bunge la tanzania majadiliano ya bunge mkutano wa...

305
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Ishirini na Sita – Tarehe 16 Mei, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae, Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Upload: others

Post on 20-Aug-2020

0 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE____________

MKUTANO WA SABA

Kikao cha Ishirini na Sita – Tarehe 16 Mei, 2017

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua

MWENYEKITI: Tukae, Katibu.

NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI:

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:

Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka waFedha 2017/2018.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka waFedha 2017/2018.

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB- MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NAUSALAMA):

Taarifa ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalamakuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshila Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamojana maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumiziya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM (K.n.y. MHE. JUMAHAMAD OMAR - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANIKUHUSU WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA):

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusuWizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa juu ya Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha2017/2018.

MWENYEKITI: Ahsante. Katibu.

NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza naOfisi ya Rais (TAMISEMI) na swali linaulizwa na MheshimiwaDkt. Pudenciana Wilfred Kikwembe.

Na. 209

Dhana ya Ugatuaji Madaraka kwa Wananchi

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE aliuliza:-

Serikali imekuwa na dhana ya ugatuaji madarakakwa wananchi ili kuharakisha maendeleo, hususan katikasekta za afya na elimu:-

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

Je, Serikali inasema nini kuhusu mfumo huo kutokuwana tija endelevu katika sekta hizo?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali laMheshimiwa Dkt. Pudenciana Wilfred Kikwembe, Mbunge waKavuu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Dhana ya Ugatuaji waMadaraka kwa Wananchi (Decentralisation by Devolution)inatokana na Ibara ya 145 na Ibara 146 ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Madhumuni yakupeleka madaraka kwa umma yakiwemo madaraka yakisiasa, kifedha na kiutawala ni kusogeza madaraka yakufanya maamuzi kwa wananchi ili kuboresha, kuimarishautoaji wa huduma kulingana na matakwa yao ya kuboreshamaisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeweza kupatamafanikio katika sekta ya afya na elimu kwa kuwashirikishawananchi katika kutekeleza Mipango ya Maendeleo ya Elimuya Msingi na Sekondari (MMEM na MMES) na Mpango waMaendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM). Kupitia utekelezajiwa hiyo fursa ya elimu ya msingi na sekondari zimewezakuongezeka kutokana na ujenzi wa miundombinu ya elimuna kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Vilevilehuduma za afya zimeimarishwa kwa kuratibiwa kwa karibuna Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuanzia ngazi ya zahanati,vituo vya afya pamoja na hospitali ya wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo wa ugatuaji wamadaraka kwa wananchi bado ni dhana muhimu kwa nchiyetu kwani ndio mfumo unaotoa fursa kwa wananchi kuwezakushiriki katika maamuzi na utekelezaji wa vipaumbele vyaokatika mchakato mzima wa maendeleo yao na Taifa kwaujumla.

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Dkt. Kikwembe.

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kunipatia nafasi niweze kuuliza swali lanyongeza. Kwanza kabisa, napenda nimshukuru MheshimiwaNaibu Waziri kwa majibu yake mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, suala hili ni lakikatiba kwa maana ya kwamba linahusisha Serikali yawananchi kwa maana ya Serikali za Vijiji. Kwa kuwa wananchiwamekuwa wakichangia takribani 20% ya maendeleo katikamaeneo yao ya vijiji. Je, Serikali sasa inafikiria nini kupelekapesa za maendeleo kwa wakati ili wananchi hawa wawezekujua sasa ile miradi ni mali yao? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli dhanahii inapeleka fursa kwa wananchi na ni kweli tumeshuhudiawananchi katika maeneo mbalimbali wakishiriki vyemakatika kutekeleza dhana hii kwa kujitolea katika miradimbalimbali ya maendeleo. Hata hivyo, naomba nilihakikishieBunge lako Tukufu kwamba Serikali kwa kipindi cha sasa nanina maana itakapofika mwezi wa Sita mtaona jinsi ganiimepeleka nguvu kubwa sana katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano katika sekta ya afyamwaka huu peke yake fedha tulizopeleka katika mifukombalimbali ikiwepo Basket Fund ni zaidi ya shilingi bilioni 79na sasa hivi tumeshapeleka fedha za quarter ya nne ambapotunaenda kukamilisha shilingi bilioni 106, hii ni sekta ya afyapeke yake. Tumefanya hivyo pia katika sekta ya elimu namaeneo mbalimbali na juzi juzi hapa tumenunua vifaa vyamaabara katika maabara zote zaidi ya 1,000 ambapo vyotevilikuwa vinagharimu shilingi bilioni 16.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kuna fedhanyingine za LDGD ambazo zimeenda moja kwa mojaambazo hazina ukakasi katika kuzitoa kwake. Serikali

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

imepeleka hela za kutosha na ni mara ya kwanza baada yamiaka minne iliyopita tulikuwa hatufanyi hivyo. Kwa hiyo,Serikali itaendelea kuweka nguvu kubwa ya kutosha, lengokubwa ikiwa ni kuwawezesha wananchi kutekeleza miradiyao.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Gekul na MheshimiwaChumi.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza.Mpango wa Afya ya Msingi (MMAM) muda wake ilikuwa uishemwaka huu 2017 lakini fedha hizo haziji kwa muda mrefu,takribani kama miaka mitatu nyuma fedha haziji. Ni kwa ninimpango huu wa MMAM ambao ulikuwa unasaidia kujengazahanati zetu umekwama na anawaambiaje Watanzaniakwa sababu maboma/zahanati nyingi badohazikajamilishwa?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema hapasio suala la maboma ya afya peke yake hata maboma yanyumba za Walimu halikadhalika madarasa. Kipindi fulanihapa takribani miaka mitatu, minne fedha hizi zilikuwahaziendi. Ndiyo maana nimesema kupitia Mfuko ule wa LDGDambapo kwa sasa mwaka huu kwa mara ya kwanza,namshukuru Mheshimiwa Waziri wangu alilisimamia kwakaribu sana, ndiyo maana hivi sasa Wabunge kamatumepitia katika Kamati zetu za Fedha katika Halmashaurizetu tunaona kuna fedha nyingi zimekuja ambazo zimesaidiakwa kiwango kimoja au kingine kuweza kuhakikisha mabomamengi sana yameweza kujengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeshuhudia hili kwaninilipopita maeneo mbalimbali nilikuwa nikipata taarifambalimbali kutoka kwa Wakurugenzi jinsi gani fedha hizi sasa

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

wameweza kuzielekeza katika kuhakikisha zile nguvu zawananchi ambazo wamezitoa hazipotei kwa kukamilishaviporo hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwashukuru sanaWaheshimiwa Wabunge, naomba tushirikiane kwa pamoja.Lengo kubwa ni kutekeleza mpango wa D-by-D kamaalivyosema Mheshimiwa Dkt. Kikwembe, tufanye hili kwa ajiliya mustakabali mzuri kwa kuunganisha nguvu za wananchikatika kuhakikisha Taifa hili linaenda mbele.

MWENYEKITI: Ahsante. Waziri wa Afya.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja namajibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nataka tukumfahamisha Mheshimiwa Gekul kwamba tayaritumeshaanza kuufanyia mapitio Mpango wa Afya ya Msingi(MMAM). Kwa hiyo, tunategemea kabla ya mwisho wamwaka tutakuwa tumetoa mpango wa pil i ambaoutatueleza kama, je, ni lazima tuwe na zahanati kila kijijiwakati sasa hivi barabara zinapitika? Je, ni lazima tuwe nakituo cha afya kila kata? Kwa hiyo, hayo maeneo yotetutayaangalia kwa upana wake. Lengo letu ni kuhakikishatunasogeza huduma bora kwa wananchi. Ahsante sana.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Chumi.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kuniona. Pamoja na majibu mazuri yaMheshimiwa Naibu Waziri na jitihada za Serikali kupelekafedha za maendeleo, ugatuaji lazima uende sambamba naupelekaji wa resources hususan fedha za OC. Fedha za OCzimekuwa haziendi kwa kiwango kinachokusudiwa matokeoyake imekuwa inaathiri mipango inayopangwa naHalmashauri kwa kutekelezwa kutokana na makusanyo yandani. Matokeo yake fedha za makusanyo ya ndani sasazinatumika kuendeshea ofisi badala ya kuelekezwa kwenye

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

shughuli za maendeleo kama inavyoelekeza ile 50%, ikiwepo5% ya vijana na wanawake. Je, Serikali imejipangajekuhakikisha kwamba inapeleka fedha za OC ipasavyo ilikusudi makusanyo ya ndani yasiathiri utekelezaji wa shughuliza maendeleo, kama ambavyo zimepangwa na Halmashaurizetu? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli nanakumbuka kwamba tulipokuwa katika kikao chetu chaALAT kule Musoma, concern kubwa ilikuwa siyo fedha za OCpeke yake hata pesa za maendeleo. Waheshimiwa Wenyevitiwa Halmashauri na Wakurugenzi wali-raise jambo hili katikaofisi yetu na ndiyo maana katika kipindi cha katikati baadaya harakati hizi kufanyika mmeona tumepeleka fedha nyingisana za maendeleo na pesa za OC.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama ambavyoMheshimiwa Waziri wangu siku zote amekuwa akisemadefinition ya OC maana yake ni Own Source plus zile fedhanyingine zinazotoka Serikali Kuu. Kwa hiyo, sisi Serikalitutajitahidi kwa kadiri iwezekanavyo OC iweze kwenda, lakininiwaombe sana Waheshimiwa Wabunge katika maeneoyetu vilevile tuhakikishe makusanyo ya ndani hayayanaimarika kwa kiwango kikubwa kwa sababutumeshuhudia hivi sasa kuna Halmashauri zingine zimefanyavizuri lakini nyingine zinasuasua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hili ni jambo letusisi sote. Upande wa Serikali tutajitahidi kufanya kilaliwezekanalo kuziwezesha Halmashauri zetu ziweze kufanyakazi vizuri kwa sababu bila ya hivyo maana yake utekelezajiwa Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi utakuwa unamatatizo. Kwa hiyo, naomba niwahakikishie kwamba Serikaliitafanya kila liwezekanalo, tutakusanya mapato lakinitutayapeleka katika Halmashauri zetu ili miradi iwezekutekelezeka vizuri.

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana swali la Wizara hiyo hiyo la Mheshimiwa Nditiye.

Na. 210

Hitaji la Mganga wa Meno – Hospitali ya Wilaya ya Kibondo

MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE aliuliza:-

Kwa muda wa zaidi ya miaka miwili, Hospitali yaWilaya ya Kibondo haina mganga wa meno licha ya hospitalihiyo kuhudumia wagonjwa wengi kwa sasa ikiwemowakimbizi kutoka nchini jirani ya Burundi:-

Je, ni lini Serikali itapeleka mtaalam wa meno katikahospitali hiyo?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali laMheshimiwa Injinia Atashasta Justus Nditiye, Mbunge waMuhambwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekwishapelekamtaalam wa meno (Daktari Msaidizi wa Meno) tangu tarehe12/4/2016. Kwa sasa yupo katika Hospitali ya Wilaya yaKibondo na anaendelea kutoa huduma kwa wagonjwa.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Nditiye.

MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE: MheshimiwaMwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, ninamaswali mawili madogo ya nyongeza. Kwa kuwa Hospitaliya Wilaya ya Kibondo ndiyo hospitali vilevile inayotumikakama Hospitali ya Rufaa kwa Wilaya ya Kakonko, lakiniinatumika kama Hospitali ya Rufaa kwa wakazi kutoka nchiniBurundi, kwa maana ya wakimbizi wapatao laki mbili. Serikali

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

ina mpango gani wa kuongeza majengo kwenye hospitalihiyo ambayo hayajawahi kuongezwa kutoka mwaka 1971?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwa sababu hiyohiyo Serikali ina mpango gani wa kuongeza mgawo wa dawaili kuweza kukidhi mahitaji ya wananchi wa Wilaya yaKibondo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli hospitaliya Mheshimiwa Mbunge ya kama Kibondo, ni kweli na miminilifika tulienda kukagua hospitali ile, kuna changamoto yamiundombinu pale na hata wenzetu wa Kakonko kwamwalimu wangu pale, mara nyingi sana wanatumia kamandio referral hospital yao katika eneo lile, changamoto hizotumeziona. Siku ile nilivyokuwa pale site niliwaambiawaangalie upungufu uliokuwepo (needs assessment) maanahata vifaa tiba na X-Ray lilikuwa ni changamoto na nilitoamaelekezo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, imani yangu nikwamba wenzetu pale Halmashauri watafanya hiyo needsassessment ambapo mchakato utaanza katika vikao vyaHalmashauri, tutaangalia nini kwa pamoja kitafanyika kwaajili ya kuboresha hospitali ile kwa sababu idadi ya wagonjwaniliyoikuta pale ni kubwa sana na ni kweli anachosemaMheshimiwa Mbunge. Kwa hiyo, Serikali inasubiri jinsi ganimichakato itawekwa katika kipaumbele cha Halmashauriyenyewe na sisi tutaweka nguvu kwa kadri iwezekanavyo ilihospitali ile iweze kutoa huduma vizuri.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Genzabuke.

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swalila nyongeza, pamoja na majibu mazuri ya MheshimiwaNaibu Waziri.

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Mkoa wa Kigomakwa muda mrefu umekuwa haupati watumishi kwa sababuupo pembezoni lakini pia wakimbizi wameingia kwa wingikatika Mkoa wa Kigoma pamoja na kwamba wana hospitalizao kwenye makambi lakini kutokana na binadamuwasivyoweza kuzuiliwa wanaingia kwa wingi katika miji yetuhali inayosababisha wagonjwa kuwa wengi kwenye hospitalizetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Ummyalipofanya ziara Mkoa wa Kigoma…

MWENYEKITI: Mheshimiwa uliza swali.

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: MheshimiwaMwenyekiti, Mheshimiwa Ummy alipofanya ziara Mkoa waKigoma alikumbana na tatizo la ukosefu wa waganga katikahospitali zetu. Ni lini sasa Mkoa wa Kigoma utapewakipaumbele cha kupatiwa waganga wa kutosha? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kulikuwana suala la concern ya dawa katika Hospitali ya Kibondoambalo mwanzo nilili-skip. Hata nilivyofika pale site Kibondonilitoa maelekezo kuhusu matumizi mazuri ya Basket Fund.Maeneo yote nilikopita nimekuta kwamba japokuwatumepeleka fedha za kutosha kwenye Basket Fund, lakiniWaganga wetu wa Wilaya wameshindwa kuhakikisha zilefedha zinatumika kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wetu.Ndiyo maana nimetoa maelekezo kwamba itakapofikamwezi wa Sita, Halmashauri yoyote ambayo Serikaliimepeleka fedha lakini zile fedha zimeshindwa kununua dawana vifaa tiba kuwasaidia wananchi, tutasema kwamba, ma-DMO wao hawatoshi katika maeneo yetu hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini suala la watumishi,japokuwa tatizo la watumishi ni tatizo kubwa sana, lakiniukiangalia katika mgawanyo wa Madaktari, Kigoma

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

tumepeleka madaktari 10 lakini mikoa mingine imepatamadaktari watano. Tunajua japokuwa Madaktari kumiwameenda katika Mkoa mzima wa Kigoma, bado hawatoshi,lakini tutakapokuja katika ajira mpya Mkoa wa Kigomatutaupa kipaumbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba muelewe nduguzangu, Kibondo pale kwa ndugu yangu Mheshimiwa Nditiyetumepeleka Madaktari watatu, Kasulu tumepeleka Madaktariwawili, halikadhalika Uvinza tumepeleka Madaktari na RASKigoma tumepeleka takribani Madaktari wanne. Lengo letuni kuhakikisha Mkoa wa Kigoma na mikoa mingine yapembeni iweze kupata…

MWENYEKITI: Mheshimiwa jibu kwa kifupi tu sababuswali lake la nyongeza yeye kadandia, mjibu kwa kifupi tu.(Kicheko)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tutawapakipaumbele watu wa Kigoma kupata Madaktari wa kutosha.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Almas na MheshimiwaParesso.

MHE. ALMASI A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nikushukuru sana kuniruhusu kuuliza swali. Kituo chaAfya cha Upuge ndiyo peke yake Hospitali ya Wilaya Jimbonikwangu, hakuna hospitali kabisa isipokuwa Kituo kile chaUpuge na hakina wataalam wa dawa za usingizi, wanaitwaanesthesia kitaaluma, kwa hiyo, hatuwezi kufanya operesheni.Je, Serikali inafikiria nini kupeleka mtaalam wa dawa zausingizi ili operesheni zifanyike? Ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwakifupi, watu ni wengi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kituo chaAfya cha mtani wangu pale, katika idadi ya wataalam

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

ambao tutawaajiri hapa katikati kutokana na nafasi nyingizilizotolewa na Mheshimiwa Rais tutaangalia mahitaji halisiya kituo hiki then tutawapa kipaumbele ili mradi wampatemtaalam huyo wa usingizi.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Paresso.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.Kumekuwa na tishio kubwa la ugonjwa wa sukari hapa nchiniambao umekuwa ukiwakumba watu wa rika mbalimbalina hatuna wataalam wa kutosha katika hospitali zetu.Vilevile hata dawa wanazopewa ikifikia hatua mgongwawa sukari anatakiwa apate insulin dawa hizo zimekuwazikiuzwa ghali, watu hawawezi ku-afford. Je, Serikali inatoakauli gani kuhusiana na tatizo hili?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Afya najuaukijibu utapata tabu bora ukae waseme hawa halafu ndiyoujibu, mimi style yangu ni tofauti kidogo. MheshimiwaMwijage, maana utakuwa unasimama kila saa hapa.

MHE. SAVELINA S. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwa kuwa matatizo ya Kibondo ya Madaktariwa meno ni sawasawa na matatizo ya Wilaya ya BukobaVijijini ya Izimbya - Katekana hawana Daktari wa meno hatammoja wakipata tatizo la ugonjwa mpaka waende BukobaMjini na ni mbali sana kutoka pale kwenda Bukoba Mjini. Nilini Serikali itaona umuhimu wa kuwaletea Madaktari wameno wa kuwasaidia hao watu wa Bukoba Vijijini?

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa Mheshimiwa Waziri waAfya, yajibu yote.

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujibuswali la nyongeza la Mheshimiwa Cecilia Paresso kuhusuupatikanaji wa dawa za kisukari na ongezeko la wagonjwawa kisukari nchini. Ni kweli sasa hivi tunashuhudia ongezekola wagonjwa wa kisukari lakini kwa sababu kwanza ya

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

mfumo wa maisha ambao watu wanaishi, watu hawafanyimazoezi, wanakula vyakula bila kuzingatia lishe lakini bilaku-check afya zao mara kwa mara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kubwa badala yakujikita kwenye kutibu tumejikita kwenye kuzuia Watanzaniawengi wasipate maradhi ya ugonjwa wa kisukari. Paleambapo Mtanzania ana ugonjwa wa kisukari kwa mujibu waSera ya Afya dawa ya mgonjwa wa kisukari inatakiwakupatikana kwa bei nafuu. Kwa hiyo, tunawaelekezaWaganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanapoandaamaoteo ya dawa basi wahakikishe pia wana-order dawaza kutosha kwa ajili ya wagonjwa wa kisukari. Kamahawawezi ku-order za kutosha sisi hatuwezi kuwapelekea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili la uhaba waMadaktari wa Meno, kama alivyosema Mheshimiwa NaibuWaziri na hata wakati wa bajeti ya Mheshimiwa Waziri waUtumishi alitoa maelezo kwamba Mheshimiwa Rais ameridhiakuajiri watumishi wa Serikali takriban 52,000 na kati ya haotunategemea kupata watumishi wa sekta ya afya. Kwa hiyo,Mheshimiwa Savelina Mwijage tutakapopata kibalitutawapanga pia kwa ajili ya hospitali za Mkoa za Kagera.Ahsante sana.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na Wizara yaUjenzi, Mheshimiwa Daniel Edward Mtuka.

Na. 211

Ujenzi wa Kituo cha Ukaguzi wa MizigoMuhulala Manyoni

MHE. DANIEL E. MTUKA aliuliza:-

Eneo la Muhalala katika Wilaya ya Manyoni ni mojaya maeneo matatu yaliyoteuliwa na Serikali kujenga vituovya ukaguzi wa mizigo katika barabara ya kati; maeneomengine ni Vigwaza Pwani na maeneo mawiliyameshajengwa kimebaki kituo cha Muhalala tu:-

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

(a) Je, ni lini wananchi ambao maeneo yaoyametwaliwa tangu mwaka 2012 watalipwa fidia?

(b) Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo chaUkaguzi wa Mizigo Muhalala baada ya kituo cha Vigwazakukamilika?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Daniel Mtuka, Mbunge wa Manyoni Mashariki,lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja, kama ifuatavyo:-

Mheheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali imeamuakujenga vituo vya pamoja vya ukaguzi wa mizigoinayokwenda nje ya nchi katika barabara ya Ukanda wa Katina Ukanda wa Dar es Salaam. Katika Ukanda wa Kati vituovitajengwa Muhalala, Mkoani Singida na Nyakanazi MkoaniKagera chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya. Aidha, katikaUkanda wa Dar-es Salaam, vituo vitajengwa Vigwaza,Mkoani Pwani, Ruaha-Mbuyuni, Mkoani Morogoro,Makambako, Mkoani Njombe na Iboya - Mpemba MkoaniMbeya chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha wa2016/2017, Serikali ilitenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 5.86kwa ajili ya malipo ya fidia kwa watu watakaoathirika naujenzi wa vituo hivyo. Tathmini ya maeneo ya watuwalioathirika na ujenzi huo katika Ukanda wa Kati yaani(Muhalala - Manyoni na Nyakanazi - Kagera) imefanyika namalipo kwa waadhirika wa ujenzi wa vituo hivyoyamefanyika na kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, mkataba wa ujenziwa vituo vilivyopo Ukanda wa Kati ulisainiwa tarehe 16Disemba, 2016 kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania na mkandarasi M/s IMPRESA DI CONSTRUZIONI INGE. MANTOVANI wa Italia. Mpaka sasa mkandarasi yupo

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

katika eneo la kazi na yupo katika hatua za awali za ujenziwa vituo hivyo. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Septemba,2018.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mtuka.

MHE. DANIEL E. MTUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri. Niipongezepia Serikali ni kweli majuzi tumepokea ugeni na shughuli hiyoimeanza mara moja. Hiyo ndiyo Serikali ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo maswali mawili yanyongeza. Swali la kwanza, kuna nyumba zinatakiwakubomolewa maeneo ya Kintinku, Chikuyu, Mawenibarabara kuu zimewekewa alama ya kijani tangu 2013 nakijani maana yake ni kwamba kuna malipo ya fidia, lakinihawajalipwa fidia, Serikali inasema nini? Ni lini wananchihawa watalipwa?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

MHE. DANIEL E. MTUKA: Samahani Mwenyekiti, swalila pili.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri subiri tumpefursa.

MHE. DANIEL E. MTUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu2013 tuliomba barabara inayoanzia Chikuyu – Chibumagwa- Mpandagani - Ikasi ambayo ina urefu wa kilomita 84ipandishwe daraja lakini tangu kipindi hicho naona ni kimyaSerikali haijaleta majibu. Hata hivyo, tarehe 17/3/2015wataalam kutoka Wizara husika walikuja kukagua barabarahii. Tulitegemea majibu yatoke lakini mpaka sasa hivi ni kimya.Ni lini sasa Serikali itapandisha hadhi barabara hii?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwakifupi.

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo ya Kintinku- Chikuyu na Maweni ambayo yapo katika barabara kuuyamewekewa alama ya ‘X’ ya kijani kama ambavyotumeweka alama za ‘X’ za kijani na nyekundu katikabarabara nyingi sana humu Tanzania tokea Sheria ile ya 2007ilipopitishwa na Kanuni ya 2013 ilipopitishwa. Maana ya zile‘X’ ni kwamba tunakujulisha eneo hilo liko ndani ya hifadhiya barabara kwa mujibu wa Sheria mpya ya mwaka 2007lakini eneo lako liko kati ya mita 22.5 ambayo ni hifadhi yabarabara kwa sheria ya zamani na mita 30 kwa sheria yasasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu upanuzi huuumefanyika wakati wewe tayari ulishajenga unastahilikulipwa fidia lakini unachotakiwa kufanya ni kuhakikishakwamba huongezi maendeleo yoyote katika eneo hilo, hiyondiyo maana yake. Sasa fidia inakuja wakati eneo hilolinapohitajika. Eneo hilo linapohitajika kupanua barabaratunawalipa fidia kabla hatujaanza kazi ya upanuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kama ambavyoyeye alisimama na mimi nikasimama, barabara inayoanziaChikuyu - Chibumagwa na kuendelea ombi la kwambaipandishwe hadhi nimwombe tu avute subira majibuyatolewa. Tuna maombi mengi tu yamekuja na marayatakapokamilika tutatoa taarifa barabara zipizimepandishwa hadhi na zipi hazikupandishwa hadhikutokana na vigezo ambavyo tumejiwekea wenyewe kwamujibu wa sheria.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mpakate.

MHE. MPAKATE D. IDDI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Naomba niulize swali la nyongeza, kama ifuatavyo.Tatizo la Manyoni linafanana kabisa na mazingira ya tatizola barabara ya Mtwaro - Pachani - Lusewa - Mchoteka - Nalasi- Mbesa - Tunduru Mjini ambayo iliwekewa alama za ‘X’ zaidiya miaka saba iliyopita. Je, ni lini ujenzi wa barabara hii kwakiwango cha lami utaanza?

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naona MheshimiwaMbunge ameanza kutaja maeneo ambayo yako katikaJimbo langu katika kuongeza umuhimu wa swali lake.Naomba tu niseme masuala ya fidia ni ya Kitaifa na wakatiambapo tutaanza kujenga na sasa hivi siwezi kusematunaanza lini kwa sababu fedha zilizotengwa kwa sasa ni zaupembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa sababu kazi hiyobado haijakamilika. Naomba kwanza tuikamilishe kaziupembuzi yakinifu na usanifu wa kina kabla hatujaanzakutafuta fedha za kujenga hiyo barabara.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na swali laMheshimiwa Mussa Bakari Mbarouk.

Na. 212

Ukarabati wa Bandari ya Tanga

MHE. MUSSA B. MBAROUK aliuliza:-

Bandari ya Tanga siku hadi siku inafanya kazi chini yakiwango:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza kina,kuipanua na kuifanya bandari ya kisasa il i kuvutiawafanyabiashara kushusha mizigo yao na wasikimbilieMombasa Kenya?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali laMheshimiwa Mussa Bakari Mbarouk, Mbunge wa Tanga, kamaifuatavyo:-

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuvutia wafanyabiasharakushusha mizigo yao na kutokukimbilia bandari ya nchi jirani,Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) ina mpango wa muda mfupi na wa kati wa kuboreshabandari ya Tanga kwa kutekeleza mradi wa kuimarisha gatinamba mbili (2).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa kuboresha Bandariya Tanga ulianza Februari, 2016 na unatarajiwa kukamilikaJuni, 2017. Mradi huu unatekelezwa na Kampuni yaUkandarasi ya COMARCO kutoka Kenya. Maboresho yabandari yanayofanyika katika mradi huu ni pamoja nakuongeza kina cha gati kwa kuchimba (dredging) kiasi chamita 1 na kufanya kina cha gati kufikia mita 4.5; kuimarishagati na kuweka mfumo wa kuzuia kutu katika nguzo (cathodicprotection).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu ukikamilikautasaidia kuongeza uwezo wa bandari kuhudumia meli zenyewastani wa ukubwa wa tani 1,200 kuingia bandarini. Aidha,Serikali kupitia TPA ina mpango wa muda mrefu wa kujengabandari katika eneo la Mwambani ambayo ina kina kirefuna uwezo wa kuhudumia meli kubwa. TPA tayari inamiliki ardhiyenye ukubwa wa hekta 92 katika eneo la Mwambani.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mbarouk.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na bandari iliyokuwepo Serikali ilipata uwezekezajiwa ujenzi wa bandari mpya ya Mwambani na kama sikoseiilikuwa ni Serikali ya Uganda na Serikali ya Kuwait. Swali lakwanza, kwa kuwa feasibility study pia ilikwishafanyika, je,ujenzi huu wa bandari mpya wa Mwambani nao umefikiahatua gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, zipo systems zaFIFO na LIFO method, First In First Out na Last In First Out, kwanini naambiwa kwamba itaanza kujengwa bandari yaBagamoyo katika siku za karibuni isianze kujengwa ile bandariya Tanga? Nataka kujua hilo.

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu, anatakakujua kwa nini tu, sasa usimzungushezungushe.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, bandari yaMwambani kama ilivyo bandari ya Bagamoyo tulikuwatunatarajia ijengwe kwa njia ya PPP. Unapokwenda kwenyemasuala ya PPP inategemea na yule aliyeonesha nia yakujenga. Wapo watu wameonesha nia Bagamoyo na Tangapia lakini tatizo lililotokea kwa Mwambani ni kwambaupembuzi yakinifu na usanifu wa kina uliofanyika ulioneshakwamba bandari ile haina faida. Sababu yake hawakufikiriamizigo ambayo italetwa na reli inatokea Musoma hadi Tanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sasa tumeanzakazi upya ya kuipitia hiyo taarifa ya upembuzi yakinifu nausanifu wa kina il i waunganishe na uwekezaji mpyauliojitokeza pale Tanga ili hatimaye bandari ile ya Mwambaniionekane ina faida kuijenga. Kwa hiyo, ni kweli kuna huoutaratibu wa FIFO na kadhalika lakini hatimaye kwa sababuunatumia PPP ni lazima ufuate wale wateja wakowanaotaka kuwekeza pale unaendana nao vipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa swali la pili,nalo nadhani nimelijibu wakati najibu hili kwa kirefu kwasababu hoja ni ileile. Nakushuruku sana.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Saumu naMheshimiwa Kakoso.

MH. SAUMU H. SAKALA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuuliza swali lanyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Pangani kamazilivyo wilaya nyingine zilizoko pembezoni mwa bahari inabandari bubu nyingi. Bandari hizi zinatumika kuingiza mizigoambayo ni halali na ambayo pia siyo halali kama vilemadawa ya kulevya, wahamiaji haramu hata na bangi kituambacho kinasababisha bandari hizi zinakuwa ni chanzo

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

kikubwa cha rushwa. Je, Serikali haioni umuhimu wakuzitambua bandari hizi i l i zi le zenye vigezo ziwezekurasimishwa na kutambulika rasmi ikiwa ni pamoja nakuzikarabati na zile ambazo hazifai zifungwe kwa maslahiya Taifa na watu Pangani? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, anayoyasema nisahihi na nadhani anafahamu kwamba ndichotunachotekeleza ndani ya Serikali kwa sababu tuna timu yaWakuu wa Mikoa yote iliyoko kwenye mwambao na upandewa Zanzibar wanakutana kila wakati kuhakikisha wanapitiazile bandari bubu kuona zipi zinaweza zikaendelezwa nakurasimishwa na zipi ambazo zinatakiwa kufungwainasimamiwa kufungwa. Nadhani ni kitu ambachoanafahamu tunakitekeleza na nimushukuru sana kwa sababukwa kuuuliza hivyo maana yake anaunga mkono hatuatunayoichukua.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kakoso.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nishukuru kunipa nafasi ya kuuliza swali ndogo la nyongeza.Serikali iliazimia kufanya marekebisho ya kuziboresha bandariza Maziwa Makuu kwa maana ya Ziwa Victoria, Nyasa naLake Tanganyika. Serikali iliazimia kujenga bandari ya Kalemaili iweze kuunganisha na nchi jirani ya DRC. Ni lini bandari yaKalema itakamilika kama Serikali ilivyokuwa imetoa hoja yakujenga bandari hiyo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzanimpongeze sana Mheshimiwa Kakos, Makamu Mwenyekitiwa Kamati ya Miundombinu, kwa namna anavyofuatiliamaendeleo ya bandari za Mwambao wa Ziwa Tanganyika.Amekuwa mstari wa mbele sana katika kulihangaikia hilo

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

na sisi tunamuunga mkono katika hilo, tutahakikisha dhamirayake ya kuwatumikia watu wa Mwambao wa ZiwaTanganyika inatimia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu kwambakazi inayofanyika sasa ni kufanya upembuzi yakinifu na usanifuwa kina wa reli na bandari, reli kutoka Kaliua mpaka Kalemapamoja na bandari yake ili hatimaye tujenge reli na bandarituweze kuhudumia mizigo mingi kutoka Kalemie upandewenzetu wa DRC Kongo. Nimwombe akubali kwamba yaleambayo tunakubaliana katika Kamati ndiyo Serikaliitakayoyatekeleza. Ahsanteni sana.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na swali naMheshimiwa Dkt. Ndugulile, kwa niaba yake MheshimiwaDkt. Chegeni.

Na. 213

Mtambo wa Kudhibiti Takwimu zaMawasiliano ya Simu

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI (K.n.y. MHE. DKT.FAUSTINE E. NDUGULILE) aliuza:-

Katika Kamati ya Bunge la Kumi Serikali iliahidi kufungamtambo kwa lengo la kudhibiti takwimu za simu za nje nandani ili kudhibiti mapato ya Serikali:-

(a) Je, utekelezaji wa suala hilo umefikia wapi?

(b) Je, ni kiasi gani Serikali imekusanya tanguutaratibu huo uanze na kabla yake mapato yalikuwaje?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri Ujenzi,Uchukuzi na Mawasil iano, napenda kujibu swali la

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mamlaka yaMawasiliano Tanzania iliweza kusimika mtambo wa kuhakikina kusimamia huduma za mawasiliano yaani TTMS hapanchini mwishoni mwa mwaka 2013. Mtambo huu umeisaidiaMamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuongeza ufanisikatika kusimamia sekta ya mawasiliano pamoja na kwendasambamba na kasi ya mabadiliko yanayotokea katika sektaya mawasiliano duniani kote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa mtambo waTTMS umeiwezesha TCRA kuwa na uwezo wa kusimamiamawasiliano ya simu za kimataifa na zile za mwingiliano;kudhibiti mawasiliano ya simu za ulaghai za kimataifa;kusimamia ubora wa mitandao katika kutoa huduma borakwa wananchi; kudhibiti namba tambulishi za vifaa vyamawasiliano nchini pamoja na usimamiaji wa miamala yafedha inayopita katika mitandao ya simu hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mafanikio hayo,jitihada za kuboresha zaidi mfumo huu ili kuweza kubaini nakujiridhisha juu ya mapato yote yaani revenue assuranceyatokanayo na huduma za mawasiliano kwa maana ya simuza sauti, data na SMS yanakidhi mahitaji ya Mamlaka yaMapato Tanzania TRA, Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na TCRAyanaendelea. Kwa vile vifungu vya mkataba wa TTMSvinamtaka mkandarasi kuweka mfumo wa kubaini nakujiridhisha juu ya mapato yote (Revenue Assurance System),Serikali kupitia TCRA imemwagiza mkandarasi aweke mfumohuo bila gharama za ziada kwa Serikali. Mkandarasi hatimayeamekubali kuweka mfumo wa Telecom Revenue Assuranceambapo unategemewa kukamilika mwishoni mwa mweziAgosti, 2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuanzia Oktoba, 2013 hadiFebruari, 2017 kiasi cha sh.63,015,450,230.40 zilipatikana nakatika hizo sh.56,987,368,631.08 zimewasilishwa Hazina nash.6,028,081,599.41 zimewasilishwa Tume ya Sayansi na

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

Teknolojia (COSTECH) kwa aji l i ya kugharamia tafitimbalimbali zenye manufaa kwa nchi yetu. Kabla ya mfumohuu, mapato haya hayakuwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendeleakuwajengea uwezo wataalam wa TCRA ili waweze kuendanana kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasilianohususan katika eneo hili la kuchakata taarifa mbalimbali zahuduma za mawasiliano zinazopatikana kutoka kwa watoahuduma ili kuweza kubaini na kujiridhisha juu ya mapato yote.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Chegeni.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: MheshimiwaMwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa NaibuWaziri wa Ujenzi, nina swali moja dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa baadhi yamakampuni haya kwa muda mrefu sana yamekuwayakifanya udanganyifu na hasa katika miamala ya simupamoja na muda wa maongezi kwa wateja na kwa kuwaSerikali tayari imeshaanza kudhibiti suala hili. Je, Serikali haionikwamba ni busara na ni vyema kuendelea kudhibitimakampuni yote haya ya simu yaweze kulipa kipato sahihina kutokuwanyonya wananchi katika suala la miamala yasimu pamoja na muda wa maongezi? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana nayena ndivyo tunavyotaka kufanya na tunavyoEndelea kufanyakwa kutumia huu mtambo wa TTMS na makampuni yotehatutaacha hata moja tutayaingiza katika mfumo huu nakuhakikisha mapato yao yote yanayopatikanatunayafahamu na tunapata haki yetu.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Martha Mlata,Mheshimiwa Haonga na Mheshimiwa Selasini.

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Napenda kujua kama mfumo anaosemaMheshimiwa Naibu Waziri unasaidia pia kukusanya data zamalipo ya nyimbo za wasanii ambazo zinatumika kama miitokwa sababu ni mara nyingi wamekuwa wakidhulumiwa nakutokujua ni kiasi gani wameuza? Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, hatujaanzakulifuatilia eneo hilo, lakini tukishakamilisha mfumo huu waTotal Revenue Assurance, nina uhakika tutaingia huko.Kikubwa hapa ni mikataba kati ya wasanii na hawa watoahuduma. Ni kazi ya sisi kupitia huu mtambo kuhakikishatunasimamia mikataba yao na hatimaye tunawanufaishawasanii. Hilo nadhani litaweza kufanyika, ngoja tusubirimtambo huu ukamilike katika mfumo wake wa Total RevenueAssurance.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Haonga.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kumekuwa na wizi unaofanywa na baadhi ya makampuniya simu, yanakata fedha za wateja yakidai kwambatumekuunganisha na huduma fulani ambayo mtejahakuomba. Je, Serikali imejipanga vipi kudhibiti hali hii yawizi unaofanywa na makampuni haya? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo ni namnatunavyotumia simu hizi. Mara nyingi sana huwa tunaulizwamaswali fulani na tunapojibu tunahalalisha makato bilawenyewe kujijua au unapobonyeza baadhi ya buttonunajikuta unakubali ukatwe bila mwenyewe kujua. Kwa hiyo,tumewataka watu wa TCRA wahakikishe wanatoa elimu ya

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

kutosha ili wananchi wasifike mahali fedha zao zinakwendabila ridhaa yao wakati wao wana utaalam wa kuwajulishawananchi na wakatuelewesha ni namna gani tuzitumie hizigadgets hasa hizi za android za siku hizi…

MWENYEKITI: Ahsante. Ameshakuelewa, MheshimiwaSelasini.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Nauliza swali hili nadhani ni mara ya sabatangu nimekuwa hapa Bungeni. Makampuni ya simu ya nchijirani kwa mfano MTN ya Zambia na Safaricom ya Kenya yananguvu kiasi kwamba ukiwa Tunduma huwezi kupatamitandao kutoka kwenye makampuni ya hapa kwetu naukiwa kule Rombo karibu nusu ya eneo la Rombo Safaricomndiyo inayosikika na mbaya zaidi hata Redio yetu ya Taifahaisikiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa inaonekana kamawananchi wa mipakani tumetengwa fulani hivi na hudumahizi za simu pamoja na Redio ya Taifa. Naomba hii iwe maraya mwisho, ni lini Serikali itarekebisha tatizo hili ili kutoingizawananchi wanaokaa mipakani kwenye roaming facility nahivyo kuibiwa muda wao wa maongezi bila wao wenyewekutaka? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani wakatitunapitisha bajeti ya Wizara ya Habari mtakumbuka kwambatuliongelea sana uimarishaji wa TBC. Tatizo ni kwambamitambo yetu hatujaifikisha katika maeneo ya mipakani kwakiwango cha kutosha. Tukishaifikisha mitambo yetu katikamaeneo ya mipakani frequency haziwezi kuingiliana, uki-tuneTBC utapata TBC, ingawa bado ukitaka ku-tune ya upandewa pili nayo utaisikia kwa sababu wenyewe watakuwawapo kwenye frequency tofauti.

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutahakikishatunaimarisha ile miundombinu ya TBC ili isikike vizuri maeneoyote ya mipakani. Vilevile wenzetu wanaotoa huduma zamawasiliano ya simu na internet nao wakiimarisha hudumazao tatizo hili litakwisha. Kwa hiyo, tupo katika mazingira hayoya kuimarisha na nadhani atakumbuka tulichokubaliana autulichopitisha kwenye bajeti ile ya Wizara ya Habari. Ahsantenisana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na Wizara yaElimu, Sayansi na Teknolojia na swali linaulizwa na MheshimiwaFrank Mwakajoka.

Na. 214

Uhitaji wa Chuo cha VETA Tunduma

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA aliuliza:-

Mji wa Tunduma una vijana wengi wanaohitimukidato cha nne lakini wanakosa nafasi za kuendelea namasomo ya juu:-

Je, Serikali inasema nini kuhusu kujenga Chuo chaUfundi VETA ili vijana wengi waweze kupata ujuzi na kujiajirina kuongeza kipato chao?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali laMheshimiwa Frank George Mwakajoka, Mbunge waTunduma, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali haitaweza kujengaChuo cha VETA katika Halmashauri ya Tunduma kwa sasakwa sababu ya ukosefu wa fedha. Wakati juhudi mbalimbalizinaendelea za kutafuta vyanzo vya ufadhili wa kujenga Vyuovya Ufundi Stadi kupitia VETA, wananchi wa Mji wa Tunduma

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

waendelee kutumia vyuo vilivyopo katika mikoa jiranihususan Mkoa wa Mbeya wenye Chuo cha VETA cha Mkoana Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) vya Nzovwekilichopo katika Manispaa ya Mbeya na Katumba katikaWilaya ya Rungwe. Aidha, wananchi wanashauriwakuendelea kutumia vyuo vingine vilivyosajiliwa na Mamlakaya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika mikoambalimbali nchini ili kupata mafunzo ya ufundi stadi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Frank.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Kutokana na majibu ya MheshimiwaWaziri, naomba niulize maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kauli mbiu ya Serikali sasa niviwanda, lakini viwanda havitakuwepo katika nchi hii kamahatutoweza kuzalisha mafundi mchundo wengi ili wawezekutekeleza majukumu mbalimbali ndani ya viwanda hivyo.Je, Serikali haioni kwamba inapoteza muda wa kutamkakwamba itakuwa ni Serikali ya viwanda wakati haitakikuzalisha mafundi mchundo wengi ili waweze kutekelezawajibu wao? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika hali halisiya majibu ya Mheshimiwa Waziri jana wakati anajibu hojambalimbali za Waheshimiwa Wabunge alisema kwambaSerikali imejipanga kujenga Vyuo vya VETA nchi nzima namaeneo mbalimbali katika Taifa hili. Leo katika majibu yakeanatuambia kwamba Serikali haina mpango wa kujengaChuo cha VETA katika Mji wa Tunduma. Je, jana alikuwaakiwadanganya Wabunge katika majibu yake ya msingialiyokuwa akiyatoa ndani ya Bunge hili? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri majibu kwakifupi, ajiandae Mheshimiwa Mbatia, Mheshimiwa Chuachua,Mheshimiwa Halima Bulembo na Mheshimiwa Esther Matiko.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi Serikali inatambua juu ya

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

umuhimu huo wa kuendelea kuzalisha mafundi sanifu namafundi mchundo pamoja na wahandisi, lakini njia zakuzalisha mafundi hao haziko tu kupitia VETA, zipo pia kupitiavyuo binafsi lakini pia kupitia mafunzo ya muda mfupiambayo wanafundishwa na kuweza hata kujitegemea katikaviwanda vidogo vidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango huo upo, kwamfano mwaka huu, kuna mafunzo ya vijana wapatao 23,000ambayo yanaendeshwa na VETA ambayo ipo chini ya Wizarayetu lakini pia kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira,Vijana na watu Wenye Ulemavu kuhakikisha kwamba vijanawengi wanapata fursa hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusiana na majibuyangu kwamba jana nimesema tutajenga vyuo nchi nzima.Kwanza naomba nipende kuliomba Bunge lako Tukufu,naona kuanzia jana hiyo kama ulivyosema na pengine sikuzote Waheshimiwa Wabunge pengine huwa hawanisikilizivizuri ninapotoa majibu yangu kiasi kwamba wameanzakuniwekea maneno ambayo sijazungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachosema ni hivi Serikaliina dhamira ya kujenga Vyuo vya VETA katika kila Wilayalakini vilevile kuhakikisha kwamba inaimarisha Vyuo vyaWananchi kila mahali vilipo ambapo vipo 55. Hata hivyo,kwa sasa kutokana na hali halisi ya kibajeti tumesematutaimarisha kwanza vyuo vilivyopo na vile ambavyovilishakuwa vimeanza mchakato wa kuanza kuvijenga. Kwahiyo, sio kwamba tutajenga tu kila mahali bila utaratibu aubila fedha, naomba nieleweke hivyo tafadhali. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Chuachua,wajiandae Mheshimiwa Mbatia, Mheshimiwa Halima Bulembona Mheshimiwa Esther Matiko.

MHE. RASHID M. CHUACHUA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwa kuwa hali i l iyoelezwa Tundumainafanana sana na hali iliyopo katika Wilaya ya Masasi. Serikaliina mpango gani sasa wa kuhakikisha kwamba kutakuwa

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

na Chuo cha VETA ambacho kitahudumia karibu asilimia 54ya watu wa Mkoa wa Mtwara pamoja na wale wanaotokeakatika Wilaya ya Nanyumbu? Majibu ya Naibu Wazirihayaoneshi ni lini sasa mpango huo utaanza. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachohitajika ni wananchi kupatamafunzo na mafunzo sio majengo peke yake. Kwa hiyo, kwaupande wa Masasi au Nanyumbu tunacho Chuo chaMaendeleo ya Wananchi Masasi ambacho tayari kimo katikampango wa kukiboresha kwa kukifanyia ukarabati wa zaidina kukiongezea uwezo ili kiweze kutoa mafunzo ambayoyanafanana pia na yale yanayotolewa VETA. Vilevile kunaChuo cha Ndanda, naomba pia wananchi waweze kutumiachuo hicho ili kuweza kupata mafunzo yanayostahili.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mbatia.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Swali la msingi linaulizia kupata ujuzi na kujiajiri naifikapo mwaka 2030 kwenye Maendeleo Endelevu ya Dunia,Lengo la Nne ni elimu bora sawa kwa wote. Je, Serikaliimejipangaje kuwa na uendelevu wa kutoa masomo kwenyesekondari zetu yaani kwenye mitaala ya sayansi, biasharana kilimo badala ya kulazimisha watoto kuchukua sayansi tuili iweze ikawa ni endelevu watoto wakaweza kujikita kwenyeuelewa wao na stadi ambazo wanazipenda zaidi?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwakifupi, wajiandae Mheshimiwa Bulembo na MheshimiwaEsther Matiko.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru pia kwa swali zuri.Kimsingi hata sasa hivi kwenye baadhi ya maeneo tunazoshule hata za msingi ambazo zinatoa pia mafunzo ya ufundi,lakini vilevile tunaona kwamba kuna haja ya kuwapandikiza

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

watoto wetu ujuzi kuanzia katika ngazi za elimu za msingi,sekondari na kuendelea ikiwemo masuala yanayohusiana nasayansi na mazingira au kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachokiona tuni kwamba, kuna ugumu wa kusema kwamba kila jambotunalolihitaji litawekwa kwenye mtaala kwa ajili ya huyomwanafunzi. Kupitia vipindi vyetu vya elimu ya kujitegemeana mafunzo nje ya vipindi vya kawaida bado hawawanafunzi wanaweza wakapata pia mafunzo kama hayo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Halima Bulembo.

MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Ilani ya Chama cha Mapinduzi moja ya ahadikubwa iliyotolewa ilikuwa ni kujenga VETA katika kila WilayaTanzania nzima. Kwa kuwa Mkoa wa Kagera unaongoza kwaidadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba nakidato cha nne lakini wanashindwa kujiendeleza kutokanana ukosefu wa vyuo hivyo. Je, ni lini sasa Serikali itahakikishavijana hawa wanajengewa vyuo hivyo angalau hata katikaWilaya tatu za Mkoa wao? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, ni lini?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa Mkoa wa Kagera nikweli kuna uhitaji wa fursa hizo, lakini tayari kuna Chuo chaVETA pale Makao Makuu ya Mkoa. Vilevile kuna Chuo chaWananchi Karagwe (KVTC) ambacho tunaendelea kukifanyiaukarabati na sasa hivi tayari tupo kwenye hatua za mwishoili kiweze kuchukua wanafunzi wengi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna Chuo chaMaendeleo ya Wananchi cha Gera ambacho nacho kilikuwakatika hali mbaya sasa hivi kimeshafanyiwa ukarabati natutaendelea kukiboresha ili kiweze kuchukua wanafunzi wengizaidi.

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa nisemekwamba, kwa Mkoa wa Kagera kuna fursa kubwa ambapotuna chuo tunategemea kukijenga kule Muhengele ambachokitakuwa kinatoa mafunzo ya ujuzi wa juu zaidi kidogokulingana na mahitaji ya soko kwa kushirikiana na nduguzetu wa China.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Matiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Tarimemiundombinu yake ni mibovu sana na haina hadhi ya kuwaChuo cha Maendeleo ya Wananchi. Kwa bajeti ya mwakajana 2016/2017, Serikali iliahidi hapa kwamba Vyuo vyote vyaWananchi vitapandishwa hadhi na kuwa VETA. Napendakujua sasa ni lini Serikali itaenda kutimiza azma yake yakupandisha Vyuo hivi vya Wananchi kuwa VETA kwa kuanziana Chuo cha Wananchi cha Tarime? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba kuna dhana yakufikiria kwamba labda mafunzo yanayotolewa na VETA nibora zaidi kuliko yale yanayotolewa na Chuo cha Wananchi.Nitake tu kusema kwamba Vyuo vya Wananchi vina uwezomzuri na mkubwa sana katika kutoa mafunzo isipokuwa kwamuda mrefu vilikuwa havijapewa haki yake ya kuendelezwana kufanyiwa ukarabati unaostahili pamoja na kuwekewamiundombinu na vitendea kazi vya kufundishia kamainavyostahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka huu Wizaraimetenga jumla ya shilingi bilioni 12 kwa ajili ya kufuatilia vyuohivyo na kuvirekebisha. Kwa hali hiyo, tutafuatilia pia Chuocha Tarime kama alivyoeleza Mheshimiwa Mbunge ili kiwezekusaidiwa.

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

MWENYEKITI: Ahsante Waheshimiwa. Tunaendelea naWizara ya Nishati na Mheshimiwa Ester Mmasi aulize swalilake.

Na. 215

Mradi wa Bomba la Mafuta Mkoani Tanga

MHE. ESTER M. MMASI aliuliza:-

Kupitia fursa ya ujenzi wa bomba la mafuta MkoaniTanga, ni dhahiri kwamba vijana takribani 15,000 watapataajira kwenye mradi kwa upande wa Tanzania:-

(a) Je, Serikali imejipangaje kuona kuwa vijanawa Kitanzania wanapata ajira katika soko la Tanzania kupitiafursa hii ya uwekezaji?

(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuingizamtaala wa mafuta na gesi katika mitaala ya VETA i l ikuwajengea uwezo, maarifa na ujuzi vijana wa Kitanzaniakatika sekta hiyo muhimu?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNishati na Madini, napenda kujibu swali la Mheshimiwa EsterMichael Mmasi, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a)na (b), kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa ujenzi wabomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda)hadi Bandari ya Tanga (Tanzania) uko katika hatua yamajadiliano ya jinsi mradi huo utakavyotekelezwa. Katikamajadiliano hayo, suala la ajira kwa Watanzanialitazingatiwa ili Watanzania wanufaike na ajira kupitia ujenzina uendelezaji wa mradi huo. Mradi unatarajiwa kutoa ajira10,000 wakati wa ujenzi na ajira kwa watu 1,000 wakati wauendeshaji.

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2012 na 2013Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Kampuni yaPetrobras ya Brazili, iliendesha mafunzo maalum ya ufundiwa plumbing, uchomeaji, upakaji rangi pamoja na mambomengine katika Chuo cha VETA huko Mtwara na Lindi.Mafunzo hayo yalilenga kuwaongezea weledi wanafunziwapatao 350 wa VETA ambao wamepatiwa vyeti vyakimataifa na wanaweza kuajiriwa ndani ya nchi na nje yanchi. Gharama za mafunzo yote ni Dola za Marekani milioninne.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wizara yaElimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Serikali yaNorway, chini ya Mradi wa Mafuta kwa Maendeleo (Oil forDevelopment) imekamilisha taratibu za kuingiza mtaala wamafuta na gesi katika vyuo vya VETA hapa nchini. Mtaalahuu utaanza kutumika katika baadhi ya vyuo vya VETA hapanchini mwaka 2018. Utekelezaji wa mpango huu utagharimuDola za Marekani milioni 20.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mmasi ajiandaeMheshimiwa Shekilindi.

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwakuwa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima (Uganda)kuja Bandari ya Tanga nchini Tanzania ulitarajiwa kuanzamwezi Juni, 2017. Kwa kuwa pia majibu ya Mheshimiwa NaibuWaziri ni kwamba Serikali itakuwa tayari kuwaandaa vijanawetu kupitia mitaala ya oil and gas kwenye Vyuo vya VETAmnamo mwaka 2018. Je, Serikali kwa kufanya hivi haioni nisawa kabisa na kuweka rehani ajira ya kijana wa Kitanzaniahususan vijana wanaotoka katika Mkoa wa Tanga?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, mchakato wauchimbaji, uchanjuaji na uchakataji wa zao la oil and gasMikoani Lindi na Mtwara ulitarajia kuanza mwaka 2013, lakinihakuanza kutokana na sababu za ndani ya Serikali na kubwaikiwa ni ukamilishwaji wa local content policy pamoja namsamaha wa kodi. Nini kauli ya Serikali kwa vijana wahitimu

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

kwa nchi ya Tanzania hasa ukiangalia kwamba vijana wengiwanahangaika kutafuta kazi pasipokuwa na imani yoyote?Ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza kabisa nimpongeze Mheshimiwa Mmasi,tumekuwa na yeye tangu mwaka 2013 katika jitihada zakufungua mafunzo kwa VETA kwa wanafunzi wa oil and gas.Kwa hiyo hongera sana Mheshimiwa Mmasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na maswali yakehaya mawili, la kwanza, Serikali haioni kwamba ni muhimusasa kuwapatia mafunzo hasa wanafunzi wa VETA kwa oiland gas. Ni kweli kabisa upo umuhimu na mwaka 2012/2013kama nilivyosema, tulianza kutoa mafunzo hayo kwa ajili yakuwafundisha vijana wetu wa VETA Lindi na Mtwara kwa ajiliya uchomeleaji, ufundi sanifu pamoja na theories za kawaidaza utafiti wa kuchimba na kutafiti mafuta na gesi hapa nchini.Kwa hiyo, tunaona umuhimu Mheshimiwa Mmasi natumeshafika hatua nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, matarajio yampango wa Serikali, kweli kabisa mwaka 2018 tunatarajiataratibu zote za taaluma ili kuingiza sasa mtaala katika Vyuovya VETA kwa upande wa mafuta na gesi itafika sasa mudamuafaka hasa kwa VETA ambavyo ni vyuo vipya ukiondoavile vyuo ambavyo vimeshaanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninavyowasiliana na Wizaraya Elimu, Sayansi na Teknolojia, tumefika hatua nzuri, Serikaliya Norway pamoja na Serikali yetu itatenga shilingi milioni 20kwa ajili ya kukamilisha hatua hii. Kwa hiyo, MheshimiwaMmasi, tutakapofika katika hatua hiyo tutashirikiana pamojatuone namna ya kuwapatia vijana wetu mafunzo hayaambayo ni muhimu sana kwa ustawi wa nchi yetu.

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Shekil indi,ajiandae Mheshimiwa Khadija.

MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kuniona ili niweze kuuliza swali mojala nyongeza. Kwa kuwa bomba hili la mafuta ghafi linaishiaBandari ya Tanga, je, Serikali imejipangaje kuona kuwa vijanawa Kitanzania hasa vijana wa Mkoa wa Tanga wanapataajira hii katika soko la Kitanzania kupitia fursa hii ya uwekezaji?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Shekil indi,hongera, tumekuona unabeba mawe unasafisha barabara.Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza kabisa nimhakikishie MheshimiwaShekilindi, hili bomba la mafuta kutoka Hoima (Uganda) kujaTanga (Tanzania) lina urefu mpana sana, lina jumla yakilometa 1,443, lakini sehemu kubwa ya bomba hilo ambayoni urefu wa kilometa 1,047 ni za hapa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, bomba hilo litapitakaribu mikoa sita ya Kagera, Geita, Shinyanga, Dodoma hadiTanga, kwa hiyo ni manufaa makubwa sana. Hivyo basi, ipofursa kubwa sana kwa bomba hili kutoa ajira kubwa kwaWatanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie MheshimiwaShekilindi na wananchi wa Tanga kwamba ajira na fursanyingi sana za kazi zitapatikana. Sambamba na hayo,tunawasiliana kwa karibu sana na Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji i l i kutoa fursa nzuri sasa kwaWatanzania kuwekeza kwa kutumia fursa hiyo ya bomba laHoima hadi Bandari ya Tanga.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Khadija.

MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kwa kuwa ajira hizi zimekuwa zikitajwa kwa

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

ujumla wake, je, ni lini Serikali itatengeneza mchanganuo ilikupata uwakilishi mzuri kwa pande zote mbili za Muungano?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, kuhusu ni lini, kinachofanyika sasa tupo katikahatua ya pili, hatua ya kwanza tumekamilisha utambuzi waeneo ambapo bomba litapita. Hatua ya pili, tunakamilishamazungumzo ili kuainisha maeneo na fursa muhimu kwa nchizetu mbili lakini pia kwa nafasi za Tanzania Bara na TanzaniaZanzibar kwa masuala ya mafuta. Kwa sababu suala la ajirasiyo la Muungano lakini fursa ziko palepale, utaratibuutakamilika baada ya majadiliano ndani ya mwaka huulakini hatua ya pili itakuwa kuainisha fursa. Kwa hiyo,tutakapofikia hatua hiyo Mheshimiwa Mbunge tutawasilianaili tuone namna ya kukamilisha na kuzinufaisha pande zoteza Muungano.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na swali laMheshimiwa Profesa Norman Adamson.

Na. 216

Ujenzi wa Bwawa la Maji kwa ajili ya Kuzalisha Umeme

MHE. PROF. NORMAN A. S. KING aliuliza:-

Utafiti uliofanywa na Serikali unaonesha kuwa MtoLumakali unaozalisha maji katika Wilaya ya Makete unawezakuzalisha megawatts 640 za umeme na hasa ikizingatiwakuwa Wilaya ya Makete inapata mvua kwa miezi nane (8)kwa mwaka:-

Je, ni lini ujenzi wa bwawa ambao ni mpango waSerikali wa tangu mwaka 2005 utaanza ili kusaidia kujengauchumi wa kudumu huko Makete, Mkoa wa Njombe naMbeya kwa ujumla?

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNishati na Madini, napenda kujibu swali la MheshimiwaProfesa Norman Adamson Sigalla King, Mbunge wa Makete,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, upembuzi yakinifuuliofanyika mwaka 2012 kupitia Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) ulibainisha kuwepo uwezekano wa kuzalishaumeme wa nguvu za maji wa megawati 222 katika eneo laMwakauta kwenye Maporomoko ya Mto Rumakali. Juhudimbalimbali zimefanywa na Serikali ikiwemo kuingia mikatabambalimbali ya Makubaliano ya Awali ya uendelezaji wa Mradihuu kwa kushirikisha Kampuni mbalimbali za nje za JSC yaUrusi pamoja na kampuni ya China. Kampuni hizo hazikuwezakutekeleza mradi huo kutokana na gharama kuwa kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea nataratibu za kumpata mshauri mwelekezi kwa ajili ya kuandaamakabrasha ya zabuni kwa ajili ya kumpata mbia wa ujenziwa mradi huo. Kazi ya kumpata mbia itakamilika mwezi Junimwaka huu wa 2017 na ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanzamwaka 2019 na utakamilika mwaka 2026. Gharama za mradihuu ni Dola za Marekani milioni 936.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Profesa.

MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Naibu Waziriyanayoleta matumaini. Hata hivyo, nina maswali madogoya nyongeza. Kwa kuwa mradi huu ulitegemewa kuzalishaumeme na wananchi wote wa Tanzania kunufaika, ni linisasa Serikali itapeleka umeme kwenye vijiji 76 ambavyo havinaumeme Wilaya ya Makete? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni lini Serikaliitakamilisha upelekaji wa umeme kwenye vitongoji ambavyohavikupata umeme Awamu ya Kwanza ya REA? (Makofi)

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Profesaanavyotupa ushirikiano katika jimbo lake na awali ya yotenimhakikishie vijiji vyake 76 vitapata umeme kwenye Awamuya Tatu ya REA inayoanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini sasa vijiji vilivyobakivitapelekewa umeme, katika majibu yetu ya kila sikutumekuwa tukisema Mradi wa REA Awamu ya Tatu umeanzatangu mwezi Machi, 2017 na vijiji vyote vilivyosalia pamojana vya Mheshimiwa Profesa King vya Makete pamoja namaeneo mengine vitapelekewa umeme kati ya mwaka huuwa 2017 hadi 2020. Kwa hiyo, Mheshimiwa Profesa, vijiji vyakevyote vitapata umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua sana Kata zaMang’oto, Lupende, Kambata na Mabacha pamoja namaeneo mengine ambayo anayataja yatapatiwa umemekatika awamu hii. Vilevile vitongoji na taasisi zake za ummavitapatiwa umeme na mradi huo ni mmoja umeshaanza,tumezindua kwa Mkoa wa Iringa na Njombe kwaMheshimiwa Mbunge wa Kilolo na kwake wameshaanza,naambiwa wiki ijayo watafika kwa Mheshimiwa Profesa.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea, MheshimiwaSusane Maselle kwa niaba yake Mheshimiwa Mgonukulima.

Na. 217

Vijana Walionyang’anywa AjiraMachimbo ya Ishokelahela

MHE. SUZANA C. MGONUKULIMA (K.n.y. MHE. SUSANEP. MASELLE) aliuliza:-

Je, kwa nini Serikali imewanyang’anya ajira vijanawaliokuwa wamejiajiri kwenye Machimbo ya Ishokelahela nabaadaye ikaamua kubadili umiliki wa leseni kwa siri?

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNishati na Madini, napenda kujibu swali la Mheshimiwa SusanePeter Maselle, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, wachimbaji wadogowaliokuwa wanachimba Ishokelahela hawakuwa na leseniya uchimbaji bali walikuwa wanachimba katika eneo lautafiti la leseni ya Kampuni ya Carlton Kitongo TanzaniaLimited.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, mwaka 2014,Serikali ilifanya mazungumzo na kampuni hiyo na kuwapatiawachimbaji wadogo hao leseni mbili za uchimbaji zenyejumla ya hekta 20. Wananchi hao waliweza kuunda kampuniyao inaitwa Isinka Federation Miners Co-operative Limited.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2015 kikundi kiliamuakubadilisha leseni zake mbili za uchimbaji mdogo na kuzifanyakuwa leseni moja ya mgodi wa uchimbaji wa kati lakini chiniya Kampuni yao ya Isinka Federation Miners Co-operativeLimited. Umiliki wa leseni hizo haujabadilishwa hadi leo upochini ya umiliki wa wachimbaji hao wadogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi kufikia mwezi Machi,2017, mgodi ulikuwa umeshakusanya tani 35,000 za mbale(ore) kwa njia ya ubia wa Kampuni ya Busolwa Mining pamojana wachimbaji hao na waliweza kutoa fursa za ajira 164 zamoja kwa moja.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Suzana.

MHE. SUZANA C. MGONUKULIMA: MheshimiwaMwenyekiti, nitauliza maswali mawili ya nyongeza kwa niabaya Mheshimiwa Susane Maselle, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, kutokana namajibu ya Naibu Waziri kuwa wachimbaji hawa wadogo

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

walipata leseni, je, Serikali inatoa kauli gani juu ya Jeshi laPolisi lililotumia nguvu kupiga mabomu wachimbaji haowadogo na kuwanyanyasa wenyewe na familia zao nakufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia wanawake nawatoto? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, je, Naibu Waziri yupotayari kuongozana na Mheshimiwa Susane Maselle kwendaeneo hilo kuongea na wananchi hao kuhusu vitendowalivyofanyiwa na Jeshi la Polisi kuwa hawakufanyiwakiusahihi kwa sababu walikuwa na leseni? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwakifupi sana.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, nianze na swali la pili, niko tayari kufuatana naMheshimiwa Susane na kwa ridhaa yako kama itapendezabasi nitafuatana naye, nitembelee maeneo yale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na wachimbajihao kupigwa mabomu pamoja na kufanyiwa harassment nisuala ambalo linatakiwa litazamwe kwa kina sana unawezausiwe na jibu la moja kwa moja. Ninachoweza kusema nikwamba pale inapotokea kunakuwa na vurugu katikamaeneo ya uchimbaji kazi ya Jeshi la Polisi ni kutuliza ghasiaili kuhakikisha kwamba kunakuwa na amani na utulivu katikamaeneo yale. Inawezekana ilifanyika katika hatua hiyo, lakiniMheshimiwa Mbunge tutakaa pamoja tuone ni hatua ganizilichukuliwa ili tushirikiane na wenzetu wa Mambo ya Ndanituone nini cha kufanya zaidi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Rhoda Kunchela naMheshimiwa Msabaha.

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Nami nataka niulize swali la nyongeza. Kwawachimbaji wadogowadogo waliopo katika Mkoa waKatavi hususan katika Machimbo ya Ibindi na Kapanda,vijana hawa wamekuwa na changamoto kubwa nyingi mno

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

ikiwepo gharama kubwa ya kukata leseni za uchimbaji lakinipia gharama kubwa ya dawa za kusafishia dhahabuwanazopata na gharama za umeme pia ziko juu. Je, ninimkakati wa Serikali kuhakikisha sasa inawasaidia hawa vijanakupunguziwa gharama hizi ambazo ni kero? Tamko la Serikalil inasema nini i l i kuwasaidia vijana kupata mikopo iliwajiendeleze kiuchumi na kupata kipato?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, wewe ni mtaalam,lijibu.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, la kwanza, ni kweli kabisa maeneo ya uchimbajimaarufu sana kwa maeneo ya Mpanda ni pamoja na Ibindi,Kapanda pamoja na Dil ifu. Hata hivyo, nimtaarifaMheshimiwa Mbunge kwamba hatua ambazo Serikaliimechukua, la kwanza kabisa ni kurasimisha maeneo hayoambayo nimeyataja kuwa maeneo maalum kwa ajili yawachimbaji wadogo na wapo wachimbaji wadogo wazurisana kwenye eneo lako ikiwa ni pamoja na MheshimiwaKapufi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusu mkakati ambaotunafanya…

MWENYEKITI: Swali moja tu unajibu.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Niseme tu, tumetoa ruzuku mwakajuzi kwa wachimbaji wa Ibindi na Kapanda na badotunawapatia elimu na uwezeshaji kwa ajili ya uchimbaji mzurikwa wachimbaji hawa wadogo.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Msabaha.

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Nami naomba kumuuliza NaibuWaziri swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa kuna migodiambayo inakuwa imeshafungwa na inakuwa si salama kwawachimbaji wadogowadogo na hawa wachimbaji

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

wadogowadogo wamekuwa wakikiuka sheria na kuvamiamigodi hii na kuhatarisha maisha yao. Je, Serikali ina mikakatigani kuhakikisha uvamizi huu wa wachimbajiwadogowadogo unakwisha na kuchukulia hatua zakisheria?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwakifupi sana.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza kabisa, kwa mujibu wa Sheria ya Madiniya 2010, hairuhusiwi kufanya uchimbaji wowote bila lesenina kwa hiyo uvamizi kwa hali ya kawaida hauruhusiwi. Hatahivyo, yapo mazingira ambapo wananchi wamekuwawakivamia maeneo na hasa ambao wao wameanzakuchimba mapema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu na mkakati waSerikali, kwanza ni kufanya mazungumzo na hao wachimbajiwadogo kuwaelewesha lakini hata wale wenye leseniambao wameyashikilia bila kuyaendeleza nao kuzungumzanao. Tunachofanya sasa, maeneo ambayo yanachukuliwana watafiti bila kuyaendeleza Serikali inayachukua nakuwagawia wachimbaji maalum wadogo kwa utaratibu wakisheria ili kufanya uchimbaji huu uwe wa manufaa kwawachimbaji wadogo pamoja na wachimbaji wakubwa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Wabunge, muda wetuumekwisha tunaendelea na Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Na. 218

Tatizo Kubwa la Maji – Mkoa wa Simiyu

MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:-

Kumekuwa na tatizo kubwa sana la ukosefu wa majisafi na salama katika Mkoa wa Simiyu pamoja na Wilayazake ambao ni Bariadi, Itilima, Busega, Maswa na Meatu:-

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia majiwananchi wa Mkoa wa Simiyu?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Majina Umwagiliaji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa EstherLukago Midimu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeshaanzautekelezaji wa mradi wa majisafi kutoka Ziwa Victoria katikaMkoa wa Simiyu kwa miji mikuu ya Wilaya za Bariadi, Maswa,Meatu, Itilima, Busega na vijiji 253 vilivyopo umbali wakilometa 12 kandokando ya bomba kuu. Tayari MtaalamMshauri anakamilisha upembuzi yakinifu, usanifu na uandaajiwa makabrasha ya zabuni. Gharama za utekelezaji wa mradimzima zinakadiriwa kuwa kiasi cha Euro milioni 313. Mradihuu utawanufaisha wakazi wapatao 834,204 na unatarajiwakutekelezwa katika awamu mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awamu ya kwanzaitahusisha kufikisha maji katika Wilaya ya Bariadi, Itilima naBusega pamoja na vijiji vilivyopo kando kando ya bombakuu ambapo Benki ya Maendeleo ya Ujerumani imeahidikutoa Euro milioni 25 na tayari mkataba wa fedha (financialagreement) umesainiwa. Fedha zingine kiasi cha Euro milioni80 zitatolewa na Global Climate Fund na ujenzi wa mradihuu unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2017/2018na utachukua miaka miwili hadi kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awamu ya pili ya mradiitafikisha maji katika Wilaya za Meatu, Mji wa Mwanhuzi naMaswa kwa gharama ya Euro milioni 208. Fedha hizi piazinatarajiwa kutoka katika Global Climate Fund.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Midimu.

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza.Kwanza kabisa, namshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

yanayotia moyo. Kwa kuwa mradi wa maji wa Ziwa Victoriautachukua muda mrefu ili kuwezesha Wilaya zote za Mkoawa Simiyu kupata maji, je, Serikali ina mpango gani wadharura wa kuwapatia maji ya uhakika wananchi wa Mkoawa Simiyu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa Mjiwa Maswa sasa hivi una matatizo makubwa ya maji,wanakunywa maji machafu na kuna mradi wa chujio ambaoni wa muda mrefu. Je, ni lini Serikali itakamilisha ili wananchiwa Maswa wapate maji safi na salama? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza amesema kwasababu mradi huu utachukua muda mrefu, je, Serikali inampango gani wa kuhakikisha sasa wananchi wanapatahuduma ya maji? Kupitia mpango wa uendelezaji wa hii sektaya maji, tayari tumeshatekeleza miradi mbalimbali katikaMkoa wa Simiyu na kuna maeneo ambayo kwa mfano,Nyangili, Mwamanyili, Bukapile, Bulima, Lamadi, Lukugu,Manara, kuna ambayo imekamilika na mingine inaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia juzi tumepitisha bajetina katika Mkoa wa Simiyu tumeweka shilingi bilioni tisa iliHalmashauri ziendelee kutekeleza miradi ya maji kuhakikishakwamba wakati tunasubiri ule mradi mkubwa, lakiniwananchi wanaendelea kupata huduma ya maji. VilevileBariadi kuna huu mradi wa visima vya Misri tumechimbavisima pale na nimeenda mwenyewe Simiyu majiyanapatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Maswa, ni kweliukiangalia ule mradi hata utakapoanza eneo la mwishoutakwenda Maswa. Kutokana na hilo, hata jana tulikuwana kikao, tayari tumeagiza KASHWASA washirikiane naHalmashauri ya Maswa ili tuweze kuona uwezekano wa kutoamaji kutoka bomba lile pale Shinyanga kupeleka maji kwamuda pale Maswa wakati tunasubiri mradi mkubwa. (Makofi)

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tumeshatumiadakika 25 za mijadala ambapo tumeshavuka kile kiwangokilichotakiwa. Nampa Mheshimiwa Mulugo peke yake,wengine nakushauri Waziri wa Maji hili suala la maji ni zitoukae na Wabunge wote hawa ujaribu kuyamaliza,Mheshimiwa Mulugo.

MHE. PHILLIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa upendeleo wa kuuliza swalimoja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Songwe lina uhabamkubwa sana wa maji lakini niongelee Kata moja inaitwaTotowe ambapo mimi mwenyewe kwa juhudi za Mbungeniliomba mradi wa Mheshimiwa Sabodo nikachimba kisimakikubwa sana na kisima hicho mpaka ninavyosema hivibomba hilo linatoa maji kutoka mwaka 2012 mpaka leoyanatiririka na yamesambaa pale kijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimejaribu kuomba paleHalmashauri angalau watupe fedha hata shilingi milioni 50tuweze kujenga tanki la kutunzia maji yale angalau yawezekusambaa vizuri kwa kujenga mabomba kwa wananchi waTotowe na maeneo ya Namambu. Je, Serikali inanisaidiajemimi kama Mbunge nimefanya juhudi kutafuta maji halafumaji yanatiririka bila kujengewa tanki ili angalau wanipefedha nikajenge tanki maji yaweze kuenea pale Totowe?Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri,majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI:Mheshimiwa Mweyekiti, alichokisema ni kweli. Baada yakumaliza Bunge mwezi wa Julai, nitamwomba MheshimiwaWaziri nianze na Mkoa wa Songwe kwa sababu Halmashauriza Mkoa wa Songwe katika suala la utekelezaji wa miradi yamaji hawakufanya vizuri.

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Katibu Mkuu anaongeanao kule Morogoro ili kuona hizi Halmashauri ambazo haziku-perform vizuri zina matatizo gani wakati tulitoa maelekezobaada ya bajeti wanatakiwa kufanya manunuzi, lakinihawakufanya manunuzi kabisa. Nitakapokuwa nimekwendatutaliangalia hili na Mheshimiwa Mbunge ili tuweze kuwekautaratibu wa kwenda haraka wananchi wapate maji.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Nakumbusha tena rulling ya Kitiya kuwa Waziri wa Maji atakapoitwa kwenye Kamati yaBajeti wadau wa maji wote waalikwe waendewakazungumzie hoja za maji kwenye Majimbo yao.

Waheshimiwa Wabunge, maswali yamekwisha. Tunawageni waliopo Bungeni asubuhi hii.

Kuna wageni sita wa Naibu Spika wa Bunge,Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, kutoka Shirika la KimataifaLisilo la Kiserikali linalotekeleza miradi mbalimbali ya afyahapa nchini ya kuzuia vifo visivyo vya lazima kwa wanawakena wanafamilia, uzazi wa mama na mtoto pamoja naUKIMWI lijulikanalo kana Jhpiego ambao ni Dkt. LeslieMancuso-Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego wa Dunia; Dkt.Alain Damiba-Makamu wa Rais Mwandamizi; Dkt. JeremieZoungrana-Mkurugenzi wa Jhpiego Tanzania; Dkt. DustanBishanga-Mkuu wa Mradi wa USAID wa Boresha wa Afya; Dkt.Albert Komba – Mkuu wa Mradi wa SAUTI wa Jhpiego naNdugu Owen Mwandumbya-Meneja Mawasiliano naUshirikishaji Wadau. (Makofi)

Tunao wageni 19 wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi lakujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi kutoka Wizaraya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakiongozwa na Dkt.Florens Turuka-Katibu Mkuu; Ndugu Immaculate Ngwale-Naibu Katibu Mkuu; Jenerali Venance Mabeyo-Mkuu waMajeshi ya Ulinzi na Usalama, Luteni Jenerali JamesMwakibolwa-Mnadhimu Mkuu wa Jeshi; Meja Jenerali MichaelIsamuyo-Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa; Meja Jenerali SimonMumwi-Mkuu wa Mipango na Maendeleo Jeshini; Meja

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

Jenerali Harrison Masebo-Mkuu wa Utumishi Jeshini; MejaJenerali E. Athanas-Mkuu wa Jeshi la Akiba; Ndugu EgbertNdauka-Kamishina wa Sera na Mipango pia wamoMabrigedia Jenerali na Makanali. Wameambatana naWakurugenzi, Wakuu wa Taasisi, Idara, Vitengo na Maafisambalimbali waliopo chini ya Wizara hiyo. (Makofi)

Pia tunao wageni mbalimbali wa WaheshimiwaWabunge pamoja na wanafunzi waliotembelea Bunge kwaajili ya mafunzo Bungeni na Madiwani ambao wanatokakwenye Jimbo la Mheshimiwa Mulugo. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea, Katibu.

MWONGOZO WA SPIKA

WABUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.

MWENYEKITI: Subiri Katibu, Waheshimiwa Kitikikishatoa maelekezo kwa Katibu, ninyi mnachelewa kamauna mwongozo si unasema mapema?

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mapema ndiyo hii.

MWENYEKITI: Msibishe.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,mapema ndiyo hii.

MWENYEKITI: Msibishe itakula kwenu. HayaMheshimiwa Bilago. (Kicheko)

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Bobali.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Haonga.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Bobali.

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bobali. MheshimiwaHaonga endelea.

WABUNGE FULANI: Ditopile.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba mwongozo wako kwa Kanuni ya 68(7) lakini pianaomba iweze kusomwa na Kanuni ya 101(4). Naombaniisome Kanuni ya 101(4) ambayo inasema:-

“Kwa kuzingatia masharti ya fasili ya (3), Kamati zaVyama zitawasil isha kwa Spika majina ya Wabungewatakaoomba kupata ufafanuzi wa suala mahususi la sera,na Spika atatoa nafasi kwa Wabunge kwa kuzingatiauwiano.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku ya jana kuna jambolimejitokeza hapa Bungeni ambalo wako Wabungembalimbali waliosimama kwa ajili ya kuweza kuombaufafanuzi wakati tunajadili Wizara ya Elimu. WalisimamaWabunge mbalimbali ambao ulikuwa umewasoma kwamajina ambapo upande wa CHADEMA alisimamaMheshimiwa Susan ambaye ni Waziri Kivuli lakini pia kwaupande wa CCM wapo pia waliosimama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lililotokea kwa kwelil i l ishangaza sana. Tunaomba kujua kama hil i sualalinaruhusiwa hapa Bungeni na wakati huo tuone kwa mujibuwa Kanuni hii ya 101(4) kama uwiano ulizingatiwa jana kwawale Wabunge waliokuwa wamesimama. Kwa hiyo, sualahili kidogo limeleta shida na sintofahamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tulikuwa tunaombakama kuna uwezekano kulingana na uwiano uliotajwahapa, akiomba mmoja labda Mbunge kutoka CCM aje waCHADEMA, aje wa CUF mmoja then turudi kwa wengine kulikokuchukua wa upande mmoja wote wanne halafu baadayeukasema muda umeisha. Suala hili kwa kweli tunaomba

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

ufafanuzi kwa sababu limelete sintofahamu na siyo jana tuna siku nyingi za nyuma kidogo limeweza kujitokeza. Ahsantesana.

MWENYEKITI: Ahsante nimeshakuelewa. MheshimiwaBobali.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nasimama kwa Kanuni ya 68(7) pamoja na 69ikikupendeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimboni kwangu Mchingahivi sasa ninapoongea kuna tembo 18 wamevamia kwenyevijiji wanakula mashamba ya wakulima lakini lililo baya usikuwa kuamkia leo wamevamia kijiji na wamevunja nyumbaza wananchi bahati ni kwamba hawakuua raia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili nimeshawahikumwambia Waziri mara nyingi, jana usiku nikampigia simuhakupokea, nikamtumia na meseji, hatua hazichukuliwi naJimbo la Mchinga halipakani na mbuga yoyote, ni tembowanaopotea kama hawa ambao walipotea wakaja hapaUDOM.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa suala hili la tembo…

WABUNGE FULANI: Ndovu.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Sawa ndovu ili mwelewe,kuvamia vijiji na kula vyakula vya wakulima katika kipindi hikiambacho mavuno yenyewe siyo mazuri, mwaka jana zililiwahekari 183 hakuna hata mkulima mmoja amelipwa walakupewa kifuta jasho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mwongozo wako,kama Waziri ameshindwa kusimamia hii Wizara aseme kwasababu kero za namna hii ziko katika Majimbo mengi lakinipia nataka kujua hawa wakulima watafidiwaje. Naombamwongozo wako.

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Bobaliumeshaeleweka. Mheshimiwa Bilago.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba mwongozo wako kwa Kanuni ya 68(7) nisiisomelakini ni jambo ambalo limetokea eneo la Masaki janamapema tu ambapo Askari Polisi ametumia risasi tisakumdhibiti Adam Malima aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedhakwa sababu ya gari tu lililokuwa limepakiwa vibaya (wrongparking).

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya risasi tisaambazo ni fedha za walipa kodi bila sababu yoyote ya msingina Malima hakuwa adui wala na silaha yoyote na vitendohivi tumevisema muda mrefu, matukio kama hayayanaendelea kuimarika nchi hii. Tulianza na TV ya Cloudsikatekwa, akatekwa Mheshimiwa Nape na bastola sasaMalima ametekwa na risasi tisa zimetumika. Naombamwongozo wako…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa

MHE. KASUKU S. BILAGO: Tunakoipeleka nchi hii…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Ndiyo huku tulikokuwatunajivunia?

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Bilagoumeshaeleweka.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Naam.

MWENYEKITI: Tumeshakuelewa.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante.

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nimeombwamiongozo mitatu, miongozo yote, mwongozo waMheshimiwa Haonga mambo yaliyotokea jana leo hayahusikilakini nitakusaidia. Kanuni zetu ziko very clear, Kanuni ya 5(4)kama Kiti kinafanya kitu hakikuridhishi ni wajibu wakokuandika barua kwa Katibu na mimi nitaitwa kwa Katibuna wewe utaitwa tutaelezana vizuri tu utaratibu wa Bungelinavyoendeshwa. Kwa hiyo, nakushauri kama unaona Kitihakijakutendea haki, tumia Kanuni ya 5(4), hiyo ndiyo rullingyangu.

Mheshimiwa Bobali mambo ya tembo, hizi Kanuni zetuziko very clear, Kanuni ya 67 ni jambo lililotokea mapemaBungeni, lakini naelewa masuala haya yanawagusaWabunge kwenye Majimbo yao na sehemu ya kilio chao nihumu ndani. Kwa hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii utakaa naMbunge ili mtazame ni namna gani mtalimaliza tatizo hilina kusaidia wananchi wake wasipate matatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Bilago suala la Mheshimiwa Malima,vilevile Kanuni zetu haziruhusu lakini pia Bunge hatuna taarifarasmi juu ya suala hili na ili mradi umelisema Serikali ipowamelisikia, watalifanyia kazi, watatupa maelekezo. Katibu.

NDG. THEONEST RUHILABAKE - KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikalikwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri

wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa. (Makofi)

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leohapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu yaBunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, naomba kutoa

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea, kujadilina kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumiziya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wafedha 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kuchukuafursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema,kwa kuniwezesha kuwasilisha hotuba yangu ya bajeti kwamwaka huu wa 2017/2018 mbele ya Bunge lako Tukufu. Pili,namshukuru kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli, kwa kuniamini kuendelea kuiongoza Wizara ya Ulinzina Jeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekeenachukua fursa hii kuungana na Watanzania kwa ujumlakumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kuchaguliwa kwake kwakishindo kuwa Mwenyekiti wa Tano wa Chama chaMapinduzi kufuatia Uchaguzi wa Viongozi wa Chamauliofanyika tarehe 23 Julai, 2016 mjini Dodoma. Watanzaniawana matumaini makubwa na safu ya uongozi wa chamachini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, napendakuwashukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu,Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kwa miongozo namaelekezo wanayonipatia katika kutekeleza majukumu yaWizara yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahadi yangu kwaMheshimiwa Rais, kwenu Waheshimiwa Wabunge naWatanzania wenzangu ni kuwa, nitaendelea kutekelezamajukumu niliyokabidhiwa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Mheshimiwa Mwenyekiti, uongozi wa Awamu ya Tanochini ya Mheshimiwa Rais na Wasaidizi wake Wakuu katikakipindi cha takriban mwaka mmoja na nusu tangu uingiemadarakani umekuwa ni mfano wa kuigwa na umewekahistoria ya kipekee nchini kwa kuendelea kutekeleza kwa kasina ufanisi mkubwa ahadi zilizomo kwenye Ilani ya CCM yaUchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie fursa hii piakumpongeza Jenerali Venance Mabeyo kwa kuteuliwa kuwaMkuu wa Majeshi ya Ulinzi. Aidha, nimpongeze Luteni JeneraliJames Mwakibolwa kwa kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuuwa Majeshi ya Ulinzi. Kipekee, napenda kumshukuru Mkuu waMajeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange kwautumishi wake uliotukuka na kwa namna tulivyoshirikianakatika kuliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzaniakwa mafanikio makubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpongeza Spikawa Bunge hili Mheshimiwa Job Ndugai; Naibu Spika,Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson; pamoja na Wenyeviti waBunge kwa kuendesha vizuri shughuli za Bunge. NamwombaMwenyezi Mungu azidi kuwapa maarifa, hekima, busara nanguvu za kuendelea kuongoza Bunge hili katika kutekelezamajukumu yake mazito na nyeti.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, napenda kutumianafasi hii kuwashukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu yaBunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mheshimiwa BaloziAdadi Rajabu, Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa KanaliMstaafu Ally Khamis Masoud na Wajumbe wote wa Kamatihii Tukufu kwa kuendelea kunipa ushirikiano mkubwa katikakuiongoza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. (Makofi)

Kamati hii imetupatia ushauri mzuri wakati wakuchambua mapendekezo ya makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara yangu kwa mwaka 2017/2018. Maoni namapendekezo yao yametusaidia sana katika kuandaampango na bajeti hii.

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hiikuwapongeza Waheshimiwa wafuatao: Alhaji AbdallahBulembo, Profesa Palamagamba Kabudi, Mheshimiwa AnneKillango Malecela, Mama Salma Rashidi Kikwete, Dkt. GetrudeLwakatare na Mheshimiwa Catherine Ruge kwa kuteuliwakuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri la Muungano waTanzania na Mheshimiwa Juma Ali Juma kwa kuchaguliwakuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani. Aidha, nampongezaMheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi kwa kuteuliwakuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie fursa hii kutoasalamu za pole kwako Mheshimiwa Spika, WaheshimiwaWabunge na Watanzania wote kwa kuondokewa nampendwa wetu Mheshimiwa Samwel Sitta, Mbunge Mstaafuwa Jimbo la Urambo Mashariki na Spika wa Bunge la Tisa laJamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia natoa pole kwaMheshimiwa Spika kufuatia kifo cha Mheshimiwa Hafidh AliTahir aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibarkilichotokea tarehe 11 Novemba, 2016 na Mheshimiwa Dkt.Elly Marko Macha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumkilichotokea tarehe 31 Machi, 2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naungana na wenzanguwote waliotangulia kuwapa pole wale waliopatwa namajanga, pamoja na kufiwa na ndugu, jamaa na wapendwawao katika matukio mbalimbali yaliyotokea nchini yakiwemotetemeko la ardhi lililotokea Kagera tarehe 10 Septemba,2016 na ajali mbalimbali za vyombo vya usafiri yakiwemomabasi ya abiria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekeenatumia fursa hii kuwapa pole Wazazi, Walimu naWatanzania wote kutokana na vifo vya wanafunzi 32,Walimu wawili na Dereva wa shule ya Msingi Lucky Vincentya Mjini Arusha vilivyotokana na ajali ya basi iliyotokea tarehe6 Mei, 2017, katika eneo la Rhotia Wilayani Karatu. NaombaMwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pemapeponi na kuwajalia majeruhi wote kupona haraka nakurejea katika masomo yao.

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo yautangulizi, napenda sasa kuchukua fursa hii kuwasilishahotuba yangu ambayo kiujumla imejikita katika maeneomakuu yafuatayo:-

Malengo na majukumu ya Wizara; Hali ya Usalamawa Mipaka katika mwaka 2016/2017; Utekelezaji wa Maonina Ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo yaNje, Ulinzi na Usalama; Utekelezaji wa Mpango na Bajeti yamwaka 2016/2017 na Mpango na Makadirio ya Bajeti kwamwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, malengo na majukumu yaWizara; kama ilivyo katika Dira ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa, Wizara imeendelea kuwa Taasisi iliyotukukaya kulinda na kudumisha amani na usalama wa Taifa letu.Vivyo hivyo, dhima ya Wizara ni kuendelea kulinda Jamhuriya Muungano wa Tanzania dhidi ya adui wa aina yoyotekutoka ndani na nje ya nchi na kuhakikisha kuwa mamlakana maslahi ya nchi yetu yanakuwa salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kufanikisha dhimayake, malengo ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifayameendelea kuwa kama ifuatavyo:-

(i) Kuwa na Jeshi dogo na mahiri la Ulinzi waNchi lenye weledi, zana bora, vifaa vya kisasa namawasiliano salama;

(ii) Kuendelea kuwajengea vijana wa Kitanzaniamoyo wa uzalendo, ukakamavu, maadili mema, utaifa nakuwafundisha stadi za kazi;

(iii) Kuendeleza utafiti na kujenga uwezo katikateknolojia za kijeshi;

(iv) Kuimarisha Jeshi la Akiba;

(v) Kusaidia mamlaka za Kiraia katika kukabiliana

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

na athari za majanga na matukio yanayoweza kuhatarishamaisha amani na utulivu wa nchi; na

(vi) kudumisha amani na usalama kwakushirikiana na nchi nyingine duniani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, i l i kufikia malengoyaliyoainishwa, Wizara itaendelea kusimamia utekelezaji wamajukumu yafuatayo:-

(i) Kuandikisha Wanajeshi wenye sifa stahiki kwalengo la kuwa na Jeshi dogo, mahiri kwa ajili ya Ulinzi waTaifa na kuwapatia mafunzo na mazoezi ya kinadharia nakivitendo;

(ii) Kuwapatia wanajeshi makazi bora, zana,vifaa na vitendea kazi bora na vya kisasa pamoja nakusimamia matumizi na matunzo yake;

(iii) Kuendesha mafunzo na mazoezi ya Mgambo;

(iv) Kuboresha mitaala ya mafunzo ya JKT kwavijana ili kuwaandaa kuwa wakakamavu, wenye nidhamuna kuwajengea moyo wa uzalendo na mshikamano waKitaifa na kutekeleza shughuli za kujitegemea;

(v) Kuendeleza utafiti na uhawilishaji wateknolojia za Kijeshi kupitia Mashirika ya Mzinga na Nyumbu;

(vi) Kuwezesha Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi laKujenga Taifa (SUMAJKT); kuwa na tija na faidaitakayochangia katika uendeshaji wa shughuli za Jeshi laKujenga Taifa.

(vii) Kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katikakukabiliana na majanga na dharura za Kitaifa paleinapohitajika kufanya hivyo; na

(viii) Kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine katikanyanja za Kijeshi na kiulinzi kupitia Jumuiya za Kimataifa,

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

Kikanda na ushirikiano na nchi moja moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa maoni naushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama. Wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge yaMambo ya Nje Ulinzi na Usalama ilipokaa na kujadiliMakadirio ya Mapato, Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ulinzina Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2016/2017ilitoa maoni, ushauri na maelekezo kadhaa kwa Wizara hiiyaliyolenga kuboresha utendaji na utekelezaji wa majukumuyake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa maoni, ushauri na maelekezo yaliyotolewayamefanyiwa kazi na hoja mbalimbali zilizotolewa naWaheshimiwa Wabunge wakati wa mjadala huo piazimezingatiwa katika mpango wa bajeti ya mwaka wafedha 2017/2018 inayowasilishwa leo hapa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya Ulinzi na Usalama wamipaka ya nchi yetu kwa ujumla ni shwari. Hata hivyo,kumekuwa na changamoto ya kutotengamaa kwa hali yausalama kwenye baadhi ya nchi za Ukanda wa AfrikaMashariki, Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika ikiwa ni pamojana Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi, Somaliana Sudan Kusini. Aidha, uwepo wa hali ya matishio ya ugaidiwa Kimataifa umevilazimu vyombo vya Ulinzi na Usalamakwa kushirikiana na nchi jirani na raia wake kuendelea kuwakatika hali ya tahadhari na umakini endapo kutajitokeza daliliyoyote inayotishia usalama, hatua stahiki ziweze kuchukuliwaharaka iwezekanavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya mipaka ya nchi yetuyenye jumla ya urefu wa kilomita 5,390 ambayo inahusishaeneo la nchi kavu na eneo la maji imeendelea kuwa shwari.Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana nawananchi vimeendeleza jitihada za kuimarisha usalama wamipaka hiyo hatua ambayo imechangia kudhibiti nakupunguza matukio na vitendo vyenye kutishia usalamakama vile, ugaidi, biashara ya dawa za kulevya, usafirishaji

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

haramu wa binadamu, uhamiaji haramu na ujambazi. Haliya mipaka yetu katika kipindi kinachopitiwa imekuwa kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpaka wa Mashariki; katikampaka huu ambao una urefu wa kilomita 1,413, nchi yetuinapakana na Bahari ya Hindi na pia nchi za Kenya, Visiwavya Ushelisheli, Comoro na Msumbiji. Kwa ujumla hali yausalama katika mpaka huu imeendelea kuwa shwarikutokana na kudhibitiwa kwa vitendo vya uharamia ambapokumeambatana na kuongezeka kwa doria katika Bahari yaHindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpaka wa Kaskazini; kwenyeeneo la mpaka huu Tanzania imepakana na nchi za Kenyana Uganda. Hali ya usalama katika mpaka huu wenye urefuwa kilomita 1,221 kwa ujumla ilikuwa shwari licha ya tatizola uingiaji wa wahamiaji haramu kutoka nchi za Ethiopia,Eritrea na Somalia ambao hujipenyeza kuingia nchini wakiwasafarini kuelekea maeneo ya Kusini mwa Afrika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpaka wa Magharibi; mpakahuu wenye urefu wa kilomita 1,220 ambako Tanzaniaimepakana na nchi za Burundi, Rwanda na Jamhuri yaKidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na kuwa shwari kwaujumla umekuwa pia na changamoto kadhaa. Mojawapoya changamoto hizo ni kutokukamilika kwa mazungumzoya upatanishi ya pande zinazosigana nchini Burundi haliinayosababisha hali ya kiusalama kutotengamaa. Aidha,uwepo wa vikundi vya waasi vyenye silaha vinavyoendeshaharakati za kimapigano dhidi ya Majeshi ya DRC na Majeshiya Umoja wa Mataifa (MONUSCO) ambako kunasababishaongezeko la wakimbizi hali ambayo inahatarisha usalamakwenye eneo la mpaka huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpaka wa Kusini; kwenyempaka wa Kusini ambao una urefu wa kilomita 1,536Tanzania inapakana na nchi za Msumbiji, Malawi na Zambia.Pamoja na hatua zinazoendelea za usuluhishi wa mgogorowa mpaka uliopo baina ya Tanzania na Malawi, kwa ujumla

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

hali ya mpaka huu imeendelea kuwa shwari na wananchiwanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Utekelezaji wa Mpango waBajeti ya Mwaka 2016/2017. Katika mwaka wa fedha wa2016/2017, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ilikadiriakukusanya mapato ya jumla ya sh.68,406,000.00 kupitiamafungu yake matatu ya 38-NGOME, 39- JKT na 57-Wizara.Kufikia mwezi Aprili, 2017 Mafungu hayo yalifanikiwakukusanya mapato ya jumla ya sh.43,516,561.80 sawa naasilimia 63.6 ya makadirio. Chanzo kikuu cha makusanyo hayoni mauzo ya nyaraka za zabuni ambayo yameendeleakupungua kwa kuwa utangazaji wa zabuni sasa unafanywapia na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti ya mwaka wafedha 2016/2017, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifail i idhinishiwa na Bunge lako Tukufu jumla yash.1,736,578,102,510.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida namaendeleo kwa mafungu yake matatu. Kati ya fedha hizo,bajeti ya kawaida inayojumuisha mishahara na matumizimengineyo ni sh.1,488,578,102,510.00 na bajeti kwa ajili yashughuli za maendeleo ni sh. 248,000,000,000.00. Mchanganuowa bajeti kwa kila Fungu umeoneshwa katika Jedwali Na.1.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi kufikia mwezi Aprili, 2017Wizara ilikuwa imepokea jumla ya sh.1,199,292,622,613.00sawa na asilimia 69.1 ya bajeti yake yote. Kati ya fedha hizo,sh.1,163,392,622,613.00 sawa na asilimia 78.2 ya bajetiiliyoidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida zilipokelewa.Fedha hizo zimetumika kutekeleza majukumu na mipangoya kazi, kulipia mishahara na posho mbalimbali muhimu ikiwani pamoja na kugharamia huduma mbalimbali zikiwemostahili za Wanajeshi na Watumishi wa Umma, uendeshaji waOfisi na kulipa madeni ya Wazabuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa matumiziya maendeleo, fedha zilizopokelewa ni sh.35,900,000,000.00sawa na asilimia 14.5 ya fedha zote zilizoidhinishwa kwa ajili

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

ya matumizi hayo. Fedha hizo zimetumika kulipia madeni yakimkataba, ujenzi wa miundombinu ya maji safi na maji takavikosini, kuingiza huduma ya maji na umeme katika baadhiya nyumba 6,064 zilizojengwa kwa makazi ya Wanajeshi nauingizaji umeme katika minara ya mawasiliano iliyosimikwakatika Mikoa ya Morogoro na Dodoma. Kuendelezaukarabati wa maghala ya silaha na milipuko na ukarabatiwa kambi mpya tano za Milundikwa na Luwa (Rukwa), Itaka(Songwe), Mpwapwa (Dodoma) na Makuyuni (Arusha).Mchanganuo wa fedha zilizopokewa kwa ajili ya matumiziya kawaida na maendeleo hadi mwezi April i, 2017umeoneshwa katika Kiambatisho Na. 1.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuangalia mchanganuowa fedha zilizopokelewa hadi kufikia mwezi Aprili, 2017,mwenendo wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya matumiziya kawaida kwa mafungu yote matatu ya Wizara hususanfedha za mishahara na chakula kwa Wanajeshi katika kipindihicho ulikuwa ni wa kuridhisha. Fedha kwa ajili ya mishaharana marupurupu zilipokelewa kulingana na makisio ya bajeti.Kwa upande wa fedha za shughuli za maendeleo, fedhazilizopokelewa hazikuweza kukidhi mahitaji na hivyo kuathiriutekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja naulipaji wa madeni ya kimikataba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mafanikio ya Utekelezaji waMpango na Bajeti ya Mwaka Wa Fedha 2016/2017. Matumiziya shughuli za kawaida; katika mwaka wa fedha 2016/2017,Wizara imefanikiwa kulipia mahitaji na huduma muhimu kwaMaafisa, Askari, Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa na Watumishiwa Umma. Aidha, kwa kutumia fedha hizi majukumumbalimbali ya kiulinzi yaliyotekelezwa ni pamoja na kufanyamafunzo na mazoezi ya Kijeshi, mafunzo ya Mgambo,ushirikiano wa kiulinzi na kijeshi na nchi nyingine, ushirikianona Jumuiya za Kikanda na Kimataifa, ushirikiano wa Jeshi naMamlaka za Kiraia na Mafunzo ya JKT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mafunzo na Mazoezi yaKijeshi; katika mwaka 2016/2017, Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania, limeendelea kutoa mafunzo na mazoezi kwa

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Wanajeshi wake ili kujiimarisha kiulinzi. Jeshi letu lilifanikiwakufanya mazoezi mbalimbali ya kimataifa na ya ndaniyafuatayo: “Exercise Eastern Accord” ililofanyika Tanzaniakuanzia tarehe 10 hadi 12 Julai 2016, Exercise AmphibiousLanding” lililofanyika Bagamoyo kuanzia tarehe 19 Agosti,2016 hadi tarehe 5 Septemba, 2016 ikiwa ni sehemu yamaadhimisho ya sherehe za miaka 52 ya JWTZ; “Exercise -Ushirikiano Imara” lililofanyika Mombasa nchini Kenya kuanziatarehe 17 - 19 Novemba, 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Jeshi liliendelea kutoamafunzo kwa Maafisa na Askari kwenye vyuo, shule na vituombalimbali vya mafunzo kwa wanajeshi katika ngazimbalimbali ndani na nje ya nchi. Mazoezi na mafunzo hayayalilenga kuwajengea Wanajeshi wetu uwezo, weledi naumahiri wa kiutendaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Mafunzo yaMgambo; mafunzo ya Mgambo kwa wananchiyameendelea kutolewa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi waTanzania. Katika kipindi cha mwaka 2016/2017, JWTZ kwakushirikiana na Vyombo vya Usalama limeendesha mafunzokatika ngazi mbalimbali ambapo jumla ya wananchi 13,997walifuzu. Hili ni ongezeko la wahitimu 7,241 sawa na asilimia51.7 ikilinganishwa na wananchi 6,756 waliopata mafunzohayo mwaka 2015/2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kutoa wito kwaViongozi wa ngazi mbalimbali kuhamasisha wananchikushiriki katika mafunzo ya Mgambo. Kwa maagizo yaMheshimiwa Rais, jumla ya Askari Mgambo 48 walioshirikikatika “Exercise- Onesha Uwezo wa Medani” lililofanyikakatika Mkoa wa Arusha na “Exercise - Amphibious Landing”lililofanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwaniwaliandikishwa katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi waTanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Huduma za Afya na Tiba;katika kipindi husika, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifaimeendelea kutoa huduma za matibabu kwa Maafisa, Askari,

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

Watumishi wa Umma, familia zao na wananchi kwa ujumla.Huduma hizo zimekuwa zikitolewa katika hospitali na vituovya tiba vya Jeshi hapa nchini. Katika kipindi hicho jumla yawananchi 217,887 walipata matibabu katika zahanati, vituovya afya na hospitali za Jeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Wizara imeendeleana maboresho ya huduma za matibabu kwa Wanajeshi nafamilia zao, ambapo mchakato wa kuanzisha Mfuko waBima ya Afya kwa ajili ya Wanajeshi ulioanza mwaka wafedha 2015/2016 umeendelea kufanyiwa kazi. Hati Maalum(instrument) ya mapendekezo ya uanzishwaji wa Mfuko huona mabadiliko ya Kanuni Namba 26 na 27 ya Juzuu ya Kwanza(I) Utawala vimeandaliwa ili viweze kuwasilishwa kwaMheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu kwa ajili ya kuridhiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ushirikiano wa Kiulinzi naKijeshi na Nchi nyingine;ushirikiano kati ya nchi yetu na nchinyingine katika nyanja za Kijeshi ni suala muhimu katikamustakabali wa ulinzi na usalama. Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania limeendelea kuwa na ushirikiano mzuri naMajeshi ya nchi nyingine hususan katika eneo linalohusu nafasiza mafunzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka fedha wa2016/2017 Maafisa na Askari zaidi ya 350 wamekwendakusoma kozi mbalimbali katika nchi rafiki zikiwemo AfrikaKusini, Burundi, Canada, China, Falme za Kiarabu, India,Kenya, Marekani, Misri, Morocco, Rwanda, Uganda, Uingereza,Ujerumani, Urusi na Zambia. Aidha, Maafisa kutoka katikabaadhi ya nchi hizi wapo hapa nchini katika vyuo vyetu vyaKijeshi kwa mafunzo. Vyuo hivyo ni Chuo cha Maafisa Monduli,Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Arusha na Chuo chaUlinzi wa Taifa - Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ushirikiano na Jumuiya zaKikanda na Kimataifa; Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania,limeendelea kushiriki katika operesheni za ulinzi wa amanichini ya Umoja wa Nchi za Afrika (African Union) na Umojawa Mataifa. Nchi yetu imeendelea kuwa na vikosi vyake

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Darfur nchini Sudan maeneo ya Khor-Abeche; Shangli Tobayina Menawash chini ya UNAMID. Aidha, Jeshi letu limeendeleakuwepo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongokama sehemu ya MONUSCO “Force Intervention Brigade”.Pia, Kombania mbili za Polisi Jeshi zipo nchini Lebanon kwamajukumu kama hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kikosi na Maafisa wa JWTZwaliopo kwenye Operesheni za Ulinzi wa Amani katikamaeneo hayo wote wanaendelea vizuri na utekelezaji wamajukumu yao. Vilevile, katika kudumisha mahusiano nakuzuia matishio ya utekaji wa meli katika Bahari ya Hindi,tumeendelea kushirikiana na nchi mbalimbali zikiwemo, nchiza Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleoya Nchi za Kusini mwa Afrika, Afrika Kusini, Australia,Bangladesh, China, Hispania, India, Iran, Italia, Pakistan,Ufaransa, Netherlands, Uingereza na Urusi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ushirikiano wa Jeshi naMamlaka za Kiraia; katika kudhihirisha utayari wa Jeshi letukushikiri katika shughuli mbalimbali za kiraia na utoaji wahuduma na misaada wakati wowote inapohitajika, katikamwaka wa fedha 2016/2017, Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania limeshiriki katika kutoa misaada kwenye maafaya tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.

Mheshimiwa Mwenyekiti, misaada hiyo imehusishakurejesha miundombinu iliyoharibika, ujenzi wa majengo yaTaasisi za Serikali pamoja na kusaidia wananchi. Aidha, Wizarailichangia sh.76,125,000.00 kwa waathirika wa tetemeko hilo.Nachukua fursa hii kuzipongeza Mamlaka za Kiraia na Taasisizote kwa kutoa ushirikiano mzuri kwa Jeshi wakati wakutekeleza majukumu hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana navitendo vya kihalifu, Wizara, kupitia JWTZ, imeendeleakushirikiana na Vyombo vingine vya Usalama na Mataifamengine katika kupambana na matishio ya kiusalamayakiwemo ugaidi, uharamia na biashara haramu ya dawaza kulevya. Aidha, JWTZ limeshiriki katika Operesheni Amboni

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

Mkoani Tanga iliyoanza mwezi Mei, 2016 na kufungwa rasmimwezi Desemba, 2016 ambapo wahalifu hao walidhibitiwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imekuwa mstari wambele katika kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais la kutatuatatizo la uhaba wa madawati katika shule za Serikali zamsingi na sekondari. Aidha, kupitia taasisi za Mashirika yakeWizara ilipewa jukumu la kutengeneza madawati 60,000. Kazihiyo ilifanyika kwa ufanisi na weledi mkubwa. Katika zoezihilo, JKT ilichangia madawati ya ziada 5,005. Wizara kupitiaJWTZ imesimamia ujenzi wa shule ya Sekondari Ihumwailiyopo Dodoma na inaendelea kusimamia ujenzi wa shuleya Sekondari ya Ihungo iliyopo Kagera iliyoathirika natetemeko la ardhi mwaka 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mafunzo ya Jeshi la KujengaTaifa kwa vijana yameendelea kutolewa kwa vijana wakujitolea na wale wa mujibu wa sheria kwa lengo la kujengauzalendo, ukakamavu, maadili mema, utaifa pamoja nakutoa stadi za kazi. Katika mwaka 2016/2017, Jeshi laKujenga Taifa limefanikiwa kuendesha mafunzo kwa vijana14,748 kwa mujibu wa sheria, ambapo kati yao Wavulanawalikuwa 10,863 na Wasichana 3,885 waliohitimu Kidato chaSita mwaka 2016. Idadi hiyo ni sawa na asilimia 73.7 ya lengola kuchukua vijana 20,000. Pia, JKT limefanikiwa kuchukuavijana wapya wa kujitolea 9,848 kwa ajili ya mafunzo, katiyao Wavulana ni 7,154 na Wasichana ni 2,694. Idadi hiyo nisawa na asilimia 98.5 ya lengo la kuchukua vijana 10,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa kuandikisha vijanawa kujitolea kwa ajili ya kujiunga na mafunzo hayo,hutakiwa kujaza na kusaini fomu maalum ya mkataba yenyemasharti kwamba kijana awe tayari kurudi nyumbani maraamalizapo mkataba wake. Pamoja na dhamira ya Serikaliya kutoa ajira kwa vijana wanaohitimu mafunzo ya Jeshi laKujenga Taifa, siyo vijana wote wanaohitimu mafunzo hayowanaweza kupata ajira katika vyombo vya Ulinzi, Usalamaau Taasisi zake. Hivyo, napenda kutoa rai kwa vijanawanaopata mafunzo ya JKT wazingatie maarifa na ujuzi

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

wanaoupata hususan wa stadi za kazi ili waweze kujiajiri nakuweza kujitegemea na hata kuajiri wao wenyewe.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya shughuli zamaendeleo; fedha zilizopokelewa hadi mwezi Machi katikamwaka wa fedha 2016/2017, kwa Mafungu yote matatuil ikuwa sawa na takribani asil imia 14.5 ya bajetiiliyoidhinishwa. Wizara imeweza kutekeleza miradi ifuatayo:-

Kukamilisha mradi wa ujenzi wa nyumba 6,064awamu ya kwanza kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi; kulipiasehemu ya madeni ya kimkataba; kukarabati majengopamoja na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na makazikatika makambi na vikosi vya JKT; ukarabati wa zana za ulinziwa anga; ujenzi wa bwalo la Maafisa katika shule ya Kijeshiya Ulinzi wa Anga Tanga; kuweka umeme katika baadhi yaminara ya mawasiliano salama Jeshini katika mikoa yaMorogoro na Dodoma. Aidha, kupitia ushirikiano baina yaTanzania na China, ujenzi wa uwanja wa ndege vitaNgerengere umekamilika na kituo cha mafunzo maalum yakijeshi Mapinga Bagamoyo ili kukabiliana na matishio mapyaya kiusalama kinaendelea kujengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa nyumba, maghalana miundombinu mbalimbali. Wizara imeendelea kutekelezamradi wa ujenzi wa nyumba 6,064 ambapo katika mwakawa fedha 2016/2017, huduma za maji na umeme katikanyumba hizo zimepelekwa na hivyo kuwezesha kuanzakutumika kwa nyumba hizo katika kambi zilizopo Mikoa yaArusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kagera, Kaskazini Pemba,Kigoma, Morogoro, Pwani na Tanga. Juhudi za kupata fedhaza kukamilisha ujenzi wa nyumba 3,936 ili kufikia lengo la ujenziwa nyumba 10,000 katika kambi zilizobaki zinaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Wizara inaendeleana ujenzi wa maghala ya kuhifadhia milipuko, ambapomaghala 12 yamejengwa Makambako-Njombe na maghalaSita yamejengwa Dunga- Zanzibar. Aidha, katika kipindihicho, upanuzi wa uwanja wa ndege vita Ngerengereulikamilika na kuzinduliwa rasmi na Rais na Amiri Jeshi Mkuu

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Machi, 2017.Mradi wa ujenzi wa kituo maalum cha mafunzoComprehensive Training Centre nao unaendelea vizuri nahadi sasa ujenzi umefikia asilimia 30.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ununuzi wa zana na vifaavya kijeshi; katika juhudi za kuliongezea uwezo wa kiutendajina kuimarisha mazingira ya kufanyia kazi Serikali imeendeleakulipatia Jeshi zana na vifaa mbalimbali. Katika mwaka wafedha wa 2016/2017, Jeshi limepokea zana na vifaambalimbali kwa ajili ya ulinzi wa nchi kavu, anga na majini.Kupatikana kwa zana na vifaa hivyo kumeongeza uwezowa Jeshi kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kiulinzi.Mpango wa ununuzi wa zana na vifaa vya kisasa na borapamoja na mafunzo ya namna ya kutumia na kutunza zanana vifaa hivyo utakuwa endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Uzalishaji Mali laSUMAJKT. SUMAJKT limeendelea kutekeleza shughuli zakekatika misingi ya kibiashara kupitia Kampuni Tanzu, Idara namiradi yake ifuatayo:-

Kampuni ya Ulinzi SUMA JKT Guard Limited; Kampuniya Ujenzi National Service Construction Department; Kampuniya Ubia; Idara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo; Idara ya Viwandana mradi wa matrekta. SUMA JKT kupitia kampuni yake yaUlinzi SUMA JKT Guard Limited, inaendesha shughuli za ulinzikatika Ofisi za Serikali, Mashirika ya Umma na sekta binafsi,zikiwemo Benki na Migodi. Kwa mwaka 2016/2017,imefanikiwa kuongeza huduma za ulinzi kwa wafuatao:-

Wakala wa Serikali Mtandao, Air TanzaniaCorporation Limited Julius Nyerere International Airport,Mamlaka ya Chakula na Dawa, Local Authority PensionFund, Wakala wa Ndege za Serikali, Medical StoresDepartment, Tanzania Insurance Regulatory Authority, Wakalawa Nishati Vijijini, TANROADS, Procurement and SuppliesProfession Technician Board, Tanzania Forests Services, Bankof Africa, BOT –Dodoma, FINCA, DCB Bank, Dar es SalaamMaritine Institute na KUDU Resources Limited.

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kampuni SUMA Guardimetoa mchango kwa Serikali kwa kupunguza tatizo la ajiranchini kwa kuajiri vijana 4,150. Kupitia Bunge lako Tukufunatoa rai kwa Kampuni zinazodaiwa kulipa madeni yaomapema iwezekanavyo ili kuwezesha SUMA JKT SeedsCompany Limited kufikia malengo yake na kuendeleakuzalisha mbegu bora kwa faida ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Mzinga; katikamwaka wa fedha wa 2016/2017, Shirika hili limeendelea nautekelezaji wa majukumu yake ya msingi ya kufanya utafitiwa kuwezesha uzalishaji wa mazao ya kijeshi kwa kutumiamalighafi zinazopatikana hapa nchini na kufanyamatengenezo na ukarabati wa zana za Kijeshi. Pamoja nachangamoto ya upatikanaji wa fedha za maendeleo, shirikalimeendelea kupanua uzalishaji wa mazao ya Kijeshi kwagharama nafuu ikilinganishwa na kuagiza bidhaa hizo kutokanje ya nchi.

Mheshimiwa Mweyekiti, katika kutekeleza azma yaSerikali ya kuwa na uchumi wa viwanda, na pia kukabilianana changamoto za upatikaji wa malighafi za kistratejia namtaji, shirika limeendelea kuchukua hatua za kujiimarishaikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya kutekeleza mpangomkakati wa kipindi cha miaka mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango mkakati huounakusudia kupanua wigo wa uzalishaji wa mazao ya Kijeshi,kuongeza wigo wa shughuli za Shirika kwa kuanzisha viwandavipya vya kutengeneza baruti na kupanua mradi wakutengeneza mashine ndogondogo kwa aji l i yakuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo na wa katikufanya uchakataji na kuongezea thamani ya mazao yakilimo na misitu. Vilevile Shirika limekusudia kuboreshakarakana ya utengenezaji samani na kuiimarisha kampunitanzu ya Mzinga Holding Company Limited kwa kuipatia mtajina vitendea kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Nyumbu; katikakipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017, pamoja na

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

kutekeleza majukumu yake ya msingi ya utafiti na uhawilishajiwa teknolojia, shirika limechangia kupunguza gharama kwaJWTZ kwa kufanya matengenezo ya zana za kijeshi kwagharama nafuu ambazo zingepaswa kusafirishwa kwendanje kwa matengenezo na kuzalisha vipuli vya magari,mitambo na mashine mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Shirika limekuwalikihusika na matayarisho ya zana, mitambo na vitendea kazikwa vikundi vinavyokwenda katika operesheni za ulinzi waamani. Aidha, shirika limeshiriki katika zoezi la Kitaifa lautengenezaji wa madawati kwa ajili ya shule za msingi nasekondari za Serikali. Katika hatua nyingine, Shirikalimetengeza vitanda 652 kwa ajili ya Maafisa na Askariwaliohamia Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika pia lilifanikiwakufanya ukarabati mdogo wa nyumba za makazi namitambo ya karakana ya shirika, kununua vifaa vya TEHAMAna kukarabati mfumo wa umeme kiwandani. Vilevile, Shirikalimeendelea kutekeleza shughuli zake za kufanya utafiti katikateknolojia ya magari na mitambo ya kijeshi, kuimarisha nakuongeza uwezo wa kuhawilisha teknolojia mbalimbali zautafiti na kukarabati miundombinu ya shirika. Shirikalimeandaa mpango wa maendeleo wa miaka kumi wenyelengo la kuliimarisha na kulirejeshea shirika hadhi yake ili liwezekushiriki katika maendeleo ya uchumi wa viwanda nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtandao wa mawasilianosalama Jeshini; Wizara imeendelea kutekeleza Mradi waMawasiliano Salama Jeshini ambapo hadi kufikia Machi, 2017jumla ya minara 132 ilikuwa imesimikwa Tanzania Bara naVisiwani. Mawasiliano kupitia mtandao huo yanapatikanakatika maeneo ya Zanzibar, Pwani, Dar es Salaam na baadhiya maeneo ya Morogoro. Kazi ya kuunganisha maeneomengine ya nchi ikiwemo Mkoa wa Dodoma kwenyemtandao huo inaendelea. Aidha, uunganishaji wamawasiliano haya salama katika vikosi vyote Jeshiniutakamilishwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

Mheshimiwa Mwenyekiti, kudhibiti uvamizi wa maeneoya Jeshi, upimaji na ulipaji wa fidia. Katika mwaka wa fedha2016/2017, Wizara haijaweza kupima na kulipa fidiawananchi kwa maeneo yaliyotwaliwa kwa matumizi ya Jeshikama ilivyopangwa kutokana na upatikanaji mdogo wafedha za maendeleo. Aidha, kwa lengo la kudhibiti uvamizizaidi katika maeneo ya Jeshi Wizara kupitia vikosi, vyuo nashule za Kijeshi, imeendelea kupanda miti na kuwekamabango kuzunguka maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto za utekelezajiwa mpango na bajeti katika mwaka wa fedha 2016/2017.Katika mwaka wa fedha 2 016/2017, Wizara iliidhinishiwajumla ya sh.248,000,000,000 kwa ajili ya shughuli za maendeleona hadi kufikia mwezi Machi, 2017 kiasi kilichotolewa nish.35,900,000,000 sawa na asilimia 14.5 ya bajeti hiyo.Kutokana na kiwango cha fedha kilichopokelewa, Wizaraimeweza kulipa sehemu ya madeni ya kimkataba na kuingizahuduma za maji na umeme katika baadhi ya nyumba 6,064pamoja na ukarabati wa miundombinu katika baadhi yakambi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtiririko wa fedha kwa ajiliya matumizi mengineyo katika mwaka wa fedha 2016/2017,umeleta changamoto katika kutekeleza kikamilifu mpangokazi kulipia kwa wakati huduma na mahitaji muhimu kwaWanajeshi, vijana wanaohudhuria mafunzo ya JKT naWatumishi wa Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango na Mwelekeo wabajeti kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Mpango naMwelekeo wa bajeti wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa katika mwaka wa fedha 2017/2018 unakusudiakuimarisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi wa Jeshi katikakutekeleza majukumu yake kulingana na dira na dhima yaWizara, Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka2015, mpango wa pili wa Taifa wa maendeleo na maelekezoya Mheshimiwa Rais wakati wa kuzindua Bunge la 11 laJamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Novemba,

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

2015. Hivyo, Wizara itaendelea kutekeleza majukumu yakemuhimu katika maeneo yafuatayo:-

(i) Kuliongezea uwezo Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania utendaji kivita kwa kulipatia vifaa na zana borapamoja na kutoa mafunzo stahiki kwa Wanajeshi dhidi yaadui wa ndani na nje;

(ii) Kuimarisha mazingira mazuri yakufanyiakazi, makazi na kuimarisha upatikanaji wa huduma, stahilina mahitaji ya msingi kwa Wanajeshi na Watumishi raia;

(iii) Kuwapatia vijana wa Kitanzania mafunzoya uzalendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa na stadi za kazi,utafiti na uhawilishaji wa teknolojia kwa madhumuni yakuzalisha bidhaa na huduma kwa ajili ya matumzi ya kijeshina kiraia; na

(iv) Kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine Dunianikatika nyanja za Kijeshi na kiulinzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shukrani; kabla sijahitimishahotuba yangu naomba kutoa shukrani zangu za dhati kwawale wote walioniwezesha kufanikisha na kutekeleza jukumula kuongoza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa. Aidha,napenda kutoa shukrani kwa wale wote waliotoa michangoiliyosaidia kufanikisha maandalizi ya makadirio ya matumiziya fedha ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwamwaka wa 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti naomba kutoa shukrani zapekee kwa wafanyakazi wenzangu wa Wizara ya Ulinzi naJeshi la Kujenga Taifa nikianzia na Katibu Mkuu Dkt. FrolenceTuruka; Naibu Katibu Mkuu Bi. Immaculate Ngwale; Mkuu waMajeshi ya Ulinzi ,Jenerali Venance Mabeyo; Mnadhimu MkuuLuteni Jenerali James Mwakibolwa; Mkuu wa Jeshi la KujengaTaifa, Meja Jenerali Michael Lisamuyo; Wakuu wa Kamandi,Wakuu wa Mashirika, Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma.Aidha, naishukuru Kamati ya Wizara iliyoandaa hotuba hiikwa ushirikiano walionipatia.

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile naomba niwashukuruwapigakura wangu wa Jimbo la Kwahani, kwa ushirikianowao walionipa katika mwaka wa 2016/2017. Ni matumainiyangu kuwa tutaendelea kushirikiana zaidi kwa manufaa yaJimbo letu na Taifa kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Serikali naombapia kutoa shukrani zangu za dhati kwa Serikali za nchimbalimbali, Mashirika na Wahisani kwa ushirikiano wao naWizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Wahisani hao nipamoja na Jamhuri ya Watu wa China, Ujerumani, Canada,Marekani, Ufaransa, India na Uturuki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, tunazishukuru nchi rafikikwa ushirikiano wao katika shughuli zetu mbalimbali zakiulinzi. Nchi hizo ni pamoja na Afrika Kusini, Bangladesh,DRC, Ghana, Falme za Kiarabu, Indonesia, Misri, Nigeria,Uingereza, Urusi na nchi wanachama wa Jumuiya ya AfrikaMashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.Nchi rafiki na wahisani wamekuwa wakishirikiana na Jeshikatika mafunzo, mazoezi ya Kijeshi, na kuimarishamiundombinu ya mawasiliano, makazi na tiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, makadirio ya mapato namatumizi ya bajeti ya mwaka 2017/2018. Makadirio yamapato. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na taasisizake haina chanzo cha uhakika cha mapato kinachowezakuingia kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa maduhuliikizingatiwa majukumu ya msingi ya Wizara hii. Chanzo kikuucha mapato ni makusanyo ya mauzo yanayotokana nanyaraka za zabuni, suala ambalo kwa sasa linashughulikiwapia na Wakala wa Serikali wa Ununuzi na Ugavi (GPSA) kwakiasi kikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha wa2017/2018, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inakadiriakukusanya jumla ya sh.69,706,000 katika mchanganuoufuatao:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fungu 38 – NGOME -

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

Sh.15,601,000/= Fungu 39 JKT Sh.54,003,000/= na Fungu 57Wizara Sh.102,000/=. Matumizi ya kawaida na maendeleo,Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inaombakuidhinishiwa jumla ya Sh.1,725,517,816,225 kwa ajili yamatumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo ili iwezekutekeleza majukumu yake katika mwaka wa fedha wa2017/2018. Kati ya fedha hizo Sh.1,506,517,816,925 ni kwa ajiliya matumizi ya kawaida na Sh.219,000,000,000 ni kwa ajili yaMatumizi ya Maendeleo. Mchanganuo kwa kila Fungu niifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fungu 38 - Ngome Matumiziya Kawaida ni Sh.1,205,244,289,563; Matumizi ya MaendeleoSh.8,000,000,000, jumla Sh. 1,213,244,289,563. Fungu 39 - JKT,matumizi ya kawaida Sh.283,362,530,783; matumizi yamaendeleo ni shil ingi 6,000,000,000; jumla niSh.289,362,530,783. Fungu 57 - Wizara; Matumizi ya Kawaidani sh.17,910,996,579; Matumizi ya maendeleoSh.205,000,000,000. Jumla Sh. 222,910,996,579.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: MheshimiwaMwenyekiti, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

MWENYEKITI: Ahsante. Hoja imeungwa mkono.

HOTUBA YA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFAMHESHIMIWA DKT. HUSSEIN ALI MWINYI (MB) AKIWASILISHABUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHAKWA MWAKA 2017/2018 KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leohapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, naomba kutoa hojakwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea, kujadili na

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka waFedha 2017/18.

2. Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua fursahii kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwakuniwezesha kuwasilisha hotuba yangu ya bajeti kwa mwakawa fedha 2017/18 mbele ya Bunge lako Tukufu. Pili,namshukuru kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. John Pombe JosephMagufuli, kwa kuniamini kuendelea kuiongoza Wizara yaUlinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Kwa namna ya pekeenachukua fursa hii kuungana na watanzania kwa ujumlakumpongeza Mhe. Rais kwa kuchaguliwa kwake kwakishindo kuwa Mwenyekiti wa Tano wa Chama chaMapinduzi kufuatia Uchaguzi wa Viongozi wa Chamauliofanyika tarehe 23 Julai, 2016 mjini Dodoma. Watanzaniawana matumaini makubwa na safu ya uongozi wa Chamachini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu. Vilevile,napenda kuwashukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na WaziriMkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) kwa miongozona maelekezo wanayonipatia katika kutekeleza majukumuya Wizara yangu.

3. Mheshimiwa Spika, ahadi yangu kwa Mhe. Rais,kwenu Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wenzanguni kuwa, nitaendelea kutekeleza majukumu niliyokabidhiwakwa uadilifu na uaminifu mkubwa. Uongozi wa Awamu yaTano chini ya Mhe. Rais na wasaidizi wake wakuu katikakipindi cha takriban mwaka mmoja na nusu tangu uingiemadarakani umekuwa ni mfano wa kuigwa na umewekahistoria ya kipekee nchini kwa kuendelea kutekeleza kwa kasina ufanisi mkubwa ahadi zilizomo kwenye Ilani ya CCM yaUchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

4. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii piakumpongeza Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kwakuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi. Aidha,

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

nimpongeze Luteni Jenerali James Aloyce Mwakibolwa kwakuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.Kipekee, napenda kumshukuru Mkuu wa Majeshi ya UlinziMstaafu Jenerali Davis Adolf Mwamunyange kwa utumishiwake uliotukuka na kwa namna tulivyoshirikiana katikakuliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwamafanikio makubwa.

5. Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe,Spika wa Bunge hili Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb), NaibuSpika Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) pamoja na Wenyeviti waBunge kwa kuendesha vizuri shughuli za Bunge. NamuombaMwenyezi Mungu azidi kuwapa maarifa, hekima, busara nanguvu za kuendelea kuongoza Bunge hili katika kutekelezamajukumu yake mazito na nyeti.

6. Mheshimiwa Spika, vile vile, napenda kutumia nafasihii kuwashukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Balozi Adadi Rajabu(Mb), Makamu Mwenyekiti Mhe. Kanali Mstaafu Ally KhamisMasoud (Mb) na Wajumbe wote wa Kamati hii Tukufu kwakuendelea kunipa ushirikiano mkubwa katika kuiongozaWizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Kamati hiiimetupatia ushauri mzuri wakati wa kuchambuamapendekezo ya makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara yangu kwa mwaka 2017/18. Maoni na mapendekezoyao yametusaidia sana katika kuandaa mpango bajeti hii.

7. Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kuwapongezaWaheshimiwa wafuatao: Alhaji Abdallah Majura Bulembo(Mb.), Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi(Mb.), Anne Killango Malecela (Mb.), Salma Rashidi Kikwete(Mb.), Dkt. Mch. Getrude Lwakatare (Mb.) na Catherine Ruge(Mb) kwa kuteuliwa kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri laMuungano wa Tanzania na Mhe. Juma Ali Juma (Mb.) kwakuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani. Aidha,nampongeza Prof. Palamagamba John Aidan MwalukoKabudi (Mb.) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

8. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kutoa salamu za

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

pole kwako Mhe. Spika, Waheshimiwa Wabunge naWatanzania wote kwa kuondokewa na mpendwa wetu Mhe.Samweli John Sitta Mbunge Mstaafu wa Jimbo la UramboMashariki na Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muunganowa Tanzania. Pia, natoa pole kwako Mhe. Spika kufuatia kifocha Mhe. Hafidh Ally Tahir aliyekuwa Mbunge wa Jimbo laDimani, Zanzibar kilichotokea tarehe 11 Novemba, 2016 naMhe. Dkt. Elly Marko Macha aliyekuwa Mbunge wa VitiMaalum kilichotokea tarehe 31 Machi, 2017.

9. Mheshimiwa Spika, ninaungana na wenzangu wotewaliotangulia kuwapa pole wale waliopatwa na majanga,pamoja na kufiwa na ndugu, jamaa na wapendwa waokatika matukio mbalimbali yaliyotokea nchini yakiwemotetemeko la Ardhi lililotokea Kagera tarehe 10 Septemba,2016 na ajali mbalimbali za vyombo vya usafiri yakiwemomabasi ya abiria. Kwa namna ya pekee natumia fursa hiikuwapa pole wazazi, walimu na watanzania wote kutokanana vifo vya wanafunzi 32, walimu 2 na dereva wa Shule yaMsingi Lucky Vincent ya mjini Arusha vilivyotokana na ajali yabasi iliyotokea tarehe 06 Mei, 2017 katika eneo la RhotiaWilayani Karatu. Naomba Mwenyezi Mungu azilaze roho zamarehemu mahali pema peponi na kuwajalia majeruhi wotekupona haraka na kurejea katika masomo yao.

10. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo yautangulizi, napenda sasa kuchukua fursa hii kuwasilishahotuba yangu ambayo kiujumla imejikita katika maeneomakuu yafuatayo: Malengo na majukumu ya Wizara; Hali yaUsalama na Mipaka katika mwaka 2016/17; Utekelezaji waMaoni na Ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mamboya Nje, Ulinzi na Usalama, Utekelezaji wa Mpango na Bajetiya mwaka 2016/17 na Mpango na Makadirio ya Bajeti kwamwaka 2017/18.

MALENGO NA MAJUKUMU YA WIZARA

11. Mheshimiwa Spika, kama ilivyo katika Dira ya Wizaraya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara imeendelea kuwaTaasisi iliyotukuka ya kulinda na kudumisha amani na usalama

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

wa Taifa letu. Vivyo hivyo, Dhima ya Wizara ni kuendeleakulinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya adui waaina yoyote kutoka ndani au nje ya nchi na kuhakikisha kuwamamlaka na maslahi ya nchi yetu yanakuwa salama.

12. Mheshimiwa Spika, katika kufanikisha Dhima yake,malengo ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifayameendelea kuwa kama ifuatavyo:

i. Kuwa na Jeshi dogo na mahiri la Ulinzi waNchi lenye weledi, zana bora, vifaa vya kisasa na mawasilianosalama;

ii. Kuendelea kuwajengea vijana wakitanzania moyo wa uzalendo, ukakamavu, maadili mema,utaifa na kuwafundisha stadi za kazi;

iii. Kuendeleza utafiti na kujenga uwezo katikateknolojia za kijeshi;

iv. Kuimarisha Jeshi la Akiba;

v. Kusaidia Mamlaka za Kiraia katikakukabiliana na athari za majanga na matukio yanayowezakuhatarisha maisha, amani na utulivu nchini; na

vi. Kudumisha amani na usalama kwakushirikiana na nchi nyingine duniani.

13. Mheshimiwa Spika, ili kufikia malengo yaliyoainishwa,Wizara itaendelea kusimamia utekelezaji wa majukumuyafuatayo:

i. Kuandikisha wanajeshi wenye sifa stahiki kwa lengola kuwa na Jeshi dogo na mahiri kwa ajili ya Ulinzi wa Taifana kuwapatia mafunzo na mazoezi ya kinadharia nakivitendo;

ii. Kuwapatia wanajeshi makazi, zana, vifaa na

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

vitendea kazi bora na vya kisasa pamoja na kusimamiamatumizi na matunzo yake;

iii. Kuendesha mafunzo na mazoezi ya Mgambo;

iv. Kuboresha mitaala ya mafunzo ya JKT kwa vijana ilikuwaandaa kuwa wakakamavu, wenye nidhamu nakuwajengea moyo wa uzalendo na mshikamano wa kitaifana kutekeleza shughuli za kujitegemea;

v. Kuendeleza utafiti na uhawilishaji wa teknolojia zakijeshi kupitia Mashirika ya Mzinga na Nyumbu;

vi. Kuwezesha Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la KujengaTaifa (SUMAJKT) kuwa na tija na faida itakayochangia katikauendeshaji wa shughuli za Jeshi la Kujenga Taifa;

vii. Kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kukabilianana majanga na dharura za kitaifa pale inapohitajika; na

viii. Kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine katika nyanjaza kijeshi na kiulinzi kupitia Jumuiya za Kimataifa, Kikandana ushirikiano na nchi moja moja.

UTEKELEZAJI WA MAONI NA USHAURI WA KAMATI YA KUDUMUYA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA

14. Mheshimiwa Spika, wakati Kamati ya Kudumu yaBunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ilipokaa na kujadiliMakadirio ya Mapato, Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ulinzina Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2016/17 ilitoamaoni, ushauri na maelekezo kadhaa kwa Wizara hiiyaliyolenga kuboresha utendaji na utekelezaji wa majukumuyake. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa maoni,ushauri na maelekezo yaliyotolewa yamefanyiwa kazi na hojambalimbali zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge wakatiwa mjadala huo pia zimezingatiwa katika mpango na bajetiya mwaka wa fedha 2017/18 ninayowasilisha leo hapaBungeni.

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

HALI YA ULINZI NA USALAMA WA MIPAKA YA NCHI

15. Mheshimiwa Spika, hali ya Ulinzi na Usalama wamipaka ya nchi yetu kwa ujumla ni shwari. Hata hivyo,kumekuwa na changamoto ya kutotengamaa kwa hali yausalama kwenye baadhi ya nchi za Ukanda wa AfrikaMashariki, Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika ikiwa ni pamojana Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi, Somalia naSudan Kusini. Aidha, uwepo wa hali ya matishio ya ugaidiwa kimataifa umevilazimu vyombo vya Ulinzi na Usalamakwa kushirikiana na nchi jirani na raia wake kuendelea kuwakatika hali ya tahadhari na umakini ili endapo kutajitokezadalili yoyote inayotishia usalama, hatua stahiki ziwezekuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

16. Mheshimiwa Spika, hali ya mipaka ya nchi yetu yenyejumla ya urefu wa kilomita 5,390 ambayo inahusisha eneo lanchi kavu na eneo la maji imeendelea kuwa shwari. Vyombovyetu vya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na wananchivimeendeleza jitihada za kuimarisha usalama wa mipakahiyo hatua ambayo imechangia kudhibiti na kupunguzamatukio na vitendo vyenye kutishia usalama kama vile,ugaidi, biashara ya dawa za kulevya, usafirishaji haramu wabinadamu, uhamiaji haramu na ujambazi. Hali ya mipakayetu katika kipindi kinachopitiwa imekuwa kama ifuatavyo:

Mpaka wa Mashariki

17. Mheshimiwa Spika, katika mpaka huu ambao unaurefu wa kilomita 1,413 nchi yetu inapakana na Bahari yaHindi na pia nchi za Kenya, Visiwa vya Ushelisheli, Komoro naMsumbiji. Kwa ujumla hali ya usalama katika mpaka huuimeendelea kuwa shwari kutokana na kudhibitiwa kwavitendo vya uharamia ambapo kumeambatana nakuongezeka kwa doria katika Bahari ya Hindi.

Mpaka wa Kaskazini

18. Mheshimiwa Spika, kwenye eneo la mpaka huuTanzania imepakana na nchi za Kenya na Uganda. Hali ya

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

usalama katika mpaka huu wenye urefu wa kilomita 1,221kwa ujumla ilikuwa shwari licha ya tatizo la uingiaji wawahamiaji haramu kutoka nchi za Ethiopia, Eritrea na Somaliaambao hujipenyeza kuingia nchini wakiwa safarini kuelekeamaeneo ya Kusini mwa Afrika

Mpaka wa Magharibi

19. Mheshimiwa Spika, mpaka huu wenye urefu wakilomita 1,220 ambako Tanzania imepakana na nchi zaBurundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)pamoja na kuwa shwari kwa ujumla umekuwa pia nachangamoto kadhaa. Mojawapo ya changamoto hizo nikutokukamilika kwa mazungumzo ya upatanishi ya pandezinazosigana nchini Burundi hali inayosababisha hali yakiusalama kutotengamaa. Aidha, uwepo wa vikundi vyawaasi vyenye silaha vinavyoendesha harakati za kimapiganodhidi ya Majeshi ya DRC na Majeshi ya Umoja wa Mataifa(MONUSCO) ambako kunasababisha ongezeko la wakimbizihali ambayo inahatarisha usalama kwenye eneo la mpakahuo.

Mpaka wa Kusini

20. Mheshimiwa Spika, kwenye mpaka wa Kusini ambaouna urefu wa kilomita 1,536 Tanzania inapakana na nchi zaMsumbiji, Malawi na Zambia. Pamoja na hatuazinazoendelea za usuluhishi wa mgogoro wa mpaka uliopobaina ya Tanzania na Malawi, kwa ujumla hali ya mpakahuu imeendelea kuwa shwari na wananchi wanaendeleana shughuli zao kama kawaida.

UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA MWAKA 2016/17

21. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2016/17Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ilikadiria kukusanyamapato ya jumla ya shilingi 68,406,000.00 kupitia mafunguyake matatu ya 38-NGOME, 39-JKT na 57-Wizara. Kufikia mweziAprili, 2017 mafungu hayo yalifanikiwa kukusanya mapatoya jumla ya shilingi 43,516,561.80 sawa na asilimia 63.6 ya

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

makadirio. Chanzo kikuu cha makusanyo hayo ni mauzo yanyaraka za zabuni ambayo yameendelea kupungua kwakuwa utangazaji wa zabuni kwa sasa unafanywa pia naWakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).

22. Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha2016/17, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa iliidhinishiwana Bunge lako Tukufu jumla ya shilingi 1,736,578,102,510.00kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwamafungu yake Matatu. Kati ya fedha hizo, bajeti ya kawaidainayojumuisha mishahara na matumizi mengineyo ni shilingi1,488,578,102,510.00 na bajeti kwa ajili ya shughuli zamaendeleo ni shilingi 248,000,000,000.00. Mchanganuo wabajeti kwa kila fungu umeoneshwa katika Jedwali Na. 1

Jedwali Na. 1: Mchanganuo wa Bajeti ya Mwaka waFedha 2016/17

23. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Aprili, 2017Wizara ilikuwa imepokea jumla ya shilingi 1,199,292,622,613.00sawa na asilimia 69.1 ya bajeti yake yote. Kati ya fedha hizoshilingi 1,163,392,622,613.00 sawa na asilimia 78.2 ya bajetiiliyoidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida zilipokelewa.Fedha hizo zimetumika kutekeleza majukumu na mipangoya kazi, kulipia mishahara na posho mbalimbali muhimu ikiwani pamoja na kugharamia huduma mbalimbali zikiwemostahili za Wanajeshi na Watumishi wa Umma, uendeshaji waOfisi na kulipa madeni ya Wazabuni.

24. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi yamaendeleo, fedha zilizopokelewa ni shilingi 35,900,000,000.00

Fungu Matumizi Kawaida Maendeleo Jumla NGOME 1,187,543,710,510 10,000,000,000

1,197,543,710,510

JKT 282,034,214,000 8,000,000,000

290,034,214,000

Wizara 19,000,178,000 230,000,000,000

249,000,178,000

Jumla 1,488,578,102,510 248,000,000,000 1,736,578,102,510

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

sawa na asilimia 14.5 ya fedha zote zilizoidhinishwa kwa ajiliya matumizi hayo. Fedha hizo zimetumika kulipia madeniya kimikataba, ujenzi wa miundombinu ya maji safi na majitaka vikosini, kuingiza huduma ya maji na umeme katikabaadhi ya nyumba 6,064 zilizojengwa kwa makazi yaWanajeshi na uingizaji umeme katika minara ya mawasilianoiliyosimikwa katika mikoa ya Morogoro na Dodoma,kuendeleza ukarabati wa maghala ya silaha na milipuko naukarabati wa kambi mpya tano za Milundikwa na Luwa(Rukwa), Itaka (Songwe), Mpwapwa (Dodoma) na Makuyuni(Arusha). Mchanganuo wa fedha zilizopokewa kwa ajili yamatumizi ya kawaida na maendeleo hadi mwezi Aprili, 2017umeoneshwa katika Kiambatisho Na. 1

25. Mheshimiwa Spika, kwa kuangalia mchanganuo wafedha zilizopokelewa hadi kufikia mwezi Aprili, 2017,mwenendo wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya matumiziya kawaida kwa mafungu yote matatu ya Wizara hususanfedha za mishahara na chakula kwa wanajeshi katika kipindihicho ulikuwa ni wa kuridhisha. Fedha kwa ajili ya mishaharana marupurupu zilipokelewa kulingana na makisio ya bajeti.Kwa upande wa fedha za shughuli za maendeleo, fedhazilizopokelewa hazikuweza kukidhi mahitaji na hivyo kuathiriutekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja naulipaji wa madeni ya kimikataba.

MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YAMWAKA WA FEDHA 2016/17

Matumizi ya Shughuli za Kawaida

26. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2016/17,Wizara imefanikiwa kulipia mahitaji na huduma muhimukwa maafisa, askari, vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa nawatumishi wa umma. Aidha, kwa kutumia fedha hizimajukumu mbalimbali ya kiulinzi yaliyotekelezwa ni pamojana: kufanya mafunzo na mazoezi ya kijeshi, mafunzo yaMgambo, ushirikiano wa kiulinzi na kijeshi na nchi nyingine,

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

ushirikiano na Jumuiya za Kikanda na Kimataifa, ushirikianowa Jeshi na Mamlaka za Kiraia na Mafunzo ya JKT.

Mafunzo na Mazoezi ya Kijeshi

27. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17 Jeshi laUlinzi la Wananchi wa Tanzania, limeendelea kutoa mafunzona mazoezi kwa wanajeshi wake ili kujiimarisha kiulinzi. Jeshiletu lilifanikiwa kufanya mazoezi mbalimbali ya kimataifa naya ndani yafuatayo: “Ex - Eastern Accord” lililofanyika Tanzaniakuanzia tarehe 10 – 22 Julai, 2016 chini ya USARAF, “Ex -Amphibious Landing” lililofanyika Bagamoyo kuanzia tarehe19 Agosti, 2016 hadi tarehe 5 Septemba, 2016 ikiwa ni sehemuya maadhimisho ya sherehe za miaka 52 ya JWTZ, “Ex -Ushirikiano Imara” lililofanyika Mombasa nchini Kenya kuanziatarehe 17 - 19 Novemba, 2016. Aidha, Jeshi liliendelea kutoamafunzo kwa Maafisa na Askari kwenye vyuo, shule na vituombalimbali vya mafunzo kwa wanajeshi katika ngazimbalimbali ndani na nje ya nchi. Mazoezi na mafunzo hayayalilenga kuwajengea wanajeshi wetu uwezo, weledi naumahiri wa kiutendaji.

Mafunzo ya Mgambo

28. Mheshimiwa Spika, mafunzo ya Mgambo kwawananchi yameendelea kutolewa na Jeshi la Ulinzi laWananchi wa Tanzania. Katika kipindi cha mwaka 2016/17JWTZ kwa kushirikiana na vyombo vya Usalama limeendeshamafunzo katika ngazi mbalimbali ambapo jumla yawananchi 13,997 walifuzu. Hili ni ongezeko la wahitimu 7,241sawa na asilimia 51.7 ikilinganishwa na wananchi 6,756waliopata mafunzo hayo mwaka 2015/16. Naendelea kutoawito kwa Viongozi wa ngazi mbalimbali kuhamasishawananchi kushiriki katika mafunzo ya Mgambo. Kwamaagizo ya Mhe. Rais, jumla ya askari Mgambo 48 walioshirikikatika “Ex - Onesha Uwezo wa Medani” lililofanyika katikaMkoa wa Arusha na “Ex - Amphibious Landing” lililofanyikakatika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani waliandikishwakatika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.Huduma za Afya na Tiba

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

29. Mheshimiwa Spika, katika kipindi husika, Wizara yaUlinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imeendelea kutoa huduma zamatibabu kwa maafisa, askari, watumishi wa umma, familiazao na wananchi kwa ujumla. Huduma hizo zimekuwazikitolewa katika hospitali na vituo vya tiba vya Jeshi hapanchini. Katika kipindi hicho jumla ya wananchi 217,887walipata matibabu katika zahanati, vituo vya afya nahospitali za Jeshi. Aidha, Wizara imeendelea na maboreshoya huduma za matibabu kwa Wanajeshi na familia zao,ambapo mchakato wa kuanzisha Mfuko wa Bima ya Afyakwa ajili ya Wanajeshi ulioanza mwaka wa fedha 2015/16unaendelea kufanyiwa kazi. Hati Maalum (instrument) yamapendekezo ya uanzishwaji wa Mfuko huo na mabadilikoya kanuni namba 26 na 27 ya Juzuu ya Kwanza (I) Utawalavimeandaliwa ili viweze kuwasilishwa kwa Mhe. Rais na AmiriJeshi Mkuu kwa ajili ya kuridhiwa.

Ushirikiano wa Kiulinzi na Kijeshi na Nchi Nyingine

30. Mheshimiwa Spika, ushirikiano kati ya nchi yetu na nchinyingine katika nyanja za kijeshi ni suala muhimu katikamustakabali wa ulinzi na usalama. Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania limeendelea kuwa na ushirikiano mzuri namajeshi ya nchi nyingine hususan katika eneo linalohusu nafasiza mafunzo. Katika mwaka fedha 2016/17 Maafisa na Askarizaidi ya 350 wamekwenda kusoma kozi mbalimbali katikanchi rafiki zikiwemo Afrika Kusini, Burundi, Canada, China,Falme za Kiarabu, India, Kenya, Marekani, Misri, Morocco,Rwanda, Uganda, Uingereza, Ujerumani, Urusi na Zambia.Aidha, maafisa kutoka katika baadhi ya nchi hizi wapo hapanchini katika vyuo vyetu vya kijeshi kwa mafunzo. Vyuo hivyoni Chuo cha Maafisa Monduli, Chuo cha Ukamanda naUnadhimu (CSC) Arusha na Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC)Dar es Salaam.

Ushirikiano na Jumuiya za Kikanda na Kimataifa

31. Mheshimiwa Spika, Jeshi la Ulinzi la Wananchi waTanzania, limeendelea kushiriki katika operesheni za ulinzi waamani chini ya Umoja wa Nchi za Afrika (African Union) na

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

Umoja wa Mataifa. Nchi yetu imeendelea kuwa na vikosivyake Darfur nchini Sudan maeneo ya Khor-Abeche; ShangliTobayi na Menawash chini ya UNAMID. Aidha, Jeshi letulimeendelea kuwepo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasiaya Kongo (DRC) kama sehemu ya MONUSCO “ForceIntervention Brigade” (FIB). Pia, Kombania mbili za Polisi Jeshizipo nchini Lebanon kwa majukumu kama hayo. Vikosi namaafisa wa JWTZ waliopo kwenye Operesheni za Ulinzi waAmani katika maeneo hayo wote wanaendelea vizuri nautekelezaji wa majukumu yao. Vilevile, katika kudumishamahusiano na kuzuia matishio ya utekaji wa meli katikaBahari ya Hindi, tumeendelea kushirikiana na nchi mbalimbalizikiwemo, nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya yaMaendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, Afrika Kusini,Australia, Bangladesh, China, Hispania, India, Iran, Italia,Pakistan, Sierra Leone, Ufaransa, The Netherlands, Uingerezana Urusi.

Ushirikiano wa Jeshi na Mamlaka za Kiraia32. Mheshimiwa Spika, katika kudhihirisha utayari wa Jeshiletu kushikiri katika shughuli mbalimbali za kiraia na utoajiwa huduma na misaada wakati wowote inapohitajika,katika mwaka wa fedha 2016/17, Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania limeshiriki katika kutoa misaada kwenye maafaya tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera. Misaada hiyoimehusisha kurejesha miundombinu iliyoharibika, ujenzi wamajengo ya Taasisi za Serikali pamoja na kusaidia wananchi.Aidha, Wizara ilichangia shilingi 76,125,000.00 kwa waathirikawa tetemeko hilo. Nachukua fursa hii kuzipongeza Mamlakaza Kiraia na Taasisi zote kwa kutoa ushirikiano mzuri kwa Jeshiwakati wa kutekeleza majukumu hayo.

33. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na vitendo vyakihalifu, Wizara kupitia JWTZ, imeendelea kushirikiana naVyombo vingine vya Usalama na mataifa mengine katikakupambana na matishio ya kiusalama yakiwemo ugaidi,uharamia na biashara haramu ya dawa za kulevya. Aidha,JWTZ limeshiriki katika Operesheni Amboni 2 Mkoani Tangailiyoanza mwezi Mei, 2016 na kufungwa rasmi mwezi Desemba2016 ambapo wahalifu hao walidhibitiwa.

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

34. Mheshimiwa Spika, Wizara imekuwa mstari wa mbelekatika kutekeleza agizo la Mhe. Rais la kutatua tatizo lauhaba wa madawati katika shule za Serikali za msingi nasekondari. Aidha, kupitia Taasisi na Mashirika yake Wizarailipewa jukumu la kutengeneza madawati 60,000. Kazi hiyoilifanyika kwa ufanisi na weledi mkubwa. Katika zoezi hilo,JKT ilichangia madawati ya ziada 5,005. Wizara kupitia JWTZimesimamia ujenzi wa Shule ya Sekondari Ihumwa iliyopoDodoma na inaendelea kusimamia ujenzi wa Shule yaSekondari ya Ihungo iliyopo Kagera iliyoathirika na tetemekola ardhi mwaka 2016.

Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Vijana35. Mheshimiwa Spika, mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifayameendelea kutolewa kwa vijana wa kujitolea na wale waMujibu wa Sheria kwa lengo la kujenga uzalendo,ukakamavu, maadili mema, utaifa pamoja na kutoa stadiza kazi. Katika mwaka 2016/17, Jeshi la Kujenga Taifalimefanikiwa kuendesha mafunzo kwa vijana 14,748 wamujibu wa sheria (Compulsory National Service Training),ambapo kati yao wavulana ni 10,863 na wasichana 3,885waliohitimu Kidato cha Sita mwaka 2016. Idadi hiyo ni sawana asilimia 73.7 ya lengo la kuchukua vijana 20,000. Pia, JKTlimefanikiwa kuchukua vijana wapya wa kujitolea 9,848 kwaajili ya mafunzo ambapo kati yao, wavulana ni 7,154 nawasichana ni 2,694. Idadi hiyo ni sawa na asilimia 98.5 yalengo la kuchukua vijana 10,000.

36. Mheshimiwa Spika, wakati wa kuandikisha vijana wakujitolea kwa ajili ya kujiunga na mafunzo hayo, hutakiwakujaza na kusaini fomu maalum ya mkataba yenye mashartikwamba kijana awe tayari kurudi nyumbani mara amalizapomkataba wake. Pamoja na dhamira ya Serikali ya kutoaajira kwa vijana wanaohitimu mafunzo katika Jeshi laKujenga Taifa, sio vijana wote wanaohitimu mafunzo hayowanaweza kupata ajira katika vyombo vya ulinzi, usalamaau Taasisi zake. Hivyo, napenda kutoa rai kwa vijanawanaopata mafunzo ya JKT wazingatie maarifa na ujuziwanaoupata hususan wa stadi za kazi ili waweze kujiajiri nakuweza kujitegemea na hata kuajiri wengine.

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

37. Mheshimiwa Spika, Wizara, kupitia JKT imeendeleakutoa mchango katika kuwapatia vijana wa Kitanzania fursambalimbali za ajira kwa kujiajiri wenyewe au kuajiriwa katikaVyombo vya Ulinzi na Usalama, Taasisi za Umma na KampuniBinafsi. Katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais na Amiri JeshiMkuu kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama la kuajiri vijanawaliohitimu mafunzo ya JKT, jumla ya vijana 732 waOperesheni Miaka 50 ya Muungano na vijana idadi 6,072 waOperesheni Kikwete wamenufaika na utaratibu huo katikamwaka wa fedha 2016/17. Aidha, vijana 46 walioshiriki Zoezila Miaka 52 ya JWTZ waliandikishwa katika Jeshi la Ulinzi laWananchi wa Tanzania.

38. Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mafunzo yaujasiriamali na kuwajengea uwezo vijana wanaohitimumafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa, Baraza la Taifa laUwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kushirikiana na JKT,liliendesha mafunzo ya ujasiriamali na uendeshaji biasharakwa wakufunzi wa vijana wa JKT 134 kwa lengo lakuwafundisha vijana wa kujitolea ili waweze kupata stadizitakazowawezesha kujitegemea na kujiajiri wenyewe pindiwamalizapo Mkataba. Mafunzo hayo yaliendeshwa nawataalam wanaotambuliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO)katika Vituo vya 831KJ –Mgulani, 834KJ –Makutopora na 841KJ–Mafinga. Kwa kupitia Bunge lako Tukufu, napenda kutoawito kwa vijana hao kujiunga katika vikundi ili Baraza la Taifala Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi waweze kuwaunganishakatika mabenki na taasisi nyingine za kifedha kwa lengo lakupata mikopo yenye masharti nafuu.

Mapambano dhidi ya UKIMWI

39. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamiakikamilifu mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vyaUKIMWI (VVU) kwa Maafisa, Askari, Vijana, watumishi waumma na familia zao. Mapambano dhidi ya maambukizi yaVirusi vya UKIMWI yanaendelea kwenye Wizara na Taasisi zake.Baadhi ya mikakati ya mapambano hayo ni pamoja na kutoaelimu kwa wahusika wote kupitia mpango wa Elimu Rikakwa vikundi ili kujadili kwa undani namna ya kujikinga na

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

maambukizi ya UKIMWI na kupitia mpango wa Tohara kwavijana wa kiume kwenye kambi za JKT. Mkakati mwingine niupimaji wa hiari wa VVU kwa maafisa, askari, vijana nawatumishi wa Umma na utoaji wa dawa za kufubaisha VVUna lishe kwa wale waliokwishaathirika.

Utawala Bora

40. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa imeendelea kutekeleza dhana ya Utawala Bora katikamaeneo ya kazi kwa kushirikisha watumishi wake na wadauwengine wa Wizara. Wizara imeendelea kuwaelimisha nakuwakumbusha mara kwa mara Maafisa, Askari naWatumishi wa Umma kuhusu kuzingatia sheria na maadili yautendaji kazi, uzalendo na kutokujihusisha kwa namna yoyotekatika kutoa au kupokea rushwa. Aidha, vikao mbalimbalikwenye vikosi vya JWTZ kuanzia ngazi ya patuni hadi kikosihufanyika. Pia, viongozi wamekuwa wakifanya ziarambalimbali vikosini ambapo masuala mbalimbali ya kiserana kistratejia hutolewa ufafanuzi. Wizara imeendeleakushirikisha wadau wa ndani na nje ya Wizara katikakuboresha huduma kwa wananchi na wadau wote kwaujumla.

Utunzaji wa Mazingira

41. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mazingira,Wizara kupitia Jeshi imeendelea kushirikiana na jamiikutekeleza Sera ya Utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira kwakuhakikisha maeneo yake yanapandwa miti pamoja nakuchukua tahadhari ya moto. Katika mwaka wa fedha 2016/17 jumla ya miti 270,980 imepandwa kwenye vikosimbalimbali.

Matumizi ya Shughuli za Maendeleo

42. Mheshimiwa Spika, fedha zilizopokelewa hadi mweziMachi katika mwaka wa fedha 2016/17 kwa mafungu yotematatu, ilikuwa sawa na takriban asilimia 14.5 ya bajetiiliyoidhinishwa. Wizara imeweza kutekeleza miradi ifuatayo:

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

kukamilisha mradi wa ujenzi wa nyumba 6,064 awamu yakwanza kwa ajili ya makazi ya wanajeshi, kulipia sehemu yamadeni ya kimikataba; kukarabati majengo pamoja nakuboresha mazingira ya kufanyia kazi na makazi katika kambina vikosi vya JKT; ukarabati wa zana za ulinzi wa anga, ujenziwa Bwalo la Maafisa katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa AngaTanga; kuweka umeme katika baadhi ya minara yaMawasiliano Salama Jeshini katika mikoa ya Morogoro naDodoma. Aidha, kupitia ushirikiano baina ya Tanzania naChina ujenzi wa uwanja wa ndege vita Ngerengereumekamilika na kituo cha mafunzo maalum ya kijeshiMapinga, Bagamoyo ili kukabiliana na matishio mapya yakiusalama kinaendelea kujengwa.

Ujenzi wa nyumba, maghala na miundombinumbalimbali

43. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekelezamradi wa ujenzi wa nyumba 6,064 ambapo katika mwakawa fedha 2016/17 huduma za maji na umeme katikanyumba hizo zimepelekwa na hivyo kuwezesha kuanzakutumika kwa nyumba hizo katika kambi zilizopo mikoa yaArusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kagera, Kaskazini Pemba,Kigoma, Morogoro, Pwani na Tanga. Juhudi za kupata fedhaza kukamilisha ujenzi wa nyumba 3,936 ili kufikia lengo la ujenziwa nyumba 10,000 katika kambi zilizobaki zinaendelea. Vilevile, Wizara inaendelea na ujenzi wa maghala ya kuhifadhiamilipuko, ambapo maghala 12 yamejengwa Makambako(Njombe) na maghala 6 yamejengwa Dunga (Zanzibar).Aidha, katika kipindi hicho, upanuzi wa uwanja wa ndegevita Ngerengere ulikamilika na kuzinduliwa rasmi na Rais naAmiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufulitarehe 06 Machi, 2017. Mradi wa ujenzi wa kituo maalumcha mafunzo (Comprehensive Training Centre) naounaendelea vizuri na hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 30.

Ununuzi wa Zana na Vifaa vya Kijeshi

44. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuliongezeauwezo wa kiutendaji na kuimarisha mazingira ya kufanyia

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

kazi, Serikali imeendelea kulipatia Jeshi zana na vifaambalimbali. Katika mwaka wa fedha 2016/17, Jeshilimepokea zana na vifaa mbalimbali kwa ajili ya ulinzi wanchi kavu, anga na majini. Kupatikana kwa zana na vifaahivyo kumeongeza uwezo wa Jeshi kutekeleza majukumuyake ya msingi ya kiulinzi. Mpango wa ununuzi wa zana navifaa vya kisasa na bora pamoja na mafunzo ya namna yakutumia na kutunza zana na vifaa hivyo utakuwa endelevu.

Shirika la Uzalishaji Mali la JKT (SUMAJKT)

45. Mheshimiwa Spika, SUMAJKT limeendelea kutekelezashughuli zake katika misingi ya kibiashara kupitia KampuniTanzu, Idara na miradi yake ifuatayo: Kampuni ya Ulinzi(SUMAJKT Guard Ltd); Kampuni ya Ujenzi (National ServiceConstruction Department); Kampuni ya Ubia; Idara ya Kilimo,Uvuvi na Mifugo; Idara ya Viwanda na mradi wa matrekta.

46. Mheshimiwa Spika, SUMAJKT kupitia kampuni yake yaUlinzi SUMAJKT Guard Ltd, inaendesha shughuli za ulinzi katikaOfisi za Serikali, Mashirika ya Umma na sekta binafsi zikiwemoBenki na Migodi. Kwa mwaka 2016/17 imefanikiwa kuongezahuduma za ulinzi kwa wafuatao: Wakala wa SerikaliMtandao (eGA); Air Tanzania Corporation Limited (ATCL);Julius Nyerere International Airport (JNIA); Mamlaka yaChakula na Dawa (TFDA); Local Authority Pension Fund (LAPF);Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA); Medical StoresDepartment (MSD); Tanzania Insurance Regulatory Authority(TIRA); Wakala wa Nishati Vijijini (Rural Energy Agency);TANROADS; Procurement and Supplies Profession TechnicianBoard (PSPTB); Tanzania Forests Services (TFS); Bank of Africa(BOA); BOT-Dodoma; FINCA; DCB Bank; Dar es Salaam MaritineInstitute na KUDU Resources LTD.

47. Mheshimiwa Spika, Kampuni imetoa mchango kwaSerikali kwa kupunguza tatizo la ajira nchini kwa kuajiri vijana4,150 mwaka 2016/17 ikilinganishwa na vijana 2,777 mwaka2015/16. SUMAJKT Guard Ltd pia limeboresha mfumo wa ulinzikwa kutumia teknolojia ya kisasa (CCTV systems). Katikamwaka wa fedha 2017/18, Kampuni imekusudia kuimarisha

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

shughuli zake kwa kununua vitendea kazi vipya kama vile;vifaa vya kupambana na moto na uokoaji (Fire fighting andrescue equipment), vifaa vya kudhibiti vurugu (anti riotequipment), vifaa vya kuhakikisha usalama katika usafirishajifedha (cash in transit equipment) na gari la kusafirishiawagonjwa (Ambulance) ili kuongeza tija kwa shirika kwaujumla.

48. Mheshimiwa Spika, mradi wa matreka mpaka sasaumeshasambaza matrekta 2,222 yenye thamani ya shilingi87,878,744,388.00. Matrekta hayo yaliuzwa kwa mkopo nafedha taslimu. Mpaka kufika Machi, 2017 jumla ya shilingi46,513,791,226.72 zilikuwa zimekusanywa sawa na asilimia52.9. SUMAJKT imekuwa ikitumia vyombo vya habari kutoamatangazo kwa umma ya kuwataka wakopaji kulipamadeni yao ili mradi huu uwe endelevu. Hadi kufikia mweziMachi, 2017 matrekta mapya 80 na majembe 120yameshawasili kwa ajili ya kuwauzia wananchi.

49. Mheshimiwa Spika , SUMAJKT, kupitia Kampuni yaUjenzi (NSCD), inatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wamajengo na barabara kama ifuatavyo: ujenzi wa Ofisi zaChama cha Walimu Tanzania (CWT) katika mikoa 8 yaTanzania, ujenzi wa bandari kavu Vigwaza yenye hekta 125,na ujenzi wa miundombinu ya Kiwanda cha Sukari MkulaziMorogoro. Kampuni hiyo imeshiriki katika ujenzi wa uzio katikamabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaamambayo yalizinduliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania tarehe 15 Aprili, 2017.

50. Mheshimiwa Spika, Idara ya Kilimo, Ufugaji na Uvuviya Shirika inashughulika na uzalishaji wa mazao ya chakulana biashara, mbegu bora, ufugaji na uvuvi. Katika mwakawa fedha 2016/17 Shirika limelima mazao ya chakula nabiashara ekari 4,787 na jumla ya mifugo 7,982 kati yakeng’ombe ni 1,471, mbuzi 302, kuku 5,885, kondoo 240 nanguruwe 174. Aidha, Shirika lina boti tatu za uvuvi moja yatani 5 iko 836 KJ Mbweni JKT (Dar es Salaam) na boti mbiliziko 822 KJ Rwamkoma (Mara). Katika mwaka wa fedha2017/18, Shirika limepanga kujielekeza kwenye kilimo cha

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

umwagiliaji (Irrigation System) katika vikosi vya JKT ili kuongezauzalishaji na kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabianchi. Kupitia shughuli za kilimo cha mboga mboga, SUMAJKTlimeweza kuchangia kiasi cha shilingi 500 kwa siku kwa kilakijana anayehudhuria mafunzo ya JKT.

51. Mheshimiwa Spika, Shirika kupitia kampuni yake Tanzuya SUMA JKT Seed Co. Ltd limeendelea na uzalishaji wa mbegubora za mazao mbalimbali. Mbegu hizo huuzwa kwakampuni mbalimbali zinazojishughulisha na uuzaji wa mbegu.Hata hivyo, kampuni hii imekuwa ikikabiliwa na changamotoya kutolipwa kwa wakati kutoka kwa washitiri wake. Hadikufikia Mei, 2017 kampuni ilikuwa inadai jumla ya shilingi494,131,226.00. Kwa kupitia Bunge lako Tukufu, natoa rai kwakampuni zinazodaiwa kulipa madeni yao mapemaiwezekanavyo ili kuliwezesha SUMA JKT Seed Co. Ltd kufikiamalengo yake na kuendelea kuzalisha mbegu bora kwafaida ya Taifa letu.

52. Mheshimiwa Spika , katika masuala yaviwanda, SUMAJKT imeimarisha viwanda vyake vya ushonaji(Ruvu na Mgulani), utengenezaji wa samani (ChangómbeFurniture Factory) na mradi wa ubia wa kokoto (SUMAJKT -ANIT ASFALT CO. LTD). Aidha, Shirika lipo katika mchakatowa kuanzisha viwanda vifuatavyo: Kiwanda cha Maji yaKunywa ya Chupa; Kiwanda cha Mess tin; Masufuria na bidhaanyigine za Aluminium; Kiwanda cha Utengenezaji Bidhaa zaNgozi; Kiwanda cha Usindikaji Minofu ya Samaki na Kiwandacha Kusindika Minofu ya Nyama.

53. Mheshimiwa Spika, katika kuongeza ufanisi wautendaji wake wa kazi, SUMA JKT imeendelea kuhuishamuundo wake. Hii ni pamoja na kutenganisha shughuli zavikosi vya Jeshi la Kujenga Taifa na zile za SUMAJKT pamojanan a kwamba zinaweza kuwa katika sehemu moja. Aidha,ili kuongeza ufanisi na tija, mikataba ya utendaji imewekwabaina ya Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu wa Jeshi la KujengaTaifa.

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

Shirika la Mzinga

54. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2016/17Shirika la Mzinga limeendelea na utekelezaji wa majukumuyake ya msingi ya kufanya utafiti wa kuwezesha uzalishajiwa mazao ya kijeshi kwa kutumia malighafi zinazopatikanahapa nchini na kufanya matengenezo na ukarabati wa zanaza kijeshi. Pamoja na changamoto ya upatikanaji wa fedhaza maendeleo, Shirika limeendelea kupanua uzalishaji wamazao ya kijeshi kwa gharama nafuu ikilinganishwa nakuagiza bidhaa hizo kutoka nje ya nchi.

55. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza azma ya Serikaliya kuwa na uchumi wa viwanda, na pia kukabiliana nachangamoto za upatikaji wa malighafi za kistratejia na mtaji,Shirika limeendelea kuchukua hatua za kujiimarisha ikiwa nipamoja na kuongeza kasi ya kutekeleza Mpango Mkakatiwa Kipindi cha Miaka Mitano (2016/17 – 2020/21). MpangoMkakati huo unakusudia kupanua wigo wa uzalishaji wamazao ya kijeshi, kuongeza wigo wa shughuli za Shirika kwakuanzisha viwanda vipya vya kutengeneza baruti nakupanua mradi wa kutengeneza mashine ndogo ndogo kwaajili ya kuwawezesha wajasiriamali (wadogo na wa kati)kufanya uchakataji na kuongezea thamani ya mazao yakilimo na misitu. Vile vile, Shirika limekusudia kuboreshakarakana ya utengenezaji samani na kuiimarisha KampuniTanzu ya Mzinga Holding Co. Ltd kwa kuipatia mtaji navitendea kazi.

Shirika la Nyumbu

56. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wafedha 2016/17, pamoja na kutekeleza majukumu yake yamsingi ya utafiti na uhawilishaji wa teknolojia, Shirikalimechangia kupunguza gharama kwa JWTZ kwa kufanyamatengenezo ya zana za kijeshi kwa gharama nafuu ambazozingepaswa kusafirishwa kwenda nje kwa matengenezo nakuzalisha vipuli vya magari, mitambo na mashine mbalimbali.Pia, Shirika limekuwa likihusika na matayarisho ya zana,

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

mitambo na vitendea kazi kwa vikundi vinavyokwendakatika operesheni za ulinzi wa amani. Aidha, Shirika limeshirikikatika zoezi la kitaifa la utengenezaji wa madawati kwaajili ya shule za msingi na sekondari za Serikali. Katika hatuanyingine, Shirika limetengeza vitanda 652 kwa ajili ya maafisana askari waliohamia Dodoma.

57. Mheshimiwa Spika, Shirika pia lilifanikiwa kufanyaukarabati mdogo wa nyumba za makazi na mitambo yakarakana ya Shirika; kununua vifaa vya TEHAMA na kukarabatimfumo wa umeme kiwandani. Vile vile, Shirika limeendeleakutekeleza shughuli zake za kufanya utafiti katika teknolojiaya magari na mitambo ya kijeshi, kuimarisha na kuongezauwezo wa kuhawilisha teknolojia mbalimbali za utafiti nakukarabati miundombinu ya Shirika.

58. Mheshimiwa Spika, Shirika limeandaa Mpango waMaendeleo wa Miaka Kumi (Ten Years Development Plan2017/18 – 2026/27) wenye lengo la kuliimarisha na kulirejesheaShirika hadhi yake ili liweze kushiriki katika maendeleo yauchumi wa viwanda nchini. Rasimu ya kwanza ya mpangohuo imeandaliwa na kuwasilishwa kwa wadau mbalimbaliili kupata maoni na ushauri ili hatimaye kuweza kuwasilishwakwenye ngazi za maamuzi.

Mtandao wa Mawasiliano Salama Jeshini

59. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekelezaMradi wa Mawasiliano Salama Jeshini (Independent MobileSecured Communication Network) ambapo hadi kufikiaMachi, 2017 jumla ya minara 132 ilikuwa imesimikwa TanzaniaBara na Visiwani. Mawasiliano kupitia mtandao huoyanapatikana katika maeneo ya Zanzibar, Pwani, Dar esSalaam na baadhi ya maeneo ya Morogoro. Kazi yakuunganisha maeneo mengine ya nchi ikiwemo Mkoa waDodoma kwenye mtandao huo inaendelea. Aidha,uunganishaji wa mawasiliano haya salama katika vikosivyote Jeshini utakamilishwa mwaka wa fedha 2017/18.

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

Kudhibiti Uvamizi wa Maeneo ya Jeshi, Upimaji naUlipaji Fidia

60. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2016/17,Wizara haijaweza kupima na kulipa fidia wananchi kwamaeneo yaliyotwaliwa kwa matumizi ya Jeshi kamailivyopangwa kutokana na upatikanaji mdogo wa fedha zamaendeleo. Aidha, kwa lengo la kudhibiti uvamizi zaidikatika maeneo ya Jeshi, Wizara kupitia vikosi, vyuo na shuleza kijeshi, imeendelea kupanda miti na kuweka mabangokuzunguka maeneo hayo.

CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETIKATIKA MWAKA WA FEDHA 2016/17

61. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2016/17Wizara iliidhinishiwa jumla ya shilingi 248,000,000,000.00, kwaajili ya shughuli za maendeleo na hadi kufikia mwezi Machi,2017 kiasi kilichotolewa ni shilingi 35,900,000,000.00 sawa naasilimia 14.5 ya bajeti hiyo. Kutokana na kiwango cha fedhakilichopokelewa, Wizara imeweza kulipa sehemu ya madeniya kimkataba, na kuingiza huduma za maji na umeme katikabaadhi ya nyumba 6,064 pamoja na ukarabati wamiundombinu katika baadhi ya kambi.

62. Mheshimiwa Spika, mtiririko wa fedha kwa ajili yamatumizi mengineyo katika mwaka wa fedha 2016/17,umeleta changamoto katika kutekeleza kikamilifu mpangokazi, kulipia kwa wakati huduma na mahitaji muhimu kwawanajeshi, vijana wanaohudhuria mafunzo ya JKT nawatumishi wa Umma.

MPANGO NA MWELEKEO WA BAJETI KWA MWAKA WAFEDHA 2017/18

63. Mheshimiwa Spika, Mpango na Mwelekeo wa Bajetiwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa katika mwaka2017/18 unakusudia kuimarisha utendaji kazi na kuongezaufanisi wa Jeshi katika kutekeleza majukumu yake kulinganana Dira na Dhima ya Wizara, Ilani ya Uchaguzi ya Chama

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

cha Mapinduzi ya mwaka 2015, Mpango wa Pili wa Taifa waMaendeleo na Maelekezo ya Mhe. Rais wakati wa kuzinduaBunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20Novemba, 2015. Hivyo, Wizara itaendelea kutekelezamajukumu yake muhimu katika maeneo yafuatayo:

i. Kuliongezea uwezo Jeshi la Ulinzi la Wananchi waTanzania utendaji kivita kwa kulipatia vifaa na zana borapamoja na kutoa mafunzo stahiki kwa wanajeshi dhidi yaadui wa ndani na nje;

ii. Kuimarisha mazingira mazuri ya kufanyia kazi, makazina kuimarisha upatikanaji wa huduma, stahili na mahitaji yamsingi kwa wanajeshi na watumishi raia;

iii. Kuwapatia vijana wa Kitanzania mafunzo yauzalendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa na stadi za kazi;

iv. Utafiti na uhawilishaji wa teknolojia kwa madhumuniya kuzalisha bidhaa na huduma kwa ajili ya matumzi ya kijeshina kiraia na

v. Kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine duniani katikanyanja za kijeshi na kiulinzi.

SHUKRANI

64. Mheshimiwa Spika, kabla sijahitimisha Hotuba yangunaomba kutoa shukrani zangu za dhati kwa wale wotewalioniwezesha kufanikisha na kutekeleza jukumu lakuongoza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Aidha,napenda kutoa shukrani kwa wale wote waliotoa michangoiliyosaidia kufanikisha maandalizi ya makadirio ya matumiziya fedha ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwamwaka 2017/18.

65. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa shukrani za pekeekwa wafanyakazi wenzangu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa nikianzia na Katibu Mkuu Dkt. Florens M. Turuka,Naibu Katibu Mkuu Bi. Immaculate P. Ngwale, Mkuu wa

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance S. Mabeyo, Mnadhimu MkuuLuteni Jenerali James A. Mwakibolwa, Mkuu wa Jeshi laKujenga Taifa Meja Jenerali Michael J. Isamuhyo, Wakuu waKamandi, Wakuu wa Mashirika, Maafisa, Askari na Watumishiwa Umma. Aidha, naishukuru Kamati ya Wizara iliyoandaahotuba hii kwa ushirikiano walionipatia.

66. Mheshimiwa Spika, vile vile naomba niwashukuruwapiga kura wangu wa Jimbo la Kwahani kwa ushirikianowao walionipa katika mwaka 2016/17. Ni matumaini yangukuwa tutaendelea kushirikiana zaidi kwa manufaa ya Jimboletu na Taifa kwa ujumla.

67. Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Serikali naomba piakutoa shukrani zangu kwa Serikali za nchi mbalimbali,Mashirika na Wahisani kwa ushirikiano wao na Wizara yaUlinzi na JKT. Wahisani hao ni pamoja na Jamhuri ya Watuwa China, Ujerumani, Canada, Marekani, Ufaransa, India naUturuki. Aidha, tunazishukuru nchi rafiki kwa ushirikiano waokatika shughuli zetu mbalimbali za kiulinzi. Nchi hizo nipamoja na Afrika Kusini, Bangladesh, DRC, Ghana, Falme zaKiarabu, Indonesia, Misri, Nigeria, Uingereza, Urusina nchiwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya yaMaendeleo ya Kusini mwa Afrika. Nchi rafiki na wahisaniwamekuwa wakishirikiana na Jeshi katika mafunzo, mazoeziya kijeshi, na kuimarisha miundombinu ya mawasiliano,makazi na tiba.

MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA BAJETI YA MWAKA2017/18

Makadirio ya Mapato68. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa na Taasisi zake haina chanzo cha uhakika cha mapatokinachoweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukusanyajiwa maduhuli ikizingatiwa majukumu ya msingi ya Wizara hii.Chanzo kikuu cha mapato ni makusanyo ya mauzoyanayotokana na nyaraka za zabuni suala ambalo kwa sasalinashughulikiwa pia na Wakala wa Serikali wa Ununuzi naUgavi (GPSA) kwa kiasi kikubwa.

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

69. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18 Wizara yaUlinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inakadiria kukusanya jumla yashilingi 69,706,000.00 katika mchanganuo ufuatao:

Fungu 38 – NGOME shilingi15,601,000.00Fungu 39 – JKT shilingi54,003,000.00Fungu 57 – Wizara shilingi 102,000.00

Matumizi ya Kawaida na Maendeleo

70. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa inaomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi1,725,517,816,925.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida namatumizi ya maendeleo ili iweze kutekeleza majukumu yakekatika mwaka 2017/18. Kati ya fedha hizo shilingi1,506,517,816,925.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida nashilingi 219,000,000,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi yaMaendeleo. Mchanganuo kwa kila Fungu ni ufuatao:

Fungu 38 – NGOME

Matumizi ya Kawaida shilingi 1,205,244,289,563.00Matumizi ya Maendeleo shilingi 8,000,000,000.00Jumla shilingi 1,213,244,289,563.00

Fungu 39 – JKT

Matumizi ya Kawaida shilingi 283,362,530,783.00Matumizi ya Maendeleo shilingi 6,000,000,000.00Jumla shilingi 289,362,530,783.00

Fungu 57 – Wizara

Matumizi ya Kawaida shilingi 17,910,996,579.00Matumizi ya Maendeleo shilingi 205,000,000,000.00Jumla shilingi 222,910,996,579.00

2.0 MWISHO

71. Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa Hoja.

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

MWENYEKITI: Sasa namwita Mwenyekiti wa Kamati yaUlinzi na Usalama.

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB – MWENYEKITI WA KAMATIYA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA: MheshimiwaMwenyekiti, kabla sijaanza kusoma taarifa yangu ningependakuwapongeza kwa dhati kabisa Majenerali ambaowamepandishwa Vyeo na Mheshimiwa Rais kwa wakati huu.Tunampongeza sana Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuuwa Majeshi, tunampongeza pia Luteni Jenerali JamesMwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi natunampongeza Meja Jenerali Michael Isamuyo kuwa Mkuuwa Jeshi la Kujenga Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni ya99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016,naomba kuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bungeya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu utekelezaji waBajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwakawa fedha 2016/2017, pamoja na maoni ya Kamati kuhusumakadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwamwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kifungu chaSita 6(3) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu zaBunge, kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Wizara yaUlinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ni jukumu la Kamati ya Mamboya Nje, Ulinzi na Usalama. Aidha, Kifungu cha 7(1)chaNyongeza hiyo kimeainisha kuwa Kamati za Kudumu zaKisekta, pamoja na mambo mengine, zina jukumu lakushughulikia Bajeti za Wizara zinazosimamia. Kwa utaratibuwa kibajeti, Wizara hii inahusisha Mafungu matatu (3): Fungu38- Ngome, Fungu 39- Jeshi la Kujenga Taifa na Fungu 57-Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo yaawali, sasa naomba kubainisha mpangilio wa Taarifaninayoiwasilisha kwa kutaja mambo makuu manne. Mambohayo ni:-

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

(i) Matokeo ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo;

(ii) Mapitio ya taarifa ya utekelezaji wa mpangowa bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/2017;

(iii) Uchambuzi wa makadirio ya mapato namatumizi ya Wizara hii kwa mwaka wa fedha 2017/2018; na

(iv) Maoni na ushauri wa Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia masharti yaKanuni ya Kifungu cha 98(1), Kamati ilitembelea na kukaguamiradi ya maendeleo iliyo chini ya Wizara tatu inazozisimamiaikiwemo Wizara hii, kuanzia tarehe 22 hadi 24 Machi, 2017.Tulitembelea Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifaambayo ilikuwa na Miradi kumi na tatu (13) ya Maendeleoiliyotengewa fedha katika Mwaka wa Fedha 2016/2017,Kamati ilitembelea na kukagua mradi mmoja tu chini yaWizara hii kutokana na ufinyu wa muda uliotengwa kwa ajiliya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi yamaendeleo inayotekelezwa na Wizara tatu zinazosimamiwana Kamati hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi uliokaguliwa ni Mradinamba 6103 uliojulikana kama ‘Defence Scheme’ nakutekelezwa chini ya Kifungu namba 2002 – ‘Military Researchand Development’ chini ya Fungu 57. Matokeo ya Ukaguzihuo yanadhihirisha mambo makuu mawili ambayo ni kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, upatikanaji wa fedha kwakiasi kidogo. Upatikanaji wa fedha kwa kiasi kidogoikilinganishwa na Bajeti iliyoidhinishwa ni jambo lililobainikakatika utekelezaji wa mradi huu. Kwa Mwaka wa Fedhaunaoisha, jumla ya bilioni 151.1 zilitengwa kwa kuidhinishwana Bunge lako kwa ajili ya mradi huu. Hata hivyo, Kamatiilielezwa kuwa hadi kufikia mwezi Machi, 2017 ikiwa ni roboya tatu ya mwaka wa fedha, Wizara ilikuwa imepokea kiasicha shilingi bilioni 30 tu ambazo ni sawa na asilimia 20 tu yafedha zilizotengwa.

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kuwa asilimia 80ya bajeti iliyotengwa kwa ajili ya mradi huu haikuwaimepokelewa kutoka Hazina jambo ambalo limeathiri ratibaya utekelezaji kwa kiwango kikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili ni kutoanzishwa kwamaabara za utafiti. Vilevile katika ziara hiyo Kamati ilibainikuwa Shirika la Nyumbu limeshindwa kuanzisha maabarahizo licha ya kuwa utafiti ni shughuli zake za msingi. Hali hiiimetokana na kutopatikana kwa fedha za kutekelezashughuli hiyo kwa kipindi cha miaka saba mfululizo. Shirikala Nyumbu halikupelekewa fedha zozote kwa ajili yamaendeleo tangu mwaka 1996 hadi 2003. Athari yachangamoto hiyo, ni upungufu na uchakavu wamiundombinu ya kiteknolojia na kushindikana kuanzishwakwa maabara za utafiti katika Shirika hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni ya jumla kuhusuutekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha2016/2017; Kutokana na matokeo ya ziara ya ukaguzi wamradi uliotekelezwa chini ya Fungu 57, Kamati inatoa maonikwamba mwenendo wa upatikanaji wa fedha kwa ajili yamiradi ya maendeleo ni jambo linalohitaji kuboreshwa zaidi.Kwa kuwa, utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye tijakwa Taifa ni jambo muhimu ni vema Serikali ikaweka uzitounaostahili dhidi ya miradi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Serikaliimeendelea kuimarisha ulinzi wa Taifa letu, ni vema miradiyote inayohusu sekta ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa iendeleekupewa kipaumbele kibajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa taarifa yautekelezaji wa mpango wa bajeti na uzingatiaji wa maoniya Kamati kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Uchambuzi waKamati katika mapitio ya utekelezaji wa mpango wa Bajetiya Wizara kwa mwaka wa fedha 2016/2017, ulijielekeza katikamakusanyo ya mapato ikilinganishwa na lengo la makusanyopamoja na upatikanaji wa fedha za matumizi kwa ajili yashughuli zilizopangwa kutekelezwa, hususan fedha za

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

matumizi mengineyo (OC) na fedha za miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Kamati ilizingatiataarifa mbalimbali zilizowasilishwa mbele ya Kamati kwakipindi cha Oktoba, 2016 na Januari 2017 na mahojianoyaliyochangia upatikanaji wa taarifa muhimu na za ziadawakati wa vikao vya Kamati. Naomba kuwasil ishauchambuzi huo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka wa fedha 2016/2017,Wizara il ikadiria kukusanya mapato ya jumla yash.68,406,000.00 kutokana na mauzo ya nyaraka za zabuni.Kamati ilijulishwa kuwa hadi mwezi Machi, 2017, Wizarailifanikiwa kukusanya jumla ya sh.30,169,863.80 sawa naasilimia 44.1 ya lengo. Uchambuzi wa Kamati umebainishamchanganuo wa makusanyo kama inavyoonekana katikaJedwali Namba Moja (1).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchanganuo huoKamati imebaini yafuatayo:-

(i) Makusanyo katika Fungu 38 – Ngome,yalikusudiwa kuchangia katika lengo la Wizara kwa asilimia22.8 lakini taarifa ya makusanyo ilionesha kuwa Fungu 38limechangia kwa asilimia 45.1 ya kiasi kilichokusanywa.

(ii) Makusanyo ya Fungu 39 –JKT, yalikusudiwakuchangia katika lengo la Wizara kwa asilimia 76, lakini halihalisi imeonesha kuwa makusanyo ya JKT yamekuwa ni asimia54.9 ya makusanyo ya kiasi kilichokusanywa.

(iii) Makusanyo ya Fungu 57 – Wizara, yalikusudiwakuchangia katika lengo la makusanyo kwa asilimia 1.2, lakinitaarifa ya Wizara imeonesha kuwa hakuna kiasikilichokusanywa kwenye Fungu hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ulinganisho huo wa malengoya makusanyo kwa kila Fungu ikilinganishwa na kiasikil ichokusanywa na kila Fungu, ulisababisha Kamatikuchambua zaidi ili kupata sababu za mwenendo huo wa

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

ufikiaji malengo. Kubwa lililobainika ni kuwa chanzo kikuucha mapato kwa mafungu yote ya Wizara hii ni mauzo yanyaraka za zabuni jambo linalosababisha makusanyo kuwachini na yasiyo ya uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upatikanaji wa fedhakutoka Hazina; Pamoja na Bunge lako Tukufu kuendeleakusisitiza kila mwaka kuhusu umuhimu wa Serikali kutoa fedhazilizoidhinishwa na Bunge kwa ajili ya matumizi ya Serikali,upatikanaji wa fedha hizo umeendelea kuwa changamotokwa Wizara nyingi. Kwa kuzingatia hilo, Kamati ilitakakujiridhisha kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ulinzina Jeshi la Kujenga Taifa kwa kufanya ulinganisho wa fedhazilizoidhinishwa kwa ajili ya matumizi yote ya Wizara kwamwaka wa fedha 2016/2017 na kiasi kilichopatikana hadikufikia mwezi Machi, 2017. Uchambuzi huo ulibainishayafuatayo:-

(i) Hadi kufikia mwezi Machi, 2017, Wizara ilikuwaimepokea asilimia 69.6 ya bajeti ya matumizi ya kawaidailiyoidhinishwa na asilimia 14.5 ya bajeti ya maendeleo.

(ii) Kiasi kilichopokelewa na Wizara kwa ajili yamiradi ya maendeleo ni pungufu kwa asil imia 10.25ikilinganishwa na Sh.40,000,000,000/= zilizotolewa kwamwaka wa fedha 2015/2016.

(iii) Pesa kwa ajili ya bajeti ya matumizi yauendeshaji (OC) ilipokelewa kwa asilimia 69.6 ikiwa niongezeko la 6%, ikilinganishwa na fedha za Matumizi yaUendeshaji zilizotolewa katika kipindi cha 2015/2016.

(iv) Kati ya Sh.35,900,000,000 zilizopokelewa kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendelo, asilimia 94 ya fedhahizo ni kwa ajili ya Fungu 57- Wizara, asilimia sita tu kwa ajiliya Fungu 38 na Fungu 39 ikiwa ni asilimia tatu ya fedha hizokwa kila Fungu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na uchambuzihuo, Kamati ina maoni kuwa mwenendo huu wa upatikanaji

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

wa fedha za maendeleo kwa Fungu 38 -Ngome na Fungu39-Jeshi la Kujenga Taifa, siyo mzuri na unaathiri ratiba nampango wa utekelezaji wa miradi muhimu ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilipopitia mpangona makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa kwa mwaka 2016/2017, ilitoa ushauri katika maeneokumi na nne (14) yanayohusu utekelezaji wa majukumu yaWizara hii. Naomba kulijulisha Bunge hili kuwa ushaurikuhusiana na baadhi ya maeneo umezingatiwa kikamilifuna unaendelea kuzingatiwa na ushauri mwinginehaujazingatiwa kabisa kama inavyoonekana katikaKiambatisho Namba Moja (1).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano wa ushauriuliozingatiwa kikamilifu ni kuhusu kurasimishwa kisheria kwamaeneo yote yaliyotolewa na Mamlaka za Mikoa kwa ajiliya matumizi ya Jeshi. Taarifa ya Utekelezaji imeonesha kuwaushauri huu umeanza kutekelezwa kwa kurasimishwamaeneo ya Jeshi Mkoani Singida, Korutambe - Tarime MkoaniMara, yaliyotolewa na Mamlaka ya Mikoa hiyo kwa ajili yamatumizi ya Jeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano wa pili ni utekelezajiwa ushauri kuhusu kulipa madeni yote ya Wizarayaliyohakikiwa. Naomba kutoa taarifa kuwa Serikaliimejiwekea utaratibu wa kutenga fedha kila mwaka kwaajili ya kulipa madeni hayo kwa awamu. Kamati ilijulishwakuwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017, jumla yaSh.151,146,888,000.00 zilitengwa kwa ajili ya kulipa madeniya kimikataba. Hata hivyo, Mheshimiwa Waziri wa Ulinzialiijulisha Kamati kuwa hadi kufikia mwezi Machi, 2017 nishilingi bilioni 30 tu zilikuwa zimetolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano huu wa ushauriambao haukuzingatiwa kikamilifu ni kuhusu Serikali kutoashilingi bilioni 35 kwa ajili ya kulipa fidia kwa maeneoyaliyochukuliwa na Jeshi. Sababu zilizotolewa ni ufinyu wabajeti na kutokutolewa kwa fedha iliyoidhinishwa. Taarifa yaWizara inaonesha kuwa katika Mwaka wa Fedha 2016/2017,

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

Wizara iliidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 27 kwa ajili yakupima na kulipa fidia wananchi ambao maeneo yaoyalitwaliwa kwa matumizi ya Jeshi. Hadi kufikia mwezi Machi,2017 fedha hizo zilikuwa hazijatolewa kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia madarakaya Bunge yaliyoainishwa katika Ibara ya 63(2) ya Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Kamatiinaendelea kusisitiza kuwa ushauri ambao haujazingatiwaunapaswa kufanyiwa kazi na kuwa sehemu ya ratiba yautekelezaji wa majukumu ya Wizara hii kwa mwaka wa fedha2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa mpangona makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha2017/2018. Ili kujiridhisha na makadirio ya mapato na matumiziya Wizara hii, Kamati ilirejea Hati Idhini ya Mgawanyo waMajukumu ya Wizara za Serikali, Toleo la tarehe 22 Aprili, 2016na kuoanisha na malengo ya Bajeti ya Wizara hii kwa mwakawa fedha 2017/2018. Kamati ilibaini kuwa katika kutekelezamajukumu ya msingi manne yaliyoainishwa katika Hati Idhini,Wizara inalenga kuimarisha utendaji kazi na ufanisi katikautekelezaji wa majukumu yake kulingana na Dira na Dhimakwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo hili limepangwakufikiwa kwa kutekeleza majukumu saba ikiwemo kuendezautafiti na teknolojia kwa madhumuni ya kuzalisha bidhaana huduma kwa ajili ya matumizi muhimu pamoja na kupimaardhi inayotumika kwa shughuli za Jeshi na kulipa fidia katikamaeneo yaliyotwaliwa kwa ajili ya matumizi ya kijeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi umeoneshakuwa majukumu yaliyopangwa yatawezesha ufikiaji walengo kwa ufanisi endapo tu Serikali itazingatia mpango namakadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa kutoafedha zitakazoidhinishwa na Bunge kwa ukamilifu na kwawakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uchambuzi wa

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

Makadirio ya Mapato kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018,Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mafungu yotematatu inategemea kukusanya mapato ya jumla yaSh.69,706,000.00. Mchanganuo wa lengo hilo la makusanyounaonekana katika Jedwali Namba Mbili (2) la Taarifa hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika uchambuzi huo,Kamati imebaini yafuatayo:-

(i) Lengo la makusanyo kwa Mafungu yote yaWizara limeongezeka kwa asilimia 1.9 ikilinganishwa na lengola makusanyo kwa mwaka wa fedha unaoisha.

(ii) Mwaka wa fedha 2016/2017, lengo lilifikiwakwa asilimia 44.1 hadi robo ya tatu ya mwaka wa fedha,lengo la makusanyo kwa Mwaka 2017/2018 limeongezekakidogo badala ya kupungua.

(iii) Fungu 38 – Ngome linategemewa kwa kiasicha asilimia 22.38 na mwaka 2016/2017 linategemewa kuwaasilimia 22.8.

(iv) Fungu 39 – JKT linategemewa kuwa katikamakusanyo kwa kiasi cha 77.47% kwa mwaka 2016/2017linategemewa kuwa asilimia 76.

(v) Fungu 57 linategemewa kuwa na makusanyokwa kiasi cha asilimia 0.015 wakati mwaka 2016/2017linategemewa kuwa na asilimia 1.2.

(vi) Makadirio ya mapato kwa Fungu 57yamekuwa yakipungua kila mwaka na makusanyo yakeyameendelea kuwa siyo ya kuridhisha. Kwa mfano, mwaka2015/2016, Wizara (Fungu 57) ilikusanya Sh.100,000.00 sawana asilimia 0.9 tu kati ya Sh.11,002,000.00 zilizokadiriwakukusanywa. Kwa kuoanisha na mwenendo wa upatikanajiwa fedha kwa Mwaka 2016/2017, inawezekana kabisa hadikufikia mwezi Machi, 2018, Wizara hii ikawa imekusanya kiasicha Sh.30,740,346.00.

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maelezo hayo, ni maoniya Kamati kuwa lengo la ukusanyaji linapaswa kuzingatiamambo mengi ili kuwa na uhalisia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa makadirio yamatumizi. Maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi kwenyeKamati yalionesha kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018,Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifainayoombwa kwa mafungu yote matatu niSh.1,725,517,816,925.00. Kati ya fedha hizo,Sh.1,506,517,816,925.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaidana Sh.219,000,000,000.00 ni kwa ajili ya kugharamia miradi yaMaendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ya Wizara hii kwamwaka wa fedha 2017/2018 imepungua kwaSh.11,012,596,075 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wafedha 2016/2017. Hata hivyo, tofauti hiyo ni pungufu kwaasilimia 0.6.

Pili; Wakati bajeti kuu ya Mwaka wa Fedha 2017/2018,kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Fedhatarehe 28 Machi, 2017, imeongezeka kwa asilimia 6.64 bajetiya Wizara hii imepungua kwa asilimia 0.6.

Tatu; Asilimia 12.7 ya bajeti ya Wizara hii kwa mwakawa fedha 2017/2018 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo naasilimia 87.3 ya bajeti hii ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Nne; Wakati asilimia 38 ya bajeti kuu kwa mwaka2017/2018 ni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo,asilimia 12.7 ya bajeti ya Wizara hii ni kwa ajili ya kugharamiamiradi ya maendeleo.

Tano; Wakati mwaka 2016/2017 asilimia 3.2 ya bajetiya Wizara hii ilikuwa ni kwa ajili ya uendeshaji, mwaka wa2017/2018 asilimia tatu ya bajeti ya Wizara hii ni kwa ajilikugharamia uendeshaji wa shughuli za Wizara.

Sita; Wakati jukumu la msingi la Wizara hii kwa mujibu

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

wa Hati Idhini ni kusimamia Sera zinazohusiana na Ulinzi naJeshi la Kujenga Taifa, hakuna kasma zilizotengwa maalumkwa ajili ya utayarishaji na ukamilishaji wa Sera ya Ulinzi,Marekebisho ya Sheria ya Ulinzi wa Taifa wala Marekebishoya Sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa; na

Saba; Licha ya azma ya Serikali ya kuongeza vijanawanaokwenda mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria, Kasmazinazohusika na mafunzo hayo kwa Fungu 39 hazijaongezewafedha ikilinganishwa na mwaka 2017. Fungu 39 – JKT,limetengewa Sh.26,100,000,000 kwa mwaka wa fedha wa2016/2017 na mwaka 2017/2018 limeombewaSh.12,500,000,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maelezo hayoyametokana na uchambuzi wa Kamati baada ya kupitiarandama za Mafungu matatu ya Wizara hii na kwa kuzingatiamasharti ya Kanuni ya Kifungu cha 98(2) ya Kanuni za Kudumuza Bunge. Naliomba Bunge lako Tukufu kupokea maelezohayo yatakayosaidia majadiliano kuhusu hoja iliyowasilishwana Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa mapema hii leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni na ushauri waKamati; kwa kuzingatia taarifa ya utekelezaji wa maoni yaKamati kwa mwaka wa fedha 2016/2017, sambamba namajadiliano ya kina kuhusu makadirio ya mapato, mipangona bajeti ya Wizara ya Ulinzi na JKT kwa mwaka 2017/2018,ikilinganishwa na Dhima ya Wizara ya kulinda uhuru, maslahina mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamatiinatoa ushauri kwa kila Fungu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fungu Namba 38 - Ngomeambalo linahusika na mambo ya msingi kwa uwepo wa nchiyetu na kwa kuwa kasma za matumizi muhimu zipo katikaFungu hili, Kamati inashauri kama ifuatavyo:-

Moja, kwa kuwa mpaka kufikia mwezi Machi, 2017Serikali ilitoa asilimia 14.5 tu ya fedha zote za maendeleozilizoidhinishwa na Bunge, jambo lililoathiri utekelezaji wa

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

miradi ya maendeleo, Fungu 38 - Ngome lipatiwe fedha zotezilizopaswa kutolewa kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Pili, Serikali itafute uwezekano wa kutoa shilingi bilioni27 zilizotengwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili yakulipia fidia kwa maeneo yaliyochukuliwa na Jeshi kabla yatarehe 30 Juni, 2017 ili kuwezesha wananchi ambao maeneoyao yametwaliwa, kulipwa fidia. (Makofi)

Tatu, Serikali ione umuhimu wa kuliwezesha Jeshikumiliki ardhi kisheria kwa kufanya tathmini na upimaji wamaeneo ya zamani na maeneo mapya yaliyotwaliwa naJeshi na kuyapatia Hatimiliki. Umuhimu huu utaonekanaendapo Serikali itatoa Sh.27,700,000,000.00 zilizotengwa katikamwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya kutekeleza shughulihiyo, lakini hadi hadi kufikia Machi, 2017 hakukuwa na fedhazozote zilizokuwa zimetolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fungu 39 - JKT. Kwanza;Serikali ikamilishe mchakato wa kufanya marekebisho katikaSheria ya Jeshi la Kujenga Taifa, Sura Namba193 The NationalService Act, Cap. 193 ili iweze kuendana na wakati, mifumoya utawala na mahitaji ya sasa ya kisheria katika Sekta yaUlinzi.

Pili; Kamati inaendelea kuishauri Serikali ione umuhimuwa suala la fidia kwa vijana wanaopata mafunzo ya JKTkutekelezwa chini ya Sheria ya JKT ya mwaka 1964 ili kuondoachangamoto zilizopo kwenye malipo ya fidia kwa vijana hao.

Tatu; Fungu 39 liwezeshwe kibajeti ili kumudu mahitajiya kuwezesha vijana wengi zaidi kujiunga na Jeshi la KujengaTaifa.

Nne; Serikali itoe kipaumbele kwa vijana waliopitiamafunzo ya JKT wakati wa kuajiri vijana kwa ajili ya shughuliza ulinzi katika shirika la SUMA JKT.

Tano; Serikali ilipe madeni ya Shirika la SUMA Guard ililiendelee kujiendesha kwa ufanisi. Aidha, Serikali ione

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

umuhimu wa kuweka utaratibu kwa Taasisi za Serikali wakutumia huduma za ulinzi za SUMA Guard badala ya kuajirimakampuni binafsi.

Sita; Serikali itoe fedha zote zilizotengwa katikamwaka wa fedha 2016/2017, kwa ajili ya ujenzi wa ukarabatiwa miundombinu katika makambi mapya kwa ajili yamafunzo na makazi ya vijana wanaotakiwa kujiunga kwamujibu wa sheria. Aidha, kwa kuwa bajeti ya maendeleo yaJeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018imepunguzwa ikilinganishwa na bajeti hiyo kwa mwaka wafedha 2016/2017. Kamati inaishauri Serikali kuongeza bajetihiyo ili Jeshi la Kujenga Taifa liweze kuchukua vijana wengiwanaohitimu kidato cha sita na kuwapatia mafunzo ya JKTkama sheria inavyotaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Hazina ioneumuhimu wa kuongeza kasi ya kulipa madeni yote ya Wizarayaliyohakikiwa yenye jumla ya Sh.212,375,287,250 ili kuzuiamgogoro unaoweza kutokea kati ya Wizara na wazabuniwaliotoa huduma mbalimbali. Hadi kufikia mwezi Februarizilikuwa zimetolewa Sh.31,628,607,462.47 zilikuwa zimetolewana Hazina sawa na asilimia 18.8 tu ya madeni yote.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itoe shil ingi10,500,000,000 kwa ajili ya kulipa madeni ya kimikataba kablaya mwaka wa fedha 2016/2017 kwisha. Hii itaepushaongezeko la deni linalotokana na ongezeko la riba.

Tatu, Ili kutatua tatizo la uchakavu na upungufu wamiundombinu kwa mashirika ya Nyumbu na Mzinga kwalengo la kuwezesha ufanisi zaidi katika shughuli ya utafiti nauhawilishaji wa teknolojia pamoja na uzalishaji wa bidhaakwa matumizi muhimu, Serikali itenge bajeti ya kutosha kwaajili ya ukarabati wa ujenzi huo.

Nne, Shirika la Nyumbu kimsingi lipo chini ya Wizaraya Ulinzi na JKT na kwa wakati huo huo linamilikiwa kisheriana Msajili wa Hazina. Serikali iangalie uwezekano wa kulifanya

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

Shirika hilo kumilikiwa kisheria na kuwajibika chini ya Mamlakamoja ili kuondoa mkanganyiko uliopo.

Tano, katika kutekeleza majukumu ya msingi yaWizara hii, Sera ya Ulinzi na Usalama (The National DefencePolicy) ni jambo la msingi. Serikali ikamilishe mchakato wakuandaa Sera hiyo muhimu kwa Taifa.

Mwisho, Serikali ikamilishe mchakato wa kufanyamarekebisho katika Sheria ya Ulinzi wa Taifa, Sura 198 (TheNational Defence Act, Cap. 192) ili iweze kuendana nawakati, mifumo ya utawala na mahitaji ya sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho, napendakukushukuru kwa kunipa nafasi hii kwa ajili ya kuwasilishataarifa hii. Napenda kuwashukuru Wajumbe wa Kamati yaMambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ambao maoni yao, ushauriwao na ushirikiano wao, umewezesha kukamilisha kwa taarifahii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Wajumbe waKamati hii napenda kutumia fursa hii kumshukuru Waziri waUlinzi na JKT, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi kwa ushirikiano wakemzuri katika kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yaKikanuni ya Kamati. Waziri huyu ni mfano kila Kamatiilipokuwa inakwenda Waziri anakuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, namshukuru KatibuMkuu Ndugu Florence Turuka, Mkuu wa Majeshi JeneraliVenance Mabeyo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni JeneraliJames Mwakibolwa, Mkuu wa JKT Meja Jenerali MichaelIsamuyo pamoja na Watendaji wote wa Wizara kwaushirikiano wao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, tunapendakumshukuru Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah kwakuratibu vema shughuli za Kamati za Bunge. Aidha,nawashukuru Mkurugenzi wa Kamati Ndugu AthumaniHussein, Mkurugenzi Msaidizi Bi. Angelina Sanga na Makatibuwa Kamati hii Ndugu Ramadhan Abdallah na Bi. Grace Bidya

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

wakisaidiwa na Bi. Rehema Kimbe kwa kuratibu vema,shughuli za Kamati na kuhakikisha Taarifa hii inakamilika kwawakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo,sasa naliomba Bunge lako Tukufu likubali kuidhinishamakadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ulinzi na JKTkwa mwaka wa fedha 2017/2018 kama yalivyowasilishwa namtoa hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja nanaomba kuwasilisha. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante.

TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YANJE, ULINZI NA USALAMA KUHUSU UTEKELEZAJI WA BAJETI YAWIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA MWAKAWA FEDHA 2016/2017; PAMOJA NA MAONI YA KAMATI KUHUSUMAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA HIYO KWAMWAKA WA FEDHA 2017/2018 KAMA ILIVYOWASILISHWAMEZANI

3.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99 (9) ya Kanuniza Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016, naombakuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mamboya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu utekelezaji wa Bajeti yaWizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka waFedha 2016/2017, pamoja na Maoni ya Kamati kuhusuMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwakawa Fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Kifungu cha 6 (3) chaNyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge,kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Ulinzi naJeshi la Kujenga Taifa ni jukumu la Kamati ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama. Aidha, Kifungu cha 7 (1) cha Nyongeza yaNane ya Kanuni za Kudumu za Bunge kimeainisha kuwa

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

Kamati za Kudumu za Kisekta, pamoja na mambo mengine,zina jukumu la kushughulikia Bajeti ya Wizara inazozisimamia.Kwa utaratibu wa kibajeti, Wizara hii inahusisha Mafungumatatu (3): Fungu 38- Ngome, Fungu 39- Jeshi la Kujenga Taifana Fungu 57- Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Spika, Baada ya Maelezo hayo ya awali, sasanaomba kubainisha mpangilio wa Taarifa ninayoiwasilishakwa kutaja mambo makuu manne (4) katika Taarifa hii.Mambo hayo ni:-

(i) Matokeo ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo;(ii) Mapitio ya Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajetikwa Mwaka wa Fedha 2016/2017;(iii) Uchambuzi wa Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara hii kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018; na(iv) Maoni na Ushauri wa Kamati.

4.0 MATOKEO YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEOILIYOTENGEWA FEDHA KWA MWAKA 2016/2017

4.1 Maelezo kuhusu Miradi ya Maendeleoiliyokaguliwa

Mheshimiwa Spika, Kwa kuzingatia masharti ya Kanuni ya98 (1), Kamati ilitembelea na kukagua miradi ya maendeleoiliyo chini ya Wizara tatu inazozisimamia ikiwemo Wizara hii,kuanzia tarehe 22 hadi 24 Machi, 2017. Pamoja na kuwaWizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ilikuwa na Miradikumi na tatu (13) ya Maendeleo iliyotengewa fedha katikaMwaka wa Fedha 2016/2017, Kamati ilitembelea na kukaguamradi mmoja tu chini ya Wizara hii kutokana na ufinyu wamuda uliotengwa kwa ajili ya kutembelea na kukaguautekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa naWizara tatu zinazosimamiwa na Kamati hii.

Mradi uliokaguliwa ni Mradi namba 6103 uliojulikana kama‘Defence Scheme’ na kutekelezwa chini ya Kifungu namba2002 – ‘Military Research and Development’ cha Fungu 57.

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

4.2 Matokeo ya Ukaguzi wa Mradi Namba 6103

Mheshimiwa Spika, Matokeo ya ukaguzi wa Mradi huuyanadhihirisha mambo makuu mawili ambayo ni:-

4.2.1 Upatikanaji wa fedha kwa kiasi kidogo

Mheshimiwa Spika, Upatikanaji wa fedha kwa kiasi kidogoikilinganishwa na Bajeti iliyoidhinishwa ni jambo lililobainikakatika utekelezaji wa Mradi huu. Kwa Mwaka wa Fedhaunaoisha, jumla ya Shilingi Bilioni 151.1 zilitengwa nakuidhinishwa na Bunge lako tukufu kwa ajili ya Mradi huu.Hata hivyo, Kamati ilielezwa kuwa hadi kufikia Mwezi Machi,2017 ikiwa ni robo ya tatu ya Mwaka wa Fedha, Wizara ilikuwaimepokea kiasi cha Shilingi Bilioni 30 sawa na asilimia 20 tuya fedha zilizotengwa. Ni dhahiri kuwa asilimia 80 ya bajetiiliyotengwa kwa ajili ya Mradi huu haikuwa imepokelewakutoka Hazina jambo ambalo limeathiri ratiba ya utekelezajikwa kiwango kikubwa.

4.2.2 Kutoanzishwa kwa maabara za Utafiti

Mheshimiwa Spika, Vilevile, katika ziara hiyo Kamati ilibainikuwa Shirika la Nyumbu limeshindwa kuanzisha maabarahizo licha ya kuwa utafiti ni shughuli zake za msingi. Hali hiiimetokana na kutopatikana kwa fedha za kutekelezashughuli hiyo kwa kipindi cha miaka 7 mfululizo. Shirika laNyumbu halikupelekewa fedha zozote kwa aji l i yamaendeleo tangu mwaka 1996 hadi 2003. Athari yachangamoto hiyo, ni upungufu na uchakavu wamiundombinu ya kiteknolojia na kushindikana kuanzishwakwa maabara za Utafiti katika Shirika hili.

4.3 Maoni ya Jumla kuhusu Utekelezaji wa Miradi yaMaendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

Mheshimiwa Spika, Kutokana na matokeo ya ziara yaukaguzi wa mradi unaotekelezwa chini ya Fungu 57, Kamatiinatoa maoni kwamba mwenendo wa upatikanaji wa fedhakwa ajili ya miradi ya maendeleo ni jambo linalohitaji

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

kuboreshwa zaidi. Kwa kuwa utekelezaji wa miradi yaMaendeleo yenye tija kwa taifa ni jambo muhimu, ni vemaSerikali ikaweka uzito unaostahili kwa miradi hiyo.

Mheshimiwa Spika, Vilevile, kwa kuwa Serikali imeendeleakuimarisha ulinzi wa taifa letu, ni vema miradi yote inayohususekta ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa iendelee kupewakipaumbele kibajeti.

5.0 UCHAMBUZI WA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WAMPANGO WA BAJETI NA UZINGATIAJI WA MAONI YA KAMATIKWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017

5.1 Uchambuzi wa Mapitio ya utekelezaji wa mpangowa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

Mheshimiwa Spika, Uchambuzi wa Kamati katika Mapitioya utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya Wizara kwa Mwakawa Fedha 2016/ 2017, ulijielekeza katika makusanyo yamapato ikilinganishwa na lengo la makusanyo pamoja naupatikanaji wa fedha za matumizi kwa ajili ya shughulizilizopangwa kutekelezwa, hususan fedha za matumizimengineyo (OC) na fedha za miradi ya maendeleo. Vilevile,Kamati ilizingatia taarifa mbalimbali zilizowasilishwa mbeleya Kamati kwa kipindi cha Oktoba, 2016 na Januari 2017, namahojiano yaliyochangia upatikanaji wa taarifa muhimu naza ziada wakati wa vikao vya Kamati. Naomba kuwasilishauchambuzi huo kama ifuatavyo:-

5.2 Uchambuzi wa Taarifa kuhusu ukusanyaji wamapato

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2016/2017,Wizara ilikadiria kukusanya mapato ya jumla ya Shilingi68,406,000.00 kutokana na mauzo ya nyaraka za zabuni.Kamati ilijulishwa kuwa hadi mwezi Machi, 2017, Wizarailifanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi 30,169,863.80 sawa naasilimia 44.1 ya lengo. Uchambuzi wa Kamati umebainishaMchanganuo wa makusanyo kama inavyoonekana katikaJedwali Na. 01.

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

Mheshimiwa Spika, Katika mchanganuo huo, Kamatiimebaini yafuatayo:-

(i) Makusanyo katika Fungu 38 – Ngomeyalikusudiwa kuchangia katika lengo la Wizara kwa asilimia22.8 lakini Taarifa ya Makusanyo ilionesha kuwa Fungu 38limechangia kwa asilimia 45.1 ya kiasi kilichokusanywa.

(ii) Makusanyo ya Fungu 39 –JKT yalikusudiwakuchangia katika lengo la Wizara kwa asilimia 76.0, lakinihali halisi imeonesha kuwa makusanyo ya JKT yamekuwa niasimia 54.9 ya makusanyo ya kiasi kilichokusanywa.

(iii) Makusanyo ya Fungu 57 – Wizara, yalikusudiwakuchangia katika lengo la makusanyo kwa asilimia 1.2, lakinitaarifa ya Wizara imeonesha kuwa hakuna kiasikilichokusanywa kwenye Fungu hili.

Mheshimiwa Spika, ulinganisho huo wa malengo yamakusanyo kwa kila fungu ikil inganishwa na kiasikil ichokusanywa na kila fungu, ulisababisha Kamatikuchambua zaidi ili kupata sababu za mwenendo huo waufikiaji malengo. Kubwa lililobainika ni kuwa chanzo kikuucha Mapato kwa mafungu yote ya wizara hii ni mauzo yanyaraka za zabuni jambo linalosababisha makusanyo kuwachini na yasiyo ya uhakika.

5.3 Upatikanaji wa Fedha kutoka Hazina

Mheshimiwa Spika, Pamoja na Bunge lako Tukufu kuendeleakusisitiza kila mwaka kuhusu umuhimu wa Serikali kutoa fedha

FUNGU

MA

KAD

IRIO

% YA JUMLA YA LENGO

MA

KUS

AN

YO % YA

JUMLA YA MAKUSANYO

38 - Ngome 15,601,000.00 22.8 13,613,561.00 45.1 39 - JKT 52,003,000.00 76.0 16,556,302.80 54.9 57 - Wizara 802,000.00 1.2 0 0.0 JUMLA 68,406,000.00 100.0 30,169,863.80 100.0

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

zilizoidhinishwa na Bunge kwa ajili ya matumizi ya Serikali,upatikanaji wa fedha hizo umeendelea kuwa changamotokwa Wizara nyingi.

Kwa kuzingatia hilo, Kamati ilitaka kujiridhisha kuhusuutekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa kwa kufanya ulinganisho wa fedha zilizoidhinishwa kwaajili ya matumizi yote ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na kiasi kilichopatikana hadi kufikia mwezi Machi, 2017.Uchambuzi huo ulibainisha yafuatayo:-

(i) Hadi kufikia Mwezi Machi, 2017 Wizara ilikuwaimepokea asilimia 69.6 ya bajeti ya matumizi ya kawaidailiyoidhinishwa na asilimia 14.5 ya Bajeti ya Maendeleo.

(ii) Kiasi kilichopokelewa na Wizara kwa ajili yamiradi ya maendeleo ni pungufu kwa asil imia 10.25ikilinganishwa na shilingi 40,000,000,000/= zilizotolewa katikaMwaka wa Fedha 2015/2016.

(iii) Pesa kwa ajil i ya Bajeti ya Matumizi yaUendeshaji (OC) ilipokelewa kwa asilimia 69.6 ikiwa niongezeko la asilimia 6 ikilinganishwa na fedha za Matumiziya Uendeshaji zilizotolewa katika kipindi cha 2015/2016.

(iv) Kati ya Shilingi 35,900,000,000 zilizopokelewakwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendelo, asilimia 94ya fedha hizo ni kwa ajili ya Fungu 57- Wizara, na asilimia 6 tukwa ajili ya Fungu 38 na Fungu 39 ikiwa ni asilimia 3 ya fedhahizo kwa kila Fungu.

Mheshimiwa Spika, Kutokana na uchambuzi huo, Kamati inamaoni kuwa mwenendo huu wa upatikanaji wa fedha zamaendeleo kwa Fungu 38-Ngome na Fungu 39-Jeshi laKujenga Taifa, si mzuri na unaathiri ratiba na mpango wautekelezaji wa miradi muhimu ya maendeleo.

5.4 Mapitio ya utekelezaji wa ushauri wa KamatiMheshimiwa Spika, Kamati ilipopitia Mpango na Makadirioya Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

Mwaka 2016/2017, ilitoa ushauri katika maeneo kumi na nne(14) yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara hii.Naomba kulijulisha Bunge hili kuwa ushauri kuhusiana nabaadhi ya maeneo umezingatiwa kikamilifu au unaendeleakuzingatiwa na ushauri mwingine haujazingatiwa kabisakama inavyoonekana katika Kiambatisho Namba 1.

Mheshimiwa Spika, Mfano wa ushauri uliozingatiwa kikamilifuni kuhusu kurasimishwa kisheria kwa maeneo yoteyanayotolewa na Mamlaka za Mikoa kwa ajili ya matumiziya Jeshi. Taarifa ya Utekelezaji imeonesha kuwa ushauri huuumeanza kutekelezwa kwa kurasimishwa maeneo ya jeshimkoani Singida na Korutambe- Tarime mkoani Marayaliyotolewa na Mamlaka za Mikoa hiyo kwa ajili ya matumiziya Jeshi.

Mfano wa pili ni utekelezaji wa ushauri kuhusu kulipa madeniyote ya Wizara yaliyohakikiwa. Naomba kutoa taarifa kuwaSerikali imejiwekea utaratibu wa kutenga fedha kila mwakakwa ajili ya kuyalipa madeni hayo kwa awamu. Kamatiilijulishwa kuwa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017, jumla yashilingi 151,146,888,000.00 zilitengwa kwa ajili ya kulipa madeniya kimikataba. Hata hivyo, Mheshimiwa Waziri wa Ulinzialiijulisha Kamati kuwa hadi kufikia mwezi Machi, 2017 shilingibilioni 30 zilikuwa zimetolewa.

Mheshimiwa Spika , Mfano wa Ushauri ambaohaukuzingatiwa kikamilifu ni kuhusu Serikali kutoa shilingibilioni 35 kwa aji l i ya kulipa fidia kwa maeneoyaliyochukuliwa na Jeshi. Sababu zilizotolewa ni ufinyu wabajeti na kutokutolewa kwa fedha iliyoidhinishwa. Taarifa yaWizara ilionesha kuwa katika Mwaka wa Fedha 2016/2017Wizara iliidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 27 kwa ajili yakupima na kulipa fidia wananchi ambao maeneo yaoyalitwaliwa kwa matumizi ya Jeshi. Hadi kufikia mwezi Machi,2017 fedha hizo zilikuwa hazijatolewa kabisa.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia madaraka ya Bungeyaliyoainishwa katika Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Kamati inaendelea

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

kusisitiza kuwa ushauri ambao haujazingatiwa unapaswakufanyiwa kazi na kuwa sehemu ya ratiba ya utekelezaji wamajukumu ya Wizara hii kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

6.0 UCHAMBUZI WA MPANGO NA MAKADIRIO YAMAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018

6.1 Mpango wa Utekelezaji wa Majukumu ya Wizarakwa Mwaka wa Fedha 2017/ 2018

Mheshimiwa Spika, ili kujiridhisha na Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara hii, Kamati ilirejea Hati Idhini yaMgawanyo wa Majukumu ya Wizara za Serikali, Toleo la tarehe22 Aprili, 2016 na kuoanisha na malengo ya Bajeti ya Wizarahii kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. Kamati ilibaini kuwakatika kutekeleza majukumu ya msingi manne yaliyoainishwakatika Hati Idhini, Wizara inalenga kuimarisha utendaji kazina ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake kulinganana Dira na Dhima kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Lengo hili limepangwa kufikiwa kwa kutekeleza majukumusaba ikiwemo kuendeza utafiti na teknolojia kwamadhumuni ya kuzalisha bidhaa na huduma kwa ajili yamatumizi muhimu pamoja na kupima ardhi inayotumika kwashughuli za Jeshi na kulipa fidia katika maeneo yaliyotwaliwakwa ajili ya matumizi ya kijeshi.

Mheshimiwa Spika, uchambuzi umeonyesha kuwamajukumu yaliyopangwa yatawezesha ufikiaji wa lengo kwaufanisi endapo tu Serikali itazingatia mpango na makadirioya mapato na matumizi ya Wizara kwa kutoa fedhazitakazoidhinishwa na Bunge kwa ukamilifu na kwa wakati.

6.2 Uchambuzi wa Makadirio ya Mapato kwa Mwakawa Fedha 2017/2018Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018, Wizaraya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mafungu yote matatuinategemea kukusanya mapato ya jumla ya shilingi69,706,000.00. Mchanganuo wa lengo hilo la makusanyounaonekana katika Jedwali Na. 2 la Taarifa hii.

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

Jedwali Na. 02 : Mchanganuo wa mapato

Chanzo: Taarifa ya Wizara

Kwa uchambuzi huo, Kamati imebaini yafuatayo:-

(i) Lengo la makusanyo kwa mafungu yote yaWizara limeongezeka kwa asilimia 1.9 ikilinganishwa na lengola makusanyo kwa Mwaka wa Fedha unaoisha.

(ii) Wakati Mwaka 2016/2017 lengo lilifikiwa kwaasilimia 44.1 hadi robo ya tatu ya Mwaka wa Fedha, lengo lamakusanyo kwa Mwaka 2017/2018 limeongezeka kidogobadala ya kupungua.

(iii) Fungu 38 – Ngome linategemewa kwa kiasicha asilimia 22.38 na Mwaka 2016/2017 lilitegemewa kwaasilimia 22.8.

(iv) Fungu 39 – JKT l inategemewa katikamakusanyo kwa kiasi cha asilimia 77.47 na Mwaka 20116/2017 lilitegemewa kwa asilimia 76.

(v) Fungu 57 linategemewa kwa makusanyo kwakiasi cha asilimia 0.15 wakati Mwaka 2016/2017 lilitegemewakwa asilimia 1.2

(vi) Makadirio ya mapato kwa Fungu 57yamekuwa yakipungua kila mwaka na makusanyo yakeyameendelea kuwa si ya kuridhisha. Kwa mfano, kwa Mwakawa Fedha 2015/2016, Wizara (Fungu 57) ilikusanya shilingi100,000.00 sawa na asilimia 0.9 tu kati ya shilingi 11,002,000.00zilizokadiriwa kukusanywa.

(vii) Kwa kuoanisha na mwenendo wa ukusanyaji

Fungu Makadirio Asilimia ya lengo la Wizara

38 - Ngome Shilingi 15,601,000.00 22.38 39 - JKT Shilingi 54,003,000.00 77.47 57 - Wizara Shilingi 102,000.00 0.15 JUMLA Shilingi 69,706,000.00 100.00

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

wa fedha kwa Mwaka 2016/2017, inawezekana kabisa hadikufikia mwezi Machi, 2018 Wizara hii ikawa imekusanya kiasicha shilingi 30,740,346.00.

Mheshimiwa Spika, kwa maelezo hayo, ni maoni ya Kamatikuwa lengo la ukusanyaji linapaswa kuzingatia mambomengi ili kuwa na uhalisia.

6.3 Uchambuzi wa Makadirio ya Matumizi

Mheshimiwa Spika, Maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Ulinzikwenye Kamati yalionesha kuwa katika Mwaka wa Fedha2017/2018, Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifainayoombwa kwa mafungu yote matatu ni shil ingi1,725,517,816,925.00. Kati ya Fedha hizo, shil ingi1,506,517,816,925.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida nashilingi 219,000,000,000.00 kugharamia miradi ya Maendeleo.

Mheshimiwa Spika, ili kukidhi mantiki ya Masharti ya Kanuniya 98 (2) ya Kanuni za Bunge, Kamati ilifanya uchambuzi wamakadirio hayo kwa kupitia kasma(Items), vifungu (Subvotes)na Mafungu (Votes) zote ikil inganishwa na bajetiiliyoidhinishwa na kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Naomba kubainisha yafuatayo:-

i) Bajeti ya Wizara hii kwa Mwaka wa Fedha2017/2018 imepungua kwa shilingi 11,012,596,075ikilinganishwa na bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017. Hatahivyo tofauti hiyo ni pungufu kwa kiwango cha asilimia 0.6.

ii) Wakati bajeti kuu kwa Mwaka wa Fedha2017/2018 kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Waziriwa fedha tarehe 28 Machi, 2017, imeongezeka kwa asilimia6.64 Bajeti ya Wizara hii imepungua kwa asilimia 0.6.

iii) Asimia 12.7 ya bajeti ya Wizara hii kwa Mwakawa Fedha 2017/2018 ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo naasilimia 87.3 ya bajeti ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

iv) Wakati asilimia 38 ya bajeti kuu kwa Mwaka

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

2017/2018 ni kwa ajili ya kugharamia miradi ya Maendeleo,asilimia 12.7 ya bajeti ya Wizara hii ni kwa ajili ya kugharamiamiradi ya maendeleo.

v) Wakati Mwaka 2016/2017 asilimia 3.2 ya bajetiya Wizara hii ilikuwa ni kwa ajili ya uendeshaji (OC), Mwaka2017/2018 asilimia 3 ya bajeti ya wizara hii ni kwa ajilikugharamia uendeshaji wa shughuli za Wizara (OC).

vi) Wakati jukumu la msingi la Wizara hii kwamujibu wa Hati idhini ni kusimamia Sera zinazohusiana naulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, hakuna kasma zilizotengwamaalumu kwa ajili ya utayarishaji na ukamilishaji wa Sera yaUlinzi, Marekebisho ya Sheria ya Ulinzi wa Taifa walaMarekebisho ya Sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa.

vii) Licha ya azma ya Serikali ya kuongeza vijanawanaokwenda mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria, Kasmazinazohusika na mafunzo hayo katika Fungu 39hazijaongezewa fedha ikilinganishwa na mwaka 2016/2017.Fungu 39 – JKT, lilitengewa shilingi bilioni 20,100,000,000 kwaMwaka wa Fedha 2016/2017, na Mwaka 2017/2018linaombewa shilingi bilioni 12,500,000,000.

Mheshimiwa Spika , maelezo hayo yametokana nauchambuzi wa Kamati baada ya kupitia randama zaMafungu matatu ya Wizara hii na kwa kuzingatia mashartiya Kanuni ya 98 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge. NiliombeBunge lako tukufu kupokea maelezo hayo yatakayosaidiamajadiliano kuhusu hoja iliyowasilishwa na Waziri wa Ulinzina Jeshi la Kujenga Taifa mapema leo hii.

7.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia taarifa ya utekelezaji wamaoni ya Kamati kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017sambamba na majadiliano ya kina kuhusu Makadirio yaMapato, Mipango na Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na JKT kwamwaka 2017/2018 ikilinganishwa na Dhima ya Wizara ya

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

kulinda uhuru, maslahi na mipaka ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Kamati inatoa ushauri kwa kila fungu.

7.1 Fungu 38 - Ngome

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Fungu 38 Ngome, linahusikana mambo ya msingi kwa uwepo wa nchi yetu, na kwa kuwakasma za matumizi muhimu zipo katika fungu hili, Kamatiinashauri kama ifuatavyo:-

i) Kwa kuwa mpaka kufikia mwezi Machi, 2017Serikali ilitoa asilimia 14.5 tu ya fedha zote za maendeleozilizoidhinishwa na Bunge jambo linaloathiri utekelezaji wamiradi ya maendeleo, Fungu 38 Ngome lipatiwe fedha zotezilizopaswa kutolewa kwa Mwaka wa Fedha 206/2017.

ii) Serikali itafute uwezekano wa kutoa shilingibilioni 27 zilizotengwa katika Mwaka wa Fedha 2016/2017kwa ajili ya kulipa fidia kwa maeneo yaliyochukuliwa na Jeshikabla ya tarehe 30 Juni, 2017 ili kuwezesha wananchi ambaomaeneo yao yametwaliwa, kulipwa fidia.

iii) Serikali ione umuhimu wa kuliwezesha Jeshikumiliki ardhi kisheria kwa kufanya tathmini na upimaji wamaeneo ya zamani na maeneo mapya yaliyotwaliwa naJeshi na kuyapatia hati miliki. Umuhimu huu utaonekanaendapo Serikali itatoa shilingi 27,700,000,000.00 zilizotengwakatika Mwaka wa Fedha 2016/2017 kwa ajili ya kutekelezashughuli hiyo. Hadi kufikia mwezi Machi, 2017 hakukuwa nafedha zozote zilizokuwa zimetolewa.

7.2 Fungu 39 JKT

i) Serikali ikamilishe mchakato wa kufanyamarekebisho katika Sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa, Sura 193(The National Service Act, Cap. 193) ili iweze kuendana nawakati, mifumo ya utawala na mahitaji ya sasa ya kisheriakatika sekta ya Ulinzi.

ii) Kamati inaendelea kuishauri Serikali ione

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

umuhimu wa suala la fidia kwa vijana wanaopata mafunzoya JKT kutekelezwa chini ya Sheria ya JKT ya Mwaka 1964 ilikuondoa changamoto zilizopo kwenye malipo ya fidia kwavijana hao.

iii) Fungu 39 liwezeshwe kibajeti ili kumudumahitaji ya kuwezesha vijana wengi zaidi kujiunga na Jeshila Kujenga Taifa.

iv) Serikali itoe kipaumbele kwa vijana waliopitiamafunzo ya JKT wakati wa kuajiri vijana kwa ajili ya shughuliza ulinzi katika shirika la SUMA JKT.

v) Serikali ilipe madeni ya shirika la SUMA GUARDili liendelee kujiendesha kwa ufanisi. Aidha, Serikali ioneumuhimu wa kuweka utaratibu kwa Taasisi za Serikali wakutumia huduma za ulinzi za SUMA GUARD badala ya kuajirimakampuni binafsi.

vi) Serikali itoe fedha zote zilizotengwa katikaMwaka 2016/2017 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wamiundombinu katika makambi mapya kwa ajili ya mafunzona makazi ya vijana wanaotakiwa kujiunga kwa mujibu waSheria. Aidha, kwa kuwa bajeti ya maendeleo ya Jeshi laKujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018imepunguzwa ikilinganishwa na bajeti hiyo kwa Mwaka waFedha 2016/2017, Kamati inaishauri Serikali kuongeza bajetihiyo ili Jeshi la Kujenga Taifa liweze kuchukua vijana wengiwanaohitimu kidato cha sita na kuwapatia mafunzo ya JKTkama Sheria inavyotaka.

7.3 Fungu 57 – Wizara

i) Serikali kupitia Hazina ione umuhimu wakuongeza kasi ya kulipa madeni yote ya Wizara yaliyohakikiwayenye jumla ya shilingi 212,375,287,250.69 ili kuzuia mgogorounaoweza kutokea kati ya Wizara na wazabuni/wakandarasiwaliotoa huduma mbalimbali. Hadi kufikia mwezi Februari,2017, shilingi 31,628,607,462.47 zilikuwa zimetolewa na Hazinasawa na asilimia 14.8 tu ya madeni yote yaliyohakikiwa.

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

ii) Serikali itoe shilingi 10,500,000,000 kwa ajili yakulipa madeni ya kimikataba kabla ya Mwaka wa Fedha2016/2017 kuisha. Hii itaepusha ongezeko la deni litokanalona ongezeko la riba.

iii) Ili kutatua tatizo la uchakavu na upungufu wamiundombinu kwa mashirika ya Nyumbu na Mzinga kwalengo la kuwezesha ufanisi zaidi katika shughuli za utafiti nauhawilishaji wa teknolojia pamoja na uzalishaji wa bidhaakwa matumizi muhimu, Serikali itenge bajeti ya kutosha kwaajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu kwa mashirikahayo.

iv) Shirika la Nyumbu kimsingi lipo chini ya Wizaraya Ulinzi na JKT na wakati huo huo linamilikiwa kisheria naMsajili wa Hazina. Serikali iangalie uwezekano wa kulifanyaShirika hilo kumilikiwa kisheria na kuwajibika chini ya Mamlakamoja ili kuondoa mkanganyiko uliopo.

v) Katika kutekeleza Majukumu ya msingi yaWizara hii, Sera ya Ulinzi wa Taifa (The National Defence Policy)ni jambo la msingi. Serikali ikamilishe mchakato wa kuandaaSera hiyo muhimu kwa Taifa.

vi) Serikali ikamilishe mchakato wa kufanyamarekebisho katika Sheria ya Ulinzi wa Taifa, Sura 192 (TheNational Defence Act, Cap. 192) ili iweze kuendana na wakati,mifumo ya utawala na mahitaji ya sasa ya kisheria katikasekta ya Ulinzi.

8.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru kwa kunipa nafasikwa ajili ya kuwasilisha Taarifa hii. Napenda kuwashukuruWajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalamaambao maoni, ushauri na ushirikiano wao umewezeshakukamilika kwa taarifa hii. Naomba niwatambue kwa majinakama ifuatavyo:-

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

1. Mhe. Balozi Adadi Mohamed Rajabu, Mb, Mwenyekiti2. Mhe. Kanal (Mst) Masoud Ali Khamis, Mb, M/Mwenyekiti3. Mhe. Capt. George Huruma Mkuchika, Mb4. Mhe. Salma Rashid Kikwete, Mb5. Mhe. Mussa Hassan Mussa, Mb6. Mhe. Prosper J. Mbena, Mb7. Mhe. Mhe. Victor Kilasile Mwambalasa, Mb8. Mhe. Mch. Peter Simon Msigwa, Mb9. Mhe. Cecilia Daniel Paresso, Mb10. Mhe. Alphaxad Kangi Lugola, Mb11. Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Mb12. Mhe. Cosato David Chumi, Mb13. Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mb14. Mhe. Bonnah Kaluwa, Mb15. Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mb16. Mhe. Kiswaga Boniventura Destery, Mb17. Mhe. Rose Cyprian Tweve, Mb18. Mhe. Joel Mwaka Makanyaga, Mb19. Mhe. Haji Khatib Kai, Mb20. Mhe. Lucy Simon Magereli, Mb21. Mhe. Masoud Abdalla Salim, Mb22. Mhe. Sophia Hebron Mwakagenda, Mb23. Mhe. Lazaro S. Nyalandu, Mb24. Mhe. Stephene J. Masele, Mb25. Mhe. Machano Othman Said, Mb26. Mhe. Hasna Sudi Katunda Mwilima, Mb27. Mhe. Khamisi Yahya Machano, Mb28. Mhe. Yahya Omari Masare, Mb

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Wajumbe wa Kamatinapenda kutumia fursa hii kumshukuru Waziri wa Ulinzi naJKT Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi (Mb) kwa ushirikiano wake mzurikatika kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu ya kikanuniya Kamati. Aidha, namshukuru Katibu Mkuu Ndugu FlorensTuruka pamoja na watendaji wote wa Wizara kwa ushirikianowao.

Mheshimiwa Spika, mwisho napenda kumshukuru Katibu waBunge Dkt. Thomas Kashililah kwa kuratibu vema shughuli zaKamati na Bunge. Aidha, nawashukuru Mkurugenzi wa Idara

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

ya Kamati za Bunge Ndg. Athumani Hussein, MkurugenziMsaidizi Bi. Angelina Sanga na Makatibu wa Kamati hii Ndg.Ramadhan Abdallah na Bi. Grace Bidya wakisaidiwa na Bi.Rehema Kimbe kwa kuratibu vema shughuli za Kamati nakuhakikisha Taarifa hii inakamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, sasa naliombaBunge lako Tukufu likubali kuidhinisha Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na JKT kwa Mwaka wa Fedha2017/2018 kama yalivyowasilishwa na mtoa hoja.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na naombakuwasilisha.

Balozi Adadi Mohamed Rajabu, MbMWENYEKITI

KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA16 Mei, 2017

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge,maelezo ya Spika kuhusu taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambiya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujengaTaifa, naomba mnisikilize vizuri.

Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita MsemajiMkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Ulinzi na Jeshila Kujenga Taifa, ili awasilishwe taarifa yake naomba nitoemaelezo machahe.

Mheshimiwa Spika amesoma taarifa ya Msemaji Mkuuwa Kambi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Ulinzi naJeshi la kujenga Taifa juu ya makadirio ya mapato namatumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018iliyowasilishwa mezani asubuhi ya leo na ameelekeza baadhiya aya ziondolewe.

Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Spikaalikwishatoa maamuzi (rulling) hapa Bungeni na akatoawaraka rasmi kwa Wanadhimu Wakuu wa Kambi zote

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

Bungeni kwamba maudhui ya hotuba zote zinazowasilishwahapa Bungeni hayatakiwi kupingana na masharti ya Kanuniya 64(1) ya Kanuni za Bunge, Toleo la Januari, 2006; nakwamba hotuba yoyote au sehemu ya hotua yoyoteitakayoonekana kuwa kwa ujumla wake inakinzana namasharti ya kanuni hiyo haitakubalika wala kusomwaBungeni. (Makofi)

Hivyo, aya ya tatu katika ukurasa wa pili na aya yatatu katika ukurasa wa kumi wa taarifa ya Msemaji waUpinzani, aya hizo zimeondolea. Kwa mantiki hiyo nakala zataarifa mlizogawiwa Waheshimiwa Wabunge nakalaambazo Msemaji Mkuu wa Upinzani ataisoma hapa Bungenina ambayo ndiyo itaingia katika Taarifa Rasmi za Bungehaitakuwa na aya hizo.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Msemaji Mkuu wa Kambi yaUpinzani naomba uzingatie sababu tunazungumzia Wizaranyeti na kuna mambo yameoneka na yana ni classifiedinformation hayatakiwi kuanikwa katika Bunge hili katikahadhara hii kwa kipindi hiki. Kwa hiyo rulling ya Kiti ni hiyo,nakuomba uyachukulie hivyo, kama utakuwa na mamboyoyote muhimu kwa Taifa hili yawasilishe katika sehemuzinazohusika siyo katika mjadala ambao maadui wa nchi hiiwanaweza wakachukua advantage ya mambo hayo.

Mheshimiwa Msemaji wa Kambi ya Upinzani, karibu.(Makofi)

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Mwenyekiti,nitazingatia kisu cha ngaliba kimepitia baadhi ya maeneokwa hiyo sitayasoma. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Msemaji Mkuuwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa JumaHamad Omar Mbunge, naomba kuwasilisha maoni ya KambiRasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu mapitio ya utekelezaji wabajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

2016/2017 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi yafedha ya Wizara hiyo, kwa mwaka wa fedha 2017/2018

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijawasilisha maonihayo, napenda kuchukua fursa hii, kumshukuru MwenyeziMungu kwa kutujalia sote uhai na kutuwezesha kushiriki katikaMkutano huu wa Bunge, kujadili Bajeti ya Serikali tukiwasalama. Aidha, napenda kutumia fursa hii kwa niaba yaKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kulipongeza Jeshi laWananchi wa Tanzania kwa jinsi walivyojitoa kwa moyo wauzalendo kabisa, kusaidia kuratibu zoezi la kuaga miili yawanafunzi 32, Walimu wawili na Dereva mmoja wa shule yaLucky Vincent waliofariki kwa ajali ya gari huko Karatu –Arusha. Sambamba na hilo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinatoa salamu za rambirambi kwa wote walioguswa namsiba huo mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa sina fadhila, kamasitawashukuru kwa dhati ya moyo wangu, wapiga kurawangu wa Jimbo la Ukonga, kwa imani na ushirikianomkubwa wanaonipa, katika utekelezaji wa majukumu yanguya Kibunge. Naendelea kuwaahidi utumishi uliotukuka nakamwe sitawaangusha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekeenapenda kuishukuru familia yangu, kwa kunifariji na kunitiamoyo katika kutekeleza majukumu yangu, lakini zaidi sanakwa kunivumilia, hasa pale ninapokuwa mbali nao, kutokanana shughuli zangu za Kibunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu inayofuata ngalibaamepitia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia nimshukuruKiongozi wa Kambi wa Kambi ya Upinzani Rasmi BungeniMheshimiwa Freeman Aikael Mbowe Mwenyekiti waCHADEMA Taifa na Mbunge wa Jimbo la Hai, kwa kuwa naimani na mimi na kuniteua kuwa Naibu Msemaji wa KambiRasmi ya Upinzani Bungeni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa.

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

Mheshimiwa Mwenyekiti, muda wa kufanya kazikatika Taasisi za Serikali ni masaa nane kuanzia saa moja nanusu asubuhi hadi saa tisa na nusu alasiri. Ikiwa mtumishiyeyote ataendelea kufanya kazi baada ya saa tisa na nusualasiri kwa sababu yoyote ile, atahesabika kwambaamefanya kazi katika muda wa ziada wa kazi na atastahilikulipwa posho ya masaa ya ziada ya kazi yaani overtimeallowance.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kawaida Wanajeshiwalikuwa wanafanya kazi hadi saa tisa na nusu alasiri nakurejea nyumbani au kambini, lakini kimsingi Wanajeshi wapokazini masaa yote, kwa kuwa kukitokea dharura yoyote,huwa wanaitwa na kushughulikia dharura iliyojitokeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni, kwa haliambayo siyo ya kawaida, Wanajeshi wa Jeshi la Wananchiwa Tanzania wamepewa amri ya kuwepo kazini hadi saakumi na mbili jioni bila kuelezwa sababu ya kufanya hivyo.Kutokana na hali hiyo, Wanajeshi wamepokea taarifa hiyokwa taharuki kubwa na kwa mtazamo hasi, jambo ambalosiyo afya kwa utendaji katika Jeshi letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la msingi hapa nikwamba, dhamira ya kuongeza muda wa kazi ni nini? Je,kuna tangazo la hali ya hatari nchini ambapo sasa inabidiWanajeshi wafanye kazi ya ziada? Je, kuna mission yoyotewaliyopewa ikafeli, kwa hiyo sasa wanapewa adhabu kwakufanya kazi ya ziada?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikumbukwe kwamba Jeshiletu limesifiwa kote duniani kuwa ni Jeshi lenye weledi nanidhamu ya hali ya juu, hata Waziri hapa amewapongezakwa hilo. Kama Jeshi hilo lina weledi mkubwa na nidhamuya hali ya juu, hata kusifiwa katika medani za Kimataifa,kumetokea nini cha ajabu hadi wafanyishwe kazi kwa masaayote hayo? Au weledi wao na nidhamu yao imeshuka? Kwahiyo, wako katika prorogramu maalum ya kuongeza weledina nidhamu? Kama hivyo, ndivyo, programu hiyo itadumukwa muda gani.(Makofi)

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vema Serikali ikawekabayana dhamira na lengo la kuongeza muda wa kazi Jeshinihadi kufikia saa 12 jioni, ili Wanajeshi wafanye kazi kwa moyomkunjufu. Bila kufanya hivyo, watakuwa na dukuduku nakibaya zaidi ni kwamba, wataweza kuwa na mgomo baridikutokana na kutoridhika na uamuzi huo na hivyo kuathiriufanisi na tija ya Jeshi zima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, athari za kuongeza mudawa kufanya kazi kwa Wanajeshi ni nyingi na zinamgusaMwanajeshi mmoja mmoja na Taifa zima kwa ujumla. Atharimojawapo kubwa ni kuhatarisha ulinzi na usalama nchini.Katika mazingira ya Dar es Salaam, mathalani, ambako kunashida ya usafiri, hali ya ulinzi na usalama kuanzia saa 12 jionihadi saa nne usiku wakati Wanajeshi wanapokuwa wanarudinyumbani, inakuwa ngumu sana Polisi wanapata shidakufanya doria kwa kuwa wanakuwa na Wanajeshi wengi, kwahiyo itawawia vigumu wakati mwingine kutambua naniMwanajeshi nani siyo Mwanajeshi katika mazingira hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, athari nyingine kubwa yakuongeza muda wa kufanya kazi ni kudorora kwa mahusianoya kifamilia miongoni mwa Wanajeshi. Tukichulia tena mfanowa changamoto ya usafiri Dar es Salaam, ili Mwanajeshiaweze kufika kazini saa moja asubuhi ni lazima aweameondoka nyumbani kwake angalau saa kumi au saa kumina moja alfajiri. Muda huo watoto wake bado wamelala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa changamoto hiyo yausafiri, atarudi nyumbani saa nne mpaka saa tano usikuanakuta watoto wameshalala. Kwa mwendelezo huo, kunasiku watoto hao wanaweza kumwita Baba Mjomba auMama wakamwita Shangazi kwa kuwa hawajui kama kwelihao ndiyo wazazi wao halisi... [Maneno haya sio sehemu yaTaarifa Rasmi za Bunge]

MHE. KAPT. (MST) GEORGE H. MKUCHIKA: Mwongozowa Mwenyekiti

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara….

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y MSEMAJI MKUU WAUPINZANI WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA):Mheshimiwa Mwenyekiti naomba niendelee…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara hebu subiri, kaakatika kiti chako.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. KAPT. (MST) GEORGE H. MKUCHIKA: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nataka ku-declare interest kwamba mimini Mwanajeshi Mstaafu. Naomba huo mwongozo wakokwamba, katika kazi za Jeshi tunaapa kulinda nchi mudawa saa 24 usiku na mchana. Katika kazi za Jeshi tunatii amriya mkubwa wako bila kuuliza maswali. Katika kazi za JeshiKamanda anaruhusiwa kutoa amri atakayoona ina manufaakwa nchi. (Makofi)

MHE. HALIMA J. MDEE: Kuhusu utaratibu.

MHE. KAPT. (MST) GEORGE H. MKUCHIKA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa hiyo aliyotoa Kamandi ya kuongeza mudawa kufanya kazi hapaswi kuhojiwa na mtu yeyote. Kwa hiyo,naomba mwongozo wako, naomba tu upande wa pili muwena nidhamu, mkae. Naomba mkae na Mheshimiwa Mbungeyule amewasha kipaza sauti, Mheshimiwa amewasha…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mkuchika unazungumza naKiti unazungumza na Wabunge? Zungumza na Kiti .

MHE. KAPT. (MST) GEORGE H. MKUCHIKA: Sijamalizakuomba mwongozo.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge subirini,Kwanza Mheshimiwa Halima Mdee kaa chini, tabia yakusimama bila kuitwa ni kosa la Kibunge, kama una hojamuache azungumze hoja yake, simama nawe utapewanafasi.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

MWENYEKITI: No no no! bado mnabisha? jengolimezungukwa na pingu leo hil i. Subirini, kaa chini.Mheshimiwa Mkuchika.

MHE. CAPT. (MST) GEORGE H. MKUCHIKA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa hiyo…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliendeleakuongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, hamuwezikukiongoza Kiti, Kiti kinawaongoza ninyi kama unaonaunapoteza muda toka nje, ukakae nje ama nenda kantini.Ndio maana yake! Kwa sababu mnakosa nidhamu, mnatakakuingilia shughuli za Kiti. Unasikitika kitu gani MheshimiwaRukia.

MHE. CAPT. (MST) GEORGE H. MKUCHIKA:Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo ninaouomba nikwanba…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mkuchika subiri kaakwanza..

(Hapa baadhi ya Wabunge waliendeleakuongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kama kunamtu anasimama kuomba mwongozo kwenye Wizara hii nyeti,ziko taratibu za kuuliza, kama ni Mwongozo au kama niTaarifa. Mheshimiwa Mkuchika kama unatoa taarifa auunatoa mwongozo toa sasa nikusikilize na isiwe ni mjadala.Haya nayasema mimi siyo ninyi, msubiri amalize.

MHE. CAPT. (MST) GEORGE H. MKUCHIKA: MheshimiwaMwenyekiti, mwongozo ninaouomba kutoka kwako nikwamba Kamanda ametoa amri kwa jinsi ilivyoona inafaa.Je, Bunge hili lina majukumu ya kumpangia Kamanda liniatoe amri na lini asitoe.(Makofi)

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

MWENYEKITI: Ahsante, haya Mheshimiwa Paresso,hapa anasimama Chief Whip, wewe Halima kaa. (Kicheko)

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,tunaomba Kiti chako kisiyumbe, kwa sababu…

MWENYEKITI: Kwanza ukishasema Kiti kinayumbatutayumba mimi na wewe hapa, ukisema Kiti kinayumbanitayumba na wewe. Wewe sema hoja yako. (Kicheko)

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,hoja yangu ni kwamba, kwa mujibu wa Kanuni na Taratibuzetu na kwa mujibu wa uendeshaji wa Bunge, Msemaji waKambi ya Upinzani au hata Waziri akiwa anasoma pale huwahakuna Taarifa wala Mwongozo. Mwongozo na Taarifaunakuja baada ya uwasilishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tayari Ofisi yakoimeshapitia, ikaondoa, ikakata baadhi ya maneno kwa ninibado baadhi ya Wabunge akiwepo Mheshimiwa Mkuchikaanaingilia. Kwa hiyo, tunaomba Kiti chako kiruhusu isomwe,kama Mbunge yeyote ana hoja zaidi ya hapo ataielezabaadae wakati wa uchangiaji. (Makofi)

MWENYEKITI: Sawa. Waheshimiwa Wabunge, Taarifahii ameshapitia Mheshimiwa Spika, lakini haizuii Mbungeyeyote mwingine akiona kuna kasoro ndani ya Taarifa na pili,hatuzungumzii taarifa za Wizara ya Maji wala Wizara yaUmeme humu ndani. Mheshimiwa haya maneno yanaallegation nzito sana. Unaweza ukaulizwa uthibitisheumezitoa wapi, Bunge linaweza likasema tunaombauthibitisho wa hizi tuhuma. Kwa hiyo, ninachokuombaMheshimiwa Waitara…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa, msicheze na impatienceyangu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Waitara, kuna vitu humu ndani vinaweza

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

vikakubana mwenyewe. Kuna maneno ambayo unayatumiayanaweza yakakubana mwenyewe, utashindwa kabisakuyathibitisha haya maneno unayosema. Siyo mazuri kwako.Nilitoa ruling mwanzo kama kuna vitu ambavyo unavionavinaathiri (vina changamoto) yako maeneo ambayounaweza ukazipeleka hizi taarifa zikashughulikiwa. Kunamaneno ambayo unaweza ukayabeba, ukayaokota mitaani,yatakuathiri mwenyewe ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Mbunge, kwa hiyo, nakuomba, maeneoyote haya yaliyosemwa hapa ya watu kuchelewa nyumbaniyote nayatoa kwenye Hansard. Endelea na taarifa yako.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naombamuda wangu ulindwe. Haya ambayo hampendi kuyasikiandiyo hoja na malalamiko ya Wanajeshi huko waliko. (Makofi)

MWENYEKITI: Wewe endelea.

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA):: Mheshimiwa Mwenyekiti, atharinyingine ni ya kiuchumi. Wanajeshi wanapokuwa wakitokakazini saa tisa na nusu alasiri walikuwa na muda wa kufanyashughuli za kijasiriamali ili kupunguza ukali wa maishakutokana na posho zao kuwa ni kidogo. Kwa mabadilikohaya ya muda wa kufanya kazi, hakuna muda tena kufanyakazi hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maelezo yote hapo juu,itoshe kusema Serikali itoe maelezo ya sababu za kuongezamuda wa kufanya kazi Jeshini ili kuwe na ufahamu wapamoja baina ya Serikali na Jeshi na hivyo kuondoamanung’uniko miongoni mwa Wanajeshi na hatimayekuongeza ufanisi Jeshini. Aidha, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni, inaitaka Serikali kulieleza Bunge hili, iwapo

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

imewalipa Wanajeshi posho ya masaa ya ziada ya kazi(overtime allowance) tangu walipoanza kutekeleza amri yakufanya kazi hadi saa 12 jioni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kusitishwa kwa utoaji wa fedhaza likizo kwa Wanajeshi. Likizo ni stahiki ya kisheria ya mtumishiyoyote iwe ni katika Sekta ya Umma au Sekta Binafsi. Msingiwa likizo ni kumpatia mtumishi muda wa kupumzika, kubadilimazingira ya kazi na hivyo ku-refresh akili na hatimaye kurudikazini akiwa na ari na nguvu mpya ya kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo likizo zenye malipo naambazo hazina malipo. Yapo malalamiko miongoni mwaWanajeshi kwamba malipo ya fedha za likizo, kwa likizo zenyemalipo yamesitishwa kimya kimya bila Wanajeshi kupewataarifa ya kinachoendelea. Kwa mujibu wa taarifa kutokakwa baadhi ya Wanajeshi ni kwamba, mara tu walipoanzakuulizia fedha zao za likizo walitishwa na Chief of Staff kuwani marufuku kuulizia na kuzungumzia popote kuhusu fedhahizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inaitaka Serikali kulieleza Bunge hili, kama haitakiWanajeshi watoe malalamiko yao kwa ngazi husika ndaniya Jeshi wanataka wakatoe malalamiko yao wapi? Kitendocha kuwatisha Wanajeshi, kwa kuwapiga marufukukuyazungumzia maslahi yao halali, tena ndani ya mamlakaza ndani ya Jeshi, ni cha kulaaniwa na anayefanya hivyoachukuliwe hatua, kwani anachochea hasira miongoni mwaWanajeshi, jambo ambalo linaweza kupelekea uasi ndaniya Jeshi na kuhatarisha amani na usalama wa nchi yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinapenda kuitahadharisha Serikali kuwa, vikosi vya waasikama vile Boko Haram, Al-Shaabab na M23 vilianza kutokanamadai madogo madogo ndani vya vikosi vyao vya Jeshiambayo hayakuthaminiwa wala kushughulikiwa. Hadininapozungumza hapa, kwa mujibu wa taarifa ya DW naBBC ya jana asubuhi ni kwamba, Jeshi la Ivory Coast limeasi

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

kutokana na madai ya malipo ya fedha ambayo Serikali yaIvory Coast haikufanyia kazi mapema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kushughulikia madai na mahitaji mengineya msingi yanayowahusu Wanajeshi kwa wakati, kwa kuwayanapoanza kusikika nje yanashusha hadhi ya Jeshi letu.Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, haikupaswa kujua madaihayo, lakini imeyajua kwa kuwa, hayapewi uzito unaostahilina wala hayashughulikiwi na Wanajeshi hawaruhusiwikuandamana, hivyo lazima watafute sehemu ya kupumuliana ni kupitia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhana ya kubana matumiziSerikalini inavyoathiri misingi ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi.Kutokana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kubanamatumizi ya Serikali, tayari Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi naUsalama ameanza kutekeleza azma hiyo, kwa kuwaagizaWakuu wa Vikosi kumuunga Rais mkono kubana matumiziya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, akiwa katika ziara ya kutembelavikosi mbalimbali baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo,Mkuu wa Majeshi alinukuliwa akiwaagiza Wakuu wa Vikosikuanza kubuni miradi ya uzalishaji mali ili waweze kujiendeshakwa matumizi madogo madogo kama vile vifaa vya ofisiyaani stationaries.

Mheshimiwa Mwenyekiti, agizo hilo la kufanya shughuliza uzalishaji mali linakiuka msingi mkuu wa uanzishwaji wawa Jeshi la Wananchi, Jeshi la Ulinzi ambalo ni ulinzi nausalama wa mipaka ya nchi yetu. Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inatambua kwamba kipo kitengo cha uzalishaji malikatika Jeshi la Kujenga Taifa yaani SUMA JKT, na kinafanyakazi nzuri. Jambo la msingi ni kuiwezesha SUMA JKT ili izalishekwa wingi na kuchangia gharama hizo siyo kulifanya Jeshizima kuwa la uzalishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, manunuzi ya vifaa mbalimbaliJeshini. Ninapozungumzia vifaa Jeshini nadhani naeleweka,

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

vifaa Jeshini siyo vifaa vya kawaida, ni vifaa ambavyo nisensitive na kwa maana hiyo, manunuzi yake pamoja nautunzaji wake, lazima ufanywe kwa makini na weledi wahali ya juu ili kuepuka madhara yanayoweza kutokeakutokana na mismanagement.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo taarifa kwamba Maafisawa ngazi za juu waliopo kwenye Bodi ya Manunuzi ndiyowanaojipa nafasi ya kwenda nje kununua vifaa hivyo nakuwaacha Maafisa wenye utaaalam na vifaa hivyo. Matokeoyake ni kwamba vinanunuliwa vifaa vinavyogharimumabilioni ya fedha, ambavyo ama vimepita muda wake wamatumizi au havifai kutumiwa katika mazingira yetu na hivyokuisababishia hasara Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu inayofuata kisu chaNgariba kimepitia. Kwa hiyo nitaparuka kwa heshima ya Kitichako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inatokana na Bodi yaManunuzi kutofuata taratibu za manunuzi na sababu kubwaya kutokufanya hivyo, ni tamaa ya kifedha na imebainikakwamba wanajipangia kwenda kufanya manunuzi hayo iliwapate posho ya safari na maslahi mengine. Kambi Rasmiya Upinzani inaitaka Serikali with a serious note kwambaisifanye mzaha kwenye eneo hili la manunuzi ya vifaa, kwanilicha ya eneo hilo kutumia fedha nyingi pengine kulikomaeneo hayo yote.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusuutaratibu.

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nafasi yaMkuu wa wa Majeshi katika kujenga Jeshi imara lenyenidhamu, utii na mshikamano.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusuutaratibu.

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

MWENYEKITI: Waheshimiwa Subirini, kaeni.

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Mwenyekiti, wakatiMkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyangeakimkabidhi Mkuu mpya wa Majeshi alimwambia kwambaamelitoa Jeshi kwenye tope na kulifikisha sehemu nzuri nakwamba, Mkuu huyu wa sasa alifikishe kwenye lami.

MHE. KAPT. (MST) GEORGE H. MKUCHIKA: MheshimiwaMwenyekiti, Mwongozo wa Spika.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara subiri. MheshimiwaMkuchika, Mheshimiwa Gulamali kaa chini.

MHE. KAPT. (MST) GEORGE H. MKUCHIKA: MheshimiwaMwenyekiti, mimi nimesoma hiyo paragraph yote namba sita.Nataka kusema yafuatayo kabla sijaomba mwongozo wako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza CDF Mkuu waMajeshi anateuliwa na Rais kwa jinsi anavyoona inafaa. CDFtuliyenae kabla hajateuliwa alikuwa number two, kwa hiyoamepandishwa kutoka number two kuwa namba moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ninalotaka kusemani Sheria ya National Defence Act ya Mwaka 1966 inasema nimarufuku mtu kusema mambo ya Jeshi kama siyo Msemajiwa Jeshi. Nataka kurudia tena… (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mkuchika Endelea.

MHE. KAPT. (MST) GEORGE H. MKUCHIKA: MheshimiwaMwenyekiti, Watakomaa lini hawa?

MWENYEKITI: Zima hiyo microphone pembeni yakohapo.

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

MHE. KAPT. (MST) GEORGE H. MKUCHIKA: MheshimiwaMwenyekiti, Sheria ya Ulinzi ya Mwaka 1966 inasema: Marufukumtu ambaye si Msemaji wa Jeshi kusema mambo ya Jeshi.Hata Wanajeshi wenyewe, hata awe Meja Jenerali, hata awenani, marufuku kuongea masuala ya Jeshi kwa vyombo vyahabari, kwa umma kama si Msemaji wa Jeshi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, paragraph hii yoteinazungumza mwenendo wa Jeshi na utendaji kazi wa CDF.Kwa hiyo, najua ningeliweza watoe kwa sababu siyoWanajeshi. Ningeweza kuomba waeleze maneno hayowameyatoa wapi, watapata matatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo ninaouomba auushauri, paragraph yote ya sita inazungumza mwenendo waJeshi ifutwe katika kitabu hiki na usiruhusu kusomwa. NaombaMwongozo wako. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Paresso unatakakusema nini?

(Hapa Mbunge fulani aliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Mheshimiwa usiingilie kazi ya Kiti.(Makofi)

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,tunaomba Mwongozo wako kwa sababu hizo hojaanazosema Mheshimiwa Mkuchika, nadhani ni fursa ya Waziribaadae kuja kujibu kama kuna hoja ambazo zimekuwa raisedna Kambi ya Upinzani. Ndiyo utaratibu wa uendeshaji borawa Bunge humu ndani umekuwa ukitumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana Kiti chakokizingatie haya.

MWENYEKITI: Waheshimiwa nimepitia ukurasa wa 11paragraph ya sita. Ni kweli anachosema MheshimiwaMkuchika haya mambo hayatakiwi yawe public, this isclassified information. Kwenye masuala ya kujibu, kuna

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

mambo mengi ya Jeshi hayazungumzwi humu wala pesazao hazitoki humu including utendaji huu ambaoameuandika Mheshimiwa Waitara kama haukuonekanamwanzo mimi nauona. Kwa mamlaka ya Kiti, paragraph hiiya sita, ukurasa wa 11 yote nayatoa, na wewe usiyasome.(Makofi)

Mheshimiwa Waitara kwa hiyo, anza ukurasa wa 12.Twende.

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa, kaeni chini wote.

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Hii ni shida ya kupokea taarifa vipande vipande,lakini ujumbe umefika. Hatujadil i utendaji wa CDFtunazungumza mambo yakafanyiwe kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuelewa lakini ujumbeumefika, naenda sasa ukurasa wa 13 namba saba; hudumaya nishati ya umeme…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Mwacheni asome, mngetaka simngekuja msome ninyi hapa mbele?

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naombaTaarifa kama ilivyowasilishwa iingie kwenye Hansard yotepamoja na marekebisho yake…

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

MWENYEKITI: Msipige kelele hapa siyo sokoni walacanteen hapa. No, no! kutokuwa na nidhamu, kwa mujibuwa Kanuni keep quiet.

MBUNGE FULANI: Acha ubabe.

MWENYEKITI: Ndiyo maana yake.

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Mwenyekiti, hudumaya nishati ya umeme katika Kambi za Jeshi. Ni jambolinalofahamika kwamba, Taasisi za Umma hulipia gharamaza huduma mbalimbali kama vile huduma za maji naumeme, kupitia bajeti ya matumizi mengineyo (OC)inayotolewa na Hazina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, Taasisi nyingi zaUmma yakiwemo Majeshi yetu yamekuwa yakishindwa kulipiahuduma hizo kutokana na bajeti ndogo ya matumizimengineyo na mbaya zaidi fedha za OC hazitolewi kwaukamilifu wake na hata hizo kidogo zinazotolewahuchelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, dawa ya kuondokana naudaiwa sugu kwa Taasisi za Umma yakiwemo Majeshi niSerikali kutoa fedha za matumizi mengineyo kwa utoshelevuna kwa wakati na siyo Serikali kuyaamuru makampuni aumashirika yanayotoa huduma kukata huduma hizo kwaTaasisi za Umma kwa kutumia neno ‘KATA’. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inatafsiri kitendo cha Mkuu wa Nchi kuiamuruTANESCO kukata umeme kwenye kambi za Jeshi kuwa nikuhatarisha usalama wa nchi. Jeshi ni taasisi nyeti katikausalama wa nchi, na kwa maana hiyo, Serikali inatakiwakuhakikisha kuwa, huduma zote zikiwemo maji, umeme, afyana kadhalika zinapatikana kwa utoshelevu ili Jeshi liwezekuendelea kufanya kazi zake za kulinda usalama wa nchi yetudhidi ya adui yeyote. Ikiwa Jeshi limeshindwa kulipia huduma

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

hizo, basi Serikali ndiyo inayotakiwa kuwajibika kwa kutotoafedha za kutosha za OC kulipia gharama hizo…. [Manenohaya siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

Mheshimiwa Mwenyekiti, usalama wa mipaka ya nchi.Kumekuwa na mvutano kuhusu mpaka wa Malawi naTazania hususan katika Ziwa Nyasa. Hata hivyo, Serikali kwanyakati tofauti imekuwa ikisema kwamba mgogoro huounashughulikiwa kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya Serikali kusemakuwa, kuna dalili njema ya maafikiano kuhusu mgogoro huo,kuna viashiria kwamba majirani zetu wa Malawi hawaafikianina usuluhishi wowote utakaowafanya wasimiliki Ziwa lote laNyasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Mtandanowa extractives ni kwamba Serikali ya Malawi imewekamsimamo kwamba haitakubaliana na usuluhishi wowoteambao utaipa Tanzania sehemu ya Ziwa Nyasa. Jambo hililinathibitishwa na Kauli ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongoziwa Serikali ya Malawi, Ndugu George Mkondiwa kwamba;“Malawi will never, and has never, at any time, acquiescedto Tanzania’s unwarranted and unjustified territorial claims,”

Mheshimiwa Mwenyekiti, kauli kama hiyo, kutoka kwaKiongozi mkubwa katika Serikali ya Malawi, hukumazungumzo ya usuluhishi yakiendelea, kwa vyovyote vileni kauli nzito na Tanzania haipaswi kuipuuza. Kwa sababuhiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kujuamazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kuhusu usuluhishi wamgogoro wa mpaka katika ya Tanzania na Malawi yamefikiawapi, na ni nini hatma ya mgogoro huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inaitaka Serikali kueleza hali ya usalamawa mipaka ya Tanzania kwa ujumla wake, ambayo kwa sikuza nyuma iligundulika kuwa beacons za mipaka hiyo zilikuwa

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

zimeng’olewa na pia raia kutoka nchi jirani walikuwawanaingia nchini mwetu kwa njia za panya kutokana namipaka yetu kupenyeka kirahisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafasi ya Jeshi katikakupambana na matukio ya kigaidi nchini.’

MHE. KAPT. (MST) GEORGE H. MKUCHIKA: KuhusuUtaratibu.

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA): Sawa Jecha.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mkuchika.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. KAPT. (MST). GEORGE H. MKUCHIKA: MheshimiwaMwenyekiti, nimesimama kwa mujibu wa Kifungu Namba 64majadiliano yetu Bungeni, ambacho kinasema: Mbungehatatumia jina la Rais kwa dhihaka katika mjadala kwamadhumuni ya kutaka kulishawishi Bunge kuamua jambololote kwa namna fulani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ukurasa wa 14Msemaji wa Kambi ya Upinzani anasema Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inatafsiri kitendo cha Mkuu wa nchi kuamuruTANESCO kukata umeme kwenye Kambi za Jeshi kuwa nikuhatarisha usalama wa nchi. Mkuu wa Nchi hapaanatuhumiwa kwa kuhatarisha usalama wa nchi.Ninavyofahamu agizo la Mheshimiwa Rais amesema watuwote ambao wametumia umeme hawajalipa, walipe.Hajaamrisha kukata…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. KAPT. (MST). GEORGE H. MKUCHIKA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa hiyo kwa maoni yangu…

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Subiri kwanza, subiri, MheshimiwaMkuchika endelea.

MHE. KAPT. (MST). GEORGE H. MKUCHIKA: MheshimiwaMwenyekiti, kwa maoni yangu maneno haya yanazungumziamwenendo wa Rais ambaye tumekatazwa kuzungumzahapa ndani.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Matiko.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwaheshima kabisa kwanza nimpe Taarifa baba yangu palenaona ameamua kupata dakika tatu, nne za kuchangia nakupoteza muda wetu wa Bunge…

MWENYEKITI: Kaa chini huna Taarifa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwasababu Mheshimiwa Rais alisikika akisema kabisa na akatajaJeshi kwamba likatiwe umeme.

MWENYEKITI: Kaa chini.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Kwa hiyo, asipotoshe naasitupotezee muda wa Bunge.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, natakatumalize kwa usalama hapa.

MHE. UPENDO F. PENEZA: Kuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Kaa chini, Upendo kaa chini. Naombatumalize kwa usalama. Yapo maneno ambayo kwa kwelikwa mujibu wa Kanuni zetu hayaruhusiwi na ninyi mnayafanyasi sababu hamjui. Unaposema inatafsiriwa kitendo cha Mkuuwa Nchi kuiamuru TANESCO... Hawakuambiwa waendekwenye vyombo vya ulinzi…

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Ilikwenda yote kwa ujumla. Kwa hiyo,Mheshimiwa Waitara utaendelea na Taarifa yako na baadhiya haya maneno natoa kwenye Hansard. EndeleaMheshimiwa Waitara.

MHE. UPENDO F. PENEZA: Kuhusu Utaratibu…

MWENYEKITI: Kaa chini.

MHE. UPENDO F. PENEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba Kuhusu Utaratibu…

MWENYEKITI: Nazungumza na Chief Whip wenu tubasi. Kaa chini.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naombamuda wangu ulindwe.

MWENYEKITI: Utalindwa, endelea.

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Mwenyekiti,wazingatie tu, cha muhimu hapa ni umeme urudishwe Jeshini,usikatwe, basi! Kelele zote zitakwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uteuzi wa Wanajeshi katikanafasi za kisiasa. Katika hotuba yake mwaka jana, MsemajiMkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alizungumziaathari za kuwateua Wanajeshi katika nafasi za kisiasa.Alionesha jinsi ambavyo Mwanajeshi anayeteuliwa kuwaMkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa anavyounganishwa naChama Tawala, kwa kutakiwa kuwa Mjumbe wa Kamati yaSiasa ya Chama katika Wilaya au Mkoa husika.

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuunganishwa huku naChama, kumewekwa bayana na Katiba ya CCM ya mwaka1977, katika Ibara ya 80(1)(c) inayowataja Wakuu wa Wilayakuwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM katika Wilayahusika na Ibara ya 94(1)(c) inayowataja Wakuu wa Mikoakuwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM katika Mikoahusika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitendo cha Katiba ya CCMkuwatambua Wakuu wa Wilaya na Mikoa kama Wajumbewa Kamati ya Siasa ya Wilaya au Mkoa husika, kinadhihirishakwamba, Wakuu hao ni wanachama wa chama cha siasa,na kwa maana hiyo ni wanasiasa. Kwa hiyo, Mwanajeshianayeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya au Mkoa automaticallyanakuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maelezo yake,alinukuu Ibara ya 147(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania inayosema kwamba:

“Itakuwa ni marufuku kwa Mwanajeshi yeyotekujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kamaatakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika Ibara yaTano (5) ya Katiba hii.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Ibara ndogo ya (4)inasema kwamba:

“Kwa madhumuni ya Ibara hii Mwanajeshi maanayake ni Askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au yakudumu katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magerezaau Jeshi la Kujenga Taifa.”

Uteuzi huu wa Wanajeshi kushika nafasi za kisiasaumetanuliwa wigo wake, ambapo sasa Wanajeshiwanaanza kuteuliwa na Chama Tawala kuwa Viongozi waChama. Uteuzi wa Kanali Ngemela Eslom Lubinga kuwaKatibu wa NEC ya Chama cha Mapinduzi Siasa na Uhusianowa Kimataifa ni uthibitisho kwamba Jeshi linaingizwa kwenyesiasa kidogo kidogo (Politicization of the army). (Makofi)

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

Mheshimiwa Mwenyekiti, athari za jambo hili nikwamba Jeshi litaanza kupoteza ile sifa yake ya kuwa Jeshila Wananchi na badala yake litaanza kufanya kazi kwa bias– kwa kupokea amri na maagizo ya Chama Tawala. Atharikubwa zaidi ni kwamba, utawala wa kiraia (CivilGovernance) utapoteza maana yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inatafsiri kitendo cha kuendelea kuwateua Wanajeshikushika nafasi za kisiasa hata baada ya kutahadharishwa nimwendelezo wa vitendo vya Serikali hii ya Awamu ya Tanovya kupuuza Katiba ya nchi yetu, jambo ambalo halina afyasana katika utawala bora. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa maelezo mbeleya Bunge hili, ni kwa nini haiheshimu katazo la Ibara ya 147(3)na (4) ya Katiba kuhusu Wanajeshi kujihusisha na kazi za siasa?

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Kuhusu taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lukuvi. MheshimiwaWaitara, hebu subiri kwanza kwani hunisikii, basi kakae.

T A A R I F A

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampa taarifa Kada wetuwa zamani, huyu alikuwa Katibu wa Vijana wa Umoja waVijana CCM. Nadhani ameisoma vibaya Katiba yetu.Mwanajeshi anapoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu waMkoa hapewi kadi ya CCM, Mheshimiwa Mbunge unapoitwaDiwani kuingia kwenye Council, uligombea Udiwani? Nasemani kama Mheshimiwa Diwani anapoingia kwenye Kikao chaCouncil lakini bado anaitwa Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu Mkuu wa Wilaya naMkuu wa Mkoa anaingia kwa sababu ya utaratibu wakikatiba. Chama Tawala ndicho kinachoisimamia Serikali.Kwa vyovyote vile, Chama chochote kinachotawala lazimakinakuwa na utaratibu wa watendaji waliowekwa kwenye

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

madaraka kwenda kutoa taarifa za utekelezaji wa Ilani. Siokwa maana ya wanachama. Ndiyo maana na ninyi mnaingiakwenye Council unawekwa kwenye Kamati zile za Madiwanimkijua ninyi ni Wabunge. Kwa hiyo, tusipotoshe hapakwamba wanapewa kadi, hawapewi kadi na CCM, mtuyoyote mwenye uthibitisho huo atuletee hapa. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante wameshakuelewa, MheshimiwaChief Whip wa Upinzani

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,tunakuomba kwa heshima kubwa sana, hizi hoja zinawezakujibiwa baadaye wakati fursa ya uchangiaji ikisha fikiatunaomba hotuba yetu isomwe imalizwe, hoja hizo zijibiwebaadaye.

MWENYEKITI: Kaa chini nimeshakuelewa, MheshimiwaWaitara endelea na taarifa unaipokea hiyo?

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifaya ndugu yangu kada wa Chama cha Mapinduzi na Waziriwa Nchi, siipokei kwa sababu ya uwongo inapotesha ukweli.

MWENYEKITI: Endelea na taarifa yako.

MHE. MWITA C. WAITARA (K.n.y. MHE. JUMA HAMADOMAR - MSEMAJI MKUU WA UPINZANI WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyonaomba niendelee, hawa ni Wajumbe wa Kamati za Siasawa Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba hilo KambiRasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa maelezo ni kwa niniWanajeshi wanaoteuliwa kushika nafasi za kisiasawanaendelea kuvaa uniform za Kijeshi wakati ilitakiwawastaafu kwanza Jeshi ili sasa wawe Watumishi wa Umma?

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu posho ya chakula(ration allowance). Mheshimiwa Mkuchika vipi hajasimama!(Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa miaka mingi, KambiRasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa mstari wa mbele kuteteamaslahi ya Wanajeshi wetu ikiwemo posho ya chakula (rationallowance). Msingi wa kutetea maslahi ya Wanajeshi nikuwapatia Wanajeshi wetu lishe bora na kuwafanya wawena nguvu ya kuhimili mazoezi na kazi mbalimbali za kiaskariwanazofanya. Aidha, lengo lingine ni kuwafanya wawe nautulivu wa ndani ili waweze kufanya kazi yao ya kulindausalama wa nchi yetu wakiwa hawana mawazo ya kwambawatakula nini pamoja na familia zao na nduguwanaowategemea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu uliopo ni kwamba,posho hii ya chakula hutolewa moja kwa moja kwa Askarikila mwezi. Askari anayepokea posho hii huwa na uhuru wakuitumia au kutokuitumia pamoja na familia yake. KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inazo taarifa kwamba kunamkakati wa kubadili mfumo wa utoaji wa posho hiyo kwaWanajeshi. Utaratibu mpya unaotaka kuanza kutumika nikwamba Wanajeshi hawatapewa tena posho badala yakeitapelekwa Kantini na wataanza kula chakula kamawanafunzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi Bungeniinaitaka Serikali kuufuta utaratibu huo na kuendelea kutoaposho ya chakula moja kwa moja kwa Wanajeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema mwanzotaarifa yangu yote iingizwe kwenye Hansard kama itashindwakumalizika ndani ya muda uliopangwa baada ya shughulinyingi za kusumbuasumbua katika hotuba hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushirikiano wa Jeshi naMataifa mengine. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinatambua Jeshi la Wananchi wa Tanzania linashiriki katikaoperesheni za Kijeshi katika mataifa mengine kupitia katika

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika na ule waUmoja wa Mataifa. Pamoja na kwamba ushiriki huuunaliongezea Jeshi letu uzoefu wa kufanya kazi katikamazingira tofauti, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitakaSerikali kutafakari upya faida hususan za kiuchumi nakiteknolojia ambazo kama Taifa tunanufaika nazo kwa Jeshiletu kushiriki katika operesheni hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinapendekeza hivi kwa sababu kama Taifa tusipojipangakimkakati zaidi, tutaishia kupokea miili ya Wanajeshi wetuwaliokufa katika operesheni hizo huku Taifa likibaki bilamanufaa yoyote. Kwa sababu hiyo, tunapendekeza kwambakuwe na malengo mahsusi na ya kimkakati Jeshi letulinapokwenda kushiriki operesheni katika Mataifa mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikakati hiyo iwe ni pamojana kufanya utafiti wa masuala ya kiuchumi na kiteknolojiayaani kwa maneno mengine wafanye ujasusi wa kiuchumi(economic espionage) ili baada ya operesheni hizo kuwe nafaida ya kidola itakayopatikana na siyo tu maslahi ya kifedha,wanayopata Wanajeshi baada ya kushiriki opereshenihizo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Kujenga Taifa naUzalishaji wa Chakula; ni aibu kwa Taifa hili kuwa na matukioya ukosefu wa chakula na njaa huku kukiwa na Jeshi laKujenga Taifa. Miaka iliyopita tulipendekeza kuwa pamojana mambo mengine, Jeshi hili lipimwe kwa uzalishaji ambaolitakuwa limefanya. Tulieleza kwamba dhima ya Jeshi laKujenga Taifa ni kwamba pamoja na mambo mengine, linawajibu wa kuwafunza vijana wetu kufanya kazi za uzalishajimali kwa ajili ya kujenga uchumi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni imekuwa ikishauri miaka nenda, miaka rudi kwambaSerikali itumie nguvukazi iliyopo kwenye Jeshi la Kujenga Taifakatika kujenga uchumi wa kweli nchini na hasa kipindi hikicha uchumi wa viwanda Jeshi la Kujenga Taifa ndilo lilitakiwalitoe dira ya namna ya kuwa na uchumi wa viwanda.

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

Tulishauri kwamba Serikali itenge mashamba makubwa ilivijana hawa wawapo mafunzoni, wafanye mafunzo kwavitendo ya kilimo ili nchi iweze kujitegemea kwa chakula.

Mheshimwa Mwenyekiti, aidha, tuliishauri Serikaliiwaagize Wakuu wa makambi ya JKT kutengeneza programumaalum za uzalishaji mali katika sekta mbalimbali kama vilekilimo, viwanda, ufundi, uvuvi na kadhalika kila mwaka.Tulipendekeza pia kwamba, Waziri mwenye dhamana aweanatoa taarifa ya kazi zilizofanywa na uzalishaji uliofanywana JKT na mapato maalum (maduhuli) yaliyopatikanakutokana na eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa Bajeti yaWizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka waFedha 2016/2017.Kumeanza kutokea mazoea mabaya yautekelezaji duni wa bajeti ya maendeleo katika Wizara hiijambo ambalo linatia wasiwasi kama kweli Serikali ina niaya dhati ya kupandisha ubora na ufanisi wa Majeshi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa taarifa yautekelezaji wa bajeti ya mwaka huu, fedha ya kutekelezamiradi ya maendeleo liyoidhinishwa na Bunge katika Fungu38 - Ngome ilikuwa ni shilingi bilioni 10, hadi Machi 2017 ilikuwaimetolewa shilingi bilioni moja tu sawa na asilimia 10 ya fedhailiyokuwa imeidhinishwa.

Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kulielezaBunge hili, hiyo bilioni moja iliyotolewa, ndiyo itawezakununua zana za kisasa zinazoendana na teknolojia ya sasa,kutoa mafunzo ya Kijeshi ya kisasa na kupandisha ubora naufanisi wa Jeshi la Wananchi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Fungu 39 -JKT, fedha ya maendeleo iliyoidhinishwa ilikuwa ni shilingibilioni nane, fedha iliyopatika mpaka sasa ni shilingi bilionimoja tu, sawa na asilimia 12.5 ya fedha iliyokuwaimepitishwa na Bunge hili. Hii ina maana kwamba bajeti yamaendeleo katika Fungu hili haijatekelezwa kwa asilimia87.5.

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinahoji JKT itawezaji kutekeleza miradi yake ya maendeleokwa madhumuni ya kujenga Taifa ikiwa mwenendo wautekelezaji wa bajeti uko namna hii? Aidha, Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa maelezo ni kwa niniJKT imekusanya maduhuli kidogo asilimia 31.8 tu wakati inamiradi mingi ya uzalishaji mali chini ya SUMA JKT?

Mheshimiwa Mwenyekiti, halikadhalika kwa upandewa Wizara, fedha iliyokuwa imeidhinishwa na Bunge ilikuwashilingi bilioni 230, lakini hadi kufikia Machi, 2017 shilingi bilioni33.9 tu sawa na asilimia 14.7 ilikuwa imetolewa. Tafsiri nyepesiya utekelezaji huu duni wa bajeti ya maendeleo, unairudishanyuma Wizara na unapunguza ufanisi, ubora na tija yaMajeshi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inataka Serikali, kwa kadri ile ambayo inalisifu Jeshiletu kuwa ni imara, lenye weledi na ufanisi mkubwa, basi sifahizo zionekane katika kutenga fedha na kupeleka fedha yotekutekeleza miradi ya maendeleo katika eneo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika randama yay aWizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Fungu 57 kuna baadhiya vitengo havikutengewa fedha kabisa tena fedha zamishahara. Kwa mfano, Subvote 1005 – ProcurementManagement, ukurasa wa 18 hakuna fedha yoyoteiliyotengwa kwa ajili ya mshahara; Subvote 2003 – BuildingConsulting Unit, ukurasa 36 haikutengewa fedha za mshaharakabisa na Subvote 2004 – Estate Management andDevelopment Unit ukurasa 39 hakuna fedha ya mshahara.Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kulielezaBunge hili ni kwa nini vitengo hivyo havijatengewa fedha zamishahara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho, naomba nimaliziehotuba yangu kwa kulipongeza Jeshi la Wananchi waTanzania kwa umahiri mkubwa, kwa jinsi linavyoendeshaoperesheni zake mbalimbali, lakini zaidi j insilinavyojishughulisha na masuala ya kijamii kunapotokea

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

maafa na majanga mbalimbali. Hata hivyo, Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni ingependa kujua Jeshi limesaidia vipikutoa msaada kwa wananchi waliokumbwa na mafurikokipindi hiki cha masika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni matamanio ya kila raiawa Tanzania kuona Jeshi letu likiendelea kupanda viwangovya ubora na ufanisi na hivyo kuwa na tija. Hata hivyo, iliviwango vipande, lazima mambo kadhaa yashughuliwekikamilifu. Kwanza, Serikali ihakikishe kwamba, bajetiinayoidhinishwa na Bunge kwa ajili ya Majeshi yetu inatolewakwa wakati na kwa ukamilifu wake. Pili, Serikali ihakikishekwamba, maslahi na stahiki zote za Wanajeshi zinatolewakwa wakati na kwa ukamilifu wake il i kuondoamanung’uniko miongoni mwa Wanajeshi na hivyokuwangezea morali ya kufanya kazi kwa moyo.

MWENYEKITI: Ahsante. Nimekuongezea dakika nnezimeshakwisha. Kwa hiyo nenda kaketi, upumzike, usubirimajibu.

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANIBUNGENI WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA MHE.JUMA HAMAD OMAR AKIWASILISHA MAONI YA KAMBI RASMIYA UPINZANI BUNGENI KUHUSU BAJETI YA WIZARA KWAMWAKA FEDHA 2017/2018 KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa KambiRasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Juma Hamad Omar(Mb), naomba kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni kuhusu mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya Wizaraya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka 2016/17 pamojana makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizarahiyo, kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Mheshimiwa Spika, kabla sijawasilisha moani hayo, napendakuchukua fursa hii, kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwakutujalia sote uhai na kutuwezesha kushiriki katika Mkutano

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

huu wa Bunge, kujadili Bajeti ya Serikali tukiwa salama. Aidha,napenda kutumia fursa hii kwa niaba ya Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni, kulipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzanikwa jinsi walivyojitoa kwa moyo wa uzalendo kabisa, kusaidiakuratibu zoezi la kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu wawilina dereva mmoja wa shule ya Lucky Vincent waliofariki kwaajali ya gari huko Karatu – Arusha. Sambamba na hilo, KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inatoa salamu za rambi rambikwa wote walioguswa na msiba huo mkubwa.

Mheshimiwa Spika, nitakuwa sina fadhila, kamasitawashukuru kwa dhati ya moyo wangu, wapiga kurawangu wa Jimbo la Ukonga, kwa imani na ushirikianomkubwa wanaonipa, katika utekelezaji wa majukumu yanguya kibunge. Ninaendelea kuwaahidi utumishi uliotukuka, nakamwe sitawaangusha.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee napendakuishukuru familia yangu, kwa kunifariji na kunitia moyo katikakutekeleza majukumu yangu, lakini zaidi sana kwakunivumilia, hasa pale ninapokuwa mbali nao, kutokana nashughuli zangu za kibunge.

[MANENO YAMEONDOLEWA KWA MAELEKEZO YA SPIKA]

Mheshimiwa Spika, nimeona nilisemee hilo, kwa kuwamatukio kama hayo, aghalabu yanahatarisha usalama wanchi yetu, na yanatoa taswira mbaya kwa mataifa mengine,kwamba, Tanzania pengine si mahali salama tena pa kuishi!Ni rai yangu na rai ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungenikwamba, Serikali ifanye uchunguzi wa matukio hayo, nakuleta taarifa ya uchunguzi huo hapa Bungeni, ili kurejeshaimani ya wananchi kwa Serikali yao, ambayo kwa sasainapungua kwa kasi, kutokana na Serikali kutoonekanaikichukua hatua za haraka, za kupambana na uhalifu huudhidi ya raia wake. Na hii inatokana na ukweli kwamba,jukumu la msingi la Serikali yoyote duniani ni kuwahakikishiawananchi wake ulinzi na usalama.

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

2. SAA ZA KUFANYA KAZI JESHINI

Mheshimiwa Spika, muda wa kufanya kazi katika taasisi zaSerikali ni saa nane (8) – yani kuanzia saa moja na nusu asubuhihadi saa tisa na nusu alasiri. Ikiwa mtumishi yeyote ataendeleakufanya kazi baada ya saa tisa na nusu alasiri kwa sababuyoyote ile, atahesabika kwamba amefanya kazi katika mudawa ziada wa kazi, na atastahili kulipwa posho ya masaa yaziada ya kazi (overtime allowance).

Mheshimiwa Spika, kwa kawaida wanajeshi walikuwawanafanya kazi hadi saa tisa na nusu alasiri na kurejeanyumbani au kambini, lakini kimsingi wanajeshi wapo kazinimasaa yote, kwa kuwa kukitokea dharura yoyote, huwawanaitwa na kushughulikia dharura iliyojitokeza.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni, kwa hali ambayo si yakawaida, wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzaniawamepewa amri ya kuwepo kazini hadi saa kumi na mbilijioni bila kuelezwa sababu ya kufanya hivyo. Kutokana nahali hiyo, Wanajeshi wamepokea taarifa hiyo kwa taharukikubwa na kwa mtazamo hasi, jambo ambalo sio afya kwautendaji kazi jeshini. Swali la msingi hapa ni kwamba; dhamiraya kuongeza muda wa kazi ni nini? Je, kuna tangazo la haliya hatari nchini, ambapo sasa inabidi wanajeshi wafanyekazi ya ziada? Na je, kuna mission yoyote waliyopewa ikafeli,kwa hiyo sasa wanapewa adhabu kwa kufanya kazi yaziada?

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kwamba Jeshi letu limesifiwakote duniani kuwa ni Jeshi lenye weledi na nidhamu ya haliya juu, na hata waziri hapa amewapongeza kwa hilo. KamaJeshi letu lina weledi mkubwa na nidhamu ya hali ya juu hatakusifiwa katika medani za kimataifa, kumetokea nini chaajabu hadi wafanyishwe kazi kwa masaa yote hayo? Auweledi wao na nidhamu yao imeshuka, kwa hiyo wako katikaprorogramu maalum ya kuongeza weledi na nidhamu?Kama hivyo, ndivyo, program hiyo itadumu kwa muda gani?

Mheshimiwa Spika, ni vema Serikali ikaweka bayana dhamira

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

au lengo la kuongeza muda wa kazi jeshini hadi kufikia saakumi na mbili jioni, ili wanajeshi wafanye kazi kwa moyomkunjufu. Bila kufanya hivyo, watakuwa na dukuduku, nakibaya zaidi ni kwamba, wanaweza kuwa na mgomo baridikutokana na kutoridhika na uamuzi huo, na hivyo kuathiriufanisi na tija ya Jeshi zima.

Mheshimiwa Spika, athari za kuongeza muda wa kufanyakazi kwa Wanajeshi ni nyingi, na zinamgusa Mwanajeshimmoja mmoja na Taifa zima kwa jumla. Athari mojawapokubwa ni kuhatarisha ulinzi na usalama nchini. Katikamazingira ya Dar es Salaam, mathalani, ambako kuna shidaya usafiri, hali ya ulinzi na usalama kuanzia saa 12 jioni hadisaa nne usiku wakati Wanajeshi wanarudi nyumbani, inakuwangumu sana. Polisi wanapata shida kufanya doria kwa kuwakunakuwa na Wanajeshi wengi kwa hiyo inawawia vigumuwakati mwingine kutambua nani mwanajeshi na nanijambazi. Kuna uwezekano mkubwa kwa majambazi kutumiamwanya huo wakavaa kombati za Jeshi na kufanya uhalifuna itakuwa vigumu kuwabaini kutokana na uwepo waWanajeshi wengi mitaani muda huo waliovalia sare zaowakirudi majumbani kutoka kazini.

Mheshimiwa Spika, athari nyingine kubwa ya kuongezamuda wa kufanya kazi ni kudorora kwa mahusiano yakifamilia miongoni mwa wanajeshi. Tukichulia tena mfanowa changamoto ya usafiri Dar es Salaam, ili mwanajeshiaweze kufika kazini saa moja asubuhi ni lazima aweameondoka nyumbani angalau saa kumi na moja alfajiri.Muda huo watoto wake bado wamelala. Kwa changamotohiyo hiyo ya usafiri, atarudi nyumbani saa nne mpaka saatano usiku. Anakuta watoto wamewameshalala. Kwamwendelezo huo, kuna siku watoto hao wanawezawakamwita baba mjomba au mama wakamwita shangazikwa kuwa hawajui kama kweli hao ndio wazazi halisi, kwakuwa hawawaoni.

Mheshimiwa Spika, athari nyingine ni ya kiuchumi. Wanajeshiwalipokuwa wakitoka kazini saa tisa na nusu alasiri walikuwana muda wa kufanya shughuli za kijasiriamali ili kupunguza

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

ukali wa maisha kutokana na posho zao kuwa ni kidogo.Kwa mabadiliko haya ya muda wa kufanya kazi, hakunamuda tena wa kusimamia miradi ya kiuchumi, na matokeoyake hali za kiuchumi za wanajeshi tayari zimeshaanza kuwambaya. Kama Serikali haioni umuhimu wa miradi hii, katikakuwapunguzia wanajeshi ukali wa maisha, basi wawapatiewanajeshi mahitaji yao yote kwa asilimia mia moja iliwaachane na miradi hiyo na kutumikia hadi saa 12 jioni.

Mheshimiwa Spika, athari ya mwisho lakini si kwa umuhimu,ni hatari ya kupungua kwa uwezo wa kuzaa na kupatawatoto miongoni mwa wanajeshi kutokana na uchovumwingi unaosababishwa na muda mrefu wa kazi. Na hiindiyo athari mbaya kuliko zote.

Mheshimiwa Spika, utakumbuka kwamba maandikomatakatifu yanasema kwamba, waana wa Israeliwalipokuwa utumwani Misri, Farao aliwafanyisha kazi nyingii l i wasizaane na kuongezeka kwa kuwa walikuwawanaonekana kuwa tishio kwa wamisri kutokana na wingiwao na uhodari wao katika kufanya kazi. Hivyo ni dhahirikwamba mtu akichoka sana kwa kazi, ile kazi nyingine mbayoni amri ya Mwenyezi Mungu pia, ya kuzaa na kuijaza dunia,inakuwa ni ngumu zaidi kwa kuwa inahitaji nguvu nyingi.

Mheshimiwa Spika, kwa maelezo yote hayo, itoshe tu Serikaliitoe maelezo ya sababu za kuongeza muda wa kufanya kazijeshini ili kuwe na ufahamu wa pamoja baina ya Serikali naJeshi na hivyo kuondoa manung’uniko miongoni mwawanajeshi na hatimaye kuongeza ufanisi jeshini. Aidha, KambiRasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kulieleza Bungehili, iwapo imewalipa wanajeshi posho ya masaa ya ziadaya kazi (overtime allowance) tangu walipoanza kutekelezaamri ya kufanya kazi hadi saa 12 jioni.

3. KUSITISHWA KWA UTOAJI WA FEDHA ZA LIKIZO KWAWANAJESHI

Mheshimiwa Spika, likizo ni stahili ya kisheria ya mtumishiyoyote iwe ni katika sekta ya umma au sekta binafsi. Msingi

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

wa likizo ni kumpatia mtumishi muda wa kupumzika, kubadilimazingira ya kazi na hivyo ku-refresh akili na hatimaye kurudikazini akiwa na ari na nguvu mpya ya kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, zipo likizo zenye malipo na likizo ambazohazina malipo kutegemeana na aina ya kada na taratibuwalizojiwekea. Utaratibu uliopo kwa upande wa Jeshi nikwamba, wanajeshi wanatakiwa kulipwa fedha ya likizo kilabaada ya miaka mitatu, ingawa wanaenda likizo kilamwaka. Hii ina maana kwamba miaka miwili wanakwendalikizo bila malipo na mwaka unaofuata wanakwenda likizoyenye malipo.

Mheshimiwa Spika, yako malalamiko miongoni mwawanajeshi kwamba; malipo ya fedha za likizo, kwa likizozenye malipo yamesitishwa kimyakimya bila wanajeshikupewa taarifa ya kinachoendelea. Kwa mujibu wa taarifakutoka kwa baadhi ya wanajeshi ni kwamba, mara tuwalipoanza kuulizia fedha zao za likizo walitishwa na Chiefof Staff kuwa ni marufuku kuulizia au kuzungumzia popotekuhusu fedha hizo.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikalikulieleza Bunge hil i, kama haitaki wanajeshi watoemalalamiko yao kwa ngazi husika ndani ya Jeshi wanatakawakatoe wapi malalamiko yao? Kitendo cha kuwatishaWanajeshi,kwa kuwapiga marufuku wasizungumzie maslahiyao halali, tena ndani ya mamlaka za ndani ya Jeshi, ni chakulaaniwa na anayefanya hivyo achukuliwe hatua, kwanianachochea hasira miongoni mwa wanajeshi, jamboambalo linaweza kupelekea uasi ndani ya jeshi na kuhatarishaamani na usalama wanchi yetu.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinapenda kuitahadharisha Serikali kuwa, vikosi vya waasikama vile Bhoko Haram, Alshaabab na M23 vilianza kutokanamadai madogo madogo ndani vya vikosi vyao vya Jeshiambayo hayakuthaminiwa wala kushughulikiwa. Hadininapozungumza hapa, kwa mujibu wa taarifa ya DW naBBC ya jana asubuhi ni kwamba, Jeshi la Ivory Coast limeasi

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

kutokana na madai ya malipo ya fedha ambayo Serikali yaIvory Coast haikuyafanyia kazi mapema.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikalikushughulikia madai na mahitaji mengine ya msingiyanayowahusu wanajeshi kwa wakati, kwa kuwayanapoanza kusikika nje yanashusha hadhi ya jeshi letu. KambiRasmi ya Upinzani mathalani, haikupaswa kujua madai hayo,lakini imeyajuwa kwa kuwa, hayapewi uzito unaostahili nawala hayashughulikiwi, na wanajeshi hawaruhusiwikuandamana, hivyo lazima watafute sehemu ya kupumulia.

4. DHANA YA KUBANA MATUMIZI SERIKALINIINAVYOATHIRI MISINGI YA KUANZISHWA KWA JESHI LA ULINZI

Mheshimiwa Spika, kutokana na azma ya Serikali ya awamuya tano kubana matumizi ya Serikali, tayari Mkuu wa Majeshiya Ulinzi na Usalama ameanza kutekeleza azma hiyo, kwakuwaagiza wakuu wa vikosi kumuunga Rais mkono kubanamatumizi ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, akiwa katika ziara ya kutembela vikosimbalimbali baada ya kuapishwa kushika wadhfa huo, Mkuuwa Majeshi alinukuliwa akiwaagiza wakuu wa vikosi kuanzakubuni miradi ya uzalishaji ili waweze kujiendesha kwamatumizi madogomadogo kama vile vifaa vya ofisi(stationeries).

Mheshimiwa Spika, agizo hilo la kufanya shughuli za uzalishajimali linakiuka msingi mkuu wa uanzishwaji wa wa Jeshi laUlinzi ambao ni ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi yetu.Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatambua kwamba kipokitengo cha uzalishaji katika Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT),na kinafanya kazi nzuri. Jambo la msingi ni kuiwezesha (SUMAJKT) ili izalishe kwa wingi na na kuchangia gharama hizo nasio kulifanya Jeshi zima kuwa la uzalishaji.

5. MANUNUZI YA VIFAA MBALIMBALI JESHINI

Mheshimiwa Spika, ninapozungumzia vifaa jeshini nadhani

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

naeleweka, vifaa jeshini siyo vifaa vya kawaida, ni vifaaambavyo ni ‘sensitive’, na kwa maana hiyo, manunuzi yakepamoja na utunzaji wake, lazima ufanywe kwa makini naweledi wa hali ya juu ili kuepuka madhara yanayowezakutokea kutokana na ‘mismanagement’.

Mheshimiwa Spika, zipo taarifa kwamba maafisa wa ngaziza juu waliopo kwenye bodi ya manunuzi ndio wanojipanafasi ya kwenda nje kununua vifaa hivyo na kuwaachamaafisa wenye utaaalam na vifaa hivyo. Matokeo yake nikwamba vinanunuliwa vifaa vinavyogharimu mabilioni yafedha, ambavyo ama vimepita muda wake wa matumizi,au havifai kutumiwa katika mazingira yetu na hivyokuisababishia hasara Serikali.

[MANENO YAMEONDOLEWA KWA MAELEKEZO YA SPIKA]

Mheshimiwa Spika, hii inatokana na bodi ya manunuzikutofuata taratibu za manunuzi, na sababu kubwa yakutokufanya hivyo, ni tamaa ya fedha. Imebainika kwambawanajipangia kwenda kufanya manunuzi hayo, ili wapateposho ya safari, na maslahi mengine. Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali ‘with a serious note’ kwamba; isifanye mzahakwenye eneo hili la manunuzi ya vifaa, kwani licha ya eneohilo kutumia fedha nyingi, pengine kuliko maeneo yote, lakinimadhara yanayoweza kutokea kutokana na kununua vifaavibovu, au vilivyopitwa na wakati ni makubwa zaidi. Aidha,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaishauri Serikali,kuitazama upya bodi hiyo ya manunuzi – kwa maana yauhakiki wa taaluma zao ili kujiridhisha kama bado ina uwezona weledi wa kufanya kazi hiyo.

6. NAFASI YA MKUU WA MAJESHI KATIKA KUJENGA JESHIIMARA LENYE NIDHAMU, UTII NA MSHIKAMANO

Mheshimiwa Spika, wakati Mkuu wa Majeshi Mstaafu GeneraliDavis Mwamnyange anamkabidhi Mkuu mpya wa Majeshialimwambia kwamba amelitoa jeshi kwenye tope nakulifikisha sehemu nzuri na kwamba, mkuu huyu wa sasaalifikishe kwenye lami.

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

Mheshimiwa Spika, bila shaka maneno hayo ya Mkuu waMajeshi Mstaafu yanaashiria kwamba alijali sana maslahi yawanajeshi wake, na kwa maana hiyo, nidhamu ilikuwa juu,jeshi lilikuwa na mshikamano wa hali ya juu, utii wa hali yajuu na zaidi ya yote walimpenda Mkuu wao wa Majeshi. Jeshilinapokuwa na nidhamu ya hali juu, utii na mshikamanohakuna shaka jeshi hilo linakuwa imara pia.

Mheshimiwa Spika, yapo malalamiko miongoni mwawanajeshi kwamba mara tu baada ya Mkuu mpya wa Majeshikuanza kazi, kuna mabadiliko mengi yametokea ambayoyanawaathiri wanajeshi na familia zao moja kwa moja.Miongoni mwa mabadiliko hayo ni kama vile kuongeza mudawa kufanya kazi bila kutoa sababu yoyote, nafasi zawanajeshi kujiendeleza kielimu (elimu za kiraia) ambazozilikuwepo kipindi cha nyuma sasa zimefutwa; wanajeshiwanaokwenda kwenye kozi za kijeshi hawapewi rationallowance ingawa fedha hiyo iliidhinishwa na bunge. Aidha,wakati uliopita wanajeshi walihimizwa kumiliki vyombobinafsi vya usafiri ili kuwasaidia kurahishisha shughuli zaonyingine, lakini sasa inasemekana vyombo hivyo vya kiraiani uchafu kwenye mazingira ya jeshi na kwa maana hiyohavitakiwi.

Mheshimiwa Spika, siku za nyuma bidhaa katika madukaya bei nafuu jeshini (duty free shops) zilikuwa na ruzuku yaSerikali na hivyo wanajeshi walikuwa wanapata bidhaa hizovikiwemo vinywaji, kwa bei nafuu. Sasa hivi maduka hayoyameondolewa kwa ahdi kwamba wanajeshi wangepewashilingi laki tatu ili kuweza kujinunulia bidhaa kwa bei zauraiani. Hii shilingi laki tatu imetolewa mara moja tu, na hainamaelezo kama itakuwa inatolewa kila mwezi au kila baadaya miezi sita au vinginevyo. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,inataka Serikali kulieleza bunge hili, hiyo shilingi laki tatuitakuwa inatolewa kila baada ya muda gani?

Mheshimiwa Spika, malalamiko mengine ni pamoja nakutopandishwa vyeo hata kwa wale waliokidhi vigezo vyakukaa kazini kwa miaka minne, na wenye sifa stahiki zakupandishwa vyeo. Aidha, nauli kwa safari za kikazi

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

hazitolewi. Askari akipangiwa safari inabidi ajitafutie nauli,na nauli hiyo hairudishwi. Inasemekana jambo hil ilinawaumiza sana askari wa vyeo vya chini ila wakubwawakisafiri wanapewa nauli mara moja. Yapo pia malalamikokwamba wanajeshi waliohamishiwa Dodoma hawajalipwafedha zao za uhamisho, na wanaishi kwa taabu.

Mheshimiwa Spika, mambo haya yote, kwa tafsiri nyepesi,ni kwamba, hayatalipeleka jeshi kwenye lami, baliyanalirudisha kule kwenye tope ambapo lilikuwa limeshatokahuko. Kutokana na hali hii, kuna viashiria vingi vyamanung’niko na hali ya kutoridhika miongoni mwawanajeshi, jambo ambalo linaweza kusababisha kupunguakwa utii au imani (loyalty) kwa uongozi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaishauri Serikalitena kwa msisitizo mkubwa kuhakikisha kwamba suala lamahusiano mazuri miongoni mwa wanajeshi na hususanuongozi na wanajeshi wengine linafanyiwa kazi harakaiwezekanavyo ili kuwe na jeshi moja lenye upendo namshikamano. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Seirikali kutatua kero zote zinazolalamikiwa nawanajeshi ili wafanye kazi kwa ari zaidi.

7. HUDUMA YA NISHATI YA UMEME KATIKA MAKAMBI YAJESHI

Mheshimiwa Spika, ni jambo linalofahamika kwamba, taasisiza umma hulipia gharama za huduma mbalimbali kama vilehuduma za maji na umeme, kupitia bajeti ya matumizimengineyo (OC) inayotolewa na hazina. Hata hivyo, taasisinyingi za umma yakiwemo majeshi yetu zimekuwazikishindwa kulipia huduma hizo kutokana na bajeti ndogoya matumizi mengineyo na mbaya zaidi fedha za OChazitolewi kwa ukamilifu wake na hata hizo kidogozinazotolewa, hazitolewi kwa wakati. Kutokana na hali hiyo,taasisi nyingi za umma zimekuwa wadaiwa sugu wa shirikala umeme (TANESCO), na makampuni au mashirikambalimbali yanayotoa huduma za maji.

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

Mheshimiwa Spika, dawa ya kuondokana na udaiwa sugukwa taasisi za umma yakiwemo majeshi ni Serikali kutoafedha za matumizi mengineyo kwa utoshelevu na kwawakati na sio Serikali kuyaamuru makampuni au mashirikayanayotoa huduma kukata huduma hizo kwa taasisi zaumma.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinatafsiri kitendo cha Mkuu wa Nchi kuiamuru TANESCOkukata umeme kwenye makambi ya Jeshi kuwa nikuhatarisha usalama wa nchi. Jeshi ni taasisi nyeti katikausalama wa nchi, na kwa maana hiyo, Serikali inatakiwakuhakikisha kuwa, huduma zote zikiwemo maji, umeme, afyan.k zinapatikana kwa utoshelevu ili Jeshi liweze kuendeleakufanya kazi zake za kulinda usalama wa nchi yetu dhidi yaadui yoyote. Ikiwa jeshi limeshindwa kulipia huduma hizo,basi Serikali ndiyo inayotakiwa kuwajibika kwa kutotoa fedhaza kutosha za OC kulipia gharama hizo.

8. USALAMA WA MIPAKA YA NCHI

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na mvutano kuhusu mpakawa Malawi na Tazania hususan katika Ziwa Nyasa. Hatahivyo, Serikali kwa nyakati tofauti imekuwa ikisema kwambamgogoro huo unashughulikiwa kwa ajil i ya kuupatiaufumbuzi.

Mheshimiwa Spika, licha ya Serikali kusema kuwa, kuna dalilinjema ya maafikiano kuhusu mgogoro huo, kuna viashiriakwamba majirani zetu wa Malawi hawaafikiani na usuluhishiwowote utakaowafanya wasimiliki ziwa lote la Nyasa.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Mtandano wa‘extractives’ ni kwamba Serikali ya Malawi imewekamsimamo kwamba haitakubaliana na usuluhishi wowoteambao utaipa Tanzania sehemu ya Ziwa Nyasa. Na jambohili linathibitishwa na Kauli ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongoziwa Serikali ya Malawi, Bwana George Mkondiwa kwamba;“Malawi will never, and has never, at any time, acquiescedto Tanzania’s unwarranted and unjustified territorial claims,”

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

Mheshimiwa Spika, kauli kama hiyo, kutoka kwa kiongozimkubwa katika Serikali ya Malawi, huku mazungumzo yausuluhishi yakiendelea, kwa vyovyote vile ni kauli nzito naTanzania haipaswi kuipuuza. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inataka kujua mazungumzo yaliyokuwayakiendelea kuhusu usuluhishi wa mgogoro wa mpaka katikaya Tanzania na Malawi yemefikia wapi, na ni nini hatima yamgogoro huo. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kueleza hali ya usalama wa Mipaka ya Tanzania kwaujumla wake, ambayo kwa siku za nyuma iligundulika kuwabeacons za mipaka hiyo zilikuwa zimeng’olewa na pia raiakutoka nchi jirani walikuwa wanaingia nchini mwetu kwanjia za panya kutokana na mipaka yetu kupenyeka kirahisi.

9. NAFASI YA JESHI KATIKA KUPAMBANA NA MATUKIOYA KIGAIDI NCHINI.

Mheshimiwa Spika, siku za hivi karibuni kumekuwa namatukio ya kigaidi ya kuvamiwa kwa vituo vya Polisi na watuwasiojulikana na kupora silaha, kuwauwa askari Polisi nakuporwa silaha, pamoja na wananchi kuuawa na hususanviongozi wa Serikali za Mitaa katika Wilaya ya Rufiji mkoaniPwani.

Mheshimwa Spika, matukio haya yanaashiria kwamba watuwanaoyafanya ni watu wenye mafunzo ya kijeshi na mbinuza kivita ndio maana wameweza kutekeleza uhalifu huo bilakukamatwa na bila kujulikana kwa majina yao, na hatawalikoelekea.

Mheshimiwa Spika, kuna kila dali l i kwamba Polisiwamezidiwa mbinu na nguvu ya kukabiliana na magaidihao. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinashauri na kupendekeza Jeshi la Ulinzi liingilie kati na hususankitengo cha upelelezi wa kijeshi (Millitary Intelligence) ili kutoamsaada wa ki-pelelezi na hatimaye kuwabaini nakuwashughulikia wahalifu hao.

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

10. UTEUZI WA WANAJESHI KATIKA NAFASI ZA KISIASA

Mheshimiwa Spika, katika hotuba yake mwaka jana, MsemajiMkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alizungumziaathari za kuwateua wanajeshi katika nafasi za kisiasa.allionyesha jinsi ambavyo mwanajeshi anayeteuliwa kuwaMkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa anavyounganishwa nachama tawala, kwa kutakiwa kuwa mjumbe wa Kamati yasiasa ya chama katika Wilaya au Mkoa husika. Kuunganishwahuku na chama, kumewekwa bayana na Katiba ya CCM yamwaka 1977, katika ibara ya 80(1) (c) inayowataja Wakuuwa Wilaya kuwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCMkatika Wilaya husika, na Ibara ya 94(1) (c) inayowataja Wakuuwa Mikoa kuwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM katikamikoa husika.

Mheshimiwa Spika, kitendo cha katiba ya CCM kuwatambuaWakuu wa Wilaya na Mikoa kama wajumbe wa Kamati yaSiasa ya Wilaya au Mkoa husika, kunadhihirisha kwamba,wakuu hao ni wanachama wa chama cha siasa, na kwamaana hiyo ni wanasiasa. Kwa hiyo, Mwanajeshianayeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya au Mkoa automaticallyanakuwa mwanachama wa CCM.

Mheshimiwa Spika, katika maelezo yake, alinukuu Ibara ya147 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniainayosema kwamba, “Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshiyeyote kujiunga na chama chohote cha siasa, isipokuwa tukama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibaraya 5 ya Katiba hii”. Aidha, Ibara ndogo ya (4) inasemakwamba; Kwa madhumuni ya ibara hii, “mwanajeshi” maanayake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au yakudumu katika Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magerezaau Jeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Spika, uteuzi huu wa wanajeshi kushika nafasiza kisiasa umetanuliwa wigo wake, ambapo sasa wanajeshiwanaanza kuteuliwa na chama tawala kuwa viongozi wachama. Uteuzi wa Kanali Ngemela Eslom Lubinga kuwaKatibu wa NEC ya CCM - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

ni uthibitisho kwamba Jeshi linaingizwa kwenye siasakidogokidogo (Politicization of the army)

Mheshimiwa Spika, athari za jambo hili ni kwamba jeshilitaanza kupoteza ile sifa yake ya kuwa Jeshi la Wananchi nabadala yake litaanza kufanya kazi kwa bias – kwa kupokeaamri na maagizo ya chama tawala. Athari kubwa zaidi nikwamba, utawala wa kiraia (civil governance) utapotezamaana yake.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinatafsiri kitendo cha kuendelea kuwateua wanajeshi kushikanafasi za kisiasa hata baada ya kutahadharishwa, nimwendelezo wa vitendo vya Serikali hii ya awamu ya tano,vya kupuuza Katiba ya nchi yetu, jambo ambalo halina afyasana katika utawala bora. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoa maelezo mbeleya Bunge hili, ni kwa nini haiheshimu katazo la ibara ya 147(3)na (4) ya Katiba kuhusu wanajeshi kujihusisha na kazi za siasa?

Mheshimiwa Spika, sambamba hilo, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kutoa maelezo ni kwanini wanajeshiwanaoteuliwa kushika nafasi za kisiasa wanaendelea kuvaauniform za kijeshi wakati ilitakiwa wastaafu kwanza jeshi ilisasa wawe watumishi wa umma?

11. POSHO YA CHAKULA KWA WANAJESHI (RATIONALLOWANCE)

Mheshimiwa Spika, kwa miaka mingi, Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni imekuwa mstari wa mbele kutetea maslahiya wanajeshi wetu ikiwemo posho ya chakula (rationallowance). Msingi wa kutetea maslahi ya wanajeshi nikuwapatia wanajeshi wetu lishe bora na kuwafanya wawena nguvu ya kuhimili mazoezi na kazi mbalimbali za kiaskariwanazofanya. Aidha, lengo jingine ni kuwafanya wawe nautulivu wa ndani ili waweze kufanya kazi yao ya kulindausalama wa nchi yetu wakiwa hawana mawazo ya kwambawatakula nini pamoja na familia zao.

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

Mheshimiwa Spika, utaratibu uliopo ni kwamba, posho hiiya chakula hutolewa moja kwa moja kwa akari kila mwezi.Askari anayepokea posho hii huwa na uhuru nayo wakuitumia kwa namna yoyote ile ikiwa ni pamoja na kuitumiana familia yake.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazotaarifa kwamba kuna mkakati wa kubadili mfumo wa utoajiwa posho hiyo kwa wanajeshi. Utaratibu mpya unaotakakuanza kutumika ni kwamba wanajeshi hawatapewa tenaposho hii moja kwa moja kwenye akaunti zao za benki,isipokuwa ataitwa mzabuni wa kuwapatia wanajeshichakula, na ile posho ya chakula atapewa mzabuni.

Mheshimiwa Spika, tafsiri ya utaratibu huo ni kwamba sasawanajeshi wanalazimishwa kula chakula kwa mzabuni nawasipofanya hivyo, posho hiyo itakuwa haiwahusu. KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inaona kwamba huo ni udhalilishajiwa hali ya juu kwa wanajeshi wetu. Wanajeshi ni watuwazima wanajua ni saa ngapi wale chakula na kwa kiasigani hivyo lazima tuwaheshimu, na tusiwachukulie kamawatoto wa shule ya msingi. Ikumbukwe pia kwamba poshohii inavyolipwa kwa mwanajeshi moja kwa moja anakulapia na familia yake. Kumlazimisha mwanajeshi ale kazini pekeyake ni kuikosesha familia yake riziki ya chakula pia. Huu niubinafsi na uchoyo wa hali ya juu kabisa unatoka kufanywana Serikali.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka serikali kuufuta utaratibu huo, na kuendelea kutoaposho ya chakula moja kwa moja kwa wanajeshi.

12. USHIRIKIANO WA KIJESHI NA MATAIFA MENGINE

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinatambua Jeshi la Wananchi wa Tanzania linashiriki katikaoperesheni za kijeshi katika mataifa mengine kupitia katikaMpango wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika na ule waUmoja wa Mataifa.

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba ushiriki huounaliongezea jeshi letu uzoefu wa kufanya kazi katikamazingira tofauti tofauti, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Serikali kutafakari upya faida hususan za ki-uchumina ki-teknolojia ambazo kama taifa tunanufaika nazo kwaJeshi letu kushiriki katika operesheni hizo.

Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa kuwa sera ya uchumiya nchi yetu kwa sasa inasisitiza mapinduzi ya viwandaambapo ili tufanikiwe, ni lazima tuwe na mkakati maalumwa uvumbuzi na ugunduzi wa sayansi na teknolojia ambayokwa kiasi kikubwa inapatikana katika nchi zilizoendelea.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilielezakatika hotuba yake mwaka jana kwamba, nchi ambazozimeendelea tayari kama vile Marekani na Uingerezahazipeleki majeshi yao kupigana vita au kulinda amani katikanchi nyingine kama hakuna maslahi yoyote na hasa ya ki-uchumi kwa mataifa yao. Na ndio maana sera zao zamambo ya nje ziko bayana kwamba ni maslahi ya nchi zaokwanza ndio mambo mengine yafuate.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekezahivi kwa sababu kama taifa tusipojipanga kimkakati zaidi,tutaishia kupokea miili ya wanajeshi wetu waliokufa katikaoperesheni hizo huku taifa likibaki bila manufaa yoyote. Kwasababu hiyo, tunapendekeza kwamba kuwe na malengomahsusi na ya kimkakati Jeshi letu linapokwenda kushirikioperesheni katika mataifa mengine. Mikakati hiyo iwe nipamoja na kufanya utafiti wa masuala ya kiuchumi nakiteknolojia – yaani kwa maneno mengine wafanye ujasusiwa kiuchumi (economic espionage) ili baada ya opereshenihizo kuwe na faida ya kidola itakayopatikana na sio tumaslahi ya kifedha wanajeshi wanayopata kwa kushirikioperesheni hizo.

13. JESHI LA KUJENGA TAIFA NA UZALISHAJI WA CHAKULA.

Mheshimiwa Spika, ni aibu kwa taifa hili kuwa na matukioya ukosefu wa chakula na njaa huku kukiwa na Jeshi la

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

Kujenga Taifa. Miaka iliyopita tulipendekeza kuwa pamojana mambo mengine, jeshi hili lipimwe kwa uzalishaji ambaolitakuwa limefanya . Tulieleza kwamba; dhima ya Jeshi laKujenga taifa ni kwamba pamoja na mambo mengine, linawajibu wa kuwafunza vijana wetu kufanya kazi za uzalishajimali kwa ajili ya kujenga uchumi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniimekuwa ikishauri miaka nenda miaka rudi kwamba; Serikaliitumie nguvu kazi iliyopo kwenye Jeshi la Kujenga Taifa katikakujenga uchumi wa kweli nchini, na hasa kipindi hiki chauchumi wa viwanda Jeshi la Kujenga Taifa ndio lilitakiwalitoe dira ya namna ya kuwa a uchumi wa viwanda. Tulishaurikwamba Serikali itenge mashamba makubwa ili vijana hawawawapo mafunzoni, wafanye mafunzo kwa vitendo yakilimo ili nchi iweze kujitegemea kwa chakula. Aidha,tuliishauri Serikali iwaagize wakuu wa makambi ya JKTkutengeneza programu maalum za uzalishaji mali katikasekta mbalimbali kama vile kilimo, viwanda, ufundi, uvuvink kila mwaka. Tulipendekeza pia kwamba, Waziri mwenyedhamana awe anatoa taarifa ya uzalishaji uliofanywa naJKT na mapato (maduhuli) yaliyopatikana kutokana nauzalishaji huo katika kila Bunge la bajeti.

Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa ushauri huo kwa sikunyingi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kupewamrejesho wa utekelezaji wa ushauri huo. Serikali ilieleze Bunge,JKT imekeleza miradi mingapi ya uzalishaji na imeingiza fedhakiasi gani kutokana na uzalishaji huo, na ina mpango wakuteleza miradi mingapi kwa mwaka wa fedha 2017/18.

14. UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA YA ULINZI NA JESHILA KUJENGA TAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17

Mheshimiwa Spika, kumeanza kutokea mazoea mabaya yautekelezaji duni wa bajeti ya maendeleo katika wizara hiijambo ambalo linatia wasiwasi kama kweli serikali ina niaya dhati ya kupandisha ubora na ufanisi wa majeshi yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

bajeti ya wizara hii, fedha ya kutekeleza miradi ya maendeleoliyoidhinishwa na bunge katika fungu 38 (Ngome) ilikuwa nishilingi bilioni 10, lakini hadi machi 2017 ilikuwa imetolewashilingi bilioni 1 tu sawa na asilimia 10 ya fedha iliyokuwaimeidhiniswa. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikalikulieleza Bunge hili, hiyo bilioni moja iliyotolewa, ndiyoitaweza kununua zana za kisasa zinazoendana na teknolojiaya sasa, na kutoa mafunzo ya kijeshi ya kisasa na kupandishaubora na ufanisi wa jeshi kwa kiwango tunachokusudia?

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa fungu 39 (JKT), fedha yamaendeleo iliyoidhinishwa na Bunge ilkuwa ni shilingi bilioni8, lakini hadi machi, 2017 ilikuwa imetolewa shilingi bilionimoja tu, sawa na asilimia 12.5 ya fedha iliyoidhinishwa nabunge. Hii ina maana kwamba bajeti ya maendeleo katikafungu hili haijatekelezwa kwa asilimia 87.5. Kambi Rasmi yaUpinzani inahoji, JKT itawezaji kutekeleza miradi yake yamaendeleo kwa madhumuni ya kujenga taifa ikiwamwenendo wa utekelezaji wa bajeti uko namna hii? Aidha,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutoamaelezo ni kwani nini JKT imekusanya maduhuli kidogo(asilimia 31.8 tu) wakati ina miradi mingi ya uzalishaji chini yaSUMA JKIT?

Mheshimiwa Spika, halikadhalika kwa upande wa wizara,fedha iliyokuw imeidhinishwa na bunge ilikuwa shilingi bilioni230, lakini hadi kufikia machi, 2017 shilingi bilioni 33.9 tu sawana asilimia 14.7 ilikuwa imetolewa.

Mheshimiwa Spika, tafsiri nyepesi ya utekelezaji huu duni wabajeti ya maendeleo, unairudisha nyuma wizara naunapunguza ufanisi, ubora na tija ya majeshi yetu. KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inataka Serikali, kwa kadri ile ileambayo inalisifu jeshi letu kuwa ni imara, lenye weledi naufanisi mkubwa, basi sifa hizo zionekane kwenye utekelezajiwa bajeti ya maendeleo ya majeshi hayo. Vinginevyoitakuwa tunajifurahisha tu kwa maneno kumbe hali halisi nimbaya.

Mheshimiwa Spika, katika randama yay a wizara ya Ulinzi

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

na Jeshi la Kujenga Taifa (Fungu 57) kuna baadhi ya vitengohavikutengewa fedha kabisha tena fedha za mishahara. Kwamfano Subvote 1005 – Procurement Management, uk. 18hakuna fedha yoyote iliyotengwa kwa ajili ya mshahara;Subvote 2003 – Building Consulting Unit, uk. 36 haikutengewafedha za mshahara na Subvote 2004 – Estate Managementand Development Unit uk.39 hakuna fedha ya mshahara.Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kulielezaBunge hili, ni kwa nini vitengo hivyo havijatengewa fedha zamishahara kwa muwa wa fedha 2017/18 au vitengo hivyohavina watendaji?

15. HITIMISHOMheshimiwa Spika, naomba nimalizie hotuba yangu kwakulipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa umahiriwake; kwa jinsi linavyoendesha operesheni zake; lakini zaidisana kwa jinsi linavyojishughulisha na masuala ya kijamiikunapotokea maafa na majanga mbalimbali. Hata hivyo,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ingependa kujua Jeshilimesaidia vipi kutoa msaada kwa wananchi waliokumbwana mafuriko kipindi hiki cha masika.

Mheshimiwa Spika, ni matamanio ya kila raia wa Tanzaniakuona Jeshi letu likiendelea kupanda viwango vya ubora naufanisi na hivyo kuwa na tija. Hata hivyo ili viwango vipande,lazima mambo kadhaa yashughuliwe kikamilifu. Kwanza,Serikali ihakikishe kwamba, bajeti inayoidhinishwa na Bungekwa ajili ya majeshi yetu inatolewa kwa wakati na kwaukamilifu wake. Pili, Serikali ihakikishe kwamba, maslahi nastahiki zote za wanajeshi zinatolewa kwa wakati na kwaukamilifu wake ili kuondoa manung’niko miongoni mwawanajeshi na hivyo kuwangezea morali ya kufanya kazi kwamoyo. Tatu, Serikali ihakikishe kwamba kuna mahusianomazuri kati ya uongozi wa Jeshi na maafisa wengine wa Jeshiili kuwa na Jeshi imara lenye mshikamano, utii na nidhamuya hali ya juu.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaamini kwamba, mambo hayo yakifanyiwa kazi kwa dhati,Jeshi letu litaendelea kupanda viwango vya ubora na hivyo

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

kuendelea kushikilia nafasi yake katika medani za kimataifakwamba, ni miongoni mwa majeshi yenye weledi nanidhamu ya hali ya juu duniani.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombakuwasilisha.

Mwita Mwikwabe Waitara (Mb)Kny. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA

UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA ULINZI NAJESHI LA KUJENGA TAIFA

16 Mei, 2017

MHE. UPENDO F. PENEZA: Mwongozo wa Spika.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kuna tangazodogo hapa, nawatangazia kuwa Kampuni ya simu TTCL ipohapa katika viwanja vya Bunge kuanzia tarehe 15 hadi 19,wanatoa huduma mbalimbali za mawasiliano, tafadhalimnaombwa kwenda kuonana nao.

Waheshimiwa Wabunge, mnatangaziwa piamchukue nyaraka zenu kwenye visanduku vya kuhifadhinyaraka ili Bunge lipate nafasi ya kuweka nyaraka zingine.Kwa hiyo, mnakuja humu ndani, mnazozana nyarakahamzisomi ziko kwenye pigeon hole.

Tangazo kwa Waheshimiwa Wabunge wote wa Imaniya Kikristo, Waheshimiwa Wabunge wote wanatangaziwakuhudhuria Ibada katika eneo la Chapel yetu ya Pius Msekwaghorofa ya pili. Aidha, tutakuwa na Mtumishi Laizer katikaIbada hiyo na kwaya ya Jerusalem kutoka Kanisa la AnglikanaKisasa. Waheshimiwa Wabunge wote wanakaribishwa.

Waheshimiwa Wabunge, tunaanza mjadala.

MHE. UPENDO F. PENEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mwongozo wa Spika.

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

MWENYEKITI: Pendo unasemaje?

MHE. UPENDO F. PENEZA: Mheshimiwa Mwenyekitinasimama na Kanuni 68(7).

MWENYEKITI: Wewe hata usisome sema tu.

MHE. UPENDO F. PENEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,sawa. Wakati Mheshimiwa Waitara akisoma hotuba yaKambi Rasmi ya Upinzani, kuna eneo la ukurasa Na. 12ambalo lilifutwa kwa kutokana na mwongozo alioombaMheshimiwa Mkuchika, lakini maelezo ambayo yanatokanana ukurasa Na. 12 yapo katika Ukurasa Na. 19 katika sehemuya posho ya chakula ya Wanajeshi kwa maana ya rationallowance. Ukiangalia katika ukurasa huo wa 12 hakuna kituambacho kipo classified kama ambavyo inaelezwa zaidi yakuelezea maslahi na huduma bora kwa ajili ya Wanajeshiwetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba Mwongozowako, kama ukurasa na 19 aya 11 imekubalika kwa ninisehemu hiyo ya ukurasa Na. 12 imeondolewa wakatiinaongelea manufaa hayo ya Wanajeshi. Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante. Nimeshakuelewa kaa chini.Viwango vya level za classified information. Kaa kwanzaunasimama! Tafsiri ya classified Information wewe huwezikujua, kaa chini.

MWENYEKITI: Waheshimiwa tunaanza Fakharia,Shomar Hamis, Jasson Rweikwiza na Mheshimiwa MasoudSalim atafuata.

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Kwanza sina budi kumshukuruMheshimiwa Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bungekwa kazi nzuri mnayoifanya humu ndani ya Bunge, kwauweledi mliokuwa nao na kazi nzuri iliyotukuka, lazimampongezwe.(Makofi)

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina budi kumpongezaMheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa naWatendaji wake kwa kazi aliyotuletea hapaametufahamisha, tumeelewa, lakini wenzetu wa upande wapili walikuja na kashfa hawakuja na maelezo ya kuujulishaumma. Kwa mfano, mtu anazungumza Jeshini wanafanyakazi saa moja na nusu….

MWENYEKITI: Mheshimiwa Fakharia subiri, mnasemaje

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,tunaomba Msemaji anayesema ama afute maneno yake,asitoe kashfa kwa upande wa pili kwa hicho anachokiongeakwamba hatujaja na point, tumekuja tu na mambo yasiyoya msingi kwa kweli kama ana hoja ajibu hizo.

MWENYEKITI: Kaa chini ahsante nimekuelewa.

Waheshimiwa Wabunge, hoja za Upinzani zitajibiwana Serikali. Jielekezeni kwenye hoja za msingi za masuala yaWizara ya Ulinzi, hakuna sababu ya kusimama kusema huyukasema hiki, huyu kasema hiki. Tupo kwenye Bunge,Wapinzani wana wajibu wa Kikatiba kusema ambayowanataka kuyasema na wameyasema yaliyoruhusiwayatajibiwa na Serikali, mamlaka ambayo ipo competent naina majibu sahihi ya kuwajibu.

Kwa hiyo, nakuomba Mheshimiwa Fakharia endeleana mjadala wako kwenye hoja za msingi. Kuna matatizomengi Zanzibar yazungumzie hayo, acha mambo mengineambayo Serikali itafanya kazi ya kujibu. (Makofi)

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante, lakini habari ndiyo hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hil i suala nil itakakulizungumza kwa sababu tayari Wanajeshi walikuwawanagombanishwa na Serikali yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina budi kumpongeza

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

Mheshimiwa Waziri kwa sababu Zanzibar iko kwenye hali yaamani na utulivu, kuanzia uchaguzi uliofanywa wa marudiowalikuwepo Wanajeshi wakaweza kuiweka hali ya salamana utulivu na hadi leo hali hiyo inaendelea ya usalama nautulivu, tunashukuru. Sina budi kuzungumza...

TAARIFA

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Naomba nimpe taarifa mzungumzaji Mamayangu anayeongea siyo kazi ya Jeshi la Wananchi kusimamiauchaguzi, hiyo ni kazi Jeshi la Polisi. Kwa hiyo, kama anatakakuwashtaki kwamba walifanya uchaguzi wa Zanzibaratuambie vizuri, kazi ya Polisi ndiyo ya kusimamia Mambo yaNdani.

MWENYEKITI: Ahsante umeshaeleweka. MheshimiwaFakharia.

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Taarifa yake siipokei kwa sababu ilikuwaishara tayari walishaonesha upande wa pili na waliowezakutuliza ni Jeshi waliofanya kazi na tukaenda kwa amani nautulivu. Polisi walikuwepo wakifanya shughuli zao na waowalikuwa wakiangalia amani na utulivu wa nchi yetu na hadihii leo tunaendelea kuwa na amani na utulivu katika nchiyetu. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Fakharia hebu kaa kwanza.

Waheshimiwa Wabunge, nataka tumalize hii bajetini ya siku moja tu, tunamaliza leo jioni. Hizi interruptionambazo naziona zinataka ku-delay mpango wa bajeti hiisitokubali na maneno ya Wabunge mnaochangia humundani, Mbunge yeyote atakayeenda kinyume na taratibu wachama chochote humu ndani, nitamdhibiti.

Waheshimiwa Wabunge, hivyo sitaki taarifa, sitakimwongozo, nitasikiliza watu wawili tu, Chief Whip waUpinzani na wa Serikali basi. Mheshimiwa Fhakharia endelea.

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante, nilindie muda wangu. Naombakuzungumzia habari ya viwango vidogo vya pensheniwanavyolipwa askari wastaafu wa zamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila siku tunavyokwenda haliya maisha inapanda na siku zinavyokwenda mishaharainapanda, lakini wale wastaafu wa zamani kiwangokinakuwa kiko kile kile, ambapo hakiongezeki. Sasaningemwomba Mheshimiwa Waziri awe anaangalia, baadaya muda na wale askari wastaafu wa zamani viangaliweviwango vyao. Kama kuna Koplo/Sajenti/Luteni Kanali wasasa kastaafu basi na wale kiwango kile kile kwa mwaka ulewaweze kuwapa wasiwaachie kile kiwango duni ambachowanacho na kinaweza kuwapa maradhi, labda akapatasukari, pressure matumizi yake yatakuwa madogo wakatimatumizi yako juu na yamepanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja na suala lingine laJKT. JKT Mheshimiwa Waziri kaizungumza katika ukurasa wa26 na amezungumza vizuri, tunakupongeza. Lakininingekuomba Mheshimiwa Waziri idadi ya vijana wa Zanzibarwanaokwenda JKT utuongezee. Kwa sababu umesema kulewanapata elimu ya ukakamavu, elimu ya kujiajiri na elimuya kuajiri wenzi wao. Sasa ukituongezea idadi ya vijana wetuwakaenda kule wakarejea tena kufanya kazi hiyo ya kwendakujiajiri, wakawa wakakamavu watapata ajira nyingi zaukakamavu, watapata kujiajiri wao na wenzi wao. NaombaMheshimiwa Waziri ulipokee ili uweze kutusaidia kwa upandewa Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumzia eneo lamambo ya kuingiliana baina ya majeshi na raia mitaani. Kunamaeneo kimazingira ni magumu, kuna maeneo ambayowanayo jeshi lakini maeneo yale yalikuwa ya raia hapo wakatiwa mabibi na mababu zetu, lakini jeshi sasa hivi imehodhi.Watu wa pale ilikuwa inabidi walipwe kwa kutoa viwanjavyao lakini huwa hawalipwi hivyo kunakuwa na mvutanobaina ya raia na Jeshi. Sasa liangalie hili na kwa upande

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

wenyewe tuangalie, kama upande wa Unguja Ukuu,Kisakasaka matatizo hayo yapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna mengine,wanajeshi wanawalipa raia, lakini baada ya kuwalipa raiahawaondoki sehemu ile na ninyi mnakuwa hamna uthibitiwa kuyazuia yale maeneo yenu; sasa kunakuwa mvutanomwingine mpya. Utayakuta haya kama kule Dunga, MgeniHaji, sasa na hayo myaangalie. Kama mtu mmeshamlipaaondoke, kama hamjawalipa na wamekubali kuondokaitabadi muwalipe ili kuweka amani na utulivu uliokuwepo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo ya Jeshi lazimamfanye utafiti kwa sababu hivi sasa maeneo ya Jeshiyameshaingiliana na ya raia. Bila kufanya utafiti mkawezakujua sehemu zenu ziko wapi na za raia ziko wapi hapomwisho kutazuka mtafaruku baina ya Jeshi na raia. Mimininajua Ninyi Wanajeshi ni wasikivu, walinzi na piamnawapenda raia wenu. Sasa naomba Mheshimiwa Wazirina hili mliangalie ili kuondoa mtafaruku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machachenaunga mkono hoja, sina matatizo. (Makofi)

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia katikaWizara hii, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naombanimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ulinzi naUsalama, JKT na wasaidizi wake wote na Wakuu wa Majeshikwa kazi nzuri wanayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze MheshimiwaRais Magufuli kwa kazi nzuri sana ya kuendelea kuiweka nchiyetu katika hali ya usalama na amani. Unaposikia amaniinakuwepo si kazi rahisi, ni kazi ya Mheshimiwa Magufuli.(Makofi)

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaenda kwenyemchango wangu, na leo nitaongelea mikataba yakimataifa; kwanza niweke vizuri Taarifa ya Kambi Rasmi yaUpinzani ambayo imepotosha mambo mengi. Moja ya eneoambalo imepotosha wanashauri kwamba jeshi litumikekufanya economic espionage; hii si kazi ya jeshi, economicespionage si kazi ya jeshi, tuwaachie wanaohusika na hiyowafanye si wanajeshi. Lakini maeneo mengine ambakowamepotosha yako mengi...

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: …wanazungumzia kuhusuAl-Shabab na Boko Haram.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa nimeshasema taarifa sasahivi nimezizuia napokea za watu wawili tu Chief Whip waOpposition na Chief Whip wa Serikali, period.

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: …bahati mbaya hawajuihata historia ya Somalia wala ya Nigeria. Al-Shabaab nikikundi cha kikabila kiko Somalia, ni watu wa kabila fulanihuwa wanapingana na kabila lingine wamejiandaa na silahazao ndiyo wanafanya mambo ya Al- Shabaab.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Boko Haram vilevile inaukabila, ina element za ukabila kule Nigeria, lakini pia nikutokana na matatizo ya kiuchumi, wanajiona kwambawametengwa, wako marginalized ndiyo maana wameundakikundi cha Boko Haram wanashambulia wananchi wenginewenzao wa Nigeria si mambo waliyoyasema wao ambao niupotoshaji mtupu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamezungumzia suala laMalawi, kwamba Malawi imesema haitakubali usuluhishi,wameyapata wapi? Usuluhishi huu bado, unafanywa na

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

Kamati Maalum inaongozwa na Mheshimiwa JoaquimChissano, Rais Mstaafu wa Msumbiji na usuluhishihaujatolewa. Sasa kusema Malawi wamekataa wamekataawapi na lini? Kwa hiyo, hili wao ndio wachonganishi,wanachonganisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamezungumzia wakuu wamikoa, wakuu wa wilaya kuingia kwenye Kamati za Siasa zaCCM, huu ni uchonganishi na upotoshaji. Tumewahi kuwana Wakuu wa Mikoa ambao si wana-CCM, tuna mifano hai.Mkuu wa Mkoa wa Geita hakuwa mwana-CCM, alikuwahaingii kwenye Kamati ya Siasa. Tulikuwa na Mkuu wa Mkoawa Kigoma hakuwa mwana-CCM alikuwa haingii kwenyeKamati ya Siasa ya Mkoa, labda kama anaitwa kutoa taarifamaalum kwa sababu CCM ndicho Chama Tawala, kinamajukumu ya kusimamia Ilani ya Uchaguzi. Hata weweWaitara leo ukiwa Mkuu wa Wilaya ukaitwa kwenye Kamatiya Siasa utakwenda tu, huna ujanja kwa sababu CCM ndiyoinayoendesha Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona niyaweke sawahaya ili kuondoa upotoshaji.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa. Wewe umesema kwamba tutajibiwa na Serikali yuleni Waziri? Haiwezekani hii ni double standard hii. Hii ni doublestandard.

MWENYEKITI: Waheshimiwa, Mheshimiwa Rweikizaendelea.

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nizungumzie suala la usalama na ulinzi. Nimesemanamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuweka nchi yetu katikahali ya usalama, lakini nishauri kidogo, usalama upo lakinilazima tuzidi kuuimarisha na kuulinda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasikia hivi karibuni kunamashambulizi pale Mikoa ya Pwani, hasa Mkoa wa Pwaniwenyewe, Rufiji, Kibiti watu wanauawa, jana au juzi kauawa

Page 180: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

Katibu wa CCM mmoja na wengine, lakini miaka miwiliiliyopita tulisikia mauaji ya watu kule Tanga na mengineyalitokea pale Mwanza ya watu wengi na inaaminikakwamba haya mauaji yalifanywa na Al-Shabaab.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hii inayofanywa kulePwani hatujui lakini inawezekana ikawa ni Al-Shabaabwanakuja wanaingia kwenye maeneo yetu, wanaletamadhara ambayo ni kuua watu. Sasa kuna taarifa kwambaAl-Shabaab wanaanza kufanya ushirikiano na Boko Haram,na kuna taarifa kwamba haya makundi mawili ya kigaidiwanajaribu kutafuta silaha za sumu (biological weapons),ambazo wazitumie kwenye mapambano yao na raiawasiokuwa na hatia huko Somalia, Nigeria na kwingineko.Tunasikia wanavyofanya Kenya wanaua watu huko shuleni,wanaua wanafunzi vyuo vikuu, wanafanya maangamizisehemu mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama watapata silahaza sumu kama wanavyojitahidi kufanya, itakuwa ni hatarikubwa sana hata kwetu. Kama kweli waliingia wakafanyamauaji pale Tanga miaka miwili iliyopita, halafu wakiwa nasilaha za sumu tutakuwa katika hali ngumu sana yakiusalama. Tanzania na Somalia haziko mbali sana, kati yetukuna Kenya tu kama kilometa 400 kutoka Somalia mpakaTanga pale kwa kwenye Maji; kwa hiyo kuna haja yakuimarisha ulinzi katika maeneo haya.

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuna mkataba…

MWENYEKITI: Ahsante, muda wako umekwisha.

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,dakika kumi zimeisha?

Page 181: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

MWENYEKITI: Mheshimiwa Masoud Abdalla Salim.

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru nimepokea taarifa kwa MheshimiwaFakharia Shomar akisema kwamba uchaguzi wa Zanzibarulitawaliwa na Jeshi la Wananchi la Tanzania, hongera sanaMheshimiwa Fakharia tumepokea taarifa na sisi upande wapili tujiandae zaidi kwa kushinda kura si kwa njia nyingineyoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rweikizanikwambie tu kwamba Jeshi la Marekani wakati wa amanilinafanya shughuli za uchumi, watu waliotembea sanashughuli hizo wanajua na majeshi mengi duniani wakatiamani yanafanya shughuli za uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ukarasa sabaMheshimiwa Waziri anasema dhima kubwa ni kuwa na jeshidogo na mahiri la ulinzi wa nchi lenye weledi. Hatuwezi kuwana jeshi dogo, mahiri na lenye weledi ikiwa bajeti yamaendeleo yenye shilingi bilioni kumi unatoa shilingi bilionimoja, hakuna kitu. Hatuwezi kuwa na jeshi lenye weledi namahiri ikiwa bajeti ya maendeleo ya JKT shilingi bilioni naneunatoa shilingi bilioni moja, hakuna kitu, hapo hakunaweledi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatutaki kuona sisi umemeunakatwa kwenye Kambi za Jeshi la Wananchi wa Tanzania,hatutaki. Hatutaki kuona kabisa wanajeshi wanafanya kazipamoja na mkataba wao kula kiapo ndani ya masaa 24lakini kwamba baada ya saa tisa na nusu ration allowanceyao nayo inaondoka, hatutaki. Tunataka kuona rationallowance ya wanajeshi wetu inapandishwa si kwambaration allowance inaondolewa kiaina aina hatutaki. Hiyoilikuwa ni chombeza ya kwanza mambo hasa yanakuja.(Makofi)

Page 182: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna malalamiko ya mudamrefu sana juu ya fidia kwa wananchi ambao maeneo yaoyamechukuliwa na Serikali kwa ajili ya Jeshi la Wananchi.Maeneo haya ambayo wanajeshi wana shughuli zao jumlayake ni maeneo 262, kati ya maeneo haya ambayoyamepimwa ni maeneo 17 tu. Kwa kweli hii ni njia yadhuluma, wananchi wamenyanganywa, wananchiwamedhulumiwa na mpaka leo Jeshi la Wananchi katikamaeneo 262 maeneo 17 waliyoyapima na kuthamini hakunafidia na mengine hayajapimwa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu mwaka 1966, 1970mpaka leo miaka 50, wananchi wengine wameshakufawameacha watoto wao wanadai, wala hawajui waendewapi, mmechukua maeneo yao mbalimbali, mbona mambomnayotaka kufanya mnayafanya? Mbona hawa hamuwapifedha zao? Hamtoi fidia zao? Kuna mambo mengineambayo mnayafanya na fedha zinapatikana, kwa ninihamtoi fidia kwa hawa na tatizo ni nini? NakuombaMheshimiwa Waziri utuambie utakapokuja hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Fungu 57 - Wizara, katikamwaka 2016/2017 ulikuwa na shilingi bilioni 27.7 ni kasma2004, zilitengwa hizi fedha hakuna shilingi iliyotoka! Wananchiwasemee wapi sasa? Wananchi wanadhulumiwa nawananyonywa hawana mdomo wa kusema, mdomo waoni sisi, lakini Serikali inasema inatafuta fedha, fedhaikipatikana, mbona fedha za kuhamia Dodoma mlizipata,zilikuwa kwenye bajeti? Fedha za kuhamia Dodomamlizipata wapi na hazikuwa kwenye bajeti? Kwa nini hawafedha zao hamuwapi? Kuna wazee wamekufa wameachawatoto wao nao wamekufa, shida kweli Tanzania jamani!Twende wapi sasa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ndiyo mambo yamsingi ya kuwasemea wananchi wetu na kuwaonea huruma,kwamba Serikali inasema inawapenda wananchi wake,inawathamini wananchi wake lakini wapi! Miaka 50 fedhazao hamuwapi mnawatesa kwa njaa, tutafika kweli?Hatufiki, shida kweli.

Page 183: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee, ni miakakadhaa tumesema, tunajifunzaje baada ya mlipuko wamabomu kule Mbagala na Gongo la Mboto? Baada ya hapowakasema wanajenga maghala fedha mimi ni mmoja wawalioidhinisha, maghala yamekuwa magofu hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mabilioni ya fedhayamepotea, maghala hayaendelezwi yako vilevile. Munguasijaalie kutokea, likitokea la kutokea nani ataulaumiwa?Maghala mengi ambayo tumetoa fedha yakianzwahayamalizwi. Mheshimiwa Waziri wa Ulinziutakapokuja naomba hili uliseme ni kwa nini mpaka sasamaghala haya bado hayajamalizwa na fedha hizozimetumika zote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Sera ya Ulinzi waTaifa, umesema sana kwenye kitabu chako hiki. Mambo yaSera bado hujakaa vizuri. Tangu mwaka 1966 mpaka leo serani ya zamani. Unataka jeshi la weledi lakini sera ndiyoitakayopelekea sheria, Sheria ya Ulinzi ni ya zamani. Kwa hiyohili nalo ni tatizo kubwa. Mheshimiwa Waziri sasa utuambiehii sera lini itaweza kukamilika? Tatizo wewe unalijua zaidi,tena sana, tu kwamba utuambie hii sera ya ulinzi wa Taifa nilini itakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pengine ningesema jambolinguine, wanajeshi wanakwenda kulinda amani Darfur, DRCna Lebanon wengine wameshaletwa tumeshawazika. Sawani kazi zao na wajibu wao lakini mbona familia zaohamzitunzi? Mnawapa fedha za muda wa miezi minne walevizuka mpaka leo lakini watoto wao hawasomi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa inakuwa ni tatizokubwa, kwamba tumeshaletewa hapa sisi wale maititumeshazika lakini watoto hawasomi, familia zimekuwamasikini imekuwa kama wale wanajeshi wastaafu auwengine ambao walikwenda kwenye vita. TunawapelekaLebanon, Darfur na kwingine.

Page 184: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziriutuambie mpango mkakati wa ziada kuona kwamba watuhawa hasa wajane wanapatiwa fedha zinazostahili.

MWENYEKITI: Endelea bado dakika moja.

MHE. MASOUD ABDALLA SALIM: Yes?

MWENYEKITI: Malizia dakika moja.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: MheshimiwaMwenyekiti, katika hayo basi ningeomba kusema kwambasambamba na hilo Mheshimiwa Waziri utakapokujautuambie wastaafu walio kuanzia ngazi ya private hadiBrigadier General kwa nini hamrekebishi maslahi yao, tatizoni nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ngazi nyingine wanalipwavizuri wengine hawa mnawadhulumu na wewe ulisha ahidimwaka wa jana kwamba kuanzia Private hadi BrigadierGeneral, wastaafu hawa wa Jeshi hasa wale wa zamani basimafao yako katika machakato na mkasema kwamba yakokatika hatua ya mwisho ni hatua ipi, mbona mnachelewasana na hakuna kitu? Naomba Mheshimiwa Waziri na hiliuliseme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hayo machache,nashukuru lakini muda wangu naona kama mmenibia.

MWENYEKITI: Ahsante.

Waheshimiwa jioni tutaanza na Rhoda Kuncheladakika tano, Sophia Mwakagenda dakika tano, MheshimiwaSaada Mkuya dakika na Martha dakika tano. Nasitishashughuli za Bunge mpaka saa kumi na moja jioni.

(Saa 6.57 Mchana Bunge lilisitishwa hadi Saa 11.00 Jioni)

Page 185: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Tukae.

Niliwataja asubuhi wachangiaji wetu wa kwanzaatakuwa Mheshimiwa Rhoda Kunchela dakika tano naMheshimiwa Sophia dakika tano.

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti,na mimi nilitaka nichangie machache kuhusiana na Wizaraya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Kwanza nataka niungehoja asilimia 100 hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzanikutokana na hotuba hii kuonesha mwelekeo wa namna ganiWizara inaweza kutatua kero ambazo zinalikabili Jeshi letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumzia suala lausalama wa nchi kama wapinzani lakini pia kamaWatanzania ambao tuna haki ya kuzungumza na kuikosoaSerikali hatuna maana mbaya, tunathamini kabisa michangoya Jeshi, tunaelewa kabisa kazi ambazo zinafanywa na Jeshiletu, kwa hiyo, si kwamba tunapinga kila kitu. Tunachotakani kuikosoa Serikali katika yale mapungufu ambayo tunaonakabisa kupitia Jeshi hili basi linaweza likafanya marekebishokatika baadhi ya sehemu ili tukaenda sawa na wananchiwakawa na amani hiyo ambayo mnaisema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nataka nizungumziekidogo kuhusiana na migogoro ya ardhi kati ya wananchina Jeshi. Kumekuwa na changamoto kubwa kwenyemaeneo mengi ya Jeshi ambayo sasa wananchi wamekuwawanayalalamikia, kwamba Jeshi limeingilia kwenye makaziya watu, lakini unakuta tena Jeshi hilo hilo linasemawananachi wamevamia maeneo ya Jeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunaiomba Serikali naMheshimiwa Waziri atakapokuja kuhitimisha aeleze nimkakati gani ambao sasa Wizara au Serikali hii imepanga ilikutatua migogoro hii ya ardhi ambayo imesababishwa naJeshi, aidha, wananchi kuvamia maeneo ya Jeshi au Jeshikuvamia maeneo ya wananchi.

Page 186: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nilitaka niseme kidogo,katika Mkoa wangu wa Katavi kuna kata ya Misunkumilopamoja na Kata ya Mpanda Hoteli. Katika maeneo hayakuna wananchi wako pale wamejenga wana miaka zaidiya 60 mpaka leo. Vilevile kuna viwanda pale na pia kunawananchi wana mashamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii wamezuil iwakuendelea kufanya shughuli za kiuchumi kwenye maeneoyale, wameshindwa kulima, wananchi wanakufa na njaakatika kata zile. Eneo lile lina mgogoro lakini Serikali mpakasasa haijawahi kusema ni lini sasa mgogoro huu utakwishaili hawa wananchi sasa waache kupigwa, waachekunyanyaswa na Serikali ambayo mnasema ni Serikali yaamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la malipo yawanajeshi. Hivi tunavyoongea kuna wanajeshi zaidi ya 250ambao wamehamishwa kutoka Makao Makuu kuja Dodomahapa katika Mji wa Dodoma, hawajalipwa na wengine wakohumu ndani. Serikali ina mkakati gani wa kuwalipa hawawanajeshi? Mmewahamisha, mmewaleta hapa watuwameacha familia zao. Tunaomba sasa katika bajeti hiiitengwe fedha kwa ajili ya kuwalipa hawa wanajeshi,wanateseka na familia zao zinateseka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niongelee pia sualala mwisho linalohusu utawala bora. Tunathamini kabisa kazizinazofanywa na Jeshi, lakini tunaomba hawa wanajeshibajeti hii sasa ilenge maana ya kuwajengea nyumba iliwatoke katika makazi ya watu, maana imekuwa ni kero;wananchi wanakuwa wanaogopa, lakini na Jeshi nalo zilekambi zake zinashindwa kufanya yale majukumu kama Jeshikwenye maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na migogoromingi. Ni kweli, wanajeshi wana haki kabisa endapomwananchi anakuwa amekosea, lakini kero nyingineinapokuja kuna makosa madogo madogo, unakutamwananchi amemuudhi huyu mwanajeshi basi hicho kipigo

Page 187: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

atakachokipata, wengine ni vilema. Ukiangalia katika fukwezetu unakuta mwanajeshi anamlazimisha mwananchi kulasamaki mbichi, leo hii tumefikia hapa! Wananchi wetuwanateseka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaliomba Jeshi, ni kweliwananchi wanakosea, sasa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa SophiaMwakagenda

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante na mimi nichukue nafasi hii kuwezakuchangia katika Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, binafsi ninayo maswali kwaWaziri atakapokuja hapa kuhitimisha. Tunataka tujue, Jeshil ina madeni makubwa sana linayodaiwa na watuwaliohudumia Jeshi. Sasa sifahamu ni lini Serikali itaweka pesatunazozipitisha hapa Bungeni na kuhakikisha fedha hizozinakwenda kwenye Wizara hii kuweza kutimiza majukumuyao? Leo hii mnajinasibu kwamba mnahitaji Jeshi lisiaibike,lakini wakati huo huo shilingi bilioni 200 lakini mnatoa chiniya asilimia 14. Sielewi mnaongea nini na mnafanya nini?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo,tunafahamu Kiwanda cha Nyumbu ni sehemu ambayoTanzania yetu ingweza kujivunia, wanatengeneza magari,lakini ukifika pale utashangaa sana mashine ni toka Nyerereyupo, alipokuwa akitegemea mkonge na sasa tunadhahabu. Mnasema Tanzania ya viwanda, kwa ninitusiwekeze kwenye jeshi pale upande wa nyumbu tukaonahiyo dhamira ya viwanda ikitekelezwa kwa kutumia jeshi lile?(Makofi)

Page 188: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda pale vifaa havifanyikazi, mashine ni mbovu, lakini pesa bado ni ndogo. Nduguzangu mimi ninaomba tuache siasa katika mambo ambayoni ya msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huohuo wanajeshihawa, amezungumza aliyepita, unawezaje kuhamishawanajeshi ukawaleta, ni kweli wao wanatii, wakati wakuhama unaambiwa uondoke asubuhi unaondoka, lakini nilazima tufikirie hawa watu wana familia zao! MheshimiwaWaziri utakapokuja kutujibu, utuambie ni lini wanalipwa, kwasababu si kweli kwamba tunasubiri bajeti hii; kama pesa niza bajeti iliyopita lazima utuambie wanalipwa lini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapinga UKIMWI kamaTaifa, leo mwanaume mwanajeshi yuko Dodoma, familiayake iko Dar es Salaam, hajui anarudije kwa sababu kazizao zinaenda kwa order, usipompatia hela unataka nini? Mkewake kule atatafuta mtu, atatafuta mbadala na yeye hukuatatafuta mbadala. Kwa hiyo, ninaomba walipwe sawasawa na stahiki yao wanayotaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jeshini kulikuwa kunamaduka ambayo yana punguzo la bei, lakini tunaambiwakwamba yale maduka yamefungwa. Wanajeshi hawahawana muda wa kufanya biashara, wanahitaji kupataincentives, kumuwekea duka lenye bei nafuu ni kumtia moyowa utendaji kazi. Sasa sijajua hizo bajeti na jinsi ya kufungamikanda kama kunafika hadi kwenye Jeshi, tukifika hapo nchiinaangamia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kauli zinasemwa naWaheshimiwa Wabunge wengine, sitaki kuwatajaumekataza, tunapozungumzia haki sisi sio Wazambia, sisi niWatanzania, ni wazawa, tunazungumzia mustakabali waTaifa hili bila kupendelea. Si sawa kutuona sisi ni magaiditunapozungumzia na kusema tunawachonganisha wanajeshina wananchi, kwani wanajeshi hawajui kama waowanakosa haki zao? (Makofi)

Page 189: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna haki ya kuzungumzapasipo kupendelea; na msijifiche kwenye kichaka chakwamba sisi ni wapinzani, tunayo haki, tunalipwa mshaharasawa na ninyi na lazima tulalamike na lazima msimamie hakina muifanye kazi hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Wananchi linajitahidisana kutetea Taifa letu, lakini ijapokuwa hii inahusika namiundombinu pia, kwenye mipaka yetu madaraja nimabovu. Leo hii tukipata shida kama nchi mimi nakwambiahivyo vifaru ambavyo wanavyo kwa kupitisha hawana. Sasahapa Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi uonane na Waziri waMiundombinu uone ni jinsi gani utaweka mipakani madaraja.Kule kwetu Kyela madaraja ni mabovu, Malawi wameoneshachokochoko kuja kwetu, je, wakifanya kweli, tunapita wapi?Ninaomba unapokuja kuhitimisha ujaribu kuliweka hili wazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna vijana wanafanya kaziya ulinzi kwenye SUMA JKT, mishahara wanayopata nimidogo. Sote tunajua kuna makampuni ya ulinzi yanalipahadi shil ingi 500,000 wafanyakazi wao, vijana hawawanapata chini ya shilingi 200,000, mimi nafikiri si sawa.Ninaomba Mheshimiwa Waziri kwa bajeti inayokuja ufikiriejinsi gani vijana wale wataongezewa mshahara. Naninaomba pia na ninashauri kama ikiwezekana makampunibinafsi mengine yapunguzwe, ili tuongeze idadi ya vijanakwenye JKT na kuchukua tender, ikiwezekana zote kwenyeSerikali, lakini pia hata makampuni binafsi tulazimishewachukue SUMA JKT. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Wananchi pamoja…(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa

muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Saada dakikatano, Mheshimiwa Mattar dakika tano.

MHE. SAADA SALUM MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Mimi pia nachukua fursa hii kumpongeza sanaMheshimiwa Waziri kwa kazi kubwa ambayo anaifanya.

Page 190: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

Nadhani hatuna budi vile ile kulipongeza Jeshi letu laWananchi wa Tanzania, hususan kwa upande wetu waZanzibar nadhani limejitahidi sana kurejesha disciplineambayo il ikuwa imeanza kutetereka, kwa hivyotunalipongeza sana Jeshi letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziriatakapokuja atueleze, kuna hospitali abazo zinaendeshwana Jeshi. Ni Hospitali za Kijeshi ambazo wananchi wamekuwana confidence nazo kwa kiasi kikubwa. Mwananchiukimwambia aende katika hospitali ya kawaida na Hospitaliya Jeshi anakwenda katika Hospitali ya Jeshi kutokana naconfidence kubwa aliyokuwanayo juu ya utendaji wawanajeshi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hospitali hizi ziko katikahali mbaya sana, dawa hakuna, hakuna vifaa, lakini hatawale madaktari ambao si wanajeshi ambao wanapangiwakatika vituo vile wanakuwa hawakai kutokana na mazingiraduni ambayo yapo katika vituo vile. Sasa tunaombaMheshimiwa Waziri atakapokuja kuhitimisha atuambie nimkakati gani hasa umewekwa kuhakikisha kwamba hivivituo ambavyo vinatoa huduma kwa wananchivinaimarishwa ili viwe na ufanisi zaidi kwa watendaji lakinivilevile kwa vifaa na dawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, inafika hadi kwa mwezivituo kama vile vinapata OC ya shilingi 100,000, haviwezikuendesheka kwa namna kama ile. Jimboni kwangu kipokituo cha namna hiyo, inafika hadi hata panadol ya kuwapawale wananchi wanaowatibu hawana. Kwa hiyo,Mheshimiwa Waziri nadhani hil i l ichukuliwe specialconsideration na utuambie mkakati ambao unatarajiakufanya katika bajeti hii ya mwaka 2017/2018. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumzia kuhusiana nawanajeshi wastaafu. Wanajeshi wetu wastaafu MheshimiwaWaziri wanahangaika sana kufuata mafao yao. Oncewanapostaafu tu ile connection baina yao na yule aliyekuwamwajiri wao inakatika. Kwa hiyo, anapostaafu huyu

Page 191: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

mwanajeshi, na hii ni kwa sababu ya experience ninayo,anakuwa hana msaada wowote zaidi ya kuanzakuhangaika kwenda kurudi, kwenda Hazina kudai mafaoyao. Pengine wale ambao walikuwa wakihangaika katikakudai mafao yao kwa muda mrefu huenda taarifa zaozimepotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kule jimboni kwangukuna mwanajeshi amestaafu muda mrefu, ni mtu mzima,amenipa namba yake ya file nimekwenda Hazina, nambaya file ndio, lakini jina silo kabisa. Hii inaashiria kwamba, walewanajeshi wetu wakistaafu inakuwa ile connection hata ziletaarifa zao zinakuwa hazipo, zinapotea, hakuna mtu wakuwafuatilia. Kwa hiyo, tunaomba sana Mheshimiwa Wazirihawa wanajeshi wetu kuwe kuna mkakati maalum wakutunza taarifa zao wakati ambapo wapo kwenye ajira,lakini wanapostaafu lazima kuwe kuna usaidizi kutoka katikataasisi zao walizokuwa ili wasiende kule kupata taabu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa ni watu ambaowamefanya kazi nzuri kwa Taifa hili, ni watu ambaowameweza kulinda mali pamoja na roho za raia kwa kipindikirefu na katika wakati mgumu. Haiwi vyema na haiwi busarakuona kwamba wakistaafu ndiyo sasa waanze waowenyewe kuhangaika, waende Hazina, wapande ngaziwarudi; na mara nyingine, hususan familia zile zinazoathirika.Wakati mwingine mwanajeshi anakuwa amefariki na familiaile kuanza kufuatilia mafao ya marehemu inakuwa ni kazikubwa sana, wanakuwa hawapati usaidizi wowote kutokakatika jeshi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu, kama walivyosemawengi kwamba sasa hivi kumekuwa kuna mchanganyikobaina ya makazi ya raia na Kambi zetu za Jeshi. Tunapatataabu sana sisi ambao tuna majimbo na tukiwa tunatakakukarabati miundombinu ambayo raia wao wenyewe piawanatumia, lakini zimepita katika maeneo ya Jeshi, tunapatatabu sana. Sasa Mheshimiwa Waziri tunaomba hili naloliangaliwe vizuri, jinsi gani sasa kama tukitaka kukarabati

Page 192: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

miundombinu katika sehemu ambazo Kambi za Jeshi zinapitalakini na raia wanatumia, tunafanya nini? Kwa sababu hiiimekuwa ni changamoto kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la mwisho ni kuhusianana mafunzo haya ya JKT. Upande wetu kule Zanzibar hizi nafasizinakuja…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mattar.

MHE. SAADA SALUM MKUYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja.

MHE. MATTAR ALI SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia katikaWizara ya Ulinzi. Kwanza nimpongeze Waziri wa Ulinzi, kakayangu Mheshimiwa Hussein Mwinyi kwa kazi nzuri ambayoanaifanya katika kuliendesha Jeshi hili, nikupongeze sanakaka yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nigusie suala la…

MWENYEKITI: Ajiandae Mheshimiwa Khadija Aboud!

MHE. MATTAR ALI SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,Naam!

MWENYEKITI: Endelea, endelea!

MHE. MATTAR ALI SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Mimi nigusie katika uchukuaji wa vijana kwendaJKT. Kwa upande wa Zanzibar uchukuaji wa vijana kwendaJKT tulikuwa tukilipigia kelele sana, nafikiri hata Bunge lililopitanimelizungumzia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wetu waZanzibar bado uchukuaji wa vijana hawa ni kidogo sana.

Page 193: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

Kwa hiyo nimuombe sana Mheshimiwa Waziri, awezekutusaidia kwa hili, aliangalie kwa macho mapana ilikuhakikisha vijana wetu kutoka Zanzibar wanaongezekakatika kuchukuliwa, na hasa kuangalia kwa sasa kama kauliyake juzi alivyoisema kwa makini kuwa vikosi vyote vya ulinzi,hata Jeshi la Polisi, basi watakuwa wanachukua vijana hawakutoka ndani ya JKT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimuombe sanaMheshimiwa Waziri aweze kutuongezea kwa upande waZanzibar kuchukua vijana hawa wa kwenda JKT angalautufike vijana 600 kutoka vijana 300 ambao wapo sasa hivi.Nimuombe sana Mheshimiwa Waziri kwa hili aliangalie.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Mheshimiwa Wazirinikuombe sana, nilikuwa nikilizungumza sana Zanzibar tunaKikosi chetu cha JKU ambacho kinafanana sana na Kikosihiki cha JKT, nikuombe sana Mheshimiwa Waziri katikamipango yako na mazungumzo yako vijana hawa wa JKTukitaka kuwachukua kwa kutoka upande wa Zanzibar nibora sana kuchukua eneo hili la JKU kwa sababu unapatavijana ambao wanakuwa wameshapata mafunzo mazuri,vijana ambao wana mwelekeo mzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nikuombe sanaMheshimiwa Waziri uweze kulifikiria hili. Mheshimiwa Wazirihili hata bajeti iliyopita mimi nililizungumzia sana kuhakikishakama vijana unapotaka kuchukua basi uelekee katika kikosihiki cha JKU kwa sababu, hiki kikosi tayari kuna vijanawameshaandaliwa kwa muda mrefu, vijana wazuri ambaowana haki ya kupelekwa katika JKT na kupata ajira ya jeshi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nigusieupandishaji wa vyeo vyeo vya juu kwa askari kutoka Zanzibar.Ni jambo la kushangaza sana kwamba hata hawa askariwetu kutoka Zanzibar bado upandishaji wao wa vyeo vyajuu umekuwa hafifu sana katika jeshi hili. Kwa hiyo, nimuombesana Mheshimiwa Waziri aweze kuliangalia hili kwa makini,

Page 194: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

hata akija akatoa maelezo yake hapo atueleze kuna askariwa vyeo vya juu wangapi kutika Zanzibar, kwa sababutuangalie katika uwiano mzuri, ili tuweze kufika pazuri.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu nigusie ilepension ya askari wastaafu wa zamani. Hili ni jambo kubwasana Mheshimiwa Waziri, hawa wazee wanapostaafu hukowanalalamika sana. Kuna Sajenti aliyestaafu, sasa hivipensheni yake analipwa takriban zaidi ya shilingi 600,000, lakinijambo la kushangaza sana yule yule Sajenti wa zamaniambaye ameondoka katika hili Jeshi hata nusu yake hafiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe sana hawa ni wazeewetu ambao wamefanyakazi kwa nguvu zao katika Jeshihil i lakini hatimaye basi malipo yao ni madogosana.Wanapata taabu na wanaadhirika sana. NimuombeMheshimiwa Waziri aweze kuliangalia kwa makini suala hilii l i kuhakikisha kwamba hawa wazee wetuwanapandishwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Mattar,Mheshimiwa Khadija Aboud, ajiandaye Mheshimiwa MoshiSelemani Kakoso

MHE. KHADIJA HASSAN ABOUD: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Awali ya yote kwanza naombakuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza na Kambi ambazozimezungukwa na maeneo ya raia. Naomba Serikaliilishughulikie suala hili kwa haraka kwa sababu tayari kunabaadhi ya maeneo ya kambi ukipita nje yanayofanyika ndaniya Kambi ya Jeshi yote raia wanayaona. Mfano Kambi yaMwanyanya inahitaji ukarabati wa kujengewa ukuta. Pianaomba Serikali sasa ilipe fidia lakini pia izungumze na Serikalikupata maeneo mengine kwa ajili ya Jeshi, maeneo yawe ni

Page 195: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

ya Serikali yasiyohitaji watu kulipwa fidia ili kuweka akiba kwahapo baadaye kwa ujenzi wa Kambi na matumizi mengineya Jeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ajira za JKT, nashauripia isiwe kwenye vikosi vya Jeshi tu lakini pia hata ajira zataasisi nyingine za Serikali na Serikali kwa ujumla iwafikirievijana wetu hawa wanatoka katika Jeshi la Kujenga Taifa iliwapewe kipaumbele kwa sababu vijana hawa tayariwameshafunzwa uzalendo, ujasiri pamoja na maandili yakuitumikia nchi na Taifa kwa jumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nalipongeza Jeshi letu kwakukabiliana na vitendo mbalimbali viovu vinavyofanyikakatika mipaka yetu ndani na nje ya Tanzania ikiwemo kudhibitimambo ya uharamia na mambo mengine yoteyanayojitokeza yanayoashiria mambo ya kigaidi namengineyo. Nalipongeza sana Jeshi letu kwa kazi nzurilinayoifanya katika kusaidia mambo mbalimbali yakiwemomajanga na maafa yanayotokea ndani ya nchi, wamekuwamstari wa mbele sana kutoa msaada wa hali na mali nanguvu zao zote katika kuhakikisha wananchi wanaishi kwaamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe pongezi zadhati kabisa kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania,Waziri wa Ulinzi, Mkuu wa Majeshi, Kamanda wetu wa Majeshina Majeshi yote nchini Tanzania kwa kazi nzuri wanayoifanyaya kulinda nchi yetu, mipaka yetu na raia kwa ujumla. Kamailivyotokea kuashiria kwa uvunjifu wa amani uliotokeaZanzibar wakaenda pale kwa ajili ya kulinda amani ya nchina hawakwenda kushiriki uchaguzi wamekwenda kusimamiaamani ya nchi na wameifanya kwa uzalendo mkubwa nanchi sasa iko shwari nchi iko salama, mipaka ya nchi yetu ikosalama, tunawashukuru wanajeshi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachokiomba mahitaji yaoya msingi tuwasaidie, yakiwemo marupurupu na mambomengine ya kupandishwa vyeo na madaraja ili wawezekufanya kazi zao kwa weledi. (Makofi)

Page 196: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

Mheshimiwa Mwenyekiti, l ingine ninaloliomba,mwenzangu alichangia kuhusu vituo hivi vya afya, ni kwelivituo vya afya na Hospitali za Jeshi zinatoa msaada mkubwasana kwa raia. Naomba ziongezewe vifaa na ziongezewewatalaam na kuwapatia mafunzo zaidi ikiwemo kuwapatiamafunzo wanajeshi wetu il i kukabiliana na hatarizinazojitokeza za kimataifa za uharamia na ugaidi. Naombamafunzo hayo yaendelee kutolewa zaidi kwa wanajeshiwetu na hasa vijana wadogo ambao ni nguvu kazi kubwaya Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho niongezee tu kwakusema kwamba Jeshi letu ni imara, Jeshi letu linafanya kazinzuri, na ninakipongeza kwa dhati kikosi kile ya Makomandoowa Jeshi. Mheshimiwa Waziri kikosi kile ukione kwa jicholingine zaidi la huruma kwa sababu ndicho kikosi ambachotunakitegemea yatakapotokea majanga na maafamakubwa ndani ya nchi yetu, lakini Mwenyenzi Mungunaomba yasitokee hayo, nchi yetu iendelee kuishi tuishi kwaamani na salama, mipaka yetu iwekwe salama, na nchi yetuiwekwe salama. (Makofi)

Mheshimwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja,ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: ahsante, Mheshimiwa Kakoso jiandaeMheshimiwa Maryam Msabaha

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nishukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwenye Wizara yaUlinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Awali ya yote nimpongezesana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa sana anayoifanyapamoja na Waziri husika wa Ulinzi na Usalama pamoja nawanajeshi kwa ujumla. Niwapongeze kwa kazi nzuriwanayoifanya ya uzalendo kwa nchi yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nizungumzie sanasuala la ulinzi na usalama hasa kwenye mipaka yetu.Mheshimiwa Waziri alipokuwa anawasilisha amezungumziampaka mrefu wa Mashariki. Mimi niiombe tu Wizara hii

Page 197: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

ielekeze nguvu sana kwenye mpaka wa Mashariki hasakwenye maeneo ya Mkoa wa Pwani, Lindi na Mtwara ilikuhakikisha mipaka hii inaimarishwa vizuri. Maeneo haya kwasasa yameanza kuwa na dalili za ugaidi. Ni dalili ambayoJeshi la ulinzi ni vema likajipanga vizuri kudhibiti yaleyanayojitokeza ili kuokoa Watanzania wenzetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambaloningependa kuzungumzia ni mpaka wa Magharibi, kwamaana ya Ziwa Tanganyika. Niipongeze sana Serikali kwakutuletea kituo cha Jeshi la Ulinzi kwenye eneo la jimbo langupale Kata ya Ikola. Kituo hiki ni kituo muhimu na kimesaidiavitu vingi sana hasa mali za raia ambao kipindi cha nyumawalianza kuwa na wasiwasi mkubwa baada ya Waasi waKongo wale waliokuwa wakizidiwa wanakimbilia nchinikwetu na kufanya uhalifu kiasi kwamba wananchi wamwambao wa Ziwa waliishi bila amani lakini baada yakuweka kile kituo, ukweli kimewasaidia sana wananchi naamani ipo ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu kwa Serikali hasakupitia Wizara hii, tunaomba kile kituo mkiangalie kwa makinisana vitendea kazi ambavyo wanafifanyia shughuli palehavitoshelezi. Wanajeshi ambao wako pale hawana gari zurila kufanyia kazi, hawana boti za doria ambazo kimsingi nivitendea kazi vinavyohitajika ili viweze kusaidia usalama wanchi yetu. Mimi nilikuwa naomba eneo hili liangaliwe sana,sambamba na kuwawekea umeme kwenye kituo chaoambacho wanafanyia kazi. Hata hivyo, bado wanajeshiwanaofanyakazi kwenye maeneo haya ni wazalendo kwelikweli; hata zahanati hawana. Mimi nilikuwa naomba Wizaraiangalie umuhimu wa kuweka angalau kituo kidogo paleambacho kitasaidia afya za wanajeshi kwenye maeneo yale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kuishukurusana Serikali kupitia SUMA JKT ambao tumewapa maeneomakubwa sana kwenye Wilaya ya Mpanda kwa ajili yauwekezaji. Kuwapa nafasi ya kutengeneza mazingira yauwekezaji kwenye Wilaya yetu kutasaidia sana kutoa elimukwa wananchi hasa wa Mkoa wa Katavi.

Page 198: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inapojipangakuwekeza kupitia SUMA JKT, niombe yale maeneo ambayowatakuwa wamepewa wafanye kazi ya kuwasaidiawananchi wanaozunguka miradi ile ya maendeleo kwenyeeneo hilo. Hii ni sambamba na kuwashirikisha, kuwapa elimuhasa kwenye suala zima la kilimo,ufugaji pamoja na kusaidiapembejeo kama watakuwa wanazo kwenye maeneo yaleili Jeshi liwe na dhamana ya kutengeneza mazingira ya kwaona kusaidia wananchi ambao kimsingi Halmashauri imetoaeneo bure bila kutoza gharama ya aina yoyote. Ninaombasana katika hili Serikali kupitia JKT lisaidie kwenye maeneohayo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe sana Serikali, JKTwamepewa maeneo yale ni pamoja na kuomba msaadawa kusaidia suala zima la uhifadhi mazingira. Eneo hilo nimiongoni mwa maeneo ambayo yamekuwa na uvamizi wamazingira ambayo wananchi wanaingia kwenye misitu; sasatunaamini ujio wa SUMA JKT utasaidia pamoja na kutatuatatizo lile la uharibifu wa mazingira ambayo kila maraunakuwa inajitokeza kwenye maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hali yausalama, tuna misitu mikubwa sana ambayo ni pamoja naMsitu wa Tongwe Mashariki, Msitu wa Tongwe Magharibi.Kimsingi eneo hili linahitaji msaada sana ambao tutahitajiSUMA JKT watakapokuwa wanafanya shughuli zao zauzalishaji watusaidie na hali ya kutunza usalama kwenyemaeneo yale na ikizingatiwa maeneo ambayo tayaritulikuwa ni maeneo yaliyokuwa na wakimbizi, kwa sasa hivini maeneo ambayo tayari wamekuwa Watanzania wapya.Hata hivyo wapo wachache ambao wanafikiria mazingirabado ni yale yale. Kwa hiyo, tutaiomba Serikali idhibiti walewachache wenye malengo mabaya tofauti na Serikali iliwaweze kutusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho niombe sanaushirikiano na Serikali kwa ujumla, kwamba tunaomba sasanafasi za kazi zitakapotoka wananchi wa maeneo yalewapewe kipaumbele ili waajiriwe na Jeshi la Kujenga Taifa

Page 199: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

kwa sababu ni nafasi pekee ambayo tumeipataitakayowasaidia Watanzania wote kwa ujumla na Mkoa waKatavi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja,ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Maryam Msabaha.

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa hii ili nichangiekwenye Wizara ya Ulinzi na Usalama. Kabla ya yote nimshukuruMwenyenzi Mungu kwa kunipa uhai na pumzi, nimesimamatena katika Bunge lako hili, ni shukrani ya pekee nairudishakwa Mwenyenzi Mungu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nimpe polekaka yangu Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi kwa kutotendewahaki katika Wizara yake kwa sababu tumekuwa tukipitishabajeti hewa, kwa sababu Wizara haitendewi haki. Hii Wizarani Wizara nyeti, na Wizara hii mnategemea miujiza gani nahawa mnasema wasiseme, lakini wataandamana kwenyemioyo yao. Niiombe Serikali ihakikishe Wizara hii inatendewahaki kama wizara nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe Serikali iangalieWizara ya Ulinzi pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa. Hili si Jeshitu la kutuma wakati wa uchaguzi bali niseme Jeshi hili lipokwa ajili ya kulinda mipaka ya nchi na kwamba halipo kwaajili ya kulinda uchaguzi. Niwapongezea pia kwa welediwao mzuri wa kulinda mipaka ya Nchi ambayo iko salamampaka sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la kukata nishatiya umeme katika Kambi za Jeshi. Mimi nashangaa sana, kwanini Serikali isipeleke pesa kwa wakati? Kama Wizara ilikuwainatengewa pesa kwa wakati fedha zinazotengwa hapazinapitishwa zinapelekwa kama zilivyo pia deni hili la nishatiya umeme lingepunguzwa, lakini nasijaabu mnasemamnakata umeme mkikata umeme jueni Jeshini kuna kazi nyeti

Page 200: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

kazi nyingine haziwezi kutajwa zile kazi zitafanyika vipi aumnategemea miujiza gani? Hawa wanajeshi wawashetochi? Kuna sehemu nyingine hawawezi kuwasha tochi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima wawe na umememasaa ishirini na nne, lazima umeme uwake Jeshini, hakunakusema hapa kazi Jeshini kazini umeme ni lazima uwake,Mheshimiwa Rais akate umeme sehemu zote, lakini si Jeshini.Kuna vitu nyeti vya ndani ya Serikali viko Jeshini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna kufunga luku, lukumtawafungia vipi wanajeshi jamani? Tangu enzi ya Nyererembona akujafungwa luku hiyo luku inatoka wapi? Angalienimkipeleka pesa haya masuala yote yataondoka, na kamakuna pesa za kurudishwa kwenye nishati zitarudishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine mnasema wanajeshiwanaripoti kazini kuanzia saa 12 asubuhi anakaa mpakajioni. Kwa mfano, anatoka Kibaha na kurudi Dar es Salaam,labda Mbagala au wapi, sasa huyu mmemfanya yeyerobbot? Toeni stahiki ambazo zinapaswa kwa wanajeshi. Leomnahamisha wanajeshi mnawapeleka vituo vingine vya kazilakini huku nyuma wanaacha familia, mnategemea nini?kuna matukio mbalimbali yametokea wanajeshi kuua wakezao; hawawaui kwa makusudi ni hasira huko alikokwendapesa hajapewa huku mke wake labla kafanya michepuko,ninyi ndio mnasababisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naomba fedhaitolewe kwa wanaopata uhamisho wapewe stahiki zaowaende na familia zao hakuna kutengeneza mambomengine vifo kwa wanawake visivyokuwa na sababu nakutengeneza UKIMWI usiokuwa na sababu. Kwa hiyo,naombeni chonde chonde muangalie kwa makini, isiwe leotunapitisha shiingi bilioni kumi na moja lakini hata shilingibilioni moja hampeleki mnategemea nini? Yale magwandanayo yanahitajika yafuliwe, viatu vinataka vibrashiwe (bebrushed) kama mlivyosema kwamba huko barabarani trafficwakikamata nao wanataka ya brush na hawa pia wanatakabrush.

Page 201: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

Mheshimiwa Mwenyekiti tuangalie hospitali; hizihospitali, kwa mfano Lugalo. Hospitali ya Lugalo imekuwani hospitali hata viongozi wengi wa kitaifa wakifawanapelekwa kule. Lakini tuangalie changamoto zilizopokatika hospitali ya Lugalo. Naomba Serikali iziangalie hospitalihizi kwa jicho la makini, na bajeti inayopagwa tuhakikisheina madaktari wanajeshi wanapata stahiki zao wanapatamafunzo, wanapata masomo, wapewe kila kinachopaswakwa sababu hospitali hizi hazihudumii wanajeshi tu,zinahudumia na raia wa kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Zanzibar unakujua naMigombani unakujua. Hospitali ile ya Jeshi ya Migombani niya siku nyingi kituo kile ni cha siku nyingi na kipo sehemu nyetisana wewe mwenyewe inaijua iko karibu na Ikulu yaMigombani, lakini kituo kile kimekuwa kinapokea watu wengimpaka majeruhi, kituo kile ni cha tangu enzi ya ukoloni.Angalieni namna gani ya kuboresha kituo kile ili kiende nasayansi na tecknolojia. Tusikae tu kituo kile ni kidogo na kikobarabarani kubwa, sehemu yenyewe ni nyeti, lakini kituohakiko katika ubora wowote. Kwa hiyo, hilo pia naombalifanyiwe kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kuhusu mipaka ya Jeshiumeangalia migogoro nakushukuru, migogoro ya Zanzibarmingi umeishughulikia, lakini bado kuna migogoro umebakiwakati wa kwenda kulenga shabaha mwangalie na kulewakishalenga shabaha na vile vitu ambavyo vinavyobakikule viondoshwe ili visiwadhuru…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Matiko dakikatano.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kuweza kunipatia nami fursa kuchangiabajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizaraambayo ni muhimu sana kwa ulinzi wa nchi yetu.

Page 202: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa masikitikomakubwa kwamba tunakaa hapa tunapitisha bajetiambazo hazina uhalisia na hatimaye utekelezaji wakeunakuwa ni wa kusuasua. Waziri wakati anawasilisha bajetiyake hapa ameainisha bayana kwamba fedha zamaendeleo ambazo zilikuwa ni shilingi bilioni 248 zimetolewaasilimia 14.5 tu ambazo ni sawa na shilingi bilioni 35.9

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii kuna wazabuni wengisana wanaidai Serikali ambao wametoa huduma kwenyeJeshi letu la JKT pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.Hawa wazabuni wamekopa fedha kwenye benki,wanafilisiwa na wengine wanafariki kwa sababu ya pressure.Nilikuwa naomba Serikali tunapokuja hapa tunatenga hizibajeti hasa za maendeleo ziwe na uhalisia ili ziweze kwendakukidhi mahitaji kwa muda wa mwaka nzima kamatunavyokuwa tumepanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine napendakuzungumzia fedha ambazo zinatolewa kwa ajili ya kupima,kuthamini na kulipa fidia kwa yale maeneo ambayo Jeshiimeyatoa kwa wananchi, tena wakati mwingine bila kufuataSheria za Ardhi. Katika hili nitajikita zaidi katika eneo ambaloJeshi la Wananchi wa Tanzania wamejitwalia kule Tarimekatika kata ya Nyamisangura na kata ya Nkende ambapokwa kweli kila mwaka ninakuwa ninasimama hapa naelezea,na Mheshimiwa Waziri amekuwa akiniambia kwambawanakuja kumaliza kuwalipa fidia. Mwaka jana tulitengashilingi bilioni 27.7 Mheshimiwa Waziri ameeleza hapa na wotetunaona kwamba haikutolewa hata shilingi 1,000 kwendakufanya hii kazi; shilingi bilioni 27.7 hata shilingi 1,000haijatolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nilikuwa nashauri,kwa sababu wanajeshi kwa mfano kwa Tarime kile kosikilipewa eneo kubwa sana Kata ya Nyandoto; tunaombawaondoke kwa sababu mmeshindwa kulipa kwa miaka yotehii kuanzia mwaka 2008, tunaomba hawa wanajeshi warudikwenye maeneo yao kule Nyandoto eneo ni kubwa sana nipori kubwa kuliko kuja kuchangamana na wananchi.

Page 203: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi yao iko kuleNyandoto ya kikosi cha 28KJ warudi kule, wakakae kule iliwaweze kulinda vizuri dhidi ya mipaka ya Nchi yetu kwaupande wa Kenya. Huku kwenye kata ya Nyamisangura naNkende wanachangamana sana na wananchi nammeshindwa kulipa. Kwa hiyo naomba leo MheshimiwaWaziri uniambie either mnatulipa kwa kipindi cha bajeti yamwaka huu au mwende mkawaombe wale wanajeshiwaondoke.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanachokifanya sasa hivikwanza wanakodisha yale maeneo kwa raia yaaniwamepoka maeneo ya wananchi halafu wanakodisha kwakufanya biashara, zaidi ni maslahi ya watu binafsi kule.Naomba uje na wewe mwenyewe Tarime ukae na wataalamwako tulimalize suala hili. Mimi binafsi kama mwakilishiinaniuma sana ninapoona wananchi wanakaa kwa miakamingi bila kufanya shughuli za maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, wale ndugu zetuwanajeshi ambao wanakwenda kusoma nje ya nchimnachelewesha kuwapelekea fedha za kijimu, wanakuwawanateseka sana. Kwa hiyo, naomba kabisa wakatimnapanga bajeti muweze kuzingatia mjue kwambamnapeleka wanajeshi wangapi kusoma nje ya nchimuwapelekee fedha za kujikimu ili wamalize mafunzo yaowakiwa na utulivu wa akili na kurudi Tanzania kuweza kulindanchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wale wanajeshi ambaounakuta wanatumwa kwenda kulinda amani kwenye nchizingine; Kambi za Tanzania za wale wanajeshi wetuwanaokwenda kukaa kule ni mbovu, hazina hadhiukilinganisha na kambi za nchi zingine ambazo wameendakulinda amani kwenye sehemu husika.

Tunaomba wakati mnawatuma wanajeshi wetukwenda kulinda amani huko basi na wenyewe muwapehadhi, wawe na makambi mazuri kama wale wengine

Page 204: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

ambao wametoka nchi zingine. Ukienda ukiangalia kambiza wanajeshi kule zinatia fedheha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mwisho nimalizie kwenyetop up allowance. Wanajeshi mara ya mwisho wamelipwahizi top up allowance ni mwaka wa jana mwezi wa tatu.Sasa hivi ni zaidi ya mwaka hamuwalipi hizi stahiki zao.Tunarudi pale pale, tunapopanga bajeti zetu tupange bajetiyenye uhalisia, tujue kwamba katika Wizara hii tuna mahitajihaya na haya. Tuweze kutimiza yale mahitaji ambayo ni yamuhimu, kwa mfano hii top up allowance ni hitajio ambalomtu anapokuwa anafanya kazi anajua kabisa anatakiwaalipwe. Sasa inapita mwaka bila kuwalipa; na ndiyo maanahotuba ya kambi rasmi ya Upinzania imejikita zaidi kuelezeamatatizo na maslahi ya wanajeshi wetu.

Kwa hiyo, naomba kipekee kabisa; Hotuba ya KambiRasmi ya Upinzani Bungeni imeelezea kwa kina sana, dakikatano ni chache kuchambua, naomba Mheshimiwa Waziriuifanyie kazi yale yote ambayo yamebainishwa kwenyeHotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni yafanyiwe kazi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni kuhusu wanajeshiwetu wastaafu na wale ambao unakuta wameaga dunia.Ni dhahiri na mimi mwenyewe nina ndugu ambao wenginewaliaga dunia na wengine ni wastaafu wanakuwawanaangahika sana kupata mafao yao; naombamuwatendee haki. Hawa ndugu unakuta wametumikia nchihii kwa uaminifu zaidi, lakini ikija kwenye mafao inakuwawanatendewa ndivyo sivyo, nashukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Elibariki Kingu,ajiandae Mheshimiwa Deo Ngalawa. Kama Kingu hayupoMheshimiwa Deo Ngalawa, Ajiandae Mheshimiwa VedastusManyinyi.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kusimama kwenyeBunge lako Tukufu kwa ajili ya kuchangia mjadala wa Wizara

Page 205: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

ya Ulinzi na Usalama. Kwanza nilipongeze Jeshi letu kwa kaziambazo linazifanya, kwa kweli ni kazi zilizotukuka nazinastahili kupewa pongezi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nijikite moja kwa mojakatika suala la ulinzi na usalama. Mimi natoka Ludewaambako Ziwa Nyasa lipo na kama kwenye hotuba ya Kambiya Upinzani kwenye ukurasa wao wa 14 na 15 walizungumziajuu ya mgogoro wa Ziwa Nyasa. Labda tu nipende kuwekavizuri taarifa yao kwamba Ziwa Nyasa limezungukwa na nchitatu; limezungukwa na Tanzania, Malawi na Msumbiji. Kwahiyo, katika hali ya kawaida Malawi hawezi ku-demand eneola Msumbiji, analo-demand ni eneo la Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ulinzi na usalamaeneo lile ni pana hasa eneo la upande wa Ludewa. Eneo laupande wa Ludewa bado ninaendelea kusisitiza kwambalina urefu wa kilometa zisizopungua 250 around the shore ofthe lake, lakini kiusalama na kiulinzi bado limewekwa nyuma.(Makofi) (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ukijaribukuangalia eneo lote hilo lenye urefu huo mkubwa badohakuna vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo vipohuko. Napenda kuchukua tu fursa hii kuliomba jeshi, kuiombawizara na kumuomba Mheshimiwa Waziri kwamba kuna hajaya kuweka mkakati wa makusudi kwa ajili ya kuimarisha ulinzina usalama wa eneo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nazungumza hivyo?Nazungumza hivyo kwa sababu eneo lile halina mawasilianoya simu; eneo hilo halina miundombinu ya barabara kwaurefu wote huo niliokua nimeuzungumza. Kwa hiyo basi, ifikemahali sasa kwa sababu ya haya mambo yanayoendeleahapa sasa hivi inakuwa ni ngumu sana incase ikitokea kituchochote wananchi kuripoti, incase kuchukua kitu chochote,wananchi hata kukimbia basi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imekuwa ikizungumzwakwamba hapa pana mgogoro na ilifika mahali kipindi kile

Page 206: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

yanachimbwa mafuta, unakuta ndege ya Malawi inakujaTanzania na wananchi hawana facilitation yoyote ya kusemakwamba wanaweza wakaripoti. Kwa hiyo, ina maana kuwakama litatokea janga lolote uwezekano ni mkubwa sanakwenda hayo maeneo na ukakuta kwamba mamboyameshaharibika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napende tu kuisihiWizara ikiwezekana sasa na kama itakuwa imeruhusu basikuwepo na vyombo vya kiulinzi ambavyo vina-patrol,angalau kuwepo hata na marine boats ambazo zitakuwazinazungukia kule kwa ajili ya kuimarisha usalama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalonaweza kulizungumzia ni juu ya Uwanja wa Ndege Sagalu,uwanja ule ni wa Jeshi lakini kwa mara ya mwisho inawezakuwa ni miaka 30 iliyopita, ule uwanja umeshakuwa ni pori.Sasa kwa sababu kuna ujio wa makaa ya mawe Mchuchumana chuma cha Liganga naamini kabisa facility ya uwanja nimuhimu. Labda twende kuliuliza Jeshi kwamba incase kamautakuwa hauna matumizi kwa sasa, turudishieni Halmashauriili tuweze kuandaa mazingira ya kufanya kazi nyingine yoyoteya kimaendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kwa kusema hivyobasi naamini; tuna kambi moja ya Jeshi pale Manda ambayoipo mpakani kabisa mwa Mto Ruhuhu. Sasa ukiangalia lileeneo lote mpaka unakuja unaigusa Kyela hakuna chombochochote cha ulinzi, hakuna mawasiliano ya simu na hakunamawasiliano ya miundombinu ya barabara. Kwa hiyo,nichukue tu nafasi hii kuishauri Serikali kwamba ipelekevyombo vya usalama kule angalau basi hata wananchiwafarijike incase kama kitatokea kitu chochote waweze ku-accommodate. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ambachoningependa kukizungumzia hapa ni juu ya dhana yaviwanda…

MWENYEKITI: Endelea.

Page 207: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: … ni juu ya dhanaya viwanda kwa Jeshi. Ifike mahali sasa Jeshi letu lijiendeshekisayansi, kwa sababu ninaamini kwamba Jeshi letu lina multiprofessionals, lina madaktari na ma-engineer. Kwa hiyo nalolipange mpango mkakati na ifike mahali jeshi lenyewe kamaJeshi lijitegemee na lisiwe inategemea ruzuku tu peke yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi ninaaminikabisa jeshi lina uwezo wa kujiendesha kisasa kama ilivyoanzaule Mradi wa Nyumbu bado unaweza likaanzisha miradimingine yoyote ambayo inaweza ikaliingizia kipato japokwamba litaendelea kupata ruzuku kutoka Serikalini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machache miminiishie hapo, ila napenda tu kwa dhati ya moyo wangu, eneolile la Ziwa Nyasa sasa hivi lipewe kipaumbele kwaniwananchi wameamua kulima barabara wenyewe. Kwa hiyo,tunaiomba Wizara ya Ulinzi maeneo ambayo ni magumu basitutakapoomba baruti watuletee, na maeneo ambayo yanamadaraja ikiwezekana basi tupate hayo madaraja. Kunabaadhi ya maeneo Jeshi huko nyuma lilishaweka madaraja;sasa bahati nzuri maeneo yale imeshapita barabara yalemadaraja yanakuwa sasa hivi ni kama hayana kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tungeomba sisitutakapokuwa tunaomba yale madaraja basi tuletewe kwaajili ya kufanya facilitation ya wananachi wetu kule ili pawezekupitika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naungamkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Manyinyi ajiandaeMheshimiwa Dau Mbaraka.

MHE. VEDASTUS M. MANYINYI: MheshimiwaMwenyekiti, na mimi nichukue nafasi hii kukushukuru kwakunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia kidogo katika hiihotuba ya bajeti ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Page 208: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli usiopingikakwamba wote tunajua kazi kubwa ya ulinzi inayofanywa naJeshi letu, ni kazi nzuri na niseme tu kwamba hasa kwetu sisiambao wakati mwingine tumekuwa watembezi tembezikidogo katika nchi za wenzetu, ukija Tanzania ndiyo unawezakujua kwamba kweli Jeshi letu linafanya kazi nzuri kwasababuukilala una uhakika wa kuamka kesho yake. Kwa hiyo baadaya kuwapongeza kwa hiyo kazi nzuri lakini kuna baadhi yamambo ambayo tunapaswa tuendelee kuwasaidia naambayo yatahakikisha kwamba kazi zao zinakwenda vizuri.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja; Jeshi letu bado linamatatizo makubwa ambayo ni pamoja na madeni.Tunaamini kwamba wanashindwa kufanya mipango yaomizuri kutokana na madeni na kwa maana ya ukwasi wafedha. Kwa mfano kati ya miradi mizuri waliyonayo ni pamojana kile kiwanda cha kutengeenza magari kile cha Nyumbu,ni kiwanda ambacho tulitakiwa tuone matokeo yake yaharaka, lakini naamini kwamba kinasua sua hii yote si kwasababu nyingine lakini ni kwa sababu ya ufinyu wa bajeti.Kwa hiyo, ningeomba Serikali iangalie uwezekano wakuwasaidia ili waweze kufanya kazi zao vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua kwamba Jeshiwanayo madeni, kwa maana ya wale wazabuni. Kwa hiyo,napo kuna tatizo kubwa kwa sababu fedha wanazopatahazikidhi mahitaji yao, kwa hiyo, Serikali inahitaji kuangalianamna ya kuendelea kuwasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tu niseme kwambakatika miradi waliyonayo, kwa mfano hawa wenzetu wa JKT;JKT kwangu mimi ninavyofahamu leo tukiamua kuitumia vizuriinaweza ikaleta impact kubwa hasa kwa vijana wetu.Nadhani Waheshimiwa Wabunge wenzangu watakubalianana mimi kwamba kila linapotoka tangazo kwamba sasakuna nafasi za kwenda JKT katika kila Wilaya unakuta wapovijana zaidi ya 1,000 wanajipanga pale msululu kwa ajili yakuomba waende JKT. (Makofi)

Page 209: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

Mheshimiwa Mwenyekiti, na wote tunakubalianakwamba katika nchi hii kama kuna tatizo kubwa tulilonaloni tatizo la ajira kwa vijana. Sasa basi JKT kwanzawanafundisha maadili, lakini wanaendelea kufundisha vijanakuipenda nchi yao. Kwa hiyo, katika yale mafunzowanayofundisha ambayo ni pamoja na mafunzo ya kufanyakazi ambayo ni ya ujuzi ni imani yangu kwamba kama Serikaliitaweka nguvu kubwa kwa JKT basi kwa kiasi kikubwaitapunguza tatizo la ajira kwa hawa vijana wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni imani yangu kwambakwa yale mafunzo ambayo vijana wangekuwa wanayapatapale mfano unazungumzia mafunzo ya kilimo. Ingekuwa nirahisi zaidi vijana wakafika pale wakapata mafunzo ya uvuvina mafunzo mbalimbali, sasa wakitoka hapo ni rahisi zaidiwakasaidiwa kidogo na wakaenda kuanza maisha yao kulikohivi ambavyo tunavyowaacha vijana wanahangaikamtaani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ninaamini kwambaJKT ni mahali pekee ambapo panaweza pakaleta impactkubwa. Unaona tunafikia mahali tunakuwa na upungufu wachakula, lakini tunayo mabonde mazuri, na mengine; labdaniseme tu moja, kwa mfano ukiangalia pale kwenye Wilayaya Musoma walipewa eneo kubwa lakini hawakupewauwezo; kwa hiyo, mwisho wa yote wameendelea tukuliangalia lile eneo mpaka mwisho. Kwa hiyo, tunadhanikwamba hayo ni baadhi ya mambo ambayo Serikaliikiwasaidia basi wataweza kufanya mambo mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja karibu na mwisho;kwa bahati nzuri hili tulishalizungumza na Mheshimiwa Waziri;ni suala la fidia kwa ajili ya wale wananchi walioombwawaondoke kwenye eneo ambalo Jeshi imelichukua, eneo laMakoko. Hili ni suala ambalo tumehangaika nalo sasa zaidiya miaka 15. Tangu mwaka 2005 tumekuwa tukilizungumzialakini hadi leo. Jeshi walishakubali kwamba wanalipa fidia,kwa maana ya Serikali, lakini hadi leo kila leo wale wananchiwameshindwa kuyaendeleza maeneo yale, lakini vile vile

Page 210: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

wameshindwa kuhamia mahali pengine kwa sababu badohawajalipwa fidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mwisho, nadhani ni wikitatu zilizopita wale wananchi walituma wawakilishi wao,bahati nzuri baada ya kuona nimezidiwa niliwapeleka mojakwa moja tukakaa na Mheshimiwa Waziri na akahaidikwamba kwenye bajeti hii tutawalipa fidia. Sasa MheshimiwaWaziri naomba commitment yako utakaposimamakuzungumza uwahakikishie hawa wananchi ili wakaewakijua, kama ulivyoniambia siku ile, wawe na uhakikakwamba kama kweli watapata hizi fedha zao. Maana sasaukiangalia ni muda mrefu na hata kati ya hao wenye hizofamilia wengine walishafariki, sasa familia zao nazo zipo palezile nyumba zinaelekea kuanguka lakini wameshindwawaende wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni imani yangukwamba baada ya kupata hayo majibu mazuri kwa mwakahuu tunaweza kumaliza hilo tatizo la wananchi ambalolimewasumbua kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo namimi naungana na wenzangu kusema naipongeza Serikaliyangu kwa kazi nzuri ambayo inaifanya, na ninaendeleakusema tupo pamoja na ni jukumu letu sisi kuendeleakuisaidia ili waendelee kutekeleza majukumu hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayonaunga mkono hoja, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Dau dakika tano,ajiandae Mheshimiwa Mwantumu Dau.

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. Nianze kwanza kwakumpongeza Mheshimiwa mtoa hoja, Waziri Dkt. HusseinMwinyi kwa kutuletea hotuba nzuri sana yenye kuletamatumaini kwa Taifa letu. (Makofi)

Page 211: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natokea Kisiwa chaMafia ambacho kipo mpakani kabisa na Comoro kule.Takribani miezi miwili, mitatu iliyopita tulipata bahati yakutembelewa na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi JeneraliMwamunyange, katika juhudi za kuhakikisha kwambawanafungua kikosi pale cha Jeshi katika Kisiwa cha Mafia ilikuhakikisha kwamba suala la ulinzi na usalama linaimarikapale kisiwani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni jambo jema sana nasisi watu wa Mafia tumelipokea kwa mikono miwili. Lakinikuna mambo mawili hapa ni vizuri niyaweke kwa attentionya Mheshimiwa Waziri ayaangalie yaweze kutusaidia ili hilijambo liwe jema zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza; siteambayo wameichagua pale sisi na wenzetu pale Wilayanitumeiona kwamba sio site nzuri kwa sababu ni katikati yaMji wa Kilindoni pale. Lakini kuna site ambayo iko maeneoya Jimbo takribani kilometa 30 kutoka Mjini Kilindoni pale;tulikuwa tunapendelea na tungefurahi sana kama jeshilingekwenda kule ili kukataa hizi crush na wananchi kwasababu kule kidogo kumejitenga na watu wapo wachache.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini angalizo la pilitungependa pia Kikosi cha Maji kiwepo pale kwa sababu sisitunapakana na bahari kuu na kule kuna maharamia walewa Kisomali na pia kuna meli za uvuvi ambazo zinakuja kuvuakule bila ya kibali cha mamlaka husika. Kwa hiyo, tungependasana kije kikosi cha maji pale ili waweze ku-patrol ile baharina kuhakikisha kwamba hakuna aina yoyote ya uvuvi wakuvamia wa meli kubwa zinazokuja kuvua pale KisiwaniMafia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuyasema hayoningependa nijielekeze sasa kwenye suala la vijanawanaoingia kwenye JKT. Mimi kwa ufahamu wangu kilawilaya imetengewa sehemu yake ya vijana watakaokwendaJKT kila mwaka, lakini kwa bahati mbaya na masikitiko

Page 212: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

makubwa sana Mheshimiwa Waziri, inapofika Wilaya ya Mafiawale washauri wa mgambo sijui wanatoka wapi, sijui wapochini yenu au wako chini ya nani, Mshauri wa Mgambo waMafia siku zote lazima ataandikisha vijana kutoka nje yaMafia. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri, hili tunaomba sana mwaka huulisijirudie, na kama litajirudia basi kuna hatari ya kuvunjikakwa amani katika Kisiwa cha Mafia, kwa sababu vijanawenye qualification wapo, lakini Mshauri wa Mgamboanalazimisha kuwaleta vijana kutoka nje ya Mafia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanapowachukua walehuku nyuma tunaanza kuulizwa na wazazi, vijanawamemaliza shule za kata hizi, form four wanakosa nafasi,kwa nini nafasi hizi wanakwenda kuzichukua watuwanaotoka nje ya Mafia? Serikali imefanya hivi kwa makusudikwa sababu ya kuleta uwiano ili Jeshi letu liwe na uwakilishimzuri, kwamba kijana kutoka kila wilaya ya Tanzaniaanakuwepo katika Jeshi. Sasa zinapokuja nafasi zetu sisimshauri wako wa mgambo Mheshimiwa Waziri anatuleteawatu kutoka nje ya Mafia, inatukera. kwa hiyo kwa mwakahuu sasa tunasisitiza, hili jambo lisijirudie, kama ni kuvumiliatumevumilia kwa miaka ya nyuma huko inatosha sasa,enough is enough. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti,…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante kwa mchango wako mzuri.Mheshimiwa Mwantumu Dau, ajiandae Mheshimiwa Kinguna wewe kwa dakika tano. (Makofi)

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja.

MHE. MWATUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kuniona. Awali ya yote nimshukuru MwenyeziMungu kwa kunijalia kuwa na hali ya uzima na afya. Nishukuru

Page 213: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

ukumbi huu leo wote tuliopo hapa pia tupo wazima wa afyampaka hivi sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi naomba kuchangiaHotuba hii ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nachangia kuhusu JKThasa kwa vijana na kule kwetu Zanzibar. Kule Zanzibar kunavijana wetu ambao wanakwenda JKT na wanakuwa wazuritu wakirudi kule wameiva, lakini wakifika kule wanakuwahawana ajira rasmi za kujiajiri, wanahangaika isipokuwa ajirazao ziwe mikononi mwao. Vijana hawa wanakuwawanatupigia kelele sana sisi wazazi au kama hivi sasa mimini Mheshimiwa, lakini huko nyuma nakumbuka sisi Wabungewaliopita walikuwa wanapata hizi ajira kama kwa mtotowake au mtoto wa ndugu yake lakini ajira walikuwawanapata kwa mtu mmoja mmoja, kwa hiyo zoezi hililimeondoka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi naomba hili zoezilirudi tena sisi Wabunge tuwe mfano wa kupata kwa kilamtoto kama mmoja mmoja au katika jamii tulizonazowapate ajira hizi za Jeshi ili na wao wajiajiri na wajisikie. Nawanakuwa na hamu sana ya kwenda Jeshini, lakini ajirakama tunavyozungumza ni ngumu. Hili lirudi na lizingatiwesana ili wale vijana wawe na imani na Nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niwapongeze Jeshikwa kazi zao wanazozifanya na hasa jana tu, wakati miminakuja huku Bungeni nipo maeneo ya Mlandizi, ilitokea ajalimbaya kati ya basi la Tanga na coaster inayotokea Morogoro,walisaidia roho za binadamu pale… (Makofi)

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

T A A R I F A

MWENYEKITI: Taarifa.

Page 214: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,mzungumzaji anayezungumza anasema kwamba zamaniwatoto au jamaa za Wabunge walikuwa wanapewa ajiraJeshini, hii haijatokea hata kidogo. Wanapewa ajira Jeshinikutokana na uwezo wao, bila upendeleo, hakuna kitu kamahicho wala haitatokea wala haijatokea. Anapewa ajiraJeshini kutokana na uwezo wake, si mtoto wa Mbunge walamtoto wa DC wala mtoto wa Rais. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dau, taarifa hiyounaipokea?

MHE. MWATUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa hiyo siikubali kwa sababu mimi sikusema kwambahuyo Mbunge ndiye anayetoa hiyo ajira hapo.

MWENYEKITI: Endelea.

MHE. MWATUM DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nieleweke.

MWENYEKITI: Endelea na mchango wako.

MHE. MWATUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,umesikia, mimi naomba kwamba sisi Wabunge hivi sasatunaomba kwamba zikitokea hizi ajira za Jeshi basi kamakuna uwezekano tuzipate ili tuwasaidie wale vijana na walewatoto wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea na hotuba yanguhii…

MBUNGE FULANI: Majimboni!

MHE. MWATUMU DAU HAJI: …majimboni, hata ikiwamajimboni ikiwa kwa jamii lakini tunaomba kwambatupatiwe na sisi hizi ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi jana limeokoa roho zabinadamu pale Mlandizi kati ya basi la Tanga na basi la

Page 215: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

coaster linalotokea Morogoro, ana-overtake basi la Tangakwa bahati yule amejitahidi kulivusha lakini hakufanikiwalikaenda uso kwa uso dereva katoka miguu hana. Kwa hiyo,pale watu walishindwa kumtoa kila mmoja na imani yakebasi walitokea vijana wetu hawa wa Jeshi na wakaendapale wakaokoa roho zile wakawakwamua na palepaleikatokea gari wakapelekwa hospitali. Mimi ninawashukurusana na ninawapongeza sana kwa kitendo kilewalichokifanya jana. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Dau, badoWaheshimiwa Wabunge wako hapa unaweza ukawafuataukawaambia vilevile kuwashukuru. Mheshimiwa Kingu,dakika tano.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kutoa mchangowangu mdogo kwa ajili ya bajeti hii ya Wizara ya Ulinzi naJeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwa dhatiya moyo wangu nianze kwa kuipongeza Serikali yetu yaChama cha Mapinduzi kwa kazi kubwa inayofanywa navyombo vyetu vya ulinzi na usalama hasa Jeshi la Wananchiwa Tanzania na waswahili wanasema ukiona vinaelea ujuevimeundwa, nidhamu kubwa inayooneshwa na Jeshi laWananchi wa Tanzania ni kielelezo cha utekelezaji bora wasera za Chama cha Mapinduzi katika kipindi chote toka Taifalimepata uhuru. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, si siri, Jeshi la Wananchi waTanzania ni miongoni mwa majeshi duniani yenye nidhamuya hali ya juu. Taifa letu la Tanzania tumepata sifa kitaifa nakimataifa, tumeshiriki operesheni mbalimbali duniani na Jeshiletu; ninataka nijivunie hata makamanda mliopo humukwenye ukumbi; tunasema ya kwamba Chama chaMapinduzi kinatakiwa kipongezwe kwa kuwa katika kipindi

Page 216: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

cha takribani miaka 50 ya Uhuru Jeshi letu limekuwa nanidhamu… (Makofi)

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: …na dunia yoteimetutambua kwa kazi kubwa inayofanywa na wapiganajiwetu.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Alberto.

T A A R I F A

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Napenda kumpa taarifa msemaji kwaba si sahihikulihusisha Jeshi na chama cha siasa, Jeshi lipo kwa ajili yanchi, halipo kwa ajili ya chama na ndiyo maana tunasemazamani kabisa Jeshi limetolewa katika chama. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kingu, endelea.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,ukweli wa Chama cha Mapinduzi chini ya nidhamu ya Jeshila Wananchi Tanzania huwezi ku-exclude kwa sababuutendaji na utekelezaji wa sera zote toka tumepata uhurunchi hii imekuwa ikitawaliwa na Chama cha Mapinduzi,unawezaje ukakitenga Chama cha Mapinduzi, unawezajeukaitenga CCM na mafanikio makubwa yanayopatikanakutokana na nidhamu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja niwaambieWaheshimiwa Wabunge, nidhamu ya Jeshi letu na ndiyomaana hata leo mchana wakati kuna hoja zimetolewa juuya vijana wa Jeshi la Polisi wamepigapiga risasi pale juukidogo jana kwa sababu ya tukio lilikuwa limetokea kwaMheshimiwa Malima. (Makofi)

Page 217: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

Mheshimiwa Mwenyekiti, let me tell you one thing,tunapozungumzia nidhamu ya vyombo vya dola, unajuakuna mataifa mimi nimejaribu kutembeatembea kidogoduniani, kuna mahali haya mambo tunayoyaona Tanzaniasisi tunayapuuza lakini nataka niwaambieni hawa wapiganajiwa Tanzania kama ni Bunge tukiamua leo tukasema kwambakwa nidhamu wanayoionesha mimi natoa rai kabisaWaheshimiwa Wabunge kwa bajeti zinazokuja naomba Jeshila Wananchi wa Tanzania tulipe kipaumbele cha kwanzakwa sababu wapiganaji hawa wameonesha nidhamu yahali ya juu na Taifa letu limepata sifa kitaifa na kimataifa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niende katika sektanzima ya suala la JKT.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba hizo interruption uzipuuze ili niweze kuendelea namchango wangu kwa sababu nina muda mfupi.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, JKTkama moja ya sehemu ya kuzalisha ajira, ninaomba nitoeushauri kwa Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi. JKT,ninatoa ushauri, kwa sababu JKT ina-recruit vijana wengiwanakwenda kupata mafunzo, naiomba Serikali tutengefedha za kutosha, vijana wanapokwenda JKT wakafanyatraining ya kijeshi, wakamaliza kwa kipindi cha miezi sitawapelekwe na watafutiwe mashamba makubwa wafanyeuzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii italisaidia Taifa kupatachakula lakini pia vijana hawa kwa kipindi hicho watakuwawanapata ajira in phase, wamemaliza walichozalishakinakuwa mali yao wanaondoka wanaingia wengine, hivi

Page 218: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

218

ndivyo wanavyofanya mataifa makubwa kama China namataifa mengine duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ninatoa ushauri,wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania sasa hivi kunachama chao kinaitwa MUWAWATA, huu ni umoja wawastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kwa maslahiya usalama wa nchi si sahihi sana umoja huu kuwa nje yamfumo wa usimamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.Hatari hii inaweza ikajitokeza wakaingiliwa na kuanzakulishwa sumu na kusababisha uasi kwenye nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikaliya Chama cha Mapinduzi, MUWAWATA waendelee kuwa nauratibu chini ya Serikali kupitia Jeshi la Wananchi kwa sababuhawa ni wapiganaji wa akiba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina takwimu, miakamichache ya nyuma MUWAWATA ulikopeshwa bajaji nawakalipishwa hela nyingi na vikundi vya wafanyabiashara,this is very dangerous kwa security ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa ushauri, kaka yanguKamanda Mabeyo najua uko hapa, kaka yangu MheshimiwaDkt. Mwinyi, najua uko hapa kipenzi cha Watanzania,ninaomba upeleke hii proposal mkahakikishe kwambaMUWAWATA inakuwa chini ya usimamizi wa Jeshi la Wananchiwa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nianze kwa kuunga mkono hoja ya Wizara ya Ulinzi

Page 219: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

219

na Jeshi la Kujenga Taifa kuhusiana na makadirio ya matumiziya fedha ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dunia inashuhudiamabadiliko makubwa katika mifumo ya maisha na mazingiraya kiusalama yasiyotabirika. Katika mazingira haya, ulinzi wamipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na uhuru wanchi yetu ni jambo la kufa na kupona linalopaswa kupewaumuhimu mkubwa na wa kipekee sasa kuliko wakatimwingine wowote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika zama hizi zamabadiliko makubwa ya teknolojia na changamoto zaushindani katika ukuzaji uchumi wa viwanda, kama nchiusalama wetu na uhuru wetu unategemea sana uwepo wajeshi imara la kisasa lenye weledi, vifaa vya kisasa, uzalendona nidhamu ya hali ya juu. Hivyo basi ni wajibu wetu kamaTaifa kuhakikisha inakuwepo bajeti ya kutoshaitakayoliwezesha jeshi letu kukabiliana kikamilifu nachangamoto za sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Mkinga inapakanana nchi jirani ya Kenya. Katika jitihada za kuimarisha ulinziHalmashauri ya ilitenga fedha za kujenga daraja ili kuwezeshaulinzi na ukaguzi wa mpaka wetu. Hii ni kutokana na ukwelikuwa kabla ya uwepo wa daraja hilo, ukaguzi wa mpakawetu ilibidi ufanyike kwa kupitia Kenya. Kazi ya kujenga darajahilo ilikabidhiwa kwa JWTZ. Natoa pongezi kwa JWTZ kwakukamilisha kazi ya kujenga daraja hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie fursa hii kuiombaSerikali iongeze nguvu katika ulinzi wa mipaka yetu kwakuweka miundombinu muhimu kama barabara na madarajayanayokidhi viwango na mahitaji ya kijeshi katika maeneoyote ya Wilaya za mipakani.

Aidha, fedha na jukumu la kujenga miundombinumuhimu katika maeneo haya ya kimkakati, kiulinzi nakiusalama lisiachwe mikononi mwa Halmashauri bali liwejukumu la moja kwa moja la JWTZ.

Page 220: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

220

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Mwakijembe nimiongoni mwa kata 22 za Wilaya ya Mkinga. Kata hii ipokatika mpaka wetu na nchi ya Kenya na kwa miongo kadhaawananchi hawa wamefanya kazi kubwa ya kuwa walinziwa mpaka wetu. Naipongeza sana Serikali kwa uamuzi wakewa kuimarisha ulinzi katika Kata ya Mwakijembe kwenyempaka wetu na nchi ya Kenya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, wakatinaipongeza Serikali kwa hatua hii, utekelezaji wake umekuwana dosari na hivyo kuitia doa Serikali. Doa hili linatokana naJWTZ kutwaa mashamba ya wananchi bila kutoa fidia stahikikwa wananchi. Inasikitisha kuwa Jeshi lilitumia mabavukuwapora wananchi ardhi yao tena kwa kufyeka mazaoyaliyokuwa mashambani. Hali hii imeleta manung’uniko nawananchi wanaona wamedhulumiwa na Serikali yaowenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kihistoria eneo hili limekuwamali ya wananchi kwa miongo na vizazi kadhaa. Hata paleHalmashauri ilipoamua kuanzisha skimu ya umwagiliaji,iliamua kuyajumuisha maeneo haya ya wananchi kwenyeskimu lakini ikahakikisha umiliki wa maeneo hayo unaendeleakuwa mikononi mwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba sana Serikali ifanyetathmini ya haraka kwa ardhi ya wananchi iliyotwaliwa iliwananchi hawa waweze kulipwa fidia stahiki. Wananchiambao mashamba yao yametwaliwa ili kuwekwa kambi/makazi ya jeshi ni Ndugu Benard Kinyili (ekari moja); NduguNgoma Joseph (ekari moja na nusu); Ndugu Hamisi Joseph(ekari moja na nusu); Ndugu Mlewa Malonza (ekari mbili) naNdugu Mwanza Kiziku (ekari mbili).

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hojanikiamini kuwa malalamiko ya wananchi wa Mkingayatapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Page 221: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

221

MHE. MGENI JADI KADIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afyanjema na kuniwezesha kuchangia hotuba hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanajeshi wanaostaafuwanahangaika, hawapati stahili zao mapema, wanapatataabu sana. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali iwaangalie kwajicho la huruma. Hawa ni watumishi wetu kamawatumishi wengine mpaka wengine wanafariki bila kupatahaki zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu huduma ya umemekatika Kambi ya Jeshi, Jeshi ni taasisi kubwa leo kukatiwaumeme itakuwa hawajatendewa haki. Wanajeshi ndiowanatulinda sisi ndani ya nchi yetu na mipaka ya nchi yetu nilazima tuwape heshima. Tunalipongeza Jeshi letu kwa kazikubwa. Kwa hiyo, wanastahili kulipwa maslahi makubwa namarupurupu wapewe pamoja na kupandishwa vyeo iliwaweze kuitumikia nchi yetu kwa weledi mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Vitongoji Ali Haji Campwaboreshewe nyumba zao, ni za zamani na nyingi ni mbovuna nyumba zilizoko Matangatuani Pemba nazo ziboreshwe.Kambi na Wanajeshi iliyoko Matangatuani ina wanajeshi walioimara na wanafanya kazi kwa weledi mkubwa.

Nashauri wanapopata uhamisho wapewe fedha zakutosha ili watoto wao wasipate shida na matatizo yakuendesha maisha yao. Pia nataka kujua ni kwa niniwanajeshi wanapopata uhamisho wasichukue familia zaoili kuwapunguzia matatizo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nichangie kwa kutoa masikitiko yangu katikamaeneo mawili tu. Moja ni suala la kutumia vibaya Jeshi letula Ulinzi (JWTZ). Si sahihi hata kidogo kwa jeshi letu kutumiwakuvuruga shughuli za kidemokrasia nchini hasa chaguzi.

Page 222: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

222

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ni mbaya na ya kutishaZanzibar. Binafsi nilipata fursa ya kuwa Zanzibar wakati wauchaguzi mdogo wa marudio Jimbo la Dimani. Nilishuhudiamalori ya JWTZ yaliyobeba “mazombi” watu waliovalia sareza jeshi na soksi usoni (wakijificha) walioshikilia silaha juuyakienda na kurudi barabara ya Fumba. Kwa hakikanilishtushwa sana na tukio hili na kwa heshima kubwanamwomba Mheshimiwa Waziri akomeshe vitisho hivi namatumizi mabaya ya jeshi letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili linalonisikitishani Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kushindwa kujitegemea kiuchumina kulisaidia Taifa. Hili ni jeshi lenye makambi karibu nchi nzimana nguvu kazi ya kutosha ya vijana wetu wanaokwenda hukokaribuni muda wote. Jeshi lina mashamba makubwa, miradiya mifugo, ujenzi na kadhalika. Ni vipi Jeshi hili lishindwekuendesha kilimo cha kisasa na chenye tija? Waziri kwa kwelialifanyie kazi suala hili ipasavyo. Kwa wataalam wa fanimbalimbali waliojaa JKT ni aibu kubwa kuwa na jeshi la ainahii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine dogoninalopenda kuchangia kwa leo ni kuomba Bunge kuipaWizara hii hadhi yake stahiki yaani kuwa Wizara ya Muungano.Kwa hadhi hii Wizara hii inastahiki kupewa muda wa kutoshakwa Wabunge kuchangia kwa nafasi badala ya kupangiwasiku moja tu ambayo inaanza kwa kipindi cha maswali namajibu. Nililisema Mkutano wa Bunge la Bajeti ya mwakauliopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni Bunge la Jamhuri yaMuungano na siyo la Tanzania Bara. Imekuwa ni tabia/mazoea ya Bunge hili kutumia muda mwingi (mpaka sikutatu) kujadili masuala ya Tanzania Bara tu (Kilimo, TAMISEMI,Afya na kadhalika) badala ya masuala ya Muungano (Ulinzi,Mambo ya Nje, Ofisi ya Makamu wa Rais na kadhalika).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho naomba Wazirimhusika aipitie vizuri hotuba ya Kambi ya Upinzani, kwauadilifu na bila hiyana kwa maslahi mapana/ya jumla ya nchi

Page 223: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

223

yetu na maslahi mahsusi ya walinzi wetu (wanajeshi) wamajeshi yote mawili –JWTZ na JKT.

Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru na naungamkono hotuba ya Kambi ya Upinzani na kumtakia kila la kheriWaziri wa Ulinzi kwa jukumu nyeti na muhimu alilopewa nanchi yetu.

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, washauri wa mgambohawatendi haki katika kuchukua vijana wanaojiunga na JKTna wengi wao wanatuhumiwa kuchukua rushwa kwakuwapa vijana nje ya eneo la Wilaya husika. Jambo hililinachafua jeshi letu. Hatua ichukuliwe kuchunguza mambohaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tunduru Kusini inapakana naMto Ruvuma na Msumbiji lakini eneo lote la mpaka huuhakuna ulinzi wowote wa jeshi na wala hamna mawasilianoyoyote ya simu jambo ambalo ni hatari kwa nchi. Hata ilebarabara ya mpaka ambayo ilikuwepo miaka 1970 na 1980haipo kabisa, barabara hiyo imekufa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tunduru kulikuwa na Kambiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania maeneo yale yamebakikuwa mapori. Hivyo tunaomba Serikali iyakabidhi maeneoyale kwa Halmashauri ya Wilaya ili yatumike kwa shughulizingine za wananchi ikiwa ni pamoja na makazi ya wananchi.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza naunga mkono hotuba ya Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Kujenga Taifa ni laWatanzania wote na inapotokea Kambi ya Jeshi inapokuwakatika kata au jimbo au vijiji naona ni fursa na faraja kwajamii inayopakana na kambi hizo. Hali imekuwa tofauti kwa

Page 224: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

224

mahusiano kati ya Chita JKT ndani ya Jimbo la Mlimba, Wilayaya Kilombero na Kata ya Mngeta, Kijiji cha Ikule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya wananchi wa Kijijicha Ikule inasikitisha. Ni kwa miaka mingi wananchi wa kijijihicho wanaishi na kufanya shughuli zao za kilimo kwa maishayao yote. Hivi nichangiapo hapa na Waziri anajua wananchiwale wamenyang’anywa maeneo yote ya kilimo. Kibayazaidi hata mazao yao ya chakula, mahindi, ndizi, mihogo,viazi, miwa, mpunga na kadhalika vyote vilifukiwa na trektana baadhi ya wanajeshi na kuzuia kabisa kufika huko wakidaini maeneo ya jeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ingawa wananchi naviongozi wa Serikali ngazi ya kijiji waliopo na waliopitawanasema na wako tayari kuongea popote kuwahawajawahi kuidhinisha mashamba yao waliyokuwawanalima miaka yote kabla hata ya kambi hiyo kuwepohapo kuwa walikubaliana katika Mkutano wa Kijiji kwamujibu wa Sheria ya Ardhi kwamba wameridhia kukabidhihiyo ardhi kwa jeshi. Hivi niwasilishapo, tokea mwaka 2016Desemba hadi leo, wananchi na viongozi wa kijiji, kataakiwemo na Diwani wa Kata hiyo wapo mahabusu kwamadai mbalimbali na hawajui hatma yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuundwe Tumehuru kwenda kijijini hapo kutafuta ukweli wa masualambalimbali yanayoendelea huko, kwani inasemekana katikavurugu za kugombania mashamba, yuko mwanajeshialiyeuawa. Pia zipo taarifa kwamba wananchi wengi naowameuawa (habari ambazo hazijathibitishwa) na hali yakijijini hapo si shwari hata kidogo, kwani wakati wowotewanajeshi huingia kijijini na kukamata na kupekua nyumba,hata wakati wa usiku na kuleta mashaka kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia kusema uwepo waKambi ya Chita ni faraja kwetu na uhakika wa kiulinzi kwaraia, isipokuwa manyanyaso ndiyo karaha kwa majirani waKijiji cha Ikule.

Page 225: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

225

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nipate majibu yaSerikali. Ahsante.

MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nianze kuchangia kuhusu JWTZ wanaolinda mpaka - Wilayaya Kakonko. Wapo wanajeshi wanaolinda mipaka ya nchiyetu kufuatia ujio wa wakimbizi Wilayani Kakonko. Wanajeshihawa husumbua raia wanaotoka Burundi kuja kwenyemasoko ya ujirani mwema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nimepata taarifa juu yaJWTZ kupiga Warundi waliokuja soko la Kabare, Kata yaGwarama. Nashauri askari hawa watekeleze majukumu yaobila kuvunja sheria za nchi, wawe karibu na wananchi ilikujenga mahusiano mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ma-DC na RC kuvaasare za jeshi; Wakuu wa Wilaya na Mikoa ambao ni wanajeshiwamekuwa wakivaa mavazi ya kijeshi wanapokuwawanatekeleza majukumu yao ya Kiserikali ofisini. Jambo hilihuwapa hofu sana wananchi ambao hawajazoea kuonaMkuu wa Wilaya/Mkoa akawa ndani ya vazi la kijeshi na hivyokushindwa kupeleka shida zao kwa wakuu hao. Huu siutawala bora pale ambao mtawala anaogopwa na waleanaowaongoza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mchakato wa vijanakujiunga na JKT; zoezi la kusajili vijana wanaojiunga namafunzo ya JKT linagubikwa na vitendo vya rushwa sana nahivyo zoezi zima kutokuwa huru kwa raia wote.

Mheshimiwa Mwenyeikiti, Kambi ya JKT Kamembwabado mipaka yake haijakaa vizuri kwani raia waKazilamihunda wanadai eneo lao linavamiwa na jeshi nahivyo kuleta malalamiko mengi. Nashauri ufanyike upimajirasmi wa kuweka mipaka ukishirikisha viongozi wa Kijiji chaKazilamihunda na uongozi wa Jeshi (Kambi ya Kanembwa).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa SUMA JKT ambaponi jeshi la uzalishaji mali lielekeze miradi yake kufanyika/

Page 226: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

226

kupatikana kila kambi ili JKT zote nchini ziweze kutekelezamajukumu ya mradi huo bila kutegemea toka Dar es Salaam.

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamojana Jeshi letu kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba hii naombanichangie kwa kumuomba Mheshimiwa Waziri maana anajuana kama amesahau nimkumbushe, ni ukweli usiofichikaWilaya ya Kilindi katika Mkoa wa Tanga ni eneo ambalolinanyemelewa na watu wabaya wenye kuhatarisha usalamawa nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wapo wananchi takribani50 au pungufu wamekamatwa kwa kujihusisha na vikundivya ugaidi na kwa kuzingatia jiografia ya Wilaya ile yenyemisitu, milima mingi, hivyo kuwa ni sehemu ya kujificha.Nimuombe Mheshimiwa Waziri kwa kushirikiana na viongoziwetu wa Jeshi la Ulinzi kama taratibu zitaruhusu basi tupatiweKituo cha Jeshi ambacho kitasaidia kulinda amani ya eneohili pamoja na Taifa kwa ujumla, tusisubiri mpaka hali mbayaikatokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeyasema hayanikifahamu kabisa katika Mkoa wa Tanga tuna Kambi ya JKTiliyopo Wilaya ya Handeni lakini pana umbali baina ya Wilayahizi mbili. Mimi naamini kabisa kuna gharama ya kuanzishavituo hivi lakini usalama wa eneo hili ndiyo wa muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia hoja hii muhimuya ulinzi wa nchi yetu na mipaka yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hiikumshukuru Rais, Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli na Serikali yake hasa Waziri wa Ulinzi na wataalam

Page 227: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

227

wake kufika katika Jimbo langu la Morogoro Kusini Masharikikatika Wilaya ya Morogoro Vijijini kufuatilia uwanja wa ndegewa Jeshi letu pale Kizuka Ngerengere. Tunasema ahsantesana.

Mheshmiwa Mwenyekiti, pia namshukuru Rais,Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufulu kwamaamuzi yake ya kuagiza kutujengea barabara ya lamikutoka Ubena – Zomozi – Kizuka mpaka Ngerengere kupitiauwanja wa Kizuka.

Mheshiwa Mwenyekiti, baada ya shukrani hizo za watuwa Morogoro Kusini Mashariki hususani wananchi wa Tarafaya Ngerengere na Tarafa ya Mvuha, naomba sasa nitoe ombilangu rasmi kwa Serikali hasa kwa Rais, Mheshimiwa Dkt. JohnPombe Joseph Magufuli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa tuna Kambi mbiliza Jeshi pale Ngerengere yaani ya Kizuka na Sangasanga nakwa kuwa barabara itakayowekwa lami ni ya Ubena –Zomozi – Kizuka - Ngerengere na kwa kuwa umbali kutokaKizuka - Ngerengere - Sangasanga siyo mbali na Kambi yaSangasanga wanatumia barabara ya Mdaula – Sangasangayenye urefu wa kilometa 10, kwa hiyo basi, naomba barabarahii nayo iwekwe lami kwani watoto hawa wa Sangasangana Kizuka ni baba na mama mmoja ili wale Sangasangawasione wametengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali yangukulipa uzito suala hili na hasa kwa umuhimu wa jeshi letu nahasa kikosi hiki cha Sangasanga kutokana na uzito wamajukumu yake. Naomba barabara ya Mdaula – Sangasanga- Ngerengere kuwekwa lami ili kuunganika na ile ya Ubena -Kizuka - Ngerengere na kurahisisha usafiri kwa jeshi letu nawananchi kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja,ahsante.

Page 228: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

228

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuchangia kuhusu hali ya usalama nchini. Kwa sasahivi unaweza kusema kuna utulivu tu; kwa sababutumeshuhudia siku za hivi karibuni pamekuwepo na matukiomengi sana ya watu kuuawa bila sababu, kwa mfano askariwaliouawa huko Kisarawe kwa kupigwa risasa na watuwasiojulikana, matukio kama haya yametokea Pangani naMwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali imeshafanyauchunguzi wahusika ni akina nani? Watu hawa wanawezakuanza taratibu uhalifu huu kwa kuanzia pembezoni mpakawakafika mjini, tutakuwa tumechelewa, je, Serikaliinawaeleza nini Watanzania kuhusu matukio hayayanayotishia usalama wa Watanzania?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Jeshi hil ilinajishughulisha na kazi za maendeleo kupitia vikosi vyakekama ujenzi wa barabara, mpaka gari wamewahi kuunda,na kwa kupitia Jeshi hili tunaweza kuokoa fedha nyingi sanahata kuwapa tender za samani za ofisi za Serikali kamawalivyotengeneza madawati, nawapongeza sana. Hatahivyo changamoto kubwa ni utolewaji wa fedha zamaendeleo ndiyo unawakwamisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano waliombashilingi 248,000,000,000/= kwa ajili ya maendeleo lakiniwamepata shilingi 35,000,000,000/=, sawa na asilimia 14.5 yabajeti waliyoomba. Je, kwa ufinyu huu unaotolewawataweza kutimiza majukumu yao? Hii ni kuwarudishanyuma, badala ya kuendelea wamebakiwa na kulipamadeni. Tukumbuke Jeshi hili kwa sasa ndilo linalotusaidiakuwajenga vijana wetu kimaadili kwa kwenda jeshini, walewanaomaliza kidato cha sita. Je mpaka sasa hivi Serikaliimeweza kuchukua vijana wangapi kwenda jeshini?

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii niWizara muhimu kwa uhai na mustakbali wa nchi yoyote,bado naafiki Jeshi halisi la JKT kimuundo. Ningependa Jeshiletu liende katika usawa kivifaa, lakini imeonekana Jeshi kwa

Page 229: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

229

sasa halina powerful public branding ili kusimama kama taasisiyenye chapa ya Kitaifa. Wananchi hupata public relationsya Jeshi only wakati wa sherehe tu, na si vinginevyo na hivyoJeshi hubakia katika obscurity. Bila shaka mazoezi ya kijeshini moja ya njia hizo kama ile amphibious iliyofanywaBagamoyo. Ningependa Jeshi liji-brand pia kwenye kufanyakazi za dhamana mara zinapotokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa kuna dharura zamvua/upepo lakini Jeshi halijitokezi kikamilifu. Kazi hizohufanywa kwenye matukio ya big magnitude tu. JKT inapaswaipitie upya jukumu li le la kujenga uzalendo ambalolinaonekana limeshindwa hata katika hili, inafaa JKT ijitathminiupya.

MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja. Sehemu kubwa ya mpakakati ya Tanzania na Uganda iko Wilaya ya Misenyi – Kagera.Kama unavyofahamu kuna mambo mengi yanayoendeleakatika mpaka huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Serikali iwe karibuzaidi na ifuatilie kila siku yanayoendelea kwenye mpaka huokwa nia ya kuimarisha ulinzi, ujirani mwema na kuimarishautangamano. Aidha, suala la ng’ombe wanaoletwa kutokanchi jirani (Uganda) na kuja kula majani Tanzania inabidiliangaliwe kwa umakini na lidhibitiwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo uwe kwambaardhi ya Tanzania itumiwe na Watanzania tu na kwambawanaoleta mifugo kutoka nchi jirani wadhibitiwe na watumieardhi ya nchi zao. Jambo hili la kudhibiti mifugo kutoka nchijirani litawezekana tu kama wale tunaowapa majukumu yakulinda mipaka wakizingatia miongozo wanayopewa nakuzingatia maadili ya Tanzania. Aidha, usalama waWatanzania wanaoishi maeneo ya mipakani na mali zaoupewe kipaumbele pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

Page 230: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

230

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninatambua umuhimu wa Wizara hii na kazi kubwa sana nanzuri inayofanyika. Aidha, nianze kwa kumpongezaMheshimiwa Waziri kwa namna anavyoongoza Wizara hiikwa hekima na utulivu mkubwa . Pamoja na pongezi hizinaomba nimpongeze pia Jenerali Venance Salvatory Mabeyokwa heshima kubwa aliyopewa na Mheshimiwa Rais, kwakumteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, hongera sana. Kwaimani kubwa aliyonayo Rais wetu kwake ndivyo na sisiWatanzania tuna imani sana na yeye. Tunaamini ataendeleakushirikiana na viongozi wote walio chini yake na walio juuyake ili kuendelea kuwa na utulivu na amani tuliyo nayo nchinipamoja na usalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi hizi pianiwapongeze wanajeshi wote kwa kazi nzuri ya kulindamipaka ya nchi yetu, hakika tunawapongeza kwanitunatambua kazi kubwa waliyonayo. Wakati wenginetunaendelea na shughuli zetu wao wakiwa katika shughulinzito ya kutulinda wakati wengine tukiwa tumelala, waowakiwa macho kutulinda. Hakika tunawashukuru sana. Tunaimani na Jeshi letu, Mungu awabariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya pongezi hizinaomba nitoe maoni yangu kwa ufupi kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa hapa Tanzania vijana walioko sekondarina hasa wanaohitimu kidato cha nne, mitihani yao huwainafanyika mwishoni mwa mwezi wa kumi kila mwaka. Hivyowatoto hawa wanaotajarajia kuendelea na masomo yakidato cha tano husubiri kwa takribani miezi minane na zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo hali hiyo huwa ni kipindicha mpito mgumu sana kwa wazazi na hata watoto piakwani mazingira yanaweza kumuathiri mtoto na kujikutaanabadili nia yake ya kuendelea na masomo yake ya kidatocha tano ama wengine kuangukia kwenye tabia za amakupata mimba au dawa za kulevya au ulevi na tabia nyinginezitakazokwamisha ndoto yake.

Page 231: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

231

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo kutokana na hali hiyo,naomba nishauri kuwa watoto hawa wanaomaliza kidatocha nne, mara baada ya matokeo yao ya mitihani Wizaraiandae namna ya kuwachukua watoto hawa kujiunga naJKT kwa miezi kati ya sita na mitatu ili wasipoteze muda burena pia kutunza uadilifu na nia yao njema ya kuendelea nashule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Jeshi la KujengaTaifa ya mwaka 1964 (na marekebisho yake) kifungu cha 5(2)kinatoa nafasi kwa kijana mwenye umri wa miaka 16kujiunga na Jeshi hilo; hivyo haitakuwa tatizo kuwachukuawanafunzi hawa. Kwa sheria hiyo Wizara iongee/ishirikianena Wizara ya Elimu ili kubadili mfumo wa kuwapeleka JKTvijana wanaomaliza kidato cha sita badala yake tunaanzana wanaosubiri kwenda kidato cha tano kwani hawa wanamuda wa kutosha sana kuliko wa kidato cha sitawanaosubiri kwenda vyuo vikuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu, vijanawatakaofaulu kuanzia division one hadi division three ndiowaweze kupata nafasi ya kujiunga na JKT. Pia itawezakurahisisha kuwapata wanaotaka kujiunga na Majeshi yetukama Polisi, Magereza, Uhamiaji, Jeshi la Wananchi nakadhalika kuliko utaratibu wa sasa unaotumika kuwasakamitaani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho najua jambo hililinaweza kuonekana ni gumu sana, lakini ninaona manufaayake ni makubwa zaidi, kwani tunaokoa Taifa letu na nguvukazi pamoja na wasomi na tunapata waadilifu zaidi kwaniwatoto hawasahau.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa naungamkono hoja asilimia mia moja.

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hotuba hii.

Page 232: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

232

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Tabora una Kambiya muda mrefu ambayo inaitwa Milambo Barracks.Kumekuwa na changamoto za uchakavu wa miundombinuya barabara zinazozunguka kambi hiyo ya muda mrefu.Niombe Serikali iangalie mambo yafuatayo:-

Kwanza, ukarabati wa barabara, pili, ukarabati wanyumba zao na tatu, ukarabati wa jengo la geti lililoko kablaya kuingia ndani ya kambi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha niiombe Serikalikupeleka vifaa vya kisasa kwa ajili ya Hospitali ya Jeshi, ipelekeMadaktari Bingwa hususani wa magonjwa ya wanawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuomba msaada huokunatokana na kutokuwa na Hospitali ya Manispaa ya Wilayana hivyo kusababisha watu wengi kwenda Jeshini kupatahuduma hiyo. Miundombinu ya maji ikarabatiwe kwani nimichakavu sana.

Vilevile Serikali ilipe madeni ya maji/TANESCO ilikusitokee ukataji wa huduma hizo kwenye majeshi kwanikukatiwa huduma hizo ni aibu kubwa. Fedha za matumizihayo zipelekwe kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Serikali kupelekafedha zilizoombwa bila kupunguza, pia kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hotuba hii.

MHE. RISALA S. KABONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kupata nafasi ya kuchangia katika Wizara hiimuhimu kwa nchi yetu. Kama ilivyo katika dira ya Taifa yakulinda na kudumisha amani na usalama wa Taifa letu;pamoja kuendelea kulinda Jamhuri ya Muungano waTanzania dhidi ya maadui wa ndani na nje ya nchi yetu;usalama wa mipaka ya nchi, mgogoro wa mpaka wa ZiwaNyasa kati ya nchi ya Tanzania na Malawi umekuwa wa mudamrefu hivyo kuendelea kuathiri ukuaji wa uchumi kwa nchiyetu hasa kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Page 233: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

233

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro huo unaendeleakuathiri shughuli za uwekezaji katika eneo la Ziwa Nyasa nahivyo kufanya mdororo wa kiuchumi kwa wananchi nakupoteza mapato katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba MheshimiwaWaziri atakapokuja kuhitimisha aniambie mgogoro huuumefikia wapi ili kuweka mahusiano mazuri kati ya nchi yaTanzania na Malawi na pia kuinua uchumi wa nchi yetukupitia fursa zilizopo katika Ziwa Nyasa na mikoa ya Nyandaza Juu Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ajira kwa vijanawaliopata mafunzo ya JKT; kumekuwa na changamotokubwa ya ajira nchini na hii ni pamoja na vijana wanaomalizamafunzo JKT na kupelekea vijana hawa kujiingiza katikavitendo vya uvunjaji wa amani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka ya nyuma taasisi zaKiserikali, kwa mfano TANAPA ilikuwa ikichukua vijana wengiwaliomaliza JKT na kuwapatia ajira hali ambayo kwa sasaimepungua na kufanya nidhamu kupungua sana kwa taasisizinazojihusisha na masuala ya ulinzi na usalama wa maliasilizetu.

MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nianze kuchangia kuhusu kuyapa uwezo wa kifedhamashirika ya Nyumbu, Mzinga na SUMA JKT. Nikiwa mjumbewa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama nilitembeleaNyumbu na wajumbe wenzangu na kujionea kazi nzuriinayofanywa na shirika hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo Shirika lingewezakufanya kazi kwa ufanisi zaidi kama lingekuwa huru hasakwa mujibu wa sheria. Ilivyo sasa shirika hili kwa mujibu washeria liko chini ya Msajili wa Hazina hali hii inasababisha si tumgongano wa kimaagizo, lakini pia utekelezaji wa mipangona maono (vision) ya shirika unachelewa kwa sababu yamlolongo wa kiutawala, kwa mfano kuna nchi zilioneshania ya kushirikiana na Shirika la Nyumbu tangu mwaka 2007,

Page 234: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

234

hata hivyo uamuzi haukutolewa kwa wakati kutokana nasababu za kisheria na kiutawala na hivyo kupoteza fursa hiyomuhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo nashauri Serikali ioneuwezekana wa kuleta mabadiliko ya sheria ili Shirika laNyumbu liwe chini ya Wizara/Jeshi kwa asilimia moja.Ninaamini uchambuzi wa kina ulifanyika, itathibitika kuwamabadiliko ya sheria yataleta tija kwa Shirika na Taifa kwaujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sikufanikiwa kutembeleaMzinga kama ilivyokuwa kwa wenzangu, lakini uhalisia nikuwa kuna fursa za wazi za kiuchumi na kimapato ikiwaMzinga itawezeshwa, ninaamini kuna soko kubwa nje ya nchikutokana na bidhaa zitakazozalishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu SUMA JKT, binafsinimetembelea kila mwaka maonesho na huwa sikosikutembelea mabanda ya SUMA JKT. Pia nimefanya ziarabinafsi ya mafunzo katika Kambi ya Ruvu nikiwa na baadhiya vijana kutoka Jimboni. Hakika iwe ni katika kilimo,ufugaji,ufundi na kadhalika, SUMA JKT inafanya kazi nzuri mno.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ulinzi tumeshaurimara kadhaa kuwa maeneo yote ya Serikali na taasisi zaumma ulinzi ufanywe na SUMA JKT, lakini pia Serikali ihakikishewote wanaodaiwa wanalipa kwa wakati, ikibidi fedha zaoza OC zikatwe zikalipe deni. SUMA JKT ipewe wigo mpanakatika kushiriki suala la kuelekea uchumi wa viwanda hasaviwanda vidogo vidogo. Hil i l itawezekana tu ikiwaitawezeshwa kifedha kwa namna (mechanism) ambayoSerikali itaona inafaa; kwa mfano kuidhamini kwa mikopoya riba nafuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mafunzo ya vijana -JKT; katika ukurasa wa tano wa kitabu cha Taarifa ya Kamatiimeeleza kuwa ikiwa fedha kiasi cha shilingi bilioni nanezitatolewa JKT itaweza kukarabati makambi na hivyokuongeza vijana wa kujiunga na JKT. Mpaka tunajadili bajeti

Page 235: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

235

hii ni kiasi kidogo cha shilingi bilioni moja tu kimetolewa. Sualala mafunzo ya JKT kwa vijana wetu ni muhimu sana kwasababu linaongeza uzalendo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo wengi waowanaingia katika ajira na kujiajiri. Ushauri wangu, katikawakati huu ambapo matumizi ya mitandao yamekuwayakichangia kumomonyoa maadili ya vijana, mafunzo hayani muhimu katika kujenga Taifa la kesho linalojitambua.Ninaamini kila kijana anayepitia JKT anajenga ushawishi(influence) kwa vijana wengine na wasiopungua 100 katikakijiji au mtaa anaoishi na kwa ushawishi huo wapo vijanawaliohamasisha vijana wenzao kujiunga katika vikundi vyakuzalisha mali. Naomba kuwasilisha.

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza kabisa napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri,Mkuu wa Majeshi Jenerali Mabeyo na makamanda wote kwakazi nzuri ya ulinzi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili naunga mkono hoja hiikwa asilimia mia moja. Pamoja na kuunga mkono hoja hiinaomba kuchangia maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sanaMheshimiwa Waziri kwa kurudisha kambi ya JKT yaMpwapwa. Hata hivyo kambi hiyo ina mapungufu yafuatayo:-

Kwanza ni kuhusu upungufu wa majengo, hivyonashauri Serikali iwajengee majengo ya kutosha kwa ajili yamakazi yao na ofisi za kufanyia kazi. Pili, vitendea kazi kamavile magari, matrekta kwa ajili ya kilimo kwa kuwa eneo hiloni zuri kwa kilimo na chakula kinachopatikana watumiewenyewe ili kupunguza gharama ya Serikali kupeleka chakulakambini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, JKT Mpwapwa ianzekuchukua vijana wa kujitolea wa form four na form six kamamakambi mengine ya JKT. Katika JKT Makutupora majengoyafanyiwe ukarabati, vyombo vya usafiri viongozwe kama

Page 236: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

236

vile magari na kadhalika. Posho za askari Wanajeshi wa JKTna JWTZ ziongezwe. Majeshi yote yajengewe makazi badalaya kupanga uraiani, kambi zijengwe za kutosha ili wanajeshiwote wasipange mitaani. Usafiri katika majeshi yote hautoshihivyo nashauri magari yaongezwe katika kambi zote ikiwemoKambi ya Ihumwa, Makutupora na Mpwapwa. Posho yachakula ya wanajeshi wote iongezwe haitoshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia huduma ya majiiboreshwe na barabara zikarabatiwe katika Kambi ya JKTMpwapwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii kwaasilimia mia moja.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kumekuwa na matukio kadhaa hapa nchini ya wananchikuokota mabomu ambayo yalikuwa ardhini tangu wakatiwa Vita ya Majimaji na Vita vya Dunia. Mifano ni mingi, lakinikwa Mkoa wa Lindi maeneo ya Mahiwa, Kiwalala na Ndandayamekuwa yakitokea mara kwa mara .

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Jeshi lifanyeutafiti wa kutosha hususan katika maeneo yote ambayo Vitavya Majimaji vilipigana pamoja, Vita vya Kwanza na vya Pilivya Dunia. Wanajeshi wa Ujeremani katika maeneo mengiwalizika silaha zao ardhini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafadhali suala hili mlipeuzito unaostahili mfanye utafiti wa kutosha ili kuepushamadhara zaidi. Mifano mizuri ni maeneo ambayo Wajerumaniwalikuwa na mashamba ya mkonge na baadhi ya sehemuya ngome zao. Ahsante sana.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, ni vyema Serikali ikatoa fedha kwa wakati zamaendeleo kwa Jeshi letu ili liweze kutekeleza majukumuyake ya kila siku, kwani kwa kuchelewesha, tunarudishanyuma maendeleo ya Jeshi letu.

Page 237: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

237

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeshangaa kuonamaduka yenye gharama nafuu yaliyokuwa yanasaidia familiahizi yamefungwa. Naomba Serikali itoe majibu, ni kwa nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana wetu walioajiriwakwenye Shirika la SUMA JKT hasa kwenye ulinzi wa makampuni,wanalipwa kiasi kidogo cha mshahara kwani hii linawezakuleta ushawishi mbaya wa vijana wetu na kuweza kuletamadhara kwa makampuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiwanda cha Mzinga nimuhimu kwa Taifa na Jeshi lenyewe, ila hakipati fungu lakutosha kutekeleza majukumu yake na kwa kuwa Serikali hiiimetangaza mwaka wa viwanda, inabidi iwekeze sanakwenye kiwanda hiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kwamba Serikaliifuatil ie hati mil iki za makambi yote ya Jeshi i l ikuondoa sintofahamu na wananchi wanaovamia makambihayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka ya 2000 Jeshi lilianzishashule za sekondari nyingi na zilisaidia sana kutoa elimu borakwa vijana wengi na hata michezo ilifanyika na kutoawachezaji bora. Hivyo, Serikali iendeleze uwekezaji huu kwanini muhimu kwa Taifa hili.

MHE. VEDASTUS M. MANYINYI: MheshimiwaMwenyekiti, naipongeza Serikali yangu kwa kazi nzuri sanaya maendeleo ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lipo tatizo kubwa MusomaMjini kwani wananchi waliombwa kupisha eneo la Jeshikatika eneo la Makoko na wameendelea kupata ahadi yakulipwa fidia. Sasa ni zaidi ya miaka kumi hadi leo badohawajapata chochote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Wazirianakumbuka wale wananchi walituma mwakilishi wao. Namimi nilimleta kwake na tukakaa pamoja akaahidi kwamba

Page 238: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

238

katika bajeti hii hao wananchi wa Musoma watalipwa fidia.Naomba kauli yake hapa Bungeni, kwani wamehangaikakwa muda mrefu sana ili suala hilo tulimalize.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naunga mkonohoja ya bajeti ya Wizara hii.

MHE. CAPT. ABBAS ALI MWINYI: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kupata nafasi ya kuchangiakatika Wizara hii muhimu kwa Taifa letu ambayo imeendeleakudumisha amani na utulivu kwa Taifa letu pamoja na kulindaMuungano dhidi ya maadui wa ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na ufinyu wa bajetikumekuwa na upungufu mkubwa wa makazi ya wanajeshiwetu na wale waliobahatika kupata makazi, hayapo katikahali ya kuridhisha. Upungufu huo wa makazi unapelekeabaadhi ya wanajeshi kuishi nje ya Kambi za Jeshi, jamboambalo ni hatari kwa askari wetu. Suala la askarikuchanganyika na raia kunawashushia hadhi yao kwawananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na changamotokubwa ya ajira kwa vijana wanaomaliza JKT Bara na Visiwani.Nashauri Wizara ya Ulinzi zishirikiane na Wizara nyingine kutoavipaumbele vya ajira kwa vijana wanaomaliza JKT. Hiiitasaidia kwa kiwango kikubwa kurudisha nidhamu yautumishi wa umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri,atakapokuja kuhitimisha (kufanya majumuisho) ananiambienafasi za ajira zinazopelekwa kwa Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar ziko kwa uwiano gani ukilinganisha na TanzaniaBara?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na uwianomdogo kati ya wanawake na wanaume kwa maafisa wangazi za juu wa uongozi wa JWTZ. Naomba kujua kutokakwa Mheshimiwa Waziri, anapokuja kuhitimisha, ni kwa ninihali hii inajitokeza?

Page 239: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

239

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, hali ya ulinzi nausalama wa mipaka ya nchi yetu ni shwari kwa mujibu wahotuba ya Mheshimiwa Waziri. Napenda kujua mgogoro wampaka wa Malawi na Tanzania kupitia Ziwa Nyasa ambaoumechukua muda mrefu, ambao unaweza kuleta athari zauwekezaji katika nchi yetu, na hivyo kupelekea hasa Ukandawa Nyasa kudorora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.Naunga mkono hoja.

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia moja. NaipongezaWizara kupitia wanajeshi wetu kwa kazi nzuri wanayoifanyaya kuilinda nchi yetu na kubaki katika hali ya utulivu na amani.Hongereni sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vijana wanaojiungana JKT mara wamalizapo mafunzo ya kujitolea (kujitegemea),baadhi yao huajiriwa na vikosi vyetu vya ulinzi, lakini baadhihurudi katika maeneo yetu na kuzurura bila kazi maalum yakufanya. Je, Serikali haioni sasa wakati umefika kwa vijanahawa wanaopitia JKT kuwa na mfuko maalum wakuwasaidia vijana hawa mara tu wamalizapo mafunzo,kupewa na kuanzisha miradi na kujiajiri wenyewe?

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile wakati wakiwa JKTwapewe mafunzo ya ujasiriamali ili wakitoka wawe tayarikujiajiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii.

MHE. DESDRIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naanza kwa kuunga mkono hoja iliyoko mbele ya Bunge lakoTukufu. Nampongeza Mheshimiwa Waziri, mchapakazi,mtulivu na mwenye tabia ya pekee kimaadili. Hongerakiongozi, unakubalika ukiitwa mtoto wa Rais Mstaafu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni Serikali ilifutaShule ya Milundikwa Sekondari kupisha makazi ya Kambi ya

Page 240: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

240

Jeshi JKT. Pamoja na kukubaliana kwa shingo upande,uamuzi huo umetuathiri wananchi wa Kata ya Nkandasi naJimbo la Nkasi Kusini kutokana na miundombinu mbalimbaliya elimu kutwaliwa pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tuna sekondari changasana ile ilikuwa inajitosheleza kwa miundombinu mingi ikiwani pamoja na maabara, mabweni ya wasichana nawavulana, madarasa na nyumba za walimu pamoja nakisima cha maji.

Pamoja na msaada wa nguvu kazi kwa wanajeshi,tunaomba Wizara hii inisaidie kujenga mabweni na maabarakwa kadri wanavyoweza ili kutuwezesha kukamilishamiundombinu pungufu. Pia Serikali izingatie familia za askariwetu, nao pia watasoma katika shule hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi la pili ni kwamba Jeshilisitwae eneo lote, yale maeneo ambayo wananchi wanalimawasiwafukuze, wawaachie waendelee kulima kwa yaleambayo yako mbali na Kambi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi la tatu, naombaWizara isaidie kujenga mnara wa mawasiliano katika Katamoja ya mpakani mwa Congo DRC; Kata ya Kala ilikuimarisha ulinzi wa mpakani na vilevile kuboreshamawasiliano ya simu za mkononi. Hii ni Kata pekee iliyobakibila mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kazi nzuri sanaya wanajeshi, zipo dosari ndogo ndogo mfano, Wilayani Nkasiimewahi kutokea kama mara mbili wanajeshi kuwapigawananchi na mara nyingi ni ugomvi wa mapenzi na marazote raia huumizwa na wakati mwingine kuuawa. Siyo jambozuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hapa Dodomaimewahi kutokea mahali pengine nchini. Naomba wapewe

Page 241: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

241

somo la maadili, kwani siku zote raia akimwona mwanajeshihuona kama mkombozi wake, huu ndiyo utamaduni waKitanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza wanajeshiwote.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi naJeshi la Kujenga Taifa. Baada ya kuunga mkono hotuba hiyo,napenda kulipongeza Jeshi letu kwa kazi kubwa linazofanyakatika kulinda usalama wa mipaka yetu na kujishughulishana shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa letu na kushirikikatika kukabiliana na majanga mbalimbali yanayolikumbaTaifa letu kwa nyakati mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikalini kuwa Serikali iongeze bajeti kwa Wizara hii ili kuziwezeshataasisi ndani ya Wizara hii za Nyumbu na Mzinga ili zijikitekikamilifu katika shughuli za utafiti wa kisayansi na ugunduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, historia inaonesha dhahirikuwa taasisi za ulinzi na usalama hasa Majeshi ya Ulinzi katikanchi mbalimbali duniani zimeshiriki kikamifu katika kuletamapinduzi ya viwanda na zana za kivita. Mfano, mifumo yacomputer ilibuniwa na Jeshi la Marekani kabla ya kuingizwakatika shughuli za kiraia. Ugunduzi na ubunifu wa vifaa vyakivita kama vile vifaru, ndege za kivita, meli za kivita,makombora ya masafa mafupi, ya kati na marefu yote nimatokeo ya shughuli za kijeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine napenda kuishaurikulitumia vema Jeshi la Wananchi katika harakati za uvuviwa bahari kuu (deep sea fishing) ili meli za kivita ambazozinakaa muda mrefu bila kufanya kazi, zitumike katika kukuzauchumi wa Taifa letu wakati huu amani ikitamalaki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naishauri Serikalikulitumia vizuri Jeshi la Kujenga Taifa kwa kulipatia zana za

Page 242: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

242

kisasa za uzalishaji mali, yakiwemo matrekta ili kuzalishamazao ya chakula na biashara kama vile kahawa, mahindina mpunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri JKT iwezeshwekuwa chimbuko la ufugaji bora wa ng‘ombe wa nyama namaziwa. Ni imani yangu kuwa Serikali ikiliwezesha Jeshi letuwakati huu, upo uwezekano mkubwa wa kuwa mchangiajimkubwa katika shughuli za ukuzaji uchumi kama majeshi yanchi nyingine yanavyofanya, mfano, Ethiopia hapa BaraniAfrika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naiomba Serikali iwalipe maslahi wanajeshi yanayoendanana gharama za maisha, kwani gharama za maishazimepanda. Naiomba Serikali imalize migogoro ya ardhi katiya Kambi za Jeshi na wananchi ili wananchi waweze kuishikwa amani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali ishughulikiemafao ya wanajeshi waliostaafu. Mfano, kuna wanajeshikatika Mkoa wa Njombe ambao wamestaafu, lakinihawajalipwa mafao yao. Naomba kuwasilisha.

MHE. HALIMA ALI MOHAMMED: MheshimiwaMwenyekiti, katika ukurasa 33 aya 46 Mheshimiwa Waziriameelezea kuhusiana na SUMA JKT kupitia kampuni yake yaSUMA JKT Guard Ltd. kuendesha shughuli za ulinzi katika Ofisiza Serikali, Mashirika ya Umma na sekta binafsi zikiwemo Benkina Migodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, walinzi hawa maisha yao nimagumu, posho ni ndogo sana, mishahara hawana naSerikali iliwaahidi itawapatia mishahara kamili kama askariwengine. Nitoe mfano, walinzi wanaoimarisha ulinzi Ofisi yaTRA Bandarini, kazi wanayofanya ni nzuri tena katika ofisi nyeti,lakini Serikali haijali kitu.

Page 243: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

243

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Serikali iangalieupya maslahi ya walinzi hawa, iwaboreshee mishahara,iwapatie vitendea kazi pamoja na stahiki nyingine, kwanisehemu ya bandari ni muhimu katika kuingiza mapato yaSerikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu malipo yawastaafu wa JWTZ. Hawa ni watumishi ambao walifanya kazikubwa ya kulinda nchi yetu, kuweka heshima, lakini piakuimarisha ujirani mwema. Siyo vyema kuwa sasa hivi waoni ombaomba. Nashauri wapewe stahiki zao kwa kuzingatiathamani ya shilingi ya Kitanzania kwa sasa au mnawasubiriwafe wote? Hilo siyo jambo zuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wako wananchi eneo laKengeja, Jimbo la Mtambile, Wilaya ya Kusini Pemba ambaoardhi yao imechukuliwa na JWTZ. Hadi hii leo ni kimya, hakunahatua yoyote il iyochukuliwa na ni maeneo ambayowanayategemea kwa kilimo cha chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali uthaminiufanyike kwa haraka. Mheshimiwa Waziri atoe kauli ni liniwananchi hawa watapatiwa haki zao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya majeshi ya JWTZwakati wa uchaguzi kwa mfano, uchaguzi mdogo wa Jimbola Dimani - Zanzibar ni uthibitisho kuwa na matumizi mabayaya Jeshi letu, matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi,lakini siyo hivyo tu, ni uminyaji wa demokrasia, kwaniwalikuwa wakipita njiani na silaha. Hii inawatisha wananchina matokeo yake wapo wananchi wengi tu ambaowaliogopa na hawakujitokeza kutimiza haki yao ya kupigakura. Hii ni aibu kwa nchi inayojigamba kama inademokrasia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe ushauri,Serikali isitumie madaraka vibaya, badala yake wanajeshiwa JWTZ waachiwe wafanye majukumu yao kwa mujibu washeria za nchi yetu kwa manufaa ya ustawi wa nchi yetu nawanasiasa wafanye siasa. Kutumia fedha za walipakodi kwa

Page 244: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

244

jambo ambalo halina msingi, ni kuwanyima wananchikutumia haki yao ya maamuzi na kuwanyima nafasi yakupata maendeleo. Ahsante sana.

MHE. MARY D. MURO: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali kuimarishaJeshi la Kujenga Taifa ili liweze kuwa na tija kama miaka yazamani lilipojenga uchumi badala ya kuwa consumer waPato la Taifa. Miaka hiyo Mlale ilitoa mahindi mengi, Mafingapia, Ruvu ilikuwa wazalisha mpunga na ufugaji ambaoulileta faida kwa jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Serikali kuwekauwazi katika ajira zinazotolewa ili kuondoa minong’onoiliyopo ya kuwa rushwa inatolewa ili vijana wetu kupataajira bila usumbufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, nashauri Kiwandacha Nyumbu kifufuliwe ili watendaji walioajiriwa kwa ajili yakiwanda wasiligharimu Taifa bila kazi yoyote. Serikali iwezekuona kiwanda hiki kilikuwa na uwezo wa kuongeza ajirana Pato la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali kwambaVituo vya Jeshi viwekwe mbali na mazingira ya wananchi ilikutoleta migongano na mazoea yaliyopitiliza kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nashauri Serikaliiwapatie posho na vitendea kazi askari wetu ili kufanya kazizao kwa urahisi zaidi.

Vilevile naishauri Serikali kulipa madeni kwa Jeshilinayodaiwa kwa kuwapa fedha zile zilizopitishwa na Bungebadala ya kusitishwa huduma muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali itoeushawishi wa Watanzania kutumia bidhaa zao ili kuwezakuwaongezea pato.

Page 245: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

245

MHE. RASHID M. CHUACHUA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuhusu suala la Bima ya Afya kwa wanajeshi, kuna malalamikoya wanajeshi kuhusu kutibiwa kwenye hospitali zao pekeebila ya kuwa na Bima ya Afya, ni lini Serikali itawapatia bimaza afya wanajeshi na familia zao?

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Jeshi la Kujenga Taifa kazi yake kuu ni kulinda usalama waTaifa, wananchi na mipaka yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majukumumakubwa ya Wizara hii bajeti hii bado haitoshi ili tuendeleekuwa na amani na utulivu tulionao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu migogoro ya mipakana Jeshi, Jeshi likiwa imara na wananchi wanakuwa salamakatika Taifa. Ni lini Serikali kupitia Wizara hii itatatua mgogorouliopo katika Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda naJeshi kuchukua eneo ambalo wananchi wamejenga? Ni liniSerikali itatatua mgogoro huu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi liliwakuta wananchilikaazima eneo hili, leo hii linadai eneo ni la Jeshi na wananchiwamekatazwa kujenga na kulima katika eneo hili.

Je, Serikali haioni kwamba Jeshi linataka kuwaporawananchi maeneo yao na mashamba, nani atawalipa fidiawananchi hawa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, kiusalama kuweka vifaavya usalama vya kijeshi karibu na makazi ya watu yaliyopokatika Kata ya Mpanda Hoteli, Misunkumilo, Milala naMakanyagio; je, hamuoni huku ni kuhatarisha usalama kamaulivyotokea mlipuko wa mabomu Mbagala? Naombamajibu kuhusiana na suluhisho hili ili wananchi waondokanena unyanyasaji huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu wanajeshikuboreshewa maslahi yao kama mshahara, pensheni nanyumba zao; kuchelewesha maslahi yao haya kunapelekea

Page 246: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

246

baadhi yao kujihusisha na matukio ya ujambazi na uhalifukatika Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matukio ya uhalifu wa watukuuawa, mauaji ya Kibiti, nini tamko la Serikali ili kuondoana kumaliza uhalifu huu unaofanywa na baadhi ya wastaafuwanajeshi ambao siyo waaminifu. Ni aibu kuona nguo/vazila Jeshi kutumika katika matukio ya aibu, Watanzania wanaimani na Jeshi hili lakini kwa baadhi ya matukio ya kijingayanayofanywa na baadhi ya watu yanalichafua Jeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Paulo Makonda, alipoendakuvamia Clouds Radio alikuwa na watu au wanajeshi wawiliwaliovaa vazi la Jeshi kwa hili lililotokea hamuoni kwambaimelichafua Jeshi hili, nini tamko la Wizara na Serikali ilikumwajibisha huyu Bashite katika tukio hili, hamuoni kwaJeshi kukaa kimya linaonesha Jeshi linahusika kufanya hayamatukio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ulinzi wa mipaka nawananchi katika maeneo yanayopakana na nchi jirani je,mkakati gani unatumika pamoja na kuwashirikishawananchi elimu kwa raia namna ya kutoa taarifa kuhusuulinzi na usalama wa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Jeshi hili lijikitezaidi katika kulinda usalama wa Taifa na lisitumiwe na watuwenye nia mbaya kwa raia. Maonyesho ya makomandohadharani hamuoni kwamba inawapa mwanya watuwaovu kujua ubora na udhaifu wa Jeshi letu. Mazoezi ya Jeshihadharani yenye tija na sio ya kutisha wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho Jeshi laKujenga Taifa lisitumike vibaya na utawala wa CCM kwamaslahi ya Chama Tawala, bali Jeshi hili liangalie maslahimapana ya Taifa.

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kablaya yote ninaunga mkono hoja kwa asilimia zote. Napendakuwapongeza Waziri na Katibu Mkuu wake kwa kusimamia,

Page 247: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

247

kuiongoza na ufuatiliaji wao wa karibu zaidi wa majukumuya Wizara yao, pamoja na changamoto zote na ukosefu wakupatiwa bajeti katika ukamilifu wake kama ilivyopitishwana Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikizungumza kwa uchungukuhusu Mkoa wetu, hapo awali tulikuwa na makambi ya JKTMilundikwa na Luwa, Rukwa ambayo yalitusaidia kuwawekavijana wetu ndani ya maadili ya uzalendo na ulinzi uliotukukawa ushirikishwaji na wananchi wetu, sasa kama itakuwaSerikali (Hazina) haitoi fedha za kukidhi mahitaji kwa angalauasilimia 75 kwa umuhimu wa Wizara hii, kwani hawana masaamaalum ya utumishi wao, hivyo kuna umuhimu wa kupewafedha za maendeleo kwa asilimia hiyo ili makambi hayayakarabatiwe na kuanza kutumika mapema, kwani vijanawanaongezeka mitaani/Vijijini baada ya kumaliza masomoyao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2016/2017zimetolewa fedha za maendeleo shilingi 35,900,000,0000 ikiwani asilimia 14.5 ya bajeti iliyoidhinishwa mwaka 2017/2018.Bajeti imepungua kwa shilingi 29,000,000,000 kwa bajeti yamwaka 2016/2018 iliyokuwa shilingi 248,000,000,000 na sasakuwa 219,000,000,000 kwa mwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni kwambafedha za maendeleo ni vema zikatolewa kwa wakati nakatika ukamilifu wake, kutokana na umuhimu wa:-

(i) Kukamilisha ukarabati wa makambi ndani yamwaka 2017/2018, kuchelewa zaidi kutatuathiri.

(i i) Tuondokane na migogoro ya wananchiwaliochukuliwa maeneo yao kwa matumizi ya Jeshi, walipwefidia zao waweze kujiendeleza. Hizo bilioni 27 ni muhimu kwasasa kabla ya Juni, 2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, madhumuni ya kukamilishamakambi ni kuwajenga vijana wetu kiuzalendo, kiulinzi nanaishauri Serikali inapohitaji kuajiri Polisi, Wanajeshi, Maafisa

Page 248: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

248

Usalama wa Taifa, Uhamiaji, Jeshi la Zimamoto na Magerezausaili ufanyike kwa vijana waliopitia JKT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa vijanawanaopitia JKT baadhi wanabaki mitaani/vijijini ni boravijana hawa wakaunganishwa kwenye huduma za ulinzi zaSUMA Guard badala ya kurudi kujiunga na jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. LOLESIA J. M. BUKWIMBA: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza napenda kuchukua fursa hii kumshukuruna kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa kwa kuwasilisha hotuba vizuri juu ya maendeleona utekelezaji kwa ujumla wa Wizara. Vilevile niwapongezekwa dhati watumishi wote wa Wizara kwa kazi nzuri ya ulinziwa Taifa letu. Hii imewezesha kuwepo kwa hali ya utulivu naamani ya nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuishukuru Wizarakwa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa vijana wetu kwaniwanapata maarifa na ujuzi hasa katika stadi za kazizinazowawezesha kujiajiri na kujitegemea. Hivyo, ninaombana kuishauri Serikali kuongeza idadi ya vijana wa kujiungana JKT kutoka 20,000 hadi 25,000 kwa mwaka 2017/2018, hiiitasaidia vijana wengi zaidi kujishughulisha kutokana na ujuziwanaoupata kutokana na mafunzo ya JKT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo muhimu ninalopendakuwasilisha ni juu ya wapiganaji vita vya Kagera. Wapowanajeshi wengi nchini Tanzania wanadai mafao yao.Mwaka jana niliuliza juu ya suala hili na katika maelezo yawanajeshi hawa ni kwamba Serikali Awamu ya Nne yaMheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete waliahidiwa kulipwamafao yao, mpaka sasa hakuna chochote. Nimeangaliakwenye bajeti iliyowasilishwa ya mwaka 2017/2018 sijaonakabisa kuzungumziwa suala hili. Ninaomba MheshimiwaWaziri, nipate maelezo ya kina juu ya suala hili.

Page 249: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

249

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimelileta suala hili kutokanana wanajeshi walioko Jimboni kwangu Busanda wamekuwawakifuatilia sana juu ya suala hili, ninaomba nipate maelezoya kina na ufafanuzi juu ya suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo haya,naunga mkono hoja.

MHE. ESTER M. MMASI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwaheshima na unyenyekevu mkubwa naomba niunge mkonohoja ya wasilisho la bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi lakujenga Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kwa moja niendekwenye hoja ya msingi juu ya masuala ya ulinzi na usalamawa raia na mali zao. Ni ukweli usiopingika kuwa bado tunachangamoto kubwa juu ya kukabiliana na majanga yaujambazi kutokana na vifaa duni katika Jeshi la Kujenga Taifana hata kwa askari wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye bajeti ya mwaka2016/2017 hususani kwenye bajeti ya Jeshi la Askari tuliombaSerikali iidhinishe bajeti ya manunuzi ya magari mawili ya bulletproof ili kuweza kupambana na uhalifu nchini Tanzania, lakinicha kusikitisha hadi tunaelekea mwisho wa mwaka wa fedha30 Juni hakuna hata gari moja lililonunuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata ninapoandikamchango wangu huu ni kweli kuwa Taifa limepoteza nguvukazi ya Jeshi la Askari hadi sasa tuna jumla ya askari 13 -15waliopoteza maisha kwenye uharamia wa Rufiji, lakini piatuna takribani jumla ya wananchi 20 - 30 waliopoteza maishakwenye sakata la ujambazi Rufiji siyo hivyo tu uharamia waBenki Mbagala na Dar es Salaam City Centre, wapo wananchiwengi waliopoteza maisha pamoja na Jeshi la Wananchina hata askari kwa ajili ya kukosa magari ya bullet proof.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia kikosi cha Jeshila Wananchi nchini Kenya pamoja na Jeshi la Askari ni ukweli

Page 250: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

250

kwa nchi ya Kenya ina hazina ya magari ya bullet proof zaidiya mia mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mauaji yanayoendeleani dhahiri kwamba kama Wizara kupitia Jeshi la Wananchina JKT kama vile Ngome na JKT hatutajipanga vizuri ni ukweliusiopingika kwa changamoto hizi hazitafika kwenye ukomo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji Jeshi la Wananchilipewe fedha ya kutosha ili waweze kununua vifaa vya kisasakatika kukabiliana na uhalifu nchini kwetu. Wizara ya Jeshi laKujenga Taifa haijatengewa fedha katika kununua magariya bullet proof na silaha muhimu za kijeshi katika kukabilianana uhalifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika wasilisho la ripotiya Kamati pia tumesikia kuwa Wizara ya Jeshi la KujengaTaifa pia liko katika hatua za mwisho za ukamilishaji waNational Defense Policy. Pamoja na ukweli kuwa tumeonajuhudi nzuri na utendaji kazi mzuri wa Mheshimiwa Wazirikwenye Wizara yake, lakini kwa kutokuwepo kwa sera hiimuhimu ni ukweli usiopingika kuwa pengine kuna uzembemkubwa katika kitengo cha sheria katika Jeshi la KujengaTaifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni maombi yangu kuwaMheshimiwa Waziri atakapokuwa anahitimisha hoja yaWizara yake atuambie ni kwa nini hadi leo Sheria ya Ulinzi yamwaka 1966 imepitwa na wakati. Je, nini tamko la Wazirimhusika kwenye changamoto hii? Naomba kuwasilisha.

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujua kuna maeneo ya wananchi katikaWilaya ya Ilemela ambayo Jeshi liliyapima ili kuyachukua kwamiaka mingi bila kulipa fidia na kuwaondoa wananchi katikamaeneo hayo, Mheshimiwa Waziri naomba kufahamuuthamini uliofanyika maeneo ya Nyagunguku - Ilemela,Nyanguku, Lukobe kwa miaka miwili sasa umefutwa au badoupo valid?

Page 251: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

251

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama lengo la JWTZ lilikuwakufanya uthamini na baadaye kuwaacha wananchi katikamaeneo yao kwa muda mrefu bila kujua hatima yao,naomba kujua watalipwa lini au Jeshi limejiondoa kwenyenia ya kumiliki maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatana na timu za OrjoroJKT na Kanembwa JKT kushushwa daraja kwa tuhuma zarushwa ambazo zimeshindwa kuthibitishwa na chombo chakisheria cha uchunguzi wa makosa hayo (PCCB). Je, ni hatuagani Wizara yako imechukua kupigania haki ya vijana wakona heshima ya vyombo hivyo nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na kudorora sanakwa michezo ya aina mbalimbali, mfano, riadha, sarakasi,ngumi, mitupo, volleyball, nimetaja kwa uchache tu kwanini kuanzia sasa kipaumbele cha kijana kujiunga na JWTZna JKT au vyombo vingine isiwe ni kipaji kimojawapo chamichezo ili kuufanya umma wa Watanzania kupendamichezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, i l i vi jana hao wawecompetent ni vizuri Wizara yako ikatafuta wabia (marafiki)kutoka nje ya nchi kusaidia kuongeza taaluma, mfano, China,Cuba, Urusi na Korea, ambapo vijana wetu waweze kupataujuzi mpya au nyongeza ya ujuzi walionao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Wizara yako ina mpangomkakati upi wa kusaidia kuimarisha michezo nchini?

MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema kubwa ya uhaina uzima. Ninakushukuru wewe kwa kunipatia nafasi na miminichangie ingawa kwa muhtasari. Nianze kwa kupongezautamaduni mzuri wa vijana wetu wanaomaliza vyuo na walewengine kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, kwa mujibu washeria na wale wa kujitolea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili ni jema sanakwani vijana wetu hupata mafunzo mbalimbali yakiwemo

Page 252: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

252

ya ulinzi na usalama na yale ya ujasiriamali, vijanawanaopatiwa mafunzo ya ujasiriamali katika shughuli zakilimo, ufugaji, fundi uashi, fundi uchongaji, na menginemengi hufanikiwa vizuri wakiwa kambini, wakishaondokakambini elimu yote waliyopata hupotea kwa sababu vijanahawawezeshwi wanabakia vijiweni tu hawajui la kufanyana elimu waliyopata inapotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu vijana hawawakusanywe vikundi mbalimbali, wasajiliwe kisheria, Serikaliiwalee na kuwawezesha ili wajiajiri na kuendeleza elimuwaliyopata kambini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa vijana wanapatamafunzo ya kijeshi na wana uwezo wa kutumia silahambalimbali, Serikali haiwezi kuwaajiri vijana wote, wengi waohurudi nyumbani wakiwa hawajui la kufanya, vijanawanakuwa rahisi kujiunga na makundi ya uhalifu, hivyo nihatari kwa Taifa na usalama kwa ujumla wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu vijana hawawawekwe katika orodha maalum sekta za ulinzi zinapohitajikuajiri wafanyakazi, kwa mfano, Polisi, Magereza, Zimamoto,Usalama wa Taifa hata kampuni za ulinzi wa binafsi basiwapewe kipaumbele vijana wetu ambao wamepitia Jeshila Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile wabakie kama Jeshila Akiba hivyo wapangiwe utaratibu kila baada ya mudafulani wanakusanywa kwa kukumbushwa majukumu yao juuya wajibu wa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie muingiliano wakambi za Jeshi na makazi ya raia. Hili ni tatizo ambalo linahitajikuangaliwa kwa makini sana. Shughuli za kijeshi ni maalumkwa Jeshi mambo mengi ya hatari ambayo yanawahusuwenyewe, mfano maghala ya milipuko mbalimbali ambapoikitokea bahati ambayo inasababisha maafa makubwa kwa

Page 253: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

253

wote. Mfano, mkubwa na hai ni ule wa Gongo la Mboto naMbagala taharuki kubwa kwa nchi na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali ifanye juhudiza makusudi, kuepusha kambi zote za Jeshi zenye ghala zamilipuko zitengwe na makazi ya raia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie ajirakatika Jeshi na vyeti fake. Tatizo hili ni la Taifa zima na katikataasisi mbalimbali, lakini taasisi hii muhimu ina athari kubwana ni hatari kuwaajiri askari na ukawapa mafunzo yote nasiri zote za Jeshi wanazifahamu wamefanya kazi zaidi yamiaka 10 au 15 ndiyo unakuja kugundua vyeti vyao ni fakena kumfukuza kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii siyo vizuri kwa sababu hilini kundi kubwa sana tunalolikufukuza na tunalifukuza wakiwana taaluma. Naomba Serikali iangalie kwa umakini suala hilimwanzo wa kuajiri wabaini kasoro zote ambazo hazifaiikiwemo vyeti fake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho niombe usawa waajira kati ya pande mbili za Muungano kwa kuwa Muunganowetu ndiyo unaunda taasisi hii muhimu ya ulinzi naomba ajirazake zifanywe kwa uwazi mkubwa tena kwa uwiano mzuri.Hii itajenga heshima na uimara katika Jeshi letu na kupataushirikiano kwa pande zote na kwa watu wote.

MWENYEKITI: Waheshimiwa tunaanza sasa na majibuya Serikali, tunaanza na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleoya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto dakika tano, Naibu Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki dakikatano, AG dakika kumi.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsantekwa fursa hii. Naomba nichangie kidogo Hoja hii yaMheshimiwa Waziri wa Ulinzi kama ifuatavyo:-

Page 254: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

254

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitachangia kwenyemaeneo mawili, eneo la kwanza linahusu hoja ambayo ipokatika kitabu cha Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzanikwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, ambapokwenye ukurasa wa 17 na kuendelea anazungumzia kuhusuuteuzi wa wanajeshi, ama wanajeshi ambao bado niwanajeshi au wanajeshi waliostaafu kwenye nafasimbalimbali za kiuongozi kama wakuu wa mikoa na wakuuwa wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Msemaji huyu wa KambiRasmi ya Upinzani anazungumzia kwamba hii ni sawasawana dhana ya politicization of the Army. Napenda kupingananaye kwa sababu politicization of the Army haipo katikazama hizi kwenye nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema haipo kwa sababukinachofanyika kwa sasa kimsingi ni kwamba MheshimiwaRais anatumia mamlaka yake ambayo yamekuwa providedfor kwenye Katiba yetu kuteua watu ambao anaona watafaakwenye maeneo mbalimbali ya uongozi na kuwapamadaraka ya kumsaidia kazi ya kuongoza nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuna maeneoyamekaa kimkakati (strategic regions) kama Kigoma nimpakani, Kagera pamoja na maeneo ya Ruvuma. Maeneoambayo yamekaa kimkakati kwa maana ya kiulinzi zaidiMheshimiwa Rais anaona watu ambao wana inclination yakijeshi aidha ni wanajeshi au ni wanajeshi wastaafu wanafaakwenda kumsaidia kuongoza katika maeneo yale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa napenda kumpongezaMheshimiwa Rais… (Makofi)

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

Page 255: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

255

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: …kwa kazi nzuri anayofanya…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara, hebu kaa kwanza.Jamani tusipoteze muda, hii bajeti inatakiwa iishe leo.

T A A R I F A

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimpe taarifa ndugu yangu, shemeji yangu,Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla kwamba sisi hatupingiwanajeshi kuteuliwa katika nafasi mbalimbali, tunachotakani kwamba wakiteuliwa wafuate utaratibu wa kawaida.Kama ameshakuwa mwanajeshi amekuwa mtumishi waumma maadili wa kawaida yafuatwe, ndicho tunachosemasisi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla, endelea.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenyekitabu hakuna mahali ambapo wanaelezea mwanajeshihata mmoja ambaye ameteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwaMkuu wa Mkoa ambaye amekiuka taratibuanazozizungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi, tunachokiona nikwamba Mheshimiwa Rais amewateua watu ambaoanaona watafaa kumsaidia kutekeleza majukumu yake yakuongoza nchi yetu na kulinda mipaka yetu na kuleta amanindani ya nchi na kusaidia kuleta amani kwa watu ambaowanatuzunguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa msingi huo nashindwakuelewa wanatoa wapi dhana kwamba Jeshi letu linakuwapoliticized. Kwa sababu hawezi leo hii Mheshimiwa Waitarakuweka Mezani hapa hata photocopy tu ya kadi ya

Page 256: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

256

mwanajeshi hata mmoja ambaye amejiunga na CCM,hawezi kuweka Mezani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachoweza kuzungumzikani kwamba anahisi kwa sababu kwenye Katiba ya CCMukiwa Mkuu wa Mkoa ama Mkuu wa Wilaya unakuwaMjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi anahisina hao wanajeshi pengine baada ya kuteuliwa kushika hayamamlaka mbalimbali kama Mkuu wa Wilaya ama Mkuu waMkoa basi wanaingia kwenye vikao vya Kamati ya Siasa yaChama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna ushahidi wowote wahilo na naweza kusema kwamba kwa sababu Ilaniinayoongoza Taifa letu ya mtu ambaye amechaguliwa nawananchi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ni yaChama cha Mapinduzi na ili ilani hii isimamiwe na chamaambacho kinaongoza dola ni lazima wale ambaowamepewa nafasi ya kusimamia utekelezaji wa ilani hiyowaweze kutoa taarifa ndani ya chama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama italazimikaMkuu wa Mkoa kwenda kutoa taarifa ya utekelezaji wa Ilaniya Uchaguzi kwenye Kamati ya Siasa na yeye ni mwanajeshi,atakwenda kutoa taarifa hiyo. Kwa sababu huwezikutenganisha uongozi wa nchi hii ambao Chama chaMapinduzi kimepewa dhamana na wananchi kupitia kurakwa kumchagua Mheshimiwa Rais anayetokana na Chamacha Mapinduzi na utendaji wa kila siku wa chama,haiwezekani, ni dhana ambayo haipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na kwamba,Chama cha Mapinduzi kilimsimamisha Mheshimiwa Rais,Mheshimiwa Rais akachaguliwa na wananchi na baada yakuchaguliwa sasa anatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chamachake, watu aliowateua ni lazima waende wakakielezechama nini wanafanya kwenye nafasi mbalimbaliwalizopewa kwenye maeneo yao. (Makofi)

Page 257: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

257

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Dkt. Kolimba.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuunga mkono hoja.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANOWA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naombakuchangia Hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshila Kujenga Taifa, lakini nitakwenda kwenye hotubailiyotolewa na Kambi ya Upinzani katika ukurasa ule wa 14ambapo walikuwa wanazungumzia suala la usalama wamipaka ya nchi na hasa mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe taarifaifuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuanzia mwaka 2014 tarehe20 mpaka tarehe 21 Machi, mkutano wa kwanza ambaounasimamiwa na jopo la Marais wastaafu watatu ulifanyika.Nataka tu nitoe status kwa sababu swali lao linaulizia status,lakini sitaweza kuwaambia yale ambayo yanazungumzwandani ya jopo lile kwa sababu bado linaendelea na linatoataarifa kwenye ngazi maalum inayohusika lakini sio mahaliambapo ni pa wazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kulikumbushana kuliambia Bunge lako Tukufu kwamba mahusiano yaTanzania na Malawi yako vizuri, ninyi ni mashahidi na yakovizuri kwa ushahidi wa kwamba sisi kama Wizara ya Mamboya Nje na kwa niaba ya Serikali tumeweza kufanya mikutanona Malawi kwa pamoja na yapo vizuri katika mahusiano yakiuchumi na kijamii na ninyi ni mashahidi.

Page 258: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

258

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukienda katika suala lamgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa, niseme tu kwamba,mgogoro ule ulisitishwa mwaka 2014 na sababu ya kusitishwamgogoro ule ni kwamba Malawi ilikuwa unaingia kwenyeuchaguzi mwezi Julai na kwa hiyo, Mwenyekiti wa jopo lile lausuluhishi akaona kwamba ni hekima Malawi wangekuwahawana nafasi ya kuweza kuhudhuria vikao vile kwa hiyo,wakasitisha. Ilipofika mwaka 2015, Tanzania iliingia pia kwenyeuchaguzi Mkuu, kwa hiyo, Mwenyekiti wa jopo pia alisitishamazungmzo ya kujadili usuluhishi wa mgogoro huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hivi nchi zote hizihaziko kwenye uchaguzi na utaratibu sasa hivi unafanyika ilikuweza kuendelea na mazungumzo haya katika mwaka huu.Kwa sasa hivi Mwenyekiti wa jopo hili anajaribu ku-consultna wadau watakaohusika katika Mkutano huu ili kuwezakuendelea na mazungumzo ya usuluhishi. Hiyo ndiyo statusya mgogoro huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba,naomba sana kwa Waheshimiwa Wabunge pamoja naWatanzania kwa ujumla wake, diplomasia iachwe ifanye kaziyake. Tunapokuwa tunaiingilia kwa kuangalia labdamitandao au nani kasema nini, nasema kwa niaba ya Wizarayangu kwamba jambo hili linashughulikiwa na lipo katikamikono ya jopo na tuiache diplomasia ifanye kazi yake. Hii nikwa nia njema tu, kwa sababu tunapokuwa tunashabikiakuchukua maneno yanayosemwa huku, sisi tunasema kutokakwenye Ofisi husika kwamba usuluhishi wa jambo hiliunaendelea na hivi karibuni mtaambiwa lini watakapo-consult kwamba wadau watakuwa na nafasi kwa siku gani.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la mipaka;kuna Kamati ambayo inaendelea kufanya kazi yake, lakinikama mnavyojua kwamba mpaka wa Ziwa Nyasa badohaujaweza kupata usuluhishi wa kusema kwamba mpakaunapitia wapi mpaka hapo usuluhishi utakapokuwaumekwisha, jopo litakapomaliza kazi yake ndipo mpaka waZiwa Nyasa utakapokuwa umesemwa. Kwa hiyo, siwezi

Page 259: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

259

kuzungumzia suala la mpaka kama lilivyoandikwa kwenyehotuba ya Kambi ya Upinzani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kwenye hotuba ileile ya Kambi ya Upinzani, katika ule ukurasa wa 15, Kambi yaUpinzani inauliza ni nini hatima ya mgogoro huu? Hivi kwelitunaweza tukatoa jibu saa hizi, kama mgogoro huuunaendelea kujadiliwa na usuluhishi wake unaendelea!Wawe na subira, Kamati hiyo na jopo litakapomaliza kaziyake, ndipo tutakapojua kwamba lini tutapata jibu na mwishowa mgogoro.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya,naomba kuunga mkono hoja hii. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa AG.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa nami niwezekuchangia, lakini pia namshukuru Mwenyezi Mungu kwakunipa fursa hii. Yapo mambo kadhaa yamezungumzwahapa ya Kikatiba na Kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwanza niseme hivi;Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka1977 inatoa haki za msingi, lakini na wajibu. Hivi vituvinakwenda pamoja; haki na wajibu.

Katiba hiyo hiyo ndiyo inayoipa Bunge mamlaka yakusimamia na kuishauri Serikali. Ibara ya 100 ina vifungu viwili;cha kwanza na cha pili. Kimoja kinatoa uhuru wa majadiliano,lakini kifungu kidogo cha pili kinasema, bila kuathiri mashartiya Katiba hii na Sheria na huo ndiyo msingi wa kanuni ya 64.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naombakuwakumbusha Waheshimiwa Wabunge Ibara ya 29(5) yaKatiba ya Jamhuri ya Muungano inasema hivi;

“Il i watu wote waweze kufaidi haki na uhuruvilivyotajwa katika Katiba hii, kila mtu ana wajibu wa kutenda

Page 260: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

260

na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo hataingiliahaki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya Umma.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, yamezungumzwa mambohapa ambayo kimsingi yanawadhalilisha Wanajeshi na Jeshila Wananchi wa Tanzania. Bunge lisiruhusu hiki kitu. Bungelimetunga Sheria; tunayo Sheria ya Usalama wa Taifa (TheNational Security Act) na sheria hii, Kifungu cha (4) inataja“Public officer” ikiwajumuisha na Wabunge. Yako mamboambayo huwezi ukayasema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha (4) cha Sheriaya The National Security Act; na hata kama umeambiwa hizohabari, ndiyo maana tuna fursa hapa za kuchangia hata kwamaneno na kwa maandishi kwa sababu haya mambo yapoprotected. Someni Kifungu cha (4) cha Sheria ya Usalamawa Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais Kikweteenzi zake aliwahi kutuambia; “akili za kuambiwa, changanyana ya kwako.” Hamwezi mkazungumza mambo ambayohata yanadhalil isha wanawake wa Wanajeshi; HaoWanajeshi wenyewe wako humu halafu tunakaa kimya!

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi nilikuwanataka kusema hivi…

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa naomba…

MWENYEKITI: Mheshimiwa AG hebu subiri kidogo,Mheshimiwa Lissu.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,maneno anayosema Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu waSerikali ni makubwa sana na ni ya hatari sana. Kusemakwamba Bunge haliwezi likazungumzia masuala ya ndani yaUkumbi wa Bunge kwa sababu ni masuala ya usalama waTaifa, maana yake ni kusema kwamba Bunge halinamamlaka tena ya kuisimamia Serikali. Serikali ni pamoja naJeshi. Kwa hiyo, kauli inakwenda kinyume na msingi mkuu

Page 261: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

261

wa Katiba yetu kwamba Bunge ni chombo cha kuisimamiana kuishauri Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, Bunge hili siyo tu linamamlaka ya kuisimamia na kuishauri Serikali, lina mamlakavile vile ya kuiwajibisha Serikali pale inapokosa. Mamlakahayo ya kuiwajibisha Serikali ni pamoja na mamlaka yakupitisha azimio la kutokuwa na imani na Waziri Mkuu nakusababisha Baraza zima la Mawaziri kuvunjwa. (Makofi)

Mwisho, Bunge hili lina mamlaka ya kumwondoaMheshimiwa Rais madarakani kwa ku-move a motion ofimpeachment. Kwa hiyo, mamlaka ya Bunge ya kuisimamiaSerikali ni makubwa sana, ni mamlakaya Bunge… (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lissu, ahsante. MheshimiwaAG.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, hii taarifa naikataa. Yeye alikusudia kueleza tumamlaka. Nimesema hapa, Ibara ya 100(2) inasema:

“Bila kuathiri Katiba hii au masharti ya Sheria nyingineyoyote inayohusika.”

Nimesema hivi, Katiba yetu inatoa haki na wajibu.Kwa mfano, huwezi ukapiga mtu au ukatukana mtu,ukasema nina uhuru wa hapa. Haiwezekani! TunatambuaKatiba inatoa mamlaka hayo na tumetunga sheria hizi hapa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami ngoja niwashaurihapa. Najua hapa wakati fulani mnapotoshwa. Uhuru huomnaotafsiri Katiba vibaya, kuna siku nyingine mtajikutapabaya, that is it! Eeh! (Kicheko/Makofi)

Hamuwezi, kwa sababu Katiba iko wazi, nakupelekatu Mahakamani. (Kicheko)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

Page 262: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

262

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, maneno yakwenye Ibara ya 10 ya hotuba hii, yanasema “Vinanunuliwavifaa vibovu ambavyo havifai kutumika kwa ajili ya matumiziya Jeshi…

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kumwambia Mwanasheria Mkuu wa Serikalikwamba maneno anayozungumza kwanza Spika aliyaondoatukakubaliana hapa, lakini kwa upande wenu wa CCMmlitoa hoja tukaunga mkono. Sasa anarudia mamboambayo tulishafunga na wewe uliagiza yakaondolewakwenye Hansard. Kwa hiyo, anarudi tulikotoka. Nadhani kamaamemaliza kuchangia, ampe mtu mwingine tufunge mjadalahuu. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa AG. MheshimiwaAG maneno yaliyotolewa yote yasisemwe. (Makofi)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, aliyasema; lakini ninachotaka kusema ni hivi,Waheshimiwa Wabunge watumie uhuru wao kuishauri nakuisimamia Serikali kwa hekima. Eeh! Haya mambo yapohapa. Siku hizi wameanzisha utaratibu…

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, yale unayoyakataa, wanaweka kwenyemitandao. Wakiweka kwenye mitandao, nitawachukuliahatua za kisheria.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

Page 263: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

263

MWENYEKITI: Mheshimiwa Rhoda, kaa chini.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, hawawezi kuwa protected.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Rhoda, kaa chini.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Naitwa Sophia, siitwiRhoda.

MWENYEKITI: Kaa chini!

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, naitwa Sophia.

MWENYEKITI: Sophia kaa chini.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Taarifa!

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, kwa hiyo, nasimamia ununuzi hata Mikataba yoteinapita hapa, vifaa vya kisasa wananunua; unawekamaneno hayo, una-expose Taifa hili kwa watu wenginekwamba Jeshi la Tanzania lina vifaa duni, kwa hiyo tunawezatukaenda tukawavamia kule. Haiwezekani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, limezungumzwa hapa nakukubali kwamba Katiba Ibara 147 imepiga marufukuWanajeshi kujiunga na Vyama vya Siasa. Hiyo ni kweli kwasababu ni sharti kabisa la Kikatiba lakini, Ibara ya 45, Kifungucha 25 cha Sheria ya Ulinzi wa Taifa (The National DefenceAct)…

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa!

Page 264: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

264

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: …kimetoaMamlaka kwa Rais ku-second mtu yoyote.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Sophia nimesema kaa chini.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: …Wanajeshi nakipindi chote hicho amekuwa…

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: MheshimiwaMwenyekiti, taarifa!

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Wewe unatafuta matatizo.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: …kuwa niMwanajeshi. Kipindi chote hicho, huyo mtu anaendelea kuwaMwenyekiti. Sasa kwa mfano, kama ameteuliwa kuwa Mkuuwa Wilaya au Mkuu wa Mkoa, tunajua yuko Mwenyekiti waChama wa Mkoa; Mwenyekiti wa Chama wa Wilaya anamajukumu yake, hawezi kuchukuliwa na Mkuu wa Mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Katiba yenyewe yaChama cha Mapinduzi imesema kwenye Ibara ya 94 na Ibaraya 80; “Mkuu wa Mkoa atakuwa Mjumbe wa hizo Kamatikama anatokana na Chama cha Siasa.” Eeh, na wotetunafahamu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa sababu huyuanakwenda kufanya mambo ya Serikali kule siyo ya Chama.Katiba iko wazi. Huyu anatokana na Chama cha Siasa.(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa AG. MheshimiwaWaziri.

Page 265: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

265

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kukushukurukwa kunipa nafasi hii ya kusimama mbele ya Bunge lakoTukufu jioni ya leo ili niweze kuhitimisha hoja yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuwashukuruWaheshimiwa Wabunge wote waliochangia katika hoja hiina michango ilikuwa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, waliochangia kwamaandishi ni Waheshimiwa Wabunge 38 na waliochangiakwa kuzungumza ni Waheshimiwa Wabunge 21.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekeenaomba niishukuru kwa dhati Kamati ya Kudumu ya Bungeya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama chini ya uongozi thabitiwa Mheshimiwa Balozi Adadi Rajabu kwa ushirikiano waomkubwa katika kutekeleza mambo ya kikanuni kamailivyoainishwa katika kanuni za Bunge, Toleo la Januari, 2016kupitia masuala yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza walitembeleamiradi ya maendeleo chini ya Wizara yangu; pili, walifanyatathmini ya utekelezaji wa mipango ya bajeti ya mwaka wafedha 2016/2017, walifanya uchambuzi wa makadirio kwamwaka wa fedha 2016/2017; na mwisho, walitoa maoni naushauri wa Kamati ambayo yalitolewa kwa kuzingatiauchambuzi wa mambo yaliyozingatiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naungana na Kamati katikamaoni yake kuhusu miradi ya maendeleo kutopatiwa fedhakadri ya makadirio na hili limekuwa ni changamoto kubwakwetu. Tunaendelea kuwasiliana na Wizara ya Fedha naMipango ili kuona kwamba miradi hiyo inapatiwa kipaumbelekabla ya mwisho wa mwaka wa fedha 2016/2017. Tatizokubwa kwa muda mrefu limekuwa ni ufinyu wa makusanyo

Page 266: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

266

na kipaumbele kwa matumizi ya Serikali na vipaumbelembalimbali vinavyoikabili nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama ilivyo ada,naomba nianze kujibu baadhi ya hoja ambazo zimetolewana Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi naUsalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa kuna hoja yakwamba Serikali iyapatie mafungu ya Ngome JKT na Wizara,fedha zote za maendeleo kwa mwaka wa 2016/2017.Kulingana na upatikanaji wa fedha zinazotokana hasa namapato ya ndani, Serikali imekuwa ikitoa fedha zamaendeleo kwa Wizara ili kuweza kutekeleza shughuli zamaendeleo. Mfano, hadi kufikia mwezi Machi, 2017 Wizarailikuwa imepokea jumla ya shilingi 35.9 bilioni sawa na asilimia14.5 ya bajeti ya maendeleo. Kumekuwa na mawasiliano katiya Wizara yangu na Hazina kuhusu Wizara kupatiwa fedhaza maendeleo zilizobakia ili kukamilisha utekelezaji wamipango yake ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili ni Serikali itoeshilingi bilioni 27 zilizotengwa mwaka 2016/2017 kwa ajili yakulipia maeneo yaliyochukuliwa na Jeshi kabla ya terehe 30Juni, 2017. Katika mwaka wa fedha 2016/2017, Wizara ilitengashilingi bilioni 27.7 kwa ajili ya kupima na kuwalipa fidiawananchi ambao maeneo yao yalitwaliwa kwa matumizi yaJeshi. Hata hivyo, fedha hizi bado hazijatolewa hadi kufikiamwezi Machi, 2017. Wizara imekuwa ikiwasiliana na hazinakuhusu kupatiwa fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli zamaendeleo ikiwemo fedha kwa ajili ya fidia za ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadaye nitatolea maelezoyale maeneo yote ambayo Waheshimiwa Wabungewameyazungumza kwa uchungu kabisa kuhusu fidia kwamaeneo yaliyochukuliwa na Jeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ni kwambaSerikali ipime ardhi inayomilikiwa na Jeshi na kuimilikisha kwaJeshi Kisheria. Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka

Page 267: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

267

1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999, hakunakipengele cha utoaji wa hatimiliki kwa Taasisi za Serikalilikiwemo Jeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, mazungumzoyanaendelea kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifana Mamlaka husika ili hatimaye maeneo yote ya Jeshiyapewe hatimiliki bada ya kuzifanyia marekebisho Sheria hizo.Serikali kupitia Wizara husika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,inaendelea na taratibu za kuibadilisha Sheria ya Ardhi Na. 4na 5 ya mwaka 1999 ili kuziwezesha Taasisi za Umma likiwemoJeshi kumilikishwa maeneo kwa hatimiliki ili kuondokana nautaratibu wa sasa wa kusajiliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la Sera na Sheriaya Ulinzi; Kamati ilitaka Serikali ikamilishe mchakato wakufanya marekebisho katika Sheria ya Jeshi la kujenga Taifa,Sura ya 193 na Sheria ya Ulinzi wa Taifa, Sura ya192 ili iwezekuendana na wakati, mifumo ya utawala na mahitaji ya sasaya Kisheria katika Sekta ya Ulinzi.

Mheshimiwa mwenyekiti, kwa kuwa suala la Sera yaUlinzi wa Taifa ni la Muungano, kukamilika kwakekunategemea ridhaa ya pande zote mbili za Muungano.Hatua iliyofikiwa kwa sasa ni kupata maoni kutoka Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar, marekebisho ya Sheria ya Ulinzi waTaifa na Sheria ya JKT yatafanyika baada ya kukamilika kwaSera ya Ulinzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili, napenda nilielezeBunge lako Tukufu kwamba tumefikia sehemu nzuri sana,nimefanya mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisanayeshughulika na vikosi vya SMZ kule Zanzibar naameniahidi kwamba sera hii sasa inakaribia kupata maoniya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili tuweze kukamilisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni Serikali ionemuhimu wa suala la fidia kwa vijana wanaopata ulemavuwakiwa katika mafunzo ya JKT. Napenda kuliarifu Bunge lakokwamba malipo ya fidia hufanyika kwa mujibu wa Sheria ya

Page 268: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

268

Ulinzi wa Taifa ya mwaka 1966 ambapo mapendekezo yamarekebisho ya Sheria tajwa yatafanyika baada yakukamilika kwa Sera ya Ulinzi wa Taifa. Kwa sasa, kijanaanalipwa fidia kwa kutumia kiwango cha mshahara wa Askariwa cheo cha Private kwa mwaka wa kwanza. Maana yakeni kwamba vijana wanaokwenda JKT wakiumia, siyo kwambahawalipwi fidia, wanalipwa fidia kwa kutumia kigezo hiki chakwamba tunawalipa sawa na aliyeajiriwa katika ngazi yaPrivate anapokuwa ni mwaka wake wa kwanza Jeshini. Kwahiyo, fedha hizi huwa wanazipata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni Serikali itoekipaumbele kwa vijana waliopitia mafunzo ya JKT wakati wakuajiri vijana kwa ajili ya shughuli za ulinzi katika Shirika laSUMA JKT. Hivi ndivyo hasa ilivyo. Napenda kutoa taarifakwamba SUMA JKT Guard Limited linatoa kipaumbele kwavijana waliopitia mafunzo ya JKT wakati wa kufanya ajirazao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni Serikaliiboreshe miundombinu ya kambi za JKT ili vijana wengi kwamujibu wa Sheria waweze kufanya mafunzo hayo na kutengafedha kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa mafunzo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara inaendeleakuwasiliana na Mamlaka husika ili kuona uwezekano wakuongeza fedha kwa mafunzo hayo kadri hali ya kifedhaitakavyoruhusu. Sisi sote tunapenda kwamba vijana wotewanaokamilisha masomo yao ya kidato cha sita wawezekuingia Jeshini kwa mujibu wa sheria kabla hawajaendeleana elimu ya juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu eneo la madeni,Kamati imeitaka Serikali ilipe madeni ya Wazabuni na madeniya Kimkataba. Serikali ione umuhimu wa kuongeza kasi yakulipa madeni yote ya Wizara yaliyohakikiwa kiasi cha shilingibilioni 212.3. Maelezo ni kwamba kiini cha madeni ya Jeshi niufinyu wa bajeti katika maeneo mbalimbali ya utekelezajiwa majukumu ya kijeshi. Jumla ya madeni yaliyohakikiwa naambayo yanapaswa kulipwa ni shilingi bilioni 95.6. Mpaka

Page 269: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

269

sasa Serikali imechukua hatua ya kuanza kulipa madeni hayoambapo imetoa shilingi bilioni 5.16. Aidha, madeni ambayohayajalipwa ni shilingi bilioni 90.4.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara katika mwaka wafedha 2016/2017, imelipa shilingi milioni 61.2 kwa ajili ya malipoya Wazabuni wa ndani ambao wametoa hudumambalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwa upande waWazabuni wa nje Wizara imelipa shilingi bilioni 30. Aidha,Wizara inadaiwa deni la kimkataba, mikataba mbalimbalikiasi cha shilingi bilioni 785.2. Kwa hiyo, katika mwaka wafedha 2017/2018 Wizara imekasimia shilingi bilioni 120.7 kwaajili ya kulipa madeni ya kimkataba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu fungu 39 la JKT jumlaya madeni ya fungu hili hadi kufikia mwezi Aprili, 2017 ni shilingibilioni 101 na madeni yaliyohakikiwa ni shilingi bilioni 79.8.Serikali imeweza kulipa shilingi bilioni 4.2, hivyo kufanya denihilo lililohakikiwa kubaki shilingi bilioni 75.6.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni kuhusu SUMAGuard ilipwe madeni yake na wale ambao wamepewahuduma naye. Tumepokea ushauri wa Kamati kuhusiana naKampuni ya SUMA JKT Guard Limited, kampuni itaendeleakufuatilia madeni kwa washitiri wake kwa kutumia Wakalawa kukusanya madeni na kuimarisha kitengo chake chaukusanyaji madeni kwa ajili ya kufuatilia na kuwakumbushawateja wake kulipa madeni yao.

Mheshimiwa Mwenyeki, kuhusu Mashirika ya Jeshi;Kamati imetaka Shirika la Mzinga kumilikiwa kisheria nakuwajibika chini ya mamlaka moja. Shirika la Mzinga ni Taasisiiliyo chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, lakinikama taasisi nyingine za Serikali au za Umma, linawajibikakuwa kwa Msajili wa Hazina vile vile. Wizara itashughulikiaushauri uliotolewa ili Shirika hili liweze kuwajibika chini yamamlaka moja kwa kuanza utaratibu wa kubadilisha sheria.

Page 270: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

270

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Serikali itenge fedhaza kutosha kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinuili kuongeza ufanisi wa utendaji wa Mashirika ya Nyumbu naMzinga; Serikali katika mwaka wa fedha 2017/2018 imetengashilingi bil ioni 8.8 kwa ajil i ya kufanya ukarabati wamiundombinu ya teknolojia ya Shirika la Nyumbu na shilingibilioni 1.5 kwa ajili ya Shirika la Mzinga. Hata hivyo, mashirikahaya yataendeleza juhudi za mashirika yenyewe binafsi iliwaweze kuzalisha fedha zaidi ambazo zitawasaidia katikakuboresha hali ya miundombinu ya mashirika haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ilikuwa ni sehemu yakujibu hoja zilizotolewa na Kamati na sasa naomba niingiekatika hoja zilizotolewa na Kambi ya Upinzani. Kabla sijaingiakwenye hoja zenyewe naomba niseme maneno machacheya utangulizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi ni Taasisi ambayo nitofauti sana na taasisi nyingine za kiraia hasa kutokana namajukumu yake. Kila Mwanajeshi anapoingia Jeshinianafunzwa miiko na taratibu zake ambapo kwa sehemukubwa ni kumwezesha Mwanajeshi kutumika vyema wakatianapohitajika kutekeleza majukumu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasikitika kwamba sehemukubwa ya hotuba ya Kiongozi wa Upinzani au Msemaji waUpinzani, imetokana na hisia na baadhi ya matamshi ambayohayana ukweli wowote au hayajafanyiwa utafiti na matokeoyake yanaweza kuzua majungu au utovu wa nidhamu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikumbukwe kwamba Jeshihuendeshwa kwa kuzingatia mambo yafuatayo:-

(1) Katiba ya Nchi;

(2) Sheria ya Ulinzi wa Taifa;

(3) Kanuni ya Majeshi ya Ulinzi; na

Page 271: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

271

(iv) ni Forces Routine Orders zinazotolewa na Mkuuwa Majeshi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, rejea zote zilizotajwa hapojuu, zinatoa utaratibu kamili wa namna ya kuendesha Jeshikama Taasisi ya Nidhamu na Utii chini ya uongozi wa AmiriJeshi Mkuu na pia uongozi wa Kisiasa wa Waziri wa Ulinzi naJeshi la Kujenga Taifa katika uhalisia wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Ulinzi wa Taifa naKanuni za Majeshi ya Ulinzi, volume ya kwanza, ya pili na yatatu, zinatoa maelekezo ya namna Wanajeshiwatakavyotenda kazi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba ya Kiongozi waKambi ya Upinzani inaingilia mno shughuli za uendeshaji wajeshi. Hatari iliyopo ni kwamba Kiongozi wa Upinzaniamechukua maneno kutoka kwa Askari wasiozingatianidhamu na bila ya kufanya utafiti wa kutosha, amegeuzakuwa ndiyo taarifa yake. Ni vyema tutambue kwamba kaulikama hizi zinaweza kupelekea kuligawa jeshi bila sababuyoyote au kupandikiza mbegu za utovu wa nidhamu jeshini.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanajeshi wamejiunga najeshi kwa masharti yaliyopo na wanapaswa kuyazingatiawakati wote wa utumishi wao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia kusema,nimesikitishwa sana na maneno yenye lengo lakuwagombanisha wanajeshi na Serikali yao pamoja naWanajeshi na Uongozi wao wa juu. Hili halipaswi kuvumiliwana ni vyema Bunge lako liangalie utaratibu wa kikanuni zakumtaka Msemaji athibitishe maelezo aliyoyatoa katikawakati muafaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo yautangulizi, sasa naomba nizijibu hoja zilizotolewa na Msemajiwa Kambi ya Upinzani kama ifuatavyo:-

Page 272: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

272

Kwanza, kuongeza muda wa kufanya kazi Jeshinibaada ya muda wa kawaida kwisha. Siyo sahihi kuwaWanajeshi hawakupewa au hawakuelezwa sababu zakuendelea kufanya kazi baada ya muda wa kazi za kawaida.Wanajeshi wote walipewa taarifa na hakuna taharuki yoyote.Muda wa kazi uliongezwa kwa ajili ya michezo na mazoeziya viungo. Aidha, ikumbukwe kuwa wanajeshiwanaandikishwa kwa masharti ya kufanya kazi masaa 24.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la usalamawao; wanajeshi wanasafirishwa kwenda na kurudi kazini kwakutumia mabasi maalum ya usafiri. Hapa nataka kusemakwamba, baada ya saa za kazi, ili Wanajeshi hawa wawena utimamu wa kimwili na kiafya, wanatakiwa wafanyemazoezi ya viungo na hasa wajihusishe na michezo. Ndiyosababu ya kuongeza muda wa kutoka kazini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zamani, ama kuna wakatipengine ilizoeleka kwamba watu wanamaliza baada yamuda wa saa za kazi wanakwenda bar wanakunywa pombena kadhalika. Hii haina afya kwa jeshi letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, viongozi wanapokujakurudisha taratibu stahili hatupaswi sisi kama viongozikuwaona wanafanya makosa, badala yake tuwapongezekwa hatua hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ilikuwa nikusitisha utoaji wa fedha za likizo kwa wanajeshi. Malipo yafedha za likizo kwa wanajeshi hayajasitishwa na ni haki kwawanajeshi wote. Aidha, siyo kweli kwamba Mnadhimu Mkuuwa Majeshi ya Ulinzi, yaani Chief of Staff amezuia madai yawanajeshi ya kulipwa malipo ya likizo. Mnadhimu Mkuu waJeshi amekuwa mstari wa mbele katika kufuatilia stahiki hizo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi kila mwaka wa fedha,fedha za likizo zinatengwa kutoka bajeti ya Jeshi kila mwakawa fedha. Changamoto kubwa imekuwa ni ukomo wa

Page 273: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

273

bajeti, hali inayosababisha kutokidhi kuwalipa wanajeshiwote wanaostahili kwenda likizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara itaendeleakuwasiliana na Hazina iweze kusaidia kuongeza bajeti katikaeneo hili ili wanajeshi wote waweze kwenda likizo. Aidha,Wizara inajaribu kubuni njia nyingine kwa kushirikiana naHazina ili kuhakikisha kuwa wanajeshi wote wanalipwa fedhaza likizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuongezea katikaeneo hili; mimi binafsi wakati nikifanya ziara zangu katikaKambi za Jeshi, napata nafasi ya kuzungumza na Wanajeshi;katika kero kubwa ambayo imekuwa ikizungumzwa naWanajeshi, ni kero ya fedha za likizo. Nimekuwa nikiwaambiakwamba hakuna mtu, siyo Wizarani wala Jeshini ambayeangependa wasipate. Sote tunapenda wapate,tunawapigania sana na tukifanikiwa katika kupata fedha hizitutawalipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wale wote ambaohawajalipwa kwa kipindi ambacho walistahili, zinahesabiwakama ni madeni. Fedha za madeni zikilipwa, watapewafedha zao. Kwa hiyo, hatuoni sababu kwa nini kuja na dhanakwamba Chief of Staff anataka watu wasilipwe? Hili litahitajikuthibitishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hoja nyingineiliyotolewa kwamba Wajumbe wa Bodi ya Manunuziwanajipa safari za ununuzi wa zana nje ya nchi. Bodi yaWazabuni ya JWTZ imeundwa kisheria kwa kuzingatia Sheriaya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na Kanuni zake. Bodihiyo ina wajibu wa kutoa idhini ya manunuzi ya vifaambalimbali kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wajumbe wa Bodi hiyohawana wajibu wa kununua vifaa na hakuna Mjumbe waBodi ya Manunuzi ambaye amesafiri kwenda nje ya nchi kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya JWTZ. Utaona kwamba hoja hiinayo inataka ithibitishwe. (Makofi)

Page 274: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

274

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani mtu mmojabarabarani akasema maneno ambayo kwa kweli yanahaributaswira ya Jeshi zima, halafu tukayachukua tukayawekakwenye hotuba halafu wengine tukanyamaza kimya. Kwakweli hili litakuwa siyo jambo la busara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ilikuwa nikuondolewa kwa maduka ya bei nafuu Jeshini, yaani MilitaryDuty Free Shops. Maduka hayo yaliondolewa rasmi na Serikalitarehe 1 Julai, 2016 baada ya kuonekana kutowanufaishaWanajeshi na pia baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu kutumia mwanya wa maduka hayo kukwepa kodi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuondoa madukahayo, Serikali imekuwa ikiwalipa Wanajeshi fedha za ruzukukama sehemu ya kupunguza makali ya misamaha ya kodiiliyoondolewa. Siyo kweli kwamba fedha hizo zimetolewamara moja tu, fedha hizo bado zimeendelea kutolewa kilabaada ya miezi mitatu kama Serikali ilivyoahidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli usiopingika, katikaziara zangu katika makambi ya Jeshi, ukiuliza matatizo yaWanajeshi, wao wenyewe watakiri kwamba maduka hayayalikuwa yanawanufaisha wafanyabiashara siyo wao.Maduka mengi ya Jeshi, ilikuwa gharama wanazolipa waoni sawa na kununua mtaani, wakati wao wametolewaushuru. Kwa hiyo, aliyekuwa anafaidika ni walewafanyabiashara. Serikali imegundua hil i, sasa hiviwanatakiwa kulipwa; wameanza fitina na hili linaonekanakama vile Wanajeshi wanaonewa. Siyo kweli, waliokuwawananufaika siyo Wanajeshi na tutaendelea kuwapa hiyoruzuku ili kuweza kuwapunguzia makali ya maisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la tano, kuhusuWanajeshi kutopandishwa vyeo. Suala la Wanajeshikupandishwa vyeo, linazingatia sheria, kanuni na taratibuzilizopo bila ubaguzi wowote. Maafisa na Askari ambaowanastahil i na wamekidhi vigezo, wamekuwawakipandishwa vyeo mara kwa mara kwa kufuata taratibu

Page 275: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

275

zilizopo. Mara ya mwisho Maafisa na Askari wamepandishwavyeo katika ngazi mbalimbali mwezi Aprili, 2017. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii maana yake nini? Maanayake, katika Hotuba ya Kambi ya Upinzani walitaka kuashiriakwamba, kuna Mkuu wa Majeshi mpya ameacha kupandishawatu vyeo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepandisha watu vyeo.Kwanza kwa taarifa yenu, upandishwaji wa vyeo unafanywana Kamati ya Ulinzi ya Taifa, ambayo Mwenyekiti wake niWaziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Aprili mwezi uliopitatumekaa na tumepandisha vyeo Wanajeshi wotewanaostahili kupandishwa vyeo. Kwa hiyo, siyo kweli hatakidogo kwenda mitaani kuchukua maneno ambayo hayanachembe ya ukweli kuyaleta na kuyazungumza ndani yaBunge lako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, malipo ya fedha za chakulakwa Wanajeshi (Ration Allowance); fedha za chakula kwaWanajeshi hulipwa kwa kuzingatia Sheria ya Ulinzi ya Taifa yamwaka 1966; na Kanuni za Majeshi ya Ulinzi, Utawala ambapochakula hutolewa kwa Wanajeshi kwa kuzingatia majukumuanayopewa Mwanajeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwanajeshi anawajibikakula chakula stahiki na mahali stahiki kwa mujibu wa kanunina taratibu zilizopo. JWTZ kwa kushirikiana na Serikali,litaendelea kuhakikisha kuwa Wanajeshi wanapewa chakulastahili kwa kuzingatia majukumu wanayopewa. Fedha zachakula anazolipwa Mwanajeshi, siyo kwa ajili ya familia yakebali ni kwa ajili yake mwenyewe ili awe na afya imara,isiyotetereka ili aweze kutekeleza majukumu ya ulinzi wa Taifakikamilifu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niongezee kusemakwamba, wale ambao wapo kazini, wale ambao wapokambini, wale ambao wana kazi maalum (operation), lazimawale ndiyo wakatekeleze operations. Wale ambao wapokatika maeneo mengine, wanapewa fedha zao kwenye

Page 276: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

276

mishahara yao. Hakuna tatizo hapa. Kwa hiyo, haya manenopia hayana ukweli Mheshimiwa. Naomba sana siku nyingineukipata maelezo kama haya, nione kwanza, nitakupa taarifakabla hujaweka kwenye hotuba yako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine inahusu ufinyuwa bajeti ya umeme. Suala la ufinyu wa bajeti ya umeme,linatokana na ukomo wa bajeti unayotolewa na Serikali.Tunapenda kuishukuru Serikali kwa hatua iliyochukua yakuweza kupunguza madeni ya umeme ili JWTZ liendeleekupata huduma ya umeme katika makambi. Wizaraitaendelea kuwasiliana na Hazina ili waweze kutoa fedha zakutosha, katika eneo la umeme na maeneo mengine muhimuambayo tunadaiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo kweli kwamba Jeshihalilipi kwa kutotaka, wala siyo kweli kwamba Amiri Jeshi Mkuuameamua hata Kambi za Jeshi zikatiwe umeme. Alichosemani kwamba watu lazima walipe na baada ya hapo Hazinawalitoa fedha na jeshi likalipa; na tutaendelea kufanya hivyo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee na eneolingine la utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/2017. Kambiya Upinzani wanasema fedha za maendeleo zimetolewapungufu, hili tunakiri. Fedha za Maendeleo hutolewa kilamwezi kutegemeana na mapato ya Serikali kila mwezi, Wizarainaendelea kuwasiliana na Wizara ya Fedha na Mipango ilifedha zote ambazo hazijatolewa, ziweze kutolewa katikakipindi kilichobaki ili tuweze kutimiza majukumu yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu makusanyo kidogoya maduhuli ya JKT; maduhuli ya JKT yaani Fungu 39yanatokana na matunzo ya mazao ya shamba darasa, uuzajiwa nyaraka za zabuni na siyo kutoka katika shughuli zauzalishaji mali za SUMA JKT. Yaani kwa maana nyinginetutofautishe kati ya SUMA JKT na Fungu 39, yaani MakaoMakuu ya JKT.

Page 277: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

277

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii taarifa ya asilimia 31.8 nimaduhuli ya JKT, yaani Fungu 39 hadi kufikia Machi 2017.Aidha, hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2017 fedha zilizokusanywakutokana na maduhuli zimefikia asilimia 67.5 ya lengo. Kwahiyo, tunakwenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika randama ya Fungu57 subvote 1005 na subvote 2004 hazikutengewa fedha zamishahara. Je, vitengo hivi havina watendaji? Lilikuwa ni swali,ambalo jibu lake ni kwamba vitengo hivi kwa sasa havinawatumishi wa umma ambao mishahara yao ingepaswakuonekana hapo, bali kwa sasa wapo Wanajeshi ambaomishahara yao inalipwa kutoka Fungu 38 la Ngome.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni Uteuzi waWanajeshi katika nafasi za Kisiasa. Ndugu yangu Naibu Waziriwa Afya amenisaidia kujibu hili eneo, lakini niseme tu hivikwamba, uteuzi wa viongozi unazingatia weledi na hitajio lauongozi katika eneo husika na kwa kuzingatia Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania. Majukumu ya Viongozihawa siyo ya kisiasa, bali ni kutekeleza kazi za Kiserikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, uteuzi unaofanywasiyo tafauti na majukumu ambayo Serikali imekuwa marakwa mara ikiliagiza Jeshi kusaidia mamlaka za kiraia. Kwamaana nyingine, mara kadhaa tumeshaombwa namamlaka za kiraia kutoa msaada hususan katika maeneoya mipakani. Kwa hiyo, inaleta mantiki unapomwekaMwanajeshi kusimamaia pale akiwa kiongozi kwa sababuatakuwa na uharaka wa kuchukua hatua kama hizitunazozizungumzia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wapo baadhi ya Wanajeshiambao wameteuliwa na Chama Tawala katika nafasimbalimbali za uongozi. Hata hivyo, uteuzi huo hufanyika kwamakubaliano ya Chama Tawala na Wanajeshi husika baadaya kustaafu utumishi Jeshini na siyo wanapokuwa katikautumishi wa Jeshi. Mfano, uteuzi wa Kanali Lubinga kuwaKatibu wa NEC ya Chama Tawala, ulifanyika baada ya AfisaMkuu huyo kustaafu rasmi utumishi Jeshini. (Makofi)

Page 278: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

278

Wanajeshi wanateuliwa kushika nafasi za Kiserikali nasiyo za kisiasa, hivyo wanaruhusiwa kuvaa sare za Kijeshikulingana na majukumu na matukio maalum. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ushiriki wa Jeshikatika operation za ulinzi wa amani; napenda nisemekwamba, ushiriki wa Jeshi katika operation za Umoja waMataifa umekuwa na faida kubwa hususan kwakuwawezesha Wanajeshi wetu kuongeza weledi, kuongezauzoefu na exposure, teknolojia na kuitangaza Tanzania katikatasnia ya ulinzi na usalama duniani. Tumekuwa tukipata sifanyingi na ni mategemeo yetu kwamba tutaendelea kutumavijana wetu wakalinde amani katika maeneo mbalimbaliduniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu eneo la JKT kwambaSUMA JKT limetoa mchango gani kwa Jeshi katika kukabilianana changamoto za bajeti? SUMA JKT linashiriki kupunguzachangamoto za kibajeti kwa Jeshi kwa kuchangia katikauendeshaji wa Kambi na pia kuchangia gharama za chakulakwa vijana JKT ambapo mpaka sasa asilimia 55 ya gharamainalipwa na itaongezeka kufikia asilimia 100 siku zijazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, SUMA JKT kupitiakampuni yake ya ujenzi imekuwa ikishiriki ukarabati na ujenziwa Kambi na miundombinu bila kutoza gharama ya kazihizo. Mchango wa SUMA kuipunguzia Serikali gharama zauendeshaji, ni kwamba jukumu la SUMA ni kuipunguzia Serikaligharama za kuendesha JKT. Jukumu hilo l imeanzakutekelezwa kwa kuchangia kulisha vijana na gharama zauendeshaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, idadi ya miradi ya uzalishajiwa mali wa SUMA JKT, iko mingi ikiwemo kilimo na mifugo,uhandisi wa ujenzi, kutoa huduma za ulinzi kwa jamii,uunganishaji na usambazaji wa matrekta na uzalishaji samani,kokoto na ushonaji wa nguo. Fedha zilizoingizwa kutokanana uzalishaji ni jumla ya Shilingi bilioni 7.8 na zinaonekanakatika audit report ya SUMA JKT .

Page 279: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

279

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie eneo hilila Kambi ya Upinzani kwa hoja hii ya Jeshi la Kujenga Taifa,kwamba Jeshi hili ni pamoja na kuwa na dhima ya kuwafunzavijana, kuzalisha mali ikiwemo kuzalisha chakula. Jeshi lipimwekwa uzalishaji mali na kupunguza njaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, JKT l ina program yakuongeza uzalishaji mali na mafunzo ya uzalishaji mali hasachakula kwa vijana wake kupitia mashamba darasayaliyopo. Aidha, vijana waliopo kwenye makambi ya JKTwameanza kujitegemea kwa awamu katika gharama zachakula kutokana na chakula wanachokizalisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ni nyingi, sitowezakuzimaliza zote, lakini nataka kuwahakikishia Waheshimiwakwamba tutazitoa kwa maandishi kabla ya mwisho wa Bungehili. Kuna eneo moja muhimu sana ambalo limechangiwana Wabunge wengi, nalo ni migogoro ya ardhi na fidia kwamaeneo ambayo Jeshi limeyatwaa. Eneo hili limechangiwana Waheshimiwa Wabunge wengi akiwemo MheshimiwaEster Matiko, Mheshimiwa Manyinyi, Mheshimiwa Mabula,Mheshimiwa Deo Sanga na wengi ambao orodha yao ninayohapa.

Waheshimiwa Wabunge, ninachoweza kusema nanaomba mnielewe vizuri kwamba nia ya kulipa ipo, tathminikatika baadhi ya maeneo imeshafanyika, upimajiumeshafanyika, kwa hiyo, kilichobaki ni kulipa tu hiyo fidiainayotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliweka katika bajeti yetukama nilivyosema shilingi bilioni 27.7, bahati mbaya badohatujapokea, lakini mazungumzo yanaendelea. Tunamategemeo kwamba kabla ya mwisho wa mwaka huu wabajeti, fedha zitakazopatikana tutaanza kulipa fidiazinazotakiwa katika maeneo ambayo nimeyazungumziahapa. Kwa hiyo, kuna maeneo mengi mno na nawezanikaitoa ile orodha, lakini kwa sababu ya muda, naombaniendelee na maeneo mengine.

Page 280: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

280

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa kuna hoja yapensheni ndogo kwa wastaafu waliostaafu zamani.Tunakubaliana kabisa na hoja hii na nataka niseme kwambaSerikali imeanza kulifanyia suala hili ili hatimaye tuwezekurekebisha penisheni hizo. Ila ni lazima tuelewe kwambawastaafu wako wengi sana na fedha zitakazohitajika ni nyingisana. Kwa hiyo, lazima zoezi hili liende awamu kwa awamu,ndiyo maana Serikali imeanza na ngazi za juu. Imeanzakutoka cheo cha Meja Jenerali hadi Jenerali kamili natutaendelea kwa awamu hadi hapo ambapo tutawezakutimiza jukumu hili la Serikali la kuweza kuwatazama waleambao wamestaafu muda mrefu uliopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hoja za MheshimiwaFakharia, kuhusu idadi ndogo ya wanaojiunga na JKT kutokaZanzibar. Mpaka sasa hivi wanaojiunga na JKT kwa mwakatunapeleka nafasi 300. Kila tukiongeza idadi ya wanaoingiaJKT, pia tutaongeza idadi ya wale wanaotoka Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawashauri tuWaheshimiwa Wabunge kwamba utaratibu ule wa ugawaji,siyo jukumu la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wala siyo laJeshi. Tunazikabidhi kwa Serikali ya Zanzibar na kuwataka waowazigawe kwa kadri watakavyoona inafaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa nilizokuwanazo,kwa sasa zinagawiwa katika Wilaya na Mikoa na kama kunamatatizo huko, likiwemo lile alilozungumzia Mheshimiwa Daukule Mafia kwamba Mshauri wa Mgambo ndio anachukuawatu kutoka nje, hapa naweza kusema kwamba zoezi hililinafanywa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.Halipaswi kufanywa na mtu mmoja. Kwa hiyo, namshauriMheshimiwa Dau kwamba kama ni kweli haya yanatokea,basi ahakikishe anakaa na DC kama Mwenyekiti ili wawezekudhibiti hii hali, kwa sababu suala hili ni jukumu la Kamatiya Ulinzi na Usalama, siyo suala la Mshauri wa Mgambo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Jasson Rweikizaalitaka kujua tuna-ratify lini ile Biological Weapon Treaty

Page 281: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

281

ambayo, tumeshaisaini? Naweza kumwambia MheshimiwaMbunge kwamba wakati tunaleta hoja hii kwa ajili yaratification tulipewa ushauri, kwamba kuna treaties nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Chemical WeaponsTreaty; kuna Biological Weapon Treaty kuna Nuclear WeaponTreaty; hizi zote ni weapon of mass destruction. Tukashauriwakwamba ziwekwe kwa pamoja ili ziwe zina sheria moja. Iliziweze kufanya hivyo, kwa hiyo, tumekubaliana kwambazoezi hilo sasa lianze kwa haraka ili hatimaye tuweze kui-ratifytreaty hii na tuweze kupitisha sheria ili tuweze ku- domesticatesheria zote hizi kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Masoudaliungana na Wabunge wengine kusema kwamba bajeti yaWizara hii ni ndogo na tunakubaliana na hilo, lakini hiyo ndiyohali ya uchumi wa nchi. Tuna uhakika kwamba kila uchumiukikua na Wizara hii itaongezewa fedha kwa umuhimu wake.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Ration Allowancekwamba isiondolewe; tunasema kwamba Ration Allowancehaijaondolewa; ipo na itaendelea kuwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la fidia ya maeneoyaliyochukuliwa na Jeshi, nimeshalitolea taarifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ujenzi wa maghalakwamba hayajakamilika na yatakwisha lini? Niseme hapakwamba maghala yako katika hatua nzuri sana, yaliyobakini mambo machache sana ya kuunganisha umeme hapana pale na kadhalika, isipokuwa lile ghala la Pemba, ambapokumetokea mgogoro na Mkandarasi. Sasa hivi utaratibuunafanywa wa kuuvunja mkataba ule ili apewe Mkandarasimwingine mwenye uwezo alikamilishe lile ghala na silahazetu ziweze kukaa sehemu salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya ulinzi wa Taifanimeshalitolea taarifa.

Page 282: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

282

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu eneo la Hospitali zaJeshi kuwa katika mazingira ambayo hayaridhishi nakadhalika. Waheshimiwa Wabunge wengi wamechangia hili.Naweza kusema hapa kwamba tuko katika mchakato wakuanzisha Bima ya Afya kwa Wanajeshi. Sisi tuna imani kubwakwamba huo ndiyo utakuwa mwarobaini wa matatizo yoteya kiafya Jeshini. Tutapata fedha za kutosha kuboresha vituovyetu, kuongeza dawa kuajiri Madaktari na kuwalipa hatawale Madaktari ambao wanakuja kufanya part time. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naona muda wangu umekwisha,bado nina hoja nyingi sana ambazo sijajibu; lakini kamanilivyoahidi, tutazitoa kwa maandishi ili WaheshimiwaWabunge wote wapate majibu ambayo tulikuwatumeyaandaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

MWENYEKITI: Hoja imeungwa mkono. Katibu.

NDG. ASIA P. MINJA – KATIBU MEZANI:

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 57 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Kif. 1001 – Admin. & HR Mgnt..................Sh. 16,314,720,125/=

Page 283: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

283

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nimepokeamajina ya Vyama vyote. Tunaanza na Martha Mlata.

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Naomba kwanza nimshukuru MheshimiwaWaziri, lakini nilitoa mchango wangu na kwa sababu yamuda, naamini alishindwa kujibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu MheshimiwaWaziri anipatie ufafanuzi, nawe unatambua kwamba vijanawetu wanaofanya mtihani wa kidato cha nne, wanafanyamtihani mwezi wa Kumi lakini wanakaa miezi nane wakisubiriwale waliofaulu kwenda form five mwezi wa Saba. Kwa hiyo,ni kipindi kirefu sana vijana hawa wanakaa nyumbani namatokeo yake tunaweza wengine tukawapoteza njiani.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa JKT wamefanyakazi kubwa sana, kwanza kwa wale wanaojitolea kwendaJKT target yao ilikuwa ni 10,000 lakini wamechukua 9,800.Wale wanaomaliza kidato cha sita, waliomaliza ni 65,000,lakini wakawachukua 14,000 na hawa ni sawa na waleambao wanatakiwa kwenda kidato cha tano; kwa hiyo,namwomba Mheshimiwa Waziri atusaidie kuweka ufafanuzikwa sababu Sheria ya Mwaka 1964 inatambua mtoto wamiaka 16 kujinga na Jeshi la Kujenga Taifa. Je, isingekuwa nisahihi, watoto hawa waweze kutumia muda huu kupatamafunzo ya Jeshi kwa maana ya JKT? Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Mheshimiwa Mlataalileta hoja hiyo, kwa bahati mbaya sana sikupata muda wakuifafanua, lakini ukweli ni kwamba Sheria ya Jeshi la KujengaTaifa inataka vijana waliomaliza form six na vile vile walewaliomaliza form four lakini wakapata elimu ya ziada, sioform four peke yake, hiyo ni kwa mujibu wa Sheria. Kwa hiyo,ninachoweza kusema hapa ni kwamba hoja ya MheshimiwaMartha ni nzuri kwa sababu ukiangalia sasa hivi

Page 284: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

284

wanaomaliza Form Six mpaka kuanza Vyuo Vikuu muda nimfupi mno, lakini wale wa form four wana muda mrefu zaidi.Kwa hiyo, tunachoweza kusema ni kwamba tutaliangaliakwa umakini kwa kushirikiana na wenzetu wa JKT lakini vilevilehata kama litaonekana linafaa litahitaji mabadiliko ya Sheria.Kwa hiyo,…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Matha.

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru na naunga mkono hoja kwa majibu yaMheshimiwa Waziri. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Richard Mbogo.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Langu ni fupi tu, nitahitaji kujua mkakati wa Serikaliau mipango. Wakati Mheshimiwa Waziri anajumuisha,ameelezea migogoro mbalimbali ya maeneo na watuwanaopewa fidia, lakini tunajua kwamba maeneo ya Majeshihasa maeneo ya Mijini yamezungukwa na raia kutokana nakuongezeka kwa idadi ya watu na kuwa karibu; nakumekuwa ni migogoro mpaka Majeshi yanakaa kwenyemaeneo ya Manispaa, yaani Mijini. Sasa je, Serikali haioni hajaya kupunguza haya maeneo na ikabaki na huduma za kijamiikama vile upande wa afya, elimu na hata kuweza kupewamaeneo mengine?

Kwa mfano, Manispaa ya Mpanda waliwezakupunguza toka ekari 3,000 na kitu mpaka 1,000 na kitu. 1,100zilienda Manispaa. Sasa je, Serikali haioni mpango wakuondoka Mijini na kwenda sehemu nyingine kuondoa hatarikwa wananchi?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri, majibu.

Page 285: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

285

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimjibu MheshimiwaMbogo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vema ikaelewekakwamba Kambi za Jeshi zina madhumuni tofauti tofauti, siyozote zenye kazi moja. Kuna kambi ambazo ni za kimapiganoambazo zinahitaji maeneo makubwa kwa sababu yausalama wa wananchi. Kuna kambi nyingine ambazo ni zakiutawala; na kuna kambi nyingine ambazo ni za logistics.Kwa hiyo, kusema kwamba kambi zote ziondoke mjini,tutakwama katika upande wa logistics na mambo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachowezakumwambia Mheshimiwa Mbogo ni kwamba tutaangaliacase by case, hatuwezi kutoa maamuzi ya jumla ili kuona niwapi ambapo hicho anachoshauri kinawezekana na wapiambapo hakiwezekani?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Masoud.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Nami naomba kupata maelezo yaziada na kama sikuridhika, natoa shilingi mapema jioni yaleo. Kuna malalamiko ya muda mrefu; pamoja na maelezoya Mheshimiwa Waziri kwamba wananchi wanachukuliwamaeneo yao, sasa ni karibu miaka 50; na maeneo haya Jeshila Wananchi wa Tanzania ambayo wameyachukua kwawananchi ni maeneo 262.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waliyoyafanyia tathiminiambayo mpaka sasa hakuna fidia iliyotolewa ni maeneo 17.Sasa ndani ya miaka 50 ambapo Jeshi la Wananchilimechukua maeneo ya wananchi na wananchi wenginewameshafariki, wanaendelea kudai haki zao, MheshimiwaWaziri anasema kwamba nia ya kulipa ipo; kama ingekuwani yeye binafsi Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi ningekubali,lakini siyo ni Serikali. (Kicheko)

Page 286: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

286

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu mambo hayani tangu mwaka 2006. Kuna kitabu kimeandikwa, “Taarifaya Ahadi za Serikali,” mimi nikiwa Waziri kivuli, tena kivuli chasaa 11.00 jioni, kitafika huko kivuli changu. Tangu mwaka2006, sasa ni miaka 11, mnasema mtayatekeleza; maeneommeyataja; Bulombola, Mlale JKT, Turuti, maeneo ya Jeshikibao, yote mmesema, lakini hamtoi fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara hii ya 2016/2017 shilingibilioni 27.7 ambazo zimetengwa, hakuna hata shilingi moja.Mheshimiwa Waziri, aniambie sasa; ana lipi kubwa ambaloatafanya juu ya kukamilisha shughuli hizi?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika maelezoyangu, kwa kweli sina maelezo ya ziada. Fedha tulizotenga,shilingi bilioni 27.7, hili tatizo linajulikana, tumezungumza nawenzetu wa Hazina, wametuahidi kututafutia kiwango fulanicha kuweza kulipa katika bajeti ya mwaka huu; na vilevilekatika bajeti ya mwakani, tumeweka fedha vilevile. Kwa hiyotunachosema Mheshimiwa, maelezo zaidi ya hapositakuwanayo isipokuwa naomba mtuamini kwamba fedhahizi zitapatikana kwa awamu ili tuweze kuondoa hilo tatizo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Masoud.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: MheshimiwaMwenyekiti, pamoja na maelezo ya Mheshimiwa Waziri naamesema kwamba tuwaamini, lakini hii ni robo ya tatu yamwaka tunamalizia; na kwa kuwa wananchi wenginewameshafariki na sisi ndio sauti zao, naomba WaheshimiwaWabunge mniunge mkono tujadili kwa kina namna bora yakuwapatia wananchi fedha hizi ambao wamelalamika mudamrefu, maeneo yao yamechukuliwa na mpaka sasa hakunafidia iliyotolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba naomba kutoahoja.

Page 287: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

287

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwigulu, MheshimiwaChegeni, Mheshimiwa Ashatu, Chief Whip utakuwa wamwisho, Mheshimiwa Waitara, Mheshimiwa Matiko,Mheshimiwa Riziki, Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Halima.

MWENYEKITI: Waheshimiwa hamwezi kupata wote.Naandika tu, halafu nitakuwa nachagua hapa.

Haya, tunaanza na Mheshimiwa Matiko.

MHE. ESTER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nimesimama kuunga hoja ya MheshimiwaMasoud kuhusiana na maeneo ambayo Wanajeshiwameyachukua. Ni dhahiri kuwa ni takriban miaka yotetunaweka bajeti hapa, Serikali inashindwa kutoa hela. Kwahiyo, kusema tumwamini Mheshimiwa Waziri inakuwa ningumu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba haya maeneo yawananchi ambayo Wanajeshi wamechukua, kwa sababummeshindwa kuyalipa kwa sababu hamna hela,muwarudishie wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri leo nimekutana na wananchi waTarime; na kuna mmoja ni babu kabisa ana miaka karibia 80;huwezi ukajua wako pale juu. Wamemweleza na amesikiakilio chao. Kwa hiyo, naunga mkono hoja, maeneo yarudikwa wananchi. Serikali haiwezi kulipa fidia kwa hawawananchi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Dkt. Kigwangala.

Page 288: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

288

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Napenda kumsihi Mheshimiwa Masoud asiichukueshilingi ya Mheshimiwa Waziri kwa hoja kwamba yeye kamaMbunge senior humu ndani atakuwa anafahamuchangamoto ambazo Taifa letu linapitia katika kutekelezabajeti yetu katika nyakati nyingi mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto hizi haziwezikuwa mahsusi tu kwa Wizara hii ya Ulinzi, mambo mengitunayapanga kama aspiration za nchi yetu sisi hapa Bungeni,tukiamini kwamba tutafanikiwa kukusanya pesa za kutoshakutatua changamoto zote ambazo zinatukabili; lakinihutokea mara chache, tukashindwa kufikia malengo na hiihaiwezi kuwa ni sababu ya makusudi, ni sababu za kiuchumina ziko nje ya uwezo wa binadamu.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Riziki.

MHE. RIZIKI S. MNGWALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nami nisimame kuunga mkono hoja yaMheshimiwa Masoud. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nia lazima ifuatiwe navitendo. Nia tu, nia, hii nia mpaka lini? Miaka 50, mnasemawenyewe tunatenga shilingi bilioni 27, hata senti mbilihaijapangwa; sasa nia hii itafika mwisho kweli! Hebu tufikemahali hii Serikali ione aibu kwa wananchi wake. Wananchiwanyonge walipwe pesa hizi, wanashikilia maeneo menginewala hawana kazi nayo; Buza, sijui wapi, mengine yapo mjinikabisa, wanachukua tu maeneo ya watu, fidia hawalipi. Kwakuwa wananchi ni wanyonge!

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa leo shilingi itaondoka.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waitara.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Naunga mkono hoja ya Mheshimiwa

Page 289: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

289

Masoud. Mheshimiwa Waziri anasema tangu mwanzo wamaelezo mpaka mwisho kwamba Serikali kwa sasahaitakuwa na uwezo wa kulipa watu hawa; na hawa niWatanzania wenzetu ambao wanapata shida. Nadhaniingekuwa ni busara tu kuwaachia maeneo waendeleekujiendeleza kiuchumi; siku watakapopata fedha, wakatihuo watazungumza kwa bei ya wakati huo ya soko la ardhi.Ni hivyo tu. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mwigulu.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza niwakumbushe tu WaheshimiwaWabunge kwamba Wizara tunayoongelea ni ya Jeshi laWananchi. Mnaposema maeneo hayo yachukuliwe nawananchi; hili ni Jeshi la Wananchi na wananchi wanatakiwamara zote watambue kwamba Jeshi la Wananchi liko kwaajili ya wananchi. Kiusalama tu, hata wanapopata eneo, sisikiraia mnaweza mkadhani halina kazi, lakini kiusalama nausalama wa wananchi wenyewe, ni vyema shughuli za kijeshizinapoendelea zisiwe karibu sana na uraia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo, Serikaliinasema itayalipia yale maeneo. Kwa hiyo, linalotakiwakufuatana na vipaumbele; na kwenye eneo hili nawaombaWaheshimiwa Wabunge, wala hatuna hata haja ya kuvutanakwa sababu ya uzito wa jambo tunaloliongelea. Hatuna hajahata ya kuvutana, tukubaliane tumpe fursa MheshimiwaWaziri huku tukiwa tumeshaona concerns zenu kamaWabunge kwa sababu mnatimiza wajibu wenu wa kuielekezaSerikali.

Mheshimiwa Waziri ameshapokea, Serikali imepokea,atakwenda kulipa, lakini hatuna haja ya kuvutana kwa shilingikwa ajili ya umuhimu wa Wizara tunayoijadili.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Chegeni.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: MheshimiwaMwenyekiti, Mheshimiwa Masoud alikuwa Mjumbe

Page 290: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

290

mwenzangu wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.Tumezunguka naye katika baadhi ya maeneo nayaliyozungumzwa na Mheshimiwa Waziri nadhani ameonani hoja ya msingi kabisa, kwa sababu Mheshimiwa Waziriameonesha nia kama Waziri na Serikali iko tayari kujaribukufanya fidia ya haya maeneo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri Mheshimiwa Masoudhoja yake, tulizunguka kwenye Kamati wakati ule, kwa niniasimwachie Mheshimiwa Waziri akafanye kazi na kauliameshasema hapa sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ashatu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na napendanimwombe tu Mheshimiwa Masoud kama alivyosemaMheshimiwa Waziri wa Wizara husika, kwamba nia ya Serikalini njema, nasi tumejipanga kulipa fedha hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo naomba muichukuehivyo; na tulisema tangu mwanzo, tangu tumeanza kipindihiki kwamba tulikumbana na changamoto ya kupanda kwariba katika Soko la Dunia, lakini sasa imeshuka na sasa tukosehemu nzuri, hizi ni pesa za maendeleo, zimepatikana nazitalipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namwombaMheshimiwa Masoud, nia ya Serikali yetu ni njema, nawananchi wote watalipwa, siyo ndani ya Wizara hii tu, Wizarazote ambazo tunatakiwa kulipa compensation, Serikali inatoacommitment, tutafanya malipo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba MheshimiwaMasoud amwachie Mheshimiwa Waziri shilingi yake ili tuwezekutekeleza bajeti hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)

Page 291: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

291

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri majibuyako ndiyo yale yale, huna tena la kuongezea. Au una laziada ambalo umelipata sasa hivi?

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba nashukurucommitment ya Serikali imepatikana na mimi mwenyewenimewaahidi Waheshimiwa Wabunge wengi kwambanitafika katika maeneo yao binafsi kuzungumza na wananchiwao ili nami kuweza kufikisha commitment hizi za Serikali kwawananchi ili wanisikie moja kwa moja. Kwa hiyo, nitafanyahivyo baada ya kikao hiki cha Bunge. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Masoud, baadaya commitment ya Serikali, nafikiri ni ubinadamu tu ukubalituwape muda na sasa hivi mambo yanakuwa mazuri na niaya Serikali ni kulipa hizi pesa sababu ni wajibu wananchi hawasiku nyingi hawajalipwa. Kwa hiyo, commitment ya Waziri waFedha na Waziri mwenyewe…

Chief Whip nilikuwa sijakupa nafasi! Umeridhika!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (SERA,BUNGE, AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU): Ndiyo.

MWENYEKITI: Kwa hiyo, nakusihi tu umrudishie pesayake, tutashirikiana kuitafuta hiyo pesa pamoja ili wananchiwalipwe hela zao.

Mheshimiwa Masoud.

MHE. MASOUD A. SALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, sinapingamizi na maelezo yako, lakini mara nyingi Mawaziriwanapojibu, wanasema Serikali ya Awamu ya Tano haisemiuongo. Mimi nataka tu kusikia ni lini? Wanasema kwambafedha inatafutwa na sasa tupo katika robo ya tatu ya mwaka;nataka mniambie tu, ni lini wananchi hawa; mniambie tu timeframe, muda gani? Ni hiyo tu siyo kingine. Shilingi nitarudishajioni hii sina pingamizi, sema ni lini? basi ni hilo tu.

Page 292: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

292

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Masoud,commitment imeishawekwa. Serikali ikitoa commitmentndiyo kauli ya Serikali. Nashukuru shilingi imerudi. (Makofi)

Tunaendelea. Mheshimiwa Lolesia Bukwimba (Makofi)

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi ili nami niweze kutoa hoja.Sina nia ya kutoa shilingi kwa Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango wangu wamaandishi, nimeulizia kwa habari ya wapiganaji wa Vita vyaKagera vya mwaka 1978/1979, ni kipindi kirefu sasawapiganaji hawa wa vita wamekuwa wakifuatilia haki zao,mafao yao na wanahitaji kulipwa pension.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipindi chote hichoSerikali imekuwa ikiwaahidi tu mara kwa mara lakini hakunakinachoendelea. Vile vile katika Serikali ya Awamu ya Nneya Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Serikali ilioneshamatumaini kutaka kuwalipa mafao hawa wapiganaji wa Vitavya Kagera, lakini mpaka sasa utekelezaji badohaujaonekana.

Sasa ningependa kujua kwamba Serikali inasemajekuhusu jambo hili? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimjibu MheshimiwaBukwimba kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha anazozungumziaMheshimiwa Mbunge ni vizuri awe amewaelewa wahusikawanazungumzia fedha gani? Kuna fedha ambazo zililipwakama ahsante baada ya watu kurudi kutoka vitani na zililipwakwa wote, hakuna anayedai fedha hizo.

Page 293: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

293

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye suala la pension;pension wanapata wale ambao walikuwa ni waajiriwa waJeshi. Mtakumbuka wakati wa vita vile, kuna wenginewalikuwa sio waajiriwa wa Jeshi. Kwa hiyo, hawahawastahili pension. Sasa kama kuna ambao ni waajiriwawa Jeshi, ambao hawana pension, napenda kumwambiaMheshimiwa Mbunge atuone ili tuangalie taratibu zao lakiniwanastahili pension yao kama walikuwa ni waajiriwa waJeshi.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Lolesia, bado unahoja?

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa Mheshimiwa Waziri kuonesha nia ya dhatikuweza kuwaona wale wahitaji kuweza kuwasikiliza. Kwa hiyo,nashukuru sana, nami binafsi nitawaomba wale watu wajekumwona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mathayo.

MHE. DKT. VEDASTUS M. MANYINYI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Nami hoja yangukubwa ilikuwa inahusiana na fidia ya wale wananchi waliokokatika Kata ya Makoko ambapo Jeshi lilichukua nafasi yao.Sasa kama nilivyosema, bahati nzuri niliwaleta wakaonanana Mheshimiwa Waziri, naye akatoa commitment, lakinijambo moja kubwa ambalo limenipa faraja ni majibu yaMheshimiwa Waziri, lakini na Serikali kwa ujumla kwa maanaya Waziri wa Fedha alivyosema kwamba ataleta fedha. Kwahiyo, ni imani yangu kwamba hilo limeisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waziri.

NDG. ASIA MINJA - KATIBU MEZANI: Hajatoa hojaameshukuru.

Page 294: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

294

MWENYEKITI: Aah, wewe hukutoa hoja, siyo!

MHE. DKT. DAVID M. DAVID: Sikutoa hoja.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Waitara.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kwanza, namshukuru sana Mheshimiwa Waziriwa Ulinzi. Hoja zangu zote za Upinzani amejibu ipasavyo, vizuri,hayo ndiyo niliyokuwa nataka. Ndiyo kazi ya Upinzanikuchokoza, unaleta majibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili namshukuru sana Mkuuwa Majeshi kwa kuokoa maisha yangu, nimempa ng’ombe25 kwa mke wangu kutoka Nyakabindi pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, hoja yanguni kuhusu wale Wateuzi wa Kisiasa; Wakuu wa Wilaya naWakuu wa Mikoa ambao wanaendelea kuvaa Sare za Jeshi.Nahitaji kauli yako. Kama hakuna majibu mazuri, nakusudiakutoa shilingi ili tujadili kwa mapana yake. Kwa wale wateuleambao ni Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa ambaowameshatoka Jeshini, wanafanya kazi za Utumishi wa Umma,lakini wanaendelea kuvaa sare za Jeshi; naomba kauli yako,utaratibu ukoje Jeshini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati najibu hoja hapa, hili sualanililizungumzia, pengine Mheshimiwa Mbunge hakusikia.Nilisema hivi, Wanajeshi ambao wameshikizwa katika kazi zaKiserikali kwa maana ya Wakuu wa Wilaya na Wakuu waMikoa, bado wanaweza wakavaa uniform pale ambapowanahitajika kufanya hivyo, kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.Sasa ukimwona RC au DC amevaa, amepata kibali cha Mkuuwa Majeshi kutokana na kazi ambayo anatakiwa kuifanya.(Makofi)

Page 295: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

295

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, leo katikamipaka yetu kule kuna operation maalum ya kushughulikialabda wahamiaji haramu au wakimbizi au nani, huyuKamanda anaamua kuvaa uniform ili awaongoze vijanawake kwenda kufanya kazi maalum kule. Sioni kama kunatatizo, kwa sababu yuko katika majukumu yake ya kiulinzi.Hiyo ndiyo sababu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa kanuni nataratibu ni kwamba, kinachotakiwa ni kibali, asivae kwamaamuzi yake. Kama ameshapata kibali, nami najuakwamba Mkuu wa Majeshi alishatoa hicho kibali, kwa hiyo,hakuna tatizo. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara, majibu haya ndiyosahihi. Nafikiri Mheshimiwa Waziri amejibu vizuri sana,professionally kabisa. (Makofi)

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,siyo kweli, kama ni kweli, sijaelewa vizuri. Kwa hiyo, naombanitoe hoja Bunge lijadili na tupate maelezo sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.

MHE. TUNDU A. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

MWENYEKITI: Sawa ni kwa mujibu wa Kanuni walahata hamna taabu, lakini nami nina kitabu changu chaKanuni hapa.

Mheshimiwa Mwigulu, Mheshimiwa Almas,Mheshimiwa Mayenga, Mheshimiwa Martha bado upo?Mheshimiwa Bilago, Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla,Mheshimiwa Frank, Mheshimiwa Marwa, Mheshimiwa Albeto,Mheshimiwa Haonga, Mheshimiwa Bashe; bado mkowengine? Haya tunaanza na Mheshimiwa Albeto.

Page 296: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

296

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Leo nimepata conflicting messages kutoka kwaSerikali hasa wakati wa kuleta bajeti asubuhi. Kwa maanaya kwamba mimi nilifikiri nchi hii Wanajeshi lazima wakaembali katika mambo ya kiutawala, lakini taarifa niliyopatahivi asubuhi ni kwamba hata hivi jioni tumesikia kwambahata kuna makubaliano baina ya Serikali na Wanajeshinamna ya kuwachukua kuingia katika Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ina-send very wrongmessage. Tunaona nchi nyingine, watu waliokuwa Wanajeshi,baada ya kutoka kwenye Jeshi hakuna suala la kuvaauniform kwa sababu ni vitu viwili vinavyotengana. Hatukatainafasi yake kama Mwanajeshi, hatukatai nafasi yake,anaweza akaongoza kikosi lakini ina-send wrong messagekwa maana kwamba kumbe Jeshi bado linahusika katikasiasa. Hili ndilo tunaona kwamba halifai, litenganishwe kabisaJeshi na siasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Albeto, mimi sio Waziri, lakinikwenye masuala mengine nyeti ya Serikali kunakuwa na jointforces zinaunganishwa. Ukienda Marekani utakuta Mkuu waMajeshi Admiro anakuwa ni National Security Adviseranakuwa incharge wa CIA, anafanya uraiani lakini bado niMwanajeshi. Kwa hiyo, kuna vitu kwenye Serikali ili kulindamaslahi, lazima kuwe na uwiano fulani wa Kiserikali ikiamua…

(Hapa Mheshimiwa Ally Saleh Ally alisimama)

MWENYEKITI: Kaa tu, wala sikupi tena nafasi yakusema kwa sababu muda wako umekwisha.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Kwa sababu Waziri wa Nchi,ndio mtu wa kujibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa kaa. Mimi ndio Mwenyekiti.Mwenyekiti anatakiwa ajue kila kitu, kaa.

Page 297: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

297

Kwa hiyo hivi ni vitu vya kawaida tu. MheshimiwaWaziri atakujibu lakini these are normal positions ambapoSerikali inaweza kumteua mtu wa Jeshi kufanya kazi kwenyemaeneo maalum.

Baada ya maneno hayo, tunaingia kwenye guillotine.(Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasauliotuteua inakuwaje?

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, huo ubabebwana!

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MWENYEKITI: Waheshimiwa sikilizeni vifungu. Sikilizenivifungu.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MBUNGE FULANI: Tunasikiliza!

MWENYEKITI: Katibu Soma.

NDG. ASIA MINJA - KATIBU MEZANI: Hawasikii,wanapiga kelele.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hapoumetumia Kanuni gani? Tuambie Kanuni uliyotumia.

NDG. ASIA MINJA - KATIBU MEZANI: Narudia Fungu57 - Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, fedhailiyoombwa shilingi bilioni mia tisa na…

MBUNGE FULANI: Kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Kaa chini.

Page 298: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

298

Fungu 57 – Wizara ya Ulinzi naJeshi la Kujenga Taifa

Kif. 1001 – Administration and HR Mgt....Sh. 16,314,720,125/=Kif. 1002 – Finance and Accounts … … ... .Sh. 265,096,300/=Kif. 1003 – Policy and Planning … … … … .Sh. 405,580,000/=Kif. 1004 – Internal audit Unit.. … … … … ..Sh. 154,878,000/=Kif. 1005 – Procurement Mgt Unit..… … … Sh. 55,273,200/=Kif. 1006 – Legal Services Unit.. … … … … ..Sh. 46,137,200/=Kif. 1007 – Govern’t Comm. Unit..… … … ..Sh. 49,300,000/=Kif. 1009 – Independent Tel. Network. … … .Sh. 54,164,000/=Kif. 2001 – Industries, Construction& Agriculture .........… … … … … Sh. 280,585,000/=Kif. 2002 – Military Research &Dev. … … … Sh. 177,362,754/=Kif. 2003 – Building Consulting Unit … … …..Sh. 41,260,000/=Kif. 2004 – Estate MGT and Dev. Unit … … ..Sh. 66,640,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 38 – Ngome

Kif. 1001 – Defence Forces Headquarters’ Command... ... ... ... ... Sh. 1,199,446,006,118/=

Kif. 1007 – Land Forces Command … … Sh. 2,087,265,726/=Kif. 1008 – Air Defence Command … … Sh. 1,850,195,124/=Kif. 1009 – Navy Command… … … … … .Sh. 815,295,195/=Kif. 1010 – Military Hospitals… … … … …Sh. 1,045,527,400/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 39 – Jeshi la Kujenga Taifa

Kif. 1001 – The National Service Force.. Sh. 283,362,530,783/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Page 299: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

299

MIPANGO YA MAENDELEO

Fungu 38 – Ngome

Kif. 1001 – Defence Forces Headquarters’ Command … … … … ... .... Sh. 8,000,000,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila Mabadiliko yoyote)

Fungu 39 – Jeshi la Kujenga Taifa

Kif. 1001 – The National Service Force… ..Sh. 6,000,000,000/=

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

Fungu 57 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Kif. 1003 – Policy and Planning .. … … ……. Sh. 400,000,000/=Kif. 1009 – Indep. Telecom. Network…….Sh. 15,418,000,000/=Kif. 2001 – Industries Construction and Agriculture ..................………..Sh. 21,300,000,000/=Kif. 2002 – Military Research and Dev... Sh. 147,593,180,000/=Kif. 2003 – Building Consulting Unit . … … …Sh. 250,000,000/=Kif. 2004 – Estate Mgt Dev. Unit ..………...Sh. 20,038,820,000/=

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)

NDG. ASIA MINJA - KATIBU MEZANI: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kutoa taarifa Kamati imemaliza kazizake.

MWENYEKITI: Bunge linarejea.

(Bunge lilirudia)

MWENYEKITI: Tukae, Mtoa hoja. (Makofi)

Page 300: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

300

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa taarifa kwambaBunge lako limekaa kama Kamati ya Matumizi nalimekamilisha kazi zake. Naomba Taarifa ya Kamati yaMatumizi ikubaliwe na Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

MWENYEKITI: Hoja imeungwa mkono, sasa nitawahoji.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka2017/2018 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

yalipitishwa na Bunge)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chief Whip.

MWONGOZO WA SPIKA

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, nasimama kwa kanuni ya 68 (7) nikiombamwongozo kuhusu jambo ambalo limetokea Bungenimapema; na jambo hili kwa kweli limetokea mapema leona limeendelea kuchukua nafasi mpaka tunapomalizakuhitimisha hoja hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja iliyotolewa leo hapaBungeni ilikuwa inahusu Wizara ya Ulinzi na kwa mujibu wakanuni, hoja hii ilipaswa kutolewa hotuba ya MheshimiwaWaziri, Mwenyekiti wa Kamati inayohusika lakini na Msemajiwa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo ninaotakakuuomba kutoka katika kiti chako ni kuhusu utaratibu wa

Page 301: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

301

kikanuni ambao pia unaendana na kanuni ya 64(1)(a)ambayo inakataza Wabunge kusema uongo ndani ya Bungelako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kanuni hiyo pia inamtakamtu ambaye anataka kuthibitisha uongo wowoteunaosemwa Bungeni arudi kwenye kanuni ya 63 nakuthibitisha kwamba maneno ambayo ama Mbunge amamtu yeyote atakayezungumza ndani Bunge anabakia katikakusema ukweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeshukuru sana Msemajiwa Kambi ya Upinzani wakati anaingia kwenye mafungu yasera amesema kabisa hapa kwamba anamshukuruMheshimiwa Waziri amejibu yale aliyoyachokoza kuyasema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Msemaji wa Kambi yaUpinzani alipokuwa anazungumzia eneo la fedha ya chakula,alitaka kuwathibitishia Watanzania kitu ambacho hakikuwahalisia na siyo cha ukweli. Alipokuwa anazungumza eneo lafedha za likizo kwa ajili ya wapiganaji wetu, alitakakuwathibitishia Watanzania kupitia Bunge lako kwamba eneohilo halikuwa likisimamiwa vizuri, lakini taarifa yake haikuwana ukweli. Eneo la muda wa kazi za ziada katika Jeshi letu laUlinzi wa Tanzania vivyo hivyo, eneo la manunuzi vivyo hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, MheshimiwaWaziri wakati anahitimisha hoja hii ametoa ufafanuzi naamesema ukweli wa mambo hayo jambo ambalo kanunizetu zinatupasa, unapotaka ku-prove aliyesema kitu fulaniamesema uongo ni lazima wewe useme ukweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Ulinziameeleza ukweli wa maeneo hayo yote na kuoneshakwamba yale yaliyoandikwa kwenye hotuba ya Kambi yaUpinzani hayakuwa maneno ya kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba mwongozowako, katika hali ya namna hii, hotuba hii ya Kambi yaUpinzani imeshatolewa na ni public document ambayo

Page 302: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

302

inaweza ikasomwa na mtu yeyote, lakini ina maneno hayaambayo siyo ya ukweli. Kwa nini kiti chako kisimtakealiyeyasoma maneno haya Bungeni ayafute maeneo hayakwamba siyo maneno ya kweli na ikiwezekana awaomberadhi wapiganaji wetu kwa kusema maneno ambayohayana ukweli, ambayo yalikuwa yanataka kuchonganishaSerikali, Jeshi na Watanzania, ama ayafute maneno hayo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hatayafuta, utupemwongozo, kanuni zetu zinasema nini ili tuweze kujifunzanidhamu ndani ya Bunge ya kuandika na kusema manenoyenye ukweli ndani ya Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara, ni kweli mwongozounaoombwa uko sahihi na nilitoa tahadhari wakati unasoma.Kwa hiyo, yako maneno na hasa Wizara hii, siyo jambo jemakuzungumza vitu ambavyo havina uthibitisho au vitu vyakuokotea tu mitaani.

Licha ya sensitivity ya Wizara yenyewe, kanuni zetuhizi haziruhusu hata kama kuna Wizara nyingine, hairuhusiwikuzungumza vitu ambavyo siyo vya ukweli. Sasa kanuni zetuziko very clear, either usimame ufute maneno uliyoyasemaau kiti kikupe muda uende uthibitishe haya manenounayoyasema. Vitu viwili tu; simama ufute maneno yako; nawahusika wenyewe wako hapa na kama unafikiri unaouthibitisho, nikupe muda wa siku mbili; Ijumaa ulete uthibitisho,kwa sababu limewagusa watu wengi sana na hasalimewagusa viongozi wenyewe wa Jeshi, kidogo wamepatashida. Kwa hiyo ni vitu viwili; futa maneno yako uliyoyasemaau nikupe muda ukathibitishe. (Makofi)

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kwanza Wanajeshi unaowasemea kwambawamekwazika, labda kama wamekuandikia. Ninachosema,haya maneno, hii document ilienda kwa Ofisi ya Spika na

Page 303: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

303

imesomwa hapa Bungeni. From time to time wakatiwanasoma hatua kwa hatua, kulikuwa na mwongozo namaneno yote yaliondolewa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara…

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Wazirialipokuwa anazungumza hapa, kuna vitu amekiri kwambavilikuwa havijalipwa. Sasa unasema nifute maneno yapi?Labda awe specific na neno lipi ambalo limesemwa, kwasababu maneno yote tumeongozwa hapa, yamefutwawakati wa mjadala.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara, ni very simple.Nanyi mnaompigia makofi mtamwacha peke yake hapa.(Kicheko)

Mheshimiwa Waitara, very simple! Futa maneno yako,twende tukapumzike, ni hilo tu basi. Futa maneno; ni manenomachache tu; futa maneno yako uliyoyasema tuondoke.

(Hapa Waheshimiwa Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ninachosema, ni maneno yapi? Kwa sababu manenomengine yamefutwa na Spika na mengine yamefutwa hapa.Muwe specific maneno yapi natakiwa nifute hapa? Ndiyohoja yangu. Au basi nikupe nafasi wewe ambayo unaonahayafai, uyaondoe kwenye Hansard. Wewe unifutie kwaniaba yangu, kwa sababu siyajui ni yapi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa hebu msomee manenoyake.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, namheshimu sana Mheshimiwa Waitara.Mheshimiwa Waitara ni Mbunge mahiri, mwakilishi mzuri wawananchi wake, lakini ninachotaka kusema, niko very specificna nimesema hapa very specific.

Page 304: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

304

Mheshimiwa Waitara eneo lililokuwa linazungumzakuhusu…

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mwenyekiti taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Frank, hebu kaa.Mheshimiwa Frank hebu kaa; usitake nikupe manenomengine, kaa.

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mwenyekiti kila wakatiunatupa maelezo hapa …

MWENYEKITI: Wewe kaa chini! Wewe kaa chini!

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Kuthibitisha anatakiwaathibitishe…

MWENYEKITI: Wewe kaa chini! Ukisimama tena,nitakuchukulia hatua. (Kicheko)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU: MheshimiwaMwenyekiti, wala sitaki kurudi kwa Mheshimiwa Mbungealiyekaa, tumeshathibitisha haya yote ambayo ninayasemahapa. Eneo linalohusu manunuzi, eneo la fedha za chakula,eneo la fedha za likizo, eneo la muda wa saa za ziada;yaliyosemwa Mheshimiwa Waitara uyaondoe kwa sababuMheshimiwa Waziri ameshatoa ufafanuzi na kutoa ukweli wamaeneo hayo. (Makofi)

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nawashukuru sana, mimi sina ugomvi na Jeshi laWananchi kwanza. Nasi unajua ndio wenye Jeshi, linaitwaJWTZ, yaani Jeshi la Wakurya Tanzania. NimesemaMheshimiwa Mabeyo ni shemeji yangu. Kwa hiyo, miminasema yale maelezo ya Mheshimiwa Waziri yasimame,yangu yaondolewe. Ahsante sana. (Makofi)

Page 305: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA …parliament.go.tz/polis/uploads/documents/1502795458-16 MEI 2017.… · MHE. KIBERA J. KISHIMBA (K.n.y. MHE. ADADI M. RAJAB - MWENYEKITI

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

305

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waitara, sema nafutamaneno yangu. Sema nafuta maneno yangu tumalizane.Hayo yote yafute, utabaki peke yako humu! Haya basi toa.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naweza nikabaki peke yangu, natosha sana, lakini kwasababu nakuheshimu Mbunge mwenzangu kule Ilala jiraniyangu na Mwenyekiti wa Kamati hii, naomba kwa heshimakubwa nifute maneno hayo, tuko pamoja na nyie. (Makofi)

MWENYEKITI: Kwanza nakushukuru Mheshimiwa Waziri,umefanya kazi nzuri sana, uko peke yako, lakini umewezakujibu maneno yote na umeyajibu kwa ufasaha. (Makofi)

Nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wotewaliochangia, ndiyo uzuri wa Bunge hili, kanuni ni kanuni.Nimeingia kwa guillotine si kwa mapenzi ya mke wangu, nikwa kanuni. (Makofi)

Kanuni zinanipa fursa mimi kuamua muda ganiniahirishe Bunge kwa mujibu wa kanuni. Kwa hiyo, kanuniinasema, “Mwenyekiti anaweza.” Nimekuona MheshimiwaBilago unapiga makelele, unataka nikufundishe tu. Somakanuni ya 104 utanielewa.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya maneno hayomachache, naahirisha Bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi.

(Saa 1.48 Usiku Bunge liliahirishwa mpaka Siku yaJumatano, Tarehe 17 Mei, 2017 Saa Tatu Asubuhi)