katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka … · katiba ya jamhuri ya muungano wa...

65
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 _______ YALIYOMO ______ Ibara Kichwa cha Habari UTANGULIZI SURA YA KWANZA JAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA, WATU NA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA SEHEMU YA KWANZA JAMHURI YA MUUNGANO NA WATU 1. Kutangaza Jamhuri ya Muungano. 2. Eneo la Jamhuri ya Muungano. 3. Tangazo la Nchi yenye mfumo wa Vyama Vingi. 4. Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi. 5. Haki ya kupiga kura. SEHEMU YA PILI MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI 6. Ufafanuzi. 7. Matumizi ya Masharti ya Sehemu ya Pili. 1

Upload: others

Post on 19-Feb-2020

3 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA YA MWAKA 1977

_______

YALIYOMO______

Ibara Kichwa cha Habari

UTANGULIZI

SURA YA KWANZA

JAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA,WATU NA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA

SEHEMU YA KWANZAJAMHURI YA MUUNGANO NA WATU

1. Kutangaza Jamhuri ya Muungano.2. Eneo la Jamhuri ya Muungano.3. Tangazo la Nchi yenye mfumo wa Vyama

Vingi.4. Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi.5. Haki ya kupiga kura.

SEHEMU YA PILI

MALENGO MUHIMU NA MISINGI YAMWELEKEO WA SHUGHULI ZA SERIKALI

6. Ufafanuzi.7. Matumizi ya Masharti ya Sehemu ya Pili.

1

Page 2: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

8. Serikali na Watu.9. Ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea.10. Nafasi na mamlaka ya Chama.11. Haki ya kufanya kazi, kupata elimu, na

nyinginezo.

SEHEMU YA TATU

HAKI NA WAJIBU MUHIMU

Haki ya Usawa

12. Usawa wa Binadamu.13. Usawa mbele ya sheria.

Haki ya Kuishi

14. Haki ya kuwa hai.15. Haki ya uhuru wa mtu binafsi.16. Haki ya faragha na ya usalama wa mtu.17. Uhuru wa mtu kwenda atakako.

Haki ya Uhuru wa Mawazo

18. Uhuru wa maoni.19. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo.20. Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine.21. Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.

Haki ya Kufanya Kazi

22. Haki ya kufanya kazi.23. Haki ya kupata ujira wa haki.

2

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 3: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

24. Haki ya kumiliki mali.

Wajibu kwa Jamii

25. Wajibu wa kushiriki kazini.26. Wajibu wa kutii sheria za nchi.27. Kulinda mali ya Umma.28. Ulinzi wa Taifa.

Masharti ya Jumla

29. Haki na wajibu muhimu.30. Mipaka kwa haki, uhuru na hifadhi kwa haki

na wajibu.

Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi

31. Ukiukaji wa Haki na uhuru.32. Madaraka ya kutangaza hali ya hatari.

SURA YA PILI

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA

RAIS

33. Rais wa Jamhuri ya Muungano.34. Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka

yake.35. Utekelezaji wa shughuli za Serikali.36. Mamlaka ya kuanzisha na kuwateua watu

wa kushika nafasi za madaraka.

3

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 4: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais.38. Uchaguzi wa Rais.39. Sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais.40. Haki ya kuchaguliwa tena.41. Utaratibu wa uchaguzi wa Rais.42. Wakati na muda wa kushika madaraka ya

Rais.43. Masharti ya kazi ya Rais.44. Madaraka ya kutangaza vita.45. Uwezo wa kutoa msamaha.46. Kinga dhidi ya mashtaka na madai.46A Bunge laweza kumshtaki Rais.46B Wajibu wa Viongozi Wakuu wa Vyombo vya

Mamlaka ya Utendaji kudumisha Muungano.

SEHEMU YA PILI

MAKAMU WA RAIS

47. Makamu mmoja wa Rais, kazi na mamlakayake.

48. Wakati wa Makamu wa Rais kushikamadaraka.

49. Kiapo cha Makamu wa Rais kushikamadaraka.

50. Muda wa Makamu wa Rais kushika Madaraka.

SEHEMU YA TATU

WAZIRI MKUU, BARAZA LA MAWAZIRI NA SERIKALI

51. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.52. Kazi na Mamlaka ya Waziri Mkuu.

4

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 5: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

53. Uwajibikaji wa Serikali.

Baraza la Mawaziri na Serikali

53A. Kura ya kutokuwa na imani.54. Baraza la Mawaziri.55. Uteuzi wa Mawaziri.56. Kiapo cha Mawaziri na Naibu Mawaziri.57. Wakati na muda wa Mawaziri kushika

madaraka.58. Masharti ya kazi ya Mawaziri.59. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri

ya Muungano.59A. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.59B. Mkurugenzi wa Mashtaka.60. Katibu wa Baraza la Mawaziri.61. Wakuu wa Mikoa.

SURA YA TATU

BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA

BUNGE

62. Bunge.63. Madaraka ya Bunge.64. Madaraka ya kutunga Sheria.65. Muda wa Bunge.

5

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 6: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

SEHEMU YA PILI

WABUNGE, WILAYA ZA UCHAGUZI NA UCHAGUZI WA WABUNGE

66. Wabunge.67. Sifa za mtu kuwa Mbunge.68. Kiapo cha Wabunge.69. Tamko rasmi la Wabunge kuhusu maadili ya

Viongozi.70. Wabunge kutoa taarifa ya mali.71. Muda wa Wabunge kushika madaraka.72. Watu wenye madaraka Serikalini kukoma

utumishi wanapochaguliwa.73. Masharti ya kazi ya Wabunge.74. Tume ya Uchaguzi.75. Majimbo ya Uchaguzi.

Uchaguzi na Uteuzi wa Wabunge

76. Uchaguzi katika Majimbo ya Uchaguzi.77. Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge wa

Majimbo ya Uchaguzi.78. Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge

Wanawake.79. Utaratibu wa uchaguzi wa Wabunge wa

kuchaguliwa na Baraza la Wawakilishi.80. Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge wa

Taifa waliopendekezwa na Jumuiya zaWananchi.

81. Utaratibu wa kupendekeza majina yawagombea Uchaguzi wa WabungeWanawake.

82. Wabunge wa kuteuliwa na Rais.

6

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 7: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

83. Uamuzi wa suala kama mtu ni Mbunge.

SEHEMU YA TATU

UTARATIBU, MADARAKA NA HAKI ZA BUNGE

Spika na Naibu wa Spika

84. Spika na Mamlaka yake.85. Naibu wa Spika.86. Utaratibu wa kumchagua Spika na Naibu wa

Spika.

Ofisi ya Bunge

87. Katibu wa Bunge.88. Sekretarieti ya Bunge.

Utaratibu wa shughuli Bungeni

89. Kanuni za Kudumu za Bunge.90. Kuitishwa kwa mikutano ya Bunge na

kuvunjwa kwa Bunge.91. Rais aweza kulihutubia Bunge.92. Mikutano ya Bunge.93. Uongozi wa vikao vya Bunge.94. Akidi ya vikao vya Bunge.95. Viti vilivyo wazi katika Bunge.96. Kamati za Bunge.

Utaratibu wa Kutunga Sheria

97. Namna ya kutumia madaraka ya kutungasheria.

7

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 8: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

98. Utaratibu wa kubadilisha Katiba hii na baadhiya sheria.

99. Utaratibu wa kutunga Sheria kuhusu mamboya fedha.

Madaraka na Haki za Bunge

100. Uhuru wa majadiliano na utaratibu washughuli.

101. Kuhifadhi na kutilia nguvu uhuru wamajadiliano na wa shughuli.

SURA YA NNE

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, BARAZALA MAPINDUZI LA ZANZIBAR NA BARAZA

LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR

SEHEMU YA KWANZA

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA RAIS WA ZANZIBAR

102. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlakayake.

103. Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar na Mamlaka yake.

104. Uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar.

8

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 9: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

SEHEMU YA PILI

BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR

105. Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Kazi zake.

SEHEMU YA TATU

BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR

106. Baraza la Wawakilishi la Zanzibar namadaraka ya kutunga Sheria za Zanzibar.

107. Madaraka ya Baraza la Wawakilishi.

SURA YA TANO

UTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO,MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO, TUME

YA KUAJIRI YA MAHAKAMA YA TANZANIA BARA,MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR, MAHAKAMA YA

RUFANI YA JAMHURI YA MUUNGANO NAMAHAKAMA MAALUM YA KATIBA YA

JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA

UTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO

107A. Mamlaka ya Utoaji Haki.107B. Uhuru wa Mahakama.

9

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 10: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

SEHEMU YA PILI

MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO

108. Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano naMamlaka yake.

109. Majaji wa Mahakama Kuu na uteuzi wao.110. Muda wa Majaji wa Mahakama Kuu kushika

madaraka.110A. Utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji

wa Mahakama Kuu.111. Kiapo cha Majaji.

SEHEMU YA TATUTUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA

112. Tume ya Utumishi wa Mahakama.113. Majukumu na madaraka ya Tume.113A. Uanachama katika Vyama vya Siasa.

SEHEMU YA NNE

MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR

114. Mahakama Kuu ya Zanzibar.115. Mamlaka ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.

SEHEMU YA TANO

MAHAKAMA YA RUFANI YA JAMHURI YA MUUNGANO

116. Tafsiri.117. Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya

Muungano na Mamlaka yake.

10

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 11: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

118. Jaji Mkuu Majaji wa Mahakama ya Rufani nauteuzi wao.

119. Mamlaka ya Majaji wa Mahakama ya Rufani.120. Muda wa utumishi wa Majaji wa Rufani.120A. Utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji

wa Rufani.121. Kiapo cha Majaji wa Mahakama ya Rufani.122. Akidi ya vikao vya Mahakama ya Rufani.123. Mashauri yanayoweza kuamuliwa na Jaji

mmoja wa Mahakama ya Rufani.

SEHEMU YA SITA

UTARATIBU WA KUPELEKA HATI NA KUTEKELEZA MAAGIZOYALIYOMO KATIKA HATI ZILIZOTOLEWA NA MAHAKAMA

124. Utekelezaji wa maagizo ya Mahakamautafanywa nchini Tanzania kote.

SEHEMU YA SABA

MAHAKAMA MAALUM YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO

125. Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano.

126. Mamlaka ya Mahakama Maalum ya Katiba.127. Muundo wa Mahakama Maalum ya Katiba.128. Utaratibu katika vikao vya Mahakama Maalum

ya Katiba.

11

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 12: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

SURA YA SITA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORANA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

SEHEMU YA KWANZA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

129. Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora.130. Majukumu ya Tume na Taratibu za Utekelezaji.131. Mamlaka ya Tume na utaratibu wa shughuli

zake.

SEHEMU YA PILISEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

132. Sekretarieti ya Maadili.

SURA YA SABA

MASHARTI KUHUSU FEDHA ZAJAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA

MCHANGO NA MGAWANYO WA MAPATO YA JAMHURIYA MUUNGANO

133. Akaunti ya Fedha ya Pamoja.134. Tume ya Pamoja ya Fedha.

12

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 13: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

SEHEMU YA PILI

MFUKO MKUU WA HAZINA NA FEDHAZA JAMHURI YA MUUNGANO

135. Mfuko Mkuu wa Hazina yaSerikali ya Jamhuri yaMuungano.

136. Masharti ya kutoa fedha zamatumizi kutoka Mfuko Mkuu waHazina ya Serikali.

137. Utaratibu wa kuidhinishamatumizi ya fedha zilizomokatika Mfuko Mkuu wa Hazinaya Serikali.

138. Masharti ya kutoza kodi.139. Utaratibu wa kuidhinisha

matumizi ya fedha kabla yaSheria ya matumizi kuanzakutumika.

140. Mfuko wa Matumizi ya dharura.141. Deni la Taifa.142. Mishahara ya watumishi fulani

wa Serikali kudhaminiwa naMfuko Mkuu wa Hazina yaSerikali.

143. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu naHesabu za Serikali wa Jamhuriya Muungano.

144. Kumwondoa kazini Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu.

13

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 14: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

SURA YA NANE

MADARAKA YA UMMA

145. Serikali za Mitaa.146. Kazi za Serikali za Mitaa.

SURA YA TISA

MAJESHI YA ULINZI

147. Marufuku kuunda majeshi ya ulinzi yasiyomajeshi ya ulinzi ya Umma.

148. Madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu.

SURA YA KUMI

MENGINEYO

149. Maelezo ya mambo yanayohusika namadaraka ya kazi mbalimbali zilizoanzishwana Katiba hii.

150. Maelezo kuhusu utaratibu wa kukabidhimadaraka ya kazi katika Utumishi wa Serikali.

151. Ufafanuzi.152. Jina kamili la Katiba, tarehe ya kuanza

kutumika na matumizi ya Katiba hii.

NYONGEZA YA KWANZA

[Mambo ya Muungano]

14

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 15: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

NYONGEZA YA PILI

ORODHA YA KWANZA

(Sheria ambazo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono natheluthi

mbili ya Wabunge wote)

ORODHA YA PILI

(Mambo ambayo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono natheluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na

theluthi mbili ya Wabunge kutoka Tanzania Visiwani)

15

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 16: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA YA MWAKA 1977

[26 Aprili, 1977]*Sura ya 500; [Toleo la 1965.]*Sura ya 598; [Toleo la 1965.]Sheria Na-14 ya 1979;1 na 28 za 1980;21 ya 1982;15 ya 1984;14 na 16 za 1990;4 na 20 za 1992;7 ya 1993;7 na 34 za 1994;12 ya 1995;3 ya 2000;1 ya 2005;*T.S Na.133 ya 2001T. S. Na.150 ya 2005

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

16

Page 17: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

UTANGULIZIMISINGI YA KATIBA

KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwadhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatiamisingi ya uhuru, haki, udugu na amani:

NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tukutekelezwa katika jamii yenye demokrasia, ambayoSerikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbewaliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, napia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibuwa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote,na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamuzinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtuunatekelezwa kwa uaminifu:

KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE

MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, kwa niabaya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kamahiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzaniainaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi yademokrasia, ujamaa na isiyokua na dini._________________________________________________* Sura zilizofanyiwa urekebu mwaka, 1965.* T. S. Na. ina maana ya Tangazo la Serikali Namba.

Sheria ya1984 na.15ib.32005 Na. 1ib. 3

17

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 18: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

SURA YA KWANZA

JAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYASIASA,WATU NA SIASA YA UJAMAA NA

KUJITEGEMEA

SEHEMU YA KWANZA

JAMHURI YA MUUNGANO NA WATU

1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri yaMuungano.

2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneolote la Tanzania Bara na eneo lote la TanzaniaZanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahariambayo Tanzania inapakana nayo.

(2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli zaSerikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar, Rais aweza kuigawaJamhuri ya Muungano katika mikoa, wilaya namaeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibuuliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheriailiyotungwa na Bunge.

Sheria ya1984 na.15ib.5

KutangazaJamhuri yaMuunganoya 1984Na.15 ib.6

Eneo laJamhuri yaMuunganoSheria ya1984 Na.15ib.6

Sheria ya1992 Na.4ib.4

18

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 19: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanzana Rais wa Zanzibar kabla ya kuigawa TanzaniaZanzibar katika mikoa, wilaya au maeneo mengineyo.

3.-(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi yakidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenyekufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.

(2) Mambo yote yahusuyo uandikishaji nauendeshaji wa vyama vya siasa nchiniyatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hiina ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo.

4.-(1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katikaJamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwana vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji,vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoajihaki, na pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutungasheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli zaumma.

(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendajivitakuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano naSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; vyombo vyenyemamlaka ya kutekeleza utoaji haki vitakuwa niMahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano naMahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, navyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria nakusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwani Bunge na Baraza la Wawakilishi.

19

Tangazola Nchiyenyemfumo waVyamaVingiSheria ya1992Na.4 ib.5Sheria ya2005Na.1 ib.4

UtekelezajiwashughulizaMamlakaya NchiSheria ya1984na.15ib.6Sheriaya 2005Na.1 ib.25

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 20: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli zaumma katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili yamgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo bainaya vyombo vilivyotajwa katika ibara hii, kutakuwana Mambo ya Muungano kama yalivyoorodheshwakatika Nyongeza ya Kwanza iliyoko mwishoni mwaKatiba hii, na pia kutakuwa na mambo yasiyo yaMuungano, ambayo ni mambo mengine yote yasiyoMambo ya Muungano.

(4) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hiikitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwakufuata masharti mengine yaliyomo katika Katiba hii.

5.-(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umriwa miaka kumi na minane anayo haki ya kupiga kurakatika uchaguzi unaofanywa Tanzania na wananchi.Na haki hii itatumiwa kwa kufuata masharti ya ibarandogo ya (2) pamoja na masharti mengineyo yaKatiba hii na ya Sheria inayotumika nchini Tanzaniakuhusu mambo ya uchaguzi.

(2) Bunge laweza kutunga sheria na kuwekamasharti yanayoweza kuzuia raia asitumie haki yakupiga kura kutokana na yoyote kati ya sababuzifuatazo, yaani raia huyo -

(a) kuwa na uraia wa nchi nyingine;

(b) kuwa na ugonjwa wa akili;

(c) kutiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai;

20

Haki yakupigakura Sheriaya 1984na.15 ib.6Sheria ya2000 Na.3ib.4

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 21: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(d) kukosa au kushindwa kuthibitisha au kutoakitambulisho cha umri, uraia au uandikishwajikama mpiga kura,mbali na sababu hizo hakuna sababu nyingineyoyote inayoweza kumzuia raia asitumie hakiya kupiga kura.

(3) Bunge litatunga Sheria ya Uchaguzi na kuwekamasharti kuhusu mambo yafuatayo -

(a) kuanzisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,na kuweka utaratibu wa kurekebishayaliyomo katika Daftari hilo;

(b) kutaja sehemu na nyakati za kuandikishawapiga kura na kupiga kura;

(c) utaratibu wa kumwezesha mpiga kuraaliyejiandikisha sehemu moja kupiga kurasehemu nyingine na kutaja masharti yautekelezaji wa utaratibu huo;

(d) kutaja kazi na shughuli za Tume ya Uchaguzina utaratibu wa kila uchaguzi ambaoutaendeshwa chini ya uongozi na usimamiziwa Tume ya Uchaguzi.

21

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 22: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

SEHEMU YA PILI

MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEOWA SHUGHULIZA SERIKALI

6. Katika Sehemu hii ya Sura hii, isipokuwakama maelezo yahitaji vinginevyo,neno “Serikali”maana yake ni pamoja na Serikali ya Jamhuri yaMuungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, serikaliza mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka aumamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote.

7.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya(2), Serikali, vyombo vyake vyote na watu wote aumamlaka yoyote yenye kutekeleza madaraka yautawala, madaraka ya kutunga sheria au madarakaya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wakuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yoteya Sehemu hii ya Sura hii.

(2) Masharti ya Sehemu hii ya Sura hiihayatatiliwa nguvu ya kisheria na mahakama yoyote.Mahakama yoyote nchini haitakuwa na uwezo wakuamua juu ya suala kama kutenda au kukosa kutendajambo kwa mtu au mahakama yoyote, au kamasheria, au hukumu yoyote, inaambatana na mashartiya Sehemu hii ya Sura hii.

8.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niNchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki yakijamii, na kwa hiyo –

22

UfafanuziSheria ya1984Na.15ib.6

Matumiziyamashartiya Sehemuya Pili.Sheria ya1984na.15 ib.6

Serikalina WatuSheria ya

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 23: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, naSerikali itapata madaraka na mamlaka yakeyote kutoka kwa wananchi kwa mujibu waKatiba hii;

(b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wawananchi;

(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;

(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikaliyao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

(2) Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano naSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, au wa cho chote katiya vyombo vyake na uendeshaji wa shughuli zakeutatekelezwa kwa kuzingatia umoja wa Jamhuri yaMuungano na haja ya kukuza umoja wa kitaifa nakudumisha heshima ya Taifa.

9. Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi waJamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibarau wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu naamani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa naKujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingiya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katikaJamhuri ya Muungano. Kwa hiyo, Mamlaka ya Nchi navyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera nashughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha -

(a) kwamba utu na haki nyinginezo zote zabinadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;

(b) kwamba sheria za nchi zinalindwa nakutekelezwa;

23

UjenziwaUjamaanaKuji-tegemeaSheriaya 1984Na. 15ib6SheriaNa 4 ya1992in.6

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 24: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(c) kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwanjia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri waTaifa unaendelezwa, unahifadhiwa naunatumiwa kwa manufaa ya wananchi wotekwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtumwingine;

(d) kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifayanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu nakwa pamoja;

(e) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanyakazi anafanya kazi, na kazi maana yake nishughuli yoyote ya halali inayompatia mtu rizikiyake;

(f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwana kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazola Dunia kuhusu Haki za Binadamu;

(g) kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vyaumma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote,wake kwa waume, bila ya kujali rangi, kabila,dini au hali ya mtu;

(h) kwamba aina zote za dhuluma,vitisho, ubaguzi,rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewanchini;

(i) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatiliamkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidiyanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondoshaumaskini, ujinga na maradhi;

24

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 25: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(j) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwikwa njia zinazoweza kusababishaulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumikatika mamlaka ya watu wachache binafsi;

(k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuatamisingi ya demokrasi na ujamaa.

10. [Ibara ya 10 ya Katiba imefutwa na SheriaNa.4 ya 1992].

11.-(1) Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibuunaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa hakiya mtu kufanya kazi, haki ya kujipatia elimu na haki yakupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee,maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali nyinginezoza mtu kuwa hajiwezi. Na bila kuathiri haki hizo,Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa kuhakikishakwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake.

(2) Kila mtu anayo haki ya kujielimisha,na kilaraia atakuwa huru kutafuta elimu katika fanianayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana nastahili na uwezo wake.

(3) Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwambawatu wote wanapata fursa sawa na za kutoshakuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundikatika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vyamafunzo.

25

Nafasi namamlakaya ChamaSheria ya1984Na.15 ib.6

Haki yakufanyakazi,kupataelimu nanyinginezoSheria ya1984Na.15 ib.6

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 26: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

SEHEMU YA TATU

HAKI NA WAJIBU MUHIMU

Haki ya Usawa

12-(1) Binadamu wote huzaliwa huru, na woteni sawa.

(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwana kuthaminiwa utu wake.

13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria,na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwana kupata haki sawa mbele ya sheria.

(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwana mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muunganokuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wadhahiri au kwa taathira yake.

(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtuna jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa namahakama na vyombo vinginevyo vya Mamlaka yaNchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu washeria.

(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa namtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka

Usawa wabinadamuSheria ya1984na.15 ib.6

Usawambele yaSheriaSheriaNa.15 ya1984 ib.6

SheriaNa.4 ya1992 ib.8Sheria ya2000 na.3ib.5

Sheria ya1994 na7.Fungu la8[1], [k].

26

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 27: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezajiwa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi.

(5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti yaibara hii neno “kubagua” maana yake ni kutimiza haja,haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwakuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoniyao ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maishakwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywaau kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewavikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu waaina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewafursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima,isipokuwa kwamba neno”kubagua” halitafafanuliwakwa namna ambayo itaizuia Serikali kuchukua hatua zamakusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo mahususikatika jamii.

6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbeleya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaaau zinazozingatia misingi kwamba -

(a) wakati haki na wajibu kwa mtu yeyoteinapohitajika kufanyiwa maamuzi namahakama au chombo kingine chochotekinachohusika, basi mtu huyo atakuwa nahaki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwaukamilifu, na pia haki ya kukata rufani aukupata nafuu nyingine ya kisheria kutokanana maamuzi ya mahakama au chombo hichokinginecho kinachohusika;

(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosala jinai kutendewa kama mtu mwenye kosahilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatiaya kutenda kosa hilo;

27

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 28: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(c) ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa sababuya kitendo chochote ambacho alipokitendahakikuwa ni kosa chini ya sheria, na piakwamba ni marufuku kwa adhabu kutolewaambayo ni kubwa kuliko adhabu iliyokuwapowakati kosa linalohusika lilipotendwa;

(d) kwa ajili ya kuhifadhi haki ya usawa wabinadamu, heshima ya mtu itatunzwa katikashughuli zote zinazohusu upelelezi nauendeshaji wa mambo ya jinai na katikashughuli nyinginezo ambazo mtu anakuwachini ya ulinzi bila uhuru, au katika kuhakikishautekelezaji wa adhabu;

(e) ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwakinyama au kupewa adhabu zinazomtwezaau kumdhalilisha.

Haki ya Kuishi

14. Kila mtu anayo Haki ya Kuishi na kupata kutokakatika jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu washeria.

15.-(1) Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishikama mtu huru.

(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtukuwa huru na kuishi kwa uhuru, itakuwa ni marufukukwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa,kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu aukunyang’anywa uhuru wake vinginevyo, isipokuwa tu-

Haki yakuwa haiSheria ya1984Na.15 ib.6

28

Haki yauhuruwa mtubinafsiSheriaya 1984Na.15ib.6

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 29: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(a) katika hali na kwa kufuata utaratibu uliowekwana sheria; au

(b) katika kutekeleza hukumu, amri au adhabuiliyotolewa na mahakama kutokana na shauriau na mtu kutiwa hatiani kwa kosa la jinai.

16.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupatahifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familiayake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi yamaskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.

(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwamujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibuwa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki yamtu ya faragha na ya usalama wa nafsi yake, mali yakena maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiriibara hii.

17.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayohaki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano nakuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi nakuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama aukufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.

(2) Kitendo chochote cha halali au sheria yoyoteyenye madhumuni ya -

(a) kupunguza uhuru wa mtu kwenda atakako nakumweka chini ya ulinzi au kifungoni; au

(b) kuweka mipaka kwa matumizi ya uhuru wamtu kwenda anakotaka ili -

Haki yafaraghanausalamawa mtuSheriaya 1984Na.15ib.6

Uhuruwa mtukwendaatakakoSheriaya 1984Na.15 ib.6

29

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 30: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(i) kutekeleza hukumu au amri ya mahakama;au

(ii) kumlazimisha mtu kutimiza kwanza wajibuwowote anaotakiwa na sheria nyinginekuutimiza; au

(iii) kulinda manufaa ya umma kwa jumlaau kuhifadhi maslahi fulani mahususi aumaslahi ya sehemu fulani ya umma.kitendo hicho hakitahesabiwa au sheriahiyo haitahesabiwa kuwa ni haramu auni kinyume cha ibara hii.

Haki ya Uhuru wa Mawazo

18. kila mtu-(a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza

fikra zake;

(b) anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoahabari bila ya kujali mipaka ya nchi;

(c) anao uhuru wa kufanya mawasiliano na hakiya kutoingiliwa katika mawasiliano yake; na

(d) anayo haki ya kupewa taarifa wakati wotekuhusu matukio mbalimbali muhimu kwamaisha na shughuli za wananchi na piakuhusu masuala muhimu kwa jamii.

30

UhuruwamaoniSheriaya 2005Na. 1ib. 5

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 31: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

19.- (1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wamawazo, imani na uchaguzi katikamambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtukubadilisha dini au imani yake.

(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada nakueneza dini itakuwa ni huru na jambo lahiari la mtu binafsi, na shughuli nauendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwanje ya shughuli za mamlaka ya nchi.

(3) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika ibara hiiitakuwa chini ya taratibu zilizowekwa nasheria ambazo ni muhimu katika jamii yakidemokrasia kwa ajili ya usalama wajamii, amani katika jamii, maadili ya jamiina umoja wa kitaifa.

(4) Kila palipotajwa neno “dini” katika ibara hiiifahamike kwamba maana yake ni pamojana madhehebu ya dini, na manenomengineyo yanayofanana aukuambatana na neno hilo nayoyatatafsiriwa kwa maana hiyo.

20.- (1) Kila mtu anao uhuru wa kukutana na watuwengine kwa hiari yake na kwa amani,kuchanganyika, kushirikiana na watuwengine, na kwa ajili hiyo kutoa mawazoyake hadharani na kuanzisha na kujiungana vyama au mashirika yaliyoanzishwakwa madhumuni ya kuhifadhi aukuendeleza imani au maslahi yake aumaslahi mengineyo.

31

Uhuruwa mtukuaminidiniatakayoSheriaya 1984Na. 15ib.6Sheria1992Na. 4ib.9Sheriaya 2005Na. 1ib.6

Uhuru wamtukushiri-kiana nawengineSheria ya1984 Na.15 ib.6Sheria ya2005 Na.1 ib.7

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 32: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) naya (4), haitakuwa halali kwa chama chochotecha siasa kuandikishwa ambacho kutokanana katiba au sera yake

(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-

(i) imani au kundi lolote la dini;(ii) kundi lolote la kikabila, mahali watu

watokeapo, rangi au jinsia;(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya

Jamhuri ya Muungano;(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya

Muungano;(c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu

au mapambano kama njia za kufikiamalengo yake ya kisiasa;

(d) kinapigania au kinakusudia kuendeshashughuli zake za kisiasa katika sehemumoja tu ya Jamhuri ya Muungano;

(e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwakwa vipindi na kwa njia za kidemokrasia.

(3) Bunge laweza kutunga sheria inayowekamasharti yatakayohakikisha kuwa vyama vyasiasa vinazingatia mipaka na vigezovilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya(2) kuhusu uhuru na haki ya watu kushirikianana kujumuika.

(4) itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyotekulazimishwa kujiunga na chama chochote aushirika lolote au kwa chama chochote cha siasakukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadiau falsafa ya chama hicho.

32

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 33: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

21.- (1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 39, ya47 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria zanchi kuhusiana na masharti ya kuchaguana kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwakushiriki katika shughuli za utawala wa nchi,kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo hakiya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi,ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishiwaliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao,kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheriaau kwa mujibu wa sheria.

(2) Kila raia anayo haki na uhuru wa kushirikikwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu yamambo yanayomhusu yeye, maisha yake auyanayolihusu Taifa.

Haki ya Kufanya Kazi

22.- (1) Kila Mtu anayo haki ya kufanya kazi.

(2) Kila raia anastahili fursa na haki sawa,kwa masharti ya usawa, ya kushika nafasiyoyote ya kazi na shughuli yoyote iliyo chini yaMamlaka ya Nchi.

23.- (1) Kila Mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa ainayoyote, anayo haki ya kupata ujiraunaolingana na kazi yake, na watu wotewanaofanya kazi kulingana na uwezowao watapata malipo kulingana na kiasina sifa za kazi wanazozifanya.

33

UhuruwakushirikishughulizaummaSheriaya 1984Na. 15ib.6Sheriaya 1994Na. 34ib. 4

Haki yakufanyakaziSheriaya 1984Na. 15ib. 6

Haki yakupataujira wahakiSheriaya 1984Na. 15ib. 6

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 34: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(2) Kila Mtu anayefanya kazi anastahili kupatamalipo ya haki.

24.- (1) Kila Mtu anayo haki ya kumiliki mali, nahaki ya hifadhi ya mali yake aliyonayokwa mujibu wa sheria.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogoya (1), ni marufuku kwa mtu yeyotekunyang’anywa mali yake kwamadhumuni ya kuitaifisha au madhumunimengineyo bila ya idhini ya sheria ambayoinaweka masharti ya kutoa fidiainayostahili.

Wajibu wa Jamii

25.- (1) Kazi pekee ndiyo huzaa utajiri wa malikatika jamii, ndilo chimbuko la ustawi waWananchi na kipimo cha Utu. Na kila Mtuanao wajibu wa –

(a)kushiriki kwa kujituma na kwa uaminifukatika kazi halali na ya uzalishaji mali; na

(b)kutimiza nidhamu ya kazi na kujitahidikufikia malengo ya uzalishaji mali yabinafsi na yale malengo ya pamojayanayotakiwa au yaliyowekwa nasheria.

(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya(1), hakutakuwapo na kazi ya shurutikatika Jamhuri ya Muungano.

34

Haki yakumilikimaliSheriaya 1984Na. 15ib. 6Sheriaya 2005Na. 1ib. 9

WajibuwakushirikikaziniSheriaya 1984Na. 15ib. 6Sheriaya 1994Na. 7Fungula 8(1),(k)

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 35: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(3) Kwa madhumuni ya ibara hii, na katikaKatiba hii kwa jumla, ifahamike kwambakazi yoyote haitahesabiwa kuwa nikazi ya shuruti au kazi ya kikatili au yakutweza endapo kazi hiyo, kwamujibu wa sheria ni -

(a) kazi inayobidi ifanywe kutokanana hukumu au amri ya mahakama;

(b) kazi inayobidi ifanywe na askari wajeshi lolote katika kutekelezamajukumu yao;

(c) kazi ambayo mtu yeyote inabidiaifanye kutokana na kuwapo hali yahatari au baa lolote linalotishia uhaiwa ustawi wa jamii;

(d) kazi au huduma yoyote ambayo nisehemu ya –(i) majukumu ya kawaida ya

kuhakikisha ustawi wa jamii;(ii) ujenzi wa taifa wa lazima kwa

mujibu wa sheria;(iii) jitihada za taifa za kutumia

uwezo wa kila mtu kufanyakazi kwa ajili ya kuimarishajamii na uchumi wa taifa nakuhakikisha maendeleo natija ya kitaifa.

26.- (1) Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kuitiiKatiba hii na sheria za Jamhuri yaMuungano.

(2) Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu

35

Wajibuwa kutiisheriaza nchiSheriaya 1984Na. 15ib. 6

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 36: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

uliowekwa na sheria, kuchukua hatua zakisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba nasheria za nchi.

27.- (1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asiliaya Jamhuri ya Muungano, mali yaMamlaka ya Nchi na mali yoteinayomilikiwa kwa pamoja na wananchi,na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.

(2) Watu wote watatakiwa na sheriakutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchina ya pamoja, kupiga vita aina zote zauharibifu na ubadhilifu, na kuendeshauchumi wa taifa kwa makini kama watuambao ndio waamuzi wa hali ya baadayeya taifa lao.

28.- (1) Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhina kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi naumoja wa taifa.

(2) Bunge laweza kutunga sheria zinazofaakwa ajili ya kuwawezesha wananchikutumikia katika majeshi na katika ulinziwa taifa.

(3) Mtu yeyote hatakuwa na haki ya kutiasahihi kwenye mkataba wa kukubalikushindwa vita na kulitoa taifa kwamshindi, wala kuridhia au kutambuakitendo cha uvamizi au mgawanyiko waJamhuri ya Muungano au wa sehemu

36

UlinziwaTaifaSheriaya 1984Na. 15ib. 6

Kulindamali yaummaSheriaya 1984Na. 15ib. 6

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 37: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

yoyote ya ardhi ya eneo la taifa na bilaya kuathiri Katiba hii na sheriazilizowekwa, hakuna mtu atakayekuwana haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri yaMuungano kupigana vita dhidi ya aduiyeyote anayeshambulia nchi.

(4) Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheriautakuwa ni kosa la juu kabisa dhidi yaJamhuri ya Muungano.

Masharti ya Jumla

29.- (1) Kila mtu katika Jamhuri ya Muunganoanayo haki ya kufaidi haki za msingi zabinadamu, na matokeo ya kila mtukutekeleza wajibu wake kwa jamii,kama zilivyofafanuliwa katika ibara ya12 hadi ya 28 za sehemu hii ya Sura hiiya Katiba.

(2) Kila mtu katika Jamhuri ya Muunganoanayo haki ya kupata hifadhi sawachini ya sheria za Jamhuri yaMuungano.

(3) Raia yeyote wa Jamhuri ya Muunganohatakuwa na haki, hadhi au cheomaalum kwa misingi ya nasaba, jadi auurithi wake.

(4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoahaki, hadhi au cheo maalum kwa raiayeyote wa Jamhuri ya Muungano kwamsingi ya nasaba, jadi au urithi.

Haki nawajibumuhimuSheriaya 1984Na. 15ib. 6

37

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 38: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki nauhuru vilivyotajwa na Katiba hii kila mtuana wajibu wa kutenda na kuendeshashughuli zake kwa namna ambayohaitaingilia haki na uhuru wa watuwengine au maslahi ya umma.

30.- (1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyomisingi yake imeorodheshwa katikaKatiba hii havitatumiwa na mtu mmojakwa maana ambayo itasababishakuingiliwa kati au kukatizwa kwa hakina uhuru wa watu wengine au maslahiya umma.

(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomokatika Sehemu hii ya Katiba hii,yanayofafanua misingi ya haki, uhuruna wajibu wa binadamu,hayaharamishi sheria yoyoteiliyotungwa wala kuzuia sheria yoyotekutungwa au jambo lolote halalikufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo,kwa ajili ya -

(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuruwa watu wengine au maslahi yaumma haviathiriwi na matumizimabaya ya uhuru na haki za watubinafsi;

(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii,amani katika jamii, maadili ya jamii,afya ya jamii, mipango yamaendeleo ya miji na vijiji,ukuzaji na

38

Mipakakwahaki nauhurunahifadhikwahaki nawajibu.Sheriaya 1984Na. 15ib. 61994Na. 34ib. 6

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 39: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

matumizi ya madini au ukuzaji nauendelezaji wa mali au maslahimengineyo yoyote kwa nia ya kukuzamanufaa ya umma;

(c) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu auamri ya mahakama iliyotolewa katikashauri lolote la madai au la jinai.

(d) kulinda sifa, haki na uhuru wa watuwengine au maisha binafsi ya watuwanohusika katika mashaurimahakamani; kuzuia kutoa habari zasiri; kutunza heshima, mamlaka nauhuru wa mahakama;

(e) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibitiuanzishaji, uendeshaji na shughuli zavyama na mashirika ya watu binafsinchini; au

(f) kuwezesha jambo jingine lolotekufanyika ambalo linastawisha aukuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.

(3) Mtu yeyote anayedai kuwa shartilolote katika Sehemu hii ya Sura hii aukatika sheria yoyote inayohusu hakiyake au wajibu kwake, limevunjwa,linavunjwa au inaelekea litavunjwa namtu yeyote popote katika Jamhuri yaMuungano, anaweza kufungua shaurikatika Mahakama Kuu.

39

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 40: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyoyaliyomo katika Katiba hii, MahakamaKuu itakuwa na mamlaka ya kusikilizakwa mara ya kwanza na kuamuashauri lolote lililoletwa mbele yake kwakufuata ibara hii; na Mamlaka ya Nchiyaweza kuweka sheria kwa ajili ya -

(a) kusimamia utaratibu wa kufunguamashauri kwa mujibu wa ibara hii;

(b) kufafanua uwezo wa Mahakama Kuukatika kusikiliza mashauriyaliyofunguliwa chini ya ibara hii;

(c) kuhakikisha utekelezaji bora wamadaraka ya Mahakama Kuu, hifadhina kutilia nguvu haki, uhuru na wajibukwa mujibu wa Katiba hii.

(5) Endapo katika shauri lolote inadaiwakwamba sheria yoyote iliyotungwa auhatua yoyote iliyochukuliwa na Serikaliau mamlaka nyingine inafuta auinakatiza haki, uhuru na wajibu muhimuzitokanazo na ibara ya 12 hadi 29 zaKatiba hii, na Mahakama Kuu inaridhikakwamba sheria au hatua inayohusika,kwa kiwango inachopingana na Katibani batili au kinyume cha Katiba basiMahakama Kuu ikiona kuwa yafaa auhali au masilahi ya jamii yahitaji hivyo,badala ya kutamka kuwa sheria au

40

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 41: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

hatua hiyo ni batili, itakuwa na uwezowa kuamua kutoa fursa kwa ajili yaSerikali au mamlaka nyingine yoyoteinayohusika kurekebisha hitilafu iliyopokatika sheria inayotuhumiwa au hatuainayohusika katika muda na kwa jinsiitakavyotajwa na Mahakama Kuu, nasheria hiyo au hatua inayohusikaitaendelea kuhesabiwa kuwa ni halalihadi ama marekebishoyatakapofanywa au muda uliowekwana Mahakama Kuu utakapokwisha,mradi muda mfupi zaidi ndio uzingatiwe.

Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi

31.- (1) Mbali na masharti ya ibara ya 30(2),sheria yoyote iliyotungwa na Bungehaitakuwa haramu kwa sababu tukwamba inawezesha hatuakuchukuliwa wakati wa hali ya hatari,au wakati wa hali ya kawaida kwawatu wanaoaminika kuwa wanafanyavitendo vinavyohatarisha au kudhuruusalama wa taifa, ambazo zinakiukamasharti ya ibara ya 14 na ya 15 zaKatiba hii.

(2) Ni marufuku kwa hatua zilizotajwakatika ibara ndogo ya (1) ya ibara hiikuchukuliwa kwa mujibu wa sheriayoyote wakati wa hali ya hatari, auwakati wa hali ya kawaida kwa mtu

41

Ukiukajiwa hakinauhuruSheriaya 1984Na. 15ib. 6

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 42: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

yeyote isipokuwa tu kwa kiasiambacho ni lazima na halali kwa ajili yakushughulikia hali iliyopo wakati wahali ya hatari au wakati wa hali yakawaida kushughulikia haliiliyosababishwa na mwenendo wamtu anayehusika.

(3) Ifahamike kwamba masharti yaliyomokatika ibara hii hayataidhinisha mtukunyang’anywa haki yake ya kuwa haiisipokuwa tu kwa kifo kama matokeoya vitendo vya kivita.

(4) Kwa madhumuni ya ibara hii na ibarazifuatazo za Sehemu hii “wakati wahali ya hatari” maana yake ni kipindichochote ambapo Tangazo la Hali yaHatari, lililotolewa na Rais kwa kutumiauwezo aliopewa katika ibara ya 32,linatumika.

32.- (1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheriailiyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo,Rais aweza kutangaza hali ya hatarikatika Jamhuri ya Muungano au katikasehemu yake yoyote.

(2) Rais aweza tu kutangaza kuwa kunahali ya hatari iwapo -

(a) Jamhuri ya Muungano iko katika vita;au

42

Madarakayakutan-gaza haliya hatariSheriaya 1984Na. 15ib. 6Sheriaya 1992Na. 4 ib.11

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 43: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(b) kuna hatari hasa kwamba Jamhuri yaMuungano inakaribia kuvamiwa aukuingia katika hali ya vita; au

(c) kuna hali halisi ya kuvurugika kwaamani ya jamii au kutoweka kwausalama wa jamii katika Jamhuri yaMuungano au sehemu yake yoyotekiasi kwamba ni lazima kuchukuahatua za pekee ili kurejesha amani nausalama; au

(d) kuna hatari dhahiri na kubwa, kiasikwamba amani ya jamii itavurugika nausalama wa raia kutoweka katikaJamhuri ya Muungano au sehemu yakeyoyote ambayo haiwezi kuepukikaisipokuwa kwa kutumia mamlaka yapekee; au

(e) karibu kutatokea tukio la hatari au tukiola balaa au la baa ya kimazingiraambalo linatishia jamii au sehemu yajamii katika Jamhuri ya Muungano; au

(f) kuna aina nyingineyo ya hatari ambayokwa dhahiri ni tishio kwa nchi.

(3) Endapo inatangazwa kwamba kunahali ya hatari katika Jamhuri yaMuungano nzima au katika TanzaniaBara nzima au katika TanzaniaZanzibar nzima, Rais atatuma maranakala ya tangazo hilo kwa Spika wa

43

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 44: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

Bunge, ambaye baada ya kushaurianana Kiongozi wa shughuli za SerikaliBungeni, ataitisha mkutano wa Bungendani ya siku zisizozidi kumi na nne, ilikuitafakari hali ya mambo na kuamuakupitisha au kutopitisha azimio,litakaloungwa mkono na kura zawajumbe wasiopungua theluthi mbiliya wajumbe wote, la kuunga mkonotangazo la hali ya hatari lililotolewa naRais.

(4) Bunge laweza kutunga sheriainayoweka masharti kuhusu nyakati nautaratibu ambao utawawezesha watufulani wenye kusimamia utekelezaji wamamlaka ya Serikali katika sehemumahususi za Jamhuri ya Muunganokumuomba Rais kutumia madarakaaliyopewa na ibara hii kuhusiana nayoyote kati ya sehemu hizo endapokatika sehemu hizo kunatokea yoyotekati ya hali zilizotajwa katika aya ya(c), (d) na (e) za ibara ndogo ya (2)na hali hiyo haivuki mipaka ya sehemuhizo; na pia kwa ajili ya kufafanuautekelezaji wa mamlaka ya Serikaliwakati wa hali ya hatari.

(5) Tangazo la hali ya hatari lililotolewa naRais kwa mujibu wa ibara hii litakomakutumika -

(a) iwapo litafutwa na Rais;

44

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 45: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(b) endapo zitapita siku kumi na nne tangutangazo lilipotolewa kabla yakupitishwa azimio lililotajwa katikaibara ndogo ya (3);

(c) baada ya kupita muda wa miezi sitatangu tangazo hilo lilipotolewa;isipokuwa kwamba kikao cha Bungechaweza, kabla ya muda wa miezi sitakupita, kuongeza mara kwa maramuda wa tangazo hilo kutumika kwavipindi vya miezi mingine sita kwaazimio litakaloungwa mkono na kura zawajumbe wa kikao hichowasiopungua theluthi mbili yawajumbe wote;

(d) wakati wowote ambapo mkutano waBunge utalitangua tangazo hilo kwaazimio litakaloungwa mkono na kura zawajumbe wasiopungua theluthi mbiliya wajumbe wote.

(6) Kwa madhumuni ya kuondoa mashakajuu ya ufafanuzi au utekelezaji wamasharti ya ibara hii, masharti yasheria iliyotungwa na Bunge na yasheria nyingine yoyote, inayohusuutangazaji wa hali ya hatari kamailivyotajwa katika ibara hii, yatatumikatu katika sehemu ya Jamhuri yaMuungano ambapo hali hiyo ya hatariimetangazwa.

45

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 46: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

46

SURA YA PILI

SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO

SEHEMU YA KWANZA

RAIS

33.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri yaMuungano.

(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongoziwa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

34.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri yaMuungano ambayo itakuwa namamlaka juu ya mambo yote yaMuungano katika Jamhuri yaMuungano, na pia juu ya mambomengine yote yahusuyo TanzaniaBara.

(2) Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano yatahusu utekelezaji nahifadhi ya Katiba hii na pia mambomengineyo yote ambayo Bunge linamamlaka ya kuyatungia sheria.

(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano juu ya mambo yote yaMuungano katika Jamhuri yaMuungano, na pia juu ya mambo

Rais waJamhuriyaMuunganoShria ya1984 Na.15 ib. 9

SerikaliyaJamhuriyaMuunganonaMamlakayakeSheria ya1984 Na.15 ib. 9

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 47: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

mengineyo yote yahusuyo TanzaniaBara, yatakuwa mikononi mwa Raiswa Jamhuri ya Muungano.

(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaKatiba hii, madaraka ya Serikali yaJamhuri ya Muungano yatatekelezwaama na Rais mwenyewe moja kwamoja au kwa kukasimu madaraka hayokwa watu wengine wenye madarakakatika utumishi wa Serikali ya Jamhuriya Muungano.

(5) Ifahamike kwamba masharti yaliyomokatika ibara hii hayatahesabiwakwamba -

(a) yanahamishia kwa Rais madarakayoyote ya kisheria yaliyowekwa nasheria mikononi mwa mtu au mamlakayoyote ambayo si Rais; au

(b) yanalizuia Bunge kukabidhi madarakayoyote ya kisheria mikononi mwa mtuau watu au mamlaka yoyote ambayo siRais.

35.- (1) Shughuli zote za utendaji za Serikali yaJamhuri ya Muungano zitatekelezwana watumishi wa Serikali kwa niabaya Rais.

47

Utekele-zaji washughulizaSerikaliSheriaya 1984Na. 15ib. 9

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 48: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

48

(2) Amri na maagizo mengineyanayotolewa kwa madhumuni yaibara hii yatathibitishwa kwa namnaitakavyoelezwa katika kanunizilizowekwa na Rais, kwa kuzingatiamasharti ya Katiba hii.

36.- (1) Bila ya kuathiri masharti mengineyoyaliyomo katika Katiba hii na ya sherianyingine yoyote, Rais atakuwa namamlaka ya kuanzisha na kufutanafasi za madaraka ya namnambalimbali katika utumishi wa Serikaliya Jamhuri ya Muungano.

(2) Rais atakuwa na madaraka ya kuteuawatu wa kushika nafasi za madarakaya viongozi wanaowajibika kuwekasera za idara na taasisi za Serikali, nawatendaji wakuu wanaowajibikakusimamia utekelezaji wa sera zaidara na taasisi hizo katika utumishi waSerikali ya Jamhuri ya Muungano,nafasi ambazo zimetajwa katika Katibahii au katika sheria mbalimbalizilizotungwa na Bunge kwambazitajazwa kwa uteuzi unaofanywa naRais.

(3) Bila ya kuathiri masharti ya ibarandogo ya (2), masharti mengineyoyaliyomo katika Katiba hii na ya sheriayoyote inayohusika, mamlaka yakuwateua watu wengine wote

Mamlakayakuanzi-asha nakuwat-euawatu wakushikanafasizamada-rakaSheriaya 2000Na. 3 ib.6

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 49: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

wasiokuwa viongozi wala watendajiwakuu, kushika nafasi za madarakakatika utumishi wa Serikali ya Jamhuriya Muungano, na pia mamlaka yakuwapandisha vyeo watu hao,kuwaondoa katika madaraka,kuwafukuza kazi na mamlaka yakudhibiti nidhamu ya watuwaliokabidhiwa madaraka, yatakuwamikononi mwa Tume za Utumishi namamlaka mengineyo yaliyotajwa nakupewa madaraka kuhusu nafasi zamadaraka kwa mujibu wa Katiba hii aukwa mujibu wa sheria yoyoteinayohusika.

(4) Masharti ya ibara ndogo ya (2) na ya(3) hayatahesabiwa kuwa yanamzuiaRais kuchukua hatua za kudhibitinidhamu ya watumishi na utumishikatika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

37.- (1) Mbali na kuzingatia masharti yaliyomokatika Katiba hii, na sheria za Jamhuriya Muungano katika utendaji wa kazina shughuli zake, Rais atakuwa huruna hatalazimika kufuata ushauriatakaopewa na mtu yeyote, isipokuwatu pale anapotakiwa na Katiba hii auna sheria nyingine yoyote kufanyajambo lolote kulingana na ushaurianaopewa na mtu au mamlaka yoyote.

49

Utekele-zaji wakazi nashughuliza Rais.Sheriaya 1984Na. 15ib. 9,Sheriaya 1992Na. 4 ib.12

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 50: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(2) Endapo Baraza la Mawaziri litaona;kuwa Rais hawezi kumudu kazi zakekwa sababu ya maradhi ya mwili auya akili, laweza kuwasilisha kwa JajiMkuu azimio la kumwomba Jaji Mkuuathibitishe kwamba Rais, kwa sababuya maradhi ya mwili au akili, hawezikumudu kazi zake. Baada ya kupokeaazimio kama hilo, Jaji Mkuu atateuaBodi ya utabibu ya watu wasiopunguawatatu atakaowateua kutoka miongonimwa mabingwa wanaotambuliwa nasheria ya matabibu ya Tanzania, naBodi hiyo itachunguza suala hilo nakumshauri Jaji Mkuu ipasavyo, nayeaweza, baada ya kutafakari ushahidiwa kitabibu kuwasilisha kwa Spika hatiya kuthibitisha kwamba Rais, kutokanana maradhi ya mwili au ya akili,hamudu kazi zake; na iwapo Jaji Mkuuhatabatilisha tamko hilo ndani ya sikusaba kutokana na Rais kupata nafuuna kurejea kazini, basi itahesabiwakwamba kiti cha Rais ki wazi, nayaliyomo katika ibara ndogo ya (5)yatatumika.

(3) Endapo Rais atakuwa hayupo katikaJamhuri ya Muungano au atashindwakutekeleza majukumu yake kwasababu nyingine yoyote, kazi nashughuli za Rais zitatekelezwa nammojawapo wa wafuatao kwakufuata mpangilio ufuatao, yaani -

50

Sheriaya 1992Na. 20ib. 4,Sheriaya 1994Na. 34ib. 6,Sheriaya 2005Na. 1ib. 9 T.SNa. 133lamwaka2001 T.SNa. 150lamwaka2005

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 51: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yakeiwazi au kama naye hayupo au nimgonjwa; basi;

(b) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

(4) Endapo Waziri Mkuu ndiye atatekelezakazi na shughuli za Rais kutokana nasababu kwamba Makamu wa Raishayupo basi Waziri Mkuu ataachakutekeleza kazi na shughuli hizoendapo lolote kati ya mambo yafuatayolitatokea mwanzo -

(a) Rais atakaporejea katika Jamhuri yaMuungano au atakapopata nafuukutokana na maradhi na kuanzakutekeleza kazi za Rais;

(b) Makamu wa Rais atakaporejea katikaJamhuri ya Muungano.

(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazikutokana na Rais kufariki dunia,kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguziau kutomudu kazi zake kutokana namaradhi ya mwili au kushindwakutekeleza kazi na shughuli za Rais,basi Makamu wa Rais ataapishwa naatakuwa Rais kwa muda uliobaki katikakipindi cha miaka mitano na kwamasharti yaliyoelezwa katika ibara ya40, kisha baada ya kushauriana nachama cha siasa anachotoka Rais

51

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 52: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

52

atapendekeza jina la mtu atakayekuwaMakamu wa Rais na uteuzi huoutathibitishwa na Bunge kwa kurazisizopungua asilimia hamsini yaWabunge wote.

(6) Ifahamike kwamba kiti cha Raishakitakuwa ki- wazi na Raishatahesabiwa kwamba hayuko katikaJamhuri ya Muungano au hawezikumudu kazi zake endapo -

(a) atakuwa hayupo katika mji ambao ndiomakao makuu ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano;

(b) atakuwa hayupo katika Jamhuri yaMuungano kwa kipindi cha muda wasaa ishirini na nne; au

(c) atakuwa ni mgonjwa lakini anatumainikuwa atapata nafuu baada ya muda simrefu.

(7) Iwapo kutatokea lolote kati ya mamboyaliyotajwa katika ibara ndogo ya (6)na Rais akiona kuwa inafaa kukasimukutoa maagizo kwa maandishi yakumteua yeyote kati ya watuwaliotajwa katika aya ya (a) au ya (b)za ibara ndogo ya (3) ya ibara hii kwaajili ya kutekeleza madaraka ya Raiswakati yeye hayupo au ni mgonjwa,na mtu huyo atakayeteuliwa

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 53: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

atatekeleza madaraka hayo ya Raiskwa kufuata masharti yoyoteyatakayowekwa na Rais; isipokuwakwamba masharti yaliyomo katika ibarahii ndogo yafahamike kuwahayapunguzi wala kuathiri uwezo waRais alionao kwa mujibu wa sherianyingine yoyote wa kukasimumadaraka yake kwa mtu mwingineyeyote.

(8) Rais aweza, akiona inafaa kufanyahivyo, kumwagiza kwa maandishiWaziri yeyote kutekeleza kazi nashughuli zozote za Rais ambazo Raisatazitaja katika maagizo yake na Wazirialiyeagizwa hivyo kwa mujibu wamasharti ya ibara hii ndogo, atakuwana mamlaka ya kutekeleza kazi nashughuli hizo kwa kufuata mashartiyoyote yaliyowekwa na Rais, lakinibila ya kujali masharti ya sherianyingine yoyote; isipokuwa kwamba -

(a) Rais hatakuwa na mamlaka yakukasimu kwa Waziri kwa mujibu wamasharti ya ibara hii ndogo kazi yoyoteya Rais aliyokabidhiwa na sheriayoyote inayotokana na masharti yamkataba wowote uliotiwa sahihi naJamhuri ya Muungano iwapo kisheriaRais haruhusiwi kukasimu kazi hiyokwa mtu mwingine yeyote;

53

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 54: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

54

(b) ifahamike kwamba maagizoyanayotolewa na Rais kwa mujibu wamasharti ya ibara hii ndogo, yakumwagiza Waziri yeyote kutekelezakazi yoyote ya Rais, hayatahesabiwakwamba yanamzuia Rais kutekelezakazi hiyo yeye mwenyewe.

(9) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wamasharti ya ibara hii -

(a) mkutano wa Baraza la Mawaziriuliofanywa kwa ajili ya kuwasilishakwa Jaji Mkuu azimio kuhusu hali yaafya ya Rais utahesabiwa kuwa nimkutano halali hata kama mjumbeyeyote wa Baraza hilo hayupo aukiti chake ki wazi, na itahesabiwakuwa Baraza limepitisha azimio hiloikiwa litaungwa mkono kwa kauli yawajumbe walio wengi waliohudhuriamkutano na kupiga kura;

(b) Rais hatahesabiwa kuwa hayupokatika Jamhuri ya Muungano kwasababu tu ya kupitia nje ya Tanzaniawakati yuko safarini kutoka sehemumoja ya Tanzania kwenda sehemunyingine, au kwa sababu kwambaametoa maagizo kwa mujibu wamasharti ya ibara ndogo ya (7) namaagizo hayo bado hayajabatilishwa.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 55: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

55

(10) Bila ya kujali masharti yaliyoelezwahapo awali katika ibara hii mtuatakayetekeleza kazi na shughuli zaRais kwa mujibu wa ibara hiihatakuwa na mamlaka ya kulivunjaBunge, kumwondoa yeyote kati yaMawaziri katika madaraka yake, aukufuta uteuzi wowote uliofanywa naRais.

(11) Mtu yeyote atakayetekeleza kazi nashughuli za Rais kwa mujibu wamasharti ya ibara hii kama ni Mbungehatapoteza kiti chake katika Bungewala hatapoteza sifa zake zakuchaguliwa kuwa Mbunge kwasababu tu ya kutekeleza kazi nashughuli za Rais kwa mujibu wamasharti ya ibara hii.

38.- (1) Rais atachaguliwa na wananchi kwamujibu wa masharti ya Katiba hii nakwa mujibu wa sheria itakayowekamasharti kuhusu uchaguzi wa Raisambayo itatungwa na Bunge kwakufuata masharti ya Katiba hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaKatiba hii, kiti cha Rais kitakuwa ki-wazi, na uchaguzi wa Rais utafanyikaau nafasi hiyo itajazwa vinginevyokwa mujibu wa Katiba hii, kadriitakavyokuwa, kila mara litokeapololote kati ya mambo yafuatayo:-

Uchaguziwa RaisSheriaya 1979Na. 14ib. 3;Sheriaya 1984Na. 15ib. 9;

Sheriaya 1992Na. 20ib. 5Sheriaya 1994Na. 34ib. 7 T.Sna. 133la 2001

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 56: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

56

(a) baada ya Bunge kuvunjwa;

(b) baada ya Rais kujiuzulu bila ya kuvunjaBunge kwanza;

(c) baada ya Rais kupoteza sifa zakushika nafasi ya madaraka yakuchaguliwa;

(d) baada ya Rais kushtakiwa Bungenikwa mujibu wa Katiba hii nakuondolewa katika madaraka;

(e) baada ya kuthibitishwa kwa mujibuwa masharti ya ibara ya 37 ya Katibahii kwamba Rais hawezi kumudu kazina shughuli zake;

(f) baada ya Rais kufariki.

(3) Kiti cha Rais hakitahesabiwa kuwa ki-wazi kwa sababu tu ya Bungekupitisha hoja ya kutokuwa na imanikwa Waziri Mkuu.

39.- (1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiticha Rais wa Jamhuri ya Muunganoisipokuwa tu kama –

(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri yaMuungano kwa mujibu wa Sheria yaUraia;

(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;

Sifa zamtukucha-guliwakuwaRaisSheriaya 1984Na. 15ib. 9,

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 57: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

57

(c) ni mwanachama, na mgombeaaliyependekezwa na chama cha siasa;

(d) anazo sifa za kumwezesha kuwaMbunge au Mjumbe wa Baraza laWawakilishi;

(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla yaUchaguzi Mkuu hajawahi kutiwahatiani katika Mahakama yoyote kwakosa lolote la kukwepa kulipa kodiyoyote ya Serikali.

(2) Bila ya kuingilia haki na uhuru wa mtukuwa na maoni yake, kuamini diniatakayo, kushirikiana na wengine nakushiriki shughuli za umma kwa mujibuwa sheria za nchi, mtu yeyotehatakuwa na sifa za kuchaguliwakushika kiti cha Rais wa Jamhuri yaMuungano kama si mwanachama namgombea aliyependekezwa na chamacha siasa.

40.- (1) Bila ya kuathiri masharti mengineyoyaliyomo katika ibara hii, mtu yeyoteambaye ni Rais anaweza kuchaguliwatena kushika kiti hicho.

(2) Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi yamara mbili kushika kiti cha Rais.

(3) Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibarhatapoteza sifa za kuweza

Sheriaya 1994Na. 34ib. 8Sheriaya 2000Na. 3 ib.7

Haki yakucha-guliwatenaSheriaya 1984Na. 15ib. 9SheriaNa. 34ya 1994ib. 9

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 58: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuriya Muungano kwa sababu tu kwambaaliwahi kushika madaraka ya Rais waZanzibar.

(4) Endapo Makamu wa Rais anashika kiticha Rais kwa mujibu wa masharti yaibara ya 37(5) kwa kipindikinachopungua miaka mitatuataruhusiwa kugombea nafasi ya Raismara mbili, lakini kama akishika kiti chaRais kwa muda wa miaka mitatu auzaidi ataruhusiwa kugombea nafasi yaRais mara moja tu.

41.- (1) Baada ya Bunge kuvunjwa aukukitokea jambo jingine lolote lililotajwakatika ibara ndogo ya (2) ya ibara ya38 na inalazimu uchaguzi wa Raiskufanyika, kila chama cha siasakinachopenda kushiriki katika uchaguziwa Rais kitawasilisha kwa Tume yaUchaguzi, kwa mujibu wa sheria, jinala mwanachama wake mmojakinayetaka asimame kama mgombeakatika uchaguzi wa Rais wa Jamhuriya Muungano na jina la mwanachamawake mwingine kinayempendekezakwa nafasi ya Makamu wa Rais.

(2) Mapendekezo ya majina ya wagombeakatika uchaguzi wa Raisyatawasilishwa kwa Tume yaUchaguzi katika siku na saa

58

Utaratibuwauchaguziwa RaisSheriaNa. 20ya 1992ib. 5SheriaNa. 34ya 1994ib. 10

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 59: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

itakayotajwa kwa mujibu wa sheriailiyotungwa na Bunge, na mtuhatakuwa amependekezwa kwa halaliisipokuwa tu kama kupendekezwakwake kunaungwa mkono nawananchi wapiga kura kwa idadi nakwa namna itakayotajwa na sheriailiyotungwa na Bunge.

(3) Endapo inapofika saa na sikuiliyotajwa kwa ajili ya kuwasilishamapendekezo ya majina yawagombea, ni mgombea mmoja tuambaye anapendekezwa kwa halali,Tume itawasilisha jina lake kwawananchi, nao watapiga kura yakumkubali au kumkataa kwa mujibu wamasharti ya ibara hii na ya sheriailiyotungwa na Bunge.

(4) Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri yaMuungano utafanywa sikuitakayoteuliwa na Tume ya Uchaguzikwa mujibu wa sheria iliyotungwa naBunge.

(5) Mambo mengine yote yahusuyoutaratibu wa uchaguzi wa Raisyatakuwa kama itakavyofafanuliwakatika sheria iliyotungwa na Bungekwa ajili hiyo.

59

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 60: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Raisatatangazwa kuwa amechaguliwakuwa Rais iwapo tu amepata kuranyingi zaidi kuliko mgombea mwingineyeyote.

(7) Iwapo mgombea ametangazwa naTume ya Uchaguzi kwambaamechaguliwa kuwa Rais kwa mujibuwa ibara hii, basi hakuna mahakamayoyote itakayokuwa na mamlaka yakuchunguza kuchaguliwa kwake.

42.- (1) Rais mteule atashika madaraka ya Raismapema iwezekanavyo baada yakutangazwa kwamba amechaguliwakuwa Rais, lakini kwa hali yoyoteitabidi ashike madaraka kabla ya kupitasiku saba.

(2) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafarikimapema zaidi mtu aliyechaguliwakuwa Rais, bila ya kuathiri mashartiyaliyo katika ibara ndogo ya (3),atashika kiti cha Rais kwa muda wamiaka mitano tangu sikualipochaguliwa kuwa Rais.

(3) Mtu aliyechaguliwa kuwa Raisatashika kiti cha Rais hadi–

(a) siku ambapo mtu atakayemfuatia katikakushika kiti hicho atakula kiapo chaRais; au

60

Wakatinamudawakushikamada-raka yaraisSheriaya 1984Na. 15ib. 9;

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 61: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(b) siku ambapo atafariki dunia akiwakatika madaraka; au

(c) siku atakapojiuzulu; au

(d) atakapoacha kushika kiti cha Raiskwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

(4) Iwapo Jamhuri ya Muungano inapiganavita dhidi ya adui na Rais anaonakuwa haiwezekani kufanya uchaguzi,Bunge laweza mara kwa marakupitisha azimio la kuongeza muda wamiaka mitano uliotajwa katika ibarandogo ya (2) ya ibara hii isipokuwakwamba muda wowoteutakaoongezwa kila mara hautazidimiezi sita.

(5) Kila Rais mteule na kila mtuatakayeshikilia kiti cha Rais, kabla yakushika madaraka ya Rais, ataapambele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri yaMuungano kiapo cha uaminifu na kiapokingine chochote kinachohusika nautendaji wa kazi yakekitakachowekwa kwa mujibu washeria iliyotungwa na Bunge.

61

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 62: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

43.- (1) Rais atalipwa mshahara na malipomengineyo, na atakapostaafu atapokeamalipo ya uzeeni, kiinua mgongo auposho, kadri itakavyoamuliwa na Bunge,na mshahara, malipo hayo mengineyo,malipo ya uzeeni na kiinua mgongohicho, vyote vitatokana na Mfuko Mkuuwa Hazina ya Serikali ya Jamhuri yaMuungano na vitatolewa kwa mujibuwa masharti ya ibara hii.

(2) Mshahara na malipo mengineyo yoteya Rais havitapunguzwa wakati Raisatakapokuwa bado ameshika madarakayake kwa mujibu wa masharti yaKatiba hii.

44.- (1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheriayoyote iliyotungwa na Bunge kwa ajilihiyo, Rais aweza kutangaza kuwapokwa hali ya vita kati ya Jamhuri yaMuungano na nchi yoyote.

(2) Baada ya kutoa tangazo, Raisatapeleka nakala ya tangazo hilo kwaSpika wa Bunge ambaye, baada yakushauriana na Kiongozi wa Shughuliza Serikali Bungeni, ndani ya siku kumina nne kuanzia tarehe ya tangazo,ataitisha mkutano wa Bunge ilikutafakari hali ya mambo na kufikiriakupitisha au kutopitisha azimio lakuunga mkono tangazo la vitalililotolewa na Rais.

62

Mashartiya kaziya RaisSheriaya 1984Na. 15ib. 9

Madarakayakutan-gaza vitaSheriaya 1984Na. 15ib. 9Sheriaya 1992Na. 4 ib.14

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 63: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

45.- (1) Bila ya kuathiri masharti mengineyoyaliyomo katika ibara hii, Rais anawezakutenda lolote kati ya mamboyafuatayo:-

(a) kutoa msamaha kwa mtu yeyotealiyepatikana na hatia mbele yamahakama kwa kosa lolote, na awezakutoa msamaha huo ama bila yamasharti au kwa masharti, kwa mujibuwa sheria;

(b) kumwachilia kabisa au kwa mudamaalum mtu yeyote aliyehukumiwakuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ilimtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyoau asitimize adhabu hiyo wakati wamuda huo maalum;

(c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewamtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabutahafifu;

(d) kufuta adhabu yote au sehemu yaadhabu yoyote aliyopewa mtu yeyotekwa ajili ya kosa lolote au kufutaadhabu yote au sehemu ya adhabu yakutoza, au kuhozi (au kuchukua) kitucha mtu mwenye hatia ambachovinginevyo kingechukuliwa na Serikaliya Jamhuri ya Muungano.

63

Uwezowakutoamsa-mahaSheriaya 1984Na. 15ib. 9

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 64: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

(2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajiliya kuweka utaratibu utakaofuatwa naRais katika utekelezaji wa madarakayake kwa mujibu wa ibara hii.

(3) Masharti ya ibara hii yatatumika kwawatu waliohukumiwa na kuadhibiwaTanzania Zanzibar na kwa adhabuzilizotolewa Tanzania Zanzibar kwamujibu wa sheria iliyotungwa naBunge inayotumika Tanzania Zanzibar,hali kadhalika, masharti hayoyatatumika kwa watu waliohukumiwana kuadhibiwa Tanzania Bara kwamujibu wa sheria.

46.- (1) Wakati wote Rais atakapokuwa badoameshika madaraka yake kwa mujibuwa Katiba hii, itakuwa ni marufukukumshitaki au kuendesha mashatakaya aina yoyote juu yake mahakamanikwa ajili ya kosa lolote la jinai.

(2) Wakati wote Rais atakapokuwa badoameshika madaraka yake kwa mujibuwa Katiba hii, haitaruhusiwa kufunguamahakamani shauri kuhusu jambololote alilolitenda au alilokosa kulitendayeye binafsi kama raia wa kawaidaama kabla au baada ya kushikamadaraka ya Rais, ila tu kama angalausiku thelathini kabla ya shaurikufunguliwa mahakamani, Raisatapewa au atakuwa ametumiwa

64

Kingadhidi yamashtakayamadaiSheriaya 1984Na. 15ib. 9Sheriaya 1992Na. 20ib. 7

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 65: KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA … · Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 37. Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais. 38. Uchaguzi wa Rais. 39. Sifa za

kwanza taarifa ya madai kwamaandishi kwa kufuata utaratibuuliowekwa kwa mujibu wa sheriailiyotungwa na Bunge, na taarifa hiyoikiwa inatoa maelezo kuhusu chanzocha shauri hilo, kiini cha madaiyenyewe, jina lake na anwani yamahali anapoishi huyo mdai na jambohasa analodai.

(3) Isipokuwa kama ataacha kushikamadaraka ya Rais kutokana namasharti ya ibara ya 46A(10), itakuwani marufuku kumshtaki au kufunguamahakamani shauri lolote la jinai au lakumdai mtu aliyekuwa anashikamadaraka ya Rais baada ya kuachamadaraka hayo kutokana na jambololote alilofanya yeye kama Raiswakati alipokuwa bado anashikamadaraka ya Rais kwa mujibu waKatiba hii.

46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitishaazimio la kumuondoa Rais madarakaniendapo itatolewa hoja ya kumshtakiRais na ikapitishwa kwa mujibu wamasharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaibara hii, hoja yoyote ya kumshtakiRais haitatolewa isipokuwa tu kamainadaiwa kwamba Rais -

65

Bungelawezakumsh-taki RaisSheriaya 1992Na. 20ib. 8Sheriaya 1995Na. 12ib. 4

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania