sikika.or.tzsikika.or.tz/uploads/2013/10/publication403.pdf · huduma zote za afya kwa umma...

36
Mwongozo wa Mwananchi Leta Mabadiliko Boresha Huduma za Afya

Upload: others

Post on 24-Feb-2020

41 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Mwongozo wa Mwananchi

Leta MabadilikoBoresha Huduma za Afya

SHUKURANIIdara ya Utawala na Usimamizi wa Fedha za Afya inapenda kuwashukuru kwa dhati wote walioshiriki katika kufanikisha kutayarisha chapisho hili la Mwongozo wa Mwananchi la Leta Mabadiliko katika Kuboresha Huduma za Afya .

Kwanza tunamshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Sikika Bw. Irenei Kiria kwa mchango wake katika kufanikisha uandaaji wa Mwongozo huu.

Pia tunatoa shukrani za dhati kwa Watendaji wa Serikali za Mitaa wa Dar Es Salaam na vijana wa Kujitolea waliowawakilisha wananchi kwa kuufanyia majaribio na kuboresha mwongozo huu. Pamoja na Nathan Mpangala (Kijast) kwa michoro ya katuni na Mhariri Joseph Kulangwa kwa kuhariri mwongozo huu.

Mwisho, tunapenda kutambua michango na juhudi za pamoja za wafanyakazi wa Sikika walioshiriki katika kutayarisha mwongozo huu ambao ni Eva Emmanuel, Florian Schweitzer, Nicholas Lekule, Daniel Mugizi, Godwin Kabalika, na Geline Fuko, Simon Moshy, Lilian Kallaghe na Scholastica Lucas.

Ahsanteni sana!

Irenei KiriaMkurugenzi Mkuu

©2013Shirika la Sikika, Haki zote zimehifadhiwaChapisho la Septemba, 2013Limeandaliwa na: Idara ya Utawala na Usimamizi wa Fedha za Afya

Katuni: Nathan MpangalaMchapishaji: Digitall Ltd.

iiiMwongozo wa Mwananchi

YaliYomoShukurani ..................................................................................................................... ii

Orodha ya Vifupisho ....................................................................................................iii

Dibaji ............................................................................................................................1

Sehemu A: WAnAnchi ni mAWAkAlA WA mAbADilikO .......................................2

Sehemu b: mAbADilikO huAnzA nA upAtikAnAji WA tAArifA.........................5

1. mizania jumuifu iliyokaguliwa .........................................................................5

2. taarifa ya mapato na matumizi ........................................................................7

3. ripoti yoyote iliyotiwa saini na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali ...........................................................................................9

4. mpango mkakati ............................................................................................10

5. bajeti iliyoidhinishwa ......................................................................................11

6. taarifa ya utekelezaji ......................................................................................12

7. taarifa ya matumizi ya fedha ........................................................................13

Sehemu c: furSA zA kuletA mAbADilikO ........................................................14

1. mchakato wa kuibua fursa na Vikwazo kwa maendeleo .............................14

2. kamati za kusimamia huduma za Afya .........................................................18

3. kamati za kudhibiti ukimWi ..........................................................................19

4. masanduku ya maoni ....................................................................................20

5. mkutano mkuu wa kijiji ..................................................................................21

6. mkutano mkuu wa mtaa ................................................................................22

kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko! ................................................................24

Viambatisho ..............................................................................................................25

1. Watendaji wakuu wa Serikali za mitaa ...........................................................25

2. ratiba ya mchakato wa fursa na Vikwazo kwa maendeleo .........................26

iv Mwongozo wa Mwananchi

orodha Ya Vifupisho

Amk Afisa mtendaji wa kijiji

Dmt Dira ya maendeleo ya taifa (2025)

fVm fursa na Vikwazo kwa maendeleo

kkhA kamati za kusimamia huduma za Afya

kku kamati ya kudhibiti ukimwi

kmk kamati ya maendeleo ya kata

ktm katibu tawala wa mkoa

mmmhS mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali

mmW mkurugenzi mtendaji wa Wilaya

mSm mamlaka za Serikali za mitaa

tAmiSemi Ofisi ya Waziri mkuu- tawala za mikoa na Serikali za mitaa

tuh timu ya uendeshaji ya halmashauri

VAt thamani ya kodi

1Mwongozo wa Mwananchi

Sikika ni shirika lisilo la kiserikali lenye lengo la kufanya ushawishi na utetezi ili kufikia upatikanaji wa huduma bora za afya kwa kila mtanzania. Huduma bora za afya ni haki ya kila mwananchi na Serikali ina wajibu wa kutekeleza haki hii. Ili kuhakikisha kwamba haki hii ya msingi inatekelezwa, wewe kama mwananchi una jukumu la kufuatilia mipango mikakati ya serikali na bajeti na hakikisha kuwa serikali inawajibika kwa vitendo.

Usimamizi wa huduma za afya ya jamii unaweza kufanikiwa kutokana na ushiriki wako katika mchakato wa bajeti. Upatikanaji wa taarifa za bajeti utakuwezesha kufahamu vema kazi za serikali, na kutumia fursa zilizopo kushawishi mipango ya maendeleo na bajeti ya jamii yako.

Hata hivyo, ufuatiliaji wa uwajibikaji wa jamii unaweza kuwa ni kazi ngumu na yenye changamoto nyingi. Ili kutimiza wajibu huu kikamilifu, unapaswa kujua ni jinsi gani unaweza pata nyaraka za bajeti, na unatakiwa kuwa na uwezo wa kufanya hitimisho kutokana na taarifa hizo kwa kutumia maarifa na uzoefu ulionao katika mikutano ya jamii. Andiko hili linajaribu kusisitiza jukumu hilo.

Baada ya kupitia Mwongozo huu, tunakuhimiza wewe kushirikisha familia na marafiki zako katika kujadili jinsi gani mnaweza kuuboresha mwongozo huu. Sikika inakuomba utushirikishe uzoefu wako ili tujifunze kutoka kwako na kuboresha machapisho yetu yajayo.

Dibaji

2 Mwongozo wa Mwananchi

Huduma Bora za Afya kwa Watanzania wote Ili kuishi maisha marefu na ya furaha, kila mtu anahitaji kupata huduma bora za afya. Kwa bahati mbaya, Tanzania ni nchi masikini na mfumo wake wa huduma za afya unakabiliwa na uhaba wa fedha ambao husababisha vikwazo kama vile; mazingira magumu ya kufanyia kazi na utendaji usio na tija. Wewe kama mwananchi unaweza saidia kuboresha mfumo wa huduma za afya kama utashiriki kikamilifu katika mchakato wa bajeti.

Huduma za Afya Zinahitaji FedhaUnatakiwa uelewe kwamba, kila huduma huhitaji fedha, na huduma za afya ni mojawapo. Serikali inapaswa kugharamia ujenzi na matengenezo ya vituo vya huduma, kulipa mishahara waganga na wauguzi pamoja na kununua dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Fedha zinatoka wapi? Zinatoka kwako! Kila wakati unaponunua au kuuza kitu (kwa mfano sukari, unga, mchele, mafuta n.k.) serikali hupata sehemu ya pato ambayo hujulikana kama (Thamani ya Kodi, kwa lugha nyepesi ni VAT), na fedha hizo hutumiwa kulipia huduma za jamii kwa mfano huduma za afya. Pia inakutoza wewe ada ya huduma fulani (kama vile maji na umeme) ili kugharamia uwekezaji wa umma (kama miradi ya miundombinu). Serikali pia inaweza kukopa fedha kutoka taasisi za fedha (benki). Hata hivyo, wakati wa kurudisha mikopo hiyo, serikali hutumia fedha zako unazokatwa katika huduma mbalimbali.

Pia kuna kiasi kikubwa cha fedha hutoka kwa walipa kodi wa nchi tajiri (zilizoendelea) ambazo hutoa misaada ya kimaendeleo kwa watu wa nchi maskini ikiwamo Tanzania.

Mzunguko wa Bajeti Bajeti ni zana ya kuchanganua matumizi ya fedha ambayo serikali huitumia katika kufikia malengo yake. Bajeti hupangwa kutumika kwa kipindi cha mwaka mmoja wa fedha ambao hugawanywa katika hatua tatu:

1. Hatua ya Mipango,2. Hatua ya Utekelezaji, na3. Hatua ya Ufuatiliaji.

Sehemu a: Wananchi ni maWakala Wa mabaDiliko

3Mwongozo wa Mwananchi

Katika hatua ya mipango, serikali huandika mapendekezo ikieleza jinsi inavyopanga kupata fedha kutoka vyanzo mbalimbali na jinsi inavyopanga kuzitumia; mpango huu wa awali unaitwa ‘mapendekezo ya bajeti’. Baada ya mapendekezo ya bajeti kuwasilishwa na kupitishwa na Bunge, mpango huwa sheria na kuitwa ‘bajeti iliyopitishwa’. Je, unashirikije katika hatua ya kupanga mipango ya bajeti?

Katika hatua ya utekelezaji, serikali huanza kutoa huduma kwa jamii kwa kuzingatia mpango wa bajeti ulioidhinishwa. Hata hivyo, ubashiri ni mgumu kwani mara nyingi kuna uchelewaji katika ukusanyaji mapato na ugawaji fedha kutoka Wizara ya Fedha kwenda kwa maelfu ya ofisi za serikali na zile zitoazo huduma kwa jamii. Hivyo, yaweza kutokea kwamba mpango wa awali wa bajeti ukashindwa kutekelezwa hadi mwishoni mwa mwaka. Je, unasimamiaje hatua ya utekelezaji wa bajeti?

Katika hatua ya ufuatiliaji, serikali huangalia utendaji wake na kuelezea kwa wananchi kama kuna hitilafu zozote zilizojitokeza katika bajeti iliyopitishwa. Kazi kubwa na muhimu hufanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (MMKHS) ambaye hukagua hesabu zote za serikali ili kuhakikisha kwamba taarifa zote za kifedha ni za kweli. Je, unafuatiliaje hatua ya usimamizi wa bajeti na mapendekezo yaliyotolewa kama yamefanyiwa kazi kikamilifu?

Baada ya mwaka wa fedha kukamilishwa na hatua hii ya ufuatiliaji, mwaka mwingine wa fedha huanza kwa kupanga bajeti mpya. Utaratibu huu hurudiwa kila mwaka na ndiyo maana huitwa ‘mzunguko wa bajeti’.

Wananchi ni sehemu muhimu ya mzunguko wa bajetiWananchi wana nafasi kubwa katika mchakato wa kuboresha utoaji huduma na hakuna mtu anayetakiwa kuzuiwa kushiriki katika maamuzi muhimu yanayoathiri jamii. Kila mtu anatakiwa kuhakikisha kwamba mahitaji yake ya maendeleo yanatimizwa na watoa huduma na kwamba mafanikio yanapatikana. Ushiriki katika mchakato wa mipango, utekelezaji na ufuatiliaji katika huduma za afya ni muhimu, lakini ni wananchi wachache tu ndio wanaotambua jinsi gani wanaweza tumia taasisi zilizopo kwa ukombozi wao.

Huduma zote za afya kwa umma zinafadhiliwa na bajeti ya Serikali ambayo hupitishwa na Bunge baada ya mchakato mrefu wa mipango ambao huanzia katika ngazi ya kijiji na kumalizikia katika Wizara ya Fedha. Ni kawaida katika mchakato wa kidemokrasia kwa makundi tofauti kuwa na maoni tofauti juu ya matumizi ya fedha zilizopo. Wananchi wanahitaji kujifunza jinsi wanavyoweza kuchangia mchakato wa upangaji bajeti katika hatua za awali kwa kuamua ni sekta gani muhimu (afya, maji, elimu, usafirishaji na kilimo) zinatakiwa kupewa kipaumbele. Pia, wanahitaji kutumia nguvu zao za kisiasa dhidi ya madiwani na wabunge kuhakikisha kwamba fedha hizo zinawanufaisha watu masikini na wasiojiweza, watoto na wazee na si wale wanaotaka kujitajirisha wenyewe.

Aidha, wananchi wanahitaji kuona viongozi wao wakitekeleza bajeti kupitia matumizi ya fedha za umma katika shughuli mbalimbali. Lakini baadhi ya wananchi hawaonyeshi shauku ya kuhudhuria mikutano ya jamii, kwa kuwa hawana uelewa

4 Mwongozo wa Mwananchi

mzuri juu ya masuala yanayojadiliwa au kwa sababu hawatarajii maboresho katika utoaji wa huduma.

Ili kutimiza wajibu wao kikamilifu, upatikanaji rahisi wa taarifa za bajeti ni jambo la msingi. Ni dhahiri, kuna sheria, kanuni na miongozo kadhaa inayoitaka Serikali za Mitaa kutoa taarifa ya matumizi ya fedha za umma, ila ni wananchi wachache ndio wenye uelewa wa mambo hayo au hawajui jinsi ya kutumia taarifa hizo katika kuboresha huduma hususani huduma za afya.

Wananchi; mnaweza kuwa mawakala wa mabadiliko! Mwongozo huu umeandaliwa kama nyenzo kwa watumia huduma za afya wanaohitaji maelekezo na kufahamu jinsi wanavyoweza kujielimisha juu ya vikwazo vilivyopo katika jamii yao na namna gani wanaweza kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo.

Tunatumaini kwamba, baada ya kusoma mwongozo huu, utakuwa unajiamini na kuchangia katika mchakato wa mipango. Vilevile utaweza kuhakikisha kwamba maofisa wa Serikali za Mitaa/Vijiji na watoa huduma za afya wanatimiza wajibu wao kikamilifu.

5Mwongozo wa Mwananchi

Kwa nini upatikanaji taarifa ni jambo la msingi?

Ili kushiriki vema katika masuala ya kijamii, wananchi wanahitaji kupata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu mikakati na maendeleo ya jamii yao, rasilimali zilizopo na uhalisia wa utoaji huduma.

Kulingana na kifungu cha 90 (i-ii) cha Memoranda ya Fedha ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1997, Halmashauri zinatakiwa kuchapisha na kutangaza katika ofisi zao na katika magazeti yaliyopo katika maeneo yao ya wilaya, kata, vijiji na mitaa taarifa mbalimbali za bajeti ili kurahisisha upatikanaji na matumizi ya taarifa hizo kwa umma; Taarifa za bajeti zinazotakiwa kuchapishwa ni kama zifuatazo:

�� Mizania jumuifu iliyokaguliwa

�� Taarifa ya mapato na matumizi (muhtasari wa hesabu) na

�� Ripoti yoyote iliyotiwa saini na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

Katika kurasa zinazofuata, tutaelezea malengo ya nyaraka hizi, nini wananchi wanachoweza kujifunza kutoka katika nyaraka hizi na jinsi gani wanaweza kuzitumia katika kushiriki katika masuala ya kijamii.

1. Mizania Jumuifu Iliyokaguliwa

Hii ni aina gani ya nyaraka?

‘Mizania’ ni ufupisho wa taarifa ya hali ya kifedha ya taasisi kwa kila mwisho wa mwaka wa fedha. Taarifa hii inaelezea aina ya rasilimali ambazo taasisi inamiliki (mali), kiasi gani cha rasilimali ambacho taasisi husika inadaiwa na wengine (madeni) na rasilimali zilizobaki (mali halisi) ambazo zinamilikiwa na serikali.

Neno ‘Jumuifu’ linamaanisha nyaraka inayojumuisha mali na madeni ya taasisi mama na matawi yake yote kana kwamba yako katika shirika moja. Neno ‘Iliyokaguliwa’ linamaanisha kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, ambaye hupitia mahesabu yote ya serikali, alihakikisha uhalali wa taarifa zilizowasilishwa baada ya utafiti na kujiridhisha; hii inaonesha kwamba tunaweza kuamini taarifa zilizomo kwenye mizania hii.

Sehemu b: mabaDiliko huanza na upatikanaji Wa taarifa

6 Mwongozo wa Mwananchi

Nitaitumiaje nyaraka hii?Unaweza ukaitumia kubaini ni madeni mangapi taasisi ya umma imejilimbikizia huko nyuma. Pia itakusaidia kufanya tathmini kama taasisi ya umma inauwezo wa kujiongezea madeni zaidi.

Ni aina gani ya taarifa zinazopatikana katika nyaraka hii?

Mizania ina sehemu tatu: Mali = Madeni + Mali halisi

Jumla ya ‘mali’ siku zote huwa sawa na jumla ya ‘madeni’ kujumlisha ‘mali halisi’; hivi ndivyo, dhana ya ‘mizania’ inavyotumika.

Mali na madeni kwa kawaida hugawanywa katika makundi mawili ambayo ni ‘fedha’ au ‘mali zinazohamishika na zisizohamishika’:

�� ‘Mali fedha zinazohamishika’ (mathalani ‘fedha na vitu vinavyoendana na hivyo’) vinaweza kutumiwa kirahisi kununulia vifaa vya ofisi au kulipa wafanyakazi.

�� ‘Mali zisizokuwa fedha’ au ‘mali zisizohamishika’ (Kama vile ‘jengo, kiwanda na mitambo’) zenye kudumu kwa muda mrefu. Mali nyingi kati ya hizi ni muhimu katika utoaji huduma kwa umma.

�� ‘Madeni ya fedha taslimu’ ni yale ambayo taasisi inadaiwa kama ‘malipo’ na yanatakiwa kulipwa ndani ya mwaka mmoja ili kufanya wadai waendelee kutoa huduma.

�� ‘Madeni yasiyo ya fedha taslimu’ ambayo yanatakiwa kulipwa baadaye (mathalan pensheni kwa wafanyakazi).

�� ‘Mali halisi’ ni mali fedha zinazomilikiwa na serikali.

Nawezaje kutumia taarifa hizi? Unaweza kulinganisha kiasi cha mali husika (‘mathalan kilichopokelewa au malipo ya kabla’), kutokana na kinachoendelea au mwaka uliotangulia na kisha uliza serikali yako kwanini kuna mabadiliko (zingatia kwamba zilizopokelewa ni fedha zilizopo ambazo zimelipwa baada ya utoaji bidhaa au huduma, wakati malipo ya awali yanafanyika pale unapolipia kabla bidhaa au huduma hujaipata.)

Unaweza pia kulinganisha ‘madeni’ na ‘mali halisi’ kwa mwaka uliopo na uliotangulia na kuiuliza serikali yako kwa nini uwiano nao umebadilika. Kama ‘madeni’ yanazidi ‘mali halisi’, basi taasisi ya umma inadaiwa zaidi na wasambazaji na ina wadeni wengi kuliko inachomiliki na hivyo basi, inaweza kukabiliwa na ugumu wa kulipa madeni yake kwa fedha ilizonazo.

7Mwongozo wa Mwananchi

2. Taarifa ya Mapato na Matumizi

Hii ni aina gani ya nyaraka? Taarifa ya mapato na matumizi inamaanisha muhtasari wa utendaji wa taasisi ya umma kifedha kwa mwaka uliopita, ambao ni kipimo cha jinsi taasisi inavyoweza kutumia mali zake kutokana na aina ya kazi yake ya msingi na uzalishaji mapato. Kwa maneno mengine, inahusu upimaji matokeo ya shughuli za taasisi na sera zake kifedha.

Nitaifanyia nini nyaraka hii? Lengo la Taarifa ya mapato na matumizi ni kupima uwezo wa kifedha wa taasisi katika kipindi fulani. Unaweza kuitumia taarifa hii kufanya tathmini ya uwezo wa taasisi wa kutoa huduma kwa umma kwa kipindi kingine cha mwaka kutokana na matumizi na kipato inachojikusanyia.

8 Mwongozo wa Mwananchi

Napata aina gani ya taarifa ndani ya nyaraka hii? ‘Mapato’ yanapatikana kutokana na kodi na ada zinazolipwa na wewe mwananchi, mahamisho kutoka taasisi za juu za serikali, mikopo kutoka kwa washirika wa maendeleo na vyanzo vingine vya mapato.

‘Matumizi’ yanaonesha ni kwa malengo gani taasisi imetumia mapato yaliyokusanywa. Miongoni mwake ni kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi, vifaa na bidhaa zinazotumika na taasisi, na gharama za matumizi ya uendeshaji wa shughuli za taasisi (ambazo zinajulikana kama ‘uchakavu’).

Katika mstari wa faida/hasara wa Taarifa, kama Mapato yanazidi Matumizi, hii inakuwa ni ziada/faida na kama Matumizi yanazidi Mapato hii huitwa nakisi/hasara. Faida inamaanisha ongezeko la ‘mali halisi’ katika mizania wakati hasara ni upungufu wa mali.

9Mwongozo wa Mwananchi

Nawezaje kutumia taarifa hii? Kwa kulinganisha mapato kutoka katika vyanzo vyote, unaweza kujua ni yapi muhimu zaidi.

Unaweza pia kulinganisha mapato fulani (au matumizi) katika miaka miwili iliyofuatana ili kujua kama mapato yote (au matumizi) yanaongezeka au kupungua. Kisha, unaweza kuwauliza viongozi wako wa serikali Mbunge/Diwani na Mtendaji ni kwa nini mapato (au matumizi) kwa ajili ya malengo fulani yamebadilika.

Kama Taarifa ya mapato na matumizi ya fedha inaonesha faida/ziada?, unaweza kuuliza kwa nini taasisi ya umma haikuweza kutumia mapato yake yote.

Aidha, unaweza kuuliza ni kiasi gani ‘mikopo ya fedha’ imetumika kwa huduma za maji, afya, elimu, kilimo na miundombinu kwa sababu ni huduma muhimu kwa maendeleo ya jamii yako.

3. Ripoti yoyote iliyotiwa saini na Mdhibiti na Mkaguzi

Mkuu wa Hesabu za Serikali

Hii ni nyaraka ya aina gani?Tangu kuanza kutolewa kwa taarifa za fedha na maofisa wa fedha wa taasisi za umma, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amekuwa akitathmini kama taarifa hizo ziko sahihi na zinaendana na sheria zilizopo. Baada ya kutathmini hali ya kifedha na matokeo yake, Mkaguzi huthibitisha kama taarifa ziko sahihi; hii huitwa ‘hati ya ukaguzi’. Kuna aina tano za maoni ya ukaguzi1:

�� Hati InayoridhishaHati hii ni matokeo bora ya ukaguzi. Hutolewa kama tu Mkaguzi ataridhika na taarifa zilizowasilishwa kwa mujibu wa kanuni za utoaji taarifa za fedha zinazokubalika.

�� Hati Inayoridhisha na Suala la Kutiliwa MkazoWakati mwingine, Mkaguzi ‘huongeza msisitizo wa jambo’ aya inayotaja suala linaloathiri taarifa za fedha. Nyongeza hiyo ya aya huwa haiathiri maoni ya ukaguzi na kwa kawaida huongezwa baada ya aya ya maoni ya Mkaguzi.

�� Hati Yenye ShakaHati hii hutolewa iwapo Mkaguzi atakuta mambo fulani ambayo yanakinzana na kanuni za mahesabu zinazokubalika. Hata ivyo pamoja na upekee wa mambo hayo, taarifa za fedha huwa zinakuwa zimewasilishwa vizuri.

1 Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (June, 2009), Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu taarifa za fedha za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2009.

10 Mwongozo wa Mwananchi

�� Hati IsiyoridhishaHati hii ni kinyume cha hati inayoridhisha. Hutolewa endapo Mkaguzi atakuta taarifa za fedha zilizotolewa haziendani na kanuni za kimahesabu zinazokubaliwa na taarifa hizo si za kweli, haziaminiki na si sahihi.

�� Hati Mbaya/ChafuHii ni hati mbaya zaidi. Hutolewa kama Mkaguzi ameshindwa kupata udhibitisho wa ukaguzi unaofaa kuhusu taarifa za fedha zilizotayarishwa na kukaguliwa. Hivyo huathiri taarifa hiyo ya fedha kiasi cha kushindwa kutoa maoni yake kuhusiana na taarifa za fedha.

Ninapata taarifa gani ndani ya nyaraka hii? Taarifa nyingi za ukaguzi zilizosainiwa huwa na sehemu tatu:

1) Wajibu wa mkaguzi na taasisi iliyokaguliwa,

2) Wigo wa ukaguzi, na

3) Maoni ya mkaguzi.

Taarifa ya Ukaguzi inaweza pia kujumuisha barua ya utawala yenye mapendekezo kwa utawala wa taasisi iliyokaguliwa, ambayo yanatakiwa kutekelezwa ili kuepuka hoja nyingi za kiukaguzi baadaye.

Nawezaje kutumia taarifa hii? Inapotokea kama maoni ya ukaguzi si safi, unaweza kuwauliza viongozi wako wa serikali Diwani/Mbunge/Mtendaji wako hoja zipi zimeibuliwa na kama kuna mtu amewajibishwa. Pia unaweza kuuliza juu ya maudhui ya barua ya utawala na kuchunguza jinsi utawala ulivyofanyia kazi mapendekezo ya Mkaguzi.

Nyaraka zingine muhimuMbali na nyaraka hizo tatu ambazo kisheria zinatakiwa kuwa wazi kwa kila mtu, kuna nyaraka zingine nyingi muhimu zinaweza pia kutolewa kwa wananchi ili kuwapa uelewa zaidi na kuweza kufuatilia vizuri uwajibikaji katika jamii. Nyaraka hizo ni:

�� Mpango Mkakati,

�� Bajeti iliyoidhinishwa,

�� Taarifa ya Utekelezaji, na

�� Taarifa ya Matumizi ya fedha.

4. Mpango Mkakati

Hii ni aina gani ya nyaraka? Mpango Mkakati ni mwongozo ambao unaongoza taasisi kutoka iliko kuelekea ambako inataka kuwa katika kipindi fulani. Mpango mkakati unatakiwa uwe katika misingi ya tathmini ya fursa na vikwazo vilivyopo, unapaswa uwe na malengo ya wazi

11Mwongozo wa Mwananchi

ya maendeleo yenye mpango wa kina unaoeleweka wa jinsi gani ya kuyafikia, na pia unapaswa kutoa muda wa kutosha wa utekelezaji.

Nitaifanyia nini nyaraka hii? Unaweza kujifunza kutoka kwenye mpango mkakati jinsi viongozi wako wanavyotaka kufikia malengo ya maendeleo katika jamii. Unaweza kutathmini shughuli zilizopangwa, kufuatilia mchakato wa utekelezaji na kuomba marekebisho kama ikibidi.

Ni aina gani ya taarifa utazipata ndani ya nyaraka hii? Mpango mkakati unapaswa kujumuisha:

�� Uchambuzi wa hali; ukielezea nguvu, udhaifu, fursa na changamoto,

�� Taarifa ya Dhamira; ikielezea sababu ya kuwapo kwa taasisi,

�� Shabaha; ambayo inafafanua dhahiri mwingiliano wa vitengo mbalimbali katika taasisi,

�� Malengo; (ya muda mrefu na ya muda mfupi) ambayo yanaweza kutumiwa kupima utendaji wa taasisi.

Pia Mpango Mkakati unajumuisha:

�� Mpango kazi (au Utekelezaji); ambao unaainisha shughuli ambazo zimewekwa ili kufikia dhamira kwa njia nyoofu na inayopimika; na

�� Mfumo wa Ufuatiliaji na tathmini, ambao unaruhusu kutathmini kama Mpango Mkakati umetekelezwa vizuri.

Ninawezaje kutumia taarifa hii? Unaweza kuhoji shughuli ambazo zinatekelezwa na hazihusiani moja kwa moja na shabaha za taasisi. Itokeapo malengo hayakufikiwa, unaweza kudai maelezo kutoka kwa serikali yako.

5. Bajeti iliyoidhinishwa

Hii ni nyaraka ya aina gani? Bajeti iliyopitishwa ni mpango wa kifedha wa mwaka wa fedha. Unaainisha jinsi taasisi ya umma inavyoweza kufanya matumizi yake kwa shughuli fulani (kwa mfano afya). La muhimu ni kwamba bajeti inajumuisha maoni kutoka kwa wadau mbalimbali.

Nitaifanyia nini nyaraka hii? Bajeti huonesha vipaumbele vya taasisi na mgawanyo wa fedha. Pia hutumika kama kipimo cha kutathmini utendaji wa taasisi kifedha baada ya bajeti kutekelezwa.

Ni aina gani ya taarifa nitazipata ndani ya nyaraka hii? Bajeti iliyopitishwa inaainisha mapato ambayo taasisi ya umma inatarajia kuyapata kutoka katika vyanzo tofauti na jinsi yanavyopangwa kutumika kwa shughuli mbalimbali.

12 Mwongozo wa Mwananchi

Ninawezaje kuitumia taarifa hii? Unaweza kuuliza ni kiasi gani cha fedha taasisi inatarajia kukusanya na kutumia ikilinganishwa na mwaka uliotangulia au ni kiasi gani cha fedha taasisi imetenga kutumia kwa jambo fulani (kwa mfano katika manunuzi ya dawa na vifaa tiba).

6. Taarifa ya utekelezaji

Hii ni aina gani ya nyaraka? Mwisho wa mwaka wa fedha, taarifa ya utekelezaji hutoa habari juu ya utendaji halisi wa taasisi ya umma na maendeleo kuelekea kufikia malengo ya mpango mkakati na bajeti iliyopitishwa.

Nitaifanyia nini nyaraka hii? Taarifa ya utekelezaji inakuonesha kiasi gani cha bajeti kilichopitishwa kimetumika na ni aina gani ya shughuli zilizotekelezwa katika mwaka wa fedha uliomalizika. Inapaswa pia kutoa sababu za kwanini utekelezaji ulichelewa.

Ni aina gani ya taarifa nitazipata ndani ya nyaraka hii? Taarifa ifuatayo kwa kawaida huwasilishwa mezani.

•� Idara Nani anatumia fedha?

•� Chanzo cha fedha Nani anatoa fedha?

•� Lengo Kwa lengo gani?

•� Shughuli Kwa shughuli ipi?

•� Hali ya utekelezaji Imeanza au imekamilika?

•� Kiasi cha fedha Kiasi gani cha fedha kilicho idhinishwa?

•� Zilizopokelewa Kiasi gani cha fedha kilichopokelewa?

•� Zilizotumika Kiasi gani cha fedha kilichotumika?

•� Baki Kiasi gani cha fedha kilichobaki?

•� Maoni Kueleza hali ya utekelezaji

Ninawezaje kutumia taarifa hii?‘Baki’ inaonesha tofauti kati ya kiasi ‘kilichopokelewa’ na ‘kilichotumika’. Kutoka kwenye ‘baki’ au ‘sifuri’ ya utekelezaji wa shughuli fulani unaangalia katika ‘maoni yaliyotolewa’ na unaweza kuiuliza serikali ili kutoa ufafanuzi zaidi.

13Mwongozo wa Mwananchi

7. Taarifa ya Matumizi ya Fedha

Hii ni aina gani ya nyaraka? Taarifa ya Matumizi ya Fedha inaonesha jinsi fedha zinavyoingia na kutoka katika taasisi ya umma; hivyo, inaonesha mapokezi na malipo ya fedha.

Naweza kufanya nini na nyaraka hii? Unaweza kutumia Taarifa ya Matumizi ya Fedha kutathmini uwezo wa taasisi katika kulipia ankara na mishahara.

Ni aina gani ya taarifa ninazopata katika nyaraka hii?Taarifa inaripoti aina tatu za shughuli:

�� ‘Shughuli za uendeshaji’ ambazo zinajumuisha utoaji huduma, kama vile za afya na elimu, zaidi kupitia kuwalipa watoa huduma na wafanyakazi;

�� ‘Shughuli za uwekezaji’ ambazo zinajumuisha ununuzi wa mali kama vile ardhi na majengo;

�� ‘Shughuli za ufadhili’ ambazo zinajumuisha fedha zitokazo serikalini, washirika wa maendeleo na mapato mengine ya ndani.

Kwa kujumlisha pamoja shughuli hizi ndipo linapopatikana ‘ongezeko halisi la fedha na mambo mengine yahusuyo fedha’

Nawezaje kutumia taarifa hii? Angalia matumizi halisi (kama ‘ununuzi wa mali, mitambo na vifaa’ vya kuendeshea shughuli za taasisi) na waulize viongozi wako wa serikali Diwani/Mbunge/Mtendaji wako kama matumizi hayo yalifanyika kwa madhumuni gani.

14 Mwongozo wa Mwananchi

Kama watumiaji wa huduma za umma, wananchi wana uelewa mzuri ambao wanaweza kuchangia katika hatua zote za mzunguko wa bajeti.

Katika hatua ya upangaji wa bajeti, wananchi wanatakiwa kubaini na kutaja mahitaji na vipaumbele vyao kwa kushirikiana na viongozi wao ili kuboresha mipango ya jamii na bajeti. Zoezi hili hujulikana kama ‘Mchakato wa kuibua Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (FVM)’.

Katika hatua ya utekelezaji wa bajeti, wananchi wanaweza kusaidia kufuatilia na kutoa mrejesho juu ya utendaji kazi wa watumishi, pia wanapaswa kutoa taarifa ya matatizo yaliyopo kwa kamati husika kupitia masanduku ya maoni na kwa kushiriki katika kamati na vikao mbalimbali (mfano kupitia kamati za kusimamia huduma za afya za vituo).

Katika hatua ya usimamizi, wananchi wanatakiwa kuwabana viongozi wao ili watimize majukumu yawapasayo katika kuhakikisha wanatatua matatizo yaliyopo. Hii inawezekana kwa kushiriki katika mikutano mikuu ya vijiji/mitaa na kata.

1. Mchakato wa Kuibua Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (FVM) kwa Mjini na Vijijini

Huu ni mchakato wa aina gani? Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo ni mchakato unaoiwezesha jamii kuandaa na kutekeleza mipango yao ya maendeleo kulingana na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 (DMT). Mchakato huu unahitaji Mamlaka za Serikali za Mitaa na wananchi kwa pamoja kutambua fursa zilizopo na vikwazo kwa maendeleo, kubainisha malengo ya jamii na kuamua shughuri za kufanya ili kufikia malengo hayo

Mchakato huu una hatua zipi muhimu? Mchakato wa Kuibua Fulsa na vikwazo kwa maendeleo vijijini na mijini hufanana, ingawa hutofautiana kidogo katika muundo wa kiutawala. Maeneo ya vijijini yamegawanyika katika vijiji na kata wakati maeneo ya mijini (miji) yamegawanyika katika mitaa na kata. Wakati mwingine, mijini mitaa huwekwa katika makundi ya kanda kabla ya kuanza kwa mchakato wa Kuibua Fulsa na vikwazo kwa maendeleo mijini.

Sehemu c: furSa za kuleta mabaDiliko

15Mwongozo wa Mwananchi

Kwa vijijni, mkutano mkuu wa kijiji ndiyo unapaswa kuidhinisha mipango ya maendeleo ya kijiji wakati, kwa mijini Kamati ya Maendeleo ya Kata ndiyo inahusika na uidhinishaji wa mipango ya maendeleo2.

Mchakato wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo una hatua kadhaa:

a) Kuwaalika wananchi katika mkutano mkuu wa kijiji/mtaa Wawezeshaji wa mchakato huu wanaandika barua rasmi kwa uongozi wa kijiji/mtaa kuujulisha kusudi la kuendesha mchakato huo katika maeneo yao. Viongozi wanatangaza na wanaitisha mkutano mkuu maalumu wa kijiji/mtaa utakaokutanisha makundi yafuatayo: viongozi, na watu wote wa jamii hiyo ambao wamefikisha umri wa miaka 18 na zaidi.

b) Uchaguzi wa shabaha za maendeleo ya jamiiMwanzoni mwa mkutano, mwezeshaji anaelezea kiundani shabaha za Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 kwa washiriki na kuelezea jinsi gani shabaha hizi za kitaifa zitawaongoza katika maandalizi ya mpango wao wa maendeleo ya jamii. Kwa maandalizi ya mipango, washiriki wanapaswa kuchagua shabaha ambazo zinaonekana kuwa na kipaumbele cha juu katika jamii.

Zaidi, mkutano unaunda makundi mahususi ambapo wanawake na wanaume, vijana na wazee watawakilishwa sawa ili kutoa nafasi kwa makundi yote kutoa maoni yao.

c) Utambuzi wa fursa na vikwazo vya maendeleoMakundi mahususi yaliyoundwa yatatumia zana shirikishi kutambua fursa zilizopo na vikwazo kwa maendeleo. Miongoni mwa zana tofauti ni umilikaji rasilimali kijinsia, uchambuzi wa vyanzo vya mapato na matumizi, matembezi mkato (Kataa ya njia), uchambuzi wa taasisi, kalenda ya msimu, historia ya matukio muhimu, na mgawanyo wa shughuli za kila siku kwa misingi ya kijinsia, kuzitaja kwa uchache.

Kumbuka: Kiutaratibu, zana shirikishi zinazotumika katika mchakato wa mipango vijijini pia hutumika katika mchakato wa mipango mjini. Ingawa zana kama Kataa ya njia na Matukio ya kihistoria hazitumiki katika mipango ya mjini kwa sababu;

�� Kataa ya njia (matembezi mkato): Maeneo ya mjini yalikwishapimwa na kujengwa kwa kuzingatia fursa na vikwazo wakati wa mipango miji. Aidha, katika maeneo ambayo hayajapimwa lakini yamejengwa sio rahisi kupitika wakati wa zoezi hili.

�� Matukio ya kihistoria: Maeneo ya Mjini, miji imejengwa kwa kufuata mpango mji. Kwa hiyo wakazi wa mjini hawawezi kujifunza kutokana na matukio ya kihistoria kupanga matumizi ya ardhi ya baadae. Pia wakazi wengi wa mjini ni wale wanaoingia na kutoka na shughuli zao hutofautiana na si za muda mrefu3.

2 International Development Centre of Japan (2008), The Study on Improvements of Opportunities and Obstacles to Development (O&OD) Planning Process, Final Report, PMO-RALG & JICA, p. 38.3 Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (2007), TAMISEMI: Uandaaji wa Mpango Shirikishi Jamii kwa Mfumo wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo, Kiongozi cha Mchakato wa Mjini, Dodoma-Tanzania.

16 Mwongozo wa Mwananchi

d) Maandalizi ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitatu

Baada ya fursa na vikwazo kwa maendeleo kutambuliwa, mpango wa miaka mitatu wa jamii lazima utengenezwe kwa kutumia taarifa zilizokusanywa kwa kutumia zana shirikishi na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2015 (DMT).

Kwa vijijini, maandalizi ya rasimu ya mpango wa jamii wa miaka mitatu inajumuisha makundi ya watu wafuatao; makundi mahususi (wanawake, vijana, walemavu), baraza la kijiji na Kamati ya Maendeleo ya Kata.

Kwa mjini, maandalizi ya rasimu ya mpango wa jamii wa miaka mitatu inahusisha watu kama; makundi mahususi, Mtendaji wa Kijiji na Kamati ya Maendeleo ya Kata.

e) Mkutano Mkuu wa Kijiji/Mtaa Kijijini: Mkutano mkuu wa Halmashauri ya Kijiji utaitishwa kujadili, kupitisha au kukataa mapendekezo ya Rasimu ya Mpango wa Maendeleo wa miaka mitatu. Baada ya mpango kuidhinishwa na mkutano mkuu wa kijiji, unatakiwa ubandikwe katika mbao za matangazo.

Mjini: Mkutano wa mtaa utaitishwa kuwasilisha mapendekezo ya Rasimu ya Mpango wa Maendeleo wa miaka mitatu na wana mtaa watapewa fursa kutoa maoni na ushauri. Baada ya hapo, michango yao itaingizwa katika mpango kabla ya kukabidhiwa na kuidhinishwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata (KMK).

Ni upi wajibu na majukumu ya washiriki wa mchakto huu? Mchakato wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo unahitaji watu/washiriki kadhaa ili kutimiza majukumu tofauti. Majukumu muhimu zaidi yanabebwa na mwezeshaji wa mchakato, viongozi wa kijiji/mtaa na makundi mahususi.

�� Mwezeshaji anawasaidia washiriki kuelewa shabaha za maendeleo ya taifa na kuwasaidia kutengeneza mikakati ya kufikia shabaha za maendeleo ya jamii bila ya kuwa na msimamo fulani wakati wa majadiliano. Mwezeshaji ana majukumu yafuatayo:

¿ Kuandika barua rasmi kwa uongozi wa kijiji/mtaa kuufahamisha juu ya nia ya kuendesha mchakato wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo katika eneo lao. Mwezeshaji anauelezea uongozi watu muhimu ambao wanapaswa kualikwa kwenye mkutano huo wa kujadili mchakato wa fursa na vikwazo kwa maendeleo.

¿ Kuelezea kiundani shabaha za Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 (DMT 2025) na kuwafanya wanajumuiya kuelewa kwamba shabaha hizi ndizo zitakazowaongoza katika maandalizi ya mpango wao wa maendeleo.

�� Viongozi wa kijiji/mtaa ndio waandaaji wa mikutano hiyo miwili. Hivyo, wanahitajika kuwaeleza washiriki kwa nini ni muhimu kwao kuhudhuria mikutano hiyo. Majukumu ya viongozi wa kijiji/mtaa ni:

¿ Kuitisha mkutano mkuu utakaokutanisha washiriki wote wa mchakato.

¿ Baada ya zoezi la kukusanya taarifa kukamilika, wanaandaa mpango wa

17Mwongozo wa Mwananchi

maendeleo wa jamii kwa kushirikiana na makundi mahususi.

¿ Kisha, wanaitisha mkutano mkuu wa kijiji/mtaa ili kujadili mpango wao wa maendeleo.

¿ Hatimaye, wanaandaa muhutasari mkutano mkuu wa kijiji/mtaa na kuuwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya (MMW).

�� Makundi mahususi ya mchakato wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo ni pamoja na wanajamii wakiwakilisha wanawake na wanaume, vijana na wazee, na makundi yaliyo katika mazingira hatarishi n.k. Majukumu ya washiriki hao ni:

¿ Kutambua fursa na vikwazo kwa maendeleo Kwa kutumia zana shirikishi Kuandaa rasimu ya mpango wa jamii kwa kushirikiana na viongozi wao.

Ni nyaraka gani hutengenezwa wakati wa mchakato huu kwa kumbukumbu?

�� Barua rasmi iliyoandikwa kwa uongozi wa kijiji/mtaa kuufahamisha juu ya nia ya kuendesha mchakato wa kuibua Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo.

�� Taarifa zilizokusanywa wakati wa mchakato wa kuibua fursa na vikwazo kwa maendeleo.

�� Mpango wa maendeleo wa miaka mitatu.

�� Muhtasari wa mikutano mikuu ya kijiji/mtaa.

18 Mwongozo wa Mwananchi

Nawezaje kuhakikisha kama mchakato huu unafanya kazi? Wakati wa mkutano mkuu wa pili wa kijiji/mtaa, unatakiwa kulinganisha rasimu ya mpango wa maendeleo mtakaosomewa na kile ambacho mlikubaliana wakati wa mkutano uliotangulia. Pia unaweza kupendekeza kuongezwa au kupunguzwa kwa baadhi ya vitu kulingana na makubaliano yenu. Mkutano wa kijiji/mtaa utaamua kama mabadiliko haya yanapaswa kufanyika katika mpango wa maendeleo.

2. Kamati za Kusimamia Huduma za Afya (KKHA)

Hizi ni kamati za aina gani? Kamati za kusimamia huduma za afya zipo katika ngazi za hospitali, kituo cha afya na zahanati. Kamati hizi zinaundwa na maofisa kutoka katika vituo vya huduma za afya na wajumbe kutoka katika jamii wakiwawakilisha watumiaji wa huduma za afya.

Nafasi hizi hutangazwa katika ngazi ya kijiji. Wananchi wanaweza kuomba kama wanakidhi sifa zifuatazo:

�� Kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

�� Kuwa na elimu ya shule ya msingi au zaidi pia uwe unaweza kusoma na kuandika Kiswahili;

�� Kuwa na umri wa miaka 25 na zaidi kwa kamati ya hospitali na miaka 21 na zaidi kwa kamati ya kituo cha afya na zahanati na si zaidi ya miaka 65;

�� Kutokuwa na wadhifa wowote wa kisiasa;

�� Kuwa mwananchi wa kawaida (mtumia vituo vya huduma za afya vya umma) na mkazi wa eneo husika.

19Mwongozo wa Mwananchi

Ni yapi majukumu na wajibu wa kamati? Kamati za kusimamia huduma za afya zilianzishwa ili kuboresha uwajibikaji kati ya watoa huduma za afya na jamii. Hivyo, wanatakiwa kuhakikisha kwamba mahitaji ya jamii yanashughulikiwa vema na vituo vya huduma za afya. Aidha, kamati zinatoa mrejesho kwa wananchi kuhusu mipango ya maendeleo na uendeshaji wa kituo.

Kamati zinazosimamia hospitali zinapaswa kukutana angalau mara moja kwa mwezi. Na kwa kamati za vituo vya afya na zahanati hukutana angalau mara moja kwa miezi mitatu.

Ni nyaraka zipi hutolewa na kamati? Kunapaswa kuwapo na muhutasari ya vikao vya kamati hizo ili kutoa ushahidi wa nani alihudhuria na nini kilijadiliwa na kuamuliwa katika vikao hivyo.

Nawezaje kuhakikisha kwamba KKHA inafanya kazi zake barabara? Kwa kuwa kamati ina wajumbe watatu wa kuchaguliwa kutoka katika jamii, unaweza kukutana nao kama unataka kuwasilisha malalamiko au maombi ya taarifa juu ya upatikanaji wa huduma au dawa katika kituo cha tiba husika. Hususani, kwa wananchi ambao wanapaswa kupata huduma za tiba bure (watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, wajawazito, wazee, watoto wa mitaani, na wengine ambao wanastahili huduma bure) wanapaswa kuhakikisha kwamba huduma hizo zinapatikana.

3. Kamati za Kudhibiti UKIMWI (KKU)

Hii ni aina gani ya kamati? Kamati za UKIMWI zinapaswa kuwa na wajumbe wengi wakiwamo wanaoishi na VVU, wawakilishi wa kidini, wawakilishi wa vijana, wawakilishi kutoka mitandao na asasi zinazoshughulikia VVU na Mamlaka za Serikali za Mitaa (kama vile mwenyekiti wa serikali ya kijiji/mtaa au Diwani na Afisa Mtendaji wa Kata). Kamati hizo zipo kwa ajili ya kuhimiza ushiriki wa jamii katika mipango na shughuli za kupambana na VVU/UKIMWI.

Ni upi wajibu na majukumu ya kamati hiyo? Kamati za UKIMWI zinaundwa katika ngazi za kijiji (Kamati ya UKIMWI ya kijiji, kata (Kamati ya UKIMWI ya kata) na wilaya (kamati ya UKIMWI ya wilaya). Kila moja ina wajibu wake:

�� Katika ngazi ya kijiji, Kamati ya UKIMWI ya kijiji huainisha na kujadili mahitaji yaliyopo na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kushughulikia VVU ambayo yanapelekwa katika kamati za kukabiliana na UKIMWI ngazi ya kata (Kamati ya UKIMWI ya kata).

�� Katika ngazi ya kata, Kamati ya UKIMWI ya kata inaandaa mpango wa shughuli za pamoja katika kukabiliana na VVU/UKIMWI na kuziwasilisha katika kamati za baraza (Kamati ya UKIMWI ya wilaya).

20 Mwongozo wa Mwananchi

�� Katika ngazi ya wilaya, Kamati ya UKIMWI ya wilaya zinachagua shughuli muhimu zaidi katika mipango iliyowasilishwa kutoka vijiji na kata kutegemeana na upatikanaji wa fedha. Kisha Mipango ya mwisho hupitishwa na baraza la Madiwani.

Kwa mujibu wa Mwongozo wa Kuanzishwa kwa Kamati za UKIMWI katika ngazi ya serikali za mitaa, Kamati za UKIMWI zinahusika na shughuli zifuatazo:

�� Kusimamia uundwaji wa Kamati za UKIMWI katika ngazi za chini za serikali;

�� Kuruhusu wadau mbalimbali kuchangia kudhibiti UKIMWI;

�� Kutathmini mipango ya kazi na utekelezaji wake na kutoa mapendekezo;

�� Kutathmini hali ya UKIMWI kwa kuangalia idadi ya wagonjwa, yatima, wajane na wagane, na mazingira yanayochangia maambukizi ya UKIMWI na uelewa wa wananchi juu ya janga hili.

4. Masanduku ya maoni

Sanduku la maoni ni kitu gani? Sanduku la maoni kwa kawaida huwekwa nje ya majengo ya ofisi za umma. Linaweza kutumiwa kukusanyia ujumbe ulioandikwa na wananchi ili kutoa maoni, mapendekezo na kuuliza maswali ya jinsi ya uendeshwaji wa kituo ama ofisi husika.

21Mwongozo wa Mwananchi

Ni nini shabaha ya sanduku la maoni?Unaweza kutumia masanduku ya maoni yaliyopo ili kuelezea mtazamo wako juu ya huduma zinazotolewa na kituo. Hii inawezesha watoa huduma kuboresha utoaji wa huduma zao kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na watumiaji huduma.

Nani anawajibika na ufunguzi wa masanduku hayo?Watu wafuatao wanawajibika na ufunguzi wa sanduku kwa vituo vya huduma:

�� Mwenyekiti wa kamati ya afya ya kituo

�� Mwakilishi kutoka kwa wananchi

�� Mjumbe mwingine yeyote wa kamati

�� Mganga Mfawidhi

Muhimu kukumbuka: Sanduku la maoni halipaswi kufunguliwa na mtu mmoja. Hivyo, linapaswa kufunguliwa wakati wa mkutano wa kamati ya afya ambapo wanakamati hukutana. Kamati hukutana mara nne kwa mwaka (kila robo ya mwaka). Mapendekezo na malalamiko yaliyotolewa yanajadiliwa na wajumbe wote wa kamati katika mkutano huo na mrejesho unapaswa kutolewa kwa wananchi kupitia mikutano ya kijiji/mtaa na kata.

Nawezaje kuhakikisha kwamba mapendekezo yangu yamefanyiwa kazi vema? Unaweza kuibua masuala yoyote yanayohusu utendaji kazi wa masanduku ya maoni kupitia wawakilishi wa wananchi wa kamati ya afya au moja kwa moja katika mikutano ya kijiji/mtaa au kata. Unapaswa kutafuta mrejesho kutoka kwa kamati au kufuatilia katika mkutano mkuu wa kijiji/mtaa ujao kama maoni, mapendekezo au malalamiko yako yamefanyiwa kazi ili kuhakikisha kuna maboresho katika utoaji huduma.

5. Mkutano Mkuu wa Kijiji

Huu ni mkutano wa aina gani? Mkutano wa kijiji (Vijijini) ni chombo cha juu cha uamuzi katika jamii. Kinaundwa na wanajamii ambao wamefikia umri wa miaka 18 na zaidi na wakaazi wa kijiji husika. Mkutano huu hukutana mara moja kwa miezi mitatu isipokuwa Mkutano wa dharura wa kijiji unaweza kuitishwa ikilazimika. Kwa kila miaka mitano mkutano hukutana kuchagua wajumbe wa baraza la kijiji.

Ni nini shabaha ya Mkutano Mkuu wa Kijiji? Mkutano wa kijiji ni sawa na Bunge. Mkutano huu husimamia baraza la kijiji ambalo huendesha shughuli zote za maendeleo na bajeti za kijiji. Ili kutekeleza jukumu lake la ufuatiliaji vema, mkutano mkuu wa kijiji unawajibika kwa shughuli mbalimbali kama:

�� Kuchagua wajumbe na mwenyekiti wa baraza la kijiji au mtaa;

�� Kupokea, kujadili na kupitisha au kukataa mapendekezo ya kukusanya mapato (kodi na ada) kwa ajili ya kijiji au mtaa;

22 Mwongozo wa Mwananchi

�� Kupokea, kujadili na kupitisha au kukataa taarifa ya baraza juu ya mapato na matumizi ya fedha za kijiji;

�� Kusimamia utekelezaji wa mipango ya shughuli za kijiji.

�� Kupokea na kujadili sheria ndogo zilizopendekezwa na halmashauri ya kijiji.

Nyaraka zipi hutolewa kwenye mkutano huu? Afisa Mtendaji wa Kijiji anawajibika kuandaa muhutasari wa majadiliano na maamuzi yaliyofikiwa katika mkutano wa kijiji.

6. Mkutano Mkuu wa Mtaa

Huu ni mkutano wa aina gani? Mtaa ni sehemu ndogo ya uongozi wa serikali za Mitaa katika maeneo ya mijini4. Mkutano wa Mtaa unajumuisha watu wazima na wakaazi wote wa mtaa husika. Kila mtaa una mwenyekiti wa mtaa ambaye kimsingi ni kiongozi anayechaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa mtaa ambao unajumuisha watu wazima na ni wakaazi wa mtaa huo. Mwenyekiti wa mtaa anapaswa kuitisha mkutano wa Mtaa angalau mara moja kila baada ya miezi miwili kisha huwasilisha muhutasari wa mkutano kwa Kamati ya Maendeleo ya Kata.

4 Kifungu cha 14 (3) cha Sheria za Serikali za Mitaa Namba 8 ya 1982 (Mamlaka za Mjini) (Toleo la 2000) inatamka kwamba, eneo la kata litagawanywa katika “mtaa” au “kijiji” vinavyojumuisha idadi ya kaya, ambazo mamlaka ya mji itazitambua.

23Mwongozo wa Mwananchi

Ni nini shabaha ya Mkutano wa Mtaa?Mkutano wa Mtaa husimamia kazi za Mwenyekiti wa Mtaa na Kamati teule ya Mtaa ambao huendesha shughuli zote za maendeleo hususani katika mipango na kusimamia utekelezaji wa sera za mtaa. Ili kutekeleza majukumu yake na ufuatiliaji mzuri, mkutano mkuu wa mtaa unawajibika kwa shughuli zifuatazo:

�� Kumchagua na kumuondoa katika nafasi yake Mwenyekiti wa Mtaa.

�� Umepewa uwezo wa kubuni na kupitisha sheria ndogo ndogo na sera kwa ajili ya maendeleo ya Mtaa husika.

�� Kufanya kazi chini ya Mwenyekiti ambaye huchaguliwa na wakaazi wa mtaa huo.

�� Kufanya kazi katika mfumo wa kamati za watu 9 zilizochaguliwa ambazo zinahusika na kazi maalum kama vile; ulinzi na usalama, elimu, afya, mazingira, wanawake na watoto, maji na nidhamu.

�� Kuimarisha amani na kukuza demokrasia ya uwakilishi na kushiriki pia hutambua na kutatua mizozo yoyote ambayo inaweza kutokea miongoni mwa wakazi wa Mtaa.

24 Mwongozo wa Mwananchi

Nyaraka zipi hutolewa kwenye Mkutano wa Mtaa? Mwenyekiti wa Mtaa anawajibika kuandaa muhtasari wa majadiliano ya mkutano na maamuzi yaliyofikiwa katika mkutano wa mtaa na kuziwasilisha kwa Kamati ya Maendeleo ya Kata.

Nitahakikishaje kwamba mkutano wa Kijiji/Mtaa unafanya kazi kama ilivyokusidiwa? Kama mwananchi, unawajibika kuwabana viongozi wako ili wawajibike. Kupitia mkutano wa kijiji/mtaa, unaweza kuomba maelezo na kuchukua hatua za kisheria dhidi yao kama hujaridhishwa na kazi zao.

Kama una matatizo ya kupata taarifa za bajeti, au kama vipaumbele vilivyoainishwa katika mchakato wa kuibua fursa na vikwazo kwa maendeleo havijabainishwa katika mpango wa maendeleo wa kijiji/mtaa wako; au kama kamati za kusimamia huduma za afya au zile za kusimamia mapambano dhidi ya UKIMWI haziwakilishi watumiaji wa huduma kikamilifu; au kama unadhani kwamba masanduku ya maoni hayatumiki ipasavyo, unaweza ukayawasilisha mambo hayo mapema wakati wa mkutano wa kijiji/mtaa ili kuona kama yanaweza kuingizwa kwenye ajenda ya mkutano kwa majadiliano kwa ufumbuzi zaidi.

Mjadala unapofikia mada yako, elezea suala lako kwa utaratibu lakini ukishikilia msimamo wako. Unahitaji kushawishi wajumbe wengine wa mkutano kwamba hali hiyo haikubaliki ili kushinikiza viongozi wenu warekebishe matatizo hayo mara moja. Hakikisha kwamba mkutano unaamua nani anawajibika kutatua tatizo hilo na ni muda gani mtu huyo apewe ili kukamilisha kazi hiyo.

Katika mkutano ufuatao wa mtaa/kijiji, angalia kama muhtasari wa mkutano uliopita unaelezea kwa usahihi suala uliloibua katika mkutano uliopita. Mtu ambaye alipewa dhamana ya kazi hiyo anapaswa kuripoti katika mkutano huu juu ya maendeleo ya kushughulikia mambo yaliyojadiliwa na kuamriwa katika mkutano uliopita.

Iwapo maendeleo si ya kuridhisha, jadilini katika mkutano huu kama mtu huyo anapaswa aongezewe muda au asaidiwe na wengine kushughulikia suala hilo.

25Mwongozo wa Mwananchi

Viambatisho

1. Watendaji wakuu wa serikali za MitaaWafuatao ndio watendaji wakuu ambao wanahusika katika mchakato wa kuandaa bajeti ya Serikali za Mtaa nchini Tanzania.

Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ndicho chombo cha Serikali Kuu; kinazipa m amlaka za Serikali za Mitaa (MSM) sera na miongozo. Ofisi hiyo inawajibika kusimamia uendeshaji wa halmashauri zote nchini.

Sekretarieti ya mkoa, inaongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa (KTM), inaratibu uhusiano uliopo kati ya Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa .Pia inawajibika katika usambazaji taarifa kwa ngazi zote za serikali.

Mamlaka ya Serikali za Mtaa (MSM) inawajibika kukuza na kuhakikisha ushiriki wa kidemokrasia wa wananchi katika utoaji maamuzi kwa umma.

Wakurugenzi wa Halmashauri (wakurugenzi watendaji wa wilaya au manispaa) wanawajibika kuandaa na kutekeleza bajeti ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa (MSM).

Timu ya Uendeshaji ya Halmashauri (TUH) na wakuu wa idara kisekta wanatoa michango ya kitaalamu katika mchakato wa bajeti na wanawajibika katika vitengo vyao.

Baraza la Madiwani linajumuisha wabunge, madiwani wa kuchaguliwa na wakurugenzi watendaji wa wilaya/manispaa. Baraza hilo linawajibika kupitia na kupitisha bajeti iliyopendekezwa. Mikutano ya baraza la Madiwani iko wazi pia kwa umma; hivyo; wananchi wanahimizwa kuhudhuria mikutano hiyo.

Kamati ya Maendeleo ya Kata (KMK) inaundwa na diwani, wenyeviti wa vijiji au mitaa, na Afisa Mtendaji wa Kata (Afisa Ugani wa Kata). Chombo hiki kinaunganisha halmashauri ya wilaya au manispaa na kijiji au mtaa na vitongoji.

Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) zilizoko vijijini, kila kijiji kina halmashauri ya kijiji ambayo inaundwa na wenyeviti wa vijiji na viongozi wa vijiji wa kuteuliwa.

Viongozi wa kijiji wanachaguliwa na mkutano wa kijiji ambao unaundwa na watu wote katika kijiji husika wenye umri wa miaka 18 na zaidi. Mkutano wa kijiji ndiyo wamiliki hasa wa rasilimali zote za kijiji. Kwa mujibu wa sheria, mkutano huu hupaswa kufanyika angalau mara nne kwa mwaka. Kwa upande wa mjini (halmashauri za majiji, manispaa na miji), chombo kama mkutano wa kijiji kinajulikana kama Mkutano wa mtaa ambao huitishwa angalau mara moja kila baada ya miezi miwili.

Wananchi ni walipa kodi na wana jukumu maalumu la kuhakikisha kwamba fedha zao zinatumika vizuri. Ndio watumiaji wa huduma zote na wanapaswa kuhakikisha kwamba wanaridhika na huduma zitolewazo. Aidha, ndio wapiga kura wanaoweka baraza la kijiji madarakani. Hivyo pia, wana madaraka ya kupiga kura dhidi ya viongozi ambao wanashindwa kuboresha ustawi wa jamii zao.

26 Mwongozo wa Mwananchi

2. Ratiba ya Mchakato wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo

Siku Mjini5 Vijijini6

1 Maandalizi ya Jamii na Kukusan-ya Takwimu

Maandalizi ya Jamii na Kukusanya Takwimu

2 Maandalizi ya Jamii na Kukusan-ya Takwimu

Maandalizi ya Jamii na Kukusanya Takwimu

3 Mkutano Mkuu Maalum wa kanda/mtaa

Kuchagua Wawezeshaji wa Jamii

Kuchagua makundi mahususi

Kuchora Ramani ya Kijiji

Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji

Kuchagua Wawezeshaji wa Jamii

Kuchagua makundi mahususi

Kuchora Ramani ya Kijiji

4 kukusanya takwimu kwa kutumia Zana Shirikishi Jamii kama;

- Kuchora ramani ya Kata

- Tathimini ya uwezo wa kaya

- Uchambuzi wa Taasisi

- Umilikaji rasilimali kijinsia

- Shughuli za kutwa kijinsia

- Uchambuzi wa vyanzo vya mapato na matumizi katika Kata

- Uchambuzi wa shughuli za ki-jamii na kiuchumi zenye athari katika mazingira

kukusanya takwimu kwa kutumia Zana Shirikishi Jamii kama;

- Matembezi Mkato (Kataa ya njia)

- Ramani ya Umilikaji Rasilimali Kijinsia

- Uchambuzi wa vyanzo vya Mapato na Matumizi

- Uchambuzi wa Taasisi

- Kalenda ya Msimu

- Historia ya Matukio Muhimu

- Shughuli za Kutwa za Kijinsia

5 Makundi mahususi kujadili Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025: Lengo la 1: Maisha Bora na Mazuri

Makundi mahususi kujadili Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025: Lengo la 1: Maisha Bora na Mazuri

6 Makundi mahususi kujadili Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025: Lengo la 1: Maisha Bora na Mazuri

Makundi mahususi kujadili Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025: Lengo la 1: Maisha Bora na Mazuri

7 Makundi mahususi kujadili Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025: Lengo la 2: Uongozi Bora na Utawala wa Kisheria

Makundi mahususi kujadili Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025: Lengo la 2: Uongozi Bora na Utawala wa Kisheria

8 Makundi mahususi kuandaa Ra-simu ya Mpango

Makundi mahususi kuandaa Rasimu ya Mpango

9 Mkutano wa Kanda/Mtaa Ku-pokea Rasimu ya Mpango, na Kutoa Maoni

na Ushauri

Kufanya Mkutano wa Halmashauri ya Kijiji

kuandaa Rasimu ya Mpango wa miaka mitatu

27Mwongozo wa Mwananchi

10 Mtendaji wa Kata Akishirikiana Wawezeshaji wa Jamii Kujumui-sha Maoni na Ushauri wa Jamii Kwenye Rasimu ya Mpango

Mkutano maalum wa Kamati ya Maendeleo ya Kata kutoa

ushauri wa kitaalamu

11 Mkutano wa Kamati ya Maende-leo ya Kata Kuweka Vipaumbele na

Kuandaa Mpango wa Miaka 3

Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji ku-pokea, kujadili na kupitisha

mpango.

12 Maafisa wa Kata Kuandaa Muhtasari wa Shughuli za utekelezaji kisekta

Kuandaa Muhtasari wa Shughuli za utekelezaji kisekta ngazi ya Kata

5 Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (2007), uandaaji Mpango Shirikishi Jamii kwa Mfumo wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo, kiongozi cha Mchakato wa Mjini, Dodoma-Tanzania, Kiambatanisho II.

6 Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (2007), uandaaji Mpango Shirikishi Jamii kwa Mfumo wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo, kiongozi cha Mchakato wa Kijijini, Dodoma-Tanzania, Kiambatanisho II.

28 Mwongozo wa Mwananchi

Baada ya kusoma mwongozo huu, tunataraji kwamba utajiamini zaidi katika kutafuta taarifa za bajeti na utakuwa mshiriki makini katika mikutano ya jamii yako.

Kama huridhiki na utoaji huduma za afya katika eneo lako, tunakushauri kutumia fursa zote zilizopo kama zilivyoelezewa vema katika chapisho hili na tuma maoni/malalamiko yako kwa shirika la Sikika kupitia namba 0688 493 882.

Pia tunakuhimiza ushirikiane na kila mmoja katika jamii yako; familia yako, marafiki na majirani zako kutumia mwongozo huu, ili nao wawe mawakala wa mabadiliko katika jamii yenu.

Tunawatakia kila la heri!

tunaweza kuleta

Mabadiliko kwa Pamoja

Notes:

Notes:

Nyumba Na.69Ada Estate, KinondoniBarabara ya TunisiaMtaa wa WaverleyS.L.P 12183Dar es Salaam, Tanzania.

Nyumba Na. 340Mtaa wa KilimaniS.L.P 1970Dodoma, Tanzania.Simu: 0262321307Faksi: 0262321316

Simu: +255 22 26 663 55/57 Ujumbe mfupi: 0688 493 882Faksi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected]: www.sikika.or.tzBlog: www.sikika-tz.blogspot.comTwitter: @sikika1Facebook: Sikika Tanzania

Sikika inafanya kazi kuhakikisha usawa katika

upatikanaji wa huduma bora za afya, kwa kutathimini

mifumo ya uwajibakaji katika ngazi zote za serikali.