aida a aadii - tanzania · umma ilianzishwa kwa mujibu wa ibara ya 132 ya katiba ya jamhuri ya...

25
Mkuchika awataka wahitimu kufanya kazi zao kwa weledi na uadilifu Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yakutana na Wadau kujadili marekebisho ya Sheria ya maadili. NDANI: Toleo la Tatu | Februari 2013 Tanzania SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA YAZINDUA TOVUTI YAKE

Upload: others

Post on 26-Dec-2019

18 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Mkuchika awataka wahitimu kufanya kazi zao kwa weledi na uadilifu

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yakutana na Wadau kujadili marekebisho ya Sheria ya maadili.

NDANI:

Toleo la Tatu | Februari 2013 Tanzania

SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMAYA ZINDUA TOVUTI YAKE

JARIDA LA MAADILI

OFISI ZA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMAMAKAO MAKUU:

Mtaa wa Ohio; S.L.P 13341, Dar es Salaam.Simu: +255 22 211 1810/11 | +255 22 213 6422Nukushi: +244 22 211 9217

Barua Pepe: [email protected] | Tovuti: www.ethicssecretariat.go.tz

KANDA YA ZIWA:(Mikoa ya Geita, Kagera, Mara na Mwanza)Jengo la Mfuko wa Hifadhi ya jamii(NSSF) - Mwanza,Mtaa wa Kenyata,S.L.P 1473,Mwanza.Simu: +255 28 250 5005Nukushi: +255 28 250 5004

KANDA YA KUSINI:(Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma)Jengo la Mkuu wa Mkoa,S.L.P 218,Mtwara.Simu: +255 23 233 3963Nukushi: +255 23 233 3962

KANDA YA MAGHARIBI: Mikoa ya Tabora, Kigoma Shinyanga na Simiyu)Jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) - Tabora,Mtaa wa Jamhuri,S.L.P 1126,Tabora.Simu/Nukushi: +255 26 260 5323

KANDA YA KASKAZINI:(Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga)Audit House Mtaa wa Kware/SakinaS.L.P 3174,Arusha.Simu: +255 27 244 4534Nukushi: +255 27 254 4780

KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI:(Mikoa ya Katavi, Mbeya, Njombe, Iringa na Rukwa)Jengo la Wakala wa Majengo,Mtaa wa Saba Saba,S.L.P 6311,Mbeya.Simu: +255 25 250 2714

KANDA YA KATI:(Mikoa ya Dodoma na Singida)Jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) - Dodoma,Mtaa wa Askari,S.L.P 1887,Dodoma.Simu: +255 26 232 1059Nukushi: +255 26 232 3838

OFISI ZA KANDA

1. Bibi Emma P. Lyimo - Mwenyekiti2. Bibi Johanither Barongo - Katibu3. Bibi Sheiba Bulu - Mhariri4. Bibi Zahara Guga - Mjumbe5. Bibi Mwanarabu Talle - Mjumbe6. Bw. Rocky Setembo - Mjumbe7. Bw. Ally Mataula - Mjumbe

BODI YA UHARIRI

YALIYOMO1. Ujumbe wa Kamishna wa Maadili ........................................................................................

2. Tahariri ........................................................................................................................................

3. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yazindua tovuti yake ...............................

4. Kamati 260 za Uadilifu zaanzishwa Nchini ........................................................................

5. Maadili kwa Viongozi wa Umma ni njia pekee ya kuleta ufanisi na kukuza uchumi

Nchini ..........................................................................................................................................

6. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawara Bora Mh George Mkuchika amewataka

Wahitimu kufanya kazi zao Kwa Weledi na Uadilifu ...................................................

7. Maadili ya Viongozi wa Umma ni Nguzo Muhimu katika kuleta maendeleo Nchini

8. Viongozi waelimishwe kuhusu maadili ya kazi zao ........................................................

9. Sekretarieti ya Maadili yaendesha Warsha na Wadau kuhusu marekebisho ya Sheria

ya Maadili ya Viongozi a Umma ...........................................................................................

10. Maadili ni msingi wa Utawala bora Nchini .......................................................................

11. Jamii iliyooza kimaadili huzaa viongozi wasio waadilifu ..............................................

12. Jukumu la kujenga misingi ya Maadili ni la wote ............................................................

13. Matumizi mabaya ya madaraka yanayohusisha unyanyasaji wa kijinsia (Sextortion”)

ni tatizo la mmomonyoko wa Maadili Nchini ....................................................................

14. Kuna vitendo mbalimbali vinavyotofautisha “Sextortion” na makosa ya kawaida ya

unyanyasaji wa kijinsia ...........................................................................................................

15. Marekebisho ya Seria ya Maadili ..........................................................................................

16. Habari katika picha ..................................................................................................................

1.

3.

4.

5.

6.

8.

9.

10.

11.

13.

15.

16

17.

18.

20.

21.

1

Katika toleo hili la jarida letu la MAADILI napenda niongelee kuhusu vipengele ambavyo tumeona ni bora vikafanyiwa marekebisho ili kuendana na mahitaji ya wakati au uhalisia. Ikumbukwe kuwa Sheria hii ilifanyiwa marekebisho mwaka 2001 kupitia Sheria Na. 5 ya mwaka 2001. Ni wazi kuwa changamoto nyingi zimejitokeza tangu wakati huo na hivyo kusababisha utekelezaji wa sheria hii kuwa mgumu ama hafifu. Pia Mhe. Rais, mwaka 2008, aliagiza kwamba Sheria ya Maadili ifanyiwe mapitio ili kuweka taratibu za namna ya kudhibiti mgongano wa maslahi miongoni mwa viongozi wa umma hususan suala la kutenganisha biashara na uongozi. Kutokana na hali hii Serikali kupitia Sekretariet ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeona ni vema Sheria hii ya Viongozi wa Umma ikafanyiwa marekebisho ili kuondoa mapungufu yaliyobainika.

Marekebisho ya Sheria hii yamegawanywa katika makundi mawili moja ni mapendekezo yanayolenga kurekebisha vipengele mbalimbali

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania na ni Idara ya Serikali inayojitegemea chini ya Ofisi ya Rais ambapo ilianza kazi zake rasmi mwezi Julai mwaka 1996. Sekretarieti ya Maadili ilianzishwa ili kutekeleza Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Na. 13 ya mwaka 1995 kama ilivyo rekebishwa na Sheria Na. 5 ya mwaka 2001.

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilitungwa na Bunge ili kutekeleza matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, ibara ya 132 (4) ambayo inasema kuwa Bunge litatunga Sheria itakayoainisha misingi ya Maadili ya Viongozi wa Umma itakayozingatiwa na watu wote wanaoshika nafasi za madaraka zitakazotajwa na Bunge.

Pia, katika Ibara 132 (5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ililipa Bunge mamlaka ya kuweka misingi ya Maadili ambayo:

(a) Itafafanua nafasi za madaraka ambazo watu wenye kushika nafasi hizo watahusika nayo;(b) Itawataka watu wanaoshika nafasi fulani za madaraka kutoa mara kwa mara maelezo rasmi kuhusu mapato, rasilimali na madeni yao;(c) Itapiga marufuku mienendo na tabia inay opelekea kiongozi kuonekana hana uaminifu, anapendelea au si muadilifu au inaelekea kukuza au kuchochea rushwa katika shughuli za umma au inahatarisha maslahi au ustawi wa jamii;(d) Itafafanua adhabu zinazoweza kutolewa kwa kuvunja misingi ya maadili;(e) Itaelekeza taratibu, madaraka na desturi zitakazofuatwa ili kuhakikisha utekelezaji wa maadili;(f) Itaweka masharti mengine yoyote yanayofaa au ambayo ni muhimu kwa madhumuni ya kukuza na kudumisha ua minifu, uwazi, kutopendelea na uadilifu

katika shughuli za umma na kwa ajili ya kulinda fedha na mali nyinginezo za Umma.

Ujumbe wa Kamishna wa Maadili

Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda,Kamishna wa Maadili.

2

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutokuwa na nguvu ya kisheria ya kuendesha mashauri mahakamani isipokuwa kwa ridhaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali (DPP), Watumishi wa Sekretarieti kutokuwa na kinga ya kushtakiwa wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kutokuwapo kwa utaratibu wa usalama kwa wananchi wanaotoa taarifa za ukiukwaji wa maadili.

Maoni ya wadau mbalimbali ni kwamba ni vema Sheria irekebishwe ili kuendana na mazingira ya sasa. Hivyo, Sekretarieti imeandaa mchakato wa marekebisho ya Sheria kwa lengo la kukidhi matakwa hayo. Hatua hiyo ni pamoja na kuandaa warsha ya wadau iliyokuwa na lengo la kujadili marekebisho ya Sheria iliyofanyika Dar es Salaam tarehe Mosi Oktoba, 2012.

Katika Warsha hiyo Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilipata fursa ya kuwasilisha mapendekezo ya marekebisho ya vifungu vya Sheria ambavyo vina mapungufu na vinahitaji kufanyiwa marekebisho. Pia, kulikuwa na nyongeza ya vifungu vya Sheria ambavyo havikuwepo katika Sheria ya sasa kwa lengo la kuipa nguvu Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya kusimamia maadili ya uongozi katika nchi yetu.

Kupitia warsha hiyo wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na Asasi za Kiraia walipata nafasi ya kutoa michango yao kuhusu mapendekezo ya Sheria yaliyowasilishwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Ninaamini kuwa mchakato huu muhimu tuliouanza utatuwezesha kupata Sheria ambayo itakuwa inaendana na wakati na hivyo kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza.

Ni matarajio ya Sekretariet ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwa wadau wataendelea kutoa ushirikiano kwa ofisi yetu ili kuwezesha kupatikana kwa Sheria hiyo mpya ya Maadili ya viongozi ambayo inaaminika kuwa itakuwa mbadala wa sheria hii ya sasa na hivyo kukabili changamoto zinazojitokeza sasa na hivyo kuendana na wakati .Mwisho napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia wananchi na wadau wetu kwa jumla usomaji mwema wa Jarida letu hili, kwani kupitia hapa mtapata kujua mambo mbalimbali tuliyoyafanya na ambayo tunatarajia kuyafanya katika siku za usoni.

vya sheria ili kukuza uadilifu, uwajibikaji na uwazi katika utekelezaji wa majukumu ya umma na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Sekretariet ya Maadili ya viongozi wa Umma na Baraza la Maadili. Kundi la pili linahusu mifumo ya kutenganisha uongozi na biashara. Ni wazi kuwa marekebisho ya Sheria hii yatawezesha upatikanaji wa Sheria mpya ambayo itafanya mambo yafuatayo;-

• Itaimarisha uadilifu, uwajibikaji na uwazi katika kutekeleza majukumu ya umma,

• Itadhibiti matumizai mabaya ya madaraka hususani migongano ya maslahi kati ya

• shughuli za serikali na shughuli binafsi,• Itaiwezesha Sekretarieti ya Maadili ya • Viongozi wa Umma kutekeleza majukumu

yake kwa ufanisi,• Kuliwezesha Baraza la Maadili kutekeleza

majukumu yake kwa ufanisi,• Kulinda amani ya wananchi juu ya uadilifu• wa Viongozi wa Umma na Serikali kwa

ujumla.

Ni miaka 16 sasa tangu Sheria hii ianze kutumika rasmi hapa nchini , na hii ilikuwa mwezi Julai, 1996 ambapo katika kipindi hiko Sheria ya Maadili ya Maadili ya Viongozi wa Umma imefanyiwa marekebisho mara moja kwa nia ya kuipa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma madaraka zaidi na kurahisisha utendaji kazi zake, taratibu za kuwasilisha malalamiko, kuongeza adhabu za ukiukwaji wa maadili na kuongeza idadi ya viongozi wanaowajibika na sheria hii.

Pia, katika kipindi hicho kumekuwa na mafanikio kadhaa yaliyopatikana hususani katika suala zima la kusimamia mienendo ya Viongozi wa Umma walioatajwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Hata hivyo, kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika Utumishi wa Umma na mapungufu katika utekelezaji wa Sheria hii. Aidha, changamoto kubwa zilizopo sasa ni kukua kwa kasi kwa uelewa wa umma juu ya haki za kisiasa kwa upande mmoja na tatizo la mmonyoko wa maadili kwa viongozi wa umma ambapo kumekuwa na taarifa za kuongezeka kwa tuhuma za rushwa, kuibuka kwa ufisadi, ubadhilifu wa mali za umma na matumizi mabaya ya mamlaka kwa viongozi wa umma.

Changamoto nyingine ambazo ni mapungufu ya kisheria katika Sheria ya sasa ni pamoja na

3

TahaririTarehe 9 Desemba ya

kila mwaka ni siku ya Maadili Duniani. Tanzania

huungana na nchi nyingine Duniani katika kuadhimisha siku hii kila mwaka, ikiwa ni njia mojawapo ya mapambano dhidi ya rushwa duniani. Lakini siku hii hapa nchini huadhimishwa Disemba 10 , hii inatokana na ukweli kuwa Disemba 9 ni siku ya Uhuru wa Tanzania bara. Ukweli huu ndio ambao unafanya maadhimishio ya siku ya maadili duniani kuadhimishwa Disemba 10 kwa hapa nchini,

Hivyo, Octoba 31, 2003 Kupitia tamko namba 58/61 Umoja wa Mataifa ulitambua umuhimu wa nchi wananchama kushirikiana katika kukabili tatizo la rushwa. Hatua hii ilitokana na Umoja wa Mataifa kutambua kuwa rushwa siyo tatizo la nchi ama taifa moja bali ni tatizo lanaloathiri mataifa mbali mbali na hivyo kuwepo umuhimu wa nchi kushirikiana kulikabili.

Mapatano hayo yalisainiwa na nchi wananchama Desemba 9, 2003 huko Merida, Mexco. Tanzania imesaini na kuridhia mapatano haya.

Kufuatia kusainiwa kwa Mapatano haya, Umoja wa Mataifa uliipitisha Desemba 9 ya kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya kupambana na Rushwa hatua inayotoa fursa muhimu kwa mataifa kushirikiana katika kuzuia na kupambana na rushwa. Hatua hii inadhihirisha kuwa Serikali za Mataifa haya zinatambua ubaya wa rushwa.

Aidha nchini Tanzania Maadhimisho haya yatakuwa yakifanyika Desemba 10 badala ya Desemba 9 na yanaitwa siku ya Kimataifa ya kuzuia na kupambana

na Rushwa. (Siku ya Maadili) Hatua hii ilifikiwa na Serikali mwaka 2005 kwa sababu Desemba 9 kila mwaka Tanzania huadhimisha Sikukuu ya Uhuru na Jamhuri.

Siku hii huadhimishwa kwa kufanya vitu mbalimbali ambavyo kwa njia moja ama nyingine huwakumbusha wananchi umuhimu wa kuendelea na kuimarisha mapambano dhidi ya Rushwa nchini na haja ya kuimarisha maadili ili kuwa na watu waadilifu.

Maadhimisho ya Siku ya Maadili Duniani yana lengo la kuelimisha umma kuhusu Maadili na Mapambano dhidi ya rushwa katika kuimarisha Utawala Bora nchini.

Maadhimisho ya siku hii huambatana na utoaji wa machapisho mbalimbali yanayohusu Maadili, Midahalo na makongamano yenye kubeba ujumbe wa kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuendeleza mapambano ya rushwa na kuimarisha maadili miongoni mwa wananchi.

Kuandaa vipindi vya redio na televisheni, kuhusu Maadili, Makala mbali mbali za masuala ya maadili katika magazeti mbalimbali, uandaaji wa mabango yenye ujumbe wa Maadili, vipeperushi na majarida mbalimbali yenye ujumbe wa Maadili ikiwa ni njia mojawapo ya kuadhimisha siku hiyo.

Hivi vyote hufanyika kwa minajili ya kutoa elimu kwa umma na kuonyesha harakati ambazo zimekuwa zikifanyika nchini katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Wakati tukiadhimisha siku ya maadili , itakuwa vyema kama

tukiangalia kidogo undani na maana ya maadili. Maadili inahusu kanuni ambazo zinatumika kutofautisha kati ya mwenendo mwema na mwenendo mbaya/ usiofaa miongoni mwa jamii husika. Maadili ndiyo dira inayoiongoza jamii katika kufanya maamuzi bora ambayo yanaleta maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Chimbuko la Maadili ni kutoka katika jamii husika. Mara nyingi Kanuni za Maadili zinaanishwa katika katiba ya nchi, Sheria na kanuni za Maadili.

Nchi nyingi Duniani ziko katika mkakati wa kujenga na kuimarisha Maadili kama njia ya kupambana na rushwa pamoja na maovu mengine ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa jamii ili kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Serikali ya Tanzania imechukua hatua mbali mbali za kusimamia Maadili nchini ikiwa ni pamoja na kuunda vyombo vya kusimamia, kudhibiti na kukuza Maadili na Utawala Bora nchini, vyombo hivyo ni pamoja na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Idara ya Maadili ya Watumishi wa Umma katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kamati za kusimamia Uadilifu katika wizara, Idara na Taasisi za Umma na kuadhimisha siku ya Maadili Duniani .

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma safari hii iliungana na taasisi zingine zinazosimamia masuala ya maadili nchini za Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa nchini (TAKUKURU), Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Idara ya Maadili katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika kuadhimisha siku hii.

4

kuweza kukidhi mahitaji mbalimbali ya wadau ambayo yanaongezeka kwa kasi”, alifafanua Bibi Mlawi.

Awali, akimkaribisha Mgeni Rasmi, Kamishna wa Maadili, Mhe. Jaji Mstaafu Salome Kaganda alisema, tovuti hiyo itawapa wananchi fursa ya kujisomea na kuifahamu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995, pamoja na upatikanaji wa haraka wa Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni zinazopaswa kujazwa na Viongozi wa Umma Nchini.

Mhe. Kaganda alitoa wito kwa Viongozi wa Dini kuwa mstari wa mbele katika kukemea uvunjaji wa maadili miongoni mwa waumini wao hali ambayo itasasidia kujenga na kulinda maadili nchini.

“Nachukua nafasi hii kuwaomba Viongozi wa dini, tusaidiane kukemea vitendo

vya ukosefu wa maadili kwa waumini wao. Kama kuna desturi ya kuungama dhambi basi muwakumbushe kufanya hivyo “ alisema.

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imezindua tovuti yake, hatua ambayo imelenga kuharakisha

uwasilishaji wa taarifa za kukuza maadili kwa umma. Tovuti hii inapatikana kupitia www.ethicssecretariat.go.tz.

Akizindua tovuti hiyo, Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Bibi Susan Mlawi ameitaka Sekretarieti ya Maadili kuhakikisha tovuti hiyo inakuwa hai na kuwawezesha wadau kupata taarifa stahili ambazo zinazoendana na wakati.

“Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni moja kati ya Taasisi chache

zilizofanikiwa kuwa na tovuti yake, sasa ni jukumu lenu kuhakikisha tovuti hii inakuwa hai wakati wote na kufanya wadau wote kupata taarifa kwa wakati ili kuendana na wakati,” alisema.

Amesema kuanzishwa kwa tovuti hii kunakuwa kiungo tosha cha mawasiliano kati ya Taasisi, wadau mbalimbali na jamii kwa ujumla na hivyo kutoa fursa ya kujifunza na kujionea kazi zinazofanyika , yakiwemo mafanikio ya Taasisi.

Pia, Bibi Mlawi alisema kupitia tovuti hiyo wadau watapata fursa ya kuwasilisha maoni, mapendekezo na taarifa zao mbalimbali kwa urahisi zaidi, ambazo zitasaidia kufichua maovu dhidi ya Viongozi wa Umma, hatua ambayo ni muhimu katika kupambana na umaskini na hatimaye kuleta maendeleo ya Taifa.

Bibi Mlawi aliendelea kusema kuwa, hatua ya Serikali ya kuleta mabadiliko kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ’TEHAMA’ imetokana na kukua

kwa Serikali na kuongezeka kwa majukumu yake na hivyo kuhitajika gharama kubwa ya kuwahudumia wananchi.

“Hayo yanadhihirika hata kwa Taasisi hii kwani inazidi kukua na majukumu

yake yanazidi kuongezeka, hivyo mbinu na mikakati mbalimbali inabidi itafutwe ili

SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA YAZINDUA TOVUTI YAKE.

Naibu Katibu Mkuu Ikulu Suzzan Mlawi akikata utepe kuzindua rasmi tovuti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya www.ethicsecretariet.go.tz , nyuma yake ni Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda.

na Rocky Setembo

yalipokelewa kutoka vyombo vya upelelezi vya TAKUKURU na Jeshi la Polisi ambapo majalada 82 yaliandaliwa hati za mashtaka na kupewa kibali cha kushtaki mahakamani. Kutolewa kwa kibali hicho kunafanya mashauri ya rushwa yaliyofikishwa Mahakamani nchini kote kufikia 369.

Pia alisema kuwa Serikali kupitia TAKUKURU imeendeleza juhudi za kutoa elimu kwa umma kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa ambapo vyombo vya habari, machapisho mbali mbali na shughuli nyingine za kijamii katika ngazi za kitaifa, mikoa na wilaya zilifanyika.

Akiongelea suala la kuwawezesha wananchi kupata taarifa mbali mbali kuhusiana na rushwa Mhe Pinda alisema Takukuru pia imeanzisha mtandao wa mawasiliano ya kisasa ya teknolojia ya habari ambapo sasa inapokea na kutuma taarifa za masuala ya rushwa ikiwa ni pamoja na kufungua klabu 2,030 za wapambanaji za rushwa zenye wajumbe 178, 142 katika shule za sekondari nchini kuanzia 2009.

Maadhimisho hayo yaliambatana na maonyesho ya shughuli za taasisi zinazosimamia mapambano ya dhidi ya Rushwa, Maadili na upatikanaji wa Haki na Sheria nchini ambapo Taasisi kutoka Ofisi ya Rais Wizara ya Utawala Bora za Takukuru, Maadili na Tume ya Haki za Binadamu zilishirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi zake RITA, Sekretariet ya Msaada wa Sheria,Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Katiba na Mahakama zilishiriki, maonyesho hayo yalifanyika kuanzia Desemba 5 hadi 10 jijini Dar es salaam ambapo wananchi walipata nafasi ya kufafanuliwa shughuli mbalimbali za Serikali na huduma za msaada wa kisheria.

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda amesema Serikali imedhamiria kuimarisha utawala bora na

kuiongoza jamii katika mapambano dhidi ya rushwa nchini . Dhamira hiyo inatokana na hatua ya kuanzishwa kwa Kamati 260 za uadilifu katika ofisi za mbalimbali za serikali. Kamati hizo zimeanzishwa katika Wizara,Idara na Wakala zinazojitegemea (MDA’s), Miji, Majiji na Halmashauri za wilaya mbalimbali nchini.

Mhe. Pinda amesema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu/Maadili duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa anaelezea mafanikio katika harakati za kupambana na rushwa nchini.

“Kama tafiti mbalimbali zinavyoonesha, mafanikio katika kupambana na rushwa

yametokana na kuzingatia utekelezaji wa Lengo Namba 3 la Mkakati wa Kitaifa wa kupambana na Rushwa Awamu ya Pili unaosimamiwa na TAKUKURU, kuna vitu vingi vimefanyika,” alisema.

Alisema Kamati hizo zimepata mafunzo juu ya majukumu yao ili kuziwezesha kusimamia kikamilifu masuala ya rushwa na maadili katika maeneo yao ya kazi.

Aidha aliongeza kuwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano, Majaji wa Mahakama Kuu na Wahadhiri wa Vyuo Vikuu wamepatiwa mafunzo ya miundombinu ya maadili kuhusiana na sehemu zao za kazi ikiwa ni harakati za Serikali za kuchochea na kujenga uadilifu ndani ya vyombo hivyo.

Akitoa msisitizo juu ya mapambanao dhidi ya rushwa nchini Mhe. Pinda alisema majalada 192 ya rushwa kubwa na ubadhirifu

Kamati 260 za Uadilifu Zaanzishwa Nchini

5

Na Sheiba Bulu

wasingekuwa makini katika kutimiza majukumu yao ya kuwaongoza wananchi na badala yake wangetumia muda wao mwingi kutumia rasilimali za Umma kwa Maslahi yao binafsi. Hii ikiwa ni pamoja na kujilimbikizia mali pamoja na rushwa.

Katika hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa kwenye kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam mwaka 2011, alisema “Napenda kutumia nafasi hii kusisitiza kwa viongozi na watumishi wa Umma kuwa, Serikali iendelee kupambana na uzembe kwa nguvu zake zote hadi Utumishi wa Umma utakapokuwa safi na uliotukuka., pia tuhakikishe kuwa mifumo na taratibu zilizowekwa za kuendesha Serikali ni lazima ziimarishwe na kutumiwa na watu wote na asasi zote za Serikali.”

Aidha, katika kusisitiza maadili kwa viongozi wasijilimbikizie mali, utaona kuwa katika kifungu cha 9 kifungu kidogo cha (3) cha sheria ya Maadili ya viongozi , kiongozi wa Umma atatakiwa kutaja mali zake na za mke wake au mume wake, au zile ambazo si za unyumba, au ambazo hazimilikiwi kwa pamoja, iwapo anadaiwa kwamba kiongozi huyo wa Umma au mwanafamilia anayemhusu sana, anaelekea kutajirika kwa haraka au kusikoelezeka kwa mujibu wa vyanzo vinavyoonekana vya mapato yake.

Aidha kiongozi wa Umma atatakiwa kutaja

Katika kuleta ufanisi na kukuza uchumi wa nchi yetu, ni muhimu kwa viongozi waliopewa jukumu

la kuongoza Umma, kuwa na Maadili katika utendaji wao wa kazi za kila siku wanazozifanya kwa manufaa ya wananchi, lengo kuu ni kuwaongoza wananchi katika misingi ya haki na usawa katika kuwaletea maendeleo.

Aidha, lengo hilo halitaweza kufikiwa, iwapo kiongozi huyo hatokuwa na maadili mema yanayomwongoza . Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kifungu cha NNE (4) cha sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995, Neno “Maadili,, lina maana ya kuwa ni maadili ya Viongozi wa Umma yaliyowekwa kwa Mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa Azimio la Arusha la mwaka 1967, liliainisha miiko ya Uongozi kwa viongozi wa chama na serikali ambayo ilitumika kwa kila kiongozi wa chama na serikali kuzingatia miiko hiyo kikamilifu wakati wa kutimiza majukumu yao, na uadilifu kwa wananachi. Kitu kikubwa katika miiko hiyo ilikuwa ni kukataza kiongozi yoyote wa Umma kutumia madaraka aliyopewa na Umma kwa maslahi yake binafsi na pia kuwanyonya wananachi anaowatumikia.

Hii inatokana na ukweli kwamba endapo Azimio la Arusha la mwaka 1967 lisingeweka miongozo yake, viongozi wa chama na Serikali kwa wakati ule

Maadili kwa Viongozi ni Njia Pekee ya Kuleta Ufanisi na Kukuza Uchumi Nchini.

6

Na Johanither Barongo

jamii au katika utekelezaji wa majukumu yake, katika taasisi yoyote iwe ya binafsi, au ya Umma.

Katika kifungu cha nne (4) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na. 13 ya mwaka 1995 inatamka kwamba ‘Maadili” maana yake ni maadili ya viongozi wa Umma yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria. Kila kiongozi wa Umma anatarajiwa kuepukana na mwenendo ambao haukubaliki na hasa ikiwa kiongozi aliyekabidhiwa madaraka na wananchi.

Ni ukweli usiopingika kuwa, ili taifa lolote ambalo linataka kuwa na amani kwa watu wake ni muhimu kwa viongozi wa Umma wa Taifa hilo kuwa na maadili katika utendaji wao wa kazi. Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka masharti ya kimaadili ambayo viongozi wa Umma hawana budi kuyazingatia. Moja ya masharti hayo yapo katika ibara ya 69 ambayo inatamka kuwa.

• Kila kiongozi wa Umma atatakiwa kuwa kabla ya siku 30 tangu aapishwe kushika madaraka kuwasilisha kwa kamishna wa maadili tamko rasmi la rasilimali na madeni yake.

• Tamko rasmi linalotakiwa kuwasilishwa kwa Kamishna kwa mujibu wa masharti ya ibara hii litatolewa kwa kutumia fomu maalum itakayowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

Kwa kuzingatia haya taifa lolote linalotaka amani endelevu kwa watu wake ni muhimu kwa viongozi wenye jukumu la kuongoza wananchi wa taifa hilo kuwa na maadili katika kazi zao na kwa kufuata misingi ya haki za binadamu na pia kwa kufuata miiko hiyo kikamilifu wakati wa kutimiza majukumu yao kwa wananchi.

kama mali yake, na mali haitahesabiwa kuwa ni mali inayostahili kutajwa na viongozi wa Umma endapo:

• Mali hiyo si mali iliyopatikana wakati wa ndoa,

• Mali hiyo haimilikiwi kwa pamoja na mume, mke wa kiongozi,

• Kiongozi wa Umma amejipatia kwa ghafla na kwa namna isiyoelezeka, utajiri mkubwa kulingana na vyanzo vinavyoonekana vya mapato yake.

Ni wajibu kwa viongozi wa Umma kuwa waadilifu, ili kuwawezesha wananchi kuwa na imani nao katika utendaji wao wa kazi kwa maslahi ya wananchi, na Taifa kwa ujumla. Kiongozi wa Umma aliyepewa majukumu ya kuwaongoza wanachi lazoma awe mwadilifu katika utendaji wa kazi zake. Ni jambo la muhimu sana, UADILIFU, kwa kiongozi wa Umma.

Hata hivyo Rais Kikwete katika usemi wake huo, aliutoa kwa kutambua dhahiri kuwa Maadili kwa viongozi wa Umma, ndio muhimili muhimu wa kuleta amani endelevu katika nchi yetu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba endapo viongozi wa Umma watatekeleza majukumu yao kwa ‘Kasi Mpya na Ari mpya’. Kwa uadilifu mkubwa hasa kwa kufikia viwango vya maadili vinavyotakiwa kama vile uaminifu, huruma, umakini, kujizuia tamaa ya mali, kutokuwa na upendeleo wakati wa kufanya maamuzi na kuridhia na kuzingatia viwango vya juu vya maadili kadri iwezekanavyo, itapelekea wananchi kuwa na imani na Serikali yao iliyopo madarakani pamoja na viongozi wao wanaowaongoza.

Kimsingi Neno ‘Maadili’ linahusu tabia na mwenendo mwema ,wa mtu katika

7

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Mhe George

Mkuchika amewataka wahitimu wa mafunzo ya uchunguzi na upelelezi ambao ni watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutumia ujuzi walioupata katika zoezi la uhakiki wa mali wanazozitamka viongozi kwa weledi, Uadilifu, na nidhamu katika kuwafichua viongozi wanaodanganya kuhusu mali wanazomiliki.Mheshimiwa Mkuchika alitoa kauli hiyo alipokuwa akifunga mafunzo ya Maafisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika chuo cha Maafisa wa polisi Kidatu mkoani Morogoro mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka 2012.

Waziri Mkuchika aliongeza kuwa kazi ya uchunguzi na upelelezi ni nyeti kwani ina manufaa ya pekee katika kuzuia vitendo vya ukiukwaji wa maadili hususani vitendo vya rushwa, ubadhirifu wa mali za umma, matumizi mabaya ya rasilimali za umma, unyanyasaji, ukiukwaji wa haki za binadamu, wizi, uzembe, ulevi, kutowajibika na mengine mengi ya aina hii. Na kwamba ili kazi hii iwe na manufaa lazima wachunguzi wawe waadilifu, weledi na wazalendo kwa nchi yao, na kazi hii isipofanyika vyema inaweza kuwa chanzo cha kupoteza taswira ya Taasisi kwa umma na kwa Taifa kwa ujumla.

Naye Kamisha wa Maadili Mhe. Jaji Mstafu Salome Kaganda katika hotuba yake alifafanua kwamba Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu kimeweza kufikia lengo la kuwapatia watumishi wa Sekretarieti mbinu za kisasa za uchunguzi ambazo zitawasaidia katika kuboresha utendaji wa kazi kwa kuwa moduli zilizofundishwa zina uhusiano wa moja kwa moja na majukumu yanayotekelezwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Mhe. Kaganda aliongeza kuwa lengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni kuendelea kuwapatia watumishi mafunzo endelevu ya uchunguzi katika ngazi ya juu zaidi, kutoka ngazi ya cheti hadi ngazi ya Stashahada.

Aidha, Mhe. Kaganda alitoa

ombi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Mhe. Mkuchika ambaye alikuwa mgeni rasmi kuiwezesha Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika upatikanaji wa majengo yeye hadhi inayolingana na ofisi ya Rais, kuanzia Makao Makuu na katika Ofisi za Kanda ili kuiwezesha ofisi kutekeleza majukumu yake ya msingi katika suala zima la kukuza Maadili ya Viongozi na kuiwezesha Taasisi kutunza vyema nyaraka muhimu za viongozi.Mafunzo hayo yaliwashirikisha watumishi 33 wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutoka Ofisi za Kanda ambazo ni Dodoma, Mwanza, Arusha, Mtwara, Mbeya, Tabora na Makao Makuu Dare-es-salaam.

8

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Mhe. George Mkuchika (katikati) akifunga Mafunzo ya Awali ya uchunguzi kwa Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma (hawapo pichani) waliohitimu mafunzo hayo yaliyofanyika chuo cha Maofisa wa Polisi Kidatu mkoani Morogoro, kulia kwake ni Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS UTAWALA BORA MH GEORGE MKUCHIKA AMEWATAKA WAHITIMU

KUFANYA KAZI ZAO KWA WELEDI NA UADILIFUNa Johanither Barongo

utendeji wa kazi zao za kila siku.

Ikumbukwe kwamba mwaka 1995 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilifanyiwa marekebisho kwa kuweka Ibara ya 132 ambayo pamoja na mambo mengine iliweka misingi ya maadili kwa Viongozi wa Umma na kuunda Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Uongozi ni dhamana na siyo mradi wa kiuchumi. Kiongozi yoyote wa kuchaguliwa, kuteuliwa, au wa kuajiriwa amekabidhiwa madaraka na watu kwa hiyo anatakiwa atumie wadhifa wake kwa manufaa ya watu wote na siyo kwa manufaa yake binafsi au kikundi cha watu.

Aidha, katika kifungu cha 12 cha Sheria ya Maadili, kiongozi wa umma haruhusiwi kufanya mambo ambayo ni kinyume na Sheria ya Maadili kama vile:

• Kutoa taarifa za kikazi ambazo hazitolewi kwa umma au kwa watu wasioruhusiwa.

• Kutoa upendeleo wa aina yoyote ile.• Kutumia mali ya Serikali kwa manufaa

binafsi ya kiuchumi.• Kupokea zawadi zozote zenye manufaa

makubwa ya kiuchumi. Inaruhusiwa tu kupokea zawadi ndogo au zenye thamani ndogo kama ukarimu wa kawaida au zawadi za kijadi. Zawadi au takrima zinaweza kutumiwa vibaya kwa kutolewa kama rushwa kwa nia ya kutaka fadhila au upendeleo.

Sheria ya Maadili imeweka kanuni za maadili ambazo kila kiongozi wa Umma anatakiwa kuzifuata. Sheria pia imeweka utaratibu wa kudhibiti maadili ya viongozi wakati wote wanapokuwa madarakani.

Uadilifu, tabia njema, uaminifu, kuheshimu haki za msingi za raia, nidhamu, uwazi, uwajibikaji na kuepuka mgongano wa maslahi. Kwa kuzingatia Sheria hii ya Maadili katika nchi yetu hatuna budi kuongozwa na viongozi wanaofuata sheria ya maadili ili kuleta ufanisi na kukuza uchumi wa nchi kwa kufuata misingi

ya Haki za Binadamu na Demokrasia ya kweli.

Ni matarajio ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa viongozi wake ni waadilifu na wako mstari wa

mbele katika kukemea vitendo visivyo vya uadilifu kama vile kutoa rushwa au kushawishi watumishi wa Umma kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa, kwa kukataa kutoa rushwa pamoja na kutoa taarifa sehemu inayohusika.

Ili Utumishi wa Umma uweze kuwa na maadili mema kinachotakiwa kwanza kabisa ni kuwa na viongozi waadilifu. Dhamira hii siyo kwa viongozi wa kisiasa kuanzia ngazi ya shina hadi uongozi wa Kitaifa, dhamira ya viongozi, hasa wanasiasa wanayo nafasi nzuri ya kuwahamasisha wanachi.

Aidha, viongozi wa Umma wakiwa na dhamira timilifu juu ya uadilifu, ni rahisi kwa wananchi kujifunza na kuiga maadili mema kutoka kwao kwa vile maneno na matendo yao yanatoa ujumbe mmoja tu, yaani wanawataka wananchi wawe waadilifu na wao wenyewe ni mfano mzuri wa uadilifu. Kutokana na kuwapo kwa dhamira hiyo basi ni rahisi kwa viongozi hao kusimamia Sheria ya Maadili na mikakati ya kukuza uadilifu kwa maslahi ya Taifa.

Hata hivyo ili Taifa liweze kuwa na viongozi waadilifu halina budi kuweka msisitizo wa maadili mashuleni kuanzia ngazi ya shule ya msingi mpaka vyuo vikuu, kwa kufundisha somo la “Maadili“ ili kusaidia kujenga jamii ya watu wenye maadili mema.

Makala hii ina lengo la kueleza mikakati ya sasa ya kukuza uadilifu kwa viongozi wa Umma na kwa wananchi wake. Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa” TAKUKURU” ni sehemu ya mikakati mipana ya Serikali ya kuhakikisha kuwa huduma kwa Umma zinatolewa kwa kufuata misingi imara ya Kimaadili.

Serikali pia inaamini kuwa vijana ni Taifa la kesho hivyo basi kuna sababu za msingi za kujenga maadili katika ngazi za shule, kwa njia hii itachangia kabisa kuwa na viongozi wa Taifa la kesho ambao wanafuata maadili katika

9

MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA NI NGUZO MUHIMU KATIKA KULETA

MAENDELEO NCHINI.Na Johanither Barongo

wenye umri wa kuanzia miaka 18 kuwa mali hizo ni zao wakati si sahihi waache tabia hiyo mara moja kwani kiongozi kukataa kutaja mali alizo nazo ni kukiuka Maadili .

Ni vema Viongozi wa Umma wakafuata maadili katika utendaji wao wa kazi ili kuwawezesha wananchi kuwa na imani nao, na pia kuwawezesha kufanya kazi zao vizuri na kwa ufanisi mzuri kwa maslahi ya Taifa na pia kwa wanachi wanaowaongoza.

Ikumbukwe kuwa Sheria ya Maadili ya mwaka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ilianza kazi rasmi mwezi wa Julai mwaka 1996.

Sekretarieti ilianzishwa ili kutekeleza Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Na. 13 ya mwaka 1995 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 5 ya mwaka 2001.

Msingi wa kudhibiti maadili ya Viongozi wa Umma unatokana na ibara ya 132 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa Ibara hiyo, Bunge limetakiwa kutunga Sheria ya Maadili kwa kuanisha misingi ifuatayo:-

• Kufafanua nafasi za madaraka ambazo watu wenye kushika nafasi hizo watahusika nayo.

• Kuwataka watu wanaoshika nafasi fulani za madaraka kutoa mara kwa mara maelezo rasmi ya mapato, rasilimali na madeni yao.

• Kupiga marufuku mienendo na tabia zinazopelekea kiongozi aonekane hana uaminifu, anapendelea au si muadilifu au anaelekea kukuza au kuchochea rushwa katika shughuli za umma au anahatarisha maslahi au ustawi wa jamii.

• Kufafanua adhabu zinazoweza kutolewa kwa kuvunja misingi ya maadili.

• Kuelekeza taratibu, madaraka na desturi zitakazofuatwa ili kuhakikisha utekelezaji wa maadili.

• Kuweka masharti mengine yoyote yanayofaa au ambayo ni ya muhimu kwa madhumuni ya kukuza na kudumisha uaminifu, uwazi, kutopendelea na uadilifu katika shughuli za umma na kwa ajili ya kulinda fedha na mali nyinginezo za umma.

Kwa kuzingatia msingi wa kudhibiti maadili ya viongozi wa umma, jukumu mojawapo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni:-Kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi yoyote wa umma.

Maadili ni nyenzo muhimu na nguzo kwa viongozi wa Umma katika kuleta ufanisi katika utendaji wa kazi zao kwa manufaa

ya wananchi na kwa taifa kwa ujumla.

Hakuna maendeleo yoyote katika nchi ambayo yanaweza kupatikana iwapo viongozi ambao ndio watendaji wa kazi watashindwa kufuata maadili ya kazi zao katika kutekeleza majukumu yao. Hivyo ni jukumu letu sote kama wananchi na viongozi wetu kukumbushana Maadili ya kazi zetu ili kuleta Amani, Usawa na Haki ya kidemokrasia nchini.

Utakumbuka katika hotuba aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika siku ya kilele cha wiki ya utumishi wa Umma iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam, alisema kuwa viongozi na watumishi wa Umma wanalo jukumu la kubadili mitazamo na tabia zao ili kupambana na mianya inayofanya rushwa na vitendo vya utovu wa maadili kushamiri mahali pa kazi.

Rushwa ni adui wa haki, hivyo viongozi wa Umma kwa kushirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mnapaswa kuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo vinavyokiuka maadili ya viongozi ikiwemo rushwa.

Aidha, Mheshimiwa Kikwete katika hotuba yake aliongeza kuwa hili ni lazima lifanyike kwa sababu vitendo hivi ndivyo vinavyozorotesha utendaji na kufanya huduma kuwa hafifu. Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 imeweka bayana mipaka ya viongozi katika kutumia madaraka yao ili kuondoa migongano kwao kama watumishi wa Umma na shughuli zao binafsi. Sheria hii ni muhimu izingatiwe na kila kiongozi wa wa umma ili utendaji serikalini ujali maslahi ya watanzania wote.

Katika ziara ya Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utawala bora Mheshimiwa George Mkuchika alipotembelea ofisi ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dar es salaam alisema kuwa kiongozi yoyote aliye madarakani hakatazwi kuwa na mali ili mradi tu mali hizo ziwe zimepatikana kihalali na zinatambulika kisheria . Alisema zoezi zima la kukagua mali za viongozi litakua la kudumu na Viongozi wa kukaguliwa wataongezeka kwa kadri hali itakavyoruhusu

Mheshimiwa Mkuchika alisema kuwa viongozi wanaotumia majina ya wake zao au watoto wao

10

VIONGOZI WAELIMISHWE KUHUSU

MAADILI YA KAZI ZAONa Johanither Barongo

11

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeendesha warsha iliyowakutanisha wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na Asasi za

Kiraia ikiwa ni sehemu ya mchakato wa Mabadiliko ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995.

Warsha hiyo iliyofanyika Oktoba, 2012 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam ilifunguliwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki (Mb). Akifungua Warsha hiyo, Mhe. Naibu Waziri alianza kwa kuipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa hatua ilizochukua ambazo ni pamoja na kukata kiu ya wananchi na kutekeleza dhamira ya dhati ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayotambua kwamba bila ya kuwa na viongozi na watumishi wa umma wenye maadili mema itasababisha usawa, haki na maendeleo katika taifa kuwa njozi.

Akielezea madhumuni ya Warsha hiyo, Mhe. Kairuki alisema kuwa ni sehemu ya mchakato muhimu sana katika Marekebisho ya Sheria ya Maadili na kwamba maoni watakayotoa wadau yatakuwa ni sehemu ya viambatisho muhimu vya Waraka wa Marekebisho ya Sheria utakaowasilishwa katika Baraza la Mawaziri na hatimaye kupelekwa Bungeni kwa ajili ya marekebisho, hivyo aliwaasa wajumbe kutoa maoni yao kwa uwazi kabisa.

Akitoa maoni yake kuhusu mada ambayo ingewasilishwa katika warsha hiyo, Mhe. Naibu Waziri alisema kuwa mada hiyo itakuwa ni msingi wa majadiliano yao na itawawezesha kutoa michango ambayo anaamini itawafikisha mahali ambapo wataweza kuwa na Sheria inayoendana na wakati.

Kuhusu utendaji kazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Naibu Waziri alionesha kuridhishwa na kusema kuwa tokea kuanzishwa kwake mwaka 1995, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imefanya kazi kubwa ya kusimamia maadili ya viongozi nchini ambapo mafanikio mengi yamepatikana katika kipindi hicho. Hata hivyo, pamoja na mafanikio mengi ambayo imeweza kuyapata katika kipindi hicho, Mhe. Naibu Waziri alisema kuwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imekabiliana na changamoto nyingi na kuwaasa wajumbe kutumia vizuri mchakato wa Marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuipa mamlaka na nguvu za kutosha Sekretarieti ya Maadili ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Akizungumzia umuhimu wa kupanua wigo wa Sheria,

Mhe. Kairuki alisema kuwa toka tupate uhuru mwaka 1961, Sheria za Maadili zimeweka mkazo kwa viongozi peke yao na kushauri kuwa katika mazingira ya sasa ipo haja ya kupanua wigo wa kuifanya Sheria hii iwamulike pia watumishi wa umma wasio viongozi. “Ni wazi kwamba wapo watumishi wa umma ambao wamejilimbikizia mali nyingi zisizolingana na vipato vyao. Wanatumia ofisi zao kujinufaisha isivyo halali, hivyo basi, ninatoa wito kwa wadau katika warsha hii kuangalia kama inawezekana kupanua wigo kujumuisha watumishi wote wa umma.” alifafanua Mhe. Naibu Waziri.

Kuhusu umuhimu wa somo la Maadili kwa watumishi, Mhe. Kairuki alisema kuwa ni vema wanapofanya mabadiliko ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma waangalie uwezekano wa kujumuisha somo la maadili kwa watumishi wa umma wanaoajiriwa serikalini. “ Hawa ndio viongozi wa kesho. Si vibaya kuanza kuwapika wawe watumishi wenye maadili mema toka mwanzo ili wanapopata nafasi za uongozi, kazi ya Sekretarieti inakuwa rahisi. Vile vile itakuwa vema kwa somo hilo likarejewa kila Afisa anapopandishwa cheo.” alisisitiza Mhe. Naibu Waziri.

Pia, Mhe. Naibu Waziri alizungumzia suala la kutenganisha Uongozi na Biashara ambapo alionesha kufurahishwa na Mchakato wa sasa wa Mabadiliko ya Sheria ya Maadili ya Viongozi kwa kutoa fursa ya kutekeleza dhamira ya Serikali ya kutengeneza utaratibu wa kutenganisha shughuli za biashara na shughuli za uongozi wa umma. Aidha, Mhe. Naibu Waziri aliirejea kauli ya Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, kuhusu nia ya Serikali ambayo ni kuwaondolea viongozi hatari ya kujikuta wana mgongano wa kimaslahi.

“Nchi nyingi duniani zenye mfumo wa uchumi huria kama tulivyo sisi, wanazo taratibu za namna hiyo. Ni sehemu ya hatua muhimu katika kujenga maadili mema ya uongozi wa umma. Ni matumaini yangu kwamba katika warsha hii, wadau mtapata fursa ya kujadili kwa kina namna bora ya kutimiza azma hii ya kutenganisha biashara na uongozi ili tuweze kupata mfumo bora utakaotumika bila kukinzana na mazingira ya sasa ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.” alimalizia kusema Mhe. Naibu Waziri.

Naye Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Salome Kaganda akifunga Warsha hiyo alianza kwa kuwashukuru Waandishi wa Habari kwa ushiriki wao kwani anaamini kuwa Vyombo vya Habari vitayafikisha malengo na

SEKRETARIETI YA MAADILI YAENDESHA WARSHA YA WADAU KUHUSU

MAREKEBISHO YA SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA.

na Ally Mataula

12

Ikumbukwe kuwa Mabadiliko ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995 kwa kiasi kikubwa yamechochewa na dhamira ya Serikali ya kujaribu kutengeneza utaratibu wa kutenganisha shughuli za biashara na shughuli za uongozi wa umma kama alivyowahi kuahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifunga mafunzo ya uchunguzi na upelelezi katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu, Morogoro mwezi Oktoba, 2011. Lengo la erikali kuweka utaratibu huo ni kuwaondolea viongozi wa umma hatari ya kujikuta wana mgongano wa kimaslahi wakati wanatekeleza majukumu yao.

Maeneo mengine ambayo yalifanyiwa marekebisho na kuongezwa katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika kusimamia utekelezaji wa Sheria hiyo ni pamoja na fungu la 4(1) kuhusu tafsiri ya maneno ambapo Sheria haitoi tafsiri ya neno mtoto wa kiongozi wa umma. Aidha, ilielezwa kuwa hali hii inaleta mkanganyiko kwa kiongozi kubainisha ni nani hasa mtoto wake kisheria maana tafsiri ya neno hili ni pana kwa mazingira, tafsiri ya sheria mbalimbali, hasa kwa familia za kiafrika hususan Tanzania.

Pia, Wajumbe walipata fursa ya kufanya marekebisho katika maeneo mengine ya Sheria ambayo ni Fungu la 6 kuhusu misingi ya maadili, Fungu la 6(j) kuhusu mienendo ya viongozi wa umma wastaafu, Fungu la 8 kuhusu adhabu kwa kukiuka maadili na Fungu la 9 kuhusu matakwa ya kiongozi kuwasilisha Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Kamishna wa Maadili.

matokeo ya Warsha hiyo kwa usahihi kwa umma wa watanzania ili uweze kushirikishwa vema na kupata uelewa.

Pia, Mhe. Kaganda alitumia fursa hiyo kutambua mchango wa wadau mbalimbali walioshirikiana na Sekretarieti ya Maadili katika kubainisha maeneo mbalimbali ya Sheria yenye mapungufu ambayo yanakwamisha utekelezaji wa majukumu ya Sekretarieti ya Maadili kwa ufanisi.

“Kama mlivyofahamishwa katika Hotuba ya Ufunguzi, warsha hii ni sehemu ya mchakato muhimu sana katika marekebisho ya Sheria. Maoni

yaliyotolewa leo ni idhini ya kuendelea na hatua nyingine ya Marekebisho ya Sheria ya Maadili na hatimaye kukamilisha mchakato wa Marekebisho ya Sheria hii”. aliendelea kufafanua Mhe. Kaganda.

Akielezea matokeo ya Marekebisho ya Sheria hiyo, Mhe. Kaganda alisema kuwa ni pamoja na kupata sheria halali ili kuimalisha uadilifu, uwajibikaji na uwazi katika utekelezaji wa majukumu ya Umma. Aidha, matokeo mengine ni kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka hususan migongano ya maslahi kati ya shughuli za Serikali na masilahi binafsi, kuiwezesha Sekretarieti ya Maadili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Mhe. Kaganda aliendelea kutaja matokeo mengine kuwa ni kuliwezesha Baraza la Maadili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na mwisho ni kulinda imani ya wananchi juu ya uadilifu wa Viongozi wa Umma na Serikali kwa ujumla.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah J. Kairuki, akiwa na Viongozi mbalimbali pamoja na Wadau, mara baada ya Ufunguzi wa Warsha ya Wadau kuhusu Marekebisho

ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995, iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, mwezi Oktoba 2012.

13

MAADILI NI MSINGI WA UTAWALA BORA NCHINI.na Ally Mataula

kuguswa na matatizo ya wananchi.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jaji Mstaafu Stephen Ihema, utafiti alioupa kichwa cha habari, “Ethics Management as an Important Aspect of Democratic Development and Public Administration: A Case Study of Tanzania” aliouwasilisha katika Mkutano wa Mwaka kuhusu Maadili katika Maendeleo ya Demokrasia, ulioandaliwa na taasisi ijulikanayo kama The Institute of Public Administration of Canada (IPAC) alinukuu kutoka kwa Mwanafalsafa wa zamani Plato ambaye alijaribu kuzitaja sifa za kiongozi bora wa umma aliyekuwa akimfikiria yeye kuwa ni kwanza kiongozi wa umma lazima awe mwingi wa busara na hekima. Jaji Ihema aliendelea kumnukuu Plato kuwa viongozi wa umma ni walezi wa taifa na lazima wawe wameelimika vya kutosha pamoja na kuwa na kalba ya uadilifu wa hali ya juu. Pia viongozi wa umma wanaoelezwa na Plato ni lazima wawe tayari kujitoa mhanga katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaendeleo katika nchi.

Kwa msingi huo basi, Jaji Ihema kupitia Kamati ya Nolan ya mwaka 1995 ambayo ilitaja Kanuni Saba zinazotakiwa kuzingatiwa na kiongozi wa umma kuwa ni pamoja na awe huru katika kufanya maamuzi, mtenda haki, muwajibikaji, muwazi, muaminifu na uongozi. Kanuni hizo ndizo zinazochukuliwa kuwa ni msingi katika kanuni zinazohusu maadili katika uongozi wa umma.Umuhimu wa maadili katika maendeleo ya nchi unatokana na ukweli kwamba maadili ni suala mtambuka, kwa maana kwamba inagusa katika kila sekta za kimaendeleo kwa mfano kilimo, afya, ujenzi, elimu, maliasili n.k. Sekta zote hizi zinahitaji uadilifu wa hali ya juu wa viongozi na watumishi wa umma waliopewa dhamana ya kuongoza.

Mathalani, sekta ya afya isipokuwa na viongozi na watumishi waadilifu itapelekea wananchi kukosa huduma bora za afya hali itakayochangia kuzorotesha afya zao pamoja na kutokea vifo vinavyoweza kuzuilika, hivyo basi taifa litakosa nguvu kazi katika mchakato wa kujiletea maendeleo, hivyo hivyo na kwa sekta nyingine zote.

Kwa kuzingatia ukweli huo basi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika suala zima la kusimamia na kuendeleza dhana nzima ya Utawala Bora kwa kuweka mkazo zaidi kujenga misingi ya maadili kwa viongozi na watumishi wa umma.

Ujenzi wa Misingi ya Maadili nchini ulianza tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo kwa mujibu wa maelezo yake kupitia hotuba zake mbalimbali ni kwamba baada ya nchi yetu kupata uhuru mwaka 1961 muda mfupi tu baadae pengo kati ya wenye nacho na wasionacho

Kimsingi ni vigumu kutoa maana ya moja kwa moja ya neno Maadili. Kuna baadhi ya wanataaluma wanatafsiri neno Maadili kama mienendo mema

iliyokubaliwa na jamii fulani kuwa sehemu ya maisha yao. Kwa mfano kuna maadili ya jamii ya waandishi habari, maadili ya jamii ya wanasheria, maadili ya jamii ya madaktari na hata maadili ya makabila mbalimbali kwa mfano Wahehe, Wamasai, Wanyamwezi nk.

Lakini maana hiyo inaleta maswali hapo kuwa hivi ni kweli kuwa kikundi cha jamii fulani inatosha kuamua upi ni mwenendo mwema na upi sio mwendo mwema? Je vipi jamii hiyo ikikubaliana kuwa tohara kwa wanawake iwe ni sehemu ya maisha yao? Au mauaji ya wanawake wazee iwe pia ni sehemu ya maisha yao, jamii hiyo itakuwa inafuata maadili kweli?

Labda tuseme maana ya Maadili isitokane na kile kinachokubaliwa na kikundi cha jamii fulani kuwa ni sehemu ya maisha yao, lakini itokane na kile mtu binafsi anachokijua kutoka moyoni kwake kuwa ni sahihi. Hata hivyo, bado swali lingine litaibuka tena hapo, je itakuwaje mtu huyo akijua kutoka moyoni kuwa ubadhirifu wa mali za umma, ufisadi, rushwa, upendeleo na ubaguzi wa aina yeyote ile kuwa ni halali, mtu huyo atakuwa anafuata maadili?

Kwa kuzingatia msingi wa maelezo hayo ya awali hapo juu, ni wazi kuwa neno maadili lina maana pana zaidi kwani kila mtu au kikundi cha watu wanaweza kuwa na maana zao. Kwa kuwa kila mtu au kikundi cha watu wanaweza kutoa maana ya maadili kwa makubaliano yao basi maana hizo zisiishie kuwa ni mienendo mema waliyokubaliana kuwa ni sehemu ya maisha yao tu lakini pia mienendo hiyo lazima ikidhi viwango vya kitaifa na kimataifa vinavyozingatia usawa, haki za binadamu, amani na utulivu wa jamii hiyo na taifa kwa jumla.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995 neno Maadili maana yake ni Maadili ya viongozi wa umma yaliyowekwa na, au kwa mujibu wa Sheria hiyo. Mathalani, Sheria hiyo imeweka misingi ya maadili yanayotakiwa kuzingatiwa na viongozi wote wa umma walioorodheshwa katika Sheria hiyo kama kufanya kazi kwa uadilifu, kutoa tamko la Mali na Madeni, kufanya maamuzi kwa kufuata Sheria na Kanuni, kuepuka mgongano wa maslahi, matumizi sahihi ya taarifa na kuepuka rushwa na matumizi mabaya ya Madaraka.

Kimsingi ili jamii yoyote iweze kuendelea kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni, maadili ni chachu katika kufanikisha hilo kufikiwa, hususani uwepo wa safu ya viongozi wanaozingatia maadili na kusimamia vema rasilimali za nchi kwa kizingatia vigezo vya utawala bora ambavyo ni uwazi, uwajibikaji, usawa pamoja na

14

Utawala Bora ni nguzo ya tatu katika Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania ambao pamoja na Mkakati wa Taifa wa Kupambana na Rushwa (NACSAP II) vinalenga katika kuongeza uwazi, uwajibikaji, uadilifu na ufanisi katika kutoa huduma kwa umma katika ngazi zote za sekta za umma katika Serikali Kuu pamoja na Serikali za Mitaa.

Katika kutilia mkazo suala la Maadili katika uongozi wa nchi, serikali imeanzisha Kamati za Maadili katika kila Wizara, Idara na Wakala za Serikali ili ziweze kuhakikisha kuwa maadili katika sehemu zao za kazi yanazingatiwa kikamilifu. Lengo ni kuhakikisha kuwa Utawala Bora unaimarika katika sekta ya utumishi wa umma hivyo kuharakisha kasi ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Hivyo kufanikiwa kwa mipango yote hiyo ya taifa itategemea kuwepo na kuimarika kwa Utawala Bora na ili Utawala Bora uweze kuwepo ni lazima wale walioshika dhamana ya uongozi katika nchi wafuate na kuzingatia misingi ya maadili iliyowekwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni wanapotimiza majukumu yao ya kila siku.

Lakini uwepo wa Sheria pekee zinazosimamia mienendo na tabia za viongozi na watumishi wa umma hazitoweza kuzaa matunda ikiwa viongozi na watumishi wenyewe hawatabadilika wao wenyewe. Umefika wakati kwa Viongozi na Watumishi wa Umma kuwa na wito kutoka katika mioyo yao pamoja na misingi ya imani za dini zao ambazo kimsingi zinahimiza waumini wao kuwa waadilifu katika kila wanalolifanya katika maisha yao hapa duniani

Ni wajibu pia wa kila kiongozi na mtumishi wa umma kuwa na moyo wa kizalendo kwa nchi yake kwa kutumia nafasi zao katika utumishi wa umma kwa uadilifu mkubwa ili waweze kuitoa nchi mahali ilipo ili iweze kupiga hatua zaidi kimaendeleo kwa maslahi na ustawi wa nchi yetu na wananchi wote.

Pia, viongozi na watumishi wa umma wanapaswa kuguswa na umaskini wa kundi kubwa la wananchi unaosababishwa aidha kwa uzembe, ubinafsi, tamaa, kukosa uadilifu au kukosa uzalendo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa umma wakati wanapofanya maamuzi hususani maamuzi yanayogusa maisha ya kila siku ya wananchi hao. Serikali kwa upande wake imekuwa ikijitahidi kubuni mipango mbalimbali yenye nia ya kuwaletea maendeleo wananchi wake, lakini mipango hiyo haitaweza kuzaa matunda bila viongozi pamoja na watumishi wa umma kuwa waadilifu.

Mwisho viongozi na watumishi wa umma wanatakiwa kutokuwa wasaliti wa wananchi wa Tanzania katika vita vilivyotangazwa na serikali ya awamu ya kwanza mara baada ya kupata uhuru dhidi ya maadui watatu ambao ni Maradhi, Umaskini na Ujinga. Pia, viongozi na watumishi wa umma wanatakiwa kuzingatia kikamilifu dhamira ya dhati kabisa ya serikali ya awamu ya nne ya kuwaletea maisha bora wananchi wa Tanzania. Hayo yote yatawezekana ikiwa tu viongozi na watumishi wa umma watazingatia kikamilifu misingi ya maadili iliyowekwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazowaongoza.

likaanza kutokea.

Kwa mujibu wa Mwalimu Nyerere ilibainika kuwa kundi kubwa la wenye nacho lilikuwa ni viongozi wa chama na serikali ambao kabla ya uhuru walikuwa maskini wa kutupwa, hivyo kwa kutumia nyadhifa zao katika chama na serikali walianza kujitajirisha wenyewe. Mwalimu Nyerere aliendelea kubainisha kuwa aina hiyo ya maendeleo ilikuwa ni kinyume kabisa na dhana ya uongozi kutoka kwa wananchi.

Kutokana na hali hiyo, ilionekana kuna haja ya kuweka wazi lengo la taifa kwa wakati huo ambalo lilikuwa ni maendeleo kwa wote na sio kikundi kidogo cha watu kunufaika na maendeleo ya nchi. Kwa mujibu wa Mwalimu Nyerere, ili lengo hilo la taifa liweze kufanikiwa walitunga Sheria ya Maadili iliyowadhibiti viongozi wa umma waliokuwa wakitumia vibaya nyadhifa zao kwa maslahi yao binafsi na serikali ilisimamia kikamilifu sheria hiyo ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.

Januari 29, 1967 lilipitishwa Azimio la Arusha ambalo maudhui yake yalijikita zaidi katika dhana ya Ujamaa kuwa ni Dira ya mipango ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Aidha, kwa kiasi kikubwa Azimio la Arusha lilizidi kutoa msukomo katika kuwadhibiti baadhi ya viongozi wa umma waliokuwa wabadhilifu kwani moja kati ya misingi yake, Maadili ya Viongozi wa Chama na Serikali yalizingatiwa lengo likiwa ni kujaribu kuleta usawa miongoni mwa wananchi wa Tanzania.

Hata hivyo kutokana na mabadiliko mbalimbali ya uendeshaji wa mifumo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yaliyotokea duniani mwanzoni mwa miaka ya 1980 mpaka 1990, Tanzania haikuweza kuwekwa kando katika mabadiliko hayo, bali nayo ilijikuta ikilazimika kufanya mabadiliko makubwa katika mifumo yake mbalimbali ya uendeshaji wa nchi ikiwemi uanzishwaji wa Sheria mpya ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 ambayo itakuwa inakidhi matakwa ya mabadiliko hayo. Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inasimamiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyoanzishwa kwa mujibu wa ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995 imeweka misingi ya Maadili ambayo inatakiwa kufuatwa na Viongozi wa Umma. Sheria hiyo pia inatoa muongozo kwa viongozi wa umma wa kufanya maamuzi kwa kuzingatia maadili ili kuhakikisha kunakuwa na maamuzi yenye kuleta tija katika usimamizi wa rasilimali za nchi kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi pamoja na kuimarisha hali ya maisha na ustawi wa jamii. Pia, uimarishaji wa hali ya maisha na ustawi wa jamii itaongeza uadilifu na uaminifu wa serikali kwa wananchi na Jumuia ya Kimataifa.

Kwa msingi huo basi, ikiwa misingi ya maadili iliyotajwa na Sheria hii itazingatiwa kikamilifu na viongozi wote wa umma waliotajwa pamoja na watumishi wa umma kwa jumla ni wazi kuwa Utawala Bora utaimarika katika nchi yetu. Aidha, kuimarika kwa Utawala Bora nchini itapelekea hata mipango mingine ya maendeleo kama MKUKUTA, Malengo ya Milenia pamoja na Dira ya Taifa ya 2025 kufikiwa kwa ufanisi mkubwa.

15

kuwa taasisi hizo kwa sasa hazitekelezi wajibu wake ipasavyo na badala yake kila mmoja anamtupia lawama mwenzake kitu ambacho sio sahihi alisisitiza Bw. Nzunda.

Bw. Nzunda alienda mbali zaidi kwa kuuponda mfumo wa maleza wa jamii kwa sasa kwa kuwategemea mayaya kulea watoto wao na wazazi kukimbia jukumu hilo kitu ambacho kinawajengea msingi mbaya kitabia watoto wetu ambao ndio wanaotegemewa kuwa viongozi wa nchi yetu siku za usoni.

Kuhusu Viongozi wa Umma kufanya biashara na shughuli nyingine za kujiongezea kipato, Bw. Nzunda alisema kuwa kimsingi sio vibaya kwa viongozi kufanya hivyo ila kinachokatazwa na Sheria ni viongozi kufanya biashara na Serikali hali ambayo inaweza kupelekea mgongano wa maslahi.

Akijibu swali kuhusu kuendelea au kutokuendelea kwa Azimio la Arusha pamoja na uwepo wa Azimio la Zanzibar Bw. Nzunda alisema kuwa kimsingi hakuna Sheria yeyote iliyolifuta Azimio la

Arusha na kwa maana hiyo bado lipo.

Aidha, Bw. Nzunda aliendelea kubainisha kuwa ujio wa Azimio la Zanzibar la mwaka 1991 lilitokana na msukumo kutoka nje na Asasi za kiraia uliosababisha hata ile misingi mizuri ya maadili iliyowekwa kwenye Azimio la Arusha kuachwa hali iliyopelekea kuwepo kwa mmonyoko mkubwa wa maadili nchini kati ya mwaka 1991 hadi 1995.

Hata hivyo Bw. Nzunda alisema kuwa Azimio la Arusha halijafutwa kwa mujibu wa Sheria, kinachotakiwa kufanywa kwa sasa ni kulihuishwa ili liendane na mazingira ya sasa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma Bibi Claudia Mpangala aliwasihi Watumishi Viongozi wa Tume hiyo kusimamia misingi ya Utawala Bora ambayo ni pamoja na kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu wanapotekeleza majukumu yao kwani kwa kufanya hivyo kutaondoa malalamiko kutoka kwa wadau wa nje na ndani ya Tume hiyo.

Jamii imetakiwa kuacha kukwepa jukumu lake la

msingi la kujenga misingi imara ya maadili ambayo itapelekea kupatikana viongozi waadilifu katika ngazi zote za uongozi katika nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu – Viongozi wa Utumishi wa Umma wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Tixon Nzunda wakati akizungumza na Viongozi Waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma katika muendelezo wa utoaji wa elimu kuhusu Sheria ya Maadili kwa Viongozi wa Umma katika Wizara, Idara na Wakala wa Serikali iliyofanyika tarehe 25 Oktoba, 2012.Bw. Nzunda alibainisha kuwa kitaalamu Maadili hujengwa na taasisi nne ambazo ni Familia, Taasisi za Elimu (Shule na Vyuo), Taasisi zilizoundwa kusimamia Maadili na ngazi ya Taifa.

Hata hivyo, pamoja na uwepo wa ngazi hizo nne ambazo kimsingi ndizo zenye wajibu mkubwa wa kuijenga jamii kimaadili Bw. Nzunda alisema

NZUNDA: JAMII ILIYOOZA KIMAADILI HUZAA VIONGOZI WASIO WAADILIFU

na Ally Mataula

NZUNDA: JUKUMU LA KUJENGA MISINGI YA MAADILI NI LA WOTE”

Awali akiwasilisha mada kwa viongozi hao, Katibu Msaidizi – Viongozi wa Umma Bibi Zahara Guga alisema kuwa lengo la mada hiyo ni kuwashirikisha Viongozi wa Taasisi za umma kuelewa vyema misingi ya maadili ya utumishi wa umma, kujenga misingi imara ya kiutendaji ili kuimarisha utoaji huduma na kukuza uelewa juu ya athari za kukosa uadilifu miongoni mwa Watumishi wa Umma.

Akielezea chumbuko la Maadili katika Utumishi wa Umma nchini, Bibi. Guga alisema lilianza tangu enzi ya Chama cha TANU ambacho kiliainisha ahadi za Chama ambazo kila mwanachama alilazimika kukiri na kuzitamka mbele ya viongozi wa TANU.

Akitaja ahadi hizo, Bibi Guga alisema kuwa ni pamoja na Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja, nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote, nitajitolea nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma, rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa na cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

Ahadi nyingine ni pamoja na “nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote, nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu, nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko na nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanzania na Afrika.

Bibi Guga alifafanua kuwa ahadi hizo ambazo ni misingi ya Azimio la Arusha pamoja na miiko yake ya uongozi ndio msingi au chimbuko la Maadili ya Taifa kama ilivyoasisiwa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akielezea mifumo ya kisheria ya kudhibiti Maadili ya Viongozi kabla ya mwaka 1995 ambapo ilianzishwa Sheria ya Maadili, Bibi Guga alisema kuwa kabla na baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 kumekuwa na mifumo mbalimbali ya kisheria. Aidha, Bibi Guga aliitaja mifumo hiyo ni pamoja na Kanuni za Utumishi wa Umma, Azimio la Arusha, 1967, Waraka wa Watumishi wa Serikali Na. 2 wa 1967, Sheria ya Kamati ya Utekelezaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi, Na. 6 ya 1973 na Azimio la Zanzibar, 1991.

Imeelezwa kuwa jukumu la kujenga misingi ya Maadili nchini si la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma pekee bali ni la jamii

nzima.

Hayo yamesemwa na Katibu – Viongozi wa Utumishi wa Umma wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Tixon Nzunda wakati akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa Viongozi waandamizi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika semina iliyokuwa na lengo la kutoa elimu kwa viongozi hao kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba, 2012.

Aidha, Bw. Nzunda alibainisha kuwa saula la kujenga maadili ni jukumu la kila mmoja wetu hivyo jamii inapaswa kuwa sehemu ya kutafuta suluhisho.

Pia, Bw. Nzunda alifafanua kuwa mabadiliko ya kweli yanaanza na mtu mwenyewe ikifuatiwa na jamii nzima na katika kutilia mkazo hilo Bw. Nzunda alimnukuu Mwanamapinduzi wa India Mahatma Gandhi aliyewahi kusema kuwa ikiwa kila mmoja atadhamiria kubadilika basi dunia nzima itabadilika.

Kuhusu tatiza la mmomonyoko wa Maadili nchini, Bw. Nzunda alisema suala hilo linahitaji dhamira ya dhati kuanzia ngazi ya familia hadi taifa na kwamba ili kukabiliana na tatizo la rushwa na vitendo vingine vinavyoashiria mmomonyoko wa maadili inahitaji kujitoa muhanga na kuzingatia uzalendo.

Vile vile katika kukabiliana na tatizo la mmomonyoko wa Maadili nchini, Bw. Nzunda alisema Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imefanya majadiliano na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu umuhimu wa kuingiza somo la Maadili katika mitaala ya elimu katika ngazi zote za elimu ili kuwajengea vijana msingi mzuri wa maadili.

Bw. Nzunda aliwaeleza Viongozi hao kuwa kwa sasa somo la Maadili limeanza kufundishwa katika shule za msingi na vyuo na jitihada zinafanyika ili somo la maadili liweze kufundishwa katika shule za sekondari.

16

..... na Ally Mataula.

17

MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA YANAYOHUSISHA UNYANYASAJI WA KIJINSIA (SEXTORTION”) NI TATIZO LA

MMOMONYOKO WA MAADILI NCHINI

Tendo hilo la rushwa lina sifa nyingi, nizitaje kwa uchache tatu tu ambazo ndio muhimu kama ifuatavyo”

Sifa ya kwanza ni kutumia madaraka vibaya.Madaraka haya yanaweza kuwa ya kijadi, kidini, kisheria, kikazi au kimaadili. Kwa mfano Kiongozi (“Boss”) na katibu muhtasi wake. Kitu cha kuzingatia hapa ni kwamba hayo madaraka lazima yawe ni yale ambayo yanamfanya huyo anayedai rushwa kuweza kutoa au kuzuia hicho kinachoombwa. Pia ni lazima yawe ni madaraka ambayo uvunjwaji wake unaweza kutambulika. Mfano walimu ambao kazi yao ni kufundisha na kuwalea wanafunzi, waajiri wa ajira mbalimbali, madaktari ambao kazi yao ni kutibu wagonjwa, viongozi wa dini mbalimbali, na mfano mzuri zaidi wa kufafanua sifa hii kwa ufasaha zaidi ni mtumishi wa umma ambaye kisheria amepewa madaraka(mamlaka) kama vile Afisa Uhamiaji aliyepewa madaraka ya kutoa Pasi za kusafiria kwenda nchi nyigine, au hata pale ambapo madaraka hayakubainishwa bayana lakini yanaelekeza kulingana na kazi ambayo mhusika anaifanya, mtu huyo atachukuliwa kuwa anayo madaraka. Katika kumpandisha cheo Mwajiri anapaswa kuangalia/kupima utendaji kazi wa mwajiriwa na si kudai rushwa ya ngono. Mwalimu pia hasa vyuoni

anapaswa kutoa alama stahiki kwa mwanafuzi baada ya kumpa mtihani na si kumpa alama za upendeleo hata kama uwezo hana, au kumnyima alama halali pale ambapo mwanafunzi anakataa kujitoa kingono. Utaratibu wa kupanga vituo vya kazi kwa waajiriwa wapya pia unapaswa kuzingatia Sera ya kazi na ajira na siyo rushwa ya ngono.

Sifa ya pili ya rushwa ni aina ya rushwa inayotumika katika ubadilishaji (“quid pro quo”) ikimaanisha ubadilishanaji wa “kitu kwa kitu.” Madaraka yanatumiwa kumnyanyasa mlengwa kijinsia ili aweze kupata hitaji lake. Kwa maneno mengine ni ngono kwa hitaji. Pale mlengwa anapokataa kujitoa kingono hapati hilo hitaji lake. Kama ilivyo atika kesi nyingine za unyanyasaji wa kijinsia, “sextortion” kama ilivyo fafanuliwa hapo mwanzo inahusu vitendo vingi na/ama vya moja kwa moja au vya kuyaangalia mazingira ambayo vitendo hivyo vimetendeka. Vyovyote iwavyo, kitu cha msingi cha kuangalia hapa ni yale mabadilishano ya ngono ili mlengwa aweze kunufaika na kile ambacho huyo mwenye madaraka anaweza kutoa au kukataa kukitoa pale ngono isipotolewa. Kwa maana hiyo basi, mwenye madaraka hawezi kutoa utetezi kwa mlengwa kuwa alichokuwa

“SEXTORTION” ni neno geni ambalo hakuna Kamusi ambayo imetoa maana yake.

Ni neno na/ama msemo ambao haujazoeleka sana. Hivyo basi tunaweza kusema kuwa neno “SEXTORTION” ni msemo mpya unaotumika kuelezea tabia ambayo imejengeka kwenye jamii ambayo ni ya unyanyasaji wa kijinsia unaoambatana na rushwa ya ngono. Lakini tendo la unyanyasaji wa kijinsia linalohusika katika tabia hii siyo lazima liwe kitendo cha ngono moja kwa moja; kwani linaweza kujumuisha pia kulazimisha mahusiano ya kimapenzi au upendeleo wa kimapenzi, vitendo vya kunajisi, kubaka na/au kuonesha sehemu za siri za mwili. Matendo mengine ni pamoja na kugusana, kufinyana, kusuguana, kupapasa sehemu za siri, kupiga picha za uchi au za ngono na vitendo vingine vinavyoendana na tabia kama hiyo. Kwa ujumla “Sextortion” hujumuisha tendo au tabia inayohusika na ngono au kupelekea kufanyika kwa ngono.

Kuhusu kigezo cha rushwa, mhusika wa kitendo cha kudai rushwa ya ngono lazima awe na madaraka makubwa ambayo anayatumia vibaya kwa kudai rushwa ya ngono na/au kukubali rushwa ya ngono katika kutumia madaraka hayo ili kufanikisha mahitaji yake. Hivyo ngono ndiyo hutumika kama rushwa na si fedha.

na Edson Peter Kamugisha

hoja nyingi nzuri, nanukuu tu kwa uchache:

“Matukio ya uzinzi yameongezeka kwa kasi kutokana na nyumba za kulala wageni kuachwa zitumike kama madanguro. Katika baadhi ya nchi, mke na mume hawawezi kuruhusiwa kukodi chumba kimoja bila kuonesha cheti cha ndoa au uthibitisho wowote wa kisheria. Hapa kwetu hali ni kinyume kabisa.”

Anachosema mhariri kikowazi kwani watu wengi wanaotumia madaraka yao vibaya ili kujipatia manufaa ya kingono toka kwa wasio na madaraka wanaokuwa na hitaji maalum toka kwao mwisho wake upelekwa katika nyumba za kulala wageni ili kutimiza haja za hao wenye madaraka. Hili ni tatizo la jamii nzima ambalo halinabudi kukemewa kwa nguvu zote na kila Mtanzania popote alipo. Kwa kufanya hivyo tutakuwa na jamii yenye Maadili mema. Tukumbuke kuwa viongozi wanatokana na jamii, na kama jamii hiyo itakuwa imeharibika Kimaadili, ni ukweli usiopingika kuwa hata viongozi wa Taifa letu watakuwa ni matokeo ya zao hilohilo la jamii isiyokuwa na Maadili.

18

kwenye koo la mlengwa tayari kumchinja endapo atakataa kutoa ngono anayodaiwa. Mfano endapo Ofisa wa Magereza atamdai mke wa mtuhumiwa aliyepo gerezani ngono ili aweze kumpelekea mtuhumiwa huyo dawa ambazo mke wake amempelekea, ofisa huyo atakuwa ametenda kosa la “Sextortion.”

Tujiulize, ni nini Chanzo cha “SEXTORTION”?

Kwa mtazamo wa makala hii, chanzo cha “extortion” ni kushuka/kumomonyoka kwa Maadili nchini kuanzia kwenye familia mpaka ngazi za juu za Taifa. Kuna watu ambao kwao kutumia madaraka yao kujipatia manufaa ya kingono toka kwa wasiokuwa na madaraka wanaona ni kitu cha kawaida sana, vivyohivyo kuna wale ambao wanaona ni kawaida kwao kutoa ngono ili kupata upendeleo wanaoutaka toka kwa wale wenye madaraka ili hali wakisahau kuwa kufanya hivyo ni kuendelea kumomonyoa Maadili nchini. Mhariri wa Gazeti la Mtanzania, Jumatano Mei 11, 2011 alitoa maoni yake katika Makala yenye Kichwa cha habari: “Jamii isiyo na Maadili huzaa viongozi wasio na Maadili” Mhariri huyo alitoa

anadai ni kwa ajili ya kumnufaisha mtu mwingine.

Sifa ya tatu ni unyanyasaji unaoumiza kwa ndani ambao si lazima kutumia nguvu (“physical force”).

“Sextortion” inategemea zaidi yale madaraka ya kuhimiza kwa kung’ang’ania kuliko yale ya kutumia nguvu au pesa ili kupata ngono. Kutumia madaraka vibaya kunahusika zaidi pale ambapo mwenye madaraka na mlengwa hawapo katika ngazi moja. Anayedai ngono anakuwa na madaraka lakini anayedaiwa ngono anakuwa hana madaraka. Kuna “in balance of power” kati ya mwenye madaraka na mlengwa. Kwakuwa huwa hakuna uwiano wa mamlaka kati ya mwenye madaraka na mlengwa, mwenye madaraka anakuwa katika nafasi ya kudai ngono kwa kung’anga’ania na mlengwa asiye na madaraka anajikuta yuko katika hali ya kukubali kutoa ngono ili aweze kupata hitaji lake. Mwenye madaraka anamshinda mlengwa (mtoa ngono) bila kutumia nguvu “physical force.” Kwa hiyo nguvu ya kudai kwa kung’ang’ania aliyonayo mwenye madaraka ni kama kisu kikali kinachoshikiwa

KUNA VITENDO MBALIMBALI VINAVYOTOFAUTISHA “SEXTORTION” NA MAKOSA YA KAWAIDA YA UNYANYASAJI

WA KIJINSIA.

Kama ilivyoelezwa hapo mwanzo, siyo matendo yote ya unyanyasaji wa kijinsia

au ya kijinai yanahesabika kuwa ni kosa la “sextortion”. Mifano ifuatayo inafafanua zaidi vitendo ambavyo vinahusu unyanyasaji wa kijinsia lakini siyo “sextortion.”

1. Jambazi anayejitokeza shambani au msituni

na silaha na kumvamia mwanamke anayelima au kuchanja kuni na kumbaka atakuwa ametenda kosa la kubaka na siyo “sextortion.”

2. Kubandika picha za uchi katika mazingira mbalimbali kama vile ya kazi ni unyanyasaji wa kijinsia na siyo “sextortion.”

3. Mwanaume anaye mpiga mke wake nakumuumiza sehemu yoyote ya mwili wake kutokana na mwanamke huyo kukataa tendo la ngono atakuwa ametenda kosa la ukatili wa nyumbani (“domestic violence”) na siyo “sextortion.”

4. Mtumishi wa Umma

19

(mwanaume) ambaye anajifanya kuwa ni ofisa wa ngazi za juu Serikalini na kumdanganya mwanamke kuwa atamsaidia kupata nyumba ya Serikali endapo atafanya naye ngono, anaweza kuwa na kosa la udanganyifu au la kurubuni lakini siyo “sextortion” kwakuwa mtumishi huyu hana madaraka ya kumpatia nyumba hiyo.

5. Mwanamke anayejitoa kingono kwa mtalii toka nje ya nchi ili apate fedha, anaweza kuwa anajiingiza katika kosa la umalaya lakini siyo “sextortion” kwasababu huyo mgeni hana madaraka ya kuweza kufanya lolote dhidi ya huyo mwanamke.

Mifano yote hii hapo juu inaonesha kuwa mhusika wa tendo la unyanyasaji hana madaraka ya kumpatia mlengwa hitaji lake, na wala fedha haikutumika kama hongo.

Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa kinachotofautisha “sextortion” na matendo mengine ya unyanyasaji wa kijinsia ni kwamba “sextortion” inajumuisha kitendo cha unyanyasaji wa kijinsia kwa kudai ngono na kutumia madaraka vibaya ili kumpatia mlengwa(anayetoa ngono) hitaji lake.

Tujiulize, je kuna Sheria yoyote ambayo inashughulikia kosa la “sextortion”?Jibu la swali hili ni ndiyo, kwani, kuna Sheria chache zinazogusia suala la “sextortion” kutegemeana na jinsi madaraka yalivyotumika vibaya. Mfano Kanuni ya Adhabu (Penal Code) Sura ya 16 pamoja na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.

Jamii ya Watanzania pia inapaswa kujua kuwa mashauri yanayohusiana na “sextortion” yanaweza kufikishwa na/ama kushughulikiwa na Mahakama

zetu chini ya Kifungu cha 130(3) cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 kamavile , kubaka, unyanyasaji wa kijinsia na matendo mengine ya kuvunja heshima au kutoulinda utu. Pia vitendo vya “sextortion” vinaweza kufikishwa Mahakamani chini ya Kifungu cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007. Kifungu hicho kinafanya kosa la “sextortion” kuwa kosa la rushwa. Kifungu hicho kinasema katika lugha ya Kiingereza kuwa,

na nukuu:

“ Any person being in a position of power or

authority, who, in exercise of his authority, demands or imposes sexual favours or any other favour on any person as a condition for giving employment, a promotion or a right, privilege or any other preferential treatment commits an offence and shall be liable on conviction to a fine of not less than 1million shillings but not more than 5 million shillings or to imprisonment for a term of not less than three years but not more than five years, or to both.”

Kifungu cha 25 kama kilivyonukuliwa hapo juu kilitumika katika Kesi ya Jamhuri Vs Michael Ngilangwa, Kesi Na.7 ya mwaka 2010 katika Mahakama ya hakimu Mkazi Iringa, ambapo mshitakiwa (mchungaji wa Kanisa la Kilutheri Iringa alishitakiwa chini ya Kifungu hiki kwa kudai ngono toka kwa mlalamikaji ambaye alikuwa mwanafunzi wake wa Kidato cha kwanza katika somo la Dini na Kiingereza.

Vipo vitendo vingi vya “sextortion” vinavyofanyika katika ofisi mbalimbali, shuleni, hospitalini, kwa waganga wa jadi na viongozi wa dini lakini waathirika wa vitendo hivyo hawatoi taarifa kwenye

mamlaka husika au vyombo vya sheiria nchini na hivyo kufanya taarifa sahihi za ukubwa wa vitendo hivyo kutopatikana kwa urahisi. Kutokana na hali hiyo vitendo hivyo vimepewa jina la “SEXTORTION”. Ni maoni ya Makala hii pamoja na wadau wengine hasa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) kuwa vitendo vya matumizi mabaya ya madaraka yanayohusisha unyanyasaji wa kijinsia kupewa jina la “sextortion”) itasaidia sana kuijulisha jamii ya Watanzania kuwa vitendo hivyo vipo na vinafanyika ili waathirika wa vitendo hivyo waweze kuchukua hatua stahiki za kuvitolea taarifa katika mamlaka husika. Hali hii itafanya vitendo hivyo kukemewa na kutokomezwa nchini ili kulinda utu na haki za binadamu.

Kutendeka kwa kitendo ama/vitendo vya “sextortion” kunasababisha ukiukwaji wa haki za binadamu kwasababu siyo tu hudhalilisha heshima na/au utu wa mwathirika wa vitendo hivyo ambayo ni kinyume na Ibara ya 12 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (Kama ilivyofanyiwa mabadiliko mara kwa mara) pia vinakiuka Ibara ya 13, 16 na 23 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivyo basi ni rai ya mwandishi wa makala hii kutaka juhudi za kina kufanywa na watunga sera ili kutafuta namna ya kukabiliana na “sextortion”. Sheria nilizotaja kwenye makala hii hazielezei kinagaubaka tatizo hili. Kuna haja ya wadau mbalimbali kujitokeza kutoa elimu ya kutosha juu ya tatizo hili na hapohapo kuwa na sheria madhubuti na/au kuwa na Vifungu katika Sheria nilizozitaja katika Makala hii pamoja na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vitakavyoelezea na kushughulikia tatizo la “sextortion” ili kuwa na Maadili mema katika Taifa letu la Tanzania.

20

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kushirikiana na Wadau mbali mbali wamefanya mapitio ya

maeneo mbali mbali ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kubaini mapungufu mbali mbali yanayohusu ukuzaji na usimamizi wa Maadili ya Viongozi wa Umma.Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilifanyiwa marekebisho kwa mara ya mwisho mwaka 2001 kupitia sheria na 5 ya mwaka 2001 ambapo changamoto mbali mbali zilijitokeza na kusababisha utekelezaji wa sheria hiyo kuwa mgumu au hafifu.Aidha mwaka 2008, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho kikwete aliagiza kwamba Sheria ya Maadili ifanyiwe mapitio ili kuweka taratibu za namna ya kudhibiti migongano ya maslahi miongoni mwa viongozi wa Umma hususani suala la kutenganisha uongozi na biashara.

Hata hivyo, Serikali kupitia Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeona ni vema sheria hii ikafanyiwa marekebisho ili kuondoa mapungufu yaliyokubalika.

Akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na 13 ya mwaka 1995 Naibu Waziri wa Sheria na katiba Mhe Angella Kairuki alifafanua kwamba Warsha hii ni sehemu ya mchakato muhimu katika marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kwamba maoni yatakayokusanywa yatakuwa sehemu ya viambatisho muhimu vya waraka wa marekebisho ya sheria utakaowasilishwa katika Baraza la Mawaziri.

Aliongeza kuwa mapendekezo ya awali ya Marekebisho ya sheria yamekwishaandaliwa ambapo wanawarsha walipata fursa ya kujadili mapendekezo hayo katika vipengere vilivyoainishwa.

Kamishna wa Maadili, Mhe. Jaji (Mst) Salome Kaganda akizungumza kumkaribisha Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angela Kairuki kufungua warsha ya Wadau ya marekebisho ya Sheria ya Maadili.

MAREKEBISHO YA SHERIA YA MAADILI

Aidha, Mheshimiwa Kairuki alifafanua kuwa marekebisho yanayopendekezwa yanaweza kugawanywa katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza ni mapendekezo yanayolenga kurekebisha vipengele mbali mbali vya sheria ili kukuza Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi katika utekelezaji wa majukumu ya Umma na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Baraza la Maadili ambapo mapendekezo haya ni muhimu sana kwa ajili ya kudumisha Utawala Bora Nchini na kulinda imani ya wananchi juu ya Uadilifu wa Viongozi wa Umma na Serikali kwa ujumla.

Katika Warsha hiyo vipengere kadhaa vilijadiliwa na wana warsha walipata fursa ya kuvijadili na kutoa maoni mbalimbali ambayo yatawasilishwa katika Baraza la Mawaziri kwa hatua zaidi.

Warsha hiyo muhimu ilifanyika tarehe mosi Octoba katika ukumbi wa Dar es salaam Conference Centre ambapo iliwashirikisha zaidi ya wadau 80 kutoka katika Taasisi za Umma , Wizara, na idara mbali mbali za serikali pamoja na Taasisi binafsi.

21

Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakiwa kwenye maandamano ya amani katika kuadhimisha siku ya Maadili Duniani – 2012 yaliyofanyika Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Maadili, Mhe. Jaji (Mst.) Salome S. Kaganda (mwenye kombe), Viongozi Waandamizi, baadhi ya Maafisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma pamoja na washiriki wengine kutoka Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupata ushindi katika Maonesho ya Nane Nane, yaliyofanyika Nzughuni, Mkoani Dodoma, mwezi Agosti 2012.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah J. Kairuki, akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu Msaidizi Idara ya Viongozi wa Umma Bibi Zahara Guga wakati wa maadhimisho ya Siku ya Maadili Duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaan Desemba 2012.

Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma waliokua mafunzoni Kidatu katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki sherehe za kufunga mafunzo yao huko Kidatu.

Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Peter A. Ilomo, akisalimiana na Viongozi Waandamizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kabla ya Ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi Mwezi Agosti 2012.

HABARI KATIKA PICHA

2324

Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda (katikati, waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Menejiment na Watumishi bora wa Taasisi kwa mwaka 2012.