huduma katika kanisa la agano jipyadorkas akafa na kanisa likamuita petro. wakamuonyesha vile...
TRANSCRIPT
HUDUMA
KATIKA
KANISA LA
AGANO JIPYA
Somo la 9 kwa ajili ya Agasti 31, 2019
Kuhudumia ndani ya kanisa
Kuhudumia nje ya kanisa
Kuwahudumia makutano mengine
Kuhudumia kama mtindo wa maisha
Paulo na huduma
Yakobo na huduma
Yesu ametuagiza kuihubiriinjili kwa ulimwengu, kuwafanya kuwa wanafunzina kuwabatiza.
Kanisa la awali lilifuatakielelezo cha Yesu kwakuwajali wenye uhitaji waliondani na nje ya kanisa wakatiwakihubiri injili.
Kanisa likakua sana chini ya uongozi waRoho Mtakatifu. Na waumini wapya“walikuwa na moyo mmoja roho moja.” (Matendo 4:32)
Wale ambao walikua wametoa sana nawale ambao hawakuwa na chochote, hivyohapakuwa na mtu mwenye uhitaji.
Baada ya muda, kugawanya mahitajimiongoni mwa wahitaji pakaleta ugumu, hivyo kanisa likaleta utaratibu waugawanyaji kwa kuteua mashemasi saba.
Huu mfumo-shirikishi haukuendelea katikajumuiya zingine za Kikristo zaidi yaYersalemu, lakini uliweka msingi wakusaidia wenye mahitaji.
Mji wa Yafa ulikuwa umebarikiwa sana kwahuduma ya mwanamke mkristo , Dorkas.
Alikuwa akishona nguo na kuwapatia wale waliokuwa wana uhitaji nazo. Pia alikuwaakitoa msaada kutimiza mahitaji ya maskini.
Hakusaidia washiriki wa kanisa tu, bali yeyotealiyehitaji msaada wake.
Dorkas akafa na kanisa likamuita Petro. Wakamuonyesha vile alivyowasaidia wajane namaskini.
Kuwasaidia wengine bila ubinafsi siyo rahisi. Maisha ya huduma yanahitaji kujikana nafsi, lakinimatokeo yake katika maisha ya wengine ni yaumilele.
Tofauti zikainuka pale injili ilipoanzakupokelewa kwa wamataifa. Baraza likakaakutatua tatizo (Matendo 15).
Paulo aliagizwa kuwafundisha wamataifabaadhi ya mafundisho na kuwajali maskini(Wagalatia 2:10).
Wakati kanisa la Yerusalemu lilipopatwana njaa, Paulo aliyaomba makanisa yawamataifa kukusanya sadaka ilikuwasaidia.
Makanisa mahalia lazima yasaidie kutoamisaada kwa makutano mengine, siyo tukwa mahitaji yao wenyewe.
E.G.W. (Welfare Ministry, cp. 3, p. 32)
Kwenye Warumi 12, Paulo alifundishanamna tunavyowezakuishi na kujihusishana wengine“dhabihu iliyo hai" (aya. 1):
Kama una karama ya huduma, hudumu (aya 7)
Kama una karama ya kutoa, ifanye kwa uhuru (aya. 8)
Kuwa mwenye Kurehemu kwa furaha (aya. 8)
Penda bila unafiki (aya. 9)
Lichukie lililo ovu na fanya lililo jema (aya. 9)
Mpendane kwa pendo la undugu (aya. 10)
Heshimu wengine (aya. 10)
Kuwa na bidii na si mlegevu (aya. 11)
Toa kutimiza mahitaji ya watakatifu (aya. 13)
Kuwa mkarimu (aya. 13)
Furahini pamoja nao wafurahio, lieni pamoja nao waliao (aya. 15)
Kama adui yako ana njaa, mlishe (aya. 20)
Yakobo alikuwa ndugu yake na Yesu na moja ya nguzoya kanisa (Wagalatia 2:9). Wakazi wa Yerusalemuwalimwangalia kama mtakatifu na mtu mwenye haki.
Katika barua yake alitufundisha jinsi ya kuwahudumiawengine:
Kuweka imani zetu katika matendo (1:22)Kuwasaidia wahitaji (1:27)Kuzuia upendeleo (2:1-4)Kuwavika walio uchi na kuwapa chakulawenye jaa (2:15-16)Kutenda kwa haki (5:4)
Huduma yetu ni matokeo ya mwonekano waimani yetu (2:14-17).
“Kristo atayatunza majina ya wote ambao
hawaihesabu kafara kuu itolewayo
kwake juu ya madhabahu ya imani na
upendo… Pale ambapo ubinafsi na
kujisifu vitasahauliwa, watakumbukwa;
majina yao yatahuishwa. Ili tuwe na
furaha wenyewe, ni lazima tuwafanye
wengine wafurahi. Ni salama kwetu
kutoa mali zetu, talanta zetu, na faraja
zetu katika ibada ya shukuran kwa
Kristo, na kwa njia hiyo kuwa na furaha
kwa maisha ya sasa na utukufu wa
kutokufa wa maisha ya badae.”
E.G.W. (Testimonies for the Church, vol. 3, cp. 26, p. 250)