haki ya kupata, kumiliki, na kutumia ardhi tanzania · sera na sheria zinazosimamia ardhi ya...

68
HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA Januari 2019 MWONGOZO WA MAFUNZO YA HAKI ZA ARDHI KWA WAZALISHAJI WADOGO CHINI YA MRADI WA UPIMAJI NA URASIMISHAJI ARDHI

Upload: others

Post on 05-Feb-2020

42 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI YA KUPATA,KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA

Januari 2019

MWONGOZO WA MAFUNZO YA HAKI ZA ARDHI KWA WAZALISHAJIWADOGO CHINI YA MRADI WA UPIMAJI NA URASIMISHAJI ARDHI

Page 2: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

Mwongozo huu umeandaliwa kwa ajili ya Mradi wa Upimaji na Umilikishaji Ardhi (LTSP) kwa Wilaya za Malinyi, Ulanga na Kilombero.

Mwongozo huu umeandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya Chama Cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) na Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), chini ya Jukwaa la Ardhi Tanzania (TALA). Mwongozo huu kwa kiasi kikubwa umejengwa kwenye mwongozo wa awali uliondaliwa na PELUM Tanzania. Mabadiliko machache yamefanywa na LEAT na TNRF ili kukidhi mahitaji ya Mradi wa Upimaji na Umilikishaji wa Ardhi (LTSP) unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania katika wilaya tatu za Malinyi, Ulanga, na Kilombero.

Page 3: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

i

DHIMA YA MWONGOZO NA SHUKRANI

Mwongozo huu wa mafunzo umeandaliwa mahususi kwa ajili ya watoa mafunzo ya haki za ardhi na wasomaji, ambao wanafanyakazi na jamii za wazalishaji wadogo. Mwongozo huu una lengo kuu la kukuza ufahamu wa jamii juu ya masuala ya ardhi, kuimarisha mfumo wa vyombo vya utoaji maamuzi juu ya ardhi na kuwawezesha wananchi hususani wazalishaji wadogo waishio vijijini kushiriki katika masuala ya ardhi ili waweze kudai, kutetea na kulinda haki zao za ardhi kwa manufaa yao wenyewe. Mwongozo wa mafunzo ya ardhi ni nyenzo muhimu sana kwa wawezeshaji, kwakuwa inajumuisha mifumo mbalimbali ambayo inawapa wananchi haki ya kumiliki ardhi na maelezo muhimu kuhusu Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu yanayohusu mfumo wa umiliki na matumizi ya ardhi nchini.

Mwongozo huu pia umebeba mada tatu zaidi juu ya masuala ya rasilimali za maji, misitu na wanyamapori. Kuongezwa kwa mada hizi kutasaidia kujenga uelewa wa jamii, hususani wazalishaji wadogo kutoka wilaya za Ulanga, Kilombero, na Malinyi ambao wapo kwenye zoezi la upimaji na umilikishaji wa ardhi.

Taasisi za LEAT na TNRF, zinapenda kutoa shukrani za dhati kwa wazalishaji wadogo wa wilaya tatu za Mradi wa LTSP: Malinyi; Ulanga; na Kilombero. Shukrani za pekee ziende kwa wananchi wa vijiji vya Mofu, Ihenga, Mpanga Kisawasawa (Kilombero), Mwaya, Isyaga, and Idunda (Ulanga), na Usangule B, Mtimbila, na Lugala (Malinyi).

Pia, shukrani za pekee ziende kwa Asasi ya PELUM Tanzania kwa kukubali sehemu kubwa ya Mwongozo huu utokane na miongozo yao mbalimbali iliyotolewa siku za nyuma kwa ajili ya wazalishaji wadogo. LEAT na TNRF ziliona si busara kupoteza muda na rasilimali kuandaa mwongozo mwingine ili hali kuna asasi marafiki zenye miongozo inayofanana na mahitaji ya wazalishaji wadogo kwenye wilaya za Malinyi, Kilombero na Ulanga.

Page 4: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

ii

YALIYOMO

DHIMA YA MWONGOZO NA SHUKRANI .................................................................................................... 2UTANGULIZI ............................................................................................................................................... 6MADA YA KWANZA .................................................................................................................................... 71 MFUMO WA UMILIKI WA ARDHI NCHINI TANZANIA ........................................................................ 7UTANGULIZI ....................................................................................................................................... 71.1 MFUMO WA UMILIKI WA ARDHI NCHINI TANZANIA ........................................................................ 71.2 UMILIKI WA ARDHI KABLA YA UKOLONI (KABLA YA MWAKA 1890) ................................................. 7

1.2.1 UMILIKI WA ARDHI WAKATI WA UKOLONI (1890 – 1961) .................................................. 71.2.2 UMILIKI WA ARDHI BAADA YA UKOLONI ........................................................................... 8

MADA YA PILI ..................................................................................................................................... 112 MAMBO YA MSINGI KATIKA SERA NA SHERIA ZA ARDHI ................................................................. 11

2.1 SERA YA TAIFA YA ARDHI YA MWAKA 1995 ........................................................................ 112.1.1 MALENGO MAKUU YA SERA YA TAIFA YA ARDHI ................................................................ 112.1.2 MALENGO MAHUSUSI YA SERA YA TAIFA YA ARDHI ............................................................ 11

2.2 MAANA YA ARDHI ............................................................................................................................. 122.3 MAKUNDI YA ARDHI ......................................................................................................................... 122.4. SHERIA ZA ARDHI ZA MWAKA 1999 ................................................................................................. 132.5. MGAWANYO WA ARDHI YA KIJIJI ...................................................................................................... 142.6 NJIA ZA UPATIKANAJI WA ARDHI ...................................................................................................... 142.7 UMILIKI WA ARDHI ........................................................................................................................... 15

2.7.1 UMILIKI WA ARDHI KWA HATI YA KUPEWA ......................................................................... 152.7.2 UMILIKI WA ARDHI KIMILA ................................................................................................ 162.7.3 HAKI YA ARDHI KWA WASIO WANAKIJIJI ............................................................................ 162.7.4 MATOKEO UHAMISHAJI WA UMILIKI WA ARDHI ............................................................... 17

2.8 DHANA YA UHAWILISHAJI NA UTWALIWAJI WA ARDHI ................................................................... 172.8.1 UHAWILISHAJI WA ARDHI .................................................................................................. 172.8.2 UTWALIWAJI WA ARDHI .................................................................................................... 182.8.3 UTHAMANISHAJI WA ARDHI .............................................................................................. 19

2.9 UTARATIBU WA KULIPA FIDIA YA ARDHI ........................................................................................... 202.10 SHERIA YA UWEKEZAJI NAMBA 26 YA MWAKA 1997 ....................................................................... 212.11 SHERIA YA WANYAMAPORI NAMBA 5 YA MWAKA 2009 .................................................................. 232.12 SHERIA YA BARABARA NAMBA 13 YA MWAKA 2007 ........................................................................ 242.13 KAMATI YA UAMUZI YA KIJIJI ............................................................................................................ 26

Page 5: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

iii

MADA YA TATU ................................................................................................................................... 283 UANDAAJI NA USIMAMIZI WA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI ................................................. 28 UTANGULIZI ..................................................................................................................................... 283.1. MAANA YA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI YA KIJIJI .................................................................. 283.2. FAIDA ZA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI .................................................................................. 283.3. MAMLAKA ZA UPANGAJI NA USIMAMIZI WA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI .......................... 283.4. HATUA ZA UANDAAJI WA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI KIJIJINI ............................................ 29

3.4.1 MAANDALIZI WILAYANI ..................................................................................................... 293.4.2 TATHMINI SHIRIKISHI YA MATUMIZI YA ARDHI YA KIJIJI ..................................................... 293.4.3 MIPAKA NA MATUMIZI YA ARDHI YA KIJIJI ......................................................................... 303.4.4 UPANGAJI WA MATUMIZI YA ARDHI YA KIJIJI ..................................................................... 323.4.5 UTAWALA WA ARDHI KIJIJINI ............................................................................................. 323.4.6 USIMAMIZI WA ARDHI NA UIMARISHAJI WA VYOMBO VYA USIMAMIZI WA ARDHI ......... 33

MADA YA NNE .................................................................................................................................... 344 HAKI YA ARDHI KWA MAKUNDI MBALIMBALI ................................................................................. 344.1. HAKI YA ARDHI KWA WANAWAKE .................................................................................................... 34

4.1.1. SHERIA ZA ARDHI ZA MWAKA 1999 .................................................................................. 344.1.3 HAKI YA ARDHI YA MWANAMKE WAKATI WA NDOA NA TALAKA ..................................... 36

4.2 MASUALA YA MSINGI YA URITHI KATIKA ARDHI ............................................................................... 394.3 HAKI ZA ARDHI KWA WAFUGAJI ...................................................................................................... 434.4 HAKI ZA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI. ................................................................................. 44

MADA YA TANO .................................................................................................................................. 455 MIGOGORO YA ARDHI NCHINI TANZANIA ....................................................................................... 455.1 MAANA YA MIGOGORO YA ARDHI ................................................................................................... 45

5.1.1 AINA ZA MIGOGORO YA ARDHI ......................................................................................... 455.2 VYOMBO VYA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI ......................................................................... 47

5.2.1 BARAZA LA ARDHI LA KIJIJI ................................................................................................ 475.1.2 BARAZA LA KATA ................................................................................................................ 495.1.3 BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA LA WILAYA ....................................................................... 505.1.4 MAHAKAMA KUU .............................................................................................................. 525.1.5 MAHAKAMA YA RUFANI .................................................................................................... 53

MADA YA SITA .................................................................................................................................... 536 MFUMO WA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI TANZANIA ................................................ 536.1 MGAWANYO WA SERIKALI ............................................................................................................... 546.2 MAKUNDI MAKUU SERIKALI ZA MITAA ........................................................................................... 546.3 UHUSIANO KATI YA SERIKALI KUU NA SERIKALI ZA MITAA .............................................................. 546.4 NGAZI ZA UTAWALA ZA SERIKALI KUU .............................................................................................. 54

Page 6: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

iv

6.5 NGAZI ZA UTAWALA SERIKALI ZA MITAA ........................................................................................ 556.6 MUUNDO WA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI KATIKA NGAZI YA KIJIJI .......................... 56

MADA YA SABA .................................................................................................................................. 627. SERA NA SHERIA ZINAZOHUSU USIMAMIZI WA MISITU ......................................................................... 62UTANGULIZI ........................................................................................................................................ 627.1. SERA YA TAIFA YA MISITU YA MWAKA 1998 ..................................................................................... 627.2. SHERIA YA MISITU NAMBA 14 YA MWAKA 2002 ............................................................................. 62

7.2.1. HAKI NA WAJIBU WA WADAU MBALIMBALI ..................................................................... 63

MADA YA NANE ................................................................................................................................. 678. SHERIA ZA WANYAMAPORI .................................................................................................................... 67UTANGULIZI ....................................................................................................................................... 67USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA SEKTA YA WANYAMAPORI .................................................................... 678.1 SERA NA SHERIA MBALIMBALI ZA WANYAMAPORI ............................................................................. 69

8.1.1. SERA YA WANYAMAPORI 2007 .............................................................................................. 698.1.2. SHERIA YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI ............................................................................ 698.1.2.1. MAKATAZO MBALIMBALI CHINI YA SHERIA YA UHIFADHI WANYAMAPORI ................. 708.1.2.2. CHANGAMOTO KATIKA UTUNZAJI NA UHIFADHI WA WANYAMAPORI ........................ 70

8.2 MAKOSA NA ADHABU KATIKA SHERIA ZA WANYAMAPORI ............................................................ 72

MADA YA TISA .................................................................................................................................... 749.1 SHERIA YA RASIMALI ZA MAJI 2007 .................................................................................................. 749.2 MAANA YA MAJI NA UMILIKI WA RASILIMALI MAJI ........................................................................ 749.3 VIPAUMBELE KATIKA UGAWAJI WA MAJI .................................................................................... 759.4 JUKUMU LA KUTUNZA RASILIMALI MAJI . .................................................................................... 759.5 USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA MAJI ........................................................................................... 75

9.5.1 MABONDE YA MAJI NCHINI ................................................................................................. 769.5.2 MAJUKUMU YA BODI ZA MABONDE ................................................................................... 769.5.3 KIBALI CHA KUTUMIA MAJI .................................................................................................. 769.5.4 VIBALI VYA KUTIRIRISHA MAJI MACHAFU .......................................................................... 77

Page 7: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

v

UTANGULIZI

Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi za maliasili na malikale ikiwemo ardhi, maji, misitu na wanyamapori. Kwa mujibu wa sheria za nchi, utajiri huu wa rasilimali humilikiwa na wananchi wote na Serikali ina dhamana ya kutunza na kuhifadhi maliasili hizi kwa niaba ya wananchi.

Tanzania ina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 945,000. Kati ya hizo, takribani hekta milioni 48[1] ni misitu. Miongoni mwa hizo kiasi cha hekta milioni 13[2] ni hifadhi za maji na ardhi na uhaianuai[3]. Serikali ina dhamana ya kusimamia na kuhifadhi maliasili za wanyamapori ikiwa ni pamoja na kusimamia Hifadhi za Taifa, Hifadhi ya Ngorongoro, Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu. Mpaka sasa Serikali inasimamia Hifadhi za Taifa 16, Mapori ya Akiba 38, na Mapori Tengefu 43.

Vilevile, Tanzania imejaliwa kuwa na rasilimali za maji nyingi sana. Kuna bahari, mito, maziwa, chemichemi na vyanzo vingine vingi vya maji. Rasilimali hizi zisiposimamiwa vizuri, wananchi huteseka sana kwani maji ni uhai na hutumika kwa shughuli kuu za uzalishaji mali na hayana mbadala.

Hivyo basi Mwongozo huu utawawezesha wananchi kuelewa usimamizi wa ardhi na maliasili zinazoambatana na ardhi. Ni matumaini yetu kuwa jamii na hasa wananchi wa kawaida katika wilaya za Malinyi, Ulanga na Kilombero watashiriki kikamilifu katika kulinda haki zao za ardhi na usimamizi wa maliasili zingine za nchi yao hasa wanyamapori, misitu na maji.

1 Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), 2013.2 Wakala Wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), 20133 Wakala Wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), 2013

Page 8: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 1

1. MFUMO WA UMILIKI WA ARDHI NCHINI TANZANIA

UtanguliziTanzania kama nchi zingine nyingi za Afrika imepitia mabadiliko mbalimbali katika mfumo wa umiliki wa ardhi. Mada hii inachambua mfumo wa umiliki wa ardhi katika vipindi vyote ambavyo Tanzania imepitia na kubainisha nafasi na haki za wananchi hususan wazalishaji wadogo katika kupata, kutumia, kumiliki na kusimamia ardhi kwa mujibu wa Sera na Sheria za ardhi katika vipindi vyote.

1.1 MFUMO WA UMILIKI WA ARDHI NCHINI TANZANIA Mfumo wa umiliki wa ardhi nchini Tanzania umepitia katika vipindi vitatu. Vipindi hivyo ni

kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni (baada ya kupata uhuru). Mabadiliko yaliyotokea katika kila kipindi yamekuwa na athari katika haki za wananchi kupata, kutumia na kumiliki ardhi kwa namna mbalimbali.

1.2 UMILIKI WA ARDHI KABLA YA UKOLONI (KABLA YA MWAKA 1890) Kabla ya ukoloni ardhi ilimilikiwa kimila kwa desturi na taratibu za koo na makabila

mbalimbali yanayohusika. Ardhi ilikuwa ni kwa matumizi ya kiuzalishaji na wala si kuihodhi au kujilimbikizia. Wananchi walikuwa na sauti ya mwisho katika umiliki, matumizi na ugawaji wa ardhi kwa taratibu zao za kimila. Viongozi wa kimila na kijadi walikuwa wasimamizi wa ardhi na wasuluhishi wa migogoro pale ilipojitokeza.

1.2.1 UMILIKI WA ARDHI WAKATI WA UKOLONI (1890 – 1961) Tanganyika (Tanzania) ilitawaliwa na wakoloni wa Kijerumani na Kiingereza ambao

waliweka mifumo ya umiliki wa ardhi kulingana na mahitaji yao ya wakati huo hasa kwa kuvamia na kumiliki dola pamoja na uchumi.

i. Wakoloni wa Kijerumani 1890 – 1918 Umiliki wa ardhi wakati wa Utawala wa Kijerumani ulisimamiwa na amri ya

tamko (decrees) ya mwaka 1895 iliyotamka kuwa ardhi yote ya Tanganyika iwe imekaliwa au kutokaliwa ni mali ya mfalme wa Ujerumani, hivyo kupata na kutumia ardhi ilikuwa sharti kupata ridhaa ya mfalme. Kwa nadra sana, ardhi iliyomilikiwa na machifu na baadhi ya watu binafsi iliachwa chini ya umiliki wao kwa makubaliano maalumu kati ya wazawa na serikali ya kikoloni.

ii. Wakoloni wa Kiingereza 1919 – 1961 Waingereza walitunga Sheria ya Ardhi Namba 3 ya mwaka 1923 iliyotamka

kuwa ardhi yote ni mali ya umma, chini ya usimamizi wa Gavana kwa niaba ya Malkia wa Uingereza. Sheria hii ilitambua mifumo miwili ya kumiliki ardhi, yaani mfumo wa kimila wa kufikirika (deemed right of occupancy) na mfumo kwa njia ya Hati ya kupewa (granted right of occupancy). Umiliki wa kimila haukuwa na ukomo wakati, umiliki wa hati ya kupewa ulikuwa na ukomo wa miaka 33, 66 na 99. Hata hivyo umiliki wa kimila ulikuwa wa hadhi ya chini ukilinganishwa na ule umiliki wa Hati yakupewa na hivyo kuwafanya wananchi kupoteza sauti yao katika umiliki wa ardhi. Hivyo, umiliki wa Hati ya kupewa ulikuwa wenye nguvu daima na wa uhakika kuliko ule wa kimila.

MADA YA KWANZA

Page 9: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 2

1.2.2 UMILIKI WA ARDHI BAADA YA UKOLONIi. Kuanzia mwaka 1961 – 1980 Mara baada ya uhuru, yalitokea mabadiliko mengi ambayo hata hivyo

hayakubadilisha misingi ya Sheria ya Ardhi Namba 3 ya mwaka 1923. Hivyo, ardhi iliendelea kuwa ni mali ya umma chini ya usimamizi wa Rais kama mdhamini tu kwa niaba ya wananchi.

Katika kipindi cha miaka ya 1960 ardhi ya vijiji ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Makazi ya Vijiji Namba 27 ya mwaka 1965, na kufuatiwa na Azimio la Arusha la mwaka 1967 ambalo liliweka misingi mikuu ya utawala na usimamizi wa mali mikononi mwa umma kwa maslahi ya Taifa. Sheria ya Utwaaji Ardhi Namba 47 ya mwaka 1967 ilitungwa ili kumpa Rais mamlaka ya kutwaa ardhi kwa maslahi na manufaa ya umma.

Katika kipindi cha miaka ya 1970 hadi 1980 serikali ilitekeleza mpango wa Operesheni Vijiji ambao ulihalalishwa na Sheria ya Ardhi zya Vijiji (Mipango na Matumizi) Namba 14 ya mwaka 1973. Suala la usajili na usimamizi wa vijiji hivi ulikuwa kwa mujibu wa Sheria ya Vijiji na Vijiji vya Ujamaa (Usajili, Uundwaji na Usimamizi) Namba 21 ya mwaka 1975.

Wakati kwa upande mmoja, mabadiliko haya yaliweza kutimiza malengo ya maendeleo ya kitaifa kupitia sera ya ujamaa na kujitegemea, kwa upande mwingine yaliathiri haki za wanavijiji katika ardhi yao. Baadhi waliondolewa kupisha uanzishwaji mashamba makubwa ya chakula, ardhi za hifadhi za wanyamapori na ranchi za taifa na wengine kuhamishwa kutoka kwenye maeneo yao ya asili kutokana na operesheni vijiji. Athari zilizojitokeza wakati huo, zimeendelea kusababisha migogoro ya ardhi kwenye baadhi ya maeneo hadi sasa.

ANGALIZO: Kifungu cha 3 cha Sheria Namba 22 ya mwaka 1992 kinatanabaisha kwamba haki zote za kukalia au kutumia ardhi kwa mujibu wa taratibu zozote za kimila ambazo zilikuwa zinashikiliwa au kudaiwa kushikiliwa na mtu yeyote kwenye kijiji chochote kabla ya Operesheni vijiji zinafutwa. Hivyo, sheria hii ilifuta maeneo yote ya MAHAME na watu wote waliochukuliwa maeneo yao kwa kupisha operesheni ya vijiji hawana haki ya kudai fidia wala kurudi katika maeneo yao ya awali hata kama kulikuwa na ukiukwaji wa sheria wakati wa Oparesheni vijiji.

ii. Kipindi cha miaka ya 1990 – 2000 Kutokana na kukithiri kwa migogoro ya ardhi, na mahakama kuelemewa na

mashauri ya ardhi na mwingiliano wa vyombo vya usimamizi wa ardhi, mwaka 1991 iliundwa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Masuala ya Ardhi ili kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mfumo mpya wa umiliki wa ardhi. Baada ya kukusanya maoni hayo,

Page 10: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 3

Tume ilitoa mapendekezo mengi kama ifuatavyo:• Kuingiza suala la ardhi katika Katiba ya Nchi ili kulipa ulinzi wa uhakika zaidi; • Kuweka dhamana ya usimamizi katika vyombo vyenye uwakilishi mpana wa

wananchi;• Kuunda mfumo shirikishi wa usuluhishi na utatuzi wa migogoro ya ardhi

kuanzia ngazi ya kijiji, utakaowahusisha moja kwa moja wananchi wenyewe; na

• Kutungwa kwa Sera na Sheria mpya za Ardhi.

Mapendekezo hayo, yalipelekea kutungwa kwa Sera ya Ardhi ya Taifa ya mwaka 1995 ambayo pia ilifanyiwa marekebisho mwaka 1997 ambayo ilipelekea kutungwa kwa Sheria za Ardhi Na. 4 & Na. 5 zote za mwaka 1999.

Baada ya muda mfupi tu wa kutungwa kwa Sheria Na. 4 na 5 za Ardhi za mwaka 1999 na kuanza kutumika mwaka 2001, Taasisi za kifedha hususani benki zilibaki na dukuduku kwamba sheria hazikukidhi matakwa ya kibiashara ya kibenki na hasa kuruhusu ardhi kutumika kama rehani ya mikopo ya kibenki. Miaka miwili baadaye, yaani 2003, benki zilifanikiwa kuishawishi serikali kufanya marekebisho katika Sheria ya Ardhi Namba 4 ambayo pamoja na mambo mengine;

• Yameipa thamani ardhi tupu (yaani ardhi ambayo haijafanyiwa maendelezo)• Yameruhusu ardhi tupu kuuzwa na kununuliwa kama bidhaa nyinginezo

kwa masharti nafuu• Yameruhusu ardhi tupu kutumika kama rehani ya mikopo ya kibenki• Yameruhusu pia mkopeshaji kuchukua ardhi iliyowekwa rehani kwa

masharti nafuu pale mdaiwa anaposhindwa kurejesha mkopo kwa wakati na kupunguza muda wa kutoa ilani kwa mdaiwa kutoka siku tisini (90) hadi thelathini (30).

• Marekebisho haya pia yanaruhusu mkopeshaji kujiuzia mwenyewe ardhi iliyowekwa rehani pindi mdaiwa anaposhindwa kurejesha mkopo kwa sharti tu kwamba ajiridhishe kuwa kwa kufanya hivyo maslahi yake kama mkopeshaji yatakuwa yamelindwa kuliko kufanya vinginevyo.

HITIMISHO Katika mada hii, tumeona jinsi mfumo wa umiliki wa ardhi ulivyopitia katika vipindi mbalimbali vya mabadiliko na misukumo mbalimbali iliyosababisha mabadiliko hayo kufanyika. Hata hivyo, suala la msingi lililojitokeza katika mada nzima ni kuwa mabadiliko mengi yaliyofanyika, yalitikisa na kuathiri mfumo wa kimila wa umiliki wa ardhi kwa kumpa hadhi hafifu na kuondoa uhakika wa milki kwa mwananchi wa kawaida aliokuwa nao kabla ya ukoloni. Tumeona pia kuwa mfumo wamilki ya ardhi baada ya uhuru ulirithi misingi ileile ya ukoloni na hivyo husababisha matatizo makubwa katika upatikanaji wa haki za ardhi kwa wanyonge kwani udhaifu wake uliruhusu migogoro baina ya watumiaji, mianya ya rushwa, utendaji mbovu na mwingiliano wa maslahi. Hata dhana mbalimbali zilizoingizwa katika sera na sheria ziliendeleza udhaifu huo.

Page 11: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 4

2 MAMBO YA MSINGI KATIKA SERA NA SHERIA ZA ARDHI

Utangulizi: Sheria za Ardhi Namba 4 na 5 za mwaka 1999, zimetungwa kutokana na sera ya ardhi ya Taifa mwaka 1995 ikilenga kulinda rasilimali ya ardhi katika kuwezesha wananchi kupata, kutumia na kumiliki ardhi nchini. Mada hii, inaeleza jinsi sheria hizi mbili zinazosimamia ardhi na namna zinavyotumika kulinda maslahi ya wananchi katika masuala yote yananyohusu haki za watuamiaji wa ardhi.

2.1 SERA YA TAIFA YA ARDHI YA MWAKA 1995Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 ni mwongozo wa kitaifa kuhusu mfumo wa umiliki, matumizi na usimamizi wa ardhi. Sera hii imeweka kanuni za msingi za umiliki, matumizi na usimamizi wa ardhi ambazo ni pamoja na; kutambua kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali ya umma na Rais ndiye mdhamini kwa niaba ya raia wote; kuwezesha kupatikana kwa ardhi na kugawiwa haki kwa raia wote pamoja na kushiriki katika kutoa maamuzi ya umiliki au matumizi ardhi kwa manufaa ya kiuzalishaji na yanayozingatia misingi ya maendeleo endelevu.

Kanuni nyingine ni, kuhakikisha haki zote zilizomo katika ardhi na umilikaji wa ardhi wa muda mrefu zinatambuliwa na kulindwa kisheria; kulipa fidia kamili, ya haki na ya wakati kwa mtu yeyote ambaye ardhi yake itatwaliwa na kuanzisha mfumo huru unaofanya kazi kwa haraka na wa haki katika kuamua migogoro ya ardhi.

Pia, Sera ya Ardhi imesisitiza juu ya haki ya kila mwanamke kupata, kumiliki, kutumia na kufanya shughuli yoyote kwenye ardhi ambayo itakuwa sawasawa kwa kiwango kilekile kama atakayokuwa nayo mwanaume.

2.1.1 MALENGO MAKUU YA SERA YA TAIFA YA ARDHIi. Kukuza na kuhakikisha mfumo wa uhakika wa umiliki wa ardhi,ii. Kuhimiza matumizi bora ya rasilimali za ardhi naiii. Kuwezesha kuwepo kwa maendeleo ya jamii na uchumi bila kuathiri mazingira.

2.1.2 MALENGO MAHUSUSI YA SERA YATAIFA YA ARDHIi. Kubuni mfumo ulio wazi wa kuwezesha raia wote kuwa na haki sawa katika

kupata ardhi;ii. Kuhakikisha kuwa milki za ardhi zilizopo hasa za kimila ambazo ndizo

zinazotumika na watu wengi nchini, zinatambuliwa na kulindwa na sheria;iii. Kuweka kikomo cha eneo la ardhi linaloweza kumilikishwa kwa mmilikaji mmoja

ili kuepusha watu kujilimbikizia ardhi au kuwa na ardhi kubwa kuliko uwezo wao wa kuiendeleza;

iv. Kuhakikisha kuwa kunakuwepo na matumizi bora ya ardhi ili kuongeza uzalishaji na kuleta maendeleo ya haraka ya kijamii na kiuchumi;

v. Kurekebisha na kurahisisha mifumo iliyopo ya usimamizi wa ardhi na kuboresha ufanisi wa mifumo ya upatikanaji wa ardhi;

vi. Kuboresha mpangilio wa uhusiano baina ya taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya ardhi au utatuzi wa migogoro ya ardhi ili taasisi hizo zifanye kazi kwa uwazi zaidi;

MADA YA PILI

Page 12: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 5

vii. Kukuza uwezo wa kutunza kumbukumbu za milki za ardhi na kuboresha mawasiliano kati ya taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya ardhi;

viii. Kulinda rasilimali za ardhi ili ziweze kutumika na kuleta maendeleo nchini.

2.2 MAANA YA ARDHIArdhi kwa mujibu wa kifungu cha 2 cha Sheria zote mbili za Ardhi za mwaka 1999, ni ile inayojumuisha vitu vyote vilivyo juu na chini ya uso wa nchi vikiwemo majengo, uoto wa asili na maendelezo yote yaliyofanywa isipokuwa haihusishi madini na mafuta.

2.3 MAKUNDI YA ARDHISheria za Ardhi za mwaka 1999 zimeigawa ardhi ya Tanzania katika makundi makuu matatu, yaani; Ardhi ya Kawaida, Ardhi ya Hifadhi na Ardhi ya Kijiji.

i. Ardhi ya kawaida Kwa mujibu wa kifungu cha 2 cha Sheria za Ardhi (Na 4 & 5) za mwaka 1999. Ardhi ya kawaida ni ardhi yote ya umma ambayo siyo ardhi ya hifadhi wala ardhi ya kijiji. Hata hivyo, ardhi ya jumla inajumuisha pia ardhi ya kijiji ambayo, haikaliwi wala kutumiwa na wanavijiji. Kamishna wa ardhi ndiye msimamizi wa kundi hili la ardhi kwa mujibu wa sheria ya Ardhi.

ii. Ardhi ya Hifadhi Kwa mujibu wa kifungu cha 2 na 6 katika Sheria ( Na. 4 & 5) za Ardhi za mwaka 1999 ni ardhi iliyotengwa kwa shughuli maalumu kama vile hifadhi ya misitu, mikoko na matumbawe, ardhi oevu, visiwa vilivyopo karibu na fukwe za bahari au maziwa, ardhi inayotumiwa kutupa taka zenye sumu, ardhi yote iliyo ndani ya meta 60 kutoka ukingo wa mto au ziwa, ardhi yenye miteremko mikali, hifadhi za taifa, vyanzo vya maji, barabara, ardhi yenye madhara n.k. Ardhi ya aina hii iko chini ya usimamizi wa mamlaka, na sheria mbalimbali kulingana na aina ya ardhi husika. Mfano, sheria ya Wanyama Pori, Sheria ya Hifadhi ya Taifa, Sheria ya Hifadhi za Bahari na maeneo Tengefu.

iii. Ardhi ya KijijiKwa mujibu wa kifungu cha 2 cha Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 na kifungu cha 7 katika Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5 ya mwaka 1999, ardhi ya Kijiji ni ardhi ambayo ipo ndani ya mipaka ya kijiji. Ardhi ya kijiji inajumuisha ardhi yote iliyomo ndani ya mipaka ya vijiji vilivyosajiliwa, ambapo Halmashauri za Vijiji na Mikutano ya Vijiji imepewa mamlaka ya kusimamia. Sheria ya Ardhi ya Kijiji Na 5 ya mwaka 1999 inatoa maelekezo ya namna usimamizi unavyotakiwa kufanyika

Hata hivyo, watu binafsi, taasisi au makampuni wanaweza kumiliki ardhi ndani ya kijiji kwa hati ya kupewa. Hata kama ardhi hiyo imo ndani ya kijiji itakuwa si ardhi ya kijiji.

2.4. SHERIA ZA ARDHI ZA MWAKA 1999Sheria ya Ardhi Namba 4 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5 zote za mwaka 1999 zilizoanza kutumika rasmi tarehe 1 Mei, 2001. Sheria hizi pamoja na kuigawa ardhi ya Tanzania katika makundi makuu matatu kama yalivyoelezewa hapo juu zinaonesha na kuelezea kila kundi la ardhi na utaratibu wake wa usimamizi na mamlaka husika. Msimamizi na Mtendaji mkuu wa masuala ya ardhi ni Kamishna wa Ardhi.

Page 13: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 6

Aidha, sheria zimeendelea kutambua aina mbili za umiliki wa ardhi ya Tanzania, yaani umiliki wa Kimila na wa Hati ya kupewa ingawa pia zimeruhusu kuanzishwa kwa Haki ya hatimiliki za kimila kama nyaraka. Uanzishwaji wa hati ya hatimiliki za kimila unaonekana kuwa ni hatua ya kimaendeleo inayoweza kusaidia kuwepo kwa uhakika wa umiliki ywa ardhi kwa wananchi wa kawaida ingawa kiutendaji, bado hati hizo zinatolewa kwa kasi ndogo sana.

Lakini pia, mtazamo wa kutoa hati hizo unaelemea zaidi kwenye kuifanya ardhi kuwa mtaji zaidi kuliko nyenzo ya uzalishaji mali na uhakika wa maisha kwa mmiliki wa kawaida. Ufafanuzi zaidi wa makundi hayo, aina za umiliki na masuala mengine ya msingi katika sheria za ardhi, unafanywa katika mada nyingine zinazofuata.

2.5. MGAWANYO WA ARDHI YA KIJIJIKwa mujibu wa sheria ya Ardhi ya kijiji inaelekeza Halmashauri za vijiji kugawa ardhi katika aina kuu tatu yaani; ardhi ya jumuiya, ardhi ya mtu binafsi/ familia na ardhi ya akiba ya kijiji.

i. Ardhi ya JumuiyaHii ni ardhi ambayo imetengwa na inatumiwa kwa shughuli za jumuiya au umma na kikundi katika kijiji au wanakijiji wote kwa makubaliano na Halmashauri ya Kijiji. Ardhi haitaruhusiwa kuuzwa, kugawiwa wala kutumiwa na mtu binafsi. Ardhi hii inajumuisha misitu, maeneo ya malisho au maeneo mengine yenye maliasili yanayosimamiwa na vikundi vya watu, ardhi ya jumuiya, pia inajulikana kama ardhi ya kijiji ya jumuiya.

ii. Ardhi ya mtu binafsi au familia Hii ni ardhi ambayo humilikiwa na kutumiwa na mtu binafsi, familia au kikundi cha watu kwa njia ya kimila. Ardhi hii inatumiwa pia kwa ujenzi wa nyumba, kilimo au biashara na watu binafsi au familia moja moja.

iii. Ardhi ya Akiba ya kijijiHii ni ardhi ambayo inaweza kutolewa kwa mwanakijiji binafsi au kikundi/jumuiya ya wanakijiji kulingana na matumizi kwa njia ya kugawiwa na Halmashauri ya Kijiji. Ardhi hii pia huifadhiwa kwa malengo maalum au matumizi ya baadaye ya watu binafsi au jumuiya.Halmashauri za vijiji hazina budi kuzingatia mambo haya muhimu kwa ajili ya kusimamia ardhi ya kijiji. Ardhi ya kijiji inatakiwa kutumika kwa hali ambayo itadumisha maisha endelevu ya watu na matumizi ya rasilimali hii.

ANGALIZO: Sheria za Serikali za Mitaa (Tawala za Wilaya) ya mwaka 1982 inazipa serikali za Kijiji mamlaka ya kisheria ya kutumia, kusimamia na kumiliki ardhi na mali nyingine. Aidha, inaipa mamlaka serikali ya kijiji juu ya usimamizi wa ardhi ya kijiji. Sheria hii inazipa serikali za vijiji mamlaka makubwa ya kufanya mikataba na makampuni yanayosaidia maisha na ustawi wa wanakijiji na taifa kwa ujumla.

Page 14: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 7

2.6 NJIA ZA UPATIKANAJI WA ARDHIKuna njia mbalimbali za upatikanaji wa ardhi nchini Tanzania kama zilivyoelezewa hapa chini:

a) KurithiMtu anaweza kupata ardhi kwa kurithishwa na wazazi wake au ndugu wa karibu na kuwa mmiliki halali wa ardhi hiyo iwe ni kwa mila au kwa hati.

b) Kununua Marekebisho ya Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 yaliyofanywa na Sheria Namba 2 ya mwaka 2004 yameipa ardhi tupu thamani ya soko na kuruhusu biashara ya ardhi. Hivyo mtu anaweza kupata ardhi kwa njia ya kununua kutoka kwa mmiliki mwingine.

c) Kupewa zawadiArdhi inaweza kutolewa kutoka kwa mmiliki wa ardhi kwenda kwa mtu mwingine kama zawadi kutokana na uhusiano uliopo kati yao. Mtoa zawadi anakuwa amehamisha haki yake ya umiliki kutoka kwenye ardhi aliyoitoa kama zawadi.

d) Kugawiwa na serikaliHalmashauri ya Kijiji kwa idhini ya mkutano mkuu wa kijiji au Kamishna wa Ardhi ndio wenye mamlaka ya kugawa ardhi kwa waombaji. Hivyo mtu, kundi la watu au taasisi yoyote inayohitaji kupata ardhi itatuma maombi kwa Halmashauri ya Kijiji au kwa Kamishna wa Ardhi kulingana na kundi la ardhi anayoomba.

(e) Kufyeka au kusafisha eneo lililo waziPia, mtu anaweza kupata ardhi kwa kusafisha eneo au pori lililowazi ambalo halijawahi kukaliwa au kumilikiwa na mtu yeyote kwa kipindi cha muda mrefu.

2.7 UMILIKI WA ARDHIKwa mujibu wa Sheria za Ardhi za mwaka 1999 umiliki wa ardhi upo wa aina mbili;

2.7.1 UMILIKI WA ARDHI KWA HATI YA KUPEWAHuu ni utaratibu uliotokana na Sheria ya Ardhi Namba 3 ya mwaka 1923 ya Waingereza, ambayo ilitamka kwamba ardhi yote ni mali ya umma na hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kufanya chochote juu ya ardhi hiyo bila idhini ya serikali. Utaratibu huu unatumika katika kundi la ardhi ya kawaida kwa ukomo wa umiliki wa hati ya miaka 33, 66 au 99 yenye hadhi ya upangaji.

Utaratibu wa kuandaa Hati ya kupewaKwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 pamoja na kanuni zake za mwaka 2001, mwombaji anatakiwa kuwasilisha maombi yake ya kumiliki ardhi katika fomu Namba 19 kwa Kamishna wa Ardhi kupitia kwa maofisa wateule wa ardhi waliopo Wilayani au Manispaa husika. Fomu hii huambatana na viambatanisho mbalimbali kama vile picha za mwombaji na kama ardhi hiyo imepimwa basi ramani yake na ya mipango miji. Kama ni eneo ambalo halijapimwa ni sharti lifanyiwe upimaji kulingana na taratibu za ramani kuu ya mipango miji zilizoainishwa katika eneo husika ambalo mwombaji anaomba kupatiwa hati. Mwombaji atapewa hati

Page 15: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 8

ya malipo inayoeleza gharama zinazotakiwa kulipwa na mwombaji. Na baada ya malipo hayo mchakato wa kuandaliwa hati hufanyika kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazo simamia ardhi.

2.7.2 UMILIKI WA ARDHI KIMILA.Huu ni utaratibu wa umiliki wa ardhi kwa kufuata taratibu za mila na desturi za jamii husika. Hivyo mtu mmoja, familia au kikundi cha watu wana haki ya kupata na kumiliki ardhi kwa njia ya kimila. Umiliki wa kimila unatambulika hata bila hati lakini mmiliki anaweza kupata Hati ya Hakimiliki ya Kimila kutoka Halmashauri ya Kijiji. Wafuatao wanaweza pia kuaomba umiliki wa ardhi ya kijiji:

i. Mwanamke, au mwanaume, yeyote ambaye ni mwanakijiji mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea;

ii. Mtu yeyote au familia yoyote au hata kikundi chochote cha watu kinachotambulika chini ya sheria ya mila au ambacho kimejiunga kama chama cha Ushirika;

iii. Mtu yeyote ambaye ameolewa na kuachika au ameondoka kijijini hapo kwa zaidi ya miaka miwili, na mwanandoa mwenzake aliyekuwa mwanakijiji kabla ya kufunga ndoa na wote ni raia wa Tanzania, anaweza kuomba haki ya kumiliki ardhi kijijini. Hii inaonyesha kuwepo kwa uwezekano wa mwanamke kupata ardhi katika kijiji chake na hata katika kijiji ambacho mumewe alikuwa Mwanakijiji kabla ya ndoa yao;

2.7.3 HAKI YA ARDHI KWA WASIO WANAKIJIJIVifungu vya 31, 32 na 33 vya Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999 vimeweka utaratibu kwa raia wasio wanakijiji kumiliki na kutumia ardhi ya vijiji kimila kama ifuatavyo:

(i) Mwombaji atawasilisha maombi yake kwenye Halmashauri ya Kijiji juu ya kiasi cha ardhi anachoomba na matumizi yake;

(ii) Halmashauri ya Kijiji itajadili na kukubali au kukataa kulingana na upatikanaji wa ardhi na kuzingatia mahitaji ya ardhi kwa wanakijiji. Endapo Halmashauri ya Kijiji itayakubali maombi itawasilisha mapendekezo yake kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji;

(iii) Mkutano Mkuu wa Kijiji utajadili maombi ya wahusika kwa kuzingatia mapendekezo ya Halmashauri ya Kijiji na kisha kuridhia au kukataa maombi hayo;

(iv) Endapo mwombaji atakubaliwa maombi yake, Halmashauri ya Kijiji itamwandikia rasmi kumjulisha na kumgawia ardhi husika;

(v) Mwombaji atawajibika kulipia ushuru na kodi kulingana na viwango vilivyowekwa katika kijiji husika;

(vi) Raia asiye mwanakijiji ana haki ya kununua ardhi kwa mwanakijiji yoyote, kuimiliki kimila na kuitumia kulingana na matumizi yaliyopangwa katika kijiji husika. Hata hivyo mauziano hayo sharti yaidhinishwe na Halmashauri ya Kijiji.

Page 16: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 9

2.7.4 MATOKEO UHAMISHAJI WA UMILIKI WA ARDHIMtu yeyote anayeuza ardhi anahamisha umiliki wa ardhi kutoka kwake kwenda kwa mnunuzi. Hivyo anakosa umiliki wa ardhi hiyo pale anapopokea malipo na kukabidhi nyaraka zozote muhimu za ardhi yake. Ikumbukwe pia ardhi inapanda thamani kila siku na ardhi ni mali isiyohamishika na ni ya uhakika. Hivyo, soko la ardhi linavutia watu wengi sana hasa kwa yale maeneo yenye rutuba ambayo mengi yanapatikana vijijini. Hivyo, wakati mwingine ni rahisi wanakijiji kushawishiwa kuuza maeneo yao pasipo kujua matokeo. Kabla ya kuuza ardhi ni vizuri kujua matokeo ya kuuza ardhi yako kwa mtu mwingine hasa kwa wakati huu ambapo kuuza ardhi kumetambulika kisheria.

2.8 DHANA YA UHAWILISHAJI NA UTWALIWAJI WA ARDHI.

2.8.1 UHAWILISHAJI WA ARDHIUhawilishaji wa ardhi ni utaratibu wa kubadilisha aina ya ardhi kutoka kundi moja kwenda kundi lingine. Yaani ardhi ya kawaida kuwa ya kijiji, na kijiji ya kuwa ya kawaida au yahifadhi na ya hifadhi kuwa ya kijiji au ya kawaida. Uwezo huu kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya ardhi Namba 4 na kifungu cha 4 na Sheria ya ardhi ya vijiji Namba 5 amepewa Rais. Kwa mujibu wa sheria Rais ndiye mwenye mamlaka pekee ya kufanya uhawilishaji wa ardhi.

Mambo ya KuzingatiaSheria inatoa mwongozo wa uhawilishaji wa ardhi ya jumla au hifadhi na kuwa ardhi ya kijiji. Endapo Rais anataka kuhawilisha ardhi atamuagiza Waziri kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria. Waziri atatakiwa kuzingatia yafuatayo katika kutekeleza maagizo ya Rais: a) Kutoa notisi au taarifa ya kusudio;b) Muda wa eneo lililohawilishwa kuanza kutumika ni siku 60 baada ya notisi;c) Nakala kwa mamlaka husika mf. Halmashauri ya kijiji;d) Majibu au pingamizi kutoka kwa mamlaka husika – siku zisizopungua 20 na

zisizozidi 40.

Uhawilishaji wa Ardhi ya Kijiji kuwa ya Jumla au Hifadhi unafuata taratibu zifuatazo a) Notisi;b) Muda wa kuanza kutumika eneo husika ni siku 90 baada ya notisi;c) Muda wa pingamizi ni siku 20 mpaka 40;d) Fidia.

Ikumbukwe kwamba wanakijiji wanayo nafasi kubwa katika suala la uhawilishaji wa ardhi hasa ya jumla au ya hifadhi kuwa ya kijiji kwa vile wao wamepewa uwezo kupitia Halmashauri ya kijiji kwa idhini ya mkutano mkuu wa kijiji kwa kumwandikia Rais kuomba ardhi husika ihawilishwe na kuwa ya kijiji endapo wanamahitaji ya ardhi hiyo kwa wakati huo.

2.8.2 UTWALIWAJI WA ARDHIHuu ni uwezo aliyopewa Rais kwa mujibu wa sheria, kuchukua sehemu yoyote ya ardhi ya Tanzania kwa kile ambacho sheria inakiita kwa manufaa ya Umma. Uwezo

Page 17: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 10

huu pia umewekwa mikononi mwa Rais na ni mojawapo ya uwezo wa kupanga matumizi ambapo Rais anaweza kubatilisha matumizi ya aina fulani na kupanga ardhi hiyo itumike kwa matumizi mengine. Kwa mamlaka hii, Rais anaweza kutengua haki ya umiliki wa ardhi ya kijiji na umiliki wa maeneo yoyote na kubadilisha matumizi yake au kugawa kwa wamiliki wengine kadri atakavyoona inafaa kwa manufaa ya umma. Mamlaka hayo amepewa kisheria kutokana na Sheria ya Utwaliwaji Ardhi, Na. 47 ya 1967 na Sheria ya Ardhi Na. 4 ya 1999.

Hata hivyo, sheria ya Utwaliwaji Ardhi ya mwaka 1967 inatoa maelekezo ya hatua za kufuatwa kabla ya kutwaaliwa kwa ardhi ambazo ni pamoja na:

• Kutoa notisi ya kusudio la utwaaji wa ardhi inayoainisha sababu za kutwaa ardhi hiyo pamoja na mpango mahususi wa matumizi ya ardhi hiyo pale itakapotwaliwa;

• Kutoa muda wa siku tisini (au miezi mitatu) kwa wale ambao ardhi yao inatwaliwa endapo wana sababu za msingi za kuweka pingamizi ya juu ardhi yao isitwaliwe;

• Endapo hakuna pingamizi, mtwaaji wa ardhi anatakiwa kufanya uthaminishaji na tathmini ya thamani ya mali zilizo katika ardhi husika (ikumbukwe kuwa baada ya marekebisho ya Sheria ya Ardhi ya 2004, hata ardhi tupu itabidi ithaminishwe kwa bei ya soko ya eneo husika); na

• Mtwaaji wa ardhi anapaswa kulipa fidia ya haki kulingana na viwango vya soko vya mali husika kama ilivyoainishwa katika sheria ya utwaaji wa ardhi na Sheria ya Ardhi Namba 4 ya 1999.

2.8.3 UTHAMANISHAJI WA ARDHIDhana ya uthamanishwaji wa ardhi maana yake ni kuipa ardhi thamani halisi kulingana na soko la ardhi la wakati huo. Kabla ya mabadiliko ya Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 2004 uthamanishwaji wa ardhi ulikuwa kwa namna tofauti na ilivyo sasa, yaani baada ya marekebisho hayo. Dhana hii haina maana kuwa kabla ya marekebisho haya ardhi haikuwa na thamani, na wala haina maana kuwa mabadiliko haya yameleta thamani ya ardhi. Ukweli ni kwamba hata kabla ya marekebisho ya sheria hiyo ardhi ilikuwa na thamani, ila thamani iliyokuwepo ni ile ya matumizi (use value). Maana ya thamani ya matumizi ni yale mavuno au faida itokanayo na matumizi ya ardhi kama vile chakula, majengo na shughuli nyingine katika ardhi.

Marekebisho yameleta mambo mawili makubwa ambayo yamebadilisha kabisa mfumo wa umiliki wa ardhi. Hivyo, kwanza kabisa marekebisho yameipa ardhi thamani ya soko (exchange value). Thamani ya soko inawezesha ardhi kutumika kama bidhaa katika soko. Pili, yameruhusu ardhi tupu kuuzwa kama bidhaa nyingine. Hii ni tofauti kabisa na wakati Sheria za Ardhi Namba 4 na 5 hazijatungwa, kilichokuwa kinauzwa ni uendelezaji uliofanyika katika ardhi husika (“unexhausted improvement”) kama vile majengo, miti n.k.

Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi iliyokebishwa 2004, vifungu vidogo vya 8 na 9 vya kifungu cha 37 kwa sasa vimefutwa. Badala ya vifungu hivyo, sasa kuna vifungu vipya, ambavyo vinamruhusu Kamishna wa Ardhi kuidhinisha uuzaji wa ardhi tupu endapo tu uuzaji huo utazingatia masharti yaliyopo kama yaliyoaainishwa katika

Page 18: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 11

kifungu kidogo cha 9 cha sheria ya marekebisho ya 2004 ya ardhi.

Mabadiliko yaliyofanywa yameleta misingi mipya ya mfumo wa umilikaji ardhi nchini. Ukweli ni kwamba yameanzisha utaratibu wa umiliki huria (freehold) wa ardhi, ingawa katika vitabu vya sheria unaendelea kujulikana kwa kivuli cha ardhi ni mali ya umma. Mfumo wa umiliki huria una sifa kuu mbili: Mosi, mmiliki wa ardhi ni mtu binafsi, na pili, umiliki ni pasipo/bila ukomo. Kabla ya marekebisho hayo ardhi ilikuwa inamilikiwa na dola, lakini sasa sheria inaruhusu mtu binafsi kumiliki ardhi kwavile anaruhusiwa pia kuiuza hata bila kuiendeleza kwa mantiki hii ukomo wa kumiliki ardhi uliopo kisheria hauna maana yoyote kwa vile sheria inaanzisha bila kutamka, umiliki usio na kikomo, umiliki wa milele.

2.9 UTARATIBU WA KULIPA FIDIA YA ARDHIPale ambapo ardhi yako au ardhi ya kijiji inapotwaliwa, au kuhawilishwa kuwa ya jumla au ya hifadhi na umetakiwa kuondoka wewe kama mmiliki, unastahili fidia kama inavyoelezwa katika Sera ya Taifa ya Ardhi . Katika kudai fidia wafuatao wanaweza kudai:

1. Halmashauri ya Kijiji kwa niaba ya wanakijiji kwa ajili ya ardhi ya matumizi ya pamoja, na pia upotevu au hasara inayotokana na kutwaliwa kwa ardhi ya kijiji ya pamoja.

2. Mwanakijiji yeyote anayemiliki ardhi katika ardhi iliyotwaliwa au kuhawilishwa, anayomiliki kimila iwe imesajiliwa au la.

Nini Stahiki za Fidia katika ArdhiFidia kwa kupoteza maslahi yoyote kwenye ardhi, itajumuisha thamani ya uboreshaji wa mali isiyohamishika (majengo n.k). Thamani ya ardhi hiyo itapatikana kwa kigezo cha soko (thamani ya soko). Thamani ya soko ni mlinganisho wa mauzo ya ardhi kama hiyo katika eneo husika. Je, kama ingeuzwa ungepata shilingi ngapi?a) Posho ya Usumbufu

Hii inakadiriwa kwa kuzidisha thamani ya ardhi mara wastani wa riba inayotolewa na benki kwa akaunti ya muda maalum wa miezi 12 wakati wa kupoteza umiliki wa ardhi hiyo

b) Posho ya UsafiriUtatakiwa kulipwa gharama za kusafirisha tani 12 za mizigo kwa njia ya barabara au reli kwa umbali wa km 20.

c) Kupoteza FaidaMfano: kama ulikuwa na duka biashara katika ardhi husika fidia ya upotevu wa faida itakadiriwa kwa kuangalia faida yako kwa mwezi na kuizidisha mara miezi 36. Hivyo kama faida katika biashara yako ni Sh. 100,000, itakuwa 100,000 x 36 =Sh 3,600,000

d) Posho ya Pango/ Makazi Kodi ya pango katika soko kwa jengo, itakadiriwa na kuzidishwa mara miezi 36 ili kukulipa fidia yako. Mfano, kama kodi ya pango ni Sh. 50,000 x 36 na hiyo itakuwa fidia ya upotevu wa pango.

e) Gharama za Upatikanaji wa Ardhi husikaFidia halisi ya ardhi yako itapatikana kwa kuithaminisha kwa kuzingatia na kuangalia thamani yake ya soko. Kama ikiuzwa ungepata kiasi gani?

Page 19: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 12

f) RibaUtalipwa riba pale tu ambapo fidia haikulipwa ndani ya miezi sita (6) toka ardhi yako itwaliwe au ihawilishwe. Riba inakadiriwa kwa kuangalia riba itolewayo na benki kwa akiba za muda maalum.

Madai/Kudai FidiaPale ardhi inapotwaliwa au kuhawilishwa Kamishna atatoa taarifa kwa Halmashauri ya Kijiji na watu wote ambao ardhi yao inahawilishwa kuwa watatakiwa kudai fidia. Wewe na wanakijiji wenzio mnatakiwa kujaza fomu maalum za kudai fidia. Kama mtahitaji msaada katika kuandaa madai yenu basi mnatakiwa kumwomba Ofisa Mtendaji wa Kijiji amwombe Ofisa Ardhi Mteule wa Wilaya awasaidie. Au mnaweza kuomba msaada kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayojihusisha na masuala ya Ardhi na/au haki za binadamu.

2.10 SHERIA YA UWEKEZAJI NAMBA 26 YA MWAKA 1997Sheria hii inaainisha masharti ya jumla kwa wawekezaji, kama vile viwango vya uwekezaji, mgawanyo wa mapato na umiliki wa rasilimali hasa ardhi. Sekta binafsi na watu binafsi wamepewa kipaumbele, kwani Sheria ya Uwekezaji na masharti yake yamerahisishwa ili wawekezaji wa ndani na wa nje ya nchi wawekeze katika sekta zote hapa nchini.i. Maana ya Uwekezaji Uwekezaji ni mchakato wa kuunganisha jitihada, rasilimali, muda na maarifa kwa lengo

la kulimbikiza mtaji na kupata manufaa zaidi katika uzalishaji au shughuli iliyopangwa kwa lengo la kupata faida.

ii. Aina za Wawekezaji• Wawekezaji ambao sio raia wa Tanzania wenye mtaji usiopungua dola laki tatu za

Kimarekani ($300,000).• Wawekezaji wa ndani ambao ni raia wa Tanzania wenye mtaji usiopungua dola laki

moja za Kimarekani ($100,000).iii. Taratibu za Uwekezaji kwa Asiye raia Mwekezaji asiye raia anapaswa kupeleka maombi ya kupewa ardhi kwenye Kituo

cha Uwekezaji Tanzania akiambatanisha na mpango wa uwekezaji. Endapo ardhi inayokusudiwa kumilikishwa ni ya kijiji ni sharti ihawilishwe kwanza. Kituo cha Uwekezaji ndicho hupeleka maombi kwa Waziri wa Ardhi ambaye atayawasilisha kwa Rais kubadilisha ardhi hiyo kutoka kundi la ardhi ya kijiji kwenda ardhi ya jumla. Maombi yakipitishwa mwekezaji anapaswa kumilikishwa ardhi na Kituo cha Uwekezaji (TIC) nchini kwa umiliki wa Hati hafifu (derivative right). Kwa mujibu wa kifungu cha 20 cha Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 kama kilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 2 ya mwaka 2004 mtu yeyote ambaye sio raia wa Tanzania haruhusiwi kumiliki ardhi nchini isipokuwa kwa shughuli za uwekezaji kwa mujibu wa Sheria ya Uwekezaji nchini.

iv. Taratibu za Uwekezaji kwa raia Kila raia ana haki na fursa ya kuwa mwekezaji kwa kutumia ardhi anayomiliki au kuomba

kupitia Halmashauri ya Wilaya au Manispaa. Mmiliki wa ardhi anayetaka kujisajili kama mwekezaji atawasilisha maombi ya kibali cha uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini na kufuata taratibu nyingine kama zilivyoelekezwa kwenye sheria ya uwekezaji. Wananchi wanaweza kuingia ubia na mwekezaji wakaendelea kuwa wamiliki wa ardhi zao bila kuhamisha umiliki wao.

ANGALIZO: Endapo uwekezaji una athari kwa umiliki wa ardhi kwa wenyeji wanapaswa

Page 20: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 13

kulipwa fidia ili kupisha uwekezaji. Mradi wowote mkubwa wa uwekezaji katika ardhi unapaswa kufuata taratibu za kufanya tathmini ya athari za kimazingira kabla ya shughuli za uwekezaji kuanza. Mara baada ya mwekezaji kumaliza uwekezaji wake, au mara kipindi chake cha uwekezaji kinapofika mwisho umiliki wa ardhi utarejea katika Kituo cha Uwekezaji nchini.

2.11 SHERIA YA WANYAMAPORI NAMBA 5 YA MWAKA 2009Lengo la sheria hii ni kuweka taratibu kuhusiana na maendeleo, matengenezo, maboresho na usimamizi wa barabara pamoja na kuweka taratibu za kubadilisha hadhi ya barabara. Kwa kuzingatia lengo hilo serkali imetenga maeneo na kuyafanya hifadhi za barabara.

i. Maana ya Hifadhi ya BarabaraHifadhi ya barabara ni sehemu ya ardhi pembeni mwa barabara iliyotengwa kwa ajili ya upanuzi wa barabara katika siku za usoni pale mamlaka husika itakavyoona inafaa. Hifadhi ya barabara inaweza kutumika kwa shughuli moja au zaidi kama ifuatavyo: miundombinu ya simu, umeme, maji safi na maji taka, vyoo, bafu, maegesho ya magari, gereji, nyumba za muda na n.k. Hifadhi ya barabara inaweza kutumika kwa ajili ya shughuli nyingine kwa ruhusa maalumu ya mamlaka zinazosimamia barabara husika.

ii. Aina za barabaraSheria ya barabara imeainisha aina tatu za barabara;(a) Barabara za taifa: Ni barabara zinaounganisha mkoa mmoja na mkoa mwingine,

mkoa na mji/miji nje ya Tanzania, mkoa na wilaya au makao makuu ya mkoa na makao makuu ya wilaya.

(b) Barabara za wilaya: Ni barabara zinazounganisha wilaya na tarafa, tarafa na tarafa, tarafa na kata, barabara ndogo ndani ya mji inayounganisha barabara kuu ya wilaya na barabara ndogo katika eneo hilo, barabara za jamii ndani ya vijiji na barabara inayounganisha kijiji na kijiji.

(c) Barabara binafsi: Hutengenezwa na mtu binafsi kwa ajili ya matumizi yake mwenyewe baada ya kuruhusiwa na kuidhinishwa na mamlaka za barabara. Barabara hii inaweza kuamuliwa kutumiwa na watu wengine endapo barabara kuu ya jamii itakuwa kwenye matengenezo.

iii. Upana wa hifadhi za BarabaraSheria ya Barabara ya mwaka 2007 na kanuni zake za mwaka 2009 zimeainisha kwa ufasaha upana unaotakiwa kisheria kwa ajili ya hifadhi ya barabara mbalimbali kama ifuatavyo:(a) Barabara za Taifa na barabara za mkoa zenye njia mbili: Barabara hizi sharti ziwe

na upana wa meta 60 yaani meta 30 kila upande kutoka kisiwa cha barabara. (b) Barabara kuu na barabara za mikoa zenye njia moja: Barabara hizi sharti ziwe na

hifadhi ya barabara yenye upana wa meta 60 yaani meta 30 kila upande kutoka mstari wa katikati wa kila barabara.

(c) Barabara za Mkusanyo (collector roads): Barabara hizi sharti ziwe na hifadhi ya barabara yenye upana wa meta 40, yaani meta 20 kila upande kutoka kwenye mstari wa katikati wa barabara.

(d) Barabara za mjazio (feeder roads): Barabara hizi sharti ziwe na hifadhi ya barabara

Page 21: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 14

yenye ukubwa wa meta 30, yaani meta 15 kila upande kutoka kwenye mstari wa katikati wa barabara.

(e) Barabara za jamii (community roads): Barabara hizi sharti ziwe na hifadhi za barabara zenye ukubwa wa meta 25, yani meta 12.5 kila upande kutoka kwenye mstari wa katikati wa barabara.

Mamlaka za Usimamizi wa barabaraSheria ya Barabara ya Mwaka 2007 imeainisha mamlaka za usimamizi wa barabara kuwa ni pamoja na: Wizara husika, Bodi ya Barabara ya Mkoa, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na mamlaka nyingine zinazoteuliwa na Waziri husika kupitia tangazo la serikali. Lakini pia Tangazo la Serikali namba 211 la mwaka 2017 lilianzisha wakala wa Barabara Vijijini (TARURA).

Taratibu za kupanda hadhi za barabaraTaratibu za kupanda hadhi za barabara hutegemea vigezo na matumizi ya barabara. Ili barabara ipande hadhi, ni lazima yawepo mabadiliko ya kiutawala yanayolazimu kubadilika kwa hadhi ya barabara kuanzia mwanzo wa barabara hadi mwisho wa barabara. Maombi ya kupanda hadhi kwa barabara yanafanywa na bodi za mikoa za barabara.

Masuala ya Kuzingatia kwa wananchi kuhusiana na hifadhi ya barabara• Barabara ni sehemu ya kundi la ardhi ya hifadhi ambayo hairuhusiwi kwa matumizi

binafsi kama vile kujenga nyumba za kudumu; na• Pale ambapo barabara zinapanda hadhi na kuleta athari kwa wamiliki halali wa ardhi

wana haki ya kulipwa fidia.

2.12 SHERIA YA BARABARA NAMBA 13 YA MWAKA 2007Endapo wananchi kupitia Mkutano Mkuu wa Kijiji wameafiki mapendekezo ya kuwepo utaratibu wa kufanya maamuzi yanayohusiana na ardhi katika ngazi ya kijiji, basi Halmashauri ya Kijiji itaunda Kamati ya Uamuzi wa Kijiji (Village Adjudication Committee VAC) kwa mujibu wa kifungu cha 53 (1) & (2) cha Sheria ya Ardhi ya Kijiji Namba 5 ya Mwaka 1999.

Halmashauri ya Kijiji itawateua wajumbe wasiozidi tisa (9) ambao baadaye wataidhinishwa na Mkutano mkuu wa Kijiji ili kuunda Kamati ya Uamuzi ya Kijiji (KaUKi). Miongoni mwa wajumbe hao wanawake wasiopungua wanne (4) lazima wawemo, wajumbe wote watatumikia kamati kwa kipindi cha miaka mitatu na wanaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi cha miaka mitatu, ili mradi tu taratibu zifuatwe. Akidi ya wajumbe ni watano (5) na angalau wawili (2) kati yao wawe wanawake

2.13 KAMATI YA UAMUZI YA KIJIJI Kifungu cha 53 (3) cha Sheria ya Ardhi ya Kijiji Na. 5, 1999 kimeainisha majukumu yafuatayo ya Kamati ya Uamuzi wa Kijiji:1. Kuweka mipaka ya ardhi na kushughulikia maslahi yaliyo juu ya ardhi ya kijiji2. Kutenga, au kuweka akiba ya ardhi ya kijiji na kutoa mipaka ya haki ya njia.3. Kutoa haki zingine ambazo itaziona kuwa ni bora katika matumizi ya ardhi kijijini.4. Kulinda maslahi ya wanawake, watoto wadogo, walemavu na watu wasiokuwepo

kijijini ila wana maslahi juu ya ardhi ya kijiji.5. Kuendesha mashauri madogomadogo ya ardhi na kuyatolea maamuzi kwa mujibu wa

Page 22: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 15

sheria za kimila.6. Kushughulikia maslahi yoyote kwenye ardhi ambayo kwa sababu yoyote hakuna madai

yaliyo fanyika

Baada ya Kamati kuundwa itachagua mmoja wa wajumbe wake kuwa Mwenyekiti ambaye atakuwa akiongoza mikutano kwenye mikutano yote atakayohudhuria na kama hata hudhuria kwenye mkutano wowote, wajumbe waliohudhuria wanaweza kumchagua mmoja wao kuendesha kikao hicho.

Mwananchi yeyote ambaye hataridhika na uamuzi wa Kamati ataweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo kwenye Baraza la Ardhi la Kijiji ndani ya siku thelathini (30) baada yakutolewa kwa kumbukumbu za uamuzi husika, kama inavyoelezwa kwenye kifungu cha 55 (1) cha Sheria ya Ardhi ya Kijiji.

Page 23: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 16

3 UANDAAJI NA USIMAMIZI WA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI

UTANGULIZIMada hii inajadili Uandaaji na Usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi kwa mujibu wa Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Namba 6 ya Mwaka 2007. Sheria hii imeweka misingi ya upangaji na utumiaji wa ardhi kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Ardhi pamoja na Sera ya Maendeleo ya Makazi ya Taifa ya mwaka 2000. Masuala mbalimbali yatakayojadiliwa kwenye mada hii ni pamoja na maana, faida, mamlaka na hatua za uandaaji wa mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji.

3.1. MAANA YA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI YA KIJIJIMwongozo wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi wa mwaka 2010 unatafsiri mpango wa matumizi ya ardhi kuwa ni “Utaratibu wa kutathmini na kupendekeza namna mbalimbali za matumizi ya maliasili ili kuinua hali ya maisha ya wanakijiji na kuondoa umaskini”. Ili mpango uwe na tija ni sharti uandaliwe kwa kushirikisha makundi mbalimbali yaliyopo katika kijiji.

3.2. FAIDA ZA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHIBaadhi ya faida za Mpango wa Matumizi ya ardhi ni pamoja na:• Kupunguza migogoro ya ardhi baina ya makundi mbalimbali ya watumiaji wa ardhi na maliasili

zilizomo;• Kutoa uhakika wa milki za ardhi kwa wananchi kupitia hakimiliki za kimila;• Kuboresha matumizi ya ardhi kwa kugawa ardhi katika makundi mbalimbali ya watumiaji kwa

kuzingatia mahitaji ya wananchi; na• Kusaidia utunzaji wa mazingira na hasa vyanzo vya maji, misitu na wanyamapori kwa lengo la

kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

3.3. MAMLAKA ZA UPANGAJI NA USIMAMIZI WA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHIMamlaka za uandaaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini Tanzania kwa mujibu wa Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Namba 6 ya Mwaka 2007 ni: Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Halmashauri ya Wilaya, Halmashauri ya Kijiji na mamlaka nyingine yoyote itakayotangazwa na Waziri mwenye dhamana ya ardhi kwenye gazeti la serikali. Mipango ya matumizi ya ardhi huandaliwa na kutekelezwa katika ngazi mbalimbali kama ifuatavyo:

Ngazi ya TaifaKatika ngazi hii kuna Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi inayoundwa na wajumbe wasiopungua 5 na wasiozidi 10 (kati yao wanawake wasipungue 3) kutoka sekta mbalimbali kama vile ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi; kilimo na mifugo, nishati au madini; serikali za mitaa; maji; afya; maliasili; utalii; uvuvi; sheria; fedha; mazingira; uchumi na mipango. Wajumbe hao wanateuliwa na Waziri mwenye dhamana ya ardhi na kuongozwa na Mwenyekiti wa Tume ambaye huteuliwa na Rais.

Baadhi ya majukumu ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya ardhi ni pamoja na; kuandaa mpango wa kitaifa wa matumizi ya ardhi, kuandaa mipango kabambe ya kikanda ya matumizi ya ardhi pamoja na kuratibu, kusimamia na kutoa mwongozo wa uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya wilaya na vijiji.Ngazi ya Wilaya

MADA YA TATU

Page 24: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 17

Halmashauri ya Wilaya itaunda Timu Shirikishi ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi (Participatory Land Use Management, PLUM,) yenye wajumbe 6 hadi 8 kutoka Idara zinazohusiana na ardhi kama vile kilimo, mifugo, maliasili, ardhi na maendeleo ya jamii. Timu ya PLUM inawajibu wa kuratibu na kuwezesha uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi Wilayani na kuziwezesha Halmashauri za Vijiji na kuunda Kamati za Matumizi ya Ardhi za Vijiji (VLUM).

Ngazi ya KijijiHalmashauri ya Kijiji huandaa mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji kupitia Kamati ya Usimamizi na Matumizi ya Ardhi. Katika ngazi hii ni lazima mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji uwe ni mchakato shirikishi unaozingatia ushirikishwaji wa wananchi kikamilifu kupitia Mikutano Mikuu ya Vijiji au mwananchi mmoja mmoja.

3.4. HATUA ZA UANDAAJI WA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI KIJIJINIUandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji hupitia katika hatua kuu sita (6) kama zifuatavyo:

3.4.1 MAANDALIZI WILAYANIHalmashauri ya Wilaya inatakiwa kuunda timu ya PLUM yenye wajibu wa kuandaa utaratibu wa utekelezaji wa mpango wa matumizi ya ardhi katika vijiji kulingana na rasilimali ilizonazo ili kufanikisha uandaaji wa mipango ya vijiji kwa wakati. Timu ya PLUM inatakiwa kuhusisha wadau mbalimbali, ikiwemo miradi na taasisi zisizo za kiserikali.

3.4.2 TATHMINI SHIRIKISHI YA MATUMIZI YA ARDHI YA KIJIJIHatua hii imegawanyika katika hatua nne 4 ndogondogo ambazo ni:

Moja: Elimu kwa Umma.Wataalam wa wilaya kwa kushirikiana na serikali ya kijiji na Kamati ya Usimamizi na Matumizi ya Ardhi ya Kijiji watatoa elimu kwa wananchi. Miongoni mwa mambo yatakayohamasishwa ni pamoja na madhumuni, umuhimu na utaratibu wa mpango wa kutekeleza matumizi ya ardhi, takwimu muhimu za kijiji kama vile idadi ya watu, kaya na mambo ya msingi katika sera na sheria za ardhi.

Mbili: Kufanya tathmini shirikishi ya kijiji.Timu ya PLUM kwa kushirikiana na Halmashauri ya Kijiji na Kamati ya Usimamizi na Matumizi ya Ardhi (VLUM) hufanya tathmini shirikishi ya kijiji kwa lengo la kukusanya, kuchambua na kuweka kumbukumbu za takwimu muhimu za kijiji kama vile idadi ya watu, mifugo, ukubwa wa eneo, vyanzo vya maji, misitu na huduma za kiuchumi na kijamii.

Tatu: Kuandaa mpango kazi wa jamii.Ni ratiba ya namna ya utekelezaji wa mambo yaliyopangwa kufanyika. Ieleweke kuwa huu ni mpango kazi na sio Mpango wa Matumizi ya Ardhi.

Nne: Kujenga na kuimarisha taasisi za kijiji.Taasisi hizi ni pamoja na Halmashauri ya Kijiji na Mkutano Mkuu wa Kijiji ambazo hujengewa uwezo ili kuimarisha ufanisi wa utekelezaji wa Mpango wa Matumizi ya Ardhi.

Page 25: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 18

3.4.3 MIPAKA NA MATUMIZI YA ARDHI YA KIJIJIHii ni hatua inayohusisha timu ya PLUM ya wilaya kuhakiki kama mipaka ya kijiji inatambulika au la, kupitia Idara ya Ardhi ya Wilaya na kuweka orodha ya vijiji katika makundi yafuatayo:a) Vijiji ambavyo vimeshapimwa (vina ramani) na havina migogoro ya mipaka na kisha

kuviandalia Cheti cha Ardhi ya Kijiji;b) Vijiji ambavyo mipaka yake inatambulika lakini havijapimwa na havina migogoro ya

mipaka.Vijiji hivi vinaweza kuandaliwa ramani ya mipaka kwa kutumia vyombo vya upimaji kama vile GPS au picha za Satelaiti, na kisha kuandaliwa Cheti cha Ardhi ya Kijiji;

c) Vijiji ambavyo mipaka yake ilikwishapimwa, lakini kwa sasa vina migogoro ya mipaka kwa mfano kama vimegawanyika basi migigoro yote lazima itatuliwe kwanza na kubaini mipaka inayokubalika kwa pande husika;

d) Vijiji ambavyo havijapimwa na vina migogoro ya mipaka basi ni sharti kwanza migogoro hiyo itatuliwe kwanza, na kubaini mipaka inayokubalika kwa pande unaohusika.

CHETI CHA ARDHI YA KIJIJI

Nini maana ya Cheti cha Ardhi ya Kijiji?Cheti cha Ardhi ya Kijiji ni nyaraka/hati ambayo inatolewa kwa Halmashauri ya Kijiji kuonesha usimamizi wa Ardhi ya Kijiji ambayo inamilikiwa na wanakijiji wote. Cheti hiki kinaonesha, mipaka ya kijiji, ukubwa wa Ardhi ya kijiji, aina ya matumizi ya ardhi yaani kama ardhi inatumika kwa kilimo, ufugaji au kilimo na ufugaji.

Hatua za kupata Cheti cha Ardhi cha Kijijii. Wanakijiji kupitia Mkutano Mkuu wa Kijiji watajadili na kuomba kijiji kipewe Cheti

cha Ardhi ya Kijiji. Baada ya kukubaliana wataagiza Halmashauri ya Kijiji kutekeleza agizo hilo. Halmashauri ya Kijiji inatakiwa kutekeleza maagizo hayo kwa kumwandikia barua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya husika juu ya ombi hilo;

ii. Endapo ombi litakubaliwa, Halmashauri ya Wilaya kupitia Idara ya Ardhi ya Wilaya itaitaarifu Halmashauri ya Kijiji juu ya kukubaliwa kwa ombi hilo ikitaja tarehe ambayo zoezi la uhakiki wa mipaka na uwekaji wa alama litafanyika;

iii. Halmashauri ya Kijiji baada ya kujadili kukubaliwa kwa ombi hilo katika Mkutano Mkuu wa Kijiji itatoa taarifa katika mamlaka inazopakana nazo ili mamlaka hizo zihudhurie katika zoezi la uhakiki wa mipaka katika siku na tarehe ya uhakiki wa mipaka;

iv. Zoezi la uhakiki wa mipaka litafanyika pale ambapo pande zote mbili zipo na kukubaliana mipaka. Timu ya wataalam kutoka idara ya ardhi itaweka alama pale tu ambapo pande mbili zitakuwa zimekubaliana kuweka kumbukumbu ya taarifa hizo. Timu ya wilaya haihusiki katika kubaini na kuhakiki mipaka;

v. Timu ya wilaya itachukua taarifa hizo na kuziingiza katika cheti maalum. Cheti hicho kikiwa na taarifa kitapelekwa kwa Kamishna wa Ardhi ili kutiwa saini na kusajiliwa kisha kukabidhiwa kwa serikali ya kijiji husika.

Page 26: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 19

Utoaji wa Cheti cha Ardhi ya KijijiCheti hiki hutolewa kwa jina la Rais, akikasimisha mamlaka yake ya udhamini kwa Halmashauri ya Kijiji kusimamia Ardhi ya Kijiji.

Cheti hiki huandaliwa na Ofisa Ardhi Mteule wa Wilaya kwa kutumia Fomu ya Ardhi ya Vijiji Namba 16 itakayowekwa mchoro wa mipaka ya kijiji na eneo lake na kusainiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji na Ofisa Mtendaji wa Kijiji kisha kusajiliwa Wilayani na kupewa Namba ya usajili.

Cheti hutumwa kwa Kamishna wa Ardhi ili kusainiwa na kuwekwa lakiri, na kisha kurejesha nakala moja katika Masijala ya Ardhi ya Wilaya na nyingine kubaki katika Masijala ya kijiji kwa kumbukumbu. Mipaka ya kijiji inapobadilika kwa namna yoyote ile ni wajibu wa Halmashauri ya kijiji kumjulisha Kamishna wa Ardhi ili afanye mabadiliko yaliyotokea katika cheti husika.

3.4.4 UPANGAJI WA MATUMIZI YA ARDHI YA KIJIJIUandaaji wa mpango wa matumizi ya kijiji sharti uzingatie ugawaji wa ardhi kwa matumizi mengine yoyote kuendana na mahitaji ya watumiaji kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa na Wizara ya Ardhi kama ifuatavyo:• Maeneo ya makazi na huduma za jamii. Mfano, shule, zahanati, ofisi, masoko, maduka,

nyumba za ibada, barabara, na makaburi;• Maeneo ya kilimo, Maeneo ya kilimo cha mazao ya kudumu, mazao ya msimu, mazao

ya umwagiliaji, kilimo cha misitu;• Maeneo ya kuchungia. Maeneo kwa ajili ya malisho, nyika, njia za mifugo, huduma za

mifugo kama vile majosho na maji; • Maeneo ya misitu. Huusisha mimea asilia yenye miti mingi, matumizi ya mbao,

majengo, kuni, mkaa, asali, mitishamba, na uhifadhi wa mimea asilia.

Baada ya mpango wa matumizi ya ardhi kukamilika timu ya PLUM huwezesha Halmashauri ya Kijiji kupitia Kamati ya Matumizi ya Ardhi ya Kijiji kuandaa rasimu ya mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji pamoja na rasimu ya sharia ndogo ambazo huwasilishwa kwenye Mkutano wa Kijiji na kujadiliwa.

Baada ya kuridhiwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji rasimu ya sheria ndogo hupelekwa katika Kamati ya Maendeleo ya Kata kisha hupelekwa kwa Hakimu au Mwanasheriavwa Wilaya kuhakikiwa kama zinaendana na sharia za nchi na kurudishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji kwaajili ya kuanza kutumika. Mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji hupelekwa Halmashauri ya Wilaya na kutiwa saini na Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya.

3.4.5 UTAWALA WA ARDHI KIJIJINIHalmashauri ya Kijiji ni msimamizi wa ardhi ya kijiji kwa niaba ya wanakijiji kwa mujibu ya Sheria ya Ardhi ya Vijiji. Halmashauri ya Kijiji husimamia ujenzi wa Masijala ya Kijiji ambayo hutunza nyaraka zote zikiwemo nakala za Hati za Hakimiliki za Kimila ambazo hugawiwa kwa kila mwenye ardhi katika kijiji mara baada ya mchakato wa matumizi ya ardhi kufikia mwisho. Utambuzi wa maeneo yaliyopangwa hufanyika katika hatua hii pamoja na kusimikwa kwa mabango yanayoonesha maeneo yaliyotambuliwa. Katika

Page 27: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 20

kurahisisha usimamizi wa ardhi ya kijiji inayomilikiwa kimila, ieleweke kwamba;a. Mtu, familia au kundi la watu wanaweza kuomba hati ya hakimiliki ya Kimila kwa

Halmashauri ya Kijiji kwa kujaza Fomu ya Ardhi ya Kijiji Namba 18, kisha kupewa Barua ya Ahadi Toleo yenye masharti kadhaa; na

b. Halmashauri ya Kijiji itatoa hati ya hakimiliki ya kimila kwa kutumia Fomu ya Ardhi Namba 21 baada ya siku 90 za mwombaji kukubali kupitia barua ya toleo.

3.4.6 USIMAMIZI WA ARDHI NA UIMARISHAJI WA VYOMBO VYA USIMAMIZI WA ARDHIKatika hatua hii Halmashauri ya Kijiji inatakiwa kusimamia sheria ndogondogo kwa kushirikiana na Kamati ya Usimamizi na Matumizi ya Ardhi. Wanakijiji wanatakiwa kutekeleza hatua stahiki za usimamizi wa ardhi ili kuzuia uchakavu na uharibifu wa ardhi, kuongeza uzalishaji wake na kuboresha hali zao za maisha. Aidha, wanakijiji wanatakiwa kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo, kuchungia mifugo, misitu, wanyamapori na makazi yanaheshimiwa na kutumiwa kama yalivyopangwa.

Page 28: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 21

4 HAKI YA ARDHI KWA MAKUNDI MBALIMBALI

UtanguliziArdhi ambayo ndio msingi mkuu wa uzalishaji mali pia inatumiwa na makundi mbalimbali ya watu katika jamii kama vile wanawake, vijana, wafugaji, wavuvi, wachimba madini, waokota matunda na wawindaji. Wakati mahitaji ya ardhi yakiongezeka, haki za ardhi kwa makundi haya yamekuwa yakinyimwa kutokana na kuzidiwa na maslahi mengine yaliyomo kwenye ardhi.

Mada hii inachambua haki za ardhi kwa makundi mbalimbali kama vile wanawake, vijana, wafugaji, wavuvi, wachimba madini na waokota matunda.

4.1. HAKI YA ARDHI KWA WANAWAKEMoja ya malengo ya kutungwa kwa Sera ya Taifa ya Ardhi ilikuwa ni kuleta usawa wa kijinsia katika umiliki wa ardhi. Hii ni kutokana na mifumo ya kimila iliyokuwepo katika usimamizi wa ardhi kutoruhusu haki sawa katika kupata, kutumia na kunufaika na ardhi. Katika sheria za kimila nyingi zilitoa haki ya ardhi kwa mwanaume kama msimamizi na mmiliki wa ardhi kwani yeye ndio huonekana kama Kiongozi wa familia. Pia, katika kugawa ardhi ya ukoo/familia mwanamke ana haki ya ardhi kwa kuzingatia taratibu za sheria za kimila, endapo sheria hizo hazikinzani na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Malengo hayo ya sera yamewekwa katika sheria mbalimbali kama ifuatavyo.

4.1.0 KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza kwamba, binadamu wote ni sawa na huzaliwa huru hivyo wanatakiwa kulindwa sawa na sheria za nchi. Hivyo, mwanaume na mwanamke wanahaki sawa mbele ya sheria na wanatakiwa kupewa ulinzi sawa na sheria za nchi ikiwemo kumiliki, kutumia na kupata ardhi kwa mahitaji yao. Kuwa kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria. Hivyo, mwanamke ana haki ya kumiliki ardhi kama mojawapo ya mali na kupata ulinzi wa mali hiyo kulingana na Katiba ya nchi.

Kwa maelezo hayo, ni wazi kwamba, suala la kumiliki na kutumia ardhi kwa mwanamke ni la kikatiba. Kwa upande mwingine mwanamke na mwanaume wanatakiwa kulinda mali hiyo na kulinda mali ya mtu mwingine inayomilikiwa kihalali.

4.1.1. SHERIA ZA ARDHI ZA MWAKA 1999

a. Haki ya Mwanamke kupata Ardhi. Sheria za Ardhi zinaainisha kwamba haki ya mwanamke kupata, kumiliki, kutumia na

kuuza au kuigawa ardhi ifahamike kuwa ni sawasawa na haki ya mwanaume yoyote kwa viwango vilevile na masharti yaleyale. Halikadhalika katika kupitisha uamuzi kuhusu maombi ya hakimiliki ya kimila Halmashauri ya Kijiji inapaswa kuzingatia maombi ya wanawake sawasawa na maombi ya wanaume.

b. Ulinzi wa Mali ya Familia dhidi ya rehani Katika kuweka rehani, ardhi ya familia itakuwa halali endapo itakuwa na saini

inayoonesha mke au wake kuridhia uwekaji wa rehani wa ardhi hiyo. Kama upande mmoja wa wanandoa haujaridhia basi rehani hiyo ni batili na ni kosa kisheria kutoa maelezo ya uongo.

MADA YA NNE

Page 29: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 22

c. Haki ya Mwanamke katika Umiliki wa ardhi wa pamoja Mwanandoa mmoja anapoomba hati miliki ya ardhi atatakiwa kueleza bayana kama

anachukua hati miliki hiyo kwa ajili yake binafsi au kwa ajili ya familia kwa hati miliki ya pamoja. Endapo jambo hili halitawekwa bayana, hati miliki itachukuliwa kuwa ya umiliki wa pamoja.

Inapotokea kwamba mwanandoa anamiliki ardhi au nyumba kwa jina lake mwenyewe na mwanandoa mwenzie amechangia nguvu zake katika kutunza au kuendeleza nyumba au ardhi hiyo, mwanandoa aliyechangia ana haki pia.

Katika umiliki wa ardhi ya pamoja kati ya mwanamke na mwanaume, kama mwanamke ameweka nguvu zake katika kuzalisha na kuiboresha ardhi hiyo, basi mwanamke anapata hadhi sawa ya umiliki hata kama jina lake halijaandikwa katika hati au cheti cha hakimiliki ya kimila.

d. Ulinzi wa Ardhi ya Familia dhidi ya Uuzwaji Katika ulinzi wa ardhi ya familia dhidi ya uuzwaji ni jukumu la mnunuzi kabla ya

kununua kujiridhisha kuwa ridhaa ya mke au wake halali imepatikana ili kuepusha mgogoro wa umiliki.

Mwanandoa hawezi au kuhawilisha kwa namna yoyote ardhi ya ndoa bila idhini au kuridhia kwa mwanandoa mwingine. Kama mwanandoa anakusudia kuuza ardhi ya ndoa pasipo idhini au kuridhia kwa mwanandoa mwingine, mwanandoa ambaye hajathirika anatakiwa kwenda mahakamani na kuweka pingamizi. Pale ambapo mwanandoa anataka kuuza au kuhamisha mali nyingine za ndoa zaidi ya nyumba ya ndoa idhini pia itahitajika. Pia, katika suala la kuweka rehani, kabla ya mabadiliko ya sheria ya vyombo vya fedha ilikuwa ni jukumu na wajibu wa taasisi za fedha kujithibitishia wenyewe kwamba mteja amepata idhini ya mwanandoa. Hivi sasa jukumu la kuthibitisha kwamba kuna idhini au maridhiano ya wanandoa limehamishiwa kwa mteja. Taasisi za fedha hazina jukumu la kuthibitisha idhini au kuridhia kwa mwanandoa.

e. Ulinzi dhidi ya Mila kandamizi Matumizi ya mila na desturi zinazowanyima wanawake, watoto au watu wenye

ulemavu njia halali za kumiliki, kukalia au kutumia ardhi ni batili na hazitatumika na kutekelezwa katika vyombo vya usimamizi wa ardhi na utatuzi wa migogoro ya ardhi nchini.

f. Haki ya Uwakilishi kwenye Masuala ya ardhi Katika vyombo mbalimbali vya utatuzi wa mgogoro na vya uendeshaji wa serikali

katika ngazi za kijiji na wilaya, nafasi ya mwanamke ni ya muhimu na ni ya lazima ili kuleta usawa wa maamuzi katika masuala ya ardhi.

Page 30: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 23

4.1.2 HAKI YA ARDHI YA MWANAMKE WAKATI WA NDOA NA TALAKA

Talaka ni nini?Talaka ni amri ya mahakama inayotolewa kuonesha kuwa ndoa imevunjika katika kiwango cha kutotengenezeka. Hii inamaanisha kuwa wanandoa hawawezi kuishi tena kama mume na mke.

Maana ya Ndoa Ndoa ni muungano wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke unaokusudiwa kudumu kwa muda wa maisha yao. Sheria ya ndoa inatambua ndoa za aina mbili; ndoa ya mke mmoja na ndoa ya mke zaidi ya mmoja .Ndoa hizi hufungwa kwa namna tatu; yaani Kidini, Kimila na Kiserikali.

a. Ndoa ya Kidini Ndoa hii hufungwa kwa mujibu wa taratibu ya dini husika. Ni lazima masharti yote

yatimizwe kisheria, taarifa ya nia ya kufunga ndoa itolewe, ndoa ifungwe mahali pa wazi panapokubalika kisheria na mfungishaji awe namamlaka. Kwa mujibu wa dini ya Kikristo, huwa ni ndoa ya mke na mume mmoja. Lakini kwa dini ya Kiislam ni ndoa ya mume na mke mmoja au zaidi ya mmoja.

b. Ndoa ya Kiserikali Ndoa hii hufungwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye Msajili wa Ndoa. Ndoa

itafungwa katika Ofisi ya Msajili au mahali pengine popote palipotajwa katika leseni ya kufungisha ndoa.

c. Ndoa ya Kimila Ndoa inaweza kufungwa kimila iwapo mmoja wa wanandoa au wote wawili wanafuata

sheria za mila za kabila fulani. Mdhamini wa ndoa za kimila ni Katibu Tarafa. Ndoa ya kimila hufungishwa na mtu anayetambulika kimila kuwa ana uwezo huo. Ni muhimu sana Katibu Tarafa kuhudhuria kwenye ufungishaji huo wa ndoa kwani ndiye atakayehusika na kuleta vyeti vya ndoa kutoka kwa Msajili. Mara nyingi ndoa hizi hazina vyeti kutokana na mazingira na miundombinu tunakoishi.

d. Dhana ya Kuchukulia Ndoa Kuna dhana inayokanushika kuwa mwanamume na mwanamke wakiishi pamoja

huweza kuchukuliwa kuwa ni mke na mume mbele ya sheria japokuwa hawakuwahi kufunga ndoa rasmi. Ili dhana hii iwepo ni lazima yafuatayo yathibitishwe:• Lazima ithibitike kwamba mwanamke na mwanamume wameishi pamoja kwa

muda wa miaka 2 au zaidi mfululizo;• Lazima ithibitike kuwa umma unaowazunguka unawachukulia na kuwapa heshima

kama mke na mume;• Lazima ithibitishwe kuwa watu hao walikuwa na uwezo wa kuwa mke na mume

wakati walipoanza kuishi pamoja na kama walikuwa na umri uliokubalika kisheria; na

• Ni lazima pia ithibitishwe kuwa kati ya hao wawili au wote hakuna aliye na ndoa inayoendelea.

Page 31: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 24

Mara nyingi wale wanaofunga ndoa ya kidini au kiserikali mara nyingi wamekuwa na fursa ya kufika mahakamani kirahisi zaidi. Uzoefu unaonesha kuwa, wanawake waliofunga ndoa ya kimila ndio wapo katika matatizo makubwa ya kukosa haki zao wakati wa talaka. Mara nyingi huachana kwa kufuata taratibu za kimila ambazo hufuata taratibu na tamaduni za makabila mbalimbali. Hivyo huwa vigumu kupata haki stahiki wakati wa talaka.

Katika baadhi ya makabila hayana kabisa suala la mali za ndoa, kwao mwanamke akiolewa na mahari kutolewa hana kitu chochote nyumbani kwa mumewe. Hivyo, wanashauriwa kwenda mahakamani pindi wanapopewa talaka za kimila kwani ni jukumu la mahakama kutoa talaka na kugawa mali za ndoa. Wakati wa talaka na baadaye mgawanyo wa mali za ndoa, mwanamke anashauriwa kuomba msaada kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji, Ofisa Mtendaji wa Kijiji, diwani, kiongozi wa dini, karani wa mahakama, asasi yoyote iliyopo kijiji au yeyote yule atakayekuwa na msaada.

Haki na Wajibu katika Ndoa Baada ya taratibu zote za ndoa kufuatwa na kwamba ndoa haina kasoro yoyote,

mke ana haki mbalimbali anazostahili kuzipata kisheria. Haki hizo ni kama ifuatavyo:

i. Matunzo Mke au wake wana haki ya kutunzwa na mume wao kwa kuwapatia mahitaji muhimu kama chakula, malazi, mavazi, matibabu n.k, kulingana na uwezo wa kumtunza mkewake. Kama ni kijijini mume anapaswa kumwonyesha mkewe mahali pa kulima na kumsaidia kukata miti na kung’oa visiki. Iwapo mume ana mke zaidi ya mmoja ana wajibu wa kuwatunza wote bila ya upendeleo. Pia, mume ana wajibu wa kuwatunza watoto wote waliozaliwa ndani ya ndoa.

ii. Kumiliki Mali Mke ana haki ya kumiliki mali aliyoipata kabla ya ndoa na hata wakati wa ndoa kama ameipata kwa fedha zake mwenyewe au kupewa zawadi. Mke pia ana haki ya kuingia mikataba, kufungua madai dhidi ya wadeni wake au kudaiwa, kununua mali au kuiuza. Kwa kuwa mume naye ana haki hizohizo, hii inamaanisha kuwa ndoa peke yake haibadilishi haki ya kumilikimali kati ya mke na mume. Pamoja na hali hii mke na mume wanaweza kukubaliana kuwa mali ambazo kila mmoja alikuwa nazo kabla ya ndoa au wakati wa ndoa ziwe zao kwa pamoja.

iii. Mke kukopa kwa Dhamana ya Mumewe Kwa kuwa katika hali ya kawaida mume ana wajibu wakumtunza mke na watoto kuna wakati inawezekana mume akasafiri kwa muda mrefu na hakuacha fedha au alizoacha zimekwisha, au mume amemtoroka mke na kumwachia watoto. Mke ana haki ya kukopa fedha kwa jina la mumewe au kuweka rehani mali ya mumewe. Mke ana uwezo wa kutumia mali ya mumewe ambayo inahamishika au kutumia fedha za mumewe zilizoko mikononi mwake kwa ajili ya kununulia mahitaji ya muhimu kwa ajili yake na watoto wake. Kufanya hivyo ni halali kisheria.

Page 32: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 25

Haki hizi zinakuwepo kama mke na mume wanaishi pamoja au kama wametengana kwa mapatano kuwa mume atatoa matunzo na mume amepuuzia mapatano hayo. Jambo la kuzingatia kwa makini hapa ni kuwa ili haki ya kutumia mali ya mume iweze kuwapo ni lazima mahitaji yanayonunuliwa yawe ni yale ambayo kama mume mwenyewe angekuwepo angekuwa na uwezo wa kuyanunua kulingana na pato lake.

iv. Haki ya Kuishi katika Nyumba ya Ndoa Nyumba ya ndoa ni nyumba ambayo mume na mke wanaishi wakati wa ndoa. Hata kama wana nyumba nyingi ni nyumba moja tu ndiyo inayochukuliwa kama nyumba ya ndoa. Pamoja na kuwa nyumba ya ndoa inaweza kuwa mali binafsi ya mke au mume, nyumba hiyo haiwezi kuuzwa, kuwekwa rehani au kuchukuliwa na mtu mwingine kama zawadi bila ya makubaliano ya wote wawili.

Ikiwa mume atafanya chochote kwenye nyumba hii bila ya makubaliano na mke, mke atakuwa na haki ya kuishi katika nyumba hiyo hadi hapo Mahakama itakapotoa maamuzi ya kuvunja ndoa hiyo, kutengana au amri ya matunzo. Kadhalika, mume naye anayo haki hiyohiyo iwapo mke ndiye mwenye nyumba na anataka kumfukuza mumewe. Ikumbukwe kuwa nyumba ya ndoa siyo lazima iwe nyumba ambayo mmoja wao amenunua ama amejenga. Hata kama nyumba ni ya kupanga bado itatambulika kisheria kama nyumba ya ndoa.

v. Mali iliyopatikana Wakati wa Ndoa Mali ya mke au mume iliyopatikana kutokana na jasho lao wote wawili ni mali yao kwa pamoja hata kama juhudi zao au jasho lao katika kupata mali hizi si sawasawa. Lakini pamoja na hayo kuna dhana inayokanushika kuwa kama mali hii imeandikishwa kwa jina la mmoja wao basi ni mali yake. Ni wajibu wa yule anayedai kuthibitisha kuwa ni mali ya pamoja na kwamba mali imeandikishwa kwa jina la mwenzi wake.

4.2 MASUALA YA MSINGI YA URITHI KATIKA ARDHI

Maana ya MirathiMirathi ni utaratibu wa namna mali ya marehemu itakavyogawiwa kwa warithi wake. Mgawanyo wa mirathi nchini unaongozwa na sheria tatu za mirathi ambazo ni; Sheria ya Kimila Sheria ya dini ya Kiislam na Sheria ya Kiserikali. Pamoja na sheria hizo, sheria ya mtoto ya mwaka 2009 imeeleza kuwa mtu yeyote hatakuwa na haki na uwezo wa kumnyima mtoto haki ya kurithi mali za wazazi wake.

i. Mgawanyo wa Mirathi Kwa Sheria Ya KimilaSheria ya kimila inayotumika kugawa mirathi imetokana na mila na desturi za jamii mbalimbali za Kitanzania zilizokusanywa katika makabila yanayorithi kufuata ukoo wa baba ambayo ni zaidi ya asilimia 85 ya makabila yote ya Tanzania. Sheria hii inapatikana katika Tangazo la Serikali Namba 436 la mwaka 1963

• Watanzania wote ambao ni wazawa wasio na asili ya Kiasia, Kizungu, au Kisomali hutumia sheria hii katika mirathi yao.

Page 33: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 26

• Kama ikithibitika kuwa mzawa aliacha kabisa mila na desturi za kabila lake wakati wa uhai wake Sheria ya Kiislam itatumika kugawa mali zake kiislamu kama marehemu alikuwa Muislam. Kama marehemu hakuwa Muislam Sheria ya Kiserikali itatumika kugawa mirathi

Mgawanyo wa mali katika Sheria ya Kimila umepangwa katika madaraja makuuma tatu kama ifuatavyo;

Daraja la kwanza a) Daraja la Mtoto wa kiume wa kwanza wa ndoa ya kwanza kutoka katika nyumba ya

kwanza, kama ndoa ilikuwa ni ya wake wengi. Huyu hurithi sehemu kubwa kuliko warithi wengine.

b) Mtoto wa kiume aliyezaliwa kwanza kutoka nyumba yeyote, kama marehemu hakuacha mtoto wa kiume katika nyumba ya kwanza.

Daraja la pili Daraja hili hushikwa na watoto wa kiume wote waliosalia ambao hupata fungu dogo ukilinganisha na mrithi wa Daraja la I.

Daraja la tatu Daraja hili hushikwa na watoto wa kike wote bila kujali umri na nafasi ya mama zao katika ndoa. Hawa hupata fungu dogo kuliko watoto wa kiume. Lakini pia kama watoto wa kiume hawapo hawa huongezewa urithi.

a. Nafasi ya Watoto wa Kike katika Urithi wa Ardhi Nafasi ya mtoto wa kike katika kumiliki ardhi ni sawa kabisa na nafasi ya mtoto wa kiume.

Msimamo huu pia umeelezwa katika Sheria ya Ardhi Namba 5 ya mwaka 1999, ambayo inatoa haki sawa kwa mwanaume na mwanamke katika kupata, kumiliki, kutumia, kuuza au kugawa ardhi. Pia, sheria hiyo inaeleza kuwa sheria yoyote ya kimila inayokwenda kinyume kwa kuwanyima wanawake, watoto au watu wenye ulemavu uhalali wa kumiliki ardhi, kutumia au kupata, basi sheria hiyo ya mila itakuwa batili. Kwa maana hiyo, daraja la tatu katika kugawa ardhi haliwezi kutumika dhidi ya wanawake kwa mujibu wa sheria za sasa.

b. Nafasi ya Mjane katika Mali ya familia Katika sheria ya Kimila mjane haruhusiwi kurithi mali za marehemu mume wake, sheria

hiyo inasema kuwa mjane mwenye watoto inabidi aishi kwa kutegemea watoto wake. Mjane ambaye hana watoto atabaki katika nyumba ya marehemu na kupewa asilimia 20 ya nusu ya mali ya marehemu mume wake na kuitumia wakati wa uhai wake. Akifariki au kuolewa na mtu mwingine nje ya ukoo mali hiyo na nyumba aliyokuwa anakaa itagawiwa kwa warithi halali wa marehemu. Sheria hii pia inasema mume hawezi kurithi mali ya marehemu mkewe katika urithi usio na wosia, isipokuwa pale tu ambapo mke hakuacha watoto na hakuacha kabisa mtu katika ukoo wake. Sheria hii kwa sasa inakosa uhalali wa kikatiba kwa kuwa haki za binadamu zinataka usawa bila ubaguzi.

c. Nafasi ya Watoto Waliozaliwa Nje ya Ndoa.• Watoto waliozaliwa nje ya ndoa hawaruhusiwi kurithi kwa baba isipokuwa pale

wanapokuwa wamehalalishwa kwa kutumia mila na desturi za jamii husika, vinginevyo

Page 34: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 27

hawa watoto hurithi kwa mama yao tu.• Pamoja na hayo, bado sheria za kimila zinafafanua waziwazi ya kuwa hata kama mtoto

wa nje amehalalalishwa na jamii husika na hata akiwa mkubwa kwenye familia hawezi kuwa daraja la kwanza la urithi.

ii. Mgawanyo wa Mirathi kwa Sheria ya KiislamSheria ya Kiislam inatumika kugawa mirathi kwa Watanzania wote ambao itathibitika kuwa wameacha mila na desturi zao na ambao Uislamu huwaongoza katika vipengele vyote vya maisha yao pamoja na watu wale ambao si wazawa ila ni Waislamu.

Mgawanyo wa Mirathi kwa Sheria ya Kiislamu ni kama ifuatavyo;a) Wajane/mjane hurithi 1/8 kama marehemu ameacha watoto;b) Wajane/mjane hurithi ¼ kama marehemu hakuacha watoto;c) Wazazi hupewa 1/6 ya salio baada ya kuondoa fungu la mjane/wajane;d) Mali iliyosalia hugawanywa katika mafungu matatu ambapo watoto wa kiume hupata

mafungu mawili na wa kike fungu moja; nae) Mjane hupewa ¼ ya mali ya marehemu mke wake kama kuna watoto au ½ kama hakuna

watoto.

Angalizo: Mtoto wa nje ya ndoa hawezi kurithi mali kwa baba yake kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu labda kama baba yake mzazi (marehemu) aliacha wosia.

iii. Mgawanyo wa Mirathi Kwa Sheria ya KiserikaliSheria ya Kiserikali hutumika na watanzania walioacha mila na desturi zao pamoja na watu wengine ambao si wazawa na wala si Waislam.

Mgawanyo wa urithi katika Sheria ya Kiserikali ni kama ifuatavyo:1. Marehemu akiacha watoto

• 1/3 hurithiwa na mjane.• 2/3 hugawiwa sawasawa kwa watoto wote.

2. Marehemu hakuacha watoto• ½ hupata mjane• ½ hupata wazazi wa marehemu au ndugu wa karibu iwapo wazazi hawapo.

Taratibu za Kufungua Mirathi

Wosia ukiwepo;1) Mtu anapofariki, kifo kiandikishwe katika Ofisi ya Vizazi na Vifo katika wilaya husika ndani

ya muda wa siku 30 tangu kifo kutokea.2) Endapo wosia haukumtaja msimamizi wa mirathi japokuwa si utaratibu wa kisheria

mkutano wa ukoo/familia ufanyike na kupendekeza msimamizi wa mirathi.3) Msimamizi aliyependekezwa au kutajwa katika wosia afungue mirathi katika mahakama

ya mwanzo iwapo sheria itakayotumika ni ya Kimila au ya Kiislam akiwa na nakala ya muhtasari wa kumbukumbu za kikao cha ukoo na cheti cha kifo.

4) Ukoo au ndugu wa marehemu hutoa mapendekezo tu juu ya mtu anayefaa kuwa msimamizi wa mirathi lakini ni mahakama pekee yenye uamuzi wa mwisho pale ambapo wosia haukusema nani atakuwa msimamizi wa mirathi.

Page 35: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 28

Wosia usipokuwepo;1) Mtu anapofariki, kifo kiandikishwe katika ofisi ya vizazi na vifo katika wilaya husika ndani

ya muda wa siku 30 tangu kifo kutokea.2) Mkutano wa ukoo/familia ufanyike kumpendekeza msimamizi.3) Msimamizi aliyependekezwa aende kufungua mirathi mahakamani akiwa na nakala ya

muhtasari wa kumbukumbu za kikao cha ukoo na cheti cha kifo.4) Mahakama hutoa tangazo la mirathi kwa muda wa siku 90 kama hakuna pingamizi lolote

msimamzi hukabidhiwa barua za usimamizi wa mirathi.5) Msimamizi anatakiwa kugawa mirathi kwa mujibu wa sheria, kufuatana na maisha

aliyoishi marehemu.

Wosia ni nini? Wosia ni kauli inayotolewa na mtu wakati wa uhai wake kwa hiari yake kuonyesha nia yake jinsi gani angependa mali zake zigawanywe baada ya kufa kwake.

Aina za wosia i. wosia wa maandishi ii. wosia wa mdomo

Wosia wa Maandishi Kwa mtu anayejua kusoma na kuandika, lazima atoe wosia katika maandishi. Wosia unataikiwa uwandikwe kwa kalamu ya wino usiofutika au upigwe chapa. Tarehe ya kutoa wosia ni muhimu. Kwa mtoa wosia anaejua kusoma na kuandika wanatakiwa mashahidi wawili watakao weka sahihi zao kuthibitisha wosia huo. Kwa mtu asiyejua kusoma na kuandika wasia wake pia unaweza kuandikwa ila sharti kuwe na mashahidi wanne (4) wawe ni watu wanaojua kusoma na kuandika.

Wosia unatakiwa kusainiwa na mtu alieutoa, na kama mtu hajui kusoma na kuandika aweke alama ya kidole gumba mbele ya mashahidi wake. Wosia unaweza kueleza msimamizi wamirathi ambaye mtaoaji wa wosia angependa asimamie ugawaji wa mali zake. Wosia unaweza kubadilishwa kwa kufuata taratibu za kisheria kwani hutuamika pale tu mtu anapofariki.

Wosia wa Mdomo Wosia huu unatolewana mtu asiyejua kusoma na kuandika, pia unapaswa ushuhudiwe na mashahidi wasiopungua wanne. Ambao wawili kati yao lazima wawe wanaukoo wa mtoa wosia. Wosia huo waweza kufutwa kwa kutoa wosia mwingine wa mdomo au kwa kutoa wosia wa maandishi.

4.1 HAKI ZA ARDHI KWA WAFUGAJI

Ufugaji ni nini?Ufugaji ni mfumo wa uzalishaji wa kiuchumi, kiutamaduni na kijamii ambao unategemea wanyama kama vile ng’ombe, mbuzi na kondoo n.k. Mfumo huu wa uzalishaji unategemea zaidi vitu vitatu vya msingi ambavyo ni rasilimali ardhi (maji na malisho), watu (familia na taasisi) na mifugo.

Page 36: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 29

Haki na Masuala yanayohusiana na Matumizi ya Ardhi kwa wafugajiWafugaji kama watumiaji wengine wa ardhi nchini wana haki sawa katika kupata, kumiliki, kutumia na kuuza ardhi. Kwa mfumo wa ufugaji wa asili ni vigumu kwa mfugaji mmojammoja kumiliki ardhi katika vipande kama ilivyo kwa watumiaji wengine wa ardhi. Hali hii inalazimu wafugaji wa asili kuhitaji eneo la pamoja la malisho ambalo wanaweza kulisha na kunywesha mifugo yao.

Baadhi ya changamoto zinazowakabili wafugaji wa asili ni pamoja na; namna gani wanaweza kupata ardhi kwa mfumo wa umiliki ardhi kijijini, namna ya kuweza kusajili ardhi yao na kupata cheti cha Hakimiliki ya Kimila. Ufahamu wa masuala haya utamsaidia kushiriki katika mpango wa matumizi ya ardhi vijijini ili kuweza kuhakikisha maslahi ya wafugaji katika upangaji wa ardhi kijijini yanazingatiwa. Umiliki wa Ardhi kwa WafugajiUmiliki wa ardhi ya kijiji kwa kufuata utaratibu wa kimila umeanza kurasimishwa kupitia utekelezaji wa mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji ambao huishia kutolewa kwa vyeti vya hakimiliki ya kimila kwa wamiliki wa ardhi ndani ya kijiji. Wafugaji wanatumia ardhi kwa pamoja na hivyo ni rahisi kupatiwa ardhi kama kikundi kuliko mtu mmojammoja.Hakimiliki ya Kimila kuweza kufanywa na mtu binafsi, familia au kundi la watu wanaotambulika ili mradi wawe na matumizi ya pamoja ya ardhi hiyo. Hivyo wafugaji wanaweza kuomba kumilikishwa eneo la malisho kwa pamoja na kupatiwa cheti cha hakimiliki ya kimila ya eneo hilo.

Pia, Kamati ya Maamuzi ya Kijiji inapaswa kuzingatia haki za ardhi za wafugaji katika kukalia, kutumia au kuwa na maslahi nayo katika kutafuta suluhu ya migogoro ya ardhi.

Halmashauri ya Kijiji ina wajibu wa kuhakikisha kuwa wafugaji wanapata haki zao katika ardhi, hasa katika mchakato wa kutoa vyeti vya hakimiliki za kimila baada ya kuandaa mpango wa matumizi wa ardhi ya kijiji. Ni muhimu wakati wa mchakato wa kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi ya kijiji kuwashirikisha wafugaji ili waweze kutoa maoni juu ya maslahi yao katika ardhi. Ni vema mipango ya matumizi ya ardhi ya kijiji ikaainisha wazi ardhi iliyotengwa kwa ajili ya shughuli za ufugaji ili iweze kuheshimika na wanakijiji wengine ambao siyo wafugaji.

Angalizo: Wafugaji wana haki sawasawa na watu wengine katika kumiliki, kupata, na kutumia ardhi kwa shughuli zao za kila siku.

4.2. HAKI ZA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI.Wachimbaji wadogo wa madini ni wachimbaji wanaotumia vifaa rahisi na mbinu ambazo zinawezesha uchimbaji mdogo wa madini. Wachimbaji wadogo wa madini wanatambulishwa kwa kwa kuwa na kiwango kidogo cha mitaji, dhana duni za uchimbaji na mazingira hatarishiya utendaji kazi. Ingawa madini syio sehemu ya ardhi kwa mujibu wa tafsiri ya neno ardhi kisheria ila kuna umuhimu wa kujadili haki za wachimbaji wadogo wa madini na wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanakopatikana na machimbo ya madini kwa kuwa madini hayo hupatikana ardhini. Masuala ya msingi ya kufahamu ni pamoja na;

• Kila mtanzania au kampuni ambayo wamiliki wake ni watanzania wana haki ya kuomba kwa Kamishna wa Kanda wa Madini, leseni ya uchimbaji mdogo wa madini au kutafiti

Page 37: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 30

madini sehemu yoyote nchini. Hii ina maanisha kwamba leseni ya uchimbaji mdogo wa madini haiwezi kutolewa kwa mtu au kampuni ambayo wamiliki wake sio watanzania.

• Sheria ya Madini pia imeainisha aina za leseni zinazotolewa kwenye uchimbaji madini ikiwemo, leseni ya utafiti wa madini, leseni ya utafiti wa vito, leseni ya kuhodhi haki ya uchimbaji madini, leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini, leseni ya uchimbaji wa kati wa madini na leseni kwa uchimbaji mdogo wa madini.

• Kwa mujibu wa Sheria ya eneo ambalo litapatikana kuwa na madini au litafanyiwa utafiti wa madini na kuleta athari katika haki za umiliki wa ardhi kwa mtu basi, mmiliki wa leseni hiyo ya madini anapaswa kulipa fidia kwa mujibu wa Sheria za Ardhi Namba 4 na 5 za mwaka 1999.

Page 38: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 31

5. MIGOGORO YA ARDHI NCHINI TANZANIA

Utangulizi Ongezeko la watu, maendeleo ya kiteknolojia, kiuchumi na kijamii, vimesababisha uhitaji mkubwa wa ardhi kwa makundi mbalimbali hali ambayo hufanyaardhi ipandea thamani na wakati mwingine kusababisha kuibuka kwa migogoro baina ya watumiaji wa ardhi. Mada hii inachambua vyanzo vya migogoro, athari zake, pamoja na mbinu mbalimbali zinazotumika kuitatua migogoro hiyo kwa mujibu wa sheria za nchi.

5.1. MAANA YA MIGOGORO YA ARDHIMigogoro ya ardhi ni hali ya kutofautiana baina ya pande mbili au zaidi juu ya umiliki, matumizi, upatikanaji, usimamizi wa ardhi pamoja na rasilimali zilizopo katika ardhi.

5.1.1 AINA ZA MIGOGORO YA ARDHIBaadhi ya migogoro inayofahamika ni;• Wakulima na wafugaji kugombea rasilimali adimu kama vile maji na malisho. • Kijiji dhidi ya kijiji wakigombea mipaka.• Serikali na wanavijiji, kwa mfano, mamlaka kupitisha maamuzi ya ugawaji ama

utwaliwaji wa ardhi ya kijiji bila ya kushirikisha wanakijiji.• Taasisi za kiserikali, kidini na kibinafsi dhidi ya wanavijiji hasa pale taasisi hizi

zinapopanua maeneo yao hadi kwenye maeneo ya kijiji.• Mamlaka za hifadhi dhidi ya wanavijiji kutokana na kupanuka kwa hifadhi hadi kwenye

maeneo ya wanavijiji bila mawasiliano wala kufuata taratibu.• Wachimbaji wadogo wa madini dhidi ya wachimbaji wakubwa. Hii ni kutokana na

wachimbaji wakubwa kuingia maeneo ya wachimbaji wadogo bila kufuata taratibu zinazotakiwa zikiwemo kulipa fidia inayostahili.

• Migogoro baina ya mtu na mtu.

5.1.2 VYANZO NA VIASHIRIA VYA MIGOGORO YA ARDHI• Sheria za ardhi kutofahamika vizuri miungoni mwa wananchi na viongozi na hivyo

kutofahamu haki na wajibu wao juu ya ardhi• Ukiukwaji wa sheria zinazosimamia ardhi kwa baadhi ya watendaji (mfano, kugawa

eneo moja kwa watumiaji wawili)• Kuendelea kupanuka kwa miji na kumeza maeneo ya vijiji• Ongezeko kubwa la wawekezaji katika ardhi, unafanya wananchi wengi kuondolewa

kwenye maeneo yao yenye rutuba pasipo kufuata utaratibu wa kuwalipa fidia stahiki.• Upanuzi wa barabara na miundo mbinu mingine, husababisha wananchi wengi

kuvunjiwa maeneo yao ya makazi.• Mitazamo hasi juu ya kundi la watu fulani na utaratibu wao wa kuzalisha mali, mfano,

ufugaji na ukulima,• Uhaba wa rasilimali ardhi katika eneo fulani huweza kuibua migogoro ya ardhi, mfano

kupungua kwa nyanda za malisho kwa upande wawafugaji, huwalazimisha kuingiza mifugo yao kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo.

• Wananchi kutoshirkishwa na kukosekana kwa uwazi juu ya usimamizi na maamuzi katika masuala yanayohusu ardhi.

• Kukosekana kwa mipango shirikishi ya matumizi bora ya ardhi

MADA YA TANO

Page 39: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 32

5.1.3 MADHARA YATOKANAYO NA MIGOGORO YA ARDHI• Uhasama, chuki na mgawanyiko miungoni mwa jamii na kukuza tofauti baina ya watu,

kikundi cha watu walio ndani ya migogoro ya ardhi.• Kusabaisha majeraha, na mara nyingine kupoteza uhai miongoni mwa watu • Kupungua kwa uzalishaji mali na mazao ya chakula kutokana na kupoteza muda mwingi

kwenye kutatua migogoro ya ardhi• Kupotea kwa Amani katika jamii husika• Kudumaza maendeleo ya taifa hadi kiwango cha mtu mmojammoja , kwa kuwa

rasilimali kubwa inatumika katika kutatua migogoro ya ardhi, na kuacha sekta zingine zikidumaa,

5.1.4 MBINU NA NJIA ZA KUZUIA MIGOGORO YA ARDHI• Kujenga uwezo wa kisheria kwa vyombo/mamlaka zinazohusika na usimamizi wa ardhi

ili viweze kusimamia kwa misingi ya haki.• Kuwezesha uundwaji na utekelezaji wa mipango shirikishi ya matumizi bora ya ardhi

vijijini• Watendaji wenye mamlaka juu ya ardhi kufuata sheria na taratibu katika kusimamia

ardhi ili kuepusha migogoro ya ardhi isiyo ya lazima• Kuepuka dalili zozote zinazoashiria mgogoro juu ya ardhi• Sheria zote zinanazosimamia ardhi zifundishwe kwa wananchi wote ili waweze kujua

haki zao na wajibu wa msingi juu ya ardhi• Kuandaa mipango bora ya matumizi ya ardhi katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kila

eneo lijulikane kwa kupimwa.• Wananchi washirikishwe katika kutoa maamuzi yanayohusiana na mustakabali wa

ardhi yao• Kuhimiza ushiriki, ushirikishwaji na uwazi katika usimamizi na maamuzi ya ardhi vijijini

5.1.4 UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHISheria za Ardhi Namba 4 na 5 za mwaka 1999 zina ainisha vyombo vya utatuzi wa migogoro ya ardhi kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa ambavyo uundwaji wake unaainishwa katika Sheria ya Mabaraza na Mahakama za Ardhi Namba 2 ya mwaka 2002. Mamlaka zinazosimamia mabaraza ya ardhi ya vijiji na mabaraza ya kata ni msajili wa vijiji na msajili msaidizi wa vijiji ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya husika. Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya yanasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa zinasimamiwa na Wizara ya Katiba na Sheria. Mamlaka zote hizi zina wajibu wa kuandaa makadirio na matumizi ya vyombo wanavyovisimamia.

5.2 VYOMBO VYA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHISheria ya Mabaraza na Mahakama za Ardhi Namba 2 ya mwaka 2002 inaainisha vyombo vya utatuzi wa migogoro kama ifuatavyo:

5.2.1 BARAZA LA ARDHI LA KIJIJIi. Maana na Muundo wa Baraza la Ardhi la Kijiji

Ni chombo cha usuluhishi wa migogoro ya ardhi ndani ya kijiji kwa kutumia taratibu za mila na desturi za eneo husika. Baraza la Ardhi la Kijiji linaundwa na wajumbe 7 ambao 3 kati yao watakuwa wanawake. Wajumbe hawa watateuliwa na Halmashauri

Page 40: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 33

ya Kijiji na kuafikiwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji.ii. Sifa za Wajumbe wa Baraza la Ardhi la Kijiji

• Awe na sifa nzuri na heshima kijijini kama mtu mwenye msimamo na mwenye kufahamu sheria za kimila za ardhi, na ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai kuhusiana na kukosa uaminifu au kukosa maadili.

• Awe raia wa Tanzania, mkazi mwenyeji wa kijiji, mwenye akili timamu na aliyetimiza umri wa miaka 18.

• Asiwe mbunge au hakimu mwenye mamlaka kwenye Wilaya ambayo ndimo limo baraza.

iii. Kipindi cha Ukomo wa Wajumbe wa Baraza la Ardhi la KijijiKila mjumbe atatumikia kwa kipindi cha miaka 3 lakini anaweza kuteuliwa tena kwa kuzingatia taratibu zilezile za awali.

iv. Majukumu ya Baraza la Ardhi la Kijiji Majukumu ya baraza ni pamoja na kupokea malalamiko yanayohusu ardhi kutoka kwa

wanakijiji, kuitisha vikao vya kusikiliza madai ya migogoro kutoka kwa walalamikaji, kusuluhisha migogoro ya ardhi iliyoletwa mbele yake kwa lengo la kufikia mapatano baina ya wahusika.

v. Vikao katika Baraza la Ardhi la Kijiji Kikao cha baraza kitakuwa na wajumbe 7 hata hivyo kikao kinaweza kufanyika kikiwa

na wajumbe wa 4 ambao kati yao 2 wawe wanawake. Baraza litamteua mmoja wa wajumbe kuwa mwenyekiti na mwingine kuwa mtunza kumbukumbu za baraza. Endapo mwenyekiti na mtunza kumbukumbu hawapo wajumbe watakaouhudhuria kikao watamteua mmoja wao kuendesha kikao.

vi. Mambo ya Kuzingatiwa wakati wa Suluhu,• Yafuatayo ni mambo makuu matatu ya kuzingatia wakati wa kutoa suluhu• Kuzingatia mila na desturi • Kuzingatia haki za asili za watu • Kuzingatia njia mbadala za utatuzi.

ANGALIZO: Hakuna utaratibu wakukata rufaa kutoka kwenye Baraza la Ardhi la Kijiji kwenda Baraza la Kata kama mwananchi hakuridhia suluhu iliyofikiwa. Kwa maana hiyo mwananchi yeyote ambaye hakuridhia suluhu kijijini, basi anaruhusiwa kwenda baraza la kata kwenda kufungua shauri upya. Sheria Namba 5 ya Ardhi ya Kijiji ya 1999 na Sheria ya Mabaraza na Mahakama za Ardhi Namba 2 ya 2002, zinayatambua mabaraza ya ardhi ya vijiji kama chombo cha utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa njia ya suluhu tu na siyo kutoa hukumu.

5.1.2 BARAZA LA KATAi. Maana na Muundo wa Baraza la Kata

Ni chombo cha utatuzi wa mashauri mbalimbali katika ngazi ya Kata kinachoundwa na wajumbe 4 hadi 8 ambapo kati yao wanawake wasipungue 3. Wajumbe wa Baraza huteuliwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata. Baraza la Kata linaundwa na Sheria ya Mabaraza ya Kata Namba 7 mwaka 1985. Hata hivyo katika utatuzi wa migogoro ya ardhi baraza huongozwa na Sheria ya Mabaraza na Mahakama za Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Namba 2 ya mwaka 2002.

Page 41: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 34

ii. Sifa za wajumbe wa Baraza la Kata• Mtu yeyote mkazi wa vijiji vinavyounda kata husika, raia wa Tanzania, aliyetimiza

miaka 18 na mwenye akili timamu.• Asiwe mbunge, mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji au Kamati ya Maendeleo ya Kata,

mwanasheria au mtu yeyote aliyeajiriwa katika idara ya mahakama.• Asiwe mtu aliyewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai ama utovu wa kukosa uaminifu.

iii. Kipindi cha Ujumbe na Majukumu ya Baraza la KataKila mjumbe atatumikia baraza kwa kipindi cha miaka 3 tokea tarehe ya kuchaguliwa kwake na kila mjumbe anaweza kuteuliwa tena kwa kuzingatia taratibu zilezile za awali. Jukumu la msingi la baraza ni kuleta amani, utulivu na mapatano katika eneo lake kwa mujibu wa Sheria za Ardhi za mwaka 1999 na Sheria ya Mabaraza na Mahakama za Ardhi ya mwaka 2002.

iv. Uongozi wa Baraza la KataBaraza litaongozwa na Mwenyekiti atakayeteuliwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Kata waliochaguliwa. Katibu wa baraza ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ambamo baraza hilo limo.

v. Vikao vya Baraza la Kata• Katika vikao vya usuluhishi vya baraza lazima liwe na wajumbe 3 na angalau mmoja

awe mwanamke.• Baraza litaweka kumbukumbu za vikao vyote.• Baraza litatakiwa kujitahidi kupata suluhu na linaweza kuahirisha kesi endapo

litafikiria kuwa kwa kufanya hivyo suluhu inaweza kupatikana.vi. Mambo ya kuzingatia wakati wa Suluhu

• Kuzingatia mila na desturi • Kuzingatia haki za asili za watu • Kuzingatia njia mbadala za utatuzi.

vii. Ukomo wa Mamlaka ya Baraza la Kata• Baraza lina ukomo wa aina mbili katika kufanya kazi zake. • Ukomo wa kieneo. Baraza lina uwezo wa kushughulikia migogoro ya mali au ardhi

iliyopo ndani ya kata tu inayohusika.• Ukomo wa kifedha. Baraza lina uwezo wa kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya

mgogoro wowote ambao mali au ardhi inayogombaniwa thamani yake haizidi shilingi milioni tatu (3000,000).

viii. Uwezo wa Baraza la KataBaraza linaweza kutoa amri za kimahakama kama zifuatazo:a. Kuagiza urejeshwaji wa ardhi iliyonyang’anywa.b. Kumtaka mtu atimize wajibu wake ndani ya mkataba.c. Kutoa amri au maagizo ya kisheria.d. Kuagiza ulipaji wa gharama zitakazokuwa zimetumiwa na atakayeshinda kesi au

mashahidi wake.e. Kutoa agizo lolote ambalo litakuwa la haki kwa uamuzi utakaotolewa.

(i) Ukataji Rufaa kutoka Baraza la KataUpande wowote ambao hautaridhika na maamuzi ya Baraza la Kata unaweza kukata rufaa katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ndani ya siku 45 tangu siku ya kutolewa uamuzi.

Page 42: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 35

5.1.3 BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA LA WILAYAi. Maana na Muundo wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya

Ni chombo cha utatuzi wa migogoro ya ardhi inayotokea ndani ya wilaya, mkoa au kanda husika. Baraza linaanzishwa na Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Ardhi. Baraza linaundwa na Mwenyekiti wa baraza na wazee wasiozidi 7 kati yao wanawake wasipungue 3

ii. Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la WilayaMwenyekiti atakuwa mwana sheria atakayeteuliwa na Waziri mwenye dhamana ya Ardhi, na kuapishwa na Mkuu wa Mkoa. Mwenyekiti atashika wadhifa huo kwa muda wa miaka 3 na anaweza kuteuliwa tena baada ya muda huo. Kazi za Mwenyekitini pamoja na kusikiliza na kutolea uamuzi migogoro ya ardhi itakayoletwa mbele ya baraza akishauriana na wazee wa baraza.

iii. Sifa za wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya• Awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, • Mwenye akili timamu, • Mkazi wa kudumu wa wilaya husika, • Mwenye umri usiopungua miaka 21 na ambaye hajawahi kutiwa hatiani kwa

makosa ya jinai hususan ya kufanya vurugu, kukosa uaminifu au tabia mbaya.• Asiwe mbunge, diwani, mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji, mjumbe wa Baraza la

Ardhi la Kijiji au Baraza la Kata.

iv. Ukomo wa Mamlaka ya Baraza la Ardhi na Nyumba la WilayaBaraza lina ukomo wa aina mbili katika kufanya kazi zake;• Ukomo wa Kieneo: Baraza lina uwezo wa kushugulikia migogoro ya mali au ardhi

iliyopo katika wilaya, mkoa au kanda kutegemea mahali baraza limeundwa na kutekeleza shughuli zake kieneo.

• Ukomo wa kifedha: Baraza lina uwezo wa kusikiliza kesi za urejeshaji mali isiyohamishika yenye thamani isiyozidi shilingi milioni Hamsini (50,000,000) na mali inayohamishika isiyozidi thamani ya shilingi milioni Arobaini(40,000,000).

v. Majukumu ya Baraza la Ardhi na Nyumba la WilayaKupokea ushahidi wa ziada kama utakuwa umeletwa, kuangalia kumbukumbu za maamuzi yaliyofanywa na Baraza la Kata, kufanya uchunguzi itakapoonekana ni lazima, upokea rufaa na kukazia hukumu kutoka kwenye Baraza la Kata.

vi. Utaratibu wa usikilizaji wa mashauri• Kesi itaendeshwa kwenye eneo la wazi. • Mlalamikaji au mlalamikiwa anaweza kujieleza mwenyewe au kuwakilishwa na

wakili au ndugu yeyote au mwanafamilia aliyeteuliwa na mhusika.• Baraza litatumia ama lugha ya Kiswahili au Kiingereza kusikiliza mashauri,

isipokuwa kumbukumbu na hukumu ya mashauri ya Baraza yataandikwa kwa lugha ya Kiingereza.

vii. Uwezo wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya kuhusu rufaaBaraza baada ya kusikiliza rufaa linao uwezo wa kuthibitisha, kutengua, kukataa au kurekebisha uamuzi uliotolewa na Baraza la Kata, kufuta shauri lililoamuliwa na Baraza la Kata, kuita na kuchunguza kumbukumbu za mashauri ya Baraza la Kata na kuagiza Baraza la Kata kupitia upya au kurekebisha uamuzi uliofanyika. Baraza litahusika kutoa sababu za kufikia uamuzi huo.

Page 43: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 36

viii. Ukataji Rufaa kutoka Baraza la Ardhi na Nyumba la WilayaUpande wowote ambao haukubaliani na maamuzi au amri ya baraza unaweza kukata rufaa Mahakama Kuu ndani ya siku 60 toka tarehe ya kusomwa hukumu, ikiwa kesi hiyo ilianzia Baraza la Kata na kwenda Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya kama rufani. Endapo shauri hilo lilianzia Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya itabidi rufani ikatwe ndani ya siku 45 kwenda Mahakama Kuu.

5.1.4 MAHAKAMA KUUi. Usikilizaji wa mashauri

Mahakama Kuu ina uwezo wa kusikiliza kwa mara ya kwanza;• Mashauri ya madai ya mali isiyohamishika yenye kiwango cha thamani inayozidi

shilingi milioni 50 na mali inayohamishika inayozidi thamani ya shilingi milioni 40.• Mashauri yote chini ya Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997, Sheria za Ardhi

za mwaka 1999 na Sheria ya Utwaaji wa Ardhi ya mwaka 1967 yanayohusisha serikali.

• Mashauri yote yanayohusiana na mashirika ya umma.• Mashauri yoyote ya ardhi chini ya sheria yoyote iliyoandikwa ambapo mamlaka

ya kusikiliza shauri hilo hayakupewa mahakama au baraza lingine.

ii. Uwezo wa Mahakama KuuMahakama Kuu ina uwezo wa kuamuru Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya kutafuta ushahidi zaidi, kukubaliana na maamuzi ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya, kubadili na, kubatilisha maamuzi ya awali, itakuwa mshauri mkuu wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya na ina uwezo wa kukagua kumbukumbu zake wakati wowote na kutoa mwongozo kwa baraza hilo.

iii. Ukataji Rufaa kutoka Mahakama Kuu.Upande wowote ambao hautaridhishwa na maamuzi ya Mahakama Kuu unaweza kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa ndani ya siku 30 kwa kuzingatia siku 14 za notisi ya kusudio la kukata rufaa.

5.1.5 MAHAKAMA YA RUFANIMtu yeyote ambaye hataridhishwa na maamuzi ya Mahakama Kuu anaruhusiwa kupeleka madai kwenye Mahakama ya Rufani. Kwa madai yoyote yanayotoka katika Baraza la Kata yatatakiwa kuambatanishwa na cheti kutoka Mahakama Kuu. Taratibu za uendeshwaji wa mashauri ya rufaa zitaongozwa na sheria na kanuni za Mahakama ya Rufani.

Page 44: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 37

6 MFUMO WA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI TANZANIA

UtanguliziMamlaka ya nchi imegawanyika katika mihimili mikuu mitatu ambayo ni Bunge, Serikali na Mahakama. Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi katika kusimamia utendaji wa serikali. Majukumu ya Bunge ni pamoja na kutunga sera, sheria na miongozo ya nchi. Serikali ni mhimili wa utendaji katika dola unaojihusisha na utekelezaji wa sera, sheria na miongozo iliyotungwa na Bunge. Mahakama ni mhimili unaotafsiri sheriazilizotungwa na Bunge na kutoa haki kwa mujibu wa sheria husika.

Mada hii ni inaonesha uhusiano uliopo katika utawala na usimamizi wa rasilimali kwa mujibu wa sheria mbalimbali zinazosimamia vyombo vya utawala nchini. Kipekee, mada hii itajikita katika kuchambua mhimili wa serikali na uhusiano uliopo baina ya serikali na wananchi na jinsi uhusiano huo unavyoweza kutumika kukuza misingi ya utawala bora, utoaji wa huduma bora kwa wananchi, utawala wa sheria, uwazi katika utendaji, maamuzi na heshima juu ya utu, haki za binadamu na masuala yote yanayohusu rasilimali.

Maana na Mamlaka ya SerikaliSerikali ni mhimili wenye mamlaka ya kutawala na kufanya maamuzi katika eneo lote la nchi kwa mujibu wa Katiba na sheriaza nchi. Kwa maana hiyo serikali inatunga na kutekeleza sheria, kanuni na miongozo katika kuendesha shughuli za ummana inatekeleza sheria zinazotungwa na Bunge. Jukumu mahsusi la serikali ni kutunza amani na usalama wa raia katika jamii.

6.1 MGAWANYO WA SERIKALIMuundo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umegawanywa katika sehemu kuu mbili; Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.

i. Serikali KuuIna mamlaka na wajibu wa kutunga sera na miongozo ya shughuli mbalimbali za utawala na maendeleo ya nchi na pia kuhakikisha usalama, ulinzi na amani kwa raia wake.

ii. Serikali za MitaaMadhumuni ya kuwepo kwa serikali za mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi. Vyombo vya serikali za mitaa vitakuwa na haki ya kushiriki na kuwashirikisha wananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika maeneo yao.

6.2 MAKUNDI MAKUU SERIKALI ZA MITAA;• Serikali za Mitaa za Mamlaka za Miji ambazo ni Mamlaka za Jiji, Manispaa na Miji. • Serikali za Mitaa za Mamlaka za Wilaya ambazo ni Halmashauri za Wilaya, Mamlaka za Miji

Midogo na Halmashauri za Vijiji.

Majukumu ya serikali za mitaani kutoa huduma za jamii, kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa wananchi, kuimarisha demokrasia katika eneo lake na kuleta maendeleo kwa wananchi.

6.3 UHUSIANO KATI YA SERIKALI KUU NA SERIKALI ZA MITAAUhusiano uliopo kati ya serikali kuu na serikali za mitaa ni katika kutekeleza majukumu na madaraka yake, kuhakikisha kuwa mamlaka za serikali za mitaa zinatekeleza sera, sheria na

MADA YA SITA

Page 45: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 38

taratibu zilizopo, kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya serikali za mitaa kutekeleza majukumu yake, na kupitia mipango na makisio ya bajeti za Halmashauri za Wilaya kwa mujibu wa sera na vipaumbele vya taifa.

6.4 NGAZI ZA UTAWALA ZA SERIKALI KUUKatika kutekeleza madaraka na majukumu yake, serikali kuu imegawanywa katika ngazi kuu nne ambazo ni Taifa, Mkoa, Wilaya na Tarafa.

i. Ngazi ya Taifa Rais ndiye kiongozi mkuu katika ngazi hii ambaye hutekeleza majukumu yake kwa kushauriana na kushirikiana na Baraza la Mawaziri.

ii. Ngazi ya MkoaMkuu wa Mkoa ndiye mwenye dhamana ya kuongoza mkoa akishauriwa na kushirikiana na sekretarieti ya mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala wa mkoa katika kutekeleza majukumu yake.

iii. Ngazi ya WilayaMkuu wa Wilaya ndiye mwenye dhamana ya kuongoza wilaya akishauriana katika kutekeleza majukumu yake na Katibu Tawala wa Wilaya.

iv. Ngazi ya TarafaNgazi hii ni kiungo kati ya serikali kuu, Halmashauri za Wilaya na kata. Madaraka na majukumu ya ngazi hii hutekelezwa na Ofisa Tarafa.

6.5 NGAZI ZA UTAWALA SERIKALI ZA MITAAKatika kutekeleza madaraka na majukumu yake, serikali za mitaa zimegawanywa katika ngazi kuu tatu ambazo ni Halmashauri ya Wilaya, Kata, na Kijiji.

i. Ngazi ya Halmashauri ya WilayaHalmashauri ya wilaya ni mamlaka ya utendaji katika ngazi ya serikali za mitaa inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Madiwani akisaidiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ambaye pia husimamia na kuongoza idara mbalimbali zinazotekeleza masuala ya kimaendeleo kwenye wilaya husika. Idara hizi ni pamoja na Ardhi, Maliasili na Mazingira, Maendeleo ya Jamii, Kilimo, Elimu na Afya.

ii. Ngazi ya KataNi ngazi ya uratibu wa shughuli za maendeleo kutoka katika vijiji mbalimbali vinavyounda kata husika. Uratibu wa shughuli za maendeleo hufanywa na Kamati ya Maendeleo ya Kata. Wajumbe wa kamati hii ni;• Diwani wa kuchaguliwa katika kata husika ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa kamati.• Wenyeviti wa vijiji kwenye kata husika.• Diwani wa viti maalum katika kata husika • Wajumbe wengine waalikwa ambao hawaruhusiwi kupiga kura katika kufikia maamuzi.

Wajumbe hawa ni pamoja na wataalam katika ngazi ya kata, asasi za kiraia na makundi mengine yanayojihusisha na masuala ya maendeleo kwenye kata husika.

• Ofisa Mtendaji wa kata husika ndiye Katibu wa Kamati ya Maendeleo ya Kata

Vikao vya kamati hupaswa kuitishwa na kufanyika siyo chini ya mara nne kwa mwaka; ingawa pia kamati inaweza kuitisha vikao vingine vya dharura pale itakapoonekana kuna haja ya kufanya hivyo.

Page 46: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 39

iii. Ngazi ya KijijiKijiji ni ngazi ya utawala inayotambuliwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile ni mamlaka inayotambulika kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa. Kijiji pia kinaundwa na vitongoji visivyozidi vitano kulingana na aidha idadi ya kaya au kutokana na mpangilio wa kijiografia kama ambavyo itaamuliwa na Halmashauri ya Kijiji na kuthibitishwa na Halmashauri ya Wilaya.

6.6 MUUNDO WA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI KATIKA NGAZI YA KIJIJIMasuala ya utawala na usimamizi wa rasilimali katika ngazi ya kijiji uko chini ya vyombo vikuu viwili ambavyo ni: Mkutano Mkuu wa Kijiji na Halmashauri ya kijiji

i. Mkutano Mkuu wa Kijijia. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kijiji

Ni wakazi wote wa kijiji wenye umri usiopungua miaka 18 na wenye akili timamu. Kila mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Kijiji bila kujali jinsi au hadhi yake katika jamii ana haki sawa ya kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kijiji.

b. Mamlaka ya Mkutano Mkuu wa KijijiMkutano Mkuu wa Kijiji ni mamlaka ya juu kabisa kuhusiana na masuala yote ya uundaji wa sera ya jumla kuhusu mambo ya kijiji kama ipasavyo.

Mkutano Mkuu wa Kijiji utakuwa na wajibu wa kuchagua Halmashauri ya Kijiji pamoja na uwezo wa kumwondoa kwenye halmashauri mjumbe yeyote, au wajumbe wote, na ina madaraka ya kutekeleza mambo yoyote yale uliyopewa kuyatekeleza kwa mujibu wa sheria hii au sheria andikwa yoyote nyingineyo”.

Mkutano Mkuu wa Kijiji ni chombo kinachohusika na mambo ya sera, sheria, usimamizi na kufanya maamuzi kuhusu rasilimali za kijiji, ikiwemo ardhi, misitu, vyanzo vya maji, hifadhi za misitu na wanyamapori.

c. Vikao vya Mkutano Mkuu wa KijijiVikao vya Mkutano Mkuu wa Kijiji ndiyo sehemu pekee ambapo maamuzi ya kijiji hufikiwa na wananchi wote wenye sifa za kuwa wajumbe wa mkutano mkuu. Kuna aina kuu 3 za vikao vya Mkutano Mkuu wa Kijiji;• Mkutano Mkuu wa kawaida:

Hiki ni kikao cha lazima cha Mkutano Mkuu wa Kijiji ambacho hutakiwa kufanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu (3), kwa maana hiyo ni jumla ya vikao vinne (4) kwa mwaka. Sheria haitaji akidi maalum ya kikao cha Mkutano Mkuu wa Kijiji, hata hivyo ni vyema kijiji kikajiwekea akidi maalum ili kuzuia uwezekano wa maamuzi ya msingi kufanywa na watu wachache mno kwa niaba ya wanakijiji walio wengi.

• Mkutano Mkuu wa dharura: Hiki ni kikao cha dharura cha Mkutano Mkuu wa Kijiji kinaweza kikaitishwa wakati wowote pale itakapoonekana kuwa kuna sababu maalum ya kufanya hivyo.

• Mkutano Mkuu wa uchaguzi: Huu ni mkutano ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano, kwa lengo la kuchagua viongozi wa kijiji.

d. Majukumu ya Mkutano Mkuu wa KijijiKupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kijiji, itakayotolewa na serikali ya kijiji, na kupitisha taarifa ya mapato na matumizi ya fedha ya kijiji, na

Page 47: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 40

mapendekezo ya kodi, ushuru na vyanzo vingine vya kuongeza mapato ya kijiji.

Majukumu mengine ni kupokea na kujadili taarifa ya makusanyo ya fedha za kodi na ushuru na mapato mengine yanayokusanywa kijijini na vyombo vya serikali za mitaa na serikali kuu, kutunga sheria ndogondogo,na kuyafanyia uamuzi masuala yahusuyo ugawaji na matumizi ya rasilimali za kijiji kama vile ardhi.

ii. Halmashauri ya KijijiHalmashauri ya Kijiji ni chombo kilichopewa mamlaka yote ya utendaji kuhusiana na masuala yote yanayohusu kijiji. Halmashauri ya Kijiji huchaguliwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji na kwa maana hiyo huwajibika kwa Mkutano Mkuu wa Kijiji katika utendaji na utekelezaji wa majukumu yake.

a. Wajumbe wa Halmashauri ya KijijiIdadi ya wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji inatakiwa isipungue 15 na isizidi 25. Wajumbe hawa ni pamoja na; Mwenyekiti wa Kijiji; Wenyeviti wa Vitongoji vyote ndani ya kijiji husika; na Wajumbe wengine wanaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji ambao robo ya idadi yao ni lazima wawe wanawake. Ofisa Mtendaji wa Kijiji ndiye Katibu wa Halmashauri ya Kijiji.

b. Sifa za Wajumbe wa Halmashauri ya KijijiAwe ametimiza umri wa miaka 21, ni mmoja kati ya wanafamilia iliyoko ndani ya kijiji na mkazi wa kudumu kwenye kijiji husika, awe anajua kusoma na kuandika aidha kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza, na awe na njia halali za kujipatia kipato katika kuendesha maisha yake.

c. Vikao vya Halmashauri ya KijijiKutakuwa na kikao kimoja cha lazima kila mwezi, ingawa kuna fursa ya kuitisha vikao kunapotokea suala la dharura. Kikao halali kinatakiwa kuwa na nusu ya wajumbe wote wa halmashauri. Wataalam mbalimbali wanaweza kualikwa kuhudhuria vikao vya halmashauri ili kutoa ushauri wa kitaalamu isipokuwa hawatakuwa na haki ya kupiga kura. Mjumbe yeyote wa halmashauri atakayeshindwa kuhudhuria vikao 3 mfululizo pasipo taarifa atakuwa amepoteza nafasi yake ya ujumbe.

d. Majukumu ya Halmashauri ya KijijiKupokea na kufanyia kazi taarifa za mikutano ya vitongoji na kamati mbalimbali pamoja na kuainisha masuala yanayohitaji maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Kijiji, kutekeleza (Pale inapofaa) maagizo na mapendekezo ya ngazi nyingine za utawala na utendaji, kwa mfano Kamati ya Maendeleo ya Kata, Halmashauri ya Wilaya. Majukumu mengine ni kuandaa taarifa ya mapato na matumizi, kubuni sera, mipango ya maendeleo na mwelekeo wa kijiji, kutunga sheria ndogondogo, kuweka mikakati madhubuti ya usimamizi wa rasilimali zilizondani ya kijiji.

e. Majukumu ya Mwenyekiti wa KijijiMwenyekiti wa kijiji atakuwa na majukumu kama yafuatayo:• Atakuwa ndiye mkuu wa halmashauri ya kijiji• Atakuwa na wajibu wa kuitisha na kuongoza mikutano yote ya serikali ya kijiji, na

mikutatano mikuu ya kijiji lakini, endapo mweyekiti hayupo kwenye mkutano wowote wajumbe wa mkutano wanaweza kuteua mwenyekiti wa muda

• Atakuwa ndiye mwakilishi wa kijiji kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata

Page 48: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 41

• Atawahudumia wanakijiji wote kwa usawa bila kujali tofauti zao za kisiasa, kijinsia au kidini n.k.

• Atakuwa mfano wa uongozi bora na utendaji bora wa kazi, kwa kuwa na shughuli zake mwenyewe za kujitegemea ambazo zinaweza kuigwa na wanakijiji anaowaongoza.

f. Majukumu ya Mtendaji wa KijijiOfisa Mtendaji wa Kijiji ni mtumishi wa halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji na anawajibika katika Halmashauri ya kijiji katika utendaji wake.

Majukumu makuu ya Ofisa Mtendaji wa Kijiji ni kama ya yafuatayo;• Atakuwa ndiye mtendaji mkuu wa shughuli zote za kijiji• Atakuwa ndiye mwandishi na mtunzanji wa kumbukumbu zote za vikao vya mikutano

ya kijiji, pamoja na rejesta ya kijiji na nyaraka zote muhimu za kijiji ikiwa pamoja na hati za kuandikisha kijiji na vyeti vya ardhi vya kijiji.

• Atakuwa ndiye mshauri mkuu wa kubuni na kutekeleza miradi ya maendeleo kijijini• Atakuwa msimamizi mkuu wa utekelezaji wa miradi yote iliyo kubaliwa na serikali ya

kijiji, pamoja na miradi mingine inayo tekelezwa katika eneo la kijiji chake.• Ataratibu shughuli zote za maofisa wa kisekta kijijini• Atawajibika kuwasilisha taarifa muhimu kuhusu kijiji chake kwa Ofisa Mtendaji wa

Kata

g. Wajibu na haki wa mwananchi/raia katika kijiji.Mwanakijiji/ raia kama mkazi wa eneo la kijiji ana haki na wajibu kwa kijiji chake kama inavyoonesha hapa chini:• Kuhudhuria mikutano yote katika kitongojina kijiji na kuhakikisha kuwa mikutano

inafanyika kila baada ya muda uliopangwa.• Kulinda mali, rasilimali za umma na kupambana na kila aina ya uovu ikiwemo

ubadhirifu, wizi, rushwa na mengineyo• Kumwondoa kiongozi au viongozi wasiowajibika kwa kumpigia kura ya hapana• Kujenga na kuimarisha mshikamano uliopo katika jamii yake• Kushiriki kupanga, kusimamia na kuthathimini na kuhoji matokeo ya miradi yote

katika kitongoji na kijiji • Kushiriki katika kupiga na kupigiwa kura kugombea nafasi za uongozi• Kuheshimu kiongozi au viongozi wake

iii. Kamati za Halmashauri ya KijijiHalmashauri ya Kijiji inaweza kuanzisha kamati za kudumu na kamati maalum pale itakapoonekana kuwa kuna umuhimu na ulazima wa kufanya hivyo katika utekelezaji wa majukumu yake kwa manufaa ya kijiji. a. Kamati za Kudumu

Zipo kamati tatu za kudumu ambazo ni Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango; Kamati ya Huduma za Jamii na Shughuli za Kujitegemea; na Kamati ya Ulinzi na Usalama. Kamati hizo zinaundwa na wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji.

b. Kamati MaalumKamati maalum zinaundwa na Halmashauri ya Kijiji kwa kushirikiana na Mkutano Mkuu wa Kijiji. Wajumbe wa kamati maalum si lazima watokane na wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji pekee bali wanaweza kuteuliwa kutoka miongoni mwa wanavijiji wenye uwezo wa kutekeleza majukumu ya kamati husika.

Page 49: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 42

• Madaraka na Majukumu ya KamatiKamati hazina madaraka ya mwisho katika kufanya maamuzi isipokuwa ni kama ‘wakala’ wa Halmashauri ya Kijiji katika kutekeleza majukumu yake. Lengo kuu la kamati ni kurahisisha kazi za halmashauri, kuangalia kwa undani na umakini masuala na mambo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi au maamuzi na halmashauri.

iv. KitongojiKitongoji ni sehemu ya kijiji na sio ngazi ya utawala inayojitegemea na hakina maamuzi juu ya usimamizi wa rasilimali nje ya mfumo wa utawala wa kijiji. Mkutano Mkuu wa Kijiji una madaraka ya kuamua idadi ya vitongoji katika kijiji ilimradi visizidi vitongoji vitano. Madhumuni ya kuwepo kwa vitongoji ni kupeleka shughuli za serikali ya kijiji karibu na wakazi na sio kugawa kijiji katika maeneo madogomadogo ya utawala.

Mkutano Mkuu wa Kitongoji huongozwa na Mwenyekiti wa Kitongoji ambaye huchaguliwa na wakazi halisi wa Kitongoji hicho. Dhumuni la Mkutano huu ni kuwapa wananchi fursa kujadili kero na changamoto zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku. Kufanya hivyo itawawezesha wananchi kupanga mipango yenye kuleta ufumbuzi na kuondoa kero zinazowakabili kwa kutumia mfumo shirikishi wa fursa na vikwazo.• Kitongoji ni sehemu ya kijiji • Kitongoji sio ngazi ya utawala inayojitegemea • Kuwepo kwa kitongoji ni kupeleka shughuli za serikali ya kijiji karibu na wakazi/wanakijiji.• Kila kijiji huwa na vitongoji visivyozidi vitano (5) • Mkutano Mkuu wa Kijiji una madaraka ya kuamua idadi ya vitongoji katika kijiji

Majukumu na mamlaka ya Mwenyekiti wa Kitongoji• Huchaguliwa na wakazi wa kitongoji katika Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa kitongoji • Ni mjumbe wa halmashauri ya kijiji kwa wadhifa wake • Kiongozi miongoni mwa viongozi wa kijiji • Kiungo kati ya halmashauri ya kijiji na wakazi wa kitongoji • Kuimarisha umoja na mshikamano kati ya serikali ya kijiji na wanakijiji • Kuwasilisha maoni, mapendekezo na mahitaji ya kitongoji kwa halmashauri ya kijiji • Kuitisha mikutano ya wakazi wa kitongoji pale anapoona inafaa • Mikutano ya kitongoji haina uwezo wa maamuzi inaendeleza mijadala na kuandaa maoni

na mapendekezo tu• Kuhamasisha wakazi wa kitongoji kwenye maendeleo• Kuwasilisha taarifa za halmashauri ya kijiji kwa wakazi wa kitongoji.

Page 50: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 43

7 SERA NA SHERIA ZINAZOHUSU USIMAMIZI WA MISITU

UTANGULIZITanzania ina rasilimali kubwa za misitu. Misitu nchini Tanzania imegawanyika katika makundi makuu manne ambayo ni:i Misitu ya Hifadhi ya Taifa;ii Misitu ya Halmashauri ya Wilaya;iii Misitu ya hifadhi ya vijiji; naiv Misitu Binafsi. Tanzania inaunda sheria, kanuni na taratibu mbalimbali ili kusimamia sekta ya misitu. Sheria, kanuni na taratibu zilizopo zinalenga kuhakikisha kuwa sekta ya misitu inalindwa na mazao ya misitu yanatumika kufikia maslahi ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

7.1. SERA YA TAIFA YA MISITU YA MWAKA 1998.Sera inatoa wito na kuhamasisha jamii katika usimamizi shirikishi wa misitu. Hii inafanyika kwa njia ya kuanzisha mfumo wa usimamizi wa pamoja wa misitu ya hifadhi na usimamizi wa jamii wa misitu nje ya hifadhi. Lengo la usimamizi shirikishi wa misitu ni kujenga mazingira mazuri kwa ajili ya usimamizi na maendeleo ya sekta ya misitu na mgawanyo wa majukumu kati ya jamii na Halmashauri za Wilaya. Inaongeza nafasi kwa ajili ya ushiriki mpana wa watu katika usimamizi wa misitu na mazao yake.

7.2. SHERIA YA MISITU NAMBA 14 YA MWAKA 2002Hii ndiyo sheria mama inayotoa utaratibu mzima wa usimamizi wa misitu nchini. Sheria hii inalenga kuimarisha usimamizi wa misitu katika ngazi ya jamii ili kutekeleza Sera ya Misitu ya Mwaka 1998 na dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa Serikali za Mitaa.

Kifungu cha 22(1) cha sheria hii kinampa Waziri husika, kutangaza katika Gazeti la Serikali eneo lolote lenye viumbe hai kuwa mamlaka ya hifadhi za misitu. Sheria inataja kanuni mbalimbali zitumikazo katika kutunza na kusimamia misitu na inatilia mkazo ufanywaji wa tathmini ya athari za mazingira kwa miradi yoyote ile katika maeneo ya misitu. Misitu inatajwa kuwa ni rasilimali ya taifa ambayo iko chini ya Wizara na uvunaji wake lazima uwe kwa mujibu wa leseni na vibali husika.

Haki na Wajibu wa Wadau MbalimbaliMpango Shirikishi wa Usimamizi wa Misitu unatoa haki na wajibu kwa wadau wote wanaohusika kama vile Halmashauri za Wilaya, Vijiji na wananchi. Misitu sasa inamilikiwa kwa pamoja kupitia Halmashauri za Vijiji pamoja na mamlaka za wilaya. Mpango huo unatoa haki na wajibu kwa vijiji kama ifuatavyo:• Wanakijiji wanaweza kuvuna rasilimali za misitu ili mradi matumizi ya Misitu yawe endelevu;• Kamati ya Maliasili inalazimika kufuatilia hali ya misitu pamoja na matumizi yake ili kuhakikisha

kuwa matumizi hayazidi viwango vifaavyo; na• Serikali ya kijiji na Kamati ya Maliasili wanaweza kutumia sheria ndogo ndogo pamoja na

vibali, ada na faini ili kudhibiti matumizi ya rasilimali za misitu.

MADA YA SABA

Page 51: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 44

3.2 Makosa na adhabu katika sheria za MisituSheria ya Misitu Namba 14 ya Mwaka 2002 imeainisha makosa na adhabu mbalimbali. Makosa na adhabu hizi ni kama ifuatavyo:

Kwa mujibu wa Sheria ya Misitu Namba 14 ya Mwaka 2002, ni kosa kwa mtu yeyote yule asiye na kibali au ruhusa kuingia katika hifadhi ya msitu, kutenda tendo lolote lile lililoanishwa katika kifungu cha 26 cha sheria hii; kuzuia njia au barabara au mkondo wa maji; kufunika kisiki cha mti kwa majani au udongo au kwa njia yoyote ile, kuharibu au kuondoa kisiki hicho; na kuharibu, kuchafua, kubadilisha, kuweka wigo, alama ya mpaka au notisi au ubao wa matangazo katika mti. Sheria hii inamtwika mzigo mtuhumiwa wa kosa jukumu la kuthibitisha kutokutenda kosa.

Hata hivyo sheria inasema wazi kuwa kitendo cha mtu kukutwa katika maeneo ya hifadhi ya msitu na kifaa chochote kile kinachoweza kutumika kukata, au kuchukua zao lolote la msitu ni kutenda kosa. Sheria inamruhusu Mkurugenzi wa Misitu kutoa tamko katika gazeti la serikali juu ya kutokuwa kosa kwa mtu yeyote yule anayekutwa na vifaa hivvyo katika hifadhi nzima au sehemu yake.

Ni lazima tamko hilo liwekwe katika sehemu iliyo wazi kwenye Ofisi za Halmashauri za Serikali za Mitaa/Vijiji ambako hifadhi husika ipo au iko karibu yake na litangazwe katika namna ambayo ni ya kawaida katika eneo hilo ili kuwawezesha wenyeji na wakazi wa eneo hilo kupata taarifa hiyo.

Vilevile, kama mnyama yoyote wa kufugwa akikutwa anachungwa au anaingia katika hifadhi yoyote ile ya msitu, basi mnyama huyo atachukuliwa kuwa alichungwa katika hifadhi hiyo. Mwenye mnyama huyo atahesabiwa kuwa ndiye aliyeruhusu kuchungwa au kuingia kwake katika hifadhi hiyo kinyume cha sheria. Kukiuka masharti ya kifungu 84(1) (a)-(e) na 84(2)-(3) ni kosa la jinai na mtu huyo pindi akikutwa na hatia atatozwa faini kati ya shilingi elfu thelathini na shilingi milioni moja au kifungo kisichozidi miaka miwili au kupewa adhabu ya kifungo na faini.

Kwa mujibu wa kifungu cha 85 ni kosa la jinai kwa mtu yeyote asiye na leseni au kibali kutoka mamlaka husika, kuangusha, kukata, kuharibu, kuondoa au kuuza mti uliotunzwa au kuhifadhiwa au sehemu yake kutoka katika ardhi isiyohifadhiwa. Adhabu ya kosa hili ni faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichozidi mwaka mmoja. Mwenye hatia anaweza kupewa adhabu zote mbili yaani faini na kifungo.

Kifungu cha 86 cha sheria hii kinatamka kuwa ni kosa la jinai kwa mtu yeyote yule, bila ruhusa au kibali kutoka kwa mamlaka husika, na kwa mujibu wa sheria hii; kuchuma, kuondoa, na kuchukua sampuli au kwa namna yoyote ile na kwa makusudi kutoa sumu, kuharibu au kuteketeza mimea-pori iliyoorodheshwa; kuonyesha kwa ajili ya kuuza au kununua au kuwa au kumiliki mimea pori iliyooredheshwa; kuuza nje ya nchi au kujaribu kuuza nje ya nchi mimea pori au sehemu yake au mbegu zake;

Adhabu ya kosa hili ni faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi sita na kutozidi miaka miwili. Mwenye hatia anaweza kupata adhabu zote mbili za faini na kifungo. Kifungu cha 87 kinataka makosa yote yanayohusiana na

Page 52: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 45

wanyamapori yashughulikiwe kwa mujibu wa sheria zinazohusika na mambo ya wanyamapori na sheria nyinginezo.

Kwa mujibu wa kifungu cha 88 ni kosa la jinai kwa mtu yeyote yule, asiye na ruhusa au baraka

za mamlaka husika, kukutwa na mazao ya misitu, isipokuwa kama ataweza kuthibitisha kuyapata kwake kihalali au kwa namna isiyo na kosa. Jukumu la kuthibitisha kutokuwa na hatia liko kwake. Adhabu ya kosa hili ni faini isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja. Kwa mujibu wa kifungu cha 89 ni kosa la jinai kwa mtu yeyote, asiye na ruhusa halali au sababu:

Kuvuna mazao ya misitu kwa mujibu wa sheria hii; Kuendesha au kusababisha kuendeshwa kwa gari na kuchukua, kubeba, kuondosha, au

kusafirisha mazao ya misitu kinyume na sheria hii; Kuchukua, kubeba au kuondosha kwa njia isiyo kwa chombo cha moto mazao yoyote ya

misitu kinyume na sheria hii; Kutaka kuuza, kuuza au kununua mazao ya misitu kinyume cha sheria hii; Kuhifadhi mazao ya misitu kinyume cha sheria hii; Kuweka alama za ubora na viwango katika mbao yoyote ile wakati si mtu mwenye dhamana

hiyo; na Kuuza nje ya nchi au kuiingiza zao la misitu katika mauzo ya nje, ambalo uuzaji wake nje ya

nchi unahitaji cheti husika cha uuzaji nje, bila ya kuwa na cheti sahihi cha uuzaji nje.

Dhamana au jukumu la kuthibitisha kutokuwa na hatia kwa mtuhumiwa liko kwa mtuhumiwa. Adhabu ya kosa au makosa haya ni faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja ama kifungo kisichozidi miaka miwili au adhabu zote mbili. Kifungu cha 90 kinatamka kuwa ni kosa la jinai kwa mtu yeyote yule kufanya mambo yafuatayo:

Kughushi, kubadilisha, kuharibu au kufuta au kuharibu stempu, alama, leseni, kibali, cheti, ruhusa, au risiti iliyotumika au kutolewa kwa mujibu wa sheria hii au kanuni, amri, au taarifa iliyotolewa au kutungwa kwa mujibu wa sheria hii;

Kwa udanganyifu na bila ruhusa au mamlaka halali kutumia au kutoa stempu, alama, leseni, kibali, cheti, ruhusa, au risiti iliyotumika au inayokusudiwa kutumika au kutolewa kwa mujibu wa sheria hii au kanuni, amri, au taarifa iliyotolewa au kutungwa kwa mujibu wa sheria hii;

Kuweka alama kwenye mbao, iwe mbao hiyo imewekwa alama na mweka alama aliyeruhusiwa

au mkaguzi au hapana, au kuweka alama sawa na ile inayotakiwa na sheria hii au sheria ndogo iliyotungwa kwa mujibu wa sheria hii na kuweza kuifanya kuchukuliwa kuwa ni alama inayotakiwa na sheria hii.

Pindi akikutwa na hatia mtuhumiwa atapigwa faini isiyopungua shilingi milioni moja na kutozidi shilingi milioni tatu au kifungo kisichopungua mwaka mmoja na kisichozidi miaka miwili. Mahakama inaweza kumpa adhabu zote mbili yaani faini na kifungo.

Kifungu cha 91 kinaweka wazi kuwa mtu yeyote ambaye bila ruhusa halali ya kisheria: Anawasha, au kusaidia kuwasha au kutumia au kuchochea au kuongeza mafuta katika moto

au kusababisha mambo haya kutokea; Anaacha bila uangalizi moto ambao bila ruhusa au kwa ruhusa amewasha au amesaidia

Page 53: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 46

kuuwasha au kutumia, kuchochea, au kuongeza mafuta bila kuhakikisha kuwa moto huo umezimwa kabisa;

Ameshindwa kufuata au kutekeleza amri halali iliyotolewa kwake kuhusiana na Sehemu ya Tisa ya sheria hii: ana hatia ya kosa na pindi atakapotiwa hatiani atatakiwa kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na kutozidi shilingi milioni moja au adhabu ya kifungo kisichozidi mwaka mmoja ama kupewa adhabu zote mbili.

Kifungu cha 91(2) kinatamka wazi kuwa mtu yeyote yule ambaye kwa makusudi na kwa kinyume cha sheria anawasha moto katika hifadhi ya msitu, shamba la misitu, miti iliyomea, mche, vichaka, viwe au visiwe ni vya asili anatenda kosa la jinai na pindi akikutwa na hatia atapewa adhabu kama ilivyoanishwa na kifungu cha 321 cha Sheria ya Makosa ya Jinai.

Pia ni kosa kutenda kosa hilo katika misitu iliyo katika ardhi ya kijiji ambayo inamilikiwa na mtu mmoja au watu wengi kwa mujibu wa hati miliki ya ardhi ya kimila; na Misitu katika ardhi ya jumla au ya kijiji ambayo umiliki wake ni kwa mujibu wa hati iliyotolewa kwa mtu au kampuni au ushirika kwa ajili ya kuitunza kwa mujibu wa sheria hii.

Page 54: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 47

8. SHERIA ZA WANYAMAPORI

UTANGULIZISekta ya wanyamapori ni chanzo kikubwa cha fedha za kigeni na ajira nchini lakini bado maendeleo yake ni duni ikilinganishwa na umuhimu wake. Kwasasa uhifadhi na matumizi ya wanyamapori kupitia shughuli za utalii, uwindaji, na ukamataji wa wanyamapori huchangia tabkribani asilimia 25 ya fedha za kigeni za nchi.

Toka siku za mwanzo za uhuru, pamoja na changamoto kadhaa, Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuhifadhi mazingira na wanyamapori. Tanzania imetenga takribani asilimia 30 ya ardhi yake kwa ajili ya uhifadhi wa maliasili mbalimbali ikiwemo misitu, mbuga za wanyama, mapori ya hifadhi, mapori ya akiba na hifadhi za jamii za wanyamapori.

Sera na sheria zinazosimamia sekta ya wanyamapori nchini zinatoa fursa kwa wananchi kushiriki katika usimamizi wa wanyamapori. Mathalani, Sheria ya Wanyamapori Namba 5, ya Mwaka 2009 inaruhusu kijiji/vijiji kuanzisha Jumuiya za Usimamizi wa Wanyampori (WMAs) katika ardhi za vijiji. Hii inalenga kutoa fursa kwa wananchi kunufaika moja kwa moja na rasilimali hizi. Sheria inatoa fursa hii ili kuwezesha vijiji kuendelea kupata faida za kiuchumi kutokana na wanyamapori na hivyo kuleta maendeleo vijijini. Pia, sheria inaruhusu kuanzishwa kwa Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu ambayo yamekuwa chini ya usimamizi wa Serikali kwa kuwashirikisha wananchi. Pamoja na ijtihada hizo, mamlaka mbalimbali zenye dhamana ya kuhifadhi wanyamapori kupitia programu mbalimbali zimekuwa zikiwashirikisha wananchi katika uhifadhi na usimamizi wa wanyamapori.

MADA YA NANE

Page 55: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 48

Page 56: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 49

Pia, Sera ya Wanyamapori inahimiza shughuli za uhifadhi wa wanyamapori na maendeleo ya kijiji/vijiji kwa: Kukuza matumizi halali ya wanyamapori na mazao yake; na Kuhimiza biashara halali na endelevu ya wanyamapori na mazao yake kutoka kwenye Mapori

ya Akiba, Mapori Tengefu na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa na hivyo kuwapatia wanyamapori thamani kubwa ya kibiashara huku yakizingatiwa matumizi endelevu ya aina za wanyama wauzwao.

Ingawa Serikali ina mikakati shirikishi inayoendelea kama vile Uhifadhi wa Kijamii (CBC), (Idara ya Wanyamapori), Ujirani Mwema (TANAPA), na Maendeleo ya Jamii (Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro), namna na kiwango cha ushiriki wa wananchi bado havijakidhi mahitaji na kuwafanya wananchi na jamii husika kama wadau wa kweli wa rasilimali hizi.

8.1 SERA NA SHERIA MBALIMBALI ZA WANYAMAPORI

8.1.1. SERA YA WANYAMAPORI 2007Sera hii, kwa ujumla wake, inalenga kuifanya jamii iweze kushiriki katika kuhifadhi maliasili za wanyamapori na kufaidika nazo zaidi. Sera inatoa fursa hii kwa jamii kupitia kuundwa kwa Hifadhi za Wanyamapori za Jamii (WMAs) ambazo zitatoa fursa zaidi kwa jamii kufaidika kiuchumi na rasilimali za wanyamapori zilizopo kwenye maeneo yao. Sera hii inapeleka madaraka ya kuhifadhi, kutumia na kufaidika na rasilimali za wanyamapori kwenye ngazi za kijamii (ugatuzi) kama inavyotakiwa na Sheria za Serikali za Mitaa (1982). Sera hii pia inatoa fursa kwa sekta binafsi kutunza na kuendeleza rasilimali za wanyamapori kupitia kwenye ranchi, sehemu salama za kutunzia wanyama mashamba binafsi, bustani za wanyama.

8.1.2. SHERIA YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI NAMBA 5 YA MWAKA 2009Sheria hii inahusu ulinzi na utunzaji wa wanyamapori walio nje ya Hifadhi za Taifa na Eneo la Hifadhi la Ngorongoro. Sheria hii imechukua nafasi ya iliyokuwa Sheria ya Wanyamapori 1974. Inatamka wazi wanyamapori ni mali ya umma chini ya Rais kama mdhamini tu. Inatoa fursa kwa sekta binafsi na wananchi kushiriki kwenye kutunza, kuhifadhi na kunufaika na wanyamapori. Ushiriki wa jamii katika kuhifadhi na kulinda wanyamapori ni kupitia WMAs (kifungu cha 33) Sekta binafsi inaweza kushiriki kupitia bustani za wanyama, mashamba ya wanyamapori na, sehemu salama za kutunzia wanyama.

Nani anamiliki wanyamapori?Kwa ujumla, maliasili zote ni Mali ya jamii nzima lakini zimekwa chini ya Raisi kama msimamizi mkuu. Kulingana na kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori, wanyamapori wote na mali ya jamii na wapochini ya Raisi kama msimamizi kwa niaba ya watanzania wote.

Mtu binafsi anaweza akamiliki wanyamapori kama atafuata taratibu zifuatazo za kisheria kama zinavyoanishwa chini ya kifungu cha 4 (2)-(4) cha Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori. Kifungu cha 4(3) kinasema inapotokea mtu amemchua mnyamapori kwa kufuata taratibu za kisheria anakuwa mmiliki halali, kwa kupata kibali au ruhusa inayotolewa chini ya Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori. Kifungu cha 4 (4) kinasema mtu anaweza kuwa mmiliki halali wa mnyamapori kama alikuwa anamiliki mnyama huyo kihalali kabla ya kutungwa kwa sheria hii.

Page 57: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 50

8.1.3 SHERIA YA WANYAMAPORI NAMBA 5 YA MWAKA 2009Wanyamapori kama rasilimali zinginezo, wanahitaji kuhifadhiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa katika sheria za nchi. Sheria inaweka utaratibu wa uhifadhi, ulinzi na utunzaji wa wanyamaproi katika maeneo tengefu na kuainisha mamlaka za usimamizi wa wanyamapori, maeneo tengefu ya wanyamapori na taratibu za utalii na uvunaji wa wanyamapori.

Maana ya WanyamaporiSheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009 inatafsiri wanyamapori kuwa ni wanyama, mimea na viumbe vingine vidogovidogo vilivyoko kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viumbe hao ikiwa ni pamoja na mfumo mzima wa ikolojia ya viumbe hao.

Aina za Hifadhi za WanyamaporiSheria ya Wanyamapori inaainisha aina 5 ya hifadhi za wanyamapori ambayo ni Hifadhi za Taifa, Mapori tengefu, Mapori ya akiba, Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori.

Mamlaka za Usimamizi wa Wanyamapori

Mamlaka zinazosimamia wanyamapori ni:• Wizara ya Maliasili na Utalii, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA). Kazi

yake ni kuratibu shughuli zote za uhifadhi wa wanyamapori nchini waliopo nje ya Hifadhi za Taifa.

• TANAPA ni mamlaka ya hifadhi za Taifa na husimamia maeneo kama: Serengeti, Mikumi, Manyara, Tarangire, Ruaha, Saadani, Gombe, Mkomazi, Arusha na Udzungwa.

• Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambayo inasimamia hifadhi ya Ngorongoro chini ya Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ya mwaka 2002.

JUMUIYA YA HIFADHI ZA WANYAMAPORIUanzishwaji wa Jumuiya za Wanyamapori umetokana na dhana ya ugatuzi wa madaraka vijijini ili wanakijiji waweze kushiriki kikamilifu katika kulinda, kutunza, kuhifadhi na kunufaika na rasilimali za wanyamapori kama inavyoelekezwa katika Sera ya Taifa ya Wanyamapori ya mwaka 1998.

• Uanzishwaji wa Jumuiya za WanyamaporiKifungu cha 31 cha Sheria ya Wanyamapori ya Mwaka 2009 kinaeleza kuwa Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori zinaweza kuanzishwa nje ya mapori tengefu, kwenye maeneo yanayotumiwa na jamii ndani ya ardhi ya kijiji. Halmashauri ya Kijiji au vijiji zinaweza kuomba kupitia kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori kuwa eneo fulani ndani ya kijiji au vijiji litangazwe kuwa eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori.

HATUA MUHIMU ZA KUANZISHA JUMUIYA ZA WANYAMAPORI VIJIJINI• Kijiji kitenge eneo la ardhi kuwa eneo la jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori kupitia

mpango wa matumizi ya ardhi. Kama eneo liko ndani ya vijiji zaidi ya kimoja vijiji hivyo vitaingia katika makubaliano ya pamoja juu ya kutumia eneo hilo kuwa eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori;

Page 58: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 51

• Kijiji kifanye usajili wa asasi ya kijamii baada ya kukubaliana katika Mkutano Mkuu wa Kijiji kuhusu uundwaji wa asasi hiyo;

• Asasi hiyo itaomba kuwa Chama Wakilishi cha Jumuiya kilichoidhinishwa kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori kupitia Halmashauri ya Wilaya kwa kuambatanisha katiba yake;

• Baada ya kuridhika na maombi, Mkurugenzi atatoa mapendekezo ndani ya siku 45 kwa Waziri kutangaza Asasi ya Kiraia kuwa Chama Wakilishi cha Jumuiya kilichoidhinishwa;

• Chama Wakilishi cha Jumuiya kilichoidhinishwa kitapeleka Mpango wa Usimamizi wa Jumuiya ya Hifadhi kwa Mkurugenzi ndani ya muda wa miaka mitano; na

• Waziri akikubali eneo hilo kuwa eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori na kutoa cheti cha ruhusa hiyo, Mkurugenzi atatoa haki ya kutumia eneo hilo kwa Chama Wakilishi cha Jumuiya kilichoidhinishwa.

8.1.2.1. MAKATAZO MBALIMBALI CHINI YA SHERIA YA UHIFADHI WANYAMAPORISheria hii imetoa makatazo kadhaa ambayo ni pamoja na:• Kuchunga kwenye GR - Mapori tengefu (Kifu. 15).• Inazuia kuwinda kwenye GR, maeneo oevu, Kifungu 18(2) & 21(1).• Inazuia shughuli za uchimbaji/kutafuta madini. (kifu. 20(1).• Inazuia kutenga, kuchimba au mitego kwa lengo la kuua, kuchukua n.k.• Inazuia kufanya chochote kwa viumbe adhimu/adimu.

8.1.2.2. CHANGAMOTO KATIKA UTUNZAJI NA UHIFADHI WA WANYAMAPORI Changamoto mbalimbali zinazoathiri sekta ya uhifadhi wanyamapori zinajumuisha i. Changamoto katika serikali na taasisi;

• Ukosefu wa watumishi wakutosha, mfano, watumishi wenye ujuzi wa kupambana na ujangili;

• Rushwa na ueledi mdogo katika kusimamia mashauri mahakamani;• Upungufu wa watumishi katika sekta ya uhifadhi wanyamapori;• Kushidwa kwa mpango wa uhifadhi wanyamapori ukilinganisha na mpango

wa uhifadhi Ardhi;• Ukosefu wa elimu ya uhifadhi wanyamapori kwa watumishi na vyombo vya

maamuzi;• Mfumo wa matumizi ya Ardhi na rasilimali pori zinazomilikiwa na serikali,

zinarudisha nyuma uwekezaji katika sekta ya wanyamapori na maendeleo kwa ujumla ya sekta ya wanyampori kwa watu au makampuni binafsi.

• Ujuzi mdogo wa kutatua matatizo ya wanyampori; na• Kutoshirikishwa kwa jamii katika usimamizi na utunzaji wa wanyamapori

ii. Changamoto za ikolojia • Kutoweka kwa makazi ya wanyamapori kutokana na kubadilika kwa

mazingira, mfano, baadhi ya mito imekuwa ikikakuka na kusababisha aina ya viumbe hai vinavyotegemea uwepo wa maji kutoweka;

• Kuenea kwa shughuli za uwindaji haramu pamoja na biashara haramu ya wanyamapori;

• Uhaba wa rasilimali watu katika kusimami shughuli za uhifadhi wanyamapori; na

Page 59: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 52

• Upungufu/uelewa mdogo wa matumizi juu ya haki ya matumizi ya wanyamapori hasa kwa wakazi wamaeneo ya vijijini.

iii. Changamoto za kibinadamu• Uchafuzi wa Mazingira unaosababishwa na shughuli za kibinadamu kama

uchimbaji madini, viwanda, kilimo na makazi, pia uchomaji wa mikaa na maendeleo ya miji;

• Ukosefu wa elimu hasa ya utunzaji wa wanyamapori hasa elimu ya Sheria za nchi;

• Kuendelea kwa shughuli za uwindaji haramu;• Kuongezeka kwa migogoro ianyotokana na wanyamapori hasa katika jamii

zinazoishi jirani na na maeneo ya hifadhi za wanyamapori;• Kutoweka kwa makazi ya wanyamapori kutokana na kuongezeka kwa

shughuli za kilimo, ufugaji, uchimbaji madini na kuongezeka kwa makazi ya binadamu kunako enda sambamba na ongezeko la watu.

iv. Changamoto za kifedha.• Upungufu wa fedha na rasilimali watu wanaohitajika katika kuiwezesha

serikali kusimamia wanyamapori hasa katika maeneo ya vijijini;• Kuwepo kwa bajeti ndogo katika utunzaji na uendelezaji wa sekta ya

wanyamapori; na• Mishahara midogo kwa watumishi jambo ambalo linapelekea kushuka kwa

morali ya kufanya kazi na mmomonyoko wa maadili ya kazi.

8.1.4. SHERIA YA HIFADHI ZA TAIFA, SURA YA, 282Hifadhi za taifa nchini Tanzania zinasimamiwa na Sheria ya Hifadhi za Taifa. Sheria hiyo inatoa mfumo wa kuanzisha na kusimamia hifadhi za taifa nchini. Sheria imeanzisha Bodi ya Wadhamini ambayo imesajiliwa kama kampuni kwa lengo la kusimamia, kudhibiti na kudumisha masuala ya Hifadhi ya Taifa nchini.

Sheria inaruhusu Rais, kwa idhini ya bunge, kutangaza eneo lolote kuwa Hifadhi ya taifa. Pia inamruhusu Rais wa kubadilisha mipaka ya hifadhi ya taifa. Tofauti na sheria nyingine ambayo zinamruhusu Rais kutekeleza maamuzi bila kushirikisha vyombo vingine, Sheria hii inasifa ya pekee sana kwani inamtaka kabla ya kutekeleza chochote lazima bunge liwe limezibitisha jambo hilo.

Shughuli za kila siku za kusimamia Hifadhi za taifa ni jukumu la TANAPA. TANAPA ni shirika la umma lililopewa jukumu la kusimamia uhifadhi katika hifadhi za taifa. Shughuli za TANAPA zinaongozwa na sheria mbalimbali zikiwemo: Sheria ya Hifadhi za Taifa, sura ya 282 [iliyorejewa 2002] na Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Na. 5 ya 2009. Kwa sasa, ya TANAPA inasimamia Hifadhi 16 za taifa.

Sheria inaruhusu watu ambao wameathirika na tamko la Rais wa kulipwa fidia. Rais pia anaruhusiwa na sheria kutoa haki zozote kwa mtu yeyote, ndani ya Hifadhi ya taifa. Sheria imeanzisha vizuizi katika Hifadhi za taifa kama vile: kubeba silaha katika hifadhi ya taifa, uwindaji, kuua mnyama yoyote, kuchimba, kuwekewa, au kujenga, wavu, mtego, mtego au kifaa kingine chochote chenye uwezo wa kuua, kuukamata au kujeruhi mnyama yoyote. Watu watakaopatikana kufanya matendo yaliyokatazwa wanaweza kushtakiwa na kama wakipatikana na hatia wanaweza kufungwa au kupigwa faini chini ya masharti

Page 60: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 53

ya sheria shughuli kuu inayofanywa katika Hifadhi za taifa ni utalii tofauti katika maeneo mengine ya uhifadhi.

8.1.5 MAKOSA NA ADHABU KATIKA SHERIA ZA WANYAMAPORIMtu yeyote akifanya mambo yafuatayo atakuwa amevunja Sheria ya Hifadhi ya Wanyamapori na atapaswa kupata adhabu kulingana na kosa alilofanya. Makosa hayo ni kama yanavyoainishwa hapa chini: Si ruhusa mtu kuwinda wanyamapori bila kuwa na leseni inayomruhusu kufanya

hivyo. Endapo mtu ana leseni, si ruhusa kuwinda mnyama ambaye hajaruhusiwa kulingana

na leseni, wala kuwinda idadi zaidi ya idadi inayotajwa katika leseni ya uwindaji.

Na endapo mtu atakuwa na hatia ya makosa hayo atahukumiwa kifungo cha miaka 3-5 kulingana na aina au kulipa fidia au vyote kifungo na fidia. Mtu yoyote hana ruhusa ya kumjeruhi mnyama yeyote na endapo atamjeruhi katika

harakati za uwindaji, mwindaji anapaswa kuhakikisha anamuua mnyama aliyemjeruhi kwa muda mfupi uwezekanao.

Mtu yeyote atakayemjeruhi mnyamapori, atapaswa kulipa fidia ambayo ni sawa na mara mbili ya bei ya mnyama aliyejeruhiwa au kufungwa jela kwa muda usiopumgua miezi 12.

Mtu yeyote asiye na leseni hapaswi kumiliki wala kuuza nyara za serikali, na mtu yoyote atakayekutwa anamiliki nyara za serikali kinyume na sheria na kukutwa na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka 20 na kisichozidi miaka 30 au kulipa fidia yenye thamani mara mbili mpaka mara kumi zaidi ya thamani ya nyara alizokutwa nazo, au fidia pamoja na kifungo.

Vilevile mtu yeyote anayefahamu mtu anayemiliki nyara za serikali kinyume na sheria, ana wajibu wa kutoa taarifa kwenye mamlaka ya hifadhi, asipofanya hivyo, atakuwa amevunja sheria na atatakiwa kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi shilling laki tano au kifungo kisichopungua miezi 12 na kisichozidi miezi 18 au vyote, yaani kifungo pamoja na malipo, na

Mwindaji mwenye kibali cha kuwinda, hana ruhusa ya kuwinda wanyama wadogo au wakike na wenye mimba, kufanya hivyo ni kosa kisheria. Vilevile hana ruhusa kuwinda kwa kutumia mbinu za uwindaji zilizokatazwa. Akifanya hivyo, pamoja na adhabu nyinginezo, mamlaka inaweza kumfutia leseni.

Ni vyema wananchi wafahamu kuwa, kukutwa na silaha pekee katika maeneo ya hifadhi ni kosa kisheria, na mahakama itamhukumu mtu huyo kama mtu ambaye anataka kuwinda hata kama hajakutwa na kitu kingine kinachoonesha kama kweli alikuwa anawinda au la.

Page 61: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 54

9.1 SHERIA YA RASIMALI ZA MAJI 2007Sheria hii imeanza kutumika tarehe 1 Agosti, 2009 baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali kupitia Tangazo la Serikali namba 235 la tarehe 10 Julai 2009. Sheria hii mpya imefuta sheria ya zamani iliyojulikana kama Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi ya Maji [The Water Utilisation (Control and Regulation) Act] Na. 42 ya mwaka 1974.

9.2 MAANA YA MAJI NA UMILIKI WA RASILIMALI MAJISheria imetoa maana ya neno maji kuwa ni “Maji ni maji yote yanayotiririka juu ya uso wa ardhi, au yaliyotuama kwenye uso wa ardhi, au yanayotiririka kutoka kwenye chanzo au kijito au ziwa la asili au chanzo chochote au eneo oevu chini ya ardhi na inajumuisha na maji yote yaliyo kwenye miamba chini ya ardhi”. Sheria hii inasema kuwa Rasilimali za maji ni mali ya umma chini ya Rais kama mdhamini tu kwa manufaa ya watanzania wote.

Sheria hii ilitungwa kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa rasilimali za maji hapa nchini zinatunzwa, zinatumiwa, zinaendelezwa, zinaboreshwa, zinasimamiwa na kudhibitiwa kwa kuzingatia kanuni muhimu. Kanuni za kutunza, kuhifadhi, na kudhibiti rasilimali za maji ni hizi zifuatazo:• Maji ni hitaji la msingi na haki ya kila mtu kwa vizazi vya sasa na vijavyo; • Kuweka utaratibu wa haki ya kuyafikia maji kama hitaji la kimsingi, na kuboresha upatikanaji

wa majisafi na salama; • Kuhakikisha maji yanatumika kwa ufanisi, yanahifadhiwa kwa manufaa ya matumizi ya watu

wote;• Kuwezesha shughuli za kijamii na kiuchumi; • Wadau na walengwa washirikishwe katika ngazi zote za usimamizi wa Rasilimali za Maji

hususani maamuzi yafanywe katika ngazi ya chini kadri iwezekanavyo kwa kuzingatia uwezo uliopo;

• Kuboresha usimamizi na hifadhi ya mifumo ya ikolojia na bayoanuai; • Kuwa na msingi bora na endelevu wa kusimamia maendeleo na mipango ya pamoja ya

matumizi ya rasilimali za maji ya chini na juu ya ardhi kwa kuzingatia mifumo ya kiuchumi, kimazingira na kijamii katika mipango hiyo;

• Kuzuia na kudhibiti uchafuzi na uharibifu wa rasilimali za maji; • Kutekeleza majukumu ya kimataifa kama ilivyoainishwa kwenye nyenzo mbalimbali za Sheria

ya kimataifa ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mshiriki; na • Kuwa na taratibu za kuhakikisha usalama wa usimamizi wa mabwawa na kujikinga na majanga

yasababishwayo na maafa ya Maji.

9.3 VIPAUMBELE KATIKA UGAWAJI WA MAJI Katika ugawaji au utoaji wa huduma ya maji Sheria ya Rasilimali za Maji imeweka vipaumbele kama ifuatavyo: • Matumizi ya maji kwa ajili ya binadamu yamepewa umuhimu wa kwanza; • Mgao wa maji kwa ajili ya hifadhi ya mazingira umepewa umuhimu wa pili; na• Mgao wa maji kwa shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi umuhimu unaofuata kama yapo

ya kutosha baada ya (a) na (b) hapo juu; (k. 6.(2)).

9.4 JUKUMU LA KUTUNZA RASILIMALI MAJI Sheria inamtaka kila mkazi akaaye Tanzania awe mdau na awajibike kutunza na kulinda vyanzo vya maji na rasilimali za maji na awajibike kutoa taarifa ya tukio lolote kwa mamlaka husika endapo tukio hilo linaonesha kuwa litaathiri ubora na wingi wa rasilimali za maji.

MADA YA TISA

Page 62: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 55

9.5 USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA MAJI Jukumu la ulinzi wa rasilimali za maji nchini limewekwa kwa kila mtu. Usimamizi wa rasilimali za maji unafanywa na Serikali haswa kupitia Waziri mwenye dhamana ya rasilimali za maji, Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Bodi za Maji za Mabonde na Kamati za Vidakio vya Maji. Vyombo vya Usimamizi Rasilimali Maji vilivyoanzishwa na Sheria hii ya Rasilimali za Maji ni pamoja na:

1. Waziri (Kif. 13) ambaye majukumu yake ni: • msimamizi mkuu-masuala ya sera, na sheria;• huteua wajumbe wa Bodi ya Maji ya Taifa; • huunda Bodi za Maji za Mabonde; • huteua Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, n.k.

2. Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji • Huteuliwa na Waziri na jukumu lake kuu ni mshauri mkuu wa Serikali kuhusu masuala ya

rasilimali za maji.

3. Bodi ya Taifa ya Maji (Kif.20)• Huteuliwa na Waziri kwa lengo la kumshauri Waziri husika;• Theluthi lazima wawe wanawake;• Muundo wake ni wataalam toka sekta za uvuvi, madini, ardhi, kilimo na, asasi za kiraia.• Wajumbe wa Bodi hii hukaa madarakani kwa muda wa miaka 3.

4. Bodi za Maji za Mabonde (kif. 22)• Waziri huzianzisha Bodi hizi na kuzitangaza kwenye Gazeti la Serikali;• Zikianzishwa huwa zinajitegemea na huweza kushitaki na kushtakiwa kwa majina yao

yenyewe (kif. 22); na• Mwenyekiti wa kila Bodi huteuliwa na Waziri mwenye dhamana na rasilimali za maji.

9.5.1 Mabonde ya Maji nchiniKuna mabonde ya maji tisa nchini na kila Bonde la Maji lina Bodi yake ya kusimamia rasilimali za maji. Mabonde haya ya maji ni:i. Bonde la Ziwa Nyasa;ii. Bonde la Ziwa Viktoria;iii. Bonde la Kati;iv. Bonde la Ziwa Tanganyika;v. Bonde la Ruvu/Wami;vi. Bonde la Ziwa Nyasa;vii. Bonde la Pangani;viii. Bonde la Rufiji; naix. Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini.

9.5.2 MAJUKUMU YA BODI ZA MABONDEi. Kuandaa mipango, bajeti, n.k. ya matumizi ya rasilimali maji kwenye bonde husika;ii. Kutoa vibali vya ujenzi wa miundombinu ya maji vyanzo vya maji;iii. Kutoa, kusitisha vibali vya kutumia Maji;iv. Kutunza daftari la maji;v. Kutatua migogoro ndani ya Bonde; na

Page 63: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 56

vi. Kuteua Mwenyekiti na wajumbe wa Kamati za Vidakio Maji.

9.5.3 KIBALI CHA KUTUMIA MAJI Mtu yeyote anayetaka kuchepusha, kukinga, kuhifadhi, kuchukua na kutumia maji kutoka kwenye chanzo cha maji au kujenga miundombinu yeyote lazima aombe Kibali cha Kutumia Maji (k. 43(4)) kutoka Bonde husika. Kibali kilichotolewa kwa mujibu wa sheria nyingine hakitahusisha matumizi ya maji au kuwa na uhalali wowote kwenye chanzo cha maji bila idhini ya maandishi kutoka Bodi ya Maji ya Bonde husika (k. 43(3)).

Uchimbaji wa kisima kwa ajili ya matumizi ya nyumbani hayahitaji kibali. Pia, matumizi ya rasilimali za maji kwa matumizi ya nyumbani, kupikia, kufua, kuoga na menginenyo hayahitaji vibali.

9.5.4 VIBALI VYA KUTIRIRISHA MAJI MACHAFU Mtu yeyote anayetaka kutiririsha au kumwaga maji machafu kutoka kwenye biashara yoyote, kiwanda au kilimo au kutoka kwenye miundombinu ya majitaka hivyo kukutana na maji juu au chini ya ardhi anatakiwa aombe kibali kutoka Bodi ya Maji ya Bonde (k. 63 (1)).

Page 64: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 57

Page 65: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 58

Page 66: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu

HAKI NA WAJIBU WA KUTUMIA RASILIMALI TANZANIA

page 59

Page 67: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu
Page 68: HAKI YA KUPATA, KUMILIKI, NA KUTUMIA ARDHI TANZANIA · Sera na Sheria zinazosimamia ardhi ya Tanzania. Pia, mwongozo huu utajengea uwezo, wawezeshaji na wasomaji kuhusu masuala muhimu