984 ya kuangushwa Aboud Jumbe, aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanza-nia na juu ya yote Makamu Mwenyekiti wa CCM, na baada ya kufukuzwa chamani Maalim Seif Sharif Hamad na wenzake sita miaka minne baadaye, yalitokea kip-indi kile cha nyuma kwa sababu tulikuwa kwenye kiza

Lakini leo tupo kwenye mwangaza na yanatokea yale yale. Kufukuzwa kwa Mansoor Yussuf Himid ni ishara inayoto-sha kuwa CCM inarudi nyuma badala ya kwenda mbele.

Na baada ya kumwangusha Mansoor Dodoma, sasa wanaonekana wamechan-ganyikiwa na uamuzi walioufanya wao

wenyewe.

Kama alivyosema pia Mwalimu Nyerere katika kauli nyengine maarufu, ambayo leo ukienda kwenye ukumbi wa CCM ka-tika jengo la White House, Dodoma, utai-kuta imeandikwa kwa maandishi mazito ukutani: “Bila ya CCM imara Tanzania ita-yumba.”

CCM imeyaandika maandishi haya ukuta-ni na kuyaacha hapo hapo kama sanamu lisilo na maana kwao. Hawayaheshimu. Hawajifunzi kwayo.

Matokeo yake? CCM imekuwa si imara tena na sasa ndio maana Tanzania ime-anza kuyumba. Lau ingelitambua kuwa wakati unabadilika visiwani Zanzibar na ingekubali kuibeba dhana ya Mamlaka Kamili kwa visiwa hivyo, basi leo CCM in-gejizolea wanachama wengi zaidi, ingei-marika zaidi na pingine huo ungekuwa mwisho wa vyama vya CHADEMA, CUF na vyengine humu Visiwani.

Walichobaki nacho CCM ni nini? Nguvu za vyombo vya dola na matusi ya ma-jukwaani. Leo ili uonekane mwanaCCM kindakindaki ni lazima uwe unatukana vyama vyengine hata viongozi wakuu wa nchi, bora tu wawe hawatokei kwenye kundi la kihafidhina la chama chako.

Kumtukana Maalim Seif, ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zan-zibar, hadharani na viongozi wengine ni ishara inayotosha kumpa mwanaCCM wa

Zanzibar sifa mbele ya wenziwe. Lakini kwa wenye akili ndiyo pia ishara ya ku-onyesha kuwa sasa CCM si imara tena, maana uimara wa chama haupo kwenye matusi hata kidogo.

CCM imekuwa haina adabu hata kwa Rais wa Zanzibar ambaye anatokea CCM, Dk. Ali Mohamed Shein. Hivi karibuni tuli-shuhudia bango kubwa kwenye mkutano wa Kibanda Maiti, ambao ulihutubiwa na mwenyewe Dk. Shein, limeandikwa “Wa-naotaka Nkataba wende kwao.” Hilo neno ‘Nkataba’ liliandikwa hivyo wakimaanisha wanaotaka hivyo ni Wapemba na hivyo wao ndio waende kwao Pemba. Rais wa nchi hii ni Mpemba. Ni ufedhuli mkubwa huu.

Kuelekea shinikizo la kumfukuza Man-soor, mmoja wa wanaCCM hao alisema wazi wazi mbele ya Rais Shein kwamba ati “tuuvunje muungano wa Unguja na Pemba, Pemba wawe na nchi yao na sisi Unguja tubakie kwenye Muungano wetu na Tanganyika,” huku akidai aonyeshwe hati ya Muungano wa Unguja na Pemba.

Huu ni uhaini. WanaCCM wameishiwa na hoja. Wanasema wazi wazi tuwatoe Wapemba wakaunde serikali yao. Basi na wamtoe sio tu Maalim Seif, bali pia Rais Shein, Waziri Muhammed Aboud na wenzao wengine wakaunde serikali yao Pemba na Unguja iwe wilaya ya Dar es Salaam.

Leo CCM imeacha kupigana na ufisadi na

MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI

N A S A LU M A B DA L L A H 44

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

45

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 24: Zanzibar Daima Online

imekuwa inapigana na wasema kweli, wanaotaka mabadiliko na demokrasia isimame. Kosa kubwa la hao wanaopigwa vita ni kusema kweli kwamba Wazan-zibari sasa wanataka Muungano wenye haki, usawa na heshima kati ya nchi yao na Tanganyika.

Mara kadhaa CCM Dodoma imekuwa ukiichagulia Zanzibar hata Rais, kiongozi mkuu wa nchi ambaye hakidhi matarajio ya nchi.

Chini chini CCM/Zanzibar hukwambia kuwa hawaipendi Dodoma. Ukiwau-liza kwa nini, watakwambia kuwa huwa inawaletea viongozi wasiowataka. La-kini maajabu ni kwamba wanaCCM hao hao wa Zanzibar, wakitaka kumgeuka mwenzao, hukimbilia huko huko Dodo-ma wasipokupenda kwenda kumchin-jia na kurudi na damu mikononi mwao, wakasherehekea Kisiwandui.

Tunaotaka mabadiliko ambayo kwenye CCM hatujayapata tunaisubiri kwa hamu tuizike CCM 2015, maana tayari tumesha-juwa wapi tutakapoyapata mabadiliko. CCM isahau kuwa itayazima maamuzi ya wananchi walio wengi. Umma ume-wakataa.

Kwenye akili zao wana fikra zile zile zilo-pitwa na wakati kuwa Chama kinawekwa madarakani na dola. Wamesahau kuwa Chama huwekwa madarakani na wanan-chi, ndio maana leo wanakimbilia polisi na jeshi.

Tayari CCM Zanzibar ishaleta mapandikizi watakaopiga kura katika Kura ya Maoni na katika Uchaguzi Mkuu. Lengo ni kuta-ka Mamlaka Kamili Zanzibar yasisimame na CUF isishinde kwenye Uchaguzi Mkuu.

Lakini tuwaambie kabisa yagujuu! Safari hii CUF haitapigiwa kura na wanaCUF tu. Itapigiwa kura na wanaotaka Mamlaka Kamili ya Zanzibar. Na hao hawana chapa za vyama.

Hawa wanafahamu tangu leo kwamba Maridhiano na Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoendeshwa na CCM na CUF inaandamwa kwa sababu ya hili hili la ku-dai Mamlaka Kamili kwa Zanzibar. Wana-fahamu kwamba kuna baadhi ya miradi ya maendeleo haitekelezwi kwa sababu tu kaileta Maalim Seif. Kisa ni kwamba ati wakiitekeleza itampa jina na ushindi Maalim Seif katika Uchaguzi Mkuu.

Kwao wao kheri nchi iwe masikini, kwao wao kheri vijana wasiwe na ajira lakini CCM iendelee kuwa madarakani. Lakini vijana wa sasa sio wale wa 1964. Wa sasa wanataka mabadiliko tena mabadi-liko yatayokuwa yanakwenda kwa kasi.

Ndio maana vijana wanataka Mamlaka Kamili ya Zanzibar ili wapate kuongeza ajira na ili bomu linalotaka kuripuka lisi-ripuke, maana vijana wasio ajira ni wengi na ni bomu.

Na wala vijana hawa hawaoni kama kuna haja ya kuingia barabarani kuandamana au kuchukuwa mtutu na kuingia msi-tuni. Hapana, wanataka kuionyesha du-nia kuwa Mamlaka Kamili yanapatikana Zanzibar bila ya umwagaji wa damu.

Hoja wanazozitoa ndio njia mwafaka kwao kuelekea Mamlaka Kamili. Basi bye bye CCM. Nyerere alishatuusia kuwa mabadiliko tutayapata kwengine, madhali tumeyakosa kwako. Na kama alivyosema Mansoor majuzi pale Bwawani, hayo yanakuja ‘tartiib.’

MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI

Nassor Shaame Kwa maoni yangu kufukuzwa kwa wanachama wa CCM kwa kupiga-nia maslahi ya Zanzibar si jambo geni wapo walio makundi mengi alianza na Mzee jumbe na dhana yake moja na moja tatu akawajibishwa, wakafuatia kundi la Wa-somi vijana ndani ya CCM na leo tunashuhudia kijana mansoor naye akiingia katika hishoria ya kupigania maslahi ya Zanzibar. Wazanzibari wako nyuma yake kamwe hatutakodisha nyumba kwa kupata kilo ya mchele.

Rashid Mohammed Wazanzibari ccm sio chama chetu wabunge wametoa maoni yao ya serikali tatu lakini wao ni Watanganyika hawavunji ilani ya chama.

Omar Hussein Zanzibar imekua ikisifika kama ni visiwa vya watu wastaarabu kwa karne nyingi, na ustaarabu wa watu wa Zanzibar ndio umepelekea sehemu za Bara pia kustaarabika kutokana na mchanganyiko baina yao na Wanzibari, kwa muda sasa tumeona ustaarabu huu umeanza kupotea kwa njia moja au nyengine. CCM ni chama chenye uzoefu wa kuongoza kuliko chama chochote cha siasa, mambo wanayoyafanya isingeingia akilini kwa mtu kusikia kwamba CCM ndio kinara wa mambo hayo,kejeli kashfa, matusi tena ya nguoni ambayo ni aibu jamii kukaa na kuyasikiliza ndio imegeuka kua ilani na sera ya CCM zanzibar tena watu hushangiria pale muhubiri aliye jukwaani akiporomosha mvua ya matusi na wengine humpa pesa kama ni tunza kwa ujinga anaoufanya, kwa kweli inasikitisha, CCM/UVCCM Zanzibar hawawezi kufanya mkutano bila kumwaga shehena ya matusi,kupandikiza chuki na uhasama baina ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe kwa kisingizio cha U-Pemba na U-Unguja kwa kutaka watu warudi kule walikotoka, kweli hii inaashiria kushindwa kisera na kuamua kugeuza viwanja vya siasa kua ni viwanja vya matusi, wengi wetu tungetegemea kwa kipindi hichi kigumu katika upinzani wa nyama vingi na mapendekezo ya rasimu ya katiba mpya CCM wangekuja na sera zenye mvuto na ushawishi wa hali ya juu ili kurejesha na kujenga imani kwa wananchi waliowaweka madarakani kwa kuwaeleza kwa nini wao wanapigania sera ya serikali mbili na kwa nini wanapinga sera ya serikali tatu,lakini haikua hivyo. Mimi hujiuliza hivi ni kwa sababu viongozi wengi wa CCM/UVCCM Zanzibar hawajasoma? Lakini mbona kuna wengine wana elimu zao kwa nini hawa wasiwe wakosoaji na wakatazaji kwa wale ambao hawakubahatika kupita skuli wakafuta angalau ujinga? au hawa watoaji wa matusi na uchochezi ni wahamiaji na sio miongoni mwa Wazanzibari ambao wana-sifika duniani kwa ustaarabu wao? Kwa kweli sipati jibu, kwa kweli kama wameona kufanya hivi ndio kujenga vguvu zaidi kwa wanachama wao kuelekea ushindi mwaka 2015 na ndiko kutakakozima harakati za Wazanzibari kupigania mamlaka kamili ya nchi yao kwa kweli wamegonga mbuyu, Wazanzibari walisha amshwa, wako macho na wamesha elimika na wameshachoka na siasa za chuki na uhasama na sasa wa-nataka amani upendo na mshikamano katika jamii, CCM/UVCCM Zanzibar wame-shapoteza dira na wanaelekea kugonga mwamba.

Kutoka Uk.39

46

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

47

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 25: Zanzibar Daima Online

LADHA YA BETI

Utumwa naliopewa, nende kwa jini nifike Hamshike sawasawa, nimfunge afungike Ashindwe jipapatuwa, chupani nimfundike Kisha nende panganikwe, silisili kumtia

Na vifaa nikapewa, na nyenzo za uhakika Makombe hazinguliwa, ya kunywa na ya kupaka Na kafara hasomewa, na hirizi hajivika Alipo nikamfika, lengo kwenda mchukuwa

Halikuta kubwa jini, lisilo mfano wake Tangu juu hadi chini, sioni khatima yake Katikati msituni, ‘meketi kitini pake Bali nisitetemeke, nili nikijiamini

Havitoa viapio, sauti ya kushituka Hamwamba “Hima njoo, na maguuni anguka! Ela sijesema nyoo, mdomo sijefumbuka!” Naye wala hekanuka, hekaidi ninenayo!

Hali kapinda magoti, na u chini uso wake Kwayo nyepesi sauti, na nzuri ladha yake Kanamba: “Sikaze nati, nitume nikatumike!” Nusura chozi litoke, kwa huruma na laiti

Nikawa swahibu yake, hajikuta aniteka Kama mtu na mwenzake, tulozoeana myaka Yalokuwa dhidi yake, yote yakanitoweka Naye kwangu kadhalika, nikawa ni mwenza wake

Kwetu watu wakangoja, majibu niyapeleke Nirudi nivikwe koja, shujaa nieleweke Zenda saa siku zaja, neno langu ‘sisikike ‘Lotumwa nikamshike, ‘mekuwa wangu mbeja!

Mohammed Ghassani

Bonn

Ujerumani

Kucheza tucheze kwetu, kwetu tulikozaliwa Kunako wazazi wetu, wazazi waheshimiwa Heshima asili yetu, tuiombe tutapewa

Vijana tucheze shime, hima tutaaminiwa Tucheze kike kiume, hamna kubaguliwa Tucheze tusisimame, mchezo hautakuwa

Tucheze tufanye ari, tukijua tutapewa Tuzipandishe na mori, na kwa nguvu tulizopewa Wazee wakitukiri, zawadi tutachukuwa

Hili halina ubishi, kwetu tukikuchaguwa Kwazidisha ushawishi, mchezo tukanogewa Kwetu michezo haishi, kila tutapoamua

Nasisitiza kwa leo, na maneno kufungiwa Hajuti mcheza kwao, hata akikosolewa Anayo mapendeleo, kila mchezo ukiwa

Said O. Shoka

Chake Chake – Pemba

Mcheza Kwao Kulikumba Jini

48

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

49

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 26: Zanzibar Daima Online

Nilitangulia kusema kuwa dhima ya mchambuzi/mhakiki wa kazi ya fa-sihi ni kuirejesha kazi ‘watuni’, yaani

kuisaidia jamii kujisoma baina ya mistari ya msanii. Na hili ndilo nitalolifanya sasa kwa kuwasaidia wenzangu kujiona wa-livyo kupitia mistari hii michache ya Ally Saleh katika Karamu.

Natokea Zanzibar kama alivyo mwandishi wa Jumba Maro. Ni maoni yangu kwamba Karamu hii aliyoiwasilisha Ally Saleh in-aakisi moja kwa moja chaguzi zetu katika mfumo wa vyama vingi.

Ninaamini pana mfanano mkubwa bai-na ya maandalizi, uendeshaji na matokeo ya chaguzi zetu ndani ya mfumo huu wa vyama vingi na karamu hii ya Bwan’ Ta-jir (ambaye kwa tafsiri yangu ni serikali ya chama tawala).

Ule mkasa wa kuingia kwa nyoka kati-ka chumba cha Bwan’ Tajir naufananisha na kuja kwa siasa za vyama vingi katika nchi, ambazo zilijipenyeza bila ya ridhaa ya dhati ya watawala.

Siku zote watawala wamekuwa wakiogo-pa kuwa upinzani utahatarisha maslahi

yao, kama vile Bwan’ Tajir anavyoogopa kuwa nyoka angelimfichulia aibu zake za woga na ugoigoi.

Kupitia mdomo wa Bwan’ Tajir, serikali ya chama tawala inamkaripia mtu inayedha-ni kuwa amechangia kurudi kwa vyama vingi: “Usiniambie mie habari ya (nyoka) kutoka wapi…mie nilikwambia naogopa nyoka. Nilikukabidhi kazi ya kuhakikisha nyoka sio tu hawaonekani, lakini pia wa-sikaribie nilipo”. (Uk. 91)

Ukweli ni kuwa, laiti serikali ya chama tawala ingelikuwa na uwezo wa kuzuia

vyama vingi visije, ingelifanya hivyo. La-kini kilichotokea ni kuwa wakati ulikuwa umeshafika, na hakuna ambaye ange-likinzana na matakwa ya wakati, kama

vile anavyosema Nokoa Mkuu, ambaye alituhumiwa na kuhukumiwa kwa kum-ruhusu nyoka kupita hadi chumbani kwa Bwan’ Tajir, kwamba: “Sina uwezo wa ku-

zuia kudra”. (uk. 91)

Wasemavyo wamalenga: “Muda na kudura hazina zisubirio”, ndi-vyo ambavyo wakati ulivyolazi-misha kuja kwa vyama vingi hata kama wakubwa walikuwa hawa-vitaki. Kwa hivyo, nyoka (siasa za vyama vingi) hakuweza kuzuilika kuingia katika chumba cha Bwan’ Tajir (nchini).

Watawala na mawakala wao ka-tika vyombo vya habari, vyombo vya dola, taasisi za kijamii na kwengineko, hawakuwa na uwe-zo wa kuvizuia vyama vingi visi-rudi, kwa kuwa hayo yalikuwa ni matakwa ya wakati.

Lakini ikiwa walishindwa na hi-cho, kuna chengine ambacho

waliweza kukifanya: nacho ni kuandaa mikakati na mbinu za kuvizuia vyama hivi kuwaondoa wao madarakani. Na karamu (chaguzi) za magube na varange ndiyo ikawa njia ya wao kujihalalishia kuende-lea kubakia madarakani huku wakiudan-ganya ulimwengu kuwa na wao wana de-mokrasia ya vyama vingi.

Ndivyo karamu ilivyoandaliwa katika Jum-ba Maro. Bwan’ Tajir alimtafuta Shawishi Mkuu kuwa muandaaji na mpishi wake. Shawishi huyu akawa na jukumu moja tu: kwa upande mmoja, kuhakikisha kuwa

N A M O H A M M E D

G H A S S A N I

“ Ya Zanzibar na Jumba Maro ni mama mmoja, baba mmoja.“

TUFUNGUE KITABU

50

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

51

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Karamu ya maro [Sehemu ya Mwisho]

Page 27: Zanzibar Daima Online

watu wengi zaidi wenye haki ya kula ka-ramu hiyo hawapati fursa na, kwa upande mwingine, wale wasio na haki hiyo, lakini ambao kula kwao kutakuwa kwa faida ya Bwan’ Tajir, wanaila kwa matonge na kwa kufuta sinia mbili mbili. Kwa ufupi, Sha-wishi Mkuu alikuwa na dhima ya kuifuja karamu.

Ndivyo ilivyo katika uhalisia. Kwamba katika kuandaa mazingira ya kuendelea kubakia madarakani, watawala wanawa-tafuta akina mashawishi wakuu na ku-wafanya wawe na mamlaka ya kuandaa na kusimamia chaguzi ziitwazo za vyama vingi. Kwa maana nyengine ni kuwa wata-wala wanajiundia mitandao inayohawa-kikishia kuwepo kwao madarakani dumu daima, hata pale umma (watu wazima wa mji) utakapokuwa umeshawakataa.

Hiki ndicho kinafanyika hadi leo Zanzibar, ambako mtandao madhubuti wa mas-heha, vyombo vya dola na Tume ya Ucha-guzi, unahakikisha kuwa Wazanzibari wengi wenye haki ya kupiga kura hawa-andikishwi kuwa wapiga kura, kwa upan-de mmoja na, kwa upande mwingine, wale wasiokuwa na sifa, lakini ambao wanatu-miwa kukipigia kura chama tawala wa-naandikishwa ikibidi hata zaidi ya mara moja. (Rejea ripoti ya TEMCO/REDET: The Politics of the PVR, 2005)

Mkasa wa Karamu ya Jumba Maro kuli-wa na watoto wadogo huku watu wazi-ma wakitazama macho tu, ndio mkasa wa kura za majimbo kadhaa ya Zanzibar am-bako kura zinazoambiwa zimemchagua mgombea fulani hupigwa na watu wa-siotimia umri huku washaotimia wakilia machozi.

Mkasa wa watu wachache kula sahani mbili mbili za biriani huku wengine wa-kienda miayo kwa njaa, ndiyo mkasa wa upigaji kura zaidi ya mara moja katika

maeneo kadhaa ya Zanzibar, huku zaidi ya Wazanzibari 20,000 kila uchaguzi wa-kipingwa na masheha kuwa si wapiga-kura halali, maana masheha hao “hawa-watambui kuwa wakaazi wa shehia“ zao. (Pitia ripoti ya National Democracy Insti-tute-NDI, 2005).

Mkasa wa akina Ahmed kukataliwa kuingia kwenye chumba cha karamu kwa kuwa kadi yake imeandikwa Ahmad, ndio mkasa wa Wazanzibari wanaojikuta ama majina yao yameshapigiwa kura au wa-naambiwa hawamo katika orodha ya wa-piga kura katika siku yenyewe ya kupiga kura. (Rejea makala za Christian Science Monitor, 2010).

Kwa hivyo, kwa kila hali, karamu ya Jum-ba Maro inafanana sana na chaguzi zetu ziitwazo za kidemokrasia. Ni njia ya akina Bwan’ Tajir kuutangazia ulimwengu kuwa na wao wana ukarimu wa kutosha wa kualika watu kuja kula katika makasri yao, lakini kumbe hawana uhodari huo. Kutoa na kujitolea kwataka moyo, na moyo huo akina Bwan’ Tajir (watawala wetu) ha-wanao.

Watawala wetu, kama alivyo Bwan’ Tajir, huomba pesa za kugharamikia chaguzi ati kuwapa raia fursa ya kuwaweka madara-kani viongozi wawatakao, lakini kwa hak-ka huwa ni kwa kujionyesha tu.

Katika vyembe vya nafsi zao, watawa-la hawa huwa wameshajiwekea kabisa kwamba hawataondoka madarakani kwa vyovyote vile, ikibidi hata kwa kutumia mtutu wa bunduki, ili waendelee kusalia pale walipo.

Hufanya mbinu, visa na mikasa, alimradi tu utimu muradi wao. Ya Zanzibar na ya Jumba Maro ni mama mmoja, baba mmo-ja.

KARAMU YA JUMBA MARO

52

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

53

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 28: Zanzibar Daima Online

Hakuna ajuaye wapi na lini mchezo wa kriketi (cricket) ulipoanza. La-kini inadhaniwa kuwa mchezo huu

ulianzia katika maeneo ya Kent na Sus-sex huko Uingereza katika karne ya 17. Mchezo huu huchezwa zaidi katika nchi zilizowahi kutawaliwa na Mwingereza.

Hapa Zanzibar kriketi ilianza kuchezwa rasmi mnamo mwaka wa 1890. Miaka sita baadaye mchezo huo ulizusha vita baina ya Uingereza na Zanzibar, vita vilivyodumu kwa muda wa dakika 37 na nukta 27 na ni vita vya muda mfupi kabisa hadi sasa katika historia ya vita duniani.

Katika mwaka wa 1896 mlolongo wa manuwari za Kiingereza, bila ya kuomba ruhusa ya Sultan, zilitia nanga kwenye bandari ya Zanzibar ili wanamaji wake wende kuangalia mchezo wa kriketi ulio-kuwa unachezwa.

Nahodha wa manuwari hizo Admeri Sir Harry Rawson aliwaamrisha mabahari wake wateremke ili wende kuangalia mchezo wa siku hiyo. Lakini Sultani, Seyyid Khalid bin Barghash, alikerwa kwa ujeuri wa Waingereza wa kutia nanga manuwari zao kwenye bandari ya Unguja bila ya kuomba ruhusa ya serikali yake. Ndipo alipoamrisha manuwari za Kiinger-eza zishambuliwe. Agosti 27, 1896 meli yake Sultani iliyokuwa ikiitwa ‘Glasgow’ ilifyetua mizinga kuhujumu meli za ki-vita za Kiingereza. Hapo tena manuwari

za Kiingereza nazo zikaishambulia Un-guja kando kando ya Forodhani. Kasri ya mfalme ilibomolewa na kuwa kifusi na inakisiwa watu na askari wasiopungua 500 waliuawa. Seyyid Khalid alikimbilia kwenye Ubalozi wa Ujerumani kutafuta hifadhi.

Awali mchezo huo wa kriketi ulikuwa ukichezwa na walowezi wa Kiingereza. Baadaye pakawa panafanywa mechi kati ya walowezi hao wa Kiingereza na ma-baharia wa Kiingereza waliokuwa wakitia nanga meli zao bandarini, Unguja.

Klabu ya mwanzo ya kriketi Zanzibar il-ianzishwa 1922 na hao wazungu walio-kuwa wakiishi hapa visiwani. Ya pili ilikuwa klabu ya Ithnaasheeri. Baadaye zikafwatia klabu za makabila mengine — ya Waarabu, ya Comorian yaani jamii ya Wangazija, nay a Wahindi waliokuwa wafuasi wa madhehebu ya Ismaili waki-ongozwa na Aga Khan.

Skuli nazo zilikuwa na timu za kriketi kuanzia Government School, King George VI Grammar Secondary School (sasa Lu-mumba College), Hindu Union na skuli ya Aga Khan. Hapa Zanzibar mchezo huu ukipendwa zaidi na Wahindi lakini hata wasio Wahindi nao wakiucheza na kuli-wakilisha taifa.

Miongoni mwa Wahindi waliokuwa maa-rufu katika miaka ya 1950 na miaka ya mwanzo ya 1960 walikuwa Baker Tejani, Harji Mawji, Rusi Madon, Gajendra Doshi,

Gulam ‘Golo’ Mshamba na Ahmed Ba-choo.

Kuna wenye kuamini ya kwamba Mzanzi-bari aliyekuwa stadi kuliko wote alikuwa Harji Mawji anayefananishwa na Gary Sobers, mzalia wa Barbados aliyekuwa akichezea timu ya West Indies. Kama Sobers Harji Mawji alibobea katika kriketi. Ukija kwenye kudima ndiye yeye aliyeku-wa bingwa; ukija kwenye mbio za kasi za wastani za kurushia mpira yeye alikuwa bingwa; ukija kwenye waliokuwa mastadi katika kuurusha mpira mpaka ukawa unaviringika basi ni yeye Harji Mawji ali-yekuwa bingwa.

Harji Mawji alikuwa na jengine lililomfan-ya apendwe apendeke. Alikuwa Mhindi

pekee aliyekuwa akichezea soka katika timu ya Kikwajuni tena Division One. Isi-toshe alikuwa pia hodari wa volley ball. Mfano wake ni kama ule wa kina Ahmed aliyekuwa amebobea katika michezo ya hoki, kriket na soka.

Wachezaji maarufu wa kriket wasio Wahindi walikuwa kina Chepe, Simba Makwega.

Wawili hao walianza kuiwakilisha Zanzi-bar katika mchezo huu katika miaka ya 1940. Mwingine alikuwa Mzee Saadati aliyekuwa akifanya kazi Mahakama Kuu. Huyu alikuwa mchezaji mahiri na alimvu-tia sana bosi wake Sir John Gray. Kila siku ya mechi Sir John akimpa ruhusa Mzee Saadati kwenda kucheza kriketi.

Historia fupi ya mchezo wa kriket ZanzibarMICHEZO

N A B A B U J I M B E

54

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

55

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 29: Zanzibar Daima Online

Safari moja katika miaka ya 1950 timu ya Comorian ilikuwa inacheza na kwa vile Mzee Saadati akichezea timu ya Co-morian alienda kuombewa ruhusa na mwalimu wa timu hiyo Mzee Ahmed Iddi Mjasiri, aliyekuwa pia akifanya kazi Ma-hakamani.

Kwa mshangao Sir John akauliza “Who is Saadati?” Akajibiwa “Your staff, (mfan-yakazi wako)”

Basi Sir John kwa kebehi alijibu: “Fine, I will give him permission and I will be among the spectators.”(Sawa, ntampa ruhusa na mimi ntakuwa miongoni mwa watazamaji.)

Mzee Sadati alikuwa ni mfunguaji na akafungua yeye pamoja na Ahmed Mshangama ‘Bwamkubwa Shoto’. Katika mchezo huo timu ya Co-morian ilikuwa inacheza na timu ya Ithnaasheri na siku hiyo Mzee Saadati mchezo ulimpa uso kwani mpira wa mwanzo alipeleka ‘boundary’ (mpaka) na kuweza kufikisha mizunguko (round) 60.

Katika mchezo mwingine uliobakia kwe-nye kumbukumbu ni ule mchezo wa timu ya Afrika Kusini iliyotembelea Afrika ya

Mashariki 1958 na kucheza na Zanzibar. Katika mechi hiyo Zaghloul Ajmi akiwa bado ni mwanafunzi wa Skuli ya Gulioni alichaguliwa kuwemo katika mchang-anyiko (combined) ya Zanzibar. La ku-furahisha ni kuwa siku ya mchezo huo wanafunzi wote wa Gulioni kuanzia wa chumba cha tano walipewa ruhusa ya ku-ondoka na mapema ili wende kushangil-ia. Zaghalouli alikuwa ni katika wenye ku-fungua na alifungua katika mchezo huo ambao alikutana na watupaji hatari wa Afrika ya Kusini akiwemo Nat Adcock, T.L

Goddard, , H.J Tayfield, R. J. West-cott na C.B van Ryneveld.

Kati ya hao ni wale ambao wakirusha

zinazoitwa ‘bounce’ za hatari. Mmo-

jawao alikuwa Westcott na mipira yake yote ya mwan-zo ilichezwa vya kutosha bila ya kuk-wepwa na Za-

ghloul, Zanzibar ilishindwa katika

mechi hiyo lakini walikiri wachezaji wa

Afrika Kusini kuwa kush-indwa kwa Zanzibar kuli-

kuwa ni ‘honourable defeat yaani ‘kushindwa kwa heshima au kushindwa kiume”.

Tukijaaliwa tutaendelea wiki ijayo kueleza zaidi kuhusu jinsi kriketi ilivyokua ime-shamiri Zanzibar

Kriketi ilianza kwa kuchezwa kwa mtindo wa Test ikiwa ni mchezo mmoja kuchezwa kwa siku tano na mchezo mwengine ni wa siku moja Fifty Fifty (50-50) na siku hizi umekuja mtindo ambao umepata umaarufu mkubwa

ujulikanao kama Twenty-Twenty (T20).

Kriketi ni kama mchezo wa kabumbu lakini sio kabumbu kwani kriketi nayo hu-chezwa na wachezaji 11 kwa kila timu kwa mtindo tafauti.

Katika mchezo mmoja wa kriketi hupambana timu mbili na kunakuwako waamuzi wawili wanaoitwa Empire. Siku hizi kumeongezeka mwamuzi wa 3 ambaye kama kuna utata wa uamuzi na kunatakiwa itolewe rufaa, mwamuzi huyo huangalia kwenye televisheni marejeo ya mchezo na hukata uamuzi wake — ima kuubakisha uamuzi uliotolea kiwanjani au kuutengua.

Timu itakayopata kura baada ya kurushwa fedha huamua ama kuanza kucheza au kwenda uwanjani kudima. Nahodha wa timu hutakiwa awe makini zaidi ku-jua iwapo kiwanja wanachokichezea kinatoa fursa kwa wapigaji au warushaji wa mpira. Ikiwa ni kwa wapigaji baada ya kushinda kwenye kura ataamua timu yao ianze na atawachagua watakaokwenda kufungua ikiwa ni wachezaji wawili na wengine tisa wakisubiri zamu zao zifike.

Kiwanja cha kriketi kina ukubwa wa yadi 22 (20 cm) kwa marefu na futi 10 (3.0 m) mapana. Waamuzi hukaa katika kila upande mmoja. Anayerusha mpira hukaa upande wake na mchezaji ambaye huwa na bao la kuchezea hukaa na bao lake kusubiri mpira urushwe na nyuma ya mchezaji hukuweko golikipa wa mchezo huu ajulikanaye Wicketkeeper.

Ukirushwa mpira na mpigaji akitoka alipo akenda alipo mwenzake huhesabiwa ni mzunguko mmoja (one round) na akipiga mpira ukatoka nje ya kamba maalumu iliyozungushwa kiwanjani hupata mizunguko minne (four runs). Na ukipigwa uk-enda nje na kuvuka kamba pasi kutambaa hapo mpigaji hupata mizunguko sita (six runs) pasina kwenda yaani mmoja kutoka huku kwenda kule.

Mchezaji hutolewa pale mpira uliorushwa akiupiga juu na ukadakwa au ukarush-wa mpira na kumpiga mguu wa kushoto (lbw) kabla ya kuupiga, au kuviangusha vijiti (stumps) na akitolewa mchezaji mmoja hujiunga mchezaji mwengine kati ya wale tisa waliobaki nje wakisubiri zamu zao.

Kila mrushaji mpira hurusha mipira sita kwa mara moja. Katika mchezo wa siku moja ujulikanao kama 50-50 katika mchezo mmoja kwa wastani hurushwa mipira 300. Mchezo wa kriketi hutaka mtu awe anajua hesabu kuweza kujua maendeleo yake na ili timu iweze kushinda ijipange pangaje.

Hivi ndivyo kriket ichezwavyo

56

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

57

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 30: Zanzibar Daima Online

Tutachimba mafuta, lakini tu tayari?

A L LY S A L E H

Juzi tulipata taarifa kuwa hatimaye Rais wa Zanzibar Dk Ali Mo-hamed Shein amesaini mkataba na kampuni moja ya Uholanzi kuhusu wa utafiti na pengine baadaye uchimbaji wa mafuta.

Hatua hii tulikuwa tukiisubiri sana kama si zaidi ya sana. Hapa si pa-hala pa kurudia misukosuko na mashaka ya uchimbaji wa nishati hiyo ambayo sio tu ni muhimu ila pia ni ya lazima kwa maendeleo na uchu-mi wa Zanzibar.

Hakuna popote pale duniani ambapo nishati hii haikuweza kubadilisha hali za watu wake, ingawa kuna baadhi ya sehemu ambapo petroli na mazao yake yote yanayopatikana yamekuwa ni laana kwa nchi hizo.

Lakini hizo si nchi nyingi. Kwa hivyo si mifano ya kutufanya tuogope. Nchi hizo chache ni mifano ya kutufanya tuwe na hadhari, tuwe macho kwa sababu nishati hiyo inaweza kuwa ya maumivu makubwa kwetu na vizazi vijavyo.

Kwa hivyo, wakati tunapoanza kujiweka sawa na suala zima la uchimbaji wa mafuta jambo la kwanza kabisa ni kujitayarisha kwa miun-dombinu ya uchimbaji mafuta wa salama na wa maslahi kwa watu wetu.

Ni ushauri wangu, kwa hivyo, kwamba kama ilikuwa hatujaanza basi natuanze haraka kutandika mipango na miundombinu ya ku-hakikisha kuwa rasilmali hiyo inakuwa ni ya Wazanzibari wote na tusianze kama ilivyo-anza kutokea Mtwara au Ogoni, Nigeria, au kwengineko.

Pili, ni wakati huu tunapopaswa kujitayari-sha kwa mambo yote yanayohusu uchumi na uwekezaji wake. Hili ni suala la umuhimu mkubwa na tuna mifano mingi ya kuiga du-niani kama vile nchi za Qatar ilivyofanya kwa gesi asilia, au Oman ilivyofanya kwa mafuta na kadhalika.

Pia, huu ni wakati wa kujifunza juu ya suala la uwekezaji maradufu ( re-investment) hatua ambayo ni muhimu katika kukuza utajiri ili tuweze kujitayarisha kukuza uchumi na nchi isifadhaike pale mafuta yatapokwisha.

Katika hili pia kuna mfuko wa utajiri wa taifa (sovereign wealth fund) ambayo nchi ya An-gola, kwa mfano, imeuanzisha.

Hapa kuna mifano mikubwa ya nchi kama China, Qatar, Singapore, Abu Dhabi na sasa Mauritius ambazo zimepanua na kujichimbia kiuchumi kwa kubuni mashirika kadhaa ya uwekezaji wa kitaifa kwa maslahi ya nchi yetu.

Mashirika ya ndege kama ya Qatar, Sin-gapore; makampuni ya uwekezaji tunay-oyaona yanachipuka huko China — yote ni matunda ya faida zinazotokana na gesi au petroli lakini fedha zinarudishwa kwa wazalendo kukuza uwekezaji.

Nimekuwa na fikra inayofanana na hiyo kwa muda mrefu. Na fikra hii ilitokana pia na fikra inayofanana ya marehemu Ahmed Hassan Diria kuwa aliwahi kumshauri Rais Abeid Am-

ani Karume juu ya Zanzibar kuwekeza ndani au nje kwa mintaarafu ya kuwekeza kama nchi.

Leo hivi sasa nalia tena nalia machozi nikiona fursa za kilimo na biashara ziliopo Tanzania Bara ambapo Serikali ya Zanzibar imeshindwa kuzichukua. Tulipewa eneo la Makurunge na kama nchi tukazembea sasa Makurunge kuna petroli.

Hivi sasa takwimu angalau za mwaka 2010 zinaonyesha Zanzibar ilifanya biashara na hu-duma na Bara kwa kiwango cha Shillingi bil-lion 125 wakati wenzetu Bara walihitajia kuto-ka Zanzibar bidhaa na huduma zenye thamani ya Shillingi billioni 25 tu. Hiyo ni nakisi ya wazi.

Wakati nakisi hiyo haitaki tochi, chembilecho vijana, kuna fursa lukuki ambazo Serikali ya Zanzibar inazisinzilia. Hakuna bidhaa yoyote ya Tanzania Bara ambayo imepata wanunuzi wa kutosha Zanzibar kama vile pasivyokuwa

na uhakika wa usafiri wa kubeba mazao na kuyaongeza thamani.

Ni wazi kuwa kama Serikali ya Zanzibar in-gewekeza katika eneo la kilimo Tanzania Bara

naamini ajira kadhaa zingepatikana kupitia huduma ya usafiri, viwanda na hata utafutaji wa masoko maana alizeti, korosho, mahindi, maharage, tangawizi, zabibu zote hizo zina masoko makubwa ya nje.

Pia kama Benki ya Watu wa Zanzibar ingejihu-sisha katika uwekezaji huko Bara mbona in-gekuwa rahisi kupunguza nakisi hiyo ambayo kwa kweli inaipunguzia Zanzibar nguvu lakini kwa watu wa kawaida wanaona Zanzibar ni kama tegemezi kwa Tanzania Bara.

Kwa hakika ninachosema ni hiki: inasikiti-sha kuoana Serikali ya Zanzibar haina mradi wowote huko Bara pamoja na kuwako upana wa fursa za kiuwekezaji.

Jambo la tatu la kushauri wakati huu ni lile la kuwasomesha vijana wetu uhandisi wa mafu-ta na gesi. Wiki moja nyuma nilimsikiliza Wa-ziri wa Fedha wa Tanzania, akitoa takwimu za

usomeshaji katika sekta hizo na moyo ulini-uma maana hakutaja hata mara moja juu ya kuipatia Zanzibar wataalamu.

Ni wazi kuwa wenzetu hawatatukumbuka na sisi tunapaswa kujua kuwa toka hapo tuna chumi zinazoshindana basi sasa pia tutakuwa na sekta za mafuta na gesi zitazo-kuwa zinashindana. Tusitaraji hata kwa uku-bwa wa ukucha kuwa tutapata fursa kutoka kwao.

Ni vyema tujipange, tujiandae, ingawa na-jua kuwa tumeanza. Tuna msingi mbovu wa masomo ya sayansi ni vyema tujirekebishe. Na kila ambapo tunaweza kuazima utaalamu tufanye hivyo. Tusione aibu kutumia uwezo mkubwa walio nao masahibu zetu kama Oman, Qatar, Abu Dhabi maana mhisani wako ndiye anayekufaa iwapo jirani kashu-

ghulika na yake na hana nafasi ya kukusaidia au hataki.

BARZA YA JUMBA MARO

58

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

59

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 31: Zanzibar Daima Online

Taifa lisilokumbuka misiba yake, halithamini furaha yake

Maisha yanasonga mbele. Hayakusi-mama. Watu wanazaliwa na wa-naendelea kuzaliwa siku hadi siku,

ingawa watu hawa hutofautiana na watu kwa lugha na mataifa. Hivi ndivyo mwe-nyewe Muumba alivyofanya. Maamuzi yake ambayo hakika hayakuwa na ubaya wowote baada ya kumtayarisha binad-amu huyu mazingira mazuri ya kuishi. Ni

binadamu hawa ndio maadui wakubwa kutokana na pumzi walizopewa bure na Muumba wakisahau hata siku ya mwisho siku, ambayo kila nafsi itauun-gama mbele yake Muumba.

Dunia kweli ni uwanja wa fujo, na baada yote haya pumzi zitaziba na kuwa sasa ni zamu yako kuelekea kwake Muumba. Kwa hakika, hata na wale wanaokusin-

dikiza kwenye safari yako ya mwisho, nao itafika siku yao – kama si leo basi kesho – nao watakwenda katika njia hiyo hiyo uliyotangulia kuiandama na iliyo-tanguliwa kuandama na wa kabla yako.

Hivyo mimi, kwa hakika, sitojutia kuwa Mtanzania mwenye asili ya Zanzibar, hata kama sina thamani yoyote katika taifa langu, kwani Mungu hakukosea

kuniteremsha kwa wazazi ambao ni Wa-zanzibari ambao baadae waliunganishwa na kuwa Tanzania, yumkini bila ya ridhaa yao na au kama waliridhia wenyewe, pasi kujua athari zake.

Hapa Zanzibar, hata baada ya Serikali ya Mseto, bado watu wanazidi kuteseka na kubaguana kuanzia wao wenyewe hata kitaifa na kimataifa. Hebu jiulize,

N A M UA N D I S H I M A A LU M

TANZIA

60

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

61

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Page 32: Zanzibar Daima Online

kuna sababu gani hata kufikia leo wa-husika wa ajali ya meli ya Spice Islanders wakawa hawajachukuliwa na kupelekwa katika Mahakama ya Uhalifu dhidi ya ubinaadamu (ICC) kule mjini The Hague? Kwani hivi hawa wana tofauti gani na Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake Wil-liam Ruto wa Kenya? Au pengine ni kwa kuwa wahanga wengi walikuwa ni ‘nzige’ kutoka Pemba ambao hawana thamani katika taifa lao?

Naandika kwa uchungu. Miaka miwili nyuma nilipoteza nuru ya moyo wangu – mke wangu, ambaye ndio kwanza tuli-kuwa wanagenzi kwenye maisha ya kifa-milia. Roho ya mke wangu ilikuwa mion-goni mwa maelfu ya nyengine zilizozama usiku wa manane pasipokuwa na usaid-izi wowote kwa uzembe na tamaa iliyo-tawala mkasa mzima wa kuzama kwa meli hiyo.

Bado rikodi zipo zinazoonesha kuwa ile ni ajali iliyoweza kuepukwa. Hata pale abiria walipotoa ushauri hawakuziskiliz-wa kwani wengi wao walijua meli hiyo ilikuwa na mashaka makubwa kuvuuka kufika Pemba. Hadi leo, licha ya udogo wa Zanzibar, majibu ya wapi alipo na-hodha wa meli hiyo ni kitendawili hadi leo. Hakuna ajuae maendeleo ya kesi hii ambayo imewagusa watu wengi, kwani kwa njia mmoja au nyengine hata vyombo vya habari vimesusia kutangaza maendeleo yake.

Ni kama vile kila mtu – kuanzia serikali inayoambiwa eti ndiyo mdhamini wa maisha na usalama wa raia wake, vyom-bo vya habari vinavyoambiwa eti ndiyo mdomo wa jamii, hadi asasi za kiraia zinazoambiwa eti ndiyo injini ya jamii in-ayowajibika na kuendelea, bali hata watu mmoja mmoja – wameamua kuizika Mv

Spice Islanders na roho zote Nungwi, bali hata kwenye shimo la sahau. Taifa lisilo-kumbuka misiba yake, halioni thamani ya furaha yake.

Ndiyo, sasa ni miaka miwili tokea meli hiyo yende kwenye mvungu wa bahari ya kina kirefu na roho za wapendwa wetu. Mayatima waliowachwa na wazazi wao wanataabika na wengine wakifa kidogo kidogo kutokana na kuathirika na mkasa mzima wa kupotelewa na wapenzi wao.

Lakini hadi leo, hakuna CCM, Chadema, CUF au NCCR-Mageuzi ambao wame-wahi kuishinikiza serikali angalau kuit-ambua tarehe 10 Septemba kama ni Siku ya Kumbukumbu ili japo kuwapa heshi-ma wahanga hao. Miongoni mwa majibu wanayotoa wanasiasa hao ni kwamba Zanzibar haina utamaduni wa kuombo-leza misiba yake milele kwa sababu ya mafungamano yake na dini ya Kiislamu.

Lakini hili ni jawabu jepesi la kukwepa uwajibikaji. Ni ule ule tu usaliti wetu wa kawaida wa kutoana muhanga, tunapo-kosana kutolana sadaka dhahiri shahiri, basi angalau huzisaliti hisia na nyoyo zetu. Kwa kuunyamazia kimya msiba huu, sote kwa pamoja tunaisaliti Zanzi-bar yetu.

Ni kweli kuwa Rais Ali Mohamed Shein aliunda Tume ya Uchunguzi baada ya ajali hiyo, lakini tangu mwanzo ilifaha-mika kwamba hicho kilikuwa kizungum-kuti. Ulikuwa mchezo wa kuigiza, maana Tume ilipendekeza ya kuyapendekeza, lakini hakuna lililokuwa. Tuliwasaliti wa-hanga wa Spice Islanders.

Leo hii maiti za watoto wadogo wasio-kuwa na hatia, akinamama, vijana wabi-chi, waze na watu wazima, popote zilipo, naamini zinaamini kwamba zinajua nchi

yao na viongozi wao waziteua roho hizo ziwe chakula cha samaki. Ni kama vile waliambiwa: “Kufeni, hamukuwa na tha-mani katika taifa lenu na ndio maana hata kaburi lenu lilikuwa ni meli!”

Ndiyo, tafsiri inabakia kuwa ni hiyo kwani hata baada ya kufa kwao, hakuna fikira zozote za kiutu zilizochukuliwa. Watoto wao wanateseka bila misaada na wale waliopatwa na ulemavu wa kimwili na ki-saikolojia kutokana na kukumbwa na msi-ba huu mzito, hawana matibabu yoyote. Hawakuulizwa kala wala kalamu, zaidi ya wengine – tena baadhi yao tu – kupata shilingi 500,000 miongoni mwa mamilioni yaliyokusanywa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Najua wako hawapendi kuyasikia sambe kuyaona majumba yakiwa yameachwa bila ya watoto au wazazi waliokuwamo kabla ya tarehe 10 Septemba 2011. Haya yote hayakuleta kimanzi kwa viongozi wetu angalau kuipa kisogo dunia na ku-wahurumia wahanga hawa masikini. Si wawakilishi, si wabunge waliokwenda katika majimbo yao kuwaulizia familia hizi zenye kumbukumbu ambayo inat-ambulika katika dunia kuwa ni miongoni

mwa ajali mbaya ya meli iliyoua mamia ya watu.

Lau serikali hii ingelikuwa kweli serikali ya watu, inayotokana na watu na kwa ajili ya watu, basi zamani ingelikuwa imeshatangaza kwamba siku hii ni siku ya mapumziko na, kama si kukusanyika pamoja tukasoma khitima na kuwatakia dua maiti wetu, basi angalau kiongozi wa nchi angelisoma risala ya kuwakumbuka na kulaani uzembe huu.

Lakini waliokufa mule hawakuwa viongozi wa kisiasa, hawakuwa viongozi wa kijeshi, hawakuwa watu mashuhuri. Walikuwa watu wa kawaida – vitoto, mama zao, baba zao, bibi na babu – wanyonge tu wa Mungu.

Miongoni mwa hao alikuwemo mke wan-gu. Na hata kama serikali yake hapa duni-ani imemsahau, mimi mumewe sitaacha kumkumbuka. Serikali yetu mimi naye ndani ya nyumba – mimi nikiwa Rais naye Waziri Mkuu – haitamsahau daima. Kila siku hii itamtilia ubani na kumuombea dua. Itaulaani uzembe wa serikali ya akina Dk. Shein, Maalim Seif Sharif na Balozi Seif Iddi, ambayo inajifanya haina haja naye.

62

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03>

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03>

63

ZANZIBAR DAIMA ONLINE TOLEO 03 >

WWW.ZANZIBARDAIMA.NET TOLEO 03 >

Unaweza kutangaza biashara yako kupitia Zanzibar Daima Online, jarida la kila wiki mbili lenye wasomaji wengi wenye kuzungumza lugha ya Kiswahili duniani kote.