vipi tusome tarekhe ya aal-beit na masahaba? · kifo cha nabii (s.a.w), mpaka kuanguka, kwa dola ya...
Post on 09-Sep-2019
4 Views
Preview:
TRANSCRIPT
Vipi tusome Tarekhe ya
Aal-Beit na Masahaba?
آ�� ���أ ��ر�� ال وا����ب
Kimetungwa na: Sh, Abdulkarim bin Khalid Alharbiy
Kimefasiriwa na: Sh, Juma Yussuf
Kimepitiwa na: Ustadh Talib Juma Ali
1431-2010
YALIYOMO
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
2
UTANGULIZI 3
Vipi tusome Tarekhe ya Masahaba? 3
Sababu ya mwanzo 4
SABABU YA PILI 5
SABABU YA TATU : 9
Jambo la Mosi : 11
Jambo la Pili: 12
Jambo la Tatu : 12
Jambo la nne: 14
Jambo la Tano: 15
Haya hujibiwa kwa njia mbili : 19
Wajhi wa mwanzo : 19
Wajhi wa Pili 23
Miongoni Mwa Vitabu Muhimu vyenye Kutegemewa kwenye Historia 25
Vitabu vyenye matatizo na kuchafua historia ya kiislamu 32
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
3
UTANGULIZI
Vipi tusome Tarekhe ya Masahaba?
Sifa zote njema zimemthibitikia Allah aliyejaalia historia ya waislamu
waliotangulia kuwa yenye kung’ara na iliyo safi, na Sala na Salamu
zimshukie yule aliyepelekwa na Allah kuwa Mtume na Nabii muongowaji
pia sala ziwashukie jamaa na masahaba wake, na kila aliyekuwa mchaji.
Ama baada ya hayo: Kwa hakika kuhifadhiwa kwa Historia yetu iliyosifika,
na kuihifadhi kutokana na mikono ya wachafuaji, na uongo wa wenye chuki
na ujinga wa wasioelewa, ni katika mambo ya wajibu juu ya wenye elimu na
maarifa, hivyo isiachiwe kuwa kwenye mikono ya Mustashrikina wakaifanya
kitambaa cha kufutia uchafu, wala kwenye mikono ya waliouacha mkono
uislamu –kwa kusahau au kwa makusudi –ili iwaondoe toka kweye njia
waliokuwa mababu na watukufu, wakachukuwa hili na kuwacha hili, kwa
ajili ya haja zilizomo kwenye nafsi zao na Allah ni mwenye kufichuwa
waliyokuwa wameyaficha.
Na katika zama hizi tunaona mataifa na umma zinazojaribu kujifanyia
historia yake, zinakusanya mawe na nyaraka, wanachimbuwa mabaki ya kale,
wanavunja majumba na kuharibu misikiti, kwa madai kwamba humo imo
historia na kumbukumbu, jambo lililowafanya watobowe, wachunguze na
kuteketeza wakiwa na matarajio ya kupata historia inayodaiwa. Na hii siyo
hali ya umma hizi tu ,bali ndiyo hali ya mataifa mengi katika zama hizi, bali
katika kila zama.
Jee ni ipi hali ya umma wetu; ulio na historia ing’arayo na iliyochapishwa
wala hawaipi umuhimu wowote ?!
Kwa kuanzia hapa ni lazima juu yetu kusoma Historia yetu kisomo cha utafiti
na uhakiki, kuisafisha kutokana na taka zilizopakaziwa, kuitakasa kutokana
na yaliyochanganyiwa, ili itoke ikiwa safi yenye kung’ara, watu wanufaike
nayo, na iwe kama alivyosema Mola wetu (Subhanahu Wataalah) :{Ama
povu basi hupotea, ama kile kinachowafaa watu basi hubakia kwenye
ardhi, hivi hivi Allah hupigia mifano}[Ar Ra’d:17]
Abdil Kariim bin Khaalid al ‘Harby.
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
4
Mlango wa Mwanzo Sababu za kufanya mapungufu katika kusoma Historia inawezekana
kuyarejesha mapungufu yaliyopo kwenye darasa nyingi za historia za
zama za kisasa kwenye sababu tatu1 :
Sababu ya mwanzo
Hakika watoto wengi wa Kiislamu wameangukia kuwa mihanga kwa
yale waliyoandika baadhi ya Mustashrikina, waathirika wao miongoni
mwa kizazi chetu na waandishi wengineo wasioaminika, ambao
hujikumbatizia uongo na uzushi uliozushwa kwenye Historia yetu ya
kiislam kwa ujumla, na yale yanayoambatana na Aalil Beit Nabii
(S.A.W) waliotoharika na Masahaba watukufu (r.a).
Batili hizi huzifanya kuwa ni nguzo kwa wanayoyaandika, kama
kwamba ni vyenye kusalimika, wakihamasisha usomaji wa maandishi
hayo toka kwa wasomaji wasioona kitu ndani yake, wakitegemea
sababu ya kuandikwa kwake kwenye vitabu vya kihistoria, kama
kwamba kuwa kwake kwenye matumbo ya vitabu inatosheleza
kupakia rangi sifa za ukweli na kuthibitishia upakaji matope kutokana
na uongo na batili, wakijisahaulisha kufanyia kazi misingi ya utafiti
wa kielimu na kupatikana kwa uhakika yale wanayoyakaribisha usiku
na mchana. Pamoja na kwamba mengi ya wanayoyanukuu na
kuyataja, ima yanakuwa ni yenye sanad dhaifu, uzushi, au yasiyokuwa
na asili kabisa kabisa.
Na wengi miongoni mwao wanauelewa uhakika huu isipokuwa
wanajisahaulisha tu, kwa ajili ya kutia kasoro na kuiangusha historia
yetu tukufu, wao huanza kuandika wakiwa na niya mbaya, malengo ya
kiadui, yakilenga kwenye upakaji matope, kutia shaka kwenye nguzo
za umma huu, kueneza fitina na kuanzisha uadui baina ya watoto wa
umma huu, jee vipi itajuzu kwa muislamu awafanye hawa na
1 Sababu hizi zimetajwa na Daktariri ‘Abdil ‘Aziz Khan Allah ampe salama
kwenye kitabu chake ا���� ا����� –Matukio na Matukio ya Fitna zenye kuenea –
uk. (73-74) na tumezidisha juu yake kutolea baadhi ya dalili muhimu na
maalumati ya lazima.
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
5
wanayoyaandika kuwa ni viwakilishi baina yao na kumbu kumbu, dini
na historia yake ?!Na hii haimaanishi kwamba mustashrikina wote
wako sawa, wapo wa aina mbali mbali.
Wapo miongoni mwao wanaokusudia kubadilisha, kutia kasoro na
kutia watu kwenye shaka; kwa sababu ya chuki na husuda na malengo
ni ustashriki wa kiadui wa kutawalia na kupora nchi kuuwa waja, na
kudidimiza maendeleo ya kiislamu na utamaduni wake.
Na miongoni mwao –nao ni wachache- ni wale walioingilia
kumbukumbu zetu kama kazi ya kielimu na utafiti, juu ya
kudhihirisha mapungufu wanapokuwa kwenye mazingatio machache
tu kutokana na ugeni wao kwenye dini hii, na ukosefu wa maarifa
mazuri wa Lugha yake ambayo (ndio msingi wa mwanzo wa kumbu
kumbu hizi na usukani wake), na katika haya ni uchapishaji wa kitabu
(Al Waafii bil Wafayaati) cha Swalaa’hid Diini as Swafadiyyi, na
utunzi wa (Muujamul Mufahras Lialfaadhil ‘Hadiithin Nabawiyyi
Shariif ).
SABABU YA PILI
Kuondoka kwa elimu ya kisheria, upungufu wa hima na maarifa,
kujingikiwa na njia ya maulamaa wa historia na misingi yenye
uhusiano na uandishi na kupanga riwaya ya kihistoria.
Hivyo baadhi ya maulamaa mfano wa Maimamu wawili (At Tabary
na Ibn Kathir) kamwe hawashurutishi kuleta riwaya sahihi kwenye
vitabu vyao na kupuuza dhaifu kutoka na na riwaya za visa dhaifu vya
matukio na mambo yaliyozuka, bali walifuata mpango maalum
waliouashiria kwenye tangulizi za vitabu vyao; ili msomaji awe
kwenye bayana ya jambo hili.
Lakini wengi wa mufakirina, waandishi na walioendelea kwa ujumla
walikuwa kwenye kifungo na bado wako kwenye misingi hiyo na
vitangulizi, hivyo imekuwa kutoielewa na kuipuuza ni sababu ya
kupotea tafiti zao na maandishi yao yenye kusadikisha –usahihi – na
kufikia kwenye haki ..
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
6
Hivyo ni katika mambo ya umuhimu kusoma utangulizi wa mtunzi wa
kitabu chochote kile ili tupate uwazi wa sera ya kitabu chake. Na kwa
kubainisha uhakika wa tuliyotanguliza; tunakuletea mfano wa
umuhimu wa kuzingatia misingi na sera za wanahistoria, nayo ni sera
ya Imam Ibn Jarir Tabary (r.a) kwenye kitabu chake cha Tarekhe.
Ubainishaji wa Sera ya Imam Tabary kwenye kitabu chake
( Taarekhul Umam wal Muluuk)
Huyu hapa Imam Ibn Jaririt Tabary2 anafichua sera yake kwenye
utangulizi wa kitabu chake anasema "Zilizomo kwenye kitabu changu
katika habari kutoka kwa baadhi ya waliotangulia, miongoni mwa yale
yanayokataliwa na msomaji, au yanayochukiwa na msikilizaji wake,
kwa kuwa hakuelewa njia katika usahihi wake, na wala haina maana
kwa uhakika, hivyo ieleweke kwamba haikuja toka kwetu, ila imekuja
toka kwa baadhi ya wanukuuji, na kwamba sisi hiyo tumeileta kwa
namna tulivyofikishiwa.3mpaka hapa.
Imam Tabary (r.a) anambainishia msomaji kwa uwazi kwamba
kamwe hakushurutisha usahihi katika yale anayoyaleta kwenye kitabu
chake hichi katika riwaya zake, na kwamba dhamana katika
anayoyanukuu iko kwa wasimulizi walionukuu kabla yake, nae
kwenye kitabu hichi alikuwa mnukuuji na muaminifu, na sio mhakiki
mkosoaji. Hivyo baadhi ya aliyoyasimulia Tabary toka kwao
walikusanya baina ya uongo na wingi wa riwaya, na miongoni mwao
ni:
a٢ Tabary:ni Imam :Muhammadbin Jariir bin Yaziid Abu Jaa’far
Tabary.Mfasiri ,Muha’haddith ,mwanahistoria ,na mwanazuoni wa Usuli
Fiqhi na mwanafiqhi ,Imam mujtahid .Alizaliwa Aamaal ‘Tabaristaan mwaka
(224) na kufariki (310H).Miongoni mwa tunzi zake ni (Tarekhe l Umam wal
Muluuk)na Jaami’iBayaan fii Ta-awiilQur-aan).
٣ Tarekhe l Umam wal Muluuk.(52/1)
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
7
1-Muhammad bin Hamiid Ar raazy sheikhe wa Tabary : Tabary amesimulia kwa wingi toka kwake kwenye kitabu chake (At
Taariikh) na (At tafsir) pamoja na kwamba Muhammad huyu
amerembewa kuwa ni muongo na mzushi wa hadithi, nae ni dhaifu
mwenye hadithi zisizofaa toka kwa As Sawaadil A’adhwam toka kwa
maulamaa wa Jerhe na Ta’adiil 4
2-Luut’ bin Ya’yaa Abuu Mikhnaf;
Anazo riwaya nyingi kwenye (Taariikh Tabary ) zimefikilia riwaya
(585), kwenye riwaya hizo ameingia kwenye matukio na mambo
muhimu yaliyozuka kwenye historia ya kiislamu yakianzia kwenye
kifo cha Nabii (S.A.W), mpaka kuanguka, kwa Dola ya Umawiyyah,
na Lut huyu ni mwenye kutiwa ila mbele ya maulamaa wa Hadithi.
Amesema Ibn Maiyn
Amesema ibn Ma’iin" ء �� ��� - - sio chochote "- Na akasema Ibn ‘Hibbaan "anasimulia hadithi za uongo toka kwa
wenye kukubalika . وي ا������ت �� ا����ت�� :" :
Nae Adh Dhahaby akasema:” mtowaji wa habari zilizofisidika”5”":
Kutokana na mfano huu umedhihiri umuhimu wa kuangalia sera na
masharti ya maulamaa na kuyafahamu katika uandishi wa historia, na
umuhimu wa kuzihudhurisha nyoyoni wakati wa kutalii kitabu cha
Imam huyu au yule.Hali hii inahusika pia na vitabu vyengine vya
habari na historia, bali pia kwenye vitabu vya kumbu kumbu na fani
zake tofauti .
Baadhi ya wanahistoria hawa sera yao ilikuwa ni kunukuu riwaya na
habari hizi zikiwa na sanad zake bila ya kuzingatia hali za watu wala
sanadi zake, kwa kwenda kwenye kauli iliyoenea :”Yeyote aliyeweka
sanad basi huyo ameshategemeza kauli –hiyo-”, kwa kufuata hikaya
4 Angalia Miizaan wal I’itidaal)(530/3-531).
5 Angalia kitabu :Marwiyyaat Abii Ma’hnif (Luutw’ bi nYa’yaa Abuu
MakhnafAl Azdy ) Kwenye Tarekhe at Tw’wabary :zama za khilafti
Raashidiah) (uk. ) cha Daktari Ya’hya bin Ibrahim Al Yahya (Chapa
.1.Daarul ‘Aaswimah /Ar Riyaad1410 H.)
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
8
za baadhi ya maulamaa wa hadithi katika uandishi wa hadithi, kwani
wao huandika kila riwaya kwa sanad yake ikiwa kama hatua ya
mwanzo; ama hatua inayofuatia – ni yenye kutofautisha baina ya
wanahistoria na wanahadithi –ambapo hushughulika na kuzichuja na
kuzitafiti, kuzihakiki na kuzitenganisha baina ya sahihi na dhaifu .
Imam Ibn Hajar ameashiria hilo akibainisha njia na sera za wengi wa
waliotangulia anasema "Wengi wa Muhadithina katika zama zilizopita
toka kwenye mwaka wa mia mbili na kuendelea mbele walitaja
hadithi kwa sanadi zake, wakiitakidi kwamba wamejiondolea
dhamana yao.”
Kwa kawaida Al-haafidh anakusudia wasimulizi wanukuuji, sio
maimamu wadadisi maulamaa wa Jerhe na Taadiil, walinzi wa dini
kutokana na kuchafuliwa na kubadilishwa, wenye kutumia misingi na
kanuni madhubuti za kukubalika na kukataliwa kwa msimulizi na
chenye kusimuliwa, hiyo ni misingi isiyokuwa na shubuha wala
mifano kwenye uzoefu wa kibinadamu na maendeleo yake .
Ni wajibu wa msomaji-akiwa ni mwenye kufaa-ahakikishe simulizi za
kitabu hichi au kile juu ya mwangaza wa misingi ya Muhaddithina
wadadisi, nao ni ule unaoitwa "Elimu ya Mustalahi-alhadithi"
uliojengeka juu ya kutafiti hali za masimulizi na habari na wanukuuji
wake katika hali ya kukubalika na kukataliwa, kwa kukaa kati ya
mambo mawili :
Mosi :Utafiti na upekuzi kuhusiana na wasimulizi wanukuuji wa
riwaya hizi wakitegemea kauli ya mabingwa wadadisi miongoni
mwao, maimamu wa Jarhu na Taadili 6;hivyo anaefaa huwa ni thiqah;
riwaya zake hukubalika, na asiefaa huwa dahifu riwaya zake
hazikubaliki wala hazina hadhi yoyote ile.
Pili :Kuangalia kwenye matini za riwaya hizi na kuzifanyia upekuzi
kwa kuzilinganisha na kitabu cha Allah na Sunna iliyo sahihi
iliyothibiti na misingi ya ujumla yenye kutegemewa kuhusiana na
6
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
9
mambo mawili hayo, ili kuelewa zisizofaa toka zile zenye kufaa,
zilizofuta –nasikh- toka kwenye zilizofutwa –mansukh- .
Hivyo msomaji akiwa ni mwenye sifa ya kustahikiwa na kuendesha
tafiti hizi na kuzifanyia uhakiki akiangalia wenye kushikamana na
elimu hii tukufu na ya kina; na vyenginevyo itamlazimu kumuogopa
Allah na jambo hili kulitegemeza kwa wanaofaa, watu maalum, watu
wa utafiti na maarifa ya mathiqa waadilifu .
SABABU YA TATU :
Kile wanachofanyia danadana baadhi ya waandishi ya uwezekano wa
kufanyiafanyia wepesi kwenye riwaya hasa zinazohusiana na zama za
mwanzo katika Historia ya Kiislamu zikilinganishwa na ukali katika
riwaya za Hadithi za Nabii (S.A.W) nalo wallahi likiwa ni katika
makosa makubwa yanayotokea kwa watu wetu waliostaarabika, kwa
vile ni aina katika aina za kuathirika na sera za kimagharibi ambazo
hazitilii mkazo kwenye unukuuji wa sanadi, na mfano mkubwa wa
hilo ni kwamba isnadi baina yao na (Injili) ni yenye kukatika kwa
mamia ya miaka, nacho ndicho kitabu chao kitakatifu basi unaona vipi
kwenye vitabu vyengine?!
Hakika historia ya Ahlil Beit ya Nabii (s.a.w) na Masahaba (r.a) ni
sehemu ya dini yetu na kamwe haisihi kuifanya sawa baina yake na ile
historia nyengine, au kufanyia uzembe katika kuichukuwa na
kuisimulia kwake, hivyo uzembe au kasoro yoyote katika haki ya
Historia hii na kuithibitisha kwake basi athari yake kwa vyovyote vile
itarejea kwenye dini, na juu ya kusihi kwa hadithi na usalama wake
kutokana na ubadilishwaji na ugeuzwaji wake .
Nasi tunao mfano wa wazi kwenye utiaji kasoro wa yule ambae ndani
ya moyo wake muna chuki kwenye riwaya ya kusilimu kwa Abu
Huraira Sahaba huyo mkubwa (r.a). Hakika watafiti wanajitahidi kwa
mapana katika kujadili baadhi ya matukio na mambo ya kihistoria
yaliyozuka zamani na sasa, wapo wanaothibitisha na wapo
wanaopinga, na kila upande unatanguliza dalili na hoja zake
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
10
zilizowapelekea kuona hivyo, pamoja na kwamba baadhi ya matukio
haya kamwe hayapelekei faida yoyote na amali kubwa, unadhania vipi
kuhusiana na Historia ya Aalil Bait na Masahaba (r.a) wabebaji wa
Sheria na ngome madhubuti ?!
Hii haimanishi uwajibu wa kutendea habari zote za (zama za
mwanzo) katika Historia yetu kama zinavyotendewa Hadithi katika
hali ya kukubalika na kukatalika, bali ni wajibu kutofautisha baina ya
habari na riwaya.
-Hivyo ikiwa habari na athari hizi ni kutoka kwa Aalil Bait na
Masahaba (r.a) wanasimulia zuhudi, ushujaa, ukarimu, kujitowa kwao
muhanga na wema wa tabia zao, mienendo yao bora na upole wa tabia
zao na mambo hayo hayakutoka kwenye misingi mikuu ya kisheria,
wala sio yanayokataliwa na maumbile yaliyo salama, hivyo hakuna
pingamizi kutajwa, kusimuliwa na kuandikwa kwake, kwani mambo
hayo hayagusi au kutikisa asili ya kisheria, na kamwe kwenye
kusimulia kwake hakuna madhara au mguso kwa hadhi ya Aalil Bait
na Masahaba (r.a) .
-Ama iwapo habari hizo ndani yake zimo fitina, au baadhi ya
misimamo ya kihamasa, au baadhi ya yanayochafua hadhi ya Aalil
Bait na Masahaba (r.a), au ndani yake kimo kitu kinachokwenda
kinyume na Misingi ya ujumla ya kisheria, au kumuingiza baadhi ya
kasoro zenye kukatalika na maumbile yaliyo sawa.
Hivyo aina hii ya habari ni lazima kuangaliwa kwenye sanad zake
muangalio wa umakini na wa kina na kuhukumiwa kwa hukumu ya
uadilifu .
Mikakati hii mitatu ambayo ndani yake kumeingia mapungufu katika
kusoma, kuonyesha na kunukuu historia ya kiislamu .
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
11
MLANGO WA TATU
Kanuni kuhusiana na kujibu shubuhati kuhusiana na Ahlil Bait:
Inampasia muislamu awe na tahadhari juu ya mambo sita
muhimu yanayoambatana na Aalil beit (r.a)
Jambo la Mosi :
Kwamba hadhi ya Ahlil Bait ni kubwa na imesaidia baadhi ya maadui
wa uislam kujipenyeza baina ya waislam, nako ni kukuza kielelezo
cha mapenzi ya Ahlil Bait na mawalii (wawachwa huru wao), kuzua
hadithi kwenye ubora wao, kama ni matokeo ya watu kukubali fadhila
za Ahlil Bait na mapenzi yao kwao kwa ujumla kwani wao walikubali
hadithi hizo za uzushi bila ya kuzifanyia upekuzi na utafiti na hivyo
tunaona Maimamu wa Aalil Bait ( r.a) wanalitaja jambo hili kwa kila
uwazi, na kwamba ni uhakika uliotokea hivyo inawapasa vipenzi vya
Aalil Bait ( r.a) kuchukuwa tahadhari miongoni mwa yaliyozuliwa juu
ya Aalil Bait ( r.a) katika athari na habari zilizozushwa .
Huyu hapa imamu miongoni mwa maimamu wa Aalil Bait tukufu (r.a)
nae ni Jaafari Sadiq (r.a) anasema "Hakika watu wamependezeshewa
uongo juu yetu "7 Naye (r.a) akiita kwa jina la Madwiyyatu
akasema:"Hakika ni sisi Aalil Bait (a.s) ni wa kweli kamwe
hatutovuka kutokana na muongo na anayotuzulia, basi ukweli wetu
huporomoka kwa sababu ya uongo wake juu yetu"8
Msikilize Shariih bin Abdil Lahil Qaadhy akiisifu kaumu iliyokaa
pamoja na Jaafar, na kudai kusimulia toka kwao:"Amesema Abu
Amril Kishy: Amesema Yahya bin Abdil Majid Al Hamany, kwenye
kitabu chake Al Muallafu fii ithbaati Imaamati 'Ali bin Abi Talib ( r.a)
"nilimwaambia Shariik Hakika watu wanadai kwamba Jaafar bin
7 Bihaarul Anwaar cha Al Majlisy (246/2)
8 (Jaamiur Ruwaat ) cha Muhammadil Ardiby Al Haairy (221/2) na
(Kuliyyaat fii 'ilmir Rijaal ) cha Jaafar As Sabhaany (uk.26)
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
12
Muhammad ni mdhaifu wa hadithi, akasema "Ninakupa habari ya
kisa, Jaafar bin Muhammad alikuwa mtu mwema, muislamu mchaji
basi akakumbatiwa na watu wajinga wakawa wanaingia na kutoka
kwake" na wanasema ametuhadithia Jafar bin Muhammad hadithi na
zote ni Munkarat walizozizuwa toka kwa Jaafar, ili wawatake watu
chakula kutokana na kufanya hivyo, na huchukuwa dirhamu toka
kwao, waliokuwa wakileta kila hadithi munkar, hayo yakasikiwa na
wasiokuwa na elimu, basi miongoni mwao wamo walioangalia, na
wengine wapo waliozikataa .
Vile vile akasema Imam Jafar Saadiq (r.a) :"Mughira bin Said alikuwa
akitegemea kumzulia uongo baba yangu, huchukuwa vitabu vya
wafuasi wake, na wafuasi wake walikuwa wamemficha ndani ya
wafuasi wa baba yangu" huchukuwa vitabu vya wafuasi wa baba
yangu na kuvipeleka kwa Mughira, akawa humo anaweka kufuru na
uzandiki, na kuyategemezea kwa baba yangu, kisha anayapeleka kwa
wafuasi wake na kuwaamrisha wayaeneze."9
Jambo la Pili:
Hakika hadithi za uongo zilizozushwa kwenye fadhila za Masahaba
(r.a) hatua kwa hatua – zinazidi idadi ya Hadithi sahihi kwa makumi
ya mara, hivyo sio wajibu kukubali hadithi za fadhila na kuzieneza na
kuvukia kwazo mpaka wa sifa ila baada ya kuzitafiti sanadi zake na
kuthibitisha usahihi wake.
Jambo la Tatu :
Hakika fadhila zilizothibiti kwenye haki za Aalil Bait (a.s)
hazimaanishi kupwekeka kwao kwa fadhila hizo zilizokuja bila ya
kuwashirikisha wengineo, na hivyo ni kwa kufata kanuni inayosema:(
Kufanyiwa umakhsusi kwa makarama hakumaanishi kuondolewa kwa mwengine).
9 (Al Hadaaiqin Naadhira h) cha Yusuful Bahry(50/1) Bihaarul Anwaar ccha
Al mjlisy(250/2)
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
13
Lau tutasema: Hakika Nabii (s.a.w) amesema kuhusiana na haki ya
Ali ( r.a) – nae ni katika Aalil Bait ( r.a)-: "Bendera hii nitampa mtu
ambae Allah atakomboa juu ya mikono yake anayempenda Allah na
Mtume wake, naye anampenda Allah na Mtume wake"
Jee kwenye hadithi hii ichukuliwe kwamba makarama haya
yameondoshwa na hayawezekani juu ya Aalil Bait waliobakia (r.a), na
kwamba Al Hassan na Al Hussein wao hawampendi Allah na Mtume
wake (s.a.w)
Kwa maumbile tu ni kwamba haiwezekani, bali wao ni mabwana wa
vijana wa watu wa Peponi na hakuna shaka kwenye mapenzi ya Allah
na Mtume wake (s.a.w) kwao, na kwamba lengo la habari ni kwamba
Allah amempa hadhi na kumnyanyulia cheo chake kwa kufanyiwa
umakhususi ya kutajwa, kwa mfano :
Amesema Allah Taala kuhusiana na Aalil Bait (r.a) {Hakika Allah
anataka kuwaondoshea takataka Aalil Bait na kuwasafisha msafisho ulio bora} [Al Ahzaab :33]
Na akasema kuhusiana na Masahaba {Kamwe Allah hataki
kukufanyieni uzito lakini anataka kukusafisheni na kukutimizieni neema zake kwenu }[Al Maaidah :6]
Usafishaji ni wenye kuenea kwa waumini wote, lakini Allah
amewafanyia umaalum Aalil Bait (r.a) kutokana na ubora wao, nawe
pima juu ya hili, na hakuna shaka kwamba baadhi ya Aalil Bait ( r.a)
wanayo mambo maalum na yanayowatofautisha na wengine ambayo
kwayo hawashirikiani na yeyote yule, kama ambavyo baadhi ya
Masahaba (r.a) wanayo mambo maalum na sifa za ziada
wasizoshirikiana kwazo na mwengine yeyote yule hivyo ni wajibu
kumpa kila mwenye haki; haki yake, na jambo lenyewe ni pamoja na
Hadithi ya Kisaai mashuhuri ambayo ndani yake imo sifa kubwa kwa
baadhi ya Aalil Bait ( r.a) na kuingiza baadhi ya watukufu wa Aalil
Bait ( r.a) kama vile Hassan na Hussein, nao ni katika jamaa wa
Mtume (s.a.w) ambao hawakuwa wakiishi kwenye nyumba ya Mtume
(s.a.w) kwenye hukumu ya aya tukufu, hivyo haifahamiki sio katika
wa karibu au wa mbali toka katika hadithi hii kubinya Ualil Bait ( r.a)
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
14
kuwa wa Ali pekee, Fatma, Hassan na Hussein (r.a) na tukawakusanya
pamoja nao, na pia katika hadithi hii haifahamiki kuingizwa na
kutolewa kwa wengine, sio katika sharti la kuingizwa hawa ni
kutolewa mama wa waislamu - Allah awaridhie wote- na rehema za
Allah zimepanua kila kitu, hivyo kamwe hazimbinyi mmoja kwa ajili
ya mwengine, lau mtu angesema nae anao ndugu kumi; Omar, Ali na
Khalid ni ndugu zangu. Jee hii inamaanisha kwamba saba waliobakia
sio ndugu zake? Haya huja kwenye maneno ya waarabu kwa wingi
bali hata kwenye Quran Tukufu, mfano wa kauli yake Taala :{Hakika
idadi ya miezi mbele ya Allah ni miezi kumi mbili kwenye Kitabu
cha Allah siku Allah aliyoumba mbingu na ardhi miongoni mwao imo minne mitukufu (hurum), hiyo ndiyo dini iliyonyooka } [at
Tawbah :26], yaani hiyo ndiyo dini iliyonyooka, na kwamba dini
iliyonyooka imefupishwa kwenye idadi ya miezi na kuwa miongoni
mwao imo miezi mitukufu, basi kadhalika kauli yake (s.a.w) kwenye
hadithi ya Kisaa –nguo-"Hawa ni Ahlil Bait yangu " Anamaanisha
watu wa nyumba yangu kama tulivyobainisha.
Nasi tunaweza kusema kuwa iwapo Hadithi ya Kisaai inazuwia
kuingia mmoja wa Ahlil Bait, basi vipi kaingia humo Ali bin Hassan
bin Muhammad, Muhammadi al-baaqir, na Jaafar Sadiq na wengineo?
miongoni mwa Itra watukufu waliobakia, na hawa bila shaka asilani
hawakuwepo kwenye tukio la kutukuza kwa ajili ya Kisaa.10
Jambo la nne:
Kwamba kutegemea nasabu pekee haitoshi; Kama ilivyo kuwa ni wajibu juu yetu mapenzi ya (Aalil Bait mmoja ),
kwa sababu ya imani yake kwa Allah na nasabu yake na ujamaa wake
kwa Nabii (s.a.w), basi ni wajibu pia kwetu kumchukia kwa kiwango
cha maasi yake, hali yake ni hali ya mtu mmoja mmoja wa umma huu
10
Angalia 9Aayatu tathiir cha 'Abdil Haadil Husseiny (uk. 20)
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
15
na "Na yeyote yule aliefanya upole wa amali yake basi kamwe nasabu
yake haitomuharakisha."11
Jambo la Tano:
Ufanyaji wa Ualil Bait ( r.a) kuwa wa Ali, Fatma, Hassan na Hussein
(r.a) na kwenye watoto tisa wa Hussein tu, kwa hali yoyote ile haisihi,
ufanyaji wa Ualil Bait ( r.a) kuwa wao peke yao ni kinuyume na
uhakika wa mambo . Na katika ufanyaji wa Ualil Bait ( r.a) kuwa wao
peke yao wamefutwa wengi wa walio Aalil Baitin Nabawy
iliyotukuka, na ndani yake umo unyimwaji wao wa nasabu hii
iliyotoharika, na haki zinazotokana nazo kiibada, kimazingatio na
kimali kwao na juu yao, Allah alizowateulia na kuwakadiridhia juu
yao, hapa sipo pahala pa kuzielezea kwa urefu .
Na katika yaliyokuwa hayana shaka ni kwamba ufupishaji wa ujamaa
wa juu ya waliotajwa (r.a), kwa vyovyote vile kunapelekea upunguzaji
wa kizazi cha Mtume (s.a.w) na haingii akilini mtu yeyote yule kuwa
mtu anaweza kuleta jambo hili .
Inatupasa kukuwauliza watu hawa :
• -Wako wapi maami wa Mtume (s.a.w) ?
• -Jee Hamza (r.a) sio katika watoto wa Abdil Muttalib?
• Upo wapi utajo wake jee yeye siye simba wa Allah na Mtume
wake, shahidi wa Uhud na shujaa wa Badri? Na pale
alipostashhadi Nabii (s.a.w) akahuzunika huzuni ambyo
hajawahi kuhuzunika kabla yake ?
• -Jee Nabii (s.a.w) hakusema "Bwana wa mashahidi mbele ya
Allah siku ya kiama ni Hamza"!?12
11
Sehemu ya Hadithi :aliyoismulia Muslim :Mlango wa fadhila za
kukusanyika kwenye kisomo cha Qur-n ikatika Hadithi ya Abi Hureirah(r.a)
nam. (2677) 12
Ameisimulia Hakim kwenye (mustadrak )( 120/2 ) na akasema (Swahihul
Isnad) na Dhahaby akampinga kwenye (Talkhis ) .Na Muhaddith albany
ameihukumu kwenye (As silsilati as Swahiha ) nam.(716 /nam 374)kuwa ni
sahihi kutokana sanad zake na shahid .
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
16
• Jee Abbas (r.a) sie katika watoto wa Abdul Muttalib na
ameshuhudia ukombozi wa Makka, na mwenye kuthibiti siku
ya Hunein pamoja na waliothibiti?
• Jee haikusimuliwa "Hakika Abbas (r.a) ni katika mimi na
mimi ni katika yeye?"
• Jee vile vile Nabii (s.a.w) hakusema:" Enyi watu !Yeyote
aliemuudhi ami yangu basi huyo ameniudhi mimi ; hakika
ami wa mtu ni mfano wake" 13
• Wako wapi watoto wa maami wa Mtume (s.a.w).?
• Jee Jaafar At Tayaaru – mwenye kuruka kwa mbawa – (r.a)
mtu mwenye mambo bora na yenye kushukuriwa?
• Jee yeye siye aliyesemewa na Nabii (s.a.w) (umeshabihi
umbile na tabia zangu )? 14
• Jee Yeye hakuwa mmoja wa watangulizi kwenye uislamu ?
• Jee hakuwa miongoni mwa waliohamia Uhabeshi, na
kuendelea kuwa huko mpaka Mtume (s.a.w) alipohamia
Madina, akaja siku ya ukombozi wa Khaibar, na Nabii (s.a.w)
akafurahi furaha kubwa na kumkumbatia na kumbusu baina
ya macho yake ?
Imesimuliwa kwamba alimwambia :"Sielewi ni kwa jambo lipi mimi
ni mwenye kulifurahia zaidi;ukombozi wa Khaibar au kuja kwa
Jaafar?"15
Pale Nabii (s.a.w) alipompeleka Muuta kuwa naibu wa Zaid bin
Haaritha (r.a) alifanya kazi kubwa kwenye njia ya Allah, akapigana
13
Ameismulia At Tirmidhy akasema (Hassanun Swahihun ) na (Ahmad )
(165/4), akadhoofishwa pia na Muhadith Albaany . kwenye Silsialti
Dhaiifah(446/2 nam .806 ).
14
(Hakim kwenye Mustadrak) (325/3) (Swahihul Isnaad )
Ameismulia At Tirmidhy 15
Imesimuliwa na Bayhaqy kwenye (Sunanil Kubra) (101/7) kwa Sanad
yake ni mpaka kwa shaaby toka kwa Nabii(s.a.w) kwa hiiyo.Na aksema:"Hii
ni Mursal"
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
17
mpaka akakatwa mikono yake miwili na akastashhadi, Allah
akamlipa mbawa mbili kwa sababu ya mikono yake hiyo miwili
Peponi, kama alivyotolea habari Assadiqul Masduq (s.a.w) basi tokea
siku hiyo duniani akapewa jina "Attayaar" ?
Nabii (s.a.w) zilipomfika habari za kustashhidi kwake alihuzunika
huzuni kubwa na kusema "Usiku wa jana niliingia Peponi nikamuona
Jaafar anaruka pamoja na Malaika. "16
Na akasema (s.a.w) (Jaafar alinipita kwenye kundi tukufu la Malaika,
huku mbawa zake mbili zikiwa zimepakwa damu zikiwa nyeupe).17
Hivyo baadhi ya sifa zake zinazojulisha ukubwa wa hadhi yake na
utukufu wa cheo chake duniani na akhera, Allah amridhie yeye na
yeye amridhie.
Jee Abdillah ibn Abbas wino wa umma –huu- na mfasiri wa Quran
aliyeitwa wino kutokana na wingi wa elimu yake, fahamu zake na
ukamilifu wa akili na wingi wa fadhila zake. Kwanini isiwe hivyo,
wakati Mtume (s.a.w) alimuombea dua ya kuwa na fiqhi ya dini na
elimu ya utambuzi? 18
nae alikuwa katika walioshuhudia Jamal na
Swifin pamoja na Ali (r.a), na Masahaba wakuu (r.a ) na Matabiina
walikiri ubora huu kwake –Allah awaridhie kwa wema-.!
Kiko wapi kizazi cha Ali (r.a) nacho ni wengi ?
Kiko wapi kizazi cha Hussein (r.a) kilichobakia na miongoni mwao ni
wajukuu wa Shahidil Kuufah, Zaidi bin Ali bin Hussein, na kizazi cha
watoto wake waliobakia ?
16
(Hakim kwenye Mustadrak) (196-209) na akasema (Swahihul Isnaad ) na
akahukumui usahihi wake kwenye (Mukhtaararah ) Muhadith Albaany .
kwenye (Swahiih Jaamii :3358 ) angalia Silsialt Swahiiha (227/3 chini ya
nam.1226) . 17
(Hakim kwenye Mustadrak) (312/3) na kusema (iko kwenye sharti la
Muslim ) na kuafikiwa na Muhadith Albaany . kwenye (Silsialt Swahiiha)
(226/3 chini ya nam.1226) . 18
Muttafaqun 'Alaihi
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
18
• Zipo wapi haki zao hawa ?
• Jee wao ni katika Aalil Bait ( r.a) au sio ?
• Na iwapo wao hawamo basi ni nani huyo aliyewatowa?
• Na kwa dalili na hoja ipi inajusurishia tendo hili ?
• Jee ipo njama nyuma ya ovu hili ? 19
Mjadala wa maudhui hii na uwazi wake hapa sio pahala pake, ila
tumetaja hayo kwa lengo la kumtanabahisha msomaji mpendwa
kwamba Historia ya Aalil Bait ni pana, kubwa na tukufu kuliko
wanavyoitaja baadhi.
Aalil Bait ni wengi Allah awazidishe na kuwabariki, nao ni wale
walioharamishiwa sadaka, ambao ni: Bani Hashim, wake wa Mtume
(s.a.w) nao ni katika ahli zake –jamaa wa kufuatia sio kwa uasili kama
ambavyo makumi ya nasi zilizothibiti zilizowazi zilivyojulisha hivyo;
hivyo ni kwamba kabla hawajaolewa na Mtume (s.a.w) hawakuwa
kati aali wa nyumba yake na nasi mutawatiri ni nyingi kwenye vitabu
na nasi ambazo zinabainisha tuliyoyataja ni kutowafunga Aalil Bait (
r.a) kwenye Ali, Fatmah na baadhi ya kizazi cha Hussein Allah wote
awaridhie, amesimulia Muhammad bin Sulaiman al Kuufy :" Hussein
bin ‘Uqbah alimuuliza Zaidil Aram :"Ni nani Aalil Bait yake ( r.a) jee
wake zake sio Aalil Bait wake ( r.a) ?
Akasema :"Hakika wake zake ni ahli zake, lakini Ahli beit yake ni
wale walioharamishiwa sadaka juu yao baada ya yeye akamwambia
Hussuein "Ni nani hao ewe Zaid?" akasema ni jamaa wa Jaa'far, jamaa
wa Aqiil na jamaa wa Abbas "20
Khuily nae ameeleza hivyo, na akasema kwenye Kauli yake
Taala:{Na wenye ujamaa} [Al Hashr:7] "Yaani jamaa wa Nabii
(s.a.w) nao ni aal -jamaa wa - Ali , aal-jamaa wa - "Abbas, aal-jamaa
19
Angalia Aalil Bait wa (Hukuukuhum Shariyyah ) cha Qadhi Swalih
Darwiish (uk . 9-12 ).
20
(Manaaqib Amiiril Muuminiin (a.s) (116/2) na akaashiria hivi pia arbili
kwenye Kashfil Ghummah na …. )
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
19
wa Jaafar na aal-jamaa wa- 'Aqiil (r.a), na kamwe hakushirikiana na
yeyote mwengineo, na wajhu huu ni sahihi kwani unawafikiana na
madhehebu ya Muhammad (s.a.w) "unajulisha wale waliotajwa kwao
wao"21
Amesimulia Assidiq kwamba Ali (r a) amesema "Ewe Mtume wa
Allah hakika wewe unampenda Aqiil: Akasema "Naam Wallahi,
hakika mimi ninampenda mapenzi mawili: mapenzi kwa ajili yake na
mapenzi kwa ajili ya Abi Twalib kwake, na kwamba mwanawe
atauliwa kwa sababu ya kumpenda mwanao.. mpake pale aliposema:
"Nashitakia kwa Allah kwa yatakayowakuta jamaa zangu baada
yangu"22
Hivyo akamuingiza Uqail na wanawe wawili kwenye wanaoitwa -
jamaa waliotoharika (al ataratit taahirah)-.
Jambo la Sita:
Nyingi ni kauli baina ya kurasa za vitabu vyenye shubuha ambavyo
vinadai kwamba Aalil Bait ( r.a) wamedhulumiwa na kukandamizwa
miaka kadha tokea kifo cha Nabii (s.a.w) na kupitia kwenye zama
Makhalifa waongofu mpaka kwenye Dola ya Umawiyyah na
Abbaasiyyah na hakuna yeyote yule miongoni mwa Aalil Bait ( r.a) ila
ameteseka kwa kufungwa, kuuawa, kuhamishwa, kutiliwa sumu au
madai zaidi ya hayo .
Haya hujibiwa kwa njia mbili :
Wajhi wa mwanzo :
Kwamba msingi wa ahli Sunna wal Jamaa na jambo ambalo halina
khitilafu katika hilo na kuwa makubaliano baina yao ni kuwaheshimu
Aalil Bait ( r.a) kujuwa fadhila na ujamaa wao kwa Nabii (s.a.w) na
wasia wake kwao amesema: Nabii (s.a.w) ''Na watu wa nyumba yangu
nakukumbusheni Allah kwenye watu wa nyumba" "nakukumbusheni
21
()'Umdatu'uyuunSahhahil Akhbaar)cha Hully(6-7). 22
( Amaalit Tuusy ) uk. (191 ) na Bihaarul Anwaar cha Al Majlisy
(288/22,44/287)
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
20
Allah kwenye watu wa nyumba yangu","nakukumbusheni Allah
kwenye watu wa nyumba yangu "23
Hivyo Aqida ya Ahli Sunnah wal
Jamaa imo kwenye vitabu vyao; vitabu vya Hadithi vitabu Aqidah,
vitabu vya Fiqhi, vitabu vya Tarajum na Sirah ambamo kila mwenye
kitabu hutaja kwenye sehemu iliyo na mnasaba na habari hiyo. Hivyo
kwenye vitabu vya Hadithi utaona milango kuhusiana fadhila zao,,
kwenye vitabu vya Aqida utaona ubainishaji wa itikadi kuhusiana na
wao, kwenye vitabu vya Fiqhi utaona milango kuhusiana na
yanayohusina nao katika ahkami, kama vile kuharamishwa sadaka juu
yao, na vitabu vya Tarajum na Sirah vinataja utajo wao, maelezo
kuhusiana na wao na taarifa zao.
Huu ndio msingi kwa Ahli Sunnah, msingi huu kamwe hauwezi
kuporomoka ila kwa dalili iliyo ya wazi, na tunaposoma Historia na
tutaona kwamba hayo yanayodaiwa na baadhi yao kuhusiana na
ukandamizaji wa Ahli Sunnah na viongozi wao kwa aal beit ni batili
yasiyosihi wala kuthibiti ila pale panapokuwa na kinyang'nganyiro juu
ya uongozi na madaraka kama ilivyotokea kwenye mapinduzi ya
Imam Zaid, Allah amrehemu yeye na wengine.
Amesema Sheikhul Islaam Ibni Taymiyah ( ""! ار#) "Ama yule
aliyemuuwa Hussein, au kusaidia basi huyo amethibitikiwa na laana "
ya Allah. Malaika na watu wote"24
Hivyo haisihi kabisa muislamu kupaka matope historia ya Aalil Bait
(r.a) iliyosafi na mapenzi ya waislamu kwao kwa kisa cha batili au
riwaya ya uongo kama vile anavyofanya Al Asfahaany kwenye kitabu
chake (Muqaatilut Twalibiin), kitabu cha Al Asfahaany kilichopewa
anwani ya (Muqaatilut Twalibiin) ni kitabu kilichojaa batili na uongo
wa kihistoria ambao mwandishi yeyote anashindwa kuyathibitisha
kabla hajawarembea ahli Sunna wal Jamaa uongo huu ulio mkubwa .
23
Swahihu muslim(Hadithi nam.2424) 24
Majmuu Fataawa )(487/4).
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
21
Vitabu vya kihistoria vimesheheni habari za kuheshimiwa kwa Aalil
Bait (r.a) na Makhalifa, kuwapenda na kuwapa kwao hadhi :
Amesema Abu Bakri (r.a) "Mchungieni Muhammad watu wa nyumba
yake"25
Na akasema (r.a) "Naapa na yule ambaye nafsi yangu iko
kwenye mikono yake hakika ujamaa wa Mtume wa Allah (s.a.w)
kwangu mimi ni bora zaidi kuliko asili ya jamaa wangu "26
Nae (r.a)
akasema vile vile akiwa anazungumza na Fatma na Ali "Wallahi
kamwe sikuwacha nyumba wala mali, na jamaa na watu wa
nyumbani, ila kwa kutafuta ridhaa ya Allah, ridhaa ya Mtume wake na
ridhaa ya jamaa zake"27
Abu Bakri (r.a) alipeleka mmoja wa wake zake nae ni Asmaa bint
Umeish kwenye nyumba ya Ali kwa lengo la kumuhudumia kwa tiba
Fatma (r.a) wakati wa ugonjwa wake bali pia akashiriki kwenye
kumkosha Fatma Az Zahraa na kumvisha sanda (r.a)28
Amesema Umar Ibn Al khatab (r.a) kumwambia Fatma (r.a) "Ewe
binti wa Mtume wa Allah hakuna yeyote kipenzi zaidi kwetu katika
viumbe kuliko baba yako na hakuna yeyote kipenzi zaidi kwetu katika
viumbe baada ya baba yako kwetu kuliko wewe.29
Inatosheleza
kwamba Omar alimteua Ali (r.a) kuwa katika jumla ya kundi ambalo
ndani yake muwe na khalifa wa waislamu baada yake"
Na Omar Alimuoa binti ya Ali -Ummu Kulthuum- (r.a)
Hivyo hivyo hali pamoja na Khalifatir Rashid Othman bin Affaan,
historia yake ni yenye kumeremeta kwa wingi kutokana na misimamo
25
Akasema pia (r.a) 26
Imesimuliwa na Bukhary (3713) mlango wa sifa za Hassan na Hussein . 27
Angalia (As Sunanil Kubra) cha Bayhaqy 301/6,na (Bidaaya wan Nihaaya)
cha Ibni Kathiir253/5.
Akasema Ibni Kathiir :"Hii sanad yake ni sahihi ,yenye nguvu"
28
Angalia Al Istiiaab cha Ibni 'Abdil Barri 387/4 na (Asmaal Matwaalib )
cha As Swalaaby 160. 29
(Muswannaf Ibni Abii Shaibah ) 567/14, na isnadi yake ni sahihi.
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
22
ya kushirikiana baina yake na baina ya Aalil Bait ( r.a) na namna
alivyokuwa akishauriana na Ali kwenye kadhia kadha, bali uhakika
wa uhusiano huu wa kidugu unatudhihirikia namna Ali
alipowasimamia wanawe kwenye kumlinda Othman bin Affaan siku
alipostashhadi kwenye nyumba yake (r.a) na hivyo ni kwa ajili ya
mapenzi kwake na mapenzi ya Othman bin Affaan kwake kwani
msimamo wao ni kujizuwia na vita.30
Imeelezewa kwamba Harun
Rashid alikwenda kwenye kaburi la Nabii (s.a.w) akijifakharisha kwa
watu, akasema Assalamu Alaikum Ewe Mtoto wa ami-yangu – kwani
yeye ni katika kizazi cha Al Abbas bin Abdil Muttalib, akaja Musa bin
Jaafar kamwambia; Assalamu 'alaika ewe baba yangu, Harun Rashid
anaangalia, akasema Wallahi huku ni kujifaharisha.
Harun Rashid akasema "Nimepata habari kwamba wengi
wananidhania mimi namchukia Ali bin Abi Talib, na Wallahi mimi
kamwe simpendi yeyote kama ninavyompemnda yeye."31
Khalifa Muadilifu Umar bin Abdilaziz alimwabia Fatmah bint Ali bin
Abi Talib (r.a) "Ewe bint Ali Wallahi kwenye uso wa ardhi hii hakuna
Aalil Bait ( r.a) vipenzi kwangu kuliko nyie na nyie ni vipenzi zaidi
kwangu kuliko jamaa zangu"32
Watu walijikumbusha Zuhudi na Mazuhadi basi kundi moja likasema
fulani na jengine likasema fulani Umar bin Abdilaziz akasema: zahid
kuliko yeyote yule ni Ali bin Abi Talib (r.a)"33
30
Tarekhe Dimashq cha Ibnl 'Asaakir 402/1 na Twabaqaat Ibn Saad 128/8. 31
Tarekheul Khulafaa cha as Suyuuty uk. 293. 32
Angalia Twabaqatil Kubraa cha Ibni Saad 388/5 33
Siya'Umar cha Ibnil Jawzy 292.akiwa amenakili tokakwenye(Ad Dawlwtul
Umawiyyah cha Daktari As Swallaaby .)
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
23
Wajhi wa Pili
Hakika jambo kubwa na lenye hadhi kubwa toka kwa watu na hasa
hasa akiwa ni katika wema wa umma na maulamaa wake Allah (S .W)
analomfanyia mtihani ili amnyanyulie hadhi na daraja yake kwenye
Pepo zenye neema, hivyo mwenye kupata mtihani mkubwa au kuuawa
miongoni mwa ahlil Bait kama ilivyotokea kwa Hussein (r.a) -Shahidi
mwenye kufanikiwa, basi huwa ni namna ile (Allah anapompenda mja
humfanyia mthani), na jambo hili sio maalum wala kukusudiwa ahlil
Beit (r.a) tu bali dhuluma imetokea juu ya maulamaa wengi wa Sunna
na wakuu wao kama vile Said bin Jubeir, Imam Abu Hanifa, Imam
Malik na, Imam Ahmad na wengi wengineo miongoni mwa wema wa
umma wa Muhammad (s.a.w).
Dhuluma, ukandamizaji na mabalaa yamewatokea Manabii wa Allah
(a.s) na wema waliokuja baada yao, huyu Daniel (a.s) aliekutana na
mabalaa ya aina ya mwisho ya ukandamizaji aliyofanyiwa na mfalme
mwenye kiburi "Bakhtanasir" kwa kumfunga na akamuingizia simba
wawili lakini Allah akamuhifadhi na kumlinda dhidi yao.34
Hivyo hivyo kisa cha Nabii wa Allah Yaqoub (a.s) kwa kupotelewa na
mwanawe, Nabii wa Allah Zakariyyah, Nabii wa Allah Mussa (a.s)
mbele ya mwenye kiburi Firaun, Nabii wa Allah Issa (a.s) pamoja na
mayahudi, Nabii wa Allah Muhammad (s.a.w) akiwa na Makureshi na
makafiri wa Makka, na visa vyao ni mashuhuri vyenye kujulikana.
Na baada yao ni Masahaba wa Nabii (s.a.w) waliohama toka kwenye
nchi zao, mali na jamaa zao, waliadhibiwa kwa aina za adhabu na
kuendelea mpaka baada kufariki kwake Nabii (s.a.w) yalitokea
yaliyotokea kwa waliokuwa kabla yao miongoni mwa watukufu,
Omar al Faruq (r,a) aliuawa kwa khanjari ya khiyana na chuki, akiwa
anasalisha kwenye mihirabu, hivyo hivyo Shahidudaar Othman bin
Affaan (r.a) aliyeuawa kwenye nyumba yake akiwa anasoma Quran,
hivyo hivyo ndivyo alivyouawa amiiril Muuminiin Ali (r.a) akiwa
anatangaza :"Enyi watu sala! Sala!, na wengineo katika Masahaba
34
"Al Bidaaya wa An Nihaaya " cha Ibni Kathiir 428/1
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
24
wema, na kadhalika balaa na ukandamizwaji yamewapitia maulamaa
wengi na wakuu.
Huyu hapa Imamu Al Awaza'iy –Allah amrehemu –alifikwa na balaa
kubwa mbele ya mmoja wa wenye jeuri na kukaribia kumuawa,
Habari za Imam wa Ahli Sunna Imam Ahmad–Allah amrehemu –
pamoja na Khalifa Muutaswim ni mashuhuri na zenye kujulikana,
hakika alimuadhibu na kumpiga viboko mpaka mgongo wake
ukachanika na kuchunika ngozi, akamfunga gerezani na kumbana 35
Pale Fatimiyina walipotawala Misri waliwakandamiza maulamaa na
miongoni mwao alikuwa Imam Abi Bakri An Naablisy, wakaamrisha
kupigwa kwenye siku ya mwanzo kisha siku ya pili kutundikwa mbele
ya watu, kisha siku ya tatu yake kuchunwa na kutolewa ngozi toka
kwenye nyama yake, kwa kisu cha kiyahudi .36
Imam Nuaim bin Hamad aliekufa akiwa amefungwa kwa minyororo
gerezani na kumuondowa akiwa maiti wakamrembea shimoni bila ya
kuoshwa .37
Imam al Harawyil Answaary anasema:"Nilionyeshwa upanga mara
tano, siambiwi rudi kwenye madhehebu yako, ila naambiwa nyamazia
waliokutangulia, huku nasema sinyamazi ."38
Mifano ni mingi mno, na lengo ni ukandamizaji na dhuluma juu ya
Ahli Sunna na maulamaa wake, kama ilivyotokea kwa wenginewe, na
mtukufu hufanyiwa mitihani, na kamwe hawatowachwa kufanyiwa
mitihani. .
35
Sira ya Imama Ahmad cha Ibnil Jawzy. 36
" Hashia ya Al Bidaaya wa An Nihaaya " 284/11, na "Al 'Ibar fii Akhbaaril
Ghubar " cha Ad Dhahaby 33/2 37
Angalia (As Siyari a'alaamin Nubalaa) cha Adh Dhahaby 610/10 38
(As Siyari a'alaamin Nubalaa) cha Adh Dhahaby 509 /18
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
25
MLANGO WA NNE
Miongoni Mwa Vitabu Muhimu vyenye Kutegemewa kwenye
Historia
Mwenye lengo la kujuwa vianzio vya Tarekhe vyenye kukubalika,
anaweza kupata kwenye vitabu vya tarekhe na Hadithi zenye
kuwekewa sanad maalum kwa maelezo ya historia za watu na watu
maalum na historia zao, ni sawa iwe watunzi wake wamejiwekea
sharti atika maulamaa wenye kukubalika usahihi kwenye kuzitaja
kwao, au kwa kutolea maelezo juu ya riwaya kuhusiana na usahihi na
udhaifu wake, hivyo vitabu vimemtoshelezea msomaji wake tabu za
kutafiti na uhakiki, ama vile vitabu ambavyo wasimulizi wake
wanasimulia kwa sanadi bila ya kubainisha hali zake basi ni wajibu
juu ya msomaji wake kuhakikisha usahihi wake.
• Na hivi hapa ni baadhi ya vianzio vya Kihistoria ambavyo
inawezekana kutegemewa katika usomaji na kuandika
Historia ya kiislamu ,tunavitaja minogoni mwao: 1. Kitabu" Tabaqatil Kubraa" cha Ibni Saad aliyefariki
mwaka 230 H:
Nacho ni kitabu muhimu katika mlango huu ; kwani yeye –Allah
amrehemu –anataja riwaya kwa sanadi zake, hivyo msomaji hana kazi
yoyote ile isipokuwa kufanyia utafiti sanadi hizo ikiwa ni mwenye
uwezo wakufanya hivyo, na katika sifa zenye kutofautisha kitabu
hichi na chengine ni kwamba ni katika vitabu vilivyotangulia na
vianzio vya Sira ya Nabii (s.a.w), Tarajumi na habari, mtunzi wake
aliwahi karne ya pili hijriyya pamoja na kuchukulia tahadhari riwaya
za Waaqidiy, na madhaifu na matrukina (wenye kuwachwa riwaya
zao) na wenginewe, au kama haelewi basi aulize wanaolewa kama
alivyoamrisha Allah Azza wa Jalla kwenye Kitabu chake kitukufu.
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
26
2. Taariikh Khaliifati bin Khayyaat ": Nacho hata kikiwa ni kidogo zaidi kuliko kitabu 'Tabaqatil kubra"
ila ni kwamba kinayo sifa ya ziada ya usalama wa matini zake
katika udhihirishaji wa fitina ,na mara nyingi yaliyotokea kwenye
zama za Masahaba (r.a).
3-(Tarekheil Umam wal Muluuk) maarufu (kwa Tarekhet
Twabary)
Nayo ni Tarekhe iliyojaza habari, athari na riwaya, lakini
imechanganya yaliyokonda na yaliyonona, na hakuna lawama
kwa Twabariy, kwani yeye ameweka sanadi kwenye riwaya hizi,
na mwenye kuwekea sanad basi huyo ameshajiondoshea dhima na
lawama, na tumeshabainisha kwa uwazi kwenye utangulizi wa
kitabu .
4-Al Bidaaya Wan Nihaaya Cha Imam Ibni Kathiir:
Mtunzi wa kitabu cha “Tafsiiril Quran al Karim “,kitabu hichi
hata pamoja na kwamba ananukuu riwaya zake toka kwenye
baadhi na vianzio vilivyotangulia ila tu ni kwamba kinayo
maelezo juu ya riwaya nyingi za kihistoria kuhusiana na usahihi
na udhaifu, kutokana na kuwa kwake Imamu kwenye hadithi na
elimu zake, na chapa bora zaidi ni chapa ya Daaril Hijra chini ya
usimamizi wa ‘Abdillahi Turky.
5-“Taariikh Dimashq “ cha Ibn ‘Asaakir:
Nayo ni historia iliyojaza ni makhsusi kwa walioingia Damascus
miongoni mwa maulamaa katika masahaba na wengineo mpaka
kwenye kipindi cha mtunzi, nacho kinatofautiana na vyengine
kwa kuwa na sanadi kwa kila tukio’
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
27
6-“Tarekheul Islaam” cha Shamsid Diin Adhdhahaby
Nacho ni kitabu kikubwa chenye manufaa makubwa, husimulia
kisa kamili cha historia ya kiislamu, na vielelezo vyake na
matukio yake muhimu, kina sifa ya ziada inayotokana na maelezo
ya imam juu ya taarifa za matukio ya kihistoria, matukio na athari.
Nae imam Dhahaby ni bahari kwenye elimu ya Jarhu na Taadiil
ni katika maimamu wakubwa katika fani hii, na Daktari Bishar
Awaadh Maaruuf amefanya kazi kubwa ya kufanyia uhakiki,
kitabu hichi kinahesabiwa kuwa ni katika chapa bora zaidi.
7-“Siyaru ’Alaam Nubalaa” cha Hafidh Adhdhahaby ( ! ار#)
Nacho ni kitabu chenye manufaa vilevile, kinatowa sira na habari
za nyota na muhimu katika maulamaa zilizojulikana katika
historia ya kiislamu tokea mwanzo wa kipindi cha Masahaba (r.a)
mpaka karibu ya kifo cha mwandishi ( ! ار#), nae
ameambatanisha na kitengo maalum kwa Sira ya Nabii (s.a.w) na
historia za Makhalifa wanne waongofu na chapa bora zaidi ni ile
chapa ya Muasasat Risaalah.
8.”Taariikhul Madiinah cha Ibn Abii Shaibah
Ni kitabu kilichojaa faida, Ibn Abi Shaibah ametilia umhimu
mkubwa utajaji sanadi kwenye hadithi na habari zilizo nyingi, na
ndani yake zimo riwaya muhimu kuhusiana na fitina na mauaji ya
Shahidi Othman bin Affaan (r.a), na kitabu kina kosoro ya baadhi
ya maudhui zake kutokana na kupotea kwa baadhi ya miswada,
kwa mfano ukhalifa wa Abi Bakr haumo kwenye kitabu.39
.
9- “Tarekhe Ibn Khulduun”
10-“Al Muntadham fiy Att arikh “ cha Ibnil Jawzy .
39
Angalia Mpango wa uandishi wa historia ya Kiislamu cha Muhammad
Swamil as Salmy.
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
28
11-“Awaaswim minal Qawaasim” cha Abi Bakr bin Al ‘Araby
Kimehakikiwa na kutolewa maelezo na sheikh Muhibbudini al
Khatib (r.a), na kitabu hichi kimechapishwa mara nyingi, na
kukubalika kwa wasomi wakuu na wengineo kutokana na nafasi
na hadhi ya mtunzi wake ambaye ni katika maimamu. wa
Kiislamu Abi Bakr bin Al ‘Araby na kutokana na hoja zilizowazi
na majibu yanayotosheleza kwa masuala mengi muhimu, hivyo
kitabu ni cha aina yake kwenye uwanja wake, anakuja na
(Qasima) shubuha, anaifuatanisha na uchambuzi na kuweka wazi
shubuha (‘Aswima ), na kuijibu kwa hoja, dalili sahihi.
Hivi ndivyo vitabu muhimu vilivyotolea umuhimu uelezaji wa tarekhe
na matukio ya kiislamu , na vyenginevyo vipo vingi katika uwanja
huu ,ni sawa viwe vya zamani au vya kisasa .
Kamwe haituondekei kwenye kiini chake kuashiria kwamba vipo
vitabu sio makhsusi kwa Tarekhe, na humo mumewekwa matukio
muhimu, na habari za kimsingi kwenye Tarekhe ya kiislamu, na hasa
kwenye zama za mwanzoni, mfano kama vile vitabu vya hadithi,
Masanidi Maajim, na muhimu vyao :
1-“Asahihi “ ya Imam Bukhariy .
2-“Asahihi “ ya Imam Muslim .
3-“Sunanul Arb’a” ya Abi Daud, Annasai, At Tirmidhy, na Ibn
Maajah .
4- “Al Musnad “ cha Imam Ahmad bin ‘Hanbal.
5- Al Muswannaf cha Ibni Abi Shaibah .
6-“ Mustadrak “ ya Haakim Nisapury.
• Ama vitabu vya tarajumi za Masahaba –wakiwemo Aalil
Beit- (r.a) vya kimsingi n amuhimu ni kama :-
•
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
29
1-Al Istii’aab fiil Ashaab cha Ibni ‘Abdil Barr .
2-“Usudul Ghaabah fii tamyiiz Sahaabah “ cha Ibni;l Athiir .
3- Al iswabah fi Tamyiiz Sahabah cha Ibn ‘Hajaril ‘Asqalany
.
Vitabu hivi ni vyenye habari na athari, na tunakumbusha kwamba
habari na athari hizi vinalazimikiwa na mizani ya uhakiki na utafiti
hasa katika kufahamu sanadi na kuhusiana na Jarh na Taadiil; ili
kujuwa sahihi kutokana na dhaifu .
• Ama vitabu vy kisasa :Wapo watafiti waliosafisha na
kudadisi riwaya, wakabainisha sahihi toka kwenye dhaifu
zake, hapa tunaashiria baadhi ya vitabu muhimu katika
vitabu hivi, mfano, Mtungo wa vitabu vya Daktari Ali bin
Muhammad As Swallaaby Allah amuhifadhi na ambariki
katika kuwepo kwake :
•
I -Al Inshiraah fii raf -i dhiiq siirati Abii Bakr.
2-Faswlil Khitaabi fii siirati Amiiril Mu-u- miniin Omar ibn Khatab
shakhsiyyatuhu wa Asruhu .”
3- Taysiiril Kariim fii sirati ‘Uthman bin ‘Affaan ‘’
4- Asmal Matwaalib fii siiratilAmiiril Muuniin Alibin Abi Talib “
5- Amiiril Muuniinal ‘Hussein bin Ali–Shakhsiyyatuhu wa ‘asrih I”
6-“Muawiya bin Abi Sufyaan “
7-“Omarbin ‘Abdil ‘Aziiz “
8-“Ad Dawalatul Umawiyyahtu ‘Awaamilil Idizdihaar wa
Tadaa’iyaatil anhiyaar”
Kadhalika vipo baadhi ya vitabu muhimu, mfano :
1- “Mausuatu Taariikhil Islaamy “ cha Muhammad Shaakir
2-Silsilatu KutubulMahmuud Muhammad Shaakir kuhusiana na
shakhsiyati40
za kiislamu .
40
Watu muhuhimu
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
30
3-Siiratiu ‘Aaisha bint Ummul Mu-u –miniin “ cha Annadawy .
“Ahdathi wa ahadithi fitina".cha Daktari Abdil ‘Aziiz ad
Dakhkhaan :
Nacho ni kitabu chenye umuhimu wa kiwango cha juu katika kufanyia
uhakiki msimamo wa Masahaba kuhusiana na fitina zilizotokea, na
utafiti wa udadisi kwa wingi wa riwaya zilizokuja kuhusiana na jambo
hili, pamoja na maana ya fitina, msimamo wa Masahaba kuhusiana na
fitina hiyo, kubainisha sababu na athari zake, msimamo wa muislamu
kuhusiana na fitina hiyo na kitabu ni kutokana na risala ya udaktariri
na kimechapishwa na Maktabati Swahaabah Sharjah chapa ya
Mwanzo.
5- ‘Hiqbatun minat Tarekhe “ cha Sheikh ‘Uthayman Khamis :
Kitabu hichi kinahesabiwa kuwa ni vitabu muhimu vya wakati huu
mtunzi ametolea umuhimu kutaja miongoni mwa habari zilizosihi
katika habari na athari zilizokuja baada ya kifo cha Nabii (s.a.w),
mpaka kipindi cha kuuawa kwa Al Hussein (r.a) pamoja na kuweka
rai wa usahihishaji baina ya rai hizo
Viwanda vingi vya kupiga chapa vimekipiga chapa, na chapa yake
bora ni ile chapa ya Maktabatil Imamil Bukhaary -Ismailiya Misri-.
6-“Tahqiiq Mawqifis Swahaabati minal Fitan" cha Daktari
Muhammad Amhazuun.:
Nayo ni kazi ya risala udaktari, mtafiti ameshughulikia ndani ya
kitabu hicho riwaya na athari muhimu zilizokuja kwenye Ukhalifa wa
Makhalifa wane kisiasa (r.a).
Kimepigwa chapa na Dar twayyibah, na Maktabatil Kawthar Riyadh
chapa ya tatu .
7-‘Asrul Khilaafaashidah” cha Daktari Akrau Dhiyaail ‘Umary
Nacho ni kitabu chenye kudadisi riwaya za kihistoria kilicho mbali na
kushadidia au kufanyia wepesi .Kimepigwa chapa na Maktabatil
‘Abiikaan chapa ya nne. :
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
31
8- Akhtwaa Yajibu an tusahhah Minat Tariikh “:Cha Daktari
Jamaal ‘Abdil Haady na Duktuurah Wafaau Juma .
Nacho ni kitabu chenye mtungo wa vitabu vyenye kushughulikia
makosa na ufahamu uliokosewa ni mashuhuri kwa baadhi ya
waandishi na wasomaji, humo mumetokea upakaji matope wa
kukusudiwa kwenye Tarekhe yetu kuu ya kiislamu.
9- Tarekheul Islaamiy Mawaaqifu wal ‘Ibar cha Daktari ‘Abdil
‘Aziiz ‘Humaidiy .
10- ‘Abullahi bin Saba-i wa Atharuhu fii ahdaathil Fitinah fii
Swadril Islaam .Cha Sheikh Sulaimanil ‘Audah.
11 “Li adhaa Yuziifuuna At Tariikh wa Ya’abathuuna bil
‘Haqaaiq” cha Isma’ill Kaylaaniy .
12-atharul ‘HYadiith fii Nash-tit Taariikh ‘inda l muslimiin “ cha
Daktari Bashshaar ‘Awwaad Ma’ruuf .
13- “ Manhaju Kitaabatit Taariikhl Ialaamiy “ cha Muhammad
Swaamilil Islaamiy .
14- “Abu Mi’hnaf wa Dawruh ufii Nash-ti kitaabati Tarekheiyyah
“ cha ‘Al y Kaamilil Qar’aaniy .
15- Al Mu-a-rrikhunal ‘Arab wal Fitinati lKubraa” cha Daktari
.’Adnaan Mal’ham
16- “ Marwiyyaat Abi Mi’hnaf fii Tarekheit ‘Twabariy” cha
Daktari Ibraahiim Al Ya’hya.
17- Iilaamul aanaam bima Yajibu Na’hwal A’alaam” utunzi wa
‘Abdil ‘Hamiidil ‘Hasuunaah.
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
32
Mlango Wa Tano
Vitabu vyenye matatizo na kuchafua historia ya kiislamu
Isije ikatuondokea kumbukumbu kwamba, baadhi ya vitabu ni wajibu
kwetu kuvichukulia tahadhari wakati wa kuvisoma na kunukuu toka
kwenye vitabu hivyo, kwani kuvisoma bila ya kujuwa kanuni
zilizopita au kuwa na tetesi juu ya sera za watunzi wake au kuvifanya
kuwa ndio vianzio vya msingi katika utafiti, kumewaingiza watafiti
wengi kwenye makosa mabaya na ya hatari, yenye kupelekea kufanya
vipenzi (Walaa) na kujitenga (Baraa) na uchoraji wa picha za kiza
kwa baadhi ya vielelezo vya umma wa kiislamu. Masahaba
Kwa hakika hivi ni vitabu vya kisanii sawa na asali iliyochanganywa
na sumu, watunzi wake ni wakeshaji kwenye mizaha na upuuzi, hivyo
wanapopata nukta yoyote ile huitowa bila ya kujali ni ya kweli au
uongo .
Tumetangulia kuashiria uwajibu wa kuangalia kwenye habari na
riwaya, habari na athari hizi zikiwa ni kuhusiana na Ahil Beit na
Masahaba zinasimulia zuhudi na ushujaa, ukarimu, kujitowa kwao
muhanga, tabia zao njema, uzuri wa mienendo yao na upole wa
desturi zao, na hazikuwa ziko nje ya misingi ya ujumla ya kiislamu
wala kuwa ni yenye kukaliwa na maumbile yaliyo salama, basi
hakuna pingamizi kutajwa, kusimuliwa na kuandikwa kwake, kwani
hazigusi wala kutia dosari msingi wowote ule wa kisheria, wala
kusimuliwa kwake hakuleti madhara au kasoro kwenye hadhi ya Ahil
Beit na Masahaba (r.a)
Ama habari hizo zikiwa ni zenye fitina, au baadhi ya misimamo ya
kihamasa, au baadhi ya mambo yanayotia dosari cheo cha Ahil Beit na
Masahaba (r.a) au ndani yake kimo kitu kinachokwenda kinyume na
misingi ya kiujumla ya sheria au ndani yake mumeingia baadhi ya
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
33
kasumba zinazopingana na maumbile sahihi; basi aina hii ya habari
lazima sanadi zake zifanyiwe utafiti, na kuhukumiwa kwake kwa
hukumu ya uadifu; kwani kuwatia dosari Ahil Beit na Masahaba ni
kuitia dosari sheria na walioibeba., na hasa kwamba vitabu hivi sio
asili ya tarikh ya Ahil Beit na Masahaba (r.a).na kwenye vitabu
vyenye kutegemewa yamo yanayotosheleza kwa uchoreaji wa sura
yenye kung’ara ya historia ya wema hao watukufu, kizazi bora
kilichowahi kujulikana na jamii ya mwanadamu na bado hali
inaendelea kuwa hivyo.
Miongoni mwa vitabu hivyo vimo ambavyo ni wajibu
kuvichukulia tahadhari wakati wa kusomwa kwao :
1-“Al –aghaaniy “cha Abil Faraj Al Asfahaaniy:
Hichi ni kitabu cha kukeshea –kwenye kumbi za starehe-mashairi na
taarabu, kamwe hakina uhusiano wowote ule na Tarekhe kwa hali
yoyote ile.Al Asfahani amekiingizia uongo na ukosefu wa haya,
ubaguzi wa kiuadui na pia utiaji dosari juu ya Makhalifa wa umma
huu, na kwenye baadhi ya watu muhimu katika Ahil Beit (r.a) kama
vile Sakinata bintil Hussein (r.a) na wengineo, kwenye majaribio
wenyekutiwa shubuha ili kutoboa ukuta madhubuti wenye kutilia
nguvu jamii za kiislamu kwenye kumbu kumbu zake za kiroho na
mirathi yao ya kiungu, ili kujiwepesishia kuutenganisha toka kwenye
ngome mshikamano wa uliojikita na zama zake tukufu zilizopita
baada ya hapo, ili uwe wenye kuandaliwa kwa hujuma na
mashambulizi, mara baada ya kupoteza kwake kujipa nguvu kwake
kwa misingi ya asili zake iliyopita –kwenye sura anayoitaka
Aswfahaaniy na wenginewe – pahala pa kutilia shaka, baada ya
kupata simanzi kutokana na marashi ya kitakatifu waliyokuwa
wakiyapata kutokana na kusoma historia ya Ahil Beit na Masahaba
(r.a) .
Hivyo kuvunja mipaka ya kiislamu kadha iliyowazi kwa Asfahany
katika kutaja riwaya na habari kwenye kitabu chake cha -“Al –
Aghaaniy" Kwa mwenye kuzingatia kitabu hichi na kama tulivyosema
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
34
kwamba yeye hakika amevunja mipaka ya heshima hadi akafikilia
kuvunja heshima za nyumba ya Nabii (S.A.W) iliyotawalia nafasi ya
mapenzi, heshima, utakatifu na fadhila katika nyoyo za waislamu,
hakika Asfahani ametowa taswira kwa Sukaina bint Al Imam Hussein
na mjukuu wa Az Zahraa Fatma bint Mustafa (s.a.w) amemuweka
kwenye sura anayoikataa na kuichukia kila muislam, basi iweje kwa
binti Al -Hussein bwana wa vijana wa watu wa Peponi ?!
Miongoni mwa sura hizi ni ile aliyoitaja kwenye kitabu chake -“Al –
Aghaaniy“ (42/17) kwamba Sakina bint Al Imam Hussein (r.a)
alikuwa akimpenda muimbaji aliyetubu kwa Allah kutokana na kosa
la kuimba, hivyo yeye kama alivyofanyiwa taswira na Al –Aghaaniy
ni mwenye kuumizwa na kughumishwa na toba ya muimbaji huyu,
nae anachokitaka toka kwake arejee kuimba, nae anafanya jitihada
zake katika kumpoteza –Tunajikinga kwa Allah kutokana na hayo -!!
Visa na uongo zaidi ya huo, Al Asfahaaniy, amesahau au
kujisahauliza kilichomfika Sakina bint Al Imam Hussein baada
kustashhadi kwa baba yake Al Imam Hussein na mateso ya familia
yake kule Karbalaa, kwenye mitikisiko yote haya yamo mambo
yanayotikisa akili na kutiribua nyoyo, basi uko katika hali gani moyo
wa Sakina bint Hussein ?!41
Kadhalika .Al Asfahani ameleta tendo baya sana nako ni kule kupinga
kwake kuwa ni kasida ya Firdaws ambayo kwenye kibwagizo chake
inasema “Huyu ndiye anayejulikana na Buta’haa ” iliyosemwa
kuhusiana na Zainil ‘Aabidina’Ali binil ‘Hussein (a.s) nae Daktari
Waliidul ‘Adhwamy –Allah amlipe kheri –amekishughulikia vilivyo
kwenye chake cha aina yake “As Seful Yamaany” fii Na’hril .Al
Asfahaniy Swa’hibul al Aghaaniy ” 42
41 - lA”–Aghaan iy “wa A sSeiful Yamaaniy “ cha Mu hammadub ) ! ار#(
42 Toleo la “Daarul Wafaa -Misr” .Na angalia kwenye Tarjamati .Al
Asfahaniilyowekwa pekee kwenye “Mu’jamil Mu-a-liffiin “ (234/2 chapa ya
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
35
Hivyo tunatahadharisha umma kutegemea kitabu cha “Al –Aghaaniy"
kusoma historia ya Ahil Beit na Masahaba (r.a) na kipindi cha
mwanzo miongoni mwa watu muhimu wa umma na tunatahadharisha
juu ya yale yaliyotajwa ndani yake miongoni mwa fedheha na misiba
aliyoiashiria Al Aadhamy kwenye “As Seful Yamaany”, ama
yasiyokuwa hayo miongoni ya yale yaliyo na Fasihi, ya Mashairi
yanayolingania watu kwenye tabia njema kujitenga na maovu na
kuchunga heshima, na yale yasiyokuwa na madhara kutajwa kwake,
hayo hakuna ubaya kufaidika nayo, kwani kitabu kinayo mashairi, na
habari za kifasihi zilizo nyingi na kinachotoshelezeka kwa
chenginecho.
“Al ‘Aqdil Fariid cha Ibni ‘Abdi Rabbihi”:
Hichi ni kitabu cha fasihi na hikaya za visa vigeni hakuna zaidi ya
hayo, basi inakuwaje kwa mwenye akili mwenye kuzingatia kufanya
mfano wa kitabu hichi kuwa ni kianzio cha msingi cha utafiti kwenye
zama miongoni mwa zama muhimu za kihistoria ?!
Muhakiki wa kitabu hichi anasema, "Kitabu ni chenye kuchanganywa
usahihi wake na habari zisizokuwa na msingi, ni chenye kuondolewa
isnadi na wasimulizi, na ametegemea vianzio ambavyo haijuzu
kunukuu toka humo .”43
Ar Risaalah) ,hapa tunaashiria kwenye darsa mbili kuhusiana na mtu huyu –
isipokuwa As Seiful Yamaaniy “ navyo ni vitabu viwili vya
MuhammadA’hmad Khalaful Laahi ,na Shafiiq Jabriy.
43
Angalia utangulizi wa uhakiki wa “Al ‘Aqdil Fariid” (16/1) ,Maktabatu
Ibni Taymiyyah , na pia angalia maneno ya Al ‘Allaama Muhammad
Rashiidir Ridhaa kwenye Tafsiiril cManaar fiil Kitaab (85/5) na Angalia pia
: Kutubu ‘Haddhdh minhal ‘Ulamaa cha Mashhuur ‘Hassan Salmaan” ( 45/2
) .
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
36
3-“Al Imaamah was Siyaasah" kilicho nasibishwa Na Ibni Qutaiba ) ! ار#( :
Nacho ni kitabu alichonasibishiwa kwa uongo hii imetokana na
sababu kadha muhimu zao ni wale waliotowa historia ya Ibni Qutaiba
kamwe hawakutaja au kumnasibishia kitabu chochote kile kwa jina la
“Al Imaamah was Siyaasah” .
Mtunzi anasimulia toka kwa Ibni Abi Laila kwa hali inayoonesha
kukutana toka kwake, na Ibni Abi Laila huyu ni Muhammad bin Abdir
Rahman bin Abi Laila Al Faqiih Qadhi wa Al-Kufah, aliyefariki
mwaka (148H), Anaelewa kwamba Ibni Qutaiba hakuzaliwa
isipokuwa mwaka (219H), yaani baada ya kifo cha Ibni Abi Laila kwa
miaka sitini na tano !!.
Anaeangalia kitabu ataona tokea mwanzo kwamba mtunzi wake
alikuwa ameishi Damacus na Moroco (au nchi za Magharibi ya
arabuni), wakati kinachojulikana ni kwamba Ibni Qutaiba kamwe
hakutoka nje ya Baghdad ila kuelekea Daynuur.
Na zaidi ya mmoja katika waandishi na watafiti wamefanya kazi ya
kubainisha kwamba kitabu hichi amezuliwa nacho Ibni Qutaiba ;
miongoni mwao :
1-Daktari Thawrat Ukasha kwenye uhakiki wake wa kitabu “Al
Maarif ” cha Ibn Qutayba na Daktari aliongoza “Wizara ya Elimu “
Misri katika miaka ya sitini .
2-Muhammad al Iskandaary kwenye utangulizi wa kitabu “’Uyuunil
Akhbaar” cha Ibn Qutayba.
3-Mu’hibbud Diinul Khatiib kwenye utangulizi wa kitabu
“Almaisaratu Qidaa’h “ cha Ibn Qutaiba.
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
37
4- Daktari Muhammad Najm kwenye “Al Imaamah was Siyaasah,Al Mansuubtu Li Ibn Qutaiba Man huwa Mu-a-llifuhu ”
Majallatul Ab’haath na vyenginevyo katika tafiti
.
5-Muruujudh Dhahab” cha Al Mas’uudy :
Nacho ni kitabu kisichokuwa na Isnad kilichojaa khurafati, hikaya za
kiajabu ajabu, amesema Sheikhul Islaam Ibni Taymiyyah –Allah
amrehemu- "Na katika Taariikhul Mas’uudy umo uongo asioweza
kuujuwa Ila Allah Taala, basi vipi atakuwa na imani na hikaya iliyo
katika isnadi yake, kwenye kitabu kilicho mashuhuri kwa uzushi
wake.
Akasema Ibni Khulduun, "Katika vitabu Masuudy na Al-waaqidy
ni katika vitiaji kasoro na kejeli ulio mashuhuri baina ya
mahafidhi na wanaokubalika “44
6-Sherhe Nahjul Balagha Abduhamiid bin Abil Hadiidil
Muutazily:
Nae ni dhaifu kwenye vipimo vya maulamaa wa Jerhe na Taadiil, bali
mwenye kuzingatia sababu ya kutunga kwa Ibn Alhahihid kitabu
chake hichi ataiona nafsi yake ni yenye kulazimika kwa kutilia shaka
kitabu na mtunzi wake, kwani alikiandika kwa ajili ya Waziri Ibnil
‘Al-aqam ambaye alikuwa ni sababu ya katika kuuawa kwa waislamu
milioni moja katika Baghdaad kwenye mikono ya Tataar
Amesema Al Khansaary kuhusiana na kitabu hichi cha Ibn Alhahihid:
“ Alikitunga kwa ajili ya hazina ya vitabu vya Alwazir Mu-ayyidudin
Muhammad bin ‘Al-qamy “45
44
: Taariikh Ibni Khulduun –Muqaddimah “(uk. 19) 45
“Rawdhwaatul Jannaat “ cha Alkhawansaary (20-21/5)
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
38
Mpaka imefikilia kwamba watu wengi wamemponda mtunzi wa
kitabu hichi na kitabu chake; amesema Al Mirza Habiibul Llahi Al
khaiyyu akimuelezea Ibn Alhahihid “ Yeye sio mwenye kujuwa na
athari na kwamba rai yake ni mbovu na nadhari yake ni yenye
kuporomoka na kwamba yeye ni mwingi kuliko kiza na kwamba yeye
amepoteza wengi na amepotea toka kwenye njia iliyo sawa”.
Ama kuhusiana na kitabu chake; basi Mirza amekielezea kwa sifa
kadha miongoni mwao :Ni kiwiliwili bila ya roho anazunguka kwenye
ganda bila ya nyama, hakina faida nyingi ndani yake zimo taawili na
tafsiri ngeni zenye kutetemesha maumbile, na kukimbiza masikio.46
6-Kitabu “As Saqiifah” cha Salim bin Qais:
Ni shakhsiyyah isiyoeleweka, na njia ya kufikilia kitabu chake ni
dhaifu kwa wote, ndani ya kitabu chake muna upakaji matope kwa
Aalil Beit mkubwa sana, ametaja baadhi ya riwaya za uzushi na za
batili zenye kuporomosha hadhi Amiril Mu-u-minin Ali bin Abi Talib
shujaa.
-Kwamba yeye ni mwoga –Allah atulinde- wa kunyang’anywa haki
yake.
.-Kwamba yeye alimpandisha punda Fatma Zahraa (r.a ) ili avute
huruma za Muhajiirina na Answar na wasimame pamoja nae kuvua
Ukhalifa wa Abi Bakr (r.a) .
- Kwamba yeye aliificha Quran iliyo sahihi, na kuwaacha watu
wategemee Quran iliyopungufu .
- Kwamba yeye aliwaachia Masahaba wakimpiga mkewe bibi wa
watu wa Peponi Fatamtiz Zahraa (r.a ) mbele ya macho yake bila ya
kutaharaki akiwa ametulizana, na habari nyengine ambazo akili iliyo
sahihi haizikubali wala kuziridhiwai, kama alivyobainisha hivyo zaidi
ya mmoja kama mfano wa Aayatullah Muhammad Fadhlullahi
aliyekana riwaya zinazosambazwa na wanaotaka kuhemua ghadhabu
za watu, kuwafarikisha na kuwaweka mbali na ukweli wa mambo
46
Angalia “Minhaaul Barraa’ah Sherhe Nahjul Balaagha “Mitrzaa H’biib
ullahil Al Khaw-i-y (14/1 chapa ya Daari I’hyaait Turaathil ‘Arabiy -Beruit ).
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
39
yenye kuwatenganisha, kama anavyofanya mwenye kunukuu toka
kwenye kitabu cha Salim bin Qais na wenginewe, hivyo Aayatullahi
Muhammad Fadhlullahi amechukizwa na kuenezwa mfano wa riwaya
hizi batili ambazo zinataja kwamba Omar (r.a ) alivamia nyumba ya
Ali (r.a) na kuvunja au kuunguza mlango wake, na kwamba alivunja
ubavu wa Fatma Zahraa (r.a ) na kuidondosha mimba yake, na
Fadhlullahi akabainisha kwamba jambo hili haliwezekani wala hakuna
akili inayolikubali akibainisha kwamba mapenzi ya waislamu kwa
Fatma Zahraa (r.a) ni makubwa yenye kuzuia watu kufanya mfano wa
tendo baya kama hili.47
Wengi wa wenye akili wametilia nguvu rai ya Fadhlullahi mfano
Ustadh Ahmad al Khatib48
Lakini harakati hizi za usahihishaji na zenye kutolea maelezo
zimekabiliana na hujuma kali toka kwa baadhi ya wakereketwa mpaka
kufikilia watu hawa kumkufurisha Fadhlullahi, na kutilia shaka
kwenye imani, itikadi ikhlasi yake, yote haya ni kwa ajili ya kukana
hadithi batili isiyosihi, na kwa anayetaka kuangalia fikira za
Fadhlullahi na kutiwa kwake dosari kwa sababu ya kukana kwakwe
jambo hili arejee kwenye kitabu “Fitinatu Fadhlillahi”cha Muhammad
baaqir As Swaafy. Na kitabu Maasaatuz Zahraa” cha Ja’afar Al
‘Aalamiy, na kitabu “awzatul ‘Ilmiyyatu Tadiinul In’hiraaf” cha
Muhammad Ali Haashimiy Al Mash-hadiy .
Ama kitabu cha “As Saqiifah” ambacho kinataja mfano wa hikaya hizi
batili ni chenye kutiliwa shaka mwanzo mpaka mwisho.
Amesema Sheikh wa A’Twaaifatil Mufiid:” Hakika kitabu hichi
hakikubaliki, wala haijuzu kufanyia kazi nyingi ya taarifa zake kwani,
ndani yake mumepatikana uchanganyikaji uongo na hadaa-.” 49
47
Angalia “Ummatu fii Rajuli Mu’hammad’Hussein Fadhlullahi “ cha
MuhammadAl Jazaairy (uk. 219) 48
Angalia : Makala :” Fadhlullahi anaongoza Maspinduzi ya kitamaduni na
anashuku ugaidi “ uk. 2/1/1999 M, naye Ustadh A’hmad il Kaatib anao utafiti
muhimu wenye anwani “Ustwuura Madhluumiyyatuz Zahraa” nao ni utafiti
makin iamezirekibisha habari zote na athari batili kuhusiana na jambo hili.
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
40
Amesema Al Ghadhaairy:” kwenye tarajama ya Abaan bin Ayaassh"
Ni dhaifu hazingatiwi na maulama wetu wanamnasibisha na kuzua
kwake kitabu cha Salim bin Qais"”50
Pia amesema Haashim bin Ma’aruuf al ‘Husseiniy "Salim bin Qais ni
mmoja wa wenye kutiliwa shaka na kutuhumiwa kusema uongo, na
pamekuja kwenye kitabu kilichonasibishwa nae kwamba Muhammad
bin Abi Bakr alimpa mawaidha baba yake wakati wa mauti yake
pamoja na kwamba alikuwa mwenye umri miaka sitini “.51
7- Kitabu “As Saqiifah” cha ‘Abdil ‘Azizil Jawhariy ;Ni kitabu
kisicho na uzito wala kima kwa vigezo kadhaa:
Kigezo cha Mwanzo :Kwamba mtunzi wake ni hajulikani wala
uadilifu wake haijulikani kwenye vitabu vya jarhi wa Taadiil na
Rijaal, wala hamna utakaso au ukubalikaji wowote ule isipokuwa vile
alivyotaja Ibni Abi Al-hadiid kwenye sherhe yake juu ya Nahjul
Balaagha kuhusiana na kumtakasa kwake, na tumetangulia kubainisha
hali ya Ibni Abi Dunya mwenyewe, na kwamba yeye sio katika watu
wa kujuwa na athari .
Na kamwe utakaso wake hauhesabiwi kabisa!,amesema Al Khaw-iy,
nae akiwa anapinga utakaso wa Ibni Abil Hadiid kwa Al Jawhariy”
Mtu huyu utakaso wake haukuthibiti –akimaanisha al Jawhariy kwani
utakaso wa Ibni Abil Hadiid hauzingatiwi 52
Na katika sababu zinatuzidishia uyakini kwamba Al Jawhariy hali
yake haijulikani amefanya hivyo At Tuusiy kwenye “ Al Fihrasa ”
49
Tashiih ‘Aqiidatil Imaamiyyah”(uk.149/5 ) 50
“Ar Rijaal cha ibinl Ghadhwaairy uk.(119) (uk.119) tajamah ya Salim bin
Qaisnam.193. 51
2Al Madhuuaat fiil Athaar wal Akhbaar “Haashim Maaruuf al ‘Husseiny
(uk.184) . 52
Muujamu”Rijaalil Hadiithcha Al Khau-i-y (142/2) .
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
41
pale alipomtaja Al Jawhariy, na kubainisha kwamba anacho kitabu
cha As Saqiifah. Na kwa kurejea kwenye utangulizi wa At Tuusisy
wa kitabu chake “ Al Fihrasa ” tunamuona anasema :” Hivyo
ninapomtaja kila mmoja wa watunzi na wenye vitabu asili basi lazima
niashirie kwenye kilichosemwa kuhusiana nae yanayohusiana na Jerhe
wa Taadiil, na jee anakubalika kwenye riwaya zake au laa?!”53
Na At
Tuusisy wakati wa kumtaja kwake Al Jawhariy hakutaja Jerhe wala
Taadiil na hili ni miongoni mwa yanayojulisha kutokubalika kwake” 54
Kigezo cha Pili: Wakati wa kufungua kurasa za kitabu cha As
Saqiifah tutaona kuwa muandishi analeta Munkaraat, katika riwaya na
maneno ambayo hakuna aliyeyasimulia na kamwe hazikunukuliwa na
yeyote yule asiyekuwa yeye, jambo lililotufanya tutilie shaka kuhusu
kitabu na hasa mtunzi wake, na kwamba anazungumzia kuhusiana na
awamu ya hatari na muhimu, haikubaliki kauli yoyote ile isipokuwa
kwa hoja na dalili madhubuti za wazi na sanadi sahihi.
Kigezo cha Tatu :Nyingi za isnadi a wasimulizi wa kitabu cha As
Saqiifah ni dhaifu, na ndani yake wamo wasiojulikana na madhaifu
anaowajuwa Allah -pekee- kwa mfano, Jawhary anasema
"Ametuzungumzia Ahmad bin Ishaq bin Saleh toka kwa A’hmad bin
Yasaar toka kwa Said al Answaary toka kwa wasimulizi wake”.Hivyo
Ahmad bin Is’haaq ni yupi na sisi hatumuelewi!!, na ni nani hao
wasimulizi wa Said, Allah ni Mjuzi zaidi !55
53
Muqaddimatul Mufahrisa cha At Tuusisy (uk. 12) * Jerhe wa Taadiil :Sifa za kukubalika au ktokubalika kwa msimulizi .
* Munkari ni Hadithi ambayo kwenye Isnadi yake yake yumo msimulizi
mwenye makosa yaliyozidi kipimo,sahau zake zimekuwa nyingi mno ,au
madhambi yake makubwa yamedhihiri 55 ihtidaHh eynewk ” hafiiawhD htiidaah‘A italisliS”٤٩٧٢ Al Allaamatu Al
Baaniy ) !! اا�ر# )maeeleezea kwa kirefu hadithi hii.
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
42
8-“ Taariikhul Ya’quuby:
Huchukuwa vianzio vya riwaya kama ndio vianzio vikuu toka kwa Al
Waaqidy na Abi Mi’naf Luutw bin Yahya, kitabu kinaelezea historia
ya Ahalil Beit na Masahaba (r.a) kwa namna ya Mursal hamuna isnad,
nae amezidisha kutaja ibara za udhaifu na unyonge, mfano
imesemekana, imesimuliwa, na wamesimulia baadhi yao, na
wamesema baadhi yao …”56
Ya’quuby huyu anafanya kiburi na kuchupa mpaka na kuwa na kedi
kuhusiana na kuwaita Abu Bakri na Omar na’Uthman kwa jina la
Khalifah , wakati anamuelezea Ali kuwa ni wasii wa Muhammad
(s.a.w), na huku ni ukandamizaji, na kedi kusikokubalika toka kwa
alieshika kazi ya uandishi wa historia ya Ahil Beit na Masahaba (r.a).
Mtu huyu anao msimamo wa kiadui dhidi ya Masahaba watukufu (r.a)
maamuzi ya dhana iliyotangulia kabla ya kuandika kwake historia ,
sifa ambazo ni katika mambo yanayokosesha kuaminika .
Kitabu cha Al Ya’quuby kimegawika kwenye sehemu mbili::
Sehemu ya mwanzo :Ndani yake amekusanya maneno yasiyokuwa
na kichwa wala miguu na khurafaat toka kwa umma zilizotangulia na
mara nyingi hutolea dalili Injili na Tawrati juu ya habari za Manabii
na kuwacha Quran isiyokuwa na shaka wala kutilika wasiwasi , basi
hili lizingatie.
Ama sehemu ya Pili : Humo anazungumzia kuhusu Sira ya Nabii
(s.a.w) :na Makhalifa baada ya yeye kwa muhtasari wenye mapungufu
na yenye kujaa riwaya zilizokatika na zisizokuwa na sanadi na za
uongo.
Kima cha kielimu cha kitabu hichi ni kidogo sana ;amesema Daktari
Muhammad Swaamil As Sulamiy –akiwa anzungumzia “Taariikhul
Ya’quuby" Hichi ni kitabu kinachowakilisha upotevu, na upakaji
56 Taariikhul Ya’quuby(168-171/ 2 ) .
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
43
matope uliopatikana kwenye uandishi wa historia, nayo ni marejeo ya
wengi wa mustashrikina na walioathirika na umagharibi baina ya wale
waliotukana kwenye historia ya kiislamu na Sira za watu wake .57
9-“Faraaidus Samtwiin “ Kitabu cha al Hamwaity .Amesema Al
‘Hafidhul Adh Dhahaby kuhusiana na yeye :na kuhusiana nae na
kitabu chake
"Alikuwa muokota kuni usiku, amekusanya hadithi sisizo na mashiko
bali ni za batili.”58
10- “Al Mukhtswar fii Akhbaar Seyyidil Bashar “ Cha Abil Fadaa
Hichi ni kitabu kama kile kilichokitangulia, ndani yake muna hadithi
zabatili na habari za kuzuwa kwa wingi .
57
Manhaj Kitaabatit Taariikhil Islaamy “(521) 58
Ad Durarul Kaaminah (67-68).
آ�� ���أ��ر�� ا�ول �����ب
Vipi tusome Tarekhe ya Aal-Beit na Masahaba?
44
Hatima
1-Umuhimu wa kutangulizwa wa mpango Quran na Sunna wakati
wa kuzungumzia kuhusiana na Ahil Beit na Masahaba (r.a) na
kipindi cha mwanzo cha kiislamu (r.a).
2-Kutilia umuhimu wa kusihi kwa unukuuji na masimulizi kama
ni msingi wa kisheria, haisihi kufanyia wepesi –uzembe – kwa
hali yoyote ile.
3- Kubainisha vitabu muhimu ambavyo vinapasa kutegemewa
wakati wa kupanga, kuandika na kusoma Historia ya kiislamu.
4- Kutahadhari kutokana na hatari za kutegemea marejeo
yasiyokuwa ya asili na yasiokubalika, jambo ambalo hupelekea
kupata maalumati yasiyokuwa sahihi au yenye kupaka matope, ni
sawa iwe ni kwa lengo la nia mbaya, au kutojuwa na kutochukua
tahadhari .
5- Mwisho :Inapasa juu ya muandishi na msomaji wa Tarekhe ya
kiislamu kutojiachilia, akaandika hadithi au kutowa hukumu bila
ya mpango, au kujitegemeza kwenye upande, msingi au kadhia,
katika mambo ambayo huenda yakampelekea kuangukia kwenye
kosa kubwa, na huenda utajaji wa hadithi ukawa mpungufu au wa
upakaji matope, au hukumu huenda zikaja za kudhulumu, au
zisizozakukiinaisha, au zisizokuwa na misingi na asili thabiti na
sahihi, kitu ambacho kinapelekea kupoteza haki na kuzifuta.
Na shukurani zote zimemthibitikia Allah, na sala na salamu
zimshukie Nabii wetu Al amini na jamaa na Masahaba zake Al
Ghurrul Mayaamiin..
KIMEKAMILIKA KITABU KWA IDHINI YA ALLAH
top related