ahadi za mgombea udiwani yusuf manji mbagala

12
YUSUF MANJI MGOMBEA UDIWANI - MBAGALA KUU Miaka kumi iliyopita tulianza safari na katika safari hiyo nilisema, “Kutoa ni moyo na si utajiri” na mimi nimetoa moyo wangu kwenu. Baadhi yenu mnaweza kukumbuka maneno niliyosema kwenye uwanja wa Mbagala Zakhem mwaka 2005 nilipokuwa na umri wa miaka 29, wakati nawania kuwa mbunge wa Kigamboni. Mlinikabidhi imani yenu ya dhati kutoka mioyoni mwenu na kwa kishindo nikashinda kura za chama kupitia kuwa mgombea mteule wa Ubunge wa Kigamboni tiketi ya CCM. Nikashauriwa na Wazee wa Chama nisubiri kutokana na umri wangu wa miaka 29 kuwa mdogo. Nimesubiri kwa muda wa miaka kumi na sasa nina umri wa miaka 39, na nimepewa idhini na Chama changu ya kuwania Udiwani wa kata ya Mbaga- la Kuu. Kama nilivyoahidi kuwapa moyo wangu miaka kumi iliyopita, bado ninakusudi hilo kwa kupitia thamani ya kura zenu, kuleta maendeleo ambayo nina amini Kata ya Mbagala Kuu, Wilaya ya Temeke na Mji wa Dar Es Salaam ulikuwa ukiyangojea. Katika kipindi chote cha kampeni nimetembelea matawi yote yanayounda Mbagala Kuu kuanzia Kichemchem Kaskazini hadi Makuka A, Makuka B mpaka Kizuiani, Kichemchem Kusini, Mbagala Kuu,n.k. ambapo nilipata nafasi ya kuzungumza na wengi wenu. 1

Upload: misty-collins

Post on 06-Dec-2015

289 views

Category:

Documents


0 download

DESCRIPTION

AHADI ZA YUSUF MANJI KWA WAKAZI WA KATA YA MBAGALA ENDAPO WATAMCHAGUA KUWA DIWANI WA KATA HIYO UCHAGUZI HUU.

TRANSCRIPT

Page 1: Ahadi Za Mgombea Udiwani Yusuf Manji Mbagala

MAENDELEO SIO MANENO

YUSUF MANJIMGOMBEA UDIWANI - MBAGALA KUU

Miaka kumi iliyopita tulianza safari na katika safari hiyo nilisema, “Kutoa ni moyo na si utajiri” na mimi nimetoa moyo wangu kwenu.Baadhi yenu mnaweza kukumbuka maneno niliyosema kwenye uwanja wa Mbagala Zakhem mwaka 2005 nilipokuwa na umri wa miaka 29, wakati nawania kuwa mbunge wa Kigamboni. Mlinikabidhi imani yenu ya dhati kutoka mioyoni mwenu na kwa kishindo nikashinda kura za chama kupitia kuwa mgombea mteule wa Ubunge wa Kigamboni tiketi ya CCM. Nikashauriwa na Wazee wa Chama nisubiri kutokana na umri wangu wa miaka 29 kuwa mdogo.

Nimesubiri kwa muda wa miaka kumi na sasa nina umri wa miaka 39, na nimepewa idhini na Chama changu ya kuwania Udiwani wa kata ya Mbaga-la Kuu. Kama nilivyoahidi kuwapa moyo wangu miaka kumi iliyopita, bado ninakusudi hilo kwa kupitia thamani ya kura zenu, kuleta maendeleo ambayo nina amini Kata ya Mbagala Kuu, Wilaya ya Temeke na Mji wa Dar Es Salaam ulikuwa ukiyangojea.

Katika kipindi chote cha kampeni nimetembelea matawi yote yanayounda Mbagala Kuu kuanzia Kichemchem Kaskazini hadi Makuka A, Makuka B mpaka Kizuiani, Kichemchem Kusini, Mbagala Kuu,n.k. ambapo nilipata nafasi ya kuzungumza na wengi wenu.

1

Page 2: Ahadi Za Mgombea Udiwani Yusuf Manji Mbagala

Nilipoanza kampeni, niliwasikiliza, nikauliza maswali ili kupata uelewa mzuri wa vikwazo mnavyokumbana navyo na ufumbuzi mnao upendekeza, kwa kuwa katika mtazamo wangu ninaona ni busara zaidi kuwasikiliza nyinyi kwanza, kisha tutafakari kabla ya mimi kuwaeleza mipango yangu na ahadi za safari yetu, ili mpate nafasi ya kuamua kama mimi ninafaa kushiriki kufikia ndoto mlizonazo juu ya mustakabali wetu na watoto wetu, pia kama mimi na chama changu tunastahili kura zenu tarehe 25 Oktoba, 2015.

Kwahiyo baada ya kusikiliza kwa umakini na kuhakiki vikwazo vikuu vinayoi-kumba Kata ya Mbagala Kuu, kupitia Ilani ya Chama changu, kama nikicha-guliwa kuwa Diwani, zifuatazo ni hatua nitakazozichukua ili kutatua chan-gamoto zinazoikabili Kata ya Mbagala Kuu:

inatubidi tuelewe mambo makuu mawili; - Kwanza, tuna uhaba wa ardhi katika kata yetu kukidhi takriban watu 100,000. Kwa hiyo ninacho pendekeza kitawezekana endapo tutasimamia uhamiaji wa watu kuja katika kata yetu na - Pili, kujenga daraja la kuleta uwiano katika ugawaji wa rasilimali kukidhi

idadi yetu kubwa.

Kwa mfano, tunahitaji barabara, shule, zahanati, vituo vya polisi, masoko, maji n.k. na vyote tunavihi-taji kwa wakati mmoja, kama tukisema tuitegemee Serikali na Manispaa ya Temeke kupata huduma

hizo kwa miaka 5, ambapo Serikali pia ina wajibu wa kushughulikia chan-gamoto kama hizo si kwa wilaya ya Temeke pekee bali hata kwa taifa zima. Hivyo tutapata maendeleo finyu katika barabara, shule, zahanati n.k. (kama kata zingine) na bado mwisho wa awamu yangu tutajikuta hatujaridhika, tuna njaa ya mendeleo wakati idadi ya watu itakuwa imeongezeka zaidi na ardhi yetu kuwa adimu zaidi.

2

Page 3: Ahadi Za Mgombea Udiwani Yusuf Manji Mbagala

Kwa hiyo, mapendekezo yangu ni kuwa inatubidi tuendeleze baadhi ya mambo kupitia rasili-mali za sekta binafsi (rasilimali ambazo mimi ninazo) na kuruhusu mfuko uliotengwa kwa ajili ya kata yetu kukidhi mahitaji ambayo rasilimali za sekta binafsi hazitaweza au hazitakuwa tayari kuwekeza.

Zifuatazo ni changamoto na mapendekezo yangu katika kuleta maendeleo ya Kata ya Mbagala Kuu:

1. Kuunganishwa na majiTatizo kubwa linalo tukumba ni kutounganishwa na maji kutokana na Kata yetu kutounganishwa na DAWASCO, hivyo wakazi wanategemea chanzo kimoja tu cha maji cha Taasisi ya Teknolojia ya Ubelgiji.

Endapo nitachaguliwa, suluhisho langu litakuwa ni kushinikiza moja ya kampuni zangu kuwekeza katika uchimbaji wa visima virefu vya kutumia umeme ambavyo vitaanza kazi ndani ya mwaka moja kuanzia siku nitakayo chaguliwa, na kwa gharama nafuu sana kuruhusu wakazi wa Mbagala Kuu

kuunganishwa na maji, fedha tutakazo

lipia huduma ya maji zitatumika kukidhi gharama za kuendeshea kampuni ili iweze kuendelea kuwekeza katika sekta ya maji ya taifa.

Pia kulikuwa na mradi wa maji uliopitishwa ambao mpaka sasa haufanyi kazi, nitafanya uchunguzi ili ifahamike kwanini mradi huo ulikufa na kuwahimiza kutua

-mini tena.

2. Huduma za kiafya / zahanati / vyumba vya kuhifadhi maiti:

Hivi sasa, Mbagala Kuu ina zahanati tatu (moja inaendeshwa na Serikali na mbili ni za mashirika binafsi), pia ipo hospitali moja ya Serikali ambayo inatambulika kama hospitali ya rufaa ambayo ni kinyume na hali halisi.

3

Page 4: Ahadi Za Mgombea Udiwani Yusuf Manji Mbagala

-

Kama nikiteuliwa suluhisho langu litakuwa ni kushinikiza moja ya kampuni zangu kuwekeza katika kuanzisha zahanati 20 zaidi ambazo zitaanza kazi mwaka moja baada ya mimi kuchaguliwa na kwa gharama nafuu sana ili kuwezesha wakazi wa Mbagala Kuu kupata matibabu. Uwekezaji huu wa kampuni zangu utafungua rasilimali kutoka Serikalini kupandisha daraja hospitali ya Kata kuwa ya hospitali ya rufaa kwa ajili ya matibabu makubwa

3. Ajira kwa vijanaVijana wengi hawana ajira

Pia kama sehemu ya mchango kutoka kwa familia yangu kwa kata ya Mbagala Kuu nitashiriki ujenzi wa vyumba vya kuhifadhia maiti, vitakavyokuwa na uwezo wakuhifadhi takriban maiti 15 kwa siku, ujenzi huu utakamilika ndani ya miezi 15.

4

Endapo nitachaguliwa, suluhisho langu litakuwa ni kushinikiza moja ya kampuni zangu kuandaa pikipiki imara 3,000 zitumike kama bodaboda ambazo zitauzwa kila mwaka kwa vijana, ambapo asilimia 70% ya malipo hayo itakuwa kama mkopo wa benki wa miaka mitatu (ambayo nitashiriki kuwaandalia) na 30% ya bei ya rejareja ya pikipiki itakuwa ni mchango kutoka kwa kampuni zangu, ili vijana wetu watakao tumia pikipiki hizo wapate kipato cha kupeleka nyumbani kwa familia zao.

Utekelezaji wa haya utaanza mara tu nitakapo pata idhini yenu, na kwa njia hiyo ndani ya miaka 5 tutakuwa tumewasaidia vijana 15,000 kupata ajira, watakao jishughulisha na biashara ya bodaboda.

Natambua kwamba hii itatatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa wakazi wa kata ya Mbagala Kuu, pia jitihada nyingine zitabidi zichukuliwe kupitia vyuo vya ufundi n.k.

Ninaamini kwamba, mchango huu kutoka kwangu utakuwa na manufaa mengi kwani vijana wetu watakao jishughulisha na biashara ya bodaboda wataweza kujenga uhitaji wa huduma kwa vijana wenzao ambao watahamasi-ka kuongeza ufundi wao kwa vile kutakuwa na uhitaji wa bidhaa na huduma kata ya Mbaga-la Kuu.

Page 5: Ahadi Za Mgombea Udiwani Yusuf Manji Mbagala

4. Soko la biashara / Huduma za serikali / Viwanja vya michezo: Katika kata ya Mbagala Kuu tuna ukosefu wa soko, wakazi wanalazimika kutembeaumbali mrefu kupata huduma kutoka manispaa, na pia vijana wanakosa viwanja vya

-

Endapo nitachaguliwa, ufumbuzi wangu utakuwa ni kushinikiza moja ya kampuni zangu kuwekeza katika ujenzi wa soko la kisasa litakalo fanana na jengo letu la Quality Centre, litakalo kuwa na ukubwa wa mita za mraba 30,000 litakaloanzia viwanja vya Zakhem mpaka uwanja wa wazi wa Mpakani.

Mjengo huo utakuwa kama ifuatavyo: Kutakuwa na jengo la o�si ambalo litakuwa na o�si za huduma za Serikali ili wakazi wa Mbagala Kuu tuweze kupata vibali, leseni, vyeti vya kuzaliwa n.k. na hivyo hakutakuwa na haja ya kwenda mbali. Ambalo litapangishwa kwa Manispaa ya Temeke.

Pia kutakuwa na benki ambazo zitalipa kodi ya pango kwa eneo la jengo, ukumbi wa harusi.

Sehemu kubwa ya jengo itakuwa ni kwa ajili ya Wafanyabiashara wanaoishi katika kata ya Mbagala Kuu ambao wataweza kununua maeneo hayo kupitia mikopo midogodogo.

Kila mmiliki na mpangaji katika soko atalipia huduma za uendeshaji kulinga-na na ukubwa wa eneo lake, makato hayo ya uendeshaji yatatumika si tu kutunzia soko bali hata viwanja vya mpira, bustani na viwanja vya michezo ya watoto. Mpago huu utachukua takribani miezi 24 kumalizika

5. Kuunganishwa na Umeme :

Bado kuna uhitaji mkubwa wa kuunganishwa na umeme ambao TANESCO bado hawajaweza kukidhi mahitaji ya wakazi wa Kata ya Mbagala Kuu.

.

michezo.

5

Page 6: Ahadi Za Mgombea Udiwani Yusuf Manji Mbagala

6. Vyoo vya umma:

Kwa uelewa wangu kipo choo kimoja tu cha umma katika Kata ya Mbagala Kuu.

-

Endapo nikichaguliwa, ufumbuzi wangu utakuwa ni kushinikiza moja ya kampuni zangu kukopesha kila nyumba kifaa cha kutumia umeme wa jua kwa kila nyumba au biashara ambayo watapenda kuunganishwa na umeme huo wa jua wakati ufumbuzi wa muda mrefu utakuwa ni kiufuatilia TANESCO na kuhakikisha umeme wa kuaminika unaletwa Mbagala Kuu haraka iwezekanavyo. Mpango huu wa ukopeshaji wa nyenzo za umeme wa solar utakuwa

tayari siku 60 baada ya mimi kuchaguliwa.

Endapo nikichaguliwa ufumbuzi wangu utakuwa ni kushinikiza moja ya kampuni zangu kuchangia kila mwaka vyoo 24 kama sehemu ya utumishi wao kwa jamii na kwa namna hii kutakuwepo na vyoo angalau 100 ndani ya miaka 5.

Vyoo vya kwanza 24 vitakuwa tayari siku 90 baada ya mimi kuchaguliwa.

Feni

Taa

Simu

7. Uwezeshaji wa wanawake kupitia SACCOS, Vijana kupitia mikopo, na elimu ya Ufundi kwa Vijana: Kutokana na ukosefu wa ufundi wa aina mbalimbali vijana wanashindwa kuendesha biashara hata pale wanapokuwa na mitaji.

Endapo nikichaguliwa, nitafanya kazi pamoja na mashirika yasiyo ya Serikali na Benki ndogo ndogo pamoja na mifuko ya SACCOS kulipia vijana mafunzo ya Ufundi (VETA) ili wapate mafunzo ya aina mbalimbali. Kwa mwaka takriban wanafunzi 5,000 watapata nafasi ya kupata mafunzo haya. Baada ya mafunzo haya vijana watawekewa mazingira ya kupata mikopo kutoka kwenye benki ndogo ndogo pamoja na wanawake. Katika hili inabidi tusaidiane, kwa kila mmoja kuchukua jukumu la kutekeleza wajibu wake pindi ambapo amepewa mkopo na kurudisha mkopo huo ili siku nyingine tuaminike kupewa mikopo zaidi.

Sola hii i naweza kutumika kwa:kuchaji simukuendesha pangaboiKuwasha taa

6

Page 7: Ahadi Za Mgombea Udiwani Yusuf Manji Mbagala

8. Vituo vya mabasi / Vivuko vya juu vya barabara ya Kilwa :

Watu wengi wanapoteza maisha wakivuka barabra ya Kilwa, tatizo hili linahitaji ufumbuzi.

Endapo nikichaguliwa, ufumbuzi wangu utakuwa ni kushinikiza moja ya kampuni zangu kuchangia barabara tatu za juu za watembea kwa miguu wakati wa kuvuka barabara ya Kilwa ndani ya miaka mitatu, ambazo wao watapunguza gharama kwa kupata faida kupitia matangazo yatakayo kuwa kwenye vivuko hivyo. kwa kukadiria kivuko

cha kwanza kitakuwa kimekamilika ndani ya siku 180 na vingine vitakuwa tayari ndani ya miaka mitatu baada ya mimi kuchaguliwa. Pia nitashughulikia ujenzi wa vituo vya mabasi katika milango ya kupandia na kushukia vivuko.

7

9. Mitaro, barabara, taa za mitaani kwa ajili ya ulinzi:

Kata ya Mbagala Kuu inakadiriwa kuwa na barabara ya kilomita 17.7 ambazo haziko katika hali ya kuridhisha pamoja na mitaro. Hata hivyo inatarajiwa kilometa 5 za barabara zitatengenezwa kuwa za lami kupitia mpango wa Benki ya Dunia kwa mji wa Dar Es Salaam.

Endapo nikichaguliwa, nitahakikisha kuwa barabara zilizopo chini ya mpango wa Mji wa Dar Es Salaam kwa ajili ya Kata ya Mbagala Kuu, zinapewa kipaumbele katika ukamilishaji na kupendekeza kutengewa mipango mingine kupitia programu za Benki ya Dunia, Manispaa ya Temeke na Serikali kwa ajili ya mifumo ya ukusanyaji maji na barabara kama rasilimali zinazohitajika katika huduma za matibabu, masoko, kuunganishwa kwa maji, vyoo vya

jamii, n.k. Kama nilivyo onyesha hapo juu mtazamo wangu ni kujenga chini ya Sekta za Kijamii, Shirikisho la Sekta Binafsi. Ninaamini kuwa ombi la miundombinu bora ya mfumo wa ukusanyaji maji ni moja kati ya mengi ambayo kata ya Mbagala Kuu inahitaji kutoka Serikalini na mimi nitakuwa mtu sahihi wa kuyapeleka maombi hayo.

Page 8: Ahadi Za Mgombea Udiwani Yusuf Manji Mbagala

10. Utupaji wa Taka:

Kuna tatizo kubwa la utupaji wa taka .

Endapo nikichaguliwa, suluhisho langu litakuwa ni kushinikiza moja ya kampuni zangu kukopesha magari 20 kwa Manispaa ya Temeke kwa ajili ya ukusanyaji wa taka na utupaji kwenye mahala husika. Mpango huu unakadiri-wa kukamilika ndani ya siku 120 baada ya mimi kuchaguliwa.

Ili kusaidia barabara ndogondogo za Kata ya Mbagala Kuu kuboreshwa kuwa ya kiwango cha lami nitatoa greda 5 kwa Manispaa ya Temeke kama mkopo ili kusaidia barabara ndogo ndogo kuwa za changarawe zitakazoweza kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa ambapo ujenzi huo utaanza ndani ya siku 120 baada ya mimi kuchaguliwa.

11. Wakazi wa maeneo yenye kukumbwa na mafuriko:

Kama nilivyosema awali moja ya tatizo letu kubwa ni upungufu wa ardhi, na hili limesababisha wakazi kujenga mabondeni. Hakuna suluhisho rahisi la kuongeza ardhi. Kwa mtazamo wangu suluhisho lipo moja kama ifuatavyo:

Endapo nikichaguliwa, nitamuomba Mheshimiwa Rais atusaidie kuwaomba JWTZ wahamishe Maghala yao kwenda mbali zaidi kutoka maeneo ya makazi ya watu na kama watakubali, nitahamasisha moja ya kampuni zangu kujenga ghala la vifaa vya jeshi vinavyohitajika kwenye eneo lingine tofauti. Kama �dia ya kuwa-hamisha, ambapo pia nitawajengea nyumba za

bei nafuu wale wakazi wanaokaa maeneo ya mabondeni na kuwawekea mazingira ya kuweza kupata mikopo. Kwa bahati mbaya hili ndio suluhisho pekee ninalo liona linaloweza kutatua tatizo hili

8

Page 9: Ahadi Za Mgombea Udiwani Yusuf Manji Mbagala

-

-

12. Shule za msingi na sekondari:

Mpaka sasa kuna shule 5 za msingi (Shule ya msingi Kibonde Maji, Shule ya Msingi Mbagala Kuu, Shule ya Msingi Maendeleo,

Shule ya Msingi Kizuiani na Shule ya Walemavu ya Mbagala Kuu) na ripoti zinaonyesha kuwa walimu wanao hitajika ni 296 wakati waliopo ni 276 (kuna upungufu wa walimu 20); madarasa yanayo hitajika ni 271 lakini yaliyopo ni 89 (182 yamepungua); madawati yanayohitajika ni 3779 wakati yaliyopo ni 2277 (yamepungua 1542); vyoo 541 vinahitaji-ka lakini vilivyopo ni 117 (424 vimepungua) viti vya walimu vinavyo hjitajika ni 375 wakati vilivyopo 221 (154 vimepungua); meza za walimu zinazohitajika ni 375 wakati zilizopo ni 133 (48 zimepungua); makabati ya walimu wanayohitajika ni 20 wakati yaliyo-po ni 5 (15 yamepungua) nyumba za walimu 284 wakati zilizopo ni 2 tu (282 zimepun-gua).

Pia zipo shule 2 tu za Sekondari (Shule ya Sekondari Mbagala Kuu ambayo ina Walimu 48 na Wanafunzi 1,389 wanaolazimika kubanana ndani ya madarasa 16 na kushirikiana kutumia vyoo 10 tu; nyingine ni Shule ya Sekondari Mbagala ambayo ina Walimu 65, na Wanafunzi 2,096 wanao lazimika kubanana ndani ya madarasa 27 na kushirikiana kutumia vyoo 7 tu.

Endapo nikichaguliwa, na kama nilivyo elezea hapo juu mtazamo wangu ni kujenga Sekta za kijamii, Shirikisho la Sekta Binafsi.

Mahitaji ya Kata ya Mbagala Kuu ni mengi na hivyo Manispaa ya Temeke haiwezi kukidhi mahitaji hayo peke yake, ninaamini hakuna sababu ya kuwaacha Wanafunzi wetu wakiteseka.

Sitapeleka malalamiko, jitihada zangu zote kwenda Manispaa ya Temeke kurekebisha mapungufu yanayo ripotiwa na takwimu kwa shule za msingi, na kufanya mazingira ya Wanafunzi wa shule ya

Sekondari kuwa mazuri ili waweze kujifunza kwa amani. Ndani ya miezi 12 baada ya mimi kuchagukliwa, pia kutoka kwenye rasilimali za familia yangu na mara�ki nitakusanya rasilimali zaidi ambazo:-(a) Ndani ya miezi 24 baada ya kuchaguliwa tutakuwa na Shule za Serikali zenye vifaa bora na (b) Ndani ya miezi 36 baada ya mimi kuchaguliwa, tutaweza kuvutia walimu bora ili tujenge Wanafunzi bora si tu kwa Tanzania bali hata kwa Afrika Mashariki nzima. Nitahakikisha kila mwaka nitachangia si chini ya shilingi milioni 200 kushu ghulikia hili ndani ya miaka 5.

9

Page 10: Ahadi Za Mgombea Udiwani Yusuf Manji Mbagala

13. Kusimamia ongezeko la watu:

Nimeeleza kuwa tuna tatizo la idadi ya wakazi, mimi kama Diwani wenu pamoja na jitihada zote nitakazo weka, tusipo simamia uhamiaji katika kata yetu bado tutajikuta baada ya miaka 5 hatuoni Maendeleo.

Endapo nitachaguliwa, ndani ya siku 90 nitahakikisha kuwa kuna vitambulisho muhimu kwa wakazi wote wa sasa wa Mbagala Kuu na Kamati za Ndani zitaanzishwa kusimamia, na kupitia maombi wa wakazi wapya watakao penda kuhamia katika Kata yetu. Nina amini kwa dhati kabisa, kwamba ili kuhakikisha maendeleo tunayo yataka tunaya�kia ndani ya miaka mitano inatubidi kusimamia uwiano wa wakazi katika eneo letu maana yake ni kwamba idadi ya watu wanaohamia katika Kata yetu walingane na wale wanao hama kutoka kwenye Kata yetu, na pia watu watakao ruhusiwa kuhamia katika Kata yetu waje na faida kwenye Kata yetu. Pia kuhakikisha watu wanaohamia wanawiana na miundo mbinu iliyopo katika shule, barabara, maji n.k.

MBAGALA KUU KITAMBULISHO CHA MAKAZI

MFANYA BIASHARA

Charles Alex SahimN123456780000 0000 0000 0000

Mtaa: Maturubai , Nyumba No. XX

Pamoja na kwamba mambo niliyoelezea hapo juu sio matatizo pekee niliyopata malalamiko yake kutoka Mbagala Kuu, na sio matatizo pekee nitakayo yafanyia kazi kwa sababu ninaelewa shauku ya kutaka kuleta maendeleo kwa watu wapatao 43,000 itahitaji kupiga mahesabu na Madiwani wenzangu kama nikichaguliwa ambapo nitakuwa katika nafasi nzuri zaidi kuliko kuwapa mategemeo matupu.

Mimi nina amini katika uwezeshaji na sio misaada; kwangu mimi wakazi wote wa Mbagala Kuu wako sawa na sitagawa misaada binafsi, na nawaomba msitegemee hilo kutoka kwangu, ila badala yake nitatengeneza mfuko wa dharura wa shilingi milioni 100, na mtu yeyote mwenye dharura ataweza kutuma maombi Kwenda kwa Uongozi wa mfuko huo.

Naomba mkumbuke kwamba ningependa tuwahimize Wabunge wetu watuwakilishe kuhakikisha tunapata kwenye Kata yetu rasilimali tunazo zihitaji.

Tukumbuke kwamba mshahara na posho anazopata kama Mbunge ni kwa ajili yake yeye na familia yake. Kama akijitosheleza nyumbani kwake basi hata kuwa na sababu ya kutokuja katika Kata yetu na kunisaidia kutatua matatizo ya Maendeleo yanayotu -kumba.

10

Page 11: Ahadi Za Mgombea Udiwani Yusuf Manji Mbagala

Jina Langu ni Yusuf Manji, Ninawaomba kura zenu zenye thamani kubwa kwenye uchaguzi huu mnichague kama Diwani wenuwa kata ya Mbagala Kuu, Wilaya ya Temeke, Dar Es Salaam.

Pia ninawaomba muwapigie kura Madiwani na Wabunge kupitia tiketi ya CCM sio tu kwa Dar Es Salaam pekee ambao tutapigiwa kura tarehe 25 Oktoba, 2015 ili na mimi nifanye kazi na viongozi waliochaguliwa kama timu moja. Kama ilivyo katika mpira mchezaji mmoja sio timu nzima, hivyo tumpigie kura Mgombea Urais wa chama changu Dr. John Pombe Magufuli, ili nitakapo kutana na tatizo ndani ya timu ya CCM nitaweza kwenda kwa Rais wangu wa CCM na tukaelewana kiurahisi zaidi kitu ambacho chama cha upinzani kinaweza kuchukua muda mrefu kuelewa.

Nimekuwa nikisika watu wakisema uchaguzi huu wanataka mabadiliko, na inanifanya nijiuelize, mabadiliko kutoka wapi kwenda wapi; Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961 idadi ya wakazi wake ilikuwa nchini ya milioni 10 kutoka makabila mbalimbali, ikiwa na barabara chache, kiwango cha elimu cha chini ya 20% wakati nchi nyingi za Afrika zikiwa bado ziko chini ya ukoloni. Ndani ya miaka 50 ambayo CCM imekuwa serikalini, idadi ya watu imeongezeka na ku�kia milioni 55 kutokana na huduma bora za wakina mama wajawazito, mkoa wa Dar Es Salaam peke yake umekua kutoka wakazi 100,000 kipindi cha uhuru na sasa ku�kia watu zaidi ya milioni 5, shule zikiongeza kiwango cha elimu kwa zaidi ya 80%, maelfu ya kilomita za barabara, imewakomboa majirani zake wengi kutoka kwenye ukoloni na kwa wakati huo huo kuondoa ukabila na ubaguzi wa kidini.

Mimi ninavyodhani uchaguzi huu hauhitaji mabadiliko bali unahitaji Maendeleo endelevu kwa kasi kubwa na ili hilo litendeke tunahitaji timu ya viongozi kuanzia ngazi ya chini ya Udiwani ambayo mimi ninawania hadi ngazi za juu kabisa zikifanya kazi kuelekea njia moja ya kuleta Maendeleo ya kasi.

Ninadhamira ya Kata ya Mbagala Kuu kuwa Kata bora kwenye mji wa Dar Es Salaam, Dar Es Salaam kuwa mji bora Tanzania na Tanzania kuwa nchi bora Afrika na kwa sababu hiyo ninawaomba kura zenu si tu kwa nafasi yangu kama Diwani, bali kwa timu nzima ya CCM, kama ilivyo kwenye mpira ushindi wa haraka unakuja kwa kufanya kazi kama timu na si kwa ushindi wa mchezaji mmoja.

11

Page 12: Ahadi Za Mgombea Udiwani Yusuf Manji Mbagala

KINONDONI

JIMBO LA TEMEKE

JIMBO LA KIGAMBONI

JIMBO LA MBAGALA

JIMBO LA ILALA

TEAM CCM DAR ES SALAAM

Mh. JOHN POMBE MAGUFULIMGOMBEA URAISI

Mh. IDDI AZZANIUBUNGE- KINONDONI

Mh. ABBAS MTEMVUUBUNGE - TEMEKE

Mh. MUSSA ZUNGUUBUNGE - ILALA

Mh. JERRY SILAAUBUNGE - UKONGA

Mh. FAUSTINE NDUNGULILE UBUNGE - KIGAMBONI

Mh. BONA KALUWAUBUNGE - KIPAWA

Mh. ISSAH MANGUNGUUBUNGE - MBAGALA

Mh. DIDAS MASABURUUBUNGE - UBUNGO

Mh. KIPPI WARIOBAUBUNGE - KAWE

Mh. FENERA MUKANGARA UBUNGE- KIBAMBA

Mh. HAMZA ABBAS FARAHANIMGOMBEA UDIWANI - KINONDONI

Mh. JOSEPHINA AIDAN WAGEMGOMBEA UDIWANI - HANANASIFU

Mh. JULIAN R. BUGUJOMGOMBEA UDIWANI - MAGOMENI Mh. MANYAMA GEORGE

MGOMBEA UDIWANI - KIGOGO

Mh. SONGORO HAMIS MNYONGEMGOMBEA UDIWANI - M/NYAMALA Mh. TAMIM O. TAMIM

MGOMBEA UDIWANI - TANDALE

Mh. HAJI MAKAME MNYAAMGOMBEA UDIWANI - MAKUMBUSHO

Mh. MOHAMED A. CHAMBUSOMGOMBEA UDIWANI - MZIMUNI

Mh. THADEY SIMAMAKA MASSAWEMGOMBEA UDIWANI - NDUGUMBI

Mh. FRANK KALOKOLA KAMUGISHAMGOMBEA UDIWANI - KIJITONYAMA

Mh. MUTTA ROBERT RWAKATAREMGOMBEA UDIWANI - KAWE

Mh. URION MICHAEL JOSEPHATMGOMBEA UDIWANI - KUNDUCHI

Mh. KHERI S. MISSINGAMGOMBEA UDIWANI - BUNJU

Mh. KEVIN WILIAM MBOGOMGOMBEA UDIWANI - MBEZI JUU

Mh. SUZAN MASSAWEMGOMBEA UDIWANI - MABWEPANDE

Mh. ANNA JOSEPH LUVANDAMGOMBEA UDIWANI - WAZO

Mh. HASHIM M. MBONDEMGOMBEA UDIWANI - MBWENI

Mh. ITEBA WILLIAM CHARLESMGOMBEA UDIWANI - MAKONGO

Mh. BERNARD LWEHABURA ONYERAMGOMBEA UDIWANI - MIKOCHENI

Mh. BENJAMIN KAWE SITTAMGOMBEA UDIWANI - MSASANI

Mh. WILLIAM M. MLEGEMGOMBEA UDIWANI - UBUNGO

Mh. AYOUB RAMADHAN SEMVUAMGOMBEA UDIWANI - KIBAMBA

Mh. MWANASHAHA HASSANMGOMBEA UDIWANI - MBEZI

Mh. ABEID JUMANNE KOKIOTIMGOMBEA UDIWANI - KWEMBE

Mh. GODFREY MHELUKAMGOMBEA UDIWANI - KIMARA

Mh. MWAKALILA KUMBUKAMGOMBEA UDIWANI - GOBA

Mh. YUSUPH OMARY YENGAMGOMBEA UDIWANI - MBURAHATI

Mh. RAJAB SULEIMAN HASSANMGOMBEA UDIWANI - MAKURUMLA

Mh. KASSIM MHAMADU LEMA MGOMBEA UDIWANI - MABIBO

Mh. RAPHAEL NYANGI AWINOMGOMBEA UDIWANI - SINZA

Mh. MDOE HAROUN YUSUFMGOMBEA UDIWANI - SARANGA

Mh. SIRAJU HASSAN MWASHAMGOMBEA UDIWANI - MSIGANI

Mh. OLIVERY QUIRINE SHIRIMAMGOMBEA UDIWANI - MAKUBURI

Mh. ABDULAKARIM RASHID ATIKIMGOMBEA UDIWANI - MANZESE

Mh. VICTOR M. MWAKASINDILEMGOMBEA UDIWANI - MAKANGARAWE

Mh. RAPHAEL JAMES LUANDAMGOMBEA UDIWANI - BUZA

Mh. AMIRI BAKARI SALUMMGOMBEA UDIWANI - KILAKALA

Mh. KENNY DICKUSI MAKINDA MGOMBEA UDIWANI - YOMBO VITUKA

Mh. WILFRED MORIS KIMATIMGOMBEA UDIWANI - KURASINI

Mh. JUDITH BONIFACE MAGEMBEMGOMBEA UDIWANI - MTONI

Mh. HAMIS ABDALLAH MZUZURI MGOMBEA UDIWANI - AZIMIO

Mh. FRANCIS SAMSON MTAWAMGOMBEA UDIWANI - KEKO

Mh. NOEL LUKAS KIPANGULEMGOMBEA UDIWANI - CHANG’OMBE

Mh. FEISAL SALUM HASSANMGOMBEA UDIWANI - TEMEKE 14

Mh. ABEL WILBARD TARIMOMGOMBEA UDIWANI - SANDALI

Mh. RAMADHAN LUKIMANGIZAMGOMBEA UDIWANI - TANDIKA

Mh. JUMA RAJAB MKENGAMGOMBEA UDIWANI - MIBURANI

Mh. DOTTO MSAWAMGOMBEA UDIWANI - KIGAMBONI

Mh. AMINA ALLY HAMISIMGOMBEA UDIWANI - TUNGI

Mh. ZACHARIA J. MKUNDIMGOMBEA UDIWANI - VIJIBWENI

Mh. HENRY LAZARO CHAULAMGOMBEA UDIWANI - MJIMWEMA

Mh. AMIRI MZURI SAMBOMGOMBEA UDIWANI - KIBADA

Mh. FRANCIS MASANJA CHICHIMGOMBEA UDIWANI - SOMANGILE

Mh. MAABAD SELEMAN HOJAMGOMBEA UDIWANI - PEMBA MNAZI

Mh. ISSA HEMED ZAHOROMGOMBEA UDIWANI - KISARAWE II

Mh. MUHIDIN SANYA BUHAYAMGOMBEA UDIWANI - KIMBIJI

Mh. MOHAMED SELEMAN MKETOMGOMBEA UDIWANI - TOANGOMA

Mh. ABDALLAH MTINIKAMGOMBEA UDIWANI - KIBONDEMAJI

Mh. YUSUF M. MANJIMGOMBEA UDIWANI - MBAGALA KUU

Mh. ANDERSON SAMWEL CHALEMGOMBEA UDIWANI - KIJICHI

Mh. HEMED JUMA KARATAMGOMBEA UDIWANI - CHAMAZI

Mh. SAID FELLAMGOMBEA UDIWANI - KILUNGULE

Mh. ABDALLAH JAFARI CHAUREMBOMGOMBEA UDIWANI - CHARAMBE

Mh. TITTO ELIAKIM OSSOROMGOMBEA UDIWANI - KIBURUGWA

Mh. RAMANDANI ZAMEMGOMBEA UDIWANI - MBAGALA

Mh. SAMINA PATRICK MASHAIRIMGOMBEA UDIWANI - MIAZINI

Mh. ABDULKARIM SALUM MASAKIMGOMBEA UDIWANI - KARIAKOO

Mh. KHERI MOHAMED KESSYMGOMBEA UDIWANI - KISUTU

Mh. FATUMA A. ALLYMGOMBEA UDIWANI - GEREZANI

Mh. MARIAM MOHAMEDMGOMBEA UDIWANI - MCHAFUKOGE

Mh. AZIMKHANA A.AZIMKHANMGOMBEA UDIWANI - MCHIKICHINI

Mh. SULTAN A. SALIMMGOMBEA UDIWANI - UPANGA MASHARIKI

Mh. SAADY M. KHIMJIMGOMBEA UDIWANI - ILALA

Mh. ADNAN KONDOMGOMBEA UDIWANI - UPANGA MAGHARIBI

Mh. HENRY MASABAMGOMBEA UDIWANI - KIVUKONI

Mh. YUSUPH M. LIMAMGOMBEA UDIWANI - KIPAWA

Mh. PETER JOSEPH KARIAMGOMBEA UDIWANI - LIWITI

Mh. ASSA S. HAROUNMGOMBEA UDIWANI - VINGUNGUTI

Mh. TUMIKE MALILOMGOMBEA UDIWANI - BONYOKWA

Mh. PERFECT EUGEN MASAWEMGOMBEA UDIWANI - SEGEREA Mh. BATULI M. MZIYA

MGOMBEA UDIWANI - MNYAMANIMh. SUDI K. SUDI

TABATAMh. LEAH B. MGITU

MGOMBEA UDIWANI - KINYEREZIMh. RUKIA MWENGE

MGOMBEA UDIWANI - KIMANGAMh. GODLISTEN O. MALISA

MGOMBEA UDIWANI - MIREFUMh. BONVENTURE G. MWAIPAJAMGOMBEA UDIWANI - KIWALANI

Mh. LUCY J.LUGOMEMGOMBEA UDIWANI - KISUKURU

Mh. BARUA A. MWAKILANGAMGOMBEA UDIWANI - BUGURUNI

Mh. EVA M. NYAMOYOMGOMBEA UDIWANI - KITUNDA

Mh. HARUNA H. BATENGAMGOMBEA UDIWANI - UKONGA

Mh. NYASIKA G. MOTEMA MGOMBEA UDIWANI - KIVULE

Mh. MOAHMED R. MSOPHEMGOMBEA UDIWANI - KIPUNGUNI

Mh. IMELDA T. SAMJELAMGOMBEA UDIWANI - PUGU

Mh. LUKAS MUNOBI RUTAINURWAMGOMBEA UDIWANI - GONGO LA MBOTO

Mh. TWAHA S. MALATEMGOMBEA UDIWANI - BUYUNI

Mh. KINGULA M. HASSANMGOMBEA UDIWANI - MAJOHE

Mh. DEOGLAS O.MASABURIMGOMBEA UDIWANI - CHANIKA

Mh. ABDALLAH S. MPATEMGOMBEA UDIWANI - ZINGIZIWA

Mh. MWALILE A. JAFFARIMGOMBEA UDIWANI - MSOGOLA

Mh. JOB I. IBRAHIMMGOMBEA UDIWANI - MZINGA Mh. YOHANA A. NGONGA

MGOMBEA UDIWANI - PUGU STATIONMh. ABDALLAH FARAJI

MGOMBEA UDIWANI - JANGWANI

12