tpa kufungua ofi si zake lubumbashi s - tanzania · 2015. 10. 28. · 1. tanzania ports authority....

16
1 TANZANIA PORTS AUTHORITY www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba Toleo Namba 2 2 24 - 30 Machi, 2014 Uk.10 OSHE yasisitiza matumizi ya vifaa kinga Bandarini Uk.5 Kazibure aimwagia sifa Idara ya makasha ‘Dar Port’ Uk.13 Wajumbe Bodi ya Kahawa waitembelea Bandari ya Tanga Tanzania na DRC zakubaliana kumaliza changamoto za uchukuzi Ziara ya Waziri wa Uchukuzi DRC TPA kufungua osi zake Lubumbashi Na Janeth Ruzangi S erikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimekubaliana kushirikiana kuondoa vikwazo vya usafirishaji wa bidhaa kati ya nchi hizo mbili ili kurahisisha usafirishaji wa shehena ya Kongo inayopitia bandari ya Dar es Salaam. Makubaliano hayo yalifikiwa hivi karibuni wakati Mawaziri wa Uchukuzi wa nchi hizo mbili walipokutana mjini Kinshasa Kongo. Katika kikao hicho Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe alimweleza Waziri wa Uchukuzi wa Kongo Mheshimiwa Justine Mwanangongo Kalumba kwamba Tanzania imedhamiria kuondoa changamoto mbalimbali za urasimu zinazowakabili wafanyabiashara wa Kongo wanaotumia Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akiagana na Waziri Justine Mwanangongo Kalumba mara baada ya mkutano wa pamoja. Kulia mstari wa mbele ni Gavana wa Jimbo la Kivu Kusini (DRC), Mheshimiwa Marcellin Chishambo na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini DRC, Balozi Anthony Cheche Inaendelea Uk. 2

Upload: others

Post on 23-Mar-2021

3 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

1

TANZANIA PORTS AUTHORITY

www.tanzaniaports.com | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email: [email protected] Toleo Namba Toleo Namba 22 24 - 30 Machi, 2014

Uk.10 OSHE yasisitiza matumizi ya vifaa kinga Bandarini

Uk.5 Kazibure aimwagia sifa Idara ya makasha ‘Dar Port’

Uk.13 Wajumbe Bodi ya Kahawa waitembelea Bandari ya Tanga

Tanzania na DRC zakubalianakumaliza changamoto za uchukuzi

Ziara ya Waziri wa Uchukuzi DRC

• TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi Na Janeth Ruzangi

Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya

Kongo (DRC) zimekubaliana kushirikiana kuondoa vikwazo vya usafirishaji wa bidhaa kati ya nchi hizo mbili ili kurahisisha usafirishaji wa shehena ya Kongo inayopitia bandari ya Dar es Salaam.Makubaliano hayo yalifikiwa hivi karibuni wakati Mawaziri wa Uchukuzi wa nchi hizo mbili walipokutana mjini Kinshasa Kongo.

Katika kikao hicho Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe alimweleza Waziri wa Uchukuzi wa Kongo Mheshimiwa Justine Mwanangongo Kalumba kwamba Tanzania imedhamiria kuondoa changamoto mbalimbali za urasimu zinazowakabili wafanyabiashara wa Kongo wanaotumia

Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akiagana na Waziri Justine Mwanangongo Kalumba mara baada ya mkutano wa pamoja. Kulia mstari wa mbele ni Gavana wa Jimbo la Kivu Kusini (DRC), Mheshimiwa Marcellin Chishambo na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini DRC, Balozi Anthony ChecheInaendelea Uk. 2

Page 2: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

2

Masoko

bandari ya Dar es Salaam ili kuondoa ucheleweshaji na kuongeza ufanisi wa huduma za uchukuzi wa shehena hiyo .

Mwakyembe alisema uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo mbili lazima uwe wa manufaa kwa wananchi wake na kwamba wakati ulikuwa umefika wa kuondoa vikwazo vinavyokwamisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

Waziri Mwakyembe alisema Serikali ya Tanzania inaendelea kuboresha huduma za uchukuzi kwa njia reli, barabara, bandari na usafiri wa anga ili kuhakikisha inatumia fursa yake ya kijiografia kikamilifu.

Ili kuwapunguzia usumbufu wafanyabiashara wa nchini DRC, Waziri alisema Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) hivi karibuni itafungua ofisi zake mjini Lubumbashi , DRC ambako wafanyabiashara hawatalazimika kusafiri mpaka Dar es Salaam kwa ajili ya kushughulikia utoaji wa mizigo yao.

Kuhusu adha wanayoipata wafanyabiashara wa nchi hiyo hasa baada ya kushindwa kuitoa bandarini mizigo yao kwa wakati Waziri aliitaka Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzisha Kituo cha mizigo kitakachokuwa maalum kwa ajili ya shehena ya Kongo na kuongeza kwamba TPA tayari ilikuwa na eneo la ekari 110 jijini Dar es Salaam na ardhi katika bandari ya Kigoma ambazo Serikali hiyo inaweza kuomba kiasi itakachohitaji.

Akizungumzia usafiri katika Ziwa Tanganyika ambalo pia linatumiwa na nchi za Kongo

na Burundi, Mwakyembe

alisema njia rahisi ya kumaliza tatizo la usafiri katika Ziwa hilo ni kuanzisha Kampuni ya Meli ya pamoja kati ya nchi hizo ambayo itamiliki na kuendesha meli ya abiria na mizigo na hivyo kurahisisha uchukuzi kupitia bandari za Kigoma na Kasanga.

Alisema Shirika la Reli Tanzania linatarajia kuanzisha huduma maalum ya usafirishaji shehena (Block Train) kati ya Dar es Salaam na Kigoma ambapo TPA itanunua vichwa vya treni na mabehewa kwa ajili ya huduma hiyo maalum ya reli. Katika kutekeleza makubaliano hayo, wataalam kutoka pande zote mbili watakutana pamoja na kuweka mpango na ratiba ya utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Uchukuzi wa DRC Bw. Justine Kalumba alisema Serikali yake inathamini uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili na kusema kwamba Wizara

yake itahakikisha makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili yanafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo ili kutoa fursa ya kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili.

Akiwa Lubumbashi ambapo alikutana na wafanyabiashara wa nchi hiyo wanaotumia bandari ya Dar es Salaam Waziri Mwakyembe alipata wasaa wa kupokea maoni na malalamiko mbalimbali kutoka kwa watumiaji hao ambao pamoja na mambo mengine walisifu ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam ikilinganishwa na miaka ya nyuma na kutoa malalamiko yao kuhusu usumbufu wanaoupata kutoka kwa Mawakala wa forodha wasio waaminifu ambao husababisha mizigo yao kuchelewa bandarini na kutokufanya kazi vizuri mara kwa mara kwa mtandao wa TRA jambo linalosababisha ucheleweshaji wa mizigo na hivyo kutozwa gharama kubwa za tozo za kuchelewa kutoa mizigo yao bandarini.

Inatoka Uk. 1

Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari mara baada Kukutana na Gavana wa Jimbo la Kivu Kusini (DRC), Mheshimiwa Marcellin Chishambo mwenye kofi a. Wa kwanza kulia ni Balozi wa Tanzania DRC Mhe. Anthony Cheche.

Page 3: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

33333333

Elimu

Na Focus Mauki

Mtumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Bw. Joseph Kakeneno anatarajiwa kutunikiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) Septemba 02 mwaka huu, na Chuo cha Dublin, UCD cha nchini Ireland.

Kakeneno ambaye amefaulu kwa alama za juu masomo yake hayo ni Meneja Mifumo ya Menejimenti (Chief of Management of Systems) ndani ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Yafuatayo ni mahojiano maalumu:

Swali: Ulianza lini masomo yako na umetumia muda gani kuyakamilisha?

Jibu: Nilianza Mwaka 2010. Nimetumia miezi 42, kama miaka mitatu na nusu. Nilimaliza kozi na mitihani yote mwezi Septemba, 2013. Hata hivyo, matokeo rasmi yaliwasilishwa kwangu na kwa Mamlaka mwezi Februari, 2014.

Swali: Je utafiti wako ulihusu nini hasa na je nini lengo la utafiti huo?

Jibu: Utafiti wangu ulihusu namna ya kutumia mbinu za sayansi ya ufanyaji maamuzi (Decision Science) kuwezesha, kurahisisha na kuboresha mifumo ya ufanyaji maamuzi shirikishi na michakato husika katika maamuzi yahusuyo maendeleo na miradi (Participatory Decision-Making, Project Planning and Developmental Processes).

Swali: Je ulipata msaada ‘suppport’ kutoka Uongozi wa Mamlaka kufanikisha masomo yako?

Jibu: Pengine nitumie nafasi hii kushukuru uongozi wa Mamlaka, kwanza kwa kuniruhusu kusoma hii kozi na pili kunipa msaada. Kozi hii ilikuwa inafadhiliwa na nchi ya Ireland kupitia mpango wake wa misaada uitwao Irish Aid. Hata hivyo, yako maeneo machache ambayo ufadhili haukuyazingatia, hususan gharama za kufanya utafiti na hata tiketi za ndege za kuhudhuria makongamano ya kitaaluma na kutetea matokeo

ya utatifi. Mamlaka haikusita kuniwezesha kusafiri na kujikimu kulingana na Kanuni za utumishi zilizopo.

Swali: Ungependa kuwashukuru watu gani kwa kufanikisha masomo yako?

Jibu: Napenda kushukuru marafiki zangu, Profesa Hosea Rwegoshora wa Chuo Kikuu Huria na Profesa Allen Mushi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kunishauri kusoma hii kozi na kunitia moyo nilipokata tamaa. Profesa Mushi alikuwa, pia,

Msimamizi Msaidizi (Assistant Supervisor) wa Utafiti akisaidiana na Prof. Cathal Brugha wa Ireland. Kwa upande wa Mamlaka, ninamshukuru sana Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Madeni Kipande kwa kukubali kuniwezesha kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi bila kusita. Nawashukuru, pia marafiki zangu na wafanyakazi wenzangu ndani ya TPA ambao walinitia moyo ambao ni wengi na siwezi kuwataja wote hapa, shukrani za pekee ziende kwa familia yangu.

Swali: Unatoa wito gani kwa wana TPA na hasa vijana katika kujiendeleza kwa masomo mpaka ngazi ya PhD?

Jibu: Ninawashauri vijana na wengine wenye uwezo wa kujiendeleza, kutoogopa kujisajili katika masomo hadi ngazi ya Uzamivu kwa kuwa, kwanza, ni jambo linalowezekana. Aidha, shahada ya uzamivu inamwezesha mhitimu kuwa na upeo mpana wa kuchanganua matatizo na kuyatolea uamuzi au, angalau, kutambua nani hasa anaweza kuyatatua (problem solving capability). Mhitimu wa shahada ya uzamivu, hasa yule aliyeipata kwa kufanya utafiti,

Kakeneno kutunikiwa PhD

Bw. Joseph Kakeneno

Inaendelea Uk. 4

Page 4: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

4

Elimu/Uteuzi

anakuwa amefuzu kuwa “mweledi katika utafiti” au Professional Researcher. Ninapiga chapuo na kufagilia sanaaaaa! Nitafurahi nikiona wana TPA wanajitokeza, inawezekana panapo nia na msaada wa Mwenyezi Mungu.

Swali: Umejipangaje kutumia utaalamu wako kuongeza ufanisi wa shughuli za Mamlaka na hasa katika kitengo chako?

Jibu: Kujipanga?, Hapana. Ni kwamba tayari ninatumia uwezo wangu mpya katika kuongeza ufanisi katika eneo langu la kazi. Kwa bahati

nzuri, miongoni mwa majukumu muhimu ya Idara yangu ni kutatua matatizo (problem solving) kwa kubuni na/au kuunda mifumo ya kazi, ubora wa huduma na utendaji. Zaidi ya hayo, kozi hii imeimarisha uwezo wangu katika maeneo ya ufanyaji mipango shirikishi, utatuzi wa migogoro (confl ict resolution) na uwezo wa kufanya majadiliano (negotiation).

Swali: Uliwezaje kumudu kusoma PhD na majuku yako ya kazi?

Inatoka Uk. 3

Inaendelea Uk. 5

Na Moni Msemo, Evelyn Balozi (MSJ), Mohamed Hussein (MUM), Tanga

Tawi la DOWUTA Bandari ya Tanga, limemteua Dkt. Omary Khupe kuwa Kaimu Katibu wa tawi hilo baada ya aliyekuwa Katibu Bw. Iddi Bode

kustaafu kazi kwa mujibu wa sheria.

Dkt. Khupe wa Idara ya Tiba, aliteuliwa na wajumbe wa DOWUTA tawi la Tanga kuwa mrithi wa Bw. Mfaume kutokana na kukidhi vigezo kama inavyoainishwa na katiba ya DOWUTA toleo la 2008 kifungu 6.7 (a) inayozungumzia jinsi ya kujaza nafasi zilizo wazi.

Katiba hiyo inaelekeza kuwa iwapo nafasi yoyote ya kuchaguliwa, kuteuliwa au kuajiriwa imeachwa wazi kwa sababu yoyote ile, nafasi hiyo ni lazima ijazwe ndani ya miezi mitatu (3) na mtu mwenye sifa zinazostahili.

Aidha katika Kanuni Na. 6.0 Kujaza nafasi zilizo wazi, kifungu kidogo 6.1.5 inafafanua kuwa endapo nafasi iliyowazi ni ya uongozi wa tawi, kamati ya tawi itamteua mjumbe miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo kushika nafasi

Katibu mteule wa DOWUTA Tanga, Dkt. Omary Khupe.

DOWUTA Tanga yampata mrithi wa Bw. Bode kuelekea uchaguzi

hiyo kwa muda kama ambavyo wajumbe hao wametekeleza.

Akizungumza baada ya kuteuliwa, Dkt. Khupe alisema kuwa wanachama wa DOWUTA wategemee ushirikiano uliokuwepo mwanzo kuendelezwa, amani na mshikamano katika kipindi chote hadi uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Mei 2014.

“Katika uendeshaji wa kitu chochote ushirikiano ndio jambo la msingi, kwa hiyo nitashirikiana

na wanachama wote ndani ya kamati ya Tawi,” alisema Dkt. Khupe.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa DOWUTA Tanga, Bw. Ali Hassani Sankole alibainisha kuwa uteuzi huo uliofanywa Januari 6, 2014 licha ya uchaguzi kukaribia, umetokana na umuhimu wa nafasi husika kwa sababu Katibu ndiyo Mtendaji Mkuu wa Chama.

Page 5: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

5

Elimu/Hafl a

Jibu: Kwanza, kozi ilipangwa kwamba katika kila mwaka, niwe chuoni Ireland kwa miezi mitatu ili kupata fursa ya kufanya shughuli za masomo tu. Niliporudi nchini, Mamlaka iliniruhusu wasaa wa kujisomea na kufanya utafiti kulingana na Kanuni za Utumishi. Hata hivyo, changamoto za kazi nilizokuwa napata katika Idara yangu ya Mifumo ziliniimarisha zaidi katika taaluma kwa vile nazo zinahusisha utafuti wa kazi (Operational research).

Swali: Ni watanzania wangapi umemaliza nao mwaka huu?

Jibu: Ni vigumu kujua idadi ya watanzania waliohitimu nami kwa chuo kizima. Kwa eneo la uongozi (Business Administration) wahitimu wote mwaka huu kwa ngazi ya Uzamivu ni 5; watanzania 2, yaani, mimi na mwingine mmoja. Katika eneo la sayansi ya maamuzi, ni mimi tu kwa mwaka huu.

Swali: Ungependa kuongeza jambo jingine kuhusiana na mafanikio haya?

Jibu: Ndiyo. Ninamshukuru Mungu. Nimefurahi sana.

Inatoka Uk. 4

Meneja wa fedha Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Lucy Kazibure akikata keki huku akishuhudiwa na Maafi sa wa Bandari ya Dar es Salaam wakati wa hafl a ya kitengo cha kontena iliyofanyika hivi karibuni.

Kazibure aimwagia sifa Idara ya makasha ÂDar PortÊNa Cartace Ngajiro

Meneja wa fedha Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Lucy Kazibure ameimwagia

sifa Idara ya makasha Banadari ya Dar es Salaam “Container Terminal “ kwa kuonyesha juhudi, umoja na mshikamano.

Kazibure ameyasema hayo wakati wa tafrija ya kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 iliyofanyika Mikocheni hivi karibuni na kuambatana na shughuli ya kuwaaga wastaafu katika Idara hiyo.

Kazibure amesema licha ya Idara ya makasha kuwa changa lakini wafanyakazi wa Idara hii wameweza kuonyesha juhudi na kuunganisha nguvu katika uzalishaji na kuleta tija bandarini na kuziomba Idara nyingine kuiga mfano huo.

Kwa mujibu wa Kazibure, utendaji bora umepelekea idara hiyo kutoa Mkurugenzi wa Utekelezaji na amewaomba wafanyakazi kuendelea kutoa ushirikiano kila mara.

Aidha Kazibure amempongeza Mkuu wa Idara hiyo Bw. Habel Mhanga kwa kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Utekelezaji na kuwaomba

wafanyakazi kuendelea kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya.

Kwa upande mwingine Kazibure ametoa salamu za pongezi kwa wastaafu wa Idara hiyo kwa niaba ya Meneja wa Bandari, “kwa niaba ya Meneja wa Bandari napenda kuwapongeza wastaafu ambao leo tunawaaga hapa baada ya kuitumikia

Page 6: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

6

Wafanyakazi wa Idara ya makasha katika Bandari ya Dar es Salaam wakiwa katika hafl a ya kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014.

Mamlaka kwa zaidi ya miaka 20, mmeonyesha nidhamu ya hali ya juu na mmejitunza kipindi chote mlichokuwa Bandarini.”

Naye Mkurugenzi wa Utekelezaji Bw. Habel Mhanga ambaye alikuwa mkuu wa Idara hiyo ameushukuru uongozi kwa kumpa nafasi na kuwashukuru wafanyakazi kwa kuonyesha ushirikiano na nidhamu katika kipindi chote alichokuwa mkuu wa Idara.

Katika risala yao kwa mgeni rasmi wafanyakazi wa Idara hiyo wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano na kufanya kazi kwa maarifa na juhudi ili kuongeza tija na ufanisi zaidi kuweza kuendana na mpango wa matokeo makubwa sasa (Big Result Now).

Wastaafu walioagwa na vyeo vyao kwenye mabano ni Bw. Abdulrahman Boffu (SMEO), Bw. Yusuph Ntinyi (SMEO), Bw. Mohamed Kulwa (Labour Foreman), Bw. Omary Salum (Cargo Foreman), Bw. Patrick Kunambi (Cargo Foreman), Bw. Shabani Ally (Operation Officer),

Bw. Daud Benedict (SMEO) Bw. Seleman Sheweji (SMEO), Bw. Cassian Kisatu (SMEO 11) Bw. William Michael (Operations Officer) na Bw. Ramadhani (Forklift Operator).

Bandari ya Tanga waaswa kuwa na ushirikiano

Na Moni Msemo, Evelyn Balozi (MSJ), Mohamed Hussein (MUM), Tanga

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Tanga wameaswa kuacha kuwa na tabia ya chuki, kashfa na kutoa siri za mamlaka kwenye vyombo vya habari na badala yake wawe wenye ushirikiano,

mshikamano na kuelezana ukweli pale mmojawapo anapokosea kwa lengo la kuleta tija na ufanisi katika mamlaka hiyo.

Hayo aliyasema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Taifa (DOWUTA) wa Mamlaka hiyo Bw. Edmund Njowoka wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Mamlaka ya Bandari Tanga kwenye hoteli ya Nyinda Executive iliyopo mkoani humo ikiwa ni mara ya kwanza kuitembelea mamlaka hiyo tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi.

Bw. Njowoka alitoa changamoto kwa wafanyakazi hao kufanya kazi kwa nguvu na

bidii na ushindani kutokana na kwamba Mamlaka ya Bandari Mtwara inakua kwa kasi kubwa kutokana na kuwepo kwa makampuni mbalimbali yanayojihusisha na uchimbaji wa gesi na mafuta kuitumia Bandari hiyo kwa kiasi kikubwa kwa sasa.

Vilevile alisema kuwepo kwa ujenzi wa kiwanda kikubwa cha saruji ambacho kinajengwa na tajiri nambari moja Afrika Alhaji Aliko Dangote kutoka nchini Nigeria huenda kukaifanya bandari hiyo kuipita Bandari ya Tanga kwa ukubwa.

Hafl a/Ushirikiano

Page 7: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

77777777

Na Moni Msemo, Evelyn Balozi (MSJ), Bashiru Ramadhani, Tanga

Katibu anayemaliza muda wake wa Chama cha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (DOWUTA) Tanga, Alhaji Mfaume Iddi Bode ametoa wito

kwa Wanachama kuunga mkono mpango wa ‘BRN’(Big Results Now) kwa kuwa unalengo zuri la kurudisha nidhamu na uwajibikaji mahala pa kazi.Wito huo aliutoa hivi karibuni katika mkutano wa mwaka uliokutanisha wanachama wa DOWUTA Tanga na wadau wengine wa Mamlaka ya Bandari, alipopewa nafasi ya kuzungumza na wanachama hao sanjari na kuwaaga kupitia nafasi hiyo ambayo ni ya mwisho kwake kukutana na mkusanyiko huo.

Bw. Mfaume alisema kuwa katika kipindi kifupi kilichopita na siku za usoni Mamlaka ya Bandari inatoa ajira nyingi mpya kwa vijana ambao ni wageni katika kazi, hivyo mpango huo utasaidia kuwajenga katika misingi bora ya uwajibikaji na utendaji wenye tija.

“Ndugu zangu naomba mpango huu ukija muupokee, mpango huu unawataka kuondokana na ufanyaji kazi kwa mazoea…, makusudio ni kwa vijana wa sasa wanaoajiriwa kujua kanuni na mipaka yao ya saa za uwajibikaji,” alisisitiza Bw. Mfaume na kuongeza

“Kuna watu katika maisha ya kazi wanaishi kwa mazoea, hii haifai ndugu zangu, nimekwaruzika sana na watu walioondoka kazini katika kipindi changu cha uongozi eti kutokana na masuala ya ulevi… huu mpango utakapokamilika kutakuwa na vifaa vya kuwapima wafanyakazi, hata utaratibu wa kutoka na kuingia getini utabadilika”

Kwa upande mwingine Katibu huyo aliupongeza uongozi wa DOWUTA na watendaji wote kutokana na misingi bora ya utendaji kazi waliyojiwekea ambayo kwa kiasi kikubwa imeondoa kero zilizokuwa zinakwamisha utendaji wenye tija kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari.

“Kwa mfumo na utaratibu wa kuwa na vikao vya Idara mara kwa mara, kero nyingi za wanachama zimetatuliwa…, huko nyuma tulirithi kutokuwa na vikao tabia ambayo ilisababisha migogoro

na malalamiko mengi kupelekewa Wanasiasa” alisema Katibu huyo.

Katika kipindi cha mwaka 2013 Mamlaka ya Bandari Tanga ilimuachisha kazi mfanyakazi wake mmoja kwa kosa la ulevi, akiwa amelewa saa za kazi, huku wafanyakazi 11 waliachishwa kwa kughushi vyeti.

Awali mwenyekiti wa DOWUTA Tanga, Bw. Ally Hassani Sankole, akimkaribisha Katibu huyo alisema kuwa wanachama wa DOWUTA wataendelea kumkumbuka kiongozi wao huyo waliyemchagua kwa kura nyingi kutokana na umahiri wake katika kipindi chote cha uongozi alichotumikia wanachama kwa moyo.

Akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa chama wafanyakazi wa shughuli za meli na Bandari Tanzania (DOWUTA) tawi la Tanga, Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Bw. Freddy Liundi alisema Bandari ya Tanga imeongeza ufanisi katika uzalishaji kwa kuhudumia Tani 1600 kwa zamu (shift) ikilinganishwa na Bandari nyingine.

Bw. Liundi aliendelea kusema sasa “Bandari ya Tanga inahudumia Tani 1600 kwa shift tumeweza kuishinda hata Bandari ya Dar es salaam ambayo inahudumia Tani 600 tu kwa shift”

Vilevile Kaimu Meneja huyo aliwasifa viongozi wa chama hicho kwa kuchochea ajenda nyingi zinazowahusu Wafanyakazi wa Bandari na kuzifanyia kazi kwa wakati kutokana na ushupavu wao. Mwisho Bw. Liundi alimalizia kuainisha miradi ambayo itafanyika katika mwaka huu kwa kuongeza vifaa baharini na nchi kavu kama vile “spreaders” mbili za futi 40 na futi 20 pamoja na mabaji.

ÂMatokeo Makubwa Sasa ni kurudisha nidhamu na uwajibikaji kaziniÊ

BRN

Page 8: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

8

Matukio mbalimb

Kaimu Meneja wa Masoko Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Fungo akiwa na wafanyakazi wa Idara ya Utawala Bandari ya Dar es Salaam mjini Bagamoyo wakati walipotemnbelea vivutio vya kitalii mjini humo.

Wafanyakazi wa Idara ya Marine wakipata historia fupi ya masalia ya kale yaliyopo Bagamoyo wakati walipofanya ziara hiyo ikiwa ni sehemu ya kuukaribisha mwaka 2014.

Mganga Mkuu Mwandamizi Bandarakimkabidhi zawadi mstaafu, Bi. Hawastaafu wa Bandari hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya maandaDar es Salaam, Bi. Anna Mwamakuwa jumla wa michezo ya Bandari Ikukabidhi vikombe hivi karibuni.

Page 9: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

9

mbali katika picha

ndari ya Dar es Salaam, Dkt. Abdallah Mwinyi i. Hariat Mkurumbi katika sherehe za kuwaaga

andalizi ya michezo Bandari ya makula akibeba kombe la ushindi dari Inter-ports katika sherehe za i.

Meneja Mapato Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Shaaban Mngazija akisakata rhumba sambamba na Afi sa Mkuu Utawala, Bi. Natu Shilla katika sherehe za kuukaribisha mwaka 2014 hivi karibuni.

Wafanyakazi wa kitengo cha Nafaka wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya bwawa la viboko kwenye mbuga ya wanyama ya Mikumi ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kuukaribisha mwaka 2014.

Page 10: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

10

OSHE

OSHE yasisitiza matumizi ya vifaa kinga BandariniNa Innocent Mhando

Katibu wa kamati ndogo ya OSHE bandari ya Dar es Salaam Bibi Kijana Mlege amesisitiza wafanyakazi wa Mamlaka kutumia vifaa kinga muda wote wanapokuwa bandarini kwa lengo kuboresha usalama sehemu zao

za kazi.

Mlege alisema hayo hivi karibuni mara baada ya kamati hiyo kutoa mafunzo kwa wafanyakazi walio katika jengo la Meneja wa Bandari ikiwa ni mwendelezo wa utaratibu waliouweka wa kutoa elimu ya usalama katika sehemu za kazi katika bandari ya Dar es Salaam.

Alitaja vifaa hivyo ambavyo ni kinga mathubuti kwa mfanyakazi ambavyo vinaweza kumuepusha na ajali ni pamoja na, refractor, safety boots, gloves, eye protector na helmet.

katibu huyo alisema kuwa ili kujenga bandari yenye wafanyakazi wenye afya tija na wenye kutunza mazingira ya bandari lazima wafanyakazi wazingatie matumizi ya vifaa hivyo “wafanyakazi wenye vifaa kinga wavitumie kwani usalama unaanza na mtu mmoja mmoja baadae kwa kwa shirika zima,” alisema Mlege.

Pamoja na mambo mengine Bi. Mlege alitaja umuhimu wa mafunzo hayo kwa wafanyakazi ikiwemo mfanyakazi kufahamu vihatarishi ambavyo si rahisi kuviona kwa macho kama mionzi na kemikali zinazopatikana kwenye mbolea

ambapo mfanyakazi ambaye yupo maeneo hayo anawajibu

wa kuchukua tahadhari.

Naye Bi. Rosemary Mgalula ambaye ni mwakilishi wa idara nne katika kamati hiyo zilizo katika jengo la Meneja wa Bandari ikiwemo Mawasiliano, Ukaguzi wa Ndani “Internal Audit”, Utawala, Biashara na Masoko akiongea katika mafunzo hayo alisisitiza wafanyakazi kuepuka tabia ya kuosha magari katika jengo hilo pamoja na maeneo yote ya bandari kwa lengo la kutunza mazingira.

Vilevile Mgalula alikemea tabia ya baadhi ya wenye magari kuendesha mgari yao katika mwendo mkubwa pasipo kuzingatia mwendo ulioidhinishwa na mamlaka ambao ni kilomita 20 kwa saa ili kuepusha ajali bandarini na ili bandari liwe eneo salama muda wote.

Kwa upande wafanyakazi waliopatiwa mafunzo hayo Afisa Mipango Mwandamizi Andulile Mwaisaka akiongea kwa niaba ya wengine alisema kuwa mafunzo hayo yana manufaa makubwa kwani yamewapa elimu ya kutumia vifaa hivyo na umuhimu wa kuwepo vifaa hivyo katika maeneo ya kazi.

Kwa upande mwingine Mwaisaka ameiomba kamati hiyo kuhakikisha vifaa vya kinga vinapatikana kwa wakati kwa wafanyakazi kwani elimu pekee haitoshi kumfanya mfanyakazi kuwa salama pasipo kuwepo na vifaa vya kujikinga “ni muda mrefu umepita pasipo kuwa na vifaa kama safety boots, eye protector na mask na hatari haisubiri, muda wowote yaweza kutokea hivyo ni vizuri elimu inapotolewa na vifaa vinakuwepo”.

Bandari ni sehemu salama lakini imekuwa ikitokea ajali nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine zinasababishwa na uzembe wa madereva kwa kuendesha mwendo kasi, wafanyakazi kupuuzia alama za tahadhari pamoja na kutokuvaa vifaa kinga pindi waingiapo Bandarini.

Hivyo kamati hiyo ya OSHE ikaona ulazima wa kutoa elimu hiyo kwa wafanyakazi na wakati huohuo Mamlaka kupitia vitengo vyake vya Zimamoto na Usalama na Ulinzi vipo makini kuhakikisha wafanyakazi wanavaa vitendea kazi wakati wa kuingia na muda wote wanapokuwa bandarini.

Page 11: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

11

Hafl a

Hafla ya kufunga mwaka ya ÂAudit Dar PortÊ yafana

Na Peter Millanzi

Hafl a ya kuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 ya Idara ya Ukaguzi Bandari ya Dar es Salaam imefanyika kwa mafanikio na kufaana vilivyo kwa kuacha kumbukumbu ya namna yake kwa hafl a za idara

mbalimbali ndani ya Bandari ya Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Kaimu Meneja Utekelezaji, Bw. Nelson Mlali alimwakilisha Meneja wa Bandari. Mlali aliwapongeza wafanyakazi wa Idara hiyo kwa kuandaa sherehe ya iliyofaana.

Mlali pia aliwapongeza wafanyakazi wa Ukaguzi kwa kuchapa kazi kwa uaminifu, uadilifu, bidii kubwa na kwa kuzingatia miongozo ya kazi.

Amewaambia wafanyazi kuwa mabadiliko yaliyofanyika katika fani ya ukaguzi yamesaidia kwani zamani wakaguzi walifanya kazi za kiuhasibu zaidi kwa kutafuta makosa

Mkuu wa Idara ya Ukaguzi, Bibi Amina Makoko amewashukuru wafanyakazi wa idara yake kwa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu.

Makoko amesema licha ya changamoto zilizopo, idara yake inahitaji watu wasio na tamaa ya kupokea rushwa kwani bila kufanya kazi kwa uadilifu sehemu zingine haziwezi kwenda sawa.

Bibi Makoko amempongeza Afisa Ukaguzi Mkuu, Bi. Witness Mahela kwa kuonyesha mfano mzuri kwa wafanyakazi walioko chini yake katika kuchapa kazi kwa bidii, na kumsifu Mahela katika kufanya kazi kwa ushirikiano na wana-audit.

Aidha katika kundi la wahitimu waliopata zawadi ni Bi. Edith Kihigwa aliyehitimu Shahada ya pili katika kozi ya Uhasibu na Fedha (Master of Science in Accounting and Finance) kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe. Teddy Kalolo amehitimu kwa kupata Certified Information System Auditor (CISA) ambayo inasimamiwa na taasisi ya kimataifa yenye makao makuu yake nchini Marekani inayoitwa Information System Audit and Control Association (ISACA).

hali inayosababisha wakaguzi kuogopwa.

Mlali alitoa rai kwa wana-audit wanapopanga mafunzo wasipange yale tu yanayojikita katika uhasibu bali wapange mafunzo yanayojikita katika maeneo mbalimbali.

Wakati huohuo, wana-audit wamewaaga Bw. Wilson Marwa na Bi. Rose Bendera ambao wamestaafu kwa mujibu wa sheria. Wastaafu hao wamewashukuru wafanyakazi wa idara hiyo kwa umoja, upendo na ushirikiano.

Mgeni rasmi, Nelson Mlali (katikati) akimzawadia mstaafu Wilson Marwa (kulia) na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ukaguzi, Bibi Amina Makoko.

Page 12: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

12

Bw. Freddy Liundi akimkabidhi zawadi Alhaji Mfaume Bode kutoka kwa Wajumbe wa Baraza dogo la Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga katika hafl a ya kumuaga baada ya kustaafu.

Na Moni Msemo, Evelyn Balozi (MSJ), Tanga

Baraza la Majadiliano la Mamlaka ya Bandari (TPA) Tanga limepata pengo baada ya Wafanyakazi wake ambao pia ni wajumbe wa Baraza hilo Bi.

Cecilia Korassa wa Idara ya Mawasiliano (Mjumbe Upande wa Menejimenti) na Bw. Alhaji Bode Mfaume (ambaye alikuwa Katibu wa DOWUTA) kutoka idara ya ‘Marine’ kumaliza muda wao wa utumishi ndani ya Mamlaka hiyo Desemba 2013.Wajumbe hao wa Baraza wameitumikia Mamlaka kwa zaidi ya miaka 30 bila kuwa na karipio au onyo dhidi ya utendaji kazi wao.

Kaimu Mkuu wa Bandari Tanga, Bw. Freddy Liundi amesema wastaafu hao wameacha njia nzuri ya kufuatwa na watumishi wanaobaki.

Nae Mwenyekiti wa Chama

cha Wafanyakazi wa Bandari (DOWUTA) Tanga, Bw. Ali Sankole amemtaja Alhaji Mfaume ambae alikuwa Katibu wa Chama hicho kuwa ni mtu mwenye ustahimilivu kwani pamoja changamoto za mara kwa mara alihakikisha malengo ya wafanyakazi na mamlaka yanafikiwa kwa njia ya amani.

Katika hatua nyingine Mhasibu Mkuu wa TPA Tanga, Bw. Tryphone Ntipi kwa niaba ya Wakuu wa Idara, amewapongeza wastaafu hao na kusema kuwa kustaafu ni tukio la kishujaa.

Awali Kaimu Afisa Mkuu wa Utumishi wa TPA Tanga, Bi. Thecla Malombe aliwataka wajumbe wa baraza waliohudhuria hafla hiyo kufuata nyao za wastaafu hao kwani hadi wanamaliza muda wao utumishi hakukuwepo malalamiko yoyote ya kutowajibika ndani na nje ya Mamlaka.

Hata hivyo kwa nyakati tofauti wastaafu hao walibainisha siri ya wao kumaliza kipindi cha utumishi bila kuwa na doa, kwamba ni kujituma kusikokuwa na mwisho huku

Wastaafu Tanga waagwa kishujaa

Bw. Freddy Liundi akimkabidhi zawadi Bi. Cecilia Korassa kutoka kwa Baraza dogo la Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga katika hafl a ya kumuaga baada ya kustaafu.

Wastaafu

Page 13: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

13131133311333

Na Moni Msemo, Mohamed Hussein (MUM), Winfrida Paul, Tanga

Wajumbe bodi ya kahawa Tanzania wakiongozwa na

aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Juma Ngasongwa (ambaye ni Mwenyekiti wa bodi hiyo) wameitembelea Mamlaka ya Bandari Tanga ili kujionea uendeshaji wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo.

Bwana Ngasongwa aliusisitizia uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanga kuweka mikakati zaidi ili kushindana na kasi ya mabadiliko ya Bandari inazowazunguka za Mombasa na Dar es Salaam, alisema “ Ni vyema mkatenga bajeti itayotosheleza Bandari yenu kujitangaza ndani na nje ya nchi ili mueneze taarifa bora za kwanini Wateja watumie Bandari ya Tanga na sio Bandari nyingine katika kusafirisha mizigo yao” alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Akizungumzia kuhusu uhusiano uliopo baina ya Mamlaka ya Bandari Tanga na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Afisa utekelezaji mkuu wa Bandari ya Tanga Bw. Khalifa Mkwizu alisema kuwa, Mamlaka zote hizi hushirikiana katika ukaguaji, uingizaji na utoaji wa mizigo kupitia kifaa cha kisasa kilichopo Bandarini hapo ambacho kitaalamu kinaitwa “Scanner”, chombo hiki hutumika hususani kubaini mali zisizohalali kama vile madawa ya kulevya, meno ya tembo na mengineyo katika usafirishaji wa mizigo hiyo.

Naye Bw. Amiri Hamza ambaye ni mjumbe wa bodi hiyo na Mwenyekiti wa shirikisho la kahawa Tanzania (‘Tanzania Coffee Association’) aliwaasa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa inaweka mikakati ya kuongeza ufanisi

zaidi ili iwe kivutio cha wafanyabiashara kuitumia kupitisha mizigo yao kuliko bandari nyingine za jirani.

Bandari ya Tanga inatumika vizuri sana katika usafirishaji wa kahawa nje ya nchi kama vile Japan, China, Ulaya na nchi nyinginezo.

Wajumbe wa Bodi ya Kahawa Tanzania wakipata maelezo kutoka kwa Afi sa Utekelezaji Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanga Bw. Khalifa Mkwizu (aliyenyoosha mkono). Kulia ni Bw. Freddy Liundi na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw. Juma Ngasongwa (aliyevaa suti) na Menyekiti wa Shirikisho la Kahawa Tanzania Bw. Amiri Hamza (kushoto).

Wajumbe Bodi ya Kahawa waitembelea Bandari ya Tanga

Kahawa

Page 14: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

14

Idara ya Fedha na Mapato wauaga mwaka 2013

Na Innocent Mhando

Idara ya mapato kwa kushirikiana na ya fedha wamefanya sherehe ya aina yake ya kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 iliyofanyika katika hoteli ya Palm Tree bagamoyo.

Mgeni rasmi katika sherehe hiyo Bibi. Natu Shila akiongea kwa niaba ya Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam wakati wa sherehe hiyo amezipongeza idara ya fedha na mapato kwa kuboresha huduma zake katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

Shilla alisema kuwa idara hizo awali zilikuwa zikipata changamoto mbalimbali lakini wameonesha ujasiri na kuboresha huduma zao ikiwemo kufanya kazi kwa umakini na kuendena na kasi ya matokeo makubwa sasa.“Tunashukuru kwa maboresho mliyoyafanya

katika miaka mingi na mnayoendelea kuyafanya katika katika kuwahudumia wafanyakazi”. Alisema Shilla.

Pia shilla aliwataka wafanyakazi wote kwa ujumla kujituma pasipo kusukumwa katika kutekeleza majukumu

Kiongozi wa DOWUTA, Bw. Hassan Hemedy akitoa mkono wa pongeza kwa Msataafu,Bw. Tini Padasi katika sherehe ya kuwaaga wastaafu wa idara hiyo.

Hafl a

Page 15: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

15

yao, “kila mtu ajiwajibishe na kufanya kazi kwa bidii , kwa upendo na kwa kushirikiana katika kutimiza majukumu aliyopewa”. Alisema Shilla.

Pamoja na mambo ,mengine Idara ya fedha ilimuaga mfanyakazi wake Tini Padasi aliyekuwa masimamizi wa mahesabu “Account Supervisor” katika idara ya fedha.

Katika kuwaaga wafanyakazi wenzake Padasi aliwausia vijana walioko kazini kwa sasa kuepuka vishawishi ikiwemo kushika imani za dini zao pamoja na kufuata taratibu na sheria za kazi kufika alipofikia.“vijana nawaomba mpende kazi na mfuate masharti ya kazi kwani ndio msingi wa

mafanikio katika kazi , muepuke vishawishi matafika nilipofikia ” alisema Padasi.

kwa upande mwingine Padasi aliuomba ongozi wa TPA kuwajali Wastaafu kwa kuwajulia hali mara kwa mara na wapate msaada kwa wakati pale unapohitajika.

Wakati huohuo kitengo cha utekelezaji kimefanya sherehe ya kuuga mwaka 2013 na karibisha mwaka 2014 sherehe iliyoambata na kuwaaaga Wastaafu 34 kutoka kitengo hiko iliyofanyika katika ukumbi wa lamada ilala.

Pia kitengo cha Nafaka kimefanya sherehe ya kuuaga mwaka 2013 mkoani Morogoro ambao pia wakiwa mkoani humo

walipata fursa ya kutembelea mbuga za wanyama Mikumi. Wengine ni Kitengo cha Marine na Idara ya Utawala waliofanya katika hoteli ya Livingstone Bagamoyo na baadae Idara ya Tiba walisherehekea katika klabu ya Bandari, sherehe ambayo iliambatana na kumuaga mstaafu Bi. Hariat Mkurumbi aliyekuwa “Assistant Medical Officer” katika hospitali ya Bandari.

Kila mwanzo wa mwaka idara mbalimbali katika bandari ya Dar es salaam na TPA kwa ujumla hufanya sherehe za kuuaga mwaka katika sehemu mbalimbali kwa nia ya kuuanza mwaka mpya na mikakati mipya katika kukabiliana na changamoto za kazi za kila siku.

Wafanyakazi wa Idara ya Mapato na Fedha wakicheza kwaito katika hafl a ya Idara hiyo hivi karibuni.

Hafl a

Page 16: TPA kufungua ofi si zake Lubumbashi S - Tanzania · 2015. 10. 28. · 1. TANZANIA PORTS AUTHORITY. | Bendera Tatu, S.L.P. 9184, Dar es Salaam Email:ccm@tanzaniaports.com TToleo Namba

1616

Michezo

Dar Port yakabidhi vikombe vya ushindi

Mlali asisitiza amani na ushirikiano kiwandaniNa Cartace Ngajiro

Washindi wa jumla mara tatu mfululizo katika michezo ya Inter port games

Bandari ya Dar salaam wamekabidhi vikombe vya ushindi kwa Meneja wa Bandari katika sherehe iliyofanyika katika klabu ya Bandari hivi karibuni.Vikombe hivyo vilitokana na ushindi katika michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, kamba wanaume na wanawake, Riadha, mchezo wa bao pamoja na kombe la jumla.

Akiongea katika tafrija ya kukabidhi vikombe hivyo, Mgeni rasmi aliyekuwa akimuwakilisha Meneja wa Bandari, Kaimu Meneja kitengo cha utekelezaji Bw.Nelson Mlali mbali aliwapongeza wanamichezo wote kuweza kuipeperusha vyema bendera na hatimaye kuipatia sifa Dar Port.

Mlali alisema kwamba, ushindi huo hautokani na juhudi za wanamichezo pekee bali ni ushirikiano mkubwa unaofanywa na uongozi pamoja na wafanyakazi wa Bandari katika kufanikisha michezo hiyo hivyo alisisitiza kudumisha amani, nidhamu na ushirikiano kiwandani.

Aidha Mlali aliwaambia wanamichezo hao wafanye kazi kwa bidii ili kuleta tija na ufanisi kiwandani pia waendelee kufanya mazoezi kuimarisha afya zao kwani ukiwa na afya njema hata utendaji kazi utaongezeka.

Katika hatua nyingine aliwaasa wanamichezo hao kutobweteka na ushindi huo bali waendelee kujifua zaidi“nawaomba tu msibweteke na ushindi huu mwakani tujitume zaidi na pale kwenye kasoro ambazo hatukuweza kushinda basi michezo ijayo tuweze kuibuka na vikombe vingi zaidi”. Alisisitiza Mlali.

Akisoma risala kwa niaba ya wanamichezo hao Bw.Hassan Lukuni licha ya kuushukuru uongozi wa Mamlaka kwa kutambua umuhimu wa michezo pia walipendekeza wanamichezo waongezwe hasa katika timu ya mpira wa kikapu pamoja na mchezo wa kuvuta kamba ili waweze kupata wachezaji wa ziada watakaokuwa wanabadilishana kipindi cha mapumziko.

Walipendekeza pia maandalizi yafanyike mapema ili waweze kujiandaa kwa wakati pamoja na kupewa vifaa vya kutosha kuweza kuboresha michezo hiyo.

Tafrija hiyo ya kukabidhi vikombe ilifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa klabu ya michezo Bandari ‘Bandari Sports Club’ uliopo Kurasini ambapo wanamichezo hao walikabidhiwa zawadi ya pesa taslimu.

Mgeni Rasmi, Meneja wa Utekelezaji Bandari ya Dar es Salaam Bwana Nelson Mlali akimpatia Kocha wa timu ya mpira wa miguu Bw. Mputa Zeno mkono wa pongezi na zawadi ya ushindi wakati wa sherehe hiyo.