mambo muhimu ya kuzingatia katika mchakato wa … · 2013-06-10 · zinapata bajeti ya mwisho,...

2
Misingi ya Bajeti Bajeti ni mpango au mkataba wa namna serikali itakavyokusanya na kutumia pesa za wananchi. Bajeti hujumuisha mapato ya serikali. Nchini Tanzania vipengele muhimu ni mapato ya ndani na Misaada ya nje. Kwa upande mwingine bajeti ni matumizi – namna serikali inavyotumia pesa vipaumbele na mipango mbalimbali. Bajeti huandaliwa na kutekelezwa kwa kipindi cha mwaka wa fedha, badala ya mwaka wa kalenda. Nchini Tanzania mwaka wa fedha huanzia Julai hadi – 30 Juni mwaka unaofuata. Ingawa umakini mkubwa kuhusu bajeti huelekezwa ‘’’Siku ya Bajeti’’mchakato wa bajeti ni mzunguko unaoendelea mwaka mzima. Bajeti inahusu pesa au rasilimali za wananchi, kwahiyo inatupatia dirisha la kufahamu umakini wa kweli wa Serikali katika utatuzi wa matatizo mbalimbali ya wananchi katika juhudi za kuleta maendeleo. Hivyo basi ushiriki mkubwa wa wananchi katika mchakato wa Bajeti utaboresha uwajibikaji, kuzuia fursa za rushwa na kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za umma na hatimaye kusaidia kuondoa matatizo yanayoikabili jamii ikiwemo Umasikini. Mamlaka ya Wananchi katika kuandaa Bajeti za Serikali Mamlaka yote ya Serikali na viongozi wa umma hutoka kwa wananchi. Hii ina maana kuwa Wananchi ndio wenye mamlaka makubwa zaidi ambayo hutoa Uhalali na Mamlaka kwa Serikali na vyombo vyake. Vivyo hivyo rasilimali zote za Taifa na Ugawaji wake kimatumizi vinakuwa chini ya Mwananchi. Wananchi ndio wanaolipa kodi na kutoa michango mbalimbali inayoiwezesha serikali kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Kwa mantiki hiyo, wananchi ndio wenye maslahi na rasilimali zao, kwa mustakabali wa nchi yao. Na hivyo, kuwa na haki yenye shauku ya kushiriki katika mchakato wa uandaaji wa bajeti na utekelezaji wake (matumizi) ni suala la msingi kwa kila Mwananchi kulizingatia. Takwimu zinaonesha kuwa karibu asilimia 80 ya wananchi wote wa Tanzania ni wakulima na wengi wao wakiwa wakulima na wafugaji wadogo na wa kati, ni muhimu kwa kundi hili kuzingatia Mamlaka yake na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa bajeti. Kwa upande mwingine ni wajibu wa Serikali kuzingatia na kuyafanyia kazi mapendekezo au vipaumbele vya kundi hili. Umuhimu wa kushiriki katika Mchakato wa Bajeti Kuna Umuhimu mkubwa kwa mkulima mmoja mmoja, vikundi vya wakulima, vyama vya ushirika, makundi ya kijamii na wananchi wote kwa ujumla kuuelewa mchakato mzima wa Bajeti ya serikali na kushiriki kikamilifu kutoa mapendekezo au vipaumbele vyao na baadae kufuatilia nanma ambavyo vimepewa nafasi kwenye Bajeti inayotolewa na serikali. Pia kufuatilia Bajeti inayopitishwa na serikali hasa inayohusiana na sekta ya kilimo na kuhakikisha imefanya kazi iliyokusudiwa, ikibidi kuwawajibisha wote wanaokwamisha utekelezaji wake MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA MCHAKATO WA KUANDAA BAJETI

Upload: others

Post on 24-Feb-2020

14 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Misingi ya BajetiBajeti ni mpango au mkataba wa namna serikali itakavyokusanya na kutumia pesa za wananchi. Bajeti hujumuisha mapato ya serikali. Nchini Tanzania vipengele muhimu ni mapato ya ndani na Misaada ya nje. Kwa upande mwingine bajeti ni matumizi – namna serikali inavyotumia pesa vipaumbele na mipango mbalimbali.

Bajeti huandaliwa na kutekelezwa kwa kipindi cha mwaka wa fedha, badala ya mwaka wa kalenda. Nchini Tanzania mwaka wa fedha huanzia Julai hadi – 30 Juni mwaka unaofuata. Ingawa umakini mkubwa kuhusu bajeti huelekezwa ‘’’Siku ya Bajeti’’mchakato wa bajeti ni mzunguko unaoendelea mwaka mzima.

Bajeti inahusu pesa au rasilimali za wananchi, kwahiyo inatupatia dirisha la kufahamu umakini wa kweli wa Serikali katika utatuzi wa matatizo mbalimbali ya wananchi katika juhudi za kuleta maendeleo. Hivyo basi ushiriki mkubwa wa wananchi katika mchakato wa Bajeti utaboresha uwajibikaji, kuzuia fursa za rushwa na kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za umma na hatimaye kusaidia kuondoa matatizo yanayoikabili jamii ikiwemo Umasikini.

Mamlaka ya Wananchi katika kuandaa Bajeti za SerikaliMamlaka yote ya Serikali na viongozi wa umma hutoka kwa wananchi. Hii ina maana kuwa Wananchi ndio wenye mamlaka makubwa zaidi ambayo hutoa Uhalali na Mamlaka kwa Serikali na vyombo vyake. Vivyo hivyo rasilimali zote za Taifa na Ugawaji wake kimatumizi vinakuwa chini ya Mwananchi. Wananchi ndio wanaolipa kodi na kutoa michango mbalimbali inayoiwezesha serikali kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Kwa mantiki hiyo, wananchi ndio wenye maslahi na rasilimali zao, kwa mustakabali wa nchi yao. Na hivyo, kuwa na haki yenye shauku ya kushiriki katika mchakato wa uandaaji wa bajeti na utekelezaji wake (matumizi) ni suala la msingi kwa kila Mwananchi kulizingatia.

Takwimu zinaonesha kuwa karibu asilimia 80 ya wananchi wote wa Tanzania ni wakulima na wengi wao wakiwa wakulima na wafugaji wadogo na wa kati, ni muhimu kwa kundi hili kuzingatia Mamlaka yake na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa bajeti. Kwa upande mwingine ni wajibu wa Serikali kuzingatia na kuyafanyia kazi mapendekezo au vipaumbele vya kundi hili.

Umuhimu wa kushiriki katika Mchakato wa Bajeti

Kuna Umuhimu mkubwa kwa mkulima mmoja mmoja, vikundi vya wakulima, vyama vya ushirika, makundi ya kijamii na wananchi wote kwa ujumla kuuelewa mchakato mzima wa Bajeti ya serikali na kushiriki kikamilifu kutoa mapendekezo au vipaumbele vyao na baadae kufuatilia nanma ambavyo vimepewa nafasi kwenye Bajeti inayotolewa na serikali. Pia kufuatilia Bajeti inayopitishwa na serikali hasa inayohusiana na sekta ya kilimo na kuhakikisha imefanya kazi iliyokusudiwa, ikibidi kuwawajibisha wote wanaokwamisha utekelezaji wake

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA MCHAKATO WA KUANDAA BAJETI

HATUA MUHIMU ZA MCHAKATO WA BAJETI ZA SERIKALI ZA MITAAHatua Mwezi Shughuli Maelezo Wahusika

1

Novemba-Desemba

Miongozo ya Bajeti inaandaliwa

Hatua ya kwaza kwa kawaida huchelawa, wakatimwingine hadi Aprili. Hii inaweza kuleta ugumu kuendesha mchakato shirikisho wa upangaji

Mamlaka za serikali za mitaa

2 Januari

Serikali za mitaa zinapeleka IPF kwe-nye kata na vijiji

Tarakimu za mwanzo zinazopewa serikali za mitaa maranyingi ubadilika baadae, ikimaanisha kua IPFs zinazopewa kata na vijiji mara nyingi si sahihi nazo pia, na maranyingi hakuna IPFs kabisa zinazotolewa katika kata na vijiji.

Serikali za mi-taa na vijiji

3 Februari

Mipango ya vijiji inaandaliwa kupitia fursa na vikwazo vya maendeleo

Mfumo wa fursa na vikwazo vya maendeleo(O&OD)sio mzuri na maranyingi unazaa mipango isiyo sahihi au mipango inayoacha vipaumbele vya makundi yanayotwezwa kama wanawake walemavu na maskini..

Mikutano

mikuu ya vijiji

na Mabaraza

ya vijiji

4 Machi

Mipango ya vijiji i n a j u m u i s h w a kwenye mipango ya kata

Kamati ya maendeleo ya kata mara nyingi inafanya mabadiliko kwenye mipango ya kijiji

Halmashauri za Vijiji/Kata

5Machi - Aprili Mipango na Bajeti

ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGA) inaandaliwa

Upangaji wa kuanzia chini kuja juu na mchakato wa bajeti wa juu kuja chini maranyingi vinakinza hapa, kwani vipaumbele vya vijiji havioani na vipaumbele vya maendeleo vya taifa. Na matokeo ni kwamba mipango ya vijiji inatambuliwa kidogo kwenye mpango wa mwisho wa Serikali za mitaa.

Mamlaka za Serikali za Mitaa

6Aprili

Halmashauri inajadili na kupitisha bajeti ya mamlaka ya Serikali za Mitaa

Bajeti ya serikali za Mitaa inafanana kitabu cha kurasa 400 au zaidi ,kinachopitishwa masaa machache tu ya mjadala kwenye halmashauri.

Maafisa wa Hal-mashauri kati-ka Halmashauri husika

7 Aprili

Mipango ya Serikali za Mitaa inapitiwa na sekretarieti ya mkoa

Mabadiliko mengi yanaweza kufanywa katika hatua hii, ili kwamba mipango iakisi vipaumbele vya taifa na vipaumbele vya serikali za mitaa

Sekretarieti za mikoa

8 Mei

Mpango mmoja na Bajeti ya OWM-TAMISEMI inaanda-liwa

Huu unahusisha mipango yote midogo midogo ya Serikali za mitaa

Maafisa wa TAMISEMI

9Juni - Julai

Bajeti inajadiliwa na kupitishwa na Bunge

Hii ndio hatua kuu inayotoa mstakabali wa Taifa, kutokana na bajeti iliyopangwa.

Wabunge na Mawaziri

10Agosti

Serikali za mitaa zinapata bajeti ya mwisho, upelekaji pesa unaanza

Kwa hatua hii mpango wa mwisho na bajeti iliyopitishwa mara nyingi iko tofauti sana na ule mpango uliopitishwa na baraza na mkutano mkuu wa kijiji. Katika hatua hii kuna matoleo mengi ya bajeti ya serikali za mitaa, hii inaleta ugumu wa kuelewa ipi ndio ‘’halisi

Taasisi na wiz-ara husika ze-nye Mamlaka ya kuidhinisha mafungu na malipo

11Septemba -Kuendelea

Utekelezaji wa miradi unaanza

‘miradi inayotekelezwa inaweza kuwa tofauti kabisa na ile iliyopendekezwa mwanzo na wanakijiji

Watoa huduma na wasimamizi wa sekta za huduma