kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na...

23
Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu b a a d a y a m s i m u k u p a n da l i s h e y a m i m e a u li n z i w a m i m e a

Upload: others

Post on 18-Jan-2021

9 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu

baada ya msimu kupanda

lishe ya mimea

ulinzi

wa mim

ea

Page 2: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

2

DIBAJI“Pamba kutoka Afrika” (CmiA), ni ubunifu wa taasisi ya Aid by Trade Foundation (AbTF), inayolenga kuboresha ustawi, ekolojia na uchumi wa idadi kubwa ya wakulima wa Pamba wa kiafrika na familia zao. Pamoja na kuwa na ubia na makampuni ya Pamba, CmiA inalenga kuhakikisha uwepo wa mafunzo katika ukulima wa kisasa, wenye tija na amabo ni rafiki kwa mazingira. Kupitia mfumo huru ya uhakiki, CmiA imejenga vigezo vya kiustawi, kiuchumi na kimazingira kwa kuzingatia falsafa ya: Watu-Faida-Sayari.

Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation huwezesha watumishi wa ugani wa wabia kuwa na uwelewa na stadi ambavyo iwapo vitaelekezwa kwa wakulima huongeza uzalishaji wa mazao bora na kupunguza matumizi ya viuatilifu vyenye sumu. Vigezo vya huzingatia mafunzo ya mara kwa mara ya uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu kama mwongozo wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) unavyosema. Kitabu hiki cha picha kinatafasiri uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu (IPPM) katika mfumo unaotekelezeka na kinalenga kuwa njia sahihi ya kuhanisha mafunzo na kwa vitendo.

Kitabu cha sasa cha ya “uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu” ni matokeo ya mawasiliano mapana na wabia katika Kusini mwa Bara la Afrika na wataalamu elekezi wa Huduma za Ugani, kwa majina Dr. Ben Sekamatte na Rudy van Gent, na ambao AbTF inapenda kuwashukuru kwa michango yao ya michoro ambayo imewekwa pamoja na picha katika vijitabu vya picha vya CmiA.

“Watoto na kilimo cha pamba-mazoea/matendo mazuri na Utumishaji mbaya wa watoto” na “Kijitabu cha picha cha Vidole vitano katika Ukulima bora wa Pamba”.

Uchapishaji© Aid by Trade Foundation

Bramfelder Chaussee 105

22177 Hamburg

Germany

Tel. +49 (0)40-6461-7971

Fax+49 (0)40-6461-1009

Email: [email protected]

www.cottonmadeinafrica.org

Mhariri: Alexandra PerschauMichoro: Donald Grant, 2016

Imechapwa kwa msaada wa C&A Foundation

Page 3: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

3

UTANGULIZI KWA UZALISHAJI JUMUISHI NA USIMAMIZI WA KUZUIA VISUMBUFUSwali la 1. Kuna changamoto kuu zipi kwa ufanisi wa uzalishaji jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu katika neon lako?Jibu la 1. ● Kukosekana kwa viuatilifu vya kutosha na vyenye bora kwa wakulima. ● Kwa kawaida, unyunyiziaji zaidi wa viuatilifu hufanyika wakati wa mvua nyingi na viuatilifu vingi hupotea bure. ● Kutokuwa na fedha au njia ya kupata fedha kwa ajili ya kununulia mbolea na hivyo kuwa na mimea inayokosa virutubishi.

Swali la 2. Kwa nini ni muhimu kwa wakulima kujifunza namna ya kutengeneza na kutumia viuatilifu vya kiasili?Jibu la 2. ● Kama unavyoweza kutumia mimea yenye sifa za kutibu badala ya kwenda kwa daktari na kulipia dawa, viuatilifu vya kiasili vinaweza kutumika kwa urahisi kupunguza mbinyo wa visumbufu hadi kiwango ambacho mmea unaweza kustahimili. ● Viuatilifu vya viwandani ni aghali na vina athari kwa wanadamu na vinadhuru wadudu rafiki au wenye faida. ● Viautilifu viatokanavyo na mimea hupatikana kwa urahisi kwa mkulima na vina bei nafuu.

Swali la 3. Utafanya nini ili uwe na afya?Jibu la 3. Kula chakula bora chenye lishe ambacho huwezesha kuwa na kinga imara na inayoweza kupambana na maaradhi.

Swali la 4. Kwa nini ni muhimu kuoanisha elimu juu ya visumbufu na lishe ya mimea kwa kutumia mbolea za asili? Jibu la 4. Mimea iliyostawi inaweza kukabiliana na mashambulizi ya visumbufu. Kwa kulinganisha na mtu mwenye lishe bora na afya, mmea unaweza kukabiliana peke yake na maradhi na mashambulizi ya visumbufu kwa urahisi zaidi.

Page 4: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation
Page 5: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

5

Swali la 1. Unaona nini katika picha iliyo kushoto?Jibu la 1. ● Mwanaume (Jina lake ni Nicodemus) ● Mfuko wa mbegu zenye manyoya ● Beseni lenye mavi ya ng’ombe ● Ndoo kubwa ya plastiki kwa ajili ya kuchanganyia ● Kijiti cha kukorogea wakati wa kuchanganya mavi ya ● Ng’ombe na mbegu na maji ya kutumia katika mkorogo ● Udongo wa kichuguu

Swali la 2. Mwanaume huyo anafanya nini?Jibu la 2. Mwanaume huyo anahifadhi mbegu za Pamba kwa kutumia mkorogo wa mavi ya ng’ombe, maji na udongo wa kichuguu.

Swali la 3. Anachanganyaje vitu hivyo?Jibu la 3. Kwanza, anachanganya kilo 1 ya mavi ya ng’ome na nusu kilo ya udongo wa kichuguu na kuongeza maji ili mkorogo uwe laini. Anaweka na kukoroga kipimo cha mbegu za manyoya kutosha hektari moja (kama kilo 15) katika tope hilo hadi kila mbegu imepakwa na kuonekana kama kapira kadogo.

Swali la 4. Kwa nini ni muhimu kuvaa glovu ukiwa unachanganya mbegu zilizohifadhiwa kwa viuatilifu?Jibu la 4. Mbegu zimetiwa dawa ili kuulinda mmea dhidi ya maradhi na mashambulizi ya awali ya visumbufu. Ili kujikinga na kuwashwa kwa ngozi au madhara hasi mengine, ni muhimu kuvaa glovu. Kazi hii ifanywe na watu wazima wenye afya tu; MARUFUKU kufanywa na watoto, wajawazito au mama wanaonyonyesha.

Swali la 5.Nini manufaa ya kuhifadhi mbegu kwa kutumia mavi ya ng’ombe?Jibu la 5. Mavi ya ng’ombe yana vimelea asili vingi vyenye faida ambavyo hulinda mmea dhidi ya vimelea vya magonjwa vilivyo katika udongo. Zaidi ya hapo, mavi ya ng’ombe yamejaa virutubisho na

homoni za kukua. Hii itasaidia mbegu kuota na kuupa mche mwanzo mzuri kwa kuupatia virutubisho kutoka mwanzo.

Swali la 6. Je, waweza kuhifadhi mbegu zingine zaidi ya Pamba?Jibu la 6. Ndiyo, mchakato huu unaweza kutumika kwa mbegu zamahindi au za zao lo lote unalotaka kupanda shambani mwako.

Swali la 7. Unaona nini katika picha iliyo kulia?Jibu la 7. Mwanamke, labda mke wa Nicodemus (Jina lake ni Mama.)

Swali la 8. Mama anafanya nini?Jibu la 8. Anapanda mbegu za Pamba zilizohifadhiwa kwa mavi ya ng’ombe. (Ndoo ile aliyotumia Nicodemus kukoroga mbegu inaonekana karibu na Mama.)

Swali la 9. Ni wakati gani anafanya hii kazi?Jibu la 9. Anafanya hii kazi baada ya mbegu zilizochanganywa na mavi ya ng’ombe kukauka , kama baada ya saa moja au mbili baada ya mume wake kuchanganya mbegu na mavi ya ng’ombe.

Ngazi ya juu : Swali la 10. Kuna njia nyingine tofauti za kuhifadhi mbegu?Jibu la 10. Ndiyo. Mkojo wa ng’ombe unaweza kutumiwa namna mavi ya ng’ombe yanavyotumiwa. Ni mbolea madhubuti ambayo hufanikisha uotaji wa mbegu.

KUHIFADI MBEGU ZA PAMBA KWA KUTUMIA MAVI YA NG’OMBE

Page 6: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation
Page 7: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

7

Swali la 1. Unaona nini katika picha ya kushoto?Jibu la 1. ● Nicodemus, mke wake Mama na binti yao (Nima) ● Kisanduku cha karatasi gumu ● Kis ● Rola ya kamba ● Kijiti kidogo chenye miiba

Swali la 2. Je, familia hii inafanya nini?Jibu la 2. ● Nicodemus anatoboa matundu katika kipande cha boksi alichokata mapema akitumia kisu. ● Mke wake, Mama anasokota kipande cha kamba. ● Mtoto Nima anaangalia picha ya kibao chenye vimambo katika kitabu. ● Familia inatengeneza kibao chenye vimambo kinachofanana na msichana anachoangalia katika kitabu.

Swali la 3. Unaona nini katika picha ya kulia?Jibu la 3. ● Nicodemus akiwa ameshikilia kibao chenye vimambo. ● Shamba la Pamba lenye mimea michanga ya Pamba.

Swali la 4. Je, Nicodemus anafanya nini?Jibu la 4. Anachunguza mimea ya Pamba katika shamba lao.

Swali la 5. Nini uchunguzi unapaswa kuanza?Jibu la 5. Uchunguzi ufanyike wiki 3 hadi 4 baada ya mbegu kuota. Zaidi ya kuchunguza uwepo wa visumbufu, pia angalia hali ya afya ya mimea na kama itathitaji mbolea ya majani.

Swali la 6. Kwa nini familia ianze kuchunguza mapema hivi katika hatua hii ya ukuaji wa mimea?Jibu la 6. ● Huu ndiyo wakati vidukari hushambulia miche. ● Hiki ndicho kipindi cha kuzaliana na kuongezeka kwa wadudu rafiki/wenye faida ambao hushambulia mazalia ya vidukari na kupunguza idadi ya visumbufu.

Swali la 7. Nini familia hii itafanya baada ya kuchunguza?Jibu la 7. ● Hawatafanya chc chote iwapo hawa taona mashambulizi ya vidukariy. ● Wanaweza kutumia mimea yenye viuadudu inayopatikana kiraisi kutayarisha sumu ya asili na kunyunyizia mimea iwapo idadi vidukari iko chini ya kiwango hatarishi. ● Watanyunyizia kiuadudu cha kemikali iwapidadi ya vidukari iko katika au juu ya kiwango hatarishi.

Swali la 8. Nini athari za kunyunyizia kiua vidukari cha kemikali?Jibu la 8. ● Kiua vidukari kikali kinaweza kuangamiza wadudu wenye faida ambao ndiyo huwa wanazaliana katika kipindi hiki. ● Mvua, ambayo hunyesha kila siku katika kipindi hiki, inaweza kuosha kiuadudu na manufaa yake kutopatikana. ● Familia ni lazima wanunue kiua vidukari.

Swali la 9. Nini manufaa ya kunyunyizia mchanganyiko utokanao na mimea?Jibu la 9. ● Mimea inayotoa mchanganyiko wa kutumika kutengeneza viua dudu vya mimea inapatikana kwa urahisi katika yako. ● Viuadudu vitokanavyo na mimea siyo vikali sana na huwa na madhara kidogo kwa wadudu rafiki. ● Viuadudu vitokanavyo na mimea havibaki kwenye mimea kwa muda mrefu, kwa hiyo familia haihitaji kusubiri muda mrefu kabla ya kuvuna mazao yaliyonyunyiziwa. ● Familia hainunui au kulipia Viuadudu vitokanavyo na mimea.

KUTENGENEZA UBAO WENYE VIMAMBO (KIBAO MAMBO) NA KUCHUNGUZA MAPEMA

Page 8: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation
Page 9: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

9

KUKAMUA VIUATILIFU KUTOKA KATIKA MAJANISwali la 1. Unaona nini katika picha ya kushoto?Jibu la 1. Nicodemus, Mama, binti yao Nima na kijana wao Samson wakitayarisha kiuatilifu kutoka katika mimea.(Angalizo kwa mkufunzi: zao hili laweza kuitwa “ya mimea” “kiuatilifu cha asili” “kiuatilifu cha kibailojia”)

Swali la 2. Ni majani yapi unaweza kutumia kutenengeneza kiuatilifu kitokanacho na mimea?Jiubu la 2. (Ngazi ya anayeanza) Unaweza kutumia majani ya muarobaini, “gliricidia” au “lantana”. (Ngazi ya juu) Tephrosia, au mimea mingine inayotumika na wenyeji kufukuza mbu.

Swali la 3. Zipi hatua muhimu ili kupata Viuatilifu vitokanavyo na mimea kwa ajili ya kunyunyizia?Jiubu la 3. ● Kwanza unavuna majani yaliyokomaa kutoka chini hadi eneo la kati la mmea. ● Baada ya hapo unayatwanga majani kwenye kinu. ● Jaza majani yaliyotwangwa kwenye kidumu cha lita 3. (Angalizo kwa mkufunzi: Ujazo wa lita 3 utatoa uzito wa kilo 2 wa majani yaliyotwangwa. Iwapo wakulima hawana vidumu vya lita 3, vidumu vingine kama vya lita 5 vya mafuta ya kupikia huweza kutumika. Pima ujazo wa lita 3 na iwapo hakuna kipimo, kata kulingana na ukubwa unaotakiwa.) ● Mimina kilo 2 za majani yaliyotwangwa katika ndoo yenye lita 20 za maji safi na koroga vyema. ● Funika ndoo na weka kwa muda wa saa 12-24. ● Kwa uangalifu chuja mchangayiko huo wa majani ulio nusu chachu mara mbili. Kwa mchujo wa kwanza mfuko wa plastiki unaweza kutumika. Mchanga nyiko unaweza kuwekwa kwenye ndoo ya pili ya plastiki. Baada ya hapo mchujo wa pili unaweza kufayika kwa kuziba kitundu cha bomba la kunyunyizia la mgongoni kwa kutumia kitambaa. Hii itahakikisha hakuna vipande vikubwa vitaziba nozeli za bomba. ● Sasa uko tayari kunyunyizia zao lako.

Swali la 4. Ni lini unatakiwa kunyunyizia kiuatilifu kitokanacho na mimea?Jibu la 4. ● Baada ya uchunguzi na matokeo kuashiria kuwa ni lazima kunyunyizia. ● Viuatilifu vitokanavyo na mimea amabvyo siyo vikali kama vya kemikali, vinaweza kutumika pia endapo matokeo ya uchunguzi yataonyesha idadi ya visumbufu bado iko chini ya kiwango ashirizi. ● Viuatilifu vitokanavyo na mimea vina athari hasi chache dhidi ya wadudu rafiki. Kwa hiyo, ni kwa manufaa zaidi kunyunyizia viuatilifu vitokanavyo na mimea mwanzoni mwa msimu wakati idadi ya wadudu rafiki bado inaongezeka.

Sawli la 5. Kwa nini ni muhimu kuchuja mara mbili wakati wa kumimina mchanganyiko/mkorogo katika bomba la kunyunyizia la mgongoni?Jibu la 5. Ni muhimu ili kupunguza uwezekano wa kuziba nozeli za bomba.

Swali la 6. Je, mkorogo huo unaweza kutunzwa kwa muda gani?Jibu la 6. Inashauriwa kutengeneza kiasi cha kiuatilifu kitokanacho na mimea cha kutumika mara moja au katika shamaba moja tu. Iwapo mvua itanyesha siku uliyotayarisha kiuatilifu, nyunyizia siku inayofuata. Inapendekezwa kunyunyizia kiuatilifu kitokanacho na mimea ndani ya siku 3 baada ya kukitayarisha.

Swali la 7. Ni muda gani mzuri wa kunyunyiziaJibu la 7. Kwa kuwa katika dawa zinazofanya kazi katika kiuatilifu kitokanacho na mimea huharibiwa na mwanga wa jua, inashauriwa kunyunyizia jioni au mapema asubuhi.

Page 10: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation
Page 11: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

11

KUKAMUA VIUATILIFU KUTOKA KATIKA MATUNDASwali la 1. Unaona nini katika picha?Jibu la 1. Nicodemus na mkewe Mama wakitayarisha kiuatilifu cha asili kutoka matunda ya mnavu (Solanum). (Angalizo kwa mkufunzi: Tumia jina la kienyeji la Solanum incanum.)

Swali la 2. Je, unatayarishaje hicho kiuadudu cha asili? Jibu la 2. ● Kwanza unavuna matunda yaliyoiva/komaa ya mnavu. ● Vaa glovu na mawani ya kukinga macho na tumia kisu kukata matunda katika vipande 4 na kasha jaza vipande hivyo katika kidumu cha lita 3 hadi kijae. ● Mimina vipande vya matunda (kilo 2) katika ndoo ya lita 20 ya maji safi na koroga sawasawa. ● Funika ndoo na hifadhi kwa saa 12-24. Weka ndoo mbali na watoto na wanyama. ● Kwa uangalifu chujia katika ndoo nyingine ya lita 20. Kwa mchujo wa kwanza unaweza kutumia mfuko wa plastiki. Baada ya kuchuja weka lita 10 (nusu ndoo) katika ndoo ya kwanza lakini baada ya kuisafisha kwanza. Jaza ndoo mbili zote kwa maji safi hadi liata 20. Koroga vyema. Tayari una lita 40 za kiuatilifu kitokanacho na mimea kwa ajili ya kutumia. ● Tumia kitambaa kuchuja tena wakati ukijaza bomba la kunyunyizia. Hatu hii itahakikisha kuwa hakuna vipande vikubwa vya kuziba nozeli za bomba.

Swali la 3. Kuna aina nyingine za matunda yanayoweza kutumika?Jibu la 3. Ndiyo, kuna aina nyingi za matunda na mbegu zianzoweza kutumika, kwa mfano pilipili na muarobaini.

Swali la 4. Kuna tofauti gani kati ya mkorogo unaotokana na majani na ule wa matunda?Jibu la 4. ● Huenda matunda (yaliyoiva/yaliyokomaa) yasiweze kupatikana msimu wote. ● Matunda huweza kuwa na ukali zaidi na hivyo inashauriwa mkorogo wake kupoozwa kwa kiwango cha juu zaidi (1:20/5%).

(Angalizo kwa mkufunzi: Wakati wa kukamua matunda, hatua za usalama/kinga lazima zichukuliwe. Anayeshika na kukata matunda, lazima avae glovu na mawani ya kukinga macho. Kazi hii ifanywe na watu wazima wenye afya tu. Ni marufuku watoto, wajawazito au mama wanaonyonyesha kufanya kazi hii.)

Page 12: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation
Page 13: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

13

KUTENGENEZA MTEGO WA PUYA (MAJI YA MAKAPI YA SUKARI) NA JINSI YA KUUTEGA SHAMBANI Swali la 1. Unaona nini katika picha ya kushoto?Jibu la 1. ● Nicodemus na mke wake Mama ● Dumu la kita 3 au 5 lenye rangi ya njano. ● Chupa yenye maji ya puya ● Kamba ● Kisu ● Umambo mrefu wa mti.Swali la 2. Unadhani hao watu wanafanya nini na hivyo vitu?Jibu la 2. Wanatengeneza mitego ya puya kwa kukata madumu. (Angalia picha juhakiki vipimo vya kukata)Swali la 3. Kwa nini vipande viwili viachwe bila kukatwa kutoka kwenye mtego?Jibu la 3. Vipande hivyo huzuia maji ya mvua kujaa ndani ya mtego na kupunguza ukali wa puya.Swali la 4. Kwa nini mitego ya puya ni ya muhimu kwa familia hii?Jibu la 4. Familia inaokoa fedha kwa kutengeneza mitego yao kwa gharama nafuu kutokana na malighafi zinazopatikana katika eneo lao.Swali la 5. Lakini nini umuhimu wa hii mitego?Jibu la 5. ● Inawezesha mkulima kunasa nondo wa funza vitumba kabla hawajataga mayai katika mimea ya Pamba. Hii inapunguza uharibifu wa majani na vitumba. ● Kwa kupunguza idadi ya mayai yaliyotagwa, mkulima anaweza kupunguza unyunyiziaji wa viuadudu. Hii huongeza faida kwa kupunguza gharama za uzalishaji. ● Kunasa funza vitumba kunaashiria ni lini unahitaji kuongeza bidii ya uchunguzi, haswa unaolenga funza vitumba na uchukue hatua wakati bado ni rahisi kuwadhibiti.Swali la 6. Unaona nini katika picha ya kulia?Jibu la 6. Mke na mume wanaweka mtego wa puya katika shamba lao la Pamba.

Swali la 7. Ni lini hasa unatakiwa kuweka mtego wa puya?Jibu la 7. Mitego ya puya hutegwa wiki 4-6 baada ya mbegu kuota ili kunasa nzao ya kwanza ya funza wa vitumba.

Swali la 8. Unaiwekaje katika shamba lako?Jibu la 8. Pata umambo mrefu ambao utadumu hadi mwisho wa msimu (mita 1.5-2.0) na tumia kamba yenye urefu wa mita 0.5 (nusu mita) kuning’inizia mtego wa puya.

Swali la 9. Je mtego uwe juu ya zao kwa urefu gani?Jibu la 9. Angalau sm 30.

Swali la 10. Je. Mkulima aweke mitego mingapi katika ekari/hektari ya shamba?Jibu 10. Si chini ya mitego 3 katika hektari ya shamba na si chini yamitego 2 kwa ekari moja.

Swali la 11. Unatarishaje puya?Jibu la 11. ● Weka mililita 100 za puya kali katika chupa tupu kasha ongeza robo lita (mililita 250) za maji safi. Tingisha chupa vyema hadi unapopata mchanganyiko laini wa puya. ● Mimina huo mchanganyikowa puya katika mtego.

Swali la 12. Unatakiwa kufanya nini baada ya kutega mtego wa puya?Jibu la 12. ● Mara kwa mara hakikisha kama mtego bado umening’inizwa vema kwenye umambo. ● Mara kwa mara chunguza puya na jaza mtego na maji safi ili usikauke. Baada ya kuongeza maji, koroga taratibu ili kuwa na mchangayiko huo kwa msimu wote.

Page 14: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation
Page 15: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

15

MKOJO WA NG’OMBE - KUTAYARISHA MBOLEA YA KIASILI YA MAJANI Swali la 1. Unaona nini katika picha kushoto?Jibu la 1. Nicodemus anakinga mkojo wa ng’ombe kabla ya kumkamua asubuhi.(Angalizo kwa mkufunzi: Baadhi ya wakulima wanapendekeza kuweka nyasi katika ndoo inayotumika ku-kingia mkojao. Hii inapunguza usumbufu wa ng’ombe kwa kelele isiyo ya kawaida.)

Swali la 2. Unaweza kutunza mkojo wa ng’ombe kwa muda gani?Jibu la 2. Usiweke mkojo wa ng’ombe katika mwanga wa jua. Kwa kawaida, mkojo ukichachuka kwa siku nyingi ndiyo unakuwa na matokeo bora.

Swali la 3. Unaona nini katika picha kulia?Jibu la 3. Nicodemus na mke wake Mama wakitayarisha mbolea ya majani kwa kutumia mchanganyiko wa mkojo wa ng’ombe.

Swali la 4. Unatayarishaje mbolea ya majani?Jibu la 4. ● Funika tanki la bomba la kunyunyizia la mgongoni kwa kitambaa cha Pamba kwa ajili ya kuchujia. ● Mimina lita 1 ya mkojo wa ng’ombe katika bomba na kisha ongeza lita 15 za maji safi ili kujaza bomba. Tikisa ili kuchanganya sawasawa.

Swali la 5. Ni wakati gani wa kunyunyizia mchanganyiko wa mkojo wa ng’ombe na maji?Jibu la 5. ● Mchanganyiko huu unyunyiziwe kila wiki kabla ya maua na kila wiki mbili wakati mimea inapotoa maua iwapo hutaweka mbolea ya kukuzia. ● Mchanganyiko huu unapaswa kunyunyiziwa mapema asubuhi au jioni. ● Mchanganyiko huu unaweza kunyunyiziwa kwenye mimea ya Pamba kwa kutumia mabomba 8-10 ya kunyunyizia ya mgongoni kila wiki 2 hadi 3 wakati wa kuweka vitumba. Lita 8-10 za mkojo wa ng’ombe usiochanganywa na maji zinapendekezwa kwa hektari 1.

Swali la 6. Kwa nini wakulima waongeze lita 1 tu ya mkojo wa ng’ombe katika bomba la kunyunyizia?Jibu la 6. Endapo ukali wa mkojo wa ng’ombe utakuwa zaidi, inweza kuunguza majani na kusababisha uharibifu.

Swali la 7. Kwa nini mkulima asinyunyizie mara nyingi au kwa kipindi kirefu?Jibu la 7. ● Ikiwa kutakuwa na virutubushi vya ziada, mmea wa Pamba uatendelea kuotesha majani badala ya kuuunda vitumba. ● Naitrojeni nyingi huvutia vidukari na kupelekea mashambulizi yasiyo ya lazima ya visumbufu nah ii inaweza kuhitaji kunyunyizia viuatilifu zaidi.

Page 16: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation
Page 17: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

17

MBONJI NA MTONDOO WA SAMADI - JINSI YA KUTAYARISHA MBOLEA ZA MAJI MAJI.

Swali la 1. Unaona nini katika picha kushoto?Jibu la 1. ● Nicodemus na mke wake Mama ● Ng’ombe jike ● Malundo mawili, moja la samadi na jingine la mbonji ● Mapipa mawili ya maji ya lita 200 ● Vipande vinene viwili vya mti nyenye urefu wa mita 1 ● Mfuniko wa plastiki wa pipa ● Magunia mawili ya sandarusi ambano itawekwa samadi na mbonji ● Kamba ndogo ya kufungia gunia kabla ya kulining’iniza

Swali la 2. Hao mume na mke wanafanya nini?Jibu la 2. Wanatayarisha mbolea za majimaji.

Swali la 3. Mama anafanya nini?Jibu la 3. Anajaza mbonji katika gunia kwa kutumia koleo.

Swali la 4. Nicodemus je?Jibu la 4. Anajaza samadi ya ng’ombe katika gunia kwa kutumia koleo.

Swali la 5. Unafikiri samadi ya ng’ombe ni kwa ajili gani?Jibu la 5. Mbolea za asili hutayarishwa kwa kutumia mbonji au samadi, lakini iwapo vyote viwili vinapatikana, inapendekezwa kuvichanganya.

Swali la 6. Mume na mke wanafanya nini katika picha ya kulia?Jibu la 6. Wanamimina mchanganyiko wa mbonji na samadi katika pipa la lita 200.Inawezekana pia kuwa wanageuza - geuza gunia la kilo 20-25 ili kuongeza kasi ya kuchachuka.

Swali la 7. Je kipande cha plastiki karibu na pipa hutumika kwa kazi gani?Jibu la 7. Kufukia pipa baada ya kukoroga mchanganyiko wa samadi na maji.

Swali la 8. Kwa nini ni muhimu kufunika pipa?Jibu la 8. Mfuniko huhakikisha kuwa virutubishi/naitrojeni haviyeyuki na kupotelea angani.

Swali la 9. Inachukuwa muda gani hii mbolea ya majimaji kuwatayari kutumika?Jibu la 9. Mchanganyiko wa mbonji au samadi ni lazima uchachuke kwa muda wa angalau siku 10-15. Kila baada ya siku 2 hadi 3 ni lazima ukorogwe kwa kutumia kile kipande cha mti. Maji hubadilika rangi ya kijivu au nyeusi. Zaidi ya hapo, harufu kali ni kiashiria kizuri iwapo mbolea ya majimaji iko tayari kutumika. Gunia huondolewa iwapo mchanganyiko uko tayari kwa matumizi.

Swali la 10. Je, mbolea hii ya majimaji inaweza kufaa kwa matumizi kwa muda gani?Jibu la 10. Mara inapokuwa tayari kwa matumizi, mbolea hii itumike ndani ya siku 10. Hakikisha pipa limefunikwa muda wote hadi litakapokuwa tupu.

Page 18: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation
Page 19: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

19

MBOLEA ZA MAJI MAJI - JINSI YA KUZITUMIA Swali la 1. Unaona nini katika picha kushoto?Jibu la 1. ● Nicodemus na mke wake Mama. ● Nicodemus anajitayarisha kunyunyizia mbolea ya majimaji iliyochotwa kutoka katika pipa. ● Mama anajaza mbolea ya majimaji katika chupa kubwa ya plastiki.

Swali la 2. Unaona Nicodemus akifanya nini haswa?Jibu la 2. Kwa umakini, anachujia ndani ya bomba la kunyunyizia la mgongoni mbolea ya majimaji iliyochotwa na mke wake Mama kutoka katika pipa. Anatumia kipande cha kitambaa kuchujia.

Swali la 3. Unaona Mama akifanya nini katika picha ya kulia?Jibu la 3. Anatumia chupa ya plastiki kunyunyizia mbolea ya majimaji katika misatri ya mimea. Njia hii huitwa kuloanisha. Inawezesha kuweka mbolea za majimaji hata kama bomba la kunyunyizia la mgongoni halipo. Unapoweka mbolea za majimaji zinazotokana na samadi ya kuku, njia ya kuloanisha ndiyo muafaka kwani ni muhimu kuepuka kunyunyizia samadi ya kuku kwenye majani ya mimea.

Swali la 4. Je mume wake anafanya nini?Jibu la 4. Ananyunyizia mbolea ya majimaji kwenye majani ya mimea kutumia bomba la kunyunyizia la mgongoni.

Swali la 5. Na kuhusu dumu la lita 10 lenye mfuniko uliotobolewa?Jibu la 5. Ni kwa ajili ya kumwagilia maji maji katika udongo katika mistari ya mimea badala ya kutumia bomba la kunyunyizia la mgongoni.

Swali la 6. Mchanganyiko sahihi wa mbolea ya majimaji na maji ni upi?Jibu la 6. Pooza ukali wa mbolea ya majimaji kwa kiwango cha 1:3, yaani lita 1 ya mbolea ya majimaji ichanganywe na lita 3 za maji. Kwa bomba la kunyunyizia la mgongoni la ujazo wa lita 16, tumia lita 4 za mbolea ya majimaji na lita 12 za maji.

Swali la 7. Ni kiasi gani cha mchanganyiko uliotayarishwa kinapaswa kunyunyiziwa katika ekari moja/hektari moja?Jibu 7. Kwa maksio lita 800 kwa hektari 1 au lita 300 kwa ekari 1 inapendekezwa.

Swali la 8. Je ni lini unaweza kuanza kunyunyizia mbolea za majimaji?Jibu la 8. Anza kunyunyizia siku 14 baada ya mbegu kuota, mara tu baada ya kumaliza kupunguzia miche. Badilisha kutoka mtondoo/mchanganyiko wa samadi na kutumia mtondoo wa mbonji baada ya kunyunyizia mara 4.

Swali la 9. Ni wakati gani wa kunyunyizia mbolea ya majimaji?Jibu la 9. Ni muafaka zaidi kunyunyizia mbolea ya majimaji baada ya mvua kunyesha. Inapendekezwa kunyunyizia mapema asubuhi au jioni sana (baada ya mvua kuacha kunyesha).

Page 20: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation
Page 21: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

21

KUKUSANYA MASALIA YA MIMEA KWA AJILI YA LUNDO LA MBONJISwali la 1. Unaona nini katika picha?Jibu la 1. Nicodemus na mke wake Mama.Swali la 2. Wanafanya nini?Jibu la 2. Nicodemus anakata masalia ya mimea ya mahindi na mke wake anayakusanya.Swali la 3. Kwa nini wanafanya hivyo?Jibu la 3. Wako mbioni kuandaa lundo la mbonji.Swali la 4. Wanatumia vifaa gani kufanya hiyo kazi?Jibu la 4. ● Toroli lililojaa samadi ya wanyama iliyokusanywa kutoka kwa ng’ombe, kuku na mbuzi wa hapo nyumbani ● Koleo ● Pipa la lita 200 za maji ● Vipande vya mianzi ● Majani ya mgomba ● Udongo mweusiSwali la 5.Ni vitu gani endapo vingepatikana vingekuwa vya manufaa kuongeza kwenye lundo la mbonji?Jibu la 5. ● Masalia ya mimea ya jamii ya mikunde ● Masalia ya mazao mengine yoyote ● Mawe ya fosfati ● Majivu ● Mkojo wa ng’ombeSwali la 6. Ni mahali gani panafaa kuweka lundo la mbonji?Jibu la 6. ● Inafaa kuliweka lundo la mbonji karibu na shamba ambamo mbonji itawekwa. ● Mahali hapo pawe na kivuli, k.m. chini ya mti na pawe karibu na chanzo cha maji. ● Sehemu zilizolowa maji zisitumike.Swali la 7. Ni upi wakati mzuri au muafaka wa kuandaa lundo la mbonji?Jibu la 7. Lundo liandaliwe wakati kuna masalia ya mimea ya kutosha. Baada ya kuvuna zao kuu, mabaki yanaweza kutumika. Iwapo shamba halitoi masalia ya kutosha, yanaweza kukusanywa kutoka sehemu nyingine nje ya shamba.Swali la 8.Nini ukubwa muafaka wa lundo la mbonji?Jibu la 8. Ili kuruhusu mzunguko wa kutosha wa hewa, linatakiwa liwe na upana usiozidi mita 2.5 na urefu wa mita 1.5.

Page 22: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation
Page 23: Kitabu cha picha cha uzalishaji kabambe na jumuishi na ... · Kwa mtizamo wa uzalishaji kabambe na jumuishi na usimamizi wa kuzuia visumbufu,taasisi ya the Aid by Trade Foundation

23

HATUA ZA KUTAYARISHA LUNDO LA MBONJISwali la 1. Unaona nini katika picha?Jibu la 1. Shughuli mbali mbali katika kuandaa au kujenga lundo la mbonji.

Swali la 2. Je, Nicodemus na mke wake Mama huanza kwa kufanya nini?Jibu la 2. Watajenga safu msingi ya vitu ambavyo huvivundi kwa haraka, k.m. miti ya mahindi au Pamba, vipande vya miti au mimea vikavu.

Swali la 3. Kwa nini wanahitaji kunyanyua safu msingi angalau hadi urefu wa sm 30?Jibu la 3. ● Safu msingi itahimilisha na kuimarisha lundo. ● Itahakikisha mzunguko mzuri wa hewa na kutiririsha maji katika lundo. ● Vitu ambavyo huvunda kw aharaka visiwekwe juu ya udongo mtupu.

Swali la 4. Kwa nini watumie mchanganyiko wa masalia ya mazao mbalimbali?Jibu la 4. Mchanganyiko wa masalia ya miti ya mahindi na ya zao la jamii ya mikunde, huhakikisha mchanganyiko mzuri wa vyanzo vya nitrojeni na kaboni na hivyo mbonji yenye ubora.

Swali la 5. Kuna nini ndani ya toroli?Jibu la 5. Samadi ya wanyama na mbonji ya zamani.

Swali la 6. Hivi vitu vya nyongeza hutumikaje?Jibu la 6. Wanalundika safu mbalimbali za vitu vigumu kama masalia ya miti, mizizi na halikadhalika vitu ambavyo huvunda haraka kama mavi ya ng’omba, majani ya kijani, masalia kutoka jikoni, samadi na mbonji ya zamani. Hii inaruhusu joto kutoka safu za juu kurahisisha kuvunda kwa vitu vigumu vilivyo safu za chini.

Swali la 7. Kwa nini ni muhimu kuweka kiasi kidogo cha udongo mweusi katika kila safu?Jibu la 7. Ni muhimu kuweka kiasi kidogo cha udongo mweusi katika kila safu ili kuhifadhi unyevunyevu na kuongeza kasi ya kuvunda.

Swali la 8. Maji yaliyo kwenye ndoo ni nini?Jibu 8. Lundo lote linahitaji kupata maji ya kutosha kabla ya kufunikwa. Kwa wakati wote, mbonji ni lazima iwe na unyevunyevu lakini siyo kuloanishwa kabisa. Inapominywa kwa mkono, mbonji igandamane lakini isitowe maji.

Swali la 9. Ni aina gani ya vitu huweza kutumika kufunika lundo la mbonji?Jibu la 9. Lundo la mbonji lifunikwe kwa kipande cha plastiki, mifuko ya sandarusi, majani ya mgomba, au kuezekwa kwa nyasi ili kulikinga kupoteza mvuke na mvua kubwa kwani hii huweza kupotea kwa virutubishi.

Swali la 10. Je hivyo vipande virefu vya mianzi vilivyo wima katika lundo vina umuhimu gani?Jibu la 10. Hivi ni vipande vya mianzi vya kurahisisha mzunguko mzuri wa hewa ndani ya lundo.

Swali la 11. Nini kinafuata baada ya lundo kujengwa na kufunikwa vyema?Jibu la 11. ● Wiki mbili hadi tatu baada ya kujenga lundo la mbonji, litakuwa limepunguwa hadi nusu ya ukubwa wake wa mwanzo. Huu ni wakati mwafaka wa kuligeuza kwa mara ya kwanza ili kuharakisha mchakato; ligeuzwe tena kwa mara ya pli baada ya wiki 1-2 na baada ya hapo ligeuzwe mara 2 tena. Kila baada ya kugeuzwa, lundo lazima lifunikwe. ● Mbonji itakuwa tayari kutumika baada ya kugeuzwa mara ya 4. ● Muda wa kuwa tayari hutegemea limegeuzwa mara ngapi na kama limepata maji ya kutosha.