jamhuri ya muungano wa tanzania wizara ya viwanda …€¦ · pekee imeweza kutoa mafunzo ya ujuzi...

8
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo TOLEO Na. 1, Desemba, 2012

Upload: others

Post on 18-Oct-2020

11 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA …€¦ · pekee imeweza kutoa mafunzo ya ujuzi ya usindikaji nafaka na matunda kwa wajasiriamali 1,764, usindikaji wa mafuta ya

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

Ifahamu Sekta ya

Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo

TOLEO Na. 1, Desemba, 2012

Page 2: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA …€¦ · pekee imeweza kutoa mafunzo ya ujuzi ya usindikaji nafaka na matunda kwa wajasiriamali 1,764, usindikaji wa mafuta ya

Wizara ya Viwanda na Biashara

2

Yaliyomo

Orodha ya Vifupisho ------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- 3

1.0 Utangulizi ------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- 4

2.0 Umuhimu wa Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo Katika Taifa Letu ------------- 5

3.0 Hali ya Sekta -------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- 6

4.0 Miongozo ya Kuendeleza Sekta ------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- 8

5.0 Fursa za Kuendeleza Sekta --------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- 9

6.0 Mafanikio yaliyopatikana Katika Sekta ----------------------------------------------------------------------------------------------13

7.0 Hitimisho -------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------14

Page 3: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA …€¦ · pekee imeweza kutoa mafunzo ya ujuzi ya usindikaji nafaka na matunda kwa wajasiriamali 1,764, usindikaji wa mafuta ya

Wizara ya Viwanda na Biashara

14

iii. Upatikanaji mitaji Wizara kupitia Mfuko wa Wafanyabiashara Wananchi (NEDF) unaoendeshwa na SIDO imeweza kutoa huduma ya mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 21 kwa kwenye zaidi ya miradi midogo 46,000 na kuwezesha kupatikana kwa ajira zaidi ya 160,000.

iv. Fursa za MasokoWajasiriamali wadogo 228 wanaozalisha bidhaa na huduma mbalimbali wameweza kuunganishwa na makampuni makubwa na ya kati. Aidha, zaidi ya wajasiriamali wadogo 1500 waliwezeshwa kushiriki maonesho ya biashara katika kipindi cha mwaka 2011/ 2012. Juhudi hizi zimesaidia jasiriamali ndogo kuzalisha bidhaa bora na kuweza kuhimili ushindani wa soko nchini na hata baadhi za bidhaa kupenya katika masoko ya nje ya Tanzania.

v. Elimu kwa ujasiriamali wadogo Wizara kwa kushirikiana na SIDO katika kipindi cha mwaka 2011/ 2012 pekee imeweza kutoa mafunzo ya ujuzi ya usindikaji nafaka na matunda kwa wajasiriamali 1,764, usindikaji wa mafuta ya alizeti, utengenezaji sabuni, mishumaa, chaki, utengenezaji wa mizinga ya kisasa na usindikaji wa asali kwa wajasiriamali 2,054 kupitia kozi 143. Aidha, wajasiriamali 63 walipata mafunzo ya usindikaji wa ngozi na bidhaa zake. Mafunzo hayo yamewawezesha wajasiriamali kufanya kazi kwa kujiamini na kuweza kuzalisha bidhaa bora zenye kukubalika na soko la ndani na nje ya nchi. Hali kadhalika, wajasiriamali 10,964 walipata mafunzo ya huduma za kuendeleza ujasiriamali, wajasiriamali 16,138 walipata huduma za ushauri na ugani.

7.0 Hitimisho

Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ni sehemu kubwa ya Sekta Binafsi hapa nchini. Sekta hii inabeba ahadi ya kulikomboa taifa letu kiuchumi na kijamii na kuliwezesha taifa letu kufikia Dira yake ya Maendeleo ya mwaka 2025.

Hivyo, Wizara inatoa rai kwa wadau wote wa Sekta hii wakiwemo Washirika wa Maendeleo kushirikiana katika kuiendeleza sekta hii muhimu ili iweze kuwa shindani na yenye kujenga msingi wa maendeleo ya sekta zingine.

3

Orodha ya Vifupisho

CAMARTEC Centre for Agricultural Mechanization and Rural Technology

CTI Confederation of Tanzania Industries

CoET College of Engineering and Technology

CHC Consolidated Holding Corporation

EPZ Export Processing Zone

EPZA Export Processing Zone Authority

GDP Gross Domestic Product

JICA Japan International Cooperation Agency

LAT Leather Association of Tanzania

NBS National Bureau of Stastistics

NDC National Development Corporation

PSRC Parastatal Sector Reform Commission

SEZ Special Economic Zone

SME Small and Medium Enterprise

SIDO Small Industries Development Organization

TCCIA Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture

TEMDO Tanzania Engineering and Manufacturing Design Organisation

TILT Tanzania Institute of Leather Technology TIRDO Tanzania Industrial Research and Development

Organisation TFDA Tanzania Food and Drug Association

TANTRADE Tanzania Development Authority

TAHA Tanzania Horticulture Association

TGF Tanzania Gatsby Foundation

TRA Tanzania Revenue Authority

UNDP United Nations Development Programme

UNIDO United Nations Industrial Development Organisation

Page 4: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA …€¦ · pekee imeweza kutoa mafunzo ya ujuzi ya usindikaji nafaka na matunda kwa wajasiriamali 1,764, usindikaji wa mafuta ya

Wizara ya Viwanda na Biashara

4

1.0 Utangulizi

Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (Small and Medium Enterpises - SMEs) ni mtambuka ambayo inagusa shughuli zote za kiuchumi kutegemeana na ukubwa wa shughuli husika. Baadhi ya shughuli za kiuchumi katika sekta hiyo ni kama uvuvi, uwindaji, dukawala, migahawa, maduka ya dawa, uchimbaji madini, ufugaji nyuki, usindikaji, viwanda, karakana, mawasiliano, utengenezaji vipuri, kliniki, shule, uchezaji ngoma, usafirishaji, ushauri nasaha na utafiti. Ili kuweza kufahamu kama shughuli fulani ya kiuchumi ni ya sekta Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo kuna vigezo vinavyotumika ambavyo nchi huwa zinakubaliana kulingana na mazingira halisi ya kiuchumi na kijamii. Vigezo ambavyo hutumika na nchi nyingi ni pamoja na idadi ya ajira, kiwango cha mtaji kinachowekezwa katika shughuli na mapato yatokanayo na mauzo ya bidhaa.

Kwa Tanzania, vigezo vya kuitambulisha sekta hii vilivyokubalika vimeainishwa vyema katika Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ya Mwaka 2003 ambavyo ni idadi ya ajira pamoja na kiwango cha uwekezaji katika shughuli. Kulingana na Sera hiyo, sekta hii hutambulika kama ifutavyo:

l Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo Sana (Micro Enterprises) ambazo huajiri watu wasiozidi 4 na kuwa na mtaji wa uwekezaji (mashine) wa chini ya Shilingi milioni 5 za kitanzania.

l Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (Small Enterprises) ambazo huajiri kuanzia watu 5 na 49 na kuwa na mtaji uwekezaji (mashine) wa kati ya Shilingi milioni 5 hadi milioni 200 za kitanzania.

l Viwanda vya Kati na Biashara za Kati (Medium Enterprises) ambazo huajiri kati ya watu 50 na 99 na kuwa na mtaji wa uwekezaji (mashine) wa kati ya Shilingi milioni 200 na milioni 800 za kitanzania.

Kwa kutambua umuhimu wa maendeleo ya teknolojia, tafsiri ya sekta inalichukulia suala la ajira kwa tahadhari. Endapo ajira katika shughuli inayoendeshwa itakuwa kwenye vigezo tajwa hapo juu, lakini mtaji ukawa nje ya vigezo hivyo, shughuli husika haihesabiki kama ni ya sekta hii. Kwa mfano, kama kiwanda kimeajiri watu 20 tu na mtaji wake ni Shs. Billioni moja kiwanda hiki kitahesabika ni kikubwa na kama kuna fursa maalum katika sekta kiwanda kama hicho hakitahusika.

Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo

13

Baadhi ya zana za kilimo zinazozalishwa katika karakana za SIDO pamoja na CAMARTEC

6.0 Mafanikio Yaliyopatikana Katika Sekta

Katika harakati ya kutekeleza Mikakati ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo na kuwawezesha wajasiriamali wadogo kutumia fursa zilizopo, sekta imeweza kupata mafanikio kadhaa.

i. Ufanisi katika mlolongo wa thamaniProgramu ya Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) imewezesha uanzishwaji na uimarishaji wa vyama/vikundi 319 vya wazalishaji na wakulima vyenye wanachama 15,482. Aidha, program hii imewezesha kuimarisha mifumo ya usambazaji wa mbegu bora na pembejeo katika mikoa ya mradi.

ii. Taarifa za SektaIli kuwezesha wadau wa sekta kupanga mipango endelevu ya kuendeleza sekta, na kuongeza kasi ya upatikanaji na usambazaji wa taarifa zinazohusiana na sekta, Wizara imekamilisha utafiti wa sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo nchini (SME Baseline Survey).

Page 5: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA …€¦ · pekee imeweza kutoa mafunzo ya ujuzi ya usindikaji nafaka na matunda kwa wajasiriamali 1,764, usindikaji wa mafuta ya

Wizara ya Viwanda na Biashara

12

Mjasiriamali mdogo akitumia fursa ya maonesho kuuza bidhaa zake katika moja ya Maonyesho ya wajasiriamali katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam

v. Fursa za Mitaji Wizara kupitia SIDO imekuwa ikitoa mitaji kwa wajasiriamali wadogo katika mikoa yote yenye ofisi. Mikopo hii ni pamoja na ile ya Mfuko wa Wafanyabiashara Wananchi (National Entrepreneurship Development Fund – (NEDF) na wakati mwingine baadhi ya Washirika wa Maendeleo huitumia SIDO kufikisha mikopo yao kwa walengwa wao.

vi. Teknolojia na UbunifuWizara inaratibu utafutaji, uzalishwaji kwa wingi na kusambazwa kwa teknolojia na zana za kilimo zinazoleta tija kwa wajasiriamali wadogo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wajasiriamali wadogo kujenga misingi ya ubunifu. Kupitia karakana za SIDO na Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini (CAMARTEC) zana nyingi za kurahisisha uzalishaji wa bidhaa na usindikaji wa mazao ya kilimo zimeweza kupatikana.

Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo

5

2.0 Umuhimu wa Sekta ya Viwanda Vidogo na

Biashara Ndogo katika Taifa Letu

Ni dhahili kuwa Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ina nafasi ya kipekee katika taifa letu. Hata hivyo, ni vigumu kupata maneno halisi ya kueleza umuhimu wa Sekta hii katika taifa na jumuia ya kitanzania. Ili kuyatendea haki maelezo ya umuhimu huo, inahitaji muda mrefu na kurasa nyingi katika kitabu. Katika makala hii tutaeleza kwa kifupi umuhimu wa sekta katika Tanzania tukigusia zaidi masuala ya uchumi na kijamii.

Kwanza kabisa, sekta hii ina mchango mkubwa katika ajira kwa watanzania. Katika kuajiri, sekta hii haibagui makundi yoyote ya kijamii kushiriki katika shuguli za kiuchumi na hivyo hutoa fursa kwa wananchi wa makundi mbalimbali ya kijamii hususan wanawake na vijana ambao wengi wao hawabahatiki kupata fursa za ajira rasmi katika sekta mbalimbali kutokana na sababu nyingi zikiwemo viwango hafifu vya elimu na ujuzi. Vilevile, sekta hii imekuwa ni kimbilio kubwa la kundi la vijana wengi wanaomaliza masomo katika vyuo mbalimbali hapa nchini. Na hivyo kuleta matumaini makubwa ya kuiboresha sekta hii kwa kutumia ujuzi na nyenzo wanazozipata wakiwa masomoni. Hivi sasa sekta inasemekana kuwa mwajiri namba mbili kwa watanzania baada ya kilimo na inaajiri watanzania zaidi ya millioni tano.

Pili, ushiriki wa Watanzania wengi katika shughuli za kiuchumi kumeiwezesha sekta kuchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la Taifa. Baada ya utafiti wa kina imebainika kuwa, hivi sasa sekta inachangia asilimia 27 katika pato la Taifa. Sekta hii pia imekuwa ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi katika maeneo ya vijijijni na imechangia sana katika kukuza vipato vya wananchi wengi. Kwa mantiki hiyo, Sekta ina nafasi muhimu na kubwa katika harakati za kuondoa umaskini na hata kusaidia katika kupunguza wimbi la uhamiaji wa watu toka vijijini kwenda mjini.

Tatu, sekta hii ni chimbuko la maendeleo ya ujasiriamali na sekta binafsi ya nchi yetu kwa vile inatoa mwanya mkubwa kwa watanzania kujifunza kuendesha shughuli za biashara na uzalishaji. Hii hasa imewezekana kwa kuzingatia ukweli kuwa uingiaji katika sekta hii unakuwa ni rahisi kwa kuwa wakati mwingine huhitaji mtaji mdogo na teknolojia rahisi.

Mwisho, Sekta hii ni kiungo mahiri kwa sekta ya kilimo na maliasili. Kwa hivi sasa kuna wajasiriamali wengi wanaojihusisha na uongezaji thamani wa mazao ya kilimo

Page 6: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA …€¦ · pekee imeweza kutoa mafunzo ya ujuzi ya usindikaji nafaka na matunda kwa wajasiriamali 1,764, usindikaji wa mafuta ya

Wizara ya Viwanda na Biashara

6

na maliasili. Aidha shughuli hii hufanyika kwa kutumia teknolojia rahisi na yenye gharama nafuu ambazo zinatengenezwa na baadhi ya wajasiriamali wadogo hapa nchini. Hii, imewezesha wajasiriamali kuanzisha viwanda vidogo vya usindikaji mazao ya kilimo na kuwezesha kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno (Post harvest losses).

3.0 Hali Ya Sekta

Kama ilivyotangulia kuelezwa hapo awali, Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo inahusisha shughuli za sekta zote za kiuchumi. Takriban, katika kila shughuli za kiuchumi, sekta hii inachukua nafasi kubwa. Hata hivyo shughuli nyingi za sekta hii ziko katika sekta isiyo rasmi. Kwa ujumla picha ya mgawanyo wa sekta hii unasimama kama inavyoonekana katika mchoro hapa chini:

Tasnia Ndogo Sana ZisizoRasmi

Tasnia za Kati

Tasnia Ndogo

Tasnia NdogoKabisa Rasmi

Mgawanyo wa SMEs

Kutokana na takwimu zilizopo, kuna jumla ya wajasiriamali wadogo milion 2.7 ambao wanamiliki jasiriamali milioni 3.2. Katika mgawanyo wa kijinsia, takwimu zinaonyesha kuwa washiriki wengi wa sekta hii ni wanawake kwa asilimia 54.3 na asilimia 45.7

Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo

11

Hapa chini ni baadhi tu ya bidhaa za wajasiriamali wadogo vilivyotokana na mafunzo hayo. Baadhi ya bidhaa zinapatikana katika maduka makubwa (supermarkets).

Baadhi ya bidhaa zilizosindikwa na wajasiriamali wadogo kutokana na malighafi zinazopatikana nchini

iv. Fursa za Masoko Wizara kwa kushirikiana na SIDO imekuwa ikiendesha maonesho ya biashara ya Kikanda. Maonesho haya hufanyika kila Kanda ya Tanzania mara moja kwa mwaka na hii huwarahisishia Wajasiriamali wadogo wengi kushiriki katika katika kila maonesho. Mgawanyo wa Kanda hizi ulizingatia ukaribu wa mikoa na hujumuisha Kanda sita ambazo ni: Kaskazini ijumuishayo mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara; Ziwa ijumuishayo mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara na Shinyanga; Kati ijumuishayo Mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida na Dodoma; Pwani ijumuishayo mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Pwani; Kusini ijumuishayo mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara; na Nyanda za Juu Kusini ijumuishayo mikoa ya Iringa, Rukwa na Mbeya. Aidha, Wizara inashirikiana na SIDO kuwaunganisha wajasiriamali wadogo na wafanyabiashara wakubwa ili wauze bidhaa zao.

Page 7: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA …€¦ · pekee imeweza kutoa mafunzo ya ujuzi ya usindikaji nafaka na matunda kwa wajasiriamali 1,764, usindikaji wa mafuta ya

Wizara ya Viwanda na Biashara

10

Baadhi ya Wajasiriamali waliopata fursa za kuhudhuria mafunzo ya uendeshaji biashara na ujasiriamali yaliyotolewa na SIDO mjini Dodoma

iii. Uhamasishaji wa uzalishaji na utengenezaji wa bidhaa mpyaKatika harakati za kuhamasisha wajasiriamali kutengeneza bidhaa mpya, SIDO imekuwa ikitoa huduma ya mafunzo maalum katika usindikaji wa mazao ya kilimo. Mafunzo haya yamefanikiwa na kuwawezesha wajasiriamali wengi kuingia katika huduma za usindikaji wa vyakula.

Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo

7

wakiwa ni wanaume. Hata hivyo shughuli nyingi za sekta hii zimejikita katika kununua na kuuza yaani biashara ambayo inawakilisha asilimia 55 wakati jasiriamali za huduma ni asilimia 30. Wajasirimali wachache hujihusisha na uzalishaji ambazo zinafikia asilimia 13.6 na nyinginezo zinachukua asilimia 1 kama inavyofafanuliwa katika jedwali Namba 1. Kama ilivyokwishaelezwa hapo awali pia, sekta hii imeajiri takribani Watanzania milioni 5.2 wengi wao wakiwa wamiliki wa moja kwa moja wa hizo jasiriamali kama inavyofafanuliwa na jedwali Namba 2.

Jedwali Namba1: Mgawanyo wa Jasiriamali KisektaIdadi ya Waajiriwa Biashara Huduma Uzalishaji Nyinginezo

Mwajiriwa 1- 4 1,710,884 942,596 406,426 14,830

Waajiriwa 5 au zaidi 40,012 21,639 23,965 2,534

Jedwali Namba 2: Mgawanyo wa Jasiriamali KijinsiaIdadi ya Waajiriwa Wanaume WanawakeMwajiriwa 1 833,279 1,259,817Waajiriwa 2- 4 537,546 444,295Waajiriwa 5 au zaidi 75,287 12,263

Wananchi wanaojishughulisha na sekta hii wamegawanyika katika makundi ya umri tofauti kama inavyoonekana katika jedwali Namba 3.

Jedwali Namba 3: Mgawanyo wa Umri wa Wajasriamali TanzaniaUmri Wanawake% Wanaume%

Chini ya Miaka 25 11.6 10.4

Miaka 25 - 34 34.2 38.4

Miaka 35 - 44 31.8 29.4

Miaka 45 - 54 16.0 15.4

Zaidi ya Miaka 55 6.4 6.8

Sekta hii inaendeshwa na Watanzania wa viwango na kada mbalimbali za elimu. Taarifa zilizopo zinaonyeshwa kuwa wengi wa wajasiriamali hao wana elimu ya msingi na wachache sana wana elimu ya chuo kikuu na ya ufundi. Watafiti wengi wa sekta

Page 8: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA VIWANDA …€¦ · pekee imeweza kutoa mafunzo ya ujuzi ya usindikaji nafaka na matunda kwa wajasiriamali 1,764, usindikaji wa mafuta ya

Wizara ya Viwanda na Biashara

8

hii wanadai kuwa elimu ya waendesha miradi ina mahusiano ya moja kwa moja na ukuaji wa biashara zao pamoja na urasimishaji wa biashara. Kama madai haya ni ya kweli, inawezekana yanachangia ukubwa wa sekta isiyo rasmi na umiliki mkubwa wa sekta hii kuwa chini ya mtu mmoja. Kwa ujumla viwango vya elimu vya waendesha sekta vimeainishwa katika Jedwali Namba 4.

Jedwali Namaba 4: Viwango vya elimu wamiliki wa shughuli za sekta

7.4

7.2

73.5

3.8

7.3

0.6

0.3

4.0 Miongozo ya kuendeleza Sekta

Kimsingi, Wizara ya Viwanda na Biashara na tafsiri ya Taifa ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo inahusika na sekta rasmi. Lakini kwa hali halisi, imekuwa ni vigumu kuachana na sekta isiyo rasmi kwa kuwa ni kubwa mno na yenye ufanisi mdogo. Ili kuweza kuboresha utendaji wa sekta isiyo rasmi, Wizara imekuwa na mikakati endelevu ya kuboresha mazingira ya biashara ili kuwezesha sekta isiyo rasmi kuwa rasmi.

Shughuli za maendeleo ya sekta hii zinaongozwa na Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ya Mwaka 2003, ambayo mikakati ya utekelezaji wake imejikita katika kuboresha mifumo ya sheria na taratibu; kuimarisha miundombinu na maeneo ya kufanyia kazi; Kuimarisha ujasiriamali na masoko ya huduma za uendelezaji wa biashara; kuboresha fursa za upatikanaji wa fedha kwa sekta; kuimarisha uwezo wa wadau katika kutekeleza program za sera hiyo; kuimarisha viwanda vijijini; masuala mtambuka hasa mazingira; jinsia ; makundi maalum na kukabiliana na maambukizi na usambazaji wa virusi vya ukimwi. Utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo unazingatia mipango mikuu ya kitaifa ikiwemo

Ifahamu Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo

9

Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mkakati wa Kupunguza Umaskini (MKUKUTA I &II), Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010, Mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano na Azma ya KILIMO KWANZA hasa nguzo namba 7 inayokazia masuala ya upatikanaji wa zana na pembejeo za kuboresha kilimo na uongezaji thamani wa mazao ya kilimo.

5.0 Fursa za kuendeleza Sekta

Kufuatia utekelezaji wa mikakati ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa sekta imewezesha sekta kuwa na fursa za aina nyingi zinazowasaidia wajasiriamali wadogo kuendeleza shughuli zao. Fursa hizi zinajumuisha program na huduma mbalimbali zitolewazo na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO pamoja na wadau wengine. Baadhi ya program na huduma hizo ni hizi zifuatazo:

i. Programu ya Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI)

Programu hii imejikita katika kuongeza ufanisi wa thamani ya mazao ya kilimo ikitumia njia ya mlolongo wa thamani (value chain). Bidhaa zinazohusika ni mazao ya alizeti, mihogo, mifugo, matunda na nyanya katika Wilaya 19 za mikoa sita ambayo ni:

Mkoa wa Iringa: Iringa Vijijini, Kilolo na Njombe;

Mkoa wa Manyara: Simanjiro, Hanang na Babati;

Mkoa wa Pwani: Bagamoyo, Rufiji na Mkuranga;

Mkoa wa Ruvuma: Songea Vijijini, Namtumbo na Mbinga;

Mkoa wa Mwanza: Sengerema, Kwimba na Ukerewe ; na

Mkoa wa Tanga: Muheza, Korogwe, Kilindi na Handeni.

ii. Huduma za Kuendeleza Biashara Wizara kupitia SIDO imekuwa ikitoa huduma za kuendeleza na kuendesha biashara ikiwa ni pamoja na mafunzo, ushauri na huduma za ugani. Aidha, SIDO imekuwa ikiwawezesha wajasiriamali wadogo kupata vifungashio vya bidhaa zao.

Kiwango cha Elimu Asilimia

Wasiosoma kabisa

Elimu ya Msingi bila kuhitimu

Waliohitimu Elimu ya Msingi

Elimu ya Sekondari bila kuhitimu

Waliohitimu Elimu ya Sekondari

Elimu ya Ufundi

Chuo Kikuu