jarida la maadhimisho ya miaka 23 ya kituo cha … 23.pdf · 2017-11-23 · makala za jarida la...
TRANSCRIPT
JARIDA LA MAADHIMISHO YA MIAKA 23 YA
KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR
{ZLSC}
YALIYOMO
(i) Historia ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.
(ii) Utangulizi
(iii) Malengo Makuu ya Kituo cha Huduma za sheria.
(iv) Maadili ya Kituo.
v) Kazi za Kituo.
Kutoa Msaada wa Sheria.
Kuwafundisha Wasaidizi wa Sheria.
Kufundisha Sheria na Haki za Binadamu.
Kusimamia Haki.
Kukitangaza kituo na kazi zinazofanywa na kituo.
Kutoa Majarida ya kituo.
Kutoa Elimu ya Sheria kupitia Vipindi vya Tv na Redio.
Huduma za Maktaba.
Wanafunzi wanaokuja kituoni Zlsc kwa ajili ya Mafunzo kwa Vitendo.
Mafunzo ya Haki za Binadamu kwa Makundi mbali mbali.
Uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2014.
Mafunzo ya wafanyakazi wa ZLSC juu ya ufuatiliaji na Tathmini.
Mafunzo ya Haki za Binadamu na Vyama vya wafanyakazi.
Mikutano ya Elimu ya Katiba inayopendekezwa.
Kituo na Jamii.
Makala za Jarida la Mwaka wa 23 wa ZLSC juu ya safari yako na
Kituo cha Huduma za Sheria.
Bodi ya Wadhamini ndicho chombo cha juu cha maamuzi katika
utendaji wa kila siku wa Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar.Kazi hiyo husaidiwa na Mkurugenzi wa Zlsc ambae ni
Katibu katika Vikao vya Bodi.Bodi ya wadhamini.Bodi ndicho
chombo cha juu chenye Mamlaka ya kuhakikisha
ufanisi,usimamizi pamoja na kuhakikisha mikakati ya kisera na
kiutendaji yote ya kituo imesimamiwa ipaswavyo ili kuhakikisha
malengo ya ofisi yanasimamiwa na kufikiwa kwa mafanikio
makubwa.
Bodi ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kabala ya hii
iliyopo sasa ilimjumuisha Profesa Haroub Othman,Mr.Hassan
Said Mzee na Bi.Fatma Maghimbi ambao walikiongoza kituo hadi
walipokamilisha mda wao.
Bodi kwa sasa inaongozwa na Profesa Chris Maina Peter,ambae
ni Profesa wa sheria,katika skuli ya sheria ya Chuo kikuu cha
Dar es Salaam,wakili wa Mahkama kuu ya Tanzania ambae ndie
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ZLSC.
Yupo pia Bi.Josefrieda G.Pereira,Ambae ni Muhadhiri kutoka
Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chukwani.
Bi.Salma Haji Saadat,ambae ametokea Jumuia ya Wanawake
wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA)
Nd.Daud Othman Kondo,ambae ametokea Wizara ya
Miundombinu na Mawasiliano.na
Bi.Harusi Miraji Mpatani ,Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar na Wakili wa Mahkama kuu ya Zanzibar ambae
pia ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya ZLSC.
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar hadi kufikia mda huu
kinajumla ya wafanyakazi 28,ambapo kwa Upande wa Unguja ni
wafanyakazi 20 na Pemba 8 ambapo miongoni mwao ni Maafisa
Mipango 11madereva 2,wahasibu 3,Afisa ufuatiliaji na tathmini 1
,Afisa Habari 1,Masekretari 2,Afisa Tawala 1na Msaidizi wake
1,Mkutubi 1,Afisa Sheria 1, Wakili 1,Sekretari 2 na Afisa
Teknologia na Mawasiliano 1.
Ni jambo la kujivunia kwa Wanawake, Watoto , Walemavu na watu
wasiojiwerza pamoja na Wananchi wa Zanzibar wamekua wakipata
masaada wa sheria na utetezi wa haki za binadamu bila ya malipo kwa
muda wa miaka 23 kuanzia 1992-2015 kupitia Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar.
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) ni asasi isiyo ya Kiserikali,
iliyo huru, ya kujitolea isiyofungamana na upande wowote wa kisiasa, na
isiyozalisha faida iliyoanzishwa rasmi mnamo mwaka 1992 na kufanikiwa
kupata Cheti cha Kukubalika chini ya Sheria ya Kijamii ya mwaka 1995
(yaani ‘Act' No. 6 of 1995).
Kazi kuu ya Kituo ni kutoa msaada wa Kisheria bila ya malipo kwa wanyonge, wanawake, watoto, wanaoishi na ulemavu, na watu wengine
wasiokuwa na fursa katika jamii; kueneza elimu ya Sheria; na kutayarisha machapisho katika nyanja zote za Kisheria kwa ajili ya watu wa Zanzibar.
Kituo kinaongozwa na Dira ambayo inasisitiza Haki na upatikanaji wake kwa wote.
Katika kufikia malengo yake Kituo pia kimejiwekea Dhamira ya kutofungamana na Chama chochote cha siasa, isiyozalisha faida, na
inayojitolea kwa dhati katika kukuza uelewa wa watu katika masuala ya Kisheria, kuhamasisha Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Malengo makuu ya Kituo ni:- 1. Kutoa msaada wa Kisheria, usaidizi wa Kisheria, na huduma nyengine za Kisheria kwa jamii, hasahasa kwa wahitaji, na watu wasiokuwa na fursa
katika jamii.
2. Kuhamasisha, kutetea, kuheshimiwa, kuangaliwa Haki za Binadamu, Utawala wa Sheria, misingi ya Kidemokrasia, utamaduni wa amani na kuvumuliana.
3. Kutoa elimu ya Sheria na ya Haki za Binadamu kwa jamii kwa ajili ya kukuza uelewa wa watu kuhusiana na haki zao za msingi pamoja na wajibu
wao.
4. Kuandaa, kuratibu au kufanya tafiti kuhusiana na mambo ya sheria,
na kufanya ushauri ndani ya mambo yanayolingana na kazi za Kituo.
5. Kuandaa miradi ya kisayansi ya kuelimisha kwa ajili ya kufundisha watu,
mmojammoja au makundi, ambao wameorodheshwa kuwa ni miongoni mwa watu watakaopata faida kutokana na mawasiliano yaliyo thabiti ya matokeo ya tafiti. Na
6. Kusaidia taasisi nyenginezo na mtu mmojammoja ambao malengo yao ni ya kujitolea kwa maana halisi ya ‘kujitolea’ kama ilivyoelezwa katika Sheria
za Zanzibar
Maadili ya Kituo
Kutokana na Katiba ya Kituo, kila mtu atakayeshiriki katika harakati za Kituo atatakiwa kuyalinda maadili yafuatayo:
a. Kuonesha imani nzuri na ya hali ya juu, na uvumilivu kwa wengine katika mambo yote yanayohusiana na Kituo.
b. Kuonesha utendaji wa kuridhisha, uaminifu, uwazi, na uwajibikaji wa dhati kwa harakati za Kituo.
c. Mtu yoyote, hatoruhusiwa kutumia mali za Kituo, jina au ushawishi kujipatia faida ama za kibinafsi, au za kiurafiki, kidini, kikabila, au faida
zinazolingana ambazo zinakwenda kinyume na malengo ya Kituo. d. Mtu asiwe na tabia ya kufanya kazi kwa upendeleo.
Kazi za Kituo ni pamoja na:-
1. Kutoa Msaada wa Sheria
Huduma hii inakusudiwa kusaidia watu wasiojiweza katika jamii ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za Mawakili binafsi. Huduma zinazotolewa zinahusiana na uvunjifu wa Haki za Binadamu, urithi wa mali
kwa jamaa wa marehemu, vurugu dhidi ya wanawake, unyanyasaji wa watoto, watu kufungwa kimakosa, ujabari wa Polisi, mashauri ya ajira na mengine mengi.
(Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bi.Harusi Miraji Mpatani Akiwasikiliza
wateja ikiwa ni miongoni mwa shughuli yake anayoipenda kuifanya pale anapopata fursa baada ya kupunguza Majukumu mengine ya Kiutawala)
(Bango hilo hapo juu ni miongoni mwa Bango lililovutia sana katika kuzipamba sherehe za
kuadhimisha mwaka wa 23 wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Mei 29,2015)
(Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Bi.Harusi M.Mpatani wa mwanzo kushoto
akizungumza na wadau wa kituo katika kongamano la wadau wa kituo moja ya shughuli zilizopangwa katika kuadhimisha mwaka wa 23 tokea kuanzishwa kwa ZLSC katikati ni Mjumbe wa Bodi ZLSC Bi.Salma Saadat na mwisho ni Mratibu wa Kongamano la wadau wa Kituo Bi.Jina
Mwinyi waziri)
(Wanafunzi wakiwa wanapatiwa Mafunzo ya namna ya kuishi pamoja na kwa Upendo kupitia alama ya kopa lilikiashira Upendo ni miongoni mwa Mafunzo yatolewayo na ZLSC katika Mafunzo
ya Ulinzi kwa Mtoto picha kwa msaada wa Gabriel Mkama Afisa Mipango ZLSC)
2. Kuwafundisha Wasaidizi wa Sheria
Mpango huu unakusudiwa kundi maalum ambalo litatumika kueneza, kusambaza na kukuza uelewa wa sheria kwa wanajamii. Kwa kawaida, kundi hili hupewa mafunzo ya Sheria mara moja kwa kila mwezi ili
waweze kueneza elimu ya Sheria katika maeneo mbali mbali ambayo watu wanaishi.
(Mratibu wa Mafunzo ya wasaidizi wa Sheria ZLSC Bi.Jina Mwinyi Waziri akiwafundisha wasaidizi
wa Sheria juu ya Sheria ya watu wenye ulemavu katika Ukumbi wa ZLSC Migombani.)
3. Kufundisha Sheria na Haki za Binadamu
Malengo ya mafunzo haya ni kupata watu wengi itakavyowezekana, kuweza kufahamu alama za Kitaifa na Kimataifa kuhusu uvunjwaji wa Haki za Binadamu, viwango na utendaji wa kimataifa kuhusiana na
uangalizi wa kanuni za Haki za Binadamu. Nafasi maalum inatolewa kwa Polisi, Maafisa wa Vyuo vya Mafunzo, na asasi zisizo za Kiserikali za
Zanzibar,ambazo moja kwa moja zinafanya kazi pamoja na jamii ya watu na viongozi wao.
(Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Kh.Makame wa Pili kushoto akiwa katika Picha ya Pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi mara baada ya kufungua Rasmi Mafunzo
juu ya Umuhimu wa Jeshi la Polisi kulinda Haki za Binadamu wakati wa Operesheni zao mbali mbali za kikazi Anaefata kushotoni kwake ni Mkurugenzi Mtendaji ZLSC Bi.Harusi Miraji Mpatani kushoto kwa Mkurugenzi ni Mratibu wa Mafunzo hayo Bi.Jina Mwinyi na kulia kwa Kamishna ni
Mrakib wa Polisi Madema Ndugu Kitole)
(Mafunzo ya kulinda haki za Binadamu kwa Maofisa Polisi yalifanyika pia kwa Mikoa yote ya
Kipolisi kwa Upande wa Pemba Anaetoa hotuba ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba Sheihan Mohammed Sheihan kushoto kwa kamanda ni Mwanasheria kutoka Wilaya ya Chake
Chake Omar Mcha Hamza na anaefata kulia ni Mratibu wa ZLSC Pemba Bi.Fatma Kh.Hemed kulia mwa Bi.Fatma ni Afisa Mipango wa ZLSC Pemba Bi.Safia Saleh Sultan)
4. Kusimamia Haki
Kazi hii inawajumuisha watu mbalimbali wanaohusika na usimamizi wa
Haki katika nchi.
Kuna sheria nyingi katika nchi zinazowapa watu na taasisi
nguvu/mamlaka ambayo kwa njia moja au nyingine zinaathiri haki za raia, ni muhimu kuhakikisha kuwa nguvu au mamlaka haya hayatumiwi vibaya. Majaji na Mahakimu hawatakiwi kujuwa sheria za nchini tu, bali
hata vyombo vya kimataifa ambavyo Tanzania ni mwanachama.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh.Omar Othman Makungu akiteta jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mshibe Ali Bakari na Pembeni ni Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Nd.Ibrahim Mzee Ibrahim katika Uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu ZLSC Migombani.
(Mafunzo ya Haki za Binadamu na Uchaguzi katika kuelekea Uchaguzi wa Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu October 2015 katika Ukumbi wa ZLSC Migombani.Mbele ya Picha hii ni Maofisa kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC wakiwasilisha Muongozo uliotolewa
na ZEC katika kusimamia Elimu ya Uraia na Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa)
Picha ya pamoja ya wadau wa kituo mara baada ya Mkurugenzi Mtendaji na Mjumbe wa Bodi ya
Wadhamini kuwataka wadau hao waeleze Mapungufu ya kituo pamoja na mafanikio ya kituo katika kuadhimsha miaka 23 ya ZLSC.
5. Jarida la ‘Sheria na Haki’
Malengo makuu ya jarida hili ni kuwapasha habari watu waliokaribu na Kituo na jamii kwa ujumla kuhusiana na harakati za Kituo pamoja na
taarifa za Haki za Binadamu na matatizo ya Kisheria Zanzibar.
(Majarida mbali mbali ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar yanayotolewa kila baada ya miezi
3 kwa lengo la kutoa taaluma ya sheria mbali mbali kupitia Majarida hayo)
Vipindi vya Redio na Televisheni
Kituo kinatayarisha na kurusha vipindi vya dakika 30 kwa kushirikana na
Redio ya Sauti ya Tanzania Zanzibar na Televisheni. Vipindi vya redio
vinaitwa ‘Haki na Sheria’ wakati vile vya Televisheni vinaitwa ‘Ijuwe Sheria’. Vipindi hivi vinazungumzia sheria mbalimbali za nchi, muundo wa sheria,
utawala wa sheria, elimu ya uraia na Haki za Binadamu.
Moja ya vipindi vya Televisheni vilivyorushwa na ZBC TV katika kipindi cha Ijue Sheria ambapo Tulipata nafasi ya kuelimisha jamii juu ya Sheria Mpya ya Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar
ZSTC Sheria nambari 2 ya 2014.Vipindi hivyo ni muendelezo wa elimu ya sheria mbali mbali zinazotolewa na ZLSC.Anaesalimiana na muendesha kipindi ni Mkurugenzi Fedha ZSTC Nd.Ismail Bai, katikati ni Mwanasheria wa ZSTC Nd.Ali Bilal na Mwendesha Kipindi ni Nd.Suleiman A.Salim
kutoka ZLSC.
7. Huduma za Maktaba
Kituo pia kinatoa huduma za maktaba ndani za ofisi zake mbili zilizopo Unguja na Pemba. Maktaba hizi zimesheheni sio tu vitabu vya sheria na
Haki za Binadamu, bali hata vitabu vyengine katika fani zisizokuwa za sheria. Machapisho haya huwasaidia wale wanaofanya kazi katika fani za sheria, wanaharakati wa Haki za Binadamu, na raia wa kawaida katika
kupata taarifa kuhusu sheria na Haki za Binadamu.
Jaji Mkuu wa Tanzania Nd.Mohammed Chande Othman wakati alipoitembelea Maktaba ya Kituo cha Huduma za Sheria wakati alipokuja katika Mahafali ya Pili ya Wasaidizi wa Sheria kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa kituo Prof.Chris Mainer Peter.
8. Mafunzo ya Vitendo kwa Wanafunzi
(Kutoka kushoto ni Zuwena Saleh Zubeir,Mohammed O.Kombo,Saleh M.Thabit,Haji Sungura Makame na Yumna Ali Mwinjuma wote hawa ni Wanafunzi wa Sheria na Social Work kutoka Chuo Kikuu Tunguu waliofika Ofisi zetu za ZLSC kwa Mafunzo ya Vitendo)
Pia Kituo kina kawaida ya kupokea na kuwapa mafunzo ya vitendo
wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini wanaomaliza mafunzo
yao.
shamra shamra za maadhimisho ya miaka 23 ya ZLSC
Kwa maksudi kituo kimeamua kuutumia mwezi wa Mei,2015 kufanya
shughuli mbalimbali ili kuwa miongoni mwa maadhimisho hayo;
(Picha ya kwanza kushoto ni washiriki mbali mbali waliojitokeza
katika Uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu ya Mwaka
2014.Picha ya pili ni Watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar walipokua katika picha ya pamoja walipojumuika katika
Dener ya kituo.Picha kwa msaada wa Afisa Habari ZLSC)
Picha ya kwanza kushoto ni Mkurugenzi kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC akiwa pamoja na Afisa Mipango wa kituo hicho Nd.Gabriel Mkama walipokua katika kipindi cha Live Redio Hits fm Mwandishi ni Zuhra Husein.Picha ya Pili ni watoto wa skuli za Maandalizi Kaskazini Unguja
walipopatiwa Mafunzo ya kujilinda na vitendo vya udhalilishaji katika chuo cha Amali Mkokotoni.
(Picha ya kwanza ni Afisa Habari ZLSC wa mwanzo kushoto Nd.Suleiman A.Salim ,akifuatiwa na
Afisa Mipango Bi.Jina Mwinyi Waziri,kulia ni Bi.Farhat Rashid na katikati ni Mtangazaji wa Bomba fm Redio Nd.Mohd waliposhiriki katika kipindi cha Live Redio kituo hicho.Picha ya Pili ni Mratibu
wa ZLSC Pemba Bi.Fatma Kh.Hemed wa Pili kulia akiwa na timu ya watendaji wa ZLSC Pemba walipoenda kuwatembelea wagonjwa Hospitali ya Chake Chake na kuwafariji)
Mafunzo ya haki za binadamu kwa makundi mbalimbali ya jamii ya
Zanzibar ikiwemo
Mafunzo kwa watu wenye Ulemavu
Jumla ya washiriki 40 kutoka jumuia mbalimbali za watu wenye ulemavu
walipatiwa mafunzo ya haki za Binadamu . Mafunzo hayo yalikua na lengo
la kuwaelewasha wanachama mbalimbali kutoka asisi zinazoshughulikia
ulinzi na utetezi wa haki za watu wenye ulemavu. Mafunzo hayo yalifanyika
katika ukumbi wa kituo cha ZLSC Chake Chake Pemba na yalifunguliwa na
Mratibu wa Kituo kwa Pemba Bi.Fatma Kh.Hemed ambapo aliwaeleza
washiriki hao kwamba lengo kuu ni kuadhimisha miaka 23 ya Kituo cha
Huduma za Sheria tokea kuasisiwa mwaka 1992.
Mwanasheria Mohd Ali Maalim kutoka Wizara ya Sheria na Katiba Pemba akitoa mada juu ya watu wenye ulemavu katika Mafunzo ya Haki za Binadamu na kundi la watu wenye ulemavu
katika ukumbi wa ZLSC.Chake Chake Pemba.
Mafunzo ya Haki za Binadamu kwa Watu wanaoishi na virusi vya
Ukimwi
Kwa mara ya kwanza Kituo kwa kushirikiana na Tume ya UKIMWI Zanzibar
(ZAC) kimefanya mafunzo ya haki za binadamu na sheria ya watu wanaoishi
na virusi vya Ukimwi Zanzibar Nambari 11/2015. Mafunzo hayo
yaliwajumisha watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI 39 wakiwemo
wanawake 26 na wanaume 13.wakiwemo wanawake 29 na wanaume 11 kwa
upande wa Pemba.
Washiriki walipata nafasi ya kukitambua Kituo na kuomba kuendeleza
mashirikiano na utetezi kwa watu hao kwani wanakumbana na matatizo
mengi ya unyanyapaa katika jamii ya Zanzibar.
Dr.Sihaba Saadat wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC) akiwasilisha mada katika Mafunzo ya watu
wanaoishi na virusi vya Ukimwi VVU Yaliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria ZLSC kwa ushirikiano na Tume ya Ukimwi Zanzibar.
Washiriki kutoka ZAPHA +PEMBA wakiwa katika picha ya Pamoja na Mratibu wa ZLSC Bi.Fatma
Kh.Hemed na Wanasheria wa Kituo cha Huduma za Sheria wakati wa Mafunzo ya Haki za Binadamu kwa watu wanaoishi na VVU.
Mafunzo ya Elimu ya uraia kwa walimu wa Sekondari wa Somo la Uraia.
Walimu wapatao 50 wakiwemo wanawake kutoka Mikoa mitatu ya Unguja
wameendelea kupata elimu na taaluma ya jinsi ya kufundisha mada
zilizomo katika mtaala wa somo ya Uraia kwa Sekondari. Mada mbalimbali
ziliwasilishwa zikiwemo Misingi ya Haki za Binadamu Kimataifa, Kikanda na
Kitaifa , Demokrasia ,Usalama Barabarani,Serikali ya Tanzania,Wajibu wa
Raia,Tabia Njema na utayari wakati wa kufanya maamuzi,Usawa kati ya
wanawake na wanaume na Elimu ya stadi za Maisha.
Walimu wa Mikoa Mitatu ya Zanzibar wanaofundisha somo la uraia walipopata nafasi ya Mafunzo juu ya Silibus ya somo la Uraia na Haki za Binadamu kama Mada hizo zilivyofafanuliwa kaika Somo
hilo wa Mtaala wa Sekondari.
Mafunzo ya Haki za Binadamu kwa Waandishi wa Habari
Katika kuadhimisha miaka 23 kituo kiliandaa Mafunzo maalum kwa ajili ya
waandishi wa habari na wahariri wa vyombo ya habari vilivyopo Zanzibar
kwa lengo la kukitangaza kituo lakini pia kuwafahamisha waandishi juu ya
kutumia kalamu zao na midomo yao katika kulinda na kutetea haki za
binadamu Zanzibar. Jumla ya Waandishi 39 walipatiwa Mafunzo ambapo
Wanaume walikua ni 24 na Wanawake 15 kwa Upande wa Unguja wakati
kule Pemba jumla ya Waandishi wa Habari 36 walipigwa msasa juu ya Haki
za Binadamu ambapo Wanaume walikua14 na Wanawake 22.
(Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari kisiwani Pemba wakati walipopatiwa
Mafunzo ya Haki za Binadamu katika kuzitumia vyema kalamu zao zisijekusababisha uvunjifu wa haki za Binadamu katika Ukumbi wa ZLSC Chake Chake Pemba)
(Waandishi wa Habari wa Unguja wakipigwa msasa katika mada ya Haki za Binadamu na kazi za Uandishi wa Habari ili kuhakikisha waandishi hao wanazitumia vizuri kalamu zao na Midomo yao
wakati wakiripoti matukio mbali mbali katika vituo vyao vya Utangazaji ili wasijekusababisha uvunjifu wa haki za Binadamu)
Mafunzo ya Haki za Binadamu kwa Jeshi la Polisi na Utambulisho wa
Wasaidizi wa Sheria
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kaskazini Unguja Hassan Nassir akipokea Salut ya heshima wakati akikaribishwa katika Mafunzo ya Haki za Binadamu na Jeshi la Polisi kwa Mkoa wa kaskazini yaliyoandaliwa na ZLSC Anaeshuhudia Salut hiyo wa mwanzo kushoto ni Mkurugenzi wa ZLSC Bi.Harus Miraji Mpatani ,akifuatiwa na Mrakib wa Polisi Madema Ndugu Kitole na mwisho ni
Mratibu wa Mafunzo Bi.Jina Mwinyi Waziri )
Mafunzo ya Haki za Binadamu kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba ikiwa ni miongoni mwa kazi za kituo kuwaeleimisha wasimamizi hao wa sheria katika kuhakikisha
wanazilinda Haki za Binadamu katika kutekeleza Operesheni zao mbali mbali za kikazi.
(Mafunzo ya Haki za Binadamu kwa Jeshi la Polisi Zanzibar Mkoa wa Kusini Pemba na Kusini
Unguja katika Kuhakikisha kwamba Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kinawakumbusha Askari hao juu ya Umuhimu wa Kulinda Haki za Binadamu katika Majukumu yao)
Uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu 2014
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh.Omar Othman Makungu akizindua Ripoti ya Haki za Binadamu kwa Mwaka 2014 katika Sherehe zilizofanyika katika viwanja vya ZLSC Migombani wanaoshuhudia kwa Upande wa kushoto ni Nd.Thabit Abdulla Mwanasheria ZLSC,Bi.Salma Saadati Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ZLSC,Bi.Harusi M.Mpatani Mkurugenzi Mtendaji ZLSC na Nd.Ibrahim Mzee
Ibrahim Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar.
(Makundi mbali mbali ya wananchi,Asasi,na Wanafunzi walijitokeza katika uzinduzi wa Ripoti ya
Haki za Binadamu kwa mwaka 2014 uliofanyika katika Viwanja vya ZLSC Migombani Mnamo tarehe 21.Mei .2015)
Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wafanyakazi wa ZLSC juu ya Ufuatiliaji
na Tathmini.
Mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa kituo kuhusu ufuatiliaji na
tathmini ambayo yaliandaliwa kwa wafanyakazi wa Kituo cha Huduma za
Sheria kwa Ofisi za Unguja na Pemba. Kwa upande wa Unguja mafunzo
hayo yalifanyika tarehe 17/05/2015, katika ukumbi wa ZLSC ambapo
Jumla ya wafanyakazi 14 akiwemo na Mjumbe mmoja wa bodi walishiriki
mafunzo. Pia kwa upande wa Pemba mafunzo kama hayo yalifanyika tarehe
27/05/2015 ambapo jumla ya wafanyakazi 7 na Mjumbe mmoja wa bodi
walishirki katika mafunzo. Lengo kuu ilikuwa ni kuwajengea uwezo
wafanyakazi katika masuala ya ufuatiliaji na tathmini ikiwemo masuala ya
uandishi wa Ripoti, ukusanyaji wa taarifa, namna ya kupima malengo kwa
kutumia viashiria na masuala yanayohusu uwasilishaji mzuri wa mada kwa
hadhira.
(Wafanyakazi wa Kituo cha Huduma za Sheria wakifatilia kwa karibu Mafunzo ya kuwajengea
uwezo yaliyoandaliwa na Afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa ZLSC Nd.Mohammed Khatib Mohammed.)
Sheria za Kazi na Haki za Binadamu kwa Viongozi na Wanachama wa
Vyama vya Wafanyakazi
Kituo kinaamini kuwa ''Kazi Pekee ndio huzaa utajiri wa mali katuka jamii''
Kifungu cha 22(1) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984.
Katika kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanazijua sheria za Kazi na wajibu
wao kwa mujibu wa sheria za Zanzibar Kituo wamefanya mafunzo ya sheria
za kazi kwa wanachama wa chama cha wafanyakazi ZUPHE( Chama cha
watoa Huduma na Afya) kwa tawi la Pemba. Jumla ya Wanachama 82
walipatiwa mafunzo hayo ambapo Wanaume ni 39 na Wanawake 42 .
(Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mafunzo ya wafanyakazi wa ZUPHE kisiwani Pemba Nd.
Bw. ZAHRAN MOH'D NAASOR akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo hayo kulia ni Mratib wa zlsc Pemba Bi.Fatma Kh.Hemed)
Elimu ya Katiba Inayooendekezwa
Katika moja ya mkakati wa kituo ni kuhakikisha jamii inakua na uwelewa
mpana juu ya elimu ya katiba pamoja na sheria mbali mbali za nchi.Katika
kulisimamia hilo kituo kimeweza kufanya Mikutano ya wazi katika Mikoa
yote Mitano ya Zanzibar juu ya Elimu ya Katiba inayopendekezwa Unguja na
Pemba.
(Mwanasheria Gabriel Mkama wa ZLSC na Mustafa Shariff wakiwafafanulia wananchi Jinzi Haki za Binadamu zilivyozingatiwa katika Katiba Inayopendekezwa wakati walipofika Bumbwini na Jimbo
la Mji Mkongwe kutoa Elimu ya Katiba Inayopendekezwa)
Kinamama wa kikiji cha Dunga Mkoa wa kusini Unguja waliojitokeza katika elimu ya katiba
inayopendekezwa iliyotolewa na Kituo cha Huduma za Sheria tarehe 15.05.2015
( Picha za hapo juu zinaonesha ushiriki wa Wananchi kutoka mikoa yote mitano ya Zanzibar Unguja na Pemba waliopatanafasi ya kuelemishwa juu ya Katiba Inayopendekezwa kupitia
Masheha wa Shehia husika kwa Mikoa hiyo Elimu iliyosimamiwa na Kituo cha Huduma za Sheria )
Vipindi vya kuelimisha Jamii na kutambulisha miaka 23 ya Kituo
Katika kujitangaza na kuielimisha jamii juu ya haki za binadamu na sheria
mbalimbali za Zanzibar kituo katika mwezi wa Mei mwaka 2013 pekee,
kiliweza kutembelea na kurikodi jumla ya vipindi 23 vya LIVE na vile vya
kurikodi .Aidha kituo kiliweza kujitangaza katika magazeti ya
Mwananchi,Zanzibar leo,Nipashe na Mtanzania ambapo waandishi wa vituo
vyote hivyo wamekua ni wadau wakubwa katika kukitangaza kituo.
(Picha zikionesha namna tunavyoshiriki katika vipindi vya tv na habari za Magazeti katika
kuwafikia Wananchi kihabari popote walipo katika visiwa hivi vya Unguja na Pemba)
(Katika kuadhimisha miaka 23 ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kilikwenda kuwatembelea
wagonjwa katika wodi ya watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja na kwa Upande wa Pemba walikwenda kuwatembelea wagonjwa katika Hospitali ya Chake Chake na kituo cha Kulelea
watoto yatima Mabaoni Mkoa wa Kusini Pemba)
Safari yangu na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar
Bi.Harusi Miraji Mpatani.
Niliweza kukifahamu Kituo cha Huduma za sheria Zanzibar nikiwa
mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo Kikuu cha Tunguu (Zanzibar
University). Kilichonipeleka huko kutumia maktaba ya sheria baada ya
kupewa kazi na mwalimu. Ilikua mwaka 2014. Bahati nzuri nilifanikiwa
kupata vitabu lakini pia ilikua ni bahati ya kuonana na Profesa Haroub
Othman baada ya kutambulishwa na Mkutubi bi. ..................ili aweze
kunisaidia suala langu.
Professa Haroub alinisaidia sio tu kujibu suala langu bali pia alinipa
maneno ya kunitia moyo na kuengeza juhudi katika masomo yangu ya chuo
kikuu . Nakumbuka aliniazima Kitabu chake ili kinisaidie kwa masharti ya
kukirejesha wiki inayofuata. Baada ya kukirejesha sikurudi tena Kituoni ,
wakati huo kilikua wireless Kisiwandui.
Mwaka 2005 kwa kupitia Zanzibar Youth Forum nilichaguliwa kutoa elimu
ya Uraia na Upigaji kura katika Jimbo la Mjimkongwe chini ya usimamizi wa
Kituo.
Baada ya kumaliza Shahada yangu ya Sheria niliajiriwa na Kituo kama Afisa
mipango katika sehemu ya Maktaba. Nilifanya kazi hiyo huku nikisimamia
Dawati la Watoto Kituoni hapo chini ya ufandhili wa Shirika Save the
Children .
Mwaka 2011 nilifanikiwa kuwa Kaimu mkurugenzi na mwaka 2013
nilithibitishwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji.
Licha ya Changamoto katika sehemu ya kazi nimejifunza mengi katika
maisha ya Kituo cha Huduma za Sheria.
SULEIMAN A.SALIM
Ilikua ni mwaka 2010 mwezi wa saba nikiwa muajiriwa wa Kituo cha TV cha
Zanzibar wakati huo kikijuilikana Televisheni Zanzibar (TVZ ) ambapo Mkuu wa
Vipindi wa TVZ Hiji Shajak aliponiomba niwe muendeshaji wa kipindi cha Ijue
Sheria.
Kwa vile sikuwamwanagenzi na uendeshaji wa vipindi mbali mbali katika kituo
hicho cha matangazo ya TV nilikubali na kuanza kufanya vipindi hivyo.Niwe
Mkweli kabla ya kuendesha vipindi hivyo sikuwa na uwelewa wa kutosha
kuhusu huduma zitolewazo na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.
Safari ya kutokea mwaka 2010 mpaka mwaka 2015 ni miaka 5 sasa wakati ule
nikiwa muajiriwa wa Televisheni Zanzibar na sasa mwaka 2015 nimekuwa
muajiriwa wa Kituo cha Huduma za Sheria katika nafasi ya Afisa Habari .
Awali nilikifahamu kituo kama taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na utoaji
wa msaada wa kisheria pekee ( legal Aid) lakini baada ya kushiriki vipindi mbali
mbali na shughuli mbali mbali zinazofanywa na kituo nimekuja kutambua
kwamba kumbe ile kazi ya kutoa msaada wa kisheria ni sehemu moja tu ya kazi
za kituo.
Kumbe kuna utitiri wa kazi zifanywazo na kituo hichi ikiwa ni pamoja na utoaji
wa machapisho mbali mbali ya kisheria kama vile Jarida la Kituo,Zanzibar
Yearbook of law,Ripoti ya Haki za Binadamu na Vijarida vyengine vidogo vidogo
vinavyochapishwa kwa shughuli mahsus.
Kuna sehemu kubwa ya utoaji wa taaluma ya sheria kwa ngazi ya cheti na hii
imekipa Kituo cha Huduma za Sheria sifa kubwa katika kuwasaidia wananchi wa
Zanzibar nafasi ya kuwa wasaidizi wa sheria katika maeneo yao waliyotoka pasi
na kuwa ni wenye Shahada za Sheria lakini wanafahamu kesi zote za Jinai na
Madai na wanauwezo wa kuzipokea na kuzifikisha panapostahili kwa ajili ya
hatua za upatikanakaji wa haki.
Hili si jambo dogo hata kidogo kwani kadiri kituo kinavyoendelea na utoaji wa
wasaidizi wa sheria hawa ndivyo idadi kubwa ya wananchi wasiojua sheria
inavyopungua na hatimae watu wataweza kudai haki na watatekeleza wajibu
baada ya kupata elimu ya sheria.
Kuna hili la utetezi wa haki mbali mbali za watoto ni eneo moja wapo ambalo
muda mrefu tunashuhudia kupitia vyombo mbali mbali vya habari kwamba
watoto wananyanyaswa, wanabakwa na kutumikishwa kupitia mradi wa
pamoja kati ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) na Save the Chilren
kumekua na ufuatiliaji na tathmini katika maeneo kadhaa ya Zanzibar yenye
lengo la kupunguza na hatimae kulimaliza kabisa suala la udhalilishaji na
unyanyasaji wa mtoto.
Mwisho katika makala hii nizungumzie suala la ushiriki wa Kituo cha Huduma za
Sheria katika utoaji wa Elimu ya uraia na uangalizi wa chaguzi mbali mbali za
kitaifa na Kimataifa.Mfano mzuri ni Pale Kituo kilipotuma Mwangali wa
uchaguzi katika uchaguzi uliofanyika nchini Kenya mwaka 2013 lakini pia
chaguzi za hapa kwetu tumekua tukishiriki katika timu ya waangali wa ndani na
kutoa ripoti zetu juu ya chaguzi hizo.
Haya na mengine mengi ni miongoni mwa mafanikio makubwa ambayo Kituo
cha Huduma za Sheria Zanzibar kimeweza kuyafikia na kipokatika harakati za
kuyaendeleza kwa sasa na siku za baadae ni vyema kila Mtumishi miongoni
mwa waajiriwa wa kituo hichi akawa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba
kunapatikana mafaniko zaidi katika utendaji wa kila siku wa kituo hichi.
MAFANIKIO YA MIAKA 23 KWA MAKUNDI YANAYOANGALIWA NA KITUO
CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR
JINA MWINYI WAZIRI
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar kiliazishwa mnamo mwaka 1992 na
watu watatu ambao ni Profesa Haroub Othman Miraji , Bi Ftma Magimbi na
Bwana Hassan Mzee. Ni moja ya Asasi isiyokuwa ya kiserikali ambayo ni ya
kujitolea, inayojitegemea na ni asasi ambayo si ya kibiashara. Lengo kuu la
Kituo ni kutoa huduma za sheria kwa watu wote wa Zanzibar wasiojiweza
wakiwemo;
1. Maskini 2. Wanawake 3. Watoto 4. Watu wenye ulemavu 5. Wazee.
Mafanikio na ufafanuzi kwa makundi haya ni kama
ifuatavyo:-
a. Maskini. Ndani ya miaka 23 Kituo kimeweza
kuwasiadia kisheria wananchi wengi walio masikini
kwa Unguja na Pemba, katika kazi hii wanacnhi walio
maskini wanashauriwa kisheria juu ya tatizo lolote la
kisheria ambalo linamkabidi, kama vile matatizo ya
Ardhi, ndoa, udhalilishaji na migogoro ya kazi .
Aidha kituo kiko mstari wa mbele kuwaandikia wananchi
hati mbalimbali za kisheria kama vile hati za Madai, majibu
ya Madai, hati za Viapo na Maombi ya Mahkama.
Ili kuifanikisha vyema kazi hii Kituo kimeajiri wasaidizi wa
sheria kuanzia mwaka 2007 hadi sasa katika majimbo yote
ya uchaguzi pamoja na vikosi vya serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar. Kazi zao kubwa ni kuwasidia maskini wasio na
uwezo wa kutia mawakili mahakamani wanapopata matatizo
ya kisheria.
Ili kwenda sambamba na hili Kituo kila mwaka ifikapo
tarehe 13 Disemba kinaadhimisha siku ya Msaada wa
Kisheria kwa kuwafikia wanachi wa vijijini kuwapatia elimu
hii ya kisheria na ushauri wa kisheria.
b. Wanawake. Kituo kiko mstari wa mbele kuhakikisha
kuwa wanawake wanapata haki zao, katika kipindi cha
miaka 23 kimeweza kuwatetea wanawake mbalimbali
wanaovunjiwa haki zao.
Wazo la kituo kwa kuwapa kipaumbele wanawake ni kwa
sababu ya mila za kizanzibari kuwa wanawake wengi wana
aibu na kushindwa kutetea haki zao.
Kituo kinatekeleza vyema mkataba wa kimataifa wa kupinga
ubaguzi kwa wanawake na kinaadhimisha maadhimisho ya
kimataifa ya siku ya wanawake duniani kila ifikapo tarehe 8
Machi kwa makongamano na warsha pamoja na vipindi vya
redio na Televisheni.
c. Watoto. Watoto ni hazina muhimu sana katika jamii,
kituo kimeweka nafasi maalum kwa watoto ili kulinda
haki zao. Katika miaka 23 ya Kituo, Kituo kilishirikiana
na Shirika la Kimataifa la Save the Children pamoja na
Wizara ya Ustawi wa Jamii Wanawake na Watoto
kupatikana kwa sheria ya Mtoto nam. 6 ya 2011.
Aidha kituo kilikuwa mstari wa mbele kupatikana kwa
mahakama ya watoto Zanzibar ili kuwasimamia watoto
wote wenye mikinzano na sheria.
Ili kwenda sambamba na mkataba wa kimataifa wa watoto
kituo kinaadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika kila ifikapo
tarehe 16 Juni ya kila mwaka, na kuanzisha miradi
maalum inayohusu haki na wajibu wa mtoto kisheria.
d. Watu wenye Ulemavu. Hili ni kundi linalopata tabu
sana katika kuvunjiwa haki zao na jamii pamoja na
Serikali ikiwa moja kwamoja au si moja kwa moja.
Kituo katika miaka 23 kimefanya mafunzo mbalimbali ya
kwa watu wenye Ulemavu kuhusu sheria, mikataba ya
kimataifa na masuala ya haki za binadamu.
Aidha kituo kinashirikiana na taasisi mbali mbali
zinazohudumia watu wenye ulemavu ili kuweza kutetea
haki zao wenyewe.
e. Wazee. Kundi la mwisho linaloangaliwa na Kituo ni
wazee ambao hawawezi kufuatilia na kusimamia haki
zao. Katika kufanikisha hili Kituo kinawasaidia wazee
katika kupata haki zao za kisheria kwa kuwapa
mafunzo ya haki za binadamu na sheria.
Kwa miaka 23 tokea Kituo kuanzishwa kimefikia malengo
yake kwa wazanzibari walio wengi ingawa kuna
changamoto ndogondogo zinazozikabili Kituo.
SHAIRI LA KUTIMIZA MIAKA 23 YA MSAADA WA SHERIA
akika twakipongeza Kituo chetu muruwa
Kimedumu na kuweza Huduma nyingi kutowa
Kwingi kishajitangaza Watu wengi wakijuwa
Miaka ishirini na tatu Hongera Kituo chetu.
rodha ya kazi zake Baadhi nawatajia
Kufanya itambulike Taaluma ya Sheria
Raia waelimike Haki zao kuzijua
Miaka ishirini na tatu Hongera Kituo
chetu.
akala za majarida Hutolewa kwa awamu
Mambo mengi ya faida Unayakutia humu
Kusoma hayana shida hupambwa na lugha
tamu
Miaka ishirini na tatu Hongera Kituo chetu.
harama hapa haipo hulipi hata thumni
Msaada upewapo Lako kubwa shukrani
Lakini kwenye malipo Hudaiwi abadani
Miaka ishirini na tatu Hongera Kituo
chetu.
ndapo mtu kakwama hajui pa kuanzia
Kituo kinasimama Msaada kumpatia
Na endepo ni lazima Mahakamani kungia
Miaka ishirini na tatu Hongera Kituo chetu.
atiba ya kufundisha Wasaidizi wa Sheria
Ili kwenda elimisha majimbo wanotokea
Hili limeshajiisha Umma kuwasaidia
Miaka ishirini na tatu Hongera Kituo chetu.
H O
N
G
E R
idha kinashiriki Kwenye yake majukumu
Kuzielimisha haki Zote za kibinadamu
Watu wengi kwa malaki Wameshapata elimu
Miaka ishirini na tatu Hongera Kituo chetu.
ao la Kituo hiki Ni Profesa Haroubu
Kwake aliona dhiki Jamii kupata tabu
Kwa watu kunyimwa haki Hakutaka awe bubu
Miaka ishirini na tatu Hongera Kituo chetu.
eo tunashereheka Kukua Kituo chetu
Kimeshapata miaka Ni ishirini na tatu
Kote kinatambulika Hii ni fakhari yetu
Miaka ishirini na tatu Hongera Kituo chetu.
ifa nyingi tuwapeni Viongozi wa Kituo
Ukweli wapo makini Kusaka mafanikio
Sote tunawaamini Kuleta maendeleo
Miaka ishirini na tatu Hongera Kituo chetu.
hris Maina Peter Mwenyekiti madhubuti
Bi Harusi anafata Mkurugenzi thabiti
Mambo mengi mmeleta Hongera kazeni buti
Miaka ishirini na tatu Hongera Kituo chetu.
A
Z
L
S
C