h 3183 wazo

3
Wazazi tujipange kuwapeleka watoto Sekondari Na Mroki Mroki KESHO watoto wetu wa darasa la saba katika shule mbalimbali nchini waanaza kufanya mitihani yao ya kumaliza shule ya Msingi. Mitihani hii ni kipimo tosha cha kuweza kuwapima wanafunzi hao juu ya uwelewa wao wa masuala mbalimbali waliojifunza kwa kipindi cha miaka saba waliyosoma elimu hiyo ya msingi. Baraza la Mitihani pamoja na wiozara ya elimu na Mafunzo ya ufundi nchini, hutumia matokeo ya mitihani hiyo kuweza kufanya mchujo wa wanafunzi watakao jiunga na elimu ya sekondari kwa shule za Serikali. Mwaka 2013 jumla ya watahiniwa 368,030 walifanya mitihani hiyo huku mwaka 2014 idadi hiyo ilishuka ambapo jumla ya watahiniwa 792,118 walifanya mitihani hiyo licha ya kuandikishwa 808,085. Mwaka huu huenda napo idadi hiyo ikashuka au ikapanda. Hapo zamani mtoto amalizapo shule ya msingi ilikuwa ni furaha kwa kijiji kizima kwani nguvu kazi kijijini inaongezeka na mara moja mtoto ambaye wakati huo anakuwa ni kijana wa makamo hukabidhiwa shamba la pamba alime na viongozi wakipita mitaani lazima msimu ukifika uoneshe shamba lako. Hili lilikuwa nijambo jema sana kwa wakati ule, ambapo hata shule za sekondari zilikuwa chache na kuchaguliwa kwenda Sekondari ilikuwa ni jambo la bahati na huko vijijini wananchi wengine walikuwa wakifanya sherehe kama mtoto atafaulu na kuchaguliwa kwenda Sekondari.

Upload: misty-collins

Post on 12-Dec-2015

289 views

Category:

Documents


0 download

DESCRIPTION

Wazazi tujipange kuwapeleka watoto Sekondari

TRANSCRIPT

Page 1: H  3183 WAZO

Wazazi tujipange kuwapeleka watoto Sekondari

Na Mroki MrokiKESHO watoto wetu wa darasa la saba katika shule mbalimbali nchini waanaza kufanya mitihani yao ya kumaliza shule ya Msingi.

Mitihani hii ni kipimo tosha cha kuweza kuwapima wanafunzi hao juu ya uwelewa wao wa masuala mbalimbali waliojifunza kwa kipindi cha miaka saba waliyosoma elimu hiyo ya msingi. Baraza la Mitihani pamoja na wiozara ya elimu na Mafunzo ya ufundi nchini, hutumia matokeo ya mitihani hiyo kuweza kufanya mchujo wa wanafunzi watakao jiunga na elimu ya sekondari kwa shule za Serikali.

Mwaka 2013 jumla ya watahiniwa 368,030 walifanya mitihani hiyo huku mwaka 2014 idadi hiyo ilishuka ambapo jumla ya watahiniwa 792,118 walifanya mitihani hiyo licha ya kuandikishwa 808,085. Mwaka huu huenda napo idadi hiyo ikashuka au ikapanda.

Hapo zamani mtoto amalizapo shule ya msingi ilikuwa ni furaha kwa kijiji kizima kwani nguvu kazi kijijini inaongezeka na mara moja mtoto ambaye wakati huo anakuwa ni kijana wa makamo hukabidhiwa shamba la pamba alime na viongozi wakipita mitaani lazima msimu ukifika uoneshe shamba lako.

Hili lilikuwa nijambo jema sana kwa wakati ule, ambapo hata shule za sekondari zilikuwa chache na kuchaguliwa kwenda Sekondari ilikuwa ni jambo la bahati na huko vijijini wananchi wengine walikuwa wakifanya sherehe kama mtoto atafaulu na kuchaguliwa kwenda Sekondari.

Siku hizi mambo yamebadilika shule nyingi za msingi vijijini na mijini wanafunzi huchaguliwa kwenda kidato cha kwanza na anaebaki basi huyo atakauwa na lake jambo.

Wanafunzi kesho mnaanza mitihani yenu ya kumaliza elimu ya msingi, hiyo ndo ‘LY’ ya ukweli, hebu mkafanye kile ambacho

Page 2: H  3183 WAZO

mmefundishwa pasi na kupepesa macho wala kutetemeka mikono halafu mkafaulu vyema kwenda Sekondari.

Wapo ambao hufanya udanganyifu katika vyumba vya mitihani, hilo ni kosa kubwa sana na pindi ukibainika basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yako hii ikiwa ni pamoja na kufutiwa matokeo yako au mapema tu kutolewa chumba cha mtihani.

Yanini yote hayo yakukute na kufanya miaka 7 uliyosota kupiga umande au kudamka alfajiri na mapema kugombania daladala kwenda shule iwe kazi bure? Epukeni hilo.

Aidha wazazi nao huu ni wakati muafaka wa kusugua vichwa kwa kutafuta shule bora na si bora shule ya kupeleka watoto wetu kupata elimu bora ya sekondari.

Wapo wazazi ambao wanauwezo kifedha, hivyo huwapeleka watoto kufanya mitihani katika shule tofauti tofauti lakini wapo wazazi ambao tunasubiri tuone watoto wetu watachaguliwa shule ipi ya Kata au yeyote ya serikali maana huko kuna ahueni ya ada.

Witio wangu kwenu wazazi, huu si wakati wa kubweteka na kujisahau na matokeo yake tunashtuka siku za mwisho mtoto amesha chaguliwa kwenda Sekondari lakini hatuja mafanya maandalizi hata ya daftari achilia mbali sare za shule.

Kuanzia sasa wazazi na walezi tuanze tabia ya kujiwekea akiba kwa tahadhari ili watoto wetu watakapo chaguliwa kuendelea na masomo basi tusione uzito wa kuwapeleka Sekondari.

Wapo wazazi ambao huwaambia watoto wao hasa wakike kuwa wafanye vibaya mitihani hiyo ili wasiende sekondari na badala yake waolewe. Hili si jambo jema, watoto msilikubali hata chembe hali ya sasa ya dunia ni elimu.

Chonde chonde wazazi wenzangu endapo tutaanza sasa kujiwekea akiba kidogo ya kuwapeleka watoto wetu hawa Sekondari, basi ni dhahiri kuwa hatutakosa sare za shule kwa wakati, madaftari pamoja na ada.

Page 3: H  3183 WAZO

Wapo watoto ambao hufaulu lakini wanashindwa kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na wazazi kushindwa kulipia baadhi ya gharama za masomo. Lakini ajabu ni mzazi huyo huyo unamuona kwenye vilabu vya pombe, kushona nguo mpya au hata kughamia shughuli ya ngoma kwa mtoto wake na kusahau elimu.

Mamlaka husika ni vyema nazo zikaanza kuwakumbusha wazazi na jamii kwa ujumla juu ya kuwapeleka watoto hao shule na si kufikiria kuwaoza au kuwa walima vibarua mtaani, hii haita pendeza kabisa. #Porojo hii ilichapichwa mara ya kwanza gazeti la Habarileo Septemba 8,2015 kama Wazo la Mwandishi.