bunge la tanzania majadiliano ya bunge · (nagoya – kuala lumpur supplementary protocol on...

177
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Saba – Tarehe 11 Septemba, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa, tukae. Katibu. NDG. YONA KIRUMBI – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kuhusu Azimio la Kuridhia Itifaki ya pamoja ya ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur kuhusu Uwajibikaji Kisheria na Fidia kwa Madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya Bioteknolojia ya Kisasa katika kutekeleza Itifaki ya Cartagena (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety).

Upload: others

Post on 20-Mar-2021

1 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA

________

MAJADILIANO YA BUNGE

_________

MKUTANO WA KUMI NA SITA

Kikao cha Saba – Tarehe 11 Septemba, 2019

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua

MWENYEKITI: Waheshimiwa, tukae. Katibu.

NDG. YONA KIRUMBI – KATIBU MEZANI:

HATI ZA KUWASILISHA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA:

Maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) kuhusu Azimio la Kuridhia Itifaki yapamoja ya ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur kuhusuUwajibikaji Kisheria na Fidia kwa Madhara yanayowezakutokea kutokana na matumizi ya Bioteknolojia ya Kisasakatika kutekeleza Itifaki ya Cartagena (Nagoya – KualaLumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress onCartagena Protocol on Biosafety).

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

MHE. OMAR A. BADWEL - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATIYA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NAMAZINGIRA:

Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira kuhusu Azimio la Kuridhia Itifaki yapamoja ya ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur kuhusuUwajibikaji Kisheria na Fidia kwa Madhara yanayowezakutokea kutokana na matumizi ya Bioteknolojia ya Kisasakatika kutekeleza Itifaki ya Cartagena (Nagoya – KualaLumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress onCartagena Protocol on Biosafety).

Azimio la Bunge la Mkataba wa Marakesh ya mwaka2013 unaolenga kuwezesha upatikanaji wa kazizilizochapishwa kwa watu wasioona wenye uoni hafifu auulemavu unaomfanya mtu kushindwa kusoma.

MHE. JOYCE J. MUKYA - K.n.y. MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI WA OFISI YA MAKAMUWA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA:

Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusuAzimio la Kuridhia Itifaki ya pamoja ya ziada ya Nagoya –Kuala Lumpur kuhusu Uwajibikaji Kisheria na Fidia kwaMadhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi yaBioteknolojia ya Kisasa katika kutekeleza Itifaki ya Cartagena(Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liabilityand Redress on Cartagena Protocol on Biosafety).

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):

Maelezo ya Waziri wa Kilimo kuhusu Azimio la KuridhiaItifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrikakuhusu Kulinda Hakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya zaMbegu za Mimea (The Protocol for Protection of New Varietiesof Plant [Plant Breeder’s Rights] in the Southern AfricanDevelopment Community – SADC).

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA - K.n.y.MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO,MIFUGO NA MAJI:

Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji kuhusu Azimio la Kuridhia Itifaki ya Maendeleoya Nchi za Kusini mwa Afrika kuhusu Kulinda Hakimiliki zaWagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimea (The Protocolfor Protection of New Varieties of Plant [Plant Breeder’s Rights]in the Southern African Development Community – SADC).

MHE. PASCAL Y. HAONGA - MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KILIMO:

Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusuAzimio la Kuridhia Itifaki ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwaAfrika kuhusu kulinda Hakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpyaza Mbegu za Mimea (The Protocol for Protection of NewVarieties of Plant [Plant Breeder’s Rights] in the SouthernAfrican Development Community – SADC).

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:

Maelezo ya Waziri wa Viwanda na Biashara kuhusuAzimio la Kuridhia Itifaki ya Marrakesh inayowezeshaUpatikanaji wa Kazi zilizochapishwa kwa watu wasioona,Wenye Uoni Hafifu au Ulemavu Unaofanya Mtu KushindwaKusoma wa Mwaka 2013 (The Marrakesh Treaty to FacilitateAccess to Published Works for Persons who are Blind, VisuallyImpaired or otherwise Print Disabled (MVT) 2013.

MHE. OMARY A. BADWEL - K.n.y. MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NAMAZINGIRA:

Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na mazingira kuhusu Azimio la Kuridhia Itifaki yaMarrakesh inayowezesha Upatikanaji wa kazi zilizochapishwakwa Watu Wasioona, Wenye Uoni Hafifu au Ulemavuunaofanya mtu Kushindwa Kusoma wa mwaka 2013 (The

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

Marrakesh Treaty to Facilitate Access to Published works forPersons who are Blind, visually Impaired or Otherwise PrintDisabled (MVT) 2013).

MHE. CECIL D. MWAMBE - K.n.y. MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI WA WIZARA YA VIWANDANA BIASHARA:

Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusuAzimio la Kuridhia tifaki ya Marakesh inayowezeshaUpatikanaji wa Kazi zilizochapishwa kwa Watu wasioona,Wenye Uoni hafifu au Ulemavu unaofanya Mtu kushindwaKusoma wa mwaka 2013 (The Marrakesh Treaty to FacilitateAccess to Published Works for Persons who are Blind, visuallyImpaired or Otherwise Print Disabled (MVT) 2013).

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mwambaumependeza na miwani baada ya kulipwa hela za korosho,umenunua miwani. (Kicheko/Makofi)

Katibu.

NDG. YONA KIRUMBI – KATIBU MEZANI: Maswali.

MASWALI NA MAJIBU

MWENYEKITI: Waheshimiwa tunaanza Ofisi ya WaziriMkuu Mheshimiwa Mwanne Ismail Mchemba.

Na. 84

Kukaribisha Wawekezaji Mkoa wa Tabora

MHE. MWANNE I. MCHEMBA Aliuliza:-

Serikali ya Awamu ya Tano imekaribisha wawekezajiwa nje na ndani kuwekeza sehemu mbalimbali hapa nchini:-

Je, Serikali ipo tayari sasa kuelekeza wawekezaji haokuwekeza katika Mkoa wa Tabora?

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (UWEKEZAJI)Alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya MheshimiwaWaziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa MwanneIsmail Mchemba, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira ya Serikali yaAwamu ya Tano ya kukuza uwekezaji katika sekta mbalimbalina kujenga uchumi wa kati wenye kuongozwa na Sekta yaViwanda ni suala linalotekelezwa katika mikoa yote ukiwemoMkoa wa Tabora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchukua fursa hiikuupongeza Mkoa wa Tabora na uongozi wake na Mikoamingine kwa kuwa mfano mzuri katika kutekeleza mikakatiya kuvutia uwekezaji ikiwemo uandaaji wa makongamanoya uwekezaji kama lile lililofanyika mwaka 2013 Dar es Salaamna lililofanyika mwezi Novemba, 2018 katika mjini Tabora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia makongamanohayo, tumeendelea kuhamasisha kila Halmashauri kuandaamradi wa kimkakati ambao utakuwa dira kwa wawekezajiwengine. Aidha, katika kutekeleza agizo la Serikali la kutengamaeneo ya uwekezaji, Mkoa wa Tabora umetenga ekari42,053.71 katika Halmashauri zake zote nane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kama sehemu yamatokeo ya jitihada za Serikali, takwimu zilizopo katika Kituochetu cha (TIC) zinaonesha kwamba tangu mwaka 1997,jumla ya miradi ya uwekezaji 55 imesajiliwa Mkoani Taborakatika Sekta za Kilimo, Viwanda, Ujenzi, Utalii Mawasiliano naUsafirishaji. Wilaya ya Tabora Mjini inaongoza kwa kusajilimiradi 19, Urambo 13, Nzega miradi tisa, Igunga 11, Sikongemiradi miwili na Uyui mradi mmoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kati ya miradi hiyo,miradi 30 ni ya Watanzania, miradi tisa ni ya wageni na miradi

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

16 ni ya ubia. Hivyo, napenda kipekee kumhakikishiaMheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inautambua Mkoa waTabora kama mojawapo ya maeneo ya kimkakati yenye fursaza uwekezaji katika sekta mbalimbali na tutaendeleakuwaelekeza wawekezaji kuja kuwekeza Tabora na katikaMikoa mingine nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hiikuwahamasisha Waheshimiwa Wabunge wote kushirikianakwa karibu na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Kituo chetu chaUwekezaji (TIC), Mamlaka ya EPZA na Taasisi nyingine katikakuibua miradi inayokidhi vigezo (bankable projects) na piakuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye maeneo yao.Lengo la hili ni kufanikisha malengo ya Serikali ya kuvutiauwekezaji wenye tija nchini kote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, Mikoainashauriwa sasa kuanza kutenga katika bajeti zake fedhakwa ajili ya kujenga miundombinu ya msingi kama vile maji,barabara, umeme na kadhalika. Lengo ni kuelekea kwenyemaeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji. Hatua hizizitasaidia katika kuharakisha uendelezwaji wa maeneomaalum ya uwekezaji kwa kukamilisha hatua muhimu zaawali na hivyo kuvutia wawekezaji na hata ushiriki wa sektabinafsi katika kuendeleza maeneo husika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, napendakuzihamasisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya kazi kwakaribu na Taasisi za Serikali zinazotoa huduma za ushauri wakuwezesha uwekezaji nchini ili kuweka mikakati ya pamojaya kutambua vivutio na fursa za wawekezaji wa ndani na njepamoja na kuwasilisha miradi ya kutafutiwa wawekezaji nakushirikiana na TIC katika kuandaa makongamano yauwekezaji katika Mikoa husika.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Nchemba.

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali mafupi yanyongeza. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Waziri na

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

Serikali ya Awamu ya Tano kwa kazi nzuri ambayo inafanywakwa ajili ya mambo ya uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni kwamba kwakuwa alipokuwepo Mheshimiwa Waziri wa Viwanda naBiashara, alikuwa ameandaa na alishawatayarishawawekezaji kutoka nchini China ambao walikuwa tayarikuwekeza katika Kiwanda cha Tumbaku, kwa bahati mbayawaliishia Dar es Salaam na kulikuwa na matatizo ya Uhamiaji:Je, Waziri yuko tayari sasa kuwafuatilia hawa wawekezaji waKichina ambao walikuwa tayari kabisa na maeneoyalitengwa ili waweze kuja kuwekeza kwenye zao latumbaku?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili: kwanzanampongeza sana Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, amefanyajitihada kubwa na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kwakuboresha maeneo katika mkoa mzima na Wilaya zote: Sasaje, Waziri yupo tayari sasa kuwaleta wataalamu rasmi ilikuweza kuainisha hayo maeneo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, kwa kifupi sana.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (UWEKEZAJI):Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa niseme tunashukurukwa pongezi na nikuhakikishie tutaendelea kufanya kazinawe pamoja na Waheshimiwa Wabunge wengine pamojana mikoa yetu katika kuhakikisha kwamba tunachochea nakuvutia uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pil i ni kwelinimefahamishwa kwamba alikuwepo mwekezaji kutokaChina ambaye alikuwa na nia ya kuwekeza Kiwanda chaTumbaku Tabora. Mpaka sasa tumeendelea kumfuatilia, lakinibado hajaonyesha nia.

Napenda kusema kwamba tutaendeleakumhamasisha yeye zaidi na kutafuta wawekezaji wenginezaidi kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Viwanda pamojana Wizara ya Mambo ya Nje.

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili katika swali lake la pilikuhusiana kuleta wataalam, kwanza napenda kuwapongezaMkoa wa Tabora kwa kutenga ardhi hiyo ya zaidi ya ekari 42,lakini kipekee napenda kusema tu kwamba ni takribaniasilimia tano ndiyo tayari inakidhi vigezo. Imewekwa ardhikubwa, mfano ukiangalia Kaliuwa, wana zaidi ya ekari 37,201,lakini ni asilimia tano tu ya Mkoa mzima wa Tabora katikamaeneo ya uwekezaji yaliyotengwa, ndiyo ambayo tayariyalimewekewa miundombinu wezeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutaendeleakushirikiana na Wizara ya Fedha, Wizara ya Ujenzi pamoja naMkoa husika wa Tabora kwanza kuhakikisha kwambamaeneo hayo yanawekewa miundombinu wezeshi lakini piakuhakikisha Halmashauri nazo zinaendelea kutenga fedha ilimiundombinu iweze kutengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuwapongezasana kipekee Halmashauri ya Nzega ambao tayari kwenyebajeti yao wameweka zaidi ya shilingi milioni 40 kwa ajili yasuala zima ya upimaji. Kwa hiyo, natoa rai kwa Halmashaurinyingine saba zilizobakia na nyingine nchini, basi wajitahidikutenga fedha katika bajeti yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala zima lakuleta wataalam, nimhakikishie kwamba tuko tayari kuletawataalamu, lakini zaidi niwapongeze Halmashauri zile nane,kila moja imekuja na mradi wake wa kimkakati; wako ambaowana mradi wa machinjio, wako ambao wana mradi wamashamba ya mifugo, kuweka kiwanda cha usindikaji nautengenezaji wa vyakula vya mifugo pamoja na sehemunyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza mikoa yotena Halmashauri zote ambazo tayari wameweza kubuni miradiya mikakati. Nawaomba waendelee kufuatilia, washirikianena Wizara ya Kilimo pamoja na Benki yatu ya Kilimo na benkinyingine za kimaendeleo ili kuweza kupata mitaji ya kuwezakuwekeza. Nakushukuru.

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

MWENYEKITI: Ahsante kwa majibu mazuri. MheshimiwaNjeza.

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.Napenda tu kuuliza Serikali, tuna mradi mkubwa wa uchimbajiwa madini ya niobium katika milima ya Panda Hill Songwe;na kwa bahati nzuri ile miradi ita-attract direct investmentya karibu dola milioni 200 na wawekezaji wapo tayari; nakatika ziara ya Mheshimiwa Rais alipofanya ziara kuleMbeya…

MWENYEKITI: Swali, swali!

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, swalilangu: Je, ni lini Serikali itakamilisha mchakato wa kuwaruhusuhao wawekezaji waanze kuchimba haya madini ya niobiumili vile vile wajenge na kiwanda cha kuchakata hayo madiniambacho ni cha kwanza Afrika na cha nne duniani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwenyekiti, majibu kwakifupi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (UWEKEZAJI):Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda kusemakwamba tunatambua kuhusiana na mradi huu wa Niobiumambao utafanyika katika milima ya Panda Hill na bahati nzurinami nilipata bahati ya kukaa katika Wizara ya Madini,niliweza kuwaona wawekezaji hawa; na ni madini ambayokwa kweli ni ya muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari tulishaanzakuwashughulikia, pia tumekuwa na mashauriano na Wizaraya Madini pamoja na Wizara ya Viwanda kupitia EPZ.Tutakutana pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizaraya Madini pamoja na Wizara ya Viwanda ili kuweza kuona nikwa namna gani tunakwamua mradi huu muhimu.

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

MWENYEKITI: Waheshimiwa tunaendelea na Ofisi yaRais, TAMISEMI, Mheshimiwa Richard Philip Mbogo, Mbungewa Nsimbo.

Na. 85

Kuangalia Upya Suala la Utoaji Ruzuku za Maendeleo

MHE. RICHARD P. MBOGO Aliuliza:-

Mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya Serikali za MitaaSura 290 yameleta nafuu sana kwa wakulima, lakini wakatihuo huo Halmashauri za Wilaya zenye wakulima zenyewakulima wadogo zimeathirika kimapato na kusababishakushindwa kutatua kero za wananchi kwa wakati:-

(a) Je, Serikali inaweza kuangalia upya suala la utoajiRuzuku za maendeleo?

(b) Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imeathirikakiwango kikubwa: Je, Serikali ipo tayari kuipatia ruzuku ili kutoahuduma za Elimu na Afya?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITAIRA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa ruhusayako kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Richard Mbogo,naomba uniruhusu niwatakie heri vijana wetu, watoto wetuwa Darasa la Saba ambao leo na kesho wanafanya mitihaniyao ya kumaliza Darasa la Saba na wanafunzi hao wapotakribani 947,221 wa kawaida na wale wenye mahitajimaalumu.

Nawaomba watu wote ambao wanahusika na zoezihili la mitihani, wazingatie taratibu na kanuni na miongozona kamwe wasijihusishe na udanganyifu kwa namna yoyoteile ili matokeo yawe yawe mazuri.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba sasa kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,TAMISEMI nijibu swali la Mheshimiwa Richard Mbogo, Mbungewa Nsimbo, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali ilifanyamabadiliko ya Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura 290kwa kuondoa kodi ambazo zilikuwa ni kero hasa kwawakulima wadogo. Takwimu za jumla zinaonesha makusanyoya Mamlaka ya Serikali za Mitaa yamekuwa yakiongezekakila mwaka. Mwaka wa fedha 2016/2017 Halmashaurizilipanga kukusanya shilingi bilioni 665.4 na zikakusanya shilingibilioni 544.8; mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashaurizilipanga kukusanya shilingi milioni 687.3 na zikakusanya kiasicha shilingi bilioni 553.4.

Mheshimiwa Mwenyekiti, samahani hizi zisomekebilioni, siyo milioni. Mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashaurizilipanga kukusanya shilingi bilioni 723.7 na zimekusanyashilingi bilioni 661.36. Hivyo, kwa tathmini ya jumla, inaoneshakuwa uamuzi wa kuondoa kodi kero haujaathiri ukusanyajiwa mapato kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye sekta ya afyakatika kipindi cha Mwaka 2017/2018 na 2018/2019, Serikaliimeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo shilingi bilionimoja kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya vya Kamoge naKatumba na shilingi milioni 220 kwa ajili ya ununuzi wavifaatiba. Vilevile katika mwaka wa fedha 2019/2020, Serikaliimetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuanza ujenziwa Hospitali ya Wilaya ya Nsimbo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa sekta yaelimu, mwaka wa Fedha 2018/2019, Serikali imeipelekeaHalmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kiasi cha shilingi milioni 250kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya madarasa 20 ya shuleza sekondari. Vilevile katika Mwaka wa Fedha 2018/2019kupitia Programu ya EP4R Serikali imeipatia Halmashauri yaWilaya ya Nsimbo kiasi cha shilingi milioni 205.7 kwa ajili yaujenzi wa madarasa manne, ukamilishaji ma maboma ya

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

madarasa saba na ujenzi wa matundu ya vyoo 12 katika shuleza msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kupitia EP4R, Serikaliimeipatia Halmashauri ya Nsimbo kiasi cha shilingi milioni 100.6kwa ajili ya ujenzi wa maabara na matundu sita ya vyoo shuleza sekondari. Aidha, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Serikaliimeitengea Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kiasi cha shilingimilioni 421 kwa ajili ya elimu msingi bila malipo.Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbogo.

MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa nafasi ili niweze kuuliza maswali madogomawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niishukuru Serikalikwa kuangalia na kutoa ruzuku kwenye Halmashauri zetu,hususan ambazo zina vipato vya chini. Swali la kwanza; kwakiwango hiki ambacho Serikali imetoa, bado kulingana nauhitaji kwenye Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo ni kidogo.Je, wako tayari kutuongezea ili tuweze kukidhi ukamilishajiwa maboma na uhitajikwenye upande wa elimu pamoja naafya?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; katika upandewa mahitaji haya je, Naibu Waziri yupo tayari kurejea ziarayake atembelee Halmashauri ya Nsimbo kujionea na awezekuona namna bora ya kuiwezesha Halmashauri ya Nsimbo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi.Jiandae Mheshimiwa Mwambe.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Kwanza naomba nipokee pongezihizi za Mheshimiwa Mbunge, na hii pia imezingatia sanakwamba amekuwa akilisemea sana eneo lake hili ili kuwezakuondoa kero.

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanzaanauliza kama Serikali ipo tayari kuongeza fedha. Naombanimhakikishie yeye na Waheshimiwa Wabunge wote kwambaSerikali nia yake kubwa ni kuhakikisha kwamba inaondoachangamoto ya miundombinu ya elimu na afya na kazi hiyoitakuwa inaendelea kufanyika kadri ya upatikanaji wa fedhakwa Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ananiulizakama nitarejea ziara katika eneo hili. Ni kweli nimeshapangaziara karibu mara mbili ikikaribia kwenda kule eneo la Katavina Rukwa, ziara hii imekuwa ikiahirishwa. Naombanimhakikishie ratiba nimeshaipanga, tukiahirisha Bunge hiliMheshimiwa Mbunge nitakuja Katavi na Rukwa nantatembelea majimbo yote ya ukanda ule. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwambe.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza:

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua hivi karibuniTAMISEMI wamekuwa wakitoa rating kwenye Halmashaurizetu kwa maana ya kuwapa namba kutokana na makusanyona utekelezaji wa makusanyo wanayoyafanya. Kwa bahatimbaya sanaHalmashauri nyingi ambazo walipanga mipangoyao ikitegemea makusanyo ya mazao ya kilimo hawakuwezakufanikiwa kupata hizo pesa kwa wakati kwa sababu Serikaliiliamua kuingilia mchakato fulani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka kuuliza kwaMheshimiwa Waziri, kwamba miradi mingi imesimamakwenye Halmashauri zetu, pesa za posho kwa ajili yaMadiwani hazilipwi kwa wakati na hasa miradi ya afya kwasababu hivi karibuni – na niipongeze Serikali kwambawametupatia pesa za 4PRkwa mfano Jimbo la Ndandatumepata zaidi ya madarasa 13. Sasa ninataka kufahamu;ni lini Serikali mtapeleka pesa kwa ajili ya kukamilisha mabomayaliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwenye Kata za

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

Ndanda, Lukuledi, Mihima na Mpanyani kwa ajili ya vituo vyaafya?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi, nilini?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana. Mheshimiwa Mwenyekiti,ameeleza maelezo mengi lakini kwa ufupi ni kwamba kamakuna mahitaji mahsusi unaandika TAMISEMI ili wawezekuyafanyia kazi. Lakini mpango wa Serikali ni kwamba hataMwaka wa Fedha tunapoanza 2019/2020, fedha zimetengwakwenda kumalizia maboma ambayo yapo ya msingi nasekondari katika Halmashauri zenu. Kwa hiyo tuvute subiralakini kama una jambo mahsusi tuandikie ili tuweze kuchukuahatua za haraka zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niseme hii haisemwiamesema 4PR, hii EP4R ndiyo lugha sahihi, maana yake nikwamba Education Payment For Results. Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante kwa majibu mazuri.Waheshimiwa tunaendelea, Wizara hiyohiyo swali laMheshimiwa Dkt. Rashid Mohamed Chuachua, Mbunge waMasasi.

Na. 86

Gharama za Elimu na Mafunzo

MHE. DKT. RASHID M. CHUACHUA aliuliza:-

Jimbo la Masasi lina Shule moja tu ya Sekondari yaKidato cha Tano na Kidato cha Sita ambayo ni ya Kitaifaingawa mahitaji ya Wanafunzi wanaofaulu kwenda Kidatocha Tano na Kidato cha Sita yameongezeka sana, Shulepekee ya Kidato cha Tano na Kidato cha Sita iliyopo Masasini Shule ya Sekondari ya Wasichana Masasi:-

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

(a) Je, ni lini Serikali itazipandisha hadhi Shule zaSekondari za Mwenge Mtapika na Anna Abdallah ili ziwezekupokea Wanafunzi wa Kidato cha 5 na 6;

(b) Jimbo la Masasi linahitaji vyumba 27 vya maabaraambapo hadi sasa vyumba Saba tu ndiyo vina vifaa vyamaabara katika shule Nne; Je, ni lini Serikali itapeleka vifaavya maabara katika Shule zote za Sekondari?

(c) Ikama ya Walimu wa Sayansi katika shule zaSekondari Tisa zilizopo Jimbo la Masasi ni Walimu 84 japokuwawaliopo ni 24 tu; Je, Serikali inaweza kulifanya jambo hili kamadharura inayohitaji utatuzi wa haraka kwa kutuletea Walimu60 wa Sayansi?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Dkt. Rashid Mohamed Chuachua, Mbunge waMasasi Mjini, lenye sehemu (a), (b), na (c), kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya MasasiMji inafanya jitihada kuziwezesha shule tatu za Sekondariambazo ni Sululu, Mtapika na Anna Abdallah ili ziwezekupandishwa hadhi na kuanza kutoa elimu ya Kidato chaTano na cha Sita. Tayari shule hizo zilishakaguliwa na wadhibitiubora wa shule na kukutwa na mapungufu kadhaa, hasa yamiundombinu ya maji, umeme na mabweni na hivyo kukosasifa. Halmashauri kwa kushirikiana na wadau inafanyia kazimapungufu hayo ili shule hizo ziweze kupandishwa hadhi nakutoa elimu tarajiwa.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha2017/2018, jumla ya shule za sekondari 1,800 zilizokamilishaujenzi wa maabara zilipelekewa vifaa vya maabara, na katiya hizo shule sita ni za Halmashauri ya Mji wa Masasi. Vilevile

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

katika Mwaka wa Fedha 2018/2019, jumla ya shule 1,258zilizokamilisha ujenzi wa maabara zitapelekewa vifaa vyamaabara na taratibu za manunuzi zinaendelea ambaposhule tatu kati ya shule zitakazopatiwa vifaa hivyo zipo katikaHalmashauri ya Mji wa Masasi.

(c) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwakawa fedha 2016/2017 hadi 2018/2019, Serikali imeajiri jumla yawatumishi 7,515 katika shule za sekondari nchini. KatiyaoWalimu ni 7,218 na Fundi Sanifu Maabara ni 297. Kati yawalimu walioajiriwa walimu wenye mahitaji maalum ni 29,walimu wenye elimu maalum ni 50, walimu wa masomo yasayansi na hisabati ni 7,089 na walimu wa lugha (Literature inEnglish) ni 100. Ambapo walimu 15 wa sayansi walipangwakatika Halmashauri ya Mji wa Masasi. Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nape, swali namba 86.

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana Naibu Waziriwa Elimu alitembelea Jimboni Mtama na katika ziara yakealikwenda kwenye Shule ya Sekondari Mahiwa na akaahidikutupatia fedha ya kuikarabati shule ile kwa sababu ilifanyavizuri katika mtihani wa Kidato cha Sita, pamoja na Shule yaSekondari Nyangao ambayo…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Chuachua nimekuona,samahani. Endelea tu Mheshimiwa Nape.

MHE. NAPE M. NNAUYE: …ambayo mwaka…

MWENYEKITI: Subiri Mheshimiwa Nape,samahani.Mheshimiwa Dkt. Chuachua.

MHE.DKT. RASHID M. CHUACHUA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Naomba kuuliza maswali mawilimadogo ya nyongeza:

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa kuwasasa kuna upungufu mkubwa wa walimu wa masomo yasayansi katika Halmashauri ya Masasi na walimu 46wanahitajika ili kukidhi Ikama ya walimu wa masomo yasayansi;

Je, ni lini Serikali italeta Walimu hao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni kwamba kwakuwa suala la kukosekana kwa walimu wa sayansi ni suala laKitaifa, na kwa kuwa wanafunzi wengi wanaomaliza kidatocha nne na kidato cha sita hawachagui kwenda kujiungana masomo ya ualimu wa masomo ya sayansi, hivi Serikalihaioni kunatakiwa kuwe na jitihada za maksudi za kuchocheawatoto hawa ili waweze kujiunga na masomo ya ualimu wasayansi hususan kwa kuondoa ama kupunguza ada kwamasomo ya Diplomaya Ualimu wa Sayansi na Degree yaUalimu wa Sayansi?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Kwanza nampongeza MheshimiwaMbunge kwa kuendelea kufuatilia suala la elimu hasa katikamasomo ya sayansi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanzaanataka kujua ni lini walimu wa sayansi watapelekwa katikamaeneo haya. Ni kweli kwamba kuna upungufu wa walimuwa sayansi na hisabati katika shule zetu za sekondari lakinitumepata kibali mwaka wa fedha uliopita tukaajiri walimu4,500 na sasa tunasubiria kibali kingine takribani walimu 15,000.Tukipatakibali hicho tutaajiri, namhakikishia MheshimiwaMbunge maeneo yote ambayo yana upungufu tutaanzanayo, pale palipo na upungufu mkubwa tunaanza nakuendelea katika maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nia ya Serikali ni kuwa nawalimu wa kutosha katika masomo ya sayansi ili kuweza

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

kuboresha elimu hii ya sayansi hasa kwenye dhananzimainayohusiana na Serikali ya Awamu ya Tano ya sera yamaendeleo ya viwanda na uchumi endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pil ianazungumzia kama kuna uwezekano wa kupunguza adakatika masomo na hasa katika Diplomaili wanafunzi wengina vijana wengi wajiunge katika masomo ya sayansi na hasaUalimu ili waweze kupunguza changamoto hii. Kwanzagharama inayotumika sasa siyo kubwa ni gharama yakawaida kabisa na Serikali imejitahidi sana kupunguzamichango mingi ambayo ilikuwa inafanyika. Sasa hivitumeshapeleka vijana wengi katika Vyuo hivi, wataendeleakusoma na ada ni ya kawaida. Ahsante.(Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nape.

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Mtama lina shuleza sekondari mbili ambazo zinapokea vijana waKidato chaTano na Kidato cha Sita. Shule ya Sekondari Nyangao naShule ya Sekondari Mahiwa. Mwaka jana Naibu Waziri waElimu alipotembelea Jimboni Mtama alipoenda kuiona Shuleya Sekondari Mahiwa alikuta majengo yake yamechoka nayamekuwa ya muda mrefu na akaahidi kwamba Serikaliitatoa fedha kusaidia ukarabati wa majengo hayo.

Je, Serikali iko tayari kutekeleza ahadi yake kwawananchi wa Jimbo la Mtama?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri mhusika, majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba nilitembelea Jimbola Mheshimiwa Nape na ni kweli kwamba alinisihi nimsaidieshule yake iweze kupata miundombinu ili iweze kuwa borana hatimaye kuwa shule ya Kidato cha Tano na Kidato chaSita. Naomba niendelee kumuahidi Mheshimiwa Mbunge

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

kwamba Serikali imepanga kupeleka fedha katika Awamuya Nane ya Mpango waEP4R, kwa hiyo, ahadi yetu ikopalepale na itatekelezwa.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabungetunaendelea na swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe.

Na. 87

Hitaji la Walimu wa Sayansi – Katavi

MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itapeleka Walimu wa Sayansi katikaMkoa wa Katavi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa niaba yaWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swalila Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha Mwakawa Fedha 2016/2017 hadi 2018/2019, Serikali imeajiri jumla yawatumishi 7,515 katika shule za sekondari nchini. Kati yao,Walimu 7,218 na Fundi Sanifu Maabara 297. Kati ya walimuwalioajiriwa walimu wenye mahitaji maalum walikuwa 29,walimu wenye elimu maalum ni 50 na walimu wa masomoya sayansi na hisabati ni 7,089 na walimu wa lugha (Literaturein English) walikuwa 100.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka2016/2017 hadi 2018/2019 Serikali ilipanga jumla ya Watumishi121 katika shule za sekondari Mkoani Katavi. Kati yaoWalimuwa masomo ya Sayansi na Hisabati walikuwa 115 na FundiSanifu Maabara walikuwa Sita.

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuajiriwatumishi wa kada mbalimbali ikiwemo walimu kwa kadriya upatikanaji wa fedha. Ahsante.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Lupembe.

MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimpongeze Naibu Waziri kwa majibu mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mahitaji yawalimu wa sayansi ni makubwa sana na ukizingatia wananchiambao tunaishi pembezoni unakuta shule moja kamaRungwa Sekondari pale Mpanda ina watoto 1,150, walimuwa sayansi kuanzia Form One mpaka Form Six walimu wakowanne tu. Na ukiangalia sehemu nyingine kama Usevia shuleForm One mpaka Form Six walimu wawili.

Je, Serikali itatuletea lini Mkoa wa Katavi walimu kwasababu tunahitaji sana walimu kutokana na uhitaji wawanafunzi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili,kwa kuwaSerikali ilifanya kazi kubwa ya kuhamasisha kujenga maabarakatika shule zote za Kata nchini, na wananchi walihamasikasana wakajenga maabara na maabara zile zimekamilikalakini walimu wa sayansi hakuna kabisa.

Je, lini Serikali itaweka mikakati maalum kamailivyofanya kuhamasisha kujenga maabara ili tuweze kupatasasa walimu wa sayansi?(Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Kwanza ninampongezasanaMheshimiwa Mbunge Anna Lupembe kwa kuendeleakuwasemea watu wake wa Mkoa wa Katavi ili wawezekupata elimu bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba tunachangamoto ya upungufu wa walimu wa sayansi na hasa

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

katika masomo ya sayansi na hisabati. Vilevile Serikaliimefanya kazi kubwa sana ya kuongeza juhudi ya kutafutafedha ili tuweze kuajiri walimu hawa wakasaidie kuondoachangamoto ya walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwataarifa tu mwezi Meimwaka huu Serikali ilipeleka fedha za EP4R motisha ili moja,zikamalizie maboma ya shule za msingi na sekondari, piliilikuwa ni ku-balance ikama katika shule zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwaelekezeWaheshimiwa Wakurugenzi katika Halmashauri zetu naMaafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya, zile fedha za Serikali ilikuwani kuangalia kama kuna shule moja ina upungufu, shulenyingine ina walimu wa ziada, ilikuwa ni kuwahamisha kutokaeneo moja kwenda lingine ili kuweza ku-balance Ikama nakupunguza changamoto ya Walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kamanilivyosema katika maswali yaliyopita leo asubuhi,tumeshaomba kibali cha kuajiri walimu hawa, zaidi ya 15,000.Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na maeneo mengine yapembezoni, tutakapopata kibali cha kuajiri walimu wa sayansina hisabati, maeneo ya pembezoni yatakuwa kipaumbele,tutaanza na maeneo ambayo yana upungufu mkubwa wawalimu kwenda pale ambapo pana upungufu ambao siyomkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili anauliziamaboma ya maabara zetu. Ni kweli, tumekubalianatunagawana kazi, Waheshimiwa Wabunge, Serikali na wadaumbalimbali wa elimu na maendeleo.Kazi ya kumaliziamaboma haya ya maabara ni ya kwetu sote kamanilivyotaja. Serikali tumejipanga, hapa tulipo tupo kwenyemanunuzi, wakati wowote kuanzia sasa taratibu za manunuzizitakamilika tutapeleka vifaa katika maabara zetu. Kwa hiyo,niwaombe Waheshimiwa Wabunge na wadau wenginetuendelee kuchangia kwa namna mbalimbali tumaliziemaboma yetu, vifaa tutapeleka, wataalam tutapeleka na

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

hii changamoto hatimaye itaisha ili watoto wetu wawezekusoma katika mazingira ambayo ni rafiki. Ahsante.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa tuna maazimiomengi leo. Tunaendelea na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano, Mheshimiwa David Ernest Silinde.

Na. 88

Ujenzi wa Barabara ya Mlowo – Kibaoni

MHE. PASCAL Y. HAONGA (K.n.y. MHE. DAVID E.SILINDE) Aliuliza:-

Je, ni l ini barabara ya Mlowo – Kamsamba –Kiliyamatundu – Kibaoni itajengwa kwa kiwango cha lami?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO(MHE. ELIAS J. KWANDIKWA)alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, napenda kujibu swali laMheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Mlowo –Kamsamba – Kiliyamatundu – Kibaoni yenye urefu wakilometa 369 ni barabara ya Mkoa na inahudumiwa naWakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mikoa yaSongwe, Rukwa na Katavi. Aidha, Serikali kupitia Wakala waBarabara Tanzania (TANROADS) imekamilisha ujenzi waDaraja la Momba lenye urefu wa mita 84 na barabaraunganishi zenye urefu wa kilometa 1.2.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kazi ya upembuziyakinifu na usanifu wa kina inaendelea kwa barabara kuanziaKamsamba hadi Mlowo, kilometa 130.14 na barabara yamchepuo kwa kuingia Makao Makuu ya Wilaya ya Momba,kilometa 15, kwa gharama ya shilingi milioni 765.46. Kazi hiiimefikia asilimia 75.

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika mwaka wafedha 2019/2020, Serikali imetenga jumla ya shilingi milioni 180kwa ajili ya kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wakina kwa barabara na kuijenga kwa kiwango cha lamisehemu ya barabara hii kuanzia Kiliyamatundu hadi Kasansa(sehemu ya Kilyamatundu – Muze (km 142) na Ntendo – Muze(km 37.04), taratibu za kumpata Mshauri Elekezi wa kufanyakazi hiyo zinaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu sehemu ya barabarakutoka Kasansa hadi Kibaoni (km 60), sehemu ya kuanziaKibaoni hadi Majimoto (km 34) ipo kwenye hatua za manunuziya kumpata mshauri elekezi kwa ajili ya kufanya kazi yaupembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Kibaoni– Majimoto – Inyonga (km 162). Aidha, sehemu iliyobakikuanzia Muze – Mamba – Majimoto (km 55) Serikali inatafutafedha ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wabarabara hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua umuhimu wabarabara hii kwa ajili ya usafiri wa wananchi na usafirishajiwa mazao ya chakula na biashara yanayozalishwa nawananchi wa maeneo ya Kata za Igamba, Hulungu, Itaka,Nambinzo hadi Kamsamba pamoja na maeneo yaKiliyamatundu, Muze, Kasansa, Majimoto hadi Kibaoni, Serikaliinaendelea kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuifanyiamatengenezo mbalimbali ili iendelee kupitika majira yote yamwaka na mara tu usanifu wa kina utakapokamilika, ujenzikwa kiwango cha lami kwa barabara hii utafanyika kwaawamu kulingana na upatikanaji wa fedha.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Haonga.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawiliya nyongeza. Swali la kwanza, wakati wa kampeniMheshimiwa Rais Dkt. Magufuli aliahidi kwamba kabla yakufika mwaka 2020, barabara hiyo ya kutoka Mlowo kwendaKamsamba hadi Kibaoni itakuwa imekamilika. Ukiangaliakuanzia sasa hadi mwaka 2020 bado miezi michache tu. Je,

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

ni lini sasa ahadi hii ya Serikali itatekezwa kwa vitendo badalaya maneno?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa katikamajibu ya Serikali kwamba kukamilisha usanifu wa kinahawajataja kwamba ni lini usanifu wa kina utakamilishwa.Je, Serikali kutotaja muda wa kukamilisha usanifu wa kinahaioni huku ni kutowatendea haki wananchi wa Mikoa yaSongwe, Katavi, pamoja na Rukwa?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Haonga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, umetaja ahadi yaMheshimiwa Rais wakati wa kampeni, lakini ujenzi wabarabara ni mchakato, lazima ufanye upembuzi yakinifu,usanifu wa kina, baadaye uingie mikataba uanze kujenga.Hauwezi ukafanya kabla ya kukamilisha hizo hatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vipande vyabarabara ambavyo unavizungumzia tayari kuna kimojamwezi huu wa tisa cha kutoka Mlowo kwenda mpaka paletulipokamilisha daraja, mwezi wa tisa usanifu wa kinautakamilika baada ya hapo mambo mengine yanaanza.Upembuzi yakinifu umeanzia kule Muze unakuja kuungaKamsamba, na tuna matarajio ya kuendelea huko na piatumeshaanzia Inyonga kuja mpaka Maji ya Moto. Kwa hiyo,utaratibu unaendelea ahadi ya Mheshimiwa Raisinatekelezwa. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge usiwe nawasiwasi na wananchi jirani zangu wa kule wawe na uhakikakwamba barabara ile itajengwa kwa kiwango cha lami.(Makofi)

MWENYIKITI: Ahsante, Mheshimiwa Musukuma.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Naomba kuuliza swali langu la nyongeza,

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

barabara ya kutoka Senga Ibisabageni mpaka Sima nibarabara inayotuunganisha Mkoa wa Geita na Mkoa waMwanza na Serikali ilitupa fedha upande wa Geita naupande wa Mwanza. Upande wa Geita tulishalima eneo letutukamaliza lakini upande wa Mwanza umebakiza kamakilomita tatu na leo ni mara ya tatu namuuliza MheshimiwaWaziri.

Je, Mheshimiwa Waziri uko tayari kufuatana na mimikwenda kuona zile kilomita tatu tu ambazo upande waMwanza wameshindwa kumaliza ili watu waanze kupitishamagari yao pale? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupi.

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Mwenyekiti, niko tayari kufuatana naye. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Mabula jiandaeMheshimiwa Komu.

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Naomba niulize swali la nyongeza, kwa kuwabarabara ya Kenyatta itokaya Mwanza Mjini kwenda Usagalakuelekea Shinyanga ni barabara ambayo inahudumia watuwengi na kwa sasa inaendelea kuwa finyu sana. Ni lini Serikalikupitia mipango yake ya uboreshaji miundombinu itaitoleafedha barabara hii walau iwe ya njia tatu mpaka nne ilikuweza kukidhi mahitaji makubwa ya watu wa Mwanza?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Mwenyekiti, kupanua barabara, kuongeza reli,hatuendi hivi hivi lakini mpaka traffic iweze kufikia kwambasasa yanapita magari 20,000 au 40,000 kwa siku ndiyotunaipanua ili kuiongezea uwezo. Kwa hiyo, itakapofikiaitafanyika.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Komu.

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

MHE. ANTONY C. KOMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja lanyongeza. Kama ilivyo katika Wilaya ya Momba, kule MoshiVijijini katika Kata ya Uru Shimbwe Mheshimiwa Rais, Dkt. JohnPombe Magufuli wakati anagombea alikuja pale akahutubiana akaahidi kujenga kwa kiwango cha lami barabara yakutoka Mamboleo mpaka Shimbwe. Kwa kweli ile barabarasasa hivi iko katika hali mbaya sana, sasa naomba kujua tokakwa Serikali ni lini ahadi hii ya Mheshimiwa Rais itatimizwa?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la MheshimiwaKomu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Serikali ya Chamacha Mapinduzi ni kuunganisha mikoa kwa barabara za lami,lakini na mipaka ya majirani zetu kuunganisha kwa lami halafubaadaye ndiyo tunaendelea na barabara nyingine.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tendega.

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kuniona. Barabara ya kutoka Iringa Mjinikuelekea Ruaha National Park ambayo ni Jimbo la Kalengaimekuwa ni changamoto na ni ahadi ya Mheshimiwa Raiswa Awamu ya Nne na Rais wa Awamu ya Tano. Ni lini sasabarabara hii itajengwa kwa kiwango cha lami?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la MheshimiwaMbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ile itajengwapamoja na Uwanja wa Ndege wa Nduli na itajengwa kupitiafedha za Benki ya Dunia, taratibu za kupata hizo fedhazinaendelea itakapokamilika mradi utaanza.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

MWENYEKITI: Waheshimiwa tunaendelea, Wizara yaElimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa Aida JosephKhenani.

Na. 89

Matamko Juu ya Wanafunzi Wanaopata Ujauzito

MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza:-

Kumekuwa na matamko na makatazo mbalimbali juuya wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni:-

Je, matamko na makatazo hayo yamesaidia kwa kiasigani?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijajibu swali naombakutumia nafasi hii kuwatakia vijana wetu 947,221 wanaofanyamitihani yao ya darasa la saba, naomba niwatakie kila lakheri na Mungu awaongoze katika mitihani yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali laMheshimiwa Aida Joseph Khenani, Mbunge wa Viti Maalumkama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, matamko na makatazokuhusu wanafunzi wanaopata ujauzito yanatokana na Kanuniza Elimu za Mwaka 2002, Kanuni Na. 4 ya Sheria ya Elimu yaMwaka 1978, Sura Na. 353 inayobainisha makosa yawanafunzi shuleni. Aidha, yanazingatia marekebisho ya Sheriaya Elimu Na. 25 ya Mwaka 1978 yaliyofanyika mwaka 2016.Katika marekebisho hayo, mtu yeyote atakayepatikana nahatia ya kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi ausekondari atahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela. Sheria hii

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

pia inatoa adhabu kwa mtu yeyote anayesaidia mhalifualiyempa mwanafunzi mimba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria na makatazo hayoyamesaidia jamii kufahamu umuhimu wa kulinda hadhi nausalama wa mtoto wa kike. Pia, imesaidia kujua adhabu kwamtu yeyote anayempa mwanafunzi mimba ambapo kesizimefunguliwa na baadhi ya wahusika wamehukumiwakifungo kwa kosa hilo. Aidha, elimu, matamko na sheriavimesaidia kupunguza mimba za wanafunzi kwenye maeneomengi nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeweka mikakati yakupunguza changamoto kwa watoto wa kike ikiwa ni pamojana kujenga mabweni na hosteli katika maeneo ambayowanafunzi wanalazimika kutembea umbali mrefu. Aidha,Serikali pia imeweka mpango wa kusaidia wasichanawanaoacha shule kwa sababu mbalimbali ili wawezekuendelea na masomo. Mpango huo ni kutoa elimu kupitiaVyuo vya Elimu Nje ya Mfumo Rasmi vinavyoratibiwa na Taasisiya Elimu ya Watu Waziri pamoja na Vyuo vya Maendeleo yaWananchi (FDC).

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe wito kwa wazazi najamii kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano wa kuwalindawatoto wa kike na kuhakikisha kuwa taarifa zinatolewa kwamamlaka husika il i kuhakikisha kuwa mtu yeyoteanayemsababishia mtoto wa kike kukosa elimu anakumbanana mkono wa sheria.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Khenan.

MHE. AIDA J.KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili yanyongeza. Kutokana na majibu ya Serikali, Serikali yenyeweinakiri kwamba kuna changamoto mbalimbali zinazopelekeamtoto wa kike kupata ujauzito. Lakini inasema ina mpangowa mtoto huyu wa kike aliyepata ujauzito kusoma elimu yawatu wazima ambayo ni nje ya mfumo rasmi. Kunawanawake ambao wana familia zao wanasoma degree,

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

wanapata Master’s na Ph.d ambao ni mfumo rasmi. Serikalihaioni kwa kufanya hivyo ambao tunawaita ni watotowakasome elimu ya watu wazima ni kuwaongezea adhabunyingine?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa Serikalipia imekiri kwamba umbali mrefu nao unachangia watotowa kike kupata ujauzito. Kwa kuwa Mkoa wa Rukwa naoumekuwa kinara kwa watoto wa kike kupata ujauzito, Mkuuwetu wa Mkoa amekuja na oparesheni ambayo ina kaulimbiu ambayo inasema, Niacha Nisome. Je, Serikali iko tayarikumsaidia fedha kwa ajili ya kujenga hosteli?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu kwa kifupisana.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze na hilo la pili,naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayariSerikali inasaidiana na wananchi kwenye halmashauri zaokujenga hosteli na mabweni kwa aji l i ya kuondoachangamoto ya watoto wa kike ambao wanatembeaumbali kwenda shuleni. Kwa hiyo, nimhakikishie tu kwambatuko pamoja na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kuhakikishakwamba azma yake hiyo inafanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na lile swali lakela kwanza, kwamba kwa maoni yake siyo haki kuwanyimawatoto ambao wamepata ujauzito kuendelea na masomokatika shule za kawaida. Naomba nimhakikishie MheshimiwaMbunge kwamba lengo la Serikali ni zuri kwa sababutunajaribu kumlinda hata mtoto yule anayezaliwa kwasababu watoto wale ambao wanapata mimba wanakuwabaadaye wanawabeba wenzao. Ukiwapeleka katika shuleza kawaida hawatapa mazingira mazuri ya kuweza kuwalea.Kwa hiyo, tunamjali mtoto yule aliyezaliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, tumeweza kujifunzavilevile kwamba hata watoto hao ambao wamepataujauzito, mara nyingi wakienda kwenye shule za kawaida zile

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

ambazo wametoka wanakuwa wananyanyapaliwa, kwahiyo tunawawekea mazingira mazuri ambayo yatawasaidiakusoma kwa uhuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, wanapoenda kusomakwenye Vituo vya Elimu ya Watu Wazima, inawasaidiakusoma katika utaratibu ambao…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri kwa kifupi sana.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwahakikishie kwambatutaendelea kuwasaidia na kwa kweli vituo hivyo ambavyoviko 500 nchi nzima vya watu wazima vimewasaidia watotowengi wa kike kuendelea na masomo katika ngazizinazofuata.

MWENYEKITI: Waheshimiwa tunaendelea, Wizara yaKilimo, Mheshimiwa Salum Mwinyi Rehani Mbunge wa Uzini.

Na. 90

Udhibiti wa Fangi Kwenye Mazao ya Korosho

MHE. SALUM MWINYI REHANI Aliuliza:-

Dawa ya Sulphur ndiyo dawa ya udhibiti wa fungue(fangi) kwenye mazao ya korosho na mazao mengine, naSerikali imeunda mfumo wa kuagiza dawa hii ya kupuliza kwanjia bubu procurement; na mwaka jana baadhi ya wakulimawaliathirika kwa kuchelewa na kupata dawa feki.

(a) Je, ni lini Serikali itakuwa tayari kuleta dawambadala ambazo ni rahisi zaidi?

(b) Je, ni lini Serikali itakaa na Vyama vya Msingi ilikupanga ratiba ya kuagiza na kuleta dawa na kupiga napia kuzuia dawa za msimu uliopita?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA)Alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waKilimo napenda kujibu swali la Mheshimiwa Salum MwinyiRehani, Mbunge wa Uzini lenye sehemu (a) na (b) kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali haijaanzisha mfumobubu wa ununuzi wa Salfa. Zao la korosho huathiriwa namagonjwa aina mbalimbali yakiwemo yale yanayosabishwana fungue. Miongoni mwa magonjwa tishio kwa zao hili niUbwiriunga, Blaiti, Chule na Mnyauko fusari. Hata hivyo,magonjwa hayo yamekwisha kupatiwa tiba isipokuwamnyauko fusari. Serikali inaendelea na tafiti kupitia taasisi zakeili kupata kinga na tiba stahiki za magonjwa na waduduwanaoshambulia zao la korosho hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, salfa ni miongoni mwaviuatilifu vinavyotumika kwa kinga na tiba ya ugonjwa waUbwiriunga. Serikali inakusudia kuandaa mfumo wa pamojawa ununuzi wa viuatilifu kwa ajili ya matumizi ya msimu wa2020/2021 ambapo viuatilifu vingine kwa ugonjwa huoambavyo ni triadimenol, hexaconazole, tebuconazole navinginevyo. Hata hivyo, Serikali itaendelea kuhimiza matumiziya salfa kwa kuwa kiuatilifu hiki hakiitaji ujuzi mwingi wakatiwa kukitumia shambani kwa kuwa kimezoeleka na vilevilehakiingii ndani ya mmea na hivyo kufanya koroshoinayozalishwa kuwa na sifa ya kilimo hai (Organic CashewNut).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Bodi yaKorosho itendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwani pamoja na Vyama vya Msingi vya Ushirika katika kutathminimahitaji ya viuatilifu na ratiba ya uagizaji wa viuatilifu hivyo.Aidha, Serikali kupitia TPRI itaongeza udhibiti katika ukaguziwa viuatilifu nchini ili kuviondoa sokoni viuatilifu visivyo na sifa.

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Rehani.

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante, nauliza maswali mawili ya nyongeza; Je, Serikali inamkakati gani wa ndani ambao utahakikisha kwambaviuatilifu vyote vinaagizwa kwa mfumo wa bulk procurementambao sasa hivi haujaanza. Mfumo huu ndiyo ule ambaounasaidia kulifanya zao la korosho ku-stand kwenye uzalishajimkubwa zaidi kama ulivyofanyika mwaka juzi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa udhibiti wawafanyabiashara wasio waaminifu pamoja na kutumiawatafiti ambao wengine wanashirikiana katika kutengenezabaadhi ya viuatilifu ambavyo wanavichanganya na dawakama za salfa, dawa kama za pecoxystrobin na proquinazidambazo zinachangia sana kuweza kusaidia kuongeza uwezowa kemikali na kuua wadudu lakini vinaharibu mazingirakatika maeneo yetu. Je, mkakati gani upo ambao utawezakuwadhibiti kupitia TPRA hawa wafanya biashara ambao siwaaminifu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri kwa kifupi sana.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anataka kujuamkakati wa Serikali kwa ajili ya kuanzisha mfumo wa uagizajiwa viuatilifu kwa pamoja (bulk procurement) ukoje. Natakanimtaarifu Mheshimiwa Mbunge, Serikali sasa hivi tuko kwenyehatua za mwisho wa mchakato wa kumalizia ili kwa ajili yauagizaji wa viuatilifu kwa pamoja. Nataka nimhakikishie msimuujao wa kilimo cha korosho wa mwaka 2020/2021 kamanilivyojibu kwenye jibu langu la msingi, tutaagiza viuatilifu kwapamoja kwa kutumia Mfumo wa Bulk Procurement.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili anatakakujua mkakati wa Serikali tuliokuwa nao katika kudhibitiuingizaji nchini wa viuatilifu feki. Tulishawaelekeza Taasisi yetuya TPRA na wako field wanafanya ukaguzi wa mara kwamara na ukaguzi wa kushtukiza katika maduka yote ili kubainiviuatilifu ambavyo havina sifa na kuvitoa sokoni na kuchukuliahatua kwa wale walioviingiza. Pia, vyombo vyetu vya ulinzina usalama pamoja na TRA wanadhibiti mipaka yetu kwa

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

ajili ya kuingiza viuatilifu hivi feki ili kuwalinda wakulima hawawapate viuatilifu vinavyostahili.

MWENYEKITI: Ahsante, Waheshimiwa tunaendeleamuda wetu mchache, Mheshimiwa Magdalena HamisSakaya wizara hiyo hiyo.

Na. 91

Tiba kwa Magonjwa Sugu ya Mazao

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA Aliuliza:-

Kutokana na kuwepo kwa magonjwa suguyanayoathiri mazao ya ndizi, mihogo, minazi na matundakama michungwa, miembe na kadhalika kumesababishawakulima kutozalisha kwa kiwango kinachostahili lakini piamazao haya kukosa masoko ya uhakika nje ya nchi.

Je, Serikali ina mikakati gani kuhakikisha magonjwahaya yanapatiwa suluhisho la haraka ili kilimo kiwe na tija nakupata masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. HUSSEIN M. BASHE)Alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waKilimo naomba kujibu swali la Mheshimiwa Magdalena HamisSayaka kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli magonjwa sugu yamazao yanaathiri uzalishaji, tija na ubora wa mazao hivyokusababisha hasara kwa mkulima. Katika kushughulikiachangamoto hiyo, Serikali inatekeleza mikakati mbalimbaliya kukabiliana na usugu wa visumbufu hivyo. Mikakati hiyo nipamoja na kuimarisha tafiti, kuzalisha na kusambaza kwawakulima mbegu zenye ukinzani dhidi ya magonjwambalimbali. Kwa mfano, mbegu za muhogo aina ya Kiroba,

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

Kizimbani, Kipusa, Chereko, Mkuranga 1 na Mkombozizinahimili ugonjwa wa Batobato na mchirizi kahawia, michebora ya migomba aina ya FHIA 17, FHI 23, Nshakara na Nyoyazinahimili ugonjwa wa unyanjano wa zao la migomba. Aidha,mikakati mingine ni kuimarisha huduma za ukaguzi wa mimeana bidhaa za mazao yanayoingizwa nchini ili kuzuia uingizwajiwa visumbufu vamizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utafitiwa ndani, kikanda na kimataifa ili kupata mbegu kinzani naviuatilifu katika mazao mbalimbali ikiwemo migomba(Resistant and Tolerant Cultivars). Utafiti wa ugonjwa mnyaukobakteria katika zao la migomba unaendelea katika taasisiza utafiti wa kilimo za Maruku, Uyole, Tengeru pamoja na nchiya Uganda. Aidha, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI)kwa kushirikiana na Shirika la Belgium Technical Cooperation(BTC) zimetafiti kuzalisha na kusambaza miche bora yamigomba 6,000,000 katika wilaya za Mkoa wa Kagera naWilaya za Kasulu na Kankonko Mkoani Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakulima na maafisa uganiwanaendelea kupatiwa mafunzo ya mbinu za udhibiti wavusumbufu vya mimea kwenye mazao hayo ili kuongezauzalishaji na tija. Serikali inawahimiza wakulima kutumiambegu zenye ukinzani dhidi ya magonjwa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Sakaya.

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kumuuliza Mheshimiwa Naibu Wazirimaswali mawili ya nyongeza. Pamoja na kuwepo kwawataalam watafiti wenye uwezo na weledi, taasisi nyingi zautafiti zinakabiliwa na changamoto kubwa za miundombinumibovu lakini pia ukosefu wa rasilimali fedha pamoja namadawa kwa ajili ya kufanya utafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali haioni kwambakushindwa kutenga asilimia moja ya bajeti kwenda kwenyeutafiti inasababisha Serikali kushindwa kuhudumia taasisi hizi

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

na hivyo kusababisha magonjwa kuendelea kutesa mimeana wananchi kuendelea kuathirika kwa kulima?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa Serikaliina mkakati wa kuweza kusambaza mbegu bora na michebora ambazo zinahimili magonjwa wakati huo huozinapandwa maeneo ambapo pambeni yake kuna mazaoyaliyoathirika, kuna mimea iliyoathirika. Kwanini Serikali isijena mkakati sasa na program maalum ya kuondoa mimeailiyoathirika yote na kuwezesha wakulima kupata mbegu nzurina miche bora ili kuhakikisha kwamba miche mipyainayopandwa haiathiriki na hivyo kusaidia wakulima kuinuauchumi wa familia na uchumi wa Taifa? Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. HUSSEIN M. BASHE):Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Sakaya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli ni maamuzi yaKikanda na Kimataifa kwamba tutenge asilimia moja ya patoletu kwa ajili ya research na development lakini vilevile niukweli usiopingika kwamba bado mapato ya nchi navipaumbele na matatizo yanayotukabili kama nchi ni mengi.Kwa hiyo, uwekezaji katika research pamoja na kuwa nimuhimu lakini hatujafikia lengo ambalo tumejiwekea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tulichoamua kamaWizara ya Kilimo ni kwamba all resource zinazokuja kutokakwa development partners na tarehe 19, Wizara ya Kilimotutakuwa na kikao na development partners wanaowekezakatika sekta ya kilimo, fedha zote tutaelekeza katika researchna seed multiplication program ili uwekezaji katika vyuo nataasisi za utafiti uweze kupata resource inayotosheleza.Tuondoe uwekezaji unaofanywa katika capacity buildingambao unatolewa na taasisi za Kimataifa zinazowekezakatika sekta ya kilimo. Kwa hiyo, focus yetu katika kipindi chamiaka mitatu kuanzia mwaka huu ni uwekezaji mkubwa wafedha zote za donors na development partners zinazokuja

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

katika sekta ya kilimo pamoja na uwekezaji wetu wa ndanikuwekezwa katika maeneo ya research na uzalishaji wambegu bora ambazo zitakabiliana na matatizoyanayotukabili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kunachangamoto pale ambapo ardhi imekumbwa na tatizohalafu tunapeleka mbegu mpya. Kama Wizara tumeamuakufanya mapping na tumeanza programu katika Mkoa waDodoma, Wilaya ya Kondoa ambao wameathiriwa nasumukuvu. Maeneo yote haya sasa hivi tunaanza utaratibuwa kwenda kwa wananchi katika kata zilizoathirika kuondoambegu walizohifadhi kwa ajili ya msimu ujao na kuanzautaratibu wa kuwapatia mbegu mpya na ku-treat ile ardhi ilitatizo hilo lisiweze kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, utaratibu wakufanya mapping na kuelewa wapi kumeathirika na niniunaendelea ndani ya Wizara. Tunaamini kwa mpango mpyawa miaka mitatu wa Wizara ya Kilimo wa kuwekeza katikaresearch na development katika taasisi hizi, tutaondokakatika matatizo haya yanayotukabili sasa hivi kama nchi.

MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea na swali laMheshimiwa Martin Mtonda Msuha, Mbunge wa MbingaVijijini.

Na. 92

Hitaji la Mazao ya Biashara-Mbinga

MHE. MARTIN M. MSUHA aliuliza:-

Tangu uhuru Wilaya ya Mbinga imekuwa ikitegemeazao moja la biashara ambalo ni kahawa:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka zao linginela biashara Wilayani humo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA)alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waKilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Martin MtondaMsuha, Mbunge wa Mbinga Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya utafiti waafya na tabaka la udongo katika kanda saba za kilimo zenyekuwezesha uzalishaji wa mazao mbalimbali kulingana naikolojia ya kanda husika. Kanda hizo za kiikolojia ni pamojana Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inayohusisha Wilaya yaMbinga na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na utafiti huo,Serikali imeandaa mwongozo wa uzalishaji wa mazao kwakuzingatia ikolojia ambapo Mkoa wa Ruvuma una fursakubwa ya kuzalisha mazao mengine ya biashara tofauti nakahawa ikiwemo mazao ya korosho, muhogo, alizeti, ufutana matunda yanayostawi katika ukanda wa baridi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakulima katikaHalmashauri ya Mbinga wamehamasishwa na wameanzauzalishaji wa kibiashara wa mazao ya korosho, alizeti, ufuta,soya, parachichi, miwa, tumbaku pamoja na mazao mapyakama macadamia. Aidha, Serikali inaendelea kusimamiauendelezaji wa mazao kwa kuhamasisha matumizi yateknolojia bora katika mnyororo wa thamani, kuongeza ushirikiwa sekta binafsi katika kilimo pamoja na kuimarisha ushirikana mifumo ya masoko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika msimu wa mwaka2016/2017, Serikali kupitia Bodi ya Korosho ilitoa mafunzo yauzalishaji wa miche bora ya korosho kwa vikundi sita vyawakulima vya Jembe Halimtupi Mtu group, Chapakazi Group,Twiga Group, Juhudi Group, Kiboko Group na KoroshomaliGroup ambapo kwa pamoja vilizalisha jumla ya miche bora111,336 na kuisambaza kwa wakulima kwa lengo la kuongezauzalishaji wa zao hilo. Aidha, msimu wa mwaka 2018/2019,jumla ya hekta 29,374.6 zilipandwa mazao ya biashara katika

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

Wilaya ya Mbinga ambapo kati ya hizo, hekta 265 zilitumikakuzalisha zao la korosho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika msimu wa 2018/2019,eneo la hekta 806 zilitumika kuzalisha zao la soya, hekta 317zao la alizeti, hekta 240 ufuta, hekta 32 miwa na hekta 89.5 niparachichi. Uzalishaji wa zao la soya umeongezeka kutokatani 42.6 msimu wa mwaka 2017/2018 hadi kufikia tani 403msimu wa mwaka 2018/2019. Aidha, kwa kuwa Halmashauriya Wilaya ya Mbinga inayo ikolojia inayoruhusu uzalishaji wamazao mengi ya biashara, Serikali itaendelea kuimarishahuduma za ugani ili mazao hayo yazalishwe kwa wingi natija.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Msuha.

MHE. MARTIN M. MSUHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Niipongeze Serikali kwa majibu mazuri katikaswali hilo. Pia kwa dhati kabisa nichukue fursa hii kuishukuruSerikali kwa kupeleka Mnada wa Kahawa Wilayani Mbingakuanzia msimu huu wa mwaka 2019. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa na maswalimadogo mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, ni kweliSerikali imepeleka zao la korosho katika Kata za Rwanda naLitumbandyosi. Changamoto ya wakulima hao ni upatikanajiwa miche bora na kwa bei nafuu. Je, Serikali iko tayarikuendelea kutoa miche ya mikorosho bora kwa bei nafuuau bure kwa wananchi wa Kata ya Rwanda naLitumbandyosi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika jibu lamsingi, Serikali imekiri kuwa ilitoa mafunzo ya uzalishaji wamiche bora ya mikorosho katika vikundi sita vya JembeHalimtupi Mtu, Chapakazi, Twiga, Juhudi, Kiboko na Koroshoni Mali lakini vikundi hivi bado vinaidai Bodi ya Korosho. Je, nilini madeni ya vikundi hivyo yatalipwa?

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwakifupi sana.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Napenda kujibu maswalimawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Martin Msuha, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanzaanataka kujua kwamba kama Serikali tuna…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, usirudie swalilake mjibu tu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tupo tayari kupelekamiche ya mikorosho kwa bei nafuu kwa wakulima wa Wilayaya Mbinga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pil i, kamatunavyofahamu deni likivuka mwaka madeni yote haya yaSerikali yanahamia Hazina. Sasa hivi Serikali tuko kwenyehatua za mwisho za kumalizia uhakiki na vikundi vyoteambavyo uhakiki umemalizika vimeshaanza kulipwa na hivialivyovitaja vitaanza kulipwa baada ya uhakiki kukamilika.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Genzabuke.

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa Serikali imeamua zao lamchikichi lilimwe Kigoma na liweze kuwa zao la biashara naWaziri Mkuu kwa kuweka msisitizo ameenda Kigoma maratatu kufuatilia zao hili la mchikichi; na kwa kuwa wananchiwameamua kuitikia mwito huo wa kulima zao hilo…

MWENYEKITI: Swali.

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: MheshimiwaMwenyekiti, je, Serikali iko tayari sasa kuhakikisha wananchiwanapata mbegu na kuanza kulima zao hilo?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. OMARY T. MGUMBA):Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongezala Mheshimiwa Genzabuke, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tuko tayari kwa ajiliya uzalishaji wa miche ya michikichi na kuigawa kwawakulima. Sasa hivi tumeshatenga zaidi ya shilingi bilioni 5kwa ajili ya kuanza uzalishaji mwaka huu na mwaka huumwezi Septemba, miche zaidi ya milioni moja itakwendasokoni. Tumeshaingia mkataba na sekta binafsi kuzalishamiche milioni tano kwa msimu huu unaokuja na ndani yamiaka mitatu tunategemea kuzalisha miche zaidi ya milioni20 na kuigawa Tanzania nzima.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Nishati, Mheshimiwa Zacharia Paulo Issaay,Mbunge wa Mbulu Mjini sasa uliza swali lako.

Na. 93

Mradi wa REA II - Jimbo la Mbulu Mjini

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY Aliuliza:-

Katika mradi wa REA I na II vijiji vingi vya Jimbo laMbulu Mjini havikufikiwa na umeme na katika vijiji vilivyofikiwani kaya kati ya 20 mpaka 30 pekee ndizo zilizopata umeme:-

(a) Je, ni lini REA III itapeleka umeme katika Vijiji 26vya Jimbo la Mbulu Mjini?

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

(b) Awamu ya I na II ziliruka shule nyingi, vituo vyaafya na Makanisa. Je, ni lini sasa taasisi hizo zitapelekewaumeme?

(c) Je, ni lini Serikali itarudia usambazaji wa umemekatika vijiji vyote vilivyosambaziwa sehemu ndogo sana katikaJimbo la Mbulu Mjini?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI Alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNishati, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zacharia PauloIssaay, Mbunge wa Mbulu Mjini, lenye sehemu (a), (b) na (c),kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utekelezaji waMradi wa REA III, Mzunguko wa Kwanza katika Jimbo la MbuluMjini, jumla ya Vijiji vitatu vya Gwaami, Tsaayo na Baneevitapatiwa umeme na Mkandarasi Kampuni ya AngeliqueInternational Limited.

Aidha, vijiji vitatu vya Murray, Silaroda na Gunyodavinaendelea kupelekewa umeme na Shirika la Umeme Nchini(TANESCO) kwa Mpango wa Umeme Vijijini. Vijiji 20 vilivyobakivya Jimbo la Mbulu Mjini vya Hereabi, Maheri, Kuta, Qwam,Nahasey, Hayasali, Hasama, Hayloto, Kwermusi, Amowa,Gwandumehhi, Aicho, Gedamar, Qalieda, Laghanda mur,Gidamba, Qatesh, Landa, Tsawa na Jaranja vitapatiwaumeme kupitia mradi wa REA III, Mzunguko wa Pili unatarajiwakuanza Januari, 2020.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, shule, vituo vya afya nataasisi nyingine ambazo hazijaunganishwa umeme katika vijijiau maeneo ya karibu yaliyounganishwa umeme na miradiya awali ikiwemo REA I na II yatapelekewa umeme katikakipindi hiki. Tumetoa wito kwa Halmashauri au taasisi husikazilipie gharama za kuunganisha umeme ili taasisi hizoziunganishiwe umeme.

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

(c) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maeneo ya MbuluMjini yaliyosambaziwa umeme, tunawaomba wananchi wamaeneo ya karibu na maeneo yenye umeme kuendeleakulipia Sh.27,000 ili maeneo hayo nayo yatumie umeme huouliopo katika maeneo hayo. Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Issaay.

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza nimpongezeMheshimiwa Rais wetu na Serikali nzima, Waziri, Naibu Wazirina Watendaji wote kwa kazi kubwa wanayofanya katika nchiyetu hususani Jimbo la Mbulu Mjini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali yangu madogo yanyongeza ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwamahitaji ya umeme katika Jimbo la Mbulu Mji ni makubwa;na kwa kuwa Jimbo la Mbulu Mji sehemu nyingi zilikosaumeme wakati wa REA I na II. Je, sasa Serikali inachukuahatua gani kwa wale wananchi ambao hadi sasawameendelea kuachwa na umeme umeshapita kwenyemaeneo yao na maombi yao hayajibiwi na Ofisi yangu inaorodha kubwa sana?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwamahitaji ni makubwa sana ya chombo kinachoitwa UMETA(Umeme Tayari) na kwa kuwa majengo mengi katika Jimbola Mbulu Mjini yako mbalimbali kwa maana ya nyumba zawananchi. Je, Serikali ina mpango gani wa kuleta chombohiki cha UMETA kwa kiasi kikubwa ili kuwapatia wananchiumeme ambao wana uhitaji mkubwa sana?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu kwakifupi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya MheshimiwaZacharia, Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini. Nampongeza

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

kwa kazi nzuri anayoifanya katika Jimbo lake hususani katikakufuatilia sekta ya nishati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, ameulizaSerikali ina mpango gani kwa kuwa mahitaji ya umeme nimakubwa na kwa maeneo mbalimbali ambayohayajafikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimtaarifuMheshimiwa Mbunge kwamba kupitia Serikali yetu kunaMradi wa Ujazilizi Awamu ya Pili B ambapo Mkoa wa Manyarani miongoni mwa mikoa 16 ambayo itahudumiwa. Kwa sasaMshauri Elekezi Multiconsult na Norplan wanaendeleakuhakiki vitongoji katika maeneo mbalimbali. Mradi huuutafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa Euromilioni 100 na unatarajiwa kuanza mapema mwakani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sambamba namiradi ya REA III ambayo itaendelea kupitia TANESCO,nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge kwa jitihada hizi na huuMradi wa Ujazilizi kwenye maeneo ambayo umepita vitongojivimeachwa, Jimbo lake la Mbulu Mjini nalo litazingatiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ameuliziamasuala ya kifaa kinachoitwa UMETA. Kwanza Serikali kupitiautekelezaji wa Mradi wa REA III, Mzunguko wa Kwanzavimetoa UMETA 250 kwa kila mkandarasi ambapo vinagaiwabure kwa makundi maalum. Sambamba na hilo, kwa kuwatumeona uhitaji ni mkubwa Shirika la TANESCO na REAwanaendelea na mchakato wa kuhakikisha UMETAinapatikana kwa bei nafuu ambayo ni Sh.36,000 ambapo kilamwananchi ana uwezo wa kumudu.

Kwa hiyo, niendelee kutoa maelekezo kwa niaba yaWaziri wa Nishati, TANESCO na REA kuendelea kusambazaUMETA hasa kwenye taasisi za umma ambazo hazina mahitajimakubwa na wananchi wa kawaida. Ahsante.

MWENYEKITI: Tunaendelea na swali la MheshimiwaAzza Hillal Hamad.

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Na. 94

Hitaji la Umeme katika baadhi ya Vijiji Shinyanga

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA (K.n.y. MHE. AZZA H.HAMAD) aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itawapa huduma ya umemewananchi wa Vijiji vya Buyubi, Itwangi, Imenya, Nyambui naMwankanga ambao muda mrefu wamekuwa watazamajiwa nguzo za umeme unaokwenda maeneo mengine?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waNishati, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Azza HillalHamad, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wakala waNishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa kufikisha umemekatika vijiji vyote nchini vikiwemo vijiji 126 vya Wilaya yaShinyanga Vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji 22 kati ya vijiji 126 katikaWilaya ya Shinyanga Vijijini vina umeme. Vijiji 50 vitapatiwaumeme kupitia Mradi wa REA III, Mzunguko wa Kwanzaunaotekelezwa na Mkandarasi Angelique InternationalLimited ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Agosti,2019 jumla ya vijiji 19 vimeshawashiwa umeme na ujenzi wamiundombinu unaendelea katika vijiji vilivyobaki na watejazaidi ya 211 wameunganishiwa umeme. Kazi ya kupelekaumeme katika vijiji hivi itakamilika ifikapo mwezi Juni, 2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya kupeleka umemekatika vijiji 50 vya Wilaya ya Shinyanga Vijijini inahusisha ujenziwa njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wakilometa 170.9; ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wakilovoti 0.4 yenye urefu wa kilometa 156; ufungaji wa

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

transfoma 78 za KVA 50 na KVA 100 na kuunganisha umemewateja wa awali 2,241. Gharama za mradi ni shilingi bilioni10.7 na mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji 54 vilivyobaki vikiwemovijiji vya Buyubi, Itwangi, Imenya, Nyambui na Mwankangavitapatiwa umeme kupitia mradi wa REA III, Mzunguko waPili unaotarajia kuanza mwezi Januari, 2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Asha Jecha.

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninamaswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwaSerikali ilielekeza TANESCO kwamba vijiji vyote ambavyoumeme umepita juu vipatiwe umeme. Miongoni mwa vijiji 74ambapo kuna Vijiji vya Buyungi, Imenya, Itwangi na Nyambui,je, Serikali itavipatia umeme lini katika huu msimu wa 2019/2020? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa NaibuWaziri aliahidi wananchi wa Nyambui atawapatia umeme.Je, ahadi hiyo itatekelezwa lini? Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi.

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzanimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri yaswali la msingi lakini nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwakuuliza swali kwa wananchi wa Shinyanga kwa niaba yaMheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitoe taarifa Kijiji chaItwangi kimewashwa umeme tangu juzi ingawaje swali wakatil inajibiwa kil ikuwa hakijawashwa umeme, kwa hiyo,kimeshawashwa umeme. Kwa hiyo, wananchi wa Itwangi

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

sasa wanapata umeme kupitia Shirika la Umeme Nchini(TANESCO).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kijiji cha Buyubi pamoja naMinyami kitawashwa tarehe 17 mwezi huu wa Septemba.Kwa hiyo, wananchi wa maeneo hayo wategemeekuunganishiwa umeme katika maeneo hayo kwa wikiinayokuja. Ahsante.

MWENYEKITI: Tunaendelea na Wizara ya Fedha naswali la Mheshimiwa Boniphace Getere.

Na. 95

Kudhibiti Kasi ya Ongezeko la Idadi ya Watu Nchini

MHE. BONIPHACE M. GETERE Aliuliza:-

Idadi ya watu nchini inaongezeka kwa kasi sana nawatu wanahitaji maendeleo; aidha ukuaji huu una matokeohasi na chanya:-

Je, Serikali ina mikakati gani ya kutumia au kudhibitikasi ya idadi ya watu?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO Alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waFedha na Mipango, napenda kujibu swali la MheshimiwaBoniphace Mwita Getere, Mbunge wa Bunda Vijijini, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, utafiti wa idadi ya watuduniani unaonyesha kwamba idadi kubwa ya watu ni fursakwa nchi iwapo baadhi ya mambo matano yatafanyika:-

(i) Kuboresha maisha ya watoto na kuboresha elimuna uwezeshaji kwa wanawake;

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

(ii) Kuimarisha uwekezaji katika afya ili kuwa nanguvukazi bora na yenye tija;

(iii) Kuimarisha uwekezaji katika elimu ya juu ili kuwana nguvukazi yenye elimu, ujuzi na ubinifu;

(iv) Mageuzi ya kiuchumi yanayolenga kuharakishaukuaji wa uchumi na upatikanaji wa kazi kwa ajili ya nguvukaziiliyopo; na

(v) Mageuzi ya Sera ili kuvutia uwekezaji wa kigeni nakuhakikisha uwajibikaji hasa katika rasilimali za umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhima ya Mpango wetu waPili wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2017 – 2020/2021ni kujenga uchumi wa viwanda ili kufungamanisha ukuaji wauchumi na maendeleo ya watu. Mpango huu wa Pili umejikitazaidi katika uwekezaji wa kimkakati katika Sekta ya Viwandakuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, kusambazaumeme mijini na vijijini, kusambaza pembejeo za kilimo kwawakati, kutatua changamoto ya muda mrefu ya upatikanajiwa umeme wa uhakika kwa kujenga bwawa kubwa la kufuaumeme katika Mto Rufiji na kuimarisha huduma za jamii kwakujenga na kukarabati miundombinu ya maji, hospitali naVituo vya Afya vya Umma, shule pamoja na kutekeleza kwaufanisi Sera ya Elimu Bila Malipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi inayoendeleakutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inalengakufungamanisha fursa za kiuchumi na ongezeko la idadi yawatu; na jit ihada hizi zinalandana na mamboyaliyopendekezwa kwenye ripoti ya utafiti ya idadi ya watuduniani na athari zake. Hata hivyo, matokeo chanyayataonekana kama kila Mtanzania atashiriki kikamilifu katikauzalishaji mali na huduma za jamii kuanzia ngazi ya kaya hadiTaifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo jambo baya kudhibitiongezeko la idadi ya watu kama familia au Taifa limefikiakiwango cha mwisho cha kutumia rasilimali (optimal

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

utilization) ya rasilimali zake za asili pamoja na mikakatimingine mbadala. Hata hivyo, Taifa letu bado lina rasilimaliasili za kutosha kama vile ardhi ya kulima, bahari, maziwa,mito na mabonde, madini, misitu, jiografia ya usafiri nausafirishaji pamoja na fursa za utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jukumu letu kama Taifakuanzia ngazi ya kaya kuakisi jitihada zinazofanywa na Serikaliyetu na hatimaye kutumia fursa hizi kwa ufanisi kwa lengo lakuongeza kasi ya uzalishaji mali pamoja na kuongeza kasi yakupunguza umasikini badala ya kuogopa ongezeko la idadiya watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuliarifu Bungelako Tukufu kwamba kwa sasa Serikali imejielekeza zaidi katikakuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na kufanya biasharana hivyo kutumia ongezeko la idadi ya watu kama fursa yanguvukazi ya kuzalisha mali pamoja na soko la bidhaa nahuduma.

MWENYEKTI: Mheshimiwa Getere.

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili yanyongeza. Namshukuru sana Naibu Waziri kwa majibu yakemazuri. Amejieleza vizuri, tumeyaona kwenye karatasi hapona yapo vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, idadi ya watu katika nchiyetu inaongezeka na toka tumepata uhuru mwaka 1961 naMuungano 1964 tumeendelea kupambana na maaduiwatatu ambao ni ujinga, maradhi na umasikini. Angalau hayamawili ya maradhi na ujinga tunaelekea kuyamudu ndiyomaana idadi ya watu inaongezeka.

MWENYEKITI: Swali, swali!

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti,swali; Serikali ina mpango gani sasa wa kupambana na adui

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

namba moja ambaye ni umasikini unaoongezeka katikamaeneo mengi hasa maeneo ya vijijini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kumekuwa namakundi makubwa ya vijana wanaohitimu elimu hasa Elimuya Vyuo Vikuu. Sasa ndhi yetu ipo kwenye mkakati wakujenga viwanda: Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwekezakatika viwanda vya Labor Intensive badala ya CapitalIntensive ili kukidhi makundi makubwa ya vijana yanayohitimushule na kwa sababu fursa tunazo? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Wazirui, majibu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza naomba kuliarifu Bunge lako Tukufukwamba umasikini ndani ya nchi yetu hauongezeki,unapungua kila mwaka. Hii naisema, siyo maneno yangu, nimaneno ya utafiti ambao umefanyika. Utafiti wa mapato namatumizi ya kaya binafsi uliofanyika mwaka 2018 naMheshimiwa Waziri Mkuu akauzindua utafiti huu, unaoneshakwamba umasikini wa kipato umepungua kutoka asilimia 28.2toka mwaka 2012 na sasa umefika asilimia 26.8 mwaka 2018.Hivyo siyo sahihi kuendelea kuimba wimbo wa Taifa letukwamba watu wanazidi kuwa masikini. Siyo sahihi hatakidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utafiti huu pia unaoneshaumasikini wa chakula kwa Watanzania katika kila kaya,mwaka 2012 ulikuwa asilimia 9.7; mwaka 2018 umasikini wachakula kwa kaya ya kila Mtanzania ni asilimia 4.4. Kwa hiyo,tunaomba Watanzania wafahamu kwamba jitihada zaSerikali yao na wao Watanzanzia wamejitolea kuelewajitihada hizi za Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli naSerikali yake wanafanya kazi kwa jitihada zote. Umasikini wakipato na umasikini wa chakula umepungua kutokana natafiti zilizofanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pilikwamba tuwekeze kwenye viwanda ambavyo vinatumiarasilimali watu zaidi kuliko kutumia capital intensive. Naomba

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba katika viwanda ambavyovimeanzishwa na vinaendelea kujengwa kama alivyoelezaMheshimiwa Waziri wa uwekezaji asubuhi, ni viwandavinavyotumia zaidi rasilimali watu. Viwanda hivi ni vileambavyo vipo katika maeneo ya nguo. Tunafahamuhatujafanya vizuri zaidi, lakini jitihada zinaendelea kufanyika.Viwanda vya kutengeneza tiles havitumii mashine, vinatumiarasilimali watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vingine ni vyakuchakata mazao yetu, havitumii capital, vinatumia zaidirasilimali watu. Nawaomba Watanzania wanaomaliza VyuoVikuu waweze kwenda kufanya kazi kwa tija kwenye viwandahivyo.

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa, tunaendelea naWizara ya Katiba na Sheria, Mheshimiwa Gimbi DottoMasaba.

Na. 96

Hitaji la Mahakama ya Wilaya – Itilima

MHE. ANATHROPIA L. THEONEST (K.n.y. MHE. GIMBI D.MASABA) Aliuliza:

Wilaya mpya ya Itilima haina Mahakama ya Wilaya,jambo linalosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchikwenda Wilaya jirani ya Bariadi kupata huduma hiyo:-

Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya Itilima?

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA Alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali laMheshimiwa Gimbi Dotto Masamba, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Wilaya ya Itilima kwasasa haina Mahakama ya Wilaya na wananchi wanalazimika

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

kusafiri umbali mrefu takriban kilometa 37 kufuata hudumakatika Wilaya ya Bariadi. Aidha, changamoto hii ipo kwenyeWilaya 27 nchini, ambazo zinapata huduma katika wilaya zajirani. Hii inatokana na ukweli kwamba Mahakama yaTanzania bado inakabiliwa na uhaba wa majengo katikamaeneo mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimekuwanikieleza katika Bunge lako, Mahakama imejiwekea mkakatiwa kutatua changamoto hii hatua kwa hatua kupitiampango wake wa miaka mitano na kujenga na kukarabatimajengo ya Mahakama kwa ngazi zote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakama ya Wilaya yaItilima ipo kwenye mpango wa kujengwa kwa mwaka 2019/2020 pamoja na Mahakama nyingine za Wilaya za Busega,Kyerwa, Misenyi, Gairo, Mbogwe, Songwe, Rufiji, Kibiti,Nyang’hwale, Mvomero, Uyui, Kaliua, Uvinza, Buhigwe,Kakonko, Chamwino, Chemba, Ikungi, Mkalama, Butiama,Rorya, Ubungo, Malinyi, Tanganyika, Mkinga, Kilosa,Kilombero, Hanang na Nkasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru uongozi waHalmashauri ya Wilaya ya Itilima kwa kutupatia kiwanja chakujenga Mahakama ya Wilaya yenye ukubwa wa mita zamraba 5,028. Aidha, nitoe pia shukrani zangu za dhati kwaHalmashauri za Wilaya zote nilizozitaja kwa kutupatia viwanjakwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Mahakama. Ahsante.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Masaba, kwaniaba yake Mheshimiwa Anatropia.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: MheshimiwaMwenyekiti, licha ya Serikali kuahidi kwamba inaendakujenga jengo hilo la Mahakama ya Wilaya katika kipindi chamwaka wa fedha 2019/2020, bado Mahakama ya Bariadiinapitia changamoto ya upungufu wa Mahakimu, hivyokusababisha kesi nyingi kuchelewa: Je, Serikali ina mpangogani kwa wakati huu mfupi kuisaidia Mahakama ya Bariadi iliiweze kukidhi?

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wakati wananchiwa Itilima wanatembea kilometa 37, wenzao wa Wilaya yaKyerwa wanatembea zaidi ya kilometa 100. Wananchi waMurongo, Kaisho, Bugomora, Bugara, wanatembea umbalimrefu kufuata hiyo huduma katika Mahakama iliyoko Wilayaya jirani…

MWENYEKITI: Swali! Uliza swali!

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: MheshimiwaMwenyekiti, swali. Ni mkakati gani wa muda mfupi kuwasaidiawananchi wa Kyerwa waweze kupata huduma katika wilayayao kabla ya kufikia mwaka 2019/2020. Nakushukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza kutoka kwaMheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mahakama ya Bariadiinafanya kazi nzuri sana. Hivi karibuni nilipitia kule na nikaonamsongamano wa kesi mbalimbali. Ni moja ya majukumumakubwa ya Wizara hii, siyo tu kujenga Mahakama katikangazi mbalimbali, lakini kutoa mafunzo kwa Mahakimu kadriujenzi unavyoendelea. Hii inaenda sambamba na kuwasaidiawananchi kwa kuwapa haki ya kusimamia mashauri yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili. Mahakama ya Wilayaya Kyerwa inahitaji kupata Mahakama yake mara moja.Katika mpango wa Mahakama ya Tanzania kamanilivyoeleza siyo tu tunataka kuleta Mahakama karibu nawananchi, lakini kuhakikisha kwamba tunapunguza keroambazo wananchi wanapata ili kupata haki yao na kwawakati. Kutokana na mkakati huo, tutaendelea kusomeshaMahakimu katika ngazi mbalimbali na tutaendelea kupanuaujenzi wa Mahakama katika ngazi mbalimbali hasa katikawilaya hiyo ambayo Mheshimiwa umeizungumzia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

MWENYEKITI: Ahsante kwa majibu mazuri.Waheshimiwa tunaendelea na Wizara ya Maji, MheshimiwaEng. Christopher Kajoro Chiza, Mbunge wa Buyungu aulizeswali lake.

Na. 97

Kutokukamilika kwa Miradi ya Maji – Kakonko

MHE. ENG. CHRISTOPHER K. CHIZA Aliuliza:-

Serikali ilitoa zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa ajili yaujenzi wa miradi ya maji ya Nyabibuye, Gwanumpu,Muhange, Kiduduye, Nyangwijima na Kakonko Mjini. Miradihiyo sasa inahitaji ukarabati mkubwa hata kabla ya kuanzauzalishaji na mingine utekelezaji upo chini ya asilimia 10:-

(a) Je, ni kasoro gani zimesababisha miradi yote sitakutotekelezwa kwa mwaka uliopangwa?

(b) Serikali imechukua hatua gani kuhakikisha miradihiyo inakamilika?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Majinaomba kujibu swali la Mheshimiwa Christopher ChizaMbunge wa Buyungu, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamojakama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa miradi yaMuhange, Kiduduye na Nyangwijima ulikamilika lakiniulishindwa kuwanufaisha wananchi kutokana na kasorombalimbali zilizojitokeza ikiwemo eneo la kisima cha pampucha mradi wa Muhange kujaa tope; na pia kwa mradi wamaji Nyagwijima na Kiduduye eneo la chanzo kushindwakuzuia maji kuyapeleka kwenye kisima chenye pampu hiiimetokana na matatizo ya usanifu yaliyojitokeza.

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuhakikisha miradi hiiinatoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa, Serikaliimechukua hatua mbalimbali kwa miradi ya Muhange,Kiduduye na Nyagwijima, Wizara imefanya mapitio ya usanifuambapo kiasi cha shilingi milioni 300 kimekadiriwa ilikurekebisha kasoro zilizojitokeza. Tayari Serikali imetoa kiasicha shilingi milioni 120 kwa ajili ya maboresho ya mradi wamaji Muhange ambapo utekelezaji unaendelea na umefikiaasilimia 45. Serikali itaendelea kutenga na kutoa fedha kwaajili ya kuboresha pia miradi ya Nyagwijima na Kiduduye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya maji Gwanumpu,Nyabibuye na Kakonko Mjini utekelezaji wake ulichelewakutokana na wakandarasi kujenga miradi hiyo kwa kasindogo kutokana na uwezo mdogo wa kifedha. Hali hiiilisababisha baadhi kusitishwa mikataba yao. Mkandarasi waMradi wa Gwanumpu yupo eneo la mradi na anaendeleana kazi ambapo amefikia asilimia 40. Kwa Mradi wa Maji waNyabibuye na Kakonko Mjini taratibu za kusaini mikataba nawakandarasi wapya zinaendelea ili waweze kukamilishautekelezaji wa miradi hiyo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Engineer Chiza.

MHE. ENG. CHRISTOPHER K. CHIZA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kwanza niishukuru sana Serikali kwakuanza kutekeleza ahadi yak. Baada ya Waziri kutembeleana kusikia kilio cha wananchi imetenga shilingi milioni 300 natayari wamepeleka shil ingi milioni 20 na wataalamwameanza kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninayo maswali mawilimadogo ya nyongeza. Katika lot ya miradi ya Kiduduye,Nyagwijima na Muhange, kwa kuwa tayari mradi waMuhange unatekelezwa: Je, ni lini sasa Serikali itapelekawataalam na fedha kwa ajili ya miradi miwili ya Nyagwijimana Kiduduye kuanza kutekelezwa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pil i. WakatiMheshimiwa Waziri wa Maji akihitimisha hotuba yake ya Bajeti

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

ya mwaka huu, alituhamasisha Wabunge wote kupelekaorodha ya visima vinavyofaa kuchimbwa katika Majimboyetu, nami nilikuwa wa kwanza kumkabidhi orodha ya visima15 vilivyofanyiwa utafiti: Je sasa, Mheshimiwa Naibu Wazirianaweza kuniambia au kuwaambia wananchi wa Buyunguni lini sasa ligi itapelekwa katika Jimbo la Buyungu kuanzakuchimba visima hivi 15? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwakazi kubwa ambayo anaifanya kwa muda mfupi tanguamechaguliwa na wananchi wake. Kikubwa amekuwamfuatiliaji, nasi kama Wizara hatutakuwa kikwazo kum-support kuhakikisha tunatatua tatizo la maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya changamotokubwa sana kusuasua kwa miradi ya maji kulikuwakunatokana na wakandarasi wababishaji. Sisi kama Wizaraya Maji, tumejipanga, sasa hivi tumeanzisha Wakala wa Majikwa maana ya RUWASA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimhakikishie, kwamiradi ile ambayo imekuwa ikisuasua, tutaitekeleza kwakutumia wataalam wetu wa ndani ili kuweza kukamilishamiradi ile kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimhakikishieMheshimiwa Mbunge, miradi hiyo tutaifanya kwa wataalamwetu na tutawa-support kuwapatia fedha ili miradi iwezekukamilika na wananchi wako, waweze kupata huduma yamaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la ahadi yavisima, ahadi ni deni. Nataka nimhakikishie MheshimiwaMbunge, tukutane tufanye mazungumzo na wenzetu waDDC ili tuwatume waende kuchimba visima kwa wananchiwake waweze kupata huduma hii muhimu ya maji safi nasalama.

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge,tunaendelea na Wizara ya Madini, Mheshimiwa JanetMbene.

Na. 98

Kufanya Mapitio ya Geological Survey Ileje

MHE. JANET Z. MBENE Aliuliza:-

Geological Surveys za Wilaya au Mikoa mingi ni zamiaka mingi tangu enzi za ukoloni. Surveys hizi nyingi zimejikitakwenye aina moja ya migodi kwa mfano Mkoa wa SongweSurvey imezungumzia machimbo ya mawe peke yake:-

(a) Je, ni lini Serikali itafanya mapitio ili kupataGeological Surveys zenye kujumuisha aina nyingine za madiniambayo yanapatikana katika Mkoa wa Songwe hususanIleje?

(b) Je, Serikali ipo tayari kwenda kuwaelimishawananchi wa Ileje juu ya madini yaliyopo na kuhamasishauwekezaji kwa wachimbaji wadogo?

NAIBU WAZIRI WA MADINI Alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri waMadini, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Janet ZebedayoMbene, Mbunge wa Ileje, lenye vipengele (a) na (b) kamaifuatavyo:-

(a) Serikali kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa MadiniTanzania (GST) imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali za jiolojiakwa ajili ya kuainisha madini mbalimbali yaliyopo nchini tangukipindi cha mkoloni hadi sasa. Aidha, GST kwa ushirikiano naufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa Korea imeanzakufanya utafiti wa kina wa kijiolojia ili kuongeza na kuboreshataarifa za uwepo wa madini mengine katika Mkoa waSongwe na mikoa mingine nchini.

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti zilizofanyika Mkoa waSongwe zinaonesha kuwa Wilaya ya Ileje ina madiniyafuatayo; moja ikiwa ni madini ya metali aina ya dhahabuyanayopatikana katika maeneo ya Mwalisi na Ikinga, Madiniya Viwandani aina ya Ulanga, yanayopatikana katikamaeneo ya vilima vya Bundali na Ileje, madini ya nishati ainaya makaa ya mawe (Coal) yanapatikana katika maeneoya Songwe, Kiwira na madini ya apatite na niobiumyanayopatikana katika miamba ya carbonatite iliyopomaeneo ya kilima cha Nachendazwaya, ikiwa ni pamoja namadini mengine kama marble na madini mengine ya ujenzi.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Taasisi yaJiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania itaendelea kufanya tafitimbalimbali za madini katika Wilaya ya Ileje na maeneomengine ya nchi kwa kadri ya upatikanaji wa rasilimali yafedha na kutoa elimu kwa wananchi juu ya upatikanaji wamadini katika maeneo mbalimbali ya nchi ikiwa ni pamojana kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya madini kwawachimbaji wadogo.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbene.

MHE. JANET Z. MBENE: Mheshimiwa Mwenyekiti,namshukuru Naibu Waziri kwa majibu ingawa ningefurahi zaidiyangekuwa siyo ya kijumla kiasi hicho kwa sababuningependa japo nisikie tu kuwa kama wapo tayari kujakufanya hata mafunzo tu kwa ajili ya vijana wetu ambaowanajishughulisha na shughuli hizi. Hata hivyo nina maswalimawili ya nyongeza:

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ni kuhusiana na uleMgodi wa Kiwira ule waunderground. Mgodi ule umesimamakwa muda mrefu sana na hivi sasa tunavyozungumza hatunahakika yaani kuna sintofahamu ya kujua ni nani mwekezajina lini ataanza kufanya kazi ili tuweze kuona mafanikio yamgodi ule?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni kuwa mwaka2010 Kamati ya Kudumu ya Bunge ilishauri kuwa mgodi ule

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

uwekwe chini ya STAMICO na TANESCO kwa sababumadhumuni ya mgodi ule ilikuwa ni kuzalisha umeme, lakinimpaka sasa hivi tunaona uko chini ya STAMICO lakini hatuoniule ubia na TANESCO ambao ungesaidia sasa katikakuhakikisha kuwa umeme unapatikana? Ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ni kweli kabisa kwamba ule Mgodi wa Kiwira umesimamakwa muda mrefu sasa na tatizo lilikuwa ni moja tu, baada yaile kampuni ya TAN Power Resources kutoka pale ilitakiwakwamba wahamishe zile share zao ili ziweze kuchukuliwa naSerikali na share hizo tungeweza kuzipeleka STAMICO kwaajili ya kuanzisha au kuendeleza mradi ule.

Sasa wale TAN Power Resources walikuwa na deniambalo walitakiwa walipe (capital gain tax)ambayo ilikuwani deni la bilioni 2.9 hawajalipa lile deni na Serikali kupitia TRAnikwamba wanafatilia kuweza kuwabana wale wahusikawaweze kulipa deni hilo ili tuweze kupata tax clearance nakuhamisha zile share ziweze kwenda Serikalini au STAMICO ilikuweza kuanzisha mradi ule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi TRA wanaendeleakufatilia hawa TAN Power Resources na inasemekanahawapo na watu hawa ambao hawapo sasa hivi kuna hatuainayofuata ya kufatilia kuwajua ma-director wa ile TAN PowerResources na kuweza kuwabana ikiwezekana kwendakuchukua passport zao binafsi ili waweze kulipa lile deni la2.9 bilioni. Baada ya kufanya hivyo STAMICO wakishachukuamradi huo mara moja mradi ule utaanza na uchimbajiutaendelea. Ahsante sana.

MWENYEKITI: Waheshimiwa maswali yetu yamekwishasasa ni kipindi cha wageni. Wageni wa Mheshimiwa Spikaambao wako Jukwaa la Spika ni Balozi wa Pakistan nchiniTanzania Mheshimiwa Amer Mohamed Khan, welcome to theParliament of Tanzania. (Makofi)

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

Wageni waliopo Bungeni asubuhi hii wageni waliopoJukwaa la Spika wageni 11 wa Mheshimiwa Spika kutokaJukwaa la Maendeleo Endelevu Jijini Dar es Salaam ambaoni Ndugu Richard Angelo, Ndugu Getrude Mugizi, Ngd.Stephen Chacha, Ndugu Iman Khatib, Ndugu Prisca Kowa,Ndugu Reynad Maeda, Ndugu Vivian Ngowi, karibuniDodoma. (Makofi)

Wageni 18 wa Mheshimiwa Spika, kutoka Benki yaNBC ambao ni Mameneja wa Kanda, Mameneja wa Mauzona Mameneja Mahusiano wa Benki hiyo wakiongozwa naMkurugenzi wa Wateja Binafsi - NBCNdugu Elibariki Masuke,karibuni Dodoma. (Makofi)

Wageni wengine wa Mheshimiwa Spika ni waandaajiwa Kipindi cha AMINIA 255 (Najivunia Tanzania) cha Kampuniya Clouds Media, Simon Simalenga - Mwenyekiti, JeromeRisasi - Katibu, Dotto Bahema - Mjumbe, Kijakazi Yunus -Mjumbe, na Hassan Ngoma - Mjumbe, karibuni sana nahongereni kwa kazi nzuri mnayoifanya.(Makofi)

Wageni 13 wa Mheshimiwa Naibu Spika, naMheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa Mbunge Naibu Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, Utumishi ambao ni Viongozi wa CCMMbeya, wakiongozwa na Ndugu Afrey Nsomba - Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Ndugu Gervas Ndaki - Katibuwa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini na Ndugu PhilemonMng’ong’o - Katibu Mwenezi wa CCM Mbeya Mjini. (Makofi)

Wageni wa Mheshimiwa Innocent Bashungwa Waziriwa Viwanda na Biashara kutoka Chama cha WasioonaTanzania ambao wamekuja kama wageni wangukushuhudia Azimio la Kuridhia Mkataba wa Marrakeshwakifuatana na Mwenyekiti wao Ndugu Luis Benedict naEmmanuel Saimon. (Makofi)

Wageni saba wa Mheshimiwa Prof. Aderaldus Kilangi,Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao ni watumishi kutokaOfisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar wakiongozwa

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

na Naibu Mwanansheria Mkuu Ndugu Mzee Ali Haji, karibuniDodoma. (Makofi)

Wageni 11 wa Mheshimiwa Dkt. HarrisomMwakyembe Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezoambao ni vingozi kutoka Multi Choice Tanzania, Tasnia yaFilamu Tanzania na The Look Company Ltd.wakiongozwa naMratibu wa Mashindano ya Miss Tanzania na Miss WorldNduguBasila Mwanukuzi, karibuni sana. (Makofi)

Wageni wa Waheshimiwa Wabunge, wageni Wawiliwa Mheshimiwa Dotto Biteko, Waziri wa Madini ambao niwapiga kura wake kutoka Bukombe wakiongozwa naMadiwani Mheshimiwa Masanja Maduhu, karibuni. (Makofi)

Wageni Watatuwa Mheshimiwa Omary MgumbaNaibu Waziri wa Kilimo ambao ni wadau wa Sekta ya Kilimokutoka Mkoa wa Iringa Ndugu Sosthenes Mushi, Ndugu EdgerMsengi na Ndugu Joshua Muna.Wageni wa MheshimiwaMwita Waitara Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMIambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ilalakutoka Kivule jijini Dar es Salaam Ndugu Yansika Getama,karibu. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunao wageni 12 waMheshimiwa Elias Kwandikwa ambao ni Kamati ya SiasaWilaya ya Kahama kutoka Mkoa wa Shinyanga wakiongozwana Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndugu Thomas Muyonga,karibuni Waziri wenu anafanya kazi vizuri sana kwa hiyomsifanye makosa.Wageni Watatuwa Mheshimiwa HusseinBashe Naibu Waziri wa Kilimo kutoka Shirika la Chakula Duniani(WFP) Ofisi ya Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi MkaaziNdugu Michael Banford, karibuni Bungeni. (Makofi)

Mgeni wa Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulileambaye ni mpiga kura wake kutoka Jijini Dar es SalaamNdugu Yona Kilatu Msoma, karibu. Mgeni wa MheshimiwaRashid Shangazi Mbunge ambaye ni ndugu yake kutoka JijiniArusha Ndugu Likoko Piniel, Karibuni Dodoma. (Makofi)

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Wageni 47 wa Mheshimiwa Sonia Magogo ambao niWalimu na wanafunzi (Scout) wa Shule ya Msingi St. Maxmillianil iyopo Tabata Segerea kutoka ji j ini Dar es Salaamwakiongozwa na Mwalimu Constantine Magehema, karibuni.(Makofi)

Wageni Wawiliwa Mheshimiwa Anatropia Theonestambao ni ndugu zake kutoka Jijini Dar es Salaam NduguRenatha Theonest na Ndugu Brito Burere. Wageni 17 waMheshimiwa Hamida Abdallah ambao ni Wajumbe waMkutano Mkuu wa Chipukizi Taifa kutoka Mkoa wa Lindiwakiongozwa na Ndugu Paksens Kisamo. Karibuni. WageniWawiliwa Mheshimiwa Joseph Kakunda ambao ni walimu waShule ya Sekondari ya Oldonyosambo ya Jijini Arusha NduguNyangusi Kissangai na Ndugu Namnyaki Laizer, karibuni.(Makofi)

Wageni Sabawa Mheshimiwa Sikudhani Chikamboambao ni jamaa zake. Salum Mohamed mtoto wake DaliaHalid Mwenyekiti wa Wawalemavu Tunduru, Rehema BurhanTunduru, Amos Mpita ndugu yake, Amir Ngwale ndugu yakeHanifa Mkura ndugu yake,Ndugu Said Athuman ndugu yake.Wageni 2 wa Mheshimiwa Ally Ungando ambao niwapigakura wake kutoka Jimbo la Kibiti Mkoa wa PwaniNdugu Daniel Motera na Ndugu Ally Ismail, karibuni. (Makofi)

Wageni 4 wa Mheshimiwa Stanslaus Mabula ambaoni viongozi wa Machinga kutoka Mkoa wa Mwanzawakiongozwa na Ndugu Jamal Said. Pia tunao wageniwaliopo Bungeni kwa ajili ya mafunzo wanafunzi 40 kutokaChuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dodoma, karibuni. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge tunaendelea.

MWONGOZO WA SPIKA

MWENYEKITI: Mwongozo Mheshimiwa Nkamia.

MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili niombe mwongozo kwa

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

mujibu wa Kanuni ya 68 (7), na kwa kuwa muda wenyewetunakimbizana nao sina sababu ya kusoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo asubuhi wakati wakipindi cha maswali na majibu Mheshimiwa Naibu Waziri rafikiyangu Hussein Bashe akijibu swali kuhusu masuala yaSumukuvu alisema Sumukuvu iliwapata wagonjwa amailiwapata watu katika Wilaya ya Kondoa na wanahitajimsaada ikiwa ni pamoja na mbegu. Sasa naombamwongozo wako ugonjwa huu wa Sumukuvu ulitokea Wilayaya Chemba katika vijiji vya Kinkima na Mlongia ambako zaidiya wagonjwa 35 waliathirika isipokuwa walikwenda kulazwakwenye Hospitali ya Wilaya ya Kondoa kwa sababu Chembahospitali yetu bado haijaanza kazi. Sasa nilikuwa naombamwongozo wako wananchi wale vyakula vyaovimemwagwa wakitegemea kupata vyakula kutokaSerikalini, hiyo ni namba moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namba mbili, pamoja nambegu zao zote zimemwagwa, sasa nilikuwa naombamwongozo wako ni lini Serikali itawapelekea chakulawananchi hawa wa Wilaya ya Chemba na siyo Kondoanasisitiza tena ambao waliathirika, naomba mwongozo wako.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Waziri amekusikiabaadaye mtakaa, mta-caucus mtajadili. Katibu.

NDG. YONA KIRUMBI-KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

MAAZIMIO

MWENYEKITI: Sasa namwita Waziri wa Nchi, Ofisi yaMakamu wa Rais.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Azimiola Bunge la Kuridhia Itifaki ya pamoja ya ziada ya Nagoya-Kuala Lumpur kuhusu Uwajibikaji Kisheria na Fidia kwa

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi yaBioteknolojia ya Kisasa katika Kutekeleza Itifaki ya Cartagena(Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liabilityand Redress on Cartagena Protocol on Biosafety).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Itifaki ya ziada ya NagoyaKuala Lumpur kuhusu uwajibikaji Kisheria na fidia kwamadhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi yaBioteknolojia ya Kisasa ilianzishwa ili kuwezesha utekelezajiwa Itifaki ya Cartagena inayohusu matumizi salama yaBioteknolojia ya kisasa iliyopitishwa na nchi wanachama waMkataba wa Hifadhi ya Bioanuai mwaka 2000 ambapoTanzania iliridhia itifaki mwaka 2003.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo kuu la Itifaki yaCartagena ni kudhibiti na kusimamia matumizi salama yabioteknolojia ya kisasa miongoni mwa nchi wanachama.Katika kutekeleza Itifaki hii Tanzania imepata fursa yakujengewa uwezo wa kitaasisi na kitaalamu kuhusu usimamiziwa matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa hususani katikamasuala yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuweka mfumo wa Kitaifawa usimamizi wa matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa,kuandaa na kutekeleza kanuni za matumizi salama yabioteknolojia ya kisasa za mwaka 2009 na miongozombalimbali kuhusu matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasana kutoa mafunzo ya vifaa kwa taasisi zinazohusika kwa tafitipamoja na usimamizi wa matumizi salama ya bioteknolojiaya kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kupitishwa kwaItifaki ya Cartagena masuala yanayohusu taratibu zauwajibikaji kisheria na fidia hayakupata muafaka wa nchiwanachama kutokana na kuwepo kwa msimamo tofauti katiya nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Nchi Zilizoendeleazilikuwa na msimamo kuwa kusiwepo na utaratibu wa pamojawa Kimataifa wa kusimamia suala la uwajibikaji kisheria nafidia na badala yake kila nchi itumie sheria zake za ndani aumisingi ya kisheria za Kimataifa zil izopo. Aidha, nchi

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

zinazoendelea ikiwemo Tanzania zilipendekeza kuwepo namfumo wa Kimataifa kuhusu uwajibikaji kisheria na fidiaendapo madhara yatatokea kutokana matumizi yabioteknoloja ya kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na kushindwakufikia mwakafaka kuhusu suala hilo nchi wanachamazilikubaliana kuwa Ibara ya 27 ya Itifaki ya Cartagena ielekezenchi wananchama kuendeleza majadiliano ya kuwekataratibu za Kitamaifa kuhusu uwajibikaji kisheria na fidia kwamadhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi yabioteknolojia ya kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utekelezaji wamaelekezo ya Ibara ya 27 ya Itifaki hiyo mkutano wa kwanzawanchi wanachama uliofanyika jijini Kuala Lumpur mwaka2004 ulianzisha majadiliano ambayo yalikamilika katikamkutano wa tano wanchi wanachama uliofanyika JijiniNagoya Japan mwaka 2010. Kukamilika kwa majadilianokulipitisha itifaki ya ziada ya Nagoya Kuala Lumpur inayowekautaratibu wa Kimaitafa kwa wajibikaji kisheria na fidia kwamadhara yanayoweza kutokana na matumizi yabioteknolojia ya kisasa. Aidha, utekelezaji wa itifaki hii ya zaidaumeanza rasmi tarehe 5 Machi, 2018 baada ya nchi 40kuridhia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuridhia itifaki hii Tanzaniaitaimarisha ushirikiano wanchi wananchama katikakusimamia na kutekeleza masuala yanayohusu masuala yauwajibikaji kisheria na fidia kwa madhara yanayowezakutokea kutokana na matumizi ya bioteknolojia ya kisasahususan bidhaa au mazao ambayo yanatoka nje ya nchi.Vilevile, kuridhia itifaki hii kutaongeza upatikanaji wa fursa zakujenga uwezo wa wataalamu nchini katika kusimamiamatumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa. Aidha, utekelezajiwa itifaki hii utasimamiwa na sheria za Usimamizi wa Mazingiraya mwaka 2004 Sura ya 191 na Kanuni za Usimamizi waMatumizi Salama ya Bioteknolojia ya Kisasa ya mwaka 2009.Pia kwa sasa sheria na kanuni hizo hazihitaji kufanyiwamarekebisho.

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

Mheshimiwa Mwenyekiti, iwapo nchi haitaridhia Itifakihii itakuwa vigumu kutumia utaratibu huu wa uwajibishajikisheria na kupata fidia kutoka kwa makampuni,wafanyabiashara ambao bidhaa zao na mazao yatokanayona bioteknolojia ya kisasa yanaweza kuleta madhara kwaafya za binadamu na mazingira hapa nchini. Madhara hayoni pamoja na uharibifu wa viumbe ambavyo havikukusudiwa,uharibifu wa bioanuai na uoto wa asili, uchavushaji wa mazaoyasiyohusika. Ongezeko la mzio yaani allergy, usugu wabaadhi ya dawa kujitokeza kwa magugu sugu na kuibukakwa visumbufu sugu vya mazao. Vilevile nchi yetu itakosafursa ya kujenga uwezo wa kitaalamu na kisheria katikakusimamia matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na maelezo hayovipengele muhimu ya itifaki hii ni pamoja na vifuaavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 1 Lengo la Itifaki.Ibara hii inahusu lengo la itifaki hii ambayo ni kuchangia juhudiza kuhifadhi mazingira na matumizi endelevu ya bioanuai kwakutambua madhara yanayoweza kutokea katika afya zabinadamu kutokana na matumizi ya mazao au bidhaazilizofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki kwa njia ya bioteknolojiaya kisasa. Hivyo itifaki hii imeweka taratibu za Kimataifa zakusimamia masuala ya uwajibikaji kisheria na fidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, 2 Ibara ya 3 Mawanda yaItifaki. Ibara hii inahusu utaratibu wa uwajibikaji kisheria nafidia kwa madhara yanayoweza kutokea kutokana namatumizi ya mazao au bidhaa zilizofanyiwa mabadiliko yakijenetiki kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mazao au bidhaa zifuatazozinahusika na ibara hii; mazao au bidhaa zinazowezakutumiwa katika chakula cha binadamu au mifugo amakutumika viwandani na mazao au bidhaa zinazowezakutumika katika utafiti. Ibara hii pia inahusu usimamizi wamazao au bidhaa zilizofanyiwa mabadiliko ya ki-geneticambazo zinaweza kuingia nchini kutoka nchi nyingine bila

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

kukusudiwa, mfano uchavushaji wa mimea (polination) kwanjia ya upepo au wadudu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara hii inahusu pia mazaoau bidhaa zinazoweza kuingizwa nchini kinyume na sheriaza nchi. Aidha, itifaki hii itatumika kwa nchi wanachama tuna endapo kutatokea madhara yatokanayo na matumizi yamazao au bidhaa zitokanazo na bioteknolojia ya kisasazinazozalishwa hapa nchini uwajibishaji kisheria na fidiautafuata sheria za nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 4, Kisababishi chaMadhara. Ibara hii inaelekeza kutumia sheria za nchi husikakuainisha chanzo cha madhara yanayoweza kutokeakutokana na matumizi ya mzao au bidhaa zilizofanyiwamabadiliko ya ki-genetic kwa kutumia Bioteknolojia ya kisasa.Na kwa hili lina manufaa kwa nchi yetu kwani kutumia sheriaza kimataifa kuianisha chanzo cha madhara hayo kunawezakusababisha kushindwa kutoa haki stahiki kulingana namazingira ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 5, ni Hatua zaKukabiliana na madhara. Ibara hii inahusu hatua za kuchukuana kukabiliana na madhara yanayoweza kutokea kutokanana matumizi ya mazao au bidhaa zilizofanyiwa mabadilikoya ki-genetic zitakazochukuliwa kwa mujibu wa sheria ya nchihusika. Gharama za kukabiliana na madhara hayo zitakuwajuu ya kampuni, kiwanda, au mtu yeyote aliyesababishamadhara hayo. Takwa hili la itifaki lina manufaa kwa nchiyetu kwani kutumia sheria za kimataifa kuainisha hatuazakukabiliana na mdahara hayo kunaweza kusababishakushindwa kutoa haki kwa watakaoathirika na matumizi yamazao au bidhaa hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 12, Utekelezaji naUhusiano wa Mifumo ya uwajibishaji. Ibara hii inaelekeza nchiwanachama kuweka mifumo ya kisheria ya uwajibishaji nafidia kwa madhara ambayo yanaweza kutokea kutokanana matumizi ya mazao au bidhaa zilizofanyiwa mabadilikoya ki-genetic kwa kutumia njia ya Bioteknolojia ya kisasa.

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

Mifumo iliyopo ni ya aina tatu; mfumo wa kwanza nikumuwajibisha mmiliki au msambazaji wa Bioteknolojia yakisasa kwa madhara yanayoweza kutokea kwa mtumiaji wamazao au bidhaa zilizofanyiwa mabadiliko ya ki-genetic bilakujali kama mmiliki alikuwa na lengo la kumdhuru mtumiaji(Strictly Liability).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfumo wa pili unahusishakumuwajibisha aliyesababisha madhara baada ya mtumiajiwa mazao au bidhaa zilizofanyiwa mabadiliko ya ki-genetickudhibitisha kudhurika kutokana na bidhaa hizo (Fault BasedLiability) na Mfumo wa tatu ni mfumo wa uwajibishaji mseto(Strict Liability na Fault Based Liability).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Tanzaniasuala la uwajibikaji, sheria na fidia kwa madhara yanayowezakutokea kutokana na matumizi ya mazao au bidhaazilizofanyiwa mabadiliko ya ki-genetic limezingatiwa katikaSheria ya Mazingira ya Mwaka 2004, Sura ya 191 hata kablaya kupitishwa kwa itifaki hii na katika kanuni za matumizisalama za Bioteknolojia ya kisasa ya mwaka 2009. Kanuni hiiimeweka mfumo wa strict liability katika uwajibishaji kisheriana fidia kwa madhara yanayoweza kutokea kutokana namatumizi ya mazao au bidhaa hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza kanuni hiibaadhi ya wadau walikuwa na hoja kuwa, kanuni hii inaathirishughuli za utafiti kutokana na mfumo wa strict liability.Kuwakosesha fursa watafiti wa ndani ya nchi kushiriki nawadau kutoka nje ya nchi, hususan makampuniyanayojihusisha na shughuli ya utafiti wa masuala yaBioteknolojia ya kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kuona umuhimuwa masuala ya utafiti katika eneo hili kanuni za matumizi yasalama za Bioteknolojia ya kisasa za mwaka 2009zilirekebishwa mwaka 2015 kwa kuondoa mfumo wa strictliability katika shughuli za utafiti na kuweka mfumo wa faultbased liability.

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 16, inaelezeaUhusiano Baina ya Mikataba na Itifaki ya Katagena. Ibara hiiinaeleza uhusiano uliopo kati ya itifaki hii ya mikataba yahifadhi ya bioanuai na Itifaki ya Katagena katika kusimamiahifadhi ya mazingira na matumizi endelevu ya bioanuai. Itifakiya ziada ya Nagoya - Kuala Lumpur inatekeleza Ibara ya 27ya Itifaki ya Katagena na utekelezaji wa itifaki hii hauathiriwajibu na majukumu ya nchi wanachama, Mkataba waHifadhi ya Bioanuai ya wa Itifaki ya Katagena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 20, inahusu Uhuruwa Kujitoa. Nchi mwanachama ina uhuru wa kujitoa katikaitifaki ya ziada baada ya miaka miwili tangu kuanzakutekelezwa kwake. Vilevile nchi ikijitoa katika Itifaki yaKatagena itahesabika kuwa imejitoa pia, kwenye itifaki hiiya ziada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ujumla kuridhia kwaitifaki hii kutasaidia kuimarisha uhifadhi wa mazingira, kulindaafya za binadamu na wanyama dhidi ya madharayatokanayo na matumizi ya Bioteknolojia ya kisasa. Matokeomengine mahususi ni pamoja na:-

(i) Kurahisisha uwajibishaji kisheria na upatikanaji wafidia kutokana na makampuni au wafanyabiashara wa nchiwanachama wa itifaki hii ambao wameingiza mazao aubidhaa zilizofanyiwa mabadiliko ya ki-genetic na matumiziyake kuleta madhara kwa afya ya binadamu na mazingirahapa nchini;

(ii) Kuimarika kwa ushirikiano baina ya Tanzania nanchi nyingine wanachama wa itifaki hii katika kusimamiauwajibikaji kisheria na fidia kwa madhara yanayowezakutokea kutokana na matumizi ya mazao au bidhaazilizofanyiwa mabadiliko ya ki-genetic kwa kutumia njia yaki-Bioteknolojia ya kisasa;

(iii) Kukuza uelewa wa wataalam wa ndani wakiwemoWanasheria katika kusimamia masuala ya uwajibikaji kisheria

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

na fidia kwa madhara yatokanayo na matumizi yaBioteknolojia au bidhaa zilizofanyiwa mabadiliko ya ki-genetic

Mheshimiwa Mwenyekiti, itifaki hii inaweza kuathiriuwekezaji katika Bioteknolojia ya kisasa kutoka nje ya nchi,hususan makampuni au wafanyabisahara kwa kuhofia kuwa,utaratibu unaopendekezwa unaweza kuwa na gharamakubwa kwao iwapo madhara ya matumizi ya bidhaa hizoyatajitokeza kwa mazingira na afya ya binadamu nawanyama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, uwekezajiambao hauzingatii usalama wa afya na mazingira unawezakuwa na hasara kubwa kuliko faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili itifaki hii iweze kutekelezwani lazima nchi zilizosaini itifaki ziridhie. Utaratibu wa kuridhiaitifaki hii umeoneshwa katika Ibara ya 18 ya itifaki yenyeweambayo inazitaka nchi hizo kuridhia itifaki hii na kuwasilishahati ya kuridhia kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifaambaye ana jukumu la kupokea na kuhifadhi hati hizo.

Aidha, itifaki hii imeanza rasmi kutekelezwa tarehe 05Machi, 2018 baada ya nchi ya 40 kuridhia itifaki hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayasasa naomba kuwasilisha Azimio la Bunge la Kuridhia Itifakihii kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa, Tanzania ni nchi mwanachama wa Itifakiya Katagena inayohusu matumizi salama ya Bioteknolojia yakisasa ya mwaka 2000 na lengo kuu la itifaki hiyo ni kusimamiamatumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa miongoni mwanchi wanachama.

Na kwa kuwa, Tanzania iliridhia itifaki hii mwaka 2003.

Na kwa kuwa, wakati wa kupitisha Itifaki ya Katagenanchi wanachama zilikubaliana kuendeleza majadilianokuhusu utaratibu wa kimataifa wa uwajibikaji kisheria na fidia

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

kwa madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumiziya Bioteknolojia ya kisasa kuweka Ibara ya 27 iliyoelekezakuendelezwa kwa majadiliano ya suala hilo.

Na kwa kuwa, majadiliano hayo yalikamilika katikamkutano wa tano wa nchi wanachama wa Itifaki yaKatagena wa mwaka 2010 uliofanyika Nagoya, Japan nakupitishwa rasmi itifaki ya ziada ya Nagoya – Kuala Lumpurinayoweka utaratibu wa kimataifa wa uwajibikaji kisheria nafidia kwa madhara yanayoweza kutokea kutokana namatumizi ya Bioteknolojia ya kisasa miongoni mwa nchiwanachama ambayo ilianza kutekelezwa rasmi tarehe 05Machi, 2018 hadi sasa jumla ya nchi 45 zimeridhia itifaki hii.

Na kwa kuwa, kwa kuridhia Itifaki ya Ziada ya Nagoya– Kuala Lumpur Tanzania itaimarisha usalama wa afya yabinadamu na mazingira dhidi ya madhara yanayowezakutokea kutokana na matumizi ya Bioteknolojia ya kisasahususan kwa bidhaa za mazao yanayotoka nje ya nchi.

Na kwa kuwa, kwa kuridhia itifaki hii kutaongezaupatikanaji wa fursa ya kujenga uwezo wa wataalam nchinikatika kusimamia matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasakatika nyanja za kisheria, kisayansi na kiteknolojia.

Hivyo basi, kwa kuzingatia manufaa yatokanayo naitifaki hii kwa Tanzania na kwa wanachama wengine. Bungehili katika Mkutano wa Kumi na Sita na sasa liazimie kuridhiakwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Itifaki ya Ziada yaNagoya – Kuala Lumpur kuhusu uwajibikaji kisheria na fidiakwa madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumiziya Bioteknolojia ya kisasa katika kuetekeleza itifaki yaCartagena (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocolon Liability and Redress to The Katagena Protocol onBiosafety).

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha naninaomba kutoa hoja. (Makofi)

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: MheshimiwaMwenyekiti, naafiki.

MWENYEKITI: Hoja imeungwa mkono, ahsante. Sasanamuita Mwenyekiti Kamati ya Viwanda, Biashara naMazingira.

MHE. KANALI (MST) MASOUD ALI KHAMIS - K.n.y.MWENYEKITI KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA,BIASHARA NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwaniaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira, naomba kuwasilisha Maoniya Kamati kuhusu Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Ziadaya Nagoya - Kuala Lumpur ya Uwajibikaji wa Kisheria na Fidiakwa Madhara Yanayoweza Kutokea Kutokana na Matumiziya Bioteknolojia ya Kisasa Katika Kutekeleza Itifaki yaCartagena. (Nagoya - Kuala Lumpur supplementary Protocolon Liability and Redress to The Cartagena Protocol Biosafety).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni ya53(6)(b). Kanuni ya Kudumu ya Bunge ya Toleo la Januari,2016, naomba kuwasilisha Maoni ya Kamati ya Kudumu yaBunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Azimio laBunge Kuridhia Itifaki ya Ziada ya Nagoya, Kuala Lumpurinayolenga kuweka utaratibu wa uwajibikaji kisheria na fidiakwa madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumiziya Bioteknolojia ya kisasa katika kutekeleza Itifaki yaCartagena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia Masharti yaFasili ya 6(b), Kifungu cha 53, ikisomwa pamoja na Fasili ya1(b) ya Kifungu cha 7 cha Nyongeza ya 8 ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016, Kamati ya Kudumuya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira inalo jukumu lakushughulikia mikataba inayopendekezwa kuridhiwa naBunge iliyo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa hoja ya Serikali kuhusu Bunge kuridhia Itifaki yaZiada ya Nagoya - Kuala Lumpur ilileta kwenye Kamati ya

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kwa mujibu wakanuni ya 53(3) ya Kanuni za Bunge. Kamati il i jadili,kuichambua hoja hii na hatimaye kuja na maoni ya ushauriambayo yamelenga kuboresha utekelezaji wa itifaki hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kushughulikia hoja hiikamati ilikutana katika Ofisi za Bunge, Dodoma ambapoilitekeleza shughuli zifuatazo kwa ajil i ya kuwezeshauchambuzi wa kina wa itifaki hii:-

(i) Semina ya Kuijengea Uelewa Kamati Juu ya Itifakiya Ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur ambapo tarehe 01Septemba, 2019 kamati ilikutana na Ofisi ya Makamu wa Rais,Mazingira na kupatiwa semina hii. Kupitia semina hii Kamatiilipata uelewa juu ya itifaki husika na kuwa katika nafasi nzuriya kuifanyia kazi hoja hii;

(i i) Kupokea maelezo ya Serikali ambayoyaliwasilishwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu waRais, Muungano na Mazingira siku ya tarehe 04 Septemba,2019;

(iii) Kupokea maoni ya wadau. Kamati ilipokuwainatekeleza jukumu lake kuhusiana na hoja hii ilizingatiamasharti ya Kanuni ya 117(9) kuhusu utaratibu wa Kamati wakuwaalika wadau. Kamati inawashukuru sana wadau wotewalioweza kushiriki kwa kuwa maoni yao yalisaidia kuboreshamaoni ya kamati kuhusu itifaki hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ni moja ya nchimwanachama wa Itifaki kwa Hofadhi ya bioanuai (theConversation on Biological Diversity) na tuliridhia mwaka 1996.Mkataba huo ulikuwa na malengo matatu ambayo nikuhifadhi bioanuai, matumizi endelevu ya bioanuai namgawanyo sahihi wa faida zinazotokana na bioanuai namatumizi yake katika kutekeleza mkataba huu ilizaliwa Itifakiya Cartagena mwaka 2000 kwa lengo la kuhifadhi nakusimamia matumizi salama Bioteknolojia ya kisasa kwa lengola kuleta matumizi endelevu ya bio-anuai Tanzania iliridhiaitifaki ya Cartagena mwaka 2003.

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

Mheshimiwa Mwenyekiti, bada ya kupitisha Itifaki yaCartagena mwaka 2003 masuala yaliyohusu taratibu zauwajibikaji kisheria na fidia hayakufikiwa muafaka kutokanana kuwepo kwa msimamo tofauti baina ya nchi wanachama,jambo lililosababisha kukubaliana majadiliano yaendelee.Katika vikao vilivyofuata nchi wanachama walikubalianakuunda kamati ndogo ya wataalamu wa masuala yamatumizi ya Bioteknolojia ya kisasa na Wanasheria. Matokeoya kazi iliyofanywa na kamati hiyo yalohitimisha mjadalaambapo nchi wanachama walikubaliana kupitisha Itifaki yaZiada ya Nagoya – Kuala Lumpur Mwaka 2010 iliyowekautaratibu wa kimataifa wa uwajibikaji kisheria na fidia kwamadhara yanayoweza kutokea katokana na matumizi yaBioteknolojia ya kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bioteknolojia ya kisasa,technology ya uhandisi gene modern Bioteknolojia, geneticengineering ni nyenzo ya kisayansi inayoweza uhamishaji wavinasaba kutoka kiumbe kimoja kwenda kiumbe kingine ilikukipatia kiumbe kingine sifa inayokusudiwa kwa lengo lakuboresha kiumbe hicho na kuongeza tija ya uzalishaji.Pamoja na faida nyingi za matumizi ya Bioteknolojia ya kisasabado matumizi ya bidhaa zitokanazo na teknolojia hiiyanaweza kuleta madhara katika afya za binadamu namazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, il i kuliwezesha Bungekutekeleza madaraka yake ipasavyo, kwa mujibu wa Ibaraya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kamati ilizingatia mambo mbalimbali yaliyo muhimu katikakufanyia kazi Hoja ya Serikali iliyo mezani leo. Kamati iliangaliaKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja nabaadhi ya sheria zinazohusiana moja kwa moja na maudhuiya itifaki iliyopendekezwa ambapo ilibaini kuwa, itifaki hiihaikuwa inakinzana na Katiba wala sheria za nchi, bali ilikuwainaongezea nguvu Sheria ya Taifa ya Mazingira katikakusimamia uhifadhi wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia, ilitafakari faidazipatikanazo kutokana na kuridhia itifaki hii ambazo ni;

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

(i) Kurahisisha uwajibikaji wa kisheria na upatikanaji wafidia kutoka kwa makampuni, wafanyabiashara wa nchiwanachama wa itifaki hii ambao mazao au bidhaa zaozinafanyiwa mabadiliko ya ki-genetic kama matumizi yakeyameleta madhara kwa afya au mazingira na;

(ii) Kuimarika kwa ushirikiano baina ya Tanzania na nchinyingine wanachama wa itifaki hii katika kusimamiauwajibikaji kisheria na fidia kwa madhara yanayowezakutokea kwa matumizi ya mazao au bidhaa zilizofanyiwamabadiliko ya ki-genetic.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Kamati iliangaliahasara ambazo zinaweza kupatikana kutokana na kutoridhiamkataba huu. Kamati ilifahamishwa hasara moja kubwaambayo nchi inaweza kuipata kama haitaridhia ni kuwaitajinyima haki yake ya kufidiwa endapo madhara yanawezayakapatikana yakadhihirika kuwa yametokana na matumiziya bidhaa au mazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya ki--gentic.Ni vyema Tanzania tuzingatie kuwa Tanzania inaruhusuuingizwaji wa bidhaa mbalimbali nchini kwa kuwa, kati yabidhaa zinazoingia kuna baadhi yake zimefanyiwamabadiliko ya ki-genetic.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilijiridhisha pia, namaudhui ya itifaki husika. Ibara ya kwanza na mkatabaimeweka wazi dhamira ya itifaki hii kuwa inalenga kuwekamatumizi endelevu ya bioanuai kwa kutambua madhara yaafya ya binadamu kwa kuweka taratibu za kimataifa zakusimamia masuala ya uwajibikaji kisheria na fidia endapoyatapatikana madhara kutokana na matumizi ya bidhaa aumazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya ki-genetic.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nanukuu, Article 1; “Theobjective of this Supplementary Protocol is to contribute tothe conservation and sustainably use of biological diversitytaking also into account risk to human health by providinginternational rules and procedure in the field of liability andredress relating to living modified organism,” mwisho wakunukuu.

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia maudhui yaibara hiyo Tanzania ikiridhia inajiweka katika nafasi yakunufaika ukizingatia bidhaa na mzao yanayofanyiwamabadiliko ya ki-genetic yanaendelea kuingia na kutumikahapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni na ushauri wa Kamati.Tanzania haijaruhusu matumizi ya bioteknolojia ya kisasakatika uzalishaji wa bidhaa yoyote kwa maana kuwaTanzania hatuzalishi bidhaa wala mazao yatokanayo nateknolojia hiyo lakini kwa uhakika mazao na bidhaazitokanazo na teknolojia hii zimeendelea kuingia nchini natumeendelea kuzitumia. Hivyo basi, kuna haja ya nchikuridhia Itifaki hii ili tuweze kulinda haki yetu pindi madharayanapobainika. Pamoja na umuhimu wa kuridhia, yapobaadhi ya maeneo ambayo ni vyema nchi tukayaweka sawakwa lengo la kuboresha utekelezaji wa mkataba huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa Itifaki hiiumeonyesha kuwa na uhusiano na ushirikiano wa moja kwamoja na sheria za nchi husika mfano Ibara ya 6(2) inatakasheria za nchi husika kufafanua exemption na mitigation kwanamnawanavyoona inafaa. Pia Ibara ya 8 inataka sheriaya nchi husika kuweka kiwango cha fidia kwa ajili ya madharayaliyopatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inaishauri Serikalibaada ya kuridhia Itifaki hii ijipange kuzipitia na kuboreshasheria za nchi na kutunga sheria ambazo zitaendasambamba na malengo ya Itifaki hii kwa kuhakikisha kamanchi tunanufaika na siyo kupoteza. Vilevile ili kuwezakutekeleza kikamilifu masharti ya Ibara hizo, Kamati inaonaupo umuhimu kwa nchi wanachama kuangalia namna yakuoanisha sheria, sera na programu zinazohusiana katikautekelezaji wa Itifaki hii kwa lengo la kuwa na manufaalinganifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamii bado ina uelewamdogo juu ya matumizi, faida na madhara ya bioteknolojiaya kisasa. Ili kunufaika na Itifaki hii, Kamati inaishauri Serikali

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

kuweka jitihada za dhati kuhakikisha jamii inapatiwa uelewajuu ya uwepo wa bidhaa au mazao yanayofanyiwamabadiliko ya kijenetiki. Pia jamii iwekwe wazi kuwa pamojana uzuri wa jambo hili bado uwezekano wa kupata madharayatokanayo na matumizi ya bidhaa hizo. Vilevile jamii ijulishwejuu ya uwepo wa Itifaki hii na namna inavyofanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Itifaki hii imeipa nchiMwanachama nafasi kubwa ya kusimamia na kuratibuutekelezaji wa Itifaki ndani ya nchi yake (utaalamu nateknolojia ya nchi katika kupima na kubaini madhara). Kamatiinaona uwezo wa nchi katika kutekeleza Itifaki hii badohautoshelezi. Kamati inaishauri Serikali kuzijengea uwezotaasisi zake ambazo zitaenda kuratibu utekelezaji wa Itifakihii kwa kuwa ndiyo zitategemewa kusimamia na kuhakikishamhanga anapata haki zake pindi itakapotokea tukio lolote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho. Naombanikushukuru sana wewe binafsi kwa uongozi wako mahiri kwakunipa nafasi ya kuwasilisha maoni ya Kamati. NimshukuruMheshimiwa Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bungekwa kuratibu na kusimamia shughuli za Bunge kwa umakinina umahiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati inapendakuwashukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira), Mheshimiwa George BonifaceSimbachawene, Naibu Waziri wake, Mheshimiwa MussaRamadhan Sima, Makatibu Wakuu pamoja na wataalamuwote wa ofisi hiyo muhimu kwa ushirikiano walioutoa wakatiwa kujadili Azimio hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya kipekee,napenda kuwashukuru Wajumbe wote wa Kamati ya Bungeya Viwanda, Biashara na Mazingira kwa ushirikiano walioutoawakati wa kuipitia, kuchambua na hatimaye kuwasilishamaoni yao juu ya Azimio hili mbele ya Bunge lako Tukufu.Orodha yao ni kama inavyosomeka hapo chini na kwa ruhusayako naomba majina yao yaingie kwenye Kumbukumbu zaBunge.

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho lakini si kwaumuhimu, nawashukuru watumishi wote wa Ofisi ya Bungechini ya uongozi wa Katibu wa Bunge, Ndugu StephenKagaigai kwa kuisaidia Kamati kutekeleza majukumu yake.

Aidha, nawashukuru Mkurugenzi wa Idara ya Kamati,Ndugu Athuman Hussein; Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu yaFedha na Uchumi, Ndugu Michael Chikokoto; Makatibu waKamati, Bi. Zainab Mkamba na Bi. Mwajuma Ramadhani naMsaidizi wa Kamati, Bi. Paulina Mavunde kwa kuratibushughuli za Kamati

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha nanaunga mkono Azimio hili.

MAONI YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA,BIASHARA NA MAZINGIRA KUHUSU AZIMIO LA BUNGE

KURIDHIA ITIFAKI YA ZIADA YA NAGOYA – KUALA LUMPUR LAUWAJIBIKAJI KISHERIA NA FIDIA KWA MADHARA

YANAYOWEZA KUTOKEA KUTOKANA NA MATUMIZI YABIOTEKNOLOJIA YA KISASA KATIKA KUTEKELEZA ITIFAKI YA

CARTAGENA - KAMA YALIVYOWASILISHWA MEZANI

(Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol onLiability and Redress to the Cartagena Protocol on

Biosafety) Kama yalivyowasilishwa Mezani _________________

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (6) (b), yaKanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari, 2016, naombakuwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge yaViwanda Biashara na Mazingira kuhusu Azimio la BungeKuridhia Itifaki ya Ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur inayolengakuweka utaratibu wa uwajibikaji kisheria na fidia kwamadhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi yaBioteknolojia ya kisasa katika kutekeleza itifaki ya Cartagena(Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Labilityand Redress to the Cartagena Protocol on Biosafety).

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia masharti ya fasili ya 6(b),Kifungu cha 53 ikisomwa pamoja na fasili ya 1(b) ya Kifungucha 7, cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu zaBunge, Toleo la Januari, 2016, Kamati ya Kudumu ya Bungeya Viwanda, Biashara na Mazingira inalo jukumu lakushughulikia Mikataba inayopendekezwa kuridhiwa naBunge iliyo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.

Mheshimiwa Spika, naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwaHoja ya Serikali kuhusu Bunge kuridhia Itifaki ya Ziada yaNagoya – Kuala Lumpur ililetwa kwenye Kamati ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira kwa mujibu wa Kanuni ya53 (3) ya Kanuni za Bunge. Kamati iliijadili na kuichambuahoja hii na hatimaye kuja na maoni na ushauri ambaoumelenga kuboresha utekelezaji wa Itifaki hii.

2.0 NAMNA KAMATI ILIVYOSHUGHULIKIA HOJA HII

Mheshimiwa Spika, katika kushughulikia hoja hii Kamatiilikutana katika Ofisi za Bunge Dodoma ambapo ilitekelezashughuli zifuatazo kwa ajili ya kuwezesha uchambuzi wa kinawa Itifaki hii;-

i) Semina ya kuijengea uelewa Kamati juu ya Itifaki yaZiada ya Nagoya – Kuala Lumpur, ambapo tarehe 1September, 2019 Kamati ilikutana na Ofisi ya Makamu waRais - Mazingira na kupatiwa semina hii. Kupitia semina hiiKamati ilipata uelewa juu ya itifaki husika na kuwa katikanafasi nzuri ya kuifanyia kazi hoja hii.

ii) Kupokea Maelezo ya Serikali ambayo yaliwasilishwana Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muunganona Mazingira siku ya tarehe 04 September, 2019. Kikao hikikilitoa fursa kwa Ofisi hiyo kufafanua kwa kina madhumuniya Itifaki hii kwa lengo la kuishawishi Kamati na hatimayekulishawishi Bunge kuridhia.

iii) Kupokea maoni ya wadau, Kamati i l ipokuwainatekeleza jukumu lake kuhusiana na hoja hii, ilizingatiamasharti ya Kanuni ya 117 (9) kuhusu utaratibu wa Kamati

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

kuwaalika wadau. Kamati inawashukuru sana wadau wotewalioweza kushiriki kwa kuwa maoni yao yalisaidia kuboreshamaoni ya Kamati kuhusu Itifaki hii.

3.0 CHIMBUKO LA MKATABA WA MAREKEBISHO

Mheshimiwa Spika, Tanzania ni moja ya nchi Mwanachamawa Mkataba wa hifadhi ya Bioanuai (The Convention onBiological Diversity) na tuliuridhia mwaka 1996. Mkataba huoulikuwa na Malengo matatu ambayo ni kuhifadhi bioanuai,matumizi endelevu ya bioanuai na mgawanyo sahihi wafaida zinazotokana na matumizi yake. Katika kutekelezaMkataba huu ilizaliwa Itifaki ya Cartagena mwaka 2000 kwalengo la kudhibiti na kusimamia matumizi salama yaBioteknolojia ya kisasa kwa lengo la kuleta matumizi endelevuya bioanuai. Tanzania iliridhia itifaki Cartagena mnamomwaka 2003.

Mheshimiwa Spika, baada ya kupitisha Itifaki ya Cartagenaya mwaka 2003 masuala yanayohusu taratibu za uwajibikajikisheria na fidia hayakufikiwa muafaka kutokana na kuwepokwa misimamo tofauti baina ya nchi wanachama jambolililopelekea kukubaliana majadiliano uendelee.Katika vikao vilivyofuata Nchi wanachama walikubalianakuunda Kamati ndogo ya wataalamu wa masuala yamatumizi ya bioteknolojia ya kisasa na wanasheria. Matokeoya kazi iliyofanywa na Kamati hiyo yalihitimisha mjadalaambapo nchi wanachama walikubaliana kupitisha Itifaki yaZiada ya Nagoya - Kuala Lumpur ya Mwaka 2010 inayowekautaratibu wa kimataifa wa uwajibikaji kisheria na fidia kwamadhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi yabioteknolojia ya kisasa.

Mheshimiwa Spika, Bioteknolojia ya kisasa/teknolojia yaUhandisi Jeni (Modern Biotechnology/Genetic Engineering)ni nyenzo ya kisayansi inayowezesha uhamishaji wa vinasabakutoka kiumbe kimoja kwenda kiumbe kingine ili kukipatiakiumbe kingine sifa inayokusudiwa kwa lengo la kuboreshakiumbe hicho na kuongeza tija na uzalishaji. Pamoja na faidanyingi za matumizi ya bioteknolojia ya kisasa bado matumizi

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

ya bidhaa zitokanazo na teknolojia hii yanaweza kuletamadhara katika afya ya binadamu na mazingira.

4.0 MAMBO YA MSINGI YALIYOZINGATIWA NA KAMATI

Mheshimiwa Spika, i l i kuliwezesha Bunge kutekelezamadaraka yake ipasavyo kwa mujibu wa Ibara ya 63(3) (e)ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamatiilizingatia mambo mbalimbali yaliyo muhimu katika kuifanyiakazi hoja ya Serikali iliyo mezani leo.

Mheshimiwa Spika, Kamati iliangalia Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania pamoja na baadhi ya Sheria za nchizinazohusiana moja kwa moja na maudhui ya Itifakiinaopendekezwa ambapo ilibainika kuwa Itifaki hii haikuwainakinzana na Katiba wala Sheria za nchi bali ilikuwainaiongezea nguvu Sheria ya Taifa ya Mazingira katikakusimamia uhifadhi wa mazingira.

Kamati pia ilitafakari faida zipatikanao kutokana na kuridhiaItifaki hii ambazo ni pamoja na;-

i) Kurahisisha uwajibikaji kisheria na upatikanaji wa fidiakutoka kwa makampuni/wafanyabiashara wa nchiwanachama wa Itifaki hii ambao mazao au bidhaa zaozilizofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki matumizi yake yameletamadhara kwa afya au mazingira; na

ii) Kuimarika kwa ushirikiano baina ya Tanzania na nchinyingie wanachama wa Itifaki hii katika kusimamia uwajibikajikisheria na fidia kwa madhara yanayoweza kutokea kwamatumizi ya mazao au bidhaa zilizofanyiwa mabadiliko yakijenetiki.

Vilevile Kamati i l iangalia hasara ambazo zinawezakupatikana kutokuridhia Mkataba huu. Kamati ilifahamishwahasara moja kubwa ambayo nchi inaweza kuipata kamahaitaridhia ni kuwa itajinyima haki yake ya kufidiwa endapomadhara yanaweza kupatikana na yakadhihirika kuwayametokana na matumizi ya bidhaa au mazao yaliyofanyiwa

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

mabadiliko ya kijenetiki. Tuzingatie kuwa Tanzania inaruhusuuingizwaji wa bidhaa mbalimbali nchini na kuwa kati yabidhaa zinazoingia kuna baadhi yake zimefanyiwamabadiliko ya kijenetiki.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilijiridhisha pia na maudhui ya Itifakihusika ambapo Ibara 1 ya Mkataba imeweka wazi dhamiraya Itifaki hii kuwa inalenga kuweka matumizi endelevu yabioanuai kwa kutambua madhara kwa afya ya binadamukwa kuweka taratibu za kimataifa za kusimamia masuala yauwajibikaji kisheria na fidia endepo yatapatikana madharakutokana na matumizi ya bidhaa au mazao yaliyofanyiwamabadiliko ya kijenetiki.

Nanukuu: Article 1 “The objective of this SupplementaryProtocol is to contribute to the conservation and sustainableuse of biological diversity, taking also into account risk tohuman health, by providing international rules andprocedures in the field of liability and redress relating to livingmodified organisms” Mwisho wa kunukuu.

Kwa kuzingatia maudhui ya Ibara hiyo Tanzania ikiridhiainajiweka katika nafasi ya kunufaika ukizingatia bidhaa namazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki vinaendeleakuingia na kutumika nchini.

5.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spika, Tanzania haijaruhusu matumizi yabioteknolojia ya kisasa katika uzalishaji wa aina yeyote, kwamaana kuwa Tanzania hatuzalishi bidhaa wala mazaoyatokanayo na teknolojia hiyo, lakini kwa uhakika mazao nabidhaa zitokanazo na teknolojia hii zimeendelea kuingianchini na tumeendelea kuzitumia. Hivyo basi kuna haja yanchi kuridhia itifaki hii ili tuweze kulinda haki yetu pindimadhara yanapobainika. Pamoja na umuhimu wa kuridhia,yapo baadhi ya maeneo ambayo ni vyema Nchitukayaweka sawa kwa lengo la kuboresha utekelezaji wamkataba huu.

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa itifaki hii umeonyesha kuwana uhusiano na ushirikiano wa moja kwa moja na sheria zanchi husika. Mfano Ibara ya 6 (2) inaitaka Sheria za nchi husikakufafanua exemption na mitigation kwa namnawanavyoona inafaa, lakini pia Ibara ya 8 inaitaka Sheria yanchi husika kuweka kiwango cha fidia kwa ajili ya madharayaliyopatikana. Kamati inaishauri Serikali baada ya KuridhiaItifaki hii ijipange kuzipitia na kuboresha sheria za nchi aukutunga Sheria ambazo zitaenda sambamba na malengoya Itifaki hii kwa kuhakikisha kama nchi tunanufaika na sikupoteza.Vilevile, ili kuweza kutekeleza kikamilifu masharti ya Ibara hizo,Kamati inaona upo umuhimu kwa nchi wanachamakuangalia namna ya kuoanisha Sheria, sera na programzinazohusika katika utekelezaji wa Itifaki hii kwa lengo la kuwana manufaa linganifu.

Mheshimiwa Spika, jamii bado ina uelewa mdogo juu yamatumizi, faida na madhara ya Bioteknolojia ya kisasa, kwalengo la kunufaika na Itifaki hii Kamati inaishauri Serikalikuweka jitihada za dhati kuhakikisha jamii inapatiwa uelewajuu ya uwepo wa bidhaa au mazao yaliyofanyiwa mabadilikoya kijenetiki. Pia jamii iwekwe wazi kuwa pamoja na uzuri wajambo hili bado kuna uwezekano wa kupata madharayatokanayo na matumizi ya bidhaa hizo. Vilevile jamii ijulishwejuu ya uwepo wa Itifaki hii na namna inavyofanya kazi.

Mheshimiwa Spika, Itifaki hii imeipa nchi Mwanachama nafasikubwa ya kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Itifaki ndaniya nchi yake (utaalamu na teknolojia ya nchi katika kupimana kubaini madhara). Kamati inaona uwezo wa nchi katikakutekeleza itifaki hii bado hautoshelezi, Kamati inaishauriSerikali kuzijengea uwezo taasisi zake ambazo zitaendakuratibu utekelezaji wa Itifaki hii kwa kuwa ndio zitategemewakusimamia na kuhakikisha mhanga anapata haki zake pindiitakapotokea tukio lolote.

6.0 HITIMISHOMheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sana wewe binafsikwa uongozi wako mahiri na kwa kunipa ruhusa ya kuwasilisha

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

maoni haya ya Kamati. Nimshukuru pia Mheshimiwa NaibuSpika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kuratibu nakusimamia shughuli za Bunge kwa umakini na umahiri.

Mheshimiwa Spika, Kamati inapenda kumshukuru Waziri waNchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe.George Boniface Simbachawene (Mb), Naibu Waziri wakeMhe. Musa Ramadhani Sima (Mb), Makatibu Wakuu, pamojana wataalamu wote wa Ofisi hiyo muhimu kwa ushirikianowalioutoa wakati wa kujadili Azimio hili.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisa, napendakuwashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Bunge yaViwanda, Biashara na Mazingira kwa ushirikiano walioutoawakati wa kupitia kuchambua na hatimaye kuwasilishamaoni yao juu ya Azimio hili mbele ya Bunge hili tukufu.Orodha yao ni kama inavyosomeka hapo chini na kwa ruhusayako naomba majina yao yaingie kwenye kumbukumbuRasmi za Bunge: -

1. Mhe. Suleiman Ahmed Sadiq, Mb Mwenyekiti2. Mhe. Kanal (Mst.) Masoud Ali Khamis, Mb M/Mwenyekiti3. Mhe. Gimbi Dotto Masaba, Mb Mjumbe4. Mhe. Kiteto Zawadi Koshuma, Mb Mjumbe5. Mhe. Hawa Subira Mwaifunga, Mb Mjumbe6. Mhe. Richard Mganga Ndassa, Mb Mjumbe7. Mhe. Kalanga Julius Laizer, Mb Mjumbe8. Mhe. Munira Mustafa Khatibu, Mb Mjumbe9. Mhe. Musa Rashid Ntimizi, Mb Mjumbe10. Mhe. Omary Ahmad Badwel, Mb Mjumbe11. Mhe. Khamis Ali Vuai, Mb Mjumbe12. Mhe. Zainabu Mndolwa Amiri, Mb Mjumbe13. Mhe. Machano Othman Said, Mb Mjumbe14. Mhe. Josephine Johnson Genzabuke, Mb Mjumbe15. Mhe. Gibson Blasius Meiseyeki, Mb Mjumbe16. Mhe. Shamsia Azizi Mtamba, Mb Mjumbe17. Mhe. Saed Ahmed Kubenea, Mb Mjumbe18. Mhe. Sylvestry F. Koka, Mb Mjumbe19. Mhe. Godbless Jonathan Lema, Mb Mjumbe20. Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mb Mjumbe

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

21. Mhe. David Cecil Mwambe, Mb Mjumbe22. Mhe. Ahmed Juma Ngwali, Mb Mjumbe23. Mhe. Jafar Sanya Jussa, Mb Mjumbe

Mheshimiwa Spika, napenda pia kumshukuru Katibu waBunge Ndg. Stephen Kagaigai; Mkurugenzi wa Idara yaKamati Bw. Athumani Hussein; Mkurugenzi Msaidizi Sehemuya Fedha na Uchumi Bw. Michael Chikokoto; Makatibu waKamati Bi. Zainabu Mkamba na Bi. Mwajuma Ramadhani naMsaidizi wa Kamati Bi Paulina Mavunde kwa kuratibu shughuliza Kamati.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkonoAzimio.

Suleiman Ahmed Sadiq, (Mb)MWENYEKITI

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NAMAZINGIRA

11 Septemba, 2019

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa namuita Msemaji waKambi Rasmi ya Upinzani, Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) atatoa maoni ya Upinzani kuhusuAzimio hilo, Mheshimiwa Lathifah.

MHE. LATHIFAH H. CHANDE - MSEMAJI WA KAMBI RASMIYA UPINZANI BUNGENI KWA OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kwa ruhusa yako, niwakumbushe WaheshimiwaWabunge na Watanzania wote tuweze kuwakumbuka walewote waliopoteza maisha katika shambulio lililotokea nchiniMarekani tarehe kama ya leo Septemba 11, miaka 18iliyopita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni ya Kambi RasmiBungeni kuhusu Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Nyongezaya Nagoya – Kuala Lumpur Kuhusu Uwajibikaji Kisheria na FidiaKutokana na Madhara nanayoweza Kutokea Kutokana na

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

Matumizi na Bioteknolojia ya Kisasa (Nagoya – Kuala LumpurSupplementary Protocol on Liability and Redress to theCartagena Protocol on Biosafety) yanayotolewa kwa mujibuwa Kanuni za kudumu za Bunge, Kanuni ya 53(6)(c).

Mheshimiwa Mwenyekiti, bioteknolojia ya kisasainaweza kuleta manufaa mengi lakini kuna hofu kwambainaweza kuwa na madhara makubwa kwa bioanuai na kwaafya ya binadamu. Kwa sababu hiyo, lengo la kuanzishwakwa Itifaki ya Nyongeza ya Nagoya, Kuala Lumpur lilikuwa nikuendeleza uhifadhi wa mazingira na kufanya matumiziendelevu ya bioanuai yaani mtawanyiko, muingiliano nakutegemeana baina ya viumbe hai na mazingira il ikukabiliana na madhara yatokanayo na matumizi yabioteknolojia

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa bioanuai ni sualala kimataifa; na kwa kuwa athari zitokanazo na uharibifu wabioanuai zinavuka mipaka ya nchi moja kwenda nyingineilionekana ni jambo muhimu na lenye afya katika utunzajiwa bioanuai yenyewe pamoja na mazingira kwa ujumlawake kuweka kanuni na taratibu za kimataifa na hasa katikadhana ya uwajibikaji kisheria na pia kulipia fidia ikiwakutatokea madhara yanayohusiana na viumbe haivilivyofanyiwa maboresho ya vinasaba (living modifiedorganisms). Ni katika maudhi hayo ambapo kifungu cha 3cha Itifaki hii kinaeleza bayana kwamba Itifaki ya Nyongezaitahusu madhara yatokanayo na viumbe haivilivyopandikizwa vinasaba tofauti kwa lengo la kuviboreshaambavyo katika kuishi kwake vinakuwa mipaka ya nchi mojakwenda nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Itifaki hiimadhara yanayotokana na matumizi ya bioteknolojiainayopelekea uharibifu wa mazingira na bioanuaiyatahesabiwa kuwa ni madhara ikiwa yatakuwayanaonekana, yanapimika na yenye athari kwa afya yabinadamu. Aidha, Itifaki inaelekeza kwamba ili mtu awezekuwajibika na au kulipa fidia ni lazima mlalamikaji aweze

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

kuthibitisha kuwa madhara hayo yanauhusiano wa moja kwamoja na viumbe vilivyofanyiwa maboresho na vinasaba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo ya msingi yakuzingatia kabla ya kuridhia Itifaki. Pamoja na ukweli kwambaItifaki hii inaonekana kuwa na nia njema ya kupambana nakuzuia madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumiziya bioteknolojia kwa kuweka kanuni za Kimataifa zauwajibikaji kisheria na kulipia faida kwa madhara ya namnahiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ingependa Serikalina Bunge kuzingatia mambo yafuatayo kabla ya kuridhiaItifaki hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwezo wa nchi katikasayansi ya na teknolojia. Kama ilivyoelezwa hapo awali, Itifakihii katika mawanda mapana inahusu kukabiliana namadhara yatokanayo na matumizi ya bioteknolojia nahususan upandikizaji wa vinasaba katika viumbe hai. Hili nijambo linalohitaji uwezo mkubwa wa kisayansi na kiteknolojia.Tofauti na nchi zilizoendelea nchi ambazo ziko nyumakimaendeleo ikiwemo Tanzania, bado hazina uwezo mkubwakatika sayansi na teknolojia kuweza kufanya tafiti na gunduziza kisayansi kama vile genetic engineering au masualayanayofanana na hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Itifaki hii ilimlalamikaji aweze kulipwa fidia kutokana na madhara yamatumizi ya bioteknolojia ni lazima aweze kuthibitishakwamba madhara hayo yanatokana na viumbevilivyofanyiwa maboresho ya vinasaba. Kwa manenomengine ni kwamba nchi itaathirika kutokana na matumiziya bioteknolojia kutoka nje. Ni lazima tuwe na maabaramadhubuti na watafiti waliobobea katika sayansi ili kuwezakugundua kama madhara tuliyopata yanauhusiano wa mojakwa moja na viumbe vilivyopandikizwa vinasaba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni ina mtazamo kwamba jambo hili litakuwa gumusana hasa kwa nchi yetu kutokana na Serikali kutoipakipaumbele Tume yetu ya Sayansi na Teknolojia. Kwa mfano,

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa MiakaMitano 2016/2017 - 2020/2021, Serikali ilijiwekea kiwango chakutenga asilimia moja ya pato ghafi la Taifa (GDP) kwa ajiliya shughuli za sayansi, teknolojia na ugunduzi. Hata hivyo,Serikali haijawahi kutenga kiasi hicho tangu imejiwekeautaratibu huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pato ghafi la Taifa kwa sasani dola za Kimarekani bilioni 52.09 ambazo ni sawa na shilingitrilioni 119.807. Hii ina maana kwamba ikiwa Serikali ingefuatautaratibu iliyojiwekea wa kutenga asilimia moja ya pato ghafila Taifa ingetakiwa kutenga shilingi trilioni 1.19. Fedhailiyotengwa kwa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)kwa ajili ya tafiti kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ni shilingibilioni 7.57 sawa na asilimia 0.00632. Hiki ni kiwango kidogokuliko vyote tangu Serikali hii ya Awamu ya Tano iingiemadarakani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi Rasmi ya Upinzaniinatoa angalizo kwa Serikali kuwa makini katika suala hili latafiti za kisayansi kwa kuwa kuna hatari ya Tanzaniakuendelea kuwa watumwa wa teknolojia ya nje jamboambalo litazidi kuweka Watanzania mbali katika kushirikikujenga uchumi wa nchi yao. Mwenendo huu wa kuendeleakutenga fedha kidogo kwa ajili ya tafiti hauna afya hatakidogo kwa mustakabali wa sayansi, teknolojia na ugunduzikatika Taifa. Hata ndoto za Serikali za kujenga uchumi waviwanda haziwezi kufikiwa ikiwa hakuna uwekezaji wakutosha katika tafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua umuhimu watafiti katika kukuza na kuendeleza sayansi na teknolojia,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kupitia CHADEMA imeelezabayana katika Sera yake ya Elimu, Sura ya 6.1 inayohusumfumo wa ugunduzi na ubunifu juu ya umuhimu wa tafiti.Sera hiyo inaeleza kama ifuatavyo: “CHADEMA inaaminikwamba msingi wa ugunduzi na ubunifu katika elimuunajengwa katika tafiti za kisayansi. Kwa hiyo, kwa kushirikianana sekta binafsi, CHADEMA itawekeza kikamilifu katika elimu

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

ya utafiti kuanzia elimu ya awali ili kumjengea mtoto uwezowa ubunifu”. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushiriki wa wadau katikauchambuzi wa Itifaki. Kumekuwa na desturi mbaya yakupitisha Maazimio ya Kuridhia Itifaki na Mikataba mbalimbaliya Kimataifa kwa ghafla ghafla bila kuwashirikisha kikamilifuwadau katika kufanya uchambuzi wa kina wa faida na aumadhara ya Itifaki au Mikataba husika na wakati mwinginebila hata kujali kama akidi ya Bunge imetimia au la katikakupitisha uamuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala gumu na lenyeuhitaji na utaalamu wa kisayansi kama hili linalohusu matumiziya bioteknolojia na madhara yake katika bioanuai, Serikaliiwe inafanya uchambuzi wa kina juu ya athari za kuridhiaItifaki hii na kuwapatia Waheshimiwa Wabunge seminaelimishi kwa Wabunge wote ili kuweza kulishawishi Bungekuridhia jambo ambalo wanauelewa nalo. Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni, haina hakika kama uchambuzi huoumefanyika na kama Wabunge wameshirikishwa kwakiwango cha kutosha. Jambo hilo ni hatari kwa kuwa Bungelinaweza kuridhia jambo ambalo litakuwa na madharabaadaye kwa nchi yetu kutokana na kukosa uelewa kuhusujambo lenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala ambayo itifaki hiihaitahusika yaani exemptions. Kifungu cha 16 cha Itifaki hiikinasema kwamba, naomba kunukuu: “Parties may provide,in their domestic law, for the following exemptions:

a. Act of God or force majeure; andb. Act of war or civil unrest.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa tafsiri isiyo rasmi nikwamba masharti ya Itifaki hii hayatatumika katika nyakatiza vita au machafuko ya kisiasa na nyakati za majanga yaasili. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kuwamakini sana na kifungu hiki kwa kuwa kinatoa kinga yakutowajibika kisheria au kulipa fidia kwa madhara

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

yatokanayo na matumizi ya bioteknolojia nyakati za vita aumachafuko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi zilizoendelea kisayansina kiteknolojia ambazo zimefikia hatua ya kutengeneza silahaza kibaolojia (biological weapons) zinaweza kutumia mwanyahuu kupenyeza silaha za kibiolojia ambazo kwa asili ni zamaangamizi makubwa (weapons of mass destruction) nawakakwepa kuwajibika kisheria na kulipa fidia kwa kisingiziokuwa ni wakati wa vita au machafuko. Katika mazingira kamahayo, nchi zilizo nyuma kimaendeleo zitabaki kuwa wahangawa matukio kama hayo (victims of circumstance).

Mheshimiwa Mwenyekiti, haki ya kuwa na stara(reservation) katika baadhi ya vifungu. Katika kifungu cha 19cha Itifaki hii ambayo inazitaka nchi wanachama kuridhiamkataba bila stara (no reservation may be made to thisSupplementary Protocol) ni wazi kuwa ibara hii ni yakuangaliwa kwa mapana zaidi.

MWENYEKITI: Kengele ya kwanza hiyo.

MHE. LATHIFAH H. CHANDE - MSEMAJI WA KAMBI RASMIYA UPINZANI BUNGENI KWA OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sote tunatambua katikaulimwengu wa sasa vita kubwa inayopiganiwa kitaalamu nakisayansi ni vita ya kibaiolojia (biological weapons). Yapomagonjwa mengi ambayo yamezua mijadala mikubwaduniani ambapo wengi wa wataalam wanaamini nimagonjwa ya kutengenezwa ambayo kitaalamuyanatokana na genetic modification.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mantiki hiyo, endaponchi tutaridhia vifungu ambavyo tayari vinaonyesha walakinikama ilivyo katika Ibara ya 6 ya Itifaki hii, tunaweza kujikutakatika hatari kubwa. Ni dhahiri wakati wa vita, silaha zakibaiolojia ambazo zinatengenezwa na virusi au bakteria,vinaweza kupenyezwa katika maji, hewa, mifugo, ardhi, miili

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

iliyokufa na kadhalika ambazo huchukua muda mrefukuweza kutafuta ushahidi au uthibitisho wa madhara. Hivyo,ni vyema Itifaki hii ikaongezewa muda wa kujumuishwa iliwataalamu mbalimbali wa sayansi waweze kuona namnabora zaidi ya kufanya kabla ya kuridhia Itifaki hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho; pamoja na ukwelikwamba Tanzania siyo kisiwa na kwamba tunalazimikakuingia katika mikataba na itifaki mbalimbali za kimataifa, nilazima kama Taifa tuingie kwenye mikataba hiyo tukiwa natahadhari hasa kwa vipengele ambavyo vinaweza kuwa naathari kwetu. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni, inashauri na kupendekeza kwamba tuendeleekupigania haki ya kuwepo kwa kifungu kinachotoa haki yakuwa na stara katika kuridhia Itifaki (reservation) hasa kwavifungu vile ambavyo tunaona wazi kwamba vinaweza kuwana madhara kwetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuhitimisha kwakusema kwamba ushiriki mpana wa wadau ni jambo muhimukwani huko ndiko tunakoweza kupata maoni na mawazombadala na kujua faida na hasara za kuridhia Itifaki hii aumkataba wowote wa kimataifa. Kwa sababu hiyo, Serikaliiwe inajipa muda wa kutosha wa kukusanya maoni kutokakwa wadau mbalimbali na kujiridhisha kwanza na maudhuiya Itifaki au Mkataba wowote kabla ya kuuleta Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, ni kuhusuutekelezaji wa Itifaki na Mikataba ya kimataifa kwa kutungasheria za ndani za kusaidia utekelezaji huo. Imekuwa ni desturiya nchi yetu kwa miaka mingi sasa ya kuridhia Mikataba auItifaki za Kimataifa na kutozitekeleza. Hivyo ni rai ya KambiRasmi ya Upinzani…

MWENYEKITI: Sekunde 10.

MHE. LATHIFAH H. CHANDE - MSEMAJI WA KAMBI RASMIYA UPINZANI BUNGENI KWA OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Ahsante.

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo ni rai ya Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni kwa Serikali kuleta haraka iwezekanavyoMuswada wa sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya ndaniya namna ya kuwajibika kisheria na kulipa fidia kwa walewote wanaohusika na matumizi ya bioteknolojia kwa lengola kulinda na kuhifadhi bionuai na mazingira kwa ujumla wake

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayoyote, naomba kuwasilisha. (Makofi)

MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSUAZIMIO LA BUNGE LA KURIDHIA ITIFAKI YA NYONGEZA YANAGOYA – KUALA LUMPUR KUHUSU UWAJIBIKAJI KISHERIA

NA FIDIA KUTOKANA NA MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEAKUTOKANA NA MATUMIZI YA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA

KAMA YALIVYOWASILISHWA MEZANI

“Yanatolewa kwa Mujibu wa Kanuni za kudumu za Bungeya 53(6) (c)

A. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, Bayoteknolojia ya kisasa inawezakuleta manufaa mengi. Lakini, kuna hofu ya kwamba inawezakuwa na madhara makubwa kwa bayoanwai na kwa afyaya binadamu. Kwa sababu hiyo, lengo la kuanzishwa kwaItifaki ya Nyongeza ya Nagoya – Kuala Lumpur lilikuwa nikuendeleza uhifadhi wa mazingira na kufanya matumiziendelevu ya bayoanwai (mtawanyiko, mwingiliano nakutegemeana baina ya viumbe hai na mazingira) ilikukabiliana na madhara yatokanayo na matumizi yabioteknolojia.

2. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa bayoanwai suala lakimataifa; na kwa kuwa athari zitokanazo na uharibifu wabayoanwai zinavuka mipaka ya nchi moja kwenda nyingineilionekana ni jambo muhimu na lenye afya katika utunzajiwa bayoanwai yenyewe pamoja na mazingira kwa ujumlawake kuweka kanuni na taratibu za kimataifa na hasa katikadhana ya uwajikaji kisheria na pia kulipa fidia ikiwa kutatokea

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

madhara yanayohusiana na Viumbe Hai vilivyofanyiwaMaboresho ya Vinasaba (Living Modified Organisms)

3. Mheshimiwa Spika, ni katika maudhui hayo ambapokifungu cha tatu cha itifaki hii kinaeleza bayana kwambaitifaki hii ya nyongeza itahusu madhara yatokanayo naViumbe Hai vilivyopandikizwa vinasaba tofauti kwa lengo lakuviboresha ambavyo katika kuishi kwake vinavuka mipakaya nchi moja kwenda nyinge.

4. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa itifaki hii, madharayanayotokana na matumizi ya bioteknolojia inayopelekeauharibifu wa mazingira na bayoanwai yatahesabiwa kuwani madhara ikiwa yatakuwa yanaonekana yanapimika nayenye athari kwa afya ya binadamu. Aidha, itifaki inaelekezakwamba ili mtu iweze kuwajibika na au kulipa fidia ni lazimamlalamikaji aweze kuthibitisha kuwa madhara hayo yanauhusiano wa moja kwa moja na viumbe vilivyofanyiwamaboresho ya vinasaba.

B. MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIA KABLA KURIDHIA ITIFAKI5. Mheshimiwa Spika, pamoja na ukweli kwamba itifakihii inaonekana kuwa na nia njema ya kupambana na kuzuiamadhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi yabioteknolojia; kwa kuweka kanuni za kimataifa za kuiwajibikajikisheria na kulipa fidia kwa madhara ya namna hiyo; KambiRasmi ya Upinzani Bungeni ingependa Serikali na Bungekuzingatia mambo yafuatayo kabla ya kuridhia itifaki hii:-

i. Uwezo wa Nchi katika Sayansi na Teknolojia6. Mheshimiwa Spika, kama ilivyoelezwa hapo awali,itifaki hii katika mawanda mapana inahusu kukabiliana namadhara yatokanayo na matumizi ya bioteknolojia nahususan upandkikizaji wa vinasaba katika viumbe hai. Hili nijambo linalohitaji uwezo mkubwa wa kisayansi na kiteknolojia.Tofauti na nchi zilizoendelea, nchi ambazo ziko nyumakimaendeleo ikiwemo Tanzania bado hazina uwezo mkubwakatika sayansi na teknolojia kuweza kufanya tafiti na gunduziza kisayansi kama vile ‘genetic engineering’ masualayanayofanana na hayo.

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

7. Mheshimwa Spika, kwa mujibu wa itifaki hii, ilimlalamikaji aweze kulipwa fidia kutokana na madhara yamatumizi ya bioteknolojia ni lazima aweze kuthibitishakwamba madhara hayo yanatokana na viumbevilivyofanyiwa maboresho ya vinasaba. Kwa manenomengine ni kwamba kama nchi itaathirika kutokana namatumizi ya bioteknolojia kutoka nje, ni lazima tuwe namaabara madhubuti na watafiti waliobobea katika sayansiili kuweza kugundua kama madhara tuliyopata yanauhusiano wa moja kwa moja na viumbe vilivyopandikizwavinasaba.

8. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniina mtazamo kwamba jambo hili litakuwa gumu sana hasakwa nchi yetu kutokana na Serikali kutoipa kipaumbele Tumeyetu ya Sayansi na Teknolojia. Kwa mfano; kwa mujibu waMpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17– 2020/21, Serikali ilijiwekea kiwango cha kutenga asilimiamoja (1%) ya pato ghafi la Taifa (GDP) kwa ajili ya shughuliSayansi, Teknolojia na Ugunduzi1 . Hata hivyo, Serikalihaijawahi kutenga kiasi hicho tangu imejiwekea utaratibuhuo.

9. Mheshimiwa Spika, pato ghafi la taifa kwa sasa ni dolaza Kimarekani bilioni 52.09 ambazo ni sawa na shilingi119,807,000,000,000 (trilioni 119.807) Hii ina maana kwambaikiwa Serikali ingefuata utaratibu iliyojiwekea wa kutengaasilimia moja ya Pato Ghafi la Taifa, ingetakiwa kutengashilingi 1, 198,070,000,000 (trilioni 1.198).

10. Mheshimiwa Spika, fedha iliyotengwa kwa Tume yaSayansi na Teknolojia - COSTECH kwa ajili ya tafiti kwa mwakawa fedha 2019/2020 ni shilingi bilioni 7.574 sawa na asilimia0.00632. Hiki ni kiwango kidogo kuliko vyote tangu Serikali hiiya awamu ya tano iingie marakani.

11. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inatoaangalizo kwa Serikali kuwa makini katika suala hili la tafiti zakisayansi kwa kuwa kuna hatari ya Tanzania kuendelea kuwawatumwa wa teknolojia ya nje jambo ambalo litazidi

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

kuwaweka watanzania mbali katika kushiriki kujenga uchumiwa nchi yao. Mwenendo huu wa kuendelea kutenga fedhakidogo kwa ajili ya tafiti hauna afya hata kidogo kwamustakabali wa Sayansi, Teknolojia na Ugunduzi katika taifa.Hata ndoto za Serikali za kujenga uchumi wa viwandahaziwezi kufikiwa ikiwa hakuna uwekezaji wa kutosha katikatafiti.

12. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa tafitikatika kukuza na kuendeleza Sayansi na Teknolojia; KambiRasmi ya Upinzani Bungeni kupitia CHADEMA imeelezabayana katika sera yake ya elimu sura ya 6.1 inayohusuMfumo wa Ugunduzi na Ubunifu juu ya umuhimu wa tafiti.Sera hiyo inaeleza kama ifuatavyo: “Chadema inaaminikwamba msingi wa ugunduzi na ubunifu katika elimuunajengwa katika tafiti za kisayansi. Kwa hiyo, kwakushirikiana na sekta binafsi, Chadema itawekeza kikamilifukatika elimu ya utafiti kuanzia elimu ya awali ili kumjengeamtoto uwezo wa ubunifu”.

ii. Ushiriki wa Wadau katika Uchambuzi wa Itifaki13. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na desturi mbaya yakupitisha maazimio ya kuridhia itifaki na mikataba mbalimbaliya kimataifa kwa ghafla ghafla, bila kuwashirikisha kikamilifuwadau katika kufanya uchambuzi wa kina wa faida na aumadhara ya itifaki au mikataba husika na wakati mwinginebila hata kujali kama akidi ya Bunge imetimia au la katikakupitisha uamuzi.

14. Mheshimiwa Spika, katika suala gumu na lenye kuhitajiutaalamu wa kisayansi kama hili linalohusu matumizi yabayoteknolojia na madhara yake katika bayoanwai; Serikaliiwe imefanya uchambuzi wa kina juu ya athari za kuridhiaitafaki hii na kuwapatia waheshimiwa wabunge seminaelimishi ili kuweza kulishawishi Bunge kuridhia jambo ambalowana uelewa nalo.

15. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungenihaina hakika kama uchambuzi huo umefanyika na kamawabunge wameshirikishwa kwa kiwango cha kutosha. Jambo

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

hilo ni hatari kwa kuwa Bunge linaweza kuridhia jamboambalo litakuwa na madhara baadaye kwa nchi yetukutokana na kukosa uelewa kuhusu jambo lenyewe.

iii. Masuala ambayo Itifaki hii Haitahusika (Exemptions)16. Mheshimiwa Spika, kifungu cha 16 cha itifaki hiikinasema kwamba; naomba kunukuu:-“Parties may provide, in their domestic law, for the followingexemptions:a. Act of God or force majeure; andb. Act of war or civil unrest.

17. Mhershimiwa Spika, kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwambamasharti ya itifaki hii hayatatumika katika nyakati za vita aumachafuko ya kisiasa na nyakati za majanga ya asili. KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuwa makini sanana kifungu hiki kwa kuwa kinatoa kinatoa kinga ya kutowajikakisheria au kulipa fidia kwa madhara yatokanayo na matumiziya bioteknolojia nyakati za vita au machafuko.

18. Mheshimiwa Spika, nchi zilizoendelea kisayansi nakiteknolojia ambazo zimefikia hatua ya kutengeneza silahaza kibaiolojia (biological weapons) zinaweza kutumiamwanya huu kupenyeza silaha za kibaiolojia ambazo kwaasil i ni za maangamizi makubwa (weapons of massdistruction) na wakakwepa kuwajibika kisheria au kulipa fidiakwa kisingizio kuwa ni wakati wa vita au machafuko. Katikamazingira kama hayo, nchi zilizo nyuma kimaendeleo zitabakikuwa wahanga wa matukio kama hayo (victims ofcircumstance).

iv. Haki ya Kuwa na Stara (Reservation) katika Baadhiya Vifungu19. Mheshimiwa Spika, katika kifungu cha 19 cha Itifakihii ambayo inazitaka nchi wanachama kuridhia mkataba bilastara ‘No reservation may be made to this SuplimentaryProtoco’ ni wazi kuwa Ibara hii ni ya kuangaliwa kwa mapanazaidi. Sote tunatambua katika ulimwengu wa sasa vita kubwainayopiganwa kitaalamu na kisayansi ni vita ya kibaiolojiayaani biological weapons. Yapo magonjwa mengi ambayo

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

yamezua mijadala mikubwa duniani ambapo wengi wawataalamu wanaamini ni magonjwa ya kutengenezwaambayo kitaalamu yamtokana na genetic modification.

20. Mheshimiwa Spika, kwa mantiki hiyo , endapo nchitutaridhia vifungu ambavyo tayari vinaonyesha walakinikama ilivyo kwa Ibara ya sita ya Itifaki hii tunaweza kujikutakatika hatari kubwa. Ni dhahiri wakati wa vita silaha zakibaolojia ambazo zinatengenezwa na virus au bakteriavinaweza kupenyezwa katika maji, hewa, mifugo, ardhi, miiliiliyokufa n.k ambazo huchukua muda mrefu kuweza kutafutaushahidi au uthibitisho wa madhara. Hivyo, ni vyema, Itifakihii kaongezewa muda wa kujumuisha zaidi wataalamumbalimbali wa sayansi ili kuona namna bra zaidi ya kufanyakabla ya kuridhia itifaki hii.

C. HITIMISHO21. Mheshimiwa Spika, pamoja na ukweli kwambaTanzania sio kisiwa, na kwamba tunalazimika kuingia katikamikataba na itifaki mbalimbali za kimataifa; ni lazima kamataifa tuingie kwenye mikataba hiyo tukiwa na tahadhari hasakwa vipengele ambayo vinaweza kuwa na athari kwetu. Kwasababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashauri nakupendekeza kwamba; tuendeleee kupigania haki yakuwepo kwa kifungu kinachotoa haki ya kuwa na stara katikakuridhia itifaki (reservation) hasa kwa vifungu vile ambayotunaona wazi kwamba vinaweza kuwa na madhara kwetu.

22. Mheshimiwa Spika, napenda kuhitimisha kwa kusemakwamba ushiriki mpana wa wadau ni jambo muhimu kwanihuko ndiko tunakoweza kupata maoni na mawazo mbadalana kujua faida na hasara za kuridhia itifaki au mkatabawowote wa kimataifa. Kwa sababu hiyo, Serikali iwe inajipamuda wa kutosha wa kukusanya maoni kutoka kwa wadaumbalimbali na kujiridhisha kwanza na maudhuri ya itifaki aumkataba wowote kabla ya kuuleta Bungeni.

23. Mwisho kabisa Mheshimiwa Spika, ni kuhusuutekelezaji wa itifaki na mikataba ya kimataifa kwa kutungasheria za ndani za kusaidia utekelezaji huo. Imekuwa ni desturi

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

ya nchi yetu kwa miaka mingi sasa ya kuridhia mikataba naitifaki za kimataifa na kutozitekeleza. Hivyo ni rai ya KambiRasmi ya Upinzani Bungeni kwa Serikali kuleta harakaiwezekanavyo Muswada wa Sheria kwa ajili ya kuwekamasharti ya ndani ya namna ya kuwajibika kisheria na kulipafidia kwa wale wote wanaohusika na matumizi yabioteknolojia kwa lengo la kulinda na kuhifadhi bayoanwaina mazingira kwa ujumla wake.

24. Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naombakuwasilisha.

Lathifah H. Chande (Mb)MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI

KATIKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS – MAZINGIRA11 September, 2019

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa namuita Waziri wa Kilimoili awasilishe Azimio la Kuridhia Itifaki ya Maendeleo ya Nchiza Kusini mwa Afrika kuhusu Kulinda Haki Miliki za Wagunduziwa aina mpya za Mbegu za Mimea.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naombakutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupitishaAzimio la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchiza kusini mwa Afrika kuhusu kulinda haki miliki za wagunduziwa aina mpya za mbegu za mimea (Protocal for Protectionof New Varieties of Plants (Plant Breeder’s Rights) in TheSouthern African Development Community – SADC).

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote napendakutoa shukrani zangu za dhati kwa Kamati ya Bunge chini yaMwenyekiti wake, Mheshimiwa Mahmoud Hassan Mgimwa,Mbunge wa Mufindi Kaskazini kwa ushauri walioutoa wakatiwa kujadili azimio hili. Napenda kulihakikishia Bunge lakoTukufu kwamba Azimio hil i l imezingatia ushauri namapendekezo ya Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, chimbuko la Azimio hili niMkataba wa Kuanzishwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

Kusini mwa Afrika (Southern Africa Development Community– SADC). Ibara ya 22 ya Mkataba wa SADC (SADC Treaty)wa mwaka 1992 umebainisha umuhimu wa kuandaa itifakiza kutoa miongozo ya ushirikiano kwenye masuala yamaendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi wanachama wa SADCziliandaa Itifaki ya SADC ya kulinda haki miliki za wagunduziwa aina mpya za mbegu za mimea mwezi Mei mwaka 2017.Itifaki hiyo iliidhinishwa na Mawaziri wa Katiba na Sheria wanchi za SADC Julai, 2017 na baadaye ilithibitishwa na Barazala Mawaziri wa Kilimo la SADC Agosti, 2017, Mjini Izulwini,Eswatini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo kuu la itifaki hii ni kutoamwongozo kuhusu kulinda haki miliki za wagunduzi wa ainampya za mbegu za mimea ili kuhamasisha ugunduzi wambegu mpya katika ukanda wa SADC.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa nchi zilizosainiItifaki hii ni saba ikiwemo Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaambayo ilisaini tarehe 18 mwezi Agosti mwaka 2019 wakatiwa mkutano wa nchi wanachama wa SADC uliofanyikaWindhoek, Namibia. Aidha, mnamo tarehe 31 mwezi Oktobamwaka 2018, Baraza la Mapinduzi la Zanzibar liliridhiamapendekezo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania kuwasilisha Itifaki hiyo Bungeni ili iweze kuridhiwa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Itifaki hii ina sehemu kumi;sehemu ya utangulizi (preamble) ina kipengele cha kwanzakinachotoa tafsiri ya maneno mbalimbali yaliyotumika ndaniya Itifaki hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya kwanza yenyeibara tano inabainisha malengo na mawanda ya Itifaki hiyo.Miongoni mwa malengo hayo ni kutoa hakimiliki kwawagunduzi wa aina mpya za mbegu za mimea il ikuhamasisha ugunduzi wa aina mpya za mbegu za mazao

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

ya kilimo na kuwawezesha kuwa na mfumo thabiti wa kulindahakimiliki za wagunduzi wa aina mpya za mbegu za mimea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya pili yenye ibaratano, ambapo Ibara ya 7 inaweka vigezo vya masharti yakuzingatia katika utoaji wa hakimiliki za wagunduzi wa ainampya za mbegu za mimea. Mbegu itakayohusika inapaswakuwa mpya inayotofautiana na nyingine (distinct) nainayofanana (uniformity) na isiyobadilika (stable).

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya tatu na ya nnezenye ibara 14 inabainisha utaratibu utakaotumika katikautoaji wa hakimiliki za wagunduzi wa aina mpya ya mbeguza mimea na namna ya kushughulikia maombi ya hakimiliki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya tano inahusumuda wa hakimiliki uliotolewa chini ya itifaki ambao utadumukwa miaka 25 kwa mazao ya miti ya jamii ya mizabibu namiaka 20 kwa mazao mengine. Aidha, sehemu hii inahusuhaki za wagunduzi waliopewa hakimiliki. Mgunduzi atakuwana haki ya kuidhinisha uzalishaji wa mbegu husika na kuruhusukuuzwa kwa mbegu husika, kusafirisha mbegu au kuhifadhimbegu husika. Vilevile sehemu hii inaweka zuio kuwa nikinyume cha sheria kwa mtu mwingine kutumia mbegu yenyehakimiliki kibiashara bila idhini ya mgunduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya sita, saba na yanane inaruhusu utoaji wa leseni na uhaulishaji wa hakimilikiambapo Ibara ya 34 inaweka masharti kwa ajili ya uhaulishajiwa hakimiliki. Aidha, Ibara ya 35 inatoa fursa ya kurudishahakimiliki ambapo Ibara ya 36 inatoa mwongozo wakubatilisha na Ibara ya 37 inahusu kufuta hakimiliki kwa mujibuwa itifaki hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya tisa na ya kumiinahusu masuala ya jumla ambapo Ibara ya 43 inahusuusuluhishi wa mgogogo (dispute settlement) na inabainishakuwa migogoro kati ya nchi wanachama wa SADC kuhusuutekelezaji wa Itifaki hiyo iliyoshindwa kupata suluhu kwamazungumzo itawasilishwa kwa Mawaziri wa Kilimo na

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

Usalama wa Chakula wa Nchi Wanachama wa SADC. Aidha,kama hakutakuwa na suluhu katika ngazi ya Mawaziri waKilimo na Usalama wa Chakula, suala hili litawasilishwa Barazala Usuluhishi wa Migogoro la SADC (SADC Tribunal).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 44 inaruhusu hakiya nchi wanachama kujitoa kwenye Itifaki hii. Kwa mujibuwa ibara hiyo, nchi mwanachama inaweza kujitoa baadaya kupita miezi 12 kutoka siku itakayotoa notice ya kujitoa.Pia inabainisha kuwa nchi inayotoa notice haitapata hakina faida zinazoambatana na Itifaki hii katika kipindi chakusubiri maamuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mapendekezoya kuridhiwa kwa Itifaki hii, Azimio hili linaweka sharti(reservation) itakayoiwezesha Tanzania kutolazimikakutekeleza masharti ya Itifaki ambayo yanaweza kuathirimaslahi ya Taifa. Utaratibu huu unatambuliwa kimataifakupitia sehemu ya pili ya Itifaki ya Vienna Convention on theLaw of Treaties uliosainiwa mwaka 1969 ambapo Tanzania nimojawapo ya nchi iliyoridhia kutumia mkataba huu tarehe12 mwezi Aprili, 1974.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia maelezo hayo,naomba sasa kuwasilisha Azimio la Kuridhia Itifaki ya Jumuiyaya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika Kuhusu KulindaHakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimeakama ifuatavyo:-

KWA KUWA, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimiongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleoya Nchi za Kusini mwa Afrika (The Southern AfricaDevelopment Community – SADC) kwa mujibu wa mkatabaulioanzishwa jumuiya hii ambao ulisainiwa na Wakuu wa NchiWanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za KusiniMwa Afrika mnamo mwaka 1992;

KWA KUWA, Mkataba huu unazitaka nchiwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

Mwa Afrika kushirikiana kwenye masuala yenye maslahi kwamaendeleo na ustawi wa wananchi wa nchi hizo;

KWA KUWA, Ibara ya 22 ya Mkataba wa Jumuiya yaMaendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika wa Mwaka 1992umebainisha umuhimu wa nchi wanachama kuandaa itifakizitakazotumika kutoa miongozo ya ushirikiano kwenyemasuala yenye maslahi kwa ajili ya maendeleo na ustawiwa wananchi wa nchi hizo;

NA KWA KUWA, mkataba huu unaelekeza kwambakila Itifaki itakayoandaliwa itaidhinishwa na Mkutano Mkuuwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya KusiniMwa Afrika na ikapaswa kusainiwa na kuridhiwa na nchiwanachama;

KWA KUWA, katika kutoa mwongozo kuhusu kulindahakimiliki za wagunduzi wa aina mpya ya mbegu za mimea(protection on new varieties of plants), nchi wanachama waJumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ziliandaa Itifakiya Kulinda Kakimiliki ya Wagunduzi wa Aina Mpya ya Mbeguza Mimea ya Mwezi Mei, 2017 ambao iliidhinishwa na Mawaziriwa Katiba na Sheria wa Nchi za SADC mwezi Julai, 2017 nabaadaye ilithibitishwa na Baraza la Mawaziri wa Kilimo waSADC mwezi Agosti, 2017;

KWA KUWA, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimwanachama wa Shirika la Biashara Duniani (World TradeOrganization) kuanzia tarehe 1 Januari, 1995 na kamamwanachama wa WTO inalazimika kutekeleza makubalianombalimbali yaliyoridhiwa na wanachama wa shirika hilo namiongoni mwa makubaliano hayo ni kuhusu makubalianoya utekelezaji wa masuala ya hakimiliki (trade related aspectof intellectual property rights);

KWA KUWA, Itifaki ya Kulinda Hakimiliki za Wagunduziwa Aina Mpya za Mbegu za Mimea (The Protocol ForProtection of New Varieties of Plants (Plant Breeder’s Rights)in the Sothern Africa Development Community – SADC)ilisainiwa mwezi Agosti, 2018 Jijini Windhoek, Namibia katika

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya yaMaendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika;

KWA KUWA, madhumuni ya Itifaki hiyo kamayalivyoainishwa katika Ibara ya 2 ni pamoja na (a) kuwezeshakuwa na mfumo thabiti wa kulinda hakimiliki za wagunduziwa aina mpya za mbegu za mimea; (b) kuhamasishaugunduzi wa aina mpya za mbegu za mazao ya kilimo; na(c) kutoa hakimiliki kwa wagunduzi wa aina mpya za mbeguza mimea;

KWA KUWA, Tanzania imesaini kuridhia na kutekelezamikataba mingine inayohusiana na hakimiliki za wagunduziwa aina mpya za mbegu za mimea ambao ni pamoja naMkataba wa Kimataifa wa Kulinda Hakimiliki za Wagunduziwa Aina Mpya za Mbegu za Mimea (UPOV Convention)ambao mikataba hii ni muhimu ikatekelezwa kwa pamoja;

NA KWA KUWA, kuridhiwa kwa Itifaki hii kutakuwa namatokeo chanya yafuatayo: (a) Kuweka mfumo wa kulindahakimiliki za wagunduzi wa mbegu unaokubalika nakutekelezwa katika nchi za SADC na hivyo kuimarishamahusiano ya nchi yetu na nchi nyingine; (b) Hakimilikiitakayotolewa chini ya Itifaki ya SADC itatambuliwa ndaniya nchi zote wanachama wa SADC na hivyo kuchocheauwekezaji katika nyanja ya utafiti na ugunduzi wa mbegumpya za sekta binafsi; (c) Kupanua wigo na kurahisishabiashara ya mbegu na hivyo kuhamasisha ushindani katikatasnia ya mbegu; (d) Kuhamasisha na kutoa fursa za utafitiunaolenga kuongeza uzalishaji wa mbegu mpya na hatimayekuwezesha wakulima kupata mbegu bora; (e) Kuongezaupatikanaji wa mbegu bora, kupunguza gharama zausafirishaji na hivyo kupunguza bei ya mbegu kwa mkulima;na (f) Kuwezesha upatikanaji wa mbegu zenye ukinzani wamagonjwa, wadudu wa mimea na kuhimili mabadiliko yatabianchi;

KWA HIYO BASI, kwa kuzingatia manufaa yatokanayona Itifaki hii kwa Tanzania na kwa nchi wanachama waJumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika na pia

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

umuhimu wa kuridhia Itifaki hii, Bunge hili kwa mujibu wa Ibaraya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaya mwaka 1977 linaazimia kuridhia Itifaki ya Hakimiliki zaWagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimea (Protocal forProtection of New Varieties of Plants (Plant Breeder’s Rights)in The Southern African Development Community – SADC)bila kulazimika kutekeleza masharti ya mkataba ambayoyanaweza kuathiri maslahi ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo,naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kuridhia Azimioninaloliwasilisha ili kuwezesha nchi yetu kunufaika na Itifakiya Hakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu zaMimea katika Ukanda wa SADC.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

MWENYEKITI: Ahsante. Hoja imeungwa mkono, sasanamwita Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji,atawasilisha Taarifa ya Kamati kuhusu Azimio hilo. Dakika 10.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA - MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie fursa hiikumshukuru Mwenyezi Mungu aliyeniwezesha kusimamambele ya Bunge lako Tukufu. Nakushukuru wewe binafsi kwakunipa nafasi ya kuwasilisha hii taarifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni ya53 (6) (b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari,2016 na kwa niaba ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu yaBunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, naomba kuwasilisha maonina ushauri wa Kamati kuhusu Azimio la Bunge la Kuridhia Itifakiya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika Kuhusu KulindaHakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimea.

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Itifaki hii inahusuNchi Wanachama zilizo Kusini Mwa Afrika (SADC), kabla yakuanza wasilisho langu, kwa niaba ya Kamati nachukuanafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe JosephMagufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwakuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC. Kamati inaaminikutokana na uwezo wake mahiri pamoja na mambomengine wagunduzi wa Tanzania na wenzao kutoka NchiWanachama wa SADC watanufaika na maudhui yalimokwenye Itikafi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu madhumuni namalengo; Ibara ya 2 ya Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo yaNchi za SADC kuhusu kulinda Hakimiliki za Wagunduzi wa AinaMpya za Mbegu:-

(a) Kuwezesha kuanzisha mfumo thabiti wa kulinda hakimilikiza wagunduzi wa aina mpya za mbegu za mimea;

(b) Kuendeleza na kuhamasisha ugunduzi wa aina mpya zambegu za mazao ya mimea kwa manufaa ya nchiwanachama katika Jumuiya ya SADC; na

(c) Kutoa hakimiliki kwa wagunduzi wa aina mpya za mbeguza mimea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi wa Itifaki. Itifakihii imegawanyika katika sehemu kuu 10 na ina jumla ya Ibara50.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya Kamati kufanyauchambuzi kwenye sehemu hizo za Itifaki, Kamati ilitakakujiridhisha kwenye maeneo ya msingi na hivyo kuhitajiufafanuzi kwenye maeneo hayo ambayo ni pamoja na:-

(i) Kwa nini nchi zenye uchumi mkubwa na ambazo zinafanyavizuri katika tasnia ya mbegu na kilimo kama Afrika Kusini,aidha nchi za Mauritius na Seychelles ambazo zina uchumimkubwa hazijasaini Itifaki hii?

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

(ii) Kuna uharaka gani wa kuridhia Itifaki hii wakati ni nchisaba tu kati ya nchi 15 Wanachama wa SADC ndizo zimesainiItifaki hii?

(iii) Je Itifaki hii haiwezi kusababisha ukiritimba kutoka katikamakampuni makubwa ya mbegu katika tasnia ya mbegu?

(iv) Je vituo vya Afrika kwa ajili ya masuala ya hakiubunifuvya ARIPO na PAIPO (Chini ya Umoja wa Afrika) haviwezikuingiliana na kusigana na Itifaki hii?

(v) Ni kwa kiasi gani uhuru wa mkulima mdogo katika uzalishajimbegu umezingatiwa kwenye Itifaki hii?

(vi) Ni kwa kiasi gani kama nchi tumewekeza katika tafiti zambegu ili kuweza kumudu ushindani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuliarifu Bungelako Tukufu kuwa Kamati imeridhishwa na ufafanuzi uliotolewana Serikali kuhusu hoja zilizoibuliwa na WaheshimiwaWabunge. Aidha, Kamati ilifanya kikao na wagunduzi wawatafiti za mbegu waliotoka Serikalini na katika Sekta Binafsiambao Itifaki hii inawagusa moja kwa moja. Kupitia mjadalahuu wadau hao waliihakikishia Kamati kuwa kuridhiwa kwaItifaki hii kutakuwa na manufaa yafuatayo: -

(1) Serikali itanufaika na fedha ilizowekeza kwenye utafiti;

(2) Uwepo wa mrabaha utakaopatikana kutokana na gawioambapo Serikali itapata mapato yatakayotokana na gawio;

(3) Kuongeza motisha kwa Watafiti;

(4) Kuongezeka kwa ushindani na ubunifu miongoni mwawafatiti;

(5) Kutarahisisha upatikanaji wa mbegu bora, mpya kwaharaka;

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

(6) Kuridhiwa kwa Itifaki hii kutaongeza uzalishaji wa chakulakwa kuwa wakulima watapata mbegu bora na mpya nahivyo kuhakikishia Taifa usalama wa chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kufanyauchambuzi wa Azimio la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya yaMaendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika Kuhusu KulindaHakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimea,Kamati inakubaliana na dhamira njema ya Itifaki hii kwa Taifana kwa Wagunduzi wa ndani. Pamoja na dhamira njemailiyopo, Kamati ina maoni na ushauri ufuatao:-

Moja, Serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya vituovya utafiti ili kuwezesha watafiti kufanya tafiti kwa kutumiafedha zetu za ndani na siyo kama ilivyo sasa ambapo tafitinyingi hufanyika kwa kutegemea fedha kutoka kwa wadauwa maendeleo. Bila ya kuwezesha vituo vya utafiti nawagunduzi wa mbegu, Itifaki hii inaweza kunufaishawagunduzi wa mbegu kutoka Mataifa mengine na sisi kubakikuwa watazamaji tu. (Makofi)

Pili, ni muhimu kwa sera na sheria zinazohusiana nambegu zikafanyiwa mapitio ili ziweze kuendana na maudhuiya Itifaki hii.

Tatu, Serikali ifanye mapitio na maboresho ya Sheriaya Kulinda Hakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbeguza Mimea ya Mwaka 2012 ili sheria hii iweze kujumuishamaudhui ya Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za KusiniMwa Afrika na kurekebisha baadhi ya upungufu uliokokwenye sheria ikiwa ni pamoja na kipengele kinachoelezahakimiliki za Wagunduzi wa aina mpya za mbegu kutovukamipaka ya Tanzania.

Nne, Serikali iweke mazingira wezeshi kwa ajili yakuvutia uzalishaji wa mbegu nchini. Uzalishaji mbegu, pamoja

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

na mambo mengine yafuatayo kutaongeza motisha kwawagunduzi wa mbegu kugundua aina mpya za mbegu,kuokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumika kuagiza mbegunje ya nchi, kiasi cha shilingi bilioni 860 hutumika kuagizambegu kutoka nje ya nchi na kuongezeka kwa mapato yaSerikali, ajira na ujuzi kwa wananchi wazawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, napendakukushukuru kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha maoni naushauri wa Kamati kwa niaba ya Wajumbe wa Kamati yaKudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kumpongeza nakumshukuru Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Japhet HasungaMbunge, Manaibu Waziri Mheshimiwa Omary MgumbaMbunge na Mheshimiwa Hussein Bashe Mbunge, na MakatibuWakuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe naProfesa Siza Tumbo pamoja na Wataalam wote wa Wizaraya Kilimo kwa ushirikiano walioutoa wakati Kamati ilipokuwaikichambua Azimio hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee nawashukuruwadau wote waliotoa michango kwa maandishi na kwakufika katika mbele ya Kamati. Kwa dhati kabisa napendakuwashukuru Wajumbe wa Kamati kwa ushirikiano namichango yao waliyoitoa wakati wa kuchambua na kujadiliAzimio hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumshukuru Katibuwa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai, Kaimu Mkurugenzi waIdara ya Kamati za BungeNdugu Michael Chikokoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo,naliomba sasa Bunge lako lipokee na lijadili na liridhie Azimiola Bunge la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchiza Kusini mwa Afrika kuhusu Kulinda Hakilimiki za Wagunduziwa Aina Mpya za Mbegu za Mimea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja nanaomba kuwasilisha. (Makofi)

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

TAARIFA KUHUSU AZIMIO LA BUNGE LA KURIDHIA ITIFAKI YAMAENDELEO YA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA KUHUSU

KULINDA HAKIMILIKI ZA WAGUNDUZI WA AINA MPYA ZAMBEGU ZA MIMEA(THE PROTOCOL FOR PROTECTION OF NEW

VARIETIES OFPLANT [PLANT BREEDER‘S RIGHTS] INTHE SOUTHERN AFRICAN DEVELOPMENT

COMMUNITY – SADC) – KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI_____________

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (6) (b) yaKanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016. Kwaniaba ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji, naomba kuwasilisha Maoni na Ushauri waKamati kuhusu Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki yaMaendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika Kuhusu KulindaHakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu zaMimea(The Protocol for Protection of New Varieties of Plant[Plant Breeder‘s Rights] In The Southern African DevelopmentCommunity – SADC).

Mheshimiwa Spika,kwa kuwa Itifaki hii inahusu NchiWanachama zilizo Kusini Mwa Afrika (SADC), kabla ya kuanzawasilisho langu, kwa niaba ya Kamati naomba kuchukuanafasi hii kumpongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuchaguliwakuwa Mwenyekiti wa Nchi za SADC. Kamati inaaminikutokana na uwezo wake mahiri pamoja na mambomengine Wagunduzi wa Tanzania na wenzao kutoka nchiWanachama wa SADC watanufaika na maudhui yalimokwenye Itikafi hii.

Mheshimiwa Spika, Nyongeza ya Nane Kifungu cha 7(1) (b)ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016, inazipaKamati za Kisekta ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge yaKilimo, Mifugo na Maji jukumu la kushughulikia Miswada yaSheria, Maazimio na Mikataba inayopendekezwa kuridhiwana Bunge iliyo chini ya Wizara inazozisimamia. Aidha, jukumuhili pia ni jukumu la Kikatiba chini ya Ibara ya 63(3)(e) ya

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka1977.

Mheshimiwa Spika, tarehe 12 Novemba, 2018 uliiletea Kamatiya Kilimo, Mifugo na Maji kazi ya kushughulikia Azimio laBunge la kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchiza Kusini Mwa Afrika (The Protocol For Protection of NewVarieties of Plant [Plant Breeder‘s Rights] In The SouthernAfrican Development Community – SADC) kuhusu KulindaHakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimeakama lilivyowasilishwa na Serikali ili Kamati iweze kuchambuamapendekezo ya Azimio husika na hatimae kutoa maoni naushauri kwa Serikali.

Mheshimiwa Spika, kama il ivyo ada, Kamati i l ianzakuchambua Itifaki husika kwa kushirikiana na wadau waliofikambele ya Kamati na wale waliotuma maoni yao kwa njia yamaandishi i l i kufahamu madhumuni na faidazinazoambatana na kuridhiwa kwa Itifaki hii. Hata hivyo,baada ya kushauriana na Serikali ilibainika kuna umuhimuwa kuongeza muda ili Kamati iweze kufanyia kazi zaidi ilimatokeo chanya yaliobainishwa kwenye Itifaki hii yawezekuleta maslahi kwa wananchi wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, kwa hekima na busara ulir idhiakuongezwa kwa muda wa kushughulikiwa kwa Itifaki hiiambapo tarehe 28 Agosti, 2019 uliiletea tena Kamati kazi yakushughulikia Itifaki tajwa. Tarehe 04 Septemba, 2019 Kamatiilianza kazi ya kushughulikia Itifaki hii ambalo liliwasilishwambele ya Kamati na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. OmaryMgumba, (Mb).

2.0 MADHUMUNI/MALENGO YA ITIFAKI

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 2 ya Itifaki ya Jumuiya yaMaendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) kuhusukulinda Hakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu zaMimea ina madhumuni ya msingi yafuatayo: -

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

(a) Kuwezesha kuanzisha mfumo thabiti wa kulindahakimiliki za Wagunduzi wa aina mpya za mbegu za mimea;

(b) Kuendeleza na kuhamasisha ugunduzi wa aina mpyaza mbegu za mazao ya mimea kwa manufaa ya nchiwanachama katika Jumuiya ya SADC; na

(c) Kutoa Hakimiliki kwa Wagunduzi wa aina mpya zambegu za mimea.

3.0 UCHAMBUZI WA ITIFAKIMheshimiwa Spika, Itifaki hii imegawanyika katika sehemukuu kumi (10) na ina jumla ya Ibara 50 ambazo maudhui yakeni kama ifuatavyo: -

Sehemu ya Kwanza

Ibara ya 1 ya Itifaki inahusu masharti ya jumla ambayoinaanzia Ibara ya 2 hadi ya 6.

Ibara ya 2 inahusu madhumuni ya Itifaki ambayo yameelezwahapo juu.

Ibara ya 3 inahusu mawanda na maeneo ambayo itifaki hiiitatumika.

Ibara ya 4 ya itifaki inaanzisha Ofisi ya Hakimiliki za Wagunduziwa Mbegu za Mimea katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchiza Kusini mwa Afrika (SADC) ambayo itakuwa na jukumu lakusimamia utekelezaji wa itifaki hii.

Ibara ya 5 ya itifaki inaanzisha Kamati ya Ushauri ya SADCkwa ajili ya kuishauri Ofisi ya Msajili wa Hakimiliki za Wagunduziwa Mbegu za Mimea katika mambo ya jumla na mahsusikuhusiana na utekelezaji wa majukumu yake na mambomengine yanayohusiana na itifaki hii.

Ibara ya 6 inaanzisha Rejista ya Usajili wa Hakimiliki kwaWagunduzi wa Mbegu za Mimea ambayo itatunzwa naMsajili.

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

Sehemu ya Pili

Mheshimiwa Spika, sehemu hii ya itifaki inaanzia Ibara ya 7hadi 11na inahusu masharti ya utoaji wa Hakimiliki za Ugunduziambapo ibara hizo zimefafanua kwa undani vigezovitakavyotumika kutoa hakimiliki hizo.

Sehemu ya Tatu

Mheshimiwa Spika, sehemu ya tatu ya itifaki imeanzia Ibaraya 12 hadi 22 ambapo ibara hizi zimeweka utaratibu wa jinsiya kutuma maombi ya kupewa hakimiliki ya ugunduzi wambegu za mimea. Aidha, ibara hizi zimefafanua kiundaniwatu wanaostahili kuomba hakimiliki, utaratibu wa kutumamaombi, haki ya kipaumbele katika kushughulikia maombipamoja na mambo mengine yanayoendana na maombi yahakimiliki.

Sehemu ya Nne

Mheshimiwa Spika, sehemu ya nne inaanzia Ibara ya 23 hadi25 na inaeleza vigezo ambavyo vitatumika katika kufikiriamaombi ya utoaji hakimili.

Sehemu ya Tano

Mheshimiwa Spika, sehemu hii inahusu Ibara ya 26 hadi 31nainaeleza kuhusu haki za mmiliki wa hakimiliki.Aidha ukomo wamuda wa matumizi ya hakimiliki kwa mbegu za mitiumeelezwa utakuwa miaka ishirini na tano (25) tangu siku yakutolewa na kwa mbegu nyingine za mimea ukomo wahakimiliki utakuwa miaka ishirini (20). Hata hivyo ukomo wamuda kwa mbegu nyingine za mimea, unaweza kuongezwana Msajili kutokana na mapendekezo yatakayotolewa kwakena Kamati inaweza kuongeza muda usiozidi miaka mitano(5).

Sehemu ya SitaMheshimiwa Spika, sehemu hii ambayo inaIbara ya 32 na 33,inaelezea kuhusu utoaji wa leseni zinazohusiana na uzalishaji

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

wa mbegu za mimea kutoka kwa mmiliki wa hakimiliki yaWagunduzi wa mbegu za mimea.

Sehemu ya Saba

Mheshimiwa Spika, sehemu hii inaIbara moja ambayo ni ya34 na inaweka masharti kuhusu uhamishaji wa hakimiliki yaWagunduzi wa mbegu za mimea.

Sehemu ya Nane

Mheshimiwa Spika, sehemu hii inaIbara ya 35, 36, na 37 nainaeleza utaratibu wa kurudisha, kubatilisha na kufutwa kwahakimiliki.

Sehemu ya Tisa

Mheshimiwa Spika, sehemu hii inaIbara moja ya 38 ambayoinaanzisha Bodi ya Rufaa kwa ajili ya rufaa kwa mtu ambaehataridhika na maamuzi ya Msajili.

Sehemu ya KumiMheshimiwa Spika, sehemu ya kumi inaanzia Ibara ya 39 hadi50 inaelezea masharti ya jumla ikiwemo utungaji wa Kanunina taratibu za uendeshaji wa Itifaki, kulinda aina za mbeguambazo zilikuwepo kabla ya Itifaki hii, masuala ya fedha,marekebisho ya Itifaki hii, utatuzi wa migogoro, utaratibu wanchi kujiondoa katika Itifaki hii, utiaji saini wa Itifaki hii, utaratibuwa kuridhia, kuanza kutumika kwa Itifaki, uwasilishwaji wa HatiIdhini na Utekelezaji wa Itifaki.

Mheshimiwa Spika, baada ya Kamati kufanya uchambuzikwenye sehemu hizo za Itifaki, Kamati ilitaka kujiridhishakwenye maeneo ya msingi na hivyo kuhitaji ufafanuzi kwenyemaeneo hayo ambayo ni pamoja na:-

i) Kwa nini nchi zenye uchumi mkubwa na ambazo zinafanyavizuri katika tasnia ya mbegu na kilimo kama Afrika kusini,Aidha nchi za Mauritius na Shelisheli ambazo zina uchumimkubwa hazijasaini Itifaki hii?.

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

ii) Kuna uharaka gani wa kuridhia Itifaki hii wakati ni nchi saba(7) tu kati ya nchi kumi na tano (15) wanachama wa SADCndio zimesaini Itifaki hii?.

iii) Je Itifaki hii haiwezi kusababisha ukiritimba (monopoly)kutoka katika makampuni makubwa ya mbegu katika tasniaya mbegu?.

iv) Je vituo vya Afrika kwa ajili ya maswala ya hakiubunifuvya ARIPO (Harare-Zimbabwe), OAPI (Africa Magharibi) naPAIPO (Chini ya Umoja wa Afrika) haviwezi kuingiliana nakusigana na Itifaki hii?.

v) Ni kwa kiasi gani uhuru wa mkulima mdogo katika uzalishajimbegu umezingatiwa kwenye Itifaki hii?.

vi) Ni kwa kiasi gani kama nchi tumewekeza katika tafiti zambegu ili kuweza kumudu ushindani wa nchi Wanachamawa SADC katika ugunduzi, uzalishaji na biashara ya mbegu;

vii) Ni kwa kiasi gani Itifaki hii imezingatia utofauti wamaendeleo ya kiuchumi uliko miongoni mwa nchiwanachama wa SADC? na

viii) Je kuna ulazima gani wa kuridhia Itifaki ya SADC wakatikatika Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) ambayo Tanzaniani mwanachama haina utaratibu wa Kulinda Hakimiliki zaWagunduzi wa Mbegu?.

Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako kuwaKamati imeridhishwa na ufafanuzi uliotolewa na Serikalikuhusu hoja zilizoibuliwa na Wabunge. Aidha, Kamati ilifanyakikao na Wagunduzi na Watafiti wa mbegu waliotokaSerikalini na katika Sekta Binafsi ambao Itifaki hii inawagusamoja kwa moja. Kupitia mjadala huu wadao hao waliiakikishiaKamati kuwa kuridhiwa kwa Itifaki hii kutakuwa na manufaayafuatayo: -• Serikali itanufaika na fedha ilizowekeza kwenye utafiti wambegu kwa kulinda kazi za utafiti wa mbegu zilizozalishwana wataalamu wake;

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

• Uwepo wa mrabaha utakaopatikana kutokana na gawioambapo Serikali itapata mapato yatakayotokana na gawio,mgunduzi atapata gawio na kiasi kingine cha mrabahakitatumika kuendeleza ugunduzi wa aina mpya za mbegu;

• Kuongeza motisha kwa Watafiti na Wagunduzi wa mbeguna hivyo kuongeza uzalishaji wa mbegu ambazo zitatumikanchini na zingine kuuzwa nje ya nchi na hivyo kuongezamapato ya Serikali pamoja na kupunguza gharama kubwaya fedha za kigeni zinazotumika kuagiza mbegu nje ya nchi;

• Kuongezeka kwa ushindani na ubunifu miongoni mwaWafatiti/Wagunduzi wa mbegu

• Kutarahisisha upatikanaji wa mbegu bora na mpya kwaharaka na

• Kuridhiwa kwa Itifaki hii kutaongeza uzalishaji wa chakulakwa kuwa wakulima watapata mbegu bora na mpya nahivyo kuhakikishia taifa usalama wa chakula.

4.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spika, baada ya kufanya uchambuzi wa Azimiola Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusinimwa Afrika Kuhusu Kulinda Hakimiliki za Wagunduzi wa AinaMpya za Mbegu za Mimea, Kamati inakubaliana na dhamiranjema ya Itifaki hii kwa Taifa na kwa Wagunduzi wa ndani.Pamoja na dhamira njema iliyopo, Kamati ina maoni naushauri ufuatao: -

(a) Serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya vituo vya utafitiili kuwezesha watafiti kufanya tafiti kwa kutumia fedha zetuza ndani na sio kama ilivyo sasa ambapo tafiti nyingihufanyika kwa kutegemea fedha kutoka kwa wadau wamaendeleo. Bila ya kuwezesha vituo vya utafiti na wagunduziwa mbegu, Itifaki hii inaweza kunufaisha wagunduzi wambegu kutoka mataifa mengine na sisi kubaki kuwawatazamaji tu.

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

(b) Ni muhimu kwa Sera na Sheria zinazohusiana na Mbeguzikafanyiwa mapitio ili ziweze kuendana na maudhui ya Itifakihii.

(c) Serikali ifanye mapitio na maboresho ya Sheria ya KulindaHakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimeaya Mwaka 2012 ili Sheria hii iweze kujumuisha maudhui yaItifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrikana kurekebisha baadhi ya mapungufu yaliyoko kwenye Sheriaikiwa ni pamoja na kipengele kinachoeleza Hakimiliki zaWagunduzi wa aina mpya za mbegu kutovuka mipaka yaTanzania.

(d) Serikali iweke mazingira wezeshi kwa ajili ya kuvutiauzalishaji mbegu nchini. Uzalishaji mbegu, pamoja na mambomengine utaongeza:-

• Motisha kwa wagunduzi wa mbegu kugundua aina mpyaza mbegu;

• Kuokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumika kuagiza mbegunje ya nchi – kiasi cha shilingi bilioni 860 hutumika kuagizambegu kutoka nje ya nchi na

• Kuongezeka kwa mapato ya Serikali, ajira na ujuzi kwawananchi wazawa.

5.0 HITIMISHOMheshimiwa Spika, napenda kukushukuru kwa kunipa nafasiya kuwasilisha Maoni na Ushauri wa Kamati kwa niaba yaWajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugona Maji.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kumpongeza nakumshukuru Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb),Manaibu Waziri Mhe. Omary Mgumba (Mb) na Mhe. HusseinBashe (Mb), Makatibu Wakuu wa Wizara ya Kilimo, MhandisiMathew Mtigumwe na Prof. Siza Tumbo pamoja naWataalamu wote wa Wizara ya Kilimo kwa ushirikianowalioutoa wakati Kamati ilipokuwa ikichambua Azimio hili.

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

Mheshimiwa Spika, kipekee nawashukuru wadau wotewaliotoa michango yao kwa maandishi na kwa kufika mbeleya Kamati. Michango yao ilisaidia kuijengea uwezo Kamatina kuwawezesha Wajumbe kuwa na uelewa mpanakuhusiana na Azimio hili.

Mheshimiwa Spika, kwa dhati kabisa napenda kuwashukuruWajumbe wa Kamati kwa ushirikiano na michango yaowaliyoitoa wakati wa kuchambua na kujadili Azimio hili.Naomba kuwatambua kwa kuwataja majina kamaifuatavyo: -

1. Mhe. Mahmoud Hassan Mgimwa Mb Mwenyekiti2. Mhe. Dkt. Christine G. Ishengoma, Mb M/Mwenyekiti3. Mhe. Dkt. Mary Michael Nagu, Mb Mjumbe4. Mhe. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo, Mb “5. Mhe. Eng. Edwin A. Ngonyani, Mb “6. Mhe. Katani Ahmad Katani Mb “7. Mhe. Khadija Hassan Aboud, Mb “8. Mhe. Haroon Mulla Pirmohamed, Mb “9. Mhe. Ritta Enespher Kabati, Mb “10. Mhe. Mattar Ali Salum, Mb “11. Mhe. Lucy Simon Magereli, “12. Mhe. Justin Joseph Monko “13. Mhe. Omar Abdallah Kigoda, Mb “14. Mhe. Anna Richard Lupembe, Mb “15. Mhe. Pascal Yohana Haonga “16. Mhe. Salim Mbaraku Bawazir Mb “17. Mhe. Deo Kasenyenda Sanga, Mb “18. Mhe. Devotha Methew Minja, Mb “19. Mhe. Haji Ameir Haji, Mb “20. Mhe. Haji Khatib Kai, Mb “21. Mhe. Sikudhani Yasini Chikambo, Mb “22. Mhe. Juma Ali Juma, Mb “23. Mhe. Emmanuel Papian John, Mb “24. Mhe. Kunti Yusuph Majala, Mb “25. Mhe. Anthony Calist Komu, Mb “26. Mhe. Jitu Vrajlal Soni, Mb “

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

Mheshimiwa Spika, mwisho napenda kumshukuru Katibu waBunge, Ndg. Stephen Kagaigai, Kaimu Mkurugenzi wa Idaraya Kamati za BungeNdg. Michael Chikokoto kwa kuisaidiana kuiwezesha Kamati kutekeleza majukumu yake kwa weledimkubwa. Kwa namna ya kipekee naishukuru Sekreterieti yaKamati ambao ni Ndg. Virgil Mtui na Ndg. Rachel Nyegapamoja na msaidizi wa Kamati Ndg. Mwimbe John kwakuihudumia Kamati ikiwa ni pamoja na kukamilisha taarifa hiikwa wakati.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naliomba sasaBunge lako lipokee, lijadili na liridhie Azimio la Bunge laKuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za KusiniMwa Afrika kuhusu Kulinda Hakilimiki za Wagunduzi wa AinaMpya za Mbegu za Mimea.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na naombakuwasilisha.

Dkt. Christine G. Ishengoma, (Mb)M/MWENYEKITI,

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO,MIFUGO NA MAJI

11 Septemba, 2019

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa namuita Msemaji waKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Kilimo atatoamaoni ya Upinzani kuhusu Azimio hilo, MheshimiwaHaongadakika kumi.(Makofi)

MHE. PASCAL Y. HAONGA - MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KILIMO:Mheshimiwa Mwenyekiti, Maoni ya Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni kuhusu Azimio la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya yaMaendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika kuhusu KulindaHakimiliki za Ugunduzi wa aina mpya za Mbegu za Mimea(The Protocol for Protection of New Varieties of Plants (PlantBreeder’s Rights) in the Southern African DevelopmentCommunity-SADC).

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Azimio hili nidhahiri Tanzania haiwezi kujitenga na Mataifa au Jumuiyanyingine hasa katika kushirikiana kwenye masuala mbalimbaliya kiuchumi na kijamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuliona hil i laushirikiano na kuzidisha mahusiano baina ya Mataifa, Katibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 63(3),(e)inataja kuwa miongoni kwa kazi za Bunge ni “Kujadili naKuridhia Mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muunganona ambayo kwa Masharti yake inahitaji Kuridhiwa”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, japokuwa ni jukumu laBunge letu kufanya kazi hiyo, ni muhimu sana kufahamuumuhimu wa mbegu katika mustakabali mzima wa jamii yetuya Kitanzania na pia katika uchumi wetu. Hatupingani naukweli kuwa uzalishaji mazao unahitaji mbegu bora, lakini niukweli kwamba uzalishaji huo wa mbegu bora unaweza piakupatikana ndani ya jamii zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo kuja kwa Azimio hili nifursa kubwa kwa nchi yetu katika kuongeza jitihada za tafitijuu ya mbegu mbalimbali, kupanua masoko ya mbeguduniani hususani katika nchi za SADC, kuruhusu watafiti wetu,wagunduzi na wabunifu kupata hakimiliki za mbegu aumimea wanayoigundua, kuongeza ubora wa mbegu zetuna zaidi ya yote kuongeza ubora wa mbegu zetu za asili ilikupata mazao bora zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuwa moja yamalengo katika Azimio hili linasisitiza mashirikiano baina yanchi wanachama na uwekaji wa mifumo ya kisheria katikakutoa hakimiliki kwa wagunduzi bado ndani ya mkataba huuhaujazungumzia ipasavyo au kuangalia maslahi mapana yakundi kubwa la wananchi ambao ni wakulima wadogowadogo ambao pia wana aina zao za mbegu kulingana namazingira yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kuwa pamoja namalengo mazuri ya mkataba huu ambayo yanalenga

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

kuwasaidia na kuwalinda wagunduzi wa mbegu mbalimbalini ukweli usiopingika kuwa umilikishaji wa mbegu kwawagunduzi unatoa maana kwamba mnyororo mzima wambegu unakuwa ni kwa faida ya wagunduzi waliosajiliwa nakutambuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti,jambo hili la umiliki binafsilinaondoa utamaduni wa wakulima wadogo hususanimaeneo ya vijijini kuweza kuendelea na utamaduni wakubadilishana na kuuziana mbegu. Huu ni utamaduni ambaoumekuwa ukitumika kwa miaka mingi. Tukumbuke kuwakundi hili la wakulima wadogo ndilo kundi la wazalishajiwakubwa wa mazao ya chakula na yanayoingizwa mataifayetu katika nchi wanachama wa SADC.

Mheshimiwa Mwenyekiti, endapo, utaratibu huu wakutumia haki miliki usiporatibiwa vyema tutakuta wananchiwetu hususani vijijini wakipata tabu sana. Zipo jamii zenyeaina za upekee wa mbegu kama vile maharage, karangana kadhalika ambazo kimsingi kama jamii zinapaswa kupewahakimiliki kunufaika ni vyema kama Taifa tukaliangalia jambohilo kwa manufaa ya wananchi walio wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti,maslahi ya nchi nilazimayaanzie kwenye maslahi ya wananchi, kama jambo lolotetunalolifanya hapa Bungeni halina maslahi mapana kwawananchi walio wengi ni dhahiri kwamba jambo hilohalitakuwa na maslahi yoyote kwa nchi pia.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haki ya Mkulima na Jamiikatika kumiliki mbegu.Katika nchi nyingi zinazoendeleazimekuwa zikiweka masharti ya aina za mazao wanayohitajikuyanunua. Hivyo, nchi hizo zimekuwa ndiyo wazalishajiwakubwa wa mbegu ambazo ndizo huingia katika nchizinazoendelea (yaani ulimwengu wa tatu) bila kujali aina yamazingira ikiwa ni pamoja na udongo, hali ya hewa nakadhalika mbegu hizo zimekuwa zikiuzwa kiholela kitendoambacho kimeleta athari kubwa kwa mbegu zetu za asili,na pia athari za kimazingira. (Makofi)

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii yote ni kutokana naMataifa mengi barani Afrika kukosa haki miliki za mazao yao,kutangaza na kuongeza thamani ya mbegu zao ili ziwezekuwanufaisha wananchi walio wengi ambao ni wakulimawadogo. Pamoja na mabadiliko makubwa yanayotokeakatika sekta ya kilimo hususani masuala ya upatikanaji nauhifadhi wa mbegu bado nchi nyingi Barani Afrika hutumiamfumo wa asili ambao umejikita zaidi katika mila, desturi natamaduni zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti,ni ukweli kwamba katikamfumo asilia mbegu huchaguliwa mapema kutoka shambanina kuhifadhiwa kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo. Taalumana teknolojia inayotumika katika uchaguzi wa mbegu kutokashambani, utunzaji wa mbegu hizo na njia zinazotumika katikakuuziana au kupeana ni jambo ambalo ni lazima liangaliwevema katika mfumo mzima wa kisheria wa umiliki wa rasilimaliza jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wazi kuwa tumechelewasana katika kuhakikisha mbegu zetu za asili zinaboreshwa nazinapata haki miliki ili kuhakikisha wakulima wanapata mazaomengi na bora. Lakini ni lazima tuweze kutambuachangamoto zitakazokuja na mkataba huu kwa kuwawakulima watalazimika kuendana na mahitaji ya soko. Nidhahiri kuwa mkataba huu utachocheza tafiti nyingi zambegu na hivyo mbegu za asili zitatoweka. Kutokana naumaskini au ugumu wa maisha ya wakulima wetu nchini,wengi wao watajikuta wanashindwa kumudu kilimo kutokanana kuongezeka kwa mahitaji katika kilimo ikiwa na maanaya manunuzi ya mbegu na madawa na mahitaji yaumwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti,sambamba na hili ni lazimaSerikali iweke mfumo mzuri ambao jamii nzima itawezakunufaika endapo kama jamii hiyo imeweza kugunduambegu za aina fulani. Hii ikiwa na maana kwamba jamiiikishirikiana kwa pamoja wanaweza kuwa mbeguwaliyoifanyia utafiti kulingana na maeneo hayo. Hivyo, Serikali

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

haina budi kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ili jamii zanamna hii ziweze kunufaika ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti,katika kuridhia mkataba huuSerikali pia ina wajibu mkubwa wa kuwaandaa watu wakekatika soko la ushindani wa mbegu. Mpaka sasa kama nchitujiulize tumewaandaaje watalaamu wetu wanaofanya tafitiza kilimo katika soko la ushindani? Bajeti zinazotolewa kwaajili ya tafiti zote ni mashahidi kuwa bajeti hizo hazitoshelezi,vitendea kazi bado ni duni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maafisa ugani wengiwanafanya kazi katika mazingira duni sana. Maeneo mengiya wakulima hayana ofisi za maafisa ugani. Hii inatoa tafsiritosha ya kujipima kama Taifa kuwa tunapoenda kuridhiaitifaki hii tumejiandaaje kupambana katika soko la ushindaniwa mbegu ili kuhakikisha nchi yetu haitakuwa dampo lambegu.

Mheshimiwa Mwenyekiti,moja ya changamotokubwa tunayokumbana nayo katika sekta ya kilimo ni pamojana ufinyu wa bajeti. Ukirejea kifungu cha 41 ‘FinancialProvisions’ Mkataba huu umezitaka nchi wanachamakutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mkataba huu “StateParties shall endeavor to allocate the necessary funds for theeffective implementation of this Protocol at the National andRegional level.”

Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na mkataba huukukazia upatikanaji wa fedha ni dhahiri katika bajeti za serikalizilizopita katika Sekta ya Kilimo ambayo ni sekta muhimu sanakwa uchumi na ustawi na Taifa letu kiasi cha fedhazilizotengwa na zinazotolewa ni kidogo sana. Mathalani,mwaka 2016/2017 fedha iliyokuwa imeidhinishwa na Bungeilikuwa kiasi cha shilingi bilioni 100.527 lakini mpaka Machi nishilingi bilioni 2.2 tu ndio ilitolewa. Hali kadhalika kwa mwaka2017/2018 ambapo ilitolewa asilimia 11 tu ya fedha zamaendeleo zilizokuwa zimetengwa katika Sekta hiyo.Kwamantiki hiyo, utekelezaji wa mkataba huu utakuwa ni mgumuendapo Serikali na Taasisi zake zinazoshughulika na kilimo

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

hazitafanya jitihada madhubuti ya kutafuta pesa ili kuinuaSekta hii ikiwa ni pamoja na kuwekeza ipasavyo katika tafitiza mbegu.

Mheshimiwa Mwenyekiti,pamoja na Azimio hiliambalo utekelezaji wake utaenda sambamba na Sheria yetuya mwaka 2002 "The Protection of New Plants (Plant Breeder’sAct 2002) ambapo Sheria hii pia huangalia hakimiliki kwajamii na mkulima, ni vema sana Serikali ihakikishe inawekezaipasavyo katika elimu, tafiti, kutangaza na kutafuta masokokwa ajili ya mbegu zetu. Hii itawasaidia wakulima wetu kupatambegu bora zaidi, kupunguza uingizwaji wa mbegu nchiniambazo siyo rafiki kwa mazingira, itapunguza gharama kwakuwa wakulima watapata mbegu zinazozalishwa hapa hapanchini kwa bei nafuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho, pamojanaumuhimu wa kuridhia Itifaki hii ni vema Serikali ikaandaana mfumo ambao utaongeza ushindani katika masoko yambegu. Serikali haina budi kuwekeza ipasavyo katikateknolojia na tafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali italazimika kuachakuwekeza fedha nyingi katika miradi ambayo haina tija yamoja kwa moja na wananchi na badala yake kuwekezaipasavyo katika miradi yenye tija kubwa kwa wananchi ikiwani pamoja na kuwekeza katika kilimo chenye tija, kuwekezakatika mifumo yenye kulinda maslahi ya wananchi wakekatika masoko ya kimataifa na zaidi kuwekeza katikakuwasaidia wakulima wadogo wadogo ili kuondokana katikajinamizi la ujinga, umaskini na maradhi ambalo limeandamaTaifa letu kwa kipindi cha miongo mingi tangu uhuru mpakasasa.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo kwaniaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, naomba kuwasilisha.(Makofi)

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSUAZIMIO LA KURIDHIA ITIFAKI YA JUMUIYA YA MAENDELEO YA

NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA KUHUSU KULINDA HAKIMILIKIZA WAGUNDUZI WA AINA MPYA ZA MBEGU ZA MIMEA (The

Protocol for Protection of New Varieties of Plants {PlantBreeder’s Rights} in the Southern African Development

Community-SADC)- KAMA YALIVYOWASILISHWA MEZANI

(Yanatolewa chini ya Kanuni ya 53 (6) (c) ya Kanuni zaBunge, toleo la mwaka 2016)

A. UTANGULIZI1. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa azimio hili nidhahiriTanzania haiwezi kujitenga na mataifa au jumuiyanyingine hasa katika kushirikiana kwenye masuala mbalimbaliya kiuchumi na kijamii.

2. Mheshimiwa Spika, katika kuliona hili la ushirikiano nakuzidisha mahusiano baina ya mataifa, Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania Ibara ya 63(3) (e) inataja kuwamiongoni kwa kazi za Bunge ni “Kujadili na Kuridhia Mikatabayote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwaMasharti yake inahitaji Kuridhiwa”.

3. Mheshimiwa Spika, japokuwa ni jukumu la Bunge letukufanya kazi hiyo, ni muhimu sana kufahamu umuhimu wambegu katika mustakabali mzima wa jamii yetu ya Kitanzaniana pia katika uchumi wetu. Hatupingani na ukweli kuwauzalishaji mazao unahitaji mbegu bora, lakini ni ukwelikwamba uzalishaji huo wa mbegu bora unaweza piakupatikana ndani ya jamii zetu.

4. Mheshimiwa Spika, hivyo kuja kwa azimiohili ni fursakubwa kwa nchi yetu katika kuongeza jitihada za tafiti juuya mbegu mbalimbali, kupanua masoko ya mbegu dunianihususani katika nchi za SADC, kuruhusu watafiti wetu,wagunduzi na wabunifu kupata hakimiliki za mbegu aumimea wanayoigundua, kuongeza ubora wa mbegu zetuna zaidi ya yote kuongeza ubora wa mbegu zetu za asili ilikupata mazao bora zaidi.

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

B. MAELEZO YA UJUMLA

5. Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwa moja yamalengo katika azimio hili linasisitiza mashirikiano baina yanchi wanachama nauwekaji wa mifumo ya kisheria katikakutoa haki miliki kwa wagunduzi bado ndani ya mkatabahuu haujazungumzia ipasavyo au kuangalia maslahi mapanaya kundi kubwa la wananchi ambao ni wakulima wadogowadogo ambao pia wana aina zao za mbegu kulingana namazingira yao.

6. Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa pamoja namalengo mazuri ya mkataba huu ambayo yanalengakuwasaidia na kuwalinda wagunduzi wa mbegu mbalimbalini ukweli usiopingika kuwa umilikishaji wa mbegu kwawagunduzi unatoa maana kwamba mnyororo mzima wambegu unakuwa ni kwa faida ya wagunduzi waliosajiliwa nakutambuliwa.

7. Mheshimiwa Spika, jambo hili la umiliki binafsilinaondoa utamaduni wa wakulima wadogo hususanimaeneo ya vijijini kuweza kuendelea na utamaduni wakubadilishana na kuuziana mbegu (customary practices).Huuni utamaduni ambao umekuwa ukitumika kwa miakamingi.Tukumbuke kuwa kundi hili la wakulima wadogo ndilokundi la wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula nawanaoyaingia kwenye mataifa yetu katika nchi wanachamawa SADC . Endapo, utaratibu huu wa kutumia haki milikiusiporatibiwa vyema tutakuta wananchi wetu hususani vijijiiwakipata tabu sana. Zipo jamii zenye aina za upekee wambegu kama vile maharage, karanga n.k ambazo kimsingikama jamii zinapaswa kupewa haki miliki ili kunufaika. Nivyema kama taifa tukaliangalia jambo hilo kwa manufaa yawananchi walio wengi.

8. Mheshimiwa Spika, maslahi ya nchi nilazima yaanziekwenye maslahi ya wananchi, kama jambo lolotetunalolifanya hapa Bungeni halina maslahi mapana kwawananchi walio wengi ni dhahiri kwamba jambo hilohalitakuwa na maslahi yoyote kwa nchi pia.

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

C. HAKI YA MKULIMA NA JAMII KATIKA KUMILIKI MBEGU

9. Mheshimiwa Spika, Katika nchi nyingi zilizoendeleazimekuwa zikiweka masharti ya aina za mazaowanayoyahitaji kuyanunua. Hivyo, nchi hizo zimekuwa ndiowazalishaji wakubwa wa mbegu ambazo ndizo huingia katikanchi zinazoendelea (ulimwengu wa tatu). Bila kujali aina yamazingira ikiwa ni pamoja na udongo, hali ya hewa n.kmbegu hizo zimekuwa zikiuzwa kiholela kitendo ambachokimeleta athari kubwa kwa mbegu zetu za asili, na pia athariza kimazingira.

10. Mheshimiwa Spika, hii yote ni kutokana na mataifamengi barani Afrika kukosa haki miliki za mazao yao,kutangaza (promote) na kuongeza thamani ya mbegu zaoili ziweze kuwanufaisha wananchi walio wengi ambao niwakulima wadogo. Pamoja na mabadiliko makubwayanayotokea katika sekta ya kilimo hususani masuala yaupatikanaji na uhifadhi wa mbegu bado nchi nyingi baraniAfrika hutumia mfumo wa asili ambao umejikita zaidi katikamila, desturi na tamaduni zetu.

11. Mheshimiwa Spika,ni ukweli kwamba katika mfumoasilia mbegu huchaguliwa mapema kutoka shambani nakuhifadhiwa kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo. Taaluma nateknolojia inayotumika katika uchaguzi wa mbegu (massselection- technology) kutoka shambani, utunzaji wa mbeguhizo na njia zinazotumika katika kuuziana au kupeana nijambo ambalo ni lazima liangaliwe vyema katika mfumomzima wa kisheria wa umiliki wa rasilimali za jamii.

12. Mheshimiwa Spika, ni wazi kuwa tumechelewa sanakatika kuhakikisha mbegu zetu za asili zinaboreshwa nazinapata haki miliki ili kuhakikisha wakulima wanapata mazaomengi na bora. Lakini ni lazima tuweze kutambuachangamoto zitakazokuja na mkataba huu kwa kuwawakulima watalazimika kuendana na mahitaji ya soko. Nidhahiri kuwa mkataba huu utachocheza tafiti nyingi zambegu na hivyo mbegu za asili zitatoweka. Kutokana naumaskini au ugumu wa maisha ya wakulima wetu nchini ,

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

wengi wao watajikuta wanashindwa kumudu kilimo kutokanana kuongezeka kwa mahitaji katika kilimo ikiwa na maanaya manunuzi ya mbegu madawa na mahitaji ya umwagiliaji.

13. Mheshimiwa Spika, sambamba na hili ni lazima serikaliiweke mfumo mzuri ambao jamii nzima itaweza kunufaikaendapo kama jamii hiyo imeweza kugundua mbegu za ainafulani. Hii ikiwa na maana kwamba jamii ikishirikiana kwapamoja wanaweza kuwa mbegu waliyoifanyia utafitikulingana na maeneo hayo. Hivyo, serikali haina budikuhakikisha inaweka mazingira mazuri ili jamii za namna hiiziweze kunufaika ipasavyo.

14. Mheshimiwa Spika, katika kuridhia mkataba huuserikali pia ina wajibu mkubwa wa kuwaandaa watu wakekatika soko la ushindani wa mbegu. Mpaka sasa kama nchitujiulize tumewaandaaje watalaamu wetu wanaofanya tafitiza kilimo katika soko la ushindani? Bajeti zinazotolewa kwaajili ya tafiti zote ni mashahidi kuwa bajeti hizo hazitoshelezi,vitendea kazi bado ni duni n.k.

15. Mheshimiwa Spika, maafisa ugani wengi wanafanyakazi katika mazingira duni sana. Maeneo mengi ya wakulimahayana ofisi za maafisa ugani. Hii inatoa tafsiri tosha yakujipima kama taifa kuwa tunapoenda kuridhia itifaki hiitumejiandaaje kupambana katika soko la ushindani wambegu ili kuhakikisha nchi yetu haitakuwa dampo la mbegu.

16. Mheshimiwa Spika, moja ya changamoto kubwatunayokumbana nayo katika sekta ya kilimo ni pamoja naufinyu wa bajeti. Ukirejea kifungu cha 41 ‘Financial Provisions’Mkataba huu umezitaka nchi wanachama kutenga fedhakwa ajili ya utekelezaji wa mkataba huu “ State Parties shallendeavor to allocate the necessary funds for the effectiveimplementation of this Protocal at the national and regionallevel”

17. Mheshimiwa Spika, pamoja na mkataba huu kukaziaupatikanaji wa fedha ni dhahiri katika bajeti za serikalizilizopita katika sekta ya kilimo ambayo ni sekta muhimu sana

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

kwa uchumi na ustawi na taifa letu kiasi cha fedhazinazotengwa na zinazotolewa ni kidogo sana. Mathalani ,mwaka 2016/2017 fedha iliyokuwa imeidhinishwa na Bungeilikuwa kiasi cha shilingi bilioni 100.527 lakini mpaka Machi nishilingi bilioni 2.22 tu ndio ilitolewa. Hali kadhalika kwa mwaka2017/2018 ambapo ilitolewa asilimia 11% tu ya fedha zamaendeleo zilizokuwa zimetengwa katika sekta hiyo.Kwamantiki hiyo, utekelezaji wa mkataba huu utakuwa ni mgumuendapo serikali na taasisi zake zinazoshulika kilimo hazitafanyajitihada madhubuti ya kutafuta pesa ili kuinua sekta hii ikiwani pamoja na kuwekeza ipasavyo katika tafiti za mbegu.

18. Mheshimiwa Spika, pamoja na azimio hili ambaloutekelezaji wake utaenda sambamba na sheria yetu yaMwaka 2002" The Protection of New Plants (Plant Breeder’sAct 2002) ambapo Sheria hii pia huangalia hakimiliki kwajamii na Mkulima, ni vyema sana serikali ihakikishe inawekezaipasavyo katika elimu, tafiti, kutangaza na kutafuta masokokwa ajili ya mbegu zetu. Hii itawasaidia wakulima wetu kupatambegu bora zaidi, kupunguza uingizwaji wa mbegu nchiniambazo sio rafiki kwa mazingira, itapunguza gharama kwakuwa wakulima watapata mbegu zinazozalishwa hapa hapanchini kwa bei nafuu.

D. HITIMISHO

19. Mheshimiwa Spika, pamoja na umuhimu wa kuridhia Itifakihii; ni vyema Serikali ikaandaa na mfumo ambao utaongezaushindani katika masoko ya mbegu. Serikali haina budikuwekeza ipasavyo katika teknolojia na tafiti. Serikaliitalazimika kuacha kuwekeza fedha nyingi katika miradiambayo haina tija ya moja kwa moja kwa wananchi nabadala yake kuwekeza ipasavyo katika miradi yenye tijakubwa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwekeza katikakilimo chenye tija, kuwekeza katika mifumo yenye kulindamaslahi ya wananchi wake katika masoko ya kimataifa nazaidi kuwekeza katika kuwasaidia wakulima wadogowadogo ili kuondokana katika jinamizi la ujinga, umaskini namaradhi ambalo limeandama taifa letu kwa kipindi chamiongo mingi tangu uhuru mpaka sasa.

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

20. Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo kwa niabaya Kambi Rasmi ya Upinzani, naomba kuwasilisha.

………………………………Pascal Yohana Haonga (Mb)

MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENIKATIKA WIZARA YA KILIMO

10 Septemba, 2019

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa namuita MheshimiwaWaziri wa Viwanda na Biashara ili awasilishe Azimio la KuridhiaItifaki ya Marrakesh inawezesha upatikanaji wa kazizilizochapishwa kwa watu wasioona wenye uoni hafifu naulemavuunaofanya mtu kushindwa kusoma mwaka wa 2013.(Makofi)

Mheshimiwa Waziri dakika kumi.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufulikubali kupitisha Azimio la Kuridhia Mkataba wa Marrakeshwa mwaka 2013 unaowezesha upatikanaji wa kazizilizochapishwa kwa watu wasioona wenye uoni hafifu auulemavu unaomfanya mtu kushindwa kusoma yaani (TheMarrakesh Treaty To Facilitate Access To Publish Work ForPersons Who Are Blind Visually Impaired or Otherwise PrintDisabled).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkataba wa Kimataifa waMarrakesh unazingatia Kanuni Tano za haki za Binadamuambazo ni, Kutobagua, kutoa fursa sawa kwa wananchi,ufikikaji yaani accessibility ushiriki kikamilivu kwa wasioonakatika shughuli za kijamii na kuendeleza ushirikiano waKimataifa kutekeleza malengo ya watu wenye ulemavu wakuona duniani kote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maandalizi yakuridhia Mkataba huu Serikali imeshirikisha Wadau mbalimbali

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

kutoka Tanzania bara na Zanzibar Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar ambao maoni yao yalisaidia sana katika kupatauelewa mpana na kuweka mkakati wa namna bora yakutekeleza Mkataba huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkataba wa Marrakeshunazingatia Ibara za 11(1)(3) na Ibara ya 18(2) za Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazoelekeza haki yakila mtu kupata elimu na taarifa kuhusu matukio mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, malengo makuu yaMkataba wa Kimataifa wa Marrakesh ni kuwawezesha watuwasioona kabisa na wale wenye huoni hafifu kupata nakutumia kazi za uandishi zilizochapishwa kwa wino wakawaida kwenye miundo mbadala inafikika kwao, kama vilemaandishi ya nukta nundu yaani brelly kurekodi katika sauti,kuwekwa katika maandishi yaliyokuzwa n.k.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kwa nafasi ya kipekeekabisa napenda kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John PombeJoseph Magufuli kwa kuwajali ndugu zetu wenye ulemavunchini, katika kulithibitisha hilo uteuzi wa Naibu WaziriMheshimiwa Stella Ikupa, uteuzi wa Mheshimiwa Dkt.Abdallah Possi Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani, uteuziwa Bwana Amon Mpanju kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizaraya Katiba na Sheria pamoja na Watendaji wengine ndani yaSerikali ni kielelezo cha jinsi gani Rais wetu Dkt. John PombeMagufuli na Serikali ya Awamu ya Tano anayoiongozainavyotekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kujaliwananchi wote wakiwemo ndugu zetu wenye ulemavu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uandaaji na utekelezaji waMkataba wa Marrakesh upo kwenye Awamu Mbili zautekelezaji kwanza ni kuandaa na kukamilisha mchakato wakusaini na kuridhia Mkataba Bungeni jambo ambalo nimatumaini yangu kwamba Waheshimiwa Wabungemtatusaidia kukamilisha hatua hii leo hii kwenye Bunge letuTukufu.

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hatua ya pili ni kuwasilishanyenzo ya kuridhiwa na Bunge kwenye Makao Makuu yaShirika la Miliki bunifu Duniani yaani World Intellectual PropertyOrganization lililopo Geneva Switzerland kwa ajili ya kusajiliwarasmi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba kuwasilishaAzimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Marrakesh ya Mwaka2013 kama ifuatavyo:-

KWA KUWA,Tanzania ni nchi Mwanachama wa Shirikala Miliki Bunifu Duniani yaani World Intellectual PropertyOrganization Wipe ambapo ilijiunga na Shirika hilo mwaka1983, Shirika hilo linasimamia masuala ya Miliki Bunifu Dunianiambayo ni miundo bunifu yaani Industrial propery na hakimiliki yaani copyright na kwa kuwa Tanzania ni nchimwanachama iliyoshiriki Mkutano wa Marrakesh Moroccotarehe 27 Juni mwaka 2013 ambao ulipitisha Mkataba huuunaowezesha upatikanaji wa kazi zilizochapishwa kwa watuwasioona wenye uoni hafifu au ulemavu unaomfanya mtukushindwa kusoma kwa njia rahisi;

NA KWA KUWA,Tanzania ilikubaliana na Mkataba huulakini haikutia saini kwa mujibu wa Ibara ya 17 ya Mkatabahuu kwa lengo la kujipa muda ili kupata maoni ya wadau;

NA KWA KUWA,Mkataba wa Marrakesh unaendana naMikataba mbalimbali ambayo Tanzania imekwisha ridhiaikiwemo Mkataba wa Berne wa Ulinzi wa Kazi za Maandishina Kazi za Sanaa (Berne Convection for the Protection ofLiterally and Artistic Works of 1986) na makubaliano kuhusuMalengo Yanayohusu Sanaa na Biashara za Miliki Bunifu (TheTrade Related Aspects of Intellectual Property AgreementTreaty);

NA KWA KUWA,Mkataba wa Berne na TRIPSkwapamoja ina lengo la kusimamia kazi zinazolindwa na Hakimilikikatika kuzalisha, kutafsiri na kusambaza kazi za maandishiambapo mtu yeyote haruhusiwi kutumia kazi za Hakimiliki bilaidhini au kutoa malipo kwe mwenye Hakimiliki;

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

NA KWA KUWA,lengo la Mkataba huu ni kuwezeshawasioona, wenye uoni hafifu na wenye ulemavu wa kusomakupata kazi zilizochapishwa katika muundo unaofikika, kutoauelewa wa masuala mbalimbali juu ya changamoto zaupatikanaji taarifa na habari katika muundo rafiki kwawalengwa, kuwezesha walengwa kupata elimu na vifaa vyakujifunzia yaani vitabu, kufanya tafiti na mawasiliano kufikiakazi andishi zilizochapishwa katika muundo unaofikika nakuimarisha uchangamano na ushirikiano katika shughuli zakijamii na za kiutamaduni;

NA KWA KUWA,Mkataba huu unatoa fursa yaupendeleo wa pekee kwenye Sheria za Hakimiliki ili kuruhusuuzalishaji, usambazaji na kuwezesha upatikanaji wa kazizilizochapishwa katika mfumo wa rafiki kwa walengwa;

NA KWA KUWA, Tanzania kwa kuridhia mkataba huuna hatimaye kuutekeleza itanufaika na mambo yafuatayo:-

(a) Kuwezesha upatikanaji wa elimu kwa njia rahisi;

(b) Kuwezesha ubadilishanaji wa kazi nan chi nyingine;

(c) Kujenga uelewa wa namna ya kutatua changamotombalimbali zinazowapata wasioona na wenye uoni hafifuwakati wakitafuta elimu;

(d) Kuondoa umaskini na kuchangia katika pato la Taifa;

(e) Kujenga uelewa katika masuala ya haki miliki;

(f) Kurahisisha upatikanaji wa vitabu, magazeti na vituvingine vinavyowasaidia walengwa katika kupata uelewawa masuala ya kijamii; na

(g) Kuwezesha mwingiliano wa kijamii katika jamii yawasioona, wenye uoni hafifu na jamii isiyo na ulemavu huo.

HIVYO BASI, kwa kuzingatia manufaa yanayotokanana mkataba huu, Bunge hili katika Mkutano wa Kumi na Sita

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

na kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ya mwaka 1977, sasa linaazimiakuridhia mkataba wa Marrakesh wa mwaka 2013,unaowezesha upatikanaji wa kazi zilizochapishwa kwa watuwasioona, wenye uoni hafifu na ulemavu unaomfanya mtukushindwa kusoma (The Marrakesh Treaty, to Facilitate Accessto Published Works for persons who are Blind, visually impairedor otherwise print disabled.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.(Makofi)

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

MWENYEKITI: Ahsante, hoja imeungwa mkono. Sasanamuita Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, Biashara naMazingira, atawasilisha taarifa ya Kamati kuhusu azimio hilodakika kumi! (Makofi)

MHE. KITETO Z. KONSHUMA - K.n.y MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE, VIWANDA, BIASHARA NAMAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba yaMwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda,Biashara na Mazingira, naomba kuwasilisha maoni ya Kamatikuhusu Azimio la Bunge la Mkataba wa Marrakesh wa mwaka2013, unaolenga kuwezesha upatikanaji wa kazizilizochapishwa kwa watu wasioona, wenye uoni hafifu auulemavu unaomfanya mtu kushindwa kusoma (The MarrakeshTreaty to Facilitate Access to Published Works for Persons whoare Blind, Visually Impaired or Otherwise Print Disabled 2013).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kanuni ya53(6)(b), ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari, 2016,naomba kuwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bungeya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Azimio la KuridhiaMkataba wa Marrakesh unaolenga kuwezesha upatikanajiwa kazi zilizochapishwa kwa watu wasioona, wenye uonihafifu au ulemavu unaomfanya mtu kushindwa kusoma waMwaka 2013 (The Marrakesh Treaty to Facilitate Access to

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

Published Works for Persons who are Blind, Visually Impairedor Otherwise Print Disabled2013).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia masharti yafasili ya 6(b), Kifungu cha 53 ikisomwa pamoja na fasili ya1(b) ya Kifungu cha 7, cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016, Kamati ya Kudumuya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ina jukumu lakushughulikia Mikataba inayopendekezwa kuridhiwa naBunge iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuliarifu Bunge lakoTukufu kuwa Hoja ya Serikali kuhusu Bunge kuridhia Azimio laKuridhia Mkataba wa Marrakesh ililetwa kwenye Kamati yaBunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kwa mujibu waKanuni ya 53(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge. Kamati ililijadilina kulichambua na hatimaye kuja na maoni na ushauriambao Kamati imeutoa kwa lengo la kuboresha utekelezajiwa Mkataba huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namna KamatiIlivyoshughulikia hoja hii, baada ya hoja hii kuwasilishwakwenye Kamati, Kamati ilikutana katika Ofisi za BungeDodoma ambapo ilitekeleza shughuli zifuatazo kwa ajili yakuwezesha uchambuzi wa kina wa Mkataba huu;-

(i) Semina ya kuijengea uelewa Kamati juu ya Mkatabawa Marrakesh, ambapo tarehe 31 Agosti, 2019, Wizara yaViwanda na Biashara iliwapitisha wajumbe katika Mkatabahusika. Semina hii iliiwezesha Kamati kupata uelewa nakuiweka katika nafasi nzuri ya kuifanyia kazi hoja hii nahatimaye kutoa maoni yake;

(ii) Kupokea Maelezo ya Serikali juu ya pendekezo laKuridhia Mkataba wa Marrakesh wa Mwaka 2013 ambapotarehe 4 Septemba, 2019 Kamati ilikutana na kupata maelezoya Serikali kuhusu pendekezo la Kuridhia Azimio la KuridhiaMkataba wa Marrakesh, maelezo hayo yaliyowasilishwa naNaibu Waziri wa Viwanda na Biashara yalifafanua nia yaSerikali kutaka kuingia mkataba huu kwa lengo la kutatua

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

changamoto ambayo wamekuwa wakikabiliana nayowalengwa wa Mkataba huu; (iii) Kupokea Maoni ya Wadau, katika kutekeleza jukumuhili Kamati ilizingatia masharti ya Kanuni ya 117 (9) kuhusuutaratibu wa kuwaalika wadau, wadau waliokuwa na maonijuu ya Mkataba wa Marrakesh walipata fursa yakuyawasilisha. Kamati iliwashukuru wadau waliofanikiwakuwasilisha maoni yao kuhusu Mkataba huu, maoni yenuyalisaidia kuboresha maoni ya Kamati kuhusu Mkataba huuna hatimaye kuishauri Serikali kwa lengo la kuboreshautekelezaji wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chimbuko la Itifaki, Mkatabawa Marrakesh unatekelezwa na Nchi Wanachama wa WIPO(World Intellectual Property Organization) ambapo Jamuhuriya Muungano wa Tanzania ni Mwanachama. Mnamo tarehe27 Juni, 2013 nchi wanachama wa WIPO walishiriki katikamkutano uliofanyika mjini Marrakesh – Morocco kwa lengola kujadili na kupata muafaka wa kuwasaidia watu wenyeulemavu wa macho kuweza kupata haki ya kushiriki katikashughuli mbalimbali za kijamii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo ya kikao hichokilipitisha azimio la kuanzishwa kwa Mkataba wa Marrakeshambao ulilenga kuweka jitihada za pamoja ambazo zinatoafursa ya upendeleo na upekee kwenye Sheria ya Hakimiliki iliziruhusu uzalishaji, usambazaji na kuwezesha upatikanaji wakazi za uandishi kuwa katika mifumo rafiki kwa watu wenyeuoni hafifu, wasioona na wenye ulemavu unaowapelekeakutokusoma kwa urahisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo ya msingiyaliyozingatiwa na kamati, ili kuliwezesha Bunge kutekelezamadaraka yake ipasavyo kwa mujibu wa Ibara ya 63(3)(e),kamati ilizingatia mambo mbalimbali yaliyo muhimu katikakuifanyia kazi hoja ya Serikali iliyo mezani leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kamati iliangalia Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadhi ya Sheria za

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

nchi zinazohusiana moja kwa moja na maudhui ya Mkatabaunaopendekezwa. Kamati ilibaini kuwa Ibara ya 18 ya Katibaya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inaelezea haki yakupata habari na taarifa muhimu katika jamii, hivyo basikuridhiwa kwa Mkataba huu kutawezesha wanufaika kupatahaki ya kikatiba. Vilevile, Kamati ilitafakari na kujiridhisha juuya Faida zinazoweza kupatikana kutokana na kuridhia kamaulivyo. Faida hizo ni pamoja na;-

(i) Kujenga uelewa wa namna ya kutatua changamotombalimbali zinazowapata wasioona na wenye uoni hafifuwakati wa kutafuta elimu;

(ii) Kurahisisha upatikanaji wa vitabu, magazeti na vituvingine vitanavyowasidia walengwa katika kupata uelewawa masuala ya kijamii; na

(iii) Kuongeza ushiriki wa jamii ya wasioona na wenye uonihafifu katika shughuli za kijamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kamati pia ilizingatia hasaraau madhara yanayoweza kupatikana kwa kuridhia Mkatabahuu ambapo haikuona madhara ya moja kwa mojayatokanayo na kuridhia Mkataba huu. Madhara ambayoyalikuwa yakitazamwa ni kuwa mkataba ungeweza kuruhusuuingizaji wa vitabu na machapisho ambayo yanapinganana mila na desturi zetu. Hofu hii imeondolewa na Ibara ya 12ya Mkataba ambayo imeelezea kuwa, ubadilishanaji wanakala za vitabu na machapisho baina ya nchi utazingatiaSheria, taratibu na utamaduni wa kila nchi inayohitaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nanukuu: Article 12(1)“Contracting parties recognize that a contracting Party mayimplement in its National Law, other copyright limitation andexception for the benefit of beneficiary persons than areprovided by this Treaty having regard to that ContractingParty’s economic situation and its social and cultural needsin conformity with that Contracting Party’s international rightsand obligations and in the case of a least-developed countrytaking into account its special needs and its particular

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

international rights and obligations and flexibilities thereof”.Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kamati ilijiridhishahatua zilizofikiwa katika Mkataba huu ambapo ilibaini kuwaMkataba ulianza kutekelezwa rasmi tarehe 30 Septemba,2016 ambapo ilikuwa ni miezi mitatu (3) baada ya nchimwanachama wa Ishirini (20) kuwasilisha Hati ya Kuridhia,kama inavyoelekezwa na Ibara ya 18 ya Mkataba. Nanukuu,Article 18 “The Treaty shall enter into force three months after20 eligible parties referred to Article 15 have deposited theirinstruments of ratification or accession”. Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkataba pia unaruhusuNchi Mwanachama kujitoa, na hii ni kwa mujibu wa Ibara ya20 ya Mkataba, kipengele hiki kinatoa Haki kwa NchiMwanachama kujitoa. Hii inatoa uhuru kwa wanachamawake pale wanapohisi hawanufaiki na mkataba. NchiMwanachama yenye kusudio la kujitoa itawasilisha ombi lakujitoa kwa Mkurugenzi Mkuu wa WIPO na ombi hilolitakubaliwa mwaka mmoja baada ya ombi hilo kuwasilishwa.Nanukuu, Article 20’’ This Treaty may be denounced by anyContracting Party by notification addressed to the DirectorGeneral of WIPO. Any denunciation shall take effect one yearfrom the date on which the Director General of WIPO receivesthe notification’’. Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati pia ilitaka kujiridhishakuhusu uhusiano wa Mikataba mingine ya Kimataifa ambayoinashabihiana na Mkataba wa Marrakesh. Ibara ya 1 yaMkataba inafafanua kuwa hakuna kitakachobadili jukumulolote ambalo nchi mwanachama imejifunga na mkataba.Nanukuu, Article 1 “Nothing in this Treaty shall derogate fromany obligation that Contracting Parties have to each otherunder any other treaties, nor shall it prejudice any right that aContracting Party has under any other treaties” Mwisho wakunukuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maoni na Ushauri waKamati, Mkataba wa Marrakesh unalenga kuwezesha watu

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

wasioona, wenye uoni hafifu au ulemavu unaomfanya mtukushindwa kusoma kupata kazi zilizochapishwa kwa njia rahisi(maandishi ya nukta nundu, sauti zilizorekodiwa na maandishiyaliyokuzwa). Vilevile Mkataba huu unalenga kutoa uelewawa masuala mbalimbali juu ya changamoto za upatikanajiwa taarifa na habari katika muundo rafiki kwa walengwa.Pia unawawezesha walengwa kupata elimu na vifaa vyakujifunzia jambo ambalo litaongeza na kuimarisha ushiriki waokatika shughuli za kijamii na utamaduni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua umuhimu waMkataba huu, naomba nilishawishi Bunge lako Tukufu kuridhiaMkataba huu kwa lengo la kuwasaidia walengwa kuanzakunufaika. Pia naomba nitoe maoni na mapendekezo yaKamati ambayo yamegusa maeneo ambayo Kamati inaonani muhimu Serikali ikayazingatia kwa lengo la kuboreshautekelezaji wa Mkataba huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 4 ya Mkatabainapingana na Sheria ya Hakishiriki na Hakishirikishi ya Mwaka1999 ambayo inazuia upatikanaji wa Kazi zilizochapwakuwekwa kwenye muundo unaofikika kwa wanufaika kamainavyotakiwa kwenye Mkataba wa Marrakesh. Kwa kuwatunaenda kuridhia Mkataba huu Kamati inaitaka Serikalikukamilisha mchakato wa marekebisho wa Sheria yaHakimiliki ili kuhakikisha Sheria hiyo inaendana na mashartiya ibara hii kwa lengo la kutoa fursa kwa wanufaika kuanzakunufaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 4(5) ya Mkatabaimeweka wazi kazi yoyote itakayochapishwa chini yamkataba huu isifanyiwe biashara yaani isiuzwe, Kamatiinashauri Serikali kuhakikisha wanufaika wanapewa elimu juuya sharti hili la mkataba.

Pia Serikali ihakikishe chombo kitakachopewa jukumula kusimamia utekelezaji wa mkataba huu kinakuwa nauwezo wa kufuatil ia na kujir idhisha kuwa sharti hilolinazingatiwa na walengwa wanapata huduma. Vilevilekamati inashauri kuwa kama itabainika kuuzwa kazi ambazo

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

zimetolewa kwa ajili ya kuwanufaisha walengwa, hatua zakisheria zifuatwe kwa lengo la kukomesha vitendo hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho, naombanikushukuru sana wewe binafsi kwa uongozi wako mahiri nakwa kunipa ruhusa ya kuwasilisha maoni haya ya Kamati. Pianimshukuru sana Mheshimiwa Spika kwa uongozi wake mahilipamoja na Naibu Spika, pamoja na Wenyeviti wote wa Bungekwa kuratibu na kusimamia shughuli za Bunge kwa umakinina umahiri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kamati inapendakumshukuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa RaisMuungano na Mazingira Mheshimiwa George BonifaceSimbachawene, Mbunge, Naibu Waziri wake MheshimiwaMussa Ramadhani Sima Mbunge, Makatibu Wakuu, pamojana wataalam wote wa Ofisi hii muhimu kwa ushirikianowalioutoa wakati wa kujadili Azimio hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekeekabisa, kwa niaba ya Mwenyekiti, napenda kuwashukuruwajumbe wote wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biasharana Mazingira kwa ushirikiano walioutoa wakati wa kupitiakuchambua na hatimaye kuwasilisha maoni yake juu yaAzimio hili mbele ya Bunge hili tukufu. Orodha yao ni kamainavyosomeka hapa chini na kwa ruhsa yako naomba majinayao yaingie kwenye kumbukumbu Rasmi za Bunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kumshukuruKatibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai; Mkurugenzi waIdara ya Kamati Bwana Athumani Hussein; MkurugenziMsaidizi Sehemu ya Fedha na Uchumi Bwana MichaelChikokoto; Makatibu wa Kamati Bi. Zainabu Mkamba na Bi.Mwajuma Ramadhani pamoja na Msaidizi wa Kamati Bi.Paulina Mavunde kwa kuratibu vema shughuli za Kamati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha nanaunga mkono Azimio. (Makofi)

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

TAARIFA KUHUSU AZIMIO LA BUNGE LA KURIDHIA ITIFAKI YAMAENDELEO YA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA KUHUSU

KULINDA HAKIMILIKI ZA WAGUNDUZI WA AINA MPYA ZAMBEGU ZA MIMEA (THE PROTOCOL FOR PROTECTION OF NEW

VARIETIES OF PLANT [PLANT BREEDER‘S RIGHTS] IN THESOUTHERN AFRICAN DEVELOPMENT COMMUNITY – SADC) –

KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI______________________

6.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 53 (6) (b) yaKanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016. Kwaniaba ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji, naomba kuwasilisha Maoni na Ushauri waKamati kuhusu Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki yaMaendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika Kuhusu KulindaHakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimea(The Protocol for Protection of New Varieties of Plant [PlantBreeder‘s Rights] In The Southern African DevelopmentCommunity – SADC).

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Itifaki hii inahusu NchiWanachama zilizo Kusini Mwa Afrika (SADC), kabla ya kuanzawasilisho langu, kwa niaba ya Kamati naomba kuchukuanafasi hii kumpongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuchaguliwakuwa Mwenyekiti wa Nchi za SADC. Kamati inaaminikutokana na uwezo wake mahiri pamoja na mambomengine Wagunduzi wa Tanzania na wenzao kutoka nchiWanachama wa SADC watanufaika na maudhui yalimokwenye Itikafi hii.

Mheshimiwa Spika, Nyongeza ya Nane Kifungu cha 7(1) (b)ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016, inazipaKamati za Kisekta ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge yaKilimo, Mifugo na Maji jukumu la kushughulikia Miswada yaSheria, Maazimio na Mikataba inayopendekezwa kuridhiwana Bunge iliyo chini ya Wizara inazozisimamia. Aidha, jukumuhili pia ni jukumu la Kikatiba chini ya Ibara ya 63(3)(e) ya

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka1977.

Mheshimiwa Spika, tarehe 12 Novemba, 2018 uliiletea Kamatiya Kilimo, Mifugo na Maji kazi ya kushughulikia Azimio laBunge la kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchiza Kusini Mwa Afrika (The Protocol For Protection of NewVarieties of Plant [Plant Breeder‘s Rights] In The SouthernAfrican Development Community – SADC) kuhusu KulindaHakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimeakama lilivyowasilishwa na Serikali ili Kamati iweze kuchambuamapendekezo ya Azimio husika na hatimae kutoa maoni naushauri kwa Serikali.

Mheshimiwa Spika, kama il ivyo ada, Kamati i l ianzakuchambua Itifaki husika kwa kushirikiana na wadau waliofikambele ya Kamati na wale waliotuma maoni yao kwa njia yamaandishi i l i kufahamu madhumuni na faidazinazoambatana na kuridhiwa kwa Itifaki hii. Hata hivyo,baada ya kushauriana na Serikali ilibainika kuna umuhimuwa kuongeza muda ili Kamati iweze kufanyia kazi zaidi ilimatokeo chanya yaliobainishwa kwenye Itifaki hii yawezekuleta maslahi kwa wananchi wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, kwa hekima na busara ulir idhiakuongezwa kwa muda wa kushughulikiwa kwa Itifaki hiiambapo tarehe 28 Agosti, 2019 uliiletea tena Kamati kazi yakushughulikia Itifaki tajwa. Tarehe 04 Septemba, 2019 Kamatiilianza kazi ya kushughulikia Itifaki hii ambalo liliwasilishwambele ya Kamati na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. OmaryMgumba, (Mb).

7.0 MADHUMUNI/MALENGO YA ITIFAKI

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 2 ya Itifaki ya Jumuiya yaMaendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) kuhusukulinda Hakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu zaMimea ina madhumuni ya msingi yafuatayo: -(a) Kuwezesha kuanzisha mfumo thabiti wa kulindahakimiliki za Wagunduzi wa aina mpya za mbegu za mimea;

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

(b) Kuendeleza na kuhamasisha ugunduzi wa aina mpyaza mbegu za mazao ya mimea kwa manufaa ya nchiwanachama katika Jumuiya ya SADC; na

(c) Kutoa Hakimiliki kwa Wagunduzi wa aina mpya zambegu za mimea.

8.0 UCHAMBUZI WA ITIFAKIMheshimiwa Spika, Itifaki hii imegawanyika katika sehemukuu kumi (10) na ina jumla ya Ibara 50 ambazo maudhui yakeni kama ifuatavyo: -

Sehemu ya KwanzaIbara ya 1 ya Itifaki inahusu masharti ya jumla ambayoinaanzia Ibara ya 2 hadi ya 6.

Ibara ya 2 inahusu madhumuni ya Itifaki ambayo yameelezwahapo juu.

Ibara ya 3 inahusu mawanda na maeneo ambayo itifaki hiiitatumika.

Ibara ya 4 ya itifaki inaanzisha Ofisi ya Hakimiliki za Wagunduziwa Mbegu za Mimea katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchiza Kusini mwa Afrika (SADC) ambayo itakuwa na jukumu lakusimamia utekelezaji wa itifaki hii.

Ibara ya 5 ya itifaki inaanzisha Kamati ya Ushauri ya SADCkwa ajili ya kuishauri Ofisi ya Msajili wa Hakimiliki za Wagunduziwa Mbegu za Mimea katika mambo ya jumla na mahsusikuhusiana na utekelezaji wa majukumu yake na mambomengine yanayohusiana na itifaki hii.

Ibara ya 6 inaanzisha Rejista ya Usajili wa Hakimiliki kwaWagunduzi wa Mbegu za Mimea ambayo itatunzwa naMsajili.

Sehemu ya PiliMheshimiwa Spika, sehemu hii ya itifaki inaanzia Ibara ya 7hadi 11 na inahusu masharti ya utoaji wa Hakimiliki za

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

Ugunduzi ambapo ibara hizo zimefafanua kwa undani vigezovitakavyotumika kutoa hakimiliki hizo.

Sehemu ya TatuMheshimiwa Spika, sehemu ya tatu ya itifaki imeanzia Ibaraya 12 hadi 22 ambapo ibara hizi zimeweka utaratibu wa jinsiya kutuma maombi ya kupewa hakimiliki ya ugunduzi wambegu za mimea. Aidha, ibara hizi zimefafanua kiundaniwatu wanaostahili kuomba hakimiliki, utaratibu wa kutumamaombi, haki ya kipaumbele katika kushughulikia maombipamoja na mambo mengine yanayoendana na maombi yahakimiliki.

Sehemu ya NneMheshimiwa Spika, sehemu ya nne inaanzia Ibara ya 23 hadi25 na inaeleza vigezo ambavyo vitatumika katika kufikiriamaombi ya utoaji hakimili.

Sehemu ya TanoMheshimiwa Spika, sehemu hii inahusu Ibara ya 26 hadi 31na inaeleza kuhusu haki za mmiliki wa hakimiliki.Aidha ukomowa muda wa matumizi ya hakimiliki kwa mbegu za mitiumeelezwa utakuwa miaka ishirini na tano (25) tangu siku yakutolewa na kwa mbegu nyingine za mimea ukomo wahakimiliki utakuwa miaka ishirini (20). Hata hivyo ukomo wamuda kwa mbegu nyingine za mimea, unaweza kuongezwana Msajili kutokana na mapendekezo yatakayotolewa kwakena Kamati inaweza kuongeza muda usiozidi miaka mitano(5).

Sehemu ya SitaMheshimiwa Spika, sehemu hii ambayo ina Ibara ya 32 na33, inaelezea kuhusu utoaji wa leseni zinazohusiana nauzalishaji wa mbegu za mimea kutoka kwa mmiliki wahakimiliki ya Wagunduzi wa mbegu za mimea.

Sehemu ya SabaMheshimiwa Spika, sehemu hii ina Ibara moja ambayo ni ya34 na inaweka masharti kuhusu uhamishaji wa hakimiliki yaWagunduzi wa mbegu za mimea.

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

Sehemu ya NaneMheshimiwa Spika, sehemu hii ina Ibara ya 35, 36, na 37 nainaeleza utaratibu wa kurudisha, kubatilisha na kufutwa kwahakimiliki.

Sehemu ya TisaMheshimiwa Spika, sehemu hii ina Ibara moja ya 38 ambayoinaanzisha Bodi ya Rufaa kwa ajili ya rufaa kwa mtu ambaehataridhika na maamuzi ya Msajili.

Sehemu ya KumiMheshimiwa Spika, sehemu ya kumi inaanzia Ibara ya 39 hadi50 inaelezea masharti ya jumla ikiwemo utungaji wa Kanunina taratibu za uendeshaji wa Itifaki, kulinda aina za mbeguambazo zilikuwepo kabla ya Itifaki hii, masuala ya fedha,marekebisho ya Itifaki hii, utatuzi wa migogoro, utaratibu wanchi kujiondoa katika Itifaki hii, utiaji saini wa Itifaki hii, utaratibuwa kuridhia, kuanza kutumika kwa Itifaki, uwasilishwaji wa HatiIdhini na Utekelezaji wa Itifaki.

Mheshimiwa Spika, baada ya Kamati kufanya uchambuzikwenye sehemu hizo za Itifaki, Kamati ilitaka kujiridhishakwenye maeneo ya msingi na hivyo kuhitaji ufafanuzi kwenyemaeneo hayo ambayo ni pamoja na:-

i) Kwa nini nchi zenye uchumi mkubwa na ambazozinafanya vizuri katika tasnia ya mbegu na kilimo kama Afrikakusini, Aidha nchi za Mauritius na Shelisheli ambazo zinauchumi mkubwa hazijasaini Itifaki hii?.

ii) Kuna uharaka gani wa kuridhia Itifaki hii wakati ni nchisaba (7) tu kati ya nchi kumi na tano (15) wanachama waSADC ndio zimesaini Itifaki hii?.

iii) Je Itifaki hii haiwezi kusababisha ukiritimba (monopoly)kutoka katika makampuni makubwa ya mbegu katika tasniaya mbegu?.

iv) Je vituo vya Afrika kwa ajili ya maswala ya hakiubunifuvya ARIPO (Harare-Zimbabwe), OAPI (Africa Magharibi) na

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

PAIPO (Chini ya Umoja wa Afrika) haviwezi kuingiliana nakusigana na Itifaki hii?.

v) Ni kwa kiasi gani uhuru wa mkulima mdogo katika uzalishajimbegu umezingatiwa kwenye Itifaki hii?.

vi) Ni kwa kiasi gani kama nchi tumewekeza katika tafitiza mbegu ili kuweza kumudu ushindani wa nchi Wanachamawa SADC katika ugunduzi, uzalishaji na biashara ya mbegu;

vii) Ni kwa kiasi gani Itifaki hii imezingatia utofauti wamaendeleo ya kiuchumi uliko miongoni mwa nchiwanachama wa SADC? na

viii) Je kuna ulazima gani wa kuridhia Itifaki ya SADCwakati katika Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) ambayoTanzania ni mwanachama haina utaratibu wa KulindaHakimiliki za Wagunduzi wa Mbegu?.

Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako kuwaKamati imeridhishwa na ufafanuzi uliotolewa na Serikalikuhusu hoja zilizoibuliwa na Wabunge. Aidha, Kamati ilifanyakikao na Wagunduzi na Watafiti wa mbegu waliotokaSerikalini na katika Sekta Binafsi ambao Itifaki hii inawagusamoja kwa moja. Kupitia mjadala huu wadao hao waliiakikishiaKamati kuwa kuridhiwa kwa Itifaki hii kutakuwa na manufaayafuatayo: -

• Serikali itanufaika na fedha ilizowekeza kwenye utafiti wambegu kwa kulinda kazi za utafiti wa mbegu zilizozalishwana wataalamu wake;

• Uwepo wa mrabaha utakaopatikana kutokana na gawioambapo Serikali itapata mapato yatakayotokana na gawio,mgunduzi atapata gawio na kiasi kingine cha mrabahakitatumika kuendeleza ugunduzi wa aina mpya za mbegu;

• Kuongeza motisha kwa Watafiti na Wagunduzi wa mbeguna hivyo kuongeza uzalishaji wa mbegu ambazo zitatumikanchini na zingine kuuzwa nje ya nchi na hivyo kuongeza

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

mapato ya Serikali pamoja na kupunguza gharama kubwaya fedha za kigeni zinazotumika kuagiza mbegu nje ya nchi;

• Kuongezeka kwa ushindani na ubunifu miongoni mwaWafatiti/Wagunduzi wa mbegu

• Kutarahisisha upatikanaji wa mbegu bora na mpya kwaharaka na

• Kuridhiwa kwa Itifaki hii kutaongeza uzalishaji wa chakulakwa kuwa wakulima watapata mbegu bora na mpya nahivyo kuhakikishia taifa usalama wa chakula.

9.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spika, baada ya kufanya uchambuzi wa Azimiola Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusinimwa Afrika Kuhusu Kulinda Hakimiliki za Wagunduzi wa AinaMpya za Mbegu za Mimea, Kamati inakubaliana na dhamiranjema ya Itifaki hii kwa Taifa na kwa Wagunduzi wa ndani.Pamoja na dhamira njema iliyopo, Kamati ina maoni naushauri ufuatao: -

(a) Serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya vituo vyautafiti ili kuwezesha watafiti kufanya tafiti kwa kutumia fedhazetu za ndani na sio kama ilivyo sasa ambapo tafiti nyingihufanyika kwa kutegemea fedha kutoka kwa wadau wamaendeleo. Bila ya kuwezesha vituo vya utafiti na wagunduziwa mbegu, Itifaki hii inaweza kunufaisha wagunduzi wambegu kutoka mataifa mengine na sisi kubaki kuwawatazamaji tu.

(b) Ni muhimu kwa Sera na Sheria zinazohusiana naMbegu zikafanyiwa mapitio ili ziweze kuendana na maudhuiya Itifaki hii.

(c) Serikali ifanye mapitio na maboresho ya Sheria yaKulinda Hakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu zaMimea ya Mwaka 2012 ili Sheria hii iweze kujumuisha maudhuiya Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

Afrika na kurekebisha baadhi ya mapungufu yaliyoko kwenyeSheria ikiwa ni pamoja na kipengele kinachoeleza Hakimilikiza Wagunduzi wa aina mpya za mbegu kutovuka mipaka yaTanzania.

(d) Serikali iweke mazingira wezeshi kwa ajili ya kuvutiauzalishaji mbegu nchini. Uzalishaji mbegu, pamoja na mambomengine utaongeza:-

• Motisha kwa wagunduzi wa mbegu kugundua aina mpyaza mbegu;

• Kuokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumika kuagiza mbegunje ya nchi – kiasi cha shilingi bilioni 860 hutumika kuagizambegu kutoka nje ya nchi na

• Kuongezeka kwa mapato ya Serikali, ajira na ujuzi kwawananchi wazawa.

10.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, napenda kukushukuru kwa kunipa nafasiya kuwasilisha Maoni na Ushauri wa Kamati kwa niaba yaWajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugona Maji.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kumpongeza nakumshukuru Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb),Manaibu Waziri Mhe. Omary Mgumba (Mb) na Mhe. HusseinBashe (Mb), Makatibu Wakuu wa Wizara ya Kilimo, MhandisiMathew Mtigumwe na Prof. Siza Tumbo pamoja naWataalamu wote wa Wizara ya Kilimo kwa ushirikianowalioutoa wakati Kamati ilipokuwa ikichambua Azimio hili.

Mheshimiwa Spika, kipekee nawashukuru wadau wotewaliotoa michango yao kwa maandishi na kwa kufika mbeleya Kamati. Michango yao ilisaidia kuijengea uwezo Kamatina kuwawezesha Wajumbe kuwa na uelewa mpanakuhusiana na Azimio hili.

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

Mheshimiwa Spika, kwa dhati kabisa napenda kuwashukuruWajumbe wa Kamati kwa ushirikiano na michango yaowaliyoitoa wakati wa kuchambua na kujadili Azimio hili.Naomba kuwatambua kwa kuwataja majina kamaifuatavyo: -

1. Mhe. Mahmoud Hassan Mgimwa Mb Mwenyekiti2. Mhe. Dkt. Christine G. Ishengoma, Mb M/Mwenyekiti3. Mhe. Dkt. Mary Michael Nagu, Mb Mjumbe4. Mhe. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo, Mb “5. Mhe. Eng. Edwin A. Ngonyani, Mb “6. Mhe. Katani Ahmad Katani Mb “7. Mhe. Khadija Hassan Aboud, Mb “8. Mhe. Haroon Mulla Pirmohamed, Mb “9. Mhe. Ritta Enespher Kabati, Mb “10. Mhe. Mattar Ali Salum, Mb “11. Mhe. Lucy Simon Magereli, “12. Mhe. Justin Joseph Monko “13. Mhe. Omar Abdallah Kigoda, Mb “14. Mhe. Anna Richard Lupembe, Mb “15. Mhe. Pascal Yohana Haonga “16. Mhe. Salim Mbaraku Bawazir Mb “17. Mhe. Deo Kasenyenda Sanga, Mb “18. Mhe. Devotha Methew Minja, Mb “19. Mhe. Haji Ameir Haji, Mb “20. Mhe. Haji Khatib Kai, Mb “21. Mhe. Sikudhani Yasini Chikambo, Mb “22. Mhe. Juma Ali Juma, Mb “23. Mhe. Emmanuel Papian John, Mb “24. Mhe. Kunti Yusuph Majala, Mb “25. Mhe. Anthony Calist Komu, Mb “26. Mhe. Jitu Vrajlal Soni, Mb “

Mheshimiwa Spika, mwisho napenda kumshukuru Katibu waBunge, Ndg. Stephen Kagaigai, Kaimu Mkurugenzi wa Idaraya Kamati za Bunge Ndg. Michael Chikokoto kwa kuisaidiana kuiwezesha Kamati kutekeleza majukumu yake kwa weledimkubwa. Kwa namna ya kipekee naishukuru Sekreterieti yaKamati ambao ni Ndg. Virgil Mtui na Ndg. Rachel Nyegapamoja na msaidizi wa Kamati Ndg. Mwimbe John kwa

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

kuihudumia Kamati ikiwa ni pamoja na kukamilisha taarifa hiikwa wakati.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naliomba sasaBunge lako lipokee, lijadili na liridhie Azimio la Bunge laKuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za KusiniMwa Afrika kuhusu Kulinda Hakilimiki za Wagunduzi wa AinaMpya za Mbegu za Mimea.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na naombakuwasilisha.

Dkt. Christine G. Ishengoma, (Mb)M/MWENYEKITI,

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO,MIFUGO NA MAJI

11 Septemba, 2019

MWENYEKITI: Ahsante, sasa namuita Msemaji waKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa Vizara ya Viwandana Biashara, atatoa maoni ya upinzani kuhusu azimio hilo.Dakika kumi! (Makofi)

MHE. CECIL D. MWAMBE - K.n.y MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI KWA WIZARA YA VIWANDA NABIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya KambiRasmi ya Upinzani Bungeni, nimekuja mbele yako kutoaAzimio la Bunge kuridhia Itifaki ya Marrakesh inayowezeshaupatikanaji wa kazi zilizochapishwa kwa watu wasioona,wenye uoni hafifu au ulemavu unafanya mtu kushindwakusoma wa mwaka 2013 (The Marrakesh Treaty to FacilitateAccess to Publish Works for Persons who are Blind, VisuallyImpaired or Otherwise Print Disabled. “Yanatolewa kwamujibu wa Kanuni ya 53(6) (c) ya Kanuni za Bunge, Toleo lamwaka 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kuwa watu wenyematatizo ya uono ni wengi sana katika jamii. Bado katikajamii zetu ni wachache sana wenye tabia ya kuangalia afyazao mara kwa mara jambo linalopelekea matatizo haya ya

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

macho kukomaa na hata kusambaa katika jamii. Kundi hilikubwa linakumbana na changamoto nyingi ikiwa ni pamojana kukosa haki ya kupata taarifa au maarifa ambayohutolewa kwa njia ya maandishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wenye matatizo yauono ambao hawaoni kabisa au wale wenye uono hafifuhupata ugumu sana katika kutambua dhana mbalimbali zakujifunzia. Hii ikiwa ni pamoja na kupata machapisho yanyaraka mbalimbali kwa kuwa wenye taaluma ya maandishiya nukta katika jamii zetu ni kundi dogo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuja kwa Mkataba huuambao unatambua haki ya kupata elimu na maarifa kwakupitia machapisho kwa kundi hili la watu wenye matatizoya uono bila vikwazo ni jambo kubwa na la kuungwa mkonona kila mmoja kati yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua kuwa katikanchi yetu bado kundi hili kubwa halijapewa kipaumbele.Mpaka sasa kuna shule chache sana au taasisi ambazo nimaalum kwa watu wenye matatizo ya uono. Katika mazingiraya shule, vyuo au hata mahali pa kazi kuchanganya kundihili hukumbana na changamoto nyingi kwa kuwa upatikajiwa nyaraka katika maktaba au hata zile za kiserikalihazijaweza kupatikana kulingana na mahitaji ya kundi hilimaalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo ya kibajeti, ukosefuwa wataalam au uduni wa teknolojia ni miongoni mwachangamoto kubwa zinazosababisha kundi hili kuachwanyuma. Katika hii Itifaki itazilazimu nchi wanachamakuongeza bajeti zao hasa katika wizara zinazohusika nawalemavu ili azimio hili liweze kutekelezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba Marrakesh kuhusuupatikanaji wa kazi zilizchapishwa kwa watu wasioona,wenye uoni hafifu au ulemavu unaomfanya mtu kushindwakusoma wa mwaka 2013, ni ukombozi kwa watu hao kuwezakuwa sambamba na wenzao wasio na tatizo hilo.

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa muunganowa watu wasioona Duniani (The World Blind Union)inakadiriwa kuwa asilimia 90 ya nyaraka zote zilizochapishwaduniani kote, hazipatikani au haziwafikii kwa urahisi watuwenye uoni hafifu au wale wasioona kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkataba wa Marrakeshikutokana na umuhimu wake kwa mataifa mengi Duniani,katika siku ya mwisho Mkutano wa Mabalozi uliofanyika katikaJiji la Marrakesh, Nchini Morocco Juni 2013 na kukubalianakupitisha mkataba huo na hadi kufikia Julai 2016 zaidi yamataifa 75 yalikuwa yamesaini tayari hiyo ikiwa ni ishara nzurikwa kuunga mkono Mkataba huo. Aidha baada ya miezimitatu yaani Septemba 30, 2016 mataifa 20 yalikuwa tayariyameridhia mkataba huo, hili ni jambo kubwa sana kwamikataba ya kimataifa kukubalika kwa haraka sana na nchinyingi ikiwemo Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapitio ya mkataba, Ibaraya 4 ya Mkataba, inatoa kazi maalum kwa nchimwanachama, nchi ambazo zitaridhia makataba huu,kuhakikisha zinarekebisha sheria za ndani zinazohusu hakimiliki. Hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikalikuhakikisha sheria ya COSOTA inafanyiwa marejeo haraka iliMkataba wa Marrakesh uweze kuwa na maanainayokusudiwa kwa jamii nzima ya watu wasioona na walewenye uwezo wa uoni wa hafifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jema sana katikaMkataba huu ni pale unapotoa ruhusa kwa nyarakazinazoweza kutumiwa na wasioona kutoka mataifa menginekuingia katika nchi ambayo tayari imeridhia mkataba, rejeaIbara ya 5 ya Mkataba (Cross-Border Exchange of AccessibleFormat Copies). Jambo hili litaongeza mawanda ya nyarakakwa ajili ya kufanyia rejea kwa wasioona au watu wenyeuwezo hafifu wa kuona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Ibara ya 5 kifungu cha2 (a) na (b) kama zinavyosema;

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

(a) Authorized entities shall be permitted, without theauthorization of the right holder, to distribute or makeavailable for the exclusive use of beneficiary personsaccessible format copies to an authorized entity in anotherContracting Party; and

(b) Authorized entities shall be permitted, without theauthorization of the right holder and pursuant to Article 2(c),to distribute or make available accessible format copies toa beneficiary person in another Contracting Party;”

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nukuu ya aya hizo mbilizilizo kwenye Mkataba, Kambi Rasmi ya Upinzani inaonaitakuwa ni jambo zuri kutambua, haki za msingi za mmiliki wanyaraka au kazi ambayo zimewekwa kwenye muundoambao unawawezesha wasioona au wenye uoni hafifukuweza kuzitumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitendo cha kutumia aukubadilisha kazi ya mtu bila kutambua mmiliki halali wa kazihiyo ni kosa. Pia tukumbuke kuwa kazi hiyo ikishawekwa katikamuundo wa mandishi ya nukta nundu, mmiliki hawezi tenakuelewa kama kazi hiyo ndiyo yenyewe au maudhuiyamebadilishwa kwa sababu labda yeye siyo mtaalam wamasuala ya nukta nundu. Kambi Rasmi ya Upinzani inamtakaMheshimiwa Waziri atoe ufafanuzi kuhusu Ibara hiyo ya 5 kwaujumla wake ili kuondoa sintofahamu ambayo inawezakutokea hapo baadaye wakati wa utekelezaji wa Mkatabahuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Ibara ya 21 ya Itifakihii, inayozungumzia lugha 21 (Languages of the Treaty),inasema:-

1. “This Treaty is signed in a single original in English,Arabic, Chinese, French, Russian and Spanish languages, theversions in all these languages being equally authentic.

2. An official text in any language other than thosereferred to in Article 21(1) shall be established by the Director

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

General of WIPO on the request of an interested party, afterconsultation with all the interested parties. For the purposesof this paragraph, “interested party” means any MemberState of WIPO whose official language, or one of whoseofficial languages, is involved and the European Union, andany other intergovernmental organization that may becomeparty to this Treaty, if one of its official languages is involved”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na umuhimu waMkataba huu, ni vyema sana kama Mkataba huu ukawa kwalugha ya Kiswahili. Naomba kurudia, kutokana na umuhimuwa Mkataba huu, ni vyema sana kama Mkataba huu ukawakwa lugha ya Kiswahili kwa manufaa mapana ya wananchiwetu. Hii itasaidia hata kuondoa migogoro pale endapomwenye haki miliki atakapoona kazi yake imefanyiwa tafsirikwa mujibu wa masharti ya Mkataba huu bila kutambualugha ya Kiswahili kwenye Mkataba huo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho. Kama ilivyo kwamikataba mingine ni vyema sana kama nchi tukajiandaaipasavyo ili kuweza kutekeleza yale yanayokubaliwa ndaniya mikataba ya Kimataifa kwa manufaa mapana ya nchina wananchi wetu kwa ujumla. Kwa kufanya hivyo, Serikaliinapaswa kutathmini utoaji mzima wa fedha za miradi yamaendeleo katika sekta zote, uboreshaji wa miundombinumbinu na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili la Mkataba huumaalum kwa watu wenye uono hafifu, ni lazima Serikali ijikitekatika kuboresha utoaji wa elimu kwa kundi hili ikiwa nipamoja na kupata zana za kutosha kwa ajili ya kufundishia,uboreshaji wa maktaba zetu ili kundi hili nalo liweze kupatanyaraka, kutoa ruzuku au kodi kwa mashine za kisasa ambazozitasaidia kundi hili kupata elimu na maarifa kama makundimengine yoyote yaliyoko nchini kwetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya,kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, naomba kuwasilisha.(Makofi)

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSUAZIMIO LA BUNGE LA KURIDHIA ITIFAKI YA MARRAKESH

INAYOWEZESHA UPATIKANAJI WA KAZI ZILIZOCHAPISHWAKWA WATU WASIOONA, WENYE UONI HAFIFU AU ULEMAVUUNAFANYA MTU KUSHINDWA KUSOMA WA MWAKA 2013

(The Marrakesh Treaty to Facilitate Access to Publish Worksfor Persons who are Blind, Visually Impaired or Otherwise

Print Disabled (MVT) 2013) - KAMAYALIVYOWASILISHWA MEZANI

“Yanatolewa kwa Mujibu wa Kanuni ya 53(6) (c) ya Kanuniza Bunge, Toleo la mwaka 2016

a. Utangulizi

1. Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa watu wenyematatizo ya uono ni wengi sana katika jamii. Bado katikajamii zetu ni wachache sana wenye tabia ya kuangalia afyazao mara kwa mara jambo linalopelekea matatizo haya yamacho kukomaa na hata kusambaa katika jamii. Kundi hilikubwa linakumbana na Changamoto nyingi ikiwa ni pamojana kukosa haki ya kupata taarifa au maarifa ambayohutolewa kwa njia ya maandishi.

2. Mheshimiwa Spika, watu wenye matatizo ya uonoambao hawaoni kabisa au wale wenye uono hafifu hupataugumu sana katika kutambua dhana mbalimbalianazojifunzia. Hii ikiwa ni pamoja na kupata machapisho yanyaraka mbalimbali kwa kuwa wenye taaluma ya maandishiya nukta katika jamii zetu ni kundi dogo sana.

3. Mheshimiwa Spika, kuja kwa Mkataba huu ambaounatambua haki ya kupata elimu na maarifa kwa kupitiamachapisho kwa kundi hili la watu wenye matatizo ya uonobila vikwazo ni jambo kubwa na la kuungwa mkono na kilammoja wetu.

4. Mheshimiwa Spika, tunatambua kuwa katika nchiyetu bado kundi hili kubwa halijapewa kipaumbele. Mpakasasa kuna shule chache sana au taasisi ambazo ni maalum

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

kwa watu wenye matatizo ya uono. Katika mazingira ya shule,vyuo au hata mahali pa kazi kuchanganya kundi hilihukumbana na changamoto nyingi kwa kuwa upatikaji wanyaraka katika maktaba au hata zile za kiserikali hazijawezakupatikana kulingana na mahitaji ya kundi hili maalum.

5. Mheshimiwa Spika, matatizo ya kibajeti , ukosefu wawataalamu na uduni wa teknolojia ni miongoni mwachangamoto kubwa zinazosababisha kundi hili kuachwanyuma. Katika hii Itifaki itazilazimu nchi wanachamakuongeza bajeti zao hasa katika wizara zinazohusika nawalemavu ili azimio hili liweze kutekelezeka.

6. Mheshimiwa Spika, mkataba Marrakesh kuhusuupatikanaji wa kazi zilizchapishwa kwa watu wasioona,wenye uoni hafifu au ulemavu unaomfanya mtu kushindwakusoma wa mwaka 2013, ni ukombozi kwa watu hao kuwezakuwa sambamba na wenzao wasio na tatizo hilo.

7. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa muungano wawatu wasioona Duniani (The World Blind Union) inakadiriwakuwa asilimia tisini ( 90%) ya nyaraka zote zilizochapishwaduniani kote, hazipatikani au hazifikiki kwa urahisi na watuwenye uoni hafifu au wale wasioona kabisa.

8. Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Marrakeshikutokana na umuhimu wake kwa mataifa mengi Duniani,katika siku ya mwisho Mkutano wa Mabalozi uliofanyika katikaJiji la Marrakesh, Nchini Morocco Juni 2013na kukubalianakupitisha mkataba huo, na hadi kufikia Julai 2016 zaidi yamataifa 75 yalikuwa yamesaini tayari hiyo ikiwa ni ishala nzurikwa kuunga mkono Mkataba huo. Aidha baada ya miezemitatu yaani Septemba 30,2016 mataifa 20 yalikuwa tayariyameridhia mkataba huo. Hili ni jambo kubwa sana kwamikataba yakimataifa kukubalika kwa haraka sana na nchinyingi.

b. Mapitio ya Mkataba9. Mheshimiwa Spika, Ibara ya 4 ya Mkataba, inatoakazi maalum kwa nchi mwanachama (nchi ambazo zitaridhia

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

makataba huu) kuhakikisha zinarekebisha sheria za ndanizinazohusu haki miliki, hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaitaka Serikali kuhakikisha sheria ya COSOTA inafanyiwamarejeo haraka ili Mkataba wa Marrakesh uweze kuwa namaana inayokusudiwa kwa jamii nzima ya watu wasioonana wale wenye uwezo hafifu wa kuona.

10. Mheshimiwa Spika, jambo jema sana katika Mkatabahuu ni pale unapotoa ruhusa kwa nyaraka zinazowezakutumiwa wasioona kutoka mataifa mengine kuingia katikanchi ambayo tayari imeridhia mkataba, rejea Ibara ya 5 yaMkataba (Cross-Border Exchange of Accessible FormatCopies). Jambo hili litaongeza mawanda ya nyaraka kwaajili ya kufanyia rejea kwa wasioona au watu wenye uwezohafifu wa kuona.

11. Mheshimiwa Spika, katika ibara hiyo ya 5 kifungu cha2 (a) na (b) kama zinavyosema;“(a) authorized entities shall be permitted, without theauthorization of the right holder, to distribute or make availablefor the exclusive use of beneficiary persons accessible formatcopies to an authorized entity in another Contracting Party;and(b) authorized entities shall be permitted, without theauthorization of the right holder and pursuant to Article 2(c),to distribute or make available accessible format copies to abeneficiary person in another Contracting Party;”

Kwa nukuu ya aya hizo mbili zilizo kwenye Mkataba, KambiRasmi ya Upinzani inaona likatakuwa ni jambo zuri kutambua,haki za msingi za mmiliki wa nyaraka au kazi ambayoimewekwa kwenye muundo ambao unawawezeshawasioona au wenye uoni hafifu kuweza kutumia.

12. Mheshimiwa Spika, Kitendo cha kutumia aukubadilisha kazi ya mtu bila kutambua mmiliki halali wa kazihiyo ni kosa, pia tukumbuke kuwa kazi hiyo ikishawekwa katikamuundo wa mandishi ya nukta nundu, mmiliki hawezi tenakuelewa kama kazi hiyo ndiyo yenyewe au maudhuiyamebadilishwa.

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

13. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinamtaka Mheshimiwa Wazir atoe ufafanuzi kuhusu Ibara hiyoya 5 kwa ujumla wake ili kuondoa sintofahamu ambayoinaweza kutokea hapo baadae wakati wa utekelezaji waMkataba huu.

14. Mheshimiwa Spika,katika Ibara ya 21 ya Itifaki hii,inayozungumzia lugha 21. ‘Languages of the Treaty’

1. “This Treaty is signed in a single original in English, Arabic,Chinese, French, Russian and Spanish languages, the versionsin all these languages being equally authentic.

2. An official text in any language other than those referred toin Article 21(1) shall be established by the Director General ofWIPO on the request of an interested party, after consultationwith all the interested parties. For the purposes of thisparagraph, “interested party” means any Member State ofWIPO whose official language, or one of whose officiallanguages, is involved and the European Union, and any otherintergovernmental organization that may become party tothis Treaty, if one of its official languages is involved”.

15. Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu waMkataba huu ni vyema sana kama Mkataba huu ukawa kwalugha ya Kiswahili pia kwa manufaa mapana ya wananchiwetu. Hii itasaidia hata kuondoa migogoro pale endapomwenye haki miliki atakapoona kazi yake imefanyiwa tafsirikwa mujibu wa masharti ya Mkataba huu.

c. Hitimisho

16. Mheshimiwa Spika, kama ilivyo kwa mikataba mingineni vyema sana kama nchi tukajiandaa ipasavyo ili kuwezakutekeleza yale yanayokubaliwa ndani ya mikataba yaKimataifa kwa manufaa mapana ya nchi na wananchi wetu.Kwa kufanya hivyo,serikali inapaswa kutathimini utoaji mzimawa fedha za miradi ya maendeleo katika sekta zote,uboreshaji wa miundombinu mbinu n.k

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

17. Mheshimiwa Spika, katika hili la Mkataba huu maalumkwa watu wenye uono hafifu ni lazima serikali ijikite katikakuboresha utoaji wa elimu kwa kundi hili ikiwa ni pamoja nakupata zana za kutosha kwa ajili ya kufundishia, uboreshajiwa maktaba zetu ili kundi hili nalo liweze kupata nyaraka,kutoa ruzuku au kodi kwa mashine za kisasa ambazo zitasaidiakundi hili kupata alimu na maarifa kama makundi mengineyoyote.

18. Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, kwaniaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, naomba kuwasilisha.

………………………………..Cecil David Mwambe (Mb)

Kny: MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI-WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

11.09.2019

MWENYEKITI: Ahsante.

Waheshimiwa Wabunge, kwa taarifa yenu naHansard kwenye ukurasa wa 8 wa taarifa ya Kamati yaViwanda na Biashara, kwenye six paragraph ya pili kunamarekebisho. Imeandikwa hapa Mheshimiwa Spika, Kamatiinapenda kumshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira), Mheshimiwa GeorgeBoniphace Simbachawene na inaendelea. Hii ni taarifa yaWaziri inatakiwa isomeke, Kamati inapenda kumshukuru Waziriwa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Innocent Bashungwana Naibu wake Mheshimiwa Stella Manyanya na wataalamwote. Kwa hiyo, naomba kwa taarifa yenu na Hansardmfanye marekebisho hayo. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, sasa tunaanza kuchangiana tunaanza na Mheshimiwa Ally Saleh, Mheshimiwa Haonga,Mheshimiwa Mwambe, Mheshimiwa Amina Mollel,Mheshimiwa Dkt. Ishengoma na Mheshimiwa Eng. Chiza.Dakika tano, tano.

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Jana tulipokuwa katika mafunzo ya watuwanaoshiriki katika Mabunge mbalimbali ya Afrika,tuliambiwa kwamba nchi yetu inachelewa kuridhiamikataba. Kwa mujibu wa viwango vya mikataba hii ambayoimeletwa leo hapa lakini specifically huu wa Marrakeshhaujachelewa kabisa kulinganisha na mikataba mingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba huu ni muhimusana kwa sababu unakwenda kusaidia kundi kubwa la watuwetu. Maelezo yanasema kwamba watu wasioona, wenyeuoni hafifu na ulemavu wa kusoma (print disabled) na hawabaadhi ni wale ambao kwa lugha ya kiingereza wanaitwaDyslexia ambao wanaona sawasawa, wana intelligencesawasawa lakini ni slow leaners. Wale ambao kwenye shuletunasema mbona huyu haelewi, mbona huyu anachelewakuelewa, nao wamekuwa considered katika mkataba huu.Kwa hivyo, mkataba huu unakwenda ku-cover kundi kubwakatika jamii ambalo hivi sasa linakosa fursa ambazowangeweza kuzipata kwa kuwa mkataba huu umechelewakuja kidunia lakini sasa hivi tayari upo na ndani ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo mengi yakufanya kama nchi. Mojawapo ni kama ilivyosema hotubaya Kambi ya Upinzani na hotuba ya Kamati kwamba kunahaja sasa kutengeneza sheria kwa haraka kuhusu copyright.Hilo liende sambamba na kuwaambia watu wetu wa ndanikwa mafunzo, maelezo na semina juu ya umuhimu wakutengeneza kazi hizi na wao wajue kwamba kazi zaozinaweza kukuzwa ili watu kama hao waweze kuzitumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine ni namnaambavyo tunaweza kuwa na kanzi data ya uhakika ili waleambao wanafaa kupewa hizo kazi ambazo zimekuzwa nasiyo kutafsiriwa, kutafsiriwa haimo katika hili, ni kukuzamaandishi ili waweze kuona basi kuwe na uhakika kwambawanaopewa ni watu sahihi. Tunaomba pia taasisi ambayoitahusika na labda wengi wetu tunafikiri ni kama Chama chaWatu Wasiiona au Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu(SHIVYAWATA) ambao wao ni authorized kwa mujibu wa

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

mkataba huu ili na wao waweze kutumia vizuri nafasi hiyo nawasiitumie vibaya kiasi kuweza kuathiri vibaya mkataba huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nafikiri kuna haja, kwasababu tumechelewa kuingia katika mkataba huu ingawasiyo sana kama watu walivyosema kwamba zaidi ya nchi 70zilishajiunga, ya kwenda kujifunza kwenye nchi nyinginewamefanya nini hadi hivi sasa. Moja ya nchi hiyo ni Australiaambayo iko mbele sana katika mkataba huu. NaishauriSerikali ikafanya utaratibu, sidhani kama Afrika tumekwendambele sana lakini kama ziko nchi zimekwenda mbele sanabasi pia tujifunze kwenye nchi za Kiafrika nini wao wamefanyajapokuwa tumechelewa kujiunga lakini tusifanye makosa yaletukafanya vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni haja sasa ambapotunasema mara kwa mara kutengeneza kanzi data. Kila sikutunaambiwa kuna kanzi data lakini jambo kama hili sasaunakuja umuhimu sana kuonesha kwamba ili tuweze kufanyamakisio, ili hiyo kazi ichapishwe kwa haki ya kukuza vyakutosha ni muhimu kuwa na kanzi data juu ya watu wasioona,wenye uoni hafifu na wale ambao wana print disabled.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, ingawa katikahotuba ya Mheshimiwa Waziri halikuwemo kuhusu suala laMarrakesh, ametuambia hapa kwamba Zanzibarimeshirikishwa lakini ingependeza katika Waraka huu rasmiwa Bunge na record zikaonesha kwamba Zanzibarilishirikishwa. Hata hivyo, ukisoma Waraka huu hamnamaandishi hayo kwamba Zanzibar ilishirikishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa namuita MheshimiwaHaonga. Wale ambao wana nia ya kuchangia ambaohawatapata nafasi walete michango yao kwa maandishi.Jiandae Mheshimiwa Mwambe.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Nami naomba kuchangia na nitajikita zaidi

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

kwenye hii Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za SADCkuhusu Kulinda Hakimiliki za Wagunduzi wa aina mpya zaMbegu za Mimea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ni kuhusuasilimia moja ya pato ghafi la Taifa kutopelekwa kwenyeutafiti. Ni kwa muda mrefu sana Serikali yetu haipeleki asilimiamoja ya pato ghafi la Taifa kwenye mambo ya utafiti na leotunaenda kuridhia Itifaki hii, kama fedha hazitapelekwa tafsiriyake ni kwamba tunaenda kuwanufaisha wale ambaowatakuwa tayari kupeleka fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu kwamba nchikama Afrika Kusini imeendelea sana na iko serious sanakwenye mambo ya utafiti, leo tunaenda kushindana nao haokwenye suala hili lakini kwa sababu wao wako serious na sisihatujawahi kupelekea fedha huko, Serikali ituambie baadaya kupitisha Itifaki hii watakuwa tayari sasa kuanza kupelekafedha za utafiti ili tutakachopitisha leo hapa au tutaporidhiaItifaki hii isije mwisho wa siku tukashindwa kuwasaidia watafitiwetu. Kwa hiyo, nadhani hili ni jambo muhimu sana isije kuwatunasindika wenzetu ambao tuko nao lakini waowamejiandaa kuliko sisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni kuhusu fedhaza maendeleo ambazo mara nyingi hapa Bungeni tumekuwatukizipitisha au kuidhinisha lakini fedha hizi hazitolewi. Kwamfano, leo tunapozungumzia suala hili la Hakimiliki zaWagunduzi wa aina mpya za mbegu maana yake hizi nifedha za maendeleo na tunajua kwenye fedha zamaendeleo Serikali hii ya Awamu ya Tano naona haijajipangakabisa kwa sababu mara nyingi sana imekuwa ikisuasuakupeleka fedha kama Bunge linavyoidhinisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, mwaka 2016/2017, zile fedha za maendeleo zilizokuwa zimeidhinishwa naBunge hili shilingi bilioni 100.527 zilipelekwa shilingi bilioni 2.2.Sasa kama zilipelekwa fedha hizo na hapa tunapitisha Itifakihii, je, utekelezaji wa haya mambo inakuwaje? (Makofi)

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2017/2018 tulipelekaasilimia 11 tu ya fedha za maendeleo ambazo ziliidhinishwana Bunge hili. Sasa leo tunapitisha Itifaki hii na kwenye Itifakihapa tunaambiwa bajeti lazima itatumika, sasa inakuwajekama hatutatenga fedha za maendeleo kwa ajili ya kwendakutekeleza mambo haya ambayo tunaenda kuyapanga leo?Kwa hiyo, niseme tu kwamba kama Serikali haijajipangakwenye mambo kama haya ni bora tukawa na subira ilimwisho wa siku tujipange vizuri na baadaye tuangalie namnaya kuweza kufanya lakini kama watatuhakikishia naMheshimiwa Waziri yuko hapa kwamba fedha za maendeleozitatolewa vizuri basi hii Itifaki itatekelezwa lakini kamahazitatolewa kama ambavyo miaka ya nyuma zimekuwahazitolewi, nadhani tutaenda kugonga mwamba nahatutafanikiwa kwenye suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu ni suala lambegu za asili. Serikali ituambie wamepanga utaratibu ganikuweza kulinda mbegu za asili. Nafahamu kwamba nchi yetutumekuwa na mbegu za asili nyingi sana na nyinginezimeanza kupotea polepole. Tulikuwa na mchele mzuri kuleKyela na zamani mnakumbuka ulikuwa unanukia, ule waKamsamba leo Serikali imejipangaje kutunza mbegu hizimaana zinaingia mbegu hizo mpya na za kwetu za asilizinapotea.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mwambe.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia. Leonimeamua tu nichangie niweze kuongea na WaheshimiwaWabunge wenzangu kwa maana ya kukumbushanamajukumu yetu. Ukiangalia trend ya michango yetu sisi wotehumu ndani kama Wabunge kuanzia jana pamoja na leo nahotuba zetu sisi za Kambi jana pamoja na leo tumeamuakuunga mkono moja kwa moja Maazimio haya yaliyoletwambele hapa na Serikali. (Makofi)

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo makusudi ilikuweza kuwakumbusha wenzetu kwamba jukumu letu laKibunge la kwanza kabisa ni pamoja na kutunga sheria. Sualala pili ambalo ni majukumu yetu pia ni kusimamia na kuishauriSerikali katika kutekeleza mipango mbalimbali. Tukifikakwenye hiyo juncture wote tukajua majukumu yetu kimsingihatuwezi kuvutana kwenye haya mambo yanayojitokezahumu ndani na kuharibu atmosphere ya Bunge wakati fulanikwa sababu tunakaa na kusikilizana. Kwa hiyo, hali ya hewainakuwa nzuri kabisa kama ambavyo mmeona imetokea janana leo pia ilivyotokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nachotakanikiseme ni kwamba haya Maazimio ambayo yamekujambele ya Bunge lako Tukufu, wote tunaungana mkonokusema kwamba yameletwa ndani ya Bunge hili kwakuchelewa. Yangekuja mapema sana shida tunazozipatahuko Majimboni kwetu, kwa mfano, mimi natokea Wilaya yaMasasi ambapo tuna Shule ya Msingi ya Masasi ambapo miminilisoma pale darasa la pili mpaka darasa la tano. Pale ndanituna walemavu wa macho na vijana wenye uoni hafifu,wanavaa miwani lakini bado hawawezi kuona, wanatumiahaya maandishi ya nukta nundu. Kipindi cha nyuma walikuwawanatumia Braille ambazo ziko kama rula, wanachoma kwavidoti wanaendelea, baadaye waka- improve wakawekapale mashine, mashine zile kule ndani zimechakaa kabisana haziwezi kuwasaidia, vijana wapya wanaoingia palewanashindwa kupata hizi mashine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru sanaMheshimiwa Ikupa alinisaidia na Mwalimu Kamtande alisemanikushukuru kwa sababu niliweza kupata kwa kufuatiliaSerikalini mashine ya kuchapa kwa kutumia nukta nundu.Suala linalokuja na matatizo tunayoyapata, tumempelekeapale mwalimu ambaye ni mwajiriwa kabisa wa Serikalianafundisha shule ya Msingi Chibugu, bahati mbaya sanalakini kutokana na pesa anazozipata hawezi tena kutumiamshahara wake kwa ajili ya kwenda kununua karatasimaalum kwa ajili ya kwenda kuchapa.

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunapoingiza hiiteknolojia mpya tunataka sasa nukta nundu zianze kutumikamaalum kabisa na Serikali imeiridhia tuone na namna yakuongeza bajeti. Bahati mbaya sana jambo limekuja baadaya bajeti kuu kupitishwa. Sina uhakika kama Wizara kunafungu ambalo wamelitenga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalolimenipa mshangao, mimi ni Naibu Waziri wa Viwanda naBiashara na jambo hili limewasilishwa pale na Waziri wanguwa Viwanda na Biashara, hivi kuna mahusiano gani kati yanukta nundu na Waziri wa Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani hil i jambolingekwenda kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili yakulisimamia vizuri upande unaoshughulika na masuala yawalemavu na wengine, kwa mfano Wizara anayosimamiaMheshimiwa Ikupa hapa lingekuwa na maana zaidi labdana bajeti yake pale ingekwenda vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tumesema tunaungamkono Azimio hili, hatuna pingamizi lolote. Hata mawazomazuri yatakayoletwa na Serikali hapa kwa kusikilizanayakianzia kwenye Kamati zetu za mtambuka na baadayeyakaja ndani ya Bunge, wote tukaona tuna nia moja yakujenga nchi yetu, Taifa letu liweze kuongea kwa lugha mojatunaweza tukafika sehemu nzuri kushauriana kwa kusikilizana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina mengi ya kusema,nilitaka niseme tu hayo machache niwaambie kuna haja yakuridhiana na kuweza kwenda pamoja. Ahsante sana.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa namuita MheshimiwaAmina Mollel ajiandae Mheshimiwa Dkt. Ishengoma naMheshimiwa Engineer Chiza.

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangiakuhusiana na Azimio hili la Mkataba wa Marrakesh.

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 14 Novemba, 2017,niliuliza swali ambalo lilihusu Mkataba huu wa Marrakesh.Katika majibu yao, Serikali waliahidi kulifanyia kazi na kuliletahapa ili mkataba huu uweze kuwasaidia watu wenyeulemavu wa kutoona. Kipekee kabisa naishukuru Serikaliimeonesha wa vitendo kwamba kile walichokiahidiwamekifanyia kazi. Nakupongeza sana Mheshimiwa Wazirimwenye dhamana pamoja na Mheshimiwa Naibu Waziri kwajitihada hizi ambazo kwa kweli zinaleta faraja kubwa sanakwa watu wenye ulemavu pamoja na Serikali yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini Marrakesh?Marrakesh ni kwa sababu mkutano huu ulifanyika nchiniMorocco katika Mji wa Marrakesh na nchi 20 zikaridhia Azimiohili ambapo katika mkataba huo waliridhia kuhusiana nakuweza kuruhusu vitabu mbalimbali viweze kutafsiriwa kwakuchapishwa katika maandishi ambayo yatawasaidiawenzetu wenye uono hafifu na wale wasioona. Kwa kwelikama ambavyo wengine wamesema, Serikali imefanyia kazijambo hili haraka sana na tunawashukuru kwa hilo kwasababu wanafunzi wengi waliokuwa wakisoma katika vyuovikuu walikuwa wakilazimika kutafsiriwa na wakati mwinginekutafsiriwa huwezi jua nini ambacho wakati mwinginekimekosekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa mkataba huuwatu wasioona utaweza kuwasaidia kwa mapana zaidi ili basimaandishi mbalimbali iwe kwenye michoro, vitabu au kwalugha nyingine zozote zile uweze kutafsiriwa na kuwasaidiakupata elimu. Elimu ndiyo kila kitu na hasa kwa watu wenyeulemavu elimu ndiyo mtaji wake. Kwa hiyo, naipongeza sanaSerikali kwa kuleta Mkataba huu wa Marrakesh ili basi watuhawa waweze kufaidika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu tunafahamukabisa kwamba hapa nchini kwetu haki ya kupata taarifahasa kwa watu wenye ulemavu wa kutoona ilikuwa ni shidahapo awali. Kwa hivi sasa, kwa Serikali hii ya Awamu ya Tanotunaona kabisa Mheshimiwa Rais amekuwa na jitihadakubwa. Kwa hiyo, Baraza la Mawaziri pia na kwa kuwa tayari

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

katika Baraza hilo la Mawaziri tunaye pia mtu ambayeanatuwakilisha, tunaona sasa haya yote yakifanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kweli Awamuhii ya Tano imekuwa na jicho la ziada katika kuhakikishakwamba hakuna anayeachwa nyuma wakiwemo watuwenye ulamavu. Ni pongezi za pekee kwa kweli nazitoa kwaMheshimiwa Rais pamoja na Baraza la Mawaziri na Serikaliyote kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika kutafsiri hukuwakati mwingine wako wengine ambao watatakakujinufaisha. Naomba Serikali iwe makini kuhakikisha kwambakile ambacho kimekubaliwa basi watu wenye ulemavu wakutoona waweze kusaidiwa kwa haki na vile vingineambavyo havitokuwa na manufaa basi sheria iweze kufuatamkondo wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Sheria ya Hakimilikiambayo iko chini ya COSOTA tuone sasa kwamba sasa nikwa jinsi gani iendane na mkataba huu wa Marrakesh; nayenyewe pia tuna haja na kila sababu ya kuweza kubadilishavile ambavyo vinahitaji viingie huko na kusiwepo nakipingamizi chochote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwakweli kutokana na hililililofanyika, langu kubwa ni pongezi lakini pia kuona kwambasasa wakati huu tunapokwenda tuone na mikataba mingineambayo kwa namna moja au nyingine bado imeachwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge, kwamamlaka ya Kiti naongeza nusu saa. Namwita MheshimiwaDkt. Ishengoma na Mheshimiwa Chiza ujiandae. Walewengine mnaweza mkachangia kwa maandishi.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii. Nami

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

najikita kwenye Azimio la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya yaMaendeleo ya Nchi za Afrika (SADC) kuhusu kulinda hatimilikiya Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu Pamoja na Mimea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu hawa, wagunduzi,ambao wamefanya utafiti wao wa muda mrefu, kama hiiikiridhiwa itakuwa nzuri sana kwa sababu ya kupata motisha.Watakuwa wanamotisha sana na wataona kuwawametambuliwa na watazidi kufanya utafiti wao kusudiwaweze kupata huo ugunduzi na waweze kugundua ainampya za mbegu pamoja na mimea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Azimio hili likiridhiwa, nchiyetu nayo itaweza kufaidika kwa njia mbalimbali kupitiamapato kwa sababu aina mpya hii ya mbegu za mimeatunaweza kubadilishana pamoja na nchi nyingine za SADCkwa njia ya uhalali. Hapo mwanzoni ilikuwa haibadilishwi kwanjia ya halali kwa sababu tulikuwa tumejifunga kwenye nchiyetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, vijana wetuna wenyewe watapata motisha kuweza kuchukua hayamasomo ya Plant Breeding ambayo yatawawezesha kufanyautafiti na kugundua aina hizi mpya za mbegu za mimea kusudiwaweze kutambulika na waweze kuendelea vizuri pamojana nchi yetu kuweza kunufaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tulivyosema kwenyeKamati, nchi yetu itaweza kufaidika pamoja na wagunduzikwenye mrabaha ambao pia unaweza kutumika mrabahamwingine kuendeleza ugunduzi mpya kwenye mambo hayaya aina mbegu za mimea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe mwenyewe na watuwengine walikuwa wanafahamu kuwa tatizo la mbegu hasahapa nchini ni kubwa sana, lakini kwa kuridhia huu mkataba,hawa watafiti baadaye wakigundua na kuwa wagunduzi,wataweza kujikita sana kwenye tafiti zao na kugundua ainampya za mbegu za mimea ambazo zitaweza kuzalisha

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

mbegu nyingi hapa Tanzania na tutaweza kupata mbeguhizi kwa urahisi bila matatizo yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikisema wagunduzi,simaanishi wale ambao wamesoma tu, kuna wagunduziwakulima ambao na wenyewe wanagundua na hawawakulima na wenyewe itawalinda kusudi waweze kugunduaaina mpya za mimea pamoja na mbegu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajira itazidi kuwepo kwasababu vijana wengi na wakulima watajikita kwenyeugunduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalo nawezakuongelea hapa ambalo nchi yetu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Dakika tano zako zimekwisha.Mheshimiwa Eng. Chiza.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa hilo. Ahsante sana. (Makofi)

MHE. ENG. CHRISTOPHER K. CHIZA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Nami naomba niipongeze Serikalikwa kuleta maazimio haya. Kwanza hata mimi naonatumechelewa, tungeanza jana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba moja kwa mojaniipongeze Serikali kwa kufanya mabadiliko katika kanuni zileza matumizi salama ya bioteknolojia. Kwa wale ambaowalikuwa wanafuatilia kwa jambo hili, jambo hili la Strictliability, hiki kipengele kwa muda mrefu kimekuwa kikwazokikubwa sana kwa watafiti wetu katika nchi hii. Maana mtatitianapoona kwamba yeye akifanya utafiti halafu yeyemwenyewe tena anakamatwa, anashikiliwa, anaadhibiwakwa utatiti ambao ameufanya, basi amekuwa anakosanguvu ya kuendelea na utafiti.

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Ibara hii ya 12ambayo Mheshimiwa Waziri wa Mazingira ameileta, kwakweli naona imeleta ahueni na motisha kwa watafiti wetukuendelea sasa kujikita kwenye utafiti. (Makofi)

Mwenyekiti Mwenyekiti, mbegu bora, mbegu zenyeukinzani na magonjwa, mbegu ambazo zinazalisha, zinaletatija katika uzalishaji ndizo tunazozitaka. Tukijifanya sisi hatutakikufanya utafiti, tutaendelea kutumia tafiti ambazo wenzetuwamefanya uko nje ambazo haziendani na ekolojia ya nchiyetu. Kwa hiyo, tusiogope kufanya utafiti katika nchi yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hiyo, nashaurituache kabisa tabia ya kutotenga fedha za utafiti.Nakumbuka kabisa mwaka 2003 nchi yetu tulikubaliana,tuliridhia pamoja na ile nchi za SADC katika Azimio la Maputo,pamoja na nchi za AU kwamba nchi zetu zitenge kila mojaasilimia kumi ya bajeti zake kwenda kwenye kilimo. Nasitukajiongeza kwamba katika hiyo, asilimia moja iendekwenye utafiti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina uhakika jambo hilitumelifanya kwa wakati gani, lakini kama tumechelewa, basihuu ndiyo wakati sasa tuanze kutenga fedha hizi, watafitiwetu wafanye kazi vizuri kwa uhuru, wapate motisha iliangalau waweze kutupeleka mbele sasa katika kutafitimbegu za mimea ili tuweze kuongeza tija katika uzalishajihasa wakati huu ambao tutahitaji zaidi kuzalisha malighafiza kilimo kwa ajili ya viwanda vyetu vya kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe ushauri,tunapokwenda kwenye utafiti huu, tunazungumza piahakimiliki za kulinda wagunduzi. Amesema vizuri MheshimiwaDkt. Ishengoma, watafiti hawa hawafanyi kazi peke yao,wanafanya kazi na wakulima. Baadhi ya watuwatakaoathirika na matokeo ya utafiti yakiwa ni hasi auchanya, ni wakulima.

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, napendekezatuweke utaratibu, tukitenga fedha za utafiti, tutenge fedhaza kutosha za kutoa elimu kwa wagunduzi, wafanyabiasharawa mbegu pamoja na wakulima wetu ikiwa ni pamoja nakuwafundisha wakulima wetu wajue haki zao ni zipi naowanalindwaje wakati wanapopata matatizo yanayotokanana matokeo hasi yanayotokana na utafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naunga mkono maazimio haya kwa asilimia mia kwa mia.Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa namwita Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira), dakikatano.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kujumuisha aukusema kwa kifupi kwa yale ambayo yamechangiwa.Kwanza nianze kumshukuru Mwenyekiti wa Kamati yaKudumu ya Bunge ya Viwanda, Bishara na Mazingira,Mheshimiwa Saddiq Murad na Makamu MwenyekitiMheshimiwa Col. Mstaafu Masoud Ally pamoja na Wajumbewa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Aidha,nawashukuru pia Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais,Eng. Joseph Mwalongo pamoja na Naibu Katibu Mkuu BaloziJoseph Sokoine na wataalam wote wa Wizara Ofisi yaMakamu wa Rais kwa kushiriki na kuandaa azimio hili hadihatua hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi wachangiaji wengikwa pande zote mbili za Kamati ikiwepo upande wa Upinzanini kama vile wameunga mkono Nyongeza la Azimio hili lakuhusiana na masuala ya Bioteknolojia. Kusema kweli, ingawailielezwa hapa kwamba tumechelewa, lakini upande waUpinzani wamesema kwamba tulipaswa kuacha kuridhia kwasababu tumefanya hivyo kwa haraka na pengine wadauhawakushirikishwa.

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

Mheshimiwa Mwenyekiti, Azimio hili ni nyongeza tu laAzimio la Cartagena ambalo Tanzania iliridhia mwaka 2003.Nyongeza hii ilitokana na namna ambavyo hatua zauwajibikaji na ulipaji wa fidia kwa wale watakaoathirika namatumizi ya bioteknolojia ambapo kulikuwa na mvutano nakikawekwa kifungu cha 27 ili nchi ziweze kwenda kutafakari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nyongeza hiikutoka mwaka 2003 mpaka 2019 ni miaka takribani 16. Kwahiyo, tathmini na tafakari zimefanyika sana na ndiyo maanasasa limekuja kuwekwa humu kuwa eneo au sehemu yaAzimio lile la Cartagena ambalo ilipitishwa mwaka 2000 naTanzania tuliridhia mwaka 2003.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwatoe mashakakwamba ushirikiswaji haukufanyika. Siyo kweli, ushirikiswajiulifanyika kwa kiasi kikubwa sana na kwamba hatua hii nimuhimu sana kwa sababu hatuna namna yoyote ya kuzuiamadhara yanayotokana na bioteknolojia. Sisi Tanzaniabasically, hatujaanza kutumia bioteknolojia, lakini hatunanamna ya kuzuia kwa sababu bioteknolojia inawezakukuathiri kwa namna nyingi; inaweza kuwa direct or indirect.Bidhaa zake tunazitumia na wapo watu inawezekanawameathirika. Kwa hiyo, kusema tusiridhie au tusite nikuendelea kujiweka katika mazingira ambayo watu wetuwakipata madhara, hatuwezi kupata fidia au hawawezikufidiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwanzatumechelewa, lakini sasa tumeamua na Bunge lakolimeamua kukaa na kujadili na kwa kiasi kikubwa wameungamkono. Kwa hiyo, nawashukuru sana, akiwepo mchangiajimmoja Mheshimiwa Eng. Chiza ambaye amezungumziakuhusiana na suala la utafiti kwamba tafiti zimeondolewa.Kwenye ule utafiti umeweka msamaha kwa hatua za kisheriakwa utafiti katika matumizi ya bioteknolojia au shughuli zakitafiti kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niseme tu, pandezote; kwa upande wa Upinzani, Kamati na Waheshimiwa

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

Wabunge wote wametoa maoni mazuri. Sisi kama Serikalitumejipanga na maoni yale yaliyotolewa tutayazingatiakwamba lazima tujenge uwezo wa wataalam kubainimadhara lakini pia jamii kupata elimu ya faida na madharaya bioteknolojia. Maoni haya yaliyotolewa na Kamati yaKudumu ya Bunge tumeyachukua na tutayafanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo,naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

(Hoja ilitolewa Iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya pamoja ya ziada yaNagoya – Kuala Lumpur kuhusu Uwajibikaji Kisheria na Fidiakwa Madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi

ya Bioteknolojia ya Kisasa katika 14 kutekeleza Itifaki yaCartagena (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary

Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol onBiosafety, liliridhiwa na Bunge)

MWENYEKITI: Wote wameafiki. Mheshimiwa Waziri,sasa hili ni Azimio Rasmi la Bunge na linaingia kwenye record.Hongera sana Mheshimiwa Waziri na Wabunge wote ambaokwa pamoja mmeunga mkono Azimio hili.

Waziri wa Kilimo.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali yayote, naomba nichukue nafasi hii kwanza kukushukuru wewemwenye binafsi kwa kutupa nafasi. Pia nashukuru Kamati yaKilimo Maji na Mifugo kwa michango mizuri ambayowametoa kwa namna ambavyo wameishauri Serikali na sisitunasema kwamba ushauri wao wote tumeupokea,tutaufanyia kazi ili tuweze kutekeleza vizuri itifaki hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nitumie nafasi hiikumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwakuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC. Kwa kwelitunampongeza sana sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuridhia itifaki hii yamaendeleo za nchi za Kusini mwa Afrika, inatupa heshimakubwa kwamba Mwenyekiti wetu sasa atakuwa na nafasinzuri ya kuweza kutekeleza majukumu yale yote ambapoamechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Nchi za SADC. Kwa hiyo,naomba Waheshimiwa Wabunge tuunge mkono itifaki hii kwasababu ina manufaa makubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati imetoa maoni mengikuhusu uwekezaji kwenye utafiti na wengi wameshaurikwamba Serikali iangalie uwezekano wa kuwekeza asilimiamoja kwenye mapato ghafi ya Taifa. Ni kweli wazo ni zuri nawengi wameshauri hivyo, tunapokea, lakini nataka nisemetu kwamba uwekezaji kwenye utafiti tunaouzungumzia niutafiti kwa ujumla, siyo kwenye kilimo peke yake. One percentkutoka kwenye GDP ni kwenye utafiti wote katika Wizaranzima, iwe kwenye elimu iwe kwenye kilimo na maeneomengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukifanya hivyo, maanayake ukichukuwa kwa mfano sasa hivi pato la Taifa ambaloni takribani zaidi ya Dola za Marekani bilioni 54, maana yaketunahitaji karibu almost trilioni moja kwa ajili ya uwekezaji. Niwazo zuri, nasi Serikali tunalipokea, lakini wakati wa kupangavipaumbele, tunaangalia kwa sababu ya mapato kidogoyanayokuwepo, vipaumbele ni nini? Tuwekeze kiasi gani?Kwa hiyo, hili tunalichukuwa, tunaendelea kulifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ya utafiti, inatokakwenye vyazo vya ndani, inaweza ikatoka kwa Washirika waMaendeleo, inaweza ikatoka kwa watu binafsi. Sisi kamaSerikali kwa mfano upande wa kilimo, mwaka huu tumetengazaidi ya shilingi bilioni nane kwa ajili ya kuhakikisha kwambatunafanya utafiti wa mbegu; na hizi hela tutahakikisha kwakweli TARI wanafanya vizuri katika kufanikisha utafiti.

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa hivi Wagunduziwetu wa mbegu wamefanya vizuri sana. Kwa mfano, katikaAfrika sina uhakika kama kuna taasisi kama TARI kuleNaliendele, kazi ambayo wameifanya na ugunduzi ambaowameufanya na mbegu ambazo zimegundulika, sina uhakikakwenye zao la korosho kama kuna taasisi hapa Afrika ambayoimefanya kama vile; na mbegu zetu sasa hivi zinatumikakatika nchi nyingi hapa Afrika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa kuridhia itifaki hii,maana yake manufaa ya mbegu zetu ambazo zinatumikasasa hivi Zambia na nchi nyingine, tutakuwa na uwezo sasawa kupata angalau mrahaba unaotokana na ugunduzi huu.Kwa hiyo, nataka kusema kwamba mambo ni mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunayo kazi ya kufanyamapitio. Sasa hivi tunapitia Sera yetu ya Kilimo ya Mwaka2013, pia tutakuja na sheria mpya ambayo itakuwa ni jumuifu,ambayo itarekebisha vikwazo vyote ambavyo vitafanya itifakihii ishindwe kutekelezeka. Kwa hiyo, tutarekebisha kamatulivyoshauriwa na Waheshimiwa Wabunge na Kamati, hayayote tutayazingatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya WaheshimiwaWabunge, pamoja na Mheshimiwa Haonga wamechangiasana namna ya kuboresha mbegu, nami nakubaliana nasuala la kubadilishwa mbegu za asili. Mbegu za asili ndiyozimetufikisha hapa, nasi tutakuja sasa hivi na sheria nyinginekwa ajili ya kulinda hizi mbege za asili. Kwa sababu ili uje nambegu nyingine za kisasa, ni lazima hata mbegu ya asiliuitambue; na utakapokuwa una-cross, unaunganisha, basizote hizi tunataka tuwatambue na tuhakikishe tunalinda kwamaslahi mapana ya Taifa letu. Nina uhakika kama hayatutayatekeleza, mambo yatakwenda vizuri sana. Kwa hiyo,nilihakikishie Bunge hili kwamba itifaki hii itakuwa na manufaamakubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida ni nyingitumeshazisema, kwa sababu ya muda hatutaweza kusemamengi, lakini nawaomba Waheshimiwa Wabunge wote kwa

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

pamoja, turidhie Itifaki hii ya Ugunduzi wa Mbegu Mpya zaMimea ili ziwe na manufaa na wagunduzi wetu wapate kuwana motisha ya kuendelea na ugunduzi na kufanya utafiti wakila namna; nami nina uhakika mkisharidhia, wagunduziwengi au watafiti wengi wataenda kuwekeza kule kwasababu wana uhakika sasa wakiwekeza watapata faida nawatapata mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, naafiki.

(Hoja ilitolewa Iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Azimio la Kuridhia Itifaki ya Maendeleo ya Nchi zaKusini mwa Afrika kuhusu Kulinda Hakimiliki za Wagunduzi

wa Aina Mpya za Mbegu za Mimea (The Protocol forProtection of New Varieties of Plant [Plant Breeder’s Rights]in the Southern African Development Community – SADC)

liliridhiwa na Bunge)

MWENYEKITI: Walioafiki wameshinda na Bunge zimalimekubali. Mheshimiwa Waziri na Waheshimiwa Wabunge,hongereni sana. Sasa hili linaingia kwenye record ni Azimio laBunge.

Waziri wa Viwanda na Biashara, dakika tano.

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza nakushukuru kwa kunipa nafasi hii iliniweze kuhitimisha hoja ya Mkataba wa Marrakesh. Pianaishukuru sana Kamati ya Viwanda na Mazingira kwaushirikiano walioipa Wizara yangu katika mchakato mzimawa kuandaa azimio hili mpaka kufikia Bungeni leo hii.Nawashukuru sana Mheshimiwa Suleiman Saddiq Murad, Col.Masoud pamoja na Wajumbe wote wa Kamati ya ViwandaBiashara na Mazingira.

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia namshukuru sana NaibuWaziri Mheshimiwa Eng. Stella Manyanya, Katibu Mkuu,Mkurugenzi wa COSOTA na wataalam wote kwa kazi nzuriwalioifanya katika maandalizi ya azimio hili la Mkataba waMarrakesh.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nawashukuru sanaChama cha Wasioona wakiongozwa na Mwenyekiti LucyBenito pamoja na Emmanue Simon, Katibu; nawashukurusana kwa kufika kwenye Bunge letu Tukufu kushuhudia azimioletu hili muhimu sana kwa walengwa wetu, ndugu zetu, watuwenye ulemavu nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia namshukuru sana NaibuWaziri, dada yangu Mheshimiwa Stella Ikupa, MheshimiwaBalozi Venance Mwamoto, Mheshimiwa Dada Amina Mollelna Mheshimiwa Kaka Ally Saleh, wametoa mchango mkubwasana katika kusukuma azimio hili liweze kufikia hatua muhimuya leo. Nawashukuru sana Waheshimiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nawashukuruWaheshimiwa Wabunge wote waliochangia, waliotoaushauri na wale ambao hamjachangia, wote najuamnaunga mkono hoja hii. Tunawashukuru sana kwa niabaya ndugu zetu watu wenye ulemavu, nawashukuru sana kwakuunga mkono hoja hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi nimekuja kushukurukwa sababu hoja hii haijapingwa na Mbunge hata mmojazaidi ya kutoa maoni ushauri na tumeelekezwa na Kamati yaViwanda, Biashara na Mazingira pamoja na michango yaWaheshimiwa Wabunge kwamba mara tu baada ya kuridhiaItifaki, basi tujitahidi sana marekebisho ya Sheria ya COSOTAyafanyike haraka iwezekanavyo ili ndugu zetu walengwawaweze kunufaika na itifaki hii, nasi kama Serikali, ushauri huutumeuchukuwa tutasukuma kwa nguvu ili mapitio ya sheriahizi yaweze kufanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na concern yacopyright kwa mwandishi wa awali, pale ambapo maandishi

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

yake yanahamishwa kwenye muundo wa nukta nundu,kwamba copyright yake, intellectual propaties, atapotezaile haki, lakini napenda kuwaondoa wasiwasi WaheshimiwaWabunge, kuhama kwa machapisho kunahama pia kwacopyright ya author. Kwa hiyo, jambo hili nilitaka kuwaondoawasiwasi, copyright inahama pamoja na muundo wamachapisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mheshimiwa Ally Salehkama alivyopendekeza, tuna fursa ya kujifunza kutokakwenye nchi ambazo tayari zimesharidhia. Kwa hiyo,tutaangalia best practice kwenye hili pamoja na mengine ilikuhakikisha mapitio na ya sera na sheria yanakidhi kiu na niaya kuhakikisha mkataba huu unawasaidia ndugu zetuwasioona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambaloningependa kulitolea maelezo ni suala la ushirikishwaji wawadau. Mchakato mzima umeshirikisha wadau kikamilifu; nakwa mara nyingine niwashukuru sana ndugu zetu upandewa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wadau wote kupitiaCOSOZA wametupa maoni mazuri sana ambayoyamepelekea kukamilika kwa mchakato wa kushirikishawadau na kuleta azimio hili hapa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tutahakikisha maudhuiya itifaki yanatafsiriwa katika Kiswahili ili yaweze kupatikanakote nchini kwa walengwa wetu pamoja na suala zima lakanzidata kama ilivyoshauriwa. Kuwa na kanzidata ni muhimusana kwa sababu itatusaidia kuwahudumia walengwa wetuvizuri. Kwa hiyo, jambo hili nalo tumelichukuwa tutalifanyiakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,nashukuru kwa kunipa nafasi hii tena na ninaomba kutoahoja. (Makofi)

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Mwenyekiti, naafiki.

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE · (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety). NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

(Hoja ilitolewa Iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Azimio la Kuridhia Itifaki ya Marrakesh inayowezeshaUpatikanaji wa Kazi zilizochapishwa kwa Watu Wasioona,

Wenye Uoni Hafifu au Ulemavu Unaofanya Mtu KushindwaKusoma wa Mwaka 2013 (The Marrakesh Treaty to Facilitate

Access to Published Works for Persons who are Blind,Visually Impaired or Otherwise Print Disabled (MVT) 2013)

Liliridhiwa na Bunge)

MWENYEKITI: Wabunge wote wameafiki. Kwa pamojanawapongeza sana Waheshimiwa Mawaziri kwa Maazimiohaya yote matatu ambayo yamepita leo kwa mudamuafaka, sasa napenda kuwaambia tu, kazi za Bunge zoteza leo zilizopangwa zimekwisha, namshukuru MwenyeziMungu kwa kutupa wepesi wa kufanya kazi yetu kwa harakana kwa uadilifu na kwa uaminifu mkubwa sana wa Taifa letu.

Naahirisha shughuli za Bunge mpaka kesho saa 3.00asubuhi.

(Saa 7.23 Mchana Bunge liliahirishwa hadi Siku ya Alhamisi,Tarehe 12 Septemba, 2019, Saa Tatu Asubuhi)