hakimiliki © bible pathway adventures 2015 · wa joto na mji wa yudea ulikuwa na joto jingi. wezi...

21

Click here to load reader

Upload: truongnhu

Post on 27-Aug-2018

249 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi
Page 2: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015

Mwandishi: Pip Reid Mchoraji: Thomas Barnett

Mkurugenzi Mbunifu: Curtis Reid Mtafsiri: Susan Koech

Kuzaliwa kwa Mfalme Mara ya kwanza kuchapishwa 2015

Shukrani kwa kukisoma kitabu hiki na kuunga mkono Safari ya Kufana Kwa Njia ya Hadithi za Biblia (Bible Pathway Adventures). Shirika letu ni shirika lisilo la faida ambalo huwasaidia wazazi na walimu duniani kote kuwafunza watoto zaidi kuhusu Biblia kwa njia ya kufana na yenye ubunifu. Wadhamini na mashabiki kama wewe ndio hutewezesha kutengeneza app, kufadhili mradi wa utafsiri na utunzi

wa hadithi na vifaa vya elimu vya jamii zote.

Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya kitabu hiki kinachoweza kuchapishwa tena, kusambazwa, au kupitishwa kwa njia yoyote, ikiwa ni pamoja na kurekodi au njia nyingine za

kielektroniki bila idhini iliyoandikwa ya Bible Pathway Adventures, isipokuwa katika matumizi ya nukuu inayoweza kutumika wakati wa kudurusu na vilevile matumizi yasiyo ya kibiashara iliyoruhusiwa na sheria ya hati miliki. Kwa maombi ya ruhusa, wasiliana na Bible Pathway

Adventures' katika tovuti iliyoko hapo chini:

www.biblepathwayadventures.com

Page 3: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

1.

“Yuko wapi yeye aliyezaliwa nfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.”

(Mathayo mtakatifu 2:2)

Kuzaliwa kwa Mfalme

(Je wajua kuwa jina la Kiebrani la Yesu ni Yeshua? Jina lake kamili ni Yehoshua, linalo maanisha,

‘Mungu ni Mwokozi wangu’.) 

Siku moja, katika msimu wa baridi, Maria aliketi kando ya moto. Malaika wa Mungu akatokea mlangoni. Maria akamtazama na kushtuka. “Wewe ni nani?” aliuliza, huku akiyakodoa macho kwa mshangao. Hakuwa amemwona malaika hapo awali!

“Usiogope; Mungu ameridhishwa nawe,” malaika aliyeitwa Gabrieli akasema. “Tazama utamzaa mwana wa kiume, nawe utamwita Yeshua. Naye ataitwa mwana wa Bwana Mkuu!”

“Lakin i bado s i jao lewa,”Mar ia a l i sema, akimtazama malaika. “Nitamzaa mwana vipi?” Malaika alitabasamu na kumhakikishia Maria, “Mungu atamtuma Roho Mtakatifu akujie juu yako na kukukabidhi mwana.”

Page 4: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

2.

Maria alikuwa na hamaki, alikwaruza kichwa. Hakujua jinsi jambo lile lingetimia. “Je, wamkumbuka jamaa yako, Elizabeti?” Gabrieli aliendelea. “Kila mtu alifahamu hangeweza kupata mtoto, lakini yuko mjamzito kwa miezi sita sasa. Hakuna kisichowezekana, kwake Mungu!” Maria aliuma midomo yake na kukubali. “Hayo ni kweli. Mimi ni mtume wa mungu, na nakubali mipango yake katika maisha yangu,” alijibu.

Alfajiri iliyofuata, alishuka kutoka kitandani, kwenda kumtembelea mchumba wake, Yusufu. “Nitamwelezaje kuwa ntajifungua mtoto?” Maria aliwaza. Alitembea aste aste hadi nyumbani kwa Yusufu. Alifungua mlango polepole.

“Yusufu, Yusufu, malaika Gabrieli amenitembelea!” Maria alisema. Yosefu alitoka kitandani na kuteremka kwa ngazi. “Alinieleza kuwa Mungu amefurahishwa nami, na eti kwamba nitamzaa mwana!”

Yusufu hakuyaamini masikio yake. Yawezekanaje kuwa mchumba wake alikuwa amezungumza na malaika? Atamzaa mwana? Aliketi chini huku akiwaza na kuwazua. “Maria, lakini hatujaoana,” alisema. “Hili linawezaje kutendeka?”

Page 5: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

3.

Nazareti ulikuwa mji mdogo na hivyo Yusufu alifahamu wazi kuwa habari kama zile zingeenea kwa haraka sana. Hakutaka jirani zake wamsimange Maria. Je, wangefanya nini?

Usiku huo, Yusufu aligaragarakitandani. Alitaka kufanya uamuzi bora na kumshughulikia Maria kikamilifu, lakini yawezekana kumtenga Maria kungekuwa njia bora ya kutatua tatizo hilo? “Pengine yanifaa kukatiza uchumba,” alishangaa. Lakini kabla ya macheo, malaika wa Mungu akamtokea ndotoni. “Usiwe na hofu bali mchukue Maria na kumfanya mkeo,” malaika akasema. “Mtoto atakayempata atakuwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu.”

Yusufu alipogutuka, alifanya alivyoagizwa na malaika: alimpeleka Maria nyumbani na kumfanya mkewe. Alikuwa tayari kupokea mipango ya Mungu na kumuamini.

Page 6: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

4.

Baadaye katika huo mwaka, Kaisari Augusto aliamuru kusajiliwa kwa watu wote. Alikuwa mtawala mkuu wa Roma, huko Judea. Aliwashurutisha Wayahudi kuzifuata sheria za Roma. Kaisari alitaka kujua idadi ya watu alioongoza na ambao angewatoza ushuru. Hata hivyo, kulikuwa na barabara nyingi za kujenga!

“Kila mtu lazima arejee nyumbani kwake na kujiandikisha majina ili kujisajili kwa ajili ya sensa,” Kaisari aliagiza akiwa katika kasri lake huko Roma.

Yusufu alikuwa mzao wa mfalme Daudi, hivyo alilazimika kwenda Bethlehemu, alikozaliwa Daudi. Mji wa Bethlehemu ulikuwa mbali, na walihitajika kuwasili huko kabla ya mwana kuzaliwa. Kwa haraka, Maria na Yusufu walisafiri kwa punda na kuelekea Bethlehemu.

Page 7: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

5.

Kule Bethlehemu, rafiki na jamaa ya Yusufu waliwakaribisha kwa moyo mkunjufu. “Shalom, shalom,” walisema, huku Maria na Yusufu wakijikokota kwa uchovu wakipitia kwenye mitaa finyu. “Barukh haba! Karibuni!”

Yusufu alijua wazi kuwa Sikukuu za Bwana zilikuwa zimekaribia na wageni wangeanza kuwasili manyumbani. “Je, kuna mtu aliye na chumba cha ziada?” aliuliza huku jirani wakichungulia madirishani ili kujua hali ya msukosuko ilitokea kwa nini.

Wanakijiji walikuwa wadadisi sana, na Yusufu alipata jamaa ya kuishi naye. Chumba chao cha wageni kilikuwa tayari kimejaa, kwa hivyo wakawaandalia Yusufu na Maria malazi sebuleni, karibu na boma la mifugo.

Maria alitabasamu na kupapasa tumbo lake. Alikuwa karibu kujifungua, na alishukuru kwa kupata makao. Alibarizi ugani huku akiwatazama kina mama waliokuwa wakioka mikate kwa moto uliokuwa ukidata. Sikukuu za Tarumbeta zilikaribia, na hivyo basi wanakijiji walikuwa na mengi ya kufanya. Maria alihisi furaha iliyotanda.

Page 8: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

6.

Siku chache baadaye, Maria alihisi kitoto tumboni kikipiga teke. “Nafikiri mtoto yu karibu kuja!” aliwaambia wanawake waliokuwa ugani kwa wasiwasi. Maria hakuwa amejifungua awali hivyo basi hakujua la kutajarajia! Kina mama walimzingira na kukaa ange, tayari kumsaidia.

Hatimaye, mfalme alizaliwa. Ili kumlinda mtoto, Maria alimvika mavazi na kumlaza horini. Yusufu alimkumbatia Maria. “Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu,” alisema, huku akimtazama mtoto aliyekuwa usingizini. Wote waling’amua kuwa mtoto huyo alikuwa wa kipekee sana.

Page 9: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

7.

Usiku huo huo, Karibu na Bethlehemu, walikuwako wachungaji waliokuwa wakilinda mbuzi na kondoo. Ghafla, malaika wa Mungu akawatokea kwa utukufu uliong’aa pande zote! Wachungaji walijawa na hofu kuu, wakafunika nyuso zao na kutorokea kwenye mbaruti. Malaika alikuwa akifanya nini pale?

“Msiogope,” malaika akasema. “Nimewaletea habari njema, itakayoleta furaha kwa watu wote.” Wachungaji wale walilala kwenye mbaruti huku nyoyo zao zikipapa. Hofu waliokuwa nayo haingewaruhusu kusema lolote wala kufanya chochote!

Malaika aliendelea, “Leo katika mji wa Bethlehemu, amezaliwa mwana, mwokozi wenu. Mtamkuta mtoto mchanga amevikwa mavazi na amelazwa horini.”

Page 10: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

8.

Mara angani kukawa na jeshi la malaika wakimsifu Mungu na kuimba, “Atukuzwe Mungu! Na dunia iwe amani kwa watu!”

Malaika walipoondoka, wachungaji walitikisa vichwa vyao kwa mshangao. “Haya, basi twangoja nini?” waliulizana. “Twendeni kijijini tukamwone Masihi!”

Waliharakisha kuelekea Bethlehemu, wakapata nyumba iliyojengwa kwa udongo wa matofali, walikoishi Maria na Yusufu. Mtoto mchanga alikuwa amelala fo!fo!fo! horini, kama walivyoelezwa na malaika. “Malaika alitokea angani na kutupasha habari kuwa huyu mtoto ni Masihi!” walisema huku wakimuashiria mtoto.

Wanakijiji walikusanyika na kutega masikio yao, huku wakikodoa macho. Walikuwa na hamu kuu ya kumuona Masihi, na sasa alikuwa amewasili!

Page 11: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

9.

Katika mji uliokaribia Bethlehemu, palikuwa na nchi iliyokuwa kubwa na yenye nguvu. Kwa kuwa Ufalme wa Parithia ulikuwa mkubwa sana,mfalme alikuwa na makuhani na viongozi walioitwa mamajusiwaliomsaidia mfalme kufanya uamuzi. Mamajusi walikuwa mashuhuri sana; hata walichagua wafalme wa Parithia!

Mamajusi pia walikuwa stadi wa nyota. Walifahamu Mungu alikuwa amepanga na kuandika wokovu mbinguni. Kila usiku, mamajusi walitazama nyota na kungoja ishara kuwa Masihi amewasili.

Machweo moja, ishara kuu ikatokea angani. “Tazama, ishara imewadia!” mmoja wao alisema kwa furaha akiashiria angani.

Page 12: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

10.

Wote walitoka nje na kutazama angani. Kwa kweli, ilikuwa ishara ambayo Balaamu alikuwa amezungumzia katika maandishi. Nyoyo zao zilipiga kwa vishindo, walijawa na furaha.

“Hii ina maana kuwa mwokozi wa Israeli yuko hapa ,” wal inong ’onezeana , macho yao yakitazama mbingu. Walijua kuzaliwa kwa masihi kulikwa kwa maana kwa kila mtu, kila mahal i . “Twende tukamsujudie mfalme aliyezaliwa!”

Lakini iliwabidi mamajusi kusubiri. Walikuwa watu mashuhuri na safari haikuwa salama. Waliketi na kuanza kupanga jinsi wangesafiri.

Page 13: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

11.

Miezi michache baadaye, mamajusi walianza safari yao kuelekea Yerusalemu. Msimu ulikuwa wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi waliondamana nao sako kwa bako. Kwa kweli, ilikuwa safari ndefu na hatari.

Kule Yerusalemu walisafiri kwa magari ya farasi na kupitia mitaani palipokuwa na vumbi. “Yuko wapi aliyezaliwa, mfalme wa Wayahudi?” waliuliza. “Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumsujudia.”

Umati ulikusanyika marikitini na barabarani. “Je, m a m a j u s i w a n a m z u n g u m z i a n a n i ? ” walinong’onezeana kwa wasiwasi. “Wamekuja Yerusalemu kufanya nini?”

Page 14: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

12.

Mfalme Herode aliitawala Yudea wakati huo. Alighadhabika aliposikia habari za mfalme aliyezaliwa. “Yawezekanaje hawa mamajusi wanamtaka mfalme mpya?” alisema kwa hasira akigonga meza“Mimi ndimi mfalme wa Wayahudi!”

Mamajusi walimtia Herode wasiwasi. Parithia ilikuwa nchi yenye mamlaka na mamajusi walikuwa watu mashuhuri. Kaisari hangefurahi iwapo Herode angezua vita nao tena. Aliwaita wakuu wa makuhani na waandishi wa Torati faraghani katika kasri lake. “Mfalme atazaliwa wapi?” Herode aliuliza.

“Nabii Mika alitabiri kuwa mfalme atazaliwa kule Bethlehemu,” walijibu, huku wakimwonyesha ilivyoandikwa katika Maandishi ya Torati. Herode alizidi kughadhabika. “Nendeni mkawatafute mamajusi,” aliwaambia watumishi wake. ”Mtakapowapata, waambieni waje kwangu haraka!”

Page 15: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

13.

Mamajusi waliwasili katika makao makuu ya mfalme. “Nyota ilitokea lini?” Herode aliuliza huku akiwakaribia. Mamajusi walimjua Herode k u w a m f a l m e m j a n j a k a m a s u n g u r a . Walitazamana na kumjibu kwa makini sana.

Herode hakuwa na amani. “Nendeni mkamkute mfalme aliyezaliwa.” Alisema huku akiwaashiria waelekee Bethlehemu. “Mnijuze pindi mtakapo mpata, pia nami nimsujudie.”

Lakini Herode hakutaka kumsujudia Yeshua bali alitaka kumuua. Herode aliamini kulikuwa na mtawala mmoja tu, yeye mwenyewe!

Page 16: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

14.

Mamajusi waliabiri magari ya farasi na kutazama angani. Nyota iliyong’a iliangazia Bethlehemu, hivyo basi kuwaongoza. “Natuifuate nyota hii kuu!” walisema kwa furaha.

Kule malishoni, wachungaji waliwastaajabia mamajusi kwa jinsi walivyo harakisha. “Mbona mamajusi wamewasili huku?” waliulizana. Walinzi wa mamajusi waliwatia hofu. “Je, wamekuja kumtazama Yeshua?”

Mamajusi waliifuata nyota hadi ilipotua alikokuwa akikaa Yeshua. Safari hio ya kutoka Parithia ilikuwa ndefu na hivyo basi walikuwa na hamu ya kumuona Masihi. Walishuka na kuingia nyumbani.

Page 17: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

15.

“Asifiwe Mungu; kweli huyu ndiye Masihi,” walisema, wakipiga magoti mbele ya Yeshua. Huku wakitetemeka, walifungua hazina zao na kumpa tunu; dhahabu, uvumba na manemane.

Lakini hawakukaa kule kwa muda mrefu. Mungu alikuwa amewaonya wasirudi kwa mfalme Herode. Walipata njia mbadala ya kuwafikisha Parithia walikotoka. Waliabiri magari yao na kutoweka.

Page 18: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

16.

Usiku huo, malaika wa Mungu akamtokea Yusufu ndotoni. “Yusufu, ondoka umchukue mtoto na mamaye, ukimbilie Misri, ukae huko hadi nitakapo kwambia utoke”

Yusufu alimtikisa Maria polepole. “Amka,” alisema. “Mungu ametuamuru tukimbilie Misri.” Ingawa alikuwa na maumivu ya tumbo, Maria ailikubali. Mungu alikuwa amepanga yapi tena? Walizifunganya mizigo na kutoweka polepole. Mji wa Misri ulikuwa mbali sana lakini walijua Mungu alikuwa pamoja nao na angewalinda.

Page 19: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

17.

Mwisho

Herode alijawa na hasira na ghadhabu. Alihangaika huku na kule, kanzu yake ikipapatika. “Iweje mamajusi wamerudi Parithia?” alipiga kelele, akitikisa ngumi yake. “Nimehadaiwa!”

Aliwakusanya wakuu wa majeshi. “Nendeni Bethlehemu na viungani mkawauwe wana wa kiume walioko chini ya miaka miwili,” aliamuru. “Angamizeni huyo anayesifiwa kuwa mfalme. Nataka amalizwe kabisa!”

Lakini ng’o! walikuwa wamechelewa kwani Maria na Yusufu walikuwa wameshaelekea Misri. Wangerudi nyumbani baada ya muda mrefu; Yeshua alikuwa salama.

Page 20: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

Je, umefurahia Kuzaliwa kwa Mfalme? Kwa hadithi zaidi za Safari ya Kufana kwa Njia Ya Biblia, agalia vitabu hivi!

Arushwa Katika Tundu la Simba

Auzwa Utumwani

Gharika Kuu

Amezwa Na Samaki

Kutoroka Kutoka Misri

Usaliti wa Mfalme

Makabiliano Na Jitu

Shukrani kwa kukisoma kitabu hiki na kuunga mkono Safari ya Kufana Kwa Njia ya Hadithi za Biblia (Bible Pathway Adventures). Shirika letu ni shirika lisilo la faida ambalo huwasaidia wazazi na walimu duniani kote kuwafunza watoto zaidi kuhusu Biblia kwa njia ya kufana na yenye ubunifu. Wadhamini na mashabiki kama wewe ndio hutewezesha kutengeneza app, kufadhili mradi wa utafsiri na utunzi

wa hadithi na vifaa vya elimu vya jamii zote.

Unaweza kujifunza mengi zaidi kuhusu matukio na hadithi kupitia:

www.biblepathwayadventures.com

Page 21: Hakimiliki © Bible Pathway Adventures 2015 · wa joto na mji wa Yudea ulikuwa na joto jingi. Wezi walitembea huku na kule shambani, hivyo mamajusi walifurahia ulinzi mkali wa wanajeshi

www.biblepathwayadventures.com