bendera tatu, s.l.p. 9184, dar es ... · 1 tanzania ports authority | bendera tatu, s.l.p. 9184,...

16
1 TANZANIA PORTS AUTHORITY www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba 20 17 - 28 Juni, 2013 Macha awaasa wafanyakazi bora mwaka 2013 kuwa mfano wa kuigwa Uk. 16 Rais aipongeza DOWUTA Uk. 12 CHEC kutekeleza mradi wa Ga Na. 13 na 14 Uk.7 Na Cecilia Korassa B andari ya Tanga imeng’ara kwa kuibuka mshindi wa kwanza katika maonesho ya kibiashara ya Mkoa wa Tanga yanayofahamika kama, ‘Tanga Trade Fair’, yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano mjini humo hivi karibuni. Bandari Tanga yang’ara Inaendelea Uk. 2 Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe na cheti cha ushindi kwa Bi. Thekla Malombe. Ni katika maonesho ya biashara

Upload: others

Post on 15-Feb-2021

0 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 1

    TANZANIA PORTS AUTHORITY

    www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba 20 17 - 28 Juni, 2013

    Macha awaasa wafanyakazi bora mwaka 2013 kuwa mfano wa kuigwa

    Uk. 16Rais aipongeza DOWUTA

    Uk. 12CHEC kutekeleza mradi wa Gati Na. 13 na 14

    Uk.7

    Na Cecilia Korassa

    Bandari ya Tanga imeng’ara kwa kuibuka mshindi wa kwanza katika maonesho ya kibiashara ya Mkoa wa Tanga yanayofahamika kama, ‘Tanga Trade Fair’, yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano mjini humo hivi karibuni.

    Bandari Tanga yang’ara

    Inaendelea Uk. 2

    Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe na cheti cha ushindi kwa Bi. Thekla Malombe.

    Ni katika maonesho ya biashara

  • 2

    Tanga imeng’ara kwa kushika nafasi hiyo ya kwanza katika kundi la Biashara na Utoaji Huduma (Trade and Service) ambalo lilikuwa na Taasisi mbalimbali za Serikali.

    Katika maonesho hayo ambayo yalifunguliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdllah Kigoda (MB) Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lilipata nafasi ya pili huku Shirika la Mapato Tanzania (TRA) likiambulia nafasi ya tatu.

    Maonesho hayo ambayo yalikuwa ni ya kwanza na ya aina yake kwa Mkoa wa Tanga yalizishirikisha Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali pamoja na Wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na nje ya nchi.

    Akimkaribisha mgeni Rasmi,

    Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Galawa, alimwambia Waziri Kigoda kuwa lengo la kufanya maonesho hayo Mkoani Tanga ni kujiandaa na Maonesho makubwa ya Wawekezaji (Investors Forum).

    “Tunatarajia kufanya maonesho haya mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu kwa lengo la kupata Wawekezaji watakaopenda kuwekeza katika Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla,” alifafanua Galawa.

    Galawa ameongeza kwamba, “Tanga inatarajia Wawekezaji wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani watashiriki na endapo watawekeza kwenye viwanda, kilimo, uvuvi, misitu, sehemu zetu za utalii, miundombinu na Bandari basi Mkoa utapiga hatua katika

    maendeleo”.

    Kwa upande wake Waziri Kigoda aliahidi kuungana na Uongozi wa Mkoa wa Tanga na kuahidi kusaidia kufanikisha maandalizi ya maonesho hayo. “Nikiwa kama Waziri wa Viwanda na Biashara na pia kama Mdau wa Mkoa wa Tanga, nitashirikiana nanyi ndugu zangu na kuhakikisha kuwa Maonesho hayo yanafanikiwa,” alisisitiza Waziri Kigoda.

    Aidha Waziri Kigoda ameipongeza wale wote ambao wamekuwa washindi na kuwapa moyo wale ambao hawakushinda kuongeza juhudi ili mwezi Septemba wafanye vizuri.

    Katika maonesho hayo washindi walikabidhiwa zawadi za vikombe na vyeti.

    Ushindi

    Inatoka Uk. 1

    Maafisa wa Bandari ya Tanga wakiwa na furaha baada ya kukabidhiwa cheti na kikombe.

  • 3

    Miradi

    Na Focus Mauki

    Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo chini ya ufadhili wa Serikali ya Watu wa China utagharimu Dola Bilioni 10 ambapo inatarajiwa utakuwa ni uwekezaji mkubwa Barani Afrika na baada ya kukamilika kwake itakuwa kubwa kuliko zote katika Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

    Hivi karibuni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliingia mkataba na Serikali ya Watu wa China kujenga Bandari hiyo ya Bagamoyo ambapo China itawekeza kiasi cha Dola Bilioni 10 kujenga Bandari hiyo.

    Ujenzi wa Bandari hii utakwenda sambamba na uboreshaji wa Bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga pamoja na Bandari nyingine nchini. Mfano wa maboresho yatakayofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam ni pamoja na

    ujenzi wa magati mapya pamoja na ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kupakia na kupakua mizigo melini.

    Mara baada ya kukamilika kwake Bandari ya Bagamoyo inatazamiwa kuwa na uwezo wa kuhudumia shehena ya kontena milioni 20 kwa mwaka ikiziacha kwa mbali Bandari nyingine ndani ya Afrika Mashariki ambazo kwa sasa zinahudumia kati ya kontena 600,000 na 500,000 kwa mwaka.

    Bandari ya Bagamoyo kuwa kubwa Kusini

    mwa Jangwa la Sahara

    Makala Maalumu: Bandari ya Bagamoyo

    Ujenzi kutoathiri miradi katika Bandari nyingine

    Inaendelea Uk. 4

  • 4

    Katika ziara yake iliyofanyika Machi 24 na 25 mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete waliweka saini makubaliano ya ujenzi wa Bandari hii.

    Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa msaada wa Serikali ya Watu wa China sio jambo geni kwa Watanzania na katika historia ya nchi hii, kwani itakumbukwa kuwa nchi hizi mbili zimekuwa na mahusiano ya kindugu kwa zaidi ya miongo minne sasa ambapo kuna miradi mbalimbali imefadhiliwa na China.

    Katika hotuba yake ya hivi karibuni, Rais Kikwete amenukuliwa akisema, “Lengo la ziara ya Rais wa China ilikuwa ni kuimarisha uhusiano mwema uliopo baina ya China na Tanzania.

    Kutokana na ukweli huu makubaliano ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ni muendelezo wa mahusiano mazuri baina ya nchi hizi mbili hivyo basi tunapaswa kuenzi na kutunza miradi mikubwa yenye manufaa kwa Taifa hili kwa manufaa ya kizazi hiki na vijavyo.

    Katika kuonyesha jinsi ambavyo Serikali ya China inathamini uhusiano wake na Tanzania, ziara ya Mh. Xi Jinping, hapa nchini imekuwa ya kwanza katika Bara la Afrika ikiwa ni siku kumi tu baada ya Rais huyo kuchaguliwa kushika madaraka.

    Sio hivyo tu bali jambo lingine la kihistoria ni kwamba Rais huyo ametumia ziara yake hapa

    nchini kuitangazia Dunia Sera ya China kwa Afrika katika kipindi cha uongozi wake. Ni kweli kwamba Dunia ya sasa inatumia vizuri Diplomasia ya uchumi na mahusiano mazuri ili kuchochea kasi ya kukua kwa uchumi wa nchi hivyo ni vyema Tanzania ikazingatia mahusino mazuri yaliyopo na kukuza uchumi wa nchi yetu.

    Duru za kimataifa zinazungumzia namna mataifa ulimwenguni yanavyotafuta namna ya kuungana au kushirikiana kiuchumi au kijamii. Viongozi wetu wamefanya jitihada za kuirudisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuweka mazingira mazuri ya kibiashra na kijamii pamoja na kuweka wigo mpana wa soko la bidhaa na ajira ndani ya muungano.

    Pamoja na umbali wa kijografia, Tanzania na China zinashirikiana kwa kiwango kikubwa katika biashara ambapo wapo wafanyabiashara wanaoleta bidhaa kutoka China na wapo wanaopeleka malighafi na vifaa vingine China. Moja ya mambo muhimu ambayo kwa namna moja au nyingine yanasaidia kuwepo kwa mazingira mazuri ya kufanya biashara ni pamoja na Serikali kuweka sera nzuri, miundombinu imara, Bandari na huduma nzuri za viwanja vya ndege.

    Katika hotuba yake Bungeni Dodoma hivi karibuni, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe amenukuliwa akisema ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ni moja ya vipaumbele vya Serikali hii katika kuendeleza Bandari zake hapa nchini.

    Dk. Mwakyembe anasema ujenzi wa Bandari hii haukuja ghafla bali ulipewa kipaumbele katika Mpango wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), (2009 – 2028) ambao umelenga kuongeza uwezo wa kuhudumia ongezeko kubwa la shehena inayotarajiwa kukua katika Bandari ya Dar es Salaam.

    Ili kuona kipaumbele hiki kinatekelezwa kwa ukamilifu tayari Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji (EPZA) imetenga ardhi yenye ukubwa wa hekta 1,000 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

    “Ili kufikia lengo tulilojiwekea, Serikali yetu na Serikali ya Watu wa China ilisaini makubaliano tarehe 25 Machi, 2013 ya kuendeleza Bandari ya Bagamoyo na eneo lake la EPZ,” ameeleza Dk. Mwakyembe.

    Zipo taarifa zisizo rasmi zinazolenga kupotosha umma kwamba ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo utasitisha miradi katika Bandari nyingine jambo ambalo sio la kweli. Dk. Mwakyembe anasema miradi iliyobainishwa katika Bandari mbalimbali hapa nchini itaendelea kutekelezwa kama kawaida na anatoa mfano wa kazi ya ujenzi wa Bandari ya Mwambani akisema upembuzi yakinifu wa mradi umekamilika Desemba, 2012, na tayari eneo lenye ukubwa wa hekta 174 limenunuliwa kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Mwambani.

    Lengo la Serikali kujenga Bandari ya Mwambani ni kutaka itumike kusafirisha shehena za Uganda na maeneo

    Inatoka Uk. 3

    Miradi

  • 5

    mengine inakopita reli ya Tanga, Arusha hadi Musoma. Waziri ameongeza kuwa Wizara yake kupitia TPA imetangaza mradi huu ili kumpata Mwekezaji kwa ajili ya kuendeleza Bandari hii kwa mpango wa ubia.

    Kwa upande wa Bandari ya Mtwara, Waziri anasema Bandari hiyo itabaki kuwa kiungo muhimu katika kuendeleza shughuli za uwekezaji hasa uchimbaji wa mafuta, gesi, makaa ya mawe na chuma zinazoendelea katika ukanda huo.

    Kazi ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Mtwara nayo ilikamilika Oktoba, 2012 na taarifa hiyo imependekeza kuwa upanuzi wa Bandari ya Mtwara ufanyike kwa awamu mbili.

    Awamu ya kwanza ya mradi wa Bandari ya Mtwara itahusu kuendeleza eneo la Bandari lenye ukubwa wa hekta 70, ujenzi wa gati nne na uanzishwaji wa Bandari huru (free port zone) kwa ajili ya kuhudumia shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi.

    Awamu ya pili itahusisha ujenzi wa magati kwa ajili ya kuhudumia mizigo mchanganyiko (multi purpose bulk terminal) na uendelezaji wa shughuli za EPZ zinazohusiana na Bandari. Wizara ya Uchukuzi inaendelea kutekeleza mapendekezo ya utafiti huu na tayari Wizara kupitia TPA imetangaza mradi huu ili kumpata Mwekezaji kwa ajili ya ujenzi wa magati manne na uendelezaji wa Bandari huru.

    Miradi mingine itakayotekelezwa na TPA sambamba na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ni pamoja na kuboresha miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam na maeneo ya kazi kwa kuboreshaji gati namba 1 mpaka 7 katika Bandari ya Dar es Salaam na kuanza ujenzi wa magati manne (4) katika Bandari ya Mtwara.

    TPA inapanga kuanza ujenzi wa awamu ya pili ya mradi wa boya la kupakua mafuta baharini (SPM) mara baada ya awamu ya kwanza ya mradi kukamilika kwa mafanikio makubwa.

    Mamlaka pia inapanga kuanza ujenzi wa gati Na. 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam kufanya ununuzi wa chelezo (floating dock) katika Bandari ya Dar es Salaam, kuendelea na maboresho ya mradi wa kuwaweka pamoja watoa huduma wote (single window system), kuweka mfumo wa usalama Bandarini (port integrated security system) na kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya uendelezaji wa kituo cha mizigo cha Kisarawe (Kisarawe Freight Station) pamoja na ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa Bandari zote.

    Serikali kupitia TPA imetenga jumla ya Shilingi bilioni 343.223 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo. Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 137.973 zitatolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari na Shilingi bilioni 205.25 zitatoka kwa wahisani, mikopo yenye riba nafuu na wawekezaji binafsi.

    Miradi/Dondoo

    Dondoo ya Usalama Mahali pa Kazi:Jali Usalama Wako, wa Wenzako na Familia yako.

    Heshimu na kuzingatia Sera na Kanuni za Usalama katika maeneo ya Bandari.

    Usizidishe mwendo wa gari yako kwa zaidi ya kilometa 20 kwa saa, kumbuka

    Bandari ni eneo la kazi lenye vifaa hatarishi.

  • 6

    Teknolojia

    Mabadiliko yatangazwa mfumo wa malipo

    Bandari ya Dar es SalaamNa Mwandishi Wetu

    Mamlaka imetangaza mabadiliko ya mfumo wa malipo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa wateja wote wanaoutumia mfumo wa Benki ya CRDB.Katika taarifa yake kwa umma, TPA imewafahamisha wateja wake wote, wadau wa Bandari na Umma kwa ujumla kuwa kuanzia tarehe 07/06/2013, wateja wote wanaolipia kupitia Benki ya CRDB hawatatakiwa kurudi ofisi za Mapato za TPA kwa ajili ya kupeleka “Bank Pay in Slip” na badala yake watapaswa kwenda “Delivery Points” ili kuendelea na taratibu nyingine za kutoa mizigo yao.

    Taarifa hiyo imefafanua zaidi kwamba utaratibu huu mpya utawahusu Wateja wanaolipia Benki ya CRDB pekee, ambapo Wateja wa Benki nyingine wataendelea na utaratibu wa kawaida hadi hapo Benki zao zitakapounganishwa na mfumo wa malipo wa TPA.

    Uongozi wa Mamlaka umewahakikishia Wateja wake kuwa Mamlaka inaendelea na uboreshaji wa mifumo yake ya TEHAMA ili kuboresha huduma kwa Wateja.

    Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Bw. Phares Magesa

  • 7

    MiradiBaraza/Bajeti

    CHEC kutekeleza mradiwa Gati Na. 13 na 14

    Na Focus Mauki

    Kampuni ya China Harbour E n g i n e e r i n g Company Ltd (CHEC), imeteuliwa kuendeleza mradi wa gati namba 13 na 14 kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA).

    Hayo yamesemwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe Bungeni Dodoma hivi karibuni. Katika taarifa yake Waziri amesema Serikali inapanga kuanza utekelezaji wa mradi wa gati namba 13 na 14 kupitia Kampuni ya CHEC.

    “Kampuni hiyo mbadala imeteuliwa ili kuendelea na utekelezaji wa mradi huu,” amesema Dk. Mwakyembe ambaye alifafanua zaidi kwa kusema, mwezi Desemba mwaka 2012, Kampuni ya China Harbour Engineering Company Ltd (CHEC) iliteuliwa na Serikali ya Watu wa China kuendeleza mradi huu.

    Amesema mazungumzo kati ya TPA na CHEC kwa ajili ya kukamilisha kazi iliyokuwa imebaki ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina (study and detail engineering

    design) yamekamilika na sasa Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza kazi Juni, 2013.

    Pamoja na mradi wa gati namba 13 na 14, Dk. Mwakyembe amesema miradi mingine iliyotekelezwa na Mamlaka ni pamoja na kufanya upembuzi yakinifu wa kuimarisha na kuongeza kina cha gati namba 1 hadi 7 katika Bandari ya Dar es Salaam.

    Kazi ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kazi hiyo ilianza mwezi Mei mwaka 2012 na kukamilika Machi, 2013. Kazi hiyo inatarajiwa kugharamiwa na Trade Mark East Africa (TMEA) na Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini (Development Bank of South Africa - DBSA).

    Mradi huu ni moja ya miradi ya Bandari iliyotangazwa na Mamlaka itakayozishirikisha sekta binafsi katika kugharamia utekelezaji wake chini ya utaratibu wa ‘Design, Finance and Build’. Wakati huohuo Dk. Mwakyembe amesema upembuzi yakinifu wa ujenzi wa kituo kikubwa cha kuhifadhia mizigo katika eneo la Kisarawe kwa ajili ya mizigo ya kwenda Zambia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi, Uganda na Rwanda unatarajiwa kukamilika Septemba, 2013.

    Tayari ekari 1,468 zimetengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu. “Taratibu zinakamilishwa ili Bandari Kavu ya Mbeya ‘Mbeya Dry Port’ ianze kazi ndani ya mwaka wa fedha 2013/14,” amefafanua Dk. Mwakyembe.

    Kuhusu msongamano wa mizigo ya makasha Bandarini, Dk. Mwakyembe ameliambia Bunge kuwa, Serikali imeendelea na juhudi zake za kupunguza msongamano wa makasha Bandarini ambapo mwezi Aprili, 2013, TPA ilikamilisha ujenzi wa eneo la kuhifadhia makasha yanayohudumiwa na kitengo chake ndani ya Bandari ya Dar es Salaam.

    Kukamilika kwa eneo hilo ambalo lina ukubwa wa mita za mraba 22,601 kumeongeza ufanisi katika kuhudumia shehena ya makasha pamoja na magari.

    Mbali na hayo Mamlaka imenunua kreni tatu zenye uwezo wa kubeba tani 100 kila moja kwa ajili ya kuhudumia shehena ya makasha hatua ambayo itapelekea kuongeza ufanisi wa utendaji katika utoaji wa huduma za makasha.

  • 8

    Matukio mbalimbali katika picha

    Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga, Bw. Freddy Liundi na Wakuu wa Idara wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi bora wa Bandari hiyo.

    Wafanyakazi wa Idara ya Fedha ya Bandari ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa tafrija ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 iliyofanyika katika ufukwe wa Sun Rise Beach Resort Kigamboni.

    Kamati iliyofanikisha tafrija ya Idara ya Fedha ya kuukaribisha mwaka 2013 wakiwa katika picha ya pamoja kwenye fukwe ya Sun Rise Beach Resort Kigamboni.

    Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mhe. Eugen Mwaiposa akiwa na Kapteni watimu ya mpira wa Miguu ya Makao Makuu Ernest Komba wakati akimtambulisha Mchezaji Machachari Frank Simbeya “ZIZZU’’ kabla ya mchezo wa Bonanza la nne la Ujirani Mwema, anayefuata kushoto ni Karimu Sabu kiungo.

  • 9

    Matukio mbalimbali katika picha

    Kamati iliyofanikisha tafrija ya Idara ya Fedha ya kuukaribisha mwaka 2013 wakiwa katika picha ya pamoja kwenye fukwe ya Sun Rise Beach Resort Kigamboni.

    Wafanyakazi wa Idara ya Fedha Bandari ya Dar es Salaam wakicheza muziki kwenye tafrija ya kuuaga mwaka 2012.

    Meneja wa Timu ya Makao Makuu, Bw. Khalid Rubama akitoa mawaidha kwa wachezaji kabla ya mchezo wao na timu ya Ukonga wakati wa bonanza la ujirani mwema lililofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kitunda.

    Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mhe. Eugen Mwaiposa akiwa na Kapteni watimu ya mpira wa Miguu ya Makao Makuu Ernest Komba wakati akimtambulisha Mchezaji Machachari Frank Simbeya “ZIZZU’’ kabla ya mchezo wa Bonanza la nne la Ujirani Mwema, anayefuata kushoto ni Karimu Sabu kiungo.

  • 10

    Wahitimu Baraza/Bajeti

    Hazina ya wasomiBandarini yaongezekaNa Mwandishi Wetu

    Hazina ya Wasomi ndani ya TPA i m e o n g e z e k a baada ya Wafanyakazi wawili kutoka Idara za Uhandisi na Zimamoto za Makao Makuu kuhitimu Shahada ya Pili ya Uzamili ya Chuo Kikuu cha Mzumbe na mmoja wa Idara ya Ulinzi na Usalama, kutoka Bandari ya Tanga kuhitimu Shahada yake ya Kwanza ya Sheria (L.L.B) ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

    Mhitimu wa kwanza mtaalamu wa biashara, kutoka Idara ya Uhandisi, Bw. Sylvester Kanyika ambaye aliajiriwa rasmi mwaka 2009 amefanikia kuhitimu Shahada yake ya Pili ya Uzamili (Masters Degree in Corporate Management) mwaka 2012 katika Chuo Kikuu cha Mzumbe.

    Naye Bw. Abeid Gallus aliyeajiriwa mwaka 2008 katika Idara ya Zimamoto mara baada ya kuhitimu masomo yake ya Shahada ya Uhasibu na Fedha katika Chuo Kikuu cha Mzumbe amefanikiwa kusonga mbele

    kwa kuhitimu Shahada ya pili ya Uzamili (Masters Degree in Corporate Management) mwaka huohuo katika Chuo Kikuu cha Mzumbe.

    Kwa upande wa mhitimu wa masomo ya Sheria, Bw. Kharid Kitentya anasema safari yake ilianzia ngazi ya cheti katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alifanikiwa kuhitimu mwaka 2002 na baadae tena kusoma Stashahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mwaka 2006.

    Bw. Kitentya baadae alijiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza ya Sheria yanayotolewa na OUT na kufanikiwa kuhitimu hivi karibuni. “Elimu niliyoipata imenipa hamasa, faraja, ari na uwezo mkubwa wa kufanya

    kazi kitaalamu na sasa imenipa msukomo wa kujiendeleza zaidi ambapo nimeamua kuendelea na masomo ya Shahada ya Pili katika fani ya Uhalifu wa Makosa ya Jinai ya Kimataifa,” anasema Kitentya.

    Kwa upande wake Bw. Gallus anasema, “Nashauri Wafanyakazi wenzangu kujikita zaidi katika kujiendeleza kielimu ili kuweza kufaidi fursa mbalimbali zinazojitokeza.”

    Naye Bw. Kanyika ameonesha kuunga mkono kauli hii ambapo ametoa wito kwa Menejimenti kuendelea kutoa msaada kwa Wafanyakazi hasa wa kuwaendeleza kielimu kwa lengo la kuwaongezea ari Wafanyakazi ili baadae kuleta tija kwa Mamlaka.

    Wahitimu katika picha.

  • 11

    Pongezi Miradi

    Utekelezaji miradi Bandari za Maziwa

    kuendeleaNa Focus Mauki

    Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe amesema Wizara kupitia TPA inaendelea kutekeleza miradi ya ujenzi katika Bandari za maziwa. Dk. Mwakyembe ametoa kauli hii Bungeni Dodoma ambapo amesema kwa kushirikiana na Manispaa ya Kigoma Ujiji, itafanyika tathamini kwa ajili ya kulipa fidia eneo la ujenzi wa gati la Kibirizi.

    Ameongeza kuwa kazi ya kumpata Mtaalamu Mwelekezi wa kufanya upembuzi yakinifu wa kuendeleza Bandari ya Mwanza South nayo inaendelea na inatarajiwa kukamilika Juni, 2013 huku ujenzi wa gati katika Bandari ya Kiwira nao ukiendelea na unatarajiwa kukamilika Desemba, 2013.

    Kwa upande mwingine, Dk. Mwakyembe amesema ujenzi

    wa gati katika Bandari ya Mafia unaendelea na unatarajiwa kukamilika Juni, mwaka huu huku ujenzi wa gati katika eneo la Kagunga ukiendela na kutarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu.

    Miradi mingine iliyoendelea kutekelezwa katika mwaka wa fedha wa 2012/2013 ni pamoja na ujenzi wa magati katika Ziwa Tanganyika maeneo ya Kipili,

    Karema, Lagosa na Sibwesa.

    Pamoja na kasi ya maboresho zipo changamato mbalimbali kama vile kutokamilika kwa wakati kwa ujenzi wa magati hayo lakini tayari Uongozi mpya wa Mamlaka umechukua hatua kurekebisha kasoro zilizopo ikiwa ni pamoja na kuajiri Mshauri Mwelekezi kupitia upya Mkataba ili kubaini udhaifu katika masharti na taratibu za utekelezaji wa mradi.

    Dk. Mwakyembe ameliambia Bunge kuwa hatua nyingine iliyochukuliwa ni pamoja na kufanya mapitio ya michoro ya magati manne (4) na kuiboresha pale itakapolazimu pamoja na kuimarisha nguvu kazi kutoka Makao Makuu kwenda Kigoma kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa miradi katika Ziwa Tanganyika.

    Katika mwaka 2013/2014, TPA imelenga kuhudumia jumla ya tani milioni 13.84 ikijumuisha tani za makasha yatakayohudumiwa katika kitengo cha TICTS.

    Mv. Liemba ikielekea kutia nanga kwenye gati la Bandari ya Kasanga.

  • 12

    Wafanyakazi Bora

    DOWUTA wapongezwa

    Na Mathew Muniku

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amekimwagia sifa Chama cha Wafanyakazi wa Kuhudumia Meli (DOWUTA) kwa kuratibu Maonesho ya Mei Mosi yaliyofanyika Mkoani Mbeya hivi karibuni.

    Rais ameyasema hayo wakati wa kukabidhi zawadi kwa Wafanyakazi Bora kwa Taasisi za Serikali jijini Mbeya siku ya kilele cha maadhimisho ya Mei Mosi kwa mwaka huu.

    Akipokea pongezi za Rais, Mwenyekiti wa DOWUTA Kitaifa, Bw. Bwana Edmund Njowoka amesema siri kubwa ya mafanikio katika kazi ni moyo wa kujituma na ushirikiano wa hali ya juu walioupata wakati wote wa maadhimisho hayo.

    Katika sherehe hizo ambazo ziliadhimishwa Kitaifa mkoani Mbeya, Wafanyakazi wawili wa Mamlaka, Bw. Cornelis Kufahaizuru wa Idara ya Ulinzi na Usalama na Kapteni Hussein Kasuguru wa Idara ya Marine Mtwara walipata wasaa

    wa kuungana na Wafanyakazi wengine nchini na kushiriki tukio hilo kubwa la Kitaifa.

    Kufahaizuru (22) ameibuka bora Kitaifa mara baada ya

    kuonesha ujasiri wa kuzuia wizi wa shaba iliyokuwa iibwe katika Bandari ya Dar es Salaam. Kwa upande wake Kapteni Kasuguru ameonesha umahiri kwa kufanya kazi

    kwa kujituma. Wafanyakazi wote walipata nafasi ya kupokea zawadi kutoka kwa Rais Kikwete.

    Katika maadhimisho hayo Maafisa wa Idara za Masoko na Mawasiliano wa Mamlaka walipata fursa ya kuitangaza Mamlaka katika Maonesho ya Taasisi za Umma yaliyoenda sambamba na sherehe hizo. Sherehe za Mei Mosi mwaka huu zilibeba kauli mbiu isemayo “Katiba Mpya Izingatie Haki na Usawa katika Tabaka la Wafanyakazi”.

    Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi askari wa Mamlaka ya Bandari, Afande Cornelis Kufahaizuru mara baada ya kutangazwa

    kuwa Mfanyakazi Bora Kitaifa.

  • 13

    Ziara

    Wafanyakazi Bora Bandari Dar na Tanga watembelea

    mbuga za wanyamaNa Mwandishi Wetu

    Wafanyakazi Bora 16 kutoka Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni walikuwa wageni wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakati walipotembelea mbuga za wanyama za Manyara, Serengeti na Bonde la Ufa Morogoro.

    Ziara hiyo amabayo hutolewa na Utawala kila Mwaka kwa Wafanyakazi Bora walio mahiri huwawezeshwa kutembelea mbuga za wanyama hapa nchini ikiwa ni kielelezo cha kutambua mchango wao kazini na katika ujenzi wa Taifa.

    Kundi hilo la Wafanyakazi hodari lilipata fursa ya kushuhudia jinsi tabia za binadamu na wanyama zinavyoshabihiana na ilikuwa ni historia katika maisha pale walipopata fursa adimu ya kuona kipindi cha fungate.

    Kwa upande wake Mwenyekiti wa DOWUTA Bandarini, Bw. Athuman Mkangara ameendela kuiomba Menejimenti kuboresha zawadi za Wafanyakazi Bora ili kuendana na mazingira ya sasa.

    “Kero ya usafiri kutokana na hali ya barabara zetu ni kubwa tunaiomba Menejimenti kumfikiria Mfanyakazi huyo Bora kupanda ndege angalau siku hii,” amefafanua Mkangara.

    DOWUTA pia imeitaka Menejimenti kuangalia namna ya kuboresha zawadi katika Idara zenye watu wengi ili kuendana na hali halisi na kuwa na uwiano wa Wafanyakazi kutoka Idara zenye watu wachache.

    Akijibu hoja za DOWUTA kwa niaba ya Menejimenti, Meneja Rasilimali watu Bw. Macha amesema Menejimenti inatambua changamoto chache zilizopo na itaendelea kuboresha maslahi ya Wafanyakazi wake kadiri uwezo utakavyoruhusu.

    Wafanyakazi Bora wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, Tanga kwa mwaka 2013 wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya Hifadhi ya Serengeti. Hifadhi ya Serengeti inasifika kwa kuwa na wanyama wa kila aina ikiwa ni pamoja na kuhama kwa Nyumbu ambao ni kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

  • 14

    Pongezi

    Prof. Kapuya apongeza awamu ya kwanza ya

    mradi wa SPM kukamilikaNa Focus Mauki

    Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Prof. Juma Kapuya imeipongeza Serikali kwa kukamilisha mradi wa boya la kushusha mafuta lililopo baharini, unaofahamika kama ‘Single Point Mooring-SPM.’

    Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Prof. Juma Athuman Kapuya (Mb) wakati akiwasilisha maoni na ushauri wa Kamati yake kuhusu mapendekezo ya mpango na Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka ujao wa fedha 2013/14, Bungeni Dodoma hivi karibuni.

    Prof. Kapuya amesema kutokana na uamuzi wa Serikali wa kununua mafuta kwa wingi na kwa pamoja (Bulk Procurement System) ili kupunguza bei ya mafuta kwa mtumiaji, Kamati yake iliishauri Serikali kununua boya kubwa baharini ambalo litawezesha meli kubwa za tani 80,000 hadi 100,000 kushusha shehena ya mafuta ya kiasi cha tani 3,000 kwa saa.

    “Katika kuongeza ufanisi wa kuhudumia meli kubwa hapa nchini, Kamati inaipongeza Serikali kwa kukamilisha mradi wa boya hilo tangu Novemba 2012,” amesema Prof. Kapuya.

    Prof. Kapuya alifafanua zaidi kwa kusema, kukamilika kwa

    mradi kumeiwezesha Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia meli kubwa zenye uwezo wa kubeba mzigo wa tani 150,000 (DWT) kutoka 75,000 (DWT). Boya hili jipya lina uwezo wa kushusha shehena ya mafuta ghafi (crude oil) tani 3,500 kwa saa na mafuta safi tani 2,500 kwa saa.

    Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kukamilika kwa mradi wa SPM ni hatua ya kwanza na kuongeza awamu ya pili ya mradi huo itahusu ujenzi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ambapo kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza Julai, mwaka huu.

    LR2 PIONEER ikiwa katika boya jipya la SPM.

  • 15

    Uwekezaji/Mv. Liemba

    Ukaguzi Mv. LiembaKuanza mwezi Juni

    mwaka huu

    Na Focus Mauki

    Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe (MB), amesema wakaguzi kutoka Ujerumani walitarajiwa kuifanyia ukaguzi Meli ya Mv. Liemba tarehe 22 hadi 27 Aprili, 2013 lakini kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo ukaguzi huo haukufanyika.

    Waziri Mwakyembe amesema sasa kazi ya kuikagua Meli hiyo kongwe na maarufu itafanyika Juni 22 hadi 28 mwaka huu. Dk. Mwakyembe ametoa kauli hii Bungeni Dodoma ambapo alifafanua kwa kusema, “wakaguzi walitoa taarifa kuwa wasingeweza kupatikana ndani ya tarehe zilizopangwa mwanzoni kutokana na ratiba zao za kazi.”

    Waziri amefafanua madhumuni ya ukaguzi wa meli hiyo kuwa ni kutaka kujua hali yake halisi kwa ujumla ambapo wakaguzi wataangalia mwili, mkuku wa meli, mitambo na sehemu zingine zote ili kubaini gharama za matengenezo zinazohitajika.

    “Tunatarajia kuwa ukarabati wa Mv. Liemba utaanza mara baada ya ukaguzi huo,” alimalizia Dk. Mwakyembe. Wakati huohuo Serikali imesema utekelezaji wa ahadi yake ya kujenga meli mpya tatu katika ziwa Viktoria, Tanganyika na Ziwa Nyasa na ukarabati wa meli za MV. Viktoria, MV. Umoja na MV. Serengeti unaendelea.

    Waziri amesema Serikali ya Denmark imekubali kufadhili mradi huu kwa kutoa mkopo nafuu ambao Serikali ya Tanzania itagharamia asilimia 50 na Serikali ya Denmark asilimia 50.

    Ameongeza kwamba tathmini ya uhifadhi wa mazingira wa mradi huu ilikamilika Aprili, 2013. Mradi huu unatarajiwa kuanza kutekelezwa mwishoni mwa mwaka 2013 na kukamilika mwaka 2018.

    Mradi huu unatarajiwa kugharimu jumla ya Dola za Kimarekani milioni 60. wakati huohuo Serikali inawasiliana na Serikali ya Korea Kusini kupitia benki ya Exim ili kupata mkopo wenye masharti nafuu wa kujenga meli 3 za abiria na mizigo katika maziwa ya Viktoria, Tanganyika na Nyasa. Dk. Mwakyembe amesema, lengo la mradi ni kuhakikisha kwamba, ifikapo mwaka 2015 meli hizo ziwe zimekamilika.

    Dk. Mwakyembe amewaambia Wabunge kuwa uwezo wa boya jipya ni kuhudumia meli za mafuta zenye uwezo wa kubeba hadi tani 150,000 kwa wakati mmoja ni zaidi ya mara tatu ya uwezo wa Kurasini Oil Jet (KOJ), ambao ni tani 45,000.

    Alifafanua zaidi kwa kusema kwamba kwa kufanya kazi boya hilo jipya la mafuta sasa kumepunguza msongamano wa meli Bandarini, uliokuwa unachangiwa na meli nyingi ndogo ndogo lakini zenye uwezo mdogo wa kubeba mafuta.

    Dk. Mwakyembe amesema kwa sasa meli yenye tani 100,000 inahudumiwa kwa wastani wa siku 6 katika boya jipya (SPM) ambapo endapo kiasi kama hiki kingehudumiwa na KOJ basi zingetumika meli 3 ambazo zingehudumiwa kwa wastani wa siku 12.

  • 16

    Nasaha

    Macha awaasa wafanyakazi bora mwaka 2013 kuwa mfano wa kuigwaNa Cartace Ngajiro

    Meneja Rasilimali watu Bandari ya Dar es Salaam Bw. Jones Macha amewaasa wafanyakazi bora kwa mwaka 2013 kuwa mfano wa kuigwa pamoja na kufanya kazi kwa ufanisi na uadilifu.Macha ameyasema hayo hivi karibuni katika Hotel ya Ipara iliyoko jijini Arusha wakati ziara ya Wafanyakazi bora Bandari ya Dar es Salaam waliotembelea hifadhi ya Serengeti na Bonde la Ngorongoro.

    “Msibweteke na ushindi kwa kuwa bado mnakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuendeleza sifa ya kuwa wafanyakazi bora, kwanza jiulizeni tumekuaje bora? msibweteke na ushindi bali kuweni mfano kwa wenzenu,” amefafanua Macha.

    Wakati huohuo Macha ametoa pongezi kwa chama cha DOWUTA tawi la Dar es Salaam kwa kusimamia zoezi la kuchagua Wafanyakazi bora. “Natoa pongezi kwa Chama cha DOWUTA kwa kushirikiana na Uongozi kuweza kufanikisha zoezi zima na pia kufanikisha ziara hii.

    Aliongeza kwamba utaratibu uliopo wa kuchagua Wafanyakazi bora ni wa takribani miaka mitano lakini kwa mwaka huu uchaguzi umekuwa wa kiuhalisia tofauti na miaka iliyopita, ambapo mambo mbalimbali yalizingatiwa kama vile kuhusisha Idara zote na vyeo mbalimbali vya wakuu wa idara, makatibu muhtasi, makarani na wahudumu.

    Kwa upande wake Mwenyekiti wa DOWUTA Tawi la Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Athumani Mkangara amempongeza na kumshukuru Meneja Rasilimali watu huyo pamoja na Menejimenti kwa ujumla kwa kuendelea kuiunga mkono DOWUTA katika kuboresha maslahi ya Wafanyakazi. Mkangara ametoa pongezi zake kwa kusema, “DOWUTA tunajisikia furaha kufanya kazi na Menejimenti yote na tunaahidi kuendelea kuwapa ushirikiano.”

    Mkangara ameuomba Uongozi kufanyia kazi na kuboresha mambo matatu ambayo amesema ni pamoja na kuboresha utaratibu wa kupata Wafanyakazi bora katika Idara zenye Wafanyakazi wengi, kuboresha zawadi na utaratibu unaotumika kuwasafirisha Wafanyakazi bora wanapoenda ziarani.

    Akiongea kwa niaba ya Wafanyakazi bora Bw. Ally Mtambo ambaye ni Karani katika Idara ya Utekelezaji ameushukuru Uongozi wa Bandari pamoja na Wafanyakazi wenzake kwa kuwachagua kuwa Wafanyakazi bora kwa mwaka huu.

    Wafanayakazi bora wanne (4) waliotunukiwa zawadi mwaka huu ngazi ya Mkoa kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwa cheo na idara

    wanazotoka kwenye mabano ni pamoja na Bi. Cartace Ngajiro (Mapokezi, Mawasiliano), Dkt. Abdallah Mwinyi (Mganga Mwandamizi, Tiba), Bw. Elia Anyelwise (Uendeshaji, KOJ) na Bw. Cornelis Kufahaizuru (Askari, Ulinzi)

    Kwa upande wa Wafanyakazi bora waliong’ara kiidara, ni pamoja na Bi. Salma Mwamba (Katibu Muhtasi, Utumishi), Bw. John Milinga (Afisa Utekelezaji, Utekelezaji), Bw. Abdulrahiman Upande (Mooring Formen,Marine), Kimicho (Kaimu Meneja Ukaguzi, Ukaguzi), Kailembo (Afisa Ugavi Msaidizi, Ugavi), Yunus Mavura (Mwendesha pampu, zima moto na usalama), Bw. Alli Mtambo (Karani, Nafaka), Bw. Shabani Yahaya (Mhudumu, Fedha),

    Wafanyakazi wengine ni Bw. David Kessy (Karani, Biashara), Bi. Magreth Temba (Karani, Uhandisi), Bi. Yasinta Mago (Afisa Fedha, Mapato) na Bw. Wilfred Shayo (Afisa Utekelezaji, Makasha).

    Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wafanyakazi hao wamesema siri ya mafanikio katika kazi ni kujituma kwa bidii na kufanya kazi kwa moyo wa uzalendo.