52654717-lnr-swahili

Upload: martynejohn

Post on 27-Feb-2018

381 views

Category:

Documents


2 download

TRANSCRIPT

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    1/32

    Muhtasari wa Sera na Sheria za

    Ardhi na Maliasili

    Mwongozo kwa Lugha nyepesi waSera na Sheria za Ardhi, Misitu na Wanyamapori

    wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Umetayarishwa kwaWildlife Working Group (WWG)

    Agosti 2004

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    2/32

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    3/32

    Muhtasari wa Sera

    na Sheria za

    Ardhi na Maliasili

    Mwongozo kwa Lugha nyepesi waSera na Sheria za Ardhi, Misitu na Wanyamaporiwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

    Umetayarishwa kwaWildlife Working Group (WWG)

    Agosti 2004

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    4/32

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    5/32iMuhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Dibaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .ii

    Ardhi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .1Sera ya Ardhi ya Taifa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .1Sheria ya Ardhi, 1999 na Sheria ya Ardhi ya Kijiji, 1999 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .2

    Kanuni Kuu,Wajibu na Majukumu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .2Aina za Ardhi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .-4Usimamizi wa Ardhi ya Kijiji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .5Ugawaji wa Ardhi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .6Hati . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .7

    Uhawilishaji wa Ardhi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .8Usuluhishi wa Migogoro . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .9

    Misitu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .11Maendeleo ya Jumla na Malengo ya Sera . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .11Majukumu ya Jamii . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .12Usimamizi wa Misitu wa Jamii kwa Ardhi ya Kijiji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .13Usimamizi wa Misitu wa Jamii kwa Ardhi ya Akiba . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .15Namna jamii zinavyoweza kunufaika na Fursa Mpya katika Usimamizi wa Misitu . . . . . . .16

    Wanyamapori . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .17Usuli wa Sheria . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .17Sera ya Wanyamapori Tanzania . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .18Namna Sera ya Wanyamapori inavyoweza kutekelezwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .20Ushiriki wa Jamii katika Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori . . . . . . . . . . . . . . . . . . .21

    Shukrani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .25

    Yaliyomo

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    6/32

    DIBAJI

    ii Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Serikali huhitaji kuwa na mpango wa utekelezaji, unaojulikana kama Sera. Sharia husika zinatumikakusimamia utekelezaji wa sera na kuzisaidia kulinda ipasavyo rasilimali muhimu kama ardhi, misitu nawanyamapori. Kuna tofauti muhimu kati ya Sheria na Sera. Sera inazungumzia:

    Mipango ya Serikali kwa sekta mbalimbali, kama vile ardhi, elimu, afya, kilimo n.k.

    Namna Serikali itakavyotekeleza mipango yake

    Kuweka wazi sheria na kanuni zinazopaswa kudhibiti utoaji uamuzi

    Ni Sheria na wala si Sera ambazo ndizo zinaelekeza haki muhimu,mamlaka na wajibu katika kudhibiti

    utkelezaji wa sera kama ya ardhi na rasilimali. Sheria zinafafanua namna ya kutekeleza sera na pia:

    Kuamua ni asasi zipi na wahusika wenye haki na mamlaka ya kutoa maamuzi

    Zinaeleza adhabu inayotolewa kwa kuzivunja sheria na kanuni

    Kuzisaidia mahakama kuhimiza utekelezaji

    Kwa hiyo sheria zinawaonyesha wadau mipaka namajukumu yao. Sera zinatoa mwongozo tu wa namnawadau wanavyoweza kuhusishwa.

    Muhtasari huu unatoa hoja muhimu kuhusu sera nasheria zinazotawala sekta tatu muhimu za rasilimali:ardhi, misitu na wanyamapori. Taarifa iliyomo katikawaraka huu imetayarishwa ili kutoa elimu kwa umma nakuvisaidia vijiji katika jamii za vijijini. Sekta za ardhi,misituna wanyamapori zimechaguliwa kwa sababu:

    Umuhimu wa elimu kwa umma

    Sera na sheria zinazohusiana nazo zimepitia mabadiliko mengi hivi karibuni

    Rasilimali za sekta hizi huwapa wanavijiji njia zao za kuendeshea maisha

    Ni muhimu kwa jamii husika kusimamia ipasavyo rasilimali hizi

    Wadau ni kina nani?

    Wale wote wanaoshiriki katika serawakiwemo wale: wanaoathiriwa na Sera wanaotekeleza sera wanaotoa fedha za kusaidia sera.

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    7/32

    SERA YA ARDHI YA TAIFASera ya kwanza ya Ardhi ya Taifa nchini Tanzania ilipitishwa mwaka 1995 kwa sababu:

    Ongezeko la idadi ya watu nchini Tanzania lilimaanisha kuwa watu wengi zaidi walikuwawanatumia ardhi.

    Kulikuwa na migogoro mingi kati ya wakulima na wafugaji kuhusu matumizi mbalimbali yaardhi.

    Watu wa maeneo mengi ya vijijini walijikuta hawana uhakika kuhusu haki zao za ardhi.

    Kwa kuwa baada ya uchumi kuamliwakuwa na misingi ya soko huria suala lawawekezaji binafsi katika sekta yaardhi ilibidi kupewa umuhimu.

    Kwa kuwa ardhi hivi sasa inaweza kununuliwa na kuuzwa kuna haja ya kudhibiti vizuri utaratibuhuo.

    Kuna migogoro mingi kuhusu kutumia na kumiliki ardhi.

    Sera ya Ardhi ya Taifa inasema kuwa ardhi ya taifa imekuwa ikisimamiwa vizuri tangu tupate uhuru.Ili kutoa huduma nzuri kwa watu, inalenga:

    Kugawa ardhi bila upendeleo

    Kumpa kila mtu haki ya kutumia ardhi

    Kuhakikisha kuwa haki ya watu iliyopo kuhusu ardhi, hasa wale wasio na hati za kisheria,wanaeleweka kwa urahisi, wanakubalika na kupewa hadhi ya kisheria.

    Kuweka ukomo wa kiasi cha ardhi inayoweza kumilikiwa na mtu binafsi.

    Kuhakikisha kuwa ardhi inatumiwa kwa njia zitakazoboresha maisha ya kila mtu.

    Kuboresha na kufafanua zaidi namna ardhi hiyo inavyosimamiwa na namna migogoro inayohusuardhi inavyoweza kutanzuliwa.

    Kuhakikisha kuwa ardhi inasimamiwa vizuri ili isitumiwe sana na iweze kuzalisha mazao kwamuda mrefu.

    ARDHI

    1Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Changamoto!

    Kwa kuwa ardhi sasa inatengwa kwa wawekezaji binafsi, jehaki za ardhi za wafugaji na jamii za asili zinalindwa vipi?

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    8/32

    ARDHI

    2 Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Sera inasema mambo muhimu kuhusu namna ardhi inavyotakiwa kusimamiwa nchini Tanzania.

    Rais ndiye aliyepewa dhamana ya umiliki wa ardhi yote nchini Tanzania kwa niaba ya Watanzania.

    Ardhi ina thamani.

    Watu hawawezi kunyanganywa haki zao za ardhi bila ya idhini ya kisheria na malipo ya fidiakamili, ya halali na kwa wakati.

    Mabaraza ya Vijiji yatasimamia ardhi yote ya vijiji.

    Mipango haina budi kufanywa ili kuyalinda maeneo yenye umuhimu wa pekee kama vile vyanzovya maji, visiwa, fukwe, misitu, mito, njia za kuhamahama wanyama n.k.

    SHERIA YA A RDHI , 1999 NA SHERIA YA A RDHI YAVIJIJI, 1999Sheria hizi zinawaeleza watu jinsi ya kutumia, kusimamia na kumiliki ardhi Tanzania Bara.

    Kanuni Kuu,Wajibu na Majukumu

    Madhumuni ya sheria hizi ni kuhakikisha kuwa mawazo ya jumla na malengo ya Sheria ya Ardhi yaTaifa yanashughulikiwa. Sheria ya Ardhi inafafanua wazi kuwa ardhi yote nchini Tanzania ni ya ummana Rais ndiye mwenye dhamana kwa niaba ya raia wote. Katika Serikali Kuu Rais anatoa mamlakakwa Waziri wa Ardhi na Kamishna wa Ardhi kuhakikisha kuwa kila kitu kinafanywa vizuri. Kamishnaamepewa mamlaka makubwa ya kutoa uamuzi unaohusu usimamizi wa ardhi na sasa ndiyemsimamizi mkuu wa ardhi nchini.

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    9/32

    Usimamizi wa Ardhi Nani anafanya Nini

    Rais Mdhamini wa ardhi yote kwa niaba ya raia wa Tanzania.Anaweza akamnyanganya mtu haki ya kutumia ardhi.Anaweza kuchukua ardhi kwa manufaa ya umma.

    Waziri wa Ardhi Anamsaidia Raisi na kumsimamia Kamishina wa Ardhi kuhusu masualaya ardhi.

    Kamishna wa Ardhi Mhusika mkuu wa masuala ya ardhi.Humsaidia Rais kutekeleza Sheria za Ardhi.Anaweza kuwaomba watu wengine au asasi kutekeleza baadhi yamajukumu.

    Anafanya uamuzi muhimu kuhusu namna ardhi inavyogawanywa.Halmashauri za Wilaya Zinasaidia kueleza asasi zinazohusika kuhusu uamuzi wa usimamizi wa ardhi.

    Mabaraza ya Vijiji Husimamia ardhi ya kijiji kwa niaba ya Mikutano ya Vijiji.Hutoa uamuzi kuhusu maombi ya ardhi kutoka kwa wanavijiji na wageni.Hugawa ardhi ya kijiji baada ya kuidhinishwa na Mikutano ya Kijiji.Hutoa hati kwa watu ili kuonyesha kuwa wana haki ya kuishi palewalipo.

    Mikutano ya Vijiji Huangalia iwapo Mabaraza ya Vijiji yanasimamia ardhi ya kijiji ipasavyo.Hukubaliana kuhusu uamuzi wa mahitaji ya maisha ya kijijiyanayotakiwa kushughulikiwa.

    Kamati za Hukumu za Vijiji Huweka mipaka ya ardhi.Huamua nani mmiliki wa ardhi fulani.Huamua migogoro iwapo watu wataona kuwa kumefanyika kosa.Huwajibika kwa Mabaraza ya Vijiji.

    Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji Huamua migogoro kuhusu masuala ya ardhi katika ardhi ya kijiji.

    ARDHI

    3Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Changamoto! Wafugaji na Haki za Ardhi

    Mkutano wa Asasi Zisizo za Serikali kuhusu Wafugaji (PINGOs) unasema kuwa ufugaji unatoa mchangomkubwa kwa uchumi wa Tanzania, lakini manufaa yote hayo yamepuuzwa na watunga sera. Wafugajihawajashirikishwa ipasavyo katika kutunga sera zinazowaathiri.

    Ufugaji ni uti wa mgongo wa sekta ya biashara ya mifugo, hutumia kwa faida ardhi mbaya na kavu, nahuwaendeshea maisha zaidi ya watanzania 400,000. Ufugaji pia ni njia ya maisha ya kiasili ambayo ni lazimaitetewe na sheria.

    Jambo muhimu ni iwapo sheria na sera za sasa za ardhi zinashughulikia masuala ya wafugaji nawawindaji/wakusanyaji chakula, kama vile umaskini, kutokuwa na uhakika wa ardhi, kudhurika, migogoro nawatumiaji wengine wa ardhi, uharibifu wa maliasili, na kudharau maisha ya wafugaji?

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    10/32

    Aina za Ardhi

    Ardhi yote ya Tanzania imegawika katika aina tatu:

    Ardhi ya Akiba ni iliyotengwa kwa ajili ya wanyamapori, misitu, hifadhi za baharini n.k. Namna maeneohaya yanavyosimamiwa yanaelezwa katika sheria zinazolinda kila sekta (k.m. Sheria ya Hifadhi yaWanyamapori,Sheria ya Hifadhi za Taifa, Sheria ya Hifadhi za Bahari na maeneo Tengefu,n.k.).

    Ardhi ya Kijiji inajumuisha ardhi yote iliyomo ndani ya mipaka ya vijiji vilivyosajiliwa, ambapoMabaraza ya Kijiji na Mikutano ya Kijiji vimepewa mamlaka ya kusimamia. Sheria ya Ardhi ya Kijijiinatoa maelezo ya namna usimamizi unavyotakiwa kufanyika.

    Ardhi ya Kawaida ni ardhi ambayo si ya akiba wala ya kijiji na kwa hiyo, inasimamiwa na Kamishnawa Ardhi.

    Usimamizi wa Ardhi ya Kijiji

    Mabaraza ya Vijiji yana jukumu la kuangalia ardhi ya kijiji kwa niaba ya Mikutano ya Vijiji. Wanakijijiwana haki inayoitwa haki ya kimila ya umiliki inayomaanisha kuwa kama wameishi katika ardhi hiyokwa miaka mingi wana haki nayo. Sheria ya Ardhi ya Kijiji inawapa watu wenye haki ya kimila yaumiliki, haki ya ulinzi wa kisheria sawa na wale wenyeji inayojulikana kuwa haki ya umilikiwaliyopewa. Watu waliopewa haki ya umiliki nao wamepewa hadhi ya kisheria.

    ARDHI

    4 Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    11/32

    Mabaraza ya Vijiji hayana budi kuzingatia hoja hizi muhimu kwa ajili ya usimamizi wao wa ardhi za vijiji:

    Ardhi haina budi kutumika kwa hali ambayo itadumisha maisha endelevu ya watu na matumiziya rasilimali.

    Miti,maji na rasilimali nyingine vijijini na maeneo yanayozunguka vijiji havina budi kutunzwa ipasavyo.

    Kuna vyombo vingine vya umma vyenye mamlaka kwa ardhi ya kijiji na mazingira yake namaamuzi na amri zao vinaweza kuathiri matumizi ya ardhi ya kijiji.

    Ardhi ya kijiji imo ndani ya mamlaka ya serikali za mitaa ili mamlaka hiyo iweze kuombwakutoa maoni yao wakati mwingine.

    Sheria ya Ardhi ya Kijiji inaelekeza Mabaraza ya Vijiji kugawa ardhi yao katika aina tatu:

    Ardhi ya Jumuiya

    Ni ardhi inayotumiwa na watu wengi kijijini inayojumuisha misitu, maeneo ya malisho aumaeneo mengine yenye maliasili yanayosimamiwa na vikundi vya watu

    Isigawiwe kwa mtu yeyote binafsi

    Itakayojulikana kama ardhi za kijiji za jumuiya

    Ardhi inayokaliwa ambayo imegawiwa na inatumiwa kwa ujenzi wa nyumba, kilimo, biashara n.k.na watu binafsi au familia mojamoja.

    Ardhi ya matumizi ya baadaye ambayo inatengwa kwa matumizi ya baadaye ya watu binafsi au jumuiya.

    Matumizi yoyote ya sehemu ya ardhi ya kijiji ya makundi hayo huamuliwa na kuidhinishwana Mkutano wa Kijiji.

    Mabaraza ya Vijiji yanaweza kufanyamikataba ya pamoja ya matumizi ya ardhi na Baraza mojaau zaidi katika ardhi za jirani. Iwapo yanataka kufanya hivyo, kila Baraza la Kijiji halina budi kwanza:

    Kuiarifu Halmashauri ya Wilaya mipango yao.

    Kupata idhini ya kila Mkutano wa Kijiji unaohusika.

    ARDHI

    5Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Sheria ya Utawala wa Kijiji na Serikali ya Mitaa ya 1982

    Sheria hii inazipa serikali za kijiji mamlaka ya kisheria ya kutumia, kusimamia na kumiliki ardhi na malinyingine. Aidha inaipa jukumu serikali ya kijiji la masuala na shughuli za vijiji. Sheria hii inazipa serikali zavijiji mamlaka makubwa ya kufanya mikataba na makampuni yanayosaidia maisha na ustawi wa wanakijiji.

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    12/32

    Iwapo angalau wanakijiji mia moja wanaona kuwa Baraza la Kijiji chao halisimamii vizuri ardhi yakijiji na kulingana na sheria za ardhi, hawana budi kuiarifu Halmashauri ya Wilaya ambayo itamwarifuKamishna wa Ardhi. Anaweza kuunda tume itakayopendekeza kuwa ama Halmashauri ya Wilaya aukamishna mwenyewe atakuwa na jukumu la kusimamia ardhi ya kijiji. Aidha, mwanakijiji yeyoteanaweza kulishitaki Baraza la Kijiji iwapo ataona kuwa ardhi ya kijiji inasimamiwa vibaya.

    Ugawaji wa Ardhi

    Mabaraza ya Vijiji yana jukumu la kugawa ardhi ya kijiji lakini hawawezi kufanya hivyo bila ya idhini yaMikutano ya Kijiji.

    Mabaraza ya vijiji yanaweza kutoa haki zakimila za kumiliki ardhi kwa wanakijijimmojammoja, familia, asasi za kijiji auwananchi wasio wanakijiji watakaopewaHati ya Kumiliki Kimila ili kuthibitishakuwa wanamiliki ardhi.

    Vijiji vinaweza pia kukodisha ardhi kwa mtuwa nje atakayepewa haki sawa na kijiji. Hakihizi zinajulikana kama haki nyambuo.

    ARDHI

    6 Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Changamoto!

    Tayari kuna sheria zinazovipa vijiji mamlaka ya kudhibitiardhi yao na rasilimali nyingi muhimu. Tatizo ni kwambasheria hizi hazitekelezwi na mawazo mazuri yaliyomokatika sera hayatekelezwi kwa vitendo.

    Serikali itafanya nini ili kuhakikisha kuwa Sheria na Sera zilizopo zinatekelezwa na ili vijiji viweze kutekeleza haki yao ya kutumia na kudhibiti ardhi?

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    13/32

    AINA ZA UKODISHAJI

    Daraja Kiasi cha Ardhi Muda Watoa uamuziDaraja A. Hekta 5 za ardhi Miaka 5 au pungufu Huamuliwa na Baraza la Kijiji

    Daraja B. Kuanzia hekta 6 hadi 29 Miaka 6 hadi 9 Huamuliwa na Baraza la Kijiji naza ardhi Mkutano wa Kijiji

    Daraja C. Hekta 30 au zaidi Miaka 10 au zaidi Huamuliwa na Baraza la Kijiji,hukubaliwa na Mkutano wa Kijijikwa kushauriwa na Kamishna.

    Kuna aina tatu za ukodishaji zinazoweza kutumiwa na watu wa nje kulingana na kiasi cha ardhiwanachohitaji na muda wanaotaka kutumia ardhi. (Angalia jedwali la hapo juu).

    Endapo vijiji vinaamua kukodisha sehemu yoyote ya ardhi yao, havina budi kwanza kuhakikisha kuwa:

    Inalingana na mipango ya namna ardhi hiyo itakavyotumiwa.

    Vijiji vinaweka ardhi ya kutosha ya akiba na matumizi ya jumuiya.

    Wanapanga namna ukodishaji huo utakavyoweza kukinufaisha kijiji.

    Mabaraza ya Kijiji hayatatoa ardhi kwa wageni au makampuni ya kigeni. Itakuwa kinyume cha sheriana inaweza kuhatarisha haki za kimila za kijiji za kumiliki ardhi.

    Utaratibu wote hauna budi kufanywa kwenye fomu rasmi za ardhi zitakazosambazwa kwa vijiji.Utaratibu usiotumia fomu hizi rasmi hautakuwa halali.

    Sheria ya Ardhi ya Kijiji inahakikisha kuwa ardhi iliyogawiwa na Mabaraza ya Vijiji kati ya mwaka 1978na Mei 1, 2001 inapewa hadhi ya kisheria.

    Hati

    Vijiji havitapewa tena hati miliki kwa ardhi ya vijiji. Badala yake Mabaraza ya Vijiji yatapewa Hatiza Ardhi ya Vijiji ambazo:

    Zitakayotolewa kwa niaba ya Rais.

    Zitakayokuwa ushahidi wa haki ya kimila ya kumiliki katika eneo fulani la ardhi ya kijiji.

    Zitakayoyapa Mabaraza ya Kijiji mamlaka ya kusimamia ardhi za kijiji.

    Zitakayoonyesha mipaka ya ardhi ya kijiji iliyokubaliwa na kuwekwa katika ardhi.

    ARDHI

    7Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    14/32

    Uhawilishaji wa Ardhi

    Rais anaweza kuhawilisha ardhi ya kijiji kuwa ardhi ya kawaida au ya akiba ambayo haitasimamiwatena na Baraza la Kijiji. Anaweza kuamua kufanya hivyo kwa manufaa ya umma, kwa mfano iwapoardhi inahitajika kwa uwekezaji.

    Iwapo Rais na Wizara ya Ardhi wanataka kuendelea na uhawilishaji huo wa ardhi, hatua zifuatazohazina budi kuchukuliwa:

    Maelezo ya uhawilishaji uliopendekezwa hayana budi kuchapishwa katika Gazeti la Serikalina kupewa Baraza la Kijiji.

    Kamishna wa Ardhi hana budi kuhudhuria mkutano wa Baraza la Kijiji au Mkutano wa Kijijikueleza sababu za kuhawilishwa ardhi hiyo na kujibu maswali mengine yoyote watakayoulizawanakijiji.

    Aina, kiasi na muda wa kulipa fidia hauna budi kukubaliwa na Baraza la Kijiji na Kamishna waArdhi kabla ya kuhawilishwa kwa ardhi ya kijiji.

    Iwapo Kamishna wa Ardhi na Baraza la Kijiji hawatakubaliana kuhusu kiasi cha fidiaitakayolipwa,basi uhawilishaji huo utasimama mpaka Mahakama Kuu itakapotoa uamuzi kuhusukiasi cha fidia hiyo.

    ARDHI

    8 Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    15/32

    Waziri anaweza kutangaza eneo lolote la ardhi ya kijiji kuwa Ardhi ya Hatari kama ataona ni hatarimno kuimiliki au itaweza kuharibiwa kwa kukaliwa. Ardhi hiyo ni pamoja na:

    Mabwawa ya mikoko

    Maeneo chepechepe

    Ardhi iliyotengwa kwa kutupia taka za hatari

    Ardhi iliyopo katika eneo la mita sitini la kingo za mto au ziwa

    Ardhi isiyoendelezwa kutokana na udhaifu wake

    Ardhi isiyoendelezwa kutokana na umuhimu wake kwa mazingira

    Kabla Waziri hajatangaza ardhi ya hatari, hana budi:

    Kuonyesha mipaka ya eneo hilo

    Kuchapisha maelezo ya ardhi ya hatari inayopendekezwa katika Gazeti la Serikali

    Kuyaarifu mamlaka ya eneo husika

    Kuwaarifu watu wote wanaomiliki eneo hilo la hatari

    Kumwarifu Rais iwapo inakaliwa na watu wenye haki za kimila. Rais atafanya mpango wakuwalipa fidia watu hao.

    Usuluhishi wa Migogoro

    Kuna ngazi tano za mahakama zilizopangwa na sheria za ardhi kusuluhisha migogoro ya ardhi.Mahakama hizo kuanzia ya chini mpaka ya juu ni:

    Baraza la Ardhi ya Kijiji

    Mabaraza ya Kata

    Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya

    Mahakama Kuu (Kitengo cha Ardhi)

    Mahakama ya Rufaa ya Tanzania

    ARDHI

    9Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    16/32

    Vijiji vyote havina budi kuwa na Baraza la Ardhi la Kijiji litakalowasaidia watu wasiokubaliana nauamuzi utakaowanufaisha wote. Wajumbe wa Baraza:

    Watakuwa watu saba, wakiwemo angalau wanawakewatatu

    Watateuliwa na Baraza la Kijiji na kuthibitishwa naMkutano wa Kijiji

    Watatumikia kwa kipindi cha miaka mitatu

    Pale ambapo mipaka ya kijiji haikuamuliwa,wanakijiji hawana budi

    kuanza utaratibu unaojulikana kama hukumu . Ina maana kuwawanahitaji kuamua mahali patakapowekwa mipaka ya ardhi yakijiji na kuwashirikisha wale wote ambao wameathirika.

    Vijiji havina budi kuunda Kamati za Hukumu za Vijiji zenye Wajumbe:

    Watakaochaguliwa na Mkutano wa Kijiji

    Wasiozidi tisa, wakiwemo angalau wanawake wanne

    Watatumikia miaka mitatu

    Wataruhusiwa kutumikia kwa kipindi kimoja zaidi cha miaka mitatu iwapo watachaguliwa tena.

    Kamati hii itakuwa na wajibu wa kufanya yafuatayo:

    Kuamua mipaka ya ardhi ya kijiji wakati wa kutoa hukumu

    Kutenga ardhi au alama za haki za kutumia njia ya jumuiya

    Kutumia sheria ya kimila ili kuchambua haki za ardhi za watu walioathiriwa wakati wa kutoahukumu

    Kulinda maslahi ya wanawake, watoto, walemavu n.k. wakati wa kutoa hukumu

    Vijiji havina budi pia kumteua Mshauri wa Hukumu wa Kijiji ambaye:

    Ni mtu wa kuheshimika kijijini, mtaalamu, mtumishi wa umma au afisa, au hakimu

    Atateuliwa na Baraza la Kijiji

    ARDHI

    10 Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Changamoto!Vyombo vya kutoa uamuzi vyakijiji havina budi kupewa taarifakuhusu haki zao na wajibu wao nasheria na sera muhimu.

    Mafunzo ya kuongeza uwezokuhusu uongozi na stadi zakutolea maamuzi yataboreshauwezo wao wa kusimamia vizuri

    ardhi ya kijiji.

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    17/32

    MAENDELEO YA JUMLA NA MALENGOYA SERAKuna mabadiliko mengi yanayofanywa katika sheria zinazotawala misitu ya Tanzania. Sera Mpya yaMisitu ya Taifa ilitolewa Machi 1998. Tanzania imejitahidi sana kuifanya sera hiyo ifanye kazi na hatuakubwa imefikiwa kwa njia zifuatazo:

    Zaidi ya misitu ya akiba ya vijiji 600 imeanzishwa nchini.

    Mwongozo wa usimamizi wa misitu kwa kushirikisha Jamii ulichapishwa na Wizara ya Maliasilina Utalii mwezi Aprili, 2001.

    Sheria mpya ya misitu imekamilika na kupitishwa na Bunge inayoruhusu Sera ya Misitu ya Taifakuanza kutumika.

    Misitu inaweza kuwa katika ardhi ya kawaida, ya akiba au ya kijiji. Jamii itakuwa na sauti kuhusunamna misitu inavyosimamiwa, kutegemea misitu hiyo iko katika mfumo gani wa utawala. Wanavijiji

    wanatakiwa wazingatie mambo matatu:

    Namna sheria zinavyobadilika kwa namna mapori na misitu vinavyosimamiwa nchini Tanzania.

    Vijiji vinapata nafasi ya kuanza kutunza misitu ya akiba ya jirani pamoja na ile iliyoko kwenyeardhi yao.

    Vijiji vitapewa mamlaka zaidi ya kusimamia na kudhibiti rasilimali hizi.

    Madhumuni makuu ya Sera ya Taifa ya Misitu ni:

    Kuhakikisha kwamba kunaendelea kuwepo na bidhaa za misitu kunatokana na usimamizi mzuriwa maeneo ya misitu.

    Kuajiri watu wengi na kupata fedha nyingi za kigeni kwa maendeleo zaidi ya viwanda nabiashara katika bidhaa za misitu ambazo zinaweza kudumishwa bila kuathiri mazingira.

    Kuhakikisha kuwa mimea yote ya aina mbalimbali na wanyama waliyomo msituni vinahifadhiwa.

    Kulinda vyanzo vya maji katika misitu.

    Kuhakikisha kuwa udongo unaendelea kuwa na rutuba.

    Kumsaidia kila mtu anayehusika kuendeleza sekta ya misitu kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.

    MISITU

    11Land and Natural Resources Law and Policy Syllabus

    Changamoto!

    Ili tupime mafanikio, hatuna budi kujua iwapo: Misitu ya akiba ya kijiji inasimamiwa kwa mafanikio Jamii inadhibiti misitu kwa ukamilifu. Hakuna migogoro yoyote.

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    18/32

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    19/32

    Kuwa Meneja mwenza na Serikali Kuu kwa Misitu ya Akiba ya Taifa au Serikali za Mitaakwa Misitu ya Akiba ya Mamlaka ya Jumuiya. Utaratibu huu wa usimamizi wa pamojautatawaliwa na Mikataba ya Usimamizi wa Pamoja.

    Sheria ya Misitu ya 2002

    Sheria mpya ya kusimamia misitu nchini kote Tanzania bara ilipitishwa na Bunge tarehe 23 Aprili,2002. Sheria hii inatoa fursa nyingi kwa Jamii kusimamia,kutumia na kulinda misitu inayowazunguka.Sheria inasema kuwa miongoni mwa malengo yake makuu ni kuwapa wajibu na haki ya kusimamiamisitu wananchi wanaoishi ndani na kandokando ya misitu.

    MISITU KATIKA ARDHI YA K IJIJISheria zinasema kwamba misitu na mapori katika ardhi ya kijiji havina budi kusimamiwa na Mabaraza yaKijiji na Mikutano ya Kijiji. Mabaraza ya Kijiji yanaweza kutenga Misitu ya Akiba ya Ardhi ya Kijiji iwapowanataka kuhakikisha kuwa misitu na mapori katika maeneo yao yanatunzwa ipasavyo. Misitu ya Akiba yaKijiji itasimamiwa na Serikali za Kijiji au na watu wengine watakaochaguliwa na serikali za vijiji. Misitu hiiya akiba itasimamiwa ili kuzalisha rasilimali muhimu kutoka katika misitu kwa mfano miti, mbao, dawa zamitishamba, matunda n.k.Pia ulinzi wa misitu unahitajika ili kuhakikisha kwamba mazingira yanatunzwa nakwamba misitu itaendelea kuwapo. Misitu hii ya akiba itasimamiwa kulingana na mipango ya usimamizi wamisitu.

    Misitu ya Akiba ya Ardhi ya Kijiji iliyotengwa na Mabaraza ya Kijiji haina budi kusimamiwa kulingana na:

    Sera zilizoamuliwa na Mabaraza ya Kijiji.

    Sheria ndogondogo zilizotungwa na Mabaraza ya Kijiji na kupitishwa na Mikutano ya Kijiji.

    Mpango wa Usimamizi wa Msitu wa Ardhi ya Kijiji.

    MISITU

    13Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    20/32

    Lazima kuwepo na Mpango wa Usimamizi iwapo wanakijiji watashirikishwa katika usimamizi wamisitu. Hii ni kwa sababu ni muhimu kujua kinachotakiwa kufanyika ili hatua zinazofaa zichukuliwe.Sheria inasema kwamba mipango ya usimamizi wa msitu katika ngazi ya jamii inapaswa:

    Kufafanua aina tofauti zote za rasilimali za misitu, ikiwemo mimea na wanyama, udongo na majina namna watu wanavyozitumia kuendeshea maisha yao au kama sehemu ya utamaduni wao.

    Kufafanua namna rasilimali zinavyotumika na anayezitumia.

    Kueleza namna wanavyotarajia kunufaika kutokana na kusimamia misitu na namnaitakavyosaidia uchumi, jamii na mazingira.

    Kufafanua ardhi ndani ya msitu ambapo maeneo ya matumizi ya wenyeji yatatengwa na hakiwatakayokuwa nayo watu katika maeneo hayo.

    Utayarishaji wa mipango ya usimamizi ni hatua nzuri kwa jamii kutenga Misitu ya Akiba ya Ardhi yaKijiji kwa mujibu wa Sheria:

    Mipango ya usimamizi kwa ajili ya Misitu ya Akiba ya Kijiji haina budi kuidhinishwa na Mikutanoya Kijiji na kutolewa maoni na Halmashauri ya Wilaya.

    Vijiji vinaweza kutunga sheria ndogondogo ili kusaidia mipango yao ya usimamizi.

    Vijiji vinasimamia misitu yao ya akiba kwa kipindi cha majaribio.

    Vijiji vinaweza kuomba Msitu wa Akiba wa Ardhi ya Kijiji utangazwe kwenye Gazeti la Serikali.Ili hayo yafanyike, vijiji havina budi kuomba kwa Mkurugenzi wa Misitu.

    MISITU

    14 Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Maeneo ya Matumizi ya Wenyeji: Nimuhimu kujenga ufahamu kuhusu maeneombalimbali ndani ya msitu na aina mbalimbaliza matumizi ya rasilimali zinaruhusiwa.

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    21/32

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    22/32

    Watu wa upande wa tatu ni kina nani, yaani watu wenye haki ya kuingia msituni lakini sisehemu ya mkataba.

    Fedha zitakazopatikana kama matokeo ya mkataba huo zitatumika katika mambo gani.

    Jinsi migogoro itakavyosuluhishwa.

    Sehemu za misitu katika Misitu ya Akiba ya Taifa au mamlaka za jamii ambapo vijiji vinapewa haki yakusimamia misitu zinaitwa Maeneo ya Usimamizi wa Misitu ya Kijiji. Maeneo haya yanasimamiwa naMabaraza ya Kijiji iwapo watu wanataka mamlaka ya kufanya hivyo na kuidhinishwa na Mkutano waKijiji.

    Maeneo ya Usimamizi wa Msitu wa Kijiji yanaweza kutengwa na Mkurugenzi wa Misitu mara baadaya Mkutano wa Kijiji kupeleka maombi kwake. Vijiji vinavyosimamia maeneo haya pia vinahitaji kuwana Kamati ya Usimamizi wa Msitu wa Kijiji.

    N AMNA JUMUIYA ZA W ANANCHI Z ITAKAVYOTUMIAFURSA MPYA KATIKA U SIMAMIZI WA MISITUHaya ni masuala yanayotakiwa kuangaliwa ili kuzingatia haja ya usimamizi wa misitu unaowashirikishawananchi katika eneo husika:

    Rasilimali za mapori na misitu zinatumiwaje kwa upana na jumuiya za wananchi?

    Je, namna rasilimali hizo zinavyosimamiwa kwa sasa zinamaanisha kuwa zitaendelea kupatikanamiaka ijayo?

    Kama jibu ni hapana, kuna matatizo gani ya namna rasilimali hizo zinavyosimamiwa?

    Iwapo wenyeji watagundua tatizo na kujionea madhara yanayofanyika, watafanya nini ilikuiboresha hali hiyo?

    Iwapo wenyeji wangeshirikishwa zaidi katika kusimamia rasilimali, italeta mafanikio gani?

    Mara maswali haya yatakapokuwa yamejibiwa na jamii kwa kuzingatia miongozo, itawasaidia kuamuaiwapo watatumia Msitu wa Akiba wa Ardhi ya Kijiji, Msitu wa Akiba wa Jumuiya ndani ya Kijiji auMkataba wa Usimamizi wa Pamoja na wasimamizi wa taifa au serikali za mitaa wa msitu wa akiba wa

    jirani.

    MISITU

    16 Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    23/32

    U SULI WA SHERIAKatika kipindi cha miaka 25 iliyopita Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 1974imetawala usimamizi wa Wanyamapori nchini Tanzania. Sheria hii inatawala wanyamapori narasilimali nyingine kwa njia kuu mbili:

    Kwa kuanzisha na kusimamia maeneo yanayolindwa kama vile Hifadhi za Wanyamapori naMaeneo ya Wanyamapori Yaliyodhibitiwa.

    Kwa kuratibu matumizi na ulaji wa wanyamapori na upatikanaji bidhaa za wanyamapori.

    Uwindaji wa kitalii na wakazi pamoja na shughuli za utalii ni njia kuu za kutumia wanyamapori.Shughuli hizi zinadhibitiwa na Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori. Uwindaji unafanywa katika Hifadhiza Wanyamapori, Maeneo ya Wanyamapori Yaliyodhibitiwa na maeneo ya wazi. Idara yaWanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii inakodisha maeneo ya uwindaji, yaani maeneo katikaardhi ya akiba au ardhi ya kijiji kwa makampuni ya kitalii na uwindaji.

    WANYAMAPORI

    17Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Katika Hifadhi za Wanyamapori:

    Haki za Watu kuingia ni finyu. Watu hawawezi kukata uoto bila leseni. Watu hawawezi kulisha mifugo yao. Watu hawawezi kuua wanyama bila leseni.

    Katika Maeneo ya WanyamaporiYaliyodhibitiwa:

    Uwindaji unaruhusiwa ingawa unadhibitiwa. Wenyeji wanaweza kuishi na kutumia ardhi

    kwa kilimo na kulisha mifugo. Watu hawaruhusiwi kula wanyamapori bila

    kupata leseni.

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    24/32

    SERA YA W ANYAMAPORI YA TANZANIAKama ilivyo ardhi na misitu, sekta ya wanyamapori nchini Tanzania inabadilika. Mabadiliko makubwayametokana na Sera ya Wanyamapori Tanzania, iliyotangazwa na Serikali mwaka 1998. MadhumuniMakuu ya Sera ya Taifa ya Wanyamapori ni:

    Kuhakikisha kuwa aina zote za viumbe hai zinahifadhiwa.

    Kuhakikisha kwamba wanyamapori hawatumiwi kiasi cha kuifanya idadi yao ipungue.

    Kuinua mchango unaotolewa na wanyamapori katika pato la taifa na maisha ya wananchi.

    Kuhakikisha kuwa sekta ya wanyamapori inawezesha maisha yawe mazuri zaidi kwa watumasikini wa Tanzania.

    Kuhakikisha kuwa Taifa linaendelea kumiliki wanyamapori na kusimamia kwa niaba ya wananchi.

    Wanyamapori nchini Tanzania wanakabiliwa na hatari nyingi zitakazosababisha idadi yao ipungue nahata wanyama kutoweka kabisa katika baadhi ya maeneo. Sera inafafanua matatizo yanayokabiliwanyamapori kama ifuatavyo:

    Wanavijiji wanataka kutumia ardhi moja na wanyamapori; kwa uchache wa ardhi, idadi ya

    wanyamapori inaweza kupungua.

    Ushindani wa ardhi kati ya watu nawanyamapori ina maana kuwa idadi yawanyamapori inapungua.

    Kwa kuwa watu wengi wanataka kutumiaardhi kwa ajili ya makazi, kulima, kuchungawanyama, kuchimba madini na kukatamagogo, wanyamapori wanakosa mahali

    ambapo kwa kawaida wanaishi nakuzaliana.

    Kuna ongezeko kubwa la biashara haramu yawanyamapori.

    Taifa linamiliki ardhi pamoja na wanyamapori,kwa hiyo wawekezaji binafsi hawatakiwikuendeleza viwanda vinavyohusu wanyamapori.

    Wanakijiji wana fursa chache za kutumiawanyamapori na mara nyingi hali hiiinasababisha kutokujali kwao kamawanyamapori wanahifadhiwa au hapana.

    WANYAMAPORI

    18 Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Changamoto!

    Kanuni za uhifadhi wa Wanyamapori(Uwindaji wa Kitalii), 2000:

    Sheria mpya iliyoongezwa katika Sheria yaUhifadhi wa Wanyamapori ya 1974 inaelezataratibu za ugawaji wa maeneo ya uwindaji.

    Inatamka kwamba kibali cha maandishi kutokakwa Mkurugenzi wa Wanyamapori kinatakiwaili kufanya uwindaji wa kitalii, kuangaliawanyama, safari za kupiga picha, matembezi auaina nyingine yoyote ya safari za kitaliizinazohusu wanyamapori, ndani ya maeneo yauwindaji au kwenye eneo lililohifadhiwa.

    Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ndiyo sheriamama na inatamka kuwa Idara ya Wanyamaporiinaweza tu kudhibiti ukamataji, uwindaji na upigaji picha wa kibiashara wa wanyamapori. Iwapo nikweli, ina maana kuwa serikali za vijiji zinadhibiti shughuli nyingine zote za kitalii katika ardhi ya kijiji.

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    25/32

    Sera inatamka kuwa sekta ya wanyamapori inakabiliwa na changamoto zifuatazo katika kuhifadhiwanyamapori nchini:

    Kuwashirikisha wananchi katika kuhifadhiwanyamapori.

    Kupata fedha za kigeni nyingi zaidi.

    Kuhakikisha kuwa kuhifadhi wanyamapori nakuendeleza jamii za vijijini vinakwenda pamoja.

    Kuhakikisha kuwa rasilimali za wanyamaporizinatumika kisheria kwa hali itakayohakikishiakudumu kwake.

    Kuhakikisha kuwa kutunza wanyamapori ni muhimu kama ilivyo kwa matumizi mengine yaardhi kwa wanavijiji.

    Zifuatazo ni baadhi ya njia za kukabiliana na changamoto hizo, kwa mujibu wa Sera ya Wanyamapori:

    Kuwashirikisha watu wengi zaidi katika kuhifadhi wanyamapori, hasa watu kutoka vijijini na

    sekta binafsi Kuhimiza wananchi kutenga Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori ili kulinda na kuhifadhi

    wanyamapori nje ya Hifadhi za Taifa na Hifadhi za Wanyama.

    WANYAMAPORI

    19Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Changamoto!

    Nini maana ya Uhifadhi?

    Uhifadhi maana yake ni kutunza miti, mimeana wanyamapori ili vyote viendelee kuwapodaima. Ina maana kutunza vyanzo vya maji ili vibaki kuwa safi na bila kufujwa. Uhifadhi maana yake hatuwezi kutumia miti mingi au

    kuua wanyama wengi. Iwapo tutatumia miti,lazima tupande mingine.

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    26/32

    Kutoa haki zaidi ya mtumiaji kwa watu wanaoathiriwa na wanyamapori.

    Kufafanua wazi kwa wananchi maana ya sera ya wanyamapori ya Serikali.

    Kuwahimiza watu wengi zaidi katika sekta ya umma na binafsi kuwekeza katika shughuli yawanyamapori.

    Kutoa sheria na kanuni zenye kusaidia ili jamii za vijijini na sekta binafsi ziweze kushirikianakuhifadhi wanyamapori.

    Sera inatamka wazi kuhusu jumuiya za kijamii: Ni lengo la Sera hii kuziruhusu jumuiya za vijijini nawamiliki ardhi binafsi kusimamia wanyamapori katika ardhi yao kwa manufaa yao.

    N AMNA SERA YA W ANYAMAPORI INAVYOWEZAK UTEKELEZWA KWA VITENDO : Kuendelea kuwasaidia watu wanaoshiriki katika usimamizi wa ardhi na wanyamapori kuwasiliana.

    Kuanzisha njia kwa jumuiya kunufaika kutokana na wanyamapori ili wanakijiji kushiriki katikauhifadhi wa wanyamapori.

    Kukabidhi majukumu zaidi kwa vijiji na sekta binafsi kwa usimamizi wa wanyamapori katika ardhi ya kijiji.

    Kwa mujibu wa Sera, kutoa haki ya mtumiaji wa wanyamapori kwa jumuiya za vijijini ili ziwezekusimamia wanyamapori itamaanisha kuwa kuwalinda wanyamapori itaonekana kuwa ni ainamuhimu ya matumizi ya ardhi. Kuwapa watu kazi ya kuitekeleza sera kwa vitendo kutasaidia kuungamkono juhudi za serikali katika uhifadhi na usimamizi wa rasilimali za wanyamapori. Aidha kwa mujibuwa Sera, wananchi wanaoishi karibu na Maeneo Yaliyolindwa au maeneo yenye wanyamapori wengiwana jukumu katika kusimamia na kunufaika na wanyamapori kwenye ardhi yao wenyewe kwakutenga Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori.

    WANYAMAPORI

    20 Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Changamoto!

    Nani anayedhibiti uwindaji wa Kitalii?

    Uwindaji wa kitalii kwenye ardhi ya kijiji hivi sasa unadhibitiwa na Idara ya Wanyamapori. Sheria ya Uhifadhi waWanyamapori ya 1974 inasema kuwa hakuna anayeruhusiwa kuwinda au kukamata wanyama katika ardhi binafsibila leseni kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori na kibali cha mmiliki wa ardhi. Ardhi ya kijiji ni ardhi binafsi,kwa hiyo,mtu yeyote anayepewa leseni ya kuwinda katika maeneo haya hana budi pia kupata kibali cha Baraza laKijiji (mamlaka ya ardhi). Mara nyingi,makampuni ya uwindaji yanaingia katika ardhi ya kijiji bila kibali cha serikaliza kijiji, ambayo ni marufuku kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori.

    Tabia hizi huinyima jumuiya haki ya kudhibiti ardhi yao. Je sera iliyopo inaitaka Idara ya Wanyamapori kukubaliana na Serikali za Vijiji kabla ya kutoa leseni za uwindaji?

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    27/32

    MAENEO YA U SIMAMIZI WA W ANYAMAPORISera ya Wanyamapori inasema kuwa ni muhimu sana kuwashirikisha wananchi katika kulindawanyamapori wa taifa. Watapewa jukumu kubwa la kusimamia rasilimali katika ardhi yao pamoja nakunufaika kutokana na wanyamapori. Njia ya kuleta mabadiliko haya itakuwa kutenga Maeneo yaUsimamizi wa Wanyamapori katika ardhi ya kijiji.

    Sera inasema kuwa Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori yatatengwa na serikali za vijiji ili:

    Kuhifadhi na kusimamia wanyamapori.

    Kuwapa wananchi jukumu la kutekeleza hayo.

    Kuwawezesha wananchi kunufaika kutokana na rasilimali za wanyamapori.

    Kuruhusu jumuiya kunufaika kutokana na wanyamapori kama wanavyonufaika kutokana namatumizi mengine ya ardhi yao.

    Kunufaisha wananchi kifedha ili waone thamani ya kuhifadhi wanyamapori

    Serikali imetunga kanuni mpya ili kufanikisha utelekezaji wa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamaporiya mwaka 1974 kuhusu kutenga Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori. Kanuni hizi ni Kanuni zaMaeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori za 2002.

    WANYAMAPORI

    21Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    28/32

    Sheria hii mpya inaeleza namna vijiji vinavyoweza kufuata utaratibu wa kutenga Maeneo ya Usimamiziwa Wanyamapori katika ardhi yao. Jamii ina haki na majukumu gani katika Maeneo mapya yaUsimamizi wa Wanyamapori?:

    Vijiji vinaweza kutenga sehemu ya ardhi yao ya kijiji kwa uhifadhi.Matumizi mengine ya ardhiyanaweza kutokea katika Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori, lakini madhumuni makuu yamaeneo haya yatakuwa kwa kuhifadhia wanyamapori.

    Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori yatasimamiwa na Mashirika ya Kijamii yanayowakilishavijiji vinavyohusika na si Mabaraza ya Vijiji au Kamati za Maliasili za Kijiji.

    Mashirika ya Kijamii yatamwomba Mkurugenzi wa Wanyamapori kuhalalisha kisheria Maeneo

    ya Usimamizi wa Wanyamapori (kutangaza katika Gazeti la Serikali Maeneo ya Usimamizi waWanyamapori) ili vijiji vinavyohusika viweze kupata haki za mtumiaji katika mapato ya mwaka yawanyamapori. Mashirika ya Jamii yatathibitisha kuwa yanaweza kusimamia ipasavyo rasilimali zawanyamapori za ndani.

    Mara baada ya Mashirika ya Kijamii kupata haki za mtumiaji yatakuwa Washiriki Walioidhinishwakama ilivyotamkwa katika Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori. Ina maana kwamba shirikalimeidhinishwa na Mkurugenzi wa Wanyamapori kusimamia na kutumia wanyamapori katikaMaeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori.

    Mashirika ya Kijamii/Washiriki Walioidhinishwa watakuwa na wajibu wa kisheria wa kusimamiawanyamapori ndani ya Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori, kwa mujibu wa mkatabawanaoufanya na Mkurugenzi wa Wanyamapori.

    Namna ya Kutenga Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori:

    Kwanza Mikutano ya Kijiji haina budi kuamua kuwa wangependa kutenga Maeneo ya Usimamizi waWanyamapori kwa kutumia sehemu za ardhi ya kijiji. Kisha wawakilishi kutoka kijiji au vijijiwataunda Shirika la Kijamii. Shirika hili litasajiliwa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mujibu wa Sheriaya Vyama ya 1994, na halina budi kuwa na katiba halali, wanachama, sheria za maadili n.k.

    Kisha wanakijiji lazima:

    Watayarishe mipango ya matumizi ya ardhi kwa kuwashirikisha wanakijiji katika mchakato waupangaji.

    Kutenga maeneo ya matumizi ya rasilimali na eneolitakalojumuishwa katika Maeneo ya Usimamizi waWanyamapori.

    Wawe tayari kwa mipango yao kupitiwa ili kuona namna inavyoathiri mazingira (Tathmini ya

    Athari ya Mazingira).

    WANYAMAPORI

    22 Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

    Maeneo ya Matumizi ya Rasilimali:Maeneo ambayo rasilimali maalumzinatumika katika sehemu tofauti za ardhiya kijiji kutokana na mpango rahisiuliofanywa na wanakijiji.

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    29/32

    Vijiji kupitia kwa Shirika laola Kijamii, havina budikutayarisha Mpango waKimkakati kwa ajili yaMaeneo ya Usimamizi waWanyamapori, wakionyeshadira yao, dhamira, mipango yakazi n.k. Kwa manenomengine, hawana budikusema namnawatakavyosimamiaMaeneo ya Usimamizi

    wa Wanyamapori kwamanufaa ya wanavijiji.

    Shirika la Kijamii/Vijiji havinabudi kutayarisha Mpango wa

    Jumla wa Usimamizi wakieleza namnawatakavyosimamia rasilimali, rasilimali ganizitatumiwa katika maeneo tofauti n.k. Hata hivyo,Kanuni za Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamaporizinatamka kuwa mpango wa eneo la matumizi yarasilimali unaweza kutumiwa mpaka miaka mitano badala ya kutayarisha Mpango wa Jumla waUsimamizi haraka.

    Mara hatua hizi zinapokamilika,Shirika la Kijamii linaweza kuomba Idara ya Wanyamapori ilipatie hakiza mtumiaji kwa ajili ya wanyamapori katika Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori yanayotarajiwana hivyo kuwa Mshiriki Aliyeidhinishwa. Baada ya haki ya mtumiaji kutolewa Maeneo ya Usimamiziwa Wanyamapori yatatambuliwa rasmi. Wakati Shirika la Kijamii linapewa haki ya mtumiaji kwawanyamapori katika Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori, linakuwa mshiriki aliyeidhinishwa.Maana yake ni kuwa limeidhinishwa na Idara ya Wanyamapori kusimamia na kutumia baadhi yawanyama katika Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori.

    Mara baada ya Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori kuundwa rasmi kisheria kwa kufuata taratibuhizi, mshiriki aliyeidhinishwa anaweza kutafuta wawekezaji katika Maeneo ya Usimamizi waWanyamapori. Wawekezaji hawa wanaweza kuwa kwa ajili ya uwindaji wa kitalii, utalii wa upigajipicha au uwindaji wa mkazi. Iwapo mshiriki aliyeidhinishwa anataka mwekezaji wa utalii wa uwindaji,amwombe Mkurugenzi wa Wanyamapori kutenga eneo la utalii wa uwindaji katika Maeneo yaUsimamizi wa Wanyamapori. Kisha Mkurugenzi wa Wanyamapori atatoa eneo hilo kwa kampuni yauwindaji atakayochagua mshiriki, na mshiriki aliyeidhinishwa ataingia katika mkataba na kampuni hiyo.Utalii wa upigaji picha hauhitaji kutengewa eneo lolote la uwindaji, lakini uwekezaji wote wa utaliikatika Maeneo ya Usimamizi wa Wanyamapori nao lazima uidhinishwe na Mkurugenzi waWanyamapori.

    WANYAMAPORI

    23Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    30/3224 Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    31/32

    Mwongozo huu katika lugha nyepesi wa Sheria na Sera za Ardhi, Misitu na Wanyamapori za Tanzaniaulitengezwa kupitia msaada wa ukarimu wa mashirika ya African Initiatives, CRT Ujamaa na SandCounty Foundation Community Based Conservation Network. Shukrani za kipekee ziende katikashirika la Hakikazi Catalyst kwa kuwezesha utengenezaji wa mwongozo huu; Francis Stolla wa Legaland Human Rights Centre (LHRC) kwa msaada wa kitaalam; na Nathan Mpangala kwa kuchoravikaragosi.

    Imepigwa chapa na:

    Colour Print (T) Limited

    SHUKRANI

    25Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

  • 7/25/2019 52654717-LNR-Swahili

    32/32

    Kwa taarifa zaidi, wasiliana na:

    Hakikazi CatalystGhorofa ya 2, Jengo la Meru Plaza

    Barabara ya EssoSLP 781Arusha

    Simu/fax: 027-2509860B h kik i@ b