waraka wa watanzania kutoka ahera kuhusu rais jakaya kikwete
Post on 11-Apr-2017
128 Views
Preview:
TRANSCRIPT
WARAKA KWA WATANZANIA KUTOKA AHERA KUHUSU RAIS JAKAYA
MRISHO KIKWETE
Nipashe
Na Prof (Dr) Handley Mpoki Mafwenga
Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]
Alfajiri ya saa tisa, naona mtu kasimama mlangoni ananieleza kuwa ametumwa na
waasisi wa CCM Julius Nyerere, Abeid Karume, Thabiti Kombo, Rashid Kawawa
na Bibi Titi Mohamed. Akanipa Waraka niupeleke kwa watanzania wenye maneno
yafuatayo;
Ndugu Watanzania, mnaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge;
muelewe kuwa mnatekeleza wajibu wenu chini ya Sheria ya Umma Na 15 ya
Mwaka 1984 na Ibara ya 21(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuchagua au
kuchaguliwa katika shughuli za utawala wa Nchi.
Tanzania ni nchi ya kwanza kwa SADC kuwa na mfumo wa vyama vingi ikifuatiwa
na Botswana, Zambia. Ni nchi pekee iliyopigania Amani kusini mwa Afrika, na nchi
ya kwanza kupata uhuru katika SADC Mwaka 1961. Ofisi zote za wapigania
uhuru kama FRELIMO, ANC, Kamati ya Ukombozi ya OAU nk zilikuwa na makao
yao makuu Dar-Es-salaam miaka ya sabini.
Tumejijengea heshima Duniani na kuwa na sifa ya Umoja, Uvumilivu, Upendo na
Mshikamano. Hii ilitufanya Mwaka 1969 tuanzishe vijiji vya Ujamaa kwa
kuchukua mfano wa Ruvuma Development Association kilichoundwa Mwaka 1963
pale kijijini Litowa kuwa mfano (Model) na kumtumia mtaalamu wao makao
makuu ya TANU na kuwa mshauri wetu wa Uchumi na Mipango Ikulu. Kwa
sababu tulijua Uhuru bila Maendeleo ni kazi bure. Mfano huo ulitumika pia
kufundishia wanasiasa wetu chuo cha siasa kivukoni.
Tanzania ni nchi ya kwanza kuanzisha uhuru wa Bunge Mwaka 1961, Uhuru huo
ulikaa kwa muda mfupi kwa sababu hatukulenga kuwa na Serikali Imara
inatakayojali matatizo ya kijamii na kiuchumi na uwepo wa chama kushika
hatamu. Katiba ya Jamhuri ya Mwaka 1962 ilitatua matatizo ya kijamii na
kiuchumi wakati Katiba ya Chama kimoja ilitatua tatizo la chama kushika hatamu.
Hii ndiyo chanzo hasa cha kufuata mfumo (Model) ya kikatiba ya Westminster
kutofautisha Bunge na Mahakama hadi leo.
Mwaka 1958 hadi 1961 tulikuwa tukitembelea shule ya msingi ya Msonga na
kumkuta kijana akiongoza wanafunzi wenzake huyu si mwingine ni Jakaya
Kikwete. Mara nyingi alitusogelea akitaka busara zetu mara tukasikia amefauru
na kwenda Lugoba Middle School Mwaka 1962.
Tulipotembelea Kibaha Mnamo Mwaka 1966 tukamkuta akatueleza kuwa
angependa sana kuwa kama Winston Chuchil Waziri Mkuu wa Uingereza kwa vile
anapenda sana maneno yake(Maxims). Tukamwambia, kwa nia hiyo hakika
utakuwa hivyo.
Mwaka 1970 hadi Mwaka 1971 alisoma Tanga shule ya Sekondari. Alipenda somo
la “Political Economy” kwani alipenda pia kusoma maandishi ya akina Lennin, Carl
Max na wengine. Nilipokuwa nakwenda Chuo Kikuu Cha Dar-Es-Salaam (Mwal
Nyerere) kutunuku wanafunzi Mwaka 1972 hadi 1977 nilikuwa nikimkuta pale
akiuliza sana maswali hasa ya Uchumi na Maendeleo aliyokuwa akisomea akiwa
na wenzake akina Edward Lowasa ambaye alisoma pia Shahada ya Uzamili ya
Sayansi katika Maendeleo huko Bath Uingereza.
Kikwete alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama cha TANU Mwaka 1975 hadi 1977.
Nilimshangaa sana kuona ameacha hata kuajiriwa kwenye Mashirika kama
Mchumi wasomi wakiwa wachache wakati huo, hakupenda sana fedha, wala
kukimbia kondoo wa Bwana bali kuwatumikia.
Mwaka 1977 baada ya Kuunda Katiba Mpya na kuunganisha TANU na ASP nikiwa
Mwenyekiti wa Kwanza wa CCM, nilitembelea Zanzibar ambapo Ali Hassan
Mwinyi alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, niliona ni vyema aende huko
Zanzibar kuwa Makamu Katibu wa CCM. Nilifanya hivyo mara baada ya kuona
amehitimu mafunzo ya kijeshi pale Monduli kuanzia Mwaka 1976 hadi 1977.
Alipanda daraja kuwa Katibu wa CCM wa Mkoa wa Tabora Mwaka 1981 hadi
1983. Na ikizingatiwa alipigana vita ya Kagera ilikuwa vyema afundishe wanajeshi
wenzie pale Monduli Mwaka 1983 hadi 1986.
Mwaka 1986 alihamia Nachingwea na Masasi kuwa Katibu wa CCM. Mwenzangu
Ali Hassan Mwinyi aliona ni vyema Kikwete alitumikie Taifa zaidi kwa kuwa
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mwaka 1988 hadi 1990, Waziri kamili Mwaka
1990 hadi 1994, Waziri wa Fedha Mwaka 1994 hadi 1995, Waziri wa Mambo ya
Nchi za Nje Mwaka 1995 hadi 2005 na Wananchi mkaona vyema kumchagua
Mwaka 2005 kwa kura zilizoonyeshwa kwenye Jedwali Na1.
Jedwali 1: Matokeo ya Uchaguzi Mwaka 2005
Mgombea Chama Kura Asilimia
Jakaya Kikwete CCM 9,102,952 80.24
Ibrahim Lipumba CUF 1,327,125 11.7
Freeman Mbowe CHADEMA 668,736 5.89
Augustine Mrema TLP 84,901 0.75
Sengondo Mvungi NCCR-Mageuzi 55,819 0.49
Christopher
Mtikila
DP 31,083 0.27
Emmanuel
Makaidi
NLD 21,574 0.19
Anna Senkero PPT-Maendeleo 18,783 0.17
Leonard Shayo Demo-Makini 17,070 0.15
Paul Kyara SAU 16,414 0.14
Wanasaikolojia, Drs. Steven Rubenzer, Thomas Fasschingbauer na Deniz Ones,
walifanya usahili kuhusu historia ya Maraisi mia moja. Wataalamu hao wakaweka
tabia ya kisaikolojia kwa miaka mitano kabla Marais hawajawa madarakani. Hata
hivyo, hawakuangalia tabia ya marais wakiwa ndani ya ofisi kwa sababu “pressure”
za kazi zao wakiwa nje hutofautiana.
Wanasaikolojia hao walibainisha sifa za Marais kumi wa Marekani, ikaonekana
kuwa Marais hao siyo wawazi na hupindisha mambo ili mambo yao yaende vizuri.
Lakini imeonekana kuwa Marais wa Karne hii ni "extraverts," na wanajumuika
sana na jamii.
Rais anatakiwa awiwe na Mafanikio, shabaha ya kuongoza, uwezo, ufanisi pamoja
na uwezo wa kitaalamu, wenye kudhibiti hasira.,w enye imani ya kiroho na
waadilifu.
Watu kama Richard Nixon, Teddy Roosevelt Nyerere, Mkapa, Abeid Karume,
Kenyata, Salmi Amour wababe; John Adams, Nixon, Nasser, Jumbe ni “Introverts”;
Rutherfor Hays, Gerald Ford, George Washington, Nyerere, Augustine Neto,
Kaunda, Kikwete, Mwinyi, Nkrumah wana roho nzuri; Warren Harding, Nyerere,
Kikwete, Neto, Lumumba, wanyoofu; Reagan, Warren Harding, Clinton, Chisano
waigizaji; Bush, Ford, Truman, Mkapa, Kikwete, Nyerere, Chisano wana Msimamo;
Lincoln, Jefferson, Madison, Carter, Mwinyi, Nyerere, Nkrumah, Kikwete
wanafilosofia; FDR Kennedy, Clinton, Theodore Roosevelt, Nyerere, Kikwete na
Reagan ni "Extraverts".
Rais Kikwete kafanya yafuatayo; Kushusha kodi ya ongezeko la thamani kutoka
asilimia 20 hadi 18, kodi ya mapato asilimia 30 hadi 25, kuimarisha Sera ya
Medium Term Pay Policy kwa kiwango cha asilimia 60, kuimarisha ushiriki wa
Elimu ya Msingi na Sekondari kupitia Kata, kuboresha miundombinu, Kuimarisha
Umoja wa Kitaifa katika Muungano, na kuimarisha Pato la Taifa kama
ilivyooneshwa kwenye Picha Na 1,
Aidha, Kuimarisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ikiwa ni pamoja na kuanzisha
soko la Pamoja, Kudhibiti Soko la Madini hasa ya Tanzanite na Kuanzisha Ukaguzi
hivyo kusababisha baadhi ya Makampuni ya Madini kuanza kulipa kodi, Kudhibiti
Ushukaji wa Pato la Taifa wakati wa Mdororo wa Uchumi kwa wastani wa asilimia
7.0, kupunguza kasi ya mfumuko wa bei, kuongeza uwezo wa Mikopo kwa sekta
binafsi kutoka wastani wa asilimia 10 Mwaka 2005 hadi wastani wa asilimia 55
Mwaka 2009, Kuongeza wigo wa uwekezaji (FDI) kutoka Dola za Marekani
494.1milioni Mwaka 2005 hadi 695.5milioni Mwaka 2008, Kuongeza nafasi za
Uongozi kwa Wanawake (Mawaziri 7), (Wabunge 98), (Viti Maalum 75), Wakuu wa
Mikoa 3, Ma-RAS 9, Makatibu Wakuu 8, Manaibu Katibu Wakuu 2, Makamishna 4,
Wakurugenzi kutoka 133, Wakuu wa Wilaya 25, Ma-DAS 34, Majaji Mahakama ya
Rufaa 18 na Mahakama Kuu 15,
Mengine ni Kuongeza udhibiti wa umiliki wa viwanja, Mifugo na zao la samaki,
Kuimarisha Kilimo cha Umwagiliaji pamoja na usambazaji wa Maji, na Kuboresha
huduma ya Afya katika udhibiti Maradhi. Orodha ni ndefu sana.
Picha Na 1: Mapato ya Ndani kwa asilimia ya Pato la Taifa
Chanzo: Wizara ya Fedha na Uchumi
Tunawaomba mchague Rais mzoefu, atakayelipeleka Taifa mahala penye neema.
Tunawatakia safari njema.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA
top related