dawa za asili katika nchi za tropiki kwa kusema “dawa za asili,” anamed ina maana ya muungano wa...

69
anamed team DAWA ZA ASILI KATIKA NCHI ZA TROPIKI II MATIBABU Matibabu ya magonjwa ya kawaida na matumizi ya baadhi ya mimea muhimu katika nchi ya tropiki. Kitabu cha Semina Ki-suahili Numba: 119

Upload: others

Post on 20-Oct-2020

30 views

Category:

Documents


18 download

TRANSCRIPT

  • anamed team

    DAWA ZA ASILI KATIKA NCHI ZA

    TROPIKI

    II MATIBABU

    Matibabu ya magonjwa ya kawaida na matumizi ya

    baadhi ya mimea muhimu katika nchi ya tropiki.

    Kitabu cha Semina Ki-suahili Numba: 119

  • Kitabu hiki kimeandikwa na anamed team: Dr. Hans-Martin Hirt, Dr.Peter Feleshi, Philip

    Mateja, Dr. Lindsey na washiriki wengine wengi wa anamed.

    Anamed Angola: Baptista Nsenda, Margarethe Roth

    Anamed Congo – Kinshasa: Konda Ku Mbuta, Bindanda M´Pia

    Anamed Congo South Kivu: Innocent Balagizi

    Anamed Congo Prov. Equator: Dieudonne, Akuma Tande

    Anamed Eritrea: Nighisti Alazar, Micele Paliaro

    Anamed Ethiopia: Ralph Wiegand, Belay Bekele, Temesgen Choleyea

    Anamed India: Sr. Rosita Kandathil, Kambala Subramanyam

    Anamed Kenya: Roger Sharland, Rebecca Nzuki

    Anamed Mozambique : Pascoal Cumbane, Myriam Wahr

    Anamed Nigeria: YMCA Jos

    Anamed Afrika Kusini: Margrit Hirt

    Anamed Sudan: Dr. Elijah

    Anamed Tanzania: Philip Mateja, Peter Feleshi, Maike Ettling

    Anamed Uganda Christopher Nyakumi

    na msaada wa uchunguzi wa Prof. Dr. Christoph Schäfer

    Kwa toleo hili la ki-swahili tunamshukuru Emmanuel Biligeya kwa kazi yake ya utafsiri na

    Mchg Hezron Shimba na Maike Ettling kwa kuhariri. Pia tunaishukuru HUYAMU (Idara ya

    Afya ya AICT – Dayosisi ya Mara & Ukerewe) kwa ushirikiano wao wa karibu.

    Toleo la tatu September 2015

    © 2008 Hakimiliki na anamed

    Anamed ingependa taarifa zilizo katika kijitabu hiki zisambazwe mahali popote zinapowezekana

    kufika. Tunawahamasisha watumiaji wa kitabu hiki kukitafsiri katika lugha zao. Hata hivyo kwa

    kuwa mambo yaliyomo yanaboreshwa mara kwa mara, tafadhali wasiliana na anamed kwanza.

    Haki miliki ya tafsiri zote inabaki na anamed. Hakuna sehemu ya kitabu hiki inayoruhusiwa

    kuchapwa na kuuzwa tena.

    Mabango ya rangi (anamed No. 403) vinaonyesha mimea iliyoelezwa katika kitabu hiki.

    Toleo la pili la kitabu hiki linapatikana katika lugha ya kifaransa, kireno, kijaluo, kiamharic,

    kiateso na kichichewa. Baadhi ya vitabu vya anamed vinapatikana katika baadhi ya nchi za

    Afrika.

    Wafuatao wanaunganisha anamed na ndio wauzaji na wasambazaji wa vitabu na vifaa vya

    anamed:

    anamed, Schafweide 77, D – 71364 Winnenden, Germany

    Email: [email protected]

    Website: www.anamed.net

    mailto:[email protected]://www.anamed.net/

  • YALIYOMO

    Sehemu I: Kuzuia magonjwa ya kawaida Sura 1: Kuzuia magonjwa ya kawaida....................…………………………..3

    Sehemu II: Tiba ya magonjwa ya kawaida Sura 2: Vidonda, kuungua, majipu na uvimbe………………………………...5

    Sura 3: Magonjwa ya ngozi……………………………………………………8

    Sura 4: Kuharisha…………………………………………………………….11

    Sura 5: Malaria ………………………………………………………………16

    Sura 6: UKIMWI: Imarisha mfumo wa kinga mwilini………………………19

    Sehemu III: Matumizi ya baadhi ya mimea

    muhimu ya nchi za Tropiki Sura 7: Allium Sativum (kitungu saumu)……………………………………21

    Sura 8: Artemisia annua anamed (A – 3)…………………………………….23

    Sura 9: Azadirachta Indica (Mwarobaini)…………………………………….38

    Sura 10: Carica papaya (Mpapai)…………………………………………….42

    Sura 11: Moringa oleifera (Mlonge)

    Sehemu IV: Utengenezaji wa baadhi ya madawa Sura 12: Mafuta na dawa za mafuta …………………………………………47

    Sura 13: Jiwe jeusi……………………………………………………………49

    Sehemu V: Msingi wa matumizi ya dawa za asili Sura 14: Kazi ya kikundi – Maendeleo ni nini?...................................

    Sura 15: Anzisha bustani ya mimea ya madawa……………………………...50

    Sura 16: Mawazo ya ki-biblia ………………………………………54

    Sura 17: Mwongozo na maadili kwa “Waganga wa asili”.……………………55

  • anamed

    Madawa ya asili katika nchi za Tropiki: Matibabu II

    Matibabu, mimea, madawa, kazi ya vikundi na maadili.

    Kitabu cha maelezo kwa semina ya madawa ya asili

    kwa muda wa juma moja.

    Na anamed team na

    Washiriki wengi wa anamed duniani kote.

    anamed (Action for Natural Medicine) ni shirika la Kikristo na Muungano wa huduma

    unaolenga kusaidia watu katika nchi za Tropiki kujitegemea kadri iwezekanavyo, hasa kwa

    masuala ya kiafya. anamed inafanya kazi na watu wa imani zote waliojitoa kuinua hali ya afya

    ya majirani zao, mkoa na taifa.

    anamed inafanikisha lengo hili kwa kuwasikiliza waganga wa jadi, kufanya uchunguzi wake

    binafsi, na kuboresha mchanganyiko wa madawa kwa matibabu. Tunatoa matokeo katika kitabu

    kiitwacho “Dawa za asili katika nchi za tropiki.” Kwa hiyo tangu 1985, tumeweka wazi kwa

    watu wote ujuzi wetu wote juu ya afya na uponyaji kwa kutumia mimea inayopatikana bure kwa

    jamii nzima. Hatuna siri, na hakika hatuna sheria inayozuia kuigwa!

    anamed inatoa ujuzi na uzoefu huu, hasa katika Afrika, kwa kuendesha semina za “Dawa za

    asili” kwa muda wa juma moja kwa wafanya kazi wa afya, madaktari, waganga wa jadi, viongozi

    wa dini, wahudumu wa jamii na kadhalika. Semina inapitia utambuzi na uchunguzi zaidi wa

    baadhi ya mimea ya dawa, utayarishaji wa madawa kutokana na mimea hiyo, matumizi yake

    katika tiba na matatizo ya kawaida ya kiafya na magonjwa.

    Kwa kusema “dawa za asili,” anamed ina maana ya muungano wa faida za madawa ya jadi na

    zile za huduma za tiba za kisasa zenye msingi wa kisayansi.

    Kitabu kiki, kitabu cha pili katika mfululizo wa “Dawa za asili katika nchi za Tropiki,” ina

    karibu masomo yote yanayohitajika kwa mafunzo ya semina kwa juma zima la kwanza katika

    dawa za asili. Nafasi hairuhusu maelezo zaidi juu ya falsafa ya kazi yetu, ingawa jambo hili ni la

    muhimu sana. Jambo hili limeelezwa katika kitabu cha kwanza, ambacho pia kinaeleza mimea

    mengi zaidi na kina maelezo zaidi juu ya kujitengenezea dawa nyumbani. Kitabu cha tatu ni

    msaada wenye taarifa nyingi kwa viongozi wa semina. Kitabu cha nne kimetolewa kwa ajili ya

    huduma kwa wanaoishi na VVU/UKIMWI.

    Sehemu I ya kitabu hiki inaelezea jinsi ya kuzuia baadhi ya matatizo ya kitabibu yaliyo ya

    kawaida katika nchi za tropiki, na sehemu ya II ni juu ya kutibu. Sehemu III inaelezea mimea na

    miti mitano maalumu, ambayo yote inaweza kustawi katika nchi za tropiki. Kwa miti hii mitano

  • tu matatizo mengi ya kiafya yanaweza kutibiwa. Kwa nyongeza, unaweza kupata chakula chenye

    virutubisho, kusafisha maji, kurutubisha ardhi na kutengeneza kiuatilifu kizuri. Sehemu ya IV

    inaeleza jinsi ya kutengeneza baadhi ya madawa. Na sehemu ya V inatoa baadhi ya msaada kwa

    ajili ya semina, pamoja na mtiririko muhimu wa rejea kwa ajili ya waganga wa dawa za asili.

    Ukishahudhuria semina ya anamed juu ya dawa za asili, tafadhali endelea kuwasiliana na

    wengine katika mkoa wako na nchi yako ambao wanatibu kwa madawa ya asili. Panga

    kutembeleana, endesha mafundisho, na julisha anamed International huku Ujerumani juu ya

    mafanikio yako! Asante!

    Sehemu I

    Sura 1:

    Kuzuia magonjwa ya kawaida. Kama tukijali mtindo wetu wa maisha, lishe, afya na mazingira tunayoishi tunaweza kutoa

    mchango mkubwa sana katika afya bora ya familia zetu, mimea yetu na wanyama.

    1.1.Kula vizuri!

    Mara nyingi ni tatizo kwamba, watu wakitajirika kidogo, ubora wa lishe yao unashuka.

    Vyakula bora (angalia jedwali hapo chini) vinatujengea nguvu na mfumo wetu wa kinga

    mwilini – yaani uwezo wetu kushambulia maambukizi na magonjwa. Vyakula visivyo

    bora kama vile sukari nyingi, unga uliokobolewa, mkate mweupe, soda mbalimbali,

    vyakula vya kwenye makopo, hupelekea ukosefu wa vitamini na protini. Kwa hiyo

    tunakuwa na uwezekano mkubwa kupata maambukizi yoyote na magonjwa.

    Jedwali I: Vyakula vya ki-msingi

    Kwa kupata nguvu kwa

    urahisi

    Mizizi ya wanga: Mihogo, viazi vitamu, “Taro”

    Matunda ya wanga: Ndizi, “breadfruit”

    Kwa kupata nguvu na

    protini

    Nafaka na mbegu: Ngano, mahindi, mchele, mawele,

    mtama, mkate. Kula mkate wa unga usiokobolewa na

    unga wa mahindi yasiyokobolewa.

    Epuka mkate uliotengenezwa kwa unga mweupe na

    mahindi yaliyokobolewa!

    Kwa chakula chenye protini

    kwa wingi

    Mbegu za mafuta: boga, tikitimaji, ufuta na alizeti.

    Jamii ya kunde: maharage, njugu, dengu, soya zenye

    kokwa, karanga, korosho, “almonds”

    Mazao ya wanayama: maziwa, mayai, jibini, samaki,

    kuku, na nyama yoyote.

    Kwa vitamini na madini Mboga: majani ya kijani – nyeusi, majani ya mihogo,

    viazi vitamu na majani ya viazi vitamu, nyanya, karoti,

    maboga, majani ya mlongelonge, mbegu za amaranth na

    mengine zaidi.

    Matunda: maembe, machungwa, limao, mapapai, mapera,

    passion fruit n.k.

    Jusi ya matunda.

    Kwa kinga imara ya mwili Kula vitunguu swaumu vibichi, unga wa majani ya

    mlonge, mbegu za amaranth, nyama laini ya jamii la

  • msubili.

    Lima matunda, mbogamboga na mimea ya madawa wewe mwenyewe! Siyo jambo lililopitwa na

    wakati wala rahisi! Vyakula vya kujitengenezea kutokana na bustani ya nyumbani ndivyo

    vyenye virutubisho bora zaidi.

    Lisha watoto mara kadhaa kwa siku. Wanahitaji vyakula kidogo kidogo mara kwa mara.

    Kunywa jusi ya matunda halisi – nchi za Tropiki zina wingi wa matunda !

    Hatari za lishe mbaya

    a) Watu wa Afrika kwa sasa wanakula sukari zaidi kuliko ilivyowahi kutokea. Soda zina sukari

    nyingi, hata wanga katika mkate mweupe unabadilishwa na vimengenya kuwa sukari mdomoni.

    Matokeo yake watu wengi sasa wameoza meno na kupata kisukari au matatizo mengine ya afya.

    Wengi hawawezi kugharimia matibabu yake. Kwa hiyo punguza utumiajii wa sukari ya

    kiwandani. Na jaribu kunywa chai na kahawa bila sukari!

    b) Watoto wanaokula mkate mweupe, ugali wa mahindi na mihogo wanaweza kuingia katika hali

    ya utapiamlo kwa sababu ya upungufu wa protini, vitamin na madini.

    c) Kama kwa vyovyote ikiwezekana, nyonyesha mtoto kwa maziwa ya titi – usishawishiwe na

    matangazo ya biashara juu ya maziwa ya chupa kwa mtoto. Uchafu na maambukizi mengine

    yananywewa na mtoto kwa urahisi kupitia hizi chupa, ambapo hupelekea kuharisha na

    magonjwa mengine. Vyakula vya madukani vya watoto hudhoofisha mtoto wako na uchumi wa

    familia yako!

    d) Matukio ya saratani na madhara ya ki-afya yanaongezeka kwa sababu ya kuongezeka kwa

    idadi ya madawa ya viwandani kutengenezwa. Soda na vinywaji vitamu vingine pamoja na

    bidhaa zingine za kibiashara zinakuwa na madawa na sukari ya kiwandani ambazo zinaweza

    kuharibu afya yako. Vyakula vya makopo pia vinakuwa na madawa hatarishi ya kuhifadhi

    chakula. Hata Blue Band ya mikate ina hayo madawa ya kuhifadhi chakula. Ni vizuri zaidi

    kupaka embe mafuta kwenye mkate wako!

    Madawa hatarishi ya viwandani yanakuwepo sio tu kwenye vyakula vya madukani, lakini pia

    kwenye kilimo (kama mbolea ya madawa ya kuulia wadudu), katika moshi ya magari na hata

    kwenye nguo na vifaa vya ujenzi.

    1.2. Angalia maji yako! Hakikisha maji unayokunywa ni salama. Kutokana na ubora wa maji yako, unaweza kutengeneza

    chujio la maji kwa mchanga, unaweza kutumia mbegu za mlongelonge zilizosagwa kama

    ilivyoelezwa katika sura ya 11, au unaweza kuchemsha maji katika jiko la jua.

    Shirikiana na wengine kuhakikisha mto wako unabaki msafi. Toeni matakataka yote! Kama

    watu wakifulia nguo zao, au hata baiskeli na magari, katika maji ambayo wengine wanakwenda

    kutumia kwa kunywa, basi wanasababisha matatizo ya afya!

    1.3. Rutubisha ardhi yako – kiasili.

    a) Panda mimea jamii ya kunde (ambayo huongeza naitrojeni kwenye udongo). Mimea jamii ya kunde ni pamoja na mboga kama vile maharage na karanga, miti kama vile

    Lusina. Lusina inaweza kupandwa kufuata kontua kuzuia mmonyoko wa ardhi, na zikatwe

  • ncha zake mara kwa mara ili kutengeneza uzio. Matawi yanayokatwa yanasaidia

    kurutubisha udongo.

    b) Ozesha takataka za mimea, maganda yote ya matunda, majani ya mboga, takataka za shambani (lakini epuka mbegu za magugu), samadi ya kuku na wanyama wengine

    virundikwe (siyo karibu sana na nyumbani lakini). Kama vikidumishwa katika hali ya

    unyevu na uvuguvugu, udongo mzuri mweusi utapatikana ndani ya miezi 3, ambao,

    ukichanganywa katika shamba lako, utaweka virutubisho (naitrojeni na madini) taratibu

    kwenye shamba lako.

    c) Tandazia nyasi – angalia sura ya 14. d) Epuka matumizi ya madawa hatarishi ya kilimo. Usitumie au tumia kiasi kidogo sana

    cha mbolea za viwandani au dawa za kuua wadudu. Zinachafua maji, zinaua viumbe,

    wanyama na mimea visivyo na madhara (na zaidi vyenye umuhimu) na zinadhuru rutuba

    ya asili katika udongo.

    1.4. Vyoo vya kienyeji ni visafi na ni rahisi kutumia!

    Kinyesi na mkojo vinaweza kuwa vyanzo vya maambukizi mengi. Chimba shimo, jenga kijumba

    juu yake. Tundu la shimo lazima lifunikwe wakati wote. Kama ukiweka dohani ambayo

    huchukua hewa kutoka kwenye shimo hadi juu ya paa, choo hakitatoa harufu. Shimo likijaa,

    lifunike kwa udongo na upande mwembe juu yake! Kisha tengeneza choo kingine cha kienyeji

    mahali pengine. Vyoo vya kienyeji vinatunza rutuba ndani ya ardhi, wakati ambapo vyoo vya

    maji vinachafua vijito na mito. Na vinatumia maji kidogo, ambayo katika sehemu nyingi

    yamezidi kuwa adimu.

    1.5. Tupa takataka kwa uangalifu !

    Katika miji mingi unaweza kuona “moto wa milele”, ambao mara chache unazima na ambamo

    takataka - ikiwa ni pamoja na plastiki na metali – vinatupwa. Moto huu una moshi mweusi mzito

    wenye sumu kali zinazoitwa dioxins.

    Takataka zinazozagaa hazipendezi. Vitu vyenye ncha kali vinaweza kukata watu, betari na

    baadhi ya vifaa vya umeme vina sumu, ni pamoja na maji ya mvua yaliyotuama katika mifuko ya

    plastik, magurudumu yaliyochakaa ambamo pia hutengeneza sehemu za mbu wa malaria

    kuzaliana.

    Kwa hiyo tupa takataka zako kama ifuatavyo:

    Mara utakapozoea kutenganisha takataka zako namna hii nyumbani kwako, wafundishe mfumo

    huu kijijini kwako au hata mjini unapoishi.

    a) NDOO YA KIJANI: Tupa kila siku: Kwa ajili ya takataka za ki-mimea kutoka bustani yako au jikoni (“0rganic waste”). Uziozeshe kupata mbolea. Au afadhali zaidi: uwalishe

    kuku zako na takataka za ki-mimea ili panya na nyoka wasikaribishwe karibu na nyumba

    yako

    b) NDOO YA BLUE: Tupa kila wiki: Kwa ajili ya karatasi. Ukusanye kwenye ndoo na mara moja kwa wiki choma karatasi pamoja na plastiki inayoweza kuchomwa ndani ya dakika 5.

    Majivu yatupwe pamoja na metali.

    c) NDOO NYEKUNDU: Tupa kila mwezi. Kwa ajili ya metali, vioo, plastiki, betari. Kama kuna uwezekano wowote wa kuvitumia tena au kuvibadilisha kuwa vitu vingine, fanya

    hivyo. Sisitiza serikali yako idai fedha za kuwekesha kwa kila mfuko wa plastiki na chupa za

    vioo inayouzwa, ili kwamba ziweze kutumika tena au kurudishwa viwandani. Vikusanye

  • kwa uangalifu, na kama hakuna mfumo wa kuweza kuvitumia tena kila mwezi uvizike chini

    sana kwenye udongo. Betari hasa zina sumu! Usipande mboga zako juu ya shimo hilo!

    d) Mbao: Uchome na uweke majivu yake shambani, yana madini yenye thamani.

    1.6. Mifuko ya Plastiki

    Baadhi ya nchi za kiafrica sasa zinazuia matumizi ya mifuko ya plastiki. Katika miji mifuko ya

    plastiki pamoja na chupa zimekuwa zikichafua mazingira na yanapochomwa yanatoa hewa za sumu.

    Imekuwa ikiziba mifereji ya maji na kusababisha mafuriko mvua kubwa zinaponyesha.

    Mashambani, mifuko ikiliwa na ng´ombe na mbuzi inaziba matumbo yao na wanyama wanakufa.

    Hata watoto wanaweza kufa baada ya kuchezea mifuko ya plastiki au chupa zilizoathiriwa na mate

    au kinyesi.

    1.7.Usafi na Afya

    Wakati wote osha mikono yako kwa sabuni na maji kabla ya kula au kutayarisha chakula, na baada

    ya kutoka chooni. Kama huna sabuni jitengenezee, au sugua mikono yako kwa maji ya majani ya

    mpapai.

    Kuoga mwili mzima kila jioni hufanya mwili na kitanda kuwa safi.

    1.8. Kwa upishi wa ndani, weka dohari!

    Kama wakati mwingi chumba chako kimejaa moshi basi uko katika hatari kubwa ya kupata matatizo

    makubwa ya macho na magonjwa ya mapafu. Ufumbuzi bora zaidi wa tatizo hili ni kutengeneza jiko

    linalotumia nishati kidogo (maana yake matumizi ya kuni kidogo ) pamoja na dohani.

    1.9. Mazoezi na uimara wa mwili

    Watu wengi wana mazoezi mengi, mfano wanawake wanaotembea kilometa nyingi kila siku

    kutafuta kuni na maji. Wengine wana mazoezi kidogo sana. Je familia yako “ina maendeleo“au

    “haijaendelea”? Katika familia “zilizoendelea” mwanaume na mwanamke wanafanya kazi kwa

    pamoja, hivyo wana mazoezi yanayofanana. Kwa njia hii mke hawi dhaifu sana, wala mme hanenepi

    sana. Kama ukiuweka mwili katika hali inayofaa, utakuwa na kinga bora zaidi kwa magonjwa.

    1.10. Zuia ajali za barbarani

    Kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya magari inaongeza matukio ya ajali zinazosababisha majeraha

    makubwa na vifo katika nchi za joto. Himiza kampeni za kuangalia usalama wa magari, vidhibiti

    mwendo, vipunguza moshi wa magari na njia za ziada kwa wote watembea kwa miguu na

    waendesha pikipiki

    SEHEMU II MATIBABU YA MAGONJWA YA KAWAIDA

    SURA 2 Vidonda, kuungua, majipu na uvimbe

    Tumia kitambaa kilicho safi. Wakati wa dharula, kama unahitaji huduma lakini ukawa huna

    kitambaa, chukua vipande vya nguo hasa za pamba. Ili kuzifanya salama zichemshwe katika

  • maji kwa dakika 20 na zikaushe kwa kutumia kaushio la jua (sola) lililo safi au kama huna

    kaushio la jua zikaushe kwa kuanika kwenye kamba ya nguo juani.

    Muhtasari ya tiba ya vidonda, kuungua na uvimbe:

    Aina ya Ugonjwa Chaguo la kwanza Chaguo la pili Chaguo la tatu

    Vidonda

    Vidonda

    vipya

    Tibu kwa sukari Tibu kwa asali Tibu kwa papai

    lililoiva

    Vidonda

    vyenye

    uambukizo

    Papai na sukari Tibu kwa papai

    bichi ukibadilisha

    na tiba ya sukari

    Embwe la majani

    ya mpera

    Kuungua

    Kuungua

    kupya

    Ute wa Aloe

    (msubili)

    Maji ya chumvi Osha kwa chai ya

    mpera

    Kuungua

    kuliko na

    uambukizo

    Utomvu mweupe

    wa mpapai, maji

    yenye chumvi

    Ute wa Aloe

    (msubili)

    Dawa ya mafuta ya

    vitunguu

    Jipu

    Jipu

    lililofungwa

    Vitunguu saumu

    vilivyopondwa

    pondwa

    Dawa ya pilipili ya

    mafuta

    Dawa ya mafuta ya

    vitunguu

    Jipi lililo wazi Papai na sukari Tibu kwa papai

    bichi ukibadilisha

    na tiba ya sukari

    Embwe la jani la

    mpera

    A. Vidonda

    Lengo kuu la tiba hii ni kuzuia kidonda kupata maambukizi, hivyo kuruhusu mchakato wa mwili

    kujiponya wenyewe vizuri iwezekanavyo.

    a) Kwanza osha kidonda.

    Kwa Vidonda vilivyo wazi, visafi, vipya, visivyo na usaha

    Tumia ama i) Maji baridi yaliyochemshwa na kuwekewa chumvi kidogo,

    au ii) Chai ya mpera:

    Chemsha kiganja 1 cha majani ya mpera kwenye lita 1 ya maji kwa muda wa

    dakika 15. Yapoe na baadaye yachuchwe. Osha kidonda kwa kutumia maji haya.

    Tengeneza upya kila unapoosha kidonda.

    Kwa kidonda kinachoonesha dalili za maambukizo,

    tumia maji yenye utomvu wa mapapai

    Maji yenye utomvu wa mapapai: Kama kidonda ni kichafu ukioshe mara kadhaa kila siku kwa

    kutumia maji yenye utomvu wa mapapai. Osha papai bichi lililopo mtini kwa kutumia kitambaa

    safi na maji safi ya moto. Weka lita 1 ya maji yaliyochemshwa na kupoa kwenye chupa safi.

    Ongeza kijiko 1 cha mezani cha chumvi na koroga vizuri. Kata papai na kukusanya matone 3 – 5

    ya utomvu wake kwenye chupa ile (kama ilivyooneshwa kwenye picha ya kitabu hiki). Usitoe

    tunda kwenye mti, kwa sababu utomvu unakauka kwa haraka papai linapovunwa. Lakini

    ukiliacha kwenye mti unaweza kuendelea kulitumia mara kwa mara.

  • A. 1. Vidonda safi, vilivyowazi na visivyo na usaha

    A.1.a. Sukari pekee

    Rundika sukari kwenye kidonda. Funga kidonda kwa kitambaa ili kuzuia sukari isitoke. Sukari

    huondoa unyevu kwenye vimelea vya magonjwa kwa mchakato uitwao mfyonzo (osmosi) na

    vimelea hivyo hufa.

    Kihudumie kidonda mara 3 kwa siku kwa kuongeza sukari, usikioshe.

    A.1.b. Mchanganyiko wa asali na sukari

    Hakikisha una asali halisi. Njia bora ni kununua sega la nyuki, na ukamue asali mwenyewe. Hii

    inafanyika kwa namna hii: Pondaponda sega hilo. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia kinu

    kipya au chombo cha kusagia nyama ikiwa kimeondolewa kitufe cha kusagia. Ni vizuri kufanya

    hivyo usiku ili kuepuka kusumbuliwa na nyuki. Sambaza mchanganyiko huu kwenye kitambaa

    safi cha pamba kilichofungiwa juu ya bakuli safi la metali. Viweke kwenye jiko la jua (solar

    oven) mchana kutwa hadi asali na nta vyote vivujie kwenye bakuli. Vitaunda matabaka tofauti.

    Jioni funua jiko la jua na ondoa nta, ambayo inaweza kutumika baadaye kwa kutengeneza dawa

    za mafuta (angalia sura ya 12).

    Sasa asali ni tayari kwa matumizi. Weka kiwango sawa cha asali na sukari. Sukari huzuia asali

    kusambaa kwa urahisi. Asali huua bakteria na kuacha kidonda kikiwa safi. Kidonda kitibiwe kwa

    mchanganyiko wa asali na sukari mara kadhaa kwa siku pasipo kukiosha tena.

    A.1.c. Papai lililoiva (Carica papai)

    Weka kipande chembamba na laini cha papai lililoanza kuiva juu ya kidonda.

    A.2. Vidonda vyenye maambukizo, majipu yaliyopasuka ya siku nyingi, vidonda vya wazi

    Papai (Carica Papai)

    Kwa matayarisho ya papai yafuatayo, vidonda vya wazi vilivyokuwa sugu kwa miaka mingi

    vimeweza kupona, kwa kawaida hata ndani ya wiki 1. Hii ni moja kati ya mifano kadhaa ambapo

    dawa za asili zimekuwa bora kuliko madawa ya hospitalini.

    Tumia matayarisho yafutayo ya mapapai hadi kidonda kisiwe na usaha tena. Kisha tibu kidonda

    kwa sukari au mchanganyiko wa asali na sukari.

    A.2.a. Sukari ya papai

    Changanya gramu 10 za sukari (nusu ya kikopo cha mikanda ya picha) na matone 10 ya utomvu

    wa papai bichi. Tengeneza upya kila siku. Tusemapo sukari „halisi“ tuna maana ya sukari

    ambayo imechukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye mfuko mpya kwenye kiwanda. Weka hii

    sukari ya papai kwa wingi kwenye kidonda, na mara tu inapoanza kuwa na majimaji ongeza

    nyingine. Kidonda kinaweza kuhitaji huduma hii mara kadhaa kwa siku.

    A.2.b. Papai bichi

    (i) Kipande chembamba: Weka kitambaa kwenye maji yanayochemka, wakati kikiwa bado cha

    moto sana osha papai bichi vizuri ambalo bado liko mtini. Osha kisu, kiweke ndani ya maji

    yanayochemka kwa dakika kadhaa, kisha kata kipande chembamba cha papai chenye unene wa

    kidole kidogo cha mtoto. Kiwekwe juu ya kidonda na ukishikize kwa kukifunga kwa kitambaa.

    Usikiondoe kwa masaa 8. Kama kikisababisha maumivu sana kiondoe mapema! Fanya huduma

    hii mara 3 kwa siku kwa siku kadhaa hadi kusiwe na usaha tena. Endeleza tiba hii na pia tumia

    tiba ya sukari kama tiba mbadala kwa hii. Baada ya kila huduma ya sukari rudi kwenye mti,

  • ondoa sehemu ile nyembamba ya lile papai ambayo kwa sasa itakuwa chafu, kisha kata na weka

    kipande chembamba kinachofuata kwenye kidonda.

    (ii) Vijiti: Vidonda vyembamba vyenye kina mara nyingine hutokea, kwa mfano, kwenye

    migongo ya wagonjwa waliolazwa muda mrefu. Katika mazingira yasiyo na maambukizo,

    waganga katika hospitali wanaweza kukata vipande vyembamba vya papai bichi na kuviingiza

    kwenye kidonda.

    A.2.c. Embwe la majani ya mpera (Psidium Guajava)

    Tiba hii haina gharama yoyote. Kwa hiyo inapatikana kwa wale wasioweza hata

    kununua dawa za gharama ya chini kabisa. Twanga kiganja kizima cha majani ya mpera

    yaliyooshwa. Yachemche taratibu pamoja na kikombe cha maji kwenye chungu kilichofunikwa

    kwa dakika 15. Iache ipoe. Weka embwe kwenye kidonda na vifunge. Rudia tiba hii asubuhi na

    jioni.

    A.2.d. Papai lililoiva

    Weka kijiko na bakuli katika maji yanayochemka kwa muda wa dakika 10 na kisha uvitumie

    kusaga nyama za papai lililoanza kuiva na kusambazia embwe lake kwenye kidonda. Fanya

    hivyo kwa kufuata kila hatua, asubuhi, mchana na jioni. Jinsi kidonda kinavyoonesha kuwa na

    maambukizo zaidi ndivyo unavyotakiwa kutumia papai bichi zaidi.

    A.2.e. „Gel“ ya Aloe (Msubili)

    Kwa vidonda vya siku nyingi vilivyo wazi na vilivyokataa kupona, kifunike kidonda kwa gel ya

    Aloe iliyochukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye jani lililo kwenye mmea mara 3 kwa siku.

    A.2.f. Mafuta ya Kitunguu saumu

    Tumia mafuta ya kitunguu saumu (Allium Sativum), angalia sura ya 7.5. Weka mara kadhaa kwa

    siku. Kwa kutengeneza kiasi kidogo cha mafuta ya kitunguu saumu changanya kijiko 1 cha

    mezani kitunguu kilichokatwakatwa vipande vidogovidogo sana na vijiko 2 vya mezani vya

    mafuta ya mimea. Weka kwenye chombo cha kioo, tikisa vizuri. Yatumike ndani ya masaa 24.

    A.2.g. Mafuta au dawa ya mafuta ya vitunguu maji (Allium cepa):

    Angalia sura ya 12

    A.2.h. Kwa vidonda na majipu yanayotoa usaha tumia jiwe jeusi (angalia sura ya 13)

    B. Kuungua

    B.1. Kidonda kipya cha kuungua

    Kwanza poza kidonda kwa maji safi ya baridi. Kumbuka, lengo kuu la huduma hii ni kuzuia

    maambukizo. Mweke mgonjwa kwenye chandarua ili kuzuia inzi kwenye kidonda.

    B.1.a. Aina za Msubili (Aloe barbadensis, Aloe ferox au Aloe arborescens)

    Osha jani vizuri bila kuliondoa kwenye shina. Kisha likate toka kwenye shina. Osha kisu kikali

    na ukiweke kwenye maji yanayochemka. Kwa kutumia kisu hiki, kata ile sehemu iliyo wazi tena

    ili kuifanya iwe safi kabisa, na pia kata na kuondoa ncha zenye miiba. Kisha ukate katikati kwa

    kufuata urefu ili kuweka wazi sehemu kubwa ya „gel“ iliyokatikati, ndani ya jani. Paka sehemu

    ya majimaji ya jani la msubili kwenye sehemu yote iliyoungua. Rudia mara kadhaa kwa siku.

  • Mweke mgonjwa ndani ya chandarua kuzuia inzi. Msubili hufanya kazi ya kuzuia maambukizo

    na kuzuia kuvimba.

    B.1.b. Chumvi ya mezani

    Yeyusha gramu 9 (kijiko 1 cha mezani kilichojaa kabisa) za chumvi ya mezani katika lita 1 ya

    maji, chemsha kwa dakika 20 na iache ipoe. Mwagie mchanganyiko huu kwenye sehemu

    iliyoungua mara kadhaa kwa siku. Kama kidonda kina kina kirefu, kifunge kwa „bandaji“ au

    kitambaa kisafi (kilichoondolewa maambukizo). Mwaga haya maji ya chumvi mara kadhaa kwa

    siku juu ya kitambaa hicho. Matone kadhaa ya utomvu kutoka kwenye papai bichi yanaweza

    kuongezwa kama kuungua kunaonekana ni hatari sana. Kwa dharula, kama huna chumvi,

    chemsha mkojo wa mgonjwa na utumie! Mkojo una chumvi!

    B.1.c. Chai ya mpera (Psidium guajava)

    Chemsha taratibu kiganja 1 cha majani mabichi yaliyooshwa ya mpera kwenye lita 1 ya maji

    katika chungu kilichofunikwa kwa dakika 15. Acha ipoe na uichuje. Baada tu ya kuchuja osha

    kidonda kwa chai hii. Rudia mara 3 kwa siku. Itakayobaki uimwage – tengeneza chai mpya kila

    inapohitajika.

    B.1.d. Mafuta na dawa ya mafuta ya kitunguu maji: Angalia sura ya 12.

    B.2. Kuungua kuliko na maambukizo

    B.2.a. Maji yenye utomvu wa papai na chumvi

    Kama sehemu iliyoungua ni chafu, isafishe mara kadhaa kwa siku kwa kutumia maji ya utomvu

    wa papai kama iliyoelekezwa hapo juu (A). Tumia pia “Gel” ya Aloe (angalia B.1.a.) au mafuta

    ya vitunguu maji (angalia B.1.d.)

    C. Majipu Jipu ni maambukizo yanayosababisha kifurushi kidogo cha usaha chini ya ngozi.

    C.1. Jipu lililofungwa usaha chini ya ngozi, ni pamoja na majipu yaliyo na mdomo,

    vidonda vilivyofungwa, maambukizo ya ngozi kuzunguka makucha ya vidole vya mkono

    au miguu n.k.

    C.1.a. Vitunguu saumu (Allium sativum)

    (i) Kata vipande vyembamba vya vitunguu saumu na uvifungie kwenye sehemu iliyoathirika

    (fanya hivi kwa usiku mzima kwa siku kadhaa) au

    (ii) Pondaponda kitunguu saumu na upake sehemu iliyoathirika au

    (iii) Tumia mafuta ya kitunguu saumu (angalia sura 7)

    Vitunguu saumu vina nguvu sana kuliko vitunguu maji. Uwe mwangalifu: Mgonjwa mwenye

    udhaifu wa ngozi anaweza kupata mabaka. Kufungia kitunguu saumu kwenye ngozi ndiyo njia

    bora zaidi, lakini pia iletayo maumivu zaidi. Kupaka ngozi kwa mafuta ya vitunguu saumu ni

    tiba dhaifu kidogo lakini pia isiyosababisha maumivu sana.

    C.1.b. Dawa ya mafuta ya pilipili: Angalia sura ya 12

    C.1.c. Kitunguu maji (Allium cepa)

  • Fuata matumizi ya vitunguu saumu hapo juu (C.1.a.). Badala ya mafuta ya vitunguu saumu tumia

    dawa ya mafuta ya vitunguu maji (angalia sura ya 12). Dawa ya vitunguu maji siyo kali kama

    dawa ya vitunguu saumu.

    C.2. Jipu lililo wazi

    Utibu kama vidonda vyenye maambukizo, angalia A.2.hapo juu.

    Sura 3: MATATIZO YA NGOZI

    A. Utangulizi: Matunzo ya ngozi na usafi Tengeneza na tumia sabuni inayolinda ngozi. Kwa kufua, tumia sabuni ya kujitengenezea

    iliyotengenezwa kama ifuatavyo: Chukua vipimo 4 vya sabuni ya kawaida, na kipimo 1 cha

    mafuta ya mboga na kipimo 1 cha maji. Pondaponda sabuni, ichanganye na mafuta na maji.

    Chemsha mchanganyiko polepole hadi sabuni itakapoyeyuka. Koroga mchanganyiko huo mpaka

    utakapopoa, kisha uumwage kwenye vyombo vya chapa. Acha kwa majuma 2 kabla ya

    kuutumia. Sabuni hii inaweza kuwekewa dawa kwa kudondoshea matone kadhaa ya mafuta ya

    mwarobaini, au majani makavu yaliyopondwa yanayotokana na mwarobaini au mlongelonge

    kabla ya kuimwaga kwenye vyombo vya chapa.

    B. Matatizo mbalimbali ya ngozi

    Kwa matatizo ya ngozi yasiyojulikana chanzo chake, kunywa mchanganyiko wa aina mbalimbali

    za chai za dawa, hasa Rozela na Artemisia, ili kuondoa sumu mwilini. Zinasaidia kusafisha

    damu, kulainisha takataka kwenye utumbo mkubwa, na kuzisaidia kutolewa nje hadi chooni.

    Uchafu na takataka mwilini zinaweza kusababisha matatizo ya ngozi.

    Kwa matibabu ya ngozi, tunapendekeza uanze na matibabu rahisi zaidi yanayonawirisha ngozi

    (yaliyotajwa mwanzoni), na endelea kwa utaratibu hadi kwenye zile zenye nguvu - lakini pia

    madhara - zaidi.

    Persea americana (avocado/ embe-mafuta) Upakaji wa nyama ya embe-mafuta lililoiva hufanya kazi kama huduma ya msingi ya kuanzia

    au dawa nzito ambayo hunawirisha ngozi yenye maambukizo au ngozi kavu. Dawa hii

    inaweza kutayarishwa jioni kwa kutumiwa kwa urembo; lakini lazima itumike haraka baada

    ya kutengenezwa. Changanya nyama ya embe-mafuta lililoiva na matone kadhaa ya limau na

    upake kwenye sehemu iliyoathirika kwa muda wa masaa 12 kwa siku; kwa mfano usiku

    mzima. Nyama ya embe-mafuta inaweza pia kutumika kama kiungo cha msingi kwa madawa

    au vipodozi, mfano: kwa kuchanganya na maji ya limau, mafuta ya mbegu za mwarobaini,

    nyama ya msubili n.k.

    Mafuta ya mbegu, kama vile mafuta ya mbegu za mchikichi, mafuta ya alizeti, mafuta ya karanga. Changanya kijiko 1 cha chai cha mafuta kwa kipimo kilekile cha maji kwenye

    kiganja cha mkono wako na usugue kwenye sehemu iliyoathirika.

    Nyama ya msubili: angalia sura ya 2.

    Brassica oleracea (kabeji): Tengeneza uzingo kutokana na jani la kabeji liliooshwa, na ulizungushe sehemu iliyoathirika. Huko Nigeria, mtoto mmoja aliamka mara 4 kila usiku

    akitoka damu, mwenye ngozi kavu. Kumzinga kwa jani la kabeji kulileta nafuu haraka.

  • Mafuta au dawa ya mafuta iliyotengenezwa kutokana na mafuta ya mbegu na mimea kama vile mpera, chamomila au artemisia. Kwa mchanganyiko huu angalia sura ya 12.

    Mafuta ya mbono (kutokana na Ricinus Commonis), ama iliyotengenezwa kiwandani, iliyotengenezwa kienyeji kijijini au iliyotengenezwa kwa kutumia mchanganyiko kutoka

    “Madawa ya Asili katika Nchi za Tropiki I”.

    Cassia alata (ringworm bush): Tengeneza embwe kwa kutumia majani yaliyopondwa na mafuta.

    Azadirachta Indica (Mwarobaini): Tumia kama embwe la majani na mafuta au maji, au dawa ya mafuta kutokana na majani, au mafuta ya mbegu za mwarobaini.

    Allium Cepa (Kitunguu maji): Tumia mafuta yake au dawa ya mafuta. Angalia sura ya 12.

    Capsicum frutescens (pilipili): Paka mafuta ya pilipili au dawa ya mafuta yake kwenye sehemu iliyoathirika. Pilipili ina viasili vinavyoua maambukizo na mara nyingine huondoa

    maumivu. Angalia sura ya 12.

    Allium Sativum (vitunguu saumu – kama mafuta ya vitunguu saumu). Angalia sura ya 7.

    “Mafuta ya upele”: Kipimo cha 50:50 cha mchanganyiko wa mafuta ya taa na mafuta ya mbegu hautumiki kwa upele pekee, bali pia kwa matatizo mengine, k.mf. maumivu

    yanayosababishwa na filaria. Angalia D.1.

    Allium Sativum (kitunguu saumu): Sugua kipande chembamba, au kifungie, kwenye sehemu iliyoathirika.

    C. Maambukizi ya mba Maambukizi ya mba yanaweza kutokea kwenye sehemu yoyote ya mwili, lakini mara nyingi

    yanapatikana katikati ya vidole vya miguu (athlete’s foot), au vidole vya mikono na katikati ya

    paja. Baka (alama nyeupe ya mviringo kichwani) pia ni maambukizi ya mba. Sehemu

    zilizoathirika zioshwe kila siku kwa maji na sabuni. Baadaye ziwekwe katika hali ya ukavu na

    zihudumiwe kama ilivyoelekezwa hapo chini. Ikiwezekana, ukae kwenye hewa nzuri na mwanga

    wa jua. Vaa nguo zilizotengenezwa kutokana na malighafi asilia, yaani pamba. Endelea na

    matibabu hayo mpaka majuma 2 baada ya dalili kupotea.

    C.1. Vigunguu saumu (Allium sativum)

    Sugua mafuta ya vitunguu saumu (angalia sura ya 7.5) kwenye sehemu iliyoathirika. Kwa mba

    wa kwenye vidole vya miguu unaweza kuweka kikonyo cha kitunguu saumu katikati ya vidole

    vya miguu.

    C.2. Ringworm bush (Cassia alata) na mbono au mafuta ya mawese.

    Twanga majani mabichi ya Cassia alata, na uchanganye vijiko vyake 10 na kijiko 1 cha mafuta

    ya mbono. Kama mafuta ya mbono hayapatikani, tumia mafuta ya mawese au mafuta mengine

    ya mimea. Weka mara 3 kila siku. Tengeneza upya kila siku. Kama huna mafuta kabisa, twanga

    haya majani mabichi na uyasugue kwenye sehemu iliyoathirika mara 3 kwa siku.

    C.3. Ringworm bush (Cassia alata), papai na mafuta

    Twanga kiganja kizima cha majani mabichi na machanga ya ringworm bush, ongeza matone 10

    ya utomvu wa papai bichi na kijiko kizima cha mezani cha mafuta ya mbono au ya mawese.

    Changanya na usugue kwenye sehemu iliyoathirika mara 3 kwa siku. Tengeneza dawa mpya kila

    siku.

    C.4. Dawa ya mafuta ya kuzuia mba. Tumia mwarobaini, melia au ringwormbush (Angalia

    sura ya 12).

  • D. Upele (Scabies)

    Upele hutambulishwa na uvimbe mdogomdogo unaowasha, ambao unaweza kutokea mwili mzima.

    Katikati ya uvimbe huu kuna vipele vyeusi vidogovidogo zaidi vyenye vichwa vyenye ukubwa wa

    vichwa vya sindano. Upele ni kawaida kwa watoto. Unapatikana zaidi katikati ya vidole vya

    mikono, kwenye kiungo cha mkono na kitanga, kiuno, na sehemu za siri. Husababishwa na vijidudu

    vidogo vinavyotengeneza njia chini ya ngozi. Unaambukiza kwa urahisi sana. Kama mtu mmoja

    katika familia akiwa na upele, lazima familia nzima itibiwe. Usafi ni muhimu. Oga mwili mzima na

    badilisha nguo zako kila siku. Nguo zote na matandiko lazima yafuliwe na kuanikwa juani. Njia

    rahisi ni kuziweka kwenye jiko la jua. Safisha sehemu za chuma au za mbao za kitanda chako kwa

    mafuta ya taa.

    D.1. Mafuta ya taa na mafuta ya mboga (“Mafuta ya upele”)

    Tayarisha mafuta ya upele kwa kuchanganya kikombe 1 cha mafuta ya taa na kikombe 1 cha mafuta

    ya mboga. Mara 2 kwa siku na kwa siku 2 hadi 3, oga mwili mzima na upake mafuta ya upele

    kwenye sehemu iliyoathirika. Mchanganyiko huu wa anamed kwa sasa unatumiwa na hospitali

    nyingi. Matibabu haya ni mazuri pia kwa mwasho unaosababishwa na filariasis (minyoo

    midogomidogo kwenye damu) kuzunguka kiuno. Filaria husafiri hadi sehemu nyingine za mwili.

    Weka mafuta ya taa na haya mafuta ya upele mbali na moto na watoto pia.

    D.2. Mafuta ya Vitunguu saumu (Allium sativum) Angalia C.1. hapo juu

    D.3. Mwarobaini (Azadirachta indica). Angalia sura ya 9.

    D.4. Mimea mingine

    Kwa watu wazima wenye upele, na kwa upele kwenye sehemu ndogo, bila kuwa na fedha ya

    kununua mafuta ya taa, na kama vitungu saumu na mwarobaini havipatikani, kuna njia tatu: Iliyo na

    sumu ndogo zaidi ni Tephrosia vogelii (kibaazi). Chaguo la pili ni Rauwolfia vomitoria

    (kimusukulu) na la tatu ni Nicotiana tabacum (tumbaku). Matumizi ya kila mmea ni kusugua majani

    safi yaliyokomaa kwenye sehemu zilizodhurika. Mbadala ni bora zaidi kwa ngozi kuponda majani

    haya na kuyachanganya na kiasi fulani cha mafuta ya mboga. Sugua mchanganyiko huu kwenye

    sehemu iliyoathirika mara 3 kwa siku. Tengeneza mpya kila siku. Uwe mwangalifu, karibu mimea

    hii yote ina sumu!

    SURA 4: KUHARISHA

    Mtu anaharisha wakati haja kubwa inapokuwa ya majimaji. Kama haja kubwa pia itakuwa na

    kamasi na damu, tatizo linaitwa “kuharisha damu” (Dysentry).

    Kuharisha ni ugonjwa hatari sana. Inahusika na vifo vya zaidi ya watoto millioni 3 katika nchi

    zinazoendelea kwa mwaka. Karibu mara zote watoto wasingekufa – kama tu wazazi wao au hata

    klinki zingejua matibabu yaliyoelezwa katika sura hii. Kuharisha ni hatari hasa kwa watoto

    waliopungukiwa lishe.

    Kuharisha kunaweza kuwa dalili za magonjwa mengine, ambayo pia yanahitaji matibabu,

    angalia jedwali hapo chini 4.1. Kama ukienda chooni mara moja, lakini ukakaa huko siku nzima,

    una kipindupindu!

    Watoto wanapoharisha, wakati wote wapewe maji ya chumvi (Oral)! Watu wazima wangependa

    kwanza kujaribu dawa rahisi zaidi kama vile dawa ya mkaa, matunda ya mpera mabichi n.k.,

  • lakini kama kuharisha kukiendelea, au kwa matatizo makubwa zaidi, maji ya chumvi ni ya

    lazima kwa watu wazima pia! Mgonjwa lazima aendelee kula vyakula vinavyoongeza vitamini

    na madini ya kutosha.

    Mara nyingi kuharisha kunaweza kuzuiwa, hasa kwa kujali suala la usafi.

    4.1. Jinsi ya kuzuia uharishaji.

    a) Osha mikono yako kwa sabuni (au majani ya mpapai) na maji yanayotiririka kabla ya kula na baada ya kutoka chooni.

    b) Usitumie chupa za watoto za kunyonyeshea kwa watoto - zina uwezekano mkubwa wa kusababisha maambukizo. Maziwa ya mama ni bora zaidi!

    c) Wakati wote tupa chooni kinyesi cha watoto wachanga na wakubwa. d) Oga kila jioni na ulale sehemu iliyo safi. e) Watu wazima na watoto lazima watumie vyoo kwa haja kubwa na ndogo. Tundu la choo lazima

    lifunikwe na kifuniko ili kuzuia inzi kusambaza maambukizo kutoka kwenye kinyesi kwenda

    kwenye chakula. Pambana na mila na desturi zinazozuia matumizi ya vyoo.

    f) Kula chakula kizuri, chenye lishe kamili na hamirojo (mfano: mahindi na mawele), protini (mfano: nyama na mayai) na vitamini (mfano: mboga na matunda). Angalia sura ya 4.

    g) Kula vitunguu saumu mbichi na/au kipande cha jani la mpapai chenye urefu wa sm 5 za mraba kila siku ili kuzuia minyoo na maambukizo ya amiba. Njia hii ni msaada hasa kwa wale wenye

    matatizo ya kuharisha mara kwa mara.

    4.2. Jinsi ya kutibu kuharisha

    A. Rudishia maji yaliyopotea, nguvu na madini kwa maji ya chumvi (Oral).

    Kwa kuharisha, jambo la muhimu zaidi ni kufidia maji yaliyopotea. Kwa watu wazima na watoto,

    wakati wote tumia maji ya chumvi na wakati wote jitengenezee maji ya chumvi mwenyewe.

    Usitumie ya madukani (ORS) - ni gharama kubwa. Hatufurahishwi pia na viroba vya chumvi za

    haya maji vinavyotolewa bure na umoja wa mataifa, maana jambo hilo linachochea hali ya

    utegemezi! Kila mzazi lazima ajue jinsi ya kutengeneza maji-chumvi

    A.1. Yaliyomo katika maji-chumvi.

    Maji chumvi yana vitu 3: Maji, sukari, na chumvi. Maji ni muhimu kwa shughuli zote za mwili,

    sukari kwa ajili ya nguvu, na chumvi kufidia chumvi iliyopotea wakati wa kuharisha.

    Jedwali 4:1: Jinsi ya kutambua na kutibu kuharisha.

    Dalili Sababu zinazoweza

    kusababisha.

    Tiba

    Hakuna damu

    kwenye kinyesi,

    hakuna homa.

    Sumu kwenye chakula. Watoto: maji-chumvi;

    Wazima: maji-chumvi/ mkaa.

    Kuharisha

    kunakosababishwa na

    virusi

    Watoto: maji-chumvi,

    Wazima: maji-chumvi/ mkaa

    Kipindupindu (kuharisha Tumia maji-chumvi kwanza kisha

  • kwa nguvu ambako mharo

    wake ni kama maji ya

    mchele).

    mpeleke hospitali.

    Hakuna hospitali? Tumia antibiotic (ni

    dawa za kuua bacteria).

    Hakuna anti-biotic? Jaribu chai ya

    anamed ya kuharisha (angalia B.3. chini)

    au chai ya Artemisia.

    Hakuna damu

    kwenye kinyesi,

    homa

    Malaria Wakati wote tumia maji-chumvi; chai ya

    mchachai wakati wote na dawa za kutibu

    malaria (angalia sura ya 5).

    Homa ya matumbo Maji-chumvi na antibiotic. Hakuna

    antioitic? Jaribu maji-chumvi na chai ya

    majani ya Azadirachta indica, au

    Artemsia annua, au Vernonia amygdalina

    au Melia azedarach.

    Damu kwenye

    kinyesi – hakuna

    homa

    Kuharisha damu sababu ya

    amiba.

    Maji-chumvi na chai ya mziwaziwa

    (euphorbia hirta). Kuharisha kukiendelea:

    Maji chumvi na chai ya kuharisha ya

    anamed (angalia B.3 chini).

    Damu kwenye

    kinyesi au mkojo.

    Hakuna homa.

    Kichocho. Maji-chumvi. Jaribu chai ya artemisia

    annua. Nenda kwenye Zahanati au

    hospitali kwa matibabu.

    Damu kwenye choo

    na homa.

    Kuharisha kwa sababu ya

    bacteria (“Bacterial

    Disentery”)

    Maji-chumvi na chai ya kuharisha ya

    anamed (angalia B.3. chini). Kama

    hakuna maendeleo yoyote, nenda

    Hospitali.

    Hakuna Hospitali? Tumia antibiotic, maji-

    chumvi na chai ya kuharisha ya anamed.

    Hakuna antibiotic? Tumia maji-chumvi,

    na ongeza Vinca rosea kwenye chai ya

    kuharisha ya anamed hadi kuharisha

    kukome. Angalia B.6. chini.

    MAJI: Tumia maji mazuri, kama hakuna maji safi ya chemchemi, tumia maji yaliyochemshwa au tengeneza chai ya majani ya mpera na uitumie badala ya maji.

    SUKARI: Hasa tumia asali, isipokuwa kwa watoto walio chini ya mwaka mmoja, ambao kwao haishauriwi kutumia asali. Kama hakuna asali, tumia sukari ya nyumbani (baadhi

    ya hospitali zinatumia glucose). Kama huna sukari au mgonjwa ana kisukari, badala ya

    gramu 30 za sukari kwenye mchanganyiko ulioelezwa hapo chini (A 2), unaweza

    kutumia na kuchanganya vizuri moja kati ya vifuatavyo katika lita 1 ya maji:

    a) Gramu 100 za ndizi tamu zilizosagwa (kama nusu kiganja, usichemshe). b) Gramu 100 za viazi vitamu (kama nusu kiganja, chemsha kwa dakika 10). c) Gramu 30 (vijiko 3 vya chai vilivyojaa sana) vya unga wa ngano, mchele

    uliotwangwa au mtama. Chemsha kwa dakika 5.

    CHUMVI: Hasa, tumia ile inayoitwa “chumvi ya kienyeji.” Hii inatengenezwa kwa kienyeji kwa kuchukua majivu ya miti iliyochomwa, ongeza maji, chemsha hadi maji

  • yakauke kwenye chungu cha udongo (kwa sababu vyombo vya metali vinaweza

    kuharibika) na kukusanya chembechembe zinazojitokeza. Hii ni nzuri, kwa sababu ina

    potassium. Ama sivyo tumia chumvi ya mezani (sodium chloride).

    POTASSIUM: Ni kitu kinachopaswa kuongezwa kama chumvi ya mezani ikitumika na kama kuharisha kutaendelea kwa siku kadhaa. Potassium inasaidia misuli ya utumbo na

    matumbo kufanya kazi vizuri. Vyanzo vizuri vya potassium ni pamoja na mchicha, embe-

    mafuta, ndizi, boga, maji ya nazi, karoti, soya iliyopikwa, njugu, moringa na majani ya

    mboga za kijani-nyeusi yaliyochemshwa.

    Kwa watoto wadogo ambao hawawezi kula chakula kingi, ongeza kijiko 1 cha chai cha

    majivu safi (kutokana na miti au nyasi zisizo na sumu, au kutokana na magugu maji

    yaliyokaushwa, ambayo yana potassium nyingi) kwenye lita 1 ya maji inayotumika

    kutengenezea maji-chumvi (angalia chini). Baada ya dakika kadhaa, chuja maji.

    Angalizo: Chumvi za potassium ziongezwe tu kama mgonjwa anaweza kukojoa.

    Kama chochote kati ya vifaa vyako (maji, sukari au chumvi) siyo safi kikamilifu,

    chemsha mchanganyiko huo kwa dakika chache ili kuua bacteria. Nyongeza ya rangi na

    harufu havisaidii kwa lolote.

    A.2. Kutengeneza maji-chumvi

    Nyumbani: Ama, ongeza vijiko 4 vya mezani vya asali au vijiko 2 vya mezani vilivyojaa sana

    vya sukari (gramu 30) na nusu kijiko cha chai kilichosawazishwa cha chumvi, kwenye lita 1 ya

    maji. Au, kwenye kikombe kikubwa cha maji (ml 500), ongeza vijiko 2 vya mezani vya asali au

    kijiko 1 cha mezani cha sukari kilichojaa sana, na mbinyo 1 wa chumvi kiasi cha chumvi laini

    unachoweza kubeba kati ya kidole gumba na shahada.

    Hospitalini: Kwenye lita 1 ya maji ongeza gramu 20 za glucose au gram 30 za sukari ya

    nyumbani, gramu 2.9 za trisodium citrate dihydrate, gramu 3.5. za chumvi ya mezani (NaCl) na

    gram 1.5 za potassium chloride.

    A.3. Maji-chumvi: Kipimo cha kunywa.

    Kwa siku: ml 200 (glass moja) kwa kila kilo 1 ya uzito wa mtoto wako. Kama hujui uzito wa

    mtoto wako, na huwezi kupima ml, jedwali lifuatalo litakusaidia: Vikombe ni vipimo vizuri zaidi

    kuliko chupa, kwa sababu ni vigumu kuosha chupa vizuri.

    Jedwali 4:2: Matumizi ya kila siku ya maji-chumvi.

    UMRI ML IDADI YA VIKOMBE AU CHUPA ZENYE

    UKUBWA WA ………….

    LITA 0.33 LITA 0.5 LITA 0.7 LITA 1

    Chini ya miezi 6 700 2 1.5 1 ¾

    Miezi 6 – miaka 2 1,400 4 3 2 1½

    Miaka 2 – 6 2,100 6 4 3 2

    Miaka 7 na zaidi 2,800 8 6 4 3

    Watu wazima 3,500 10 7 5 3½

  • Kunywa taratibu kwa uaminifu kutwa nzima. Kwa watoto wachanga lazima uendelee

    kunyonyesha maziwa ya mama.

    B. Kutibu kwa chai ya mimea ya dawa au mkaa wa dawa.

    B.1. Mpera (Psidium guajava)

    Mpera huzuia maambukizo, huzuia mshituko wa mwili, na ina kemikali ya hudhurungi

    inayosaidia usukumaji wa damu kwenye misuli. Sifa zote hizo ni nzuri kwa kutibu kuharisha.

    Kutengeneza chai ya mpera, chukua kiganja (maana yake: kiasi cha majani ambayo mgonjwa

    mwenyewe anaweza kuzinga katika kiganja chake) cha majani ya mpera, yachemshe katika lita 1

    ya maji kwa dakika 2. Baadaye uache ikolee kwa dakika nyingine 30, chuja na tumia ndani ya

    masaa 24.

    a) Kuharisha kwa kawaida kwa watu wazima: Kunywa lita 1 ya chai ya majani ya mpera ya kawaida. Hii husaidia katika 90% ya matukio yote ya kuharisha.

    b) Kwa kuhara kunakodumu kwa watu wazima na watoto tumia “maji-chumvi ya mpera” kwa kiasi kilichotolewa kwenye jedwali 4.2. Tayarisha chai ya mpera kama ilivyoelezwa

    hapo juu, na ongeza sukari na chumvi kama ilivyoelezwa kwenye A.2. hapo juu.

    c) Chai ya mpera inasaidia pia kwa vidonda vya tumbo: Kunywa kidogokidogo kila baada ya saa 1.

    B.2. Mziwaziwa (Euphorbia hirta)

    Kama chai ya mpera haisaidii: Chemsha kiganja 1 cha

    majani mabichi (kata kwa mkasi, ukiacha mizizi ili mmea

    uweze kustawi tena) kwenye lita 1 ya maji kwa dakika 2

    (Kama una mzani: tumia gramu 10 za majani mabichi au

    gramu 2 za majani yaliyokauka) na uache ikolee kwa dakika

    nyingine 30. Chuja na unywe kwa awamu kutwa nzima.

    Endelea na tiba hii kwa siku 8.

    Hii inafaa sana, hasa kwa maambukizi ya amiba. Ni muhimu

    kuutambua mmea huu kama ulivyo. Umeenea katika nchi za

    tropiki. Unakua kati ya sm 30 na sm 40 kwa urefu, na una

    majani (yenye menomeno mafupi) kwenye vikonyo vifupi. Mashina yamefunikwa na

    nywelenywele ngumu zilizotapakaa zenye rangi ya njano.

    Unafanana na magugu mengine mengi, lakini una tofauti tatu zinazoonekana:

    a) Utomvu mweupe unaovuja kutoka katika shina linapokatwa. b) Kitita cha maua madogo madogo sana ya kijani yanakuwa kwenye shina fupi ambao

    linatokeza mahali ambapo jani linaungana na shina.

    c) Matunda yana mbegu zenye rangi nyekundu, ambazo zina urefu usiofikia milimeta 1 na zenye kingo 3.

    B. 3. Kuhara sana na kuhara damu. “Chai ya kuhara ya anamed”

    Chai ya kuhara ya anamed inafaa sana, na imeokoa maisha ya watu wengi. Hata hivyo,

    inatakiwa kutumika pale tu unapokuwa umetumia chai ya mpera na ukaona haitibu. Osha na

    changanya kiganja 1 (maana yake: kiasi ambacho mgonjwa mwenyewe anaweza kushika

    katika kiganja chake) cha kila vifuatavyo:

  • Mziwaziwa (Euphorbia hirta – mmea mzima lakini siyo mizizi)

    Majani ya mpera

    Majani ya mwembe machanga ya kijani.

    Jedwali 4:3 - Kipimo cha anamed cha dawa ya kuhara.

    Umri Kipimo cha kila siku

    Mwaka 1 – 3 ¼ lita kila siku

    Miaka 4 – 6 ½ lita kila siku

    Miaka 7 – 12 ¾ lita kila siku

    Miaka 13 – watu wazima lita moja

    Chemsha kwa dakika 2 katika lita 1 ya maji, na uache ikolee kwa dakika nyingine 30. Kama mwembe au mpera haupatikani tumia majani ya mpapai. Lakini chai hiyo itakuwa

    chungu na mtoto anaweza kuikataa.

    Kunywa kiasi hiki cha chai kwa masaa 24. Endelea kwa siku 8 hata kama dalili zimetoweka. Tiba inayoendelezwa huondoa mayai yaani amiba kutoka kwenye matumbo.

    Mara nyingi inaondoa minyoo ya kwenye matumbo pia.

    Bakavu, huko Kongo, mahali ambako kumbukumbu zimetunzwa kwa uangalifu, walikuwa na mafaniko ya 99% katika kutibu zaidi ya wagonjwa 200 wanaosumbuliwa na amiba na

    kuharisha damu kwa kutumia chai ya majani ya Euphorbia Hirta, mpera na mwembe.

    Dokezo kwa Mahospitali: Unaweza kupendelea kutayarisha chai hii ya kuharisha ya anamed

    kutokana na majani makavu. Vuna mimea hii kwa kiwango kilicho sawa kuelekea mwisho wa kipindi

    cha mvua, ikaushe vizuri na uisage. Kipimo sasa kitakuwa kuchemsha kijiko 1 kilichojaa katika lita 1

    ya maji kwa dakika 2 na baadaye uache ikolee kwa dakika nyingine 30. Kama unga wa majani makavu

    ukitunzwa kwenye chombo kisichoruhusu hewa kuingia, itadumu salama kwa mwaka mmoja.

    B.4. Mimea mingine

    Mimea iliyotajwa juu isipopatikana, chai inaweza kutengenezwa kwa kutumia majani ya

    mwarobaini (angalia sura ya 9), kutokana na Artemisia annua (angalia sura ya 8) au kutokana

    na majani mabichi ya kijani ya mwembe (Mangifera indica).

    Majani ya mpapai (Carica papai) pia yanatibu: Chemsha kiganja 1 kilichojaa cha majani

    katika lita 1 ya maji kwa dakika 1, kisha acha ikolee kwa dakika 20. Chuja na unywe kwa

    sehemu sehemu kutwa nzima. Watoto hupendelea chai ya majani ya mpera kwa sababu chai

    ya majani ya mpapai ni chungu. Kama hakuna kingine kinachopatikana, kunywa maji

    uliyotumia kupika mchele.

    B.5. Mkaa wa dawa

    Mkaa unatumika kwenye matukio ya chakula chenye sumu au kwa kuhara polepole. Uwe

    mwangalifu kwa watoto, hata mkaa lazima wakati wote unywewe ukiambatana na maji-

    chumvi. Tengeneza mkaa kutokana na mti ambao hauna sumu. Kwa mfano, tumia matawi

    yanayoota kuelekea katikati ya mwembe ambao kamwe hayazai matunda, au tumia maganda

  • ya karanga yaliyopondwapondwa. Yachemshe katika chombo cha chuma kilichofunikwa

    hadi mti au maganda yawe mkaa. Uwe mwangalifu wakati unafunua, unga unaweza kushika

    moto kwa ghafla! Ponda mkaa, uchekeche, uchemshe tena ili kuhakikisha hauna

    maambukizo. Kunywa kijiko 1 cha chakula, mara 3 kwa siku katika maji. Endelea kunywa

    maji mengi au maji-chumvi wakati wote (angalia A.2. juu).

    B.6. Vinca rosea

    Katika hali zinazotishia maisha, ambapo hata chai ya kuzuia kuhara ya anamed haisaidii,

    tayarisha chai ya anamed ya kuzuia kuhara kama ilivyoelekezwa hapo juu. Kisha, mara moja

    baada ya kushusha chai kutoka kwenye moto, ongeza kiganja kizima cha majani mabichi ya

    Vinca rosea kwenye chai na uiache ikolee kwa dakika 30. Chuja na kunywa kwa awamu kwa

    muda wa siku nzima.

    Angalizo: Vinca rosea ina sumu!

    SURA 5: MALARIA

    5.1. Utangulizi

    Katika dunia nzima karibu watu milioni 500 hupata malaria kila mwaka. Kati ya hao, millioni 1

    hadi 2 hufa. Wengi kati yao ni watoto chini ya miaka 5.

    Malaria huambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine na mbu wa jamii ya Anopheles.

    Wanapochukua damu kutoka kwa mtu aliyeambukizwa wanachukua vimelea vya malaria

    (vijidudu viitwavyo plasmodium). Kisha wanapochukua damu kutoka kwa mtu mwingine,

    wanaingiza plasmodium pamoja na mate yao. Plasmodium husafiri hadi kwenye ini, na kutokea

    hapo huingia hadi kwenye chembe nyekundu za damu. Mtu huugua baada ya siku 7 hadi 10

    baada ya kuumwa na mbu.

    Kwa kawaida mgonjwa wa malaria huhisi baridi na mara nyingine hutoka jasho. Inawezekana

    lakini kwamba dalili mojawapo ikawa na nguvu zaidi, kiasi kwamba haidhihiriki haraka kwamba

    mgonjwa ana malaria. Kwa njia hii malaria inaweza kujificha nyuma ya safu ya dalili za

    magonjwa, mfano: kuharisha na kutapika, matatizo ya kiakili, kupoteza fahamu, upungufu wa

    damu au homa.

    Mimea inayotibu inaweza kuokoa maisha ya wengi. Mfano wa kushangaza unatokea Kongo

    D.R.C.: Mwaka 1997 Askofu wa Dayosisi ya Bolungu–Ikela ilimbidi kuwakimbia waasi na

    kujificha porini kwa majuma 4, akiwa na watu wengine 20. Hawakuwa na nyumba wala

    chandarua, wala madawa. Waliishi chini ya miti! Walipopata homa walikunywa chai za dawa

    zilizoorodheswa hapa chini. Askofu alisema, “Pamoja na hofu yetu, hakuna mmoja wetu

    aliyekuwa mgonjwa sana kwa malaria.”

    5.2. Jinsi ya kuzuia malaria

    1. Punguza idadi ya mbu nyumbani kwako na katika mazingira yaliyo karibu.

    Usiwe na maji yaliyo wazi katika mapipa au matenki yote; yanahitaji vifuniko au nyavu za kuzuia mbu.

    Kusiwe na maji yaliyosimama ya aina yoyote.

    Kusiwe na taka zinazozagaa – mfano mbu huzaliana katika taili zilizochakaa na makopo.

    Tunza msitu wako kwa sababu huko wanaishi maadui wa asili wa mbu.

  • Usiwe na mimea mirefu (mfano nyasi) karibu na nyumba, isipokuwa mimea yenye harufu nzuri kama vile Cymbopogon citrates (mchaichai), jamii za tururu, (Tagetes

    erecta, Tagetes minuta) au Artemisia annua. Inashauriwa hata kuwa na mimea hiyo

    ndani ya nyumba (ikiwa imeoteshwa kwenye vyombo).

    2. Punguza mgusano kati ya mbu na watu.

    Tumia chandarua, hasa wakati wa kulala na nyavu za kuzuia mbu kwenye madirisha. Weka kiasi kidogo cha mafuta ya mwarobaini katika mafuta ya kuwashia taa.

    Weka maua ya pyrethrum yaliyokaushwa na kupondwapondwa kwenye kona ya chumba chako.

    3. Punguza idadi ya vimelea.

    Tibu wagonjwa Zuia vimelea kuwa sugu – tumia tiba za aina mbalimbali (angalia jedwali Na. 5).

    4. Jenga kinga nzuri ya mwili

    Unapokuwa na malaria – itibu inavyopaswa. Kula matunda na mboga kwa wingi – ambavyo vina vitamini C. Weka vitunguu saumu vingi kwenye chakula chako hasa vibichi. Angalia sura ya 6. Epuka uvutaji sigara na pombe

    Jedwali 5 Madawa ya asili kwa ajili ya kutibu Malaria

    Jina la mmea Utumike hadi

    joto la mwili

    (°C)

    Sehemu

    ya mmea

    Jinsi ya kutumia Nguvu ya

    mmea

    Madhara

    Cymbopogon

    citratus

    (mchaichai)

    wakati wote Majani chai (angalia point 3) + Hakuna

    Allium Sativum

    Vitunguu

    saumu

    (angalia sura

    ya 7)

    Wakati wote Vitunguu vijiko 3 vya vitunguu

    saumu

    vilivyokatwakatwa

    ++ Maumivu ya

    tumbo

    Zingiber

    officinale

    (tangawizi)

    37.5 Mizizi kula tangawizi bichi

    kiganja 1 au chemsha

    kwa dakika 10.

    Usichuje, kula na

    kunywa kila kitu

    + Hakuna

    Psidium

    guajava

    (mpera)

    37.5 Majani chai (decoction) + Hakuna

    Carica Papaya

    (mpapai)

    angalia sura ya

    10

    38.0 Majani chai (infusion) ++ Kuna

    uwezekano wa

    kutapika au

    kupata allergic

    readtion

    Vernonia

    amygdalina

    38.5 Majani au

    mizizi

    majani: infusion

    mizizi: decoction

    ++ Haijajulikana;

    ina aina ya

  • (bitter leaf) (angalia

    maelezo

    No 4 na 8)

    sumu lakini

    Azadirachta

    indica

    (mwarobaini) –

    angalia sura ya

    9

    38.5 Majani

    (angalia

    maelezo

    No 4 na 8)

    majani: infusion

    ++ Inaathiri ini

    Cinchona

    officinalis

    39.0 Gome

    (angalia

    maelezo

    No

    5 na 8)

    chai (decoction) +++ Mlio masikioni

    Wakati

    mwingine

    kichefuchefu na

    kutapika. Dawa

    ikizidishwa

    kiziwi kinaweza

    kujitokeza au

    kutoka kwa

    damu masikioni

    Artemisia

    Annua (angalia

    sura ya 8)

    39.0 Majani

    (angalia

    maelezo

    No 8)

    chai (infusion) +++ Hakuna

    5.3.Kutibu kwa mimea

    Tumia mimea ya dawa ya aina nyingi ili kuzuia vimelea vya malaria kuwa sugu kwa

    tiba.Tunapokwua na maambukizi, vijidudu vinasababisha homa, hasa vinapokufa na kuanza kuoza.

    Vitu vyovyote vinavyosababisha homa vinaitwa “pyrogens.” Unywaji husaidia mwili kuondoa

    pyrogens. Pyrogens pia hutolewa nje kupitia kwenye ngozi kwa njia ya jasho. Chai ya moto ya

    mchaichai hasa husababisha mwili kutoa jasho na kukojoa sana, kwa jinsi hiyo husafisha damu na

    mwili. Kutokwa jasho hasa kunaondoa sumu mwilini. Tunapendekeza kwamba mtu mzima mgonjwa

    wa malaria anywe lita 2 za chai ya mchaichai kwa nyongeza kwenye lita 1 ya chai ya dawa ya

    mimea iliyotajwa kwenye jedwali Na. 5. Hata hivyo, tunapendekeza kwamba mtu mzima ye yote

    mwenye joto kali anywe lita 2 za mchaichai kila siku - kwa tatizo lolote.

    Kila tiba ya hii mimea iendelezwe kwa siku 7. Sukari au asali inaweza kuongezwa kwenye aina zote

    za chai. Malaria huharibu sukari mwilini, na kwa hiyo kufidia sukari katika damu ni jambo

    linalosaidia. Pia wagonjwa wa malaria ni vyema wapewe chakula kwa kuwa mara nyingi hupoteza

    hamu ya chakula na hivyo kupungukiwa lishe.

    Muhtasari wa matibabu

    1. Watu wazima wanatakiwa kunywa jumla ya lita 3 kwa siku. Watoto nao ni lazima pia wanywe sana kiwango kikitegemea uzito wa miili yao.

    2. Chai ya dawa inaweza kutengenezwa kwa kuchemsha dawa katika maji au kumwagia maji ya moto.

    Kumwagia maji ya moto (Infusion): Mwaga lita 1 ya maji yanayochemka kwa kiganja

    kizima cha majani mabichi ya dawa, au gramu 15 ya majani makavu (kama ni Artemisa

    annua au Azadirachta indica iwe gramu 5). Iache kwa dakika 10 hivi, kisha ichuje.

  • Kuchemsha (Decoction): Kipimo ni kama katika kumwagia maji ya moto. Chemsha

    maji na mimea kwa pamoja kwa dakika kama 20 hivi. Poza na uchuje.

    3. Kwa mchaichai, chemsha majani yake kwa dakika 2. Acha itulie kwa angalau dakika 10, kisha ichuje.

    4. Vernonia amygdalina. Majani yake ni machungu sana. Magamba ya mizizi yake lina nguvu zaidi. Tumia mizizi yenye unene wa kidole, mizizi ya pembeni, siyo mzizi mkuu, ili mti

    usife. Tumia kiganja 1 cha magamba ya mizizi na uchemshe kwenye lita 1 ya maji kwa

    dakika 20. Chuja na unywe kwa awamu 4 kwa siku 1. Endeleza tiba hii kwa siku 7.

    5. Cinchona officinalis: Chemsha gram 10 au vijiko 3 vya chai vya magamba yaliyopondwapondwa katika lita 1 ya maji kwa dakika 10, chuja na unywe kwa awamu ndani

    ya masaa 24. Watoto wanywe kiasi kidogo zaidi kufuatana na uzito wao.

    6. Katika hali ambayo mimea yote hii haisaidii, endelea kutumia lita 2 za mchaichai kila siku, na pia tumia dawa za hospitalini (k.mf. Amodiaquine au Fansidar). Hakikisha pia kwamba ni

    malaria kweli inayomsumbua mgonjwa na si ugonjwa mwingine.

    7. Kumbuka kuwa hakuna wagonjwa wawili wanaoweza kuwa na hali zilizo sawasawa kamwe. Ingawa watu wawili wanaweza kuwa na dalili zile zile, wanaweza wasitibiwe na dawa ile ile

    ya mmea.

    8. Akina mama wajawazito wasitumie Azadirachta indica (mwarobaini) au Vernonia amygdalina (mtukutu). Katika miezi 3 ya mwanzo ya ujauzito tumia Cinchona officinalis

    (mkwinini) au Artemisia annua chini ya uangalizi wa Daktari tu.

    SURA 6: UKIMWI: Imarisha mfumo wa kinga mwilini

    Ili kudumu katika afya njema, kila mtu anatakiwa kuhakikisha mfumo wake wa kinga mwilini

    uko imara kadri iwezekanavyo. Jambo hili ni la muhimu hasa kwa watoto wadogo, wajawazito

    na watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).

    Jali haya yote yafuatayo:

    a) Ishi kwa matumaini, uwe na uhusiano mzuri na majirani zako na uwe karibu na Mungu. b) Hakikisha kuwa chakula chako ni kizuri na kina lishe kamili. Kunywa maji ya matunda

    na maji salama kwa wingi. Jiepushe na aina mbalimbali za soda. (angalia sura ya 1)

    c) Usivute sigara, na kama unakunywa pombe, kunywa kiasi kidogo sana. d) Fanya mazoezi ya viungo. Tembea kwa miguu, endesha baiskeli au fanya shughuli

    kwenye bustani kila siku.

    Mimea na mazao ya asili yafuatayo yanasaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini. Vinafaa

    kwetu sote. Kama unaishi na VVU, tumia mimea miwili au mitatu kati ya ifuatayo. Washiriki

    wa anamed katika nchi nyingi wametoa taarifa za mafanikio mazuri katika matumizi ya kila siku

    ya unga wa majani ya mlonge na chai ya artemisia – bila kujali kama wanatumia madawa ya

    kupunguza makali ya VVU (ARV´s) au la.

    1. Allium Sativum (kitunguu saumu) Tia vitunguu saumu kisichopikwa (kibichi) kingi kiasi uwezacho katika chakula chako cha kila

    siku. Unaweza kuvikata vipande vidogovidogo na kuvichanganya katika chakula chako

    unapotaka kula.

  • Vitunguu saumu vina kiasili cha kuua bacteria (antiseptic, antibiotic, antiviral, antifungal na

    antidiabetic). Umuhimu wake kwa UKIMWI ni kwamba vitunguu saumu vimeonekana kuzuia

    jamii za ugonjwa wa mkanda wa jeshi (herpes simplex) ambao ni kirusi kinachochochea

    kuzaliana kwa VVU. Watu wanaopata maumivu ya tumbo wanapokula kiasi kikubwa cha

    vitunguu saumu wanashauriwa kula kiasi kidogo cha mafuta ya maji kama vile mafuta ya alizeti

    au samuli ambayo hufunika ukuta wa tumbo na kusambaza viini vinavyoleta maumivu. Huko

    China vitunguu saumu vinatumika kutibu vidonda vya tumbo.

    2. Aloe Vera (Msubili) Aloe ina acemannon, kiini kinachoharibu VVU kwa kubadilisha ngozi yake ya protini kiasi

    kwamba hakiwezi kujishikiza kwenye T-lymphocytes, ambayo ni sehemu muhimu kwenye

    mfumo wa kinga ya mwili. Kata jani kubwa lililokomaa sana la aloe kama ilivyoelezwa katika

    sura ya 2, kisha parua ute wake mzito kwa kijiko. Chukua kijiko 1 hadi 2 vya mezani vya ute

    mzito wa msubili. Kula kijiko 1 hadi 2 vya mezani vya ute mzito wa msubili kila siku,

    ikiwezekana kabla hujala chochote.

    3. Artemisia annua Washiriki wa anamed wanaoishi na VVU walitumia chai ya artemisia kama ifuatavyo:

    a) Wakati wa hali mbaya ya ayfa (acute phase): Mwaga maji ya moto kwenye gramu 5 (yaani

    vijiko 4 vya chai vilivyojaa sana) za majani makavu ya artemisia, acha itulie kwa dakika 15,

    chuja na unywe chai hii kwa awamu 4 ndani ya siku moja. Kutegemea hali ya mgonjwa njia hii

    inaweza kuendelea kwa muda wa wiki kadhaa au hata miezi.

    b) Baada ya hapo (chronic phase): Mwaga robo lita ya maji ya moto kwenye gramu 1,25 (yaani

    kijiko 1 cha chai) ya majani makavu ya Artemisia, acha itulie kwa angalau dakika 15, chuja na

    unywe chai hii wakati wa asubuhi. Unaweza kuendelea hivyo kwa wiki au hata miaka.

    Kama una mimea ya Artemisia kwenye bustani yako unaweza kutumia gramu 25 (acute phase)

    au gramu 6,25 (chronic phase) ya majani mabichi kila siku.

    4. Azadirachta indica (mwarobaini) Mradi wa permaculture huko Malawi na Kuluva Hospital huko Uganda vyote hutengeneza unga

    wa majani ya mwarobaini yaliyokaushwa na huwapa wagonjwa wa UKIMWI kijiko 1 hadi 2 vya

    chai kila juma.

    5. Citrus limon (Limau) Limau lina vitamin C nyingi. Kunywa maji ya limau 1 kila siku, ama katika maji vuguvugu (siyo

    ya moto ili usiharibu vitamin C) au lililokamuliwa katika chakula chako.

    6. Cymbopogon Citratus (mchaichai) Chai ya mchaichai: Chemsha kiganja 1 cha majani ya mchaichai mabichi katika lita 1 ya maji

    kwa dakika 2, acha ikolee kwa dakika 15 na kisha uichuje kwa chujio. Kunywa lita 2 kwa

    awamu kwa siku nzima. Huko Afrika kusini kwenye Moretele Sunrise Hospice, Mpho

    Sebanyoni na wenzake wamegundua kwamba wagonjwa wa UKIMWI ambao wanakunywa

    mchaichai kila siku wanapata tena hamu ya chakula, wanaongeza uzito na wanakuwa na nguvu

    tena.

    7. Lishe: Moringa Oleifera na/ au mbegu za Amaranth

  • Majani ya Moringa Oleifera (mlongelonge) na Moringa Stenopetala yanajulikana sana kwa

    kuwa yana kiasi kikubwa cha vitamin, protini na madini pamoja na amino acids. Kwa sababu hii

    kula mlongelonge kila siku, ama mbichi iliyotayarishwa kama mboga au kama unga wa majani

    (angalia sura ya 11) unaochanganywa katika chakula cha kila siku. Mlongelonge unaonesha

    mafanikio makubwa kurudisha afya ya watoto walioathirika kwa kukosa lishe. Unasaidia sana

    pia kwa wajawazito na kina mama wanaonyonyesha. Kutumia unga wa majani ya mlongelonge

    siyo tu kwamba kunajenga upya mwili, bali mara nyingi huondoa matatizo nyemelezi kama

    kuharisha na matatizo ya ngozi.

    Ongeza kijiko 1 cha chai kilichojaa cha unga wa mlongelonge kwenye chakula mara 3 kwa siku.

    Wagonwja wa UKIMWI wafanye hivi kila siku katika maisha yao.

    Amaranth ni mboga inayozalisha mbegu na majani yenye virutubisho inayofanana kabisa na

    mlonge. Mbegu zinaweza kusagwa kutengeneza unga na kuliwa kama uji pamoja na unga wa

    ulezi au mahindi, au unaweza kutumika katika kuumua mikate, keki na biskuiti.

    8. Mazao ya asili ya nyuki Asali: anamed Bukavu huko D. R. Kongo hutibu kwa chai ya artemisia na mchanganyiko wa

    asali na aloe pamoja na kitunguu saumu kwa siku 20 kila mwezi. Kila siku, changanya kijiko 1

    cha chakula cha ute mzito wa msubili na vijiko 2 vya mezani vya asali na unywe katika siku

    moja. Mara 3 kwa siku, kata kata vikonyo 3 vya kitunguu saumu na unywe kwa maji kiasi. Chai

    ya artemisia inanywewa kama kwa malaria.

    Propolis: Gundi hii ni fukizo la kiasili linalotengenezwa na nyuki katika mizinga yao, na

    imeonekana kuwa ni antibiotic, anti-fungal, antiseptic na antiviral. Changanya gramu 10 za

    propolis na ml 100 za kileo halisi cha kutengenezea dawa (98%) kwa matumizi ya ndani

    (kunywa). Tikisa mara moja kwa siku kwa muda wa siku 30. Chuja. Kipimo: kunywa matone 20

    mara 1 hadi mara 3 kwa siku.

    Kwa maelezo zaidi angalia katika kitabu cha anamed “Ukimwi na madawa ya asili”

    Jani, mbegu na vitumba vya Moringa oleifera, unga wa majani ya mlongelonge unaweza pia kunywewa kama chai.

  • SEHEMU III: MATUMIZI YA BAADHI YA MIMEA MUHIMU

    KATIKA ENEO LA TROPIKI

    SURA 7: Allium Sativum (Kitunguu saumu)

    7.1. Maelezo ya kibotania (asili ya mimea) Familia: Liliaceae

    Vitunguu saumu ni zao linalostawi mwaka hadi mwaka. Hurefuka hadi kati ya sm

    30 na 90, na shina lake huwa na vikonyo kati ya 5 na 15. Asili yake ni Ulaya na

    Afrika kaskazini, lakini jamii mpya kwa sasa zinaweza kustawi katika maeneo ya

    tropiki.

    7.2. Ulimaji

    Vitunguu saumu hupendelea udongo wenye rutuba unaopitisha maji vizuri. Pogoa kikonyo kwa

    uangalifu kutoka kwenye shina la saumu, na ukipande kwenye eneo yenye kivuli kwa kina cha

    sm 5, na umbali wa sm 15 mche hadi mche kwenye mstari wa sm 30 mstari hadi mstari. Kama

    mmea ukianza kutoa maua likate ua kusudi nguvu ya mmea iende kustawisha shina. Vuna wakati

    majani yakianza kuwa na rangi ya hudhurungi na kuanza kunyauka. Kausha vitunguu kivulini

    mahali ambapo kuna hewa nzuri inayopita, na kwa uangalifu vifute udongo na majani ya juu

    (ukifanya hivi wakati vitunguu vina unyevu, vikonyo vitaharibika). Vitunze katika chombo cha

    udongo.

    7.3. Nguvu ya uponyaji ya vitunguu saumu

    Imekuwa ikisemwa kwamba kitunguu saumu ndio mfano mzuri zaidi wa falisafa inayosema

    kwamba dawa yako ndiyo iwe chakula chako, na chakula chako kiwe dawa yako.

    Kuna hadithi juu ya nguvu za dawa za vitunguu saumu tangu mapema miaka ya 1700. Wezi

    wanne walikuwa wamegundua njia ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa tauni na walikuwa

    wanaishi maisha mazuri kwa kuiba maiti za wahanga wa tauni. Mara alipokamatwa, wale wezi

    waliokoa maisha yao kwa kufichua siri yao – walikunywa siki kingi kilichochanganywa na

    vitunguu saumu. Wachunguzi wanaamini kwamba allicin ndicho chanzo kikubwa sana (lakini

    siyo yote) cha nguvu ya uponyaji – ikiwa pia ndio chanzo cha harufu yake. Inatengenezwa

    kutokana na muungano wa alliin na mmeng’enyo wa alliinase, ambao hutokea mara kitunguu

    saumu kinaposagwa, kinapokatwa vipande vyembamba au vidogovidogo.

    Kuna madai kwamba kitunguu saumu kinaweza kutumika kutibu matatizo mengi, pamoja na

    kifaduro, maambukizi ya njia ya hewa na njia ya mkojo, matatizo ya uyeyushaji wa chakula na

    kutapakaa kwa vidudu vibaya mwilini, matatizo ya ngozi, magonjwa yanayoshika watu wengi

    kwa mara moja (epidemic) na homa. Katika vita vya kwanza vya dunia vilitumika kuzuia kuoza

    kwa vidonda na damu kupata sumu sababu ya maambukizo ya kidonda. Huko China imekuwa

    ikitumika kutibu kuharisha, kuharisha damu, kifua kikuu, diptheria, ugonjwa wa ini, ringworm,

    homa ya matumbo na trachoma. Katika nchi za magharibi vimekuwa vikitumika kutibu

    magonjwa sugu ya njia ya hewa.

    7.4. Vilivyomo:

    Allicin: Vitunguu saumu vinaposagwa, enzaimu alliinase inaibadilisha alliin na kuwa allicin.

    Allicin ni dawa ya bakteria na fangasi yenye nguvu. Alisini pia inatibu kukaza kwa mishipa ya

    moyo (Arteriosclerosis).

  • Ajoene: Pamoja na kuwa na asili ya kuua vidudu na fangasi (anti-bacterial na antifungal) pia

    inazuia kuganda kwa damu na kupunguza uwezekano wa kutokea magonjwa ya moyo

    Flavonoids: Ni vizuizi vya kupotea kwa oksijeni na inapunguza hatari za saratani, magonjwa ya

    moyo na baadhi ya magonjwa ya mishipa ya fahamu.

    7.5. Kujenga mfumo wa kinga

    Ulaji wa vitunguu saumu wa kila siku umeonyesha kupunguza uwezekano wa kutokea

    kwa:

    o Magonjwa ya moyo o Stroke (kupooza upande mmoja wa mwili) o Saratani o Shinikizo la damu o Mafua

    Vinafanya hivyo kwa:

    o Kupunguza kiasi cha “cholesterol” katika damu o Kuvunja fibrin ambayo ni moja kati ya vilivyomo katika vigandisha damu. o Kupambana na vijidudu, mba na jamii za virusi. Kwa baadhi ya magonjwa

    ‘antiobitic’ zinaweza kuwa na nguvu zaidi, lakini mara nyingi vitunguu saumu

    vina nafasi kubwa ya kutibu na vinapenya kwa urahisi zaidi katika sehemu

    iliyoambukizwa. Vitunguu saumu pia vina madhara kidogo zaidi.

    Wakati wa maambukizo ya watu wengi ya ugonjwa wa uti wa mgongo katika eneo fulani huko

    Ethiopia, wenyeji wa eneo hilo walihamasishwa kula vitunguu saumu vibichi. Kati ya wale

    waliokula hakuna aliyekufa, lakini wale wengine wengi wao walikufa. Harufu ya vitunguu

    saumu katika pumzi ya mtu inaweza kupunguzwa kwa kula tangawizi kwa njia yoyote.

    7.6. Kutayarisha tiba ya vitunguu saumu

    Kula vitunguu saumu vibichi. Hii ndiyo njia bora zaidi.

    Vipike katika chakula.

    Asali ya vitunguu saumu. Jaza chupa kubwa ya kioo kwa vikonyo vya vitunguu saumu vilivyomenywa na kukatwa katwa. Taratibu mimina asali ili ijaze nafasi zote kati ya

    vikonyo. Weka chupa hiyo kwenye joto la wastani na nyuzi 20ºC. Kati ya majuma 2 na

    4 asali itafyonza maji ya vitunguu saumu hivyo vitakuwa tepetepe na visivyo vyeupe

    tena. Vichuje. Tumia ndani ya miezi 3.

    Mchanganyiko wa kitunguu saumu na sukari. Pondaponda kijiko 1 cha chai cha vikonyo vya kitunguu saumu. Changanya na kiwango

    kile kile cha sukari au asali. Tumia haraka.

    Mafuta ya vitunguu saumu Chukua sehemu 1 ya vitunguu saumu vlivyokatwakatwa na changanya na sehemu 2 za

    mafuta ya mimea. Koroga vizuri. Kama huna fridge, tumia ndani ya wiki 1. Hatushauri

    tena kuyatunza kwa muda wa mwezi 1 kutokana na hatari ya kuingilia kwa vijidudu

    vinavyoweza kusababisha sumu ya botulism. Botulism inaweza kusababisha kupooza

    kwa mwili.

  • Saumu ya kileo (Tincture): Tumbukiza gramu 200 za vikonyo vilivyomenywa na kukatwa katwa katika lita 1 ya mvinyo au 40% ya kileo kingine kwa siku 14 katika eneo

    lililo na joto kama nyuzi 20ºC katika chupa yenye kifuniko kisichopitisha hewa. Tikisa

    chupa mara kadhaa kwa siku. Chuja vipande vya vitunguu. Dawa ya aina hii inaweza

    kutumika mwaka mzima.

    7.7. Magonjwa ambayo vitunguu saumu vinaweza kutibu:

    A. Kikohozi, mafua na koo linalouma 1. Kula kikonyo cha kitunguu saumu kutwa mara 3. 2. Kunywa kijiko 1 cha chai kilichojaa cha dawa ya asali ya vitunguu saumu kila

    baada ya masaa chache.

    3. Tumia kijiko kizima cha chai cha mchanganyiko wa sukari na vitunguu saumu kila baada ya masaa machache.

    4. Kunywa kijiko cha chai cha mafuta ya vitunguu saumu mara 6 kwa siku.

    B. Maambukizi sugu ya ‘sinus’, maumivu ya kichwa, maumivu ya kichwa ya upande mmoja yaumayo kwa vipindi.

    Mara kwa mara dondosha tone la mafuta ya vitunguu saumu katika kila tundu la pua, au

    kata ncha za vikonyo 2 vya vitunguu na uweke kikonyo 1 katika kila tundu la pua.

    (Angalizo: ni muhimu kuacha ganda la kitunguu saumu, vinginevyo kitunguu saumu

    kitaunguza ngozi nyepesi (mucose membrane) ndani ya pua).

    C. Sprains, maumivu, maambukizo ya mba, matatizo madogo madogo ya ngozi Sugua mafuta ya vitunguu saumu moja kwa moja kwenye eneo lililoathirika. Angalia

    sura ya 3

    D. Kisukari: Kula kitunguu saumu kila siku. Vitunguu saumu na vitunguu maji hupunguza sukari kwenye damu na shinikizo la damu.

    E. Shinikizo la damu: Kula vitunguu saumu vibichi, au tumia matone kati ya 5 na 25 ya vitunguu saumu ya kileo (tincture) mara kwa mara kwa siku, kiasi kinachohitajika.

    F. Malaria: Katakata kitunguu saumu vizuri. Meza kijiko 1 cha mezani cha vitunguu hivi mara 3 kwa siku, na unywe lita 2 za chai ya mchaichai kwa siku. Endeleza tiba hii kwa

    siku 5. Ikibidi ongeza tiba nyingine ya malaria.

    G. UKIMWI: Changanya vitunguu saumu vingi kiasi iwezekanavyo katika chakula chako cha kila siku ili kuimarisha mfuno wa kinga mwilini. Vitunguu saumu kwa sasa vinazidi

    kutumika kama tiba ya msaada kwa malaria na UKIMWI.

    H. Kuumwa na wadudu: Wadudu wana vidudu vya maambukizo. Maambukizo au mzio vinaweza kufuata baada

    ya kuumwa na mdudu. Sugua sehemu iliyoumwa kwa kitunguu saumu kibichi, au fungia

    kipande bapa chembamba cha kitunguu saumu kwenye sehemu iliyoumwa kwa kutumia

    plaster.

    I. Maumivu ya jino Kwa dalili ya kwanza ya maumivu ya jino (kutokana na usaha chini ya jino) weka

    kipande bapa chembamba cha kitunguu saumu kwenye sehemu iliyoathirika. Kiweke kati

    ya shavu na jino. Upande uliokatwa uwe upande wa jino, upande mwingine uwe upande

    wa shavu. Badilisha kila siku na ukiacha kwa muda wa siku kadhaa wakati wa mchana au

    usiku. Athari ya kuungua kwenye taya au ulimi itatoweka baada ya dakika chache.

    Kitunguu saumu huua bacteria wanaosababisha meno kuoza kwa sababu kinaweza

    kupenya katika nyama na katika tabaka gumu la juu la jino.

  • Pia kula vitunguu saumu vibichi mara kwa mara.

    J. Majipu yasiyo na mdomo; usaha chini ya ngozi (pamoja na maumivu na usaha kwenye vidole au kucha)

    Tumia kitunguu saumu kilichosagwa au mafuta ya kitunguu saumu (angalia sura a 2).

    Kitunguu saumu kina tabia ya kupambana na bacteria kupitia ngozi. Hata hivyo,

    unatakiwa kuwa makini, kwa sababu kitunguu saumu kina nguvu sana na kinaweza

    kuunguza ngozi na kuacha makovu ya kudumu.

    SURA 8: Artemisia annua anamed “A-3” (Sweet annie)

    8.1. Maelezo ya kibotania: Familia Asteraceae.

    Artemisia annua anamed (A-3) ni zao la mwaka 1 linaloweza kurefuka hadi meta 3. A – 3 ni

    zao la mchanganyiko wa aina za Artemisia annua, ambalo linapolinganishwa na aina zake za

    porini, yenyewe ina faida nyingi zaidi:

    Inarefuka zaidi Ina majani mengi zaidi Inastawi kwa muda mrefu zaidi kabla ya kutoa maua na kufa Ina kiwango kikubwa cha viasili vya dawa. Muhimu zaidi ni kwamba inastawi katika eneo la tropiki

    8.2. Ulimaji

    Hifadhi mbegu zikiwa kavu na zidumu kuwa kavu. Tumia kiasi chake kidogo sasa, na kilichobaki kwa kila mwezi. Kama zikitunzwa katika hali ya

    ukavu kabisa, hazitaharibika. Kiwango cha kuota kinapungua kwa 10% kwa mwaka. Mbegu na

    miche inayozaliwa ni midogo sana na dhaifu. Vinahitaji uangalizi mkubwa! Usijaribu kulima A

    – 3 mpaka wewe au mtunza bustani yako awe amejitayarisha kutoa muda wake mwingi kwa

    jambo hili, ni pamoja na Jumamosi na Jumapili.

    Tayarisha kitalu cha mbegu.

    Ni vyema kutayarisha kitalu kinachobebeka. Mfano: Ubao bapa mpana wenye ukingo wenye

    urefu wa sm 6, au tumia kingo za plastiki za ndoo. Kwa mbegu 500 unahitaji kitalu cha mbegu

    cha sm 50 × sm 50. Au trei chache ndogo ndogo. Kamwe usisahau kutoboa matundu ya kutosha

    kwenye kitako ili maji ya ziada yaweze kutoka na ili maji yaweze kunyonywa kupitia kitako.

    Weka tabaka la udongo mzuri lenye unene wa sm 3 kwenye kitako cha trei, na ufunike kwa

    tabaka nyingine la mchanga la sm 3. Mchanga huu uchemshwe kwa dakika lisizopungua 5 ili

    kuua mbegu za magugu ambazo zinaweza kuwemo. Mbegu zenyewe zina virutubisho vya

    kutosha vinavyohitajika wakati wa hatua za mwanzo za kukua.

    Hakikisha kwamba kitalu kina unyevu sana lakini hakina maji yaliyotua. Mbegu zisambazwe

    kwa usawa kwenye uso wa udongo – chujio la jikoni linaweza kusaidia mchakato huu. Usifunike

    mbegu.

    Mbegu za Artemisia huhitaji mwanga na unyevu ili kuota na kustawi.

  • Weka kitalu chini ya paa ili kuzuia mvua. Kiwe mahali ambapo kitapata mwanga wa jua moja

    kwa moja. Joto la kadri kwa uotaji ni kati ya nyuzi 20 na 30ºC lakini uotaji pia umefanikiwa

    katika joto la chini kiasi cha nyuzi 10ºC na joto kali kiasi cha nyuzi 40ºC. Kama kuna hatari

    yoyote kutoka kwa ndege, panya au kuku, funika kitalu kwa waya wa mbu.

    Kuhakikisha kwamba udongo una unyevu wakati wote, mara kwa mara weka kitalu chako katika

    trei kubwa lenye maji kidogo kwa dakika 10, ili maji yaingie kupitia kwenye kitako.

    Majani ya kwanza ya kijani hutokeza baada ya siku 3 na 7. Artemisia annua ni “dicotyledon”,

    maana yake ni kwamba inapoota majani mawili hutokea. Kwa hiyo inaweza kutofautishwa na

    miche ya majani ambayo huchipua jani moja tu. Siku 8 baada ya kupanda miche iotayo karibu

    karibu sana inatakiwa ing’olewe kwa kutumia kikoleo na ipandwe sehemu nyingine kwenye

    kitalu cha mbegu tena.

    Kuweka miche katika viroba

    Kati ya wiki 1 hadi 4 baada ya kupanda, ihamishe kwenye viroba. Unaweza kutumia vyungu vya

    kupandia, vifijo vya plastiki au vyungu vilivyotengenezwa kwa majani ya migomba. Udongo

    huu uwe na rutuba nyingi; mchanganyiko wa sehemu zilizo sawa za mboji iliyooza vizuri ( au

    udongo mweusi) na mchanga ndio bora zaidi.

    Kuhamishia shambani

    Mimea ikifikia urefu wa sm 15, kama majuma 8 baada ya kupanda, tayarisha

    shamba lako.

    Artemisia hustawi vizuri katika aina mbalimbali za udongo na hali ya hewa.

    Inastawi vizuri zaidi katika udongo wa hali ya kati au wa hali ya “alkaline” kidogo,

    lakini inavumilia udongo wenye hali ya acid kidogo.

    Zao zuri kulima kabla ya artemisia ni viazi vitamu au viazi mviringo, kwa sababu

    viazi huufanya udongo uingize hewa nzuri . Artemisia ni mmea wa jalalani, maana

    yake ni kwamba inastawi vizuri kwenye udongo unaopitisha hewa vizuri ambao una

    nitrojeni nyingi kama vile udongo kutoka kwenye rundo la mboji. Kwa hiyo lainisha udongo.

    Kama ardhi ni ngumu sana na ina udongo wa mfinyanzi, chimba kwanza shimo ambalo ni kubwa

    zaidi sana ya kipimo ulichotaka, tuseme sm 70 × sm 70 × sm 70 na ndani yake tupia vijiti na

    majani mengi (lakini siyo yatakayo katika mimea yenye “acid” kama vile conifers au mkaratusi)

    na kwenye udongo changanya mbolea iliyooza ambayo ina kinyesi cha ng’ombe au kuku. Kama

    ukipanda miche ya artemisia kwa umbali wa sm 60 toka mche hadi mche, utapata miche 30,000

    katika hekta. Kama nafasi itaruhusu panda kwa umbali wa meta 1. Kati ya miche ya artemisia

    unaweza kupanda maharage au karanga, ambavyo hurutubisha udongo, au panda mpapai,

    mahindi au mtama katika mistari kwa kubadilishana na mstari wa artemisia. Katika udongo

    wenye rutuba artemisia itakua na kufikia upande wa meta 1 na urefu wa meta 3!

    Badala ya kupanda artemisia katika shamba moja kubwa, ipande katika maeneo mbalimbali,

    kwenye jua, kwenye kivuli, karibu na mlima, kwenye ardhi tambarare, ili ugundue mwenyewe ni

    sehemu ipi inayofaa zaidi. Kwenye eneo lenye joto ni bora zaidi ardhi ikikaa na unyevu. Kama

    joto litakuwa zaidi ya nyuzi 30º wakati wote na hakuna uwezekano wa kumwagilia wakati wote,

    tengeneza kivuli. Hili linawezekana kwa kutengeneza kiunzi cha mianzi ambacho kwacho

    unaweza kustawisha mimea yenye virutubisho kama maharage yanayotambaa, Passion fruit na

  • maboga, au kwa kubadilishana katika mistari kati ya mistari ya A – 3, na mistari ya mapapai au

    mahindi.

    Kama unaishi katika eneo kame sana, pandikiza miche kwenye mistari kama sm 5 chini ya uso

    wa ardhi. Kama unaishi katika eneo ambalo mara nyingine maji hutua kwa siku kadhaa

    mfululizo, panda miche kwenye mistari juu kidogo ya usawa wa kawaida wa ardhi.

    Tumia jembe na umwagilie mara kwa mara. Ardhi lazima ikae na unyevu, hasa majuma 2 ya

    kwanza baada ya kupanda. Mmea huitikia matatizo, hasa ya ukame mkali, kwa kutoa maua kabla

    ya kukomaa. Mimea ikifikia sm 50 kwa urefu, unaweza kuiwekea mbolea ya asili, kama vile

    kinyesi cha wanyama kilichoozeshwa vizuri. Tumia mbolea za viwandani pale tu unapokuwa

    huna njia nyingine. Kwa hali hii, jaribu kutumia mbolea ya N-P-K.

    Kuzalisha artemisia annua

    Kama ilivyoelezwa hapo juu, A-3 ni chotara, kwa hiyo mbegu zake haziwezi kutumika. Zingine

    zitaota lakini mimea yake itakuwa dhaifu, ikiwa na sura mchanganyiko na upungufu wa 30% wa

    viasili vya dawa. Hii inaweza kuwa ndogo sana kiasi cha kutoweza kutibu malaria.

    Kwa hiyo artemisia lazima izalishwe kwa vipandikizi! Miezi 2 au zaidi baada ya kupanda,

    chagua mimea 3 yenye nguvu na afya zaidi. Kata matawi katika vipande vyenye urefu wa sm 2

    hadi 3 kwa kutumia wembe. Kwa njia hii, katika mmea moja unaweza kupata vipandikizi 1,000

    vyenye uwezo wa kutibu wagonjwa 5,000 na zaidi! Tengeneza vipandikizi kila mwezi. Kamwe

    usitumie mimea yenye maua, au chipukizi. Ukitumia hivyo, mimea yako itaanza kutoa maua

    mapema!

    Ondoa majani yote makubwa katika vipandikizi hivi. Tayarisha udongo na uvipande sm 1

    udongoni kwenye kitalu cha kile kilichotayarishwa kama ilivyoelezwa hapo juu lakini kikibeba

    udongo ambayo ni mchanganyiko wa mchanga na mboji iliyoozeshwa vizuri.

    Kila kipandikizi lazima kiwe na vifundo visivyopungua 2. Mkato wa chini lazima uwe chini

    kidogo tu ya kifundo ama sehemu ya kipandikizi iliyo

    udongoni itaoza. Ondoa majani yote kwenye kifundo cha chini, na kwenye kifundo cha juu.

    Ondoa jani kubwa tu, na uache kichipukizi cha pembeni salama. Vichomeke vipandikizi hivi

    udongoni ili mizizi iote kuanzia kwenye kifundo cha chini, na ili kipandikizi hicho kiwe kwenye

    ulalo wa nyuzi 30º kutoka kwenye wima. Kama hewa ni kavu sana, funika vipandikizi kwa

    plastiki ambayo umeitoboa vitundu. Lakini kama hali ya hewa ina unyevu sana, acha wazi.

    Vipandikizi lazima viwe kwenye mwanga, lakini visiwekwe kwenye jua moja kwa moja. Jambo

    zuri ni kuwa na vitalu 2 ambavyo unavihudumia kwa namna tofauti kidogo, ili kujifunza namna

    nzuri katika mazingira yako.

    Wakati watu wengine hawana tatizo kabisa katika kuzalisha kwa kutumia vipandikizi, wengine

    wanaona ni vigumu sana. Kama ni hivyo, weka vipandikizi vyako, kama ilivyoelekezwa hapo

    juu – katika maji ambayo yana matone kidogo ya mbolea ya viwandani au mbolea ya asili.

    Mbolea ya maji ya asili inaweza kutengenezwa kwa kuchanganya maji na kinyesi cha mbuzi na

    kuachwa kitulie kwa majuma 6.

  • Kutoka katika mimea inayokua unaweza kuchukua vipandikizi zaidi, na katika mimea mipya vile

    vile, unaweza kuchukua vipandikizi kwa njia hii mwaka hadi mwaka bila kupoteza kiasi

    chochote cha “artemisinin” katika mmea.

    Njia mbadala (stone-method), wakati mmea ukifikia urefu wa sm 50, ni kupinda matawi ya chini

    na kuzika sehemu zake za kati kwa udongo. Jiwe linaweza kuhitajika kuzuia lisifyatuke. Mara tu

    tawi lililozikwa likianza kuota mizizi, likate kutoka kwenye shina mama na ulipande shambani.

    Kama kawaida tumia mmea wenye afya zaidi, na mimea isiyo na maua pekee au hata vitumba.

  • 1. Changanya vikombe kumi kumi kila kimoja cha udongo, mchanga na maji. 2. Chemsha mchanganyiko huu kuua mbegu za magugu. 3. Tengenza kitalu kinachochukulika kutokana na miti na uweke vitundu vidogovidogo kwenye kitako. 4. Weka udongo kwenye kitalu. 5. Fungua mfuko wenye mbegu – ambazo ni ndogo sana!! 6. Sambaza mbegu kwa usawa. Usizifunike, na uweke kitalu kwenye sehemu yenye mwanga. Udongo

    ukianza kukauka, weka kitalu ndani ya maji.

    7. Mbegu huota kati ya siku 3 hadi 7. Zinahitaji jua la kutosha. 8. Punguza mimea.

    9. Juma 1 baada ya kupanda, weka kila mche kwenye kifuko chake. 10. Mara mmea ukifikisha urefu wa sm 10, ukaupande bustanini au shambani.

    11. Achanisha mimea kwa umbali wa mita 1.

  • 12. Kutoka katika mimea bora, chukua vipandikizi. 13. Au zalisha mmea kwa njia ya “stone – method.” 14. Mmea unahitaji kiasi cha kutosha cha mwanga wa jua, maji mengi, na mboji nyingi. 15. Mara tu unapochanua maua, vuna mmea mzima. Kata majani kuanzia kwenye ncha za matawi hadi kwenye

    kitako.

    16. Ondoa matawi yote, katakata majani katika vipande vidogovidogo, na yakaushe kwa siku 3 tu. 17. Sugua majani makavu kupitia kwenye chekecheo na mabaki uipe mifugo wako. 18. Majani ya artemisia, katika kifuko chenye maelezo, kilichozibwa, tayari kwa matumizi. Tunza sehemu

    kavu.

    Picha: Bindanda Tsobi, Kinshasa. Taarifa na hakimiliki: www.anamed