jarida la wiki nishati na madini toleo la 48

Upload: ahmad-issa-michuzi

Post on 02-Jun-2018

437 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 8/10/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 48

    1/9

    BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali

    kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizar a ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA

    NISHATI &MADINI

    Toleo No. 48 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe Januari 1-7, 2015

    Mwaka 2015 uwe wa mafanikio zaidi Uk3

    Uingereza yaimwagia

    sifa Tanzania

    Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo

    nThe Guardian UKyaitangaza kimataifanUgunduzi wa gesi kuchagiza uwekezaji

    The Guardianimeyataja makam-puni makubwa yauwekezaji katikasekta ya mafutana gesi ya Uin-gereza ambayo

    yanafanya utatikatika sekta hiyohapa nchini kuwani pamoja na BGGroup, Statoil,

    Exxon Mobil naShell.

    Habari Uk. 2

  • 8/10/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 48

    2/9

    2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI

    Na Veronica Simba

    Gazeti la The Guardian laUingereza hivi karibunilimechapisha toleo maalu-mu lenye makala mbalim-

    bali zinazoielezea Tanza-nia kama nchi yenye vivutio vingi vyauwekezaji ikiwemo sekta ya nishatiinayochagizwa na ugunduzi wa gesiasilia.

    Toleo hilo la The Guardian la No-vemba 25, 2014 limeweka bayanakuwa kwa mujibu wa tafiti walizo-fanya pamoja na mahojiano na watumbalimbali, Tanzania ina sifa nyingina mazingira mazuri yanayovutiawawekezaji, ikiwa ni pamoja na amaniiliyopo pamoja na hali ya usalama.

    Katika mahojiano na Gazeti hilo,Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Dianna Melrose alisema Serikali yakeimedhamiria kuelekeza misaada yakekwa Tanzania katika sekta za nishatina elimu, ambapo inawezekana kupi-ma matokeo (measure results) badalaya kuchangia katika bajeti ya nchi kwaujumla wake kama ambavyo imekuwaikifanya.

    Lengo letu katika maendeleo yakiuchumi ni kuhakikisha nchi zinaon-dokana na utegemezi wa misaada, ali-

    sisitiza Balozi Melrose.Akizungumzia suala la Uingereza

    kuwekeza Tanzania, Balozi Melrosealisema nchi yake inawekeza kwa kiasikikubwa Tanzania na kuongeza kwam-

    ba uwekezaji huo utaongezeka zaidihasa kutokana na ugunduzi wa gesiasilia unaoendelea.

    Kwa upande wake, Waziri mpyawa Serikali ya Uingereza aliyeteuliwakusimamia Afrika, James Duddridgeameelezewa kukiri kuridhishwa na

    jitihada chanya za Tanzania katika ku-saidia kuimarisha amani na usalamakatika Ukanda wa Afrika hususankatika Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC).

    Naye Mwakilishi wa Biashara waUingereza kwa nchi za Kenya na Tan-zania, Clive Hollick alipoulizwa na

    The Guardian kuhusu hatua wanazo-chukua katika kukuza biashara bainaya Uingereza na Tanzania, alisemakuna mambo mengi yanafanyika, mo-

    jawapo ikiwa ni kuhakikisha uwepo wafursa muhimu katika sekta ya gesi namafuta.

    The Guardian imeyataja makam-puni makubwa ya uwekezaji katikasekta ya mafuta na gesi ya Uingerezaambayo yanafanya utafiti katika sektahiyo hapa nchini kuwa ni pamoja naBG Group, Statoil, Exxon Mobil naShell.

    Aidha, imeelezwa kuwa Kampuniya BG na mshirika wake Ophir mpakasasa wamewekeza zaidi ya Dola za ki-marekani bilioni moja katika shughuli

    za utafiti wa gesi na mafuta hapa nchinitangu mwaka 2010 na kwamba kwakiasi kikubwa utafiti huo umeleta ma-tokeo yenye kutia moyo.

    Uingereza yaimwagia

    sifa Tanzania

    Vijiji 45 mkoani Mara kupatiwa umemeNa Greyson Mwase

    Waziri wa Nishati na Ma-dini Profesa SospeterMuhongo amesema

    kuwa vijiji vipatavyo45 vilivyopo katika

    mkoa wa Mara vinatarajiwa kuungan-ishiwa na huduma ya umeme kupitiaWakala wa Nishati Vijijini (REA)

    Profesa Muhongo aliyasema hayokatika ziara yake ya siku sita katikamkoa wa Mara lengo likiwa ni kukaguana kuzindua miradi ya umeme vijijiniawamu ya pili inayosimamiwa na Waka-la wa Nishati Vijijini (REA) kwa kush-irikiana na Shirika la Umeme Nchini(TANESCO)

    Profesa Muhongo alisema ziarayake ambayo ilihusisha wilaya za Mu-soma Vijijini, Tarime, Rorya, Bundana Serengeti ililenga pia kubaini na ku-kagua mahitaji ya umeme katika wilaya

    hizo ili vijiji vilivyokosa umeme katikautekelezaji wa awamu ya pili viingizwekatika awamu nyingine ya umeme viji-

    jini.Alieleza kuwa Wizara imekuwa

    ikisambaza umeme katika kila mkoa nawilaya za Tanzania kwa awamu kulin-gana na mahitaji na idadi ya watu katika

    maeneo husika.Alisema kwa sasa umeme unaosam-

    bazwa upo katika awamu ya pili ambapoawamu ya tatu itakuja baada ya awamuya pili kumalizika.

    Aidha alitaja maeneo yanayopewavipaumbele katika uunganishaji waumeme vijijini kuwa ni maeneo yenyehuduma muhimu za kijamii kama vileshule, vituo vya afya, makanisa, misiki-ti, ofisi za vijiji na kata, na sehemu zenyemiradi ya maji.

    Lengo letu kuu la kwanza ni ku-hakikisha kuwa wananchi wanapata hu-duma za jamii kwa urahisi na baada yakuboreshwa kwa huduma hizo tunak-wenda kuwaunganishia umeme mwa-nanchi mmoja mmoja ikiwa ni mkakati

    wa kuhakikisha maisha ya wananchiyanaboreshwa kupitia nishati ya umeme, alisema Profesa Muhongo

    Profesa Muhongo aliongeza kuwa,ili nchi yoyote duniani iweze kupiga

    hatua katika ukuaji wa uchumi wake,inahitaji nishati ya umeme na kuongezakuwa kwa kutambua hilo serikali im-eanza kuunganisha umeme kwa upandewa vijijini ili wananchi hao waweze kuji-

    ingizia kipato kwa kujiajiri.Alifafanua kuwa wananchi wa viji-

    jini kupitia nishati ya umeme wanawezakuwekeza kwenye mashine za kusaganafaka, kukamua mafuta, kuhifadhivyakula vya kuuza kwenye majokofuna kujipatia fedha na kuongeza kuwaitapunguza wimbi la watu kukimbiliamjini kutafuta ajira.

    Wakati huohuo Mwenyekiti wakijiji cha Bukabwa Thomas Makweraalisema kuwa wananchi wa kijiji chakewamekuwa wakikabiliwa na changamo-to ya kutokuunganishwa na nishati yaumeme kwa muda mrefu hali inayopele-kea maendeleo ya kijiji hicho kudorora.

    Hata hivyo aliongeza kuwa wa-kandarasi wamekuwa wakionekana

    wakisimika nguzo za umeme hali inay-otia hamasa kwa wananchi ya kutakakujua ni lini wataunganishwa na hudu-

    ma hiyo ya umeme.Akijibu swali la Mwenyekiti huyo

    Profesa Muhongo alimtaka mkandarasianayesimamia mradi huo kutoka kam-puni ya Derm Electrical Huseni Ayubu,

    kutoa ufafanuzi ambapo mkandarasihuyo alieleza kuwa kazi ya kusimikanguzo pamoja na kuunganisha umemeinatarajiwa kukamilika mapema, mweziFebruari mwakani.

    Naye Profesa Muhongo aliwatakawanakijiji wa Bukabwa kuchangamkiafursa ya kuunganishiwa umeme kwagharama nafuu ya shilingi 27,000.wakati mradi wa umeme ukiwa badoupo katika kijiji chao.

    Alisema kuwa lengo la utekelezajiwa miradi ya umeme vijijini kupitiaWakala wa Nishati Vijijini (REA) nikuhakikisha kuwa vijiji vyote ambavyoumeme umepita lakini havijaunganishi-wa vinaunganishiwa ili kuhakikisha vi-jiji vyote vilivyopitiwa umeme vinapata

    umeme kwa kufuata utaratibu huo.

    Kushuka kwa bei ya mafuta kuna atharikatika utafiti wa mafuta na gesi nchini TPDC

    Na Malik Munisi,TPDC

    Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania huenda ikalazimika kupitiaupya mkataba wa uzalishaji na utafu-taji wa mafuta na gesi (ProductionSharing Agreement-PSA) kuvutia zaidi

    uwekezaji katika utafutaji wa mafuta na gesinchini.

    Kupitiwa upya kwa mkataba huo kunato-

    kana na kushuka kwa kasi kwa bei ya mafutakatika soko la dunia hali ambayo itayalazimu

    Makampuni ya Kimataifa ya Utafiti wa mafutana gesi kupunguza bajeti zao za utafutaji kwakiasi kikubwa. Kwa miezi kadhaa sasa bei yamafuta ghafi katika soko la dunia imekua ikishu-ka hadi kufikia takribani dola za kimarekani 61kwa pipa (61 US Dollar per barrel) kutoka dolaza marekani 100 kwa pipa mwaka jana.

    Hayo yalielezwa na Kaimu Mkurugenzi waMikakati na Mipango wa Shirika la Maendeleoya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. WellingtonHudson wakati akitoa mada juu ya uanzish-waji wa mkataba wa uzalishaji na utafutaji wamafuta na gesi hapa nchini katika semina iliyo-washirikisha wadau kutoka Wizara na Taasisimbalimbali iliyoandaliwa na shirika hilo mjiniBagamoyo hivi karibuni .

    Kama bei ya mafuta itaendelea kushukakwa kasi ya sasa tunaweza kulazimika kupitiaupya vipengele vya mkataba wa uzalishaji nautafutaji wa mafuta na gesi (PSA) ili kuvutia

    zaidi uwekezaji katika utafiti wa mafuta na gesinchini, alisema Dkt. Hudson.

    Aidha, aliongeza kuwa, mkataba unaotu-mika sasa uliboreshwa mwaka 2013 kutokana naugunduzi mkubwa uliofanyika katika maeneo yakina kirefu cha bahari mwaka 2010 pamoja nanchi jirani za Msumbiji, Uganda na Kenya.

    Kama hali ya kushuka kwa bei ya mafutaitaendelea hivi basi Makampuni yatapunguzakwa kiasi kikubwa bajeti yao katika utafutaji wamafuta na gesi, alisisitiza Dkt. Hudson.

    Vilevile alisema kuwa, mfano wa mkatabawa mwanzo wa uzalishaji na utafutaji wa mafutana gesi (MPSA) uliandaliwa mwaka 1989 kwamsaada wa Sekretariati ya Jumuia ya Madolaya Uchumi na Sheria ( Economic and Legal Ser-vices of the Common wealth Secretariat), Mka-taba ambao ulilenga kuvutia uwekezaji nchini,ambapo Tanzania ilikuwa inachukuliwa kamaeneo ambalo bado halijafanyiwa utafiti (Frontirepetroleum province).

    Aliongeza kuwa, hata hivyo kwa wakati huohakukuwa na ugunduzi wa aina yoyote katikaeneo la kina kirefu cha maji hali ambayo ilito-kana na kutokana na vikwazo vya teknolojia.

    Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na

    Mikakati kutoka TPDC, Dkt. HudsonWellington akitoa mada katikasemina ya wadau kutoka Serikaliniiliyofanyika Bagamoyo mwishoni mwawiki iliyopita.

  • 8/10/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 48

    3/9

    3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    MAONI

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    FIVEPILLARS OFREFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    INCREASE EFFICIENCY

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OFTHE CLIENT

    SATISFACTION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OFSHAREHOLDERS

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Mwaka 2015 uwewa mafanikio zaidi

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Wizara ya Nishati na Madinikupata tuzo ya kimataifa

    Hatimaye tumeingia mwaka 2015. Mwaka 2014 ulikuwawa mafanikio makubwa kwa Wizara ya Nishati na Ma-dini (MEM) na taasisi zake.

    Kwa mfano, malengo ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Serikali yalikuwa kuhakikisha kuwa asilimia 30 ya wa-nanchi wanapata huduma ya umeme ifikapo 2015 lakini lengohilo limeshavukwa na kufikia asilimia 36 mwaka jana (2014).

    Ikumbukwe kuwa Mwaka 2005 watanzania waliokuwa nafursa ya kutumia umeme walikuwa ni asilimia 10 tu na sasa ni

    asilimia 36, hayo ni mafanikio makubwa sana.Pia suala la mgawo wa umeme limeendelea kubaki historiabaada ya kuwa utamaduni miaka kadhaa iliyopita. Hali ya kuka-tika umeme kwa sasa inatokana na uchakavu wa miundombinu yausafirishaji umeme ambayo Shirika la Umeme Tanzania (TANE-SCO), linaendelea na kazi ya ukarabati na kupanua miundombinuhiyo ili kuweza kuwa na umeme wa uhakika.

    Mwaka jana pia tumeshuhudia mgodi wa STAMIGOLD uli-opo chini ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ukianza ku-zalisha dhahabu ukiwa chini ya wazawa.

    Aidha, hadi ilipofika mwaka jana 2014, Wakala wa Ukaguziwa madini nchini (TMAA) uliweza kukamata madini yaliyokuwayakisafirishwa nje ya nchi bila kibali ya thamani ya zaidi ya shilingibilioni 15. Hii ni hatua ya kupongezwa katika shughuli za udhibitimadini.

    Vilevile, mwaka jana Chuo cha Madini (MRI) kilicho chiniya Wizara kimefanya mahafali yake ya kwanza ambapo wahit-imu 368 walitunukiwa vyeti katika ngazi ya shahada katika faniza jiolojia na utafutaji madini; uhandisi wa uchimbaji madini; nauhandisi wa uchorongaji madini.

    Kuhitimu kwa wataalamu hao si jambo la kubeza ukizingatiakuwa fani hizo ni adimu nchini na mahitaji ya wataalamu hao kwa

    sasa ni makubwa sana kutokana na kukua kwa kasi kwa sekta yamadini. Tunaupongeza uongozi wa Wizara ya Nishati na Madinikwa kukiwezesha Chuo hicho katika masuala mbalimbali yali-yowezesha kufikia hatua hiyo kubwa.

    Mwaka jana pia tumeshuhudia Wakala wa Nishati Vijijini(REA) ikiendeleza juhudi za usambazaji umeme vijijini kwa kasiya ajabu. Awali, ilipotangazwa miradi ya REA, baadhi ya watuwalifikiri ni ndoto lakini sasa wameamini, kwani, vijiji vingi nchinihivi sasa vimeanza kuona neema ya nishati hiyo ya umeme.

    Mafanikio mengine ni pamoja na kuanza kutolewa ruzukukwa wachimbaji wadogo; kuendelea kugundulika kwa gesi asilia;utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme; na kupitiwa kwamikataba ya madini kwa kufanya majadiliano na Kampuni zauchimbaji madini zenye mikataba ili kurekebisha vipengele vyamikataba ambavyo vinalenga kuleta manufaa zaidi kwa Taifa.

    Na matunda ya mapitio ya mikataba ilionekana tarehe 9 Ok-toba, mwaka jana ambapo Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM)ilitiliana saini mkataba na Serikali wa kurekebisha vipengele katikamkataba uliosainiwa huko nyuma baada ya majadiliano kukami-lika.

    Kwa kweli mafanikio ni mengi, mengi sana na makubwa am-bayo hayahitaji jicho la tatu kuyaona.

    Lakini mafanikio hayo ya mwaka jana ndio changamoto zetukwa mwaka huu. Ni matarajio ya watanzania kuwa mwaka huulengo la watanzania wenye fursa ya kutumia umeme kufikia asil-imia 45 hadi 50 litawezekana.

    Eneo jingine la kutiliwa mkazo mwaka huu ni wachimbajiwadogo. Mwaka huu uwe ni mwaka wa kuwasaidia wachimbajiwadogo kwa nguvu zote ili wajikwamue kiuchumi na hivyo ku-changia pato la Taifa.

    Aidha mwaka huu ni wakati wa kuutumia kikamilifu uchumiwa gesi kwa kutumia fursa zote zinatokana na uchumi huo. Kupi-tia uchumi wa gesi, nchi yetu itatoka hapa ilipo kiuchumi Duniani.Hasa ikizingatiwa kuwa bomba la gesi litaanza kusafirisha gesihiyo ili kutumika katika shughuli mbalimbali ikiwemo kuzalishaumeme.

    Mwaka 2015 uwe pia kwa ajili ya kuipa kipaumbele nishatijadidifu. Maendeleo ya nishati itokanayo na mionzi ya jua, upepo,tungamotaka na jotoardhi yatachochea maendeleo ya sekta zauzalishaji na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.

    Tuungane pamoja kuufanya mwaka 2015 kuwa wa mafani-

    kio makubwa zaidi. Heri ya mwaka mpya!

    Na Mwandishi Wetu

    Wizara yaNishati naM a d i n iimeshindaTuzo ya Ki-

    mataifa ya mwaka ya maende-leo ya udhibiti wa sekta ndogoya mafuta na gesi.

    Tuzo hiyo inayotolewa

    na Kampuni ya Kimataifaya Wildcat International,ya nchini Marekani kupitiamachapisho yake maarufuDuniani ya The Oil & GasYear (TO&GY), itakabidhiwarasmi mwezi Februari mwaka2015 jijini Dar es Salaam.

    Kwa mujibu wa Jarida laTO&GY, Wizara imeshindatuzo hiyo kutokana na mafan-ikio yake katika kushughulikiachangamoto za udhibiti katikasekta ndogo ya mafuta na gesina hivyo kuchochea maende-leo ya sekta hiyo.

    Mafanikio hayo ni pamojana kuwa na sera mpya ya gesi

    asilia; kuwa na muundo mpyawa makubaliano ya gharamaza utafutaji na uzalishaji wamafuta na gesi (Production-Sharing Agreement); na kuwana Rasimu ya Sera Uweze-shaji na Ushirikishaji Wazawa(local content policy).

    Hayo ni baadhi tu yamaendeleo yaliyofanya sektahii kueleweka zaidi na kuku-balika zaidi kwa wawekezaji

    na wadau vilevile, imesemasehemu ya Jarida la TO&GY.

    Ushindi wa Tuzo hiyoni mwendelezo wa vielelezombalimbali vinavyoonyeshamafanikio makubwa yali-yofikiwa na Wizara katikasekta za Nishati na Madini.

    Mwaka 2014, Wizara piailishika nafasi ya pili kamataasisi ya Serikali inayofanyavizuri zaidi katika utoaji taar-ifa kwa umma nchini.

    Matokeo hayo ni kutokanana Utafiti wa 2014 wa Upati-kanaji Taarifa kutoka taasisi zaserikali uliofanywa na Taasisiya Vyombo vya Habari Kusinimwa Afrika (MISA), Tawi laTanzania (MISA-TAN).

    Utafiti huu hufanywa kilamwaka na MISA katika nchi11 wanachama wa Jumuiyaya Maendeleo Kusini mwaAfrika (SADC).

    Wizara ilishika nafasi yakwanza katika utafiti kamahuo mwaka 2013.

    Pamoja na Tuzo ya Wiz-ara ya T0&GY, Mkurugen-zi Mtendaji wa Shirika la

    Umeme nchini (TANESCO)Mhandisi Felchesmi Mrambanaye ameshinda Tuzo ya Mtuwa Mwaka (Person of theYear) ya machapisho hayo.

    Mhandisi Mrambaameshinda Tuzo hiyo kutoka-na na mipango yake ya Dolaza Kimarekani Bilioni Sitaitakayowezesha TANESCOkuongeza uzalishaji umememara tatu zaidi ya sasa na

    kuondokana na utegemeziwa uzalishaji umeme kwa ku-tumia mafuta.

    Aidha Shirika la Maende-leo ya Petroli nchini (TPDC)limeshinda Tuzo ya Shirika laMpito la Mwaka kutokana nampango wake wa kutokuwamdhibiti pekee wa sekta ndo-go ya mafuta na gesi bali piamwekezaji baada ya kushindatenda na kupata vitalu viwilikwa ajili ya utafiti wa mafuta

    na gesi.Pamoja na Jarida laTO&GY, machapisho men-gine ya TO&GY ni pamoja navitabu, magazeti na majaridambalimbali.

    Usambazaji wa machap-isho hayo unakaguliwa naTaasisi ya Marekani ya BPAWorldwide inayokaguamachapisho maalum zaidi ya2600 katika nchi 30 Dunianiyakiwemo majarida maarufuya Toronto Star, Wall StreetJournal na Gulf News.

    Machapisho hayo yanawasomaji zaidi ya 69,000 ka-tika nchi 81 Duniani ambapo

    asilimia 79 ya wasomaji haoni viongozi waandamizi ka-tika menejimenti ya kampuni,taasisi na mashirika mbalim-bali Duniani.

    Kampuni ya WildcatInternational ni kampuniya kimataifa ya habari in-ayojishughulisha na ku-toa machapisho, kuandaamatukio ya kimataifa, uten-genezaji wa filamu na ushauri

    BODI YA UHARIRI

    MHARIRI MKUU:Badra Masoud MHARIRI : Leonard Mwakalebela

    MSANIFU: Essy OgundeWAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase

    Teresia Mhagama, Mohamed Saif na Nuru Mwasampeta

  • 8/10/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 48

    4/9

    4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Paul Masanja wa pili kuliaakifuatilia ibada ya misa ya mazishi ya Mke wake Marehemu PhildaMasanja. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madinianayeshughulikia Madini Stephen Masele, Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini Eliakim Maswi na watoto wa Kamishna Masanja Patrikna Mary Masanja.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Stephen Maseleakimpa mkono wa pole Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Paul Masanjabaada ya kufiwa na mke wake hivi karibuni na mazishi kufanyika mkoaniShinyanga.

    Habari Ktk Picha

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pilikutoka kuhoto, waliovaa makoti) akizungumza na wananchi wakijiji cha Kitaramaka mkoani Mara ambapo aliwaahidi kuwa umemeunategemewa kuwashwa katika kijiji hicho ifikapo tarehe 15/3/2015.Katika kufanikisha hilo Waziri aliwaagiza watendaji wa Shirika la Umemenchini (TANESCO) kufika kijijini hapo tarehe 10/1/2015 kutoa elimu kwawananchi kuhusu taratibu za ufungaji Umeme.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, EliakimMaswi akisalimiana na baadhi ya watumishiwa Wizara waliohudhiria katika msiba wa Mkewa Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi PaulMasanja mkoani Shinyanga. Anayeongozananaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini,Richard Kasesera.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa nnekutoka kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kitaramakamkoani Mara (hawaonekani pichani ) ambapo aliwaahidi kuwa umemeunategemewa kuwashwa katika kijiji hicho ifikapo tarehe 15/3/2015.Katika kufanikisha hilo Waziri aliwaagiza watendaji wa Shirika laUmeme nchini (TANESCO) kufika kijijini hapo tarehe 10/1/2015 kutoaelimu kwa wananchi kuhusu taratibu za ufungaji Umeme.

    u

    u

  • 8/10/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 48

    5/9

    5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Kikao kazi cha wakaguzi wamigodi kilichofanyika Mwanza

    Pichani ni baadhi ya wakaguzi wa migodi nchini wakifuatilia hotubaya kufunga rasmi kikao kazi cha kuandaa ckecklist ya ukaguzi wamigodi nchini.

    Mmoja wa wakaguzi wa migodi nchini akiwasilisha kazi ya kikundi wakati wakikao kazi cha kuandaa checklist za ukaguzi wa migodi nchini

    Kamishna wa Madini Uratibu John Shija akiongea jambo wakatiwa hotuba ya kufunga kikao kazi cha wakaguzi wa migodinchini kilichoandaa checklist kwa ajili ya shughuli za ukaguzi wamigodi nchini

    Kamishnawa MadinianayeshughulikiaUkaguzi wa MigodiMhandisi AllySamaje akisisitiza

    jambo wakati wakufunga kikaokazi cha kundaa

    checklist zaukaguzi migodikilichohudhuriwana wakaguziwa migodikutoka maeneombalimbali nchini.Anayesikiliza niKamishna MsaidiziUratibu, MhandisiJohn Shija.

    Wakaguzi wa migodi nchini wakijadiliana juu ya namnabora ya kuandaa checklist zitakazotumika katikashughuli za migodi nchini. Baadhi ya wakaguzi wa migodi nchini wakiwa katika kazi ya makundi kuandaa checklist

    zitakazotumika kwa ajili ya shughuli za ukaguzi wa migodi nchini.

    u

  • 8/10/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 48

    6/9

    6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    u

    Maazimio ukaguzi migodikupewa kipaumbele

    Na Asteria Muhozya,Mwanza

    Kamishna wa Madini anayes-hughulikia Ukaguzi waMigodi, Mhandisi Ally Sa-maje ameeleza kuwa, ameya-chukua maazimio yaliyo-

    tolewa na Wakaguzi wa migodi nchinikwa uzito mkubwa kutokana na umuhimuwake katika utekelezaji wa shughuli za mi-

    godi nchini.Mhandisi Samaje aliyasema hayowakati akifunga kikao kazi cha wakaguziwa migodi nchini kilichofanyika hivi ka-ribuni kikilenga kuandaa check list yaukaguzi wa migodi itakayotumiwa katikashughuli hizo.

    Nimeridhishwa na namna kazi yakuandaa checklist ilivyofanyika, nitajita-hidi kuhakikisha maazimio yaliyotolewaleo yanasaidia katika kuleta mabadiliko ka-tika shughuli za ukaguzi migodi pamoja nakubadilishana uzoefu, aliongeza Samaje.

    Aidha, aliwataka wataalamu hao kuan-za kuyafanyia kazi masuala ambayo wame-

    jifunza katika kikao hicho na kuongeza,twende na mtazamo utakaoleta mabadi-liko, masuala haya ni muhimu na yana-

    takiwa kutekelezwa kitaalamualisisitizaKamishna Samaje.Wakati huo huo, Kamishna Msaidizi

    wa Madini, Uratibu Mhandisi John Shija

    akizungumza wakati wa kufunga kikaohicho alieleza kuwa uwepo wa miongozouna mchango mkubwa katika shughuli zaukaguzi migodini kutokana na kwambaitatumika kama nyenzo muhimu za kufan-ya shughuli hizo.

    Kazi imefanyika kwa ustadi ni jambozuri kutengeneza kitu ambacho tukikitumiakinaleta utofauti. Unaweza usikitumie leolakini kesho utakitumia na mchango wakeunakuwa mkubwa, alisema MhandisiShija.

    Naye Mratibu wa kikao hicho,

    Mhandisi Assa Mwakilembe aliwatakawashiriki wa kikao hicho kutumia Sheriana taratibu zilizopo katika sekta ya madinikatika shughuli za ukaguzi jambo ambalolitawaongezea ujuzi na kuwa wataalamuwaliobobea katika shughuli hizo.

    Sisi sote tutanufaika na matokeobaada ya kuandaa checklist hizi. Tukum-buke kuangalia sheria na taratibu zilizopo.Jambo hili litatuongezea nafasi ya kuwawataalamu zaidi kwasababu utaalamuunajengwa na mambo mengi, alisisitizaMhandisi Mwakilembe.

    Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwakatika kikao hicho ni pamoja na uwepo wampango Kabambe endelevu wa ukaguziwa Madini.

    Azimio jingine lililopendekezwa ni

    kuanzishwa kikosi kazi maalum cha wak-aguzi wa migodi na uokoaji wa dharurahuku msisitizo ukilenga kukijengea uwezokikosi hicho.

    Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi Mhandisi Ally Samajeakisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya kufunga kikao kazi cha kuandaa checklist yaukaguzi migodini. Wanaofuatilia pichani ni baadhi ya wakaguzi waliohudhuria kikao hicho

    Kijiji cha Kabasa kupata umeme Machi 2015Na Teresia Mhagama

    Wananchi wa kijiji cha Ka-basa mkoani Mara wamea-hidiwa kupata huduma yaumeme ifikapo tarehe 15Machi 2015.

    Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishatina Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakatialipofika kijijini hapo katika ziara yake ya sikusita katika mkoa wa Mara lengo likiwa ni ku-kagua na kuzindua miradi ya umeme vijijiniawamu ya pili inayosimamiwa na Wakala waNishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana naShirika la Umeme Nchini (TANESCO)

    Waziri Muhongo alitoa ahadi hiyo baadaya baadhi ya wananchi kuwa na hofu ya kupati-wa Umeme huku wengi wao wakiwa wameji-andikisha kwa ajili ya kufungiwa Umeme.

    Pamoja na ahadi hiyo Waziri wa Nishatina Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliwaa-giza watendaji wa Shirika la Umeme nchini(TANESCO) kurudi kijijini hapo kutoa elimuya taratibu za kufunga Umeme ifikapo tarehe12/1/2015 Saa 8:15 mchana.

    Aidha, wananchi hao walielezwa kuwaawamu ya tatu ya mradi wa umeme vijijiniutaanza mwezi Julai, 2015 na vijiji ambavyohavipo kwenye awamu ya pili vitaingizwa kwe-nye awamu ya tatu ya Mradi huo.

    Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo wa kwanza kulia akisikiliza maelezoya mmoja wa wananchi katika kijiji cha Kabasa mkoani Mara wakati alipofika kijijini hapokwa ajili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini Awamu ya Pili.inayosimamiwana Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini(TANESCO).

  • 8/10/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 48

    7/9

    7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Waziri wa Nishati na Madini,

    Profesa Sospeter Muhongo

    (mwenye fulana ya bluu)

    akizungumza na baadhi

    ya watendaji wa kijiji cha

    Kiagata mkoani Mara

    pamoja na maafisa wa

    Shirika la Umeme nchini

    (TANESCO). Waziri wa Nishati

    na Madini amefanya ziara

    ya kikazi mkoani humo ku-

    kagua maendeleo ya miradi

    mbalimbali ya umeme.

    Vijiji ambavyo havijashushiwaumeme kutathminiwa

    Na Teresia Mhagama

    Waziri wa Ni-shati na Madini ,Profesa SospeterMuhongo ame-liagiza Shirika

    la Umeme nchini (TANESCO)pamoja na Wakala wa NishatiVijijini (REA) kufanya tathminiya vijiji vyote ambavyo umemeumepita bila kushushwa katikavijiji hivyo.

    Waziri wa Nishati na Madini

    aliyasema hayo alipokuwa katikakijiji cha Kiagata mkoani Maraakiwa katika ziara ya siku sitakatika mkoa huo. Ziara hiyo ili-lenga katika kukagua na kuzinduamiradi ya umeme vijijini awamu yapili inayosimamiwa na REA kwakushirikiana na TANESCO.

    Agizo hilo la Waziri lime-kuja baada ya wananchi katikakijiji hicho kuonesha wasiwasi namashaka kuwa umeme unawezausishuke kijijini hapo kwani kuna

    baadhi ya vijiji ambavyo nguzo zaumeme zimepita barabarani lakinihavipati nishati hiyo.

    Profesa Muhongo aliwaelezawanakijiji hao kuwa Serikalikupitia Wizara ya Nishati na Ma-dini, imeliona tatizo hilo na tayariimeshaziagiza Taasisi zake za TA-NESCO na REA kufanya tathminiili kutambua vijiji vyote ambavyoumeme umepita lakini wananchi

    hawapati huduma hiyo.Alieleza kuwa lengo kubwa

    la Serikali ni kuhakikisha kuwakila kijiji kilichopitiwa na nguzoza umeme kinapata nishati hiyomuhimu.

    http://www.mem.go.tz

    Na Samwel Mtuwa-Dodoma.

    Wizara yaNishati naMadini kupi-tia Wakalawa Jiolojia

    Tanzania (GST) imefanikiwakukamilisha maandalizi ya ri-poti ya mawe ya nakshi Kandaya Ziwa.

    Kwa mujibu wa Meneja waMawe, Madini na Uchakatajikatika Maabara ya Uchunguziwa Madini GST Bw. BazilMomburi, ripoti hiyo itatoafursa kwa wazawa na wadaumbalimbali kuwekeza katikamadini ya nakshi.

    Bw . Momburi alisema

    kuwa Ugunduzi huo unaonye-sha kuna zaidi ya aina kumi(10)za mawe ya nakshi ambayoni Slate, Sandstone, Granite ,Granodiorite , Diorite , Basalt,Dolerite, Quartzite , Synitena Alaskite katika Kanda yaZiwa.

    Bw. Momburi alifafanuakuwa ugunduzi utatoa hamasana fursa kubwa kwa wadaukuweza kuwekeza katika sektaya mawe ya nakshi, hii ni kuto-kana kuwa mpaka sasa Kandaya Ziwa ina kiwanda kimoja tucha mawe ya nakshi kilichopomkoani Mwanza.

    Bw. Momburi alieleza kuwakuna faida nyingi zitokanazo

    na mawe ya nakshi ambazoni pamoja na kuwa rafiki wamazingira hii ni kutokana nakutokuwa na uharibifu unao-

    fanyika katika uwekezaji namatumizi ya mawe ya nakshina kuongeza kuwa uwekezajihuo hauna gharama sana nahauhitaji teknolojia kubwa yakiwanda.

    Aliongeza kuwa mawe yanakshi hayana madhara ya afyakwa jamii na bidhaa husika yamawe ya nakshi ni endelevu nainadumu kwa muda mrefu.

    Pia alisema kuwa tayaritafiti tatu za aina hiyo zime-fanyika Tanzania zikijumuishaKanda ya Kati katika mikoa yaDodoma, na Singida; Kandaya Magharibi katika mkoa waTabora na Kanda ya Nyandaza juu kusini katika mikoaya Iringa, Mbeya, Rukwa naMpanda.

    Takwimu zinaonyeshakuwa mpaka sasa Tanzania ina

    viwanda sita vya mawe ya nak-shi ambavyo vipo katika mikoaya Mbeya, Morogoro, Pwani,Mwanza na Dodoma.

    Kukamilika kwa ripoti hizini kufuatia agizo la Rais Dk.Jakaya Kikwete alilotoa katikamaonesho ya Wakulima naWafugaji (Nane nane) mwaka2007 mkoani Dodoma lakutaka utafiti juu ya maweya nakshi ufanyike ili kubainikiasi na maeneo yanapopatika-na ili kuwezesha wawekezajikupata taarifa muhimu kablaya kuwekeza katika mawe yanakshi

    GST pia ina mpango wa ku-malizia kukamilisha maandal-

    izi ya ripoti ya mawe ya nakshiKanda ya Mashariki na mikoaya kusini ambayo ni Mtwara,Ruvuma na Lindi.

    GST yakamilisha maandalizi ya ripoti ya mawe ya nakshi Kanda ya Ziwa

    Watalaam wa utafiti wa miamba

    kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania

    (GST) wakisoma ramani kama moja

    ya shughuli za utafiti wa madini

    katika moja ya eneo lililopo katika

    mkoa wa Lindi.

  • 8/10/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 48

    8/9

    8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

    MINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

    Invitation for Bidsfor

    PROPOSED REFURBISHMENT AND EXPANSION OFMTWARA MINE OFFICE BUILDING

    (Bid No. .ME/008/SMMRP/W/11

    1. This Invitation for Bids follows the General Procurement Notice for thisProject which appeared in United Nations Development Business Issueno. 775 dated 31st May 2010.

    2. The Government of the United Republic of Tanzania through the Ministry of Energy and Minerals received funds from the International Development Association (IDA) towards the cost of the SustainableManagement of Minerals Resources Project (SMMRP)and it intendsto apply part of the proceeds of this credit to cover eligible paymentsunder the contract for Proposed Refurbishment and Expansion ofMtwara Mine Ofce Building.

    3. The Ministry of Energy and Minerals now invites sealed bids fromeligible Building Contractors registered or capable of being registered inClass four and above for carrying out the Proposed Refurbishment andExpansion of Mtwara Mine Ofce Building.

    4. Bidding will be conducted through the National Competitive Bidding

    procedures specied in the Public Procurement Act 2011 (Goods, Works,Non Consultancy Service and Disposal of Public Assets by Tender)Regulations, 2011 and is open to all Bidders as dened in theRegulations (2013).

    5. Interested eligible Bidders may obtain further information from and

    inspect the Bidding Documents at the ofce of the Secretary,Ministerial Tender Board; Ministry of Energy and Minerals Plot No:754/33 Samora Avenue; Tanesco Building, Wing B, Room No. 10,P.O.Box 2000 Dar Es Salaam Tanzania. Telephone +255-22-2121606,Facsimile No. +255-22-2123688, e-mail address: [email protected] from0830 to 1530 Hours local time on Mondays to Fridays inclusiveexcept on public holidays.

    6. A complete set of Bidding Document(s) in English and additional setsmay be purchased by interested Bidders on the submission of a writtenapplication to the address given under paragraph 5 above and uponpayment of a non-refundable fee of Tshs. 150,000.00 (TanzaniaShillings One Hundred Fifty Thousand Only). Payment should be by

    Cash or cheque payable to Permanent Secretary, Ministry of Energy andMinerals.

    7. All Bids must be accompanied by a Bid securing Declaration in a formatprovided in the bidding document.

    8. All bids in one original plus two (2) copies, properly lled in, and en

    closed in plain envelopes must be delivered to the address below at orbefore 10.00 hours local time on 12th January 2015. Bids will be openedpromptly thereafter in public and in the presence of Biddersrepresentatives who choose to attend in the opening at The Ministry ofEnergy and Minerals, 5 Samora Machel Avenue, 5th Floor inthe Board Room, P.O. Box 2000, 11474 Dar es Salaam Tanzania.

    9. Late bids, portion of bids, electronic bids, bids not received, bids notopened at the bid opening ceremony shall not be accepted for evaluationirrespective of the circumstances.

    Address:Permanent Secretary,

    Ministry of Energy and Minerals,5 Samora Machel Avenue;

    P.O. Box 2000, 11474 Dar Es Salaam, Tanzania.Telephone: +255 22 2121 606

    Facsimile No.: +255 22 212 3688email: [email protected]

    KATIBU MKUU

    Tangazo

    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

    MINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

    Invitation for Bidsfor

    PROPOSED REFURBISHMENT OF NACHINGWEA ANDTUNDURU MINE OFFICES

    (Bid No. .ME/008/SMMRP/W/10

    1. This Invitation for Bids follows the General Procurement Notice for thisProject which appeared in United Nations Development Business Issueno. 775 dated 31st May 2010.

    2. The Government of the United Republic of Tanzania through theMinistry of Energy and Minerals received funds from the InternationalDevelopment Association (IDA)towards the cost of the SustainableManagement of Minerals Resources Project (SMMRP)and it intendsto apply part of the proceeds of this credit to cover eligible payments

    under the contract for Proposed Refurbishment of Nachingwea andTunduru Mine Ofces.

    3. The Ministry of Energy and Minerals now invites sealed bids fromeligible Building Contractors registered or capable of being registeredin Class ve and above for carrying out the Proposed Refurbishment ofNachingwea and Tunduru Mine Ofces.

    4. Bidding will be conducted through the National Competitive Biddingprocedures specied in the Public Procurement Act 2011 (Goods, Works,Non Consultancy Service and Disposal of Public Assets by Tender)

    Regulations, 2011 and is open to all Bidders as dened in the Regulations.

    5. Interested eligible Bidders may obtain further information from andinspect the Bidding Documents at the ofce of the Secretary,Ministerial Tender Board; Ministry of Energy and Minerals Plot No:754/33 Samora Avenue; Tanesco Building, Wing B, Room No. 10,P.O.Box 2000 Dar Es Salaam Tanzania. Telephone +255-22-2121606,Facsimile No. +255-22-2123688, e-mail address: [email protected] from0830 to 1530 Hours local time on Mondays to Fridays inclusive excepton public holidays.

    6. A complete set of Bidding Document(s) in English and additional setsmay be purchased by interested Bidders on the submission of a writtenapplication to the address given under paragraph 5 above and uponpayment of a non-refundable fee of Tshs. 150,000.00 (TanzaniaShillings One Hundred Fifty Thousand Only). Payment should be by

    Cash or cheque payable to Permanent Secretary, Ministry of Energy andMinerals.

    7. All Bids must be accompanied by a Bid securing Declaration in a format

    provided in the bidding document.

    8. All bids in one original plus two (2) copies, properly lled in, andenclosed in plain envelopes must be delivered to the address below ator before 10.00 hours local time on 12th January 2015. Bids will beopened promptly thereafter in public and in the presence of Biddersrepresentatives who choose to attend in the opening at The Ministry ofEnergy and Minerals, 5 Samora Machel Avenue, 5th Floor in theBoard Room, P.O. Box 2000, 11474 Dar es Salaam Tanzania.

    9. Late bids, portion of bids, electronic bids, bids not received, bids notopened at the bid opening ceremony shall not be accepted for evaluationirrespective of the circumstances.

    Address:Permanent Secretary,

    Ministry of Energy and Minerals,5 Samora Machel Avenue;

    P.O. Box 2000, 11474 Dar Es Salaam, Tanzania.Telephone: +255 22 2121 606

    Facsimile No.: +255 22 212 3688email: [email protected]

    LOT DESCRIPTION QTY

    1 Refurbishment of Nachingwea Mine Office 1

    2 Refurbishment of Tunduru Mine Office 1

  • 8/10/2019 JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 48

    9/9

    9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano SerikaliniWasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    UJUMBE WA WAZIRI WIKI HIIUJUMBE WA WAZIRI WIKI HIIWAFANYAKAZI WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, KAMPUNI NA

    TAASISI ZETU TUENDELEE KUCHAPA KAZI KWA UMAKINI, UADILIFU NAUBUNIFU MKUBWA SANA KWA KUSUDIO LA KUFUTA UMASIKINI NCHINIMWETU. TUTASHINDA, TUSIKATISHWE TAMAA.

    Waziri wa Nishati na MadiniProf.Sospeter Muhongo(katikati)akipokewa kwashamrashamra mara

    baada ya kuwasili katikakituo cha ushirika wakutokomeza ukeketaji chaMasanga kilichopo kata yaGoronga Wilayani Tarimemkoani Mara.Wasichanawanaopata mafunzo katikakituo hicho walimpokeaProfesa Muhongo kwamabango kuoneshaombi lao la kuwekewaumeme katika kituo hichoambapo Profesa Muhongoaliwaahidi kuwa umemeutawashwa mwezi Mei,mwaka 2015.

    Kituochakutoamafunzombadalakuhusuukeketajikupatiwaumemebure

    Na Teresia Mhagama

    Waziri wa Nishati na MadiniProf. Sospeter Muhongoametoa ahadi ya kufungiwaumeme bure kwenyekituo cha Ushirika wa

    kutokomeza ukeketaji cha Masanga kilichopowilayani Tarime mkoani Mara kinachohi-fadhi na kutoa elimu kwa wasichana juu yakupinga ukeketaji.

    Waziri Muhongo alitoa ahadi hiyo wakatialipotembelea kituo hicho akiwa katika ziaraya siku sita katika mkoa huo ambayo ililengakukagua na kuzindua miradi ya umeme viji-

    jini awamu ya pili inayosimamiwa na Wakalawa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikianana Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).

    Muhongo alisema kuwa kituo hichoambacho hukusanya wasichana wanaokim-

    bia ukeketaji, hakitalipa gharama zozote za

    kuvutiwa umeme na kwamba TANESCOitawapa umeme bure ili uwasaidie kupatamwanga katika shughuli zao mbalimbalizikiwamo za mafunzo.

    Profesa Muhongo alitoa ahadi ya umemekuwashwa katika kituo hicho ifikapo tarehe15 Mei, 2015 na kuwataka wanafunzi haokuweka bidii katika elimu ili kuondokanana umasikini na kuweka kipaumbele katikamasomo ya sayansi.

    Waziri Muhongo alitumia fursa hiyopia kuwashukuru wamiliki wa kituo hichokinachomilikiwa na kanisa katoliki jimbo laMusoma kwa ubunifu wao wa kuanzishakituo husika ambacho kinasaidia wasichanahao katika kuepuka kukeketwa.

    Wasichana hao walisema kuwa wame-fika kituoni hapo kwa ridhaa ya wazazi waolakini wapo wasichana wengine ambao wapo

    kituoni hapo baada ya kukimbia majumbanikwao wakikwepa kukeketwa kwa kuwa wan-aporudi majumbani wazazi wao huwatengana kutowasomesha.

    Wasichana hao waliiomba serikali kupi-tia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi naWizara ya Katiba na Sheria kuwachukuliahatua Mangariba, Wazee wa Mila na wazaziwanaolazimisha wasichana kukeketwa kwanikitendo hicho kinachochea ongezeko laukeketaji nchini.

    Naye Mkurugenzi wa Kituo hicho SistaBaibika alisema kuwa mafunzo ya elimu yaukeketaji na athari zake hutolewa kila mwakamwezi wa Desemba ambao shughuli za uke-ketaji zinafanyika.

    Wasichana wanaopata mafunzokatika kituo cha ushirika wakutokomeza ukeketaji cha Masangakilichopo kata ya Goronga WilayaniTarime wakimsikiliza Waziri waNishati na Madini Prof.SospeterMuhongo wakati alipotembeleakituo hicho katika ziara yake ya sikusita katika mkoa wa Mara. Ziara yaProfesa Muhongo mkoani humoililenga kukagua na kuzinduamiradi ya umeme vijijini awamuya pili inayosimamiwa na Wakalawa Nishati Vijijini (REA) kwakushirikiana na Shirika la Umemenchini (TANESCO).

    u

    u

    Waziri wa Nishati na Madini Prof.Sospeter Muhongo (wa nne kutoka kushoto) akiwa katikapicha ya pamoja na watendaji mbalimbali kutoka Halmashauri ya wilaya ya Tarime, Shirikala Umeme nchini (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) , pamoja na watendaji katikakituo cha ushirika wa kutokomeza ukeketaji cha Masanga kilichopo kata ya GorongaWilayani Tarime. Profesa Muhongo alitembelea kituo hicho akiwa katika ziara ya sikusita katika mkoa wa Mara ambayo ililenga kukagua na kuzindua miradi ya umeme vijijini

    awamu ya pili inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana naShirika la Umeme nchini (TANESCO).