kizazi chenye usawa: simama dhidi ya ubakaji · 2020. 4. 20. · vinavyotokea kazini, mashuleni,...

12
Simama dhidi ya Ubakaji KIZAZI CHENYE USAWA: SIMAMA DHIDI YA UBAKAJI

Upload: others

Post on 24-Oct-2020

28 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • Simama dhidiya Ubakaji

    Kizazi chenye usawa: simama dhidi ya ubaKaji

  • SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

    asanTe Kwa KuunGana nasi KaTiKa Kuadhimisha KamPeni ya siKu 16 za KuPinGa uKaTiLi wa Kijinsia

    Wewe ni sehemu muhimu ya kuchochea na kuleta mabadiliko katika harakati hizi; Tumeandaa kijarida hiki kukupa taarifa muhimu kama vile;

    + Kampeni + Jumbe muhimu + Hali ya ukatili wa kijinsia + Shughuli za kampeni

    • Huduma za msaada• Ushiriki wa wadau wa kimataifa• Taarifa za mitandao yetu ya kijamii• Kopi ya tovuti

    Tuungane katika kumtetea kila mwanamke na mtoto Anayefanyiwa Ukatili, Inaweza Kuwa Moja Ya Njia Nzuri Ya Kuleta Mabadiliko Na Kujenga Uelewa Kwenye Jamii Kuhusu Masuala Ya Ukatili Wa Jinsia.

  • SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

    unGana nasi Kwenye miTandaO ya Kijamii KuPiTia aKaunTi zeTu

    Badili rangi ya mpangilio wa tovuti na akaunti zako katika mitandao ya kijamii na kuwa rangi ya chungwa katika kipindi hiki cha siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia. Ungana nasi kwenye mitandao ya kijamii kupitia akaunti zetu:

    FacebOOK: www.facebook.com/WiLDAFTzTwiTTeR: www.twitter.com/WiLDAFTz /insTaGRam: www.instagram.com/WiLDAFTz websiTe: www.wildaftanzania.org

    Twitter, Facebook na instagram: @16DaysTanzania

    jiunge na mazungumzo.Kuwa sehemu ya mabadiliko na uangalie maudhui yaliyoshirikishwa kupitia alama zareli (hashtags) zifuatazo:

    #OrangeTheWorld#GenerationEquality

  • SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

    Kuna njia nyinGi za KushiRiKi KaTiKa KamPeni hii:1. unGa mKOnO haRaKaTi

    za siKu 16 za KuPinGa uKaTiLi wa Kijinsia. + Onesha ishara ya Amani! vaa

    fulana au shati lenye ya rangi ya chungwa (Orange).

    + Shawishi familia, marafiki, majirani kushiriki katika kampeni.

    + Ungana na wafanyakazi wenzio katika mijadala mbalimbali kama wakati wa chai ya asubuhi au chakula na kujadili kuhusu ukatili wa kijinsia mahala pa kazi na hata kutumia njia ya majadiliano katika mitandao ya kijamii.

    + Shirikishana jumbe na picha mbalimbali za kupinga Ukatili wa Kijinsia kupitia mitandao ya kijamii ili kampeni iweze kuwafikia watu wengi zaidi

    2. ibua mijadaLa ya uKaTiLi wa Kijinsia + Anzisha dawati la jinsia shuleni

    kupitia klabu za afya na jinsia, fema au masomo(subject clubs).

    + Anzisha klabu za kupinga ukatili sehemu yako ya kazi, michezoni, sehemu za ibada kama makanisani, na misikitini, ili kujadili na kupinga ukatili wa Kijinsia unaotokemajumbani.

    3. jiunGe KaTiKa maadhimishO haya ya KamPeni ya siKu 16 za KuPinGa uKaTiLi wa Kijinsia POPOTe PaLe unaPOsiKia. + Shiriki katika kampeni ya siku 16

    popote pale kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania isiyo na Ukatili.

    + Anzisha mijadala katika maeneo ya jamii, vijiwe, sokoni, sehemu za ibada, michezoni dhidi ya mila

    potofu zinazobagua wanawake na wasichana katika kupata rasilimali na kushiriki katika nafasi za uongozi.

    + Shawishi jamii yako juu ya fikra chanya kuhusu umuhimu wa ushiriki wa wanawake kushika nafasi za uongozi kisiasa katika ngazi ya kijiji, kata, tarafa na taifa kwa ujumla.

    + Hamasisha wanawake na wasichana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za kijiji, kata, tarafa na taifa ili kuongeza juhudi ya kuleta maendeleo ya nchi na kufikia uchumi wa viwanda.

    4. wezesha uPaTiKanaji wa huduma za msaada wa KisheRia + Huduma mkoba (outreach

    program) za msaada wa kisheria maeneo ya vijijini ili kuwafikia wanawake wanaohitaji msaada wa kisheria, pia kuwajengea uwezo kuhusu haki na sheria mbalimbali.

    + Huduma ya dawati la jinsia kwenye taasisi za elimu kama vile vyuo vikuu.

    5. chuKua haTua na vunja uKimya, + Wasaidie wahanga wa Ukatili wa

    Kijinsia kuepuka manyanyaso katika jamii na kupatiwa huduma za msaada wa kisheria, kisaikolojia na hata matibabu ya afya.

    + Toa taarifa kwa vyombo vya dola, serikali na hata asasi za kiraia pindi unapofanyiwa au kushuhudia vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwa msaada zaidi wa kisheria.

  • SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

    KamPeni

    madhumuniMwaka huu 2019, kampeni inadhamiria kuibua tafakuri na kupaza sauti, kuhimiza majukumu ya kila mtu katika kukabiliana na vitendo vya ubakaji, rushwa ya ngono pamoja na unyanyasaji wa kingono katika jamii. Pia inalenga kuhamasisha jamii kuweka mazingira salama kwa wanawake, na watoto kwa sababu kila mtu anastahili kujisikia salama na kuheshimiwa. Lengo la mwaka huu ni kuhamasisha kila mtu katika nafasi yake bila kujali umri kuchukua hatua juu ya matendo ya ubakaji, unyanyasaji wa kigono pamoja na rushwa ya ngono. Tunategemea kuhama kutoka kwenye kuongeza uelewa mpaka kwenye vitendo. Kila mtu katika jamii ana uwezo wa kutenda jambo dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia, ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia

    muda wa KamPeni Kampeni hii itaanza na uzinduzi wa tarehe 25 Novemba ambayo ni siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na kuhitimishwa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu Desemba 10.Tunahitaji jamii yote kuhoji ubaguzi na, kuunga mkono usawa wa kijinsia katika mtazamo wa kijinsia. Kila mtu ana jukumu la kuzuia ukatili unaofanyika kwenye familia,watu binafsi, shule, mahali pa kazi, nyumba za ibada, vilabu vya michezo na serikali. Ikiwa wewe, au mtu unayejua, amefanyiwa ukatili wa kijinsia, unaweza kufika katika vyombo husika vinavotoa msaada wa Kisheria. Unga mkono usawa wa kijinsia, heshimu na usiwe sehemu ya ukatili. Vaa nguo zenye rangi ya chungwa kuonesha ishara ya Amani katika kipindi cha kampeni.

    KauLi mbiuKizazi Chenye Usawa Simama Dihidi ya UbakajiKauli mbiu ya mwaka huu imelenga kutoa wito kwa kila mmoja bila kumuacha mtu yoyote nyuma (Watoto, vijana na wazee) kuchukua hatua, kuhoji, kupaza sauti, kupinga vitendo vya ukatili wa kingono vinavyotokea kazini, mashuleni, taasisi mbalimbali, mitaani, hospitali, kwenye usafiri wa umma n ahata mitaani. Kauli mbiu mwaka huu inasisitiza mambo yafuatayo; + Kuheshimu na kutambua harakati

    za wanawake na uongozi wao katika siku 16 za kampeni na katika kuzuia na kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kwa ujumla.

    + “Kutomuacha hata mmoja nyuma” Kutumia mbinu ya haki ya binadamu na mtazamo makini juu kuyafikia makundi yote ya watu hasa makundi wanawake na wasichana waliochwa nyuma na wasiopewa nafasi.

    + Ushiriki wa Sekta mbalimbali: kila mtu katika jamii ana jukumu muhimu la kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na wasichana na sote lazima tufanye kazi pamoja katika sekta zetu ili kushughulikia masuala mbalimbali ya ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana.

    + Kuchukua hatua, kuingilia kati kwa kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili wa kingono.

  • SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

    jumbe

    haLi ya uKaTiLi wa Kijinsia.

    Takwimu zinaonyesha ukatili wa kijinsia + 40% ya wanawake wenye miaka 15-49

    wamefanyiwa ukatili wa kimwili.(TDHS 2015-2016)

    + 10% ya wanawake wenye umri kati ya mika 15-49 wamefanyiwa ukeketaji (THDS 2015-2016)

    + 37% ya wanawake wenye umri kati ya miaka 20-24 waliolewa kabla ya kufikia mika 18 (UNFP 2014)

    + Matukio 7617 ya ubakaji yaliripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi katika kipindi cha Januari mpaka Desemba 2018 (Ripoti ya Takwimu za Hali ya Uhalifu na Matukio ya usalama Barabarani Januari-Desemba 2018). Namba hii ya kuogofya ni sawa na asilimia 64.7 ya matukio yote ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyoripotiwa katika kipindi tajwa.

    + Hata hivyo, matukio mengi ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji, rushwa ya ngono na unyanyasaji kingono hayaripotiwi kwenye vyombo husika hivyo kuwanyima wahanga fursa ya kupata msaada na huduma stahiki na

    hivyo kuongeza madhara zaidi ikiwemo maambukizi ya virusi vya UKIMWI, Mimba zisizotarajiwa na athari za kisaikolojia.

    + Ukatili wa kijinsia hugharimu baadhi ya nchi mpaka asilimia 3.5 ya pato ghafi la taifa hivyo kuleta matokeo hasi kwenye ukuaji wa uchumi (Benki ya Dunia) Duniani kote, ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto unafanyika ndani ya jamii, nyumba na familia.

    + Msingi mkuu wa ukatili dhidi ya wanawake ni mamlaka tofauti ya umiliki kati ya wanaume na wanawake katika jamii, mifumo na kanuni ambazo zinasimamia mfumo dume.

    + Tanzania, ukatili dhidi ya wanawake inabaki kuwa changamoto kubwa na kizuizi kwa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.

    + Ukatili dhidi ya wanawake ni jambo linalohitaji mwamko wa kisiasa ili kubadilisha mifumo dume katika ngazi ya mtu binafsi, watu walio kwenye mahusiano ya kimapenzi, familia, jamii na taasisi kwa ujumla.

    + Ukatili dhidi ya wanawake huathiri wanawake katika kutambua uwezo wao na kuchangia maendeleo ya nchi.

  • SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

    je, unaFahamu mPanGO Kazi wa TaiFa wa KuTOKOmeza uKaTiLi dhidi ya wanawaKe na waTOTO Tanzania (mTaKuwwa)?

    shabaha

    Hadi kufikia mwaka 2021 – 2022 MTAKUWWA umedhamiria pamoja na mambo mengine yafuatayo:

    KuimaRisha uchumi wa Kayai. Kuogeza idadi ya wanawake wanaofikia

    huduma za kifedha kutoka 51.2% hadi 65%

    ii. Kuongeza vikundi vya wanawake wanaojiunga na SACCOS kutoka 1% hadi 15%

    iii. Kuongeza idadi ya wanawake wanachama wa VICOBA kutoka 795 hadi 85%

    iv. Kupunguza idadi ya watoto wanaoishi mitaani, wapatao 35,916

    v. Kupunguza ajira kwa watoto kutoka 29% hadi 9%

    vi. Kuongeza msaada wa kielimu kwa wasichana wanaotoka katika familia masikini kutoka 23.4% hadi 53.4%

    miLa na desTuRii. Kuongeza uwiano wa waathirika wa

    vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake waliofanyiwa aina yoyote ya ukatili kutoa taarifa ndani ya saa 72 baada ya tukio kutoka asilimia 30 hadi 65.

    ii. Kuongeza uwiano wa halmashauri zenye programu za kijamii za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake kutoka asilimia 0 hadi 20.

    iii. Kuongeza uwiano wa wanakaya wenye umri kati ya miaka 15-49 waliopata taarifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake, kutoka asilimia 0 hadi 55.

    iv. Kupunguza ukatili wa kingono kutoka asilimia 17.2 hadi 8.

    v. Kupunguza ukatili wa kimwili dhidi ya wanawake wenye umri kati ya miaka 15-49 toka asilimia 39 hadi 10.

    vi. Kupunguza ukatili wa kihisia kutoka asilimia 36.3 hadi 18.

    vii. Kupunguza mimba za utotoni kutoka asilimia 27 hadi 5.

    viii. Kupunguza kiwango cha ukeketaji kutoka asilimia 32 hadi 11.

    ix. Kupunguza ndoa za utotoni kutoka asilimia 47 hadi 10.

    maLezi ya wazazi/waLezi, misaada wa KiFamiLia na mahusianO.i. Kuongeza stadi za malezi kwa wazazi/

    walezi na kwa watoa huduma za malezi kutoka wilaya 72 hadi wilaya 113.

    ii. Kuongeza programu/huduma za elimu ya awali kwa watoto chini ya miaka mitano kufikia asilimia 50 kutoka kwa watoto 122,500.

    uTeKeLezaji na usimamizi wa sheRiai. Kuongezeka idadi ya watu waliotiwa

    hatiani kwa kesi za ukatili dhidi ya wanawake kutoka asilimia 8 hadi 50.

    ii. Kuongeza idadi ya watu waliotiwa hatiani kwa kesi za ukatili dhidi ya watoto kutoka asilimia 7 hadi 50.

    iii. Kupunguza muda wa uendeshaji wa kesi za ukatili dhidi ya wanawake kutoka miaka 4 hadi miezi 12.

    iv. Kupunguza muda wa uendeshaji wa kesi za ukatili dhidi ya watoto kutoka miaka 4 hadi miezi 12.

  • SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

    uTOaji huduma Kwa waaThiRiKa wa uKaTiLi dhidi ya wanawaKe na waTOTOi. Kuongeza vituo vya utoaji huduma rafiki

    kutoka 4 hadi 26ii. Kuongeza uwiano wa kutolea taarifa

    za wahanga wa ukatili dhidi ya watoto ndani ya saa 72 baada ya tukio toka 30% hadi 65%

    iii. Kuongeza madawati ya jinsi na watoto ya polisi yanayofanya kazi kutoka vituo vys polisi 417 hadi 600

    usaLama shuLeni na sTadi za maisha iLi KuTOKOmeza uKaTiLi dhidi ya waTOTO.i. Kupunguza idadi ya wanafunzi

    wanaoacha shule kutokana na kupata ujauzito kwa nusu ya idadi ambayo ni 251 kwa shule za msingi na 3,439 kwa walio Sekondari.

    ii. Kuongeza idadi Mabaraza ya watoto ya Wilaya kutoka 108 hadi 185.

    iii. Kuongeza idadi ya klabu za watoto

    shuleni kutoka 398 hadi 13,200.iv. Kuendeleza usawa wa kijinsia kwa

    wahitimu shuleni wa 1:1.v. Kuongeza mafunzo ya stadi za maisha

    toka asilimia 0 hadi 70.vi. Kuongeza utoaji wa msaada wa pedi

    za kujisitiri watoto wa kike wanaotoka katika familia maskini toka asilimia 1 hadi 20.

    uRaTibu, uFuaTiLiaji na TaThimini ya uKaTiLi dhidi ya wanawaKe na waTOTOi. Kuongeza ukusanyaji wa takwimu za

    msingi kuhusiana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto ili kuhabarisha vyombo vya kuchukua maamuzi toka 24% hadi 85%

    Unga mkono juhudi za serikali kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake ili kufikia malengo ya Mtakuwwa.

  • SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

    unGana na wadau KuPiTia

    Rutgers - 16 Days Campaign - USA https://16dayscwgl.rutgers.edu/ #16Days

    UN Women - 16 Days Campaign - USA https://www.unwomen.org/en/what-we-do/ending-violence-against-women/take-action/16-days-of-activism

    Prevent GBV Africa - 16 Days Campaign - UGANDA http://preventgbvafrica.org/understanding-vaw/

    UNITE Campaign http://www.unwomen.org/en/what-we-do/endingviolence-against-women/ take-action/uniteSouth Africa Government – South Africa https://www.gov.za/16DaysofActivism2019

    Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children (MoHCDEC) - Tanzaniahttp://www.mcdgc.go.tz/data/NPA_VAWC.pdf

    Embassy of Ireland https://www.dfa.ie/irish-embassy/tanzania/news-and-events/latestnews/leave-no-one-behind-end-violence-against-women-and-girls.html

    WiLDAF Tanzania https://wildaftanzania.org/16-days-2018/Legal and Human Right Center (LHRC) https://www.humanrights.or.tz/posts/b/News/16-days-of-activism-against-gender-based-violence-end-violence-in-the-world-of-work

    Kivulini - Mwanza http://kivulinitz.org/?s=16+days

    Tanzania Network of Legal Aid Providers (TANLAP) http://www.tanlap.or.tz/

    KWIECO - Kilimanjaro http://www.kwieco.org/our-programmes/support-forvictims-of-gender-based-violence/

    Maendeleo ya Jamii Idara Kuu MAADHIMISHO YA UFUNGUZI WA KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA https://www.youtube.com/watch?v=NHw0ZXJEloI

  • SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

    unaPOFanyiwa viTendO vya uKaTiLi wa Kijinsia au KuOna mTu aKiFanyia viTendO hivO basi chuKua haTua ziFuaTazO:

    + Ripoti tukio la ukatili katika madawati ya polisi ya kijinsia (Police Gender Desks) yanayopatikana kwenye vituo vya polisi vilivopo nchini au katika huduma ya mkono kwa mkono (One stop centre).

    + Unaweza pia kutoa taarifa za tukio katika ofisi zaustawi wa jamii, serikali za mitaa, vituo vya afya ili kupata huduma kwa wakati.

    + + Vituo vya msaada wa kisheria vilivoenea nchi nzima vinaweza kuwa ni msaada mkubwa

    kwa waathirika wa ukatili. Msaidie mwathirika kuripoti tukio lake. + Baadhi ya asasi za kiraia zinatoa msaada wa kisheria wa dharula. Piga bure namba

    zifuatazo:

    0800750035 | 0800751010 | 0800780100 | 0800780070

    LeGaL and human RiGhTcenTRe (LhRc)

    Piga Bure Namba : 0800750035www.humanrights.org

    Tanzania wOmen LawyeRs assOciaTiOn(TawLa)

    Piga Bure Namba : 0800751010www.tawla.or.tz

    wOmen and LeGaL aid cenTRe (wLac) :Piga Bure Namba : 0800780100

    www.wlac.or.tz.

    namba za msaada wa KisheRia wOmenin Law and deveLOPmenT in aFRica (wiLdaF)

    Piga Bure Namba : 0800780070www.wildaftanzania.org

    namba ya msaada na uLinzi KwawaTOTO c-sema

    Piga Bure Namba 116www.sematanzania.org

    waPi Pa KuPaTa msaada?

  • SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

    unGana nasi KuPiTia

    Website Linkhttp://wildaftanzania.org/campaign/

    Facebook Pagehttps://www.facebook.com/WiLDAFTz

    Twitter pagehttps://twitter.com/WiLDAFTz

    Instagram Pagehttps://www.instagram.com/wildaftz/

  • Kauli Mbiu ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia

    unaweza FiKa KaTiKa OFisi zeTu Kwa ajiLi ya ushauRi namsaada wa KisheRia KuPiTia anwani ziFuaTazO:

    Women in Law and Development in Africa (WiLDAF) : National CoordinatorMikocheni A area, WiLDAF Street, Block F, Plot No. 635

    P . O. Box 76215, Dar es salaam, Tanzania mobile: +255 22 270 1995

    KIZAZI CHENYE USAWA: SIMAMA DHIDI YA UBAKAJI