adhabu ya viboko

52
Je, Adhabu ya viboko ina madhara gani? Viboko havikubaliki hapa! TRV-Bk 1 Jishindie kompyuta Jishindie kompyuta ndani! ndani!

Upload: vukiet

Post on 29-Jan-2017

285 views

Category:

Documents


4 download

TRANSCRIPT

Page 1: Adhabu ya viboko

Je,

Adhabu ya viboko

ina madhara gani?

Vibokohavikubaliki

hapa!

TRV-Bk1

Jishindie kompyuta

Jishindie kompyuta

ndani!ndani!

Page 2: Adhabu ya viboko

Adhabu ya kuchapa wanafunzi ni:Adhabu yoyote inayosababisha maumivu ya kimwili.

Kuchapa kwa mikono, vitu, kupiga teke, kuunguza, kusukuma,

ku nya, nk.

Vilevile ni adhabu yoyote ile isiyo ya kimwili ambayo

hudhalilisha, hutishia, huogopesha

na humuaibisha mtoto.

1

Page 3: Adhabu ya viboko

Asilimia 98 ya watoto wamedai

kuwa wameshakumbwa

na adhabu hii...

Mtoto mmoja kati ya watatu

hukumbwa na adhabu hii kila wiki.

2

Page 4: Adhabu ya viboko

Kwahiyo? Jambo hili lina ubaya gani?

Ni jambo ambalo tumekuwa nalo, hivyo tunadhani ni jambo zuri kwa malezi ya watoto wetu!

Mwalimu wangu alinichapa kwa sababu alitaka nijifunze!

3

Page 5: Adhabu ya viboko

Wala hatuwaumizi watoto wetu!

Kweli! Tunawashikisha

adabu!

4

Page 6: Adhabu ya viboko

Lakini adhabu ya kuchapa wa

Kimwili

Kihisia

Kimahusiano

Huumiza mwili wangu!

Huumiza moyo wangu!

Inanifanya nisiamini watu!

5

Page 7: Adhabu ya viboko

anafunzi ina madhara mengi!

Kitabia

Ugumu wa

kujifunza

Hunisababisha nifanye mambo mabaya!

Hufanya nishindwe kujifunza!

Tazama ninacho maanisha!

6

Page 8: Adhabu ya viboko

Madhara ya kimwili

Ninapaswa nichote maji na kusa sha nyumba kabla ya kwenda shule. Mara nyingi ninachelewa ku ka shuleni!

Mara nyingi ninachapwa ninapochelewa. Siku moja niliji cha kichakani mpaka mwisho wa vipindi.

7

Page 9: Adhabu ya viboko

Mwalimu alinikamata na akakasirika sana! Alinichapa viboko 20!

Rose, nitakukomesha uache utoro!

Nisame-he!

Alinichapa sana nikaumia, wazazi wangu wakanipeleka hospitali na nilishindwa kwenda shule wiki nzima.

Najisikia maumivu mwilini!

8

Page 10: Adhabu ya viboko

Maumivu ya hisia

Stella! Kila siku wewe ni mchafu! Kwanini huwezi kuwa msa kama wanafunzi wengine?

Lakini mwalimu....

9

Page 11: Adhabu ya viboko

Naona unataka kujifunza kufua! Sasa, nenda nyumbani kwa matroni ukafue nguo zake zote...

Na ndiyo maana umefeli mtihani wa hisabati, mjinga wewe!

Hakuna anayenijali! Sijui maisha yangu yatakuwaje!

Inaniumiza rohoni!

10

Page 12: Adhabu ya viboko

Madhara ya kitabia

Peter, nilikwambia ufagie darasa. Bado tu!

Mwalimu… nita….

Mvivu wewe! kalete fagio na ufagie sasa hivi!

11

Page 13: Adhabu ya viboko

Baadaye siku hiyo…

We mpumbavu! Huwezi kucheza, uko legelege!

Embu leta maji yako! Nina kiu!

Kwanini mimi tu? Kosa langu nini?

Inasababisha nifanye mambo

mabaya

12

Page 14: Adhabu ya viboko

Madhara ya kimahusiano

Hassan, funga domo lako! Na uache kusukuma kiti cha Hasifa!

Hassan, inatosha! Sasa ngoja nikufundishe adabu! Hebu peleka tofali 100 kule kilimani!

Namchukia! Na nitaendelea kumchokoza kila siku!

13

Page 15: Adhabu ya viboko

Wiki iliyofuata…

Hassan, hebu acha kutupa ovyo karatasi! Kumbe hukukoma wiki iliyopita?

Hassan, hebu niambie nini tatizo lako? Kwanini wewe msumbufu?

Ungejua ninavyokuchukia!Sina jinsi tu!

Inanifanya nisiamini watu!

14

Page 16: Adhabu ya viboko

Ugumu wa kujifunza

Haya...Fatima, jibu?

Hivi hili darasa lina tatizo gani? Ni mara ngapi nimefundisha jambo hili?

Fatima, njoo hapa! Sasa ninawashikisha adabu muwe wasikivu!

15

Page 17: Adhabu ya viboko

Aisee! Fatima naona umelamba viboko!

Yaani, ninajisikia woga darasani! Ninaho a mwalimu ataniuliza swali huku sijui jibu!

Ninasoma kwa bidii, lakini nimekuwa mwoga kuongea darasani!

Ninatamani walimu wangeacha kututisha!

16

Page 18: Adhabu ya viboko

WIKI ILIYOFUATA

Nimesoma vya kutosha! Sasa niko tayari kujibu maswali!

Fatima, jibu?

17

Page 19: Adhabu ya viboko

We binti mjinga! Unajua kuwa nitakuchapa, na bado hutaki kujibu!

Najua hali hii itaendelea kutokea, sijui nifanyeje?

Inanifanya nishindwe kujifunza.

Ninajihisi mjinga

18

Page 20: Adhabu ya viboko

Adhabu ya kupigwa huwafanya watoto kujisikia vibaya…Lakini bado watu wazima wanatoa sababu za kuendelea kutumia adhabu hii.

Sababu

Sababu

Sababu

Sababu Sababu

SababuSababu

Sababu

19

Page 21: Adhabu ya viboko

Sababu

Kama mtoto hakuogopi, kamwe hatakuheshimu!

Mshenzi wewe! Jifunze kuheshimu wakubwa!

Lakini huwezi kumlazimisha mtu kukuheshimu!

Hicho kichapo kitakufanya uniheshimu!

20

Page 22: Adhabu ya viboko

Heshimu watu! Watakuheshimu pia!

Mwalimu, hii hapa insha yangu ya mashindano.

Sa sana!

Asante! Naona umekusanya mapema!

21

Page 23: Adhabu ya viboko

Sababu

Mwalimu mzuri ni yule anayedhibiti tabia ya mwanafunzi.

Nani anapiga kelele? Ninasikia kelele mpaka o sini kwangu!

Siyo mimi! Sielewi somo!

Kimya!

Wanafunzi huweza kukaa kimya kwa kuogopa adhabu…

22

Page 24: Adhabu ya viboko

Mara vitisho vinapoondoka

Matokeo ya nidhamu ya woga...

23

Page 25: Adhabu ya viboko

Walimu wazuri hawadhibiti tabia za wanafunzi kwa kuwachapa au kuwatukana.

Huwezi kudhibiti ubunifu… bali unaweza kuuchochea tu!

Ninadhani… Wazo zuri!

Na kuhusu hili?

U mbunifu sana!

24

Page 26: Adhabu ya viboko

Sababu

Nilikuwa nikichapwa na imenifunza nidhamu nzuri!

SASA:

Lakini…

Hutoweza kuelewa sayansi, mjinga wewe!

Mimi mwenyewe sikuelewa sayansi, wewe mjinga ndo utaelewa!

25

ZAMANI:

Page 27: Adhabu ya viboko

ZAMANI:

SASA:

Jaribu kuwaza jinsi ambavyo mafanikio yako yangeweza kuwa!

Sayansi ni ngumu kwako, hebu ngoja nikusaidie!

26

Page 28: Adhabu ya viboko

Lakini mchelea mwana kulia, hulia mwenyewe!

Mithali ya biblia kuhusu viboko ilikuwa kwa nyakati zile…

Lakini, Agano Jipya husisitiza upendo na msamaha

Sababu

27

Page 29: Adhabu ya viboko

Tunapaswa kubadilika kuendana na wakati.

Kamwe! Dini haiungi mkono kumlea mtoto kwa kumuumiza!

Maonyo huweza kuwa maneno au vitendo elekezi, na si viboko!

Na daima tusiache kuonya!

28

Page 30: Adhabu ya viboko

Sababu

Viboko ni mila na desturi zetu! Hatutaki kukumbatia maadili ya nje!

Lakini mila na desturi zetu SIYO kuumiza watoto!

Huzingatia heshima, upendo na maelekezo

29

Page 31: Adhabu ya viboko

Tunataka watoto wetu wakue na kupenda mapokeo yao...

...sio kuyaogopa!

30

Page 32: Adhabu ya viboko

Sababu

Mtaka cha uvunguni sharti ainame!

Wanafunzi wangu wamefaulu mtihani kwa sababu waliweza kukariri kila kitu kwasababu ya kuogopa viboko!

Kweli? Hivi kweli wanaelewa?

31

Page 33: Adhabu ya viboko

Salma, jana ulikariri namna ya kukokotoa hesabu ya eneo la mstatiri. Sasa namna gani unaweza kukokotoa eneo la mcheduara?

Kujifunza kwa viboko kunatulazimu kukariri!

Kweli, hatujifunzi namna ya ku kiri!

Tumekuwa wanafunzi mbumbumbu!

32

Page 34: Adhabu ya viboko

Lakini tunatumia adhabu ya viboko kidogo tu inapobidi!

Sababu

33

Page 35: Adhabu ya viboko

Jaribu ku kiria iwapo bosi wako atakuchapa ko , hata mara moja tu, kwa kuchelewa kumaliza ripoti. Utajisikiaje?

34

Page 36: Adhabu ya viboko

Ninatumia adhabu ya viboko pale inaponilazimu tu!

Aaah...nimesahau homuweki yangu!

Duh! Pole sana Saad, leo utalambwa viboko!

Hapana, mwalimu hatanichapa ataniamini. .

SHULE

Sababu

35

Page 37: Adhabu ya viboko

Saad! Umesahau homuweki yako! Hakuna njia nyingine ya kukumbusha!

Lakini nilikuamini! Ulisema hutatuchapa! Sikuelewi!

Alaa! Kumbe adhabu ya kumtandika mwanafunzi hudhoo sha kujiamini kwake!

36

Page 38: Adhabu ya viboko

Kila mmoja anakubali, adhabu ya viboko haisaidii!

37

Page 39: Adhabu ya viboko

Ulimwenguni kote, watu wameamua kuachana na adhabu ya kuchapa wanafunzi!

38

Page 40: Adhabu ya viboko

Sera za kimataifa zinaeleza kuhusu maamuzi hayo ya dhati

Tamko la kimataifa

kuhusu haki za binadamu

Watoto wana haki za kiutu

na usawa wa kimwili.

Azimio la haki za watoto• Watoto wanapaswa

kulindwa dhidi ya

mambo yote ya kuwaumiza.

• Nidhamu shuleni

inapaswa kuzingatia

utu wa watoto.• Watoto hawapaswi

kutendewa vitendo

vya kinyama wala

kunyanyaswa.Kamati ya Haki za

Watoto

Achana na adhabu ya

kuchapa wanafunzi.

39

Page 41: Adhabu ya viboko

Sera ya Afrika pia huzungumza kuhusu maamuzi haya thabiti.

Makubaliano ya Umoja wa Afrika

kuhusu haki za watoto na malezi bora.

Watoto wanapaswa kulelewa

kwa heshima na utu pindi

wanapoonywa nyumbani au

shuleni.

Makubaliano ya haki

za binadamu Afrika

• Watoto wana haki ya

utu na kuishi.• Watoto wana haki

ya kulindwa dhidi ya

uonevu.

40

Page 42: Adhabu ya viboko

Sera ya Tanzania ina mkanganyiko

Katiba ya Tanzania• Binadamu wote huzaliwa huru, na

wote ni sawa.• Kila mtu anastahili heshima ya kutam-

buliwa na kuthaminiwa utu wake.

• Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuad-

hibiwa kinyama au kupewa adhabu

zinazomtweza au kumdhalilisha.

Sheria ya Haki za

Mtoto, 2009

• Mtu yeyote hataruhusiwa kumfanya mtoto

apate mateso, au adhabu ya kikatili, au

afanyiwe matendo yenye kumshushia hadhi.

• Hakuna adhabu kwa mtoto inayokubalika am-

bayo haiendani na kiwango cha umri, afya /hali ya

mwili na akili yake. Hakuna adhabu inayokubalika

kwa mtoto mwenye umri mdogo asiyeelewa

kusudio la adhabu hiyo.

41

Page 43: Adhabu ya viboko

Waraka wa Elimu, wa Serikali namba

24 wa mwaka 2002 unaruhusu viboko

japo imewekewa masharti:• Viboko ni kwa ajili ya makosa

makubwa tu. • Mwalimu mkuu ndiye mwenye

mamlaka kuruhusu kimaandishi.

• Viboko visizidi vinne na

viandikwe katika kitabu cha

kumbukumbu. • Mwanafunzi wa kike atachapwa

na mwalimu wa kike tu au

Mwalimu mkuu.

Licha ya kuridhia mikataba ya kimataifa ya haki za watoto, Tanzania bado inatumia adhabu hii!Waraka huu unapingana na Katiba na sera ya mtoto.

42

Page 44: Adhabu ya viboko

Shule nzuri huzingatia sera za kimataifa, kitaifa na kikanda.

43

Page 45: Adhabu ya viboko

Shule nzuri huunda sera inayopinga adhabu ya viboko kwa wanafunzi.

44

Page 46: Adhabu ya viboko

Katika shule

Ninajisikia huru na ninalindwa!

Ninajifunza vizuri bila woga!

Ninaheshimiwa na ninaheshimu pia!

Shule nzuri HAINA adhabu ya kuchapa wan

45

Page 47: Adhabu ya viboko

nzuri…

nafunzi! Je, shule yako ni nzuri?

Nina watu wazuri wanaonivutia kubadili tabia yangu!

Ninawaamini walimu!

46

Page 48: Adhabu ya viboko

Je, unaweza kufanya nini kuhusu adhabu ya kuchapa wanafunzi?

• Amua kuachana na adhabu hii kwa kudhamiria moyoni.

• Jenga mazingira ya kuepuka adhabu hii shuleni.

• Jifunze kuhusu nidhamu isiyo ya uoga na kisha tumia mbinu za kusisitiza nidhamu hiyo.

• Wasikilize wanafunzi na kutatua matatizo yao.

• Jadili na watu wengine kuhusu faida za utulivu.

• Kuwa mbunifu! Jaribu kutumia mbinu mpya darasani.

47

Page 49: Adhabu ya viboko

Jinsi ya kutumia kijitabu hiki…

• Soma kijitabu hiki pamoja na wanafunzi au walimu wengine. Kisha jadilini madhara ya adhabu ya viboko.• Fanya uta ti kuhusu sheria na sera zinazoongoza shule, wilaya, mkoa na nchi nzima kwa ujumla. Jadili undani wa sheria na sera hizo.• Fanya mijadala ukitumia sababu watu wanazotoa kuhusu kuendelea kutoa adhabu hii na kisha fafanua madhara yake. • Fanya maigizo kuhusu adhabu hii na kisha onesha jinsi watoto wanavyoadhirika kutokana na adhabu hii.• Shirikisha familia yako kujua athari za adhabu hii. • Tumia sera zinazopaswa kuzingatiwa ili shule iwe nzuri.

48Mchoraji : [email protected]

Page 50: Adhabu ya viboko

49

Toa maoni, shiriki na

Kila baada ya miezi mitatu kwa mwaka 2012, maoni ya wanafunzi yatakayo-tumwa kupitia shule zao yatashindanishwa. Maoni kumi bora yatachaguliwa na yatachapishwa kwenye vitabu pamoja na tovuti. Kila shule itakayoshinda itapata kompyuta ndogo mbili (laptops).

Zawadi:

Msomaji, Serikali yako inataka kukusikia! Shiriki kwa kutuma maoni yako. Mawazo yako yanaweza kuboresha huduma kwa jamii na utawala bora. Pia, hii itakuza ushirikiano kati ya wananchi na Serikali. Maoni yako yatahusiana na mafunzo uliyopata kupi-tia kitabu hiki. Kigezo cha kupata washindi ni ubunifu au wazo jipya.

Page 51: Adhabu ya viboko

50

jishindie kompyuta!Mwisho wa maoni yako weka taarifa zako:

a) Tareheb) Majina kamili, umri wako na jina la shule/taasisic) Jinsia - Mwanaume/Mwanamked) Anuani (SLP) kamili, makazi (Kata, Wilaya, na Mkoa)e) Simu yako na/au Barua pepe (kama unayo).

Unangoja nini! Shiriki basi kwa njia zifuatazo. Tuma kwa:

• Barua: OGP Ikulu, S.L.P 9120 Dar es Salaam• Barua pepe: [email protected] au [email protected]• Tovuti: www.wananchi.go.tz

Fikiria. Paza Sauti. Twaweza!

Page 52: Adhabu ya viboko

Vibokohavifai!

Kuthaminiwa zaidi!

Kitabu hiki kimeandaliwa na:

Jadili na wenzio ulichojifunza humu au shiriki mjadala kupitia:

Twaweza_Nisisi

Twaweza Tanzania

www.twaweza.org www.raisingvoices.org