wakala wa vipimo - tanzania...mwelekezi (consultant) akikabidhi funguo za jengo. kituo cha kupimia...

Post on 19-Mar-2020

1 Views

Category:

Documents

0 Downloads

Preview:

Click to see full reader

TRANSCRIPT

WAKALA WA VIPIMO

TAARIFA ZA MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA NNE KWA SEKTA YA

VIWANDA NA BIASHARA KIPINDI CHA MWAKA 2005-2015

UTANGULIZI

Wakala wa Vipimo ilianzishwa mwaka 2002 kwa sheria ya Wakala wa Serikali Sura

Na. 245 ya mwaka 2002. Kabla ya kuwa Wakala, ilikuwa Idara chini ya Wizara ya

Viwanda na Biashara

Wakala wa Vipimo inafanya majukumu yake kwa kutumia sheria Sura Na. 340 na

kupitiwa upya mwaka 2002.

Wakala ina jukumu kubwa moja ambalo ni kumlinda mlaji (mwananchi) kupitia

vipimo sahihi.

Katika kipindi cha mwaka 2005-2014 Wakala ilitekeleza majuku yake na kupata

mafanikio mbalimbali kama inavyooneshwa katika picha mbalimbali hapo chini

MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA KIPINDI HIKI

1. Kuanzishwa kwa Kitengo cha Bandari kwa ajili ya kusimamia vipimo

vitumikavyo kupimia mafuta yanayoingizwa nchini pamoja na gesi

2. Kununua vifaa mbalimbali vya kitaalam kwa ajili ya kuboresha huduma ya

ukaguzi wa vipimo vinavyotumika katika biashara ili kumlinda mlaji (

mwananchi)

3. Ununuzi wa viwanja kumi na tisa ( 19) vya Wakala kwa ajili ya kujenga ofisi

na vituo vya kupimia magari yabebayo mafuta

4. Ukarabati wa ofisi mbili (2) za Morogoro na Tanga

5. Kufanya utafiti wa jinsi mfumo wa vipimo katika sekta ya gesi asilia ( Natural

gas) kwa ajili ya kusimamia sekta hiyo

6. Ujenzi wa vituo vya kupimia magari ( Calibration bays) yabebayo mafuta vya

Iringa na Mwanza, na kukiboresha kituo cha zamani cha Ilala

7. Kujenga vituo vya kukagua bidhaa zilizofungashwa mipakani (Sirari,

Namanga, Horiri, Horohoro na bandari za Mwanza, Tanga,Dar es Salaam).

8. Maandalizi ya kujenga kituo cha kukagulia magari Misugusugu mkoani Pwani

( michoro ipo tayari mchakato wa kumpata mjenzi unaendelea)

9. Wakala imepanua wigo wa maeneo ya kufanyia kazi hivyo imeongeza ajra

kwa watanzania. Kabla ya 2015 watumishi walikua ……….. na mpaka mwaka

uliopita wa fedha 2013/2014, watumishi walikuwa………………

10. Wakala imefanikiwa kununua magari mazuri ya kufanyia kazi tofauti

na ilivyokuwa hapo awali.

BAADHI YA VIFAA VYA KITAALAM VILIVYONUNULIWA NA WAKALA KATIKA KIPINDI HICHO

Vifaa vya kitaalam vilivyonunuliwa na Wakala

Vifaa vya kitaalam vilivyonunuliwa na Wakala

Vifaa vya kitaalam vilivyonunuliwa na Wakala

Vifaa vya kitaalam vilivyonunuliwa na Wakala

WAKALA INASIMAMIA VIPIMO VINAVYOTUMIKA KATIKA SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA

ILI KUPATA BIDHA ZENYE VIPIMO SAHIHI

Ukaguzi wa Bidhaa

zilizofungashwa, viwandani,

bandarini na baadhi ya vituo

vya mipakani

Ukaguzi wa Bidhaa zilizofungashwa, viwandani, bandarini na baadhi

ya vituo vya mipakani

Upimaji wa bidhaa viwandani kupata usahihi wake.

Ukaguzi wa Bidhaa zilizofungashwa, viwandani, bandarini na baadhi

ya vituo vya mipakani( maafisa Vipimo wakikagua)

WAKALA KUSIMAMIA USALAMA

Upimaji wa mwendo kazi wa magari kwa kutumia vifaa vya

kitaalam ( maarufu tochi)

WAKALA HUSIMAMIA VIPIMO VINAVYOTUMIKA KUPIMIA MAFUTA YAINGIAYO NCHINI

Usimamizi na udhibiti wa kiasi cha mafuta ya petrol na gesi

yaingiayo nchi kupitia vipimo sahihi (Wakala inasimamia)

WAKALA HUSIMAMIA VIPIMO VITUMIKAVYO KUPIMIA MAFUTA KWENYE SOKO

Upimaji wa matenki kwa kutumia kifaa cha kitaalam (Prover)

Upimaji

wa

matenki

ya ardhini

Upimaji wa matenki ya treni

Upimaji wa matenki makubwa ya kuhifadhia mafuta na gesi

WAKALA HUTOA ELIMU WA WANANCHI KUHUSU MATUMIZI YA VIPIMO

SAHIHI

Afisa vipimo bw. akitoa elimu kwa naibu Katibu Mkuu wa Viwanda na

Biashara Bi…………..

Kaimu meneja wa Habari Bi. Irene John akifafanua jambo kwa waandishi wa

habari kuhusu matumizi ya vipimo ( Hawapo pichani)

Utoaji wa elimu kwa wananchi kwenye maonyesho kuhusu

vipimo

MAENEO MAPYA YA KAZI ZA VIPIMO YAMEONGEZA AJIRA KWA VIJANA

Maeneo mapya maafisa wakipima urfu wa mabati kama yanakidhi matakwa

ya sheria ya vipimo

Maafisa wakipima ili wajiridhishe vipimo vyake

MAGARI YA WAKALA KIPINDI CHA NYUMA KABLA YA 2005

MAGARI YA WAKALA KATIKA KIPINDI KUANZIA 2005

WAKALA INATEKELEZA MIRADI MBALIMBALI

Ofisi ya Morogoro baada ya kukarabatiwa, Picha mshauri

mwelekezi (Consultant) akikabidhi funguo za jengo.

Kituo cha Kupimia magari yabebayo mafuta kilichojengwa

mkoani Iringa

Mfano wa kituo cha kupimia magari yanayobeba mafuta

kitakachojengwa eneo la Misugusugu mkoani Pwani

(Impression drawings)

Ofisi itakayojengwa eneo la Misugusugu kwa ajili ya kazi za

kituo hicho

WAKALA IMEPATA TUZO MBALIMBALI ZA KITAIFA NA KIMATAIFA

(1)

(2)

(1). The Most Accountable and Transparent Organization Award receive in

Ghana during African Public Services Exhibitions

(2) OIML Award for Excellent Achievements in Legal Metrology in Developing

Countries

top related