kimefasiriwa na profesa/ ayman ibrahim alaasar · 2016-04-10 · wizi wa kielimu na athari zake kwa...

150
Wizara ya Mambo ya Waqfu ya Misri Baraza Kuu la Mambo ya Kiislamu ANGA ZA UTAMADUNI MAKALA KATIKA DINI NA MAISHA Profesa/ Muhammad Mukhtaar Juma Waziri wa Mambo ya Waqfu Raisi ya Baraza Kuu la Mambo ya kiislamu Mjumbe Wa Baraza la Tafiti Za Kiislamu AL-azhar Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar Kairo 1437 AH & 2016 CE

Upload: others

Post on 10-Jul-2020

3 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

Wizara ya Mambo ya Waqfu ya Misri

Baraza Kuu la Mambo ya Kiislamu

ANGA ZA UTAMADUNI

MAKALA KATIKA DINI NA MAISHA

Profesa/ Muhammad Mukhtaar Juma

Waziri wa Mambo ya Waqfu

Raisi ya Baraza Kuu la Mambo ya kiislamu

Mjumbe Wa Baraza la Tafiti Za Kiislamu

AL-azhar

Kimefasiriwa Na

Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar

Kairo

1437 AH & 2016 CE

Page 2: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

2

Yaliyomo

1 Mtume Muhammad ni nabii wa rehema

7

2 Kuelekea pamoja kwa jamii safi ya kisasa

13

3 Makosa yatokanayo na hutuba za dini

20

4 Utendaji wa dini kwa muonekano wa nje na

wa kisiasa

25

5 Umuhimu wa juhudi za pamoja

32

6 Vyama vingi na utawala usiomil

38

7 Maana ya Usalama wa taifa

42

8 Miji mikuu, mipaka na ujenzi wa taifa

47

9 Sinai Ndani ya Kurani tukufu

50

10 Uhakiki kati ya marekebisho na ubomoaji

55

11 Vyombo vya habari vyenye malengo

62

12 Hofu ya kuzembea

65

Page 3: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

3

13 Kisa cha masanamu na ubomoaji wa ustaarabu

71

14 Kati ya utendaji bora na utii 78 15 Mfano mzuri wa kugawanya mali ya zaka 85

16 Mfano mzuri wa kugawanya mali ya zaka 89

17 Baina ya Matumaini na Kazi 93 18 Uzuri, furaha na hisia njema 107

19 Rafiki tumtafutaye

112

20 Haki ya mwanamke katika kurithi na maisha

mazuri

117

21 Ujeuri na mwisho mbaya

125

22 Misri ni nchi kubwa kwa maadili yake na ustaarabu wake

130

23 Wizi wa mali za umma na kuzifuja 134

24 Mazungumzo ya ijumaa

Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa

139

25 Wito wa kuwa na matumaini

144

Page 4: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

4

Utangulizi

Shukurani zote njema anastahiki mwenyzi Mungu, rehma na

amani zimshukie Mtume wa mwisho na mjumbe wake sayidna

Muhammad bin Abdillah, na jamaa zake na masahaba zake na

kila aliyemfuata mpaka siku ya mwisho.

Huu ni mkusanyiko wa makala za matukio mapya mbalimbali

: ya kidini, kitamaduni, kifikra, kijamii na kitaifa, nimependelea

kuyaandika chini ya anuani “Anga ya Utamaduni”. Nayo ni kwa

ajili ya kutilia mkazo juu ya makosa yaliyomo katika akili za

watu ya kutoelewa kutafautisha kati ya dini na tamaduni. Kuna

tafauti kubwa na kwa kuwa msomi anatakiwa awe na kiwango

kikubwa cha ufahamu wa vitu mbali mbali. Kwa kuwa hukumu

ya kitu ni sehemu ya ujuzi (ili uhukumu kitu inatakiwa uwe na

ujuzi nacho). Pamoja na kuchunga hali na sehemu ambazo pia

ni nguzo muhimu za ufikishaji, kitu kinachopelekea kwa msomi

awe na ufahamu wajamii iliyomzunguka na kwa matukio na

changamoto zinazojiri duniani.

Ulimwengu wa kiarabu na kiisilamu umefikwa na mbano

mkubwa wa taaluma au kiwango kidogo cha taaluma kwa watu

Page 5: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

5

wengi, pengine ni kwa sababu ya kutowafikia kwa njia sahihi

kwa baadhi ya wakati. Na tatizo hili imebidi kuzungumziwa kwa

kuwa mtafutaji au msomi wa somo

maalumu huwa anazingatia ile fani yake pekee na kuacha kujua

ima kifikra au hata kimitaala fani nyengine kitu ambacho

huzalisha kizazi ambacho –pengine- huwa hakijaelimika au

kutoweza kufanya kazi kwa pamoja kwa roho ya timu au kuwa

na uhusiano wa karibu na jamii. Kwa sababu hajabobea kw

nyenzo za kitaaluma na ujuzi wa kisasa. Na huenda mwandishi

au msomi akatibu kimakosa baadhi ya kadhia au hata

akapelekea mkangamano sawa iwe kwa mihadhara ya

kusikikana au ya kuonekana.

Na nimejitahidi katika kuleta fikira mbalimbali katika makala

hizi ambazo ninaziandika katika kitabu hiki, hali ya kumuomba

Mwenyezi Mungu anikubalie, na niongeze kitu katika taaluma

za fikra ya kiisilamu, nikiwa niko sawa basi kwa fadhila za

Mwenyezi Mungu na kama si hivyo basi ni kwangu nami

nimejitahidi na kujaribu.

Page 6: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

6

Mwenyezi Mungu yu nyuma ya kila lengo naye ni Mwafikishaji

na Msaidizi.

Prof. Muhammed Mukhtari Juma

Waziri wa Wakfu

Na Mjumbe wa Utafiti wa Al Azhar Sharif

Page 7: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

7

Mtume Muhammad Ni Nabii Wa

Rehema

Mwenyezi Mungu Mtukufu amemleta Mtume Muhammad

(rehma na amani zimshukie) kuwa ni rehema kwa ulimwengu

mzima, akasema: {na wala hatujakutuma isipokuwa ni rehema

kwa ulimwengu mzima} na Mtume akajieleza mwenyewe kwa

kusema “enyi watu hakika mimi ni rehema yenye kuongoa.” Na

Qur’ani Tukufu inasisitiza kuhusu hilo na kusema { Hakika

amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe;

yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana.

Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma. }

Na kitabu chake alichoteremshiwa Mtume ni kitabu chenye

uongofu kwani Mweneyzi Mungu anasema {Na tunateremsha

katika Qur'ani yaliyo ni matibabu na rehema kwa Waumini.

Wala hayawazidishii madhaalimu ila khasara}

Dini yake ni dini ya rehema,amani na usalama kwa viumbe

wote, dini yenye misingi thabiti ya kuwawezesha watu wote

waishi kwa amani. Inahifadhi kutomwaga damu, inahifadhi mali

Page 8: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

8

zote kwa misingi ya kiutu bila ya kutafautisha watu kwa misingi

ya dini, rangi, jinsia na kabila, nafsi zote zimehifadhiwa,

heshima na mali pia zimehifadhiwa. Na amana zote hurejeshwa

kwa weneywe bila ya pingamizi. Na Mtume wetu (rehma na

amani zimshukie) wakati wa kuhamia kwake Madina alimuacha

Ali bin Abi Twalib nchini Makka ili azirudishe amana kwa

watu wake ingawa walimnyanyasa na kumkera.

Na siku walipokuwa mji wa Taifu watu wa mji ule

walipowaamuru watumwa na watoto wamrembee kwa mawe

mpaka akamwagika damu nyingi miguuni mwake, wakamjia

malaika wa majabali na kumwambia : “Ewe Muhammad hakika

Mweneyzi Mungu amesikia maneno ya watu wako kuhusu

wewe na mimi ni malaika wa majabali Mwenyezi Mungu

amenituka kwako ili uniamrishe kwa amri yako pindi ukitaka

niwagandamize katika majabali mawili. Mtume (rehma na

amani zimshukie) akasema: “lakini ninaema,ewe Mweneyzi

Mungu waongoe watu wangu kwani hawajui walitendalo, nami

ninataraji kuwa Mwenyezi Mungu atatoa katika migongo yao

atakaesema Lailaha illa llahu (hapana wa kuabudiwa kwa haki

isipokuwa Mweneyzi mungu).” Na alipoambiwa. “Waombee

Page 9: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

9

washirikina” akasema: mimi sikutumwa kuwa ni mweneye

kulaani lakini nimetumwa kuwa ni rehema.

Uisilamu ni dini ya rehema na amani wa ulimwengu wote,

hakuna mauaji kwa sababu ya itikadi hata kidogo, na Mtume

(rehma na amani zimshukie) alipomuona mwanamke wa

kikafiri ameuliwa katika uwanja wa vita akasema: “ni nani

amemuua? Huyu haikupasa kuuliwa.” Hii inathibitisha kuwa

ukafiri si sababu ya kuuliwa, isipokuwa mauaji hutokea kwa

sababu ya kuondoa uadui kwani dini hailazimishi mtu na wala

haina maneno ya kejeli, Mweneyzi Mungu anasema

. Na lau ungeli kuwa mkali, kumwambia Mtume wake {

mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi

ika wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao kat

mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi

Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao

} na Qur’ani ilipowazungumzia makafiri kupitia mtegemea.

ulimi wa Mtume (rehma na amani zimshukie) na kwa ndimi za

masahaba wake akasema { Na hakika sisi au nyinyi bila ya

shaka tuko kwenye uwongofu au upotofu ulio wazi.} na wala

hakusema “sisi tupo katika uongofu na nyinyi mupo katika

Page 10: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

10

upotevu wa wazi, na misemo kama hii inajulikana kwa wasomi

wa ufasihi wa maneno kuwa ni “ kunyeyekea”. Na hii ndio

tamaduni yetu ambayo inamfanyia uadilifu mwengine hata

katika kuzungumza.

Uisilamu umeamrisha kusema maneno mazuri, mwenyezi

Mungu akasema Semeni na watu vizuri} na watu inakusudiwa

kwa ujumla pia semeni maneno mazuri {na sema kuwaambia

waja wangu waseme maneno ambayo ni mazuri} na watende

pia vitendo vyema. { Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu

kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana

uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu} huyu

ndiye Mtume wetu na hizi ndizo tabia zake akasema

“nimetumwa kukamilisha tabia njema”

Na iwapo dini yetu ni dini ya rehema na kitabu chetu ni kitabu

cha rehema na Mtume wetu (rehma na amani zimshukie) ni wa

rehema sasa vipi kuhusu sisi? Tumefikwa na nini? Na ni kipi

kilichowafika wenye nyoyo dhaifu juu ya dini yetu hata

wakafikia kuwa wana nyoyo ngumu kiasi hiki? Na utatuzi wake

ni upi?

Page 11: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

11

Hapana shaka kuwa vitendea kazi vingi vinahusika juu ya hili,

ikiwemo wasomi wasio na fani husika kuwa na mamlaka katika

kutoa hutuba za ulinganio na kushika nafasi hizo kwa muda

mkubwa. Na wengine kuamisi sivyo na kuzidisha itikadi kali

katika dini, yote haya ni ufahamu usio sahihi na ipo haja ya

kusahihisha pamoja na kusisitiza kuwa uisilamu ni dini ya

msamaha, rehema na wepesi. Na wasomi wamesema kuwa

“Fiqhi” ni utambuzi na uwepesishaji kwa dalili, na hakuna

aliyesema yeyote katika wenye kutegemewa elimu zao sawa

katika wale wa zamani au wa somi wa kisasa kuwa “fiqhi” ni

elimu yenye itikadi kali. Mweneyzi Mungu anasema {

Mweneyzi Mungu anakutakieni wepesi wala hakutakieni uzito}

na anasema {Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika

Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi

Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii

(Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe

mashahidi kwa watu}. Pia anaendelea kusema {Na jueni kuwa

Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nanyi. Lau angeli kut'iini

katika mambo mengi, bila ya shaka mngeli taabika. Lakini

Mwenyezi Mungu amekupendezeeni Imani, na akaipamba

Page 12: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

12

katika nyoyo zenu, na amekufanyeni muuchukie ukafiri, na

upotovu, na uasi. Hao ndio walio ongoka, 8. Kwa fadhila za

Mwenyezi Mungu na neema zake. Na Mwenyezi Mungu ni

Mwenye kujua, Mwenye hikima. }. Na Mtume wetu (rehema na

amani zimshukie) hakuwa akichagua kati ya mambo mawili

isipokuwa akichagua lililo jepesi lao ilivyokuwa si katika maasi

au kuvunja undugu, na Mtume (rehema na amani zimshukie)

alikuwa ni mwenye kujiepusha sana katika maasi

Page 13: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

13

Kuelekea Pamoja Kwa Jamii Safi Ya

Kisasa

Usafi ni maadili ya kisasa lakini hasa ni anuani ya ustaarabu, na

haiwezekani kwa wananchi wenye kuwa na ustarabu wa aina

mbili nazo zote ni kubwa mno ambazo historia ya mwanadamu

imezielewa wapuuzie jambo hili. Sisi ni wana wa ustarabu

tuliobobea na uliokita zaidi ya miaka elfu saba. Na ustaarabu

mwegnine ni wa kuwepo uisilamu, na zote mbili hizi

zimekusanyika pamoja na kutengeneza mwanaraia wa Misri.

Ustaarabu huu una wito wa kuwa watu wazuri na wenye haiba,

na kujiweka mbali na kila lenye makero na kuudhi na ambalo

halitakikana kwa mtu mwenye akili timamu. Mwenyezi Mungu

amewasifu watu wa msikiti wa Qubaa kwa pupa zao za kuwa

wasafi, Mwenyezi Mungu akasema: “ndani yake muna vijana

wanaopenda kujisafisha, na Mwenyezi Mungu huwapenda

wajisafishao ”

Na Mwenyezi Mungu ametuamrisha kuchukua mapambo yetu

kila tuendapo misikitini akasema, {Enyi wanadamu, chukueni

mapambo yenu kila muendapo msikitini}. Na kutuamrisha

Page 14: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

14

kujisafisha miili yetu na nguo zetu akasema {enyi mlioamni

mukisimama kwenya sala basi osheni nyuso zenu na mikono

yenu mpaka katika visugudi na pakeni vichwa vyenu na miguu

yenu mpaka kwenye visigino na muwapo na janaba basi ogeni}

. na pia Mweneyzi Mungu akasema kumwambia Mtume wake

(rehma na amani zimshukie {1 Ewe uliye jigubika! 2 Simama

uonye! 3 Na Mola wako Mlezi Mtukuze! 4 Na nguo zako,

zisafishe.}

Na Mtume (rehma na amani zimshukie) ameweka wazi kuwa

usafi ni nusu ya dini akasema: “Usafi ni nusu ya imani.” Si

hivyo tu bali uisilamu umefanyaa usafi wa mwili na nguo na

mahali ni sharti ya kukubaliwa ibada muhimu katika maisha ya

muisilamu na ni nguzo ya kimatendo iliyo ya juu kabisa katika

uisilamu baada ya kutoa shahada mbili, nayo ni sala. Mtume

(rehma na amani zimshukie anasema: “ Hakika Mweneyzi

Mungu Mtukufu haikubali sala bila ya tohara (usafi) na sadaka

kutoka mali haramu.

Na Mtume (rehma na amani zimshukie) kaenda mbali zaidi ya

hapoa katika hadithi ya usafi aliposema kuwa kuacha

kujisafisha baada ya kwenda haja ndogo ni sababu ya kupata

Page 15: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

15

mtu adhabu ndani ya kaburi lake, na hii ni pale alipopita (rehma

na amani zimshukie) katika makaburi mawili akasema: “ hawa

wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama

mmoja wao alikuwa ni msengenyaji na mwengine alikuwa

hajisafishi kutokana na haja ndogo.”

Na dini yetu tukufu imekataza kutumia kila kinachoharibu maji

au sehemu au kuweka vizuizi kwa watu katika maisha yao au

lolote lenye kusababisha makero na kudharau. Imekataza pia

kukojoa ndani ya maji au kivulini au katika njia wapitazo watu

au maeneo ya watu wote. Mtume (rehma na amani zimshukie)

amesema: “waogopeni walaanifu wawili, wakasema: “Ni nani

hao ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” akasema: “ambao

wanajisaidia njiani na katika vivuli vya (kupumzikia) watu.”

Kama ambavyo uisilamu umekataza pia mtu kufanya haja

ndogo katika eneo analoogea sawa iwe ni mtoni, baharini au

hata katika bwawa la kuogelea au kufanya haja ndogo upande

unaotokea upepo, na jambo hili ukaliwekea adabu zake, zaidi

juu ya maudhui hii imeelezwa kwa kina katika vitabu vya fiqhi,

sehemu za tohara (usafi).

Page 16: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

16

Na atakaehesabu idadi ya majosho ya lazima kwa mfano,

mwanamke anapomaliza hedhi, au damu ya ugonjwa, au ujusi

(baada ya kujifungua) au baada ya kukutana (mtu na mkewe),

aukutokwa na manii. Au hata majosho yasiyo ya lazima kwa

mfano; kuoga kwa ajili ya sala ya Ijumaa kwa wanaosema kuwa

ni sunna (baadhi ya wasomi), ingawa wengine wanasema kuwa

ni jambo la lazima, na kuoga kwa ajili ya sala za idi mbili, na

kuoga kwa anayeosha maiti, na kuingia Makka, na majosho

mengineyo yasiyo ya lazima (sunna), itafahamika kuwa ni

namna gani uisilamu umelipa uhuhimu jambo la usafi.

Na jambo jengine ni kuwa uisilamu umehimiza urembo na

kujipamba Mtume (rehma na amani zimshukie) aliposema “

hatoingia peponi mwenye chembe ya kiburi ndani ya moyo

wake, kijana mmoja akasema: “ kuna mtu hupenda nguo zake

na viatu vyake viwe vizuri.” Mtume (rehma na amani

zimshukie) akasema: “Mwenyezi Mungu ni mzuri na hupenda

uzuri, kiburi ni kukana ukweli na kudharau watu.”

Uisilamu umefanya usafi wa kinywa (upigaji mswaki) kuwa ni

jambo la sunna, na ukasema pia ni wajibu kuosha katika mikato

ya nje na ya ndani ya mikono na miguu, na kueleza kuwa iwapo

Page 17: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

17

itakuwa ni msimu wa baridi basi kutumia maji katika

kujitahirisha kunazidishiwa malipo mara mbili, Mtume (rehma

na amani zimshukie) akasema: “ Je niwafundishe

atakayokufutieni Mweneyzi Mungu makosa yenu na kukuinueni

daraja? Wakasema:” ndio ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.

Akasema: “kueneza udhu wakati wa baridi, na kuenda sana

misikitini, na kungojea sala baada ya sala hayo ndiyo malipo

makubwa.”

Na uisilamu umetaka usafi wa njia (barabara) na kuondoa

uchafu na kuacha kabisa kuutupa (kiholela) kwani usafi ni

sehemu ya imani akasema: “imani ni sehemu sabini au ni

sehemu sitini, bora yao ni tamko la “Lailaha illa llahu (hapana

apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mweneyzi Mungu) na

ya chini yake ni kuondosha uchafu njiani.” na hadithi hii

inaweka wazi kuwa kuondosha uchafu njiani humpa mtu imani

na haya yanasisitizwa na kijana alipomuuliza Mtume (rehma na

amani zimshukie) kuhusu matendo yatakayomuingiza mtu

peponi akamwambia: “ondosha uchafu njiani”. Na katika

hadithi nyengine “kuondosha uchafu njiani ni sadaka.”

Page 18: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

18

Na hayo yote yanatilia mkazo juu ya ustaarabu wetu kuhusu

usafi na uzuri, na kukataza aina zozote za uchafu na makero, na

katika mambo ambayo inabidi tuyaangalie kwa undani zaidi ni

usafi katika maisha yetu ili tusijikere na kuwakera wengine. Na

iwapo hatutasaidiana katika usafi wa mazingira yetu, jamii yetu

na mandhari yetu basi kwa uchache na tusiwe ni sababu ya

kuwakera watu sawa iwe kwa kutupa taka au masalio ya ujenzi

katika barabara (njiani) au kurembea matakataka katika njia

ipitayo maji-taka au kumwaga maji ya viwandani katika mto wa

Nile, na kutupa masalio na uchafu ndani yake na kuchafua uzuri

wake na kuharibu kingo zake.

Kila mmoja wetu ajitahidi katika usafi wa mwili wake, nguo

zake, sehemu yake, shule yake, sehemu afanyayo kazi na

asaidie pia katika usafi wa jamii, kwa kuondoa uchafu njiani, na

ajitahidi kadiri awezavyo katika kuifanya jamii ionekane nzuri

na safi na ya kisasa.

Na kwa jamii zilizoendelea zinaweza kuzibadilisha taka na

kuzifanya kuwa ni rasilimali yenye kurudisha faida kwa jamii

yake, je, sisi tuko tayari kwa hili? Na tunaweza? Bila shaka,

“ndio” tunaweza, lakini kwa sharti la kuacha maneno na

Page 19: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

19

kufanya vitendo, na kuanza kila mmoja wetu.. na iwe kauli

mbiu yetu.. jamii safi ya kisasa."

Page 20: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

20

Makosa Yatokanayo Na Hutuba Za Dini

Hapana shaka kuwa mabadiliko na urekebishaji wowote wa

utoaji wa hutuba za dini kwa kupitia historia ya viumbe

haiwezekani uwe ni kadhia ya jamii au makubaliano pasi na

kuainisha muda au wakati ambao huenda ukarefuka au ukawa

mfupi kwa mujibu wa wasomi wa wakati ule kupitia juhudi zao

na misimamo yao na pia uwezo wao wa kukinai kwa mawazo

mapya. Na kwa upande wa wasomi wa zamani na wenye

kunufaika kwa matukio ya hali iliyopo kwao inakuwa ni

vigumu kukubaliana kirahisi na kwa wepesi na wasomi wa

kisasa, na kwa mujibu wa mawazo ya wasomi wa kisasa na

mwenendo wao wa kimawazo uliofikia mbali (mara nyinyi)

jamii huwa tayar kuambatana nao kimawazo na kuacha njia ya

wasomi wenye mawazo mgando yasiyoleta tija. Isipokuwa njia

nyepesi ya kati na kati nayo imekuwa ni kitu chenye utata kati

ya makundi mawili haya.

Maudhui hii kwa upande huu itagawanyika katika mafungu

matatu makuu, nayo:- ufahamu uliosahihi (uliotakasika), hatari

Page 21: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

21

ya kuacha maudhui husika na kumuelekea mtu binafsi, na uhuru

wa itikadi na wa maoni.

Fungu la kwanza: ufahamu uliosahihi (uliotakasika), wa zamani

na mtazamo wake kwa kuwa ni wa zamani kiasi ambacho

inakaribia kuonekana maneno yaliyozungumzwa na baadhi ya

wasomi wa zama hizo kwa mujibu wa nyakati zao na maeneo

yao yanaonekana kama ni maneno matukufu. Ama kwa nyakati

hizi itahitajika kuwepo kwa jitihada

mpya yenye kwenda sambamba na wakati tulionao na matukio

yake pamoja na matakwa yake, na tunakaribia kuona

wanaoyatukuza maneno ya baadhi ya wanahistoria na kile

walichokiandika katika vitabu vya ukoo (majina) na historia.

Na kwa upande mwengine tunaona wenye kuvuka mipaka kwa

njia ya kejeli kuhusu yale mambo yaliyothibiti (kidalili) au yapo

karibu sana na kuwa yamethibiti kwa kisingizo cha urekebishaji

kiasi ambacho baadhi yao huharibu kabisa kabisa. Na hili

huenda likawa kwa sababu ya uoni mdogo au kwa manufaa na

makusudia mabaya ingawa hatukanushi au kukubali kwani

nyoyo na nia zote zipo katika mikono ya Mwenyezi Mungu

(S.W) .

Page 22: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

22

Msisitizo wetu tunaourejea rejea mara kwa mara ya kuwa sisi

tunahitajika turekebishe na kuifanyia akili kazi nasi tupo

kinyume na mawazo mgando na fikira za kizamani na kufunga

mlango wa jitihada na kudunisha upeo au kuufunga kabisa na

kuuziba. Na tupo kinyume na kuwaona kuwa wao ni makafiri

na kuwatuhumu kuwa wapo kinyume na taifa lao isipokuwa

kama mahakama itatoa hukumu ya jambo hilo. Na mimi

nakumbushia kuwa hakuna yeyote katika watu na itikadi zao

kuwa atakubali kuingiliwa katika kile anachokiamini na

kumfanyia uadui ndani yake hata kama itakuwa kwa kubatilisha

itikadi yake kwa njia za akili na dalili.

Fungu la pili: Na miongoni mwa makosa makubwa yatokanayo

na hutuba za dini ni kuacha kuacha maudhui na kumuelekea

mtu binafsi na kumdhalilisha mpaka inafikia kuonekana kuwa

ni matusi, au kurudishiana matusi ya nguoni kama si matusi ya

waziwazi. Sawa kati ya wanaogombana na wanaozungumza kati

ya maulamaa na wasomi. Iwapo msomi atakapozungumzia

maudhui Fulani na akawa nachunga heshima ya mazungumzo

na kutoa mawazo yake kisomi na kwa akili huyu itajulikana

kuwa anasema kwa mujibu wa upeo wa hoja, rai na akili ya

kimantiki. Lakini iwapo msomi au mtafutaji au mhakiki

Page 23: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

23

atakapozungumzia maudhui na akawa anamzungumzia

mwengine kwa njia ya kumkweza sawa na iwe katika wasomi

wa zamani au wa kisasa na sawa awe kati wasomi wa dini au si

wa dini jambo hili katu halitakubaliwa. Na haiwezekani

kulikalia kimnya au kilisubiria, na hili linaweza kuwa ndio

chanzo cha kukujeliana na audui wa kifikra. Na kwa wafuasi wa

anayeshambuliwa wanaweza kutoka nje ya mipaka na wakaona

kuwa ni wajibu wao kisheria, kiakili na kiutu kuwakinga

wasomi wao, jambo ambalo huenda likapelekea kuzuka kwa

vita ya maneno na mijadala mipya au ya zamani yenye

kujirudiarudia au hata kusababisha matukio yenye kutenganisha

ndani ya historia ya taifa letu.

Fungu la tatu: ni lile lenye kuzungumzia ufahamu sahihi na

ufahamu usio sahihi kuhusu uhuru wa maoni, sisi

tunatenganisha uhuru wa itikadi na uhuru wa maoni, kama

tunavyotafautisha kati ya uhuru unaodhibitiwa na sheria au akili

au kanuni na machafuko ambayo hayana mipaka. Pamoja na

kuwa dini yetu haijambebesha mtu mzigo au kumlazimisha

kuikubali, mweneyzi Mungu anasema { Hapana kulazimisha

katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na

upotofu } na pia anasema : { Na Mola wako Mlezi angeli

Page 24: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

24

penda angewafanya watu wote wakawa umma mmoja.

Lakini hawaachi kukhitalifiana} na anaendelea kusema {

Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi

Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua

zaidi waongokao}, pia anasema { Si juu yako ila kufikisha

Ujumbe tu.}Na anasema pia {3. Huenda labda ukajikera

nafsi yako kwa kuwa hawawi Waumini. 4. Tunge penda

tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea

shingo zao.}

Uisilamu umeweka vidhibiti vya uhuru vilivyo imara na

vyenye kusisitiza msamaha wake mkubwa, lakini jambo hili na

ufahamu wa uhuru wa maoni halitakiwi liwe la kuvuka mipaka

au kuzidi kiwango juu ya yale yaliyothibiti kidalili au yale

yanayotukuzwa au hata kugusa heshima za watu kwa kisingizio

cha uhuru wa maoni . na kwa kuwa sisi tunahitajika zaidi

kufanya kazi na si kulombana na kujiweka pamoja kwa

lililokubaliwa pande zote, na kukubaliana juu ya kutofautiana

kwa maoni

yawengine, na wala tusielekee katika lugha ya matusi na

kurushiana madongo au kurudishiana matusi na mfano wake

hili ni kwa ajili ya kulinda uzuri wa jamii kwa ujumla. Kitu

Page 25: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

25

ambacho (kulumbana) hakikubaliki katika akili na ni kigeni

katika jamii yetu na katika ustaarabu wa kiarabu na wa

kiisilamu.

Utendaji Wa Dini Kwa Muonekano Wa

Nje Na Wa Kisiasa

Page 26: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

26

Hapana shaka kuwa utendaji wa dini kwa muonekano wa nje na

kwa muonekano wa kisiasa hii ni changamoto kubwa sana

ambayo umma wa kiarabu na wa kiisilamu unakabiliwa nayo.

Na iwe sawa kwa hawa ambao wanazingatia umbo au

muonekano hata kama itakuwa ni kwa kuacha asili. Na kufanya

kuwa muonekano ndio kila kitu, na hata kama mwenye kujidai

muonekano huo hana utu wala tabia ambazo humfanya awe ni

kigezo na mfano wa kuigwa. Na hii inatokana na kuwa mwenye

kujionesha huwa tabia yake haiendani sambamba na mafunzo

ya kiisilamu na hii huzingatiwa kuwa moja ya uvunyaji na

ukiukwaji wa dini, kwani iwapo muonekano wa wenye

kujionesha ni tabia mbaya au uongo au kutengua ahadi au

khiyana au kula mali za watu kwa dhuluma, hapa jambo hili

kwa hakika huwa ni hatari sana.

Isitoshe mwenye tabia hizi huwa ni katika wanafiki, kwani

Mtume wetu (SWA) amesema : ”alama za mtu mnafiki ni tatu;

akizungumza husema uongo, akitoa ahadi haitimizi na

akiaminiwa hufanya khiyana. (imepokewa na Bukhari).

Vile vile kwa waichukuliao dini kuwa ni ibada na kufanya

jitihada ambazo zitapelekea kuifahamu dini vibaya na kufikiria

zaidi mambo yasiyohitajika na kubeba silaha na kujitenga na

Page 27: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

27

watu wenzao, kama ilivyokuwa kwa madhehebu ya Khawarij

ambao walikuwa wakisali sana, kufunga na kusali usiku

isipokuwa wao hawajaisoma elimu ya sheria kama itakiwavyo

ambayo ingeweza kuwakinga na umwagaji wa damu na

kupelekea watu wawapinge kwa kutumia panga zao. Lau kama

wangetafuta elimu kwanza kama alivyosema imam shafii

“Mwenyezi Mungu amrehemu”, wangejikinga na mengi, kwani

uisilamu ni dini ya upole kabla ya chochote, na kila ambacho

kitakuweka mbali na upole basi hicho hukuweka mbali na

uisilamu, na kinachozingatiwa ni tabia njema si maneno

matupu. Kwani wamesema “Muungwana hujulikana kwa

matendo na si kwa maneno.”

Na hakika ibada zote haziwezi kuleta matunda yake isipouwa

tabia ya mwenyewe itakapokuwa njema, na yeyote ambae swala

yake haitamkataza juu ya uovu na machafu basi huwa hana

swala, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “hakika ya swala

inakataza maovu na machafu, na utajo wa Mwenyezi Mungu ni

mkubwa, naye Mwenyezi Mungu anajua yote muyatendayo”

(Ankabut, aya 45)

Na yeyote ambae funga yake haimzuii na maneno machafu basi

huwa hana funga, kwani Mtume SWA anasema “asiyeacha

Page 28: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

28

maneno machafu na matendo machafu, basi hakika Mwenyezi

Mungu huwa hana haja ya mja huyo kuacha chakula chake na

kinywaji chake” (Imepokewa na Bukhari)

Mwenyezi Mungu huwa hakubali zaka wala sadaka isipokuwa

kwa mali halali, Mtume wetu (SWA) anasema “Hakika

Mwenyzi Mungu ni Mzuri na wala hakubali isipokuwa kizuri”

(Imepokewa na Muslim).

Mtume (SWA) anasema “ Swala haikubaliwi bila ya tohara na

wala sadaka haikubaliwi iwapo ina husuda (Imepokewa na

Muslim).

Na hata ibada ya Hijja ili ikubaliwe itategemea kipato cha halali

na tabia njema “Atakaehiji na akawa hajafanya uovu wala

machafu basi hurejea (na madhambi yake hufutwa) kama siku

aliyozaliwa na mama yake”. Na Mtume (SWA) ametaja “Mtu

ametoka safari ya mbali amejaa vumbi kisha ananyosha mikono

yake mbinguni anasema “Ewe Mola wangu ewe Mola wangu,

hali ya kuwa chakula chake ni haramu kinywaji chake haramu,

nguo zake ni haramu na amekula haramu iweje basi mtu huyu

kujibiwa” (Imepokewa na Muslim).

Na utendaji ulio mbaya zaidi ni utendaji wa dini kwa

muonekano wa nje kwa ajili ya kisiasa, hapa tunakusudia hili

Page 29: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

29

kundi ambalo wameifanya dini kuwa ndio njia ya kupitia

kuelekea kwenye uongozi kwa kutumia upenzo wa dini na

kuwapendezesha watu hasa wale wasiojua kitu kuhusu dini yao.

Na kuwahadaa kuwa lengo la kushika madaraka ni kwa ajili ya

kuitumikia dini ya Mwenyezi Mungu pekee na kuinusuru na

kuifanya iwepo. Pamoja na kuwa sisi huwa hatuhukumu kupitia

nia na wala hatuingilii chochote kuhusu nia ya mtu kwani nia ni

kati ya mja na Mola wake, na kila mmoja wetu ana malengo

yake (nia yake), lakini ujuzi tulionao wa kuishi na kundi la

kigaidi la Ikhiwani na kwa wale wenye mwenendo kama wao au

kuwaunga mkono katika makundi mengine ya kiisilamu

tumejihakikishia mambo mawili, nayo:-

1. Tukio kwa upande wao si tukio la kidini hata kidogo

isipokuwa ni kupigania uongozi kwa makeke na mabavu,

hatukuwahi kuona mfano wake na kuwatendea wengine

kwa kujeli, kiburi na maguvu, kitu ambacho watu wengi

wakakipinga kwa kuwa ni mzigo katika dini, na ikawa

hakuna budi isipokuwa kuifuta sura hii mbaya ambayo

imeenea katika akili za wengi kati ya watu ambayo

imefungamana na tabia za watu wa kundi hili pamoja na

dini.

Page 30: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

30

2. Jambo la pili jingine ni kuwa, wao wameiharibu dini yao

na kuipa sura mbaya pamoja na kuwa dini ina tamaduni

nzuri na ya upendo, na wakajithibitishia kuwa wao si

watu wa dini na wala hawawezi uongozi, kwa sababu, je

ni dini gani inayowakhini watu wake na taifa lake na

kutoa siri na kuuza hata nyaraka muhimu na kuwa

wapelelezi wa nchi yao kwa wasioitakia manufaa. Na je

kuna dini inayochochea vurugu, mauaji, ufisadi na

kuunda vituo vyenye lengo la kueneza maovu kwa

wafuasi wake pamoja na kufanya khiyana ambayo

haijawahi kutokea, ikiwemo khiyana ya taifa na

kutendeana na maadui wa nchi yake?

Imethibiti na ninazidi kuthibitisha kuwa kundi hili ambalo

limeifanya dini kuwa ndio chombo cha kuwahadaa watu na

kunufaisha malengo yao ya kuutaka uongozi si zaidi ya

kuungana na shetani, ili kutekeleza na kuhakikisha malengo

yao na tamaa zao za kutaka utawala na uongozi kwa kupitia

dini, au nchi au kwa umma.

Page 31: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

31

Umuhimu wa Juhudi za Pamoja

Jamii yetu imeingiliwa na fatwa ngeni pamoja na rai zisizo

sahihi na baadhi ya wenye husuda na wasio na ujuzi na wenye

Page 32: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

32

nafsi dhaifu ambao wanawaingilia maulamaa, kwa madhumuni

ya kupata umaarufu, vyeo na kutaka kuonekana tu, wakazitumia

rai zote zisizo sahihi na zilizo ngeni ili wapate kuonekanwa na

kwa ajili ya masilahi yao pamoja na makundi yao.

Na kwa kutokana na wingi wa kadhia pamoja na matukio

mapya yanayojiri na kugawanyika kwake na vuguvugu lake

pamoja na kutowafikiana kwa baadhi yake katika rai za

wanazuoni na wasomi waliotangulia ambao wao walitoa fatwa

kwa mujibu wa zama zao na wakati wao pamoja na sehemu zao.

Ukizidisha na ujinga wa wasio wasomi wa fani hiyo ambao

hawana ujuzi wa kuchambua na kufanya uhakiki, pia kuacha

kutendea baadhi ya hukumu bila ya vigezo, na hii ni kwa

sababu ya ujinga wa tukio pia ujinga wa kutofahamu sharti za

vipimo sahihi. Kwa sababu hizi ndio imepelekea kuwepo kwa

ulazima wa upatikanaji wa juhudi za pamoja.

Kwa ajili hiyo. Huu ukawa ndio wito wa Imamu Mkuu Prof.

Ahmed Twayyib, kiongozi wa Al Azhar Shariyf, katika hotuba

yake ya ufunguzi kwenye mkutano wa Kikao kikuu cha masuala

ya Waisilamu, uliofanyika katika mji wa Luxur, wenye anuani:

“Mtazamo wa viongozi na maulamaa katika kurekebisha hotuba

za dini, na kutengua fikira zisizo sahihi,” na kuwepo juhudi ya

Page 33: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

33

pamoja ambayo itawaita wasomi wakubwa katika nchi tafauti

ulimwenguni, na kwa kila mwenye kuwa na hisia juu ya umma

na matatizo yake, ili wapinge kwa ushujaa wao wote masuala

yaliyopo kwa mfano; ugaidi, ufahamu wa hukumu juu ya pahala

pa kiisilamu, kujiunga na makundi ya kigaidi yenye kutumia

silaha, kuacha kuwa pamoja na wanajamii na kuwachukia,

kuhalalisha damu za raia wasio na hatia kwa kuwaua au kwa

kuwaripua, au kila chenye kuhusika na haki za kibinadamu na

uhuru, na kila lenye kuhusika katika masuala ya kijamii kwa

mfano, suala lenye kupewa kipaumbele ni masuala ya

mwanamke, kuanza kujua mwezi upi wa kiarabu ndio

unaotangulia kwa kupitia makadirio ya falaki, masuala ya Hijja

na hasa katika kuanza kuhirimia Jiddah kwa wale waendao

(kuhiji) kwa kupitia vyombo vya anga au kwa vyombo vya

bahari, pia kulenga mawe katika nyakati zote nyengine , na

masuala mengineyo ambayo yanashikana na haki za nchi, na

yanashikana na wakati na pia mahitajio ya watu.

Na ili umma uinuke inapasa kutoa fat-wa zenye kuwezekana

kutendeka na zenye kuharamisha kujibweteka na uvivu, na hii

ni kwa masharti isije ikatolewa fat-wa yenye kuhitaji

mazingatio ya kina kwa kuitolea fat-wa iliyokuja kwa ujumla na

Page 34: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

34

kwa maelezo ya ujumla ambayo hayaendani na uhalisi uliopo na

ambazo pia hazitaweza kutoa jibu juu ya masuala au hata

kubadilisha kilichopo.

Na bila shaka juhudi za pamoja zitasaidia sehemu kubwa na

zitaweka wazi sana ili kufuta rai zisizo sahihi, na kwa ajili ya

kuondosha sababu za uasi, Kikao kikuu cha masuala ya

Waisilamu katika mkutano wake wa mwisho kimezungumzia

mambo muhimu, nayo ni:-

1. Kufunga, kuzuia, na kuacha kufuata bila ya mwelekeo, na

kuweka wazi ufahamu wa kuyafasiri maelezo kama

yalivyo katika asili yake na kujiepusha na uelewa wa

matukio ambayo matokeo ya fat-wa yake hayatafanana

na tukio, na kutofahamu misingi ya sheria kiujumla (pasi

na kujua asili yake), pia kuwapa nafasi wasio na elimu

katika kueneza ulinganio.

2. Baadhi ya watu kuitumia dini kama biashara, na kuitumia

kwa malengo ya kisiasa na kwa vikundi vya vyama, pia

kwa kujipatia faida katika vikundi na miasasa yao kwa

jina la dini na taifa, na kujifanya watendaji wa dini lakini

Page 35: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

35

kwa mtazamo wa nje na wa kisiasa badala ya kuitendea

dini kwa ajili yake Mwenyezi Mungu pekee.

3. Kufanikiwa kwa baadhi ya watawala katika kuwatumia

vibaraka wao katika nchi nyingi za kiarabu na za

kiisilamu, sawa kama ni kwa ajili ya kubadilishana

masilahi, au kupewa ahadi za uongo kwa baadhi ya

makundi, au kwa njia ya kununuliwa na kuwa kama

watumishi.

Ikifanyika juhudi ya pamoja basi itapelekea kufikia lengo

kubwa hasa katika upande wa kuwepo pamoja kwa wasomi,

na sababu nyingi za mtengamano zitaondoka, na hii

itapelekea, bila shaka, umma kuwa kitu kimoja, na hasa hasa

katika kupambana na fikira zisizo sahihi, za uasi na zenye

kupotosha.

Vyama Vingi na Utawala Usiomili

Anuani hii inakusanya mambo mawili yanayokaribia kuwa

ni yenye kukinzana kwa kutowafikiana na kutokubalika, moja

wapo likiwa ni lazima lipatikane katika Nyanja za kidemokrasia

Page 36: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

36

na jengine linaonekana kuwa ni hatari kubwa kwa kutengeneza

taifa kwani huenda likasababisha kuporomoka na kuanguka na

kudhoofisha. Kwa upande wa vyama vingi hili ni jambo la

kiadilifu kwa upande wa kidemokrasia, kwani ulimwengu wa

sasa ni sawa na mhimili mmoja (kijiji kimoja). Na mara nyingi

kukosekana kwa kujadili mambo kwa uadilifu hutokea hali ya

kidikteta na udhaifu na hasa pale inapokuwa hakuna upinzani

wa kweli wa kuweza kutimiza ahadi ya kweli juu ya kile

alichokiahidi na kukalifishwa.

Ama kwa kuwepo utawala unaomili katika nchi yoyote au

kuwepo kwa makundi yenye kujali masilahi yao pekee, hii

husababisha hatari kubwa sana ya ujenzi wa mshikamano wa

taifa. Na hasa iwapo utawala utajisitiri kwa vazi la kidini na

kujaribu kutumia madaraka yake na ushawishi wake kwa njia

hiyo.

Na kipimo pekee cha kujua kuwa utawala au jamii haina

au ina utawala unaomili ni kwa kuangalia kwa kina gani

wanatekelea sheria bila ya upendeleo au uficho na bila ya kusita

au kudhulumu. Na kutoruhusu kundi lolote au mtu yeyote

kushajiisha wafuasi wake waende kinyume na sheria au

kuiharibu sheria kwa nguvu.

Page 37: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

37

Na kwamba wote wanahitajika kufuata mkondo wa sheria

katika kuelezea matakwa yao, na wafanye vile sheria nakanuni

ilivyoruhusu katika Nyanja zote, pia kuhakikisha kuwa

hairuhusiwi kutumia udanganyifu kwa kupitia sheria. Na kama

mfano wa kundi la kiisilamu la kisiasa linavyodai ya kuwa

“kwenye lengo hupatikana njia”, kwa kutumia njia hii jamii

ilishuhudia kutetereka na kuyumba na kama si usaidizi kutoka

kwa Mwenyezi Mungu taifa lingelikuwa lishatoweka. Na kwa

kutokana na umakini wa Mheshimiwa raisi Abul fatah Al sisi na

wasaidizi wake pamoja na jeshi lake shujaa na wengine wenye

kuipenda nchi yao, kitu ambacho kinachofanya kurudi kwa

kundi la kigaidi la Ikhwani katika kutengeneza dola lenye

kumili kuwa ni jambo lenye kupingwa na lazima lipingwe kwa

nguvu zote kwa ajili ya kuhifadhi heshima ya nchi.

Na iwapo tunaamni kuwa hakuna kulazimishana katika

dini, na nafasi ya wasomi ni kufikisha ujumbe kwa njia sahihi

na wao ni walinganiaji na si mahakimu au majaji basi jambo hili

linahitaji kuwekwa wazi katika mahusiyano yaliyopo kati ya

walinganiaji na watawala, kwa kuzingatia kuwa utawala wenye

kumili hujaribu kuutengeneza kwa wafuasi wake unaweza

ukawa umemili katika kisiasa au kifikira au kitamaduni na

Page 38: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

38

inaweza kuwa pia kiuchumi au kijamii kwa kupitia baadhi ya

vitega uchumi vyake au kwa njia nyengine yoyote.

Kiufupi, kundi lolote ambalo litakuwa linahisi kwamba

lipo juu ya sheria na kuwa halishtakiwi jambo hili litapelekea

kuonekana kuwa utawala uliopo ni wa kumili nalo ni jambo la

hatari sana kwa serikali na kwa sheria zake. Kinachohitajika ni

kutimiza sheria kwa yeyote bila ya kumili hili ni jambo la

uadilifu kwa ajili ya kuokoa taifa na sheria zake. Na mtume weu

(rehma na amani zimshukie juu yake) anasema: “hakika

wliokuwa kabla yenu waliangamia kwani walikuwa akiiba mtu

mwenye cheo walimuachilia huru na akiiba mnyonge walikuwa

wakimpa adhabu ya wizi, nami ninaapa kwa Yule ambae nafsi

yangu ipo mikononi mwake lau kama Fatuma bint Muhammad

angeliiba basi ningelimkata mkono wake.”

Na sayidna Ali (Mwenyezi Mungu amwie radhi) anasema

pale alipopewa uongozi: “enyi watu mimi nimepewa madaraka

juu yenu hali ya kuwa si mbora wenu, nikidhoofika basi nitieni

nguvu, nikifanya vyema basi nisaidieni, ukweli ni amana, uongo

ni khiyana, dhaifu kwenu basi kwangu ni mwenye nguvu mpaka

apewe haki yake kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, na mwenye

nguvu kwenu kwangu ni dhaifuampaka apate haki yake kwa

Page 39: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

39

uwezo wa Mwenyezi Mungu.. nitiini kadiri nitakavyokuwa

ninamtii Mwenyezi Mungu na mtume wake, na nikimuasi

Mweneyzi Mungu na mtume wake basi musinitii.”

Na mfano mwengine ni sayidna Umar bin Khatab

(Mwenyezi Mungu amwie radhi) anamuandikia Abi Musa Al

ash ariy (Mwenyezi Mungu amwie radhi) barua ya kihistoria

kuhusu uongozi, anasema: “ baada ya hayo, hukumu ni jambo la

lazima lenye hekima na ni mwenendo wenye kufuatwa, elewa

pindi ukifikwa na jambo kuwa usiseme isipokuwa ya

kweli,fanya usawa kwa watu kwenye uso wako na kikao chako

na uadilifu wako na wala dhaifu asikate tamaa katika uadilifu

wako, na wala mwenye cheo asiwe na tama katika uadilifu

wako.

Sayidna Omar bin Al Khatwab alimuandikia kingozi wa Kufa

Abi Mussa Al ashary kwamba awafanyie usawa watu katika

hukumu, akamwambia: “ fanya usawa kwa watu kwenye kikao

chako na katika uso wako.” Akikusudia hata katika mwenendo

na uwapo nao na hata

unapowaangalia. Usimpokee mmoja kwa kumchukia na

mwengine kwa bashasha, au mwengine ukamuita kwa jina lake

la kawaida na mwengine kwa jina la ukoo na la kupanga, ili

Page 40: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

40

watu wasije wakawa na tamaa ya kusifiwa au madhaifu wasione

kuwa wanadhalilishwa bila ya haki yoyote.

Uadilifu ni kwa wote na kwa ajili ya kuhifadhi sheria

(kanuni) na kuinua taifa. Na kuhifadhi uongozi na hukumu. Ili

amani ya nafsi na utulivu wa jamii upatikane, kwani wasomi

wamesema: “ Hakina ya Mwenyezi Mungu huhifadhi nchi

yenye uadilifu hata kama ni ya makafiri na wala hainusuru nchi

yenye kudhulumu hata kama ni waumini.”

Na hatari kubwa inayokumbana na taifa lenye kumili ni ile

ya kuwepo makundi au vikundi vya madhehebu au ukabila

ambavyo hupata nguvu zake kwa kupitia nchi nyengine, kama

mfano tuonavyo kwa baadhi ya makundi ya kishia ambayo

hupata nguvu zake kutoka kwa Wafursi. Na kufanya uongozi

wa mwanzo na wa mwisho ni haki yao pekee na hujiimarisha

kwa kila hali.

Na la kushangaza kabisa ni kuona nchi ya Saudi Arabia

kutekeleza hukumu zake juu ya mwananchi wake na kisha

kujitokeza wanaowaunga mkono Wairani wakiingilia mambo

ya ndani ya nchi hiyo, na kufikia ujinga wa wafursi wa kisufi

hadi kuvunja mikataba ya kimataifa ya kuwahifadhi

wanadiplomasia, na hali ingekuwaje lau kama (Saudi

Page 41: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

41

Arabia) angefanya hukumu ya kumnyonga raia wa Irani?

Na je, yupo yeyote anayeingilia kati kama hivi juu ya nchi ya

Iran na upotefu wake dhidi ya nchi za kiarabu kwa kuwanusuru

madhehebu ya sunni katika Ahwaz na sehemu nyengine? Au

haya ni maonyesho tu ya Irani kuonyesha nguvu zake kwa ajili

ya kutaka kudhihirisha nyama zake za kutaka kueneza fitina

katika eneo la mashariki ya kati kwa ajili ya adui mayahudi na

ubepari wa majigambo wa kifursi?

Maana ya Usalama wa Taifa

Hapana shaka kuwa taifa lolote ili liwe na utulivu ni lazima liwe

na utulivu na usalama wa taifa. Na kila mwananchi awe na

pupa katika kuhakikisha usalama wa taifa, bila ya kusita na

hasa pale taifa linapofanya maamuzi, na hasa maamuzi ambayo

Page 42: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

42

yanahusika na utendaji wa ulimwengu wa nje au ambayo

yataathiri katika utendaji huu.

Iwapo usalama wa taifa lolote ni mstari mwekundu usiopaswa

kutengeukwa au kuupuuzia pasi na kuathiri kwa msitari huu

itapekelea kuwepo na ufahamu na elimu ya kuendelea ya

kuuelezea umuhimu wa usalama wa taifa. Ninaweza kusema: “

kufanya vipindi vya mara kwa mara kwa lengo hilo kwa kila

aliye na chezo au nafasi ya uongozi itakuwa ni jambo la lazima

sana na lenye msisitizo, kwa kuwa ujuzi wa fani, uendeshaji wa

idara na utendaji pekee hautofalia kwa ajili ya kuleta muono

ambao utapelekea kuelekea katika njia sahihi, na hii iwapo

hakuna muono mwengine mkubwa zaidi wenye athari ambao

utatekelezwa kwa asili ya usalama wa taifa.

Na wengi hawazingatii akilini katika yale maamuzi wayafanyayo

au wayasimamiayo yanayoshikamana na mahusiana ambayo

yanaweza kuleta athari katika usalama wa taifa. Inaweza kuwa

si kwa kukusudia isipokuwa kwa kutojua yanayohitajika katika

ulinzi wa usalama wa taifa, au yanayohitajika yakawa hayupo

kwa muhusika kwa kiwango kitakiwacho. Na kwa kipindi

ambacho taifa na eneo la Mashariki ya kati lilivyo, na

Page 43: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

43

ulimwengu unahitaji mwananchi wa kawaida ukiachana na

mtoa maamuzi kwamba awe na ufahamu wa usalama wa taifa

lake. Sawa atoapo maamuzi au kuweka mahusiano au katika

makubaliano na itifaki.

Na iwapo umuhimu wa kujua ni jambo kubwa litakiwalo na ni

la hatari kwa kule kushikamana kwake na usalama wa taifa na

kutafautiana kati ya mtu na mwengine kwa kuzingatia vielelezo

tafauti kama; utamadunim hima ya kutaka masilahi ya taifa,

kujali shida za taifa, na kuweka masilahi ya taifa mbele zaidi ya

kila kitu, hivyo jambo hili litapelekea:

a. Kuelimisha zaidi kuhusu usalama wa taifa kwa kupitia

vipindi vya mara kwa mara kwa kila kiongozi.

b. Kuzindua umuhimu wa usalama wa taifa na ulazima

wa kuulinda hasa kwa wanasiasa na wasomi na

waandishi na wataalamu na vyombo vya habari, na

hasa kwa wale wenye kumiliki uoni mkubwa wa elimu

juu ya fani hii. Na kuweka katika mazingatio yao kuwa

hili nalo ni moja ya yaletayo utulivu wa taifa.

Page 44: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

44

c. Ulazima wa kuwepo ushirikiano kwa vyombo husika

kabla ya kufanya makubaliano au itifaki pamoja na

vyombo vya nje, kwa kuzingatia isije ikatokea aina

yoyote ya uvujaji au athari zitakazoathiri masilahi ya

taifa hata kama itatokezea bila ya kukusudia.

Kwa kusisitiza ufahamu wa usalama wa taifa kwa nchi

yoyote itabidi pia kuzingatia hali ya kisiasa ya ndani na nje

na kimaeneo na kimataifa. Kutokana na kina chetu sisi

waarabu na kina chetu waafrika na ulimwengu wetu wa

kiisilamu pamoja na mahusiano yetu ya kimataifa yote hayo

inabidi yawekwe katika mazingatio wakati wa kuchukua

(kufanya) maamuzi muhimu na tendaji, pamoja na kusoma

upeo wa athari juu ya mahusiano hayo, na kujua faida zake

au hasara zake kwa pande zote, pamoja na kusoma yaliyo

muhimu na kumjuvya mwananchi uzito wa kila hatua

inayofanyika.

Hakuna shaka ya kuwa mahusiano ya kisiasa, kipolisi,

kiuchumi, kitamaduni, kifani na vyombo vya habari athari

zake zinaathiri wenyewe kwa wenyewe, kwa kuwa

haiwezekani kutenganisha kimoja na kuacha chengine,

Page 45: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

45

ilivyokuwa kila taasisi inajitegemea kama vile ni ulimwengu

uliojikamilisha. Hivyo basi, inabidi kwa kila taasisi kuzingatia

utendaji wake na kuchunga utendaji wa taasisi nyengine. Na

bila shaka jambo hili linahitaji hisia za kizalendo za hali ya

juu na utambuzi mkubwa na kufanya kazi sote kwa pamoja

kwa roho ya timu na kufahamu usemi kuwa “ ufahamu wo

wote na utendaji wa baadhi”, kwa kuhakikisha kila

muhusika anahusika ipasavyo juu ya kazi alizoachiliwa na

tahasusi yake anaifanya kwa kiwango cha uelewa kwa roho

ya pamoja (timu) na wote alionao, na kutoa maamuzi kwa

mujibu wa jambo husika.

Na kwa kuhakikisha kuwa taifa haliwezi kuendelea kwa

kuwa tu tuna nia njema bila ya kuwa na mipangilio na

uamko, katika ulimwengu ambao asiyejikinga na mbwa

mwitu basi ataliwa naye.” Sayidna Umar bin Khatab (Mungu

amwie radhi) anasema: “ mimi si mjanja na mtu mjanja

hawezi kunihadaa.” Na Mughira bin Shuuba alikuwa

akisema: “ lau kama si uisilamu basi ningelifanya vitimbwi

visivyowezekana katika bara arabu.”

Page 46: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

46

Na nia njema haina budi kuwepo ili matendo yakubalike,

Mwenyezi Mungu anasema: {Sema: Je, tukutajieni wenye

khasara mno katika vitendo vyao? 104. Ni wale ambao juhudi

yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani

kwamba wanafanya kazi nzuri.} na kwa ajili hiyo kurani

imesisitiza sharti za amana na utendaji bora kwa kuwa

zinatoshelezana, kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu anasema

kupitia ulimi wa mtoto wa nabii Shuaib (rehma na amani juu

yake) { Akasema mmoja katika wale wanawake: Ewe baba

yetu!Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumuajiri ni mwenye

nguvu na muaminifu.} na pia anasema { Yusuf akasema:

Nifanye mshika khazina za nchi.Kwani hakika mimi ni mlinzi

mjuzi.

Miji Mikuu, Mipaka na Ujenzi wa Taifa

Uhusiano kati ya miji mikuu na mipaka yake ni uhusiano wa

kukamilishani na si wa kugombana na wala haitakikani iwe

hivyo, kwa kuwa hakuna taifa lolote ambalo linaweza

Page 47: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

47

kujitosheleza kufanya kuwa mji mkuu ndio kitovu na kusahau

pande nyengine za taifa kwani bila ya mipaka taifa haliwezi

kusonga, isipokuwa tu mataifa mengi huifanya miji mikuu kuwa

ni kituo kikubwa walichokipa kipaumbele na mifano ya

kihistoria inaweka wazi ushahidi wa jambo hili. Isipokuwa kuna

tafauti kati ya mataifa yaliyoendelea na mataifa yasiyoendelea

katika kutoa umuhimu wa miji mikuu. Mataifa yaliyoendelea

haiwezekani kuzembea hata kidogo kuhusu hata kipande cha

ardhi, jengo au sehemu na kuiacha ikiharibika au kufanyia

uharibifu au hata fikira tu za kutaka kujitenga (kama ni

maeneo).

Mshairi mmoja alikwenda kwa Umar bin Abdul Aziz (Mungu

amwie radhi) akamsomea shairi akasema:

Iwapo unahifadhi unaowamiliki basi elewa

Wafanyakazi wa ardhi yako ni mbwa mwitu

Hawajaitikia wito wako uliowaita

Mpaka wapigwe viboko na kukatwa shingo

Na kwa kuwa ukuaji wa maeneo na sehemu za mipakani si

jukumu la serikali pekee au viongozi wa kisiasa, kwani hifadhi

na umuhimu pamoja na kazi za ukuzaji ni jukumu linalokusanya

taasisi zote za nchi, sawa na iwe taasisi rasmi au mashirika ya

kijamii, wafanyabiashara, watega uchumi, sekta za elimu, sekta

za afya, za ujenzi, za tamaduni, wizara ya wakfu, na wizara

nyengine na mashirika pia, pamoja na jumuiya za huduma za

kijamii.

Wote hawa inabidi watilie umuhimu mkubwa na hasa maeneo

ya mipaka. Na walipe kipaumbele na kuona kuwa ni suala

linalohusu usalama wa taifa kwa upande mmoja na la ukuzaji

kwa upande wa mwengine. Na inatakikana sote kwa pamoja

Page 48: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

48

tuyageuze maeneo ya mipakani iwe ni maeneo ya kuvutia na si

ya kukimbiwa. Na inapotokezea taifa kutojali maeneo haya basi

huwa ni nafasi kwa makundi kufika katika maeneo haya na

kufanya kambi zao na kusababisha msongamano usio wa

kawaida kwa vituo vya huduma za kijamii na kupatikana uwepo

wa ujenzi wa kiholela, na hata kusababisha kukuwepo kwa

maisha ya kitabaka, maradhi na matatizo mengine ya kijamii

ambayo yatahitaji udhibiti usio wa kawaida ili kuyatatua.

Ama kwa upande wa taifa kujali na kutoa umuhimu wa maeneo

haya ya mipakani kwa upande wa vitega uchumi, ni kule

kuweka huduma za lazima kwa wananchi wake: makazi, afya,

elimu, utamaduni, na huduma nyenginezo ambazo zinahitajika

kuendeleza maisha katika ardhi yao. Pamoja na kuwepo kwa

nafasi za kazi na uzalishaji. Hayo yote yatapelekea kwa

wananchi kuipenda ardhi yao (taifa lao) na kuhifadhi chembe

ndogo ya mchanga ili isipotee pamoja na kuwafanya wawe

wazalendo.

Na panapokuwepo kwa vivutio na ushajiishaji wa kazi katika

maeneo haya na kuwepo kwa vitega uchumi madhubuti kama

nchi inayotilia mkazo ilivyo hivi sasa katika maeneo ya Sinai,

Matruh na Ismailia mpya, Halayib, Shalatin na Wadi Jadid, na

maeneo mengine kama yale ya jangwani. Maeneo haya karibuni

yatabadilika na kuwa ya kuvutia. Kitu ambacho kitapelekea

kuwepo kwa ugawaji sawa wa kijiografia, kimakazi na pia

utawezesha kuwepo kwa maisha mazuri kwa wananchi wa

maeneo hayo. Na kupunguza msongamano wa utoaji wa

huduma kwa wakazi wa maeneo hayo, au kupatikana huduma

kama zile zipatikanazo katika miji sawa huduma za kisiasa au

za kiuchumi. Na kuwepo kwa vivutiaji vitakavyowezesha

kuvutia watalii na kuushangaza ulimwengu na kuonyesha

ukubwa na upevu wa wanachi wa ukuaji wao.

Page 49: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

49

Sinai Ndani ya Kurani Tukufu

Kurani tukufu imezungumzia kuhusu Sinai maneno ambayo

yanahitaji mazingatio, maelezo yanayotilia mkazo umuhimu wa

Page 50: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

50

eneo kwa upande wa kidini na kihistoria. Maelezo ambayo

yanatufanya tufikirie sana umuhimu wa eneo hilo, na ukuaji

wake na uwekezaji wake na mali asilia zake pamoja na alama

zake kwa upande wa kitalii, kidini kitabia nchi na kimatibabu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameuapia mlima Sinai ndani ya

kitabu chake kitukufu aliposema: {1 Naapa kwa mlima wa T'ur.

2 Na Kitabu kilicho andikwa. 3 Katika ngozi iliyo kunjuliwa. 4

Na kwa Nyumba iliyo jengwa. 5 Na kwa dari iliyo

nyanyuliwa,} (At tuur; 1-5). Na ametangulia kuapa kwa Tuur na

kuacha vyengine kutokana na umuhimu wake na nafasi yake

tukufu, si hivyo tu bali sura nzima imepewa jina na kuitwa

“sura at tuur”.

Na Mwenyezi Mungu anaapa kwa uwazi zaidi ndani ya kitabu

chake katika sura ya “At tiyn” aliposema {3 Na kwa mji huu

wenye amani! 2 Na kwa Mlima wa Sinai! 1 Naapa kwa tini na

zaituni!} (At tiyn;1-3). Na ametanguliza kuapia mlima Sinai

kabla ya kutaja mji wenye amani pamoja na kuwa ni mji wenye

utukufu mkubwa.

Kama ilivyoashiria Kurani Tukufu juu ya baadhi ya kheri na

neema zilizopo katika mlima Sinai, Mwenyezi Mungu anasema,

{ Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unatoa mafuta na kuwa

Page 51: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

51

kitoweo kwa walao.} (Al muuminun; 20) na kuhusu mti huu

Mtume wetu (rehma na amani zimshukie) anasema: “ kuleni

mafuta, na jipakeni nayo, kwani ni katika mti wenye Baraka.”

(Tirmidhy)

Na ndani mwake muna sehemu ya ardhi iliyobarikiwa na

imetajwa katika Kurani Tukufu Mwenyezi Mungu anasema kwa

kupitia mazungumzo yake na Mtume Mussa (rehma na amani

zimshukie) { Basi alipo ufikia aliitwa kutoka ng'ambo ya

bonde la kulia ni katika eneo lilio barikiwa kutoka kwenye

mti: Ewe Musa! Hakika Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mola

Mlezi wa walimwengu wote.} (Al qasas; 30). Na kuna jangwa

tukufu la Tuwa ambalo Mwenyezi Mungu amelieleza ndani ya

kitabu chake alipokuwa akizungumza na Mussa (rehma na

amani zimshukie) aliposema {Basi alipo ufikia akaitwa: Ewe

Musa! 12. Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu

vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T'uwa.} (Taha; 11-

12).

Eneo hili la Sinai ambalo Mwenyezi Mungu amelitaja maalumu

linapasa kuwepo ndani ya nyoyo zetu, na kulilinda na kujitolea

muhanga kwa ajili yake kwa kila tunachokimiliki.

Page 52: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

52

Hapana shaka ya kuwa jeshi letu kakamavu limevumilia kwa

ushujaa wa hali ya juu na limejitolea muhanga na halijaacha

kufanya hivyo kwa ajili ya kuhifadhi damu za wananchi wake

kwa ujumla. Pia kwa ajili ya kuihifadhi Sinai na kuisafisha

kabisa na makundi ya itikadi kali, kitu ambacho wanastahiki

pongezi na hongera kwa upande na kuwa safu moja yenye

nguvu na kutoa kila kinachobidi kwa ajili ya kuilinda kwa

upande wa pili, sawa iwapo hifadhi hii ni ya kimali au isiyo ya

kimali.

Na kwa jaribio letu la kuangazia upande wa kidini, na kitalii,

tabia nchi, kiustaarabu na kihistoria kuhusu kusini mwa mlima

Sinai tumeamua kama Wizara ya Wakfu ya Misri kufanya

mashindano ya kimataifa ya Kurani tukufu katika mji wa

Sharmi Alshaekh kwa kusaidiana na wizara ya Vijana na

Michezo na mkoa wa Kusini mwa Sinai pamoja na Taasisi ya

gazeti la Jamhuria ambayo itakuwa ni mmoja wa washirika

muhimu, na kundaa matembezi ya mandhari za kidini na

kiustaarabu, kihistoria na tabia nchi kwa kuwa Misri itapokewa

wageni kutoka mataifa mbalimbali ya ulimwenguni katika mji

wa At Tuur (Sinai) na Uyuun Mussa, na Saint Catherina na

Page 53: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

53

alama mandhari mengine. Pamoja na kuwaelezea umuhimu wa

maeneo haya kwa upande wa dini na kihistoria.

Na kwa kuwa mashindano ya mkwa huu yatakuwa na mtindo

mpya utakaukuwa wa aina mbili: Aina ya kwanza; mashindano

ya kuhifadhi kurani tukufu ya vijana chini ya umri wa miaka

kumi na mbili na, aina ya pili; ni mashindano ya kuhifadhi

kurani kwa wenye ulemavu kwa uchache juzuu tatu. Na

mashindano haya yanafanyika kwa kusisitiza kuwa mji wa Sinai

ni mji wa amani na utabakia hivyo kwa Uwezo wa Mwenyezi

Mungu. Na kwa kuwa upo moyoni na akilini mwa kila Mmisri

mwenye kuipenda nchi yake. Na kuhusu majaribio ya kuvunja

tamaa ya baadhi ya maadui hayatotuzuia tusiweze kuiendeleza

Sinai nakuijenga na kuihifadhi kwa mapenzi yetu yote na

kushikamana na ardhi yake, pamoja na kuwa macho katika

kuondosha kabisha chimbuko la ugaidi.

Na hapa ninahimiza kwa maimamu ambao watapata nafasi ya

kuongoza eneo la Sinai wafanye kazi kwa ajili ya kuondoa

shinikizo la kigaidi, kama ninavyohimiza kwa wale wote ambao

watakuwa na kazi ya kueneza wito (ulinganio) sawa wawe ni

kutoka katika wizara ya Wakfu ndani ya mkoa wa Kusini mwa

Sinai au kutoka katika sehemu nyengine ambazo zipo chini ya

Page 54: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

54

uangalizi wa Wizara ya Wakfu kuwa wafanye kazi zao kwa

mtindo wa kupishana.

Uhakiki Kati ya Marekebisho na

Ubomoaji

Page 55: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

55

Mwanzo kabisa hatuna budi kutenganisha kati ya uhakiki ulio mzuri na ule mbaya, Na kinyume chake ambacho ni ubomoaji. Maana ya neno la kwanza nalo limechukuliwa katika mfano ule wa kusema “ dhahabu na fedha zimesafishwa” ikimaanisha kuwa zimetenganishwa kati ya dhahabu / fedha nzuri na ile siyo nzuri. Na maana ya neno la pili likiwa na maana ya ubomoaji (maporomoko) ni kama kusema “mtu Fulani amefariki chini ya maporomoko: ikiwa na maana yupo chini ya mabaki ya nyumba iliyoyabomoka. Na neno uhakiki katika lugha lina maana mbili: ya kwanza: aibu, tusi na lawama, mfano kama alivyosema Abi Dardai (Mwenyezi Mungu amwie radhi) “ukiwatusi watu nao watakutusi na ukiwaacha nao watakuacha: ikiwa na maana iwapo utawatia aibu na lawamani nao pia watafanya hivyo, kwani iwapo kama una ulimi basi watu wana ndimi. Ama maana ya pili ni ile inayokusudiwa ya kupambanua kati ya jema na baya, inaweza kuwa ni kusifia na kupendezeshea na inaweza kuwa pia kukejeli na kutusi na inaweza kukusanyika ikakusanya yote mawili. Na uhakiki unaweza kuwa ni wa kibinafsi au wa kitabia, na unaweza kuwa ni wa kielimu na kimitaala na kimaudhui. Mfano

Page 56: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

56

wa uhakiki wa kibinafsi ni; kwa mfano kusoma makala au kusikiliza hotuba au neno au hadithi au kuona ubao ulochorwa na fanani na ukashangazwa nao bila ya kutaka kujua undani wa fani au kujua sababu za uzuri wake, na unaweza usishangazwe kwa kutotaka kujua undani wa fani ile ambayo kwa mtazamo wako haina kiwango cha uzuri. Ama kwa upande wa uhakiki wa kielimu na kimitaala na maudhui ni ule uliopo na uliosimamia misingi ya kielimu na kimaudhui na kifani na uhakiki wa namna hii unahitaji nguzo tatu kuu:- Nguzo ya kwanza: Zana zenye kuhusika na utengenezaji au fani. Mhakiki wa kazi za ufasihi anahitajika kujua sana lugha kwa mfano nahau, sarufi, elimu ya mashairi, elimu ya ufasaha wa usemaji, na elimu ya uhakiki, na fasihi pamoja na kujua baadhi ya elimu nyengine za kibinaadamu, kijamii, kisaikolojia, fani za historia , ustaarabu wa jamii na ujenzi na masome mengine kwa ujumla. Mhakiki wa mahesabu au wa kisiasa au wa fani au uchoraji hana budi kuwa na kiwango kikubwa sana cha misingi ambayo anataamali nayo. Kinyume chake atakuwa anafanya uhakiki wa kijuujuu tu na atahitajika kuwepo wa

Page 57: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

57

kumhakiki na wa kumkosoa pia, na pengine afikwe na kejeli kutoka kwa atakaemueleza vibaya na hata kumdharau. Nguzo ya pili: kwa mhakiki awe na utambuzi na ujuzi na umiliki, je huoni kuwa unaweza kusikia msomaji anasifia hutuba mbili nzuri zenye mvuto mkubwa au ukasoma vitabu viwili vya makala vya waandishi wakubwa ukawa una zana zote za ufahamu (inakusudiwa elimu kwa fani tafauti) au ukapata kuhakiki kazi za kielimu na kifani zilizo na ufanisi wa hali ya juu, isipokuwa unaweza ukapambanua kazi hizo kwa kitu chenye kufahamika lakini ikawa ni vigumu kuelezeka. Mfano kama alivyosema Al Amindiy: “ huoni kuwa unaweza kukutia farasi wawili wazuri wakawa na sifa zilizofanana kwa upande wa uhodari werevu na nguvu na uasili na ikawa kwa mwenye akili ni vigumu kuwapambanua, isipokuwa kwa wale wenye ujuzi wa farasi kwao ikawa wanaweza kuwatenganisha mmoja kutoka mwengine, vile vile mbao zilizochorwa kwa ustadi mkubwa na majengo yaliyojengwa kwa kiwango kwa wenye ujuzi ni rahisi kujua uzuri uko wapi na kasoro iko wapi kwa kuwa wanamiliki zana za utambuzi wa fani hiyo. Ama kuingilia tu fani ya uhakiki kwa wasio na ujuzi nayo na wala wasio miliki zana zake au hata kuisomea hili huwa ni

Page 58: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

58

tatizo kubwa ambalo huchelewesha na lisiloleta maendeleo na lenye kuharibu na lisilojenga na humpa sifa mbaya mhakiki kabla ya alichokihakiki. Nguzo ya tatu: nayo ni muhimu sana nayo ni kutenda kwa moyo wote na kujiepusha na matamanio na kusifika kwa watu, kwani kuingia katika matatizo na matamanio na kuacha kutenda yanayotakikana ni janga kubwa ambalo inapasa kujiepusha nalo. Hii ni kwa kuwa baadhi ya nyoyo ni gonjwa hazielewi isipokuwa njia ya ubomoaji pekee na kama alivyosema Imamu Ali Bin Abdiaziz Al jarjani katika utangulizi wa kitabu chake, kinachoitwa Alwasatwatu baina almutanabiy wakhusumuhu. Ametaja kuwa upungufu upo wa makundi mawili: kundi hufanya kwa ajili ya kurekebisha mapungufu yao na kuficha aibu, na jambo hili ni jema kwa kuwa mhakiki amejishughulisha zaidi na nafsi yake na kujaribu kujiweka katika nafasi nzuri. Ama kundi la pili ni la wale wenye mapungufu ikawa wamejikali ima kutokana na kushindwa au kwa hiyari yao au kwa udhaifu au kwa uvivu na hakuna kitu kinachowalazimisha wawe na mapungufu au kuweza kuhifadhi aibu zao kutokana na mapungufu hayo, na wakawa

Page 59: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

59

wanadhania kuwa na mwenendo huo kutawafanya waweze kunyanyuka na kupata vyeo vya juu. “ Na wengi wamefikwa na jaribio hili hata katika zama zilizotangulia ikawa wanachumia pato lao kwa kupitia sifa wanazosifiwa na maneno mazuri wanayopambiwa, na kujipatia pato kwa njia ya kusifiwa jambo hili lilikuwa ni maarufu tangu zama za kijahili kwani wapo waliojulikana kama chuo cha utunzi au cha uchumaji kupitia mashairi kwa mfano Zuheyri bin Abi Salma, Nabia Adhubiyan na wengineo, na wengine walijulikana kwa ufasaha hata mwanzoni mwa kuja kwa uisilamu kama Hutwaya ambae alikuwa akiwatishia watu kutokana na ufasaha wake wa kuweza kumsema mtu vibaya, mpaka kiongozi Umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) akamtishia sana pindi asipoacha kuhujumu tabia za watu, akasema: “ basi na wafariki watoto lakini nitanunua kutoka kwake (Hutwaya) heshima za watu kwa dirhamu elfu arobaini ili asije akamvunjia heshima yeyote. Na Hutwaya akaacha kuwakejeli watu kwa muda wa uongozi wa Umar kisha akarudia tena baada ya kufariki kwake. Haya yote hayawezi kutengeneza ustaarabu wa kweli au kuendelea kwa jamii yenye usawa ambayo inastahiki kusifiwa

Page 60: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

60

na pongezi za kweli, lakini uhakiki wa aina hii hubomoa. Na uhakiki wa kweli wa kimaudhui uliojengeka kwa misingi ya kielimu na ujuzi wa utaalamu na uadilifu huu ndio utakaojenga. Kwa mfano kusema kwa aliyefanikiwa: “ umefanikiwa” na kwa aliyekosea, kumwambia kwa heshima kuwa “umekosea na umepunguza. kwani huenda akajirekebisha na kuitafuta njia ilizo sawa. Na huu ndio uhakiki wenye malengo ambao haubomoi bali hujenga na wenye uadilifu na kushajiisha na wakati huohuo unaweka wazi pamoja na kutahadharisha. Na iwapo uongozi ni majukumu na ni amana basi kuhakikisha uhakiki na uchambuzi ni amana na majukumu vilevile. Nasi sote tutaulizwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kila mtu ataulizwa juu ya amana ambayo Mwenyezi Mungu amempa. Kama ambavyo tutaulizwa juu ya ujenzi wa taifa letu na kazi za uimarishaji wake na ukuaji wake kupitia njia za ujenzi na marekebisho na si kwa njia za uvunjaji na ubomoaji. Na si kwa njia ya kujinufaisha au kupenda kuonekana, kwa wengi wetu sasa wanaweza kutambua nini ngano na nini pumba. Na Mwenyezi Mungu anasema katika kitabu chake kitukufu: “Basi lile povu linapita kama takataka tu basi. Ama kinacho wafaa watu hubakia kwenye ardhi.

Page 61: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

61

Vyombo Vya Habari Vyenye Malengo

Page 62: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

62

Hapana shaka kuwa nafasi ya vyombo vya habari duniani ni

muhimu sana na tendaji kubwa na wala haiwezekani

kuvizembea na kuvipuuzia, na vyombo vya habari vyenye

malengo ni vile vyenye kujenga na sio vile vyenye kubomoa.

Na hakuna yeyote apingaye kuwa vyombo vya habari vya

kisasa vinapita katika mikondo tafauti, baadhi yake

vinajishughulisha na masuala ya kitaifa, vyengine vya kisiasa

sawa imechama tawala au upinzani, viko pia visivyomili upande

wowote au vya kuajiriwa na baadhi ni vya biashara na vyengine

ni vya kijamii na kibinafsi.

Na kila chombo kinapimwa kutokana na kazi zake zifanyazo

kwa jamii na kujiweka kwake katika kufuata misingi ya kikazi

na maadili ya kiutangazaji, na kuacha kumili pamoja na kujadili

mambo kwa kina na kwa mitazamo ya viongozi na waandishi

wake na wasomi wake pamoja na wahabari wake pia kuzingatia

ubora wa wafanyakazi wake katika fani hiyo.

Na nilazima kwa kila taasisi ya utangazaji au isiyo ya utangazaji

iwe na chombo cha uchunguzi ambao utachunga namna za

ubora wa wafanyakazi wake katika kila sekta zake, kitu

kitakachopelekea kuzidisha ufanisi na uwezo wake wa kuweza

kushindana na vyombo vya habari sawa viwe vya kitaifa au vya

Page 63: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

63

kimataifa. Na kikusudiwacho ni ufuatiliaji wa kweli wenye hisia

za kitaifa na dhamiri ya kikazi.

Na hapana shaka kuwa ulimwengu wa kimaarifa upo wazi zaidi

na una uwezo mkubwa wa kujipambanua, na kuweza kumjua

nani mwenye ujuzi wa kazi hii na nani asiye na ujuzi wa kazi hii

(ya utangazaji) kwa kuwa ni kazi yenye kuhitaji uwezo wa

kifikra na maarifa.

Na hakuna shaka kuwa taasisi za magazeti ya kitaifa yamesaidia

kwa kiwango kikuba katika kurekebisha mwenendo wa

utangazaji na ushirikiano wake wa kutoa huduma katika kujadili

masuala ya kitaifa. Na kuzifanya taasisi hizi kuwa na heshima

kubwa kwa wananchi kwa ujumla na kwa wasomi kwa

kuwahusisha wao pekee.

Na hapana shaka pia mikutano ya kiuchumi na ya kisomi

ambayo inafanywa na baadhi ya taasisi za magazeti makubwa

ni mojawapo ya shajiisho kubwa lenye kustahiki pongezi na

hongera. Vilevile kuzingatia masuala ya kisomi na uchambuzi

wa kina kwa kusaidia kuweka wazi sura na mitazamo. Na

pengine hata fikira zilizo nje ya sanduku kuziweka wazi mbele

ya watengenezao maamuzi.

Page 64: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

64

Pamoja na kuweka wazi tafauti kati ya uhakiki ambao

unakusudia kubomoa na uhakiki wa maudhui ambao huleta

nyongeza kubwa sana katika Nyanja za kisomi nakitamaduni na

kiidara na kiuchumi nacho ni kitu ambacho kinahitajika

tukikaribishe sote na kukishajiisha na tufaidike nacho. Na kuona

kuwa ni nyongeza isiyo na upungufu ilivyokuwa inachunga

misingi ya kazi na masilahi ya taifa.

Na kumiliki hisia za kutosha za kupanga mambo, na katika

mambo ya kuzingatia pia ni kuendesha mafunzo ya vizazi

virithishane . Na wale wenye ujuzi wa kazi wawafunze vijana

na kuwajuvya uhumimu wa kuwasiliana na mazungumzo yenye

kuendelea kati ya wahusika na waandishi wa habari

(wanahabari), na kuwepo na uhusiano uliokamilika wenye kuwa

na masilahi ya kitaifa pamoja na kuhakikisha umaridadi. Na

kama alivyosema mmoja wa waandishi wa habari” “

nimejifunza kutoka kwa walimu wangu kuwa ni afadhali

kuzikosa habari mia moja kuliko kupoteza ukweli wangu katika

kueneza habari moja kwa njia isiyo sahihi.

Hofu ya Kuzembea

Page 65: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

65

Taabira hii inamaanisha kuwa kuzembea ni jambo kubwa

mno kwani huhofisha mwili na roho pia, na si hivyo tu bali

inazidi mipaka ya kutia hofu ndani ya nafsi na kufikia hatua ya

umwagaji wa damu, kuteketeza mali za watu pengine hata na

heshima zao. Mambo haya yote yaweza kuwa kweli kwa bidii

katika kazi kwa ajili ya manufaa ya watu wote na nchi nzima.

Na lau kama tungeshikamana na hadithi ya mtume (rehma na

amani zimshukie juu yake) “nyote ni wachungaji na nyote

mutaulizwa juu ya mulivyovichunga..” (Bukhari) Mume ni

mchungaji wa nyumba yake na watu wake naye ataulizwa juu

ya aliowachunga. Mwalimu ni mchungaji kwa wanafunzi wake

na ataulizwa juu ya aliowachunga, mwalimu mkuu ni

mchungaji juu ya shule yake na ataulizwa juu ya

aliowachunaga, mkuu wa idara, mkurugenzi, mkuu wa sekta

wote hawa ni wachungaji na wataulizwa juu ya waliowachunga.

Katika sekta ya elimu, afya, usafi wa mazingira, kilimo, na

sekta nyenginezo lau kuwa tungeshikamana na hadithi hii basi

uzembe ungebadilika na kuwa mafanikio

Page 66: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

66

Nasi tunaomba juhudi zizidishwe ndani ya taasisi za kitaifa na

kuweka sheria kali za kupambana na ugaidi, tunataka sheria hii

iwabane wote wenye kuzembea na pia kuwazuia wahalifu. Na

lau kuwa nafsi ya wanadamu tumeipa nafasi yake na kuelewa

heshima hii ina thamani gani basi tusingelimwaga damu na wala

kuidhulumu si kwa kuzembea wala kwa kuiogopesha. Na lau

kama tungeelewa kuwa mali ni mali ya Mwenyezi Mungu na

mali zote kwa ujumla sawa iwe ya mtu binafsi ya umma

inapaswa kuhifadhiwa na kuitunza na ni amana iliyo katika

mikono yetu mwenye kuilinda na kuijali na kunufaika nayo, na

kuwa sisi tuna majukumu juu ya mali hizo na ya kuwa

hautanyanyuka mguu wa mja siku ya kiyama mpaka aulizwe,

basi tungelizihifadhi sawa ziwe mali zetu au za wenzetu.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu wenye kufanya

ubadhirifu kuwa wao ni ndugu wa mashetani akasema, {

Hakika wabadhirifu ni ndugu wa Mashet'ani. Na Shet'ani ni

mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi.} Israa,27. Sasa ni

vyema zaidi kujiepusha na kujiweka mbali na uzembe na

kuzembea kwani adhabu zake ni kali. Na Mtume (rehma na

amani zimshukie juu yake) amekataza kuwa nimemsikia huyu,

Page 67: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

67

nimemsikia Yule na kufuja (kupoteza) mali, pasipo na haki kwa

kufanya isirafu na kwa kuzembea.

Sisi tunahitajika kuondoa utamaduni wa kutojali sawa kama

itakuwa ni kwa njia kueleweshana na kwa mafundisho ya kidini

na kuhisi jukumu la taifa. Kwa upande wa sheria itahitajika

kuweka adhabu kubwa itakayokuwa ni fundisho kwa kila

afanyaye ufisadi katika ardhi, kwani kuzembea ni ufisadi na {

Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi }Al baqara 205.

Na kuna matukio ambayo baadhi ya watu watayaona kuwa ni

mepesi lakini ukweli yanahitaji kuchukuliwa tahadhari, na

yanaweza kusababisha hatari kubwa au tukio kubwa. Kuacha

taa za barabarani wakati wa mchana zinawaka huku ni

kuzembea na kupoteza nguvu ambazo tunazihitajia sana, nayo

pia ni kupoteza mali za jamii ambazo jamii inahitajia.

Pia kufanya isirafu katika kutumia maji na kuacha kutengeneza

njia za maji taka na kuacha na inawezekana kutengeneza kwake

ni rahisi sana ama madhara yake ni makubwa kwa mfano nyaya

za umeme zilizo wazi, au mashimo ya maji taka yaliyo wazi au

kutozingatia yanayopaswa kuangaliwa kwa mfano kuacha

kuangalia matairi ya magari breki zake, vioo vya pembeni na

Page 68: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

68

vya kuonea nyuma au kuacha vioo vya gari hali ya kuwa vina

ufa, na kuacha kuchukua tahari ipasavyo. Yote haya yanaweza

kusababisha hatari kubwa ambayo tungeweza kuepukana nayo

lau kama tungelijiepusha na sababu za kizembe na kutojali.

Na uzembe wa hali ya juu kwa mtu kuacha kile ambacho

Mweneyzi Mungu kampa akishughulikie, kwani jamii (taifa)

litamshitaki mbele ya Mwenyezi Mungu. Vyeo na uongozi wa

idara si burudisho la kitaifa na la kijamii – hakuna cha kufurahia

kwa wakati wowote – bali vyeo ni amana, na siku ya kiyama

itakuwa ni fedheha na majuto isipokuwa kwa yule aliyechukua

nafasi ya uongozi na kutekeleza amana hiyo kama itakiwavyo.

Athari za matatizo ya kuzembea zimezidi mara dufu na tishio la

mihadarati na vileo ambavyo vimeshafunika akili, na

kudhoofisha miili na kutuletea aina tofauti za kuzembea na

kutojali. Muhadarati ni mama wa madhambi kwani mtu pindi

akili yake ikatoweka na akawa anaenedelea na ugonjwa wake

huu hatoacha kutafuta mali kwa ajili ya kutaka kununua kwa

njia yoyote ile hata kama itakuwa ni kwa kufanya uadui kwa

jamaa zake wa karibu na hufikia hata kuua. Baadhi ya magazeti

na mitandao imeeleza kisa cha yule kijana muovu ambae

Page 69: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

69

amejaribu kutaka kumvunjia heshima mama yake mzazi mzee

kwa sababu akili yake haipo.

Na hatari hii kubwa inahitajika msimamo madhubuti wa

jamii nzima kwa ajili ya kupambana na kutojali na kuzembea na

wale wote wasiotekeleza majukumu yao. Uuzaji wa madawa ya

kulevya ni kitendo kidogo chenye kupelekea ufisadi mkubwa na

ni chanzo kikubwa cha kuharibu akili za vijana wetu na

mustakbali wa taifa letu. Hii, inahitajika kwa taasisi za kidini,

kitamaduni, kielimu na vyombo vya habari kuchukua jukumu

lake ipasavyo bega kwa bega na vyombo vya serikali, vya

uchunguzi na vya kimahakama. Na kufahamu ya kuwa

apotezaye akili yake basi hatari huwa kwa nafsi, heshima na

mali na daktari pengine katika kutibu atahitajika kukata sehemu

katika mwili kwa ajili ya kuhifadhi usalama wa roho yake. Na

mwanadamu anaweza kuwa mkali kwa baadhi ya wanawe kwa

ajili ya kuwahifadhi na kuwalinda na kuwalea malezi bora. Na

mshairi wa kiarabu anasema:

Haki ya taifa na haki ya jamii ni kuwa salama kwa namna zote,

na usalama tunaouzungumzia hauwezi kupatikana kwa upande

na kuachika katika upande mwengine, lakini kwa jamii nzima.

Page 70: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

70

Na itapendeza zaidi lau kama kila mtu atakuwa na pupa ya

kuheshimu usalama wa jamii, kwani kuna maelfu kama si

mamilioni ambao wananufaika na usalama, na kama

utadumishwa basi kuna wengine pia wataudumisha na kama

utazembewa na kila mtu akawa hajali basi uzembe utaenea

katika jamii, na wa zamani walisema “mtendee mwengine vile

upendavyo kutendewa”. Wakasema “fanya utakavyo, kama

ulivyokopa utalipwa.” Na kwa asiyejua masilahi ya nafsi yake

jamii italazimika kumsaidia kulijua hili na kumrudisha katia

uongofu, kwani Mwenyezi Mungu humuondoshea kitu sultani

kila si chomuondoshea msomi wa kurani.

Kisa Cha Masanamu na Ubomoaji wa

Ustaarabu

Page 71: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

71

Kwa kuanzia, hakuna muisilamu duniani mwenye kuabudu

sanamu. Au hata kuamini jambo hilo pia hata kulingani

kuabudiwa au kufikiria tu jambo hilo, si muisilamu tu mwenye

kuamini hivi lakini pia hata wale wa dini zilizoteremshwa.

Na iwapo uisilamu umekataza kutengeneza masanamu

mwanzoni mwa uisilamu basi hili lilikuwa kwa sababu mbili; Ya

kwanza. Watu walikuwa bado ni wapya katika uisilamu na

walikuwa wameacha kuabudu masanamu kwa muda mchache

(tangu kuingia kwao katika uisilamu) kwa kudhania kuwa

yanawaweka karibu na Mwenyezi Mungu mtukufu. Kama

iliyoeleza kurani tukufu kwa ndimi zao pale Mwenyezi Mungu

aliposema { Sisi hatuwaabudu ila wapate kutujongeza tu

kumkaribia Mwenyezi Mungu }.

Page 72: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

72

Sababu ya pili:Iwapo masanamu haya hutengenezwa

kwa ajili ya kuabudiwa au kutengenezwa kwake ni kwa ajili ya

kumfananisha na Mwenyezi Mungu. Na kati ya yenye

kuthibitisha hayo na kuwa tukiachilia mbali kuondosha

masanamu yaliyokuwa yakiabudiwa ndani ya Alkaaba kwa ajili

ya kuisafisha haikuthibiti kuwa kuna sahaba yeyote aliyevunja

sanamu au athari yoyote ile ya sanamu katika nchi yoyote

katika zile walizozifungua. Hii ni kwa kuwa walifahamu

malengo ya makusudio ya uisilamu ufahamu ulio sawa na wala

hawakusita kusimamia ufasiri wa aya kijuujuu.

Lakini waliangalia kwa undani zaidi juu ya makusudio na

malengo kwa dalili ya kuwa walijua madhumini ya aya, hata

sayidna umar (Mwenyezi Mungu amwie radhi) pale alipozuia

fungu la sadaka kwa wale wanaozoweshwa nyoyo zao katika

Page 73: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

73

uisilamu pamoja na kuwa imethibiti ndani ya kurani, Mwenyezi

Mungu aliposema { Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na

masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao,

na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika

njia ya Mwenyezi Mungu,) na alipoulizwa Umar( Mwenyezi

Mungu amwie radhi) iweje unasimamisha fungu ambalo Mtume

(rehma na amani zimshukie juu yake) alikuwa akilitoa?

Akasema: “ tulikuwa tukiwapa na uisilamu ni dhaifu na kwa

lengo la kuwazowesha lakini sasa Mwenyezi Mungu Mtukufu

ameupa nguvu uisilamu kwa fadhila zake kwa ajili hili fungu hili

halina kazi tena.

Na zaidi ya haya, alizuia kutimizwa hukumu ya wizi katika

mwaka wa njaa pale alipomwandkia mmoja wa wafanya kazi

wake, utafanya nini akikujia mwizi (mtu kaiba)? Akasema:

Page 74: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

74

nitamkata mkono wake.” Akasema: “ mimi akinijia mwenye

njaa basi nitaukata mkono wako.

Isipokuwa umma wetu wa kiisilamu umefikwa na mitihani

mikubwa akili za watu wake zikasimama wakaanza kuhalalisha

na kuharamisha bila ya elimu, ufahamu na wala kujua,

wakajidhatiti kwa nafsi zao na za wanafunzi na wafuasi wao

kwa yale wasiyo kuwa na elimu nayo kwa kutoa fatwa,

wakapotea na kupoteza wengine, pia kufungua mlango mpana

wa kuwapa mwanya watawala na mabeberu kufuta athari za

ustaarabu wetu sawa ustaarabu wa kiarabu, kiisilamu,

kikiristu, kifirauni, kiashuri, kibabeli, kiyunani, kirumi na

ustaarabu mwengine. Hii ni kwa kufuta utajo wa waarabu na

pia ustaarabu wake na ustaarabu wa kiisilamu na pia wa

kikiristu. Kwa kuwa wao ni wajinga wa tabia na

Page 75: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

75

wasio na dini na wala maadili. Kwao wao ni kufikia

malengo yao pasi na kutizama sababu na hata kama

kuangamiza wanadamu na majengo na kila kikavu na kibichi

pia hata kubomoa ustaarabu wa kibinaadamu.

Mbaya zaidi ni kuwa haya yanatendeka kwa jina la dini na

baadhi ya watu huidhania dini vibaya na kuona ni ya kiadui

kumbe dini ipo mbali sana na mambo haya. Na hata kama

watajidanganya wenyewe na kuwahadaa wahanga wao

(wafuasi wao) katika vijana wenye kujiunga nao kwamba wao

wapo sawa. Hao ni kama wale aliosema Mwenyezi Mungu

Mtukufu, {na kundi jengine limethibitikiwa na upotofu. Kwa

hakika hao waliwafanya mashet'ani kuwa ndio marafiki walinzi

badala ya Mwenyezi Mungu, na wanadhani kuwa wao

wameongoka} na anasema {Sema: Je, tukutajieni wenye

khasara mno katika vitendo vyao? 104. Ni wale ambao

Page 76: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

76

juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao

wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri} {. Na katika

watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya

kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi

Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye

mkubwa wa ukhasimu. 205. Na anapo tawala hufanya

juhudi katika nchi kwa kufisidi humo na kuteketeza mimea

na viumbe. Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.}

Na kiongozi mkuu wa Al Azhar Profesa Ahmad Al-Twayib

amesisitiza kama alivyosisitiza waziri wa wakfu na Dar Al-Iftaa

ya Misri, kuwa haifai kuharibu alama hizi za ustaarabu kwa

namna yoyote ile sawa iwe kwa kuzivunja, kuziharibu

mkuziuza, kuziiba au kuzibomoa na kuziharibu ni sawa na

kuharibu ustaarabu wa mwanadamu.

Na katika jambo lenye kuhitaji mazingatio na lenye kuleta hisia

na mshangao na kuleta masuala mengi ni msimamo wa nchi

za magharibi na mashirika ya kimataifa juu ya kimya chao

Page 77: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

77

kikubwa juu ya makosa haya ambayo lau kama yangelitokea

sehemu yoyote hapa ulimwenguni ukiachilia mbali eneo la

mashariki ya kati (ukanda wa kiarabu) basi ulimwengu wote

ungelijua. Basi hii ndio tabia ya maadui zetu ambao

wanatushajiisha katika vita visivyo vya sheria, na lenye kuuma

zaidi ni zile Fatwa ambazo hutilia mkazo matendo ya aina hii,

hivyo basi tunahakikisha na kuthibitisha tena na tena kuwa

kuna haja

kubwa ya kuweka sheria ambazo zitazingatia utoaji wa

Fatwa kwa kutolewa na wale tu wenye ujuzi nazo na si

wengine.

Page 78: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

78

Kati ya Utendaji Bora na Utii

Pindi nchi ikiwa na uetndaji bora pamoja na utiifu, utiifu

wa kazi, utendaji bora wa kazi na sehemu afanyayo kazi mtu

basi jambo hili huwa ndilo litakiwalo. Ama ikiwa ni utendaji kwa

ajili ya mtu Fulani au kundi Fulani au hata chama Fulani basi

jambo hili huwa ni la kujiweka rehani kwa kutumia utendaji

nalo huwa ni hatari sana, sawa kwa kipimo cha sheria au kwa

Page 79: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

79

kipimo cha taifa. Utendaji bora na utiifu ni mambo mawili

yaliyoshikamana pamoja na wala hayatengani. Mtume wetu

(rehma na amani zimshukie juu yake) anasema: “ yeyote

mwenye kumtumia mtu juu ya kundi naye akawa anatambua

kuwa (kufanya hivyo ni) kumtumikisha, basi atakuwa

amemfanyia khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume wake na

waisilamu wote.” Na uongozi uwe wa aina yoyote sawa uwe

mkubwa au mdogo huwa ni amana na huhitajika ufanisi na

utendaji bora. Mwenyezi Mungu anasema kwa ulimi wa mtoto

wa nabii Shuayb (rehma na amani juu yake) kuhusu Mtume

Mussa (rehma na amani juu yake): { Akasema mmoja katika

wale wanawake: Ewe baba yetu!Muajiri huyu. Hakika mbora

wa kumuajiri ni mwenyenguvu na muaminifu.} uaminifu pekee

hautoshi pia na elimu pekee haitoshi ,Abu dhari alipomtaka

Mtume (rehma na amani zimshukie) ampe uongozi, mtume

Page 80: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

80

(rehma na amani zimshukie) akamwambia: “ ewe Aba dhari

wewe ni dhaifu uongozi ni amana na siku ya kiaya ni fdheha

na majuto isipokuwa kwa atakaeuchukua kwa haki na

kutekeleza yapasayo.” Na Mtume akawapa uongozi wa

kuongoza jeshi Khalid bin Al-Walid na Amru binAl- A`s na

wengineo pamoja na kuwa walisilimu muda mchache sana

kutokana na utendaji wao na ujuzi wa fani za kivita na

mazingira ya mapigano na malumbano.

Ama utendaji wa ubinafsi huturudisha katika miaka ya

kiza iliyokuwa makabila na watu maalumu ndio wakiongoza

kupitia utiifu wa watu maalumu na kuacha kutii wengine. Pia

huturudisha katika kipindi ambacho ufisadi ulienea katika idara

zote na hadi hivi sasa bado tunaendelea kupata athari zake,

kwani ilikuwa hutangulizana wenyewe kwa wenyewe na baadhi

Page 81: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

81

ya wanafiki na wenye kusifiana wenyewe kwa wenyewe na

wale wenye kuamini njia ya ulaji rushwa kuwa ndio njia pekee.

Dhuluma na uvunjaji moyo zikawa ndio vilivyopo na kusitiriana

pamoja na kujiweka mbali na utendaji wa unaostahiki na ikawa

wanafichiana aibu zao, pamoja na kuhakikisha kuwa kile

walichokitoa katika mali (kipindi cha kampeni) wanahakikisha

kuwa kinarudi tena mifukoni mwao kwa njia yoyote. Hivyo, vita

kuu ya raisi ni kupambana na ufisadi na mafisadi wote na

kung`oa ufisadi kabisa kutoka katika mashina yake.

Hapana shaka kuwa utiifu kwa wale wapandao mabega

ya watu watii kwa njia zisizo za kisheria wala za kikanuni hawa

huwa hawaelewi zaidi ya kuwanufaisha wakubwa wao pekee

hata kama ni kwa kuitumia dini yao na dhamira zao watafanya

hivyo kwa masilahi ya pande zao na kuacha masilahi ya taifa.

Page 82: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

82

Na hapana shaka kuwa hawa wenye kujitakia manufaa ya

nafsi zao hawawezi katu kulinufaisha taifa na wala taasisi kwa

amana ya aina yoyote. Kwa kuwa hawastahiki na wala hawana

shime ya kutekeleza uamnifu, isipokuwa kwa nafsi zao zilizo

na chuki kwa kuwatendea wale walio na utii. Na wala

haiwezekani kuwakosoa au kuwaingilia kwa lolote katika

matendo yao au hata kuwasahihisha ukosefu wa matendo yao.

Na katika kosa kubwa sana lililofanywa na chama cha

kisiasa cha kiisilamu ni kule kuwahadaa watu kwa mtazamo wa

nje na kuitumikisha dini kwa juujuu na kufanya kuwa

kujilazimisha kuitendea dini katika baadhi ya mambo ni

sehemu ya uongozi bali pia ni shuruti muhimu na mambo ya

lazima kufanyika. Watu wengi walotii kundi la kisiasa la kidini

wakawa ndio wengi waliopata vyeo, unaweza muona yule

Page 83: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

83

ambae jana hakuwa akijua kitu chochote katika dini leo hii

keshapata nafasi kubwa na hatari sana ya uongozi. Cheo

ambacho hana iuhusiano unacho wala ujuzi nacho. Na mfano

mkubwa ni yale yaliyotokea katika Wizara ya Wakfu ya Misri

pale kilipotawala chama cha Kigaidi. Waliwaweka watu wasio

na ujuzi wowote kwenye wizara hiyo wala katika idara zake ili

tu ionekane kuwa kundi hilo ndilo lenye kuongoza. Na si

katika wizara ya wakfu pekee bali pia khiyana ilienea katika

vyombo vya dola kwa mfano bei kupanda na uroho wa kutaka

madaraka.

Na utengwaji pengine historia ya nchi haijawahi

kushuhudia namna hiyo isipokuwa baada ya kutawala kundi hili

uongozi wa taifa, kitu ambacho kikapelekea kuanguka kwao

kukawa ni kukubwa historia ya karibuni haijawahi kuona tukio

Page 84: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

84

kama hilo na kuweka wazi ukweli wao mbele ya ulimwengu

wote. Kitu ambacho kinatupa uhakika kuwa mwisho wa kundi

hili kuwa limeitumia dini kama biashara na kuiweka katika

mnada ulio rahisi, na lilikuwa likiwadanganya watu kwa muda

mwingi mpaka Mwenyezi Mungu akafichua mambo yao, kila

mtu akaelewa ubaya wa nia zao, na pole za wale

wanaowatetea hazikusaidia kitu.

Na juu yetu kukunufaisha kwa kukuweka mbali na utiifu

usio wa kweli na wa uongo na usiokubalika kisheria na taifa.

Na kuwapa wenye kustahiki kulisimamia jambo hili kwani

wakati tulionao unahitaji nguvu madhubuti za mwenye ujuzi na

mpenda nchi.

Mfano Mzuri wa Kugawanya Mali ya

Page 85: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

85

Zaka

Hapana shaka kuwa iwapo zaka itagaiwa kama itakiwavyo

kisheria basi itaziba pengo kubwa la mahitajio ya mafakiri na

wenye shida sana na masilahi ya taifa zima. Pindi nafsi za

matajiri na wenye uwezo wakifanya ukarimu na kutenda

wajibu wao wa kuwalisha wenye njaa, kuwavesha wasio na

nguo, kuwatibu wagonjwa, kuwasaidia wenye kuhitaji na kutoa

mchango wa kuboresha na kudumisha kwa taifa basi ni lazima

nchi ibadilike. Na hapatakuwa na raia ambaye atakuwa

anahitajia na kuomba, imamu Ali (mwenyezi Mungu amwie

radhi) anasema: “Hakika ya Mwenyezi Mungu Mtukufu

amegawa chakula cha masikini katika mali za matajiri, na katu

masikini hatokuwa na njaa isipokuwa tajiri atakuwa ameshiba,

na akipatikana masikini mwenye njaa, tambua kuwa pana tajiri

dhalimu na hakutoa haki ya Mwenyezi Mungu katika mali yake,

na hakutekeleza wajibu wake kwa upande wa jamii yake.”

Na iwapo (tajiri) ataekeza vitega uchumi kwa njia sahihi kwa

ajili ya masilahi ya taifa lake jambo hili litapelekea kuinuka

kwa taifa letu zuri kama itakiwavyo. Bali pia huenda manufaa

Page 86: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

86

yakaenea katika nchi nyengine nyingi za kimasikiniambazo nasi

tunahitajika kuzisaidia kwa mfano wa nchi za mto wa Nile

ambazo inatubidi kuwa na mawasiliano nazo na kusaidiana

kielimu, kitamaduni, kimanufaa na kiutu kwa kiwango cha

kiserikali na cha kiraia na kwa taasisi zake za kitaifa ambazo

tunaweza kufanya vitega uchumi vikubwa na imara katika nchi

hizi na nyenginezo katika nchi za Afrika zilizo na umasikini,

kama ni mojawapo ya mbinu na himaya ya usalama wa raia

wetu. Na kwa jambo hili kuna mifano mingi inyoshukuriwa

kwa upande wa taasisi za kiraia.

Page 87: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

87

Zaka ni Haki ya Lazima Katika Mali

Nasisitiza juu ya ukweli, na wa kwanza ni: hakika ya zaka ni

hali ya lazima katika mali na ni nguzo kuu kati ya nguzo za

kiisilamu mfano wa sala na funga bila ya kutafautiana, na

Sayidna Abdallah Ibn Abbas (Mwenyezi Mungu awawie radhi)

amesema: “Vitu vitatu ndani ya kurani tukufu vimeteremshwa

kwa kuambatanishwa sambamba na vitu vitatu (vyengine)

kimoja wapo hakikubaliwi bila ya chengine, navyo neno lake

Mwenyezi Mungu “Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtiini

Mtume wake.” Na neno lake, “Na Simamisheni sala na toeni

zaka” mwenye kuacha kutoa zaka pamoja na kuwa anajua

kama ni lazima basis ala yake haitomnufaisha kitu mbele ya

Mwenyezi Mungu. Na neno lake, “na unishukuru mimi na

wazazi wako wawili na kwangu ni marejeo.”

Asiyewashukuru wazazi wake wawili kwa wema wao na

matendo mazuri yao basi pia hatomshukuru Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema kuhusu wanaoweka hazina za mali

na kujizuia na utoaji wa zaka {Na wanao kusanya dhahabu na

fedha, wala hawazitumii katika Njia yaMwenyezi Mungu,

Page 88: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

88

wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu. 35. Siku zitapo

tiwa moto katika Moto wa Jahannamu, nakwazo

vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao namigongo

yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mlio jilimbikia nafsi zenu,

basi onjeni mliyo kuwamkilimbika. }

Jambo la pili: hakika uisilamu umetoa wito wa kutoa sadaka

kwa wingi, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema { Mfano wa

wanao tumia mali zao katika Njia yaMwenyezi Mungu ni

kama mfano wa punje moja iliyochipuza mashuke saba.

Katika kila shuke zimo punjemia. Na Mwenyezi Mungu

humzidishia amtakaye, naMwenyezi Mungu ni Mwenye

wasaa na Mwenye kujua.} ( Surat Albaqarah.Aya,261). Na

Mtume (rehma na amani zimshukie juu yake anasema) “ mali

haipungui kwa kutoa sadaka.” Na anasema: “sadaka bora ni

ile uitaoyo hali ya kuwa ni mzima kabisa, unataraji utajiri

na kuogopa umasikini, usiicheleweshe hadi pale roho

inafikia kooni kasha ndio unasema, Fulani apewe hiki na

Fulani hiki na ilikuwa kwa Fulani (hiki) na ilikuwa kwa

Fulani (hiki).” Na pia anaendelea kusema: “hakuna siku

isipokuwa malaika wawili huita na mmoja wao husema

“ewe Mola mpe kila atoe (mpe) ziada, ewe Mola mpe kila

Page 89: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

89

ajizuiaye uharibifu.” Na anasema Mwenyezi Mungu

Mtukufu:{ Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya

Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanao fanya

ubakhili. Na anaye fanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili

mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio

wahitaji. Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu,

nao hawatakuwa kama nyinyi}. ( Surat Mhammad,Aya 38) .

Huondosha na kutibu mwanya:

Hapana shaka kuwa mwanya utakuwa ima katika vyombo

(taasisi) vyenye kutoa zaka au vyenye kupokea zaka au

vyombo vyenye kuunganisha na sawa iwe ni mtu, jumuiya au

taasisi.

Mwanya unaopatikana kupitia vyombo vitoavyo zaka itakuwa

ima kwa kutotoa hiyo zaka kabisa, au kwa kuipunja au itakuwa

inatolewa lakini si kwa umakini kwa wahusika wake.

Hivyo basi, ni wajibu kuzingatia katika hutuba za dini juu ya

ulazima wa kutoa zaka na umuhimu wake na madhambi

makubwa ayapatayo mwenye kuzuia kutoa zaka mbele ya

Mwenyezi Mungu, pamoja na kusisitiza ya kuwa tajiri

hatoepukana na dhima yake kwa kuitoa mali yake kiholela. Na

baadhi ya wasomi wa elimu ya sheria wameona ya kuwa iwapo

Page 90: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

90

tajiri amempa mali yake kwa anayedhania kuwa ni masikini

kasha akaja kuelewa kuwa si masikini basi itamlazimu kutoa

tena zaka. Ni wajibu wake ahakikishe kuwa anatoa kwa mujibu

wa sheria na kwa amana na kwa uchunguzi na kwa vyombo vya

kisheria ambavyo hupewa zaka ili dhima yake iondoke mbele

ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ili zaka yake ilete matunda

mazuri ambayo yanapatikana kwa utoaji wa zaka.

Na mwanya upatikanao kwa upande wa mpokeaji, unakuja

kutokana na udhaifu wa ugawaji kwa baadhi ya wenye nia

mbaya za kutaka kujilimbikizia mali kwa njia yoyote hata kama

ni kwa kulaghai. Ni wajibu wetu kuwakumbusha muongozo

sahihi wa kiisilamu na utu wa kibinaadamu ambao unakataza

kwa mwenye uwezo kulaghaia na kujidhalilisha. Mtume

(rehma na amani zimshukie juu yake) anasema “haifai kuomba

isipokuwa kwa Yule mwenye ufakiri uliopindukia mipaka,

au mwenye madeni makubwa, au mwenye damu ya

maumivu ”. Na anasema; “Mwombaji ni kama pambo

ambalo mtu hujipambia usoni mwake, akitaka huliacha

usoni mwake na akitaka huliondoa.” Na ima Ali (radhi za

Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) anasema;

Page 91: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

91

Ni afadhali kubeba kima cha jabali * kuliko kufadhiliwa na

watu

Watu hunambia kazi ni aibu * nami huwambia “aibu ni kuomba

watu”

Na Mtume wetu (rehma na amani zimshukie juu yake) anasema

“ katika mambo ambayo watu waliyapata kutokokana na

maneno ya utume ya mwanzoni ni kuwa, usipokuwa na

haya basa fanya utakacho.”

Lazima tuhakikishe ya kuwa uisilamu umekataza kuomba pasi

na sababu ya msingi, na mtu mwenye heshima hawezi

kuishusha nafsi yake kwa kuomba, na mkono wa juu (utaoa) wa

juu ni bora kuliko wa chini (usiotoa). Pamoja na kuhakikisha

umuhimu wa kufanya kazi na thamani yake na msisitizo wa

uisilamu juu ya kazi. Na kuweka wazi ya kuwa anayekwenda

mbio kwa ajili ya wajane na masikini ni sawa na apiganiaye

jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na mbora wa watu ni

Yule alaye kwa mkono wake na si kwa kuomba kwa wengine.

Ama kwa upande wa mwanya wa tatu: ni ukusanyaji na

ugawaji, pamoja na imani yetu kwa baadhi ya taasisi za kijamii

kuwa zinapunguza mzigo mkubwa kwa mafakiri na wasi na

uwezo sawa kwa upande wa kuwapa mahitajio kwa kupitia

Page 92: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

92

vitega uchumi na hasa kwa upande wa matibabu, isipokuwa

nionavyo kuwa taasisi hizi zinahitaji yafuatayo:-

A. View chini ya uangalizi wa vyombo vya kiserikali, na

vyombo hivi viwe vinafutilia na kuchunguza ipasavyo, na

kuwe na uwazi wa kutangaza uwezo wake, mahitajio

yake na mafao yake pamoja na kuwaongoza katika

utendaji wa kiidara kadiri wawezavyo.

B. Kuwe na ramani ya wazi juu ya taasisi hizi, na upeo

wake wa kijiografia na utendaji wake, ili ijulikane

mipaka yake na kikomo chake na isije ikatokezea

kupatikana uzembe kwa baadhi ya sehemu pengine

zingelikuwa zinahitaji msada mkubwa zaidi.

C. Kuwe na idara ambayo itashughulikia taasisi hizi kwa

mfano Wizara ya Ushirikiano wa jamii. Kuwe na

kiunganishi chenye kuwaunganisha watoaji na wapokeaji

na taasisi za kijamii kwa mwelekeo wake wa kijiografia

au mwelekeo wa kihuduma, ili pia wahusika wajulikane

na iepukane kutowafikia walengwa halisi wanaohitajia

zaka.

D. Malengo na madhumuni yawe wazi yajulikane kwa wote,

au kila chombo au jumuiya ijulikane ina dhumuni gani

Page 93: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

93

iwapo ni kuwalisha wasio na uwezo au kuwatibu

wagonjwa, kulipia madeni ya watu, nahyo haya ni

miongoni mwa malengo wanayoyaendea mbio Wizara ya

Wakfu ya Misri.

Baina ya Matumaini na Kazi

Maisha yamejaa matumaini. Hakuna kukata tamaa

maishani. Na wala maisha hayawi pamoja na kukata tama. Na

mwenye akili hupata jibu kwa kila jambo gumu au kwa uchache

huwa anajaribu kufanya hiyo. Na mjinga huwa anaona katika

kila suluhisho lina msongo (fundo) uliokamatana. Basi huwenda

jambo lililo sahihi kisheria haiyumkini kupingana na usahihi wa

akili kwani sheria zote zinaelekea kuwa ni kwa masilahi ya

watu. Basi wanachuoni wanachukulia kuwa kukata tamaa na

kukatisha tamaa ni kutoka katika rehema ya Mwenyezi Mungu

Page 94: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

94

Mtukufu na ni miongoni mwa madhambi makubwa. Basi

kutoka kwa Ibn Abaas R.A. anasema kwamba mtu mmoja

alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni yapi Madhambi

makubwa? Mtume S.A.W. akasema: Kumshirikisha Mwenyezi

Mungu na kukatia tamaa kwa Nguvu ya Mwenyezi Mungu, na

kukata tamaa kwa rehema za Mwenyezi Mungu, aliyelindwa na

Mwenyezi Mungu kwa mambo hayo na kuepushwa nayo

nimemuhakikishia kuingia peponi.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema kwa ulimi wa

Bwana wetu Ibrahim (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu

yake) katika mazungumzo yake pamoja na Malaika

waliombashiria Ishaq (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu

yake): {Akasema: "Oh!" Mnanipa khabari hii, na hali yakuwa

uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanipa khabari njema

hivyo?" (54) Wakasema: "Tumekupa khabari njema iliyo haki;

basi usiwe miongoni mwa wanaokata tamaa." (55) Akasema:

"Na nani anayekata tamaa ya rehema ya Mola wake isipokuwa

wale waliopotea?" [AL HIJR 54-55-56]

Na huyu ni Yaaqub (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu

yake) anawaambia watoto wake: {"Enyi wanangu! Nendeni

mkamtafuta Yusuf na nduguye na wala msikate tamaa na

Page 95: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

95

rehema ya Mwenyezi Mungu. Hawakati tamaa na rehema ya

Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri"} [YUSUF 87].

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema; {Sema, "Enyi

waja wangu mliojidhulumu nafsi zenu! msikate tamaa na

rehema ya Mwenyezi Mungu, bila shaka Mwenyezi Mungu

husamehe dhambi zote; hakika yeye ni mwingi wa kusamehe

(na) mwingi wa kuehemu."} [AZ ZUMAR 53].

Basi mwenye dhambi asikate tamaa kwa usamehevu,

kwani Mwenyezi Mungu alifungua wazi mlango wa toba, na

katika Hadithi ya Qudisi kwamba Mtume S.A.W: asema "Ewe

mwanadamu! Wewe ukiniomba na ukinitarajia Mimi

nikakusamehe madhambi yako na sisiti, ewe mwanadamu

ukinijia kwa kiasi cha ardhi makosa lakini hunishirikii na kitu

cho chote basi tutakupa msamaha kiasi chake" [Imetolewa na Al

Tarmiziy].

Na mgonjwa hakati tamaa kwa kutopona hata kama

ugonjwa wake ni mkali kabisa, basi lazima atafute njia ya

kujitibu, pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu katika

uponyaji, na sisi tuna mfano wa Ayyubu (amani ya Mwenyezi

Mungu iwe juu yake), Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

{Na (mtaje) Ayyubu alipomwita Mola wake (akasema) "Mimi

Page 96: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

96

yamenipata maradhi, nawe ndiwe unayehurumia kuliko wote.

(83). Basi tukamkubalia (wito wake) na tukamwondolea

ugonjwa aliyokuwa nao, na tukampa rehma yeye na watu wake

na mfano wao pamoja nao. Ni rehemu inayotoka kwetu, na

ukumbusho (mzuri) kwa wafanyao ibada.} [AL ANBIYAA 83-

84].

Na kama ulikuwa tasa huzai, basi usikate tamaa kwa

rehema ya Mwenyezi Mungu mwingi wa utoaji. Basi

mwangalie huyu ni mke wa Ibrahimu (amani ya Mwenyezi

Mungu iwe juu yake) alipobashiriwa mtoto na Malaika ingawa

umri wake ulikuwa mkubwa, anasema: {(mkewe Ibrahimu)

akasema: "Ee Mimi we! Nitazaa na hali mimi ni mkongwe, na

huyu mume wangu ni mzee sana? Hakika hili ni jambo la

ajabu." (72). Wakasema (wale Malaika): "Je, Unastaajabu amri

ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka

zake juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye

(Mwenyezi Mungu) ndiye anayestahiki kusifiwa na

kutukuzwa"} [HUD 72-73].

Na Zakaria (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake)

alipomwomba Mola wake basi akasema: {Akasema: "Mola

wangu! Bila shaka mifupa yangu imekuwa dhaifu na kichwa

Page 97: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

97

kimejaa mvi, wala sikuwa mwenye bahati mbaya, (mwenye

kuhasirika, Mola wangu, kwa kukuomba wewe." (4). "Na

hakika mimi nawahofia jamaa zangu baada yangu (kuharibu

dini). Na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi (anijie) kutoka

kwako."} [MARYAM 4-5]. Jibu lilimjia kutoka kwa Mola

wake kwa haraka... {(Akaambiwa) "Ewe Zakaria! Tunakupe

habari njema ya (kuwa utazaa) mtoto, jina lake ni Yahya:

Hatujafanya kabla yake aliye na jina namna hilo.} [MARYAM

7].

Na Zakaria (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake)

alipoulizia: {Akasema (Zakaria) "Mola wangu!) Nitapataye

mtoto, na hali uzee umenifikia, na mke wangu ni tasa?"

Akasema: (Mwenyezi Mungu) "Ndiyo vivyo hivyo; Mwenyezi

Mungu hufanya apendavyo."} [AALI IMRAN 40]. Basi jibu

lilimjia: {Akasema: "Ni kama hivyo. Akasema Mola wako.

"Haya ni sahili kwangu. Na kwa yakini Nilikuumba zamani

nawe hukuwa cho chote.} [MARYAM 9].

Na kama ulikuwa masikini, basi jua! kuwa fakiri wa leo

labda atakuwa tajiri wa kesho, tajiri wa leo pengine atakuwa

fakiri wa kesho, na siku huzunguka, na kwamba Mwenyezi

Mungu Mtukufu atakapo jambo kwa mja hulipitisha: {Hakika

Page 98: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

98

amri yake anapotaka cho chote (kile kitokee) ni kukiambia

"kuwa" basi mara huwa.} [YASIN 82]. Na Mwenyezi Mungu

Mtukufu anasema: {Rehema Anayoifungua Mwenyezi Mungu

kwa watu, hakuna wa kuizuia na Anayoizuia hakuna wa

kuipeleka mbele (isipokuwa Atake) Naye ni Mwenye nguvu,

Mwenye hikima.} [FATIR 2].

Na hata nyakati za hasiri zinapokuwa na ugumu katika

maisha yako basi ushikamane na kamba ya Mwenyezi Mungu

Mtukufu. Basi huyo ni Maryam (amani ya Mwenyezi Mungu

iwe juu yake), dunia ilipoingia giza machoni mwake na

hakupata kimbilio kutoka kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa

kwake akasema: {Akasema: "Laiti ningekufa kabla ya haya, na

ningekuwa ni mwenye kusahaulika kabisa.} [MARYAM 23].

Basi msaada na rehema zilikuja kutoka kwa Mwenyezi Mungu

Mtukufu katika kauli yake: {Mara ikamfikia sauti kutoka chini

yake (inamwambia): "Usihuzunika! Hakika Mola wako

Ameweka kijito cha maji chini yako." (24) "Na litikisie kwako

shina la mtende huo, litakuangushia tende nzuri, zilizo mbivu."

(25) "Kisha ule na unywe na litue jicho (lako) (furahi, pumua

moyo wako). Na kama ukimwona mtu yoyote (anataka

kukuuliza habari ya mtoto huyu), sema: "Hakika mimi

Page 99: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

99

nimeweka nadhiri ya kufunga kwa ajili ya (Mwenyezi Mungu)

Mwingi wa rehema, kwa hivyo leo sitasema na mtu."}

[MARYAM 24-25-26].

Na wale waislamu katika vita vya Ahzabu; mushrikina

waliwazingira kila upande, lakini ushindi uliwajia ambapo bila

kutegemea kama vile Quraani tukufu ilivyoyazungumzia haya

katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlioamini

kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu;

yalipokufikieni majeshi, Tukayapelekea upepo na majeshi

msiyoyaona (ya Malaika), na Mwenyezi Mungu Anayaona

(yote) mnayoyafanya." (9) Walipokujieni (kukushambulieni)

kutoka juu yenu na kutoka chini yenu, na mlipoyakodoa macho

yenu na nyoyo zikapanda kooni nanyi mkaanza kumdhania

Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali. (10). Hapo waislamu

walitiwa mtihani (kweli kweli) na wakatetemeshwa kwa

matetemesho makali.} [AL AHZAB 9-10-11].

Na huyu ni Bwana wetu Ibarahim (amani ya Mwenyezi

Mungu iwe juu yake) watu wake walipomtupia motoni kuokoka

kwake kulitoka kwa Mwenyezi Mungu: {Tukasema; "Ewe

moto! kuwa baridi na salama juu ya Ibrahim. (69) Na walimtaka

Page 100: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

100

ubaya, lakini tukawafanya wao ndio wenye kupata hasara.} [AL

ANBIYAA 69-70].

Na huyu ni Yunus (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu

yake) alipomezwa na nyangumi basi alielekea kwa Mwenyezi

Mungu Mtukufu, na aliendelea kumtegemea Mwenyezi Mungu,

na ikawa rehema na uokovu kutoka kwa Mwenyezi Mungu

Mtukufu, anasema: {Na (mtaje) Dhun-Nun (Yunusi) alioondoka

hali amechukia, na akadhani ya kwamba hatutamsaidia. Basi

(alipozongwa) aliita gizani (akasema): "Hakuna aabudiwaye

isipokuwa wewe, Mtakatifu, hakika mimi nilikuwa miongoni

mwa wenye kudhulumu (nafsi zao)" (87) Basi tukampokea na

tukamwokoa katika huzuni ile. Na hivyo ndivyo tuwaokoavyo

walioamini.} [AL ANBIYAA 87-88].

Na miongoni mwa rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu

nasi kuwa anatuamrisha juu ya kutafuta njia, ama matokeo ya

kinachofanyiwa kai tuyarudishe kwake Mwenyezi Mungu

Mtukufu, basi kama tukifanya mema kwa kufuata njia

inayotakiwa na tukifanya mema katika kumtegemea Mwenyezi

Mungu Mtukufu atatufungulia milango ya rehema zake katika

dunia na Akhera. Imepokelewa na Omar Bin Al Khattab R.A.

kuwa yeye alimsikia Mtume S.A.W akisema: "Kama nyinyi

Page 101: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

101

mtamtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea

atawaruzuku kama afanyavyo kwa ndege ambao huondoka

matumbo yao yakiwa matupu na hurejea yakiwa yamejaa."

[Imetolewa na Imamu Ahmad].

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na anaye

mwogopa Mwenyezi Mungu, (Mwenyezi Mungu)

humtengenezea njia ya kuokoka (katika kila balaa). Na humpa

riziki kwa namna asiyoitazamia.} [AT TALAQ 2, 3]. Na

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {"Na anayemtegemea

Mwenyezi Mungu Yeye humtosha, kwa yakini Mwenyezi

Mungu anatimiza kusudio lake (lo lote alitakalo; hakuna wa

kumpinga). Hakika Mwenyezi Mungu amekwisha kiwekea kila

kitu kipimo chake.} [AT TALAQA 3].

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na

anayemwogopa Mwenyezi Mungu, (Mwenyezi Mungu)

humafanyia mambo yake kuwa mepesi.} [AT TALAQA 4]. Na

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Je, Mwenyezi Mungu

hamfikii (hamtoshelezi) mja wake? Na wanakuogopesha kwa

aliye duni (masanamu; kuwa watakudhuru kama hutawaabudu,

wanaweza wapi kudhuru, ukiachana na kunufaisha!. Na

Page 102: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

102

aliyehukumiwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hana wa

kumuongoa.} [AZ ZUMAR 36].

Lakini matumaini bila ya kazi ni matumaini matupu, na

ni amani ya uongo yenye makosa. Na Bwana wetu Omar Bin Al

Khattab R.A anasema: "Asijibwetekee yeyote miongoni mwenu

na akaacha kutafuta riziki, na kisha anasema ewe Mola wangu,

niruzuku! na hakika ni kwamba mbingu hainyeeshi dhahabu na

wala fedha na wala haitoshi kufanya kazi tu, bali kazi ni lazima

iwe kamilifu na kwa ujasiri zaidi na ifanywe vizuri. Na kutoka

kwa Aisha R.A. amesema kwamba Mtume S.A.W. anasema:

"Hakika Mwenyezi Mungu anampenda yule ambaye afanyapo

kazi huifanya kwa ukamilifu." [Musnad Abi Yaaliy], na

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Hakika wale walioamini

na kufanya vitendo vizuri (tautawalipa mema ya hayo). Hakika

sisi hatupotezi ujira wa wale wanaofanya vitendo vizuri.} [AL

KAHF 30].

Na Uislamu haukutoa wito wa kufanya kazi tu, bali kazi

lazima ifanyike vizuri na kwa kuikamilisha. Na kutoka kwa

Aisha R.A kwamba Mtume S.A.W. anasema: "Kwamba

Mwenyezi Mungu Mtukufu anampenda yule ambaye afanyapo

Page 103: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

103

kazi huifanya kwa ukamilifu." [Ilipokelewa na Al Baihaqiy

katika Al Shaab].

Na hivyo ni pamoja na udharura wa kumwogopa

Mwnyezi Mungu Mtukufu, kwa siri na wazi wazi, kwani ni

vigumu mno bali pengine ilikuwa jambo lililoepushwa au labda

ni muhali kwamba tutajaalia mlinzi kwa kila mwanadamu ili

amlinde, au mwangalizi ili amwangalie, na hata lau tuliyafanya

hayo, basi mlinzi pengine anahitaji mlinzi mwingine ili

amlinde, na mwangalizi anahitaji mwangalizi ili amwangalize,

lakini ni jambo jepesi kujenga malezi ya dhamira njema kwa

kila mwanadamu, dhamira iliyo hai inapumua haki na inatoa

msukumo wa kuelekea katika heri. Kwani dhamira hiyo

inalindwa na asiyepatwa na usingizi wala wala kulala.

Na kwa kukazia umuhimu wa kazi, Uislamu umetutolea

wito kuwa tufanye kazi hadi mwisho wa maisha yetu. Hata

kama hatutayapata matunda ya kazi hiyo. Na jambo hili

halikuwa isipokuwa kwa ajili ya kubainisha thamani ya kazi na

umuhimu wa uzalishaji kwa watu na mataifa. Na kutoka kwa

Anas Bin Malik R.A. anasema: Mtume S.A.W.

amesema;"Kama kikija Kiyama na katika mkono wa mmoja

Page 104: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

104

wenu kuna mche basi akiweza kuupandikiza kabla ya kuja

Kiyama basi aupande." [Katika Al Adab Al Mufrad].

Kama ambavyo Quraani imetoa wito wa kufanya kazi, na

ikaifanya kazi hiyo kuwa katika kiwango cha ibada. Na

Mwenyezi Mungu Mtukufu ametutolea wito kwa ajili ya sala ya

siku ya Ijumaa -ibada hiyo tukufu- kwa amri, kisha

ametuelekeza kufanya kazi baada ya swala kwa amri iliyo sawa

na nyingine, ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

{Enyi mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya sala ya siku ya

Ijumaa, nendeni upesi kumtaja Mwenyezi Mungu na acheni

biashara. Kufanya hivi ni bora kwenu. Ikiwa mnajua hivi, basi

fanyeni!" (9) Na itakapokwisha sala, tawanyikeni katika ardhi

mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni

Mwenyezi Mungu kwa wingi (ili msipate kufanya mabaya), ili

mpate kufaulu.} [AL JUMUA 9-10]

Na Bwana wetu Iraak Bin Malik R.A alikuwa pindi

anapomaliza kuswali sala ya siku ya Ijumaa huondoka na

akasimama katila mlango wa msikiti kisha akasema: Mola

wangu! Mimi niliuitikia wito wako na nikaswali faradhi yako,

na nikaondoka kama ulivyoniumuru, basi niruzuku fadhila zako,

na wewe ndio mbora wa kuruzuku. [Tafsiri ya Ibn Katheer]. Na

Page 105: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

105

kwa kuwa Uislamu unatoa wito wa kufanya kazi na uzalishaji

basi pia unapinga -na kwa nguvu- ukosefu wa ajira, uzembe na

kuombaomba, kwani hayo ni miongoni mwa sababu ya

kuchelewa kwa taifa na uharibifu wa watu, na Mtume S.A.W.

alikuwa akijikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na

kushindwa na uzembe. Na kutoka kwa Anas Bin Malik R.A.

akasema: Mtume S.A.W. alikuwa akisema: "Mola wangu!

Najikinga kwako kutokana na kushindwa na uzembe, woga,

uzee na ubahili, na najikinga kwako kutokana na adhabu ya

kaburini, na fitina za uhai na umauti." [Muslim akaitoa].

Kwa hivyo Mtume S.A.W alikuwa akiwavutia watu

katika kufanya kazi, na alikuwa akikataza ukosefu wa ajira na

uzembe. Na kutoka kwa Abi Huraira R.A. anasema: Mtume

S.A.W. anasema: "Kwani kuwa mtu mmoja miongoni mwenu

anakata kuni, na kuubeba mzigo wa kuni juu ya mgongo wake

ni bora zaidi kuliko kuwa anaombaomba, anaweza kupewa au

asipewe." [Al Bukhariy aliitoa]. Na kutoka kwa Ibn Omar R.A.

kwa wote wawili, alisema: Mtume S.A.W. aliulizwa juu ya

chumo zuri zaidi kuliko yote, basi akasema: "Kazi ya

mwanamume kwa mikono yake, na kila uuzaji bora."

Page 106: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

106

[Imetolewa na Imamu Ahmad katika Musnadi yake na Al

Ttabaraniy katika Al Muajam Al Kabeer].

Na kutoka kwa Al Meqdaam R.A. kutoka kwa Mtume

S.A.W. anasema: "Hakuna Mtu yeyote aliyekula chakula kizuri

zaidi isipokuwa anapokula chakula kutokana kazi ya mkono

wake, na kuwa Nabii wa Mwenyezi Mungu Dawud (amani ya

Mwenyezi Mungu iwe juu yake) alikuwa akila kutokana na kazi

ya mkono wake." [Al Bukhariy aliitoa]. Na kutoka kwa Abi

Huraira R.A alisema: Mtume S.A.W. anasema: "Hakika kuna

madhambi miongoni mwa madhambi yasiyofutwa na sala wala

kufunga (saumu), wala Hija na wala Umra." Wakasema basi ni

yepi yanayoyafuta ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?

Akasema: " Shime ya kutafuta maisha." [Al Ttabaraniy aliitoa].

Na kutoka kwa Abi Huraira R.A., kutoka kwa Mtume

S.A.W anasema: "Mwenye kumkimbilia mjane na masikini ni

kama mpiganaji wa jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu -na

nilidhani kuwa alisema: na kama vile mwenye kusali sala bila

ya kupumzika, na kama vile mfungaji hafuturu." [Inaafikiana

juu yake].

Na hayakuwa hayo yote ila kwa sababu ya kutilia mkazo

umuhimu wa kazi na uzalishaji. Na kwamba nchi yoyote haina

Page 107: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

107

kauli na wala utashi isipokuwa kwa watu wake wote kufanya

kazi ili kuiendeleza na kuistawisha. Na ili iweza kuzalisha

chakula chake, vinywaji chake, mavazi yake, dawa zake, silaha

zake na misingi yote ya maisha yake. Na haya yote

hayawezekani isipokuwa kwa elimu, kazi na mikakati mizuri.

Nayo ndio tutakayoyazungumzia kwa kirefu katika hotuba yetu

ijayo kama Mwenyezi Mungu Mtukufu akipenda.

Uzuri, Furaha na Hisia Njema

Uisilamu ni dini ya ustaarabu na upendo, dini ya furaha na

maelezo yake na njia zake zote zinathibitisha hili na hata kurani

tukufu na hadithi za mtume (rehma na amani zimshukie juu

yake) pia zinathibitisha hili. Mwenyezi Mungu anasema katika

kurani { Na nyama hoa amekuumbieni. Katika hao mna vifaa

vya kutia joto, na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala.

6. Na wanakupeni furaha pale mnapo warudisha jioni na

mnapo- wapeleka malishoni asubuhi.}

Page 108: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

108

Na anasema pia { Ambaye amekufanyieni ardhi kuwa tandiko,

na akakupitishieni humo njia, na akakuteremshieni kutoka

mbinguni maji. Na kwa hayo tukatoa namna mbali mbali za

mimema.} na kuendelea kusema { na tukaiotesha mimea mizuri

ya kila namna.} {, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni,

na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi

hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja

na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu walio potoka.} na

kusema pia {17. Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo

umbwa?18. Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?19. Na milima jinsi

ilivyo thibitishwa?20. Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?} na

anasema pia { Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi

wa Rehema.}ama kuhusu mbingu zilizo juu anasema { na

tumezipamba kwa wenye kuangalia.} { Na kwa hakika

tumeipamba mbingu ya karibu kwa mataa,}

Kurani tukufu imetuamrisha kujipamba kwa mapambo mazuri

na tuchukue mapambo yetu kila tuendapo misikitini (tusalipo).

Mwenyezi Mungu anasema { Enyi wanaadamu! Chukueni

pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada, na kuleni, na

kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye

hapendi wanao fanya israfu 32. Sema: Ni nani aliye harimisha

Page 109: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

109

pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo

vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai

wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna

hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua.} Na Mtume (rehma

na amani zimshukie juu yake) aliposema: “ haingii peponi mtu

mwenye chembe ndogo ya kiburi (dharau). Mtu mmoja

akasema: “kuna mtu hupendelea nguo yake iwe nzuri na viatu

vizuri.” Mtume akasema: “ Mwenyezi Mungu ni mzuri hupenda

uzuri, kiburi ni kukana ukweli na kudharau watu.” (muslim). Na

sayidna Mughira bin Shuuba (Mungu awie radhi) alipomueleza

kuwa yeye amemchumbia mwanamke, mtume (rehma na amani

zimshukie juu yake) akamwambia: “mwangalie kwani

itapelekea kudumu kati yenu.” (Tirmidhiy).

Mtume (rehma na amani zimshukie alikuwa kipenda uzuri, na

alilingania pia uso wa bashasha akasema: “jambo jema lolote

usilidharau hata kama utakutana na mwenzio basi iwe kwa uso

wa bashasha.” (Muslim). Na kusema kuwa kuingiza furaha kwa

watu ni kitu kimuwekacho mtu karibu na Mwenyezi Mungu

akasema: “ mwenye kuingiza furaha katika nyoyo ya muisilamu

basi ni haki ya Mwenyezi Mungu kumridhisha siku ya kiyama.”

Na akasema “ amali zipendwazo sana na Mwenyezi Mungu ni

Page 110: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

110

furaha uiingizayo kwa muisilamu.” Na akawataka masahaba

zake kuvaa nguo nzuri wakati wanapokutana na katika sherehe

na minasaba

Pamoja na kuwa uzuri wa kweli haupo katika mandhari ya

muonekano na uzuri wa vitu lakini unavuka mipaka zaidi nao ni

uzuri tabia na mwuonekano. Mustafa Saadiq Rafii (Mungu

amrehemu) anasema: “ mwanamke mbora ni yule mwenye sura

nzuri kama tabia zake na akili yake ikawa uzuri wake wa tatu.

Mwanamke huyu akiwa na mwanamke mwenye kuendana nae

basi atamfurahisha na kumfurahisha na kumfurahisha. Mshairi

anasema

Mtu iwapo hajalaumiwa kwa heshima yake

Basi nguo yoyote aivaayo huwa nzuri

Tunaelewa kuwa kidogo huwa ni kingi

Nikasema kuwa ukarimu huona kidogo

Sikudhurika kwa kidogo na jirani yetu

aliye mwema ni mwenye nguvu

na jirani mwenye wengi ni dhalili

Inatulazimu sote kujipamba kwa tabia za kiisilamu katika

muonekano wetu, mazingira yetu, mashule yetu, vhuo vyetu,

Page 111: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

111

bustanini mwetu, matembezini mwetu na katika sehemu zote.

Na wala tusifanye yenye kuondosha furaha na ucheshi.

Na katika alama kubwa sana za ucheshi na ziletazo furaha ni

neno zuri lililo jema, sayidna Umar bin Khatab (Mungu amwie

radhi) alipita kwa watu waliokuwa wakiota moto akachukia

kuwasalimia kwa kusema “amani iwe juu yenu enyi watu wa

motoni” isipokuwa akasema” amani iwe kwenu enyi watu wa

kivulini”. Na kama ulivyotulingania uisilamu kuwa tuchague

majina yenye maana nzuri na kujiepusha na majina mabaya

yasiyoendana na hisia za kiutu, kwani kurani imetuamrisha

kufanya kila lililo zuri na jema na kusema kila lililo jema.

Mwenyezi Mungu anasema { nasemeni na watu kwa wema,}

Albaqara 83. Na akasema { Waambie waja wangu waseme

maneno mazuri,} Israa 53. Basi kauli mbiu yetu ni “hisia njema

na uzuri”. Hisia nzuri ni kigezo cha kujua uzuri na kuueneza

kwa waliotuzunguka katika wanajamii.

Page 112: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

112

Rafiki Tumtafutaye

Rafiki tumtafutaye ni yule aliyesema Mustafa Sadik Al rafiy

(Mungu amrehemu): ni yule anapokuwa hayupo husemi kuwa

Fulani hayupo bali unasema kuwa sehemu katika wewe haipo,

sehemu katika wewe, si rafiki akupakae mafuta kwa mgongo wa

chupa na kukuhadaa kama anavyohadaa fisi au kudonoa kama

anavyodonoa kalunguyeye (aina ya mnyama mfano wa panya)

na marafiki hawa huwapatikani isipokuwa pale tatizo

linapokuwa limeshamalizika nao ni kama inzi hawaonekani

isipokuwa pale penye asali.

Page 113: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

113

Rafiki wa kweli tumtafutaye ni kama alivyosema Imam Shafi

(Mungu amrehemu) :

Rafiki wa kweli ni Yule anaekuwa nawe

Na kuidhuru nafsi yake kwa ajili yako

Ambaye wako unapokuwa mgumu hukusaidia

Na hujikimu nasfi yake ili akuunge.

Na siyo kama alivyosema kadhi Abu-Surur:

Mbona uko hivyo nami nilikuona kuwa ni rafiki,

wakati ukanitenganisha na kwa haki zote,

Nilikuwa ninakuhesabu kuwepo katika tabu zangu ,

hata kama wakati utanitafuna kwa dhiki,

Ulipata habari kama wakati ulinikaba,

ukabakia wewe kunipigia makofi,

Na ulipofahamu yakini kuwa mimi,

nimepata nafasi kubwa,

Ukanijia na kunipongeza kwa furaha,

unashangaza sana mambo yako ya kuvunja undugu,

Hakika upendo sehemu yake ni moyoni,

Page 114: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

114

lakini ukweli wake huonekana pale penye matatizo

Mmoja wao aliulizwa: “ ni nani rafiki yako? Akasema:

“simjui” akaulizwa: “kwa nini” akasema: “kwa kuwa dunia

imenigeukia na itakapogeuka upande mwengine nitamfahamu

nani rafiki yangu kwani watu wengi huzunguka na dunia kila

iendapo, ukiwa nao basi wapo nawe na ukiwa mbali nao huwa

kinyume nawe. Na ndio maana wakasema: rafiki wa kweli

hujulikana wakati wa shida. Na mshairi akasema:

Mweneyzi Mungu ayalipe matatizo heri zote,

kwani kupitia hayo nimeelewa rafiki yangu na adui yangu

Na mwengine akasema:

Nimewaona watu wameenda,

kwa wenye dhahabu.

Na kwa wasio na dhahabu,

wakawa wananyenyekea kwa wenye fedha.

Nimeeona watu wameenda,

kwa wenye fedha kuelekea.

Page 115: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

115

Na kwa asiye na fedha ,

wakawa wananyenyekea kwa wenye fedha.

Nimeona watu wamemili,

kwa wenye mali .

Na kwa wasio na mali ,

wakawa wananyenyekea kwa wenye mali .

Na mwengine akasema:

Tajiri husalimiwa kwa salamu ,

na bakhili hunyimwa salamu .

Kwani mauti kwao si mamoja tu ,

pindi wakifa na wakiwa makaburini?

Neno rafiki ni mnyumbuliko wa neno Sidqi (Ukweli) nalo

lina ujumbe wa anayekuamini katika hali ya siri na dhahiri na

katika hali ya raha na tabu katika uchangamfu na

unyongonyevu, anayekupendelea kile akipendacho nafsi yake

na kukichukia kwako kile akichukiacho katika nafsi yake.

Page 116: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

116

Mtume wetu (rehma na amani zimshukie) anasema: “

hatoamini mmoja wenu mpaka ampendelee mwenzake kile

anachokipenda katika nafsi yake.” (Bukhari). Na anasema

(rehma na amani zimshukie): “ mambo matatu mwenye kuwa

nayo basi atapata utamu wa imani; awe Mwenyezi Mungu

na Mtume wake anawapenda kuliko wengine wasiokuwa

hao. Na ampende mtu asimpendee kwa chochote isipokuwa

kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na achukie kurudi katika

ukafiri kama anavyochukia kutumbukizwa motoni.”

(Bukhari) na pia anasema (rehma na amani zimshukie):” watu

saba Mwenyezi Mungu atawafunika kwa kivuli chake siku

isiyokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake; kiongozi

muadilifu, Kijana aliyeishi katika kumuabudu Mwenyezi

Mungu. Na mtu moyo wake umefungamana na misikiti. Na

watu wawili waliopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu

wanakutana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kuagana kwa

ajili ya Mwenyezi Mungu. Na kijana aliyeitwa na

mwanamke mwenye cheo na uzuri (kwa ajili ya kufanya

maovu) akasema (kijana) “Mimi ninamuogopa Mwenyezi

Mungu.” Na kijana anaetoa sadaka akaificha mpaka mkono

wake wa kushoto ukawa haujui kinachotolewa katika

Page 117: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

117

mkono wa kulia. Na kijana anaemtaja Mwenyezi Mungu

hali ya kuwa yu pekee mpaka akatokwa na machozi.”

(Bukharin a Muslim).

Na imepokuwa kuwa kuna mzee mmoja alimtembelea

mwenzake katika kijiji chengine Mwenyezi Mungu akamwekea

katika njia yake malaika, alipomfikia akamwambia:

“unakwenda wapi?” akasema “kwa ndugu yangu aliye katika

kijiji hiki.” Akasema: je unaneema yoyote unayoitaka kutoka

kwake? Akasema: “ hapana, isipokuwa mimi nimempenda kwa

ajili ya Mwenyezi Mungu mtukufu. Akasema: “hakika mimi ni

mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwako na hakika ya

Mwenyezi Mungu anakupenda kama unavyompenda ndugu

yako kwa ajili yake (Mwenyezi Mungu).” (Muslim). Nakatika

hadithi Kudsiy, “mapenzi yangu yamewajibika kwa

wapendanao kwa ajili yangu, na wakaao pamoja kwa ajili

yangu, na wenye kutembeleana kwa ajili yangu.” (Ahmad).

Na mtume wetu (rehma na amani zimshukie): “wapendanao

kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wana mimbari za nuru siku

ya kiyama wanapendwa na mashahidi.” (kitabu cha

Mustadrik). Hivyo, ni uzuri ulioje kuwepo kwa mahusiano na

urafiki kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee, uhusiano

Page 118: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

118

utakayokuwa na upendo na utu na athari iliyojengekwa kwa

maadili na tabia njema, mbali na aina yoyote ua ubinafsi na

masilahi na kujinufaisha kimasilahi.

Haki ya Mwanamke Katika Kurithi na

Maisha Mazuri

Kadhia ya urithi ni moja kati ya kadhia kubwa sana amabazo

mtume wetu (rehma na amani zimshukie juu yake) ameisisitiza

katika hotuba yake ya kuagana aliposema: “hakika Mwenyezi

mungu amempa kila mweye haki amempa haki yake, tambueni

kuwa hakuna wasia kwa anaerithi.” (Ibn Majah). Naye

Mwenyezi Mungu ameweka wazi mafungu ya wanaorithi na

suala hili hakumuachia yeyote katika viumbe vyake, akasema

{11. Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu:Fungu

la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili.Na ikiwa

wanawake zaidi ya wawili, basi watapata thuluthi mbili za

Page 119: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

119

alichokiacha maiti. Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja,

basi fungu lake ni nusu. Na wazazi wake wawili, kila mmoja

wao apate sudusi ya alichokiacha, ikiwa anaye mtoto. Akiwa

hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi

wake, basi mama yake atapata thuluthi moja. Na akiwa anao

ndugu, basi mama yake atapata sudusi. Haya ni baada ya

kutolewa alicho usia au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu,

nyinyi hamjui ni nani baina yao aliye karibia zaidi kwenu kwa

manufaa. Hiyo ni Sharia iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu. Bila

ya shaka Mwenyezi Munguni Mjuzi na Mwenye hikima.}.

Na haikuishia hapo kutaja mafungu tu, lakini pia kurani tukufu

imetaja na adhabu kali mno kwa kila atakaefanya dhuluma

katika haki hizi, akasema Mwenyezi Mungu mtukufu, {13.

Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anaye mt'ii Mwenyezi

Mungu na Mtume wake, Yeye atamtia katika Pepo zipitazo

mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu

kukubwa.

14. Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na

akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni

adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.}. Na

ikawakemea watu majahili kwa kule kula kwao mali za baadhi

Page 120: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

120

ya warithi bila ya haki, akasema {Sivyo hivyo! Bali nyinyi

hamuwakirimu mayatima, 18. Wala hamhimizani kulisha

masikini; 19. Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa, 20. Na

mnapenda mali pendo la kupita kiasi. 21. Sivyo hivyo! Itakapo

vunjwa ardhi vipande vipande, 22. Na akaja Mola wako Mlezi

na Malaika safu safu, 23. Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo,

siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa

nini? 24. Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu!

26. Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake. 25. Basi siku

hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.}. Na mtume

wetu (rehma na amani zimshukie juu yake) anasema “mwenye

kukata mirathi ambayo mwenyezi Mungu na Mtume wake

wamefaradhisha, basi Mwenyezi Mungu atamkatia urithi wake

peponi.”

Na inasimuliwa kuwa kuna mtu alimnyima mtoto wake wa kike

mirathi, akangoja hadi muda wa kufariki (kwa mzazi wake) na

kukutana na Mola wake, alipoingizwa sehemu ya kuoshwa

(naye mtoto wa kike) akaingia, akawa anamwangalia na

kusema: “ewe Mola wangu hakika unaelewa kuwa ameninyima

baadhi ya neema za dunia name nakuomba umnyime neema za

akhera.”

Page 121: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

121

Kasha kitendo cha kuwanyima wanawake urithi huenda ikawa

kinasababishwa na tabia ovu au tamaduni na mila zilizopitwa na

wakati ambazo hazina asili yoyote katika sheria, na kama

kwamba Yule anayemnyima mwengine na kumpa mwengine

anadhani ya kuwa amefanya jambo la masilahi kwa

anayestahiki na kwa siye stahiki kwa Mola wa viumbe vyote,

muumbaji wa kila kitu na Mbora wa mahakimu, na kama

kwamba (anayegawa mirathi kwa dhuluma) anasema ndani ya

moyo wake: “mgao wa Mwenyezi Mungu haunipendezi” au

“mimi nitagawa vizuri zaidi kuliko hata Mwenyezi Mungu” –

Mungu atuepushe mbali- kwani angelikuwa ni muumini wa

kweli na kuamini kuwa mgao wa mwenyezi Mungu ni bora na

wa haki basi mtu huyu asingelifadhilisha mwengine na

kumuacha mwengine.

Ama kuhusu mwanamke kwa ujumla sawa awe ni dada,mke,

mtoto wa kike au yeyote, ieleweke kuwa dini yetu imekataza

kuwadhulumu na kupunja haki zao, bali ikasema kuwa uadilifu

kwao na kwa watoto wa kiume ni njia nzuri ya kupata radhi za

Mwenyezi Mungu na kupata pepo yake, mtume (rehma na

amani zimshukie juu yake) anasema: “Yeyote atakaekuwa na

mwanamke na akawa hajamzika akiwa haina wla

Page 122: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

122

hakumdhulumu ْ na wala mzazi wake hakumpendelea zaidi ya

mwengine (kamfanyia usawa) basi Mwenyezi Mungu

atamuingiza peponi.” Na katika hadithi hii kuna maana kubwa

na ufasaha wa hali ya juu kabisa kwani mtume amesema

“yeyote” ambayo inamaanisha mjumuiko na pia akasema

“mwanamke” na wala hakusema “mtoto wa kike” kwa sababu

mwanamke inakusanya jinsia ya kike sawa awe mtoto,

dada,mtoto wa kike n.k.

Na mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) ameusia

kuwakirimu na kuwatendea wema wanawake katika nyanya

zote, kwani katika hadithi kudisiy ambayo imepokewa na

mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) kutoka kwa Mola

mtukufu anasema: “Niridhisheni kupitia madhaifu wawili,

mwanamke na yatima.” Na mtume (rehma na amani zimshukie

juu yake anasema: “mwenye kuwa na watoto wa kike watatu,

akawa na subira kwao, akawalisha, na kuwavisha kwa kipato

chake, basi hao watakuwa kwake ni kinga ya moto siku ya

kiama.” Na katika mapokezi mengine, mwenye kuwa na watoto

wakike wawili au ndugu wa kike wawili. Na katika mapokezi

mengine pia inasisitiza hata kama atakuwa na mtoto wa kike

mmoja tu akamfundisha na kumpa malezi mema atakuwa

Page 123: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

123

kwake ni kinga ya moto siku ya kiama. Na alipokuwa mzee

mmoja amekaa pamoja na mtume (rehma na amani zimshukie

juu yake) akaja mtoto wake wa kiume,akamchukua na kumbusu

na kumuweka mapajani mwake, kasha baadae akaja mtoto wake

wa kike akamchukua na kumuweka ubavuni mwake, mtume

(rehma na amani zimshukie juu yake) akasema: “ unaonaje lau

kama ungeliwafanyia uadilifu”. Hapa anakusudia kama

ulivyomuweka mtoto wa kiume mapajani ilibidi pia ufanye

hivyo hivyo kwa mtoto wa kike kwa kumuweka kwenye paja

jengine.

Ingawa kwa wakati tulionao tunaona aina tafauti za

utenganishaji usiohitajika, ndani ya nyumba moja ya familia

kwa baadhi ya watu, mtoto wa kiume huwa ni bora kuliko wa

kike, na katika sekta ya elimu hushughulikiwa zaidi wavulana

kuliko wasichana, kwenye mirathi –ambayo tunatoa tolea lake-

ima atakuwa hapewi kabisa au atapewa lakini kwa kuridhisha tu

(na si kama haki yake), nalo ni jambo lisilokubalika hata kidogo

hiyo ni aina ya kumkandamiza na kutumia mabavu au

unyanyasaji. Ita utakavyo isipokuwa kinachohitajika ni mirathi

ya haki kwa ajili ya kumfuata sheria ya uadilifu wa Mwenyezi

Page 124: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

124

Mungu na kwa ugawaji kama ambavyo sheria, haki, uadilifu

inavyotaka.

Ujeuri na Mwisho Mbaya

Ujeuri na mwisho mbaya ni mambo mawili yaondayo

sambamba wala hayatengani. Mwenyezi Mungu Mtukufu

anasema :{ Enyi watu! Jeuri zenu zitakudhuruni wenyewe.

Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni

kwetu, na hapo tutakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.}

(Yunus; 23). Na anasema pia {Ama kina A'di walijivuna

katika nchi bila ya haki , na wakasema: Nani aliye kuwa na

Page 125: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

125

nguvu kushinda sisi ? Kwani wao hawakuona kwamba

Mwenyezi Mungu aliye waumba ni Mwenye nguvu

kushinda wao? Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu!.

16 Basi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika sikuza

ukorofi, ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwa hizi katika uhai wa

duniani, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ina

ukali(khezyy) zaidi, na wala wao hawatanusuriwa.}

(Fussilat; 15-16). Na anaendelea kusema { Walipo

jifakharisha katika waliyo kanywa tuliwaambia: Kuweni

manyani wa kudharauliwa } (Al aaraf; 166). Na wasomi

wameeleza kuwa Mwenyezi Mungu huunusuru umma ulio

na uadilifu hata kama ni wa kikafiri na wala haunusuru

umma ulio na dhuluma hata kama ni waumini.

Ujeuri unaweza kuwa ni kwa mtu au kwa kundi nalo ni lile

liitwalo “kundi la kijeuri” na inaweza pia kuwa ujeuri kwa

taifa. Ama kuhusu mtu au kikundi au makundi

yatakayofanya ujeuri na kuvuka mipaka ya haki basi

mwenyezi Mungu hatowaacha anatashika na kuwapa

malipo wanayostahiki, kwani anasema: { Na ndio kama

hivyo ndivyo inavyo kuwa Mola wako Mlezi anapo ikamata

Page 126: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

126

miji inapo kuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni

mchungu na mkali.} (Hud;102).

Na anasema Mwenyezi Mungu kuhusu Qaruni, {Hakika

Qaruni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia

dhulma. Na tulimpa khazina ambazo funguo zake

zinawatopeza watu wenye nguvu kuzichukua. Walipo

mwambia watu wake: Usijigambe! Hakika Mwenyezi

Mungu hawapendi wanao jigamba. 77. Na utafute, kwa

aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala

usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama

Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala

usitafute kufanya ufisadi katika ardhi.Hakika Mwenyezi

Mungu hawapendi mafisadi. 78. Akasema: Kwa hakika

nimepewa haya kwa sababu ya ilimu niliyo nayo. Je!

Hakujua kwamba Mwenyezi Mungu kesha waangamiza,

katika vizazi vya walio kabla yake, watu walio kuwa wenye

nguvu zaidi kuliko yeye,na wenye makundi makubwa zaidi

kuliko yake. Na wakosefu hawataulizwa khabari ya dhambi

zao. 79. Basi akawatokea watu wake katika pambo

lake.Wakasema wale walio kuwa wanataka maisha ya

duniani:Laiti tungeli kuwa tunayo kama aliyo pewa Qaruni!

Page 127: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

127

Hakika yeye ni mwenye bahati kubwa. 80. Na wakasema

wale walio pewa ilimu: Ole wenu!Malipo ya Mwenyezi

Mungu ni bora kwa mwenye kuamini naakatenda mema.

Wala hawatapewa hayo isipo kuwa wenye subira. 81. Basi

tukamdidimiza yeye na nyumba yake katika ardhi; wala

halikuwepo kundi lolote la kumnusuru kwa Mwenyezi

Mungu, wala hakuwa miongoni mwa wanaojitetea.}(Al

qasas; 76-81)

Na kuhusu kisa cha nabii Saleh pamoja na watu wake,

Mwenyezi Mungu anasema {Na wakamuuwa yule ngamia,

na wakaasi amri ya Mola Mlezi wao, na wakasema: Ewe

Saleh! Tuletee unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa

Mitume. 78. Basi tetemeko la ardhi likawanyakua, na

kulipokucha wakawa majumbani mwao kifudifudi

wamekwishakufa.} (Alaaraf; 77-79).

Ama kuhusu kisa cha nabii Shuib (rehema na amani

zimshukie) pamoja na watu wake Mwenyezi Mungu

anasema {95. Kama kwamba hawakuwamo humo. Zingatia

walivyoangamia watu wa Madyana, kama walivyo angamia

watu waThamud!Na ilipo fika amri yetu, tulimwokoa

Page 128: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

128

Shua'ibu na wale walio amini pamoja naye kwa rehema

yetu. Na ukelele uliwanyakua walio dhulumu, na

wakapamba ukiwa majumbani mwao wamekufa

kifudifudi!} (Hud; 94-95)

Na Mtume wetu (Rehma na amani zimshukie) “Mwenyezi

Mungu humpa muda dhalimu mpaka anapoamua

kumchukua basi hapo hatowezatoroka.” Dhuluma ni kiza

siku ya kiyama, na vitimbwi havirudi isipokuwa kwa

wenyewe.

Hivyo basi, ninasisitiza zaidi kuwa mwisho wa taifa lenye

dhuluma ni kutoweka, na amesema kweli mashairi Hafidh

Ibrahim aliposema katika ushairi wake mzuri:

Misri inajieleza wenyewe.

Nchi ngapi zimenifanyia ujeuri

Kisha zikatoweka, kwani huo ndio mwisho

wake

Na hakuna aliyenilenga kisha akawa salama

Mwenyezi Mungu amelihifadhi jeshi lake tokea zamani.

Nchi itendayo dhuluma na mataifa yaliyojijenga kidhuluma

zinajiwekea sababu za kuporomoka na kuanguka kwa

haraka sana.

Page 129: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

129

Na makundi ambayo yanayofanya utumiaji wa mabavu,

dhuluma, ujeuri na kuvuka mipaka katika kutenda maovu

kwa mfano wa yale makundi yanayotelekeza mauaji ya

kujitolea muhanga na kungamiza, na kurikodi namna

wanavyowachinja watu na kuunguza mwili wake. Pamoja

na kudhalilisha watu, na kuuza wanawake kama ni mateka

wa kivita, kubomoa tamaduni na majengo na kuangamiza

kila kilicho na roho na kisicho na roho, hao wanajibebesha

sababu za kuanguka kwao na kuangamia, kwani Mwenyezi

Mungu hapendi uharibifu wala wenye kufanya uharibifu.

Na kwa ajili hiyo mimi ninatoa bishara ya kuwa kuangamia

kwa kundi la wapiganaji wa dola la kiisilamu na makundi

mengine ya Alqaida na maadui wa nyumba tukufu ya

Qudsi, boko haramu na makundi mengineyo ya kikatili -

kuangamia – kwao kupo karibuni, {NaMwenyezi Mungu

ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu

wengi hawajui.} (Yusuf; 21)

Page 130: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

130

Misri ni Nchi Kubwa Kwa Maadili Yake

na Ustaarabu Wake Hakuna shaka kuwa Misri ni nchi kuwa kwa uongozi

wake, wasomi wake, wanaume wake, wanawake wake,

wavulana wake, wasichana wake, historia yake, ustaaarabu

wake, nafasi yake ya uongozi katika eneo la mashariki ya kati

kimawazo, kielimu, kitamaduni kijeshi na kiutu. Na pengine

kitu kinachofanya kuonekana kuwa ni nchi kubwa ni masafa

yake makubwa na uwezo wake wa mkubwa na msamaha ulip

Page 131: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

131

nao na kuachana na mambo madogo madogo na yasiyo na

uhumimu kwani hutaamali kiakili. Wapo wasemao:

Mjinga hunikabili kwa kila njia * nami nachukia kumjibu

Ujinga wake ukizidi nami hekima zangu huzidi * kam ujiti

wa udi unapo kila unapounguzwa ndio huzidi kutoa harufu

nzuri

Lakini kuna tafauti kubwa kati ya upole na nguvu, na kati

ya udhaifu na unyenyekevu . Misri ina upole na wala si dhaifu,

ni kaka mkubwa kwa anaetaka mafanikio na iko tayari kusaidia

kwa kila anachomiliki bila ya kutenganisha familia na kuvunja

udugu na haiku tayari kumuacha mkono wakati wa shida hata

kwa Yule aliyemfanyia ubaya katika ndugu zake.

Na iwapo hii ndio hali ya kaka mkubwa juu ya ndugu zake,

basi Misri itabakia kuwa ni kiongozi na haitoachana kutaamali

na matukio ya taifa lake na wakati huohuo haitojiingiza katika

matatizo ambayo yatafanya makundi hasimu kuwemo katika

machafuko zaidi yenye mwisho mbaya.

Misri kwa kipindi chote cha historia yake kubwa na

iliyojaa utu na maadili, watu wake hawakuelewa khiyana na

uvunjaji ahadi, na wala kumfanyia mwengine uadui bila ya

haki, isipokuwa ilisimama wima kwa ndugu zake na marafiki

Page 132: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

132

zake na kipindi chote cha historia ilijulikana kwa ujirani

mwema, na usamehevu wa watu wake na ujirani mwema na

upole wa roho zao, haikuwa ukifahamu matumizi ya nguvu na

wala itikadi kali. Ama yanayojiri katika matumizi ya nguvu

haya ni matukio ya kupita na ni mageni ambayo jamii ya kimisri

katu hawajayashuhudia na ni kama mawingu tu ambayo

mwisho wake yatatoweka.

Misri imechukua ustaarabu wa nchi nyingi, na ikafaidika

kwa ustaarabu huo sana, na kupitia msamaha wa Al zhar na

usawa wake unaojulikana kwa mujibu wa historia ambayo

imelea kwa kipindi cha maelfu ya miaka imekuwa ni moja ya

dhamana ya usamehevu na usawa huu, si Misri pekee na wala si

katika ulimwengu wa kiarabu pekee na wala si katika

ulimwengu wa kiisilamu pekee lakini ni kwa ulimwengu wote

kwa ujumla.

Na kwa hili nimeandika beti zifuatazo:

Misri tukufu iliyohifadhika

Kitabu kitukufu kimetaja amani yake

Na ikidhoofisha siku moja itapona haraka haraka

Na uisilamu utarudi hali ya kuenea

Page 133: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

133

Na umma wa kiarabu utakuwa na nguvu zake

Atakaekuja kwa amani atapokewa

Na atakaekuja kwa vita basi sisi ndio wenyewe

Hatufanyi uadui na wala haturidhii khiyana

Nguzo yeu ni ujanadume

Moja ya mawili ndio tutakacho

Ushindi mkubwa au kuonekana mashahidi

Iulizeni historia kuhusu mashujaa wake

Na lieleweni jeshi la mtume

Jeshi bora ni jeshi la Misri, liheshimuni

Ardhi bora ni haki yake na ni cheo chake

Na Azhari yake ni ni yetu pia na ambayo

Imehifadhi elimu kwa karne

Ikawa inafundisha kila sehemu duniani

Usamehevu ni dini yetu na anuani yake

Msalieni aliyechaguliwa Ahmad

Kwani yeye ni mbora wa viumbe na ni kiongozi wao

Page 134: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

134

Wizi wa Mali za Umma na Kuzifuja

Hapana shaka kuwa uisilamu umeweka uharamu wa mali

kama ulivyoweka uharamu wa kumwaga damu, pale Mtume

(rehma na amani zimshukie) aliposema katika hijja ya kuaga

akiwahutubia watu wote: “enyi watu hakika ya damu zenu na

mali zenu ni haramu kwenu kama ilivyokuwa ni haramu

siku yenu hii (siku ya Arafa) na katika mji wenu huu

(Makka mji wa Mwenyezi Mungu), ewe Mola wangu

shuhudia, tambueni, na aliyekuwepo amfikishie

Page 135: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

135

asiyekuwepo. Na anasema: “mwili wowote uliojengeka kwa

haramu basi moto ni bora kwake.” Na pia anasema Mtume

(rehma na amani zimshukie): “ Hakika ya watu wenye

kulumbukiza mali za Mwenyezi Mungu bila ya haki

watakuwa na moto siku ya kiyama.” Na Mwenyezi Mungu

anasema. {Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa

dhulma,isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe.

Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye

kuwarehemuni.30. Na mwenye kutenda hayo kwa uadui na

udhaalimu,basi huyo tutamwingiza Motoni. Na hilo ni jepesi

kwa Mwenyezi Mungu.} (Anisaa, 29-30).

Na hapana shaka ya kuwa kuiba mali za umma na kuzitumia

vibaya ni katika makosa makubwa kuliko kutumia mali za mtu

binafsi. Kwa kuwa mali za umma zina haki nyingi ni mali ya

jamii kwa pande zote. Na atashtakiwa mbele ya Mwenyezi

Mungu siku ya kiyama kila mwenye kuzinyooshea mkono wake,

Mwenyezi Mungu anasema: { Na haiwezekani kwa Nabii

yeyote kufanya khiyana.Na atakaye fanya khiyana, atayaleta

Siku ya Kiyama aliyo yafanyia khiyana, kisha kila mtu

atalipwa kwa aliyo yachuma, kwa ukamilifu; wala

hawatadhulumiwa.} (Al Imraan, 161).

Page 136: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

136

Na wakati Abdallah bin Umar bin Al-Khatwab (Mwenyezi

Mungu awawie radhi) alipoingia kwa Ali bin Amir Al-

hadharamiy kumuangalia alipokuwa katika kitanda cha umauti

akasema Al-hadharamiy: “Tuombee Mwenyezi Mungu ewe

mtoto wa Umar (Mwenyezi Mungu awawie radhi) akasema Ibn

Umar: “ hakika ya Mwenyezi Mungu haipokei swala bila ya

udhu (tohara) na wala sadaka kwa kujionesha mnawe ulikuwa

kiongozi nchini Basra na huenda ukawa umechanganya mali za

umma na mali zako kitu kitakachopelekea kubadilisha hali ya

maombi ya dua zako na kukubaliwa kwako hii iwapo kama

dhamira yako ilikuwa iko safi, na imeepukika na vijikasoro na

iko mbali na shaka au kutiliwa wasiwasi, na kwa namna hiyo

imesemwa,: wacha Mungu wameitwa wacha Mungu kwa sababu

wao huogopa vile ambavyo watu wengine hawaviogopi. Na

baadhi ya masahaba na wanaowafuata na wafuasi wao katika

wachaji Mungu walikuwa wakiacha baadhi ya vitu vya halali

kwa kuogopea isije ikawa ndani yake muda wasiwasi wa

kuwepo kitu cha haramu. Na Mtume wetu (rehma na amani

zimshukie) anasema: “ halali ipo wazi na haramu ipo wazi, na

katikati yake pana vitu vinavyoshabihiana, watu wengi

hawavielewi, na ajiepushae na vitu vyenye utata (shubuhati)

Page 137: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

137

basi atakuwa ameilinda dini yake na heshima yake, na

atakaeingia katika vitu vyenye utata atakuwa ameingia katika

haramu, kwa mfano mchungaji anayechunga kandokando ya

mipaka, inaogopewa asije akaivuka, tambueni kila mmiliki ana

mipaka, eleweni mipaka ya Mwenyezi Mungu ni yale

aliyoyaharamisha. Na katika mwili kuna pande, pindi

likitengemea basi nao mwili wote hutengemea, na likiharibika

nao mwili mzima huharibika, tambueni pande hilo ni moyo.”

(Bukharin a Muslim)

Na pengine wengine wanaweza kudhani kuwa wizi wa mali za

umma unakusudiwa ni ule wa kuiba au ubadhirifu lakini ni zaidi

ya hapo, kwani kuacha kulipa kodi zenye kustahiki katika

wizara husika na taasisi husika nayo pia hujulikana kama ni wizi

wa mali za umma bali ni wizi uliokamilika vitendo kabisa.

Na tumetoa toleo la Wizara ya wakfu kubainisha kuwa wizi wa

huduma hauhitilafiani na wizi wa mali na kuzitumia vibaya.

Kwani uhalisi wa huduma ni mkusanyiko wa mali, aibaye

umeme, maji, au kuacha kulipa nauli ya garimoshi au metro na

vyengine, huwa sana na aibaye mali.

Na kama afanyae ujanja wa kutumia pesa bandia ili apate ruzuku

zake huyu nae ni mla haramu, kwani anachukua mali

Page 138: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

138

asiyostahiki. Na iwapo sheria imeweka kiwango maalumu na

pato maalumu kwa mwezi kwa bidhaa za mgao unaotolewa na

serikali basi kila atowaye bidhaa hizi kwa kwenda kinyume na

shuruti itakuwa nae yumo makosani. Kwa kuwa atakuwa ametoa

kwa wasiostahiki na kuwaacha wenye kustahiki au kwa wale

wenye kuhitaji zaidi. Vilevile kwa upande wa makazi wenye

kufanya hila za kutaka kujinufaisha wao na kuhalifu shuruti

zilizowekwa.

Hawa na kila anayewasaidia watakuwa ni washirika katika

makosa au wakawa wanazembea katika kutaka kurekebisha

kasoro au wakawa wana nia ya kupata kitu chochote kutoka

katika mali za umma kupitia uzembe wanaoufanya.

Siku zote na tukumbuke maneno ya Mtume wetu (rehma na

amani zimshukie): “nyote ni wachungaji, na nyote mutaulizwa

juu ya mulivyovichunga. Imamu ni mchungaji naye ataulizwa

juu ya aliowachunga, mume ni mchungaji juu ya watu wake

naye ataulizwa juu ya aliowachunga, mke ni mchungaji katika

nyumba ya mumewe naye ataulizwa juu ya aliowachunga,

mtumishi ni mchungaji juu ya mali ya bwana wake naye

ataulizwa juu ya alichokichunga.” (Bukhari). Na Mwenyezi

Page 139: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

139

Mungu atauliza kila mchungaji kwa kile alichokichunga iwapo

amekihifadhi au amekipoteza.

Mazungumzo ya Ijumaa

Wizi wa Kielimu na Athari Zake Kwa

Taifa

Kila tendo lina jawabu lake lililo sawa, na pia lina jawabu la

kinyume, kushajiisha kufanyika kwa utafiti, uchunguzi na

ugunduzi wa kielimu na kuendelea nao kwa ajili ya mustakabali

wa kweli inahitajika kuwepo nguvu na kuchukua hatua

madhubuti za kuweza kupambana na wizi wa kielimu na mfano

wake. Na hasa katika Nyanja za mafunzo ya taaluma na utafiti

Page 140: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

140

wa kielimu, kuwepo na adhabu kali kwa kila aibae matokeo ya

utafiti wa mwengine na izingatiwe kuwa ni moja kati ya makosa

yenye kuondosha heshima ambayo hayahitajiki kwa mtu

ambaye atapewa wadhifa wa uongozi kwani uongozi unahitaji

uaminifu na usafi na kuwa na tabia njema na heshima.

Na kujifunza kuwa muaminifu katika Nyanja za kielimu

inapaswa ianze mapema katika shule za msingi mpaka mwisho

wake na kuendelea katika Nyanja zote za kielimu.

Tukingalia uhalisi wetu tutafahamu kuwa baadhi ya sekta

ambazo hutoa elimu za ukamilisho kama zile zifunzazo malezi

na mafunzo ya mwisho kwa mfano, ukiongeza vyuo vitoavyo

vyeti vya sanaa huenda vikawa vinatoa mitihani isiyo kwenda

sambamba na hali halisi ya uwezo unaohitajika, jambo hili

inabidi lipelekee kuwepo kwa nidhamu ya ufatiliaji na

uchunguzi.

Tukikiri kuwa baadhi ya wahitimu wa diploma (uzamili) ya

sanaa hawawezi kusoma na kuandika kama ipasavyo na miaka

ambayo wamesoma tutaelewa kuwa ipo haja ya kubadili

mwenendo wa kitaaluma kwa namn ya utoaji wa mitihani na

upasishaji. Na kuhakikisha kuwa khifadhi nidhamu za kisayansi

na kielimu na utafiti na hasa nay ale yanayoshikamana na

Page 141: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

141

mitihani na namna ya kuitathmini kwani nayo pia ni amana. Na

kukengeuka ni khiyana na kumpa kwa asiyestahiki na

asiyekuwa na uwezo wa kumiliki, kitu ambacho kunatoa

wanafunzi wasio na uwezo hali ya kubeba vyeti visivyokwenda

sambamba na ukweli wa elimu zao, na wala hawawezi kuingia

katika soko la la wafanyakazi. Na kupelekea vyuo vilivyotoa

vyeti hivi kukosa thamani yake na nafasi yake na ubora wake

ndani ya nchi na nje pia. Si hivyo tu, bali hata mwanafunzi

mwenyewe kukosa hisia za kujua thamani ya cheti ambacho

amekipata na thamani ya nafsi yake, na kukosa uwezo wa kuishi

kwa mujibu wa hali halisi.

Na iapo udanganyifu umekatazwa katika hali zote, kwani

mtume (rehma na amani zimshukie juu yake) anasema:

“adanganyae si katika sisi”. Udanganyifu katika fani ya elimu

na fikira ni haramu zaidi na huondoa heshima na utukufu wa

mtu.

Na japokuwa kuna aina mbaya sana za udanganyifu ambazo

wengi hawawezi kuzijua (kwa mfano) ile ya kuiba kazi za tafiti,

kwa kumtaka mmoja wa wanafunzi au rafiki yake kumuandika

jina lake katika kazi ya utafiti ambayo hakushiriki hata kidogo

na wala hakutumia juhudi yoyote, kitu ambacho ninaomba

Page 142: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

142

ipatikane juhudi ya kumuhoji mtafiti kwa utafiti alioufanya kwa

njia ya mazugumzo ili tuhakikishe uwezo wake wa ufahamu.

Kwa ajili hiyo inapasa kwa pande zote husika zenye

mfungamano na fikira na elimu kuweka mipangilio ambayo

itafanyika bila ya kuiba elimu, au kumzuia asiye na uwezo

kupatia asichostahiki. Na ni lazima kutekelezwa sheria kwa

umakini na ukali kwa kila anayevunja sheria na nidhamu za

kielimu na kimalezi katika vyuo, na kuwepo na ufuatiliaji

unaoendelea kwa walimu na wengine. Ufuatiliaji uwe wa kweli

na sio wa kuzuga ili anayejitahidi aone matunda ya juhudi zake.

Na kwa siyejitahidi nae apate kujikaza kaztika juhudi na kuinua

kiwango chake au apewe kazi kwa mujibu wa uwezo wake, na

liwe hili waziwazi na si kwa ajili ya upendeleo wa aina yoyote.

Iwapo tunaamini thamani ya elimu kuwa ni njia pekee

itakayotuwezesha kuvuka na kuelekea katika usalama, basi njia

hii inapasa iwe ya ukweli na tuipe juhudi ya kweli inayostahiki

na kutaabika nayo, na kujikaza na kushikamana mabega hadi

tufikie katika manufaa yanayotarajiwa. Na tupate kigezo kizuri

kutokana nayo, na kuanzisha katika kila kituo cha elimu utafiti

au kuwepo na idara yenye kushughulikia suala la wizi wa

kielimu, ili tuelekee katika ulimwengu wa kielimu na taaluma,

Page 143: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

143

na taifa letu na watu wake wapate kusimama katika ulimwengu

ambao nguzo kuu za maendeleo ni elimu na teknolojia na kujua

anga za nje na ili vita yetu kubwa iwe ni ya kifikra na elimu na

teknolojia vita ambayo mshindi wake ni Yule mwenye kumiliki

vyanzo madhubuti na endelevu.

Kwa kutilia mkazo kuwa uisilamu umeipa elimu thamani

Mwenyezi Mungu anasema {Je huwa sawa wanaojua na

wasiojua, hakika wenye kukumbuka ni wale wenye akili}. Na

mtume wetu (rehma na amani ziwe juu yake anasema: “wasomi

(maulamaa) ni warithi wa mitume, na hakika ya mitume

hawakurithiwa dinari wala dirhamu (mali) lakini wamerithiwa

elimu na atakaeichukua basi kachukua fungu kubwa.” Na

akasema (rehma na amani zimshukie): “mwenye kupita elimu

yenye kushikamana na elimu basi Mwenyezi Mungu

atamuwepesishia njia ya kwenda peponi.” Na neno “elimu”

limekuja bila ya kuhusishwa elimu Fulani bali elimu yoyote ile.

Ikiwa na maana kuwa makusudio ni ile faida ipatikanayo

kupitia elimu, na msomi wa kweli, na mwanafunzi mwenye

juhudi na sio kwa mwenye kubeba cheti cha uongo au

kilichopatikana kwa njia ya udanganyifu na kilichokosa ukweli

na heshima.

Page 144: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

144

Wito Wa Kuwa na Matumaini

Uzuri ulioje wa kuwa na tama, na ubaya na hatari ilioje ya

kukata tama, kukata tamaa kuangamiza nafsi, na kuondosha

matarajio na huzalisha unyongevu na kutia simanzi. Kwa ajili

hiyo uisilamu umekataza kukata tamaa na kukatisha tamaa na

kujichangabya na kuchangaya na baadhi ya wasomi wakasema

hilo ni miongoni mwa madhambi makubwa.

Mwenyezi Mungu mtukufu anasema kwa ulimi wa Mtume

Yakubu (rehma na amana zimshukie juu yake: { Enyi wanangu!

Nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye,wala msikate tamaa na

Page 145: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

145

faraji ya Mwenyezi Mungu. Hakikahawakati tamaa na faraji ya

Mwenyezi Mungu isipo kuwa watu makafiri } na anasema

kupitia ulimi wa mtume Ibrahim (rehma na amani zimshukie

juu yake) { Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika!

Basikwa njia gani mnanibashiria? 55. Wakasema:

Tunakubashiria kwa haki; basi usiwemiongoni mwa wanao kata

tamaa. 56. Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema

yaMola wake Mlezi ila wale walio potea?

Na kutoka kwa Ibn Abass (radhi za Mwenyezi mungu

ziwashukie) amesema: Kijana mmoja alisema: “ ewe mjumbe

wa Mwenyezi Mungu, ni yepi madhambi makubwa? Akasema:

“ kumshirikisha mwenyezi Mungu na kutokuwa na matumaini

na upole wa Mweneyzi Mungu na kukata tamaa katika rehema

za Mwenyezi Mungu

Na tunamwambia mgonjwa hata kama ni maradhi ya

kudumu au ya vipindi kuwa usikate tamaa ya kutopona, na

kumbuka Mwenyezi Mungu alivyomponya mtume Ayubu

(rehma na amani ziwe juu yake) na akashikamana kwa

kumuomba mola wake na akamfanya kuwa ni kigezo pale

aliposema Mtukufu: { Na Ayyubu, alipo mwita Mola wake

Mlezi, akasema:Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye

Page 146: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

146

unaye rehemukuliko wote wanao rehemu. 84 Basi tukamwitikia,

na tukamwondolea madhara aliyokuwa nayo, na tukampa watu

wake na mfano wao pamojanao kuwa ni rehema inayo toka

kwetu, na ukumbusho kwa wafanyao ibada.}

Na iwapo ni tasa basi usisahau neema ya Mwenyezi Mungu

kwa mtume Zakariyya (rehma na amani zimshukie juu yake)

pamoja na umri wake mkubwa na utasa ambao hakutarajia

kupata mtoto, nah ii ni pale alipoita zakaria (rehma na amani

zimshukie juu yake) Mola wake “{Akasema: Mola wangu

Mlezi! Mafupa yanguyamedhoofika, na kichwa

kinameremeta kwa mvi; wala,Mola wangu Mlezi, sikuwa

mwenye bahati mbaya kwakukuomba Wewe 5. Na hakika

mimi nawakhofia jamaa zangu baada yangu.Na mke wangu

ni tasa. Basi nipe mrithi kutoka kwako. 6. Atakaye nirithi

mimi na awarithi ukoo wa Yaaqub.Ewe Mola wangu Mlezi!

Na umjaalie awe mwenyekuridhisha.} na anasema Mwenyezi

Mungu mtukufu {89 Na Zakariya alipo mwita Mola wake

Mlezi: Molawangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe

ndiye Mborawa wanao rithi. .90 Basi tukamwitikia, na

tukampa Yahya natukamponyeshea mkewe. Hakika wao

Page 147: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

147

walikuwa wepesi wakutenda mema, na wakituomba kwa

shauku na khofu. Naowalikuwa wakitunyenyekea.}

Na kikawaida kuwa mwanamke anapokuwa ni gumba ambae

hazai huwa anafanyiwa dawa kwanza ili azae. Lakini aya za

kurani hazikusema hivi isipokuwa mwenyezi Mungu anasema:

{ Basi tukamwitikia, na tukampa Yahya natukamponyeshea

mkewe.} wamebashiriwa mtoto kwa kutibiwa mke, na kama

kwamba Mwenyezi Mungu ana uwezo wa kumpa mtoto bila ya

sababu, sawa mke akitibiwa au hapana {hakika jambo lake

atakapo huwa anasema kuwa likawa}. Nayo ni kama

ilivyoelezwa katika kisa cha Nabii Ibrahimu (rehma na amani

zimshukie juu yake) wakati malaika walipombashiria mtoto

pamoja na kuwa alikuwa na umri mkubwa, Mweneyzi Mungu

anasema { Na mkewe alikuwa kasimama wima, akacheka.

Basitukambashiria (kuzaliwa) Is-haq, na baada ya Is-

haqYaaqub 72. Akasema: Je, hivyo mimi nizae, na hali

yangu nikikongwe na huyu mume wangu ni kizee? Hakika

haya nimambo ya ajabu! 73. Wakasema: Je, unastaajabia

amri ya Mwenyezi Mungu?Rehema ya Mwenyezi Mungu na

baraka zake ziko juu yenu,enyi watu wa nyumba hii!

Hakika Yeye ndiye Msifiwa wa kutukuzwa.}

Page 148: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

148

Na mtu awapo katika tabu au maafa aelewa kuwa hazina

za Mwenyezi Mungu ni nyingi na wala hazishi, na masiku

huzunguka kati ya mazuri na mabaya, tajiri wa leo huenda

akawa masikini kesho, na masikini wa leo huenda akawa tajiri

kesho.

Page 149: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

149

Huoni Kuwa Fakiri Hutaraji Utajiri

Na Tajiri Huogopea Ufakiri

Mwenyezi Mungu anasema {Na anaye mcha Mwenyezi Mungu

humtengezea njia ya kutokea. .3 Na humruzuku kwa jiha asiyo

tazamia. Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu Yeye

humtosha.} na anasema pia { Na anaye mcha MwenyeziMungu,

Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi.} na

anaendelea kusema {Rehema ambayo Mwenyezi Mungu

anawafungulia watu hapana wa kuizuia. Na anayo izuia hapana

wa kuipeleka isipo kuwa Yeye. Naye ndiye Mwenye nguvu,

Mwenye hikima.}

Na kwa kuupokea mwaka mpya hapana budi tujiweke

kuwa na tamaa ya muda ujao ulio bora na wenye kuchomoza,

kwani ufunguzi wa Mwenyezi mungu upo karibu. Tusikate

tamaa wala kufadhaika na wala tusiwe wa kutarajia mabaya.

Kwani dui wetu huwa anataka tukate tamaa na kuvunjika moyo,

na kwa kuwa dini yetu haijatufundisha kukata tamaa na wala

haijui kuvunja moyo sisi ni umma wenye tamaa kubwa.

Page 150: Kimefasiriwa Na Profesa/ Ayman Ibrahim Alaasar · 2016-04-10 · Wizi wa kielimu na athari zake kwa taifa 139 25 Wito wa kuwa na matumaini 144 . 4 Utangulizi Shukurani zote njema

150

Mbingu yenye huzuni imesema kwa ubaya

Nikasema: tabasamu wacha ubaya uwepo juu

Ikasema: Nyusiku zimeniumiza

Nikasema: wewe tabasamu tu hata kama zimekuumiza

Kwani mwengine wakikuona upo sawa

Basi huzuni huweka kando na wao huwa sawa.