haliuzwi - ccp home pageccp.jhu.edu/documents/si mchezo 63 nov-dec low res.pdf · baadhi ya watu...
TRANSCRIPT
ISSN
: 0
85
6-8
995
Maishaya kijani
Haliuzwi
KATUNI:
2 Si Mchezo! SEPTEMBA-OKTOBA 2012
Si Mchezo! Huzalishwa na kusambazwa.
Si Mchezo! husambazwa.
Lilikozalishwa toleo hili.
Yapo madhara mengi yanayosababishwa na ukataji miti bila utaratibu kama kukauka kwa vyanzo vya maji, kuleta ukame, kukosa hewa safi, n.k. Chukua hatua kukataa ukataji miti hovyo.
Misitu ni urithi mzuri tunayotakiwa kuilinda ili itulinde. Kila mmoja wetu ana jukumu la kulinda kwa faida yetu na vizazi vijavyo.
3
TAHARIRIMwaka ndiyo huoooo umesepa na mishemishe bado zinaendelea. Mbali na hayo, lazima niwatakie heri ya Krismasi na Mwaka mpya wasomaji wetu popote pale mlipo. Safari hii hatukucheza mbali na Bongo kwani ni mashariki kidogo tu mwa Tanzania, yaani Pwani ndiko tulitia kambi kusikiliza kilio cha misitu! Nani anaweza kudai kwamba hakuwahi kutumia mti au mazao yatokanayo na mti? Pata stori humu ndani
Majuka
YALIYOMO4 Stori Yangu: Maisha ya kijani
6 Mambo Mapya
8 Mambo ya Fedha: Tuyavune kwa njia salama
9 Nguvu ya Mwanamume: Puchu kwa faragha!
10 Hadithi ya Picha: Wizi mtupu
14 Je, Wajua: Kataa katakata kukatakata miti
16 Tulichovuna: Mabalozi wa mazingira Rufiji hawa
18 Chezasalama: Jiulize tuko wangapi?
20 Burudani: Kabwela na Stamina ft Mavocal
22 Pasipo na Daktari: Msaada unapoumwa na nyuki
23 Huduma: Wafahamu MJUMINGU
24 Katuni: KICHAPO!
27 Ukweli wa Mambo: Kilio cha miti
30 SEMA, TENDA!: Misitu yetu, uhai wetu
31 Ushauri
Mhariri Majuka Ololkeri
WaandishiBetty LidukeRaphael NyoniRebeca Gyumi
WashauriTimu ya Femina HIP
Mkurugenzi MtendajiDr. Minou Fuglesang
Mkurugenzi wa Habari Amabilis Batamula
Meneja MachapishoJiang Alipo
Meneja MahusianoLilian Nsemwa
Katuni na UsanifuBabaTau, Inc.
Mpiga Chapa Jamana Printers Ltd
Usambazaji EAM Logistic LtdFemina HIP na Washirika
Si Mchezo! limefanyika kwa hisani kubwa ya Serikali za Sweden (Sida), Denmark (DANIDA), HIVOS, RFSU, Twaweza na JHU-CCP/TCCP.
Toleo hili limefanyika kwa kushirikiana na Serikali ya Finland na Norway kupitia Kampeni ya Mama Misitu.
Yaliyomo humu ndani ni jukumu la Femina HIP na hayawakilishi maoni au mitazamo ya wafadhili.
Wasiliana nasi kwa:S.L.P. 2065, Dar es SalaamSimu: (22) 212 8265, 2126851/2 Fax: (22) 2110842email: [email protected]
Si Mchezo! huchapishwa na Femina HIP.Sms: 0715 568222
Hiyo ngalawa mpande wenyewe, bora nitembee kuzunguka
Maji kwenye Mto Rufiji yamepungua kwa kiasi kikubwa hata kusimami-sha kivuko kutovusha abiria
Umbali kutoka hapa hadi Ikwiriri si chini ya kilo-meta 65 tofauti na hapa kilometa 20
4 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
STORI YANGU
Tangu wakati nasoma nilikuwa navutiwa na mambo ya utunzaji wa mazingira.
Wilaya yetu imejaaliwa uoto mzuri wa asili, lakini changamoto ni uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea kwa miaka mingi. Hivyo, kutokana na azma yangu ya utunzaji wa mazingira, nilitafakari ni kitu gani nitakifanya kusaidia jamii yangu ambayo ndiyo waathirika wakubwa wa uharibifu huo wa mazingira.
Naitwa Ally Mussa Mkumbege (23), mtoto wa kwanza katika familia yetu. Nimezaliwa katika Kijiji cha Mloka, Rufiji. Nilipata elimu ya sekondari katika Shule ya Ruaruke mwaka 2007, baadaye nilihamishiwa Shule ya Sekondari Zimbini, zote za Rufiji ndipo nikahitimu mwaka 2010.
Wakati nasoma kuna wataalamu mbalimbali ambao walikuwa wakitutembelea shuleni kutoa elimu kuhusu mazingira, VVU na Ukimwi n.k. Hizi zote zilinijenga katika makuzi lakini nilifurahia zaidi elimu ya mazingira ambayo Kikundi cha Mazingira cha Rufiji (REG) walitupa.
Utakubaliana na mimi kuwa suala la uharibifu wa mazingira limekithiri katika maeneo mengi Tanzania hasa katika Wilaya yetu ya Rufiji ambayo imezungukwa na misitu mizuri ya asili. Mara nyingi tunaona malori makubwa yakisafirisha magogo yaliyovunwa hapa kwetu. Mengine ni halali na mengine yanapitishwa mlango wa ‘uwani’! Ndiyo si tunaona!? Sipendi kuona miti inakatwa na kuisha kwani nimejifunza madhara yake kama vile vyanzo vya maji kukauka, mfano mto wetu Rufiji ambao tunategemea kwa mambo mengi kukauka, kukosa hewa safi,
Nahamasisha maisha ya kijani
Ally Musa (kulia) akiwa na mkewe Bi Sharfa Said na mtoto wao Rahma Ally.
5NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
Nahamasisha maisha ya kijani
kukosa matunda, kusababisha kipindi cha kiangazi kuongezeka.
Si hayo tu yaliyonigusa kunifanya kuwajibika kimazingira, bali nimeona nionyeshe mfano kwa vijana wenzangu kuwa wanaotakiwa kuchukua hatua ya kulinda mazingira ni sisi wenyewe hasa vijana ambao ndiyo huenda kuwinda na kuchoma moto ili kuwatimua wanyama na kupata kitoweo.
Nilipomaliza kidato cha nne, sikufanikiwa kuendelea na masomo kwani sikufaulu mtihani. Sikukata tamaa, niliona ndiyo fursa ya kuwatafuta REG ili wanielimishe juu ya utunzaji wa mazingira. Walinipokea vizuri na kuona ujio wangu ni wa
kipekee kwani nimekuwa kijana mwenye umri mdogo kujiunga na kikundi hicho. Nilifurahishwa na shughuli zao na ilinisaidia kujifunza mengi kama vile kupanda aina mbalimbali za miti asili na ya kisasa na kutambua umuhimu wa utunzaji mazingira. Mpaka sasa ni miaka miwili tangu nijiunge na wanamazingira hawa. Ni kijana pekee kwenye kundi na napiga kazi kwa bidii hadi najulikana kama ‘jembe’ la mazingira.
Kutokana na elimu ya VVU na Ukimwi ambayo niliipata nikiwa shuleni, niliamua kuoa baada ya kumaliza shule na tumebahatika kumpata mtoto mmoja. Tumepima pamoja na tuko kamili gado. Nampenda mke wangu na tunaishi kwa uaminifu.
Ally akiwa kwenye shamba lao la miti huko Kibiti, Rufiji. Ally akijaza mifuko ya mbolea ili kupandikiza miche
6 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
MAMBO MAPYA
Mbinu za maharamia wa misitu zapanguliwaKatika hali isiyo ya kawaida, tuliibukia Kijiji cha Muyuyu na kukaribishwa na magogo kibao yakiwa yamepangwa kana kwamba yanasubiri mnunuzi. Tulipoonana na Afisa Mtendaji wa Kijiji alitusimulia kisa cha magogo hayo. Mmoja wa wanakijiji aliyakuta magogo hayo 637 yakiwa yameshakatwa kwenye Msitu wa Hifadhi ya Ngumburuni tayari kwa kusafirishwa. Mwananchi hakukaa kimya, aliripoti ofisi ya Serikali ya Kijiji. Mkakati wa kuwakamata maharamia hao ulipangwa lakini haukufanikiwa labda wakishtukia ‘ishu’. Wananchi wayasafirisha magogo hayo kwenda kijijini na kuyalinda yakisubiri utaratibu mwingine wa kisheria. Kwa sasa, vijiji saba ambavyo vizunguuka msitu huo vimejipanga kulinda msitu huo ikiwa ni pamoja na kuweka uzio kwenye barabara zinazotoka.Timu ya Si Mchezo inawapongeza sana wanakijiji hao kwa kazi nzuri.
Mazingira yalivyochomwa moto
Kivuko cha Utete kikionekana kusi-mamisha shughuli zake za kuvusha huko Utete kutokana na Mto Ru-fiji kupungua kina cha maji kwa kiasi kikubwa. Hali hiyo inasababishwa na kuongezeka kwa kipindi cha kiangazi sababu ikiwa ni uharibifu wa misitu.
7NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
Hawa wanapaswa kuigwa…Tulipotembelea Rufiji tulipata fursa ya kutembelea vijiji kibao tukajionea utajiri uliyoifunika Wilaya hiyo ambao umepewa mgongo na binadamu. Ni wachache wanaofahamu kuwa Mkoa wa Pwani ambayo Rufiji ndiyo moja ya Wilaya zake ni moja ya maeneo yenye maajabu duniani. Si hayo tu, pia imejaaliwa na rutuba kubwa ambayo huzalishwa chakula kwa wingi kama vile mpunga, nazi, mboga za majani, korosho, mahindi, nanasi na matunda mengine kibao. Wanafanya nini?
Pamoja na kwamba wanapata fursa ya kupigwa tafu na mashirika kama vile vile WWF, wamehamasika na kuanzisha utaratibu wa kuotesha miti ya asili na kupanda kwenye shamba lao lenye hekari 60 huko Nyambili. Vile vile wana vitalu vyao vya kuotesha miti ya asili ambao hupanda kwenye shamba lao kwa ajili matumizi mbalimbali ikiwamo uchomaji mkaa. Wanatoa elimu kwa wanakijiji wenzao juu ya uchomaji mkaa kwa njia za kisasa
Nini kinaendelea?Kikundi cha uchomaji mkaa endelevu (KIUME) wamechukua hatua baada ya kuona uharibifu unaoendelea katika kijiji chao cha Nyambili na vijiji vya karibu kuanzisha utaratibu wa kutunza mazingira ambao ni wa aina yake. Waliona kuwa uchomaji mkaa ni suala ambalo ni gumu kuachana nalo. Sasa wamekuja na njia kabambe za kunusuru miti katika uchomaji mkaa kwa kiasi kikubwa
Tuhifadhi, tutunze na tuyalinde mazingira yetu ili yatutunze.
8 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
MAMBO YA FEDHA
Pamoja na kwamba tunaunga mkono juhudi za kutunza mazingira, ni vizuri pia kutoa elimu juu ya uvunaji salama wa misitu yetu. Ndiyo, kwani kwa asilimia kubwa bado tunatumia misitu kwa mahitaji
muhimu. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) Rahima Njaidi, alisema zipo njia nyingi ambazo tukizitumia zitasaidia kuhifadhi mazingira huku jamii ikinufaika kwa kujiingizia kipato kutokana na misitu.
Baadhi ya njia hizo ni;• Ufugaji wa nyuki; Jamii inashauriwa itumie
njia za kisasa za ufugaji wa nyuki ambazo inatumia mizinga ya kisasa inayosaidia nyuki kujaa kwa wingi na kuweza kutoa asali nyingi zaidi tofauti na mizinga ya kienyeji. Ufugaji nyuki ni rafiki kwa misitu kwani inapunguza uchomaji moto, kwa kuwa watu/mtu au kikundi kinafahamu kwamba watahatari-sha uwepo wa nyuki na ubora wa asali kwa ujumla
• Uchimbaji na uchumaji wa dawa mbalim-bali za asili ambazo zimekuwa na soko kila pande ya nchi
• Uchomaji mkaa kwa kutumia njia za kisasa. Kutumia matanuri maalumu am-bayo hutumia miti michache na kupata mkaa mwingi. MJUMITA na Tanzania Forest Conservation Group (TFCG) wanashirikiana kutekeleza mradi wa utengenezaji wa mkaa endelevu Wilaya ya Kilosa.
• Ufugali vipepeo; Wananchi wa Amani, Muheza hufuga vipepeo ambao imewanu-faisha sana kwa kujipatia kipato kwa kuuza hata nje ya nchi.Hukaushwa na kutengen-ezwa vidani
• Utalii wa mazingira; ambayo wananchi wanaweza wakatenga sehemu yenye bayo-anuwai likawa kivutio cha watalii
Tuyavune kwa njia salama
J K u m b u k aJuhudi za utunzaji wa mazingira zinahitaji ubunifu wa wananchi wenyewe kuanzisha njia rafiki za matumizi ya misitu ili kuondokana na uharibifu wa misitu itutunze sisi na vizazi vijavyo. Kuwa mstari wa mbele kutetea uhifadhi wa mazingira ili wengine nao waige kwa vitendo.
9NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
NGUVU ZA MWANAMUME
Mengi yanasemwa kuhusu kupiga ‘puchu’, lakini ukweli unabaki palepale kuwa, wake kwa
waume wanajichua wakiwa faragha, na wengine wanahofia kutokana na tetesi wanazozisikia mitaani.
Puchu kwa faragha!
Je kuna madhara?
Wataalamu wa afya wanasema kwamba ni kitendo cha kawaida kisichokuwa na madhara yoyote.
Punyeto inaweza ikawa ni tatizo ikiwa utaifanya hadharani au ikiwa itaingilia shughuli zako za kawaida katika maisha. Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe ndiye mwa-muzi.
Hivi inakuwaje kwani?• Kujichuaaukupigapunyetonikitendo
cha kujisisimua uke au uume kwa kusugua taratibu hadi kufikia mshindo.
• Vijanaambaowanabalehenawanaanzaku-pata hamu ya kujamiiana hujikuta wakipata msukumo wa kupiga punyeto.Hata watu wazima hupiga punyeto na haijalishi wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi au la.
Ukweli wa kitaalamu kuhusu kujichua;
• Husaidiakupunguzamsongowamawazo.• Kingasahihidhidimagonjwayamaambukizi
ya ngono na ya VVU.
• Kutulizahamuyamapenzikwamtuambayehayuko tayari kufanya mapenzi.
• Husaidiakufurahiazaidikitendochakujamii-ana kwa kuwa unakuwa unajua nini kinacho-furahisha
Hizi ni baadhi ya imani potofu eti;•Wasiowezakutongozandiyowanaopiga punyeto
• Husababishamatatizoyaakili,upofunakupoteza uwezo wa kufanya mapenzi
• Nywelekuotakatikaviganjavyamikono.
• Wanaumekuishiwanguvuzakiumekama watapiga punyeto sana.
• Kunenepaupandemmoja.
• Watuwenginewanawezakufahamukama unapiga punyeto kwa kukuangalia.
J K u m b u k aHakuna mtu aliyezaliwa akijua jinsi mwili wake unavyoitikia msisimko wa kimapenzi. Inabidi kupata ushauri nasaha.
10 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
Wizi mtupu!Sakata la mabadiliko vyanzo vya maji kukauka, lilileta tafrani katika Kijiji cha Mtiki. Wanakijiji walianza kunyoosheana vidole kumtafuta mchawi huku kila moja akitafakari pa kuanzia. Haikuwa kawaida lakini kilichotokea baadaye kilikamilisha ule useme usemayo; kikulacho kinguoni mwako. Fuatilia mchezo huu.
Mchezo huu umeigizwa na Pamoja Art Group kutoka Ikwiriri, Rufiji. Huu ni mchezo wa kuigiza na hauna uhusiano wa moja kwa moja na maisha halisi ya waigizaji
Sawa mume wangu
Haya sasa, Ogama na Jindai wamekubaliana kufanya kazi pamoja. Jindai hajauliza ni kazi gani kwa kuwa anamwamini rafiki yake Ogama hivyo haikuwa kitu muhimu kuuliza bali aliona bora ‘liende’! Twende pamoja…
Aaah! Tuko pamoja
Hofu ya Jindai imeanza siku ya kwanza tu kuingia msituni. Si kwamba anaogopa kukamatwa, bali anahofia wanyama wakali. Tuendelee na stori.
Mke wangu sasa hivi endelea na shughuli za shamba, nami nikafanye shughuli nyingine
Usije ukaniangusha kama unaogopa useme mapema
Unajua kuwa tunavyotunza haya mazingira ndiyo haya maji hayakauki
Huu ni muujiza kabisa.
Mwaka huu hayataisha
Msitu mkubwa sana, hakuna wanyama kweli?
Acha uoga bwana twende!
KIKAO CHA KAMATI YA MISITU…
Kila mwananchi analo jukumu la kulinda rasilimali za kijiji chetu ikiwamo misitu.
Siku hizi kuna malori mengi ya magogo hapa kijiji
11NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
YUKO NA RAFIKI YAKE WAKIP-ANGA KWENDA MSITUNI…
Jana kwenye kikao cha misitu tumetakiwa kufanya doria kwenye msitu
Niko ‘busy’ na mambo yangu
Labda kuna mti mkubwa maeneo hayo
Mwaka huu mzee umejipanga!
Maisha ni kuhangaika!
Hilo ndiyo kiboko ya miti.
Mwaka huu una mpango gani na miti ndugu yangu? Mmh!
Kawaida tu
Unaweza kazi za hatari
Kama inalipa niko tayari
Huu ni muujiza kabisa.
Mbona leo njia tofauti na sisi?
Ogama amenunua msumeno mpya ameamua safari hii
Hata vifaa siunaona ni vipya?
UWAZI BAADA YA MITI KUKATWA ENEO LA HIFADHI…Kila mwananchi analo jukumu la kulinda
rasilimali za kijiji chetu ikiwamo misitu.
12 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
TUENDELEE ILI TUONE MWELEKEO WA KILA MMOJA. MWINDAJI APIGWA NA BUTWAA MSITUNI…
MAMBO YAMEBADILIKA KISIMANI…
Ogama na Jindai wameuza mkaa. Maisha yamebadilika kwani kwa masuala ya mshiko sasa wako vizuri. Ni jukumu la kila mmoja kupangilia matumizi ya pesa zake.
Matokeo ya uharibifu wa vyanzo vya maji umeanza kujitokeza lakini wenyeji bado hawajui ‘mchawi’ ni nani. Tuendelee
Hapa tukivuna umaskini kwisha!
Nashukuru sana kwa kunishirikisha hili dili kaka
Hiki kisima miaka yote hakijawahi kuishiwa maji hivi
Vipi Ogama mbona siku hizi hatukuoni kwenye maeneo yetu ya mkaa?
Nahisi waliokata ule msitu ni kina Ogama kwani siku hizi hatuwaoni kwenye eneo la siku zote la mkaa
Labda wamekiloga ndugu yangu
Nikifanikiwa nitakuambia uwe ‘mpole’.
Pesa nilizonazo kwa sasa nitakununulia nyumba
Nami nitakupenda milele
Daaaah!! Yaani msitu wa hifadhi ndiyo umekatwa hivi?
Inawezekana hawa ndiyo wamesababisha maji kuisha haraka
Nimepewa taarifa ya kusikitisha sana na inatubidi tukawatege huko huko msituni
Hawa lazima tuwapate
Inawezekana kwani ni majuzi tu nimesikia wameshusha mzigo mkubwa na hakuna anayejua umetoka wapi.
13NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
Watu kama hawa ambao hupenda kuharibu mazingira kwa ufinyu wa uelewa wao wako wengi sana katika vijiji vyetu. Tutoe taarifa pale tunapoona uharibifu wowote kwenye vijiji vyetu.
MWINDAJI KWA MTENDAJI WA KIJIJI…
BAADA YA SIKU KADHAA…
TATIZO LA MAJI LINAZIDIKUWACHANGANYA WANAKIJIJI…
MZIGO UKATUA KIJIJINI…
Zile gunia mia mbili za mkaa? Subiri konda wangu aje.
Twende tukachukue ule mzigo niliyokuambia jana
Huyu sasa atatuletea balaa
Lazima mchawi ametoka mbali
Ngoja tukufikirie tutakupa jibu
Kumbe una mzigo wa maana hivi? Naomba niwe nakuja kununua kwenye eneo la uzalishaji
Mtendaji huwezi kuamini msitu wa bonde la kisimani umefyekwa karibu unaisha
Inawezekana ndiyo iliyosababisha maji kukauka kisimani mwaka huu
Hivi tutaishije bila maji?
Tusipotafuta suluhu la tatizo hili tutakwisha
Msimuumize jamani tuwapeleke ofisini
Nilijua tu ni wewe ngoja nikuvunje kiuno
Mtendaji tuokoe! Usilolijua ni sawa
na usiku wa kiza. Kumbe mume wangu alikuwa akifanya kazi za uharibifu wa mazingira?
Mambo hayo. Wahenga wanasema usione vyaelea ujue vimeundwa! Matanuzi ya Jindai hayakuwa ya kitoto
14 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
Hapa tukivuna
umaskini kwisha!
Nashukuru sana kwa
kunishirikisha hili dili kaka
Niko ‘busy’ na mambo yangu
Jana kwenye kikao cha misitu tumetakiwa kufanya msako kwenye msitu
JE, WAJUA?
Kataa katakata kukatakata miti
Suala la mabadiliko ya tabia nchi limekuwa likipigiwa kelele na wadau
wa mazingira sehemu mbalimbali duniani. Utunzaji wa mazingira na utumiaji endelevu wa misitu umekuwa ukihimizwa mara kwa mara duniani kote. Kwa baadhi ya watu, suala la utunzaji wa mazingira limekuwa ni kama hekaya za abunuwasi. Wengine wanafikiri kuwa kama si mashirika au taasisi fulani, basi ni wenyeviti wa Serikali za Vijiji na viongozi wengine wa Serikali ndiyo wanaohusika na suala la utunzaji wa misitu na mazingiria kwa ujumla. Tunasahau kwamba misitu hii inapoangamizwa jamii yote inaathirika na majanga kama vile, ukame na njaa yanatukumba sote
Fahamu ya kuwa:
• Misitunichanzochakikubwa mvua amba-zo sikuhizi zimekuwa ni za msimu kutokana na kutokomea kwa misitu mingi hapa nchini
• Misitunichanzoki-zuri cha mapato ikiwa itatumika kwa ufugaji wa nyuki.
• Paleunapokatamti,unatakiwa kupanda miti.
15NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
Maisha ya mwanadamu yamezungukwa na miti, miti hii hutuletea mvua,kivuli na hata matunda. Kwa ufupi ni kuwa kama tutaitunza hii miti, basi na yenyewe itatutunza, lakini kama hatutaituza, maisha yatakuwa ni majanga tu.
Tuyafahamu haya:
Misitu inatokomea kwa kasi ya ajabu hapa Tanzania. Shughuli za ukataji wa miti kwa ajili ya kutengenezea samani za ndani na magogo yanayosafirishwa nje ya nchi, zimesababisha kutokomea kwa miti ya asili na sasa, samani hizo hutengenezwa kwa kutumia miti kama miembe na mikorosho. Uchomaji wa mkaa kwa staili ya Ogama na mwenzake Tindare unawakilisha vijana wengi ambao huamua kujilipua na kujaribu zali bila kufikiria matokeo yake kwao na kwa jamii inayowazunguka.
Nani awajibike?
• Kilammojawetuanatakiwakuipa misitu kipaumbele
• Elimuyamisituiendeleekutolewa mara kwa mara ili watu watambue umuhimu wa misitu.
• Watuwanapoambiwawasikatemiti, waonyeshwe njia mbadala ya kujiingizia kipato.
• Tuwafichuewatuwanaoingiakukata mitit kwa siri kwenye misitu iliyohifadhiwa.
SwaliJe,unadhani ni mbinu gani zitumike ili kulinda misitu ya hifadhi isiharibiwe na majangili?
Tuma maoni yako kwa ujumbe mfupi kwenda namba 0715568222
Hivi tutaishije
bila maji?
Tusipotafuta suluhu la
tatizo hili tutakwisha
TATIZO LA MAJI LINAZIDI KUWACHANGANYA WANAKIJIJI…
16 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
Mabalozi wa mazingira Rufiji ndiyo hawa…
Baada ya kuona mabadiliko yasiyo ‘rafiki’ yakiendelea kutokea kila mwaka, walikaa chini na kutafakari ni kitu gani wangeweza kukifanya ili kuokoa ‘jahazi’. Muungano wa watu 12 ndiyo uliounda Rufiji
Environmental Group (REG), mwaka 2006 ambayo umejikita katika kutunza mazingira hasa vyanzo vya maji na upandaji miti. Makao makuu yao ni Kibiti lakini wanahudumia maeneo yote ya Wilaya ya Rufiji. Ukiwakuta utafurahishwa na uchapaji kazi wao. “Tunafanya kazi mfano wa nyuki na kila mtu anajua majukumu yake. Hafuatiliwi mtu hata kidogo,” alisema Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Musa Mapesa.
Walianza hivi...
Walipopata wazo la kuwa mabalozi wa mazingira, walipeleka maombi kwenye ofisi ya Serikali ya Kijiji ili watumie Bonde la Bwawa Kibibi kupanda miti na kuwauzia wananchi wa Rufiji ili wapande. Walipokubaliwa, walianza kufanya utafiti wa mbegu za miti ya asili na kuzikusanya na kuzihifadhi kwenye kituo walichokianzisha. Waliomba msaada wa mafunzo huko Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Idara ya Maliasili jinsi ya kuandaa na kuendeleza vitalu. Walipewa mafunzo na wakaanza kazi rasmi ya upandaji miti.
Wanashughulika na haya
• KuhifadhiBwawaKibibilililoko Kibiti ambalo ni chanzo kikubwa cha maji.
• Kutengenezaajirakwavijana kwa kutumia maji hayo kwa kupanda miti ya biashara.
• Kuelimishajamiiijueumuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.
• Kuuzamitinakujipatiakipato rafiki kwa mazingira.
TULICHOVUNA
Baadhi ya miti wanayopanda…
• Mkongo• Mpingo• Mpangampanga• Mkuruti• Mtondoro• Mtanga• Mkenge• Mwarobaini
Moja ya miche inayooteshwa na REG kwenye vitalu vyao huko Kibiti, Rufiji.
17NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
Haya ndiyo mafanikio yao
• Wamepandahekarinanezamiti• Wamepataujuziwaupandajimitina
sasa wanawaelimisha watu wengine hapo kijiji Kibiti
• Wamekuwa kituo cha mafunzo yautunzaji mazingira na upandaji miti kwa shule za Rufiji na wananchi wake
• Wamefanikiwa kuonyesha kazi zaokwenye maonyesho ya kitaifa ya Nanenane na zimeleta hamasa kubwa
• Wamejiajiri
Changamoto zipo;
• Mwamkowawananchijuuya utunzaji mazingira bado ni mdogo
• Ukosefuwausafiriambaoun-gewasaidia katika ukusanyaji wa mbegu za miti za asili msituni
• Baadhiyawanakikundikutoji-amini juu ya kazi wanayofanya ingawa ni wachache wenye hofu hiyo
Malengo
• Kununuakiwanjanakujengaofisi na nyumba za wanachama
• Kufuganyuki• Kuanzishamashambayamitina
matunda ya asili• Kufugakukunasamakiiliku-
jiongezea kipato
J K u m b u k a
Utunzaji wa miti hutupa maisha marefu na yenye furaha hivyo tunawahamasisha wananchi wote wazingatie kuwa kuharibu mazingira kwa lengo la kupata faida binafsi ni hatari kwa jamii. Kuwa wa kwanza kusema hapana kwa uharibifu wa mazingira.
Wafanya kazi wa REG wakionyesha eneo wanalotumia kupanda miti na kutun-za chanzo cha maji cha Bwawa Kibibi walipotembelewa na timu ya Si mchezo, Majuka (wa pili kushoto) na Suleyman ( kwanza kulia)
18 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
CHEZASALAMA
Jiulize, tuko wangapi?
Kuwa katika mtandao wa kimapenzi imekuwa kama ‘fashion’ siku hizi, vijana wanakuwa ndani ya uhusiano lakini
wanapotakiwa kuwataja wapenzi wao hupatwa na kigugumizi. Si umeshawahi kusikia nyumba ndogo, kidumu, kicheche, chipsi funga, ATM, buzi, serengeti boys, mario, kibustani na ‘sugar mami?Hapa sizungumzii walio nje ya ndoa tu, maana kuna wanandoa wasio waaminifu kwenye ndoa zao. Uaminifu ni suala nyeti kwenye uhusiano wa kimapenzi, kama umesahau kuwa mwaminifu, jiulize swali moja tu je, tuko wangapi? Tulizana.
Madhara ya kuwa katika mtandao wa mapenzi…
• Kuvunjikakwauhusianokatika familia.
• Kupatamsongowamawazo.• Kusambazavirusivya
ukimwi.• Kujishushiaheshimakatika
jamii.
Mwanamume yeyote rijali namwanamke yeyote anayeshirikikatika mapenzi anahusikakwenye kampeni hii.
Mlengwa ni nani hasa?
19NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
Kwa nini ujiulize?
Inawezekana mpaka sasa hivi una imani kuwa uko peke yako, kumbe upo na ‘wenzako’ ni vyema ukajifahamu upo katika mazingira gani ya kiuhusiano na mpenzi wako. Wengine wako kwenye mtandao huku wakijua lakini wanapuuzia. Badilika! Madhara yake ni kujiweka katika hatari ya kuambukizwa magonjwa ya maambukizi ukiwemo Ukimwi.
Sababu za mtandao
• Mara nyingi hutokana na misukumo mbalimbali iliyopo katika makundi rika ili kuwezakukubalika kihisia, kingono na kiuchumi ili kuonyesha kwamba umekamilika.
• Sababuzakihisiazinakuwapalemtuanapohisihakunamapenzikatiyakenamwenzawake.Unawezaje kuepuka hii? Ni kwa kutenga muda mwingi wa kuwa pamoja na kuzungumza mara kwa mara na hata kutumiana meseji za simu mnapokuwa mbali.
• Kutoridhishanakingononimojayamatatizomakubwakwenyemahusiano.Wengihunyamazana kujikaza ‘kisabuni’ wakiogopa kuwaambia wenzi wao ili mahusiano yasiingie dosari. Hilo sio suluhisho, cha kufanya ni kuzungumza na mwenza wako kwa njia ya upole mnapokuwa faragha bila kumkwaza,fanyeni maandalizi ya kutosha ,na jitahidi kuongeza ‘mautundu’.
• Tamaazamkwanjawafastafastanamaishayaanasakulikouwezobinafsihuwaunganishawengi katika mtandao. Ukitaka kujinasua hapa, ridhika na ulichonacho pia muheshimu huyo uliyenaye. Pangeni kwa pamoja mkakati wa kujinasua kiuchumi, tengenezeni bajeti na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.
JK u m b u k aKama mtu mmoja katika
mtandao ameathirika, kila mmoja aliye katika mtandao yupo katika hatari ya kupata maambukizi hata kwa wale ambao ni waaminifu kwa wapenzi wao lakini wapenzi wao wanasaliti uhusiano wao.
20 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
BURUDANI
Uuuu, Aaaa, oooYou know what Kevy, this is my life man, Stamina
Ubeti wa KwanzaNapigwa msumari wa kichwa mwili unangoja kaburi,Maisha yamenipiga picha nega zimetoka vivuli,Dunia tambara bovu nalidekia kwa shida,Jitahidi kuisolve bila kutumia four figure,Natamani nisimame ili nione magharibi,Moyo umejawa ukame, kuhema unajitahidi,Macho yote yanaukungu utadhani chungu cha bibi,Nata-kumuomba Mungu shetani anazidi spidi (Men) Vizuri viko wapi, navisaka havionekani (dah)Napata makapi vinono navitamani,Sina baba, sina mama, sina babu, sina bibi,Uchumi wangu umesimama kama behewa la itigi,Umasikini unanipodoa bila kutumia cosmetics,Daily unanizodoa unanivuta bila magnetics,Maisha yangu hayana swaga kama masai wa njiro,Natamani kula burger naishia viazi vya Gairo,
KiitikioLeo nimepata kesho nimekosa,Nachohifadhi maumivu tu, laifu ni ngumu bado inan-ichosha,Nakula mbichi sili mbivu,Uweza mimi bado ni kabwela, sina uhuru kama niko jela x 2Ubeti wa piliKusoma kitajiri, kichwa kimejaa madufu,Maisha hayana tafsiri usidhani yanamjua rufufu,Naichora lami na mkaa kwa kudhani nitaona chochote,Atleast class ningekaa, nisingeitwa kiokote,Pesa imegeuka Yuda, daily inanisaliti,Mishale inazidi muda, utajiri unaninyima siti,Maisha kama gwaride, Kuna wa mwisho na wa kwanza,Yakisema nyuma geuka, wa mwisho anakuwa wa kwanza,Taifa la kichwa changu rais wake naona kichaa,Na kitabu cha dhambi zangu kwa Mungu kimeshajaa,Napatwa wazimu shida zinanitia madoa, pesa imekuwa adimu kama bikra kwa changudoa,Banda ninalofugiwa sihemi halina dirisha,Wasichana wananikimbia, wananiita nyoka wa kibisa,
Msosi wangu sio wa draft, sili mpaka nijitumeMaisha yana supa shafti yashanizidi nguvu za kiume.
Kiitikio
Ubeti wa tatuUshindi wangu ni uchafu, kwenye vita ya wasafi,Kila ninayemuomba tafu anataka nifanye naye ulafi,Maisha ni kombolela, maskini ndio mlinda kopo,Cha msingi ni kuunga tela mpaka nitoke kwenye msoto,Jua linapozama natamani pasikuche, hasi inageuka chanya,Kapeto anageuka sunche, naona alama za mlango ila sioni pa kutokea,Hii pesa imetoka jando inataka kunibabu Seya,Nimegeuka konokono natembea na mzigo shida,Silali nimekuwa pono maisha yanakwenda na mida,Shida zishanipa ustaa zaidi ya kanda ya Loketo,Utumbo umezoea njaa hadi shibe naiona mseto,Vikombe vya uaminifu nishavivunja mtaani,Na vijiko vy uhalifu nishaviweka kwenye sahani,Mi nadhani haya maisha yana ramani, ila aliyewachorea masikini peni iligomea njiani
Kiitikio
Wimbo: KabwelaMsanii: Stamina ft Richard Mavocal
!
21NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
J
!!! !
Asiyesikia la mkuu…
Afisa mmoja wa misitu alikwenda kwenye shamba la miti kukagua, msimamizi akamwambia usiingie sasa hivi. Afisa akatoa kitambulisho cha kazi akamwam-bia “wewe ni nani wa kunizuia?” Unaona kitambulisho? Msimamizi akamwambia pita wewe ni mtu mzito bwana. Kupita tu akaanza kupiga makelele “nyuki nakufaa nisaidieee” Jamaa akamwambia wao-nyeshe kitambulisho!
Jamaa na mtoto
Jamaa aliingia kwa kinyozi na mtoto mdogo akase-ma anyolewe yeye kwanza. Alipomalizwa ,akasema, “poa endelea kumnyoa mwanangu naenda dukani halafu nakuja kumpitia” Mtoto akanyolewa. Baada ya saa moja jamaa hakurudi!! Kinyozi akamwuliza mtoto, “Kwani baba yako anarudi saa ngapi?” Mtoto akajibu, “huyo si bàbangu, amenipata hapo nje akaniambia tuje hapa tunyolewe bure”.
J
Mwanafunzi amchanganya mwalimu
TICHA: Kati ya pesa na akili wewe ungechagua nini? Haya Juma tuambieJUMA: Ningechagua pesa mwal-imuTICHA: Ningechagua akili. Sasa Juma kwa nini umechagua pesa badala ya akili?JUMA: Kila mtu huwa anachagua kitu ambacho hana
Wanafunzi ‘wamtesa’ konda…
Usiku mmoja konda alikuwa amelala, ghafla mdogo wake akaamka na kwenda chooni, alivyorudi ile anafunua neti tu, Konda akamzuia na kumwambia wanafun-zi wanatosha..
JMdada agonga mwamba
Mdada na mkaka walikuwa wan-apita madukani, si mdada akakiona kiatu kimoja kizuri, bei 60,000/-.
MDADA: Mweee kiatu kizuri ningekuwa sijasahau pesa nyumbani ningeki-nunua, ninunulie jamaniMKAKA:Chukua hii 5,000/-, kodi taxi uka-chukue hela yako ‘sweety’ naku-subiri hapahapa.
22 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
PASIPO NA DAKTARI
Msaada unapoumwa na nyuki…
Wahenga wanasema fuata nyuki ule asali, lakini wakati mwingine unaweza
ukajikuta umeambulia maumivu ya ajabu kwa kuumwa na nyuki. Pamoja na kwamba asali yao ni tamu lakini si rahisi kuipata, lazima ujipange ili ufanikiwe la sivyo manundu yatakuhusu.
Uking’atwa na nyuki;
• Ondokaeneohiloharakakwaninyukihutoa harufu maalumu ya kuwaita wen-zake hivyo ukiendelea kuwepo mahali hapo watakudhuru zaidi
• Ondoamshalewanyukikwamakuchaharaka, usitumie kibanio, kinaweza kufinya sumu ndani ya mwili.
• Wekabarafuaukitambaakilichototase-hemu uliyoumwa na nyuki kuzuia kuvimba na kupunguza maumivu.
• Jipakemchanganyikowamajinahamiraulipoumwa kuzuia maumivu.
• Mezatembezakupunguzamaumivuaumuwasho
• Endapounamzio(Allergic)ukang’atwananyuki ni vyema ukawahi kituo cha afya bila kusubiri dalili za mzio
Madhara ya kung’atwa na nyuki
Madhara hutofautiana kwa kila mtu kwani mfumo na kinga hutofautiana haya ni baadhi;• Maumivumakalisehemuuliyong’atwana
wakati mwingine kusambaa mwilini• Kuvimba• Kuwashwa• Endapomshalewanyukiutabakimwilini
kwenye pua, mdomo au koo huweza kukusababishia upate shida ya kupumua.
J K u m b u k aKung’atwa kwa nyuki inauma sana na wakati mwingine husababisha kifo kwa wale ambao wana mzio wa sumu ya nyuki. Njia salama ya kupunguza na kuondoa maumivu au mmenyuko ni kuondoa mshale haraka iwezekanavyo.
23NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
HUDUMA
Wafahamu MJUMINGU
Ni kifupi cha Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Msitu wa Ngumburuni
uliopo wilayani Rufiji. Mtandao huu ulianzishwa mwaka 2005 ili kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zilianza kujitokeza baada ya kuanzisha utekelezaji wa usimamizi shirikishi wa misitu. Mjumingu unajumuisha vijiji saba vinavyozunguka Msitu wa Ngumburuni ambavyo
ni Mayuyu, Ruaruke A, Mangwi, Mkupuka, Umwe Kaskazini, Umwe Kusini na Umwe Kati.“Tunaiomba Serikali kurudisha misitu kwa jamii badala ya kumilikishwa kwa halmashauri ya wilaya, kwani wanajamii ni rahisi kuisimamia kwa ukaribu, tofauti na wilayani ambapo uwajibi-kaji wa moja kwa moja unakosekana” anasema Katibu wa Mjumingu Bw Mwarami Kwangaya.
Wamefanikiwa
• Kukamatamagogonakuyataifi-sha
• Kupataelimuyakufanyashughuli mbadala ya namna ya kutunza misitu.
• Kupatamafunzokutokase-hemu mbalimbali yahusuyo uongozi na uhifadhi wa misitu.
• Kupunguzakasiyauvunajiharamu wa magogo.
• Kuwashirilishawananchikatikakusimamia misitu na kuwafi-chua wahalifu wanaokata na kusafirisha magogo toka msitu wa Ngumburuni.
Changamoto
• Kukosekanakwavizuizikwenyemaenenoyamali-asili.
• Kukosekanautawalaborawausimamiziwamisitu.• Jamiikutegemearasilimaliyamisituilikupatamahi-
taji muhimu.• Ukosefuwaelimuyamisitunafaidazakekwawana-
jamii.• Ukosefuwavifaanamafunzokwaaskaridoria.• Vijijihavinufaikinamsitu
Kuna sapoti za wadau
Mjumita (Mtandao wa Usimam-izi wa Misitu Tanzania) imekuwa ikiwapiga tafu upande wa kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kuhusu suala zima la uhifadhi wa misitu.
Baadhi ya viongozi wa MJUMINGU huko Ikwiriri, Rufiji
24 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
KATUNI
Michoro: babatau cartoons 2012
KICHAPO!Miti imeleta noma baada
ya kuona kuwa kitendo wanachofanyiwa na binadamu hakistahili. Ni mchezo wa kuigiza lakini ukifuatilia kwa undani utaelewa wanachomaanisha miti hiyo huko kijiji cha Mburuni
25NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
26 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
Miti imewabadilikia wanadamu kwa kile wanachodai kuwa wamekuwa wakiwaonea bila ya kujali faida wanayowapa. Naona ni sawa kabisa kwani wakati mwingie inabidi tuseme hapana!
27NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
UKWELI WA MAMBO
Kilio cha miti
Utawala wa mwanadamu umekuwa na tabaka mbali mbali kiasi kwamba anawanyima viumbe vingine uhuru wa kuishi. Mimea ndiyo wenye kilio kikubwa hasa misitu ambayo hufunika ardhi na kutunza
ardhi yenye viumbe vingine vingi.Kwenye mchezo huu wa katuni tumewajengea uwezo miti ili iweze kujitetea. Ni sehemu ya burudani lakini tukifikiria kwa kina, miti ina kilio kikubwa ambacho ingetamani siku moja izungumze kuwaeleza binadamu juu ya uangamizaji wanaoufanya.
J K u m b u k aTunaweza kutumia bidhaa mbadala tukauacha mti uendelee kuishi ili utusaidie kuleta mvua, kuhifadhi vyanzo vya maji, hewa safi na hifadhi ya viumbe vingine. Kwa kufanya hivyo, itasaidia ama kuacha au kupunguza matumizi ya miti.
Miti wana ujumbe gani?
Inasema kuwa watu wanasahau misaada wanaowapatia na viumbe vingine. Wanyama, ndege na hata wadudu wanauhitaji kwa ajili ya kupata hifadhi na msosi.
Miti hulia kwa kufanyiwa haya;• Kukatwailikututumiakujenganyumbanahatama-
banda ya mifugo• Kuchomwakupatamkaakwaajiliyakupikia.Wen-
gine hutumia kuni kupika.• Mitihukatwanakutengenezaviti,meza,makabati,
vitanda, vijiko, vitana na hata vinyago hutengenezwa kwa kutokana na miti
Njia mbadala zipo?
Kwa dunia ya sasa, teknolojia imeongezeka na zimegundulika njia mbalimbali ambayo mti anaweza akanusurika ingawa bado anahitajika kwa kiasi kikubwa kwa mwanadamu. Hizi ni baadhi tu;• Kutumiagesiaumajikoya
kawaida yanayotumia kiasi kidogo cha mkaa kupikia
• Kutumiaviti,mezan.kvyaplastiki
• Tunawezakupunguzaidadiyavinyago vya miti kwa kutumia udongo ya kutengeneza vinyago
28 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
Wewe pia unaweza kulonga na vijana wenzako. Tuandike maoni, ushauri,
vichekesho,maswali nk, weka anuani yako na tuma ukiambatanisha
na picha yako kwa Mhariri, Jarida la Si Mchezo!,
S.L.P 2065 Dar es [email protected] tumbukiza katika boksi
la Si Mchezo! kama lipo katika eneo unaloishi.
SAUTI YANGU Kama una chochote unachotaka kusema tuandikie ili upate fursa ya kuwaelimisha wengine
Maoni yaliyotolewa katika ukurasa huu ni ya wasomaji, si lazima yalingane na msimamo wa Femina.
Si Mchezo!Femina HIPSLP 2065,
DSM
Biashara yangu
Kero yangu ni kuhu-siana na biashara yangu ya mashine yetu ya kukoboa nafaka. Kumekuwa na majungu sana. Tumekuwa hatu-pendani, tumekuwa hatuna msimamo katika bei zetu za kilo kwa mpunga. Unakuta mtu anapunguza bei ilimradi wateja wote waende kwake, wakati siyo taratibu zetu, kama tunataka kushusha bei basi wote tuwe tunakubali-ana na wote kwenda sawa. Naomba wote tunaohusika tujirekebishe.Abdallah Issa, Rufiji
Polisi punguzeni mzukaKwa nini polisi wanaua watu bila ya hatia? Ina maana uongozi hautam-bui? Kama ni hivyo basi wananchi hawatakuwa na imani na jeshi la polisi. Rais inabidi atambue hili, polisi wanawafundisha watu kuchukua sheria mkononi wakati hii ni nchi ya amani na inaendeshwa kisheria.Shabani MapekweRufiji
Msimamo
Naomba Serikali yetu iwe na msimamo mzuri kwa wananchi wao. Kwa sababu vitu vingi vichafu vinafanyika, naomba waache kudharau. Kama hapa kijiji chetu kinasumbuliwa na wafugaji wanaua watu bila ya kuchukuliwa hatua yoyote ileHaji Omari,Ikwiriri, Rufiji
Magonjwa ya ngono yamezidi!
Vijana wapewe elimu ya kutosha kuhusu masuala ya magonjwa ya ngono kama gono, kaswende na pangusa kama Ukimwi unavyopewa kipaumbele katika kue-limisha jamii kwa kutumia vipeperushi, semina mbal-imbali hasa kwa Wilaya ya Rufiji.Florida MwechiRufiji
29NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
Unamshaurije rafiki yako anayejihusisha kwenye mtandao wa kimapenzi aache?
30 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012
SEMA, TENDA!
“Maliasili” wengi wanaposikia hili neno hili wanafikiri kuwa viongozi wa Serikali na taasisi zinazojishughulisha na mazingira pekee ndiyo wenye wajibu wa kutunza misitu. HAPANA! Misitu ni mali ya jamii yote.Tanzania ni moja ya kati ya nchi ambazo zina neema ya kuwa na misitu mingi ya asili, lakini jambo la kusikitisha ni kuwa jitihada za haraka zisipochukuliwa, misitu hii inaweza kubaki katika vitabu vya historia tu.Misitu hii inatakiwa kutuletea ustawi na utajiri katika jamii. Lakini wakati mwingine maliasili hizi hazitumiki katika njia isiyo ya kidemokrasia na uwazi ili ziwanufaishe watu wote.
Misitu yetu, uhai wetu
Vijana hili ni letu…
Kijana kuwa mfano wa kuiga! Uharibifu wa misitu inabidi usitishwe kwa kuzingatia ushiriki wetu endelevu katika kutunza mazingira kwa kuanza kuyajali mazingira ya mahali tunapoishi kwa kupanda miti zile sehemu zote tulizokata miti, pia kwa kuwafichua wale wote wanaoshirki biashara haramu ya ukataji wa magogo katika misitu ya hifadhi.Kama wewe unafahamu umuhimu wa kutunza mazingira na una muona jirani yako au rafiki yako anaharibu mazingira, mfuate na umuelimishe bila hiyana, kama elimu umempa na bado anaendelea na vitendo vyake, nenda kamripoti maliasili.
Mazingira bora
Hivi umeshawahi kujiuliza kwenye mazingira unayoishi kwa nini kuna vyanzo vingi vya maji na hali ya hewa ya kuvutia? Ni kwa sababu ya misitu inayotuzunguka. Hivyo basi, kutunza misitu hii ni jukumu letu sote kama wana jamii kwa kuwa tunanufaika nayo.Ukataji wa miti tena usiokuwa na mpangilio, unaathiri kwa kiasi kikubwa mazingira tunayoishi na njia muhimu za kujipatia mahitaji yetu ya kila siku. Ardhi imekumbwa na ukame wa kutisha na hata hali ya hewa katika mazingira tunayoishi imebadilika kwa joto kupanda kwa kasi ya ajabu
S w a l iNjia gani zitumike ili kuwahamasisha vijana washiriki katika utunzaji wa mazingira yanayowazunguka?Tuambie kwa kutumia mawasiliano hapa chini:Barua pepe: [email protected] Sms: 0715568222
31NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!
USHAURI
Betty Liduke ni rafiki mkubwa wa vijana, hata wewe unaweza kulonga naye. Ni msambazaji mkubwa wa Jarida la Si Mchezo! Mkoani Njombe. Ni mshauri nasaha na ni Mratibu wa Kitengo cha Udhibiti Ukimwi katika Kampuni ya TANWAT, Njombe.Mwandikie kupitia Jarida la Si Mchezo!Si Mchezo! S. L. P. 2065 Dar es Salaamau tuma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba 0715 568222 na utuambie kama ungependa uchapishwe.
Swali
Kwanza inaonyesha huyo mama haku-pendi, hivyo unatakiwa mkae chini muongee ili akuambie ana msimamo gani juu yako. Beatrice Leonard
Kinachotakiwa ni kumchunguza mpen-zi wako ana msi-mamo gani juu yako. Hapo inaoneka huyo mama yake hakupen-di na hataki mwa-naye akuoe, ndiyo maana anakuzushia maneno ya uongo. Sihaba Mohamedi ,Rufiji
Nina mpenzi, tunapendana, ninafanya kazi Morogoro yeye yuko Dar. Huku niliko kuna wazazi wake, tatizo mama yake amekuwa akinizushia maneno ya uongo kila
siku. Nimemwambia mpenzi wangu, naye anamtetea mama yake, kinachonisikitisha mama yake amesema mtoto wake hatonioa. Naomba ushauri wenu. Nairath.
Hapo hakuna ndoa, cha msingi tafuta mtu ambaye atakupenda na wewe utampenda ili mfunge ndoa.Abdallah Adam,Ikwiriri, Rufiji
Mimi ni msichana wa miaka 24, Nilibahatika kumpata mvulana ambaye tulianza uhusiano. Katika uhusiano wetu sikuwa na haraka ya kutambalishwa kwani nilijua kila kitu kinakwenda na wakati. Mpenzi wangu aliniambia anakaa na mama yake na dada yake na mimi nilimweleza kuwa naishi na mama yangu. Kwa kuwa alikuwa ni mwanamume aliyenionyesha ulimwengu wa mapenzi nilimpenda na kumheshimu. Baada ya miaka miwili ya uhusiano wetu ndipo nilipogundua kuwa mpenzi wangu ameoa na ana mtoto mmoja. Kweli nilipomuona mke wake nilijiuliza mengi. Mama alinishauri niachane naye lakini nampenda sana huyo kijana na sidhani kama kuna mwanamume atakayechukua nafasi yake. Naomba ushauri wenu.Msomaji wa Si mchezo Mbulu, Manyara
Pole kwa maswahibu hayo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa mpenzi wako bado hajawa na uamuzi wa kukuoa kama wewe unavyofikiria. Kuwa na subira, fanya uchunguzi wa kina kuhusu upendo wa mpenzi wako kwako halafu jadiliana naye usikie uamuzi wake. Mara nyingi katika uhusiano wa vijana wazazi wengi huingilia. Ni vyema wazazi watambue kuwa uamuzi wa nani ataishi na mwanaye ni wa kijana mwenyewe, Mpenzi wako akiwa na msimamo tatizo hili litakwisha.
Msubiri arudi ili akwambie kama anataka kuwa na wewe au la. Kama hataki kumbadili-sha mama yake basi achana naye na kila mtu aendelee na maisha yake.Omary Kasim,Rufiji
SWALI LA TOLEO LIJALO