chuo cha serikali za mitaamuki.lgti.ac.tz/documents/lgti_mwezeshaji_mwongozo_swahili.pdf · za...
TRANSCRIPT
-
CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA
MWONGOZO WA MWEZESHAJI
Mwongozo huu wa Mwezeshaji umetayarishwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (ORTAMISEMI), Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Mradi wa
Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani
(USAID), uliopo Dar es Salaam, Tanzania
© Chuo cha Serikali za Mitaa, 2018 Toleo la kwanza ,(Elimu masafa), 2018
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili au kukitoa kitabu hiki kwa njia yoyote ile bila
idhini ya maandishi ya Chuo cha Serikali za Mitaa.
-
Yaliyomo 1.0 Fahamu namna ya kutumia Moodle(MUKI) .................................................................................... 3
2.0 Sajili kozi mpya ................................................................................................................................ 3
2.1 Anza .............................................................................................................................................. 4
3.0 Uhariri wa Vipengee vya Kozi Yako ................................................................................................ 6
4.0 Maelekezo ya ujumla ya upakiaji wa kozi. ....................................................................................... 6
5.0 Mahitaji Katika Utengenezaji wa Kozi ............................................................................................. 8
6.0 Uongezaji wa bloku kwenye kozi yako .......................................................................................... 10
7.0 Usimamizi wa kozi yako................................................................................................................. 12
8.0 Kuongeza Rasilimali ....................................................................................................................... 12
9.0 Kuweka Kazi .................................................................................................................................. 14
10.0 Kazi ............................................................................................................................................... 15
10.1 Hatua kwa ajili ya kupangilia kazi ............................................................................................ 15
10.2 Matini ya Mtandaoni ................................................................................................................. 17
10.3 Upakiaji wa faili wa juu ............................................................................................................ 17
10.4 Kupakia faili moja .................................................................................................................... 18
11.0 Kusahihisha Kazi .......................................................................................................................... 19
12.0 Zoezi la Papo kwa Papo ................................................................................................................ 20
12.1 Kutengeneza Maswali ............................................................................................................... 20
12.2 Mipangilio ya kawaida kwa aina zote za maswali .................................................................... 21
13.0 Aina ya Maswali ........................................................................................................................... 22
13.1 Swali la insha ............................................................................................................................ 23
13.2 Majibu yaliyounganishwa na (Vaana) Maswali ....................................................................... 23
13.3 Maswali ya kuchagua ................................................................................................................ 24
13.4 Swali la Nambari ...................................................................................................................... 24
13.5 Maswali ya Kweli/Si kweli ...................................................................................................... 25
14.0 Jukwaa .......................................................................................................................................... 25
15.0 Soga .............................................................................................................................................. 29
16.0 Faharasa ........................................................................................................................................ 30
17.0 Kitabu cha alama .......................................................................................................................... 33
17.1 Kuingiza na kuweka alama ........................................................................................................ 33
18.0 Tathmini ........................................................................................................................................ 34
19.0 Hariri wasifu wako........................................................................................................................ 36
20.0 Kutuma ujumbe wa faragha ......................................................................................................... 38
-
3
1.0 Fahamu namna ya kutumia Moodle(MUKI)
Nenda kwenye wavuti ya Moodle (elms.lgti.ac.tz). Hii itakupeleka kwenye ukurasa wa kuingia ndani ya mfumo:
Ingiza "jina la mtumiaji" na “Nywila,” bofya kwenye kitufe “Ingia.” Itakupeleka kwenye ukurasa wa mwanzo wa mfumo.
2.0 Sajili kozi mpya
Jukumu la mwalimu linaweza kuhariri au kuongeza maudhui kwenye kozi ambayo
imeshasajiliwa. Kama unahitaji kua na kozi mpya ni lazima umuombe msimamizi
wa mifumo asajili kozi mpya kwa ajili yako ama vinginevyo akupe haki ya msajili
kozi.
Ukishaingia ndani ya mfumo unaweza kufungua kozi yako kwa kubofya “Kozi za
Madiwani” kwenye kategoria ya kozi kisha bofya kwenye kozi yako.
-
4
2.1 Anza
Ukurasa wa mwanzo wa kozi unafanana na picha ya kiwamba ifuatayo. Upande wa
kulia chini kuna bloku ambazo zinaweza kuongezwa ama kuondolewa, na kushoto ni
"eneo la kufanyia kazi".
-
5
Unaweza kuanza kufanya kazi kwa kuruhusu uhariri, kwenye kitufe kilichopo juu kulia
kwenye menyu ibukizi chagua “Ruhusu uhariri”:
Ukurasa wa mwanzo wa kozi baada ya kuruhusu uhariri;
-
6
3.0 Uhariri wa Vipengee vya Kozi Yako
Wakati uhariri umewezeshwa, Kila kipengee kwenye ukurasa wa mwanzo wa kozi yako na
kila sehemu/bloku kutakua na ikoni pembeni yake ambazo zote ninafanya kazi mbalimbali
kama vile kuhariri /hamisha / durufu/ futa/ ficha.
Alama Kazi
Ikoni ya uhariri inakuwezesha kubadili maneno au mipangilio wa kipengee
Ikoni ya onyesha/ficha inawezesha kipengee kionkane au kisionekane kwa wanafunzi
Ikoni za mishale ya kushoto na kulia inatumika kujongeza vipengee vya kozi
Ikoni za mishale ya Juu na Chini zinatumika kuhamisha vipengee na bloku kwenda juu ama chini.
Ikoni ya kuhamisha inawezesha kuhamisha kipengee kwenda kwenye mada au bloku nyingine.
Ikoni ya"crosshairs" inakuwezesha kuhamisha vipengee au sehemu kwa kukokota na kuachia.
au
Ikoni ya kufuta inaondoa kabisa vipengee ama bloku kwenye kozi yako Delete.
Groups icon allows you to change between no groups or separate/visible groups
Roles icon allows you to assign roles locally in the item.
Ikoni ya msisitizo inakuwezesha kusisitiza sehemu kama eneo lililopo kwa wakati huu.
4.0 Maelekezo ya ujumla ya upakiaji wa kozi.
Utakapo bofya kwenye ikoni hapo juu ukurasa ufuatao utaonekana;
Bofya hapa kuongeza taarifa za jumla
za kozi. Jina la kozi, Maelezo na
Madhumuni.
-
7
Weka Muhtasari wa kozi hapa
Kama tayari,Bofya
hapa kuhifadhi
mabadiliko
Andika jina la kipengele
-
8
5.0 Mahitaji Katika Utengenezaji wa Kozi
Ona Mfano Hapo chini
-
9
Msimbo na Jina la Kozi
Maelezo na
Malengo ya
Kozi
Maelezo ya
Kozi
4. Mada ya Mafunzo na
Maudhui Yake (Vidokezo,
PPT, Video, Maswali,
Marejeleo na Shughuli)
-
10
6.0 Uongezaji wa bloku kwenye kozi yako
Bloku zinatokeza upande wa kushoto chini wa eneo la kufanyia kazi ambamo unaongeza
kazi na vitendea kazi vyako.
Kuna bloku nyingi za kawaida ambazo zinakuwezesha, kwa mfano, kuonyesha kalenda,
shirikisha matokeo ya zoezi, onyesha RSS feeds, ongeza maudhui binafsi, o n y e s h a
m t u m i a j i a l i e k o h e w a n i , o n y e s h a m a o n i k w e n y e k o z i y a k o nk. M w a l i m u
a n a w e z a k u o n g e z a b l o k u m p y a w a k a t i u h a r i r i u k i w a u m e w e z e s h w a k w a
Mada iliyogawanywa katika sehemu sita
Faharasa
Marejeo
Tathmini
http://docs.moodle.org/22/en/Remote_RSS_feeds_block
-
11
k u b o f y a "Ongeza Bloku" kwenye menyu chini kushoto mwa ukurasa:
Hiyo ni mifano ya bloku, pia
unaweza kuongeza bloku
kutegemeana na Matukio
unayohitaji kuyaonesha kwa
mwanafunzi.
-
12
7.0 Usimamizi wa kozi yako
Sehemu ya usimamizi wa kozi ya mipangilio ya bloku inamuwezesha mwalimu kusimamia
nyanja mbalimbali za kozi zao. Watumiaji –wanaweza kuwaandikisha watuamiaji wapya. Vichujio - inaweza kuwezesha au kuzima vichujio vilivyoruhusiwa vya kozi yako. Alama-inawezesha kuona,kuongeza na kuhariri alama za wanafunzi wako. Cheleza/Rejesha - v iu n g a n i sh i h i v i v in a ku w e z e sh a ku d u r u f u k o z i ya k o a u
k u re je sh a k oz i ku t ok a mah a l i p op ot e .
Ingiza ndani - unaweza kuingiza shughuli kwenye kozi yako hapa. Anzisha upya–inawezesha kuondoa taarifa za watumiaji wa zamani mwishoni mwa mwaka
wa masomo au kipindi ili kuanza upya
8.0 Kuongeza Rasilimali
Pamoja na kuongeza zoezi shirikishi kwa wanafunzi wako, unaweza kuwapa rasilimali
tuli.
Kuongeza rasilimali, wezesha uhariri, chagua sehemu kwenye ukurasa wako wa kozi
ambapo ungelipenda ionekane na bofya kwenye menyu kunjufu "Ongeza rasilimali au
shughuli".
Kitabu - inamuwezesha mwalimu kuweka rasilimali yenye kurasa nyingi kama kitabu chenye
sura.
Faili - Kama unataka kupakia nyaraka za kozi katika mtindo mwingine, unaweza
kuzihifadhi katika Moodle na ukarahisisha wanafunzi kuzifikia.
Folda - Kama ukipakia maudhui mengi , ungeweza kuyakusanya kwenye
makabrasha. Unaweza kuyaonyesha maudhui ya folda lote badala ya fail i
moja baada j ingine.
Maudhui ya IMS - Maudhui ya IMS inaruhusu maudhui yaliyowekwa kulingana
na maudhui ya IMS y a o n e k a n e k w e n y e k o z i . IMS n i c h o m b o
k i n a c h o s a i d i a k u a i n i s h a k a n u n i z a k i t a a l a m z a v i t u
m b a l i m b a l i , maudhui ya kimtandao ya kujifunzia.
Lebo - L e b o i n a w e z e s h a m a t i n i n a t a s w i r a z i c h o m e k w e m i o n g o n i m w a v i u n g a n i s h i v y a s h u g u l i .
Urasa- Ukurasa unawezesha ukurasa wa tovuti uonekane na kuhaririwa ndani ya kozi.
URL - Unaweza kutengeneza kiurahisi viunganishi vya tovoti nyingine nje ya kozi ya Moodle.
-
13
Orodha ya Rasilimali na kazi
Chagua Rasilimali au Kazi
kisha Bofya hapa kuweka
-
14
9.0 Kuweka Kazi
Moodle inatoa idadi kubwa ya shuguli za kujifunzia kwa wanafunzi. Kuweka kazi wezesha
uhariri, chagua sehemu kwenye ukurasa wa kozi yako ambapo ungependa ionekane kisha
bofya kwenye menyu kunjufu "Weka kazi"
K a z i : Kuwaambia wanafunzi watume kazi
S o g a : Pangilia chumba cha kusogoa kwa wanafunzi
Chaguo: Pangilia kura kwa wanafunzi
K a n z i d a t a : Pangilia kanzi data ya wanafunzi ya kuchangia
J u k w a a : Pangilia majukwa ya wanafunzi washiriki kwenye majadiliano
F a h a r a s a : Pangilia faharasa ambamo wanafunzi wanaweza kuchangia.
S o m o : Pangilia somo la kujisahihisha.
Z o e z i : Pangilia jaribio la kujisahihisha mwenyewe kwa kutumia maswali ambayo
umetunga kwa kutumia akiba ya maswali ya moodle.
-
15
10.0 Kazi
Kazi inatumika wakati unataka wanafunzi wako watume kazi kupitia Moodle (isipokua kazi za
nje ya mtandao). Kazi ikishatumwa unaweza kutoa alama na kutoa mrejesho kupitia Moodle.
Alama zinatunwa kwenye kitabu cha alama cha kozi. Kuna aina nne za kazi. Chaguo lako la
aina ya kazi inategemea unataka wanafunzi wako wafanye nini.
M a t i n i y a M t a n d a o n i
Mwanafunzi anachapa ndani ya kiboksi kwenye Moodle – wanakua na kihariri cha
Moodle WYSIWYG hivyo wanatumia vitendea kazi vilivyomo; kujiunganisha kwenye
tovuti, kuonesha picha, nk.
P a k i a f a i l i m o j a
Wanafunzi watapaswa kupakia faili. Mwalimu ataamua ukubwa wa mwisho wa faili la
kupakia wakati akipanga kazi.
Pakia faili zaidi ya moja
Mwalimu anaweza kuruhusu upakiaji wa faili zaidi ya moja. Kwa aina hii ya kazi,
mwanafunzi anaweza kufuta kazi ambayo tayari ilikua imepakiwa na kutuma
upya.
Kwahiyo aina hii ya zoezi ni muhimu hasa kama unataka wanafunzi wako watume
nakala ya rasimu ambayo unaweza kutoa mrejesho kabla hijaboreshwa na
mwanafunzi kisha atume upya. Mara toleo la mwisho litakapokua limepakiwa,
wanafunzi wanaweza kubofya ‘tuma kwa ajili ya usahihishaji’.
10.1 Hatua kwa ajili ya kupangilia kazi
Kupangilia zoezi kunafanana kwa aina zote za mazoezi isikuwa kuna sehemu maalumu yenye
mipangilio mahsusi kwa ajili ya aina ya kazi iliyochaguliwa.
Mipangilio ya Ujumla (Inafanana kwa aina zote za kazi)
• Wakati uhariri umewezeshwa kwenye kozi yako, nenda kwenye sehemu
ambapo ungependa kuweka kazi bofya ‘ongeza kazi...’
• Chagua aina ya kazi.
• Weka jina la kazi (jina litakua kiunganishi ambacho wanafunzi wako watabofya)
• Kwen ye k isanduku cha maelezo wap e wanafunz i wako maelekezo wan ayoh ita j i kukamil i sha kaz i .
-
16
Bainisha ni namna gani utasahihisha kazi kwa kutumia ‘alama’ kwenye menyu kunjufu.
• Amua kama unataka kudhibiti ni wakati gani wanafunzi wako wanaweza kuanza
kutuma kazi kwako. Unaweza pia kupangilia ni lini iwe mwisho wa kutuma kazi au
ukazima hali tumizi hii kwa pamoja (kwa kutumia vijisanduku vya chaguzi).
• A m u a k a m a u t a w a r u h u s u w a n a f u n z i w a t u m e k a z i k w a k u c h e l e w a a u i s i t u m i w e
mipangilio ‘zuia utumaji uliocheleweshwa’ (kama umechagua kutumia tarehe ya mwisho hapo kwanza). The next section of settings is specific to the assignment type you chose.
Andika Maelezo ya kazi yako hapa
Unaweza kuweka tarehe ya
kukamilisha kazi hapa
-
17
10.2 Matini ya Mtandaoni
10.3 Upakiaji wa faili wa juu
Endelea kufanya Machaguo mbali
mbali na ukamilishe kazi yako.
-
18
Ukubwa unaoruhusiwa wa faili : Chagua ukubwa wa juu wa faili ambao
wanafunzi wanaweza kupakia kwa kila faili moja.
R u h u s u u f u t a j i : Mwanafunzi anaweza kufuta faili lilitomwa au la?
I d a d i y a j u u y a m a f a i l i y a t a k a y o p a k i w a : Amua ni mafaili
mangapi yatumwe kwaajili ya kazi.
Ruhusu notsi: Je unataka kuwapa wanafunzi wako mahali pakuandika notsi notes,mf. maelezo ya kuainisha faili.
F i c h a m a e l e z o k a b l a t a r e h e k u f i k a : Kama utachagua hili,
maelekezo ya kazi yatafichwa na kubadilishwa na: ‘Samahani, kazi hii haipatikani
bado. Maelekezo ya kazi yataoneshwa hapa kwenye tarehe ilioonesha chini.
T a a r i f a z a b a r u a p e p e k w a w a l i m u : K a m a Moodle i n a f a h a m u
anuani yako ya barua pepe na umechagua ndio utapokea barua pepe kila wakati
mwanafunzi akituma kazi kwako.
W e z e s h a u t u m a j i k w a a j i l i y a k u s a h i h i s h a : K a m a u k i c h a g u a n d i o mwan af u n z i a t ab of ya k i t u f e k i l i ch oan d i kw a
‘Tuma kwaajili ya kusahihisha’ wakati watakapopakia mafaila yaliyotayari. Kama
hapana, kazi itaonekana kama imeshatumwa mara tu mwanafunzi anapopakia
faili
10.4 Kupakia faili moja
Ruhusu kutuma upya: Kama ‘Ndio’ wanafunzi wanaweza kutuma upya kazi
zao. Kama ‘Hapana’ na mwanafunzi ametuma kazi kimakosa hakuna
namna ya kuanza upya.
T a a r i f a z a b a r u a p e p e k w a w a a l i m u : Hii inafanana na aina
zingine za kazi juu. Kama Moodle inafahamu anuani yako ya barua pepe
na uchague ndio utapokea barua pepe kila wakati ambapo mwanafunzi
atatuma kazi kwako.
Ukubwa wa juu wa faili: Inafana na pakia faili zaidi ya moja. Chagua ukubwa
wa juu wa faili ambao mwanafunzi anaweza kupakia.
-
19
11.0 Kusahihisha Kazi
Wanafunzi wanapowasilisha kazi unaweza kuipata kwa kubonyeza kazi na kufuata
kiungo chini ya "Muhtasari wa alama" ambayo inasema 'Angalia maoni yote au'
Hakuna majaribio yamefanywa juu ya kazi hii '. Kiungo hiki kinakuwekea kuwa
orodha ya wanafunzi waliojiandikisha kwenye kozi.
Unapoanza kuweka alama kuna machaguo ya aina mbili.Utaratibu ni ule ule kwa
machaguo mawili.
Ni juuu yako kuchagua uchaguzi upi wa uwekaji wa alamaKutegemea na unachosahihisha
unaweza kupendelea mmoja
Uwekaji wa alama wa msingi:
1. Bofya ‘alama’ katika safu ya hali ya mwanafunzi wa kwanza, hii inaleta dirisha jipya
2. T o a a l a m a n a j a z a k a t i k a m r e j e s h o
3. Bofya ‘hifadhi na onyesha kinachofuata t’ kuona mwanafnzi anayefuata
-
20
Utoaji wa haraka wa alama:
1. Ingiza daraja na maoni moja kwa moja kwenye ukurasa ambapo unaweza kuona
orodha ya wanafunzi wote.
2. Kutoa alama kwa haraka hakutakuwezesha kutoa maoni ndani ya maandishi ya
kazi ya maandishi ya mtandaoni. Hata hivyo, kupiga haraka mara kwa mara
kunafaa wakati wa kuingiza alama na maoni kwa faili zilizopakiwa au shughuli za
nje ya mtandao
3. . Kubadili uwekaji wa alama wa haraka 'Chagua kweye kisanduku' (chini ya kulia)
na kisha bonyeza 'Hifadhi mabadiliko yote ya haraka'.
12.0 Zoezi la Papo kwa Papo
Tumia mazoezi kama unataka kutunga mtihani wa kujitegemea kwa wanafunzi wako,
ukitumia mchanganyiko wa aina za maswali (maswali ya kuchagua, kweli na uongo,
majibu mafupi ... nk). Kwa moduli ya mazoezi unahitaji kuunda benki ya maswali kabla
ya kufanya mazoezi
12.1 Kutengeneza Maswali
Katika sehemu yako ya uendeshaji wa kozi bofya kwenye benki ya maswali.
-
21
12.2 Mipangilio ya kawaida kwa aina zote za maswali
1. Katika benki ya mswali bofya kichupo
2. Amua ni aina gani / folda unayotaka kuuliza maswali
3. Choose the type of question you wish to make using the ‘create new question’ drop
down menu , Chagua aina ya swali unalotaka kutumia ‘tengeneza swali jipya ’
4. . Lipe swali jina linalojieleza
5. Andika swali kwenye boksi la ‘Swali la maandishi’ . Unachokiandika hapa kitatofautiana na aina ya swali lilichogaliwa (kweli/si kweli, mlinganisho….n.k
6. ‘Muundo wa msingi wa uwekaji wa alama “ ni alama ya tuzo itakayopewa kwa jibu sahihi .
7. ‘Adhabu’ Ni alama itakayokatwa kwa sababu swali limejibiwa kimakosa na likajaribu kujibiwa tena
-
22
8. Unapotunga swali una nafasi ya kuiweka 'mode adaptive' ifanye kazi au isifanye kazi
Maana yake mwanafunzi anakua na kitufe kinachomuwezesha kutuma jibu moja moja anapomaliza kufanya swali (badala ya kujibu maswali na kuyatuma mwishoni wa zoezi)
13.0 Aina ya Maswali
Kuna aina 10 tofauti za aina ya maswali ambazo zinawea kutumika katika maswali ya moduli.
Aina Matumizi
Maswali ya kimahesabu To create lots of versions of a mathematical
question with different value
Maelezo Kutoa maelezo ambayo yanaweza
yakasaidia swali linalofuata ambalo
mwanafunzi anaweza akalijaribu.
Insha Kuuliza maswali ambayo yanakua na aya
kadhaa, Aina hii ya maswali yanakutaka
usahihishe bila kufuata mtiririko Fulani
yaani kwakusoma wazo na kuliona kama
lipo sahihi.
Mlinganisho Orodha ya sentensi ambayo inaweza
ikalinganishwa na orodha nyingine ya
sentensi.
Majibu yaliyounganishwa (vaana) Kujaza nafasi zilizo wazi katika aya ya maandishi
Maswali ya kuchagua To answer questions where there is a list of
answers to choose from,Kujibu maswali ambapo kuna orodha ya majibu
Majibu mafupi Kutunga swali la kimahesabu ambapo
wanafunzi watajaza majibu kwenye boksi
la maandishi
Nambari Kutunga swali ambalo jibu lake ni neno au misemo
Majibu yanayolingana Unapokua na majibu mafupi kwenye
benki ya Moodle na unataka
kuyabadilisha kwemye maswali
yanayolingana
-
23
Kweli/Si kweli Kuamua kwamba sentensi ni kweli au sio
kweli
Maelezo (Hili sio swali) Hii inatumika wakati unapotaka kutoa maelezo ambayo yatakua na umuhimu kwenye
maswali.
Hili sio swali –Ni kama alama katika benki ya maswali.
Haiwezi kufanya kazi vizuri ikiwa umechagua kuzuia maswali bila mpangilio
1. Chagua ‘Maelezo’ kutoka ‘Tunga swali’ menyu kunjunzi
2. Yape maelezo jina la maelezo
3. Katika nakala ya swali jaza maelezo unayotaka kuwapa wanafunzi.
4. Hifadhi mabadiliko
13.1 Swali la insha
Swali la muundo huu linahitaji jibu ambalo sio lenye aya kadhaa. Hili swali huhitaji
usahihishaji usio na mpangilio zaidi ya kuangalia wazo lililojengwa na mwanafunzi. Alama za
wanafunzi zitakua 0 hadi utakaposahihisha
1. Chagua ‘swali la insha kutoka ‘Tunga swali jipya menyu kunjunzi
2. Yape maelezo jina la maelezo
3. . Katika nakala ya swali jaza swali lako
4. Badilisha daraja la msingi kwa idadi ya alama swali linalofaa
5. kama unataka kutoa malezo bila kujali jibu lilitolewa, w e k a m a j u m u i s h o y a
p a m o j a k a t i k a s a n d u k u l a k u w e k e a . Kumbuka kwamba hii itaonekana
utakaposahihisha swali bila mpangilio mahsusi..Chochote utakachoandika
kitaonekana moja kwa moja wakati swali litakapowasilishwa.
6. Unaposahihisha swali una sehemu pia ya kuandika maoni yako.
13.2 Majibu yaliyounganishwa na (Vaana) Maswali
Aina hii ya maswali inatumika unapotaka wanafunzi wajaze nafasi zilizo wazi katika aya ya
maandishi.Wanafunzi wanapaswa kuandika kwenye visanduku au kwenye menyu kunjuzi
1. Chagua ‘Majibu yaliyoungwa (vaana)’ Kutoka ‘Tunga swali jipya’ menyu kunjunzi
2. Lipe swali maelezo ya jina
3. Katika sehemu ya aya andika aya yako na huisha kwa kutumia msimbo wa Moodle ili
kuzalisha aina tofauti za mapungufu Unaweza kupata maelezo ya kumbukumbu juu
ya hili kwa kubonyeza alama ya swali juu ya ukurasa (upande wa “ Majibu
mjumuiko’).
-
24
13.3 Maswali ya kuchagua
1. Maswali ya aina hii hutumika unapotaka wanafunzi wajibu maswali panapokua na
orodha ya majibu ya kuchagua.. Kunaweza kuwa na jibu moja sahihi au
majibukadhaa sahihi.
2. Chagua ‘Uchaguzi mwingi’ kutoka ‘Tunga swali jipya’ menyu kunjuzi.
3. Lipe swali maelezo ya jina.
4. Katika sehemu ya swali andika swali lako.
5. Unaweza kuamua kubadilisha daraja la msingi la swali – hasa hasa kama unataka
kuchagua zaidi ya jibu sahihi moja.
6. Amua ni majibu sahihi mangapi yatakuwepo katika orodha ya majibu 7. Orodha ya majibu sio mara zote inaonekana katika mpangilio unaofanana. 8. Unaweza kubadilisha njia ambazo uchaguzi huchapishwa kwa kutumia 'Idadi ya chaguzi'katika menyu kunjuzi
9. Kwa kila moja ya majibu ya kuchagua unahitajika kujaza jibu kwa daraja lililofanana
na maoni. Inawezekana kuongeza majibu / uchaguzi zaidi kwa kubofya Vipengele 3
Zaidi vya kuchagua'
10..Mrejesho kitengo wa jumla ni wa muhimu kwa sababu unaweza kuweka jumbe za
mrejesho kwa wanafunzi wakati wanpojibu swali walilopewa kwa usahihi ,sio sahihi
sana au sio sahihi kabisa.
11. Hifadhi mabadiliko
13.4 Swali la Nambari
Aina hii ya swali inatumika kutunga swali la kimahesabu ambapo mwanafunzi huweka jibu
katika kisanduku. Hili swali linafanana na swali la majibu mafupi isipokua ni la kimahesabu.
1. Chagua ‘namnari’ kutoka ‘Tunga swali jipya’ menyu kunjuzi.
2. Lipe swali maelezo ya jina
3. Katika sehemu ya swali andika swali lako
4. In the answers section put the correct answer, its corresponding grade (100%),
accepted error and feedback (optional).Katika sehemu ya majibu weka majibu sahihi
5. Hifadhi mabadiliko
-
25
13.5 Maswali ya Kweli/Si kweli
Maswali ya aina hii yanatumika unapotaka kujua kama sentensi ni kweli ama sio kweli
1. Chagua ‘Jibu fupi’ kutoka ‘Tunga swali jpya’ menyu kunjuzi.
2. Lipe swali maelezo ya jina.
3. Katika sehemuya maandishi tengeneza sentensi iliyo sahihi au isiyo sahihi
4. Chagua kama sentensi uliyoandika ni sahihi au siyo sahihi kwa kutumia ‘jibu sahihi’ menyu kunjuzi
5. Toa mrejesho sambamba wakati wanafunzi wanapochagua Kweli au Sio kweli
6. Hifadhi mabadiliko
14.0 Jukwaa
Unapoongeza jukwaa la majadiliano kwenye kozi ya Moodle.unatengeneza ujumbe wa
taarifa za mtandaoni kw ajili ya wanafunzi wako kuongea wao kwa wao au kuongea na
wewe.Jukwaa la majadiliano ni rahisi sana kutengeneza na zipo aina tano tofauti. Jukwaa lipi
linalochaguliwa inategemea ni kwa namna gani majadiliano yatafanyika.
Aina tofauti za majadiliano ni :
Mjadala moja rahisi - Mada moja ya majadiliano ambayo kila mtu anaweza kujibu
Kila mtu anaandika mjadala mmoja - Kila mwanafunzi anaweza kuchapisha mada
moja katika majadiliano mapya, ambayo kila mtu anaweza kujibu
Q na A jukwaa la mjadala - Wanafunzi wanapaswa kwanza kuweka maoni yao kabla ya kuangalia maoni ya wanafunzi wengine
Mijadala ya kawaida inaonyeshwa kwenye muundo wa blogu wa wazi ambapo
mtu yeyote anaweza kuanza majadiliano mapya wakati wowote, na ambapo mada
ya mjadala inaonyeshwa kwenye ukurasa mmoja na kiungio "Jadili mada hii".
Mjadala wa kawaida kwa matumizi ya jumla - Jukwaa wazi ambapo mtu yeyote anaweza kuanza majadiliano mapya muda wowote
H a t u a za kutengeneza mjadala wa majadiliano
1. Kwenye sehemu ya kuhariri kwenye kozi yako nenda kwenye mada / sehemu ambapo ungependa
Jukwaa la kuonyesha na bonyeza 'Ongeza shughuli ...' kisha 'Mjadala'
2. Lipe jina jukwaa la majadilano (Hii inakua ni kiungio ambacho wanafunzi wako wata
bofya kuingia kwenye jukwaa la mjadala )
3. Chagua aina ya mjadala unayopendelea kutumi kutoka kwenye menyu kunjunzi.
4. Lipe Jukwaa la mjadala Utanguliz
-
26
5. Utakapokua umejaza utangulizi unapaswa kuchagua kutoka kwenye mipangilio ifuatayo.
Unaweza kuacha mpangilio uliokua umewekwa mwanzoni
-
27
Hapo utakuwa tayari umeshaweka mjadala, sasa Fungua kwa kubofya Jukwaa hapo chini
Andika Jina la jukwaa
la majadiliano hapa
Andika maelezo ya Jukwaa hapa
Hifadhi kumbukumbu
-
28
Kwa mara ya kwanza hakutakuwa na Mada iliyowekwa mezani, hivyo unapaswa kuweka mada kwa ajili ya majadiliano.
Dirisha lifuatalo litafunguka
Bofya hapa kuweka mada
Andika kichwa cha habari cha
mjadala
Andika ujumbe hapa
Pia unaweza kuambatanisha
mafaili ya mjadala hapa
Baada ya kumaliza, Bofya hapa
kuingia kwenye mjadala
-
29
15.0 Soga
Moduli ya sogoa inakuwezesha kutengeneza sogoa yamtanadaoni ambapo wanafuzni wako
watafanya mijadala kwa kutuma na kupokea mazungumzo ya papo kwa papo..Wale
wanafunzi waliosajiliwa tukwenye kozi yako ndio wataweza kushiriki. Kama mwalimu
unaweza kushauriana nao nakala za mazungumzo ya zamani, unaweza hata kuanzisha
chumba cha mazungumzo ili wanafunzi waweze kuona mazungumzo yaliyopita.
T e n g e n e a z a c h u m b a c h a m a z u n g u m z o : Katika Moodle kozi yako weka kihariri kifanye kazi na nenda katika sehemu unayotaka
kuongeza chumba cha mazungumzo.
Chagua ‘Soga’ Kutoka ‘Ongeza shughuli...’ menyu kunjuzi.
-
30
Kipe chumba cha mazungumzo jina. Kama kawaida , hii itakua kiunga kwa wanafunzi
watakayobofya kila mara.
16.0 Faharasa
Kwa kutengeneza faharasa katika kozi yako unatoa maana ya maneno yaliyotumiwa katika
kozi.
Kawaida faharasa inaruhusu wanafunzi wako kuchangia ufafanuzi wao wenyewe (unaweza
kuacha hii kama unataka) hivyo walimu wanaweza kuuliza wanafunzi kufafanua maneno
mapya ambayo yanaweza letwa na wanafunzi. Kwa upande mwingine, ufafanuzi huu unaweza
kuwa bora na kupelekwa kwenye ghala kuu ambayo wanafunzi hawawezi kuhariri
Jaza sehemu za wazi kisha bofya
chini kuweka soga
-
31
Machapisho yana uwezo wa 'kuunganisha moja kwa moja '. Hii inamaanisha kuwa ikiwa
neno, lililopo kwenye faharasa, linawekwa mahali fulani katika kozi, neno hilo litahusishwa
moja kwa moja na ufafanuzi wake katika faharasa. Hivi ndivyo faharasa inavyoonekana:
Namna ya kutengeneza faharasa
-
32
Andika jina hapa
Weka Maelezo ya Faharasa
Bofya Kuchagua Aina
ya Faharasa
Bofya Kuhifadhi Bofya Kuhifadhi
Kama Umemaliza ,Bofya
hapa Kuhifadhi
-
33
17.0 Kitabu cha alama
Alama kwa kila mwanafunzi kwenye kozi zinaweza kupatikana kwenye'Taarifa ya alama' chini
Alama’ Chaguo katika Utawala wa Kozi
17.1 Kuingiza na kuweka alama
1. Nenda kwenye kozi unayotaka kuongeza alama
2. Bofya ‘Alama’ na halafu ‘Taarifa ya alama’ katika Utawala wa kozi.
3. Kulia kwako juu kwenye kona utaona kitufe cha "Washa kiharirio"
button. Bofya hiki kitufe kuwezesha kuingiza ingozo za alama.
4. Nenda sehemu ya mazoezi ambayo ungependa kuingiza alama na andika alama za
wanafunzi katika boksi husika la maandishi
5. Kwa alama ambazo tayari zimeingizwa moja kwa moja kwa mazoezi yaliyopewa alama
, bofya kitufe cha kuhariri mbele ya boksi la maandishi
6. Katika ukurasa unaofuata , angalia screen, check the "overridden" check box and na
ingiza alama katika alama za mwisho katika sanduku la maandishi
-
34
18.0 Tathmini
Moduli ya shughuli ya tathmini inatoa nyenzo kadhaa za ukusanyaji taarifa ambazo
zimethibitishwa kuwa zinafaa kupima na kuchochea usomaji kwa njia ya mtandao.
Mwalimu anaweza kutumia nyenzo hizi kukusanya taarifa kutoka kwa wanafunzi ambazo
zitawasaidia kujifunza kuhusu kozi yao na kujitahmini ufundishaji wao..
Kuweka Tathmini fanya yafuatayo,
Baada ya kubofya weka Tathmini, Dirisha lifuatalo litafunguka.
-
35
Weka Jina la Tathmini
Andika Maelezo ya Tathmini hapa
Jaza taarifa nyingine za
Tathmini
Kama umeshamaliza kujaza ,Bofya
hapa Kuweka Tathmini
Weka Tathmini Weka
Tathmini
-
36
19.0 Hariri wasifu wako
Watumiaji mmoja mmoja wanaweza kuhariri nyasifuzao kwa kubofyakiungo cha Hariri
wasifu wako inayopatkana katika ukurasa wa katika menyu ya mtumiaji ( juu kulia )
Bofya jina la mtumiaji;
Hariri Maelezo Mafupi
Bofya kuhariri taarifa
zako
Hariri taarifa zako
Badili nywila
-
37
Unaweza
kuhariri
taarifa zako
hapa
Pia Unaweza kuweka Picha yako kwa
kubofya mshale huu hapa Ukimaliza kuweka taarifa
zako sawa ,Bofya hapa
kuhuisha taarifa
-
38
20.0 Kutuma ujumbe wa faragha
Moodle inaruhusu watumiaji kutuma ujumbe wa faraghakwa wanafunzi , walimu , wahadhiri na
kwa mtumiaji yoyote Yule .Kutuma ujumbe wa faraghafuata hatua zifuatazo chini hapa mara
unapokua kwenye kozi yako , bofya washiriki wa kozi
1. Bofya jina la mtu unayetaka kumtumia ujumbe.
Bofya hapa
kuona
washiriki
-
39
Bofya kitufe au kiungio cha Tuma ujumbe
Baada ya kutuma ujumbe wako, unaweza kuangalia ujumbe ulotuma au kama kuna ujumbe uliotumiwa, kufanya hivo angalia picha chini.
Bofya Kutuma ujumbe
Sehemu ya kuandika ujumbe Sehemu ya kutuma ujumbe
Tazama ujumbe uliotuma au
kutumiwa hapa