“akawa na virusi vya ukimwi?” je, huenda mtoto wangu · nenda kwenye kituo cha afya kilicho...

2
Watoto walio na virusi vya ukimwi wanaweza kuwa na siku za usoni zenye matumaini Nenda kwenye kituo cha afya kilicho karibu bila kuchelewa! Utapata maelezo kuhusu jinsi ya kupima virusi vya ukimwi, utaambiwa wakati wa kutarajia matokeo, na utasaidiwa kuelewa matokeo. Nimpeleke mtoto wangu wapi ili apimwe? Ziada za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi zimesababisha faida nyingi, lakini baadhi ya watoto bado wanaambukizwa wanapozaliwa au kupitia maziwa ya mama. Wengine huambukizwa na mama asiyefahamu hali yake ya ukimwi, ama na mama anayeambukizwa na ukimwi baada ya kujifungua. Watoto walio na maambukizi ya virusi vya ukimwi wakiwa bado wachanga wanaweza kuonekana wenye afya au wanaweza kugonjeka mapema. Watoto wanaopimwa ili kujua hali yao ya ukimwi, na kupata matibabu mapema, wanaweza kuku awakiwa na afya. Je, huenda mtoto wangu akawa na virusi vya ukimwi? Iwapo una maswali, wasiliana na: National Empowerment Network of People living with HIV/AIDS in Kenya (NEPHAK) Nambari ya simu 0720209694 International Community of Women Living with HIV Kenya Chapter (ICW-K) Nambari ya simu 0713963106 Kenya National AIDS & STI Control Programme (NASCOP) Nambari ya simu 0202630867 Barua pepe: [email protected] Mimi ni yatima. Wazazi wangu waliaga kwa sababu ya Ukimwi, na sikufahamu hali yangu hadi wakati nilipogonjeka sana. Ndugu yangu aliyenilea aliogopa sana kutoa ruhusa ili nipimwe hali yangu ya ukimwi. Kwa bahati njema, nilipata kujua hali yangu, iwapokaribu nichelewe kuanzishwa matibabu. Wazazi na walezi, tafadhali msidhani kuwa watoto hawana uwezo wa kukabiliana na ukimwi. Tafadhali msisahau kuwa watoto wanaoanzishwa matibabu mapema, bila kupoteza wakati, wanaweza kukuwa wakiwa wenye afya, nilivyokuwa mimi! Juliana, Msichana aliye na ukimwi, Msemaji wa Vijana

Upload: others

Post on 28-Jul-2020

27 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: “akawa na virusi vya ukimwi?” Je, huenda mtoto wangu · Nenda kwenye kituo cha afya kilicho karibu bila kuchelewa! Utapata maelezo kuhusu jinsi ya kupima virusi vya ukimwi, utaambiwa

Watoto walio na virusi vya ukimwi wanaweza kuwa na siku za usoni

zenye matumaini

Nenda kwenye kituo cha afya kilicho karibu bila kuchelewa! Utapata maelezo kuhusu jinsi ya kupima virusi vya ukimwi, utaambiwa wakati wa kutarajia matokeo,

na utasaidiwa kuelewa matokeo.

Nimpeleke mtoto wangu wapi ili

apimwe?

“”

Ziada za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi zimesababisha faida nyingi, lakini baadhi ya watoto

bado wanaambukizwa wanapozaliwa au kupitia maziwa ya mama. Wengine huambukizwa na mama

asiyefahamu hali yake ya ukimwi, ama na mama anayeambukizwa na ukimwi baada ya kujifungua.

Watoto walio na maambukizi ya virusi vya ukimwi wakiwa bado wachanga wanaweza kuonekana wenye

afya au wanaweza kugonjeka mapema.

Watoto wanaopimwa ili kujua hali yao ya ukimwi, na kupata matibabu mapema, wanaweza kuku

awakiwa na afya.

Je, huenda mtoto wangu akawa na virusi vya ukimwi?“ ”

Iwapo una maswali, wasiliana na:

National Empowerment Network of People living with HIV/AIDS in Kenya (NEPHAK)

Nambari ya simu 0720209694

International Community of Women Living with HIV Kenya Chapter (ICW-K) Nambari ya simu 0713963106

Kenya National AIDS & STI Control Programme (NASCOP) Nambari ya simu 0202630867

Barua pepe: [email protected]

Mimi ni yatima. Wazazi wangu wal iaga kwa sababu ya Ukimwi, na sikufahamu hal i yangu hadi wakati ni l ipogonjeka sana.

Ndugu yangu al iyeni lea al iogopa sana kutoa ruhusa i l i nipimwe hal i yangu ya ukimwi . Kwa bahati njema, ni l ipata kujua hal i yangu, iwapokaribu nichelewe kuanzishwa matibabu. Wazazi na walezi , tafadhal i msidhani kuwa watoto hawana uwezo

wa kukabi l iana na ukimwi . Tafadhal i msisahau kuwa watoto wanaoanzishwa matibabu mapema, bi la kupoteza wakati , wanaweza kukuwa wakiwa wenye afya, ni l ivyokuwa mimi !Juliana, Msichana aliye na ukimwi, Msemaji wa Vijana

Page 2: “akawa na virusi vya ukimwi?” Je, huenda mtoto wangu · Nenda kwenye kituo cha afya kilicho karibu bila kuchelewa! Utapata maelezo kuhusu jinsi ya kupima virusi vya ukimwi, utaambiwa

Mtoto wako atapewa matibabu ya bure na atakuwa akionekana na madaktari na wauguzi ili kuhakikisha

kwamba anaendelea vyema, na anakua vizuri bila matatizo.

Dawa za aina nyingi zimetengenezwa kwa ajili ya watoto. Dawa hizi ni salama na rahisi kutumia na

pia zinasaidia watoto kuwa na afya njema. Mtoto atatumia dawa hizi siku zote za maisha yake.

Dawa hizi zinapatikana katika kituo cha afya.

Watoto walio na virusi vya ukimwi hupata magonjwa kwa urahisi kwa sababu miili yao haiwezi kupambana na magonjwa yanayowashambulia. Baadhi ya watoto wenye

virusi vya ukimwi wanaweza kuonekana wenye afya, lakini wakianza kuonekana wagonjwa, inaweza kuwa tayari wameadhirika sana. Wasipopata matibabu watakufa.

Kupimwa virusi vya ukimwi kwa mtoto wako kunaweza

kukupatia wasiwasi. Hata hivyo, ni jambo la muhimu kwa mtoto wako kupimwa tena kupitia maagizo ya daktari.

Ni muhimu kupima watoto mapema na kuanza matibabu bila kuchelewa. Kwa hivyo, usisubiri mpaka uchelewe,

mtoto anaweza kupata usaidizi.

Mtoto wangu anaoneka kuwa mwenye afya nzuri. Ni kwa nini unanihimiza

kupima hali yake ya ukimwi?

“”

Iwapo mtoto wangu atapatikana kuwa na virusi va ukimwi, nini kitatendeka?

“”

Matibabu gani yanapatikana, na yana gharama gani?“ ”

Dawa zitasaidia mwili wa mtoto wako kupata nguvu ya kupigana na virusi vya ukimwi. Baadhi ya watoto

huenda wakawa na madhara kama upele au kuendesha - hii inalingana na madawa.

Haya madhara huwa si makali na hupunguka kwa muda na kwa urahisi.

La muhimu ni kumweleza muuguzi au daktari kuhusu dalili yoyote ya madhara. Watakusaidia na kuhakikisha mtoto wako yuko salama na anapata

matibabu yanayo faa, anapoendelea kukua!

Matibabu haya yatamsaidiaje mtoto wangu?“ ”

Watoto walio na virusi vya ukimwi wakipimwa na kupewa matibabu, wana nafasi kubwa ya kukuwa

wakiwa na afya njema.

Watoto walio na virusi vya ukimwi wanaweza kuishi maisha ya furaha na afya.

Usichelewe! Mpeleke mtoto wako apimwe.