mapitio ya matumizi ya umma (per) ya matumizi ya...1 mapitio ya matumizi ya umma (per) makala kwa...

Post on 26-Dec-2019

39 Views

Category:

Documents

0 Downloads

Preview:

Click to see full reader

TRANSCRIPT

1

Mapitio ya Matumizi ya Umma (PER)

Makala kwa ajili ya Semina ya Mafunzo kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi,

Zanzibar

Limetayarishwa na

Dk. Joseph L.M.Shitundu Mkurugenzi, Kitengo cha Utafiti wa Uchumi

Chuo Kikuu , Dar es Salaam

12 May, 2008

Dar es Salaam

2

Mapitio ya Matumizi ya Umma (PER)

1.0 Utangulizi

2. Mapitio ya Matumizi ya Umma (PER) ni nini?

3. Vitu muhimu katika PER nzuri

4. Kwa nini tunaanda PER?

5. Madhumuni ya mafunzo haya mafupi

6. 6. Utayarishaji wa PER Tanzania Visiwani

6.1 Nini Madhumuni yake

6.2 PER na utaratibu wa Budget

(PER and Budget Process)

3

• Muundo wa matumizi ya muda wa Wastani (MTEF)

• Mzunguko wa kuandaa budget and PER

Mchoro No. 2.1

Mchoro na 2.2

6.3 Ripoti ya PER ikoje?

6.4 Mapungufu ya PER

7.0 Mfano wa vitu/maswali muhimu ya sekta ya

elimu

4

8.0 Matokeo (impact) ya PER

9.0 Tumejifunza nini kutokana na PER

5

Mapitio ya Matumizi ya Umma (PER)

1.0 Utangulizi

• Katika kusukuma mbele maendeleo

serikali mbalimbali huzingatia utoaji wa

huduma bora (goods and services) na pia

husimamia na kusaidia ukuaji wa sekta

binafsi.

6

• Serikali hufanya matumizi (ya pesa) ili

kufikia malengo mbalimbali ya kiuchumi,

kijamii na kisiasa. Miongoni mwa malengo

hayo ni:

• Kuondoa umaskini

• Kujenga mazingira bora/wezeshi kwa

sekta binafsi

7

• Matumizi ya serikali/umma (Public

spending) ni nyenzo muhimu ya kuondoa

umaskini. Lakini inahitaji kwamba:

- Matumizi yapangwe na kulengwa

katika maeneo muhimu yanayoongeza

maskini kupata huduma na pia kuongeza

uwezo wao wa kujipatia kipato.

8

- Utafiti/uchambuzi wa kina kufanyika

- Ziwepo taasisi, taratibu madhubuti

katika utandaji kazi wa serikali.

• Mageuzi yamechochea ari ya kutaka

kudhibiti/kusimamia vyema matumizi ya

umma

- Jinsi fedha za umma zinavyopatikana

9

- Malengo ya matumizi

- Faida itokanayo na matumizi

• Tutambue kuwa:

- mara nyingi “mahitaji” ni makubwa

kuliko “pesa”.

- Chaguzi zetu za vitu/mahitaji

zinabanwa

10

- Matumizi ya umma pia hubanwa i.e.

kiwango ambacho serikali inaouwezo wa

kutumia.

• Kwa hali hiyo ni muhimu kwamba

“matumizi ya umma” yanatumika

vizuri/ubora iwezekanavyo kupata huduma

nyingi na nzuri za kutosha.

11

2.0 Mapitio ya Matumizi ya Umma (PER)

ni nini?

• PER hufanya kazi ya kuchambua

matumizi ya umma, hususani kuhusiana

na “kutosha” na “usahihi” wake katika

kufikia malengo ya maendeleo.

• PER inawakilisha “mfumo” na

“mazao/matoikeo” ya uchambuzi wa

mfumo wa mapato na matumizi, ikiainisha

na kupendekeza mbadiliko muhimu katika

12

mgano wa matumizi ya umma na

taasisi/taratibu na sheria zitumikazo.

• PER inaimarisha mfumo wa bajeti

• PER inatoa fursa ya `kukodineti’ misaada

na kupima matokeo yake

• Zipo PER za kitaifa (macro) na za kisekta

13

3.0 Vitu muhimu katika PER nzuri

• PER nzuri inapatikana kwa kutumia mfumo bora wa uchambuzi, ukihusisha:

- Uchambuzi wa ushirikiano sahihi wa sekta ya umma na sekta binafsi katika kutooa huduma na mahitaji. Na pia ukionyesha umuhimu wa uhalali (rationale) wa sekta ya umma kuingilia pale nguvu za soko huru zinaposhindwa kuleta ufanisi na usawa.

14

- Kuchambua na kupima vipa-umbele vya

matumizi ya umma katika sekta mbalimbali huku

ikizingatiwa ufinyu wa rasilimali na mgao wenye

usawa.

- Kuangalia kwa ukaribu mfumo, taasisi na sheria

pamoja na malengo ya kisiasa ili kuboresha vitu

hivyo vilivyo muhimu katika kuhakikisha kuwa

matumizi ya umma yanakuwa bora na ya

kudumu (sustainable).

15

4.0 Kwa nini tufanye PER

- Hutoa mchango muhimu katika mfumo wa bajeti

- Inashughulia vitu muhimu katika maendeleo ya

muda wa kati na mrefu

- Inapima na kuchambua madhara ya “mambo ya

jumla” (cross cutting issues)

- Inatoa fursa ya kuchunguza kwa makini jinsi

Wizara, Idara na Taasisi zingine za umma

zinavyotumia fedha na raslimali zingine.

16

- Inatoa fursa ya kupima mafanikio ya sera

na mipango yetu kwa mfano jinsi serikali

na umma kwa ujumla kupitia wizara,

sekta, idara na taasisi zake

zinavyotekeleza Mpango wa Kupunguza

Umaskini Zanzibar (MKUZA).

17

5.0 Kutayarisha/Kuandaa PER

• Mfumo wa budget unahusisha utayarishaji

wa mipango ya matumizi ya umma,

mapitio ya matumizi ya umma (PER)

“miongozo ya bajeti”, Muundo wa

Matumizi ya muda wa wastani (MTEF)na

bajeti ya mwaka. PER na MTEF hususani

inasaidid akuhakikisha kwamba MKU\A ni

sehemu ya mfumo wa mipango na bajeti

18

uliokamilika unaoongozwa na upembuzi

wa mambo ya kupewa umbele na kuwa na

nidhamu ya kuangalia hyali halisi ya bajeti.

- Lengo la jumla ni kuongeza idadi ya

raslimali zinazoelekezwa kwenye

maeneo muhimu zaidi katika zoezi la

upunguzaji umaskini.

19

- Hivyo uandaji wa PER huhusisha wadau

na taasisi mbalimbali

- Kwa kawaida “mzunguko wa uandaaji wa

bajeti” unahusisha utayarishaji na utoaji

wa “miongozo ya bajeti (BGL) kwa ajili ya

MTEF kutoka kwa :Kamati ya taifa ya

Miongozo ya Bajeti”.

20

• Miongozo ya Bajeti inatoa: picha

maendeleo ya kiuchumi kitaifa na kisekta.

- sera au vipengele muhimu vya sera

vinavyopaswa kutiliwa maanani wakati wa

kuandaaa bajeti

- Majukumu ya taasisi mbalimbali katika

uandaaji wa bajeti

21

• Mfumo wa bajeti kwa kipindi cha kati na

format ya kutayarisha makadirio ya bajeti

kwa wizara, idara na taasisi za umma.

• Mfumo wa bajeti huonyesha rasilimali

(funds) zilipo na mapendekezo ya

“ceilings” kwa wizara, idara, sector and

taasisi za umma.

22

• Kwa kufupi Miongozo ya Bajeti (BGL) ina vitu muhimu vifuatavyo:

- muhtasari wa hali ya jumla kiuchumi na makisio (macro-economic performance and projections)

- muhtasari wa utendaji katika sekta na sera na mikakati husika

- “ceiling” za kasma (vote) za matumizi kulingana na upatikanaji wa raslimali

23

- taratibu/mfumo wa kuandaa na

kuwasilisha riport ya awali (draft) ya

bajeti huko Wizara ya Fedha.

• Wadau wakuu wanaoshiriki katika PEWR

ni: Serikali, wawakilishi kutoka World

Bank, Wafadhili, Taasisi zisizo za

Kiserikali.

24

- Wadau hawa huunda “PER Sector Working

Group na PER Working Group na kwa sasa ni

“PER Cluster WG” na `PER Macro Group”

- PER Macro Group huishauri kamati ya taifa ya

miongozo ya bajeti kuhusu.

- Kipewa umbele katika mgawanyo wa matumizi,

bajeti, na muunda na matumizi ya muda wa

wastani na uandaaji wa miongozo ya bajeti.

25

• Mzunguko wa utayarishaji wa MTEF/PER

Bajeti

- Husika na Chati 2.1

- Husika na Chati 2.2

26

6.0 Ripoti ya PER ikoje?

• Ripoti ya PER siyo ya aina moja lakini sehemu muhimu za Ripoti kwa ujumla ni:

(i) Utangulizi

(ii) Uchambuzi kwa kifupi wa maendeleo ya utekelezaji wa mapendekezo ya PER iliyotangulia

• Muhtasari wa mapendekezo

• Uchambuzi wa utekelezaji na maendeleo yaliyofikiwa

• Vipewa-umbele vikuu

27

(iii) Upitiliaji wa mfumo wa Bajeti katika sekta husika

(iv) Uchambuzi wa mgao wa Bajeti na matumizi katika vipaumbele vya utekelezaji kwa miaka mitatu ya nyuma na mwaka husika wa fedha

• Uchambuzi wa bajeti kwa mambo ya jumla na athari za kutokuyaingiza katika bajeti

• Uchambuzi wa mahitaji ya sasa na yanaotakiwa kuimarisha uwezo (capacity) na ujuzi wa wafanyakazi katika sekta husika.

28

(v) Kutathmini/kuboresha ukadinaji wa

gharama za kutekeleza mikakati

mbalimbali katika sekta husika ili kufikia

malengo ya kupunguza umaskini

• Uchambuzi wa fedha zinazotakiwa

kulinganisha na makadirio ya pesa

zinazoweza kupatikana.

29

• Njia mbadala za kupanga matumizi ili

kufikia malengo husika

• Kuangalia maana/matokeo ya njia

mbadala zilizopendekezwa.

(vi) Kutathmini mfuko wa raslimali kwa

sekta pamoja na maeneo ya kupewa

umbele katika kupewa za matumizi

30

• Uchambuzi wa huduma muhimu zinazotolewa

na sekta

• Uchambuzi wa wapi pesa inaweza kupatikana

• Uchambuzi wa muko wa rasilimali za kutekeleza

MTEF ikilinganishwa na pengo la raslimali

• Uchambuzi wa maeneo ya kupewa umbele

katika matumizi ya raslimali katika sekta husika

31

(vii)Uchambuzi wa mambo ya jumla na jinsi

ya kuyaweka katika bajeti

(viii)Majumuisho na mapendekezo na

wahusika wa kutekeleza/kusimamia

utekelezaji wa yaliyopendekezwa.

32

7.0 Mapungufu ya PER

• PER kwa ujumla inafaa kupanga vyanzo

vya mapato, mgawanyo na matumizi.

Lakini PER haiwezi kuhakikisha kuepukwa

yafuatayo:

- mgao au uwekezaji usiosahihi kwa

huduma halisi itolewayo

- huduma duni ukilinganisha na fedha

zilizotolewa

33

- huduma kutokutumika na walengwa

• Hivyo ipo mifumo mingine kusaidiana na PER

- PETS

- QS

Mifano wa Mambo muhimu katika PER ya Sekta ya Elimu

• Maelezo kwa kifupi kuhusu mipaka ya sekta itakayohusishwa na PER

34

• Vipengele muhimu kwa ujumla:

(i) Kiasi gani kinatumika katika sekta ya

elimu? Na serikali inatumia kiasi gani

(ii) Ni vipi serikali inalipia/kutoa fedha kwa

sekta ya elimu?

(iii) Ni sehemu/mambo yapi ambayo serikali

inalipia katika sekta ya elimu?

35

(iv) Je matumizi ya umma katika elimu

yanalinda usawa katika jamii?

(v) Je raslimali za umma (fedha, watu,

majengo, vitabu) vinatumika kwa ufanisi

na kwa manufaa?

(vi) Je matumizi ya umma katika sekta ya

elimu yanatosha na yanaweza

kuendelea kwa muda mrefu?

36

• Vipengele muhimu kwa undani

(i) Kuhusu kiasi kinachotumika katika

sekta ya elimu:

• Ni kiasi gani cha pesa kinapatikana

kutoka vyanzo vyote (serikali, sekta

binafsi, wafadhili na mashirika yasiyo ya

kiserikali) kwa matumizi katika elimu?

37

• Ni kiasi gani kinatumika katika elimu

kutoka vyanzo vya umma?

• Matumizi katika elimu ni asilimia ngapi ya

pato la taifa?

• Je matumizi ya umma katika elimu

yanatokana na mapato ya jumla au kodi

maalumu?

38

• Ni kiasi gani cha matumizi katika elimu

kinalipwa na sekta binafsi?

• Uandikishaji wa watoto/wanafunzi

kiasilimia kwa shule za binafsi na za

umma ukoje?

• Ni kwa kiasi gani sekta ya elimu

inategemea fedha za wafadhili? Na ni

maeneo yapi ya bajeti?

39

(ii) Serikali inalipiaje sekta ya elimu?

• Mgawanyo wa fedha za elimu ukoje kwa

serikali kuu na serikali za mitaa?

• Katika mgao huo ni nini kinacholipiwa?

• Je wanaotoa maamuzi ya bajeti ya elimi ni

watu wa kuchaguliwa au la na wanawajibika

kwa nani?

• Je serikali za mitaa zinayomamlaka kamili ya

kukusanya pesa na kuzitumia katika elimu?

40

• Ni kiasi gani cha fedha kutoka serikali kuu

hupelekwa katika elimu serikali za mitaa? Je

fedha hizo huka kama fungu maalumu la elimu

au kama fungu la jumla?

• Mfumo wa kuripoti mapato na matumzi ya fedha

za elimu ukoje?

• Je shule zina bajeti zao na wanayo mamlaka ya

jinsi ya kutumia? Je shule zinamapato kutoka

vyanzo vyake? Na pesa hiyo hupelekwa wapi?

41

(iii)Serikali hulipia nini?

• Mgano wa fedha za elimu ukoje katika ngazi mbalimbali za elimu?

• Ni nini “unit cost” katika ngazi mbalimbali za elimu? Linganisha na pato la mtu.

• Mgao wa fedha za umma ukoje kwa huduma mbalimbali za elimu?

• Je fedha kutoka kwa wafadhili zinatumika wapi zaidi?

42

• Ni kiasi gani cha fedha hutolewa kwa

matunzo/matengenezo na ukarabati wa

shule? Je kinatosha kulingana na

gharama halisi?

• Je vitabu vinatosheleza kwa kila

mwanafunzi. Kila na wanafunzi wangapi?

43

(iv)Sera na Matumizi ya Umma na Usawa

• Nini tofauti ya uandikishwaji, kumaliza na mafunzo kati ya makundi mbalimbali katika jamii?

• Je serikali hutoa ruzuku kwa shule za binafsi? Kwa sheria na utaratibu upi?

• Je kuna mianya na vitendo vya rushwa katika kupata nafasi shuleni na kufaulu? Katika kutoa huduma?

44

(v) Je Raslimali za umma zinatumika kwa manufaa na ufanisi?

• Je serikali hupima “inputs”, utaratibu na matokeo ya matumizi ya umma?

• Je serikali hupima mafanikio yatokanayo na matumizi ya umma katika elimu? Na je njia mbadala hupendekezwa.

• Mgao wa waalimu ukoje? Je ni sahihi kwa kila ngazi?

45

• Nini ratio kati ya waalimu, wanafunzi na

watumishi wasio waalimu?

• Waalimu wanatumikaje? Nini mzigo wao wa

kufundisha? Wanafundisha kwa kiasi gani?

• Kwa wastani mwalimu mmoja hugharimu kiasi

gani?

• Ni gharama ya mitaala ukizingatia vitabu na

mafunzo maalumu kwa walimu ili waendane na

mitaala mipya?

46

• Je fedha za ujenzi (capital) zinatumikaje?

- Vigezo gani hutumika kuamua kujenga

shule mpya na wapi?

- Ni nini gharama halisi za kujenga

darasa moja?

- Ni gharama za kutengeneza/kukarabati

darasa? Je shule inayo bajeti hiyo?

47

Wastani ukoje kwa shule zingine?

- Je juna uwazi na ufuataji wa taratibu na

kanuni za manunuzi katika utoaji wa

tenda katika ujenzi, ukarabati na utoaji

wa vifaa vikiwemo vitabu? Je hakuna

rushwa au mazingara ya rushwa?

• Nini wastani wa watoto katika darasa moja

kati ya mijini na vijijini?

48

• Je ni shule ngapi zina “shift” mbili?

• Je wanafunzi wangapi wanaacha shule?

Wararudia? Na gharama zake zikoje.

49

9.0 Impact ya PER

• Kutayarisha vipa umbele vizuri zaidi

• Kuongezeka kwa taarifa na hivyo kuboresha maamuzi

• Kuboresha “coordination” ya wafadhili na uingizaji wa misaada katika bajeti kwa njia bora zaidi?

• Mfumo mzuri zaidi wa programmu za maendeleo kisekta

• Kujenga uwezo miongozi mwa wadau mbalimbali wa bajeti

50

10.0 Tumejifunza nini?

• Ushirikiano (Partnership) miongoni

mwa wadau wa PER

- Faida za ushirikiano huu ni:

- Wadau kuelewa vizuri sekta

mbalimbali

- Pesa za wafadhili katika kuandaa

PER

51

- Kuibuliwa kwa masuala muhimu ya

bajeti

- Kusambazwa miongoni mwa Wadau

ripoti za PER katika mikutano na vikao

mbalimbali

52

• Majadiliano na Ushiriki

- Majadiliano yameboresha uandaaji na utumiaji wa PER katika bajeti

- Fursa kwa wadau mbalimbali wa PER katika kushiriki maandalizi ya PER na MTEF za kisekta

- Fursa kwa taasisi/mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, sekta binafsi, wabunge/wawakilishi wanataaluma kuchangia mawazo na mapendekezo yao katika bajeti ikiwa ni pamoja na “consultative meeting”

53

• Uhusiano na kusaidia Taasisi na nchini

- Taasisi za ndani zinashiriki kuandaa na kuchambua PER. Hiyo mfumo na mawasiliano yanaboreshwa kuhusiana na menejimenti na sera za kibajeti.

• Maboresho ya bajeti

- Namna nzuri zaidi yakupanga na kulipia vipa umbele katika sekta mbalimbali.

54

- Mgao bora zaidi “strategic allocation” kwa kutumia PER na MTEF.

- Kuimarisha uandaji na usimamizi wa bajeti

- Kuboresha uwajibikaji katika bajeti

- Kuelewa kwa undani zaidi hali halisi ya bajeti na usimamizi wa matumizi ya umma katika sekta mbalimbali na hasa serikali za mitaa.

- Fursa ya kupitia/evaluate mafanikio ya bajeti imeboreshwa.

55

Ahsanteni Sana

top related