husseinsengu.files.wordpress.com · web viewkatika sheria ya mtoto uthibiti wa ajira mbaya...

14
................. Tafsiri Rahisi ya Mkataba wa Haki na Ustawi wa Mtoto wa Afrika

Upload: others

Post on 04-Jan-2020

21 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: husseinsengu.files.wordpress.com · Web viewkatika sheria ya mtoto uthibiti wa ajira mbaya inayoongezeka barani Afrika na kuathiri watoto kiafya na kielimu kwa kuwazuia kupata elimu

.................

Tafsiri Rahisi ya Mkataba wa Haki na Ustawi wa Mtoto wa Afrika

Page 2: husseinsengu.files.wordpress.com · Web viewkatika sheria ya mtoto uthibiti wa ajira mbaya inayoongezeka barani Afrika na kuathiri watoto kiafya na kielimu kwa kuwazuia kupata elimu

YALIYOMO

Utangulizi ...................................................................................................... 1

Maudhui ........................................................................................................ 2

SURA YA KWANZA

Majukumu ya nchi wanachama .................................................................... 2

Maana/tafsiri ya mtoto ................................................................................. 3

Haki za kuzingatia baada ya mtoto kuzaliwa................................................. 3

Haki ya elimu kwa mtoto .............................................................................. 4

Haki za kuzingatia katika kumjenga mtoto kiafya na kimwili ........................... 5

Ajira kwa mtoto, mateso na unyanyasaji ...................................................... 5

Taratibu za kumuadabisha mtoto aliyevunja sheria ...................................... 6

Ulinzi toka kwa familia ................................................................................... 6

Ulinzi dhidi ya mila na tamaduni gandamizi .................................................. 7

Haki ya ulinzi kwa mtoto katika mazingira ya vita/ukimbizi .......................... 7

Kuasili ............................................................................................................ 7

Mtoto aliyepotezana/kutengana na wazazi/walezi ....................................... 8

Ulinzi dhidi ya ubaguzi na manyanyaso ......................................................... 8

Biashara haramu dhidi ya watoto ................................................................. 8

Adhabu kwa mama mwenye mtoto .............................................................. 8

Wajibu wa mtoto ........................................................................................... 8

SURA YA PILI:Kuanzishwa na mamlaka ya kamati ............................................................... 9Mamlaka na taratibu za kamati .................................................................... 10

MFASIRI Hussein F. Sengu

CONSULTANT CHILDREN’S RIGHTS

Tafsiri Rahisi ya Mkataba wa Haki na Ustawi wa Mtoto wa Afrika

Maarifa ni Ufunguo na Children in Crossfire

2012

Page 3: husseinsengu.files.wordpress.com · Web viewkatika sheria ya mtoto uthibiti wa ajira mbaya inayoongezeka barani Afrika na kuathiri watoto kiafya na kielimu kwa kuwazuia kupata elimu

UTANGULIZI:

Utangulizi

Kijitabu hiki ni fasili ya maudhui ya ya Mkataba wa Haki na Ustawi wa Mtoto wa Afrika, ambayo yanaendana / kufananishwa na sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 ya Tanzania. Huu ni mkataba wa kwanza wa kikanda uliotungwa kukuza / kueneza / kuendeleza maudhui ya Mkataba wa Haki za Mtoto wa Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia uhalisia wa maisha ya mtoto wa Afrika.

Madhumuni ya fasili ni kukuza uelewa kwa wasomaji walengwa vipengele muhimu vya Mkataba wa Haki na Ustawi wa Mtoto wa Africa na sheria ya Mtoto ya 2009.

Mktaba unainisha hali ya baadhi ya watoto wa Afrika kuwa katika mazingira yanayowapa fursa ya kukua, kujifunza na kufurahia upendo wa familia zao wakati kubwa la watoto wengi wanataabika kutokana na umasikini, maradhi na kukosa huduma muhimu za kijamii kutokana na vita, majanga ya kiasili na umasikini.

Kama ulivyo Mkataba wa Haki za Watoto wa Umoja wa Mataifa (Convention on the Rights of the Child - CRC), Mkataba wa Afrika wa Haki za Mtoto umetungwa kama chombo cha kutoa ulinzi kamili kwa mtoto wa Afrika.

Mkataba wa Haki na Ustawi wa mtoto wa afrika uliridhiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika yaani Umoja wa Afrika mwezi Julai 1990, na kuanza kufanya kazi rasmi mwezi

November 1999. Hivyo nchi zote za ukanda wa mashariki na kusini mwa Afrika zimerithia mkataba huu isipokuwa Somalia na Zambia ambazo wamesaini bila kuridhia.

Mkataba ulitungwa kwa kuzingatia uhasilia wa mazingira ya kiafrika tofauti na mkataba wa kimataifa uliotungwa kwa ushiriki hafifu wa wa nchi za kiafrika kutokana nauwakilishi mdogo.

Maeneo yaliyosahauliwa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kuzingatiwa na mkataba wa Afrika ni: unyanyasaji na ubaguzi wa rangi hasa kwa watoto, mila gandamizi hasa kwa watoto wa kike kama vile ukeketaji, ndoa za utotoni na kuachishwa masomo, haki ya mtoto aliyetumboni wakati mama yake amefungwa akiwa mjazito, umasikini na mazingira safi na salama ya kuishi kwa watoto, nafasi ya familia katika makuzi na ustawi bora wa mtoto.

MAUDHUI

Mkataba umesheheni haki za msingi za mtoto ukilenga kuhimiza ustawi bora wa mtotokwa kuweka misingi ya kuthibiti mazingira ya unyanyasaji wa kijinsia kwa kunyimwa haki ya kupata ya elimu, afya, kulindwa, na kadhalikwa, kulazimishwa kufanya majukumu mazito ya kivita na ajira za watoto kama biashara haramu ya ngono. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la umoja wa mataifa la kutetea watoto (UNICEF), watoto million 150 duniani walio na umri kati ya miaka 5 mpaka 14 wanafanyishwa kazi katika mazingira magumu na kukosa haki zao zingine za msingi..Mfano thelusi ya idadi ya watoto katika nchi za ukanda wakusini mwa Sahara wanatumikishwa katika ajira haramu za watoto.

SURA YA KWANZA

Page 4: husseinsengu.files.wordpress.com · Web viewkatika sheria ya mtoto uthibiti wa ajira mbaya inayoongezeka barani Afrika na kuathiri watoto kiafya na kielimu kwa kuwazuia kupata elimu

HAKI NA WAJIBU:

Mkataba umeainisha haki za msingi za mtoto na wajibu kwa wahusika wa kukuza ustawi bora wa mtoto, hivyo kutoa wito kwa nchi kutunga sheria kulinda ustawi huo. Nchi na hasa Tanzania ilitunga sheria ya Mtoto ya 2009 kuitikia wito huo kwa kuzingatia mambo muhimu ifuatavyo:

Katika kifungu cha 1 (Aya ya 1 – 3) mkataba unatamka majukumu ya nchi wanachama ya kutambua haki, uhuru, na ulinzi wa maslahi kwa ustawi bora wa mtoto, pamoja kutimiza majukumu kama sehemu ya sheria za nchi bila kuathiri sheria nyingine zinazohusu kulinda haki na maslahi bora ya mtoto kwa kupambana na mila na desturi potofu zinazopelekea ukatili na unyanyasaji wa moto.

Katika vifungu cha 2, 3, 4 na 5 tafsiri sahihi ya mtoto inatolewa na haki zake za msingi ili kuondoa utata wa tafsiri wa nchi na nchi kimtazamo na kupelekea baadhi ya haki kupuuzwa. Kwa mujibu wa kifungu cha 2 cha Mkataba. Mtoto ni binadamu yoyote aliye na umri chini ya miaka 18.

i. Mkataba umebaini haki na mambo ya nchi mwanachama kuzingatia yakiwa ni kuhakisha kuwaWatoto hawabaguliwi kwa misingi yoyote ya kijinsia, kikabila, kilugha, kiudini, utaifa au ueneo na hivyo kukomesha aina yoyote ya ubaguzi.

ii. Kipaumbele kinatolewa kwa watoto katika kufanya maamuzi, na mipango mbalimbali hasa inayowahusu

watoto, kwa mfano maamuzi ya mahakama pale ambapo kutakuwa na mgogoro wa kisheria na mtoto, au katika mipango ya maendeleo ambayo kwa njia moja au nyingine itawagusa watoto.

iii. Haki ya uhai na usalama wa mtoto zinalindwa na sheria na taratibu mahsusi za kulinda usalama wa mtoto ikiwa ni pamoja na kupinga adhabu ya kifo kwa watoto.

Kwa mujibu wa vifungu vya 6 hadi 10, mkataba unaainisha haki za kuzingatia baada ya mtoto kuzaliwa za kuzingatiwa kwa kuziwekwa kwenye sheria za mtoto na utekeleza wake kusimamiwa kikamilifu ili kuhakikisha kuwa mtoto anapata haki ya

Page 5: husseinsengu.files.wordpress.com · Web viewkatika sheria ya mtoto uthibiti wa ajira mbaya inayoongezeka barani Afrika na kuathiri watoto kiafya na kielimu kwa kuwazuia kupata elimu

i. Utaifa, na kutambuliwa rasmi kwa mujibu wa sheria, hivyo kupatiwa jina na kusajiliwa mara tu baada ya kuzaliwa,

i. ii. Uhuru wa kusikilizwa, kukusanyika, kutoa mawazo na kuabudu.

ii. Iii. M Kuwa na faragha na kutoingiliwa na kutwezwa utu wake.

Kuhusu haki ya mtoto kupata elimu bora yenye sifa ya kulenga .1. Kukuza haiba, ujuzi, akili na maarifa ya mtoto.

ii. Kumjengea mtoto utamaduni wa kupenda na kuheshimu haki za binadamu iii. Kumjenga mtoto katika maadili na mitazamo bora na sahihi ya kiafrika.

iv.Kumuandaa mtoto kuingia katika maisha huru na jamii yoyote kwa kuheshimiana na kuvumiliana katika tofauti za kidini, mitazamo ya kisiasa na tamaduni hasa kukitoa tofauti ya hoja za makundi ya kidini, kisiasa au kikabila.

i. Kumjengea mtoto uzalendo, heshimu na kuthamini utaifa wake na umoja wa waafrika, kuthamini na kulinda mazingira na maliasili za nchi yake na bara la Afrika kwa ujumla pamoja na umuhimu wa huduma za Afya ya msingi.

Kwa utekelezaji wa malengo mkataba umeagiza nchi wanachama kutimiza majukumu ya:

a. Kutoa elimu ya msingi bure kwa watoto wote walio katika umri stahili.

b. Kuboresha elimu ya ngazi ya sekondari iwe itolewa bure na lazima kwa watoto wote.

c. Kuwezesha elimu ya juu kupatikana kwa wote wanaofuzu bila vipingamizi.

d. Kufanya jitihada ya kuhakikisha kuwa makundi yote yaliyopembezoni na kusahauliwa kama wasichana, walemavu, na vipaji maalumu yanapata fursa sawa ya kupata elimu.

Mkataba imetoa rai kwa nchi wanachama kutoa kipaumbele katika sheria ya mtoto kwa wazazi walezi kutimiza majukumu kuwapatia elimu bora watoto wote ikiwa pamoja na. na wasichana waliopata mimba wakiwa mashuleni kuruhusiwa kupata elimu japo kwa mpango maalumu.

Page 4

Page 6: husseinsengu.files.wordpress.com · Web viewkatika sheria ya mtoto uthibiti wa ajira mbaya inayoongezeka barani Afrika na kuathiri watoto kiafya na kielimu kwa kuwazuia kupata elimu

Katika vifungu 12, 13 na14 haki za kuzingatia katika kumjenga mtoto kimwili na afya zilizoainishwa ni:

Haki ya kila mtoto ikiwa na mlemavu kupata huduma ya elimu na afya bora.

Haki ya kila mtoto kucheza. Haki ya kila mtoto kushiriki kufanya kazi inayokuza

utaalamu na ujuzi, basi katika mazingira hayo sheria za nchi zihakikishe kuwa mtoto hafanyishwi kazi itakayohatarisha afya yake, na ilenge kumjenga na si kumnyonya..

Mkataba umeainisha majukumu ya wadau mfano wazaz, walezi na hasa serikali katika kusimamia na kutekeleza mikakati ya kutoa haki kwa watoto. .

Kuhusu haki ya ajira kwa mtoto na ulinzi dhidi mateso na unyanyasaji, vifungu 15 na 16 vinaagiza nchi wanachama kuweka katika sheria ya mtoto uthibiti wa ajira mbaya inayoongezeka barani Afrika na kuathiri watoto kiafya na kielimu kwa kuwazuia kupata elimu.

Kuhusu taratibu za utoaji wa haki na uwajibishaji kwa mtoto aliyevunja sheria, kifungu 17 cha Mkataba. kinahimiza nchi kuhakikisha utoaji wa haki/ kwa mtoto unaendana na wajibu wake. Pia kimeelekeza namna ya kuhakiki upatikanaji wa haki kwa mtoto na uwajibikaji wake. Maelekezo kwa nchi mwanachama ni

a. Kuzingatia haki ya asili kuwa mtoto yoyote anayetuhumiwa kufanya kosa hatoadhibiwa mpaka ithibitishwe pasipo na shaka na chombo maalumu kilichopewa dhamana ya kusimamia haki za mtoto.

b. Mtoto asiwekwe mahabusu moja na watu wazima, ila sehemu maalumu ya watoto naa asiadhibiwe au kuteswa.

c. Utaratibu wa kuendesha mashitaka ulenge kuimarisha ustawi wa mtoto na si kuutweza utu wake na kuathiri maisha yake ya baadae. Lengo liwe kumjenga na si kumuumiza.

d. Kuhakikisha kuwa mtoto anapata uwakilishi wa Wakili wa kumsimamia katika utetezi wake.

e. Lazima kuwe na umri maalumu utaowekwa kisheria kwamba kuanzia hapo ndio mtoto anaweza kushitakiwa.

Kuhusu Ulinzi toka kwa familia na majukumu ya wazazi / walezi, vifungu 18, 19 na 20 vya mkataba vimeweka bayana majukumu yao katka kumpatia mtoto ulinzi ili akue akiwa na maadili na mipango endelevu ya maisha yake.

Majukumu ya wazazi wa familia ikiwachombo cha asili na cha muhimu sana katika ustawi bora wa mtoto ni a. Kuhakikisha kuwa haki zote za msingi anazostahili mtoto katika ngazi ya familia anapatiwa na zinalindwa mfano wa haki ya kupata jina, haki ya kupata elimu haki ya kucheza na, haki ya matunzo ya wazazi, na kwa

Page 5

Page 7: husseinsengu.files.wordpress.com · Web viewkatika sheria ya mtoto uthibiti wa ajira mbaya inayoongezeka barani Afrika na kuathiri watoto kiafya na kielimu kwa kuwazuia kupata elimu

kukaa na wazazi bila kutenganishwa. Isipokuwa pale vyombo vya kisheria vitakapoamua ipasavyo.

Kwamba wazazi/walezi watakuwa na jukumu la msingi la kuhakikisha kuwa katika malezi na makuzi ya mtoto wanazingatia;

a. Maslahi bora ya mtoto ndio kipaumbele chaob. Kwa kadri ya uwezo wao wa kifedha wanampatia mtoto

mahitaji muhimuc. Wanamjenga mtoto kimaadili kwa mujibu wa tamaduni bora

za kiafrikaPamoja na jitihada hizo za mlezi/mzazi pia wadau wengine mbali na serikali wanapaswa kuunga mkono jitihada za mzazi/mlezi katika kuhakikisha kuwa mzazi anaweza kuyatekeleza hayo kwa kuwa mzazi/mlezi peke yake hatoweza kukamilisha yote.

Kifungu cha 21: Ulinzi dhidi ya mila na tamaduni gandamizi

Nchi wanachama zihakikishe kuwa zinafanya njia zote kutokomeza mila na tamaduni gandamizi zinaathiri utu, maisha na ustawi bora wa mtoto ambazo kwa ujumla;

a. Zinapelekea athari za afya kwa mtotob. Zinapelekea kuutweza utu na heshima ya mtoto hasa kwa

maisha yake ya baadaec. Zinamdhalilisha mtoto hasa katika hali maumbile, kijinsia na

hali zingineNdoa za utotoni zipingwe na nchi wanachama wahakikishe kuwa wanawalinda watoto kutokana na ndoa za utotoni.

Kifungu cha 22 na cha 23: Haki za mtoto katika mazingira ya kivita na ukimbizi. Japokuwa kwa Tanzania tumekuwa tukifurahia amani ilidumu kwa muda mrefu, lakini kwa nchi za wenzetu barani africa kumekuwa na vita vikiendelea na kusababisha madhara makubwa hasa ukizingatia kuwa waathirika panapotokea vita huwa ni kina mama na watoto, hivyo Umoja wa africa ukaona kupitia mkataba huu ni bora kuzisisitiza nchi wanachama kuhakikisha kuwa katika mazingira ya kivita na hali ya ukimbizi haki za mtoto ziendelee kulindwa kwa kuhakikisha kuwa;

1. Watoto wanapewa ulinzi wakati wa vita, na wasihusishwe na shughuli za kijeshi

2. Kuhakikisha kuwa nchi wanachama wanatoa ruhusa na hifadhi kwa mtoto mkimbizi atayekimbilia nchi yoyote kwa hifadhi, na kupatiwa mahitaji yote ambayo mkimbizi anastahili

3. Pale ambapo mtoto atakuwa amepotezana na wazazi/walezi wake, nchi mwanachama kwa kushirikiana na mashirika na jumuiya zozote wadau wa masuala ya wakimbizi

Page 8: husseinsengu.files.wordpress.com · Web viewkatika sheria ya mtoto uthibiti wa ajira mbaya inayoongezeka barani Afrika na kuathiri watoto kiafya na kielimu kwa kuwazuia kupata elimu

watahakikisha kuwa wanafanya jitihada za kuwakutanisha mtoto na wazazi/walezi wake. Haki hizo na zingine zote za mtoto mkimbizi, pia atatakiwa kupata mtoto ambae atakuwa ni mkimbizi wa ndani. Ambaye atakuwa kapotezana na wazazi/walezi kutokana na majanga ya kiasili, matatizo ya ndani ya nchi au sababu nyingine yoyote.

Kifungu cha 24: Kuasili Katika kuasili mtoto nchi wanachama wametakiwa kuhakikisha kuwa zinakuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa zinaweka sheria nzuri za kuasili mtoto zitakazolinda haki na kwa maslahi ya mtoto anayeasiliwa kwa kufanya yafatayo;

i. Waleza/wazazi wanatoa ridhaa yao kwa mtoto anayetaka kuasiliwa

ii. Kufuata sheria na kimataifa, za kikanda au za nchi kama zipo zinzolinda maslahi ya mtoto anayeasiliwa

iii. Kuhakikisha kuwa mtoto anayeasiliwa nchi ingine anapatiwa fursa na haki kama mtoto wa nchi aliyeasiliwa anavyopatiwa mahitaji.

iv. Kuwe na utaratibu wa kufuatilia maendeleo na matunzo ya mtoto aliyeasiliwa

Kifugu cha 25: mtoto aliyetengana/kupotezana na wazazi/walezi Katika mkataba huu ili kulinda haki za mtoto ambaye atakuwa mbali na wazazi/walezi wake na kwa kutambua umuhimu wa mtoto kuwa karibu na wazazi/walezi wake. Nchi wanachama wamesisitizwa katika mkataba huu kuhakikisha kuwa wanaweka mazingira mazuri ya kisheria na ya kitaasisi kuhakikisha kuwa:

a) Mtoto anapata hifadhi katika taasisi au kituo maalumu na mahitaji ya muhimu wakati taratibu zingine zinafanywa.

b) Wazazi/walezi wanatafutwa na kuunganishwa na mtoto waoc) Yote hayo yafanyike kwa kujali maslahi na ustawi bora wa

mtoto.

Kifungu cha 26: Ulinzi dhidi ya ubaguzi na manyanyasoNchi chache barani Afrika zimekuwa zikilaumiwa kwa kushindwa kuzuia mifumo ya ubaguzi wa rangi na manyanyaso, pia hata nchi zingine japo hazikutajwa sana ila zimekuwa na baadhi ya watu au taasisi zinazoendelea ubaguzi na manyanyaso, kwa kutambua hilo mkataba huu unalenga kulinda maslahi ya mtoto katika mazingira ya ubaguzi na manyanyaso kwa kuwataka nchi wanachama;

1. Nchi wanachama zinachukuwa jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa zinazuia ubaguzi na unyanyasaji wa hali yoyote kwa mtoto.

2. Kuhakikisha zinawachukulia hatua madhubuti na kutokomeza watu, taasisi au makundi yoyote yanayoendelea kuendeleza ubaguzi na manyanyaso

Page 7

Page 9: husseinsengu.files.wordpress.com · Web viewkatika sheria ya mtoto uthibiti wa ajira mbaya inayoongezeka barani Afrika na kuathiri watoto kiafya na kielimu kwa kuwazuia kupata elimu

Kifungu cha 27, 28 na 29: Biashara haramu dhidi ya watoto.Nchi wanachama wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanapambana vikali na biashara zote haramu zinazohatarisha afya, ustawi na maisha ya mtoto, kwa kuweka sheria kali na kuzisimamia ili kutokomeza biashara hizo haramu zinazofahamika kama:

1. Biashara ya ngono kwa watoto2. Madawa ya kulevya na mihadarati3. Biashara haramu ya watu

Kifungu cha 30: adhabu ya Kifungo kwa mama mwenye mtoto

Mkataba huu umeenda mbali zaidi na kuona haki ya mtoto ambae mama yake anaweza kutwa na hatia na kufungwa zitapotea, kwa kuhakikisha kuwa japo Mama wa mtoto atakuwa amekutwa na hatia basi maslahi ya mtoto yawekwe mbele kwa kuhakikisha kuwa

Mama huyo anapewa adhabu zingine na si ya kifungo. Kwa kumfunga mama kutapelekea mtoto akose haki zake za msingi kutoka kwa mama kama zilivyo orodheshwa katika mkataba huu.

Hivyo basi nchi wanachama wametakiwa kuangalia adhabu mbadala na si ya kifungo kwa mama atakaye kutwa na hatia wakati ana mtoto mdogo.Kifungu cha 31: wajibu wa mtotoBila kuathiri haki zake zingine mtoto pia anawajibu wa kufanya na si haki tu, kifungu hiki pia kimejumuishwa katika sheria ya mtoto ya mwaka 2009 ya Tanzania, kikiwa na malengo ya kumjengea mtoto utamaduni wa kuheshimu na kufuata taratibu zilizowekwa ili pamoja na kulinda haki zake pia kumjenga kuwa mzalendo na

anayeheshimu sheria na haki za binadamu, katika mkataba wajibu wa mtoto umeorodheshwa kuwa ni;

a) Kusaidiana na wanafamilia kuijenga familia yake.b) Kuwa na heshima kwa wazazi/walezi na wakubwa wake pia

kwa wadogoc) Kutumia uwezo wake wote kulitumikia Taifa lake kwa

mujibu wa nafasi yaked) Kuwa mbele katika kutunza na kuzikuza taratibu na

tamaduni nzuri za taifa lake na za kiafrikae) Kushiriki kadri ya uwezo wake katika kuchangia kukuza

maendeleo ya umoja wa Afrika.

SURA YA PILI

Page 10: husseinsengu.files.wordpress.com · Web viewkatika sheria ya mtoto uthibiti wa ajira mbaya inayoongezeka barani Afrika na kuathiri watoto kiafya na kielimu kwa kuwazuia kupata elimu

KUANZISHWA NA MAMLAKA KWA KAMATI YA HAKI NA USTAWI WA MTOTO YA UMOJA WA AFRIKA.

Ili kuyasimamia yaliyo katika mkataba huu, umoja wa Afrika utakuwa na kamati mahsusi yenye wataalamu waliobobea katika masuala ya haki za mtoto. Kamati itakuwa na wajumbe 11 wenye maadili na nidhamu ya hali ya juu pia ni wabobevu katika masuala ya haki za watoto, ili nchi wanachama washiriki kwa uwiano sawia, hakutatoka wajumbe zaidi ya mmoja katika nchi moja.

Katika sura hii inayozungumzia kamati ya haki na ustawi wa mtoto ya umoja wa Afrika taratibu mahsusi zimewekwa za kuwapata wajumbe ambazo zina umakini wa kuhakikisha kuwa wajumbe wataopatikana watakuwa ni wajuzi, mahiri na wabobevu, na pia mzuri utaopelekea kutoa manung’uniko kwa nchi wanachama wengine. Ili kuhakikisha hilo yafuatayo yamebainishwa kwa uwazi, demokrasia na umahiri;

1. Uchaguzi wa wajumbe2. Sifa za wagombea3. Muda wa kuhudumu4. Panapokuwa na nafasi pael ambapo mjumbe amejitoa

Ifahamike tu kuwa kamati hii ni kiungo muhimu sana kati ya nchi wanachama na utekelezaji wa mkataba huu, kwa kuwa sheria za kimataifa ni tofauti na sheria za kitaifa ambazo utekelezaji wake si wa hiyari.

SURA YA TATU

MAMLAKA NA TARATIBU ZA KAMATI

Utekelezaji wa sheria za kimataifa ni tofauti sana na utekelezaji wa sheria za nchi, hivyo basi mamlaka waliyopewa kamati na kwa kuzingatia kuwa hii ni sheria ya kimataifa ni pamoja na;

1. Kukuza na kupelekea utekelezwaji wa mkataba huu na nchi wanachama

2. Kufanya tafiti mbalimbali juu ya haki na ustawi wa mtoto barani Afrika ikiwa ni pamoja na kushirikiana na kuzihimiza taasisi na mashirika mbalimbali yanayofanya kazi za ulinzi wa haki za watoto barani Afrika

3. Kuandaa taratibu na miongozo mbalimbali inayolenga kukuza na kulinda haki na ustawi wa mtoto kama ambavyo mkataba utavyohitaji

4. Kutoa tafsiri sahihi ya vifungu vya mkataba huu kwa nchi wanachama, wanazuoni na umoja wa mataifa

5. Pamoja na majukumu mengine watakayopangiwa na baraza la wakuu wanchi za umoja wa Afrika

Kamati itakuwa inapokea taarifa zitakazokuwa zinawasilishwa na nchi wanachama juu ya utekelezaji wa mkataba na hali halisi ya haki za watoto katika nchi hizo. Lakini pia mkataba umewapa nguvu kamati ya kupokea taarifa kutoka katika vyama vya kiraia, asasi mbalimbali pia hata kutoka kwa mtu binafsi mwenye utashi juu ya haki za watoto.